Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

79
1 Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz Imekusanywa Na Kufasiriwa Na: Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush

description

Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

Transcript of Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

Page 1: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

1

Fataawa Za Shaykh

al-Imaam Ibn Baaz

Imekusanywa Na Kufasiriwa Na:

Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush

Page 2: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

2

Swali:

Kuna kundi la at-Twariyqah at-Tijaaniyyah wanakusanyika kila siku ya

Ijumaa na Juma tatu na wanamdhukuru Allaah kwa Dhikr hii: "Laa ilaaha illa

Allaah", na mwisho wake wanasema: "Allaah! Allaah!" kwa sauti ya juu. Sijui

ni nini hukumu ya Kishari´ah kwa kitendo chao hichi?

Imaam Ibn Baaz:

at-Twariyqah at-Tijaaniyyah ni Twariyqah iliozushwa. Ni Twariyqah ya batili.

Wako na mambo ya kufuru. Haijuzu kuifuata, bali ni wajibu kuiacha.

Tunamnasihi yule aliyeshikamna nayo aachane nayo na ashikamane na njia ya

Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Njia iliyopita

Maswahabah wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Na

wakaipita maimamu wa Uislamu; kama mfano wa Imaam Maalik, Shaafi´iy,

Abu Haniyfah, Ahmad, al-Awzaa´iy, Ishaaq Rahawayh, ath-Thawriy na

wengine katika wanachuoni. Waliifuata njia hiyo, wakiwemo Ahl-us-Sunnah

wal-Jamaa´ah. Njia hiyo ambayo ni kumpwekesha Allaah na kumtakasia

´Ibaadah Yake, kusimamisha Swalah, kutoa Zakaah, kufunga Ramadhaan,

kwenda kuhiji Nyumba na kutii amri na makatazo aliyokuja nayo Mtume

Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hii ndio njia aliyokuja nayo

Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ama Twuruq as-

Suufiyyah ni wajibu kuziacha. Isipokuwa tu kile kitu ambacho kimeafikiana

na Shari´ah. Wakiwa na kitu kilichoafikiana na Shari´ah, kitachukuliwa kwa

sababu Shari´ah imekuja nacho. Ama kitu walichozua Suufiyyah kitaachwa.

Na katika hayo ni kule kukusanyika kwao na kuleta Dhikr za pamoja: "Allaah!

Allaah! Allaah!", au "Huu! Huu!". Yote haya ni Bid´ah na hayana asli. Ilikuwa

inatakikana kusema: "Laa ilaaha illa Allaah", au "Subhaana Allaah,

Ahmadulillaah, Laa ilaaha illa Allaah na Allaahu Akbar." Ama fujo za: "Huu!

Huu!", au "Allaah! Allaah!", haya ni Bid´ah na hayana asli. Nakunasihi ewe

ndugu muulizaji kuachana nao na ushikamane na njia ya Muhammadiyyah

aliyokuja nayo Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Nayo

Page 3: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

3

ni zile Dhikr maarufu; "Subhaana Allaah, Alhamdulillaah, Laa ilaaha illa

Allaah na Allaahu Akbar." Sawa ukiwa nyumbani kwako, Msikitini, njiani na

kila mahali. Kama ilivyokuja kutoka kwa Mtume Muhammad (Swalla

Allaahu ´alayhi wa sallam). Au wakakusanyika na kuanza kusema: "Allaah!

Allaah!", au "Huu! Huu!". Yote haya nu munkari.

Swali:

Ninapokuwa katika muda wa hedhi husoma Qur-aan zile Suurah

nilizohifadhi. Je, inajuzu kwangu kufanya hivyo?

Imaam Ibn Baaz:

Hakuna neno kufanya hivyo. Kauli yenye nguvu katika kauli za wanachuoni

ni kuwa inajuzu kwa mwenye hedhi kusoma Qur-aan bila ya kuushika

msahafu, asome kimoyoni kwa kuwa muda wa hedhi unakuwa mrefu na ni

hali kadhalika kwa mwenye nifasi. Hakuna ubaya akasoma kimoyoni. Ama

yule mwenye janaba, hapana. Mwenye janaba hasomi mpaka akoge, kwa

kuwa muda wake yeye ni mdogo na anaweza kukoga. Hali kadhalika kwa

yule mwenye hadathi ndogo. Asome kimoyoni na wala asisome katika

msahafu mpaka atawadhe.

Swali:

Je, ni wajibu kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kila pale

anapotajwa au hilo ni Sunnah?

Imaam Ibn Baaz:

Wajibu ni kumswalia pale anapotajwa jina lake (´alayhis-Swalaat was-Salaam).

Kutokana na yaliyothibiti kutoka kwake:

"Ameangamia yule ambaye litatajwa jina langu kisha asiniswalie."

Page 4: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

4

Hii ni dalili ioneshayo ya kuwa kumswalia ni wajibu kumswalia pale

anapotajwa (´alayhis-Swalaat was-Salaam).

Page 5: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

5

Swali:

Ni ipi hukumu ya Twuruq katika Uislamu? Kwa kuwa kuna ambao

nimewauliza wakasema kuwa ni Haramu, na wengine wakasema sio faradhi

wala Haramu. Naomba jibu la wazi Allaah Akuwafikishe.

Imaam Ibn Baaz:

Swali haliko wazi. Ikiwa muulizaji anamaanisha Twuruq as-Suufiyyah ni

munkari na Bid´ah; na baadhi yazo ni kufuru na zingine ni Bid´ah na sio

kufuru. Kwa kuwa njia ambayo ni wajibu kuifuata ni njia ya Mtume wetu

Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Anasema Allaah (Jalla wa

´Alaa):

بعوه ذا صراطي مستقيما فات ـ وأن ه

"Na kwamba hii njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni." (06:153)

ذا كتاب أنزلناه مبارك ـ بعوه وه فات

"Na hiki Kitabu (Qur-aan) Tumekiteremsha kilichobarikiwa, basi kifuateni."

(06:155)

سول فخذوه وما نهاكم عنه فانتهوا وما آتاكم الر

"Na lolote (lile) analokupeni Mtume (Muhammad (صلى هللا عليه وآله وسلم) basi

lichukueni, na (lolote lile) analokukatazeni, basi acheni." (59:07)

Wajibu kwa Waislamu ni kufuata mfumo wa Mtume Muhammad (Swalla

Allaahu ´alayhi wa sallam), na waelekee katika njia yake na Dini yake.

Anasema (Ta´ala):

بع ه فات ه ويغفر لكم ذنوبكم قل إن كنتم تحبون اللـ وني يحببكم اللـ

"Sema (ee Muhammad صلى هللا عليه وآله وسلم): “Mkiwa mnampenda Allaah, basi

nifuateni, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu." (03:31)

Njia ya Allaah iliyonyooka ni ile aliyokuja nayo Mtume wetu Muhammad

(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), na ndio njia waliyoneemeshwa kwayo.

Kama ilivyo katika Kauli Yake (Jalla wa ´Alaa):

راط المستقيم صراط الذين أنعمت عليهم اه دنا الص

Page 6: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

6

"Tuongoze katika njia iliyonyooka. Njia ya wale Uliowaneemesha" (01:06-07)

Nao ni Mitume, maswadiki, mashahidi na watu wema. Kama ilivyokuja

katika Kauli Yake (Ta´ala):

يق د بيين والص ن الن ه عليهم م ئك مع الذين أنعم اللـ ـ سول فأول ه والر اين ومن يطع اللـ هداء والص لحين وحسن والش

ئك رفيقا ـ أول

"Na atakayemtii Allaah na Mtume, basi hao watakuwa pamoja na wale

ambao Allaah Amewaneemesha miongoni mwa Manabii, na asw-Swiddiqiyna

na Mashahidi na (waja) wema, na uzuri ulioje hao kuwa ni rafiki (zake)."

(04:69)

Hii ndio njia ya sawa. Ama Twuruq as-Suufiyyah zina Shirki; kama

kuwaabudu baadhi ya Mashaykh wao, kuwaomba msaada baadhi ya

Mashaykh wao na yasiyokuwa haya katika Bid´ah zao nyingi. Kuna mmoja

katika wao anasema:

"Ni juu yako kujisalimisha kwa Shaykh huyu, kumpenda, na wala usimpinge

kwa lolote, na uwe kwake kama maiti kwa mwoshaji." Twuruq zote hizi ni

batili na potofu.

Swali:

Kulipitika majadiliano na maneno wakati wa ghadhabu baina yangu mimi na

mke wangu nikawa nimemwambia mara tatu: "Kuishi kwako wewe na mimi

ni Haramu" ilihali aliendelea kuishi nami. Je, nina kafara kwa hili?

Imaam Ibn Baaz:

Ni juu yako kwa hili kutoa kafara ya yamini. Kauli yako "Kuishi kwako na

mimi ni Haramu" ni juu yako utoe kafara ya yamini kwa jambo hili na wala

hulazimiki kitu baada ya hapo. Kwa kuwa hili hukumu yake ni yamini. Toa

kafara ya yamini; nayo ni kulisha masikini kumi, au kuwavisha au kuacha

mtumwa huru. Na kuwalisha maana yake ni kuwa utampa kila mmoja

takriban 1,5 kg katika tende au chakula kingine chochote ambacho

kimezoeleka mjini. Ukifanya hivi yatosheleza, Alhamduli Allaah. Na ni juu

Page 7: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

7

yko Tawbah na Istighfaar. Kwa kuwa Muislamu haijuzu kwake

kujiharamishia Aliyomhalalishia Allaah.

Swali:

Niliswali Dhuhr peke yangu, na katika Rakaa ya pili baada ya Suurat al-

Faatihah sikusoma Suurah nyingine katika Qur-aan kwa kusahau.

Nikakumbuka kabla ya kutoa Salaam nikasujudu Sijda mbili za kusahau. Je,

nina lolote katika hili?

Imaam Ibn Baaz:

Huna juu yako kitu. Na wala sio wajibu kuleta Sijda ya kusahau. Kwa kuwa

kusoma Suurah nyingine baada ya al-Faatihah sio wajibu, muhimu ni kusoma

al-Faatihah. Ama kusoma Suurah au Aayah baada yake ni jambo

lililopendekezwa tu. Hivyo akiiacha mtu sio lazima alete Sijda ya kusahau au

pindi atapoisahau. Swalah yake ni sahihi na wala haina neno.

Swali:

Kauli ya Allaah (Ta´ala):

يعلمون ل والذين يعلمون الذين يستوي هل قل

“Je, wanalingana sawa wale wanaouja na wale wasiojua?” (39:09)

Na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

"Wanachuoni ndio warithi wa Mitume (´alayhis-Swalaat was-Salaam)."

Je, makusudio ni wanachuoni wa utabibu, kemia au wasiokuwa hao? Au

makusudio ni wanachuoni wa Shari´ah?

Imaam Ibn Baaz:

Page 8: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

8

Makusudio kwa makubaliano ya wanachuoni wote ni ma´ulamaa wa Shari´ah,

wanaochukua kutoka katika Kitabu na Sunnah. Wana fadhila kubwa na kheri

nyingi. Ama kuhusiana na elimu ya udaktari, uhandisi na elimu zingine za

dunia zinazofafana na hizo, ni elimu ambazo watu wao hukumu yao ni kiasi

cha makusudio yao. Yule ambaye atajifunza uhandisi au udaktari ili

awanufaishe Waislamu dhidi ya maadui wao, huyu ni mwenye kupewa ujira

kwa kiasi cha nia yake. Hali kadhalika, kwa yule mwenye kusomea

uanaskari, vita ili aje kuwanufaisha Waislamu, au akasomea uanajeshi ili

makusudio yake ni kuwanufaisha Waislamu, huyu ni mwenye ujira na

hukumu yake itakuwa kama ya wanachuoni wa Shari´ah. Ujira itategemea nia

yake. Ama mwenye kusomea elimu ya dunia kwa makusudio ya kupata dunia

ili aweze kula, au kupata kazi na kuishi, hili limeruhusiwa na hana juu yake

kitu. Kwa kuwa Shari´ah imeamrisha kutafuta riziki. Lakini mtu huyu hawi

kama yule aliyejifunza ili aweze kula pato la Halali na ajitosheleze na

kuwaomba watu au awanufaishe Waislamu dhidi ya maadui wao, nia

inatofautiana. Mwenye kujifunza kwa nia nzuri atakuwa ni mwenye ujira. Na

mwenye kujifunza nayo ili ajiepushe na Haramu na achume pato la Halali, ni

mwenye ujira. Na mwenye kujifunza nayo, hana makusudio yoyote ila tu ili

apate kuishi, kula na kunywa, na makusudio yake sio kuwanufaisha

Waislamu, yeye kajifunza nayo kwa maslahi ya kidunia tu, huyu kwake

itakuwa inaruhusiwa tu.

Swali:

Nimeolewa na kijana na wala hakuniingilia baadae, na mimi kwa sasa nataka

Talaka kutoka kwake kwa sababu nyingi, miongoni mwanzo:Ni mtu

asiyekuwa na adabu na ni mjinga, wakati ninakaa nae katikatikatika kikao

ananishutumu na kunitukana mbele ya watu. Hili ni jambo la kwanza. Jambo

la pili, tokea tufunge ndoa imekuwa miezi mitano lakini hanihudumii jambo

ambalo linalilazimu kwenda kuwaomba wazazi wangu pesa. Na jambo la

tatu, ni kuwa ni mtu ambaye haswali na hata akiswali anaswali siku mbili na

anaacha kwa muda wa mwezi. Nifanye nini? Nimeshamnasihi mara nyingi.

Inajuzu kuomba Talaka au nitakuwa mwenye kupata madhambi?

Page 9: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

9

Imaam Ibn Baaz:

Ikiwa hali ni kama hii, kama ulivyotaja ewe dada muulizaji, anaswali wakati

fulani na wala haswali kwa muda mrefu, huyu haijuzu kwako kubaki naye.

Kwa kuwa kuacha Swalah ni kufuru kubwa kutokana na kauli yenye nguvu

ya wanachuoni, hata kama hakupinga uwajibu wake. Ni wajibu kwako

kuachana nae na wala haijuzu kwako kumwingilia wala kubaki katika ndoa,

bali ndoa hii ni batili kutokana na kauli yenye nguvu ya wanachuoni. Ni juu

yako [... sauti haiko wazi... ]. Na ikiwa hakukupa Talaka, ni juu yako kupeleka

kesi hii mahakamani watatue ila hii. pamoja na kwamba, umesema ana

mdomo mchafu wa kutusi na kulaani, hii ni ila nyingine. Lakini ila ya kuacha

Swalah ni kubwa na iliyo wazi zaidi.

Swali:

Qadhiya ya mume kusafiri na kumuacha mke zaidi ya mwaka au miezi sita na

kwamba hili ndani yake lina kitu kama mapungufu kwa upande wa mume,

pamoja na kuwa baadhi ya watu wanalazimika kusafiri na kwa ajili ya kutoka

kwenda kutafuta riziki. Anauliza hukumu ya hilo?

Imaam Ibn Baaz:

Hakuna ubaya kwa mume kusafiri kutoka kwenda kutafuta elimu au riziki na

wala hakuna mpaka wa (muda wa) safari yake, si kwa miezi sita wala

kinyume na hilo. Lakini afanye vovyote itavyowezekana kusafiri pamoja nae

ikiwa hali itaruhusu, hapo itatakikana kwake kusafiri nae ikiwa anaweza hilo.

Ama ikiwa haiwezekani, amuache mahali ambapo ni pa amani na asafiri

kutoka kwenda kutafuta elimu au riziki, na ajitahidi kuharakisha kumrudilia

ili awe nae karibu na wala asicheleweshe muda.

´Umar bin al-Khattwab (Radhiya Allaahu ´anhu) aliweka mpaka kwa mume

wa kubaki nje kwa kipindi cha miezi sita. Hiyo ilikuwa Ijtihaad yake. Akiweza

kumjia baada ya miezi sita, miezi mine, miezi mitano au mitatu, hili ni jambo

zuri. Na hali za wanawake zinatofautiana. Anaweza kuwa mahala pa amani

na wala hakhofiwi juu yake kitu hata safari ikiwa ndefu, na anaweza kuwa

Page 10: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

10

mahala ambapo si pa amani na anakhofiwa, katika hali hii inatakikana

kujitahidi kumrejelea na kutazama amani ya hali yake ilivo. Jambo hili

linatofautiana kutokana na hali ya mume na hali ya mke na hali ya nchi.

Swali:

Miaka mitano ya kabla nimeolewa na mwanaume mmoja hivi, na kabla ya

ndoa nimemuuliza kuhusu Swalah akanambia kuwa haswali na akaniahidi

kuwa ataanza kuswali baada ya ndoa In Shaa Allaah.

Lakini kwa masikitiko makubwa, baada ya ndoa imedhihiri kuwa hatimizi

ahadi yake na wala hatimizi Swalah za faradhi isipokuwa Swalah ya Ijumaa

peke yake ndio anaswali Msikitini. Na daima humuombea kwa kuwa mimi

namcha Allaah. Na nimesikia kuwa haijuzu kuishi na mtu ambaye ni kafiri

mwenye kuacha Swalah. Je, hili ni sahihi?

Imaam Ibn Baaz:

Ndio, haijuzu.

Swali:

Kuna mwanamke alienda mahakamani kuomba Talaka kuachana na mume

wake, wakamuuliza yuko wapi mume wako, akasema hayupo na wala sijui

alipo. Mahakama wakawa wamemuomba alete mashahidi wawili wathibitishe

hilo. Mashahidi hao wawili wakathibitisha ya kwamba bwana huyo hayupo

na kwamba hawajui alipokwenda. Lakini wao (mahakamani) wanajua kuwa

yupo katika mji huo na anafanya kazi, na ni wenye uhakika mkubwa kwa

hilo. Mahakama wakawa wamempa Talaka.

Baada ya hapo, akaolewa huyu mwanamke na mume wapili na mume wapili

anajua maudhui hii kuanzia mwanzoni. Ipi hukumu ya mashahidi wawili,

mwanamke huyu na mume wapili?

Page 11: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

11

Imaam Ibn Baaz:

Kesi hii wairudishe kwenye mahakama ambapo walihukumu, wawarejelee na

wawabainishie hali ya sasa na mahakama iangalie hukumu yake. Masuala

haya yanahusiana na mahakama, mahakama ibainishiwe hali ilivyo na

kwamba mume yupo, walidanganya wakati walisema kuwa hayupo. Kwa

vyovyote, kesi hii ipelekwe kwenye mahakama iliyohukumu mpaka waweze

kutazama hukumu yake.

Muulizaji:

Shaykh, vipi kuhusu madhambi?

Imaam Ibn Baaz:

Mashahidi ikiwa walidanganya (kwa kujua), wako juu yao na madhambi,

pamoja na manamke huyo.

Muulizaji:

Vipi na mume huyu wapili ambaye anajua hali ilivyo?

Imaam Ibn Baaz:

Na huyu pia ana madhambi. Na wala haijuzu kwake kumuoa naye anajua

kuwa mume wake bado yupo, akamchukulia haki yake.

Swali:

Alimtaliki mke wake Talaka tatu, kisha akamrejea na kuishi nae miezi mingi.

Kisha atamtaliki mara ya pili Talaka tatu, akabaki kwenye nyumba ya baba

Page 12: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

12

yake miezi miwili. Kisha akamrejea tena bila ya ndoa upya na bila ya kuolewa

na mume mwingine. Je, kumrejea kwake huku ni sahihi kwa hali hii au kuishi

nae ni Haramu?

