Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu...

32
ISSN: 0856-8995 Maisha ya kijani Haliuzwi KATUNI:

Transcript of Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu...

Page 1: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

ISSN

: 0

85

6-8

995

Maishaya kijani

Haliuzwi

KATUNI:

Page 2: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

2 Si Mchezo! SEPTEMBA-OKTOBA 2012

Si Mchezo! Huzalishwa na kusambazwa.

Si Mchezo! husambazwa.

Lilikozalishwa toleo hili.

Yapo madhara mengi yanayosababishwa na ukataji miti bila utaratibu kama kukauka kwa vyanzo vya maji, kuleta ukame, kukosa hewa safi, n.k. Chukua hatua kukataa ukataji miti hovyo.

Misitu ni urithi mzuri tunayotakiwa kuilinda ili itulinde. Kila mmoja wetu ana jukumu la kulinda kwa faida yetu na vizazi vijavyo.

Page 3: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

3

TAHARIRIMwaka ndiyo huoooo umesepa na mishemishe bado zinaendelea. Mbali na hayo, lazima niwatakie heri ya Krismasi na Mwaka mpya wasomaji wetu popote pale mlipo. Safari hii hatukucheza mbali na Bongo kwani ni mashariki kidogo tu mwa Tanzania, yaani Pwani ndiko tulitia kambi kusikiliza kilio cha misitu! Nani anaweza kudai kwamba hakuwahi kutumia mti au mazao yatokanayo na mti? Pata stori humu ndani

Majuka

YALIYOMO4 Stori Yangu: Maisha ya kijani

6 Mambo Mapya

8 Mambo ya Fedha: Tuyavune kwa njia salama

9 Nguvu ya Mwanamume: Puchu kwa faragha!

10 Hadithi ya Picha: Wizi mtupu

14 Je, Wajua: Kataa katakata kukatakata miti

16 Tulichovuna: Mabalozi wa mazingira Rufiji hawa

18 Chezasalama: Jiulize tuko wangapi?

20 Burudani: Kabwela na Stamina ft Mavocal

22 Pasipo na Daktari: Msaada unapoumwa na nyuki

23 Huduma: Wafahamu MJUMINGU

24 Katuni: KICHAPO!

27 Ukweli wa Mambo: Kilio cha miti

30 SEMA, TENDA!: Misitu yetu, uhai wetu

31 Ushauri

Mhariri Majuka Ololkeri

WaandishiBetty LidukeRaphael NyoniRebeca Gyumi

WashauriTimu ya Femina HIP

Mkurugenzi MtendajiDr. Minou Fuglesang

Mkurugenzi wa Habari Amabilis Batamula

Meneja MachapishoJiang Alipo

Meneja MahusianoLilian Nsemwa

Katuni na UsanifuBabaTau, Inc.

Mpiga Chapa Jamana Printers Ltd

Usambazaji EAM Logistic LtdFemina HIP na Washirika

Si Mchezo! limefanyika kwa hisani kubwa ya Serikali za Sweden (Sida), Denmark (DANIDA), HIVOS, RFSU, Twaweza na JHU-CCP/TCCP.

Toleo hili limefanyika kwa kushirikiana na Serikali ya Finland na Norway kupitia Kampeni ya Mama Misitu.

Yaliyomo humu ndani ni jukumu la Femina HIP na hayawakilishi maoni au mitazamo ya wafadhili.

Wasiliana nasi kwa:S.L.P. 2065, Dar es SalaamSimu: (22) 212 8265, 2126851/2 Fax: (22) 2110842email: [email protected]

Si Mchezo! huchapishwa na Femina HIP.Sms: 0715 568222

Hiyo ngalawa mpande wenyewe, bora nitembee kuzunguka

Maji kwenye Mto Rufiji yamepungua kwa kiasi kikubwa hata kusimami-sha kivuko kutovusha abiria

Umbali kutoka hapa hadi Ikwiriri si chini ya kilo-meta 65 tofauti na hapa kilometa 20

Page 4: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

4 Si Mchezo! NOVEMBA-DESEMBA 2012

STORI YANGU

Tangu wakati nasoma nilikuwa navutiwa na mambo ya utunzaji wa mazingira.

Wilaya yetu imejaaliwa uoto mzuri wa asili, lakini changamoto ni uharibifu mkubwa wa mazingira unaoendelea kwa miaka mingi. Hivyo, kutokana na azma yangu ya utunzaji wa mazingira, nilitafakari ni kitu gani nitakifanya kusaidia jamii yangu ambayo ndiyo waathirika wakubwa wa uharibifu huo wa mazingira.

Naitwa Ally Mussa Mkumbege (23), mtoto wa kwanza katika familia yetu. Nimezaliwa katika Kijiji cha Mloka, Rufiji. Nilipata elimu ya sekondari katika Shule ya Ruaruke mwaka 2007, baadaye nilihamishiwa Shule ya Sekondari Zimbini, zote za Rufiji ndipo nikahitimu mwaka 2010.

Wakati nasoma kuna wataalamu mbalimbali ambao walikuwa wakitutembelea shuleni kutoa elimu kuhusu mazingira, VVU na Ukimwi n.k. Hizi zote zilinijenga katika makuzi lakini nilifurahia zaidi elimu ya mazingira ambayo Kikundi cha Mazingira cha Rufiji (REG) walitupa.

Utakubaliana na mimi kuwa suala la uharibifu wa mazingira limekithiri katika maeneo mengi Tanzania hasa katika Wilaya yetu ya Rufiji ambayo imezungukwa na misitu mizuri ya asili. Mara nyingi tunaona malori makubwa yakisafirisha magogo yaliyovunwa hapa kwetu. Mengine ni halali na mengine yanapitishwa mlango wa ‘uwani’! Ndiyo si tunaona!? Sipendi kuona miti inakatwa na kuisha kwani nimejifunza madhara yake kama vile vyanzo vya maji kukauka, mfano mto wetu Rufiji ambao tunategemea kwa mambo mengi kukauka, kukosa hewa safi,

Nahamasisha maisha ya kijani

Ally Musa (kulia) akiwa na mkewe Bi Sharfa Said na mtoto wao Rahma Ally.

Page 5: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

5NOVEMBA-DESEMBA 2012 Si Mchezo!

Nahamasisha maisha ya kijani

kukosa matunda, kusababisha kipindi cha kiangazi kuongezeka.

Si hayo tu yaliyonigusa kunifanya kuwajibika kimazingira, bali nimeona nionyeshe mfano kwa vijana wenzangu kuwa wanaotakiwa kuchukua hatua ya kulinda mazingira ni sisi wenyewe hasa vijana ambao ndiyo huenda kuwinda na kuchoma moto ili kuwatimua wanyama na kupata kitoweo.

