ANNUUR 1142

16
ISSN 0856 - 3861 Na. 1142 DHULQAAD, IJUMAA , SEPTEMBA 12-18, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu www.annuurpapers.co.tz Jamani Zanzibar hakuna magaidi! Zanzibar kuna watu wanaotaka mamlaka kamili ya nchi yao. Muundo wa Muungano wa Serikali mbili, unalenga kuitia kitanzi Zanzibar kama nchi. Masheikh wa Uamsho waligundua hilo na walisimama kidete kuidai Mtuhumiwa wa ugaidi akatwa mguu Yadaiwa ni kutokana na mateso ya kutisha Mwingine mahututi, asomewa kesi kitandani Waislamu wawasilisha malalamiko Ikulu Hiyo ndiyo gharama ya kutaka Zanzibar huru! Hata Mzee Aboud Jumbe yalimkuta Alikwenda Dodoma Rais akarudi raia Fitna hii Kisonge kwa faida ya nani? Zanzibar yao huru. Masheikh hao, siyo wa kwanza kupata misukosuko kutokana na kuidai Zanzibar huru. Hata Mzee Aboud Jumbe alipohoji tu muundo tata wa Muungano wa Serikali mbili alionja joto ya jiwe! (Soma uk. 8) Sheikh Bassaleh ataka Serikali ichukue hatua Asema aliyofichua Farid ni mazito Kongamano Kichangani Jumapili Uk. 4 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Uhusiano, Mh. Steven Wasira. Sheikh Rajabu Katimba Hakuna kitu kinachowaliza wenye akili zaidi kuliko wasiwasi wa kuokoka na Moto na kupata Pepo! Hijja peke yake ndiyo inayoweza kumsafisha muislamu na madhambi yote, akarudi kama siku aliyozaliwa na mama yake, na akapata Pepo katika muda wa siku tano. Gharama zote ni Dola 4,500. Karibuni Ahlu Sunna wal Jamaa kwa mipango mizuri na huduma bora. Karibuni kwa Hijja "mabroor". Tafadhali wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0655/0765/0682/0777 - 462022; Zanzibar: 077 7468018/0685366141/0657606708. (18) KUPATA PEPO KWA SIKU TANO!

Transcript of ANNUUR 1142

  • ISSN 0856 - 3861 Na. 1142 DHULQAAD, IJUMAA , SEPTEMBA 12-18, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

    Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz

    Jamani Zanzibar hakuna magaidi! Zanzibar kuna watu wanaotaka mamlaka kamili ya nchi yao.

    Muundo wa Muungano wa Serikali mbili, unalenga kuitia kitanzi Zanzibar kama nchi.

    Masheikh wa Uamsho wa l i g u n d u a h i l o n a walisimama kidete kuidai

    Mtuhumiwa wa ugaidi akatwa mguuYadaiwa ni kutokana na mateso ya kutishaMwingine mahututi, asomewa kesi kitandaniWaislamu wawasilisha malalamiko Ikulu

    Hiyo ndiyo gharama ya kutaka Zanzibar huru!

    Hata Mzee Aboud Jumbe yalimkutaAlikwenda Dodoma Rais akarudi raia

    Fitna hii Kisonge kwa faida ya nani?

    Zanzibar yao huru.Masheikh hao, s iyo

    w a k w a n z a k u p a t a misukosuko kutokana na kuidai Zanzibar huru.

    Hata Mzee Aboud Jumbe alipohoji tu muundo tata wa Muungano wa Serikali mbili alionja joto ya jiwe! (Soma uk. 8)

    Sheikh Bassaleh ataka Serikali ichukue hatua

    Asema aliyofichua Farid ni mazitoKongamano Kichangani Jumapili Uk. 4

    WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Uhusiano, Mh. Steven Wasira. Sheikh Rajabu Katimba

    Hakuna kitu kinachowaliza wenye akili zaidi kuliko wasiwasi wa kuokoka na Moto na kupata Pepo! Hijja peke yake ndiyo inayoweza kumsafisha muislamu na madhambi yote, akarudi kama siku aliyozaliwa na mama yake, na akapata Pepo katika muda wa siku tano. Gharama zote ni Dola 4,500. Karibuni Ahlu Sunna wal Jamaa kwa mipango mizuri na huduma bora. Karibuni kwa Hijja "mabroor". Tafadhali wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0655/0765/0682/0777 - 462022; Zanzibar: 0777468018/0685366141/0657606708.

    (18) KUPATA PEPO KWA SIKU TANO!

  • 2 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 12-18, 2014AN-NUUR

    S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.

    www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected] zetu zipo: Manzese Tip Top

    Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

    Tahariri/Habari

    SHEIKH Ponda Issa Ponda (kushoto) akiteta jambo na Wakili wake Juma Nassor, katika Mahakama Kuu Dar es Salaam hivi karibuni.

    SIKU za hivi karibuni, serikali imelazimika kuingia gharama za dharura ili kukabilia na ugonjwa wa Dengue, ambao uliibua wasiwasi na kuwa tishio la maisha ya watanzania ,hususan wakazi wa jiji la Dar es Salaam.

    Haukupi ta muda, hivi sasa tunaishuhudia ser ikal i ik i lazimika tena kuingia gharama za dharura, kujiandaa kukabiliana na hatari ya ugonjwa wa Ebola, ambao tayari umekuwa tishio na umeshagharimu maisha ya maelfu ya watu katika nchi za Afrika magharibi.

    Hata hivyo, wakati t u k i e n d e l e a n a maandalizi haya, maisha ya watanzania yanazidi kuteketea kila uchao kutokana na kukithiri ajali za barabarani.

    Kipindi hiki , kwa muda mfupi tu, tayari zimetokea ajali mbaya na za mfululizo zaidi ya tatu za mabasi ya abiria na kuangamiza maisha ya watu.

    Wiki iliyopita, zaidi ya watu hamsini walipoteza maisha yao katika ajali iliyohusisha mabasi ya abiria ya kampuni za J4 Coach na Mwanza Coach, ajili iliyotokea k w a m a b a s i h a y o kugongana uso kwa uso katika barabara ya Mwanza Musoma.

    Licha ya kusababisha vifo vya watu, ajali hiyo mbaya kabisa ilijeruhi a b i r i a we n g i n e n a kusababisha uharibifu na kupotea mali.

    Haukupi ta muda, tukasikia ajali nyingine mbaya imetokea huko Kilosa mkoani Morogoro, ambayo ilihusisha basi la abiria la kampuni ya Air bus, linalofanya safari zake Dar -Tabora.

    Tusifanye mzaha ajali zinatumaliza

    Katika a ja l i h iyo, iliarifiwa kuwa abiria w a n n e w a l i p o t e z a maisha katika eneo la tukio na wengine 35 kujeruhiwa.

    Wiki hii, ikatangazwa ajali nyingine kutokea huko Songea mkoani Ruvuma, ambapo basi dogo la abiria liligonga mt i na kupinduka . Taarifa zimeeleza kuwa basi hilo lilipata ajali, baada ya dereva wake kumkwepa mwendesha baiskeli na kushindwa kulimudu basi hilo na hatimaye kuparamia mti na kupinduka.

    Tumeelezwa kuwa abiria watatu walipoteza maisha yao na wengine 24 kujeruhiwa katika ajali hiyo.

    Juzi tu huko mkoani L i n d i , t u l i a r i f i w a kwamba gari la jeshi liliparamia nyumba za raia na kusababisha vifo.

    Matukio ya ajali hizi yamefuatana sana. Hizo ni baadhi tu ya ajali za barabarani , ambazo zinatokea na kuripotiwa kat ika vyombo vya habari.

    Tunaamini kabisa kwamba kila siku, maisha ya wengi yanapotea sehemu mbal imbal i nchini , na wengine kujeruhiwa au kupata ulemavu kutokana na kukithiri kwa ajali hizo, lakini taarifa za ajali hizo zinakuwa hazivifikia vyombo vya habari kuripotiwa.

    A j a l i z a p i k i p i k i pekee zimegharimu na zinaendelea kuangamiza maisha ya wengi kila siku, achilia mbali za magari binafsi, ya abiria na ya mizigo.

    Hata hivyo, pamoja n a k u w e p o k w a ushahidi wa kutosha wa kuteketea maisha ya watanzania kwasababu

    ya kukithiri ajali za barabarani, bado serikali haionekani kushtushwa na kasi ya ajali hizi kama inavyoshtushwa na ebola au dengue, na hatimaye kuamua kuchukua hatua zinazotekelezeka za kudhibiti ajali hizi.

    Wengi tunashuhudia n a m n a a s k a r i w a usalama barabarani wanavyotumia makosa ya waendesha vyombo vya moto barabarani, k u v u n a f e d h a z a mifukoni.

    Kuna tetesi kwamba wapo wanaombatana na vitabu viwili vya faini (notification), vitabu halisi na dublicated, hizo ni tetesi na s i tunazichukulia kuwa ni tretesi.

    Yaani kosa linaloweza k u l e t a m a d h a r a barabarani, linaweza k u f u m b i wa m a c h o likaachwa tu liendelee hata likidhuru maisha ya wengine alimuradi afande kafutika senti zake mfukoni.

    N a k u m b u k a tulishawahi kuandika maoni katika gazeti hili na kushauri serikali kufanya kila iwezalo, kuhakikisha kunakuwa na vifaa vya kutosha na vya uhakika kwa ajili ya kuchunguza na kufuatilia masuala ya usalama barabarani ( Ve h i c l e t r a c k i n g system), kama ilivyo katika nchi za wenzetu.

    Kwa kutumia vifaa

    hivi , i takuwa rahisi kuwangamua madereva wazembe, wavuta bangi au walevi akiendesha gari kihasara, bila hata ya kuwa na haja askari wa usalama kila kona barabarani.

    Tunaamini kabisa kwamba mfumo huo pekee, ndio utakaosaidia k u r e j e s h a h e s h i m a barabarani na hatimaye k u o k o a m a i s h a ya maelfu ya wananchi yanayopotea kila mwaka kwa ajali za kizembe barabarani.

    Pia tukumbushe tu kuwa, lingekuwa jambo la maana zaidi kwa serikali kuliwezesha jeshi la polisi, hususan kikosi cha usalama barabarani kuwa na vifaa vya kutosha vya uokoaji.

    Hii itasaidia mara baada ya ajali kutokea, iwe ni rahisi kuokoa m a j e r u h i , k u o n d o a maiti, mizigo na gari au magari yaliyopata ajali katika eneo la tukio na huduma kuendelea bi la usumbufu kwa watumniaji wengine wa barabara.

    Jeshi la Polisi kama lilivyo na magari ya patro, linaweza kuwa na magari yake ya break down na ambulance zao, ambayo yanaweza kutoa huduma katika maeneo ya matukio ya ajali kwa wakati. Kama ni malipo, yanaweza kufanywa na wenye vyombo vilivyohusika

    na ajali na maduhuli kuingia katika mfuko wa serikali au katika kitengo hicho cha usalama ili kumudu kujiendesha.

    Kama kwa muda mfupi tu, serikali imeweza kutumia mabilioni ya fedha kwa dharura ya kujipanga kukabilia na ebola, kama serikali kwa muda mfupi ilipata fedha kugharamia mlipuko wa dengue, na tunaamini likitokea afa jingine inaweza kuingia katika gharama za kukinga wananchi wake, kwa nini isitumie dharura hiyo hiyo kugharamia u w e k e z a j i k a t i k a usalama barabarani, ili kuokoa maisha ya maelfu ya wananchi wanaokufa kila mwaka kwa ajali za kizembe barabarani?.

    Hata hivyo, tunashauri kwamba kwa maslahi ya usalama wa maisha ya watu wetu, ni vyema pia elimu ya usalama b a r a b a r a n i i k a w a inatolewa tangu shule za msingi, ili kujaribu ku jenga ta i fa watu wenye ufahamu mzuri wa sheria za usalama barabarani siku za usoni.

    Hii i tasaidia sana kupunguza kwa kiasi kikubwa ajali zisizo za lazima, zinazotokana na ujinga wa kujua sheria za barabarani, kwa kuwa raia wote watakuwa wanajua sheria hizi wawe ni madereva au watembea kwa miguu.

  • 3 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 12-18, 2014Habari

    Mtuhumiwa wa ugaidi akatwa mguuM M O J A w a Wa i s l a m u waliopo mahabusu kwa tuhuma za ugaidi, imedaiwa k u wa a m e k a t wa m g u u kufuatia jeraha alilolipata katika kile kilichodaiwa kuwa ni mateso na vipigo wakati wa kukamatwa na akiwa rumande.

    Wakati mtuhumiwa huyo aliyetajwa kwa jina la Sudi Nasibu Lusuma, akipoteza mguu wake, mtuhumiwa mwingine, Abulkarimu Thabiti, inadaiwa kuwa yu mahututi.

    Hayo yamebainishwa na msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T) Sheikh Rajabu Katimba, akiongea na vyombo vya Habari, katikati ya wiki hii, katika Ofisi za TAMPRO, Magomeni, Jijini Dar es Salaam.

    Katimba amesema kuwa katika zoezi la kamata kamata dhidi ya Waislamu inayoendelea katika miji ya Zanzibar, Arusha na Dar es Salaam, wamebaini kuwa limekuwa likiambatana na utesaji uliovuka mipaka.

    A l i s e m a , u t e s a j i h u o unafanyika wakatika wa kuhojiwa, kwani alidai hadi sasa wapo waliovunjwa miguu, waliopigwa hadi kupoteza fahamu, na wengine kuhojiwa wakiwa uchi na mbaya zaidi alidai kuna waliotumbukiziwa vitu katika sehemu zao za siri.

    Katika hao, Sudi Lusuma, kutoka Arusha imepelekea kukatwa mguu kufuatia mateso makubwa yaliyopelekea mguu wake uliopondwa kuoza, lakini Muislamu mwingine Abudulkarimu Thabiti, ni mahututi ambapo alisomewa mashitaka akiwa taabani kitandani. Alisema Katimba.

