Haliuzwi - Johns Hopkins Center for Communication Programsccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 67 Jul-Aug...
-
Upload
duongquynh -
Category
Documents
-
view
372 -
download
13
Transcript of Haliuzwi - Johns Hopkins Center for Communication Programsccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 67 Jul-Aug...
2 Si Mchezo! JULAI-AGOSTI 2013
Si Mchezo! Huzalishwa na kusambazwa.
Si Mchezo! husambazwa.
Lilikozalishwa toleo hili.
Kuja mjini bila mpango ni kujidhalilisha na pia unakuwa mzigo kwa
wengine. Tuliza akili na anza kuangalia fursa zilizoko huko kijijini kwako kisha zifanyie
kazi. Omba ushauri kwa wataalamu ikibidi
Maisha ni kama mchezo wa kuigiza kwani kila
wakati unatakiwa ubuni kitu kipya na kukiendeleza. Lengo lako litatimia kama
utakuwa mbunifu wa kuboresha yale uliyolenga
kuyatimiza.
3
TAHARIRIJiji la Dar es Salaam hupokea vijana zaidi ya laki moja kila mwaka ambao
huja ‘kusaka’ maisha. Wengine kabla ya kuingia mjini husikia kwenye
nyimbo ujumbe ‘usije mjini’. Huenda hofu inatanda katika nafsi zao na
kukosa malengo. Wengine huishia mikononi mwa mgambo wa jiji! Sawa
basi peruzi kitu kipya kilichopikwa katika jiji la Bongo kisha tujadili
mustakabali wa maisha yetu vijana.
Majuka
YALIYOMO
4 Stori Yangu: Usije mjini, jipange kwanza
6 Mambo Mapya:Unaishi vipi Dar?
8 Hadithi ya Picha: Mjini mipango
12 Je, Wajua: Jiangalie, utapotea jombaa
14 Sauti yangu
16 Burudani: Karibu Dar
18 Ruka Juu: Joseph nd’o jembe!
20 Nguvu za mwanamume: Ngono na mapenzi
21 Nguvu za mwanamke: Kweli, inawezekana
22 Cheza salama: Kona ya mtaa
24 Katuni: Jilinde...
27 Ukweli wa mambo: Sema hapana, mlinde mwenzako
28 Sema Tenda:Tusilalamike, tuchakarike
30 Ushauri
Mkurugenzi MtendajiDr. Minou Fuglesang
Mkurugenzi wa HabariAmabilis Batamula
Meneja MachapishoJiang Alipo
Mhariri Mkuu Majuka Ololkeri
WaandishiRaphael NyoniGaure MdeeBetty LidukeJosephat Mwambula
WashauriTimu ya Femina HIP
Meneja UhusianoLilian Nsemwa
Katuni na UsanifuBabaTau, Inc.
Mpiga Chapa Jamana Printers Ltd
Usambazaji EAM Logistic LtdFemina HIP na Washirika
Si Mchezo! limefanyika kwa hisani kubwa ya Serikali za Sweden (Sida), Denmark (DANIDA), HIVOS, RFSU, TWAWEZA na JHU-CCP/TCCP
Yaliyomo humu ndani ni jukumu la Femina HIP na hayawakilishi maoni au mitazamo ya wafadhili.
Wasiliana nasi kwa:S.L.P. 2065, Dar es SalaamSimu: (22) 212 8265, 2126851/2 Fax: (22) 2110842email: [email protected] Mchezo! huchapishwa na Femina HIP.Sms: Andika SM acha nafasi andika maoni yako kisha tuma kwenda 15665
Ukiingia kichwa kichwa mjini uta-
potea! Shauri yako.
Mmh kweli, tupeane michongo lakini
4 Si Mchezo! JULAI-AGOSTI 2013
Kusaka maisha kunahitaji utulivu wa akili na
kugundua fursa zinazokuzunguka vinginevyo
utajikuta upo kwenye wakati mgumu. Wengine
wana bahati zao lakini kama wahenga walivyosema,
“Bahati ya mwenzio, usiilalie mlango wazi”.
Naitwa Hamad Masoud (27), nilizaliwa Urambo,
Tabora. Nilipozaliwa tu, baba na mama
wakatengana. Mama alishindwa kunisomesha.
Nilipofikisha miaka 12 nilianza kusaka pesa ili
kumsaidia mama kutunza familia. Nilipata ajira
ya kuuza maandazi nikiwa nalipwa 2,000/= kwa
mwezi. Nilijifunza kutengeneza maandazi pia.
Baada ya miaka miwili, binamu yangu anayeishi
Tabora mjini aliniita nikafanye kazi ya kuuza
mitumba. Nilifika na kuanza kazi hiyo kwa ujira wa
1,000/= kwa siku. Pesa hiyo ndiyo chakula, malazi
na mavazi. Nilifanya kwa miaka mitatu lakini
nikaona hainilipi kulingana na gharama za maisha
ya mjini. Wakati huo nilikuwa nikisikia kwamba Dar
es Salaam panalipa. Sikuwa na nauli lakini nilisafiri
hadi Dar kwa treni kwa kumkwepa mkaguzi wa
behewa ili nisikamatwe mpaka nikafika. Mfukoni
nilikuwa na 500/= tu ambayo nilinunulia mihogo.
Nilifika stendi ya Mnazi Mmoja na kupanda basi
liendalo Tabata. Lilikuwa basi linalonadiwa na
wapiga debe nikajua watu wote wanakwenda
huko. Niliposhuka Tabata sikuwa na ndugu wala
rafiki wa kufikia kwake. Njaa iliuma na sikuwa
hata na senti mfukoni. Nilimuona dada aliyekuwa
dukani. Nilimfuata kumwomba msaada na baada
ya mahojiano na kumweleza ukweli alinipa kazi
ya kuuza maji. Nilipeleka mapato jioni. Malipo
yangu kwa mwezi yalikuwa 30,000/= Baada
ya miaka mitatu nilishindwana na bosi wangu
nikaacha kazi na kurudi Tabora. Maisha hayakuwa
kama nilivyotarajia.
