KANUNI ZA UTHIBITISHAJI MADEREVA NA USAJILI WA ......Ada ya Maombi 10.-Malipo ya vyeti yatafanyika...
Transcript of KANUNI ZA UTHIBITISHAJI MADEREVA NA USAJILI WA ......Ada ya Maombi 10.-Malipo ya vyeti yatafanyika...
KANUNI ZA UTHIBITISHAJI MADEREVA NA USAJILI WA WATENDAJI WA
TRENI ZA MWAKA 2019
MPANGILIO WA KANUNI
Kanuni Jina
SEHEMU YA KWANZA
MAELEZO YA AWALI
1. Jina la Kanuni.
2. Matumizi ya Kanuni.
3. Tafsiri ya Kanuni.
SEHEMU YA PILI
UTHIBITISHAJI WA MADEREVA
4. Uthibitishaji wa Madereva.
SEHEMU YA TATU
UTARATIBU WA KUPATA VYETI
5. Maombi ya Cheti.
6. Utoaji wa Cheti.
7. Kamati ya Uthibitishaji.
8. Majukumu ya Kamati ya Uthibitishaji.
SEHEMU YA NNE
UTOAJI USIMAMISAJI NA UFUTAJI WA CHETI
9. Utoaji wa Cheti cha Umahiri wa Dereva.
10. Ada ya Maombi.
11. Kibali cha Kuvuka Mipaka.
12. Alama Jumuishi.
13. Kusimamisha au Kufuta Cheti.
14. Kuhuisha Cheti.
15. Kuhamisha Matumizi ya Cheti.
SEHEMU YA TANO
USAJILI WA WATENDAJI WA TRENI
16. Maombi ya Usajili.
17. Matakwa ya Usajili.
18. Utoaji wa Vitambulisho vya Usajili.
19. Kuhamisha Matumizi ya Kitambulisho.
20. Kupotea kwa Kitambulisho.
SEHEMU YA SITA
MASHARTI KWA WATENDAJI WA TRENI
21. Masharti kwa Madereva na Treni Gadi.
22. Katazo kwa Watendaji wa treni.
SEHEMU YA SABA
MAKOSA NA ADHABU
23. Makosa na adhabu
24. Uwezo wa kufifisha makosa
MAJEDWALI
NOTISI YA SERIKALI………………imetolewa …………………
SHERIA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (SHERIA NA. 3
YA MWAKA 2019)
Kanuni
(Zimetengenezwa chini ya kifungu cha 45)
KANUNI ZA UTHIBITISHAJI MADEREVA NA USAJILI WA WATENDAJI WA
TRENI ZA MWAKA 2019
SEHEMU YA KWANZA MAELEZO YA AWALI
Jina la kanuni 1. Kanuni hizi zinaweza kutambuliwa kama Kanuni za Uthibitishaji wa Madereva wa
Treni na Usajili wa Watendaji wa Treni za Mwaka 2019 Matumizi ya Kanuni 2. Kanuni hizi zitatumika kudhibiti madereva na Watendaji wa treni
Tafsiri 3. Katika kanuni hizi, endapo matakwa hayatahitaji vinginevyo:-
Sheria Na. 3 ya mwaka 2019
“Sheria” inamaanisha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini;
Act No. 3 of 2019 “Mamlaka” inamaanisha Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Ardhini (LATRA) kama
ilivyoanzishwa kupitia kifungu cha 4 cha sheria “Cheti cha Umahiri” kinamaanisha kibali kilichotolewa na Mamlaka kwa Dereva wa treni
GN. No…… “cheti” inamaanisha cheti kinachotolewa kwa dereva wa treni;
“Kamati ya Uthibitishaji ” inamaanisha kamati yenye jukumu la kuthibitisha madereva wa sekta
inayodhibitiwa kupitia sehemu ya 7 ya kanuni hizi
“Watendaji” inamaanisha Dereva, Treni Gadi, Mtunza Behewa na Mkaguzi wa Tiketi;
Sheria Na. 3 ya Mwaka
2019
“Mkurugenzi Mkuu” inamaanisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka chini ya kifungu cha 15 cha
sheria
“nyaraka” inamaanisha nyaraka yeyote iliyotolewa au kupokelewa na Mamlaka;
