ANNUUR 1064

12
ISSN 0856 - 3861 Na. 1064 JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 29-APRILI 4, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu www.annuurpapers.co.tz Umoja ni nguvu, na Hijja ni nguzo ya umoja wa Uislamu. Hijja inawakusanya waislamu kutoka kila pembe ya dunia. Qur’ani (22:27) inatwambia Allah Anatuita huko tukapatemanufaa Aliyotuandalia. Utukufu, nguvu na ushindi ni vya Allah!Twenda wengi kutoka kila pembe ya nchi yetu tukapate nguvu zitokazo kwa Allah!KaribuniAhlu Sunna wal Jamaa.Gharama zote ni Dola 4,300.Tafadhaliwasiliana nasi ifuatavyo: Tanzania Bara: 0717224437; 0777462022;Unguja: 0777458075;Pemba: 0776357117. (9) HIJJA IMEBEBA NGUVU YA WAISLAMU Walio Jela wapata Sunna ya Mitume Kesi yao yaweka rekodi nchini, lakini… Makafiri watatumia mabavu watashindwa Uamsho, Sheikh Ponda hayajapoteza kitu Hata Ibarahim alitupwa katika moto mkali Dhambi kubwa ya serikali yafichuliwa TATIZO la ‘udini’ lipo tangu wakati wa Mwalimu Nyerere. Ndio mfumo aliotujengea ndani ya serikali yetu! Sasa tukianza kumlaumu Rais Kikwete, tutakuwa tunafanya ushabiki tu. ZANZIBAR watangaze tu kwa Tamko la Rais (Presidential Decree) kuwa Ijumaa ni siku ya mapumziko. Kumtii Mungu ni bora zaidi kwao kuliko kuheshimu na kuhofia mambo ya kidunia kama kweli ni watu wenye kutafakari. Watakuwa Maanswari; watupokee Muhajirina kutoka Bara tuje tumwabudu Allah kingamiangamia! Tutahamia huko Zanzibar msisubiri Tume ya Warioba Anzeni kupumzika Ijumaa Hili si la muungano, ni Dini Katiba yenu ya sasa inatosha kama baadhi ya watu wa Uingereza walivyohamia Marekani katika karne ya 16 ya kipindi kile cha Great Awakening na Reconnaisance (uamsho mkubwa), kwa kumkimbia King George aliyekuwa akiwafanyia ukatili pale walipokuwa hawakubaliani naye alipoanzisha Kanisa lake la Anglikana na kujipa mwenyewe ukuu (self- imposed) wa kanisa hilo. (Soma Uk. 5, 9) Tusimuonee Kikwete Udini ndio mila yetu Tuache ushabiki. Tufumue ‘Mfumo’ kwanza Tatizo la udini lipo ndani ya mzunguko wa damu wa mfumo wetu wa utawala. Tukitaka kulitatua kiukweli, tufumue mfumo mzima wa utawala na kuunda upya! (Soma Uk. 6) Na hii ndiyo itakayolisambaratisha Taifa MUFT Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kabi akiongoza viongozi wa serikali na Waislamu katika swala.

Transcript of ANNUUR 1064

Page 1: ANNUUR 1064

ISSN 0856 - 3861 Na. 1064 JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 29-APRILI 4, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz

Umoja ni nguvu, na Hijja ni nguzo ya umoja wa Uislamu. Hijja inawakusanya waislamu kutoka kila pembe ya dunia.

Qur’ani (22:27) inatwambia Allah Anatuita huko tukapatemanufaa Aliyotuandalia. Utukufu, nguvu na ushindi ni vya Allah!Twenda

wengi kutoka kila pembe ya nchi yetu tukapate nguvu zitokazo kwa Allah!KaribuniAhlu Sunna wal Jamaa.Gharama zote ni

Dola 4,300.Tafadhaliwasiliana nasi ifuatavyo: Tanzania Bara:

0717224437; 0777462022;Unguja: 0777458075;Pemba: 0776357117.

(9) HIJJA IMEBEBA NGUVU YA WAISLAMU

Walio Jela wapata Sunna ya MitumeKesi yao yaweka rekodi nchini, lakini…Makafiri watatumia mabavu watashindwaUamsho, Sheikh Ponda hayajapoteza kituHata Ibarahim alitupwa katika moto mkali

Dhambi kubwa ya serikali yafichuliwa

TATIZO la ‘udini’ lipo tangu wakati wa Mwalimu Nyerere.

N d i o m f u m o aliotujengea ndani ya serikali yetu!

S a s a t u k i a n z a kumlaumu Rais Kikwete, tutakuwa tunafanya ushabiki tu.

ZANZIBAR watangaze tu kwa Tamko la Rais (Presidential Decree) kuwa Ijumaa ni siku ya mapumziko.

K u m t i i M u n g u n i bora zaidi kwao kuliko kuheshimu na kuhofia mambo ya kidunia kama kweli ni watu wenye kutafakari.

Watakuwa Maanswari; watupokee Muhajirina kutoka Bara tuje tumwabudu Allah kingamiangamia!

T u t a h a m i a h u k o

Zanzibar msisubiri Tume ya Warioba

Anzeni kupumzika IjumaaHili si la muungano, ni DiniKatiba yenu ya sasa inatosha

kama baadhi ya watu wa Uingereza walivyohamia Marekani katika karne ya 16 ya kipindi kile cha Great Awakening na Reconnaisance (uamsho mkubwa), kwa kumkimbia King George aliyekuwa akiwafanyia ukatili pale walipokuwa hawakubaliani naye alipoanzisha Kanisa lake la Anglikana na kujipa mwenyewe ukuu (self-imposed) wa kanisa hilo. (Soma Uk. 5, 9)

Tusimuonee KikweteUdini ndio mila yetu

Tuache ushabiki. Tufumue ‘Mfumo’ kwanzaTatizo la udini lipo

ndani ya mzunguko wa damu wa mfumo wetu wa utawala.

Tukitaka kuli tatua kiukweli, tufumue mfumo mzima wa utawala na kuunda upya! (Soma Uk. 6)Na hii ndiyo itakayolisambaratisha Taifa

MUFT Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kabi akiongoza viongozi wa serikali na Waislamu katika swala.

Page 2: ANNUUR 1064

2 AN-NUURJAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 29 - APRILI 4, 2013

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

MAONI YETU

Tahariri/Habari/Tangazo

Dhambi kubwa ya serikali yafichuliwaIMEELEZWA kuwa dhambi kubwa inayofanywa na viongozi wa serikali, ni kutambua kuwa upo ‘Mfumokristo’ lakini wakipanda katika majukwaa ya kisiasa hupiga porojo kuwa haupo.

Hayo yamesemwa na Ustadhi Sa l im Khamis i Machano, akiwahutubia Waislamu katika Msikiti wa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam, katika ibada ya swala ya Ijumaa, wiki iliyopita.

Ameyaeleza hayo kufuatia mwendendo wa vyombo vya dola na vya kisheria ambavyo vimeonyesha ubalakala, ubaguzi na upendeleo katika kutekeleza sheria moja kwa watu tofauti.

Hiyo ni kufuatia kitendo cha watuhumiwa wa Kiislamu kunyimwa dhamana huku waliofanya makosa makubwa zaidi au kama hayo, wakipewa haki yao ya dhamana na kwa upande mwingine Waislamu wakifungwa jela huku waliofanya kosa kama lao wakiachiwa au kutokufunguliwa kesi kabisa.

Ust . Machano, a l ikuwa akiongelea hukumu dhidi ya Waislamu waliohukumiwa M a c h i 2 1 , 2 0 1 3 , k a t i k a Mahakama ya Kisutu, kifungo cha mwaka mmoja, jela kwa kosa la kuandamana kwenda kwa DPP, kujua sababu za kuzuia dhamana ya Sheikh Ponda Issa na Mukadam Swaleh.

Ust. Machano, alisema tokea kukamatwa Waislamu hao, kisha kushitakiwa na hatimae kuhukumiwa kifungo ndani ya siku chache kimemshangaza na kuhoji kama adhabu za nchi hii zipo kwa ajili ya Waislamu au na makundi mengine?.

Alisema, kama kosa ni kuandamana bila kibali wapo pia watu na Taasisi zinazoratibu maandamano na kuandamana pamoja na jeshi la Polisi kuzuia lakini hawakamatwi wala husikii wameshitakiwa katika Mahakama yoyote.

“ W a l e w a l i o f a n y a maandamano yasiyo na kibali kabla ya Waislamu zipo wapi kesi zao, kwani sheria za nchi hii zina makengeza? Kwa mwenendo huu sidhani kama ndiyo njia sahihi ya kujenga usawa na haki miongoni mwa makundi katika jamii.” Alisema na kuhoji Ust. Machano.

Ust. Machano, alibainisha

Na Bakari Mwakangwale kuwa, Waislamu hawaogopi mateso au vifungo, wala kufa kwa ajili ya dini yao bali wanachotaka ni kutendewa haki na wala si upendeleo, na kwamba sheria ifuatwe pasi ya kuangalia dini ya mtu, kabila au rangi yake.

Lakini alidai vyombo vya dola, vimekuwa vikiwashukia zaidi Masheikh na Waislamu kuliko mtu mwingine yoyote hata kama makosa yatakuwa yanafafa.

Alisema, haya yanayotokea hivi sasa yanawapa Waislamu msimamo, imani na utiifu kwa dini yao, sambamba na kuelewa aina ya viongozi wanao waweka madarakani kwani alidai itakumbukwa kuwa katika utawala wa Mzee Ally Hassan Mwinyi, Wahadhiri wa Kiislamu walifungwa miaka mine, jela.

Ust. Machano alisema, haya yanayojiri hivi sasa nchini dhidi yao, (Waislamu) wanapaswa kuyaangalia kwa umakini na kwa undani zaidi kisha kuyatolea majibu yaliyo sahihi.

Akirejea matukio mbalimbali yanayofanana na makosa yalipelekea kufungwa Waislamu, Ust. Machano, alikumbushia sakata la mgomo wa madaktari, waliogoma wakidai kuboreshewa mazingira ya kazi na kuongezewa mshahara nakusabisha vifo vya raia wasio na hatia na wengine kuteseka.

Katika kipindi hicho, Ust. Machano alisema, baadhi ya Taasisi za kiraia ziliratibu maandamano wakishinikiza Serikali ikubaliane na madai ya madaktari, maandamano ambayo hayakupata kibali kisheria na yalifanyika kupitia barabara ya Salenda, Jijini Dar es salaam, lakini mpaka sasa alidai haifahamiki waandamanaji wale, walichukuliwa hatua gani.

Ust. Machano, alitolea mfano tukio lingine la wanafunzi wa IFM, walioandamana bila kibali maeneo ya Kigamboni, lakini nao mpaka sasa haijulikani kama walikamatwa na kesi yao kwa kosa hilo inasikilizwa katika Mhakama gani.

Aidha, alisema Chama Cha Chadema, kimewahi kufanya maandamano Jijini Arusha, wakipinga uchaguzi wa Meya wa Jiji hilo na katika maandamano yale raia walipoteza maisha.

Kama haitoshi Ust. Machano, alisema kwamba, chama hicho kilifanya maandamano yasiyo na kibali Mkoani Singida, wakafanya tena maandamano

Morogoro, akafa mtu na kisha walifanya maandamano ya lazima Mkoani Iringa, licha ya kupigwa marufuku na IGP, Said Mwema, lakini hakuna kesi ya walioandamana bila kibali wala kukamatwa na vyombo vya sheria vipo.

“Hawa wote wamevunja sheria, wameharifu maagizo ya Polisi, kama walivyodaiwa kukiuka Waislamu waliofungwa kwa kosa hilo, kesi za waandamaji hawa wengine ziko katika Mahakama gani, haki ipo wapi, ni hatua gani zilizochukuliwa dhidi ya makundi haya ya kiraia walioandamana huku Polisi wakiwa wamepiga maruku au sheria hizo zipo kwa ajili ya waislamu tu?”. Alisema na kuhoji Ust. Machano.

Alisema, katika sura hiyo hiyo ya kudai haki na kuwasilisha kilio chao kwa mujibu wa Katiba kama walivyofanya wengine, Wais lamu nao wal i ra t ibu maandamano, lakini alidai pamoja na kwamba Waislamu hawakuandamana, zaidi ya kukamatwa kwa muonekano wao, walifikishwa Mahakamani kisha kuhukumiwa.

Ust. Machano, alibainisha kwamba, maandamano hayo yalikuwa yanalengo kufika kwa DPP, ili kutaka kujua sababu za kuzuiwa dhamana ya Sheikh Ponda Issa Ponda na Ustadh Mukadam Swaleh.

Ust. Machano, alisema yapo matukio ya kuvamia na pengine kuchomwa moto vituo vya Polisi na raia wanaoitwa wenye hasira kali, lakini huwezi kusikia vishindo vya kuwashughulikia watu hao kama ambavyo Waislamu wakiamua kuandamana au kudai haki zao kwa mujibu wa sheria. Ust. Machano, alisema viongozi wa nchi hii wasidhani kuwa kuwafunga, kuwatesa na kuwanyima haki zao Waislamu kutasababisha woga miongoni mwao na kurudi nyuma.

Alisema, kwa mujibu wa historia ya nchi hii hizo ni changamoto kwa Waislamu, kwani al idai tokea Uhuru upatekane wameshafungwa sana kwa makosa ya kudai haki au kupinga dhulma.

