ANNUUR 1145e

17
ISSN 0856 - 3861 Na. 1145 DHULHIJJA , IJUMAA , OKTOBA 3-9, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu www.annuurpapers.co.tz UNAPOTAKA kupiga kura fikiria, wazia na pimia juu ya uzito wa mchoro wako mmoja tu wa kalamu utavyokuwa na athari kwa nchi yako, watu wako na watoto na wajukuu wako. Fumba macho, rudisha nyuma fikra zako, kumbuka wema na ihsani za waliokuzunguka, “BIBLIA yasema Irak ina pepo shujaa wa vita. Walipigana na malaika wa Mungu siku 21. Ilibidi Malaika Mkuu Mikaeli ashuke kuingilia kati. Rais Bush asoma Biblia kabla ya kutangaza vita.” Hivi sasa yaelekea Bush na makamanda wake wa kupigana vita dhidi ya ugaidi, ndio ‘Malaika Mkuu’ wa kuangamiza Waislamu. (Uk. 6) EID MUBARAK! Mhariri na Watendaji wa gazeti la AN-NUUR wanawatakia Waislamu wote Eid Mubarak njema. EID MUBARAK!!! KAULI ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa Katiba, Mh. Andrew Chenge, kuwa Mahakama ya Kadhi haistahili kuingia katika Rasimu ya Katiba, ni sawa na kuwaambia Waislamu kuwa Qur’ an ni kitabu kidogo. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Jopo la Masheikh na Wanazuoni Ni ‘Hapana’ kwa Rasimu  Asema kiongozi Bara za Kuu Baraza la Idd Kichangani Jumapili Shura ya Maimamu yajipanga Masheikh wapo Golgotha ni yale yale ya Constantino  Alisema kweli George W Bush ni ‘Crusa de’ Haishangazi leo kwa akina Sheikh Farid Eid Mubaraka Wajumbe... Bunge la Katiba kutoka Zanzibar Chenga twawala, lakini twafungw a Kura yako ‘Maangamizi Daima’ uliokuwa nao pamoja katika maisha yako na uwakirie khatma njema ya muda mrefu. Kumbuka jukumu lako kwa Mwenyenzi Mungu na kiria kama hicho ni kitendo cha mwisho cha maisha yako ili ukitie katika mizania nzuri ya maamuzi yako. (Uk. 7)  Amesema kw eli Mataka Qur’an imedhalilishwa Kamati ya Chenge imedharau Waislamu Wakristo wanaweza kuhukumiwa na Pilato Na Bakari Mwakangwale Inaendelea Uk. 2 wa Kiislamu Tanzania, Sheikh Hamisi Mataka, akiongea katika kipindi cha Baraza la Katiba, kinachorushwa na Radio MUM ya Chuo Kikuu Cha Waislamu Morogoro. She ikh Mat aka akizungumzia kauli hiyo ya Mh. Chenge, alisema kwamba unaposema Mahakama ya Kadhi ni Mahakama ndogo maana yake unawaambia SHEIKH Farid Hadd. SHEIKH Ayman al-Zawahiri. MWENYEKITI wa Bunge la Katiba, Samwel Sia (kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya uandishi Bunge la Katiba, Mtemi Andrew Chenge.

Transcript of ANNUUR 1145e

  • ISSN 0856 - 3861 Na. 1145 DHULHIJJA, IJUMAA , OKTOBA 3-9, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

    Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz

    UNAPOTAKA kupiga kura fikiria, wazia na pimia juu ya uzito wa mchoro wako mmoja tu wa kalamu utavyokuwa na athari kwa nchi yako, watu wako na watoto na wajukuu wako.

    Fumba macho, rudisha n y u m a f i k r a z a k o , kumbuka wema na ihsani za waliokuzunguka,

    B I B L I A ya s e m a I r a k ina pepo shujaa wa vita. Walipigana na malaika wa Mungu siku 21. Ilibidi Malaika Mkuu Mikaeli ashuke kuingilia kati. Rais Bush asoma Biblia kabla ya kutangaza vita.

    Hivi sasa yaelekea Bush na makamanda wake wa kupigana vita dhidi ya ugaidi, ndio Malaika Mkuu wa kuangamiza Waislamu. (Uk. 6)

    EID MUBARAK!Mhariri na Watendaji wa gazeti la AN-NUUR wanawatakia Waislamu wote Eid Mubarak njema.

    EID MUBARAK!!!

    KAULI ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa Katiba, Mh. Andrew Chenge, kuwa Mahakama ya K a d h i h a i s t a h i l i kuingia katika Rasimu ya Katiba, ni sawa na kuwaambia Waislamu kuwa Qur an ni kitabu kidogo.

    Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Jopo la Masheikh na Wanazuoni

    Ni Hapana kwa Rasimu Asema kiongozi Baraza KuuBaraza la Idd Kichangani Jumapili Shura ya Maimamu yajipanga

    Masheikh wapo Golgothani yale yale ya Constantino

    Alisema kweli George W Bush ni CrusadeHaishangazi leo kwa akina Sheikh Farid

    Eid Mubaraka Wajumbe...Bunge la Katiba kutoka ZanzibarChenga twawala, lakini twafungwaKura yako Maangamizi Daima

    uliokuwa nao pamoja katika maisha yako na uwafikirie khatma njema ya muda mrefu.

    Kumbuka jukumu lako kwa Mwenyenzi Mungu na fikiria kama hicho ni kitendo cha mwisho cha maisha yako ili ukitie katika mizania nzuri ya maamuzi yako. (Uk. 7)

    Amesema kweli MatakaQuran imedhalilishwa

    Kamati ya Chenge imedharau WaislamuWakristo wanaweza kuhukumiwa na Pilato

    Na Bakari Mwakangwale

    Inaendelea Uk. 2

    wa Kiislamu Tanzania, Sheikh Hamisi Mataka, akiongea katika kipindi cha Baraza la Katiba, kinachorushwa na Radio MUM ya Chuo Kikuu Cha Waislamu Morogoro.

    S h e i k h M a t a k a akizungumzia kauli hiyo ya Mh. Chenge, alisema k wa m b a u n a p o s e m a Mahakama ya Kadhi n i M a h a k a m a n d o g o maana yake unawaambia

    SHEIKH Farid Hadd.SHEIKH Ayman al-Zawahiri.

    MWENYEKITI wa Bunge la Katiba, Samwel Sitta (kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya uandishi Bunge la Katiba, Mtemi Andrew Chenge.

  • 2 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 2014AN-NUUR

    S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.

    www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected] zetu zipo: Manzese Tip Top

    Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

    Tahariri/Habari

    AWALI ya yote tuchukue fursa hi i kuwatakia Wa i s l a m u w o t e E i d Mubarak. Lakini pia tuwatakie kila la kheri mahujaji wetu waliopo Makka, wakitekeleza ibada ya Hija, ambayo ni nguzo ya tano ya Uislamu.

    Idd el Hajj ni sikukuu ya Ki is lamu ambayo h u s h e r e h e k e wa k i l a mwaka katika siku ya kumi ya mwezi wa Dhul Hijjah, mwezi ambao ni wa Hajj.

    Kwa Waislamu sikukuu hii hujulikana zaidi kama Idd-a l -Adhha , yaan i s ikukuu ya kuchin ja au Idd-al-Kabir, yaani sikukuu kubwa.

    Idd Hajj husheherekewa kama kumbukumbu ya sadaka ya Ibrahimu, ambaye alipewa mtihani na Mwenyezi Mungu na kuamriwa kumchinja mwanaye kipenzi Ismail. Mtihani huu ulilenga kupima imani ya Nabii Ibrahim na mwanaye Ismai l , ambaye naye Mwenyezi Mungu alimpa Unabii.

    Nabii Ibrahim aliridhia a m r i y a A l l a h w a kumchinja mwanaye, naye Ismail akaridhia baba yake kutekeleza maamrisho aliyopewa na Mola wake. Lakini wakati Ibrahim anaanza kutekeleza amri hiyo, alisikia sauti ya takbira.

    M w e n y e z i M u n g u alishashuhudia utii wa waja wake hawa, Malaika Jibril akamzuia Ibrahim asimchinje mwanaye na akampatia kondoo kutoka kwa Allah (sw) amchinje na kuwa sadaka badala ya mwanaye.

    Kwa kisa hiki, kimekuwa ni funzo kubwa la utii kwa Allah (sw) na ibada kubwa kwa Waislam. Hapo ndipo lililozaliwa somo la kuchinja katika Hija na kwenye sikukuu ya Eid el Haji.

    H i k m a y a k e n i kujikurubisha kwa Allah

    Eid Mubarak(SW) kama anavyosema katika kauli yake: Basi swali na uchinje kwa ajili ya Mola wako. (Al-Kawthar: 2)

    Leo tuchukue fursa hii kukumbushana na kuelekezana Waislamu juu ya umuhimu wa kutekelezwa ibada ya kuchinja katika Eid el Udhhiya.

    Kama tunavyofahamu, sherehe ya Idd huanza na swala ya Eid Msikitini au eneo la wazi (uwanjani). Baada tu ya swala ya Eid kubwa, Waislamu wenye uwezo wanapaswa kuchinja mnyama wa sadaka siku hiyo.

    Mafundisho yanasisitiza kwamba kuchinja kondoo n i b o r a z a i d i l a k i n i a k i k o s e k a n a , m b u z i , n g ' o m b e n g a m i a n a mnyama mwingine halali kuliwa anaweza kufaa katika kutekeleza ibada hii.

    Tusisahau kuwa sehemu ya nyama ya sadaka hii h u g a w i w a m a s i k i n i wasio na uwezo, majirani na marafiki na nyingine hutumiwa katika karamu ya familia.

    Kuchinja ni moja ya ibada za Kiislamu ambayo inatukumbusha Tawhid ya Allah (SW) na baraka zake kwetu, pamoja na kutupa mafunzo ya utiifu wa baba yetu Ibrahim kwa Mola wake na kumpwekesha Allah. Hivyo ibada ya k u c h i n j a n i m u h i m u sana kwa Muislamu na inatupasa tuizingatie kwa makini na kuitekeleza.

    Nyama zao hazimfikii Allah wala damu zao, lakini unamfikia uchaji Allah wenu. Namna hivi tumewadhalilisha kwenu i l i mumtukuze Al lah kwa alivyokuongoeni. Na wabashirie wafanyao mema. (Al-Hajj: 37).

    Na kafara ni kuchinja kwa kujikurubisha kwa Allah (SW). Kuihuisha Sunnah mojawapo ya Tawhid, wakati Allah alipompa wahyi Ibrahim

    (as) amchinje mwanawe Ismail. Kisha Allah (SW) akampa fidia ya kondoo, akamchinja badala yake. Al lah (SW) anasema: Basi tukamtolea fidia kwa dhabihu mtukufu (Aswaaffaat: 107).

    M u i s l a m k u w e z a kuwalisha nyama familia yake pamoja Na jamaa zake siku ya Eid na kueneza rahma miongoni mwa masikini na mafakiri.

    Kutoa shukurani kwa Allah (SW) kutujaalia kuwa na wanyama wafugwao k a m a a n a v y o s e m a : Na ngamia wa sadaka tumekufanyieni kuwa ni kudhihirisha matukuzo k wa A l l a h ; k wa h a o mna kheri nyingi. Basi litajeni jina la Allah juu yao wanaposimama kwa safu. Na waangukapo ubavu kuleni katika hao na walisheni waliokinai n a w a n a o l a z i m i k a k u o m b a . N d i o k a m a hivi tumewafanya hawa wanyama dhalili kwenu ili mpate kushukuru.

    Nyama zao hazimfikii Allah wala damu zao, lakini unamfikia uchaji Allah wenu. Namna hii tumewadhalilisha kwenu i l i mumtukuze Al lah kwa alivyokuongoeni.

    Na wabashirie wafanyao mema. (Al-Hajj: 36-37).

    Hata hivyo tuwe na tahadhari kuwa wanyama w a n a o p e n d e k e z w a kuchinjwa, lazima wawe wanono na wenye afya, wasiokuwa na maradhi au kilema au kasoro za kumfanya awe duni.

    N i v y e m a p i a t u k a k u m b u s h a n a n a m a p e m a k w a m b a kuchinja ni asubuhi ya siku ya Idd baada ya swala. Hairuhusiwi kuchinja kabla ya swala kama alivyosema Mtume (Saw) Kutoka kwa Anas (ra) kwamba, Mtume (Saw) amesema, Atakayechinja kabla ya swala atakuwa amejichinjia kwa ajili yake mwenyewe. Na Atakayechinja baada ya swala atakamilisha kafara (kichinjo) yake na atapata (atatekeleza) Sunna ya Waislam (Bukhari na Muslim).

    I n a p e n d e k e z w a M u i s l a m u k u c h i n j a m w e n y e w e , l a k i n i a k i m w a k i l i s h a m t u k u m c h i n j i a p i a inaruhusiwa. Hakuna hitilafu katika jambo hili baina ya Maulamaa.

    Mchinjaji anatakiwa kuigawa nyama aliyochinja k a t i k a s e h e m u t a t u .

    S e h e m u y a k w a n z a watatumia familia, sehemu ya pili itatolewa sadaka na sehemu ya tatu itagawiwa marafiki, majirani n.k. kama anavyosema Allah (Sw), Ili washuhudie manufaa yao na walitaje jina la Allah katika siku maalumu juu ya nyama hao aliowaruzuku. Basi kuleni katika hao na mlisheni mwenye shida aliye fakiri (Al-Hajj: 28).

    Pia inaruhusiwa pia kuigawa nyama yote sadaka. Inaruhusiwa pia kubakisha sehemu.

    A i d h a t u n a p e n d a kuwakumbusha Waislamu na kuwapa nasaha ya kufunga siku ya Arafah ya Dhul-Hijjah 1435 Inshaa-Allaah. Fadhila zake ni kufutiwa madhambi ya miaka miwili ; mwaka uliopita na unaofuatia.

    P i a t u n a k u m b u s h a kuwa katika siku ya Eid kubwa, ni vyema kila Muislamu akafunga kwa muda kuanzia asubuhi hadi baada ya swala. Inapomaliza swala ya Eid aendelee kula na kunywa na kusherehekea sikukuu yake. Itakuwa dhambi kuendelea kufunga baada ya swala.

    Eid Mubarak

    Amesema kweli MatakaInatoka Uk. 1

    Waislamu kuwa Quran yao ni kitabu kidogo jambo ambalo si sahihi.

    Sheikh Mataka alisema Mahakama ya Kadhi sio Mahakama ndogo kama anavyodhani Mh. Chenge, pengine na kamati yake kwani inapaswa ichukuliwe kama Mahakama maalumu na kwa mambo maalum ya kiimani.

    Mahakama ya Kadhi inahukumu kwa mujibu wa Qur an na Sunna, hivyo unaposema Mahakama ya Kadhi ni ndogo na Katiba haishughuliki na Mahakama ndogo huku ni kuwadharau Waislamu lakini ndani yake pia kuna namna ya kuidharau zaidi Qur an. Alisema Sheikh Mataka.