Imaam Ibn Baaz:

Haya ni masuala makubwa na ya khatari. Tunaona kuwa, huyu muulizaji na

walii wa mwanamke warejee kwa Qadhiy walio naye huko Yemen, mpaka

Qadhiy aweze kuangalia maudhui hii na atutue tatizo hili na awakhabarishe

lililo la wajibu juu yao. Na wala haitoshi kulijibia hapa kwa njia ya idhaa.

Swali:

Ni upi usahihi wa mahala pa kaburi la Nabii Yuunus (´alayhis-Salaam) ni

Iraaq?

Imaam Ibn Baaz:

Ama Yuunus (´alayhis-Salaam) haijulikani kaburi lake na wala hili halina

usahihi. Bali makaburi ya Mitume wote hayajulikani,ila tu kaburi ya Mtume

wetu Muhammad (´alayhis-Salaam) inajulikana, alizikwa nyumbani kwake

Madiynah (´alayhis-Salaam).

Hali kadhalika kaburi la Mtume Ibraahiym (´alayhis-Salaam) alizikwa

Palestina. Ama wasiokuwa hao wawili, wamebainisha wanachuoni ya

kwamba hayajulikani makaburi yao. Na mwenye kudai ya kwamba hii ni

kaburi ya fulani au fulani, ni muongo. Halina asli wala usahihi. Na mwenye

kusema kaburi la Yuunus liko mahali fulani, halina asli. Inatakikana lijulikane

hili.

Swali:

Page 13: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

13

Nimesoma Hadiyth katika baadhi ya vitabu vya Du´aa ya kwamba mwenye

kusoma Suurat ad-Dukhaan usiku, watamuombea maghfirah Malaika 7.000.

Upi usahihi wa Hadiyth hii?

Imaam Ibn Baaz:

Sijui usahihi wake. Haina asli kutokana na ninvyojua.

Swali:

Je, ni sahihi kwangu kufanya ndoa na msichana wa shangazi yangu au

hapana?

Imaam Ibn Baaz:

Kufanya ndoa na msichana wa shangazi na mjomba, wote hawa inajuzu. Lililo

la Haramu ni kumuoa shangazi yako au mama yako mdogo. Ama msichana

wa shangazi yako na mtoto wa mjomba, hakuna ubaya wa hilo.

Swali:

Nilianza kupata ndoto nilipokuwa na umri wa miaka 13, na sikuswali wala

kufunga ila nilipofikisha miaka 15, na hilo ni kutokana na ujinga wangu. Je, ni

juu yangu kulipa Swalah na Swawm ya miaka miwili hii iliyopita au hapana?

Imaam Ibn Baaz:

Mtu akibalaghe miaka kumi na tatu kwa kuteremsha manii, kisha akaacha

Swalah na Swawm kwa ujinga, hana juu yake kulipa. Kwa kuwa kuacha

Swalah ni kufuru. Ni juu yako kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jalla). Mtu

Page 14: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

14

aliyebaleghe kuacha Swalah ni kufuru kubwa kwa wanachuoni wahakiki, na

hii ndio Ijmaa´ ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum).

Na linatolewa dalili hilo na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa

sallam):

"Ahadi iliopo baina yetu sisi na wao (makafiri) ni Swalah, atakayeiacha

kakufuru." (Hadiyth Swahiyh, kaipokea Imaam Ahmad na Ahl-us-Sunan)

Kauli yake tena (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

"Baina ya mja na baina ya kufuru na Shirki ni kuacha Swalah." (Kaipokea

Muslim)

Tawbah inatosha, maadam katubu kwa Allaah Tawbah ya kweli, inatosha na

huna juu yako kulipa, si Swawm wala Swalah. Kwa kuwa aliyeritadi halipi

kitu, na mwenye kuacha Swalah anazingatiwa kuwa ni mwenye kuritadi

kutokana na kauli sahihi ya wanachuoni. Ni juu yake kutubu kwa Allaah

upya na wala asilipe kitu. Achunge jambo hili katika Mustaqbal, kwa kuleta

Tawbah ya kweli na kujilazimisha na ´amali njema.

Swali:

Nimemuapia mke wangu Talaka kwenye mkanda na nikamtumia nao, na

kusema: "Ni juu yangu Talaka ikiwa sintoenda na nikachukua kiwango hichi

kwa kaka yako, basi mimi nitakuwa nimekutaliki." Na baada ya hapo

nikasafiri kwenda Misri na sikufanya lolote kuhusiana na yamini hii. Naomba

faida.

Imaam Ibn Baaz:

Ikiwa kwa yamini hii, ulikusudia nafsi yako usifanye kitu hiki, au ulikusudia

uweze kufanya kitu hiki. Ikiwa makusudio ni kuihimiza nafsi yako kufanya

au kutofanya kitu, na makusudio haikuwa kufarakana nae na kumtaliki,

hukumu ya hili ni hukumu ya yamini kutokana na kauli sahihi ya

wanachuoni. Ama ikiwa ulikusudia kupita kwa Talaka ikiwa utafanya au

Page 15: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

15

hutofanya, katika hali hii Talaka inapita ikiwa hukufanya. Ikiwa kama

ulikusudia kupita kwa Talaka.

Swali:

Nilioa nami nilikuwa bado mdogo, na baada ya kuoa kwa takriban miezi

kama mitatu nikwamwambia mke wangu mara nyingi: "Mimi sikutaki!".

Waambie wazazi wako kuwa mimi sikutaki", pamoja na kuwa ni mke

mwema. Na sasa sijui maneno niliyomwambia mke wangu huchukuliwa

nimemtaliki au hapana? Kwa kuwa sikukusudia kumtaliki kwa kumwambia

hivyo. Na ikiwa kama nimemtaliki, je nifunge nae ndoa upya kwa mara ya

pili?

Imaam Ibn Baaz:

Maneno haya haiwi Talaka, uliyasema bila ya kukusudia hivyo, haiwi Talaka.

Maadamu hakunuwia Talaka, si Talaka. Bado ni mke wake.

Muulizaji:

Je, ana kafara yoyote kwa hilo?

Imaam Ibn Baaz:

Hana juu yake kitu.

Swali:

Mke wangu alienda kwenye nyumba ya jirani mmoja nikakariri kumtaliki

kwa sababu ya kwenda kwake bila ya idhini yangu. Nikamwambia chukua

kila chako kwenye nyumba hii na mimi ni Haramu kwako. Lakini wazazi

Page 16: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

16

wangu wawili hawakukubaliana na mimi, wakanambia: "Wewe ndiye utatoka

kwenye nyumba hii na yeye (mke wako) atakaa na sisi". Sikutamka Talaka

lakini nilimwambia tu: "Mimi ni Haramu kwako." Nimewauliza baadhi ya

watu wakanambia kuwa hii sio Talaka na wala sina juu yangu kafara.

Naomba unipe kauli ya sahihi katika maudhui hii.

Imaam Ibn Baaz:

Ikiwa hali ni kama alivyosema muulizaji, hakika juu yako una kafara ya

Dhwihaar kwa kauli yako: "Mimi nimeharamika kwako". Ni kama mfano wa

kusema: "Wewe ni kama mgongo wa mama yangu." Ni juu yako kutoa kafara

ya Dhwihaar ikiwa hukukusudia Talaka kwa kusema kwako hivi. Ikiwa kwa

hili hukukusudia Talaka, basi hukumu yake ni kama ya Dhwihaar. Kutokana

na kauli sahihi ya wanachuoni. Ni juu yako kutoa kafara ya Dhwihaar, nayo ni

kuacha mtumwa huru ambaye ni Muislamu, ikiwa hukupata utafunga miezi

miwili mfululizo, ikiwa hilo ni gumu kwako na wala huwezi, utalisha

masikini sitini ambao ni mafakiri. Kila mmoja utampa 1,5 kg ya tende, ngano

au chakula chochote ambacho kimechozoeleka hapo unapoishi. Kila masikini

mmoja utampa takriban 1,5 kg kabla ya kumgusa mke wako, kabla ya

kumjamii. Huu ndio wajibu wako ikiwa hukukusudia Talaka. Ama

uliposema: "Wewe ni Haramu kwangu" ikiwa ulikusudia Talaka, hili

kutokana na kauli sahihi, ni kwamba ni Talaka moja itakuwa imepita ikiwa

hapo mwanzo ulikuwa hujamtaliki, unaweza kumrejea kwa kusema:

"Nimemrejea mke wangu, au mimi namrejea mke wangu, au namrejea mke

wangu", au maneno mfano na hayo. Kwa kushuhudisha mashahidi wawili

waadilifu ya kwamba umemrejea.

Swali:

Mimi nina rafiki kazini, ananambia ameoa tangu miaka kumi. Na mwanzoni

wakati wa ndoa alikuwa haswali na sasa ameshakuwa na watoto watatu.

Ndoa hii ni sahihi au hapana? Na kwa sasa - Alhamdulillaah - anaswali.

Afunge ndoa upya?

Page 17: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

17

Imaam Ibn Baaz:

Ikiwa mke wake anaswali naye (mume) haswali, mke wake alikuwa ni

Muislamu na mwenye msimamo, anaswali naye (mume) haswali wakati wa

ndoa, ndoa hii si sahihi kwa wanachuoni wote. Kwa kuwa mwenye kuacha

Swalah ni kafiri, kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)

katika Hadiyth Swahiyh: Ahadi iliopo baina yetu sisi na wao ni Swalah,

atakayeiacha amekufuru." (Kaipokea Imaam Ahmad, Ahl-us-Sunan kwa

isnadi sahihi kutoka kwa Buraydah (Radhiya Allaahu ´anhu)

Na kapokea Muslim katika Swahiyh yake, kutoka kwa Jaabir (Radhiya

Allaahu ´anhu) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)

kasema:

"Baina ya mtu na baina ya kufuru na Shirki ni kuacha Swalah."

Ni wajibu kufunga ndoa upya kutokana na kauli yenye nguvu ya

wanachuoni. Na kuna wanachuoni wengine ambao wanaona kuwa hakufuru

kwa hilo ikiwa anaamini kuwa (Swalah) ni haki na ni wajibu, lakini kaiacha

kwa kuzembea na uvivu, wanaona kuwa ni muasi na ni kufuru ndogo, lakini

si kufuru kubwa. Kutokana na kauli hii ya pili, itakuwa si lazima kufanya

upya ndoa. Lakini kauli yenye nguvu inayosapotiwa na dalili, ni kuwa kufuru

yake ni kubwa. Itakuwa ni juu yake kufanya ndoa upya kwa njia za Kishari´ah

baada ya kutubia na Allaah Kumneemesha uongofu. Ama ikiwa mke wake

alikuwa ni kama yeye kipindi cha ndoa, naye alikuwa haswali, ndoa yao hii

itakuwa ni kama ndoa za Ahl-ul-Kitaab (mayahudi & wakristo) wengine.

Ndoa yao ni sahihi na wala kutakuwa hakuna haja ya kufanya upya. Itakuwa

ni juu yao wote wawili kutubu kwa Allaah kwa kuleta Tawbah ya kweli.

Swali:

Ipi hukumu ya madhiy yakiingia kwenye nguo, yaoshwe au yanyunyuziwe

maji na kusafisha?

Imaam Ibn Baaz:

Page 18: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

18

Madhiy ni najisi, lakini najisi yake ni khafifu. Akinyunyuzia maji kwenye

nguo yake, yatosha. Ama manii, ambayo ndio asli ya binaadamu, yanayotoka

kwa nguvu na kwa shahawa na ladha, haya ni Twahara. Yakiingia kwenye

nguo au mwili, utatwahirisha. Lakini, kuifanya nguo ikawa safi au kuiosha

kabisa ndio bora zaidi.

Swali:

Ipi hukumu ya mwenye kuswali au kutekeleza ´Ibaadah yoyote katika

´Ibaadah naye mkononi mwake amevaa hirizi?

Imaam Ibn Baaz:

Hirizi ni Haramu na wala haijuzu. Na ni katika Shirki ndogo, na inaweze

kwenda katika Shirki kubwa. Swalah yake ni sahihi, ikiwa hakuufanya moyo

wake kuitegemea hirizi hiyo na akaitakidi kuwa inadhuru na kunufaisha.

Hajatumbukia katika Shirki kubwa. Shirki ndogo haiporomoshi matendo

(yote), isipokuwa Riyaa tu ndio inaporomosha ´amali iliyochanganyika nayo.

Ama akivaa hirizi kwenye shingo yake au kwenye mkono wake... na at-

Tamiymah baadhi ya watu wanaiita kwa majina mbali mbali kukiwmo jina la

hirizi. Wanawavalisha watoto wao kuwakinga na kijicho, jini na huenda

akavalishwa hata mgonjwa. Yote haya ni makosa na hayajuzu.

Lakini halimzuii kusihi kwa Swalah yake kwa kuwa ni Muislamu, Swalah

yake ni sahihi. Na hili ni kosa lake, kwa kuwa ni katika Shirki ndogo na

makatazo. Na wala haiwi Shirki kubwa na wala haiwezi kwenda katika Shirki

kubwa isipokuwa tu ikiwa ataufanya moyo wake kuitegemea (hiyo hirizi) na

akaitakidi kuwa yenyewe ndio inaendesha, inaponya au inanufaisha yenyewe.

Na hii ni I´tiqaad khatari yake ni kubwa, ni Shirki kubwa. Lakini mara nyingi

Muislamu haamini hivyo, isipokuwa huwa anadhania kuwa ni katika

kuchukua sababu. Amesema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yeyote atakayevaa hirizi [au atakayejiambatanisha na kitu], basi Allaah

Hatomtimizia matakwa yake kutimia kamwe. Na yule atakayevaa au

kutundika chaza ndogo."

Page 19: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

19

"Yeyote atakayevaa hirizi kafanya Shirki."

Mtume kabainisha uharamu wa hirizi hii na uharamu wa kuivaa. Ni wajibu

kwa Muislamu kutubu kwa Allaah ikiwa amefanya hili. Hali kadhalika

muumini mwanamke atubu kwa Allaah kwa jambo hili na akate hirizi hii na

mtu atahadhari nayo kabisa. Hata kama itakuwa ni hirizi iliyo na Aayah za

Qur-aan. Ni wajibu kuikata. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa

sallam) kakataza hirizi na akaonya zote, na wala hakubagua hiriizi yoyote. Na

ni kwa kuwa, kuvaa hirizi ya Qur-aan ni njia inayopelekea katika kuvaa hirizi

nyinginezo.

Ni wajibu kufunga njia zote za Shirki. Hii ndio nasaha zangu kwa kila

Muislamu. Ya kwamba ni wajibu kwake kutahadhari na hirizi, na wala asiivae

na kuitundika popote pale; si kwenye bega lake, kwenye shingo yake, mtoto

wake, mkewake na kadhalika. Badala yake, ashikamane na Allaah na aombe

kinga na hifadhi kwa Maneno ya Allaah yaliyotimia kwa shari ya

Alivyoviumba na afanye sababu za Kishari´ah; Du´aa, dawa n.k., na

vinatosheleza. Na wala hakuna haja ya hirizi. Huu ndio wajibu kwa kila

Muislamu.

Swali:

Tatizo langu ni kuhusiana na mume wangu, ni mwanaume ambaye ana

mapungufu katika Dini yake, haswali. Na pindi ninapomwita kuswali

anakasirika na ananifanyia istihzai. Na anaendelea kuacha Swalah kwa hoja

kuwa baba yake alikuwa haswali, hii ndio sababu na yeye haswali.

Niliendelea na hali ya kumkumbusha na siku moja akanambia: "Ukiendelea

kwa hali hii, mlango uko wazi", hapo ndio nilifika namuomba Talaka.

Na mara ya pili ilikuwa takriban sababu hiyo hiyo. Akanambia:

"Usiniongeleshi mpaka siku ya Qiyaamah". Ipi rai yako kwa mtu huyu na kwa

maneno yake aliyosema kwa minasaba miwili, wa kwanza na wa pili? Je,

huchukuliwa ni Talaka au nini? Na je, inajuzu kwangu kubaki nae katika hali

hii?

Page 20: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

20

Imaam Ibn Baaz:

Mwanaume huyu haijuzu kubaki nae. Maadamu anaacha Swalah kama

ulivyosema, kwa hilo anakuwa kafiri. Ikiwa baba yake naye haswali, kaiga

kwake. Na wala haijuzu kumuiga kafiri asiyeswali, anatukana Dini, au

anafanya kitu miongoni mwa vitu vinavyovunja Uislamu wa mtu au maasi

katika maasi ya kumuasi Allaah. Watu wote hawa ni mamoja. Mwanaume

huyu ni kafiri na kamuiga kafiri mwenzake kutokana na kauli yake. Na

imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba

kasema:

"Baina ya mtu na baina ya kufuru na Shirki ni kuacha Swalah." (Kaipokea

Muslim katika Swahiyh yake)

Na kasema (´alayhis-Swalaat was-Salaam):

"Ahadi iliopo baina yetu sisi na wao ni Swalah, mwenye kuiacha amekufuru."

Kauli yenye nguvu katika kauli za wanachuoni ni kwamba, mwenye kuiacha

kwa kuzembea na uvivu ni kafiri, hata kama hakupinga uwajibu wake. Na

ikiwa mwanaume huyu anapinga uwajibu wake, ni kafiri kwa Ijmaa´. Kwa

hali yoyote, mwanaume huyu ni mwanaume mbaya na ni kafiri kwa kuacha

kwake Swalah kutokana na kauli yenye nguvu ya wanachuoni. Haijuzu

kwako kubaki nae. Bali ni wajibu kwako kuachana nae na wala usimpe kitu.

Na kauli yake kusema kuwa mlango uko wazi, hii ni kinaya. Ikiwa

amekusudia Talaka, anakusudia utoke kwa nia ya Talaka, itakuwa ni Talaka.

Na ikiwa hakukusudia Talaka, itakuwa sio Talaka.

Lakini kwa hali yoyote, hata kama hakukutaliki, haitakikani kwako kubaki

nae. Bali ni wajibu kwako kumuacha na umuachie [... sauti haiko wazi... ], na

watoto wako uwachukue na yeye (mume) hana haki ya (kubaki na) watoto

kutokana na ukafiri wake. Wewe ndiye aula zaidi ya watoto wako. Ni

mwanaume mbaya kwa kumkufuru kwake Allaah (´Azza wa Jalla). Huenda

Allaah Akamsamehe. Akitubu nawe bado ungali ndani ya eda, akarejea,

akatubu kwa Allaah na akajuta kwa aliyoyafanya na akaanza kuswali, hakuna

ubaya kwako kurudi kwake na maadamu ungali ndani ya eda. Ama baada ya

eda hapana (kurudi kwake), isipokuwa kwa ndoa mpya.

Page 21: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

21

Swali:

Sisi ni familia, tunakaa kwenye sinia moja wakati wa kula na hili ni jambo

limezoeleka kwa ndugu - wanawake na wanaume sote tunakaa na kula

kwenye sinia moja. Je, hili lina hukumu ya Kishari´ah inayokataza

mchanganyiko? Mimi kwa hakika sina raha kwa hili, lakini ni mambo ya ada

tu na kufuata kichwa mchunga ndio yameenea kwetu. Tufanye nini?

Imaam Ibn Baaz:

Hii ni ada chafu. Ni wajibu kuiacha. Na wala haijuzu kwa mtu kukaa na

mwanamke ambaye sio Mahram wake, kama kwa mfano msichana wa ami

yako, mjomba wako, shangazi yako. Ni wajibu kwa wanawake wawe upande

wao kwenye sinia lao na wanaume wawe kwenye sinia lao upande mwingine.