Alisema, Ust . Machano kwamba , U i s l amu n i wa mapambano tokea enzi na enzi, kwani hata Nabii Yusuph alifungwa jela kwa uonevu tu ambapo naye Nabii Ibrahim, alichomwa moto kwa kukataa kufuata mila za Makafiri.

WAKATI ile sikukuu ya Kikristo ya Pasaka ikiwa imefika, tayari zimeanza kuzagaa propaganda za woga na za kichonganishi na kizushi, ambazo tunaona zinatokana chuki na uchonganishi wa kijinga.

Tunasema wa kijinga kwa sababu fitna iwe ya kikabila au kidini ikikolea, hakuna atakaye kuwa na salama.

Propaganda iliyopo sasa ni kwamba eti kuna watu wanakusudia kushambulia nyumba za ibada, bila shaka yakikusudiwa makanisa wakati wa sherehe hizo za Pasaka.

Ta a r i f a h i z o t a y a r i zimeripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari mapema wiki hii. Hii inatupa kumbukizi ya propaganda kama hizi huko nyuma ambapo jeshi la polisi lilipa kazi ya kulinda makanisa baada ya lenyewe kupiga propaganda kuwa kuna Waislamu wanataka kushambulia makanisa wakati wa Krisimasi.

Lengo la propaganda kama hizi, kama ulivyokuwa ule urongo wa wachungaji na mapadiri kuwa kuna makanisa yamechomwa moto Yombo; ni kuchochea chuki za kidini na pengine kutafuta fursa na mazingira ya kufanya shambulio la kigaidi la kupanga (false flag terror attack) ili kipatikane kitisho cha kweli na kupata sababu zaidi ya kuwabamiza Waislamu.

Kwa bahati mbaya vyanzo vya taarifa hizi au waasisi wa propaganda hizi, hawaonyeshi kama wanakusudia kuzuia uhalifu zaidi ya kuonyesha nia ya kuzua na hofu na taharuki na hatimaye kuhandisi uhasama usiokuwa na maana wala manufaa.

Tunasema hivyo kwa sababu kiutaratibu, wanaotoa taarifa za uhalifu kwa jeshi la polisi, hufanya hivyo kwa siri ili kutoa nafasi kwa jeshi hilo kufanya kazi yake bila watuhumiwa kushtuka, i l i kurahisisha kuwanasa.

Kwa anayefahamu mpango wa uhal i fu , haiwezekani akakimbilia kwanza kwenye

Hawa ndio waharibifuTuwazomee, tusalimike

Wapo viongozi wa serikali, wachungaji na ‘masheikh maadhura’v y o m b o v y a h a b a r i n a kubwabwaja kuhusu kuwepo njama za uhalifu huo, badala ya kuzipeleka taarifa hizo katika chombo husika cha dola cha kupambana na uhalifu, ambacho ni Jeshi la Polisi.

Hapa ndipo tunapopata mashaka juu ya nia za wenye kusambaza propaganda hizi, ni kwa nini wasiwasilishe taarifa hizi Polisi kwa mujibu wa taratibu, juu ya mpango huo wa kushambulia Makanisa wakati wa Pasaka ili wanaohusuka mpango huo wadhibitiwe na mapema.

Hapa ndipo inapodhihiri kuwa taarifa hizi zinatokana na watu wazushi, wanaolenga kuleta fitna na farka kati ya Waislamu na Wakristo.

Tayari tumeshashuhudia namna uzushi wa namna hii ulivyofaulu kule Geita na Ukerewe Mwanza, Zanzibar na hata hapa Dar es Salaam.

Tutoe ushauri wetu kwa jeshi la Polisi kwamba, ni vyema zinapotolewa taarifa zozote zinazoashir ia kuandaliwa uhalifu hasa wa kiimani, basi waanze uchunguzi wao na watoa taarifa hizo kabla ya kwenda kwenye vyanzo vingine.

Kwa mfano, lingekuwa jambo la manufaa zaidi iwapo askari wa jeshi la Polisi wangewatafuta na kuwapata waliotoa taarifa za kuwepo hatari ya kushambuliwa hizo nyumba za ibada wakati wa Pasaka, ili waeleze wasiwasi wao msingi wake nini.

Hata hivyo hili nalo lina matatizo tukizingatia rekodi za utendaji wa vyombo vetu vya Dola. Imetokea mara kadhaa fitna huanzia kwa viongozi wa serikali, wao ndio huzua urongo ukadakwa na polisi na vyombo vya usalama. Mfano halisi ni ule wa aliyekuwa Waziri Mkuu Bwana Sumaye.

Hebu fikiria unapokuwa na kiongozi mkuu wa serikali ambaye ndiye wa mwanzo kuleta fitna na uzushi wa kuchochea chuki miongoni mwa raia huku anajifanya kuwa ndiye mpigania umoja wa kitaifa!

Imesema kweli Qur ’an:

“Na wanapoambiwa msifanye uharibifu ulimwenguni, husema “Sisi ndio watengezaji. Hakika wao ndio waharibuji lakini hawatambui.” (2:11-12)

Kwa Waislamu tunasema kuweni macho. Hawakawii hawa kufanya kile kinachoitwa “Inside job” ili wapate kufanya ‘fisadi’ katika ardhi.

Hawashindwi kujipachika u-Alqaqida, Al-Shabab na Boko Haram ili wakusingizie

nyinyi. Wanao vijana wengi wa kuwapachika majina ya Al-Zarqawi, Abdul Aziz na fazul.

Na hawa dawa yao ni kuwazomea mapema na kuchoma vichaka vyao.

Ama kwa wale ‘Masheikh maadhura’ ambao hukimbilia kutoa nasaha kwa Waislamu kuwa eti waache chuki na kushambulia makanisa, hawa tuwaombee dua huenda hata kinachotokea duniani hivi sasa

hawakijui. Wapo gizani. L a k i n i p i a t u s i k o s e

k u w a f a n y i a ‘ F a d h a k i r ’ maana kama wapo gizani huku wakijifanya kuwa ndio wasemaji wa Waislamu, zaidi ya kutusaliti, wanatutukanisha sote mbele ya walimwengu.

Wai s l amu wame ta jwa katika Qur’an kuwa ni watu wenye akili. Sio mbumbumbu wanaoparamia kila propaganda na kutumiwa kijinga.

Page 3: ANNUUR 1064

3 AN-NUURJAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 29 - APRILI 4, 2013Habari

Walio Jela wapata Sunna ya MitumeW A I S L A M U waliohukumiwa kwenda j e l a m w a k a m m o j a wamepata Sunnah ya Mitume. Na hiyo ni katika kufuzu kukubwa.

Hayo yamebainishwa na wazungumzaji mbalimbali katika Itiqaaf iliyofanyika katika Msikiti wa Tungi, jijini Dar es Salaam.

I m e e l e z w a k a t i k a Itiqaaf hiyo kuwa katika kupigania haki, katika kufikisha ujumbe wa Allah na kupambana na ukafiri na ushirikina, kupata mateso na hata kuuliwa ni katika jumla ya changamoto zake na Sunna ya Mitume.

Ndio tunaona kuwa Nabii Yusuf aliwekwa ndani bila ya kosa na Nabii Ibrahim akahukumiwa kuchomwa moto wakati akipigania kusimamisha Tawheed.

Ni kwa mtizamo huo, Waislamu wametakiwa k u w a o m b e a D u a n a k u w a o n a w a m e f u z u Masheikh wa Uamsho na wengine walio ndani au katika mateso ya namna mbalimbali mikononi mwa makafiri.

Kwamba, Waislamu na hasa Masheikh wasitamani kukumbatiwa na kuwa karibu na watawala wa tawala za kidhalimu kwani huo utakuwa ushahidi kuwa wao wamepotoka badala ya kuwausia haki watawala wao sasa wanatumiwa kulinda watawala wasio tenda haki na kufuata amri za Mungu na huo utakuwa upotofu mkubwa na maangamizi kwao.

Kuhusu hukumu ya kifungo cha mwaka mmoja kwa Waislamu waliodaiwa k u a n d a m a n a k w e n d a kwa DPP, ilielezwa kuwa Waislamu hao wanakwenda kutimiza sunna na hakuna hata mmoja anayesikitikia h i l o k w a s a b a b u walilitegemea na kwamba Wais lamu wategemee makubwa kuliko hayo.

“Kwanza kwa sasa tunapata ithibati kubwa ku toka kwa wenze tu waliopo katika mtihani, kwa kesi iliyoendeshwa chini ya siku 32, hii ni historia katika nchi hii, haijawahi kutokea. Wa i s l a m u t u t e g e m e e

Na Bakari Mwakangwale makubwa zaidi ya hukumu hiyo, lakini kamwe msitoke katika lengo la kudai haki zenu.” Aliasa msemaji Ustadh Rajabu Mussa Katimba.

K a t i m b a a l i s e m a , Waislamu wanapaswa kufahamu kuwa katika kudai haki zao katika utawala ambao msingi wake ni Mfumokristo, wategemee madhila na changamoto nyingi, hata hivyo akasema kuwa kwa Muumini wa kweli hayo ni mambo ya kawaida.

Pamoja na hayo Katimba a l i w a t a k a Wa i s l a m u wasitoke katika malengo yao, na watambue kuwa Allah (sw) ataendelea kuwapa mitihani na hata wengine itafika wapoteze uhai, lakini lengo ni kudai haki zao.

Sheikh Katimba, alisema Wais lamu wamekuwa wakiililia Serikali yao kwa muda mrefu, pamoja na kuainisha sekta zenye matatizo dhidi yao lakini badala ya kuwasikiliza na kutafuta ufumbuzi m a d a i y a o , S e r i k a l i imekuwa ikiwaadhibu na kuwakejeli.

A l i s e m a , I t i q a f zinazoendelea hivi sasa zitatoa majibu hususani kwa

viongozi au watu ambao wamekuwa ni kikwazo kwa makusudi kuona Waislamu wanapata haki zao.

Alikumbushia miaka y a n y u m a a m b a p o , aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu wa wakati huo, Bw. Augastino Mrema, aliwazushia Waislamu na kuwavalia njuga kisha kuanza kukamatwa hovyo, na kufika wakati Waislamu kujiona wanyonge katika nchi yao na kujihisi ni raia wasiotakiwa nchini.

“ B a a d a y a k u o n a madhila yanatuzidi, kwa fitna za Agastino Mrema, pamoja na juhudi zingine za kujinasua katika udhalili ule, Waislamu waliamua kumlilia Mwenyezi Mungu kwa dha t i . ” Al i sema Katimba.

Alitanabaisha kwamba anarejea kumbukumbu hiyo ili Waislamu na umma waweze kufahamu uzito na umuhimu wa kumlilia Allah (s .w), pale wanapohisi kudhulumiwa baada ya juhudi zingine kukwama.

Al i sema , baada ya Itiqafu hizo, Waislamu watatangaziwa Itiqafu ya Kitaifa, mipango ambayo inafanywa na Shura ya

Maimam, kwa utaratibu maalum.

Huku ak i r ea j a aya mabalimbali katika Qur an, alisema Mwenyezi Mungu anaeleza, kwamba muda mwingine unaweza ukafikiria mambo fulani yana kheri nawe lakini kumbe yana shar i na mengine ukaona yana shari, kumbe yana heri.

Akifafanua hukumu hiyo kwa Waislamu, Katimba, a l i s e m a k u m e k u w a na utata kuhusu muda waliohukumiwa kwamba sheria yenyewe inasema wamefungwa miaka mitatu baada ya kuonekana wana makosa matatu.

Al i sema kwa kuwa adhabu yenyewe inakwenda p a m o j a i n a m a a n a watatumikia kifungo cha mwaka mmoja jela na muda huo ina maana ni wastani wa miezi minane ndani.

Pamoja na hali hiyo, Mawakili wa Waislamu wapo katika mchakato wa kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa, ili haki itendeke.

A k i t o a r i p o t i k w a W a i s l a m u k u h u s u mwenendo wa kesi ya Sheikh Ponda, Mukadam na Waislamu wengine, katika kesi hiyo, Katimba alisema

“vyovyote itakavyokuwa, Waislamu wapo pamoja na kuangalia njia yoyote mbadala ya kujipanga na kuendelea na harakati za kudai haki za Waislamu”.

Naye Imamu wa Msikiti wa Tungi, Sheikh Shaaban Ibrahim, alisema, tawala zozote ambazo misingi yake ni dhulma, ubabe na uonevu, Mwenyezi Mungu huwadhalilisha hapa hapa duniani.

Imamu Shaaban, alirejea utawala wa Firauni, na k u w a t a k a Wa i s l a m u watafakari mwisho wake, lakini pia alimtolea mfano mmoja wa viongozi wa Serikali ya Zanzibar, na kusema hali yake sasa inahuzunisha, na kudai kuwa hali yake imekuwa ikielezwa kuwa ni matokeo ya vilio vya Waislamu katika utawala wake.

“Hivi sasa kiongozi huyo hata uwezo wa kuhudhuria hafla za Kitaifa hana, yupo katika hali ngumu, wote hawa waliwatenda Waislamu katika utawala wao, Waislamu waliamua kuinua mikono kumlilia na kumshtakia Allah (s.w), na hayo ndiyo majibu yake.” Alisema Imam Shaaban.

WANAFUNZI wa shule ya sekondari ya Benjamini Mkapa ya Jijini Dar es Salaam, mapema wiki hii wamejikuta mikononi mwa askari shirikishi b a a d a y a k u k u t w a wakicheza kamari muda wa masomo.

