Fataawa Za Wanachuoni (17)
-
Upload
wanachuoni -
Category
Documents
-
view
267 -
download
3
description
Transcript of Fataawa Za Wanachuoni (17)
1
������� ���
Fataawa Za Wanachuoni
[17]
Imefasiriwa Na Kutayarishwa Na:
Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush
©
2
Dibaji:
Hizi ni Fataawa za wanachuoni mbali mbali ambazo nimezikusanya ili
kuweza kuwasahilishia ndugu zetu Waislamu na khaswa wale watafutaji
elimu. Fataawa ni mchanganyiko kuhusiana na masuala mbali mbali ya
Tawhiyd, ´Aqiydah, Manhaj, Fiqh na mengineyo.
Hivyo, ninamuomba Allaah (´Azza wa Jalla) ziweze kuleta faida kwa ndugu
zetu Waislamu, na ninamuomba Allaah (´Azza wa Jalla) Ajaalie kazi hii niwe
nimeifanya kwa kutafuta Radhi Zake (Subhaanahu wa Ta´ala), na Amlipe kila
Aliyeisambaza kwa ndugu mwengine na Awalipe ndugu wasomaji wote kwa
jumla.
Tanbihi: Fataawa zote hizi tumezifasiri kwa njia ya Video na zinapatikana
Youtube waweza kusoma na huku wasikiliza. Kwa mwenye kutaka hizo
Fataawa za Video aende Alhidaaya au Youtube kwa juu sehemu ya kutafuta
aandike au kukopi kichwa cha habari cha Fatwa (kama ilivyo hapo chini kwa
kila Fatwa ina kichwa chake cha habari) na atafute itajitokeza In Shaa Allaah.
Jazaakumu Allaahu Khayra
Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad, na ahli zake na
Maswahabah zake na watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah.
3
Fataawa zilizomo ni hizi zifuatazo:
1. Mtume Hakufanya Da´wah Kwa Kutenga Siku Maalumu
2. Msingi Wa al-Ikhwaan al-Muslimuun Hauna Maana
3. Rabiy´ al-Madkhaliy Ni Salafiy
4. Shaykh al-Jaabiriy Kuhusu ´Abdul-Maalik Ramadhaaniy
5. Mfano Wa Khawaarij Wa leo
6. Kusoma Kwa Mtu Asiyefanya Tabdi´ Kwa ´Ar´uur, al-Ma´ribiy Na al-
Maghraawiy
7. ´Allaamah al-Fawzaan Anakanusha al-As'ilah al-´Iraaqiyyah Cha al-
Halabiy
8. Ibaadhi Na Mashia Ndio Vijukuu Vya Jahmiyyah
9. ´Allaamah Ahmad an-Najmiy Kuhusu Picha Na Mawaidha Ya Video
10. Salafiy Haina Maana Mtu Kalindwa Na Madhambi
11. Allaamah al-Fawzaan Akimradi al-Qaradhwaawiy Anaesema Uhuru
Ni Bora Kuliko Shari´ah
12. Allaamah Rabiy´ Kuhusu Muhammad Mukhtaar ash-Shanqiytwiy
13. Hizi Mbwa Zenye Fujo Haziwezi Kudhuru Salafiyyuun
14. Kumnasihi Mtawala Au Mtu Kwa Dhati Yake Kwenye Mimbari
15. Da´wah Haianzi Kwa Maonyo
16. Hukumu Ya Mwenye Kupinga Kuja Kwa Dajjaal?
17. Imaam Ibn Baaz Kuhusu Utiifu Kwa Mtawala Wa Kuwait
18. Ni Wajibu Kusambaza Radd Za Wanachuoni
19. Tunaonya Hizbiyyuun Kwa Maslahi Yao Wenyewe
20. Haya Hawayajui Wale Walioghafilika Kuhusu Hizbiyyuun
21. Ni Sharti Wakubaliane Wanachuoni Katika Kumjeruhi Mtu? (1)
22. Radd Kwa Dr. Zakir Naik Asemae Kuwa Manaswara Ni Ndugu Zetu
Kibinaadamu
23. Radd Ni Dawa
24. Mdogo Anaweza Kumpiga Radd Mkubwa?
25. Ni Sharti Wakubaliane Wanachuoni Katika Kumjeruhi Mtu? (2)
26. Mume Kumpa Talaka Mke Bila Ya Sababu
27. Ikiwa Ni Radd Ya Haki, Haijuzu Kwako Kuiacha
28. Shaykh as-Suhaymiy Kuhusu Facebook
4
29. Mwanachuoni Tu Ndiye Awezae Kupiga Radd?
30. Shubuha Zinazotumiwa Na Wale Wanaopinga Radd
31. Allaamah an-Najmiy Kuhusu Yule Anaewatuhumu Maimamu
Watatu Kuwa Ni Murji-ah
32. Nasaha Ya Shaykh Fawzaan Kwa Dada Ambaye Anapata Tabu Kwa
Ajili Ya Dini Yake
33. Je Awwaam Ni Salafiyyuun?
34. Jabriyyah Na Jahmiyyah Ni Watu Wa Bid´ah Au Makafiri?
35. Awwaam Watahadharishwe Dhidi YaWatu Wa Bid´ah
36. Allaamah al-Fawzaan Kauli Ya as-Suwaydaan Kupingana Na Allaah
Na Mtume Wake
37. Allaamah ´Abdul-´Aziyz Aal ash-Shaykh Kuhusu Kauli Ya as-
Suwaydaan Uhuru Wa Dini
38. Haitoshi Kujiita Tu Salafiy
39. Nasaha Za al-´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy Kuhusu Baadhi Ya
Mashaykh
40. Ni Yapi Madhehebu Ya al-Ikhwaan al-Muslimuun?
41. Allaamah Rabiy´ al-Madkhaliy Kuhusiana Na Maandamano
42. Ipi Hukumu Ya Kuweka Camera Msikitini?
43. Masanduku Ya Swadaqah Msikitini
5
Wanachuoni waliomo ni hawa wafuatao:
1. ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
2. Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
3. Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
4. Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
5. ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aal ash-Shaykh
6. Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
7. Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
8. Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
9. Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy
10. Muhammad bin Swaalih al-Luhaydaan
11. Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
12. Swaalih bin Sa´iyd as-Suhaymiy
13. Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy
14. Muhammad bin ´Abdillaah al-Imaam:
15. Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy
6
Bismillaahi Rahmaani Rahiym
1. Mtume Hakufanya Da´wah Kwa Kutenga Siku Maalumu
Swali:
Yapi maoni yako kuweka mpaka siku maalumu kufanya Khuruuj katika njia
ya Allaah na Jamaa´t-ut-Tabliygh?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) haikuthibiti kwake kwamba
aliamrisha hilo kabisa. Na Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walikuwa
ni watu wenye hima kwa kheri na watu wenye kujikurubisha kwa yale Allaah
Anayoyapenda. Haikupokelewa kutoka kwa mmoja katika yao (Radhiya
Allaahu ´anhum) kitu katika hayo. Na ikiwa tutashindwa kufanya baadhi ya
´amali, tuko na mizani kamili; Maneno ya Allaah na maneno ya Mtume wake
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hivyo basi, tukimbilie kujifunza Dini. Na
mmoja wetu akitaka kubobea katika kitu, basi anaweza kuhifadhi na
kufahamu Maneno ya Mola wa viumbe na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam). Kwa hakika atakaeruzukiwa kufahamu Kitabu cha Allaah
(Jalla wa ´Alaa) na Sunnah za Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)
atakuwa ameruzukiwa kheri kubwa.
Chanzo:
http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=130109&st=40
7
2. Msingi Wa al-Ikhwaan al-Muslimuun Hauna Maana
Swali:
Yapi maoni yako kwa mwenye kusema:
"Tushirikiane kwa yale tunayoafikiana, na tusameheana kwa yale
tunayokhitilafiana."
´Allaamah al-Luhaydaan:
Haya maneno hayana maana. Wala haifai kuyafanyia kazi.
Haya maneno, ina maana wanamaanisha kama kuna mtu ambaye anadai ni
Muislamu ilihali ni Mulhid (kafiri) na mwengine katika Ahl-us-Sunnah wako
na kituwanaafikiana cha maslahi na mji wao, washirikiane kafiri huyu na yule
mwengine. Ingelikuwa sawa kama ni kuhusiana na kuulinda mji na
wavamizi, ama baadhi ya Madu´aat wanaosema tushirikiane kwa yale
tunayoafikiana, na tusameheana kwa yale tunayokhitilafiana, hichi ni kitendo
ambacho si sahihi.
