ANNUUR 1033

16
ISSN 0856 - 3861 Na. 1033 SHAWWAL 1434, IJUMAA SEPTEMBA 7-13, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu Jamani hawa ndio Polisi wetu Ndio wale wale waliouwa Mwembechai! Mkawapongeza 2001 walipouwa watu 27 Mngepiga kelele kama hizi za Daudi labda… Waziri Haji atolewa jasho Ikulu Zanzibar Uamsho wampiga Da’wah kubwa katika sensa Wataka Mawaziri waingie ofisini na Uislam wao Pemba mambo yazidi kuwa magumu Sensa ‘yageuka’ Jihad Sumbawanga Adhana yakusanya Waislamu Polisi Baada ya Swala, Dua, mmoja asilimu Gari Polisi ‘yagoma’ kubeba watuhumiwa Mwanza: DC, Masheikh waviziwa Butimba Uandikishaji unaendelea. Gharama za Hijja ni kama Hijja iliyopita mwaka jana, USD 3850. Tarehe za safari ni 19 Oktoba, 2012 na kurudi tarehe 11 Novemba, 2012. Wahi kujiandikisha sasa. Kwa mawasiliano: +255 22 2181577, +25 22 2182370, 0717 000065, 0786383820, 0754 261910 E-mail: [email protected], info@hajjtrusttz. org Website: wwwhajjtrusttz.org Safari ya Hijja Hijiria 1433 Waislamu kuandamana Dar leo? Ni kupinga kamatakamata ya sensa Mbunge Kilwa naye atiwa nguvuni Viongozi wa Jumuiya waitwa wizarani Waziri wa Mambo ya Ndani, Dkt. Emmanuel Nchimbi BAADHI ya viongozi wa UAMSHO.

Transcript of ANNUUR 1033

Page 1: ANNUUR 1033

ISSN 0856 - 3861 Na. 1033 SHAWWAL 1434, IJUMAA SEPTEMBA 7-13, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Sauti ya Waislamu

Jamani hawa ndio Polisi wetu

Ndio wale wale waliouwa Mwembechai!Mkawapongeza 2001 walipouwa watu 27Mngepiga kelele kama hizi za Daudi labda…

Waziri Haji atolewajasho Ikulu Zanzibar

Uamsho wampiga Da’wah kubwa katika sensaWataka Mawaziri waingie ofisini na Uislam waoPemba mambo yazidi kuwa magumu

Sensa ‘yageuka’ Jihad SumbawangaAdhana yakusanya Waislamu PolisiBaada ya Swala, Dua, mmoja asilimuGari Polisi ‘yagoma’ kubeba watuhumiwaMwanza: DC, Masheikh waviziwa Butimba

Uandikishaji unaendelea. Gharama za Hijja ni kama Hijja iliyopita mwaka jana, USD 3850. Tarehe za safari ni 19 Oktoba, 2012 na kurudi tarehe 11 Novemba, 2012. Wahi kujiandikisha sasa.Kwa mawasiliano:+255 22 2181577, +25 22 2182370, 0717 000065, 0786383820, 0754 261910E-mail: [email protected], [email protected]: wwwhajjtrusttz.org

Safari ya Hijja Hijiria 1433

Waislamu kuandamana Dar leo?Ni kupinga kamatakamata ya sensaMbunge Kilwa naye atiwa nguvuniViongozi wa Jumuiya waitwa wizarani

Waziri wa Mambo ya Ndani, Dkt. Emmanuel Nchimbi

BAADHI ya viongozi wa UAMSHO.

Page 2: ANNUUR 1033

2 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 7 - 13, 2012

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0755 260 087 0713 110148, DSM. www.ipctz.org E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

MAONI YETU

Tahariri/Tangazo

DAUDI Mwangosi, aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo c h a t e l e v i s h e n i c h a C h a n n e l Te n mkoani Iringa, tayari ameshazikwa Jumanne ya Septemba 3, kijijini kwao Busoka, Rungwe mkoani Mbeya.

Mwangosi alifikwa na mauti Septemba 2 wakati akiwa kazini. Maisha yake yamekatishwa na kile kinachoelezwa kuwa ni baada ya kupigwa na kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu wakati po l i s i wa l ipokuwa waki tawanya wa tu w a l i o k u w a k a t i k a mkutano wa hadhara wa CHADEMA huko Mufindi mkoani Iringa.

W a k a t i p o l i s i w a n a u s a m b a t i s h a mkutano huo, watu wengine kumi nao w a l i j e r u h i w a n a kukimbizwa hospitali ya Mafinga, Iringa.

Kwa kiasi kikubwa polisi wanahusishwa na kifo cha mwandishi huyo kulingana na mazingira ya kifo chenyewe, hasa ikizingatiwa kwamba kitu kinachosadikiwa kumuua ni bomu.

Kama ilivyo ada ya polisi, tukio la mauaji lilitokea baada ya polisi kuanza kusambaratisha w a t u w a l i o k u w a mkutanoni. Kabla ya kuanza usambaratishaji, r a i a w a l i k u w a wamekusanyika kwa amani.

Mara nyingi mikutano ya hadhara, hasa ya vyama vya upinzani imekua ikiingia dosari za vurugu pale tu polisi wanapoamua kuzuia

kwa nguvu mikutano hii au maandamano. Bila wao, ni nadra sana kutokea vurugu.

Kwa jinsi hali ilivyo, hatudhani kwamba raia waliokuwepo katika mkutano huo walibeba silaha za moto kama bunduki na mabomu a m b a z o k w a z o zingeweza kumdhuru Mwangosi. Silaha za ina hiyo walikuwa nazo polisi.

Wa l a h a t u d h a n i kwamba ni jiwe, mkuki, pinde, panga au kisu, kilichotumika kuondoa uhai wa Mwangosi. Maana hizi ndizo silaha ambazo raia anaweza kuwa nazo au kuzimiliki na kuzibeba bila hofu.

Tunajiuliza, Mwangosi kauliwa na bomu kutoka kwa nani kama si mmoja katika polisi miongoni m w a w a l i o k u w a wakitawanya watu?

Ni katika mantiki hii, ndio maana polisi wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya mwandishi huyo ambaye alikuwa kaz in i kuhakik isha kwamba umma unapata habari kuhusu matukio mbalimbali yaliyokuwa yakijiri katika mkutano huo wa CHADEMA.

Tukire jea nyuma, mwaka 1998 pol is i walidaiwa kuua watu wawili na kusababisha vilema kwa baadhi ya raia akiwemo Chuki Athumani, ambaye sasa ni mlemavu baada ya kupewa ulemavu kwa risasi za polisi alipokuwa mtoto mdogo kabisa.

Pamoja na po l i s i kuua tena hadharani, serikali ilipiga kimya

na zaidi iliwapongeza p o l i s i w a l i o f a n y a mauwaji yale. Waislamu wakataka iundwe tume huru ya kuchunguza mauaji katika tukio lile la Mwembechai, lakini hakuna aliyewasikiliza na kuishia kupuuzwa.

Aidha tunakumbuka pia mauaji yaliyofanywa na Polisi Zanzibar Januari 26 na 27 mwaka 2001. Hiki kilikuwa kipindi cha uongozi wa Rais M s t a a f u B e n j a m i n William Mkapa. Makumi kwa makumi ya raia wa Zanzibar waliul iwa. Kama ilivyo ada, wauaji w a l i p o n g e z w a k w a ‘kazi nzuri’ na watawala n a k u p a n d i s h w a vyeo, na hakuna kesi iliyofunguliwa dhidi ya wauaji.

Kat ika awamu ya kwanza ya Rais Jakaya Kikwete, polisi waliua wafanyabiashara ya madini kutoka Morogoro jijini Dar es Salaam na kupora fedha zao. Tume ikaundwa na Rais Kikwete kuchunguza Tukio hilo. Majibu ya tume yalionyesha kuwa kuna kesi ya kujibu kwa polisi wakiongizwa na Kamishna wao wa Upelele ambaye alikuwa Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Dar es Salaam Abdallah Zombe.

Lak in i kwa kuwa mpelelezi, mwendesha mashitaka, ndiye huyo h u y o m s h i t a k i w a , ushahidi wa uhakika h a u k u w a s i l i s h w a m a h a k a m a n i n a watuhumiwa wa mauaji wakashinda kesi. Leo w o t e w a p o n j e n a wanaendela na maisha huku marehemu wakikosa haki.

Siku za nyuma huko Arusha, matukio ya polisi kuua raia yalishawahi kuripotiwa na vyombo vya habari . Lakini kwa mazoea haya ya polisi wetu kuua bila kufikishwa mahakamani, hatudhani kwamba kuna hatua zozote za kisheria zilizochukuliwa kwa wauaji hao. Hii ni mifano kiduchu tu ya polisi

kuhusishwa na mauaji lakini wauaji wakiachwa bila kuchukuliwa hatua stahiki.

Kwa ujumla tunaweza k u s e m a k w a m b a l imekuwa n i jambo la kawaida au hulka k w a a s k a r i p o l i s i kuua na kuachwa bila kuchukuliwa hatua za kisheria hapa nchini.

Upolisi umekuwa kazi inayoweza kumkinga muuaji dhidi ya sheria. Ndio maana kuua kwao si taabu wala si jambo la kuogofya. Ni suala la kuamua tu na kuweka mazingira ya kupoteza ushahidi. Na mara nyingi wanapotuhumiwa kuua, hutoa visingizio kama vile marehemu alikuwa jambazi, askari walikuwa wakijihami, aliyeuliwa alikuwa na silaha ya moto akiwashambulia askari nk. na mwishowe kesi huishia hapo hapo polisi. Kwa staili hii ndio maana wanaendelea kuua raia pale wakijisikia kufanya hivyo na wana uhakika

wa usalama wao mbele ya sheria.

Tunaambiwa kuwa tayari Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Emmanuel Nchimbi ameshateua Tume ya uchunguzi wa mauaji ya mwandishi Daud Mwangosi.

Lakini kutokana na utamaduni wa watumishi h a w a , h a t u d h a n i k a m a w a u a j i w a mwandishi Mwangosi watachukuliwa hatua stahiki japo wapo kazini. Wasiwasi wetu ni kwamba h a t a w a k i p a t i k a n a , yanaweza kuwa kama yale ya Afande Zombe.

Ni kwa sababu hiyo, tunadhani ingekuwa vyema Tume iliyoundwa ikajaribu kuwa makini, ikazingatia ukweli wa mambo, ikajali haki na kuweka mbele masilahi ya ta i fa hi l i kul iko kuangalia mazoeya ya huko nyuma.

A m a n i y a n c h i h i i h a i t a d u m i s h w a kwa ‘kuwaficha’ au kuwafumbia macho wauwaji.

Tusipokuwa makini polisi itakuwa kichaka cha wauaji

P.O. Box 55105, Tel: 2450069, 0754 260241 Fax: 2450822 Dar es Salaam

E-mail: [email protected]

UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL

Maandalizi ya Kidato cha Kwanza 2013

Shule ya Kiislamu ya Ubungo (Ubungo Islamic High School) inatangaza PROGRAMU maalum ya maandalizi ya kujiandaa na Kidato cha Kwanza 2013 kwa wanafunzi Waislamu.Programu hii itaanza tarehe 15/09/2012 hadi tarehe 10/12/2012 Jumatatu hadi Jumamosi saa 3:00 asubuhi hadi saa 8:30 mchana.Masomo yatakayofundishwa katika programu hii ni:1. Elimu ya Dini ya Kiislamu2. English Language3. Arabic Language4. Mathematics6. Introduction to ComputerNi programu maalumu ya miezi mitatu (15/09/20212 hadi 10/12/2012)Ada ya masomo kwa programu yote ni Tshs 50,000/= inalipwa yote mwanzoni mwa programu.

Fomu za kujiunga zinapatikana Shuleni - BURE

Kwa mawasiliano zaidi: 0714 888557, 0659 204013, 0717 295107

MLETE MWANAO APATE ELIMU BORA NA MALEZI MEMA YA KIISLAMU

Wabillah TawfiiqMKUU WA SHULE

Bismillahir Rahmaanir Rahiim

Page 3: ANNUUR 1033

3 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 7 - 13, 2012Habari

Waziri Haji atolewa jasho Ikulu ZanzibarWAZIRI Ofisi ya Rais Zanzibar Mheshimiwa Mwinyi Haji Makame amejikuta akikabiliwa na wakati mgumu wakati Masheikh wa Uamsho walipompa madai mazito wakituhumu serikali kutokujali masilahi ya Zanzibar na zaidi Uislamu na Waislamu.

M a s h e i k h h a o w a Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu wakitoa msimamo wao juu ya Sensa ya watu na Makazi wamesema kuwa, wao hawapingi sensa kwa sababu wanajua umuhimu wake, lakini wanaamini kuwa muhimu kwanza ni kupata nchi na serikali.

W a k i f a f a n u a wal imwambia Wazi r i Makame kuwa, hivi sasa Zanzibar imekuwa kama nchi isiyo na ardhi na serikali isiyo na mamlaka kwani kila kitu chake kinategemea matashi na kutaka kwa serikali ya muungano.

W a k a s e m a , k i l a asiyepanga, anayesubiri kupangiwa mara zote huharibikiwa.

Ni kwa sababu hiyo wakasema kuwa, wao wanachotaka ni kuona kuwa Zanzibar inapata mamlaka yake kamili ndio ifanyike sensa.

Kwa upande mwingine Masheikh hao wakasema k u w a w a n a s h a n g a a inakuwaje viongozi wa Ser ika l i ya Zanz ibar w a n a k u w a w e p e s i kulinyenyekea Kanisa, lakini wakati huo huo wakichukua hatua za kuwadhalilisha Masheikh.

W a k i t o a m f a n o wakataja kitendo cha Rais Mheshimiwa Dr. Shein k u w a p o n g e z a P o l i s i waliowapiga mabomu na kuwadhalilisha Waislamu na Masheikh.

Na kwa upande mwingine akitoa kauli kali za kulani wa l ioda iwa kuchoma makanisa na kuwaangukia kwa kuomba radhi Wakristo ilihali hakusema chochote juu ya Misikiti iliyopigwa na kubomolewa.

K a t i k a h a l i h i y o , Masheikh wakasaema kwamba kinachoonekana ni kuwa wakati viongozi wa serikali Wakristo (Bara) wakiingia katika serikali na Ukristo wao na wakiwa karibu na kupanga mambo

Na Mwandishi Wetu na Wakr is to wenzao, Waislamu wao wanapoingia serikalini hutupa Uislamu wao na kama ni kufanya dini hufanya kama jambo la dharura.

Kufuatia makombora hayo, i l imbidi Waziri Mhesh imiwa Mwiny i k i l a m a r a k u k a t i s h a wazungumzaji kufafanua mambo aliyodhani kuwa yanapotoshwa.

Awali , katika kikao hicho kilichofanyika Agosti 24, Waziri aliwaambia Masheikh hao wa Uamsho kuwa alikuwa amewaita ili washauriane juu ya namna ya kufanikisha sensa.

Katika kile walichosema kuwa sensa hiyo haitakuwa na manufaa kwa Wazanzibari walisema kuwa, ilivyo hivi sasa kuna watu sio Wazanzibari waliowaita wa kutoka Msumbij i , lakini wana vipande vya ukaazi wakati Wazanzibari wenyewe halisi hawapewi.

Wakasema, Zanzibar h a k u n a m a m l a k a y a kudhibiti wanaoingia na wanaotoka, kwa hiyo hata ikifanyika sensa kupanga mambo kwa mujibu wa idadi ya watu itakayopatikana, inakuwa sawa na kutia maji katika pakacha badala ya ndoo.

Wa k a s e m a h u w e z i kuweka harusi ya kuingia kwa kadi wakati mahali i napofany ika hakuna m a d i r i s h a , m i l a n g o wala watu wa kudhibiti waingiaji.

Wakadai kuwa hivyo ndivyo ilivyo Zanzibar kwa sasa. Kwa hiyo ili sensa iweze kuwa na maana, basi Zanzibar yenye mamlaka na dola kamili ipatikane kwanza.

Pamoja na jitihada za Mufti wa Zanzibar ambaye naye alikuwa katika kikao hicho kujaribu kuwarai masheikh hao, lakini mpaka mwisho wa kikao msimamo wa Masheikh wa Uamsho ulibaki kuwa ule walioingia nao Ikulu.

Wakati huo huo, hali si shwari Pemba na jana Polisi walikuwa katika heka heka kuwakusanya watu katika kituo cha Polisi Wete na kuwarai kuandikishwa.

Habari zilizotufikia jana zinafahamisha kuwa watu takriban 200 waliitwa katika kituo cha Polisi kwa barua ya OCD.

H a t a w a l i p o f i k a waliambiwa kuwa ilikuwa waonane na Waziri wa

Sher ia na Mambo ya Katiba.