Ama kukaa na mke wako, mama yako, shangazi yako, msichana kukaa na

mjomba wake na kaka yake hakuna ubaya. Lakini wanawake ambao wewe sio

Mahram wao, haifai kwako kukaa nao kwenye sinia la chakula kimoja,

isipokuwa wanawake hao wanatakiwa kukaa kwenye sinia la chakula kingine.

Na wala mchanganyiko huu haijuzu jambo ambalo linapelekea mwanaume

kugusana na mwanamke ambaye sio Mahram wake au kumtazama na

yanayofuatia katika hayo.

Mwili wa mwanamke wote ni ´Awrah (uchi). Hivyo haijuzu kwake kukaa na

ambaye sio Mahram wake, akawa anaona anavyokula, uso wake n.k. Kwa

vovyote, huu ni munkari na ni wajibu kuachana nalo. Na kila ada chafu ni

wajibu kuiacha. Na ada ambayo inakwenda kinyume na Shari´ah na wala

haijuzu kuitanguliza kabla ya Kishari´ah. Ni wajibu kuziweka ada kinyume na

Shari´ah. Ile inayoafikiana na Shari´ah inakubaliwa na kubaki, na ile

inayokwenda kinyume na Shari´ah ni wajibu kuiacha.

Swali:

Tunaomba kutoka kwenu kutuwekea wazi Aayah au Hadiyth ambazo

zinaharamisha nyimbo.

Page 22: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

22

Imaam Ibn Baaz:

Ndio. Anasema Allaah (Jalla wa ´Alaa) katika Kitabu Chake kitukufu:

ه سبيل عن ليضل الحديث لهو يشتري من الناس ومن خذها علم بغير اللـ ئك هزوا ويت ـ ه عذاب لهم أول ين م

"Na katika watu (wako) wanaonunua maneno ya upuuzi (muziki, nyimbo

n.k.) ili wapoteze (watu) njia ya Allaah bila elimu, na wanaichukukilia (njia ya

Allaah) mzaha. Hao watapata adhabu ya kudhalilisha."

أليم بعذاب فبشره وقرا أذنيه في كأن يسمعها لم كأن مستكبرا ولى آياتنا عليه تتلى وإذا

"Na anaposomewa Aayah Zetu, hugeuka huku akitakabari kama kwamba

hazisikii, kama kwamba kuna uzito (uziwi) masikioni mwake, basi mbashirie

adhabu iumizayo." (31:06-07)

Wamesema wanachuoni wengi, ya kuwa makusudio ya "... maneno ya

upuuzi" ni nyimbo, ndio maneno ya upuuzi. Na wengine wakasema

kuhusiana na Aayah hiyo, kunaingia ndani yake firimbi na matari na

yanayofanana na hayo. Haya ndio maneno ya upuuzi yaliyoharamishwa. Na

ni katika sababu ya kupotea kutoka katika Njia ya Allaah. Hakika ya moyo

ukisibiwa na nyimbo unagonjweka, unakuwa mgumu na unapinda, jambo

hilo likamkosesha kusikiliza Qur-aan. Jambo hilo likamsababishia moyo wake

kupinda na kuihama kusikiliza Qur-aan, na badala yake ukajaa nyimbo na

maneno machafu. Na imekuja kuhusiana na maana ya Hadiyth jambo ambalo

linaonesha uharamu wa nyimbo. Katika hayo, ni yale aliyopokea al-Bukhaariy

katika Swahiyh yake, ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)

kasema:

"Kutajitokeza katika Ummah wangu watu watakaohalalisha Zinaa, Hariri,

Pombe na Nyimbo."

Mtume (´alayhis-Salaam) kaelezea ya kuwa, kutajitokeza katika zama za

mwisho watu ambao watahalalisha Haramu hii, kutokana na udhaifu wa

Imani yao. Laa Hawla wa laa Quwwata illa biLlaah.

Swali:

Page 23: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

23

Sisi tunajua ya kwamba, kutumia mkono kwa kujitoa manii ni Haramu na ni

jarima kubwa. Lakini vipi ikiwa mtu kalazimika kufanya hivyo kutokana na

amri ya tabibu kwa maslihi ya kidawa au mengineyo, inajuzu kwake kufanya

hivyo mwenyewe au kufanyiwa na mwingine?

Imaam Ibn Baaz:

Kujitoa manii ambako unatumiwa mkono ni jambo la Haramu na halijuzu. Na

linaingia ndani ya Kauli Yake (Ta´ala):

لك وراء ابتغى فمن ئك ذ ـ العادون هم فأول

"Basi yeyote yule atakayetaka kinyume ya hayo, basi hao ndio warukao

mipaka." (70:31)

Anasema Allaah:

هم أيمانهم ملكت ما أو أزواجهم على ل حافظون لفروجهم هم والذين ملومين غير فإن

"Na ambao wanahifadhi tupu zao. Isipokuwa kwa wake zao, au wale

iliyowamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi." (70:29-30)

Kisha Akasema:

لك وراء ابتغى فمن ئك ذ ـ العادون هم فأول

"Basi yeyote yule atakayetaka kinyume ya hayo, basi hao ndio warukao

mipaka." (70:31)

Kujitoa manii linaingia ndani ya hili. Isitoshe, madhara yake ni makubwa

ambayo wameyabainisha matabibu. Ni wajibu kutahadhari na hilo. Na hili ni

Haramu kwa mwanamke na mwanaume wote wawili. Lakini, kukihitajika

haja ya kufanya hivyo kwa ushauri wa matabibu atoe manii yake kutokana na

madhara yaliyo nayo, hii ni dharurah na hakuna neno. Atafanya wakati wa

haja. Ama kufanya hiyo ndo ikawa ada yako, kama wanavofanya baadhi ya

wapumbavu, hili halijuzu. Ni wajibu kutahadhari. Ama hilo likihitajia haja ya

kimatibabu na dawa, litakuwa halina neno.

Page 24: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

24

Swali:

Yatosheleza kwa mwanamke kuswali nyumbani kwake kwa adhaana peke

yake, au kwa adhaana na ´Iqaamah? Hali kadhalika mwanaume

akichelewesha Swalah yake na akaiswali nyumbani kwake, kinyume na

wakati wake au katika wakati wake, inatosheleza kwake ´Iqaamah au ni

lazima atoe adhaana na ´Iqaamah?

Imaam Ibn Baaz:

Ama mwanaume inatosha kwake ´Iqaamah, kwa kuwa kishasikia adhaana.

Wakati wa kuswali atakimu tu. Ama mwanamke, hana juu yake ´Iqaamah

wala adhaana. Ni juu yake kuswali bila ya ´Iqaamah wala adhaana.

Swali:

Kuko ambao wako katika Chuo Kikuu wanachukua elimu, lakini anataka

kujua hukumu ya Uislamu, naye amechanganyika na wanawake, kwa kuwa

masomo katika Chuo Kikuu hichi ni ya mchanganyiko, yaani ni wanaume na

wanawake. Na wanawake wengi katika Chuo Kikuu hichi sio wenye kujisitiri

na wanavaa nguo zinazoonesha.

Imaam Ibn Baaz:

Nasaha zetu kwa huu mwanafunzi ni kwamba asisome na wanafunzi wakike

na wala asichanganyike nao. Kwa kuwa hii ni njia inayopelekea katika

kufitinika nao. Ni juu yake atafute njia nyingine ya kujifunza. Ama kusoma na

wasichana, hakika hii ni njia inayopelekea katika khatari kubwa. Ni wajibu

kwake kutahadhari na hilo.

Masomo ya mchanganyiko yana shari kubwa na ufisadi mkubwa. Na wala

haijuzu kwa mtawala kulichukulia sahali. Bali ni wajibu kwa watawala

masomo yasiwe mchanganyiko. Namna hii ndio inapaswa kuwa, watawala

wa Waislamu ni wajibu kwao kufanya masomo ya wanawake yawe upande

Page 25: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

25

wake pamoja na ulinzi na kuhifadhiwa, na masomo ya wanavulana yawe

upande wake.

Swali:

Wakati fulani nina swali (Swalah za) faradhi mimi mwenyewe kwa kutokuwa

na Msikiti ulio karibu na mimi. Je, inanilazimu kwangu adhaana na ´Iqaamah

katika kila Swalah au naweza kuziswali bila ya adhaana au bila ya ´Iqaamah?

Imaam Ibn Baaz:

Sunnah ni wewe uadhini na ukimi. Hii ndio Sunnah. Ama kuhusu uwajibu,

kuna tofauti kwa wanachuoni. Lakini aula na bora zaidi kwako ni wewe

uadhini na ukimu, kutokana na ujumla wa dalili. Lakini, ni lazima kwako

kuswali pamoja na Jamaa´ah (Msikitini)vovyote itavyokuwa, ukisikia adhaana

Msikiti ulio karibu nawe, ni wajibu kwako kumuitikia muadhini na

kuhudhuria pamoja na Jamaa´ah. Ikiwa husikii adhaana na wala huna Msikiti

ulio karibu, Sunnah ni wewe uadhini na ukimu.

Swali:

Mimi ni mjane wa Kiislamu Alhamduli Allaah ambaye ninafunga na kuswali.

Nilisibiwa na maradhi makubwa siku miongoni mwa siku katika Ramadhaan

ambayo yalikuwa yanataka kuniua. Nikawa nimekula kutokana na ukubwa

wa maradhi kisha nikalipa siku hii. Anauliza kama kula kwake (siku hii ya

Ramadhaan) ana madhambi?

Imaam Ibn Baaz:

Page 26: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

26

Hana madhambi, bali ni mwenye kupewa ujira. Mtu akisibiwa na maradhi,

na Swawm ikamkuwia kwake nzito inajuzu kwake kula na ni mwenye ujira

kwa kuchukua rukhusa (ya Allaah). Anasema Allaah (Subhaanah):

ريضا منكم كان فمن ة سفر على أو م ن فعد ام م أخر أي

"Basi atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu, au yuko safarini (akafunga

baadhi ya siku); basi (akamilishe) idadi (ya siku anazotakiwa kufunga) katika

siku nyinginezo." (02:184)

Na anasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

"Hakika ya Allaah Anapenda kuchukuliewa (mambo ya) rukhusa Zake kama

Anavyochukia kufuatwa maasi Yake (Aliyokataza)."

Mtu akichukua rukhusa kwa kumtii Allaah na kufanyia kazi Aliyoyaweka

katika Shari´ah (Ta´ala), ni mwenye ujira na hana madhambi. Wewe dada

muulizaji huna dhambi juu yako kwa kula kwako kutokana na hali ya

maradhi. Na ni juu yako kulipa na umekwishafanya hivyo Alhamdulillaah.

Swali:

Nilimtaliki mke wangu mara tatu. Mara ya kwanza ilikuwa wakati wa

Maghrib aliponambia maneno yaliyonikasirikisha nikawa nimemtaliki na

(baadae) nikamrejea na kumrudisha nyumbani kwa kuwa ni mama wa watoto

wangu wawili.

Na baada ya siku kukatokea baina yetu magomvi, nikawa nimemtaliki.

Akaingia kwangu na kuniomba nimrudi kwa ajili ya (maslahi ya) watoto.

Nikamrudisha. Na baada ya siku kukatokea magomvi baina yetu kama

ilivyokuwa katika hali ya kwanza na ya pili, nikamtaliki mara ya tatu.

Naomba unifaidishe kwa hili.

Imaam Ibn Baaz:

Ni juu yako kurejea mahakamani au Muftiy aliye katika mji wenu waangalie

suala hili. Na asli ni kuwa, baada ya Talaka tatu hakuna kurudiana. Lakini

Page 27: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

27

apelekewe Qadhiy au Muftiy aangalie hilo. Ama ikiwa uko Saudi Arabia

unaweza kuturejelea kwa kutuandikia, ili tuweze kukusaidia wewe na yeye

kuyaangalia maudhui hii na tutazame uhakika, wewe, mwanamke na walii

wake, mpaka fatwa iwe juu ya jambo la wazi ikiwa uko Saudi. aAma ikiwa

uko katika mji mwingine na ikawa unaweza, rejea mahakamani au Muftiy

wenu, na In Shaa Allaah Atawafikishwa kutoa fatwa inayoafikiana na

Shari´ah.

Swali:

Akitalikiwa bikira kabla ya kuingiliwa, je itaandikwa katika ndoa yake ya

mara ya pili kwa mume wa pili kuwa ni bikira au ni mwanamke ambaye

kishaingiliwa?

Imaam Ibn Baaz:

Ni bikira. Ikiwa hakumwingiliani bikira. Ndoa mpya aliyofanya ikiwa

hakuingiliwa, haimtoi katika ubikira wake. Maadamu (mume huyo)

hakumwingilia, atabaki katika ubikira wake.

Swali:

Du´aa al-Istifaah (ya kufungulia Swalah) inasomwa katika faradhi na

Naafilah, au ni katika faradhi tu?

Imaam Ibn Baaz:

Sunnah ni katika yote mawali, asome Du´aa al-Istifaah katika yote mawili

faradhi na Naafilah. Hii ndio dhahiri ya Hadiyth ya Hadiyth kutoka kwa

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Page 28: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

28

Swali:

Je, Duyyuuth ni yule ambaye anaelezea yanayopitika baina yake yeye na mke

wake kitandani au ni nani Duyyuuth kwa mtazamo sahihi wa Kiislamu?

Imaam Ibn Baaz:

Duyyuuth ni yule ambaye anaridhia machafu ya mke wake, anaridhia

kuchukuliwa mke wake, anaridhia mke wake kufanywa Zinaa. Huyu ndiye

Duyyuuth. Ni yule ambaye anaridhia kuchukuliwa mke wake na kutumiwa,

pasina kuwa na wivu wala kujali. Kwa kuwa na na Imani pungufu au

kutokuwa nayo kabisa. Huyu ndiye huitwa Duyyuuth. Ama yule ambaye

anaelezea hali yake na mke wake, haya ni maasi na anaweza kuwa fasiki kwa

hilo. Lakini hawi Duyyuuth. Duyyuuth ni yule ambaye anaridhia machafu ya

mke wake.

Swali:

Ipi hukumu kwa mwanaume ambaye ni Muislamu kumpa mke wake Talaka

kwa kuandika jina la mwanaume mwingine naye (mke huyo) yuko katika

dhimma yake ili wapewe pesa kutoka serikali?

Imaam Ibn Baaz:

Ni kama tulivyotangulia kusema, yote haya ni maovu na ni mali ya Haramu.

Swali:

Nataraji utanielekeza katika kitabu cha Hadiyth kizuri?

Page 29: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

29

Imaam Ibn Baaz:

Katika vitabu vizuri kwa mwanafunzi ni kitabu "Buluugh-ul-Maraam". Ni

kitabu kizuri na ni chenye faida katika milango ya Ahkaam. Ni kitabu kizuri

na chenye faida, "Buluugh-ul-Maraam" cha Haafidhw Ibn Hajar. Hichi tunatoa

nasaha kihifadhiwe na khaswa kuzingatia yaliyomo katika Hadiyth ambazo ni

Swahiyh. Na kuna Hadiyth ambazo ni dhaifu lakini ni ndogo na

kumebainishwa na kutanabahishwa hali zake.

Kuna vitabu vingine vizuri ambavyo ni mukhtasari, "Umdat-ul-Hadiyth" cha

´Abd-ul-Ghaniy bin ´Abd-ul-Waahid bin ´Aliy al-Maqdisiy (Rahimahu

Allaah). Kuna jumla ya Hadiyth nzuri. Kuna Hadiyth karimu 400 na zaidi

kidogo zenye manufaa na faida. Lakini kilicho cha manufaa zaidi ni "Buluugh-

ul-Maraam". Kwa kuwa chenyewe ni chenye faida zaidi na kina Hadiyth

nyingi.

Swali:

Tumejua kupitia barnamiji hii ya kwamba haipiti Talaka kwa mwenye hedhi

na mwenye mimba. Je, ni kuwa haipiti kabisa au inapita baada ya Twahara?

Imaam Ibn Baaz:

Talaka ya mwenye hedhi haipiti kutokana na kauli sahihi (yenye nguvu) ya

wanachuoni, tofauti na kauli ya jamhuri. Jamhuri ya wanachuoni wanaona

kuwa inapita. Hali kadhalika kwa mwenye nifasi.

Lakini kauli ya sahihi katika kauli za wanachuoni, na ndio waliokuwa

wakifutu baadhi ya Taabi´iyn na Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) na

akaichagua Shayk-ul-Islaam bin Taymiyyah, mwanafunzi wake Ibn al-Qayyim

na kundi katika wanachuoni, kuwa Talaka hii haipiti. Kwa kuwa inakwenda

kinyume na Shari´ah ya Allaah, kwa kuwa Allaah Kawekea Shari´ah

kumtaliki mwanamke katika hali ya Twahara ya nifasi, hedhi na katika

Twahara ambayo mume wake hakumjamii. Hii ndio Talaka ya Kishari´ah.

Akimtaliki katika hedhi, nifasi au Twahara ambayo amemjamii, Talaka hii ni

Page 30: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

30

Bid´ah na wala haipiti kutokana na kauli ya sahihi ya wanachuoni. Kwa Kauli

ya Allaah (Jalla wa ´Alaa):

ها يا بي أي تهن فطلقوهن النساء طلقتم إذا الن لعد

"Ee Nabii! Mtakapowataliki wanawake, basi watalikini katika wakati wa eda

(twahara na si katika hedhi) zao." (65:01)

Bi maana katika Twahara ya jimaa. Namna hii ndivyo walivyosema

wanachuoni kuhusu (maana ya) "watalikini katika wakati wa eda." Wawe

Twahara hawakuingiliwa au wawe na ujauzito. Hii ndio Talaka ya katika eda.

Ama Talaka ya mjamzito wanachuoni wanaona kuwa inapita, na mwenye

kusema kuwa haipiti kakosea. Talaka ya mjamzito inapita kwa wanachuoni,

Talaka isiyopita ni ya mwenye hedhi na nifasi na Twahara ambayo

mwanamke kaingiliwa na hakujadhihiri mimba yake. Talaka hizi (sampuli

tatu) hazipiti kutokana na kauli ya sahihi ya wanachuoni, kwa kuwa

zinakhalifu na Shari´ah ya Allaah na vile vile ni katika hali ambayo

haikuwekwa Talaka kama tulivyotangulia kusema.

Na baadhi ya ´Awwaam wanastaajabu na kusema Talaka ya mjamzito haipiti,

hili ni kosa. Hii ni katika kauli za ´Awwaam zisizokuwa na asli katika Shari´ah

wala maneno ya wanachuoni. Mjamzito Talaka inapita. Ni wajibu kujua hilo.

Swali:

Baadhi ya migahawa na vinywaji vinaandikwa "haina-nguruwe", au "haina-

pombe". Je, mtu atosheke na maandiko kama haya na kuvitumiaau kuna

neno?

Imaam Ibn Baaz:

Hakuna neno, maandiko haya yanatosha ikiwa ni katika mji wa mayahudi na

manaswara, yanatosha maandiko haya. Asli ni kuwa, chakula (vichinjo) vyao

ni Halali hata kama hakikuandikwa kitu. Na ikiwa kimeandikwa, inakuwa ni

aula zaidi. Isipokuwa tu ikijulikana ya kuwa haya (waliyoyaandika) ni uongo

na katika kitu hichi kuna nguruwe au kuna kitu kingine cha najisi, maandiko

Page 31: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

31

haya yatakuwa hayana maana yoyote. Ikijulikana kwa dalili kutoka kwa

waaminifu ya kwamba, huu ni uongo. Ama maadamu hakujajulikana kitu,

asli ni kwamba inaruhusu na ni salama.