Askari hao waliokuwa w a m e o n g o z a n a n a Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Karume Ilala, jijini Dar es Salaam, Bw. Mohammed Zukher i , waliwakamata wanafunzi hao maeneo ya mitaa ya L ind i na Tabora , sehemu inayofahamika kwa jina la Calipso Game Centre, wakicheza kamari wakati wenzao wakiwa

Wanafunzi wafikishwa polisi kwa kucheza kamariNa Mwandishi Wetu madarasani.

M a r a b a a d a y a kukamatwa, Mwenyekiti Zukheri alisema vijana hao wamekuwa na tabia ya kutoroka shuleni na kwenda kucheza kamari, kuvuta bangi na kufanya mambo mengine ambayo hayastahiki kwa mwana funzi kuyafanya.

A l i s e m a h a l i h i y o inachangia kwa kias i fulani

Walimu kuonekana kwa wazazi kuwa hawafundishi wakati wanafunzi wenyewe hawafiki shuleni.

Alisema tat izo hi lo ni sehemu ya matokeo yanayopatikana katika mitihani ya mwisho , ambapo hushudiwa baadhi yao wakiandika madudu na

matusi katika karatasi za kujibu mitihani.

Kutokana na tukio hilo, Mwenyekiti wa mtaa wa Karume, amewaomba wazazi kujitahidi kufuatilia watoto wao wanaporudi m a j u m b a n i k w a kuchunguza madafutari yao ili kubaini kama wanapotoka majumbani wana f ika shu l en i au wanaishia njiani.

“Ni muhimu ukajengwa uhusiano wa karibu kati ya walimu na wazazi, wazazi wawe na namba za simu za walimu ili kurahisisha mawasiliano na ufuatiliaji wa wanafunzi”. Alisema Mwenyekiti huyo.

Wanafunzi waliofikishwa Kituo cha Polisi Pangani Ilala, walikuwa watano

baada ya mmoja kuponyoka na kukimbia.

Wanafunzi hao ni Wilfred Antony, Festo Joackim, Aloyce Nyangenyange, Peter William Muhaji, Hamidu Saidi na Muumini Hafidhi, wote wanasoma kidato cha tatu shuleni hapo.

Hata hivyo baada ya wanafunzi hao kufikishwa kituo cha Polisi Pangani, walishauriwa suala la vijana hao kurudishwa kwa uongozi wa shule, ili kutoa fursa kwa wazazi wa wanafunzi hao na uongozi wa shule kulipatia ufumbuzi wa kudumu.

Naye Mwalimu wa zamu wa shuleni hapo aliahidi kuwa suala hilo la utovu wa nidhamu litashuhughulikia kwa mujibu wa sheria za Shule yake.

Page 4: ANNUUR 1064

4 AN-NUURJAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 29 - APRILI 4, 2013Makala

Q U R ’ A N Tu k u f u n i chanzo cha uongozi chenye kuendelea, na muongozo i n a o u t o a u p o k a t i k a muktadha wa kile msomaji anachotafuta. Kujifunza kutoka kwenye Qur’an ni mchakato wenye kuendelea na hiyo ndiyo sababu tunaendelea kuisoma katika mazingira na mahitaji yote.

Q u r ’ a n T u k u f u inatufundisha kwa namna nyingi, na moja ya namna hizo ni kupitia visa vya Mitume, Wafalme na hata watu wa kawaida. Kwa hiyo watu tofauti katika nyakati tofauti na mitazamo tofauti ya mawazo, wanaweza kuvuna mafunzo tofauti kutoka kwenye visa hivi.

Leo ningependa tuangalie kidogo mafunzo ya uongozi kutoka kwenye visa kama hivyo - Kisa cha Dhul Qarnayn. Kwa nini tutafute mafunzo ya uongozi? Kwa sababu sisi sote kama Waislamu, tunafanya majukumu ya uongozi katika namna moja au nyingine. Moja ya hadithi mashuhuri za Mtume wa Mwenyezi Mungu inasema: “Kullu kum ra’in was kullu ra’in mas’uul an rai’yatay-hi...”, ikimaanisha kwamba, “Kila mmoja wenu ni mchunga na kila mchunga ataulizwa juu ya kile alichokichunga”.

Kisa cha Dhul Qarnayn k i m e e l e z w a n d a n i y a Qur’an katika Surat Kahf. Inaelezwa kwamba makafiri wal ikuwa wakimjar ibu Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa kuwataka Waislamu w a m u u l i z e b a a d h i y a maswali, ambayo walidhani asingekuwa na majibu yake, isipokuwa tu kama angekuwa Mtume wa kweli.

Kwa hiyo walimuuliza kuhusu vijana walioishi pangoni, na mtu mmoja aliyesafiri huko na kule na kuhusu roho. Haya ndiyo mazingira yaliyosababisha kushushwa kwa Sura Kahf, ambapo Mwenyezi Mungu anamfahamisha Mtume wake kuhusu majibu ya maswali hayo.

Hatujui kwa hakika hasa Dhul Qarnayn alikuwa nani. Baadhi ya Wanahistoria

Mafunzo ya uongozi ndani ya Qur’an Kisa cha Dhul- QarnaynNa Said Rajab w a n a s e m a a l i k u w a

‘Alexander the Great’, na wengine wanasema alikuwa Cyrus, Mfalme wa Persia. Lakini hata hivyo, si muhimu sana kujua alikuwa nani, ili kuweza kuvuna mafunzo yanayotolewa na kisa chake. Qur’an inasema:

“Na wanakuuliza habari za Dhul - Karnain. Waambie, “Nitakusomeeni baadhi ya hadithi yake.”(Qur18:83). Na kisha inasema, “Sisi tulimmakinisha (tumlitia nguvu) katika ardhi, na tukampa njia za kupata kila kitu” (Qur- 18:84).

Kupi t i a aya h izo za Qur’an, tunajifunza kwamba u o n g o z i n i k u k a s i m u m a m l a k a ( D e l e g a t i n g authority), na kanuni ya msingi katika kukasimu ni kwamba, mamlaka lazima yakasimiwe pamoja na rasilimali zinazoendana nayo. Yaani njia na nyenzo za kukamilisha kazi ambayo mtu amekasimiwa.

Katika kisa cha Dhul Qarnayn, tunakumbushwa kwamba Mwenyezi Mungu ndiye mwenye mamlaka yote. Anakasimu mamlaka yake kwetu kwa viwango tofauti. Anakasimu kazi kwetu, na kukamilisha kile anachotaka kupitia sisi.

Lakini Mwenyezi Mungu, hatodai kukamilishwa kwa kazi iliyokasimiwa, bila ya kutupa nyenzo stahiki au rasilimali muafaka za kukamilisha kazi hiyo. Mwenyezi Mungu anasema alimuweka Dhul Qarnayn katika ardhi na alimpa nyenzo za kila kitu. Yaani uwezo na rasilimali alizohitaji k u k a m i l i s h a j u k u m u alilopewa.

Upande wa pili wa sarafu ni kwamba Mwenyezi Mungu hawezi kutudai, kile ambacho hatuna uwezo wa kufanya, pale aliposema katika Sura Baqarah: “Laa yu kallifu-lahu nafsan illa was - aa - ha” (Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi kwa lile ambalo haina uwezo nalo).

Kwa hiyo, katika mazingira ya kibinadamu, hili ni funzo kwetu kila tunapojikuta kwenye nafasi yoyote ya uongozi, kwamba tutarajie mafanikio kutoka kwa wale tuliowakasimu kazi, iwapo tu

masharti mawili yatakuwepo. Kwanza, tusitarajie zaidi ya kile tunachojua wanaweza kufanya, na pili tuwape nyenzo, rasilimali na mafunzo yanayohitajika kufanya kazi hiyo.

Qur’an Tukufu inaendelea, “Basi akaifuata njia. Mpaka alipofika machweo ya jua (nchi za magharibi) aliliona linatua katika chemchem (ziwa) yenye matope mengi. Na pale akawakuta watu.Tu k a s e m a “ E w e D h u l - Karnain! Waadhibu au wafanyie wema” Akasema: “ A m a a n a y e d h u l u m u basi tutamuadhibu, kisha atarudishwa kwa Mola wake, naye atamuadhibu adhabu mbaya kabisa.” Na yule mwenye kuamini na kufanya vitendo vizuri, atapata ujira mwema nasi tutamwambia (tutamfanyia) lililo jepesi katika amri yetu” (Qur- 18:85-88).

Uongozi unaambatana na mitihani wakati wote. Hapa tunaona Dhul Qarnayn anawekwa katika mtihani. Amepewa mamlaka makubwa na Mwenyezi Mungu na uwezo wa kufanya analotaka, halafu anapewa changamoto ya kuamua cha kuwafanyia watu ambao amewazidi kwa kila kitu. Anaonyesha sifa za kiongozi bora - kuwatenganisha walio wema na waovu.

A n a o n y e s h a s i f a z a

uongozi bora za kutenda hak i na ku topende lea . Wakosaji lazima waadhibiwe, lakini watu wema lazima wazawadiwe na kuheshimiwa. Angalia hatua mbili hizo katika kila kundi. Katika kundi la wakosaji, adhabu ya kwanza inatoka kwake, lakini adhabu kubwa zaidi itakuja baadaye kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Katika kundi la watu wema, kwanza watapata zawadi bora kutoka kwake, na zaidi ya hapo atazungumza nao kwa wema. Kwa hiyo lazima kuwe na tofauti katika kuwashughulikia watu wema na waovu. Qur’an inaendelea kusema: “Kisha akaifuata njia. Hata alipofika katikati ya milima miwili, alikuta nyuma yake (milima hiyo) watu ambao waliweza kwa shida kufahamu neno (wanaloambiwa). Wakasema: “Ewe Dhul - Karnain! Hakika Yaajuu na Maajuju wanafanya uharibifu katika ardhi. Basi je, tukupe ujira ili utie baina yetu na baina yao kuzuizi” (Qur- 18:92-94).

Uongozi siyo kuwanyonya wanyonge. Wakati Dhul Qarnayn alipokutana na watu wanaozungumza lugha tofauti kabisa na yake, na kwa hakika ni wageni kwake, aliwachukulia kwa moyo wa kuwahudumia zaidi kuliko kuwanyonya. Ingawa watu wale walikuwa tayari kumlipa

ili awawekee kizuizi baina yao na wavamizi wa kigeni, lakini hakudai zaidi, na wala hakukubali kile ambacho wao wenyewe walimpa, kwa sababu hakutaka kutumia udhaifu wao kujinufaisha.

Pengine kama angewapiga na kuwashinda, huenda angetarajia kitu kutoka kwao, lakini siyo katika mazingira ambayo wao wenyewe wamejisalimisha kwake na kumuonyesha udhaifu wao. Kwa hiyo, kama kiongozi bora, Dhul Qarnayn ni mkarimu. Katika ukarimu wake p ia , anaonyesha unyenyekevu, kwa sababu anakumbuka kwamba hata kile alichonacho amepewa na Mwenyezi Mungu na anasema hivyo.

Pia anatambua kwamba nguvu ambazo Mwenyezi Mungu amemjaa l i a n i nyenzo tu ya kumtumikia Yeye. Kwa hiyo anamtumikia Mwenyezi Mungu kwa kuwa ‘kiongozi - mtumishi’ kwa watu wake, yaani kiongozi anayeshughulikia mahitaji ya watu wake.

Akasema: “Yale ambayo Mola wangu amenimakinishia (amenipa) ni bora kuliko (ujira wenu. Nitakufanyieni bure); Lakini nisaidieni kwa nguvu zenu (wafanyaji kazi). Nitaweka baina yenu na baina yao kizuizi imara” (Qur-18:95)

Inaendelea Uk. 11

JUMLA ya Maimamu thelathini kutoka sehemu mbalimbali Unguja wameshiriki katika semina elekezi iliyoandaliwa na Chuo cha Kiislamu cha Markaz Chang’ombe cha jijini Dar es Salaam na kufanyika visiwani Zanzibar Ijumaa iliyopita. iliyokuwa na anuani, “Ufahamu sahihi wa Uislamu ni lazima ujulikane na watu wote”. Dk. Ossama Mahmoud Ismail,, Mkurugenzi wa Markaz Chang’ombe (katikati).

Page 5: ANNUUR 1064

5 AN-NUURJAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 29 - APRILI 4, 2013Habari za Kimataifa

MWEZI Januari mwaka huu, niliandika gazetini makala iliyobeba anuani: HIJA IBADA KONGWE KWA WANADAMU WOTE. Watu wengi, walijitokeza kunipongeza baaada ya kuguswa na maudhui ya makala ile. Nachukua fursa hii kuwashukuru wale wote, ambao kwa njia ya simu, sms na baruapepe (e-mail) walinitumia pongezi zao.

Wakati huu tukielekea katika kukamilisha mchakato wa kupata katiba mpya ya nchi yetu, nimeonelea vyema na mimi nifanye haraka kupeleka mawazo yangu kwa Tume ya Warioba, nikiwalenga wale wananchi watakaopata nafasi ya kuwamo katika mabaraza ya kupitia rasimu ya katiba hiyo, watambue utukufu wa siku ya Ijumaa na hivyo kuiomba iwe siku ya mapumziko kwa wote.

Tukirudisha kumbukumbu (retrospect) katika miaka i l i y o p i t a , w e n g i w e t u tumeshuhudia katika sehemu nyingi za miji, vijiji na vitongoji, hasa vya maeneo ya Pwani ya Tanzania, ambao wakazi wake wengi ni Waislamu, shughuli za kuuza na kununua zikisimama, pa le l inapochomoza jua kuashiria Ijumaa imeingia.

