Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
-
Upload
wanachuoni -
Category
Documents
-
view
163 -
download
1
description
Transcript of Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
1
Uwajibu Wa Kuwachukia
Makafiri Na Kutofanya
Nao Urafiki
Kauli Za Wanachuoni Mbali Mbali
Imefasiriwa Na Kukusanywa Na:
Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
2
Kuwapenda makafiri ni namna mbili:
1) Kuna mapenzi yanayolazimisha kuritadi na kutoka katika Uislamu. Haya ni
mapenzi ya kuwapenda kwa ajili ya dini yao.
2) Kuna mapenzi ambayo ni haramu, lakini hayomtoi mtu katika Uislamu. Haya ni
mapenzi ya kuwapenda makafiri kwa sababu ya mambo ya dunia yao. Wakati
mwingine kunatokea kuchanganya na kutatizika kati ya kuishi vizuri na makafiri
(wasio katika vita na Waislamu) na kati ya kuwachukia na kuwakataa. Ni lazima
kutofautisha kati ya mambo mawili. Kuwatendea haki, kuishi nao vizuri bila ya
mapenzi ya ndani, kama kumuonea huruma mnyonge wao, kuwa na kauli nzuri kwao
kwa njia ya kuwa mpole kwao na kuwa na huruma, ni jambo linalofaa. Allaah
Mtukufu kuhusu jambo hilo Amesema kuwa: "Allaah Hakukatazeni kuhusu wale
ambao hawakupigeni katika dini na hawakukutoeni katika nyumba zenu,
(hakukatazeni) kuwafanyia wema na kuwafanyia uadilifu” [al-Mumtahinah 60 : 08].
Ama kuwachukia na kuwafanya adui ni jambo jingine. Jambo hilo Ameliamrisha
Allaah Mtukufu kwa kauli Yake isemayo kuwa: "Enyi ambao mmeamini, msiwafanye
maadui wangu na maadui wenu wapenzi mnaokutana nao kwa upendo". [al-
Mumtahinah 60 : 01] Kwa hiyo inawezekana kufanya uadilifu katika kushirikiana
nao pamoja na kuwachukia na kutowapenda, kama alivyofanya Mtume kwa Mayahudi
wa Madiynah.” (Imenukuliwa kutoka kwenye kitabu ”Maswali muhimu katika
maisha ya Muislamu” uk. 56 footnot ya 07)
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
3
Fataawa zilizomo:
Kuwapenda makafiri ni namna mbili
01. al-Walaa´ wal-Baraa
02. Hukumu Ya Kumuita Kafiri Kuwa Ni Rafiki!
03. "Nchi Za Waislamu Hazina Uislamu, Uislamu Unapatikana Ulaya"