Chanzo:
http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=130109&st=20
3. Rabiy´ al-Madkhaliy Ni Salafiy
Swali:
Ipi rai yako kwa anayemponda Shaykh Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy?
8
Imaam Ibn ´Uthaymiyn:
Ni kosa hili. Ni kosa.
Swali:
Unasemaje kuhusiana na Shaykh?
Imaam Ibn ´Uthaymiyn:
Mtu huyu namjua. Ni Salafiy.
Swali:
Ipi hukumu ya kueneza mikanda ambayo Serikali imekataza, mfano wa
mikanda ya baadhi ya Madu´aat ambao wamepigiwa marufuku?
Imaam Ibn ´Uthaymiyn:
Haijuzu.
Swali:
Haijuzu?
Imaam Ibn ´Uthaymiyn:
Ndio.
Chazo: http://youtu.be/c6vBiepR1Y0
9
4. Shaykh al-Jaabiriy Kuhusu ´Abdul-Maalik Ramadhaaniy
Swali:
Kuna swali kuhusu Shaykh ´Abdul-Maalik Ramadhaaniy.
Shaykh Dr. ´Ubayd al-Jaabiriy:
´Abdul-Maalik Ramadhaaniy imekuwa siku hizi anachanga sana mambo na
anakosa nia. Hafai.
Swali:
[Swali haliko wazi]
Shaykh Dr. ´Ubayd al-Jaabiriy:
Hapana, hapana. Siwanasihi kushikamana naye. Ni katika wafuasi wa al-
Halabiy sasa.
Swali:
Vitabu vyake vya zamani vipo hapa Libya.
Shaykh Dr. ´Ubayd al-Jaabiriy:
Vitabu vya zamani mtu anaweza kuchukua elimu akastafidi kwavyo, na
khaswa vile ambavyo vina Radd dhidi ya Khawaarij. Ni vizuri. Kwa mfano
kitabu "Madaarik-un-Nadhwar". Ni kizuri.
10
Swali:
Ana kitabu hata cha Hijaab...
Shaykh Dr. ´Ubayd al-Jaabiriy:
Hakuna neno kusoma vitabu vya zamani. Lakini mtu huyu kwa sasa,
amekuwa kama nimevyokwambia. Kuanzia miaka ya nyuma amekuwa hana
tena nia. Anasapoti maneno na sifa za al-Halabiy kwa The Amman Message
ambayo imejaa Kufuru.
Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=127471
5. Mfano Wa Khawaarij Wa leo
Swali:
Mtu anaweza kusema ya kwambawanachama wa al-Qaa´idah ni Khawaarij?
Shaykh Dr. Muhammad bin ´Abdillaah al-Imaam:
Ndio. Ni Khawaarij. al-Ikhwaan al-Muslimuun ni Khawaarij. Hizb-ut-Tahriyr
ni Khawaarij. Suruuriyyah ni Khawaarij. Suruuriyyuun wamefanya uasi
Algeria na katika miji mingine.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=6785
11
6. Kusoma Kwa Mtu Asiyefanya Tabdi´ Kwa ´Ar´uur, al-Ma´ribiy Na al-
Maghraawiy
Swali:
Inajuzu kuchukua elimu kwa mtu ambaye hambadi´ Ar´uur, Abul-Hasan al-
Ma´ribiy na al-Maghraawiy na anasema shirika la Ihyaa' at-Turaath ni Salafiy?
Hajasoma na wala hana Tazkiyyah kutoka kwa wanachuoni. Anachukua
elimu kwenye mikanda na vitabu vya Ibn Baaz, Al-Albaaniy na Ibn
´Uthaymiyn (Rahimahumu Allaah).
´Allaamah Yahyaa an-Najmiy:
Kwa hakika ni kwamba yule ambaye hawabadi´ watu hawa, yeye ni kama
wao. Kwa kuwa watu hawa ni watu wa Bid´ah. Na al-Maghraawiy imethibiti
kwake kuwa ni Takfiyriy
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=865
7. ´Allaamah al-Fawzaan Anakanusha al-As'ilah al-´Iraaqiyyah Cha al-
Halabiy
Swali:
Sisi tuko magharibini, tumepata kitabu chenu kwa jina la "al-As'ilah al-
´Iraaqiyyah"...
12
´Allaamah al-Fawzaan:
Tumesema kwamba ni cha uongo. Nimekipiga Radd. Ni cha uongo, uongo,
uongo.
Chanzo: http://alfawzan.ws/sites/default/files/bryhari--1427-2-12.mp3
8. Ibaadhi Na Mashia Ndio Vijukuu Vya Jahmiyyah
Swali:
Ipi tofauti kati ya ´Aqiydah (Itikadi) ya Jahmiyyah na ya Ibaadhi? Je, ni
kikundi kimoja kwa jina jipya?
Shaykh Dr. Swaalih as-Suhaymiy:
Katika mlango wa Sifa za Allaah, ni takriban kundi moja. Wote wanakanusha
Sifa za Allaah (Jalla wa ´Alaa) na wanakanusha waumini kumuona Mola Wao
Aakhirah. Wanakubaliana (Ibaadhi) na Raafidhwah (Mashia) na Jahmiyyah
katika masuala mengi.
Lakini katika mlango wa Ijraa´, wanatofautiana na Jahmiyyah. Jahmiyyah
wakali wanaamini ya kwamba ´amali si katika Imani, na kutokana na hili
wanakufuru kwani ni Ijraa´ ya Kufru. Nayo ni kuamini ya kwamba ´amali si
katika Imani, na kwamba inatoka nje ya Imani. Bila ya shaka mwenye kuamini
hivyo amekufuru. Na Jahmiyyah ni katika mkumbo huu. Ama Ibaadhi wao ni
Khawaarij, wako kinyume chao (na hao Jahmiyyah) hata hivyo
wanakubaliana katika masuala mengi; kama kukanusha Sifa za Allaah
(Subhaanahu wa Ta´ala).
13
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=nT5Yqm-DM4o
9. ´Allaamah Ahmad an-Najmiy Kuhusu Picha Na Mawaidha Ya Video
´Allaamah Ahmad an-Najmiy:
Haijuzu kwa yeyote kunichukua picha (Video). Ni Haraam juu yenu. Haijuzu
kwa yeyote kunichukua picha, sitaki yeyote anichukuepicha.
Mwanafunzi wa Shaykh:
"Ni ndugu zetu wenye simu za Camera wamezifugua na kutaka kumchukua
picha (sasa Shaykh amewakataza), kwa kuwa Shaykh haonelei kujuzu kwa
hilo."
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=rZz8NsqYqAw
10. Salafiy Haina Maana Mtu Kalindwa Na Madhambi
Swali:
Ikiwa mtu ana Manhaj safi na anapenda Salafiyyuun, lakini ana madhambi
mengi. Je, anaweza kuitwa Salafiy?
´Allaamah al-Waswaabiy:
14
Kinachoangaliwa ni ´Aqiydah na Manhaj. Salafiy haina maana mtu kalindwa
na madhambi. Lakini ikiwa ana ´Aqiydah sahihi na Manhaj sahihi, ni Salafiy
na Sunniy. Tunamuusia kuwa na msimamo na kuachana na maasi.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=3436
11. ´Allaamah al-Fawzaan Akimradi al-Qaradhwaawiy Anaesema Uhuru Ni
Bora Kuliko Shari´ah
Yuusuf al-Qaradhwaawiy:
"Kwa hakika, hakuna dawa kwa Ummah huu isipokuwa mpaka kwa Uhuru
(Demokrasia). Kama nilivyotangulia kusema katika baadhi ya barnamiji
zangu, mimi ninaipa kipaumbele Uhuru (Demokrasia) juu ya kutekeleza
Shari´ah ya Kiislamu. Haiwezekani kutekeleza Shari´ah ya Kiislamu na Uhuru
(Demokrasia) inakosekana."
Swali:
Ipi hukumu ya mwenye kusema ya kwamba Uhuru ni bora kuliko Shari´ah?
´Allaamah al-Fawzaan:
Mna shaka ya kwamba ni kafiri? Mwenye kusema ya kwamba Uhuru ni bora
kuliko Shari´ah, huyu ni kafiri ukafiri mbaya - A´udhubi Allaah.
Chanzo http://alfawzan.ws/sites/default/files/bryhari--1427-10-14.mp3
Tarehe: 1427-10-14/2006-11-06
15
12. ´Allaamah Rabiy´ Kuhusu Muhammad Mukhtaar ash-Shanqiytwiy
Swali:
Ndugu mmoja ametupa mkanda wa Sharh ´Umdat-ul-Ahkaam cha Shaykh
Muhammad [al-Mukhtaar] ash-Shanqiytwiy na una mikanda 400. Tuache
ibaki Msikitini?