Siku hiyo ikifika, wakulima huwa hawaendi shamba; wavuvi hawaendi kuvua; wajenzi hawajengi; mafundi cherehani hawatoi vyarahani vyao barazani na watoto hawaendi madrasa kusoma. Kila mmoja huwa katika harakati za kujiandaa kwenda kushiriki Ibada ya Ijumaa pamoja na waumini wengine kuanzia asubuhi mapema.

Akiwahutubia waumini kwenye khutba yake ya Ijumaa, Novemba 21, mwaka jana kuhusu utukufu wa siku ya Ijumaa, Sheikh Ahmed Haidar Mwinyimvua, Imam Mkuu wa Msikiti wa Mwinyikheri Akida, Dar es Salaam amesimulia hadithi kwamba siku moja Mtume Muhammad (S.A.W), alijiwa na Malaika Jibril akiwa ameshika kioo kilichokuwa kinaonyesha siku ya Ijumaa kuwa n i S ikukuu. J ibr i l alimwambia Mtume kwamba Mola wake amemtaka aifanye siku hiyo kuwa ni Sikukuu kwa umma wake mpaka mwisho wa dunia hii. (Angalia

hadithi ya Atirmidhi).Amesema Sheikh Haidar:

“Wakati huu wa kutengeneza katiba kaombeni Ijumaa iwe mapumziko kwa sababu ni siku bora miongoni mwa siku zilizochomozewa na jua…Baba yetu Adam aliumbwa siku ya Ijumaa, alitiwa Peponi siku ya Ijumaa, alitolewa Peponi Ijumaa, na Kiyama hakitatokea mpaka ifike Ijumaa…

“Ijumaa iwe ni mapumziko nchini na siyo kama ilivyo

Katiba mpya itoe mapumziko Ijumaa Na Alhaji Abdallah

Tambazamazoea kwamba ni siku ya kuabudu kwa waumini wa Kiislamu peke yao kwa kupewa ruhusa kazini saa 6 mchana muda mchache tu kabla ya sala yenyewe.”

Amri hii ya kuitukuza Ijumaa ilikuja kwa Mtume hata kabla ya ile aya iliyotutaka kuanza kwenda msikitini kusali sala mahsusi ya Ijumaa kwa pamoja, iliyomteremkia Mtume nje kidogo ya Mji wa Madinna alipokuwa njiani kutoka Makka katika lile tukio mashuhuri la Hijria.

Habari zinasema, ilikuwa kama siku ya Jumatatu au Jumanne hivi, msafara wa Mtume ulipojiwa na Jibril na kutakiwa kusimama na kuadhimisha Ijumaa ya mwanzo mahali hapo kabla ya kuingia Madinna. Ingawa sasa umejengwa msikiti mkubwa, lakini mahala pale iliposaliwa Ijumaa ya mwanzo n i sehemu ambayo wote wanaokwenda ziara Madinna, hufika kupashuhudia kutokana na utukufu wa Ijumaa ulivyo duniani leo hii.

Kwa mujibu wa kitabu cha mwongozo wa Hi j ja kilichoandaliwa na Taasisi ya Tawheed Development Network, ukurasa wa 48, na kwa maelezo ya Alhaj Yusuf Macherenga, katika msafara wa mahujaji kwenye Masjid Quba, huo ndio msikiti wa mwanzo kujengwa na Mtume katika ardhi iliyomilikiwa na familia ya Kalthum bin Al Hadm, ambao ndiyo waliompa hifadhi ya sehemu ya kukaa alipohamia Madina. Masjid Quba umetajwa kwa sifa katika Quran Sura ya Tauba Aya ya 108.

Mtume (SAW) amesema, yule ambaye atajitoharisha nyumbani na kwenda Masjid Quba, na akaswali rakaa mbili, basi thawabu zake ni sawa kama amefanya Umrah.

Tangu ulipojengwa enzi za Mtume (SAW) umeendelea kupanuliwa na leo hii una uwezo wa kuchukua jumla ya waumini 20,000. Mwandishi huyu amepata bahati ya kuswali katika msikiti huo.

Sala ya Ijumaa ni waajibu kwa kila Muislamu, isipokuwa kwa watu wanne: mwenye kumilikiwa kwa maana ya mtumwa, mwanamke, mtoto mdogo na mgonjwa. Pia mwenye tumbo la kuendesha na hawezi kujizuia; na kama kuna maiti itakhofiwa kuharibika, watu wataacha kwenda kusali Sala ya Ijumaa na kumshughulikia maiti mpaka kuzikwa.

Ukiangalia upande mwingine, utukufu wa siku ya Ijumaa unapatikana kwenye maandiko yanayosema kwamba Nabii Issa (Yesu) A.S.W alifikwa na mauti pale msalabani siku ya Ijumaa Kuu (Good Friday) ambayo Wakristo duniani huitukuza kwa ibada mbalimbali. Vyovyote vile iwavyo, huo ni ushahidi (clear manifesto) mwengine wa ukubwa wa Ijumaa.

Sasa kama kweli binadamu

tunaamini kuumbwa (birthday) ya Adam; kutiwa na kutolewa peponi kwake; ni matukio ambayo yanatugusa na sisi kama kizazi chake yaliyopelekea kushushwa kwake duniani kuanzisha uzao wetu huu wa kibinadamu yalitokea siku ya Ijumaa, basi ni sababu tosha ya kuienzi na kuitukuza siku ya Ijumaa kwa mapumziko.

Siku ya Ijumaa Waislamu tumetakiwa kusali sala maalumu ya pamoja. Sala hiyo hutanguliwa na khutuba mbili zilizoandaliwa kwa Ijumaa hiyo na kamwe mtu hawezi kusali Ijumaa peke yake kama zilivyo sala zingine za asubuhi, dhuhri, laasiri… za siku na nyakati za kawaida.

Kabla ya kwenda msikitini siku ya Ijumaa waumini hutakiwa kujiandaa kwa mambo kadhaa muhimu (kuoga, kuvaa nguo maridadi, kutia manukato na udhu) majumbani mwao tokea mapema ambayo yote huwa na malipo lukuki kwa Mungu. Huwezi kupata sehemu ya kuoga na kuvaa nadhifu ukiwa utaanzia safari ya Ijumaa kutoka ofisini, mkutanoni au shuleni.

Kwa kutoifanya siku ya Ijumaa kuwa siku ya mapumziko, Wa i s l a m u w a Ta n z a n i a wamekuwa waki i tekeleza ibada hii muhimu na yenye fadhila na thawabu kemkem kwa mapungufu makubwa kwa kutofikia vigezo na hivyo kutopata chochote miongoni mwa ahadi—Mungu hachezewi ka t ika ibada kwa namna tufanyavyo.

M o j a y a m a m b o yanayotakikana siku ya Ijumaa ni kusoma Qurani kwa wingi (hasa Surat l’qaaf) ukiwa msikitini ambayo kila herufi moja usomayo utalipwa thawabu kumi. Ruhusa ya saa 6 mchana haikupi muda wa kufanya hivyo. Hata kuwahi kukaa safu za mbele pia kuna thawabu zake.

Ruhusa ya saa 6 mchana mara zote hupelekea muumin kukosa kusikiliza zile khutba mbili za Ijumaa ambazo huwa na thawabu nyingi sana na humpa mja nafasi ya kuomba dua moja kwa moja (direct) kwa Mola wake bila ya kizuizi katikati wakati inapomalizika khutba ya mwanzo.

Kuukubali na kuuachia m f u m o u l i o p o u e n d e l e e kutukosesha mambo haya ni uzembe mkubwa maana thawabu hizi tunazoziachia zipite kizembezembe pengine ndizo zingekuwa mwokozi siku ile ya ‘Ijumaa ya hesabu’ mbele ya Allah.

Kwa kupewa ruhusa saa 6 mchana kwenda msikitini, Waislamu wanakosa kabisa au kuchelewa kutimiza mambo muhimu yanayowataka kufanya kabla kuelekea msiki t in i kusali:

Kwa mfano mtu unaweza usiwe umeoga mwili mzima siku zote za wiki, lakini Ijumaa inakutaka uwe umekoga na siyo kuchukua udhu tu na kuingia msikitini kusali. Ijumaa pia inakutaka uwe umevalia nadhifu kwa nguo unazozipenda pamoja na kujitia manukato mazuri kabla ya kuelekea msikitini.

Baada ya kufanya hayo utakuwa unapata thawabu kila hatua moja utakayotembea kutoka kwako kuelekea msikitini ambako thawabu hutolewa kwa wingi kwa wale walioingia mapema na kuanza kusali sala za sunna zisizo na idadi pamoja na kusoma Qurani kwa wingi. Malaika waliomo huwa wanamworodhesha kila mtu anayeingia na kufanya ibada tokea mapema.

Habari zinasema kwamba, waliowahi mapema kwenye saa 4 mpaka 5 wao wanapata thawabu kipimo cha ngamia; wanaofuata ng’ombe; mbuzi;

kuku; na mwisho ni yai au hakuna kitu.

Waislamu wa Tanzania, kwa sababu za kimfumo tu wa nchi, miaka yote tumekuwa tukiambulia yai au sifuri kwa sababu kazi inatutaka tufike msikitini saa 6:30 au zaidi na pengine kukosa kabisa Ijumaa.

N i l a z i m a k u z i n g a t i a hapa, kwamba thawabu zote hizi ambazo siku ya hesabu zingetuokoa zinapotea kwa sababu wenyewe tumeridhia ku tup i l i a mbal i hak i h i i ya kuabudu na kujiongezea thawabu.

Ni lazima tufanye ibada kwa usahihi maana ndiyo vitu tutakavyohisabiwa navyo siku ya malipo. Mtume amesema; “Je tukwambieni watu ambao watapata hasara siku ya hesabu? Ni wale ambao wamefanya ibada zao bila ya mpango”.

Kat ika h i l i l a I jumaa , Mwenyezi Mungu hakuna mahala aliposema kwamba a t a k u s a m e h e a u k u k u p a thawabu sawa na wengine kama utashindwa kufika msikitini kwa wakati, eti bosi hakukuruhusu! Ukiikosa umeikosa na huwezi kusali kadha.

C h a k u s h a n g a z a h a p a ni kwamba hata viongozi waandamizi wa Kiis lamu nchini, wamekuwa wakifumbia macho jambo zito kama hili la kuabudiwa Mwenyezi Mungu kwa wao wenyewe pia kutofanya hima kwenda misikitini kwa wakati kwa kisingizio cha vikao na mikutano! Inna Lillah!

Mara nyingi tumewashuhudia ‘live’ wabunge Waislamu pale Dodoma wakiendelea kukaa kwenye viti vya Bunge wakati muda wa sala umekwenda wakimsubiri Spika aahirishe B u n g e s a a 6 : 3 0 n d i p o wakimbilie msikitini kupata labda yai. Udhalili gani huu!

Inaendelea Uk. 9

MUFT Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kabi (kulia) akiongoza viongozi wa serikali na Waislamu katika kisomo.

Page 6: ANNUUR 1064

6 AN-NUURJAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 29 - APRILI 4, 2013MAKALA

MKUU wa Chuo cha Waislamu Morogoro (MUM), Hajat Mwantumu Malale akihutubia siku ya uzinduzi wa Kitivo cha Sayansi Chuo Kikuu cha Waislamu, Morogoro na sio Hajat Mwantumu Mahiza kama tulivyoandika toleo lililopita.

IMANI ni nafsi, na nafsi ni ubinafsi! Taifa lolote lile duniani, ili liishi na liendelee kuwepo, ni lazima lithamini raia wake kulingana na imani za watu wake. Taifa ambalo lina watu wenye imani za kiroho tofauti, au mi la na des tur i tofauti, ni lazima taifa hilo lijengwe kwa juhudi za kufanya kazi kwa dhati kwa madhumini ya kulijenga taifa kiuchumi, k i m a e n d e l e o n a kitekinolojia. Taifa lenye watu wanaojitambua kwamba ilikuwepo jana, ipo leo na kutakuwepo kesho; ni lazima kuwe na mikakati na malengo ya kitaifa hasa likiweka msisitizo kuhusu kesho, lakini bila ya kusahau leo kukoje na jana kulikuwa vipi? Taifa lenye maono ya namna hii ni taifa lenye akili!

Wa a n d i s h i w e n g i w a m e a n d i k a s a n a kuhusu tatizo la udini, na wengine wamediriki moja kwa moja kumshutumu Rais Kikwete kwamba anapendelea dini yake ya Kiislamu katika serikali yake! Mimi nawapinga wale wote waliomshutumu M h e s h i m i w a R a i s Kikwete kuhusiana na tatizo la udini hapa nchini, na wanaonekana aidha hawauju i mfumo wa utawala wa nchi hii kwa ujumla tangu nchi imepata uhuru au ni miongoni mwa wana mfumo ambao wapo upande wa pili wa imani ya Kikwete hivyo wanaona maslahi yao yameathirika!