Nilipomaliza kidato cha nne, sikufanikiwa kuendelea na masomo kwani sikufaulu mtihani. Sikukata tamaa, niliona ndiyo fursa ya kuwatafuta REG ili wanielimishe juu ya utunzaji wa mazingira. Walinipokea vizuri na kuona ujio wangu ni wa

kipekee kwani nimekuwa kijana mwenye umri mdogo kujiunga na kikundi hicho. Nilifurahishwa na shughuli zao na ilinisaidia kujifunza mengi kama vile kupanda aina mbalimbali za miti asili na ya kisasa na kutambua umuhimu wa utunzaji mazingira. Mpaka sasa ni miaka miwili tangu nijiunge na wanamazingira hawa. Ni kijana pekee kwenye kundi na napiga kazi kwa bidii hadi najulikana kama ‘jembe’ la mazingira.

Kutokana na elimu ya VVU na Ukimwi ambayo niliipata nikiwa shuleni, niliamua kuoa baada ya kumaliza shule na tumebahatika kumpata mtoto mmoja. Tumepima pamoja na tuko kamili gado. Nampenda mke wangu na tunaishi kwa uaminifu.

Ally akiwa kwenye shamba lao la miti huko Kibiti, Rufiji. Ally akijaza mifuko ya mbolea ili kupandikiza miche

Page 6: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

6 Si Mchezo! NOVEMBA-DESEMBA 2012

MAMBO MAPYA

Mbinu za maharamia wa misitu zapanguliwaKatika hali isiyo ya kawaida, tuliibukia Kijiji cha Muyuyu na kukaribishwa na magogo kibao yakiwa yamepangwa kana kwamba yanasubiri mnunuzi. Tulipoonana na Afisa Mtendaji wa Kijiji alitusimulia kisa cha magogo hayo. Mmoja wa wanakijiji aliyakuta magogo hayo 637 yakiwa yameshakatwa kwenye Msitu wa Hifadhi ya Ngumburuni tayari kwa kusafirishwa. Mwananchi hakukaa kimya, aliripoti ofisi ya Serikali ya Kijiji. Mkakati wa kuwakamata maharamia hao ulipangwa lakini haukufanikiwa labda wakishtukia ‘ishu’. Wananchi wayasafirisha magogo hayo kwenda kijijini na kuyalinda yakisubiri utaratibu mwingine wa kisheria. Kwa sasa, vijiji saba ambavyo vizunguuka msitu huo vimejipanga kulinda msitu huo ikiwa ni pamoja na kuweka uzio kwenye barabara zinazotoka.Timu ya Si Mchezo inawapongeza sana wanakijiji hao kwa kazi nzuri.

Mazingira yalivyochomwa moto

Kivuko cha Utete kikionekana kusi-mamisha shughuli zake za kuvusha huko Utete kutokana na Mto Ru-fiji kupungua kina cha maji kwa kiasi kikubwa. Hali hiyo inasababishwa na kuongezeka kwa kipindi cha kiangazi sababu ikiwa ni uharibifu wa misitu.

Page 7: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

7NOVEMBA-DESEMBA 2012 Si Mchezo!

Hawa wanapaswa kuigwa…Tulipotembelea Rufiji tulipata fursa ya kutembelea vijiji kibao tukajionea utajiri uliyoifunika Wilaya hiyo ambao umepewa mgongo na binadamu. Ni wachache wanaofahamu kuwa Mkoa wa Pwani ambayo Rufiji ndiyo moja ya Wilaya zake ni moja ya maeneo yenye maajabu duniani. Si hayo tu, pia imejaaliwa na rutuba kubwa ambayo huzalishwa chakula kwa wingi kama vile mpunga, nazi, mboga za majani, korosho, mahindi, nanasi na matunda mengine kibao. Wanafanya nini?

Pamoja na kwamba wanapata fursa ya kupigwa tafu na mashirika kama vile vile WWF, wamehamasika na kuanzisha utaratibu wa kuotesha miti ya asili na kupanda kwenye shamba lao lenye hekari 60 huko Nyambili. Vile vile wana vitalu vyao vya kuotesha miti ya asili ambao hupanda kwenye shamba lao kwa ajili matumizi mbalimbali ikiwamo uchomaji mkaa. Wanatoa elimu kwa wanakijiji wenzao juu ya uchomaji mkaa kwa njia za kisasa

Nini kinaendelea?Kikundi cha uchomaji mkaa endelevu (KIUME) wamechukua hatua baada ya kuona uharibifu unaoendelea katika kijiji chao cha Nyambili na vijiji vya karibu kuanzisha utaratibu wa kutunza mazingira ambao ni wa aina yake. Waliona kuwa uchomaji mkaa ni suala ambalo ni gumu kuachana nalo. Sasa wamekuja na njia kabambe za kunusuru miti katika uchomaji mkaa kwa kiasi kikubwa

Tuhifadhi, tutunze na tuyalinde mazingira yetu ili yatutunze.

Page 8: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

8 Si Mchezo! NOVEMBA-DESEMBA 2012

MAMBO YA FEDHA

Pamoja na kwamba tunaunga mkono juhudi za kutunza mazingira, ni vizuri pia kutoa elimu juu ya uvunaji salama wa misitu yetu. Ndiyo, kwani kwa asilimia kubwa bado tunatumia misitu kwa mahitaji

muhimu. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) Rahima Njaidi, alisema zipo njia nyingi ambazo tukizitumia zitasaidia kuhifadhi mazingira huku jamii ikinufaika kwa kujiingizia kipato kutokana na misitu.

Baadhi ya njia hizo ni;• Ufugaji wa nyuki; Jamii inashauriwa itumie

njia za kisasa za ufugaji wa nyuki ambazo inatumia mizinga ya kisasa inayosaidia nyuki kujaa kwa wingi na kuweza kutoa asali nyingi zaidi tofauti na mizinga ya kienyeji. Ufugaji nyuki ni rafiki kwa misitu kwani inapunguza uchomaji moto, kwa kuwa watu/mtu au kikundi kinafahamu kwamba watahatari-sha uwepo wa nyuki na ubora wa asali kwa ujumla

• Uchimbaji na uchumaji wa dawa mbalim-bali za asili ambazo zimekuwa na soko kila pande ya nchi

• Uchomaji mkaa kwa kutumia njia za kisasa. Kutumia matanuri maalumu am-bayo hutumia miti michache na kupata mkaa mwingi. MJUMITA na Tanzania Forest Conservation Group (TFCG) wanashirikiana kutekeleza mradi wa utengenezaji wa mkaa endelevu Wilaya ya Kilosa.

• Ufugali vipepeo; Wananchi wa Amani, Muheza hufuga vipepeo ambao imewanu-faisha sana kwa kujipatia kipato kwa kuuza hata nje ya nchi.Hukaushwa na kutengen-ezwa vidani

• Utalii wa mazingira; ambayo wananchi wanaweza wakatenga sehemu yenye bayo-anuwai likawa kivutio cha watalii

Tuyavune kwa njia salama

J K u m b u k aJuhudi za utunzaji wa mazingira zinahitaji ubunifu wa wananchi wenyewe kuanzisha njia rafiki za matumizi ya misitu ili kuondokana na uharibifu wa misitu itutunze sisi na vizazi vijavyo. Kuwa mstari wa mbele kutetea uhifadhi wa mazingira ili wengine nao waige kwa vitendo.