    Katimba alisema kuwa watu hao ni watuhumiwa tu, na haoni ni kwa sababu gani wateswe tena ndani ya nchi ambayo inaongozwa kwa utawala wa haki na sheria na kuheshimu misingi ya haki za binaadamu.

    Alisema, kimsingi umma unatambua wazi kuwa sheria ya ugaidi ya mwaka 2002, kwa kiasi kikubwa ipo dhidi ya Waislamu nchini, hata hivyo akasema Jumuiya hiyo haipingi watu kukamatwa na kuhojiwa kwa taratibu za kisheria zinazozingatia maadili na utawala bora.

    Tunachopinga vikali na kulaani ni kuteswa watuhumiwa na kuwadhalilisha kwa hisia tu, mtu ahesabiwe kuwa ni

    Na Bakari Mwakangwale mkosaji baada ya Mahakama kuthibitisha tuhuma zake kisha apewe adhabu kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi. Alisema Sheikh Katimba.

    Akaongeza kuwa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu inajiuliza, hawa watendaji wanaokiuka taratibu za sheria za nchi wana mwakilisha nani katika zoezi hili la kutesa watuhumiwa.

    Akabainisha kuwa Jumuiya na Taasisi, katika kufuatilia kadhia hiyo, wamelazimika kukutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uhusiano, Mh. Steven Wasira, ili kuwasilisha malalamiko ya Waislamu juu ya yanayojiri kwa Waislamu wanaoteswa wakiwa mikononi mwa vyombo vya dola.

    Alisema, katika kikao chao na Waziri Wasira, Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T), imetoa mapendekezo yake na namna ya kulishughulikia

    jambo hili la tuhuma za Ugaidi ambazo kwa asilimia kubwa linathiri kundi moja katika jamii jambo ambalo ni hatari kwa mustakabali wa Taifa kwa ujumla.

    T u n a i t a k a S e r i k a l i kusimamia uadilifu katika utendaji ili kutoleta hisia za

    kundi fulani la wananchi kuhisi kuonewa, hii ni kutokana na historia ya kuwa ni viongozi wa Kiislamu tu wanaokutwa na masaibu haya. Alisema Katimba.

    Jumla ya Waislamu 46, kutoka Jijini Arusha, Dar es Salaam na Visiwani Zanzibar, wamekamatwa na kufikishwa Mahakamani kwa tuhuma mbalimbali za Ugaidi.

    Hata hivyo Agosti, 21. 2014, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Sheikh Farid Had Ahmed, na wenzake walitoa tuhuma nzito mbele ya Mahakama hiyo kwamba, Jeshi la Polisi na Vyombo vya Usalama, baada ya kuwakamata waliwatesa na kuwadhalilisha huku wakidai kufanyiwa mambo machafu ya wale waovu wa Qaumu Lut.

    Hatimaye rufaa ya Sheikh Ponda Issa Ponda sasa itaanza kusikilizwa Septemba 22, 2014 Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.

    Jaji anayesikiliza shauri hilo, Augustino Shangwa, alisema kuwa shauri la rufaa hiyo litasikilizwa katika chumba (chamber ) , ambapo sasa mawakili wa pande zote mbili, yaani upande wa Jamhuri na ule wa Sheikh Ponda, watawasilisha hoja zao kwa maandishi.

    M a m i a y a Wa i s l a m u walifurika mahakamani hapo kufuatilia kesi hiyo huku msafara wa Waislamu kutoka Morogoro ukiongozwa na Sheikh Ibrahimu Makange.

    Hata hivyo Jaji anayesikiliza rufaa hiyo Mhe. Augustino Shangwa, amewata Waislamu kutosumbuka tena kuja kwa wingi mahakamani hapo kwa kuwa sasa kesi hiyo itakuwa ikisikilizwa katika chumba (Chamber) na sio katika vyumba

    Rufaa ya Ponda Septemba 22Waislamu waridhia ushauri wa Jaji Shangwa

    Na Abdulkarim Msengakamba vya kawaida vya mahakamani hapo walivyovizoea.

    "Tukubaliane kuwa siku ya tarehe 22 hakuna haja ya kuja kwakuwa mawakili watakuja kuleta shauri lao kwa maandishi, sasa hakuna haja ya kuja. Lakini siku ya hukumu mtaruhusiwa kuja wote. Hiyo ndiyo siku muhimu, sio siku za kusikiliza shauri kwakuwa siku hiyo Sheikh hamtamuona kwasababu kesi itakuwa ikisikilizwa chamber. Nawashauri tu lakini siwazui kuja, alifafanua Jaji Shangwa.

    Naye Sheikh Ponda alisimama na kumuomba Jaji atoe ushauri wake, ambapo alisema kuwa yeye anakubaliana na ushauri wa Ja j i , lakini akashauri kuwa itakuwa vyema Jaji a k a wa r u h u s u Wa i s l a m u watano au sita kuwawakilisha wenzao kusikil iza shauri lake mahakamani hapo, nao watawapelekea wenzao yale yatakayojiri mahakamani hapo.

    Jaji Shangwa alikubaliana na ombi la Sheikh Ponda.

    Kufuatia maelezo ya Jaji Shangwa na Sheikh Ponda, Wa i s l a m u w a l i o f u r i k a mahakamani hapo kwa pamoja waliridhia ushauri wa Jaji pamoja na ombi la Sheikh.

    Sheikh Rajabu Katimba.

    Sheikh Ponda Issa Ponda.

  • 4 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 12-18, 2014Habari

    JUMUIYA ya Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini K e n ya ( M O A) , i m e t i s h i a kuchukua hatua za kisheria ikiwa mswada unaolipa Bunge nguvu za kuwaadhibu waandishi wa habari wanaolikosoa Bunge hilo utapitishwa, liliripoti gazeti la Daily Nation la Kenya.

    Mswada wa Madaraka na Fursa za Bunge wa Mwaka 2014, uliowasilishwa na Mbunge wa Eldas, Adan Keynan, unalipa Bunge nguvu kubwa za kuubana uwezo wa waandishi wa habari katika kuandika habari za Bunge na unatoa adhabu kali kwa kile walichokiita iwapo uandikaji wao wa habari utaonekana una matatizo.

    Mswaada huu mpya una vifungu hatari ambavyo kama vikiruhusiwa kupita, vitabana uandishi wa habari za Bunge na pia kukandamiza maandamano ya asasi za kijami," alisema Mwenyekiti wa MOA nchini humo

    Wanahabari Kenya vyapinga rasimu ya sheria 'kandamizi' ya habari

    Sheikh Bassaleh ataka Serikali ichukue hatua

    MAALIM Ally Bassaleh, a m e s e m a m a m b o yaliyoelezwa na Sheikh Farid, mbele ya Mahakama ni mazito, na kwamba mtu mzima kutoa malalamiko ya kutendewa vitendo visivyo vya kibinadamu si suala la kupuuzwa.

    Ni kwa sababu hiyo, ameitaka Serikali ilipe uzito suala hilo bila kujali yule aliyetoa tuhuma hizo ni mtu wa namna gani katika jamii kwa kuzingatia utawala wa Sheria na haki za binadaamau.

    Tuhuma hizo zimetolewa Mahakamani sio mtaani , na waliosema ni Masheikh a m b a o n i v i o n g o z i wa Kiislamu wanaojua kwamba kusema uongo ni haramu na haifai, bado Serikali mpaka leo haishituki ipo kimya tu. Alisema Maalim Bassaleh, akionyesha kustaajabu.

    H a t a h i v y o a l i s e m a , k u o n y e s h a k w a m b a wanachola lamikia ak ina Sheikh Farid, kuwa ni cha kweli, kwa mara nyingine tena katika Mahakama hiyo (Kisutu) mmoja wa washitakiwa hao ameionyesha Mahakama nguo yake ya ndani jinsi ilivyojaa damu, akimwambia Hakimu, Angalia hii.., naomba nifanyiwe uchunguzi. Alisema Maalim Bassaleh, akimnukuu mtuhumiwa huyo.

    A l i s e m a , n i v y e m a Serikali ikaunda tume huru uchunguzi ukafanyika ili ijulikane yale yamefanyika kweli au hayajafanyika na kama yamefanyika hatua gani zinachukuliwa dhidi ya wale waliofanya.

    Kwa upande mwingine, Waislamu Jijini Dar es Salaam, wanatarajia kukutana Jumapili ya Septemba 14, 2014 (Kesho kutwa), katika Kongamano litakalo zungumzia madhila wayapayo Sheikh Farid Had na wenzake waliopo gerezani, kwa tuhumza za Ugaidi.

    K o n g a m a l o h i l o lililoandaliwa na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T) litafanyika katika Msikiti wa Kichangani, Magomeni Jijini Dar es Salaam, kuanzia majira ya saa nane mchana (baada ya swala ya Adhuhur) ambapo Masheikh wa Jumuiya hiyo watalitolea taarifa suala hilo na hatua ambazo hadi sasa wameshazichukua.

    Akizungumzia Kongamano hilo, Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T) Sheikh Ramadhani

    Na Bakari Mwakangwale

    Sanze, amesema baada ya taarifa hizo kusikika kupitia Mahakamani, Jumuiya na Taasisi za Kiislamu zilikutana na kutafakari madai ya Sheikh Farid Hadi.

    Alisema, katika vikao vyao chini ya uwakilishi wa Jumiya hiyo inayoundwa na taasisi zipatazo 30, walikubaliana mambo kadhaa ya kulifuatilia suala hilo, ikiwamo Kongamano la kukutana na Waislamu.

    Sanze, amesema Kongamano hilo ni hatua ya mwisho katika makubaliano ya viongozi wa Jumuiya na Taasisi, ikitanguliwa na kukutana na viongozi wa Serikali na kulifikisha katika asasi mbalimbali zisizo za Kiserikali, wakiwemo Mabalozi wa nchi mbalimbali nchini.

    Alizitaja sehemu ambazo tayari taarifa hiyo imefikishwa kwa maandishi kuwa ni asasi za kutetea haki za binaadamu kama vile Tanzania Human Right Legal Centre pamoja na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

    Pia alisema, wamefika kwa Balozi mbalimbali zilizopo nchini, miongoni mwa hizo ni Ubalozi wa Finland, Norway, Ujerumani, Uingereza pamoja na Marekani.

    Kwa upande wa Vyama vya siasa, alisema wameonana na viongozi wa vyama vya vya CCM, CHADEMA, CUF na NCCR, kote huko alidai

    kuwa wameleza hatari ambayo inaweza kutokea endapo unyama na udhalili kama huo hautokomeshwa.

    Na kwa upande wa Serikali, alisema Viongozi wa Jumuya hiyo wameonana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi, Mh. Steven Wasira, pamoja na kumuandikia Jaji Mkuu wa Serikali, na kuwafahamisha juu ya kadhia hii na.

    Sasa hatua inayofuata n i k u f a n ya K o n g a m a n o kubwa kabisa ili kuweka w a z i h a t u a a m b a z o viongozi tumeshazichukua huku tukisubiri majibu na utekelezaji wake hususani kutoka Serikalini. Kabla ya hatua hii tuliona ni vyema kwanza tuonane na kuzifikisha katika mamlaka mbalimbali za Serikali na zisizo za Serikali. Alisema Shkh. Sanze.

    Alisema, Jumuiya na Taasisi hazihoji hatua ya vyombo vya dola kukabiliana na tuhuma za kuwepo viashiria vya kuwepo ugaidi, bali tatizo lao ni kuona jinsi haki za binadamu zinavyovunjwa tena chini ya vyombo vya sheria huku mamlaka za Serikali zikiwa kimya kana kwamba hakuna utawala wa Sheria.

    Sanze, alikumbushi tukio la kuuwawa Waislamu katika Msik i t i wa Mwembecha mwaka 1998, jambo ambalo lilikaliwa kimya huku wengine wakifurahia na kupongezana.

    na Mkurugenzi wa Standard Media Group, Sam Shollei, Siku ya Jumatatu.

    "Kama vyombo vya habari, tuna haki ya kuchukua hatua dhidi ya uanzishwaji wa mswada huu na tutachukua hatua za kisheria kuvitangaza vifungu husika kuwa ni kinyume cha sheria." Alisisitiza Mkurugenzi huo ambaye pia aliwahi kuwa M k u r u g e n z i M t e n d a j i wa Mwananchi commonication hapa nchini.

    Alisema kuwa katika mswada huo, kulitukana Bunge ni kipengele kilichoorodheshwa kuwa ni kosa linaloweza kuadhibiwa kwa faini ya hadi shilingi 500,000 za Kenya (dola 5,650).

    "Dhamira ya adhabu kama hizo inaonekana wazi inatokana na kampeni za hivi karibuni za vyombo vya habari na asasi za kijamii dhidi ya tabia za kibinafsi (za wabunge), ikiwepo ile ya kujiongezea mishahara yao," alisema Bw. Shollei.

    MAALIM Ally Bassaleh (kulia) akielezea jambo katika kongamano lililofanyika Msikiti wa Kichangani hivi karibuni.

    Katikati ni Sheikh Katimba.

  • 5 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 12-18, 2014Habari

    MAHAKAMA moja ya Misri imewahukumu vifungo kwa miaka 20 jela viongozi wawili wa harakati ya Ikhwanul Muslimin nchini humo kwa kosa la kujaribu kuwaua polisi wawili.

    Mahakama hiyo Jumanne wiki hii iliwatia hatiani Bw. Mohamed al Biltaji, kiongozi w a I h w a n u l M u s l i m i n na Safwat Hijazi kiongozi wa kidini wa ngazi ya juu wa harakati hiyo kwa kosa lililoelezwa kuwa ni kujaribu kuwaua polisi wawili katika maandamano yaliyofanyika huko Cairo mwezi Julai mwaka jana.

    Aidha mahakama hiyo imewawahukumu madaktari wawili kifungo cha miaka 15 jela, kwa kosa la kuwatibu waandamanaji waliojeruhiwa kat ika ghasia kubwa za maandamano huko Cairo.

    Bw. Mohamed Bi l ta j i , ambaye anafahamika kama mkosoaji mkubwa wa kitendo cha kuondolewa madarakani Bw. Muhammad Mors i , ametuhumiwa pia kwenye kesi nyingine kadhaa.

