ANNUUR 1147

17
ISSN 0856 - 3861 Na. 1147 DHUL-HIJJA , IJUMAA , OKTOBA 17-23, 2014 BEI TShs 500/=, Ksh s 50/= Sauti ya Waislamu www.annuurpapers.co.tz Uk. 8 MAALIM Seif Shariff Hamad amesema kuwa Katiba inayopendekezwa imepora mamlaka yote ya Zanzibar na kuyahamishia Dodoma, jambo ambalo halikubaliki. Kwa upande mwingine akasema kuwa, katiba hiyo imeweka vipengele ambavy o, dhahi ri 'Kufa kupona' sasa kuitetea Zanzibar Wasema Mzee Moyo, Mansour Tanganyika yazidi kuimarishwa... ‘Katiba ya Sitta’ itapora ardhi ya Z'bar- Maalim Seif  Wananchi wajiandae kusema ‘Hapana’  Nchi na Dola yenye mamlaka lazima  Njia pekee ya kudumisha muungano Na Mwandishi Maalum  MAALIM S eif Shari  Hamad. Inaendelea Uk. 4 Sheikh Msel em azirai gerezani Mwingine amuonyesha hakimu usaha Polisi bado wagoma kutoa PF3 Utetezi watinga Mahakama Kuu Innalillah wa inna ilaihir rajiuun: Tusubiri  yal iyo msibu Siad Bare, Wasomali  Haitawasibu viongozi tu, lakini…  Hata Masheikh waliokaa kimya  Kosa gani kafanya Sheikh Mselem?  Vipi italipwa dhulma hii kwa haki? SHEIKH Mselemu Ali  Mselem. ‘Mujahidina’ Shimon Elliot a.k.a Abu Bakr al-Qurashiy  MMOJA wa Waislamu anayetu humiwa kwa kesi ya ugaid i (mwenye kilemba ) akionyesha suruali yenye usaha sehemu iliyozungushiwa duara katika Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam juzi. Kushoto ni baad hi ya watuhumiwa wenzake. Uk. 16 Uk. 2 Uk. 3

Transcript of ANNUUR 1147

  • ISSN 0856 - 3861 Na. 1147 DHUL-HIJJA, IJUMAA , OKTOBA 17-23, 2014 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

    Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz

    Uk. 8

    MAALIM Seif Shariff Hamad amesema kuwa Katiba inayopendekezwa imepora mamlaka yote ya Zanzibar na kuyahamishia Dodoma, jambo ambalo halikubaliki.

    Kwa upande mwingine akasema kuwa, katiba hiyo imeweka vipengele a m b a v y o , d h a h i r i

    'Kufa kupona' sasakuitetea Zanzibar

    Wasema Mzee Moyo, MansourTanganyika yazidi kuimarishwa...

    Katiba ya Sitta itaporaardhi ya Z'bar-Maalim Seif Wananchi wajiandae kusema Hapana Nchi na Dola yenye mamlaka lazima Njia pekee ya kudumisha muunganoNa Mwandishi Maalum

    MAALIM Seif Shariff Hamad.

    Inaendelea Uk. 4

    Sheikh Mselem azirai gerezani

    Mwingine amuonyesha hakimu usahaPolisi bado wagoma kutoa PF3Utetezi watinga Mahakama Kuu

    Innalillah wa inna ilaihir rajiuun:Tusubiri yaliyomsibuSiad Bare, Wasomali Haitawasibu viongozi tu, lakini Hata Masheikh waliokaa kimya Kosa gani kafanya Sheikh Mselem? Vipi italipwa dhulma hii kwa haki?

    SHEIKH Mselemu Ali Mselem.

    Mujahidina Shimon Elliota.k.a Abu Bakr al-Qurashiy

    MMOJA wa Waislamu anayetuhumiwa kwa kesi ya ugaidi (mwenye kilemba) akionyesha suruali yenye usaha sehemu iliyozungushiwa duara katika Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam juzi. Kushoto ni baadhi ya watuhumiwa wenzake.

    Uk. 16

    Uk. 2Uk. 3

  • 2 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 17-23, 2014AN-NUUR

    S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.

    www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected] zetu zipo: Manzese Tip Top

    Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

    Tahariri/Tangazo

    MUSLIM UNIVERSITY OF MOROGOROP.O. BOX 1031 Morogoro, Tanzania.

    Tel: +255 23 2600256; Fax: +255 23 2600286Website: www.mum.ac.tz, E-mail address: [email protected]

    SEVENTH GRADUATION CEREMONY FOR UNDERGRADUATE DEGREES AND CERTIFICATES

    CONFERMENT 2014The seventh graduation ceremony will be held at the campus of the Muslim University of Morogoro on SATURDAY, 8th November, 2014. The ceremony is expected to start at 2.00 pm and end at 5.30 pm.

    Students eligible to attend the ceremony are undergraduates and certificates students who successfully completed their studies in 2014.

    Parents, relatives and guests of the students as well as interested members of the general public are welcome to attend the graduation ceremony at the playground. Guests are expected to dress modestly and decently. Lady guests attending the ceremony are advised to wear the hijab or any dress that does not expose the body other than the face, hands and feet.

    All eligible students are requested to attend the occasion, regardless of whether or not they bring guests. However, they must inform the office of DVC (Academic) of their intent to participate in the ceremony NOT LATER THAN 1st November, 2014.Preferably call Mobile No: 0712 - 277598

    Academic costumes (gowns, hoods and caps) are available for hire by the graduands starting from 1st to 7th November 2014.The University cashiers office must receive from each of the participating students a total of Tsh. 40,000 (Ts. 20,000 for hiring the costumes, Ts. 10,000 deposit security which is refundable, and Ts. 10,000 convocation fee).

    Graduands, who do not have costumes on, will not be allowed to participate in the Ceremony.

    Strictly, we shall not issue Academic costumes on the Graduation day, each and every Graduand shall have his/her gowns between 1st and 7th November, 2014.

    Graduands are required to bear in mind that the hired gowns shall have to be returned after the ceremony. A heavy fine will be imposed in case the costumes are damaged, or not returned and/or in time. A hiring Contract Form will be provided for completion by those intending to hire the costumes.

    For the safety of all participants and their guests, close-up picture taking and video recording near the stage is restricted.

    REHEARSALSince the rehearsal is an integral part of the ceremony, all graduands who wish to attend the graduation ceremony MUST attend the rehearsal which is scheduled on Saturday morning (8th November, 2014) at 8.30 at the graduation site. Failure to attend rehearsals by students will result in to such students graduating in absence which implies they will not be official presented to the guest of honor.

    Certificates and transcripts of the graduands will not be given at the ceremony. These can be received at another convenient day from the Office of the DVC (Academic) upon signing register books and presenting an ID card.

    K.K. KONDODEPUTY VICE CHANCELLOR (ACADEMIC)

    SIKUFIKIRIA wala kuwaza kuwa Wairaki ni binadamu. Anasema Steven Green, askari wa Marekani aliyembaka binti wa miaka 14 wa Iraq na kisha kumuuwa yeye na wazazi wake.

    An Iraq War veteran serving five life terms for raping and killing a 14-year-old Iraqi girl and killing her parents and sister, says he didn't think of Iraqi civilians as humans. (Daily Mail)

    Limeripoti gazeti la Daily Mail ikimaanisha kuwa askari Steven Green (former 101st Airborne soldier), wakati akimbaka binti Muislamu wa Iraq wa miaka 14 na kisha kumuuwa pamoja na kuwauwa wazazi wake na dada yake, hakuwa akiwaza kuwa watu hao ni binadamu.

    Ilikuwa ni mwaka 2006 al ipofanya ukati l i na unyama huo kumbaka na kisha kumuuwa Abeer Qassim al-Janabi, katika eneo la Mahmoudiya, Iraq.

    Mbakaji na muuwaji huyo aliyasema hayo kama utetezi wake ili asipewe adhabu ya kunyongwa akisema kuwa mafunzo a l iyopewa ya kuuwa na uzoefu aliopata wa kuuwa bila ya kuwa na huruma kule Iraq katika kile alichokiita Triangle of Death, alikuwa kama mtu aliyepata wazimu aliyetokwa na ubinadamu kabisa.

    Ukipita barabara ya Mwenge-Tegeta, daraja la kwanza kukutana nalo ni la Mlalakuwa. Ukilitizama, hapana shaka litakupelekea kuwaza kuwa hiyo ni alama na mfano mmoja tu wa mafanikio makubwa aliyopata Rais Jakaya Mrisho Kikwete, na kwa hakika atakumbukwa k w a m e n g i m a z u r i y a k i w e m o h a y a y a ujenzi wa barabara. Yapo maelezo kuwa barabara alizojenga, ukipima kwa

    Innalillah wa inna ilaihir rajiuun:

    Tusubiri yaliyomsibuSiad Bare, Wasomali

    kilometa, ni zaidi ya barabara zote kwa ujumla zilizojengwa na marais wote waliomtangulia.

    Hata hivyo, unapofikiria mafanikio haya ya serikali ya Mheshimiwa Rais Kikwete na kutabasamu, mara nafsi inapiga kiza, ikaingia huzuni na furaha yote kutoweka inapokujia video ya hali iliyomkuta S h e i k h M s e l e m j u z i Jumatano alipoanguka pale nje ya gereza la Segerea na kuzirai wakati akitolewa kupelekwa mahakamani. Wakati tukiandika maoni h a y a , b a d o i l i k u w a haijajulikana hali yake inaendeleaje na kama alipelekwa hospitali au la.

    M a e l e z o y a l i y o p o ni kuwa hii si mara ya kwanza Sheikh Msellem kuanguka na kuzimia na hii ni kutokana na maradhi na kunyimwa matibabu. Mpaka juzi wakat i wanaf ik ishwa mahakamani, Sheikh huyo pamoja na watuhumiwa w e n z a k e w a l i k u w a hawajapatiwa matibabu na taarifa i l iyotolewa na hakimu ilidai kuwa fomu za kuwaruhusu k u p e l e k wa h o s p i t a l i zilikuwa hazijachukuliwa na mamlaka husika hapo mahakamani.

    Ukiacha maradhi ya kawaida, kama malaria na mengine ambayo, ama watuhumiwa waliingia n a y o r u m a n d e a u waliyapata wakiwa huko katika hali ya kawaida tu ya kibinadamu, lakini yapo maradhi mengine na mgogoro wa kiafya a m b a y o wa m e d a i wa kuyapata kutokana na mateso waliyokumbana nayo wakiwa mikononi mwa vyombo vya Dola. Japo mambo mengine ni ya aibu na shida kutamkika hadharani, lakini baadhi ya watuhumiwa walikuwa na ujasiri wa kusema mbele ya mahakama waliyotendewa yakiwemo ya kufanyiwa

    vitendo vya kihabithi vya Kaumu Lut pamoja na kutiwa majiti sehemu zao za siri.

    Ilivyo katika ulimwengu wa k i s t a a r a b u , h a t a mtuhumiwa wa uhaini ana haki zake za kibinadamu a m b a z o a n a s t a h i k i kutekelezewa. Tuhuma au uhalifu wake hauondoi ubinadamu wake. Kwa hiyo, hata kama tukijaaliya kuwa watuhumiwa hao wana kesi ya kuj ibu, hatudhani kuwa tuhuma hizo zinahalalisha mateso waliyodai kufanyiwa au kunyimwa matibabu.

    Tu n a v y o a m i n i s i s i ni kuwa kama Sheikh Msellem ana kosa la kujibu au yupo ndani kwa sababu za kisiasa za ndani ya nchi ama zile za nje au zote mbili kwa pamoja, viongozi wetu wanajua kwa uhakika.

    Wasiwasi wetu upo katika sehemu moja tu: kama tuhuma zinazomkabili, h a z i n a m s i n g i , n a n i atalipa dhulma hii? Ni muda mfupi tu Sheikh Msellem na Masheikh wenzake wametoka jela baada ya kukaa rumande kwa zaidi ya miaka miwili, bila ya kesi yao kusikilizwa wala kuhukumiwa jambo linalojenga tuhuma kuwa

    wal ikuwa ndani kwa sababu za kisiasa au kesi za kupanga.

    Yapo maelezo kuwa yanayotokea Somalia, ni kutokana na laana au kipigo kutoka kwa Allah kutokana na dhulma iliyofanyika huko nyuma na jamii haikuchukua hatua za kuikanya. Inaelezwa kuwa al iyekuwa Rais wa nchi hiyo Siad Bare alikuwa akiuwa na kutesa Masheikh aliowatuhumu k u wa wa n a h a t a r i s h a masilahi yake ya kisiasa. Dhulma na mauwaji hayo yakifanyika, Maseikh waliokuwa vipenzi wa serikali hawakufunua mdomo kusema. Jamii nayo ya Waislamu Somalia, ilijikuta ikipuuza ile kanuni muhimu kat ika jamii kuwa watu wamsaidie mwenye kudhulumiwa halikadhalika wamsaidie dha l imu kwa kumpa nasaha na kumkanya kuacha dhulma. Nini matokeo yake?

    Quran inasema kuwa watu waogope adhabu ya duniani ambayo ikija haitawathubutikia wale tu waliodhulumu nafsi zao, bali hata waliokaa kimya, wasiwakanye. Sote, tunajua ki l ichomsibu Bare na

    waliofuatia katika viongozi wa serikali ya Somalia na hata yanayoendelea kuwasibu Wasomali hivi sasa.

    Wa k a z i w a M t o n i Kidatu, hasa waumini wa Masjid Sahaba, waliokuwa wakihudhuria Darsa za Quran za Sheikh Msellem Ali Msellem, je, inaweza k u w a p i t i k i a a k i l i n i kuwa Mfasiri huyo wa Quran anaweza kufanya japo sehemu tu ya hayo anayotuhumiwa kwayo?

    Masheikh wetu wa Zanzibar na Bara, hapana shaka wanamjua vyema Sheikh Msellem na ufahamu wake juu ya Kitabu cha Allah na Uislamu kwa u j u m l a , j e , wa k i k a a inaweza kuwapi t ik ia katika akili zao kuwa Sheikh mwenzao huyo, anaweza kuporomoka kiasi cha kufanya vitendo vya kigaidi, kwa maana ya kupanga kuuwa watu wasio na hatia kwa sababu zozote zile?

    Na kama nilivyotangulia kusema, viongozi wetu wa kisiasa, wakitaka kujua ukweli, wana namna zao za kujua ukweli, tena kwa uhakika, kama mtuhumiwa

    Inaendelea Uk. 3

  • 3 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 17-23, 2014Habari/Tangazo

    'Kufa kupona' sasa kuitetea ZanzibarJOTO la kisiasa limepanda Zanzibar huku likitawaliwa na suala la Katiba inayopendekezwa.

