Fataawa Za Wanachuoni (31)
-
Upload
wanachuoni -
Category
Documents
-
view
313 -
download
10
description
Transcript of Fataawa Za Wanachuoni (31)
1
فتاوى العلماءFataawa Za Wanachuoni
[31]
Imefasiriwa Na Kutayarishwa Na:
Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush
©
2
Dibaji:
Hizi ni Fataawa za wanachuoni mbali mbali ambazo nimezikusanya ili
kuweza kuwasahilishia ndugu zetu Waislamu na khaswa wale watafutaji
elimu. Fataawa ni mchanganyiko kuhusiana na masuala mbali mbali ya
Tawhiyd, ´Aqiydah, Manhaj, Fiqh na mengineyo.
Hivyo, ninamuomba Allaah (´Azza wa Jalla) ziweze kuleta faida kwa ndugu
zetu Waislamu, na ninamuomba Allaah (´Azza wa Jalla) Ajaalie kazi hii niwe
nimeifanya kwa kutafuta Radhi Zake (Subhaanahu wa Ta´ala), na Amlipe kila
Aliyeisambaza kwa ndugu mwengine na Awalipe ndugu wasomaji wote kwa
jumla.
Tanbihi: Fataawa zote hizi tumezifasiri kwa njia ya Video na zinapatikana
Youtube waweza kusoma na huku wasikiliza. Kwa mwenye kutaka hizo
Fataawa za Video aende Alhidaaya au Youtube kwa juu sehemu ya kutafuta
aandike au kukopi kichwa cha habari cha Fatwa (kama ilivyo hapo chini kwa
kila Fatwa ina kichwa chake cha habari) na atafute itajitokeza In Shaa Allaah.
Jazaakumu Allaahu Khayra
Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad , na ahli zake na
Maswahabah zake na watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah.
3
Fataawa zilizomo:
1) Kukufurisha Na Kubadiy´ Ni Kazi Ya Wanachuoni
2) Kuhiji Kwanza Au Kufanya Hijrah?
3) Tuko Ufaransa Na Hatuna Wanachuoni, Twaomba Nasaha Zenu
4) Tofauti Ya Wanawake Wa Leo Na Maswahabah Wa Kike
5) Swali Kuhusiana Na Sijda Ya Kusahau
6) Je, Salafiyyuun Wanafarakanisha Waislamu?
7) Nasaha Ya Shaykh Rabiy´ Kuhusiana Na Mashaykh Wawili
8) Nasaha Kwa Watafutaji Elimu (Wanafunzi)
9) Mwanamke Kupanda Gari Ya Mwanaume Na Mke Wake Bila Ya Mahram
10) Ibara "Lau Bila Ya Allaah Kisha Wanachuoni"
11) Hukumu Ya Raafidhwah (Mashia) Wote Ni Moja
12) Hukumu Ya Kusikiliza Mawaidha Ya Watu Wa Bid´ah Kama ´Aa´idh al-Qarniy
13) Hukumu Ya Kufuturu Kabla Ya Kuzama Jua
14) Da´wah Na Acha Kuingilia Makundi Potofu
15) ´Allaamah al-Fawzaan Kuhusu Bia Isiyokuwa Na Pombe
16) Shaykh Mahiyr Qahtwaaniy Kuhusu Kumsikiliza Khaalid ar-Raashid
17) Hukumu Ya Wanawake Kuzuru Makaburi -2-
18) Tofauti Ya Hadiyth al-Qudsiy Na Hadiyth Za Mtume Za Qur-aan
19) Mke Wangu Anasema Uongo Sana
20) Kujifunza Mwenyewe - Maradhi Khatari Ya leo Je, Katika Zama Hizi Kuna
Maulamaa Wa al-Jarh Wa Ta´adiyl?
21) Je, Katika Zama Hizi Kuna Maulamaa Wa al-Jarh Wa Ta´adiyl?
22) Haijuzu Kwa Mwanamke Kuvaa Suruwali Yoyote Kwa Hali Yoyote
23) Shaykh Yahyaa al-Hajuuriy Kuhusu al-Halabiy
24) Wale Wasiopenda Kuzungumziwe Manhaj Ahl-is-Sunnah wal Jamaa´ah
25) Mwanamke Kuvaa Punjabi Yenye Suruwali
26) Lipi La Kufanya Unapojiwa Na Mawazo Mabaya?
27) Kufunga Siku Ya Maulidi Ya Mtume (´alayhis-Salaam)
28) Ipi Hukumu Ya Kutawadha Bafuni?
29) Hukumu Ya Kulala Kwa Tumbo (Kifudifudi)
30) Hadiyth Dhaifu Ya Mu´aadh (Radhiya Allaahu ´anhu)
31) Anampiga Binti Yake Kwa Kumtomsikiliza Yeye Na Mama Yake
32) ´Allaamah ´Abdul-Muhsin al-´Abbaad Kuhusu Anashiyd
33) Usufi Si Katika Uislamu
34) Radd Kwa Jabriyyah Na Qadariyyah
35) Muislamu Aliyeacha Swalah Ni Kafiri Na Lazima Auawe
36) Lini Kuhukumu Kinyume Na Aliyoteremsha Allaah Mtu Anakuwa Kafiri?
37) Kitabu Na Sunnah Vinatangulizwa Kabla Ya Ijmaa´
38) Imaam Abu Haniyfah, Imaam Wetu, Kiigizo Chetu
39) Kumtolea Mtu Swadaqah Kwa Kuswali Naye Baada Ya Swalah Ya ´Aswr Na Fajr
40) Ipi Bora Kwa Wanawake Kuswali Jamaa´ah Au Kila Mtu Kivyake?
41) Inajuzu Kumhukumu Mtu Moja Kwa Moja Kuwa Ni Mnafiki?
4
42) Hukumu Ya Kufanya Mazoezi Katika Ukumbi Za Muziki
43) Anashiyd (Qaswiydah) Ni Haramu
44) Mume Na Mke Wanadanganya Serikali Wameachana Ili Wapate Pesa Zaidi
45) Msikiti Unaokhatimu Qur-aan Na Usiyokhatimu, Wapi Nifanya I´tikaaf?
Wanachuoni waliomo:
1) Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
2) Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
3) ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
4) ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
5) ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz Aal ash-Shaykh
6) ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
7) ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy
8) Shaykh Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
9) ´Allaamah Swaalih Aal ash-Shaykh
10) Shaykh Ahmad bin ´Umar Bazmuul
11) Shaykh Abu ´Abdul-Haliym ´Abdul-Haadiy
12) Shaykh Yahyaa al-Hajuuriy
13) Shaykh Mahiyr al-Qahtwaaniy
14) ´Allaamah ´Abdir-Rahmaan al-Baraak
5
Bismillaahi Rahmaani Rahiym
1) Kukufurisha Na Kubadiy´ Ni Kazi Ya Wanachuoni
Swali:
Ni haki ya Muislamu kumkufurisha [Takfiyr] au Tabdiy´ kwa kila ambaye
atatumbukia katika kufuru au Bid´ah?