04. Asiyemkufurisha Kafiri Na Yeye Ni Kafiri Kama Yeye
05. Mtu Kuwaambia Ndugu Zake Manaswara "Mimi Nawapenda"
06. Khatari Ya Kusema Manaswara Na Mayahudi Ni Ndugu Zetu?
07. Kuwasifia Makafiri Na Kuwaponda Waislamu
08. Hii Ndio Sababu Ya Wasilamu Kuwachukia Makafiri
09. Kutangamana Na Makafiri
10. Kujifananisha Na Makafiri Kimavazi
11. Kuvaa Nguo Yenye Picha Ya Kafiri?
12. Inajuzu Kuwapenda Wazazi Ambao Ni Makafiri?
13. Kuwapenda Na Kuwanusuru Makafiri Yanapokutana
14. Kumpenda Mke Kafiri Kwa Dini Yake
15. Kuwasifia Manaswara Na Mayahudi Kwamba Wanachunga Ahadi
16. Atakayejifananisha Na Makafiri Basi Yeye Ni Katika Wao
17. Kutabasamu Na Kumkumbatia Kafiri
18. Tafsiri Sahihi Ya Aina Za Kufanya Urafiki Na Makafiri
19. Kuita Nchi Ya Kikafiri Kuwa Ni Nchi Rafiki
20. Wanaosema "Heshimuni Dini Ya Kinaswara Na Kiyahudi"
21. Kwanini Wastaajabu Kwa Teknolojia Walio Nayo Makafiri
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
4
22. Kukubaliana Na Makafiri Juu Ya Kitu Cha Shirki
23. Kuleta Kicheko Na Makafiri
24. Kuangalia Mazoezi Ya Makafiri Kwenye TV Na Kutamani Washinde
25. Ibara Ya Kusema "Makafiri Ni Waislamu Bila Ya Uislamu"
26. Kumpenda Raisi Wa Nchi Ambaye Ni Kafiri
27. Ni Kupi Kujifananisha Na Makafiri?
28. Kuwapenda Makafiri Pamoja Na Kuwasaidia Dhidi Ya Waislamu Na
Uislamu
29. Uwajibu Wa Kuchukia Makafiri Na Ukafiri Wao
30. Hukumu Ya Kusema Dini Zote Ni Sawa Twamuabudu Mungu Mmoja
31. Kafiri Anajijongeza Kwangu Na Kusema "Ndugu Yangu", Nifanye Nini?
32. Kubusu Kichwa Cha Mzazi Asiyeswali
33. Kusoma Elimu Ya Dini Katika Miji Ya Makafiri
34. Tofauti Kati Ya Nchi Ya Kiislamu Na Ya Kikafiri
35. Kuvaa Nguo Yenye Msalaba
36. Kumtembelea Kafiri Ambaye Ni Mgonjwa Kwa Lengo La Da´wah
37. Ufaransa Imepiga Marfuku Kuvaa Hijaab, Tuhame?
38. Kuishi Katika Miji Ya Kikafiri Pamoja Na Kudhihirisha Dini
39. Makafiri Ni Ndugu Zetu Kibinaadamu
40. Kwa nini Sisi Tu Ndo Twavaa Mavazi Ya Makafiri Wao Hawavai
Mavazi Yetu?
41. Hukumu Ya Kusema Mayahudi Na Wakristo Ni Ndugu Zetu
42. Hukumu Ya Kujiita Majina Ya Makafiri
43. Kuongea Lugha Za Makafiri Pasina Haja
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
5
44. Kuvaa Nguo (Jezi) Yenye Jina Au Picha Ya Kafiri
45. Kuvaa Suruwali Ni Kujifananisha Na Makafiri
46. Maandamano Ni Kujifananisha Na Makafiri Kikamilifu
47. Hukumu Ya Kushiriki Sikukuu Za Makafiri Na Kuwapongeza
48. Kula Pamoja Na Kafiri Na Kumpa Swadaqah
49. Jinsi Ya Kutangamana Na Makafiri Katika Shirika Unapofanya Nao Kazi
50. Mwanamke Kafa Baba Yake Mdogo Kafiri
51. Kuvaa Nguo Za Makafiri Za Kumalizia Masomo
52. Hukumu Ya Muislamu Kuwa Na Urafiki Na Makafiri
53. Kumuomba Kafiri Msaada Kwa Kitu Anachokiweza
54. Kumualika Jirani Kafiri Katika Walima
55. Kuwapa Mkono Wa Pole Makafiri Wanapofiwa
Wanachuoni waliomo:
01. Imaam Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
02. ´Allaamah Muhammad Amaan al-Jaamiy
03. ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkaliy
04. ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
05. ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
06. ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
6
بسم اللـه الرحمـن الرحيم
01. al-Walaa´ wal-Baraa´
Swali:
Kumekuja maswali mengi kuhusiana na watu ambao wanachukulia sahali al-
Walaa´ wa-Baraa´. Tunatarajia kutoka kwako kutuwekea wazi jambo hili.
´Allaamah al-Fawzaan:
Muislamu anatakiwa kuwapenda Waislamu na kuwanusuru. Na wachukia
makafiri, kuwabughudhi na akawakate katika mapenzi. Ama kuamiliana nao
katika mambo ambayo yanaruhusiwa; kama kuuza na kununua (biashara),
kujifunza kutoka kwao elimu na mambo mengine yasiyokuwa hayo - katika
mambo ya kidunia - hili halina ubaya. Hali kadhalika kumlipiza wema pindi
anapowatendea Waislamu jambo ambalo Waislamu watafaidika kwalo, au
kujizuia kuwadhuru Waislamu, nao watalipizwa wema. Anasema Allaah
(Jalla wa ´Alaa):
وه ن دياركم أن تبر ين ولم يخرجوكم م ه عن الاذين لم يقاتلوكم في الد م وتقسطوا إليهم إ لا ينهاكم اللـا ه ي نا اللـا
المقسطين
"Allaah Hakukatazeni kuwafanyia wema na uadilifu wale wasiokupigeni vita
katika Dini, na wala hawakukutoeni kutoka majumbani mwenu. Hakika
Allaah Anapenda wafanyao uadilifu." (60:08)
Hili ni kwa ajili ya kulipiza wema tu na sio kwa ajili ya mapenzi. Hili ni kwa
ajili ya kulipiza wema kutokana na wema wao watakaokuwa wamefanya. Hili
ndilo wanalostahikimakafiri. Kuwafanya ni maadui na kuwachukia. Ama
kuamiliana nao katika mambo ambayo yanawafaa Waislamu, hakuna ubaya.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/4292.mp3
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
7
02. Hukumu Ya Kumuita Kafiri Kuwa Ni Rafiki!
Swali:
Ipi hukumu ya neno rafiri kumwambia kafiri?
´Allaamah al-Fawzaan:
Haijuzu. Haijuzu kumwambia kafiri rafiki. Rafiki maana yake ni kipenzi.
Haijuzu hili.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/alldroo...
03. "Nchi Za Waislamu Hazina Uislamu, Uislamu Unapatikana Ulaya"
Swali:
Kuna mlinganizi mmoja anasema:
"Uislamu uko huku kwetu na roho yake [Uislamu huo] iko Ulaya."
Sikiliza maajabu:
"Dhati na udhahiri wa Uislamu tuko nao sisi huku katika nchi za Kiislam -
kwa mfano katika nchi hii [Saudi Arabia] - na nchi zingine katika nchi za
Waislamu, lakini roho ya Uislamu iko Ulaya."
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
8
´Allaamah Muhammad al-Jaamiy:
Maneno haya yana maana? Huu ni upotofu. Ni maneno yasiyokuwa na
maana yoyote. Hali kadhalika, kuna baadhi ya wengine wanasema:
"Katika nchi za Kiislamu kuna Waislamu bila ya Uislamu na kuna Waislamu
pasina Waislamu."
Ibara hii zamani aliisema Muhammad ´Abd [aliyekuwa Muftiy wa Misri].
Aliishi Ufaransa na akawa na ada za watu wa Ulaya akarejea katika nchi yake
[Misri] akasema hivi. Na wafuasi wake - walikuwa wanamwita ni Imaam -
walikuwa wanachukulia maneno haya ni maneno ya mtu mwenye busara
sana. Ya kwamba Uislamu unapatikana Ulaya pasina Waislamu, na katika
nchi za Waislamu kuna Waislamu pasina Uislamu. Ni kina nani ambao wako
Ulaya? Ikiwa katika zama za Muhammad ´Abd anasema maneno haya
ambayo leo yanasemwa na vijana, kuna nini Ulaya? Kumejaa pombe, maasi na
Fusuuq. Uislamu uko wapi unaopatikana Ulaya? Watu wa Ulaya wenyewe
lau watapelekewa maneno haya watayakadhibisha. Watu wa Ulaya wenyewe
lau watapelekewa maneno haya watayakadhibisha. Wao wenyewe
watayakadhibisha. Watu wa Ulaya wanajua kuwa Uislamu uko huku, dhati
yake na roho yake. Hivyo, maneno haya ni batili. Yasiwadanganye vijana.
Watanabahi.
Chanzo: http://www.eljame.com/mktba/catplay.php?catsmktba=3
04. Asiyemkufurisha Kafiri Na Yeye Ni Kafiri Kama Yeye
Swali:
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
9
Amejitokeza mmoja wa wanachuoni ambaye anamsifu mkristo anayeit-wa
Edward Sa´iyd. Na anamuomba Allaah aufaidishe Ummah kupitia kwake. Na
akasema:
"Sisi tunawachukulia wakristo wa kiarabu ni Waislamu kwa utamaduni na
ustaarabu, ingawa sio Muislamu kwa ´Aqiydah yake na Dini yake." Je,
maneno haya haya ni sahihi na huchukuliwa ni moja katika mambo
yanayovunja Uislamu wa mtu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Maneno haya ni batili na wala hayawagusi Waislamu. Bali yanamgusa
aliyeyasema. Ikiwa yeye hamkufurishi mnaswara basi yeye ndiye kafiri. Yule
asiyemkufurisha kafiri, basi na yeye ni kafiri kama yeye.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/9660
05. Mtu Kuwaambia Ndugu Zake Manaswara "Mimi Nawapenda"
Swali:
Mimi nina ndugu manaswara. Ni ninapoongea nao daima hunambia kuwa
wananipenda. Je, inajuzu kwangu kuwaambia pia kuwanawapenda, lakini sio
mapenzi ya Kishari´ah bali ni ya kimaumbile?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana. Usiwaambie kuwa mimi nawapenda, usiwaambie kuwa mimi
nawapenda. Kamwe! Waambie ikiwa kweli mnanipenda basi ingieni katika
Uislamu. Mimi nawapendelea Uislamu na muokoke na Moto.
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
10
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/7622_0.mp3
06. Khatari Ya Kusema Manaswara Na Mayahudi Ni Ndugu Zetu?
Swali:
Ipi rai yako kwa yanayosemwa na baadhi ya wenye kufutu na khaswa kupitia
chaneli za satellite wanasema: "Ndugu zetu manaswara au mfano wa maneno
haya, ibara inayoashiria kwamba sote ni waumini?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hii ni kufuru na upotofu. Allaah Atukinge. Yule anayeona kuwa manaswara
na mayahudi ni Waislamu na kwamba ni waumini na kwamba ni ndugu zetu,
huyu anaritadi kutoka katika Dini ya Uislamu. Kila yule ambaye hakumfuata
Mtume Muhammad ( صلى هللا عليه وسلم) ni kafiri, ambaye hakumfuata Mtume
Muhammad ( صلى هللا عليه وسلم) ni kafiri. Sawa ikiwa ni myahudi au mnaswara
au wasiokuwa hao. Baada ya kutumwa Mtume Muhammad ( صلى هللا عليه وسلم)
hakuna Dini wala Imani ila kumfuata Mtume Muhammad ( صلى هللا عليه وسلم).
Yule anayesema baada ya kutumwa Mtume Muhammad (صلى هللا عليه وسلم) watu
sio lazima kumuamini, wanaweza kubaki katika uyahudi na unaswara na ni
Dini sahihi, huyu huchukuliwa ni kafiri na karitadi kutoka katika Dini ya
Kiislamu.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/9657
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
11
07. Kuwasifia Makafiri Na Kuwaponda Waislamu
Swali:
Je, kuwapaka mafuta makafiri, kuitikia matendo yao na mambo yao, na kutaja
aibu za Waislamu mbele yao ni katika kuwafanya marafiki na ni katika
kuwapenda?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio. Ndani ya hili kuna kitu kama kuwasifia makafiri na kuwaponda
Waislamu. Hili ni jambo lisilojuzu. Hili dogo tuwezalo kusema ni kwamba ni
dhambi na ni maasi, hata kama uinje wake linaonekana kuwa ni kufuru.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/7618_0.mp3
08. Hii Ndio Sababu Ya Wasilamu Kuwachukia Makafiri
Muulizaji:
Ipi hukumu ya kumpenda kafiri?