    K u p a n d a k wa j o t o h i l o kunadhihirisha jambo moja kuwa, licha ya katiba hiyo kupitishwa kwa mbwembwe Dodoma na kutangazwa kuwa ni ushindi, hali si shwari.

    Wale wajumbe waliojinadi ndani ya Bunge hilo kuwa wao ndio wawakilishi wa Wazanzibari, na waliwakilisha mawazo na matakwa yao hadi kupatikana katiba hiyo, hali halisi inaonyesha vingine.

    Mitaani watu wanagugumia wakiwaona wasaliti, huku watu mashuhuri katika siasa za Zanzibar wakijitokeza kupingana nao.

    M m o j a wa wa t u h a o n i Mwenyeki t i wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar,Mzee Nassor Moyo aliyesema kuwa Wazanzibar waliungana na Tanganyika kwa hiari yao hivyo hakuna mtu yeyote wa kuwalazimisha kufanya mambo yanayokwenda kinyume na matakwa ya Wazanzibar.

    Ameyasema hayo Mzee Moyo hoja ya muungano wa serikai tatu kuzimwa na kupitishwa mfumo wa serikali mbili ukiwa umeboreshwa zaidi kwa kupora na kumega zaidi madaraka ya Zanzibar ikibaki kinadharia nchi, yenye Rais, lakini kisheria na kikatiba, mkoa au sehemu ya Tanzania.

    Kwa upande mwingine, Mjumbe wa kamati hiyo ya maridhiano Mansour Yussuf Himid, yeye alisema kuwa ataendelea kuitetea Zanzibar popote na bila ya kuogopa mpaka Zanzibar ipate mamlaka yake kamili.

    Alisema kuwa ataendelea kupinga mfumo wa muungano wa CCM mpaka siku ya kiama kwani ni muungano uliojaa ukatili dhidi ya Wazanzibar.

    Akijiapiza kulifanya hilo bila ya woga, Mansour alisema kuwa, kufa kila nafsi itaonja mauti, kwa hiyo hakuna kuogopa chochote katika kuipigania Zanzibar.

    Ki l ichobakia ni kuingia mitaani kuwambia Wazanzibar wasikubali kuipitisha katiba hiyo. Alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema.

    Nasaha na maoni ya wakongwe hao wa siasa za Zanzibar, walizitoa katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kibanda mait i , mwishoni mwa wiki iliyopita.

    Awali Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Sa l im Abdallah Bimani alisema kuwa rasimu inayopendekezwa sio ya Wazanzibar na haitofika Zanzibar, bali itaishia Kisiwa cha Chumbe .

    A k a wa t a k a Wa z a n z i b a r i kuungana pamoja na kuikataa kwa nguvu zote rasimu ya Chenge na wenzake kwani, kama alivyodai,

    Na Mwandishi Wetu imekuja kuiangamiza Zanzibar.Wakati huo huo, Jaji Warioba

    ameonyesha wasiwasi wake juu ya hatma ya muungano kutokana na mambo yaliyoingizwa katika Katiba yakipingana na hali halisi ya siasa za Zanzibar.

    Akiongea na baadhi ya vyombo vya habari Jaji Warioba alisema kuwa Katiba inayopendekezwa imeendelea kuivisha Tanganyika koti la Muunganio, bali na kuliboresha zaidi.

    Alitoa mfano kuwa kwa kuweka suala la kodi ya mapato, ushuru

    wa forodha na bidhaa katika mambo ya muungano, ambayo maana yake ni kwamba kodi yote inayokusanywa, ikiwamo ya kutoka Zanzibar itaingizwa kwenye mfuko wa muungano, kutazidi tu kuimarisha tatizo la Tanganyika kuvaa koti la Muungano.

    Alisema, ni jambo la kushangaza Zanzibar imepewa uwezo wa kusimamia mambo yake yenyewe na ili iweze kulitekeleza hilo ni lazima iwe na vyanzo vyake vya mapato. Sasa watasimamiaje

    wakati mapato yote yanaingia kwenye mfuko wa muungano.

    Akifafanua zaidi alisema kuwa kwa jinsi ilivyo sasa Katiba ya Zanzibar, hakuna namna ya Katiba inayopendekezwa inaweza kutekelezeka mpaka i le ya Zanzibar ibadilishwe.

    Na kwa maana hiyo, itakuwa pia vigumu kupata theluthi mbili ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitisha mabadiliko hayo, ambayo kimsingi hayatatui kero ya Tanganyika kuvaa koti la Muungano, bali kuiimarisha zaidi.

    Tusubiri yaliyomsibu Siad Bare, WasomaliInatoka Uk. 2Sheikh Msellem, kuna sababu za kutosha kumtia katika tuhuma za ugaidi au la.

    Hoja yetu hapa sio kuhoji sheria wala kuingilia taratibu za kimahakama. Wala hoja sio kupinga kuwa kuna watu wanaweza kufanya vitendo vya kigadi. Wapo watu kweli walistahiki tuhuma hizo, lakini yaweza pia kuwa wapo waliokumbwa tu na mkumbo. Aidha, kama tunavyojua, Sheria iliyopo ya kupambana na ugaidi inampa nguvu, ruhusa na uhalali afisa wa polisi au chombo husika cha dola, kuwa akimtuhumu mtu kwa ugaidi, hata akimdhuru ikiwemo hata kutoa uhai wake, kuharibu afya yake kwa mateso au kuharibu mali yake, hawezi kushitakiwa mahakani, muda wa kuwa amesema kuwa alimdhania ni gaidi au anakusudia kufanya vitendo vya kigaidi.

    Kwa hiyo, inaweza kuwa yanayofanyika hivi sasa dhidi ya Sheikh Msellem yapo ndani ya sheria kwa mujibu wa sheria husika iliyotokana na USA PATRIOT Act (Uniting and Strengthening America by Providing Appropriate Tools Required to Intercept and Obstruct Terrorism Act of 2001.)

    Kwa hiyo, tunachoomba hapa ni kuruhusu ubinadamu wetu kutawala katika jambo hili. Yule askari Steven Green aliyembaka Abeer Qassim al-Janabi, na kisha kumuuwa alisema, 'I was crazy. I Didn't Think of Iraqis as Humans.

    Imani yetu ni kuwa sisi kama jami i , kama b inadamu wa Zanzibar na Tanzania Bara, sio crazy, wala hatujapandwa na shetani wa aina yoyote kututoa ubinadamu na utu wetu. Ila tukiruhusu matendo ya kinyama na kishenzi kama haya wanayodai kufanyiwa akina Sheikh Farid, bila kukemewa, nafsi zitaota kutu, zitazoeya na hatimaye tutaona si mambo mabaya. Tutakuwa sawa na yule muuwaji aliyedhani kuwa binadamu wenzake hawana uhai wala damu kama yeye.

    Tu z i n g a t i e k u wa d a m u ,

    heshma na uhai wa mtu ni vitu vitakatifu. Kamwe dua ya mwenye kudhulumiwa haianguki patupu. Turejee historia, tuangalie, nini ilikuwa hatma ya dhulma.

    Twaweza kujidanganya kuwa tunatekeleza sheria, lakini tujue pia kuwa ipo Siku ya Malipo. Yupo Mfalme wa Siku ya Malipo.

    Na Quran inasema: Je , hakuwa Mola wako ni Hakimu wa Mahakimu?

    Nimalizie kwa kukariri kuwa ile kuwa tuna sheria ya kupambana na ugaidi inayoweza kuruhusu

    kufanyika wanayofanyiwa Sheikh Msellem na wenzake, haitakuwa utetezi mbele ya Hakimu wa Mahakimu na Mfalme Siku ya Malipo.

    Kinachoweza kutunusuru ni kuupa nafasi ubinadamu wetu kufanya kazi na kujiuliza iwapo tunayowafanyia wenzetu, ni sahihi?

    Je, kuna ukweli juu ya tuhuma zinazowakabili? Na hata kama tuhuma hizo ni kweli, ubinadamu unatuelekeza tuwatendee vipi?

    Sifa na masharti ya kujiunga Muombaji atimize sifa na masharti yafuatayo:(i) Awe Muislamu aliye tayari kuishi Kiislamu(ii) Awe anajua kusoma Quran kwa ufasaha.(iii) Awe amemaliza juzuu ya 1 na 2 ya Maarifa ya

    Uislamu, Darasa la Watu Wazima kabla ya kujiunga.(iv) Awe na uwezo wa kusoma na kuandika lugha ya

    Kiswahili kwa ufasaha.(v) Awe amehitimu darasa la saba au kidato cha nne

    na awe anafundisha madrasa au kipindi cha dini katika shule za Msingi au Sekondari. Patakuwanausaili namtihani siku ya tarehe

    29/11/2014 saa 2:00 asubuhi katika chuo cha Ubungo na Kirinjiko na katika vituo mbalimbali vya mitihani kote nchini. Mwishowakuchukuafomunitarehe28/11/2014. Fomuinalipiwashilingi5,000/-tu.

    Fomu zinapatikana katika vituo vilivyoorodheshwa ukurasawa15wagazetihili.

    MKURUGENZI

    ISLAMIC PROPAGATION CENTRE

    NAFASI ZA KUJIUNGA NA KOZI FUPI YA UALIMU KATIKA VYUO VYA UBUNGO NA KIRINJIKO-2015

  • 4 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 17-23, 2014Makala

    KAMA wajuavyo Watanzania wote, Alhamisi iliyopita Bunge Maalum la Katiba lilipigia kura ya kuipitisha rasimu ya katiba, ambayo hatimaye watapelekewa Watanzania kwa ajili ya kura ya maoni, na ambayo sasa tunaambiwa kuwa itafanyika kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

    R a s i m u h i y o ya K a t i b a ilipokelewa kwa shangwe na nderemo ndani ya kuta za ukumbi wa bunge. Ndani ya shangwe hizo, mulikuwa na mambo ya kumtafishi mtu ya l iyovungwavungwa kwenye nyimbo na kupongezana kinafiki kwa marafiki wa kitambo, pamoja na hotuba zilizodhamiria kujenga hofu miongoni mwa wale wote wanaothubutu kupinga.

    Lau ungeliisimamisha vidio ya yaliyotokea kwenye ukumbi ule siku hiyo, ukazivuta kwa karibu picha za wahusika mmoja baada ya mwengine na kisha kuichunguza kila moja kwa undani, mithali ya vile mwanasayansi amchunguzavyo bakteria kwenye kioo cha kukuzia picha cha maabara, ungeliona makubwa zaidi ya yaliyoshuhudiwa kwenye ukumbi. Kwamba ungeliona khofu na uharaka ambavyo viliutanda mchakato huu mzima wa mashujaa wetu.

    Lakini kwa nini kuna khofu na wasiwasi wa kiasi hiki? Nilijiuliza huku nikiwa nimekaa naangalia mkasa ule kwa mashaka na ikanipitikia kwamba khofu hizi zinatokana na hali ya kutengwa kwa mashujaa wetu, yaani Chama tawala cha Mapinduzi (CCM) licha ya kujuwa pasina na tone la shaka kwamba Rasimu hiyo ya Katiba iliandikwa nao CCM, ikajadiliwa nao CCM na kupitishwa na wao wenyewe CCM.

    Hoja nyengine zote kinyume na zile za CCM aidha zilitupiliwa m b a l i , a u k u p o n d w a a u kulazimishwa zishindwe kabisa. Matokeo ya siasa za utengano ni hali ya kutengwa, na gharama ambayo CCM itapaswa kulipa kwa kumuuzia roho yake jini huyo wa siasa za utengano ni kuishi kwenye hali ya wasiwasi na khofu.

    Matokeo yake ni kuwa endapo nasi tutataka kutikisa mapiringiti ya miili yetu kucheza ngoma ya CCM kwa maslahi tu ya kuonesha kuwa tunaiunga mkono, basi tutakuwa tu maadui na sio raia wa nchi hii wanaostahiki heshima ya chama hiki.

    Ukiivuta kwa ukaribu zaidi picha ya vidio ile ukumbini Dodoma na ukaanza kuwachunguza wapigadebe waliomo, utaona khofu zao pia. Kama ilivyo CCM, nami pia ninawafahamu wapigadebe wasio majina ambao waliipigia kura ya Ndio Rasimu ya Katiba ya CCM, kwa sababu wanajuwa kuwa ni maamuma tu, ambao bila ya makombo yatakayodondoka kutoka Meza Kuu, watakufa njaa. Lakini kinyume na CCM, mimi silazimiki kikatiba kuwataja wale waliopigia

    Sauti ya Zanzibar lazima isikizweFatma Karumekura Rasimu hiyo.

    Ndipo hapo sote mimi na wao tunapojikuta tumeganda kwenye nakama iliyoumbwa kwa khofu tukiwa tunaogopa kusema, tunaogopa kupiga kura, tunaogopa hata kuonesha hisia zetu; na baya zaidi tuna khofu mno kiasi cha kwamba tunaogopa hata kuandika maoni yetu ambayo yatatuweka huru na utumwa huu wa khofu tuliojitia. Wakati huo huo, tunaambiwa na tunajidai kukubali kwa lengo la kuwashawishi walioko nje ya nchi waamini kuwa eti hii ni nchi ya amani. Mimi nasema, si kweli.

    Si kweli kwamba hii ni nchi ya amani. Badala yake hii ni nchi iliyolemazwa kwa khofu na woga, aidha ambayo chini ya mvungu wake kumelala ghadhabu ambazo zinajijenga taratibu lakini kwa uhakika. Mara ya mwisho, Watanzania walipohisi ghadhabu kama hizo, Mwalimu Nyerere alistaafu uraisi. Pamoja na yote, Mwalimu alikuwa ameweka kidole chake kwenye mshipa unaoratibu mapigo ya moyo wa Tanzania, na kwa hivyo aliweza kuzihisi ghadhabu hizo na akajuwa kuwa Watanzania walitaka mabadiliko. Naye, kwa hivyo, kwa njia za amani kabisa, akakabidhisha hatamu za utawala kwa wengine.

    Kwangu mimi, Jaji Mstaafu Joseph Warioba anafahamu hili na kama ilivyo kwa (aliyekuwa) Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud, naye ni mtu ambaye hakuiruhusu khofu kumuamulia njia ya kupita. Wote wawili wamechagua njia ya heshima badala ya khofu.