Swali:

Nimechumbia mwanamke wa umri wa miaka ishirini, na niliwahi kumsaidia

kwa kumpa damu pindi alipokuwa mgonjwa kabla sijamchumbia. Je, inajuzu

kwangu kumchumbia?

Imaam Ibn Baaz:

Damu haiathiri, sio kama kunyonya. Mwanamke kuolewa na mwanaume

ambaye ana damu yake, au mwanaume kuoa mwanamke ambaye ana damu

yake aliyompa wakati wa haja ya hilo, hili halina hukumu kama ya kunyonya.

Mwanamke haharamiki kwake (mwanaume) wala (mwanaume) haharamiki

kwake (mwanamke) kwa yaliyopitika katika kunufaishana kwa damu ambayo

anaihitajia mgonjwa.

Swali:

Mimi naishi na ndugu zangu ambao hawaswali na mimi ninawapenda sana

na wala siwezi kutengana nao kwa kuwa sina wengine badala yao. Je, inajuzu

kuishi nao?

Imaam Ibn Baaz:

Ikiwa haswali hutakikani kuwapenda na wala hulazimiki kuwa na mapenzi

juu yao kwa ajili ya Allaah, kwa kuwa watu hawa udhahiri wao ni ukafiri.

Kwa kuwa mwenye kuacha Swalah anakufuru. Hivyo, ilikuwa haitakikani

kuwapenda, bali uwachukie kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Na

Page 32: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

32

wala hutakiwi kuishi nao. Isipokuwa tu ikiwa kama ni jambo la kidharurah,

hivyo utawanasihi daima, na kuwaogopesha Allaah, na kuwaambia

"muogopeni Allaah enyi watu, swalini, zihifadhini Swalah, mcheni Allaah".

Saidiana na aliye karibu yako katika ndugu zako; kama baba zao, babu zao,

mama zao na mfano wa hao mpaka waweze kukusaidia katika kuwapa

nasaha na kuwaelekeza katika kheri. Wakiendelea kuacha Swalah, watu hawa

watakuwa hawana kheri yoyote. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla

Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa kasema:

"Ahadi iliopo baina yetu na wao ni Swalah, atakayeicha basi amekufuru."

Fanya vovyote utavyoweza usiishi nao, hata ikibidi kuishi katika nyumba ya

wewe mwenyewe au baadhi ya ndugu zao wengine fanya hivyo. Hili ndilo la

wajibu kwako kadiri na utakavyoweza.

Swali:

Mke wangu anaishi pamoja nami Saudi na anataka kuwatumia mzazi wake

picha wanaoishi Misri ili apate utulivu. Na nimesikia Fatwa kuwa picha kwa

ala ya picha ni Haramu. Je, hii ni dharurah?

Imaam Ibn Baaz:

Hii sio dharurah. Haifai kwake kutuma picha yake, sawa kwa mama yake

wala asiyekuwa mama yake. Kwani hii sio dharurah. Amuandikie [barua],

aongee nae kwenye simu. Alhamduli Allaah. Ama kutuma picha haijuzu.

Swali:

Je, ni sahihi ya kwamba jini linaweza kumwingia mtu na likamfanya akaongea

kwa sauti yake?

Page 33: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

33

Imaam Ibn Baaz:

Ndio. Jini linaweza kumwingia mtu. Likamwingia kwa sifa maalumu na

likamfanya mtu akatamka kwamambo, hujulikana sauti ya jini na ya sauti ya

mtu. Hili ni jambo hutokea tangu zamani mpaka sasa. Hali kadhalika

mwendawazimu. Aliyeingiwa na jini na mwendawazimu hutamka kwa

maneno: "Nipeni kadhaa", "Fanyeni kadhaa" n.k., kwa sauti wanayoisikia

watu isiyokuwa sauti ya mwanaadamu. Hili ni jambo ambalo hutokea, na

mwenye kupinga hili kakosea. Jini humwingia mtu na kwa hili anakuwa kama

mwendawazimu akili zake zinatoweka. Linapomtoka (jini hilo) na kutengana

nae, akili zake hurudi.

Swali:

Anapomaliza mwenye kuswali Swalah yake na akataka kutoa Salaam, je

aseme "as-Salaam ´alaykum wa Rahmatullaahi wa Barakatuh", kuliani kisha

kushotoni." Au niseme "as-Salaam ´alaykum wa Rahmatullaahi", tu? Na ni ipi

hukumu ya mwenye kufanya hivyo kwa kuzidisha "... wa Barakatuh"?

Imaam Ibn Baaz:

Lililothibiti katika Sunnah ni kusema "... wa Barakatuh" tu, hii ndio iko katika

Shari´ah, kusema "as-Salaam ´alaykum wa Rahmatullaah" tu, hili ndilo liko

katika Shari´ah. Nako ni kusema "as-Salaam ´alaykum wa Rahmatullaahi",

kuliani na kushotoni. Ama kuzidisha "... wa Barakatuh", wanachuoni

wametofautiana. Na kapokea ´Alqamah (Radhiya Allaahu ´anhu) kutoka kwa

baba yake kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba

amesema namna hii: "as-Salaam ´alaykum wa Rahmatu-llaahi wa Barakatuh".

Lakini Riwaayah hii ya ´Alqamah ina tofauti. Kuna wanachuoni ambao

wameisahihisha kutoka kwake, na kuna wanachuoni ambao wamesema kuwa

imekatika (isnadi yake).

Muislamu anatakiwa asizidishe, aula na bora zaidi aishie kwa kusema "... wa

Rahmatullaah." Na mwenye kuzidisha kwa kudhani kuwa ni sahihi au hajui

mambo haya, hakuna neno na Swalah yake ni sahihi. Lakini bora zaidi ni

Page 34: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

34

kutozidisha. Hivi ndivyo walivyosema wanachuoni. Na kufanyia kazi jambo

lililothibiti na lenye nguvu.

Swali:

Mimi nimemuoa mwanamke ambaye anaasi amri zangu na wala hanitii kwa

kitu. Na daima anatoka nyumbani bila ya idhini yangu nakwenda kufanya

baadhi ya kazi ambazo zimenifanya kunighadhibisha na kufikiria kumtaliki.

Ikawa nimeandika karatasi ambapo nimeandika kuwa "nimekutaliki Talaka

mbili" na nikamtaja kwa jina lake na la baba yake. Wakati huo nilikuwa

nyumbani peke yangu na sikuwa na yeyote. Lakini baada ya hapo nikawa

nimeichana hiyo karatasi na wala hakuna yeyote aliyejua kilichokipitika wala

yeye. Na wakati huo ilikuwa ni kabla ya miezi mitano. Talaka imepita au

hapana?

Imaam Ibn Baaz:

Ndio, zimepita Talaka mbili. Ukimtaliki kwa kuandika au kwa kumtakia,

Talaka inakuwa imepita hata kama hukushuhudisha. Lakini umebaki na

Talaka moja, ikiwa ulikuwa hujamtaliki kabla ya hapo umebaki na Talaka

moja. Unaweza kumrejea, na unaweza kumchumbia tena ikiwa kishatoka

ndani ya eda. Muhimu ni kuwa kumebakia Talaka moja, ikiwa ulikuwa

hujamtaliki kabla ya Talaka hii uliyoandika.

Muulizaji:

Kulikuwa kumeshapita miezi mitano kuanzia muda ule ambapo aliandika.

Siatakuwa kishatoka ndani ya eda?

Imaam Ibn Baaz:

Page 35: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

35

Ndio, mara nyingi ni kuwa atakuwa kishatoka ndani ya eda kwa kupata hedhi

au kwa miezi mitatu ikiwa ni eda ya mwanamke aliyokoma hedhi. Isipokuwa

tu ikiwa kama ni mjamzito na hajajifungua, ni juu yake (aendelee) kukaa eda.

Muulizaji:

Vipi lakini kuhusiana na muda ule tangu aandike karatasi hiyo ya Talaka,

ikiwa kwa mfano (alimtaliki) katika Twahara ambayo kamwingilia.

Imaam Ibn Baaz:

Kauli ya sahihi ni kuwa, ikiwa ni katika Twahara aliyomjamii au ilikuwa ni

wakati wa hedhi, kauli ya sahihi ni kuwa (Talaka) haipiti. Tofauti na kauli ya

wanachuoni wengi (wanaoonelea kuwa inapita).

Swali:

Hukumu ya mwenye kuacha Swalah na je anazikwa katika makaburi ya

Waislamu?

Imaam Ibn Baaz:

Kuhusiana na mwenye kuacha Swalah kwamba atazikwa katika makaburi ya

Waislamu, wanachuoni wametofautiana kuhusiana na hukumu yake.

1) Akiacha kwa uvivu na wala hapingi uwajibu wake, anaamini kuwa Swalah

ni wajibu lakini akaacha kwa uvivu na kuzembea, kuna ambao wanaona

kuwa hakufuru kufuru kubwa, bali ni kufuru ndogo. Na kwamba anazikwa

pamoja na Waislamu wengine, kuoshwa na kuswaliwa. Hii ni kauli maarufu

kwa kundi kubwa la wanachuoni.

2) Kauli ya pili ni kuwa, anakufuru kufuru kubwa. Na hii ndio kauli iliyo ya

sahihi. Kutokana na hili, hatozikwa pamoja na Waislamu, bali atatafutiwa

mahali afukiwe na asiachwe juu ya ardhi. Atazikwa kama ilivyo kwa makafiri

Page 36: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

36

wengine. Kutokana na kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika

Hadiyth Swahiyh:

“Ahadi iliopo baina yetu sisi na wao ni Swalah, atakayeiacha amekufuru."

Na wala hakubagua yeyote, na wala hakusema ikiwa anapinga uwajibu wake

(hakufuru). Na hii ni Hadiyth Swahiyh imepokea Ahmad na Ahl-us-Sunan

kwa isnadi Swahiyh. Na Muslim kapokea katika Swahiyh yake, kutoka kwa

Jaabir (Radhiya Allaahu ´anhu) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi

wa sallam) kasema:

"Baina ya mja na baina ya kufuru na Shirki ni kuacha Swalah."

Shirki na kufuru inapokuja kwa sampuli hii inakuwa kubwa. Hii ndio kauli

iliyo sahihi na yenye nguvu pamoja na kuwa kuna dalili zingine nyingi

ambazo zinaonesha kuwa hata kwa mwenye kuacha Swalah kwa uvivu, hana

lolote katika Uislamu.

Swali:

Mwanzoni wa mwaka katika ndoa yetu nilipatwa na khasira nyingi

nikamuapia mke wangu Talaka, nikamwambia: "Mama yako akiingia hapa

utakuwa ni mwenye kutalikika", na nilikuwa nimekusudia kumkataza

asifanye hivyo na si Talaka. Na baada ya hapo mama yake akaingia na ndoa

yetu ikaendelea mpaka sasa ni zaidi ya miaka 20 na nikazaa nae watoto na

sikumuapia Talaka mara nyingne kwa kiasi cha muda wote huu. Ni ipi

hukumu ya Talaka hii, imepita au hapana?

Imaam Ibn Baaz:

Kauli iliyo ya sahihi ni kuwa, Talaka hii hukumu yake ni ya yamini. Kwa

kuwa hukukusudia kumtaliki, bali ulikusudia kum-kataza mama yake

asiingie. Talaki hii hukumu yake inakuwa ya yamini kutokana na kauli sahihi

ya wanachuoni. Ni juu yako kukafiria yamini yako hata kama muda

umekwishapita; kwa kulisha masikini 10 au kuwa-visha nguo, au kuachia

mtumwa huru. Kama Alivyobainisha Allaah katika Kitabu Chake Kitukufu

Page 37: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

37

katika Suurat-ul-Maaidah. Na kila masikini mmoja utampa 1,5 kg ya tende,

mchele au visivyokuwa hivyo katika vyakula (vilivyozoeleka) katika mji,

watapewa masikini 10. Au kuwakatia nguo, kuwapa kanzu au kikoi na nguo

ya juu. Kufanya kwako hivi yatosha. Alhamduli Allaah. Na wala Talaka

itakuwa haikupita na mke atabaki kuwa ni wako. Na wala haidhuru kwa

muda wote huu mrefu. Isipokuwa tu ulikosea kwa kukawia kutoa kafara kwa

muda wote huu mrefu. Ama kauli inayosema kuwa Talaka inapita (katika hali

kama hii), ni kauli dhaifu. Kauli iliyo ya sahihi ni kuwa haipiti, maadamu

makusudio yako ilikuwa ni kumkataza na kumzuia na haikuwa kumtaliki.

Swali:

Kuna siku nilihudhuria nyumbani, nikamkuta mke wangu amefanya kazi

ambayo ilinikasirikisha. Nikamwambia "ukikaa nyumbani siku hii ya leo,

nitakuwa nimekutaliki". Akawa ametoka siku hiyo hiyo na kisha akarejea

baada ya wiki. Je, ametalikika au hapana? Na je, nina kafara yoyote?

Imaam Ibn Baaz:

Ikiwa makusudio ilikuwa ni kumkataza kubaki siku hiyo na usiku wake tu,

hakupiti kitu, kwa kuwa alitoka na hakurudi isipokuwa baada ya wiki. Ama

kama makusudio yako ilikuwa ni kutengana nae, makusudio yako sio siku na

usiku huu, bali makusudio yako ilikuwa ni kutengana nae na kumtaliki, basi

Talaka itakuwa imepita ambayo ulikusudia. Nayo ni Talaka moja, haikupita

isipokuwa Talaka moja tu. Ikiwa mwanzoni alikuwa hajamtaliki Talaka mbili,

anaweza kumrejea maadamu bado angali ndani ya eda. Hali hii ni kama

alikusudia Talaka. Ama ikiwa makusudio yake ilikuwa ni kumkataza siku

hiyo tu, kutakuwa hakukupita kitu.

Swali:

Page 38: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

38

Mimi ni mwanaume ambaye nimeoa na nina matangamano na mke wangu

mazuri sana kwa daraja ambayo nilimwambia "uso kukutana na wangu ni

Haramu ukinificha kitu kinachohusiana na maisha yetu ya kindoa." Lakini

nimekuja kuona kuwa jambo hili ni khatari, na nataka kuelekezwa katika

jambo ambalo litanitoa katika sharti hii. Ipi hukumu ikiwa mke wangu

atanificha kitu bila ya mimi kujua?

Imaam Ibn Baaz:

Ikiwa makusudio ni kumkataza asikufiche chochote, inatosha kwako kutoa

kafara ya yamini. Na wala sio lazima kwake kukubainishia kila kitu, ikiwa ni

mambo yaliyopita. Akubainishie mambo yenye faida. Ama yanayoweza

kumdhuru katika mambo ambayo ni maslahi maalumu yanayomuhusu yeye

au yakakudhuru wewe, sio lazima kwake kukubainishia. Lakini akubainishie

yanayohusiana na maslahi yako na maslahi ya nyumba yako.

Na ikiwa unataka kujitoa katika hilo ni juu yako kutoa kafara ya yamini, ni juu

yako kutoa kafara ya yamini na inatosha. Kwa kuwa makusudio yako

(kusema hivyo) ni kumhimiza kukubainishia kila kitu na wala asikufiche kitu.

Ukitoa kafara ya yamini inatosha. Anasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi

wa sallam):

“Kama utakula yamini ukaona lingine ni bora kuliko hilo basi lifanye hilo bora

na fanya kafara la yamini yako.”

Na hii hukumu yake ni kama ya yamini. Ni juu yako kuleta Tawbah juu ya

hilo, kwa kuwa kuharamisha ni jambo lisilojuzu. Ni juu yako kutubu kwa

Allaah (Ta´ala) na utapotoa kafara ya yamini yako hakuna neno. Muhimu ni

wewe utoe kafara kwa yamini yako.

Muulizaji:

Hata kama kwa kusema kwake huko amekusudia (mke huyo) kuharamika

kwake?

Imaam Ibn Baaz:

Page 39: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

39

Ikiwa amekusudia kuharamika kwake, huyu ni juu yake kutoa kafara ya

Dhwihaar. Ama ikiwa amekusudia kumhimiza (kufanya au kutofanya kitu)...

Na hii ndio dhahiri (ya makusudio ya muulizaji). Watu wengi kwa mfano wa

hili, wanakuwa wanakusudia kuhimiza ili kumtisha (mke wake). Kwa hali hii

atatoa kafara ya yamini. Ama ikiwa ndani ya moyo wake amekusudia

kuharamika kikamiifu, hii itakuwa ni Dhwihaar na ni juu yake kutoa kafara ya

Dhwihaar. Nayo ni kuacha mtumwa huru, asiyeweza afunge miezi miwili

mfululizo na asiyeweza alishe masikini sitini kwa chakula kimechozoelekea

mjini; kila masikini atampa 1,5 kg kabla ya kumgusa (kumjamii). Ikiwa

alikusudia hili - kuharamika - naye akathibitisha kuwa amemficha kitu, atatoa

kafara hii na yatosha. Ama akithibitisha ya kuwa hakumficha kitu, hana juu

yake kitu.

Muulizaji:

Vipi ikiwa atamficha na asimwambie hilo?

Imaam Ibn Baaz:

Ikiwa anajua kihakika ya kuwa kamficha kitu, ni juu yake kutoa kafara...

Muulizaji:

Lakini nakusudia ikiwa (mke) amemficha kitu wala yeye (mume) hakujua

kitu...

Imaam Ibn Baaz:

Hana juu (mume) kitu. Lakini akimweleza, ni juu yake atoe kafara.

Swali:

Page 40: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

40

Nimemtaliki mke wangu na kumwambia: "Ukimuomba mwanaume kukuoa,

olewa" na nikampa karatasi yake (ya Talaka). Je, naweza kumrudi mara ya

pili?

Imaam Ibn Baaz:

Talaka ikiwa ni kwa matamshi kama haya, inakuwa imepita mara moja.

Akimwambia: "Ukikubaliana na mwanaume mwengine waweza kuolewa",

"mwanaume mwengine akikichumbia, olewa" au mfano wa matamshi kama

hayo, au "wewe nimekutaliki", au "wewe umetalikika" au mfano wa hayo, hii

huchukuliwa ni Talaka moja tu. Anaweza kumrudi maadamu bado angali

ndani ya eda, kwa kushahidisha mashahidi wawili ya kwamba kamrejea mke

wake. Bora zaidi, awashuhudishe mashahidi wawili ambao ni waadilifu,

washuhudie ya kuwa kamrudi mke wake maadamu bado angali ndani ya eda,

yaani maadamu katwaharika hedhi mara tatu ikiwa ni mwanamke mwenye

kupata hedhi. Na ikiwa ni mwanamke ambaye hapati hedhi, eda yake ni miezi

mitatu. Akimrudi ndani ya miezi hii mitatu, mwanamke huyo anakuwa ni

Halali kuwa mke wake.

Ama ikiwa ni mwanamke wa kupata hedhi, eda yake (inaisha) kwa kupata

hedhi tatu, ikiwa ni mwanamke wa kupata hedhi. Na ikiwa ni mzee na hapati

hedhi, eda yake ni miezi mitatu. Ama ikiwa ni mwanamke wa kupata hedhi,

eda yake (inaisha) kwa kupata hedhi tatu, ikiwa ni mwanamke wa kupata

hedhi.

Na ikiwa ni mzee na hapati hedhi na binti mdogo (ambaye hajaanza kupata

hedhi), eda yake ni miezi mitatu. Ikiwa hakumuwahi ndani ya muda wake

huyo wa eda, basi mwanamke huyo atakuwa ni ajinabi kwake. Hatokuwa

Halali kwake isipokuwa kwa ndoa nyingine mpya kama wanawake wengine

ambao anaweza kuwachumbia. Hawi Halali isipokuwa kwa kufunga ndoa

mpya na masharti yanayokubalika Kishari´ah.