    Alisema, maj ibu ya Mh. Chenge, juu ya suala hilo ni jibu la kiufundi kwa Waislamu, kwani mtu akitaka kulikwepa jambo kiufundi atatumia ufundi katika jibu lake

    akitegemea kueleweka zaidi, lakini kinyume chake afahamu kuwa kwa jibu hilo ameidharau Qur an.

    K i l a s i k u j i b u l a kiufundi haliwi ni jibu halisi, bali ni jibu la kumtoa mtu katika mtengo fulani alionasa, maelezo ya Mh. Chenge, si maelezo sahihi kwa umma wa Kiislamu. Alisema Sheikh Mataka.

    Alisema, hoja ya Mh. Chenge, haina mantiki kwani ni hoja dhaifu katika jambo zito kama hili linalo gusa imani ya moja ya kundi kubwa katika umma wa Watanzania, ambao nao ni miongoni mwa watumiaji wa katiba hiyo.

    Shkh. Mataka, alisema kwa kuwa suala hi lo ni hitajio la kiimani na kiibada hivyo Waislamu w a t a e n d e l e a k u i d a i Mahakama ya Kadhi na ana imani kwamba siku moja watafanikiwa kama ilivyo Kenya, Uganda na nchi nyingine jirani na Tanzania zenye Mahakama za Kadhi zinazotambulika

    Kikatiba.Mataka alisema huko

    nyuma wakati Waislamu w a n a d a i u w e p o w a Mahakama hiyo walielezwa kuwa haiwezekani kwa sababu Katiba iliyopo haiitambui, cha ajabu akasema katika muda huu wa kutengeneza Katiba mpya zinakuja sababu na hoja zisizo na mantiki tena kwa viongozi wenye heshima.

    Tanzania ingetaka kuangalia na kulimaliza suala la Ukadhi ingeangalia nchi jirani kwamba ni jambo ambalo l inawezekana kuingizwa katika Katiba. Mahakama ya Kadhi imetajwa katika katiba ya Kenya, na ibara ya nane katika Katiba ya Uganda, kwa nini wasiangalea mfano katika nchi hizo. Alisema na kuhoji Sheikh Mataka.

    K wa u p a n d e wa k e akichangia katika kipindi hicho, Bw. Magesa Japhet,

    Inatoka Uk. 1

  • 3 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 2014Habari

    Ni Hapana kwa Rasimu WAISLAMU hawatokuwa na kura ya NDIYO katika zoezi la kuipigia kura Rasimu ya Katiba iwapo maoni yao ya uwepo wa Mahakama ya Kadhi hayatoingizwa katika Katiba mpya.

    Mwishoni mwa wiki iliyopita, Mwenyeki t i wa Kamati ya Uandishi ya Bunge la Katiba, Mh. Endrew Chenge, aliwasilisha Rasimu ya mwisho ya Katiba, ambapo ilibainika kuwa maoni ya Waislamu juu ya Mahakama ya Kadhi hayajaingizwa katika Katiba inayopendekezwa.

    Rasimu hiyo ni ya mwisho katika mtiririko wa kupatikana Katiba mpya, ambapo katika hatua zote za awali za Rasimu, maoni ya Waislamu mengi, likiwemo pia la Mahakama ya Kadhi hayakuonekana.

    Kwa mujibu wa taratibu, kinachosubiriwa sasa ni Rasimu hiyo kurudi kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura jambo ambalo tayari Waislamu wameweka msimamo wa kuikataa rasimu hiyo kwa kupiga kura ya hapana.

    Akizungumza na An nuur, msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Rajabu Katimba, al isema kutokana na maamuzi hayo ya Bunge na kutiliwa mkazo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waislamu hawatoiunga mkono rasimu hiyo ya Katiba.

    Kwa hili hatuna kura ya ndiyo, tutakuwa na kura ya hapana na hili linaanza kufanyiwa kazi katika Baraza la Eid, (kesho kutwa) tutawaeleza Waislamu msimamo juu ya hatua hiyo ya Bunge na Serikali yake, tutawaeleza maoni yetu yamekataliwa na sisi tuikatae Rasimu hiyo katika kupiga kura. Alisema Katimba.

    Alisema, njia na mikakati iliyotumika kugomea Sensa ya watu na makazi baada ya Serikali kugoma kuingiza kipengele cha Dini ndizo zitakazotumika kuwaeleza Waislamu kupiga kura ya hapana.

    Katimba alisema kuanzia sasa Jumuiya na Tasisi za Kiislamu, zinaratibu hotuba za Ibada ya swala ya Ijumaa zitakazo kuwa na ujumbe mmoja, ambazo zitasomwa mfululizo kila Ijumaa, katika muda utakaopangwa zikielezea kupuuzwa kwa maoni ya Waislamu katika Katiba mpya.

    Alisema, uzuri wa bahati kauli na msimamo huo wa Bunge Maalum na Serikali, umekuja wakati Shura ya Maimamu, ikiwa katika vikao na Maimamu kutoka Mikoa mbalimbali nchini hivyo moja ya maazimio waliyo ondoka nayo (Maimamu) ni mikakati kuhusu Waislamu kupiga kura ya hapana.

    Wajumbe kutoka Mikoa yote iliyojumuishwa Kikanda kwa Tanzania bara na Visiwani, kazi itafanyika na ujumbe utafika tutakutana nao mitaani katika masanduku ya kura. Alisema Shkh. Katimba.

    Al isema, kat ika kupinga Rasimu hiyo ya Chenge, wataanza kusambaza vipeperushi na vitabu mbalimbali nchi nzima kama ilivyokuwa katika sakata la Sensa

    Na Bakari Mwakangwale

    na kazi itakayo anza katika Baraza hilo la Eid, ambalo litafanyika siku ya Jumapili (kesho kutwa) katika Msikiti wa Kichangani TIC Magomeni jijini Dar es Salaam, kuanzia majira ya saa nane mchana.

    Kat imba amesema, ik iwa wajumbe katika kamati ya uongozi wa Bunge hilo wamejiridhisha kuwa madai ya Waislamu kuhusu Mahakama ya Kadhi ni ya msingi, kwa nini wasubiri mpaka Januari mwakani.

    Akitoa tamko la Ser ikal i Bungeni baada ya maoni ya Waislamu kuhusu Mahakama ya Kadhi kutokuwemo katika Rasimu iliyowasilishwa na Mh. Andrwe Chenge, Waziri Mkuu Mzengo Pinda, alisema Januari mwakani Sheria ya Kiislamu sura ya 375 itafanyiwa marekebisho ili kutambua uamuzi wa Mahakama ya Kadhi, ikiwemo maeneo saba yanayolalamikiwa na Waislamu.

    Waziri Mkuu (Mh. Pinda) akisema kuwa itaboreshwa hapo baadae, anamaanisha kwamba Mahakama ya Kadhi sio jambo muhimu kwa mtazamo wao lakini kwetu sisi Waislamu ni muhimu sana lazima watambue hivyo na ni muda mrefu Waislamu wameonyesha umuhimu wa suala hili lakini wanapuuzwa. Alisema.

    Alisema, ukiyatafakari maelezo ya Waziri Mkuu Pinda, na maelezo ya Mh. Chenge, ni maelezo ambayo yanagongana na kuashiria lengo ni kuwatoa Waislamu katika msimamo wao au kuwafanya daraja la kupitishia mambo ya wengine.

    Shkh. Katimba, alisema kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa Rasimu ya Katiba ya Bunge hilo (Mh. Chenge) alieleza bayana kwamba kila kitu kilicho muhimu kimeingizwa katika Rasimu hiyo

    ya Katiba.Kwa hiyo Jumuiya na Tasisi

    za Kiislamu tunaona kuwa hili ni changa la macho, hamna chochote watakacho kipata Waislamu, kwani hizo zimekuwa ndio kauli zao kwani walianza katika ilani yao ya CCM ya uchaguzi waliahidi hivyo hivyo lakini hakuna utekelezaji, sasa sisi tunasema msimamo wetu upo pale pale, Hapana kwa Rasimu. Alisema.

    Jumamosi ya wiki iliyopita, Sheikh Hamid Jongo kutoka kundi la 201, anaewakilisha dini ya Kiislamu, aliomba mwongozo akionyesha wasiwasi wake kwamba huenda ubora wa Katiba mpya ukawa mashakani endapo maoni ya Waislamu kuhusu Mahakama ya Kadhi hayatoingizwa katika Katiba mpya.

    Sisi tulileta marekebisho yetu, Waislamu tunataka tujue yataingizwa au hayaingizwi kama hayaingizwi, basi (Waislamu) tunao msimamo wetu ambao pengine ule ubora wa katiba inayopendekezwa utabomokea hapa. Alisema Sheikh Jongo.

    Amesema kweli MatakaInatoka Uk.2

    aliwataka Wakristo wenzake kutotaka jambo ambalo kwao halipo wala dini yao haijaamuru kuhukumiana kwa mujibu wa Biblia.

    Tusione kwa kuwa Waislamu wanataka haki yao ya msingi ambayo imo katika kitabu chao (Qur an) na sisi ndio tuanze kujipenyeza kudai kitu ambacho hatunacho kiimani, kwa nini isifike mahali tukaungana nao kuitaka Serikali wapewe haki yao. Alisema Bw. Japheti.

    Bw. Japheti, aliyedai kuwa amefanya utafiti wa kina juu ya suala hilo na kuona halina tatizo kuingizwa katika Katiba ya nchi, akaitaka Serikali kuziruhusu Mahakama hizo kikatiba na kuzigharamikia hata kwa asilimia 75 tu, kama sio kwa asilimi mia moja.

    Al isema, haoni sababu kwa Ser ika l i kushindwa kuzigharamikia Mahakama hizo ikiwa ni huduma kwa sehemu ya raia wake, ili hali inatumia mabilioni ya pesa bila sababu za msingi.

    Alisema, kutokana na utafiti alioufanya, amebaini kuwa tatizo watu wengi husasani wa upande wa pili hawajaelimishwa na endapo wataelimishwa vizuri nini maana ya Mahakama ya Kadhi, hukumu yake na mipaka yake lingechukuliwa kuwa ni jambo la kawaida na ni haki ya Waislamu na hata uwepo wake Kikatiba hakuathiri imani ya watu wengine.

    Akizungumzia kauli ya Askofu Mapunda, aliyedai kuwa endapo Mahakama ya Kadhi itaingizwa katika Katiba basi, hata Wakristo nao watahitaji pia Mahakama yao ya Kikristo, alisema hakuna sababu ya kufanya hivyo kwani wao Wakristo Dini yao haina amri ya kuhukumiana Kikristo.

    Mimi kama Mkristo na msomaji mzuri wa Biblia nataka kuuthibitishia umma unaonisikiliza kwamba katika Biblia kunzia kitabu cha kwanza kinachoitwa Mwanzo na cha mwisho kinaitwa Ufunuo wa Yohana hakuna mahala popote ambapo sisi Wakristo katika imani yetu tumelazimishwa na Mungu ama panapozungumza Wakristo wanatakiwa kuwa na Mahakama zao. Alisema Bw. Japheti.

    Akifafanua Bw. Japheti, alisema kwamba hata hukumu ya Kristo (Yesu) pale msalabani hakuhumiwa na Kanisa au kwa sheria za Kikristo, bali alihukumiwa na kina Pilato (watawala) kwani alidai wakati ule (mtawala) ndiye aliyekuwa Jaji (mwamuzi).

    K w a h i y o K r i s t o h a k u h u k u m i w a k a t i k a M a h a k a m a ya K i k r i s t o , h a k u n a m a h a l a p o p o t e ambapo Wakristo wanatakiwa w a h u k u m i w e K i k r i s t o kama ambavyo Waislamu wanaelekezwa katika Qur an yao. Sisi (Wakristo) tunaweza kabisa tukahukumiwa na hizi Mahakama za Seriakali, wala

    dini ya Kikristo haizumgumzi c h o c h o t e v i p i M k r i s t o ahukumiwe Kikristo. Alisema Bw. Japheti.

    Kwa mana hiyo alisema, ukisoma kat ika Mathayo utakuta inasema Tiini mamlaka kwa kuwa hakuna mamlaka iliyowekwa yenyewe mamlaka zote zimewekwa na Mungu.

    Kiongozi huyo (Askofu Mapunda) nadhani alikuwa anajaribu kujenga hoja ili hii Mahakama ya Kadhi isiweze kuingizwa katika Katiba, lakini hakuna sababu yoyote ile ya msingi ya kuzuia Mahakama hiyo isiruhusiwe kikatiba ili Waislamu wakahukumiana kwa mujibu Quran yao inavyotaka. Alisema.

    Bw. Japheti, akitilia mkazo kua Wakristo hawana lazima ya kuhukumiana Kikristo, alitoa changamoto kwa kiongozi yoyote wa juu wa Kanisa hata kama ni Papa, ajitokeze kumthibitishia kwa maandiko kama Wakristo wanatakiwa kuwa na Mahakama zao zilizo amliwa na Mungu au Yesu kwa ajili ya kuhukumiana Kikristo, na endapo akijitokeza atakuwa tayar i kuwa mjakazi wa kiongozi huyo bila malipo kwa maisha yake yote yaliyobaki.

    Hili ni sawa na suala la kuchinja, kwani wenzetu kuchinja ni ibada lakini kwa Mkristo nichinje nisichinje hainiathiri, kwa nini tusimuachie yule ambaye kuchinja kwake ni ibada akafanya shughuli hiyo ili kujenga umoja na mshikamano wa Kitaifa. Alisema Bw. Japheti.

  • 4 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 2014Habari/Tangazo

    TAASISI ya Taqwa Orphans Trust Tanzania imepokea hundi yenye thamani ya dola za kimarekani 13,690 pamoja na nguo mpya za watoto kutoka kwa wahisani wao taasisi ya Qamer ya nchini Canada, kwa ajili ya sikukuu ya Idd el Hajj.

    Msaada huo ulitolewa katika hafla ya kuwakutanisha watoto hao yatima na wahisani wao kutoka nchini Canada, iliyofanyika katika ukumbi wa Al-Hilal jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita na umewalenga watoto yatima wanaoishi majumbani pamoja na walezi wao.

    Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Dk. Salha, wakati wa kupokea msaada huo alisema kuwa, jambo la kuwalea yatima ni la kila mtu na linalompendeza sana Mwenyezi Mungu, hivyo kila Muislamu anatakiwa kujitahidi kuchukua nafasi hiyo popote pale.

    Qamer Foundation imechukua dhamana ya kuwalea watoto 34 kati ya watoto 100 wanaolelewa na taasisi ya Taqwa, ikitoa mahitaji yao yote ya nyumbani, shule na madrasa pia.