´Allaamah al-Fawzaan:
Msukumo wa kuwahukumu watu na Takfiyr na Tabdiy´, hili halijuzu
isipokuwa kwa wanachuoni, ambao wanajua mipaka ya kufuru, Bid´ah,
kuritadi na sababu zake wanazijua wanachuoni. Hili ni jambo khaswa kwa
wanachuoni. Haijuzu kwa yeyote kumhukumu mwenzake kwa Bid´ah,
kufuru, Shirki naye hajui sharti za Takfiyr, Tabdiy´ na madhambi. Mtu
auhifadhi ulimi wake. Kuna khatari akamwambia mtu ambaye siye, kwamba
ni kafiri, mtu wa Bid´ah, mpotofu, fasiki. Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi
wa sallam) anasema:
"Atakayemwambia ndugu yake "wewe kafiri!" naye si hivyo, maneno yake
yatarejea kwake".
Maneno yake yatarejea kwakwe mwenyewe, A´udhubi Allaah. Ni juu ya
Muislamu kuhifadhi ulimi wake na asiuache ukawa huru katika masuala
kama haya. Ni jambo khatari. Yanahitaji mtu kwanza asome na ajue masharti
ya Takfiyr, Tabdiy´, Tafsiyq na si kuongea tu kwa ujinga, hisia, hamasa au
ushujaa. Anaweza kutumbikia katika makosa na maneno yake yakamrejea
mwenyewe. Masuala haya ni khatari sana. Na haya maneno ambayo ulisema
katika kukufurisha watu, Tabdiy´ au Tafsiyq hayaachwi hivi hivi. Ikiwa
wanastahiki hayo, yanaenda kwao. Na kama hawayastahiki yanakurejelea
wewe. Ni juu yako kuuhifadhi ulimi wako katika masuala haya.
Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=127359
6
2) Kuhiji Kwanza Au Kufanya Hijrah?
Swali:
Mimi nina mali inayotosha kwa Hajj tu, na mimi naishi katika mji wa kikafiri,
lipi aula zaidi kwangu Hajj au kufanya Hijrah kwa kuzingatia ya kwamba
mali hii haitoshi kufanya Hijrah?
´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy:
Ikiwa mali hii haikutoshi kufanya Hijrah na wewe unataka kutanguliza
kwanza kufanya Hajj, hakuna ubaya kutanguliza kwanza Hajj. Kwa kuwa
Hijrah inahitajia kwako kujikalifisha na safari, kuandaa nyumba ambapo
utaishi na mfano wa hayo, uzito utakuwa mwingi. Ikiwa hali ni kama hivyo,
ni juu yako kwanza kutanguliza kufanya Hajj. Lakini kadiri utavyoweza
katika siku za mbele ni wajibu kwako kuhama, kwa kuwa kufanya Hijrah ni
wajibu.
Chanzo: http://youtu.be/LNQ1ozM7OUo
3) Tuko Ufaransa Na Hatuna Wanachuoni, Twaomba Nasaha Zenu
Swali:
Mi naishi Ufaransa, kwa ukosefu wetu wa wanachuoni twatafuta elimu
kupitia vitabu kama cha Tawhiyd cha Shaykh Ibn ´Abdil-Wahhaab, kitabu
Sharh al-Mumtiy´ cha Ibn ´Uthaymiyn na visivyokuwa hivyo kama (vitabu)
vya Ibn Baaz, al-Albaaniy, al-Fawzaan, ´Abdu-´Aziyz Aal ash-Shaykh na mimi
huwa nikirejea kwa wanachuoni ninapokuwa na swali na masuala ya utata,
ipi nasaha yako kwetu?
7
´Allaamah Ahmad an-Najmiy:
Endelea kutafuta kwako [elimu], na tunawaombea kwaAllaah mafanikio.
Chanzo: http://youtu.be/DAlq8d8YNek
4) Tofauti Ya Wanawake Wa Leo Na Maswahabah Wa Kike
Swali:
Siku hizi twasikia sana kwamba mke si lazima kumhudumia mume wake
kama vile kupika na kufua nguo. Tunaomba kutoka kwako ufafanuzi
kuhusiana na suala hili.
´Allaamah al-Fawzaan:
Mwanamke leo kaendelea na wala hamhudumii mume wake. Leo wakati una
haja ashughulikie moja katika haja zako, hayupo nyumbani. Mume anakuja na
kukaa nyumbani na kusubiri, mke haji ila mpaka ifike mwisho wa usiku.
Wanawake wa leo wamekuwa waasi. Ni katika Sunnah wanawake
kumhudumia mume wake. Maswahabah wa kike (Radhiya Allaahu
´anhunna) walikuwa wakiwahudumia waume zao; walikuwa wakipika,
wakiangalia mambo ya nyumbani. Isitoshe ni Maswahabah wa kike,
wanawake bora katika Ummah. Fatmah bint Muhammad (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam) na (Radhiya Allaahu ´anha) alikuwa akibeba maji kwenye
mgongo wake mpaka kamba ikaacha alama kwenye mgongo wake.
Alimuomba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ampe mtumishi
akakataa, akakataa kumpa mtumishi. Akamuamrisha atafute msaada kwa
Dhikr na Istighfaar, naye ni binti wa Muhammad (´alayhis-Salaam).
Chanzo: http://youtu.be/J49hX6Z6HrI
8
5) Swali Kuhusiana Na Sijda Ya Kusahau
Swali:
Je ni juu ya maamuma kuleta Sijda ya kusahau wakiswahili Jamaa´ah na
Imamu?
´Allaamah Ahmad an-Najmiy:
Hapana; akisahau mwenyewe hana juu yake [Sijda] ya kusahau [kama si
jambo la wajibu], wala Imamu. Lakini akisahau Imamu, ni juu ya Imamu na
walionyuma yake.
Chanzo: http://youtu.be/Njq6BZYbkck
6) Je, Salafiyyuun Wanafarakanisha Waislamu?
Swali:
Je ni sahihi wanayoyasema baadhi yao kwamba kuwakosoa watu wa Bid´ah
katika Suufiyyah au wengineo ndio katika sababu za kufarakanisha watu na
kufarakanisha Ummah?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio tunataka kufarakanisha watu wa Bid´ah na washirikina na waabudu
makaburi. Sisi hatutaki wakusanyike na sisi. Hatuwezi kuwa pamoja ila na
watu wa Tawhiyd. Hili ndilo tunalotaka, mfarakano huu ni wakukusudia.
Allaah Kafarakanisha baina ya waumini na makafiri.
يستوون ل فاسقا كان كمن مؤمنا كان أفمن
9
“Ati aliye Muumini atakuwa sawa na aliye mpotovu? Hawawi sawa.” (32:18)
كالفجار المتقين نجعل أم الرض في كالمفسدين الصالحات وعملوا آمنوا الذين نجعل أم
“Je! Tuwafanye walioamini na wakatenda mema kama wafanyao uharibifu
katika nchi? Au tuwafanye wacha Mungu kama waovu?” (38:28)
Sisi tunakusudia hili, tunakusudia kutenganisha baina ya yule asiyekubali
haki atutenge na tujiweke mbali naye, mtengo wa wazi kabisa.