´Allaamah Rabiy´ al-Madkhaliy:
Mtu mtu huyu, mimi sijasoma Sharh hii. Sijui. Nimeambiwa kuwa mtu huyu
hawezi kupambanua baina ya Ahaadiyth Swahiyh na Dhaifu, na kwamba
anatangamana na Hizbiyuun na Sufiyyuun nawala hana mawasiliano na Ahl-
us-Sunnah. Ndio maana siwezi kuzitakasa wala kumtakasa mtu huyu. Kwa
kuwa sijazisoma. Nanyi hamna haja... Ni nani anaesambaza mikanda ya mtu
huyu? Sio Ahl-us-Sunnah wanaosambaza mikanda yake. Wanaozisambaza ni
Hizbiyyuun. Yeye mwenyewe hajionyeshi kuwa ana vikundi vikundi. Lakini
wakati unapoona watu hawa wamemzunguka na mikanda yake na
wanamchukulia kuwa Imaam wa Waislamu, ni dalili ionyeshayo kuwa mtu
huyu ni katika wao. Ni njia ya khatari inayowafanya vijana kuwa vikundi
vikundi. Mko na vitabu vya Salaf. Vinawatosheleza.Fiqh ya Salaf
inawatosheleza. Kwa kuwa hayo yatakuja kuwapeleka katika mambo
mengine.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=Pknjz6e_fEo
13. Hizi Mbwa Zenye Fujo Haziwezi Kudhuru Salafiyyuun
Swali:
16
Siku zilizopita waliongea sana watu wapotofu maneno ambayo wanadai
wanaiweka Salafiyyah kwenye usawa. Unasema nini kuhusu hilo?
´Allaamah al-Fawzaan:
Jambo hili ni kitu ambacho watu mfano wao; katika wanafiki na makafiri
walikuwa wakilifanya. Walikuwa wakitukana watu wa Dini. Wanawatukana
Waislamu wanaoshikama na Dini yao. Tokea zamani. Hakuna jipya.
Wanafuata njia ya watu hawa. Hawakudhuru Salafiyyah wala Salafiyyuun na
lolote. Wanajidhuru wenyewe. Salafiyyah ya kweli kweli - Alhamdulillaah -
iko thabiti juu ya Qur-aan na Sunnah. Haikudhurika na fujo za mbwa.
Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=133045
Tarehe: 1431-04-11/2010-03-27
14. Kumnasihi Mtawala Au Mtu Kwa Dhati Yake Kwenye Mimbari
Swali:
Je, ni katika nasaha kumpa mtawala na kuamrisha mema na kukataza maovu
kukataza maovu wanayoyafanya juu ya mimbari?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Sio katika nasaha kumkosoa mtu au mtawala kwenye mimbari. Nasaha
hutolewa kwa njia ambayo itanufaisha. Ama ikiwa makusudio ni kuleta
tashwishi na kueneza aibu na chuki, hii sio katika nasaha. Ikiwa mtu anaweza
kumnasihi mtawala kuacha yale anayoyaona ni maovu au kumfanya akataza
maovu, amuombee Allaah Amuafikishe kufanya hivyo, au amwambie
17
anaedhania anaweza kumnasihi ya kwamba kuna kasoro kadha na kadha,
ikiwa anajua kwa yakini makosa hayo.
Chanzo:
http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=130109&st=20
15. Da´wah Haianzi Kwa Maonyo
Swali:
Vipi tutajumuisha kati ya kutotaha-dharisha wanaokhalifu na kuelezea Njia
iliyonyooka? Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa ni
mwenye kutoa bishara na mwenye kutahadharisha. Tukinyamazia
wanaokhalifu na wala hatubainishi...
´Allaamah al-Fawzaan:
Wewe kitu cha kwanza, wafunze njia sahihi. Watakuja kujua wanaokhalifu.
Ama kuanza tu kuwakataza na wao hawana msingi wala hawana elimu, hili
halina faida. Litakuja kupelekea kwenye chuki tu. Wafunze njia sahihi.
Wafanye waifahamu Dini ya Allaah. Halafu baada ya hilo, ima wao wenyewe
watakuja kujua ni nani anaekwenda kinyume au wewe uwatanabahishe ikiwa
hawajui. Lakini haifai kuanza wao na kuwatahadharisha dhidi ya fulani na
fulani wakati hawafahamu lolote.
Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=133027
18
16. Hukumu Ya Mwenye Kupinga Kuja Kwa Dajjaal?
Swali:
Ipi hukumu kwa mwenye kupinga kuja kwa Dajjaal?
´Allaamah al-Fawzaan:
Huyu ikiwa anajua dalili na akapinga, ni kafiri. Kwa kuwa kapinga kitu
ambacho ni Mutawaatir kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa
sallam). Ama ikiwa ni mjinga na wala hajui dalili, huyu abainishiwe.
Akiendelea kupinga baada ya kubainishiwa, anahukumiwa ukafiri. Kwa
kuwa anamkadhibisha Allaah na Mtume Wake (´alayhis-Salaam).
Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=124546
17. Imaam Ibn Baaz Kuhusu Utiifu Kwa Mtawala Wa Kuwait
Swali:
Kiongozi wa Kuwait ni mtawala na ni lazima kumtii kwa yale yanayoruhusu
kwa vile hahukumu kwa kutumia Shari´ah?
Imaam Ibn Baaz:
Ndio, ni watawala, sawa wa Kuwait, Jordan au Syria. Ni watawala. Ni wajibu
kuwatii kwa yale yanayoruhusu kama alivyosema pia Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam). Ni wajibu kuwatii kwa yale yanayoruhusu na wala
hawatiiwi kwa yale ambayo ni maasi, si wao wala wengineo. Kwa mfano
wakisema kunyweni pombe, wasitiiwe. Chukueni Ribaa, wasiitiwe. Wakisema
zinini, wasitiiwe. Ama wakiamrisha kumtii Allaah na Mtume Wake au
19
wakaamrisha kwa kitu kinachowanufaisha Waislamu na wala hakikhalifu
Shari´ah au sheria za barabarani ili kuepuka ajali, ni wajibu kuwatii.
Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=133070
18. Ni Wajibu Kusambaza Radd Za Wanachuoni
´Allaamah al-Fawzaan:
Ikiwa Radd hizi ni za kielimu na zimetoka kwa wanachuoni waaminifu na
zina faida kwa Waislamu na zina nasaha na muongozo, basi ni wajibu
kuzisambaza ili watu wanufaike kwazo, na kwa ajili ya kuwanasihi Waislamu
na kuondosha utata, kwa vijana na kwa wale wasiojua utata huu. Radd hizi
kutoka kwa wanachuoni na Baswiyrah, kuna faida kwa watu wote. Kuna
kuondosha utata. Ni nasaha kwa Waislamu. Yule mwenye kuzisambaza ana
ujira kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).
Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=133178
19. Tunaonya Hizbiyyuun Kwa Maslahi Yao Wenyewe
´Allaamah al-Waadi´iy:
Ama kuhusu Hizbiyyuun, Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Anasema kwenye
Kitabu Chake Kitukufu:
و�و وا ����س ����
20
"Na semeni na watu kwa wema." (02:83)
Sisi tunaonya watu dhidi yao kwa ajili ya maslahi yao wenyewe. Na lazima
kuwepo kujeruhiwa na kusifiwa, Jarh wa Ta´diyl. Wanachuoni wanaojulikana
wamekubaliana kujeruhiwa na kusifiwa, Jarh wa Ta´diyl, na kuonya dhidi ya
Ahl-ul-Bid´ah. Wao wenyewe wanaonya dhidi yetu mchana na usiku. Sisi
tunaonya dhidi ya watu wa Bid´ah na tunalingania watu kwenye Sunnah ya
Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Chanzo: http://muqbel.net/sounds.php?sound_id=39
Tarehe: 1420-05-28/1999-09-09
20. Haya Hawayajui Wale Walioghafilika Kuhusu Hizbiyyuun
´Allaamah al-Waadi´iy:
Ndugu! Hatuna muda wa kujadili. Katika sisi kuko wenye kutaka kuhifadhi
Qur-aan. Wengine wanataka kuwa mabingwa wa lugha ya kiarabu. Wengine
wanataka kuwa mabingwa wa Sunnah na kupambanua Swahiyh, dhaifu na
yenye kasoro. Hatuna muda. Wakati Hizbiy anakujia anataka kujadiliana na
wewe, mwambie aende kwa mwenye shaka kama yeye, mimi niko thabiti
kwenye Dini yangu. Wao hawana mengine zaidi ya haya; mjidala na
kukamata wenye kughafilika. Kuna wenye kughafilika katika wao. Hatutaki
kuwa na wenye kughafilika katika Ahl-us-Sunnah. Hatujui wapi mpaka
unapokwenda - kwetu Ahl-us-Sunnah au Hizbiyyuun? Wanasema:
"Hawa wamaamini ya kwanba Allaah Kastawa juu ya ´Arshi Yake. Wanaamini ya
kwamba Allaah Ana macho mawili. Wanamaani ya kwamba Allaah Ana mikono
miwili."
