ANNUUR 1177A

20
ISSN 0856 - 3861 Na. 1177 RAJAB 1436, IJUMAA , MEI 15-21, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu facebook: [email protected] AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST Hali za Masheikh mbaya Segerea Sheikh Mselem adhalilishwa vibaya Farid atoboa siri ya kukamatwa kwao Wamtaka Mwanasheria Mkuu wa Z’bar Tusiparamie vikosi vya ATPU kama vile vya Uhuru Kenyatta Kasema kweli Askofu Lebulu Tusipojifunza kwa waliotangulia… Yakitukuta, tutulie, tusipige kelele RAIS Siad Bare wa Somali aliwakamata Maulamaa akawatesa na akawaua hadharani. Somalia ilikumbwa na vita na mauaji. Mpaka leo Wasomali wanauana wenyewe kwa wenyewe. Saddam Hussein aliua Masheikh na kuwatesa. Haikuchukua muda Iraq iliingia katika vita vilivyoua mamilioni ya watu na kuharibu makaazi na mpaka leo Iraq haijatulia. Rais Gadafi wa Libya naye alifanya kosa hilo hilo la kuwakamata Maulamaa kuwaweka ndani na kuwaua. Naye aliuliwa kama alivyowaua wenzake na nchi nzima imetumbukia katika umwagaji damu mkubwa usiomalizika. (Soma Uk. 4) Laana ya Siad Bare inatunyemelea Kuteswa Masheikh wasio na hatia… Maafa Zanzibar, Dar huo ni mwanzo Makosa ya laana, balaa lake linakuja Toka lini ‘Alamtara’ ikawa kasida ya dufu? RAIS wa zamani wa Somalia, Siad Bare. Kwa vile baadhi yetu wana uwezo na hawaendi Hijja, Allah Anaonesha hasira Zake kwa kusema, "Hana haja na viumbe sote" (Aal Imran:97). Hivyo, tuhimizane, wakienda wengi faida tunapata sote, na wasipokwenda hasara ni yetu sote! Muda unakwisha! Gharama zote kwa Hijja ni Dola 4,500. Umra ya Ramadhani ni Dola 2,300. Karibuni Ahlu Sunna Wal Jamaa kwa huduma nzuri na uongozi bora. Wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0765462022;0782804480; 0717224437. (10) HASARA ZA KUTOHIJI NI ZETU SOTE! MWANASHERIA Mkuu wa Zanzibar Saidi Hassan Said Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu. Sheikh Mselem Ali Mselem, kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho. Kushoto Kadhi Mkuu Sheikh Khamis Haji akifuatiwa na Mufti Sheikh Saleh Omar Kabi

Transcript of ANNUUR 1177A

  • ISSN 0856 - 3861 Na. 1177 RAJAB 1436, IJUMAA , MEI 15-21, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

    Sauti ya Waislamufacebook: [email protected]

    AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST

    Hali za Masheikh mbaya SegereaSheikh Mselem adhalilishwa vibayaFarid atoboa siri ya kukamatwa kwaoWamtaka Mwanasheria Mkuu wa Zbar

    Tusiparamie vikosi vya ATPU kama vile vya Uhuru Kenyatta

    Kasema kweli Askofu LebuluTusipojifunza kwa waliotanguliaYakitukuta, tutulie, tusipige kelele

    RAIS Siad Bare wa Somali aliwakamata Maulamaa akawatesa na akawaua hadharani.

    S o m a l i a i l i k u m b w a na vita na mauaji. Mpaka leo Wasomali wanauana wenyewe kwa wenyewe.

    Saddam Hussein aliua Masheikh na kuwatesa. Haikuchukua muda Iraq iliingia katika vita vilivyoua m a m i l i o n i ya wa t u n a kuharibu makaazi na mpaka leo Iraq haijatulia.

    Rais Gadafi wa Libya naye alifanya kosa hilo hilo la kuwakamata Maulamaa kuwaweka ndani na kuwaua.

    N a ye a l i u l i wa k a m a alivyowaua wenzake na nchi nzima imetumbukia katika umwagaji damu mkubwa usiomalizika. (Soma Uk. 4)

    Laana ya Siad Bareinatunyemelea

    Kuteswa Masheikh wasio na hatia

    Maafa Zanzibar, Dar huo ni mwanzoMakosa ya laana, balaa lake linakujaToka lini Alamtara ikawa kasida ya dufu?

    RAIS wa zamani wa Somalia, Siad Bare.

    Kwa vile baadhi yetu wana uwezo na hawaendi Hijja, Allah Anaonesha hasira Zake kwa kusema, "Hana haja na viumbe sote" (Aal Imran:97). Hivyo, tuhimizane, wakienda wengi faida tunapata sote, na wasipokwenda hasara ni yetu sote! Muda unakwisha! Gharama zote kwa Hijja ni Dola 4,500. Umra ya Ramadhani ni Dola 2,300. Karibuni Ahlu Sunna Wal Jamaa kwa huduma nzuri na uongozi bora. Wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0765462022;0782804480; 0717224437.

    (10) HASARA ZA KUTOHIJI NI ZETU SOTE!

    MWANASHERIA Mkuu wa Zanzibar Saidi Hassan Said

    Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu.

    Sheikh Mselem Ali Mselem, kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho.

    Kushoto Kadhi Mkuu Sheikh Khamis Haji akifuatiwa na Mufti Sheikh Saleh Omar Kabi

  • 2 AN-NUURRAJAB 1436, IJUMAA MEI 15-21, 2015AN-NUUR

    S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.

    www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected] zetu zipo: Manzese Tip Top

    Usangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

    Tahariri

    WIKI iliyopita tuligusia j a m b o a m b a l o n i maarufu hivi sasa kwa yoyote anayetaka kujua u k we l i n a a m b a ye hajageuzwa kuwa kifaa cha mabeberu (Asset) cha kuwarahisishia kupata masilahi yao wala hajatekwa na kuwa msaliti wa nchi yake na watu wake.

    Jambo lenyewe ni k a m a a l i v y o s e m a Zbigniew Brzezinski, kwamba ugaidi sio adui lakini mbinu chafu za kufikia malengo fulani ambapo watu wasio na hatia huuliwa. Zaidi akasema kuwa msemo huo umefanywa usiwe na maana inayoeleweka sio kwa bahati mbaya, bali umefanywa hivyo makusudi na walioubuni na wanaoendeleza vita hiyo ili kufikia malengo yao ya kusimika kitisho (culture of fear).

    Kwa nini imekuwa ni lazima kuwatisha wa t u ? K a c h e r o n a m w a n a d i p l o m a s i a , Zbigniew Brzezinski anafafanua akisema kuwa:

    Fear obscures reason, i n t e n s i f i e s e m o t i o n s and makes it easier for demagogic politicians to emotions mobilize the public on behalf of the policies they want to pursue.

    K w a m b a ukishawatisha watu, unaondoa uwezo wao wa kufikiri, unawaburuza unavyotaka kwa sababu, badala ya kuyatizama mambo kwa akili na k u t a f a k a r i , k u h o j i , w a n a o n g o z w a n a

    Tusiparamie vikosi vya ATPU kama vile vya Uhuru Kenyatta

    Kasema kweli Askofu LebuluTusipojifunza kwa waliotanguliaYakitukuta, tutulie, tusipige kelele

    mihemko (emotions).Tunachofahamishwa

    h a p a n i k u w a kinachoitwa ugaidi hivi leo na msamiati vita dhidi ya ugaidi, h a u w a k i l i s h i a d u i yoyote anayetambulika a u k w a m a a n a nyingine, haiwakilishi adui wa kweli. Kama w a l i v y o c h a m b u a wasomi na wachambuzi wengi ni kuwa, huo umekuwa tu ni moja ya mikakati ya mabeberu kataka kufikia masilahi yao.

    Na kama ambavyo imeelezwa pia kwa mare fu na mapana ikiwemo kuandikiwa vitabu, machapisho na kufanyiwa midahalo m b a l i m b a l i k a t i k a vyombo vya habari iliyohusisha wanazuoni m a s h u h u r i w a kuaminika kimataifa, kinachoitwa mbinu za kupambana na ugaidi, nacho inakuwa kiini macho kingine ambacho, pamoja na kuwekewa bajeti kubwa, haisaidii lolote katika kutokomeza huo unaoitwa ugaidi. Bali kuuchochea zaidi na kutunisha mifuko ya wana-usalama na vikosi vya ulinzi. Namna yake ni kama kuwepo kwa vikosi hivyo kunachochea zaidi kuwepo kwa ugaidi. Na hiyo huendana na ho ja za wanazuoni kuwa kinachotakiwa ni kuwepo huo ugaidi i l i ipatikane sababu ya kufanyika mambo mengi ya kurahisisha mikakati ya mabeberu ikiwemo kusambaza

    utando wa kijeshi na kikachero dunia nzima kutimiza lengo lao la u d h i b i t i wa d u n i a Hegemony. Na pili kupitia utando huo wa kijeshi unaowawezesha kuwepo kila mahali kwa kizingizio cha kusaidia kupambana na ugaidi, waweze kuzidhibit i nchi mbalimbali pamoja na rasilimali zao hasa mafuta, gesi na madini.

    Baada ya miaka mingi ya machafuko, kuna wakati Somalia ilikuwa imef ik ia mahal i pa kuondokana na vurumai hizo zilizoangamiza mamia ya maelfu ya roho za Wasomali. Ghafla mabeberu wakawaundia vikosi vya kupambana na magaidi. Vikawa vinapewa mapesa mengi na silaha nzito nzito. Amani na hali ya utulivu i l iyokuwa inanukia Somalia, ikatoweka. Walipofikishwa Allah ndiye mjuzi watatokaje.

    K e n y a wametutangulia sana katika mchezo huu wa mabeberu. Waliundiwa vikosi vya kupambana na magaidi-Anti Terror Pol ice Unit (ATPU) n a m a p e m a . AT P U ndio wanaotuhumiwa kuuwa Masheikh wengi na vijana wa Kiislamu kwa k is ingiz io cha kupambana na ugaidi. Kwa mujibu wa makala ya Jipo Pevu iliyokuwa ikirushwa na kituo cha televisheni cha KTN, hawa ATPU walikuwa wakiwafuata Masheikh majumbani mwao na kuwauwa kikatili kwa kuwapiga risasi, kisha hutoa taarifa za uwongo k w a v y o m b o v y a habari kuwa Masheikh hao waliuliwa wakati wakipambana na polisi.

    Lakini pia kwa mujibu wa makala ya Aljazeera, hawa ATPU na vikosi v ingine vya namna hiyo, wao hutamba kuwa ni vikosi vya wauwaji (elimination), s i o v y a k u k a m a t a watu na kuwapeleka mahakamani. Na zaidi wanasema kuwa hao hao mabeberu ambao n d i o w a l i m u n a wafadhili wao, wao ndio huwaambia nani wa kumuuwa. Wakipewa t a a r i f a k a m u u we n i Fulani, humuuwa na

    kutoa taarifa kwa vikosi vya hao hao mabeberu kuwa washatekeleza kazi waliyowatuma.

    Ni muda mrefu sasa toka uanze uhusiano huo kati ya Kenya na mabeberu, lakini kadiri siku zinavyokwenda, ndio hali huwa mbaya zaidi. Wala hizo ATPU zao na huo uhusiano wao na mabeberu na mipango yao ya Counter Terrorism, haijaweza kuzuiya shambulio la Garissa.

    K w a m u j i b u w a KTN, ukiangalia wale Masheikh walivyokuwa wakiuliwa na kuteswa, inakupitikia kichwani kuwa ulikuwa ni mkakati wa kuchochea hasira za Waislamu na kuleta ghasia katika nchi. Lakini tizama pia yalipotokea m a s h a m b u l i z i y a Westgate , Mandera na Garissa. Ilikuwa ni vyombo vya habari vya mabeberu hao hao viliokimbilia kutuambia k u w a m a g a i d i walikuwa wakiwatenga Waislamu mbali, kisha huwauwa Wakr i s to kikatil i . Kama kuna chombo cha habar i cha Kenya au Tanzania kiliripoti mambo kama haya, ni kwa kunukuu taarifa za vyombo hivyo vya mabeberu. Katika moja ya matoleo yetu, tuliarifu jinsi televisheni m o j a y a U f a r a n s a ilivyokuwa ikipandikia jambo la kuzua kuwa magaidi wa Al-Shabaab walikuwa wakiwachinja Wakristo Garissa.

    N a h a p a n d i o p a n a t a k i k a n a tupazingatie vizuri . Gazeti la Msamaria Mwema, la Jumapili Mei 10, l i l ikuwa na habari iliyonadi Kanisa Katoliki lafichua siri mabomu Arusha.

    K a t i k a h a b a r i hiyo kuna nasaha za M h a s h a m u A s k o f u Lebulu. Akirejea tukio la shambulio la bomu katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Mtakatifu Josefu Mfanyakazi, Olasiti , Arusha, Mei 5, 2013, Askofu Lebulu aliwataka waumini wa Kikatoliki na Watanzania kwa ujumla kuheshimiana n a k u p e n d a n a

    k a m a b i n a d a m u . A k a k u m b u s h a n a k u s i s i t i z a k u w a wanaofanya matendo ya kigaidi wanalenga kutufarakanisha na kule ta f i tna mbaya miongoni mwetu lizuke balaa la machafuko.

    Alisema, waliorusha bomu lile walitaka kuliingiza Taifa kwenye migogoro ya kidini, lakini kupitia nguvu za Mwenyezi Mungu, walishindwa.

    K w a h a k i k a h i l i n i s o m o a m b a l o Watanzania tunatakiwa t u l i z i n g a t i e s a n a . Kenya watalaumiwa k w a k u i n g i z w a kichwakichwa katika biashara hii kichaa. Tunaweza kusema kuwa hawawezi kuepuka lawama ya kuuziwa mbuzi wa mikakati ya Counter Terrorism ya mabeberu na ATPU zao katika gunia.

    Lakini sisi Watanzania, itabidi tujilaumu sana kama hatutajifunza kwa yanayowakuta wenzetu Kenya. Wameuwa na kutesa sana watu wao kupitia mipango hii ya kupewa ya ki- ATPU na kupi t ia aki l i ya kupewa na kushikiwa na mabeberu. Lakini pia kadiri walivyopewa mikakati, ndivyo damu ya Wakenya inavyozidi kumwagika na kuwa k a m a m i h a n g a y a kulinawirisha Subiani ugaidi.

