ANNUUR 1210A

20
ISSN 0856 - 3861 Na. 1210 RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA , JANUARI 1 - 7, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu www.annuurpapers.co.tz au facebook:[email protected] Mhitimu Segerea aguswa na huruma ya Masheikh Shuwari inayoitumbukiza shimoni Zanzibar Soma Uk. 3 Soma Uk. 10 KATIBU Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad. Hakuna nchi iliyoendelea kwa soko huria Maalim hatoshiriki Sherehe za Mapinduzi CCM watakiwa kufungasha virago Ikulu Watakiwa kusubiri 2020 wajaribu tena Amesema kweli Mzee Moyo, Bi Sakaya MZEE Hassan Nassor Moyo MANSOUR Yusuf Himid Soma Uk. 9

Transcript of ANNUUR 1210A

Page 1: ANNUUR 1210A

ISSN 0856 - 3861 Na. 1210 RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA , JANUARI 1 - 7, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz au facebook:[email protected]

Mhitimu Segerea aguswa na huruma ya Masheikh

Shuwari inayoitumbukiza shimoni Zanzibar

Soma Uk. 3

Soma Uk. 10

KATIBU Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.

Hakuna nchi iliyoendelea kwa soko huria

Maalim hatoshiriki Sherehe za Mapinduzi

CCM watakiwa kufungasha virago IkuluWatakiwa kusubiri 2020 wajaribu tenaAmesema kweli Mzee Moyo, Bi Sakaya

MZEE Hassan Nassor MoyoMANSOUR Yusuf Himid

Soma Uk. 9

Page 2: ANNUUR 1210A

2 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 1- 7, 2016Mafundisho ya Qur'an/Uwanja wa Maarifa

Aal Imran: 117

Fethullah-Gulen“Na hakuwadhulumu wao

Mwenyezi Mungu isipokuwa nafsi zao, wanazidhulumu”. [Aali-Amran 117]

Mara nyingi huja masuala haya katika Qur’an tukufu kwa maneno yaliyo katika muundo huu “Na hakuwa dhulumu wao Mwenyezi Mungu, isipokuwa walikuwa nafsi zao wanazidhulumu”. Kama inavyoonekana , tofauti kati ya maana haya mawili ni kitendo cha kuwa “walikuwa”.

Ndiyo hakipatikani kitendo kuwa “walikuwa” katika ambayo iko hapo juu. Na jambo hili linatukumbush,a na Mwenyezi Mungu ndiye mjuzi zaidi mambo yafuatayo:

Dhulma ya watu hawa kwa nafsi zao haitakuwa katika uficho na siri, bali itakuwa kwa uwazi na kwa kuonekana, kwa sifa ya kuwa haki, na kuepuka dhuluma yao na hapana mfano kwa nafsi zao kutakuwa kwa uwazi mpaka daraja ambalo hapatakuwa na haja ya kulifichua jambo hilo, kwa sababu watu wote wataliona na watalielewa.

Hakika kitendo “kuwa” k i n a f i d i s h a m a a n a ya kutokuwepo huko nyuma, na kupatikana kwake hivi sasa. Ama makafiri wao wanazidhulumu nafsi zao tokea zamani na mpaka sasa. Hili ndilo jambo ambalo wanalishuhudia watu wote. Kwa sababu hiyo, imeepukana aya hii na kitendo cha kuwa “walikuwa”.

1. Kwa ajili ya kuyaweka wazi maana ya kifungu cha pili, tunasema kwamba hakika wale ambao walipewa kitabu baada ya kufika kwa sababu ya vitabu hivi kwenye uongofu katika kipindi katika zama, walipondoka wakaacha uongofu huu na wakatumbukia katika ukafiri na upotevu. Maana h a wa k u wa m a d h a l i m u tokea mwanzo, kwa sababu hii, kumekuwa na uwiano kukitumia kitendo cha kwa

ajili ya kuliweka wazi jambo hili. Ama hali ya madhalimu, tokea mwanzo haina haja ya kufungwa kwa namna yoyote wala kwenye kuwekwa wazi kwingine.

“Kisha akakuteremshieni baada ya huzuni amani – amani yenyewe ni usingizi, hali ya kulifunika kundi moja katika nyinyi na kundi jingine ziliwashughulisha nafsi zao wanamdhania Mwenyezi Mungu, isiyokuwa haki dhana ya kikafiri, hali ya kuwa wanasema: Jee tuna sisi katika jambo hili kitu chochote? Sema: Hakika mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu wanayaficha katika nafs i zao yale ambayo hawayadhihirishi kwako, wanasema lau tungekuwa tuna sisi katika jambo hili kitu chochote tusingeuliwa h a p a . W a a m b i e l a u m n g e k u wa m a j u m b a n i mwenu wangetoka wale a m b a o w a m e a n d i k w a kuuawa kwenda mahali pa maangamizi yao na ili Mwenyezi Mungu ayajaribu yaliyomo vifuani mwao na ili ayasafishe yaliyomo katika nyoyo zao na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliyo vifuani”. [Aali-Imaran 154]

Walikuwa ni wanafunzi wa A-Naur wakati wanapopatwa na maudhi yoyote au dhulma yoyote na kutendewa jambo lisilofaa, anawakumbusha Al-Ustadh Badiu A-Zamani, ulazima wa kurudia rudia kuisoma aya hii na kuifasiri. Na kama mtu mfano wangu ambaye amefaidika na somo la Al-Ustadh A-Noursy, na tuisome aya hii mara nyingine na tuchukue kutokana nayo somo ambalo kunapasa kulikuchukua.

Hakika kuzama kundi lolote linalosumbuana na hofu na kuyumba kuliko kukubwa katika usingizi na kufika kwao kwenye amani na utulivu wa roho na moyo, na kwenye upole uliyokamilika; hakika si jambo jingine huo ni msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu na fadhila kutoka kwake kwa kundi hili. Hiyo ni hoja na ushahidi wa kujiamini kwa kundi hilo, na kujisalimisha na kuyategemea mambo kwa Mwenyezi Mungu na kutegemea katika mambo hayo kutoka kwa kundi hili juu ya Mwenyezi Mungu mtukufu. Katika vita vya Badri na Uhud, kulikuwa kudhihiri kwa mfano wa utulivu huu na ahadi hii ya Mwenyezi Mungu na kutuka kwa upole huu wa Mwenyezi Mungu kwa kiwango cha kushikamana na dini na kwa kiwango cha kuelekea nyoyo

kwenye mihrabu yake. Hili limekuja katika kila hali na katika kila kuelekea kuliko kwa kweli.

Ndiyo, hakika dini ndiyo roho ya maisha, na kuliweka juu tamko la Mwenyezi Mungu, ndiyo kazi takatifu sana, na kuyatoa maisha na kuyamaliza katika njia hii, ndiyo njia ya kuugonga mlango wa maisha ya milele na kupatikana kwa milele. Kwa kipimo cha radhi ya Mwenyezi Mungu mtukufu kuweka kama lengo la malengo yote katika mkabala huo, utavuna msaada wake na uchungaji wake na himaya yake. Huku kusaidiawa na kuchungwa kumeonyeshwa kila zama na kila mahali , na kwa kiwango chenye kukaribiana n a k u s a i d i wa k w e n y e kutajwa kwa maswahaba kila yanapokamilika mashariti ya msaada huu na mazingira ya k e n a s a b a b u z a k e . Atakayekuwa katika waumini katika mfano wa kiwango hiki cha imani na kujisalimisha, na kumtegemea Mwenyezi Mungu, anaweza kuingia hata moto wa Namrudh kwa kifua kilichofunguliwa na moyo uliyotulizana bali huenda akaugeuza moto huo na kuwa ni baridi na salama. Katika mkabala wa maisha haya yaliyopoa na yaliyotulizana ya watu hawa, tunalikuta kundi jingine linashirikiana na watu hawa katika mazingira hayo hayo isipokuwa ni kwamba kundi hilo halivuti hewa hiyo hiyo. Kwa sababu hii tunaliona kundi hilo limebobea katika matakwa kwa nafsi zao. Kwa hiyo, huonekana matatizo yaliyo katika hisia zao na fikra zao ili yakawachoree njia ya maisha ambayo imejaa mambo yenye kupingana yenye kutahayariza. Kwa sababu hii, hawaoni hawa uso wa mapumziko na raha milele, bali wataishi katika hali ya kuyumba, kwa sababu ya kuwa vichwa vyao vimejazwa kwa fikra za kijahiliya – kikafiri. Hata kama wangeamini hawa, kwa hakika fikra zao, kuhusiana na utulivu, kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, zitakuwa ni zenye kuchanganywa na ubaya wa dhana ya aya tukufu:

“Na kundi jingine kwa hakika zimewashughulisha nafsi zao, wanamdhania Mwenyezi Mungu isiyokuwa haki dhana ya kikafiri”

Inaweka wazi hali ya kukata tamaa iliyo nyeusi katika hisia zao na yale ambayo wanasumbuana nayo miongoni mwa kizingazinga na kuharibikiwa.

Jee Unajua?

MASUALA1.Mtume Muhammad (SAW) alikufa akiwa na umri wa miaka mingapi? 53, 63, 73 Jawabu: 632.Sahaba yupi akiitwa Al-Farooq? Jawabu: Umar (bin Khatab)3.Sahaba gani akiitwa upanga wa Mungu? Jawabu: Khalid bin Walid4.Sura ipi ukiendeleza kuisoma katika nyakati za Al-Asri utaondokewa na umaskini? Jawabu:Waaqiyah5.Sahaba gani alimshauri Mtume Muhammad (SAW) kuchimba Khandaki katika vita vya Khandaq? Jawabu: Suleman Farsy6.Mji wa Madina kabla ya kuhamia Mtume Muhammad (SAW) ukiitwaje? Jawabu: Yathrib7.Alipokuwa Mtume Muhammad (SAW) anaumwa nani akiongoza Sala, akiwa Imamu? Jawabu: Abubakar8.Msikiti unaoitwaje alioujenga Mtume Muhammad (SAW) mara tu alipowasili Madina? Jawabu: Masjid Quba9.Jina la mwanzo la Imam Abu Hanifa? Jawabu: Numaan10.Mtume gani alirembewa kwenye moto? Jawabu: Ibrahim

JAWABU CHEMSHA BONGO NAMBA: 32

CHEMSHA BONGO: 33Weka duara kwenye jawabu ilio sawa. Jawabu kamili wiki ijayo.

MASUALA1.Itaje Sura inayotaja juu ya matunda mawili?2.Jina kamili la Imam Shafi.3.Sura ipi ya Quran inayomalizia kwa majina ya Mitume wawili?4.Alipohama Mtume Muhammad (SAW) Makka kwenda Madina alimtaka sahaba yupi alale kwenye kitanda chake?5.Suratul Faatiha ina aya ngapi?6.Ashuraa ipo katika mwezi gani wa Kiislamu?7.Mtume Hud (AS) alitumwa kwa Umma upi?8.Mtume Saleh alitumwa kwa Umma upi?9.Mtume Mussa alifwatana na Mtume gani kwenda kukabiliana na Firauni?10.Jina la ngamia Mtume Muhammad (SAW) alimpanda alipoingia Madina?

1. Pyrimad la Giza lilihesabiwa kuwa ni jengo lilokuwa refu duniani kabla hayajaja mapinduzi ya viwanda, jengo hili lilijengwa kwa kutumia hesabati za hali ya juu na kudhihirisha kuwa elimu ya hesabati ilikuwa imeshajikita katika bara la Afrika miaka 2560 kabla ya kuzaliwa Myume Issa (AS): http://www.curiosityaroused.com/history/how-were-the-pyramids-built/2. Meli ya kitalii ya Tatanic ambaye mjenzi wa meli hii alithubutu kutamka kuwa ni jambo lisilowezekana kwa meli hio kuzama kwa ufundi alioutumia katika ujenzi wake, ilizama mwezi wa April 15, 1912 ikiwa na abiria 2,227 abiria pamoja na mabaharia waliosalimika walikuwa ni 702 tu: http://www.curiosityaroused.com/history/how-many-people-survived-the-titanic/3. Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia vilianza mwaka wa 1914 na chanzo chake kilitokana na kuuliwa kwa Archduke Franz Ferdinad kuondolewa katika kiti cha Ufalme akiongoza kwa nchi ya Austria na Hungary hapo tena mapambano yakaanza baina ya Wa-Austria, Wa-Hungary na Wa-Serbia: http://www.curiosityaroused.com/politics/what-started-world-war-1/4. Bahari ya Dead Sea inafahamika kama "Bahari iliyokufa" ambayo iko katikati ya Jordan na upande wa magharibi inapakana na Israeli. Sifa ya bahari hii ni watu wakiingia hawawezi kuzama: http://www.curiosityaroused.com/nature/why-is-the-dead-sea-called-the-dead-sea/5. Meet the Press ndio kipindi cha Televisheni kilichoonyeshwa kwa kipindi kirefu kuanzia mwaka wa 1947 hadi leo ikiwa na umri wa kipindi hicho miaka 68, kutoka mwaka wa 1947 hadi 1992 ishakuwa na maonyesho 5,100, kipindi hiki kipo mahabubu kinapendwa na watu.: http://www.curiosityaroused.com/culture/the-longest-running-tv-show-of-all-time/6. Ikulu ya Marekani ijulikanao kwa jina la White House ina vyumba 132, sehemu za kukogea 35, ngazi za kupandia kama 8, maeneo 28 ya kuepukana na moto, madirisha 147 milango 412, kiwanja cha kuchezea Tennis, kufanya mazowezi ya Jogging, Chumba cha Snema, Bwawa la kuogolea: http://www.curiosityaroused.com/politics/how-many-rooms-are-in-the-white-house/7. Ngozi ndio kiungo kikubwa cha umbo la mwanadamu koliko kiungo chochote chengine: http://www.curiosityaroused.com/health/what-is-the-largest-organ-in-the-human-body/8. Barabara iliopo Bolivia ni barabara ilio ya hatari zaidi kuipita ikiwa ni nyembamba na kila mwaka ukipita sehemu ya barabara hii humomonnyoka: http://www.curiosityaroused.com/world/10-of-the-worlds-most-dangerous-roads/

U T H M A N M U A D H K N U

I B R A H I M A D D U L U M

J A M A L U R W A S A D M A

K H A L D U N R I D H A A R

S U L E M A N F A R S Y A A

A B U B A K A R J A M A N L

W A A Q I Y A H M I K I D I

M A S J I D Q U B A A A M U

K H A L I D B I N W A L I D

63 73 P Y A T H R I B 53 N U R

.

A T T I N B A Q A R A A A A

M U H A M A D I D R I S S A

S U R A T U L A L A L A A K

A L I A B I T A L I B 7 8 9

M U H A R A M A A D U M A R

T H A M O O D A I S H A A A

H A R O O N S A F I A A A A

T H A M O O D J A B A L I I

K A S W A H H I J R A A H T

M U S S A K U S A I B A N U

Page 3: ANNUUR 1210A

3 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 1- 7, 2016

Habari

M U F T I wa B a k wa t a A b u b a k a r Z u b e r i amewataka Waislamu kuwa na mazingatio juu ya kifo na kujua kwamba hilo ni jambo lililo katika mamlaka ya Allah.

Akiongea katika maziko ya Muhadhiri Mahawia Karenga, Mufti Zuberi amesema kuwa kifo ni jambo linalotokana na Allah na hivyo lililo kwa Muislamu anapopatwa na msiba ni kukiri Imani hiyo kwa kusema kuwa “sisi sote ni waja wa Allah na kwake tutarejea.”

“ H i y o n i k a z i y a M w e n y e z i M u n g u ambayo anaifanya kwa viumbe na ametuumbia uhai na umauti hivyo mwandaamau atambue kuwa ataishi kwa muda fulani katika ardhi kisha a taondoka na kuish i katika maisha mengine ya Barazaq.” Alisema Mufti Zuber.

Alisema kwa Muislamu baada ya kupatwa na msiba kikubwa anatakiwa kuambatana na subra sambamba na kumuombea m a g h i f i r a n a r a h m a marehemu.

A k i m z u n g u m z i a M a r h u m K a r e n g a , Mufti Zuberi, alisema anamuelewa kwa jitihada na juhudi zake katika Dini wakati wa uhai wake akiishughulikia jamii kwa muda mrefu akiwa ni mtu ambaye alikuwa pamoja na Waislamu katika kila jambo.

Muft Zuber alisema kwa sasa ni vizuri kuangalia mema yake na juhudi zake alizokuwa akizifanya wakati wa uhai wake na kuwataka wengine kuiga ili kuweza kuendeleza harakati za kuhuisha Uislamu kwa hoja kwa kurejea vitabu vya dini zote.

Kwa upande mwingine, kifo cha Sheikh Mahawia Karenga, kimekumbushia dhulma waliofanyiwa Wahadhiri wa Kiislamu na Ser ikal i baada ya k u w a s h i t a k i k i s h a kufungwa je la miaka miwili, mwaka 1992.

K a t i k a s a k a t a h i l o W a h a d h i r i k a d h a a akiwemo Al-Marhumu S h e i k h K a r e n g a , walijumuishwa katika kadhia ya uvunjwaji wa

Mufti Zuberi awahimiza Waislamu kuzingatia mautiNa Bakari Mwakangwale Mabucha ya Nguruwe,

katika eneo la Manzese Jijini Dar es Salaam, ili hali wao walikuwa Temeke, wakiendesha Muhadhara.

W a k i l i m a a r u f u anayeshughulikia kwa karibu kesi mbalimbali za Waislamu, Juma Nassoro, akizungumzia tukio hilo, alisema wahadhiri hao ni kama vile walihusishwa kwa kukomolewa kutokana na kasi yao wakati huo kuingiza watu wengi katika Uislamu.

Alisema, katika harakati z a k e z a k u u l i n g a n i a Uislamu kwa kutumia Biblia na Qur an, mbali ya umahir i wake wa kutumia vitabu hivyo, lakini atamkumbuka zaidi Shkh Karenga, kwa tukio la kuhusishwa katika sakata la Mabucha ya Nguruwe, ili hali hawakuwepo kabisa katika eneo la tukio lakini walihukumiwa kifungo.

A l i s e m a Wa i s l a m u watakumbuka kwamba siku hiyo waliyolazimika kuvunja mabucha ilikuwa ni baada ya watoto wa K i i s l a m u , k u u z i w a nyama ya Nguruwe kwa makusudi.

A l i s e m a , h a t u a hiyo ilifikiwa baada ya Waislamu kutoa taarifa Serikalini, juu ya hatari na athari ya uwepo wa mabucha ya Nguruwe katika makazi ya imani za watu mchanganyiko, lakini Serikali ilipuuzia.

Alisema, siku ambayo wa t o t o wa K i i s l a m u walipouziwa nyama hiyo, iliwalazimu Waislamu kuvunja mabucha hayo na wakati huo kulikuwa kuna muhadhara unaendelea Temekea chini ya Wahadhiri Sheikh Mahawia Karenga, Hamim Boza, Said Ricco, pamoja na Ustadhi Othman Mazinge.

“Lakini cha ajabu Sheikh Mahawia na wenzake hao walijikuta wakikamatwa na Polisi kisha kufikishwa M a h a k a m a n i n a kuhusishwa moja kwa moja na kadhia hiyo kwa walishiriki kuvunja mabucha hayo.” Alisema Wakili Nassoro.

Alisema, anakumbuka kat ika Mahakama ya Kisutu, Jijini Dar es salaam, mbele ya Hakimu ambaye alikuwa ni Mheshimiwa Mama Kimaro, (sasa ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania) , a l is imama Askari Polisi na kutoa

ushahidi kwa upande wa Jamhuri akidai kwamba, alimuona Sheikh Mahawia, Mazinge na Sheikh Boza, wakivunja mabucha ya nguruwe Manzese, katika

bucha ya Mbokomu, jambo ambalo halikuwa kweli.

“Mwisho wa siku katika kesi hiyo yeye (Marhum K a r e n g a ) p a m o j a n a wenzake walihukumiwa

miaka miwili jela, hata hivyo walikuja kutoka kwa msamaha wa Rais wa wakati huo Alhaj Ally Hassan Mwinyi.” Alisema Wakili Nassoro.

“NILISHANGAA jinsi walivyo wakarimu mle walimo, sijawahi kusikia wakilalamikiwa kwa ukatili ukilinganisha na uzi to wa tuhuma wa l i z o p e wa p a m o j a n a u l i n z i m z i t o w a n a p o p e l e k w a Mahakamani.”

Anasimulia kijana Issa Mohammed (23), akiongea na An nuur, mara baada ya kutoka jela katika gereza la Segerea Jijini Dar es Salaam, Ijumaa ya wiki iliyopita.

Mohammed, alisema ameweza kurejea uraiani kutokana na juhudi za Sheikh Mselem Ally na timu yake baada ya kusikia kisa chake kilichosababisha kuhukumiwa kwenda jela miezi nane au kulipa faini ya Shilingi 30,000/-

Alisema, kitendo cha k u w e z a k u m s i k i l i z a na kumfari j i na kisha kumuwezesha kutoka, kinaashiria kuwa Masheikh h a o h a wa we z i k u wa magaidi, kwa maana ya sifa za magaidi zinavyoeleweka kwa kutokuwa na huruma na upendo.

Alisema pamoja na kuwa

Mhitimu Segerea aguswa na huruma ya MasheikhNa Bakari Mwakangwale amekaa nao kwa muda

mchache, lakini imetosha kuj i funza na kubaini mambo mengi ya wema kutoka kwao na kustaajabu uzito wa tuhuma zinazo wakabili, kwani alidai ni vitu viwili tofauti.

Ki jana Mohammed, alisema alishangaa sana jinsi Masheikh na Waislamu hao walivyo wakarimu katika maisha ya humo gerezani na hajapata kusikia wafungwa au mahabusu wakiwalalamikia kwa ukatili zaidi ya kuwasifia kwa ukarimu na wema wao.

A l i s e m a , k u t o k a n a na uz i to wa tuhuma walizopewa na jinsi umma unavyojaribu kuaminishwa pindi wanapo pelekwa Mahakamani wakiwa chini ya ulinzi mzito wa Askari wenye silaha nzito, unaamini kabisa kuwa hao (Masheikh) ni watu hatari sana katika jamii.

“ K i l a m m o j a m l e g e r e z a n i a n a l a a n i kuwekwa mle Masheikh na Waislamu wale, kwani ni watu wakarimu sana n a wa n a a m i n i k u wa wamesingiziwa tu, kwani kwa jinsi walivyo huwezi k u w a l i n g a n i s h a n a majambazi waliomo mle

ndani wao ni wakarimu z a i d i . ” A m e s e m a Mohammed.

Alisema, awali na kwa muda mrefu a l ikuwa anasikia taarifa zao kupitia vyombo vya habari kuwa Masheikh hao na Waislamu wapo gereza la Segerea w a n a t u h u m i w a k w a vitendo vya Kigaidi na siku nyingine hukutana na msafara wao ukienda Mahakamani wakiwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi.

Al i sema, a l ipopata mtihani wa kesi kisha kuwekwa mahabusu na hatimae kuhukumiwa alipata bahati ya kuonana nao kwa karibu na ndipo al ipogundua kwamba tuhuma wanazopewa hazilingani kabisa na watu hao.

Akifafanua alisema, wao humo gerezani wamekuwa ni watetezi wakubwa wa wa n y o n g e k wa n i hawapendi kabisa kuona mambo yanaenda katika njia ya dhulma na kwamba wakiona kitu kinakwenda sivyo huongea na kukemea kwa haraka.