    Akitoa maelezo ya taasisi hiyo na shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo, Dk. Salha alisema kazi yao kubwa ni kuhakikisha watoto

    Taqwa watoa Eid Mubarak kwa yatima Dar es Salaam

    Na Azza Ally Ahmed mwao pamoja na michango ya wanachama na watu mbalimbali, ambao wanasaidiana kuwalewa watoto hao kwa mapenzi na huruma ili na wao wajisikie wapo na wenzao.

    Aidha amewataka kina mama na wafadhili kujitokeza zaidi kuwafadhili watoto hao, hata kwa kumlea mtoto moja au kupeleka chochote anachojaaliwaa mtu katika ofisi zao.

    Alikumbusha kuwa watoto hao wanawalea hali ya kuwa wako katika familia zao na ndugu zao, na sio katika vituo vya kuwalelea watoto yatima.

    Alisema wanachofanya ni kuwapelekea misaada na mahitaji muhimu inayohitajika katika malezi yao pale wanapolelewa.

    Naye mwakilishi na mwanzilishi wa Qamer Foundation kutoka nchini Canada, Ukht Bilkis Abdulkadir, aliwataka Waislamu kulitilia mkazo suala la kuwasaidia na kuwalea watoto yatima na kudai kuwa ni jambo la kila mtu na sio kuachia taasisi au watu fulani.

    Alisema Waislamu, mtu moja moja au vikundi ni vyema wakawa na tabia ya kujiwekea malengo, hata kwa kuchangishana shilingi mia mia kwa kuwa hiyo mia inaweza kufanya jambo kubwa katika kuwasaidia yatima hao bila ya mtoaji kujua.

    wanapata chakula, wanawatafuta wahisani ili kusaidiana kuwalea watoto hao kuhakikisha wanapata matibabu pamoja na mahitaji yao

    muhimu ya shule.Dk. Salha alisema pesa

    wanazotoa kwa watoto hao ni fedha zinazotoka mifukoni

    JUMUIYA ya Istiqama for Devolopment ikishirikiana na Zanzibar Children Fund (ZCF) wiki hii kwa mara nyengine tena wameendelea kutoa misaada mbalimbali ya kijamii ikiwemo fedha taslimu na masurufu mengine, ikiwa ni kwa lengo l a k u wa s a i d i a wa n a j a m i i kufanikisha maandalizi ya kusherehekea sikukuu ya Iddi-elhaji.

    Kiongozi mkuu wa jumuiya h i z o S h e i k h M o h a m m e d Suleiman Altiwaniy mapema aliweza kuongoza hafla hiyo kwa kuwakaribisha wageni waalikwa ambao ni pamoja na maafisa tawala, masheha, madiwani kutoka Wilaya zote nne za kisiwa cha Pemba, ujumbe kutoka ofisi ya mufti, ujumbe kutoka ofisi ya wakfu na mali ya amana, maimamu, wanachama wa jumuiya ya Istiqama na wanajimii.

    S h e i k h M o h a m m e d amefahamisha kuwa misaada wanayoendelea kutoa kwa jamii ni kwa ajili ya kujenga ushirikiano mapenzi mshikamano na umoja miongoni mwao kama Mwenyezi Mungu alivyoamrisha.

    Mwenyezi Mungu ametutaka tushikamane na tushirikiane, hakika Waislamu wanapokaa pamoja na kuacha tofauti zao, umoja wao na mshikamano

    Istiqama watoa misaada PembaNa Mwaandishi wetu wao huongezeka mara dufu pia

    nakushukuruni kwa kukubali kukaa pamoja kwa mambo ya k u s a i d i a n a k u n ya n y u a Waislamu kisiwani Pemba. Sheikh Mohammed.

    Mapema akifungua hafla hiyo mgeni rasmi Ndugu Ahmed Khalid, ambaye ni Afisa Tawala wa Wilaya ya Micheweni, alisema wamefurahishwa mno wao kama viongozi wa serikali kwa jinsi ya mshikamano ambao ndugu zao wa Istiqama wanauonesha kwa jamii huku akikumbushia jinsi walivyoweza kutoa msaada kwa janga la moto lililowahi k u w a k u m b a w a k a z i w a Micheweni mwaka jana.

    Alisema ihsani ya namna hiyo ni ya kuigwa na taasisi nyengine kisiwani Pemba hata zile zisokuwa za kidini.

    Tul impelekea r ipot i i l e Balozi Seif Ali Iddi ambaye ndie aliyekuwa kiongozi wa kwanza kututemblea mara baada ya janga lile kututokea na alifurahishwa mno na ripoti ile juu ya namna taasisi hii ilivyojitolea pamoja na wengine wote waliotusaidia Alisema Ahmed

    Aidha alisifu jitihada hizo na kuwasihi kuendelea na moyo waliounesha huku akiahidi mashirikiano pindi watakapo hitaji msaada kwa serikali juu ya shuhuli zao.

    Zaidi ya shilingi milioni ishirini zimetumika kwa msaada huo kwa jamii.

    BAADHI ya watoto yatima wanaohudumiwa na taasisi ya akinamama ya Taqwa.

  • 5 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 2014Makala

    Rasimu i l iyotangazwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa Katiba, Andrew Chenge, inatusuta na kuwafanya wale wengine ambao hawataki Muungano wowote kati ya Tanganyika na Zanzibar wawe na hoja juu yetu. Wanatwambia kuwa tangu mwanzo walijua pasingelikuwa na kheri yoyote inayoweza kupatikana kupitia mikono ya Chimwaga.

    Sisi tujionao kuwa Waliberali wa Muungano tumeshindwa. Kushindwa kwetu, hata hivyo, hakumaanishi ushindi kwa wale wa siasa kali zinazoelemea u p a n d e wa k u l i a k we n ye Muungano, ambao sauti yao ndiyo inayoakisika kwenye Rasimu hii ambayo tayari imeshapagazwa lakabu ya Rasimu ya Vijisenti.

    Tumeshindwa Waliberali , ambao licha ya upinzani wetu kwa mfumo uliopo wa Muungano, tulitaka uendelee kubakia ukiwa na mageuzi ya kimsingi. Lakini hawakushinda wahafidhina ambao wanataka mfumo uliopo ubakie na bali usonge mbele zaidi kuelekea serikali moja kama ilivyokuwa ndoto ya mmoja wa waasisi wake, Mwalimu Julius Nyerere. Hawakushinda hata kama waliyoyataka ndiyo yaliyomo kwenye Rasimu ya Tatu na ambayo huenda ikapitishwa Bungeni na yumkini ikapelekwa kwa wananchi kwa ajili ya kura ya maoni.

    Kile ambacho Rasimu hii ya Vijisenti imefanya ni kuuchora mstari katikati ama wanaotaka Muungano kwenye tafsiri yake ya awali ambayo ni Tanganyika kushika hatamu (Tanganyika supremacy) au wale wasioutaka kabisa Muungano huu, na ambao wanaona jambo bora na la salama ni ya mataifa haya mawili kwenda njia mbalimbali na kukutana kwenye ujirani na ushirikiano mwengine wa kikanda.

    Kwa maneno machache ni kuwa sasa nguvu zilizopo kwenye siasa za Muungano zimo kwenye matapo mawili tu wale wenye siasa kali za mrengo wa kushoto kuelekea Muungano na wale wenye siasa kali za mrengo wa kulia kuelekea Muungano. Sisi waliberali wa Muungano tunapaswa sasa ama kuchagua moja kati ya makundi hayo mawili au kujikubalisha kufa na kuachana kabisa na siasa za Muungano. Ingawa nalo pia halimaanishi kwamba nchi itakuwa salama. Panapokosekana watu wanaopigania wastani wa mambo, mambo yote huharibika. Afdhalul-umuri ausatuhaa. ubora wa mambo ni wastani wake, ndivyo tunavyousiwa!

    Rasimu ya Jaji Joseph Warioba ilikuwa imesimama katikati baina

    Rasimu ya 'vijisenti itakavyouvunja kabisa MuunganoNa Mohammed Ghassani

    ya uliberali na mrengo wa kulia panapohusika suala la Muungano. Bado iliupa Muungano nafasi ya juu kwenye kila jambo, lakini pia ikapuruzia baadhi ya utashi wa nchi washirika. Haikuwa ya kiliberali moja kwa moja.

    Kinyume chake ni kuwa Rasimu ya Vijisenti imeelemea moja kwa moja kwenye mrengo wa siasa kali za kulia. Imechukuwa kila kitu kwenye Muungano na haikuacha lolote kwa nchi washirika. Na hapo panaifanya Zanzibar kufa dungu msooni, kwa kutumia maneno ya Arham Ali Nabwa. Inaambiwa mchezoni haimo na ilokwishakula iziteme.

    Mwandishi wa siku nyingi na mwanasheria wa Zanzibar, Ally Saleh, ambaye pia aliwahi kuwa mjumbe wa tume iliyokusanya na kuratibu maoni ya wananchi juu ya katiba mpya (Tume ya Warioba), anaandika hivi kwenye waraka wake kwa wabunge wa Zanzibar waliomo kwenye Bunge Maalum la Katiba:

    Si kweli, na si kweli kabisa, kuwa Katiba inayopendekezwa ina maslahi na Zanzibar. Haina, haina katu, haina abadan, kamwe haina. Ni katiba ambayo inatuweka pabaya na pagumu zaidi na imeendelea kuyachukua mamlaka ya Zanzibar na kuyatia katika Muungano. Vipi Katiba hi i i takuwa na maslahi na sisi (ikiwa) . kuondosha au kuukataa mfumo wa Shirikisho ina maana (a) Zanzibar haiwezi kuwa na hadhi na haki sawa na Serikali ya Muungano, ( b) Tumejibakisha pale pale Zanzibar haina mshirika mwenziwe kwenye Muungano , (c) Tumerudi pale pale mshirika wa Zanzibar ni Tanzania na kwa hivyo hakuna usawa , (d) Tumeganda pale pale kuwa Tanganyika inasimamiwa na Serikali ya Muungano , (e) Tumesalia papo kuwa Bunge la Muungano linatunga sheria za Tanganyika na tunajua kuwa sheria kama hizo hazina nguvu

    Zanzibar , (f) Tumejizuga vile vile kumwita Waziri wa Muungano hata asiyesimamia jambo la Muungano kama kilimo bila ya kuwa na hadhi kama hiyo, ( g) Tumekwama pale pale Mahakama Kuu ya Tanganyika inaitwa ya Muungano, ( h) Tumejidanganya vile vile wafanyakazi wote wa Tanganyika wanabaki ni wa Muungano na wale wa Zanzibar mwisho wao ni Chumbe.

    Ally Saleh, kama nilivyo mimi, ni mliberali wa Muungano. Anataka Muungano ubakie ukiwa na mageuzi ya kimsingi. Anataka nguvu ya Serikali ya Muungano kwa mambo yasiyokuwa ya Muungano katika nchi washirika zipungue kama si kuondoka kabisa. Anataka mgawanyiko wa wazi wa ipi Tanganyika (kama nchi mshirika) na ipi Tanzania (kama Muungano wenyewe). Anataka hadhi na heshima ya Tanganyika, kwa upande mmoja, na Zanzibar, kwa upande mwengine, zitambulike na ziheshimike.

    Rasimu ya Vijisenti inafanya kinyume chake na hapo ndipo unapolifanya kundi la mrengo wa siasa kali za kushoto ndani ya visiwa vya Zanzibar kuwa na nguvu kwenye hoja yake. Baada ya Rasimu hii, sasa ni rahisi zaidi kuushawishi umma kuamua dhidi ya Muungano kwa ujumla wake kuliko kuamua juu ya baadhi ya mambo na kuacha baadhi ya mengine ndani Muungano huo, kama ambavyo Rasimu ya Warioba ilikuwa imefanikiwa kuweka mizania.

    Danganya-toto, kwa mfano, ya kumfanya Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Tanzania, lakini wakati huo huo kuyapeleka madaraka ya Muungano kwa Makamu wa Kwanza na wa Tatu (ambao si lazima wawe Wazanzibari na hata wakiwa hawawakilishi matashi ya Zanzibar kwenye Muungano) kumedhihirisha tu hoja ya wenye

    siasa kali za kushoto kuelekea Muungano, kwamba Dodoma haitapata usingizi hadi imalize kila alama ya uhuru, uwezo na hadhi ya Zanzibar.

    Waliberali wa Kizanzibari wa Muungano kama tulivyo mimi na Ally Saleh ambao kila siku tuliamini kuwa njia ya kati na kati inawezekana kupitika kuelekea Muungano mzuri zaidi kati ya Tanganyika na Zanzibar, tumeambiwa na Rasimu ya Vijisenti kwamba hilo halipo wala haliwezekani kabisa. Tumekhiyarishwa baina ya kuisalimisha kabisa heshima ya nchi yetu au kuukataa kabisa Muungano na Tanganyika.

    Wakati Rasimu hii imetunyima sisi waliberali tunachokitaka, na ambacho tunaamini ndicho pekee kinachoweza kuudumisha na kuunusuru Muungano, imewapa kila kitu wale wenye siasa kali za mrengo wa kulia, ambao mtazamo na siasa zao ni kuelekea nchi moja na serikali moja na ambao wala si waumini wa Muungano kwa dhati yake, bali Muungano kwa jina lake tu. Kwa dhati kabisa, kundi hili linaamini kuwa Zanzibar haipaswi hata kuishi kama sehemu muhimu na yenye upekee kwenye Muungano, bali inapaswa tu kuwa kama vile zilivyo Arusha, Tanga na Shinyanga.

    Tuliokosa si sisi Waliberali tu, bali pia kundi jengine ambalo si dogo ndani ya visiwa vya Zanzibar ambalo liliivumilia mizania ya Rasimu ya Warioba licha ya kwamba haikuwapa kila wakitakacho la siasa kali za kushoto kuelekea Muungano. Lile ambalo linaamini juu ya k u t o k u w e p o k a b i s a k w a Muungano. Lakini kwa kuwa kundi hili l i l i tegemea sana matokeo hayo, halikushitushwa isipokuwa tu limethibitisha na kupata hoja ya kutusuta sisi wengine. Na kwa msingi huo, sasa linapata uhalali zaidi kuliko kundi la akina miye na Ally Saleh.

    Matokeo yake ni kuwa Rasimu ya Vijisenti inatufanya na sisi waliberali tuangalie upya siasa zetu kuelekea Muungano kwa mara ya kwanza. Je, ni kweli hapa njia ya kati na kati kuelekea kwenye Muungano wa heshima, haki na usawa kama tulivyokuwa tukiamini siku zote? Je, nasi tuelemee kushoto kabisa au kulia kabisa?

    Maj ibu ya maswali haya yametolewa kwa njia isiyo sahihi ndani ya Rasimu ya Vijisenti; na haitakuwa ajabu kwamba Rasimu hii, kwa hivyo, ndiyo itakayouvunjilia mbali Muungano huu uliodumu kwa nusu karne.