    Sisi tunaamini kuwa hakuna gaidi s i wa kutoka Al-Shabaab au AlQaida au wa jina lolote lile, awe wa ndani au wa nje, anayeweza kuja kuipiga Tanzania, kama sio hao wa kutengenezwa na mabeberu.

    N a k w a m a a n a hiyo, kama ikitokea kupigwa, Mwenyezi Mungu atuepushe na balaa hilo, sisi imani yetu itabaki kuwa ni ugaidi wa kupanga. Na kwa maana hiyo hiyo, mipango yoyote tutakayofanya ikipewa jina lolote lile, maadhali itakuwa mithili ya ile ya Kenya, itakuwa ni ya kutuangamiza zaidi. Haya ni maoni yetu na tutasimama nayo.

  • 3 AN-NUURRAJAB 1436, IJUMAA MEI 15-21, 2015Habari

    Hali za Masheikh mbaya Segerea S H E I K H ( M s e l e m ) kafanyiwa udhalilishaji mkubwa wa kuachwa uchi wa mnyama huku amening' inizwa kwa pingu.

    H u y u n i S h e i k h a n a y e s o m a k i t a b u kitakatifu cha Mwenyezi Mungu, akisikika akisoma Qur'an tukufu katika Redio nyingi Afrika Mashariki, lakini anafanyiwa ushenzi kama huo-Sheikh Farid

    Hali za watuhumiwa wa ugaidi mbaya. Hivi sasa baadhi yao wamegoma kula.

    Ni katika hali hiyo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam, imeambiwa isubiri kupokea maiti za watuhumiwa hao, ikiwa hatua za makusudi hazitachukuliwa kunusuru afya zao ndani ya gereza la Segerea.

    Kauli hiyo imetolewa na Sheikh Farid Had Ahmed, mbele ya Hakimu wa M a h a k a m a h i y o anayesikiliza kesi yao, Renatus Rutta, Jumatatu wiki hii.

    S h e i k h F a r i d H a d akimpa Hakimu histori fupi ya kesi yao iliyopo mbele yake, alisema kuwa, wamebambikiziwa kesi ya ugaidi kwa kudai nchi yao huru ya Zanzibar na kusema mfumo wa M u u n g a n o u l i o p o hawautaki.

    Alisema, kesi yao ni ya kisiasa na si vinginevyo na kwamba, walikamatwa na kuletwa bara kuja kudhalilishwa tu na polisi wa kike na wakiume.

    S h e i k h F a r i d alimtambulisha Hakimu huyo kuwa wao ni Viongozi wa Taasisi mbalimbali na yeye akiwa ni kiongozi Umoja wa Mihadhara na Sheikh Mselem Ali Mselem ni kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho, zote za Zanzibar.

    Sheikh Kama huyu ( M s e l e m ) k a f a n y i wa udhalilishaji mkubwa wa kuachwa uchi wa mnyama huku amening'inizwa kwa p ingu , huyu n i Sheikh anayesoma kitabu kitakatifu cha Mwenyezi Mungu, akisikika akisoma Qur'an tukufu katika R e d i o n y i n g i k a t i k a Afrika ya Mashariki, lakini anafanyiwa ushenzi kama huo Alisema Sheikh Farid mbele ya hakimu huyo.

    Naye mshitakiwa Salum alimkumbusha Hakimu Rutta kuwa wiki iliyopita

    Na Bakari Mwakangwale aliahidi kuwa atafuatilia hali zao gerezani na kuhoji mbona hawakumuona?.

    Alisema yeye ni moja wa wa l i o d h a l i l i s h wa na Polisi kwa kutiwa chupa na majiti, lakini alisikitishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe ambaye alisema hawajatendewa chochote huku akijua sio kweli.

    Awali, kabla ya kupanda kizimbani watuhumiwa hao, siku ya Jumamosi wiki iliyopita, zilienea taarifa kuwa watuhumiwa wa ugaidi katika Gereza la Segerea wamegoma kula.

    Wakati taari fa hizo zikitoka, taarifa nyingine zilibainisha kuwa mmoja wa watuhumiwa hao aliyetajwa kwa jina la Said, anaumwa jambo ambalo l i m e i l a z i m u K a m a t i ya Maafa ya Shura ya Maimamu kupambana k u t a k a k u s i m a m i a matibabu yake.

    Sheikh Farid, ambaye ni Amir wa Jumuiya ya Uamsho Zanzibar, alisema Mahakamani hapo kuwa k u n a w a t u h u m i w a wamegoma kula huku wengine wanne hali zao kiafya zikiwa sio nzuri kiasi cha kuhifadhiwa katika chumba maalum.

    Kulingana hali hiyo Sheikh Farid, aliiomba Mahakama kufika katika gereza hilo kuangalia hali halisi ya watuhumiwa hao i l i hatua s tahiki zichukuliwe.

    Tunaiomba mahakama k u j a k u l e g e r e z a n i mjionee hali halisi, ili hatua s tahiki z iweze kuchukuliwa, vinginevyo subirini kupokea maiti na muingie katika historia ya Zanzibar. Alisema Sheikh Farid Mahakani hapo bila kufafanua zaidi.

    A s k a r i M a g e r e z a a m b a y e h a k u w e z a kufahamika jina lake mara moja, alikiri kuwepo kwa hali hiyo kwa watuhumiwa hao wa ugaidi baada ya Hakimu wa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam anayesikiliza kesi hiyo Renatus Rutta, kupokea maelezo na taarifa hiyo ya Amir Hadi na kumuhoji askari huyo.

    Hakimu alimtaka Ofisa wa Magereza aeleze ni kwa nini watuhumiwa hao watatu hawakufika mahakamani.

    Afisa huyo aliieleza m a h a k a m a k u w a wameshindwa kuf ika k u t o k a n a m g o m o n a wametoa masharti kuwa wanahitaji Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa Zanzibar na wa Tanzania bara pamoja na Jaji Mkuu,

    wa wa t e m b e l e e h u k o gerezani.

    Watuhumiwa ambao hawakuweza kufika ni Said Amour, Salum na Said Shehe, Sharifu na Abdallah Hassani Hassani.

    Hata hivyo Sheikh Farid Had Ahmed, ambaye ndiye mshitakiwa namba moja alimweleza Hakimu yale wanayohi ta j i na kumwambia, washitakiwa watatu ambao hawakuweza kufika mahakamani ni kwa sababu ya mgomo na wengine hawakuweza kufika kwa maradhi.

    H a k i m u R u t t a a l ipofanya juhudi za kuwasihi waliohudhuria m a h a k a m a n i h a p o k u wa s i h i wa l i o g o m a waache na kumtaka Sheikh F a r i d a wa f a h a m i s h e kwamba waje mahakamani, j ibu la She ikh Far id lilikuwa kwamba wenzao w a m e a n z a n a w a o watakwenda kumaliza kwa kuwa lao ni moja.

    Akiongea na gazeti la An-nuur kufuatia taarifa za watuhumiwa hao kugoma kula gerezani na wengine kuugua, Katibu wa Kamati ya Maafa ya Shura ya Maimamu, Ustadhi Ally Mbaruku, alisema taarifa h i z o wa m e z i p a t a n a wanazifanyia kazi.

    Alisema wanayo taarifa ya kuugua kwa Said Amour na wapo katika mchakato wa kumshughulikia.

    Kuhusu kugoma kula, alisema ni suala ambalo lipo nje ya uwezo wao kwani madai yao yameelekezwa katika mamlaka husika.

    Alisema baada ya kupata taarifa za kuugua kwa Amour , wal i laz imika k u u a n d i k i a u o n g o z i wa M a g e r e z a b a r u a ya kupatiwa kibali cha kumtibia chini ya uangalizi w a o ( m a g e r e z a ) n a Waislamu watagharamikia matibabu yake.

    Ust. Mbaruku, alisema kwa mujibu wa maelezo waliyo nayo kutoka kwa mtuhumiwa huyo, anadai kuwa sehemu zake za siri zimevimba na zina dalili ya kuwa na usaha kutokana na kuminywa na askari wa usalama baada ya kukamatwa kabla hajafikishwa gerezani.

    Hiki ni ki l io chao cha muda mrefu kuwa wanahitaj i kufanyiwa uchunguzi afya zao kwa u j u m l a k u t o k a n a n a madhila waliyoyapata lakini hakuna anayejali, kwa sasa tunahitaji kibali (ruksa) ya uongozi wa Magereza ili tumpatie matibabu. Alisema Ust. Mbaruku.

    A l i s e m a A m o u r n i m i o n g o n i m w a w a t u h u m i w a walioshindwa kuhudhuria Mahakamani s iku ya Jumatatu (Mei 11, 2015) kutokana na maradhi yanayomsumbua, huku wengine ikiripotiwa kuwa wameshindwa kuf ika kutokana na kukosa nguvu.

    Alisema Kamati ya Maafa ilikuwa inategemea kupata majibu mapema wiki hii, lakini mpaka Jumanne wiki hii bado hawajajibiwa, jambo ambalo linazidi kuchelewesha t iba ya uhakika kwa mtuhumiwa huyo.

    Hata hivyo kwa mujibu wa Ust. Mbaruku, alisema mke wa Said Amour, alifika gerezani hapo kujua hali ya mumewe na kuelezwa k w a m b a J u m a t a n o (wiki hii) kuna daktari atakwenda kumwangalia kwa ajili ya kumpatia matibabu.

    Pamoja na majibu hayo lakini mle ndani wanapewa h u d u m a z a h a p a n a pale ambazo kwakweli hazikidhi haja ya matatizo waliyonayo, ndio maana athari zinazidi kujitokeza.

    Hata hivyo tunaendelea kuwasiliana na uongozi mara kwa mara juu ya kupatiwa majibu ya barua ya maombi yetu ya kutoa huduma kwa Muislamu h u y o . A l i s e m a U s t . Mbaruku.

    Akizungumzia mgomo wa watuhumiwa hao kula gerezani humo, Ust. Mbaruk alisema waliuanza tangu Jumamosi ya wiki iliyopita na kutoa masharti

    kadhaa.Alisema baadhi ya madai

    yao ni kutaka wafutiwe mash i taka ya uga id i kwa sababu ni tuhuma za kubambikizwa zisizo na ukweli wowote, ndio maana ushahidi mpaka sasa hakuna.

    J ingine n i kwamba wamechoshwa kupigwa danadana kwa rufaa yao, wakihoji ni kwa nini haitolewi maamuzi kwa wakati huku wakiendelea kunyimwa dhamana.

    Ust. Mbaruku, alisema mgomo huo umeanza k w a w a t u h u m i w a w a c h a c h e m i o n g o n i mwa watuhumiwa hao n a k wa m b a , s i w o t e waliogoma kwa sasa.

    H a t a h i v y o U s t . Mbaruku alisema, tayari Sheikh Farid Hadi, ametoa kauli kuwa watuhumiwa wote wataungana na wenzao ikiwa madai yao hayatotekelezwa.

    W a k a t i h u o h u o kulikuwa na Kesi nyingine inayomkabli mtuhumiwa mwingine Ust. Sharifu S u l e i m a n S h a r i f u kutoka Zanzibar nayo imeahirishwa huku akiwa kwenye mgomo wa kula.

    W a i s l a m u wanaotuhumiwa kwa Ugaidi, wapo gerezani h u m o k wa m a k u n d i tofauti tofauti kulingana na tuhuma zinazowakabili, ambapo inakadiriwa kuwa mpaka sasa wapo zaidi ya arobaini katika gereza la Segerea. Kesi imeahirishwa hadi Mei 24.

    Sheikh Mselem Ali Mselem, kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho,

  • 4 AN-NUURRAJAB 1436, IJUMAA MEI 15-21, 2015MakalaKUENEA kwa mambo ya laana kunasababisha maafa. Mfano rushwa ikienea sana mpaka kusajiliwa kwa vyombo vya baharini itakuwa kwa rushwa, kupanda kwenye chombo kwa rushwa hatimaye chombo kinazama.

    Wa m e l a a n i wa n a Allah (SW) wanaotoa na wanaopokea rushwa (Mj 2313 T1337 Amesahihisa Tirmidhy).

    L a k i n i a t h a r i y a r u s h wa we n ye h a k i wataporwa haki zao, wenye makosa ya kuuza ulevi na kokeni watatoa rushwa na kusalimika, aliyebaka atatoa rushwa na hatofungwa. Itaenea dhulma itakayomkasirisha Allah SW na mwisho wataadhibiwa.

    Wa n a w a k e k u v a a masuruali na fulana, ni laana na hii ndiyo sare katika makundi ya mazoezi takriban yote.

    A m e s i m u l i a A b u u Hurayra (RA) amesema Mtume (SAW) amemlaani M t u m e m w a n a m m e anayevaa nguo za kike na mwanamke anayevaa nguo za kiume(D 4098). Pamoja na wanawake kuchanganika ovyo na wanaume waki fanya m a z o e z i p a m o j a , wanawake hujilaza miguu juu, huku wakibenuliwa na wanume. Huko ngazi mia mamia ya wanawake na wanaume kwenye fukwe huchanganika w a k i i k a r i b i a z i n a a k w a k u k a a p a m o j a kufundishana kuogolea. K w e n y e f u k w e h a k u s e m e k i . Z i n a a hadharani. Wanawake na wanaume hukodi magari wakachukua na ulevi na wanawake walio uchi na kucheza ngoma na kuzini kwenye fukwe.

    Wakati wa mchana mchanganiko mbaya wa wanawake na wanaume k w e n y e s e h e m u z a wazi na bustani kama Jamhuri Garden ambayo imegeuzwa ni bustani ya mapenzi. Jinsia mbili hukaa faragha kukamatana na kuchezeana hadharani. Wakati wa usiku maeneo y a w a z i h u g e u z w a kuwa viwanja vya zinaa. Wanawake na wanaume huzini ovyo kwenye viwanja, majengo ya shule na mambo hayo yakienea yanasababisha maafa kwa ushahidi wa hadithi sahihi ya Mtume SAW.

    Aliuliza Zaynab binti Jahshi RA Hivi tutahiliki na miongoni mwetu wako watu wema? Akasema

    Mambo ya laana

    ndiyo ikiwa yatakithiri maovu (Muttafaq SB 3346 SM 2880).

    Amesimulia Hudhayfa (RA) kutoka kwa Mtume (SAW) amesema Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake, mtaamrishana mema na mtakatazana maovu, laa s ivyo n i k a r i b u n i A l l a h S W a t a w a l e t e a a d h a b u kisha mumuombe na asikukubalieni. (T 2169 D4338 Mj 4008 ameisahisha Albani).