“Wamekuwa ni msaada k w a w a n y o n g e m l e gerezana na kwa wale ambao hawana msaada

Inaendelea Uk. 14

MUFT Abubakar Zuberi (katikati).

Page 4: ANNUUR 1210A

4 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 1- 7, 2016

Tahariri/Habari

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

B I N A D A M U t o f a u t i n a v i u m b e w e n g i n e , t u m e j a a l i wa a k i l i , i l i kufikiri , kutambua na kuamua tukiwa na ufahamu, na hatimaye kupata matokeo chanya au maslahi na faida kwa kile tulichokitenda kwa kufikiri.

Wataalam wanatuambia kwamba wastani wa umri wa kuishi kwa Watanzania ni miaka 61 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012. Mwaka 1988 wastani wa umri kwa Mtanzaia ulikuwa ni miaka 50.

Mwaka 2009 kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na serikali ya Marekani, wastani wa matarajio ya umri wa kuishi (Life expectancy) wa Mmarekani umefikia miaka 77.9.

Kwa maana hiyo, takwimu zinatuonyesha kwamba wastani wa umri wa kuishi mwanadamu wa dunia ya leo ni kati ya miaka 61 hadi 80.

Katika ulimwengu wa sasa, mwanadamu anapokufa akiwa na umri wa miaka 70 au 80, huwa ametimiza mambo machache sana kati ya mambo ambayo angeweza kufanya.

Ikiwa alipenda michezo, inawezekana alikuwa mahiri katika mchezo mmoja au miwili tu. Ikiwa alipenda kuzungumza na watu katika lugha yao, pengine alimudu kuzungumza kwa ufasaha lugha mbili au tatu tu, huku akitamani kuzungumza lugha nyingi zaidi.

M w a n a d a m u h u y u anatamani kuishi umri mrefu zaidi ili pate wasaa wa kufurahia mambo mengi zaidi, kufurahia maisha ya dunia.

Lakini wengi hawatamani k u i s h i u m r i m r e f u i l i wamtukuze yule anayewapa u h a i n a k u f u r a h i a hayo maisha. Tumeona mifano mingi ya watu kupata unyenyekevu wa kumwabudu na kumtukuza Mwenyezi Mungu, baada ya kupata matatizo hasa maradhi na hapo ndipo hujiwa na abadu ya kutaka k u m t u k u z a M we n ye z i Mungu zaidi hata baada ya matatizo kwisha.

Huenda tukajiuliza, kwa nini Mwenyezi Mungu amuumbe mwanadamu akiwa na akili yenye uwezo wa kufurahia mambo mengi hivyo, kisha amkatishe tamaa kwa kutomwezesha kuishi muda mrefu vya kutosha kufurahia mambo hayo?

Tunafurahia kupungua umri wa kuishiBila kujali tumetanguliza nini kwa Allah (sw)

Pia huenda tukajiuliza, kwa nini Mwenyezi Mungu amuumbe mwanadamu akiwa na sifa za pekee kama vile kuwa na akili kuliko viumbe wengine, lakini akamjaalia kuijua haki na kumpa huruma na wakati huo huo ampe mwelekeo wa kutenda mabaya na asiwe tena na hafu ya Muumba?

Sote tuna hakika kwamba maisha ya mwanadamu wa leo ni mafupi, lakini mwanadamu huyo huyo akajaa kibri, kiasi kwamba amefanya ni jambo la kawaida badala ya kumshukuru M w e n y e z i M u n g u , akajikita katika kumuasi na kusherehekea kumaliza mwaka, lakini asitambue k u w a a n a s h e r e h e k e a kupungua umri wake wa kuishi hapa duniani.

Maisha ye tu mafupi na mwelekeo wa kutenda mabaya ni kama uhalifu. Hatuta fakar i , za id i ya kuendeshwa na mihemko ya matamanio ya nafsi na kumsahau mwenye nafasi yake, aliyetupa hayo maisha, yaani Mwenyezi Mungu Muumba.

Tunaelezwa katika vitabu vyetu vya dini kwamba Nabii Adamu aliishi miaka 930. Nabii Ibrahimu aliishi 175. Inaonekana kwamba hatua kwa hatua muda wa maisha ya wanadamu unapungua kadir i miaka na zama zinavyopita.

Tubadilike, katika matukio ya kuadhimisha miaka, basi hatua ya kwanza ni kumjua Mungu. Jitihada inahitajiwa ili kupata fikra kwa Mwenyezi Mungu. Tunafanya kazi ili kupata ujira kwa ajili ya maisha ya familia zetu. Lakini ni jambo la msingi kujenga hofu kwa Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye mwamuzi wa maisha yetu.

Wale wanaoshangil ia m wa k a m p ya , h a l i ya kuwa hakuna la maana w a n a l o l i f a n y a k w a kusherehekea kwao ambalo linamfurahisha Mwenyezi Mungu, wala wasijidanganye maana wanavyofanya ni sawa na kufurahia kupungua miaka ya kuishi hapa duniani, hali ya kuwa maisha mafupi waliyoishi hayakuwa ya kumfurahisha Mwenyezi Mungu.

Tutumie akili zetu vizuri na tuwe makini. Mwaka m p ya h u a m b a t a n a n a kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kufikisha umri uliofikia ukiwa salama.

Pia itumike fursa hii kuongeza ibada na kuandaa mazingira bora ya maisha yetu ya baadae baada ya kwisha umri wa kuishi hapa duniani.

Lakini ni vyema kwa wale wanaokufurahia huo mwaka mpya, wakatafakari zaidi juu

ya nini walifanya mwaka uliopita, walifanikiwa wapi, walikwama wapi na nini kifanyike ili kujikwamua. Ni muda wa kuweka mipango na mikakat i mizuri ya kimaisha katika familia na jamii zao kwa ujumla kwa mwaka huo.

Maisha b i la hofu ya Mwenyezi Mungu, bi la mipango ni sawa na gari lililokosa dereva.

Tujifunze na tubadilike. Tutambue kuwa maisha ni milki ya Mwenyezi Mungu. Mwembwe za saa sita usiku hazina msaada kwetu.

Maalim hatoshiriki Sherehe za MapinduziCHAMA cha Wananchi, CUF, kimesema kuwa hakitashiriki shughuli zozote za Sherehe za Mapinduzi, bila ya kuwa na Rais halali wa nchi, kwani kufanya hivyo ni kuyasaliti mapinduzi yenyewe.

Hayo yamebainishwa katika taarifa ya Chama hicho iliyotolewa na Mansour Yusuf Himid, katika wadhifa wake wa mshauri wa Katibu Mkuu.

Katika taarifa hiyo kwa vyombo vya habari jana, Mansour amesema kuwa “Chama Cha Wananchi (CUF) kimekuwa kikishiriki kikamilifu katika maadhimisho ya siku hiyo kila mwaka kwa kutambua kwamba Mapinduzi ya tarehe 12 Januari, 1964 ni Mapinduzi ya Wazanzibari wote.”

Na kwamba Viongozi wa CUF wakiongozwa na Maalim Seif Sharif Hamad wanaamini katika msingi mkuu wa Mapinduzi ya tarehe 12 Januari, 1964 chini ya uongozi wa Baba wa Taifa la Zanzibar, Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume, “ni kuleta utawala wenye ridhaa ya wananchi walio wengi.”

Akifafanua akasema kuwa Msingi huo umewekwa wazi na kutiliwa nguvu na Katiba ya Zanzibar kwamba, “Mamlaka ya kuendesha nchi ni ya wananchi wenyewe ambapo nguvu na uwezo wote wa Serikali kufuatana na Katiba utatoka kwa wananchi wenyewe.”

Mansour akasema kuwa “Mamlaka hayo ya wananchi yalitekelezwa tarehe 25 Oktoba, 2015 kwa kuwachagua

Na Mwandishi Wetu viongozi watakaoongoza Serikali yao kwa miaka mitano ijayo.”

Kwa hiyo, “Kitendo chochote cha kupindua mamlaka hayo ya wananchi ni kwenda kinyume na misingi ya Mapinduzi na misingi iliyowekwa na Baba wa Taifa la Zanzibar, Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume.”

Na kwa hiyo, CUF hawako tayari “kushiriki katika kuisaliti misingi hiyo na kuisaliti dhamira ya Mzee Karume.”

Katika ufafanuzi wake Mansour amesema kuwa hivi sasa Zanzibar haina Rais halali wala Baraza la Wawakilishi kwa vile mamlaka zote hizo zilishamaliza muda wake.

“Kwa sasa, hatuna viongozi wenye uhalali wa kikatiba kuweza kutekeleza majukumu ya kiserikali. Kwa hivyo, kushiriki katika ratiba hizo kwa kutumia nafasi ambazo hazina uhalali tena wa kikatiba ni kwenda kinyume na dhamira ya waasisi wa Mapinduzi, jambo ambalo hatuko tayari kulifanya.”

Alisema Mansour na kusisitiza kwamba “viongozi wa CUF hawatoshiriki katika ratiba walizopangiwa mpaka pale chaguo la wananchi wa Zanzibar walilolifanya tarehe 25 Oktoba, 2015 litakapoheshimiwa.”

Wakati huo huo, imeelezwa kuwa umefika wakati usanii na kuchezeana akili, ufike mwisho wake.

CCM waseme wazi kuwa wao ni ‘Kamuzu Banda’, na CUF wajivue gamba waseme wazi kuwa wao wanacheza ‘gemu’.

La sivyo, matokeo ya

uchaguzi yatangazwe kama wananchi walivyopiga kura.

Hayo yamebainishwa na mzee mmoja mkereketwa wa moja ya vyama vya upinzani nchini akisema kuwa itakuwa ni usaliti mkubwa kwa wananchi iwapo mabilioni ya kodi zao zitachotwa tena kufanya ‘kiini macho’ cha uchaguzi.

Alisema ni kiini macho kwa sababu Uchaguzi Mkuu unaodaiwa kuwa na dosari na hivyo kufutwa, ulifanyika vizuri na waangalizi wote wamethibitisha hilo na ndio maana kura za Wazanzibari ndio pia zimetumika kumpa Mheshimiwa JPM Urais na kulipa Bunge la Jamhuri Wabunge kutoka Zanzibar.

Akasema, kisichotakiwa katika Uchaguzi huo ni kushindwa Dr. Ali Mohammed Shein na kushindwa CCM.

Kwa hiyo bora kuondoa kiini macho cha kuwa tuna demokrasia na uchaguzi, ili kunusuru pesa za walipa kodi.

Itangazwe tu kwamba tuna viongozi na chama cha kutawala maisha kama alivyokuwa amejitangaza Hastings Kamuzu Banda wa Malawi.

Alisema, kwa kuheshimu, kulinda na kuzingatia matakwa ya Katiba ya Nchi, na matakwa ya mfumo wa demokrasia ya vyama vingi, mabilioni ya pesa (inasemekana bilioni 7), zilitumika kwa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar.

Wakati taarifa na hali halisi iliyoonekana uchaguzi huo ulienda vizuri hadi kufikia hatua ya kutangaza matokeo

Inaendelea Uk. 7

Page 5: ANNUUR 1210A

5 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 1- 7, 2016Habari za Kimataifa

WIZARA ya Ulinzi ya Urusi imeikabidhi Ufaransa nyaraka zinazothibitisha kuwa, Uturuki inalisaidia kifedha kundi la kigaidi la Daesh huko Syria.

Taarifa iliyotolewa wiki iliyopita na Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema kuwa, nchi hiyo imeikabidhi Ufaransa taarifa za dharura kuhusu mchango wa Uturuki katika kupora maliasili na utajiri wa Syria na misaada yake ya kifedha kwa kundi la kigaidi la Daesh.

Taarifa hiyo imesema kuwa, Mkuu wa Majeshi ya Urusi, Jenerali Valery Gerasimov, ndiye aliyetoa taarifa hizo kwa Ufaransa zinazoonesha jinsi maliasili z i n a v y o p o r w a n c h i n i Syria kwa ushirikiano wa Uturuki na mapato yake yanavyotumika kulisaidia kundi la Daesh.

M o s c o w i m e t a n g a z a kuwa, serikali ya Ankara ndio mnunuzi mkubwa wa mafuta ya magendo yanayoporwa na makundi ya kigaidi katika nchi za Syria na Iraq.

Urusi inasema kuwa Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki na familia yake wanahusika moja kwa moja na biashara ya mafuta na kundi hilo la kigaidi.

Urusi yakabidhi nyaraka za ushirikiano Uturuki na DaeshAidha Urusi imetangaza

k u w a m a k o m b o r a y a kulenga vifaru ambayo Marekani inadai imewapa wanamgambo wanaoitwa w e n y e m i s i m a m o y a wastani wa Syria, kwa sasa yanatumiwa na kundi la kigaidi la Daesh.

Siku kadhaa zilizopita k u l i s a m b a z w a p i c h a katika vyombo vya habari vyenye uhusiano na kundi la Daesh, zinazowaonesha wanachama wa kundi hilo wakitumia makombora dhidi ya vifaru ya Tow, ambayo yametengenezwa Marekani.

Kundi la Daesh lilikuwa likitumia makombora hayo katika mkoa wa Aleppo kwenye kituo cha anga cha Kweyris. Kituo hicho kilikombolewa na jeshi la Syria siku chache zilizopita.

Haijajulikana bado Daesh imepata vipi makombora hayo, lakini ripoti zilizotolewa hapo kabla zilisema kuwa makumbora hayo yalitumwa na Marekani kwa makundi ya wanamgambo wanaoungwa mkono na nchi hiyo huko Syria.

H i v i k a r i b u n i m w a n a c h a m a m m o j a a l i ye j i t e n g a n a k u n d i la Daesh alikiri kwamba, wapiganaji waliokuwa chini ya usimamizi wake walipata mafunzo nchini Uturuki. irib

MKUU wa Majeshi ya Urusi, Jenerali Valery Gerasimov.

J E S H I l a Ye m e n limefanikiwa kutungua ndege isiyo na rubani ya Saudi Arabia katika mkoa wa Ta'izz, Kusini Magharibi mwa nchi hiyo ya Kiarabu.

Televisheni ya al-Mas i rah ya Yemen imeripoti kuwa, drone h i y o y a A a l - S a u d ilitunguliwa na vikosi vya Yemen vikishirikiana n a h a r a k a t i y a Ansarullah katika eneo la Jahmaliyeh.

W i k i i l i y o p i t a , Wapiganaji wa harakati ya Ansarullah ya Yemen, wakishirikiana na jeshi la nchi hiyo walifanikiwa kuangamiza askar i karibu 150 wa Saudi A r a b i a b a a d a y a kushambulia kambi mbili za Wasaudia na washirika wao kwa makombora mawili ya balestiki.

Mashambulizi hayo ya wa p i g a n a j i wa Ansarullah yamefanyika kujibu uchokozi na m a s h a m b u l i z i y a anga yanayoendelea kufanywa na ndege za Saudi Arabia dhidi ya maeneo mbalimbali ya

Yemen yatungua drone ya Saudi Arabia

DRONE ya Saudi Arabia iliyoangushwa na majeshi ya Yemen.

nchi hiyo. Zaidi ya Wayemeni

7500 wameuawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa kutokana na mashambulizi hayo ya kivamizi ya Saudi A r a b i a ya l i y o a n z a mwezi Machi mwaka huu, kwa lengo eti la kumrejesha madaraka rais wa zamani wa Yemen aliyejiuzulu na kukimbia nchi, Abdi Rabbuh Mansur Hadi.

NCHI tatu zenye maadili ya Kiislamu zimetangaza kuwekea wananchi wake marufuku ya sherehe za mwaka mpya.

Nchi hizo zilizochukuwa uamuzi wa kuzuia sherehe za mwaka mpya ni Brunei na Tajakistan za bara la Asia na Somalia kutoka bara la Afrika.

Sultan Hassanal Bolkiah wa Br u n e i , a l i t a n g a z a marufuku hiyo kutokana na kuwa kinyume na maadili ya Kiislamu, na kuweka adhabu ya kifungo cha miaka 5 gerezani kwa raia watakaokiuka sheria.

Wizara ya E l imu ya Tajakistan nayo ilitangaza k u w e k a m a r u f u k u ya m i t i y a m a p a m b o y a Krismasi na sherehe za mwaka mpya ingawaje adhabu ya washerehekeaji haikubainishwa.

Kwingineko katika nchi ya Somalia, sherehe za Krismasi na mwaka mpya pia zilipigwa marufuku kwa madai ya kuwa ni misingi ya dini ya Kikristo.

K i o n g o z i m m o j a wa Wizara ya Masuala ya Dini Mohammed Hayrow, alitoa maelezo na kusema kwamba watazuia sherehe zozote zitakazofanyika kwa ajili ya

Nchi tatu zapiga marufuku sherehe za mwaka mpya

Krismasi au mwaka mpya.Gazeti la the Guardian

l imeripoti kuwa sheria iliyowekwa na Wizara ya Elimu Tajikistan inazuia, matumizi ya mil ipuko, vyakula vya hadharani, k u p e a n a z a w a d i n a kuchangishana fedha kwa ajili ya sherehe za mwaka mpya pamoja na kuweka miti ya krismas iwe ni ya asili au ile ya bandia katika shule na vyuo vikuu.

Aidha imearifiwa kwamba nchi ya Brunei imeweka vizuizi kusherehekewa mwaka mpya wa Kichina kwa kupita na vinyago mitaani.

K a t i k a b a r u a i l i y o s a m b a z wa k a t i k a vyombo vya habari na mitandao nchini humo imeeleza kuwa maonyesho dansi ya asili ya kichina ambapo watu wanacheza wakiwa wamevaa vinyago na kutembea kama simba katika kusherehekea mwaka mpya wa kichina yanaweza kufanyika kwa saa kadhaa zilizopangwa kwa siku tatu kuanzia Februari 19 hadi 21 – na katika maeneo matau pekee ambayo ni kwenye mahekalu, mabwalo ya shule na katika nyumba za familia za kichina.

TAASISI ya al Azhar nchini Misri imelaani kitendo cha kuchomwa moto nakala za kitabu kitakatifu cha Qur'ani katika kisiwa cha Corsica nchini Ufaransa.

Taari fa i l iyotolewa mwishoni mwa wiki i l iyopita na al Azhar imelaani vikali hatua ya kundi moja lenye misimamo ya kibaguzi iliyovuka mipaka kuvunjia heshima eneo la ibada ya Swala katika kisiwa cha Corsica, huko Ufaransa, kwa kuharibu eneo hilo na kuchoma moto nakala za Qur'ani Tukufu.

Vilevile taasisi hiyo ya kidini ya Misri imelaani kauli mbiu za kibaguzi zilizokuwa zikitolewa na kundi hilo dhidi ya Waislamu nchini Ufaransa.

Al Azhar imei taka ser ika l i ya Ufaransa kuchunguza kwa makini vitendo hivyo, ili kuzuia mivutano zaidi ambayo itayanufaisha makundi yenye misimamo mikali.

Ijumaa iliyopita kundi la Wafaransa lilifanya m a a n d a m a n o k a t i k a k i s i wa c h a C o r s i c a , likipinga kuwepo raia wa kigeni hususan Waislamu katika nchi hiyo.

M a a n d a m a n o n a m a c h a f u k o h a y o y a l i e n d e l e a k w a kushambuliwa eneo la kuswalia la Waislamu na kuchomwa moto nakala za k i tabu k i takat i fu cha Mwenyezi Mungu, Qur'ani.

Al Azhar yalaani kuchomwa Qur’ani

Page 6: ANNUUR 1210A

6 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 1- 7, 2016Hoja ya Juma Kilaghai

MOJA ya mambo ambayo yametikisa sana

kwenye vyombo vya habari katika siku za hivi karibuni, ni mashambulizi yaliyoanzishwa na viongozi wakuu wa Wizara ya Afya dhidi ya matabibu wa tiba mbadala na waganga wa jadi. Japo inaonekana kama vita hii ilianza pale Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Hamisi Andrea Kigwangwala alipofanya ziara ya kustukiza katika kliniki ya Foreplan inayoendeshwa na tabibu Juma Mwaka, lakini ukweli wa mambo ni kwamba hiyo ni raundi mpya tu katika vita ambayo imekuwa ikiendelea kwa muda mrefu sasa.

Kihistoria mamlaka za Tanzania haziwapendi kabisa watu wa tiba mbadala na tiba asilia. Ukifanya uchunguzi utagundua kuwa mamlaka hizi zinawavumilia tu kwa sababu hamna jinsi. Ushahidi juu ya hili unapatikana pale mtu anaporejea visa kama vile vya dawa ya NGETWA na MAFUTA YA UBUYU. Ngetwa ilikuwa ni dawa iliyopata maarufu mkubwa sana kiasi kwamba wateja wake walisambaa hadi nchi jirani za Kenya na Uganda. Katikati ya umaarufu huu, ghafla serikali iliingilia kati na kusema kuwa Ngetwa haikuwa dawa ya kweli na badala yake ilikuwa na madhara kwa watumiaji. Kwa kuwa Wananchi wengi huwa wana imani kubwa na kile kinachosemwa na serikali yao, huo ukawa ndiyo mwisho wa Ngetwa.

Hatua hii ya serikali ilinishangaza sana ukizingatia kuwa kwa kawaida serikali huwa zinachukua hatua kama hiyo pale kunapokuwa na malalamiko ya wateja, na baada ya uchunguzi ikabainika kuwa malalamiko hayo ni sahihi. Ukweli wa mambo ni kwamba hakukuwa na malalamiko yoyote ya watumiaji wa Ngetwa na wala hakukuwa na uchunguzi wowote. Ni kama vile wakubwa enzi zile hawakufurahia mafanikio ya kiuchumi ya mzalishaji wa hiyo Ngetwa, na kwa hivyo wakaamua kutumia mamlaka yao kumtibulia.

Jambo hilo hilo lilijitokeza kwa mafuta ya

Lengo letu ni moja, kwa nini tunagombana?

DKT. Hamisi Andrea Kigwangwala. TABIBU Juma Mwaka.

ubuyu. Baada ya mafuta hayo kupata umaarufu mkubwa na baadhi ya watu wakaanza kuvuna uchumi mkubwa kutokana na uwekezaji waliofanya kwenye eneo hilo, ghafla serikali kupitia Taasisi ya Chakula na Dawa (TFDA), ikaingilia kati na kudai kuwa mafuta hayo yana madhara. Kama ilivyotokea kwa Ngetwa, huo ukawa ndiyo mwisho wa umaarufu wa mafuta ya ubuyu!

Katika madai yake, TFDA ilidai kuwa katika mafuta ya ubuyu kuna baadhi ya viambata ambavyo vilikuwa na uwezekano wa kusababisha saratani. Hatukatai. Lakini kama hiyo ndiyo iliyokuwa sababu ya msingi, mbona vichocheo vya saratani vimejaa kila mahala, ikiwamo na katika bidhaa mbalimbali maarufu zinazotumiwa na wananchi kila siku, lakini hawajasema chochote? Mbona hatujawasikia wakizungumzia acryl amide katika chips, mikate na maandazi? Mbona hatujawasikia wakizungumzia heterocyclic amines kwenye mishikaki inayochomwa hadi ikakaukia? Mbona hatujawasikia wakizungumzia aflatoxins katika nafaka zetu huko masokoni? Mbona hatujawasikia wakizungumzia zebaki (mercury) katika michanganyiko ya kuzibia matundu kwenye meno? Alimradi ukitaka kuhoji vitu ambavyo vinaweza kuwa ni visababishi vya saratani ambavyo TFDA walitakiwa wavizungumzie lakini kwa sababu wanazozijua wao wamechagua kukaa kimya, ni vingi mno na unaweza

hata kujaza kitabu!Sakata la matangazo

ya tiba mbadala na tiba asili katika vituo vya runinga na radio pia ni kielelezo cha jinsi mamlaka zinavyohangaika kuminya shughuli za matabibu wa tiba mbadala na wanganga wa jadi hapa Tanzania.