Swali:

Page 41: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

41

Kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah inajuzu? Kwa kuwa huku kwetu watu

wanamchinjia mtu ambaye anaitwa "Mujalliy". Na tunapowauliza ni nani

Mujalliy? Wanasema kuwa ni Nabii katika Manabii wa Allaah. Tunaomba

utupe faida.

Imaam Ibn Baaz:

Kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah ni munkari mkubwa na ni Shirki

kubwa, sawa ikiwa kachinjiwa Nabii, walii, nyota, jini, sanamu au

visivyokuwa hivyo. Kwa kuwa Allaah (Subhaanah) Anasema:

ه ومماتي ومحياي ونسكي صلتي إن قل لك له شريك ل العالمين رب للـ ل وأنا أمرت وبذ المسلمين أو

"Sema (ee Muhammad وسلم وآله عليه هللا صلى ): “Hakika Swalaah yangu, na

Nusukiy (kuchinja kafaara na ‘ibaadah zangu) na uhai wangu na kufa kwangu

ni kwa ajili ya Allaah (Pekee) Mola wa walimwengu. Hana mshirika, na kwa

hayo ndio nimeamrishwa, nami ni Muislamu wa kwanza (waliojisilimisha

kwa Allaah).” (06:162-163)

Akaelezea (Subhaanah) kuwa kuchinjiwa ni kwa ajili Yake kama Swalah ilivyo

Yake. Atakayechinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah, ni kama aliyeswali kwa

ajili ya asiyekuwa Allaah. Atakuwa kamshirikisha Allaah (´Azza wa Jalla).

Hali kadhalika Anasema (Subhaanah):

ا وانحر لربك فصل الكوثر أعطيناك إن

"Hakika Sisi Tumekupa (ee Muhammad وسلم وآله عليه هللا صلى ) Al-Kawthar (mto

katika Jannah). Basi swali kwa ajili ya Mola wako na chinja (kwa ajili Yake)."

(108:01-02)

Swalah na kuchinja ni ´Ibaadah mbili muhimu sana. Atakayewachinjia walio

ndani ya makaburi, Manabii, nyota, sanamu, jini au Malaika, basi atakuwa

amemshirikisha Allaah. Ni kama mfano wa kuswali kwa ajili yao, au

kuwataka msaada (kwa wasiyoyaweza) au kuwawekea nadhiri, yote haya ni

kumshirikisha Yeye (Subhaanah). Na Allaah (Subhaanah) Anasema:

ه المساجد وأن ه مع تدعوا فل للـ أحدا اللـ

"Na kwamba Misikiti ni (kwa ajili) ya Allaah, basi msiombe (msimuabudu)

yeyote pamoja na Allaah." (72:18)

Page 42: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

42

Na Anasema (Subhaanah):

ليعبدون إل والنس الجن خلقت وما

"Na Sikuumba majini na watu wa isipokuwa waniabudu." (51:56)

Na Anasema (Subhaanah):

اه إل تعبدوا أل ربك وقضى إحسانا وبالوالدين إي

"Na Mola wako Amehukumu kwamba: “Msiabudu (yeyote) isipokuwa Yeye

Pekee na (Ameamrisha) kuwafanyia wema wazazi wawili." (17:23)

´Ibaadah ni haki ya Allaah Pekee; na kuchinja ni miongoni mwa ´Ibaadah,

kutaka msaada ni katika ´Ibaadah na Swalah ni katika ´Ibaadah. Na imethibiti

kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema:

"Allaah Amlaani mwenye kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah." (Swahiyh

Muslim, Hadiyth kutoka kwa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu))

Ni juu yenu kuwakataza watu hawa na kuwafunza ya kwamba hii ni Shirki

kubwa na kwamba lililo la wajibu juu yao ni kuacha hilo. Hawafai kwao

kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah, kama ambavyo hawafai kuswali kwa

ajili ya asiyekuwa Allaah. Na hili, ni kwa ajili ya kusaidia katika wema na

uchaji Allaah, kukataza maovu, na kulingania katika Dini ya Allaah na

kumpwekesha Allaah kwa kumtakasia ´Ibaadah Yake. Kwa minajili ya

Tawhiyd.

Ni wajibu ´Ibaadah iwe kwa Allaah Mmoja (Subhaanahu wa Ta´ala). Ni

wajibu kwa wanachuoni, wanafunzi na Waislamu kusaidiana juu ya wema na

uchaji Allaah na wakataze Shirki kwa yule mwenye kuifanya, mpaka iweze

kudhihiri Tawhiyd na kushikwe vikwazo kwa sababu zinazopelekea katika

Shirki.

Swali:

Ni yapi maoni yako kufuatilia kisimo cha Qur-aan Tukufu katika idhaa ya

Qur-aan na kusoma pamoja naye na mimi huku niko nafanya kazi?

Page 43: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

43

Imaam Ibn Baaz:

Hakuna ubaya kufuatilia Qur-aan, lakini iwe kwa kunyamaza na isiwe kwa

kusoma. Allaah (Subhaanah) Anasema:

ترحمون لعلكم وأنصتوا له فاستمعوا القرآن قرئ وإذا

"Na inaposomwa Qur-aan, basi isikilizeni kwa makini na mkae kimya

(mzingatie) mpate kurehemewa." (07:204)

Wewe sikiliza na uzingatie anayosoma msomaji na ustafidi kwayo. Ama

kusoma pamoja naye hapana. Sunnah ni kunyama, kuzingatia maana yake na

kusikiliza mpaka uweze kustafidi kwa Maneno ya Mola Wako (´Azza wa

Jalla). Lakini usisome pamoja na msomaji, nyamaza. Hii ndio Mashru´ah.

Swali:

Nikiwa katika safari ambayo mtu anaweza kufupisha Swalah, na Swalah ya

´Aswr ikanifikia na sikuiswali mpaka wakati wake ulipokwisha na nikafika

kwa ahli zangu. Je, nilipe Swalah ile kwa kufupisha au kikamilifu?

Imaam Ibn Baaz:

Msafiri akifika kwa ahli zake, analipa (Swalah) zilizompita kikamilifu na

hafupishi. Anafupisha tu katika hali yake ya safari, ama akichelewesha kwa

mfano ´Aswr, au Dhuhr au ´Ishaa mpaka akafika kwa ahli zake, ataswali

Rakaa´ nne, kwa kuwa rukhusa alikuwa nayo katika hali ya safari.

Swali:

Ikiwa mtu ametawadha au yuko katika Wudhuu, akamgusa mama yake au

dada yake. Je, Wudhuu wake unavunjika?

Page 44: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

44

Imaam Ibn Baaz:

Kauli sahihi ni kwamba, kumgusa mwanamke hakuvunji Wudhuu, sawa

ikiwa ni mke wake au wanawake wengine. Hii ndio kauli sahihi. Na kuna

tofauti kwa wanachuoni. Wanachuoni kuhusiana na hili wana kauli tatu:

1) kumgusa mwanamke kunavunja Wudhuu kabisa, 2) hakuvunji Wudhuu

kabisa na 3) kuna ufafanuzi, kunavunja Wudhuu ikiwa amemgusa kwa

matamanio, vinginevyo hapana.

Na kauli yenye nguvu katika kauli hizi tatu ni kwamba, (kumgusa

mwanamke) hakuvunji Wudhuu kabisa. Kutokana na yaliyothibiti kutoka

kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa aliwabusu baadhi ya wake

zake kisha akaswali na wala hakutawadha. Na ni kwa sababu, asli ni kuwa

mtu anabaki na Twahara na wala haivunjiki isipokuwa kwa kitu cha wazi. Na

ni kwa sababu jambo hili wanakumbana nalo sana katika manyumba yao, na

lau kumgusa mwanamke kungekuwa kunavunja Wudhuu angelibainisha hilo

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ubainisho wa wazi na asingelificha.

Ama Kauli Yake (´Azza wa Jalla):

النساء ستم لم أو

"Au mmewagusa (mmewaingilia) wanawake." (04:43)

Makusudio ya hilo ni Zinaa, kama alivyosema hilo Ibn ´Abbaas (Radhiya

Allaahu ´anhumaa) na wengineo. Makusudio ni jimaa, Allaah Kaiita kwa jina

na kugusa. Allaah Kaipa jimaa kunya kwa lafdhi kama hii na kwa "kukutana".

Hii ndio kauli sahihi, ya kuwa kumgusa mwanamke hakuvunji Wudhuu

isipokuwa tu mtu akitokwa na kitu, kama madhiy. Vinginevyo hakutengui

Wudhuu.

Swali:

Huku kwetu watu wanawasomea Qur-aan maiti na wanachukua ujira kwa

hilo. Anapokufa mmoja wao wanamsomea Qur-aan kwa siku tatu,

wanamchinjia na kumfanyia walima. Je, maiti wanafaidika kwa lolote na je hili

ni katika Shari´ah?

Page 45: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

45

Imaam Ibn Baaz:

Hili ni Bid´ah. Kumsomea maiti na kuchukua ujira kwa hilo, hili ni Bid´ah na

wala halijuzu. Hakuna cha ujria na wala haifai kwake kumsomea maiti na

wala hakuna dalili ioneshayo kuwa atanufaika kwayo, bali hili ni munkari na

Bid´ah. Hali kadhalika, kumchinjia na kumfanyia chakula, yote haya ni Bid´ah

na munkari na hayajuzu. Ni wajibu kutahadhari hilo na kuwatahadharisha

watu kwa hilo. Hili ndilo la wajibu kwa wanachuoni na kwa watawala.

Wawatanabahishe watu kwa Aliyokataza Allaah, na wawachukulie hatua

wajinga na wapumbavu mpaka waweze kunyooka katika njia iliyonyooka

ambayo Allaah Kawawekea nayo waja Wake. Kwa hilo, hali na jamii

itatengemaa, na itadhihiri hukumu ya Kiislamu na mambo ya Kijaahiliyyah

yataisha.

Swali:

Mwanaume wa Kiislamu akimtukana mke wake au Dini yake anakuwa ni

mwenye kutalikika Kishari´ah kama tunavyosikia kwa watu wengi?

Imaam Ibn Baaz:

Akimtukana mke wake hatalikiki. Lakini ni juu yake atubu kwa Allaah na

apatane na mke wake. Na ikiwa watasameheana, hakuna kitu. Na ikiwa

atamtusi kama (mke) alivyomtusi kwa kulipiza kisasi bila ya kuzidisha juu ya

hilo, haina neno. Na ikiwa atamsamehe ndio bora zaidi. Kwa kuwa Allaah

Anasema:

للتقوى أقرب هو اعدلوا

"Fanyeni uadilifu; hivyo ni karibu zaidi na taqwa." (05:08)

Ama kumtukania Dini yake ilihali naye (mwanamke huyo) ni Muislamu, huu

ni ukafiri. Tunamuomba Allaah afya. Ikiwa mume ni Muislamu na mke ni

Muislamu, kutukana Dini yake ina maana kautukana Uislamu. (Mke) asiishi

naye (huyo mume). Atiwe adabu (huyo mume) na apigwe kwa kitendo chake

Page 46: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

46

hichi kibaya na aambiwe kutubia.Akitubu kwa kitendo chake hichi kibaya (ni

vizuri) la sivyo ni wajibu (mume huyo) kuuawa. Ni wajibu kwa mtawala wa

Waislamu au kiongozi wa nchi wamfanye atubu, la sivyo auawe. Kwa kuwa

kutukana Dini ya Kiislamu ni katika aina mbaya kabisa za ukafiri zinazovunja

Uislamu (wa mtu). Hali kadhalika kumtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi

wa sallam) na kutukana Qur-aan.

Swali:

Je, kukata kucha baada ya Wudhuu na kunyoa ndevu kunavunja Wudhuu au

hapana?

Imaam Ibn Baaz:

Kukata kucha hakutengui Wudhuu, hali kadhalika kunyoa ndevu na kichwa.

Kunyoa kichwa hakuvunji Wudhuu na wala sio katika mambo yanayovunja

Wudhuu. Lakini kunyoa wala kupunguza ndevu haijuzu. Kwa kuwa (Swalla

Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:

"Punguze masharubu na zirefusheni ndevu, mjitofautishe na washirikina."

Na anasema (´alayhis-Swalaat was-Salaam):

"Punguzeni masharubu na zirefusheni ndevu mjitofautishe na Majuus

(waabudu Moto)."

Kasema:

"... zirefusheni ndevu."

Kaamrisha (´alayhis-Swalaat was-Salaam) kuzirefusha, kuzifanya kuwa ndefu

na kuzifuga. Haijuzu kwa Muislamu kuzinyoa wala kuzipunguza, kamwe.

Badala yake, ni wajibu kuzirefusha, kuzifanya kuwa ndefu na kuzifuga. Kwa

kuwa, katika kufanya hivyo kuna kwenda kinyume na washirikina na

kushikamana na mafunzo ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na

kuna kujitofautisha na wanawake.

Page 47: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

47

Swali:

Akitawadha mtu kwa ajili ya Swalah, na njiani akakutana na mnaswara au

myahudi na wakapeana mikono. Je, Wudhuu wake unatenguka? Na ipi

hukumu kuwaalika manaswara kula chakula katika nyumba ya Muislamu?

Imaam Ibn Baaz:

Akipeana mikono na manaswara au mayahudi na makafiri wengine

atakaokutana nao, Wudhuu hautenguki. Atabaki na Twahara yake. Lakini

haifai kwake kupeana nao mikono wala kuanza yeye kuwaongelesha.

Anasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

"Msianze kuwapa mayahudi wala manaswara Salaam."

Na kupeana mikono ni baya zaidi. Tusemeje kupeana nao mikono? Asianze

kuwapa Salaam wala kupeana nao mikono. Lakini, wao wakianza kutoa

Salaam na kukupa mkono, hakuna ubaya kumjibu. Ama yeye kuanza, hapana

asianze. Ama kuwaalika katika walima na kula chakula, hili linahitajia

ufafanuzi. Ikiwa malengo ni kutaka kumkaribisha katika Uislamu, kumpa

nasaha na kumlingania katika Uislamu, hili halina neno. Ama kumualika

katika chakula kwa ajili ya Swadaqah na urafiki, hapana. Kwa kuwa baina

yetu sisi (Waislamu) na wao kuna uadui na chuki.

Swali:

Je, inajuzu kusoma kwa sauti katika Swalah za kusomwa kwa siri?

Imaam Ibn Baaz:

Kujuzu inajuzu, lakini kusoma kwa siri ni bora. Wakati fulani alikuwa

akisoma kwa sauti, anasoma kwa sauti Aayah. Lakini mara nyingi, alikuwa

Page 48: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

48

akisoma kwa siri (´alayhis-Swalaat was-Salaam). Hii ndio Sunnah. Alikuwa

akisoma kwa siri kama katika Swalah ya Dhuhr na ´Aswr, lakini kusoma kwa

sauti katika baadhi ya nyakati, hivi ndio bora.

Swali:

Je, inajuzu kusoma Qur-aan sokoni katika wakati ambapo ninakuwa sina kazi?

Imaam Ibn Baaz:

Hakuna ubaya kusoma Qur-aan katika duka lako au mahali pa kazi kwako,

ukiwa na uwezo wa hilo utasoma utachoweza katika Kitabu cha Allaah, au

utamdhukuru Allaah au utamswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa

sallam). Unapokuwa huna kazi, jishughulishe na kumdhukuru Allaah (´Azza

wa Jalla); kwa kusoma Qur-aan, kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi

wa sallam) au kwa kusoma vitabu vyenye faida. Mambo yote haya ni mazuri.

Swali:

Sisi katika mji wetu ikiwa mtu anaitakidiwa kuwa ni mwema, basi

wanamfanya mtoto wake kuwa Khalifah baada yake. Na akifa mtoto huyu,

wanaweka Khalifah mwingine badala yake kutoka katika watoto wake, hali

inaendelea hivi wanarithiana Ukhalifah. Na wote hawa, (watu) wanaamini

kuwa ni wema na wana baraka, na watu wanabusu mikono yao. Na

wanawaletea mali na kuwawekea nadhiri kwa kuomba baraka. Ipi hukumu ya

Kishari´ah kwa hilo?

Imaam Ibn Baaz:

Page 49: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

49

Haya ni katika matendo ya baadhi ya Suufiyyah. Na hili ni jambo lisilokuwa

na asli katika Shari´ah. Bali haya ni katika mambo ya ukhurafi ambayo

yamezushwa na baadhi ya watu wa Ahl-ul-Taswawwuf kurithiana Ukhalifah.

Haya hayana asli. Na baraka kuchukuliwa kutoka kwa baadhi ya watu, hili

halina asli na ni jambo lisilojuzu. Bali hili ni katika maovu na njia

inayopelekea katika Shirki kubwa. Baraka zinatoka kwa Allaah (Ta´ala). Yeye

ndiye Huleta baraka (Subaanahu wa Ta´ala). Na wala baraka haitafutwi

kutoka kwa asiyekuwa Yeye. Kuitafuta kutoka kwa Zayd au ´Amr akupe

baraka, hili ni jambo lisilokuwa na asli. Bali ni katika Shirki, ikiwa utamuomba

nayo na ukaamini kuwa anawabariki watu na mwenye kuleta baraka ni yeye,

hii ni katika Shirki kubwa. A´udhubi Allaah.

Ama akidhani (mwenye kufanya hivyo) kuwa, kumtumikia au kumtii kuna

baraka kwa kuwa ni katika watu wema na anataraji kwa hili kupata thawabu

akimtii au kumsaidia kwa kitu, hili yategemea. Ikiwa huyu mwenye kutiiwa

ni mwanachuoni katika wanachuoni wa Waislamu au ni katika watu wema

wanaomuabudu Allaah ambao wanajulikana ni wenye misimamo na anamtii

Allaah na Mtume Wake, akamsaidia kwa ajili ya Allaah, akamtatulia haja yake

na akamtembelea kwa ajili ya Allaah na si kwa ajili ya kutafuta baraka kutoka

kwake, au akamtembelea mgonjwa, haya ndio maadili ya Waislamu na ni

jambo limependekezwa. Kwa minajili ya kutembeleana, kumtembelea

mgonjwa, kumtembelea ndugu yako kwa ajili ya Allaah, hili ni haki. Ama

(kumtembelea) kwa minajili ya kumuomba baraka, hili ni jambo lisilojuzu.

Kwa kuwa hili halina asli yoyote, isipokuwa hili ni kwa haki ya Mtume

(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) peke yake. Allaah Kamfanya kuwa ni

mwenye baraka. Hakuna ubaya mtu akakusudia kutafuta baraka kutoka

katika maji yake, nywele zake n.k., yeye ana baraka (´alayhi-Swalaat was-

Salaam).

Na hili la kutabaruku kwake lilikuwa linafanywa na Maswahabah. Hili ni

jambo ambalo ni maalumu kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na si

kwa mwingine yeyote. Ni wajibu kwa Waislamu wajue hili, na wajiepushe na

ukhurafi huu ambao unafanywa na Suufiyyah, Tijaaniyyah na Shaadhiliyyah

na Ukhalifa huu ambao wanarithiana, halina asli na ni jambo la batili. Ni

jambo ovu na njia inayopelekea katika Shirki. A´udhubi Allaah.