    Waswahili husema: kheri i matumboni mwa shari!

    (Makala hii imetolewa kwa hisani ya Mohammed Ghasani kama ilivyopatikana katika mtandao wa Mzalendo.)

  • 6 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 2014Makala

    Inaendelea Uk. 12

    NENO msalaba linatokana na neno sulubu, kwa maana ya tabu, mateso, shida n.k. Hivyo kama ni kazi, ni kazi ya mateso, kama ni maisha ni maisha ya mateso, kama ni kipigo ni kipigo cha mateso na kama ni kifo au kuuawa ni kifo au kuuawa kwa mateso ya aina yoyote, si lazima yawe ya aina fulani.

    K u u n g a n i s h w a k i l e kinachoaminika kuwa Yesu alisulubishwa kwa maana ya kuwa alipigiliwa msalabani, na kuunganishwa kuwa msalaba ni nembo ya ukombozi kwa dini ya Kikristo, inawezekana kuwa si sahihi, kwa kuwa, kuwasulubisha watu kulikuwa hata kabla ya Yesu kuzaliwa, na ilikuwa ni sheria ya ukatili uliotendwa na serikali ya Kirumi kwa enzi hizo. Ndiyo maana walikuwa na mahali maalumu pa kusulubishia watu palipoitwa Golgotha, yaani mahali penye mafuvu ya watu walio teswa na kufia hapo na kuozea hapo.

    N d i y o m a a n a s h e r i a ya Taurat i ikatofaut isha unyongwaji wa mtu aliyestahili kunyongwa na ile sheria ya Kirumi, pale ilipoandikwa hivi:

    Akiwa mtu ametenda dhambi ipasayo kufa, akauawa, nawe ukamtundika juu ya mti, mzoga wake usikae usiku kucha juu ya mti; lazima utamzika siku hiyo hiyo kwani aliyetundikwa amelaaniwa na Mungu; usije katia unajisi katika nchi yako akupayo BWANA Mungu wako, iwe urithi wako. (Kum. 21:22-23.)

    Kwa maana hiyo, alama ya pande nne au jumlisha, sio msalaba. Neno hilo la msalaba, limeingizwa na mfalme wa Rumi ili kuchochea askari wake wakati wakipigana vita kwa kuvamia mataifa mengine ili wahakikishe kuwa wanawasulubu wale wote waliowaita kuwa ni maadui zao, wasiwahurumie na baadaye likatiwa rasmi katika Vita vya Msalaba. Kilichozungumziwa hapo, ni , kutundikwa mtini au kunyongwa, iwe ni kwa kamba au nduano (ndwana).

    Vita vya Msalaba vilikuwa v i ta vya kuwaangamiza Waislamu vya mwaka wa 1096, vilivyo idhinishwa na Pope Urban II na ambavyo vinaendelezwa hadi sasa kwa kutumia misamiati mbalimbali kama tutakavyoona baadaye.

    M w a k a A . D . 3 1 2 C o n s t a n t i n e a l i k w e n d a kupigana vita na Maximian, aliyekuwa amejitwalia kwa hila ufalme wa Italy, na wa Afrika. Constantine alipokuwa akisafiri kwenda vitani, alisema kwamba aliona maono ya ajabu: maana mbinguni ilitokea dalili au ishara, kama ya msalaba wa mwanga ukizungukwa na

    Masheikh wapo GolgothaWanabebeshwa msalaba wa Pope Urban II

    Na Khatib J. Mziray

    WATUHUMIWA wa kesi ya ugaidi wakiwa katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

    maneno ya moto yaliyongaa. Maneno yenyewe ni haya: Kwa msalaba huu utapata ushindi. Basi Consitantine akaamuru kwamba mfano wa msalaba ushonwe katika bendera zote za majeshi yake. Akaenda akamshinda Maxsentius, kisha aliporudi Rumi akasimamisha sanamu humo mjini mfano wake yeye mwenyewe; sanamu aliyechorwa katika jiwe kuu. Na sanamu huyo alikuwa na msalaba mkononi; nao umeandikwa chini anwani yake ya kusema kwamba msalaba huo ulimshindia vitani. (Historia ya Kanisa uk.55, cha Canon H.J.E. Butcher.)

    Ndiyo maana Peter the Hermit, alipozusha poropoganda, za kuwa, Waislamu wanawauwa Wakristo kule Yerusalemu, na akaomba kibali kwa Pope Urban II; alifanya kazi hii hii inayofanywa na Marekani, na mataifa ya Ulaya ya kuzunguka nchi za Ulaya, na kukusanya Maaskofu na ma Padre wengi wa k a k u s a n ya Wa k r i s t o wengi wake kwa waume, watoto kwa wakubwa wakavaa alama ya msalaba katika nguo zao, wakenda vitani. Ikimanisha kuwa wanaenda kuwasulubu Waislamu wa Yerusalemu, katika Crusades ya mwaka wa 1096. Na wanaandika wenyewe jinsi walivyowasulubu, hata pale Waislamu walipotaka suluhu, Wakristo na kanisa na viongozi wao hawakutaka suluhu, bali sulubu. Canon anatufahamisha akisema:

    Kisha askari hao wakaenda zao wakafika Antiokia, katika nchi ya Palestine, wakauzunguka muda wa mezi minane. Wakautwaa mji huo, wakawaua wote waliokataa

    kuishika dini ya Kikristo. (Historia ya Kanisa, u.k. 85.)

    Pia, walikuwako wengi kati ya Waislamu ambao walitaka kuishi kwa amani kati yao na Wakristo, vile vile Wakristo wenye mashamba eneo za Mashariki waliona haja ya kupatana. Lakini, maaskari waliotoka nchi za Magharibi w a l i t u m a i n i k u w a o k o a Waislamu wote kwa upanga, wakaacha chuki kat i ya Waislamu na Wakristo hata siku hizi zetu. (u.k.87).

    Wafundishaji wa Ukristo, wanatwambia kuwa msalaba ni alama ya ukombozi, na askari hao wa Crusades walivaa mavazi yaliyochorwa misalaba kama alama ya ukombozi, lakini kazi waliyofanya ni hiyo hapo juu; ya kuwaokoa (kuwauwa) Wais lamu kwa kuwakata vichwa kwa upanga.

    Ukatili huo unaotokana na sera za kuasisiwa kwa Kanisa, chini ya mfumo wa Kirumi, na viongozi wa Ukristo, ndio huu huu unaoendelezwa sasa katika vita vinavyoitwa vya magaidi, wanavyofanyiwa Waislamu. Chakusikitisha ni kuwa, kwa sasa, viongozi wa nchi za Kiislamu na hata na viongozi wa Waislamu, wanakusanywa pamoja na nchi za Ulaya na kuchangia Vita vya Msalaba (Crusades) kwa kisingizio cha kutokomeza magaidi. Labda hapa nitoe mfano hai wa vita vya Iraq vilivyomwondoa Rais Sadam Husseni, tuone jinsi vita hivyo vilikuwa vya msalaba; na jinsi viongozi wa Makanisa walivyokuwa wakifurahia kuona Waislamu wakiokolewa kwa kulipuliwa vichwa kwa risasi na mabomu.

    S a d a m H u s s e n i alisingiziwa kuwa ana silaha za maangamizi. Rais Bush akishirikiana na mataifa ya Ulaya, Umoja wa Mataifa na baadhi ya nchi za Kiarabu (Waislamu) wakakokotwa kwa kutishwa kuwa atakayekataa kushirikiana na Marekani, atachukuliwa kuwa huyo ni gaidi. Na viongozi wa Makanisa na mashirika ya kanisa na vyombo vyao vya habari vikieneza poropoganda na kusherehesha na kufafanua lengo la vita hivyo. Kwa ujumla vikikoleza propaganda, uzushi na uwongo.

    N i l i a n d i k a m a k a l a zilizoelezea lengo la vita hivyo tarehe 28/10/2005. Inawezekana waliozisoma wakati huo hawakuzingatia ukwel i huo, n imeonelea nizinukuu hapa ili wasomaji walinganishe hali iliyopo sasa na mambo yalivyokuwa na lengo lilivyokusudiwa. Moja ya gazeti la Kanisa liliandika kichwa cha habari hiv:

    Biblia yasema Irak ina pepo shujaa wa vita. Walipigana na malaika wa Mungu siku 21. Ilibidi Malaika Mkuu Mikaeli ashuke kuingilia kati. Rais Bush asoma Biblia kabla ya kutangaza vita.

    Chini ya maandishi hayo iliwekwa picha ya askari wa Iraki aliyetekwa na askari wa Marekani wakimnywesha maji kutoka katika chupa zao za kijeshi na mmoja wa askari hao amemwekea mtutu wa bunduki kichwani; lakini inavyoonekana ni kuwa askari huyo wa Iraki alishakufa, na hizo ni kejeli na mbwembwe za askari wa vita vya msalaba.

    Mwandishi wa makala hiyo alikuwa ni Mchungaji Teghua akithibitisha kuwa anachofanya Bush ni cha Kanisa -Ukristo, na kuwa ametumwa na Mungu kuwaangamiza Waislamu (mapepo) wa Iraki. Alinukuu kitabu cha Danieli (10:1-19), ili kuonyesha uhalali wa Rais Bush wa kuivamia Iraki huku akimwelezea kuwa ni mkombozi aliyetumwa na Mungu kuyaondoa mashetani wa Iraki. Hivyo kuangamizwa watu wa Iraki ni halal i . Mchungaji Teghua aliandika hivi:

    Rais Bush wa Marekani, ambaye ni Mlokole alikaa kwanza kusoma Biblia katika kitabu cha Mwanzo 18:17; BWANA AKANENA, JE! Nimfiche Ibrahimu jambo nilifanyaloHaikuelezwa na yeyote kuwa ni nini alichokikusudia Rais Bush kusoma andiko hilo kisha kunyanyuka kwenye kiti na kutangaza vita.

    Hata hivyo Mchungaj i Teghua, alifafanua kidogo kwa kuandika hivi:-

    Kama vile alivyosema Bwana Yesu kuwa siku za mwisho zitakuwa

  • 7 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 2014Makala

    Barua ya wazi kwa Wajumbe wa Bunge la Katiba kutoka Zanzibar27 Septemba, 2014Assalam alaykumNatumai hamjambo ndugu, kaka na dada zangu. Inshallah Mwenyenzi Mungu akupeni afya na uzima kuelekea kipindi hiki muhimu cha kupiga kura kuamua Katiba inayopendezwa na pia Mola akupeni busara na maamuzi mema.

    Nakuandikieni barua hii kama M z a n z i b a r i m we n z e n u s i n a zaidi ya hilo. Ni kutokana na Uzanzibari wangu nimeona kuwa nijaribu kukuaidhini, kunasihini, kukushawishini, kukusemesheni, kukuombeni kuwa msiikubali Katiba inayopendekezwa na muipigie kura ya HAPANA.

    Ta f a d h a l i n i we k e n i m b a l i ushindani, itikadi na mitazamo ambayo inatutenganisha Wazanzibari na muamue kwa maslahi makubwa, mapana na ya muda mrefu ya Zanzibar. Msitizame tulipojikwaa bali tizameni tulipoanguka. Msitizame nyuma mkahesabu visa na mikasa, ila nyinyi hapo mlipo ndio wenye fursa ya kuiokoa, kuinusuru na kuihuisha Zanzibar.

    Naam, ni kura ya HAPANA ndio ambayo itaibakisha, itaiokoa, itaisimamisha Zanzibar. Mjue mkipigia kura ya NDIYO maana yake ni kuwa Zanzibar tuipendayo inazidi kupungua, kuchukuliwa na kumezwa kama ambavyo imekuwa khofu yetu kwa miaka kadhaa ya Muungano huu.

    Nataka muamini ndani ya dhati yangu mimi ni muumini wa Muungano. Nataka Muungano wa haki na hadhi sawa baina ya Washirika wa Muungano Tanganyika na Zanzibar- ili kila nchi ipate fursa sawa za kuhudumia watu wake.

    Wengi wenu kwa kauli zenu mara kadhaa mmekuwa mkisema Muungano hauakisi hali ya usawa, haki na hadhi sawa, lakini mkawa mnatumia neno KERO kuwasilisha fikra zenu hizo, na wengi tukawa na matumaini kwamba fursa hii ya kuunda upya Katiba yetu itapunguza kama si kuondosha kabisa KERO hizo.

    Ila baada ya kuiona Katiba inayopendekezwa, nimeona kuwa andiko hilo halina msaada, halina muelekeo na halina wema na Zanzibar. Kulikubali andiko hilo ni kujitia kitanzi wenyewe na sasa imekuwa ni kusokotwa, kubanwa na kudhibitiwa Zanzibar lakini mara hii itakuwa kwa kujitakia wenyewe.

    Huko nyuma tumekuwa tukisema kuwa kumekuwa na hadaa, sijui ujanja, sijui ghalat, sijui unyemela wa kuongeza Mambo ya Muungano ambayo yamekuwa yakipunguza madaraka ya Zanzibar, lakini mara hii tunajichinja wenyewe kwa mikono yetu.

    Hii ilikuwa ni fursa kubwa kwetu kusimama kama Zanzibar. Zanzibar ilipaswa kusimama kama kundi zima ndani ya Bunge na kukaa na kundi zima la upande wa pili yaani Tanganyika, na watu wa pande mbili hizi kuamua umbo, hadhi na sifa gani tunataka Tanzania iwe.

    Hili la pande mbili lilikuwa lisionewe aibu kwa sababu ndio ukweli na uhalisia kwamba tuko pande mbili. Haiwezekani kuwa na Muungano, ambapo upande mmoja

    WAJUMBE wa Bunge la Katiba kutoka Zanzibar walipokuwa Bungeni Dodoma. (Picha kwa hisani ya mtandano wa IPP)

    una kila sifa za kuwa nchi, halafu upande mwengine uwe na sifa za kuwa dola na nchi ifichwe ndani yake.

    Ilikuwa ni nafasi nzuri kwa Zanzibar kudai haki zake, stahiki zake, fursa zake ili iweze kukidhi mahitaji ya watu wake, maana hata kama tumo ndani ya Muungano, basi bado tuna chumi mbili zinazoshindana na kwa kweli zinazopigania na kunyanganyiana rasilimali karibu zile zile.

    Ilikuwa ni wakati wa kufanya kila njia ili Zanzibar ijitengenezee fursa ya kuwa na mafanikio kama ya Visiwa vya Seychelles au Mauritius ambavyo wastani wa kipato cha mwananchi wa nchi hizo mbili ni zaidi ya dola 14,000 na dola 15,000 mtawalia.

    Najua hoja itakuja basi haya yangefanywa kwa umoja , na mbona umoja huo haukuwepo, nakiri kuwa hilo kweli limetokea, lakini ni kama katika mchezo iwapo mchezaji mmoja ametolewa ama kwa kuonewa na mwamuzi au kwa kitendo chake cha makusudi, haina maana kuwa waliobakia uwanjani wakubali kupoteza mchezo, badala yake hujibidiisha kushinda ili iwe njia moja ya kumsuta mwenzao aliyetolewa na sifa kwa kweli inakuja kwa waliobakia uwanjani.