Kulingana na uzoefu wangu kwenye mfumo huu wa utawala wa Nyerere ni kwamba walalamikaji wenye majukwaa ya kulalamika na kukasikika kile wanacholalamika siku zote wamekuwa upande wa pili wa imani ya Kikwete hivyo kwa vile wana jukwaa lenye vipaza sauti vya kisasa ambavyo wakipayuka kila mtu husikia na kuona kwamba kweli kuna tatizo,

Tuvunjilie kwa mbali ‘mfumo Kristo’ ndio tutakuwa salama

Na Dr. Noordin Jella lakini ni kwamba tatizo hili lipo tangu wakati wa Nyerere na lina msukumo mkubwa katika mfumo wa serikali yetu kwa ujumla! Sasa tukianza kumlaumu Kikwete kama Kikwete na imani yake ya kiroho t u t a k u w a t u n a f a n y a ushabiki tu wa kiroho. Tatizo la udini lipo ndani ya mzunguko wa damu wa mfumo wetu wa utawala, hivyo ukitaka kulitatua k i u k w e l i u n a t a k i w a uufumue mfumo mzima wa utawala na kuunda upya!

Wa k a t i t u m e y a kuandika katiba mpya inasema madaraka ya rais yasiguswe, na watawala wote wastaafu wa nchi hii wanasema madaraka ya rais yasiguswe; naomba tufikiri zaidi. Hivi katika mazingira kama haya tunamlaumu Rais Kikwete kwa vile amezaliwa Msoga au tunamlaumu kwa sababu gani!

Mwasisi wa serikali za udini hapa nchini n i Mwalimu Nyerere na amejenga mis ingi madhubuti ya udini kiasi kwamba huwezi kuumaliza udini hapa nchini mpaka uufumue mfumo wote wa utawala! Wakati wa u t awa la wa Nyere re udini ulionekana, lakini waliokuwa upande wa pili wa imani ya Nyerere walikuwa hawana jukwaa maalumu la kulalamika ndiyo maana pamoja n a m a l a l a m i k o y a o mengi waliyotoa, lakini hayakusikika kwa vile j ukwaa l ao l i l i kuwa dogo na halina vipaza sauti! Kulikuwa hakuna magazeti, redio na taasisi za Kiislamu zilibanwa na kuachwa msemaji kuwa Bakwata pekee. Na tunaijua Bakwata ni nini. Alipoingia Mzee Mwinyi na kuanza kupunguza malalamiko ya udini ya miaka 23 kwa upande wa Waislamu, akaonekana yeye ndiye anayeleta udini, na waliokuwa wanamlaumu ni wale waliokuwa upande wa pili wa imani yake! Turejeshe kumbukumbu zetu jinsi alivyoandamwa

Almarhum Alhaj Kighoma Ali Malima. Na tukumbuke p i a j i n s i b a a d h i y a wachungaji kama Mtikila walivyomsambulia Mzee Mwinyi.

N i m e w a h i k u s e m a kwamba Profesa Kighoma Malima aliyewahi kuwa Waziri wa Elimu wakati wa ser ikal i ya Mzee Mwinyi aliwahi kusema kwamba kuna “waraka” aliouandika Nyerere wa kuisisitiza serikali kwamba iwape kipaumbele katika elimu waumini wote wa Kikristo, na waraka huu ndiyo unaotumiwa tangu nchi hii imepata uhuru hadi leo hii! Sasa sijui kwa nini Nyerere aliona kwamba Wakristo wana sababu za kupendelewa na kupewa fursa maalum! Je, aliona kuna udhaifu wa kufikiri na kuelewa kwa upande wa Wakristo au alifanya hivyo ili Wakristo wawe werevu zaidi, na Waislamu wawe mbumbumbu au alifanya hivyo kwa makusudi gani? Angelikuwepo hai ningelipenda maswali haya akayajibie ndani ya ukumbi wa bunge kule Dodoma. Lakini kwa vile hayupo, si vibaya kama warithi wake watamsaidia kuyajibu maswali haya!

Suala la kuwepo kauli ya Nyerere kuwapa ‘fursa ya upendeleo’ Wakristo lipo, lakini hakuna anayetaka kulizungumzia, kwa vile Watanzania tumezoea mambo ya ubinafsi na ubinafsi ni uchache, na

kwenye uchache kuna kufaidi zaidi! Tukitaka kutatua tatizo la udini hapa nchini tuhoji uhalali wa waraka wa Mwalimu Nyerere!

Waislamu wanalalamika kuhusu kubaguliwa kwao kielimu kwa vigezo vya udini, lakini walijibiwa na majukwaa makubwa na yenye vipaza sauti vya kisasa kwamba wapo nyuma kielimu kwa vile w a m e e n d e k e z a s a n a kusoma Qur ’an zaidi badala ya kusoma masomo ya sayansi au hawataki kusoma! Haya yalikuwa si majibu sahihi.

Malalamiko ya Waislamu hayakujibiwa kiukweli kwa vile walitoa hoja na ushahidi na wanaendelea kutoa ushahidi mpaka leo, lakini waliojibu na wanaojibu hivi leo, hujibu kisiasa za kukataa ukweli bila kugusa wala kukanusha ushahidi unaotolewa.

Sitetei imani ya Kikwete, bali tu nasema kwamba watu katika taifa moja hawathaminiwi kwa sababu ya dini yao.

M a r e k a n i n i t a i f a lililoendelea sana duniani kwa kila hali ya maendeleo ( k i u c h u m i , k i s i a s a , kitekinolojia, kijamii na kifikra), lakini pamoja na mendeleo hayo kila mwaka wanachezesha bahati nasibu (Green Card) ambayo hujumuisha nchi zote duniani bila ya kuchagua kwamba ni nchi ya Kiislamu au Kikiristo.

Bahati nasibu hii ina lengo moja kubwa la kutafuta vipaji nje ya Marekani kwa vile kizazi kipya cha Kimarekani pamoja na kwamba wameendelea sana, lakini kizazi hiki kipya hakijishughulishi kabisa na masomo ya sayansi kitu ambacho Wamarekani wameona ni hatari kwa taifa lao (wengine hukiita kizazi cha muziki wa R&B na Hip Hop), hivyo wakaamua k u a n z i s h a u t a r a t i b u huu wa Green Card ili kuibua vipaji vipya toka nchi mbali mbali duniani watakaoweza kuendeleza sayansi ya Wamarekani. Ukienda kwenye idara nyeti ya udadisi wa sayansi ya hali ya juu ya mambo ya anga ya Marekani (NASA) utakuta watu wenye asili ya kila kona ya dunia, na imani tofauti za kidini, lakini pamoja na kuwa na rangi za ngozi tofauti na imani za dini tofauti, bado wote hawa Amerika inajivunia kwamba ni raia wake na inawatendea haki sawa. NASA kuna Wa a f r i k a , Wa a r a b u , Wa z u n g u , Wa h i n d i , Wachina na Wajapani; wote hawa kila mmoja ana imani yake ya kidini, lakini hawathaminiwi na serikali ya Marekani kutokana na imani zao za kiroho, hapana, b a l i w a n a t h a m i n i w a kulingana na mchango wao wa kimaarifa kwa taifa lao. Sasa sisi tukianza

Sahihisho

Inaendelea Uk. 9

Page 7: ANNUUR 1064

7 AN-NUURJAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 29 - APRILI 4, 2013TANGAZO

Page 8: ANNUUR 1064

8 AN-NUURJAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 29 - APRILI 4, 2013

Makala/Tangazo

Na Khalid S Mtwangi

H I V I k a r i b u n i n i k i w a nimesaidiwa kupelekwa nyumbani ndani ya gari nzuri ya kisasa RAV4, gari ambazo leo hii ndio zinatumiwa na wengi wenye mapesa ya wale ‘walioula’ hivi karibuni. Safari yetu ilianzia sehemu moja ya Tabata…tukielekea Mwenge mpaka Mikocheni “B” hapo Dar es Salaam. Hapo Tabata ilibidi tupite karibu ya lile Kanisa kubwa la Katoliki likiitwa Christ the King.

Hakika huyu Rasul-ul-Llah (A.S) wanayemwita YESU kapewa majina na sifa nyingi sana ambazo nyingine ni kufuru tupu. Wakati mwingine hufikiria kuwa kama angerudi leo akaona na kusikia yale yanayoelezwa kumhusu yeye na akapoona picha na sanamu ambazo zinasemekana kuwa ndiye yeye, basi bila shaka angejifinya kwa nguvu kujihakikishia kama kweli yuko macho na akili timamu na hayo anayoyaona na kuyasikia na sio ndoto.

Tusubiri wakati atakaporudi h u k u d u n i a n i k a m a tunavyofundishwa na Qur’an. Kwa sasa turudi kwenye gari na hawa waliyonipa ‘lift’, wote wakiwa wanandugu damu. Karibu na kanisa hilo kuna bango li l i loandikwa CATHOLIC UNIVERSITY OF…(yaani CHUO KIKUU CHA KIKATOLIKI CHA…). Kila aliyekuwemo ndani ya gari hilo aliliona hilo bango na ni mmoja wao ndiye alilisoma kwa sauti na sote tuliokuwemo ndani ya gari tulisikia. Mimi nilishtuka na kusema kuwa hawa jamaa watatutawala milele, hicho labda ni Chuo Kikuu chao cha “kumi” nchini humu. Kingine wameanzisha huko Bagamoyo, ambako hakika ni mji wa Kiislamu.

Basi hapo nilichokoza nyuki. Hawa jamaa walionipa ‘lift’ walianza kinishambulia mimi na Waislamu wote wa nchi hii. Wanandugu hawa, wakiwa mmoja mwanamume na wawili wanawake, walinisuta wakisema kuwa Waislamu imekuwa kazi yenu ni kulalamika tu hamfanyi lolote kujiendeleza. Haiwezekani hawa waKatoliki ama waKristo wote kwa jumla wasite kuleta maendeleo yao ili kuwasubiri ninyi Waislamu mkipiga domo tu.

Nijaribu sana kujitetea na

Waislamu acheni kulalamika tu!kuwatetea Waislamu kama vile kuwatambulisha historia ya nchini humu ikiwahusu Waislamu tangu kabla ya uhuru mpaka baada ya uhuru, jinsi walivyokuwa mbele na namna walivyodhoofishwa. Hayo kweli wao wasingeweza kuyafahamu; wao wote wamezaliwa baada ya uhuru na labda ni bahati mbaya kuwa walipopata fahamu, hasa ya kujua kuna nini duniani humu walikuwa nje ya nchi.

Halafu kama inavyojulikana miongoni mwa Waislamu wengi, historia ya nchi hii imeandikwa na kufundishwa kutegemea na nani anaieleza. Wote hawa waliokuwa wakinishambulia wana elimu ya chuo kikuu. Lakini inastaajabisha jinsi gani walivyo ‘tupu’ kuhusu historia ya Waislamu na Uislamu na nchini humu kuwa ujumla.

Inawezakana kuwa mzazi naye alaumiwe kukosa kuwaeleza angalau machache juu ya hayo yanayowasibu Waislamu nchini humu kwa muda mrefu sana. Lakini ukweli ni kwamba, hawa wote ni wasomi wenye shahada za vyuo vikuu, hivyo wanategemewa kujua mengi yanayoendelea humu Tanzania, hasa baada ya kelele nyingi zinazopigwa na Waislamu ambazo wao wamezisikia. Hata hivyo si vibaya tukijaribu kutafakari hoja walozitoa huku wakinishambulia.

Ukweli ni kwamba Waislamu wa nchi hii hawajitutumui vya kutosha katika kuwatafutia elimu watoto wao, hasa wakati huu ambao kila Muislamu anafahamu kuwa kuna dhulma kubwa inapitishwa nchini humu dhidi ya Waislamu.

Ikubalike kuwa hivi sasa kuna shule nyingi zaidi zimejengwa na zinazoendeshwa na Waislamu kuliko wakati wowote katika historia ya nchi hii. Pengine huu ni ukweli ambao wale jamaa walionipa ‘lift’ ndani ya gari yao hawalifahamu au hawakulikumbuka.

Hii maana yake ni kuwa sio kwamba Waislamu wanalalamika tu, bali nao wanafanya kwa vitendo kujiendeleza katika elimu. Lakini swali la kujiuliza ni kama Waislamu nao wana kasi ya kutosha kukabiliana na nia ya Makanisa kuendelea kuitawala nchi hii. Nadhani hilo ndilo lilikuwa linawatuma hawa vijana kunishambulia kiasi kile.

L i l ikuwa n i juhudi ya kujivunia sana pale hivi karibuni palipoitishwa tamasha pale uwanja wa taifa kuchangisha pesa kujenga na kuanzisha kituo cha television cha Waislamu n c h i n i h u m u . Wa i s l a m u waliitikia wito huo kwa shauku kubwa sana. Uwanja ulifurika, takriban kila aliyekuwa na nguvu ya kutembea alifika na kila aliyeweza kuchangia angalau kwa shilingi moja alijitolea.

Hapa jambo linalijitokeza

ni kwamba Waislamu wako tayari kujitolea kwa hali na mali kuuendeleza Uislamu na kujiendeleza wao wenyewe. Sasa Kitu gani kinatokea mpaka kunatokea hawa wasomi walionipa ‘lift’ kunishambulia kiasi kile?

U k w e l i n i k w a m b a Wa i s l a m u w a n c h i h i i wanakosa uongozi uliothabiti na wenye ukereketwa wa hali ya juu sana juu ya Uislamu wao. Uongozi unaojulikana nchini na uliopewa ulingo peke yao kwa muda mrefu umekuwa ni BAKWATA. Lakini historia ya kusikitisha ya chombo hicho ambacho kimekuwa kikidai kuwa ndicho kinachowawakilisha Waislamu, imekuwa ya kusikitisha sana.