‘Herbalists, TV Stations, face legal action over adverts’.

Hiki ni moja ya vichwa vya habari vilivyolipamba gazeti la Serikali la Daily News la Jumatano, tarehe 23, Julai 2014. Kichwa hiki kilimaanisha kuwa matabibu wa dawa za miti shamba, na vituo vya runinga kwa pamoja walikuwa wanakabiliwa na mashitaka, kufuatia matabibu hao kutoa matangazo ya tiba zao kupitia vituo hivyo.

Kwa mujibu wa habari iliyobebwa na kichwa hicho, kuwepo kwa hali hiyo kulithibitishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) kwa pamoja na idara inayohusika na tiba asili na tiba mbadala katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

TFDA ilidai kuwa ni kinyume kabisa cha sheria kwa tabibu yoyote wa miti shamba kutoa tangazo lolote kwa umma kuhusu dawa zake iwapo dawa hizo hazikuthibitishwa na mamlaka hiyo. Msemaji wa taasisi hiyo, Gaudensia Simwanza, alilalamika kuwa pamoja na kuchukua hatua mara kadhaa za kuwaita matabibu wanaohusika na kuwaonya, na pia kuvitembelea vituo vya runinga vinavyorusha matangazo hayo na kuvionya pia, hali haikuwa imebadilika.

Kitendo cha Idara inayohusika na Tiba Asili

na Tiba Mbadala katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kukaa meza moja na TFDA, kuwapiga vita wadau wa tiba mbadala na tiba asili kwa kweli ni cha kustua na kushangaza. Kitendo hiki ni cha kustua na kushangaza kwa sababu idara hii kama msajili wao, ndiye mlezi wa hawa wadau wa tiba mbadala na tiba asili. Ni lazima ustuke na kushangaa pale mlezi wako, ambaye kimsingi anatakiwa awe ndiyo mtetezi wako, anapoungana na wale wasiokupenda kukupiga vita!

TFDA inadai kuwa imekuwa ikichukua hatua hizi kwa sababu ya kulinda usalama wa watumiaji wa dawa za tiba mbadala na tiba asili ambazo hazijasajiliwa. Hoja ya TFDA inalenga kutuambia kuwa kwa sababu matabibu wengi wa tiba mbadala na waganga wa jadi hawataki kuzisajili dawa zao, dawa hizo ni hatari kwa watumiaji, na TFDA haiwezi kukaa kimya bila kuchukua hatua. Hoja hii ni nzuri. Lakini je, inaendelea kuwa nzuri pale unapotenda haki na kuusikiliza upande wa pili?

Kimsingi, matabibu wa tiba mbadala na waganga wa jadi wanadai kuwa wamekuwa wakisita kutoa ushirikiano kwa TFDA katika suala la usajili kwa hofu ya kuibiwa FORMULA za dawa zao. Wanadai kuwa hofu yao inatokana na utaratibu uliowekwa na TFDA wakati wa kusajili, unaomtaka mmiliki wa dawa kutaja viambata vilivyomo katika dawa, kiasi cha kila kiambata, na jinsi dawa inavyotengenezwa.

Ni vema TFDA ikakubali kuwa hofu ya matabibu wanaokataa kusajili tiba zao TFDA ina mashiko, na ushahidi juu ya hilo uko wa kutosha. Ushahidi uliopo unaonyesha kuwa TFDA ni kero kubwa kwa matabibu wanaowasilisha tiba zao kwao kwa nia ya kutaka kuzisajili, kwani mara nyingi, kama siyo zote, TFDA hukataa kuzisajili kwa visingizio dhaifu kabisa. Nini kinachomthibitishia tabibu ambaye dawa yake imekataliwa kupata usaji kuwa FORMULA

ya dawa yake, ambayo amelazimishwa na utaratibu uliowekwa kuiweka hadharani, haitatumiwa kwa manufaa ya kiuchumi ya maofisa wa TFDA waliohusika na kutathmini maombi yake?

Kwa kweli hoja kuwa dawa za asili siyo salama kwa sababu hazijasajiliwa ni hoja dhaifu kabisa na isiyoungwa mkono na ushahidi wowote wa kisayansi. Matabibu wengi sana wako makini kuhusu suala la usalama na mara nyingi huhakikisha kuwa kabla ya kuanza kutoa dawa zao huziwasilisha kwa Mkemia Mkuu wa serikali ili kupimwa na kujua usalama wake. Haiwezekani Mkemia Mkuu wa Serikali aseme dawa fulani haina madhara (japo huwa mwangalifu asiseme kuwa inatibu), lakini TFDA waseme kuwa dawa hiyo siyo salama kwa kuwa tu hawajaisajili!

Msimamo huu wa TFDA ni sawa na kuzipigia debe dawa za kifamasia ambazo kabla ya kuanza kutumika ni lazima zipitie kwao na wao wazisajili. Ingekuwa ni vizuri iwapo TFDA wangetuchapishia orodha ya dawa hizi ambazo kwa sababu za kiusalama kwa watumiaji, wamekataa kuzisajili! Nina mashaka makubwa kuwa orodha hiyo ipo, ukizingatia uhusiano wa karibu uliopo baina ya makampuni yanayozalisha dawa mbalimbali za kifamasia, na mamlaka mbalimbali za kitaifa zinazohusika na usimamizi wa dawa, katika nchi mbalimbali.

Makampuni yanayozalisha dawa za kifamamisia, au mawakala wao wa kuzisambaza ni taasisi zenye fedha nyingi. Kuna ushahidi mwingi kuwa sehemu ya fedha hizo imekuwa ikitumika kununua mamlaka mbalimbali za kusimamia dawa, au kuwanunua madaktari na maofisa wa mamlaka hizo ili kufifisha upinzani dhidi ya dawa zao.

Kwa mfano, mwaka 1992 Bunge la Marekani lilipitisha sheria iliyojulikana kama ‘the Prescription Drug User Fee Act (PDUFA)’. Sheria hii ilikuwa inatoa ruksa

Inaendelea Uk. 16

Page 7: ANNUUR 1210A

7 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 1- 7, 2016HABARI

Maalim hatoshiriki Sherehe za MapinduziInatoka Uk. 4

huku wengine wakiwa washapewa vyeti vya ushindi, ilitangazwa kufutwa uchaguzi huo na sasa yanaandaliwa mazingira ya kutumia mabilioni mengine tena kufanya ‘kiini macho’ kingine cha uchaguzi.

“Mimi nadhani katika hali hii, tufikie mwisho wa usanii. Tusiwadanganye wananchi kuwa tupo katika mfumo wa siasa za vyama vingi, wala tusiwadanganye wananchi kuwa tunafanya uchaguzi, tukatumia pesa zao chache ambazo zingetumika kuboresha huduma za afya na mambo mengine, isemwe tu kwamba ‘viongozi wa CCM’ ni Kamuzu Banda wa Zanzibar (Tanzania), ni ‘marais wa Maisha.’ Hii angalau itakuwa imesaidia kuokoa kodi za wananchi.”

Alisema Mzee huyo alipotembelea ofisi za gazeti hili kutoa maoni yake juu ya kile alichosema ‘kukerwa na tamko la CCM’ la kurudiwa uchaguzi halikadhalika ‘kukerwa na mwenendo wa CUF’ katika kinachodaiwa kuwa mazungumzo na CCM.

Akichambua zaidi anavyoyatizama mambo, alisema, CUF na hasa mgombea wake wa Urais, ifike mahali ama wajisajili wajulikane kuwa wao ni wapinzani wa kweli na wanautaka Urais ili kuhudumia Wazanzibari, vinginevyo nao wajivue gamba.

“Kadiri ninavyowatizama hawa CUF, nao wananitia wasiwasi. Suala la matokeo ya uchaguzi sio la mtu, sio la Katibu Mkuu wa Chama au mgombea pekee, ni la chama. Lakini kila nikitizama kinachoitwa mazungumzo, ni mtu mmoja Vs Sita wa upande wa pili, ambao tafsiri yake ni kuwa hao CUF wenyewe kamwe hawatajua kinachozungumzwa!”

Alisema Mzee huyo akihitimisha kwa kusema kuwa hajawahi

kuona wala kusikia mahali popote duniani ambapo mgogoro wa kisiasa unatatuliwa kwa kufanywa mazungumzo ya sura ya jambo binafsi na bila kuzingatia uwiano wa ushiriki wa pande mbili husika katika mgogoro.

Katika hali hiyo akasema kuwa, kama CCM, viongozi wa CUF nao wanatakiwa kuwa waadilifu na kuwatendea haki wafuasi wao na wananchi kwa ujumla.

Kwamba ama wajivue ‘gamba’ wajulikane kwamba wanafanya kazi ya kuwapandisha ‘presha’ wananchi na kuishusha, au wafanye siasa za kweli za upinzani, na siasa za kweli za chama cha upinzani ni kupigania kushika serikali.

“Wananchi washawasafishia njia, lakini kuna mashaka iwapo hao ‘wagombea’ wa CUF wenyewe wapo tayari au hilo ndio walilokuwa wakitaka.” Alisema Mzee huyo ambaye hata hivyo hakutaka jina lake litajwe gazetini.

Wiki iliyopita, CCM, Zanzibar ilitoa kauli ikiwataka wanachama wake kujiandaa kwa marudio ya uchaguzi mkuu na kukiandalia chama hicho mazingira ya kupata ushindi wa

kishindo.Kauli hiyo ya CCM

imekuja siku chache baada ya mazungumzo ya Maalim Seif na Rais John Pombe Magufuli, Ikulu, jijini Dar es Salaam, jambo ambalo limetafsiriwa na baadhi ya watafiti na wachambuzi wa mambo kwamba huenda hilo ndio walilokubaliana katika mazungumzo hayo.

Na kwamba kitendo cha CCM ni katika kuandaa mazingira ya kukubalika na kutekelezeka hilo na hasa ile kauli ya CCM kwamba eti nao hawatakubali uchaguzi urudiwe chini ya Tume ya Jecha.

“Ukiangalia mfuatano huu wa matukio baina kikao cha Rais na Kamati ya CCM, Zanzibar na kutolewa tamko la kurudiwa uchaguzi, lakini pia ukisikiliza msisito wa CCM, Zanzibar kwamba eti nao hawamkubali Jecha na Tume yake, kuna wasiwasi kwamba hapa kuna mchezo.”

Alisema mchambuzi mmoja ambaye zamani alikuwa mwanachama katika chama cha CUF, lakini akahamia chama kingine cha upinzani.

“Sioni ni kwa namna gani CCM wangekuwa na ujasiri wa kutangaza

marudio ya Uchaguzi Mkuu bila ya kupata ‘ushirikiano’ na viongozi wa CUF, sioni namna ambavyo CCM wanaweza kuibuka na kutangaza habari za marudio ya uchaguzi iwapo katika vikao vyao na CUF wanauona msimamo thabiti usio yumba wa kupinga jambo hilo.” Alisema.

Wakati huo huo, Mzee Hassan Nassor Moyo amesema kuwa “kamwe hatamuunga mkono Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, ikiwa ataridhia kurudiwa Uchaguzi Mkuu” Zanzibar.

Mzee Moyo amesema hayo akijenga hoja kuwa dunia nzima inajua kuwa Uchaguzi ulifanyika vizuri na kwamba mshindi anajulikana.

Alisema, kuitisha Uchaguzi Mkuu mwingine, ni dhulma, dhambi na kutowatendea haki wananchi waliopiga kura zao.

Akiongea na baadhi ya vyombo vya habari wiki iliyopita nyumbani kwake Fuoni, Mzee Moyo amesema kuwa mazungumzo yanayodaiwa kuendelea hivi sasa ni jambo jema.

Hata hivyo akasema kuwa hayatakuwa na maana yoyote iwapo hayatazingatia haki na ukweli.

Akasisitiza kuwa haki na ukweli ni

kumtangaza aliyeshinda na aliyeshindwa akubali kushindwa.

Kwa upande mwingine, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Magdalena Sakaya amesema kuwa msimamo wa CUF ni kwamba hawatakubali uchaguzi urudiwe.

Alisema Baraza Kuu la Uongozi Taifa, ambalo ndio chombo cha mwisho kutoa uamuzi, limeshatoa uamuzi na msimamo kwamba hakuna kurudiwa uchaguzi, bali kilichopo ni kukamilishwa utangazaji wa matokeo.

Akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari amesema, kwa sasa CUF haishughulishwi iwapo Maalim Seif anakwenda katika vikao peke yake au na mtu.

“Uamuzi wa kwenda au kutokwenda na mtu ni wa Maalim Seif.”

Hata hivyo akasisitiza kuwa msimamo wa CUF ni ule ule kwamba hawatakubali uchaguzi urudiwe.

Katika hatua nyingine, Chama Cha Wananchi, CUF, kimewataka wanachama wao na wananchi kwa ujumla kupuuza taarifa ya CCM kwamba kutakuwa na marudio ya Uchaguzi Mkuu.

Taarifa ya chama hicho iliyotolewa na Ismail Jussa imesema kwamba kilichopo sasa ni kutoa nafasi ya mazungumzo yanayoendelea halikadhalika kumpa nafasi Rais John Pombe Magufuli katika jitihada anazofanya kuleta ufumbuzi.

Hata hivyo, Jussa alijikita zaidi katika kuchambua na kukosoa tamko la CCM badala ya kutoa msimamo wa wazi wa CUF juu ya uwezekano wa kushiriki au kutokushiriki Uchaguzi Mkuu wa marudio.

Alichosema Jussa kama kauli ya chama ni kuwa “CUF inawahakikishia Wazanzibari kwamba haitotetereka na itasimamia kwa dhati maamuzi yao waliyoyafanya kwa njia za kidemokrasia kupitia Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na italinda chaguo lao la Rais wa Zanzibar, Wawakilishi na Madiwani wao.”

NAIBU Katibu Mkuu wa CUF, Magdalena Sakaya (katikati) akiwa na Wakurugenzi wa Chama hicho. Shaweji Mketo (kushoto) Bw. Kambaya (kulia).

Page 8: ANNUUR 1210A

8 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 1- 7, 2016Makala

WAFALME wa Rumi na wa ki- Giriki, walishirikiana sana na viongozi wa dini ya Kiyahudi katika mambo mengi ya kubuni mifumo ya kuitawala dunia ndani ya kivuli cha dini kwa kiasi kwamba mambo mengi yametiwa katika maandiko na kuaminishwa kuwa ni ufunuo. Kumbe ni sheria, mila na tamaduni za falme za nchi hizo. Na ndiyo maana unakuta kuwa maandiko ya kwanza ya Ukristo yaliandikwa kwa lugha ya Kigiriki badala ya Kihibru-ki Ibrania au ki- Yahudi. Tusidhani kuwa kuandikwa maandishi ya kwanza ya Biblia kwa lugha ya Kiyunani (Kigiriki), kuwa ni kwa kubahatisha.

Wakati tunamwona Kaisari Consitantino mwaka wa Rumi 325 B.K. akishughulikia Injili, kuwa ifutwe Twheed (Upeke wa Mwenyezi Mungu), iliyofundishwa na Nabii Musa na Isa (Yesu) A.S, huko nyuma mwaka wa 198 K.K. (kabla ya kuzaliwa Yesu), mfalme Antioko Epifani wa Ugiriki naye alihakikisha mafundisho ya Nabii Musa (Torati) hayafatwi tena na wana wa Israeli; Biblia inatueleza hivi:

“Antioko Epifani anateka nyara Hekaluni na anawadhulumu Wayahudi wachaji wa Torati. Akaingilia Misri na jeshi kubwa…akaiendea Israeli akafika Yerusalemu na jeshi kubwa. Akaingia katika hekalu kwa jeuri, akachukua madhabahu ya dhahabu,…Akawadanganya kwa maneno ya amani wakamwamini. Lakini aliuangukia mji kwa ghafla akaupiga pigo kubwa, akawaharibu watu wengi wa Israeli. Aliuteka mji akauchoma moto, akazibomoa kuta zake pande zote.” (Makabayo 1:14-31.)

‘Neno Amani’ tunalolisikia katika kila taifa hapa duniani, tusidhani ni ile amani

Leo sio mwaka mpya, ni ibada ya kikafiri ya Mungu ‘Januari’

Na Khatib J. Mziray

yenye maana ya ‘Assalaam’, iliyokuwa na maana ya, Amaani, Salaama, na Kusalimika, katika Uislamu. Ni amani kwa mtazamo wa mfumo tangu enzi za mfalme Antioko Epifani, miaka 198 kabla ya kuzaliwa Yesu.

Msomaji kumbuka kuwa walibadilisha kila kitu kinachowezekana kubadilishwa. Ndiyo maana hata miaka walikuwa wanahesabu kinyumenyume, kwa kuanzia 2000, kurudi hadi moja, ndiyo maana unaona inaandikwa ‘198 k.k.’ Sera hizo ndizo hizi tunazoshuhudia, zimetutia shemere vichwani. Tunayakufuru matarakimu, hata wale walio na Ph.D katika fani mbalimbali haziwasaidii kutu.

Katika ulimwengu wa leo ili mtu aonekane kuwa ameelimika, nilazima ajidanganye mwenyewe. Akitaka kujua majira ni lazima moja ibadilike, iwe saba, na saba iwe moja; lakini ukimpa shilingi moja ukimwambia kuwa ni saba, atakuona u- mwehu, au hujaenda shule. Huna maarifa ya

KKK (Kusoma, Kuandika na Kuhesabu).

Ndiyo haya yanayoitwa, mwaka mpya, wasomi na wafuasi wa sera za ‘ma-Antioko, wanakesha usiku hadi saa sita na dakika moja, wakisubiri mwandamo wa mwezi wa kwanza. Ambapo kila mwaka ni lazima uandame saa hizo hizo. Lakini wakati huo ukiangalia juu mbinguni, utaukuta mwezi asilia una umri wa siku kumi na tano. Ila wasomi hawa macho yao hayana hata zile tongotongo za aibu ya kunadi kuwa mwezi umeandama, na asubuhi yake ni siku kuu. Kwa dunia nzima, ni mwaka mpya-Januari 1 wakiamini kuwa wanasherehekea mwezi wa kwanza, unaoitwa Januari, kumbe wanasherehekea ‘mungu mtu, wa Warumi.’

Mfalme huyo aliyejifanya mungu mtu, alisema, kuwa, yeye jina lake litakuwa ndilo la mwezi wa kwanza, na mwezi huo utakuwa na siku 31. Ili raia wa himaya yake wafanye kazi siku moja bila malipo. Ili serikali yake iongezeke kipato

kisicholipiwa ujira; na watumishi wasijihisi kuwa wanadhulumiwa, kwa kuwa mwezi haujaisha maana

Waporaji.Hizo ndio sera

zao na malengo yao- “Wakawachukua wanawake na watoto utumwani na kuwakamata ng’ombe. Wakauzungusha mji wa Daudi ukuta mkubwa,…wakachukua nyara zote za Yerusalemu…Walimwaga damu isiyo na hatia.” (Makabayo 1:32-37.)

Uroho wa mali uliokithiri, kiasi kwamba, watu wakiona mali hawajali roho za watu. Hekaluni walianza na madhabahu ya dhahabu, na kila chenye thamani walikichukua. Majumbani walichukuwa wanawake, watoto na kuwafanya watumwa. Sasa ukisikia wanatetea haki za kina mama na watoto, utadhani ni mke na mtoto wako na wangu, kumbe sivyo, wao ndio watu tu. Na hayo ndiyo tunayoshuhudia wakati huu kimataifa:

“Mfalme Antioko akaziandikia milki zake zote, kwamba wote wawe taifa moja, kila mtu aache sheria zake za asili. Watu wote wa

haujafikia siku 31. Shemere hizo, ndizo hizi tunazoendeshewa nazo hadi sasa. Za kukesha hadi saa sita usiku tukisubiri kuandama kwa mwezi wa ‘Janus’.

Wasomi na Ph.D zao wameshindwa kuwakwamua wanadamu katika ujinga huu. Kisa ni nini? ‘Umagharibi’ ndio maendeleo!

Shemere hizo, ndizo hizi, tunazoendelea kutiwa vichwani, kuwa kuna, ‘Baraza’ la Usalama la Umoja wa Mataifa, kumbe ni Baraza ka Mataifa ‘Watemi’, Wakandamizaji, Wanyonyaji, Majambazi, Wavamizi, Wauwaji na

mataifa wakaikubali amri ya mfalme, hata wengi katika Israeli wakaifuata ibada yake, wakitoa dhabihu kwa miungu ya uongo na kutia unajisi Sabato…Tena wajenge madhabahu na mahekalu na viwanja vitakatifu vya miungu ya uongo, na kutoa dhabihu za nguruwe, na wanyama wachafu; waache wana wao bila kutahiriwa, na kujitia nafsi zao unajisi kwa uchafu na ukafiri wa kila namna; kusudi waisahau sheria na kuzibadili kawaida zao. Naye asiyelitii neno la mfalme atakufa.” (atauawa) (Makabayo

Page 9: ANNUUR 1210A

9 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 1- 7, 2016Makala

SIKU 90 zilizohalalishwa katika Katiba ya Zanzibar ya

1984 zinakwisha, nchi ikiongozwa na Dk. Ali Mohamed Shein ambaye kuwepo kwake kunatetewa na wasaidizi wake baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 kufutwa kimaajabu. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaongoza peke yake tangu hapo baada ya kuunga mkono tamko la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta uchaguzi na kushikilia kuwa ni halali Dk. Shein kuongoza mpaka rais mpya atakapoapishwa.

Dk. Shein anajitokeza kutekeleza shughuli za urais ndani ya mgogoro wa kisiasa unaoendelea huku akikutana na mshindani mkuu wa urais, Maalim Seif Shariff Hamad pamoja na marais wastaafu Zanzibar.

Kule wananchi kunyamaza wakiendelea na maisha kama vile hakuna kilichotokea; kunapumbaza mgeni asione tatizo. Wenyeji wanaviona viashira vya hatari ya mgogoro kuzaa balaa kwa kukosekana ufumbuzi haraka. Mshindi wa uchaguzi hajatangazwa miezi miwili uchaguzi ulifanyika. Wanaojua sababu ni watawala wa CCM.

Kabla ya hapo, maisha ya kisiasa Zanzibar yamekuwa ya kushuhudia Maalim Seif akigeuzwa jamvi la kutupiwa matusi ya nguoni na maneno ya kibaguzi kwa watu wenye asili ya Pemba kama yeye.

