Tz Kukuza Soko La Madini Ya Vito Kwa Kufuata Nyayo Za Thailand Makala

download Tz Kukuza Soko La Madini Ya Vito Kwa Kufuata Nyayo Za Thailand Makala

of 7

Transcript of Tz Kukuza Soko La Madini Ya Vito Kwa Kufuata Nyayo Za Thailand Makala

  • 8/20/2019 Tz Kukuza Soko La Madini Ya Vito Kwa Kufuata Nyayo Za Thailand Makala

    1/14

     

     TANZANIA KUKUZA SOKO LA MADINI YA VITO NCHINI KWA

    KUFUATA NYAYO ZA THAILAND 

  • 8/20/2019 Tz Kukuza Soko La Madini Ya Vito Kwa Kufuata Nyayo Za Thailand Makala

    2/14

     

    SOKO LA MADINI YA VITO NCHINI THAILAND

     Thailand ni nchi iliyoendelea ikilinganishwa na nchi nyingine

    zinazoizunguka.Sababu kadha wa kadha huzungumzwa ikiwa ni pamoja na

    sera ya ubepari iliyosababisha mataifa ya magharibi kuwekeza nchini humo

    katika miaka ya awali ya Uhuru pamoja na Marekani kujenge miundo mbinu

    mingi ili kuitumia nchi hiyo kama kituo katika vita ya Vietnum.

    Aidha ugunduzi wa Gesi uliongeza kwa kiasi kikubwa sana maendeleo ya

     Thailand kwa kuwa na staha ya kusubiri mabadiliko ya sera ya uwekezaji

    katika nyaja hiyo na mwishowe kuweza kupata sera nzuri iliyowanufaisha

    kama taifa. 

    Baada ya kuwa na uhakika wa miundo mbinu na nishati ya kutosha, Thailand

    iliazimia kuanzisha uchumi imara wa viwanda vidogo,vya kati na vikubwa.

    Viwanda vya nguo na viatu ilikuwa ndiyo chaguo lao la kwanza pamoja na

    uanzishwaji wa vyuo vya kati (Polytechnic/Vocational Colleges  ).Hatua ya pili ,

    walitangaza vivutio vilivyopo nchini humo na kuruhusu nchi zinazopeleka

    watalii wengi zaidi kupata pasi ya kusafiria mara wafikapo nchini Thailand( on

    arrival VISA).

    Baada ya uchumi kuimarika, Serikali ya Thailand ilitunga sheria; shughuli

    zote za uchimbaji na biashara ya madini vito itakuwa chini ya wazawa nakupiga marufuku usafirishaji wa madini vito ghafi nje ya Thailand bali ina

    ruhusu uingizwaji wa madini ghafi ya aina yoyote ndani ya Thailand bila

    kibali.Hatua iliyofuata ni kutengwa kwa mji wa CHANTHABURI   kama kitovu

    cha biashara ya madini hususan madini ya Vito.

    Serikali ya Thailand kwa kushirikiana na taasisi za elimu walianzisha mafunzo

     ya utengenezaji na uvumbuzi wa mashine za bei nafuu zitakazotumika kukata,

    kuchonga na kung’arisha madini vito ili kuyaongeza thamani.Zoezi hili lilianza

    kwa kuwatumia Wahunzi wa Jadi.Kwa kuwatumia hao, ilikuwa rahisi kuweza

    kutengeneza mashine kwa kutumia tekinolojia ya ndani.Zoezi hilo lilipata

    mwitikio mkubwa na mashine mbalimbali na ujuzi tofauti wa kukata madini

     ya vito vilivumbuliwa zaidi.

    Nchi ya India pia ilifuata mfano huu kwa kuwachukua baadhi ya Wahunzi wa

    mashine za kutengeneza nguo na kuwapeleka nchini Thailand kujifunza

  • 8/20/2019 Tz Kukuza Soko La Madini Ya Vito Kwa Kufuata Nyayo Za Thailand Makala

    3/14

     

    namna ya kutengeneza mashine za kuchonga na kung’arisha madini  ya vito

    ikiwa ni pamoja na kujifunza kukata.