    Hadithi hizo mbili ni ushadidi tosha wa kuwa yakikithiri maovu, basi lazima majanga yatatokea.

    Ama jambo la tatu ni kukithiri maovu maalumu ya liwati, riba, ulevi na muziki ambayo yakienea madhambi hayo, basi Allah SW hasubiri akhera, ila atawaonja kwanza kwa adhabu kabla ya akhera. K u e n e a k wa m a b a a ambayo hata wananchi wakiyapinga kisheria, b a d o ya n a r u h u s i wa . Kuenea kwa wavutaji bangi na wala unga, liwati, watoto kubakwa, wanaume kuoana na wanaume na wanawake kuingiliwa kinyume na maubile, ndiyo mitindo iliyoenea sasa. Mambo h a y a y a k i f a n y i k a Muumba wa Ulimwengu hughadhibika na kuamua kuwaletea watu majanga.

    Allah (SW) anasema Basi ilipofika amri yetu tuliifanya (ardhi hiyo iwe juu chini) juu yake kuwa chini yake , na tukawanyeshea mvua ya changarawe za udongo m g u m u wa m o t o n i . Zilizotiwa alama (kila mtu kwa jina lake) na adhabu

    hii haiko mbali kwa (kwa wanaofanya uovu huu kwa uma huu) (Huud 82-83).

    A m e s i m u l i a A n a s (RA) amesema Mtume (SAW) watakapofanya umma wangu mambo matano imewastahikia k u n g a m i z w a , itakapodhihiri kulaaniana, (kuenea vi tendo vya laana na kulaaniana wao wenyewe) ukanywewa ulevi, (ukaenea ulevi na kunywewa hadharani) n a i k a va l i wa h a r i r i n a w a t a k a p o t u m i a a l a z a m u z i k i , n a w a t a k a p o i n g i l i a n a wanaume kwa wanaume n a wa n a wa k e k wa wanawake. (Ameipokea Bayhaq ST2054).

    K u t o k a k w a A b i i Mal ik (RA), kwamba amemsikia Mtume (SAW) Watakunywa watu ulevi na watauita si kwa jina lake, zitapigwa juu ya vichwa vichwa vyao, ala za muziki na wanawake waimbaji , Allah (SW) atawadidimiza ardhini na atawajaalia masokwe na maguruwe.(Mj 3384 ST 2377, 2378).

    Imepokewa kutoka kwa Ubadah bn Samit(RA), kutoka kwa Mtume (SAW) amesema Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake watakesha watu katika batara na shari, na kucheza na pumbao, na wataamka asubuhi wamegeuzwa masokwe na maguruwe, kwa kuhalalisha mambo yal iyayoharamishwa, na kuchukua wanawake waimbaji, na kunywa ulevi na kula riba na kuvaa harir i . (Abdil lahi bn Ahmad ST2377). Batara ni

    kufanya israfu na kuwa na kibri katika mambo mbali mbali kama kula , kunywa na mengineyo.

    Ames imul ia Imran I b n u H u s s a y n ( R . A) kwamba katika umma huu yatatokea (maafa ya) kudidimizwa watu ardhini, kugeuzwa sura za wanyama, kurembelewa mvua ya mawe, akaulizwa mtu katika Waislamu ewe Mtume (SAW) lini yatatokea hayo? Akasema Zitakapoenea ala za mziki na wanawake waimbaji na utakaponywewa ulevi ( imepokelewa T 2212 Albany ameipa draja la hasan).

    Yaliyotokea Indonesia ni funzo, kuwaachia watalii wakafanya watakavyo mpaka wakaandaa hafla ya kufanya liwati fukweni, basi hapo ndipo adhabu ya Allah ilipokuja. Mtindo wa liwati unatisha kiasi kwamba watoto wengi wameingia katika masuala haya wengine kwa hiari na wengine wanabakwa. Kaseti za ngono na liwati zinauzwa bila kificho. Katika mitandao liwati na zinaa haisemeki na watoto huangalia mambo hayo. Humo Waislamu hujifundisha laana ya kuwaingilia wanawake kinyume na maumbile na hawaelewi kuwa hiyo ni laana na ni liwati.

    A m e s i m u l i a A b u u Hurayra (R.A) kutoka kwa Mtume (S .A.W) At a k a e m u i n g i l i a m w e n y e h e d h i a u mwanamke k inyume n a m a u m b i l e , ( k wa nyuma) au akamsadiki k u h a n i a m e k a n u s h a a l i y o t e r e m s h i w a Muhammad (SAW) (Mj 639 T135, ameisahihisha Albany).

    A m e s i m u l i a A b u u Hurayra (R.A) hutoka kwa

    Mtume (SAW) amesema, a m e l a a n i w a m t u atakayemuingilia mkewe kinyume na maumbile. (D 2162, ameisahihisha Albany).

    Amesimulia Abdillahi b n u A m r u ( R . A ) , amesema Mtume (SAW) Hiyo ni liwati ndogo y a a n i m w a n a m m e atakayemuingilia mkewe kwa nyuma. (Ahmad ST2420).

    Katika simu na komputa mna michezo michafu ya zinaa na liwati. Picha za wanaofanya liwati na zinaa husambazwa kwenye mitandao na watu hurushiana wakitizama b i l a k i f i c h o . Wa t u huingiliana wakapigana picha na kuzitia kwenye m i t a n d a o a m b a p o mamilioni wanazitizama, h a wa j u i wa t u k u wa kutizama picha za uchi ni haramu.

    A m e s i m u l i a A b i S a i d i ( R A) k wa m b a Mtume (SAW) amesema Asiangalie mwanamme utupu wa mwanamme wala mwanamke utupu wa m wa n a m k e wa l a mwanamme asilale na mwanamme wakajifunika n g u o m o j a , w a l a mwanamke asilale na mwanamke mwenziwe wakajifunika nguo moja (SM 338).

    Anasema Ibn Hajar A s q a l a n y A m e s e m a Nawawyndani ya hadithi hii (SM338), kuna makatazo ya mwamamme kutizama utupu wa mwanamme, na mwanamke kutizama utupu wa wamamke, k a t i k a h o j a a m b a y o h a i n a k h i t i l a f u , n a mwanamme kutizama utupu wa mwanamke, na mwanamke kutizama utupu wa mwanamme, ni haramu kwa makubaliano ya Ulamaa wote.

    Imekosekana haya na aibu tumewazidi wanyama kwa ufuska tutegemee nini? Kama si mafuriko au upepo uvumao kwa kasi . Maafa ya mvua n i m a d o g o a n g a l a u , lakini jee mawimbi ya bahari yakatokea pande zote za v is iwa wapi t u t a k i m b i l i a ? N a n i atamuokoa mwenzake? Ni miundombinu ipi tutairekebisha wakati huo?.

    Basi tahadhari kabla ya hatari. Ni wajibu wetu kutubu kwa makosa yetu, na tujiweke katika njia iliyosawa kabla ya adhabu ambayo ha i tachagua mwema na muovu hapa duniani.

    Hukumu kamili iko kesho akhera, kwa wale wasiotubia.

    (Mussa Ame Mussa 0773 834 795)

    SHEIKH Farid Hadd. Sheikh Mselem Ali Mselem. RAIS wa zamani wa Somalia, Siad Bare.

  • 5 AN-NUURRAJAB 1436, IJUMAA MEI 15-21, 2015Habari za Kimataifa

    WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Saudia, Adel al-Jubeir, amesema kuwa nchi yake inafikiria kusimamisha m a s h a m b u l i z i ya k e n c h i n i Ye m e n k w a kipindi cha muda wa siku tano na kwamba, tayari Riyadh imewasilisha pendekezo hilo kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, ambaye alifanya safari nchini humo.

    Tumeiomba Marekani tusimamishe vita siku tano Yemen Bw. Adel alisema hayo katika mkutano na waandishi wa habari akiwa na Waziri huyo mwenzake wa Marekani huko Riyadh, mji mkuu wa Saudia.

    Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry, alizitaka pande husika nchini Yemen kukubali pendekezo hilo la Saudia.

    Hata hivyo Bw. Kerry alisema kuwa, hadi sasa Washington na Riyadh h a z i j a j a d i l i s u a l a l a kutumwa vikos i vya nchi kavu nchini Yemen, kufuatia Rais wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kutoroka nchi, Abdu Rabuh Mansur Hadi, k u i t a k a S a u d i a n a washirika wake, kutuma askari wa nchi kavu nchini humo.

    Baada ya kuwas i l i m j in i R iyadh , Kerry a l i z u n g u m z a n a Muhammad bin Nayef bin Abdulaziz, mrithi wa kiti cha Ufalme wa Saudia juu ya masuala tofauti ukiwemo mgogoro wa Yemen.

    H i i n i k a t i k a h a l i ambayo licha ya Saudia kuendeleza mashambulizi yake Yemen ambayo sasa yameingia wiki yake ya sita, lakini imeshindwa kufikia malengo yake, suala ambalo limedaiwa kuibua mgogoro kati ya wanafamilia wa ukoo wa Aal Saud nchini humo.

    Wakati hali ya Yemen ikiwa hivyo, Kamati ya Maulamaa nchini Yemen nayo imeitaka Saudia is i t ishe hujuma zake nchini Yemen bila masharti yeyote.

    Sheikh Abdus Salaam al Wajih, Katibu Mkuu wa Kamati hiyo alisema kwamba, mashambulizi ya Saudia lazima yasitishwe na kusisitiza kwamba, wananchi wa Yemen w a t a k a b i l i a n a k w a utukufu na izza na hujuma hizo za ukoo wa Aal Saud.

    Abdus Salaam alisema

    Saudia yadhihirisha kuipiga Yemen kwa niaba ya Marekani

    MAKUNDI 10 ya wabeba silaha huko Jamhuri ya Afrika ya Kati yametia saini mapatano ya kuweka chini silaha na kumaliza mgogoro a m b a o u m e s a b a b i s h a maelfu ya watu kupoteza maisha nchini humo.

    Kundi la wanamgambo wa Kikristo la Anti-Balaka na lile la Waislamu la Seleka ni miongoni mwa makundi hayo kumi ya l iyosa in i makubaliano ya kusalimisha silaha zao kwa serikali ya mpito mjini Bangui.

    K w a m u j i b u w a m a k u b a l i a n o h a y o , w a n a m g a m b o watakaosalimisha silaha zao watajumuishwa katika jeshi la taifa na kwenye mashirika mengine ya kiraia.

    April i 9 mwaka huu, v i o n g o z i wa m a k u n d i ya Seleka na Anti-Balaka w a l i s a f i r i h a d i m j i n i Nairobi Kenya na kusaini makubaliano ya usitishaji vita pamoja na mpango wa kuweka chini silaha.

    Marais wote wa zamani

    kuwa, kushambulia kaburi la Sayyid Hussein Badrud Din al Huthi, Mwasisi wa Harakati ya Answarullah ya nchi hiyo, hakuwezi kufuta hata kidogo fikra

    yake kwa Wayemen, bali kutapelekea raia wengi wa taifa hilo kuzidi kumuenzi kiongozi wao huyo.

    Licha ya Saudia na washirika wake kama

    Marekani, utawala wa Israel na nchi kadhaa za Kiarabu kuanzisha wimbi kubwa la mashambulizi d h i d i ya Ye m e n n a kusababisha maelfu ya

    watu wa taifa hilo kuuawa na kuharibu miundombinu y a k e , l a k i n i b a d o imeonekana kushindwa kufikia malengo yake huko Yemen.

    Seleka, Anti Balaka wakubaliana amaniwa m e a f i k i h a t u a h i y o ya kusalimisha silaha na kumaliza uhasama nchini humo, japo kuna wasiwasi wa utekelezwaji wa hatua hiyo.

    Michel Djotodia, Kiongozi wa Seleka aliyempindua Rais Francois Bozize mwezi Machi mwaka 2013 na kisha kujitangaza Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, ameafiki mpango wa kusalimisha silaha.

    Uamuzi kama huo pia umetangazwa na Bw. Bozize lakini wafuatiliaji wa siasa za CAR wanatilia shaka utekelezwaji wa makubaliano hayo. Hii inatokana na ukweli kwamba, Djotodia na Bozize wamepoteza ushawishi wao kwenye makundi ya Seleka na Anti Balaka na kwa mantiki hiyo, uamuzi wa makundi hayo kusaini makubaliano hayo huenda usiwe na athari yoyote.

    Baadhi ya wachambuzi w a n a s e m a k u s a i n i w a makubaliano ya Nairobi pasina kuweko mwakilishi

    wa Umoja wa Mata i fa pamoja na Rais wa serikali ya mpito ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bi. Catherine Samba Panza, kunayafanya maafikiano hayo kukosa itibari ya kimataifa na hata kutilia shaka uwezo wake wa kuhitimisha mapigano ya kikabila na kidini katika nchi hiyo ya kati mwa Afrika.

    Makubaliano ya Nairobi ya l i k u wa m a t u n d a ya mazungumzo kati ya pande hasimu chini ya upatanishi wa serikali ya Kenya. Baadaye viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Kati mwa Afrika ECCAS walimteua Dennis Saso Nguesso, Rais wa Kongo Brazzaville kuwa mpatanishi wa mgogoro wa CAR.

    Ni chini ya upatanishi wake ndipo pande hasimu zilipokutana mjini Brazzaville Mei 4 na kusaini makubaliano mengine ya usitishaji vita na kuweka chini silaha.

    Jamhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013 wakati kiongozi

    wa Seleka, Michel Djotodia alipompindua dikteta wa zamani, Francois Bozize.

    Kundi la kikristo la Anti-Balaka lilianzisha vita na mauaji dhidi ya wanachama na wafuasi wa Seleka, ambao wengi walikuwa Waislamu. Vita hivyo vilibadilika na kuwa vya kidini ambapo Waislamu wengi waliuawa na wengine wakalazimika kuikimbia katika Taifa hilo lenywe wafuasi wengi wa Ukristo.

    Wa c h a m b u z i w e n g i w a n a a m i n i k u w a , makubaliano ya usitishaji vita na kusalimisha silaha yaliyosainiwa na makundi ya wanamgambo wa CAR, hayatoshi kumaliza mgogoro wa nchi hiyo.

    Wafuatiliaji wa mgogoro wa nchi hiyo wanasema muarubaini wa tatizo lililoko ni kufikiwa maridhiano kati ya jamii ya Waislamu na Wakristo, kwani jamii hizo bado zinaangaliana kwa jicho la chuki na uhasama kutokana na yaliyojiri kati yao miaka miwili iliyopita.