Chanzo: http://youtu.be/SUWfE7z5lmo
7) Nasaha Ya Shaykh Rabiy´ Kuhusiana Na Mashaykh Wawili
Shaykh Ahmad al-Bazmuul:
Mimi nanawanasihi na kuinasihi nafsi yangu mwenyewe kwa nasaha za
Shaykh Rabiy´, nayo ni qadhiya ya Shaykh ´Ubayd al-Jaabiriy na Yahyaa al-
Hajuuriy. Ninawanasihi kwa aliyoniusia Shaykh Rabiy´ na kuwausia vijana
wa Salafiyiyn, waache kuongelea masuala haya. Kuacha kuongelea masuala
haya. Shaykh ´Ubayd ni mwanachuoni, muheshimiwa na ni maarufu kwa
elimu yake na Manhaj yake. Hali kadhalika Shaykh Yahyaa al-Hajuuriy ni
maarufu pia kwa elimu yake, heshima yake na ni katika wanafunzi wa Shaykh
Muqbil (bin Haadiy al-Waadi´iy). Na mzozano baina yao si tofauti ambazo
zinamuingiza mmoja wao katika Tabdiy´ au Tadhwliyl (upotofu). Bali ni
tofauti ambayo, yawezekana wameyaingilia watu waovu na kusababisha
matatizo na mfano wa hayo. Tunataraji kwa Allaah (´Azza wa Jalla) na
tunamuomba Allaah Atengeneze baina yao na Azikutanishe nyoyo zao. Na
tunataraji kwa vijana wote wa Salafiyiyn waache kuingia katika mambo
haya... kuingia katika masuala haya yatawaathiri. Na ninawanasihi kwa
nasaha za Shaykh Rabiy´ kuacha mambo haya. Na bila shaka Shaykh ´Ubayd
al-Jaabiriy manzilah yake yajulikana, na kusifiwa na baadhi ya watu kwa
majina mabaya haifai... Haifai, Shaykh ´Ubayd ni maarufu Allaah Amhifadhi.
10
Chanzo: http://youtu.be/1JefmMwXklM
8) Nasaha Kwa Watafutaji Elimu (Wanafunzi)
Swali:
Ipi nasaha zako kwa watafutaji elimu (wanafunzi) wanaoanza?
´Allaamah Ahmad an-Najmiy:
Nasaha zangu kwao wakimbilie kutafuta elimu na wachukue [elimu] kama
Alivoamrisha Allaah, nako ni dalili kutoka katika Kitabu, Sunnah, kauli za
Salaf (Rahihamu Allaah).
Chanzo: http://youtu.be/IC-S42xXMK8
9) Mwanamke Kupanda Gari Ya Mwanaume Na Mke Wake Bila Ya
Mahram
Swali:
Je, inajuzu kwa mwanamke kupanda gari bila ya Mahram wake na ni safiri
[huku akiwa pamoja na] mwanaume ajinabi na mke wake akihitaji hilo kwa
kuzingatia ya kuwa ni waaminifu, na jua kuwa amejisitiri uso wake?
´Allaamah Ahmad an-Najmiy:
Kujuzisha mwanamke kupanda gari na [mwanaume] mwaminifu ikiwa
atakuwa pamoja na mke wake hili ndilo wanalosema na kulikariri
wanachuoni na Shaykh Muhammad bin Ibraahiym Muftiy aliyetangulia na
11
kusema kuwa kila mtu anapaswa kuwa na mume wake, na ni wajibu awe
mume.
Chanzo: http://youtu.be/Qq9RWXVDEWI
10) Ibara "Lau Bila Ya Allaah Kisha Wanachuoni"
Swali:
Ibara hii, lau bila ya Allaah kisha wanachuoni tungelikuwa watu wapotofu, je
kusema hivi ni katika matamshi ya kishari´ah au ni katika matamshi ya
kishirki?
´Allaamah al-Fawzaan:
Lau bila ya Allaah kisha Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam),
wanachuoni kuna uwezekano sehemu zote mbili: Kuna wanachuoni ambao
wako katika uongofu na kheri, na kuna wenye wako katika upotofu. Si
wanachuoni wote. Lakini ni Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)
ndiye kalindwa na madhambi tu.
Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=127660
11) Hukumu Ya Raafidhwah (Mashia) Wote Ni Moja
Swali:
Ipi hukumu ya watu ´Awwaam wa Raafidhwah? Je, hukumu yao ni kama
hukumu ya maulamaa wao?
´Allaamah al-Fawzaan:
12
Enyi ndugu acheni maneno haya, Raafidhwah hukumu yao ni moja, hukumu
yao ni moja. Wote wanasikilzia Qur-aan, wote wanasoma bali wengi wao
wanahifadhi Qur-aan, hoja imekwishawasimamia. Wacheni falsafa hii na fikra
ambayo imeenea kwa vijana na wanafunzi, acheni hili. Aliyefikiwa na Qur-
aan hoja imekwishasimama kwake.
بلغ ومن به لنذركم القرآن هذا إلي وأوحي
"Na nimefunuliwa Qur-aan hii ili kwayo nikuonyeni nyinyi na kila
inayomfikia." (06:19)
Mpaka siku ya Qiyaamah.
Chanzo: http://aloloom.net/show_fatawa.php?id=247
12) Hukumu Ya Kusikiliza Mawaidha Ya Watu Wa Bid´ah Kama ´Aa´idh
al-Qarniy
Swali:
Je inajuzu kwetu kusema mtu fulani si Salafiy ikiwa ´Aqiydah yake ni
Salafiyyah lakini anasikiliza mikanda kwa mfano ya ´Aa´idh al-Qarniy?
´Allaamah Ahmad an-Najmiy:
Ikiwa huyu anayesikiliza mikanda ya ´Aa´idh al-Qarniy na hajanasihiwa na
yeyote na yeye hajui na anadhani kuwa ´Aa´idh al-Qarniy ni Salafiy, katika
hali hii atanasihiwa. Ikiwa atakataa kunasihiwa na akaendelea katika alioemo,
Hivyo ataambiwa ni mmoja katika Hizbiyyuun.
Chanzo: http://youtu.be/spapJXJpyKc
13
13) Hukumu Ya Kufuturu Kabla Ya Kuzama Jua
Swali:
Tulikuwa katika Swawm ya Ramadhaan, akaadhini muadhini kabla ya
kuzama jua kwa makosa sisi tukafuturu, lipi la wajibu kwetu?
´Allaamah Yahyaa al-Hajuuriy:
Ni wajibu kwenu kulipa siku hio kutokana na kauli sahihi, kwa kauli ya
Allaah (´Azza wa Jalla):
وا ثم يام أتم الليل إلى الص
"Kisha timizeni Swawm mpaka usiku." (02:187)
Na atakayefuturu kabla ya kutimia Swawm ni wajibu kwake kurudi siku hio.
Chanzo: http://www.sh-yahia.net/show_sound_1431.html
14) Da´wah Na Acha Kuingilia Makundi Potofu
Swali:
Ipi rai yako kwa anaesema: "Ni juu ya mwanachuoni kufunza Manhaj Salaf-
us-Swaalih bila ya kuingilia makundi potofu na watu wa Manhaj potofu? Je
hili silinaingia katika msemeo wa ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhu):
"(Uislamu) utameguliwa seheumu kwa sehemu."
´Allaamah Swaalih ´ Aal ash-Shaykh:
Jibu ni kuwa, maneno haya si sahihi bali ni makosa. Kwa kuwa kuwapiga
Radd wanaokhalifu katika Dini ya Kiislamu ni katika misingi ya Dini hii. Kwa
kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye wa kwanza kuwaradi
14
wanaomkhalifu Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Kuwapiga Radd wanaokhalifu ni katika mambo makubwa.