    Baada ya mafunzo husika walirudi na serikali ya India ikatenga mji wa Jaipur 

    kuwa eneo la kuanzia shughuli husika.Ndani ya muda mfupi Jaipur ukawa mji

    maarufu kwa uuzaji na ukataji wa madini ya vito.Itakumbukwa madini ya Tanzanite hukatwa kwa wingi na kuuzwa katika mji huu sababu kuu ikiwa ni

    hizo zilizotajwa –  Manguli wa Kukata,kuchonga na kung’arisha Madini ya Vito

    kwa ustadi wa hali ya juu pamoja na Gharama nafuu.

     Thailand imeendelea kuboresha biashara ya madini ya vito kwa kuanzisha

    huduma fungamano; vyuo vinavyotoa elimu ya Madini ya vito, viwanda

    vinavyotengeneza bidhaa (mapambo) zinazotumia madini ya vito, uanzishwaji

    wa maeneo rasmi ya uuzaji na ununuzi wa madini (Minerals Bourses),

    maonesho ya biashara ya madini ya vito mwaka mzima katika vipindi tofauti.

    Katika nchi zote zinazo jishughulisha na madini ya vito, ‘ Bourses ’   imekuwa

    ndiyo suluhisho la makusanyo badala ya ‘ Individual Broker and Delears’ .

    Masharti yamewekwa ya kuongeza kodi zaidi kwa ‘ Individual Broker and

    Delears’ na kuondoa au kupunguza kodi kwa wafanyabiashara katika

    ‘ Bourses ’ .

    Bourses ni eneo linalotengwa na kujengwa na serikali na kuandaa meza

    ambazo wafanyabiashara huruhusiwa kufanya mauzo na manunuzi ya madini

    na watumishi wa serikali kutoza kodi na kutoa vibali vyote katika eneo hilo.Piawafanyabiashara hupata fursa ya kujua bei halisi na masoko ya nje.Taarifa

    hizi hutolewa na watumishi wa serikali katika eneo hilo.Falsafa ya uanzishwaji

    wa bourse ulianzia katika nchi ya Ubeligiji na mantiki kuu ikiwa ni kufifisha

    biashara ya mtu mmoja mmoja katika maeneo mbalimbali na kuweka motisha

     ya wafanyabiashara kufanya biashara ya madini ya vito sehemu moja na pia

    kwa kutumia minada.1 

    1My personal point of view is that : ‘ Dealing with individual, means dealing with

    his/her mind set but dealing with organization means dealing with underlined formal

     procedures’ which are easy to control, improve and benefits the country in a multi - 

    effects. Therefore always let’s encourage economic groups’. 

  • 8/20/2019 Tz Kukuza Soko La Madini Ya Vito Kwa Kufuata Nyayo Za Thailand Makala

    4/14

     

    SOKO LA MADINI YA VITO NCHINI TANZANIA

    Samaruga Inc: Madini aina ya Rhodolite garnet

     Tanzania licha ya kuwa na wingi wa Madini ya Metali, pia imejaliwa kuwa na

    mashapo ya kutosha ya Madini ya vito.Uelewa wa wananchi katika

    kujishughulisha na biashara ya Madini, umejikita zaidi katika aina moja ya

    Madini.Watanzania wanauelewa mkubwa wa Madini ya metali kama dhahabu,Shaba na fedha.

    Hii imetokana na uhitaji wa Madini hayo kuwa wa kiasi kikubwa sababu

    Madini hayo mbali ya kutumika kama mapambo, hutumika pia katika nyanja

     ya viwanda na matumizi mengine ya vifaa vya kielektroniki.Uhitaji huu

    umesababisha Madini hayo kupata wawekezaji na wanunuzi wakubwa kwa

    urahisi. 