Hakika wao sio wawakilishi wa Waislamu hata kidogo. Kuna vyama vingine vimeibuka kwa minajili ya kuutumikia Uislamu na Waislamu; navyo ufanisi wao umekuwa duni ingawa wao labda sio wasaliti wa Uislamu. Hivyo sivyo ilivyo miongoni mwa waKristo.

Wasomaji watakumbuka kuwa Kanisa Katoliki na v i o n g o z i w a m a k a n i s a mengine walipoamua kukiunga mkono chama cha siasa cha CHADEMA, sio Mapadri tu ndio waliingia ulingoni. Ilikuwa wazi kabisa wasomi wengi, kama sio wote, walio waKristo waliunga mkono harakati hizo.

Ni wao ndio waliotunga kwa fasaha lile tamko la kanisa juu ya uchaguzi. Hilo halikutosha walitoa pia Ilani ya Uchaguzi

ambayo iliandikwa na wasomi pamoja na wale walio katika utumishi Serekalini. Bila shaka itakumbukwa kuwa nyaraka zote hizo mbili zilikuwa za ubaguzi mkubwa wa kidini ukilenga kutaka Mfumo Kristo uendelee kuitawala nchi hii.

Hebu turudi tena kwa wale wanadungu walionishambulia wakisema kuwa kama walivyo Waislamu wengine mimi pia nimezoea kulalamika tu.

Kuna jambo moja ambalo lazima Waislamu walitafakari kuwa hakika jamii ya Kikristo huwa tayar i kuutumikia Ukristo wao kwa hali na mali. Ndugu yangu mmoja Mkristo ananiambia kwamba katika lile kanisa la Lutheran lililopo Tangi Bovu, huweza kukusanya mpaka shilingi milioni sita siku ya Jumapili. Hiyo ni ngwe ambayo Waislamu hawawezi kuikata. Hakika ziko sababu.

Lakini pia i tambulike kuwa maendeleo yote haya wanatutambia waKristo ni misaada kutoka kwa ndugu zao nje ya nchi na serikali. Kanisa Katoliki likiwa mfano linajulikana kuwa tajiri sana takriban kushinda makanisa mengine yote. Walokole walio Marekani wako tayari kutumia kiasi chochote cha mapesa kujaribu kuuwa Uislamu.

Nimewahi kuhakikishiwa mara mbili na viongozi wawili wa makanisa tofauti kuwa mara nyingi kazi za maendeleo

kama vile ujenzi wa shule na kadhalika, miradi hiyo husimamiwa na waumini kutoka nje ya nchi. Yaani Wazungu.

Suala hapa analoweza kujiuliza Muislamu ni kiasi gani mashirika ya Kiislamu yaliyo nje ya nchi hii yako tayari kuwasaidia Waislamu wa Tanzania kupambana na dhoruba ya Mfumo Kristo unaowaathiri sana Waislamu wa Tanzania.

Bado turudi kwa hawa waheshimiwa walionipa ‘lift’ na jinsi walivyowakosoa Waislamu wenzao, ati kazi yao ni kulalamika tu. Haya ni pamoja na jitihada yote wanayoifanya Waislamu leo kujaribu kujenga shule zao nyingi nchini.

J a m b o m o j a a m b a l o niliwakumbusha na ambalo hawakunipa jibu ni kuwa, wote hao ni wanachama wa chama cha wanataaluma wa Kiislamu Tanzania (TAMPRO). Niliwauliza lini walihudhuria kikao cha chombo hicho muhimu kinachojikita kwa ari zote kutafuta maendeleo ya Waislamu.

Mimi nafahamu kuwa hata pale palipoitishwa mkutano w a k u c h a g u a v i o n g o z i wapya, hawa wanadugu hawakuhudhuria.

Kweli wanaweza kuwa na haki ya kunikosoa mimi na Waislamu wengine kiasi kile?

Inawatangazia Waislamu wote Kuwa Imeandaa Safari ya Hijja Mwaka 2013 Sawa na Mwaka 1434 Hijria kwa Dola US$ 3550 tu.Umra kwa Mwezi wa Ramadhani itakuwa ni Dola US$ 1995 Fomu zinapatikana katika ofisi zifuatazo:-1. Ofisi ya Ahlul Daawa Dar es salaam Mtaa wa Dosi na Mkadini Nyumba Namba 26 Mkabala na Showroom ya Magari Tel 0713 730 444, au 0773 804101 au 0785 930444 na 0773 930444.2. Ofisi ya Ahlul Daawa Zanzibar Rahaleo Tel 0777 484982 au 0777 413 987.3. Abubakar Maulana wa Markaz Kiwalani Dar es salaam 0784 4538384. Abdallah Salehe Mazrui ( HOKO) Dar es salaam 0715 724 4445. Salim Is-haq Dar es salaam 0754 286010 au 0774 7861016. Dukani kwa Abdala Hafidh Mazrui wete pemba 0777 482 6657. Dukani kwa Mohamed Hafidh Mazrui Mkoani Pemba 0777 4569118. Sheikh Daudi khamis sheha 0777 6796929. Maalim Seif Humoud Hamed Kijichi Zanzibar 0777 417736Wahi kulipia. Ofisi ya Ahlul Daawa Dar es salaam 0713 730 444 au 0773 804101 au 0785 930444.Ofisi ya Ahlul Daawa Zanzibar Rahaleo 0777 484982 au 0777 413 987.Maalim Seif Humoud Hamed Kijichi Zanzibar 0777 417736 Sheikh Salim Mohamed Salim 0774 412974 au Kupitia ACCOUNT NAMBA 048101000030 NBC

Tanbih:Atakae maliza Taratibu zote kuanzia sasa Mpaka 15 July 2013 atapata Punguzo la asilimia 16% atalipia $ Dola 2982 tu.Atakae maliza Taratibu zote kuanzia Tarehe 16-july Hadi Tarehe 15 Augost 2013 atapata Punguzo la Asilimia sita 6% atalipia Dola $3337 tu.Kutakuwa na umra ya utangulizi kabla ya Umra ya Hijja kwa atakae maliza kufanya hivyo.Atakae maliza taratibu zote mwanzo ndie atakae shughulikiwa mwanzo.Ukilipia kwa njia ya Account kwanza piga simu 0774 412975. Kumbuka Kikundi cha Ahlul Daawa Kwa Bei nafuu kuliko wote na Huduma bora Kuliko wengi.

Nyote mnakaribishwa

Ahlul Daawa Hajj And Travel Agency

Page 9: ANNUUR 1064

9 AN-NUURJAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 29 - APRILI 4, 2013Makala

Katiba mpya itoe mapumziko Ijumaa Inatoka Uk. 5

Udhaifu gani huu wa kiimani? Mbona ha tumuoni Sp ika Jumapili akiendesha Bunge? Je, ndugu Wabunge mmeridhika kuchelewa kufika msikitini na kuwakuta malaika weshafunga vitabu vyao? Mnataka thawabu sifuri kwa Mungu ilimuradi Spika anawapa posho? Na siku ya kutoka roho mtamwabia Malaika wa kutoa roho asubiri ruhusa ya Mheshimiwa Spika?

Mara nyingi ukizungumzia jambo hili la kutaka kuifanya Ijumaa iwe mapumziko watu wengi sana, wakiwamo Waislamu pia, wanadhani kufanya hivyo kutaifanya nchi yetu ionekane kama nchi ya Kiislamu. La hasha!

Duniani nchi ya Kiislamu zaidi ya Saudia na labda Iran nadhani hakuna. Nchi zote zile za Arabuni kama vile za Falme za Kiarabu (Sharjah, Dubai na Abudhabi… UAE yote), Misri, Oman, Morocco, Sudan n.k, hawafanyi kazi siku ya Ijumaa. Hii ni kwa sababu ya utukufu tu wa siku yenyewe na kwamba raia wa nchi hizo ni Waislamu. Hakuna hata moja ya nchi hizo mwizi hukatwa mkono au mzinifu huuawa kwa mawe.

Hivyo wakati huu tukielekea kwenye kutengeneza katiba mpya, ni muhimu kuti l ia maanani jambo hili maana leo hii idadi ya Waislamu Tanzania imeongezeka sana kuliko wenzetu Wakristo ambao mfumo uliopo tuliourithi kwa wakoloni

unawapendelea. Kama mkoloni alikuwa Muanglikana aliyetutaka t u m u h e s h i m u y e y e k w a kupumzika Jumapili kwa mujibu wa dini yake, leo kaondoka kwa nini tusibadilike?

Pamoja na kuwaomba sana wajumbe wa Tume ya Warioba kulitazama hili kwa mtizamo chanya (positive) na kutafuta njia ya kuwafanya Waislamu wa Tanzania wawe na haki ya kuabudu katika nchi yao, niwaombe pia ndugu zetu wa Zanzibar (zaidi ya asilimia 98% ya watu wake ni Waislamu) watangaze tu kwa Tamko la Rais (Presidential Decree) kuwa Ijumaa ni siku ya mapumziko. Kumtii na kumfurahisha Mungu ni bora zaidi kwao kuliko kuheshimu na kuhofia mambo ya kidunia kama kweli ni watu wenye kutafakari.

H i v i k w e l i — e n y i Wazanzibari— mmeridhika kupata thawabu mfano wa yai la kuku au sifuri badala ya kupata thawabu za ngamia kwa jambo ambalo mnaweza kulitekeleza? Au mnadhani Mungu na Mtume wake hawasemi kweli kwamba kuna malipo makubwa ya Ijumaa?

Zanzibar kimsingi wana mambo ya Muungano na yale mahsusi ya Kizanzibari, sidhani kama watakuwa wanamkwaza mtu yeyote kama hawatafanya kazi Ijumaa. Hii ni kama vile ambavyo wamejitangazia kuwa shule zote ziwe zimefungwa unapoanza Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ; na kula

hadharani mwezi wa Ramadhani u n a f u n g w a j e l a m p a k a Ramadhani nyengine.

Kwa tamko la Serikali tu, Visiwani, Elimu ya msingi Zanzibar imekuwa Form III badala ya Std 7 kama ilivyo Tanzania Bara; na kwamba elimu yote pamoja na gharama za vitabu ni jukumu la Serikali ya Mapinduzi— huku Bara siyo hivyo.

Wa z a n z i b a r i m t a k u w a mmeutukuza na kuupandisha chati Uislamu kama leo hii mtatoa tamko hili ambalo halihitaji nyinyi kumsubiri Jaji Warioba kutangaza. Huku kwetu si rahisi kusikilizwa. Maana pamoja na kwamba ni haki yetu, tutaambiwa, kama tulivyoambiwa katika Kadhi na OIC; upande wa pili hawataki!

Wazanzibari msisubiri katiba ya Warioba; yenu ya sasa inatosha kutoa tamko hilo haraka. Kwa kumsubiri Jaji Warioba, punde hivi mtakuja kulishwa nyamafu au hata nguruwe huku mkiona. Jamaa sasa wanadai na wao wawe na haki ya kuchinja na nyama iuzwe mabuchani kwa kila mtu.

Wazanzibari mkiweza kufanya hili, la Ijumaa kuwa sikukuu, basi mtakuwa mmetufungulia njia na sisi kwa kupata pa kuanzia kutokana na kigezo chenu. Si la Muungano hili; Mungu Muumba ndiye aliyetutaka kutekeleza ibada ya Ijumaa. Visingizio vya ruhusa kazini havitomridhisha Mungu.

Wapi na wapi nyinyi na

sikukuu za Boxing day, Easter Monday (Pasaka) na Good Friday (Ijumaa kuu) ambazo hata Marekani hazisherehekewi Kiserikali? Mkiwa idadi kama hiyo hamwoni kama ni bora kwenu kuishi Kiislamu zaidi?

“Enyi mlioamini! Ikiadhiniwa Sala ya Siku ya I jumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu na wacheni biashara…”.(Suratul Jumu’a :9)

“Mwenye kuacha kusali sala ya Ijumaa, Ijumaa tatu (mfululizo), Mwenyezi Mungu hupiga muhuri ndani ya moyo wake”.

(Imehadithiwa na Abu Daud na Al Tirmidhy na Al Nissaai).

Na amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu:

“Niliazimia nimuamrishe mtu asalishe, kisha niende nikawachomee moto nyumba zao watu wasiokwenda kusali Sala ya Ijumaa”. (Imepokewa na Muslim)

K w a d h a t i k a b i s a tunamwomba Mungu muweza wa yote awazindue Wajumbe wa Tume ya Warioba wafikie kile kinachoitwa ‘win-win situation’ kwa kutupatia Ijumaa mapumziko. Muda wa kazi utakaopotea Ijumaa unaweza kufidiwa kiaina kwa kubadili saa za kuingia na kutoka kazini siku za kawaida.

Kama ikishindikana, basi sote tutahamia Zanzibar, kama Zanzibar watatekeleza hili kwa kutaraji radhi za Allah,

ili tukatekeleze ibada zetu kwa nafasi huko kama Mtume a l ivyowape leka waumin i Abbysinia (Ethiopia) baada ya kukumbana na vikwazo vingi kwao Makka.

Mfalme wa Ethiopia (Najash) al iwapa hifadhi na uhuru mkubwa wa kuabudu mwenyewe akiwa bado ni Mkristo, ingawa alisilimu baadaye.

Tutahamia huko tukafanye ibada sahihi kama alivyofanya Mtume na maswahaba zake walipohama kutoka Makka kwenda Madinna, si kwa jengine, bali ni kwa kutafuta wepesi wa kumwabudu Allah ambako mji wa Madinna ulikuwa unatoa.