Zanzibar kwa sababu ya siasa za chuki, imekuwa kijiwe cha siasa chafu na ubarakala wa kutukanana. Hakuna heshima tena sio tu kwa viongozi wa vyama vya siasa, Serikali ama wananchi mitaani, matusi imekuwa nyimbo kila mahali. Wingu la siasa chafu, na hofu ya usalama kwa raia limeathiri uhusiano wa mtu na mtu na hata ule moyo wa kuhurumiana na kusaidiana. Kama vile mgogoro huo unavyoathiri Tanzania Bara kwa kuzuiwa msaada wa fedha na Marekani kupitia mpango wa MCC kwa kile Marekani, Ulaya na

Shuwari inayoitumbukiza shimoni ZanzibarNa Enzi T. Aboud

Jumuiya za Kimataifa zinavyotoa shindikizo na husisitiza mshindi wa urais Zanzibar atangazwe ili kuinusuru na kutumbukia katika vurugu kama ilivyotokea Ivory Coast au Burundi kutokana na watawala kung’ang’ania madaraka.

Huu ni mgogoro zaidi ya riwaya ya mfalme wa Misri Ramases au Farau na Mtume Mussa au Mkombozi wa Wanaisraeli (Wayahudi wa kale). Dk. Shein mshikilia madaraka makubwa ya urais wa Zanzibar bila ya kikomo anajivuna kwa kubebwa na makada wa CCM na serikali ya muungano. Wanamlinda kwa nguvu, na kweli, nani wa kumuondoa kwenye kiti alichokalia? Na kwa upande wa Maalim Seif, Katibu Mkuu wa CUF, chama chenye nguvu kubwa Pemba na hata Unguja kama ilivyotokea uchaguzi uliofutwa, ameongeza nguvu. Ni nguli kisiasa, asiyeshikika. Nani wa kumkamata na kumuweka gerezani kama ilivyokuwa huko nyuma? Demokrasia ya vyama vingi inamhifadhi.

Lakini, kajitokeza Jaji Mstaafu Mark Bomani akijigamba kuwa mshauri; anamuoneshea kidole kwa kujitangaza mshindi, anataka akubali uchaguzi urejewe kwani “alivunja Sheria ya Uchaguzi,” bila ya mwanasheria mkuu wa kwanza wa Tanganyika huru huyu kutaja Mahakama iliyomtia hatiani na kumhukumu kwa kosa hilo. Anamdhihaki anaogopaje uchaguzi anaotamba ameshinda? Aina ya kumuunga mkono Mwenyekiti

wa Tume, aliyeufuta uchaguzi wote akidai ulikumbwa na matatizo mengi. Anashiriki kusaidia kumfunika shuka usoni Jecha kwa uhuni alioutenda. Anakingwa, hajapelekwa Mahakamani kwa kutaka kuingiza Zanzibar katika maafa makubwa ya kufuta uchaguzi kinyemela kama wanasheria wanavyothibitisha.

Kama hilo halitoshi, Jaji Bomani akatoa ushauri liundwe jopo la wataalamu na watu wenye kuaminika, liwe chini ya Jaji Mkuu mstaafu mmoja na kuishirikisha Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (NEC) na kupata wataalamu wa uchaguzi kutoka nchi chache rafiki na za Jumuiya ya Madola au Umoja wa Afrika (AU) kuja Zanzibar kutatua mgogoro. Jaji mstaafu Bomani yumkini anaumwa. Mgonjwa wa maradhi ya uzee ya kupoteza kumbukumbu. Amesahau huu si mgogoro wa kisiasa wa kwanza Zanzibar, ni zaidi ya mmoja na kwa visiwani migogoro ya kisiasa ni kama utamaduni wake kutokana na migawanyiko ya wananchi wa asili ya Unguja na wale watokao Pemba.

Lakini wanaoishi Unguja kwa mchanganyiko wao ni wengi zaidi na wanaitikadi tofauti za kisiasa hasa vyama vyao vya CCM na CUF zinatokana na vyama vya kistoria – Afro Shirazi Party (ASP), Zanzibar Nationalist au Hizbu (ZNP) na Muungano wa Watu

JAJI Mstaafu Mark Bomani

wa Pemba na Unguja (ZPPP) vinavyozidisha ugumu wa siasa zenyewe na utatuzi unapotokea mgogoro. Yote anayoyashauri yalifanyika wakati wa mgogoro uliotokea kwa Dk. Salmin Amour Juma na Maalim Seif baada ya uchaguzi mkuu wa 1995. Dk. Salmin alitangazwa mshindi wa urais na kupingwa na Maalim Seif na CUF; na kutangaza kutomtambua. CUF ilishikilia kuwa imeporwa ushindi.

Kwa historia ya siasa ilivyo, Zanzibar hakujatulia na kule kushuhudia wafadhili wakisitisha misaada huku mataifa yakishinikiza Tume ikamilishe kumtangaza mshindi wa uchaguzi, na safari za kitalii zikifutwa na kampuni za uwakala za Ulaya na Marekani, kunathibitisha.

Zanzibar chini ya Dk. Salmin ilifutiwa misaada yote ya maendeleo na kuathiri huduma nyingi za kijamii ikiwemo afya na elimu. Kulizuka upungufu mkubwa wa bidhaa, kukatokea mfumuko wa bei na hatimae Serikali kushindwa hata kulipa mishahara ya watumishi wake. Ndani ya madhila yote hayo, mgogoro uliodumu kwa miezi 34 ulibaki ukiwashinda Dk. Moses Anaf na Chief Emeka Anyaoku kutoka Jumuiya ya Madola, mpaka Dk. Salmin akamaliza miaka mitano Oktoba 2000 akiwa dhoofu wa afya na mwishoni akapoteza uwezo wa kuona.

Hizo ndizo siasa za Zanzibar za mizengwe na vurugu zinazoshupaliwa na watawala wahafidhina ambazo sijui kama ni kweli Jaji Bomani amezisahau. Fikra zake zinafanana na za Samuel Sitta alipokuwa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba mwaka 2014 alipoamini angeweza kuiburuza Zanzibar kwa kubuni uongo wa kupatikana theluthi mbili ya wajumbe kutoka Zanzibar na kuipitisha Katiba Inayopendekezwa. Kwa kuwa kulifanyika uongo na dhulma, Katiba hiyo haikupigiwa kura ya maoni na wananchi. Sitta kwa sababu ya kufanya dhambi na dhulma, ameporomoka kisiasa kwa kupuuzwa hata na CCM aliyoinufaisha kwa matendo yake. Hayo pia ni malipizo kwa dhulma na maonevu aliyomfanyia Edward Lowassa alipokuwa Waziri Mkuu na kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni.

Watawala wa CCM hasa wa Zanzibar wamekuwa na tabia ya kukandamiza wananchi na kuonea wakiamini hawataondoka madarakani. Kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar na Rais Dk. Shein kuendelea kubakia madarakani wakati muda wake kikatiba umemalizika, ni ushahidi tosha wa kiburi cha kung’ang’ania madaraka. Mgogoro hautoamulika kwa kurejewa uchaguzi ila ni kuzidisha migogoro zaidi ya hasa pale itakapotokea uchaguzi kurudiwa na CCM kutangazwa mshindi.

Sina shaka CUF hawatakubali kuutambua ushindi huo na ndipo Zanzibar itapotumbukizwa shimoni, na sasa kutarajiwa ukandamizaji viongozi wake na wafuasi wao, bali ikawa chanzo cha mauaji ya kisiasa. Kwa kuwa wananchi wa Zanzibar ni wamoja na imejitokeza wanataka mamlaka kamili ili waweze kujiamulia mambo yao, lazima Dk. Magufuli asimame imara kuona haki ya Maaliam Seif kutangazwa mshindi na kupewa nafasi kuunda serikali inatekelezwa.

(Makala kwa hisani ya Mtandao wa Mzalendo.)

Page 10: ANNUUR 1210A

10 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 1- 7, 2016

Makala

TAREHE 15 Disemba mwaka huu ulifanyika mkutano wa Shirika la Biashara Duniani (WTO). Mawaziri wa Biashara kutoka nchi 162 wanachama walikutana jijini Nairobi ili kuzungumzia mfumo wa biashara kimataifa. Jumla ya wajumbe 7,000 walimiminika Nairobi, wakiwemo wanaharakati na wawakilishi wa asasi za kiraia ambao walihudhuria kama watazamaji.

Kama kawaida ya mkutano huu, kulikuweko na malumbano makali, hasa baina ya nchi za magharibi (tajiri) na nchi za kusini (masikini). Ilibidi mkutano urefushwe kwa siku moja na ukamalizikia tarehe 19 Disemba. Malumbano haya yalianza mwaka 2001 wakati WTO ilipokutana mjini Doha na yangali yanaendelea

Mkutano wa Nairobi ulihudhuriwa na mataifa 43 ya Afrika. Kati yao 33 yanatambulika kama mataifa ‘masikini’, pamoja na Tanzania, Uganda, Sudan Kusini na Ethopia

Mwaka 2001 WTO ilianza mazungumzo mjini Doha (Qatar) kuhusu soko huria kwa lengo la kuondoa vikwazo vya biashara. Tangu wakati huo mazungumzo yamekuwa yakiendelea kwa muda wa miaka 14 bila ya mafanikio, kutokana na pingamizi zinazowekwa na nchi tajiri za magharibi. Wenyewe wanayaita mazungumzo ya Doha (Doha Round)

Hili suala la soko huria huwa linahubiriwa sana na nchi tajiri, wakidai kuwa ili nchi zetu ziendelee ni lazima tuondoe vikwazo kama kodi na ushuru ili kuruhusu mashindano ya kibiashara, yaani biashara holela. Je, hii ni kweli? Tuanze na mfano wa India ambayo hivi karibuni imeamua kueneza umeme vijijini

Raia milioni 400 nchini India hawana umeme. Hii ni robo ya raia wote. Sera ya serikali yao ni kuwafikishia umeme vijijini lakini sera ya WTO (ikiongozwa na Marekani) imekuwa kikwazo kikubwa

Ni kwa sababu serikali ya India inakusudia kutoa ruzuku na msamaha wa kodi kwa uzalishaji wa umeme kutokana na mionzi ya jua (sola). Umeme huu wa sola siku hizi unatiliwa mkazo ili kuepukana na umeme wa mkaa ambao unachafua mazingira kwa kutoa hewa ukaa (kaboni) kwa wingi.

Wachafuzi wakuu wa mazingira ni nchi tajiri. Kwa mfano nchini India kaboni inayozalishwa ni wastani wa tani 1.7 kwa kila raia, wakati nchini Marekani ni tani 17 kwa kila raia. Hata hivyo ni nchi kama India ndizo zinazobanwa na nchi tajiri. Ndio maana India imeamua kupunguza umeme wa mkaa na kuendeleza umeme wa sola kwa kuwawezesha wawekezaji/wazalishaji wa ndani badala ya kutegemea teknolojia hiyo kutoka nje.

Hakuna nchi iliyoendelea kwa soko huriaNa Nizar Visram

Lakini kanuni za WTO haziruhusu utoaji wa ruzuku, la sivyo India inaweza kuwekewa vikwazo vya kibiashara na mataifa tajiri kama Marekani. Matokeo yake India ikalazimika kusitisha ruzuku kwa umeme wa sola. Hii ni baada ya Marekani kuishitaki India katika WTO mnamo 2013, ikidai kuwa eti ruzuku ya India inazuia uagizaji wa vifaa vya sola kutoka nje (magharibi)

Hivi sasa India inazalisha asilimia 71 ya umeme kutokana na mkaa. Ni sehemu ndogo sana inatokana na sola. Makubaliano ya kimataifa yaliyofikiwa mjini Paris hivi karibuni yanazitaka nchi zote zipunguze utumiaji wa mkaa na badala yake zitumie njia mbadala na endelevu kama vile sola na upepo. Ndio maana India ikaanzisha mradi wa kuendeleza umeme wa sola.

Chini ya mradi huu India imekaribisha wawekezaji wa ndani na nje kuanzisha viwanda vya kutengeneza vifaa vya sola. Serikali ikaweka masharti kuwa sehemu kubwa ya bidhaa ghafi na vipuli kama vile beteri na mabango ya sola ni lazima yatoke ndani ya nchi badala ya kuagiza kutoka nje. Hii ni sera ya kujitegemea kiuchumi kwa kutengeneza vipuli ndani ya nchi. Serikali ikatoa ruzuku ili kuwawezesha wenye karakana za vipuli wazalishe kwa bei nafuu

Hapa ndipo Marekani ilipokuja juu. Wakaona watakosa soko, kwani hivi sasa sehemu kubwa ya bidhaa ghafi za sola zinaagizwa kutoka Marekani. Ndipo Marekani ikalalamika kwa WTO kwa kusema eti India inawabagua

Cha ajabu ni kuwa Marekani yenyewe “inaisaidia” India kuzalisha umeme wa sola. Imetoa dola bilioni 4 ili kuendeleza sekta hii nchini India. Makubaliano yalitiwa saini tarehe 18 Novemba 2014. Lakini India imetakiwa itumie fedha hizo kuagiza vipuli kutoka Marekani. Kwa maneno mengine Marekani inatoa “misaada” ili kukuza biashara yake.

Ni sawa na kutoa ruzuku kwa wazalishaji wake ili waweze kutawala masoko

ya kimataifa. Yaani hizo fedha za “misaada” kwa India zisitumiwe kuwezesha wazalishaji wa India bali zitumiwe kwa maslahi ya kampuni za Marekani

Wakati Marekani “inaisaidia” India kuendeleza sola, wakati huohuo inaishitaki kwa WTO kuwa eti inazibagua kampuni za Marekani kwa kuzuia uagizaji kutoka nje

Kwa vile WTO (kwa shinikizo la Marekani) imeikataza India isitoe ruzuku kwa wazalishaji wa ndani, maana yake sasa India italazimika kununua vipuli na mali ghafi kutoka Marekani. Yaani ilichofanya Marekani ni kutoa mkopo kwa India ili kuzisaidia kampuni za Marekani ziweze kuzalisha na kuuza bidhaa kwa India. Hiyo ni ruzuku ya Marekani kwa kampuni za Marekani

Msimamo wa Marekani kuikataza India isitoe ruzuku kwa wazalishaji wake ni unafiki. Ni kwa sababu Marekani yenyewe inatoa ruzuku kwa kampuni zake zinazosafirisha bidhaa za sola nje ya nchi. Katika muda wa miaka mitano iliyopita ruzuku iliyotolewa ni wastani wa dola bilioni 39 kila mwaka. Idara yao ya kodi inatoa msamaha wa asilimia 30 kwa wawekezaji wa sola

Wakati Marekani inalalamika kuwa India inawalinda wazalishaji wake wa ndani, wakati huo huo Marekani inazilinda kampuni zake za sola. Kwa mfano nchi hiyo inatoza kodi kubwa kwa vifaa vya sola kutoka China. Lakini China haikunyamaza kimya, kwani iliishitaki Marekani kwa WTO na ikafanikiwa. Kwanini India nayo isifanye hivyo?

Ni kwa sababu India inahitaji uwekezaji wa dola takriban bilioni 100 ili kufanikisha mradi wake wa sola. Zaidi ya nusu ya fedha hizi ni kutoka nje, hasa Marekani. Sasa iwapo India itailalamikia Marekani katika WTO maana yake itakosa mtaji huo. Haya ndio matatizo ya Waziri Mkuu Modi. Analazimika kupeana mikono na rais Obama na kutabasamu mbele ya camera

Ikiwa India inakabiliwa na masharti kama haya kutoka magharibi, sembuse nchi zetu za Afrika ambazo

ni tegemezi zaidi. Ndio maana utakuta rais wetu akikimbilia Washington mara kwa mara ili kupeana mikono na Obama na kutabasamu. Kwa maelezo zaidi ni vizuri tukaangalia mifano ya Afrika.

Mwaka 2003 katika mkutano wa baraza kuu la WTO, Burkina Faso ilizungumza kwa niaba ya nchi za Kiafrika zinazozalisha pamba kwa wingi. Walilalamika sana jinsi uchumi wao ulivyokuwa ukididimia kutokana na sera ya Marekani ya kutoa ruzuku kwa wakulima wake wa pamba. Kwa kweli bei ya pamba ulimwenguni iliporomoka kwa asilimia 10 kutokana na ruzuku hii ya Marekani.

Bei ikianguka kwa asilimia 10 duniani, maana yake mkulima wetu wa Mwanza na Geita anapungukiwa asilimia 20. Matokeo yake anaachana na pamba na kutafuta ajira mijini

Katika nchi za Afrika Magharibi mashamba 900,000 ya pamba yaliathirika, yakiwa yanaajiri wakulima milioni 7 hadi 8. Ukichanganya na familia zao ni jumla ya watu milioni 13 waliathirika kutokana na kuanguka kwa bei ya pamba kulikosababishwa na ruzuku nchini Marekani.

Hili si tatizo la mwaka 2003 tu bali linaendelea hadi leo. Katika mkutano wa WTO jijini Nairobi Burkina Faso na nchi zingine zilirudia tena madai yao na mara nyingine Marekani ikakataa kuacha kutoa ruzuku kwa wakulima wake wa pamba. Halafu wanatufundisha kuwa soko huria eti ni sera bora kwa maendeleo yetu

Mfano mwengine ni nchi ya jirani ya Kenya ambako zao moja kubwa linalosafirishwa hadi Ulaya ni maua. Huzalishwa kwa wingi karibu na ziwa Naivasha ambalo hupata maji yake kutoka mito ya Malewa na Gilgil. Msomi mashuhuri wa Uganda, Profesa Tandon anasema katika ujana wake mnamo 1957 alitembelea maeneo hayo na akashuhudia ardhi yenye rotuba. Aliona mito yenye maji safi, iliyojaa miti na wanyama wa kila aina, kuanzia ndege aina

ya korongo, flamingo hadi viboko na vipepeo.

Aliona maelfu ya wavuvi wakivua samaki kwa wingi na wakulima wakiapata maji ya kutosha kwa mashamba yao yaliyosheheni nafaka

Anasema mwaka 2009 alitembelea tena na kuona vyote hivi vimetoweka. Badala ya vipepeo, samaki na ndege sasa kuna mashamba makubwa ya maua yanayomilikiwa na makampuni makubwa yanayoajiri vibarua. Hata nyakati zile mamia ya wakulima walikuwa wakilima maua pamoja na chakula chao. Leo wanaajiriwa na wawekezaji kutoka nje waliovamia ardhi ya wakulima wadogo. Matajiri wanatajirika na vibarua wanaishi maisha duni.

Kuna watakaosema haya ni maendeleo. Lakini ni maendeleo baada ya kuteketeza mazingira na maisha ya wananchi wa kawaida. Hapa kwetu kuna wanaohubiri ‘maendeleo’ ya aina hii. Wanayaita ‘Kilimo Kwanza.’

Wanadai maendeleo yatakuja kwa kupitia soko huria na wawekezaji wakubwa. Huko vyuoni wanafunzi wetu watalazimishwa kumeza ‘nadharia’ hiyo na kujibu masuali wakati wa mitihani. Ni wachache kati yao wataambiwa ukweli kuwa hakuna kitu kama hicho. Soko huria haikuwepo hata wakati Ulaya ilipoingia katika mfumo wa kibepari, sembuse leo wakati wa uliberali mambo-leo

Wanafunzi wetu hawatafundishwa kuwa wakati Marekani ilipoanza kujenga ubepari ilikataa katukatu soko huria. Nchi hiyo ilipojikomboa kwa mtutu wa bunduki kutoka ukoloni wa Uingereza mwaka 1776, watawala wapya wa Marekani wakawaambia wakoloni wa Uingereza:

“Hatutakubali tena kuendelea kuwazalishieni pamba na tumbaku, na kisha tukanunua bidhaa kutoka viwanda vyenu. Kwani nasi pia tunataka kujenga viwanda.”

Ndipo Marekani ikapiga marufuku bidhaa kutoka Uingereza na badala yake wakaanza kuunda bidhaa zao wenyewe. Hivi ndivyo walivyoleta mapinduzi ya viwanda, siyo kwa kupitia soko huria.

Huu ni mfano mmoja tu wa Marekani. Kuna nchi nyingi ambazo pia zimeendelea kwa kuviwezesha viwanda vya nyumbani na kuzuia bidhaa kutoka nje. Ni pamoja na nchi za Asia kama Japani na Korea.

Leo Afrika tunaambiwa turuhusu biashara holela, eti hivi ndivyo tutakavyoendelea. Tutapokea ‘misaada’ itakayotumika kununua bidhaa kutoka kwao na kuwalipa mishahara na posho za kufuru ‘washauri’ kutoka kwao.

(0713-562181 [email protected])

RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta (katikati).

Page 11: ANNUUR 1210A

11 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 1- 7, 201611 AN-NUURSafu ya Ben Rijal

WIKI iliopita tuliliangalia suala zima la taka na tatizo la taka kurundikana katika maeneo yanayotuzunguka. Kwa kweli suala la taka linataka umakini mkubwa kutoka kuzikusanya hadi zinapotupwa. Kinyume chake ndipo taka huwa taka na mashaka katika mazingira yanayotuzunguka na kupambana na maradhi ambayo yanasababishwa na taka.

Wengi wetu hushindwa kutambua kuwa maji machafu nayo ni taka na husababisha maradhi na moja ya maradhi ambayo yanayochukua maisha ya watu mara mmoja ni Kipindupindu ambayo husababishwa na maji yalio sio safi na salama. Tunapozungumza taka na kipindupindu, ni vyema tukasema ni maji machafu, kwani taka ngumu hazisababishi kipindupindu.

Kati ya matatizo yanayotukabili wananchi ni kutokuwa weledi wa kujikinga na uchafu na utupaji wa taka na pili ni kule waliowajibika kutuongoza ikiwa Manispaa, Wapanga Miji na Vijiji, watu wa Afya na Mazingira kutofanya kazi zao inavyotakikana na taasisi hizo zote nilizoziorodhesha kila mmoja ina jukumu lake la kusaidia kuratibiwa kwa taka, lakini utaona mchango wao sio ule unaohitajika katika kuleta ufanisi.

Taka kwa mfano ziwe majumbani, kwenye ofisi, kwenye viwanda n.k. Kuanzia hapo ndipo taka zinapohitajiwa kuratibiwa. Kivipi? Tunatakiwa tunapokuwa majumbani mwetu tunatakiwa tujuwe taka zipi ni zile zinazooza na zipi zile zisizooza. Hayo hayaji hivi hivi bila ya wananchi kuelimishwa na kuna njia tele ambazo zinahitajika kutumiwa kutoa elimu kwa wananchi, kwa kuanzia

Yawe endelevu - 2

kwenye Mikutano ya Shehia/Kaya, vijiji, semina, vipindi vya radio na TV, makala katika magazeti, kutolewa vipeperushi na jumbe katika simu za mkononi.

Elimu ya utupwaji taka inahitajika ingawa wengi wataona ni kichekesho kusema leo tunaelimishwa namna ya utupaji wa taka. Ndio, lazima hayo yafanyike watu kuelimishwa taka zinavyohitajika kutupwa na kwa kuanzia elimu hio inahitajika kuchukuliwa Shehia/Kaya mmoja kuwa ni kiegezo wa kuelekezwa watu namna ya utupaji wa taka kisha mafanikio yake kuanza kupelekwa kwa upana kwenye Wilaya, Mkoa na hapo ndio kusema nchi nzima itakuwa imeilimishwa.