Page 50: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

50

Swali:

Je, inatosha kusema "Bismillaah" bila ya kuelekea Qiblah, au ni lazima kufanya

yote mawili (kusema Bismillaah na kuelekea Qiblah)? Kwa kuwa mahala

ambapo nafanya kazi ni pafinyu na wala siwezi kuelekea Qiblah wakati wa

kuchinja.

Imaam Ibn Baaz:

Kusema "Bismillaah" wakati wa kuchinja ni jambo la wajibu, kwa kuwa Allaah

(Jalla wa ´Alaa) Kaamrisha hilo, na namna hii ndivyo alivyoamrisah Mtume

(´alayhis-Swalaat was-Salaam). Haijuzu mtu kukusudia kuacha kusema

"Bismillaah". Mtu anatakiwa kusema wakati wa kuchinja "Bismillaah Allaahu

Akbar". Hii ndio Sunnah. Na lau atasema "Bismillaah" yatosha. Haifai kwake

kukusudia kuacha kusema "Bismillaah". Akiiacha kwa kusahau au kwa ujinga

wa kutokujua, hakuna neno kwa hilo na kichinjo kitakuwa ni Halali. Lakini

haifai kwake kuiacha kwa kukusudia. Ama kuelekea Qiblah ni jambo

limependekezwa na wala sio lawajibu. Lau atachinja bila ya kuelekea Qiblah,

ni sahihi na inajuzu. Lakini kuelekea kwake Qiblah wakati wa kuchinja ndio

bora.

Swali:

Baadhi ya maamuma wakitoa Salaam moja upande wa kulia kabla ya Imamu

kwa kusahau. Je, Swalah zao zinabatilika?

Imaam Ibn Baaz:

Swalah yake haibatiliki. Lakini itabidi watoe Salaam baada yake mara mbili.

Swali:

Page 51: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

51

Ni yapi mahari ya Kishari´ah kwa msichana ambaye hajaolewa na mwanamke

ambaye kishatalikiwa?

Imaam Ibn Baaz:

Mahari hayana mpaka maalumu. Hakukutengwa mahari maalumu kwa yule

ambaye hajaolewa, ambaye katalikiwa wala yule ambaye kafiwa. Atayowekea

hata kama yatakuwa ni madogo, yatosha. Sawa mwanamke huyo alikuwa ni

bikira hajaolewa, alikuwa amekatalikiwa au alikuwa amefiwa. Watayopatana

mwanaume na mwanamke yanatosha, sawa yakiwa madogo au yakiwa

mengi.

Swali:

Baada ya kukoga janaba, natokwa na kitu kama manii. Je, ni wajibu kwangu

kurudi kukoga tena?

Imaam Ibn Baaz:

Hapana sio wajibu, maadamu umekwishakoga manii haya hayana maana

yoyote. Kwa kuwa yametoka bila ya shahawa, hukumu yake ni kama ya

mkojo, hayana maana yoyote. La wajibu ambalo ni kukoga

umekwishatekeleza, haidhuru kutoka kwa manii ambayo ni athari ya jimaa

uliofanya. Hali kadhalika mwanaume, lau atakoga kisha yakamtoka baada ya

hapo pamoja na mkojo, haidhuru hilo maadamu alikoga kwa jimaa aliofanya

mwanzoni. Ama yakitoka kwa shahawa nyingi, au kwa kupapa sana, au kwa

kubusu au kwa mfano wa hayo katika mambo ambayo ni sababu ya kutoka

kwa manii kwa shahawa, haya yatakuwa ni manii mapya ambayo yanahitajia

kukoga. Ikiwa yametoka kwa shahawa mpya; sawa ikiwa ni kwa kuangalia,

kupapasa au kubusu, haya hukumu yake itakuwa ya janaba mpya. Ni juu ya

yule ambaye yamemtoka akoge upya sawa ikiwa ni mwanaume au

mwanamke. Ama ikiwa ni (athari ya) yaliyobaki kwa (kitendo) alichokifanya

nyuma, hayadhuru na wala hayahitajii kukoga upya.

Page 52: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

52

Wanaosema Kuwa Qur-aan Imeumbwa Na Kutoonekana Allaah Qiyaamah

Swali:

Ipi hukumu kwa mwenye kujinasibisha na madhehebu ambayo yanaamini

kuwa Qur-aan imeumbwa, na kwamba watu hawatomuona Allaah siku ya

Qiyaamah, kwa kuzingatia ya kwamba yule anayejinasibisha na madhehebu

haya mara nyingi hawakiri kuumbwa kwa Qur-aan wala hawaamini hivyo

[wao] na wanasema sisi hatuamini kuwa Qur-aan imeumbwa, lakini sisi

tunajinasibisha na madhehebu haya kwa kuwa baba zetu walikuwa

wakijinasibisha kwayo tu. Na je, ipi hukumu ya mwenye kuamini kuwa Qur-

aan imeumbwa? Je, anachukuliwa katoka katika Uislamu?

Imaam Ibn Baaz:

Ndio, mwenye kuamini kuwa Qur-aan imeumbwa ina maana anapinga kuwa

sio Maneno ya Allaah. Hii ni Shirki kubwa. Hukumu hii hali kadhalika kwa

yule mwenye kupinga kuonekana kwa Allaah siku ya Qiyaamah Peponi. Hii

ni Shirki kubwa. Kwa kuwa amemkadhibisha Allaah na amemkadhibisha

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hivyo kila kikundi au mtu asemae

Qur-aan imeumbwa, ina maana [anapinga] si Maneno ya Allaah. Bali anaona

ni maneno ya kiumbe yameumbwa atamka nayo. Na Allaah Kasema kuwa ni

Maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Na Allaah Kasema kuwa ni

Maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Katika Kauli Yake:

ن أحد وإن هللا كلم يسمع حتى فأجره استجارك المشركين م

"Na ikiwa mmoja wapo katika washirikina akikuomba ulinzi, basi mpe ulinzi

apate kusikia Maneno ya Allaah." (09:06)

Kasema tena Allaah (Ta´ala):

لوا أن يريدون هللا كلم يبد

"Wanataka kuyabadili Maneno ya Allaah.” (48:15)

Page 53: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

53

Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwaambia watu:

"Aletwe kwanza mpaka afikishiwe Maneno ya Allaah."

Ilikuwa ni wakati bado wanasubiri kufanya Hijrah kutoka Makkah,

akaawambia:

"Wasimhame kwanza mpaka afikishiwe Maneno ya Allaah."

Makusudio ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na

Maswahabah wote walikubaliana kuwa Qur-aan ni Maneno ya Allaah. Na

Qur-aan yenyewe inaonesha dalili kuwa ni Maneno ya Allaah. Atakayedai

kuwa Qur-aan imeumbwa basi amedai kuwa sio Maneno ya Allaah.

Anakufuru kwa hili. Kwa kuwa kamkadhibisha Allaah na Mtume Wake na

Ijmaa´ [makubaliono ya Maswahabah] ya Waislamu.

Hali kadhalika kwa mwenye kupinga Sifa za Allaah na akapinga kuonekana.

Mwenye kusema [Allaah] sio Al-Haliym, Al-Hakiym, Al-´Aziyz, Al-Qadiyr na

Sifa Zake zingine. Huyu ni kafiri kama Jahmiyyah.

Hali kadhalika mwenye kupinga kuonekana kwa Allaah, kuwa hatoonekana

Aakhirah wala Peponi. Huyu ni kafiri kufuru kubwa. A´udhubi Allaah.

Tunamuomba Allaah afya. Kwa kuwa kamkadhibisha Allaah na Mtume

Wake. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Kasema kwa haki ya makafiri:

هم كل بهم عن إن لمحجوبون يومئذ ر

"Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa kumuona Mola

Wao." (83:15)

Asiyemuitikia Allaah [katika hili] ni kafiri, ina maana waumini watamuona

Mola Wao (Subhaanahu wa Ta´ala).

اضرة يومئذ وجوه ناظرة ربها إلى ن

"Zipo nyuso siku hiyo zitaong'ara, zinamwangalia Mola Wao." (75:22-23)

"Kungara" kutokana na Uzuri Wake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Na

Kasema tena Allaah (Jalla wa ´Alaa):

وزيادة الحسنى أحسنوا للذين

"Kwa wafanyao wema ni wema na zaidi." (10:26)

Page 54: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

54

Maana ya "Ziada" katika Hadiyth sahihi kasema Mtume (Swalla Allaahu

´alayhi wa sallam):

"Husna [wema] ni Pepo, na ziada ni kuangalia Uso wa Allaah."

Na imekuja katika Hadiyth Swahiyh Mutawaatir kutoka kwa Mtume (Swalla

Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa amesema:

"Hakika nyinyi mtamuona Mola Wenu kama mnavyouona mwezi mpevu.

Hakuna kitu kitakachowazuia kumuona siku hiyo."

Na akasema tena (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika upokezi

mwingine:

"Kama mnavyouona mwezi mpevu. Na kama mnavyouona mwezi usiku wa

al-Badr. Na hakuna kitu kitakachowazuia kumuona siku hiyo."

Ina maana kuonekana kwa Allaah ni jambo la wazi kabisa, ni kitu hakina utata

wala shaka. Makusudio ni kuwa waumini siku ya Qiyaamah watamuona

Mola Wao waziwazi kama uonekanavyo mwezi wazi kabisa bila ya pazia.

Hali kadhalika Peponi watamuona Mola wao (Jalla wa ´Alaa). Atakayepinga

hili na kusema hatoonekana kamkadhibisha Allaah na Mtume Wake hivyo

anakuwa kafiri. Tunamuomba Allaah afya.

Chanzo: http://www.binbaz.org.sa/mat/10243

Swali:

Kuna mtu katika mji wetu hafungi wala haswali. Na nimemuona kwa macho

yangu anacheza kamari. Na watu wake wanadai kuwa ni katika mawalii na

watu walio karibu ya Allaah. Na kuna watu waaminifu wamenieleza ya kuwa

anamtukana Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Wakati nilipomkataza kitendo hichi kichafu, wakadai watu wake ya kuwa hii

ni hali yake kwa uinje, ama kwa udani ni muumini. Ipi hukumu ya Kishari´ah

kwa mfano wa huyu?

Page 55: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

55

Imaam Ibn Baaz:

Huyu ni mnafiki na wala sio muumini. Mfano wa watu kama hawa ni katika

mawalii wa Shaytwaan. Mawalii wa Allaah ni wale wenye Imani na Taqwa.

Anasema Allaah (Subhaanah):

ه أولياء إن أل قون وكانوا آمنوا الذين يحزنون هم ول عليهم خوف ل اللـ يت

"Tanabahi! Hakika awliyaa wa Allaah (vipenzi Vyake wanaoamini Tawhiyd

ya Allaah na kufuata amri Zake) hawana khofu juu yao, na wala

hawatohuzunika. Wale walioamini na wakawa wana taqwa (wanafuata amri

za Allaah na Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

( (26:01-06

Namna hii ndivyo ilivyo katika Suurat Yuunus, hizi ndizo sifa za mawalii wa

Allaah; ni wenye Imani na Taqwa kwa nje na kwa ndani. Na Akasema tena

(´Azza wa Jalla):

كن المتقون إل أولياؤه إن أولياءه كانوا وما ـ يعلمون ل أكثرهم ول

"Na hawakuwa walinzi (awliyaa) wake (Msikiti huo). Hawakuwa walinzi

(awliyaa)wake isipokuwa wenye taqwa; lakini wengi wao hawajui." (08:34)

Anasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

"Watu wa (... sauti haiko wazi... ) sio katika mawalii wangu, isipokuwa

mawalii wangu ni waumini."

Mawalii wa Allaah na mawalii wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)

ni waumini na watu wa Taqwa. Yule mwenye kujidhihirisha kwa kuacha

Swalah, Swawm na anamtukana Allaah na Mtume Wake, huyu sio katika

mawalii wa Allaah, bali ni katika mawalii wa Shaytwaan.

Na ni wajibu aambiwe kutubu vinginevyo auawe, ni wajibu kwa mtawala wa

Waislamu amwambie atubie la sivyo auawe. Kwa kuwa mwenye kuacha

Swalah ni kafiri, aambiwe kutubu la sivyo auawe.

Na mwenye kumtukana Allaah na Mtume wake, huyu anauawa hata bila ya

kuambiwa kutubia kutokana na wanavyoona kundi katika wanachuoni.

Muhimu ni kuwa, mtu huyu na watu mfano wake sio katika mawalii wa

Allaah, isipokuwa ni katika mawalii wa Shaytwaan. Na wale wanaomtetea na

kumhami na kusema kuwa kwa nje ni namna hii tu, lakini kwa ndani ni

Page 56: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

56

muumini, watu hawa ni katika jinsia yake nao ni mawalii wa Shaytwaan. Na

ni watetezi wa shari na ufisadi.

Baadhi ya Suufiyyah waliodanganywa ndio hufanya hivi. Ni wajibu

kutanabahi kwa hili. Wanachuoni wa Sunnah (Rahimahumu Allaah)

wamesema kwa yule mwenye kudai ni walii:

"Lau atatembea angani, akatembea juu ya maji, hazingatiwi kuwa ni katika mawalii

wa Allaah mpaka matendo yake yatazamwe kwanza na kupimwa kwa mizani ya

Kishari´ah.”

Akisimama katika mipaka ya Kishari´ah na kujulikana kuwa ni mwenye

msimamo juu ya utiifu wa Allaah na Mtume Wake na kujiweka mbali na

maharamisho ya Allaah na Mtume Wake, huyu ndiye muumini na walii. Na

yakionekana kwake mambo ya ufasiki, kufanya ya haramu au kuacha ya

wajibu, haya ni dalili tosha kuwa ni katika mawalii wa Shaytwaan na sio

katika mawalii wa Allaah." Kama alivyosema haya Imaam Shaafi´iy na

Ahmad (Rahimahuma Allaah) na wasiokuwa wao katika wanachuoni.

Muhimu ni kuwa, mfano wa watu kama hawa ni katika mawalii wa

Shaytwaan. Na ni wajibu kwa mwenye kujua hilo kupeleka suala lake kwa

kiongozi wa Waislamu mpaka ampe kinachomstahiki; amwambie kitubu la

sivyo amuue.

Swali:

Kulitokea baina yangu mimi na mke wangu tofauti kisha siku hiyo nikampiga

kutokana na ghadhabu niliokuwa nayo, akalia na kunambia "nataka unitaliki".

Nikamwambia "vaa nguo zako nikupeleke kwa familia yako". Alipokuwa

anataka kuvaa nguo zake nikawa nimemkataza kufanya hivyo na tukapatana

siku hiyo hiyo kama kwamba hakukupitika kitu. Na hapo ilikuwa miezi

miwili iliopita. Lakini nafsi yangu inanambia mara kwa mara mbali na muda

wote huu kuhusu hukumu ya Kishari´ah kutokana na tulioambizana. Na je,

kwa hayo Talaka itakuwa imepita?

Imaam Ibn Baaz:

Page 57: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

57

Ikiwa hali ni kama alivyosema muulizaji, hakuna Talaka, kwa kuwa nia peke

yake haipitishi Talaka. Isipokuwa Talaka inapita kwa kufanya moja ya mambo

mawili; ima kwa kutamka maneno au kuandika. Au nia peke yake haipitishi

Talaka. Kutokana na kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

"Hakika ya Allaah Kausamehe Ummah wangu, yanayohadithiwa na nafsi zao

maadamu hawajayafanya wala kuyatamka."

Nia peke yake wanachuoni wanaona kuwa Talaka haiwezi kupita. Kuwa na

utulivu ewe ndugu na umshukuru Allaah kuwa na usalama. Na ninamuomba

Allaah Atupe sote Tawfiyq.

Swali:

Walii wa mwanamke akimuwekea sharti asioe (mwanamke mwingine) juu ya

binti yake, kisha akafanya. Je, ni haki kwa mke kuomba Talaka?

Imaam Ibn Baaz:

Ndio, akimuwekea sharti asioe mwanamke mwingine, sharti ni sahihi

kutokana na kauli sahihi ya wanachuoni. Na anaweza kuomba watengane

akioa. Na akiendelea kuishi nae, Alhamdulillah.

Swali:

Mke wangu kwa sasa haswali na wala haswali. Na hii ilikuwa ni sharti yangu

kwake kabla ya kufunga nae ndoa. Na baada ya ndoa nikawa nimemwacha

kwa kiasi cha muda miezi mitano. Ipi hukumu ya Kishari´ah kwa mke kama

huyu?

Imaam Ibn Baaz:

Page 58: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

58

Mwanamke asiyeswali hazingatiwi kuwa ni Muislamu, bali anazingatiwa

kuwa ni kafiri kutokana na kauli yenye nguvu ya wanachuoni. Kwa kuwa

kuacha Swalah ni kufuru kubwa, kwa kuwa Swalah ndio nguzo ya Uislamu.

Na imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba

amesema:

"Ahadi iliopo baina yetu sisi na wao (makafiri) ni Swalah, atakayeiacha

amekufuru."

Na hili linawahusu wanaume na wanawake. Na kauli yenye nguvu ni kuwa ni

kufuru kubwa, hii ndio kauli sahihi na ndio kauli waliokubaliana

Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kama

alivyosema ´Abdullaah bin Shaqiyq:

"Maswahabah wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)

hawakuwa wanaona kitu mtu akikiacha ni kufuru isipokuwa kuacha Swalah."

Hii ni dalili inaonesha kuwa [Maswahabah] (Radhiya Allaahu ´anhum)

walikubaliana juu ya hili. Asiyeswali hana kheri yoyote. Ni wajibu kutengana

nae kabisa.

لهن يحلون هم ول لهم حل هن ل

"Wao si (wake) halaal kwao (hao makafiri), na wala wao si (waume) halaal

kwao." (60:10)

Na wala usilale nae katika kitanda kimoja, kwani mwanamke huyu hana kheri

yoyote, bali ni wajibu kuachana nae.

Swali:

Nilioa mtoto wa mjomba wangu nikafunga nae ndoa na wala sikumwingilia.

Na mke huyu (niliyemuoa) ni dada wa kaka yangu katika kunyonya, yaani

alinyonya kwa mamangu na mimi sikunyonya kwa mama yake. Je, ndoa hii ni

Halali au Haramu?

Imaam Ibn Baaz:

Page 59: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

59

Ndoa hii haina neno. Maadamu yeye hakunyonya kwa mama yako na wewe

hukunyonya kwa mama yake, haina neno. Ama kaka yako kunyonya ziwa

moja na mke wako, hili halizingatiwi. Muhimu ni kuwa, hili halina neno ewe

muulizaji.

Swali:

Mke wangu mimi haswali. Na nimeshamwamrisha Swalah zaidi ya mara moja

lakini hapokei (nasaha). Hali kadhalika havai Hijaab, na nywele zake

zinaonekana na watu wote. Naomba unipe faida nimfanye nini?

Imaam Ibn Baaz:

Mwanamke huyu, kakusanyikiwa na shari mbili kubwa. Na moja wapo ni

kubwa zaidi kuliko nyingine.

1) Shari ya kwanza ni kutoswali kwake kwake na hii ni kufuru kubwa

kutokana na kauli ya sahihi.