Page 9: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

9NOVEMBA-DESEMBA 2012 Si Mchezo!

NGUVU ZA MWANAMUME

Mengi yanasemwa kuhusu kupiga ‘puchu’, lakini ukweli unabaki palepale kuwa, wake kwa

waume wanajichua wakiwa faragha, na wengine wanahofia kutokana na tetesi wanazozisikia mitaani.

Puchu kwa faragha!

Je kuna madhara?

Wataalamu wa afya wanasema kwamba ni kitendo cha kawaida kisichokuwa na madhara yoyote.

Punyeto inaweza ikawa ni tatizo ikiwa utaifanya hadharani au ikiwa itaingilia shughuli zako za kawaida katika maisha. Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe ndiye mwa-muzi.

Hivi inakuwaje kwani?• Kujichuaaukupigapunyetonikitendo

cha kujisisimua uke au uume kwa kusugua taratibu hadi kufikia mshindo.

• Vijanaambaowanabalehenawanaanzaku-pata hamu ya kujamiiana hujikuta wakipata msukumo wa kupiga punyeto.Hata watu wazima hupiga punyeto na haijalishi wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi au la.

Ukweli wa kitaalamu kuhusu kujichua;

• Husaidiakupunguzamsongowamawazo.• Kingasahihidhidimagonjwayamaambukizi

ya ngono na ya VVU.

• Kutulizahamuyamapenzikwamtuambayehayuko tayari kufanya mapenzi.

• Husaidiakufurahiazaidikitendochakujamii-ana kwa kuwa unakuwa unajua nini kinacho-furahisha

Hizi ni baadhi ya imani potofu eti;•Wasiowezakutongozandiyowanaopiga punyeto

• Husababishamatatizoyaakili,upofunakupoteza uwezo wa kufanya mapenzi

• Nywelekuotakatikaviganjavyamikono.

• Wanaumekuishiwanguvuzakiumekama watapiga punyeto sana.

• Kunenepaupandemmoja.

• Watuwenginewanawezakufahamukama unapiga punyeto kwa kukuangalia.

J K u m b u k aHakuna mtu aliyezaliwa akijua jinsi mwili wake unavyoitikia msisimko wa kimapenzi. Inabidi kupata ushauri nasaha.

Page 10: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

10 Si Mchezo! NOVEMBA-DESEMBA 2012

Wizi mtupu!Sakata la mabadiliko vyanzo vya maji kukauka, lilileta tafrani katika Kijiji cha Mtiki. Wanakijiji walianza kunyoosheana vidole kumtafuta mchawi huku kila moja akitafakari pa kuanzia. Haikuwa kawaida lakini kilichotokea baadaye kilikamilisha ule useme usemayo; kikulacho kinguoni mwako. Fuatilia mchezo huu.

Mchezo huu umeigizwa na Pamoja Art Group kutoka Ikwiriri, Rufiji. Huu ni mchezo wa kuigiza na hauna uhusiano wa moja kwa moja na maisha halisi ya waigizaji

Sawa mume wangu

Haya sasa, Ogama na Jindai wamekubaliana kufanya kazi pamoja. Jindai hajauliza ni kazi gani kwa kuwa anamwamini rafiki yake Ogama hivyo haikuwa kitu muhimu kuuliza bali aliona bora ‘liende’! Twende pamoja…

Aaah! Tuko pamoja

Hofu ya Jindai imeanza siku ya kwanza tu kuingia msituni. Si kwamba anaogopa kukamatwa, bali anahofia wanyama wakali. Tuendelee na stori.

Mke wangu sasa hivi endelea na shughuli za shamba, nami nikafanye shughuli nyingine

Usije ukaniangusha kama unaogopa useme mapema

Unajua kuwa tunavyotunza haya mazingira ndiyo haya maji hayakauki

Huu ni muujiza kabisa.

Mwaka huu hayataisha

Msitu mkubwa sana, hakuna wanyama kweli?

Acha uoga bwana twende!

KIKAO CHA KAMATI YA MISITU…

Kila mwananchi analo jukumu la kulinda rasilimali za kijiji chetu ikiwamo misitu.

Siku hizi kuna malori mengi ya magogo hapa kijiji

Page 11: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

11NOVEMBA-DESEMBA 2012 Si Mchezo!

YUKO NA RAFIKI YAKE WAKIP-ANGA KWENDA MSITUNI…

Jana kwenye kikao cha misitu tumetakiwa kufanya doria kwenye msitu

Niko ‘busy’ na mambo yangu

Labda kuna mti mkubwa maeneo hayo

Mwaka huu mzee umejipanga!

Maisha ni kuhangaika!

Hilo ndiyo kiboko ya miti.

Mwaka huu una mpango gani na miti ndugu yangu? Mmh!

Kawaida tu

Unaweza kazi za hatari

Kama inalipa niko tayari

Huu ni muujiza kabisa.

Mbona leo njia tofauti na sisi?

Ogama amenunua msumeno mpya ameamua safari hii

Hata vifaa siunaona ni vipya?

UWAZI BAADA YA MITI KUKATWA ENEO LA HIFADHI…Kila mwananchi analo jukumu la kulinda

rasilimali za kijiji chetu ikiwamo misitu.

Page 12: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

12 Si Mchezo! NOVEMBA-DESEMBA 2012

TUENDELEE ILI TUONE MWELEKEO WA KILA MMOJA. MWINDAJI APIGWA NA BUTWAA MSITUNI…

MAMBO YAMEBADILIKA KISIMANI…

Ogama na Jindai wameuza mkaa. Maisha yamebadilika kwani kwa masuala ya mshiko sasa wako vizuri. Ni jukumu la kila mmoja kupangilia matumizi ya pesa zake.

Matokeo ya uharibifu wa vyanzo vya maji umeanza kujitokeza lakini wenyeji bado hawajui ‘mchawi’ ni nani. Tuendelee

Hapa tukivuna umaskini kwisha!

Nashukuru sana kwa kunishirikisha hili dili kaka

Hiki kisima miaka yote hakijawahi kuishiwa maji hivi

Vipi Ogama mbona siku hizi hatukuoni kwenye maeneo yetu ya mkaa?

Nahisi waliokata ule msitu ni kina Ogama kwani siku hizi hatuwaoni kwenye eneo la siku zote la mkaa

Labda wamekiloga ndugu yangu

Nikifanikiwa nitakuambia uwe ‘mpole’.

Pesa nilizonazo kwa sasa nitakununulia nyumba

Nami nitakupenda milele

Daaaah!! Yaani msitu wa hifadhi ndiyo umekatwa hivi?

Inawezekana hawa ndiyo wamesababisha maji kuisha haraka

Nimepewa taarifa ya kusikitisha sana na inatubidi tukawatege huko huko msituni

Hawa lazima tuwapate

Inawezekana kwani ni majuzi tu nimesikia wameshusha mzigo mkubwa na hakuna anayejua umetoka wapi.

Page 13: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

13NOVEMBA-DESEMBA 2012 Si Mchezo!