Taka zinataka kutupwa kwa namna ambayo nchi zilizoendelea ndio wanavyofanya na kufanikiwa. Wengine watasema ya nchi zilizoendelea huko huko wao wanaweza kwasababu matajiri, wana teknolojia. Lakini mtu huyo huyo hasemi anapopewa gari kubwa lenye kunywa mafuta kwa wingi na huduma zake ni sawa na kulisha familia 20 za watu nchi ya maskini kupata mlo wa mfuto wala sio ule wakujisikia. Mtu huyo atasingizia hayo ni ya Wazungu ndio yao, lakini kupanda gari la Serikali la kifakhari, kukaa kazini kwenye kiyoyozi, kuvaa tai au mjusi shingoni hayo sio kitu cha Wazungu.

Elimu inayozungumzwa ni kuwa lazima kila nyumba iweze kuwa na mifuko mitatu meusi mikubwa ya kukusanya taka mifuko hiyo itakuwa inaiingizwa taka zinazooza (organic) ikiwa maganda ya mihogo, mbatata, viazi, makaratasi, mabaki ya

samaki, machichira, maganda ya ndizi n.k. Taka hizo ziwe hazichanganywi na taka nyengine huingizwa katika mfuko mmoja, kisha taka zote za Plastiki pamoja na chupa za Plastiki hizi huingizwa katika mfuko wa aina nyengine, kisha mfuko wa tatu taka zote za vibati na makopo huingizwa katika mfuko wake, kisha kitachofwatia ni kuwa, unapofika kwenye kiburuji (slab) cha kutupa taka kuwe na tabaka tatu zimewekwa nazo ni ile ya taka zinazooza, pili nitaka za Plastiki na sehemu ya Vikopo na mabati, mtupaji wa taka atazibeba taka zake na atapofika atajua taka ipi aitupe wapi?

Utaona ni kazi kufanya hivyo lakini sio kazi hata chembe kama tutafundishana na tukawa tayari kuitikia wito huo. Tuseme tukawa na nidhamu. Kinachobaki baada ya elimu ni ujenzi wa sehemu hizo na kwa kuanzia Serikali ifidie manunuzi ya mifuko hio, kwani Serikali inahitajia kuliweka sawa suala hili la taka kwa hio mfuko mmoja thamani yake isizidi shilling 200/= hakutokuwa na shida ya kuununua na mtu anaweza kutumia moja ya njia mbili, moja ni kuuwacha mfuko wa taka alizokwenda nazo kuzitupa na njia ya pili ni kuzimwaga na kurudi nyumbani na mfuko wake kisha akauosha na kuwa tayari kuendelea kuutumia.

Manispaa wanapofika katika ukusanyaji wa taka wanahitajiwa wawe na magari ambayo yataendana na mpango huu, iwe inachukua taka zenye kuoza mbali na taka za plastiki mbali na

mabati na makopo mbali.Njia nyengine ni zile

taka zinazooza itakiwe kila Shehia/Kaya kuwe na sehemu ya kuchukua baadhi ya taka hizo kutengeneza mbolea kisha serikali ikaja na ule wito uliopata kuwepo katika miaka ya 60 kila mwananchi kuwa na bustani ambayo bustani hio atapanda mchicha, tungule, nyanya chungu, bilingani, mabamia na vipando vyengine, mwananchi mmoja mmoja awe na bustani yake na Shehia/Kaya wawe na eneo lao ambalo watakuwa wanapanda vipando hivyo. Kufanya hivyo ndio inaelekeza nini? Ndio pale tuliposema taka sio taka na taka ni mali kwasasa. Ikiwa mtu mwenye familia ya watu 5 anatumia kwa mwezi shilling 20,000/= kwa matumizi ya mboga mboga, atasita na manunuzi hayo na hio shilling 20,000/= sasa itatumika katika matumizi mengine na hata kuweza kusema katika mwezi angalau anakuwa ana akiba ya shilling 20,000/= taka hizo sasa zinaelekea katika wigo wakupunguza umasikini ikiwa ni MKUZA na MKURABITA mipango ya kupunguza makali ya umasikini kwa sehemu ndogo yanaweza kurekebishwa kutokana na taka, hapo inahitajia kuwapata mabingwa wa uchumi kuwaelekeza na wao kutoa maelekezo yao na kufanya muelekeo wa siku za baadaye (projection).

Shehia/Kaya inaweza kufanya mpango wa kugeuza chupa za plastiki kuwa ni miradi kwa njia mbili, mmoja ni kuzikusanya na kwenda kuziuza na nyengine chupa hizo sasa kutengeneza vitu mbalimbali, ikiwa vigari, mapambo, vijimeza na viti vidogo vya kupamba, hayo tunaweza kwenda kujifunza kule Rodrigers nchini Mauritius au Mohele katika visiwa vya Comoro, vijana wanaweza kukusanywa na kufundishwa kufanya hayo na ikawa ndio ajira

yao, kwa kuzingatia kuwa taka zinazalishwa kila siku.

Makopo kabla ya kuyataftia suluhisho Serikali itatakiwa iweke ushuru mkubwa vitu vya makopo ili kuupunguzia mzigo Mazingira yetu yaliotuzunguka, soda za vikopo zinaweza zikapigwa marufuku, soda zote ziwe za chupa au plastiki, kwa kuwa chupa za viage ni rahisi kurejezwa (recycling) aidha chupa za plastiki. Jengine kunaweza kuanzishwa viwanda vidogo ambavyo makopo huafanywa likawa busati kubwa likakunjwa na kisha kurejeshwa viwandani kutumiwa tena kwa njia nyengine.

Ukitizama mtizamo huo tukajaribu kuutumia kwa kiasi Fulani, mzigo wa taka tunaweza kuupunguza na hapo hapo tukapata ajira kutokana na taka. Kuna njia nyingi zinazotumika za kimambo leo ambazo taka huweza kugeuzwa na kuweza kuzalisha nishati, nishati ndogo hio katika mitaa itaweza kutumiwa katika mfano kukaushia samaki, kuwasaidia mama lishe (mama ntilie), kumefika wakati hata hawa kina mama wanaouza vyakula wakawekwa kwa njia za ushirika na kuwa kitu kimoja, bingwa wa maharagwe akatakiwa apike maharagwe tu, bingwa wa mpunga iwe pilau, wa nazi apike wali tu, ushirika wa watu watano watano na kupata nishati kutokana na taka watajikuta wanapika haraka, chakula kizuri na kuyasaidia mazingira kuwa safi.

Unapoandika fikra kama hizi wengine watakuambia hizi ni ndoto za Ali Nacha, lakini Ali Nacha katika kuota kwake alikuwa anavyo vitu akawa amelala anaota na kisha kupiga teke kapu lake na vitu vyake kuvunjika. Sisi tupo kama Ali Nacha, taka zimetuzunguka sasa lilokuwepo ni kuzigeuza na kuwa mali. Hapo ndio yataanza kuwa yale Yawe Endelevu na taka zinazofika kwenye jaa kuu ni kidogo nazo zinafukiwa kitaalamu.

Fatwana na mie wiki ijayo katika kuendeleza kuchambua Yawe Endelevu. (Kwa mawasiliano 0777 43 69 49)

Aina ya Mashine itumiwayo kutoa nishati kutokana na taka

Page 12: ANNUUR 1210A

12 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 1- 7, 201612 Safu ya Ben Rijal

KATIKA kumuelezea kuzaliwa kwake na maisha yake ya kwanza ya utotoni, nitadokoa sehemu ya simulizi cha kitabu “Mzanzibari asimlia hadithi yake” kitabu kilichoandikiwa na mdogo wake Shaaban Saleh Farsy.

Sheikh Abdalla Saleh Farsy alizaliwa mwezi wa Februari mwaka 1912 katika mtaa wa Jongeyani uliopo eneo la Malindi, Unguja. Kutokana na Sheikh Shaaban Saleh Farsy katika kitabu chake hicho anaeleza kuwa baba yao akiitwa Saleh Abdallah Saleh bin Kassim bin Mansour bin Haydar bin Ahmad Al-Farsy, mama yao akiitwa Bibi Fatma Binti Jabir bin Saleh Bin Kassim bin Mansour bin Haydar bin Ahmad Al-Farsy. Katika ukoo wa Sheikh Saleh Farsy walizaliwa watoto 6 akiwemo Bi. Farashuu S. Farsy aliozaliwa mwaka wa 1908 akiwa ndio mkubwa wa ndugu zake Sheikh Abdalla Saleh Farsy kisha akazaliwa Bi. Amina katika mwaka wa 1910, akafwatia Sheikh Abdalla katika mwaka wa 1912, Sheikh Shaaban mwaka wa 1914, Sheikh Jabir mwaka 1923 na kitinda mimba wao akiwa Maalim Muhammad Jabir ambaye alizaliwa mwaka wa 1925.

Sheikh Shaaban anaendelea kusimulia kama ifwatavo “Sisi tumezaliwa Malindi Jongeani nyumbani kwa Babu yetu, Marehemu Sheikh Jabir bin Saleh Al-Farsy, tulilelewa na kukulia huko huko, pia tukasoma Qr’ani na kuhitimu hapo jirani, kwenye chuo cha Marehemu Bimwalimu Bint Hamadi. Lakini baadaye tukahamia Funguni, kwa Babu yetu mimi na Sheikh Abdalla Saleh Farsy na katika nyumba hii ndio tukatahiriwa sisi tu wawili peke yetu.”

Sheikh Shaaban anaeleza kuwa kati ya ndugu zake wote, Sheikh Abdalla alikuwa na fahamu pana na akiwapita ndugu zake wote. Katika maandiko ya Sheikh Shaban na mengineyo yanafahamisha kuwa Sheikh Abdalla aliweza kuihifadhi Qur’an yote pamoja na hadithi nyingi za Mtume Muhammad (SAW) katika umri wa miaka 20 na akaanza kusalisha Tarawehe kwa kutumia Msahafu kila siku mmoja Juzuu mmoja. Sheikh Abdalla alikuwa na wasaidizi wake akiwemo

Masheikhe wetu: Sheikh Abdalla Saleh Farsy-10Makala iliopita nilimuandika Sheikh Fatawy bin Issa Sheikhe ambaye alikuja kuchukua

makamo ya Sheikh Abdallah Saleh Farsy ambaye ni mmoja wa Masheikhe wa karibuni katika karne ya 20 aliofanya kazi kubwa ya kueneza Uislamu kwa njia mbili kuu mmoja ikiwa kusomesha na kutoa mawaidha na ya pili ni kuweza kuandika vitabu mbalimbali. Sheikhe Abdalla alifanya kazi kubwa ya kuandika na moja ya kazi yake kubwa kati ya nyingi alizozifanya, ni kule kutafsiri Qur’an kwa Kiswahili tafsiri ambayo imewafaa wengi wasiojuwa Kiarabu kuweza kujifunza yaliomo kwenye Qur’an. Tafsiri hio ikijulikana kwa jina la “Qurani Takatifu” ambalo Chapisho la mwanzo lilichapishwa katika mwaka wa 1969, chapisho la tatu likichapishwa nakala 15,000 na Chapisho la nne lilichapishwa nakala 36,000 na Islamic Foundation of Kenya. Sheikh Abdalla Saleh Farsy tafsiri yake hio ilikuwa ya kujibu mapigo ya tafsiri ya Qur’an ilioandikwa na Ahmadiya ikiwa utangulizi wake ulitokana na ‘Fi Tafahamul Qur’an’ yaani Msingi wa kufahamu Qur’an ulioandikwa na Sayyid Abdul A’la Maududi wa Pakistan (1903-1979) akiwa ni mwanaharakati aliofanya Daawah kubwa nchini Pakistan na kupambana na utawala wa nchi hio na kuwekwa jela kama maulamaa wengine niliokwisha kuwaeleza katika makala zilizopita.

SHEIKH Abdalla Saleh Farsy.Maalim Mohammed Juma, Dr. Saleh Khasiby, Sheikh Saleh Zagar, Abdalla Himidi na Mohammed Hamid. Alikuwa ni yeye peke yake akisalisha pasi na kukamata juzuu kwa kutizamia.

Zanzibar ya leo sio ile iliopita, kwani katika

WASWAHILI wajivunia kwa ulamaa Sheikh Abdalla Saleh Farsy.

mji wa Unguja katika Manispaa yake kulikuwa na sio chini ya Maktaba za kujisomea na kuazima vitabu isiopungua 5 na kila skuli iliopo katika mji kulikuwa na Maktaba yake. Sheikh Abdalla alikuwa kipumzikio chake ni kwenda katika

Maktaba mbalimbali kujisomea na kuazima vitabu. Alikuwa na shauku kubwa ya kujisomea na hio ilimuwezesha kuweza kuzimudu vilivyo lugha tatu nazo zikiwa ni lugha ya Kiswahili, Kiarabu na Kiengereza. Sheikh Abdalla akipenda lugha na hata

akipenda kutaniyana na baadhi ya wanafunzi wake kwa lugha ya Kigujirati, Kingazija na Kiurdu kwa maneno ya kutupa ya hapa na pale.

Walimu wake na kusoma kwake

Alisoma kwa Masheikhe wafwatao ambao walikuwa

Maalim wakupigiwa mfano, akiwemo Sheikh Abu Bakar bin Abdullah bin Bakathir, Sayyid Hamid bin Mansab, Sayyid Alawy bin Abdul Wahab, Sheikh Ahmed bin Muhammad al-Mlomry ambaye nishamuelezea kigogo huyu aliosafiri na kwenda Misri hadi Makka kwenda kusoma dini ya Kiislamu.

Alianza kujifunza kwa Sheikh Hamid Mansab ambaye nilishamzungumza makala zilizopita aliokufa akisomesha darsa katika mwezi wa Ramadhani. Alikuwa akenda pahala panapojulikana Msikiti Barza ambapo ndipo akisomeshwa na Sayyid Hamid akitoka kwao Funguni na kwenda Mkunazini kwenda kujifunza kitabu hicho katika nyakati za Magharibi. Sheikh Abdalla alianza kusoma kitabu cha mwanzo cha Fiqhi kijulikanacho kwa jina la Risalatul Jamia, alianza

kupata mafunzo ya Fiqhi kwa Sheikhe huyu ambaye akipenda kusoma na aliwavutia wanafunzi wake pale anaposomesha kuwa na mifanyo ya dini, historia, jografia na kuwa na maelezo ya sadiki ukipenda. Sheikh Abdalla alimaliza kwa haraka kusoma kitabu hicho na kukielewa kushinda wengi wa wanafunzi waliosoma hapo kwa Sayyid Hamid. Aidha alisoma somo la Fiqhi kwa Sayyid Alawi bin Abdul Wahab Sheikhe ambaye inaelezewa hakutokea mtu wa mfano wake alioshikamana na Sunna za Mtume Muhammad (SAW) kwani tangu anakwenda kulala husoma zile dua na sura ambazo Mtume Muhammad (SAW) akisoma, akiamka kwa sala za usiku, na anapoamka asubuhi alikuwa akisoma “Alhamdu Lillaahi lladhiy ahyaana baada maa amatana Wailayhi nnushuur, asbahna waasbaha mulku Lillaahi Allahumma innaa nasaluka khayra hadha lyaum nuurahu wabarakatahu wanaswarahu wahudahu wanaudhubika min Sharii hadha lyaum Washari maa Fiihi washari maa kablahu Washari maa baadahu Birahmatika yaa Arhama Rraahimiin; Allahumma ftah lana abwaba Rahmatika Birahmatika yaa Arhama Rraahimiin.” Tuipendelee kuisoma dua hii kila tunapoamka. Aidha

Inaendelea Uk. 13

Page 13: ANNUUR 1210A

13 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 1- 7, 2016Safu ya Ben Rijal

Masheikhe wetu: Sheikh Abdalla Saleh Farsy-10Inatoka Uk. 12Sayyid Alawi alikuwa kila analolifanya ni kama Mtume Muhammad (SAW) alivyotufunza anapoingia msalani husoma dua aliokuwa akisoma Mtume Muhammad (SAW) na anapotoka hufanya hivyo hivyo, akivaa viatu hufwata taratibu ambazo Mtume Muhammad (SAW) akisoma na akihakikisha akitoka kwa mguu wa kulia kwenda safari zake atokapo nyumbani, kwa ufupi Sayyid Alawi maisha yake yote yalikuwa hivyo na aliwavutia wengi kwa kuwa na taratibu hizo na Sheikh Abdalla akiwa mmoja wa hao.

Sheikh Abdalla alisoma kwa Sayyid Alawi vitabu 12 vya Fiqhi pamoja na Sharhi ya Mardfin Rabbiyyah ambayo imeambatana na elimu ya mirathi. Sheikh Abdalla alifunzika vilivyo kwa Sheikhe huyu kwani alipokuwa anasomesha Mirathi wanafunzi hawakuwa wanapata tabu kuuelewa mlango ambao ni mgumu kufahamika.

Aliweza kujifunza vya kutosha lugha ya Kiarabu kwa Masheikhe mbalimbali na alipotimu umri wa

miaka 20 tu, alikuwa akiweza kuandika Mashairi mbalimbali kwa lugha ya Kiarabu. Uandishi wa Mashairi ni katika moja ya uwezo wa mtu kumudu lugha yoyote ile.

Sheikh Abdalla alibahatika kumdiriki mmoja wa Ulamaa aliokamilika Sheikh Ahmad Muhamamd Mlomry ambaye Sheikhe huyu aliwahi kukutana na Mufti wa Misri Sheikh Muhammad Abdoo na kusoma kwake. Aidha Sheikh Mlomry alikutana na Sheikh Muhammad Bin Suleiman Hasballah mtunzi wa kitabu “Riyadhal-Badia.” Aidha Sheikh Mlomry alikutana na Sheikh Muhammad Bin Suleiman Hasballah mtunzi wa kitabu “Riyadhal-Badiah.” Alipata bahati kukutana na Seyyid Ahmad Bey-Al-Husseyny mtu wa mwanzo kupiga chapa ‘Al-Umm’ ya Imam Shafi. Kwa Sheikhe huyu Sheikhe Abdallah alisoma vitabu 25 vikiwemo Tafsiri ya Jalalayn kilichoandikwa na Jalal al-Din Mahali (1389-1450) kutoka Misri na Jalal

al-Din Suyuti (1445-1505) wa Syria. Hao wawili ni Maulamaa wakubwa na maarufu wa madhehebu ya Imam Shafi.

Sheikh Abdalla Alijifunza pia kutoka kwa Sheikh Abu Bakar (1881-1943), mtoto wa Sheikh Abdullah bin Abu Bakar Bakathir (1860-1925), mwanafunzi wa Sheikh Ahmed bin Abu Bakar al-Sumait. Kwa Sheikh Sheikh Abu Bakar bin Abdullah bin Bakathir alijifunza elimu ya Fiq'hi. Sheikh Abu Bakar akamchagua Sheikh Abdalla kuwa Imamu wa Swala ya Witri kutoka mwaka 1933 mpaka terehe 28 October 1939, alipomruhusu pia kusomesha Qur’an katika Msikiti Gofu ambapo wanafunzi walikuwa wengi na hata wasikilizaji na Msikiti ukifurika na wengine kukosa nafasi wakikaa nje. Nilishuhudia darsa hii kwani mie nilikuwa nikisoma Chuwoni hapo Masjid Barza.

Sheikh Abdullah alisoma vitabu vingi vya Fiq'hi kutoka kwa Sheikh Muhammad Abdul Rahman al-Makhzuymy vikiwemo

vitabu vya Fathul Muin na Iqnai, ambavyo mwanzo vilikuwa vikisomeshwa na Sheikh Abdullah bin Abu Bakar bin Bakathir hapo Msikiti Gofu katika mwaka 1917. Alijifunza aidha kwa Sheikhe huyu elimu ya kupanga nyakati za Swalah na kuujua upande wa Qiblah.

Sheikh Abdalla aidha alisoma kwa Sheikh Muhsin bin Ali bin Issa Barwany aliyekuwa kati ya vigogo vya Ukutani, Sheikh Muhsin alikuwa mwanachuoni wa mwanzo katika mwaka 1944 kumruhusu Sheikh Abdullah Saleh Farsy kusomesha Jalalayn Msikiti Barza katika mwezi wa Ramadhani. Baadaye Sheikh Abdullah Saleh Farsy alijifunza kwa Sheikh al-Amin Ali bin Abdullah bin Nafi al-Mazrui (1875-1947).

Sheikh Abdullah Saleh Farsy alipewa Ijaza (Shahada) na Sheikh ‘Umar bin Ahmad bin Abu Bakar al-Sumait aliyemsomesha vitabu vya Fiq'hi, Mantiq (Logic) na Hadith, pamoja

na vitabu vingine. Sheikh Umar bin Ahmad bin Suamayt mbali ya kuwa alim alikuwa ni mcha Mungu wakupigiwa mfano, akiwa mzalia wa visiwa vya Comoro mwenye asili ya wazee kutoka Yemen, alikuwa kila mtu akimkubali Sheikhe huyu. Bahati mbaya alihama visiwani Zanzibar na kwenda kuhamia visiwa vya Comoro katika mwaka wa 1965, penye wimbi kubwa la Masheikhe kukihama kisiwa cha Zanzibar.

Sheikh Abdalla mbali ya kusoma elimu ya dini, katika mwaka wa 1924 alijiunga na Central Primary School, inasemekana kuwa alipokuwa Skuli ya msingi (Primary) alikuwa akikimudu Kiengereza vilivyo na alisoma elimu ya msingi kwa miaka 9 ambayo ilikuwa mwanafunzi anaanza na darasa likijulikana kama Qu’ran Class kisha anaanza darasa la kwanza na kuendelea hadi darasa la 8.

(Makala hii inaendelea tafadhali fwatana na mie katika toleo lijalo-0777 43 69 49)

S H U K U R A N I z o t e a n a s t a h i k i M we n y e z i Mungu mola mlezi wa ulimwengu, rehema na amani zimfikie mbora wa manabii na mitume wote.

Upole wa Mtume (s.a.w) ni umbali muhimu katika utu wake na katika ulinganiaji wake, na katika jambo la kuzingatia kuwa yeye ni nabii na Mtume na ndiye mfikishaji ujumbe toka kwa mola wake (na hatukukutumiliza wewe isipokuwa ni rehema kwa ulimwengu wote).

Hembu tujikumbushe vipi mtume huyu alikuwa na vipi maisha yake yalikuwa aya hii inatueleza kwa upana wake, akinasibiana na mazoea yake kwa daraja la baina ya ujumbe na utume katika upole huu, ili isionekane kuwa hakufikisha ujumbe miongoni mwa upole kwa walimwengu isipokuwa ni kuthibitisha kuwa kweli huyo ni Mtume wa watu wote uliotimia alisambaza upole huo kwa njia zote na kupambana katika moyo

Mazazi ya Mtume (s.a.w) na maisha yake

Na Sheikh Mohamed Ubaidillahi Mohamed Ally

wake na maumbile yake yote .

A m e s e m a M we n ye z i M u n g u ( k w a h a k i k a amekujieni Mtume kutokana na nafsi zenu wenyewe yanamsumbua mlionayo anapupa nanyi kwa waumini ni mpole mwenye (huruma) (128) Surat Tauba.

Mtume ni kiigizo chema kwa upole wa kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kwa hivyo amemsifu kwamba yeye ni mpole mwenye huruma kwa yakini amemleta Mwenyezi Mungu kuwa ni rehema kwa ulimwengu wote.

Kwa upole uliotimia kwa wote waliokamilika kwa ujumla wao, wanaweza waumini kupata fa ida k u t o k a n a n a u p o l e alioshikamana nao Mtume (s.a.w).