    Madini ya vito hayafahamiki sana miongoni mwa wa Tanzania ikilinganishwa

    na Madini ya Metali (Precious metal).Sababu kubwa ni kutokana na uhitajiwake kuwa mdogo ikilinganishwa na Madini mengine kwa sababu Madini ya

    vito hutumika kwa mapambo tu ukiachilia mbali kwa sasa ambapo kutokana

    na ukuwaji wa teknolojia, Madini ya Vito nayo yameanza kutumika katika vifaa

    vya viwandani.Hali hii imeongeza uhitaji wa Madini ya vito na hivyo soko lake

    kuimarika kama la Madini ya metali.Ni wakati sasa watanzania kujikita kwa

    dhati katika biashara ya Madini ya vito yapatikanayo Tanzania kwa wingi

  • 8/20/2019 Tz Kukuza Soko La Madini Ya Vito Kwa Kufuata Nyayo Za Thailand Makala

    5/14

     

    kama yalivyo ainishwa katika vitabu na majarida mbalimbali ikiwamo

    GEMSTONES OF TANZANIA( Google Gemstones of Tanzania by Gilay Shamika)

    Faida moja wapo kubwa ya Madini ya Vito ni kwamba mara baada ya

    kuchimbwa unaweza uza moja kwa moja (direct to the market like harvested

    crops ).Huitaji hatua nyingine kama dhahabu kuichakata na kuichoma ili upatezao la mwisho kwaajili ya kuuza.Kwa mantiki hii, uwekezaji katika shughuli ya

    biashara ya Madini ya vito ni rahisi sana ikilinganishwa na Madini ya metali.

    Mbali ya faida hiyo, pia kuna faida nyingine ambayo Madini ya vito

    inayo.Madini ya vito mengi yana bei kubwa sana zaidi ya Madini ya metali.Kwa

    ujumla, uwekezaji katika Madini ya vito ni njia mahususi katika kuondoa

    umaskini kwa wananchi na kuongeza mapato kwa serikali.

    Aidha suala la uharibifu wa mazingira hasa vyanzo vya maji, ni mdogo kwa

    sababu madini ya vito hayahitaji kemikali maana haya chakatwi kama madini ya metali.

     JITIHADA ZA SERIKALI ILI KUKUZA SOKO NA BIASHARA YA MADINI YA VITO NCHINI

    Samaruga Inc: Tanzanite the Uniqueness of Tanzania, the stones on the foot of Mount Kilimanjaro 

  • 8/20/2019 Tz Kukuza Soko La Madini Ya Vito Kwa Kufuata Nyayo Za Thailand Makala

    6/14

     

    Kitendo cha nchi nyingine kuwa na mauzo ya Madini yaliyo juu zaidi ya

     Tanzania na wakati huohuo Madini husika yanapatikana ama Tanzania tu au

    ndipo yalipo kwa wingi, imekuwa ni kitendawili cha muda mrefu.

    Wafanyabiashara pamoja na wataalamu wa Serikali wamekuwa wakijadili

    kuona namna ya kuboresha hali ya soko na mifumo nchini ili kuondokana na

    kitendawili hicho.Hivyo jitihada na udhati wa pande hizo mbili ni wa muhimu

    ili kufikia lengo la kupata jibu la kitendawili husika. 

    Kwa kufuatilia Taarifa zinazotolewa na Serikali katika vyombo vya habari ni

    wazi kuwa jitihada za Serikali zinazoendelea kuhusu kukuza soko la ndani na

    nje la Madini ya Vito ni kama ilivyo ainishwa.

    SHERIA YA MADINI YA MWAKA 2010

    Katika sheria hii mpya ya Madini, Serikali kwa makusudi kabisa ya kusaidia

    wananchi kiuchumi imeeleza wazi shughuli za Madini ya Vito kuwa chini ya

    Watanzania.Aidha sheria imetoa mwanya kwa wageni kujihusisha na shughuli

    za Madini ya Vito kwa shariti la kuingia ubia na wazawa.Sheria imezuia

    mwanya wa Wawekezaji wa nje kumiliki shughuli za uzalishaji na biashara ya

    Madini ya Vito kwa asilimia mia moja.

    Kuna mantiki mbili katika kipengele hiki cha sheria ya Madini.Kwanza ni

    kuinua wazawa kiuchumi kwa kuwapa fursa pana ya kuwekeza katika Madini

     ya vito bila kuingiliwa na wawekezaji wa nje mpaka pale wazawa wanapo amua

    kuingia ubia kwa utashi wao.

    Pili ni kutatua kitendawili husika cha utoroshwaji wa Madini ya Vito. Kwakuwa

    Madini ya Vito yapo katika miliki ya Wazawa ama kwa asilimia miamoja au

    kwa ubia, hakuna uwezekano wa wawekezaji kutorosha au kukiuka sheria bila

    wazawa kujua au kushiriki maana wao ndiyo wamiliki.Hivyo ikitokea kuna

    utoroshaji maana yake wazawa wameridhia kufanya hivyo na kuhujumu Taifa.

    Kero ya nchi nyingine kusafirisha Tanzanite zaidi ya Tanzania, kwa muhtadha

    wa hapo juu, ni juhudi zinazofanywa na watanzania wenyewe.Ni muda

    muafaka tutumie fursa tuliyopewa na Serikali ya kumiliki Madini ya Vito na

    kuiletea nchi manufaa na si kinyume chake.

    Sheria hii pia ndiyo iliyopo nchini Thailand ya Wazawa kumiliki Madini ya Vito

    na kuhusika kudhibiti utoroshwaji kinyume cha sheria.Wamiliki wote ndiyo

    waangalizi kwa niaba ya Serikali na anaekiuka hufutiwa Umiliki na

    kuadhibiwa.

  • 8/20/2019 Tz Kukuza Soko La Madini Ya Vito Kwa Kufuata Nyayo Za Thailand Makala

    7/14

     

    MAONESHO YA MADINI YA VITO JIJINI ARUSHA KILA MWAKA

    Kwa bahati mbaya au mazoea ni sekta moja tu ambayo inamaeneo rasmi ya

    Masoko kwa ajili ya bidhaa zao: Sekta ya Kilimo na Mifugo wana maeneo rasmi

    (minada na maghala ya Serikali) ya kuuza mazao na mifugo na serikalikusimamia kutoa Vibali pamoja na kutoza ushuru wa shughuli husika.

    Samaruga Inc: Madini ya Vito katika moja ya banda kwenye maonesho ya Madini ya Vito

    yaliyofanyika Mwaka huu jijini Arusha katika hoteli ya Mt.Meru.

    Sekta nyeti ya Madini kwa muda mrefu haina ama sehemu maalumu ya kuuza

    na kununua na vilevile hakuna minada kwa ajili ya Madini.

    Watu binafsi (dealers,brokers and jewellers) wanavibali kwaajili ya shughuli

    hiyo ya kununua na kuuza Madini.Ni vema, lakini bado kuna uhitaji wa eneo

    maalumu kwa yeyote mwenye Madini kuuza na kununua (minerals bourses)

    kwa uwazi ili kuzuia utapeli unaojitokeza kwa baadhi ya watu binafsi

    wanaoendesha shughuli hizo.

    Kwa kulijua hilo Serikali imeanzisha Maonesho ya Madini ya Vito kila mwaka

     jijini Aruha ili kukuza soko la Madini ya Vito. Wauzaji na wanunuzi wa ndani

    hufanya biashara zao kwa mujibu wa taratibu husika.Aidha maonesho hayo

     yamekuwa ni kiunganishi muhimu kati ya wafanyabiashara wa ndani na nje

    pamoja na kutangaza Madini ya Vito kwa wageni.

  • 8/20/2019 Tz Kukuza Soko La Madini Ya Vito Kwa Kufuata Nyayo Za Thailand Makala

    8/14

     

     Jitihada hii ya kuanzishwa kwa Maonesho ya Madini ya Vito yamekuza mauzo

     ya Madini ya Vito kadri maonesho yanavyoendelea.Mwakani maonesha hayo

     yatafanyika kuanzia tarehe 19-21/04/2016. Ni vema watanzania

    kuchangamkia fursa hii kwa kupata Taarifa zaidi Wizarani pamoja na Ofisi za

    Kanda za Madini.Aidha waweza tembelea tovuti ya www.arushagemshow.com 

    kwa Taarifa zaidi.

    Nchini Thailand, maonesho ya Madini ya Vito hufanyika mara tatu kwa

    mwaka.Aidha Thailand imetenga mji wa Chanthaburi kuwa eneo maalumu

    kwaajili ya kuuza na kununua Madini ya Vito.Vilevile katika jiji la Bangkok

    kuna maeneo Maalumu ya kuuza na kununua Madini ( Minerals bourses).

    Nchi za Asia,Ulaya na Marekani zinamaeneo hayo pamoja na Minada ya Madini

    kila baada ya muda kadhaa mara nyingi baada ya miezi 3.Minada ya Madini

    huvuta wanunuzi kutoka sehemu mbali mbali ikiwa ni pamoja na Madini

    kuuzwa kwa bei ya juu kutokana na ushindani katika Mnada.

    Niwazi kuwa Serikali ipo mbioni kuanzisha maeneo hayo ya kuuzia na

    kununulia Madini pamoja na Minada ya Madini nchini kutokana na maelezo

     yaliyotolewa na Kamishna wa Madini Eng.Paul Masanja wakati wa ufunguzi wa

    Maonesho ya Madini ya Vito Arusha kwa kuanzisha Jengo maalumu

    kuendeshea shughuli hizo. Maofisa wa Serikali watakuwepo ili baada ya

    kununua au kuuza wahusika wapate vibali husika (Madini and TRA Officials).

    Pamoja na mpango huo Kamishina wa Madini Eng.Paul Masanja ameanzisha

    pia utaratibu wa kisasa wa kuomba Leseni za Madini kwa njia yamtandao.Jambo hili nila kupongezwa kwa kwenda na wakati pamoja na kuwa

    mbunifu.

    WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA (TMAA)

    Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), kwa kuzingatia sababu tajwa,

    umekuwa ukitoa elimu ya Madini ya Vito kwa wananchi, kuanzisha Maabara

    za kisasa kwaajili ya kutambua Madini ya Vito kwa Gharama nafuu,kutoa bei

    elekezi kwa wananchi ili wauze kwa mujibu wa thamani halisi badala ya

    kutapeliwa na wafanyabiashara wasio waaminifu. 

    http://www.arushagemshow.com/http://www.arushagemshow.com/http://www.arushagemshow.com/

  • 8/20/2019 Tz Kukuza Soko La Madini Ya Vito Kwa Kufuata Nyayo Za Thailand Makala

    9/14

     

    Samaruga Inc : Mitambo yakisasa ya kupimia madini katika Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA)

    Maabara za Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania zinapatikana Dar es

    Salaam,Arusha,Mwanza na Mbeya.Kwa habari zaidi kuhusu huduma za

    Maabara ya Madini ya Vito na Metali zitolewazo na Wakala wa Ukaguzi wa

    Madini Tanzania (TMAA) tembelea Ofisi Kuu jijini Dar es Salaam Chole

    Road,Masaki (+255 22 2601819 ) pamoja na Ofisi za Kanda za Wakala kama

    zilivyotajwa hapo juu.Tovuti ya Wakala ni www.tmaa.go.tz. 

    Aidha mbali ya jitihada husika hapo juu, Wakala pia umesomesha wataalamu

    katika Nyanja hiyo ambao hushiriki katika maonesho ya Madini ya Vito jijini

    Arusha na kutoa elimu ya masoko na utambuzi wa Madini kwa kutumia Vifaa

    vya kisasa pamoja na kuhudumu Maabara tajwa.Jitihada hizo zimeongeza

    uelewa kwa wananchi na pia makusanyo ya maduhuli ya Serikali.

    Ni jukumu la watanzania kutumia taasisi za serikali kupata huduma

    mahususi.Baadhi ya Maabara nyingine ni ile ya Madini Dodoma, GST na

    SEAMIC.

    http://www.tmaa.go.tz/http://www.tmaa.go.tz/http://www.tmaa.go.tz/

  • 8/20/2019 Tz Kukuza Soko La Madini Ya Vito Kwa Kufuata Nyayo Za Thailand Makala

    10/14

     

    Samaruga Inc : Mitambo yakisasa ya kupimia madini katika Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA)

    Huduma fungamano: Mbali ya kuwa na soko au eneo maalumu kwa ajili ya

    biashara ya Madini,huduma pia hazina budi kupatikana hapo, Gem-min

    Lab,Gem-treatment,Gem-valuation and Pricing .Huduma hizi hurahisisha na

    kuvutia wafanyabiashara wengi na ni mnyumbuliko wa 4Ps ( Place, Product,

    Price and Promotion).Huduma fungamano husaidia mtu kununua Madini

    akiwa na uhakika wa anachonunua pamoja na thamani halisi.Huduma za

    kupima na kuthaminisha Madini kutolewa kwa bei nafuu.

    Nchini Thailand huduma fungamano za Madini ya Vito zipo kila mtaa na

    wanausemi kuwa huwezi nunua nguo bila kupima kama inakuenea na vivyo

    hivyo si busara kununua Madini bila kupima thamani yake kwa kuthibitisha

    na kujua ubora wake.

    Kwa minajili hiyo, upatikanaji wa huduma fungamano za kupima Madini

    sehemu yanapouzwa au kununuliwa ni wazi ule msemo wa Tanzania wa aliye

    uziwa cheni feki nae katoa fedha feki hauta dhihirika maeneo hayo  

    (Minerals bourses) maana cheni feki hazitaletwa kwasababu Madini

     yanapimwa kuthibitishwa.

  • 8/20/2019 Tz Kukuza Soko La Madini Ya Vito Kwa Kufuata Nyayo Za Thailand Makala

    11/14

     

    Samaruga Inc : Mitambo yakisasa ya kupimia madini katika Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) 

    TANSORT

     Tanzania Sorters (Tansort) kwa tafasiri ya moja kwa moja ni Wachambuzi wa

    Madini ya Vito Tanzania. Sort: ni kitendo cha kuchambua Madini ya Vito na

    kuyatenga kwa mujibu wa madaraja ya ubora wakwanza, wapili, watatu,wanne

    na mwisho makapi.

    Mara baada ya kuanzishwa kwa STAMICO ili kusimamia shughuli za

    uendeshaji migodi na biashara ya Madini nchini, Serikali iliona umuhimu wa

    kuwa na kitengo hicho ili kuisaidia kuthaminisha Madini ya Vito na kujua

    thamani halisi kwa ajili ya kodi.

    Baada ya muda Serikali iliona umuhimu wa kuongeza thamani ya Madini ya

    Vito kwa kuyakata na kung’arisha, hivyo ilianzishwa pia Tanzania Cutters  –  

    Almasi (Tancut-Almasi).Mlio wengi mtakumbuka pia Band ya Music ya shirika

    hilo ikiitwa Tancut Almasi Band   –  Wazee wa kukata na kung’arisha. 

  • 8/20/2019 Tz Kukuza Soko La Madini Ya Vito Kwa Kufuata Nyayo Za Thailand Makala

    12/14

     

    Vitengo hivi viwili vilifanyakazi na mwishowe TANSORT shughuli zake

    mahususi kwa ajili ya kuthaminisha Almasi za Mgodi wa Mwadui zilihamia

    Uingereza ambapo mauzo yalikuwa yakifanyika mpaka hivi karibuni kitengo

    kilipo rejea na utaratibu wa sasa ni mtumishi kuongozana na Mzigo mpaka

    sokoni nchi ambayo itauzwa ili kudhibiti Mapato ya Serikali.

    Kitengo hiki kinafanyakazi nzuri sana kwa mujibu wa Taarifa ambazo

    zimekuwa zikitolewa katika vyombo vya habari hususan kipindi Wizara ya

    Madini inapotoa Taarifa ya utendaji kwa kila idara.

     Tancut Almasi ilikufa ila uhitaji wa kukata,kuchonga na kung’arisha Madini ya

    Vito ni mkubwa sana.Jijini Arusha ambapo ndiyo soko kuu la Madini ya Vito,

    uhitaji huo unaonekana dhahiri.Ni fursa kwa sekta binafsi kuchangamkia eneo

    hili na kuwekeza kwa kutumia mashine za bei ndogo wanazotumia Jaipur

    zinazo gharimu takriba dola 800 kwa mashine moja.

    Hivyo tutumie kitengo cha TANSORT, TMAA na Ofisi za Madini Kanda katika

    kutambua thamani za Madini ya Vito.Itategemea na taasisi ipi kati ya hizo ipo

    karibu na eneo lako. Hizi ni jitihada za Serikali kuleta huduma karibu na

    wananchi katika kukuza biashara ya Madini ya Vito.

    Ukipata jiwe lenye rangi yeyote, peleka katika taasisi hizo kwa uchunguzi

    huenda una mali ya thamani mikononi mwako.

    STAMICO

    STAMICO ni moja kati ya taasisi kongwe nchini zilizo anzishwa mara baada ya

    uhuru kuisaidia Serikali kuu katika jitihada za kumiliki na kukuza uchumi wa

    nchi.Baada ya sheria mpya ya Madini ya mwaka 2010, STAMICO ilihuishwa

    kuwa msimamizi wa Hisa za serikali katika migodi mikubwa itakayo anzishwa

    au kuhuishwa Leseni zao mara baada ya sheria husika.Tumeshuhudia mpaka

    sasa STAMICO ikimiliki hisa katika Mgodi wa TanzaniteOne Mkoani Manyara

    Mererani.Pia ikimiliki kwa asilimia miamoja Mgodi wa STAMIGOLD uliopo

    Biharamuro.

    Katika kukuza Soko la Madini ya Vito, STAMICO imeamua kumiliki asilimia

    hamsini ya Mgodi wa TanzaniteOne katika kuendesha shughuli za uchimbaji

    na biashara ya Tanzanite kwa kushirikiana na Wazawa wanaomiliki asilimia

    hamsini pia.Juhudi zinaonekana katika kusimamia soko la Tanzanite

    zitokanazo na mgodi husika.

  • 8/20/2019 Tz Kukuza Soko La Madini Ya Vito Kwa Kufuata Nyayo Za Thailand Makala

    13/14

     

    CHUO CHA JIMOLOJIA JIJINI ARUSHA – TANZANIA GEMOLOGICAL CENTRE

    Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imeanzisha chuo cha kisasa

    kinachotoa mafunzo yahusuyo elimu ya Madini ya Vito. Wahitimu katika chuo

    hicho wanapata ujuzi wa kutambua,kupanga madaraja ya Madini vito,kuthaminisha Madini ya vito pamoja na uwezo wa kutumia mashine za

    kukata,kuchonga na kung’arisha Madini ya Vito. Hii ni hatua kubwa

    inayopaswa kupongezwa. Aidha ni wajibu wa Sekta binafsi kuwatumia

    Wahitimu katika kuwekeza kwenye fursa hii ya Madini ya Vito.Chuo husika

    pia kinatoa huduma za Kimaabara kwa wananchi wanaohitaji kutambua

    Madini yao ya Vito.

    Samaruga Inc: Wanafunzi wakijifunza aina ya Madini ya Vito

    Kwa maelezo yote hapo juu, inaonesha ni kwa namna gani Serikali

    imedhamilia kukuza shughuli na biashara ya Madini ya Vito

    nchini.Kilichobakia ni utayari wa sisi wananchi kutumia huduma za taasisi za

    serikali tajwa hapo juu na pia kuanza kujikita katika biashara ya Madini ya

    Vito ambayo haijakuwa nchini.

    Pia fursa katika uwekezaji wa kukata na kung’arisha Madini ya Vito,

    unahitajika kupewa mkazo kwa kutoa elimu kwa wananchi ili watambue na

    kuwekeza.

    CHUO CHA MADINI DODOMA

    Miongoni mwa taasisi za Serikali zilizotoa mchango mkubwa katika kuimarisha

    Wizara ya Nishati na Madini ni chuo cha Madini Dodoma.Chuo hiki ndicho

    chuo cha mwanzo kabisa nchini kutoa mafunzo ya Madini pamoja na Maabara

  • 8/20/2019 Tz Kukuza Soko La Madini Ya Vito Kwa Kufuata Nyayo Za Thailand Makala

    14/14

     

     ya kupima Madini na Sampuli za udongo pamoja na miamba.Mpaka leo hii

    chuo hicho bado kinatoa huduma hizo na kwasasa zimeboreshwa zaidi.

    Serikali imeongeza kozi za Madini zinazotolewa chuoni hapo na ufanisi wake

    unaonekana kwa kutoa wahitimu walio bobea wa ngazi ya kati.Migodi mingi

    nchini inapendelea kuchukua wafanyakazi waliohitimu chuo cha MadiniDodoma (MRI) pamoja na wanao hitimu VETA kwaajili ya nafasi za ngazi ya

    operators.

    Aidha huduma za Maabara ambazo zimekuwa zikitolewa tangu miaka ya

    1970’s zinaendelea katika jitihada za kuimarisha huduma za Madini kwa

    wananchi.

    GST

    Geological Survey of Tanzania (GST) ni muhimili muhimu sana katika kukuzabiashara na shughuli za Madini nchini.

    Huduma ya uhakiki wa mashapo ya Madini nchini kote ni muhimu ili

    kutambua maeneo yenye Madini na kiasi husika kwa ajili ya uendelezaji na

    uwekezaji wa uhakika badala ya kubahatisha.

    Uhakiki na Upimaji wa maeneo yenye Madini unaoendelea kufanywa na GST

    nchini, unaongeza kasi ya uwekezaji na mipango ya serikali kuhusu sekta ya

    Madini.

    Wananchi tutumie huduma za GST kujua kiasi kilichopo kwenye maeneo yetu

     yenye Madini.

    Fanya sasa biashara ya Madini ya Vito ambayo ni changa nchini (niche market)

    na kuepuka ushindani uliopo katika biashara nyingine .

    Kwa jitihada hizi za Serikali, ni wazi kuwa mwisho wa ule usemi wa

    ALIEUZIWA ‘CHENI FEKI’ KATOA ‘FEDHA FEKI’   utafikia ukomo kutokana na

    huduma fungamano za kutambua na kupima ubora wa madini zitolewazo na

    taasisi za serikali.

    Mwandishi wa Makala;

    Eng.Gilay Charles Shamika [email protected]

    Mhandisi Mwandamizi Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA)

    mailto:[email protected]:[email protected]