Hata hivyo, hakutokea Waziri huyo na badala yake walioongea ni Polisi na baadhi ya maofisa wa serikali wa Wilaya.

Katika kikao hicho, takbira zilikuwa zikivuma mara kwa mara wakati waliohudhuria wakitoa hoja za kuonyesha mantiki ya msimamo wao wa kususia sensa.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinafahamisha kuwa ilibidi OCD, SSP Juma S Khamisi, pamoja na kuwa ni Muislamu kusimama na kutaka Takbira hizo ziachwe akidai kuwa zinakera, kauli ambayo ilileta mtafaruku watu wakitaka kutoka na kususia kilao hicho.

Kwa upande mwingine, p o l i s i w a m e k u w a wak i tumia mtu tu wa bunduki kuhakikisha kuwa sensa inafanikiwa kama ilivyopangwa.

Katika tukio moja huko Pemba, Sheikh na Imam mmoja, Sheikh Omar Swaleh alijikuta akinaswa kibao na kutiwa pingu kabla ya mkewe naye kuelekezewa mtutu wa bunduki akitakiwa kutoa taarifa zilizotakiwa na karani wa sensa.

Akisimulia tukio hilo, Sheikh Swaleh amesema kuwa akiwa kazini kwake

J u m a m o s i i l i y o p i t a Septemba 1, alipigiwa simu na mtu asiyemjua akimwambia kuwa mke wake ameanguka na hali yake mbaya.

Anasema, alikimbilia nyumbani lakini alipofika alikuta kikosi cha polisi kikiongozwa na OCD wa Wete ambaye alimwambia kuwa ndiye aliyempigia simu.

B a a d a y a k u k a t a a k u h e s a b i w a k i b a b e anasema kuwa alipigwa kibao na OCD huyo na kisha kuwekwa pingu.

Akisimulia zaidi Sheikh Swaleh anasema kuwa baada ya kumtia pingu walimfuata mkewe na kumwelekezea mtu tu wa bunduki wakimtisha kuwa kama hatatoa taarifa naye watamtia pingu na kumpeleka rumande.

K a t i k a h a l i h i y o , ilibidi mkewe atoe taarifa zilizohitajika na kisha kuachiwa.

Mumewe naye aliachiwa pia baada ya kuhesabiwa k u p i t i a m a e l e z o yaliyotolewa na mkewe.

Matukio kama hayo yamee l ezwa ku tokea sehemu mbalimbali Unguja na Pemba baada ya watu wengi kukataa kuhesabiwa wakisema kuwa wanafuata maelekezo ya viongozi

wao.Ni kutokana na hali hiyo,

awali kabla ya zoezi la sensa kuanza hapo Agosti 24, Masheikh wa Uamsho waliitwa Ikulu ambapo walikutana na Waziri katika Ofisi ya Rais, Mheshimiwa Mwinyi Haji Makame.

“Uzanzibari kwanza sensa baadae; mwenye sensa hii ndiye anayetuibia. Wenzenu (Bara viongozi wa serikali Wakr i s to) wanafanya kazi na Ukristo wao, nyie Uislamu wenu mnautupa mkiingia serikalini (vipi?)”, w a n a d a i w a k u s e m a Masheikh hao wakimkabili Waziri Makame.

I l i k u w a b a a d a y a Masheikh wa Uamsho k u k a t a a t e n d a y a kuhamasisha Waislamu kushiriki sensa, Polisi walimjia Sheikh Abdallah Madawa usiku wa saa 6 w a k a m k a m a t a n a kumpeleka k i tuo cha Polisi.

Hali hiyo ilipelekea m a m i a y a Wa i s l a m u kufurika Madema kutaka kujua nini hatma ya Sheikh wao.

Haikupita muda Sheikh Abdallah akaachiwa lakini Polisi wakahamishia vipigo na vitisho kwa wananchi wa Mashamba, hasa Nungwi ambapo inadaiwa kuwa watu wengi walikuwa wamekataa kushesabiwa.

RAIS wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akiwa na Makamu kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad.

Page 4: ANNUUR 1033

4 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 7 - 13, 2012Habari

Inawatangazia Mahujaji wake wote kuwa Safari ya kuondoka ni tarehe 09/ 10/2012 na 11/10/2012Kurudi ni tarehe 03/ 11/2012 na 05/11/2012Mahujaji wote wamalize kuchanja haraka iwezekanavyoPaspoti zipelekwe ofisini kwa ajili ya Viza na SafariSemina Dar es salaam siku ya Jumapili tarehe 30/ 09/ 2012 Madrasatul Jabalhira Magomeni karibu na ofisiniZanzibar ni Suni Madrasa Mkunazini tarehe 08/09/2012.Wamalize malipo na taratibu zote za safari.Nafasi bado zipo bei zetu ni USD 3,375 tu kwa huduma zote pamoja na mahema maalumu ( VIP). Kwa mawasiliano zaidi piga simu.FOMU ZINAPA TIKANA A. Ofisi ya Ahlul Daawa Dar es salaam Mtaa wa Dosi na Mkadini Nyumba Namba 26 Mkabala na Showroom ya Magari Tel- 0713 730444 au 0773 804 101 AU 0785 930 444 AU 0773 930444.B. Ofisi ya Ahlul Daawa Zanzibar Raha leo Tel- 0777 484 982 0777 413987C. Abubakari Maulana wa Markaz wa Kiwalani Dar es salaam Tel- 0784 453 838D. Abdallah Salehe Mazrui (Hoko) Dar es Salaam Tel-0715724444E. Salim Is-Haq Dar es Salaam Tel-0754 286010 au 0774 786101F. Dukani kwa Abdalla Hafidh Mazrui Wete-Pemba Tel-0777482665G. Dukani kwa Mohammed Hafidh Mazrui Mkoani Pemba Tel-0777456911H. Sheikh Daud Hamis Sheha Tel-0777 679692I. Maalim Seif Humoud Hamed Kijichi Zanzibar Tel-0777 417736

Wahi kulipiaUsisahau kikundi cha Ahlul Daawa ni cha bei nafuu kuliko vingine na huduma bora kuliko wengi

Wabillah Tawfiq

AHLUDAAWA HAJJ AND TRAVEL AGENCY

Sensa ‘yageuka’ Jihad SumbawangaW A K A T I m u d a ulioongezwa wa sensa y a w a t u n a m a k a z i ukimalizika, matuki yasiyo ya kawaida yameendelea kuripotiwa yakitawaliwa na msuguano kati ya vyombo vya dola na Waislamu waliogoma kuhesabiwa.

Kutoka Sumbawanga inaripotiwa kuwa mtu mmoja amesilimu nje ya kituo cha Polisi Sumbawanga mjini baada ya kushuhudia Waislamu wakiswali na kuleta Dua ndefu.

Dua hiyo ilifuatia Swala ya Alasiri iliyoswaliwa nje ya kituo hicho cha Polisi wakati mamia ya Waislamu wakisubiri kujua hatma ya Wais l amu wenzao waliokuwa wamefikishwa kituoni hapo baada ya kukamatwa kutoka vijiji vya Muze, Laela na Kirando, Sumbawanga Vijijini.

Awali kabla ya tukio hilo ilikuwa imetolewa taarifa katika swala ya Ijumaa iliyopita kuwa kulikuwa na Waislamu waliokamatwa katika maeneo mbalimbali ya Sumbawanga vijijini.

Taarifa hiyo ilitolewa katika misikiti ya Qiblatain, Salaam, Rahmaan, Rawdha, Jadidah, Tawba, Taq’wa na Ibaadhi, ambapo waumini walitakiwa kuwa tayari tayari wakisikia Adhana isiyo na ‘haiya ala swalaa’ watoke

k w a w i n g i k w e n d a kuwanusuru Waislamu w e n z a o w a l i o k u w a wamekamatwa tangu jana yake.

Wa k a t i Wa i s l a m u wakitawanyika, Maimamu walikaa Shura na ndio katika kikao chao zikaja habari kuwa Waislamu w a l i o k a m a t w a t a y a r i wamefikishwa kituoni.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya mji wa Sumbawanga i l is ikika adhana tofauti na ya kawaida ya siku zote huku Muadhini akisema Hayyaalal jihad…Hayyaalal Jihaad.

Katika muda usiozidi dak ika 15 , Wais l amu w a k a w a w a m e f u r i k a katika Msikiti wa Qiblatain ambao ndio Msikiti Mkuu wa Ijumaa huku wengine wakikusanyika na Masjid Taq’wa na kwa pamoja

Na Waandishi Wetu, Mwanza, Rukwa,

Tanga

wakaelekea kituo cha polisi. Wakiwa katika barabara kuu iendayo mbeya, Waislamu hawa wali tembea kwa nidhamu wakiwa wawili wawili.

Ilikuwa baada ya kuona umati huo wa Waislamu, harakati za kuwapatia dhamana waliokamatwa ziliharakishwa.

Hata hivyo, muda wa swala ulifika kabla ya zoezi kukamilika ndio ikapigwa Adhana Waislamu wakasimama safu kuswali na kisha kuleta Dua iliyowaliza Waislamu wengi.

Kitendo hicho kiliwaacha n a m s h a n g a o w a t u waliokuwepo eneo hilo ambapo mtu mmoja alipoona Waislamu wakiswali nje ya kituo cha polisi tena katika vumbi na mchanga aliuliza kuna nini na kufahamishwa kuwa hawa Wais lamu wamewafua ta wenzao waliokamatwa na polisi kwa ajili ya kugoma kuhesabiwa sensa, sasa muda wa sala yao umefika wanaswali.

Mtu yule baadae alisilimu na kufuatana na Waislamu wenzake kwa shangwe baada ya kuachiwa Waislamu kurejea msikitini.

Tukio hilo lilifanya mji kuzizima kwa shangwe, maandamano na kivumo cha “Hakuna Sensa!” “Hakuna Sensa!!!!”, hususan katika barabara ya Mbeya-Mpanda na maeneo ya soko kuu la Manispaa.

W a l i o k u w a wamekamatwa na kuwa sababu ya tukio hili la kihistoria Sumbawanga ni Abdalla Masoud alokamatwa Laela, Zuena Juma na Hassan Said wa Kirando, na Omary Ally, Ashura Kasonso, Haji Kiyoso, Amru Sinah na Hassan Mohamed, wote wakazi wa Muze, Sumbawanga Vijijini.

Mwanza

Wa k a t i h u o h u o , habari kutoka Mwanza zinafahamisha kuwa zoezi la sensa limefanikiwa kwa kiwango kikubwa baada ya muda kuongezwa na serikali kupiga propaganda kubwa.

Hata hivyo inakisiwa kuwa bado wamebaki Waislamu, si haba ambao hawakuhesabiwa mpaka

sasa.Katika kuonyesha jinsi

hali ilivyokuwa ngumu, mapema wiki hii ilibidi M k u u w a Wi l a y a y a Nyamagana akiandamana na baadhi ya Masheikh kwenda katika Mahabusu y a B u t i m b a k w e n d a kuwashawishi Waislamu waliokuwa wakishikiliwa wakubali kuhesabiwa.

Kabla ya hapo Waislamu walikuwa wamepata habari kuwa zoezi hilo lingefanyika na hivyo wakakusanyika gerezani Butimba kuwasubiri wapate kupambana nao.

Hata hivyo, baada ya Mkuu wa Wilaya kupata taarifa hakwenda muda aliokuwa ametarajiwa, badala yake wakavizia baada ya Waislamu kuondoka wakafika Butimba saa tisa Alasiri.

Masheikh wanaotajwa kuandamana na DC huyo ni Sheikh Hassan Kabeke na Sheikh Amani Mahuba ambaye ni Imam Masjid N-nuur uliopo mtaa wa

Uhuru.Taarifa zinafahamisha

kuwa baada ya Waislamu kupata taarifa kwamba Masheikh hao walishiriki katika msafara wa DC kwenda kuhamasisha sensa kwa mahabusu, hali yao si shwari mitaani.

K w a u p a n d e w a Sheikh Mahuba, waumini walipomwendea na kumkosa walimwendea anayedaiwa kuwa ‘mfadhili’ (jina tunalo) wake ambaye walimwambia amwonye Sheikh huyo na kumwachia ujumbe mzito wa maneno na maandishi.

Uchunguzi wa kina wa mwandishi wa habari hizi, unaonyesha kuwa kabla ya kuongezwa siku za sensa, idadi kubwa ya Waislamu walikuwa hawajahesabiwa.

Hata hivyo kufuatia vitisho na propaganda iliyopigwa baada ya kuongezwa siku, idadi kubwa ya waliogoma w a m e h e s a b i w a k w a vitisho.

H a t a h i v y o , b a d o inaaminika kuwa kuna wengi hawajahesabiwa.

Wakati huo huo, hali si shwari Tanga hasa katika Wilaya ya Mkinga na Tanga mjini.

Habar i z i l izotuf ik ia jana zinafahamisha kuwa takriban watu wote katika kijiji cha Kichalikani wilaya ya Mkinga wamegoma kuhesabiwa hali iliyopelekea timu ya Mkuu wa Mkoa na viongozi wa wilaya kufunga safari kuonana na wazee wa kijiji hicho.

Baada ya wazee na vijana kusimama katika msimamo wao, kesho yake ikaja gari ya polisi na kukamata baadhi ya vijana na wazee.

Hata hivyo gari hiyo ilipofika katika “wangwa” ilikwama.

W a t u h u m i w a w a k a s h u s h w a , g a r i l i k a w a s h w a n a kukwamuka.

Safari ya watuhumiwa kupelekwa polisi Tanga mjini ikaishia hapo.

Kwa upande mwingine, b a d o k a m a t a k a m a t a inaendelea Tanga mjini ambapo miongoni mwa waliowekwa rumande ni mama, Mwanaidi Hariri na mtoto wake wa mwaka miwili.

Aliwekwa ndani pia Shukurani Issa na mtoto wa miezi 6 pamoja na Saida Ali wote wa Makorora.

Page 5: ANNUUR 1033

5 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 7 - 13, 2012Habari za Kimataifa

CAIRO WAKAZI wa eneo la Bo-Kaap wameandamana kupinga kutolewa leseni ya kuuzwa pombe katika mgahawa na bar jirani na msikiti wa Nurul Islam.

Waislamu wa jiji la Cape Town wameandamana na kudai kuwa kutolewa kwa leseni ya kuuza pombe jirani kabisa na msikiti wao ni kudharau haki za Waislamu za kuabudu.

“Mamlaka zimeruhusu bar ya kwanza hapa Bo-Kaap kuwa jirani na msikiti,” alieleza Mwenyekiti wa Bo-Kaap Civic Association, Osman Shabodien alipoieleza Cape Times wiki iliyopita.

“Tunataka kujua kwa nini hatukujulishwa.”

Leseni ya kuuza pombe imetolewa kwa muuza bar ikiwa ni mita moja kutoka msikiti wa Nurul Islam, moja ya misikiti ya zamani zaidi uliojengwa mwaka 1834 katika kitongoji cha Bo-Kaap jijini Cape Town.

Wakazi wanaozunguka msikiti huo wameonyesha kuchukizwa na kitendo cha kutolewa leseni hiyo ya kuuzwa ulevi mahali ulipo msikiti wao, ambapo wakazi 100 wameandamana nje ya mgahawa na Bar ya Abantu, kupinga kuuzwa pombe katika eneo hilo.

“ Tu m e z u n g u m z a n a mmiliki wa bara bw. Sam, ambaye alisema madhali amepewa l e sen i , ba s i ataendelea na biashara yake ya pombe, Tumekasirika sana ,” a l i sema Osman Shabodien.

Waislamu nchini Afrika ya Kusini ni asilimia 1.5 ya idadi ya watu wote nchini humo, ambapo ni milioni 49 kwa mujibu wa takwimu za CIA fact book.

Uislamu umekataza aina zote za vileo. Waislamu wanazuiwa kunywa na kuuza pombe.

Sheria ya Uislamu katika vileo ni kwamba kinyeaji cha aina yeyote kinachosababisha watu kulewa wanapokunywa k i n a k a t a z w a , i w e n i kwa kiwango kidogo au kikubwa.

Ikiwa umbali wa mita moja kutoka ulipo msikiti huo mkongwe, Waislamu wamesema wamekuwa wakilalamikia bar hiyo mara

Afrika Kusini waandamana kupinga Bar kufunguliwa jirani na Msikitini

kwa mara kutokana na kelele na harufu mbaya ya vileo eneo la msikiti.

“Hali sasa imekidhiri, usafi na mazingira ya msikiti hakuna anayejali” alisema Imamu wa Msikiti huo Serag Johaar.

Mwenyekiti wa Bo-Kaap Civic Association, Shabodien, alisema kuwa maandamano ya yaliyotokea hayatakuwa ya mwisho dhidi ya uwepo wa bar hiyo jirani na msikiti huo.

Alisema maandamano yataendelea hadi katika baraza la Jimbo.