Hayo ni kwa sababu (kwa waumini ni mpole mwenye huruma) na pia anaweza kafiri na mnafiki kupata faida kutokana na upole hii ni pale alipoambiwa walaani mushirikina.

Akasema Mtume (s.a.w) (mimi s ikutumwa kuja kulaani, bali nimetumwa niwe rehema kwa viumbe wote).

Kama ilivyokuwa upole wa k e u m e e n e a k a t i k a familia yake na uma wake na masahaba wake kwa hakika alikuwa Mtume (s.a.w) ni mbora wa watu ni mbora kwa familia yake, na ni mbora wao

kwa umma wake kutokana na uzuri wa maneno yake na uzuri wa kuchanganyika kwake na wake zake kwa uzuri na heshima pale aliposema Mtume (s.a.w) (mbora wenu kwa watu wake na mimi ni mbora wenu kwa watu wangu)

Kama alivyokuwa akiishi na watu wake na akiwafanyia upole na akicheza nao na kama alivyokua akiwasaidia wake zake katika mambo ya nyumbani na anawapa mahitaji yao alikuwa mama aisha (r.a) akioga maji pamoja nae katika chombo kimoja na akimwambia (nibakishie).

Mtume al ikua mpole kwa wote, kwa watoto bali alikuwa akisikia kilio cha mtoto. hupunguza kisimamo cha swala kwa kuogopa fitina ya kilio hicho kwa mama wa mtoto ndani ya swala na alikuwa akipita kwa watoto huwasalimia na walikuja hassan na hussein nao ni watoto wa binti yake fatuma naye alikuwa juu ya mimbari (jukwaa) akihutubu akawabeba na kuwaweka mikononi mwake akasema amesema kweli Mwenyezi Mungu na Mtume wake (na jueni hakika ya mali zenu na watoto wenu ni fitina na kwa hakika Mwenyezi Mungu kuna kuwa na malipo makubwa) (28) Surat Anfali

Niliwatazama watoto hawa wawili wakiwa wanatembea n a k u a n g u k a n a m i nimeshindwa kusubiri hadi

nimekatisha mazungumzo na kuwanyanyua.

Basi upole wa Mtume (s.a.w) ukamfanya kuwa na huruma hakuwa muovu wala mwenye kusababisha uovu wala mwenye kunyanyua sauti na kupiga kelele sokoni na wala hakulipiza mabaya kwa mabaya lakini alisamehe.

Bali Anas Ibin Maliki (r.a) anasema (nilimuhudumia Mtume (s.a.w) kwa muda wa miaka kumi (10) namuapia Mwenyezi Mungu hajapata kunigomba (kunilaumu) hata mara moja, na wala hajawahi kuniambia katika jambo kwa nini umefanya ivi na kwa nini hukufanya hivi” na toka kwa Aisha (r.a) amesema (hajapatapo Mtume kumpiga mtumishi wake wala mke wake kwa mkono wake isipokuwa katika jihad tuu, na katika mapokezi mengine (hajapatapo Mtume kumpiga mtu yeyote kwa mikono yake hata mara moja si mke au mtumwa isipokuwa vita vya jihad tuu).

Qur-ani imesema juu ya hilo (na kwa rehema za Mwenyezi Mungu umekuwa laini kwao na laiti ungekuwa mkali na mwenye roho mbaya basi wangekukimbia wote ulio nao basi wasamehe na waombee msamaha na shauriana nao katika mambo na unapotaka kufanya jambo tegemea kwa Mwenyezi Mungu.

Mtume (s.a.w) mpole kwa waja kuwapunguzia na

kuwaondolea ugumu naye katika haya anasema Mtume (s.a.w) wenye kuona huruma atawahurumia Mwenyezi Mungu, wahurumieni walio ardhini atakuhurumieni Mwenyezi Mungu mbinguni).

Lakini pia alikuwa ni mtu mwenye upole mkubwa, alikuwa mwanasiasa, lakini wakati huo huo ni mtu mwenye heshima kubwa na mwenye subira, hebu tutupie macho katika vita vya Uhud, alipouliwa ami yake Hamza (Simba wa Mungu na Mtume wake (ra) na kuchanwa chanwa mwili wake kama ulivyochanwa mwili wa mama yake shangazi yake Abdilahi bin Jahshi, na kupasuliwa kichwa chake.

M w e n y e z i M u n g u wasamehe watu wangu kwani wao hawajui walitendalo) je, kuna mtu mpole kuliko Mtume Muhamad kwa mfano wa nyakati hizi zote?

Na wakati wa kuikomboa Makka aliamkiana nao wale watu waliomfukuza na kumtoa na wakasaidiana na kumuudhi, ona ni namna gani aliamkiana na wale wagomvi wake katika watu wa Abii Twalib na wakasababisha kifo cha mke wake mpenzi naye ni mama Khadija Kubraa (r.a)

Na wakati wa kifo cha ami yake Abii Twalib na alitendeana vipi watu wa Makka baada ya historia yote hii iliyojaa uadui na dharau?

Page 14: ANNUUR 1210A

14 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 1- 7, 2016

MAKALA/MASHAIRI

Ni ala ala jirani, msemo wetu wa ada, Lengo kuu kuthamini, ya ujirani ibada, Bali si kwa kufurani, na kutengua aqida, Tusitengue AQIDA, kwa nembo ya ujirani.

Kausia Adinani, kuwafanyia saada,Si kwa imani kukhini, tena kwa yao irada,Bali kwa dini kuwini, na kuilinda aqida,Tusitengue AQIDA, kwa nembo ya ujirani.

Kushiriki noelini, ni kukiuka kaida,Kisa eti ujirani, usijepata kudoda!Twaiwekaje rehani, ya dini yetu aqida?Tusitengue AQIDA, kwa nembo ya ujirani.

Sikuyo waloibuni, si ya Issa maulida, Muhali maandikoni, kuitolea shuhuda, Kulikoni na kwanini, tububuswe kiaqida? Tusitengue AQIDA, kwa nembo ya ujirani.

Ya ala ala jirani, yaendane na aqida,Yasiwe ya ujirani, dhidi ya yetu aqida,Kushiriki noelini, ni hilaki kwa aqida,Tusitengue AQIDA, kwa nembo ya ujirani.

Tuachane ikhiwani, na ya ujahili ada,Ya kuchanganya imani, UTATU na TAUHIDA,Imara tusimameni, kuin'goa hii ada,Tusitengue AQIDA, kwa nembo ya ujirani.

Haya shime waumini, kulinda yetu aqida,Si kwa mtutu vitani, kwa kughairi fuada,Nimefika ukingoni, sina kwenu la ziada,Tusitengue AQIDA, kwa nembo ya ujirani.

ABUU NYAMKOMOGI-MWANZA.

KRISMASI SI YAKO Kalamu nimeishika, kunena na Islamu, Noeli wanoiweka, mbele na kuiadhimu, Sawasawa kuwaweka, ni letu sote jukumu, Si yako haikuhusu,haifai kushiriki.

'Christ' laambatika, na 'mass' neno fahamu, Pamoja yafasirika, kwa lugha yetu adhimu, 'Jumuiko' pasi shaka, la ya 'kristo' kaumu, Si yako haikuhusu, haifai kushiriki.

Si sikukuu tajika, kwa wenye njema fahamu,Ila kwa walojivika, usungo waizuumu,Eti! ndio kazalika, 'mungu' mwana 'muadhamu', Si yako haikuhusu, haifai kushiriki.

'Mungu' mwana msifika, hudai wanaadamu, Yu eti! ni mzalika, wa aso mwana Rahimu,Mipaka wameivuka, kwa ghururi za rajimu,Si yako haikuhusu, haifai kushiriki.

Kwa madai kuropoka, dhidi yake ya haramu, Zi karibu kupasuka, mbingu zenye nujumu,Soma upate zinduka, suratul-Mariamu, Si yako haikuhusu, haifai kushiriki.

Lengo risala kufika, kwenu nyote Islamu,Mpate kuwaidhika, kwa kweli kuifahamu,Muepuke ushirika, wa misingi ya haramu,Si yako haikuhusu, haifai kushiriki.

Leo hii kwa hakika, chonde chonde Islamu, Msije kughururika, noeli kuiadhimu, Kalamu chini naweka, nimetimiza jukumu, Noeli haikuhusu, ni haramu kushiriki.

ABUU NYAMKOMOGI-MWANZA.

ALA ALA JIRANI !

Mhitimu Segerea aguswa na huruma ya MasheikhInatoka Uk. 3kutoka nje kwani huwapa m a h i t a j i k wa n i wa o (Masheikh) wanamahitaji muhimu karibia yote kutoka kwa ndugu zao na kwa Waislamu kupitia Kamati ya Maafa.

Mohammed, alisema ni wao (Masheikh) ndio waliorudisha matumaini y a k u r u d i u r a i a n i badaa ya maongezi yao n a k u wa e l e z a k u wa amelazimika kutumikia kifungo cha miezi nane baada ya kushindwa kulipa faini ya Shilingi 30,000/-.

A l i s e m a , p a m o j a na kumsihi kuwa na subra kwa tatizo hilo, wal imuunganisha na Kamat i ya Maafa ya Wa i s l a m u i n a y o t o a huduma hapo gerezani k w a W a i s l a m u n a kuwaeleza wamsaidie kutoka kwa kumlipia faini inayotakiwa.

“Baada ya kushindwa kulipa faini na kwenda jela sikuwa na njia ingine zaidi ya kusubiri kutumikia kifungo cha miezi minane gerezani, hapa Jijini sina ndugu, wazazi wangu na ndugu wapo Mkoani L i n d i , n a wa s h u k u r u sana Masheikh pamoja na Kamati .” Alisema Mohammed.

Mohammed, anaeleza sababu za yeye kujikuta anakwenda jela ni baada ya kukamatwa na Polisi wa Usalama barabarani, Julai 19, 2015, maeneo ya daraja la Salenda, Jijini Dar es Salaam, baada ya daladala yake kukodiwa kutoka Buguruni kwenda ufukweni (Beach) na kudaiwa kutumia barabara hiyo bila kuwa na kibali maalumu kutoka Sumatra.

Alisema, alipelekwa Polisi kisha Mahakamani baada ya kukaa mahabusu na bosi wake kutoweka bila kumsaidia na kujikuta hana msaada mwingine na hata kushindwa kulipa faini ya kiasi cha Shilingi 30,000/- na kulazimika kwenda jela miezi nane.

Hata hivyo alisema, kwa kuzingatia muongozo wa Masheikh aliwasiliana na Kamati ya Mafaa akiwa humo gerezani, ambapo Kamati hiyo ilifanya juhudi kwa kufuata taratibu za Magereza na hatimae kuweza kumtoa baada ya Kamati kulipa faini iliyotakiwa na Mahakama.

Mohahamed, alitoa wito kwa Waislamu kuiunga mkono Kamati ya Maafa ili wasife moyo katika kuwasaidia Waislamu, kwani wanafanya kazi

kubwa ya kuisaidia jamii iliyopo gerezani pamoja n a k u w a m i c h a n g o yao ni kidogo, lakini inawanusuru wanyonge k a m a y e y e wa l i o p o gerezani.

“Ukiangalia, msaada wanaoutoa hauegemei u p a n d e m m o j a w a Masheikh au Waislamu ambao ni wa mlengo wao, kila wanapo sikia au kuambiwa fu lan i anahitaji msaada, kweli w a n a m u h a n g a i k i a . ” Alisema Mohammed.

Hata hivyo kijana huyo kwa masikitiko alisema, baada ya kutoka gerezani na kwenda alipokuwa akiishi amekuta tayari chumba chake kimepangishwa mtu mwingine na mama mwenye nyumba na vifaa vyake vikihifadhiwa stoo.

Al i sema, kwa sasa anaishi kwa Katibu wa Kamat i ya Maafa ya Waislamu Ustadhi Ally Mbaruku, huku akijipanga kuanza maisha upya, akitafuta ajira mahala pengine.

Alisema, kazi yake ni dereva mwenye lesi daraja ‘C’ hivyo yupo t a ya r i k u f a n ya k a z i popote ili aweze kuanza kujikimu kimaisha baada ya kunasuliwa kutoka gerezani na Kamati ya Maafa.

Katika hatua nyingine, Mohammed alielezea ziara ya Mawaziri gerezani humo siku chache kabla hajatoka na kuongea na mahabusu pamoja na wafungwa ambapo walitoa malalamiko yao.

Aliwataja Mawaziri w a l i o f i k a G e r e z a n i ni Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Charles Kitwangi , pamoja na Wazir i wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison M wa k ye m b e , a m b a o walionana na wafungwa pamoja na Mahabusu na kupata maelezo ya maisha

yao kwa ujumla humo gerezani.

Akinukuu maelezo ya Mawaziri hao wakiwa g e r e z a n i , a l i s e m a w a l i w a e l e z a k u w a wamelazimika kuonana nao na kusikiliza matatizo yao ili kuyafanyia kazi na kuahidi kurudi baada ya mwezi mmoja kwa ajili ya mongezi zaidi.

Alisema, Mawaziri hao waliwaeleza wafungwa na mahabusu kuwa, wasiwe na hofu kwamba wao wamewafikia kwa ajili ya kazi na si kwa ajili ya maslahi ya watu wengine.

K w a u p a n d e w a mahabusu na wafungwa waliwaeleza viongozi h a o t a t i z o l a r a i a kubambikiwa kesi, jambo ambalo l inasababisha mrundikano mkubwa wa wafungwa na mahabusu unaosababishwa na baadhi ya Askari Polisi kutokuwa waadilifu.

“Lingine walielezwa ni juu ya kulazimishwa kukiri makosa baada ya kukamatwa na Polisi wakati wa mahojiano ama wakati wa kuandika maelezo huku ukipata adhabu kali na mateso.

Walifafanua kwamba hali hiyo imewaathiri watu wengi na hata wengine k u f i k i a k u a h a r i b i k a vizazi kufuatia mateso na adhabu wanazopata wakiwa mikononi mwa Jeshi la Polisi.” Alisema Mohammed.

A i d h a , w a l i e l e z a masikitiko yao katika suala la ukandamizwaji watuhumiwa, hususani k a t i k a k e s i a m b a z o wanashtakiwa na Jamhuri (Serikali) kwa kukaa muda mrefu kwa kigezo cha ushahidi kutokamilika sambamba na kunyimwa dhamana kwa makosa yenye haki ya kupata dhamana.

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe.

Page 15: ANNUUR 1210A

15 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 1- 7, 2016Makala

kiongozi wao Mkuu lazima awe Muangilikana, Saudi Arabia dini yao rasmi ni Uislamu lakini si Uislamu tu, ila ni Uislamu-suni na Mfalme lazima awe Suni. Tanzania si nchi ya namna hiyo. Ina utaratibu wa tofauti ambao haufangamani na dini yoyote.

Katika hili mantiki yake ni kwamba kuna tofauti kati ya Jakaya Mrisho Kikwete na urais wake Tanzania. Maana yake ni kwamba Kikwete alikuwa ni Muislamu lakini urais wa Tanzania hauna dini yaani kiti cha Urais hakina dini. Katika katiba Ibara ya 19 Naomba Kwa idhini ya wahusika niinukuu.

UHURU WA MTU KUAMINI DINI ATAKAYO

19(1) Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa Mawazo, imani na Uchaguzi katika mambo ya dini pamoja na uhuru wa mtu kubadilisha dini au imani yake.

(2) Bila ya kuathiri sheria zinazo husika za Jamhuri ya Muungano kazi ya kutangaza d in i ,kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu binafsi,na shughuli za uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za Mamlaka ya Nchi.

(3) Kila palipotajwa neno dini katika ibara hii ifahamike kwamba Maana yake ni pamoja na madhehebu y a d i n i n a m e n e n o mengineyo yanayofanana au kuambatana na neno hilo nayo yatatafsiriwa kwa maana hiyo.

Katika ibara hii ya 19(1)(2)(3) kuna maneno ambayo tunapaswa kuyazingatia kimantiki ili kukidhi haja ya takwa au hitajio la sheria hii . Katika ibara ndogo ya (1) tunaona kuna neno la Mazingatio ambalo ni

uhuru. Tafsiri ya uhuru ni hali ya kutoingilia, maana yake ni kwamba hastahili m t u k u m w i n g i l i a m t u mwingine katika suala la Imani, mawazo na maamuzi yake juu ya imani hiyo ili mradi tu anakidhi matakwa ya kikatiba. Cha kufanya ni kumshauri kwa hoja juu ya maamuzi, mawazo na imani juu ya hilo.

Katika ibara ndogo ya (2) tunaona pia kuna suala la kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini ni jambo huru na hiari. Neno uhuru tumeshaona ni hali ya kutoingiliwa katika maamuzi lakini katika ibara hii kuna neno lingine jipya ambalo ni hiari. Hiari maana yake ni hali ya uchaguzi binafsi wa mambo yaani ukiamua kufanya hakuna mtu wa kukuzuia kufanya lakini pia ukiamua kutokufanya hakuna mtu wa kukulazimisha kufanya. Ibara hiyo pia inaendelea kusema kuwa shughuli za uendeshaji wa jumuiya za dini itakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi. Hii maana yake ni kwamba serikali haina mkono katika shughuli za uendeshaji wa jumuiya za dini yaani katika shughuli zote zinazohitaji kuendeshwa na serikali shughuli za kidini si mojawapo. Kazi ya serikali katika hili ni kulinda haki hii ya raia wa Tanzania kupitia katiba isinyang’anywe na mtu yeyote kwa misingi ya namna yoyote iwe ni tofauti za kiimani au vyeo au mali.

Kat ika nch i ye tu ya Tanzania raia wake wanazo dini kuu mbil i ambazo ni Uislamu na Ukristo. Waislamu wanaongozwa na kitabu chao ambacho ni Quran na hadithi za Mtume Muhamad (S.A.W) wakati Wakristo wanatumia

MWA K A 1 9 7 0 Rais wa kwanza wa Jamuhuri ya Muungano wa

Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitoa hotuba kwa Maaskofu M j i n i Ta b o r a k a t i k a Ukumbi wa Mihayo, jina ambalo lilotokana na jina la aliyekuwa Askofu wa Jimbo la Tabora Maiko Mihayo. Katika Mkutano huo Mwalimu Nyerere kwa mara ya kwanza aliwaambia Maaskofu maneno ambayo t a n g u s i k u h i y o h a d i sasa ninaandika makala h i i , ya m e k u wa n d i y o wimbo wa Watanzania wote. Najua unahamu ya kutaka kuyajua maneno hayo ambayo Nyerere aliwaambia Watanzania kupitia Mkutano wake na Maaskofu, maneno hayo ni haya hapa: “TANZANIA HAINA DINI.”

Baada ya maneno hayo Wakatoliki wakaandika kitabu walichokipa jina la Tanzania na dini. Sitaki kuzungumza kilichoandikwa ndani ya kitabu kile lakini naomba nijikite kwenye kauli ya J.K Nyerere na Maneno haya nataka yawe ndiyo kiini hasa cha lengo la Makala hii. Maneno haya ya Mwalimu Nyerere yamezoeleka sana kwenye Midomo ya Watanzania wa aina zote Wasomi na wasio Wasomi. Lakini pengine wengi huwa hawajui maana ya maneno haya kimantiki. Wapo wanaoyabeba kama yalivyo na kuyatumia kama yalivyo ama kwa ujinga au kwa kujua lakini kwa ajenda zao za siri. Lakini wapo wanaoyabeba kimantiki na kuyatumia kimantiki. Kundi la wale wanaoyabeba kama yalivyo na kuyatumia kama yalivyo kwa ujinga l ikieleweshwa l i taingia katika kundi la pil, kundi ambalo linayabeba kimantiki na kuyatumia kimantik na wengine watabaki katika kundi lile linaloyabeba na kuyatumia kama yaliyo kwa kujua lakini kwa ajenda zao maalumu. Kundi hili ndilo ninalotaka kulizungumzia kwani ni kundi hatari ambalo kwa namna yoyote ile, lazima mwisho wa kazi yao hiyo utakuja kuleta machafuko ambayo yataligharimu taifa.

Mwl. Nyerere aliposema Nchi haina dini alifafanua kwamba utawala Uongozi na Uendeshaj i wa nchi hautokani na Miongozo ya dini. Zipo nchi zina dini Rasmi Mfano dini rasmi ya Uingereza ni Anglicanism na

Jicho mbadala

Nyaraka za serikali katika ofisi za serikali, zinafuta Katiba?na kuongozwa na kitabu kinachoitwa Biblia. Misingi na taratibu za dini hizi mbili zinatofautiana ingawa yapo baadhi ya mambo ambayo yanafanana Mfano wa mambo yanayofanana ni kama hili, Waislamu na Wakristo wanakubaliana kuwa Musa, Daudi na Wengine ni Mitume wa Mungu ingawa Wakristo w a k i f i k a k w a Ye s u (Issa) wanatofautiana na Waislamu juu ya Yesu (Issa) ni nani, na miongoni mwa mambo ambayo Waislamu na Wakristo hutofautiana ni swala. Wakristo husali mara moja kwa wiki kwa mujibu wa muongozo wao ambapo siku maalumu kwao huwa ni Jumamosi na wengine Jumapili tofauti na Waislamu ambao huswali kila siku mara tano ambapo siku ya Ijumaa huwa na Swala Maalum. Pamoja na tofauti zote hizo zilizopo, katiba ya nchi ibara ya 19 inaondoa migongano ambayo ingeweza kujitokeza baina ya pande hizi mbili, kwani inatoa uhuru wa kila upande kufanya lile ambalo wao wanaliamini ili mradi tu hawavunji sheria za nchi.

Hata hivyo, binadamu tunatofautiana utashi na upenzi katika dini. Binadamu anaweza kuipenda dini yake sana hata akafikia mahali kutamani binadamu wengine wa tofauti na dini yake wasifanye ibada tofauti na dini yake. Yaani M k r i s t o a n g e t a m a n i sana kuwaona Waislamu wanaswali kama yeye mara moja kwa wiki na pengine ni Jumamosi au Jumapili. Muumini wa namna hii kuna wakati hufikia hatua ya kuzungumza na nafsi yake kwamba ningekuwa na uwezo ningeamuru watu wote waswali siku moja tu. Lakini pia Mkristo a n a p o t a m a n i h i v y o , muumini wa Kiislamu naye angetamani kuona watu wote wanakuwa Waislamu. Watu wa aina hii huwa wana ugomvi wa kisaikolojia hata kabla hawajakutana na pengine mmojawapo akipata nafasi ya namna ambayo atakuwa juu ya mwingine hutumia nafasi ile kuwakandamiza watu wa upande wa pili kufuata dini yake hata kama sikuihama kabisa dini yao.

M i k a t a b a y o t e y a kimataifa inasema wazi kuwa muhimili wa hili ni kuvumiliana katika imani ya a n i k a m a a m b a v y o Muislamu anavyomvumulia Mkristo kwa kuona kuwa

a n a k o s e a k u s a l i m a r a moja kwa wiki ndivyo ambavyo Mkristo anapaswa kumvumil ia Muis lamu anaposwali mara tano kwa siku na ni kila siku. isitokee upande mmoja unataka kuvumiliwa ila wenyewe haupo tayari kuwavumilia wenzake

Pamoja na hayo yote niliyosema, katika nchi yetu bado lipo tatizo la kiufundi la kikatiba ingawa serikali imejitahidi kuliwekea viraka ili kulipoza. Tatizo lenyewe ni kwamba siku za ibada kwa waumini wa Kikristo ni siku ambazo karibu nchi nyingi duniani ofisi za umma hufungwa ili waumini wa dini ya Kikristo wafanye ibada. Kwa lugha nyingine, siku hizi zinatambulika kimantiki kama siku za ibada na hivyo waumini hawapaswi kufanya kazi ila ni nafasi ya kufanya ibada. Lakini dola hiyo hiyo iliyosema haina dini ila watu wake wana dini, haitoi haki hii ya kupumzika na kufanya ibada kwa Waislamu siku ya Ijumaa kama wavyopumzika waumini wanaoabudu siku ya Jumamosi na Jumapili.

Hata hivyo, baada ya Mgogoro wa muda mrefu baina ya Waislamu na Serikali juu ya haki hiyo Serikali ilitoa waraka namba ED/OK/C.2/4/77 ambao u l i w a l e n g a Wa i s l a m u walioko tasisi ya elimu (shule) juu ya haki ya swala ya Ijumaa pamoja na suala la uvaaji wa Hijab. Waraka huu unaelekeza na kuagiza wanafunzi wa K i i s l a m u kupewa fursa ya kwenda Msikitini muda wa kati ya saa 6 na saa8. Jambo hili ni jambo jema kwani waraka huu unajaribu kukidhi mahitaji ya katiba ibara ya 19(2) ambayo tayari nimeshaelezea awali. Lakini ni kumbushe swali langu ambalo ndiyo kichwa cha makala hii, je nyaraka za serikali kwenye ofisi za serikali zinafuta katiba?

Sasa naomba ufuatane nami nikujuze kisa kimoja kilichotokea katika Mkoa wa Kilimanjaro Wilaya ya Siha kata ya Ndumeti katika shule ya Msingi Roseline. Ni kisa ambacho kimebeba swali ambalo ndilo kichwa cha makala yangu. Shule ya Msingi Roseline kama nilivyoeleza kwamba ipo Mkoa wa Kilimanjaro Wilaya ya Siha kata ya Ndumeti Kijiji cha Roseline Kitongoji cha Roseline B. Ni shule yenye jumla ya Wanafunzi zaidi ya 620. Ina walimu 10 tu na

HAYATI Mwalimu Nyerere DKT. Jakaya Kikwete.

Inaendelea Uk. 16

Page 16: ANNUUR 1210A

16 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 1- 7, 2016Makala

ina vyumba vya madarasa vinavyotumika 6 tu kila darasa moja lina wastani wa wanafunzi zaidi ya 100. Shule hii ina walimu wa Kiislamu 3 na Wakristo 7.

Kwa mujibu wa ratiba ya shule, swala zote za Waislamu ukiondoa swala ya dhuhuri zinaswaliwa nyumbani au muda ambao wanafunzi wametawanyika. Na kwa mujibu wa ratiba ya shule, utaona swala hii inaangukia wakati wa mapumziko na chakula saa 6:30 – 8:00. Kama haki yao ya kikatiba ibara ya 19(2) lakini pia ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa amri ya Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa imani yao, aidha ikiwa ni sehemu ya wajibu wao kama walimu wa kuwalea wanafunzi kiakili kimwili na kiroho, Wal imu na Wanafunzi Waislamu hutumia muda wa dakika kati ya 7 na 15 kuswali swala yao moja yaani swala ya dhuhuri kuanzia saa7:00 7:7/14. Lakini pia kwa kujua wajibu wake kama mwalimu na pia kwa kuona umuhimu wa jambo hili katika kudumisha nidhamu shuleni, mwalimu mmoja wa Kikristo ambaye ndiyo kwanza alikuwa

anaanza kazi, nae aliamua kuingia na wanafunza wa madhehebu ya Kikristo darasani kufanya maombi kwa muda uleule uliotumiwa na Waislamu kuswali. Hata h i v y o m wa l i m u h u y u kijana hakupata ushirikiano kutoka kwa walimu Wakristo wenzake akakata tamaa na kusitisha zoezi lile.

Waislamu wameendelea kufanya ibada yao hadi alipokuja mwalimu mkuu mwingine January 2015 a m b a ye k wa u s h a b i k i na upenzi wa dini yake uliopitiliza na akiwa miongoni mwa yale makundi mawili niliyokwisha kuyazungumza yaani wanaobeba na kuitumia kauli ya Mwalimu Nyerere kama ilivyo kwa ujinga au kwa kujua ila wanafanya makusudi kwa msukumo wa kidini, aliamua kuwapiga marufuki wanafunzi wa Kiislamu kuswali muda ule wa mapumziko. Baada ya kuulizwa na walimu wa Kiislamu sababu za k u z u i a i b a d a , s a b a b u zake zinachekesha ngoja nimnukuu: Kwanza natumia mamlaka niliyopewa, pili kwenye ratiba hakuna mahali palipoandikwa kuswali. Hizi ndiyo sababu zake mbili alizotoa.

Lakini katika kuiangalia sababu hi i ya kwanza, utagundua kile nilichokisema

awali kwamba mtu anaweza kutumia madaraka yake kuwalazimisha watu waishi m a i s h a ya n a y o e n d a n a n a m i s i m a m o ya d i n i yake ingawa watu wale wataendelea kubaki katika dini yao. Hawa pia ndio wale ambao ama waliibeba na kutumia kauli ya Mwl. Nyerere kama ilivyo kwa ujuha au kwa kujua lakini anafanya h ivyo kwa msukumo wa upenzi wa dini yake.

Ukiitazama sababu ya pili nayo inafurahisha k w a n i w a n a f u n z i wakitokea wakati wa mapumziko kila mmoja hufanya lake ilimradi tu halina madhara kwa wengine na kwake pia. Wapo wanafunzi ambao huamua kwenda uwanjani kucheza mpira , kuruka Kamba, kucheza rede, mdako, na wengine hubaki darasani wakijisomea na wengine hulala. Kama ilivyo swala la kusali lisivyotajwa kwenye ratiba ya shule, na haya nayo hayajatajwa kwenye ratiba hiyo. Lakini jiulize swali, kwanini haya hayazuiliwi ila swala tu?-Itaendelea.

(Makala hii imeandikwa na Ismail Musa Mche-0755 224 921, [email protected])

Inatoka Uk. 15

Nyaraka za serikali katika ofisi za serikali, zinafuta Katiba?

Lengo letu ni moja, kwa nini tunagombana?Inatoka Uk. 6kwa FOOD AND DRUG ADMINISTRATION (FDA), ambayo ni mamlaka ya chakula na dawa ya Marekani, kuyatoza tozo makampuni ya dawa yaliyokuwa yamewasilisha maombi kwa taasisi hiyo kwa ajili ya mapitio na usajli wa dawa zao, ili kuharakisha zoezi hilo! Sheria hii inataka mapitio na usajili sasa vifanyike ndani ya miezi 12, tofauti na ilivyokuwa mwanzo ambapo ilihitajika miezi 30!

Wachambuzi wanasema tangu sheria hii ianze kutumika kumekuwa na ongezeko kubwa la madhara kwa dawa zinazopitishwa na taasisi hiyo. Takwimu zinaonyesha kuwa katika kila miezi 10 iliyopunguzwa katika muda wa mapitio ya maombi ya dawa, madhara ya dawa kwa watumiaji yameongezeka kwa 18.1%. Aidha kumekuwa

na ongezeko la 10.9% la watu waliolazwa hospitali kutokana na madhara yaliyosababishwa na matumizi ya dawa hizo, na ongezeko la 7.2% la vifo kwa watumiaji wa dawa hizo!

Katika kitabu chake, Deadly Medicines and Organized Crime: How Big Pharma Has Corrupted Healthcare, Peter Gøtzsche, kiongozi wa taasisi ya Nordic Cochrane Centre (ambayo ni taasisi huru maarufu ya kufanya mapitio ya matokeo ya tafiti mbalimbali za kisayansi) anafananisha ufisadi unaofanywa na makamupuni yanayozalisha dawa za kifamasia na uhalifu unaoendeshwa na magenge ya kihalifu ya kimafia.

Katika kitabu chake Peter anasema:

"Ukiondoa ukweli kuwa makampuni yanayozalisha dawa za kifamasia yanauza

madawa ya hatari zaidi ukilinganisha na watumiaji wanavyotangaziwa, makampuni haya pia yanahusika kwa kiasi kikubwa na kubomoa misingi ya sayansi ya tiba, kwa kuwa ndiyo wafadhili wakubwa wa tafiti zinazohusika. Kuna ushahidi mwingi kuwa matokeo ya tafiti mbalimbali yamekuwa yakiathiriwa na matakwa ya wale wanaofadhili”

Kwa mujibu wa takwimu kutoka katika taasisi ya Thomson Reuters, idadi ya matokeo ya tafiti za kisayansi yaliyoondolewa kwenye matumizi ya umma baada ya kuchapishwa imekuwa ikiongezeka kwa zaidi ya mara 15 tangu mwaka 2001. Mapitio ya tafiti hizi yameonyesha kuwa zaidi ya 75% yaliondolewa kwenye matumizi ya umma kwa sababu yalikuwa na taarifa za uongo, waandishi hawakuzingatia maadili,

na au waandishi waliiba na kuweka taarifa za kitafiti za watu wengine kwenye machapisho hayo, kama zao wenyewe!

Ukweli ni kwamba ukilinganisha usalama wa dawa za kifamasia na dawa za mitishamba au virutubisho (nutritional supplements), kwa mujibu wa takwimu za kisayansi zilizopo, taasisi kama TFDA zinatakiwa kuomba radhi kwa upotoshaji mkubwa wanaoufanya kwa umma. Kwa mfano, kwa mujibu wa taasisi ya International Campaign Group ya Uingereza, ambayo ni sehemu ya taasisi ya Natural Health International (ANH-Intl), dawa za kifamasia zina uwezekano mara 62,000 zaidi wa kumuua mtumiaji ukilinganisha na virutubisho, na mara 7,750 zaidi ukilinganisha na dawa za miti shamba.

Aidha takwimu hizi pia zimebainisha kuwa ukilinganisha na matumizi ya virutubisho, kuna uwezekano wa zaidi ya mara 900 kwa mtu kufa kutokana na kula chakula kibaya (food poisoning); na uwezekano wa zaidi ya mara 300,000 kwa mtu kufa kutokana na makosa ya kidaktari yanayozuilika yanayotokea kwa wagonjwa wanaolazwa katika hospitali za Uingereza.

Takwimu hizi zilizokusanywa kutoka vyanzo vya kiserikali vya Uingereza na Jumuia ya Ulaya zinaonyesha kuwa idadi ya vifo vinavyotokana na matumizi ya virutubisho na miti shamba ni chini ya mtu 1 katika kila watu milioni 10! Bila ya shaka hali hii inaonyesha wazi kuwa virutubisho na miti shamba ni miongoni mwa vitu vyenye usalama wa hali ya juu sana kwa watumiaji, pale tunapolinganisha na matumizi ya dawa za kifamasia!

Sasa kama hali iko hivi, ni kwa nini mamlaka za nchi zihangaike kuwabana na kuwadhibiti watoa huduma inayohusisha virutubisho na miti shamba badala ya kuwaunga mkono? Sababu zinaweza kuwa nyingi lakini kubwa mbili ni ushindani wa kibiashara na kibri cha kitaaluma. Unapokuwa kwenye ulimwengu wa biashara, kuna kanuni inayokutaka kufuatilia kwa karibu washindani wako wa

kibiashara. Tiba mbadala na tiba asilia hivi sasa wamekuwa ni washindani wakubwa wa kibiashara wa tiba za Kimagharibi ambazo zinajumuisha madaktari wa kawaida, hospitali za kawaida, watengenezaji wa vifaa tiba, na makampuni ya kutengeneza dawa za kifamasia. Kwa kuwa mamlaka nyingi za kinchi ziko upande wa tiba za Kimagharibi (kama sehemu ya urithi wa kikoloni), ni jambo la kutarajiwa kuwa zitachangia nguvu upande huo katika vita hii ya kibiashara.

Tatizo la kiburi cha kitaaluma linatokana na mfumo ambao umeendekeza sana elimu ya darasani na vyeti. Huu ni mfumo ambao unawaona watu wote ambao hawakupitia darasani na kutunukiwa vyeti kuwa hawajui na wanapojaribu kufanya jambo lolote linalohusisha taaluma, basi ni matapeli. Huu ni mfumo ambao umejisahaulisha kuwa milango ya fahamu ni mingi, na huo wa darasani ni mmoja tu katika milango hiyo.

Matabibu wengi wa tiba mbadala ni watu wenye elimu kubwa juu ya tiba mbadala, japokuwa hawakusoma rasmi darasani na kutunukiwa vyeti. Ni watu ambao wametumia vizuri milango yao ya fahamu kujua mambo mengi sana yanayohusu siha na tiba. Kwa kuwa wamejikita katika uwanja ambao ni mbadala, mara nyingi wamejikuta katika mazingira ya kutatua matatizo ya kiafya ya watu ambao wamekosa ufumbuzi huko katika mfumo wa tiba wa Kimagharibi. Kutokana na kuwa katika nafasi ya kipekee ya kutatua shida zilizoshindikana kwingine, wamejikuta pia wakipata mafanikio ya harakaharaka ya kiuchumi. Japo haisemwi, lakini haya mafanikio ya kiuchumi yamekuwa ni chanzo kikubwa cha chuki toka kwa wadau wengine wa sekta ya afya, hususan wale wenye shahada zao walizozipata baada ya kutumikia miaka mingi ndani ya mfumo wa elimu ya darasani.

Hata hivyo hakuna haja ya kugombana na kufanyiana uadui, ikizingatiwa kuwa pande zote mbili malengo yao ni mamoja, yaani kumfanya mwanadamu aishi maisha ambayo yuko mbali na magonjwa.

(Kwa mawasiliano zaidi piga namba 0754281131/0655281131)

Page 17: ANNUUR 1210A

17 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 1- 7, 2016

MAKALA/TANGAZO

Inawatanganzia Waislam wote kuwa imeandaa safari ya Hijja mwaka 2016 sawa na mwaka 1437 Hijria kwa Dola US$ 3,555

Kutakuwa na punguzo la asilimia 16% kuanzia muda huu mpaka Feb 29/2016. Itakuwa Dola $2986 tu.

Kuanzia mwezi Machi 01-2016 mpaka Juni 12-2016 kutakuwa na punguzo la asilimia 6% sawa na Dola $3,341 tu.

MAMBO YATAKAYOGHARAMIWA1. Semina za Hija, 2. Huduma za afya na kuchinja 3.Airport Charge na ticket

za Ndege 4.Nyumba Makkah na Madina 5.Irham na Kuchinja kwa ajili ya Tama-tuu 6.Chakula wakati wote 7.Usafiri na ziara Makkah na Madina 8.Mahema Mina na Arafa.UMRA MWEZI WA RAMADHANI ITAKUWA NI DOLA US $1995

Fomu zinapatikana sehemu zifuatazo:-1.Ofisi ya Ahlul Daawa Dar es Salaam Mtaa wa Dosi na Mkadini nyumba Namba 26 mkabala na Showroom ya magari Tell. 0713 730 444, 0773 804 101 ,0785 930 444 au 0773 930 444.2. Ofisi ya Ahlu Daawa Zanzibar Rahaleo Tel: 0777 484 982, 0777 413 987.3. Abubakr Maulana wa Markaz Kiwalani Dar es Salaam, Tel: 0784 453 8384. Abdallah Salehe Mazrui (Hoko) Dar es Salaam, Tel: 0715 724 444 5. Abdallah Hafidh Mazrui, Wete Pemba Tel: 0777 482 6656. Mohammed Hafidh Mazrui Mkoani Pemba 0777 456 9117. Sheikh Daud Khamis Shekha Tel: 0777 679 6928. Maalim Seif Humoud Hamed (Kijichi Zanzibar) 0777 417 736WAHI KULIPIA1. Ofisi ya Ahlul Daawa Dar es salaam Tel: 0713 730444, 0773

804101,0785 930444.2. Ofisi ya Ahlul Daawa Zanzibar Rahaleo Tel: 0777 484982, 0777 413

987.Maalim Seif Humoud Hamed (Kijichi Zanzibar) Tel: 0777 417 736

TANBIH(a) Atakaemaliza taratibu zote mwanzo ndie atakayeshughulikiwa

mwanzo(b) Ili uwemo katika fungu la kwanza unatakiwa umalize taratibu

zote kabla ya punguzo (c) Kumbuka kikundi cha Ahlul Daawa kwa bei nafuu kuliko wote

na huduma kuliko wengi.Wabillah Tawfiq

Ahlu Daawa Hajj and Travel Agency

OKTOBA 14, 2015 miladia sawa na Muharam 1, Waislamu waliadhimisha mwaka mpya wa Kiislamu ambao ni 1437. Katika kalenda ya Kiislamu, sherehe za kuadhimisha mwaka mpya wa Kiislamu zilifanyika sambamba na kumbukumbu ya kuhama kwa Mtume Muhammad (s.a.w) kutoka Mji wa Makka kwenda Madina. Kalenda hii inafuata mwezi mwandamo, kwa maana mwezi huanza kwa kuandama mwezi na mwezi huisha kabla ya kuandama mwezi mpya.

Kat ika ka lenda ya Kiislamu, siku huanza baada ya kupinduka jua, (magharibi) kadhalika kuisha kabla ya kuingia Magharibi. Kwa kawaida k a t i k a m a a d h i m i s h o ya mwak a mp ya wa Ki i s lamu, hufanyika ibada mbalimbali ikiwa ni pamoja na Masheikh, Maimam na Maulamaa kutoa elimu, hasa historia ya Uislamu, matukio yaliyofanyika kwa kipindi hicho likiwemo na tukio kubwa la Hijra ya Mtume kutoka Makka kwenda Madina, ambayo ndio chanzo cha kuasisiwa mwaka mpya wa Kiislamu n a k u s o m wa Q u r’a n tukufu.

W a i s l a m u t a y a r i walishasherehekea mwaka wao mpya tangu Oktoba 14, 2015 Miladia, na Mazazi ya Mtume Muhammad (saw), tena kwa stara, utulivu, bila fujo wala laghawi na starehe za kufuru. Hakuna athari mbaya za kutokea ajali na majeruhi, kuchoma moto matairi, ajali. Mwaka wao mpya ulienda salama salmin.

Hata hivyo, leo Januari 1, 2016 Miladia, sawa na tarehe ya mwaka wa Kiislamu Rabbiul Awwal 1437, kulikuwa na sherehe nyingine za mwaka mpya zilizoanza jana saa 6:00 usiku, mwaka ambao unaojulikana kwa asili yake kuwa ni mwaka wa Gregory. Kalenda ya Gregory inaanzia kwa Papa wa Kikatoliki Gregory XIII, ambaye aliunda mpango wa kalenda mpya katika Kanisa la Mt. Petro huko Vatikani. Mwaka mpya unaosherehekewa sasa ni matokeo ya Kalenda ya Gregory, kalenda ambayo i m e k u wa i k i t u m i wa zaidi kimataifa hadi leo. Jina limetokana na Papa Gregory XIII, aliyeamua

Mwaka mpya wa Papa GregoryMbona unasherehekewa Kirumi

Na Shaban Rajab

kutumia kalenda hiyo tangu 15 Februari 1582, b a d a l a y a K a l e n d a i l iyokuwa iki julikana kuwa ni ya Julius Caesar.

Kalenda ya Gregoy inahesabu mwaka wa siku 365. Mwaka una miezi 12. Miaka inahesabiwa tangu kuzaliwa kwake ‘Kristo’ kufuatana na makadirio ya Dionysius Exiguus. Siku hizi ni kawaida kuanzisha mwaka tarehe Mosi Januari, lakini hii ni mapatano ya baadaye si utaratibu wa kalenda ya Gregory yenyewe. Wachunguzi wanasema kuwa katika mwaka unaosherehekewa, utaratibu wa wiki (au juma) au siku saba umeendelea kutokuwa na uhusiano na utaratibu wa mwaka.

Kalenda ya Gregory kufuata mzunguko wa dunia kwenye mzingo wake, ambao tumeambiwa kuwa ni siku 366. Kile k i l i c h o e l e z wa k u wa sababu za matengenezo ya kalenda ya Papa Gregory ni kutokana na madai ya kuwepo kasoro za Kalenda ya Julius. Papa Gregori XIII kama kiongozi wa kiroho wa dunia ya kikatoliki (sehemu kubwa ya Ulaya) alitaka kusahihisha kasoro z i l izoonekana kat ika kalenda ya awali.

Inaelezwa kwamba tangu zama za Waroma wa Kale, hesabu ya wakati ilifuata kalenda ya Julius iliyoanzishwa na Julius Caesar mwaka 46 KK. Ilidaiwa kuwa Kalenda hii ilikuwa na tatizo la urefu wa mwaka wake, kwamba ulipita muda kamili ya mwaka wa jua kwa dakika 11 na sekunde 14 , yaani mwaka wa kalenda hii ulikuwa mrefu kwa muda wa dakika 11 kila mwaka. Tatizo kwa maisha ya Kanisa lilikuwa kwamba tarehe ya Pasaka iliendelea kusogea nyuma polepole na haikufuata tena utaratibu uliowekwa na mtaguso wa Nicea.

Azimio hili la mwaka 325 BK lilisema kwamba Pasaka itasheherekewa J u m a p i l i ya k wa n z a baada ya mwezi mpevu wa kwanza baada ya 21 Machi (yaani tarehe ya siku sare katika machipuo, ambayo ni siku ya usawa wa mchana na usiku hivyo mwanzo wa majira ya

kuchipua katika kaskazini ya dunia). Wakati wa Papa Gregori XIII tarehe ya siku sare ilikuwa imewahi siku 10 na kufika tayari 11 Machi! Kwa sababu hiyo mtaguso wa Trento wa Kanisa Katoliki mwaka 1563 uliamua kusahihisha kalenda.

Inaelezwa kuwa ni Papa Gregori XIII aliyeita wataalamu waliofanya makadirio mapya. Alifuata mapendekezo ya mtabibu wa Kitaliano Aloisius Lilius pamoja na Padre na mwanahisabati Mjerumani Christopher Clavius.

Pe n d e k e z o l i n g i n e l i l i k u w a n a m n a y a k u s a h i h i s h a k o s a l i l i loingia tangu siku z a k a l e . Wa t a a l a m u walipendekeza kufuta siku 10 ambazo tarehe

ya siku sare machipuo ilikuwa imesogea mbele. Baada ya marekebisho hayo ya Papa Gregory, awali ni nchi chache tu zilizofuata kalenda mpya. Nje ya Italia, zilifuata Hispania na Ureno Oktoba 1582, Ufaransa mwisho wa 1582. Kwa ujumla nchi za Kikatoliki ziliwahi kutumia kalenda mpya lakini nchi za Kiprotestant zilichelewa kukubali, zilizo nyingi zilipokea kalenda mpya kuanzia mwaka 1700. Kwa karne nyingi kalenda hii ilikuwa suala la Ulaya ya Magharibi tu, lakini baadae lilienea kupitia ukoloni.

Nchi za Kiorthodoksi za Ulaya ya Mashariki zilikataa kalenda mpya hadi karne ya 20. Muda uliopokelewa Kalenda

ya Gregory katika nchi za Ulaya: Hispania na Ureno 1582, Uholanzi ya K i k a t o l i k i 1 5 8 2 , Ufaransa 1582 Venesia (Italia) 1582, Ujerumani wa Kikatoliki tangu 1583, Uholanzi wa Kiprotestanti 1 7 0 0 , U j e r u m a n i wa Kiprotestanti tangu 1700, Denmark 1700, Uingereza pamoja na koloni zake na Marekani 1752, Sweden 1753, Urusi 1918, Ugiriki 1924, Uturuki 1926.