“Tabibu” inamaanisha Tabibu aliyesajiliwa na “Baraza la Matabibu la Tanganyika” au aliyethibitishwa na mamlaka kukagua madereva wa treni;
“Alama Jumuishi” inamaanisha mfumo wa kuratibu umahiri wa dereva ambapo alama
zitapunguzwa kulingana na makosa na endapo alama zitakuwa chini ya kiwango kilichowekwa
kikanuni Dereva atafutiwa usajili
Kifungu Na. 95 “Dawa za kulevya” inabeba maana kama ilivyofafanuliwa kwenye Sheria ya Kuzuia Usafirishaji
wa Dawa Haramu (Drugs and Prevention of Illicit Traffic in Drugs Act);
“Afisa wa Mamlaka” inamaanisha Mkurugenzi, Meneja au Afisa yeyote wa Mamlaka;
“Abiria” inamaanisha mtu yeyote anayesafiri kwenye treni na ana Tiketi halali ya kusafiria;
“rejista” inamaanisha mchanganuo wa taarifa za usajili wa Watendaji wa treni
“ratiba” inamaanisha nyaraka iliyotolewa na Mtoa Huduma za reli ikionyesha muda wa treni
kuanza safari na muda wa kufika kwenye vituo vilivyoainishwa;
“Dereva wa Treni” Mtu aliyethibitishwa na Mamlaka kuendesha treni;
“treni” inajumuisha kichwa cha treni, kichwa cha treni kinachopanga mabehewa, kichwa cha
treni na mabehewa au kiberenge kilichoruhusiwa kusafiri;
SEHEMU YA PILI
UTHIBITISHAJI WA MADEREVA Uthibitishaji Madereva
4-(1) Mtu yeyote hatoruhusiwa kuendesha treni pasipo kuwa amethibitishwa na Mamlaka.
(2) Dereva atakayeendesha treni na kuvuka mipaka ya Tanzania Bara atatakiwa kuhakikisha
ana vitu vifuatavyo -
(a) Cheti cha usajili kilichotolewa na Mamlaka kwa mujibu wa kanuni hizi; au (b) Cheti cha Usajili kilichotolewa na mamlaka husika kwenye nchi anakotoka.
SEHEMU YA TATU UTARATIBU WA KUPATA VYETI Maombi ya Cheti 5.-(1) Mtu yeyote anayekusudia kupata usajili wa Mamlaka kuwa Dereva wa treni anatakiwa
kuwasilisha maombi kwa Mamlaka katika muundo ulioonyeshwa kwenye Jedwali la Kwanza
(2) Maombi yatakayotumwa kwa mujibu wa kanuni ya (1) yataambatana na:
(a) nakala iliyothibitishwa ya cheti cha kuzaliwa au nyaraka nyingine ; (b) nakala iliyothibitishwa ya cheti cha elimu ya sekondari; (c) nakala iliyothibitishwa ya cheti cha mafunzo ya awali ya udereva wa treni toka kwenye
chuo cha reli kinachotambuliwa na serikali; (c) uthibitisho toka kwa mwajiri juu ya utendaji kazi usiopungua miaka miwili kwenye
udereva wa treni; (e) uthibitisho wa malipo ya ada ya usajili kwa Mamlaka; (f) Ripoti ya afya ya hivi karibuni iliyotolewa na Tabibu.
(3) bila kuathiri masharti ya kanuni ya (1) dereva yeyote - (a) aliyemaliza mafunzo ya awali ya kuendesha treni; na (b) mwenye uzoefu wa kuendesha treni usiopungua miaka mitano Atawasilisha maombi yake kwa utaratibu maalum utakaowekwa na Mamlaka.
Utoaji wa Vyeti
6. - (1) Mamlaka baada ya kujiridhisha kwamba mwombaji amekidhi matakwa ya maombi ya vyeti, itatoa cheti kwa mwombaji.
(2) Cheti kitakachotolewa na mamlaka chini ya kanuni (1) kitabeba taarifa zifuatazo–
(a) Jina na Anwani ya dereva wa treni aliyethibitishwa; (b) Muda wa uhai wa cheti husika; na (c) Masharti ya cheti.