Watu kama hawa ambao hupenda kuharibu mazingira kwa ufinyu wa uelewa wao wako wengi sana katika vijiji vyetu. Tutoe taarifa pale tunapoona uharibifu wowote kwenye vijiji vyetu.

MWINDAJI KWA MTENDAJI WA KIJIJI…

BAADA YA SIKU KADHAA…

TATIZO LA MAJI LINAZIDIKUWACHANGANYA WANAKIJIJI…

MZIGO UKATUA KIJIJINI…

Zile gunia mia mbili za mkaa? Subiri konda wangu aje.

Twende tukachukue ule mzigo niliyokuambia jana

Huyu sasa atatuletea balaa

Lazima mchawi ametoka mbali

Ngoja tukufikirie tutakupa jibu

Kumbe una mzigo wa maana hivi? Naomba niwe nakuja kununua kwenye eneo la uzalishaji

Mtendaji huwezi kuamini msitu wa bonde la kisimani umefyekwa karibu unaisha

Inawezekana ndiyo iliyosababisha maji kukauka kisimani mwaka huu

Hivi tutaishije bila maji?

Tusipotafuta suluhu la tatizo hili tutakwisha

Msimuumize jamani tuwapeleke ofisini

Nilijua tu ni wewe ngoja nikuvunje kiuno

Mtendaji tuokoe! Usilolijua ni sawa

na usiku wa kiza. Kumbe mume wangu alikuwa akifanya kazi za uharibifu wa mazingira?

Mambo hayo. Wahenga wanasema usione vyaelea ujue vimeundwa! Matanuzi ya Jindai hayakuwa ya kitoto

Page 14: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

14 Si Mchezo! NOVEMBA-DESEMBA 2012

Hapa tukivuna

umaskini kwisha!

Nashukuru sana kwa

kunishirikisha hili dili kaka

Niko ‘busy’ na mambo yangu

Jana kwenye kikao cha misitu tumetakiwa kufanya msako kwenye msitu

JE, WAJUA?

Kataa katakata kukatakata miti

Suala la mabadiliko ya tabia nchi limekuwa likipigiwa kelele na wadau

wa mazingira sehemu mbalimbali duniani. Utunzaji wa mazingira na utumiaji endelevu wa misitu umekuwa ukihimizwa mara kwa mara duniani kote. Kwa baadhi ya watu, suala la utunzaji wa mazingira limekuwa ni kama hekaya za abunuwasi. Wengine wanafikiri kuwa kama si mashirika au taasisi fulani, basi ni wenyeviti wa Serikali za Vijiji na viongozi wengine wa Serikali ndiyo wanaohusika na suala la utunzaji wa misitu na mazingiria kwa ujumla. Tunasahau kwamba misitu hii inapoangamizwa jamii yote inaathirika na majanga kama vile, ukame na njaa yanatukumba sote

Fahamu ya kuwa:

• Misitunichanzochakikubwa mvua amba-zo sikuhizi zimekuwa ni za msimu kutokana na kutokomea kwa misitu mingi hapa nchini

• Misitunichanzoki-zuri cha mapato ikiwa itatumika kwa ufugaji wa nyuki.

• Paleunapokatamti,unatakiwa kupanda miti.

Page 15: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

15NOVEMBA-DESEMBA 2012 Si Mchezo!

Maisha ya mwanadamu yamezungukwa na miti, miti hii hutuletea mvua,kivuli na hata matunda. Kwa ufupi ni kuwa kama tutaitunza hii miti, basi na yenyewe itatutunza, lakini kama hatutaituza, maisha yatakuwa ni majanga tu.

Tuyafahamu haya:

Misitu inatokomea kwa kasi ya ajabu hapa Tanzania. Shughuli za ukataji wa miti kwa ajili ya kutengenezea samani za ndani na magogo yanayosafirishwa nje ya nchi, zimesababisha kutokomea kwa miti ya asili na sasa, samani hizo hutengenezwa kwa kutumia miti kama miembe na mikorosho. Uchomaji wa mkaa kwa staili ya Ogama na mwenzake Tindare unawakilisha vijana wengi ambao huamua kujilipua na kujaribu zali bila kufikiria matokeo yake kwao na kwa jamii inayowazunguka.

Nani awajibike?

• Kilammojawetuanatakiwakuipa misitu kipaumbele

• Elimuyamisituiendeleekutolewa mara kwa mara ili watu watambue umuhimu wa misitu.

• Watuwanapoambiwawasikatemiti, waonyeshwe njia mbadala ya kujiingizia kipato.

• Tuwafichuewatuwanaoingiakukata mitit kwa siri kwenye misitu iliyohifadhiwa.

SwaliJe,unadhani ni mbinu gani zitumike ili kulinda misitu ya hifadhi isiharibiwe na majangili?

Tuma maoni yako kwa ujumbe mfupi kwenda namba 0715568222

Hivi tutaishije

bila maji?

Tusipotafuta suluhu la

tatizo hili tutakwisha

TATIZO LA MAJI LINAZIDI KUWACHANGANYA WANAKIJIJI…

Page 16: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

16 Si Mchezo! NOVEMBA-DESEMBA 2012

Mabalozi wa mazingira Rufiji ndiyo hawa…

Baada ya kuona mabadiliko yasiyo ‘rafiki’ yakiendelea kutokea kila mwaka, walikaa chini na kutafakari ni kitu gani wangeweza kukifanya ili kuokoa ‘jahazi’. Muungano wa watu 12 ndiyo uliounda Rufiji

Environmental Group (REG), mwaka 2006 ambayo umejikita katika kutunza mazingira hasa vyanzo vya maji na upandaji miti. Makao makuu yao ni Kibiti lakini wanahudumia maeneo yote ya Wilaya ya Rufiji. Ukiwakuta utafurahishwa na uchapaji kazi wao. “Tunafanya kazi mfano wa nyuki na kila mtu anajua majukumu yake. Hafuatiliwi mtu hata kidogo,” alisema Mwenyekiti wa kikundi hicho Bw. Musa Mapesa.

Walianza hivi...

Walipopata wazo la kuwa mabalozi wa mazingira, walipeleka maombi kwenye ofisi ya Serikali ya Kijiji ili watumie Bonde la Bwawa Kibibi kupanda miti na kuwauzia wananchi wa Rufiji ili wapande. Walipokubaliwa, walianza kufanya utafiti wa mbegu za miti ya asili na kuzikusanya na kuzihifadhi kwenye kituo walichokianzisha. Waliomba msaada wa mafunzo huko Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Idara ya Maliasili jinsi ya kuandaa na kuendeleza vitalu. Walipewa mafunzo na wakaanza kazi rasmi ya upandaji miti.

Wanashughulika na haya

• KuhifadhiBwawaKibibilililoko Kibiti ambalo ni chanzo kikubwa cha maji.

• Kutengenezaajirakwavijana kwa kutumia maji hayo kwa kupanda miti ya biashara.

• Kuelimishajamiiijueumuhimu wa kutunza vyanzo vya maji na mazingira kwa ujumla.