    Mwezi Aprili mwaka huu, Bw. Bil ta j i al ihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kuvitukana vyombo vya mahakama vya Misri.(www. irib.ir)

    Mahakama Misri yawahukumu viongozi wa Ikhwan

    P O L I S I n c h i n i K e n y a imewakamata raia wawili wa Kijerumani kwa kuwashuku kuwa na uhusiano na al-Shabaab, liliripoti gazeti la The Standard la Kenya Jumanne wiki hii.

    U j e r u m a n i y a k a m a t a washukiwa 3 wa al-Shabaab wakirejea kutoka Kenya

    Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Polisi cha Kupambana na Ugaidi nchini humo, John Mulaulu, alisema watuhumiwa hao wawili walikamatwa jijini Nairobi Agosti 29, siku kadhaa baada ya kuwasili kutoka Somalia ambako walikuwa wakiishi tangu mwaka 2012.

    "Kunaweza kuwepo na wapiganaji zaidi wa kigeni ambao sasa wanarejea kwenye nchi zao kwa sababu kundi walilokuwa wakilipigania linasambaratika," alisema Mulaulu.

    Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, Wizara y a M a m b o y a N j e y a

    Wajerumani wakamatwa Kenya wakihusishwa na al-Shabaab

    Ujerumani ilithibitisha kuwa raia hao wawili walikuwa wamekamatwa, lakini haikutoa k wa u n d a n i s a b a b u z a kukamatwa kwao.

    S i k u y a J u m a m o s i , W a j e r u m a n i w a t a t u wa l i k a m a t wa b a a d a ya kurudi nyumbani wakitokea Kenya, wakishukiwa kuwa na mafungamano na al-Shabaab.

    Walikamatwa kwa tuhuma za ugaidi kwenye uwanja wa ndege wa Frankfurt na kupelekwa mahakamani siku iliyofuata, ambapo Jaji aliamuru wawekwe kizuizini wakingojea kesi yao, ilisema ofisi ya mwendesha mashtaka wa serikali ya shirikisho.

    Raia kadhaa wa kigeni kutoka mataifa ya magharibi wamekamatwa Afrika ya Mashariki kwa kuhisiwa kuwa na mafungamano na al -Shabaab, huku Kenya ikionekana kama njia kuu ya kupitia kuingia Somalia.(www.sabahionline)

    RIPOTI ya uchunguzi wa ajali ya ndege ya Malaysia - MH17, iliyotokea Mashariki mwa Ukraine imesema kuwa ndege hiyo iligongwa na vitu vya kasi kubwa na kwamba, ilivunjika ikiwa angani.

    Habari hizo zilizotangazwa k a t i k a r i p o t i m o j a iliyochapishwa na idara ya

    Ndege ya Malaysia ilitunguliwa Ukraineusalama wa safari za ndege mj ini The Hague nchini Uholanzi, inaonyesha kuunga mkono dhana kwamba ndege hiyo ilitunguliwa.

    Abiria wote 298, wakiwa ni pamoja na raia 193 wa Uholanzi waliuawa wakati ndege hiyo ilipoanguka Julai 17, wakati ikiwa njiani kutoka Amsterdam kuelekea Kuala Lumpur.

    N c h i z a M a g h a r i b i z i l i w a s h u t u m u w a a s i wa n a o u n g wa m k o n o n a Urusi kwa kuitungua ndege hiyo wakitumia mtambo wa kufyatua makombora kutoka ardhini.

    Hata hivyo Urusi ilililaumu jeshi la Ukraine kwa kuhusika na ajali hiyo.(www.irib.ir)

    KIONGOZI wa kundi moja la waasi nchini Syria ameuawa Jumanne wiki hii katika mlipuko wa bomu pamoja na maafisa wengine wa ngazi ya juu wa kundi hilo.

    Hata hivyo mpaka sasa hakuna kundi lililojitokeza k u d a i k u h u s i k a n a shambulizi hilo lililomuua Bw. Hassan Aboud na wanachama wengine wakuu wa Ahrar al-Sham.

    A i d h a i m e e l e z w a kuwa haidhaniwi kuwa wanajeshi watiifu kwa serikali ya Rais Bashar al-Assad wnaweza kuhusika na tukio hilo, ikidaiwa kuwa katika operesheni zao huwa hawatumii walipuaj i wa kuj i toa mhanga.

    K u n a w a s i w a s i kwamba inaonekana majeshi yaliyopo ndani ya makundi ya upinzani katika mgogoro wa Syria uliodumu miaka mitatu sasa, ndiyo yalihusika.

    S h a m b u l i z i h i l o liliulenga mkutano wa ngazi ya juu wa kundi l a A h r a r a l - S h a m ulioandaliwa katika mji wa Kaskazini Magharibi wa Ram Hamdan, mkoa wa Idlib nchini Syria.

    Taarifa kutoka kwa kundi hilo zimesema mlipuko huo ulimuuwa Aboud, anayefahamika pia kama Abu Abdullah al-Hanwi, pamoja na viongozi wengine wakuu kumi na moja.

    Mlipuko wa bomu waua viongozi wa waasi Syria

    AL-HAMAWI Hassan Aboud Abu Abdullah

  • 6 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 12-18, 2014Habari

    SHIRIKA la kutetea haki za binadamu limesema katika ripoti yake kuwa, wanajeshi wa Umoja wa Afrika wanaolinda a m a n i n c h i n i S o m a l i a wamewadhalilisha kijinsia wasichana na wanawake wa kisomali wanaoishi katika mazingira magumu mjini Mogadishu.

    Shirika hilo la Human Rights Watch, limesema nchi za kiafrika zilizochangia askari katika jeshi hilo pamoja na wafadhili wa AMISOM, wanapaswa kushughulikia ukiukaji huo wa haki za binadamu haraka iwezekanavyo na kuimarisha utaratibu ndani ya Somalia wa kutafuta haki ya wanawake hao.

    Ripoti hiyo yenye kurasa 71 iliyopewa jina la The Power These Men Have Over Us' yaani nguvu walizonazo wanaume hawa dhidi yetu, inaonesha waz i v i sa wal ivyofanya wanajeshi hao kwa kutumia misaada ya kibinadamu, kuwadhal i l i sha k ingono wanawake na wasichana tangu mwaka wa 2013.

    W a n a j e s h i h a o wa n a se me k a n a k u t u m i a misaada hiyo ili kuwashinikiza wanawake kushiriki vitendo vya ngono.

    Ripoti hiyo imeendelea kufafanua kuwa wanajeshi hao wamewabaka baadhi ya wanawake waliokuwa wa k i t a f u t a m s a a d a wa matibabu pamoja na maji katika kambi za AMISOM.

    Umetolewa mfano kuwa mwaka 2013, mmoja mwenye umri wa miaka 15 alikwenda k a t i k a e n e o wa n a l o k a a wanajeshi wa Burundi katika kambi ya AMISOM, kuomba msaada wa dawa kwa ajili ya mama yake aliyekuwa m g o n j w a . I m e e l e z w a kuwa baadaye mkalimani wa kisomali aliamuamuru kuwafuata wanajeshi wawili waliokuwa na dawa hizo, kijana huyo aliliambia shirika la HRW kwamba badala ya kupewa dawa alizohitaji , alipelekwa katika maeneo ya misitu na kubakwa na mmoja wa wanajeshi hao, kisha baada ya kitendo akapewa dola kumi na aliyemtendea unyama huo.

    HRW limewahoji wanawake 21 waliopitia masaibu hayo.

    A i d h a s h i r i k a h i l o l a

    Kashfa nzito vikosi vya AMISOMWanawake wabakwa SomaliaNa Amina Abubakar,HRW

    kutetea haki za binadamu limekusanya vielelezo vyake kwa kuwafanyia mahojiano wanawake 21 na wasichana ambao wameelezea kubakwa au kudhalilishwa kijinsia na wanajeshi kutoka Burundi na Uganda, wanaofanyakazi na wanajeshi wa Umoja wa Afrika.

    B a a d h i ya wa n a j e s h i w a U m o j a w a A f r i k a wanatumia nafasi zao vibaya kwa kuwafanyia maovu wanawake na wasichana mjini Mogadishu, alisema Liesl Gerntholtz, Mkurugenzi wa Haki za Wanawake katika

    shirika hilo.Gerntholtz, amesema kwa

    sasa Somalia ina matatizo mengi, lakini uongozi wa Somalia na Umoja wa Afrika unaweza kubadilisha hali ilivyo kwa kuwawajibisha wanajeshi waliotekeleza vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia.

    Imeelezwa kuwa kwa miaka mingi ya mapigano na ukosefu wa chakula nchini Somalia, yamesababisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao huku wakiishi bila kazi au kipato chochote cha kumudu maisha. Wengi wanategemea usaidizi

    kutoka nje na wanalazimika kushawishika katika visa vya udhalilishaji ili kujikimu kimaisha pamoja na watoto wao.

    Mwaka wa 2007 Baraza la Usalama la Amani la Umoja wa mataifa liliwapeleka wanajeshi wa kulinda amani nchini Somalia wanaojulikana kama AMISOM, chini ya maelekezo ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulinda miundo mbinu ya Somalia, pamoja na maafisa wa serikali na pia kusaidia katika kutoa misaada ya kibinadamu.

    Wanajeshi wa AMISOM wanachangiwa na mataifa ya Uganda, Burundi, Kenya, Ethiopia, Djibouti, na Sierra Leone.

    Hata hivyo wanaharakati wanasema Umoja wa Afrika, hauwezi kulifungia j icho suala hili maana ya kwamba watakuwa wanaupotezea uaminifu umoja huo katika mpango wake wa kulinda amani Somalia.

    Shirika hilo limeeleza kuwa kinachohitajika hivi sasa ni serikali zinazounga mkono uwepo wa vikosi vya AMISOM Somalia, kufanya kazi na Umoja wa Afrika kumaliza visa vya udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya wasichana na wanawake nchini humo na kuchukua hatua kwa wanajeshi wanaosemekana kutekeleza hujuma hiyo, huku wakifanya kila wawezalo kukomesha kabisa visa hivyo.

    KIJANA Ali Mahmoud wa Tomondo Wilaya ya Magharibi Unguja, amefanya utafiti wa namna ya kuzalisha umeme nafuu wa upepo kuanzia mwaka 1999. Mwaka 2009 kwa uwezo wake Allah (sw) utafiti wake ulimwezesha kufanikiwa kugundua namna ya kuzalisha umeme nafuu kwa upepo.

    Hivi sasa anaunda mtambo wa majaribio wa kuzalisha umeme huo huko Tomondo na kuthibitisha kipaji chake.

    Mpaka sasa ameshatumia kiasi cha shilingi 6,000,000, katika kuunda mtambo huo

    Mvumbuzi huyu anahitaji msaadaikiwa ni michango ya Waislamu.

    Awali aliwasilisha mchoro wa uvumbuzi wake Tume ya Sayansi na Teknolojia Dar baada ya kuitwa Julai 31, 2012 kuonyesha uwezo wake.

    Tume ilithibitisha ubunifu wake na akashauriwa kuacha mchoro kwa ajili ya kupelekwa Chuo cha Ufundi Dar Tech ili ufanyiwe kazi.

    Hata hivyo hakuwahi kuitwa tena wala kupewa taarifa yeyote kuhusu kuendelezwa ugunduzi wake. Hali hiyo ndiyo iliyomfanya kuamua kuundeleza ugunduzi wake

    yeye mwenyewe kwa msada wa michango ya Waislamu.

    Majaribio ni gharama na Bw. Ali Mahmoud hana uwezo. Hivyo anawaomba Waislamu, k u m c h a n g i a c h o c h o t e watakachojaaliwa ili aweze kukamilisha uvumbuzi wake huo na hatimaye kuzalisha umeme nafuu wa upepo utakaotokana na teknolojia ya Mtanzania.

    Msaada unaweza kufika kupitia namba zifuatazo:

    0774 775189, 0659 382025A/c No 54110100021946

    Benki ya Watu wa Zanzibar Ltd.

    RAIS Museven. Jeshi lake linaunda jeshi la Afrika.

    RAIS Uhuru Kenyatta. Jeshi la nchi yake lipo Somalia.

  • 7 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 12-18, 2014Makala

    KITABU kitakatifu cha Qurani kinawapigia mfano wa kiigizo waumini, mke wa Firauni kama ni kiigizo cha juu.

    Asia, mke wa Firauni a l i k u w a m u u m i n i n a m w a n a m k e m w e n y e ufahamu mkubwa. Licha ya kuishi katika mazingira mabaya kabisa ya dhulma na uonevu, yaani katika kasri ya Firauni, hakuachana na imani yake thabiti na wala hakuathirika kifikra na dhulma iliyokuwa ikifanywa na Firauni na wasaidizi wake.

    M w a n a m k e h u y o alitawakali na kumtegemea Mwenyezi Mungu na hivyo kushikamana na njia ya haki. Bila shaka Bibi kama huyo anaweza kuwa miongoni mwa viigizo vyema na bora kwa wanadamu kwa ajili ya malezi. Mwenyezi

    Mungu anasema katika aya ya 11 ya Surat at-Tahrim kwamba: Na Mwenyezi Mungu amewapigia mfano walio amini - mkewe Firauni, alipo sema: Mola wangu mlezi! Ni jengee kwako nyumba peponi, na uniokoe na F irauni na v i tendo vyake, na uniokoe na watu madhaalimu.

    Bi. Maryam (AS), mama yake Nabii Issa (AS) ni mfano na kiigizo kingine chema kwa waumini tunachoarifishiwa n a Q u r a n i t u k u f u . Qurani inamuarifisha na kumtambulisha Bibi Maryam kwamba ndiye mwanamke bora zaidi katika zama zake. Moja kati ya sura za Qurani imeitwa kwa jina na Bibi mwema huyo.

    Kwa hakika Bi. Maryam, ni mwanamke wa peponi. Miongoni mwa sifa njema za Bibi mwema huyo ni usafi, tabia njema, kulinda heshima yake, ukweli, uaminifu na utakasifu.

