Haliuzwi - The Compass...kwetu sote kujua ni jinsi gani kila mmoja alivyoanza maisha ya mtaani na...
Transcript of Haliuzwi - The Compass...kwetu sote kujua ni jinsi gani kila mmoja alivyoanza maisha ya mtaani na...
2 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
Si Mchezo! Huzalishwa na kusambazwa.
Si Mchezo! husambazwa.
Lilikozalishwa toleo hili.
Changamkia jembe kwa sababu kilimo ni fedha! Kifanye kuwa shughuli yako rasmi ufaidike na kilimo.
Kilimo kina thamani na kinaweza kuwa sekta yenye faida kubwa kwa sababu watu wanahitaji kula, soko la bidhaa za kilimo linakuwepo kila wakati hususani mazao cha ya chakula.
Ramani ya Tanzania
3
TAHARIRIHeri ya Mwaka Mpya wapenzi wasomaji wetu. Mwaka huu tumetuliza vichwa na kubadilisha vitu vingi kwenye jarida lengo likiwa kukuletea vitu adimu kivingine. Yote haya yametokana pia na mawazo yenu mnayotutumia. Toleo hili tumezungumzia masuala ya kilimo. Bila shaka kila mmoja anajua kuwa kilimo ndiyo uti wa mgongo wa Mtanzania. Tufunguke katika kilimo! Karibu. Majuka
YALIYOMO4 Stori Yangu: Kilimo kinalipa
6 Mambo Mapya
8 Hadithi ya Picha: Ujanja shambani!
12 Je, Wajua: Maofisa ugani ndiyo nguzo ya kilimo
14 Sauti yangu
16 Burudani: Moro All Stars
18 Ruka Juu: Ruka juu na jembe
20 Nguvu za mwanaume
21 Nguvu za mwanamke
22 Chezasalama: Jipange, usije ukavuna mabua!...
24 Katuni: Chakarika jembe likutoe
27 Ukweli wa mambo: Kilimo ni tumaini la wengi
28 Sema Tenda: Kilimobiashara ni zaidi ya ujuavyo
30 Marie Stopes: Waelimisharika Zanzibar, walia na utoaji mimba
31 Ushauri
Mhariri Majuka Ololkeri
WaandishiRaphael NyoniRebeca Gyumi
WashauriTimu ya Femina HIP Betty Liduke
Mkurugenzi MtendajiDr. Minou Fuglesang
Mkurugenzi wa Habari Amabilis Batamula
Meneja MachapishoJiang Alipo
Meneja UhusianoLilian Nsemwa
Katuni na UsanifuBabaTau, Inc.
Mpiga Chapa Jamana Printers Ltd
Usambazaji EAM Logistic LtdFemina HIP na Washirika
Si Mchezo! limefanyika kwa hisani kubwa ya Serikali za Sweden (Sida), Denmark (DANIDA), na mashirika ya HIVOS, RFSU, Marie Stopes, Mama Misitu, TWAWEZA na JHU-CCP/TCCP.
Yaliyomo humu ndani ni jukumu la Femina HIP na hayawakilishi maoni au mitazamo ya wafadhili.
Wasiliana nasi kwa:S.L.P. 2065, Dar es SalaamSimu: (22) 212 8265, 2126851/2 Fax: (22) 2110842email: [email protected] Mchezo! huchapishwa na Femina HIP.Sms: Andika SM acha nafasi andika maoni yako kisha tuma kwenda 15665
...Peta maishani
Kijana jitume shambani...Ruka Juu kijanja
4 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
Mtanange wa kusaka maisha nilianza siku nyingi na niliyoyapitia ni mengi lakini
nataka nizungumzie machache tu kati ya hayo. Najua vijana wengi tumepitia magumu kama yangu na ni haki ya kila mmoja kuwa huru kutoa historia yake. Nimeamua kufunguka ili kuwaelimisha wengine juu ya umuhimu wa kubadili uamuzi pale ‘unapobugi step’.
Naitwa Nesho Festo Madepana (25), mzaliwa wa Kijiji cha Zombo, Kilosa. Nilimaliza elimu ya msingi mwaka 2002 hapa Zombo na sikufaulu kuendelea na elimu ya sekondari. ingawa nilikuwa na nia ya kujiendeleza kielimu. Nilijishughulisha na vibarua mbalimbali nikiwa na lengo la kuwa na pesa ya kianzio kwani wazazi wangu hawakuwa na uwezo wa kunisomesha. Nilipata pesa kiasi ambazo nilitumia kufuatilia kujiunga VETA Mikumi ambapo baba alikubali kunilipia ada. Nilikubaliwa chuoni hapo nikaanza masomo ya ufundi magari mwaka 2003. Baada ya miezi kadhaa nilifukuzwa chuo kwani baba hakuweza kulipa ada na sikuwa na uwezo wa kujilipia. Hapo ndipo nikaanza kuonja ‘joto ya jiwe’ katika maisha.
Nilikaa Mikumi kwa kipindi fulani nikisoma ‘ramani’ ya jinsi gani naweza kuendelea. Nilijiunga na Kikundi cha Sanaa cha Wanyonge Family kama mwanamuziki nikawa natunga na kuimba nyimbo. Hatukufanikiwa kiviile kwani hatukuwa na mtaji. Mwaka 2004 nikarudi nyumbani, safari hii nikamuomba baba shamba la kulima na akanipatia hekari moja. Nilianza kulima mahindi peke yake, nilipovuna mara ya kwanza nilipata magunia 12 kwa hekari
moja. Niliuza yote nikapata 230,000/- nikiwa na lengo la kwenda Bongo kufungua biashara ya kuuza chipsi. Nilitua Jijini mwaka 2005 nikaweka kambi Tabata. Nilijaribu zali la chipsi pale Mwenge lakini niligonga mwamba baada ya kupiga mahesabu na kugundua kuwa gharama za kufungua banda
Kilimo kinalipa
Mambo yote shambani: Nesho akiwa na mkewe wakionyesha mazao yao.
STORI YANGU
5JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo!
la kuuzia chipsi ni 180,000/- na pesa nitakazobaki nazo hazitanitosha kujikimu Jijini. Nilipoona hivyo nilibadilisha mawazo na kwenda Kariakoo, nikanunua belo la suruali kadhaa za ‘jeans’ kwa ajili ya biashara, nikanunulia na mbegu za matikiti maji, nikaamua kurudi nyumbani.
Niliporudi nyumbani mwaka 2006 niliwakuta wenzangu ambao tulimaliza wote elimu ya msingi waliotulia wakaamua kuwa wakulima wamepiga
hatua kimaendeleo. Waliniumiza akili sana. Niliuza zile jeans na pesa hiyo nikafungua banda la kuuza chipsi hapa Zombo huku nikiendelea na kilimo.
Mwanzoni tulishirikiana na baba kulima pilipili kwa ajili ya biashara. Nilikuwa nikizipeleka Bongo tatizo likawa soko duni. Hatukuwahi kupata faida kwani bei zilikuwa ndogo sana. Biashara ya chipsi haikuendelea kwani nilishindwa kuendesha zote kwa pamoja. Niliamua kulima nyanya maji, huku nikijishughulisha na vibarua ili niweze kupata pesa za kununua dawa ya kuua wadudu shambani. Nilipovuna, nikabahatisha msimu mzuri wa biashara nikauza plastiki moja kwa bei ya 4000/- nikapata 280,000/-. Nikaanza kujitegemea mwaka 2007. Nilinunua shamba la hekari tatu. Baadaye nikaweza kununua pampu ya kumwagilia. Mpaka sasa nimegundua siri iliyopo kwenye kilimo kuwa kinalipa! Imenifanya niwe na matumaini ya maendeleo hapo baadaye. Mbali na kilimo hicho pia nafuga nguruwe watatu sasa.
Wengine wana fikra potofu kuwa kilimo hakina tija lakini nimekuwa mmoja wa wale wanaoombwa buku kitaani! Hivyo kijana jipange na anza upya sasa. Nina mengi ya kuwashauri vijana. Unapojaribu kitu ukagundua kuwa hakina tija, usione ujinga kuanza upya! Tuepukane na makundi rika yanayotupotosha.
Nimeoa, mimi na mke wangu tunapendana, tunaheshimiana, tunalindana na tunasaidiana kazi.Najipanga ili niweze kujenga nyumba ya kuishi na pia kujiendeleza kielimu ili kuongeza ufanisi kwenye kilimo.
Maisha ni kupeta kwa Nesho na mkewe, baada ya kujikita kwenye kilimo.
6 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
MAMBO MAPYA
Majengo yanakaa bure haya!
Hivi Tanzania tutaendelea kutegemea misaada mpaka lini? Yaani inatia uchungu kuona haya majengo ya Ilonga Youth Centre yamekaa tu bila ya hata ya kutumika kwa kukosa fedha na hata yakitumika basi ni kwa kipindi kifupi cha mafunzo ya wiki mbili tu! Majengo haya pamoja na mand-hari yake yanafaa yakatumika kwa kuwa chuo cha elimu ya juu kuanzia ngazi ya stashahada ya kilimo kama tu wizara husika itaamua kufanya kweli.
Boda boda
Waendesha pikipiki wa mikoani wanasifika kwa kuzingatia sheria za barabarani, lakini huyu braza wa Gairo yeye sijui vipi? Lori linaovateki na jamaa nae akaona ‘apige mande,. Haraka izin-gatie usalama na sheria za barabarani. Wakati unawahi ishu zako, kumbuka na majukumu yako kwa watu wanao-kutegemea katika jamii.
Uchumi Flower
Wajumbe walikaa na kuunda kikundi cha Uchumi Flower mwaka 2009 chenye makao yake makuu kijiji cha Mhenda, Kilosa. Jamaa wamejipanga ile mbaya kujikwamua kwa kutumia mashamba ya wanachama kulima alizeti. Penye nia pana njia, wamepa-ta mkopo wa mashine ya kukamua alizeti kutoka halmashauri ya wilaya. Unajua nini? Imesaidia sana wanaki-jiji kupunguza gharama za kwenda kukamua alizeti na wao wanajiingizia kipato kutokana na kilimo.
7JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo!
Young Farmers in Business
RUKA jUU
Kuanzia Machi 2013,Femina itakuletea Ruka Juu TV showUsicheze mbali na luninga yako
ITV kila Jumamosi saa 1 usiku
TBC1 Kila Jumapili saa 3 usiku
Funguka shambani peta maishani na Fema Radio. RFA kila Jumatatu saa 2.45 usikuTBC FM kila Jumanne saa 3 usiku
8 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
azikiwe na wanija ni marafiki tangu wanasoma.wanashirikishana mambo mengi, japo wanasikilizana na wakati mwingine kutofautiana. Wamemaliza kidato cha nne na sasa wameanza maisha ambayo ni funzo kwetu sote kujua ni jinsi gani kila mmoja alivyoanza maisha ya mtaani na sasa anafanya nini. Tufuatilie mchezo huu na tujielimishe
haya sasa, azikiwe na wanija
wamemaliza masomo na matokeo ya
mtihani yameshatoka na
wamefeli.Changamoto iko mbele yao juu ya maisha ya baadae, hebu
tuwafuatilie kuona nini
kitajiri kwaohaya sasa, kila
mmoja yuko bize na maisha yake. kuna
aliyepanda kwenye starehe na
aliyepanda kwenye kilimo, tuone watavuna nini?
unaonaje tukianzisha bustani ya
mbogamboga ili tujipatie kipato?
aku bibi eeh! ya nini
kujizeesha na juma ananihudumia kila
kitu?
unauhakika nae? shauri yako! baadae usije lia
wakati mwenzio nachekelea mavuno!
shoga mbona hivyo! subiri majibu yatoke ndio
tutajua
baada ya matokeo ya mtihani
hata kama nimepata division four. Siwezi nikashika
jembe
kwani jembe litakataa?
sasa kulima ndio
kufeli maisha?kulima ndio
mpango mzima, utaona!
…baba hekari moja tu inatosha kwa
kuanzia.
sawa mwanangu,
usihofu umeshapata hilo
basi eti azikiwe alinishauri
tulime, mi nkakataa .
he, yule sio shoga yako?
mbona na jembe jioni yote hii?
achana naye, kafulia yule
wanija akionywa na wazazi
hivi kwa nini umekuwa mazururaji,
siku nne sasa hujaonekana hapa
nyumbani
bora useme wewe
azikiwe akiwa na bwana shamba
mtaalamu msaidie mwanangu awe mkulima wa
kisasa
akizingatia haya, atavuna
vizuri
panda mbegu kwenye
mstari kwa kuzipa nafasi ili zistawi
vizuri
ameukataa huu ujauzito, sijui
nifanyaje
baada ya miezi kadhaa
jikaze hivyo hivyo
mpaka ujifungue mwaya
kufeli mtihani sio
kufeli maisha
ungezeeka, shauri yako
kilimo ni suluhu ya ajira kwa
vijana
duh! kumbe bora nimestuka
mapema
9JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo!
azikiwe na wanija ni marafiki tangu wanasoma.wanashirikishana mambo mengi, japo wanasikilizana na wakati mwingine kutofautiana. Wamemaliza kidato cha nne na sasa wameanza maisha ambayo ni funzo kwetu sote kujua ni jinsi gani kila mmoja alivyoanza maisha ya mtaani na sasa anafanya nini. Tufuatilie mchezo huu na tujielimishe
haya sasa, azikiwe na wanija
wamemaliza masomo na matokeo ya
mtihani yameshatoka na
wamefeli.Changamoto iko mbele yao juu ya maisha ya baadae, hebu
tuwafuatilie kuona nini
kitajiri kwaohaya sasa, kila
mmoja yuko bize na maisha yake. kuna
aliyepanda kwenye starehe na
aliyepanda kwenye kilimo, tuone watavuna nini?
unaonaje tukianzisha bustani ya
mbogamboga ili tujipatie kipato?
aku bibi eeh! ya nini
kujizeesha na juma ananihudumia kila
kitu?
unauhakika nae? shauri yako! baadae usije lia
wakati mwenzio nachekelea mavuno!
shoga mbona hivyo! subiri majibu yatoke ndio
tutajua
baada ya matokeo ya mtihani
hata kama nimepata division four. Siwezi nikashika
jembe
kwani jembe litakataa?
sasa kulima ndio
kufeli maisha?kulima ndio
mpango mzima, utaona!
…baba hekari moja tu inatosha kwa
kuanzia.
sawa mwanangu,
usihofu umeshapata hilo
basi eti azikiwe alinishauri
tulime, mi nkakataa .
he, yule sio shoga yako?
mbona na jembe jioni yote hii?
achana naye, kafulia yule
wanija akionywa na wazazi
hivi kwa nini umekuwa mazururaji,
siku nne sasa hujaonekana hapa
nyumbani
bora useme wewe
azikiwe akiwa na bwana shamba
mtaalamu msaidie mwanangu awe mkulima wa
kisasa
akizingatia haya, atavuna
vizuri
panda mbegu kwenye
mstari kwa kuzipa nafasi ili zistawi
vizuri
ameukataa huu ujauzito, sijui
nifanyaje
baada ya miezi kadhaa
jikaze hivyo hivyo
mpaka ujifungue mwaya
kufeli mtihani sio
kufeli maisha
ungezeeka, shauri yako
kilimo ni suluhu ya ajira kwa
vijana
duh! kumbe bora nimestuka
mapema
10 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
baada ya miezi kadhaa : kila mmoja amevuna alichokipanda
azikiwe akimshukuru bwana shamba
asante sana maana
ushauri wako umenisaidia kuongeza mavuno
acha tu, kwa kuwa sasa ni wapenzi, wewe
chukua tu
nimeshasema mimi na wewe sasa bhaaaas!
baada ya kipindi flani
mmh! hivi nitaishi
maisha haya mpaka lini?
Kilimo kinalipa,ingia shambani tu!
dah! sijui kwa
nini sikuanza mapema
Haya nikiuza
yatanisaidia sana
nimeshajenga,na sasa naenda
kusomea kilimo
usikate tamaa, kwa kilimo unaweza kumudu familia na kujisomesha pia.
miaka miwili baadae
huku mambo shwari, na mimi nataka kuja kusoma
huko
maisha yananamchapa
wanija,. anaamua kujirahisisha kwa
wanaume ili aweze kumhudumia
mwanae, je hili ndio suluhisho? hebu tujionee
baada ya misukosuko mingi ya kimaisha, wanija ameamua kutafakari upya maisha yake,Je
atabadilika? hebu tuendelee na stori
Karibuni wageni,
wanijaaa,kuna wageni
karibuni, waoo, na
zawadi kabisa asante, hongera jamani
mazao yako tayari,
tuma gari lije kubeba
asante sana
naomba unisamehe
mpenzi
…watoto baba zao wamewakataa, maisha yamekuwa magumu sana
kwangu
herí yako, mi na
hawa watoto siwezi tena
sawa nitajitahidi
haya,mambo ya kilimo hayo. Wanija
amebadilika na sasa ni mkulima mzuri
kabisa.huu ni mfano mzuri
vijana wengi wanaona
kama kilimo hakilipi. ila ukweli ni kwamba
Ukizingatia njia za kilimo
cha kisasa unatoka
jitahidi na kilimo uje, elimu
ndio mpango mzima
ushauri wa wataalamu wa
kilimo ni muhimu
kuuzingatia
baada ya miezi 3
fumanizi!!!
11JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo!
baada ya miezi kadhaa : kila mmoja amevuna alichokipanda
azikiwe akimshukuru bwana shamba
asante sana maana
ushauri wako umenisaidia kuongeza mavuno
acha tu, kwa kuwa sasa ni wapenzi, wewe
chukua tu
nimeshasema mimi na wewe sasa bhaaaas!
baada ya kipindi flani
mmh! hivi nitaishi
maisha haya mpaka lini?
Kilimo kinalipa,ingia shambani tu!
dah! sijui kwa
nini sikuanza mapema
Haya nikiuza
yatanisaidia sana
nimeshajenga,na sasa naenda
kusomea kilimo
usikate tamaa, kwa kilimo unaweza kumudu familia na kujisomesha pia.
miaka miwili baadae
huku mambo shwari, na mimi nataka kuja kusoma
huko
maisha yananamchapa
wanija,. anaamua kujirahisisha kwa
wanaume ili aweze kumhudumia
mwanae, je hili ndio suluhisho? hebu tujionee
baada ya misukosuko mingi ya kimaisha, wanija ameamua kutafakari upya maisha yake,Je
atabadilika? hebu tuendelee na stori
Karibuni wageni,
wanijaaa,kuna wageni
karibuni, waoo, na
zawadi kabisa asante, hongera jamani
mazao yako tayari,
tuma gari lije kubeba
asante sana
naomba unisamehe
mpenzi
…watoto baba zao wamewakataa, maisha yamekuwa magumu sana
kwangu
herí yako, mi na
hawa watoto siwezi tena
sawa nitajitahidi
haya,mambo ya kilimo hayo. Wanija
amebadilika na sasa ni mkulima mzuri
kabisa.huu ni mfano mzuri
vijana wengi wanaona
kama kilimo hakilipi. ila ukweli ni kwamba
Ukizingatia njia za kilimo
cha kisasa unatoka
jitahidi na kilimo uje, elimu
ndio mpango mzima
ushauri wa wataalamu wa
kilimo ni muhimu
kuuzingatia
baada ya miezi 3
fumanizi!!!
12 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
JE, WAJUA?
Maofisa ugani ndio nguzo ya kilimo vijijini
Katika mchezo huu tumeona jinsi Azikiwe alivyopiga hatua
kwa kujikita katika kilimo. Wanija ‘alibugi step’ alivyokuwa akivinjari kwenye uhusiano, baadaye alijutia uamuzi wake. Kuna mengi tunaweza kujifunza katika mchezo huu lakini ningependa tujadili kidogo kuhusu umuhimu wa maofisa ugani ambao ndiyo waliompiga tafu kubwa Azikiwe katika mafanikio yake.
Hawa ndiyo wanaweza kuwa maafisa ugani...
Maofisa ugani wapo katika sekta nyingi. Wanaweza kuwa;• Washauriwamisitu• WashauriwaUkimwikwenyejamii• Washauriwakilimo• Maofisamifugokwenyejamii• Maofisaafyakatikajamii• Wakungawajadi Lakini katika stori hii, tunazungumzia wale wanao-
husika na kilimo tu.
Shughuli zao hizi hapa;
Pamoja na kwamba maofisa ugani wana shughuli nyingi kwenye jamii, hizi ni baadhi tu;• Kutoahabarinakuenezateknolojiakatikajamii• Kuunganishajamiinamasoko,jamiinyinginenawatoahuduma• Kuhamasishajamiikujifunzamambombalimbali• Kuwezeshauundwajiwavikundi• Kutoamafunzokatikajamiinakufuatilia• Kutoaufafanuzikwakutumiamashambayaowenyewe
Jamii ina nafasi kubwa katika kuchagua ofisa ugani
Yapo mambo mengi ambayo jamii inataki-wa kushiriki katika mchakato wa kumcha-gua ofisa ugani. Haya ni machache tu;• Jamiiiwemstariwambelekushiriki
kwenye uteuzi, ufuatiliaji na tathmini ya shughuli za maofisa ugani ili ku-hakikisha ubora wa utoaji huduma.
• Muhimukujuamipakayahudumazinazotakiwa kutolewa na maofisa ugani.
• Jamiiitoemotishakwamaofisaugani kwa kutoa ushirikiano mzuri ili wafurahie kazi zao.
Maofisa ugani ni nani?
Ofisa ugani ni mshiriki mkuu, anayeishi na kupata riziki kwenye jamii, lakini si lazima awe mzaliwa wa eneo hilo. Anatakiwa awe anapatikana na anaelewa uwezo, udhaifu na matarajio ya jamii hiyo kwa kutumia utaalamu alioupata na kuwa wakala wa kilimo. Awe anafahamu lugha, awe na uelewa halisi wa utamaduni, kanuni, mila na desturi za jamii hiyo. Awe na uwezo wa kuhamasisha kushawishi au kuwavutia wengine kutumia njia sahihi za kilimo kwa kuwafundisha, kuwatembelea na kuwaonyesha katika mchakato wa kufanya kazi zao za kilimo.
Swali;Je unawajua maofisa ugani wa eneo lako? Wanaku-saidiaje? Jadili na wenzako na utuambie kwa kutuma ujumbe mfupi; andika SM acha nafasi, andikia maoni yako kisha tuma kwenda namba 15665
14 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
Wewe pia unaweza kulonga na vijana wenzako. Tuandike maoni, ushauri,
vichekesho,maswali nk, weka anuani yako na tuma ukiambatanisha
na picha yako kwa Mhariri, Jarida la Si Mchezo!,
S.L.P 2065 Dar es [email protected] tumbukiza katika boksi
la Si Mchezo! kama lipo katika eneo unaloishi.
SAUTI YANGU Kama una chochote unachotaka kusema tuandikie ili upate fursa ya kuwaelimisha wengine
Maoni yaliyotolewa katika ukurasa huu ni ya wasomaji, si lazima yalingane na msimamo wa Femina.
Si Mchezo!Femina HIPSLP 2065,
DSM
Migongano ya wafugaji na wakulima itakwisha lini?
Serikali itusaidie kutatua suala la uhaba wa maji kwenye wilaya yetu ya Kilosa kwani hali hii inatusaba-bishia kutokuelewana baina ya sisi wafugaji na wakulima pindi tuna-potumia chanzo cha maji pamoja. Endapo kitatengenezwa chanzo kingine cha maji kwa ajili ya mifugo, itaepusha migongano na tutaishi kwa amani na upendo. Dani Zakayo MumbiKimamba, Kilosa
Wadada mnaojiuza badilikeniTabia ya wadada wengine kujiingiza katika biashara ya ngono si jambo jema na linapingana na maadili ya Kitanzania. Mnatoa tham-ani ya utu wenu na kujid-halilisha kijinsia na kuwa watumwa. Mara nyingi wakihojiwa wanasingizia ugumu wa maisha lakini pesa wanayoipata haibadili-shi mfumo wa maisha yao, bali huishia kununua mavazi na mapambo ili kuwavutia wateja wao.Elizabeth J. MollelKilosa
Jembe ndiyo mpango mzima!
Vijana wenzangu tutumie sana ardhi aliyotu-patia Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kilimo ili kitusaidie kwa maisha yetu ya kila siku na siyo kukimbilia mjini bila kuwa na mipango. Serikali iwafuatilie mawakala wa mbegu na dawa ili wa-tusambazie bidhaa zenye ubora pia ikumbuke kuwa vijana ni Taifa la leo na si la kesho.Francis Denis MtawatawaKilosa
Mabosi wengine ni kero!
Kuna mabosi wengine ni wasum-bufu sana hasa ukifika wakati wa kutoa posho au mishahara ya wafanyakazi wao. Mara ukatwe mshahara na kutafutiwa sababu zisizo na msingi ili mradi tu asikupe posho yako yote. Wakati mwingine anakuja na vitisho na kutaka ufanye naye ngono ndio akupe mshahara wako. Hii ni kero hasa kwa vijana wa kike walio-ajiriwa na wanaume. Eda Joseph IbarajaKilosa
15JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo!
Miaka 20, anaishi Buguruni Madenge, DSMTunu Ramadhani
“Niliamua kuja kliniki ili kujua maendeleo ya ujauzito wangu, kupima damu na kujua kama nimeambukizwa VVU. Ningegundulika kuwa nina maambukizi ya VVU, ingekuwa rahisi kumlinda mtoto asipate maambukizi hasa wakati wa kujifungua. Nimepata ushauri mzuri sana kutoka kwa watoa huduma, na nina amani sana baada ya kujua sijaambukizwa VVU” “Hii ni mimba yangu ya kwanza. Nilimweleza mume wangu baada ya kugundua, yeye akamwomba dada yake anisindikize kituo cha afya kwa ajili ya kupima. Imekuwa ni vigumu yeye [mume wangu] kunisindikiza kutokana na majukumu ya kazi kwani inabidi awe dukani na hakuna mtu wa kumsaidia na hawezi kufunga duka”
“Ushauri wangu kwa akina mama ni kwamba waende kliniki. Huduma ni nzuri, unapata kujua maendeleo ya afya zao. Pia nimefahamu damu yangu ni kundi gani, na nimeanza kujiandaa kwa kuwa nimefahamu tarehe ya kujifungua”
Ana ujauzito wa miezi mitano. Ameolewa na Ramadhani Shabani ambae ana miaka 30
Miaka 30, anaishi Buguruni, DSMHalima Salim
“Ni muhimu kwenda kliniki mara baada ya kugundua u-mjamzito. Nilikwenda kupata matibabu ili kukilinda kiumbe kilichopo tumboni. Nilipimwa Virusi vya Ukimwi, magonjwa ya zinaa pamoja na kupewa dawa za malaria na za kuongeza kiwango cha damu kwa kuwa nilikuwa na upungufu”
“Ushauri wangu kwa akina mama wajawazito na wale wanaopanga kuwa na watoto, waende kliniki kujua afya zao. Hii itawapa fursa kujua kama wana maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na kupewa ushauri wa namna ya kumlinda mtoto asipate maambukizi”
“Mume wangu alikuwa wa kwanza kumtaarifu kwamba nina ujauzito. Alifurahi sana ukizingatia kwamba tumekaa muda mrefu bila kupata mtoto mwingine. Alizipokea habari hizi kwa mtazamo chanya”
“Sababu ya mimi kuja kliniki ni kutaka kujua maendeleo ya ujauzito wangu na kufahamu mtoto anavyokua, wingi wa damu, kupima Virusi vya Ukimwi. Baada ya kupatiwa huduma huwa napatiwa kadi ndogo yenye tarehe ya kurudi”
“Mtu wa kwanza kumwambia nina ujauzito alikuwa mume wangu kwa sababu ndiye mtu wa karibu sana kwangu na mtu muhimu katika maisha yangu. Mume wangu ndiye mhusika mkubwa wa mimba hii. Lakini nakwenda kliniki peke yangu. Hajawahi kunisindikiza kutokana na kazi yake, mara nyingi huwa anakuwa safarini”
“Nawashauri akina mama wajawazito waende kliniki wapime afya na umri wa mimba zao. Pia wataweza kujikinga na maambukizi ya magonjwa kwa kupata kinga sahihi na ushauri toka kwa watoa huduma”
Ana ujauzito wa miezi mitano. Ana mtoto wa kike Amina mwenye miaka sita, ameolewa na Hamis Said mwenye miaka 30
Ana ujauzito wa miezi tisa. Ana mtoto Kiume Arafat mwenye miaka mitatu, Salama na mumewe Said Kassim wanaishi Buguruni, Dar es Salaam
Pich
a zo
te n
a Ze
char
iah
Mla
cha
SaumuAbiud Miaka 19, anaishi Buguruni,
DSM
ThuwebaAbbasMiaka 27, anaishi Buguruni Kisiwani, DSM
“Niliamua kuja kliniki kujua kama mtoto aliye tumboni ni mzima, kupima damu pamoja na virusi vya ukimwi, kupewa dawa za malaria na vidonge vya kuongeza damu”
“Nilimwambia mume wangu, siku ya kwanza alinileta hapa hospital kufanya vipimo”
“Wanawake wajawazito waje kliniki kupata chanjo ili kuwakinga watoto kutokupata magonjwa, kujua afya zao kama hawana maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na kujua siku zao za kujifungua”
“Nilikuja kliniki kupata huduma za afya na kutaka kujua mwanangu anaendeleaje, pia kupimwa damu na kujua umri wa mimba”
“Kwa kuwa nilikuja mara ya kwanza kliniki na wifi yangu, alikuwa wa kwanza kujua nina ujauzito baada ya kupimwa. Niilipofika nyumbani nilimwambia mume wangu”
“Akina mama waje kliniki kwa sababu ni hatari. Unaweza kujifungua bila kujua siku yako ila ukija hospitali unajua mambo yote”
Wazazi Nipende Advert
Miaka 22, anaishi Buguruni, DSMySalma Ally
Ana ujauzito wa miezi sita
Ana ujauzito wa miezi nane na mtoto wa kike aitwaye Nahia mwenye miaka mitatu. ameolewa na Bw. Hassan Rashid mwenye miaka 30.
Tuma SMS neno “mtoto” BURE kwenda 15001 kwa taarifa zaidi
16 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
BURUDANI
Na na na na na na na naa na na na na naaa M-O-R-OOoh, moro town yeah! Home sweet home x2 (uuh)
Ubeti wa kwanza - StaminaChunga usipitilize stendi suka acha watu msamvu,Moro imenipa mengi, washkaji pesa na shavu, hatuna mpango na bahari, Mbona hata mindu ina fukwe,Milima kwetu fahari, mwaka mzima kwetu full kipupwe,Ausindile anoga ndio swagga za waluguru, hata ufunge kwa kuroga ila Moro itaniacha huru,sihitaji tena Baga utamu naupata Gairo,Masai wote huu wana swagga karibu kama upo Njiro,
Toka enzi za Mbaraka mpaka wa-jukuu wa Mwinshehe,Mkude kusimama Pastor, Mbokeleni kuwa sheikh,Nina haki ya kujisifu, Moro imenipa kitalu,Namwaga Pombe kwa Chifu wa Moro Babu Kingalu,Sina bifu na Mngoni, Mpogoro ndio napodeka,Anzisha tifu ulingoni usande tukupe Cheka,Mliotutoka kimwili kiroho tupo pamoja,Karibu Moro mswahili uzalendo uende kwa hoja, (uuuuuh hu huuu)
KiitikioKaribu Morogoro, watu wote wa bara, visiwani mpaka Zanzibar,Bahari sio kasoro, wageni karibuni
hapa kwetu mtapata furaha, x2Urithi burudani vyote shwariiiiii, ka-ribu mji kasoro,Udzungwa ujionee ehee hee hee hee hee heee he mwenyewe,Usisubiri usimuliweee, mwenyeweee (Yoo) Njooow
Ubeti wa pili – O - tenYeah! mji unaweza poa, niko rock juu mlimani, Na mimi ndio mkuu wa mkoa kar-ibuni madizini,Matonya alifukuzwa Dar breki ya kwanza akaja shaini,Mandela alikuwa shujaa, moro akaifanya maskani,Si unajua? Miji kibao haipati mvua,tofauti kubwa hapa kwetu inanyesha mpaka inaua,Mzinga, Ndigutu, Kichangani, Kiguru nyembe, hapa kwetu haina uzembe,Hata star anashika jembe, Natokea matombo kilosa narudi mzumbe,Nampitia Mkude, makala yuko wapi Msinde,Moro Bambam ila vichwa visivimbe, narudi shamba hata muziki nisiimbe,No, mi na moro tupo kama pacha, yes karibu moro tuishi kama kacha,Mbuga zipo na hata madini yapo, palipo na amani ndo mi nilipo
KiitikioUbeti wa tatu- Afande Sele Morogoro,mjini kwetu,Karibuni wote rafiki na ndugu zetu(shua)Toka pande zote iwe ndani, mpaka nje ya nchi yetu,Karibuni kwetu mtembeee, harakati zetu mjionee,Kama mimi na mtu chee, kuna mashamba tunalimaga,Mboga mboga na mipunga, kuna mahindi, kuna matunda, viazi miwa na karanga,
Wimbo: Moro All StarsWasanii: Afande Selle, Stamina, O – Ten,Belle 9,Samir, Chriss Wamaria, Nassa, Dynna na Zilla
17JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo!
Karibuni nyote Morogoro mchote, hekima za Selemani mtangaze mataifa yote,Mkawaambie, mlichokiona hapa, mkawasimulie siri ya cheka kuwa chapa,Na habari kibao za wakali wa hapa-hapa, kwa soka kwa hip hop, ma streika marapa,Maboxer, madensa wote waliotoka hapa, wahapahapa, tangu kitambo kile,Kabla ya Afande Sele, Kabla ya O ten na Belle, kabla ya Supa Ngedere Moro Bado Chapa IlaleNgoma inogile, tuna historia tele, hata Mwalimu Nyerere alikuwaga mbunge wa kwanza wa Moro miaka ile,kwa wasiotambua hilo. Karibuni Moro, hata tommorowkaribuni mjionee maajabu ya mzimu wa Kolelo, Ifakara Kilombero,Turiani, Mvomero, Kilosa na Msowero, Masombo mpaka GairoYeaaah hii ndio Morogoro mpaka Nyachiro kwa mjomba KobeloNa Mahenge kwa shangazi wa kipo-goro, twende mahewaa
Kiitikio
Kibwagizo Morogoro mji kasoro bahari kwetu bado shwariMorogoro, Mgeta Mzumbe Mlali Moro imetuleaNilipokula gimbi na kachumbari, mwenzenu mimi naona fahariHata ninapokwenda mbali nitarudi moro nyumbaniNimelelewa angali bado kichanga, bado mimi sijajua kuimbaMpaka sasa mimi natamba, tena Moro nimepata Mchumba mie x2Nitazikwa Moro, Nitakufa Moro, Naipenda Moro, nitaishi Moro
Wimbo: Moro All StarsWasanii: Afande Selle, Stamina, O – Ten,Belle 9,Samir, Chriss Wamaria, Nassa, Dynna na Zilla
J!!! !
Muulize mama’ko...Baba flani mlevi alirudi nyumbani mwake jioni akamkuta mwanawe anafanya ‘homework’.Mtoto akamuuliza babake, “Baba Indian ocean iko wapi?”Baba akajibu “Muulize mamako sababu ye ndio anapenda kusafi-sha nyumba saa zote,hata mimi viatu vyangu sivioni!”
Nakusaidia hata nikiwa gerezaniMzee mmoja alimtumia mjukuu wake aliyefungwa gerezani barua, na ilisomeka hivi:-
“Mjukuu wangu mpendwa nina huzuni sana mwaka huu sitoweza kulima viazi kwenye shamba kwa sababu wewe uko gerezani na sina uwezo wa kulima shamba lote peke yangu”.Mjukuu alipopata barua akajibu hivi:-“Babu usijaribu hata kidogo kulima hilo shamba...zile pesa zote nilizoiba nilizificha kwenye hilo shamba”.Mapolisi wa gereza walipoona ile barua kesho yake wakaenda kwe-nye shamba la mzee wakalilima lote wakitafuta pesa.Baada ya wiki mjukuu akamuan-dikia babu yake barua nyingine:-“Unaweza kupanda viazi vyako sasa babu...unaona jinsi ninavy-oweza kukusaidia hata nikiwa huku gerezani?
Nafata chenji yangu!Basi lilipata ajali katika daraja lika-zama kwenye mto...watu wakaanza kuogelea kujitoa nje.Jamaa mmoja akajitahidi kujitoa. Alipofika nje ya mto ghafla akavua nguo na kujitupa tena kwenye mto.Rafiki yake alipomuona akashangaa akamuuliza,”JUMA unaenda wapi?”JUMA,”Nataka kumtafuta konda...hajanirudishia chenji yangu!”
J
J
18 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
RUKA JUU
Ruka Juu na jembe!Unakumbuka shindano la ujasiriamali la Ruka Juu, kwenye luninga mwaka 2010? Habari ya mjini ndio hii, Ruka Juu imerudi tenaaa… na sasa ni kuhusu vijana wanaofanya kilimo kama biashara. Kipindi kipya cha radio pia kitazinduliwa kikilenga kuelimisha kwenye masuala haya haya ya kilimo.
Kilimo ni uti wa mgongo:
Unafahamu kuwa 85% ya Watanzania wanaishi kwa kutegemea ardhi? Muda umefika wote tuweke msisitizo kwenye kilimo na kukifanya kiwe na faida.
Kilimo ni utajiri:
Kila mtu ni lazima ale ili aishi, hakuna kazi nyingine yenye umuhimu kuliko kilimo. Soko la kilimo haliishi, kuna kipato kwenye kilimo. Lima kwa usahihi na ubora.
Kilimo ni maisha:
Chakula kinajenga miili yetu, kinatupa nguvu. Kwa kutumia chakula tunakua, tunakidhi njaa zetu, tunaponya magonjwa mbalimbali. Tupo tulivyo kwa sababu ya chakula.
19JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo!
Msimu mpya
Msimu mpya utakaoanza kurushwa Machi, 2013, umejaa mambo kibao ya kijanja, tumezunguka sehemu mbalimbali Tanzania na kukutana na vijana wakulima ambao wako tayari kukushirikisha mbinu za kutoka na kilimo.
Amabilis Batamula, mtangazaji wako wa msimu uliopita amerudi tena akiwa na Bwana Ishi anayetaka kuingia kwenye kilimo. Bila kumsahau Bahati, atawabahatisha wote watakaowasiliana nasi kupitia Wasiliana na Bahati Ubahatike.
Kwenye redio utakutana na vijana wenzako; Michael Baruti na Rebeca Gyumi wakiwa tayari kukuelimisha kuhusu masuala mbalimbali ya kilimo. Hii si ya kukosa.
JK u m b u k a
Kilimo siyo ushamba, kilimo ni ajira na kinaweza badili maisha yako.
Kilimo Bomba!
Unaweza kuita kilimo bomba au Kilimo Kwanza, kama kampeni inayoendeshwa na serikali. Tuungane wote na kukipa kilimo kipaumbele. Tulishe kizazi kijacho, tujenge maisha yetu.
Ardhi kubwa yenye rutuba:
Nchi yetu imebarikiwa ardhi yenye fursa kibao za kuendeleza kilimo. Wakulima wajanja wanaofahamu nini cha kupanda wanaweza kubadilisha ardhi hii kuwa pesa.
20 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
NGUVU ZA MWANAMUME
Pwani kuna msemo unaosema “Ushalipiwa weye”ambao watu wengi wakiambiwa, hung’aka na kuwa wakali kama vile wamekula pilipili mbuzi. Ndiyo. Hata wewe unapopewa ofa zisizoeleweka na watu
unaowafahamu au usiowafahamu. Kuwa makini. Chunga sana hizo ofa, wengi huwa wanakuja kudai vyao na kutaka vyako pia.
Imeshalipiwa hiyo, unaitaka?
Kupenda ofa husababisha:
• Kuwamtumwawangono,hasa pale unapolazimishwa kulipa vitu ambavyo ulipewa kama ofa na huna uwezo wa kuvilipa, hii inakuweka katika mazingira hatarishi.
• Vijanawengikudhanikuwazali la mentali litawadon-dokea na kufanikiwa kimaisha bila ya kufanya kazi na ku-wajibika kikamilifu na ma-tokeo yake ni kukosa ubunifu wa kukabiliana na changa-moto za maisha na ‘fainali’ ni uzeeni.
• Kutokuwanamisimamothabiti juu ya maisha yako.
• Kujiingizakatikatabiahatari-shi.
Jihadhari
• Kamamtuusiyemfa-hamu anakupa ofa, kabla ya kukubali muulize kwanza ana lengo gani hadi anatoa ofa kwako.
• Nimuhimukutafakarimahusiano uliyonayo na huyo mtu anayekupa ofa
J K u m b u k a
Ofa zinatengeneza mazingira ya kukosa utashi na ufinyu wa maamuzi. Tafakari kabla ya kutenda.
Vijana wengi wa kiume hudhani kuwa ofa kwao ni “zali la mentali” na ni akina dada peke yao ndiyo wanaohongwa na hizo ofa huwatokea puani hao kina dada, Hapana! Hata wewe kidume unaweza kukumbwa na madhara yale yale ambayo yanaweza kuwakumba akina dada ukiangukiwa na hilo zali la ofa, mentali.
21JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo!
NGUVU ZA MWANAMKE
Huzuni kubwa imetanda. Ni vilio huku na kule, wakubwa kwa watoto, wote wanalia. “Mama Wawili umetutoka, Mama Wawili” wanasikika wanawake wakilia.Mama Wawili, mwanamke mcheshi, mama wa watoto wawili amefariki wakati akijifungua mtoto wa tatu. Mtoto pia amefariki. Mama na mtoto kufariki wakati wa uzazi si mara ya kwanza kutokea katika kijiji hicho; na wala si jambo jipya nchini kwetu, lakini si jambo la kuvumilia.
Wazazi nipendeni!
J K u m b u k a
Maandalizi ni kitu muhimu kwenye kila kitu. Kwa mama mjamzito, maandalizi ya uzazi salama yanaanza kwa kuhudhuria kliniki mapema.
Ni wajibu wetu sote
Pamoja na juhudi za serikali kuimarisha huduma za afya kwa wajawazito, mafanikio bado ni kidogo. Kina mama na watoto wengi wanaendelea kufa kutokana na matatizo wakati wa ujauzito na kujifungua!Ila serikali haiwezi kufanya juhudi za kupambana na tatizo hilo peke yake. Ni wajibu wa kila mmoja wetu, kama taifa zima, jamii, familia, baba wa mtoto na mama mjamzito pia.
Tufanyeje?
Hakuna anayependa kifo, hasa pale uhai mpya unapotazamiwa kuchipua. Wazazi na jamii nzima mpendeni huyo mtoto kabla na baada ya kuzaliwa.
Kliniki kwanza
Mjamzito anatakiwa kuhudhuria kliniki katika wiki 16 (miezi minne) za kwanza za ujauzito. Pia mjamzito anatakiwa ahudhurie kliniki angalau mara nne katika kipindi chote cha ujauzito.
Mahudhurio ya kliniki kwa wakati unaofaaa yatamuweka mjamzito pamoja na mtoto wake katika nafasi bora zaidi ya uzazi salama.
Wazazi Nipendeni ni nini?
Kampeni ya “Wazazi Nipendeni” ina lengo la kutekeleza kampeni ya kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi Afrika, kwa kuwawezesha wajawazito na wenza wao kuchukua hatua muhimu kwa afya ya mama mjamzito na uzazi salama.
Kuhudhuria kliniki mape-ma ndiyo usalama wako!
Kwa mjamzito ni muhimu kutambua mapema kwamba u-mjamzito. Hii itakusaidia kujiwekea mikakati ya jinsi ya kutunza mimba yako na maandalizi ya kuhakikisha kwamba unajifungua salama.
22 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
CHEZASALAMA
Jipange, usije ukavuna mabua!...Baada ya kuisha kwa msimu wa mavuno, wakulima hupata muda wa kufanya tathmini na kupumzika kwa ajili ya kujiandaa na msimu mwingine wa kilimo. Kipindi hiki mara nyingi hutawaliwa na chereko chereko kwani mazao yanakuwa yameshauzwa na watu wameshavuta mkwanja wao na kuusunda kibindoni. Kinachofuata…
Ushauri wa bure
Ukilima na kuvuna, pesa inayopatikana ni bora ikaongezewa katika mtaji wa kilimo kwa kununua mbegu na pembejeo nyingine za kilimo. Kumbuka kuwa msimu wa kilimo ni mrefu zaidi kuliko msimu wa mavuno. Ni vyema basi ukajiandaa mapema kwa msimu unaofuata badala ya kujisahau na kujirusha kwa sana.
Msimu wa sherehe
Hapa ndio utasikia ‘vishughuli’ kila nyumba;
• kumtoamwali,• ngoma,• ndoa/harusi• Safarizakwendamjini
kusalimia nduguNa siyo kwamba huwa zinafanyika hivihivi tu, bali wengine hutafuta hata sababu ili mradi tu wafanye sherehe.
Hatari ipo jirani!
Utumiaji wa vileo kama vile pombe huongezeka sawa sawa na idadi ya wapenzi, ukizingatia pesa ipo. Kipindi hiki ndio utasikia, Tumia pesa ikuzoee, jenga heshima baa! Vipi lakini jembe, umeshajiandaa kwa kilimo katika msimu unaofuata? Una uhakika msimu unaokuja utakuwa wa neema kama huu ulioisha? Jihadhari kabla ya hatari!
23JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo!
Jipange, usije ukavuna mabua!...
JK u m b u k aKuna mabadiliko ya hali ya hewa, mabadiliko ya bei ya mazao sokoni, mabadiliko ya bei za zana za kilimo na magonjwa ya mazao. Jipange kwa msimu ujao!
Muhimu kuzingatia
Baada ya kuuza mazao na kudaka huo mkwanja, tuliza ubongo na kujiongeza kifikra namna ya kujiletea maendeleo. Fikiria kuhusu biashara nyingine ambazo zinalipa msimu wa mavuno ili kujazia kwenye kilimo. Achana na mawazo potofu ya ushawishi kutoka kwa marafiki wanaokutaka mkapige ‘tungi’ au kushinda kijiweni kutwa nzima bila kuwa na shughuli ya kufanya.Msimu wa kilimo ni mfupi lakini ni mrefu kama hautakuwa makini upande wa matumizi ya fedha, Usije ukashtuka wakati jua ndio linaanza kuchwa, pasua kichwa.
24 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
Mich
oro:
bab
atau
car
toon
s 201
3
chakarika na jembe likutoe!Kijana Chema anatafuta jinsi ya kutoka kimaisha na washkaji.
Ametoka kijijini kwenda mjini kucheza mdundo wa muziki wa mjini. Ni muziki gani huo? Je, atatoka? Fuatilia...
BAADA KUSHINDWA MUZIKI WA MJINI
25JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo!
CHAMA AKIKOMAA NA MTEJA
BALAA!
KILIMO KIMEJIBU, CHEMA ANASAFIRISHA MAZAO KWENDA
KUUZA MJINI
26 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
Umeonaeee? Michongo ya maisha si lazima kuifukuzia mjini, hata kijijini ipo. Umemwona Chema? Wengine tulibugi kama Chema, tuko mjini tunasota, kila kukicha afadhali ya jana! Umeshafikiria kuhusu kilimo? Tafakari!
ANAKUTANA NA WASHKAJI, BADO WANAHANGAIKA NA MDUNDO WA MUZIKI WA MJINI
27JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo!
UKWELI WA MAMBO
Kilimo ni tumaini la wengi
Wengi wetu tumekuwa tukiimba nyimbo lakini hatuujui tunachezaje, kwa kuwa hata mdundo wake hiyo inatupiga chenga. Kwa kawaida kila wimbo una uchezaji wake na
hivyo kama wimbo utabadilishwa ghafla basi ni wazi kuwa hata uchezaji utabadilika.Vijana wanakimbilia mjini wakidai kuwa eti kilimo hakilipi wakidhani mjini ndiko maisha bora yaliko.
J K u m b u k aWapo vijana ambao wameweza kunufaika kupitia kilimo na sasa wanaendesha maisha yao vizuri. Usikubali kuachwa nyuma, kilimo ndio mdundo wa uhakika!
Tudadisi haya yanayotokea
• Vijanakukimbiliamjinikumefanyakilimokudumaana kusababisha wakulima wengi na wengine ambao maisha yao yanategemea kilimo wakaanza kubadili-sha wimbo
• Wakatikilimokinadumaakutokananavijanawenyenguvu kukimbilia mjini mambo yakabadilika na kutokea kwa nyimbo mbili tofauti. Ukaanza ule wimbo wa ukitaka maisha mazuri yapo mjini
• Hukomjininakovijanawalikimbiliakaziyakuuzanguo yaani umachinga, ulinzi n.k baadaye wakaji-kuta wakilazimika kuimba wimbo mmoja na askari wa jiji yaani Jeshi la Mgambo.
• Sasawimbohuuwamgambosiwakawaidakwaniuliwafanya baadhi ya vijana kuukumbuka ule wa shambani ambao ulikuwa rahisi hata kuucheza.
Twende sawa basi;
• Vijanatukiachananavuruguza mgambo wa jiji na kurudi mashambani tutakuwa na wimbo mmoja, tutacheza pamoja na kitaeleweka.
• Tuanzekubadilikatu-changamkie kilimo cha um-wagiliaji na kuacha kutegemea mvua za msimu
• Tukopepesakwenyeasasimbalimbali ili tuwekeze katika kilimo.
28 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
SEMA. TENDA!
Mengi yanasemwa kuhusu kujihusisha na kilimo. Wengine wanakandia kilimo na saa nyingine wana sababu ambazo zinaweza zikakushawishi
kukubaliana nao. Tulitia timu Kilosa na tukachonga na vijana kuhusiana na kilimo, soko lake, namna ya kujiendeleza katika kilimo na kadhalika.
Kilimobiashara ni zaidi ya ujuavyo
Changamoto zinazo wakabili wakulima ni hizi
• Wakulimawengiwanalimabilakuwanamalengo• Hakunamfumowataarifazamasokokuwawezeshawakulimakujua
watauza wapi• Elimundogojuuyajinsiyakuongezathamanimazaowanayolima
kama vile usindikaji• Hakunautunzajimzuriwamazao• Kutojuaumuhimunafaidazakujihusishakwenyevikundinataasisiza
kifedha kama vile SACCOS na VICOBA• Kutokuwanauwezowakupangabeiyamazao• Miundombinudunihasayabarabaranamawasilianombovu• Ukosefuwavyombovyausafirishajikutokamaeneoyauzalishaji• Kutojuanamnayakutumiasimuzamikononikibiasharakatikakupata
taarifa• Uborawamazaokupunguapaleyanapofikasokoni
Mbegu mbalimbali za mahindi
Moja ya pembejeo za kilimo ambao ni mbolea ya chumvi chumvi kwenye moja duka la pembejeo za kilimo, katika Kijiji cha Msalabani, Kilosa
29JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo!
Nini kifanyike?
• Sektazinazohusikazitoeelimuyakilimobiashara ili wakulima wanufaike na kilimo
• Kuwenamsukumowamatumiziyateknolojia sahihi za kilimo kama vile kilimo cha umwagiliaji, mbegu sahihi kulingana na udongo na hali ya hewa ya eneo lako.