21
Masikini wewe! Unasahau ya kwamba wanaharibu Sunnah!
Masikini wewe! Unasahau ya kwamba wanajuzisha Demokrasia na uchaguzi
wa kikafiri!
Masikini wewe! Unasahau ya kwamba wako na al-Ikhwaan al-Muslimuun!
Masikini wewe! Unasahau ya kwamba wamechukua Msikiti wa ndugu zetu
Aden!
Masikini wewe! Unasahau ya kwamba wanakimbiza watu kuikimbia Sunnah
na Ahl-us-Sunnah!
Allaah Amrehemu Aliyesema:
"Ukimuona mtu anawaponda Ahl-ul-Hadiyth, basi jua ya kwamba ni mtu wa
Bid´ah."
Chanzo: http://muqbel.net/sounds.php?sound_id=39
Tarehe: 1420-05-28/1999-09-09
21. Ni Sharti Wakubaliane Wanachuoni Katika Kumjeruhi Mtu? (1)
Swali:
Kujeruhi (Jarh) kumeshurutishwa Ijmaa´?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hii ni kazi ya wanachuoni wa Hadiyth. Sio sharti iwe Ijmaa´ ya kwamba mtu
huyu kajeruhiwa. Bali mwenye kuthibitisha anatangulia kabla ya mwenye
kupinga. Mwenye kutakasa, huyu ndiye anayepinga; na yule mwenye
kujeruhi (Jarh), huyu ni mthibitishaji na ndiye mwenye kutangulia.
22
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=JgxnJbCQGLc
22. Radd Kwa Dr. Zakir Naik Asemae Kuwa Manaswara Ni Ndugu Zetu
Kibinaadamu
Swali:
Mwenye kusema makafiri ni ndugu zetu wa kibinaadamu na si katika Dini. Je,
maneno yake haya ni sahihi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Haitoshi kiubinaadamu. Hakuna undugu wa ubinaadamu. Wala mtu hasemi
hivi kwa kutaka kuwapaka mafuta au hisia zao. Hapana! Mtu asisemi hivi.
Inatakiwa kusema wao ni maadui zetu wala mtu asisemi ni ndugu zetu wa
kibinaadamu. Bali mtu anatakiwa kusema ni maadui zetu. Ikiwa ni maadui
zetu katika Dini, udugu wa kibinaadamu utafidisha nini? Utafidisha nini?
Fir´awn alikuwa pia binaadamu. Au sio? Je alikuwa pia ndugu yetu?
Haitakikani kusema hivi.
Chanzo: http://alfawzan.ws/node/1875
Tarehe: 1431-04-14/2010-03-29
23. Radd Ni Dawa
Swali:
23
Mi napenda Sunnah na nnachukia Bid´ah na ukhurafi. Lakini Shaykh
kuwapiga Radd Ahl-ul-Bid´ah na watu waliopinda, baadhi ya watu hawako
katika Manhaj Salaf, na wanapopigwa Radd kuna watu wanaosema haifai
kuzisambaza isipokuwa tu zisambazwe kwa wanafunzi. Tunaomba nasaha
kwa swali hili.
´Allaamah al-Fawzaan:
Kama amevyosema muulizaji, Ruduud hakuna budi lazima ziwe zimetoka
kwa wanachuoni ambao wanajua mambo ya Radd, wanajua kosa na
wanaweza kulirudi kwa dalili katika Qur-aan na Sunnah. Kusambaza Ruduud
hili ni jambo la wajibu kwa kuwa ni kuwafunza Waislamu. Ikiwa mtu kaeneza
Bid´ah yake na akaeneza kosa lake kwa watu, ni lazima kusambaza Ruduud
sahihi [... sauti imepotea... ] kwa ajili kuondosha madhara ya Bid´ah na kosa.
Hili ni lazima na ni dawa. Radd ikifichwa shari itaenea kwa watu, Bid´ah
kuzidi kuwa kubwa n,k. Ni lazima kusambaza Ruduud zilizo sahihi na si kila
Ruduud. Ruduud sahihi zilizotoka kwa wanachuoni ambao wanajua Bid´ah
na wanajua kosa na wanajua vipi watalirudi kwa Qur-aan na Sunnah.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=Tvpvs9oXl5s
24. Mdogo Anaweza Kumpiga Radd Mkubwa?
´Allaamah Rabiy´ al-Madkhaliy:
Sawa ikiwa ni mkubwa au mdogo, ikiwa atabainisha kwa elimu hakuna
ubaya, sawa ikiwa ni mdogo au mkubwa. Kinachotazamwa ni yule
aliyepigwa Radd. Inaweza kuwa ni mtu mpotevu anayepoteza Ummah,
akampiga Radd aliye mdogo kuliko yeye na wala hakuna ubaya kufanya
hivyo.
24
Chanzo: http://youtu.be/tARw5OfeH8E
25. Ni Sharti Wakubaliane Wanachuoni Katika Kumjeruhi Mtu? (2)
Swali:
Je, ni sharti katika kuwajeruhi Ahl-ul-Bid´ah Ijmaa´a (wakubaliane
wanachuoni wote) wa zama hizo? Au anatosha mwanachuoni mmoja tu?
´Allaamah Rabiy´ al-Madkhaliy:
Huu ni mfumo wa ulegezaji mchafu. Ni zama zipi zilizoshurutisha Ijmaa´ hii?
Na dalili iko wapi ya sharti hii? Kila sharti isiyopo katika Kitabu cha Allaah
sharti hiyo ni batili. Anapomjeruhi Imaam Ahmad bin Hanbal, au Yahyaa bin
Ma´iyn, wakamjeruhi Mubtadi´ah, je ni lazima wakubaliane wanachuoni wa
Sunnah wote duniani kote ya kwamba mtu huyu ni Mubtadi´ah? Ataposema
Ahmad bin Hanbal huyu ni Mubtadi´ah watakiwa kupokea hivyo. Na hivyo,
ilikuwa anaposema fulani ni Mubtadi´ah, watu wote wanakubali hilo.
Mashahidi wawili wanapotoa ushahidi kwa Qadhi kuhusu fulani ya kwamba
amemuua fulani, je ni sharti iwe Ijmaa´ (wakubaliane na wengine) ya kwamba
kweli ameua? Bali ni wajibu kwa Haakim kutoa hukumu kwa Shari´ah ya
Allaah, ima atoe Diyah au Qiswaas. Ni wajibu ahukumu kwa Shari´ah ya
Allaah (´Azza wa Jalla). Imeshurutishwa Ijmaa´ kwa ushahidi wa mtu huyu?
Na hili ni jambo kubwa kuliko kuwabadi´ Mubtadi´ah. Hawa ndio walegezaji,
Ahl-ul-Baatwil na Madu´aat wa shari. Msisikilize porojo hizi. Anapomjeruhi
mwanachuoni mwaminifu mtu, ni lazima kukubali Jarh hii. Mwanachuoni
mwengine mwaminifu anapopinga hilo, hapo ndipo kunaangaliwa nini
kasema huyu na huyu, kunatazamwa Jarh hii na Ta´diyl hii. Ikiwa Jarh hii
imefafanulia na kuwekwa wazi, basi inatangulizwa juu ya Ta´diyl, hata ikiwa
wanachuoni waliomsifu mtu huyo ni wengi. Mwanachuoni mmoja ametoa
Jarh iliyofafanuliwa, wakasema kinyume chake wanachuoni ishirini mpaka
khamsini pasina dalili, hawana zaidi ya kumdhania vizuri na kuchukulia kwa
25
uinje wanavyomuona, na huyo mwanachuoni mwengine ana dalili kwa
kumjeruhi mtu huyu kwa dalili, basi Jarh hii inatangulizwa. Kwa kuwa
aliejeruhi ana hoja na hoja ndio inayotangulia. Na wakati mwingine
inatangulizwa hoja hata kama wataikhalifu mamia au maelfu ya watu.
"Jamaa´ah ni ile iliyoko juu ya haki hata kama mtu atakuwa peke yake."