    Kwa kuendelea kujigandisha katika ubavu, kuendelea kuamini kuwa hatuwezi kujitegemea na kwa hivyo mambo kadhaa kuyabakisha katika Muungano ni kujiviza akili, ni kujidhalilisha kimkakati na kujidogosha kihadhi.

    Si kweli na si kweli kabisa kuwa Katiba inayopendekezwa ina maslahi na Zanzibar. Haina, haina katu, haina Abadan, kamwe haina. Ni katiba ambayo inatuweka pabaya na pagumu zaidi na imeendelea kuyachukua mamlaka ya Zanzibar na kuyatia katika Muungano.

    Vipi Katiba hii itakuwa na maslahi na sisi? Hebu tutizame mambo machache:

    1. Kuondosha au kuukataa mfumo

    wa Shirikisho ina maana kuwa Zanzibar haiwezi kuwa na hadhi na haki sawa na Serikali ya Muungano. Pili, tumejibakisha pale pale Zanzibar haina mshirikia mwenziwe kwenye Muungano. Tatu, tumerudi pale pale mshirika wa Zanzibar ni Tanzania na kwa hivyo hakuna usawa. Nne, tumeganda pale pale kuwa Tanganyika inasimamiwa na Serikali ya Muungano. Tano, tumesalia papo kuwa Bunge la Muungano linatunga sheria za Tanganyika na tunajua kuwa sheria kama hizo hazina nguvu Zanzibar. Sita, tumejizuga vile vile kumwita Waziri wa Muungano hata asiesimamia jambo la Muungano kama kilimo bila ya kuwa na hadhi kama hiyo. Saba, tumekwama pale pale Mahakama Kuu ya Tanganyika ina i twa ya Muungano . Nan , tumejidanganya vile vile wafanyakazi wote wa Tanganyika wanabaki ni wa Muungano na wale wa Zanzibar mwisho wao Chumbe.

    Fikiria, hii ndio Zanzibar tuitakayo?2. Tunajipa moyo kuwa kumfanya

    Rais wa Zanzibar kuwa ni Makamo wa Rais wa Muungano kuna manufaa kwa Zanzibar ilhali hakutakuwa na msaada wowote.

    Tumewapa watu matumaini kuwa hilo litawezesha Rais wa Zanzibar akitoka nje atakuwa na hadhi ya kimuungano wakati tunajua hilo litaleta utata mkubwa zaidi huko mbele. Kwanza kwa suala la gharama pili kutakuwa na mgongano wa maslahi na majukumu yake kama Rais wa Zanzibar vs Umakamo wa Muungano

    3 . H a i w e z e k a n i R a s i m u inayopendekezwa iwe imenyofoa mamlaka zaidi yaliokuwa yameanza kuikaribia Zanzibar kutokana na Rasimu ya Warioba, halafu isemwe kuwa kuna maslahi kwa Zanzibar. (Mfano) kuondoa uwezo wa Zanzibar kuunda Benki yake. Kurudisha nguvu za kuigawa Zanzibar kwa Rais wa Muungano. Kukubali ardhi

    kurembwa. Tumerudisha suala la Tume ya Pamoja ya Fedha ambayo imeshindikana kwa miaka kadhaa toka nia hiyo ilipotiwa kwenye Katiba ya 1977.

    4. Uamuzi wa kuyatia madaraka ya Serikali ya Zanzibar ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ilhali hakuna sehemu yoyote ya Katiba inayopendekezwa ambapo madaraka ya Serikali ya Tanzania Bara kama inavyoitwa yameainishwa ni kuendelea kujidanganya.

    Pili, kwa kufanya hivyo tunarudi tena pale pale ambapo Zanzibar inaonekana inakiuka Katiba ya Jamhuri pale inapotaka kufanya mabadiliko yenye maslahi yake, ilhali jambo kama hilo halionekani na wala halipo kwa upande wa mshirika mwenziwe, maana mshirika ni huyo huyo Serikali ya Jamhuri na Serikali ya Tanzania Bara.

    Ndugu, kaka na dada zangu ujue wazi kuwa maamuzi unayotaka kuyafanya ni makubwa na yana athari ya muda mrefu kwa vizazi vingi vya Zanzibar, ambayo pamoja na tofauti zetu, lakini naamini tunakubaliana kuwa Zanzibar tuipendayo iwepo. Na kuwepo kwake lazima iwe na nguvu na matao yake.

    Na kwa dalil i zote, Rasimu inayopendekezwa inapopotoa nguvu na matao ya Zanzibar. Inaondosha uzuri na haiba yake kwa kuifanya kuwa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano badala ya kuwa ni nchi moja kamili ndani ya Muungano huu.

    Fikirini, pimeni na muvuke nje ya itikadi na mitizamo. Fanya uamuzi ili nafsi yake iwe na amani kwa sababu umefanya uamuzi wako bila ya shindikizo, maelekezo au utashi wa kisiasa, maana wewe kwanza ni Mzanzibari kisha mengine ndio yanafuata.

    Nawaomba radhi kwa uamuzi huu wa kuandika barua ya wazi maana isingewezekana kumfika kila mmoja wenu, lakini nataka muamini kuwa barua hii nimeiandika kwa sababu nimeona kuna wajibu kwangu kufanya hivyo.

    Unapotaka kupiga kura fikiria, wazia na pimia juu ya uzito wa mchoro wako mmoja tu wa kalamu utavyokuwa na athari kwa nchi yako, watu wako na watoto na wajukuu wako. Fumba macho, rudisha nyuma fikra zako,

    kumbuka wema na ihsani za waliokuzunguka, uliokuwa nao pamoja katika maisha yako na uwafikirie khatma njema ya muda mrefu.

    Kumbuka jukumu lako kwa Mwenyenzi Mungu na fikiria kama hicho ni kitendo cha mwisho cha maisha yako ili ukitie katika mizania nzuri ya maamuzi yako.

    Piga HAPANA kwa faida ya Zanzibar na usinitizame mimi kama Ally Saleh, la. Mimi ni mtu mmoja tu tena tunaweza kuwa tuna mzigo wa tofauti zetu, lakini pamoja na yote mimi na wewe ndio Zanzibar.

    Kwa maslahi ya Zanzibar piga HAPANA.

    Ally SalehZanzibar

  • 8 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 2014Makala

    Inaendelea Uk. 9

    HALI si shwari. Ni hamkani tupu. Polisi, jeshi, taasisi za kikachero na viongozi wa serikali katika nchi mbalimbali duniani, wapo hai hai kuweka mikakati ya kukabiliana na kitisho cha al Qaida, al-Shabab, Boko Haram na ISIS. Vikao vinafanyika na kutumia gharama kubwa, nini? Kujadili kitisho cha ugaidi, iwe ni Boko Haram, al Qaida, ISIS au al Shabab.

    Kwa upande mwingine, wapo wale ambao ndio waathirika wa k u b wa n a wa m wa n z o kuathiriwa na mikakati hii ya wakubwa ya kupambana na magaidi. Waathirika hawa ni Waislamu. Nao miongoni mwao wapo wale waliomezeshwa propaganda ya Jihad ya Boko Haram, al Shabab na ISIS, wakaipokea na sasa wapo tayari kuacha familia zao kwenda kushika bendera nyeusi yenye kalimt Tawheed kusimamisha Khilafah. Lakini hata kama hilo, halitawezekana, basi wamebaki k u wa m a s h a b i k i a m b a p o katika ushabiki huo wanajikuta wakifanya vitendo ambavyo vinawapeleka Goligotha, wao binafsi na jamii ya Waislamu kwa ujumla.

    Makundi yote haya mawili, yanafanya kazi kama mawakala

    Tumemeza al Qaida, ISISBoko Haram, al Shabab

    Sasa tunaletewa Khorasan Group

    Na Omar Msangi

    tu, iwe kwa kutambua au kwa kutumiwa bila kujijua.

    Hivi sasa Marekani ipo katika kampeni kubwa ya kuwapiga

    IS ndani ya Syria. Lakini katika kufanya kazi hiyo inajikuta ikikabiliwa na vikwazo viwili. Kwanza ni kuwa inafanya

    mashambulizi hayo bila idhini ya Bunge lake yenyewe wala kibali kutoka Umoja wa Mataifa (U.N. authorization). Kwa hiyo hakuna uhalali wa kisheria (lack of legal justification- No viable claim of self-defense or U.N. approval.)

    Pili, ni kuwa itakuwa vigumu sana kudumisha uungwaji mkono kutoka kwa wananchi wake iwapo kampeni hiyo itachukua muda mrefu. Na hiyo ni kwa sababu hao ISIS hawaonekani kama ni kitisho cha karibu na cha uhakika kwa Marekani (imminent threat to the homeland). Wanaonekana tu kuwa ni adui na zimwi, lakini lililopo mbali. Nini ufumbuzi? Kutafuta zimwi jipya.

    Kundi la KhorasanHivi sasa Marekani imekuja na

    madai kuwa kuna kundi jipya la kigaidi linalojiita The Khorasan Group, ambalo ni hatari zaidi ya ISIS. Na kwamba kundi hili linapanga kufanya mashambulizi Amerika na Ulaya mfano wa lile la Septemba 11. Katika madai hayo, wakuu wa Marekani wanasema kuwa hao The Khorasan Group wana utaalamu wa kutengeneza milipuko midogo lakini yenye nguvu sana na ambayo haiwezi kugundulika kirahisi na mitambo ya ukaguzi kwa hiyo wanaweza kuingia nayo katika ndege za abiria

    MAUAJI kushoto kulia. Hakuna anayehesabu tena ni watu wangapi wanauliwa. Libya imetoka katika habari zinazongara za mfumo. Imeshavurugwa. Waliotumika wakidhani akiondoka Gadhafi w a t a s i m a m i s h a D o l a y a Kiislamu (Khilafah), wameachwa wakiuwana wenyewe kwa wenyewe. Amani hakuna tena Libya. Nia na lengo la makafiri mabeberu limefikiwa. Mapigano yamefanikiwa. Kuisambaratisha nchi nyingine ya Waislamu ili kuinyonya kwa urahisi. Sasa Libya ni Congo (DRC) ya Afrika Kaskazini.

    Vita na mtambo wa mauaji vinasonga mbele. Waislamu h a m n a z o h a w a j a k o m a w a l a k u t a n a b a h i . S a s a wanatumika tena kuivuruga na kuisambatarisha Syria. Damu ya maelfu kwa mamilioni ya akina mama na watoto wasio na hatia inamwagwa ili kufanikisha malengo ya mabeberu makafiri. Waliotangulizwa kufanya kazi hii chafu ni wanaojiita Waislamu mujahidina, IS.

    Kwa kisingizio cha kuangamiza n a k u t o k o m e z a u g a i d i unaohatarisha amani duniani, vita ya kuuwa na kuhujumu Waislamu inaendelea. Masheikh wanakamatwa na kufanyiwa matendo ya kudhalilisha ikidaiwa kuwa hiyo ni katika vita kwa ajili ya kudumisha amani na utulivu. Ni hivyo. Hakuna jipya. Gazeti la Washington Post linavisifu vita

    Mauaji kushoto kuliaMtambo wa mauaji unasonga mbele Tumekuwa wacheza mduara wa maadui

    Na Omar Msangi

    ni pendekezo lenye faida.Ukienda kule Nchi za Ghuba,

    tayari ni wacheza mduara wa Marekani, kama alivyothibitisha Waziri wa Mambo ya Nje John Kerry katika safari yake ya hivi karibuni kwenda Mashariki ya Kati kupata mifungamano mipya. Mashine ya kutotoa

    uwongo inafanya kazi nzuri kuwachanganya watu. Kufikiri binafsi ni kama kumeuawa. Watu wanafuata propaganda ya habari ya nchi za Magharibi ambayo inashikiliwa kwa asilimia 90 na mashirika sita ya habari ya Wayahudi. Ukweli huu na hali halisi vinabidi kurudiwa kila wakati vinginevyo tutasahau ni wapi uwongo unaochuruzika unapotokea.

    Tangu 9/11, kati ya watu milioni 10 na milioni 15 wameuawa, iwe ni moja kwa moja kwa mikono ya mtambo wa vita wa Marekani na NATO, au kupitia machafuko yaliyosukumwa na kuwezeshwa kifedha kote duniani na Marekani. Yote katika j ina takatifu la kupigana na ugaidi, bila shaka. Ni kisingizio chema sana. Nchi zote za Magharibi zinashiriki. (Kipande hiki kimetafsiriwa na kuhaririwa kutoka makala The Mass Media and ISIS vs Syria, vs Ukraine, vs Iraq, vs Gaza: A Game Of Confusion And Killing By Propaganda kama ilivyoandikwa na Peter Koenig)

    Balaa lililoletwa na ISMapema wiki hii ndani ya

    Baraza la Umoja wa Mataifa, Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alisema kuwa Islamic State, kwa maana ya Dola ya Kiislamu, ndio kitisho kikuu cha dunia hivi sasa. Akaongeza kuwa IS na Hamas, ni matawi ya mti ule ule wa sumu akiutaja kuwa ni Uislamu akiubatiza kwa jina la militant Islam.

    "ISIS and Hamas are branches of the same poisonous tree. ISIS and Hamas share a fanatical creed.

    Alisema Netanyahu, ufupi wa maneno akimaanisha kuwa ISIS na Hamas, ni matawi ya mti wa sumu na mti huo akautaja kwa ishara kuwa ni Uislamu.

    Japo ameijumuisha Hamas hapa, lakini muhimu hapa ni kuwa hapa ndipo walipotufikisha ISIS. Kwamba leo hata Netanyahu ambaye punde tu ametoka kuchinja Wapalestina takribani 2000, anakuwa na ujasiri wa kusimama mbele ya Baraza la Umoja wa Mataifa kudai kuwa kuna watu katili na wauwaji kuliko Israel.

    Ukiacha kauli hii ya Netanyahu, lakini kinachofanyika hivi sasa, ni kufuta rekodi i l iyokuwa imewekwa na wauwaji katili wote waliotangulia katika historia ya mwanadamu wakiwemo wale wa makuruseda, na kuandika historia mpya kuwa watu katili na wauwaji washenzi kuliko wote, ni hao IS wanaotajwa kwa jina linalowakilisha Uislamu na Waislamu. Hii pekee ni msiba kwa Waislamu.

    Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu.

    Inaendelea Uk. 9

  • 9 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 2014Makala

    Tumemeza al Qaida, ISISBoko Haram, al Shabab

    Inatoka Uk. 8bila kugundulika. Wanaendelea kudai kuwa Khorasan Group wameingia Syria, si kwa lengo la kupigana bega kwa bega na ISIS, lakini kutafuta namna ya kutoa mafunzo kwa wapiganaji wa ISIS kutoka Ulaya na Marekani ili iwe rahisi kwa wapiganaji hao kuingia katika nchi zao kufanya mashambulizi ya kigaidi.