Anasema Shaykh-ul-Islaam:
"Na ni katika aina kubwa ya Jihaad." Na hili ni sahihi.
Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=126696
15) ´Allaamah al-Fawzaan Kuhusu Bia Isiyokuwa Na Pombe
Swali:
Kinywaji kinachoitwa "Beer/Bia" ambacho kipo katika baadhi ya maduka. Je
hichi kinywaji huchukuliwa ni katika alcohol (pombe) au inajuzu kukinywa?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ikijulikana kuwa kina alcohol kisinywe, ama ikujulikana kuwa hakina alcohol
asili itakuwa ni Halali.
Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=126775
16) Shaykh Mahiyr Qahtwaaniy Kuhusu Kumsikiliza Khaalid ar-
Raashid
Shaykh Mahiyr al-Qahtwaaniy:
Ama Daa´iy aitwae Khaalid ar-Raashid hatujui kuwa yuko katika Da´wah ya
Salafiyyah, khaswa (kama inavyojulikana) yuko na mikanda ambayo
15
inahamasisha kumfanyia uasi mtawala na Jihaad za Bid´ah kama
nilivyowaambia. Siwanasihi kusikiliza mikanda yake.
Chanzo: http://youtu.be/hdzzU79RlV0
17) Hukumu Ya Wanawake Kuzuru Makaburi -2-
Swali:
Dada huyu anauliza kuhusiana na kuzuru kaburi la baba yangu na
kumuombea Du´aa. Sisi katika ada yetu ni kwenda kuzuru kaburi lake na
kumuombea Du´aa na kuweka baadhi ya miti katika kaburi lake?
´Allaamah al-Fawzaan:
Yote haya hayajuzu. Kwanza mwanamke kuzuru makaburi haijuzu. Kwa
kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwalaani wanawake wenye
kuzuru makaburi, wanayachukuliwa kuwa ni Misikiti na sehemu zao za
mwanga. Mwanamke hazuru makaburi. Hali kadhali kuweka (kupanda) mti
kwenye kaburi haijuzu. Kwa kuwa hii ni Bid´ah na ni njia katika Shirki.
Chanzo: http://youtu.be/B3Lw-SQ2Sbs
18) Tofauti Ya Hadiyth al-Qudsiy Na Hadiyth Za Mtume Za Qur-aan
Swali:
Ipi tofauti kati ya Hadiyth al-Qudsiy na Hadiyth za Mtume, na ipi tofauti kati
ya Qur-aan na Hadiyth al-Qudsiy?
16
´Allaamah al-Fawzaan:
Hadiyth al-Qudsiy ni aliyoipokea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)
kutoka kwa Mola Wake kwa lafdhi na maana yake. Ama Hadiyth ya Mtume
ni aliyoisema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na maana yake
inamrudilia Allaah (´Azza wa Jalla). Tofauti kati ya Hadiyth al-Qudsiy na
Qur-aan, vyote viwili ni Maneno ya Allaah (´Azza wa Jalla). Lakini Qur-aan ni
Mutawaatir, Hadiyth al-Qudsiy inaweza kuwa si Mutawaatir, inaweza kuwa
Ahaad, dhaifu, hasan. Hadiyth al-Qudsiy inaweza kukumbwa na yanayoweza
kuikumba Hadiyth ambayo sio Qudsiy kwa kukataliwa mapokezi yake. Ama
Qur-aan yenyewe ni Mutawaatir kwa Ijmaa´ ya Waislamu. Hili ni jambo la
kwanza. Jambo lingine ni kuwa Qur-aan mtu anafanya nayo ´Ibaadah kwa
kisomo chake, kwa Swalah na mengineyo tofauti na Hadiyth al-Qudsiy
hakufanywi ´Ibaadah kwa kisomo chake.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2514
19) Mke Wangu Anasema Uongo Sana
Swali:
Mke wangu anasema uongo sana mbele yangu na mbele ya watoto wake na
familia yake, na anasema kuwa hawezi kuacha hilo. Una ninasihi nini Shaykh?
´Allaamah ´Abdul-´Aziyz Aal ash-Shaykh:
Mbainishie jarima ya kusema uongo, na hadhi ya uongo, na kuwa ni katika
tabia ya wanafiki na kuwa ni katika yanayopugunza uaminifu kwa
mwanamke au mwanamume. Usikae kimya kwa uongo wake, na usikubali
kitu kwake mpaka akubali kosa lake ajikerebishe na atubie kwa Allaah kwa
aliyofanya.
Chanzo: http://youtu.be/vkg2dX2mC8U
17
20) Kujifunza Mwenyewe - Maradhi Khatari Ya leo
Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab kasema:
"34- Usiamini Dini yako katika vitabu na wale wanaojinasibisha kwa elimu."
´Allaamah al-Fawzaan:
Usiamini vitabu moja kwa moja. usiviamini. Kwa kuwa kuna haki na batili.
Usiviamini vitabu. Bali rejea kwa maulamaa (wanachuon) waliobobea katika
elimu. Usichukue elimu yako tu katika vitabu, au ukasoma kwenye vitabu
vyenyewe. Baadhi ya watu wanahifadhi mujaladi na maandishi, lakini
hawafahamu yaliyomo ndani yake na wala hawajui maana yake. Kwa kuwa
hawakusoma kwa maulamaa ambao wanasherehesha na wanabainisha
muradi wake. Wanaweza kufahamu ufahamu ambao ni wakimakosa. Hili ni
khatari! Usiamini hivi vitabu. Vitabu ni njia tu katika elimu. Usiviamini katika
kujifunza kwako. Si vitabu vyote vinakuwa sahihi. Hata kama kitabu ni sahihi
ufahamu wako una mpaka. Fahamu inatofautiana hata kama kitabu kitakuwa
sahihi. Je Khawaarij hawakupotea nao ni walikuwa ni wenye kuhifadhi Qur-
aan na wanasimama na kuisoma usiku katika Tahajjud wakiswali? Lakini
wamepotea. Allaah Atulinde. Kwa kuwa hawafahamu maana ya Qur-aan na
hawakuchukua elimu kwa maulamaa. Walijitenga na Maswahabah na
wakatosheka na kusoma Qur-aan na ufahamu wao kivyao. Ndo maana
wamepatwa na yaliyowapata. Na haya maradhi ya leo ni khatari. Mtu
kudhani kuwa anajua ni maradhi khatari, nako ni kuchukua elimu kwenye
vitabu au kwa watu wasiofahamu kwa wale wanaodhani kuwa wanajua na
wanaoanza. Hii ni khatari kwa mtu mwenyewe na ni khatari kwa Ummah.
Kwa kuwa atatoka aanze kutoa Fatwa, aanze kufasiri Qur-aan au afasiri
Sunnah apoteze watu.
Chanzo: http://alfawzan.ws/node/12520
18
21) Je, Katika Zama Hizi Kuna Maulamaa Wa al-Jarh Wa Ta´adiyl?
Muulizaji:
Assalaam ´alaykum warahmtullaahi wa Barakatuh
´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy:
Wa ´alaykum-us-Salaam warahmtullaahi wa Barakatuh
Muulizaji:
Hayaak Allaah Shaykh, vipi hali yako?