    MAUAJI nchini Yemen yanayofanywa na Saudi Arabia nchini humo.

  • 6 AN-NUURRAJAB 1436, IJUMAA MEI 15-21, 2015Makala

    KATIKA safari zangu nil ikutana na mtoto mmoja wa Kitanzania mwenye asili ya Kiarabu a l i y e k u wa a k i s o m a darasa la tano. Katika kumwulizia kukhusu masomo ya utumwa, alibadilika sura yake, akanielezea manyanyaso anayoyapata darasani wakati wa somo hilo. Moja ya manyanyaso hayo ni kutambulishwa darasani kuwa babu yake ndiye aliyekuwa m f a n ya b i a s h a r a ya utumwa, ingawa kuwa ukoo wake haukukhusika na biashara ovu hiyo, lakini alikhusishwa kwa sababu alikuwa na asili ya Kiarabu tu.

    Naamini hii sio sera rasmi Tanzania ambayo raia wake wote wana haki sawa, lakini yule mwal imu mwenyewe kapandikizwa khabari za uwongo kichwani tokea utotoni mwake na hivyo chuki moyoni mwake na amepewa nyenzo za kuuonesha ubaya unaotokana na siasa kali za udini na kuziendeleza siasa hizo katika bongo za watoto wadogo ambao wataendelea kuishi nazo maishani mwao na hivyo kuendeleza chuki nchini. Tujiulize: Huyo mtoto wa shule wa leo, anakhusiana n i n i n a b i a s h a r a ya utumwa ya karne zilizopita hata aadhiriwe mbele ya wenziwe darasani kuwa anakhusika na ni mtu muovu? Walio waovu si wanafunzi , bal i ni hao wenye kutapakaza

    propaganda kali za udini shuleni, katika vitabu na magazeti na katika majukwaa ya siasa.

    Ukiwa unaelewa taarikh kwa kiasi tu na ni mtu unayetumia akili yako na mantiki, hutaacha kuona propaganda dhidi ya Uislamu inavyotapakazwa Tanzania. Hapana ubaya kufikisha ujumbe, ikiwa u j u m b e we n ye we n i sahihi, lakini ikiwa ujumbe si sahihi au umekusudia kupotosha ukweli au kuleta chuki au kuigawa jamii, basi ujumbe huo utakuwa unasikitisha na kutisha sana, na khasa ikiwa wanaofikishiwa ujumbe ni wanafunzi watoto wadogo na vijana ambao watakuwa viongozi wetu kesho.

    Lakini basi, picha hii iliyochorwa na Cloudy Chatanda inaelezea ukweli wa mambo yalivyokuwa? Jawabu ni kuwa mchoraji amebirua ukweli kabisa na kuwanyooshea kidole c h a k e c h a l a w a m a asiowapenda, nao ni Waislamu. Wakati wowote tunapoficha ukweli na

    kuwakinga madhalimu na vitendo vyao vya d h u l m a n a w a k a t i h u o h u o k u wa l a u m u wengineo wasiokhusika na kitendo hicho, uwongo h u o h u i n g i a k a t i k a kumbo la propaganda, na propaganda ni silaha mbaya sana yenye kukuza chuki ambazo aghlabu humalizikia kuulisha watu wengi bila ya sababu.

    Hapana shaka yoyote kuwa propaganda hizi zinazosomeshwa shuleni Ta n z a n i a n a k a t i k a magazeti na majukwaa ya siasa na katika khutba za makanisa na misikiti, z i m e s h a a n z a k u l e t a khasama kubwa baina ya Waislamu na Wakristo. Kwa sasa nakuachilia m we n ye we u f u n g u e masikio yako usikilize vizuri wanaokhubiri na ufungue macho yako usome magazetini uangalie vizuri sana Tanzania inakotokomezwa. Kama u n a i p e n d a Ta n z a n i a k i k w e l i k w e l i , b a s i utatafuta kila njia ya kuziondosha propaganda kila mahala zinakotumiwa,

    tena vibaya sana. Kuna wachache kati ya Waislamu na Wakristo wanaofaidika na propaganda hizi na ninajua fika kuwa waovu hawa wasioipendelea mema Tanzania watatafuta kila njia ya kuhakikisha kuwa ukweli utaendelea kunyongwa na upotoshaji.

    K a t i k a p i c h a h i i t u n a y o i z u n g u m z i a , hapana shaka yoyote kuwa mchoraji ametumia picha zilezile zilizochorwa zaidi ya miaka 130 nyuma na kubadi-l isha, kwa makusudi, mkamataji Mzungu katika picha ya kwanza na katika picha ya pili akaona awatoe Wazungu Wakristo na Waafrika wasiwemo na badala yake ampachike Mwarabu Mwislamu. Hapana shaka kuwa w a m e o n a M w a r a b u atawafaa zaidi katika propaganda zao dhidi ya Waislamu.

    Je, watu kama hawa wenye kubirua ukweli wa kihistoria wanafaa kuachi l iwa wawe na u h u r u w a k u w a p a vidonge vya propaganda za sumu vijana wa shule Tanzania kwa kuandika na kuchora propaganda za f i tna zitakazokuja kuwaulisha watu wasio na hatia baadaye?

    Iangalie vizuri na hii picha ya zamani ambayo inaonesha wazi kabisa kuwa wakamataji khasa wa wanyonge ni kutoka katika makabila ya hao Waafrika yaliokuwa na nguvu. Angalia vizuri na utaona kuwa mkamataji amevaa suruwali, yaani ni mtu ambaye alikuwa na ukhusiano na Wazungu Wakristo na si Waarabu Wa i s l a m u . A n g a l i a pia ukweli wa mavazi waliyovaa mateka utaona kama ilivyokuwa wakati huo Waafrika wanawake katika sehemu nyingi walikuwa hawavai sidiria wala vitambaa kifuani kufunika maziwa yao kama utakavyoona baadae humu katika picha zilizochorwa na wachoraji wa leo wa Kitanganyika wenye siasa kali za udini (wa Kikristo) katika juhudi zao za

    kupindua ukweli. Picha hii inaonesha mlolongo wa watumwa wa kike waliobebeshwa mizigo ya kwenda kuuziwa Wareno Msumbiji pamoja na hao mateka.

    Kwa wenye kui jua historia ya ulimwengu v i z u r i n a w e n y e k u t u m i a a k i l i z a o wataelewa mara moja kuwa wanapropaganda we n ye s i a s a k a l i z a u d i n i w a k i a c h i l i w a kuendelea na mipango yao dhidi ya Uislamu na Waislamu isiyokhusiana na kuelezea ya ukweli wala kufuata mafunzo ya Ukristo wala Uislamu, basi wataelewa mara moja kuwa yanayosomeshwa katika shule hayatachukua muda mrefu yatailetea Tanzania maafa mapevu. Picha za kipropaganda na uzushi si hizo chache tu tulizozinakili kabla, la, zipo nyingi tu. Angalia mifano mingine michache inayofuata:

    Hakuna Mwarabu a l i y e k w e n d a b a r a k u k a m a t a wa t u m wa na kuwapeleka Pwani. Lakini wenye udini lazima wa m t w i k e M wa r a b u Mwislamu lawama za ukamataji wanyonge pia.

    Tumeshaelezea kabla kuwa Mwarabu wala Mswahi l i hakuwemo kat ika ukamata j i wa wanyonge Bara, lakini wenye propaganda zao kwa lengo lao maalumu linalotokana na siasa kal i za udini lazima wamshirikishe Mwarabu na Mswahili. Picha hii hakika ni ya kuchekesha. Kwanza anayeoneshwa ni Mwarabu aliyevaa agali kichwani, kivazi ambacho si cha Kiomani wala cha Kiyemen, na ni Waarabu wenye asili ya nchi mbili hizi ndio waliokuweko Pwani ya Afrika Mashariki kwa wingi. Koti alilovishwa ni la baridi la Kiulaya na viatu vinashabihi vya Kihindi. Mwarabu huyu ni wa wapi?

    H a i d h u r u k i t u k u w a c h o r e a w a t o t o w a d o g o w a s h u l e

    Profesa Ibrahim Noor Shariff

    Propaganda za udini shuleni Tanzania-2

    PICHA inaonesha Waafrika wamewakamata watumwa. Mkamataji amevaa suruali na shati inaonesha ametokea upande uliotawaliwa na Wazungu.

    Inaendelea Uk. 7

  • 7 AN-NUURRAJAB 1436, IJUMAA MEI 15-21, 2015Makala

    Inatoka Uk. 6

    Propaganda za udini shuleni Tanzania-2uwongo wowote! Yaani, wanazivuruga akili na nyoyo za wanafunzi wa shule Tanzania na kuwaelekeza, kwa makusudi, kunako fitina na mauwaji ya watu wa jamii Fulani. Jee, haya hayakuwa ya wajinga n d i o w a l i w a o ? Khalafu tusisahau kuwa wanazungumzia Karne ya 19 na labda kabla ya hapo, sasa hii bunduki aliyoishika Mwarabu ya semi-automatic kaipata wapi na bunduki za aina hiyo zilikuwa bado hazijaundwa?

    M r a d i u c h o r a j i unapotosha ukwel i kwa kadiri kubwa sana, lakini pia ingelikuwa ni wa vichekesho sana ingelikuwa maudhui yenyewe na athari zake si za khatari ya kuweza kuulisha watu bure baada ya kujenga chuki zisizokuwa na ukweli.

    Halikadhalika, na picha hii inayofuata ya kuchora kutoka ukurasa wa 74 wa kitabu cha History for Secondary Schools, Form Two, ya wafanyabiashara ya utumwa wanakiingilia kijiji inapingana sana na yale yaliyothibitishwa kutoka

    K w a m a b i n g w a wa historia. Picha hii inaonesha kuwa ni Waarabu peke yao waliokuwa wakiviingilia vijiji vya Kiafrika na kuwauwa Waafr ika hao kiholela. Ukweli ni kuwa kitendo hicho kilifanywa sana, tena sanasana, na machifu wa Kiafrika waliokuwa na nguvu pamoja na Wa p o r t u g i z i . K wa hivyo, inahitajia tupewe jawabu ya sababu ya kuwanyooshea kidole cha lawama Waarabu Waislamu peke yao kwa vitendo vilivyofanywa zaidi na makabila ya Kiafrika yaliyokuwa na nguvu pamoja na Waportugizi Wakristo? Nini lengo la wachoraji kuuficha ukweli huu?

    Tena, na picha hii

    PICHA hii ya juu inaonesha kuwa hakuna wa kulaumiwa katika ukamataji wa watumwa ila Waarabu Waislamu peke yao.

    imechorwa kuonesha k u w a h a k u n a w a k u l a u m i wa k a t i k a ukamataji wa watumwa ila Waarabu Waislamu.

    N a h i i y a j u u p ia inamshir ik i sha M w a r a b u k a t i k a ukamataji. Na inayofuata i n a w a s h i r i k i s h a Waarabu na Waswahili k a t i k a k i t e n d o k i l i c h o f a n y w a n a Waafr ika wa Bara . Dhahiri kuwa ukhabithi wa wakamataji wa kweli, yaani makabila ya Waafrika wa Bara

    yaliyokuwa na nguvu wanatupiwa Waarabu na Waswahili. Kisa ni kwa kuwa ni Waislamu.

    Na katika picha hii pia, wenye kulaumiwa kwa ukamataji wa wanyonge wa Kiafrika ni Waarabu na Waswahili Waislamu.

    N a h i z i p i c h a zinazofuata kutokana na vitabu vya kusomeshea historia Tanzania hali ndiyo hiyohiyo. Mtwike M w a r a b u l a w a m a zote za ukamataji wa wanyonge wa Kiafrika na kuwatia utumwani

    n a k w a k u f a n y a hivyo lengo khasa la kuichukiza dini yao ya Kiislamu litafikiwa katika bongo za watoto vijana katika shule za Tanzania. Lakini hilo halitafikiwa kwa sababu kila kukicha wengi wenye kutumia akili zao wanazidi kuuona ukweli. Lakini wenye lengo lao la siasa kali za udini ni sawa kwao wanaona kuwa haidhuru kitu wakija Waislamu na Wakristo kuuwana siku za mbele, na Tanzania

    ikawa nchi isiyokalika. Siasa zao kali za udini ni masikitiko makubwa kwa nchi nzima.

    Mwarabu hajulikani wa wapi! Wanawake wa Kiafrika katika zama hizo kweli walikuwa wakivaa vitambaa kifuani kama sidiria? Vichekesho kwa mwenye kuujua ukweli.

    Angal ia na picha inayofuata. Tena na tena picha za kuchora zinamlaumu Mwarabu k w a u k a m a t a j i wanyonge wa Kiafrika na kuwatia utumwani.

    Na hii inayofuata ndiyo naipa nishani kubwa kabisa. Maelezo yanasema, kwa tafsiri: Watumwa wakiwa kazini katika mashamba ya miwa katika West Indies.

    West Indies ni visiwa vilioko Amerika ambako Waarabu hawakuweko huko. Sasa inakhusu nini nokoa achorwe M w a r a b u ? H a w a waandishi na wachoraji wenye siasa kali za propaganda za udini dhidi ya Wais lamu wamefikaje kuidhibiti manhaji (karikulamu) ya kusomeshea historia Ta n z a n i a n a h u k u tunaambiwa Tanzania haina dini?

    H a t a k a t i k a mashamba ya miwa ya West Indies ambako Waarabu hawakuweko, wanawalaumu Waarabu kuwa ndio waliokuwa manokowa!

    H a p a n a u b a y a k u f i k i s h a u j u m b e , ikiwa ujumbe wenyewe ni sahihi, lakini ikiwa ujumbe si sahihi au umekusudia kupotosha ukweli au kuleta chuki au kuigawa jamii, basi ujumbe huo utakuwa ni wa khatari sana, na kila mpenda haki na usalama wa nchi na jamii zake anatakiwa aupinge kwa kupaza sauti yake, khasa ikiwa wanaofikishiwa ujumbe ni wanafunzi wadogo a m b a o w a t a k u w a viongozi wetu kesho, na wao ndio watakuwa wanatuamulia mambo yetu na kutuongoza.