• Kuuzamitinakujipatiakipato rafiki kwa mazingira.

TULICHOVUNA

Baadhi ya miti wanayopanda…

• Mkongo• Mpingo• Mpangampanga• Mkuruti• Mtondoro• Mtanga• Mkenge• Mwarobaini

Moja ya miche inayooteshwa na REG kwenye vitalu vyao huko Kibiti, Rufiji.

Page 17: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

17NOVEMBA-DESEMBA 2012 Si Mchezo!

Haya ndiyo mafanikio yao

• Wamepandahekarinanezamiti• Wamepataujuziwaupandajimitina

sasa wanawaelimisha watu wengine hapo kijiji Kibiti

• Wamekuwa kituo cha mafunzo yautunzaji mazingira na upandaji miti kwa shule za Rufiji na wananchi wake

• Wamefanikiwa kuonyesha kazi zaokwenye maonyesho ya kitaifa ya Nanenane na zimeleta hamasa kubwa

• Wamejiajiri

Changamoto zipo;

• Mwamkowawananchijuuya utunzaji mazingira bado ni mdogo

• Ukosefuwausafiriambaoun-gewasaidia katika ukusanyaji wa mbegu za miti za asili msituni

• Baadhiyawanakikundikutoji-amini juu ya kazi wanayofanya ingawa ni wachache wenye hofu hiyo

Malengo

• Kununuakiwanjanakujengaofisi na nyumba za wanachama

• Kufuganyuki• Kuanzishamashambayamitina

matunda ya asili• Kufugakukunasamakiiliku-

jiongezea kipato

J K u m b u k a

Utunzaji wa miti hutupa maisha marefu na yenye furaha hivyo tunawahamasisha wananchi wote wazingatie kuwa kuharibu mazingira kwa lengo la kupata faida binafsi ni hatari kwa jamii. Kuwa wa kwanza kusema hapana kwa uharibifu wa mazingira.

Wafanya kazi wa REG wakionyesha eneo wanalotumia kupanda miti na kutun-za chanzo cha maji cha Bwawa Kibibi walipotembelewa na timu ya Si mchezo, Majuka (wa pili kushoto) na Suleyman ( kwanza kulia)

Page 18: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

18 Si Mchezo! NOVEMBA-DESEMBA 2012

CHEZASALAMA

Jiulize, tuko wangapi?

Kuwa katika mtandao wa kimapenzi imekuwa kama ‘fashion’ siku hizi, vijana wanakuwa ndani ya uhusiano lakini

wanapotakiwa kuwataja wapenzi wao hupatwa na kigugumizi. Si umeshawahi kusikia nyumba ndogo, kidumu, kicheche, chipsi funga, ATM, buzi, serengeti boys, mario, kibustani na ‘sugar mami?Hapa sizungumzii walio nje ya ndoa tu, maana kuna wanandoa wasio waaminifu kwenye ndoa zao. Uaminifu ni suala nyeti kwenye uhusiano wa kimapenzi, kama umesahau kuwa mwaminifu, jiulize swali moja tu je, tuko wangapi? Tulizana.

Madhara ya kuwa katika mtandao wa mapenzi…

• Kuvunjikakwauhusianokatika familia.

• Kupatamsongowamawazo.• Kusambazavirusivya

ukimwi.• Kujishushiaheshimakatika

jamii.

Mwanamume yeyote rijali namwanamke yeyote anayeshirikikatika mapenzi anahusikakwenye kampeni hii.

Mlengwa ni nani hasa?

Page 19: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

19NOVEMBA-DESEMBA 2012 Si Mchezo!

Kwa nini ujiulize?

Inawezekana mpaka sasa hivi una imani kuwa uko peke yako, kumbe upo na ‘wenzako’ ni vyema ukajifahamu upo katika mazingira gani ya kiuhusiano na mpenzi wako. Wengine wako kwenye mtandao huku wakijua lakini wanapuuzia. Badilika! Madhara yake ni kujiweka katika hatari ya kuambukizwa magonjwa ya maambukizi ukiwemo Ukimwi.

Sababu za mtandao

• Mara nyingi hutokana na misukumo mbalimbali iliyopo katika makundi rika ili kuwezakukubalika kihisia, kingono na kiuchumi ili kuonyesha kwamba umekamilika.

• Sababuzakihisiazinakuwapalemtuanapohisihakunamapenzikatiyakenamwenzawake.Unawezaje kuepuka hii? Ni kwa kutenga muda mwingi wa kuwa pamoja na kuzungumza mara kwa mara na hata kutumiana meseji za simu mnapokuwa mbali.

• Kutoridhishanakingononimojayamatatizomakubwakwenyemahusiano.Wengihunyamazana kujikaza ‘kisabuni’ wakiogopa kuwaambia wenzi wao ili mahusiano yasiingie dosari. Hilo sio suluhisho, cha kufanya ni kuzungumza na mwenza wako kwa njia ya upole mnapokuwa faragha bila kumkwaza,fanyeni maandalizi ya kutosha ,na jitahidi kuongeza ‘mautundu’.

• Tamaazamkwanjawafastafastanamaishayaanasakulikouwezobinafsihuwaunganishawengi katika mtandao. Ukitaka kujinasua hapa, ridhika na ulichonacho pia muheshimu huyo uliyenaye. Pangeni kwa pamoja mkakati wa kujinasua kiuchumi, tengenezeni bajeti na kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima.

JK u m b u k aKama mtu mmoja katika

mtandao ameathirika, kila mmoja aliye katika mtandao yupo katika hatari ya kupata maambukizi hata kwa wale ambao ni waaminifu kwa wapenzi wao lakini wapenzi wao wanasaliti uhusiano wao.

Page 20: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

20 Si Mchezo! NOVEMBA-DESEMBA 2012

BURUDANI

Uuuu, Aaaa, oooYou know what Kevy, this is my life man, Stamina

Ubeti wa KwanzaNapigwa msumari wa kichwa mwili unangoja kaburi,Maisha yamenipiga picha nega zimetoka vivuli,Dunia tambara bovu nalidekia kwa shida,Jitahidi kuisolve bila kutumia four figure,Natamani nisimame ili nione magharibi,Moyo umejawa ukame, kuhema unajitahidi,Macho yote yanaukungu utadhani chungu cha bibi,Nata-kumuomba Mungu shetani anazidi spidi (Men) Vizuri viko wapi, navisaka havionekani (dah)Napata makapi vinono navitamani,Sina baba, sina mama, sina babu, sina bibi,Uchumi wangu umesimama kama behewa la itigi,Umasikini unanipodoa bila kutumia cosmetics,Daily unanizodoa unanivuta bila magnetics,Maisha yangu hayana swaga kama masai wa njiro,Natamani kula burger naishia viazi vya Gairo,

KiitikioLeo nimepata kesho nimekosa,Nachohifadhi maumivu tu, laifu ni ngumu bado inan-ichosha,Nakula mbichi sili mbivu,Uweza mimi bado ni kabwela, sina uhuru kama niko jela x 2Ubeti wa piliKusoma kitajiri, kichwa kimejaa madufu,Maisha hayana tafsiri usidhani yanamjua rufufu,Naichora lami na mkaa kwa kudhani nitaona chochote,Atleast class ningekaa, nisingeitwa kiokote,Pesa imegeuka Yuda, daily inanisaliti,Mishale inazidi muda, utajiri unaninyima siti,Maisha kama gwaride, Kuna wa mwisho na wa kwanza,Yakisema nyuma geuka, wa mwisho anakuwa wa kwanza,Taifa la kichwa changu rais wake naona kichaa,Na kitabu cha dhambi zangu kwa Mungu kimeshajaa,Napatwa wazimu shida zinanitia madoa, pesa imekuwa adimu kama bikra kwa changudoa,Banda ninalofugiwa sihemi halina dirisha,Wasichana wananikimbia, wananiita nyoka wa kibisa,

Msosi wangu sio wa draft, sili mpaka nijitumeMaisha yana supa shafti yashanizidi nguvu za kiume.

