Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI...

45
Elimu Bora ni Nini? Taarifa ya Utafiti kuhusu Mitazamo ya Wananchi na Stadi za Msingi za Watoto Mei 2008

Transcript of Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI...

Page 1: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

Elimu Bora ni Nini?

Taarifa ya Utafiti kuhusu Mitazamo ya Wananchi na Stadi za Msingi za Watoto

Mei 2008

Page 2: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

ii

Shukrani

Uchunguzi huu wa kitafiti uliandaliwa na wafanyakazi wa HakiElimu wakishirikiana na Suleman Sumra, mjumbe wa bodi na Profesa mstaafu wa Elimu Chuo kikuu cha Dar es Salaam. Prof. Sumra aliwapa wafanyakazi mafunzo ya taratibu za ukusanyaji wa data na kusimamia zoezi zima la utafiti. Wafanyakazi wa HakiElimu Kellie Bonnici, Emmanuel Dedu, Grace Frederick, Sylvand Jeremiah, Godfrey John, David Kagondi, Stephen Kasambo, Richard Lucas, Daniel Luhamo, Agnes Mangweha, Esther Mashoto, Fiona McGain, Robert Mihayo, Glory Mosha, Fausta Musokwa, Mariam Mwambalaswa, Rosemary Mwenda, Mary Nsemwa, Linus Nzabhayanga, Lilyan Omary, Magreth Paul, Frederick Rwehumbiza, Nyanda Shuli, Peter Tupa, and Gervas Zombwe walifanya kazi ya utafiti, walisafiri katika maeneo ya utafiti na kukusanya taarifa. Wafanyakazi Naina Vira, Gervas Zombwe, Ruth Carlitz, Fiona McGain, Rajab Kondo na Linda Scholl walisaidia pia katika uchambuzi wa taarifa na upangaji wa matokeo. Ripoti hii iliandikwa na Suleman Sumra na Linda Scholl. Uhariri, mrejesho na ushauri ulitolewa na Elizabeth Missokia, Rakesh Rajani, Rajab Kondo, Ruth Carlitz, na Gervas Zombwe. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilipitia pendekezo la utafiti na kuidhinisha utafiti tarehe 6 August 2007. Ripoti hii isingeweza kufanikiwa pasipo ushirikiano wa wanafunzi, wazazi, wajumbe wa kamati za shule, walimu na maafisa wa wilaya tuliowahoji katika mtiririko wa utafiti huu. Tunawashukuru sana kwa michango na utayari wao kufanya kazi na sisi. © HakiElimu, 9977-423-66-3 HakiElimu, PO Box 79401, Dar es Salaam, Tanzania Tel: (255 22) 2151852/3, Fax: (255 22) 2152449 Sehemu yeyote ya kitabu hiki; inaweza kutolewa kwa namna nyingine yeyote kwa madhumuni ya kielimu na yasiyo ya kibiashara, kwa kuzingatia kuwa chanzo kitatajwa na nakala mbili zitapelekwa HakiElimu.

Page 3: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

iii

Yaliyomo 1.0 Muhtasari ........................................................................................................................................ 1

2.0 Utangulizi........................................................................................................................................ 3

3.0 Mbinu za Utafiti............................................................................................................................. 4

3.1 Uchaguzi wa Sampuli ...................................................................................................... 4

3.2 Ukusanyaji wa Data ......................................................................................................... 5

4.0 Elimu Bora: Dhana na Mitazamo ............................................................................................... 6

4.1 Matokeo: Mahojiano na Majadiliano katika Makundi mjadala.................................. 6

4.1.1 Ubora wa Elimu kama vitendea kazi............................................................... 6

4.1.2 Ubora wa Elimu kama Kufaulu Mitihani ....................................................... 7

4.1.3 Ubora wa Elimu kama Walimu........................................................................ 8

4.1.4 Ubora wa Elimu kama Maandalizi ya Baadaye .............................................. 8

4.2 Majadiliano: Mahojiano na Majadiliano katika Makundi mjadala ........................... 10

4.3 Matokeo: Upimaji wa Uwezo wa Wanafunzi............................................................. 12

4.4 Majadiliano: Upimaji wa Uwezo wa Wanafunzi........................................................ 13

5.0 Uwezo wa Watoto katika Stadi za Msingi................................................................................ 13

5.1 Hisabati ........................................................................................................................... 14

5.2 Lugha............................................................................................................................... 16

5.2.1 Stadi za Kusoma............................................................................................... 16

5.2.2 Stadi za Kutafsiri .............................................................................................. 17

5.2.3 Stadi za Imla...................................................................................................... 24

5.3 Majadiliano: Stadi za Lugha.......................................................................................... 29

5.4 Kisa Mkasa cha Shule ya Kata ..................................................................................... 30

6.0 Hitimisho...................................................................................................................................... 30

7.0 Mapendekezo............................................................................................................................... 33

8.0 Marejeo ......................................................................................................................................... 35

9.0 Viambatisho

9.1 Kiambatisho A: Miongozo ya Maadili kwa ajili ya Watafiti ..................................... 37

9.2 Kiambatisho B: Itifaki ya Mahojiano ya Mtu Mmoja Mmoja kwa Washiriki........ 38

9.3 Kiambatisho C: Itifaki ya Majadiliano ya Makundi................................................... 39

9.4 Kiambatisho D: Vigezo vya Kupimia Imla................................................................ 40

9.5 Kiambatisho E: Matokeo ya Majaribio ya Hisabati ya Shule za Msingi Kiwilaya 41

9.6 Kiambatisho F: Matokeo ya Majaribio ya Hisabati ya shule za Sekondari Kiwilaya

.......................................................................................................................................... 42

Page 4: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

iv

Vifupisho DAO District Academic Officer (Afisa Taaluma wa Wilaya)

DED District Executive Director (Mkurugenzi wa Maendeleo wa Wilaya)

DEO District Education Officer (Afisa Elimu wa Wilaya)

FGD Focus Group Discussion (Majadiliano katika Makundi Mjadala)

IEG Independent Evaluation Group (Kundi Huru la Taathimini)

MDG Millennium Development Goals (Malengo ya Maendeleo ya Milenia)

PEDP Primary Education Development Plan (Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi – MMEM)

PSLE Primary School Leaving Examinations (Mitihani ya Kuhitimu Elimu ya Msingi)

SEDP Secondary Education Development Plan (Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari – MMES)

UNESCO United Nation’s Education, Scientific and Cultural Organisation (Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni)

URT United Republic of Tanzania (Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)

Page 5: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

1

1.0 Muhtasari Tanzania imefanya jitihada kubwa za kuboresha mifumo ya elimu kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES). Hata hivyo, pamoja na kwamba madarasa mengi yamejengwa na idadi ya wanafunzi walioandikishwa kuongezeka kwa kiasi kikubwa, wananchi wengi bado wanalalamika kwamba elimu wanayopewa watoto ni ya ubora wa chini na kwamba watoto hawajifunzi stadi muhimu watakazozihitaji ili kupata kazi, kuishi katika jamii zao na kutoa mchango katika maendeleo ya taifa. Wakati MMEM na MMES zinatia msukumo katika kuongeza ubora wa elimu, jitihada nyingi hadi sasa zimekuwa zikielekezwa katika wingi wa vitendeakazi. Suala la UBORA wa Elimu; sasa linahitaji kuibuliwa na kufanywa liwe kiini. “Elimu Bora” ni nini? Tunawezaje kutambua kuwa mtoto anapata elimu yenye ubora wa hali ya juu? Ni kwa kiasi gani hasa watoto wanaendeleza stadi muhimu wawapo shuleni?

HakiElimu ilimpa kazi ya utifiti mtaalamu ili kuyachunguza maswali hayo hapo juu kuhusu ubora wa elimu katika ngazi za chini. Wilaya sita zilichaguliwa kwa ajili ya utafiti huu. Katika kila wilaya, shule mbili za msingi na shule mbili za sekondari zilitembelewa. Watafiti walikusanya taarifa kutoka kwa wanafunzi, wazazi, wajumbe wa kamati za shule, walimu, walimu wakuu na wawakilishi wa ofisi ya elimu wilayani. Taarifa hii inatoa na kujadili aina mbili za matokeo ya utafiti huo:

Dhana ya Elimu Bora. Tunakusanya ufahamu wa dhana ya elimu bora katika ngazi za shule na jamii kupitia mahojiano na majadiliano katika makundi mjadala ya wananchi. Pia tunatoa matokeo ya vipimo vya ubora wa elimu wanayoipata watoto shuleni kutoka kwa washiriki kwa kutumia orodha pana ya mambo ambayo watoto wanapaswa kuwa wanayamudu hadi wanapomaliza shule.

Majaribio ya Kupima Stadi za Watoto . Tunatoa taswira ya ubora wa elimu inayotolewa shuleni kwa kuonesha matokeo ya majaribio mafupi na mepesi yaliyotolewa kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari. Majaribio haya yalipima kiwango cha stadi za wanafunzi katika Hisabati na Lugha.

1.1 Matokeo: Dhana za Elimu Bora

Washiriki katika utafiti walielezea dhana nne tofauti za elimu bora: • Ubora = vitendeakazi. Washiriki wengi walilinganisha elimu bora na vitendeakazi kama

rasilimali watu na vitu kama madarasa, maktaba, maabara, idadi ya walimu, nyumba za walimu na vitabu vya rejea.

• Ubora = kufaulu mitihani. Washiriki wengine walitaja kuwa ubora wa elimu unaweza kupimwa kwa kuangalia idadi ya wanafunzi wanaofaulu mitihani kama mtihani wa kuhitimu elimu ya Msingi, kidato cha Nne na Sita.

• Ubora = walimu. Washiriki wengine waliujadili ubora wa elimu katika muktadha wa ubora wa walimu: Hamasa wanazopewa na mazingira ya kufanyia kazi; viwango vyao vya ufahamu, ustadi na mafunzo; na ufundishaji wao darasani.

• Ubora = maandalizi ya baadaye. Washiriki wengi pia, hususani wanafunzi na wazazi, walieleza kuwa kiashiria kikubwa cha “ubora” wa elimu ni uwezo wa wanafunzi wanaohitimu kuweza kupata kazi na kuishi katika jamii.

Walipoulizwa kupima ni kwa kiasi gani wanaamini watoto wao shuleni walikuwa wakiboreshewa uwezo wao, washiriki walizipatia shule alama chini ya wastani. Wazazi na wajumbe wa kamati za shule ndio walioonesha mashaka zaidi kuhusu ubora wa elimu

Page 6: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

2

inayotolewa. Washiriki wote walikubali kuwa shule zilikuwa zikijitahidi sana katika kujenga uwezo wa kusoma, kuongea na kuandika kwa Kiswahili kuliko kwa Kiingereza.

1.2 Matokeo: Majaribio ya Stadi za Msingi za Watoto Tuliwapa wanafunzi wa darasa la 6 na kidato cha 2 majaribio sawa (yatokanayo na mtaala wa darasa la 5) ili kupima kiwango cha ustadi wao katika maeneo mawili makuu: Lugha na Hisabati. Jaribio la Hisabati lilikuwa na maswali saba yaliyopangiliwa kwa kufuata ugumu wake katika kukokotoa. Katika lugha, stadi za Kiswahili na Kiingereza zilipimwa katika maeneo matatu: kusoma, imla na kutafsiri. Pamoja na urahisi wa maswali, uwezo katika Hisabati ulibainika kuwa ni mdogo sana – kwa wanafunzi wote, wa shule za msingi na sekondari. Hata katika maswali yaliyokuwa rahisi zaidi, idadi kubwa ya wanafunzi hawakuweza kujibu kwa usahihi. Katika maswali yaliyohitaji ustadi wa kukokotoa, idadi kubwa ya wanafunzi pia hawakuweza kuyajibu. Kwa mfano, katika swali la mwisho (lililowataka wanafunzi kukokotoa umbali kati ya magari mawili yaliyokuwa yakisafiri baada ya muda fulani), ni 11% tu wanafunzi wa shule ya msingi na 10% tu wanafunzi wa sekondari waliweza kukokotoa na kupata majibu sahihi. Taathimini ya matokeo ya majaribio ya lugha ilionesha kuwa wakati wanafunzi wengi walikuwa na uwezo wa kusoma na kufanya imla kwa Kiswahili, wengi wao walidhihirika kuwa na uwezo mdogo katika lugha ya Kiingereza. Kwa mfano, miongoni mwa wanafunzi wa shule ya msingi, 75% walifikia kiwango cha “vizuri” au “wastani” wakati katika jaribio la Kiingereza ni pungufu ya 25% waliofikia viwango hivyo. Kwa wanafunzi wa sekondari, 90% walipata “vizuri” au “wastani” wakati zaidi ya 60% walipata viwango kama hivyo katika Kiingereza. Uwezo wa wanafunzi wa kutafsiri kati ya Kiswahili na Kiingereza ulikuwa unakatisha tamaa zaidi. Miongoni mwa wanafunzi wa shule ya msingi, asilimia 66 ya tafsiri kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili, na asilimia 92 ya tafsiri kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza zilikuwa katika kiwango “hafifu”. Kwa wanafunzi wa sekondari, asilimia 34 ya tafsiri kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili na asilimia 59 ya tafsiri kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza zilikuwa katika kiwango cha “hafifu”.

1.3 Hitimisho/Mapendekezo Mjadala wa kitaifa kuhusu uboreshaji wa elimu umejikita na kuelekezwa zaidi katika wingi wa vitendea kazi. Wakati msisitizo huu unaakisiwa pia katika matokeo ya utafiti huu, kuna ongezeko la uelewa pia miongoni mwa wananchi kwamba japokuwa wingi wa vitendeakazi ni muhimu katika elimu, lakini hazitoshi katika kuhakikisha kuwa watoto wanapata elimu itakayoboresha maisha yao. Ili kubadili mwelekeo wetu kutoka katika idadi na kuelekea katika ubora, mjadala wa kitaifa unahitajika ili kuweza kutengeneza dira ya elimu bora, iliyowazi na inayolenga katika matokeo. Lengo kuu la elimu bora ya msingi linapaswa kuwa kuendeleza uwezo wa aina mbali mbali ndani ya watoto ambao utawafaa bila kujali ni kazi gani ama uelekeo gani wa maisha watakaoufuata baada ya shule: ustadi wa kusoma na kuhesabu, kuelewa, na stadi za kimaadili ambazo zote ni muhimu. Ili kuweka mwelekeo mpya wa mfumo wa elimu katika matokeo haya ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa kazi kwa walimu unahitajika. Walimu wanahitaji mafunzo na msaada ili kuongeza ufahamu wao katika masomo wanayofundisha pamoja na utumiaji wa mbinu shirikishi katika kufundisha ambazo huwashirikisha wanafunzi kikamilifu. Zaidi ya hayo, mfumo wa taathimini ambao utalenga katika uwezo wa wanafunzi inabidi uundwe. Kwa kuanzia, kipimo huru na cha kitaifa cha stadi za msingi za watoto katika kusoma na kuhesabu inabidi kifanyike kila mwaka.