  • 8 AN-NUURRAJAB 1436, IJUMAA MEI 15-21, 2015Makala

    A M E TA K A S I K A , Aliyemchukua mja Wake usiku mmoja k u t o k a M s i k i t i M t u k u f u m p a k a Msikit i wa Mbali , ambao Tumevibariki vilivyouzunguka, ili Tumwonyeshe baadhi ya Ishara Zetu. Hakika ni Mwenye Kusikia na Mwenye Kuona. (Al-Israa 17: 1)

    Allaah (Subhaanahu wa Taala) Anaelezea Utukufu Wake, Ukubwa Wake na Uwezo Wake, kuwa Yeye ni Mweza wa kila kitu na Anafanya kila kitu Anachotaka kukifanya. Yeye pekee N d i y e M u n g u w a kweli na Yeye pekee Ya k e N d i ye M l e z i (Muumba, Mtoaji wa Riziki na Mwenye kutoa ukimu wa kila kiumbe). Alimchukua mja Wake Muhammad (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) kutoka Makkah na kumpeleka katika msikiti wa mbali huko Jerusalem katika usiku mmoja. (Kutoka Tafsiyr ya Ibn Kathiyr)

    M t u m e ( S w a l l a Allaahu alayhi wa a a l i h i wa s a l l a m ) alipewa miujiza mingi na Mola wake. Muujiza wake mkubwa ni Kitabu cha Qur-aan, kitabu ambacho kiliteremshwa miaka 1400 iliyopita na hakuna hata mtu mmoja a m b a y e a m e w e z a kubadilisha hata herufi moja au kuleta kitabu cha mfano wake. Allaah Amesema: Hakika Sisi ndio Tulioteremsha Ukumbusho na hakika Sisi ndio Tutaoulinda (Al-Hijr 15: 9).

    A a y a h h i i n i changamoto dhidi kwa makafiri kuwaambia kitu kinachofanana na Qur-aan ambao wal i jar ibu kufanya mifano ya Qur-aan wakawa wameshindwa vibaya sana. Vitabu vingine vya kutoka Kwa Allaah (Subhaanahu wa Taala) ni Taurati na Injili ambavyo viliharibiwa na kubadilishwa na ujumbe kubadilika ama kwa kuongeza maneno au kupunguza maneno na maana vile vile. Allaah Amesema juu ya Qur-aan kuwa Atailinda

    Israi na Miraji

    MSIKITI wa Baytul Muqas uliopo Palestina ambao ulikuwa Kibla cha kwanza kwa Waislamu kabla ya Makkah. Katika safari ya Mi'raji Mtume (s.aw) alipita katika Msikiti huu.

    na kweli Ameilinda na Ataendelea Kuilinda.

    M t u m e ( S w a l l a Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) alisema, Kila mtume aliyekuja kabla yangu alipewa muujiza na miujiza hiyo ilibakia kuwa miujiza wakati wa uhai wao hao mitume.: Mfano Iysa (Alayhis-Salaam) alikuwa na muujiza wa kutibu watu wagonjwa na kufufua wafu. Muusa ( A l a y h i s - S a l a a m ) alipewa fimbo ya miujiza na mambo mengine. N a m i n i m e p e w a muujiza wa milele , Qur-aan itabakia kuwa muujiza hadi kusimama Q i y a a m a h . H i v y o natarajia kuwa wafuasi wangu watakuwa ni wengi kat ika idadi zaidi ya wafuasi wa Mitume wengine kwa kuwa muujiza wangu utabakia na utakuwepo hadi Siku ya Qiyaamah ambao ni Qur-aan. Kila anayekisoma Kitabu hiki hata kama ni mpagani, basi yeye huvutika na kuona ukweli uliomo ndani yake na kuona hakuna aliyekiandika isipokuwa Bwana wa Mbingu na Ardhi . (Swahiyh Al-Bukhaariy na Swahiyh Muslim)

    Muujiza mwingine

    wa Mtume wa Allaah ilikuwa ni kupasuka kwa mwezi. Anas anasema katika riwaya yake, kuwa watu wa Makkah wa l i m t a k a M t u m e (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) awaonyeshe muujiza na akawaonesha kupasuka kwa mwezi. (Swahiyh Al-Bukhaariy, Juzuu ya 4 Namba 831)

    Kutoka Maji Kutoka Vidole Vya Mtume (Swalla Allaahu Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam)

    Imepokewa kutoka kwa Jaabir ibn Abdullah akisema: Nilikuwa na Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) na muda wa kuswali Swalah ya Al-Aswr ukafika. Tulikuwa hatuna maji isipokuwa maji kidogo tu ambayo ya l ikuwa ndani ya c h o m b o a m b a y o yaliletwa kwa Mtume. Basi aliweka mkono wake ndani ya maji hayo na kutandaza vidole vyake na huku akisema, Njooni Haraka watu wote ambao wanataka k u t a wa d h a H i i n i baraka kutoka kwa Allaah Nikaona maji yakibubujika kutoka katika vidole vyake. Hivyo watu walitawadha na wengine wakawa

    wa n a k u n y wa m a j i hayo na mie nilitaka kunywa maji mengi kupita kiasi (kwa sababu nilijua kuwa ilikuwa ni baraka). Mpokeaji wa hadiyth hii kutoka kwa Jaabiri alisema kuwa nilimwuliza Jaabir Je, mlikuwa watu wangapi wakati huo? Akajibu, Tulikuwa watu elfu moja na mia nne. (Swahiyh Al-Bukhaariy Juzuu 7 namba 543 na Swahiyh Muslim Juzuu 4 namba 779)

    M t u m e ( S w a l l a Allaahu alayhi wa a a l i h i w a s a l l a m ) a l i k u w a a m e p e w a miujiza mingine mingi. Muuj iza mwingine mkuu ni ule wa Israa na Miiraaj au Safari ya Usiku Makala hii ni kujaribu kuonesha faida zinazopatikana katika safari hii na mafunzo yanayopatikana katika muujiza huu mkubwa.

    Tukio la Israa na Miiraaj lina hekima kubwa sana na mafunzo makubwa. Funzo lake kubwa ni kuwa mja hapaswi kukata tamaa, l a z i m a a we d a i m a anamtegemea Mola wale na atamletea faraja hata kama kutakuwa n a m a m b o m a z i t o yanamkabi l i . Zaidi ya hapo mwanadamu

    anapaswa kuwa daima karibu na Mola wake hasa wakati anapokuwa anakabiliwa na mambo mazito na vitendo vya kuhuzunisha au mikasa mizito, kwani matatizo hayo hupotea kama vile yalikuwa hayajatokea.

    Mwaka wa HuzuniTukio la Israa na

    Miiraaj lilikuwa katika kipindi cha mwaka wa huzuni. Mwaka huu ulipewa jina hilo kutokana na sababu z i f u a t a z o : K wa n z a ni kifo cha Ami ya Mtume, Abu Twaalib. Abu Twaalib alikuwa ni mlinzi na mlezi wa Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) wakati Waislamu wakiwa Makkah na yeye alimkinga dhidi ya mashambulizi ya makafiri wa Makkah. Wa t u w a M a k k a h walipopinga ujumbe wa Muhammad kwa n g u v u n a k u a n z a kumshambulia Mtume n a Wais lamu, Ab u Twaalib alikinga kifua chake na kumhami mtoto wa nduguye. Alisema, Tunapenda kusaidia tunakubali u s h a u r i w a k o n a tunayakubali maneno yako. Hawa ni watu wa jamii yako ambao umewakusanya na mimi ni miongoni mwao, lakini mimi ni mwepesi kuliko wote kufanya kile ukitakacho. Fanya kila lile uliloamriwa kufanya. Nitakulinda na kukuhami, lakini siwezi kuiacha dini yangu Abu Lahab akapayuka: Wallaahi jambo hili ni jambo ovu Wewe lazima umkataze hayo ayafanyayo kabla y a w a t u w e n g i n e hawajamkanya. Abu Tw a a l i b a k a s e m a , Naapa n i taende lea kumlinda na kumhami katika maisha yangu yote. (Ar-Rahiyqul-Makhtuum).

    Ameeleza Al-Abbaas bin Abdul-Mutwalib (Radhiya Allaahu anhu) k u wa a l i m wa m b i a Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa s a l l a m ) , H u k u wa

    Inaendelea Uk. 12

  • 9 AN-NUURRAJAB 1436, IJUMAA MEI 15-21, 2015Makala

    KWENYE makala iliyopita tuliona kwamba pamoja na Mengineyo, mambo yafuatayo yanachangia katika uduni na unyonge wa misikiti yetu hivi leo kwa kulinganisha na ule wajibu ambao msikiti unatakiwa uutekeleze kijamii: Kukosa Dira iliyodhahiri, Kukosekana kwa s tadi /mbinu za u o n g o z i , M a z i n g i r a yanayokatisha tamaa, Uras imu wa hal i ya juu, Kukosa ubunifu, M a w a s i l i a n o d u n i , U s h i r i k i a n o m d o g o , Udhaifu katika kufanya kazi kama t imu, na Uratibu dhaifu wa fikra na maarifa mbalimbali.

    K a b l a y a k u a n z a kuyajadili mambo hayo, zipo nukta ambazo ni vema tukazijadili kwanza. Ni nukta ambazo huenda zikaamsha f ikra zetu kuweza kuuangazia msikiti wetu kwa uoni stahiki. Uoni ambao umejengwa juu ya msingi imara wa Qur-an na Sunnah ya M t u m e M u h a m m a d (s.a.w).

    W a k a t i m m o j a nilipokuwa nikiendesha mafunzo kwa baadhi ya viongozi wa misikiti nilipata kuwauliza swali moja. Ni swali ambalo liliibua mjadala mkali k idogo kat ika pande m b i l i z i l i z o p a t i k a n a wakati wa kutafuta jibu la swali lenyewe. Kila upande ulionelea kwamba maelezo yake ni sahihi zaidi kuliko ya upande wa pili. Na kwa manufaa ya darasa tukahitimisha kwamba tukubal iane kutokukubaliana.

    Swali lenyewe lilikuwa ni hili: Kipi ni bora zaidi, msikiti kumiliki shule au msikiti kumilikiwa n a s h u l e ? N a m n a utakavyoanza kutafakari maj ibu ya swali hi l i , inahusika moja kwa moja na nafasi ya msikiti wako itakavyokuwa katika jamii yako. Unaweza kutumia taasisi badala ya shule ili uweze kutafakari swali hilo kwa upana zaidi.

    Hivi leo, tunayo misikiti mingi ambayo inamiliki shule, zikiwa za ngazi tofauti. Baadhi ya misikiti inamiliki shule za ngazi fulani tu na mingine inamiliki shule za kuanzia ngazi ya awali hadi kidato cha sita.

    K w a u p a n d e w a pili, zipo shule nyingi za Ki i s lamu ambazo zinamiliki misikiti. Misikiti hiyo inakuwa ni sehemu ya majengo ya shule hizo zikiwa chini ya uendeshaji wa kawaida wa utawala ndani ya shule husika. Utaratibu unaoendelea ndani ya misikiti kama hiyo, unazingatia ratibu

    Nafasi ya Msikiti-2Na Abuu Numan Hassan

    kuu ya shule.Unaweza kutumia, kama

    tulivyotanguliza hapo awali, taasisi badala ya shule katika kuunogesha mjadala kwenye eneo lako. Kwa wakati tulionao, ipo misikiti mingi ambayo inamilikiwa na taasisi. Misikiti hiyo inatekeleza kazi zake nyingi kwa kuzingatia maelekezo na usimamizi wa taasisi mama.

    Kwa nini v iongozi Waliohudhuria mafunzo y a l e w a l i k u b a l i a n a kutokukubaliana? Ilitokea hivyo kwa sababu ya mvutano wa hoja uliojikita katika mambo muhimu m a t a n o ( 5 ) . M a m b o yenyewe ni namna ya kuyafikia malengo ya m s i k i t i / s h u l e / t a a s i s i kwa ufanisi , masuala yanayohusu usimamizi wa fedha, utambuzi na utatuzi wa migogoro, mchakato wa ukuaji wa msikiti/shule/taasisi, na mfumo wa mawasiliano kiutendaji kati ya msikiti na shule/taasisi.

    M a m b o h a y o yaliwagawa wajumbe katika pande mbili zenye kuyatazama mambo hayo kwa mitazamo mawili to faut i . Hata h ivyo , zingatia kwamba mjadala huo haukubeba hisia za chuki wala uadui kati ya pande mbili zilizokuwa zikivutana kwa hoja.

    Upande wa kwanza u l i s e m a k u w a , mambo hayo hapo juu yatafanikiwa vizuri pale ambapo msikiti utakuwa ndiyo mmiliki wa shule au taasisi. Na hali ya umiliki i takapokuwa tofaut i , basi msikit i utakuwa kwenye wakati mgumu wa kuweza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi unaotakiwa.

    U p a n d e w a p i l i wa l i k u wa n a m a o n i kwamba ili shule/taasisi i w e z e k u ya t e k e l e z a m a m b o y a l i y o t a j w a

    hapo juu, ni muhimu msikiti uwe ni sehemu ya shule/taasisi hiyo. Kwa maneno mengine, msikit i umil ikiwe na shule/taasisi, vinginevyo itakuwa ngumu sana kama itawezekana kuyatekeleza majukumu hayo hapo juu kwa ufanisi unaotakiwa.

    Je, wewe binafsi na wenzako kwenye msikiti wako mnatoa majibu gani kwa swali la kipi kinafaa zaidi kat i ya msiki t i kumiliki shule/taasisi, au msikiti kuwa chini ya umiliki wa shule/taasisi?

    J e , m n a t a f a k a r i kuchagua upande mmoja mnaoona unawafaa kati ya pande hizo mbili hapo juu; au mnatafuta majibu ya kati na kati; au mnatafuta majibu mengine tofauti? Katika mchakato wa safu ya uongozi wa msikiti kutafuta majibu ya swali hilo, ndivyo ambavyo wanazielekeza fikra zao katika kutengeneza nafasi ya msikiti wao katika jamii.

    Nilipata kuzungumza na baadhi ya maimam wa m i s i k i t i a m b a y o inamiliki shule wakiwa wanalalamika kwamba viongozi wa shule ni jeuri na hawana heshima kwa viongozi wa misikiti . Wanawachukulia kama wageni wanaofika shuleni kulia njaa. Wao kama v iongoz i wa ms ik i t i hawapewi taar i fa ya maandishi juu ya kile kinachoendelea shuleni k i la baada ya muda fulani!