Ha ta h ivyo Maof i sa wa ser ikal i wameahidi kushughulikia suala hilo a m b a p o c o u n c i l o r w a Democratic Alliance, Dave Bryant, alisema kuwa leseni hiyo ilitolewa wakati yeye akiwa bado hajapata wadhifa alio nao.

Alikubalina na Waislamu wanaopinga bar hiyo kuwa jirani na msikiti

“Hi l i tu ta l i fua t i l i a , ” aliahidi.

Sheria za Afrika Kusini zinazuia kutoa leseni ya vileo katika maeneo ya shule au sehemu za ibada.

CAIROKAMPUNI ya Uturuki ya Kuveyt Turk Investment Fund inapanga kufungua benki ya kwanza ya Kiislamu nchini Ujerumani mwezi huu na kuleta matumaini ya kuziba madhara mabaya yanayoendelea kufuatia mgogoro wa kuchumi Ulaya hivyo kutoa nafasi ya kupata nafuu kutokana na mafanikio ya mfumo wa kibenki wa Kiislamu.

“Wazo la Islamic bank ni kuwa linafuata misingi na kanuni za uwekezaji wa Kiislamu,” Zaid el-Mogaddedi, mwasisi na Mkurugenzi wa Institute for Islamic Banking and Finance (IFIBAF) ya Frankfurt, alilieleza Deutsche Welle mwishoni mwa wiki.

Kampuni ya Kuveyt Turk yenye maskani yake jijini Istanbul itafungua benki ya kwanza ya Kiislamu nchini Ujerumani mwezi huu.

Benki hiyo imetambulishwa huku nchi nyingi za Ulaya zikitumaini kuridhia taasis za kifedha ambazo zinatoa huduma za amana zinazothibit ika

Benki za Kiislamu zapiga hodi Ujerumanipekee (tangible assets) kuliko kudhibi dhamana zisizoonekana ( s p e c u l a t i v e f i n a n c i a l management) jambo ambalo l imesababisha msukosuko unaoendelea katika taasisi za fedha za Kimagharibi.

“Unaweza kuliona hilo katika mfumo wa kifedha wa Kiislamu ambao ufanyaji kazi wake unaviza madhara ya viwango vya riba,” alisema Martin Schulte, mtaalam wa Islamic Banking kutoka Association of Foreign Banks Ujerumani.

Uislamu unazuia Waislamu kujihusisha na riba, kupokea au kutoa riba katika mikopo.

Benki za Kiislamu na taasisi za fedha haziwezi kutoa fedha kwa ajili ya biashara za pombe, kamari, biashara za ngono, tumbaku, silaha au nguruwe

Biashara za kibenki kwa mujibu wa Shari`ah zinahusiana na kuweka mipango ya pamoja kati ya mteja na benki, manunuzi ya pamoja na mauzo ya pamoja au ushirika.

Wawekezaji wana haki ya kujua fedha zao zimetumika vipi huku sekta husika ikisimamiwa n a b o d i y a w a s i m a m i z i

wanaokubalika pamoja mamlaka za usimamizi za Taifa.

M f u m o h u u a m b a o umeanzishwa miaka mingi iliyopita katika nchi za Ulaya, wataalam wana matumaini kwamba utaratibu huu mpya wa kibenki wa Ki is lamu nchini Ujerumani, utakuwa na mafanikio zaidi kuliko yale yaliyopatikana katika nchi za Uingereza na Ufaransa.

“Nukta muhimu itakuwa kama Benki za Kiislamu zitatoa huduma nzuri na inayovutia,” amesema El-Mogaddedi kutoka Institute for Islamic Banking and Finance.

Ikiwa imekaidi kwa miaka mingi kujaribu mfumo huu unaokua kwa kasi, Taasisi ya mfumo wa kiuwekezaji wa Kiislamu il iundwa nchini Ujerumani Mei 2012 na kampuni moja kutoka Malaysia ya CIMB Principal. Fedha ziliidhinishwa na German Financial Supervisory Authority (BaFin).

Bidhaa za kifedha kwa mfumo was Kiislamu zimekuwa haraka zaidi kwa mara ya kwanza baada ya mashambulio ya 9/11 nchini Marekani.

WAISLAMU wakiandamana Afrika Kusini kupinga kufunguliwa Baa jirani na Msikiti.

NAIROBIKAMISHENI ya Uchaguzi ya Somalia imetangaza kuwa anayetaka kugombea Urais wa nchi hiyo na kuunda serikali

Rais Somalia sharti awe Muislamukamili ya nchi hiyo sharti awe Muislamu.

M a s h a r t i m e n g i n e n i mgombea kuwa na umri usiopungua miaka 40 na

kuungwa mkono na wabunge wasiopungua 20.

Rais wa sasa wa Somalia Sheikh Sharif Ahmad na spika wa zamani wa bunge Muhamamd Ali Gaas ni miongoni mwa watu wanaowania kiti cha Rais.

Uchaguzi wa rais wa Somalia umepangwa kufanyika tarehe 10 mwezi huu wa Septemba. Uchaguzi huo utahitimisha kipindi cha miaka 8 ya serikali ya mpito.

Ser ikal i ya kwanza ya mpito ilichukuwa madaraka nchini Somalia mwaka 2004 na haikuweza kutatua matatizo na mapigano ya ndani kutokana na uongozi duni na usiofaa.

Katika kipindi chote cha miaka 8 iliyopita Somalia imekuwa katika ghasia na machafuko ya mara kwa mara.

Wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa nchi za Magharibi hususan Marekani hazikuwasaidia wananchi wa Somalia katika kipindi chote cha mapigano ya ndani licha ya kutoa ahadi chungu nzima zaidi ya kuhusika kwa njia moja au nyingine katika kuchochea machafuko hayo.

Kwa upande mwingine, Jumuiya ya nchi za Kiarabu imetangaza kuunga mkono serikali ya Somalia kwa ajili ya kuvuka kipindi cha mpito.

Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo Nabiil al Arabi, amewataka maafisa wa serikali ya Somalia kuchukua hatua zaidi za kutimiza mwenendo wa kipindi cha mpito nchini humo.

Page 6: ANNUUR 1033

6 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 7 - 13, 2012Habari

MOTO wa kugombea Kiti cha Uwakilishi katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Bububu, Wilaya ya Magharibi Unguja, umeanza kufukuta, huku Vyama vikitunisha na kurusha ndoana za sera usoni kwa umma.

Ni kufuatia kuzinduliwa rasmi kwa Kampeni za Uchaguzi wa kuligombea Jimbo hilo, lililowachwa wazi tokea kifo cha aliyekuwa Mjumbe wake wa Baraza la Wawakilishi, Marehemu Salum Mtondoo, aliyefariki dunia mwanzoni mwa mwaka huu.

Tume ya Uchaguz i ya Zanzibar, imeitangaza Tarehe 16 Agosti, 2012, kuwa Siku ya Uchaguzi, ambapo Wananchi wa Jimbo la Bububu, watapiga kura kuchagua Mjumbe wao Mpya wa Baraza la Wawakilishi.

Wakati vyama vikianza kwa kasi na mbwembwe za namna yake, tayari vionjo vya ladha ya ushindani wa kisiasa vimeshaanza kubainika, huku Umma wa wananchi wa Bububu, na Wazanzibari kwa ujumla nao wakiperuzi kwa macho makini, nani mwenye ‘gimba’ la kutisha la kutatua matatizo na kukabiliana kikamilifu na changamoto ndani ya Jimbo hilo.

“Hapa sasa tutajua mbovu na mbichi maana Bububu yetu hasa haijapata bahati ya Kiongozi angalau wa kutunawisha uso kwa hii adha tuliyonayo ya maji ba njia (barabara) yetu”, alisema Mwananchi wa umri wa makamu hivi aliyejitambulisha

Waislamu kuandamana Dar WAISLAMU kutoka misikiti mbalimbali jijini Dar es Salaam leo wanatarajiwa k u j i t o k e z a b a r a b a r a n i kuandamana hadi Wizara ya Mambo ya Ndani kupinga vitendo vilivyokithiri hivi sasa vinavyofanywa na vyombo vya dola na watendaji vya kukamatwa, kudhalilishwa na kuwekwa ndani Waislamu wanaokataa kuhesabiwa katika zoezi la sensa ya watu na makazi inayofikia tamati leo.

Taarifa kutoka Jumuia na Taasisi za Kiislamu nchini zimeeleza kuwa tayari uongozi wa Jumuia umeshapeleka barua Wizara ya Mambo ya Ndani kumjulisha kuhusu kuyapokea maandamano hayo na ujumbe utakaotolewa na Waislamu.

Na Shaban Rajab.

Aidha jeshi la polisi tayari limeshaarifiwa kuhusu kuwepo kwa maandamano hayo.

Akizungumzana An-nuur jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Jumuia na Taasisi za Kiislamu Sheikh Ponda Issa Ponda, amesema uamuzi wa Waislamu kuandamana umefikiwa kufuatia tabia ya kukamatwa na kuwekwa ndani Waislamu katika maeneo mbalimbali ya nchi wanaokataa kuhesabiwa, huku ikifahamika wazi kwamba suala la mtu kuhesabiwa ni la shuruti bali hiari.

Imeelezwa kwamba uamuzi wa Waislamu kuandamana kupinga unyanyasaji huo unaofanywa na baadhi ya watendaji wa serikali na vyombo vya dola

dhidi ya Waislamu, umefikiwa baada ya kikao cha viongozi na Maimamu wa Jumuia hiyo kilichofanyika Ofisi za Jumuia hiyo Jumapili iliyopita, baada ya uongozi kupokea taarifa nyingi za Waislamu kukamatwa na kuwekwa ndani kwa kukataa sensa.

“Hivi tunavyozungumza, tayari kuna taarifa kwamba b a a d h i y a W a i s l a m u wamekamatwa leo (Alhamis) na kuwekwa ndani huko Kilwa Kivinje. Hata Mbunge wa Kilwa Kusini Bw. Bundala, ambaye alifika eneo hilo na kuhoji sababu za kuwekwa watu wake ndani na kutaka kuwepo suluhu, yeye pamoja na Sheikh Salim wa Kilwa tumearifiwa kwamba

wamekamtwa”. Alifahamisha Sheikh Ponda.

Amesema kuwa kabla ya kukamatwa viongozi hao, awali walikamatwa Waislamu wal iogoma kuandikishwa akiwemo mke wa Sheikh wa Kilwa Kivinje Ahmad Juma Slim aitwaye Kulthumu Abrahaman. Kufuatia kukamatwa kwa mkewe, Sheikh Slim ndipo alipokwenda kituo cha polisi kumwekea dhamana mkewe naye akaswekwa ndani.

B a a d a e t a a r i f a z a kamatakamata zikamfikia Mbunge wa Kilwa Kusini Bw. Suleiman Bungara, ambaye alikwenda kituoni kutafuta suluhu na kuwawekea dhamana waliokamatwa akiwemo Sheikh

Slim. Naye alipofika na kujaribu kuwatetea raia wa eneo lake, akaambiwa kuwa anaizuia polisi kufanya kazi yake na kuchochea fujo, naye akakamatwa. Wakati tunakwenda mitamboni, taarifa zinaeleza kuwa waliokamatwa wamepelekwa mahakamani Kilwa Masoko.

Wakati taarifa za Waislamu kuandamana kuelekea Wizarani zikiwa zimeshatua polisi na Wizara ya Mambo ya Ndani, taarifa nyingine zimeeleza kwamba viongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu wameitwa na watendaji wa Wizara hiyo kwa ajili ya mazungumzo. Imeelezwa kuwa katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ofisi za Polisi Kanda maalum Dar es Salaam, Wizara na Polisi walishauri kuwepo mjadala kati yao na viongozi wa Jumuia juu ya kadhia ya kamatakamata ya sensa inayodaiwa kufanywa na askari wa jeshi hilo dhidi ya Waislamu. Hata hivyo viongoizi hao walisema pamoja na kutakiwa yawepo majadiliano hayo, bado wanawajibika kuandamana kufikisha ujumbe kwa kuwa hadi jana bado Masheikh na Waislamu wameendela kukamatwa na kuswekwa ndani.

Hivyo Uongozi wa Jumuia umefahamisha kwamba licha ya kufanyika mazungumzo kati ya pande hizo,bado maandamano ya Waislamu leo yamebaki palepale.

Naye Sheikh Kundecha a l i d h i b i t i s h a k u w e p o maandamano hayo pamoja na kuwepo majadiliano na uongozi wa Wizara na polisi.

CUF yatunisha “gimba la gangari” Zanzibar Ni Vita ya Kampeni Jimbo la Bububu Hoja ya Muungano yaiteka Unguja

Na Waandishi wetu, Zanzibar

kuwa Mpenda Maendeleo ya Jimbo, ambaye pia aliahidi kukodolea macho kikamilifu Mikutano yote ya kampeni ili afanye maamuzi sahihi.

Jumapili ilishuhudia Vyama vya CCM na CUF vikijitupa Uwanjani kuzindua kampeni zao, ambapo Chama cha Wananchi (Civic United Front),walikuwapo katika Kiwanja cha Skuli ya Bububu, Chama cha Mapinduzi kikielekea Mtaa wa Kijichi.

Chama cha CUF, kikiongozwa na Mgeni Rasmi wa Mkutano huo, Makamo Mwenyekiti wake, Bw. Machano Khamis Al i , k i l i j inad i mbe le ya umati mkubwa wa wananchi waliofurika hapo, kwa Sera ya Haja ya Kupigania na Kurejesha Dola Huru ya Zanzibar.

“Nakwambien i hakuna Chama chochote kinachoweza kuonyesha jeuri ya kutanua kifua kikadai maslahi ya Zanzibar ndani ya Muungano isipokuwa ni Chama chenu Chama cha Wananci CUF”, alisema Bw. Machano.

Huku akishangiliwa kwa shangwe kubwa Kiongozi huyo hakuacha kugeuza uso upande wa wapinzani wao akisema, “kwanza hawa wenzetu hakuna anayethubutu kusema hata ‘nyoko’ na akiinua mdomo kudai maslahi ya Zanzibar anakaripiwa arudishe kadi…hawa hawana ubavu..ipeni kura CUF muone”.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Dokta Mohamed Gharib Bilal, alisikika akimnadi Mgombea wa Chama chake ‘Bhaa’ Ibrahim Makungu, akisema hicho nacho ni Chama pekee cha kuyalinda Mapinduzi

ya Zanzibar ya mwaka 1964. Chama cha CUF kimemteua

Bw. Issa Khamis Issa kusima katika Uchaguzi huo Mdogo wa Jimbo la Bububu, kuwa Mgombea wake.

Mbali ya CCM na CUF, vyama vingine vilivyoweka Wagombea katika uchaguzi huo ni pamoja na TADEA, ADC, na NCCR-Mageuzi, ambapo vyama vingine kikiwamo CHADEMA, walitangaza kususuia Uchaguzi huo.

Aidha, CUF wamewaomba w a n a n c h i w a J i m b o l a Bububu kumchagua Mgombea Mwakilishi kutoka Chama hicho ili aongeze idadi ya kushughulikia kero za Muungano ili kupata Muungano ulio imara Kati ya Tanganyika na Zanzibar.

Hayo yalielezwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho kwa upande wa Zanzibar Ismail Jussa Ladhu wakati wa ufunguzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa kiti cha baraza wakilishi ulifanyika katika viwanja vya Skuli ya Bububu.

Ladhu alisema ni vyema wananchi wa Bububu kumchagua Issa Khamis Issa kwani yeye ndie pekee mwenye nia ya kukubali mabadiliko ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

“Zanzibar ina matatizo mengi lakini kama mutatuongezea Issa basi mutafanya kazi yetu kuwa rahisi sana ya kuipatia maendeleo yaliyo boraq katika watu wa visiwa hivi” alisema Ladhu.

Ismail Jussa Ladhu yeye na wenzake ndio wanaongoza katika Baraza la Wawakilishi katika kupigania haki za Zanzibar ndani ya Jamuhuri ya Muungano

wa Tanzania . Ladhu alifahamisha, hivi

sasa Tanzania imo katika hatua ya kukusanya na kuratibu maoni kwa ajili ya Katiba mpya na kusema ni vyema kwa Wazanzibari kutoa maoni ambayo yataleta Zanzibar kuwa na mamlaka yake na Tanganyika pia, halafu uandaliwe Muungano wa Mkataba (shirikisho).

“Sisi hatutomnyan’ganya mtu kadi kwamba hakufuata sera za chama lakini wananchi wa Zanzibar ni vyema kutoa maoni ambayo yataleta Muungano wa mkataba baina ya Tanganyika na Zanzibar.

Akimkaribisha Mgombea, Mkurugenz i wa Haki za binaadamu, Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa CUF, Bw. Salim Bimani, aliwambia umati huo uliofurika katika viwanja vya Bububu Skuli kwamba watawaunga mkono wale wote ambao wanapigania uhuru wa Zanzibar.