    Ni kutokana na sababu hiyo ndio maana Mwenyezi Mungu akamchagua Bibi huyo kuwa miongoni mwa wanawake bora kabisa ulimwenguni.

    Mwenyezi Mungu anasema katika aya ya 12 ya Surat

    Viigizo vya tabia na malezi katika Qurani tukufu-2Na Salum Bendera

    at-Tahrim kwamba: Na Mariamu binti wa Imrani, aliye linda ubikira wake, na tukampulizia humo kutoka roho yetu, na akayasadiki maneno ya Mola wake mlezi na vitabu vyake, na alikuwa miongoni mwa watiifu.

    Subira na uvimilivu na kustahamili matatizo na mushkili, ni sifa nyingine aliyokuwa nayo Bibi mwema huyo, ambazo waumini wanaweza kujifunza na kumfanya mwanamke huyo kuwa kiigizo chao katika maisha hayo.

    V i i g i z o v i n g i n e kat ika Qurani tukufu vimetambulishwa kama ni mkusanyiko, mjumuiko wa watu wema, mataifa, jamii ya watu fulani, kama vile As-Habul Kahf, yaani watu wa pangoni. Katika Suratul Kahf, kuanzia aya ya 9 hadi 26 Mwenyezi Mungu anaelezea kisa cha vijana hao waliohajiri, wakikimbia udhalimu wa mtawala wa Kirumi. Vijana hawa wakawa ni kiigizo na ruwaza njema kutokana na msimamo wao thabiti. Vijana hao walikuwa wakiishi kat ika neema kubwa, lakini waliamua kuachana na neema zote hizo ili kulinda imani yao na kuonyesha kutoridhishwa na udhalimu na ukandamizaji uliokuwa ukionyeshwa na mtawala wa wakati huo.

    M w e n y e z i M u n g u anasema katika aya ya 13 ya Suratul Kahf kwamba: Sisi tunakusimulia khabari zao kwa kweli. Hakika wao walikuwa ni vijana walio muamini Mola wao mlezi. Na Sis i tukawazidisha uwongofu.

    Nabi i Yusuf (AS) n i miongoni mwa mifano na viigizo vingine vya malezi ndani ya Qurani tukufu, ambavyo visa vyao ni ibra na mazingatio makubwa kwa waumini. Kisa chake kinaenezwa na Qurani kuwa ni, Ahsanal Qaswas, yaani simulizi nzuri kabisa. Qurani inamtambulisha Nabii Yusuf (AS) kama bingwa na mshindi wa kukabiliana na matamanio ya kinafsi.

    Bi. Zulaikha aliyekuwa mke wa aliyekuwa mmoja wa watawala wa Misri, alimtamani na kumtaka kimapenzi Nabii Yusuf (AS). Nabii huyo wa Mwenyezi Mungu aliushinda mtihani huo kutokana na kutawakali na kumtegemea Allah. Mwenyezi Mungu anaashiria hilo katika Surat Yusuf, aya ya 23 kwa kusema: Na yule bibi wa nyumba a l i y o k u w a m o Y u s u f alimtamani kinyume cha nafsi yake, na akafunga milango. Akamwambia: Njoo! Yusuf akasema: Audhubillahi! Najikinga na Mwenyezi Mungu. Huyu bwana wangu kaniweka maskani nzuri, na

    hakika wenye kudhulumu hawatengenekewi.

    Fauka ya hayo, Nabii Yusuf bin Yaqub (AS) alikuwa tayari kuziacha raha zote na hishima aliyokuwa akipewa katika kasri la mtawala huyo aliyekuwa mumewe Zulaikha, kama anavyosema Mwenyezi Mungu katika Surat Yusuf, aya ya 33, Yusuf akasema: Ee Mola mlezi wangu! Nastahabu kifungo kuliko haya anayo niitia. Na usipo niondoshea vitimbi vya wanawake mimi nitamili kwao, na nitakuwa katika wajinga.

    Hivyo basi, watu waliotajwa katika Qurani tukufu kama ni viigizo vya malezi, ni watu wa Mungu na shakhsia bora ambao maisha yao yalijaa mambo mema na hiyo bila shaka ni natija ya kumtegemea na kumtaka msaada Mwenyezi Mungu pekee pasina ya kumshirikisha. Maisha ya watu hao yanaonyesha kwamba, mja anaweza kufikia kilele cha tabia njema, saada na ufanisi kwa kuichagua njia sahihi na ya haki.

    Mwenyezi Mungu anatutajia kiigizo kingine cha malezi, nacho ni Nabii Ismail, mwana wa Nabii Ibrahim (AS) na kumtaja Nabii huyo kuwa ni nembo ya kusalimu amri mbele ya sheria na amri ya Mwenye Mungu, mtu ambaye hakusita wala kutetereka wakati baba yake, yaani Nabii I b r a h i m , a l i p o m wa m b i a kwamba ameamrishwa na Allah amchinje.

    Aidha Nabii Ibrahim, naye pia ni mja mwema ambaye wanadamu hawana budi kumfanya kiigizo chao kutokana na subira kubwa aliyoinyesha katika maisha yake na hasa katika kisa cha kuamrishwa amchinje mwanaye kipenzi. Mbal i na vi ig izo vyema a m b a v y o m w a n a d a m u anapaswa kuvifanya kuwa mfano wake wa kuiga, kama tulivyosema katika kipindi chetu kilichopita, Qurani pia imetaja viigizo vibaya ambavyo mja anapaswa kujitenga navyo na kupata ibra na mazingatio kutokana na hatima iliyowapata watu hao.

    Firauni, Qaruun, mke wa Nabii Luti na Nabii Nuhu ni baadhi ya watu wanaotajwa ndani ya Qurani kuwa, si viigizo vyema ambavyo mtu anapaswa kuvifuata.

    Mamia ya Waislamu walifurika mahakama Kuu Dare s Salaam kufuatilia kesi inayomkabili Sheikh Ponda Issa Ponda mahakamani hapo hivi karibuni.

  • 8 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 12-18, 2014Makala

    NIMEUMIZWA kwa kiasi kikubwa na tuhuma za kudhalilishwa masheikh w a U a m s h o , w a k a t i wakiwa mikononi mwa vyombo vya dola. Jamani Zanzibar hakuna magaidi! Z a n z i b a r k u n a wa t u wanaotaka mamlaka kamili ya nchi yao. Muundo wa Muungano wa Serikali mbili, unaoshabikiwa na CCM, unalenga kuitia kitanzi Zanzibar kama nchi. Masheikh wa Uamsho w a l i g u n d u a h i l o n a walisimama kidete kuidai Zanzibar yao huru.

    Labda niwakumbushe k idogo . Mashe ikh wa Uamsho visiwani Zanzibar, siyo wa kwanza kupata misukosuko kutokana na kuidai Zanzibar huru. Hata Mzee Aboud Jumbe alipohoji tu muundo tata wa Muungano wa Serikali mbili alionja joto ya jiwe! A l i k w e n d a D o d o m a akiwa Rais wa Zanzibar, akarudishwa Mji Mwema kama raia wa kawaida! Hiyo ndiyo gharama ya kutaka Zanzibar iwe huru!

    M a r e h e m u S h e i k h Ilunga Kapungu alipata kusema katika mfululizo

    Hakuna magaidi Zanzibar

    Na Said Rajab.

    wa makongamano yake kuhusu 'Mfumo na Athari zake Tanzania kwamba visiwani Zanzibar, mfumo huo unafanya kazi kupitia Muungano wa Serikali mbili. Ukigusa tu muundo wa Muungano, utawaona wenye muungano wao waliojificha nyuma ya pazia wakija juu!

    Angalau Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge, bwana William Lukuvi amekuwa mkweli kidogo. Huyu bwana alifichua kanisani, sababu halisi ya CCM kung'ang'ania Muungano wa Serikali mbili. Kwenye hafla ya kusimikwa Askofu mjini Dodoma, Lukuvi alisema Serikali tatu zitasababisha Zanzibar kujitenga na kuunda Dola ya Kiislamu! Kwa hiyo hofu ni Uislamu Zanzibar!

    Lukuvi, bila ya kutambua,

    harakati za kuidai Zanzibar huru, basi unakuwa adui namba moja wa 'Mfumo', kwa sababu unasababisha mgongano wa maslahi. Wenye Muungano wao lazima wakunyamazishe, kupitia vitisho, propaganda, u d h a l i l i s h a j i n a h a t a

    mwake.Nelson Mandela, kama

    kiongozi wa chama cha 'African National Congress' (ANC), aliendesha harakati za kupinga mfumo wa ubaguzi wa rangi kwa kutumia njia zote, ikiwemo ushawishi na ghasia. Wakati leo Mandela akiheshimika duniani kwa kazi yake hiyo, kipindi cha harakati zake za kisiasa, yeye na chama chake cha ANC waliitwa magaidi!

    Kama ilivyokuwa kwa Mzee Nelson Mandela, bado kuna maelfu ya watu wengine hapa duniani, ambao wanapigania haki zao na kujitoa muhanga, ili kuleta mabadiliko katika jamii zao. Watu kama hao ni pamoja na wale Masheikh wa Uamsho visiwani Zanzibar. Kuna mafunzo ya kuchota kwenye harakati za kuleta mabadiliko zilizoendeshwa na Mzee Nelson Mandela.

    M z e e h u y u a l i a m i n i katika msingi kwamba Waafrika Weusi hawawezi kubaguliwa kwa sababu ya rangi yao. Imani hiyo n d i y o i l i y o m s u k u m a kufanya harakati kadhaa, ili kubadilisha mfumo huo katika mazingira ya nchi yake. Mandela aliendesha

    Inaendelea Uk. 9

    a m e t h i b i t i s h a k i l e kilichosemwa na Sheikh Ilunga Kapungu, kwamba ' M f u m o ' u n a wa t a f u n a Waislamu wa Zanzibar kupitia Muungano huu wenye utata. Masheikh wa Uamsho walikuwa wakifanya harakati za kuwazindua Wazanzibari kuhusu hatari ya Muungano huu.

    Sasa katika mazingira h a y a , u n a p o e n d e s h a

    kubambikiwa kesi. Ni jambo la hatari sana!

    Mzee Nelson Mandela, mwanaharakati mashuhuri wa kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, ameondoka hapa duniani akiwa ni mtu mwenye heshima kubwa. Heshima hiyo i l i tokana na j insi alivyojitoa muhanga, katika harakati za kupinga mfumo wa ubaguzi wa rangi nchini

    MAREHEMU Sheikh Ilunga Kapungu.

    HAYATI Nelson MandelaMZEE Aboud Jumbe (mwenye miwani) akisalimiwa na Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal.

  • 9 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 12-18, 2014Makala

    Hakuna magaidi ZanzibarInatoka Uk. 8harakati za kuhakikisha kwamba mfumo wa ubaguzi w a r a n g i ( A p a r t h e i d System), haufanyi kazi na Waafrika weusi nchini humo hawatawaliki kupitia mfumo huo.

    A l i wa k u s a n ya wa t u wengine kujiunga naye na kufichua maovu ya mfumo wa ubaguzi wa rangi, ikiwa ni pamoja na kuendesha harakati za ghasia zilizolenga kuidhoofisha serikali ya makaburu. Aliandaa watu na kuwajaza Itikadi ya ukombozi, ikiwa ni pamoja na kuwajenga, ili waweze k u k a b i l i c h a n g a m o t o zinazotokana na kusimamia msingi huu wa kupinga ubaguzi wa rangi.

    Mazingira hayo aliyoandaa Mzee Nelson Mandela, yalihakikisha kwamba kifo chake au kutokuwepo kwake, hakuwezi kukwamisha harakati za Waafrika Weusi kupinga kubaguliwa nchini mwao. Kazi hii ya kusimamia msingi wa kupinga ubaguzi wa rangi, ilimfanya Mandela alipe gharama kubwa mwaka 1962, wakati alipohukumiwa kifungo cha maisha jela.

    Chama cha (ANC) na tawi lake la kijeshi, Umqhonto we Sizwe, kiliendelea na harakati zake kama kawaida, na ilipofika mwishoni mwa miaka ya 1980, utawala wa makaburu wa Afrika Kusini, ukafahamu wazi kwamba ubaguzi wa rangi hauwezekani tena nchini humo. Huyo ndiyo Mandela. Mzee huyu ametufundisha kwamba mapambano ya kudai haki hayakomi mpaka haki ipatikane.

    Wasomaji wangu mniwie radhi, mada yangu leo siyo Mzee Nelson Mandela na ANC yake. Natumia tu harakati za Mzee huyu kama mfano hai wa kile ninachotaka kueleza. Binafsi, namkubali sana Nelson Mandela, kama mwanaharakati asiyeyumba kat ika kus imamia l i l e analoamini kuwa ni sahihi,

    RAIS wa zamani wa Marekani, Ronald Reagan.

    hata mazingira yakionekana magumu vipi. Yuko tayari kufa!

    Mandela alichukiwa na tabaka tawala la Afrika Kusini wakati ule, kwa sababu alikuwa akipigania

    mabadiliko ya kuwaondoa watawala madarakani . Ser ikal i ya Makaburu, Waziri Mkuu wa Uingereza, Margareth Thatcher na Rais Ronald Reagan wa Marekani, wote walimwita "Gaidi."

    M z e e M a n d e l a hakuchukiwa kwa sababu alipigania mabadiliko, bali kwa sababu mabadiliko a l iyopigania yal i lenga k u u n g ' o a m f u m o u l i o k u we p o . M a n d e l a al iendesha harakati za k u u n g ' o a m f u m o w a ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Harakati zake kuwahamasisha wananchi kupinga ubaguzi, ndizo zilizoishinikiza serikali ya M a k a b u r u k u a n z a mazungumzo na chama cha ANC mwishoni mwa miaka ya 1980.

    Mkakati ule ule uliotumiwa na utawala wa Makaburu nchini Afrika Kusini pia u m e k u w a u k i t u m i w a na watawala katika nchi nyingine zinazoitwa huru. Watawala hawa wamekuwa w a k i w a t u h u m u w a l e wanaopigania mabadiliko ya mfumo kuwa magaidi au wachochezi.