Kamati ya
Uthibitishaji 7. -(1) Mkurugenzi Mkuu atateua kamati ya Uthibitishaji itakayoundwa na wajumbe wafuatao-
(a) Afisa Mkaguzi wa reli; (b) Mkaguzi wa vichwa vya treni; na (c) Mwanasaikolojia au Tabibu. (2) Kamati hii itadumu kwa kipindi cha miaka mitatu na inaweza kuongezewa kipindi kingine
kimoja. (3) Mamlaka itaandaa mwongozo wa namna Kamati itakavyotekeleza majukumu yake kwa
mujibu wa kanuni hizi.
Majukumu ya Kamati
ya Uthibitishaji 8- (1) Majukumu ya Kamati yatakuwa kama ifuatavyo:
(a) Kuchambua maombi ya uthibitishaji wa madereva yaliyowasilishwa;
(b) Kuandaa taarifa ya uchambuzi wa maombi; na
(c) Kutekeleza majukumu mengine watakayopangiwa na Mkurugenzi Mkuu
SEHEMU YA NNE
UTOAJI USIMAMISAJI NA UFUTAJI WA CHETI Utoaji wa Cheti cha
Umahiri wa Dereva 9.-(1) Mamlaka baada ya kujiridhisha na uwasilishaji wa maombi kwa mujibu wa kanuni hizi,
itatoa cheti kwa ajili cha umahiri wa Dereva
(2) Kwa mujibu wa kanuni hizi Umahiri wa madereva utapimwa kulingana na:
(a) Utaratibu uliowekwa kwenye Jedwali la Pili la kanuni hizi; na
(b) Utakuwa na jumla ya alama jumuishi 100 kama inavyoonekana kwenye
Jedwali la Pili:
(3) Cheti cha Umahiri wa madereva kitatolewa kila baada ya miaka miwili
Ada ya Maombi 10.- Malipo ya vyeti yatafanyika kwa kufuata mchanganuo uliowekwa kwenye
Jedwali la Tatu la kanuni hizi .
Kibali cha Kuvuka
Mipaka 11.-(1) bila kuathiri masharti ya kanuni ya 5, Mamlaka inaweza kutoa kibali kwa madereva
wanaoendesha treni kuvuka mipaka ya Tanzania bara kwa mujibu wa mikataba ya makubaliano
ya kimataifa.
(2) Dereva wa treni wa nje ya nchi anayekusudia kuingia ndani ya mipaka ya Tanzania
atawasilisha maoni yake kwa njia za kielekroniki kama inavyoonekana kwenye Jedwali la
Nne.
Alama Jumuishi 13.-(1) Dereva wa treni atawajibika kufuata utaratibu wa alama jumuishi kama ulivyowekwa
kwenye Jedwali la Tano.
(2) Mamlaka itarekodi alama jumuishi zilizopunguzwa kwa Dereva kutokana na
makosa mbalimbali kwa kipindi cha miaka miwili tangu kukabidhiwa cheti.
(3) alama zitakazopunguzwa kwenye cheti cha umahiri wa dereva zitakuwa kwenye muundo
ulioonyeshwa kwenye Jedwali la Tano:
Kusimamisha au
Kufuta Cheti 14.-(1) endapo dereva atakiuka kanuni hizi, Mamlaka inaweza kufuta au
kusimamisha matumizi ya cheti chake kama ilivyoainishwa kwenye Jedwali la Tano
(2) bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo (1), mamlaka itatoa notisi ya siku
saba kueleza sababu za kufuta au kusimamisha matumizi ya cheti
(3) Endapo Mamlaka haitaridhika na maelezo ya dereva, inaweza kufuta au kusimamisha
matumizi ya cheti cha uthibitisho wa dereva;
(4) dereva wa treni aliyefutiwa au kusimamishiwa matumizi ya cheti atatakiwa:-
(a) endapo amesimamishiwa matumizi ya cheti, asiendeshe treni kwa kipindi chote
alichosimamishwa; na
(b) endapo amefutiwa cheti, atakoma kuendesha treni kuanzia tarehe ya kufutwa rasmi kwa
cheti husika na atatakiwa kukabidhi cheti hicho kwa mamlaka haraka iwezekanavyo
(5) Endapo mtu yeyote hatokubaliana na maamuzi ya Mamlaka anaweza kuomba marejeo ya
shauli lake kwa mujibu wa sheria ndani ya siku kumi na nne tangu maamuzi hayo kutolewa.
Kuhuisha Cheti 15.-(1) Dereva wa treni anayekusudia kuhuisha cheti chake cha umahiri anaweza
kuwasilisha maombi kwa mamlaka kufanya hivyo ndani ya siku sitini kabla ya cheti hicho kuisha
muda wake;
(2) Maombi ya kuhuisha cheti yafanyike kwa kuambatanisha vifuatavyo:
(a) Nakala ya cheti kinachoisha muda wake;
(b) Nakala ya uthibitisho wa malipo ya ada ya usajili kama ilivyoainishwa kwenye Jedwali la
Tatu; na
(c) Ripoti ya afya ya hivi karibuni kutoka kwa Tabibu.
Kuhamisha Matumizi
ya Cheti 16.- Cheti cha umahiri kinachotolewa kwa mujibu wa kanuni hizi hakiruhusiwi kuhamishiwa
matumizi kwa mtu mwingine.
SEHEMU YA TANO USAJILI WA WATENDAJI WA TRENI
Maombi ya Usajili 17.- Mtu yeyote anayekusudia kufanya kazi za utendaji ndani ya treni atawasilisha maombi kwa
Mamlaka kama ilivyoelekezwa kwenye Jedwali la Sita la kanuni hizi;
Viambatanisho vya Maombi ya Usajili
18.- Maombi ya usajili wa Watendaji wa treni yataambatana na vifuatavyo:-
(a) barua ya utambulisho toka kwa mwajiri;
(b) ripoti ya afya ya hivi karibuni kutoka kwa Tabibu; na (c) Cheti cha mafunzo kwenye kazi anazofanya. Utoaji wa Vitambulisho vya Usajili
19.- Mamlaka inaweza -
(a) Endapo imejiridhisha kwamba mwombaji amekidhi masharti ya kanuni ya 18 , itatoa
cheti kama ilivyooneshwa kwenye Jedwali la Saba; au (b) kukataa kutoa usajili na kumfahamisha mwombaji sababu za kufanya hivyo. Kuhamisha Matumizi ya Kitambulisho
20- Kitambulisho cha Usajili kinachotolewa kwa mujibu wa kanuni hizi hakiruhusiwi
kuhamishiwa matumizi kwa mtu mwingine. Kupotea kwa
Kitambulisho 21. Endapo kitambulisho kilichotolewa kwa mujibu wa kanuni hizi kitapotea, kuibiwa au
kuharibika; Mamlaka baada ya kujiridhisha itatoa kwa Mhusika nakala nyingine ya
kitambulisho.
SEHEMU YA SITA
MASHARTI Masharti kwa
Madereva na
Treni Gadi
22.-(1) Dereva na treni gadi wanatakiwa kuhakikisha yafuatayo-
(a) Wanafuata matakwa ya ukomo wa mwendokasi uliowekwa; (b) Wanahakikisha Milango imefungwa kabla ya kuondoa treni ya abiria. (c) Wanafuata ratiba iliyopangwa;
Katazo kwa
Watendaji wa
treni
23.-(1) Watendaji wote wa treni wakiwa kwenye majukumu yao wanakatazwa kuzingatia
yafuatayo-
(d) Kutozidisha abiria au mizigo juu ya uwezo wa behewa; (e) Kujaza batli na kufuata ratiba iliyopangwa; (f) Kuvaa kitambulisho cha kazi; (g) Kuvaa sare za kazi; (h) Kutokuwa na ulevi au uraibu wa aina yeyote; (i) Kutii amri halali ya Afisa wa Mamlaka; (j) Kutotumia lugha ya matusi au yenye kudhalilisha mbele ya abiria.
SEHEMU YA SABA
MAKOSA NA ADHABU Makosa na adhabu 24.-(1) Mtu atakayekiuka masharti ya kanuni hizi atakuwa ametenda kosa na endapo atatiwa
hatiani atawajibika kulipa faini isiyopoungua elfu hamsini na isiyozidi laki 1 na atafungwa jela
kwa muda usiopungua mwezi mmoja na usiozidi mwaka mmoja au vyote kwa pamoja Uwezo wa kufifisha
makosa (2) Bila kuathiri matakwa ya kanuni hizi, mtu atakayefanya makosa kwa mujibu wa kanuni hizi,
mamlaka inaweza kabla ya kumfikisha mahakamani; kufifisha makosa husika na kumpa uwezo
mtuhumiwa kulipa faini kama ilivyoonyeshwa kwenye Jedwali la Nane la kanuni hizi
Mamlaka itaweza kufifisha makosa yaliyoanishwa chini ya kanuni hizi endapo Mhusika atakiri
kwa maandishi kwamba ametenda makosa hayo na ataomba mamlaka iyafifishe
(3) Endapo mamlaka itafifisha makosa chini ya kanuni hizi, utaratibu ulioelezwa kwenye kanuni
ndogo (1)
(a) Utawekwa kwenye maandishi na utaambatanishwa kwenye wasilisho la masharti na
nakala atapewa Mhusika endapo atahitaji
(b) Utaeleza aina ya kosa lililotendwa, kiasi cha pesa kinacholipwa kama faini na tarehe ya
kulipa pesa hiyo;
(c) Utakuwa wa Mwisho na hautakatiwa rufaa mahakamani;
(d) Utakuwa ni sawa na hukumu ya kimahakama;
(2) Endapo mtu yeyote hataridhishwa na maamuzi yaliyotolewa chini ya kanuni ndogo (1)
anaweza ndani ya siku thelathini tangu kutolewa agizo hilo, kukataa rufaa dhidi ya
maamuzi hayo kwenye mahakama kuu kupitia masharti ya Sheria ya Mwenendo Wa
Makosa ya Jinai ya mwaka 1985 na mabadiliko yake yatatumika kwenye rufaa hiyo kana
kwamba ni uamuzi uliotolewa na mahakama ya wilaya yenye mamlka ya kufanya hivyo
(4)Kosa lolote lililofifishwa chini ya kanuni hizi halitakuwa na uhalali wa kupelekwa
mahakamani na endapo Mhusika atashitakiwa na kosa hilo hilo ufifishaji chini ya kanuni hizi
utatolewa kama ushahidi kuhusu shauli hilo.
MAJEDWALI
Jedwali la Kwanza
(Limetengenezwa chini ya Kanuni ya 5(1))
TRAIN DRIVING CERTIFICATE APPLICATION FORM
(a) a certified copy of birth certificate or any relevant document for proof of birth;
(b) a certified copy for successful completion of at least secondary school education;
(c) a certified copy of a successful completion of basic
(d) training in locomotive driving from a recognized railway institute;
(e) proof of completion of at least two years practical and
(f) internship training in railway operation;
(g) proof of payment of certification fees; and
(h) a recent medical examination report from a medical practitioner
Passport size
photo
PART 1: Applicant’s Details
1.1. Surname:…………………………………………………………………………..
1.2. Name(s):………………………………………………………………………….
1.3. Sex:
Male: …………… Female:…………………….
Date of birth (DD-MM-YYYY):……………………………………...............................................
1.4. Place of birth: ………………………………………………………
1.5. Nationality: ………………………………………………………...
1.6. Language spoken………………………………………………………
1.7. Postal address………………………………………………….
1.8. Application for:
a. First issue: …………… b. Replacement:………………………….
c. Renewal: …………….
NIDA Identification Number:……………………………………………………………………………………
Date of first issue …………………………………
Expiry date:……………………………………………………..
PART 2: List of documents to be appended
PART 3 Declaration
I hereby declare that to the best of my knowledge that all the information provided in this
application is true.
Applicant’s Signature …………………………….. Date………………………
12
JEDWALI LA PILI
(Limetengenezwa chini ya Kanuni ya 9 (2) (a))
Certificate of competence
The United Republic of Tanzania
Land Transport Regulatory Authority
(LATRA)
CERTIFIED TRAIN DRIVER
Passport size
photo
Drivers Name:: …………………………………….
Staff ID No. …………………………………
Department: …………………………….
CERTIFICATION:
The bearer of this card is a Certified Train Driver as per LATRA requirements.
Date of Issue ………………….. Signature
Expiry Date …………………. ……………………………..
Serial No. …………………………… Director General
13
JEDWALI LA TATU
(Limetengenezwa chini ya Kanuni ya 11)
Application Fee
S/N Particular Amount
1. Application Fee 60,000/-
2. Replacement Fee 80,000/
Note: These fee items are paid per the term of the certification
14
JEDWALI LA NNE
(Limetengenezwa chini ya Kanuni ya 12(2))
Application Form – Transit Permit for Train Driver
Part 1. Personal Details
1. First Name(s) …………………………………………..
2. Surname ………………………………………………..
3. Postal Address………………………………………….
Town/City………………………………………………
4. Nationality……………………………………………...
Place of Birth…………………………………………...
Date of birth Day………Month ………………Year…………………………..
5. Gender: Male Female
Part 2. Other Information
Telephone number……………………………………….…………………..
Email………………………………………………………………….………
Purpose of the visit……………………………………………………………
Destination ………………………………Country ………………………….
Duration of stay in days ……………………………………………………..
Entry date ………………………………Expected return date………………
Employer’s……………………………………………………………………….
Employer’s Contact Address…………………………Tel. No…………………………
Part 3. License Details
1. Driver’s Certificate number …………………………………………..……………
2. Issuing Authority……………………………………………………………………..
3. Date issued ……..…………………………………………..………………………..
4. Expiry date ……………………………………………………………………...
Part 4. Declaration
I hereby declare that to the best of my knowledge that all the information provided in this application
is true.
Applicant’s Signature …………………………….. Date……………………………
Passport size
photo
15
JEDWALI LA TANO
( Limetengenezwa chini ya Kanuni ya 13(1))
Demerit Points
1. In these Regulations, “Accumulated demerit points” means the total demerit points in
a driver’s record acquired as a result of offences committed within any period of two
years.
2. The authority shall take the following decision in relation to accumulated demerit
points:
(a) suspend for the period of three months Driver’s Certificate of competence of the
driver who’s accumulated demerit points are between forty and fifty points;
(b) suspend for the period of six months Driver’s Certificate of competence of the
driver who’s accumulated demerit points are between thirty and forty;
(c) revoke Driver’s Certificate of competence of the driver whose accumulated
demerit points are below thirty; and
(d) any driver whose Certificate of competence has been revoked, shall not be
allowed to apply for the same certificate within the period of two years.
3. A table indicating type of offences and number of points attached to each offence is
here under:
S/N
NATURE OF OFFENCE NUMBER OF
DEMERIT POINTS
1. Driving under the influence of alcohol or any other narcotic substances exceeding set limit. 20
2. Driving above sectional running speed 15
3. Failure to observe and obey safety signs and signals 15
4. Driving the train while passenger’s door is open 10
5. Improper filling of the logbook 10
6. Driving a train without a line clear ticket 10
7. Blocking or obstructing intentionally other traffic at level
crossings 10
8. Driving a train without carrying safety protective equipment 5
9. Driving a train without carrying a certificate of registration 5
Total Demerit Points 100
16
JEDWALI LA SITA
(Limetengenezwa chini ya Kanuni ya 17)
APPLICATION FORM FOR TRAIN CREW REGISTRATION
PART 1: Applicant’s Details Passport size
photo
1.9. Surname: …………………………………………….
1.10. Name(s):……………………………………….
1.11. Sex: Male: ………. Female:…………………..
1.12. Date of birth (DD-MM-YYYY):…………………………
1.13. Place of birth: …………………………………
1.14. Nationality: ……………………………….
1.15. Language spoken…………………………
Applicant Physical address …………………………………….
NIDA Identification Number:……………………….
Date of first issue (YYYY-MM-DD):………
Expiry date:………………………………….
PART 2: List of documents to be appended
(a) a letter from the employer; (b) a recent medical examination report from the medical practitioner; and (c) a certified copy of a certificate of attendance in a relevant field.
PART 3 Declaration
I hereby declare that to the best of my knowledge that all the information provided in this
application is true.
Applicant’s Signature …………………………….. Date……………………………
JEDWALI LA SABA
(Limetengenezwa chini ya Kanuni ya 19)
Crew Registration Card
The United Republic of Tanzania
Land Transport Regulatory Authority
(LATRA)
REGISTERED TRAIN CREW
Staff Name: …………………………………….
Staff ID No. …………………………………
Department: …………………………….
CERTIFICATION:
The bearer of this card is a registered …………… as per LATRA requirements.
Date of Issue ………………….. Signature
Expiry Date …………………. ……………………………..
Serial No. …………………………… Director General
Dodoma, Isack A. Kamwelwe
…….., 2019 Minister for Works, Transport and Communications
Passport
size
photo