“Tunaelewa ni wengi sasa walioguswa maslahi ya Zanzibar na wenye uchungu na hivyo hakika yetu tutawaunga mkono wale wote ambao wanaitakia mema Zanzibar kwa kuwa na mamlaka yake” alisema Machano.

Aliwaambia wananchi hao kuwa Zanzibar imo katika vita vikubwa vya kutafuta uhuru kami l i kwan i Muungano umekuwa na dhulma kubwa dhidi ya Zanzibar lakini kupitia Tume ya Kuratibu Maoni Juu ya Marekebisho ya Katiba mpya ndio njia pekee ya kupata haki hizo.

M k u t a n o h u o a m b a o ulihudhuriwa na Mawaziri wote wa SMZ kutoka Chama cha Wananchi, CUF ulikuwa kivutio kikubwa kwa umma uliofurika ambapo ulipambwa na Matarumbeta, Rusha roho, na ngoma za jadi.

ZAYEM kuhuisha utamaduni wa Mzanzibari Na Haji Mtumwa, Zanzibar

JUMUIYA ya Vijana, Elimu na Maadili Zanzibar (ZAYEM) imesema inakusukusudia kufanya kila aina ya jitihada ili kuhakikisha utamaduni wa Zanzibar unaimarika zaidi haraka iwezekanavyo.

Hali ambayo kwa kiasi kikubwa itaweza kuifanya Zanzibar kudumu katika sifa yake ya amani na upendo kwa wageni na wenyeji, ambayo inajivunia kwa kipindi kirefu.

Kauli hiyo imetolewa na Amiri wa Jumuiya hiyo Masoud Saleh Issa wakati akizungumza na gazeti hili mara baada ya kukamilika kwa kikao cha kamati tendaji cha Jumuiya hiyo kilichofanyika huko Afisini kwake Magomeni Mkoa wa Mjini Unguja.

A l i s e m a k u w a k a t i k a makusudio hayo jumuiya yao imejipanga zaidi kutoa elimu katika Shule mbali mbali za Unguja na Pemba zikiwamo za Mjini na vijijini.

Amiri huyo alifahamisha kuwa shule hizo zitakuwa zile za Serikali na binafsi hatua ambayo wanategemea kupata asilimia

Inaendelea Uk. 7

Page 7: ANNUUR 1033

7 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 7 - 13, 2012Makala

Jumuiya ya Wataalamu wa Kiislam Tanzania (TAMPRO) kupitia Kituo chake cha mafunzo na Ajira inawatangazia Semina ya Mafunzo ya Ufugaji Kuku wa Kienyeji na Ujasirimali kwa kutumia wataalamu wenye uzoefu wanaoshughulikia masuala hayo kwa muda mrefu. Semina itakuwa kama ifuatavyo:-

Walengwa: Wafugaji, wanaotaka kuanza kufuga, wajasiriamali wadogo wadogo na watakaopenda .

Siku: Kuanzia Jumamosi, JumapiIi na jumatatu terehe 15 -17 Septemba 2012

Muda: Saa 2:00 asubuhi - 10:00 jioni

Mahala: Ofisi Kuu ya T AMPRO Magomeni Usalama, Dar es Salaam

Mada: Njia za ufugaji wa kuku, Uchaguzi wa kuku kwa ajili ya kufuga, Kuandaa chakula bora, magojwa ya kuku na tiba yake, Utunzaji wa vifaranga na mayai nk. Vile vile mafunzo ya kutafuta soko la bidhaa zinazotokana na kuku, kutunza mahesabu na kumbukumbu za fedha pamoja jinsi ya kukuza mtaji yatatolewa.

Kujisajili: Shilingi 50,000/= kwa mtu mmoja. (Kwa ajili ya cheti cha ushiriki, Kitabu cha muongozo,na chakula kwa siku zote tatu)

Muhimu: Washiriki watapatiwa vyeti na kitabu cha muongozo wa ufugaji kuku kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili ili kukidhi haja.

Kujisajili: IIi kujisajili piga 0714 151 532, 0767 151 532,0716 574 266 au fika TAMPRO Makao Makuu, Magomeni Usalama, jirani na Halmshauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Wahi kuijiandikisha kwani nafasi ni chache

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia 0714 151 532,0767 151 532,0716 574 266 au info(@)tampro.org

MRATIBU MAFUNZOTAMPRO MAKAO MAKUU

SEMINA YA UFUGAJI BORA WA KUKU WA KIENYEJI

KITUO CHA MAFUNZO NA AJIRA CHA TAMPRO

SHUKRANI zote anastahiki Mwenyezi Mungu, Mola na viumbe wote mwenye k u r e h e m u m r e h e m e v u ambaye ameumba watu kutokana na nafsi moja na amewaumba kutokana na mwanamune na mwanamke na akawafanyamataifa na makabila ili mupate kujuana.

Pia nashuhudia kuwa hapana apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake na ninashuhudia p ia mtume Muhamadi n i mjumbe wake na ni mtumwa wake ambaye amesema, ‘nyote nyinyi mnaotokana na Adamu,

Muongozo wa Uislam ni kutembeleana na kuhurumiana

Na Shekh Mostapha Rashad

na Adamu anatokana na udongo mbora wenu ni yule amchao Mwenyezi Mungu sana, hakuna mwarabu wala asiye mwarabu utukufu isipokuwa uchamungu tuu kwa ahakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi na anahabari Surat – Hujurat aya 13

Kwa hakika uislam umeweka msimamo na mwongozo kwa ajili ya kuungwa watu wote

Kati ya watu wote ; huko ndiko kuunga undugu.

Baina ya muslimina wao kwa wao ni kuunga udugu kwa kutembeleana kwa ndugu zako

Kati ya mke na mume kwa kiasi cha ukubwa kwa mpangilio wa kifamilia, ni uungaji wa ukoo maalum.

Hebu tuanze na mawasiliano ya watu wote, Mwenyezi Mungu ametupangia mahusiano ya watu wote kwa binadamu ni jengo

la Mwenyezi Mungu ambalo amelijenga kwa nguvu zake na akalipulizia roho na akamuweka duniani na akamuumba na kumtukuza na kumuweka sawa na wakamsujudia malaika wake, na akaweka mahusiano ya watu wote. Ni wajibu kuungana kati ya Muislamu na kafiri kwani wote wanatokana na Adamu. Adamu ameumbwa kw audongo na kwa hakika mchamungu wenu kwa Mwenyezi Mungu ni yule mwenye kumcha sana Mwenyezi Mungu. Amesema mwenyezi Mungu mtukufu, ‘Enyi watu acheni watu, mcheni Mola wenu ambaye ndiye aliyekuumbeni kutokana na nafsi moja na akamuambia kutoka humo mke wake.

Na akasambaza kutokana na wao wanaume wengi na wanawake. Mcheni Mwenyezi Mungu ambaye atakuulizeni juu ya kuunga koo kwani Mwenyezi Mungu kwenu ni mwenye kuwasubiri. Na yeyote mwenye kumfanyia uadui kwa kumuua binadamu mwenzie au kumtukana huyo atakuwa ni sawa na aliyewafanyia uadui viumbe wote. Amesema Mtume

(S.A.W), ‘Binadamu ni jengo la Mwenyezi Mungu mwenye kulaniwa, yule mwenye kuvunja jengo la Mwenyezi Mungu. Amesema Mwenyezi Mungu katika Surat maida (32) yeyote mwenye kuua nafsi bila ya nafsi au uharibifu duniani.

Ni kama a l iyeua watu wote ameziokoa nafsi za watu wote na akafanya mapendi na huruma kwa wale wasio waislam pale aliposema Mwenyezi Mungu mtukufu hakukatazeni Mwenyezi Mungu juu ya wale wasiokupigeni vita katika dini na wala hawakutoeni katika miji yenu kuwafanyia wema na uadilifu kwao kwa hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wafanyao usawa (Uadilifu).

Na ameamrisha kuishi kwa ujirani mwema kwa waislam na wasio waislam pale aliposema Mwenyezi Mungu mtukufu ( Na muabuduni Mwenyezi Mungu na wala msimshirikishe na kitu chochote na wazazi wawili muwafanyie wema na majirani wa dini moja ma majirani wa nje ya dini na rafiki wa kando ya dini) . Na mawasiliano ya waislamu wao kwa wao. Amesema Mwenyezi Mungu, ‘Na waumini wa kiume na waumini wa kike hutawaliana wao kwa wao, wanamrishana mema na wanakatazaza mabaya, wanasimamisha swala la wana toa zaka na wanamtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao

tu ndio ambao atawarehemu M w e n y e z i M u n g u k w a hakika Mwenyezi Mungu ni mshindi na mwnye hekima’ surat Tauba – 71 na katika hadithi muislam ni ndugu wa musilamu basi asimdhulumu na wala asimlengeshe kwa adui ; na yatosha madhambi kwa mtu kumdharau ndugu yake. Na haki za kuungana na muislamu na muislamu ni jambo ambalo ameamrisha Mwenyezi Mungu na Mtume (S.A.W) pale aliposema Mtume (S.A.W) ninaapa hatokuwa muumini mara tatu alirudia neno hili. Wakauliza masahaba ni nani huyo ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu ? akasema, ‘yeyote atakayelala ameshiba na jirani yake ana njaa na yeye anajua.

Muungano wa kifamiliaPale alipowekwa mke kuwa ni

utulivu kwao na akawafanyieni kati yenu mapenzi na huruma Surat Rum aya ya 21

Mwisho : kwa hak ika Mwenyezi Mungu yeye ni mrehemevu ameiumba rehema na akapasua humo jina miongoni mwa majina yake na yeyote mwenye kuunga basi Mwenyezi Mungu atamuunga na mwenye kukata basin aye atakatwa (kutengwa) amesema Mwenyezi Mungu katika Surat Muhammad aya ya 22 (Jee mwaonaje pale mtakapotawalishwa na mkafanya uharibifu katika dunia na mkakata koo zenu) yaani mkaacha kutembeleana na kuwasiliana. Jee hili ni jambo zuri ?

ZAYEM kuhuisha utamaduni wa Mzanzibari Inatoka Uk. 6kubwa ya mafanikio kutokana na ushirikiano watakaoufanya kati yao mna walimu wa shule hizo.

Alisema kuwa wameamua wameamua kuchukua umamuzi huo wa kutoa elimu mashuleni kutokana na maeneo hayo kuwa ni miongoni mwa vyanzo vya vijana kuingia katika vishawishi vibaya, vikimo vya utumiaji wa madawa ya kulevya.

“Tumejipanga kutoa katika shule mbali mbali za Zanzibar tukiwa na shabaha ya kuwa maeneo hayo ndimo waliomo vijana wengi,huku tukiwa na matumaini kuwa lile lengo letu linaweza kufikiwa kwa wepesi zaidi” alisema Amiri huyo.

Aliongeza kusema kuwa “Njia hii kwa kiasi kikubwa tunategemea kuwa ile dhamiri yetu ya kuimarisha utamaduni wa Zanzibar inaweza kufikia kwa hatua kubwa.”

Aidha alisema kuwa pamoja na kuingia katika kutoa elimu hiyo shuleni lakini pia Jumuiya yake imejipanga kuingia hadi mitaani (Maskani), ili kuweza kufanikisha malengo yao waliyokusudia.

“ P a m o j a n a k u f a n y a shughuli zeti mjini lakini pia tutafika hadi vijijini ili nako kutoa elimu kama ilivyo mjini tukiwa na makusudio makubwa ya utamaduni wa Zanzibar unaimarika na kukuwa kwa wanajamii wote wa Zanzibar” alisema Amiri huyo.

Amiri huyo alisema kuwa hatua hiyo ya kutaka kurudisha utamaduni wa Zanzibar kupia Jumuiya yao ni miongoni mwa malengo ya jumuiya yao, malenfgo ambayo yanawahusu vijana ambao wao ndio tegemeo kubwa kwa maisha sasa na

baadae. Aidha Amiri Masoud alisema

kuwa Jumuiya yao pamoja na jitihada hizo lakini pia wanatoa elimu ya kuachana na utumiaji wa madawa ya kulevya, Elimu na maadili Michezo pamoja na elimu nyemngine mbali mbali.

Alisema kuwa hatua zote hizo hufanya kwa lengo la kuifanya jamii hasa vijana kudumu katika kufanya shughuli zao kwa kielimu zaidi huku wakiachana nay ale yote yatakayoweza kuwanfa kuingia katika matatizo hapa duniani na akhera.

“Mipango yote hiyo tuniafanya sisi wenyewe huku ndani yake tukionesha na kutangaza imani ya dini ya kiislam, ili vizazi viweze kufumbua macho na kuona maadili mazuri na si vyenginevyo”alisema Amiri huyo.

Hata hivyo alisema kuwa pamoja na hayo pia Jumuiya ina mpango wa kufungua vituo maaluma vya utoaji wa elimu ya maadili hasa kwa vijana ambao wao ndio walengwa wakubwa.

Alisema kuwa hatua hiyo kwa kiasi kikubwa itaweza kufanikisha yale malengo yao waliyokusudia kupia Jumuiya yao ya Vijana, elimu na maadili Zanzibar.

“Kabla ya kuanza shughuli zetuy za jumuiya huwa tunafanya utafiti kupitia kitengo cha utafiti cha Jumuiya yetu ili kuweza kugundua ni matatzo gani yanayowakuba wanajamii hasa vijana hadi kufikia katika njia mbaya”alisema Amiri huyo

Jumuiya ya Vijana , elimu na Maadili Zanzibar imaeanza kazi zake ikiwa na usajili halali wa Zanzibar kuanzia mwaka 2005, na hivi sasa ina Ju,mla ya wanachama 140, wakiwamo wanaume na wanawake.

Page 8: ANNUUR 1033

8 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 7 - 13, 2012Makala

Jamani hawa ndio Polisi wetuNa Omar Msangi

A W A L I y a y o t e ningependa kuchukua fursa h i i kuungana na Watanzania wote waliosalia japo na chembe ya huruma, imani na ubinadamu kulani kwa nguvu zote mauwaji yanayodaiwa kufanywa na Polisi.

H i v i s a s a w a t o t o wa Marehemu Daudi wamekuwa yatima kwa baba na mkewe amekuwa mjane. Haya ni katika m a t o k e o m a b a y a y a mauwaji haya ambayo athari yake ni ya daima dumu.

Ni matarajio yangu kuwa Tume iliyoundwa na serikali kuchunguza mauwaji haya itafanya kazi yake kwa makini na haraka na mwishowe wahusika watawajibishwa kwa mujibu wa sheria. J a p o k u w a j i b i s h w a huko hakutawaondolea uyatima watoto wa Daudi Mwangosi, kwa maana kuwa hakutamrejesha tena duniani baba yao, lakini hiyo itakuwa namna moja ya kutenda haki.

Kubwa zaidi ni kuzuiya mauwaji kama hayo yasiwe ni jambo la kuzoeleka kwa maana kuwa wauwaji wakajiona kuwa wanaweza wakauwa na isiwe lolote. Inapojengeka hali kama hiyo, uhai wa binadamu unakuwa hauna thamani tena na janga hilo huwa sasa ni balaa katika nchi ambalo litamtafuna kila mmoja kwa namna na kwa wakati wake. Ufupi wa maneno hakuna atakayesalimika.

Ndio maana kwa upande mwingine naona kuna kila sababu ya kuwapongeza wote waliojitokeza na kupaza sauti ya kulani mauwaji haya vikiwemo vyombo vya haba r i , wanasiasa na viongozi wa dini.

Katika watu waliotoa matamko makali kulaani mauwaji hayo ni waandishi w a h a b a r i a m b a p o hawakuishia hapo bali wamechukua hatua ya kusema kuwa hawatafanya kazi na Polisi kwa maana ya kuripoti habari zao angalau kwa k ip indi

hiki ambapo wanasubiri uchunguzi na kuona hatua zitakazochukuliwa.

M a t a m k o m a k a l i yametoka pia kwa viongozi wa kidini ambapo, Askofu Msaidizi Jimbo Katoliki la Bukoba, Methodius Kilaini akilani mauwaji hayo alishangaa iwapo polisi wetu wamepata mafunzo stahiki ya kipolisi.

“ Inas ik i t i sha sana , hali ni mbaya, hivi kweli ha iwezekani kuzuiya maandamano bila ya kuua, tujiulize hao wanaozuiya m a a n d a m a n o w a k o ‘trained’ vya kutosha katika kuzuiya maandamano?”

“Hivi hawawezi kuzuiya maandamano bila kutumia r isasi na mabomu ya hatari, hili liangaliwe kwani kuuwa siyo vizuri.” Alisema Askofu Kilaini.