Lau mtu atakuwa juu ya Sunnah, wakamkhalifu watu wa vijiji viwili au vitatu
- Mubtadi´ah, haki iko na mtu huyo. Na kunatangulizwa hoja alizonazo na
haki juu ya yale ya batili waliyonayo hao wengine. Ni wajibu kuheshimia haki
na kuheshimia hoja na dalili.
�ل ھ��وا �رھ���م إن ���م ��د��ن
"Sema: "Leteni ushahidi wenu kama nyinyi ni wasema kweli." (02:111)
وإن �ط+ أ�(ر )ن '& ا%رض �#�"وك ن ���ل �
"Na ukiwatii wengi katika hawa waliomo duniani watakupoteza na Njia ya
Allaah." (06:116)
Wingi hauna maana yoyote ikiwa hauna hoja. Ikiwa watu wa duniani wote
wamekusanyika katika upotofu pasina hoja, isipokuwa watu wachache tu
waliko kwenye haki, wengi hao hawana maana na wingi wao. Hata kama ni
mtu mmoja au watu idadi ya watu wachache. Hishimieni haki, shikamaneni
nayo na kubalini haki ikiwa ina hoja.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=M7DcNcQMKDA
26. Mume Kumpa Talaka Mke Bila Ya Sababu
26
Swali:
Anapata madhambi mume akimpa Talaka mke wake bila ya sababu?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Ataangaliwa kwa nini kamtaliki. Ikiwa yuko na sababu, atapewa udhuru na
wala hana juu yake kitu. Na kama amemuonea bila ya sababu miongoni mwa
sababu, si mtu mwenye aibu wala tabia katika khulka yake, anapata
madhambi bila ya shaka. Kwa kuwa kamuonea na pengine hata hana familia,
akaja kuathirika kwa taabu. Hivyo, ni juu ya mtu kumcha Allaah. Maisha ya
ndoa yamefungamana baina ya muumini mwanaume na muumini
mwanamke. Mke wa mja hapa duniani ndio mke wake huko Peponi kwa
kiwango kikubwa cha uzuri na ukamilifu; mbora kuliko hata Huur al-´Iyn
kutokana na Swalah zake, kisimamo chake na Imani yake. Hivyo ni juu ya
muumini kuwa makini, Akimsahilishia Allaah kumpa mke katika watu wa
Tawhiyd, mwema na mwenye kufunga. Na akiwa na kitu kama kasoro,
akiweke sawa kwa kadiri na uwezo wake. Na hakuna mtu isipokuwa ana
makosa na hukosea. Mtu kuwa na subira ni katika tabia ya muumini.
Muulizaji:
Anauliza pia kuhusiana na Kauli ya Allaah:
م ا���دال ز ��ن زوج وآ���م إ�داھن� ��ط�را '4 23�ذوا )0� /�.�وإن أرد�" وج )�
"Na mkitaka kubadilisha mke mahali pa mke, na hali mmoja wao mmempa
chungu ya mali, basi msichukue katika hayo kitu chochote." (04:20)
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
27
Ndio, akitaka (kubadili mke), iwe ni kwa sababu miongoni mwa sababu.
Haifai kwake (mume) kumbadili (kumtaliki) mke ambaye kamhudumia na
wakaishi naye, isipokuwa iwe kwa sababu inayomlazimu kwa hilo, hapo
atakuwa halaumiki.
Chanzo: http://youtu.be/7BKHeJNFkZI
27. Ikiwa Ni Radd Ya Haki, Haijuzu Kwako Kuiacha
Swali:
Nitapoona ya kuwa Radd itamghadhibisha na kumkasirikisha mtu fulani. Je,
kuna maslahi ya kuacha kumpiga Radd hata kama ni Radd ya haki?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ikiwa ni Radd ya haki, haijuzu kwako kuiacha. Mwenye kukasirika kwa ajili
ya Radd ya haki, mtu huyu hana kheri yoyote. Wewe usijali kuridhika kwake
na kukasirika kwake. Bali unatakiwa kujali haki ya Allaah (Subhaanahu wa
Ta´ala). Ni lazima kwako kubainisha haki bila ya kuogopa lawama za wenye
kulaumu. Ikiwa kuna kheri yoyote, atafurahi kwa hili. Ama ikiwa hakuna
kheri yoyote, usimjali.
Chanzo: http://youtu.be/SnXLKAuNr-8
28. Shaykh as-Suhaymiy Kuhusu Facebook
28
Shaykh Dr. as-Suhaymiy:
Mfano wa hayo makundi mengine ni la kisiasa, ambalo linalingania watu
kwenye maandamano. Na hiyo ni alama miongoni mwa alama za Khawaarij
Qudaamah, wao na wanaowasaidia wote, na wanaopita katika njia yao au
kuwanusuru kupitia Internet, sawa ikiwa ni (tovuti) iitwayo Facebook au
nyinginezo katika vifaa ambavyo vimekuwa ni sumu na maskani mwa watu
waasi na Ahl-ul-Bid´ah, vibaraka vya Mayahudi na Manaswara ambao
wamefanya ufisadi katika miji mingi. Hakika kuwasaidia ni katika
kusaidizana katika dhambi na uadui. Allaah (Ta´ala) Amesema:
=وى و; �8�و�وا �: ا9(م وا 8دوان �� �ر< وا و�8�و�وا �: ا
"Na saidianeni katika wema na uchaji Allaah. Wala msisaidiane katika dhambi
na uadui." (05:02)
Miongoni mwa hayo makundi maovu pia, ni yale makundi ambayo yanaona
lengo (nia) nzuri inamjuzishia mtu njia. Wanaruhusu mambo ya Haramu kwa
ajili ya kufikia mambo yao maovu.
29. Mwanachuoni Tu Ndiye Awezae Kupiga Radd?
Swali:
Upi usahihi wa maneno ya baadhi ya watu:
"Hapigwi Radd mwanachuoni isipokuwa tu na mwanachuoni mwenzake?"
´Allaamah Rabiy´ al-Madkhaliy:
29
Maneno haya ni makosa. Ina maana anyamazie kosa ikiwa hakupatikana
mwanachuoni wa kubainisha haki, na ikawa mdogo huyu (anaepiga Radd)
ana hoja na dalili! Ni wajibu kwake kubainisha aliyo nayo (dalili na hoja).
Nukta muhimu ni kuwa mwanachuoni na mwanafunzi haongei isipokuwa
kwa elimu, na wala haingii katika jambo lolote isipokuwa kwa elimu.
��ر وا @ؤاد � )+ وا �� ل" أو ـ.ك ��ن 0� )�ؤو; و; �=ف )� �س ك �0 �م إن� ا
"Wala usiyafuate usiyo na ujuzi nayo. Hakika asikio, na macho, na moyo -
hivyo vyote vitaulizwa." (17:36)
Kusema mambo usiyoyajua sawa hata ikiwa ni mwanachuoni,
maneno hayo mbali na wala hayakubaliwi na ni Haraam; na yanaweza kufikia
katika daraja ya Shirki kubwa kwa Allaah (´Azza wa Jalla). Kama Alivyosema
Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala):
م ر�<& ا @وا�ش )� ظDر )�D� و)� )� �ر� �H�ر ا �ق< وأن �/ر� �ل إ�� &H� وا�طن وا9(م وا
ل �0 ��ط��� وأن �=و وا �: م ��ز< �( 0 �ـ���0 )� ; 8��)ون ا �ـ�
“Sema: “Hakika Mola wangu Ameharamisha fawaahish (al-kabaair;
madhambi makubwa, ueasharati, zinaa, liwati, n.k.) yaliyodhihirika na yaliyo
ya siri, na dhambi (za kila aina), ukandamizaji bila ya haki, na
(Ameharamisha) kumshirikisha Allaah kwa chochote kile ambayo
Hakukiteremshia dalili, na kusema juu ya Allaah yale ambayo hamyajui.”
(07:33)
Ibn-ul-Qayyim anasema katika Tafsiyr yake kwamba "Hakika Allaah katika
Aayah hii Kafanya mambo hayo kuanzia madogo kwenda kwenye makubwa;
na kubwa ya madhambi hayo ni kusema juu ya Allaah pasina elimu. Kwa
kuwa inaingia katika Shirki, Kufuru, Bid´ah na inaingia katika maasi n.k.