2) Shari yake ya pili, ni kutojisiri kwake kwa Hijaab. Inatakikana kwako na hili

ni jambo la wajibu kutengana nae, kwa kuwa haijuzu kwa Muislamu (wa

kiume) kubaki na mwanamke kafiri. Anasema (Ta´ala):

لهن يحلون هم ول لهم حل هن ل

"Wao si (wake) halaal kwao (hao makafiri), na wala wao si (waume) halaal

kwao." (60:10)

Ni wajibu kwako kutengana nae maadamu hapokei nasaha. Ni wajibu

kuachana nae. Na ninakubashiria kuwa utapata aliye bora kuliko yeye. Na

(huyo mwanamke) tunamuombea kwa Allaah uongofu. Muhimu ni kuwa,

huyu mwanamke ana shari mbili ambazo ni kubwa, na moja wapo ndio

kubwa zaidi kuliko nyingine. Nayo ni kuacha Swalah, hii ni kubwa kwa kuwa

hii ni kufuru kubwa. Na kule kutojisitiri kwake si nywele zake wala uso wake,

hii pia ni dhambi na shari kubwa. Ni wajibu kwako kutengana nae,

kutahadhari nae na kumpa Talaka. Tunamuomba Allaah sote Atupe afya. Na

yule mwenye kuacha kitu kwa ajili ya Allaah, Allaah Humpa kilicho bora

Page 60: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

60

kuliko hicho (alichokiacha). Allaah Atakupa aliye mbora na mwema kuliko

yeye In Shaa Allaah.

Swali:

Inajuzu kwa Muislamu kunuia nia mbili kwa wakati mmoja? Kama kwa

mfano kunuia Swalah iwe ya Sunnah ikiwa atakosea katika Swalah ya faradhi,

au akakosea katika Hajj au Zakaah?

Imaam Ibn Baaz:

Hatujui kuwa hili lina asli. Bali asli ni salama na afya. Anuie Swalah

anayoswali kama anavyotaka; Sunnah ya Dhuhr, Sunnah ya Maghrib, Sunnah

ya ´Ishaa, Sunnah ya Dhuhaa bila ya kuwa na mashaka (wasiwasi)

aliyoashiria. Asli ni salama. Alhamdulillaah. Na wala hatujui kuwa hili lina

asli yoyote ya kuweka nia mbili.

Swali:

Mimi namwamini Allaah kuwa ni Mmoja asiyekuwa na mshirika, lakini

nimesikia watu wakisema kuwa kuna mtu mwenye mavazi meupe sana na

hakuonekani kwake athari za safari. Mtu huyu akikupa kitu, basi baraka ya

mali yako inazidi. Naomba faida, je, mambo haya yanaingia akilini au ni

katika Bid´ah?

Imaam Ibn Baaz:

Kauli hii ni ya batili na haina msingi wowote. Na mtu kama huyu hapatikani.

Na baadhi ya watu wanadhani kuwa aliyekusudiwa hapa ni Khidhr, na hili ni

jambo lisilokuwa na usahihi wowote. Khidhr alikufa muda tu kabla ya kuja

kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutokana na kauli ya sahihi ya

Page 61: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

61

wanachuoni. Na ukhurafi huu uliyosema, ni katika mambo ya Kishaytwaan

na hayana msingi wowote. Inatakikana ujue hilo, na usidanganyike na

maneno ya watu hawa wachawi.

Swali:

Ipi hukumu ya mwenye kunuia kumtaliki mke wake na akachelewesha

kufanya hivyo?

Imaam Ibn Baaz:

Mwanaume akinuia kumtaliki mke wake kisha akaacha hilo na asifanye kitu,

Talaka haipiti. Nia haifanyi Talaka kupita. Kutokana na kauli ya Mtume

(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

"Hakika ya Allaah Kausamehe Ummah wangu yanayohadithia nafsi zao

maadamu hawajayafanaya au kuyatamka."

Maadamu hajayatamka na wala kuyafanya - kuandika hilo - isipokuwa

kaweka nia tu, nia hii haipitishi chochote na mke atabaki katika asli yake.

Talaka haipiti mpaka aandike Talaka au aitamke.

Swali:

Ni sahihi kwa mwanaume kumuosha mke wake anapokufa au msichana wa

mwaka moja mpaka miwili hata kama atakuwa ni ajinabi kwake?

Imaam Ibn Baaz:

Page 62: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

62

Hakuna ubaya wowote mwanaume kumuosha mke wake, na mke kumuosha

mume wake kwa kufuata Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa

sallam). Ama kinyume na mke, hapana.

Lakini mdogo ni kama mfano wa mke. Hakuna ubaya mwanaume akamuosha

msichana mdogo, na wala hakuna neno akamuosha kama mke. Ama mama

yake, msichana wake, dada yake na mfano wa hao, haifai kwake kuwaosha.

Bali hawa wanaoshwa na wanawake. Lakini msichana ambaye ni mdogo

haina neno anaweza kuoshwa na wanaume. Ikiwa ni chini ya miaka saba;

kama mfano wa msichana wa miaka mitano, tatu, mine, haina neno.

Hali kadhalika, mvulana wa chini ya miaka saba anaweza kuoshwa na

wanawake pia. Watoto chini ya miaka saba wanaweza kuoshwa na wanaume

na wanawake.

Swali:

Mwanaume aliyeoa kumwaga manii nje ya tupu ya mwanamke ni Haramu au

hapana? Na khaswa anafanya hivi wakati wa hali ya hedhi au damu ya uzazi?

Imaam Ibn Baaz:

Kumwaga manii nje ya tupu ikiwa kuna manufaa, hakuna neno kufanya

hivyo. Na hii huitwa "´Azl". Na imethibiti ya kwamba Maswahabah (Radhiya

Allaahu ´anhum) walikuwa wakifanya ´Azl, na akawakubalia hilo (´alayhis-

Swalaat was-Salaam). Kukiwa na haja ya kufanya ´Azl, bi maana kumwaga

manii yake nje ya tupu, ima kwa kuwa mke wake hawezi kushika mimba

nyingine wakati ule au kwa sababu aliyoisema muulizaji. Kwa kuwa lililo la

Haramu (wakati wa hedhi na nifasi) ni kufanya nae jimaa. Akicheza nae

katika tupu yake (mke) na akamwaga manii kwa nje na wala asimjamii,

hakuna ubaya kufanya hivyo. Kwa kuwa Haramu ni kufanya jimaa. Kasema

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusiana na mwanamke wa

hedhi:

"Fanya kila kitu isipokuwa (kitendo cha) ndoa."

Page 63: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

63

Yaani jimaa. Anaweza kukutana nae, kumkumbatia, kucheza nae na kustarehe

nae kwa tupu yake, tumbo lake na yasiyokuwa hayo. Lakini bora zaidi, awe

na kizuizi kwa juu kama ´Izaar au suruwaliili kujiepusha na khatari. Kwa

kuwa mwenye kuikabili tupu, Shaytwaan anaweza kumshawishi kufanya

kitendo cha jimaa kilochoharamishwa. Bora, ni yeye (mume) akutane nae

nyuma ya ´Izaar, suruwali au kanzu. Anasema ´Aaishah (Radhiya Allaahu

´anha):

"Alikuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiniamuru nijifunge

vizuri nguo yangu kiunoni kisha akinikumbatia hata nikiwa katika hedhi."

Namna hii ndivyo alivyosema ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha). Makusudio

ni kuwa, Sunnah kwa upande wa mume ikiwa mwanamke yuko katika hedhi

au nifasi, akutana nae nyuma ya ´Izaar au nyuma ya suruwali na mfano wa

hivyo. Lakini lau akikutana nae ndani ya ´Izaar na ndani ya suruwali, hakuna

ubaya wa hili. Kumekuja katika Sunnah kitu kinachotolea dalili hilo. Kwa

kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

"Fanya kila kitu isipokuwa (kitendo cha) ndoa."

Ilikuwa ni baada ya kuambiwa kuwa mayahudi pindi mwanamke anapoingia

hedhini, basi wanamchukia, wanamtenga na kumhama nyumbani. Ndio

akawa amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

"Fanya kila kitu isipokuwa (kitendo cha) ndoa."

Yaani wakhalifuni mayahudi, bi maana fanya kila kitu ila jimaa. Hivyo

akiweka tupu yake kwenye mapaja na akaweka nje ya tupu, hakuna ubaya.

Lakini asimjamii, ni Haramu kwake kumjamii sawa ikiwa atateremsha au

kutoteremsha. Ni wajibu kujiepusha na jimaa. Ama kule kuweka kwake tupu

yake kwenye mapaja yake au karibu na tupu yake (mke) mpaka akamwaga

bila ya kuiingiza, hakuna ubaya kwa hilo. Lakini lililo bora zaidi kabisa, ni

yeye kujiepusha na hili, ili Shaytwaan asimshawishi kufanya kitendo

kilichoharamishwa. Na kwa ajili ya hili, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa

sallam) kawaamrisha wanawake wajisitiri (tupu zao) wakati wa kukutana nao

moja kwa moja (´alayhis-Swalaat was-Salaam).

Page 64: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

64

Swali:

Mtu kama alikuwa na mke akamtaliki. Je, anaweza kumuoa dada yake ndani

ya eda yake (huyo mke wake)? Na akifa anaweza kuoa katika hali hii?

Imaam Ibn Baaz:

Akimtaliki mke wake, haijuzu kwake kumuoa dada yake wala wanawake

wengine isipokuwa baada ya eda, baada ya kwisha kwa eda. Ikiwa ni Talaka

rejea, hili wamekubaliana wanachuoni wote. Ya kwamba haijuzu kwake

kumuoa dada yake wala mwanamke mwingine yeyote isipokuwa baada ya

kwisha kwa eda, kwa kuwa mwanamke rejea ni mke. Ama ikiwa ni Talaka

Baain [Talaka ambayo kakosa haki ya kumrejeakwa kuwa eda imekwisha], au

Talaka kwa mwanamke kujivua (katika ndoa), hapa kuna tofauti, lakini kauli

yenye nguvu ni kuwa asioe mwingine ila baada ya kwisha kwa eda. Ama

(mke) akishakufa, hakuna ubaya akaoa mwanamke mwingine baada ya siku

moja au mbili tokea siku ile kafariki. Ikiwa mke kafa, eda yake imekwisha kwa

kufa kwake, ndoa imekwisha kwa kufa kwake. Katika hali hii, hakuna ubaya

akamuoa dada yake au mwanamke mwingine yeyote.

Swali:

Mimi ninafanya kazi ya uguuzi, na wakati fulani ninawapa wanaume "ibar"

kutokana na sheria ya kazini kwa kukosekana muuguzi mwanaume awezae

kuwapa "ibar" hii. Na anakuwa mgojwa katika hali nzito ya kuhitajia dawa hii.

Ipi hukumu ya hili na je nina madhambi?

Imaam Ibn Baaz:

Kukihitajia haja (dharurah) ya hilo, hakuna neno In Shaa Allaah. Lakini ni

wajibu kwako kuwa pamoja na wanawake. Na wauguzi wanaume wawe

pamoja na wanaume wenzao, na kila mmoja achunge na kutimiza kazi yake.

Kukitokea dharurah ya wewe kumsimamia mwanaume kwa kukosekana

muugizi mwanaume, hakuna neno In Shaa Allaah.

Page 65: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

65

Swali:

Ipi hukumu ya mwanamke ambaye ametalikiwa kisha akaolewa na

mwanaume mwingine. Na baada ya muda mrefu akamuomba yule mume

wake wa kwanza kumwandikia Talaka ili kupata pesa kutoka serikali, pamoja

na kuwa (mwanamke huyu) kwa sasa yuko katika dhimma ya mwanaume

ambaye yuko nae sasa?

Imaam Ibn Baaz:

Ni kama tulivyosema. Hata kama itakuwa ni kweli katalikiwa, lakini akaficha

ukweli ya kwamba kaolewa (na mume mwingine) baada ya hapo, haya ni

maovu na utatizi. Ndani yake kuna hila na uadui. A´udhubi Allaah.

Kuchukua mali pasina haki ni jambo ovu na ni ulaji wa vya Haramu.

Tunamuomba Allaah afya.

Swali:

Mimi ninawasalimia na mkono watoto wa shangazi yangu na mjomba wangu

bila ya kizuizi. Je, hili linajuzu? Na ikiwa haijuzu, je naweza kuweka mkononi

mwangu abaya na vifuniko vya mikono (gloves)?

Imaam Ibn Baaz:

Haijuzu kwa mwanamke kupeana mikono na wanaume ikiwa sio Mahaarim

zake; kama mfano wa watoto wa shangazi na mjomba wake, hakika hawa sio

Mahram zake. Haifai kwake kupeana nao mikono, sawa ikiwa kwa kuweka

kizuizi au bila ya kuzuizi. Isipokuwa anaweza kupeana mikono na Mahaarim

zake; kama kwa mfano wa kaka yake, mjomba wake, shangazi yake, baba

yake au wanawake wenzake haina neno. Anasema Mtume (Swalla Allaahu

´alayhi wa sallam):

Page 66: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

66

"Mimi sipeani mikono na wanawake."

Mwanaume asipeani mokono na mwanamke, na mwanamke asipeani mikono

na mwanaume ambaye sio Mahram wake; kama kwa mfano wa mtoto wa

shangazi yake, mjomba wake, jirani yake, mume wa dada yake, kaka wa mke

wake. Wote hawa ni watu ajinabi kwake, haifai kwake kupeana nao mikono,

sawa iwe kwa kuweka kizuizi au pasina kizuizi.

Swali:

Ipi hukumu ya kutia wanja? Na je, imethibiti kwa Mtume (Swalla Allaahu

´alayhi wa sallam) ya kwamba alikuwa anaweka wanja machoni mwake?

Imaam Ibn Baaz:

Kutia wanja ni Sunnah. Na imethibiti ya kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi

wa sallam) alikuwa anatia wanja machoni mwake. Ni Sunnah.

Swali:

Kuna mtu ana watoto watatu ambao hawana mapungufu katika kumtii na

kumtendea wema, na yeye (mzazi huyo) anawaombea dhidi yao. Je, Du´aa

yake itawadhuru?

Imaam Ibn Baaz:

Haimpasi muumini kuomba dhidi ya watoto wake, bali ni wajibu kwake

kutahadhari kwa hilo, kwa kuwa anaweza kuomba katika saa ya kujibiwa.

Haimpasi kwake kuomba dhidi yao, na ikiwa ni wema jambo hili linakuwa

baya zaidi kukosa kuwaombea Du´aa. Ama ikiwa wana mapungufu,

haitakikani vilevile kwake kuomba dhidi yao. Bali kinyume chake, awaombee

Page 67: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

67

uongofu na wema na Tawfiyq. Namna hii ndivyo inavyopasa kuwa kwa

muumini.

Na kumekuja nususi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)

ambazo zinatahadharisha mzazi kumuombea Du´aa mbaya mtoto wake, ahli

zake na mali yake. Kwa kuwa anaweza kuomba saa ya kujibiwa, akawa

amejidhuru nafsi yake mwenyewe, ahli zake na mtoto wake.

Inatakikana kwako ewe muulizaji uuhifadhi ulimi wako na umkataze

unayemjua kuwa anafanya jambo hili auhifadhi ulimi wake na amche Allaah

kwa hilo, mpaka asiombe dhidi ya mtoto wake wala kuwaombea Waislamu

wengine. Bali kinyume chake, awaombee kheri, uiamara na msimamo. Na

isiwe kuwaombea Du´aa dhidi yao kwa yanayowadhuru.

Swali:

Muulizaji anasema kuwa mzazi wake kafikisha zaidi ya miaka 85 naye ni

mgonjwa hawezi kutia Wudhuu kwa maji. Tunampa udongo atayamamu

kwao. Je, inajuzu kwake kutayamamu kwa udongo huu mwezi au zaidi?

Imaam Ibn Baaz:

Ndio, hakuna neno. Atatumia udongo mpaka katika muda maalumu.

Maadamu anapata udongo, Alhamdulillaah.

Swali:

Kuna mtu kamjamii mwanamke wake ambaye alikuwa anataka kumchumbia

kabla ya kufunga ndoa, akambebesha mimba akamwambia hilo walii wa

mwanamke. Wakawa wamefunga ndoa kisha Allaah Akawaruzuku mtoto. Ipi

hukumu ya mtoto huu Kishari´ah kwa kuzingatia kuwa baba amekubali ni

wake?

Page 68: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

68

Imaam Ibn Baaz:

Mtoto huyu ni wa Zinaa. Kwa kuwa kufanya nae jimaa kabla ya kutimia kwa

ndoa, ni jambo ovu na Zinaa. Hatonasibishwa nae na wala hatokuwa mtoto

wake (baba), isipokuwa atanasibishwa kwa mama yake, au atanasibishwa kwa

´Abdullaah, ´Abdul-Latwiyf, ´Abdul-Maalik kwa minajili ya kumsitiri katika

Mustaqbal. Muhimu ni kwamba, hatonasibishwa kwa baba yake kwa kuwa ni

mtoto wa Zinaa, lakini badala yake atanasibishwa kwa mama yake. Ni juu yao

wote kufanya Tawbah. Ni juu ya mwanaume na mwanamke watubu kwa

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na wafunge ndoa upya, kwa kuwa ndoa

ilifanywa katika hali ya ujauzito wa Zinaa. La wajibu ni wafunge ndoa upya,

baada ya kujifungua. Awafungishe ndoa walii wa mwanamke, baada ya wote

wawili kutubu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

Swali:

Nikiwa ni mwenye kujiheshimu kwa vazi la Kiislamu nyumbani na wala

siachi (kuvaa) Khimaar (shela, ushungi) kichwani mwangu. Je, inajuzu

kwangu kukaa na watoto wa kiume wa ami na shangazi yangu na mfano wao

ikiwa sote ni wanaume na wanawake twakaa sehemu moja?

Imaam Ibn Baaz:

Hakuna ubaya kukaa na watoto wa ami na shangazi pamoja na kuwa na

heshima, kujisitiri na kuvaa Hijaab. Hata uso, ni ´Awrah kwa kauli ya sahihi.

Ni wajibu fuunika na kichwa, hivyo viwili ni aula zaidi atapokaa na ndugu

zake; watoto wa shangazi, mjomba au jirani yake kwa mipaka mizuri ya kidini

isiyokuwa na neno ndani yake. Pamoja na kujisitiri, kuvaa Hijaab na wala

kutoonesha kitu katika hivyo; si uso wala kingine chochote, hakuna ubaya

kwa hilo. Na wala haitoshi kufunika kichwa, bali ni wajibu kufunika uso pia.

Mwanamke anatakiwa kujiheshimu na kujiweka mbali na sababu

zinazopelekea katika fitina; (asichukulie sahali) si pamoja na watoto wa

shangazi yake, mjomba wake wala wasiokuwa wao.

Page 69: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

69

Swali:

Mimi nina kaka na ndugu ambao kwa masikitiko makubwa hawaswali na

wala hawasimamishi mipaka ya Allaah. Je, ni lazima juu yangu kuwakata?

Kila ninapowaamrisha mema au kuwakataza maovu, wanafanya mzaha na

maskhara na mimi na wanasema "je wewe unataka kuwafanya watu wote

kuwa wema?" Wao wamekataa kukaa na mimi na wamenikata, lipi la wajibu

kwangu kufanya juu yao?

Imaam Ibn Baaz:

Ni juu yako kuwahama na kuwakata. Maadamu hawakubali nasaha na

hawaswali, inatakikana kwako kuwahama na kuwakata mpaka hapo Allaah

Atapowaongoza. Hili ndilo la wajibu, bali hii ndio Sunnah iliyosisitizwa.

Baadhi ya wanachuoni wanaona hivi, uwajibu wa kuwahama na kuwakata

kutokana na upotofu wao na kuzuia njia za kheri.

Lakini ukiwasiliana nao baadhi ya nyakati kwa kutaraji pengine Allaah

Akawaongoza, kwa kuwalingania na kuwapa nasaha, hakuna neno. Na ikiwa

wataendelea, hakuna neno kwako kuwakata na kujiweka kwako mbali nao

kikamilifu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwakata Maswahabah

watatu wakati walipoacha kwenda kupigana vita pamoja naye bila ya udhuru.