    K a m a a l i v y o k u w a Mzee Mandela, Masheikh wa Uamsho, wamekuwa w a k i f a n y a h a r a k a t i z i n a z o l e n g a k u l e t a mabadiliko ya mfumo na muundo wa Muungano, ambayo yataifanya Zanzibar kuwa huru na yenye mamlaka kamili kama nchi. Muundo wa Muungano wa serikali mbili, unaopigiwa debe na CCM, hauna dhamira njema na Zanzibar.

    Harakati za kudai haki za Mzee Nelson Mandela zinatufundisha kwamba kuleta mabadiliko ya mfumo maana yake ni mapambano makali kati ya wanaonufaika na mfumo huo na wale wanaoupinga. Madhalimu huwa hawataki mabadiliko ya mfumo. Lakini katika mapambano ya Haki na Batili, Haki ndiyo itakayoshinda. Mwenyezi Mungu awape s u b i r a M a s h e i k h w a Uamsho. InshaAllah kile wanachopigania Zanzibar, iko siku kitakuwa kwa sababu ni haki.

    VIONGOZI wa Jumuiya ya JUMIKI Zanzibar.

  • 10 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 12-18, 2014Makala

    SERA ya mambo ya nje ya Marekani hailengi kupambana na kuenea kwa 'Uislamu wa siasa kali,' ni tofauti kabisa. Kuzuka kwa harakati hizo kunaendana kabisa na sera za Marekani tangu kuanguka kwa iliyokuwa Urusi na hali ya Mashariki ya Kati haikabani na mwelekeo uliofichika wa Marekani.

    Mkakati wa Marekani ni kukoleza na kudhibiti wimbi la ugaidi ili kuyumbisha jamii za mataifa tofauti na kuzuia kuzuka kwa madai ya kijamii yanayokinzana na maslahi ya himaya ya kiuchumi ya Marekani. U t a w a l a w a Wa s h i n g t o n unaendelea kuunga mkono, kwa kutumia operesheni za siri za CIA, kushamiri kwa siasa kali za Kiislamu kote Mashariki ya Kati, katika Urusi ya zamani, na hata China na India.

    P r o p a g a n d a y a v i t a : Mashambulizi ya kigaidi katika ardhi ya Marekani ya kiwango na aina ya Septemba 11 2001 yalifikia, kwa mujibu wa mkuu wa zamani wa makao makuu ya Jeshi la Marekani, Jenerali Tommy Franks ambaye ndiye aliyesimamia uvamizi wa Irak mwaka 2003, kukauka kwa mfumo wa kikatiba wa serikali nchini Marekani.

    Katika mahojiano ya Desemba 2003, ambayo yalitajwa kwa uchache mno katika vyombo vya habari nchini Marekani, Jenerali Franks aliainisha mazingira ambako kuondolewa kwa utawala wa Katiba kungefikia kuundwa kwa serikali ya kijeshi nchini Marekani.

    Alisema shambuilio kubwa la kigaidi linalogharimu maisha ya watu wengi mahali fulani katika nchi za Magharibi - iwe kwa mfano ni Marekani - ambako kunafikisha mahali watu wanahoji Katiba yetu na kuanza kuisuka upya nchi kijeshi ili kuondoa uwezekano wa shambulio jingine kama hilo, iliyochapishwa katika blogu ya 'Cigar Aficionado' (mpenda sigara nene) Desemba 2003.

    Franks alikuwa akiashiria kile kinachoitwa kitaaluma 'tukio kama la Pearl Harbour' (ambako Japan ilishambulia kwa ghafla kambi kuu ya jeshi la Marekani katika Bahari ya Pacific wakati nchi hizo hazikuwa vitani bado, mwaka 1942, ikaingiza Marekani vitani rasmi). Tukio kama hilo lingezua mchecheto katika hisia za watu kukubali kuundwa kwa serikali ya kijeshi yenye mtandao mkali sana wa usalama wa taifa.

    Tukio la kigaidi ambalo lingechukua maisha ya watu wengi lilizungumziwa na Jenerali Franks kama ambalo lingesababisha mabadiliko makubwa. Mgogoro ambao ungetokea, kuvurugika

    Dhamira iliyofichwa ya Marekani-2Na Profesa Michel Chossudovsky

    kwa mshikamano kijamii na hasira ya makundi makubwa ya watu ingewezesha kutokea mageuzi makubwa katika mifumo ya kisiasa, kijamii na kiutawala nchini Marekani. Ni muhimu kuelewa kuwa Jenerali Franks alikuwa hatoi maoni yake binafsi kuhusu suala hilo.

    Taarifa yake inaendana na hisia zinazofahamika kwa uwazi katika makao makuu ya jeshi la Marekani na Idara ya Usalama wa Ndani kuhusu jinsi ambavyo matukio yangeweza kufikia hali ya hatari kutangazwa nchini.

    "Matukio ya kusababisha maafa Makubwa."

    Tukio la kusababisha maafa makubwa ni sehemu muhimu ya ufundishaji katika ngazi za kuu za jeshi. Uharibifu na kupoteza maisha kutokana na shambulio la kigaidi kunasababisha hasira kubwa miongoni wa watu. Ni matukio ambayo yanaweka mazingira ya woga wa pamoja na tishio, hali ambayo inafananisha kuondolewa kwa uhuru wa mtu binafsi na kuingizwa kwa hatua za udhibiti wa hali ya nchi kwa mitandao ya kiusalama.

    Mashambulio ya Septemba 11 2001 dhidi ya majengo pacha ya Kituo cha Biashara cha Kimataifa na makao makuu ya jeshi la Marekani yalitumiwa kuinua uungwaji mkono na wananchi kwa uvamizi wa Afghanistan, ambao ulifanyika wiki nne baadaye. Marekani ilikataa kuwasilisha ushahidi kuhusu kuhusika kwa Al Qaeda ambao ulidaiwa na serikali ya Taliban ili kumtoa Osama bin Laden, hivyo Taliban ikabebeshwa mzigo wa kuhusika na mashambulio ya 9/11.

    Mipango ya kuanzisha vita ya upana mkubwa i l ikuwa imeanza mapema tu kabla ya 9/11. Wakati majeshi ya Marekani tayari yalikuwa katika 'hali ya juu ya utayari' wa vita. Mapema kabisa kabla ya mashambulio ya

    9/11, uamuzi wa kuingia vitani na Afghanistan ulitangazwa kesho yake asubuhi. Wakati huo huo NATO iliainisha Ibara ya 5 ya Mkataba wa Washington (wa kuunda umoja huo wa kujihami) na kutangaza vita dhidi ya Afghanistan kwa niaba ya wanachama wote wa umoja wa nchi hizo.

    Tangazo la vita la NATO l i l i loendana na kanuni ya 'kujilinda' lilichukuliwa ndani ya saa 24 baada ya mashambulio ya 9/11.

    Ibara ya 5 ya Mkataba wa Washington ilitajwa kwa suala hilo Septemba 12, 2001. Washirika wa Ulaya pamoja na Canada wal iahidia kuunga mkono mara baada ya mashambulizi ya k igaidi ya 9 /11 . NATO iliafiki mpango uliobuniwa na Marekani wa 'Vita ya Dunia dhidi ya Ugaidi. Wanachama 14 wa NATO walipeleka vikosi Afghanistan kwa mujibu wa jarida la NATO la muhula wa kiangazi, 2006, kuhusiana na 'Operation Northwoods.'

    Tukio la kuondoa maisha ya watu kwa wingi la 9/11 lilikuwa na umuhimu mkubwa katika mkondo wa mipango ya kijeshi. Ilitoa nafasi, katika macho ya wengi, sababu ya kutosha (au kisingizio cha kutosha) kwenda vitani.

    Kuzushwa kwa 'visingizio vya kwenda vitani' ni sehemu ya miongozo ya Pengaton (makao makuu ya jeshi la Marekani). Kwa kweli ni sehemu mahsusi ya historia ya kijeshi ya Marekani. Mwaka 1962, wakuu wa majeshi tofauti ya Marekani walitunga mpango wa s i r i unaoi twa ' O p e r a t i o n N o r t h w o o d s ' kutengeneza maafa makubwa ya watu ili kuhalalisha kuishambulia Cuba.

    "Tungeweza kulipua meli ya Marekani eneo la ufukwe wa Guantanamo na kudai Cuba i m e h u s i k a . " " Tu n g e w e z a kuanzisha kampeni ya kigaidi ya kikomunisti ya Cuba katika eneo la Miami, katika miji mingine ya jimbo la Florida na hata mjini Washington," hivyo "idadi ya maafa katika magazeti ya Marekani inatumainiwa ingewezesha wimbi la hasira kote nchini," kwa mujibu wa waraka uliowekwa wazi wa mwaka 1962 uitwao "Kuhalalisha Uingiliaji wa Marekani nchini Cuba." na kuelezewa katika machapisho ya Global Research, (http://www.globalresearch.ca/articles/NOR111A.html).

    Tahadhari za ugaidi na matukio ya ugaidi

    ili iwe na 'ufanisi,' kampeni za hofu na udanganyifu haziwezi kutegemea tu 'tahadhari' kuhusu uwezekano wa kushambuliwa baadaye, ila inahitaji matukio 'hal is i ' ya kigaidi , ambayo yanawezesha kuaminika kwa mipango ya vita ya utawala uliopo madarakani. Propaganda inakubalisha hitaji la kutekeleza 'hatua za dharura' pamoja na

    mashambulizi ya kujibu mapigo.Tahadhari za mashambnlizi na

    matukio ya kigaidi yamesaidia kutoa kisingizio cha kuhalalisha maamuzi makubwa ya kijeshi. Kufuatia ulipuaji jijini London mwezi Julai 2005, Makamu wa Rais Dick Cheney aliripotiwa kuiagiza kamandi kuu ya jeshi la Marekani USSTRATCOM (US Strategic Command) kuandaa mpango unaowezekana wa muda mfupi "unaoweza kutumika kama likitokea shambulio lingine la kigaidi kama lile la 9/11 nchini Marekani." Kilichoainishwa katika mpango huo wa muda mfupi ni uhakika kuwa Iran ingekuwa inahusika na shambulio la pili la aina ya 9/11.

    Mpango huu wa muda mfupi ulitumia kisingizio cha '9/11 ya pili,' ambayo bado ilikuwa haijatokea, kujitayarisha kufanya operesheni kubwa ya kijeshi dhidi ya Iran, wakati shinikizo likielekeza Iran kuhusiana na madai hewa ya mpango wa silaha za nyuklia.

    Kilicho cha kishetani zaidi katika uamuzi wa Makamu wa Rais wa Marekani ni kuwa uhalalishaji wa Cheney kuipiga vita Iran ulitegemea madai ya kuhusika kwa Iran katika shambulio la kigaidi dhidi ya Marekani, ambalo lilikuwa bado halijatokea.

    Mpango huo ni pamoja na mashambulizi makubwa ya anga juu ya Iran yakitumia silaha za kawaida na zinazoshabihiana na zile za nyuklia. Ndani ya Iran kuna zaidi ya maeneo ya kulengwa muhimu 450, ikiwa ni pamoja na yale yanayodhaniwa yanahifadhi mitambo ya kufanya majaribio ya kutengeneza silaha za nuklia. Mengi kati ya maeneo ya kulengwa yamezingirwa kwa zege ya aina maalum au yako chini sana ardhini na hayawezi kufikiwa na silaha za kawaida, hivyo kuwepo zile zinazoshabihiana na silaha za nuklia.

    Kama iliyokuwa wakati wa kushambuliwa Irak, mashambulizi hayo yasingetegemea kuhusika halisi kwa Iran katika tukio la ugaidi dhidi ya Marekani. Maofisa kadhaa wa ngazi za juu wa jeshi la anga la Marekani waliohusika na kuandaa mipango hiyo walisemekana kushtushwa na kile walichokuwa wanafanya - k u wa I r a n i n a a n d a l i wa kushambuliwa bila sababu yoyote - lakini hakuna aliyekuwa tayari kuvuruga matazamio yake kikazi kwa kuanza kuuliza maswali, kwa mujibu wa Philip Giraldi, katika jarida la 'The American Conservat ive ' (Uhaf idhina Marekani) la Agosti 2, 2005.

    Hivi tuelewe kuwa wapanga mikakati wa Marekani, Uingereza na Israel wanangojea tu itokee Septemba 11 nyingine, kuanza operesheni za kijeshi kuelekea Syria na Iran?

    Makamu wa Rais wa zamani wa Marekani, Dick Cheney.

  • 11 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 12-18, 2014Makala

    UMASIKINI katika dunia ya leo ni hangaiko kubwa kabisa l inalomtesa mwanadamu. Umasikini umeshadidi hata katika maeneo ambayo kuna ardhi nzuri yenye rutuba, maliasili na utajiri kama madini, dhahabu na almasi.

    Ni ukweli unaosikitisha kuona kuwa idadi kubwa ya wakazi wa dunia hii ni masikini na wengi wao ni masikini kupita kiasi. Ukiwa umebahatika kuwa na nyumba ya kukusitiri, basi kuna mamilioni kama wewe ambao hawana makazi, kama umebahatika wewe na familia yako kupata milo mitatu ya uhakika kwa siku, basi kuna mamilioni kama wewe ambao wanakufa kwa kukosa mlo mmoja kwa siku, kama wewe na familia yako mnapata huduma ya tiba pale mnapoihitaji, basi kuna mamilioni kama wewe ambao kupata asprini kwa ajili ya kutuliza maumivu yao ni neema kubwa kwao.

    Miongoni mwa vitisho na migogoro mikubwa na ya muda mrefu kwa jamii ya mwanadamu, umasikini ni moja ya vitu hivyo.

    Historia ya umasikiniHistoria ya umaskini ni sawa

    na takribani umri wa historia ya mwanadamu. Kuna watu wengi wamepoteza maisha yao katika vipindi tofauti kutokana na uhaba wa chakula au kushindwa kupata suhula na mahitaji ya awali kabisa ya maisha kama chakula, maji safi ya kunywa, mahala pa kuishi na huduma za kimsingi za afya.