Wa z a n z i b a r i m t a k u w a M a a n s w a r i ; m t u p o k e e Muha j i r i na ku toka Ba ra t u j e t u m w a b u d u A l l a h kingamiangamia!

Tu tahamia huko kama baadhi ya watu wa Uingereza w a l i v y o h a m i a M a r e k a n i katika karne ya 16 ya kipindi kile cha Great Awakening na Reconnaisance (uamsho mkubwa), kwa kumkimbia King George aliyekuwa akiwafanyia uka t i l i pa le wa l ipokuwa hawakubaliani naye alipoanzisha Kanisa lake la Anglikana na kujipa mwenyewe ukuu (self-imposed) wa kanisa hilo. Kwa kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu siku ya ‘Ijumaa ya ufufuo’(Yaumu Saah) bora ya hayo!

(Simu: 0715 808 864/0784 808 864

e-mail:[email protected])

Tuvunjilie kwa mbali ‘mfumo Kristo’ ndio tutakuwa salama

Inatoka Uk. 6

kubaguana kwa imani za kidini bila ya kujali uwezo na maarifa ya kitaaluma tutaipelekaje ile Satellite yetu kwenye Orbit miaka ishirini ijayo?

Mwaka 1994 kundi kubwa la Maprofesa wa Kirusi walifanya ziara maalumu nchini Marekani, ziara hiyo ilikuwa na malengo ya kuanzisha ushirikiano wa kielimu katika ngazi ya vyuo vikuu wa nchi hizo mbili. Walipokuwa nchini Marekani walipata bahati ya kuongea na wanafunzi mbali mbali wa vyuo vikuu vya nchi hiyo, na idadi ya wanafunzi wengi waliopata fursa ya kuongea nao kwamba wanapendelea masomo gani zaidi, wengi wao walidai wanapenda sana hesabu! Maprofesa wa Kirusi wakashangaa kuona kwamba kila mtu anapenda hesabu, kitu ambacho siyo cha kawaida kwa wanafunzi wengi duniani! Walipowaomba

walete vitabu na madaftari ya hesabu wanazofanya h u k o c h u o n i m w a o ; Maprofesa wa Kirusi walikuta kwamba hesabu wanazosoma wanafunzi wa vyuo vikuu vya Marekani ni hesabu ambazo kule Urusi wanasoma wanafunzi wa shule za sekondari, hivyo wakawa wamepata jibu ni kwanini kila mtu anapenda kusoma hesabu chuo kikuu! Baada ya wiki moja wakapewa fursa ya kuwapiga msasa wa hesabu darasani vijana waliokuwa wanasema wanapenda sana hesabu; walipoanza kuwafundisha h e s a b u w a n a z o s o m a wenzao wa vyuo vikuu vya kule Urusi wanafunzi wote walikimbia darasa na kusema hawataki tena kusoma hesabu, wakidai

k u m b e k u n a h e s a b u ngumu kiasi hicho! Hapa nilitaka tu nikuthibitishie

ni namna gani serikali ya Marekani inaona umuhimu wa kucheza Green Card kila mwaka na kuingiza w a t u w a p a t a o e l f u hamsini (50,000) toka kila kona ya dunia, kwa vile wasipofanya hivyo huko mbele waendako uchumi

wa Marekani utabuma.Tukitaka kutatua tatizo la

udini kiukweki hapa nchini ili nchi isije siku moja ingia kwenye vurugu na hata vita vya wenyewe kwa wenyewe, tuvunjilie kwa mbali udini ulioasisiwa na kujengwa na Mwalimu Nyerere!

Plot Hatua Eneo Mraba Bei (Tsh) Awamu 1. Awamu ya 2 Awamu ya 31 50 x 50 1341 6,705,000 3,000,000 2,000,000 170,50002 32 x 32 1136 5,680,000 3,000,000 2,000,000 160,0003 50 x 30 1470 7,350,000 4,000,000 2,000,000 575,0004 37 x 30 1115 5,575,000 3,000,000 2,000,000 575,0005 50 x 45 2259 11,295,000 6,000,000 3,000,000 2,295,0007 60 x 45 2423 12,115,000 7,000,000 3,000,000 2,115,0008 50 x 40 1984 9,920,000 5,000,000 3,000,000 1,920,0009 67 x 50 3564 17,820,000 9,000,000 5,000,000 3,820,00010 70 x 45 2842 14,210,000 7,000,000 4,000,000 3,210,00011 90 x 50 3780 18,900,000 10,000,000 5,000,000 3,890,00017 57 x 53 2423 12,115,000 7,000,000 3,000,000 2,115,000

Viwanja Vinauzwa – Vimepimwa Kongowe Kibaha TownshipREGISTERED PLAN NO. 70995 BLOCK H

Bei zote ni pamoja na hati milikiMalipo kwa Awamu tatu ( 3)

Km. 2 kutoka Barabara ya Morogoro kuelekea SogaKwa mawasiliano zaidi 0755/ 0715 090754

Page 10: ANNUUR 1064

10 AN-NUURJAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 29 - APRILI 4, 2013Mashairi/Barua/Tangazo

Ndugu Mhariri,Assalaam alaikum, “RAIS Jinping, aliyekuwa katika ziara ya siku mbili nchini na juzi usiku alisaini mikataba 17 inayohusu sekta za kilimo, afya na miundombinu.”

Miongoni mwa mikataba hiyo ni pamoja na: Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani ni kati ya miradi mikubwa iliyomo kwenye makubaliano hayo. Ujenzi wake utafanywa na Kampuni ya Merchants Holding ya China na utakwenda sanjari na u jenz i wa barabara inayounganisha bandari hiyo. Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, unatarajiwa

Jee Zanzibar imeambulia nini kufuatia ziara ya Rais Xi Jinpin?

kugharimu Dola za Marekani milioni 500 (Sh bilioni 800).

Pia katika bandari hiyo itaunganishwa na Reli ya Kati na ile ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) ili kurahisisha usafiri wa mizigo ndani na nje ya nchi. Mikataba mingine itahusiana na uboreshaji wa sekta ya viwanda, kilimo hasa kile cha tumbaku ikiwamo kuwatafutia soko wakulima kutoka Mikoa ya Tabora na Ruvuma ili waweze kuuza zao hilo katika soko la China. Msaada wa vifaa vya utangazaji vya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC). Mikopo yenye riba nafuu kwa Tanzania

katika nyanja ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Teknohama). Makabidhiano ya cheti cha JNICC, ujenzi wake umegharimu dola za Marekani milioni 29.7 (Sh. bilioni 47.5). Mikopo isiyo na riba halikadhalika Mkataba wa utekelezaji wa mpango wa ushirikiano katika utamaduni kati ya mwaka 2013-2016 na hati ya makubaliano ya kuanzishwa kwa kituo cha utamaduni cha China na Tanzania.

Naam hayo ndio wenzetu waliyonufaika nayo. Jee Zanzibar imenufaika na nini?

PASAKA SI YAKOKalamu i mkononi, namhimidi QudusuYu Khaliku wa insani, na vyote vilomuhusuWahidu ulimwenguni, uwenza kwake nukusuSi yako haikuhusu, ni haramu kushiriki.

Mushiriki wamebuni, kwa nadhari zao nusuEti mwana wa Manani, bin Mariamu YesuAso mwana kulikoni, wampachike nukusuSi yako, haikuhusu, ni Haramu kushiriki.

Pasaka wameibuni, kuwa fufuko la YesuNiwaombe kwa makini, Injili waidurusuUkweli watabaini, kamili tena si nusuSi yako, haikuhusu, ni Haramu kushiriki.

Ishna sita funguni, kumi na nane ni kisuKitowachoma mioyoni, hadi chini wajulusuNachombeza wasidhani, Matayo wakadurusuSi yako, haikuhusu, ni haramu kushiriki.

Yu awagiza mjini, wanafunzi wake YesuWende huko kubaini, Pasakayo kwa unasuHiyo ni Pasaka gani, waagizwayo na YesuSi yako haikuhusu, ni haramu kushiriki.

Ufufuko kulikoni, u wapi hapo wa YesuWagala nielezeni, msitafute ususuMuhali kuubaini, hauko kwenye nususuSi yako, haikuhusu, ni haramu kushiriki.

Zingatia dada Shani, nawe akhui Yunusu,Jitanibuni jamani, na jambo lisowahusuKushiriki Pasakani, ni kufuru kwa Qudusu,Si yako, haikuhusu, ni haramu kushiriki.

ABUU NYAMKOMOGIMWANZA.

Nabtadi kualifu, si tungo kuzibanangaJambo moja kuarifu, si mengi kutangatangaSi jingine mintarafu, hiyo siku ya wajingaSio siku ya wajinga, bali ya waongopaji.

Tarehe mosi tengefu, Aprili naipingaSi siku inosadifu, urongo wanoulongaLengolo ufisidifu, na kaumu kuivungaSio siku ya wajinga, bali ya waongopaji.

Imepachikwa wasifu, eti siku ya wajingaHadhiyo si yake kufu, mimi hilo ninapingaU mwingi udanganyifu, wala kamwe si ujingaSio siku ya wajinga, bali ya waongopaji.

Nadhifisha yako safu, kwa puya kutoziengaUsimuasi Latwifu, kwa longolongo kutungaUkweli wewe sanifu, kukomesha hili jangaSio siku ya wajinga, bali ya waongopaji.

Akhui nakuarifu, ndanimwe ‘sijejiungaEbu basi jikalifu, kutogeuka mshengaKuupamba upotofu, nini unachokilengaSio siku ya wajinga, bali ya waongopaji.

Kwa urongo kurudufu, Jahanamu tutatingaIkabu zake lufufu, shadidi zitatusongaHakuna ndanimwe ufu, wala uhai wa angaSio siku ya wajinga, bali ya waongopaji.

Haya shime dada Afu, nawe akhui MagangaTudumishe utiifu, kwa ALLAH si kwa wajingaTujenge usadikifu, kweli kutoibanangaSio siku ya wajinga, bali ya waongopaji.

Tuache ukengeufu, wa mambo kuyabananga,Ukweli tuusharifu, akhera kwetu ni kinga,Kaditama kualifu, ABUU natia nanga,Sio siku ya wajinga, bali ya waongopaji.

ABUU NYAMKOMOGIMWANZA.

SIKU YA WAJINGA

Page 11: ANNUUR 1064

11 AN-NUURJAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 29 - APRILI 4, 2013Makala

Mafunzo ya uongozi ndani ya Qur’an Inatoka Uk. 4

Uongoz i n i ku fanya kazi pamoja kwa sababu viongozi peke yao, hawawezi kufanikisha lolote bila ya wafuasi wao (na bila shaka msaada wa Mwenyez i Mungu). Baada ya kuwaambia kile alichopewa na Mwenyezi Mungu ni bora zaidi kuliko kile wanachoweza kumpa, Dhul Qarnayn akawaambia kwamba atawasaidia tu iwapo nao watamsaidia kazi hiyo kwa kushughulika pamoja kama kundi.

Kitendo hiki kinafanya mambo matatu ya msingi, ambayo v iongozi bora hufanya katika kukamilisha yale waliyopanga. Kwanza, kuwaomba watu wamsaidie, inawapa watu wale heshima kubwa na kuwafanya wajione ni washirika katika kutatua tatizo. Pili, inawafanya kuwa wadau katika mafanikio ya ufumbuzi utakaopatikana. Na tatu, inawafanya wawajibike kikamilifu katika kulinda na kudumisha ufumbuzi uliopatikana kwa kuwa nao walishiriki kuutafuta. Ni muhimu sana kuzingatia kwamba Dhul Qarnayan a l i w a o m b a w a t u w a l e wamsaidie kile walichokuwa nacho, ambacho kilikuwa ni nguvu zao.

“Nileteeni vipande vya chuma” Hata alipoijaza (kwa hicho chuma) nafasi iliyo katikati ya milima miwili, alisema: “Pulizeni (moto)”, mpaka alipokifanya (kile chuma) kuwa (kama) moto, alisema: “Nileteeni shaba iliyoyeyuka niimwage juu yake (hicho chuma)”. (Qur-18:96).

D h u l Q a r n a y n p i a anaonyesha tabia nyingine ya uongozi wake bora na uwezo mkubwa alionao wa kukamilisha mambo, kwa kuweka mchakato ulio wazi na kuufanyia kazi hatua kwa hatua, tena kwa mpangilio maalumu. Hivi ndivyo anavyofanya:

Kwanza, anawapa habari watu kuhusu kazi inayopaswa kufanyika na kuwaandaa kwa kazi hiyo. Pili, anatafuta dhamira yao (kujitoa kwao) kwa kazi hiyo na anawaambia kile anachoweza kukamilisha kwa msaada wao. Tatu, anakamilisha awamu ya kwanza ya kazi kwa kuwaagiza walete vipande vya chuma vitakavyowekwa katikati ya milima. Nne, anawasha moto na kuwaomba kuupuliza. Tano, anakamilisha hatua

inayofuatia ya kazi, kwa kuwaagiza kuleta shaba iliyoyeyuka na kuimwaga juu ya chuma cha moto.

Ukuta umekamilika sasa, kwa kutumia elimu yake na busara, pamoja na kufanyakazi bega kwa bega na watu wake, kwa kutumia nguvu zao na dhamira waliyonayo. Zingatia aya hapo juu ambapo Dhul Qarnayn anaonyesha kwamba kiongozi bora pia ni mfuasi mzuri: Anawataka watu wafuate maelekezo yake, lakini na yeye mwenyewe anashiriki kikamilifu katika kutekeleza maelekezo yale.