´Allaamah an-Najmiy:
Mzima.
Muulizaji:
Nina swali Shaykh naweza kuuliza?
´Allaamah an-Najmiy:
Ndio.
Muulizaji:
Je, kuna maulamaa wa al-Jarh wa Ta´adiyl katika zama hizi?
´Allaamah an-Najmiy:
19
Maulamaa wa al-Jarh wa Ta´adiyl wanakuwepo katika kila zama.
Muulizaji:
Na ni kina nani Shaykh?
´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy:
Maulamaa wa al-Jarh wa Ta´adiyl wanakuwepo
katika kila zama.
Muulizaji:
Na ni kina nani katika zama hizi?
´Allaamah an-Najmiy:
Wapo, kama Shaykh Rabiy´ (al-Madkhaliy), Muhammad bin Haadiy (al-
Madkhaliy), (Swaalih) as-Suhaymiy na kadhalika.
Chanzo: http://youtu.be/1XmZLDbg2WI
22) Haijuzu Kwa Mwanamke Kuvaa Suruwali Yoyote Kwa Hali Yoyote
Swali:
Ipi hukumu ya kuvaa suruwali ya “jeans” na kanzu juu yake? Je, ni katika
mavazi ya makafiri?
´Allaamah al-Fawzaan:
20
Kila ambacho hakisitiri na kina fitina haijuzu kukivaa, na suruwali ina fitina.
Kwa kuwa inabainisha viungo vya mwili wa mwanamke na maumbile ya
mwanamke, akamfitinisha yule anayemwangalia. Haijuzu kwa mwanamke
kuvaa suruwali kwa hali yoyote, kama kweli anamuogopa na kumcha Allaah.
Na haijuzu kuziuza kwa wanawake na thamani yake ni Haramu, haijuzu
kuziuza kwa wanawake. Kwa masikitiko makubwa leo sehemu za mavazi
hukuti mavazi ya Kishari´ah, bali unakuta mavazi ya kimagharibi na mavazi
yasiyositiri. Wanaziuza na wanakula thamani yake na wanakuwa tajiri kwazo.
Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=127853
23) Shaykh Yahyaa al-Hajuuriy Kuhusu al-Halabiy
Shaykh Yahyaa al-Hajuuriy:
Kuna makala ya Radd kwa ´Aliy al-Halabiy imesambazwa, hakuna ubaya
ndugu waiuze (Dammaaj) kutokana na tunavyomjua. Ndugu walinipa na
kunambia niangalie kama inaweza kuuzwa hapa. Hakuna ubaya (iuzwe).
(makala hio) ina (kauli ya al-Halabiy) kuhisiana na uchaguzi (katika ubunge),
na sisi yeyote anayehamasisha uchaguzi tunaona kuwa hakuna ubaya
kubainisha (kwa watu) makosa yake katika hilo. ´Aliy al-Halabiy bado
hajaachana na Abul-Hasan, aliachana nae au bado yuko nae?
Bado yuko nae! Bado hajaachana na ´Adnaan ´Ar´uur, hajaachana na al-
Maghrawiy, na hajaachana na Usaamah al-Quusiy, na hajaachana na Ihyaa at-
Turaath. Anasema "Bado huwa ninawazuru na tunanasihiana... " Anasema
kwa mfano "Siwezi kuwaficha ukarimu nilionao kwao... " na kadhalika. Huyu
ndiye (al-Halabiy)! ´Aliy al-Habaliy ni Mu´mayyi´ (mpaka mafuta) enyi
ndugu. Da´wah yake ni Da´wah ya Tam´yi´!
Chanzo: http://youtu.be/h4zEtZ6mlkc
21
24) Wale Wasiopenda Kuzungumziwe Manhaj Ahl-is-Sunnah wal
Jamaa´ah
Swali:
Kuna kundi la vijana katika mji wetu, hawapendi kuzungumziwe Manhaj
kabisa wala hawachanganyiki na vijana walioko katika haki katu, bali
nikakundi kamejitenga Ipi hukumu ya kushirikiana nao?
´Allaamah Muhammad al-Madkhaliy:
Ikiwa hizi ndo sifa zao tahadhari nao. Hakika yule ambaye hataki kuongelewe
Manhaj ya haki - Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, kushikamana nayo na
kutahadharisha na yanayoikhalifu huyu ni mtu wa shari. Usiwe pamoja nae.
Chanzo: http://www.youtube.com/mirathiyamitume
25) Mwanamke Kuvaa Punjabi Yenye Suruwali
Swali:
Baada ya kuangalia mavazi yaliyopo madukani na tukapata zinazositiri,
tukapata vazi linaloitwa "punjabi". Nayo ni kanzu ya wasaa inayofunika hadi
nusu ya magoti. Chini ya hio mtu huvaa suruwali ndefu na ya wasaa...
´Allaamah al-Fawzaan:
Ni suruwali?
Muulizaji:
Ndio.
22
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana, haiwezekani. Suruwali haiwezekani.
Chanzo: http://youtu.be/rKR8UyI_8AM
26) Lipi La Kufanya Unapojiwa Na Mawazo Mabaya?
Swali:
Mawazo yangu mara nyingi yanakuja katika mambo yanayomchukiza Allaah,
na mimi daima huwa nikijiepusha na mawazo haya na kusema kuwa
yanatoka kwa Shaytwaan. Je, mtu atahesabiwa kwayo?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hatohesabiwa kwayo:
"Ummah wangu umesamehewa kwa makosa yao na kwa kusahau, na
yanayohadithia nafsi zao maadamu tu hawajayatamka au kuyafanya".
Kule kuchukia kuyazungumzia na kuyasema, hii ni alama ya Imani. Ni juu
yako kutafuta kinga kwa Allaah kutokana na Shaytwaan aliyelaaniwa, na ni
juu yako kutupa mawazo hayo na kuepuka maingiliano yake.
Chanzo: http://youtu.be/waGR7ndX3IY
27) Kufunga Siku Ya Maulidi Ya Mtume (´alayhis-Salaam)
Swali:
23
Inajuzu kufunga siku ya kuzaliwa kwa Mtume (maulidi)?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana, ni Swawm ambayo haikuweka Allaah wala Mtume Wake na wala
haikuwekwa kwetu kufunga. Naam, siku ya Jumatatu unafunga, hapana ya
tarehe 12 Rabiy´ al-Awwal - unafunga Jumatatu kwa kila wiki, hii ni Sunnah.
Ama tarehe 12 ya Rabiy´ al-Awwal ikikutana na siku ya Jumatatu
unasherehekea [na kufunga] kwa kuwa imeangukia siku ya Maulidi, hapana
haijuzu hili.
Chanzo: http://youtu.be/AZNuq_-Nm7w
28) Ipi Hukumu Ya Kutawadha Bafuni?
Swali:
Ipi hukumu ya mwenye kutawadha bafuni, na je inajuzu Wudhuu wake?
Imaam Ibn Baaz:
Hakuna ubaya. Akitawadha bafuni, hakuna ubaya. Aseme kabla ya
kutawadha "Bismillaah" na atawadhe. Kwa kuwa [kusema] Bismillaah ni
wajibu kwa baadhi ya wanachuoni, na ni jambo la kusisitizwa kwa [kauli] ya
wengi. Aiseme, na ni karaha kuiacha, kwa kuwa kilicho cha karaha kinaachwa
wakati wa haja. Mtu kaamrishwa kusema Jina la Allaah mwanzo wa kutia
Wudhuu, hivyo atasema Jina la Allaah na kukamilisha Wudhuu wake. Ama
Du´aa baada ya Wudhuu inakuwa baada ya kutoka bafuni. Akimaliza anatoka
na kuomba Du´aa ya baada ya Wudhuu nje ya bafu. Lakini ikiwa bafuni ni
sehemu tu ya Wudhuu na hakuna sehemu ya kujisaidia wala kukojoa bali ni
sehemu tu ya Wudhuu, hakuna ubaya kusema jina la Allaah kwa kuwa si
sehemu ya kujisaidia.
24
Chanzo: http://youtu.be/ImTC_0ASc6Y
29) Hukumu Ya Kulala Kwa Tumbo (Kifudifudi)
Swali:
Nimeambiwa kuwa kulala kwa tumbo ni Haramu, je hili ni sahihi? Na ikiwa
ni sahihi, nifanye nini kwa kuwa siwezi kulala vizuri ila mpaka nilale kwa hali
hii?
Imaam Ibn Baaz:
Imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba
alimuona mmoja katika baadhi ya Maswahabah wake akilala kwa tumbo lake
akamtikisa kwa mguu wake na kumwambia:
"Hakika ni njia ambayo inamchukiza Allaah."
Katika Riwaayah nyingine:a
"Hakika ndo jinsi watu wa motoni wanavyolala."
Kwa hiyo ni makruhu kulala hivyo, inatakiwa kuacha isipokuwa kama
kutakuwa dharurah, kama kwa maumivu ambayo mtu anayapata ikamfanya
mtu alale hivi. La sivyo inatakiwa kuacha, dogo tunaloweza kusema ni
makruhu. Kwa kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
"Hakika ni njia ambayo inamchukiza Allaah."
Inatakiwa kuacha, dogo tuwezalo kusema ni kuwa ni makruhu kufanya
hivyo, kwa kuwa dhahiri ya Hadiyth inaharamisha. Inatakiwa kwa muumini
mwanaume na mwanamke kuacha kulala kwa njia hii, isipokuwa tu kwa
dharurah isiyowezekana.
Chanzo: http://youtu.be/RyV-HT6GiJA
25
30) Hadiyth Dhaifu Ya Mu´aadh (Radhiya Allaahu ´anhu)
Shaykh Dr. Abu ´Abdul-Haliym ´Abdul-Haadiy:
Kwa kuwa kuna baadhi ya Hadiyth ambazo Ummah wamezikubali, ila
hazikuthibiti kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama Hadityh
mashhuri wakati Mtume alipomtume Mu´aadh (Radhiya Allaahu ´anhu)
kwenda Yemen. Akamwambia utahukumu Kwa nini? Akasema "Kwa Kitabu
cha Allaah." Akamuuliza "Ikiwa hukupata katika Kitabu cha Allaah?”
Akasema "Kwa Sunnah za Mtume wa Allaah." Akamuuliza “Ikiwa hukupata
katika Sunnah za Mtume wa Allaah?” Akasema "Ntajitahidi kwa rai yangu."
Hadiyth hii enyi waja wa Allaah, haikuthibiti kwa Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam) hata kama Ummah wameikubali. Ni wajibu kutanabahi
jambo hili.
Chanzo:
http://www.assalafia.com/modules.php?name=tapes&dcategory=%C7%E1%
E3%E4%E5%CC
31) Anampiga Binti Yake Kwa Kumtomsikiliza Yeye Na Mama Yake
Swali:
Ninapotaka kumpiga binti yangu kwa tatizo baina yake yeye na dada yake au
vurugu zake nyumbani au kutosikiliza maneno ya mama yake au maneno
yangu na kadhalika; ninapompiga huogopa na husema: "Babangu mpenzi
Allaah Akuhifadhi, ninamuomba Allaah Akuingize Peponi." Naingiwa na
wasiwasi kwa Du´aa hii khaswa ninapoendelea kumpiga na ninajiambia
nafsini: "Sema, ewe Allaah Niingize Peponi ilihali na mimi niko nampiga."
´Allaamah ´Abdir-Rahmaan al-Baraak:
26
Kwa nini unampiga? Kwa nini? Usimpige! Kwa nini umpige?!
Muulizaji:
Kwa kumuasi mama yake au baba yake.
´Allaamah ´Abdir-Rahmaan al-Baraak:
Hapana, hapana usimpige. Muadhibu kwa maneno. Kumpiga si njia nzuri.
Mpige kwa kukiuka haki ya Allaah, kwa kukiuka haki ya Allaah. Kwa mfano
haswali na kishafikisha miaka kumi, muadhibu kipigo cha kumuweka adabu.
(Kumpiga kwako) ni kosa. Kuna baadhi ya watu wanachupa mipaka. Hata
kuna baadhi ya watu wanawaadhibu watoto wao kwa moto! Huu ni ujinga.
Kumuweka mtoto adabu si kumtesa! Kuwa mwenye kurehemu utarehemewa
nawe. Usimpige binti yako. Muadhibu kwa [maneno]. (Kama kusema) huoni
aibu, huoni aibu, hili si sawa, unafanya nini hivyo?
Chanzo: http://youtu.be/rEq0EZMTMEg
32) ´Allaamah ´Abdul-Muhsin al-´Abbaad Kuhusu Anashiyd
´Allaamah ´Abdul-Muhsin al-´Abbaad:
Mtu anatakiwa kuchunga wakati wake katika yatayomfaa duniani na
Aakhirah, ajishughulishe na kusoma Qur-aan, kusoma vitabu vyenye
manufaa, mashairi mazuri ambayo yanashaji´isha katika tabia nzuri na katika
adabu nzuri. Ama hizi Anashiyd ambazo zimezuka katika masiku haya
yamwisho na ambazo zinawashughulisha kila siku wengi na wanazisambaza,
haitakiwi kujishughulisha nazo na wala haitakiwi kuzisikiliza.
Chanzo: http://youtu.be/ouMuOfE0CHM
27
33) Usufi Si Katika Uislamu
Swali:
Ipi hukumu ya Usufi katika Uislamu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Katika Uislamu hakuna usufi, hili ni Bid´ah. Usufi ni Bid´ah na si katika
Uislamu. Ni wajibu wa aliyetumbukia humo atubie kwa Allaah (´Azza wa
Jalla) na arejee katika Sunnah na katika waliyokuwemo Salaf-us-Swaalih
katika kuwa na msimamo katika Dini ya Allaah na kumuiga Mtume (Swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam) na Makhalifah wake waongofu. Hii ndio Manhaj
sahihi. Kasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
"Na Ummah wangu utagawanyika katika makundi 73, yote yataingia motoni
ila moja tu. Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) wakauliza: "Ni lipi hilo
Mtume wa Allah? Akasema: "Ni wale watakaokuwa katika mfano wa yale
niliyomo leo na Maswahabah wangu."
Hakuna kusalimika wala kuokoka isipokuwa [kwa kushikamana] na mfumo
wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake. Na
usufi si katika mfumo wa Mtume (Swalla Allahu ´alayhi wa sallam) na si
katika mfumo wa Maswahabah wake, na si katika mfumo wa karne bora bali
ni kundi limezushwa katika Uislamu, na lina upotofu mwingi. Na wakati
mwingine kunakuwa na makaburi na kumshirikisha Allaah (´Azza wa Jalla)
na kuwaamini maiti (wafu). Inakuwa ni usufi na Shirki pia.
Chanzo: http://youtu.be/4SUw8OSMKVo
34) Radd Kwa Jabriyyah Na Qadariyyah
28
Shaykh Dr. Abu ´Abdul-Haliym ´Abdul-Haadiy:
Na kawaradi Allaah (Jalla wa ´Alaa) makundi mawili kwa kauli Yake (Jalla wa
´Alaa):
البصير السميع وهو شيء كمثله ليس
"Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona."
(42:11)
Anawaradi Mushabbihah (wale wanaozifananisha Sifa za Allaah za viumbe
Vyake) kwa kauli Yake Allaah:
شيء كمثله ليس
"Hapana kitu kama mfano wake." (42:11)
Hapa anawaradi mushabbihah. Na kauli Yake Allaah:
البصير السميع وهو
"Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona." (42:11)
Hapa Anawaradi Mu´attwilah (wale wanaokanusha Sifa za Allaah). Watu wa
haki (Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah) ndio wanathibitisha Sifa za Allaah (Jalla
wa ´Alaa) uthibitisho usiokuwa na mfano, na hawazifananishi na sifa za
viumbe kwa kutegemea Kauli ya Allaah (Jalla wa ´Alaa):
البصير السميع وهو شيء كمثله ليس
“Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona.”
(42:11)
Wao wako kati kwa kati, katika mlango vitendo vya Allaah baina ya Jabriyyah
na al-Qadariyyah. Jabriyyah wamechupa mipaka katika Qadar, wakapinga
matendo ya waja na wakasema:
"Binaadamu kafungwa katika matendo yake, hana khiyari wala matakwa."
Ni mwenye kuzini na wakati huohuo si yeye mwenye kuzini, anaiba na si
yeye mwenye kuiba, wananasibisha kuwa matendo haya ni majawaliwa, na
[wanasema] kwa uhakika mtendaji ni Allaah (´Azza wa ´Alaa). Na haya ni
madhehebu batili, madhehebu ya Jabriyyah, na ndio madhehebu ya Jahmiy
bin Safwaan.
29
Chanzo:
http://www.assalafia.com/modules.php?name=tapes&dcategory=%C7%E1%
E3%E4%E5%CC
35) Muislamu Aliyeacha Swalah Ni Kafiri Na Lazima Auawe
Swali:
Nina jamaa asiyeswali, nimemnasihi hakukubali. Nikamweleza msimamizi
wake na akasema anasikia uogo asije kuhamishwa. Akanambia nimsisitize
aswali na kwamba kumtisha kufukuzwa. Akanikasirikia sana. Je, kitendo
changu hiki ni kosa? Na lipi la wajibu katika hali kama hii?
´Allaamah al-Fawzaan:
Yule asiyeswali sio Muislamu. Kutokana na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam). Kasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
"Baina ya mja na kufuru na Shirki ni kuacha Swalah."
"Ahadi iliyopo baina yetu sisi na wao [makafiri] ni Swalah, atakayeiacha
amekufuru."
Na dalili za kwenye Kitabu (Qur-aan) na Sunnah zinamkufurisha aliyeacha
Swalah ni nyingi. Wala haitoshi mtu kama huyu kuhamishwa tu kazini, bali ni
wajibu kuachishwa kazi kabisa. Bali ni wajibu auawe ikiwa hatotubia kwa
Allaah na kuhifadhi Swalah; ataambiwa aleta Tawbah ikiwa hakufanya hivyo
auawe. Na ulivofanya kwake huo ndo wajibu kwako; kumnasihi,
kumkumbusha Allaah. Na ikiwa hatokubali na akaendelea kuacha Swalah, ni
wajibu (kiongozi) kumuua. Wala haitoshi tu kumhamisha kazini, bali kitendo
tu cha kumuajiri ni kosa. Haijuzu kumuweka mtu kama huyu kafiri sehemu
za Waislamu, kwa kuwa anakuwa kiigizo [kibaya] kwa wengine.
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=K2Ax448_J30
30
36) Lini Kuhukumu Kinyume Na Aliyoteremsha Allaah Mtu Anakuwa
Kafiri?
Shaykh Dr. Abu ´Abdul-Haliym ´Abdul-Haadiy:
Wale wanaowakufurisha watawala wa kiislamu, na wanawakufurisha wale
ambao hawahukumu kwa yale Aliyoteremsha Allaah (Jalla wa ´Alaa), hata
hivyo masuala haya yanahitajia ufafanuzi. Kuhusiana na kuhukumu kwa yale
Aliyoteremsha Allaah (Jalla wa ´Alaa). Hakimu anaweza kuwa kafiri - ukafiri
wa kumtoa katika Uislamu akihukumu kinyume na aliyoteremsha Allaah
huku akiitakidi kuhukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah ni bora zaidi
kuliko kuhukumu kwa Aliyoteremsha Allaah (Jalla wa ´Alaa). Huyu ni kafiri!
Atakayehukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah huku akiitakidi kuwa
[hukumu hio] iko sawa na hukumu ya Allaah huyu ni kafiri! Na
atakayehukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah huku akiamini kuwa
inajuzu kuhukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah, huyu pia ni kafiri
kufuru kubwa! Ama akihukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah huku
akiamini kuhukumu kwa Aliyoteremsha Allaah ndio bora zaidi na iliyo
kamili, lakini kwa [kupewa] rushwa, kupenda cheo au kutaka kufikia jambo
fulani la kidunia, akahukumu naye ni mwenye kuitakidi kuwa ni dhalimu na
ni muasi kwa hali hii hatoki katika Uislamu na kufuru yake ni kufuru ndogo
kama alivosema Ibnu ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kwa kauli ya
Allaah:
“Na wasiohukumu kwa Aliyoteremsha Allaah, basi hao ndio makafiri.”
(05:44)
Akasema ni kufuru ndogo. Khawaarij wanamwita mtu huyu kafiri, na
wanahalalisha damu yake na mali. Hivyo ndo maana walimkufurisha ´Aliy,
Mu´aawiyah na Maswahabah wao na wakahalalisha yanayohalalishwa kwa
makafiri. Ama Mu´tazilah wanasema mwenye kufanya dhambi kubwa
anatoka katika Imani (Uislamu) na wala haingii katika kufuru, mtu huyo yuko
katika manziylah mbili - mtu hawezi kusema ni kafiri wala kusema ni
muumini. Hii ni katika misingi ya Mu´tazilah. Wana misingi mingine
kuhusiana na Tawhiyd, makusudio ya Tawhiyd kwao ni kupinga [kuzikataa]
Sifa [za Allaah]. Hivyo akiongelea mtu kuhusu Tawhiyd ni juu yake
31
kubainisha uhakika wa Tawhiyd ambayo waliomo. Kuna ambao wanasema
Tawhiyd maana yake ni al-Haakimiyyah - maaya ya laa ilaaha illa Allaah
maana yake ni al-Haakimiyyah. Na hii ndio Itikadi ya al-Ikhwaan al-
Muflisiyn.