    Leo hii ulimwengu umepiga hatua na kila siku wataalamu wa m e k u wa wa k i f a n i k i wa kugundua mambo mengi ya kielimu na kiteknolojia, ambayo bila shaka ni maendeleo kwa nchi husika kwa ajili ya ustawi. Licha ya maendeleo yote hayo kat ika nyanja mbalimbali , lakini inasikitisha kuona kuwa, si tu umasikini, kutokuwa na kitu, uhohehahe na ulala hoi haujatokomea, bali hata kupungua haujapungua na hali ya leo huwa mbaya kuliko ya jana yake.

    Natija ya kwanza tunayoipata kutokana na uhakika huu m c h u n g u w a u m a s i k i n i ni kwamba, maendeleo ya makubwa yaliyopatikana katika nyanja mbalimbali ulimwenguni, ambayo yametokana na juhudi za huyu mwanadamu mwenyewe hasa katika miongo ya hivi karibuni, kamwe hayajaweza kusaidia sana kupunguza na kuhafifisha moja kati ya misiba mikubwa ya mwanadamu, yaani

    Umasikini tishio kwa usalama wa duniaNa Salum Bendera

    HALI ya umasikini Somalia iliyosababishwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea nchini humo.

    umasikini. Vi le v i le uvumbuzi huu

    unaoonekana na kutangazwa kila siku kuhusiana na masuala m b a l i m b a l i u l i m we n g u n i , haujaweza kufanikiwa kupunguza v i t a d u n i a n i n a k u s a i d i a kueneza amani na usalama au hata kulitatua tatizo la dawa za kulevya, magendo ya binadamu, utumwa mambo leo nk.

    Kwa nini maendeleo hayajaweza kupunguza machungu ya umasikini?

    Sababu hasa ya maendeleo haya ulimwenguni kushindwa kulitafutia ufumbuzi suala la umasikini ni kuwa, maendeleo ya mwanadamu huyu hayakuja na kupatikana kwa aji l i ya kumhudumia mwanadamu, bali ni kwa ajili ya kuyahudumia madola makubwa na tajiri ulimwenguni, yaani kwa ajili ya kuhudumia mabepari.

    Katika hali ambayo kuna watu ambao hata hawawezi kukidhi mlo mmoja kwa siku, watu wengine ni matajiri kupita kiasi na kila siku wamekuwa wakifikiria, wakiwaza na kuwazua namna ya kujilimbikizia mali na kuongeza utajiri wao,tena kwa dhulma. Lau kama matajiri hao badala ya kujifikiria wao na kuongeza utajiri wao wangekuwa wanafikiria namna ya kuwapunguzia matatizo mustadhaafu na wenye kuhitajia, sidhani kama hali ingekuwa hii tunayoishuhudia hii leo katika pembe mbalimbali duniani.

    Aina za umasikini

    Kwa ujumla wataalamu wa mambo wanaugawa umasikini katika makundi mawili makuu. Umasikini mkubwa au ulala hoi na umasikini usio mkubwa. Katika umasikini mkubwa au

    ulala hoi wa kupindukia, ni kuwa utapata watu hawana uwezo wa kukidhi mahitaji yao ya kimsingi kama vile, chakula, nyumba, mavazi na huduma za afya na matibabu. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, kigezo kinachotumika kwa ajili ya kuainisha umasikini huo ni wale watu ambao wanaishi kwa kipato cha chini ya dola moja kwa siku, ambapo kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia, zaidi ya asilimia 20 ya watu ulimwenguni wanaishi kwa kipato hicho.

    Sehemu ya pili ya umasikini unaojulikana kama umasikini usio mkubwa. Hata kama hali si mbaya ukilinganisha na ya umasikini wa aina ya kwanza, lakini katika kundi hili la umasikini pia kuna watu ambao hawapati huduma muhimu na za lazima kama elimu, afya, lishe bora na mambo mengine ambayo ni huduma za lazima na za dharura katika maisha.

    Ta k w i m u z i n a o n y e s h a kuwa, takribani nusu ya watu duniani wamo katika hali hii ya pili ya umasikini. Takwimu hizo zinazohusiana na ueneaji wa umasikini duniani ni za kusikitisha na zenye kufanya mtu ajiulize maswali mengi, hasa kutokana na maendeleo makubwa tunayoyashuhudia hi i leo ul imwenguni. Hata hivyo tunapochunguza kwa makini, tunaona kuwa tatizo hilo halisababishwi na uhaba au upungufu wa suhula, bali unatokana na siasa mbovu za mataifa pamoja na ugawaji wa utajiri usio wa kiadilifu au kuweko madarakani viongozi ambao ni vibaraka wa madola ya kibeberu, ambao huruhusu mali na utajiri wa mataifa yao kuporwa na kuhamishiwa katika madola hayo ya kibeberu.

    Kwa mujibu wa takwimu rasmi kuanzia mwaka 1990, pato la nchi zinazoendelea ongezeko lake kwa wastani lilikuwa ni asilimia 3. Lakini wakati huo huo, katika kipindi hicho pato la wastani la nchi 54 duniani lilipungua. Branko Milanovic, mmoja kati ya wanauchumi wa Benki ya Dunia ameweka wazi nukta hiyo katika uchunguzi wa kila upande alioufanya na kubainisha kwamba, pato la asilimia moja miongoni mwa watu matajiri kabisa duniani ni sawa na kiwango cha asilimia 57 ya masikini duniani.

    Katika maeneo mbalimbali duniani hali ya dhulma, ubaguzi na ukosefu wa uadilifu inaonekana wazi kabisa. Kwa mfano katika maeneo ya Amerika ya Latini kipato cha asilimia 5 cha tabaka la matajiri katika jamii ni mara mia tatu ya kipato cha asilimia 5 cha tabaka masikini kabisa katika nchi za eneo hilo.

    Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa, asilimia 60 ya watoto Kusini mwa Asia na Kusini mwa Jangwa la Sahara wanaishi katika umasikini mutlaki. Kwa kuzingatia uhakika huo, bila shaka kuna haja ya kuandaliwa mipango madhubuti kwa ajili ya kukabiliana na baa la umasikini ulimwenguni.

    Sehemu kubwa ya hali mbaya ya kiuchumi duniani inatokana na mfumo mbovu ulioenea ulimwenguni, wa ugawaji mitaji na fursa za kiuchumi na kibiashara. Katika mfumo huo wa kiuchumi, ni dhahiri inaonekana kuna fursa za uwiano na mlingano, ambazo hupatiwa watu wote lakini kwa vitendo matajiri na wenye mitaji mikubwa ndio ambao hufaidika zaidi na fursa hizo, kwa ajili ya kujiongezea nguvu zao za kisiasa na kiuchumi.

    Ukoloni wa zamani na ukoloni mambo leo umetokana na fikra hii ya kupata faida ya Kimagharibi, ambapo kupitia mfumo huo utajiri wa makumi ya nchi za ulimwengu wa tatu umeporwa na wakoloni wao. Si hayo tu, bal i kuna mambo mengine yanayotawala ulimwengu leo hii, ambayo kwa hakika hayawezi kufumbiwa mambo kutokana na kuwa na nafasi katika kueneza umasikini ulimwenguni.

    Bila shaka hakuna anayepinga kwamba, baadhi ya asasi za kifedha za kimataifa kama vile Mfuko wa Fedha wa Kimataifa ( IMF) na Benki ya Dunia , zimekuwa na nafasi katika kuenea umasikini ulimwenguni kutokana na utendaji wao kutokuwa wa uwiano na uadilifu. Asasi hizo kwa kutoa mikopo na kutwisha masharti ikiwa ni pamoja na kuchukua faida na riba kubwa kwa mikopo yake hiyo kutoka kwa nchi zinazostawi, zimekuwa zikizishinikiza mno nchi hizo.

    Kutokana na nchi hizo wakati

  • 12 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 12-18, 201412 Barua/Mashairi

    Ndugu Mhariri,N a s h a n g a z w a n a Wayahudi kila uchao kuwaua Wapalestina katika Ukanda wa Gaza. Nikiwa binadamu m w e n y e k u j a l i utu, nahuzunishwa kushuhudia mauaji ya wasiokuwa na hatia, nalaani mauaji hayo na nawausia wapenda a m a n i w e n g i n e kufanya hivyo.

    K i s h a w a l i o d h u l u m u wataambiwa ionjeni a d h a b u i k a a y o . H a m t a l i p w a i l a kwa yale mliokuwa mkyachuma. (Quran suratul Yunus).

    D h u l m a k a f a r a , chumo la hasara, amali dhaifu, kilio na hofu. Lakini matendo mema neema.

    Tu t a f a k a r i s i k u watoto watakapouliza kisa na sababu ya k u u l i w a k w a o . Waliowafanya wengine walemavu kwa vita wataonja adhabu pevu.

    Waliowaua watoto, ajuza na wanawake

    Ya Gaza yanishangazawasiokuwa na hatia watapata malipo yao kwa Allah (sw).

    W a m e a n g a m i z a m a j u m b a , s h u l e , hospitali, Misikiti hakika w a t a n a s a k w e n y e ulimbo wa kuchukiza. Huo ni ukweli, si kama naapiza. Sina sifa ya kupatiliza.

    La haki nil iseme, Waarabu na Wayahudi k w a m u j i b u w a maandiko ni ndugu wa baba mmoja. Wote ni watoto wa Nabii I b r a h i m , a m b a y e katika kipindi kabla ya kuzaliwa Nabii Isa (as), alihama kutoka Iraq na kuishi katika mji wa Khalil.

    Hapo aliruzukiwa kupata watoto wawili ambao ni Nabii Ismail (kaumu ya Waarabu) na Nabii Ishaq (Kaumu ya Wayahudi) na baadae mwaka 1750 Nabi i Yakub alizaliwa.

    W a a r a b u n a Wa y a h u d i k a t i k a kuthibitisha kuwa ni ndugu wanaotokana na baba mmoja, hata sura

    zao wanafanana.K a m a w a t a a c h a

    vita na kupatana nina hakika sehemu kubwa ya Mashariki ya Kati itakuwa salama.

    Hata hivyo, Marekani a m b a y o i m e k u w a bwana wa Wayahudi, isijivike joho la Mungu kuwatuma Wayahudi k u z i t o a r o h o z a Waarabu.

    Marekani na Israel, warudi kwa Mungu w a o . W a y a h u d i wajifunze kutoka kwa Hitler, juu ya athari za kihistoria za vita vya pili vya dunia.

    I l e n e m b o y a Marekani iliyochagizwa na maneno In God we trust , hebu ifanyieni kazi kwa uadilifu ili dunia iwe salama!

    Tumechoka na zogo la vita huku wakubwa w a k i n y a m a z a n a kuangalia kama sinema.

    Y a G a z a yanashangaza, yanaliza.

    M z e e H a s s a n M k we n d e H a s s a n (Kuchona)

    Unyama wa mazayuni, dhidi ya PALESTINA,Unyama wa mazayuni, si usiku si mchana,Unyama wa mazayuni, bila shaka mwauona,Unyama wa mazayuni, walimwengu kila kona,Tupinge uhayawani, wao japo kwa kunena. Unyama wa mazayuni, umekithirika sana,Unyama wa mazayuni, kiasi si kunga tena,Unyama wa mazayuni, kwa insi kutouona,Unyama wa mazayuni, na madharaye bayana,Tupinge uhayawani, wao japo kwa kunena.

    Unyama wa mazayuni, wahilikisha insana,Unyama wa mazayuni, MADHULUMU kwa khiyana,Unyama wa mazayuni, japo hatia hawana,Unyama wa mazayuni, kwa ya kivita mazana,Tupinge uhayawani, wao japo kwa kunena.

    Unyama wa mazayuni, pamwe na yao mazana, Unyama wa mazayuni, waogopa kupambana,Unyama wa mazayuni, na wa JESHI wale WANA,Unyama wa mazayuni, wa HAMAS tena sana,Tupinge uhayawani, wao japo kwa kunena.

    Unyama wa mazayuni, badalaye wakazana, Unyama wa mazayuni, kuua WAKE na WANA, Unyama wa mazayuni, na RAIA waso zana,Unyama wa mazayuni, japo hatia hawana,Tupinge uhayawani, wao japo kwa kunena.

    Unyama wa mazayuni, siriye moja kunena,Unyama wa mazayuni, leo aula naona,Unyama wa mazayuni, ipate tambulikana,Unyama wa mazayuni, kwa walimwengu bayana,Tupinge uhayawani, wao japo kwa kunena.

    Unyama wa mazayuni, unyuma wa yule 'bwana',Unyama wa mazayuni, ajifanyaye 'mungwana',Unyama wa mazayuni, na 'mwenye huruma sana', Unyama wa mazayuni, kila kona kupambana! Tupinge uhayawani, wao japo kwa kunena. Unyama wa mazayuni, ni kweli hajauona? Unyama wa mazayuni, hapana hilo nakana!Unyama wa mazayuni, kwanini yashindikana?, Unyama wa mazayuni, u nyumaye huyo 'bwana',Tupinge uhayawani, wao japo kwa kunena.

    Unyama wa mazayuni, si sawa kuunong'ona,Unyama wa mazayuni, tuutongoe bayana,Unyama wa mazayuni, waumanye hata WANA,Unyama wa mazayuni, kwa mawanda na kwa kina,Tupinge uhayawani, wao japo kwa kunena.

    ABUU NYAMKOMOGI-SAFARINI KAGERA.

    Kumbuka asili yako 1.Mwanadamu hutambui, asiliyako ni nini Wajifanya hubaini, hukuwa wewe manii Khasimu wa rahamani, mwanadamu punguani Twakuonya huonyeki, ipo siku utajuta.2.Kwanini wajihiliki, kutufanyia mzaha Tumekuletea haki, waifanyia fedheha Kuisadiki hutaki, iposiku utahaha Subiri yaje mauti, ndipo chamoto taona3.Twakukumbusha qiyama, tukio hili la haki Bila shaka tasimama, hakuna atayebaki Ukweli utausema, japo moyo hautaki Ndio utasimamishwa, mbele yao halaiki4.Tukio hili fedheha, litadumu kwayakini Halitojali jamaa, wala ndugu wa nyumbani Siku moja ya fedheha, ni miaka hamsini Mwanadamu we-tubia, sujudu kwa rahamani5.Hakika u-khasarani, na utatiwa motoni Hivi unavyojikhini, kwa kutupa qur-ani Hujui u-safarini, twakusubiri wanjani Tutakuvuta kwa nguvu, zako nywele za utosi.6.Utosi ulokiburi, unokupa ukafiri Utosi wenye jeuri, wakufunza ufedhuri Tutakushika vizuri, vizuri kwa ujabari Utakiona cha moto, na kusagasaga meno7.Chamoto utakiona, hilo mapema ujuwe Vizuri tutakubana, kwa yetu makubwa mawe Katu huwezi kupona, twasema ujitambue Amakweli mwanadamu, mjinga usofikiri8.Ni mjinga bila shaka, mjinga sotafakari Kwanini umeumbika, tena kwa umbo makini Iposiku bila shaka, utaipata khabari Utajuta mwanadamu, kwahili twakukariri9.Hii nema takuhoji, kwa vile yetu amana Tumekupa mahitaji, yalomengi yakufana Umekua mfujaji, watumia kwa laana Kweli tauona moto, hasa moto unochoma10.Huo ni moto mkali, unobabua ngozini Moto unoshika mwili, namna takuchomeni Hili ni onyo dhahiri, kwenu ninyi miongoni Tubia mshike dini, mola takusameheni11.Juu yake tumeweka, walinzi mekamilka Moja tisa malaika, vizuri wamefunzika Basi na atayetaka, haraka atakumbuka Hili ni letu kumbusho, tamfaa tayeshika

    Abu Nurain Al-Tanza

    UNYAMA WA MAZAYUNI!

    WAISLAMU wa Masjid Kadiria Mwasiti uliopo kijiji cha Kibuta wilayani Kisarawe mkoani Pwani wanawashukuru Waislamu na Dada Mwasiti Hamisi kwa kufanikisha ujenzi wa Msikiti wa kisasa wa matofali ambao awali ulikuwa wa miti.

    Hata hivyo wanaomba msaada wa kuchimbiwa kisima katika Msikiti huo, madrasa ya watoto na jenereta kwa ajili ya kusukuma maji kwa ajili ya matumizi Msikitini.

    Gharama za uchimbaji wa kisima hicho ni shilingi milioni tatu. Dada Mwasiti amejitahidi kuchangisha pesa kwa ajili ya kuchimba kisima hicho na mpaka sasa amefanikiwa kupata milioni moja tu. Watoto wameshapatiwa sare na Juzuu za mafunzo.

    Shime Muislamu kutoa ni moyo, unaombwa kuchangia chochote

    Msaada Masjid Kadiria

    ulichojaaliwa na Muumba wako kwa ajili ya kuweka akiba ya Akhera yako.Unaweza kuchangia kupitia Akaunti ya benki na namba za simu zifuatazo:

    0656 092 436 au 0655-906898.

    A/c No 001340085740001 Amana Bank

    Wabillah Tawfiq

  • 13 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 12-18, 2014MAKALA

    N I j a m b o l a k h e r i k w a mwanadamu, mume au mke kuwa na mwenza wake wa ndoa katika nyakati za maisha yao yote hapa duniani. Kuoa au kuolewa, ni tendo ambalo huleta faraja kubwa ya moyo kwa mwanadamu katika maisha yake, huchochea uwajibikaji, kujiamini na kujenga heshima katika jamii.

    N i j a m b o l i l i l o d h a h i r i kwamba mahusiano baina ya wanandoa, ndiyo mahusiano yaliyo bora kabisa katika maisha ya mwanadamu.

    Leo tuzungumzie umuhimu wa mume kumuenzi mkewe, mke ambaye Mwenyezi Mungu ametueleza kuwa ndio faraja na tulizo kwa mume.

    Katika maisha yetu ya kila siku, mke ndio mwenzi katika maisha yote ya mume, ndiye mwandani wake na rafiki yake kipenzi.

    Kuna kila sababu ya mume kumuenzi na kumjali mkewe, hasa ikizingatiwa kwamba kwa uwezo wa mwenyezi Mungu, mwanamke ndiye alojaaliwa kubeba sehemu kubwa ya mchakato wa kuumbwa kiumbe binadamu hadi kumletwa duniani.

    Kisha kiumbe hicho kinapewa ubini wa baba (patrinial) badala ya mama, na mama hakuona husda wala jazba katika hilo, zaidi ya kuongeza utii kwa mumewe na kumkirimu.

    Mara nyingi mke mwema anaona kuwa ana deni la kushiriki na mumewe katika nyakati zote za uhai wa mumewe, ziwe ni za furaha au huzuni, shida au raha, mafanikio au taabu, mke atakuwa pamoja na mumewe.

    Mume akiumwa, mkewe atampa huduma bora kwa kadiri ya uwezo wake. Unapohitaji msaada atafanya awezavyo kwa ajili yako, ukihitaji ushauri, atakupa ushauri kadiri itakavyofaa.

    Kwa mume anayejali, mkewe anakuwa ndio mtu wa mwisho kumuona kabla ya kulala na wa kwanza kumuona baada ya kuamka.

    Mke ndiye anayejua kwa undani aibu za mumewe zote, anayejua hulka za mumewe huyo, anayejua uwezo wake, tabia zake, mahitaji yake, machukizo yake n.k.

    Hakika Mwenyezi Mungu anajua kila jambo. Anasema katika Quran: Wao ni vazi kwenu, na nyinyi ni vazi kwao [Al-Baqarah 2:187].

    Kweli, wanandoa ni kama vazi juu ya wao kwa wao kwa sababu wanapeana ulinzi, liwazo, kinga, stara, kusaidiana n.k.

    Mahusiano ya kimapenzi ya

    NAFASI YA MWANAMKE

    Wanaume tuwaenzi wake zetuNa Shaban Rajab mume na mke ni ya kipekee

    kabisa. Ni mahusiano ambayo si rahisi kuyaelezea kirahisi. Hii inathibitishwa na Mwenyezi Mungu pale aliposema: Na Allah Amekuumbieni wake (na wenza) katika jinsi yenu) An-Nahl 16:72.

    M w e n y e z i M u n g u amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Na amejal ia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo ishara kwa watu wanaofikiri." A-Ruum 30:21.

    Lakini Allaah Subhanahu Wa Taaala Anajua kwamba moyo wa binaadamu sio kitu ambacho kiko tuli, wakati mwengine huwa dhaifu na wakati mwengine huwa na nguvu.

    Hisia zinaweza kubadilika na hubadilika pindi wakati u n a v y o s o g e a . M a p e n z i yanaweza kufifia na kupayuka mbalini. Mshikamano wa ndoa unaweza kuwa dhaifu kama haujahudumiwa vizuri. Furaha katika ndoa haiwezi kudharauliwa; furaha ya kuendelea inahitaji utowaji wa daima kutoka pande zote. Ili mti wa mapenzi ya ndoa ubaki hai na kuendelea kuishi, udongo lazima udumishwe, uhifadhiwe, umwagiwe maji na ulelewe.

    Kamwe usidharau umuhimu wa vitu vidogo vidogo kama vile kuweka chakula kwenye mdomo wa mkeo, kumfungulia mlango wa gari, na hali kadhalika. Kumbuka kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anasogeza goti lake kwa mkewe amkanyage kuweza kumpanda ngamia.

    Jaribu kutafuta wakati ili nyote wawili muweze kuswali pamoja. Kuuimarisha uhusiano kati yenu na Allaah (Subhanahu wa Ta'aala) ni hakikisho kubwa kuwa uhusiano wenu wa kindoa utabaki madhubut i . Kuwa na amani kati yenu na Allah (Subhanahu wa Ta'ala) daima kutapelekea ndani mwenu kuwa na amani zaidi. Kumbuka kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwapa habari nzuri (aliwabashiria) wanandoa wanaoamka usiku kuswali pamoja. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anamsisitiza mwanandoa anayeamka mwanzo amuamshe mwenzake, japo kummwagia maji katika uso wake.

    Ni vizuri wanaume wakajaribu kwa kadiri wawezavyo kuwa watu wazuri kwa wake zao kwa vitendo. Kimantiki mwanamke huwa mtulivu na mwenye aibu na hufarijika sana asikiapo maneno matamu yanayoonyesha kumjali kutoka kwa mumewe.

    Pia hekma ya mume katika kumkabili mkewe, daima ni silaha kubwa ya kuepusha kibri na mitafaruku baina ya wanandoa.

    K u w a t i m i z i a a h a d i tunazowaahidi ni jambo la

    msingi sana kwa mwanamme kumuenzi mkewe. Kama uliahidi kumnunulia zawadi basi timiza ahadi hiyo. Kama ulimuahidi kuzuru naye mahali fulani ni vyema ukatimiza ahadi hiyo nk.

    Pamoja na mapenzi katika ya mke na mume, pamoja na mume kutimiza jukumu la kumuenzi mke barabara na mke kuendelea utii kwa mumewe, itoshe wote kuwa na yakini kuwa kuna maisha baada ya mauti.

    K w a w e m a n a i h s a n i uliyomfanyia mkeo duniani, na kwa uvumilivu na utii aliofanya mke kwa mumewe, basi watakuwa na nafasi kubwa mbele ya Allah (sw) pale aliposema, Ingieni Peponi, nyinyi na wake zenu; humo mtafurahishwa. (Az-Zukhruf 43:70).

    Ni somo tosha iwapo tutafuata somo la mapenzi ya Mtume Muhammad (saw) kwa mkewe Bi. Hadijah aliyeishi naye kwa miaka 25.

    Pamoja na kwamba Bi. Hadijah alikuwa tajiri mkubwa na mkubwa kwa Mtume (saw), mkewe huyo alimheshimu sana, alimtii kwa kila hali hata kabla ya Mtume kupewa Utume.

    Naye Mtume alimuenzi kwa kila hali mkewe, hakumkwaza na alimkumbuka kila wakati hata baada ya kupita miaka mingi baada ya kifo cha mkewe.

    Kama alitoa zawadi hakuacha kuwakumbuka wale aliokuwa akiwapenda Khadijah. Akichinja

    mbuzi sharti atume sehemu kwa familia ya Bibi Khadijah na marafiki zake.

    Pamoja na kwamba hutoa hitilafu kati ya mume na mke, lakini Mwenyezi Mungu kaajalia subra na uvumilivu.

    Kwa wenye hekima, hitilafu za mizozo ya mke na mume huondolewa kwa kusubiri hasira, baada ya kupoa, wawili hukaa pamoja na kuombana radhi na kuelekezana palipotokea kosa na kusawazisha.

    Hata Mtume (Saw) wakati fulani i l i tokea kukerwa na wakeze, ilipotokea hali hii alikaa mbali kwa muda, kisha alirejea na kuzungumza nao hali ya kuwa wote wamepoa.

    Na wakati mwingine joto lilipopanda, Mtume alichukua kiasi cha maji na kunywa. Tendo hili husaidia kushusha hasira na kutulia.

    Pia ni vyema kuzunguza na mwezi wako nyote mkiwa mmekaa, hitilafu ya maneno kwa waliosimama haina kupoa haraka.

    Yote haya ni mafunzo ya Mtume (saw) juu ya maisha yetu ya kila siku katika jamii.

    Inshaalah mwenyezi Mungu awajaalie wanaume kuwa na wake wema, wanawake kuwa na waume wenye mapenzi ya dhati kwa wake zao na familia zao na hatimaye lipatikane zao jema katika familia.

  • 14 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 12-18, 2014Habari

    Maalim Seif aikosoa serikali kuhusumigogoro ya wakulima na wafugajiInatoka Uk. 16

    akihutubia katika mikutano ya hadhara katika vijiji vya Ngudu na Hungumalwa Wi layani humo, amefuatana na viongozi waandamizi wa CHADEMA wa mkoa wa Mwanza.

    Alisema katika kipindi cha miaka 53 tangu nchi ilipopata uhuru, kadiri siku zinavyokwenda mbele hali za maisha ya wananchi zinazidi kuwa mbaya, kutokana na nchi kukosa uongozi bora chini Chama cha Mapinduzi.

    Ujumbe wetu kwenu ni kuwa CCM imeshalewa madaraka, h a i w e z i t e n a k u w a l e t e a mabadiliko ya kimaisha, kipeni talaka na mchague vyama vyenye uwezo wa kuwaletea maendeleo, alisema Katibu Mku wa CUF.

    Alisema uthibitisho wa CCM kukosa uwezo wa kuwaletea mabadiliko ya kimaisha wananchi ni namna ambavyo wanavuruga mchakato wa kupata Katiba Mpya, ambao wananchi wa Tanzania Bara na Zanzibar walitarajia uweke misingi bora ya maisha yao ikiwemo matumizi ya maliasili za ardhi, madini, kilimo, elimu bora na utawala bora kwa jumla.

    Maalim Seif alisema CCM wa m e b a d i l i s h a m a o n i ya wananchi yaliyowasilishwa na Tume ya Mbadiliko ya Katiba chini ya Jaji Mstaafu Warioba, maoni ambayo msingi wake ni mfumo wa Serikali tatu baada ya wananchi hao kubaini ndio wenye maslahi kwao.

    Alisema badala yake, CCM kimepindua maoni hayo bila ya kujali fedha nyingi zilizotumika, lengo lao likiwa ni kulinda maslahi ya wachache na kupuuza shida zinazowakabili Watanzania ambao wameshaona mfumo wa Serikali mbili hauwafai tena.

    Alieleza kuwa wanafanya hivyo kuendeleza ufisadi unaofanywa na baadhi ya viongozi wa chama hicho, kama ule wa kuiba fedha nyingi za wananchi na kwenda kuzificha katika mabenki ya nje kama nchini Uswisi.