• Wakulimawajifunzenamnayakutafutamasoko na biashara juu ya kilimo stahiki kinacholenga hitaji la soko na walaji
• Kuwaunganishawakulimakwenyemasokokwa kutumia teknolojia na mawasiliano mfano vipindi vya redio na simu za mkon-oni
• Kufanyetafitizakuendelezakilimobiasha-ra
• Miundombinuyabarabara,vyombovyausafiri n.k iboreshwe
• Elimuyausindikajiitolewekwawakulima• Sualalakilimobiasharalipewekipaumbele
katika ngazi zote ili wakulima waweze kuingia katika soko la ushindani
• Hudumazapembejeozakilimozisogeezaidi vijijini na ziwalenge wakulima
SwaliJe, ni changamoto zipi wanazokutana nazo wakulima wa eneo lako? Unadhani nini kifanyike kutatua changamoto hizo? Tuambie kwa kutumia mawasiliano hapa chini:Barua pepe: [email protected]: andika SM acha nafasi, andikia mao-ni yako kisha tuma kwenda namba 15665S.L.P. 2065, Dar es Salaam.
Matokeo yake ni nini?
• Vijanawengihukatatamaaku-jishughulisha na kilimo kwa madai kwamba hakilipi
• Wakulimahukatatamaakuende-leza kilimo hata kuuza mashamba
• Vijanakukimbiliamijinibilakuwana malengo
• Wengihulimakwaajiliyachakulatu
Kikundi cha Jitegemee wakiwa mbele ya duka la mmoja wa wanakikundi hicho. Hawa wanajihusisha na kilimo biashara
30 Si Mchezo! JANUARI-FEBRUARI 2013
MARIE STOPES
Suala la utoaji mimba kwa njia zisizo salama, limekuwa likipigiwa kelele kila mara hapa Tanzania. Vijana waelimishaji rika huko Zanzibar wamefunguka na kuwaomba wazazi, viongozi wa dini na Serikali kuwasaidia kupambana na vifo vitokanavyo na utoaji mimba usio salama.
Waelimishaji rika Zanzibar, walia na utoaji mimba
Maandalizi ya mafanikio ya baadaye ya kijana, huanza akiwa mdogo. Sote tuwalinde vijana ili tuwe na Taifa lenye vijana wanaofaidi matunda ya malezi ya wakubwa wao.
Kwa huduma za kuokoa maisha kwa walioharibikiwa mimba fika kituo cha Marie Stopes Tanzania kilichopo Kilimani Mnara wa Mbao au kliniki yoyote ya serikali. Kwa mawasiliano piga 0767160038 au tuma ujumbe au kwa njia ya baruapepe [email protected]
Vijana hao wametoa ushauri huu...
• Wazazikuwakaribunavijanailiku-wafundisha kuhusu afya ya uzazi kwa kuwaruhusu kupata elimu hiyo kwenye vituo vya afya ya uzazi.
• Serikalinaviongoziwadinimbalimbaliwalihimizwa kuweka sera itakayomlin-da kijana hasa wa kike kupata huduma bora hasa baada ya mimba kuharibika ili wasipoteze maisha. Jamii pia ielim-ishwe juu ya matumizi ya njia za uzazi wa mpango.
Kuna madhara ukijihusisha na uhusiano wa kimapenzi kwenye umri mdogo
• Kupatamimbakatikaumrimdogo• Kujiingizakatikamazingirahatari-
shi ya kutoa mimba kwa njia zisizo salama.
• Kujishushiaheshimambeleyajamiiyako
• Kujiongezeamajukumukatikaumrimdogo
Muelimisharika akizungumza na wazazi kuhusu madhara ya utoaji mimba.
JK u m b u k a
Kuna usiri mkubwa
“Vijana wengi hushirikiana kutoa mimba kwa kutumia miti shamba,” alisema mmoja wa waelimishaji rika. Akaongeza, “vitendo hivi hufanyika kwa kificho sana ili wazazi na jamii kwa ujumla isijue. Hii hupelekea hatari ya vifo pale watoaji wanapozidiwa.” Walizungumzia pia kuhusu mila na desturi za jamii yao kuwa zinamzuia kijana kuanza mapenzi kabla ya ndoa, kwa hiyo vijana hutoa mimba mafichoni na kwa usiri ili kuepuka aibu na adhabu.
31JANUARI-FEBRUARI 2013 Si Mchezo!
Betty Liduke ni rafiki mkubwa wa vijana, hata wewe unaweza kulonga naye. Ni msambazaji mkubwa wa Jarida la Si Mchezo! Mkoani Njombe. Ni mshauri nasaha na ni Mratibu wa Kitengo cha Udhibiti Ukimwi katika Kampuni ya TANWAT, Njombe.Mwandikie kupitia Jarida la Si Mchezo!Si Mchezo! S. L. P. 2065 Dar es SalaamSMS; andika SM acha nafasi andika ujumbe wako kisha tuma kwenda namba 15665 na utuambie kama ungependa uchapishwe.
USHAURI
Swali
Ningependa kukwambia uondoe mawazo kwake na amini kuwa yupo mvulana mwenye mapenzi ya kweli, na muaminifu na huyo ndiye atakayekufaa. Vumilia tu utampata.Mwanahamisi RajabuKilosa
Kama unaishi naye sehemu moja ondoka ili kumsahau kirahisi. Jishughulishe na kazi na siyo mapenzi. Ukisema ukae nae bado itakusumbua kwani bado utakuwa kama mke mwenza na utaumia zaidi.Steven F. Mbwiss
Kilosa
Mimi ni msichana wa miaka 24. Nilibahatika kumpata mvulana ambaye tulianza uhusiano. Katika uhusiano wetu sikuwa na haraka ya kutambulishwa kwani nilijua
kila kitu kinakwenda na wakati. Mpenzi wangu aliniambia anakaa na mama yake na dada yake na mimi nilimweleza kuwa naishi na mama. Baada ya miaka miwili pamoja ndipo nilipogundua kuwa mpenzi wangu ameoa na ana mtoto mmoja. Mama alinishauri niachane naye lakini nampenda sana huyo kijana na sidhani kama kuna mwanamume atakayechukua nafasi yake. Naomba ushauri.Msomaji wa Si mchezo, Mburu-Manyara.
Tafuta muda ukae naye, muulize kama yupo tayari kuendelea na mwanamke ali-yezaa naye au kuwa na wewe na akupe sababu za msingi kwa nini amemchagua aliyem-chagua, ndipo ufanye maamuzi. Abdulrazaaq NgowoKilosa
Nina miaka 21, nina rafikiwa kike ambaye tumejuana kwa muda wa mwaka mmoja hadi sasa. Nampenda ila naogopa kumueleza kwani nitavunja urafiki wetu. Pia kuna mwa-namke anayenipenda sana ila mie simpendi na yupo jirani sana na mimi kuliko yule nimpendae ambaye ni rafiki yangu, vijana wenzangu naomba mnishauri nifanye nini katika suala hili?
Hantish JozackNjombe.
Nashukuru kwa swali. Ukweli ni kwamba mtu anayekupenda kwa dhati hawezi kukudanganya huyaweka mambo yake wazi ili muweze kuya- jadili pamoja. Ingawa unampenda sana jiulize; ‘kwa mfano mimi ningekuwa mke wa huyu bwana nitakaposikia habari hizi nitajisikiaje?’ Pia kumbuka kwamba mahusiano na watu wengi, kama anavyofanya huyo mwanaume huchangia sana katika kueneza magonjwa ya zinaa pamoja na VVU. Tafakari kabla ya kuchukua hatua hata kama unampenda.Asante.
Huyo hana mapenzi ya kweli kwako, mpe nafasi mwingine, utampata anayekupenda. Umeshajifun-za, kwa huyo mwingine utakuwa makini zaidi.Pili GeorgeKilosa
SWALI LA TOLEO LIJALO