    Mazungumzo yangu na baadhi ya wakuu wa shule ambazo ziko chini ya umiliki wa misikiti nayo hayakukosa malalamiko. Wakuu wa shule hizo wanalalamika kwamba viongozi wa misiki t i wamekuwa na kawaida ya kufanya mambo kiholela, wanapiga mno mizinga kiasi kwamba wanapoingia

    ofisini unapata wasiwasi kwamba leo watataka kiasi gani, na hata wanapopewa taarifa za maendeleo y a s h u l e h a w a n a muda wa kuzisoma na kutafakari mapendekezo yaliyotolewa na uongozi wa s h u l e n a n a m n a ya kuyatekeleza bal i wanakimbilia kuangalia kiasi gani kimekusanywa ili na wao wapate mgao bila kuzingatia wala kujali bajeti ya shule kwa kuwa tu wao ndiyo wamiliki wa shule husika!

    N a d h a n i u n a o n a namna ambavyo nafasi ya msikiti inaingia katika mkanganyiko mkubwa kwa msikiti kuwa mmliki wa shule, na kwa msingi huo huo, kumiliki taasisi. Kuna ulazima wa haraka kupata ainisho zuri la nafasi ya msikiti katika mchakato wa utekelezaji mipango ya msikiti pale ambapo msikiti ni mmiliki wa shule/taasisi.

    T a f a k u r i k u b w a i n a h i t a j i k a k a t i k a mchakato huu wa kutafuta ainisho zuri la nafasi ambayo msikiti unatakiwa kuibeba ili tutoke hapa t u l i p o , a m b a p o k i l a upande msikiti na shule/taasisi wanalaumiana na hivyo kuviza utendaji wao.

    Sasa tugeukia upande wa wale waliojenga hoja kuwa inafaa zaidi shule/taasisi kumiliki msikiti na kuwa sehemu ya utendaji wake wa kila siku.

    Katika mazungumzo yangu na baadhi ya maimam wa mis ik i t i iliyo chini ya umiliki wa shule/taasisi walikuwa wakilalamika kwamba uongozi wa shule/taasisi hautengi kabisa fungu au unatenga fungu dogo la fedha kwa ajili ya msikiti

    wakati wa kuandaa bajeti ya shule/taasisi husika, i l i h a l i s h u l e / t a a s i s i inatenga mafungu ya bajeti kwa ajili ya maeneo mengine ya utendaji.

    Halikadhalika, maimam hao walilalamika kuwa shule/taasisi zinachukulia kazi za misikiti kama kazi za ziada katika majukumu ya msingi ya shule/taasisi. Na tangu hapo msikiti upo pale kwa ajili ya kupata ukaribu wa sehemu ya kutekelezea ibada ya swala tano pekee.

    K u m b u k a k u w a maimam hao aidha ni wanafunzi wa shule/taasisi au ni watendaji wa taasisi mama.

    K w a u p a n d e w a wamiliki wa shule/taasisi niliopata kuzungumza n a o , w a l i k u w a n a mtazamo kwamba msikiti ni jambo ambalo ujenzi wake wanahitaji msaada wa fedha na vifaa kutoka kwa Waislam. Jambo la kustaajabisha hapa ni kwamba, baada ya kukamilisha ujenzi wa madarasa, ofisi, mabweni n.k. mwenye shule anahitaji Waislam wachangie ujenzi wa msikiti wa shule yake. Na mara nyingi, jengo la msikiti huwa ni la mwisho kujengwa ndani ya eneo la shule.

    Katika mazungumzo hayo na viongozi wa shule, hawakuonesha kwamba wanaitazama misikiti ya shule zao kama ni kiungo muhimu kati ya shule zao na jamii zinazowazunguka, u k i z i n g a t i a k wa m b a misikiti hiyo mara nyingi hujengwa pembezoni mwa eneo la shule ili kuwaruhusu Waislam wanaoishi jirani na shule kuweza kuhudhuria swala za jamaa.

    Tuhitimishe makala ya leo kwa kuendelea kuitafakari nafasi ya misikiti yetu hivi leo ndani ya jamii yetu. Kwa upande mmoja tuna hali ya misikiti kuendeshwa kwa mazoea na kuwa na uholela katika usimamizi wa utendaji wa shule/taasisi ambazo zinamilikiwa na misikiti hiyo.

    Na kwa upande wa pili, tunaikuta misikiti ikiwa inadogoshwa na kutelekezwa pale misikiti inapokuwa iko kwenye umiliki wa shule/taasisi.

    In sha Allah wiki ijayo tutaendelea na kujadili nukta zingine baada ya kumalizia nafasi ya msikiti kati ya kumiliki shule/taasisi na msikiti kuwa kwenye umiliki wa shule/taasisi.

  • 10 AN-NUURRAJAB 1436, IJUMAA MEI 15-21, 2015Makala/Tangazo

    NIMERAGHIBIKA k u i t u m i a p i c h a h i i l e o k u wa p a n a s a h a v i j a n a w a n a o c h i p u k i a k u p e n d a s i a s a n a a m b a o w a n a d h i h i r i s h a uzalendo mkubwa k w a n c h i y e t u Zanzibar kwamba wasome na kukaa na wazee wenye hazina ya maarifa na historia ili waweze kuijua zaidi Zanzibar na pia kuongeza maarifa yao katika siasa na historia.

    Picha hii ilikuwa ni katika mwaka 1993 nikiwa na Maalim Seif Sharif Hamad nyumbani kwake Mtoni , Zanzibar . Wakati huo Maalim S e i f a l i k u w a n i Makamu Mwenyekiti wa CUF na mimi n i l i k u wa K a t i b u (Private Secretary) wa Katibu Mkuu wa CUF Marehemu Shaaban Khamis Mloo.

    T o k e a n i k i w a mwanafunzi nilikuwa napenda kujifunza s a n a m a m b o yanayohusu siasa na historia. Kutokana na kupenda huko kujifunza nilikuwa n a k a w a i d a y a kukaa sana na watu walioshiriki harakati za siasa Zanzibar na pia kusoma vitabu na maandishi mbali mbali yanayohusu siasa na historia. N a s h u k u r u nimechota mengi kwao.

    Ni kwa sababu hiyo niliitumia kikamilifu miaka ya mwanzo mwanzo wakati CUF i n a u n d wa k u k a a na kuzungumza na kumuuliza maswali mbali mbali Maalim S e i f n a k u p i t i a mazungumzo kama h a y o n i l i j i f u n z a mengi sana.

    N i l i k u w a n a k a w a i d a y a kumtembelea Maalim nyumbani kwake Mtoni jioni baada ya saa za kazi na huko kulikuwa na barza ya mazungumzo ya siasa ambapo kwa aliyetaka kujifunza aliyapata mengi.

    Nasaha kutoka kwa Jussa kwa vijana

    Ismail Jussa na Maalim Seif Sharif Hamad (pichani mwaka 1993) nyumbani kwa Maalim Seif, Mtoni Unguja.

    Wa t u w e n g i n e a m b a o n i l i p a t a bahati ya kukaa nao, kuzungumza nao na kuchota mengi kwao ni pamoja na Mzee Ali Haji Pandu, Mzee Shaaban Khamis Mloo (Marehemu), Mzee Mkubwa Makame ( M a r e h e m u ) , Mzee Said Sal im Baes (Marehemu), Maalim Juma Ngwali (Marehemu), Maalim Masoud Omar Said (Marehemu), Mzee Machano Khamis Ali, Juma Othman Juma, Hamad Rashid Mohamed, Khatib H a s s a n K h a t i b , Maalim Soud Yussuf Mgeni (Marehemu), D k . M a u l i d i Makame Abdallah ( M a r e h e m u ) , n a Bwana Juma Haji w a M c h a n g a n i (Marehemu).

    K a t i k a v i p i n d i to faut i n imepata pia fursa za pekee na bahat i kubwa kukaa na kujifunza kutoka kwa watu kama Sheikh Al i M u h s i n B a r wa n i (Marehemu), Maalim Salim Kombo Saleh (Marehemu), Sheikh S u l e i m a n S u l t a n Malik (Marehemu), Sheikh Salim Masoud Riyami (Marehemu), Sheikh Issa Nasser I s s a A l - I s m a i l y , Mzee Mohamedali Karim J innah wa Masomo Bookshop ( M a r e h e m u ) , Bwana Ali Nabwa ( M a r e h e m u ) , B i Inaya Himid Yahya (Marehemu), Maalim M o h a m e d I d r i s (Marehemu), Prof. Ibrahim Lipumba, Prof. Haroub Othman ( M a r e h e m u ) , S h e i k h A h m e d Badawi Qullatein (Marehemu), Prof. A b d u l S h e r i f f , Maalim Salim Mzee, Ali Ameir Mohamed, Mzee Hassan Nassor Moyo, Sheikh Salim Said Rashid, Dk. Salim Ahmed Salim, na sasa Dr. Amani Karume.

    Bila shaka wapo na wengi wengine ambao nimejichanganya na kujumuika nao kwa muda mfupi mfupi n a k u f a i d i k a n a hazina na maarifa yao lakini hao niliowataja hapo juu ni katika

    waliosarif mawazo yangu na mitazamo yangu kuhusiana na mengi yanayohusu siasa na historia ya Zanzibar.

    M o j a a m b a l o l i t a b a i n i k a n i kwamba nimekaa na kujumuika na k u z u n g u m z a n a watu wa mirengo tofauti ya siasa za Z a n z i b a r ( A S P , ZNP, ZPPP, Umma Pa r t y n a a m b a o hawakujitambulisha na vyama vya siasa) na hilo limenifundisha kusikiliza mitazamo i n a y o k i n z a n a n a kisha kuchambua na kupima mwenyewe yale niliyoyasikia huku nikifanya rejea k w e n y e v y a n z o vyengine vya khabari k a m a v i t a b u n a maandiko mengine mbali mbali.

    Nawaombea kheri wote walionipa na wanaoendelea kunipa fursa kama hizi na wale waliokwisha t a n g u l i a m b e l e ya haki Mwenyezi M u n g u A wa l a z e mahala pema Peponi. Amin.

    N a w a h i m i z a vijana wa kizazi cha leo watumie fursa zilizopo kukaa na wazee na watapata mengi kutoka kwao yatakayowasaidia kupanua ufahamu wao wa mambo.

    Ukiona vyaelea, vimeundwa

    Ismail Jussa

  • 11 AN-NUURRAJAB 1436, IJUMAA MEI 15-21, 201511 AN-NUURMakala

    KUFUATIA kukithiri ghasia nchini Burundi baada ya Rais wan chi hiyo anayemaliza muda wake Pierre Nkurunziza, kutangaza kusimama tena katika uchaguzi ujao, imeripoti k u w a w a k i m b i z i zaidi ya elifu hamsini wamerundikana katika mji Kagunga, katika mwambao wa Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma, wakisubiri taratibu za kuingizwa k a t i k a k a m b i y a wakimbizi ya nyarugusu wilayani Kasulu.

    Taar i fa z inae leza kuwa mpaka sasa ni wakimbizi elfu sita tu ambao wamekamilisha taratibu na kupelekwa katika kambi hiyo.

    T a r a t i b u zinazofanyika kabla ya wa k i m b i z i h a o kuingizwa kambini ni pamoja na kukaguliwa kama kuna waliobeba s i l a h a , k a m a k u n a wanajeshi nk.

    M a h a k a m a y a Katiba nchini Burundi i m e m r u h u s u R a i s P i e r e N k u r u n z i z a kuwania muhula wa tatu madarakani ambao umegubikwa na utata.

    M a h a k a m a h i y o i l i s e m a J u m a n n e kwamba Rais ataweza kuwania tena kiti hicho bila kukiuka katiba ya nchi inayosema kurudia tena muhula w a u r a i s k u p i t i a kipengele cha moja kwa moja cha haki ya kupiga kura katika uchaguzi wa kisiasa inaruhusiwa.

    Lakini Naibu Rais wa Mahakama hiyo amepinga maamuzi hayo na kukimbilia n c h i n i R w a n d a . Sylvere Nimpagaritse aliwaambia waandishi wa habari kwamba dhana yake haimruhusu kutia saini maamuzi ambayo ni kinyume cha katiba.

    Muhula wa kwanza wa utawala wa Nkurunziza kama Rais ulitokana na matokeo ya kura ya

    Kufuatia machafuko Burundi maelfu ya raia wakimbilia TanzaniaKigoma imeelemewa

    wabunge. Wafuasi wa Rais huyo wanasema Bw. Nkurunziza ametumikia muhula mmoja pekee k w a k u c h a g u l i w a baada ya kuwa mshindi katika uchaguzi mkuu hivyo kwa misingi huo anastahi l i kuwania muhula mwingine.

    Wakosoaji wanasema B w . N k u r u n z i z a anakiuka katiba na mkataba wa amani wa Arusha wa mwaka 2000, ambao ulisaidia k u m a l i z a v i t a v ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

    J u h u d i z a R a i s huyo kuongeza muda w a k e m a d a r a k a n i z i m e c h o c h e a m a a n d a m a n o y a mi taani ka t ika mj i m k u u , B u j u m b u r a n a k u s a b a b i s h a mapambano na polisi na yaliyozaa vifo vya watu wasiopungua 12.

    Makamu Rais, Prosper Bazombanza, alisema J u m a n n e i l i y o p i t a kwamba serikali ipo tayari kuwaachia mamia y a w a a n d a m a n a j i inaowashiki l ia kwa zaidi ya wiki mbili sasa, kwa mashart i kwamba maandamano yasitishwe.

    Ukiacha warundi wanaokadiriwa kufikia 50,000 waliokimbilia Tanzania, kiasi cha w a r u n d i 2 4 , 0 0 0 wamekimbi l ia nchi jirani ya Rwanda tangu ghasia hizo zilipoanza April 26 huku maelfu ya wengine wakiingia Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC. (VOA).

    Tayari Serikali ya Ubelgiji imesimamisha misaada yake kwa nchi hiyo kwa kile ilichodai kuwa ni kuendelea machafuko ndani ya nchi hiyo.

    AlexanderDe Croo, Waziri wa Ushirikiano n a M a e n d e l e o wa Ubelgiji, amesema kuwa nchi yake imesimamisha misaada ya kifedha kwa Burundi ambayo ingetumiwa kwa ajili ya

    Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza.

    uchaguzi mkuu ujao. A i d h a a l i s e m a

    k u wa B r u s s e l s p i a i m e s i m a m i s h a ushirikiano wa pande mbili hizo katika sekta ya k u t o a m a f u n z o kwa polisi ya Burundi kufuatia kuendelea machafuko ndani ya nchi hiyo.

    Alisema uamzi huo u m e k u j a b a a d a ya ripoti iliyotolewa na Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa

    Mataifa nchini Burundi. Kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni ya K a m i s h a n a h u y o , waandamanaji 11 hadi sasa wamekwishauawa k a t i k a m a c h a f u k o kufuatia hatua ya Rais Nkurunziza wa nchi hiyo kutangazwa na c h a m a t a wa l a c h a CNDD-FDD kugombea uchaguzi mkuu mwezi ujao.