Chanzo cha balaa zote ni mtu kusema juu ya Allaah pasina elimu, na kusema
kwa jila la Allaha na kwa jina la Dini Yake pasina elimu. Ikiwa kuna
30
mwanafunzi ambaye ana elimu katika jambo fulani na ana dalili ya jambo hilo
- na wanachuoni hawakuongelea jambo hilo, anatakiwa aseme haki.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=c4K4aLHLKXY
30. Shubuha Zinazotumiwa Na Wale Wanaopinga Radd
´Allaamah al-Fawzaan:
Na kwa hili kuna UWAJIBU wa kumradi anaekwenda kinyume, kinyume na
wanavyoseme baadhi ya watu acheni Ruduud, waacheni watu kila mmoja na
abaki na maoni yake na heshima yake, uhuru wa maoni na maneno. Kwa haya
Ummah utaangamia, kwa haya Ummah utaangamia. Salaf
hawakuwanyamazia mfano wa watu kama hawa, bali waliwafedhehesha na
kuwapiga Radd, kwa kujua kwao khatari yao kwa Ummah.
Sisi hatuwezi kunyamaza kwa shari yao, ni lazima kwetu kubainisha yale
Aliyoyateremsha Allaah. La sivyo tutakuwa wenye kuficha, wale ambao
Allaah kasema kuwahusu:
�@ �� ف �D)� إن� ا و� ��ت أو ا �)ر 'K 4��ح �0� أن �ط� 0 ')ن M�� ا ع 2�را 'Pن� وا )روة )ن /�8.ر ا �ـ� و)ن �طو�0 /��ر ��م ا �ـ�
"Hakika wale ambao wanaficha yale Tuliyoyateremsha katika Hoja zilizo
wazi na Hidaaya baada ya kuwa Tumeyabainisha kwa watu katika Kitabu,
hao Anawalaani Allaah na wanalaaniwa na kila mwenye kulaani." (02:159)
Jambo hili haliishii kwa Mubtadi´ah, bali linawapata pia watu
wanaowanyamazia. Mwenye kuwanyamazia (watu wa Bid´ah) dhambi
inampata na adhabu. Kwa kuwa ni wajibu kubainisha, kuwawekea watu
wazi. Na hii ndio kazi ya Ruduud za kielimu. Ruduud za kielimu zilizoenea
31
kwenye Maktabah za Waislamu, zote zinasafisha (upotofu) kwenda katika
Njia iliyonyooka na zinatahadharisha dhidi ya watu hawa. Tusipandikizwe
fikra hii; uhuru wa maoni, uhuru wa maneno, kuheshimia wengine na
mengineyo.
Sisi makusudio yetu sio kuwaingilia watu, makusudio yetu ni haki.
Makusudio yetu sio kuwajeruhi watu na kutoa aibu za watu, makusudio yetu
sisi ni kubainisha haki. Hii ni amaana Allaah Kawapa nayo wanachuoni.
Haijuzu kunyamazia watu mfano wa hawa.
Lakini kwa masikitiko makubwa, kunapotokea mtu akawapiga Radd mfano
wa watu kama hawa, wanasema "Wewe una pupa, wewe una hili na lile, huyu
hastahiki kupigwa Radd, ungemnyamazia jambo hili lisingejulikana." Na
mfano wa maneno hayo ya kutia wasiwasi. Huyu hawezi kusitisha
wanachuoni kubainisha kwa watu shari ya watu hawa Madu´aat wapotofu.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=aw1awpALjGo
31. ´Allaamah an-Najmiy Kuhusu Yule Anaewatuhumu Maimamu Watatu
Kuwa Ni Murji-ah
Swali:
Baadhi ya watu waliolelewa kwa vitabu vya Suruuriyyah na Hizbiyyah,
wanawatuhumu maimamu watatu - Ibn Baaz, Ibn ´Uthaymiyn na Al-Albaaniy
(Rahimahumu Allaah) - Irjaa´ kwa kuwa hawawakufurishi watawala.
Unasemaje kuhusu hili?
´Allaamah Ahmad an-Najmiy:
Huu ni ujinga na upotofu. Hawa watu wa Bid´ah kila siku wanajitokeza kwa
picha nyingine. Ikiwa Al-Albaaniy, Ibn Baaz na Ibn ´Uthaymiyn ambao ni
32
wanachuoni wa Ummah, viongozi na wakubwa, ni Murji-ah - nani aliebaki?
Ni nani aliebaki? Kuna yeyote aliebaki? Hapakubaki hata mmoja. Huu ni
msiba, haya ni magonjwa. Ninavyoona kuhusu watu hawa ni kuwa,
anaeonekana na kauli kama hii, akamatwe, atiwe adabu na apigwe. Ikiwa
hakujirudi, pengine kunahitajika kutumiwa mfumo mwengine.
Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=132786
32. Nasaha Ya Shaykh Fawzaan Kwa Dada Ambaye Anapata Tabu Kwa
Ajili Ya Dini Yake
Swali:
Allaah (´Azza wa Jalla) Kaniongoza baada ya kusikilia muhadhara wa mmoja
katika wanachuoni kuhusu Aakhirah. Baada ya siku hii nilihisi utamu wa
Imani na tangu sasa naishi maisha mengine ya raha na mafanikio na raha na
watoto wangu. Nawafunza Kitabu cha Allaah na kuwaita kwa Allaah na
kumkumbuka Allaah katika hali zote.
Pia nilianza kuvaa mavazi ya Kiislamu ambayo yanaendana na mwanamke
wa Kiislamu. Lakini pamoja na uzito wote huu na njia hii mpya
nimeyochukua, familia yangu, ndugu zangu wote katika familia wananiona
kama mgonjwa na ni mwenye wasiwasi. Ndio maana nimemtumia swali
langu bwana muheshimiwa Shaykh Swaalih ili anifanye kubaki kwenye
thabati na msimamo.
´Allaamah al-Fawzaan:
Hii ni bishara ya kheri kwa mwana mke huyu ambaye aliathirika kwa
muhadhara mzuri. Allaah Amjaze alieutoa kheri. Namna hii yatakikana
muhadhara kuwa, iwe ni wenye kuibainisha Dini hii na kubainisha fadhila za
33
Dini hii na kuvutia watu kwayo. Muhadhara usizungumzia mambo mengine,
kuingia kwenye siasa na mfano wa mambo kama hayo ambayo yanapoteza tu
muda wa watu na linawaathiri na wala hawastafidi kitu. Bali wanadhurika.
Namna hii unatakiwa kuwa mihadhara na khaswa khaswa kwenye Misikiti.
Khutbah za Ijumaa na mawaidha iwe namna hii. Ikumbushe Allaah (´Azza wa
Jalla), ikiwafunza watu wasioyajua katika mambo ya Dini yao.
Na wewe mwanamke uliposema ya kwamba umetubu kwa Allaah na ukawa
na msimamo katika Dini ya Allaah na ukashikamana na Hijaab, jua kuwa hili
ni kheri kwako na maisha yako ya sasa na si kama maisha yako ya kwanza.
Maisha ya uongofu na Imani. Ni juu yako kuwa na msimamo na kuendelea
kwa hili. Jizidishie Imani. Jizidishie kusikiliza mihadhara mizuri na Dhikr.
Usibabaishwe na watu hawa waharibifu ambao wanataka kukurudisha
nyuma na uache neema Aliyokupa nayo Allaah. Hawa ni katika Mashaytwaan
wa kibinaadamu ambao wanapoteza watu na wanawakimbiza katika kheri.
Ni juu yako kushikama imara na Dini yako na kuwa na subira kwa uliyomo.
Ni juu yako kujifunza elimu yenye manufaa ili iwe kutubu kwako na ´Ibaadah
zako zimejengeka juu ya Baswiyrah na juu ya elimu yenye manufaa.
Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=133391
33. Je Awwaam Ni Salafiyyuun?
Swali:
Je ´Awwaam Waislamu tunaweza kuwaita Salafiyyuun?
Shaykh Dr. Muhammad al-Madkhaliy:
34
Hapana. Itategemea na hali zao na mji waliyomo. Mtu ataangalia mji
waliyomo. Ikiwa wengi wao ni hivi, basi ni ndiyo. Na ikiwa wengi wao wako
katika Bid´ah, hapana.
Chanzo:
http://ar.miraath.net/sites/default/files/fatawah/questions/q&a_Almadkli
_...
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=IfT1EJQybiY
34. Jabriyyah Na Jahmiyyah Ni Watu Wa Bid´ah Au Makafiri?
Swali:
Kumekuja maswali mengi yanauliza kuhusu Jabriyyah na Jahmiyyah ni watu
wa Bid´ah au ni makafiri?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ni watu wa Bid´ah. Ama makafiri ni kama nilivyowaambia, mwenye
kukusudia khaswa na analingania katika madhehebu yake potofu huyu ni
kafiri. Ama mfuata kichwa mchunga huyu hakufurishwi, lakini ni mpotofu na
abainishiwe haki.