Hata hivyo, ukiacha kalenda ya Ki is lamu pamoja na sehemu kubwa ya dunia kufuata kalenda ya Gregory kusherehekea mwaka mpya, baadhi ya nchi zimeendelea kuishi na kuheshimu tamaduni zake mbalimbali za majira na kusherehekea mwaka wao, pamoja na kwamba pia mwaka wa Gregory u n a t u m i k a . U a j e m i , Afghanistan, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan, Azerbaijan, Turkmenistan na Kashmir husheherekea

Inaendelea Uk. 18

Page 18: ANNUUR 1210A

18 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 1- 7, 2016

MAKALA/TANGAZO

Mwaka mpya wa Papa GregoryInatoka Uk. 17mwaka mpya kufuatana na kalenda ya Kiajemi k w e n y e s i k u k u u ya N o u r u z , a m b a y o n i siku sare ya bubujiko inayotokea kati ya tarehe 20 - 21 Machi kwenye kalenda ya Gregori lakini kwao mwezi na mwaka mpya unaanza.

Wachina na Wavietnam husheherekea mwaka mpya wakati wa mwezi mwandamo wa pili baada ya solistasi ya majira baridi na hii inakuwa kati ya Januari 21 na Februari 21.

Nchi ya I s rae l i na Wayahudi husheherekea mwaka mpya kufuatana na kalenda ya Kiyahudi kwa jina la Rosh hashana, ambayo ni siku inayotokea kati ya Septemba na nusu ya kwanza ya Oktoba.

Imezoeleka kuona watu wakiharakisha shughuli zao na kuzisitisha au k u m a l i z a m a p e m a majira ya alasir ya siku ya mkesha wa mwaka mpya wa Gregory, ili kuwahi kujiandaa na mkesha. Hata inapofika majira ya saa 5:30 usiku, huwa inashuhudiwa watu wengi huanza shamra shamra, huku yakianza kuo9nekana madhara kwa baadhi ya watu kuchomwa visu au kupigwa risasi, kunashuhudiwa majeruhi na vifo vinavyotokana na ajali za magari, uzinzi n a m a t a t i z o l u k u k i yanayosababishwa na ulevi.

Mara nyingi siku ya kwanza ya mwaka mpya inaonekana kama ni siku mbaya sana katika mataifa mbalimbali kwa sababu ya sherehe zilizopindukia. S h e r e h e z a M w a k a Mpya zimechukuliwa kama ni sherehe za watu wanaopenda raha na ni pambano j ingine kati ya wanadamu na ulevi, starehe zilizopindukia, na maaswi.

Ni kweli kwamba si watu wote wanaosherehekea Mwaka Mpya na kufanya m a m b o m a c h a f u , kunywa kupindukia au kwa kufanya matendo ya kipumbavu na jeuri. Lakini wengi siku hizi husherehekea Mwaka Mpya na kufanya machafu kupita kiasi, jambo ambalo limefanywa kuwa ni la kawaida.

Hata hivyo, Wakristo wanapaswa kuchunguza chanzo na maana ya sherehe hiyo maarufu. Je, mafundisho ya Biblia ya n a z u n g u m z a n i n i kifanyike katika sherehe

za Mwaka Mpya?Katika zama za kale,

i n a e l e z w a k w a m b a s h e r e h e z a M w a k a Mpya zimekuwapo kwa muda mrefu. Maandishi ya kale yaliyochongwa yameonyesha kwamba Wababiloni waliadhimisha sherehe hizo katika milenia ya tatu K.W.K. Walifanya sherehe kuu ya mwaka mpya katikati ya mwezi wa Machi.

Kitabu cha The World B o o k E n c y c l o p e d i a kinaeleza kuwa “wakati huo mungu Marduki aliamua mambo ya mwaka uliofuata.”

Sherehe za mwaka mpya za Wababiloni ziliendelea kwa siku 11 na zilikuwa na maandamano, kutolewa sadaka na ibada ya kuomba mvua na mazao.

M w a k a m p y a w a Waroma ulianza pia mwezi wa Machi katika kipindi fulani. Lakini mnamo mwaka wa 46 K.W.K, Julus Caeser (Kaisari) aliamua uanze Januari mosi. Hapo awali Januari mosi ilikuwa siku ya Janus, Mungu wa mianzo na mwaka wa 46 siku hiyo ikawa pia siku ya kwanza ya mwaka wa Waroma.

T a r e h e h i y o ilibadilika lakini sherehe haikubadilika. Kitabu cha marejeo cha Cyclopedia cha McClintock na Strong k i n a s e m a k w a m b a katika Januari mosi watu “ wa l i j i i n g i z a k a t i k a sherehe zenye fujo na ulevi, na ushirikina mbalimbali wa kipagani.”

Bib l ia inawashaur i Wakristo wajiendeshe kwa adabu, si katika sherehe zenye makelele ya ulevi. (Waroma 13:12-14; Wagalatia 5:19-21; 1 Petro 4:3).

W a p o W a k r i s t o wanaokesha Makanisani k a t i k a m k e s h a w a m w a k a m p y a w a Gregory, wakiimba na kumshukuru Mungu wao, lakini wengi wao huwa katika sherehe za Mwaka Mpya kwa sababu mara nyingi sherehe hizo ndizo zenye ulevi na mambo mengine ya kupita kiasi yanayokatazwa na Biblia. Jambo hilo halimaanishi k w a m b a W a k r i s t o wanataka kuzuia wengine wasifurahie mambo.

Badala yake, wanajua kwamba Biblia huwaambia mara nyingi wamwabudu

wa Mungu wa kwel i washangilie, na kuna sababu nyingi za kufanya hivyo. (Kumbukumbu la Torati 26:10, 11; Zaburi 32:11; Mithali 5:15-19; Mhubiri 3:22; 11:9) Biblia pia yakubali kwamba kula na kunywa hufurahisha mara nyingi.—Zaburi 104:15; Mhubiri 9:7.

Hata hivyo, tumeona k wa m b a s h e r e h e z a Mwaka Mpya hutokana na mila za kipagani. Dini zenye kuchukiza mbele ya Yehova Mungu, na kwa mujibu wa Biblia Ukristo unakataa desturi zilizo na

uhusiano wowote nazo, kuwa ndio za Mungu.

Wakristo wanajua vile vile kwamba kushiriki katika desturi za ushirikina hakutawaletea furaha na ufanisi , hasa kwa sababu kushiriki sherehe hizo kunaweza kufanya wakataliwe na Mungu. (Mhubir i 9 :11 ; I saya 65:11, 12) Isitoshe, Biblia yawashauri Wakristo wawe wenye kiasi na wenye kujidhibiti.

(1 Timotheo 3:2, 11) Bila shaka, mtu anayedai kufuata mafundisho ya Kristo hawezi kushiriki

sherehe yenye fujo na ulevi.

H a t a s h e r e h e z a Mwaka Mpya ziwe zenye kuvut ia kadir i gani , Biblia yatuambia ‘tukome kugusa kitu kisicho safi’ na “tujisafishe wenyewe kila unajisi wa mwili na wa roho.” Yehova anawapa wale wanaot i i ahadi hii yenye kutia moyo: “Nitawakaribisha ndani. . . Nitakuwa baba kwenu, na nyinyi mtakuwa wana na mabinti kwangu.” (2 Wakorintho 6:17b–7:1) Ndiyo, Mungu anawaahidi wa l e wa n a o d u m i s h a uaminifu kwake ufanisi na baraka za milele.—Zaburi 37:18, 28; Ufunuo 21:3, 4, 7.

Sheikh Mahawia Mrisho Karenga hatunaeInatoka Uk. 20N y u m b a n i k w a k e Karataka, Jijini Dar es Salaam, kabla ya kwenda k u h i f a d h i wa k a t i k a makaburi ya Kisutu.

Shkh Karenga, Alizaliwa mwaka 1952, Wilayani Kigoma Mjini, na kusoma elimu ya Msingi katika shule ya msingi Businde na alipata elimu yake ya dini kwa Sheikh Hamisi Sinongo, Butunga.

Baada ya hapo Shkh. Karenga, aliingia Jijini Dar es Salaam, mwaka 1972, na kuajiriwa katika kiwanda cha kutengeneza mablanketi ki l ichopo C h a n g ’ o m b e , J i j i n i Dar es Salaam, mpaka alipostaafu.

Huku akiwa muajiriwa Shkh. Karenga, alikuwa

a k i f a n y a h a r a k a t i mbalimbali za kuuhuisha Uislamu huku mwenyewe akijiendeleza kitaaluma zaidi katika dini yake.

Katika kujiendeleza h u k o , a l i b a h a t a i k a kujifunza elimu yake mahojiano na hoja kwa Shkh Abubakari Mwilima, na ndipo walipoafikia k u a s i s i Ta a s i s i y a kul ingania d in i kwa kutumnia Mihadhra ya Al-Malid, mnamo mwaka 1984, ambayo i l ikuja kupata usa j i r i rasmi mwaka 1992.

Katika miaka hiyo chini ya Al-Malid, mihadhra hiyo ya kulingania dini kwa kutumia Qur an na Biblia, ilikuwa na mvuto wa aina yake na kupelekea watu wa dini zote kuvutika

kuifata kwa umbali mrefu katika maeneo ya Jiji la Dar es Salaam, kwa namna Marhum Kalenga na timu yake walivyo kuwa wakiwaendesha kwa hoja wapagani na Wakristo.

Pia alikuwa ni mmoja wa waasisi wa umoja wa wahadhiri nchini Tanzania na kufanikiwa kushika nyadhifa mbal imbal i akiwa Katibu wa Al-Malid , mpaka anafariki na pia alikuwa ni Katibu wa umoja wa Wahadhiri wa Kiislamu.

Al-Marhum Sheikh Mahawia Mrisho Karenga, ameacha mke na watoto wanne.

A l l a h a m r e h e m u na amlipe amali njema alizochuma katika uhai wake na amsamehe pale alipokosea, Inshaa Allah.

BAADHI ya kina mama wa Kiislam wakiwa katika sherehe za Maulid ya Mtume (s.a.w). Maulid hayo yaliyoandaliwa na taasisi ya Bi. Aisha Sururu na kufanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Page 19: ANNUUR 1210A

19 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 1- 7, 2016

MAKALA/TANGAZO

N I M E V U T I WA m n o n a v i t a b u a m b a v y o vinapatikana katika ‘site’ ya Alhidaaya, nikaona nisiwe mchoyo kwa kutowapatia Waislamu wenzangu ambao hawakubahatika kuviona. Moja ya vitabu hivyo ni; “Dini Ya Kweli Ya Mwenyezi M u n g u ” a m b a c h o kinapatikana kwenye tovuti ya www.alhidaaya.com/sw/node/1351. Lakini pia kwa wasiokuwa Waislamu, kinawafaa zaidi ikiwa kweli wana shauku ya kupata uzima wa milele, ambao kwa hakika haupatikani kwa kuimba peke yake, bali kwa kupitia Dini sahihi.

Kitu cha kwanza ambacho m t u n i l a z i m a a k i j u e na kukifahamu barabara kuhusu Uislamu ni maana ya neno hili , “Islaam – Uislamu”. Neno hili ni la Kiarabu “Islaam” ambalo linamaanisha kunyenyekea, kut i i au ku j i sa l imisha kwa hiari yake mtu kwa Mwenyezi Mungu wa kweli tu anayeitwa kwa Kiarabu “Allah”.

Y u l e a n a y e t i i n a kunyenyekea kwa Mwenyezi M u n g u k wa k u p e n d a kwake anaitwa kwa Kiarabu “Muslim – Muislamu.” Dini ya Kiislamu haijaitwa kwa jina la mtu au kaumu wala halikuamuliwa na kizazi cha baadaye, kama ilivyo kwa Ukristo ambao uliitwa kwa jina la Yesu Kristo, Ubudha baada ya mwanzilishi wake Gautama Buddha, Ukomunisti baada ya Confucius, Umaksi baada ya Karl Marx, Uyahudi kutokana na kabila la Yuda na Ubaniyani kutokana na Mabaniyani (Wahindi). Uislamu (kunyenyekea kwa kufuata matakwa ya Allah) ni Dini aliyopewa Adam, mwanadamu wa kwanza na Nabii wa mwanzo wa M w e n y e z i M u n g u n a ilikuwa ni Dini ya Manabii na Mitume wote waliotumwa na Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwa wanadamu. Mbali na hayo jina lake (Uislamu) lil ichaguliwa n a M w e n y e z i M u n g u Mwenyewe na kutajwa kwa uwazi katika Kitabu cha mwisho kilichoteremshwa kwa watu. Katika Wahyi huo wa mwisho, unaoitwa kwa Kiarabu Qur’aan (Qur’ani), Al lah (Subhaanahu wa Ta'ala) Amesema yafuatayo:

“Leo nimekukamiliishieni D i n i y e n u , n a nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini” (5: 3).

“Na anayetafuta dini i s i y o k u w a U i s l a m u

Ijue dini ya kweliNa Juma Jumanne

haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasiri (wenye hasara)” (3: 85).

Kwa hiyo, Uislamu haudai kuwa ni Dini mpya iliyoletwa na Nabii Muhammad (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam) huko Arabuni katika karne ya saba, bali kuwa ni udhihirisho mpya katika mfumo wa mwisho wa Dini ya kweli ya Mwenyezi Mungu Muweza na Mwenye nguvu, Allah (Subhaanahu wa Ta'ala), kama i l ivyoteremshwa mwanzo kwa Adam (‘Alayhis Salaam) na baadaye kwa Manabii waliomfuata.

Kwa sehemu hii tunaweza kueleza kwa muhtasari kuhusu Dini nyengine mbili zinazodai kuwa ni n j ia za kwel i . Hakuna kifungu chochote katika B ib l ia k inachoonyesha kuwa Mwenyezi Mungu Aliwafunulia kaumu ya Nabii Musa (‘Alayhis Salaam) au vizazi vyao kuwa Dini yao inaitwa Uyahudi, na pia kwa wafuasi wa Kristo kuwa Dini yao inaitwa Ukristo. Kwa maneno mengine, majina “Uyahudi” na “Ukristo” hayatoki kwa Mwenyezi Mungu au kukubaliwa naye. Haikuwa ila baada ya muda mrefu wa kuondoka kwake ndipo jina Ukristo likapatiwa Dini ya Yesu.

Je, Dini ya Yesu kwa uhakika ilikuwa tofauti kabisa na jina lake? Dini yake iliakisiwa na kuonekana kwa mafundisho yake, ambayo aliwahimiza kwayo wafuasi wake kuyakubali kama

misingi ya uongofu katika mahusiano yao na Mwenyezi Mungu. Katika Uislamu, Yesu ni Mtume aliyetumwa na Allah (Subhaanahu wa Ta'ala), na jina lake kwa Kiarbu ni ‘Issa (‘Alayhis Salaam). Kama Mitume kabla yake, aliwalingania watu wake kwa ridhaa na hiari

Mwenyezi Mungu.“Si kila aniambiaye ,

‘Bwana, Bwana’, ataingia katika ufalme wa mbinguni; ila ni yule tu anayetimiza matakwa ya Baba yangu aliye mbinguni” (Mathayo 7: 21).

“Mimi siwezi kufanya kitu kwa uwezo wangu mwenyewe. Mimi nina

hukumu kama ninavyosikia kutoka kwa Baba, nayo hukumu yangu ni ya haki. N i a ya n g u s i k u f a n ya nipendavyo mwenyewe, bali apendavyo yule aliyenituma” (Luka 5: 30).

Zipo ripoti nyingi katika Anaajiil (wingi wa Injili) zinazoonyesha kuwa Yesu aliwawekea wazi kabisa wafuasi wake kuwa yeye hakuwa Mwenyezi Mungu mmoja wa kweli. Kwa mfano, alipokuwa akizungumza kuhusu Siku ya Mwisho (Kiyama), alisema:

“Lakini juu ya siku au saa hiyo hakuna mtu ajuaye itakuja lini; wala Malaika wa mbinguni, wala mwana; Baba peke yake ndiye ajuaye” (Marko 13: 32).

H i v y o , Ye s u k a m a Mitume wengine kabla yake na yule aliyekuja baada yake, walifundisha Dini ya Uislamu: Kunyenyekea na kutii kwa amri ya Mwenyezi Mungu mmoja tu wa kweli.

SWALI: Lugha ipi nyepesi itumike kuwafanya watu wakaiona haki, wakaikubali na wakaifuata? Na wale wanaodai kuwa dini zote ni sawa, waelewe mara baada ya kusoma ujumbe huu adhimu kwamba, madai hayo hayawafikiani na risala kutoka kwa Mungu wa kweli! Lugha ipi nyepesi kueleweka zaidi ya hii?

yao kujisalimisha k w a m a e l e k e z o y a M w e n y e z i Mungu (Uislamu unasimamia hilo). Kwa mfano, katika A g a n o J i p y a inaelezwa kuwa Yesu aliwafunza wafuasi wake kumuomba Mwenyezi Mungu kama ifuatavyo:

“Baba! Jina lako litukuzwe; ufalme wako ufike” (Luka 11: 2).

Na p ia : “Baba yetu uliye mbinguni: Jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike d u n i a n i k a m a mbinguni” (Mathayo 6: 9 – 10)

F i k r a h i i ilihimizwa sana na Yesu kwa kauli zake nyingi zilizorikodiwa k a t i k a A n a a j i i l ( G o s p e l s ) . K w a mfano, alifundisha k u w a w a l e Wanaonyenyekea Watarithi Pepo.

Yesu al iashiria k u w a y e y e p i a ananyenyekea na kutii maagizo ya

Mheshimiwa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi (Katikati) akiwa na Mabalozi kutoka nchi mbalimbali walioko nchini, na wageni waliohudhuria hafla ya kuwapongeza wahitimu waliohifadhi Qur`an wanafunzi hao kutoka kituo cha SHAFII Bunju Jijini Dar es salaam wakiwa katika picha ya Pamoja hafla iliyofanyika katika hoteli ya Serena ya Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

Page 20: ANNUUR 1210A

20 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 1- 7, 201620 MAKALA AN-NUUR

20

Soma gazeti la AN-NUUR

KWA TSH 800/=kila Ijumaa

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Ltd, Dar es Salaam.

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA JANUARI 1 - 7, 2016

HAIIBA TIMAMU TEA CHAI YA AJABU KWA AJILI YA KUKABILIANA NA

SHINIKIZO LA DAMU (HYPERTENSION/HIGH BLOOD PRESSURE)

UGONJWA WA MOYO KIHARUSI JONGO (GOUT) MAUMIVU YA VIUNGO (RHEUMATISM) MAUMIVU SUGU YA KICHWA BAWASIR (PILES/HEMORRHOIDS) MAGONJWA YA INI SARATANI MBALIMBALI UOTO/UVIMBE MBALIMBALI KATIKA VIUNGO VYA UZAZI VYA MWANAMKE (FIBROIDS, POLYPS NA CYSTS)

KUSHINDWA KUZUIA MKOJO (URINARY INCONTINENCE)

ATHARI ZA KISUKARI CHA UKUBWANI PUMU UPUNGUFU WA KINGA ZA MWILI KASI YA KUZEEKA MATATIZO YA MFUMO WA MZUNGUKO WA DAMU

MKAKAMO WA NGOZI; UDHAIFU WA MACHO KUPOTEZA KUMBUKUMBU KASI NDOGO YA KUPONA MAJERAHA MAKOVU KWENYE MAPAFU UGONJWA WA NGOZI KUCHUJA RANGI, YAANI, VITILIGO

HAIIBA TIMAMU TEA INAPATIKANA

HERBAL IMPACT

MOSQUE STREET, NO. 1574/144 (MKABALA NA MSIKITI WA SUNNI), KITUMBINI, DAR ES

SALAAM

TUTEMBELEE AU TUPIGIE SIMU NAMBA:

0754281131/0655281131/0686281131/0779281131

HAIIBA TIMAMU TEA IMENIREJESHEA MAISHA YANGU!

Na. Salim Kajenge

Miaka michache iliyopita nilikumbwa na ugonjwa mbaya sana wa kushindwa kuzuia mkojo. Ilikuwa nikijisikia tu haja ya kukojoa na mkojo huo unafuata! Hali hii ilinilazimisha kuacha kabisa kuondoka na kwenda mbali na maeneo ya nyumbani. Ukweli wa mambo ni kwamba nilikwazika sana. Jitihada zote za kutafuta tiba hazikuzaa matunda. Mwezi wa Desemba 2014 nilisoma kwenye gazeti la Annur kuhusu dawa moja iliyokuwa inaitwa chai ya ajabu. Niliamua niijaribu japo sikuwa na matumaini sana. He! Nilishangaa kuwa baada ya kuitumia kwa siku chache hali yangu ilianza kubadilika. Niliitumia hii chai kwa majuma matano na baada ya hapo nikasitisha baada ya kuona kuwa nimepona kabisa!

https://www.facebook.com/Herbal-Impact-157972014402705/

MHADHIRI maarufu w a K i i s l a m u w a mihadhara ya dini l i n g a n i s h i n c h i n i , S h e i k h M a h a w i a M r i s h o K a r e n g a , hatunae.

S h e i k h K a r e n g a , amefikwa na umauti Desemba 24 , 2015 , kat ika hospi ta l i ya Mwananyamala Jijini Dar es Salaam, akiendelea na matibabu na mazishi ya k e ya m e f a n y i k a Ijumaa (iliyopita) katika makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam.

Shkh. Karenga ni muhadhiri mwandamizi maarufu wa ulinganiaji wa Dini kwa kutumia Biblia na Qur an, na kupitia kwake watu we n g i wa m e s i l i m u huku akiacha athari kubwa kwa kufanikiwa kuufikisha Uislamu kwa wapagani na Wakristo

Innaalillah wainnaa ilayhir raajiun

Na Bakari Mwakangwale

kwa njia ya hoja.K a t i k a u h a i wa k e

S h k h K a r e n g a ,

amepata kufungwa jela akihusishwa na sakata la kadhia ya kuvunjwa kwa

Mabucha ya Nguruwe, maeneo ya Manzese Jijini Dar es Salaam, mwaka

1992.Lakini pia alikuwemo

katika purukushani y a J e s h i l a P o l i s i pale l i l ipovamia na kuwapiga Waislamu mabomu ya machozi k a t i k a M s i k i t i wa Mungu Moja Dini Moja, wakati wakiendelea na Muhadhara.

K u f a t i a u m a h i r i wake wa kulingania, Marhum Shkh Karenga, al ikuwa ana uwezo wa kuichambua Biblia akiupambanua Uislamu katika kitabu hicho kwa ufasaha na kuifanya mihadhara wakati huo kuwa na mvuto mkubwa na kuvutia wasiokuwa Waislamu wauamini Uislamu.

M a r h u m S h k h Karenga, alifanyiwa ibada yake ya mwisho M a s j i d i T a q w a , Mwanayamala kisha mwili wake ulipelekwa

Inaendelea Uk. 18

Sheikh Mahawia Mrisho Karenga hatunae

WAISLAMU wakiubeba mwili wa marehemu Sheikh Mahawia Mrisho Karenga kwenda mazikoni.