    W i k i i l i y o p i t a waangalizi wa uchaguzi

    wa Umoja wa Mataifa wal i tangaza kuwa, hali inayotawala hivi sasa nchini Burundi, hairuhusu kufanyika uchaguzi huo.

    A w a l i B r u s s e l s i l i k u w a i m e t e n g a msaada wa Euro milioni nne kwa ajili ya Burundi, huku milioni mbili kati ya fedha hizo zikiwa t a ya r i z i m e k w i s h a kabidhiwa kwa serikali ya Bujumbura.

    DURU za kuaminika z i m e f i c h u a k u wa , Saudi Arabia na Israel z i m e t i l i a n a s a i n i mkataba wa ushirikiano wa kijasusi katika suala la Yemen pamoja na kutumiwa ndege zisizo na rubani za Israel katika anga ya Yemen.

    Z i m e n u k u l i w a duru za kuaminika zilizofichua kuwa, Mkuu wa Shirika la Kijasusi la Saudi Arabia, Khalid bin Ali bin Abdullah al Hamidan, hivi karibuni alielekea katika ardhi za Palestina zinazokaliwa

    Imebainika Saudia inashirikiana kijasusi na Israel

    k w a m a b a v u n a Wazayuni na kutia saini mkataba wa ushirikiano wa ki jasusi kati ya Saudia na utawala wa Kizayuni wa Israel.

    Kabla ya hapo baadhi ya vyombo vya habari kama vile televisheni ya al Alam na gazeti la Kizayuni la Yediot Ahronot, vilitangaza habari ya kutua ndege ya Saudi Arabia katika uwanja wa ndege wa Ben-Gurion huko Tel Aviv.

    Mashirika ya habari yalisema kuwa ndege

    hiyo ilikuwa ya mwana mmoja wa ukoo wa kifalme wa Aal Saud, ingawa Saudia ilidai k u w a n d e g e h i y o ilikuwa ya shirika la ndege la Ureno.

    Hii si mara ya kwanza kuripotiwa habari za ushirikiano baina ya utawala wa Kizayuni wa Israel na ukoo wa Aal Saud.

    Habari za kuwepo ushirikiano mpya baina ya pande hizo mbili dhidi ya wananchi wa Yemen zinatilia nguvu ushirikiano wa muda mrefu baina ya Saudia na utawala wa Kizayuni wa Israel.

  • 12 AN-NUURRAJAB 1436, IJUMAA MEI 15-21, 201512 MAKALA/MASHAIRI

    Israi na MirajiInatoka Uk. 8

    mwenye kumsaidia A m i y a k o , A b u Twaalib, japo kuwa yeye alikuwa ni mtu mwenye kukuhami sana na alikuwa anachukizwa s a n a k w a m a m b o uliyokuwa unatendewa na Makureshi. Mtume akasema, Yuko katika moto mwepesi, kama si mimi angelikuwa kwenye moto wa tabaka la chini kabisa huko Jahanam. (Swahiyh Al-Bukhaariy Juzuu 5 Namba 222); Hivyo Abu Twaalib licha ya kuwa kafiri alimuunga mkono Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) kwa nguvu zake na mali zake dhidi ya makafiri. Wakati Abu Twaalib al ipokuwa hai makafiri walikuwa hawawezi kumdhuru Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam). Hata hivyo, kifo cha Abu Twaalib kilikuwa ni mwanya m wa m a k a f i r i wa kuendeleza vitimbi vyao dhidi ya Mtume pamoja na Waislamu kwa ujumla. Tabia yao ya ukatili ilimfanya Mtume aone maisha mj ini Makkah ni magumu. Kutoa shahada kwa Maswahaba wa Mtume mjini Makkah ilikuwa ni njia ya kujitangazia uadui wa wazi wazi na wakawa wanapata madhila na kuadhibiwa vibaya. Kila aliyesilimu aliambiwa afanye moja kati ya mambo mawili: aritadi au aondoke hapo nchini au sivyo basi roho yake itafariki dunia; makafiri hawakutaka njia nyingine zaidi y a h i y o . L a k i n i Maswahaba licha ya kuwa hiki kilikuwa ni kipindi kigumu sana na chenye taabu kubwa sana katika maisha yao kutokana na adhabu na madhila waliyoyapata, waliendelea kusimama imara juu ya imani ya Uislamu na walisonga mbele na Mtume wao katika msimamo huo. Kupanuka kwa Uislamu k u l i w a u d h i s a n a

    makafiri na wakajaribu kila nj ia i l i kuzuia na kukinga Uislamu usiwepo katika nchi yao. Ulinganiaji wa dini hii ukawa mzito kwa Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) na hata kuishi mjini Makkah ikawa ni hali ngumu sana kwake na kwa Waislamu.

    Jambo la pili lilikuwa kifo cha mama wa Waumini Khadiyjah (Radhiya Allaahu anha) Ni miezi miwili tu baada ya kifo cha Abu Talib, Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) alipata tatizo lingine zito lililomhusu yeye binafsi. Mke wake na Mama ya waumini, Bi Khadiyjah (Radhiya Allaahu anha) alifariki. Mama huyu, mama wa Waumini Khadiyjah, alikuwa ni rehma kwa Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Taala). Daima alikuwa n a M t u m e wa k a t i akipata madhila na maudhi ya makureshi na alikuwa naye siku zote wakati wa mitihani m i z i t o i l i p o k u w a inamwendea Mtume kutoka kwa mahasimu wake wa Kikureshi na walikuwa pamoja katika hali hiyo kwa muda wa miaka 25. Na kwa yote hayo Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) k w a u k a r i b u h u o aliokuwa nao mama wa Waumini Khadiyjah alisikitika sana kwa kifo cha mkewe mpenzi na kuna wakati alisikika akisema juu ya bibi h u y u , A l i n i a m i n i w a k a t i w e n g i n e hawakufanya hivyo, Alijiunga na Uislamu wakati watu walikuwa h a wa t a k i k u f a n ya hivyo. Pia alinisaida na kuniliwaza mwenyewe na na kwa mali zake w a k a t i k u l i k u w a hakuna hata mtu wa

    kuniunga mkono. Pia nilipata watoto kutoka k wa k e . ( M u s n a d Ahmad 6/118).

    M a t u k i o h a y a m a w i l i y a l i t o k e a m f u l u l i z o . M t u m e (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa amefikia hali ya kubabaika namna gani awaongoze Waarabu w a M a k k a h , b a s i aliangalia upande wa Twaaif mji ambao kwa wakati huo ulikuwa unahitajia msaada na uongozi. Lakini hata huko pia hakupokelewa na hali hiyo kuongeza machungu moyoni mwake (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) hata akaona kipindi hicho kuwa ni Mwaka wa Huzuni.

    Katikati ya huzuni z o t e h i z o A l l a a h Alimchukua mja Wake katika muujiza mkubwa wa Israa na Miiraaj ili amwoneshe Aayah Zake na kumpat ia msaada na himaya. Allaah Anasema, Ili Tumwoneshe baadhi ya Ishara Zetu

    Kwa muuj iza wa Israa na Mi i raa j , Allaah Aliweka msingi kwa waja Wake kuwa hata kama makafiri wangelifunga mlango wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam), Allaah Ndiye Mwenye Kumhami na ndio Mlezi Wake na milango ya Peponi iko wazi kwa ajili ya Muhammad (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam). Hakuna nguvu ambayo inaweza kumteza au kumdhuru yule ambaye yuko chini ya ulinzi wa Allaah. Israa na Miiraaj ilikuwa ni dalili ya kuonesha kufanikiwa kwa Dawah ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) na ushindi wake juu ya maadui zake pamoja na kuwepo kwa matatizo na huzuni zote hizo.

    KARIBU MWEZI SHAABANI

    "KATIBA SHERIA-MAMA", kauli-mbiu si ngeni,Kuinena lelemama, kuitenda 'uhaini',Kwa HAKI kutosimama, MAMA huyu yu rehani,KULIKONI DPP, KUWA JUU YA SHERIA ?

    Yu rehani wetu MAMA, mnadiwa kaulini,Yavunjwa yake heshima, vitendoni bila soni,Yake chini taadhima, kwa hawaa ya insani,KULIKONI DPP, KUWA JUU YA SHERIA ?

    Adogoshwa huyu MAMA, si batini hadharani,DPP 'muadhama', yu JUU MAMA yu CHINI,Yapuuzwa yake dhima, na 'WANA' wa mwake ndani, KULIKONI DPP, KUWA JUU YA SHERIA ?

    DHAMANA haki adhima, si ngeni i katibani,Kutoitoa jarima, mtenziwe hatiani,Yu awe sawa yu mwema, au muwi yu 'haini',KULIKONI DPP, KUWA JUU YA SHERIA ?

    DHAMANA haki daima, ya 'mtovu' sheriani,Kwa yeyote kuizima, hachomoki hatiani,Kwa kuauni DHULUMA, yu DHALIMU orodhani, KULIKONI DPP, KUWA JUU YA SHERIA ?

    DHAMANA haki ya zama, jana, leo na zamani,KWANINI sasa YAKWAMA, kwa MASHEKHE KULIKONI,Beti sita kaditama, MAHABUSU HADI LINI,U WAPI UADILIFU, WA DPP KWA HILI ?

    ABUU NYAMKOMOGI-MWANZA.

    RAJABU i ukingoni, aula kukujuzeni,Na SHABANI i njiani, wiki kesho si mwakani,Mbeleye i RAMADHANI, si baidi tambueni,SHABANI ikiwadia, tuienzi kwa kufunga.

    Muhammad adinani, alikifunga Shabani,Pima wake uthamani, ujisaili kwanini,Thuma ujitathmini, kwa RAHMANI u nani?SHABANI ikiwadia, tuienzi kwa kufunga.

    Hakuacha asilani, kuifunga maishani,Siku moja msidhani, bali tumbi tambueni,Mimi nawe kulikoni, kutoifunga Shabani?SHABANI ikiwadia, tuienzi kwa kufunga.

    Twaridhika ikhiwani, tuna nini nijuzeni, Rasuli tumgezeni, kwa kuifunga Shabani,Kulikoni na kwanini, tusiifunge Shabani?SHABANI ikiwadia, tuienzi kwa kufunga.

    Haya shime waumini, wa Bara na Visiwani,Sote nia tutieni, ya kuifunga Shabani,ILAHI tumuombeni, tuidiriki Shabani,SHABANI tuilakini, kwa swaumu waumini.

    ABUU NYAMKOMOGI-MWANZA.

    UADILIFU WA DPP !

  • 13 AN-NUURRAJAB 1436, IJUMAA MEI 15-21, 2015Habari

    NI masikitiko makubwa kwa watu wanaojidai kuwa ni Waislamu wenye kutaka kusimamisha Ukhalifah, kwa kuwashumu ndugu z a o k a t i k a i m a n i n a kuwapachika ukafiri kwa shutuma za uwongo.

    Mathalan i , h iv i sasa kwenye mtandao wa Somal Memo, binafsi na watu wengine, tumetuhumiwa kwa madai ya kwamba hatuna Akida (Tahweed na Man-Haj). Hizi ni shutuma mbaya za kutukufurisha na kututoa katika Uislamu.

    Mimi binafsi kwenye m a k a l a n i l i z o z i a n d i k a nimeelezea kwa mujibu wa ukweli (facts) nilizonayo na kwa mtazamo wangu na nilivyomtathimini juu ya anayedaiwa eti ni Khalifah wa Uis lamu Abubakari Baghdadi.

    Naam !!! Twaibu, baada ya kuisoma na kuielewa makala hiyo, nimepata msukumo wa kuwapa Nasaha ndugu zangu hao waliyotajwa kwa majina yao na kuwataka wawe na subira, kwani hiyo ni mitihani katika harakati za Daawah na Allah (Subhaanahu wa Taala) na awalipe ujira mwema kwa mtihani huo uliowafika.

    Hali hii uzoefu wake inaonyesha jinsi tulivyo k we n ye j a m i i ye t u ya K i i s l a m u , k u k i t o k e a sintofahamu yoyote kati ya mtu na mtu, taasisi na mtu au taasisi kwa taasisi za Kiislamu kadhia hiyo itaishia kutoleana tuhuma za kuchafuana kwa vipeperushi, mitandaoni na kutiana motoni nk.

    Abu Said na Abu Hureira (Radhiya Allaahu anhu) wamepokea kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa sallam) kuwa amesema:

    Muislamu hatapatwa na taabu, wala maradhi, wala huzuni, wala udhia na wala ghamu (sonenoko), mpaka mwiba unaomdunga isipokuwa Allah Hufutia dhambi zake kwa sababu ya hayo. (Muttafaq).

    Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa sallam) amesema:

    Malipo makubwa yapo pamoja na balaa kubwa, hakika Allah anapowapenda watu, Huwapa mitiani, ; atakaridhika, basi atapata r a d h i ( z a A l l a h ) , n a a t a k a e c h u k i a , u t a p a t a hasara . Tir imidhy, na amesema Hadithi hii ni Hasan.

    Na kwenye jamii yetu ya Kiislamu pale inapotokea kuhitilafiana/kutofautiana au kukosana rai, mtizamo na mgongano wa mawazo juu ya kutathimini mambo ya Kiislamu ni kwamba kutatokea Wa i s l a m u k u f a n y i a n a mambo maovu yanayo

    Kushutumiana kwenye mitandao sio maadili ya Uislamu

    vunja udugu na upendo na kuweza kufarikiana n a k u j e n g a u h a s a m a baina yetu Waislamu. Na kufanyiana mambo maovu kama vile: Kuzulumiana, Kusengenyana, Kudhaniana vibaya, Kuchunguzana, K u m c h u k i a m t u k w a tuhuma za kusikia juu juu, Kudharaul iana na kutukanana, Kuvunjiana heshima, Na kusalitiana kwa Matwaaghuut ama kwa kupelekena Mahakamani au kuvujisha siri kwa adui zetu kwa lengo kumuharibia mtu au taasisi au harakati zozote za Kiislamu ili ziweze kuangamia n.k.

    Hali hii tuliyonayo ni tofauti kabisa na mafunzo ya D i n i ye t u , a m b a y o imetufundisha namna ya kumaliza tofauti zetu na kupata sulhu kwa lengo la kujenga udugu wetu wa K i i m a n i . N i k we l i kwamba katika hulka za binadamu lazima kutatokea sintofahamu baina yetu kwa jambo hili au lile ichukuliwe k a m a c h a n g a m o t o n a kukabiliana nayo kama tulivyoekezwa na Dini yetu kwa Nususi mbambali za kisheria.

    Katika umri Wangu mpaka sasa ni nadra kuona watu wa Dini Nyingine isiyokuwa ya Uislamu humu mwetu, kwa kuwaona wakizozana h a d h a r a n i k wa j a m b o linahusiana na michakato mbalimbali ya harakati za dini zao na kufikia kiasi cha kutoleana vipeperushi vya tuhuma au kwenye Mass Media (Vyombo vya Habari) n.k. hawa ni binadamu kama sisi, mazingira na culture zetu ni moja na hawana Ufunuo kutoka kwa Allah (Subhaanahu wa Taala) bali wana Nidhamu kwenye Dini yao na kufuata kanuni sahihi za kibinadamu kumaliza tofauti zao.

    Mtu kama sio mweledi wa SERA za harakati zetu za Kiislamu, anaweza kupata taabu au kutatizika

    ni kwa nini? Hali hii inatokea kwenye safu zetu hali ya kuwa tunao Muongozo. Hali hii inasababiswa na mambo yafuatayo:

    M o s i , k w e n y e mikusanyinyiko yetu ya Kiislamu hatuna lengo, Vision na Mission moja, bali kila mtu ana jambo lake moyoni. Pili, hakuna Nidhamu kwa Viongozi wengi kwenye mikusanyiko yetu kwa Maamuma/wafuasi na wanakundi wenzao na au kinyume chake ni hivyo hivyo. Bali mambo mengi yanafanywa kwa msukumo wa jazba, ushabiki, kukumoana, kulipizana visasi n.k. Tatu, Baadhi Madaiyah (Mudir, Rais, Mkurugenzi, Sheikh, Ustadh, Amir n.k.) wengi kama sio wote, hakuna wanaofanya Mipango ya K i s t r a t e j i a S t r a t e g i c Plans (Mipango Mkakati) kuwalea Waislamu kiasi cha kuwawezesha kufuata N i d h a m u ya K i i s l a m u katika mfumo wa maisha yao katika kila kipengele cha k is iasa , k iuchumi , kimaadili, kitamadnni, nk. Ba l i wanawatengeneza watu kuwa washabiki wa kama wa timu za mipira na sio kuwafanya wawe ni watumwa wa Mwenyezi M u n g u . K wa m t i z a m o wangu ndio baadhi ya vyanzo vya matatizo yetu ambayo yamesababishwa na mambo yafuatayo: Ukosefu wa Elimu Sahihi ya Uislamu, Mbinu za ufundishaji Uislamu, Maslahi ya maisha binafsi na Ushabiki kama watimu ya mpira nk.

    Kadhia ya kushutumiana ina athari za kipropaganda, Upotoshaji wa taarifa/habari zisizo zenyewe, kufitinisha na kufarakanisha Waislamu n.k. kwani ni kitendo ambacho huwa kimefanywa na mtu kwa jazba na ushabiki au maadui walio nje ya safu za Waislamu katumia fursa ya udhaifu wetu wa kugomba au kwa kukusudia kuzusha Fitna kwenye safu za Waislamu ili washughulikiane wenyewe

    na huku wao wakitekeleza mipango ya kuwaangamiza Waislamu.

    Ndugu zangu, Al lah (Subhaanahu wa Taala) awasamehe (endapo mtaleta Toba) kwa kitendo chenu cha kughafilika na kughalifu juu ya mafunzo ya Uislamu yanayoelekeza namna ya kukosoana kwa nia ya kujenga na kuleta umoja na mshikamano wa udugu wa kweli katika Imani. Bali kwa dhahiri yenu mmeonyesha kusukumwa zaidi na Jazba, ghadhabu nk Hatuna budi kuwakumbusha mtizamo wa Uislamu juu ya kupokea na kutangaza habari kwani Uislamu umeweka sheria juu ya jambo hilo. Amesema Allah (Subhaanahu wa Taala):

    E n y i m l i o a m i n i ! A k i k u j i e n i F A S K I ( m p o t o v u ) n a k h a b a r i yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda. (49:6)

    Na pia amesema Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa sallam):

    Lau watu watapewa kwa kila wanachokidai (Bila Ushahidi), basi mali za watu zitapotea, damu zitamwagika sana, heshima zitapotea, hivyo basi kila anayedai na alete ushahidi, na anaye kanusha a le te Kiapo . (Muslim na Ahmad).

    A m e s e m a A l l a a h (Subhaanahu wa Taala):

    E n y i m l i o a m i n i ! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipelelezane, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anayependa kuila nyama ya nduguye aliye kufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu. (49:12)

    Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke.

    Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari. (49:13)

    Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa sallam) amesema:

    Anayevumisha maneno ambayo ameyasikia juu juu hataingia Peponi. (Bukhari na Muslim).

    Na Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa sallam) amesema:

    Muovu zaidi kat ika watumwa wa Mwenyezi Mungu ni wale wanaotangaza maneno ya kufarakanisha watu wapendanao na kutaka kutia ila wale wasiokuwa na makosa (hatia). (Ahmad).

    Na Mwenyezi Mungu ametoa kemeo kali juu ya kauli yake pale aliposema:

    K w a h a k i k a w a l e wanaopenda uenee uchafu kwa walio amini, watapata adhabu chungu katika dunia na Akhera. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui. (24: 19).

    Na Amesema Al laah (Subhaanahu wa Taala):

    Na wale wanao waudhi Waumini wanaume na wanawake pas ina wao kufanya kosa lolote, bila ya shaka wamebeba dhulma kubwa na dhambi zil io dhaahiri. (33:58).

    Abu Hureira (Radhiya Allaahu anhu) amesema: Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa sallam) amesema:

    Nawahadharisha na TUHUMA, hakika TUHUMA ni mazungumzo ya uongo. Wa l a m s i c h u n g u z a n e , wala msifanyiane ujasusi, wala msishindane, wala m s i h u s u d i a n e , w a l a msibughudhiane , wala msipane mgongo. Kuweni- enyi waja wa Allah- Ndugu moja kama alivyowaamrisha. Muislamu ni ndugu ya Muislamu, hamdhulumu wala haachi kumnusuru, wala hamdharau. Uchaji Mungu uko hapa, Uchaji Mungu uko hapa.

    Akaashiria kifuani mwake. Yatosha mtu kuwa ana shari anapomdharau ndugu ya Muislamu. Kila Muislamu ni haramu juu ya Muislamu m w e n z i e d a m u y a k e , heshima yake na mali yake. Hakika Allah hatazami miili yenu wala sura zetu, lakini Anatazama nyoyo zenu na amamli zenu. (Muslim).

    Wabbilah Tawfiq.(Makala hii imeandiskwa

    na: Abu Saumu, Kombo Hassani Kidumbu. E-Mail [email protected] Mob: 0714720965-Mikanjuni-Tanga-Tz)

  • 14 AN-NUURRAJAB 1436, IJUMAA MEI 15-21, 2015Makala

    Na Ben Rijal

    Na Ben Rijal

    Mchango wa Waislmau katika maendeleo ya Dunia - 11

    UWANJA WA VIJANA - JIONGEZEE MAARIFACHEMSHA BONGO namba 6

    MAJIBU CHEMSHA BONGO NO:51. Mtume gani alikabiliana na Mfalme Nimrod?

    Yusuff, Ebrahim, Issa. Jawabu: Ebrahim2. Mwezi wa mwanzo wa mwaka Kiislamu ni

    mwezi wa : Muharram, Ramadhan, Mfungo Mosi, Jawabu: Muharram

    3. Mtume Mussa alipoitupa Fimbo yake iligeuka: Nge, Ndege, Nyoka. Jawabu: Nyoka

    4. Waliomfwata Mtume wakati yupo hai wakiitwa: Marafiki, Wenzani, Masahaba.Jawabu: Masahaba

    5. Sura ngapi zimeanza na kalima Bismillahi Rahman Rahim? 114, 113, 720 Jawabu:113

    6. Harufu gani imetumika zaidi katika Quran? Alif, Taa, Yee. Jawabu: Alif

    7. Mwaka katika Uislamu una siku ngapi? 365.4, 354, 365. Jawabu: 354

    8. Mtume Muhamad SAW alihama Makka kwenda Madinah mwa kagani? Jawabu: 622

    9. Mtume Younus alimezwa na: Nyangumi, Papa, Ndowaro. Jawabu: Nyangumi

    10. Ni Sahaba yupi mwanamue mtu mzima alikuwa wa mwanzo kumkubali Mtume SAW na Sahaba yupi aliokuwa mtoto wa mwanzo kumfwata Mtume SAW? Jawabu: Syd Abubakar mtu mzima na Syd Ali akiwa mtoto.

    K a t i k a m a k a l a z i l i z o k w i s h a kutangulia nimejaribu kuonyesha mchango m k u b w a a m b a o Waislamu waliutoa ka t ika maendeleo y a s a y a n s i n a m w a n a d a m u . Makala ya safari hii n i t a m u e l e z e a I b n Khaldun, ili kuweza kuelewa mchango w a I b n K h a l d u n katika maendeleo ya mwanadamu itakuwa vyema kumuelezea kwa makala mbili tofauti. Makala ya kwanza itamzungumzia juu ya maisha yake na makala ya pili itamzungumzia kazi zake pamoja na ile kazi yake kubwa ijulikanayo kwa jina la Muqaddimah.

    I b n K h a l d u n j ina lake kamili ni A b d a l - R a h m a n b i n M u h a m m a d bin Muhammad bin Muhammad bin Al-H a s a n b i n J a b i r b i n M u h a m m a d b i n I b r a h i m b i n Abdurahman bin Ibn Khaldun. Nasaba yake inatokana na Hadharmi yaani watu wa Kusini ya Yemen, wengine wanasema kuwa juu ya kuwa mizizi yake yanatokana na nchi ya Yemen lakini yeye ametokana na koo za Wail Hajar likiwa katika kabila la Azal nchini Yemen kama alivyoelezea Ibn Hazam katika kitabu chake Jamharat ansb al-arab.

    Kiasili Ibn Khaldun a n a t o k e a Ye m e n kiuzawa amezaliwa nchini Tunisia katika mwaka wa 732 AH (27 May 1332), ingawa alizaliwa Tunisia lakini familia yake ilikuwa inaishi Uspani (Spain). Ilibidi kuhajiri kutoka Uspain na kuhamia Tu n i s i a k u t o k a n a

    na misukosuko ya Waislamu walioyakuta baada ya v i ta vya msalaba. Katika utoto wake kama watoto wengi Waki i s lamu katika nchi mbalimbali a l i a n z a k w a kusomeshwa Quran na aliianzia masomo yake nyumbani kwa kusomeshwa na babake kisha akasoma kwa wasomi mbalimbali maarufu wa wakati wake nchini Tunisia. Ibn Khaldun alikuwa Hafidh Quran aliweza kuusoma msahafu wote kwa ghibu alijifunza sayansi ya hadith za Mtume SAW, akajifunza nahawi, fiqhi, ufundi wa a s i l i ya l u g h a mashairi, hesabati na elimu nyenginezo.

    K a t i k a d u r u ya masomo mara nyingi k i j a n a a n a p o f i k a m i a k a 1 9 h u w a amemaliza masomo ya kati na kuelekea masomo ya juu ikiwa huko nyuma wengi walipofikisha umri wa miaka 19 walikuwa washakubuhu katika uga wa el imu. Ibn Khladun alipotimiza umri wa miaka 19 alikuwa kisha balighi kielimi na kuajiriwa katika tawala kubwa za sehemu mbalimbali alizokwenda kuishi.

    Siasa za tawala za siku za nyuma zilikuwa mara kwa mara kuwa k a t i k a m a p i g a n o baina ya nchi moja n a n y e n g i n e k w a minajili ya kutanuwa mamlaka ya viongozi hao. Matokeo kama hayo yal impelekea Ibn Khaldun kuhama kutoka Tunisia kuhamia Algeria, kisha akahamia M o r o c c o k u t o k a Morocco akaelekea Misri na kuingia Uspani nchi walioishi wazee wake kabla ya kuhamia Tunisia na mwisho Ibn Khaldun alimalizia kuishi nchini Misri na kufia hapo.

    Ibn Khaldun kama w a s o m i w e n g i n e a l i f u n g w a n c h i n i Morocco kutokana na uungaji wake mkono upande mmoja wa uongozi. Alifungwa kwa kipindi cha miaka miwili . Korokoroni kuliweza kumsaidia kupanua fikra zake na kumfanya aweze

    kufikiria juu ya mbinu za utawala na uatawala bora uweje na kugawa madaraka ya utawala.

    K u h a m a h a m a kwake kulimfikisha nchini Misri, huko Misri kulimfanya kujulikana katika ngazi kuu za taifa na kupata sifa katika kila kona za mji wa Misri, sifa hizo zilimpelekea Sultan Farouk kumtaka asafiri naye kueleka nchini Syria katika mji mkuu wake wa Damascus. Sifa ya viongozi wa m i a k a y a n y u m a walipokuwa wanasafiri w a k i p e n e d e l e a kufwatana na wasomni ili kuweza kuwasaidia katika mazungumzo na wenyeji wao, taratibu h i z i z i n a e n d e l e a k u f w a t w a l a k i n i kinyume na za zama h i z o z i l i z o p i t a , k w a n i v i o n g o z i waliopita walikuwa wakiwachagua wasomi kufwatana nao katika safari kwa uwezo wao bila ya uependeleo, wakiwachagua wasomi sio kwa kabila zao au dini zao au rangi zao.

    Safari yake hiyo Ibn Khaldun inaelezewa n a Wa n a h i s t o r i wa kuwa Sultan alibakia mjini Damascus kwa kipindi cha wiki mbili tu na kurudi Misri k wa u w o g a k u wa kulikuwa na tetesi za kupinduliwa, aliondoka na kumwacha nyuma Ibn Khaldun.

    Kutokana na umahiri wa k e wa h i s t o r i a , ufanisi wa lugha Ibn Khaldun akateuliwa k u wa m j u m b e wa upatanishi baina ya pande mbili zilizokuwa zikizozana baina ya u o n g o z i u l i o k u wa ukitumia mkono wa chuma Amir Timur wa Samarkand nchi inayojulikana kwa sasa Uzbekistan na watu wa Syria. Nchi ya Syria walitaka kuelewana na Amir Timur kwa kumchagua Ibn Muflih kuwa n