Chanzo:
http://www.assalafia.com/modules.php?name=tapes&dcategory=%C7%E1%
E3%E4%E5%CC
37) Kitabu Na Sunnah Vinatangulizwa Kabla Ya Ijmaa´
Swali:
Wakati fulani kunasemwa katika masuala "Dalili ya hili ni Ijmaa´, Kitabu na
Sunnah. Kwa nini kunatangulizwa Ijmaa´? Je, Ijmaa´ ina nguvu zaidi kuliko
Kitabu na Sunnah?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana hili ni kosa. Dalili ya hilo ni Kitabu na Sunnah na Ijmaa´. Hakuna
yeyote awezae kutanguliza Ijmaa´ kabla ya Kitabu na Sunnah.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2513
38) Imaam Abu Haniyfah, Imaam Wetu, Kiigizo Chetu
Swali:
Tulikusikia wakati wa darsa ukisema:
"Abu Haniyfah (Rahimahu Allaah)"; Ulimrehemu...
32
´Allaamah al-Fawzaan:
Rahmah kunjufu! Namuomba Allaah Amrehemu Rahmah kunjufu na
Amsamehe. Ni Imaam wetu na kiigizo chetu bora. Afurahi mwenye kufurahi
na achukie mwenye kuchukia.
Chanzo: http://youtu.be/A7KDMfJCXGY
39) Kumtolea Mtu Swadaqah Kwa Kuswali Naye Baada Ya Swalah Ya
´Aswr Na Fajr
Swali:
Aliingia mtu Msikitini baada ya Swalah ya ´Aswr nami nimekaa, akanambia
nitolee Swadaqah na uswali na mimi. Nikakumbuka kuwa ni wakati wa
makatazo [kuswali], lakini nikaswali naye. Ipi hukumu ya kitendo hiki? Na je
vipi ikiwa ni baada ya Swalah ya alfajiri?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Hukumu ni ya kitendo hiki ni thawabu na ni sahihi, sawa ni baada ya Swalah
ya alfajiri au baada ya Swalah ya alasiri. Swadaqah yake ni sahihi na wewe ni
mwenye ujira.
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2547
40) Ipi Bora Kwa Wanawake Kuswali Jamaa´ah Au Kila Mtu Kivyake?
Swali:
33
Muulizaji kutoka Sweden, je inajuzu kwa wanawake kuswali Jamaa´ah? Na
lipi bora kwao kuswali Jamaa´ah au mmoja mmoja?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Ndio waswali Jamaa´ah wakiweza hilo na waongozwe na msomi mjuzi wao
na asimame katikati yao. Kuswali Jamaa´ah katika hali zote ni bora kuliko kila
mmoja kuswali kivyake.
Chanzo: http://youtu.be/eV8zv4vsxpM
41) Inajuzu Kumhukumu Mtu Moja Kwa Moja Kuwa Ni Mnafiki?
Swali:
Muuliza kutoka Ufaransa, je atayedhihiri kuwa na alama za unafiki
atahukumiwa kuwa ni mnafiki?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Atahukumiwa kwa matendo yake kama walivyokuwa wakifanya Salaf-us-
Swaalih. Walikuwa wakisema atayefanya kadha, atakuwa kadha.
Atakayefanya ukafiri kakufuru, atakayefanya unafiki amenafaka. Inakuwa
atakayefanya kadha katumbukia katika unafiki, na mtu hasemi moja kwa
moja wewe ni mnafiki. Kwa kuwa usulubu huu si usulubu sahihi. Da´wah
inatakiwa iwe kwa hekima na mawaidha mazuri.
Chanzo: http://youtu.be/Ubv_ks-MbHA
34
42) Hukumu Ya Kufanya Mazoezi Katika Ukumbi Za Muziki
Swali:
Muulizaji kutoka Ubelgiji, mama yangu kafikwa na maradhi ya mafuta
yaitwayo "sumna", na alienda kwa daktari akamwambia ana umuhimu
mkubwa wa kufanya mazoezi, na ukumbi zote za mazoezi zina muziki.
Afanye nini?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Anaweza kufanya mazoezi nyumbani kwake, na haijuzu kwake ikiwa kweli ni
Muislamu mwanamke kwenda katika manyumba ya muziki na yaliyomo
katika ufisadi. Tahadhari! Anaweza kufanya mazoezi nyumbani kwake, au
akatoka yeye na Mahram wake mahala pazuri na akafanya mazoezi; kama ya
kutembea, kufanya harakati n.k. na akafikia lengo lake katika hayo. Na
ajiepushe na ukumbi za muziki na nyinginezo.
Chanzo: http://youtu.be/dX-_xi66OqQ
43) Anashiyd (Qaswiydah) Ni Haramu
Swali:
Ipi hukumu ya kusikiliza Anashiyd ambazo zinahalalishwa na baadhi ya
wanachuoni na baadhi ya wengine wanaziharamisha? Na ikiwa ni Haramu
vipi vikwazo vyakuharamisha?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Bila shaka Anashiyd sio katika ´Ibaadah mpaka mtu apewe ujira kwayo
mwenye kuziimba na msikilizaji, na si katika uongofu wa Salaf na
litalokwenda kinyume na hili ni batili. Kuna baadhi ya wanachuoni
wameandika kuhusiana na Anashiyd na kubainisha ubatili wake khaswa
35
katika zama hizi za mwisho kumekuwa Anashiyd za nyimbo na zimeathiri
sana kuliko Qur-aan na khaswa vijana. Ni wajibu kujiepusha nazo, na ibara
mbaya wamezipa ni pale wasemapo "Anshiyd za Kiislamu", sio za Kiislamu
kwa hali yoyote. Ni Haramu bila shaka.
Chanzo: http://youtu.be/nbfiRXqzx9o
44) Mume Na Mke Wanadanganya Serikali Wameachana Ili Wapate Pesa
Zaidi
Swali:
Muulizaji kutoka Sweden, lau ikiwa mtu ataidanganya serikali na kuwaambia
kuwa amempa Talaka mke wake kwa kuwa watampa mwanamke yule
aliyetalikiwa mali, na isitoshe akapiga saini kwa hilo. Je, kitendo hiki kinajuzu,
na je Talaka imepita?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Atachukuliwa kuwa ni muongo na uongo ni jarima munkari hata kama
itakuwa ni kwa kafiri. Watu wawe na tahadhari kwa kufikia mali kwa njia
chafu kama hii ya uongo.
Chanzo: http://youtu.be/90Ui0scVyEo
45) Msikiti Unaokhatimu Qur-aan Na Usiyokhatimu, Wapi Nifanya
I´tikaaf?
Swali:
36
Ipi bora zaidi kwa mwenye kukaa I´tikaaf, afanye I´tikaaf katika Msikiti wake
ambapo wanasoma nusu juzu katika Kitabu cha Allaah au atoke aende katika
Msikiti ambapo wanakhatimu Qur-aan?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ni mwenye khiyari kuchagua kufanya I´tikaaf katika Msikiti wowote ambapo
anaona ni bora kwake, achague Msikiti ambao anaona ni bora kwake katika
mji wake.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2655
Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad , na ahli zake na
Maswahabah zake na watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah.