Uharamu Na Hatari Ya Kupeana Mikono Na Wanawake - ´Allaamah as-Suhaymiy

3
Uharamu Na Hatari Ya Kupeana Mikono Na Wanawake Fataawa Za Wanachuoni Swali: Je, bibi kizee inajuzu kwangu kumsalimiakwa kumpa mkono, na inajuzu kumuangalia? ´Allaamah Swaalih as-Suhaymiyn: Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa sallam) alijiwa na mmoja katika ´ Maswahabah wa kike kumpa bay ah, na bay ah ni kitu kikubwa. ´ ´ Akamwambia ewe Mtume wa Allaah nipe mkono wako nikubayi, akamwambia Mtume Swalla (Allaahu alayhi wa sallam): ´ "Mimi sipeani mikono na wanawake." Na anasema Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa sallam): ´ "Mmoja wenu kudungwa kichwa kwa sindano ya chuma ni bora kwake kuliko kumgusa mwanamke asiyeruhusiwa kwake.Tahadhari na kupeana mikono, kwani hiyo ni njia inayopelekea katika Zinaa. Vipi unaweza kuridhia ikiwa ni binti yako, dada yako, mke wako, mama yako, mwanaume akampa mkono na wewe huku hushuhudia kama bwege? Akili zako ziko wapi? Haijuzu hilo. Ikiwa kuna mtu atasema, sisi hii ni ada yetu isitoshe roho zetu ziko safi - anadanganya huyo wallaahi roho yake siyo safi. Muongo mkubwa! Je roho yako ni safi kushinda roho za Maswahabah? Je roho yako ni safi kushinda roho za wake wa Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa ´ sallam) ambao wameamrisha na Allaah kutolegeza sauti zao asije kutamani yule mwenye maradhi katika nafsi yake. Sisi kwa usafi [wa nyoyo] hatujongelei kwa hata mmoja kati yao, vipi sasa tusemeje kuwakabili wanawake na kudai roho zetu ni safi, roho yako ingelikuwa safi [nzuri] ungelifuata muongozo wa Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa sallam). Hii ndo roho safi ambayo inakubali ´

description

Uharamu Na Hatari Ya Kupeana Mikono Na Wanawake - ´Allaamah as-Suhaymiy

Transcript of Uharamu Na Hatari Ya Kupeana Mikono Na Wanawake - ´Allaamah as-Suhaymiy

Page 1: Uharamu Na Hatari Ya Kupeana Mikono Na Wanawake - ´Allaamah as-Suhaymiy

Uharamu Na Hatari Ya Kupeana Mikono Na Wanawake

Fataawa Za Wanachuoni

Swali:

Je, bibi kizee inajuzu kwangu kumsalimiakwa kumpa mkono, na inajuzu kumuangalia?

´Allaamah Swaalih as-Suhaymiyn:

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alijiwa na mmoja katika Maswahabah wa kike kumpa bay´ah, na bay´ah ni kitu kikubwa. Akamwambia ewe Mtume wa Allaah nipe mkono wako nikubayi, akamwambia Mtume Swalla (Allaahu ´alayhi wa sallam):

"Mimi sipeani mikono na wanawake."

Na anasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

"Mmoja wenu kudungwa kichwa kwa sindano ya chuma ni bora kwake kuliko kumgusa mwanamke asiyeruhusiwa kwake.”

Tahadhari na kupeana mikono, kwani hiyo ni njia inayopelekea katika Zinaa. Vipi unaweza kuridhia ikiwa ni binti yako, dada yako, mke wako, mama yako, mwanaume akampa mkono na wewe huku hushuhudia kama bwege? Akili zako ziko wapi? Haijuzu hilo. Ikiwa kuna mtu atasema, sisi hii ni ada yetu isitoshe roho zetu ziko safi - anadanganya huyo wallaahi roho yake siyo safi. Muongo mkubwa! Je roho yako ni safi kushinda roho za Maswahabah? Je roho yako ni safi kushinda roho za wake wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao wameamrisha na Allaah kutolegeza sauti zao asije kutamani yule mwenye maradhi katika nafsi yake. Sisi kwa usafi [wa nyoyo] hatujongelei kwa hata mmoja kati yao, vipi sasa tusemeje kuwakabili wanawake na kudai roho zetu ni safi, roho yako ingelikuwa safi

Page 2: Uharamu Na Hatari Ya Kupeana Mikono Na Wanawake - ´Allaamah as-Suhaymiy

[nzuri] ungelifuata muongozo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hii ndo roho safi ambayo inakubali kufuata muongozo wa Mtume Swalla (Allaahu ´alayhi wa sallam). Ama kuwaiga makafiri wa magharibi na Ulaya anapokuja rafiki yako na wageni wako na kuanza kucheka "mke [wangu] anataka kukusalimia" Masikini! Akili zako ziko wapi? Halafu anakuja mke kukaa pamoja nao, kuanza kupiga vicheko, kupiga mzaha na kusema maneno ya ukhabithi na wewe uko hapo unaangalia. Huyu ni uduyuthi, duyuthi ndio anaweza kufanya namna hii. Kuwa tahadhari mja wa Allaah na uduyuthi kama huu. Usiseme roho yangu ni safi wala moyo wake [huyo mwanamke] ni msafi - hili si sahihi. Kuwa makini! Vile vile kumuangalia hata kama itakuwa inajuzu.

"Kila chenye kutupwa kina mwenye kukiokota."

Hakumuamrisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kijakazi ambaye alikuwa anajuzu kwake [kujiachia kwa mavazi n.k.], akamwambia "jisitiri ewe kijakazi."

Haijuzu kumwangalia hata bibi kizee. Na mimi najua kijana ambaye anamtamani hata bibi kizee mwenye miaka thamanini - kijana hataki wasichana anataka zake bibi kizee.

"Kila chenye kutupwa kina mwenye kukiokota."

Tahadhari, tena tahadhari tena tahadhari na kupeana mikono wanawake, au kuwatazama tazama. Akisema mtu sisi tunajua baadhi ya Madu´aat kwenye baadhi ya miji wapotofu ambao kila siku wanacheka na wanawake na wanakaa kati ya wanawake, wala nao, hawaishi ila kati ya wanawake, Da´wah yao haitoki ila tu ni kati ya wanawake. Na wanaruhusu filamu n.k., na wanasema mmoja wao tunataka wanaume na wanawake wataocheza filamu za kuigiza za Kiislamu, komeni kabisa Uislamu hausambazwi kwa filamu. Zinaitwa filamu, nini maana ya filamu? Uongo mtupu. Filamu maana yake ni "uongo". Baya zaidi kunajitokeza wajinga wanaume na wanawake, huyu anammithili Abu ´Ubaydah, ´Umar, Abu Bakr, ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhum). Na huyu anammithili ´Aaishah - ima [watu hao] ni manaswara, Shiy´ah, al-Maariqah au wajinga - wanammithili ummu ´Umaarah, ´Aaishah, Hafswah, Faatwiymah, Ummu Sulaym na wanamithili wanamithili. Je hii ni Da´wah ya Allaah, wallaahi hapana, hii ni Da´wah ya Iblisi, hii ni Da´wah ya Kishetani. Kuna kitabu kizuri cha Shaykh Bakr Abu Zayd (Rahimahu Allaah) cha hukumu ya

Page 3: Uharamu Na Hatari Ya Kupeana Mikono Na Wanawake - ´Allaamah as-Suhaymiy

filamu. Kabainisha hukumu ya hizi filamu. Usiangalii fataawa za kipotofu ambazo kazitolea fatwa ya kujuzisha mtu ambaye sipendi kumtaja jina lake hapa, kwa kuwa si watu wakutajwa. Fataawa zao ni za kipotofu.

Fatwa za kuhalalisha muziki ni za kipotofu, fatwa za kuwa filamu ni katika njia ya kufikisha Da´wah ni za kipotofu, fatwa za kuwa Anashiyd ni katika njia ya kueneza Da´wah ni za kipotofu, fatwa za kwenda kwa wachawi ili kutibiwa kwao ni za kipotofu, fatwa za kuchanganyika na wanawake, zote hizo ni za kipotofu. Kisa kilichonifika kabla ya siku mbili. Anasema huyu Daa´iyyah mjinga ambaye kawatolea wanawake fatwa, anasema je inaingia akilini Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwahutubia siku ya ´Iyd na kuwaambia [wanawake] "Haki nyinyi ni wapungufu wa akili na Dini"? Anasema "hapana hapana hili haliingii akilini."

Kisichoingia akilini ni maneno yako ewe mjinga msazi. Haya ndio hayaingii akilini. Ama maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni yenye kuingia akilini na ambayo ni wajibu kuyafanyia kazi. Mmoja katika hawa wajinga anasema "vipi tusadikishe hadiyth inayosema:

"Watu hawawezi kufaulu watapotawaliwa na mwanamke katika utawala wao."

Vipi inawezekana na sisi tunaona wanawake wafalme, wenye vyeo n.k. - tunajilinda kwa Allaah.

"Na atayejalia kunguru kuwa dalili yake atamuelekeza kwenye mzoga wa mbwa."

Tahadharini enyi waja wa Allaah na mambo kama haya na watu wenye kutoa fataawa za kumzulia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Tahadhari kwa hili. Tahadhari na fataawa kama hizi, fataawa kama hizi ni za kipotofu. Wanaichukua Hadiyth kwa kutumia akili zao fupi na uoni wao mbaya. Na ninakariri nilichoanza nacho.

"Kuwa mwangalifu ni kwa nani unaichukua Dini yako."

Imaam Muhammad bin Siriyn anasema:

"Hakika hii ni elimu ya Dini, kuwa mwangalifu ni kwa nani mnaichukua Dini yenu."

Page 4: Uharamu Na Hatari Ya Kupeana Mikono Na Wanawake - ´Allaamah as-Suhaymiy

Chanzo: http://youtu.be/93ZikKlMnrI