Kiitikio

Ubeti wa tatuUshindi wangu ni uchafu, kwenye vita ya wasafi,Kila ninayemuomba tafu anataka nifanye naye ulafi,Maisha ni kombolela, maskini ndio mlinda kopo,Cha msingi ni kuunga tela mpaka nitoke kwenye msoto,Jua linapozama natamani pasikuche, hasi inageuka chanya,Kapeto anageuka sunche, naona alama za mlango ila sioni pa kutokea,Hii pesa imetoka jando inataka kunibabu Seya,Nimegeuka konokono natembea na mzigo shida,Silali nimekuwa pono maisha yanakwenda na mida,Shida zishanipa ustaa zaidi ya kanda ya Loketo,Utumbo umezoea njaa hadi shibe naiona mseto,Vikombe vya uaminifu nishavivunja mtaani,Na vijiko vy uhalifu nishaviweka kwenye sahani,Mi nadhani haya maisha yana ramani, ila aliyewachorea masikini peni iligomea njiani

Kiitikio

Wimbo: KabwelaMsanii: Stamina ft Richard Mavocal

!

Page 21: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

21NOVEMBA-DESEMBA 2012 Si Mchezo!

J

!!! !

Asiyesikia la mkuu…

Afisa mmoja wa misitu alikwenda kwenye shamba la miti kukagua, msimamizi akamwambia usiingie sasa hivi. Afisa akatoa kitambulisho cha kazi akamwam-bia “wewe ni nani wa kunizuia?” Unaona kitambulisho? Msimamizi akamwambia pita wewe ni mtu mzito bwana. Kupita tu akaanza kupiga makelele “nyuki nakufaa nisaidieee” Jamaa akamwambia wao-nyeshe kitambulisho!

Jamaa na mtoto

Jamaa aliingia kwa kinyozi na mtoto mdogo akase-ma anyolewe yeye kwanza. Alipomalizwa ,akasema, “poa endelea kumnyoa mwanangu naenda dukani halafu nakuja kumpitia” Mtoto akanyolewa. Baada ya saa moja jamaa hakurudi!! Kinyozi akamwuliza mtoto, “Kwani baba yako anarudi saa ngapi?” Mtoto akajibu, “huyo si bàbangu, amenipata hapo nje akaniambia tuje hapa tunyolewe bure”.

J

Mwanafunzi amchanganya mwalimu

TICHA: Kati ya pesa na akili wewe ungechagua nini? Haya Juma tuambieJUMA: Ningechagua pesa mwal-imuTICHA: Ningechagua akili. Sasa Juma kwa nini umechagua pesa badala ya akili?JUMA: Kila mtu huwa anachagua kitu ambacho hana

Wanafunzi ‘wamtesa’ konda…

Usiku mmoja konda alikuwa amelala, ghafla mdogo wake akaamka na kwenda chooni, alivyorudi ile anafunua neti tu, Konda akamzuia na kumwambia wanafun-zi wanatosha..

JMdada agonga mwamba

Mdada na mkaka walikuwa wan-apita madukani, si mdada akakiona kiatu kimoja kizuri, bei 60,000/-.

MDADA: Mweee kiatu kizuri ningekuwa sijasahau pesa nyumbani ningeki-nunua, ninunulie jamaniMKAKA:Chukua hii 5,000/-, kodi taxi uka-chukue hela yako ‘sweety’ naku-subiri hapahapa.

Page 22: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

22 Si Mchezo! NOVEMBA-DESEMBA 2012

PASIPO NA DAKTARI

Msaada unapoumwa na nyuki…

Wahenga wanasema fuata nyuki ule asali, lakini wakati mwingine unaweza

ukajikuta umeambulia maumivu ya ajabu kwa kuumwa na nyuki. Pamoja na kwamba asali yao ni tamu lakini si rahisi kuipata, lazima ujipange ili ufanikiwe la sivyo manundu yatakuhusu.

Uking’atwa na nyuki;

• Ondokaeneohiloharakakwaninyukihutoa harufu maalumu ya kuwaita wen-zake hivyo ukiendelea kuwepo mahali hapo watakudhuru zaidi

• Ondoamshalewanyukikwamakuchaharaka, usitumie kibanio, kinaweza kufinya sumu ndani ya mwili.

• Wekabarafuaukitambaakilichototase-hemu uliyoumwa na nyuki kuzuia kuvimba na kupunguza maumivu.

• Jipakemchanganyikowamajinahamiraulipoumwa kuzuia maumivu.

• Mezatembezakupunguzamaumivuaumuwasho

• Endapounamzio(Allergic)ukang’atwananyuki ni vyema ukawahi kituo cha afya bila kusubiri dalili za mzio

Madhara ya kung’atwa na nyuki

Madhara hutofautiana kwa kila mtu kwani mfumo na kinga hutofautiana haya ni baadhi;• Maumivumakalisehemuuliyong’atwana

wakati mwingine kusambaa mwilini• Kuvimba• Kuwashwa• Endapomshalewanyukiutabakimwilini

kwenye pua, mdomo au koo huweza kukusababishia upate shida ya kupumua.

J K u m b u k aKung’atwa kwa nyuki inauma sana na wakati mwingine husababisha kifo kwa wale ambao wana mzio wa sumu ya nyuki. Njia salama ya kupunguza na kuondoa maumivu au mmenyuko ni kuondoa mshale haraka iwezekanavyo.

Page 23: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

23NOVEMBA-DESEMBA 2012 Si Mchezo!

HUDUMA

Wafahamu MJUMINGU

Ni kifupi cha Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Msitu wa Ngumburuni

uliopo wilayani Rufiji. Mtandao huu ulianzishwa mwaka 2005 ili kukabiliana na changamoto mbalimbali ambazo zilianza kujitokeza baada ya kuanzisha utekelezaji wa usimamizi shirikishi wa misitu. Mjumingu unajumuisha vijiji saba vinavyozunguka Msitu wa Ngumburuni ambavyo

ni Mayuyu, Ruaruke A, Mangwi, Mkupuka, Umwe Kaskazini, Umwe Kusini na Umwe Kati.“Tunaiomba Serikali kurudisha misitu kwa jamii badala ya kumilikishwa kwa halmashauri ya wilaya, kwani wanajamii ni rahisi kuisimamia kwa ukaribu, tofauti na wilayani ambapo uwajibi-kaji wa moja kwa moja unakosekana” anasema Katibu wa Mjumingu Bw Mwarami Kwangaya.