Lakini labda niseme jambo moja hapa kuwa askari hawa tunaoshangaa na kuhoji kuwa inakuwaje wazuiye maandamano kwa kutumia risasi za moto kutokana na kumuuwa Daudi Mwangosi, ndio wale wale waliozuiya maandamano Zanzibar mwaka 2001 na kuua watu zaidi ya 27.

Kwa hesabu ya serikali watu waliouliwa katika maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi Z a n z i b a r w a 2 0 0 0 , walikuwa 27 japo kwa hesabu nyingine inadaiwa idadi yao kufikia 70 na zaidi.

Katika mauwaji yale Kiongozi Mkuu wa Kanisa Ka to l ik i , Muadhama Polycarp Kadinali Pengo wakati huo akisaidiwa na Askofu Methodius Kilaini alisema kuwa ilikuwa sawaswa Polisi kuuwa Wazanzibari wale. Katika kuwapongeza na kuwatetea Polisi waliowafyatulia risasi za moto na kuuwa waandamanaji, Kardinali Pengo alidai kuwa baadhi ya waandamanaji walikuwa na mawe na kwamba hata jiwe linauwa!

Ninakumbusha haya kwa sababu roho ya Daudi, mbe le ya Mwenyez i Mungu, ni roho kama zilivyokuwa zile roho 27 zilizoangamizwa Pemba

Inaendelea Uk. 9

IGP Said Mwema.

DCI Robert Manumba.

Page 9: ANNUUR 1033

9 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 7 - 13, 2012Makala

Jamani hawa ndio Polisi wetuInatoka Uk. 8na Unguja. Damu ya Daudi, ni sawa na damu ya Wazanzibari wale 27 i l iyomwagwa Januari 2001. Uhai wa Daudi katika vipimo na mizani ya muumba, ni sawa na uhai wa yule Imam aliyepigwa risasi Januari 26, 2001 akiwa nje ya Msikiti.

Kama huo ndio ukweli, m t u u t a j i u l i z a , n i n i kilipelekea kuwapongeza Polisi waliouwa watu 27 waliokuwa wakiandamana k u l e P e m b a n a l e o tunawaona Polisi hao hao kuwa ni waovu na wabaya kwa kutumia risasi za moto na mabomu katika maandamano ya CHADEMA Iringa!

Hoja ya msingi hapa ni kuwa kama ni ubinadamu, basi kinachotakiwa ni kutetea ubinadamu bila kujali ni nani kauwawa na nani kauwa. Kama ni kuwalani Polisi kwa kutumia vibaya mamlaka na maguvu yao, tulani bila kujali kuwa walipouwa watu ni Pemba au Arusha. Utu wa mtu, ubinadamu wa mtu na thamani ya roho na damu ya mtu, haitegemei kabila wala dini yake, mahali anapotoka au chama chake cha siasa.

Leo katika kifo hiki cha Daudi Mwangosi, haraka haraka serikali imejikuta haina namna ila kuunda Tume kufanya uchunguzi. S io kwamba ser ika l i imekuwa ya kibinadamu na yenye kujali sana. La hasha! Imefanya hivyo kama namna ya kujinusuru. Zogo limekuwa kubwa na kujikuta katika wakati mgumu.

Hapana shaka kama kelele kama hizi zingekuwa zimepigwa katika mauwaji ya Watanzania wenzetu wale 27, pangekuwa na namna ambapo serikali na Polisi wangekuwa wamepata fundisho na huenda mauwaji kama haya ya Daudi Mwangozi yasingetokea.

L a k i n i P o l i s i wameuwa Mwembechai, wamepongezwa. Tena sio wanapongezwa na serikali tu, wanapongezwa

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Dkt. Emmanuel Nchimbi

ASKARI wa jeshi la polisi Zanzibar wakiwa wamemkamata mmoja wa waumini wa dini ya Kiislamu kisiwani humo kwa madai ya kufanya maandamano isiyo halali

na vyombo vya habari, v i o n g o z i w a v y a m a vya siasa na Maaskofu. Wakaja wakauwa Imam wa Msikiti Januari 2001. Huyu hakuwa kat ika maandamano wala katika

kugomea sensa. Alikuwa ndio anatoka Masjid baada ya kuswalisha Ijumaa pale Mwembetanga, Unguja. Polisi wakapongezwa.

Matokeo yake ndio haya. Polisi wanazoeya kuuwa.

Wa n a o n a w a n a w e z a kuuwa na isiwe kitu bali wapongezwe na hata kupandishwa vyeo.

Ipo kauli moja imesemwa na mmoja wa Wachungaji wa l io j i tokeza ku lan i

mauwjai haya yanayodaiwa kufanywa na Polisi ambayo nayo inahitaji kupewa uzito wa kipekee.

Mchungaji huyo wa Kanisa la Ki inj i l i la Kipentekoste Tanzania, Kanda ya Mbeya, William Mwamalanga anasema kuwa haiwezekani kwa Tanzania kuwa na Polisi wauwaji utafikiri askari wa kukodiwa wasiojali uhai wa Watanzania.

Alisema kuna haja ya kufuatilia kwa kina aina ya askari wanaopelekwa k a t i k a o p e r e s h e n i mbalimbali, kwani kuna uwezekano wa kuwepo kwa hujuma za makusudi zinaendelea bila uongozi wa juu wa serikali kujua.

Kama nilivyotangulia kusema, kaul i hi i ya M c h u n g a j i Wi l l i a m inahitaji tafakuri makini hasa tuk i re jea tuk io la majuzi tu ambapo baadhi ya askari Arusha waliotumwa kusimamia zoezi la sensa waliacha jukumu wal i lo tumwa wakatumia fursa hiyo kudhihirisha chuki yao dhidi ya Waislamu.

Mtu utajiuliza, askari aliyetema cheche za chuki kwa kumtukana mama wa Kiislamu na mwanaye mlemavu kule Nji ro , atashindwa kuwamiminia risasi Waislamu akipata fursa?

Je, hawa si ndio wale waliotoa amri ya “piga yule risasi, bado mwongeze, mpige na yule” pale Mwembechai?

Je, yawezekana ikawa afande yule aliyeamuru vijana wake wapige risasi Waislamu alitumwa na viongozi wa ngazi za juu wa serikali au ni katika wale anaosema Mchungaji William kuwa wana agenda zao za kufanya hujuma?

Sambamba na h i lo inapasa kujiuliza, ni kwa nini inapotokea zahama Zanzibar huagizwa vikosi kutoka Bara?

J e , h i i n i k a t i k a k u h a k i k i s h a k u w a wanaoshiriki operesheni kama zile za wakati wa uchaguzi mkuu kwa siku za nyuma wanakuwepo ‘polisi wanaoweza kufanya hujuma na mauwaji bila kuona vibaya bila kujali k u w a h a w a k u t u m w a na viongozi wa serikali kufanya hivyo?

Page 10: ANNUUR 1033

10 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 7 - 13, 2012Makala

SHUKRANI zote zinamstahiki Allah ambaye ana hukumu kwa ukweli na Haki na ana waongoza Awatakao kwenye Njia Iliyonyooka. Anaamua mambo yote kwa (Busara) Hekima yake na ana faradhisha mfumo wa maisha (dini), naye ni mwenye Hakima ya juu, Mjuzi wa yote.

Ali tuma Mitume kama wapasha habari za kufurahisha n a k a m a w a o n y a j i , n a aliwateremshia Kitabu il i wahukumu watu kutokana na waliyokuwa wakitofautiana miongoni mwao. Ili wahukumu kwa uadilifu na kumpa kila mtu haki stahiki bila upungufu au kuzidisha.

Nakiri kuwa hapana Mungu apasaye kuabudiwa isipokuwa Allah pekee bila washirika. Yeye ni mfalme, Anastahiki shukrani zote na ni muweza wa kila kitu. Nakiri kuwa Muhammad ni mja na Mjumbe wa Allah, Rehema na Amani za Allah zimwendee, kizazi chake na wote walio mfuata (wafuasi) kwa ubora mpaka siku ya Hukumu.

Enyi watu! Mcheni Allah aliye Tukuka, jitoeni kwa utiifu na kumuunga mkono na Atakuhakikishieni ushindi, mtiini Yeye na atakulipeni.

“ Na bila shaka Mwenyezi M u n g u h u m s a i d i a y u l e anaye msaidia yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu Mtukufu. Wale ambao tukiwapa madaraka katika nchi husimamisha Sala, na wakatoa Zaka, na wakaamrisha mema, na wakakataza mabaya. Na kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo ya mambo yote” (22:40 – 41).

Enyi watu! Imani haipatikani kwa kupenda au matarajio. Bali Imani mahali pake ni moyoni na hutekelezwa kwa vitendo ambavyo vina thibitisha ukweli wake na asili yake kwa kufanya vitendo vya ibada na kujitenga na makosa. Kila mmoja wetu anaweza kujiita Muislam na hata kudai kuwa ni Mu’min (Muumini). Kila mmoja wetu anaweza kutangaza kuwa hapana Mungu apasaye kuabudiwa isipokuwa Allah na kuwa Muhammad (S.A.W) ni Mjumbe wa Allah. Hata wanafiki, ambao watakaa chini kabisa ya Jahanamu (motoni), wana mtaja Allah kwa maneno yao. Wanafiki walikuwa wakitangaza mbele ya Mtume (S.A.W), “Tunashuhudia kuwa wewe ni Mjumbe wa Allah” . Pia waliapa kwa Mtume (S.A.W) na Maswahaba zake kuwa walikuwa pamoja nao, japokuwa walikuwa dhidi yao. Pamoja na hayo na ahadi na viapo vyote havikuwasaidia chochote; hapa wapo chini kabisa Motoni chini ya kila Mushriki (Washirikina), Mpagani, Myuhudi na Mkristo! Hii ni kwa sababu viapo vyao havikutoka mioyoni mwao iliyojaa Yaqin (uaminifu), Imani, kujisalimisha au utii.

“ Na katika watu, wako (wanafiki) wasemao; “ Tume mwamini Mwenyezi Mungu wa siku ya mwisho”; na hali ya kuwa wao si wenye kuamini” (2:8).

Imani yenye nguvu na thabiti ambayo inazaa matunda ya kauli za ukweli, vitendo adilifu, mapenzi katika Njia ya Allah, uaminifu katika utekelezaji wa

Kiini cha imani na dalili zake

Tauhid na utii kwa Mjumbe wake (S.A.W). Imani inahitaji utatuzi, maisha, juhudi, uvumilivu na moyo kujizatiti kwa inaloliona kuwa gumu; kumtii Allah na kuizuia nafsi na tamaa na kumuasi Allah.

Kuna dalili nyingi za Imani zilizo tajwa na Allah ndani ya Kitabu chake na Mjumbe wake (S.A.W) na kufafanuliwa ndani ya Sunnah yake ifuatavyo:-

Allah amesema:“Hakika wanao amini kweli

ni wale ambao anapo tajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hujaa khofu; na wanapo somewa Aya zake huwazidishia imani, na wakamtegemea Mola wao tu basi; (hawana kuamini mizimu wala pango wala shetani wala makaburi wala mengineyo). Ambao wana simamisha sala na wanatoa katika yale tuliyowapa. Hao ndio wanao amini kweli kweli. Wao wana vyeo (vikubwa) kwa Mola wao, na msamaha na riziki bora (kabisa huko Akhera) (8:2 – 4).

Aidha Allah amesema:“ N a i n a p o t e r e m s h w a

sura (mpya ya Qur’an) wako miongoni mwao (watu wanafiki) wasemao: “ Ni nani miongoni mwenu (Sura) hii imemzidishia imani?” Ama wale walioamini ina wazidishia imani, nao wa furahi. Ama wale wenye ugonjwa nyoyoni mwao, basi inawazidishia ubaya (mpya) juu ya ubaya walio kuwa nao; na wanakufa na hali ni makafiri. Je! Hawaoni ya kwamba wanatiwa mtihanini kila mwaka mara moja au mara mbili (au zaidi)? Kisha hawatubu wala hawakumbuki” (9:124 – 126).

Kwa hiyo ndugu Waislam, ni nani miongoni mwetu mwenye sifa hizi? Nani miongoni mwetu mwenye hisia za woga ndani ya nafsi yake kwa sababu ya Allah na Anatukuza utajo wake anapotajwa? Nani miongoni mwetu ambaye Imani yake imeongezeka na anaye furahia wakati akisomewa Ayat za Mola wake? Anaye hisi furaha ya

kuamini Ayat na kutekeleza Sharia zake? Nani miongoni mwetu anamhisi kwa dhati Allah, bali zaidi ya kiumbe yeyote? Nani miongoni mwetu anaye simamisha sala kama inavyo takiwa, kwa usahihi na kwa wakati? Nani miongoni mwetu anatoa katika vile alivyo ruzukiwa na Allah kwa kutoa zakat na kuwasaidia wenye kuhitaji, jamaa na masikini?

Tunapo tafakari hali ya Waislam katika zama zetu, tunawaona Waislam wengi wasiotia kwenye vitendo Imani au Uislam, isipokuwa yule aliye ridhiwa na Allah miongoni mwao kuwa na imani. Kwa ujumla, Waislam wana udhaifu, hususani katika kutimiza haki za Allah, haki za mtu kwa mtu, na kuwa na Imani za yaqin (uhakika). Waislam wengi katika ulimwengu wa Kiislam hawafuati kanuni za tabia/mwenendo au kusahihisha matendo yao na wengi wao wame athirika na utamaduni mbovu wa makafiri. Athari yake inaonekana kwa baadhi ya Waislam wenye wasiwasi na mashaka mioyoni mwao juu ya wahyi wa Allah. Ubashiri wa Mtume, uwepo wa malaika na majini na usahihi wa Ujumbe wa Mtume kwa ujumla. Baadhi yao walitilia mashaka kuwepo kwa Allah, Mola na Muumba! Utukufu ni wake Allah! kuwa yeyote mwenye mashaka na kuwepo kwa Allah, bali kutilia mashaka kuwepo kwake mwenyewe? Nani aliye muumba basi, iwapo Allah hakufanya hivyo? Hii ndio sababu tunawaona Waislam wengi leo hii ambao mioyo yao haitikisiki wakisikia Allah anatajwa, kama vile hawakusikia chochote cha kuwafanya wawe wa pole na wanyenyekevu. Baadhi ya Waislam hawaongezi imani yao wakati Ayat (Qur’an) zinasomwa. Bali wana zidisha uovu na dhambi, wakidhihaki Ayat za Allah na hawakuza kutekeleza kwa sababu ya ujinga. Baadhi ya Waislam

wa leo hawana uaminifu kwa Allah, bali wana imani na mali na maisha ya dunia. Kwa sababu hiyo hawatafuti mali kwa njia za halali, wanadhani wakifanya hivyo, fursa ya kujilimbikizia mali inapungua, wanafanya bidii kutafuta mali kutoka rasilimali zozote, ima ni halali au haramu. Baadhi ya Waislam leo wana wategemea maadui wa Allah ili kupata usalama na amani, ambayo inawafanya kuwatii makafiri kwa kuto mtii Allah na Sharia yake.

“Kwa hakika wanaorudi nyuma baada ya kwisha wabainikia uwongofu, shetani huyo amewashawish i na amewaghuri. Hayo ni kwa sababu waliwaambia waliochukia aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu: Tutakutiini katika baadhi ya mambo. Na Mwenyezi Mungu anajua siri zao. Basi itakuwaje Malaika watakapo wafisha wakawa wana wapiga nyuso zao na migongo yao! Hayo ni kwa sababu wao waliyafuata yaliyo mchukiza Mwenyezi Mungu na wakachukia yanayo mridhisha, basi akaviangusha vitendo vyao”. (47: 25 – 28)

Tunaona kuwa wale Waislam wanao watii na kuwafuata maadui zao kwenye masuala yanayo pingana na Sharia ya Kiislam, wanafanya hivyo kwa sababu ya udhaifu na imani kwa Allah na utegemezi mkubwa kwa kitu kingine minghairi yake! Wana shangazwa na nguvu za maadui wa Allah na kudhani kuwa nguvu zote ziko mikononi mwao. Wana sahau kuwa yule Aliye waumba maadui, kwa hakika ana nguvu zaidi yao lau watu hawa wangelitumia hofu yao kwa kusabilia utii wao kwa Allah pekee, na wakatafuta njia za kupata ushindi, kama kufuata dini na Sharia ya Allah inayohusu mambo yao ya maisha, watapata nguvu ya kutosha. kama wakifanya hivyo, Allah atakuwa pamoja nao, na yeyote aliye na Allah, hatoshindwa.

“Na hapana kitu kinachoweza kumshinda Mwenyezi Mungu mbinguni wala katika ardhi. Hakika yeye ni Mwenye kujua ; Mwenye uwezo”. (35:44)

Siku hizi tunawaona Waislam hawajiungi na sala za jamaa wala kuhifadhi wajibu wake. Hawahudhurii sala za jamaa Msikitini na hata wakisali hawatimizi nguzo za sala, masharti na sunna Hawajali usafi wa mwili, kusali kwa wakati, kukamilisha kisimamo, kitako, rukuu na sujud kwa utulivu na madaha. Baadhi ya watu wanaojiita Waislam hawa Sali kabisa, na baadhi yao huwa kebehi wanao Sali na sala yenyewe. Baadhi ya Waislam hawatoi zakat wala Sadaqah kutokana na walivyo ruzukiwa na Allah, wala hawatumii kwa wale waliotakiwa wawape. Bali, watu hao wanatumia kwa usirafu (kwa fujo) kwa yale yasiyo wasaidia na kwa yale walio haramishiwa na Allah.

Leo Waislam wako katika hali ya kutisha. Tunamlalamikia Al lah ku tokana na uovu walioufanya na kwa kutelekeza mipaka yake na maamrisho. Tuna mlalamikia Allah kwa kuichukulia Sharia yake kwa wepesi, tukisahau kumdhukuru, tukihisi tuko sehemu kutokana na mpango wake, waki dharau/Kupuuza lengo la kuumbwa kwao na badala yake kutelekeza na kuzama kwenye mambo ya kipuuzi. Hali hii inaelezea sababu ya maadui wa Uislam kuwa na nguvu juu yao sasa na kuwa dhalilisha, wakati wana wadhibiti kisiasa, na kiuchumi. Waislam wamekuwa kama kundi la Kondoo ambao hawasikii lolote isipokuwa miito na vilio vya mchungaji wao, ni viziwi, mabubu na vipofu, na kwa hiyo hawaelewi. kwa hakika sote tunatoka kwa Allah na kwake tutarejea.

Ewe Allah! Tuna kuomba wewe tunapo subiri kufanya ibada ambayo umetufaradhishia kama neema kutoka kwako. Tunakuomba kwa kusisitiza kuwa Wewe ni, Mmoja, Mlishaji. Yule ambaye hakuzaa wala Hakuzaliwa na hapana mfano wake (hapana kama Yeye). Ewe uliye umba mbingu na dunia, Mmiliki wa nguvu na Rehema, wa milele Asiye kufa, anayevipa uhai vinavyoishi. Tuifanye Imani itupendeze, ifanye nzuri uithibitishe nyoyoni mwetu. Tunakuomba uufanye ukafiri, dhambi na uasi chukivu kwetu na utuepushie njia hii ya uovu.

Ewe Allah! Tunakuomba uweke sawa mambo ya Ummah huu na uupat ie v iongozi waadilifu ambao wanajali ukweli na wana hukumu kwayo. Turidhie viongozi ambao hawachelei lawama za mtu yeyote wanapotekeleza Sharia ya Allah. Tupe viongozi wasio wapendelea jamaa zao kwa sababu ya uhusiano wao au kwa nguvu zao. Tunakuomba uilinde dini yetu na utuimarishe juu yake mpaka siku ya kufa kwetu. Wewe, bila shaka ni Mwema sana, Mwingi wa Rehema. Nasema haya na namwomba Allah anisamehe pamoja na wewe1.

Page 11: ANNUUR 1033

11 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 7 - 13, 2012Matangazo

Munazzamat Al- Daawa Al- Islamiyya Ofi si ya Tanzania inayo furaha kuwatangazia wafuatao kuwa wamechaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha (International University of Africa) kilichopo Khartoum-Sudan kwa mwaka wa masomo 2012/2013. Usajili tarehe 15-30/9/2012, Masomo yataanza tarehe 2/10/2012.

FACULTY OF ENGINEERING FACULTY OF SHARIA1 MARIAM ABDALLAH MOHAMMAD (ZNZ) 28 SULEIMAN KHAMIS ISSA (ZNZ)2 OMAR MBAROUK OMAR (ZNZ) 29 ASHA MOHAMED OMAR (ZNZ)3 RAMADHANI SAID (MWANZA) 30 SAID ALI SALEH (ZNZ)4 RAMADHANI ZILI RAMADHANI (DSM) 31 IBRAHIM MUSA KAVINWA (MWANZA)5 KARIM ADAM (DSM) 32 ALAWI NUHU BUKENDE (MWANZA)6 KHANIFA AMANA (DSM) 33 ISMAIL ABDALLAH NAYAMBE (MWANZA)7 SEIF HAMZA (DSM) 34 JAFARY RAJABU SHOMARY (MWANZA)

FACULTY OF PHARMACY 35 HAMIMU SHABANI MASONJO (DSM)8 UMMU-L-KHAYR SADRI ABDULLAH (ZNZ) 36 HAMISI ABRAHAMANI CHIMA (DSM)9 ASIA MOHAMED SULEIMAN (ZNZ) 37 KINANDA YUSUPH SHOMARI (DSM) 10 HADIJA ATHUMANI MBELWA (DSM) 38 OMARI YUSUFU ALLY (DSM)11 ABDALLAH NURDIN ABDALLAH (DSM) 39 JAFARI OMARI MWINDADI (DSM) 12 ALLY JUMA OMARY (DSM) 40 SULTANI SAID MUHANI (DSM)FACULTY OF PURE SCIENCE 41 SAADU ABDUL-MAJID (DSM)13 NASSOR KHAFIDH MAJID (ZNZ) 42 ABDRAHMANI HUSEINI SULEIMANI (DSM)14 ALI MAKAME AME (ZNZ) 43 MBWANA HAJI MJAJA (DSM)15 KHALID WALID BAHORERA (ZNZ) 44 ABDALLAH ALLY CHUMBE (DSM) 16 ABDALLAH MOHAMED (DSM) 45 IS-HAQ MUSA ALLY (DSM)17 AMINA ATHUMANI NADA (DSM) 46 ALLY SHOMARI RAMADHANI (DSM)

FACULTY OF DENTIST FACULTY OF EDUCATION18 WALIID RASHID SEIF (ZNZ) 47 MARIAM HUSSEIN MUSSA (MWANZA)19 HAMID HASSAN KARAMA (DSM) 48 ALAWI NUHU (MWANZA)20 HAMIS JUMA ASSEDI (DSM) 49 SAID RAJABU NYANGE (DSM)

FACULTY OF ECONOMICS 50 KHAMIS RAJABU SIMBA (DSM) 51 MAJID MAULID OMARI (DSM)21 KHADIJA MOHAMED NAWAB (MWANZA) 52 ABDALLAH HAMIS KABELELA (DSM)22 AHMAD SAID KAPAYA (MWANZA) 53 HASSANAT MANGO (DSM)23 JUMA SHABANI (MWANZA) FACULTY OF MEDICINE24 AMASHA JUMA (DSM) 54 WASILA MMANGA MUSA (ZNZ)

FACULTY OF COMPUTER SCIENCE 55 HAWA OMARY RAMADHANI (DSM)25 SALIM MOHAMED SALIM (ZNZ) FACULTY OF LABORATORY SCIENCE26 RASHID RAJABU (DSM) 56 AMEIR JAKU VUAI (ZNZ)27 ISMAIL MUSA GALAWA (DSM) 57 HAMAD JONAS (MWANZA)

Kwa maelezo zaidi fi ka kituo ulichofanyia mtihani au piga simu :Zanzibar: 0773 415 835, Mwanza: 0782 382 434, D’Salaam: 0786 806 662/ 0652 806 662.

Khamis Mohamed Liyenike KNY, Mkurugenzi- MDI

STUDENTS JOINING IN THE ACADEMIC YEAR 2012/2013 ARE HEREBYASKED TO OBSERVE THE FOLLOWING INSTRUCTIONS:

1. ADMISSION LETTER/JOINIING INSTRUCTIONS- STUDENTS ARE ADVISED TO TAKE THEIR ADMISSION LETTERS AT THEFOLLOWING POINTS:(I) ZANZIBAR (UNGUJA); – AT UKUEM OFFICES(II) PEMBA (CHAKECHAKE); - AT UKUEM OFFICES(III) D’SALAAM – AT ANNUUR OFFICES, MANZESE TIP TOP USANGI HOUSE(IV) MTWARA – CONTACT MR. LENGA; 0787501081(V) IRINGA – CONTACT MR. ZUBERI; O714522122(VI) MOROGORO – AT MUM ADMISSIONS OFFICE(VII) TANGA – CONTACT MAAWA S.S.; 0713549504(VIII) K’NJARO (MOSHI) – CONTACT MR. OMARI; 0715185285(IX) SINGIDA – CONTACT MR. KINDI; 0784841055(X) TABORA – CONTACT MR. MANGI; 0783079146(XI) MWANZA – CONTCT MR. BEN; 06558893302. PAYMENT- THE STUDENT SHOULD MAKE THE NECESSARY PAYMENTS BEFOREREPORTING TO THE UNIVERSITY FOR REGISTRATION

IMPORTANT NOTICE TO NEW STUDENTSIN THE ACADEMIC YEAR 2012/2013

- ALL THOSE WHO HAVE BEEN ALLOCATED LOANS BY THE HESLB SHOULDPAY NOT LESS THAN A QUARTER OF THE AMOUNT OF TUITION FEE NOTALLOCATED BY THE HESLB- THE SELF – SPONSORED STUDENTS SHOULD AT LEAST PAY NOT LESSTHAN HALF OF THE TUITION FEE

THE STUDENTS SHOULD ALSO PAY THE FOLLOWING:- ADMINISTRATION/REGISTRATION COST………SHS. 35,000.00- CAUTION MONEY………………………………………. “ 20,000.00- IDENTITY CARD………………………………………… “ 3,000.00

ALL PAYMENTS SHOULD BE MADE THROUGH THE FOLLOWING MUM A/CNUMBER AND NAME: 01J1013380601 CRDB MUSLIM UNIVERSITY OFMOROGORO

3. REGISTRATION- THE STUDENTS ARE REQIRED TO REPORT AT THE UNIVERSITY ON 1STOCTOBER, 2012, FOR REGISTRATION. STUDENTS SHOULD COME WITH THEIRORIGINAL CERTIFICATES, MEDICAL REPORT, FOUR (4) PASSPORT SIZEPHOTOGRAPHS AND BANK PAY IN SLIP, FOR ANY PAYMENT MADE.- THE DEADLINE FOR REGISTRATION IS 7TH OCTOBER, 2012

4. ORIENTATION WEEK

- ORIENTATION WEEK FOR THE NEW STUDENTS BEGINS ON 8TH OCTOBER, 20125. LECTURES- LECTURES BEGIN ON 15TH, OCTOBER, 2012

F. A. TAMIMFor DVC (ACADEMIC)

NB: Kwa wanafunzi waliochanguliwa MUM waliopo Dar es Salaam wafi ke katika ofi si za gazeti la AN-NUUR wakiwa na Copy ya cheti cha Kidato cha Nne. 0714 111669

Page 12: ANNUUR 1033

12 AN-NUURBarua/Shairi SHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 7 - 13, 2012

Je! Una maoni, barua au Mashairi? Tuandikie:Mhariri AN-NUUR,

S.L.P. 55105, Dar es Salaam au tutumie kwa Barua pepe

E-mail: [email protected]

Ndugu Mhariri,

Assalaam alaikum.Hakuna shaka wala hofu kwamba UDINI upo katika nchi yetu na mtu wa kwanza kabisa kuileta dhambi hii si mwingine bali ni Nyerere!

W a k o l o n i w o t e w a l i o t u t a w a l a wa l i z ihesh imu d in i zetu, lakini kuja uhuru na Nyerere, limekuwa balaa.

Sensa ya kikoloni ya mwisho iliyofanyika katika nchi hii ilikuwa

Huu si wakati wa kutishanamwaka (1957) ilionyesha Waislamu wal ikuwa asilimia 58, Wakristo 32, na wapagani asilima 10. Hizi ni takwimu za mwaka 1957 na bado hatujawa huru.

B a a d a y a h a p o Nyerere alisema suala la dini linatuhusu nini sisi Watanzania! Lakini wakati huo huo anasema atahakikisha kuwa analipa Kanisa lake Katoliki u p e n d e l e o m a a l u m linawiri. Je, huu sio udini tena uliokubuhu?

Leo hii baada ya miaka 50 ya uhuru Serikali yenyewe ina wabagua raia wake kwa itikadi ya

dini!Tunashuhudia kila

m w a k a m a k a n i s a yakichukua mabilioni ya pesa za Watanzania kama wao ndio Watanzania halisi na wengine hawana haki. Je, huo sio udini?

Watanzania wenzangu huu s io waka t i wa d a n g a n y a t o t o , n a kutoleana vitisho visiokua na maana. Huu sio wakati ule wa kusema zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa CCM.

Watu wanajua mambo mengi ambayo zamani yal ikuwa wakiyajua baadhi tu ya waheshimiwa na na watumishi fulani wa Mungu.

Serikali inawapeleka Wa t a n z a n i a m a h a l i ambapo ni vigumu kuja kuwarud i sha . Hapa mlipotufikisha pana tosha!

MwananchiDar es Salaam

Ndugu Mhariri, N ik iwa mmoja wa w a s o m a j i w a k o mkongwe wa An nuur, leo naomba na mimi unipe nafasi kidogo nitoe maoni yangu.

Kuna watu kiasi l i hata kama akifanya jambo la hovyo, hawezi kulaumiwa kutokana na asili yake kuwa ametoka kwennye jamii ya watu wa hovyo. Kuna tatizo la baadhi ya watu ambao wamejiwekea desturi ya kutokwenda shamba mpaka wanywe pombe au wavute bangi. Hii ni kasumba mbaya kabisa.

Vile vile kuna watu kiasili akifanya jambo l i s i l o f a a , l a z i m a u l i shangae kwamba hata huyu na asili yake anafanya hivi!

Rais, wetu mpendwa yupo katika kundi la watu ambao kiasili ni watu wastaarabu na waungwana. Ni vipi leo akae kimya ndugu zake wawekwe rumande tena Mwezi Mtukufu w a R a m a d h a n i , n a kusababisha kukosa ibada, kisa eti wanasusia

Ogopeni Dua ya mwenye kudhulumiwasense ya watu! Huu ni ukatili wa hali ya juu sana.

Al ikuwepo Meles Zenawi , a l iwatumia Masheikh wa ‘Bakwata’ ya Ethiopia kuangamiza Waislamu wa nchi yake. Leo kaondoka, huko aliko anapata jaza ya udhalimu wake.

Kumbuka kwamba amesema Mtume (s. a.

w), ogopa dua ya mwenye kudhulumiwa kwani haina pazia kati yake na Mola wake.

D h u l m a m n a y o w a f a n y i a Waislamu haitoenda patupu. Allah (AWT) atawaonyesha hapa hapa duniani na kesho Akhera pia mtaadhibiwa.Issa Ibrahim KimweriDar es Salaam.

Karibu tena safuni, kwa ya katiba maoni,Sehemu hii jamani, ni ya pili tambueni,ZINGATIA kwa makini, kila ubeti unani,Haya ndo yetu maoni, tambueni ikhiwani.

UHURU iuthamini, wa KUABUDU nchini,Katiba isiukhini, kwawe ufinyu uoni,Ibada si kanisani, bali kote maishani,Haya ndo yetu maoni, tambueni ikhiwani.

Na SHERIA ya kihuni, iondoshwe katibani,Si nyingine hadharani, nathubutu kubaini,Haki zetu ‘sothamini, ya UGAIDI nchini,Haya ndo yetu maoni, tambueni ikhiwani.

MAENEO ya KIDINI, katiba iyabaini,Kwa ya insafu mizani, bila kubagua dini,Si KUHODHI moja dini, HAKI kubwa ARDHINI,Haya ndo yetu maoni, tambueni ikhiwani.

NAFASI SERIKALINI, zigawiwe kwa mizani,Wasijazwe waumini, wa dini moja safuni,UWIANO wa KIDINI, uwe wazi katibani,Haya ndo yetu maoni, tambueni ikhiwani.

UWAKILISHI BUNGENI, utamkwe hadharani,Si mwingine wa KIDINI, kwa maslahi ya dini,Yawakilishwa na nani, maoni ya wanadini,Haya ndo yetu maoni, tambueni ikhiwani.

Kadhalika UDIWANI, si dhambi kwa wanadini,SERIKALI MITAANI, uwe pia mwake ndani,Lengo maoni ya dini, ‘siwe ombwe wala duni,Haya ndo yetu maoni, tambueni ikhiwani.

MAHAKAMA iwe ndani, ya KATIBA ikhiwani,Vipengele katibani, itoe yake maani,Nazo sheria kinzani, ‘batilishwe katibani,Haya ndo yetu maoni, tambueni ikhiwani.

MAHAKAMA elezeni, za HAKIMU MAKAZINI,Ziondoshwe katibani, kwa za wilaya nchini,MAMLAKAYE WIANI, kuwa MBILI kulikoni,Haya ndo yetu maoni, tambueni ikhiwani.

Na FASILI ya yakini, ya NIKAHI katibani,‘Yainishwe kwa makini, ‘sijekuwa matatani,Kwa ndoa za KISHETWANI, za jinsi moja jamani,Haya ndo yetu maoni, tambueni ikhiwani.

HAKI za KIHAYAWANI, zisiwemo katibani,LIWATWI kama kifani, si HAKI ya KIINSANI,Ni HAKI za KISHETWANI, tunopaswa kuzilani,Haya ndo yetu maoni, tambueni ikhiwani.

Ithnashara mwishoni, ‘sije dhani wa maoni,Pamoja tena tuweni, juma lijalo safuni,Kwa akthari maoni, ya kutoa katibani,Haya ndo yetu maoni, tambueni ikhiwani.

ABUU NYAMKOMOGI MWANZA.

Maoni katiba mpya (2)

Kwa mahitaji ya viroba bora vipya kabisa kwa matumizi mbalimbali sasa unaweza kupata kwa bei ya jumla na rejareja kwa saizi zote kwa bei nafuu zaidi, kwa BANDO.

Tupo mtaa wa Likoma na Pemba Kariakoo, Dar es Salaam (nyuma ya Msikiti wa Idrisa).

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana kwa simu: 0657 800999/0683 800999.

VIROBA MURUA

Page 13: ANNUUR 1033

13 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 7 - 13, 2012Makala

“(Hili ni) tangazo, ni tangazo la kujitoa katika dhima (ahadi) litokalo kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, kwa wale mlioahidiana nao miongoni mwa washirikina.” (Quran 9:1).

Hii ni Aya ya kwanza ya surat Tawba ambayo ni sura ya tisa katika mpangilio wa sura ndani ya quran tuikufu.. Kushuka kwa Aya hii kunafuatia tabia za washirikina wa Kiarabu wa Makkah ambao walikuwa hawatekelezi ahadi au mikataba waliyokubalina baina yao na Waislamu. Kwa maneno mengine ni kuwa mikataba hiyo ilikuwa ikitekelezwa na Waislamu pekee.

K a t i k a A y a y a 4 , Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema, “Isipokuwa wale mlioahidiana nao miongoni mwa hao washirikina, kisha hawakukupunguzieni chochote wala hawakumsaidi yeyote dhidi yenu…”

Katika Aya hii Mwenyezi Mungu Mtukufu anaweka bayana kuwa sio mikataba yote inayotakiwa kuvunjwa, bali ile tu ambayo washikina hawatekelezi upande wao. Lakini kwa ile ambayo washirikina walikuwa wakiitekeleza hakukuwa na sababu ya kuivunja kwa kuwa Uislamu unachunga ahadi.

Matukio yaliyofanya aya hizi kushushwa yalijiri wakati wa Mtume Muhammad SAW. Mwenyezi Mungu Mtukufu angeweza tu kumpa maelekezo mtume wake juu ya kadhia hii ya kuvunja mikataba na washirikina, lakini hakufanya hivyo, bali ameijaalia kadhia hii kuwamo ndani ya Quran, ikimaanisha kuwa ni ujumbe kwetu tunaotakiwa kuufanyia kazi.

Serikali yetu ya Tanzania haina dini, kwa maana nyingine ni serikali ya kipagani, na upagani ni ushikina. Na kwa kuwa raia wa nchi hii tuna dini zetu tofauti tofauti, basi waasisi wa dola hii wakaona ni vema tukawa na mkataba/makubaliani/ahadi baina yetu, ya kwamba serikali itakuwa ya kishirikina na raia watabaki na dini zao na kwamba ni marufuku dini ya mtu au kundi fulani la watu kuwa na ushawishi wa kimaamuzi katika serikali.

Lakini kwa bahati mbaya sana wakati Waislamu wakitekeleza ahadi, serikali ikishikiliwa na mawakala wa kanisa pamoja na Wakristo kupitia Nyerere hawakufanya hivyo. Nyerere akaanza kulipa kanisa “better chance” dhidi ya Waislamu. Hapa sitaki kwenda ndani zaidi kwani kitabu maarufu cha Dr. Sivalon chatosha kuthibitisha hoja hii. Mwislamu mmoja shujaa aliyeona mbali alimkabili Nyerere na kumwabia wewe hutatekeleza ahadi. Utawapa kipaumbele Wakristo wenzako tu. Kwa kutokujua Waislamu

Sensa: Hili ni tangazo la kujitoaNa Rajab Nkawa

wakampiga pande ndugu yao huyu, Almarhumu Sheikh Suleiman Takadiri.

Habari hizi za Sheikh Takadiri na wengineo kwa sasa tunazisoma kama historia ya mapambao ya Waislamu dhidi ya maadui wasiowatakia mema mema Waislamu na dini yao. Na kwa kweli tunawasifu watu kama hao na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu mlezi awafanyie wepesi siku ya kisimamo. Amiin.

H i v i s a s a Wa i s l a m u tunauelewa mkubwa juu ya madhila tuyapatayo kutokana na kutekeleza mkataba ilihali wengine wakihalifu. Aidha, Waislamu sisi tunazisoma katika Qur’an aya zile nilizo zitanguliza mwanzoni. Hakuna tusichokijua, tunajua kila kitu.

Baada ya utangulizi wote huo hapo juu, sasa naingia katika hoja yangu ya msingi. Nayo ni kwamba sisi Waislamu tunapopata nafasi za kiutendaji serikalini bado tunakuwa na utii mkubwa kwa dola huku tukitekeleza ahadi ilihali wengine hawatekelezi. Ni kama Quran hatuisomi au kama tunasoma basi aya tulizozitanguliza pale mwanzo tunazipita kama masimulizi ya zamani na kwamba hazina jambo lolote na sisi.

Wenzetu linapokuja suala lenye kugusa maslahi ya dini yao hawakai kimya, wote kwa pamoja, viongozi wa kidini na siasa lao linakuwa moja. Serikali iliwahi kupeleka bungeni hoja ya kufuta misamaha ya kodi katik taasisi za kidini hapa nchini. Viongozi wa makanisa na wabunge wakiongozwa na mbunge wa Karatu Mheshimiwa Slaa walipiga kelele kwa pamoja

na hatimaye serikali ikafuta hoja yake.

Aidha kuna kisa kile cha mwaka jana cha mzee mmoja wa Monduli maarufu kama Babu aliyedai kaoteshwa na “Mungu” kutibu watu wenye matatizo ya maradhi sugu. Pamoja na Wizara ya Afya chini ya Waziri Dk. ‘Alhaj’ Haji Mponda kuonya kuwa hakuna ushahidi wa kisayansi kwamba dawa ile ina uwezo wa kutibu na kutaka watu wasiende huko, hatimaye alishindwa baadaya kanisa la KKKT kutoa sapoti kubwa na viongozi wa kiserikali Wakristo na wabunge wakienda wenyewe kunywa kikombe cha Babu. Kwa kifupi ni jambo lenye maslahi na Kanisa basi wenzetu huwa kitu kimoja.

Kwetu sisi ni kitu tofauti kabisa. Kwa mujibu wa serikali nchi haipangi mipango ya maendeleo kwa kutegemea dini za watu bali utanzania wao. Lakini wakati huo huo serikali inamkataba na makanisa maarufu kama Memorandum of Understanding (MoU) ambapo serikali inayapa makanisa mamilioni ya pesa kwa ajili ya kundesha shughuli zake za ustawi wa jamii. Waislamu walipohoji hili Rais Kikwete alijibu kiwepesi tu kwamba Waislamu hawakuomba. Yaani Rais Kikwete anaona ni sawa na ni halali kwa Wakristo kuchotewa mamilioni kutoka Hazina ya taifa kupewa dini moja.

Rais Kikwete anasema takwimu zilizopo zinazotolewa na Wakristo na taasisi za serikali, Wizara na Ofisi ya Waziri Mkuu zinazoonyesha

kuwa Wakr is to n i wengi kuliko Waislamu tuzipuuzie na kwamba hazina maana yoyote. Napenda kumuuliza hapa hivi anapoteua Wakuu wa Wilaya 133 halafu kati ya hao 42 tu wakawa Waislamu, yeye haoni kama anaongozwa na takwimu hizo anazotaka sisi tusitambue? Kama siyo, je inakuwaje? Hebu aangalie Baraza lake la Mawaziri, hivi ni kweli uteuzi wake umetegemea viwango vya elimu vya wateuliwa?

Kuna wakati nilimsikia Rais Kikwete akisema kuwa urais wake hana shea na mtu, ni wake peke yake. Lakini napata wasiwasi na kauli yake kwani ni kama vile yeye ni Rais wa kuidhinisha majina wakati uteuzi umeshafanywa na watu wengine. Kwasababu huwezi kupata picha ya jinsi ya vigezo atumiavyo wakati akiteua watendaji wake iwe ni katik Uwaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu wa Wizara, Wakuu wa Mikoa nk. Hivi kwa nini haitokei kwa bahati mbaya Waislamu wakazidi upande fulani.

Swali la mwisho kwa Rais Kikwete ni kuwa hivi anaamini kabisa kile akisemamiacho katika suala zima la sensa ya watu na makazi ya 2012? Alisema alikutana na Masheikh na Wanaharakati wa Kiislamu, hivi baada ya maongezi yote hayo, hakuwaelewa kweli? Kama ndiyo hivyo basi mfumokristo ni ulevi mbaya sana kulikon pombe au madawa ya kulevya na bangi. Yaani anahangaika kutekeleza ahadi wakati wenzake hawatekelezi upande wao!

Sasa tuwageukie Waislamu Mawaziri, Wabunge, Wakuu

wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na watendaji wengine. Hivi ni kwa nini hawaioni kweli na wakaamua kuungana na Waislamu wenzi wao katika kutetea hadhi ya Waislamu na Uislamu katik nchi hii? Hivi hoja za Waislamu za kususia sensa wao wanaziona hazina maana au zina maana lakini wanashindwa kwa sababu wapo kazini? Waelewe kuwa kazi hizo wanazoogopa kuzikosa, si chochote ukilinganisha na Pepo ya Mungu aliyowaandalia waja wake baada ya maisha ya hapa duniani.

Nakumbuka siku za mwisho kuelekea katika siku za sensa Wakuu wa Mikoa na Wilaya Waislamu ndiyo walikuwa wakipamba taarifa za habari za televisheni na redio za kuandaa futari na kuwaponda Waislamu wenye msimamo wa kususia sensa.

Lau kama sensa ingekuwa inasusiwa na Wakristo, sidhani kama tungemwona kiongozi yeyote wa kisiasa Mkristo ambaye angeunga mkono. Kwanza hata huku kwa wananchi lisingefika, watendaji wangeshalimaliza katika vikao vyao. Unajua kwa nini? Kwa sababu wao ni “wengi katika serikali hii” na wingi wao unawafanya wao kuwa wengi katika vyombo vya maamuzi.

Lakini pengine wenzetu hawa katika nafasi hizo chache za juu walizo nazo wanaweza kuwa na njia bora zaidi mbadala ya hizi tunazoona sisi zinafaa. Lakini nataka kuwaambia kuwa hekima ya Mungu na Mtume wake wakati wote zitakuwa juu ya hekima zote. Mtume anatuambia munkari ukiingia katika jamii tunawajibu wa kuuzuia kwa mikono yetu, au tuseme na kuchukia japo haya ya mwisho ni katika udhaifu wa imani.

Narejea tena kuwa Mwenyezi Mungu amekwishatoa tangazo kwa Waislamu la kujivua na hizi dhima zisizokuwa na maana za kutekeleza ahadi upande mmoja huku wenzetu wakiendelea kutuhujumu katika kila sekta, mfano ule mgogoro baina ya yetu na Baraza la Mitihani. Hivi kama Waislamu wote kunzia Rais Kikwete mpaka hawa wakuu wengine tungeshikamana pamoja kutetea dini ya Mungu si ingekuwa raha! Hivi lini hili litatokea?

Namaliza makala yangu kwa maswali ambayo Mwenyezi Mungu anatuuliza sisi sote tunaojiita Waislamu:

“Enyi mlioamini! mna nini mnapoambiwa nendeni kupigana kwa ajili ya dini ya Mwenyezi Mungu mnajitia uzito katika ardhi? Je, mumekuwa radhi na maisha ya dunia kuliko ya akhera?...”

“ J e m n a d h a n i k u w a mtaachwa, na hali Mwenyezi Mungu hakuwabainishawale waliopigania dini miongoni mwenu…?

HAYATI Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati wa uhai wake.

Page 14: ANNUUR 1033

14 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 7 - 13, 2012Makala

SERIKALI imelazimika kuongeza muda wa siku saba katika zoezi la sensa ya watu na makazi. Bila shaka sababu ni ili kuondoa kasoro zilizojitokeza za watu wengi kuwa bado hawajahesabiwa katika muda wa siku saba uliopangwa awali.

Siku saba za awali kuanzia Jumapili ya Agosti 26 hadi Oktoba2, zilipangwa kutumika katika zoezi la sensa ya watu na makazi. Lakini kwa jinsi zoezi lilivyokwenda kufuatia k u j i t o k e z a k w a k a s o r o nyingi, inavyoonekana zoezi limeshindwa kufikia malengo.

Baadhi ya watu walinukuliwa wakisema kuwa hawako tayari kuhesabiwa kwa kuwa hata hayo maendeleo yanayoambiwa ndiyo sababu kubwa ya kuhesabiwa, hawayaoni zaidi ya kukithiri ugumu wa maisha, mfumko wa bei na wizi wa mali za umma.

Licha ya watu wengine kuamua kugomea zoez i kutokana na sababu mbalimbali, Waislamu nao walitangaza na mapema kugomea zoezi lenyewe na kutoa sababu za kufanya hivyo.

Kwa upande wa Waislamu, wao waliahidi kugomea sensa hii siku kadhaa kabla ya zoezi kuanza iwapo kipengele cha dini hakitakuwepo katika dodoso za sensa. Hoja ya Waislamu ni kwamba zimekuwepo kabrasha za kiserikali zilizochapishwa na kwenye mitandao ambazo tayari zilikuwa na takwimu za idadi ya Watanzania kwa dini zao. Takwimu hizo zimetiliwa mashaka kwamba si sahihi kwa kuwa hakukuwa na sensa ya idadi ya watu kwa dini zao tangu ile ya mwaka 1967, ambayo nayo ilichakachuliwa katika kipengele hicho.

Aidha Waislamu wanasema, kama takwimu za idadi ya watu kwa dini zao haina maana na inaweza kuwagawa watu, iweje serikali izitoe takwimu hizo kama ni hatari kwao na hazina maana? Pia Waislamu wanaona kuwa kujua idadi yao kwa kupitia sensa, itawarahisishia ibada zao nyingi tu ambazo zinahitaji idadi yao kitaifa. Hivyo madhali kuna zoezi la kitaifa la sensa, basi huo ungekuwa muda muafaka wa kupata takwimu sahihi.

Kwa upande wa serikali ilipinga hoja hiyo ya Waislamu kwa madai kuwa kufanya hivyo ni kuwagawa Watanzania kidini na sababu nyingine ya serikali ni kwamba sensa malengo yake ni kwa ajili ya kujua idadi ya Watanzania ili

Serikali itakuwa imejifunza jambo zoezi la SensaNa Haruna Abdul kuweza kupanga maendeleo,

na maendeleo yenyewe si kwa misingi ya kidini.

Kwa kuwa hoja za Waislamu zilipuuzwa, wakatangaza kugomea zoezi lenyewe nchi nzima. Lakini kwa kuwa serikali inaamini kuwa Waislamu wengi wanaunganishwa na BAKWATA, basi ikalitumia ‘Baa’ hilo kuhamasisha ushiriki wa Waislamu katika zoezi hilo, ikiamini kuwa Waislamu walio wengi ni watiifu kwa Baraza hilo kuliko taasisi nyingine.

Ha ta h ivyo , ku fua t i a Wa i s l a m u w a l i o w e n g i kutekeleza kwa vitendo mgomo wao, yamepatikana mafunzo matatu muhimu.

K w a n z a W a i s l a m u wana j i t ambua na wana msimamo imara. Wanamjua mwenye heri kwao na mwenye shari kwao. Wanatambua haki zao na wapi pa kuzipata.

Waislamu wa sasa wanahoji na kuamua mambo kama yana maslahi kwao au la, tofauti na siku za nyuma ambapo walikuwa hawahoji wala kuwa na nguvu ya kutoa msimamo wao zaidi ya kugugumia maumivu dhidi ya mambo yanayofanywa na serikali, ambayo inawakandamiza.

Kuna mifano iliyo wazi inayothibitisha maelezo haya. Baadhi ya mifano ni kama vile serikali kufanya mambo mengi ambayo kimsingi hayakuwa na maslahi kwa umma wote wa Watanzania zaidi ya sehemu tu ya watu wa itikadi fulani na Waislamu wakagugumia.

Kuvunjwa Mahakama ya Kadhi, chombo ambacho kilikuwa muhimu kiimani kwa Waislamu katika kutekeleza ibada zao. Licha ya katiba kutoa uhuru wa kuabudu, bado serikali kwa fikra za mtu mmoja na kwa maslahi yake, aliamuru kuvunjwa Mahakama ya Kadhi bila hata kuhoji Waislamu na Waislamu wakavumilia maumivu bila kuhoji wala kutoa msukumo kudai haki yao.

Tu c h u k u l i e k w a m b a uvunjwaji wa mahakama hizo ungefanyika leo, nini kingetokea? Bila shaka Waislamu wangehoji kwa nguvu zote umuhimu na sababu za msingi za kuchukuliwa hatua hiyo. Ni wazi kwamba wasingekubali.

Serikali ilivunja taasisi zote za Kiislamu ambazo zilikuwa na nguvu kama vile EAMWS na badala yake wakaundiwa BAKWATA, ambayo kimsingi sera na misimamo yake imeegemea zaidi kulinda maslahi ya serikali kuliko

WAISLAMU wakionesha umoja wao katika maandamano ya kupinga dhulma ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) baada ya baraza hilo kuwadhulumu wanafunzi Waislamu katika mitihani ya Kidato cha Sita 2012. Kwa umoja wao huo pia wamepinga zoezi la Sensa.

kuendeleza dini.Waislamu wa zama hizi

asilani wasingekubaliana na upuuzi huu.

Jambo j ingine ambalo lilifanywa na serikali dhidi ya Waislamu ni kuruhusu kuwepo ubalozi wa Vatican nchini, ubalozi ambao ni mahsusi kushughulikia masuala ya Wakristo Wakatoliki. Wakati hili linafanyika watawala, kuanzia Rais wa zamani hayati Mwalimu Julius Kambarage, alitutangazia kuwa nchi haina dini wala kufuata misingi ya kidini katika kuendesha shughuli zake.

Msimamo wa kususia zoezi la sensa uliotangazwa na taasisi karibu zote za Kiislamu ikiwemo hiyo BAKWATA, bila shaka serikali ilijawa na wasiwasi wa kutekelezwa msimamo huo ikiamini taasisi yenye nguvu na kuisikilizwa ni BAKWATA ambayo ipo chini ya himaya yake. Serikali ilijua kwamba msimamo huo wa taasisi za Kiislamu ungevunjika punde tu, baada ya kukutana wabia wao, viongozi wa taasisi wa BAKWATA hasa Mufti Issa Simba na jopo lake.

K w e l i p u n d e M u f t i Simba akatangaza kutengua msimamo wake alioutoa kwa Waislamu hapo awali na kukubaliana na matakwa ya serikali. Alifanya hivyo bila hata kuona haja ya kueleza sababu gani zimemfanya kubatilisha msimamo wake wa awali na wala hakuona sababu ya kuwahus isha

viongozi wenzake wa taasisi nyingine walioweka msimamo wa pamoja wa awali.

Bila shaka taasisi nyingine z i l i t a m b u a k u w a k u n a uwezekano mkubwa wa BAKWATA kubadilika wakati wowote kutokana na historia za viongozi wa baraza hilo.

Hili halikuwashtua na wakaende lea kubaki na msimamo wao ule ule wa Waislamu kutoshiriki zoezi la sensa iwapo marekebisho w a l i y o p e n d e k e z a hayatazingatiwa. Pia taasisi hizo zilijua nguvu yao kutoka kwa Waislamu katika miaka ya hivi karibuni.

Ni wazi serikali ilidhani k a m a Wa i s l a m u b i l a BAKWATA wanajidanganya, akina Ponda na Mohammed Issa , Kundecha hawana utii unaoweza kuwafanya Waislamu wampuuze Mufti Simba.

Serikali haikujua kuwa taasis i hizi mbadala wa BAKWATA sasa zimekuwa na kuimarika na kuaminiwa zaidi na umma wa Kiislamu.

L e o t u n a o n a k a m a wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutimiza azma ya Waislamu licha ya kuwepo propaganda za upotoshaji za kuwachangaya Waislamu juu ya sensa na jitihada za wanafiki.

Leo ser ikal i imeingia gharama kwa kuongeza muda wa zoezi la sensa wa siku saba zaidi, huku wakifahamu kampeni mbalimbali kwa

kuwatumia Masheikh maslahi na nguvu za dola na vitisho kujaribu kuzima msimamo wa Waislamu zimekwama.

Serikali imezoea kutumia nguvu za dola kuzima mambo mbalimbali yanayofanywa na taasisi za Kiislamu zisizounga mkono BAKWATA. Kwa mfano waliwahi kupigwa wanafunzi wa BASUTA eti kwasababu wameswali Idd kabla ya BAKWATA k u t a n g a z a k u o n e k a n a mwezi Shawal. Leo watu wanaoswali Idd isiyokuwa ya BAKWATA wameongezeka hivyo hakuna tena mweye ubavu wa kuwabughudhi.

Lakini kupitia zoezi hili, kuna haja ya serikali kujifunza j a m b o k a m a i t a h i t a j i . Kwa taasisi yao kongwe waliyoianzisha miaka zaidi ya 40 iliyopita imedhoofika na kupoteza maana ya kuwepo kwake. Lakini zaidi ni kwamba haiaminiwi na Waislamu walio wengi. Hakuna Muislamu wa kweli anayes ik i l i za Bakwata inasemaje. Hata hao Waislamu walioshiriki sensa, sio kwa kufuata kauli za Masheikh wa Bakwata bali kwa kuona tu washiriki kiserikali.

Yote hayo ni matokeo ya kuifanya taasisi hiyo kama idara ya serikali badala ya kuwa chombo cha Waislamu na kujiingiza zaidi katika kutetea maslahi ya serikali kama Baraza la Mawaziri badala ya kusimamia shida za Waislamu.

Page 15: ANNUUR 1033

15 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 7 - 13, 2012Habari

NECTA irekebishwe harakaInatoka Uk. 15

Issa.Alisema, Jumuiya na

Taaisi za Kiislamu nchini zipo katika mchakato wa kuikumbusha Serikali juu ya majibu ya Waislamu kuhusu NECTA, hivyo a l i w a t a k a Wa i s l a m u kuonyesha msimamo na kuitikia wito wa viongozi wao kama walivyoitikia katika kuigomea Sensa, p i n d i w a t a k a p o i t w a kulikabili Serikali dhidi ya NECTA.

Akizungumzia suala la Sensa, lililoanza Agosti 26, 2012, na kumalizika Ijumaa ya wiki iliyopita, kabla ya kuongezwa muda wa wiki moja mbele, ili kutoa nafasi kwa wale ambao hawaja hesabiwa, Sheikh Ponda alisema, kwa Sensa hii ni wazi, Tanzania ndio nchi ya kwanza kutoa Sensa ya ajabu duniani.

Alisema, mwitikio wa Waislamu ulikuwa mkubwa na kila mmoja ni shahidi na kwamba, kwa muda mrefu nchini haijawahi kutokea mshikamno ulionyeshwa na Waislamu kama katika tukio hili maana kila kona ya nchi Waislamu

wamesikika kuikataa Sensa.

Alisema, kitendo cha kuwakamata Waislamu k u w a p i g a n a h a t a kuwashikia mtutu wa bunduki i l i wakubal i kuhesabiwa, ni jambo ambalo halijawahi kutokea duniani kote, kwani alidai hata sheria zao za Sensa, zinataka karani kushawishi na si kushurutisha.

Alisema, baada ya kuona mambo magumu, Serikali imebidi kutumia magari ya polisi kuingia mitaani kukamata Waislamu, na kuwapeleka katika vituo vya Polisi kisha kuwaita makarani wa sensa kwa ajili kuwalizimisha kuhesabiwa, hata hivyo alidai zoezi hilo nalo limekuwa gumu.

“Kupitia zoezi hili la Sensa ni wazi kabisa Serikali iliyopo madarakani na Bakwata yake imeonyesha kuwa havitawali nyoyo za Waislamu bali inatawala viwiliwili vyao, jambo ambalo ni hatari, kwa kuwa

hawasikilizwi.” Alisema.A l i s e m a , n g u v u

i l i y o t u m i k a k u w a s h u r u t i s h a Waislamu na kuwafanyia madhila mbalimbli kwa kuwalazimisha kukubali kuhesabiwa baada ya kugoma, inadhihirisha ni jinsi gani Waislamu nchi hii ambavyo hawathaminiwi.

A l i s e m a , i m e p i t a migomo mikubwa nchini, kama vile mgomo wa Madaktari na Walimu, ambapo watu wamekufa na watoto wamekoseshwa haki zao za msingi za kusoma, lakini hakuna daktari wala mwalimu aliyepigwa au kukamatwa na kulazimishwa kwenda kazini.

“ R a i s ( K i k w e t e ) aliongea katika migomo ile kama binaadam, pamoja na Madaktari kufanya kitendo cha kinyama, watu walikufa kwa migomo yao, lakini walibembelezwa. R a i s a k i z u n g u m z i a msimamo wa Waislamu

kutoshiriki sensa, alitoa maneno mabaya sana huku akitoa agizo hatua kali zichukuliwe kwa Waislamu.” Alisema.

Alisema, moja ya faida iliyopatika katika zoezi hili la Sensa kwa Waislamu ni kuimarika kiimani, kwani alidai viongozi wa Jumuiya za Kiislamu wameliratibu zoezi hili kiimani zaidi.

A l i s e m a , k u p i t i a msimamo wa Waislamu ni kuwa neno ‘Islamu’ limesikika kwa asilimia mia moja ndani ya wiki moja ndani na nje ya Tanzania.

“Katika zoezi la Sensa, hakuna eneo lililotawala ndani na nje ya mipaka ya Tanzania kama Islamu, kila alipofikiwa Muislamu, alisema sisi au mimi ni Muislamu sihesabiwi. Kalma ya Mwenyezi M u n g u i m e s i k i k a . ” Alisema Ponda.

Adhabu kwa askari wa Marekani waliochoma moto Qur’ani yatangazwa

Inatoka Uk. 16

katika machafuko hayo. Hukumu hiyo dhaifu

iliyotolewa na mahakama ya Marekani dhidi ya wahalifu hao, pia huenda ikazusha upinzani na maandamano makubwa nchini Afghanistan na kwingineko.

Msemaji wa Rais Hamid Karzai wa Afghanistan, amesema ofisi ya kiongozi huyo inachunguza uamuzi uliochukuliwa juu ya askari hao wa Marekani na kutoa mtazamo wake kuhusu suala hilo hivi karibuni.

Aw a l i s e r i k a l i y a Afghanistan ilitoa wito wa

kupelekwa mahakamani a s k a r i w a M a r e k a n i waliochoma moto kitabu cha Qur’ani, ambapo Ofisi ya Rais Hamid Karzai ilitaka shirika la kijeshi la nchi za Magharibi N AT O k u w a f u n g u l i a mashitaka askari wa Marekani walioivunjia heshima Qur’ani na kuwahukumu katika mahakama ya wazi na ya kiadilifu.

A i d h a R a i s K a r z a i alimtaja afisa mmoja wa jeshi la Marekani kuwa ndiye aliyehusika na kitendo cha kuchomwa moto Qur’ani katika kituo cha anga cha Bagram.

NAIROBIWA L I M U w a s h u l e za umma nchini Kenya wameanza mgomo wao kwa nchi nzima mapema wiki hii wakilalamikia nyonyeza ya mishahara na mazingira duni ya kufanyia kazi.

Shule za Msing i na Sekondari zinazomilikiwa na serikali zimeanza muhula wa tatu Jumatatu ya wiki hii lakini walimu hawakufika katika maeneo yao ya kazi licha ya mahakama kutangaza siku ya Ijumaa kwamba mgomo huo si halali.

Ha ta h ivyo masomo yameanza vyema katika shule za kibinafsi. Chama cha Walimu nchini Kenya KNUT, kimesema walimu hawatorudi kazini hadi pale matakwa yao yatakapotekelezwa.

Walimu hao wanadai asilimia 300 ya nyongeza ya mishahara pamoja na kutekelezwa makubaliano ya mwaka 1997 yanayoitaka

Walimu Kenya waanza mgomo nchi nzima

serikali kuongeza marupurupu ya walimu.

W a n a f u n z i n a o wameingiwa na hofu kwani mitihani ya kitaifa katika shule za Msingi na Sekondari hufanyika katika muhula huu wa tatu.

WAZIRI Mkuu wa Kenya, Raila Odinga.

WAANDAMANAJI nchini Afghanistan wakipinga kuchomwa Qur'an na askari wa Marekani nchini humo.

Page 16: ANNUUR 1033

16 AN-NUURSHAWWAL 1433, IJUMAA SEPTEMBA 7 - 13, 2012

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

AN-NUUR16 SHAWWAL 1433, IJUMAA SEPT. 7-13 , 2012

BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) ni lazima l ifanyiwe marekebisho ili likidhi matarajio ya wananchi.

Hayo yamebainishwa na Sheikh Ponda Issa Ponda, akiongea na Waislamu mara baada ya swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Idrisa, Kariakoo Jijini Dar es Salaam, Ijumaa ya wiki iliyopita.

Sheikh Ponda, alikuwa akitoa tathmini na uhalisia wa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi, lililoanza Agosti 26, 2012, na msimamo wa Waislamu kwa ujumla na kuelezea nini kinachofuata kwa sasa.

Alisema kuwa Baraza hilo halina sura ya kitaifa na hata utendaji wake umelikosesha imani kwa wateja wake na hivyo, haliwezi kuachwa likabaki lilivyo.

Katika maelezo yake Ponda libainisha jinsi NECTA inavyohusika kutoa matokeo ya mitihani yasiyo halisi kwa maana yasiyowakilisha uwezo wa mwanafunzi halikadhalika makisi al izopewa na

NECTA irekebishwe haraka Na Bakari Mwakangwale wasahihishaji.Na kwamba kat ika

‘uchakachua j i ’ huo , w a n a o b a m i z w a n i wato to wa Ki is lamu kwa vile kamati maalum ya kutunuku madaraja imekuwa kama kitengo cha Parokia ya Kanisa.

Baraza la Mitihani la Taifa, limekuwa ni moja kati ya Taasisi za Kiserikali, ambazo Waislamu kwa muda mrefu wamekuwa wakililalamikia kuwa toka kuundwa kwake, mwaka 1973, limekuwa likiongozwa na Wakristo, na hivi karibuni kubainika kuwa kuna uchakachuaji wa mitihani ya wanafunzi wa Kiislamu.

“Lazima Baraza lile l i v u n j w e , n a w a l e w a n a o c h a k a c h u a maksi za watoto wa Ki is lamu waondoke , u m o j a t u l i o u t u m i a katika kuigomea Sensa ndio tutautumia katika kulisafisha Baraza la M i t i h a n i , B a k w a t a iacheni kama ilivyo maana imejidhirisha kuwa ni moja ya Taasisi za Serikali na si Taasisi ya Waislamu.” alisema Sheikh Ponda

KATIBU Mtendaji Baraza la Mitihani la Tanzania, Dk. Joyce Ndalichako. Inaendelea Uk. 15

MAHAKAMA ya Marekani imetangaza adhabu ya askar i wa jesh i lake waliochoma moto nakala za Qur’ani Tukufu mapema mwaka huu katika kituo cha anga cha Bagram huko Afghanistan.

Shir ika la habar i la Associated Press, limeripoti kuwa askari sita wa Marekani ambao walikana kuchoma kwa makusudi nakala hizo za Qur’ani Tukufu, mwishoni mwa wiki walitambuliwa na mahakama ya nchi hiyo kuwa hawana hatia na kwamba, watapewa adhabu ndogo ya kiidara.

Hata hivyo shirika hilo

Adhabu kwa askari wa Marekani waliochoma moto Qur’ani yatangazwa

la habar i la Marekani halikufafanua zaidi kuhusu kilichoitwa adhabu ya kiidara ni adhabu gani.

Kwa kawaida adhabu ya kiidara inahusisha adhabu za kushushwa cheo, kukatwa mshahara, kutoa ahadi ya kutorejea kosa au kufukuzwa jeshini.

Kitendo cha askari hao sita wa Marekani kuchoma moto nakala za ki tabu ki takat ifu cha Qur ’ani ki l izusha maandamano makubwa nchini Afghanistan na maeneo mengine duniani na watu kadhaa wakiwemo askari wa Marekani waliuawa

Inaendelea Uk. 15

www.tawheedtz.orgUnakuhimiza ufanye Ibada ya Hijja 2012Fanyeni Haraka Kuhiji. Maana Hajui Mmoja Wenu Kitakachomtokea – Ibn AbbasMkabala na Msikiti wa Makonde, Kariakoo, Dar es Salaam022 2182068; 0776 070770; 0719 689528

Mtandao wa Tawheed