Muhimu ni kuwa, watu hawa inatakikana kuwahama. Kwa uchache,

kuwahama kunakuwa ni Sunnah iliyosisitizwa mpaka hapo Allaah

Atapowaongoza na kuwarudisha katika usawa.

Swali:

Kijana anapotaka kumposa mmoja katika wasichana. Katika hali hii, je ni

wajibu kwake (kijana huyo) kumuona? Na je, ni sawa msichana huyo kufunua

kichwa chake ili abainishe uzuri wake zaidi kwa mposaji wake?

Page 70: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

70

Imaam Ibn Baaz:

Hakuna ubaya, lakini sio wajibu bali ni jambo limependekezwa. Ni jambo

limependekezwa (kijana huyo) akamuona na yeye (msichana huyo) akamuona

(mvulana huyo). Kwa kuwa hii ni njia ya karibu ya kukubali. Mtume

(´alayhis-Salaam) kamwamrisha mwenye kutaka kuchumbia atazame

(kwanza). Akifunua uso wake, na miguu yake na kichwa chake, haina neno

kutokana na kauli sahihi. Wamesema baadhi ya wanachuoni kuwa inatosha

uso wake na vitanga vyake, lakini kauli ya sahihi ni kuwa haina neno kufunua

kichwa na miguu atazame apendekezwe na uzuri wake. Wanaweza

kutazamana (kwa kuwepo walii wa mwanamke)kwa kuwa hii ni njia ya

karibu ya kuweza kukubali. Hili liwe pasina mchanganyiko (yaani wasiwe

wao wawili tu), bali wawe pamoja na baba yake na msichana, au kaka yake au

mwanamke mwingine. Wasichanganyike wao wawili tu.

Swali:

Kuna kijana ambaye anataka kuoa msichana ambaye hajui kuwa anaswali au

hapana. Je, ndoa hii inajuzu na ipi hukumu ya hilo?

Imaam Ibn Baaz:

Ni lazima kuthibitisha kwanza jambo hili. Aulizie kwanza, kwa kuwa kumuoa

mwanamke ambaye ni kafiri haijuzu. Kwa Kauli Yake (Subhaanah):

لهن يحلون هم ول لهم حل هن ل

"Wao si (wake) halaal kwao (hao makafiri), na wala wao si (waume) halaal

kwao." (60:10)

Na mwenye kuacha Swalah anakufuru, kutokana na kauli ya sahihi ya

wanachuoni hata kama atakuwa anakubali uwajibu wake. Akiacha kwa uvivu

na kuzembea anakufuru. Kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi

wa sallam):

"Baina ya mtu na Shirki au kufuru ni kuacha Swalah."

Page 71: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

71

Na kasema tena (´alayhis-Swalaat was-Salaam):

"Ahadi iliopo baina yetu sisi na wao ni Swalah, atakayeiacha amekufuru."

Ikiwa haswali haijuzu kumuoa. Ama akijua kuwa anaswali vizuri, anaweza

kumuoa. Kasema Kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa

sallam):

"Mwanamke anaolewa kwa mambo mane: "Kwa mali yake, uzuri wake,

nasabu yake na Dini yake, basi shikilia (chagua) mwenye sifa za Dini

utasalimika."

Kumchagua mwanamke mwenye Dini ni jambo limefaradhishwa. Na katika

Dini jambo muhimu na nguzo kubwa ni Swalah inayokuja baada ya

Shahaadah mbili.

Swali:

Je, ni wajibu kupandisha mikono wakati wa Takbiyrat-ul-Ihraam tu au ni

lazima kuipandisha katika nguzo zote za Swalah?

Imaam Ibn Baaz:

Sunnah ni kupandisha mikono wakati wa Ihraam, na wakati wa Rukuu´, na

wakati wa kutoka katika Rukuu´ na wakati wa kusimama kutoka katika

Tashahhud ya kwanza mpaka ya tatu. Na hilo sio wajibu bali ni Sunnah.

Lilifanywa na Mtume (´alayhi-Salaam), Makhalifah waongofu na lilinukuliwa

kutoka kwa Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Sunnah ni muumini mwanaume na mwanamke afanye hivyo katika Swalah

zake zote. Kwa kuwa asli ni kuwa, mwanamke ni sawa na mwanaume katika

Ahkaam isipokuwa kwa yale yaliyokhusishwa na dalili.

Sunnah ni kunyanyua mikono yake katika Takbiyrah ya kwanza mpaka

kwenye mabega au masikio yake, hali kadhalika (apandishe) mikono yake

wakati wa Rukuu´ na wakati wa kuinuka kutoka katika Rukuu´, na hali

kadhalika wakati wa kuinuka kutoka katika Tashahhud ya kwanza mpaka ya

mwisho. Kama ilivyokuja katika khabari zilizo sahihi kutoka kwa Mtume

Page 72: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

72

(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Na hili ni jambo Mustahabah na Sunnah

na sio wajibu. Na lau ataswali bila ya kupandisha, Swalah yake ni sahihi.

Swali:

Ipi hukumu ya kuwatahiri wasichana? Kwetu ni lazima tufanye hivyo, na

kuna baadhi ya watu wamenambia kuwa ni jambo lisilojuzu kwa kuwa ndani

yake kuna kama kuadhibu. Ipi hukumu ya hilo?

Imaam Ibn Baaz:

Kutahiriwa (kwa wanawake) ni Sunnah iliyosisitizwa, hali kadhalika kwa

wanaume, wote ni Sunnah iliyosisitizwa. Na kuna kundi la wanachuoni

ambao wanaona ni wajibu kwa wanaume na ndio kauli yenye nguvu.

Inatakikana kuwatahiri wanaume na wala haitakikani kulichukulia sahali, na

namna hii ni kuwa imependekezwa kuwatahiri wanawake ikiwa atapatikana

mwenye kujua hilo katika wanawake wanaotahiri.

Swali:

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiswali Rakaa ngapi

baada ya Swalah ya Ijumaa? Tunaomba faida.

Imaam Ibn Baaz:

Masru´ah ni kuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiswali baada

ya Ijumaa Rakaa mbili nyumbani kwake. Namna hii ndivyo ilivyokuja katika

Swahiyh al-Bukhaariy na Muslim, Hadiyth ya Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu

´anhumaa).

"Alikuwa akiswali Rakaa mbili baada ya Ijumaa nyumbani kwake."

Page 73: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

73

Lakini, kasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

"Mwenye kuswali baada ya Ijumaa, aswali (Rakaa) nne."

Wanasema wanachuoni, kuoanisha baina ya Hadiyth hizi mbili ni kuwa,

akiswali Msikitini ataswali Rakaa nne, na akiswali nyumbani kwake ataswali

Rakaa mbili. Kuoanisha baina ya nususi hizi mbili.

Swali:

Nilioa mwanamke nikabaki nae kwa muda, kisha nikamtaliki na akaolewa na

mwanaume mwingine baada yangu. Je, inajuzu kwake kumbusu na

kumsalimia baba yangu baadaya kumtaliki?

Imaam Ibn Baaz:

Hakuna ubaya. Kwa kuwa Allaah Kasema:

أبنائكم وحلئل

"Na (mmeharamishwa) wake wa watoto wenu." (04:23)

Ni katika wake wa watoto (walioharamishwa kwa baba). Hata kama

amemtaliki. Ni Mahram wa baba yako.

Muulizaji:

Yaani umahram wao ni wenye kubaki hata kama amemtaliki?

Imaam Ibn Baaz:

Ni kama mke wa baba yake, lau baba yake atamtaliki, bado (mama huyo)

ataendelea kuwa Mahram wake (mtoto). Allaah Kasema:

ن آباؤكم نكح ما تنكحوا ول النساء م

Page 74: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

74

"Na wala msiwaoe (wake) waliowaoa baba zenu." (04:22)

Baba akimtaliki (mke wake) au mtoto (mke wake), anakuwa ni Haraam (huyu

kwa yule, na yule kwa huyu).

Swali:

Mimi nimeoa wanawake wawili, lakini wote wawili hawaswali, wanafunga tu

mwezi wa Ramadhaan. Nimeshawaamrisha Swalah zaidi ya mara moja.

Mmoja wao aliswali siku kadhaa, na pindi niliporejea Misri nikitoka Saudi

Arabia nikakuta ameacha Swalah. Na (mke) wa pili anasema hajui kitu katika

Qur-aan hata al-Faatihah. Nifanye nini?

Imaam Ibn Baaz:

Ni juu yako uwafanye watubu na uwabainishie umuhimu wa Swalah na

kwamba ndio nguzo ya Uislamu na kwamba kuiacha ni kufuru, wakitubu

Alhamdulillaah ubaki nao. Na ikiwa hawakutubu, ni wajibu kwako

kutengana nao na Allaah Atakupa walio bora kuliko wao.

"Mwenye kuacha kitu kwa ajili ya Allaah, Allaah Humpa kilicho bora kuliko

hicho."

Na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Anasema:

ه يتق ومن يحتسب ل حيث من ويرزقه مخرجا له يجعل اللـ

"Na yeyote (yule) anayemcha Allaah Atamajaalia njia (ya kutoka katika

matatizo). Na Atamruzuku kutoka njia ambayo hatizamii." (65:02-03)

Na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Anasema:

ه يتق ومن يسرا أمره من له يجعل اللـ

"Na yeyote (yule) anayemcha Allaah Atamjaalia wepesi katika jambo lake."

(65:04)

Ni wajibu kwako uwafunze, uwafunze al-Faatihah na Suurah fupi katika

nyakati ambazo nyoyo zitakuwa zimetulia, uwafunze na ujitahidi kwa hilo na

Page 75: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

75

wewe utakuwa mwenye ujira mkubwa. Wakishindwa kusoma al-Faatihah,

walete badala yake Adhkaar; kwa kusema "Subhaanallaah","Alhamdulillaah",

"Laa ilaaha illa Allaah", "Allaahu Akbar" na "Laa Hawlah wa laa Quwwatah

illa billaah". Mtume (´alayhis-Salaam) kaamrisha asiyeweza al-Faatihah alete

Dhikr hizi. Akishindwa, alete Dhikr hizi. Lakini iwe ni pamoja na kujaribu

katika nyakati za mbele kuihifadhi (al-Faatihah) na kujifunza nayo.

Muulizaji:

Kuwafanya kwake watubu ni kwa ajili ya kuacha kwao Swalah? Na ikiwa

hawakutubu, ni juu yake kufarakana nao?

Imaam Ibn Baaz:

Ndio.

Imaam Ibn Baaz:

Mpaka hapa tumepata kujua kuwa, kusherehekea Maulidi ya Mtume ni

Bid´ah bila ya shaka. Na ni wajibu kuiacha na wala haijuzu kuifanya. Na yule

atakayeyafanya, yuko baina ya mambo mawili:

1) Ima ni mjinga hajui haki, afunzwe na kuongozwa.

2) Au ni mwenye kasumba za kufuata matamanio na kiburi. Alinganiwe

katika usawa na aombewe uongofu na Tawfiyq. Na katika watu wote hawa

wawili hakuna mwenye hoja, sawa huyu wa kwanza ambaye ni mjinga wala

huyu wa pili mwenye kasumba. Wote hawana hoja. Hoja inapatikana katika

Aliyosema Allaah na Mtume Wake. Na sio katika kauli isiyokuwa ya hao

wawili. Kisha kusema kuwa Bid´ah imegawanyika sehemu mbili; Bid´ah nzuri

na mbaya, na katika Haramu na wajibu, huku ni kutoa kauli pasina dalili. Na

wameliradi hilo Ahl-ul-´Ilm wal-Yaqiyn na kubainisha makosa ya mgawanyo

huu. Na wametumia dalili kwa kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

"Atakayezusha katika Amri yetu hii yasiyokuwemo, basi yatarudishwa."

(Muttafaq)

Page 76: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

76

Na Imaam Muslim kapokea katika Swahiyh yake, Hadiyth kutoka kwa

´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha)ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi

wa sallam) kasema:

"Atakayefanya ´amali isiyokuwa humo na Amri yetu, basi itarudishwa."

Na katika Swahiyh, Hadiyth kutoka kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ´anhu) ya

kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akikhutubu siku

ya Ijumaa akisema:

"Amma ba´ad: "Hakika maneno bora ni Kitabu cha Allaah, na uongofu bora ni

wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), na shari ya mambo ni

mambo ya kuzua na kila Bid´ah na upotofu."

Na wala hakugawa na kusema:

"Kuna Bid´ah hii na hii."

Bali kasema:

"... kila Bid´ah ni upotevu".

Bali alizidi kusisitiza hilo kwa kusema: "Tahadharini na mambo ya kuzusha!

Hakika kila kitachozushwa ni Bid´ah, na kila Bid´ah ni upotevu."

Na Bid´ah inakuwa katika mambo ya Dini ambayo ni ya kujikurubisha na si

katika mambo ya dunia. Ama mambo ya dunia; katika mambo ya kula na

kunywa, kukafanywa chakula maalumu na cha aina mbalimbali, hili halina

neno. Bali kinachozungumziwa ni katika mambo ya kujikurubisha na mambo

ya ´Ibaadah ambayo mtu anajikurubisha kwayo kwa Allaah, hapa ndio

mahala pa kuzua.

Hali kadhalika, uvumbuzi wa mambo na vifaa vya vita; wanaweza kuzua

mambo mbalimbali katika silaha za kijihami na kujitetea, hili halina neno.

Kinachozungumziwa ni katika mambo ambayo mtu anajikurubisha kwayo

kwa Allaah, na ambayo yanachukuliwa kwa watu kuwa ni ukurubisho na ni

utiifu kwa Allaah, wakitarajia kwa hayo thawabu kutoka kwa Allaah. Hapa

ndipo panapozingatiwa. Yale ambayo hayakufanywa na Mtume (Swalla

Allaahu ´alayhi wa sallam) wala Maswahabah wake na wala hakulitolea dalili

(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala kuliashiria, bali limezua watu na na

kulitia katika Dini ya Allaah, hilo ni Bid´ah. Sawa ikiwa fulani atapenda au

atachukia. Na haki ndio yenye haki kufuatwa. Katika mlango huu kuna mengi

Page 77: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

77

yamezushwa na watu; kama ya kujenga Misikiti katika makaburi na

kuyawekea kuba, hizi ni Bid´ah ambazo zimezua shari nyingi. Mpaka

imejitokeza Shirki kubwa na kufikia makaburi kuabudiwa badala ya Allaah

kwa sababu ya Bid´ah hii (ya Maulidi). Ni wajibu kwa Muislamu atanabahi na

kushikamana na Aliyoyawekea Allaah Shari´ah, na atanabahi na waliyozusha

watu na atahadhari nayo.

Swali:

Anasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

"Swalini kama mlivyoniona mimi nikiswali".

Kinachofahamika katika Hadiyth hii ni kuwa, hakuna tofauti kati ya Swalah

ya mwanaume na ya mwanamke. Sawa katika kusimama, kuinama, Rukuu´

wala Sujuud. Kwa ajili hii, mimi huwa sitofautishi, lakini huku kwetu baadhi

ya wanawake Kenya wananikasirikia na kunambia kuwa Swalah yangu sio

sahihi kwa kuwa inafanana na Swalah ya mwanaume.

Na wanataja dalili ambazo - kwa mtazama wao - zinatofautisha Swalah ya

mwanaume na ya mwanamke; kama kuweka mikono juu ya kifua au kuiacha

na namna ya kushutama katika Rukuu´ na yasiyokuwa hayo katika mambo

ambayo sikukinaika nayo. Naomba unibainishie; je, Swalah ya mwanaume na

ya mwanamke katika utekelezaji kuna tofauti?

Imaam Ibn Baaz:

Uliyosema dada muulijizaji, sahihi ni kuwa hakuna tofauti kati ya Swalah ya

mwanamke na Swalah ya mwanaume. Na waliyosema baadhi ya wanach-uoni

ya utofautishaji hayana dalili. Na Hadiyth uliyoisema katika swali lako, nayo

ni kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

"Swalini kama mlivyoniona mimi nikiswali".

Inahusu watu wote. Shari´ah za Kiislamu zinawahusu wanaume na

wanawake, isipokuwa yaliyo na dalili ya ukhusishaji. Sunnah ni mwanamke

kuswali kama anavyoswali mwanaume; sawa katika Rukuu´, Sujuud, usomaji,

Page 78: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

78

uwekaji wa mikono juu ya kifua, hivi ndio bora. Hali kadhalika, jinsi ya

kufanya Rukuu´, jinsi ya kufanya Sujuud katika ardhi, yanayosemwa katika

Rukuu´ na Sujuud, baada ya kutoka katika Rukuu´ na Sujuud ya kwanza, yote

haya (mwanamke) ni sawa kama anavyofanya mwanaume.Kwa kuifanyia

kazi dalili ya maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

"Swalini kama mlivyoniona mimi nikiswali". (Swahiyh al-Bukhaariy)

Muulizaji:

Kuhusiana na kudhihirisha kisomo na kukimu Swalah, je, Swalah ya

mwanamke siinatofautiana na ya mwanaume katika hili?

Imaam Ibn Baaz:

Kukimu kunatoka nje ya haya, ´Iqaamah na adhaana ni khususan kwa

wanaume tu. Kuna maandiko ya haya. Wanaume wanaadhini na wanakimu,

ama wanawake hawana kukimu wala kutoa adhaana. Ama kudhihirisha

(yaani kusoma kwa sauti) anaweza kusoma kwa sauti; Fajr, Maghrib na ´Ishaa.

Rakaa mbili za asubuhi, na Rakaa mbili za mwanzo za Maghrib na ´Ishaa

anaweza kusoma kwa sauti kama wanavyofanya wanaume.

Swali:

Vipi mwanamke anatakiwa kujisitirina Hijaab? Je, ni mwili wake wote? Je

anaweza kuonesha vitanga vyake vya mikono na uso wake kwa Mahram zake

wote?

Imaam Ibn Baaz:

Mwanamke anatakiwa kujisitiri kwa watu ambao sio Mahram zake; jirani

yake, watoto wa ami yake, mume wa kaka yake. Ama Mahram zake si lazima

awe na na Hijaab; hakuna neno akaonesha uso wake, vitanga vyake na miguu

yake kwa Mahram zake; kama kaka yake, ami yake na yake, hakuna ubaya.

Page 79: Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz

79

Muhimu ni yeye kujisitiri mbele ya watu ajinabi; kama kwa mfano mtoto wa

mjomba wake, kwa kuwa ni ajinabi kwake na sio Mahram. Na kama kwa

mfano mume wa dada yake, kaka wa mume wake, ami wa mume wake na

mfano wa hawa. Watu hawa ni juu yake kujisitiri mbele yao mwili wote;

kuanzia uso mpaka chini. Kwa Kauli ya Allaah (Ta´ala):

لكم حجاب وراء من فاسألوهن متاعا سألتموهن وإذا وقلوبهن لقلوبكم أطهر ذ

"Na mnapowauliza (wake zake) haja, waulizeni nyuma ya pazia. Hivyo ni

utwaharifu zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao." (33:53)

Anasema tena (Subhaanah):

بعولتهن آباء أو آبائهن أو لبعولتهن إل زينتهن يبدين ول

"Na wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa kwa waume zao, au baba zao, au

baba za waume wao... " (24:31)

Hivyo ni kuwa, kaamrishwa kujisitiri kwa Hijaab kwa watu ambao sio

Mahram zake.

Chanzo: http://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.scholarallsubjects&schid=8177

1420-01-27/1999-05-13