Wamefanikiwa

• Kukamatamagogonakuyataifi-sha

• Kupataelimuyakufanyashughuli mbadala ya namna ya kutunza misitu.

• Kupatamafunzokutokase-hemu mbalimbali yahusuyo uongozi na uhifadhi wa misitu.

• Kupunguzakasiyauvunajiharamu wa magogo.

• Kuwashirilishawananchikatikakusimamia misitu na kuwafi-chua wahalifu wanaokata na kusafirisha magogo toka msitu wa Ngumburuni.

Changamoto

• Kukosekanakwavizuizikwenyemaenenoyamali-asili.

• Kukosekanautawalaborawausimamiziwamisitu.• Jamiikutegemearasilimaliyamisituilikupatamahi-

taji muhimu.• Ukosefuwaelimuyamisitunafaidazakekwawana-

jamii.• Ukosefuwavifaanamafunzokwaaskaridoria.• Vijijihavinufaikinamsitu

Kuna sapoti za wadau

Mjumita (Mtandao wa Usimam-izi wa Misitu Tanzania) imekuwa ikiwapiga tafu upande wa kutoa elimu na mafunzo mbalimbali kuhusu suala zima la uhifadhi wa misitu.

Baadhi ya viongozi wa MJUMINGU huko Ikwiriri, Rufiji

Page 24: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

24 Si Mchezo! NOVEMBA-DESEMBA 2012

KATUNI

Michoro: babatau cartoons 2012

KICHAPO!Miti imeleta noma baada

ya kuona kuwa kitendo wanachofanyiwa na binadamu hakistahili. Ni mchezo wa kuigiza lakini ukifuatilia kwa undani utaelewa wanachomaanisha miti hiyo huko kijiji cha Mburuni

Page 25: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

25NOVEMBA-DESEMBA 2012 Si Mchezo!

Page 26: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

26 Si Mchezo! NOVEMBA-DESEMBA 2012

Miti imewabadilikia wanadamu kwa kile wanachodai kuwa wamekuwa wakiwaonea bila ya kujali faida wanayowapa. Naona ni sawa kabisa kwani wakati mwingie inabidi tuseme hapana!

Page 27: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

27NOVEMBA-DESEMBA 2012 Si Mchezo!

UKWELI WA MAMBO

Kilio cha miti

Utawala wa mwanadamu umekuwa na tabaka mbali mbali kiasi kwamba anawanyima viumbe vingine uhuru wa kuishi. Mimea ndiyo wenye kilio kikubwa hasa misitu ambayo hufunika ardhi na kutunza

ardhi yenye viumbe vingine vingi.Kwenye mchezo huu wa katuni tumewajengea uwezo miti ili iweze kujitetea. Ni sehemu ya burudani lakini tukifikiria kwa kina, miti ina kilio kikubwa ambacho ingetamani siku moja izungumze kuwaeleza binadamu juu ya uangamizaji wanaoufanya.

J K u m b u k aTunaweza kutumia bidhaa mbadala tukauacha mti uendelee kuishi ili utusaidie kuleta mvua, kuhifadhi vyanzo vya maji, hewa safi na hifadhi ya viumbe vingine. Kwa kufanya hivyo, itasaidia ama kuacha au kupunguza matumizi ya miti.

Miti wana ujumbe gani?

Inasema kuwa watu wanasahau misaada wanaowapatia na viumbe vingine. Wanyama, ndege na hata wadudu wanauhitaji kwa ajili ya kupata hifadhi na msosi.

Miti hulia kwa kufanyiwa haya;• Kukatwailikututumiakujenganyumbanahatama-

banda ya mifugo• Kuchomwakupatamkaakwaajiliyakupikia.Wen-

gine hutumia kuni kupika.• Mitihukatwanakutengenezaviti,meza,makabati,

vitanda, vijiko, vitana na hata vinyago hutengenezwa kwa kutokana na miti

Njia mbadala zipo?

Kwa dunia ya sasa, teknolojia imeongezeka na zimegundulika njia mbalimbali ambayo mti anaweza akanusurika ingawa bado anahitajika kwa kiasi kikubwa kwa mwanadamu. Hizi ni baadhi tu;• Kutumiagesiaumajikoya

kawaida yanayotumia kiasi kidogo cha mkaa kupikia

• Kutumiaviti,mezan.kvyaplastiki

• Tunawezakupunguzaidadiyavinyago vya miti kwa kutumia udongo ya kutengeneza vinyago

Page 28: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

28 Si Mchezo! NOVEMBA-DESEMBA 2012

Wewe pia unaweza kulonga na vijana wenzako. Tuandike maoni, ushauri,

vichekesho,maswali nk, weka anuani yako na tuma ukiambatanisha

na picha yako kwa Mhariri, Jarida la Si Mchezo!,

S.L.P 2065 Dar es [email protected] tumbukiza katika boksi

la Si Mchezo! kama lipo katika eneo unaloishi.

SAUTI YANGU Kama una chochote unachotaka kusema tuandikie ili upate fursa ya kuwaelimisha wengine

Maoni yaliyotolewa katika ukurasa huu ni ya wasomaji, si lazima yalingane na msimamo wa Femina.

Si Mchezo!Femina HIPSLP 2065,

DSM

Biashara yangu

Kero yangu ni kuhu-siana na biashara yangu ya mashine yetu ya kukoboa nafaka. Kumekuwa na majungu sana. Tumekuwa hatu-pendani, tumekuwa hatuna msimamo katika bei zetu za kilo kwa mpunga. Unakuta mtu anapunguza bei ilimradi wateja wote waende kwake, wakati siyo taratibu zetu, kama tunataka kushusha bei basi wote tuwe tunakubali-ana na wote kwenda sawa. Naomba wote tunaohusika tujirekebishe.Abdallah Issa, Rufiji

Polisi punguzeni mzukaKwa nini polisi wanaua watu bila ya hatia? Ina maana uongozi hautam-bui? Kama ni hivyo basi wananchi hawatakuwa na imani na jeshi la polisi. Rais inabidi atambue hili, polisi wanawafundisha watu kuchukua sheria mkononi wakati hii ni nchi ya amani na inaendeshwa kisheria.Shabani MapekweRufiji

Msimamo

Naomba Serikali yetu iwe na msimamo mzuri kwa wananchi wao. Kwa sababu vitu vingi vichafu vinafanyika, naomba waache kudharau. Kama hapa kijiji chetu kinasumbuliwa na wafugaji wanaua watu bila ya kuchukuliwa hatua yoyote ileHaji Omari,Ikwiriri, Rufiji

Magonjwa ya ngono yamezidi!