Chanzo: http://alfawzan.ws/sites/default/files/tg--1431-11-04_0.mp3
Tarehe: 1431-11-04/2010-10-11
35
35. ´Awwaam Watahadharishwe Dhidi YaWatu Wa Bid´ah
Swali:
Je ni katika misingi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kutahadharisha dhidi ya
Ahl-ul-Bid´ah?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Ama kutahadharisha Ahl-ul-Bid´ah, atahadharishwe yule asiyejua njama zao.
Ama mwenye kuijua, hahitajii mwenye kumtahadharisha nazo. Na watu
wengi wanaweza kuwa hawajui hali za Ahl-ul-Bid´ah, na hawajui ahkaam za
mapenzi juu yao na chuki juu yao. Na Bid´ah chafu na zakikafiri zinaingia
katika kauli ya Allaah (Jalla wa ´Alaa):
0 ور�و ون )ن ��د� �� وا �وم ا2Rر �واد" �S�� ; K�د �و)� �ؤ)�ون
”Huwakuti watu wanao muamini Allaah na siku ya Mwisho kuwa
wanawapenda wanao mpinga Allaah na Mtume Wake.” (58:22)
Bid´ah za kikafiri ni kumpinga Allaah na Mtume Wake.
Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=129784
36. ´Allaamah al-Fawzaan Kauli Ya as-Suwaydaan Kupingana Na Allaah Na Mtume Wake
Twaariq as-Suwaydaan:
36
"Nukta nyingine kuhusiana na uhuru, ni uhuru wa kutabiri. Ni katika haki za
watu kusema watakalo ilimradi tu hawajaharibu tabia kama kulingania katika
fikra mbali mbali, kuwa na kipingamizi kwa mji, mtawala hata Uislamu. Mimi
sina tatizo nalo. Hata kuwa na kipingamizi kwa Allaah (Ta´ala) na Mtume wa
Allaah."
Twaariq as-Suwaydaan:
"Ni katika haki ya mtu kuchagua Dini na pote apendalo. Akitaka kuwa Shia,
Sunniy, Durziy... Yuko na uhuru. Na ni haki ya kila mtu kuabudu Mungu
amchaguaye kwa njia aipendayo. Kanisa zisikatazwe. Hekalu zisikatazwe. Ni
katika haki za watu."
Twaariq as-Suwaydaan:
"Mimi hata hadd [adhabu] ya kuritadi sioni kama ni ya kidini. Naona ni kama
adhabu ya kisiasa tu."
Swali:
Kumedhihiri baadhi ya Madu´aat wasemao hadd ya kuritadi ni jambo la
kisiasa na si jambo la kisasa. Pia anasema kuwa inajuzu kuwa na kipingamizi
kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) bali hata kwa Allaah (´Azza
wa Jalla). Ipi hukumu ya kauli yake? Je ni kuritadi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Bila shaka. Hakuna kuritadi baada ya huku. Anayemfanyia mzaha Allaah,
Mtume Wake na Ahkaam za Kishari´ah. Hakuna baada ya kuritadi kama
huku. Hii ni aina mbaya ya kuritadi.
Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=129316
37
37.´Allaamah ´Abdul-´Aziyz Aal ash-Shaykh Kuhusu Kauli Ya as-Suwaydaan Uhuru Wa Dini
Swali:
Nimesikia baadhi ya Madu´aat wakisema inajuzu kuwa na kipingamizi kwa
Allaah, Uislamu na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Na anasema
tuache watu wachague Dini na waabudu wapendacho. Na anataka
waondoshe adhabu ya kuritadi na anataka kuachwe kujengwe kanisa katika
miji ya Waislamu. Ipi Radd yako shaykh?
´Allaamah ´Abdul-´Aziyz Aal ash-Shaykh:
Sijui maneno haya wayasemayo wanayasema kwa akili na Dini au upumbavu
na maradhi ya nyoyo. Je, haya yanatokwa na mtu aliyekosa Imani au kwa mtu
asiyejua alisemalo? Vipi tuwe na kipingamizi kwa Allaah? Allaah (Jalla wa
´Alaa) Katuamrishakumtii na kumtii Mtume Wake:
�ول �D ا �ذ�ن آ)�وا أط�8وا � وأط�8وا ا ر� �� أ�"
”Enyi mlioamini! Mtiini Allaah, na mtiini Mtume.” (04:59)
�D ا �ذ�ن آ) �وا أط�8وا � ور�و 0 و; �و �وا 0� وأ��م ��)8ون �� أ�"
”Enyi mlioamini! Mtiini Allaahna Mtume wake, wala msijiepushe naye, nanyi
mnasikia.” (08:20)
)وك '�)� /Kر �D��م >��� : � �#�ت و���<)وا ����)�'4 ور�<ك ; �ؤ)�ون ��� �( >( �Kم �رD�@�دوا '& أK� ; �م)
38
”La! Naapa kwa Mola wako! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye
muamuzi katika yale wanayokhitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo
zao juu ya hukumu utayo toa, na wanyenykee kabisa.” (04:65)
Akiwa na kipingamizi kwa Allaah akikusudia kukataa maneno ya Allaah na
Sunnah ya Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kupa
kipaumbele rai na matamanio kabla ya Kitabu na Sunnah, ni upotofu na
inaweza kumfanya mtu akaritadi. Tunawajibika kuamini.
0 وا )ؤ)�ون �لU آ)ن ��S و)T.0�� و���0 ور�� >� �ول �)� أ�زل إ 0� )ن ر� ��0 آ)ن ا ر� ق ��ن أ�د )<ن ر" 0 ; �@ر< �� ��وإ �ك ا )��ر و�� وا �)8�� وأطV ��8@را�ك ر
”Mtume ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola Wake, na
Waumini vile vile. Wote wamemuamini Allaah, na Malaika Wake, na Vitabu
vyake na Mitume Wake. Hatutafautishi baina ya yeyote katika Mitume Wake,
na (Waumini) husema: “Tumesikia na tumetii. Tunakutaka maghfira Mola
Wetu! Na marejeo ni Kwako”.” (02:285)
Haya maneno yana uchafu kama kipingamizi kwa Allaah na Mtume Wake, au
uhuru wa Dini!! Dini zote zimefutwa baada ya Allaah Kumtuma Muhammad
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Shari´ah yake imekhatimu Shari´ah zote
za kabla na kufuta Dini zingine zote. Ikawa ni wajibu kwa viumbe vyote
kumtii Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kufuata Sunnah
zake. Anasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
"Hatosikia yeyote kuhusu mimi si myahudi wala mnaswara kisha asiniamini
ila ataingia Motoni."
Kwa kuwa Muhammad ndiyo Mtume na Nabii wa mwisho. Tunaamini
Mitume wote waliotangulia na Risalah zao. Lakini ´amali na utekelezaji ni
kwa mujibu wa Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
39
Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=129316
38. Haitoshi Kujiita Tu Salafiy
Swali:
Baadhi ya watu wanamkataza mwenye kusema (kujiita) "Sisi ni Salafiyyuun"
na "Athariyyuun". Je, kukataza huku kunafaa? Na je, inajuzu kujinasibisha na
Salafiyyah, Athariyyah na Jaamiyyah au ni pote katika vipote?
´Allaamah al-Fawzaan:
Sijui Jaamiyyah. Hakuna kundi liitwalo Jaamiyyah. Hili ni jina lililozushwa.
Halina asili. Kila mwenye kuwakhalifu [Mubtadi´ah] kwa jambo,
wanamchukia na kumpanga majina. Achane mambo haya. Ama kujinasibisha
na Salafiyyah, ni jambo zuri. Lakini lazima uwatambue Salafiyyah ni watu
gani. Wafuate kwa wema. Lakini unatakiwa kutambua madhehebu ya Salaf ili
uweze kuwafuata. Wala hakuna haja ya kujiita "Salafiy" kwa kujisifu. Usifanye
hivyo. Shikama na waliokuwemo Salaf (Wema waliotangulia) na wala
usijitakase nafsi yako ewe ndugu.
Chanzo: Fadhl-ul-´Ilm wal-´Ulamaa'
Källa: http://alfawzan.ws/allmohadrat
39. Nasaha Za al-´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy Kuhusu Baadhi Ya Mashaykh
´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy:
40
Na ukitatizika na kitu wasiliana na wanachuoni waheshimiwa. Kama Shaykh
Ibn Baaz, Kama Shaykh Al-Albaaniy, Kama Shaykh Swaalih bin Fawzaan,
Kama Shaykh Rabiy´. Na mfano wa hawa ndugu zetu waheshimiwa wasiliana
nao na ustafidi kwao. Baaraka Allaahu fiykum. Hii ndo nasaha yangu kwa
ndugu zangu Waislamu. Na ninamuomba Allaah Atuhifadhie dini yetu na
Atufishe sote Waislamu.
Chanzo: http://muqbel.org/sounds.php?sound_id=8
40. Ni Yapi Madhehebu Ya al-Ikhwaan al-Muslimuun?
Swali:
Baadhi ya ndugu huenda wanatumia kauli yako kuwa kijana wa ki-Afghaniy
ni Malaika, na wanadai kuwa unawafananisha waabudu makaburi na
makhurafi kama Malaika Watukufu. Tunaomba tanbihi ya hili?
´Allaamah Rabiy´ al-Madkhaliy:
al-Ikhwaan al-Muslimuun ndio wanasema hivi na si mimi. Ni makhurafi.
Mimi niliona kwa macho yangu makaburi na mlolongo mkubwa. Niliona hili
kwa macho yangu. Na kulikuwa ujinga, ukhurafi na Bid´ah. al-Ikhwaan al-
Muslimuun hapa walikuwa na makhurafi, na wanakuwa baina ya Salafiyyah
na mapote yote. Na wanaharibu kwa ajili ya hili. al-Ikhwaan al-Muslimuun ni
watu waovu watu wa shari. Wao ni khatari kuliko hata makhurafi. Wao
madhehebu yao itategemea na madhehebu ya mji waliopo. Kuna mmoja
anasema:
"Ninashahidilia kuwa ´Aliy ndio mpenzi wa Allaah."
Anapokuja mtu wa Yemen, anasema:
"Njooni katika kheri za Yemen."
41
Kunapokuja kundi la Salafiyyuun, wanasema:
"Njooni katika mafanikio."
Hapana ndo walivyo. Katika kila mji na kila kundi wanakuwa na Dini yao. Na
walipokuja katika mji huu [Saudia] hivyo wakawa hawana budi kuwa
Salafiyyuun. Tatizo Iran ndo ndugu zao. Na Mayahudi ni ndugu zao na
Manaswara ni ndugu zao. Wanasema hivi kweli. Bali kasema hivi al-Banna.
Muulizaji:
Alisema pia Suufiyyah ni Salafiyyah.
´Allaamah Rabiy´ al-Madkhaliy:
Hapana! Alisema:
"Hakuna baina yetu sisi [Waislamu] na Mayahudi uadui wa kidini, bali Qur-
aan imetuamrisha kinyume chake. Na Uislamu ni Dini ya kibinaadamu. Na
Qur-aan imefanya baina yetu sisi na wao ushirikiano."
´Allaamah Rabiy´ al-Madkhaliy:
Hii ni kufuru. Hii ni kufuru tunaomba kinga kwa Allaah. Anaikadhibisha
Qur-aan.
��د وا���� أ����ا � �,+&ن أ�& ا��(س '&اوة �"��� آ ��ا ا�
“Hakika utawakuta walioshadidi kuliko watu wote katika uadui kwa
walioamini ni Mayahudi na washirikina.” (05:82)
��د وا��0(رى أو��(ء� �( أ��( ا���� آ ��ا 3 2,1�وا ا�
42
“Enyi mlioamini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristokuwa ni marafiki.”
(05:51)
Kisha huyu anasema eti ni ndugu zetu?
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=WPEJ_GRsQO0
41.´Allaamah Rabiy´ al-Madkhaliy Kuhusiana Na Maandamano
Swali:
Wanajuzisha baadhi ya watu maandamano ya amani dhidi ya mtawala
ambaye kakufuru na wanatumia hoja kwa kusema wanachuoni wamejuzisha
hilo. Je kauli yao hii ni sahihi?
´Allaamah Rabiy´ al-Madkhaliy:
Wanachuoni wamejuzisha tu kufanya Khuruuj kwa mtawala ambaye ni kafiri
dalili ziko wazi kama lionekanavyo juwa. Mpaka muone ukafiri wa wazi
kabisa wenye dalili kwa Allaah. Na demokrasia inaharibu Uislamu na si
katika Uislamu. Na maandamano si katika Uislamu. Na Waislamu hawafai
kufanya matendo kama haya. Kinachohitajika ni subira wakati wa fitina na
dhuluma za mtawala. Mpaka hapo Allaah (Ta´ala) Atapoleta nusra. Na kuna
kitabu - makala nimeandika kuhusiana na hili, wape ndugu wakisome na
wajue hukumu za Kishari´ah kwa demokrasia hizi na haya maandamano.
Mtajua hilo kwa dalili. Na nimebainisha upotofu wa wanaosema kuwa ni
katika Uislamu na ni katika kuamrisha mema na kukataza maovu. Madai haya
ni batili na si katika Uislamu. Bali katika Uislamu ni subira - kama
alivyotueleza hilo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na nimetaja kwa
dalili katika makala hii na mstaftafidi kwa jibu hili.
43
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=SI3eQTaASkg
42. Ipi Hukumu Ya Kuweka Camera Msikitini?
Swali:
Ipi hukumu ya kuweka camera Msikitini kwa ajili ya kuchunga amani?
´Allaamah Rabiy´ al-Madkhaliy:
Camera ni Haramu Msikitini na nje ya Msikiti, lakini kuiweka Msikiti ni
Haramu zaidi. Mwenye kutengeneza picha amelaaniwa, na watu wataokuwa
na adhabu kali siku ya Qiyaamah ni watengeneza picha. Na Malaika
hawaingii nyumba yenye mbwa au picha. Na Mtume kakazia sana suala hili la
picha zaidi kuliko suala la Ribaa na watu waasi na matamanio. Ni watu wenye
adhabu kali siku ya Qiyaamah, watengeneza picha. Haya ndo makemeo
waliompa Fir´awn
آل >�'�ن أ�& ا�;�اب و��م 92�م ا�7('6 أد5"�ا
“Na itapofika Saa ya Qiyaamah patasemwa: "Waingizeni watu wa Firauni
katika adhahabu kali kabisa!”." (40:46)
Watu wanachukulia sahali suala la picha, wanaweka kwenye magazeti,
camera daima - unawaona Haram [Makkah na Madiynah] wanarekodi watu.
Ni vifuata mchunga vya Mayahudi na Manaswara, ni vifuata kichwa
mchunga vya Mayahudi na Manaswara. Wamesahau Sunnah ya Mtume
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), na makemeo yake makali kuhusiana na
picha na yanayofanana na hayo. Mtume (swallaSAllaahu ´alayhi wa sallam)
44
aliona Qaram - koti lililokuwa na picha, akakasirika sana na akaamrisha
walitoe (´alayhis-Salaam). Na picha leo kwenye magazeti na TV ni fitina
kubwa na ni jambo liko wazi kabisa. Na hili ndo alikataza Mtume (Swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam). Baraka Allaahu fiykum.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=Q2ndKI5bhDs
43. Masanduku Ya Swadaqah Msikitini
´Allaamah Rabiy´ al-Madkhaliy:
Nani kaiweka Msikitini? Yapi makusudio yao kuweka sanduku hii [ndani ya
Msikiti]?
Muulizaji:
Ni kamati.
´Allaamah Rabiy´ al-Madkhaliy:
Ni kamati?
Muulizaji:
Ni kamati ya Msikiti.
´Allaamah Rabiy´ al-Madkhaliy:
45
Je, huwa wakiweka sanduku Msikitini daima [kila siku] au ni siku ya Ijumaa
tu au lini?
Muulizaji:
Ni kila siku wanaweka Msikitini.
´Allaamah Rabiy´ al-Madkhaliy:
Kila siku!?
´Allaamah Rabiy´ al-Madkhaliy:
Naona hii ni njia ya Hizbiyyuun, si katika njia ya Ahl-us-Sunnah. Asli ya
kuomba omba ni Haramu! Na haijuzu isipokuwa katika hali ya dharurah -
Baraka Allaahu fiykum. Asli ya kuomba omba ni Haramu! Na mwenye
kukithiri kuomba omba atakuja siku ya Qiyaamah akiwa hana kipande cha
uso. Mmefahamu? Na hii ni njia ya Hizbiyuun - Baraka Allaahu fiykum. Yule
mwenye kutaka [... sauti haisikiki vizuri... ] na kuswali mwache aweze
kufanya hivyo, ama kumuomba omba hapana!
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=h23UFp2SudA
Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad, na ahli zake na
Maswahabah zake na watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah.