Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda...

28
Mwongozo wa Wakufunzi A (Kazi za Awali za Tathmini) UWEZO TANZANIA 2 0 1 4

Transcript of Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda...

Page 1: Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya

1Uwezo | Elimu Bora, Jukumu LanguUwezo Elimu bora, Jukumu langu!

Mwongozo wa Wakufunzi A(Kazi za Awali za Tathmini)

U W E Z O T A N Z A N I A

2 0 1 4

Page 2: Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya

2 Uwezo | Elimu Bora, Jukumu Langu

ZITAMBUE NEMBO ZAKO

Kazi ya kikundiWakati wa mafunzo, mkufunzi wako atawapanga katika makundi ili kufanya kazi fulani maalum kwa pamoja.

Swali & Jibu Kipindi cha Maswali na Majibu ni muhimu sana. Unahimizwa kuuliza maswali mengi ili kuhakikisha wahusika wanaelewa kikamilifu shughuli mbalimbali za mafunzo.

Dhana kuuUnapoona picha hii, maana yake ongeza umakini kwa kuwa hili ni jambo muhimu kukumbuka!

Angalizo kwa MwezeshajiNembo hii inapotumika ujumbe unakuwa umemlenga mwezeshaji, ukimpa ushauri au taarifa ambazo zitamwezesha kuendesha mafunzo

Utunzaji wa MudaNembo hii inatumika mwanzoni mwa kila sura ili kusaidia kumwongoza mkufunzi atumie muda mrefu kiasi gani kuwezesha kwa kila kipengele.

JS

YALIYOMO

ZITAMBUE NEMBO ZAKO

SURA YA 1: UTANGULIZI, MATARAJIO NA MAKUBALIANO YA PAMOJA

SURA YA 2: KUHUSU UWEZO NA MCHAKATO WAKE

SURA YA 3: UCHAGUZI WA SAMPULI, MBINU NA KUWAPATA WAHOUJAJI/WATAFITI

WA KUJITOLEA

SURA YA 4: KUWASILIANA NA SHULE

SURA YA 5: MAZINGIRA MAGUMU

SURA YA 6: MASUALA YA KIMAADILI

1

4

6

12

18

23

26

Page 3: Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya

3Uwezo | Elimu Bora, Jukumu Langu

MAANDALIZI KWA AJILI YA TATHMINI RATIBA YA SHUGHULI MBALIMBALI KWA AJILI YA MRATIBU WA WILAYA/MRATIBU MSAIDIZI/ MRATIBU WA KIJIJI

• Kabla ya kufanya shughuli zozote halisi, lazima umtembelee Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya (DED)• Muoneshe barua ya utambulisho kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa (RAS)• Watembelee Mkurungenzi na Mkuu wa Wilaya mara tu upatapo barua ya utambulisho kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa (RAS).

Na. Shughuli Malengo

2. Tembelea a. Mkurugenzi wa Wilaya b. Mkuu wa Wilaya c. Afisa Elimu wa Wilaya

- Kupata kibali cha kutembelea Maeneo ya Kuhesabia yaliyochaguliwa kinasibu (EAs) katika Wilaya

1. Kuhudhuria warsha ya Mafunzo ya Kanda

3. Kutembelea Maeneo ya Kuhesabia katika Wilaya yako

- Ifahamu vizuri kalenda ya matukio - Andaa bajeti ya wilaya yako- Wasilisha bajeti ya mafunzo

- Kumtambua na kumshirikisha kiongozi wa kijiji/mtaa - Hakiki ramani ya Eneo la Kuhesabia- Orodhesha kaya zote zilizo ndani ya EA- Fanya usaili na kuajiri wahojaji wa kujitolea

Kila mshiriki katika mafunzo ya kanda atapewa Kitabu cha Mwongozo wa Waratibu wa Uwezo wa Vijiji, ambao umeandaliwa kwa ajili ya Waratibu wa Uwezo wa Vijiji kama wahusika WAKUU. Hata hivyo, mwongozo huu utatumiwa na washiriki wote ili kukamilisha shughuli muhimu za awali ambazo zinapaswa kufanyika kwa ajili ya Tathmini ya Mwaka ya Uwezo ya awamu ya mwisho.

Page 4: Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya

4 Uwezo | Elimu Bora, Jukumu Langu

1.1: USAJILI WA WASHIRIKI WA MAFUNZO

Usajili wa washiriki utakuwezesha kujua ni wilaya/mikoa gani imewakilishwa katika mafunzo yenu, na kutambua kama kuna mapungufu yoyote (washiriki wowote ambao wameshindwa kuhudhuria). Usajili pia ni sehemu ya kuwaunganisha waratibu wa kijiji wanaotoka wilaya moja, endapo walikuwa hawafahamiani hapo kabla.

1.2: LENGO LA UTAMBULISHO

Malengo ya Mafunzo ya Tathmini ya Awali yatafanikiwa vyema iwapo washiriki watafahamiana mwanzoni mwa mafunzo. Kuna njia nyingi za kuwasaidia washiriki kufahamiana, au ‘kuchangamshana’. Mchezo mfupi unaweza kutumika ili kuwezesha utambulisho na kujenga mazingira ya kirafiki. Mkufunzi ana wajibu wa kuwezesha michezo ya ‘kuchangamshana’.

Hapa kuna mapendekezo machache:

Kwa kutumia kipande cha karatasi kimoja kwa kila mshiriki, kila mtu atengeneze ndege ya karatasi na aandike jina lake, jambo alipendalo, na ukweli wa kuvutia kuhusu yeye mwenyewe. Wakiwa katika mstari, kila mtu arushe ndege yake eneo lolote ndani ya ukumbi. Kama atapata ndege, aokote na kuendelea kurusha kwa muda wa dakika 1-2. Mwishoni mwa dakika hizo, kila mtu lazima awe na ndege moja ya karatasi. Huyu ndiye mtu atakayemtafuta na kumtambulisha kwa washiriki.

Ligawe kundi katika timu za watu wawili wawili (waambie wachague mshiriki ambaye hawafahamiani vizuri). Waambie wahojiane kwa dakika kumi (Unaweza pia kuandaa maswali kabla ya kufanya hivyo au kutoa mwongozo wa jumla wa namna ya kuhojiana). Wanahitaji kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya ndoto yake ni ipi (mapendekezo mengine yanaweza kuongezwa). Baada ya mahojiano, warejeshe kuketi katika nafasi zao na kila timu watambulishane kwa washiriki.

Mchezo wa Mahojiano

Mchezo wa Ndege ya Karatasi

SURA YA 1: UTANGULIZI, MATARAJIO NA MAKUBALIANO YA PAMOJA

Dakika 45

Page 5: Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya

5Uwezo | Elimu Bora, Jukumu Langu

1.3 WASIFU WA WARATIBU WA VIJIJI

Kwa mwaka 2014, wahojaji wa kujitolea waliochaguliwa ambao waliwahi kufanyakazi na Uwezo kwa miaka kadhaa – watajulikana kama wahojaji “waandamizi” au “Wahojaji viongozi” -, watashiriki tena kwenye utafiti wa Uwezo wakiwa na nafsi ya juu; na watajulikana kama Waratibu wa Vijiji (VCs).

Waratibu wa Vijiji wana uzoefu mkubwa kwenye kazi na hujituma kwa kiwango cha juu kuitumikia Uwezo. Wao ni kiungo muhimu cha mawasiliano kati ya Uwezo na jamii - walimu, wazazi, na viongozi wa vijiji/mitaa. Kwa kawaida wao ni washiriki makini kwenye uboreshaji wa kujifunza katika jamii zao na wanatazamwa kama chanzo cha taarifa na elimu kuhusu Uwezo. Waratibu wa Vijiji ni taswira ya Uwezo katika vijiji vyao.

1.4 MADHUMUNI YA MAFUNZO WARATIBU WA VIJIJI

Kabla ya Uwezo 2014, Waratibu wa Vijiji wamekuwa wakipata mafunzo ya aina sawa na wahojaji wengine wa kujitolea. Hata hivyo, waratibu wa vijiji (VCs) sasa watakuwa na majukumu maalum ambayo watahitaji kupatiwa mafunzo yanayokidhi majukumu yao. Majukumu yao yatakuwa kama ifuatavyo:

a) Kuhudhuria mafunzo ya siku tatu ya kikanda; b) Kumsaidia Mratibu wa Wilaya kuhakiki ramani za maeneo ya kuhesabia (EAs) kuorodhesha kaya na kuajira wahojaji wa kujitolea na kuitambulisha Uwezo kwa Viongozi na Wazee wa vijiji kufuatana na maelekezo; c) Kusaidia katika kuratibu mafunzo ya siku mbili ya wahojaji wa kujitolea; d) Kusaidia utekelezaji wa tathmini katika Maeneo ya Kuhesabia; e) Kusaidia katika kukusanya na kuhakiki vijitabu vya utafiti. f) Kuwasilisha matokeo ya utafiti shuleni

Kwa hiyo, madhumuni ya mafunzo maalum kwa Waratibu wa Vijiji itakuwa ni kuimarisha maarifa na ujuzi wao; hasa, katika maeneo haya muhimu:

• Chimbuko la Uwezo na mahusiano yake na mashirika mengine – nafasi yake katika muktadha wa kitaifa, kikanda, na kimataifa) • Mchakato ambao kupitia huo Uwezo inalenga kuleta mabadiliko ya kudumu katika sera ya elimu katika Afrika Mashariki • Jinsi Maeneo ya Kuhesabia (EAs), kaya, na watoto wanavyochaguliwa kwa ajili ya tathmini kila mwaka • Jinsi ya kuhakiki ramani ya Eneo la Kuhesabia• Jinsi ya kuandaa Orodha ya Kaya• Jinsi ya kuwasilisha matokeo ya Uwezo 2014 shuleni• Jinsi ya kujibu maswali magumu na kukabiliana na mazingira au hali ngumu zinazojitokeza eneo la kazi

1.5 JINSI YA KUTUMIA MWONGOZO HUU

Mwongozo huu umeandaliwa hasa kukuwezesha wewe mkufunzi, kukupatia maarifa muhimu na ujuzi ambao utakuwezesha kuwafanyia mafunzo Waratibu wa Vijiji na Waratibu Wasaidizi wa Uwezo kwa ufanisi.

CHAPTER 2: ABOUT UWEZO AND THE UWEZO PROCESS

CHAPTER 2 : ABOUT UWEZO AND THE UWEZO PROCESS

Page 6: Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya

6 Uwezo | Elimu Bora, Jukumu Langu

Kiwango cha maarifa na ufahamu wa Waratibu wa Vijiji kuhusu Jitihada ya Uwezo kipo katika ngazi sawa na wahojaji wengine wa kujitolea, kitu ambacho kinapunguza uwezo wao kujibu maswali mengi ambayo shule na wazazi huwauliza. Madhumuni ya kifungu hiki ni kupanua maarifa yao ya sasa kuhusu Uwezo na mchakato wake.

Hadi kufikia mwishoni wa somo hili, wanapaswa kuwa na uwezo wa kushirikishana kwa kujiamini na kwa usahihi taarifa kuhusu:

• Chimbuko la Uwezo na umuhimu wake kitaifa, kikanda, na kimataifa • Manufaa kijamii ambayo Uwezo inataka kufanikisha • Mchakato ambao Uwezo inatumia kuleta mabadiliko ya kudumu katika nchi za Afrika Mashariki • Mahusiano ya Uwezo na mashirika mengine

Kabla ya kuwasilisha taarifa zilizopo katika pointi ya 2.1 na 2.2, waulize washiriki wanajua nini kuhusu Uwezo – Chimbuko lake, kuanzishwa kwake, juhudi nyingine kama hiyo duniani kote, nk. Andika majibu ubaoni. Kisha, someni pointi 2.1. na 2.2 kwa pamoja.

2.1 CHIMBUKO LA UWEZO NI NINI?

• Uwezo ni juhudi inayofanya kazi katika nchi za Kenya, Uganda na Tanzania ambayo ilianza mwaka 2009, kufuatia hamasa iliyotokana na Ripoti ya Mwaka ya Hali ya Elimu (ASER) huko India. • Tathmini zinazoongozwa na wananchi za kuhusu kujifunza kwa watoto, kama ASER na Uwezo, zinafanywa kila mwaka katika mabara 3 na nchi 8 duniani kote: Kenya, Tanzania, Uganda, India, Pakistan, Mali, Senegal, na Mexico. • Juhudi hizi huru zinafanya kazi pamoja kama familia, kukusanya na kushirikishana ushahidi kuhusu ujuzi halisi wa watoto katika kusoma na kuhesabu. • Si kwamba wanashirikishana taarifa wao kwa wao tu, lakini pia wanatoa taarifa kwa wananchi, serikali za mitaa na kitaifa, na mashirika muhimu duniani kote yenye nia ya kuboresha kiwango cha kujifunza kwa watoto. • Hadi sasa, jitihada hizi zimetathmini watoto zaidi ya milioni moja duniani kote. Ukanda wa Afrika Mashariki peke yake, takriban watoto 350,000. • Kwa pamoja, tathmini zinazoongozwa na wananchi zinashirikisha maelfu ya wafanyakazi wa kujitolea kila waka. Katika Afrika Mashariki, zaidi ya wahojaji wa kujitolea 20,000 hutembelea kaya kila mwaka. • Wewe ni sehemu ya juhudi hii, ya wananchi kufanya kitu kushughulikia tatizo la ujifunzaji linalowakabili watoto wetu.

SURA YA 2: KUHUSU UWEZO NA MCHAKATO WAKE

Dakika 45

Page 7: Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya

7Uwezo | Elimu Bora, Jukumu Langu

2.2 JE, UWEZO NI JUHUDI INAYOSIMAMA YENYEWE?• Hapana, Uwezo ni sehemu ya jitihada kubwa na huru katika Afrika Mashariki iitwayo Twaweza. • Twaweza inafanya kazi ya kutoa taarifa za kiutendaji kwa wananchi ili waweze kuleta mabadiliko katika jamii zao. • Twaweza ipo katika nchi zote tatu za Afrika Mashariki. Wape washiriki fursa ya kutafakari na kupokea taarifa hii, ambayo inaweza kuwa mpya kwa wengi wao. Waombe wajaze kipengelele hiki katika sehemu ya shughuli ndani ya kitabu chao cha mwon-gozo, mmoja mmoja au wakiwa katika jozi. Lengo la kazi ni kuimarisha kujifunza kwao sehemu hii kwa kulinganisha “nini nilikuwa nadhani” na “sasa najua nini.”

2.3 UWEZO HUFANYAJE KAZI ZAKE?

Kabla ya kuelezea mchakato ulioneshwa sehemu hii, anza kwa kuwauliza washiriki ni badiliko gani kubwa la kijamii ambalo Uwezo inataka kufanikisha?

Unaweza kupata baadhi ya majibu yafuatayo:

- kuinua ubora wa elimu katika nchi za [Kenya/Uganda/Tanzania] - kuboresha matokeo ya ujifunzaji katikanchi za [Kenya/Uganda/Tanzania] - kukusanya ushahidi juu ya matokeo ya ujifunzaji katika nchi za [Kenya/Uganda/Tanzania] - kujenga uelewa wa watu kuhusu matokeo ya ujifunzaji katika nchi za [Kenya/Uganda/ Tanzania]

Baada ya kukusanya baadhi ya mawazo; andika majibu sahihi ubaoni: Lengo la muda mrefu la Uwezo la kuleta mabadiliko ya kijamii ni kuelekeza umakini kwenye matokeo ya ujifunzaji kwa kutumia ushahidi halisi uwezo wa watoto katika stadi za msingi na kusoma na kuhesabu.

Elezea kwa wahojaji wa kujitolea yale majibu kama “kukusanya ushahidi ...” na “kujenga uelewa ...” ni hatua kuelekea lengo hilo, lakini si lengo la mwisho la Uwezo. Hata hivyo, wao ni sehemu muhimu ya mchakato wa Uwezo kwa ajili ya kufikia malengo yake yaliyokusudiwa. Sasa, uko tayari kuelezea mchakato.

Page 8: Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya

8 Uwezo | Elimu Bora, Jukumu Langu

Mara baada ya takwimu zote kukusanywa, hufanyiwa kazi katika kituo cha takwimu Nairobi na timu za kila nchi hutoa ripoti ya kila mwaka, iitwayo: “Je, Watoto Wetu Wanajifunza?” Pia huandaliwa ripoti moja ya ukanda mzima wa Afrika Mashariki, na nyingine moja kwa kila nchi.

Kila mwaka, zaidi ya wahojaji/watafiti wa kujitolea 20,000 , hutembelea kaya kwenye kila wilaya katika nchi za Kenya, Tanzania, na Uganda. Wao hutathmini viwango vya kusoma na kufanya hesabu kwa watoto wenye umri wa miaka 7-16.

1.3.

2.

Ripoti ya mwaka inatoa matokeo kwa kila wilaya. Ina maelezo ya kina ya watoto wangapi wana ujuzi au hawana ujuzi wa kusoma na kufanya hesabu kwa kiwango ambacho kingeweza kutarajiwa wafikie kulingana na ngazi za madarasa yao.

TANZANIA

Unaweza kuhitaji kuwa na nakala za Ripoti za Uwezo za kikanda na kitaifa za miaka ya nyuma kwa ajili ya kuzitumia kama vielelezo vya kuelezea mchakato ufuatayo:

Page 9: Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya

9Uwezo | Elimu Bora, Jukumu Langu

Ni matumaini ya Uwezo kwamba mazungumzo na mijadala hii itawahamasisha wananchi kuchukua hatua za kuboresha elimu katika jamii zao

Matokeo ya ripoti hizi hutumika kuchagiza mazungumzo na mijadala inayohusu kujifunza kwa watoto nchini kote.

Baada ya hapo, matokeo ya ripoti huwasilishwa kwa jamii pana kwa njia mbalimbali, ili kwamba yaweze kuwafikia viongozi wa serikali pamoja na wananchi wa kawaida: wazazi, wanafunzi, na jamii ngazi za msingi.

4.

5.

6.

Inawezekana kabisa kwamba maelezo yaliyotolewa hapo juu yatachochea mjadala kati ya washiriki, ambao watakuwa na maoni na maswali mengi ya kufuatilia.JS

Page 10: Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya

10 Uwezo | Elimu Bora, Jukumu Langu

Vidokezo kwa ajili ya kuwezesha majadiliano:

• Simamia muda vizuri ili majadiliano yasizidi dakika 10.• Jibu maswali kwa kadri ya uwezo wako, na kuhakikisha kuwa unafikisha mawazo muhimu yafuatayo kwa waratibu vijiji:

1. Mchakato ni jinsi Uwezo inavyoamini itaweza kufikia malengo yake ya muda mrefu.2. Mchakato huu ni ubunifu, au wazo jipya linalotawa kazi za Uwezo. Badala ya kusubiri ma badiliko yatokee kutoka juu kuja chini (serikali), ni wananchi wenyewe ambao wataleta mabadiliko kuanzia chini kwenda juu. 3. Kabla ya Uwezo, hakukuwa na ushahidi wa kila mwaka unaopatikana kiurahisi juu ya matokeo ya kujifunza katika nchi za Afrika Mashariki. Kukusanya na kushirikishana ushahidi ambao mtu yeyote anaweza kuelewa kuhusu viwango vya kujifunza nimafanikio muhimu sana ya Uwezo, mwaka baada ya mwaka. 4. Kabla ya Uwezo, viwango vya kujifunza vya watoto haikuwa mada iliyojadiliwa mara kwa mara katika vyombo vya habari.Uwezo imechukua hatua muhimu kuhamisha mtazamo kutoka miundombinu/vitendeakazi na kuelekea matokeo ya ujifunzaji.5. Waratibu wa Vijiji ni sehemu muhimu ya Jitihada ya Uwezo. Mawazo yao juu ya jinsi ya kuongeza ufahamu na kuwapa nguvu wananchi kuchukua hatua ya kuboresha matokeo ya ujifunzaji yanakaribishwa.

Wahamasishe washiriki kushirikishana mafanikio kutoka katika maeneo ya kazi ambayo yanaonesha kuwa inawezekana kuleta mabadiliko kwa kufuata mchakato Uwezo. Je, wameshuhudia mifano halisi ya ongezeko la mwamko kuhusu matokeo ya ujifunzaji? Je, wanajua jitihada zozote za wananchi za kuongeza ubora wa elimu katika jamii?

2.4 MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA KUHUSU MCHAKATO WA UWEZO

Swali: Baada ya wahojaji wa kujitolea kukusanya takwimu, zinakwenda wapi? Zinafanywa nini? Jibu: Takwimu zinarekodiwa katika kijitabu cha utafiti. Takwimu hizi hufanyiwa kazi katika kituo cha takwimu cha Nairobi. Wataalamu wengi wa takwimu, ikiwa ni pamoja na wanaotoka Ofisi za Tak-wimu za kila nchi husika, huchambua takwimu hizo. Mratibu wa Nchi na Meneja wa Kanda wana jukumu la msingi la kusimamia mchakato wa kuandika ripoti. Kuna ripoti moja ya kikanda na ripoti moja kwa kila nchi. Ripoti huchapishwa na kusambazwa katika kila ofisi za nchi za Uwezo.

Swali: Baada ya matokeo kuchapishwa, kwa jinsi gani Uwezo hufanya kazi na serikali na Wizara ya Elimu? Jibu: Ingawa Uwezo hushirikishana matokeo ya tathmini na serikali za kitaifa na serikali za mitaa, Uwezo siyo mshauri wa serikali wala hairatibu hatua zozote. Swali: Kama haiishauri serikali, Uwezo inafanya nini? Jibu: Lengo la Uwezo ni kuhamisha mjadala kuhusu elimu kutoka pande zote mbili katika ngazi ya taifa na / au ngazi ya mtaa. Badala ya kuuliza kuhusu madarasa mangapi yamejengwa, walimu walioajiriwa, na vitabu vilivyotolewa, Uwezo inauliza swali rahisi tu, “Je, watoto wetu wanajifunza?” Uwezo inasambaza taarifa kuhusu viwango vya kujifunza ili kujenga uelewa na kuwahamasisha wale ambao wanajali kuhusu kujifunza kwa watoto wachukue hatua kuboresha elimu ya watoto wao.

Page 11: Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya

11Uwezo | Elimu Bora, Jukumu Langu

Swali: Uwezo inanufaikaje na kile inachofanyaJibu: Uwezo haipati manufaa ya kifedha kutokana na tathmini. Uwezo inaamini kuwa wananchi wenye taarifa na motisha ni mawakala wenye nguvu zaidi katika kuleta mabadiliko. Kufahamisha na kuhamasisha wananchi kuchukua hatua kuboresha elimu katika nchi za Afrika Mashariki ndiyo dhamira kuu na tuzo muhimu ya Uwezo.

2.5: CHANGAMSHA MWILI NA TAFAKURIIli kusaidia kuimarisha yale ambayo wahojaji wa kujitolea wamejifunza katika kipindi hiki, Mchezo wa Kurusha Mpira unaweza kutumika kuwachangamsha washiriki na kuwasaidia kukumbuka kipindi kilichopita. Mchezo wa Kurusha Mpira ni nusu ya mapitio na zoezi la kutia nguvu.

1. Omba kila mtu asimame na kuunda duara. Washiriki wote wageukie ndani, ili wawe wanatazamana.

2. Rusha mpira mdogo wa karatasi au kitu chochote laini na chepesi kwa mtu fulani katika mduara..

3. Mtu yeyote atakayedaka mpira anapaswa kuwaambia washiriki jambo moja ambalo wamejifunza katika kipindi kilichokwisha.

4. Kisha anarusha mpira kwa mtu mwingine.

5. Kisha mtu huyo anaelezea niniwamejifunza katika somo lililopita.

6. Endelea na mchezo huo mpaka kila mtu awe amepata mpira angalau mara moja na kupata fursa ya kushiriki.

Page 12: Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya

12 Uwezo | Elimu Bora, Jukumu Langu

SURA YA 3: UCHAGUZI WA SAMPULI, MBINU NA KUWAPATA WAHOJAJI/WATAFITI WA KUJITOLEA

3.1 MALENGOKuna sababu kuu mbili kwa nini kipengele hiki kimejumuishwa kwenye mafunzo:

1. Waratibu wa Kijiji wanakutana na maswali mfululizo kuhusu vigezo vinavyotumiwa kuchagua EAs, shule, na kaya kwa ajili ya utafiti na tathmini ya kila mwaka. Hadi sasa, Waratibu wa vijiji hawajapata taarifa za kutosha kujibu maswali haya kwa ufanisi. Kuna wakati, maswali yanatokea kutokana na kukosekana kwa imani kutoka kwa walimu na wazazi kuhusu uwazi kwenye mbinu za Uwezo za kuchagua sampuli. Kuna nyakati walimu wanakatishwa tamma na wao kutohusishwa kwenye utafiti.

2. Waratibu wa vijiji watakuwa wakiwasidia Waratibu wa Wilaya katika kuhakiki ramani za EA na kutengeneza (au kurekebisha) orodha za kaya. Pia watakuwa wakiwasaidia wahojaji wa kujitolea wakati wa utafiti wenyewe. Kwa hiyo, wanahitaji kukumbushwa jinsi ya kutekeleza majukumu haya kwa usahihi.

Hadi mwisho wa kipindi hiki, washiriki wa mafunzo wanapaswa kuelewa: • Jinsi Maeneo ya Kuhesabia (EAS), kaya, na watoto wanavyochaguliwa kwa ajili ya tathmini kila mwaka• Jinsi ya kuhakiki ramani za EA • Jinsi ya kutengeneza (au kurekebisha) Orodha za Kaya• Jinsi ya kuwaajiri wahojaji wa kujitolea

3.2 MUUNDO WA UTAFITI WA UWEZO

Sehemu ya kwanza ya mafunzo kwenye sura hii itajikita kusaidia washiriki wa mafunzo kufahamu dhana muhimu zifuatazo na umuhimu wake katika kuandaa utafiti wa Uwezo: • Uchaguzi sampuli kinasibu • Sampuli wakilishi • “Uwiano wa uwezekano wa ukubwa wa sampuli” (kipengele cha tatu kwenye namba 2.2)

Inashauriwa kuwa utumie mifano kueleza dhana hizi. Njoo na kadi nyingi, vipande, mipira, au kitu kingine chochote ambacho unaweza kuonesha “uchaguzi sampuli”, “sampuli nasibu,” “sampuli wakilishi,” na “ Uwiano wa uwezekano wa ukubwa wa sampuli.”

Dakika 120

Lengo ni kuhakikisha waratibu wa vijiji wanajua vya kutosha kuhusu mbinu za uchaguli sampuli za Uwezo ili waweze kujibu maswali kwenye maeneo ya utafiti kwa kujiamini. Hakikisha unaelezea kwa ufupi na kwa urahisi - hakuna haja ya kuelezea kwa kina.

Page 13: Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya

13Uwezo | Elimu Bora, Jukumu Langu

3.3 NANI ANAPIMWA NA KUTATHMINIWA KILA MWAKA?

Tathmini na utafiti wa Uwezo unafanywa kwenye sampuli nasibu yenye uwakilishi wa kitaifa kwa watoto wenye umri wa miaka 7 hadi 16.

Swali: Je, sampuli maana yake nini? Jibu: Sampuli ni sehemu ndogo ya vitu au watu miongoni mwa kundi kubwa. Kwa maana ya Uwezo, ina maana kuwa si kila mtoto katika nchi anafanyiwa tathmini kila mwaka, lakini sehemu tu ya watoto wote.

Swali: Je, ‘sampuli nasibu’ maana yake nini? Jibu: Ina maana kuwa kila mtoto ndani ya sampuli ya watoto watakaotathminiwa anachaguliwa kwa bahati nasibu, kama kushinda bahati nasibu.

Swali: Je, ‘uwakilishi wa kitaifa’ maana yake nini? Jibu: Ina maana kuwa ingawa si kila mtoto mwenye umri wa miaka 7 hadi 16 atapimwa, watoto wa kutosha watapimwa kwa usahihi kuwakilisha ukweli halisi wa viwango vya kujifunza vya wato to nchini kote.

Pitia kwa haraka na washiriki kuhusu mifumo wa kisiasa nchini Tanzania; kupitia mchoro uliochorwa ubaoni. Inapaswa kueleweka kwao kuwa eneo kubwa la kisiasa ni wilaya, ambapo linaundwa na vijiji/mitaa kadhaa. Na vijiji/mitaa inagawanyika katika sehemu ndogo ndogo zinazoitwa Maeneo ya Kuhesabia(EA), ambayo hutumika kwenye sensa ya watu.

3.4 MBINU YA KUCHAGUA SAMPULI YA UWEZO NI NINI?

Mbinu ya kuchagua sampuli ni utaratibu unaotumika kuchagua Maeneo ya Kuhesabia (EAS), kaya, na watoto kwa ajili ya zoezi la Uwezo.

• Kila wilaya katika nchi za Kenya, Tanzania, na Uganda ina fursa sawa na uwezekano wa kushiriki katika jaribio na utafiti.

• Kwa Kenya, wilaya zote za sensa huchaguliwa. Hata hivyo, kwa Uganda na Tanzania ni sampuli tu ya wilaya hizi ambazo zitachaguliwa kwa ajili ya tathmini ya mwaka 2014(utaratibu huu si wa kudumu na unaweza kubadilika miaka ijayo).

• Kutoka ndani ya kila wilaya, Maeneo ya kuhesabia (EAs) 30 huchaguliwa kinasibu. Hata hivyo, wilaya na Maeneo ya Kuhesabia (EAs) yenye idadi ya juu ya watu na kaya yana uwezekano mkubwa wa kuchaguliwa kwa ajili ya utafiti.

• Kisha, ndani ya kila EA, kaya 20 huchaguliwa kinasibu kushiriki katika utafiti huo. • Kila mwaka, Uwezo huchukua sampuli 20 za Maeneo ya Kuhesabia (EAs) kutoka kwenye sampuli

ya mwaka uliopita, na kujuzimuisha na nyingine 10 mpya. Hii ndio sababu baadhi ya Maeneo ya Kuhesabia (EAs) huendelea kuwemo katika utafiti kwa miaka kadhaa mfululizo.

EAs zilizochaguliwa Mwaka wa 1 EAs zilizochaguliwa Mwaka wa 2

Page 14: Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya

14 Uwezo | Elimu Bora, Jukumu Langu

3.5 ENEO LA KUHESABIA NI NINI?

Nchi imegawanyika katika vitendo vya kiutawala chini ya serikali kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Maeneo ya Kuhesabia (EA) kimsingi yameundwa kwa lengo la kufanyia sensa ya Kitaifa. Eneo la Kuhesabia linaweza kuchukua kijiji kimoja kamili, sehemu ya kijiji au zaidi ya kijiji kimoja kwenye maeneo Fulani.

3.6 MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA KUHUSU MBINU ZA UCHAGUZI SAMPULI ZA UWEZO

Washiriki wa mafunzo sasa wana fursa ya kuyafanyiakazi kivitendo yale ambayo wamejifunza katika sehemu iliyotangulia. Waombe wafanye igizo-dhima wakiwa katika jozi kwa muda wa dakika 10. Mmoja wao atakuwa mwalimu au mzazi, na mmoja wao, Mratibu wa Wahojaji wa Kujitolea.Mmoja ambaye anacheza kama mwalimu au mzazi atauliza baadhi ya maswali ya kawaida kutoka shule na katika jamii kuhusu mbinu za sampuli za Uwezo, na mwingine atakuwa akijibu kwa kutumia taarifa alizojifunza muda mfupi.

Hapa chini kuna mifano michache ya maswali hayo, lakini washiriki wa mafunzo wanahimizwa kuja na maswali yao, kutokana na uzoefu wao kwenye maeneo ya kazi.

• Kwa nini Uwezo inaendelea kuja katika shule/eneo hili kama uchaguzi ni wa kinasibu?• Tunataka kufanyiwa tathmini, kwa nini Uwezo haijafika katika shule /EA yetu? • Kwa nini Uwezo inakusanya takwimu kutoka kaya chache tu katika EA?

Sambaza miongoni mwa timu kuchunguza kama wamejifunza vya kutosha taarifa mpya. Jibu swali lolote ambao timu inaweza kuwa nalo na andaa maelezo ya ufahamu kuhusu masomo unayohitaji kurejea upya pindi zoezi litakapofika mwisho.

Mara baada ya zoezi kufika mwisho, uliza washiriki wa mafunzo kama wana maswali yoyote. Hata kama hakuna maswali, rejea na fanya mapitio tena ya mbinu na dhana ambazo unaona zilikuwa ngumu kwa washiriki

Waratibu wa vijiji watamsaidia Mratibu wa Wilaya kuhakiki ramani ya Maeneo ya Kuhesabia na kuandaa orodha za Kaya. Ramani na orodha ya kaya vitakuwa msingi wa kazi kwa wahojaji wa kujitolea wakati wa kufanya utafiti na tathmini, hivyo ni lazima vifanywe kwa usahihi.

Kuhakikisha washiriki wa mafunzo wanafuatilia kwa makini zaidi kipindi hiki, fanya mchezo mfupi wa kuchangamsha mwili utakaowasaidia kuchangamsha mwili na akili kabla ya kuendelea na mafunzo. Unaweza kuja na mchezo wako mwenyewe au waombe washiriki kupendekeza mchezo mfupi wa kuchangamsha mwili.

JS

3.7 RAMANI ZA MAENEO YA KUHESABIA Ramani ni nini?Ramani ni uwakilishi wa vielelezo vilivyo katika uso wa dunia vikiwemo vya asili au vilivyotokana na shughuli za kibinadamu, katika kipande cha karatasi kwa kutumia uwiano au kipimo cha ramani.

Page 15: Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya

15Uwezo | Elimu Bora, Jukumu Langu

3.7.1 KUHAKIKI RAMANI ZA MAENEO YA KUHESABIAMaeneo ya kuhesabia (EA) ambayo Waratibu wa Vijiji watafanyia kazi yameshafanyiwa sampuli na Ofisi ya Taifa ya Takwimu. Watapatiwa ramani kuwaongoza kutambua mipaka ya maeneo ya kuhesabia. Kila EA lazima iwe na ramani; kama ramani haipo, lazima wamjulishe Mratibu wao wa Wilaya. Mratibu wa Wilaya atakuwa tayari alishamtembelea Katibu Tawala wa Mkoa (RAS) na Mkuu wa Wilaya kuitambulisha Uwezo na kupata kibali. Zifuatazo ni hatua ambazo Waratibu wa Vijiji watafanya katika EA. 1. Kumtembelea Mwenyekiti Mtaa/ Kijiji /Afisa Mtendaji wa Kijiji (VEO) wa Eneo la Kuhesabia lililo chaguliwa na kuwasilisha barua ya utambulisho. 2. Kumuonesha Mwenyekiti/Afisa Mtendaji wa Kijiji ramani ya EA. Muombe Mwenyekiti wa Kijiji/ Mtaa/ VEO kama watakusindikiza kwenye eneo la kuhesabia kuhakiki taarifa za ramani, ikiwa ni pamoja mipaka. 3. Kuongeza maelezo yoyote yanayokosekana kwenye ramani.

3.7.2 USOMAJI WA RAMANI YA EA HATUA KWA HATUA Kuna mambo muhimu yalioneshwa kwenye ramani ya eneo la kuhesabia watu.(Pata maelezo zaidi kwenye jalada ya nyuma ya hiki kitabu).

3.8 KAYA NI NINI?Kaya ni kundi la watu ambao wanaishi ndani ya nyumba moja kwa kawaida. Watu hawa pia lazima wawe wanapika na kula kutoka chungu kimoja, ndiyo watachukuliwa kama kaya moja.

MUHIMU! Mkuu wa kaya si lazima awe wanaume. Kuna kaya zinazoongozwa na wanawake na watoto. Kaya hizi ni pia hujumuishwa kwenye orodha ya kaya.

3.9 KUENDESHA ZOEZI LA KUORODHESHA KAYA Mara baada ya Waratibu wa vijiji kuhakiki ramani za EA, wataigawa EA katika sehemu 4 na kuanza kuorodhesha kaya.

Kadiri unavyoendelea na sehemu hii na washiriki wa mafunzo, hakikisha unasisitiza kuwa lazima wagawanye EA katika sehemu nne ili kufanya kazi kwa mpangilio mzuri. Kwa njia hii, watafanya kazi kwa ufanisi zaidi na kuhakikisha kuwa wameorodhesha kikamilifu kaya zote sehemu moja kabla ya kuendelea na sehemu nyingine.1. Kama hakuna orodha ya kaya katika EA, wanapaswa kumuomba Menyekiti wa kijiji/VEO kuwasaidia kuandaa orodha hiyo. 2. Kama orodha ya EA haina taarifa za sasa, wanapaswa kurekebisha taarifa walizonazo kwa msaada wa Mwenyekiti wa Kijiji/Afisa Mtendaji wa Kijiji 3. Ikiwa idadi ya kaya haijulikani, watajaza idadi ya wakazi na kisha kutembelea EA kujua idadi ya kaya kwa kila makazi.4. Pale ambapo watu wanashirikiana chumba au nyumba, lakini wanapika tofauti, wataorodheshwa kama watu wa kaya tofauti.5. Muombe Afisa Mtendaji wa Kijiji/Mwenyekiti wa Kijiji kuwasaidia kuorodhesha wakuu wote wa kaya kwenye EA iliyochaguliwa.

JS

Mara baada ya kumaliza maelezo ya jumla ya jinsi ya kufanya Uhakiki wa ramani ya EA na kuorodhesha Kaya, waulize washiriki wa mafunzo kama wana maswali yoyote kabla ya kuhamia kwenye sehemu ya pili, Uchaguzi wa Kaya. Kama hakuna maswali, basi uliza maswali yako mwenyewe kuwapima uelewa wao

Page 16: Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya

16 Uwezo | Elimu Bora, Jukumu Langu

3.10 JE, KAYA ZINACHAGULIWAJE KUTOKA KWENYE ORODHA YA KAYA?• Kumbuka: kaya 20 tu ndizo zinafanyiwa sampuli kwa kila EA. • Ili kuchagua kaya 20 kinasibu, unatakiwa kwanza kupata namba ya kutenganisha kaya itakayochaguliwa . Je, unatafiti kila baada ya kaya 2, kila kaya 3, n.k? hii ni namba ya kuhesabia (nth).• Ili kupata namba ya kuhesabia, gawanya kwa 20 jumla ya idadi ya kaya zote katika EA. Kwa mfano

- Kuna jumla ya kaya 117 katika EA 1. Gawanya 117 kwa 20. (117 ÷ 20 = 5.85) - Karibisha jibu hilo ili liwe kwenye namba nzima (5.85 6). Ambayo itakuwa 6 - Kwa madhumuni ya EA 1, namba 6 ndiyo namba ya kuhesabia (nth). Chagua kila kaya 6 kutoka orodha ya EA iliyopo katika sampuli ya utafiti. Endelea kufanya hivyo mpaka utakapokuwa umechagua kaya 20. • Kuchagua kaya 5 mbadala endelea na utaratibu huo huo. Kama namba ya kuhesabia (nth) imefikia kwenye kaya ambayo imeshachaguliwa, ruka na uchague kaya inayofuata. • Ili kujua sehemu ya kuanzia, zipe namba karatasi sita kuanzia namba 1 hadi 6. Ziinamishe chini na uchague moja. Hii itakuwa kaya namba moja. Kila kaya iliyoorodheshwa kati ya namba ya kuhesabia (nth) na moja inapata nafasi sawa ya kuchaguliwa kuwa sehemu ya utafiti.

Baada ya kuelezea jinsi kaya zinavyochaguliwa kwa ajili ya utafiti na tathmini, ni muhimu kufanya mapitio ya utaratibu kwa mchoro.

Kabla ya mafunzo, andaa mchoro mkubwa wa kijiji cha kaya 40, mchoro uwe mkubwa wa kutosha ili washiriki wote waweze kuona.

Pitia mchakato mzima wa kutambua namba ya kuhesabia (nth), uchaguzi wa kaya na kaya mbadala kwenye mchoro. Usitoe hotuba- ruhusu washiriki kusema hatua inayofuata, na kaya gani inayofuata inayopaswa kuchaguliwa. Watie moyo washiriki kuuliza maswali katika hatua yoyote kama hawaelewi vizuri.

Mara baada ya shughuli hii kukamilika, ruhusu washiriki kufanya jaribio lifuatalo mmoja mmoja (dakika 10). Kisha, pitieni maswali na majibu kama kikundi. Hii itakuwa nafasi ya ziada ya kufanya marudio ya somo.

Sasa, jipime mwenyewe kwa kiasi gani umejifunza katika somo hili: KWELI SI KWELI

Kaya zinazohusika katika utafiti zimechguliwa na wataalamu kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu. Maeneo ya Kuhesania yanayotembelewa hunapokea fedha na ufadhili kutoka Uwezo.Mratibu wa Wilaya ndiye mwenye jukumu kuu la kuchora ramani za EAs.Kila mwaka, Uwezo inafanya utafiti wake kwenye wilaya 20, katika Maeneo ya kuhesabia(EA) 30 kwenye kila wilaya, na katika kila kaya kwenye EA zilizochaguliwa.Watu wanaoishi pamoja lakini wanapika tofauti wanachukuliwa kama sehemu ya kaya moja.

Page 17: Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya

17Uwezo | Elimu Bora, Jukumu Langu

3.11.2 KUWAPATA WAHOJAJI WA KUJITOLEA WA UWEZOKabla ya kufika kwenye EA, inatarajiwa kuwa utakuwa umekamilisha hatua tatu zifuatazo:

1. Kutuma mabango ya ‘Tangazo la kuhitaji wahojaji wa kujitolea’ kwa watu unaowajua katika sampuli za EAs, na kuwaomba wayaweke mabango katika maeneo ya wazi- Ofisi ya kiongozi Maeneo ya maduka, Kanisa/Msikiti na kadhalika; 2. Kupokea simu au ujio wa waombaji watarajiwa na kutengeneza orodha ya watu wanaohitaji. Kama wapo zaidi ya 6, tengeneza orodha ya waombaji wa kiume na wa kike ambao unaona ni bora na wana vigezo maalumu vilivyoorodheshwa katika bango; 3 Wasiliana na waombaji unaotaka kuwafanyia usaili kabla ya kwenda kijijini, ili wakusubiri kwa siku utakayokwenda kwa ajili ya usaili.

Utakapokutana na waombaji, omba wakupatie vitambulisho vyao na cheti cha kumaliza elimu ya sekondari (CSEE) au kinachofanana na hicho. Thibitisha utambulisho na sifa zao. Waulize waombaji maswali kadhaa ili kuwajua zaidi, na kuthibitisha sifa zao, vitu wanavyopendelea na utayari wao kwa ajili ya tathmini ya Uwezo. Kumbuka kuwa utaajiri waombaji ambao lazima wawe wakazi katika kijiji hicho na kwamba mmoja atakuwa wa kiume na mmoja wa kike. Shauriana na Mratibu wa Wilaya kama kuna mazingira ambayo masharti hayo hayawezi kufikiwa.

3.11 WAHOJAJI WA KUJITOLEA WA UWEZO Wahojaji wa kujitolea ni wananchi wenye kiu na utayari wa kuboresha elimu ambao hukubali kwa ridhaa yao wenyewe kushiriki kwenye tathmini ya Uwezo kama wakusanya takwimu kwenye vijiji vyao. Ushiriki wao ni wa hiari siyo wa kulazimishwa. Wahojaji wa kujitolea hutafutwa na wadau wa Uwezo walioko wilayani. Kila Eneo la Kuhesabia (EA) lina wahojaji wa kujitolea wawili, na wahojaji hao lazima wawe mwanamke na mwanaume. Ni sehemu ya majukumu ya Mratibu wa kijiji kuwasaidia wahojaji wa kujitolea wakati wa mafunzo na wakati wa kukusanya takwimu.Jukumu kubwa la wahojaji wa kujitolea ni kukusanya takwimu kijijini, shuleni na kwenye kaya kwa kutumia zana walizopatiwa.

3.11.1 ZANA GANI HUTUMIA WAHOJAJI WA KUJITOLEA? Wahojaji wa kujitolea hutumia zana za utafiti zifuatazo:

1. Kijitabu cha majaribio: Hiki kina sampuli nne za majaribio kwa kila somo kwenye masomo yote matatu: Kiswahili, Kiingerza na Hisabati. Mhojaji wa kujitolea anatakiwa atumie sampuli moja ya jaribio kwa kila mtoto.2. Vitabu vya takwimu za utafiti: vina fomu ya taarifa za kijiji ambazo zinatumika kumhoji kiongozi wa kijiji au mtaa; fomu ya takwimu za shule; na fomu ya taarifa za kaya ambazo zinatumika kukusanya taarifa kwenye kaya na kurekodi ngazi za ujuzi wa mtoto baada ya kupimwa. Fomu ya taarifa za kaya pia hurekodi taarifa za majaribio ya ziada kama swali la ziada na kipimo cha uwezo wa macho kuona. 3. Bango la mrejesho wa papo kwa papo: Bango hili hutumika kutoa mrejesho kwa wazazi kuhusu ujuzi wa watoto katika kusoma na kuhesabu.

Waelekeze Waratibu wa vijiji jinsi wahojaji wa kujitolea wanavyofanya tathmini shuleni na kwenye kaya, huku ukirejea mwongozo wa wakufunzi B & Mwongozo wa kazi wa wahojaji wa kujitolea.

Page 18: Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya

18 Uwezo | Elimu Bora, Jukumu Langu

SURA YA 4: KUWASILIANA NA SHULE

4.1 MALENGO

Mara baada ya matokeo ya tathmini kuchambuliwa na ripoti kuchapishwa, Waratibu wa Vijiji watakuwa na nafasi ya kwenda tena shuleni na kuwasilisha matokeo. Madhumuni ya kifungu hiki ni kuwaongoza jinsi kuwasilisha matokeo shuleni kwaa ufanisi na usahihi.

Hadi mwisho wa somo hili, Waratibu wa Uwezo wa Vijiji wanatakiwa: • Kujua hatua za kuwasilisha matokeo ya Uwezo 2012/2013 shuleni• Kuwa na uwezo wa kusoma, kufafanua, na kueleza Muhtasari wa Matokeo • Kuwa na uwezo wa kusoma, kufafanua, na kueleza nafasi ya ufaulu kiwilaya • Kuwa tayari kujibu maswali magumu kutoka shuleni na kwa jamii kuhusu matokeo ya Uwezo ya 2014

Waulize washiriki wa mafunzo kama wana maswali yoyote kuhusu hatua za kuasilisha matoke ya Uwezo ya 2014 kabla ya kuhamia kwenye sehemu ya pili. Kama hakuna maswali, basi unapaswa kuuliza maswali yako mwenyewe kupima uelewa wa washiriki.

Q A

Dakika 120

1. Rudi kwenye shule ambazo zilifanyiwa utafiti. 2. Utapatiwa bango ambalo lina taarifa zifuatazo:

4.2 KUTOA TAARIFA ZA MATOKEO YA UWEZO SHULENI NA JAMII

• Mfano wa vipimo (kusoma na kuhesabu) • Muhtasari wa ya Matokeo ya Tathmini ya wilaya husika• Wilaya na daraja lililopo Kulingana na Matokeo ya Uwezo Tanzania

3. Kabla ya kubandika matokeo shuleni, kutana na Mwalimu Mkuu (au Naibu wa Mwalimu Mkuu, kama Mwalimu Mkuu hayupo).

4. Jitambulishe tena, na kwa kutumia bango, eleza matokeo kwa Mwalimu Mkuu. Anza na Muhtasari wa Tathmini ya Matokeo.

5. Mara baada ya kuelezea matokeo na kujibu maswali kutoka kwa Mwalimu Mkuu, omba idhini ya kubandika matokeo mahali panapoonekana katika mazingira ya shule.

Page 19: Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya

19Uwezo | Elimu Bora, Jukumu Langu

Ifuatayo ni mbinu inayopendekezwa kufundisha washiriki jinsi ya kusoma na kutafsiri muhtasari wa matokeo:

4.3 MUHTASARI WA MATOKEO YA TATHMINI

Muhtasari wa Tathmini ya matokeo kwa ajili ya wilaya husikautakuwa na taarifa hii (huu ni mfano tu, wala si matokeo halisi):

Kusoma silabi/herufi Darasa la 2 22%% ya watoto ambao hawawezi kusoma maneno rahisi ya ngazi Darasa la 3 39%% ya watoto ambao hawawezi kusoma aya rahisi ya mistari 4 Darasa la 3

Darasa la 458%40%

% ya watoto ambao hawawezi kusoma “hadithi” rahisi (DRS la 2 ngazi ya Nakala)

Darasa la 3

Darasa la 4

Darasa la 5

74%58%43%

UJUZI WA KUSOMA: JE, WATOTO WANAWEZA KUSOMA?

LUGHA AMBAYO WATOTO WALIYOTAKIWA KUSOMA: KISWAHILI

Wilaya: Kasulu,Tanzania

% ya watoto ambao hawawezi kutambua nambari hadi 100

Darasa la 2

Darasa la 3

Darasa la 4

52%27% 12%

% ya watoto ambao hawawezi kutoa Darasa la 2

Darasa la 3

Darasa la 4

66%40%22%

HISABATI: JE WATOTO WANAWEZA KUTAMBUA NAMBARI?

HISABATI: JE WATOTO WANAWEZA KUTOA?

Wilaya: Kasulu,Tanzania

Page 20: Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya

20 Uwezo | Elimu Bora, Jukumu Langu

1. Kama mapitio, anza kwa kuuliza washiriki kwa mujibu wa mitaala ya kitaifa, watoto wanatarajiwa kuweza nini kwenye kusoma, kuandika na kuhesabu wanapofikia darasa la 2? Jibu sahihi ni:

Hadi mwisho wa darasa la 2, watoto wanapaswa kuwa wamepata stadi za juu; yaani waweze kusoma na kuelewa hadithi na kufanya hesabu rahisi.2. Kisha, eleza chati ya matokeo (kusoma na kuhesabu), mstari kwa mstari. Hakikisha unawasaidia kuelewa dhana muhimu zifuatazo:

a. Fanya mapitio ya haraka kujua ‘asilimia’ ni nini. b. Muhtasari unaonesha idadi ya watoto ambao hawawezi kufaulu mazoezi ya darasa la 2/ Darasa la 3/Darasa la 7. Kuonesha matokeo ya idadi ya watoto ambao hawawezi kufikia ngazi ya darasa fulani ni njia fanisi zaidi kuonesha uhalisia wa tatizo linalohitaji kutatuliwa (matokeo duni ya kujifunza). c. Kwa kuwa Uwezo inawapima watoto katika kaya, matokeo yanaonyesha kiwango cha kujifunza kwa watoto wote, Bila kujali kama wameandikishwa shule au wapo nje ya shule.

3. Mwisho, wahimize washiriki wa mafunzo wakuambie maana ya matokeo (sampuli). Kujifunza kwao juu ya kusoma muhtasari wa matokeo haujakamilika bila wao kuweza kutafsiri takwimu. Wasaidie kupata jibu wao wenyewe, na wewe utaingilia pale tu tafsiri zao siyo sahihi.

Wahimize washiriki wa mafunzo kuuliza maswali katika hatua yoyote wakati unaonesha jinsi ya kusoma na kutafsiri matokeo. Kama hawana maswali, waulize maswali yako mwenyewe kuwapima uelewa wao katika kipengele hiki.

Kama msisitizo wa somo la jinsi ya kusoma na kutafsiri Muhtasari wa Matokeo, waombe washiriki wa mafunzo waandike kwenye madaftari yao jinsi wanavyoweza kuelezea kila mstari wa Muhtasari wa Matokeo (kusoma na kuhesabu) kwa mtu mwingine. Wape mfano kwa mstari wa kwanza wa matokeo ya kusoma: Kati ya kila watoto 100 wa ngazi ya Darasa la 2, watoto 22 hawawezi kutambua herufi.

Mchakato watakaofuata kuelezea matokeo kwa Walimu Wakuu utatoa picha katika kuendelea na zoezi juu ya jinsi ya kusoma Muhtasari wa Matokeo::

4.4 JINSI YA KUELEZEA MUHTASARI WA MATOKEO YA TATHMINI

1. Muoneshe Mwalimu Mkuu Mfano wa jaribio la kusoma. Mkumbushe mwalimu kuwa vipimo vya majaribio ya Uwezo vilitumia viwango vya kazi za darasa la 2.2. Elezea matokeo mstari kwa mstari. “Kama mnavyojua, watoto wote wa darasa la 2 wanapaswa kuwa na uwezo wa kusoma herufi/silabi. Matokeo ya wilaya yanaonesha kuwa kwa kila watoto 100 wa darasa la 2, watoto 22 hawawezi kutambua herufi”.3: Unaweza pia kutaka kumfahamisha Mwalimu Mkuu kuwa matokeo yanabainisha ujuzi wa watoto ambao wako shuleni na ambao hawapo shuleni, kwa kuwa watoto walikuwa wakipimwa uelewa katika kaya zao.

JS

Page 21: Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya

21Uwezo | Elimu Bora, Jukumu Langu

4.5 UPANGAJI WA UFAULU KIWILAYA KUTOKANA NA USHAHIDI WA UWEZO

Upangaji wa ufaulu kiwilaya kulingana na Matokeo ya Uwezo utakuwa na taarifa hizi (hii ni sehemu tu ya mfano, na si daraja halisi):

Upangaji wa ufaulu kiwilaya kwa wastani wa viwango vya ufaulu vya majaribio yote kwa pamoja kwa watoto wote wenye umri wa miaka 7-16Nchi: Tanzania

NAFASI MKOA WILAYA KIWANGO CHA UFAULU(%)

1 Iringa Mafinga 78%2 Kilimanjaro Muleba 75%3 Manyara Longido 70%

Karatasi ya madaraja ya ufaulu inatumia viwango vya ufaulu. Kiwango cha ufaulu kina maana kuwa na uwezo wa kufaulu majaribio yote ya kusoma na kuhesabu kwa wakati mmoja. Mwanafunzi anahitaji alama 100% katika somo la kuhesabu NA 100% katika kusoma ili kufaulu majaribio yote kwa pamoja. Kwa hiyo, wastani wa ufaulu ni kigezo muhimu.

Ifuatayo ni mbinu inayopendekezwa kwa ajili ya kufundishia washiriki jinsi ya kusoma na kutafsiri Upangaji wa ufaulu wa Wilaya:

1. Anza kwa kupitia maana ya kiwango cha ufaulu: a. Kupata 100% - maana yake ni kuwa na uwezo wa kusoma hadithi bila shida kwenye jaribio la ya kusoma na uwezo wa kufanya hesabu za kuzidisha kwenye jaribio la hisabati. b. Kufaulu majaribio YOTE ya kusoma na kuhesabu.

2. Kisha, sisitiza kuwa daraja la ufaulu kiwilaya, tofauti na Muhtasari wa Matokeo, linajikita kwenye ujuzi wa watoto wenye umri wa miaka 9-13 tu. Watoto wenye umri wa 9-13 wanapaswa kuwa na uwezo wa kufaulu majaribio yote kwa alama 100%.

3. Kama ni muhimu, rudia kwa mara nyingine kuelezea maana ya ‘asilimia’.

4. Elezea kuwa wastani wa ufaulu (asilimia kwa kila wilaya) inaonesha jinsi watoto wengi wangefaulu majaribio yote kwenye EA ya kawaida katika wilaya hiyo.

5. Mwisho, wahimize washiriki wakuambie maana ya (sampuli) matokeo ya daraja la ufaulu kiwilaya. Mafunzo yao juu ya kusoma muhtasari wa upangaji wa ufaulu kiwilaya hautakamilika bila wao kuweza kutafsiri takwimu. Wasaidie kupata jibu wao wenyewe na ingilia kati pale tu tafsiri zao siyo sahihi.

Wahimize washiriki wa mafunzo kuuliza maswali katika hatua yoyote wakati unaonesha jinsi ya kusoma na kutafsiri madaraja ya ufaulu kiwilaya. Kama hawana maswali, waulize maswali yako mwenyewe kuwapima uelewa wao katika sehemu hii.

Mchakato watakaofuata katika kuelezea matokeo kwa Walimu Wakuu utatoa mwanga wa jinsi ya kuendelea na zoezi la kusoma Muhtasari wa Matokeo:

JS

Page 22: Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya

22 Uwezo | Elimu Bora, Jukumu Langu

4.6 JINSI YA KUELEZEA UPANGAJI WA MADARAJA YA UFAULU KIWILAYA

1. Elezea kwa Mwalimu Mkuu kuwa upangaji wa madaraja ya ufaulu unatokana na watoto wangapi wenye umri wa 9-16 wanatarajiwa kufaulu majaribio yote (kusoma na kuhesabu) katika wilaya husika. Kwa mfano: Kwenye EA ya Wilaya ya mafinga, watoto 78 kati ya 100 wenye umri wa miaka 10-16 watakuwa katika ngazi ya hadithi kwenye ujuzi wa kusoma na katika ngazi ya kugawanya kwenye hesabu.2. Muoneshe Mwalimu Mkuu/Kiongozi wa kijiji/mtaa nafasi iliyoshika wilaya yake.

4.7 JINSI YA KUJIBU MASWALI KUTOKA KWA WALIMU WAKUU JUU YA USHAHIDI KUTOKA UTAFITI WA UWEZO

Pindi waratibu wa vijiji watakapowasilisha muhtasari wa matokeo na madaraja ya ufaulu kiwilaya Inawezekana Mwalimu Mkuu atakuwa na maswali mengi kuhusu matokeo. Hapa chini kuna baadhi ya majibu ya maswali magumu utakayotakiwa kujibu..

Swali: Je, Afisa Elimu wa Wilaya au Wizara ya Elimu wamepata matokeo haya? Je, wana taarifa kuhusu shule hii?Jibu: Matokeo ya Uwezo kwa miaka yote yanapatikana kwa mtu yeyote ambaye anataka kuyapitia, awe Kiongozi wa serikali au mwananchi. Yanapatikana kwenye machapisho na kwenye mtandao. Uwezo pia inawasilisha matokeo kwa upana zaidi kwa kupitia njia nyingi. Hata hivyo, Uwezo huchapisha matokeo ya wilaya tu. Matokeo ya kila shule na eneo la kuhesabia ni siri. Hata viongozi wa serikali hawawezi kupata taarifa hiyo

Swali: Uwezo itafanya nini na taarifa hii? Je, Uwezo inafanya kazi na serikali?Jibu: Uwezo inatoa matokeo ya tathmini yake kwa upana zaidi kwa sababu inaamini kuwa mabadiliko chanya hayawezi kuletwa na chombo kimoja peke yake, kama serikali. Kila mtu mwenye shauku ya kuboresha ujifunzaji wa watoto anapaswa kushiriki kuleta mabadiliko. Uwezo inatoa taarifa lakini si kuratibu hatua yoyote itakayotekelezwa na kundi lolote..

Swali: Je, Uwezo itafanyanini kusaidia kuboresha matokeo ya watoto wetu?Jibu: Lengo la Uwezo ni kuwasilisha matokeo ili serikali, na jamii, wapate ufahamu wa viwango halisi ya kujifunza vya watoto. Sisi tunatoa mapendekezo na dondoo juu ya hatua ambayo inaweza kuboresha kujifunza.

Baada ya kupitia sehemu hii juu ya jinsi ya kujibu maswali kutoka shuleni, waulize washiriki wa mafunzo kama wana maswali yoyote kwao wenyewe. Kama hawana lolote, waulize swali lako kupima ufahamu wao wa kujifunza katika sehemu hii. Washiriki wa mafunzo sasa wana fursa ya kuyafanyia kazi kivitendo yale waliyojifunza katika sehemu iliyotangulia: • Jinsi ya kueleza Muhtasari wa Tathmini ya Matokeo • Jinsi ya kueleza Muhtasari wa upangaji ufaulu kiwilaya • Jinsi ya kujibu maswali kutoka kwa Walimu Wkuu na ushahidi uliotolewa

Waombe wafanye igizodhima wakiwa katika makundi ya watu 3 au 4. Wengine wacheze kama mwalimu mkuu, wengine kama Waratibu wa Vijiji wakiwasilisha matokeo ya mwaka 2014.

Zungukia vikundi kuchunguza jinsi walivyoelewa taarifa mpya. Jibu maswali yoyote wanayoweza kuwa nayo na andaa maelezo ya ufahamu kuhusu somo lolote utakalohitaji kurejea pindi zoezi linapofikia mwisho.

JS

Page 23: Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya

23Uwezo | Elimu Bora, Jukumu Langu

SURA YA 5: MAZINGIRA MAGUMU

5.1 MALENGO

Kuifikia jamii na kukusanya takwimu siku zote siyo jambo rahisi. Watu si kila siku wako tayari kushiriki kwenye utafiti na wanaweza wasielewe malengo ya Uwezo. Hapa chini kuna aina nne kuu za mazingira magumu unayoweza kukumbana nayo, na vidokezo vya namna ya kukabiliana navyo:

Hadi mwisho wa kipindi hiki, Mratibu wa kijiji anapaswa:• Kuelewa mtazamo sahihi wa kuchukua kwa watu ndani ya jamii• kuwa amejifunza mbinu chache za jinsi ya kushughulikia mazingira na hali ngumu

Tofauti na vipengele vingine vya mafunzo ya waratibu wa vijiji, sehemu hii itajikita kujenga ujuzi, kuliko kupanua maarifa ya washiriki kwenye eneo husika. Kwa hiyo, dhumuni la kipindi hiki ni kutoa mbinu na mitazamo kushughulikia mazingira na hali ngumu watakazokumbana nazo.

5.2 CHA KUFANYA UNAPOKUMBANA NA MAZINGIRA MAGUMU

• Usiku wa jana yake, Waratibu wa vijiji watakuwa walipata fursa ya kuandaa igizo fupi la kichekesho kwa pamoja na wenzao.• Kila timu itakuwa ilipatiwa moja ya mazingira manne ya kufanyia igizo. Kazi yao ni kuandaa igizo la mazingira magumu la dakika 3 (siyo zaidi ya dakika 3!), kuigiza jinsi hali ngumu inavyopaswa kushughulikiwa. Wako huru kutumia mapendekezo yaliyo kwenye mwongozo wa kufanyia kazi au kuongeza ya kwao. Pia wanahimizwa kutumia masomo ya sehemu za mafunzo zilizopita (kuhusu Uwezo, Kuchagua sampuli na mbinu, kuwasilisha matokeo).• Watakapomaliza kuigiza, wana dakika 2 (siyo zaidi ya dakika 2!) kufanya majumuisho kwenye kikundi juu ya mbinu walizotumia kushughulikia hali ngumu.• Siku ambayo kipindi cha sehemu hii kinafanyika, timu zote zitatapata fursa ya kuwasilisha maigizo yao. • Anza na mazingira/hali yoyote unayotaka, lakini hakikisha maigizo yote yanayohusiana na hali/ mazingira hayo yanawasilishwa kwenye kundi lilelile.• Baada ya timu zote kwenye mazingira/hali A kuwasilisha maigizo yao, endesha mjadala wa dakika 5 na wanakikundi waliobaki.• Mawazo gani mazuri yamewasilishwa kwenye maigizo? Je, wana mapendekezo yoyote ya nyongeza ya jinsi ya kushughulikia hali hizi? Unaweza kumpa kazi mmoja wa washiriki kuandika maelezo kwenye ubao.• Fanya hivyo hivyo kwenye maigizo ya mazingira/hali tatu yaliyobaki

Dakika 120

Page 24: Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya

24 Uwezo | Elimu Bora, Jukumu Langu

• Daima kuwa mwaminifu kwa wazazi na kamwe usiahidi msaada au usaidizi wowote kutoka Uwezo.

• Wasaidie wazazi kuelewa umuhimu kujua ngazi za ujifunzaji za watoto wao.

• Kuwa na subira na mwenye kujali.

• Kuwa msikilizaji mzuri na kujaribu kuelewa ni kwa nini mtu anakosa imani.

• Tatua mashaka yao na hofu kwa kuwapa maelezo ya wazi kuhusu mchakato wa Uwezo.

• Kuwa rafiki na mnyenyekevu ili kupata imani ya mtu.

1. Wazazi wenye matarajio makubwa

2. Kutoaminiwa na walimu na wazazi

Je, Uwezo itafanya nini kwa ajili ya familia yangu?

Je, Uwezo itazifanyia nini taarifa inazokusanya?

• Kuifikia jamii na kukusanya takwimu siku zote siyo jambo rahisi. Watu si kila siku wako tayari kushiriki kwenye utafiti na wanaweza wasielewe malengo ya Uwezo. Hapa chini kuna aina nne kuu za mazingira magumu unayoweza kukumbana nayo, na vidokezo vya namna ya kukabiliana nayo:

Page 25: Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya

25Uwezo | Elimu Bora, Jukumu Langu

• Kuwa na subira na mwenye kujali - baadhi ya familia zinaishi katika hali ngumu sana.

• Toa vidokezo au masimulizi, kulingana na ushahidi, wa njia rahisi inayojulikana kuboresha matokeo ya kujifunza ya watoto wao.

• Wasaidie wazazi kuelewa ni kwa nini ni muhimu kujua ngazi ya kujifunza ya watoto wao.

• Daima kuwa mpole na mwenye heshima kwa wazazi.

• Usipendelee upande wowote kwa wazazi au mtoto.

• Washirikishe taarifa za matokeo ya motto kirafiki ili waweze kusaidia kuboresha matokeo ya kujifunza ya mtoto wao.

3. Hisia za Wazazi kuwa hawawezi kufanya chochote kuwasaidia watoto kujifunza

4. Wazazi kuwaadhibu watoto wao kwa matokeo mabaya ya tathmini

Je, unafikiri una uwezo wa

kushawishi jinsi shule inavyoelimisha

watoto wetu?

WEWE !!!..........

Page 26: Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya

26 Uwezo | Elimu Bora, Jukumu Langu

SURA YA 6: MASUALA YA MAADILI

6.1 MALENGO

Hadi mwisho wa kipindi hili, Waratibu wa kijiji wanatakiwa:• Wawe na uelewa wa kina kuhusu majukumu na kazi zao• Wawe na uelewa wa kina kuhusu majukumu yao dhidi ya majukumu ya wahojaji wa kujitolewa wenye uzoefu mdogo• kuelewa matarajio ya tabia na mwenendo wao kwenye maeneo ya utafiti

Sehemu muhimu zaidi kwenye mafunzo haya itakuwa ni kuwataarifu Waratibu wa vijiji kuhudu mipaka ya majukumu yao. Kwa kuelewa kikamilifu majukumu yao, watakuwa na mahusiano mazuri na Waratibu wa Wilaya, Wahojaji wadogo na jamii kwa ujumla.

6.2 KAZI ZA MRATIBU WA KIJIJI

a) Hudhuria siku tatu mafunzo ya kanda; b) Kusaidia Mratibu wa Wilaya kupitia ramani ya EA, orodha ya kaya na kuajiri wahojaji wa kujitolea na kutambulisha Uwezo kwa viongozi wa jadi na viongozi wa kijiji kama inavyoelekezwa; c) Kusaidia kuratibu mafunzo ya siku mbili ya wahojaji wa kujitolea; d) Kusaidia utekelezaji wa tathmini kwenye Maeneo ya Kuhesabia yaliyochaguliwa; e) Kusaidia katika kukusanya na kuhakiki vitabu vya utafiti. f) Kutoa taarifa za matokeo ya utafiti kwenye shule zilizofanyiwa utafiti

6.3 MAHUSIANO YAKO NA WAHOJAJI WA KUJITOLEA

Dakika 30

Wasaidie wahojajii wa kujitolea ili wafanye kazi zao kwa usahihi:

• Jibu maswali yao yote • Wasaidie kujaza vitabu vya taarifa na vitabu vya

utafiti kwa usahihi • Wasaidie kuwatahini watoto kwa usahihi • Wasaidie kutatua masuala yoyote wanayoweza

kukumbana nayo shuleni au kwenye kaya • Wasaidie kusimamia muda wao kwa usahihi

Kuwamotisha na kuwatia moyo wahojaji wa kujitolea

Wewe ni mfano wa kuigwa na kiongozi wa wahojaji wa kujitolea. Waoneshe wahojaji wa kujitolea kuwa watu wanaofanya kazi na Uwezo wanajituma, ni wachapakazi na wakarimu.

Wewe siyo bosi wala msimamizi wa wahojaji wa kujitolea. Unaweza kuwa na uzoefu zaidi, lakini wewe ni sehemu ya kundi. Hufanyi kazi peke yako.

Kudumisha nidhamu ya wahojaji wa kujitolea.

Kuwakosoa wahojaji wa kujitolea kwa kushindwa kufanya kazi yao kwa usahihi.

Kusubiri kubaini makosa ambayo wahojaji wa kujitolea huenda wakafanya

KAZI YAKO NI... KAZI YAKO SI...

Page 27: Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya

27Uwezo | Elimu Bora, Jukumu Langu

Unapaswa kuuliza kama kuna maswali yoyote baada ya kipindi. Kama hakuna maswali, waulize wewe maswali kupima uelewa wa washiriki sehemu hii.

6.4 VIWANGO VYA MAADILI

Tabia yako katika jamii inapaswa kuakisi malengo na maadili ya Uwezo.

MAADILI YA UWEZO TABIA YAKO

Uwazi Daima kuwa mkweli: usitoe ahadi za uongo, usitie chumvi, usitoe majibu ya uongo kama unapata shida na maswali

Si-kwa-faida Usitoe wala kupokea zawadi yoyote, ikiwemo fedha, ili kuwapatia takwimu na ushahidi uliokusanya.

Huru na isiyoegemea upande wowote

Usimpendelee yeyote katika jamii. Usitoe ushauri kwa shule na familia kupendelea ufumbuzi wowote wa njia ya watotokujifunza.

Heshima kwa watoto na familia

Watendee watoto na familia kwa heshima, uvumilivu, na wema, bila kujali jinsi wao wanavyokutendea wewe.

Mawasiliano Kama kuna jambo lolote kubwa, toa taarifa mara moja.

JS

Page 28: Uwezo Elimu Bora, Jukumu Langu UWEZO TANZANIA 2014 · kujifunza kuhusu nini kila mmoja anapenda kufanya katika muda wake wa ziada, anapendelea nini, anatoka kijiji gani na kazi ya

28 Uwezo | Elimu Bora, Jukumu Langu

Uwezo Tanzania iliyoko Twaweza

S.L.P. 38342 Dar Es Salaam,TanzaniaE: [email protected]

www.uwezo.net

NAMNA YA KUSOMA RAMANI YA EA HATUA KWA HATUA

Mambo muhimu yaliyoonyeshwa kwenye ramani ya eneo la kuhesabia watu ni:-1. Kichwa cha Ramani (Title); 2. Mshale wa Kuonyesha Kaskazini (Northings);

Mshale wa Kaskazini ni alama iliyowekwa kwenye ramani ya EA ili kumwongoza msoma ramani kutambuau elekeo wa ramani yake. Msoma ramani anatakiwa kutambua uelekeo wa Kaskazini wa mahali alipo na kuiweka sawa ramani ya EA aliyo nayo kufuatana na uelekeo wa mshale wa Kaskazini ulio kwenye ramani kabla ya kuanza kutambua mipaka ya EA yake. Namna rahisi ya kutambua uelekeo wa Kaskazini ni kama ifuatavyo:

mbele yako ni Kaskazini, nyuma yako ni kusini, kushoto kwako ni Magharibi na kulia kwako ni Mashariki. Mahali eneo lilipo pameelezwa kwa kutumia mfumo wa mageresho (namba 12 za kutambulisha EA). Idadi ya tarakimu kwa kila geresho, kama vile kwa Mkoa, Wilaya, Kata, Kijiji/Mtaa na EA ni kama ifuatavyo:-

Mfano wa mageresho/namba ya utambulisho: 05 06 083 01 324

Ikimaanisha mkoa 05, wilaya 06, kata ya 083, kijiji 01 na EA 324. Kwa mfano namba/ mageresho hayo hapo juu yanawakilisha:Mkoa wa Morogoro (05) Wilaya ya

(324) = 050608301324. Namba kama hizi ndizo zitakazotumika kutambulisha EA mbalimbali

3. Kipimo cha Ramani (Scale); 4. Ufunguo (Key); na5. Maelezo ya nyongeza.

Eneo la Utawala Idadi ya tarakimu Mkoa 2 Wilaya 2 Kata 3 Kijiji/Mtaa 2 EA 3Jumla 12