Pamoja na kurudi Tabora, ‘ramani pia haikusoma’.
Rafiki yangu tuliyekuwa tukiuza naye mitumba
alinishauri nirudi Dar kwa dada yake ambaye
angeweza kunipatia kazi. Niliona kuna neema
inakuja mbele baada ya kukatiwa tiketi ya safari
ya Dar. Nilipofika Dar, kazi niliyopewa kwa miezi
mitatu ya mwanzo ilikuwa ni kufua na kuosha
vyombo huku nikisubiri kazi niliyoahidiwa.
Baadaye nilipewa 10,000/= kama mtaji wa biashara
ya maji ya paketi huku kila siku jioni nikitakiwa
Hamad akiwa katika moja ya mishemishe zake huko
Magomeni, Dar es Salaam
STORI YANGU
Usije mjini, jipange kwanza
5JULAI-AGOSTI 2013 Si Mchezo!
kurudisha faida ya 25,000/=. Nilifanya kwa uvumilivu kwa muda
wa miaka miwili nikiamini ipo siku nitapewa mtaji wangu.
Kuna kipindi sikuwa na maelewano mazuri na yule dada. Niliugua
sana na baada ya matibabu na kupona, mume wa yule dada
alinihamishia kwa mke wake mwingine Magomeni. Kazi zilikuwa
zile zile ila penyewe ujira ulikuwa mkubwa hadi nikaweza kupanga
chumba cha 6,000/= kwa mwezi. Baadaye kidogo tajiri alibadili
biashara hivyo ‘nikapigwa chini’.
Maisha yakabadilika. Sikuwa na chanzo cha pesa tena. Nililala
popote kwa kushindwa kulipia kodi ya chumba. Nilikuwa navaa
nguo zangu zote tano nilizokuwa nazo. Safi ndiyo iliyotangulia
kwa juu na chafu kwa ndani.
Mwaka 2008, nilianza kazi ya kupiga debe katika vituo vya
daladala, kazi ambayo naifanya hadi sasa. Kazi hii ni ngumu sana
kwani unaishi katikati ya watu wenye dhiki na wenye mitindo
ya maisha yenye changamoto kama kutumia dawa za kulevya,
wizi na pombe. Ushauri wangu kwa vijana wenzangu ni kwamba
usije mjini kabla hujajipanga kwani utaweza ukajutia uamuzi
wako. Nina mchumba ambaye naishi naye na wote tunaishi kwa
kuaminiana na kujihadhari kwani tunajua kuwa maambukizi ya
VVU yapo.
Hamad akiwa na
mchumba wake
Fatuma Ally (24)
mitaa ya Magomeni,
jijini Dar.
6 Si Mchezo! JULAI-AGOSTI 2013
MAMBO MAPYA
Unaishi vipi Dar?
Asubuhi na jioni utaona kila mtu ‘bize’ akiwahi mishemishe zake na wengine wakirudisha
‘majeshi’. Kutokana na tatizo la ajira, wachache wamebahatika kupata ajira maofisini tofauti
na mawazo ya wengi. Labda nikuulize, hivi umeshawahi kujiuliza waliobaki huwa wanaishia
wapi? Au maisha yao wanayaendesha vipi? Hebu chekecha akili halafu upate picha ya changa-
moto ya ajira iliyopo Bongo Dar es salaam.
Matunda kwa afya
Wakati unajenga
afya, wao wanain-
giza mkwanja, ‘fea’
kabisa yaani. Ukiwaona
mtaani unaweza
kuwadharau, lakini
wengi wao wanamudu
kulipa kodi za nyumba
na kusomesha watoto
wao kutokana biashara
ya matunda.
Kujituma ndiyo mpango mzima
Baadaye ukimkuta
jamaa kanyuka pamba
za ‘ukweenh’, unaweza
kufikiri kuwa ndiye
yule mshikaji uliyeku-
tana naye kitaa anauza
maji?
Mmachinga amka!
Wewe mmachinga ni mjasiriamali unayechipukia, hivi unafahamu
kwamba kuna Vibindo? Ni jumuiya ambayo inasaidia na kuende-
leza biashara ndogondogo kwa kuwasaidia wajasiriamali wadogo
kuanzisha kuimarisha na kukuza biashara.
Ndiyo! Kama una biashara yako na hujui jinsi ya kuisajili, kiroho safi
tu wanakuelekeza mchakato mzima. Usifanye biashara yako kienye-
ji. Kama vipi wapigie 022 2152359/ 0784 546 122 kwa maelezo zaidi.
7JULAI-AGOSTI 2013 Si Mchezo!
Poza koo japo kidogo!
Unatoka zako nyumbani kuwahi shu-
ghuli zako, jua kali unajipa moyo uta-
pata sehemu ya kupumzika, upo kwenye
foleni, koo linakereketa. Ukitupa macho
dirishani unakutana na jamaa anaku-
chombeza kwa maji baridiii!
Usafi siyo wa mwili tu
Watu wengi wanakumbuka
kusafisha miili yao lakini
wanasahau kutunza mazin-
gira. Usifanye mchezo kuli-
tunza jiji na barabara zake!
Ili lionekane safi inabidi
baadhi ya watu waonekane
kivingine kabisa.