    Kwa kipindi sasa, taarifa hizo zimekuwa zikilishwa vyombo vya habari vya Marekani na kuchukua nafasi kubwa kuliko zile za ISIS. Taarifa ya Associated Press (AP) ya Septemba 13 inawanukuu maofisa wa serikali ya Marekani wakisema kuwa kumeibuka mujahidina wapya kutoka Afghanistan, Yemen, Syria na Ulaya ambao ni tishio la moja kwa moja kwa usalama wa Marekani. Wakadai pia kuwa mujahidina hao wapya wanashirikiana na magaidi wa Yemen wenye ujuzi wa kutengeneza mabomu wakiwa la lengo la kushambulia U.S. aviation.

    I n a e l e z wa k u wa t o f a u t i n a m u j a h i d i n a w e n g i n e wa n a o p a m b a n a k u m n g o a Bashar al Assad, hawa Khorasan wametumwa na kiongozi wa al-Qaida Ayman al-Zawahiri

    kuwapa mafunzo mujahidina wenye hati za kusafiria (passports) za Marekani na Ulaya ili iwe rahisi kwao kuingia katika nchi hizo

    kufanya mashambulizi bila ya kutiliwa shaka.

    The fear is that the Khorasan mi l i tants wi l l prov ide these

    sophisticated explosives to their Western recruits who could sneak them onto U.S.-bound flights.

    A P i l i e l e z a i k i w a o n y a Wamarekani kuwa tofauti na ISIS, hawa Khorasan Group ni tishio la moja kwa moja na la sasa hivi kwa Amerika .

    Katika kukoleza kitisho na propaganda hiyo, taarifa ya habari ya CBS News asubuhi ya Septemba 18, ikaja na kauli kama:

    sources warn of a more immediate threat to the U.S. Homeland.

    Sources confirm the Al Qaeda cell goes by the name Khorasantheyre developing fresh plots to attack U.S. aviation.

    Mchana wa siku hiyo hiyo, ika toka kaul i kutoka kwa Mkurugenz i wa Nat iona l Intelligence, James Clapper akidai kuwa:

    In terms of threat to the homeland, Khorasan may pose as much of a danger as the Islamic State.

    Septemba 20, The New York Times , nalo likaibuka na kichwa cha habari kilichonadi:

    U.S. Suspects More Direct Threats Beyond ISIS.

    Na kukoleza kwa kibwagizo kuwa Khorasan, ikiongozwa na mtu aliyetajwa kwa jina la Muhsin

    Inaendelea Uk. 11

    Mauaji kushoto kuliaInatoka Uk. 8H o j a h a p a s i o k a m a yanayosemwa kufanywa na IS ni kweli au la, lakini hoja ni namna Waislamu walivyotumika kufanikisha propaganda hii kupitia proxy war kutufikisha hapa. Wapo baadhi ya watu wanatoa hoja kuwa IS ni wapigania dini wenye nia ya kusimamisha Uislamu na wao (IS) wameona kuwa njia inayofaa ni hiyo ya vita na mauwaji. Wenye hoja hii wanasema kuwa hakuna haja ya kuwasema vibaya IS kwani hiyo itakuwa sawa na kueleta faraka, fitna na malumbano yasiyo na maana miongoni mwa makundi mbalimbali ya Waislamu.

    Pengine nianze kwa kusema kuwa hoja kama hizi zinatoa somo moja kubwa na muhimu sana kwa Waislamu: Kwamba maadui wa Uislamu hawalali na wameshafanya kazi kubwa sana. Tunavyostuka hivi sasa, ni kuwa inavyoonyesha kumeshafanyika kazi kubwa sana ya kusambaza mawakala (agents ) ambao wamefanikiwa kupandikiza sumu na kukoroga bongo za Waislamu kiasi cha kuleta kuchanganyikiwa kukubwa.

    Lakini pia kuna mambo mengi yenye utata mkubwa. Jaaliya kuwa mahali fulani wanaibuka watu na kusimama katika mimbari za Misikiti wakihamasisha watu kushika silaha kupambana na wasio Waislamu. Jaaliya kuwa watu hawa wanatokea kuhubiri kuwa ni halali Muislamu kupora mali ya kafiri!!! Mwelekeo na mahubiri ambayo kwa hakika yanakuwa sawa na kuwachochea watu wafanye yale yanayofanywa

    na Boko Haram kule Nigeria-kuwavamia watu (Wakristo na hata Waislamu wasio kubaliana nao) na kupora mali zao na kisha kuwauwa. Swali ni je, ikitokea watu hawa wakafanya kazi hii kwa kiasi mwaka mzima bila jamii kuwachukulia hatua, nini itakuwa tafsiri ya kitendo hicho cha jamii

    na hasa vyombo vya dola kukaa kimya? Je, inawezekana katika nchi yoyote kufanyika mambo kama hayo, serikali isijue? Na kama itakuwa inajua, swali ni je, kwa nini watu kama hao waachwe wadumu na mahubiri yao mpaka kupata wafuasi kisha baadae ndio zije operesheni za kamatakamata?

    Ni jambo lililo wazi kuwa hawa IS waliandaliwa, kupewa mafunzo, silaha na fedha na hao hao wanaokusanyana leo kuunda muungano wa kuwapiga IS hivi sasa. Je, hatuoni kuwa iwapo tulikuwa tukiwasikia watu wakitoa mahubiri ya ki-IS na hatukuchukua hatua, hii yaweza kutafsirika kuwa na sisi huku tulibeba jukumu la kushiriki katika hii Crusade ya kuangamiza Waislamu, kwa kuwapa fursa hawa akina Abu Fulani, ambao ni wenzao na akina Abu Baghdadi, kukamilisha uwakala wao unaolenga kusimika uwepo wa kitisho cha ugaidi ndio tuanze kuwakamata na kutoa fursa ya kuingiza waliokuwemo na wasio kuwemo?

    Lakini jingine la kutaja hapa ni kuwa siri iliyo nyuma katika kuicha IS ifanye iliyofanya na sasa kuanza kuipiga ndani ya Iraq na Syria, sio siri tena. Inajulikana wazi kuwa ni katika kuzisambatarisha nchi za Mashariki ya Kati, kuzichangua, na kuweka mazingira mazuri ya kupora mali kuzinufaisha Israel na mabeberu wa Marekani na Ulaya.

    Iwapo jamii yetu itakubali kuwalea akina Abu Baghdadi waliotumwa huku kwetu, halafu baadae ndio ije na mkakati wa operesheni kamatakamata na kuchukua hatua za kushadidia uwepo wa kitisho cha ugaidi, ni lazima ijue kuwa inachofanya ni kuita machafuko, mauwaji zaidi na kukaribisha drones na hatua nyingine zitakazowapa mabeberu kisingizio cha kutuvuruga zaidi na wao kutandaza makucha yao

    RAIS wa Syria, Dkt. Bashar al Asaad (katikati).

    Inaendelea Uk. 11

    WAPIGANAJI wa ISIS.

  • 10 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 2014Makala

    I K I WA n i s i k u r a s m i ya upigaji kura kwa wajumbe wa bunge maalum la Katiba kuridhia ama kutoridhia katiba inayopendekezwa, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alijitokeza hadharani kulitolea ufafanuzi suala la Mahakama ya Kadhi ambalo lilikuwa limeanza kulitafuna Bunge hilo baada ya wajumbe kadhaa Waislamu kutishia kukwamisha rasimu hiyo ya katiba.

    Alipokaribishwa kuzungumzia hilo tangu awali wa taarifa yake nilijua tu kabisa hakuna mahakama ya kadhi kwenye katiba kwa ule ule wimbo wa kutenganisha shughuli za dini na serikali, kwamba serikali haina dini, ila wakati wa shida zao wanarudi kwa viongozi wa dini kuwalilia kuhusu mambo hayo hayo ya serikali.

    Waislamu wakitaka ushirikiano wa kiuchumi na mashirika ya kimataifa kama Organisation of Islamic Conference (OIC), kupata fedha za misaada n.k kutoka Uarabuni, serikali inaingilia kati na kukemea vikali, Waislamu wanayakumbuka ya Zanzibar na OIC , East African Muslim Walfare Society (EAMWS) pamoja na aliekuwa mlezi (patron) wake mkuu Agha Khan.

    Ila kabla hatujaangalia kiundani maelezo na tamko la Waziri Mkuu Pinda pia maswali tata yanayojitokeza, naomba nianze na historia hii fupi ya hapo mwaka 2012 wakati viongozi wa Kiislamu na waumini wao walipoishinikiza serikali kuweka kipengele cha dini katika kuhesabu sensa ili kuondoa ule mkanganyiko uliofanywa na baadhi ya Taasisi na shirika la utangazaji la Tanzania (TBC) kwamba Wakristo ni wengi kuliko Waislamu.

    Kwa muda mrefu hoja nyingi za kutaka kipengele hicho kiwekwe zilitolewa, majadiliano yakafanyika baina ya viongozi wa Kiislamu na serikali, ikawa mikikimiki, wakati wote huu hakuna kiongozi mkuu wa nchi, Rais, makamu wake na hata Waziri Mkuu alijitokeza hadharani kulitolea ufafanuzi.

    Siku za lala salama ndipo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete akajitokeza hadharani katika hali ya huzuni na unyenyekevu mkubwa kuwalilia Waislamu wajitokeze kujiandikisha kwenye sensa.

    Hoja kuu ya Rais Kikwete katika kuwashawishi Waislamu

    Kutoka sensa hadi Mahakama ya kadhi, mchezo ni ule uleNa Yusufu Ahmadi

    kujiandikisha kwenye sensa i k a w a k w a m b a t a k w i m u zitakazopatikana ndio zitatumika katika kupata kitambulisho cha uraia ambacho pia kitakuwa kikitumika katika kupigia kura katika chaguzi mbalimbali za hapa nchini n.k.

    Wapo walioitika wito kwa kuhesabiwa baada ya ushawishi wa Rais na kuhofia kutopata vitambulisho vya uraia , na wengine kwa hofu ya kuchukuliwa hatua za kisheria kwani wapo waliokamatwa kwa hatua za kususia mchakato ule.

    Baadhi ya watu nikiwemo mimi, tulijiuliza wakati wote ule wa vuta ni kuvute Rais alikuwa wapi kulizungumzia jambo hili, wapo waliosema aliwaachia wasaidizi wake, hoja ikawa suala lile lilikuwa ni zito na hata hivyo wasaidizi wengi wa serikalini hawaaminiki siku hizi, kwani kauli zao nyingi zinazotolewa ni za kugongana.

    Mchakato ukapita japo wapo ambao hawakujiandikisha katika sensa , ndio maana baadhi ya watu wanasema hata takwimu zilizopatikana mfano wa idadi ya watu kuwa tupo takribani milioni 45 zina kasoro kutokana na baadhi ya Waislamu kususia.

    Leo hii vitambulisho vya Uraia vinatolewa, aliyehesabu sensa, hakuhesabu wote wanapewa, sijui tatizo lilitokea wapi mpaka takwimu za sensa hazitumiki katika zoezi hili kama ilivyoelezwa na Rais Jakaya Kikwete katika hotuba yake ile.

    Kisa kama hicho nakilinganisha na hiki cha Waziri Mkuu Pinda, wakati huu ikiwa ni suala zima la kuingizwa kwa mahakama ya kadhi kwenye katiba mpya ambapo Waislam walipiga kelele sana mahakama hiyo kuwemo ndani yake huku wengine wakipinga hilo.

    Kama ilivyokuwa kwa zoezi la sensa, ndivyo imekuwa katika mchakato wa katiba mpya ambapo hoja mbali mbali kutoka kwa Waislamu zililitolewa, mivutano ikatokea ndani ya bunge maalum la katiba kutaka kipengele cha mahakama hiyo iingizwe kwenye katiba.

    Waislam wakatoa hoja nyingi tu, moja wapo ni ile ya kwamba, kutaka kwao mahakama ya kadhi kuwemo kwenye katiba ni kuwezesha hukumu zinazotolewa na mahakama hiyo zinakuwa na nguvu za k i sher ia p ia zinaheshimiwa na mahakama za kawaida, kwani ilionekana hukumu hizo zikipelekwa katika mahakama za kawaida zinakuwa ni batili.

    Muda wote huo wa mvutano hakuna kiongozi mkuu yeyote wa nchi aliejitokeza hadharani kulitolea ufafanuzi, badala yake Kama ilivyokuwa kwa Rais Kikwete kujitokeza siku za lala salama za sensa, ndio kafanya Waziri Mkuu Pinda, kachomoza hadharani kuzungumzia suala hilo siku rasmi ya upigaji kura kama nilivyosema awali.

    Kwa mujibu wa Pinda, ambae ofisi yake ilipewa jukumu la kulishughulikia suala hilo, aliwaambia wajumbe wa Bunge na Umma kwamba wamekubaliana na Masheikh kuwa wataliingiza suala hilo katika Sheria ya Mahakimu sura ya 11 na Sheria ya Kiislamu sura ya 375 ambapo zitafanyiwa marekebisho ili kutambua uamuzi wa Mahakama ya Kadhi.

    N a k w a m b a o f i s i y a k e inaenda kuzipitia sheria hizo ili kuziboresha na kisha kuja nazo katika Bunge la Januari mwakani ili zijadiliwe na kupitiwa na wabunge kabla ya kuwa sheria rasmi baada ya Rais Kikwete kutia saini yake.

    Taarifa na ahadi ya Waziri Mkuu inazua maswali kadhaa na muhimu ya kujiuliza kwa Waislamu wote, kwa nini Waziri Mkuu kama alivyofanya Rais Kikwete amejitokeza siku ya kupigia kura katiba iliokuwa inapendekezwa na Bunge, siku zote za mivutano alikuwa wapi?

    Waziri Mkuu kakiri kuwa suala

    Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

    hilo limo ofisini mwake tangu mwaka 2005 , sasa ni takribani miaka saba imepita, ina maana ofisi yake ilikuwa haijajua tatizo liko wapi, wiki iliopita ndio kweli wamefahamu kwamba kwa nini Waislamu wanataka mahakama ya kadhi kuwemo kwenye katiba?

    Naikumbukwe suala hi l i halijaanza katika utawala wa awamu hii ya nne, tangu enzi za Rais Mstaafu Benjamini Mkapa lilikuwepo na tume iliundwa, japo Waziri Mkuu Pinda hakurejea yaliokuwemo ndani ya tume ile kujua sababu?