Muhimu zaidi, anaonyesha njia. Kiongozi anakuwa k i o n g o z i k w e l i p a l e anapoonyesha njia kwa kufanya kazi ngumu zaidi au yenye changamoto kubwa. Katika aya, tunaona Dhul Qarnayn mwenyewe ndiye aliyebeba jukumu zito na la hatari zaidi la kumwaga shaba iliyoyeyuka kwenye vipande vya chuma cha moto. Tunaweza kuiga hatua zote alizofuata Dhul Qarnayn katika utendaji kazi wetu wa kila siku.

Ni muhimu sana kuzingatia h a p a k w a m b a w a t u wanaozungumzwa katika kisa hiki cha Dhul Qarnayn, walikuwa na rasi l imali kama vile chuma na shaba, lakini hawakuwa na elimu wala ujuzi wa kuzitumia. Hii inatueleza kwamba tuna wajibu wa kujifunza jinsi ya kutumia rasilimali zote tulizojaaliwa na Mwenyezi Mungu.

Kwa hiyo maendeleo ya Sayansi na Teknolojia, na nyanja zingine za elimu, a m b a z o z i n a t u s a i d i a kunufaika na rasilimali zetu ni wajibu wa Kiislamu kwa jamii za Waislamu.

Tumeona kwamba kizuizi ambacho Dhul Qarnayn amekijenga kinaonyesha u b i n g w a w a k e k a t i k a teknolojia ya kisasa zaidi kuliko iliyokuwepo wakati wake. Kwa hiyo, elimu ya kisayansi na uhandisi ya Dhul Qarnayn ni sehemu ya nyenzo ambayo Mwenyezi Mungu amempa wakati alipommakinisha katika ardhi.

Kwa hiyo ni muhimu kwa Waislamu kuichukulia elimu ya ufundi (technical knowledge) kama zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ambayo inapaswa kukubal iwa, kuenziwa, kupaliliwa, kuhamasishwa, kuendelezwa na kutumiwa katika maisha yao wenyewe

na kuwahudumia wengine. Tofauti kabisa na mitazamo

ya kijinga inayopandikizwa kwenye jamii za Waislamu na watu wabaya, kwamba haifai kusomea taaluma za Sayansi na Ufundi, eti kwa sababu wema waliotangulia hawakufanya hivyo! Huo kama siyo uchizi ni nini?

Ni jambo la wazi kabisa na lisilohitaji dalili kwamba rejea ya Qur’an kuhusu mradi huu mkubwa wa kihandisi u l ios imamiwa na Dhul Qarnayn inaonyesha kwamba ni jambo la Kiislamu kutatua matatizo ya binadamu kwa kutumia elimu ya ufundi na busara tuliyopewa na Mwenyezi Mungu:

“Basi (Yaajuju na Maajuju) hawakuweza kuukwea wala hawakuweza kuutoboa”. Akasema: “Hii ni rehema itokayo kwa Mola wangu ( A l h a m d u l i l l a h ) . N a itakapofika ahadi ya Mola wangu (ya kufika kiama), atauvunjavunja. Na ahadi

ya Mola wangu ni kweli tu” (Qur-18:97-98).

Vilevile, kama kiongozi bora, baada ya kukamilisha kazi yake - ya kujenga kuzuizi cha kuwadhibiti wavamizi wa kigeni, Dhul Qarnayn anakumbuka na kuwakumbusha watu wake kwamba mamlaka yote ni ya Mwenyezi Mungu. Anawaambia kwamba kile alichokamilisha ni kutokana na rehema za Mwenyezi Mungu, na kama ilivyo kwa vitu vingine vyote, ukuta huu pia utasambaratika siku ya Kiama. Dhul Qarnayn anawatahadharisha watu wake kuhusu ukweli na uhakika wa siku ya Kiama.

K w a n a m n a f u l a n i , anaonyesha unyenyekevu kwamba hata ukuta ule imara alioujenga, si chochote mbele ya nguvu za Mwenyezi Mungu.

Ndugu zangu ka t ika imani, mafunzo haya ya uongozi kupitia kisa cha Dhul Qarnayn, yanaoana kwa

kiasi kikubwa na nadharia za kisasa kabisa za uongozi. Nitaziweka wazi, japo kwa muhtasari:

- Unapokasimu kazi yoyote ile, muwezeshe msaidizi wako kufanikiwa kwa kumpa nyenzo muhimu za kutenda kazi hiyo.(Hershey and Blanchard).

- Vi o n g o z i b o r a n i wa tumish i - v iongoz i . (Greenleaf).

- Viongozi hawakamilishi jambo peke yao, wanafanya kazi na timu ya wafuasi. (Dyadic research; team-building).

- Vi o n g o z i b o r a n i wafuasi wazuri. (Kouzes and Posner).

- V i o n g o z i n d i y o wanaoonyesha njia. (Kouzes and Posner).

- V i o n g o z i b o r a n i w a n y e n y e k e v u n a w a n a t a m b u a k w a m b a mafanikio yanatoka kwa M w e n y e z i M u n g u . (George).

Ofi si ya Munazzamat Al-Daawa Al- Islamiya ( MDI) iliyopo Mbezi Beach-Tangi Bovu jijini Dar es Salaam, inapenda kuwatangazia nafasi za masomo kwa wale wote wanaotaka kujiunga na Chuo Kikuu cha INTERNATIONAL UNIVERSITY OF AFRICA, Khartoum Sudan.

Kozi zinazotolewa ni; 1. Shahada ya kwanza katika Medicine, Pharmacy, Dentist, Nursing, Laboratory

Sciences, Engineering, Electronics&electrical Engineering, Computer Science, Pure Science, Applied

chemistry, Microbiology, Geology, Physics, Computer with Mathemtics.2. Shahadaya kwanza katika Law & Shari’a, Islamic studies, Economics, Administration,

Political Science, Education&Administration, Curriculum&Methods of Teaching, Arts (Mass communication, Arabic, Geography, History, and General Psychology).3. Diploma katika EducationFomu za maombi zinapatikana kwa Tsh. 10,000/= tu, kuanzia Tarehe 25 Machi- 6 Aprili,

2013 DAR ES SALAAM: katika ofisi ya Munazzamat iliopo Tangibovu- Mbezi Beach.

MWANZA: Msikiti wa Rufiji uliopo Mtaa wa Rufiji na ZANZIBAR: katika ofisi ya Munazzamat ( Kituo cha kusaidia mayatima) kilichopo eneo la Mpendae kwa mchina mwisho, mkabala na skuli ya Kijangwani, saa 3:00 asubuhi mpaka saa 7:00 mchana.

Mtihani (Written Interview) utafanyika tarehe 13/4/2013, saa 2:00 asubuhi, siku ya Jumamosi katika Ofi si za MDI Dar es Salaam, Mwanza: Shule ya Msingi Mbugani Mtaa wa Unguja na katika Chuo cha Kiislam Zanzibar.

Sifa za muombaji: Awe amemaliza Thanawiya au amemaliza kidato cha sita na amefaulu kwa kupata angalau

Division Three kidato cha Nne.

Kwa maelezo zaidi piga simu namba 0786 806662 au 0773 249015 au 0652 806662 au 0787 121283 au 0712 175985.

Kwa upande wa Zanzibar piga simu No. 0777415835 au 0715 415835.

Kwa upande wa Mwanza piga simu No. 0688 216644 au 0782 382434 au 0756 614916.

Mr. Khamisi M. Liyenike

K.n.y. Mkurugenzi, MDI, TZ

NAFASI ZA MASOMO SUDAN 2013/2014

Page 12: ANNUUR 1064

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

AN-NUUR12 JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA MACHI 29 - APRILI 4, 2013

Usikose nakala yako ya AN-NUUR kila

Ijumaa

A S K A R I w a Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam w a m e f a n i k i w a k u w a o n d o a w a f a n y a b i a s h a r a waliokuwa wakifanya shughuli zao katika makaburi ya Karume, Ilala j ij ini Dar es Salaam.

Kabla ya kuondolewa k a t i k a e n e o h i l o , wachuuzi hao walikuwa wakifanya biashara zao katika makaburi

WAKATI ajira za ualimu k w a Ta n z a n i a b a r a zikitolewa kwa mpango maalum, kwa upande wa Zanzibar ajira hizo zimekuwa giza tupu kwa wahitimu wa ualimu.

Kwa mara ya tatu sasa Wizara ya Elimu kupitia Wizara ya Utumishi wa Umma ya Zanzibar, imekuwa ikitangaza ajira hizo na kuwataka wahitimu wa vyuo vya ualimu kupeleka barua za maombi, lakini hadi leo hakuna mwalimu yoyote aliyeajiriwa.

Taarifa zinafahamisha kuwa mwezi Oktoba mwaka jana, Wizara ya Utumishi wa Umma ya Zanzibar iliwataka wahitumu hao kupeleka barua zao za maombi kwa ajili ya kupatiwa ajira katika shule zote za Zanzibar.

Majina hayo yalitangazwa kwenye mbao za matangazo za Wilaya, ambapo kwa mjini yalibandikwa Hoteli ya Bwawani na Magharibi yalikuwa wilaya ya Mwera.

Imeelezwa kuwa Desemba 2012, Wizara hiyo iliwataka wahitimu hao kupeleka tena barua za maombi na mwishoni mwa mwezi huo, Wizara ya Utumishi wa Umma ilitoa majina ya wahitimu wa ngazi za stashahada, shahada na cheti na kubandikwa tena katika Makao Makuu ya Wilaya visiwa vya Unguja na Pemba.

Hata hivyo inasikitisha kuona kuwa hadi leo hakuna muhitimu aliyeajiriwa.

K a t i k a h a l i iliyowashangaza wengi, wiki hii Wizara hiyo kwa mara nyingine tena, imetangaza kuwa wahitimu wa ualimu wapeleke tena maombi yao, jambo ambalo limezua gumzo kubwa kwa wahitimu hao kwa kuwa hawajui nini kusudio la usumbufu unaojitokeza.

K a t i k a t a n g a z o l i l i l o to l ew a w ik i h i i , wahitimu wanaotakiwa ni wale watakaoajiriwa katika

Ajira za ualimu Zanzibar kizungumkutiNa Mwandishi Wetu,

Z’barshule zote za Pemba na kwa upande wa Unguja ni Wilaya ya Kati, Kaskazini A na Kaskazini B na Kusini, huku Wilaya ya Magaharibi na Mjini wakiwa hawahusiki.

Hii itakuwa ni kwa mara ya tatu kutolewa tangazo hilo huku kukiwa hakujatolewa ajira yeyote kwa walioomba k u p i t i a m a t a n g a z o yaliyopita.

A i d h a m a j i n a h a y o ha i f ahamik i kwa n in i yanafutwa na kutakiwa wahi t imu hao kuomba tena nafasi hizo, huku kukiwa hakuna afisa yoyote aliyewahi kulizungumzia sakatata hilo, jambo ambalo limeleta sintofahamu kwa wahitimu, wanafunzi na jamii kwa ujumla.

Mmoja ya muhit imu ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, ambae amemaliza Chuo cha Ualimu cha Kiis lam Mazizini , amesema kuwa yeye hajui nini hatma ya ajira hizo kwani kila mara wanapeleka barua zao lakini hawaajiriwi na kinachosikitisha zaidi ni kwamba, kila tangazo jipya linalotoka masharti yanabadilika.

“Tunamuomba Waziri wa Elimu aingilie kati suala hili. Zaidi ya mara tatu tushapeleka barua na majina yanatoka, lakini mara tunasikia tupeleke barua nyengine tena kwa masharti mapya, hii inaturudisha nyuma wahitimu na kuona labda ni mbinu tu ya kisiasa ya kutupa matumaini”, alisema muhitimu huyo.

W a t u m b a l i m b a l i w a l i o z u n g u m z a n a mwandishi wa habari hizi wameitaka Wizara ya Ajira na Wizara ya Elimu kuwa makini na utendaji wao, kwani suala la ajira kwa walimu limeifanya wizara hizo kuonekana kutokuwa makini katika utendaji wao.

Wizara ya Elimu kwa sasa inashikiliwa na Mh. Juma Ali Juma Shamhuna, Mwakilishi wa Donge huku Wizara ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ikishilikiwa na Haji Omar Kheri, Mwakilishi wa Jimbo la Tumbatu.

Machinga waondolewa makaburi ya Karume

Na Mwandishi Wetu hayo yanayopakana n a m a j e n g o r a s m i ya kufanyia biashara ndogondogo maarufu k a m a M a c h i n g a Complex.

Salumu Said Salumu, mfanyabiashara wa mabegi katika jengo la Machinga complex, alisema kuwa wachuuzi hao walijikita katika makaburi hayo, bila kujali waliohifadhiwa katika makaburi hayo ni binadamu wenzao.

Alisema mara kwa m a r a w a m e k u w a

w a k i w a s h a u r i kuondoka eneo hilo, lakini walijibu kuwa wanaotaka waondoke, basi kwanza wafunge njia inayokatisha katika makaburi hayo ili watu wapite katika njia rasmi zilizopo sokoni hapo.

“Mgambo wamekuwa wakiwabembeleza kwa kujuana, sasa ni Polisi wa jiji tuangalie kasi yao kama watafaulu kuwaondoa wasirudi tena”, alisika akisema Sabiti Dulopio, mkazi wa jijini.

RAIS wa Zanzibar Dkt. Shein akiwa na Makamu wake wa kwanza Maalim Seif.