Page 7: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

3

2.0 Utangulizi “Ubora wa elimu katika shule nyingi siku hizi ni hafifu!” Ongea na wazazi kuhusu elimu ya watoto wao. Wasikilize wanafunzi kuhusu mambo yanayoendelea shuleni kwao. Soma taarifa za vyombo vya habari kuhusu elimu ya msingi na sekondari. Wakati ni kweli kuwa kuna dalili nzuri zinazojitokeza, Watanzania wengi wanasimulia kuhusu madarasa yaliyojaa kupindukia, utoro wa walimu, ukosefu wa vitabu, adhabu kali au vitisho, walimu wasio na sifa, usomaji usio shirikishi na viwango vya juu vya udondokaji wa wanafunzi. Zaidi ya hayo ni kwamba wanafunzi ambao humaliza muda wote wa masomo kwa kawaida huwa hawajajifunza stadi za muhimu ambazo watazihitaji ili kupata ama kubuni kazi, kuishi katika jamii zao na kuchangia katika maendeleo ya taifa. Maswali kuhusu ubora yanazidi kuongezeka. Lakini hili linawezekanaje? Kila mmoja anakubali kwamba Tanzania imefanya jitihada kubwa katika kuboresha mfumo wa elimu. MMEM na MMES zimechangia sana katika kuongeza upatikanaji wa elimu. Shule nyingi zaidi na madarasa yamejengwa na uandikishaji wa wanafunzi umeongezeka sana. Kwa bahati mbaya, wakati MMEM na MMES zimetoa msukumo katika kuongeza ubora wa elimu, jitihada za serikali kwa kiasi kikubwa zimeelekezwa katika wingi: uandikishaji wa wanafunzi wengi zaidi, kutafuta walimu zaidi na kutengeneza nafasi nyingi zaidi kwa ajili yao. Hakujawepo na uzingatifu mahususi kuhusiana na suala la ubora wa elimu. Hali ilivyo mashuleni inadhihirisha hili: kuna fedha nyingi za kujenga shule na wanafunzi wengi zaidi wanaingia madarasani lakini usomaji unaofanyika madarasani humo uko hali mbaya kiubora. Matokeo yake ni kwamba miaka mingi baada ya kuanzishwa kwa MMEM na MMES, uelewa unazidi kuongezeka miongoni mwa wananchi wanaojali kuhusu suala la ubora wa elimu. Haitoshi tena kwa watoto kwenda shuleni tu, wanatakiwa wapate elimu ambayo itaboresha maisha yao. Upataji wa elimu tu, japokuwa ni muhimu, hautoshi kuhakikisha kuwa maisha ya mtu binafsi yanaboreka ama hata maendeleo ya nchi nzima kwa ujumla. Sasa ni wakati wa UBORA – sio wingi – kuwa kiini cha elimu. Hata hivyo, tunahitaji kufikiri kwa kina zaidi kuhusu maana hasa ya elimu bora. Ni ufahamu na stadi gani ambazo ndizo kiini cha elimu bora? Ufundishaji na usomaji ukoje darasani? Ni kwa kiasi gani watoto wanaendeleza stadi za muhimu katika maisha wawapo shuleni? Tunatambuaje kwamba mwanafunzi amepata elimu yenye ubora wa juu shuleni? Ni mifumo gani ya kielimu inapaswa kuanzishwa ili kuongeza ubora? Ni kwa namna gani shule na jamii zinahakikisha kuwa wanafunzi wanapata elimu bora? Mjadala wa kitaifa ambao utawahusisha wadau mbali mbali wa elimu kama wazazi, wanafunzi, walimu, wajumbe wa kamati za shule, jamii, wataalamu wa elimu, uongozi wa elimu kimikoa na kitaifa, serikali na asasi za kiraia unahitajika. HakiElimu ilifanya utafiti huu kama hatua ya kwanza katika mjadala huu. Kwa kuwa mjadala kuhusu masuala ya elimu umekuwa ukitawaliwa na watunga sera serikalini kwa kiasi kikubwa, tulipenda kupata mtazamo kuhusu ubora wa elimu kutoka katika jamii. Tulikuwa na malengo mawili makuu katika utafiti huu. Kwanza, tulitaka kujua wananchi wanalichukuliaje suala la ubora wa elimu, ikiwa ni pamoja na iwapo watoto wao wanapata elimu bora au la. Pili, tulitaka kupata taswira ya ubora wa elimu ambayo watoto wanaipata shuleni. Kwa maneno mengine, ni kwa kiasi gani wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanajengewa stadi za msingi watakazozihitaji maishani mwao baada ya masomo? Kwa kuwa utafiti ulikuwa changamani na matokeo yake yenye kuchokoza fikra, tumeigawanya taarifa hii katika vipengere tofauti. Kwanza, tunaelezea ni kwa namna gani utafiti huu ulifanyika na ulimhusisha nani. Tunajadili mchakato wa utafiti na kuelezea zana zilizotumika katika ukusanyaji wa data. Baada ya hapo, tunakusanya na kujadili dhana za jamii kuhusu ubora wa elimu kwa kutumia matokeo ya majadiliano katika makundi lengwa na wanafunzi, walimu, wazazi

Page 8: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

4

na maafisa katika ngazi ya wilaya. Katika kipengere hiki, tunatoa pia matokeo ya vipimo vilivyotolewa na washiriki kuhusu namna ambavyo shule zinajenga stadi mbali mbali za muhimu miongoni mwa wanafunzi. Baada ya hayo, tunatoa na kujadili matokeo kuhusu ubora haswa wa elimu inayotolewa shuleni. Matokeo haya yanatokana na majaribio mafupi ya Lugha na Hisabati ambayo yalitolewa kwa wanafunzi katika wilaya husika. Kisha tunaangalia matokeo ya utafiti kwa ujumla na kujadili dira yetu ya elimu bora, ambayo inahusiana na ujenzi wa ufahamu na uwezo wa mwanafunzi. Katika sehemu ya mwisho, tunatoa mapendekezo ya muhimu katika kuchochea majadiliano zaidi na vitendo vinavyohusiana na mwelekeo huu wa elimu bora.

3.0 Mbinu za Utafiti Utafiti uliandaliwa na wafanyakazi wa HakiElimu pamoja na mtaalamu mzoefu wa masuala ya utafiti ambaye huko nyuma alishawahi kuwa mshauri mwandamizi serikalini katika ofisi ya Waziri Mkuu. Chini ya uongozi wa mtaalamu huyo, wafanyakazi wa HakiElimu walipewa mafunzo juu ya zana zote za utafiti na kisha wakasafiri kwenda katika wilaya 6 mbali mbali nchini kwa ajili ya kukusanya data katika kipindi cha juma moja. Kila wilaya ilipangiwa timu ya watafiti wanne. Taratibu za ukusanyaji wa taarifa zilijadiliwa na wafanyakazi wakati wa mafunzo na orodha ya miongozo kadhaa ambayo kila mfanyakazi alipaswa kuifuata iliandaliwa. Kwa kuwa HakiElimu ni shirika lenye misingi ya haki, mafunzo ya wafanyakazi yalizingatia umuhimu wa kuhakikisha kuwa ukusanyaji wa taarifa unafanyika kwa kuzingatia maadili. Miongozo ya kimaadili iliandaliwa na kufuatwa na watafiti wote (Angalia kiambatisho A). Wananchi wote waliohojiwa walipewa taarifa zote kuhusiana na utafiti na wakakubali kwa hiari yao kushiriki.

3.1 Uchaguzi wa Sampuli Utafiti huu ulifanyika katika wilaya sita za Tanzania bara. Wilaya hizi zilichaguliwa kwa kuzingatia nafasi zake za ufanisi katika Mitihani ya Kumaliza Elimu ya Msingi mwaka 2005. Japokuwa mitihani sio kiashirisha tosha cha ubora wa elimu, kilitumika kutokana na kutokuwepo kwa viashiria vingine ambavyo vingefaa. Lengo lilikuwa kupata sampuli yenye uwakilishi wa shule na kuwahoji washiriki. Japokuwa taarifa zinazohusu matokeo ya shule na wilaya katika mitihani ya elimu ya msingi huwa zipo, tumependelea kutokutaja majina ya wilaya na shule zilizoshiriki. Matokeo yake, kwa matumizi ya utafiti huu tu, kila wilaya inatajwa kwa herufi. Yafuatayo ni maelezo ya wilaya zilizochaguliwa katika kila eneo: Wilaya zi l izo fau l i sha vizuri

Wilaya A (ya kijijini): Wilaya A ilifaulisha wanafunzi kwa 90%kwa wavulana na wasichana. Na wastani wa maksi zaidi ya 140 (kati ya 200) kwa wavulana na wasichana pia. Wanafunzi katika wilaya hii wamekuwa wakifaulu katika mitihani kwa miaka kadhaa mfululizo sasa. Wilaya B (ya mjini): Kiwango cha jumla cha kufaulu katika wilaya hii kilikuwa 92%, huku 96% ya waliofaulu wakiwa ni wavulana na 88% wasichana. Wastani wa maksi ulikuwa 141 kwa wavulana na 129 kwa wasichana.

Wilaya zenye u fau lu wa wastani

Wilaya C (ya mjini): Kiwango cha jumla cha kufaulu katika wilaya hii kilikuwa 58%, huku 66% ya wavulana wakifaulu na 50% ya wasichana wakifaulu pia. Wastani wa alama kwa wavulana ulikuwa 124 na kwa wasichana ulikuwa 108.

Page 9: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

5

Wilaya D (ya kijijini): Kiwango cha jumla cha kufaulu katika wilaya hii kilikuwa 41% huku 65% ya wavulana wakifaulu na 26% ya wasichana wakifaulu. Wastani wa alama kwa wavulana ulikuwa 114 na wasichana 85.

Wilaya zi l izo fanya vibaya

Wilaya E (ya kijijini): Kiwango cha jumla cha kufaulu katika wilaya hii kilikuwa 29% huku 34% ya wavulana wakifaulu na 24% ya wasichana wakifaulu. Wastani wa alama kwa wavulana ulikuwa 87 na 77 kwa wasichana. Wanafunzi katika wilaya hii wamekuwa wakifeli mara nyingi. Wilaya F (ya kijijini): Katika wilaya hii, kiwango cha kufaulu kilishuka kutoka 61% mwaka 2004 hadi 45% mwaka 2005, pamoja na ukweli kwamba pamekuwa na ongezeko katika kiwango cha wavulana waliofaulu. Anguko hili kubwa lilitokana na kuporomoka kwa idadi ya wasichana waliofaulu kutoka 67% mwaka 2004 hadi 36% mwaka 2005.

Kama inavyoweza kuonekana, katika wilaya hizo sita, mbili zilikuwa za mijini na nne zilizobaki zilikuwa za vijijini. Katika kila wilaya, shule mbili za msingi na mbili za sekondari zilichaguliwa kwa ajili ya utafiti kutokana orodha ya shule zote iliyopatikana katika ofisi ya Afisa Elimu wa Wilaya. Ili kupata taarifa zilizoakisi maoni ya pande zote (vijijini na mijini), shule moja ya msingi ilichaguliwa kutoka eneo la mjini na nyingine kutoka kujijini. Kwa shule za sekondari, shule moja ya kata, na shule moja ya zamani zilichaguliwa katika kila wilaya.

3.2 Ukusanyaji wa Data Kwa sababu utafiti huu ulikuwa changamani na ulikuwa ukijaribu kuchimbua masuala tofauti yahusuyo elimu bora, taarifa kadhaa zilitumiwa:

1. Mahoj iano binafs i : Mahojiano yalitumiwa kukusanya maoni ya washiriki. Mara zote ilipowezekana, viongozi wa elimu wilayani – Mkurugenzi wa Maendeleo wa Wilaya; Maafisa Elimu wa Wilaya; Maafisa Taaluma wa Wilaya – walihojiwa kwa kuwa wanawajibika katika kufuatilia na kuongoza maendeleo ya elimu katika wilaya zao. Zaidi ya hapo, kila ilipowezekana katika kila shule walimu 4 (2 wanaume na 2 wanawake), mwalimu mkuu na mwenyekiti wa kamati ya shule walihojiwa. Mahojiano yalikuwa yamepangiliwa kwa kuwalenga washiriki ili kupata mitazamo yao kuhusu ubora wa elimu, kwa kiasi gani shule zilikuwa zinatoa ama hazitoi elimu bora na sababu za kufanya hivyo. Jumla ya washiriki 134 walihojiwa. (Angalia kiambatisho B ili kupata nakala ya itifaki ya mahojiano).

2. Majadi l iano kat ika Makundi Mjadala (FGD): (Haya ni makundi ya mahojiano

yenye idadi ndogo ya washiriki) yaliyokuwa yakitumiwa katika kila eneo la utafiti. Majadiliano haya yalifanywa kwa makundi tofauti kama: wanafunzi, wazazi, wajumbe wa bodi za shule na walimu. Sambamba na mahojiano, majadiliano haya yalilenga katika mitazamo ya washiriki kuhusu elimu bora na kwa kiasi gani shule zilikuwa zinatoa elimu bora. Jumla ya makundi 30 yaliendeshwa katika zile wilaya sita. (Angalia kiambatisho C ili kupata nakala ya itifaki ya majadiliano katika makundi lengwa).

3. Mapit io ya uwezo wa Wanafunzi : Washiriki walitakiwa kutaja ni kwa kiasi gani shule

yao ilikuwa ikihamasisha uendelezaji wa vipaji mbali mbali vya wanafunzi. Orodha ya vipaji iliyotumika katika utafiti huu ilitolewa kwenye orodha inayotambulika kitaifa na kimataifa ya mambo ambayo mtoto anapaswa kuyamudu kama sehemu ya elimu ya msingi. Orodha hii ina mambo kama kusoma, kuandika na kuongea Kiswahili na

Page 10: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

6

Kiingereza, kuelewa masuala na matukio ya kitaifa na kimataifa, umakini, utatuzi wa matatizo, kushirikiana na wengine na maadili.

4. Majaribio : Ili kupata taathimini huru ya uwezo wa wanafunzi katika maeneo

waliyoyasoma, watafiti walitoa majaribio mafupi mafupi ya Lugha na Hisabati kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari. Katika jaribio la Lugha, Lugha zote mbili – Kiswahili na Kiingereza zilipimwa. Jaribio la Hisabati lililenga kupima uwezo wa mwanafunzi kukokotoa hesabu rahisi na kutatua mitego.

4.0 Elimu Bora: Dhana na Mitazamo 4.1 Matokeo: Mahojiano na Majadiliano katika Makundi Mjadala Katika sehemu hii, tunatathimini namna ubora unavyochukuliwa na wananchi katika ngazi za shule na wilaya. Ili kupata mawazo ya washiriki kuhusiana na mada hii, maswali kadhaa yaliulizwa katika mahojiano na majadiliano na washiriki: “Elimu Bora” ni nini? Watoto wanapaswa kupata aina gani ya Elimu? Je, kuna shule inayotoa elimu bora? Ni nani anawajibika kuhakikisha kwamba shule zinatoa elimu bora? Elimu bora ina umuhimu gani wa tofauti? Kwa ujumla, majibu ya washiriki yanaweza yakagawanywa katika dhamira nne. Elimu bora ilitajwa kuwa ni: 1) vitendeakazi (kama idadi ya shule na madarasa, vifaa vya kujifunzia na kufundishia); 2) kufaulu mitihani; 3) ubora wa walimu; na 4) maandalizi ya baadaye. Hapa chini tunajadili kila moja ya dhamira hizo. 4.1.1 Ubora wa Elimu kama Vitendeakazi Washiriki wengi waliilinganisha elimu bora na vitendeakazi vya elimu kama idadi ya madarasa, maktaba, maabara, nyumba za walimu, vifaa vya kusomea na kufundishia na vyoo. Kwa ujumla huu ndio ulikuwa mtazamo uliozagaa. Kulingana na wengi wa washiriki, shule zilikuwa zinatoa elimu bora iwapo mazingira ya shule yalikuwa mazuri hususani vifaa vinavyogusika vinavyohusika katika uendeshaji. Kwa mfano, Mkurugenzi wa Maendeleo wa Wilaya alisema kuwa ubora wa elimu unaweza kuongezwa kwa kujenga shule nyingi zaidi, kuhakikisha kuwa kuna idadi ya kutosha ya walimu na kuwapatia wanafunzi vitabu vya kutosha na vifaa zaidi vya michezo. Washiriki wengi waliweka msisitizo katika nafasi ya kutosha darasani, upatikanaji wa vitabu vya kiada na idadi ya walimu. Walipoulizwa iwapo shule zao zinatoa elimu bora, na sababu zake, washiriki wengi waliyahusisha mafanikio ama kushindwa kwa shule zao na upatikanaji wa rasilimali. Kwa mfano, walimu wengi na maafisa wa elimu wilayani walitaja kuwa katika miaka ya karibuni shule zimekuwa zikitoa elimu bora zaidi kwa sababu madarasa zaidi yamejengwa, shule zimepatiwa idadi ya kutosha ya vitabu vya kiada na walimu. Maktaba zimejazwa vitabu na vifaa vya maabara kama vile kemikali zimenunuliwa. Afisa Elimu mmoja wa Wilaya alisema kwamba:

“Watoto katika wilaya yangu wanapata elimu bora kwa sababu idadi ya wanafunzi wanaojiunga sekondari imeongezeka katika miaka ya hivi karibuni. Serikali ilihusika sana katika ongezeko hili kwa sababu imetoa

pesa zaidi kwa shule ambazo zimewezesha ununuzi wa vitabu vingi zaidi, vifaa vya sayansi na hisabati. [Mojawapo ya sababu za mafanikio hayo ni kwamba] kuna vitabu vingi zaidi shuleni kwa sasa kuliko hapo

awali na hivyo wanafunzi wanaweza kujisomea wenyewe. Japokuwa wilaya yetu ilikuwa ya mwisho kimkoa kwa

idadi ya wanafunzi waliofaulu, wanafunzi wengi zaidi wamefaulu katika wilaya hii kuliko katika wilaya nyingine yoyote mkoani.