Vijana wapewe elimu ya kutosha kuhusu masuala ya magonjwa ya ngono kama gono, kaswende na pangusa kama Ukimwi unavyopewa kipaumbele katika kue-limisha jamii kwa kutumia vipeperushi, semina mbal-imbali hasa kwa Wilaya ya Rufiji.Florida MwechiRufiji

Page 29: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

29NOVEMBA-DESEMBA 2012 Si Mchezo!

Unamshaurije rafiki yako anayejihusisha kwenye mtandao wa kimapenzi aache?

Page 30: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

30 Si Mchezo! NOVEMBA-DESEMBA 2012

SEMA, TENDA!

“Maliasili” wengi wanaposikia hili neno hili wanafikiri kuwa viongozi wa Serikali na taasisi zinazojishughulisha na mazingira pekee ndiyo wenye wajibu wa kutunza misitu. HAPANA! Misitu ni mali ya jamii yote.Tanzania ni moja ya kati ya nchi ambazo zina neema ya kuwa na misitu mingi ya asili, lakini jambo la kusikitisha ni kuwa jitihada za haraka zisipochukuliwa, misitu hii inaweza kubaki katika vitabu vya historia tu.Misitu hii inatakiwa kutuletea ustawi na utajiri katika jamii. Lakini wakati mwingine maliasili hizi hazitumiki katika njia isiyo ya kidemokrasia na uwazi ili ziwanufaishe watu wote.

Misitu yetu, uhai wetu

Vijana hili ni letu…

Kijana kuwa mfano wa kuiga! Uharibifu wa misitu inabidi usitishwe kwa kuzingatia ushiriki wetu endelevu katika kutunza mazingira kwa kuanza kuyajali mazingira ya mahali tunapoishi kwa kupanda miti zile sehemu zote tulizokata miti, pia kwa kuwafichua wale wote wanaoshirki biashara haramu ya ukataji wa magogo katika misitu ya hifadhi.Kama wewe unafahamu umuhimu wa kutunza mazingira na una muona jirani yako au rafiki yako anaharibu mazingira, mfuate na umuelimishe bila hiyana, kama elimu umempa na bado anaendelea na vitendo vyake, nenda kamripoti maliasili.

Mazingira bora

Hivi umeshawahi kujiuliza kwenye mazingira unayoishi kwa nini kuna vyanzo vingi vya maji na hali ya hewa ya kuvutia? Ni kwa sababu ya misitu inayotuzunguka. Hivyo basi, kutunza misitu hii ni jukumu letu sote kama wana jamii kwa kuwa tunanufaika nayo.Ukataji wa miti tena usiokuwa na mpangilio, unaathiri kwa kiasi kikubwa mazingira tunayoishi na njia muhimu za kujipatia mahitaji yetu ya kila siku. Ardhi imekumbwa na ukame wa kutisha na hata hali ya hewa katika mazingira tunayoishi imebadilika kwa joto kupanda kwa kasi ya ajabu

S w a l iNjia gani zitumike ili kuwahamasisha vijana washiriki katika utunzaji wa mazingira yanayowazunguka?Tuambie kwa kutumia mawasiliano hapa chini:Barua pepe: [email protected] Sms: 0715568222

Page 31: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe

31NOVEMBA-DESEMBA 2012 Si Mchezo!

USHAURI

Betty Liduke ni rafiki mkubwa wa vijana, hata wewe unaweza kulonga naye. Ni msambazaji mkubwa wa Jarida la Si Mchezo! Mkoani Njombe. Ni mshauri nasaha na ni Mratibu wa Kitengo cha Udhibiti Ukimwi katika Kampuni ya TANWAT, Njombe.Mwandikie kupitia Jarida la Si Mchezo!Si Mchezo! S. L. P. 2065 Dar es Salaamau tuma ujumbe mfupi wa maandishi kupitia namba 0715 568222 na utuambie kama ungependa uchapishwe.

Swali

Kwanza inaonyesha huyo mama haku-pendi, hivyo unatakiwa mkae chini muongee ili akuambie ana msimamo gani juu yako. Beatrice Leonard

Kinachotakiwa ni kumchunguza mpen-zi wako ana msi-mamo gani juu yako. Hapo inaoneka huyo mama yake hakupen-di na hataki mwa-naye akuoe, ndiyo maana anakuzushia maneno ya uongo. Sihaba Mohamedi ,Rufiji

Nina mpenzi, tunapendana, ninafanya kazi Morogoro yeye yuko Dar. Huku niliko kuna wazazi wake, tatizo mama yake amekuwa akinizushia maneno ya uongo kila

siku. Nimemwambia mpenzi wangu, naye anamtetea mama yake, kinachonisikitisha mama yake amesema mtoto wake hatonioa. Naomba ushauri wenu. Nairath.

Hapo hakuna ndoa, cha msingi tafuta mtu ambaye atakupenda na wewe utampenda ili mfunge ndoa.Abdallah Adam,Ikwiriri, Rufiji

Mimi ni msichana wa miaka 24, Nilibahatika kumpata mvulana ambaye tulianza uhusiano. Katika uhusiano wetu sikuwa na haraka ya kutambalishwa kwani nilijua kila kitu kinakwenda na wakati. Mpenzi wangu aliniambia anakaa na mama yake na dada yake na mimi nilimweleza kuwa naishi na mama yangu. Kwa kuwa alikuwa ni mwanamume aliyenionyesha ulimwengu wa mapenzi nilimpenda na kumheshimu. Baada ya miaka miwili ya uhusiano wetu ndipo nilipogundua kuwa mpenzi wangu ameoa na ana mtoto mmoja. Kweli nilipomuona mke wake nilijiuliza mengi. Mama alinishauri niachane naye lakini nampenda sana huyo kijana na sidhani kama kuna mwanamume atakayechukua nafasi yake. Naomba ushauri wenu.Msomaji wa Si mchezo Mbulu, Manyara

Pole kwa maswahibu hayo. Kuna uwezekano mkubwa kuwa mpenzi wako bado hajawa na uamuzi wa kukuoa kama wewe unavyofikiria. Kuwa na subira, fanya uchunguzi wa kina kuhusu upendo wa mpenzi wako kwako halafu jadiliana naye usikie uamuzi wake. Mara nyingi katika uhusiano wa vijana wazazi wengi huingilia. Ni vyema wazazi watambue kuwa uamuzi wa nani ataishi na mwanaye ni wa kijana mwenyewe, Mpenzi wako akiwa na msimamo tatizo hili litakwisha.

Msubiri arudi ili akwambie kama anataka kuwa na wewe au la. Kama hataki kumbadili-sha mama yake basi achana naye na kila mtu aendelee na maisha yake.Omary Kasim,Rufiji

SWALI LA TOLEO LIJALO

Page 32: Haliuzwi - CCP Home Pageccp.jhu.edu/documents/Si Mchezo 63 Nov-Dec low res.pdf · Baadhi ya watu kwa mtazamo wa kidini hukataza kujichua hadi kufikia kusema kwamba ni dhambi. Wewe