    Je, tukisema lengo la Waziri Mkuu Pinda lilikuwa nikulainisha tu mioyo ya baadhi ya wajumbe wa Kiislamu ambao walitishia kupiga kura ya Hapana kama mahakama ya kadhi isingeingizwa kwenye katiba na badala yake waipigie kura ya Ndio kuepusha kukwama kwa katiba iliokuwa inapendekezwa, tu takuwa tunakosea? Jambo ambalo lilifanikiwa kwani walilainika haswaa.

    Je, ni kweli Pinda na serikali yake wana nia ya dhati ya kuwapa Waislamu mahakama ya kadhi ilio na meno makali kama anavyosema, au na yeye anasogeza siku tu mbele ili amalize muda wake atue mzigo chini amuachie atakaekuja?

    Nimshauri na kumsihi Waziri Mkuu Mizengo Pinda kama alivyoambiwa pale Bungeni na Sheikh Masoud Jongo kwamba wao (viongozi wa dini ya Kiislamu) hawawezi kubeba dhamira ya Waislamu, kazi yao ni kushawishi tu waumini wao.

    Hivyo basi atambue kuwa nia ya Waislamu kudai mahakama ya kadhi yenye meno makali sawa na mahakama zingine kamwe haitakufa.

    Kama tamko lile lilikuwa ni geresha tu ya kuwafanya wajumbe wa Kiislamu wapigie kura ya Ndio ili katiba iliokuwa inapendekezwa ipite, akumbuke yeye atapita ila maandiko yatabaki milele katika mioyo ya Waislamu ikibeba wito wa mahakama ya kadhi yenye uhai.

    Ni ukweli sasa mahakama y a k a d h i k w e n y e k a t i b a haiwezekani,na wanaosubiri Januari 2015 kwamba ndio watapata mahakama hiyo yenye nguvu kwa kuwemo kwenye sheria za kawaida, wasubiri tu, kwangu mimi ni ndoto!

    Si walisema Zanzibar itoke OIC ili Tanzania ijiunge. Kiko wapi! Kama hatutaamka na kutanabahi, tutafanywa madaraja ya kupitishia mambo ya wengine daima.

    Ahsanteni.

  • 11 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 2014Makala

    Inaendelea Uk. 13

    Tumemeza al Qaida, ISISBoko Haram, al Shabab

    Inatoka Uk. 9al-Fadhli, posed a more direct threat to America and Europe.

    Inadaiwa kuwa huyu Muhsin al-Fadhli, alikuwa mmoja wa viongozi waandamizi wa al Qaeda akiwa karibu sana na Osama Bin Laden, na kwamba yeye ni katika watu wachache waliokuwa wakijua mipango ya siri ya shambulio la Septemba 11, 2001 kabla shambulio halijafanyika.

    P r o p a g a n d a i l i e n d e l e a kukolezwa na mwandishi Richard Engel wa NBC News akiungana na Brian Williams, kuleta madai ya adui mpya-The New Enemy, ambapo Engel akidai kunukuu vyanzo kutoka duru za kiusalama za Marekani alisema kuwa:

    Khorstan is considered a threat to the U.S. because, U.S. intelligence officials say, it wants to bring down airplanes with explosives.

    Akimaanisha kuwa maadui hao wapya wana lengo la kulipua ndege za abiria na hivyo wanakuwa tishio kwa Marekani.

    Hebu soma nukuu zifuatazo: The United States also pounded a little-known but well-resourced al-Qaeda cell that some American officials fear could pose a direct threat to the United States. (The Washington Post)

    Among the targets of U.S. strikes across Syria early Tuesday was the Khorasan Group. The group was actively plotting against a U.S. homeland target and Western targets, a senior U.S. official told CNN on Tuesday. (CNN)

    There were indications that the militants had obtained materials and were working on new improvised explosive devices that would be hard to detect, including common hand-held electronic devices and airplane carry-on items such as toiletries.

    Osama Bin Laden.(U.S. official)

    We hit them last night out of a concern that they were getting close to an execution date of some of the plans that we have seen. (U.S.A Attorney General Eric Holder.)

    Nimeweka nukuu hizi i l i kutopotosha maana kwa tafsiri kuonyesha kinachopikwa na kupangwa hivi sasa. Tunaletewa

    gaidi mpya Khorasan Group, ambaye tunaambiwa kuwa huyu ni kitisho cha uhakika na cha sasa hivi kwa Marekani. Na kwamba hao ni wataalamu wa kutengeneza milipuko kulipua ndege za abiria za Marekani na Ulaya na kwamba wanaweza kuingia na milipuko hiyo katika ndege bila kutambulika kutokana

    na walivyoitengeneza kitaalamu!Kinachotafutwa hapa ni kile

    tulichoeleza mwanzoni. Moja, kitisho hicho kitawafanya watu wa Marekani kuiunga mkono serikali yao.

    La pili, ni kujenga mazingira ya kupata kibali kutoka Umoja wa Mataifa kama kilivyopatikana kile cha kuipiga Afghanistan. Kama mkakati huo utaonekana kuwa utazaa matokeo yanayotakiwa, h a p a n a s h a k a u t a e n d e l e a kupigiwa debe mpaka na sisi huku tutaimbishwa. Vyombo vya usalama vitakwenda mbio kuwasaka Khorasan Group. Na si ajabu zikawekwa taratibu mpya za ukaguzi wa usalama katika viwanja vya ndege. Hiyo ikiwa ni pamoja na kulazimishwa kuweka mitambo mipya itakayoamuliwa na mabeberu na tutainunua kwa bei watakayoweka mabeberu. Ukiacha ndege zinazuiwa kutua katika viwanja vyako. Mabeberu wananeemeka.

    Lakini usije ukashangaa pia kukuta vi jana wa Kiislamu wakishabikia kuwa wao ni Mujahidina wa Khorasan Group. Unajua sababu yake nini?

    Khorsan n i j ina la eneo la kihistoria linalounganisha Kaskazini mwa Iran, Turkmenistan ya Kusini na Kaskazini mwa Afghanistan. Ni eneo lililokuwa toka utawala wa Sasania kule Iran (Sasanian dynasty), jina hilo likimaanisha (Ardhi ya Jua) kwa vile ilikuwa upande wa Mashariki wa utawala huo. Wakati wa utawala wa Kiislamu chini ya Umayyah (Umayyad Caliphate), Khorsan ilikuwa moja ya maeneo ya utawala huo iliyostawi sana. Ipo Hadith yenye utata ambayo inadai kuwa Mtume (s.a.w) alitabiri

    Inatoka Uk. 13

    Mauaji kushoto kuliaInatoka Uk. 9ya ubeberu. Hili tukilifahamu, nadhani tunaweza kuwa makini zaidi tusije kuwa vibaraka na mamluki wa kuangamiza nchi zetu kwa mikono yetu wenyewe tukidhani tunapambana na ugaidi.

    Haihitaji kuwa razini sana kufichua uwongo

    Labda tujiulize, hivi kuna mtu mwenye aki l i t imamu anayeamini yale tuliyoambiwa juu ya Westgate Kenya au zile porojo za Bring Back Our Girls kule Nigeria? Wasichana 270 wamepotelea porini mpaka leo hawajapatikana-nchi ambayo ina serikali, polisi, usalama wa taifa na jeshi!! Usanii wa ki-Hollywood uliovunja rekodi. Hivi wataalamu wetu, wanausalama wetu na viongozi wetu, wanapokutana (au pengine tutumie maneno wanapokutanishwa na hawa viranja wa vita dhidi ya ugaidi d u n i a n i ) k u j a d i l i m a m b o yanayofanana na porojo hizi za Bring Back Our Girls na kisha kuibuka na kauli kalikali, wanajisikiaje?

    Tuache kuisingizia mambo Quran, Suna

    Jambo la pili linalojitokeza katika hoja zinazotolewa na baadhi ya Waislamu, inaonesha kuwa wengi wanaojidai kufuata Quran na Sunna au kuja na hoja kuwa jambo fulani halipo katika Quran na sunna, hata hiyo Quran yenyewe hawaisomi au kama wanaisoma, huisoma kibubusa.

    Inadaiwa kuwa Boko Haram na IS wanataka kusimamisha Khilafah, kwa maana ya Dola ya Kiislamu. Lakini taarifa tunazopewa kupitia vyombo vya habari na kupitia mitandao yao, ni za utekaji nyara, mauwaji, kuchinja watu, iwe ni Wakristo au Wais lamu wanaodaiwa kutokukubaliana nao. Ukiacha taarifa za vyombo vya habari, kuna video mbalimbali zinarekodiwa na wanaodaiwa kuwa viongozi wa Boko Haram na IS wakitoa taarifa za harakati zao wakithibitisha kuwa wamefanya mauwaji haya

    na yale na kutoa picha za watu waliowauwa.

    Katika tukio la kutekwa mabinti wa shule Nigeria, anaonekana anayedaiwa kuwa kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau akiwa kasimama na bendera yenye maandishi ya kalima tawheed akitangaza kuwa wasichana aliowateka amewasilimisha kwa nguvu na kutishia kuwauwa wanaokataa kusilimu. Kwa IS ni hivyo hivyo, wanarekodi picha za video wakichinja watu na kuziingiza katika mtandao wakidai ni katika harakati zao za kusimamisha Khilafah.

    Kuna namna mbil i tu za kuzipokea habari hizi. Moja, ni kuamini kuwa yaliyosemwa ni kweli. Ukijaaliya hivyo, sasa jiulize je, mambo haya yanakubalika katika Uislamu? Kwamba katika kusimamisha Khilafah, unapita mtaa kwa mtaa, kijiji kwa kijiji, mji kwa mji, ukiuwa na kuchinja watu? Jibu ni hapana.

    Namna ya pili ni kujaaliya kuwa

    hata kama kuna watu wanajiita IS wenye lengo la kusimamisha Dola ya Kiislamu, lakini sio wanaofanya vitendo hivyo. Wanasingiziwa tu. Ukijaaliya hivyo, lazima uje na taarifa mbadala ukionyesha wanachosema na wanachofanya IS. Mpaka sasa hakuna taarifa hata moja kutoka IS inayowaonyesha wakikanusha kuwa wao sio wanaofanya mauwaji hayo na wala zinazoonyesha mambo mazuri wanayofanya katika miji waliyodaiwa kuteka. Ila kilichopo ni taarifa zao wenyewe, zikiwemo za video walizojirekodi, wakithibitisha kufanya mauwaji hayo. Lakini pia ukijaaliya kuwa taarifa hizo ni uwongo, akili ya kawaida tu itakutuma kujua kuwa majina haya kama IS na madai ya kusimamisha Khilafah yakiambatanishwa na matendo mabaya ya mauwaji ya kikatili, yanatumiwa kama propaganda ya kuupaka matope Uislamu na kuutafutia sababu ya kuuangamiza. Kwa hiyo, haitakuwa busara kushabikia msamiati huo.

    Sasa leo anapoibuka Muislamu na kuja na hoja kuwa IS/Boko

  • 12 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 201412 Makala/Mashairi/Tangazo

    Inatoka Uk. 6

    Masheikh wapo Golgothakama ilivyokuwa Sodoma na Gomora, ujumbe huo aliousoma Rais Bush, ni muhimu sana hasa kwa vile ndio uliokuwa ujumbe wa utangulizi kabla ya Mungu kuziangamiza Sodoma na Gomora . Hivyo bila shaka ni ishara nyingine ya Mungu kuangamiza tena kizazi hiki kiovu na uovu wake.

    (Kizazi kiovu hapo ni Wairaki, Waislamu na Uislamu wao.)

    Mchungaji Teghua anachokieleza hapo ni imani yao kama Wakristo Walokole, k u wa wa - I r a k i n a Waislamu popote walipo wanaonekana katika imani na macho yao kuwa ni mapepo yaani mashetani, hivyo ni wa kuangamizwa kama wal ivyoangamizwa watu wa Sodoma na G o m o r a , n a B u s h ( M a r e k a n i ) n d i o kachaguliwa kufanya kazi hiyo.

    Ni vizuri ninukuu zile aya ambazo Rais Bush alizisoma, na mchungaji

    akazinukuu kwa kifupi ili msomaji asiye na Biblia aelewe mtazamo na malengo ya Mlokole Bush, wachungaji na Crusades zao:

    K i s h a wa t u h a o w a k a o n d o k a h u k o wakaelekeza nyuso zao Sodoma . I b ramhimu akaenda pamoja nao awasindikize. BWANA (Mungu) akasema, Je! Nimf i che Ibrah imu jambo hili nilifanyalo? Akiwa Ibrahimu atakuwa tai fa kuu, hodari na katika yeye mataifa ya dunia watabarikiwa? Kwa maana nimejua yakwamba atawaamuru wanawe, na nyumba yake baada yake waishike njia ya BWANA wafanye haki na hukumu, ili kwamba BWANA naye akamtimizie Ibrahimu ahadi zake. (Mw. 18:16-19).

    Tujiulize, maneno hayo hapo juu, kwa mujibu wa imani ya Wakristo, yameandikwa na Nabii Musa A.S. na yamepitia kwa manabii wengi wa wana wa

    Israe l i , na dini ya Kikristo inatokana na msingi wa kitabu cha Torati, na Rais Bush na Mchungaji Teghua ni wafuasi wa Neno la Mungu tena walokole, kwa maana ya kuwa h a w a n a d h a m b i ; Je! Kuishika njia ya BWANA (Mungu) ndio huko kuwaangamiza wa Iraki na Waislamu katika nchi zao?

    I n a v y o o n e k a n a k i n a c h o w a s i b u W a i s l a m u n a Masheikh duniani kote wa n a o b a m b i k i wa t u h u m a z a u g a i d i kisha kudhalilishwa kwa mateso na hata kunajisiwa na matendo mengine ya kishenzi, ni katika muendelezo wa vita ileile iliyoasisiwa na Albano, akina Bush ni warithi tu.

    Ni Golgotha ileile ya Warumi. Unamtesa mtu, huridhiki mpaka unamtia majiti sehemu zake za siri!!!

    P.O. BOX 80059, TEL: 022-2860694, 0754/ 0655-462777, 0754-377897 DAR ES SALAAM (TZ)

    QURAN, TAALUMA , MAADILI.

    PRE-FORM-ONE 2015.MASOMO YATAANZA TAREHE 14/10/2014 (SIKU YA INTERVIEW) HADI

    14/12/2014.

    MASOMO YATAKAYOFUNDISHWA NI QURAN, MATHEMATICS, MAARIFA YA UISLAM NA KIINGEREZA.

    WANAFUNZI WATAKAA BWENI (BOADING).

    MAHITAJI: MAVAZI YA KIISLAM, MADAFTARI (HARD COVER), MAS-HAF AU JUZUU NA MAHITAJI YA KUMUWEZESHA KUKAA BWENI.

    ADA KWA MUDA WOTE HUO NI T.SHS 200,000/= TU.

    KWA WANAFUNZI WALIOMALIZA DARASA LA SABA (7) DAARUL-ARQAM SCHOOLS WATASOMA BURE.