Page 11: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

7

Kinyume chake, washiriki wengine walidai kuwa ubora ulikuwa ukiporomoka mashuleni kwa kuwa idadi ya wanafunzi ilikuwa ikiongezeka wakati kiwango cha rasilimali kikipungua. Wanafunzi wengi, hususani katika shule mpya za sekondari za “kata” walilalamikia ukosefu wa maabara na maktaba. Mwalimu mmoja katika shule ya sekondari alisema:

“.Shule yetu haijafikia hatua ya kuweza kutoa elimu bora kutokana na sababu mbali mbali. Hatuna idadi ya

kutosha ya vitabu vya kiada. Katika somo la Kiingereza, kwa mfano, kuna kitabu kimoja tu kwa kila wanafunzi 15. Kwa kuwa vitabu vya kiada havitoshi, inabidi tuwe tunaandika notisi ubaoni na wanafunzi

wananukuu.”

Maoni ya namna hiyo yanayohusisha rasilimali na pembejeo zilizopo shuleni na kuongezeka ama kupungua kwa ubora wa elimu yalitolewa na wanafunzi, wazazi, walimu na maafisa wa elimu wa wilaya pia. Wakati wa ukusanyaji wa data, uchunguzi wa watafiti ulibaini kuwa shule nyingi zilikuwa na madarasa mapya. Hata hivyo, hata madarasa haya mapya yalikuwa hata hayajapakwa rangi na yalikuwa matupu. Wakati ni kweli kwamba kulikuwa na madawati mengi darasani, hakukuwa na kitu chochote ubaoni na madarasa mengine yalikuwa hayajasakafiwa. Walimu walionekana kutokuwa na uwezo ama kutotaka kuyaboresha madarasa na kuyafanya kuwa mahali pa kuvutia kwa wanafunzi. Watafiti pia walibaini uchache wa rasilimali nyingine na vifaa vingine katika maeneo hayo. Madarasa na vyoo hayakuwa muafaka kwa wanafunzi wenye ulemavu. Shule nyingi zilizotembelewa hazikuwa na vifaa vya kutunzia maji. Katika shule nyingi za sekondari, japokuwa kulikuwa na majengo ya maabara, majengo haya yalikuwa hayana vifaa vya kutosha na wakati mwingine yalikuwa hayatumiki kabisa. Katika shule moja kwa mfano, jengo la maabara lilikuwa linatumiwa kama ghala. 4.1.2 Ubora wa Elimu kama Kufaulu Mitihani Kwa washiriki wengi, hususani Maafisa Elimu wa Wilaya, Walimu na Wajumbe wa kamati za shule, wanaona ubora wa elimu shuleni unaweza kupimwa kwa kuangalia idadi ya wanafunzi wanaofaulu mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi ama ile ya kidato cha 4 au cha 6. Ikiwa wanafunzi walikuwa wakifaulu sana, ubora wa elimu katika shule hiyo ulisemekana kuwa ulikuwa juu, na iwapo wanafunzi walikuwa wakifeli, basi ubora ulitajwa kuwa umeshuka. Kwa mfano, mjumbe mmoja wa kamati ya shule alisema:

“.Ubora umeongezeka kwa kuwa chati inapanda. Idadi ya wanafunzi wanaofaulu mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi inaongezeka mwaka hadi mwaka”

Walimu wengi walisema kuwa shule yao ilikuwa ikitoa elimu bora kwa kuwa wanafunzi wengi walikuwa wakifaulu mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi na kuchaguliwa kwenda sekondari. Kwa mfano, mwalimu mmoja alisema kuwa ubora wa elimu ulikuwa juu kwa kuwa wanafunzi wengi walikuwa wakifaulu kwa alama za juu. Mwalimu mwingine alisema:

“”Shule yangu inatoa elimu bora kwa wanafunzi. Idadi ya wanafunzi wanaofaulu mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi imekuwa ikiongezeka katika kipindi cha miaka mitano mfululizo. Waalimu katika shule hii

wanafanya kazi kwa kujituma sana ili kuhakikisha watoto wanafaulu mitihani. Huwafundisha wanafunzi hata wakati wa likizo

Kwa ujumla, washiriki wengi walieleza kuwa, hamu kubwa ya walimu ilikuwa ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wengi wanafaulu mitihani yao ya kuhitimu. Mkuu mmoja wa shule akasema:

Page 12: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

8

“.Shule yangu inatoa elimu bora kwa kuwa nimeanzisha masomo ya ziada. Masomo haya huendelea hadi usiku.

Nimetoa darasa moja kwa ajili ya wanafunzi wasichana wakae wakati hosteli ikiwa inakamilishwa. Ni vizuri wanafunzi wasichana wakakaa shuleni ili kuwakinga na vishawishi mbali mbali wanavyokabiliana navyo.

Wasichana hawa hupata masomo ya ziada kuanzia saa 1 hadi saa 4 usiku”

Masomo ya muda wa ziada yalikuwa yakitumiwa kujibu maswali ya mitihani iliyopita na kuwafunza wanafunzi namna ya kujibu maswali ya mitihani. Walimu wakuu na walimu wengine walionekana wazi kuwa walikuwa wanajivunia kuwasaidia wanafunzi kufaulu mitihani. 4.1.3 Ubora wa Elimu kama Walimu Washiriki wengi walieleza kuwa uchache wa walimu ni tatizo kubwa katika jitihada za kuwapatia wanafunzi elimu bora. Hata hivyo, pamoja na hilo, kulikuwa na masuala mengine ya msingi yahusianayo na walimu: hamasa na mazingira ya kazi; ufahamu wao, stadi na mafunzo na ufundishaji wao darasani. Nafasi ya walimu ilionekana kutambuliwa sana na washiriki wengi. Hata hivyo, washiriki wengi walieleza kuwa walimu hupewa mishahara midogo na hamasa kidogo sana. Kutokana na mishahara kuwa midogo, walimu wengi hufanya shughuli zao nyingine za kiuchumi kama kilimo, uvuvi na biashara ndogo ndogo. Walimu wengi walionekana kutatizwa sana na mazingira ya kazi huku wakidai kuwa mazingira mabaya yalikuwa yanaathiri utendaji wao. Walitaja mara nyingi kuwa mazingira ya kazi kwa walimu yalikuwa magumu sana na kwamba walikuwa wakilemewa na madarasa makubwa. Kulikuwa na malalamiko mengi kuhusu mishahara. Akiongelea suala la mazingira ya kazi, mwalimu mmoja alikiri kuwa: “Baadhi yetu hata huwaza kuwa kuja shuleni ni sawa tu na

kuendelea kulala nyumbani.” Wakati walimu wengi walionekana kutokuwa na hamasa, kulibainika kuwa na mtazamo wa kujitolea zaidi miongoni mwa walimu wengi. Washiriki wengi walieleza kuwa ubora wa elimu unaweza kuongezwa kwa kuongeza ubora wa walimu mashuleni. Wazazi sana sana ndio waliosisitiza umuhimu wa walimu, wakisema kuwa ili elimu iweze kuwa bora, ni muhimu kwamba“walimu wakawa wameandaliwa vyema kwa kazi .” Baadhi ya maafisa wa serikali pia nao walionekana kushughulishwa na suala la ubora wa walimu.Walisema kuwa wengi miongoni mwa walimu hawakuwa na uelewa mzuri wa mbinu za kufundishia na kuonesha mashaka zaidi kuhusiana na uwezo wa walimu wa Kiingereza. Mkurugenzi mmoja wa Maendeleo wa Wilaya alisema:

“Waalimu wengi wa Lugha hawatumii mbinu nzuri za ufundishaji kwa kuwa huwa hawajafundishwa namna ya kufundisha Kiingereza. Wengi hufundisha Kiingereza kwa kutumia Kiswahili.”

Jambo kuu kwa upande wa wanafunzi lilikuwa ni tabia za walimu darasani. Wanafunzi wengi walieleza kuwa mambo ambayo mwalimu anayofanya darasani na namna anavyoyafanya ni vitu vya muhimu kuhusiana na ubora wa elimu. Wanafunzi walieleza kuwa zaidi ya kuwa na vifaa vya kutosha vya kufundishia na kujifunzia:

“Waalimu wanapaswa kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa kile kinachofundishwa. Ni muhimu wakawa marafiki zaidi kwa wanafunzi na sio kuwatisha. Mwalimu rafiki atahakikisha kuwa wanafunzi

wanajisikia “huru”. Wanafunzi hawawezi kujifunza katika mazingira ya hofu. Inabidi wajisikie “huru” ili wajifunze.” (Mwanafunzi wa shule ya Sekondari).

4.1.4 Ubora wa Elimu kama Maandalizi ya Baadaye Washiriki wengi, hususani wanafunzi na wazazi, walieleza kuwa moja ya viashiria muhimu vya “ubora” wa elimu ni kiwango cha mwanafunzi kuweza kuajiriwa anapomaliza shule. Kwa mfano, mjumbe mmoja wa kamati ya shule alisema kuwa wanafunzi katika eneo lao walikuwa wakipata elimu bora kwa sababu walikuwa wanapata ajira nzuri baada ya masomo:

Page 13: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

9

“Shule yetu inatoa elimu bora na hili linaonekana wazi kwa kuwa watu wengi waliohitimu kutoka hapa

waliajiriwa serikalini na katika mashirika. Hili linaonesha kuwa shule yetu inatoa elimu bora”

Suala la uwezo wa kuajiriwa lilionekana kuwa nyeti kwa wazazi na wanafunzi wengi. Wazazi wengi na wanafunzi walieleza kushughulishwa kwao na hali ya ajira kwa sasa kutokana na nafasi za ajira kuwa chache hata kwa wale wenye shahada. Kwa kuzingatia hilo, wazazi walisema kuwa shule, hususani za msingi, hazitoi elimu bora. Baadhi walifikia hata hatua ya kuona kuwa watoto wao walikuwa wanapoteza muda kwa kwenda shuleni. Kwa mfano, washiriki kadhaa walikubaliana na mmoja wao aliyeeleza kuwa “. iwapo mwanafunzi atamaliza shule halafu asipate ajira, basi miaka aliyoitumia shuleni ilikuwa kupoteza muda Washiriki wengine walisema kuwa kwa maoni yao elimu ya msingi ilikuwa na iko “kitaaluma mno” na kwamba shule zilikuwa haziwafunzi wanafunzi stadi za muhimu za maisha ambazo watazihitaji baada ya kuhitimu masomo. Mara nyingi, uwezo wa kuajiriwa ulikuwa unahusishwa na mafunzo ya ufundi stadi. Kwa mfano mjumbe mmoja wa kamati ya shule alisema:

“Watoto katika shule yetu ya msingi hawapati elimu bora. Wanatumia muda mwingi kujifunza mambo ambayo hayahusiani na maisha yao. Wanafunzi wanaohitimu elimu ya msingi wanapaswa kuwa na stadi kama uashi,

ujenzi, uselemara na biashara, wakati mwingine hata stadi za kilimo.”

Mjumbe mwingine wa kamati ya shule alisema:

“Watoto wanapaswa kufundishwa kusoma, kuandika na stadi za maisha. Ni muhimu wasichana

wakafundishwa sayansi kimu. Siku hizi somo hilo limesahaulika. Walimu wanapaswa kufunzwa sayansi kimu ili nao waweze kuifundisha. Wasichana wanaomaliza shule hawajui hata kushona nguo, ama hata kuweka

kifungo. Stadi hizi inabidi zifundishwe tangu darasa la 1”

Wengine walifikiri kuwa stadi za kuandika na kuhesabu zinapaswa kuwa sehemu ya stadi za muhimu ambazo wanafunzi wanajengewa wawapo shuleni. Mzazi mmoja alisema:

“Wakati wa ukoloni, kila aliyehitimu elimu ya msingi alikuwa akipata ajira. Sidhani kwamba hilo lilitokana na uchache wa shule za msingi kwa wakati huo. Naamini ni kwa sababu wahitimu walikuwa na stadi

zinazohitajika. Wale waliokuwa wakiajiriwa kama makarani katika ofisi walikuwa na uwezo wa kuandika Kiingereza na Kiswahili. Waliweza hata kutunza vitabu vya mahesabu. Wahitimu wetu wa leo wanaweza

wakafanya hivyo? Achilia mbali shule za msingi, mtu aliyemaliza kidato cha nne anaweza akaandika barua kwa Kiingereza?”

Jambo la kuzingatia zaidi pia ni kuwa, washiriki wengi walikubali kuwa moja ya stadi muhimu zinazomtofautisha msomi na asiye msomi ni uelewa wake wa Kiingereza. Kwa mfano, mwalimu mmoja wa sekondari alisema:

“.Kuna tofauti nyingi ambazo mtu anaweza akaziona kati ya mtu aliyesoma na yule asiye soma shule. Tofauti

kubwa ni kwamba aliyesoma anaweza akaongea Kiingereza vizuri”

Kauli hii iliungwa mkono na washiriki wengi waliohojiwa. Stadi za lugha ya Kiingereza zimekuwa kiashiria muhimu cha ubora wa elimu kwa watu wengi. Kwa ujumla, maoni ya wengi kuhusu kutokuwa na sifa za kuajiriwa yalilenga elimu ya msingi; hata hivyo, wengine pia walikuwa na mtazamo kama huo kuhusiana na elimu ya sekondari kwa kuwa hailengi sana katika stadi za maisha. Mwanafunzi mmoja alisema kuwa jambo pekee ambalo walikuwa wakijiandalia wanapokuwa shuleni ni kuendelea na masomo ama kufanya kazi ofisini, ambayo yote mawili ni vigumu yakatokea katika mazingira yake. Alisema kuwa kulikuwa na stadi

Page 14: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

10

kidogo sana za maisha walizokuwa wakizipata, na kama [wanafunzi] hawaendelei na masomo, basi wanakuwa kama “wanapoteza muda wao” Idadi nyingine kubwa ya wanafunzi wa sekondari walieleza kutoridhishwa kwao na jinsi ambavyo shule haziwaandai kwa ajili ya kazi za baadaye. Haya hapa ni maoni ya mmoja wa wanafunzi:

“.Mimi na familia yangu tulifurahi sana nilipochaguliwa kujiunga na shule ya sekondari. Tuliamini kwamba

nitakapomaliza shule nitakuwa mwanasayansi. Nilikuwa nayapenda sana masomo ya sayansi. Nilipoanza kidato cha kwanza, kulikuwa na mwalimu mmoja tu shuleni, Mkuu wa Shule. Alikuja siku moja tu halafu

akatoweka. Katika mwaka wa kwanza, hakukuwa na waalimu wa sayansi. Kwa sasa tunaelekea kumaliza

mwaka wa pili shuleni na hatujawahi kufanya mazoezi yoyote ya kivitendo ya sayansi. Serikali imejenga maabara, lakini haina vifaa na kemikali. Ndoto zangu zilififizwa. Kwa sasa sina tumaini tena la kufaulu

shuleni. Nitawezaje kufaulu mitihani wakati sijafundishwa? Nimepoteza miaka yangu miwili hapa.”

Washiriki wengi waliweka msisitizo kwenye umuhimu wa stadi maalumu ambazo wanafunzi wanapaswa kuziendeleza wawapo shuleni kama ujasiri, ubunifu, utatuzi wa matatizo ama umakinifu katika masuala yanayoliathiri taifa. Hata hivyo, wanafunzi kadhaa walitaja umuhimu wa shule kujenga stadi ambazo wanafunzi watazihitaji wakati wa kutafuta ajira ama katika kazi zao. Mzazi mmoja alisema:

“Elimu ya darasa la saba haimtoshi [mwanangu] kuweza kuajiriwa ama hata kujiajiri. Hana ujasiri, na kwa namna hiyo hana tofauti na mtu ambaye hajaenda shule.”

Mkuu mmoja wa shule alisema kwamba elimu bora inapaswa kumpa mwanafunzi “uwezo wa kufikiri na kushiriki katika maendeleo ya kitaifa.” Katika kusisitiza kauli hii, Mkurugenzi mwingine wa Maendeleo wa Wilaya alisema msomi huwa na ufahamu zaidi wa masuala ya kitaifa na kimataifa. Mwingine akasema:

“[mtu aliyeelimika] hatakuwa mtegemezi kwa kuwa atautumia ujuzi na ufahamu alioupata shuleni. Anapopata

tatizo la kiafya, hatamdhania mtu mwenye “macho mekundu” (mchawi). Atatafuta njia za kumaliza matatizo, atashiriki katika maendeleo ya jamii na kusaidia kupunguza ujinga miongoni mwa watu wanomzunguka.”

Maoni kama hayo hapo juu yanaashiria dira miongoni mwa watu kuhusu umuhimu mkubwa wa elimu katika kuwaandaa wanafunzi kushiriki katika shughuli mbali mbali za kijamii ambazo zinaathiri maisha ya wale wanaowazunguka.

4.2 Majadiliano: Mahojiano na Majadiliano katika Makundi Washiriki wengi walihusisha wazi wazi ubora wa elimu na viashiria vingine kama viwango vya uandikishaji; idadi ya shule, madarasa na vitabu vya kiada. Wengi katika ngazi za wilaya, jamii na shule walielezea imani yao kuwa iwapo shule zingekuwa na madarasa ya kutosha, idadi ya kutosha ya walimu na vitabu vya kutosha vya kiada basi elimu na maisha ya wanafunzi vingeweza kuwa bora. Mlengo katika vitendeakazi vya elimu katika ngazi za chini haushangazi. Hadi hivi karibuni, majadiliano ya kitaifa kuhusu ubora wa elimu yamekuwa yakilinganisha wingi wa vitendeakazi na ubora, wazo likiwa ni kwamba ‘wingi’ unamaanisha ‘ubora’. MMEM na MMES zote zinatoa msukumo na msisitizo katika ubora, lakini zinaelekeza jitihada nyingi katika kupanua upatikanaji wa elimu na kuongeza wingi wa vitendeakazi vinavyoingizwa katika elimu. Sehemu kubwa ya fedha za MMEM na MMES zimetumika kujenga shule na nyumba za walimu, kununua vitabu na kuajiri walimu wapya. Kuenea kwa msisitizo huu wa kitaifa katika wingi wa vitendeakazi umeathiri kwa kiasi kikubwa mjadala kuhusu ubora wa elimu katika ngazi za chini. Wakati tukitambua kuwa vitendeakazi hivi ni vya muhimu katika kujenga mfumo endelevu wa elimu, tunaamini pia kuwa hili tu halitoshi peke yake kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata elimu itakayoboresha maisha yao. Kwa ujumla wataalamu wengi wanaeleza kuwa msisitizo katika eneo moja tu la vitendeakazi(nyenzo) bila kuambatana na uongozi thabiti na uwekezaji katika ubora

Page 15: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

11

unaweza kusababisha kuporomoka kwa thamani ya elimu kwa ujumla. Tunaamini kwamba kuinua ubora ni zaidi tu ya kuongeza zana za kazi; inahusisha msisitizo katika matokeo pia. Kama matokeo ya utafiti wetu yanavyoonesha, washiriki wengi waliuhusianisha ubora wa elimu na kufaulu katika mitihani na kuendelea na masomo ya juu. Jambo la kufurahisha ni kwamba mtazamo huu unatambua umuhimu wa matokeo. Katika utafiti huu, tokeo kuu liliotajwa na washiriki wengi ni kuendelea na masomo. Hata hivyo, hata kwa kufikiria tu, matokeo ya mtihani yanapaswa kuonesha na kutoa taathimini sahihi ya ufahamu na ustadi wa muhitimu. Tafiti za hivi karibuni kuhusu mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi zinaonesha yale ambayo yalioneshwa na tafiti nyingine kuhusu mitihani ya mwisho: kwamba mitihani hiyo, hususani ile inayotia msisitizo katika maswali ya kuchagua, kwa kiasi kikubwa hupima uwezo wa mwanafunzi kukariri (Kitta, na wenzake, 2008). Stadi za kufikiri kwa kina – kama kuzalisha mawazo, kuchambua na kutatua matatizo, kutathimini matokeo na kutumia ufahamu katika mazingira mbali mbali – huwa hazipimwi katika mitihani hiyo. Kwa hiyo, pamoja na kwamba alama za juu huweza kumsaidia mwanafunzi kuendelea na masomo (na hili huthaminiwa sana na wazazi, wanafunzi na walimu), matokeo ya mitihani tu ni kipimo hafifu cha ufahamu na ustadi wa mwanafunzi. Mfumo thabiti zaidi wa tathimini unapaswa kuhusisha upimaji wa stadi nyingi za mwanafunzi kwa namna endelevu kupitia mtaala. Matokeo ya utafiti wetu yanaonesha kwamba, washiriki wengi walipoulizwa kuhusu elimu “bora” walienda zaidi ya vitendeakazi na mitihani ya mwisho hadi kuzingatia ufundishaji wenyewe unavyofanyika darasani. Kwa mfano, ubora wa walimu ulikuwa unatajwa kuwa ni kitu cha muhimu katika kuboresha elimu. Kulingana na walimu wengi, utendaji wao ungeweza kuongezwa kwa kuboreshwa kwa mazingira ya kazi na malipo yao. Wazazi walipendekeza kuboreshwa kwa stadi za walimu. Wanafunzi walielezea umuhimu wa walimu kujenga mahusiano mazuri na wanafunzi. Maoni haya yanahusiana kwa karibu na utambuzi wa msingi kwamba elimu bora inahusiana sana na mchakato mzima wa ufundishaji na usomaji. Namna mchakato huu unavyofanyika shuleni na darasani ndilo jambo linaloweza kueleza iwapo wanafunzi wanahamasishwa na kuhusishwa kwa vitendo katika kujifunza na kuendeleza stadi zao. Washiriki wengi walionesha kutambua kwamba kiwango ambacho mwalimu anatia jitihada katika ufundishaji, kiwango cha ufahamu, mafunzo pamoja na stadi za ufundishaji ni mambo ya muhimu sana pia katika mchakato huu wa kusoma na kufundisha. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha pia kuwa washiriki wengi waliujadili ubora wa elimu kwa mtazamo wa kuwa na sifa za kuajiriwa na kumudu maisha ya baadaye. Mahsusi zaidi ni kwamba wazazi wengi, wanafunzi na wajumbe wa bodi za shule walionekana kuhisi kwamba watoto walikuwa hawapati elimu bora kwa kuwa walikuwa hawajengewi stadi ambazo zingeweza kuyafaa maisha yao baada ya kumaliza shule. Stadi maalumu na za lugha ya Kiingereza, vilihusishwa kwa kiasi kikubwa na elimu bora. Washiriki wengine wachache pia walihusianisha elimu bora na vitu vingine kama ujasiri, utatuzi wa matatizo, fikra huru na ushiriki katika masuala ya kijamii na kitaifa. Washiriki hawa walikuwa wanauchukulia ubora wa elimu katika muktadha wa matokeo ya mwisho, hususani katika uwezo ambao wanafunzi wanaupata katika kipindi chote cha masomo. Kama itakavyojadiliwa ziadi hapa chini, tunaamini msisitizo katika matokeo ya usomaji unapaswa kuwa ndio kiini cha majadiliano ya kitaifa kuhusu ubora wa elimu. Wakati ukweli unabakia kwamba vitendeakazi vya elimu ni za muhimu, hazijitoshelezi peke yake kuhakikisha kwamba elimu bora inatolewa. Ili watoto waweze kukua na kuishi kama watu wazima, wanahitajika kuwa na stadi mbali mbali ambazo zitakuwa za muhimu kwao katika mazingira mbali mbali. Jitihada za kutoa elimu bora zinapaswa kuelekezwa kiamakusudi katika kuendeleza stadi hizi.

Page 16: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

12

4.3 Matokeo: Upimaji wa Uwezo wa Wanafunzi Katika sehemu ifuatayo, tunaangalia matokeo ya utafiti wetu kuhusiana na uendelezaji wa uwezo wa wanafunzi. Maksudi zaidi, kwa kutumia utafiti huu, tulitaka kupima ni kwa kiasi gani washiriki wanaamini siku hizi shule zinajenga na kuendeleza uwezo na stadi za wanafunzi katika maeneo fulani. Ili kuweza kufanya hili, washiriki – ikiwa ni pamoja na wazazi, wanafunzi, wajumbe wa kamati za shule na maafisa wa serikali – katika wilaya zote sita walipewa orodha yenye maeneo 19 ya uwezo wa mwanafunzi. Orodha hii iliandaliwa kwa kuzingatia viwango vya kitaifa na kimataifa vya elimu. Washiriki walitakiwa kutoa vipimo kwa jinsi wanavyodhani shule katika maeneo yao zilikuwa zikiendeleza maeneo hayo miongoni mwa wanafunzi. Washiriki walitumia skeli hii kutoa vipimo: 1=sio yote, 2=kidogo, 3=wastani, na 4=kwa kiasi kikubwa. Jedwali na. 1 linaonesha wastani wa vipimo vilivyotolewa na makundi ya washiriki

Jedwali na. 1: Maoni ya Washiriki kuhusu Kiwango namna Shule

Zinavyoendeleza Maeneo ya Uwezo mbali mbali miongoni mwa Wanafunzi

1=sio yote 2=kidogo 3=wastani 4=kwa kiasi kikubwa

WASTANI WA ALAMA UWEZO W’Funzi wa S/M

Wa’Funzi wa Sek.

Walimu Wazazi/ Waj. Wa

Kamati ya Shule

Watumishi wa Serikali

1. Kusoma Kiswahili kwa Ufasaha 3.3 3.6 3.9 3.2 3.0

2. Kusoma Kiingereza kwa Ufasaha 2.6 2.9 2.8 2.1 2.4

3. Kuongea Kiingereza Vizuri 2.1 2.4 2.3 1.8 2.3

4. Kuongea Kiswahili Vizuri 3.5 3.4 3.7 3.4 3.0

5. Kuandika Kiingereza Vizuri 2.8 2.6 2.8 2.1 1.9

6. Kuandika Kiswahili Vizuri 3.3 3.3 3.6 2.8 3.1

7. Kutumia hesabu katika maisha ya kila siku 2.5 2.5 3.5 2.1 3.1

8. Kusoma ramani; kuzitumia kupata njia 3.2 2.8 3.0 2.4 2.9

9. Kufikiri kwa umakini 2.6 2.8 3.0 2.4 3.0

10. Kutambua matatizo yaliyopo katika jamii 3.0 2.9 2.9 2.4 3.1

11. Kutatua matatizo yaliyopo katika jamii 2.3 2.3 2.8 2.6 2.9

12. Ufahamu mpana wa masuala ya Kitaifa 2.5 2.4 3.1 2.3 2.3

13. Ufahamu kuhusu nchi na watu wengine 2.2 2.1 2.7 2.0 2.3

14. Kujivunia utaifa 2.3 2.4 3.6 2.1 3.1

15. Kuheshimu maoni ya watu wengine 3.0 3.3 3.4 2.8 3.0

16. Kuwajali watu wenye shida 3.3 3.0 3.5 2.4 2.9

17. Maadili (ukweli, uaminifu) 3.4 2.7 3.3 2.4 2.9

18. Kufanya kazi na wengine ili kufikia malengo 2.9 3.0 3.6 3.1 3.1

19. Kushiriki katika masuala ya kitaifa 3.2 2.0 3.5 2.5 2.6

Jumla ya Wastani 2.8 2.8 3.2 2.5 2.8

Matokeo hayo hapo juu yanaonesha mambo kadhaa. Kwanza, washiriki katika makundi yote walizipatia shule zao viwango vya chini kwa ujumla. Kwa kuangalia tu katika jumla ya alama kwa kila kundi, mtu anaweza kubaini kuwa kwa ujumla, wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na maafisa wa serikali walitoa alama chini ya wastani kwa shule zao. Wazazi na wajumbe wa kamati za shule wanaonekana kutoridhika zaidi na ubora wa elimu inayotolewa. Kwa wastani, walizipatia alama shule zao katika ya “kidogo” na “wastani”. Walimu, kwa upande mwingine, alama walizotoa kwa shule zao ni zaidi kidogo ya wastani. Kwa ujumla vipimo vya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari vinashabihiana karibu katika maeneo yote, isipokuwa tu kwenye uwezo wa kushiriki katika masula ya kitaifa ambapo wanafunzi wa shule za msingi walitoa alama kupita

Page 17: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

13

wastani huku wale wa sekondari wakiishia katika “kidogo”. Kinyume chake, tofauti kati ya alama zilizotolewa na walimu kwa upande mmoja na zile zilizotolewa na wazazi na wajumbe wa kamati za shule kwa upande mwingine zilikuwa zinatofautiana sana, hususani katika eneo la “kujivunia utaifa” na “matumizi ya hesabu katika maisha ya kila siku”. Katika maeneo haya yote, walimu walitoa alama za juu wakati wazazi na wajumbe wa kamati za shule walitoa alama karibu kabisa na “kidogo”. Katika maeneo mengine pia, walimu walitoa alama za juu kuliko wazazi na wajumbe wa kamati za shule. Pili, washiriki wote walikubali kuwa shule zilikuwa zikifanya vizuri zaidi katika kuendeleza stadi kama kusoma, kuongea na kuandika Kiswahili kuliko Kiingereza. Vipimo vya stadi za Kiswahili vilikuwa juu (kati ya 3.0 na 3.9) wakati kwa Kiingereza vilikuwa chini sana (kati ya 1.8 na 2.9). Kwa ujumla, zaidi ya stadi za kusoma, kuandika na kongea Kiswahili, washiriki walitoa alama za juu pia katika “kuheshimu maoni ya watu wengine”, “kufanya kazi na wengine ili kufikia malengo” na “kuwajali watu wenye shida”. Vivyo hivyo, zaidi ya stadi za kusoma, kuandika na kuongea Kiingereza, washiriki walitoa alama za chini sana kwa maeneo mengine kama “Kutatua matatizo yaliyopo katika jamii”, “ufahamu mpana wa masuala ya kitaifa” na “ufahamu kuhusu nchi na watu wengine”.

4.4 Majadiliano: Upimaji wa Uwezo wa Wanafunzi Matokeo hayo hapo juu hakika hayaoneshi wazi kwamba wanafunzi wanapata elimu bora. Washiriki walionekana kukubaliana kwamba shule zinafanya kazi nzuri katika kuwafundisha wanafunzi kusoma, kuandika na kuongea Kiswahili, na katika kushirikiana na kuelewana na watu katika jamii. Hata hivyo, uchache wa alama ambazo washiriki walizitoa kwa shule katika maeneo mengine ya stadi unaonesha kwa ujumla ni kwa kiasi gani elimu bado iko duni katika eneo la ubora. Ni jambo la muhimu pia kuzingatia kwamba matokeo haya yako wazi japokuwa bado fedha nyingi zilizotengwa kwa ajili ya MMEM na MMES zinaelekezwa katika kuongeza pembejeo za kielimu. Ni wazi sasa kwamba kuongezwa kwa pembejeo hizo haimaanishi moja kwa moja kwamba sasa wanafunzi watapata stadi na kujengewa uwezo wanaouhitaji katika maisha.

5.0 Uwezo wa Watoto katika Stadi za Msingi Wakati sehemu hizo hapo juu zinachambua mitazamo ya wananchi katika ngazi za chini kuhusu ubora wa elimu, tulipenda kupata picha ya stadi halisi ambazo wanafunzi wangeweza kuzionesha katika shule walizokuwa wakisoma. Kazi kubwa ya Pratham, shirika lisilo la kiserikali lililoko India, ilitumika kama mfano wa kuigwa katika utafiti huu. Shirika hili lilianzishwa katika miaka ya 1990 huko Mumbai, India likiwa na lengo kuu la kuhakikisha kuwa watoto kutoka familia maskini pia wanapata elimu ya msingi. Kazi za shirika hili zimekuwa chachu ya harakati za elimu ndani na nje ya India. Kazi kubwa ya shirika hili imekuwa ni kufanya taathimini ya kila mwaka ya stadi za watoto za kusoma na Hisabati katika jamii za vijijini. Tathimini huamsha uelewa wa wananchi kuhusu stadi za watoto na kuhusu ubora wa elimu katika maeneo yao. Taarifa ya kila mwaka hutumika kama taathimini huru ya uwezo wa watoto nchini humo (Pratham, 2008). Japokuwa tathimini ya kina ya maeneo yaliyotajwa hapo haikufanywa katika utafiti huu, tulipenda kupata tathimini huru kuhusu ubora wa elimu kwa kupima stadi za watoto. Kwa kutumia mfumo wa Pratham, tuliwataka wanafunzi kufanya mazoezi madogo ya kupima ustadi wao katika maeneo mawili makuu: Lugha na Hisabati. Mazoezi yote yaliandaliwa kwa kufuata mtaala wa darasa la 5 na vitabu vya kiada. Jaribio la Hisabati lilikuwa na maswali saba, mchanganyiko wa maswali marahisi na mengine yaliyohitaji ukokotozi. Katika jaribio la Lugha, stadi za Kiswahili na Kiingereza zilipimwa katika maeneo makuu matatu: Kusoma, Imla na kutafsiri. Jaribio hilo hilo moja lilitolewa kwa wanafunzi wa darasa la sita na wanafunzi wa kidato cha pili. Hili lilifanyika ili

Page 18: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

14

kuweza kuelewa iwapo hiyo tofauti ya miaka mitatu huweza kuwa imeongeza ufahamu zaidi kwa mwanafunzi. Matokeo ya majaribio haya yatatolewa kwenye sehemu zinazofuata za taarifa hii.

5.1 Hisabati Msingi imara katika Hisabati ndio kiini cha mtaala wa elimu. Stadi za uchambuzi na kufikiri kwa kina vyote huongezwa kwa kusoma Hisabati. Karibu nchi zote zina mtazamo wa aina hii na huweka Hisabati kuwa ndicho kiini cha elimu. Hivyo mafunzo ya lazima ya Hisabati kwa watoto ni ya muhimu katika kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika jamii zao, na hivyo kuongeza mchango katika ushindani wa kitaifa na jamii iliyoelimika. Jumla ya wanafunzi 549 wa shule za msingi walifanya jaribio la Hisabati, na wanafunzi 491 wa sekondari. Jaribio hili lilikuwa na maswali saba rahisi, ambayo yalikuwa hayahitaji ufahamu wa kina wa Hisabati. Yalikuwa yakihitaji stadi za msingi na uwezo wa kutumia stadi hizo katika kujibu maswali. Kwa sababu lugha ya kufundishia kwa elimu ya sekondari ni Kiingereza na wanafunzi wanafanya mitihani yao kwa Kiingereza, maswali haya yalitolewa kwa Kiingereza. Hata hivyo, yalitafsiriwa kwa Kiswahili kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi.

Jaribio la Hisabati

1. Ni namba gani inayofuata?:

A. 2 4 8 16 B. 2 4 16 256 C.

2. Iwapo nina machungwa 30 na ninataka kuwagawia sawasawa watoto 7, nitahitaji

machungwa mangapi zaidi ili watoto wote wapate idadi sawa? 3. Mama yako alikupatia noti ya shilingi 10,000 kununulia vifuatavyo:

Kilo 1 ya sukari ambayo inauzwa kwa shilingi 1,300 Bunda 2 za majani ya chai ambazo zinauzwakwa sh. 500 kila moja.

Utarudishiwa shilingi ngapi na muuza duka baada ya kununua vitu hivi?

4. Gari lilianza safari toka Segera kuelekea Moshi kwa mwendokasi wa km 60 kwa saa. Gari jingine lilianza safari muda uleule kuelekea Dar es salaam kwa mwendokasi wa km 80 kwa saa. Ni umbali gani magari haya yatatengana baada ya masaa mawili?

5. Gari lilianza safari yake saa 2 asubuhi kutoka Dar es salaam kuelekea Morogoro kwa

mwendokasi wa Km 80 kwa saa. Gari jingine lilianza safari ileile saa 2:30 asubuhi kwa mwendokasi wa Km 100 kwa saa. Ni umbali gani magari haya yatatengana ifikapo saa 3 asubuhi?

Page 19: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

15

Pamoja na urahisi wa maswali, matokeo ya jumla yalikuwa mabaya. Chati na. 1 inaonesha idadi ya wanafunzi (kwa %) waliojibu maswali mbali mbali kwa usahihi. Kulikuwa na swali moja tu (1a) ambalo zaidi ya 50% ya wanafunzi wa shule za msingi walijibu kwa usahihi. Wanafunzi wa sekondari kwa ujumla walijibu vizuri zaidi kuliko wale wa msingi; hata hivyo 45% ya wale wa shule za msingi walipatia swali la 2 wakati ni 33% tu ya wanafunzi wa sekondari walipatia. Zaidi ya hayo, wanafunzi wengi zaidi wa shule ya msingi walijibu kwa usahihi swali la 5 kuliko wale wa sekondari. Ni muhimu ikaeleweka kuwa swali la 1a linahitaji ufahamu wa msingi tu. Kusingeweza kuwa na swali rahisi kupita hilo. Hata katika swali hili, 18% ya wanafunzi wa sekondari hawakuweza kujibu swali hili kwa usahihi. Matokeo yalikuwa mabaya zaidi katika maswali mawili ya mwisho. 23% tu ya wanafunzi wa sekondari na 1% tu wanafunzi wa shule za msingi walijibu swali hili kwa usahihi. Katika swali la 5, sekondari walipata 11% na shule za msingi 10%.

Matokeo hayo hapo juu yanaonesha alama za jumla za wanafunzi katika jaribio la Hisabati. Matokeo haya yakigawanywa kwa wilaya na shule, inakuwa rahisi zaidi kuona tofauti za alama. Kwa mfano, katika shule moja ya msingi katika Wilaya C, 100% ya wanafunzi walipata majibu sahihi kwa swali la 1a, wakati katika shule nyingine katika Wilaya E, ni 28% tu ya wanafunzi walipata majibu sahihi. Katika shule nyingine za msingi zilizotembelewa katika wilaya C, 62% ya wanafunzi walipata majibu sahihi kwa swali la 5 wakati katika wilaya nyingine zilizobakia wote walipata chini ya 8%. Tofauti hii pia ilionekana katika matokeo ya sekondari miongoni mwa wilaya shiriki, japokuwa tofauti haikuwa kubwa sana kama ile ya shule za msingi. Kwa mfano, katika shule moja ya sekondari katika wilaya C, 61% ya wanafunzi walipata jibu sahihi kwa swali la 2, wakati ni 8% tu ya wanafunzi katika shule nyingine ya sekondari ndani ya wilaya hiyo hiyo waliopatia. Viambatisho E na F vinaonesha matokeo ya Hisabati kwa wilaya kwa shule zote za msingi na sekondari zilizofanyiwa utafiti. Matokeo haya yanatoa ushahidi wazi wa tofauti kubwa zilizopo katika ubora wa elimu wanayoipata wanafunzi katika shule na wilaya tofauti nchini. Jambo lingine la kuzingatia ni kwamba, miongoni mwa wanafunzi wa sekondari, wale wanaosoma katika shule za zamani waliweza kupata matokeo mazuri zaidi kuliko wale wanaosoma katika shule mpya za “kata”. Chati ya 2 inaonesha tofauti ya matokeo ya wanafunzi kutoka katika aina hizi mbili za shule.

Chati 1: % ya Wanafunzi Waliojibu kwa Usahihi Hisabati

0%

10%

20%

30%

40%

50%

60%

70%

80%

90%

100%

Msingi (N=549) 66% 38% 41% 45% 49% 1% 11% Sekondari (N=491) 82% 55% 73% 33% 70% 23% 10%

1a 1b 1c 2 3 4 5

Page 20: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

16

Katika maswali yale ya mwanzo, tofauti kati ya wanafunzi wa shule za zamani na zile mpya haikuwa kubwa. Hata hivyo, kwa kadri ugumu wa maswali ulivyokuwa unaongezeka, tofauti ya alama pia ilizidi kuongezeka. Kwa mfano, wakati kulikuwa na tofauti ya 4% kwa swali la 1, kulikuwa na tofauti ya 17% ya alama kwa swali 4. Kama data zetu zinavyoonesha, uwezo wa jumla katika Hisabati ni mdogo – kwa wanafunzi wote, wa sekondari na msingi. Hata kwa maswali marahisi zaidi, kulikuwa na wanafunzi wengi walioshindwa kupata majibu sahihi. Katika maswali yanayohitaji ujuzi zaidi wa hesabu, idadi kubwa ya wanafunzi walishindwa kupata majibu sahihi.

5.2 Lugha Utafiti pia uliangalia katika uwezo wa wanafunzi katika lugha mbili: Kiswahili na Kiingereza. Ni muhimu kukumbuka kuwa lugha zote hizi mbili ni za muhimu sana. Kiswahili ni lugha ya taifa, lugha ya kufundishia shule ya msingi na lugha ya mawasiliano kwa watu wengi nchini. Kiingereza pia kina nafasi ya muhimu katika maisha ya baadhi ya Watanzania. Ni lugha ya kufundishia sekondari na lugha ya kuwasiliana kimataifa. Hivyo ni muhimu shule zikazifundisha lugha hizi kwa ustadi na kuwajengea wanafunzi uwezo wa kutosha. Hili linakuwa la muhimu kwa shule za sekondari ambapo lugha ya kufundishia ni Kiingereza. 5.2.1 Stadi za Kusoma Stadi za kusoma huwa zina nafasi kubwa sana katika masomo shuleni. Uwezo wa kusoma na kuelewa maelekezo ni hitaji la msingi ili mtu afaulu masomo yoyote. Umuhimu wa kujua kusoma hata hivyo huwa hauishii tu pale mwanafunzi anapohitimu shule. Stadi hizo pia ni za muhimu katika maeneo mengine ya maisha, shuleni na nje ya shule, kuwezesha ushiriki wa mtu katika jamii na kuchangia katika mwingiliano wa kijamii na maendeleo binafsi.

Chati 2: % ya Wanafunzi waliojibu kwa usahihi Hisabati, kwa aina ya Shule

0%

10%

20%

30%

40%

50%

60%

70%

80%

90%

100%

Za “Zamani” (N=242) 84% 57% 78% 39% 77% 31% 16% Za “Kata” (N=249) 80% 53% 72% 28% 59% 14% 4%

1a 1b 1c 2 3 4 5

Page 21: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

17

Aya mbili, moja ya Kiingereza na nyingine ya Kiswahili zilichaguliwa kutoka kwenye vitabu vya kiada vya darasa la 5, kwa kuwa ilidhaniwa kuwa wanafunzi tayari wanauelewa wa masuala husika. Wanafunzi 10 kutoka darasa la sita na wengine 10 kutoka kidato cha pili walichaguliwa bila kufuata utaratibu wowote ili kufanya jaribio hilo la kusoma. Wanafunzi hao walipewa dakika 5 za kusoma aya zote kimya, baada ya hapo wakatakiwa kusoma aya hizo kwa sauti. Watafiti walikuwa wakifuatilia namna aya zilivyokuwa zinasomwa na makosa yaliyokuwa yakijitokeza katika usomaji.

Jaribio la Kusoma Aya ya Kiswahili

Jangwa ni sehemu ya ardhi yenye mchanga mwingi sana. katika sehemu hiyo kuna mchanga mwingi sana ambao ni kikwazo kikubwa kwa maisha ya viumbe hai. Watu wanaoishi jangwani ni wahamaji. Wanalazimika kuhama kutoka sehemu moja hadi nyingine kutafuta maji kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya mifugo yao. Kuna sehemu chache zenye vichaka na miti michache tu. Kadhalika, mifugo ni michache sana jangwani kutokana na uhaba wa maji na malisho. Hali ya usafiri ni ngumu kwa sababu sio rahisi kujenga barabara juu ya mchanga. Watu wa jangawani hutegemea sana ngamia kwa usafiri na uchukuzi wa mizigo yao. Hii ndio sababu ngamia akaitwa Meli ya Jangwani.

Aya ya Kiingereza

Mohamed is a young and active boy. He is in class five at Mnazini Primary School. He is the school’s football captain. Next week will be a busy week for his team. They will play with Bondeni team on Monday. The game will start at 8:30 p.m. Mohamed’s team is known as Shining Star. On Tuesday they will play with the Lions at noon. On Thursday, they’ ll face the Bulls. The Thursday match will kick off at 3:30 p.m. On Friday, the shining Star will fight it out with the Matata Group at 11:00 a.m. and lastly, they’ll face the Winning Star from Bidii Primary school on Saturday at 10:00 a.m.

Kwa ujumla, wanafunzi wengi, kwa shule za msingi na sekondari, hawakuwa na matatizo katika kusoma aya ya Kiswahili. Wanafunzi wengi walisoma kwa ufasaha, na hata pale yalipofanyika makosa, yalikuwa ni matokeo ya kusitasita tu wakati wa usomaji. Hata hivyo, kwa upande mwingine, wanafunzi walionesha uwezo mdogo sana katika kusoma aya ya Kiingereza, hususani shule za msingi. Wanafunzi ambao awali walikuwa wakisoma kwa uhuru na kwa sauti Kiswahili walishindwa kusoma Kiingereza kwa namna hiyo hiyo. Miongoni mwa wanafunzi 120 waliofanya jaribio hili, hakuna hata mmoja kati yao aliyeweza kusoma aya hiyo kwa ufasaha. Makosa ya matamshi yalikuwa ni ya kawaida sana, kama ilivyokuwa kwa makosa katika usomaji wa muda. 5.2.2 Stadi za Kutafsiri Uwezo wa kutafsiri aya kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza na kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili unaonesha ni kwa kiasi gani mwanafunzi anazielewa lugha hizi mbili. Aya mbili, moja ya Kiswahili na nyingine ya Kiingereza, zilichaguliwa kutoka kwenye vitabu vya kiada vya darasa la 5. Vile vile aya hizi pia zilichaguliwa na watafiti kwa kuwa walikuwa wakiamini kuwa wanafunzi wote wana ufahamu wa masuala husika.

Page 22: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

18

Jaribio la Kutafsiri

Aya ya Ki ingereza: Once in a small village in Mwanza region, there lived an old man with his wife, two sons and three daughters. He was a poor man but an honest one. He had a small piece of land and was maintaining his family by growing vegetables. His eldest son Marando wanted to go for higher education but due to poverty he could not go on. He decided to look for a job in Mwanza town in order to help his father educate his brothers and sisters. Aya ya Kiswahi l i : Tarehe 14 Desemba mwaka jana, shule zote za msingi mkoani kwetu zilifungwa. Wanafunzi walipewa likizo ya majuma sita. Majuma mawili kabla ya kuanza likizo shule yetu ikafanya sikukuu ya wazazi. Siku hiyo wazazi wote walialikwa shuleni. Siku ya sikukuu ya wazazi kila darasa lilipangiwa shughuli ya kufanya. Sisi, wanafunzi wa darasa la tano, tulipewa kazi ya kuwatembeza wageni na wazazi kwenye miradi ya shule. Baadhi ya wanafunzi wa darasa letu walichaguliwa kuelezea juu ya kila mradi. Shule ilikuwa na miradi mine, ukiwemo ule wa n’gombe, kuku, samaki na nyuki. Jumla ya wanafunzi 476 wa shule za msingi na 465 wa sekondari walifanya jaribio hili. Walipomaliza jaribio, watafiti walisahihisha kazi zao kwa kuzingatia vigezo vitano: maana, tahajia, unyambuzi wa vitenzi, alama na usafi wa kazi. Baada ya hapo, jumla ya alama kwa kila kazi ilikokotolewa. Alama ya juu zaidi ilikuwa 50. Tafsiri hizi baada ya hapo ziligawanywa kwenye makundi matatu: dhaifu (alama 0-20 au 1%-40%), wastani (alama 21-35 au 41%-70%) na vizuri (alama 36-50 au 71%-100%). Chati na. 3 inaonesha alama za wanafunzi wa shule za msingi katika kutafsiri. Asilimia kubwa miongoni mwao walifanya vibaya. 66% ya wanafunzi walifanya vibaya katika kutafsiri aya ya Kiingereza kwenda Kiswahili, na 92% walifanya vibaya katika kutafsiri aya ya Kiswahili, kwenda Kiingereza. Katika hili la pili, wengi wao walishindwa kabisa hata kutafsiri.

Page 23: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

19

Hii hapa chini ni baadhi ya mifano ya majaribio ya Kutafsiri kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili kwa wanafunzi wa darasa la 6:

Tafsiri ya Wanafunzi wa Shule za msingi: Kiingereza kwenda Kiswahili - kiwango “dhaifu”

Tafsiri ya Wanafunzi wa Shule za msingi: Kiingereza kwenda Kiswahili - kiwango

“wastani”

Chati 3: Ubora wa Tafsiri - Shule za Msingi

0%

10%

20%

30%

40%

50%

60%

70%

80%

90%

100%

Vizuri Wastani Dhaifu

Vizuri 13% 4% Wastani 21% 4% Dhaifu 66% 92%

Kiingereza kwenda Kiswahili Kiswahili kwenda Kiingereza

Page 24: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

20

Tafsiri ya Wanafunzi wa Shule za msingi: Kiingereza kwenda Kiswahili - kiwango “kizuri”

Hii hapa chini ni baadhi ya mifano ya majaribio ya Kutafsiri kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza kwa wanafunzi wa darasa la 6:

Tafsiri ya Wanafunzi wa Shule za msingi: Kiswahili kwenda Kiingereza - kiwango “dhaifu”

Tafsiri ya Wanafunzi wa Shule za msingi: Kiswahili kwenda Kiingereza - kiwango

“wastani”

Page 25: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

21

Tafsiri ya Wanafunzi wa Shule za msingi: Kiswahili kwenda Kiingereza - kiwango “Kizuri”

Kwa ujumla, wanafunzi wa sekondari waliweza kutafsiri vizuri zaidi kuliko wale wa shule za msingi. Hata hivyo, matokeo yalikuwa duni kupita ilivyotarajiwa (angalia chati na.4 hapa chini). Wanafunzi watatu kati ya kumi walifanya vibaya katika kutafsiri kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili na karibu sita kati ya kumi walifanya vibaya katika kutafsiri kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Ni 22% na 10% ya tafsiri zilifikia kiwango cha “vizuri”.

Makosa yaliyojitokeza mara nyingi yalikuwa: makosa ya misamiati, matumizi yasiyo sahihi ya herufi kubwa na ndogo, alama na kuchanganya matumizi ya nafsi ya kwanza na ya tatu.

Chati 4: Ubora wa Tafsiri - Shule za Sekondari

0%

10%

20%

30%

40%

50%

60%

70%

80%

90%

100%

Vizuri Wastani Dhaifu

Vizuri 22% 10% Wastani 44% 31% Dhaifu 34% 59%

Kiingereza kwenda Kiswahili Kiswahili kwenda Kiingereza

Page 26: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

22

Ifuatayo ni mifano ya tafsiri za wanafunzi wa kidato cha 2 kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili:

Tafsiri ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari: Kiingereza kwenda Kiswahili - kiwango “dhaifu”

Tafsiri ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari: Kiingereza kwenda Kiswahili - kiwango “wastani”

Tafsiri ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari: Kiingereza kwenda Kiswahili - kiwango “kizuri”

Ifuatayo ni mifano ya tafsiri za wanafunzi wa kidato cha 2 kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza:

Page 27: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

23

Tafsiri ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari: Kiswahili kwenda Kiingereza - kiwango “dhaifu”

Tafsiri ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari: Kiswahili kwenda Kiingereza - kiwango “wastani”

Tafsiri ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari: Kiswahili kwenda Kiingereza - kiwango “kizuri”

Pamoja na hayo, kulikuwa pia na tofauri kati ya wanafunzi kwa kuzingatia aina ya shule. Wanafunzi kutoka shule za sekondari za zamani walifanya vizuri zaidi kuliko wale wa shule za kata. (Angalia chati na. 5 na 6 hapa chini).

Page 28: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

24

Kwa ujumla, uwezo wa kutafsiri wa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ni mdogo. Hii ni kwa sababu wanafunzi hawa hawajajengewa stadi hizi tangu mwanzo. Jambo kubwa zaidi la kuzingatia ni kwamba wanafunzi wengi wa sekondari wana uelewa mdogo sana wa Kiingereza japokuwa ndiyo lugha ya kufundishia sekondari. Wanafunzi wengi iliwawia rahisi zaidi kutafsiri aya kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili kuliko kinyume chake, kwa sababu hili linahitaji uelewa zaidi wa Kiingereza. 5.2.3 Stadi za Imla Ili kupima uwezo wa wanafunzi katika kusikiliza na kuandika Kiswahili na Kiingereza, wanafunzi walitakiwa kuandika aya ya Kiingereza na nyingine ya Kiswahili walizokuwa wanasomewa. Imla hii ilitolewa kwa wanafunzi wa darasa la 6 katika shule za msingi na kwa wanafunzi wa kidato cha 2. Jumla ya wanafunzi 483 wa shule za msingi na 559 wa sekondari walifanya jaribio hili. Ili kuhakikisha kwamba wanafunzi hawatatizwi na matamshi ya maneno waliyokuwa wakisomewa, walimu wa shule husika ndio waliopewa jukumu la kuwasomea. Katika shule za msingi, mwalimu wa somo la Kiingereza ndiye aliyepewea hilo jukumu. Katika shule za sekondari, walimu walichaguliwa tu bila kufuata utaratibu wowote. Walimu katika shule zote walipewa muda wa kuzisoma aya husika na kujiaanda kwenda kuzisoma mbele ya darasa. Walimu walianza kwa kuzisoma zile aya taratibu huku wanafunzi wakisikilza kabla ya kuanza kuandika. Kisha walimu walisoma zile aya taratibu na wanafunzi walianza kuandika. Mwisho, walimu walisoma zile aya kwa mara ya tatu taratibu na wanafunzi walitumia nafasi hii kusahihisha makosa. Utaratibu huu ulitumiwa ili kuhakikisha kwamba mambo mbali mbali kama tofauti ya matamshi ama kasi ya usomaji hayawaathiri wanafunzi. Baada ya imla, watafiti walitoa alama kwa wanafunzi kwa viwango vya “vizuri”, “wastani” na dhaifu kutokana na vigezo vilivyokuwa vimewekwa (angalia kiambatisho D).

Chati 5: Ubora wa Tafsiri Wanafunzi wa Sekondari: Kiingereza Kwenda Kiswahili kishule

0%

20%

40%

60%

80%

100%

Vizuri

Wastani

Dhaifu

Vizuri 34% 20%

Wastani 40% 48%

Dhaifu 26% 32%

Sekondari za Zamani

Sekondari za Kata

Chati 6: Ubora wa Tafsiri Wanafunzi wa Sekondari: Kiswahili Kwenda Kiingereza kishule

0%

20%

40%

60%

80%

100%

Vizuri

Wastani

Dhaifu

Vizuri 4% 2%

Wastani 32% 27%

Dhaifu 63% 71%

Sekondari za Zamani

Sekondari za Kata

Page 29: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

25

Jaribio la Imla

Aya ya Kiingereza

When I arrived at school that morning, I met my friend Christina. “Good morning Theresa’’ She said. “Are you prepared for the English test?’’ ‘’I can hardly remember anything’’ I said. I have revised a lot of work, but a fear of the test is making it difficult for me to remember anything’’ that is how I feel too,’’ agreed Christina. I hope the test will be easy.

Aya ya Kiswahili

Siku moja, wakati jua na upepo wakiendelea kubishana, mara akatokea Binadamu. Jua akasema, “Mabishano yetu yataisha leo.’’ Upepo ulipogeuka na kumwona binadamu akasema, “Afadhali. Tusiandikie mate na wino ungalipo.’’ Jua akauliza, “ Sasa tufanyaje? Upepo ukajibu, “Yeyote kati yetu atakayeweza kumfanya Binadamu avue koti lake alilovaa atakuwa ndiye mwenye nguvu zaidi.’’ Jua akakubali. Akaondoka taratibu kujificha nyuma ya mawingu.

Kwa ujumla, wanafunzi wote – wale wa msingi na wa sekondari – waliandika vizuri zaidi aya ya Kiswahili kuliko ile ya Kiiengereza (angalia chati na. 7 na 8 hapa chini). Miongoni mwa wanafunzi wa shule za msingi, watatu kati ya wanne walipata “vizuri” au wastani katika imla ya Kiswahili wakati ni chini ya robo ya wanafunzi wote walipata alama kama hizo katika imla ya Kiingereza. Ni 5% tu ya wanafunzi wa shule za msingi walipata “vizuri” katika imla ya Kiingereza. Miongoni mwa wanafunzi wa Sekondari, tisa katika kumi walifanya “vizuri” au “wastani” katika imla ya Kiswahili, wakati ni zaidi kidogo tu ya sita kati ya kumi walipata “vizuri” au “wastani” katika imla ya Kiingereza. Ni robo tu ya wanafunzi wa sekondari waliopata “vizuri” katika imla ya Kiingereza.

Kwa kuangalia katika imla ya Kiswahili, ni jambo linaloshitua kuona kuwa 25% ya wanafunzi wa shule za msingi walifanya “vibaya”. Wanafunzi waliofanya jaribio hili walikuwa wamekwisha kusoma kwa miaka sita kwa Kiswahili lakini bado robo yao walikuwa hawawezi kuandika kwa usahihi aya ya Kiswahili katika imla.

Chati 7: Ubora wa Imla Wanafunzi wa Shule za Msingi

0%

20%

40%

60%

80%

100%

Vizuri Wastani Dhaifu

Vizuri 38% 5%

Average 37% 19%

Dhaifu 25% 76%

Kiswahili Kiingereza

Chati 8: Ubora wa Imla Wanafunzi wa Shule za Sekondari

0%

20%

40%

60%

80%

100%

Vizuri

Wastani Dhaifu

Vizuri 58% 25%

Wastani 32% 44%

Dhaifu 10% 31%

Kiswahili Kiingereza

Page 30: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

26

Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya majaribio ya imla kwa wanafunzi wa shule za msingi:

Imla ya Kiswahili ya Mwanafunzi wa Shule ya msingi – kiwango “dhaifu”

Imla ya Kiswahili ya Mwanafunzi wa Shule ya msingi – kiwango “wastani”

Imla ya Kiswahili ya Mwanafunzi wa Shule ya msingi – kiwango “vizuri”

Imla ya Kiingereza ya Mwanafunzi wa Shule ya msingi – kiwango “dhaifu”

Page 31: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

27

Imla ya Kiingereza ya Mwanafunzi wa Shule ya msingi – kiwango “wastani”

Imla ya Kiingereza ya Mwanafunzi wa Shule ya msingi – kiwango “vizuri”

Ifuatayo ni mifano ya imla za wanafunzi wa sekondari:

Imla ya Kiswahili ya Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari – kiwango “dhaifu”

Imla ya Kiswahili ya Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari – kiwango “wastani”

Page 32: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

28

Imla ya Kiswahili ya Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari – kiwango “vizuri”

Imla ya Kiingereza ya Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari – kiwango “dhaifu”

Imla ya Kiingereza ya Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari – kiwango “wastani”

Imla ya Kiingereza ya Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari – kiwango “vizuri”

Katika imla, wanafunzi wa shule za msingi na sekondari walifanya makosa mengi sana ya alama mbalimbali, jambo lililowafanya watafiti kudhani kuwa labda masuala hayo huwa hayafundishwi shuleni. Wanafunzi mara nyingi walikuwa wakitumia herufi kubwa hata pasipohusika. Vile vile

Page 33: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

29

wanafunzi walionekana kutoelewa hata matumizi ya nafasi kati ya neno na neno ama kati ya sentensi na sentensi. Ufahamu wa alama za sarufi ulionekana kuwa mdogo. Ukilinganisha pia matokeo ya wanafunzi kutoka shule za zamani na zile za kata, hali ilionekana kuchanganya zaidi. (Angalia chati na. 9 na 10 hapa chini). Wanafunzi wengi zaidi kutoka shule za zamani walipata “vizuri” ikilinganishwa na wale kutoka shule za kata; hata hivyo nao pia walikuwa na wanafunzi wengi zaidi waliopata zaidi kidogo tu ya “dhaifu” ikilinganishwa na wale katika shule za kata.

5.3 Majadiliano: Stadi za Lugha Kwa ujumla, takwimu zinaonesha kuwa wakati ni kweli kwamba uwezo wa wanafunzi katika somo la Kiswahili unajengwa vizuri, stadi zao katika lugha ya Kiingereza ni duni sana katika ngazi zote – msingi na sekondari. Wanafunzi walipata matatizo katika kusoma, kuandika na kutafsiri Kiingereza. Jambo hili ni baya sana, hususani kwa wanafunzi wa sekondari. Nchini Tanzania, mfumo wa elimu unaelekeza mafunzo ya elimu ya msingi yafanywe kwa Kiswahili lakini mafunzo ya sekondari na elimu ya juu yafanywe kwa Kiingereza. Hali hii inasababisha kuibuka kwa matatizo ya kijamii na kielimu. Wakati wa kuingia sekondari, sio tu kwamba wanafunzi wanatakiwa kujifunza dhana zile zile kwa lugha nyingine, lakini pia kuanza kusoma masomo mengine ambayo ni magumu zaidi. Iwapo wanafunzi wengi hawawezi kusoma na kuelewa lugha inayotumiwa kuwafundisha (kama takwimu zetu zinavyoonesha), ni vigumu kuelewa ni kwa namna gani uwezo unaweza ukajengwa na kuongezwa. Ni jambo la kuzingatia kwamba kuna shule moja ya msingi katika wilaya F ambayo wanafunzi wake walifanya na kupata “dhaifu” katika mazoezi yote. Katika shule ile, wanafunzi walionekana kana kwamba hawajajifunza kitu chochote tangu walipoingia shuleni miaka sita iliyopita. Hakuna mwanafunzi hata mmoja katika shule hii aliyeweza kujibu swali hata moja katika majaribio yote matatu. Watoto hawa hawakuweza kusoma, kuandika imla wala kutafsiri. Baadhi yao hata walishindwa kuandika majina yao na ya shule zao kwenye karatasi za majaribio. Shule hii ambayo

Chati 9: Ubora wa Imla ya Kiswahili Wanafunzi wa Sekondari kishule

0%

20%

40%

60%

80%

100%

Vizuri Wastani

Dhaifu

Vizuri 56% 50%

Wastani 30% 41%

Dhaifu 14% 9%

Sekondari za Zamani Sekondari za

Kata

Chati 10: Ubora wa Imla ya Kiingereza Wanafunzi wa Sekondari kishule

0% 10% 20% 30% 40% 50% 60% 70% 80% 90% 100%

Vizuri Wastani

Dhairu

Vizuri 33% 22%

Wastani 36% 49%

Dhaifu 31% 29%

Sekondari za Zamani Sekondari

za Kata

Page 34: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

30

inawahudumia watoto wa Wamaasai na makundi megine ya wafugaji, ina rasilimali kidogo sana. Ilikuwa na walimu wawili tu wakifundisha madarasa yote saba. Japokuwa jambo hili linaonekana kutokuwa la kawaida, inasikitisha kuona kwa miaka sita ya kuwepo shuleni, wanafunzi wanaonekana hawajajifunza kitu chochote.

5.4 Kisa Mkasa cha Shule ya Kata Shule W ni shule mpya ya kata ambayo imeanzishwa hivi karibu, na iko karibu na mji. Shule inaakisi ufanisi na mapungufu ya ujenzi wa haraka haraka wa shule za Sekondari unaoendelea nchi nzima. Shule hii iko katika eneo zuri lililozungukwa na miti. Majengo ya kwanza ya madarasa yalijengwa kwa ushirikiano wa serikali na jamii. Jamii ilishiriki kwa kuleta mawe na mchanga, serikali ikamlipa mhandisi. Katika mwaka wa kwanza, madarasa manne yalijengwa. Kwa kuwa ofisi za walimu na madarasa mengine yalikuwa hayajakamilika kujengwa, ufunguzi wa shule ulichelewa kwa miezi miwili. Majengo haya yamejengwa na kuezekwa vizuri. Tatizo moja ambalo limejitokeza ni kwamba sakafu imepasukapasuka ndani ya mwaka mmoja tu wa kwanza. Mwishoni mwa mwaka 2006, madarasa mengine manne kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha 2 yalijengwa. Majengo haya pia yalijengwa na mhandisi aliyelipwa na serikali. Maoni ya wananchi yalikuwa ni kwamba majengo haya ya baadaye yalikuwa imara zaidi ya yale ya kwanza. Wananchi pia walikuwa na uhakika kwamba majengo kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha 3 yangekuwa tayari mapema. Ushirikiano kati ya serikali na jamii ulifanikiwa kuhakikisha kwamba kuna madarasa ya kutosha shuleni. Jengo la maabara pia limekamilika japokuwa bado halijawekewa vifaa vya kazi. Hakuna maktaba katika shule hii. Kuna nyumba moja ya mwalimu iliyojengwa katika eneo la shule ambayo ilikusudiwa kwa ajili ya Mkuu wa Shule. Kwa kuwa mkuu huyo hakupendelea kukaa katika nyumba hiyo, nyumba hiyo sasa wanakaa walimu wapya. Wanafunzi walichaguliwa kwa ajili ya kujiunga na shule hii mwaka 2006, lakini walipofika shuleni hawakukuta walimu. Mkuu wa shule alipangiwa kuja katika shule hii, alipokuja alikaa siku chache na akaondoka, hakurudi tena. Kaimu Mkuu wa Shule ndiye anayeisimamia shule hii kwa sasa. Katika mwaka wake wa kwanza, shule haikuwa na mwalimu wa Hisabati wala Sayansi na hivyo wanafunzi hawakufundishwa masomo hayo. Idadi ya walimu ilianza kuongezeka taratibu. Kwa sasa kuna walimu 16 shuleni, lakini wakati wa ziara ya siku mbili ya watafiti, si zaidi ya walimu watano walioonekana shuleni. Zaidi ya 80% ya wanafunzi wanatoka nje ya kata hiyo, huja kwa gari kutoka katika maeneo ya jirani. Hutumia zaidi ya nusu saa kwenye basi wakati wa kwenda shule. Walimu wengi pia huishi katika maeneo ya mbali na hivyo hupanda “dala dala” kila siku kwenda shuleni. Mahudhurio ya walimu yalikuwa ni tatizo kubwa. Katika majadiliano kwenye makundi mjadala, baadhi ya wazazi walisema “Watoto wetu walikuwa wanakuja shuleni na wakimkuta mlinzi anawaambia kuwa siku hiyo hakuna mwalimu hata mmoja”. Wanafunzi wanacheza kwa muda mfupi kisha wanarudi nyumbani. Hali katika shule hii ya kata siyo ngeni. Shule nyingi za kata zinakabiliwa na matatizo kama haya haya. Inatarajiwa kwamba hali ya namna hii katika shule za kata ni ya muda mfupi na kwamba itashughulikiwa ndani ya miaka michache ijayo. Hata hivyo ni muhimu kupanga maendeleo ya shule za kata ili kuhakikisha kwamba pale wanafunzi wanapoanza shule wanakuta idadi ya kutosha ya walimu na vifaa.

6.0 Hitimisho Tanzania ni moja ya nchi nyingi duniani zinazopitia katika mabadiliko makubwa, mabadiliko ambayo yanahitaji kufikiriwa upya na kwa makini ili kuweza kufahamu hasa lengo letu kuu katika mfumo wa elimu. Kwa muda mrefu, majadiliano juu ya uboreshaji wa elimu yamekuwa

Page 35: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

31

yakifunikwa na msisitizo katika suala moja la wingi wa rasilimali zilizopo shuleni. Kufanikiwa ama kushindwa kwa elimu mara kwa mara, kumechukuliwa katika mtazamo wa idadi za uandikishaji, alama katika mitihani na kuendelea na masomo ya juu. Msisitizo huu mkubwa katika vitendeakazi na jitihada juu ya wingi, zimejitokeza sana katika taarifa hii. Washiriki wengi walilinganisha ubora wa elimu na kongezeka kwa vitendeakazi au nyenzo za elimu na viwango vya kufaulu mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi. Wakati huo huo, washiriki walipoulizwa kuhusu stadi ambazo wanafunzi walikuwa wanajengewa shuleni, majibu yao yalionesha kuwa shule zilikuwa hazifanyi vizuri katika eneo hili isipokuwa tu katika stadi za lugha ya Kiswahili. Kwa namna hiyo, utafiti huu unaonesha kuwa pamoja na shule nyingi kujengwa, walimu wengi kuajiriwa, wanafunzi wengi kuandikishwa na wengi wao kufaulu mitihani, bado ubora wa elimu haujaongezeka sana. Zaidi ya hayo, wengine wamefikia hatua ya kuona kuwa ubora wa elimu umepungua zaidi miaka ya hivi karibuni. Kwa bahati nzuri, uelewa kuhusu umuhimu wa kuzingatia matokeo ya elimu (zaidi ya vitendeakazi tu vya elimu) wakati wa kuifanyia taathimini unazidi kuongezeka. Mtazamo huu unazidi kukubalika zaidi katika ngazi za chini, kitaifa na kimataifa. Washiriki wengi katika utafiti huu waliuzungumzia ubora wa elimu kwa mtazamo wa “maandalizi ya maisha ya baadaye”. Baadhi ya washiriki walizungumzia stadi kama kuwa na fikra huru, ujasiri, utatuzi wa matatizo na ushiriki katika masuala ya kitaifa na kimataifa. Kitaifa, washiriki wengi walikiri kuwa elimu bora lazima iwaandae wahitimu kukabiliana na changamoto za maisha watakayokutana nayo katika jamii. Kimataifa, wataalamu wa sera za elimu wamegeuza mlengo wao kutoka kwenye viwango vya uandikishaji hadi kwenye kuchunguza stadi na uwezo wanafunzi wanaojengewa wawapo shuleni. Mabadiliko haya katika mtazamo yanaenda sambamba na utambuzi wa ukweli kwamba wingi wa vitendeakazi(nyenzo) za elimu peke yake hautoshi kuhakikisha kwamba wanafunzi wanakuwa na stadi zinazohitajika. Kwa mfano, Kundi Huru la Tathimini (IEG) la Benki ya Dunia lenye historia ndefu katika kutathimini mikakati ya kielimu katika nchi zinazoendelea liliripoti kuwa:

Ufahamu na stadi za msingi – sio kuhitimu masomo – ni mambo ya msingi katika kupunguza umaskini. Kuongeza

uandikishaji na kuhitimu elimu ya msingi ni mambo ya muhimu – lakini hayatoshi – kuhakikisha kuna uelewa wa msingi wa kusoma na kuhesabu. (IEG, xiii)

Kimsingi, IEG, pamoja na kuendelea kutambua umuhimu wa elimu ya msingi, imebadilisha msisitizo wake kuelekea kwenye uboreshaji wa elimu kwa kujenga uwezo wa wanafunzi.

“Jitihada katika elimu ya msingi inabidi zielekezwe katika kuboresha matokeo ya kujifunza, hususani miongoni mwa watu maskini na makundi mengine yaliyo pembezoni. Malengo ya Maendeleo ya Milenia yanatia msisitizo

katika kuongeza uandikishaji na viwango vya kuhitimu elimu ya msingi, lakini mambo haya hayatoshi kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata ufahamu wa kusoma na kuhesabu ambao ni wa muhimu sana katika kupunguza

umaskini. Ili kupunguza umaskini, nchi… zinapaswa kufanya uboreshaji wa matokeo ya usomaji kuwa ndiyo kiini

cha mipango yao ya elimu yao ya msingi na kujikita katika kuyashughulikia mambo - yatakayobainika katika upembuzi wa kitaifa – ambayo yanaweza yakawa na mchango mkubwa katika kufikia lengo hili kwa kutambua

kuwa uboreshaji wa matokeo ya kujifunza utahitaji gharama kubwa zaidi ya kuhitimu tu” (IEG, page x)

Tunahitaji kuuvuka mtazamo finyu kuhusu elimu bora unaolenga tu wingi, na kwenda katika ule unaohusisha masuala yote ya uwezo na stadi za mwanafunzi anapohitimu. Hili halimaanishi kupuuzia uboreshaji wa miundombinu na rasilimali shuleni. Uwezo wa mfumo wa elimu kumudu kutoa nafasi za kutosha kwa wanafunzi wote inabidi uendelee kuongezwa. Mazingira ya kazi na ya kuishi kwa walimu inabidi yazidi kuboreshwa. Vifaa vya kufundishia na kusomea inabidi viendelee kutolewa. Haya yote hata hivyo sio malengo ya elimu. Ni nyenzo tu za kusaidia kufikia lengo kuu: Vijana wanahitaji kujenga stadi na ufahamu katika mambo mengi yatakayo wawezesha katika kazi, maisha katika jamii na mchakato wa baadaye wa kuendelea kujifunza. Suala la

Page 36: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

32

kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanapata elimu bora ndilo linapaswa kuwa lengo kuu la mfumo wa elimu. Amartya Sen, mchumi ambaye ni mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, ni mtetezi mkubwa wa elimu inayolenga kwenye matokeo. Anasema kuwa kuna haja ya kuitathimini elimu kwa kuangalia “maisha halisi ambayo watu wanaweza kuyapata” (Sen, 1992, 52). Dhana hii inayagusa mambo yote ambayo mtu anaweza akataka kuyafanya, tangu yale yaliyo madogo (kama kupata chakula) hadi yale yaliyo magumu (kama kuweza kushiriki kwenye maisha ndani ya jamii). Sen anaeleza pia kuwa dhana hii inahusisha mafanikio na ‘uhuru halisi’ na ‘uwezo’ wa kuchagua aina ya maisha mtu anayoyataka. Elimu ina nafasi kubwa katika kuujenga uwezo huu.

Kama ilivyokwisha tajwa, washiriki wengi katika utafiti huu walionekana kutambua umuhimu wa kuwajengea wanafunzi wawapo shule ya msingi na sekondari stadi ambazo zitakuwa na manufaa maishani mwao. Hata hivyo, pamoja na kwamba washiriki wachache waliweza kutaja matokeo machache ya mtu kusoma, wengi walishindwa kueleza hasa ni ufahamu na stadi zipi ambazo wanafunzi wanapaswa kuzijenga katika masomo yao. Hili halishangazi. Kwa sasa, hakuna mwelekeo wa kitaifa ama dira ya wazi kuhusu mambo ambayo shule zinapaswa kuyajenga ndani ya wanafunzi. Wananchi katika ngazi zote za mfumo wa elimu wanahitaji uelewa mkubwa wa tafsiri halisi ya “elimu bora”. Tunahitaji kufikiri kwa uwazi zaidi kuhusu aina za stadi ambazo wanafunzi wanahitaji kujengewa wawapo shuleni na kuhakikisha kuwa mitaala inalenga kufikia malengo hayo. Elimu bora inabidili itafsiriwe kwa kuzingatia uwezo wa wanafunzi ambao utawawezesha kuishi maisha watakayoyachagua. Kwa kuzingatia ongezeko kubwa la wataalamu wa masuala ya elimu (International Baccalaureate Organization, 2006; Calgary Board of Education, 1998), HakiElimu inapendekeza pawepo na dira ya elimu bora ya Tanzania inayolenga ujenzi wa stadi zifuatazo:

VIPAWA VYA MWANAFUNZI

Kusoma/Kuhesabu Stadi za Utambuzi

Ajue kusoma, kuelewa, kuandika na kutamka

Weza kukokotoa mafumbo

Mchunguzi na Mdadisi

Mbunifu na mfikiriaji

Mtatuzi wa Matatizo

Muwasilianaji

Maendeleo Binafsi Maadili

Mwenye kujiamini

Awe tayari kwa lolote

Mwenye msimamo thabiti

Mwenye kujali na msaidiaji

Muwazi wa fikra

Mwenye kushirikiana

Wanafunzi wanahitaji msingi imara katika lugha na Hisabati ili waweze kuielewa dunia inayowazunguka. Uwezo katika kusoma na kuhesabu ni msingi wa mtu kuweza kuelewa masomo mengine yote kama fasihi, jiografia, historia, masuala ya kitaifa na kimataifa na sayansi. Zaidi ya

Page 37: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

33

stadi hizi, hata hivyo, kuna maeneo mengine pia ambayo ni ya muhimu si tu katika kuelewa masomo mengine bali hata katika kazi. Uendelezaji wa stadi za mtoto kama za uchunguzi, ubunifu, utatuzi wa matatizo na mawasiliano ni mambo ya muhimu katika uwezo wao wa kufanya kazi katika mazingira mbali mbali. Stadi binafsi pia, kama ujasiri, ubunifu na kuwa na msimamo thabiti ni sifa ambazo hujenga uwezo wa mtoto kufikiri na kuchukua hatua haraka. Stadi za kimaadili kama kuwa muwazi kifikra na kushirikiana na wengine huchochea uwezo wa mtu kuzalisha kwa kushirikiana na wengine katika jamii. Stadi hizi zote zinaweza kujengwa kwa namna endelevu tangu shule za msingi na sekondari. Hivyo, Elimu bora, kwa mtazamo wetu, ni mfumo wa elimu ambao kiini chake ni uendelezaji wa stadi hizi. Kwa sasa, stadi haziendelezwi kwa utaratibu rasmi mashuleni. Kama ilivyoonekana katika matokeo ya jaribio kwenye utafiti huu, stadi za kusoma na kuhesabu za wanafunzi inabidi ziimarishwe. Zaidi ya hayo, uendelezaji wa stadi za utambuzi, maendeleo binafsi na za kimaadili unabidi kuwa sehemu kuu ya mchakato wa usomaji na ufundishaji. Bila stadi hizi za muhimu, inaweza kuwawia vigumu wanafunzi kuweza kufanikiwa katika maisha yao baada ya kuhitimu. Jambo hili lilitajwa pia na washiriki wengi tuliozungumza nao wakati wa utafiti. Kunahitajika jitihada za kimakusudi ili kuupangilia upya mfumo wa elimu ili kwamba wanafunzi wote waweze kuhitimu shule wakiwa na stadi hizi. Ni lazima tukabiliane na changamoto kubwa katika mchakato wa usomaji na ufundishaji. Ni mbinu gani za kiufundishaji zitahitajika ili kuendeleza stadi hizi za wanafunzi? Ni namna gani mafunzo ya walimu tarajali na mafunzo ya walimu kazini – yanaweza kutengenezwa ili kusaidia ujenzi wa stadi za watoto? Ni michakato ipi ya tathimini inaweza kutengenezwa ili ituwezeshe sisi kuchunguza na kuelewa ni kwa kiasi gani uwezo wa wanafunzi unajengwa? Kwa mtazamo wetu, walimu inabidi wajenge mbinu shirikishi zaidi na za kivitendo katika ufundishaji. Mfumo wa tathimini itabidi utengenezwe ili kwamba wanafunzi wapate fursa ya kuonesha uwezo na stadi zao katika maeneo mbalimbali. Rasilimali watu na vitu pia zitahitajika ili kufanikisha shughuli hii.

7.0 Mapendekezo Kutokana na matokeo ya utafiti huu na majadiliano hayo hapo juu, tunatoa mapendekezo yafuatayo:

1. Mjadala wa kitaifa juu ya ubora wa elimu unahitajika ili kuweza kujenga dira ya

pamoja na ya wazi kuhusu ubora wa elimu. Ukosefu wa dira kama hiyo unaendelea kutatiza uwezo wetu wa kuwajenga watoto waweze kukabiliana na mabadiliko ya kijamii na kiuchumi yanayoendelea nchini Tanzania. Mkutano wa UNESCO wa Mawaziri kuhusu elimu bora mwaka 2003 ulihitimisha kuwa:

“Ubora umekuwa ni dhana inayobadilika sana ambayo inabidi mara zote kuchukuliwa katika eneo ambako jamii zake zinapitia katika mabadiliko makubwa ya kijamii na kiuchumi. Uhamasishaji wa mfumo wa kufikiri unaolenga mbele zaidi unazidi kuonekana wa muhimu zaidi. Dhana za kizamani kuhusu ubora hazitoshi tena… pamoja na mazingira tofauti tofauti, kuna mambo mengi yanayofanana katika utafutaji wa elimu bora, ambayo yanapaswa kuwawezesha watu wote, wanaume kwa wanawake, kuwa washiriki kamilifu wa jamii zao na pia kama raia wa duniani.”

Uuundaji wa dira ya pamoja kuhusu elimu bora miongoni mwa wananchi ni wa muhimu sana katika kutuwezesha kujenga na kuboresha mustakabali wa mfumo wetu wa elimu.

Page 38: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

34

2. Elimu bora inapaswa kutafsiriwa upya kwa kuzingatia matokeo na uwezo tunaokusudia kuujenga ndani ya watoto. Wakati ujenzi wa miundombinu ya shule unaendelea kuwa ni wa muhimu, vitendeakazi(nyenzo) peke yake hazitoshi kuhakikisha kuwa watoto wanapata stadi watakazo zihitaji kwa ajili ya maisha yao ya baadaye. Lengo kuu la elimu ya msingi linapaswa kuwa kujenga uwezo ndani ya wanafunzi ambao utawafaa hapo baadaye katika maisha yao bila kujali kazi watakazokuwa wakizifanya. Uwezo wa kusoma na kuhesabu ni wa muhimu katika lengo hili kwa kumwezesha mtu kuyaelewa masomo mengine kwa urahisi. Stadi za maendeleo binafsi, stadi za utambuzi na maadili ni za muhimu sana pia kwa kuwa husaidia matumizi kamilifu ya uwezo wa mtu katika jamii na taifa kwa ujumla.

3. Uwekezaji mpana na endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kwa walimu tarajali

na walio kazini yanahitajika. Walimu wanahitaji mafunzo kwa ajili ya kuongeza ufahamu wao katika masomo wanayoyafundisha. Wanahitaji pia mafunzo na msaada katika ngazi ya shule ili kuachana na mfumo wa “chaki na kuongea” katika kufundisha. Mbinu shirikishi za kufundisha zinapaswa kuendelezwa ili kwamba watoto washiriki katika kujifunza na wapate fursa nyingi za kuendeleza stadi zao.

4. Ili kuuelekeza mfumo wa elimu kwenye kulenga matokeo, itakuwa ni muhimu

kutengeneza mfumo bora wa taathimini kuhusiana na uwezo unaotakiwa. Kama sehemu ya kwanza katika mchakato huo, utafiti huru wa kutathimini stadi za wanafunzi katika kusoma na kuhesabu unapaswa kufanyika kila mwaka. Aina ya majaribio yaliyotumiwa katika utafiti huu na mbinu ya Pratham iliyotajwa huko nyuma ni mifano muhimu ya namna ambavyo zoezi hilo linaweza likafanyika. Yakifanyika mara kwa mara, mazoezi haya yanaweza kutoa fursa ya kuelewa uwezo halisi wa wanafunzi. Matokeo ya majaribio haya yataongeza uelewa wa jamii na kutoa taarifa za muhimu na endelevu kwa wananchi, waelimishaji na watunga sera juu ya ubora wa elimu wanayoipata watoto shuleni.

Elimu bora haipatikani kwa urahisi. Itahitaji jitihada na michango ya kila mtu – wanafunzi, wazazi, wajumbe wa kamati za shule, walimu, jamii, wataalamu wa elimu, uongozi wa kielimu kimkoa na kitaifa, serikali na asasi za kiraia. Wote wanawajibika; na wote wanapaswa kuwajibishwa katika kujenga na kuendeleza elimu bora. Muda umefika wa kufanyika kwa mjadala wa wazi wa kitaifa.

Page 39: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

35

8.0 Marejeo Calgary Board of Education. (1998). Quality learning: Work in progress. Calgary, Canada. Commonwealth Secretariate (2003) Improving quality in education: Report of a workshop. League for

the Exchange of Commonwealth Teachers London: Commonwealth Secretariate European Commission (2000) European report on the quality of school education: Sixteen quality indicators.

Brussels: Director-General for Education and Culture

Independent Evaluation Group. (2006a). From schooling access to learning outcomes: An unfinished agenda. An evaluation of World Bank support to primary education. Washington DC: World Bank Group.

International Baccalaureate Organization. (March 2006). The IB learner profile. United Kingdom.

Retrieved August 22, 2007, from http://www.ibo.org/programmes/documents/learner_profile_en.pdf.

Kitta, S., Sima, R., & Sumra, S. (2008) Primary School Leaving Examinations (PSLE): What do the

examinations measure? Dar es Salaam: HakiElimu and TEN/MET. Pratham Organization. (2008). Pratham: About Us. Retrieved February 21, 2008, from

http://www.pratham.org/aboutus/aboutus.php. Sen, A. (1992). Inequality re-examined. Cambridge, MA: Harvard University Press. UNESCO (2004) EFA Global Monitoring Report: Is the World on Track? Paris: UNESCO. Unterhalter, E. (2004). Education, Capabilities, and Social Justice. Background paper prepared for the

Education for All Global Monitoring Report 2003/2004: Gender and Education for All. Paris: UNESCO.

Page 40: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

36

Kiambatisho A:

Mwongozo wa ki-maadili kwa watafiti Uchunguzi wa Ubora wa Elimu

Masuala ya Kimaadili

1. Wanafunzi na watu wazima wanapaswa kufahamishwa dhumuni la utafiti, taarifa zitakazo

kusanywa na jinsi gani taarifa zitatumika. Wapatiwe anuani ya HakiElimu kama wanahitaji taarifa zaidi kuhusu utafiti.

2. Siku zote tafuta ridhaa ya wanaojibu maswali ili washiriki katika utafiti. Haitoshi kupata

ridhaa ya mwalimu mkuu au Mkuu wa shule iwe wakala wa ridhaa ya wanafunzi 3. Iwapo unakwenda na kinasa sauti(tepu rekoda) wakati wa usaili, mfahamishe anayejibu

maswali sababu ya kuitumia tepu rekoda. Pata ridhaa yake. 4. Iwapo unakwenda kupiga picha, omba ruhusu kutoka mamlaka za shule. Kama unakwenda

kupiga picha za mtu mmoja mmoja, pata ridhaa yao hata kama mwalimu mkuu amekupa ruhusa ya kupiga picha maeneo ya shuleni

5. Usiri: hakikisha hakuna mwanafunzi au mtu mzima yeyote anakwazika kutokana na utafiti

wako. Usitoe taarifa za kile kilichosemwa na wanafunzi kwa mkuu wa shule au mamlaka zozote. Vivyohivyo, taarifa inayomhusu mwalimu (hata kama inakera) isitolewe kwa Mwalimu Mkuu au Afisa Elimu Wilaya.

6. Hakikisha hakuna shida yeyote inayosababishwa na uulizaji maswali wetu 7. Usiingilie uhuru wa wanaojibu maswali. Usilazimishe iwapo wanaojibu maswali wanaonekana

kutokuwa radhi kujibu swali fulani. 8. Ahadi zote zitakazotolewa kwa wanaojibu maswali zinapaswa kutimizwa. Usiahidi chochote

usichoweza kutimiza. 9. Usioneshe makosa kwa wanafunzi au watu wazima. Usitolee maamuzi taarifa ulizopewa.

Usijifanye Mwalimu. 10. Hakikisha uvaaji wako na tabia zinakubalika kitamaduni. 11. Kataa takrima au zawadi kiupole 12. Washukuru wote baada ya kumaliza kukusanya taarifa.

Page 41: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

37

Kiambatisho B: Itifaki ya usaili wa mtu mmoja mmoja kwa washiriki

Uchunguzi wa Ubora wa Elimu

Ubora:

1. Ungefafanuaje ubora wa elimu?

2. Je, Shule katika wilaya yako zinatoa elimu bora kwa wanafunzi? Eleza. (DEO)

3. Je, shule yako inatoa elimu bora?Fafanua(Mwalimu mkuu)

4. Nani anawajibika kwa hali hii? Tafadhali elezea.

5. Ubora wa elimu unaotolewa katika shule yako(katika wilaya yako) umebadilika miaka ya hivi karibuni? Unadhani kwanini mabadiliko haya yametokea?

6. Nani aliwajibika katika mabadiliko hayo?

Uwezo:

1. Stadi gani tatu muhimu zaidi wanazopaswa kuwanazo wahitimu wa shule?

2. Tunawezaje kujua kwamba wanafunzi wamepata stadi hizi?

3. Kama shule zinatoa elimu bora, ni aina gani ya uwezo na stadi zipi wanafunzi wanapaswa kuwa nazo wanapohitimu shule?

4. Ni jinsi gani miaka saba ya elimu ya msingi(minne ya sekondari) inawabadilisha wanafunzi waliopita katika elimu hii? Waliosoma wanaweza kufanya nini ambacho wasiosoma shule ya msingi(sekondari) hawawezi?

5. Wafuatao wanawajibu gani katika kubuni shule ambako wanafunzi wanajifunza stadi na kukuza uwezo: serikali, kamati/bodi ya shule, mwalimu mkuu,walimu, wazazi, jamii na wanafunzi? Ki- vipi?

6. Serikali inapaswa kujenga kwanza madarasa na kisha ijikite katika ubora au haya yanaweza kwenda pamoja? Au serikali inapaswa kuhakikisha kiasi fulani cha ubora wakati linafanyika ongezeko la uandikishaji? Inawezekana? Elezea tafadhali.

Page 42: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

38

Kiambatisho C: Itifaki ya Majadiliano katika makundi Mjadala Uchunguzi wa Ubora wa Elimu

Elekeza majadiliano katika dhamira zifuatazo: 1. Elimu bora ni nini? Ni kile wanafunzi wanajifunza shuleni au kile wanachoweza kufanya

pindi wamalizapo kusoma? 2. Kiwango gani cha yale wanayojifunza wanafuzni shuleni kina manufaa katika maisha baada

ya kuhitimu? 3. Stadi gani muhimu wanzaojifunza wanafunzi zenye manufaa baada ya kumaliza kusoma?Ni

stadi gani walizonazo wanafunzi wa shule ya msingi ambazo watoto wasiosoma shule hawana? Wahitimu wanaweza kutatua matatizo yanayoibuka katika jamii? Toa mifano

4. Wahitimu wa shule wanaweza kufanyakazi katika jamii baada ya kumaliza kusoma? Kama

hawawezi, kwanini? Wahitimu wa elimu ya msingi wanaweza kujumuika vyema katika uchumi wa maeneo yao kuliko wale wasiosoma?

5. Wasomi wanaotoka shule wanaweza kupata ajira? Kwanini? kama wanapata ajira ni aina gani

ya kazi wanazofanya? Kuna wahitimu wowote ambao wamekwisha pata kazi kwa miaka hii mitatu iliyopita? Kazi gani wanazofanya?

6. Ni elimu ya namna gani inahitaji kutolewa kwa wanafunzi ili kuhakikisha wanaajiriwa?Ili

waweze kuwa wajasiriamali ndani ya jamii?

Page 43: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

39

Kiambatisho D: Vigezo vya Upangaji Alama za Imla Uchunguzi wa Ubora wa Elimu

Vizuri Kwa ujumla, Imla inasomeka vizuri. Mwanafunzi ameyapata maneno mengi zaidi na kuziandika kiusahihi herufi zake(uwepo wa makosa mara mojamoja katika herufi ni sawa) Iwapo amezitumia kiusahihi alama za uandishi na kufanya makosa madogo madogo Wastani Kwa ujumla, imla inasomeka, lakini kuna makosa kiasi. Mwanafunzi ameyapata maneno mengi, lakini kuna maneno mengi pia yanakosekana. Ameweka baadhi ya alama za uandishi na anaweza kuwa na makosa katika baadhia ya maeneo. Dhaifu Kwa ujumla, Imla ni ngumu kusomeka na kufasiri. Yanakosekana maneno mengi na maneno mengine yamekosewa. Hivi ni vitambulisho vya mgawanyo wa makundi. Katika kila kundi patakuwepo kiwango fulani cha ubora.

Page 44: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

40

Kiambatisho E: Ufanisi wa jaribio la hisabati, wanafunzi wa shule za msingi ki-wilaya

Uchunguzi wa Ubora wa Elimu

Shule za msingi SWALI

1

WILAYA

SHULE

YA MSINGI

N/ %

a b c

2 3 4 5

JUMLA

N 20 1 5 3 3 0 1 1

% 58% 3% 14% 9% 9% 0% 3%

35

N 17 13 9 8 2 0 0

A

2

% 63% 48% 33% 30% 7% 0% 0%

27

N 62 36 26 15 27 1 1 1

% 87% 51% 37% 21% 38% 1% 1%

71

N 42 31 23 8 37 0 1

B

2

% 93% 69% 51% 18% 82% 0% 2%

45

N 21 0 2 3 10 0 7 1

% 100% 0% 10% 14% 48% 0% 33%

21

N 71 62 69 68 66 0 45

C

2

% 97% 85% 95% 93% 90% 0% 62%

73

N 19 0 4 4 6 0 1 1

% 45% 0% 10% 10% 14% 0% 2%

42

N 35 11 30 91 76 0 0

D

2

% 34% 11% 29% 88% 73% 0% 0%

104

N 35 20 13 8 18 0 0 1

% 69% 39% 25% 16% 35% 0% 0%

51

N 12 19 36 28 18 0 0

E

2

% 28% 44% 84% 65% 42% 0% 0%

43

N 0 0 0 0 0 0 0 1

% 0% 0% 0% 0% 0% 0% 0%

9

N 26 17 9 12 13 2 2

F

2

% 93% 61% 32% 43% 46% 7% 7%

28

N 360 210 226 248 266 3 58 Jumla

% 66% 38% 41% 45% 49% 1% 11%

549

Page 45: Elimu Bora ni Nini? - HakiElimuhakielimu.org/files/publications/Quality Education SWAHILI (2).pdf · ya usomaji, uwekezaji endelevu katika mafunzo ya kitaalamu kabla na wakati wa

41

Kiambatisho F: Ufanisi wa jaribio la hisabati, wanafunzi wa shule za sekondari ki-wilaya

Uchunguzi wa Ubora wa Elimu

shule za sekondari SWALI

1

WILAYA

SHULE YA SEKONDARI

N/ %

a b c

2 3 4 5

JUMLA

N 36 23 26 14 16 5 2 1

% 82% 52% 60% 32% 36% 11% 5%

44

N 38 17 30 19 23 5 3

A

2

% 91% 41% 71% 45% 55% 12% 7%

42

N 25 20 24 8 24 10 7 1

% 89% 71% 86% 29% 86% 36% 25%

28

N - - - - - - -

B

2

% - - - - - - -

-

N 47 34 43 31 41 16 10 1

% 92% 67% 84% 61% 80% 31% 20%

51

N 36 23 39 4 23 4 1

C

2

% 71% 45% 77% 8% 45% 8% 2%

51

N 27 18 24 12 29 8 1 1

% 60% 40% 53% 27% 64% 18% 2%

45

N 47 31 53 26 47 5 4

D

2

% 70% 46% 79% 39% 70% 8% 6%

67

N 63 44 48 19 44 12 0 1

% 94% 66% 72% 28% 66% 18% 0%

67

N 36 28 37 8 33 13 1

E

2

% 92% 72% 95% 21% 85% 33% 3%

39

N 17 12 5 7 11 5 2 1

% 65% 60% 25% 35% 55% 25% 10%

20

N 31 21 31 16 26 14 16

F

2

% 84% 57% 84% 43% 70% 38% 70%

37

N 403 271 360 164 343 111 47 Jumla

% 82% 55% 73% 33% 70% 23% 10%

491