8 Si Mchezo! JULAI-AGOSTI 2013
Maisha ni kutafuta na sio kutafutiana, na
kila mmoja inabidi achakarike ki mpango
wake. ‘Ntoke vipi’ ndio swali ambalo kila
mtu anajiuliza kichwani. Nchumali kafikiria
akaona hapana, siwezi kutoka nikiwa hapa
hapa kijijini labda niende mjini. Twende
naye huko mjini...
12 Si Mchezo! JULAI-AGOSTI 2013
JE, WAJUA?
KumbukaFanya kazi kwa bidii, jitume, maisha popote,mjini au kijijini.
Jiangalie, utapotea jombaa!
Ukweli ni huu
Fursa zilizoko vijijini hazina tofauti kubwa
na zile ambazo tunazikimbilia mjini.
Wakati mwingine, kijijini ndiyo mwake
zaidi kwani kuna ardhi kubwa ya kulima na
kufanyia vitu vingi ilimradi tuchangamshe
akili zetu kubuni kitu cha kufanya.
Bora uende mjini ukiwa na michongo
yako mizuri kijijini, kuliko kwenda kuhaha
ukaishia mikononi mwa mgambo wa jiji,
utajuta!
Jibebe
Hata kama ukipata mwenyeji
akakupa hifadhi, haimaanishi
huyo atakuwa mlezi wako ndani
ya jiji, inabidi ujue utakula wapi
na utaishi vipi. Jipange!
Zingatia haya
kwenda MJINI
unapoishi na uzitumie.
na manufaa kwako.
Eti kuzaliwa mjini ‘Form Six’ kuishi
mjini chuo kikuu! Unaacha
mipango yako ya maana ili uwahi
fasta ‘chuo kikuu.’ kakudanganya
nani?
Kuishi mjini kunahitaji ujipange na
siyo kuishi kwa kutegemea misemo
ya kale. Si wote unaowaona wako
mjini mambo yamewanyookea, la
hasha! Wengine wamepigika kweli
lakini hawataki tu kukubali matokeo
na kwenda kujipanga upya kijijini
kuliko kuishia kuhaha bila ‘ramani’
14 Si Mchezo! JULAI-AGOSTI 2013
Wewe pia unaweza kulonga na vijana wenzako. Tuandike maoni, ushauri,
vichekesho,maswali nk, weka anuani yako na tuma ukiambatanisha na picha yako kwa Mhariri, Jarida la
Si Mchezo!, S.L.P Dar es Salaam.
[email protected] tumbukiza katika boksi la
Si Mchezo! kama lipo katika eneo unaloishi.
SAUTI YANGU Kama una chochote unachotaka kusema tuandikie ili upate fursa ya kuwaelimisha wengine
Maoni yaliyotolewa katika ukurasa huu
ni ya wasomaji, si lazima yalingane na
msimamo wa Femina.
Si Mchezo!Femina HIPSLP 2065,
DSM
Tujiheshimu kwanza
Wasichana kuvaa nguo nusu utupu
mnajidhalilisha. Siyo kujidhalilisha
tu, mnatudhalilisha hata sisi wen-
gine mbele ya wazazi wetu na jamii
kwa ujumla. Mila na desturi zetu
haziruhusu kuvaa nguo nusu utupu
ila tunafanya kuiga nchi za wen-
zetu. Tubadilike tuache tabia hiyo
na tuendeleze utamaduni wetu
ili kuokoa kizazi
kijacho.
Khadija Omary,
Dar es salaam.
Mabasi ya wanafunzi ni muhimu
Kwa mtazamo wangu naona wanafunzi hasa wanaosoma mbali na shule wanapata tabu ya usafi ri hapa Dar. Tatizo hili linawa-fanya wachelewe kufi ka shule na kukosa baadhi ya vipindi darasani. Naishauri serikali ifanye jitihada za kutafuta njia mbadala kama kutoa mabasi maalumu kwa ajili yao ili kuwa chachu ya mafanikio yao ya kielimu na katika jamii.Othman Juma,Dar es salaam.
Kamari zinaharibu vijana
Kero yangu kubwa ni kwa vijana kujihusisha na mchezo
wa kamari. Vijana wengi waliopo mitaani na hata wa-
nafunzi shuleni, hucheza mchezo wa ‘kubeti’ ambao un-
awapotezea muda mwingi na kujikuta hawafanyi shughuli
za kujiingizia kipato au kusoma. Naiomba serikali kupitia
wizara inayohusika na mambo ya vijana,
wazazi, walezi na wadau wote wa vijana
waliangalie suala hili na kuchukua hatua
haraka iwezekanavyo.
Ally A. Dauka,
Dar es salaam
Dawa za kulevya ni noma
Inasikitisha vijana wengi wa-
napotea kwa kujiingiza katika
suala la utumiaji wa dawa za
kulevya.Tunapaswa kujua
kwamba vijana ndiyo nguzo
kubwa ya taifa letu. Tuepukane
na tabia hizo hatarishi zinazot-
ufanya tupoteze
malengo yetu.
Mary R.
Mwandu,
Dar es salaam.
15JULAI-AGOSTI 2013 Si Mchezo!
“Inatosha,” anasema Shukama mume wa mama wa nyumbani aitwaye Ndope kwa miaka 10 sasa. Shukama anadhani anampenda mke wake ambaye ni mjamzito, lakini kanasa kwenye mtandao wa mapenzi. Ana wapenzi wengine wa nje (nyumba ndogo). Siku ya siku, mambo yakawa si mambo, kama anavyosimulia mwenyewe:
“Juzi nilipokea ujumbe mfupi kwenye simu
yangu, mmoja kati ya wapenzi wangu
Anita alikuwa ananiulizia kuhusu kodi ya
pango na ujumbe mwingine kutoka kwa
mpenzi wangu Zawadi aliyekuwa anataka
hela kwa ajili ya kulipia karo ya shule ya
mdogo wake. Mezani nyumbani kwangu
kulikuwa kuna karatasi yenye ujumbe
kutoka shuleni kwa mwanangu wa kiume
ukinitaka kulipa karo ya shule ndani ya
siku mbili la sivyo mwanangu
atafukuzwa shule.
Jana niliamua kumsindikiza mke
wangu kliniki, baada ya kutafakari ombi
Rajafa. Kliniki tulielezwa mengi kuhusu
elimu ya afya kwa mama mjamzito na
mtoto aliye tumboni, umuhimu wa kuzuia
maambukizi ya VVU kutoka kwa mama
tumboni,
pamoja. zinazochangia
ya VVU, ikiwemo kuwa na uhusiano wa kingono na wanawake zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Mafunzo haya ya kliniki na zile kasheshe zingine za ada na pango, zilinifanya nitafakari kwa kina juu ya tabia zangu na
mtandao wa ngono.
Hii ni moja ya stori tulizowahi
kusikia mara nyingi kutoka kwa
kwenye mitandao ya kingono.
Wakati mwingine hawatambui
hatari iliyopo kwenye mitandao ya
aina hiyo ni ya kweli, mpaka
kitokee kitu cha kutisha. Sikiliza
stori hii:
ya sekondari na kwa sasa amejiunga na masomo ya chuo kikuu kitivo cha
kingono na Sikioni ambaye ni mwanachuo mwenzake wa mwaka wa kwanza.
Mbali na kuwa na uhusiano ya kingono na Sikioni, pia ana uhusiano ya kingono na Mzikombo ambaye ni mfanyabiashara maarufu. Matokeo ya mtihani wa muhula wa kwanza wa masomo yameonyesha kuwa
inamlazimu kurudia masomo matatu.
Kiboboko na kumshawishi wafanye ngono kwa masharti ya kupewa alama
kwa masomo mawili yaliyobaki.
kuwa yuko peke yake katika uhusiano ya kingono na wanaume wake. Kwa kuwa
alikuwa mzuri na mwenye akili hakuona sababu itakayomfanya mwanamume wake awe na mwanamke mwingine.
Alipatwa na mshangao siku alipomtembelea Mzikombo nyumbani kwake na kumkuta anafanya ngono na mwanafunzi mwingine aitwaye Jusiku.
Kitendo hiki kilipiga kengele akilini
kwa kina kuhusu hali ya afya yake. Akaamua kutembelea kituo cha afya ili kupata uhakika wa aina ya majanga aliyojitumbukiza. Aliamua kupima VVU na hakuwa na maambukizi.Alishangaa kwa kuwa alikuwa kwenye mtandao wa ngono na bado amefani-kiwa kuwa salama. Alijua siyo kila mtu
mwenye hiyo bahati. Akaamua kuach-ana na mitandao ya ngono. Bila shaka kuna faida nyingi za kujitoa kwenye mitandao ya ngono zikiwemo kuepuka hatari ya kupata maambukiziya VVU, kumlinda mwenza wako dhidi ya maambukizi ya VVU, kuepuka gharama zisizo za lazima za kuhudumia wana- wake wengi kwa wakati mmoja katika kukidhi mahitaji yao ya maisha, kuleta furaha na maelewano mazuri na mwenza wako nyumbani. Kwa mantiki hii, tujiangalie kwa kinasisi wenyewe, tujitathimini na kupima faida dhidi ya hasara na kusema...
KWA NINI WATU WANAACHANA NA MITANDAO YA KIMAPENZITAHARIRI AWAMU YA PILI
Pia nilijifunza tabia hatarishi
mtu kupata maambukizi
wangu mpendwa na mtoto tunayemtarajia na kisha kuamua INATOSHA. Hapana tena
lake na ushauri wa rafiki yangu.
Uhandisi. Sotafia ana uhusiano wa
kwenda kwa mtoto aliye ushauri
na kupima
Sotafia alibahatika kufaulu mitihani yake
16 Si Mchezo! JULAI-AGOSTI 2013
Utangulizi
Dada tuma eeh! Ngoja kwanza,Producer mbeziYo ha haaaa 0444
Ubeti wa 1Picha linaanza kama muvi ya Solomoni, Gafl a vumbi linazidi wajanja wanavaa miwani, Hii ndio dar karibu ili usijisikie nyumbani,Hapo Ubungo usinunue simu utauziwa sabuni, Panda daladala tukutane buguruni, kuna watu wanapiga ndole utadhania majiniGizani usiku utaona rangi zote za bikini, wanauza mwili ili wanunue wali maini, usicheke broo! Kwa sababu mi sio Mr. Bean,chunga wallet hapa kuna wizi wa mfu-koni, haukawii kushuka kwenye gari hauna phone, kuwa makini uvukapo huku gari hazipigi honi,dala dala zinaa,Bajaj zinakesha macho, Kama huamini ngoja siku ije uamini we Tomaso, Wasio na kazi wanashindia stori za freemason,Wajanja wamepanga sinza, Kino na Tabata, Mchana wanazibua vyoo usiku wanakula bata, Usikojoe ovyo bro! Mgambo watakukamata,Hii ndio dar, mbona unadata kabla hata hujapata starter?
Kiitikio x 2Mmh bata ni daily, daily’Karibu bushman kaa chini tukupashe habari Shangaa mataa Dar ugongwe na gari (Dar es salaam ya sasa)
Ubeti wa piliKaribu sana kwenye hili jiji la joto, Uswahilini chumba kimoja baba mama na watoto, Si ulisikiaga ma-bomu ya gongo la mboto?Yalifanya rafi ki yangu wa damu akafi a
Ghetto,Yaliacha kovu kubwa kama la mba-gala, Dar es salaam watu wengi tu hawanaga pa kulala,Kama unataka mirungi twen’ zetu mitaa ya ilala, Magomeni, mi ujanja wangu wote niliitwa fala,Watu wanaingiza pesa wakiwa wamelala, Watu wengi toka waje ha-wajawahi kurudi kwao,Sababu hawana nauli japo wamemisi ndugu zao, Kuhusu kushinda na njaa hapa ndo zao, Wauza sura wanaishi kwa kuuza mademu zao,Mama anauza bangi, Baba amekata ringi anashinda anacheza bao,Wake zao wanazini kulisha watoto wao, Vijana wao wanatembeza karan-ga, wanatembeza maji,wanatembeza vocha,Jioni wanakabidhi hesabu kwa bosi wao,
Hii ndio dar, ukipenda unaweza kuiita bongo, Machizi wakikosa hela ya bia wanakula gongo,See, haiwi siri uswahilini ukipata mchongo, Wapangaji watakuandama bro mpaka utahama,Ni majungu mixer wanga, utaenda tu kwa mganga, Utapo lala Ghetto kwako kasha ukamwagiwa mchanga
Kiitikio x 2Mmh bata ni daily, daily’Karibu bushman kaa chini tukupashe habari Shangaa mataa Dar ugongwe na gari (Dar es salaam ya sasa)
Ubeti wa tatuDar es salaam ingekuwa nchi, huku Rais angekuwa LowasaHuku watu washashtukia kuna mchezokwenye siasa,Usione watu wamependeza, wengine hawana hata mia,
BURUDANI
Wimbo: Karibu DarWasanii: Kala Jeremiah akimshirikisha Ben Paul
17JULAI-AGOSTI 2013 Si Mchezo!
Hapa mboga ni maharage, nyanya chungu na bamia,Brother man anatembea toka keko kwa miguu, Anakwenda mlimani city kununua mkate tu,(Are you on the facebook?) Ndo mas-wali ya maduu,Ukitaka demu wa peke yako kata mgomba lala juu,Ukimwita demu wako bar wanakuja crew, Utachunwa mpaka ubaki na raba ubaki miguu juu,Hapa bomba halijatoa maji mwezi mzima,Hii ni uswahilini tu na sio kwa jiji zima, Twende Mbezi au Masaki yanatoka mwaka mzima,Katiza Kwa Mtogole uporwe simu mchana,Siku hizi mwanaume anavaa suruali ya kubanaa, Siku hizi dada’ko anakalio za kichina, ukimtafuta humpatiAmeshakuwa wa kimjinimjini
!!! !Nimetoka wapi?DOGO: Baba kwani mimi
nimetoka wapi?
BABA: Dah! mwanangu mbona
unaniuliza swali gumu hivyo?
Hebu kaa hapo nikuhadithie.
Nilikutana na mama yako
kituo cha basi siku moja wakati
anatoka kazini mvua kubwa
ikaanza ikatulazimu tuchelewe
sana kupanda basi, hivyo tu-
kazoeana sana. Baada ya kama
miezi mitatu tukaona ni vyema
tuoane, tukawaeleza wazazi
wetu wakatukubalia, harusi
ikafanyika, tena kubwa sana,
tukaanza kuishi pamoja na kwa
kifupi ndiyo wewe ukapatikana.
Ukikua kidogo utanielewa nina
maana gani
DOGO: Haya, ila mwalimu
atanipiga nisipomwambia ke-
sho, katuambia wote tuwaulize
wazazi wetu tumetoka wapi.
Mwalimu wetu kasema yeye
ametoka Bukoba.
Ndani ya DaladalaDaladala lilipofi ka Manzese konda
akauliza;
KONDA: kuna mtu anashuka?
MREMBO: Tumeyaacha nyumbani,
hapa tuna mitandio tu!! Kufi ka
Ubungo Maziwa, yule dada aliyele-
ta nyodo akataka kushuka
MREMBO: Konda nashuka maziwa
KONDA: Kayanunulie SIDIRIA
yasishuke
Roboti laumbua!Baba mmoja alinunua roboti maal-
umu kwa lengo la kudhibiti tabia ya
uongo katika familia yake. Kwamba
mtu akisema tu uongo basi roboti
linamtandika vibao dakika hiyo hiyo.
Siku moja baba akamuuliza mwa-
nae: “Mage umekuwa wa ngapi
kwenye mtihani?” Mtoto akajibu:
“Wa kwanza!” Bila kuchelewa roboti
likampiga kibao. Baba akaanza kuji-
nadi: “Enzi zangu mimi kila mtihani
nilikuwa nashika namba moja!” Saa
hiyohiyo roboti likamnasa kibao.
Mtoto alipoanza tu kucheka, mara
mama akatokea na kumfokea: “Un-
acheka nini sasa, hujui kama huyo ni
baba yako?” Bila kuchelewa roboti,
likamtandika kibao na yule mama!
Duh...
18 Si Mchezo! JULAI-AGOSTI 2013
RUKA JUU
Joseph nd’o jembe!
Baada ya wiki 13 za kutifua ardhi, kujifunza na
kushindana, hatimaye mshindi wa msimu wa
pili wa shindano la Ruka Juu amepatikana! Joseph
Kizito, 28, kutoka Nkasi, Rukwa, ndiye mkali!
Joseph, amejinyakulia kitita cha shilingi milioni
tano, “Sikuwahi kufikiria kwamba mimi na
kilimo changu ningeweza kupata hadhi hii
au fursa ya namna hii. Kupitia Ruka Juu, watu
sasa wananifahamu na wanakuja kwangu kwa
ushauri,” anaeleza Joseph.
Joseph ni nani?
“Watu waliomzunguka walimfahamu kama
mkulima wa nyanya ambaye aliwahi kuvamiwa na
wezi, wakampora fedha, lakini hiyo haikumkatisha
tamaa ya kulima,” anasema Amabilis Batamula,
mtangazaji wa Ruka Juu ambaye aliwatembelea
washiriki wote sita katika mashamba yao wakati
wa shindano. “Sasa atafahamika kama Mshindi
wa Ruka Juu.”
Ushindi haukuwa rahisi
Joseph, anasema kuwa kushiriki shindano la Ruka Juu
haikuwa kazi ndogo, hasa lilipokuja suala la kusaka
kura. Anaeleza jinsi alivyolazimika kuwa ‘mwanasiasa’
kwa muda wote wa shindano! Alipita nyumba hadi
nyumba wilayani Nkasi, akibisha hodi, kujitambulisha
na kuomba kupigiwa kura “Nakumbuka namna
nilivyokuwa nikiwashawishi watu kwamba ushindi
huu usingekuwa wangu peke yangu, bali wa wana-
Nkasi wote na wilaya yetu na hata utaonyesha juhudi
zetu katika kilimo.”
Joseph, mwenye mke na watoto wanne,
anasema “Mke wangu hakuwa akiunga
mkono uamuzi wangu wa kushiriki Ruka
Juu na alikuwa na uhakika kwamba
sitoshinda. Alianza kubadili mawazo yake
alipoanza kuona alama zangu kwenye
TV wiki chache baadaye na baada ya
ushindi alinipigia simu kunifahamisha jinsi
alivyosherehekea pamoja na wananchi
wa Nkasi na walikuwa wakinisubiri kwa
hamu.”
19JULAI-AGOSTI 2013 Si Mchezo!
Juhudi binafsi ni muhimu.
Naweza kumsaidia mtu
yeyote atakayehitaji msaada
wangu na nimekuwa nikifanya
hivyo hata kabla ya Ruka Juu.
Mkulima ‘Mpya!’
“Nimejifunza mengi wakati wote wa shindano.
Nahitaji mbinu bora za kupata masoko, sitolima bila
kuwa na uhakika wa soko. Nitamtumia bibi shamba
na bwana shamba zaidi kuanzia sasa,” anasema.
Amejifunza umuhimu wa kuchukua mkopo benki,
“kuwa katika shindano si tu kwamba kumewawezesha
watu kuamini kwamba mimi ni mkulima mzuri,
bali pia ni mwaminifu. Meneja wa Benki ya NMB
alinipigia simu na kuniomba nionane naye mapema
iwezekanavyo kwa ajili ya mkopo.”
Hongera!
Joseph pamoja na washiriki wengine wote wa Ruka Juu; Aziza, Tatu, Mustafa, Yusta na Lawriani. Nyote mlifanya vizuri na kwa hakika mifano yenu imebadili mitazamo ya jamii juu ya kilimo.
20 Si Mchezo! JULAI-AGOSTI 2013
NGUVU ZA MWANAMUME
Ngono na mapenzi
Kumekuwa na mitazamo
mbalimbali katika jamii
ambapo inaonekana hakuna
mapenzi bila ngono. Hii
inatokana na watu kuwa na
mazoea kwamba urafiki kati
ya msichana na mvulana basi
kuna viashiria vya ngono.
Mapenzi yanaweza kujengeka
Unapomuona mtu kwa mara ya kwanza
Baada ya kupendezwa na tabia au muonekano
wa mhusika
Pia yanaweza kufifia pale unapogundua
upungufu wa mhusika
Ngono je?
na ya kiume (Japo kumekuwa na mwingiliano
wa tofauti na iliyozoeleka kunakohusisha
jinsia moja)
puchu
Msukumo unaotoka katika jamii hufanya wengi
kujiingiza katika ngono japo bado hawapo tayari
kimapenzi.
KumbukaMapenzi siyo lazima yahusishe ngono. Inawezekana pakawepo mapenzi ya dhati na yasihusishe ngono.
Mapenzi ni nini?
Mapenzi ni hisia ya upendo kwa mtu
fulani au kitu fulani. Mfano utasikia
mtu akisema, “Napenda sana mpira
wa miguu” tunapozungumzia
suala la mapenzi katika uhusiano
limegawanyika katika sehemu mbili
Mapenzi yanayohusisha hisia
za mwanamume kwenda kwa
mwanamke au mwanamke
kwenda kwa mwanamume
Mapenzi baina ya wazazi,
watoto, ndugu na marafiki.
Mapenzi ni hisia zenye msisimko wa
pendo la dhati zinazotoka moyoni
kwa mtu kwenda kwa mwingine
21JULAI-AGOSTI 2013 Si Mchezo!
NGUVU ZA MWANAMKE
Kweli, inawezekana!
Wape laivu
Kama upo katika mtandao
wa uhusiano na unataka
kuukatilia mbali, waambie
kuwa haupo tayari kuen-
delea katika uhusiano hayo
kwa sababu:
kwa dhati
kulinda afya yako na ya
mwenza wako
matumizi yasiyokuwa
na lazima
-
awishi uwe na wenzi
wengi ‘wapotezee’
Vuta picha, upo nyumbani umetulia na barafu wa moyo wako mkitaniana na kufurahi
pamoja. Simu yako ipo mezani lakini moyoni huna amani hata chembe. Kila mara mwenza
wako akitaka kuishika unatoa sababu zisizoeleweka, moyoni unajua kabisa kuwa simu yako ni
“weka mbali na mpenzi”.
KumbukaMawasiliano ndiyo msingi wa mapenzi, tengeneza mawasiliano mazuri na mwenza wako na kuvunja mtandao wa ngono.
Unaweza kuepuka hili
Mweleze mwenza wako kama ulishawahi kuwa na
uhusiano
Tumia muda mwingi na mpenzi wako baada ya shughuli
zako za kila siku
Tuma ujumbe mwingi wa kimahaba kwa simu
mnapokuwa mbali.
KUWA MUWAZI kwa mwenza wako, kama hakuridhishi
mweleze, muongeze ‘mautundu’
Kaa na mwenzi wako mpange kwa pamoja bajeti yenu ya
mapato na matumizi.
22 Si Mchezo! JULAI-AGOSTI 2013
Kona ya mtaa
Niaje mwana? Maisha ya mtaa yanasemaje? ‘Sista’
siyo kwamba nakupotezea! Nilikuwa namaliza
kusalimiana na mshkaji, halafu nije kwako, si unajua raha
ya mbio ni kumaliza! Mambo vipi? Joto la Dar linasemaje?
Umekwishaanza kuzoea mazingira au yanakuelemea? Poa
tulia basi nikupe mkanda wa jinsi picha linavyokwenda.
Tuliza boli
Usibabaike na kila unayemuona
ukamuamini, ukampa moyo wako na
mapenzi motomoto, utajikuta kaburini.
Hapa hapendwi mtu linapendwa
pochi! Kumbuka kupanga bajeti katika
mapato, matumizi na kutunza pesa.
Ukiendekeza washkaji na kula bata
utakuwa jalala la dhiki.
Kuna wazee ambao ni sukari za vijana,
chunga sana hawana maana zaidi ya
kutaka kuuchezea utu wako.
CHEZASALAMA
23JULAI-AGOSTI 2013 Si Mchezo!
Gogozembe aka kijiwe
Hapa ndiyo tunapokutana na kush-
irikishana stori zote za kitaa, kupeana
dili na michongo mbalimbali. Uki-
zubaa unaweza ukakuta jioni im-
eingia na huna kitu mfukoni wakati
mwenye kijiwe chake biashara inaen-
delea kama kawa na jioni anahesabu
‘mpunga’ wake . Inawezekana ikawa
ni saluni au kwa yule fundi viatu au
wa baiskeli pale kwenye mti wenye
kivuli murua.
Hapa hapa
dawa za kulevya wakakushawishi. Jiepushe nao.
yao wanakutafutia mabuzi. Watenge kabla
hawajakutenda.
kuiga tabia zao chafu. Kubali kuwa mshamba.
kama umekuja Dar kutafuta maisha au kufa.
Kumbuka
Kuna malengo ambayo umejiwekea wakati unakuja mjini kutafuta maisha, yazingatie hayo mengine yaache siyo yako.
24 Si Mchezo! JULAI-AGOSTI 2013
Mich
oro:
bab
atau
car
toon
s 201
3 Wenye nazo
wanavyokaba
hadi kuwaweka
wengine katika
mazingira hatarishi.
Ni Jukumu lako
kuchagua mbivu
na mbichi! Fuatilia
mchezo huu…
JIlinde...
KATUNI
26 Si Mchezo! JULAI-AGOSTI 2013
Haya yaliyomkuta binti huyu yanahitaji kufikiri na kuchukua uamuzi ambao haukudhuru wala kumdhuru mwingine. Tuombe ushauri tunapokutana na magumu yanayotushinda
27JULAI-AGOSTI 2013 Si Mchezo!
Jambo lililotokea katika katuni stori hii linatokea sana katika
maeneo mengi yenye huduma za kijamii kama vile nyumba
za kulala wageni. Kuna njia kadhaa za kukabiliana nalo kama
vile;
kinachokukabili
limevuka mipaka kama kulazimishwa kufanya kitu
usichokitaka
mwili wako
Toa taarifa kwa vyombo vya dola ili kumnasa huyo
anayejihusisha na kuwauza wasichana kwa wateja wake.
UKWELI WA MAMBO
Sema hapana, mlinde mwenzako…
Ni dhahiri kabisa kwamba
udhalilishaji wa wanawake
hapa Tanzania bado ni tatizo
kubwa. Sehemu nyingi hasa
zenye biashara ya pombe (bar),
matendo hayo huonekana hata
mchana kweupeee. Wadada
wanaohudumia wateja usiku
na mchana wameelezea kero
zao na kusema hawana jinsi.
Kumbuka
Mabadiliko chanya huanza na wewe! Ukisema hapana na kuonyesha mfano, wengi watakuiga na kuchukua hatua kisha kujikomboa huku tukitoa elimu kwa wale wachache wanaotumia madaraka yao kinyume na taratibu za ajira.
Usikubali kuburuzwa
Mwenye uamuzi wa kutumia
mwili wako vibaya au vizuri
ni wewe.
bosi kwani unahatarisha
maisha yako kwa kupata
mimba zisizotarajiwa
na magonjwa ya ngono
ikiwemo VVU
kwa kujiendeleza
katika kupata taarifa
sahihi na kupata ujuzi
utaokujengea uwezo
wa kusema hapana kwa
matendo kama hayo.
Jiamini.
28 Si Mchezo! JULAI-AGOSTI 2013
SEMA, TENDA
Mara nyingi, asilimia kubwa ya vijana wakikaa kijiweni, mbali
na stori zote, huishia kukandia baadhi ya mambo ambayo
yamekaa vibaya katika mtaa wao au karibu na eneo wanaloishi
wakisahau wao pia ni sehemu ya hilo tatizo kwa kuendelea
kuliruhusu liwepo katika jamii yao. Hii ni tofauti kwa ‘wana’
wa Tandale. Tandale Youth Centre wanapokutana, wanakuwa
na mtazamo chanya juu ya maendeleo ya kata yao ya Tandale.
Tusilalamike, tuchakarike!
Tandale Youth Centre ni nani?
Wao wanajitambulisha kama wanaharakati kutoka Kata
ya Tandale. “Harakati zetu zinahusisha vijana kutoka mitaa
sita. Vijana hawa ni wale wali o mashuleni na nje ya shule.
Wasichana kwa wavulana, alimradi tu wawe na ‘mzuka’ wa
kuleta maendeleo katika kata yetu” anaeleza Hassan Pukey
ambaye ni mratibu wa matukio katika kikundi hicho.
Uelimishaji rika
Vijana hawa wanatoa elimu katika maeneo makuu
mawili
Elimu ya afya
Utambuzi na tiba ya magonjwa ya ngono
Uzazi wa mpango
Kushawishi vijana kwenda kupima VVU kwa
hiyari.
Uraia
Wajibu na haki za msingi kwenye shule za msingi,
nyumba kwa nyumba, Camps za vijana, mata-
masha. Kwa wale ambao katikati ya wiki hawana
muda wa kupata elimu wamewatengea darasa lao
siku ya jumapili. Yote haya yanafanyika ndani ya
kata yao.
Malengo
Kuhusisha vijana kwa kuwa-
jengea uwezo wa kutambua
fursa za uchumi na kuzitumia
Kuhakikisha kila mwana
Tandale ana elimu ya afya ya
uzazi
Kutengeneza mtandao wa
vijana wa Tandale
Kutumia vipaji vya vijana
kama ajira.
Kupambana na maambukizi
mapya ya VVU
Kufungua Saccos ya vijana.
29JULAI-AGOSTI 2013 Si Mchezo!
Mafanikio
jamii
Tandale katika shughuli mbal-
imbali.
Changamoto zinazowakabili
vipeperushi n.k
kikamilifu katika shughuli mbalimbali za kijamii
kutokana na changamoto za kimaisha
30 Si Mchezo! JULAI-AGOSTI 2013
Betty Liduke ni rafiki mkubwa
wa vijana, hata wewe unaweza
kulonga naye. Ni msambazaji
mkubwa wa Jarida la Si
Mchezo! Mkoani Njombe. Ni
mshauri nasaha na ni Mratibu
wa Kitengo cha Udhibiti
Ukimwi katika Kampuni ya
TANWAT, Njombe.
Mwandikie kupitia
Jarida la Si Mchezo!
Si Mchezo!
S. L. P. 2065
Dar es Salaam
SMs; Andika SM acha nafasi, andika maoni yako kisha tuma kwenda namba 15665
na utuambie kama ungependa
uchapishwe.
USHAURI
Swali
Dada yangu inabidi umwambie mume
wako asiogope kumwambia kaka yake
juu ya uwepo wake na jinsi anavyowa-
bana. Kama haitawezekana waite wazazi
wa pande zote mbili ili kutatua tatizo
hilo lakini dada usiache
ndoa yako
Geradi G.Nyamoga,
Dar es salaam.
Unatakiwa ujadiliane na mumeo ili
muone jinsi gani mtatatua hilo tatizo.
Kama itashindikana mtafute mshenga
wenu ili awaeleze wazee.
Usichukue uamuzi wa ha-
sira na usiwe na haraka.
Farida M.Membe,
Dar es salaam.
Mpe shemeji yako mwongozo wa
ndoa jinsi unavyotaka kwa kum-
shirikisha na mumeo. Mweleze
utaratibu wa ndoa, hali yenu ya
maisha na jinsi mnavyoshindwa
kuifurahia ndoa yenu. Arudi
nyumbani au aangalie utaratibu
mwingine wakati akitafuta kazi.
Maulid
Mziwanda,
Dar es salaam.
Mimi nina shida, naomba ushauri kwa wenzangu. Mimi ni msichana wa miaka 30, nimeolewa.
Nampenda na namheshimu mume wangu. Tatizo ni kaka yake. Amekuja mjini mwaka mmoja
uliopita kutafuta kazi na hadi leo anasema hajapata. Tunaishi kwenye chumba kimoja na sebule na tunaishi naye
kwa mwaka mzima sasa. Kusema kweli nimechoka. Nahitaji kufurahia ndoa yangu. Anatubana na nakosa uhuru na
faragha. Mume wangu naona anashindwa kumwambia kaka yake aondoke japo anajua sifurahii tena uwepo wake.
Nimeamua nifungashe vilivyo vyangu niondoke au yeye aondoke. Tafadhali naomba ushauri
Msomaji wa Si Mchezo!
Dada vumilia usiondoke kwani
ukiondoka shemeji yako na ndugu
wa mwanamume watajisikia vibaya.
Mshauri mumeo aendelee kumtafu-
tia kaka yake kazi ili aweze kujitege-
mea. Hiyo ni moja ya changamoto za
maisha ya ndoa.
Zawadi Khamis,
Dar es salaam.
Mimi nina mke na mtoto mmoja ambaye nilizaa na mwanamke mwingine ni-
kiwa Ifakara. Nikimshauri mke wangu kwamba nikamchukue mtoto Ifakara ha-
taki, anasema nikienda sitarudi. Nifanyeje ili nimpate mwanangu?
Baba .K. Mmulunga
Newala
Nakupongeza kwa kuuliza swali zuri. Kuishi ni kujifunza na kuwa
kwenye ndoa kunahitaji kuvumilia na kushirikishana katika kila
jambo, kufunga mizigo kuondoka siyo suluhu. Kaa jadiliana na
mumeo pamoja na huyo kaka wa mume wako mwelezeni hali
halisi mliyonayo na baada ya hapo chukueni uamuzi ulio sahihi
utakaojenga nyumba yenu.
SWALI LA TOLEO LIJALO