    Khofu ya CCM imetawaliwa na hali ya kutengwa; khofu ya upinzani imetawaliwa na mapigo; khofu yetu inatawaliwa na uelewa kwamba licha ya uhuru wa kinadharia wa mahakama, tunaishi na kufanya kazi kwenye nchi ambako kuna hali ya wazi kabisa ya wateule wachache kutokuguswa na mkono wa sheria. Sasa inakuwaje chama ambacho kimetengwa kinaweza kupata ushindi wa theluthi mbili za kura za maoni zinazohitajika kupitisha Rasimu ya Katiba visiwani Zanzibar? Nimeambiwa kwamba kuna njia rahisi sana lakini yenye ufanisi mkubwa kuweza kufanya hivyo. Hivyo, nami nachangiana nanyi nadharia hiyo, ikiwa mngelipenda kujua.

    Kuna tume mbili za uchaguzi ambazo zina dhamana ya upigaji kura Zanzibar, yaani Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC). NEC huandikisha watu wote wanaoishi Zanzibar kwa ajili ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ZEC huandikisha Wazanzibari pekee, ambao wana haki ya kupiga kura

    kwa ajili ya Rais wa Zanzibar. Nadharia inasema kwamba, tafsiri ya Mzanzibari kwa ajili ya kura ya maoni ya kupitisha Rasimu ya Katiba itatanuliwa na kuwajumuisha wote ambao wameandikishwa na NEC na wanaodai kuwa ni Wazanzibari.

    Hilo ni licha ya ukweli kwamba kuna sheria visiwani Zanzibar ambayo inamuelezea hasa Mzanzibari ni nani. Kwa hivyo, kinadharia Watanzania wanaodai kuwa Wazanzibari, popote walipo watakuwa na haki ya kupiga kura ya maoni kama Wazanzibari. Bila ya shaka, utakubaliana nami kwamba hii ni nadharia nyepesi na yenye ufanisi kweli kwa sababu ghafla moja sauti ya Wazanzibari milioni 1.2 itamezwa kwenye tarumbeta la Watanzania milioni 44. Lakini hatimaye CCM italazimika kuwatawala Wazanzibari milioni 1.2 visiwani Zanzibar na kuizamisha sauti yao kwa muda kutaongeza tu hisia za kutoridhika na hali ya wasiwasi.

    Mimi nilipiga kura kwenye uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995, na nikaishi kuushuhudia ufukara, utengano na ukosefu wa furaha ulioundwa na kile kilichoonekana kuwa

    mpasuko wa kisiasa usiozibika, ambao uliwagawa Wazanzibari. Mpasuko huu ulizibwa mwaka 2010 pale tulipoanzisha mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar. Sitaki kamwe kuja kuona muongo mwengine ukipotezwa kwenye siasa za utengano zitakazoumba mpasuko tena kati ya Wazanzibari na Watanzania Bara.

    Kinyume na i l ivyokuwa kwenye Bunge Maalum la Katiba, Wazanzibari wanastahiki kuwa na kauli kwenye kura ya maoni. Ikiwa hatukubaliani na CCM, kuweni na uthubutu na heshima ya kukubali ukweli huo na fanyeni mabadiliko ambayo yatatupelekea kwenye Tanzania bora zaidi isiyoendeshwa kwa khofu na vitisho, bali inayoendeshwa kwa ushiriki na utayarifu wa kubadilika.

    Naweza kuonekana mtu mwenye usungo, lakini kwa hakika naamini kwamba demokrasia ndio mfumo bora kabisa wa utawala.

    (Makala hii kama ilivyopatikana katika mtandao, ni Tafsiri ya Mohammed Ghassani kutoka makala iliyoandikwa kwa Kiingereza na Fatma Karume na kuchapishwa na gazeti la The Citizen la Tanzania la tarehe 7 Oktoba 2014 ikiwa na kichwa cha habari: FATMA KARUME: Zanzibaris deserve say in referendum)

    Katiba ya Sitta itapora ardhi ya Z'barInatoka Uk. 1vinadhamira ya kupora ardhi ya Zanzibar na kuipeleka Tanganyika iliyovaa koti la muungano.

    Hata hivyo, Maalim Seif aliye Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar , amewaambia wananchi wa Zanzibar wasiwe na wasiwasi kuhusu Katiba hiyo inayopendekezwa, kwani wao ndio waamuzi wa mwisho na wana uwezo wa kuikwamisha.

    A l i ya s e m a h a y o wa k a t i akiongea na maelfu ya Wazanzibar katika viwanja vya Kibanda Maiti visiwani humo Jumapili iliyopita.

    Akiongelea suala la Rais wa Jamhuri ya Muungano kuwa na mamlaka ya kuteuwa Wakuu wa Mikoa na Wi laya kwa upande wa Zanzibar, alisema hatakuja kushangaa kumuona Rais wa Jamhuri ya Muungano anamchagua mtu Bukoba akawe Mkuu wa Mkoa katika mkoa kule Zanzibar.

    Akasema, jambo halo kamwe hali takubalika ndio maana wanapigania Zanzibar yenye mamlaka yake.

    Akizungumza katika mkutano huo , Maal im Se i f a l i sema kuwa, hakuna namna katiba inayopendekezwa itapita katika kura za maoni, labda kama matokeo yatachakachuliwa.

    Hata hivyo akaongeza kuwa na hata kama hiyo itatokea,

    basi kutakuwa na mgogoro wa kikatiba kwa sababu Katiba ya Tanzania inayopendekezwa haiwezi kutekelezwa sambamba na katiba ya Zanzibar.

    Akasema, itakuwa ni ndoto kwa Zanzibar kubadili Katiba yake, hasa kwa vile CCM kwenye Baraza la Wawakili Zanzibar hawapati theluthi mbili ya wajumbe.

    Maalim Seif Sharif Hamad katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika uwanja wa Kibanda Maiti Mjini Zanzibar, alisema rasimu hiyo imekosa uhalali wa wananchi kwa sababu ni ya CCM pekee badala ya ile inayotokana na maoni ya wananchi kama yalivyo katika rasimu ya Jaji Warioba.

    Katiba yenu (CCM) mnaitunga wenyewe, wameijadili wenyewe, wameipi t i sha wenyewe na wameichezea ngoma wenyewe, a l isema Maal im Sei f huku akishangiliwa na maefu ya wananchi.

    A l i s e m a k u w a r a s i m u inayopendekezwa na Bunge la Katiba imeinyanganya mamlaka yake Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa lengo la kulinda maslahi ya CCM na kupora mamlaka ya Zanzibar kuyahamishia Dodoma.

    Katika hali hiyo, haitakuwa katiba ya wananchi wa Zanzibar kwa sababu haikuzingat ia matakwa na maoni yao na hivyo lazima ipingwe.

  • 5 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 17-23, 2014Habari

    TAASISI isiyo ya Kiserikali ya Muqaddam Foundation, i m e s e m a i p o m b i o n i kuwawezesha watoto yatima, w a j a n e , w a l e m a v u n a wajasiriamali kujikwamua na umasikini.

    Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Bw. Kamaldeen Hussein M u c c a d a m , a l i p o k u w a akiongea na makundi hayo k a t i k a s h u l e ya m s i n g i Mchikichini, Ilala Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

    Al i se m a , Ta a s i s i ya k e imej ipanga kwa kuja na mikakati ya kuipunguzia j a m i i k e r o m b a l i m b a l i zinazowafanya waendelee kuwa masikini.

    Tumejipanga kushughulikia

    MSOMI na mtaalamu wa masuala ya kisiasa na dini ya Kislamu, Profesa Ali Mazrui amefariki mjini Binghamton, jimbo la New York, Marekani akiwa na umri wa miaka 81, baada ya kuugua kwa muda.

    Prof. Mazrui amefariki Jumatatu ya wiki hii na atazikwa Mombasa nchini Kenya alikozaliwa.

    Mwenyekiti wa Shirika la Kiislamu la Kutetea Haki za B i n a d a m u n c h i n i K e n y a (MUHURI), Khelef Khalifa, alinukuliwa akisema kuwa, mwili wa marehemu Profesa Ali Alamin Mazrui, utasafirishwa na kupelekwa Kenya kwa ajili ya mazishi.

    Mpwa wake Alamin Mazrui, a m e t h i b i t i s h a k w a m b a , marehemu alipenda azikwe nchini Kenya.

    Gavana wa Mombasa, Hassan Joho na Seneta Hassan Omar,

    Prof. Ali Mazrui afariki duniawalitangaza kifo cha msomi huyo maarufu na atazikwa huko Mombasa Kenya.

    Bw. Joho alisema kuwa Jimbo la Pwani na Kenya kwa ujumla wamempoteza mtu muhimu, msomi, profesa wa taaluma za Kislamu na masuala ya Afrika.

    Al i sema Profesa Mazur i alisihi kuzikwa Mombasa katika mtaa mashuhuri wa jumba la makumbusho la Fort Jesus.

    Katika uhai wake, aliwahi kuwa Mkurugenzi wa taasisi ya Taaluma ya Utamaduni wa Kimataifa, katika Chuo Kikuu cha Binghamton.

    A l i k u w a n i m s o m i anayefahamika kote duniani na amesomesha katika mabara yote matano ya dunia na kuandika karibu vitabu 30.

    Profesa Mazrui aliyezaliwa Februari 24, 1933, al ikuwa mchambuzi mahiri na mashuhuria katika vyombo mbalimbali vya habari ndani na nje ya Afrika. Ameacha mjane na watoto sita.

    Profesa Mazrui alikuwa msomi wa masuala ya kisiasa, utamaduni wa Kiafrika na masuala ya dini ya Kiislamu na alisifika sana kwa kutetea utamaduni wa Kiafrika kwa walimwengu.

    Kabla ya kifo chake, alikuwa ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Binghamton mjini New York.

    Kwa miaka mingi Prof. Mazrui alisifika kwa kuwashauri viongozi wa mataifa mengi ya Afrika na ya kigeni, akizungumzia masuala ya nchi za Afrika katika dunia nzima.

    Amechapisha vitabu vingi na kuandika nyaraka mbalimbali

    kuhusu siasa za Afrika, athari za siasa kwa dini ya Kiislamu na uhusiano kati ya mataifa ya Kaskazini na Kusini.

    Alikuwa mwanaharakati wa kweli wa wazo la Afrika kuwa huru na alikosoa mataifa yanayopora rasilimali za Afrika na kunyanyasa watu wake.

    WASIFU WAKEUkiacha kuwa Profesa wa Albert

    Schweitzer katika Humanities na Mkurugenzi wa Taasisi ya Global Cultural Studies huko Chuo Kikuu cha Binghamton, State University of New York, ambako alifanya kazi hadi mauti yanamfika, pia muda mwingi alikuwa akifanya kazi na Chuo Kikuu cha Jos nchini Nigeria.

    Andrew D. White Professor-at-Large Emeritus and Senior Scholar in Africana Studies katika Chuo Kikuu cha Cornell.

    Prof . Mazrui pia al iwahi kuteuliwa kuwa Chancellor wa Chuo Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta Kenya

    Ibn Khaldun Professor-at-Large, Graduate School of Islamic and Social Sciences, Leesburg, Virginia (1997-2000).

    Walter Rodney Professor at the University of Guyana, Georgetown, Guyana (1997-1998).

    Prof. Mazrui alipata shahada yake ya kwanza (B.A. with Distinction) kutoka Chuo Kikuu cha Manchester England, Shahada yake ya uzamili (M.A.) aliipata Chuo Kikuu cha Columbia, New York, na ile ya uzamivu (PhD) aliipatia Chuo Kikuu cha Oxford England.

    Kwa miaka kumi alikuwa mhadhir i Chuo Kikuu cha Makerere Kampala, Uganda, ambako alikuwa Mkuu wa Idara ya Sayanzi ya siasa, Mkuu wa idara ya sayanzi ya jamii na baadae Mkuu wa Idara ya Sheria.

    Aliwahi kuwa Makamu wa Rais International Political Science Association na kuhadhiri katika vyuo mbalimbali katika mabara matano.

    Aidha Profesa Mazrui aliwahi kuwa profesa wa political science (1974-1991) na Mkurugenzi wa Center for Afroamerican and African Studies (1978-1981) katika Chuo Kikuu Michigan, Ann Arbor, Michigan.

    Amekuwa msomi mualikwa katika vyuo vikuu vya Stanford, Chicago, Colgate , S ingapore , Australia, Malaysia, Oxford, Harvard, Bridgewater, Cairo, Leeds, Nairobi, Teheran, Denver, London, Ohio State, Baghdad, McGill, Sussex, Pennsylvania, nk.

    Pia aliwahi kuwa mshauri maalum wa Benki ya Dunia.

    Amewahi kuwa katika Bodi ya Wakurugenzi (Board of Directors of the American Muslim Council, Washington, D.C.) Mwenyekiti wa Board of the Center for the Study of Islam and Democracy, Washington, D.C., kuhudumu katika Board of the Center for Muslim-Christian U n d e r s t a n d i n g , G e o r g e t o w n University, Washington, D.C., na kuwa Fellow of the Institute of Governance and Social Research, Jos, Nigeria.

    Alipendelea kufanya tafiti za kisiasa na baadhi ya tafiti zake ni pamoja na African politics; international relations; comparative politics na political theory.

    Mwenyezi Mungu amsitiri na kumjaalia maisha mema ya Barazak.

    Innalilahi wainnaillaihir Rajiun.

    Muqaddam Foundation kuwasaidia wajasiriamali wasiojiwezaNa Bakari Mwakangwale mambo ya kijamii na hasa

    kupambana na umasikini kwa kuanza na kuwawezesha wajane, yatima, walemavu, wasiojiweza na wajasiliamali ili kuwaepusha na umasikini. Alisema Bw. Mukaddam.

    Aliongeza kuwa katika mpango wake huo, ataanza kutoa mafunzo ya ujasiliamali b i la gharama yoyote na baada ya kufuzu mafunzo hayo, walengwa watapatiwa mitaji kwa ajili ya kujiajiri kwa kufanya biashara mbalimbali.

    Bw. Mukaddam, alifafanua zaidi kwamba taasisi yake imejipanga kutilia mkazo shughuli za kilimo cha bustani na ufugaji wa kuku wa kienyeji, ambapo alieleza kuwa mipango ya taasisi hiyo kwa baadae ni kutoa mitaji ya ufugaji wa ngombe wa maziwa na mbuzi.

    A l i s e m a t a a s i s i y a k e inafahamu kuwa tatizo la ajira

    na umasikini nchini ni kubwa, hivyo zinatakiwa juhudi za makusudi ili kupambana na hali hiyo kwa lengo la kupunguza umasikini unaosababishwa na ukosefu wa ajira na mitaji.

    Tatizo la ajira na umasikini hususani kwa makundi hayo na vijana ni kubwa, hali ya kuwa kuna vyanzo vingi vya kuondoa umasikini kupitia maliasili zilizopo nchini. Alisema.

    Alisema makundi hayo wakiwemo vijana, wamekosa mambo mawi l i muhimu aliyoyataja kuwa ni elimu ya ujasiriamali pamoja na mitaji ya kufanyia biashara.

    Bw. Mukaddam alisema kwa kawaida matumaini yeyote ya kesho, hutengenezwa kwa kukarabati makosa ya leo. Aidha alisisitiza kuwa ili mtu aweze kufanikiwa, anatakiwa awe rafiki wa sayansi.

    Alitolea mfano taifa la China kuwa, limefaulu kiuchumi duniani baada ya watu wake kujikita kikamilifu katika ku jenga uchumi kupi t ia wajasiriamali.

    Alisema katika mipango yao, zoezi hilo litaanza na wakazi wa wilaya ya Ilala, kisha itafuatia wilaya ya Kinondoni na kumalizia na wilaya ya Temeke na baada ya hapo, taasisi hiyo itaanza kutembelea mikoani kwa dhamira hiyo hiyo.

    Awali taasisi hiyo ilitoa m s a a d a w a p e s a k w a vikundi vitatu, ambapo kila kikundi kilipata kiasi cha shilingi 500,000/. Vikundi vilivyobahatika kupata msaada huo ni Upendo Group kutoka Ilala Kota, Amkeni Group na Upendo Group vya Chikichini.

    PROFESA Ali Mazrui.

  • 6 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 17-23, 2014Makala

    AKIWASILISHA amri za Richard Nixon kwa upigaji mabomu mkubwa dhidi ya Cambodia mwaka 1969, (Waziri wa Mambo ya Nje) Henry Kissinger alisema chochote kinachoruka juu ya chochote kinachotembea.

    Wakati (Rais) Barack Obama anaanzisha vita vyake vya saba dhidi ya dunia ya Kiislamu tangu atunukiwe Nishani ya Amani ya Nobel, kiwewe kilichotengenezwa na uwongo unamfanya mtu atamani jinsi Kissinger alivyosema ukweli kuhusu uuaji wake.

    Kama shahidi wa athari kwa binadamu za unyama kutoka angani ikiwa ni pamoja na kulipua vichwa vya wahanga, viungo vyao vikionekana katika miti na mashamba sishangazwi na kutojali kumbukumbu na historia, kwa mara nyingine. Mfano halisi ni kuingia madarakani kwa Pol Pol na wanamapinduzi wa Khmer, ambao walikuwa wanafanana na hawa Islamic State ya Irak na Syria (ISIS). Wao pia walikuwa watu wakatili wa zama zilizopita ambao walianza kama kikundi kidogo. Wao pia walikuwa ni matokeo ya uharibifu wa kutisha uliofanywa na Marekani, safari hii barani Asia.

    Kwa mujibu wa Pol Pot , mkusanyiko wake ul ikuwa hauna zaidi ya wapiganaji 5,000 wenye silaha za hapa na pale wasiokuwa na uhakika nini wanataka kufanya, mbinu, utii na viongozi. Mara ndege za kupiga mabomu za B52 za Nixon na Kissinger zilipoanza kazi kama sehemu ya Operesheni Menu, mtu huyo aliyechukiwa kuliko wote katika nchi za Magharibi hakuamini bahati yake.

    Wamarekani waliangusha kiasi cha Hiroshima (bomu la atomiki dhidi ya Japan mwaka 1945) tano za mabomu dhidi ya vijiji vya Cambodia kati ya 1969 na 1973. Walisambaratisha kijiji baada ya kijiji, na kurudi kupiga mabomu magofu na maiti. Mahandaki yaliacha mikanda mirefu ya mauaji, bado inaokenana kutoka angani . Uharamia ul ikuwa hauwezi kufikirika.

    Ofisa wa zamani wa Khmer R o u g e ( w a n a m a p i n d u z i wa Cambodia) alielezea jinsi waliopona walivyoganda na walikuwa wakitembea kwa siku tatu au nne bila kusema neno lolote. Wakiwa na kihoro na nusu vichaa, watu walikuwa tayari kuamini walichoambiwa Ndicho kilichowezesha ikawa rahisi kwa Khmer Rouge kuungwa mkono.

    Tume ya Uchunguzi ya serikali

    Kutoka Pol Pot hadi ISIS: Chochote kinachoruka juu ya chochote kinachotembea

    Na John PilgerOktoba 9, 2014: Mtandao wa

    Kupashana Habari

    Rais Barack Obama wa Marekani.ya Finland ilikisia kuwa watu 600,000 nchini Cambodia walikufa kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyofuata na kuelezea upigaji mabomu kama hatua ya kwanza katika muongo wa mauaji ya halaiki, Kile ambacho Nixon na Kissinger walianzisha, Pol Pot, aliyefaidika nacho, alimalizia. Wakati wa upigaji mabomu, Khmer Rouge iliongezeka na kufikia jeshi la watu 200,000.

    ISIS ina historia kama hiyo na hali halisi inayofanana. Kwa makisio mengi zaidi ya wasomi, uvamizi wa Bush na Blair nchini Irak mwaka 2003 ulisababisha vifo vya watu 700,000 katika nchi ambayo haikuwa na historia ya misukumo ya jihad. Wakurdi walikuwa na makubaliano ya udhibiti wa maeneo na mfumo wa siasa; wa-Sunni na wa-Shia walikuwa na tofauti zao za kitabaka na kimadhehebu, lakini walikuwa na amani; kuoana kulikuwa jambo la kawaida. Miaka mitatu kabla ya uvamizi, niliendesha gari kuzunguka kote Irak bila woga. Njiani nilikutana na watu wanaojiamini, na zaidi, kuwa wa-Iraki , warithi wa ustaarabu uliokuwa kwao, ni kama unaendelea.

    Bush na Blair walilipua yote haya kuwa vumbi. Irak sasa ni kiota cha jihadi. Al Qaeda -.kama mujahidina wa Po Pot walidandia nafasi iliyotokana na mirindimo ya Tisha na Ogofya (jina la operesheni ya Marekani nchini humo) na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyofuata. Uasi nchini Syria ulileta faida kubwa zaidi, wakati CIA (Shirika la Ujasusi la Marekani) na serikali za Ghuba zikitoa milolongo ya silaha, vifaa na fedha kupitia Uturuki. Kuingia kwa wapiganaji

    kutoka nje kusingezuilika. Balozi wa zamani wa Uingereza, Oliver Miles, aliandika hivi karibuni serikali (ya Waziri Mkuu David Cameron) inaelekea kufuata mfano wa Tony Blair, ambaye alipuunzia ushauri usioyumba wa Wizara ya Mambo ya Nje, idara za ujasusi wa kijeshi za MI5 naM16 kuwa sera yetu ya Mashariki ya Kati na hasa vita vyetu vya Mashariki ya Kati vilisaidia sana kujisajili kwa Waislamu kwa vitendo vya ugaidi nchini humu.

    ISIS ni kizaliwa cha Washington na London, ambako wale ambao, katika kuiteketeza Irak kama nchi na kama jamii, walishiriki kufanya uhalifu mkubwa dhidi ya binadamu. Kama Pol Pot na Khmer Rouge, ISIS ni kichotara cha utisho kutoka nchi za Magharibi uliosambazwa na tabaka hodhi la wala raha lisilojali matokeo ya hatua zao zilizofanywa kutoka kwingineko kabisa kwa umbali na utamaduni. Jinai yao haitajwi katika jamii zetu.

    Ni miaka 23 tangu mauaji ya halaiki yaifunike Irak, mara baada ya vita vya kwanza vya Ghuba, wakati Uingereza na Marekani zilipoteka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kuweka vikwazo; teketezi dhidi ya watu wa Irak na kinyume chake, kuongeza nguvu za ndani za utawala wa Saddam Hussein. Ilikuwa ni kama mzingiro wa vita vya Ulaya hapo zamani. Kila kitu ambacho kinawezesha serikali ya kisasa kimsingi kilizuiwa - kutoka dawa ya chlorine ya kusafishia maji yawe salama hadi penseli za darasani, vifaa vya kubadilisha katika mashine za X-ray, dawa za kawaida za kutuliza maumivu na dawa za kupambana na saratani ambazo

    hazikuwa zimeonekana kabla ya hapo zilizopeperushwa na vumbi kutokana medani za vita kusini ya nchi hiyo yaliyoathiriwa na urani iliyodidimia.

    Kabla ya Krimasi, Wizara ya Biashara na Viwanda ya Uingereza ilizuia kuuzwa kwa chanjo zenye nia ya kuwalinda watoto wa Irak dhidi ya homa ya manjano na mkamba (diphtheria). Kim Howells, daktari na Naibu Waziri katika serikali ya Blair, alieleza kwanini. Chanjo za watoto, alisema, zinaweza kutumika katika silaha za maangamizi. Serikali ya Uingereza iliweza kukwepa kuwajibika kwa udhi kama hilo kutokana na jinsi vyombo vya habari vilivyokuwa vinatoa habari kuhusu Irak sehemu yake kubwa ikiwa inasukumwa na Wizara ya Mambo ya Nje kumshutumu Saddam Hussein kwa kila kitu.

    Chini ya mpango feki wa kibinadamu wa Mafuta kwa Chakula, kiasi cha dola 100 kilipangwa kwa kila raia wa Irak kuishi kwa mwaka mmoja. Kiwango hili ndicho kingelipia mahitaji yote ya miundombinu na huduma muhimu kama nishati na maji. Fikiria, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Hans von Sponeck aliniambia kuweka hivyo vijisenti dhidi ya ukosefu wa maji, na hali kuwa wananchi walio wengi wa Irak wakiugua hawawezi kulipia matibabu, na mshtuko wa kutoka siku hadi siku, na unapata picha kidogo ya jinamizi hilo. Na mtu asifanye kosa, yote hii ni ya kunuia. Sikuwahi siku za nyuma kutaka kutumia neno mauaji ya halaiki, lakini sasa hakuna njia.

    Akiwa ametosheka , Von Sponeck alijiuzulu kama mratibu wa shughuli za misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Irak. Aliyemtangulia, Denis Halliday, ambaye pia alifanya kazi nzuri katika Umoja wa Mataifa, pia alijiuzulu. Nilielekezwa, Halliday alisema, kutekeleza mpango ambao unaendana na tafsiri ya mauaji ya halaiki: sera ya kudhamiria ambayo kimsingi imeua zaidi ya watu milioni moja, watoto na watu wazima.

    Utafiti uliofanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF ulionyesha kuwa kati ya mwaka 1991 na 1998, wakati wa kilele cha hali nguvu kutokana na uzuiaji wa bidhaa, kulikuwa na vifo 500,000 vya ziada vya watoto wa Irak chini ya umri wa miaka mitano. Mwandishi wa habari wa televisheni wa Marekani alimhoji Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Madeleine Albright, akimwuliza bei hii ni sawa? (ya maafa hayo na malengo ya nchi hizo). Albright alijibu, tunadhani

    Inaendelea Uk. 7

  • 7 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 17-23, 2014Makala

    Kutoka Pol Pot hadi ISIS: Inatoka Uk. 6ni sawa.Mwaka 2007, ofisa mwandamizi wa Uingereza anayehusika na vikwazo, Came Ross, akiitwa Bwana Irak, aliiambia kamati ya Bunge serikali za Marekani na Uingereza zimezuia kimsingi njia ya watu takriban wote wa Irak kuweza kuishi. Nilipomhoji C a m e R o s s m i a k a m i t a t u baadaye, alikuwa amegubikwa na masikitiko na majuto. Naona aibu, alisema. Hivi sasa ni msema ukweli wa nadra kuhusu serikali zinavyodanganya na jinsi vyombo vya habari vinavyofuata mstari vinachukua nafasi muhimu katika kutawanya na kuendeleza uwongo. Tunawalisha (waandishi wa habari) vielelezo vilivyopimwa na mashirika ya kijasusi, alisema, au tungevizuia kabisa.

    Hapo Septemba 25,kichwa cha habari cha gazeti la Guardian (la Uingereza) kilisema: Mbele ya kihoro cha ISIS lazima tuchukue hatua. Hiyo lazima tuchukue hatua ni kama mzuka, inayotahadharisha kumbukumbu iliyobanwa, vielelezo, maudhui yaliyofunzwa, masikitiko au aibu. Mwandishi wa makala hiyo alikuwa Peter Hain, aliyekuwa Waziri katika Wizara ya Mambo ya Nje akishughulikia Irak chini ya Blair. Mwaka 1988, wakati Denis Halliday alipofichua kiwango cha mateso nchini Irak ambako serikali ya Blair ilikuwa inahusika kwa karibu, Hain alimtukana katika kipindi cha Newsnight cha BBC kama mtetezi wa Saddam. Mwaka 2003, Hain aliunga mkono uvamizi wa Irak iliyochoka kwa misingi ya uwongo wa wazi. Katika mkutano mkuu wa chama cha Leba baadaye, alipuuzia uvamizi kama suala la pembeni.

    Sasa Hain anahimiza mapigo ya angani, matumizi ya droni, zana za kijeshi na misaada mingine kwa wale walio hatarini kwa maangamizi makubwa nchini Irak na Syria. Hii itawezesha kufikia utatuzi wa kisiasa. Obama ana fikra kama hiyo pale alipoondoa vizuizi kwa upigaji mabomu na mashambulizi ya droni. Hiyo ina maana kuwa makombora na mabomu ya pauni 500 (kilo takriban 1000) yanaweza kuvunji l ia mbali nyumba za wakilima, ambayo yameendelea bila kizuizi huko Yemen, Pakistan, Afghanistan na Somalia kama yalivyofanya nchini Cambodia, Vietnam na Laos. Mnamo Septemba 23, kombora la Tomahawk lilipiga kijiji katika jimbo la Idlib nchini Syria, na kuuwa watu wanaofikia 12, pamoja na wanawake na watoto. Hakuna al iyekuwa anapeperusha bendera nyeusi.

    Siku makala yaHain ilipotokea,

    Denis Halliday na Hans Von Sponeck walitokea kuwa jijini London na wakaja kunitembelea. Hawakushangazwa na unafiki wa kifo wa mwanasiasa (huyo), lakini wakasikitishwa na kutokuwepo kwa muda mrefu, kusikoelezeka, kwa diplomasia ya kutafuta kuacha mapigano kwa aina fulani. Duniani kote, kuanzia Ireland ya Kaskazini hadi Nepal, wale wanaoangaliana kama magaidi na wanaokufuru wameangaliana pande mbili za meza. Kwanini isiwe hivyo sasa nchini Irak na Syria.

    Kama Ebola katika Afrika Magharibi, kijidudu kinachoitwa vita isiyoisha kimevuka bahari ya Atlantiki. Lord Richards, ambaye hadi hivi karibuni alikuwa mkuu wa majeshi ya Uingereza, anataka buti katika ardhi (yaani askari) sasa (wapelekwe Irak). Kuna kubwabwaja kusiko na maana, kutokuwa na hamu ya utu kutoka kwa Cameron, Obama na jumuiko la wanaokubali walilounda hasa Tony Abbott wa Australia asiyeeleweka kwa ushambulizi wake wanapoelezea mashambulizi kutoka futi 30,000 angani ambako damu ya uvinjari uliopita wa kijeshi haikukauka. Hawajawahi kuona upigaj i mabomu na inaelekea wanapenda sana kiasi cha kumpindua mshirika wao pekee mwenye manufaa kwao, Syria. Yote haya si mapya, kama ambavyo mawasiliano ya kijasusi ya Marekani na Uingereza yaliyovuja yanavyoonyesha:

    Ili kuwezesha kazi ya vikosi v i n a v y o k o m b o a . j u h u d i maalum ifanyike kuwaondoa baadhi ya watu na kuendelea na machafuko ya ndani nchini Syria. CIA iko tayari, na SIS (MI6) itajaribu

    kufanya hujuma na matukio ya kutumia mkono (?) nchini Syria, ikishirikiana na wapasha habari na watu binafsi. kiwango cha lazima cha woga mashambulio ya mipakani na mapigano ( ya k u p a n g wa ) ya t a t o a kisingizio cha kuingilia CIA na SIS zitumie nyenzo za kisaikolojia na medani (za kijeshi) kuongezea hali ya wasiwasi.

    Hiyo iliandikwa mwaka 1957, ingawa ingeweza kuwa imeandikwa jana. Katika dunia ya ubeberu, hakuna kinachobadilika kimsingi. Mwaka jana, waziri wa zamani wa Ufaransa wa Mambo ya Nje Ronald Dumas alifichua kuwa miaka miwili kabla ya Mchanuo wa Nchi za Kiarabu (Arab Spring) aliambiwa jijini London kuwa vita dhidi ya Syria inapangwa. Nitakuambia kitu, akisema katika mahojiani na kituo cha televisheni cha Ufaransa LPC, nilikuwa Uingereza miaka miwili kabla vita haijaanza kwa masuala mengine . Ni l ikutana na maofisa wa juu wa Uingereza, ambao walikiri kwangu kuwa wanatayarisha kitu kuhusu Syria. Uingereza ilikuwa inapanga waasi kuingia Syria. Walifika hata kuniuliza, licha ya kuwa sikuwa tena Waziri wa Mambo ya Nje, kama ningependa kushiriki. Operesheni hii inatoka mbali. Ilipangwa, ilidhamiriwa na kuandaliwa.

    Washindani halisi wa ISIS ni mapepo yanayotambuliwa na nchi za Magharibi Syria, Iran na Hezbollah. Kizuizi ni Uturuki, mshirika na mwanachama wa NATO, ambayo imefanya njama

    na CIA, MI6 na mamwinyi wa Ghuba kupeleka misaada kwa waasi wa Syria, ikiwa ni pamoja na wale ambao sasa wanajiita ISIS. Wakiwa wanaunga mkono Uturuki katika njama zake za siku nyingi za kuwa bwana mkubwa katika eneo hilo kwa kuipindua serikali ya Assad ni kutazama usoni vita kubwa ya kimataifa na kuchanwa kwa njia ya kutisha kwa nchi yenye mchanganyiko mpana zaidi wa kitaifa katika Mashariki ya Kati.

    M a k u b a l i a n o ya k u a c h a mapigano hata yangekuwa vigumu kiasi gani kufikiwa ndiyo njia pekee kuondokana na mkanganyiko huu wa kibeberu; vinginevyo kukatwa vichwa kutaendelea. Kuwa mazungumzo halisi na Syria yanaonekana kama kinyume cha maadili (The Guardian, ya Uingereza) kunaonyesha kuwa hisia za kujiamini kimaadili miongoni mwa wale waliomuunga mhalifu wa kivita Blair siyo tu hazina maana, bali ni hatari.

    Pamoja na makubaliano ya kuacha mapigano, lazima kuwe na kuachwa kabisa kwa upelekaji wa zana za kivita kwenda Israel na kutambuliwa kwa Taifa la Palestina. Suala la Palestina ni kidonda kinachovuja damu kwa wazi katika eneo hilo, na sababu inayotajwa kila mara ya kuanza kwa siasa kali za Uislamu. Osama bin Laden alisema hivyo kwa uwazi. Palestina pia inaleta matumaini. Toa haki kwa Wapalestina na unaanza kubadili dunia inayowazunguka.

    Zaidi ya miaka 40 iliyopita, kupiga mabomu kwa Nixon na Kissinger nchini Cambodia kulizusha mkondo wa mateso ambako nchi hiyo haijawahi k u p o n a . N i h i v y o p i a ilivyokuwa kwa uhalifu wa Blair na Bush nchini Irak. Kwa ubunifu wa ajabu wa muda, kitabu cha hivi karibuni cha Henry Kissinger cha kujitukuza kimechapishwa hivi karibuni kikiwa na kichwa cha kuleta tabasamu, World Order (Mfumo-dola wa Dunia). Katika mapitio ya kukinadi, Kissinger anasemekana ni mmoja wa wasukaji muhimu wa mfumo-dola wa dunia ambao umebaki thabiti kwa robo karne.

    Waambie hilo watu wa Cambodia, Vietnam, Laos, Chile, Timor ya Mashariki na wahanga wengine wote wa usukaji dola wake. Ni pale tu sisi tutakapotambua wahalifu wa vita miongoni mwetu ndipo damu itaaanza kukauka.

    (Makala imeandikwa na John Pilger na kufasiriwa kwa Kiswahili na Anil Kija-www.johnpilger.com)

    WAPIGANAJI wa ISIS wapo katika nchi za Iraq na Syria.

  • 8 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 17-23, 2014Makala

    NILIKUWA katika semina moja wiki iliyopita ambapo mtoa mada mmoja katika muda wa majadiliano aliuliza:

    Ni kwa nini suala la Mahakama ya Kadhi lilikwama kuingizwa katika Katiba inayopendekezwa kule Dodoma.

    Mshiriki mmoja katika kujibu akasema kuwa ni kwa sababu Katiba sio jambo la Kiislamu, ni la kikafiri na kwa hiyo, lazima Mwenyezi Mungu alikwamishe.

    Ilikuwa vigumu sana kwa muuliza swali kujenga hoja kwa sababu tayari mtoa jawabu alionekana kufura kwa hasira a k i o n ye s h a k u wa h a k u n a anachoweza kue lewa kwa muda ule kutokana na uoni wake ulivyokuwa. Ufupi wa maneno kilichojitokeza ni kuwa huyu ni mmoja wa majeruhi na wahanga wa harakati mpya za watu wanaojinasibu kusimamisha Khilafah, wakiharamisha takriban kila kitu. Wao ndio pekee wenye shaksiya ya Kiislamu na wao ndio walio sahihi.

    Watu hawa wapo kat ika makundi mawili. Kuna kundi moja linahamasisha Waislamu kushika silaha wakidai kuwa Uislamu hauwezi kusimama ila kwa silaha. Wapo wengine wanasema kuwa hakuna haja ya kugombana na Serikali , hakuna sababu ya kushika silaha kupambana na makafiri, lakini kusoma haramu, kulima haramu, kufanya kazi serikalini haramu, almuhimu kila kitu kwao haramu.

    Katika nchi kama hii ambapo kuna watu wa jamii mbalimbali, ni lazima mkubaliane mtakavyoishi kila mmoja akipata haki zake. Sasa kama mtaita kanuni hizo kuwa ni Katiba au mkataba, hoja si jina. Lakini pia ili kuweka kanuni hizo ni lazima mkutane mjadili mkubaliane. Sasa kama mtaita ni Bunge au Shura, jina pia si hoja. Muhimu ni kuwa ni lazima kuwe na chombo cha kuwakutanisha kuweka kanuni hizo.

    Ya Wakristo yanapita Dodoma k wa s a b a b u wa n a p o i n g i a wanaingia kama Wakristo, si kama CCM, wala Chadema. Rejea walivyosimama kupinga hoja ya aliyekuwa Waziri wa Fedha Bwana Mkulo ya kuondoa misamaha ya kodi kwa taasisi za kidini kwa sababu wanajua namna makanisa yanavyonufaika na misamaha hiyo.

    Lakini mpaka leo Waislamu hawajaingia Bungeni kama Waislamu kupinga upendeleo na namna serikali inavyotumia kodi za Watanzania kuendeleza Wakristo kupitia MoU baina ya makanisa na serikali, au kama si kupinga nao kudai mgao wa Waislamu! Lakini hao hao ambao wanasema kuwa Uislamu unawataka wasikubali kudhulumiwa. Wamsaid ie mwenye kudhulumu, kwa kumnasihi na kumkanya aache dhulma na wamtetee pia mwenye kudhulumiwa. Lakini katika

    Mujahidina Shimon Elliota.k.a Abu Bakr al-Qurashiy

    Kutoka Lawrence, aka "Lawrence of Arabia,"Hadi akina Abu Baghdadi, Abu Ismail Mwanza

    Na Omar Msangi hili la kodi zao kuchukuliwa k u p i t i a M o U k u n u f a i s h a Ukristo, wameshindwa kuisaidia serikali na Wakristo waache kudhulumu na wameshindwa kujisaidia wenyewe kwa kukataa kudhulumiwa.

    Lakini hata kama ikitokea u k a s u s a b u n g e , s h e r i a z i t a k a z o w e k w a l a z i m a utawajibika. Kama ni kodi utalipa kama ilivyopangwa na bunge, utaandikisha kiwanja cha kujenga msikiti na kama ni mjini na unataka kujenga ghorofa, hutajenga mpaka uchore ramani ipitishwe na mamlaka husika kutimiza sheria iliyopitishwa na Bunge, wala hutawaambia kuwa wewe hufuati sheria zilizopitishwa na Bunge la kikafiri! Usipokuwepo watapitisha hata ya kuudhuru Uislamu kwa sababu hakuna mtetezi.

    Lakini hata kama ni katika nchi ya Kiislamu, ni lazima iwekwe taratibu za namna ya kuishi. Iweke sera, itunge sheria, kanuni na taratibu mbalimbali. Wala haiwezi kuwa maadhali jamii ni ya Kiislamu ikasema kuwa Katiba na Sheria zake (namna ya kuendesha Mahakama, biashara, taratibu za ndoa na maisha ya kifamilia na kijamii, ni Quran.) Quran ni Mwongozo, sio Kitabu cha kuendesha mahakama, biashara, jela, na mambo kama hayo. Ndio maana maulamaa wanaandika vitabu na kutoa fatwa mbalimbali katika masuala mbalimbali ya maisha ya Muislamu. Tofauti ya mambo haya kati ya jamii ya Kiislamu na ile ya kikafiri ni kuwa kwa Waislamu, katiba, sera, sheria na kanuni zote zitawekwa kwa kuzingat ia Quran na Sunnah zinasemaje, kwa maana kuwa hazitakiuka maamrisho na makatazo ya Uis lamu. Kwa upande wa makafiri wao watatumia tu akili na matashi ya nafsi.

    Tulikuwa katika semina moja ya vijana wa Kiislamu wa Vyuo

    Inaendelea Uk. 9

    ABU Baghdad (aliyezungushiwa mduara) akiwa na veteran wa vita wa Marekani John McCain alipowatembelea huko Syria. Picha chini kulia akiwa na mkewe kabla ya kushika ukamanda wa 'Jihad'. Kushoto baada ya kushika ukamanda akiwa na madevu na kilemba cheusi.

  • 9 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 17-23, 2014Makala

    Mujahidina Shimon Elliota.k.a Abu Bakr al-Qurashiy

    Inatoka Uk. 8Vikuu, mmoja wao akaja na hoja kuwa bila silaha hakuna Uislamu utakaosimama, akatoa hoja akisema kuwa ndio maana Mohammed Mursi wa Misri kangolewa madarakani kwa sababu njia aliyopitia sio sahihi. Ilitakiwa aingie Ikulu kupitia Jihad ya Kitali. Mtu unaweza kujiuliza, hivi Fathi Makkah ilipatikana kwa Kitali? Ule umma ulioingia Makkah ikabidi akina Abu Sufyani kusalimu amri, ulipatikana kule Madina kwa Kitali?

    Mtu anayekuja na hoja kama hii na ukizingatia kuwa yupo Chuo Kikuu, kwa hakika inakuwa vigumu kuelewa ni kitu gani kimekoroga akili yake mpaka ile akili ndogo tu ya kujisaidia yeye mwenyewe anakuwa hana tena.

    Taleban, walisimamisha dola ya Kiislamu Afghanistan kupitia mtutu wa bunduki. Wapo wapi? Walingolewa na majeshi ya Marekani na washirika wake. Ukija Libya, walikusanywa waliodaiwa kuwa wapinzani wa Gadhafi na wapiganaji wa Kisalafi (Mujahidina) wakidai kuwa wakimngoa Gadhafi wa n a s i m a m i s h a K h i l a f a h . Nakumbuka mpaka huku kwetu, kila ilivyokuwa ikitolewa hoja kuwa Gadhafi kawafanyia wema watu wake, wapo waliokuwa wakidai kuwa, pamoja na hayo hatawali kwa Kitabu na amekuwa a k i w a u w a w a n a h a r a k a t i n a M a s h e i k h w a n a o t a k a kusimamisha Kitabu. Gadhafi kangoka kwa mtutu wa bunduki na makombora, Dola ya Kiislamu iwapi Libya? Imekuwa vurugu tupu, amani hakuna tena Libya. Imebaki majuto ni mjukuu.

    Kwa nini Salafi hawapigani na Israel, makafiri wengineKwa mujibu wa uchambuzi wa

    mwandishi Ali Mamouri, anasema kuwa hutawasikia hata mara moja ISIS wakizungumzia kuipiga Israel (makafiri wengine) au kuwasaidia Hamas, kwa sababu hilo sio lengo la kuundwa kwao. Lakini anasema pia kuwa kuwepo kwa ISIS, kama wanavyosema wachambuzi wengine, ni katika kutekeleza mkakati kabambe wa wagawe uwatawale. Anasema, ndio sababu Salafi, hawa kila mtu kwao kafiri ila wao tu ndio

    al-Baghdadi amekuja kufanya kazi kama aliyofanya Lawrence aliyeisaidia Saudi Arabia kujitoa katika Dola ya Kiislamu, hadi utawala wa Uthmaniyah uliokuwa na makao makuu yake Istanbul, ukaporomoka.

    Lipo jambo moja ambalo lau Waislamu hawatalitizama na kulikubali, huko mbele ni kiza kitupu. Alikuwa akiniambia

    jamaa yangu mmoja kutokana aliyoshuhudia Dodoma kuwa yalimfikisha mahali kuona kuwa labda Wazanzibari wana laana na haijulikani nani kawalani. Alisema, siasa imeshindwa kuwaunganisha Wazanzibari, w a m e b a k i C U F , C C M , wakipingana hata katika yale mambo ambayo ni kwa masilahi yao kama Wazanzibari. Lakini la kusikitisha ni kuwa hata Uislamu umeshindwa kuwaunganisha au kwa kauli sahihi zaidi, wamekataa U i s l a m u k u wa u n g a n i s h a -hawaungani hata kwa masilahi ya Uislamu wao. Sasa hiyo kama sio laana nini?

    H i l i n d i o t a t i z o k u b wa kwa Waislamu iwe Zanzibar, Tanganyika, Mashariki ya Kati na dunia kwa ujumla. Tunaowaita makafiri, wakikutana katika Umoja wa Mataifa, UN, lao ni

    wenye Shaksiya ya Kiislamu. Wanasema Hamas ni makafiri, bora hata kusimama upande wa Israel kuwapiga Wapalestina kwa sababu wanapigania uhuru, sio dola ya Kiislamu. Ni yale yale ya Tanzania mwaka 1995 kuwa usimchague Lipumba kwa sababu sio mwana Sunnah, bora Mkapa Katoliki!

    Wakati wananchi wa Gaza

    wakiuliwa kikatili na Israel hivi karibuni, kiongozi mmoja wa Salafi kule Misri (July 22, 014) Sheikh Talaat Zahran, alitangaza kuwa ni haram kuwasaidia Waislamu wa Gaza kwa sababu wanapigania uhuru na demokrasia na kwa sababu wanaungwa mkono na na Hizbullah na Iran, basi ni Mashia.

    Ni k a t ik a mt izamo hu u inaonekana kuwa Abu Bakr Inaendelea Uk. 10

    ABU Bakr al-Baghdadi, jina lake halisi ni Elliot Shimon, kachero wa Mossad.

    T.E . Lawrence , maarufu Lawrence of Arabia.

  • 10 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 17-23, 2014Makala

    Mujahidina Shimon Elliota.k.a Abu Bakr al-Qurashiy

    Inatoka Uk. 9moja. Wakikutana katika NATO, wao kama Wakristo, lao ni moja. Na hata wakikutana Dodoma Bungeni, lao ni moja. Ndio maana wanakuwa na nguvu ya kukwamisha kila wasilolitaka la Kiislamu na wanalolitaka kama Wakristo hupita, haijalishi limeletwa na CCM, CHADEMA, CUF au NCCR.

    Hii ndiyo nguvu inayokwamisha OIC na Mahakama ya Kadhi. Njoo kwa Waislamu hali ikoje!!!

    Waarabu, Waislamu walikuwa katika muungano wa kupigwa Afghanistan, wakawa katika muungano wa kupigwa Muislamu mwenzao Iraq, Libya na sasa wapo katika muungano wa kupigwa Syria. Na juzi hapa walitumiwa pia katika harakati za kuondolewa Mohammad Mursi!!!

    K a t i k a wa l e wa l i o k u wa Dodoma, wabunge wa kawaida, walio serikalini na katika vyama vya siasa, na hasa CCM, Chama tawala, Waislamu wangapi walijali maslahi ya dini yao wakasemea Mahakama ya Kadhi? Ndio kwanza walionekana wakicheza kiduku na rusha roho bungeni kusherehekea ushindi wa Wakristo kukwamisha Mahakama ya Kadhi kuingia katika Katiba ya nchi!!!

    Nilikuwa naangalia video moja iliyotumwa katika mtandao wa YouTube, ikionyesha jinsi ISIS wanavyopata wafuasi wa kuwaunga mkono. Katika sehemu moja kiongozi wa ISIS anaonekana akiingia katika Msikiti wa Ijumaa Mosoul, kule Iraq, anapanda katika mimbar anahutubia. Mada ni juu ya kupigana kwa silaha kwa ajili ya kusimamisha Khilafah. Anachosisitiza ni kuwa hakuna Uislamu bila silaha, hakuna kusimama Uislamu, ila bi silaha. Baada ya mawaidha yale watu wanapewa kiapo cha kumkubali Khalifah al-Baghdad, wanaapa-kwa maana kuwa wanachukua Baiyah ya kumkubali Abu Baghdadi (Abu Qurashiy) kuwa ni Khalifah wa Waislamu. Nje ya msikiti baada ya Baiyah hiyo watu wanahojiwa wakiwa wana nyuso za furaha wakisema kuwa wanafurahi kupata Khalifah wa Waislamu na kwamba watakuwa chini yake kupigana dhidi ya makafiri.

    Mawazo kama haya ndio hayo hayo ambayo yamefikishwa huku kwetu na mawakala (agents) waliotumwa huku, akina Abu Dawd na wenzao.

    Nani Abu Baghdadi?Kwa mujibu wa taarifa ya

    aliyekuwa kachero wa US National Security Agency (NSA), Edward Snowden, huyu anayei twa Khalifah wa Waislamu (ISIS) Abu Baghdadi, ni kijana wa M16 (Uingreza), CIA (Amerika) na Mossad (Israel). Anasema kuwa kupatikana kwa Abu Baghdadi na kundi lake la ISIS, ni katika kutekeleza mkakati utakaoipatia Israel inayodhaniwa kuwa amani na usalama wa kudumu. Mpango

    RAIS wa Syria, Dkt. Bashar al Assad.mkakati wenyewe ukiitwa "the hornet's nest".

    K wa m u j i b u wa t a a r i f a zilizofichuliwa na kachero huyo, Edward Snowden, halikadhalika na zile za makachero wa Iran, huyu Abu Bakr al-Baghdadi, jina lake halisi ni Elliot Shimon, kachero wa Mossad, aliyezaliwa na baba na mama Wayahudi.

    (Soma: The real name of Abu Bakr al-Baghdadi is Shimon Elliott. Au Shimon Elliot, aka Al-Baghdadi, son of Jewish parents, Mossad Agent.)

    K wa m u j i b u wa t a a r i f a m b a l i m b a l i z i n a z o f i c h u k a hivi sasa, huyu Shimon Elliott alipewa mafunzo ya ukachero na kijeshi, kisha akafunzwa namna ya kuongea kama Sheikh na Mujahidina wa zama hivi. Akawa na aya na hadithi za Jihad na mambo mengine muhimu katika Uislamu na kisha kuwezeshwa kuunda jeshi la Mujahidina lililo tayari kutumiwa mahali popote duniani patakapodaiwa kuwa kuna Jihad ya kusimamisha Khilafah. Moja ya mafunzo makubwa ya Shimon Elliott, ni kuwatoa wafuasi wake katika ulimwengu wa hakika, waishi ndotoni-kila kitu kwao haramu, kulima haramu, kusoma haramu, uvaaji unaodaiwa si wa shaksiya ya Kiislamu (Kiarabu) haramu, kufanya kazi serikalini haramu, katiba haramu. Lakini baya zaidi ni kuwajaza bangi na kuwaaminisha kuwa Uislamu ni

    kuuwa kila asiyefanana nawewe, awe Muislamu au kafiri. Hata kama ukiwa umetamka shahada, lakini si wa Salafi ya Ki-Abu Baghdadi al Qurashiy na Abu Islamail, basi wewe sawa sawa tu kuuliwa.

    Yupo kijana mmoja wa Zanzibar alifika kidato cha tano akaacha shule akidai kuwa amegundua ukweli kuwa alikuwa katika dhambi kusoma elimu za kikafiri. Mwanafunzi mwenzake akawa anajadiliana naye akamwambia, hebu jaaliya wewe umeoa na mkeo kapata matatizo ama ya uja uzito au magonjwa ya akina mama na kwa hiyo anahitaji mtaalamu. Je, kama Waislamu hawatasoma, huoni itakuwa vibaya zaidi kwa mkeo kutibiwa na kafiri tena mwanamume?

    Jibu la yule kijana likawa kuwa, bora kutibiwa na kafiri kuliko Muislamu ambaye hafuati sunna za kisalafi! Na akadai kuwa ipo hadithi ya Mtume (s.a.w) inaagiza hivyo!

    Sasa hapa unaweza kuona k i w a n g o c h a u j i n g a n a kuchanganyikiwa. Hebu jaaliya Waislamu wamekimbia nyanja zote maana ni za kikafiri na wategemee huduma kutoka kwa makafiri , je wakikataa kuwahudumia au kuwauzia kama ni bidhaa!

    Swali hapa ni je, nini lengo la hawa akina Shimon katika kupandikiza fikra na imani hii kuwa kila kisicho salafi wa ki-Abu Ismail ni haramu na stahiki kuuliwa? Kwa mujibu wa taarifa za kikachero za Iran na zile za Edward Snowden, huyu Abu Bakr Al Baghdadi (Elliot Shimon) akiwa na jina lingine la uwongo, Ibrahim ibn Awad ibn Ibrahim Al Al Badri Arradoui Hoseini:

    Was recruited by the Israeli Mossad and was trained in espionage and psychological warfare against Arab and Islamic societies (and) has cooperated with the U.S. Secret Service, British and Israel to create an organization capable of attracting terrorist extremists from around the world. (Soma: Simon Elliot, aka Al-Baghdadi, son of Jewish parents, Mossad Agent.)

    Pigia msitari maneno-to create an organization capable of attracting terrorist extremists from around the world.

    Ya k i wa n a m a a n a k u wa kutokana na mafunzo aliyopewa huyu Abu Baghdadi, ana uwezo wa kuunda kundi la magaidi na siasa kali wa kutoka dunia nzima. Na msingi wa hili ni ule ufundi wa kuwaita watu katika Jihad, kuwachota bongo zao mpaka

    waone kuwa hapa wanaifia dini na hakuna namna nyingine Khilafah kusimama ila kwa njia hii ya silaha. Ndio maana unaona misafara ya pikipiki ilivyokuwa kule Mwanza kwenda kila alikokuwa akienda kamanda wao kuswali Ijumaa. Na ndio maana unaona pia moto huu unasambaa kama moto nyikani wakati wa kiangazi kwa sababu ya kuunganishwa na imani. Mtu akiambiwa kuwa ni foot soldier wa proxy war ya mabeberu, wala haelewi.

    Labda swali linalobaki ni hili: Likishapatikana hili jeshi la Salafi siasa kali, nini kazi yake?

    The plan: get into the military and civilian heart of the countries that are declared as a threat to Israel in order to destroy to facilitate thereafter, the take over by the Zionist state on the entire area of the Middle East in order to establish the biblical Greater Israel.

    Hapa kuna malengo mawili. Moja, ni hilo la kuuwa Waislamu kama wanavyouliwa hivi sasa Syria na Iraq, ikielekea katika k u z i s a m b a r a t i s h a n c h i z a Waislamu, kuzidhoofisha na hivyo kuibakisha Israel kuwa ndio bosi wa Mashariki ya Kati. Pili, ni kuwa ukishazidhoofisha nchi hizo, inakuwa rahisi pia kupora mali (mafuta) utakavyo.

    Ukija huku kwetu, ukishakuwa na kundi kubwa la ki-Abu Baghdadi, ni wazi kuwa watafanya fujo zile zile wanazofanya Syria na Iraq. Watauwa Waislamu na wasio Waislamu. Jamii itakuja juu, kwa maana ya serikali. Watakao hujumiwa watakuwa ni Waislamu kwa kisingizio cha kupambana na magaidi. Kwa namna hiyo, Waislamu watateswa, watauliwa na kudhoofishwa. Wasiokuwa Waislamu watakuwa juu. Sasa ukichanganya na ule upumbafu mwingine wa kuwatoa vijana vyuoni, kukimbia kazi serikalini/taasisi za umma na kule Bungeni, utaona ni kwa namna gani mkakati huu utakavyowamaliza Waislamu.

    T.E . Lawrence , maarufu Lawrence of Arabia, akijifanya kipenzi cha Muarabu, alikuwa k a c h e r o w a U i n g e r e z a aliyewasaidia viongozi wa nchi za Kiarabu kufanya uasi na kupigana dhidi ya utawala wa Kiislamu uliokuwa na makao makuu yake Istanbul, Uturuki. Na ikawa ndio sababu ya kuanguka kwa utawala wa Kiislamu na kuanza utawala wa kifalme katika nchi hizo. Hiyo ilikuwa ni katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.

    Hivi sasa wameibuka akina Lawrence wengine, wanapigana kusimamisha Khilafah wakati wenyewe ni Mazayuni. Waislamu wamo tu. Maadhali akina Elliot Shimon wanajiita Abu Ismail, tayari washakuwa Masheikh na makamanda wa Jihad!

    Mara kadhaa Quran inauliza: H a m n a a k i l i ? H a m u o n i ? Hamtafakari? Hamzingatii?

  • 11 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 17-23, 2014Makala

    N I L I B A H AT I K A k u i s o m a barua ya wazi ya muandishi Ali Saleh aliyomuandikia rais wa Tanzania Mheshimiwa Rais Jakaya Kiketwe iliyohusiana na shutma ya udhalilishwaji wa Masheikh wa Zanzibar wanao shikiliwa juu ya shutma ya kesi ya ugaidi Tanzania Bara.

    Wakati niki isoma barua ya muandishi huyu binafsi, nilikuwa nalengwa lengwa na machozi juu ya shutma nzito za aina za udhalilishaji huo; dhana iliyoniambaia hata yule mpelekewa naye bila shaka angebubujikwa na machozi n a u c h u n g u z i wa h a r a k a ungeelekezwa ufanywe haraka.

    Hata hivyo mwandishi huyu hakuvunjika moyo na kubweteka pale tu alipoiona Rasimu ya Katiba ilio pewa jina la ya Warioba jinsi ilivyotiwa kitanzi Chimwaga huku baadhi ya Wazanzibar wakiwa ndani yake wakishangiria kwa vigele gele na hoi hoi katika azma yao ya potelea mbali wacha Zanzibar izame, lakini ilivyokuwa wazo la kuiokowa ni kutoka upinzani naizame.

    Akiona bado ipo nafasi ya kuizamuwa mara hii muandishi huyu aliijaribu bahati yake kwa Barua ya Wazi kwa Wajumbe wa Bunge la Katiba Kutoka Zanzibar kuwataka kusema HAPANA kwa rasimu ile ambayo yeye aliiona sasa Tanganyika bila soni ina dhamira hasa kuimaliza Zanzibar hata kile kidogo ambacho imesaza kiwe hakipo kabisa.

    Akawaorodheshea Wajumbe hawa wa Bunge la Katiba Kutoka Zanzibar mifano iliyo wazi mingi mingi kwa sisitizo la, Sikweli na sikweli kabisa kwamba Katiba inayopendekezwa ina maslahi na Zanzibar.

    Akawagogoteza, Rasimu ya Katiba hii, Zanzibar haiwezi kuwa sawa na ser ika l i ya Tanganyika ijiitayo ya Muungano hata kidogo. Rasimu hii haiipi Zanzibar maamuziye yote yale ya maana, hata yale maamuzi ya kumteuwa rais wa Zanzibar itabidi kuamuliwa Chimwaga. Kwa yale ambayo aliwaorozeshea muandishi huyu yalitosha kwa mtu aliye timamu kuamuwa kujinusuru maisha yake kwa kuvuka mkondo wa Nungwi kwa kuogelea au kwa kujisalimisha katika meli.

    Lakini matokeo yake ilikuwa ni mithili ya Mtume Muhamad ( s.a.w.) na ami yake Abu Jahel; pale Mtume alipo kuwa akiwaelezea watu walio mzungumka juu ya safari yake ya Miraj. Katika kulitolea ushahidi wa hili, alisema alipita Baitul Mukadas na hapa aliswali rakaa mbili. Abu Jehel katika hili akamtaka Mtume

    Ali Saleh, sema na wananchi wapokea posho washatusaliti

    Na Juma Ali Simba

    auleze jinsi ulivyo huo msikiti wa Baitul Mukadas kama kweli aliswali humo. Mtume alipo uelezea jinsi msikiti ulivyo, Abu Jehel alimwambia Mtume msikiti umeupatia sawa sawa lakini tatizo wewe ulosema siye.

    Hiki ndicho kilichojiri kwa muandishi Ali Saleh, kwa barua yake ya wazi kwa Rais na ile Barua ya Wazi kwa Wajumbe wa Bunge la Katiba Kutoka Zanzibar. Si kwamba alichokiandika ndicho kilichokuwa na mushkeli, hasha lakini tatizo lililo jitokeza ni yeye ambaye aliye andika ndiye tatizo.

    K w a b a a d h i y a w a l e tuliobahatika kuzisoma barua zote za muandishi huyu na matokeo tunayo yashuhudia tunaweza kuimithilisha kazi yake mithili ya bure ghali. Lakini mimi si miongoni mwao, hasa kwa ile barua ya Wazi kwa Wajumbe wa Bunge la Katiba Kutoka Zanzibar kuwataka kusema HAPANA kwa rasimu.

    Tatizo ni kwamba muandishi huyu maskini aliwaandikia wajumbe waliokuwa sio na wakati sio. Aliwaandikia wajumbe walio tayari rambishwa asali, tayari wameshapokea vijisenti kujisaliti nafsi zao na kuisaliti nchi yao, tayari hawaoni haja tena ya kujimualia wenyewe, tayari wameshakubali tarjisi za ndoa Zanzibar izifatiye Tanganyika. Wao wameshajikubalisha.

    Ta y a r i w a j u m b e h a w a washakubali, na wanacho kitaka kwetu sisi nasi tukubali, kwamba

    mfumo bora wa kuwa na serikali ni huu wa mbili wanao uafiki wao, na mfumo huu ndio suluhisho pekee la Watanzania t u k i we m o Wa z a n z i b a r i . Tayari tuikubali rasimu hii ya katiba ya Tanganyika ambayo imebatizwa jina la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania kumbe ni katiba ya Tanganyika inayo elekea kutoka kwenye kiitwacho serikal mbili kwenda serkali moja .

    Hivyo n ionavyo mimi ukweli ni kwamba barua ya ndugu Ali Saleh wastahiki wa kuambiwa na kugogotezwa tena na tena na kuaidhiwa tuseme HAPANA kwa rasimu ya katiba hii ni wananchi.

    Ni sisi hasa wa kusema HAPANA, kwa sababu tokea awali tulishasema kile tunacho kitaka kwa kuamini hicho ndio chenye faida nasi, maslahi bora na mustakabali mzuri. Kwa sababu tuko Wazanzibari tunaielewa katiba tuliyo nayo hivi sasa ya Muungano jinsi inavyotubana, jinsi inavyo tudhili katika maslahi yetu, jinsi ilivyo ificha Tanganyika ndani ya Tanzania, lakini bado tunafurukuta huku tukisema kero la Muungano ni kero dogo tuu. Ni udhifu wetu huu sasa ndio umetowa nafasi ya kupitishwa hadaa na ghilba ya rasimu itayo iangamiza Zanzibar.

    Ni ukweli ulio wazi katiba hii iliyo pendekezwa kwa

    kiasi kikubwa haina manufaa na mema juu ya Zanzibari na kama yamo ni mithili ya kutafuta chuwa katika mchele wa basmati. Kijuu juu ni njema lakini ki undani ni katiba iliyokunjuwa makucha yake na kukiweka kiywa chake wazi tayari kuimaliza Zanzibar kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni, na hata kielimu.

    Kwa miaka Wazanzibari tumekuwa na bado tunalilia Muunganmo ambao utakuwa na serikali mbili zenye usawa, Zanzibar yenye mamlaka yake kamili, yenye mamlaka ya kujiamulia mambo yake ya ndani na nje yenyewe. Yenye mamlaka ya kusema huyu anaweza kuwa rafiki yangu na na huyu la, na kwa upande wa Tanganyika iwe hivyo hivyo ambapo hivi sasa hivi ndivyo ilivyo kwa Tanganyika. Iwepo pia serkali, ikiwa ni ya Jumuia, Muungano, Shirikisho, au kwa jina lolote lile lakini siyo Muungano unaoitwa wa Tanzania huku Tanganyika ikijificha ndani ya koti jeusi ndani ya usiku wa kiza na kumiliki mamlaka ya Tanganyika na Zanzbar kwa kupitia mgongo wa serkali ya Muungano.

    Wazazibari tulitaka na bado tunataka rasimu ya katiba isemayo wazi wazi, Tanzania ni nchi mbili, Zanzibar na Tanganyika zinazo fanya muungano, hatukutaka rasimu isemayo, Jamhuri ya Muungano ni nchi moja yenye mamlaka kamili.

    Wengi tunajiuliza ni kwa kitu gani hasa wenzetu hawa Wajumbe wa Bunge la Katiba Kutoka Zanzibar wanacho jifakharishia, kuipigia vigere gere, hoi hoi, na vifijo rasimu ya katiba hii ambayo muelekeyo wake ni kuiondowa Zanzibar kwenye ramani ya dunia?

    Kwa sababu haya na mengi mengineo tuliyoyapendekeza wakati wa mchakato wa kuratibu rasimu iliyo simamiwa na Mwenyekiti Mheshimiwa Warioba na wenzake, siyo yale yaliyomo ndani ya rasimu hii iliyofanyiwa marekebisho na Bunge la Katiba maalum, na kwa sababu Wajumbe wetu wa Zanzibar walishindwa kuipigia kura ya HAPANA rasimu hii juu ya kwamba waliombwa kufanya hivyo kwa lugha fasaha, sasa namuomba Ali Saleh atuwaidhi, atunasihi, atushawishi, atusemeshe, na atuombe sisi wananchi wa Zanzibar tusi ikubali.

    Sisi tutakusikia na tutapiga kura ya HAPANA kwa rasimu ya katiba hii ya vijisenti. Bado hatujachelewa.

    BAADHI ya Waislamu wanaotuhumiwa kesi ya ugaidi wakiwa katika mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaama juzi.

  • 12 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 17-23, 201412 Makala/Mashairi/Habari

    Sheikh Mtupa awapa nasaha wahitimu Mzinga sekondariInatoka Uk. 16

    Aidha aliwaasa kuepuka kujihisi kuwa wao ni wasomi na kushindwa kufanya kazi za nyumbani.

    Nyinyi bado ni watoto tu na wajibu wenu kwa wazazi upo pale pale , kuweni msaada kwa wazazi wenu kwa muda wote wa

    kusubiria majibu ya mitihani yenu, kwani wao ndio walio wafikisheni hapo mlipo sasa.

    Elimu mliyoipata ni kwa juhudi zao kuwasomesha wala sio kwa ujanja wenu, mkifanya hivyo mtapata faraja na Allah atawasimamia k a t i k a m a m b o ye n u . Alisema Sheikh Mtupa.

    Akisoma r i sa la kwa

    mgeni rasmi , Us tadhi Hassan Baruchy, alisema wanafunzi wa Kiislamu wa shule hiyo wamebahatika kupata sehemu maalumu ya kufanyia ibada kutoka kwa uongozi wa shule hiyo, pamoja kupatiwa nyenzo za mafunzo ambazo ni vitabu ( Juzuu na Masahafu) na walimu wa kuwafundisha.

    Karibuni karibuni, Mahujaji wa nchini, Karibunikaribuni, wa Bara na Visiwani, Karibuni karibuni, kwa sururi karibuni,Karibuni Mahujaji, tushikamane lengoni.

    Karibuni karibuni, dhuyufu wa Rahmani, Karibuni karibuni, kiramu kwetu wageni, Karibuni karibuni, kwa heshima karibuni, Karibuni Mahujaji, tushikamane lengoni.

    Karibuni karibuni, kutoka ughaibuni, Karibuni karibuni, toka Makka ibadani, Karibuni karibuni, kwa ibada karibuni, Karibuni Mahujaji,tushikamane lengoni.

    Karibuni karibuni, kwa Hijja kutoikhini, Karibuni karibuni, kwa kumridhi Manani, Karibuni karibuni, kwa ridhaa karibuni, Karibuni Mahujaji, tushikamane lengoni.

    Karibuni karibuni, kwa nguzo kuithamini, Karibuni karibuni, kwa muudhamu thamani, Karibuni karibuni, kwa kutimiza rukuni, Karibuni Mahujaji, tushikamane lengoni.

    Karibuni karibuni, msafara uungeni, Karibuni karibuni, wa harakatiza dini, Karibuni karibuni, kwa jihadi karibuni, Karibuni Mahujaji,tushikamane lengoni.

    Karibuni karibuni, kikoa shikamaneni, Karibuni karibuni, kunusuru yetu dini,Karibuni karibuni, kwa nusura karibuni, Karibuni Mahujaji, tushikamane lengoni.

    Karibuni karibuni, mahaji twakungojeni,Karibuni karibuni, na mahajati nchini, Karibuni karibuni, kwa pamoja karibuni, Karibuni mahujaji, tushikamane lengoni.

    Karibuni karibuni, lengo lizingatieni, Karibuni karibuni, la hijja kwa tamakuni, Karibuni karibuni, kwa taadhima ya dini, Karibuni Mahujaji, tushikamane lengoni.

    Karibuni karibuni, nimefika ukingoni, Karibuni karibuni, mwa kukukaribisheni, Karibuni karibuni, kalamu naweka chini, Karibuni karibuni, Mahujaji karibuni.

    ABUU NYAMKOMOGI MWANZA.

    KARIBUNI MAHUJAJI

    S H U K U R A N I z o t e a n a s t a h i k i M we n ye z i Mungu, Mola mlezi wa walimwengu na mwisho mwema kwa wenye kumcha M we n ye z i M u n g u n a hapana uadui isipokuwa kwa madhalimu, nina shuhudia kwamba hapana Mola apasaye kuabudiwa k wa h a k i i s i p o k u wa Mwenyezi Mungu, Mola wa ulimwengu na rehema na amani zimfikie Nabii wetu na muombezi wetu bwana wetu Muhammad na jamaa zake na sahaba zake wote.

    Ama baada ya utangulizi huu mfupi mpenzi msomaji wa safu hii ya makala, hakika dini ya Uislamu inalingania juu ya upole na ulaini na huruma na ihsani kwa watu wote, bila ya kuagalia dini zao au imani zao au utaifa wao au rangi zao au lugha zako, kwani Uislamu misingi yake ni Qurani Tukufu, kitabu ambacho ni zawadi na ni rehema pia kina misingi ya kuishi maisha bora na wengine, ambayo yametengwa kwa tabia ya heshima na ihsani kwa watu wote.

    Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, Na semeni maneno mazuri kwa watu (83 Bakarat). Na uzuri ulioje wa maneno mazuri haya ya Mwenyezi Mungu.

    Na semeni kwa watu yaliyo mazuri na neno watu ni tamko kwa ajili ya watu wote Waislamu na wasio Waislamu. Pia anasema kat ika Surat Mumtahina, aya ya (8), Hawakatazini Mwenyezi M u n g u w a l e a m b a o hawakupigini vita katika dini na wala hawakutoeni katika miji yenu kuwafanyia ihsani, Mwenyezi Mungu

    Ihsani kwa wasiokuwa Waislamu

    Na Dk. Ukail Mohamed Ukail

    anawapenda wafanyao uadilifu.

    A n a s e m a U s t a d h D r . M o h a m e d S a y e d Twantwau, Sheikh wa Al-Azhari Mwenyezi Mungu amrehemu, katika tafsiri yake ya aya hii tukufu, kisha amebainisha Mwenyezi Mungu kwa waumini ambao watakwenda nao katika kupendana kwao na uadui wao na kuungana kwao na kununiana kwao, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu, hawakatazeni Mwenyezi Mungu, kisha akasema Mtume [s.a.w] ndio mpokee mama yako. Na amepokea Imamu Ahmad toka kwa A b d i l l a h b i n Z u b a i r i , amesema ilikuja Katiilatu bint Abdi Al-izi, naye akiwa mushirki (kafiri) kwa mtoto wake Asmaa binti Ab bakri ,alikuja na zawadi akakataa Asma kukubali kuipokea zawadi yake au kuingia ndani mwake hadi akaenda kwa Aisha, ili akamuulize Mtume [s.a.w] juu ya hilo.

    Akauliza, akateremsha M w e n y e z i M u n g u : Hawakatazeni Mwenyezi Mungu kwa wale ambao h a w a k u p i g e n i v i t a katika dini. Na amesema Hassani na Abuu Swalahe, imeteremka aya hii katika kabila la Kiarabu, walikuwa wa m e w e k a m a p a t a n o kwamba arudi na akasema Muhaidu iliteremka kwa watu mjini Makka waliamini lakini hawakuhama wala watu wa Makka na wale wa Madina wanasifiana kwa kulaumiana kwa wema wao na kuacha kwao faradhi ya kuhama na maana ni kwamba hawakatazani Mwenyezi Mungu Mtukufu e n y i wa u m i n i j u u ya kuwapenda na kuungana n a m a k a f i r i ( a m b a o hawapigani na nyinyi katika dini na wala hawakutoeni kat ika mi j i yenu) kwa maana hawakupigeni kwa sababu ya kuwa nyinyi ni waislamu na hawajaribu kukuudhini ni kwa maudhi yoyote kama vile kufanya juhudi za kukutoeni katika miji yetu hawakatazeni kwenu Mwenyezi Mungu k u w a f a n y i a i h s a n i k a t i k a k u h u d u m i a n a na kuwakirimu na pia m u w a f a n y e u s a w a muwahukumu kwa uadiliu (usawa) na muishi nao vizuri kama wanavyoishi nanyi

    vizuri wala msiwafanyie ujeuri katika hukumu yoyote kwa hakika Mwenyezi M u n g u a n a w a p e n d a wafanyao usawa yaani uadilifu katika kauli zao na vitendo vyao na hukumu zao ambao wanawapa watu haki zao zote kwa njia ya uadilifu nafsi zao hizo zinawafanyia wema wale ambao na wao wawafanyia wema pia na baada ya ufafanuzi huu wa kutosha na ubainifu huu mwingi toka kwa mheshimiwa Imamu, Mungu amrehemu inapambanuka kwa kila Mwenye aki l i kwamba Mwenyezi Mungu haamrishi ubabe wala kuadhibu wala uharibifu bali ameamrisha ihsani hadi kwa makafiri na wale wasio na dini kabisa.

    Hapana shaka juu ya yote hayo ndiyo mambo yanayoweza kumuathiri anayelinganiwa na kuingia na kushikamana k ias i kwamba hakumkuti asiye M u i s l a m u , i s i p o k u wa atampongeza na kukiri juu ya uwepesi wa dini hii tukufu na ametilia mkazo Mtume [s.a.w] katika wosia wake juu ya wale wanaoishi kwa amani kinyume na Waislamu na kumlingania kila anayekwenda kinyume na usia huu kuwa, watapata hasira za Mungu na adhabu zake. Ikaja kwenye hadithi yake tukufu neno lake [s.a.w] kwamba, yeyote mwenye kumuudhi huyo ameniudhi m i m i . A m e m u a h i d i Mwenyez i Mungu p ia a m e s e m a M w e n y e z i kumuudhi mimi ni mgomvi wangu nitagombana naye siku ya kiyama katika kitabu cha jamii swaghir cha Albani

    Na amesema tena Mtume [s.a.w] yeyote mwenye kumdhulumu muahida au akampunguzia haki yake akamlazimisha kazi iliyozidi uwezo wake au akamchukulia kitu chake bila ya ruhusa yake, basi mimi nitakuwa na hoja naye siku ya kiyama. Ameipokea Abuu Daudi katika suna z a k e n a wa m e e k e l e z a Makhalifa wa Mtume [s.a.w] juu ya kuzichunga haki hizi na uharamu wake.

    H i v y o t u n a m u o m b a Mwenyezi Mungu Mtukufu aturuzuku milele kulingana katika dini yake kwa hekima na mawaidha mazuri na kuwanyia ihsani watu wote.

    wabillah tawfiq

    1.Ikisomwa inapenya, ngozini hadi damuniAkilini inaonya, yaangazio moyoniWallahi nakuambiya, hiyo ndiyo qur-aniKama kuna neno zuri, halishindi qur-ani

    2. Qur-ani maajabu, maneno yenye hekimaKwa lugha ya kiarabu, kila mtu anasomaNi neema yake Rabbu, kwa mtume ametumaKamwe hayata tokea, maneno kuzidi haya

    3. Sijaona neno tamu, zaidi ya qur-aniYake nzuri ridhimu, inavyopita kinwaniKusoma haishihamu, yaburudisha moyaniQur-ani ndiyo damu, ya uhai wa milele

    4. Kipi kinakosekana, ndani yake qur-aniMaovu na yenye mana, yote kimeyabainiAjibu iliyofana, inavyokuza imaniZawadi gani twataka, zaidi ya qur-an

    5. Kitabu kilicho nuru, kimetoka kwenye nuruMesafirishwa na nuru, mepokelewana nuruKiishicho kwenye nuru, chasomwa na wenye nuruNi nuru juu ya nuru, chaongoza kwenye nuru,

    Abu nurain Al-Tanza

    LADHA ISIYO KIFANI

  • 13 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 17-23, 2014MAKALA/TANGAZO

    K I L A s i f a n j e m a zinamstahiki Mwenyezi Mungu Swala na Amani z i m f i k i y e M t u m e M u h a m m a d ( s . a . w ) Moja kati ya majina ya Mwenyezi Mungu ni As-Salaam (Chanzo cha Amani, ukamilifu na Mtoa Amani).Amesema Allah (s.w.):

    Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hakuna abudiweye kwa haki i s i p o k u wa y e ye t u ; M f a l m e , M t a k a t i f u , M w e n y e S a l a m a , mtoaji amani, mwenye kuyaendesha mwenyewe mambo yake, mwenye shani (Al-Hashr:23) :

    Hivi sasa viongozi mengi wa kisiasa hawaishi kwenye midomo yao kutamka amani, amani, amani !!!!!

    Tanzania Kisiwa chsa Amani hata walevi , wimbo ni huo huo.

    A m a n i n i h a l i inayoiwezesha jami i kusalimika na madhara ya aina zote, yawe ni ya kiimani, kimwili na kiakili. Na amani kubwa mno n i ya waumini watakayoipata kesho Akhera.

    Amesema Allah (s.w.);Hawatasikia humo

    maneno ya upuuzi wala m a n e n o ya d h a m b i . Isipokuwa maneno ya Salama na Amani. (Al-Waqiyah 25-26).

    Wacha Mungu ndio pekee watakaopata amani hapa dunia na kesho akhera. Amesema Allah (s.w.):

    ( H a p a n a s h a k a ) wale walioamini na hawakuchangaya imani yao na ushirikina, basi hao ndio watakaopata amani. (Al-Anam:82)

    Na amani itakuwa juu ya wale wanaofuata uongofu. (Ta Ha 26)

    Jamii yoyote ambayo washirikina ndio wanao tawala, haitakuwa na amani na dhuluma ndiyo itakayokuwa inatawala mfumo wa maisha ya jamii.

    Amesema Allah (s.w.): N a L u q m a n

    alipomwambia mwanaye kwa kumpa mawaidha; E w e m w a n a n g u usimshirikishe Mwenyezi

    Amani haitadumishwa kwa mechi kati ya Masheikh na Maaskofu

    Na Abu Saumu, Kombo Hassani Kidumbu.

    Mungu kwani hakika ushirikina bila shaka ni dhuluma iliyo kubwa. (Luqman 31:13)

    Dhuluma ni hali ya mtu/watu kuweka kitu mahali pasipo stahiki. Neno dhuluma unaweza kulitafsiri kwa maana pana zaidi au ndogo zaidi kiasi upendacho, lakini ukweli ni kwamba katika jamii yoyote ambayo HAKUNA UADILIFU na HAKI haitendeki, basi ni wazi kuwa dhuluma imetawala katika jamii hiyo.

    Siku zote kimaumbile watu wanao dhulumu, hupendelea kuwa katika hal i hiyo kwa muda wote, lakini ni ukweli usiopingika kuwa hakuna binadamu mwenye akili timamu ambaye huwa tayar i kudhulumiwa s iku zote . Hal i h i i imethibitishwa na ukweli wa k i h i s t o r i a p a l e ambapo tabaka la wenye kudhulumu katika jamii mbalimbali walipoamka na kudai haki zao kwa mujibu wa mazingira waliyokuwa wakiishi.

    Hapa Tanzania dhuluma kwa Waislam limekuwa jambo kongwe kabisa. Wais lam wamekuwa wa k i n ya n ya s h wa n a

    d h i d i y a L u k u v i . Chanzo: Uhuru la Siku ya Jumanne Mei 6, 2014.

    Tuhuma wanazozitoa baadhi ya Waislamu dhidi ya Serikali utatuzi wake hauwezi kwisha kwa kuchezwa mechi baina ya Masheikh na Maskofu ili kuleta amani. Bali utatuzi wa kudumu wa usuguano u l i o p o b a i n a y a Waislamu na serikali ni ule uliopendekezwa na Halmashauri Kuu ya Waislamu (1999) k a t i k a b a r u a y a o waliyomwandikia Rais, na ambao kwa ubaya wa bahati, ulikataliwa.

    Na wala si busara tena kutarajia kuwa mgogoro huu utakwisha w e n y e w e n a k w a kuwaweka gerezeni baadhi ya Waislamu n a b i l a k u c h u k u a hatua za makusudi za kuudhibiti. Kauli za hivi karibuni za baadhi ya Waislamu zinaonyesha k u w a s u b i r a y a o inaelekea ukingoni na imani yao kwa serikali inazidi kupungua. Na hii si ishara nzuri kwa mustakabali wa nchi yetu.

    Wabbilah Tawfiq.

    kupuuzwa tangu enzi ya ukoloni. Hali hii ndio imepelekea kwa Waislam p a l e w a n a p o a m k a na kutaka ku j inasua n a d h u l u m a h i y o , watashughulikiwa na kuzibwa mdomo.

    Lakini mpaka sasa S e r i k a l i i n a y o d a i kuendeshwa kwa utawala bora/sheria na uwazi, bado inatia pamba masikioni kuhusiana na malalamiko ya Waislamu juu ya madai ya dhuluma ambazo wanadai wanafanyiwa.

    Viongozi wa kisiasa wanaiaminisha jami i k wa P r o p a g a n d a ya kwamba kuna viashiria vya uvunjifu wa amani hapa nchini baina ya Waislamu na Wakristo; hii ni propaganda ya kuitoa agenda ya Wais lamu iliyopo mezani. Kufanya ni ugomvi wa Wakristo na Waislamu.

    M a t h a l a n i , S h e i k h wa BAKWATA Mkoa w a D a r e s S a l a a m , Alhad Mussa Salum, wakat i akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam, mnamo tarehe 5/05/2014 alisema: Katika siku za karibuni kumekuwepo na propaganda zinazowataka Waislamu kumchukia

    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Sera, Uratibu na Bunge) Mhe. Lukuvi, bila ya sababu ya msingi. Na alisema: hatua hiyo imewafanya baadhi ya waumini (wa Kiislamu) kuomba dua maalumu

    WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Sera, Uratibu na Bunge) Mhe. Lukuvi.

  • 14 AN-NUURDHUL-HIJJA 1435, IJUMAA OKTOBA 17-23, 2014Habari

    Sheikh Mselem azirai gerezani Inatoka Uk. 16

    Inatoka Uk. 16M a k k a k we n d a M a d i n a , alisisitiza Ust. Saleh.

    Aliongeza kuwa kabla ya hijra ya Mtume, yaani kuhama kutoka Makka kwenda Madina, Waislamu walikuwa wanajua tarehe zao kupitia kuzaliwa Mtume (s.a.w) mfano Sayyidna Uthman alizaliwa mwaka wa Sita ( 6) baada ya kuzaliwa Mtume (S.a.w).

    Baada ya Mtume (S.a.w) kupewa Utume, wakaanza na mtindo mwingine wa kuhesabu kwa mfano, Sayyidna Omar alisilimu mwaka wa tano ( 5) baada ya Mtume (S.a.w) kupewa Utume.

    Aidha Mwenyeki t i huyo alieleza kuwa chanzo cha mwaka wa Kiislamu kuwa ilipofika mwaka wa 17h katika Hilafa ya Sayyidna Omar, ndipo fikra za tarehe zikaanza.

    Alisema, Maswahaba walianza kuhesabu tarehe kutokana na kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema

    MIN AW AWAL YAUMIN ( 9:108).

    Ni siku ya mwanzo ambayo Uis lamu u l ipopata nguvu na Mtume (s .a.w) akaweza kumuabudu Mola wake kwa amani na bila misukosuko yoyote.

    Aidha alisema Ust. Salehe kuwa taasisi ya Istqama imeandaa mihadhara mbalimbali ya kuukaribisha mwaka huo mpya wa Kiislamu ambayo itafanyika kat ika Mis ik i t i tofaut i , i l i kuwafanya Waislamu waweze kuijua kalenda yao na kuifanyia kazi .

    Kwamba lengo la kufanya hafla hiyo ni kutangaza kalenda ya Kiislamu ili itumike tofauti na sasa ambapo inatumika kwa matukio maalumu kama vile ndoa, eda, kuanza na kumalizika mwezi wa Ramadhani, wakati wa Hijja na sikukuu za kidini.

    Taasisi ya Istiqama imekuwa ikifanya sherehe hizi kila mwaka na kuwa na kauli mbiu yake, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni Uislamu na Mazingira.

    Inatoka Uk. 16 K i o n g o z i b o r a n i y u l e

    a n a y e s h i r i k i a n a n a w a l e anaowaongoza kwa kupokea ushauri wao, malalamiko yao na kuyafanyia kazi kwa uadilifu, lakini leo hii, kiongozi akisikia Waislamu wana majambia, basi itatolewa amri ya kamata kamata bila hata kufanya uchunguzi na hatimaye kuwadhuru watu bila sababu za msingi. Alisema Ust. Maduga.

    A l i o n g e z a k u wa k i o n g o z i mwadilifu ni lazima awe karibu na raia wake na anapokosea, awe tayari kukubali kukosolewa ili atakapoamua jambo raia anaowaongoza waweze kuridhika. Lakini