    Vyama vya CUF, CHADEMA na NCCR Mageuzi vina viongozi makini, wenye uwezo wa hali ya juu na vimedhamiria kikweli kuwaletea mabadiliko ya kimaisha wananchi wote wa Tanzania bila ya ubaguzi kama inavyofanyika chini ya CCM, alisema.

    N a y e M w e n y e k i t i w a CHADEMA Wilaya ya Ilemela, Greyson Wanzagi Warioba,

    akihutubia katika mkutano wa N g u d u a l i s e m a C C M imejidhihirisha wazi hakikuwa upande wa wananchi kwa miaka yote tangu kupatikana uhuru, kutokana na kitendo chao cha kujifungia Dodoma na kupindua maoni ya wananchi wa Tanzania.

    Alisema chama hicho kinajali maslahi yao binafsi, na Umoja wa Kutetea maoni ya Wananchi (UKAWA) utaendela kufichua maovu wanayofanya, ili wananchi wayaelewe na wakikatae katika uchaguzi mkuu ujao.

    Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano ya Umma CUF, Hamis Kambaya alisema Serikali ya CCM haiwajali wananchi wa Kanda ya Ziwa kutokana na kitendo cha kuwapatia wananchi hao mbegu zisizofaa za zao la Pamba.

    Mbali na hilo alisema bei ya zao hilo hivi sasa ni ya chini kiasi kwamba haiwezi kumsaidia mkulima anayekabiliwa na hali duni ya maisha na kumfanya ashindwe kupata mlo kamili wa siku, mbali na huduma nyengine kadhaa wa kadhaa muhimu za kijamii zinazomkabili.

    Mwenyekiti wa Wanawake wa CHADEMA katika mkoa wa Mwanza, Suzan Masele alisema umefika wakat i wanawake waepuka kulaghaiwa kwa Khanga

    KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake mkoani Mwanza hivi karibuni.

    na Vitenge kunakofanywa na viongozi wa CCM wakati wa

    uchaguzi kwa sababu mambo hayo tayari yamepitwa na wakati.

  • 15 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 12-18, 2014Makala ya Mtangazaji

    45 children critically injured in Gaza to be treated in Germany GAZA CITY (Maan) -- Forty-five children severely injured in Israels seven-week offensive on Gaza will be transferred to Germany on Monday to receive medical treatment, a Palestinian MP said.

    Ashraf Jumaa said 45 children, some of whom underwent amputations in Gaza hospitals, will be treated abroad in Germany.

    The trip was organized and paid for by the Union of Palestinian Doctors and Pharmacists in Germany after a visit to the besieged enclave on Sunday.

    The union will also reportedly take custody of 300 children orphaned during the Israeli offensive.

    Some 90 entire families were killed during the conflict, Jumaa said.

    Over 2,100 Palestinians, most of them civilians, were killed in Israels seven-week assault on the Gaza Strip, with a further 11,000 injured.

    Up to 1,000 Palestinians are likely to suffer a permanent disability from their wounds.

    Israel must end discrimination against Palestinians: OHCHR

    The United Nations High Commissioner for Human Rights has called for an end to the Israeli regimes discrimination against the Palestinian people in the occupied West Bank and the Gaza Strip.

    Another example of the need to end persistent discrimination and impunity is the Israel-Palestine conflict, with the recurring violence and destruction evident in the repetition of crises in Gaza, Zeid Raad Al Hussein, UN High Commissioner for Human Rights, said in his opening statement at the Human Rights Councils 27th session in Geneva on Monday.

    He added that the recent Israeli aggression against the Palestinians resu l ted in a par t i cu lar ly devastating death toll, suffering and destruction, and compounded an already precarious situation due to the Gaza blockade imposed by Tel Aviv in 2007.

    Current and future generations of Palestinians in Gaza and the West Bank, including East Jerusalem, have a right to live normal lives in dignity: without conflict, without a blockade, indeed without the wide range of daily human rights infringements that are generated by military occupation, illegal settlements, excessive use of force, home demolitions, and the Wall that continues to be constructed across the occupied Palestinian

    territory, Hussein pointed out.Israel started pounding the

    blockaded enclave in early July. Some 2,140 Palestinians, mostly civilians, including women, children and elderly people, were killed in the Israeli military aggression against the Gaza Strip. Around 11,000 others were injured.

    Israeli Forces Seize Bulldozer from Stone-Cutting Factory near Bethlehem

    BETHLEHEM (WAFA) Israeli forces seized Monday a bulldozer from a stone-cutting factory in Beit Fajjar to the south of Bethlehem, said a local source.

    According to Head of the Union of Stone and Marble Industry in Palestine Subhi Thwabteh, large Israeli troops raided and cordoned off Khalit Hajja area in Beit Fajjar, where they extensively searched some stone and marble-cutting factories, opened fire on Palestinian workers, seized a bulldozer and damaged an excavator.

    Thawabteh noted that Israeli forces f requent ly targeted Palestine stone-cutting factories and industrial facilities, causing extensive losses to their owners.

    Jerusalem clashes after teens funeral

    JERUSALEM (Maan) -- Israeli forces attacked the funeral procession of slain Jerusalem teenager Abd al-Majid Sinokrot after mourners marched from his hometown of Wadi Joz to the al-Aqsa mosque on Monday.

    Mourners raised Palestinian flags and after they left the mosque, Israeli forces fired stun grenades, tear gas, and rubber-coated steel bullets toward them near al-Sahira gate.

    Clashes also broke out along Salah al-Din Street in Jerusalem.

    The clashes shut down traffic throughout much of occupied East Jerusalem.

    O v e r 7 7 0 P a l e s t i n i a n s have been detained in East Jerusalem following widespread demonstrations in the East Jerusalem neighborhood of Shufat after the murder of teenager Muhammad Abu Khdeir on July 2.

    Child Injured, Four Children Kidnapped, Near Jenin

    (IMEMC) - Israeli soldiers invaded, on Monday at night, the town of Yabad, West of the northern West Bank city of Jenin, shot and injured a Palestinian child, and kidnapped several residents.

    Eyewitnesses have reported that clashes took place between the invading soldiers and local youths, and that the soldiers fired rounds of live ammunition, rubber-coated metal bullets and gas bombs.

    The clashes took place in different parts of the town, focusing mainly in the School Area, and another area where local workshops are located.

    Medical sources said the wounded child, identified as Imad Herzallah, 14 years of age, was shot by a live round in his shoulder, and was moved to a local hospital.

    In addition, soldiers kidnapped four children in the town, and took them to a nearby military and security base.

    Eyewitnesses said the soldiers also fired dozens of rounds of live ammunition, concussion grenades and gas bombs at a number of homes, and stores, causing dozens of residents to suffer the effects of tear gas inhalation.

    Army Kidnaps Twelve Palestinians

    Near Nablus(IMEMC) - Israeli soldiers,

    stationed at the Zatara military roadblock, south of the northern West Bank ci ty of Nablus, kidnapped on Monday evening twelve Palestinians and took them to an unknown destination.

    Eyewitnesses said the soldiers were searching cars and inspecting the ID cards of dozens of Palestinians, causing a huge traffic jam, upon which they kidnapped twelve young Palestinians who remained unidentified at the time of this report.

    The army also closed the roadblock, preventing hundreds of Palestinians from crossing, and did not provide a reason for the arrests, and the temporary closure of the roadblock.

    Earlier on Monday at dawn, Israeli soldiers invaded different communities of the occupied West Bank, broke into and searched several homes and kidnapped six Palestinians.

    IOF soldiers round up Palestinian citizens in WB raids

    R A M A L L A H - I s r a e l i occupation forces (IOF) rounded up several Palestinian citizens during raids in many areas of the West Bank at dawn Monday and Sunday night.

    The Palest inian prisoner association (pps) said in a statement on Monday that IOF soldiers nabbed two Palestinians in Tubas town.

    It said that three others were detained in Bethlehem, one in Jericho and a teenager in al-Khalil.

    Israeli policemen nabbed a 17-year-old boy from his home in occupied Jerusalem.

    Meanwhile, eyewitnesses told reporter that large numbers of IOF soldiers raided the village of Burin, south of Nablus, at dawn Monday and broke into many homes.

    They said that the soldiers field-interrogated several citizens but no arrests were reported.

    In Nablus city, IOF soldiers in dozens of army jeeps raided al-Ein suburb and searched many shops and warehouses after blasting their doors.

    The PPS said in a statement on Sunday that IOF soldiers rounded up 127 Palestinians in the first week of September.

    Contact us: P.O Box 20307, 612 UN Road Upanga West, Dar es Salaam Tel: 2152813, 2150643 Fax: 2153257 Email: [email protected]: www.pal-tz.org

  • 16 AN-NUURDHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 12-18, 201416 MAKALA

    Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na POA Printing Works Limited, S.L.P. 4605 Dar es Salaam.

    AN-NUUR16 DHULQAAD 1435, IJUMAA SEPTEMBA 12-18, 2014

    Tanzania Muslim Hajj Trust. Uandikishaji unaendelea, gharama za Safari ni $ 4400Tarehe za safari ni 22 na 24 Septemba na Kurudi 16 na 19 Oktoba, 2014.Tunasafiri na Shirika la Ndege Umoja wa Falme za Kiarabu EMIRATES.

    Wahi kujiandikisha sasa.Kwa Mawasiliano: +255222181577 +2552221823700786 383820 0717 [email protected] or Website: wwwhajjtrusttz.org

    Safari ya Hijja Hijiria 1435/2014

    K AT I B U M k u u w a Chama cha Wananchi CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema migogoro inayowakumba wakulima na wafugaji na kusababisha mauaji, inatokana na Serikali i l i y o p o m a d a r a k a n i kukosa sera sahihi ya kilimo na ufugaji.

    Maalim Seif, aliyasema hayo alipokuwa akihutubia wananchi katika mikutano mbalimbali ya hadhara katika ziara yake ya siku nne mkoani Mwanza, ambapo alizindua miradi ya maendeleo iliyo katika Kata zinazoongozwa na CUF mkoani humo.

    A k i z u n g u m z a n a wa n a n c h i b a a d a ya kuzindua daraja katika Kata ya Igogo, alisema inasikitisha kuona kila siku wakulima na wafugaji wakiuana kwa kugombea maeneo ya kilimo na kulishia mifugo, huku S e r i k a l i i k i s h i n d wa kudhibiti hali hiyo.

    Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, alisema mauaji kati ya wakulima na wafugaji yasingekuwepo kama Serikali ingekuwa na Sera thabiti zinazoanisha maeneo maaluma kwa ajili ya ufugaji na maeneo maalum kwa shughuli za kilimo pekee.

    K a m a S e r i k a l i i n g e k u w a n a S e r a inayoanisha maeneo ya ufugaji na ya kilimo, t u s i n g e s h u h u d i a mapigano na mauaji haya, wakulima na wafugaji wangefanya kazi zao kwa utulivu na kazi zao zingewapatia maslahi makubwa, alibainisha Maalim Seif.

    Maalim Seif aikosoa serikali kuhusumigogoro ya wakulima na wafugaji

    Aunga mkono mgombea wa UKAWA 2015Na Mwandishi Maalum

    A l i o n g e z a k u w a Tanzania imejaliwa kuwa na maliasili nyingi kuliko nchi nyingi duniani na kwamba, iwapo serikali ingeweza kuzitumia vizuri kusingekuwa na sababu ya nchi kuwa miongoni mwa nchi masikini.

    Maalim Seif ameeleza kuwa mbali na maliasili zilizopo chini ya ardhi kama vile madini, gesi na mafuta, Tanzania imejaaliwa kuwa na hali ya hewa inayotafautiana k a t i k a m a e n e o mbalimbali, hali ambayo inaifanya nchi kuzalisha mazao tafauti tafauti.

    Hata hivyo, alisema kwa kukosekana kwa sera muafaka, kumesababisha

    wananchi walio wengi kushindwa kunufaika na neema iliyopo katika nchi yao, akatoa mfano wa watu wa kanda ya Ziwa kuwa licha ya wananchi katika ukanda huo kuongoza kwa kilimo cha pamba, lakini hakuna hata kiwanda cha nguo.

    Wananchi wa Kanda hii nyinyi ndio mnaozalisha pamba, lakini pamba hiyo inasafirishwa Ulaya, w a n a t e n g e z a n g u o wanavaa na baadaye wanatuletea sisi ikiwa ni mitumba na sisi tunaivaa, alibainisha Maalim Seif.

    A k i h u t u b i a k a t i k a mkutano wa hadhara k a t i k a u w a n j a w a F u r a h i s h a K i r u m b a ,

    K a t i b u M k u u h u y o alisema kuwa wananchi hawana budi kujiandaa kufanya mageuzi ya uongozi wa nchi, kwa kuwaweka madarakani viongozi wenye uwezo na mtazamo mpya wa kuleta

    maendeleo ya wananchi.N a ye M b u n g e wa

    N ya m a g a n a k u p i t i a C H A D E M A , E z e k i e l Wenje, akihutubia katika mkutano huo alisema njia muafaka ya kuleta mageuzi ya kiuongozi nchini ni vyama vya upinzani kuendeleza ushirikiano na kuwa na mgombea mmoja katika ngazi zote.

    Wenje alisema yeye b i n a f s i y u k o t a ya r i kufadhili safari ya viongozi wakuu wa CHADEMA, CUF na NCCR Mageuzi wa k a j i f u n g i e n c h i n i Sychelles, ili waweze kupata mgombea mmoja ambaye watamsimisha kuwania Urais katika

    u c h a g u z i m k u u wa m w a k a n i k u p i t i a muungano wa Umoja wa Katiba ya Watanzania (UKAWA).

    Hata hivyo akilifafanua hilo, Maalim Seif alisema jambo hilo wala halihitaji

    kwenda kuamuliwa nje ya nchi, na badala yake viongozi hao wanaweza kutoa maamuzi hayo hapa hapa nchini.

    A wa l i a k i h u t u b i a mkutano wa hadhara W i l a y a n i K w i m b a , Maalim Seif Sharif Ham