    USAILI (INTERVIEW) 2015.USAILI KWA WANAFUNZI WA SHULE YA AWALI, MSINGI NA SEKONDARI

    (2015) ITAFANYIKA SHULENI DAARUL ARQAM KIGAMBONI DSM JUMANNE TAREHE 14/10/2014 (NYERERE DAY) SAA 2 ASUBUHI. FORM NI TSHS 10,000/= TU.

    SIMU 0717 190 242 AU 0658 190 079.

    DAARUL ARQAM SCHOOLS

    Leo siku ashirafu, ARAFA iso na shaka,Mahujaji twawashufu, ALLAH wakimuitika,Uwanja mtakatifu, "Allahumma labbaika",ARAFA siku tukufu, tuisharifu kwa FUNGA.

    Kutwa nzima watakifu, hapo pasipo kutoka,Ndaniye itasadifu, jua likishapinduka,Khutba njema zindufu, thuma swala kuswalika,ARAFA siku tukufu, tuisharifu kwa FUNGA.

    Kasi DHIKIRI sharifu, baadiya zitashika,Na kumuomba RAUFU, MAGHFIRA kadhalika,Pamwe na DUA lufufu, mpaka kughurubika,ARAFA siku tukufu, tuisharifu kwa FUNGA.

    ARAFA siku tukufu, kwa walo ndani ya Makka,Watangaa utukufu, wake na nje ya Makka,Kwa FUNGA tuusharifu, nasi tusokuwa Makka,ARAFA siku tukufu, tuisharifu kwa FUNGA.

    Tufanye udunduifu, wa fedha nasi kuweka,Kabla ya wetu ufu, tuweze hijja kufika,Kaditama kualifu, chini kalamu naweka,ARAFA siku tukufu, tuisharifu kwa FUNGA.Tuisharifu kwa FUNGA, siku hii ashirafu.

    ABUU NYAMKOMOGI-MWANZA.

    ARAFA (TUISHARIFU KWA FUNGA)

    IDD ! (SALAMU ZA IDD)Natakadamu za IDD, salamu zipokeeni,Kesho wala si baidi, nadharini tambueni,Tutakuwa kwenye IDD, kwa utashi wa MANANI,Natoa kwa ikhiwani, salamu zangu za IDD.Salamu zangu za IDD, vyema zizingatieni,Kuzitoa sina budi, kuzindua ikhiwani,Katika yote biladi, ya Bara na Visiwani,Natoa kwa ikhiwani, salamu zangu za IDD.Sinazo tumbi zawadi, za nyote kukutosheni,Kwa timilifu idadi, yenu pasi nuksani,Kwa hiyo nimeadidi, badala cha kukupeni,Natoa kwa ikhiwani, salamu zangu za IDD.

    Chazidi hata nukudi, na vito vyenye thamani,Si lulu wala zabadi, kadhalika marijani,Kwa ukumbusho wa IDD, vyote havioni ndani,Natoa kwa ikhiwani, salamu zangu za IDD.Mwapaswa siku ya IDD, kutambua nadharini,Kwa nuru ya tauhidi, si kwa kiza cha shetani,Kwamba kwetu sisi IDD, si siku ya kufurani,Natoa kwa ikhiwani, salamu zangu za IDD.Kwa hiyo hapana budi, ALLAH tumdhukuruni,Takbira na nyiradi, masnunu tuleteni,Kwa wingi tumhimidi, sikuyo kwa shukurani,Natoa kwa ikhiwani, salamu zangu za IDD.Tusijevuka hududi, kwa kumuasi MANANI,Kwa twaa tujitahidi, kumtii RAHMANI,Pamwe na kuikalidi, ruwaza yake Amini,Natoa kwa ikhiwani, salamu zangu za IDD.

    IDD siku ajwadi, kwa twaa furahikeni,Kadhalika mawaridi, majumba yenu pambeni,Yumkini hata nyudi, kwa ndani yafukizeni,Natoa kwa ikhiwani, salamu zangu za IDD.Maakuli kuadidi, fanzeni hima nyumbani,Vinywaji kuvifanidi, vya halali sharibuni,Sharubati za kutadi, mipaka ziepukeni,Natoa kwa ikhiwani, salamu zangu za IDD.Libasi zenu jadidi, za stara valieni,Jitanibuni na jadi, ya kujivika vimini,Nanyi Abuu na Iddi, kata 'kei' ziacheni,Natoa kwa ikhiwani, salamu zangu za IDD.Zingatieni hududi, ya filamu runingani,Kushufu picha za 'nyudi', si wetu utamaduni,Kikoa tuzikaidi, 'ponografi' kwa kani,Natoa kwa ikhiwani, salamu zangu za IDD.Kadhalika ukuwadi, wa fulani kwa fulani,Nayo siyo yetu jadi, kuunganisha wahuni,Wanomuasi WADUDI, kwa zinaa pasi soni,Natoa kwa ikhiwani, salamu zangu za IDD.IDD ni siku saidi, si ya kwenda uzinzini,Wala si ya kufisidi, ajisadi ulevini,Au ya shari kuzidi, na kukesha madansini,Natoa kwa ikhiwani, salamu zangu za IDD.

    'Kiasi siku ya IDD, ja kwamba mahasharini,Ikabuyo i shadidi, akhera yaumu-dini,Juludiyo 'tajadidi, iyeyukapo narini,Natoa kwa ikhiwani, salamu zangu za IDD.

    Sinayo mengi zaidi, kwa twaa sururikeni,Ikiwa bado ahadi, tutakutana mwakani,Khamsashara sizidi, kalamu naweka chini,Salamu zidurusuni, za IDD kwa irishadi.

    ABUU NYAMKOMOGI-MWANZA.

  • 13 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 2014MAKALA/TANGAZO

    Tumemeza al Qaida, ISIS Boko Haram, al ShababInatoka Uk. 11akisema kuwa Bendera Nyeusi zitasimama kutokea Khursan na hakuna atakayeweza kuzizuiya mpaka zisimamishwe pia Ayliya (Bayt al-Maqdis).

    Hadi th hiyo inayodaiwa kusimuliwa na Ahmad, at-Tirmidhi na Nu'aym ibn Hammad, inadaiwa kusimuliwa na Abu Hurayrah.

    Kwa kuwepo Hadith hii, hapana shaka utaona kuwa makafiri mabeberu wamefanya kazi yao vizuri. Wanajua kuwa vijana wa Kiislamu watashabikia jina hili Khorsan kwa vile lipo katika Hadith inayotabiri kuwa Uislamu

    utasimama kuanzia mahali hapo. Na ndio maana unaona pia hata bendera za ISIS ni nyeusi zikiwa na Kalma Tawheed.

    Muhimu hapa s io kuwa Hadith hiyo ni sahihi au la, lakini mambo manne. Moja ni kuwa hao Khorasan Group hawapo Syria na hata kama wakitokea kuwepo watu wakijiita jina hilo, watakuwa wa kupanga kama yule mtoto na kigeleni chake cha mafuta ya taa aliyedaiwa kutaka kulipua Ubalozi mmoja maarufu Jijini Dar es Salaam.

    Pili, magaidi hawa wapya wa n a b u n i wa i l i k u t a f u t a kisingizio na sababu ya mabeberu

    kuendeleza vita yao Syria ili kumngoa Bashar Assad (another regime change).

    Ta t u , m a k a f i r i h a wa l a l i na wanapopanga mambo yao hufanya utafiti na kulenga mahali na kwa namna ambayo kama akili hazikutumika, inakuwa vigumu sana kutambua kwa haraka ulaghai wao. Tizama walivyochagua jina Khorasan lililotajwa katika Hadith ya Abu Huraira kuwa ndio mahali bendera ya Uislamu itakapoanza kusimama!

    Nne, baadhi ya watafiti kama Will McCants wa Brookings Institute, anasema kuwa utabiri

    huu unahusu mapinduzi ya wakati wa Abbasid karne ya 8 (Abbasid revolution), mapinduzi yaliyoanzia Khorasan, ambapo himaya ya Waarabu iliporomoka, utawala wa Kiislamu ukawa mikononi mwa wasiokuwa Waarabu. Lakini hata ukijaaliya kuwa Hadith hiyo ni sahihi na inatabiri kuibuka upya kwa utawala wa Kiislamu katika zama hizi, bado ukweli utabaki kuwa hao Khorasan Group hawapo hivi sasa na hawana huo ujuzi wanaodaiwa kuwa nao wa mabomu yanayotishia usalama wa ndege za abiria za Amerika na Ulaya.

    Mauaji kushoto kuliaInatoka Uk. 11Haram, wana lengo zuri la kusimamisha Uislamu wasisemwe vibaya, lazima mtu uhoji uwezo wa akili ya mtu kama huyo. Ni kama vile katika baadhi ya kesi mahakamani hutokezea zikafutwa kama watu watatuhumu kama mtuhumiwa hayuko barabara kiakili na dakitari akathibitisha hilo. Ila sasa kwa muktadha huu, jambo hili si jepesi kiasi hicho kwa sababu madhara yake ni makubwa mno kijamii. Waislamu wasiwachukulie watu hawa kuwa ni maadhura wakawaacha, ni lazima watafute namna ya kuwatibu na kuhakikisha kuwa hawaleti madhara kwa jamii ya Waislamu na nchi kwa ujumla. Hawa watakuwa wamefikishwa mbali. Watakuwa wamekorogwa vya kutosha na wale akina Abu Fulani, walioachiwa wakafanya kazi yao ya uwakala, baadae ndio tunakurupuka kuendesha operesheni za kuwasaka na kuwakamata!!!

    Wapo wasomi waliotimiza wajibu wao, siri wamefichua

    Wasomi na watafiti wengi wameandika sana juu ya hatari ya hawa mawakala na vifaa vya mabeberu-IS na Boko Haram. Lakini unapowanukuu katika zile tahadhari zao wanazotoa, baadhi ya vijana wetu, watakuambia kuwa unanukuu makafiri badala ya kuleta ushahidi wa Quran na Sunna. Namna yake ni kama unakutana njiani na John anakuambia ndugu yangu, hapo mbele kuna joka kubwa au kuna vibaka usipite, unasema mimi sisikilizi la kafiri nafuata Quran na Sunna! Sasa huu ni ujinga na kuisingizia Quran. Niliwahi kutoa mfano nikasema kuwa wanaotoa hoja hizi wachukue sumu ya cynide au sumu yoyote, watizame maelezo yake, wakiona kuwa anayetoa tahadhari juu ya sumu hiyo sio Muislamu na wala maelezo ya sumu hiyo hayapo

    kwenye Quran na Sunna, basi wanywe.

    Nihitimishe kwa kusema kuwa ukitizama hoja nilizozijadili hapa kama zinavyotolewa na baadhi ya vijana wa Kiislamu, zinabainisha mambo makubwa matatu. Moja ni kuwa mawakala wa mabeberu makafiri, wamefanikiwa sana kutukoroga, sasa wanavuna. Kwa upande mmoja wamefanikiwa kupandik iza f ikra potofu , sasa Waislamu wanakorogana wenyewe kwa wenyewe. Pili, baada ya kuchanganyikiwa huko, sasa Waislamu wanatumika kumal izana wenyewe kwa wenyewe kwa manufaa ya kafiri. Wanauwana Syria, Libya, Iraq na kwengineko. Wamefanikiwa pia kupandikiza kitisho cha ugaidi katika nchi zetu, sasa baadhi ya watu wapo ndani wakisubiri kesi zao huku kukiwa na madai ya kudhalilishwa Masheikh waliounganishwa katika kesi hizi.

    Tatu, ni kuwa mjadala huu u n a o n y e s h a k u wa u j i n g a miongoni mwetu ni mkubwa sana. Mtu anakuja na hoja kuwa hawezi kusikiliza la kutoka kwa kafiri, lakini kavaa kilemba, kaptura na kanzu iliyotengenezwa na elimu (kutoka kwa Allah) iliyofanyiwa utafiti na ugunduzi, ama na Muislamu au wasio kuwa Waislamu ikawezesha kupatikana mitambo ya kucheza na Pamba ya Msukuma mpaka ikatoa nguo. Lakini kavaa kilemba na kanzu au kikoi, ambavyo vingi vinatoka China, Thailand, Indonesia na nchi zisizokuwa za Waislamu. Badala ya kuhimiza Waislamu kusoma taaluma hizi ili hatimaye viwanda kama vya nguo na vitu mbalimbali vizalishwe na Waislamu, ili kukuza uchumi wa Waislamu; unakuja na hoja lemavu za kusema elimu ni za kikafiri ambapo maana yake ni kuwa utaendelea kununua

    kanzu na pensi yako (suruali fupi ya kufika magotini ila kidogo), ki lemba na kizibao kutoka

    viwanda vya makafiri na hivyo kuzidi kuwatajirisha!

    Au t u s e m e m w i s h o wa mawaidha haya ya elimu za kikafiri ni kuvua na nguo z i l i z o t o k a n a n a t a a l u m a (zinazosingiziwa kuwa) za kikafiri na kutembea uchi?

  • 14 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 3-9, 2014Makala

    Uchakachuaji wa Aqida ya Kiislamu - 2Na Said Rajab

    KAMA tulivyoona kwenye makala ya mwanzo, uwepo wa fikra za kikafiri kwenye jamii, umekuwa kikwazo kikubwa katika njia ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu. Na kuongeza chumvi kwenye kidonda , f ikra hizo zinasimamiwa na kunezwa na wanaharakati wa Kiislamu na makundi yao. Wakati umefika kwa Waislamu wenye ufahamu, walio waadilifu na wanaomuogopa Mwenyezi Mungu, kuendesha harakati za kusimamisha Uislamu kama alivyofanya Mtume wa Mwenyezi Mungu. Waondoe fikra hizo potofu kutoka kwenye nyoyo na fikra za Waislamu. Wale wanaolingania Uislamu kama vitendo binafsi vya Ibada (rituals) lazima wafahamishwe na waelewe kwamba Uislamu ni mfumo kamili wa maisha na dini iliyokusanya nyanja zote:

    "Si maneno yaliyozuliwa, bali ni hakikisho la yale yaliyokuwa kabla yake (miongoni mwa vitabu vingine vya Mwenyezi Mungu) na ni maelezo juu ya kila kitu..." Qur(12:111).

    "Na tumekuteremshia Kitabu hiki kielezacho kila kitu..." Qur(16:89)

    Na lazima Waislamu wazingatie kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuagiza kuuchukua Uislamu wote kama ulivyo na siyo vipande vipande, na tena amewalaani Waislamu wanaofanya hivyo:

    "Enyi Mlioamini! Ingieni katika hukumu za Uislamu zote,wala msifuate nyayo za Shetani; kwa hakika yeye kwenu ni adui dhahiri" Qur(2:208).

    "Je? Mnaamini baadhi ya Kitabu na kukataa baadhi (yake)? Basi hakuna malipo kwa mwenye kufanya haya katika nyinyi ila fedheha katika maisha ya dunia; na siku ya Kiyama watapele