´Allaamah al-Fawzaan:
Haijuzu kumpenda kafiri. Kumpenda kafiri haijuzu. Yule ambaye Allaah
Anamchukia, na wewe watakiwa kumchukia. Allaah ni adui wa makafiri, na
wewe watakiwa kuwa adui wa makafiri.
ه ورسوله ادا اللـا ون من ه واليوم الخر يواد لا تجد قوما يؤمنون باللـا
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
12
"Hutokuta (ee Muhammad صلى هللا عليه وآله وسلم) watu wanaomuamini Allaah na
Siku ya Mwisho (kuwa) wanawapenda wale wanaopinzana na Allaah na
Mtume Wake." (58:22)
كم أولياء ي وعدوا خذوا عدو ل تتا
“Msimchukue adui Wangu na adui wenu (kuwa) marafiki wandani
mkiwapelekea (siri za mikakati) kwa mapenzi." (60:01)
Haijuzu kumpenda kafiri. Kwa sababu Allaah Anawachukia, hivyo wewe
watakiwa kumchukia yule Anayemchukia Allaah. Kwa kuwa ni adui wa
Allaah. Hivyo wewe unamfanya adui yule ambaye ni adui wa Allaah.
كم أولياء ي وعدوا خذوا عدو ل تتا
"Enyi mlioamini! Msimchukue adui Wangu na adui wenu (kuwa) marafiki
wandani mkiwapelekea (siri za mikakati) kwa mapenzi." (60:01)
Muulizaji:
Na atakayempenda kafiri kwa ajili ya kitendo chake kizuri alichomfa-nyia au
kwa kuwa mwanamke kafiri ni mke wake, je pia hili limekatazwa?
´Allaamah al-Fawzaan:
Usimpende kwa ajili ya kitendo chake kizuri, lakini unamlipa kwa kitendo
kizuri alichokufanyia au kumfanyia na wewe wema.
وهم وتقسطوا إ لي هم ن دياركم أن تبر ين ولم يخرجوكم م ه عن الاذين لم يقاتلوكم في الد اللـا ل ينهاكم هللاا
"Allaah Hakukatazeni kuwafanyia wema na uadilifu wale wasiokupigeni vita
katika Dini, na wala hawakukutoeni kutoka majumbani mwenu." (60:08)
Utatangamana nae kwa wema na kumlipa kwa wema wake. Ama hilo
kukufanya wewe umpende, hapana. Usiwapende isipokuwa Waislamu peke
yao.
ه ورسوله والاذين آمنوا كم اللـا ما ولي إنا
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
13
"Hakika Waliyy (Mlinzi) wenu ni Allaah na Mtume Wake na wale
walioamini." (05:55)
Usiwapende isipokuwa Waislamu peke yao. Ama mume kumpenda mke
wake ambaye ni mkristo au myahudi, haya sio mapenzi ya ki-´Ibaadah, bali ni
mapenzi ya kimaumbile yanayokuwepo baina ya mume na mke. Hayaingii
katika mambo ya Dini. Ni kama jinsi unapenda chakula, kunywa, kumpenda
yule anayekufanyia wema. Haya ni mapenzi ya kimaumbile.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/taxonomy/term/117
09. Kutangamana Na Makafiri
Swali:
Je, inajuzu kutangamana na makafiri, kukaa nao na kuishi nao?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana. Haijuzu kutangamana nao na wala usiishi nao. Kwa kuwa hili
linaonesha dalili ya kuwapenda. Hakukuwi kutangamana nao isipokuwa ni
pamoja na kuwapenda. Kwa kuwa ungekuwa huwapendi usingelitangamana
nao. Lakini kule wewe kufanya nao biashara au kubadilishana nao faida za
kudunia, hakuna makatazo. Lakini bila ya kutangamana nao na bila ya
kuwapenda.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/8236
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
14
10. Kujifananisha Na Makafiri Kimavazi
Swali:
Ipi hukumu kwa mtu ambaye akienda katika miji ya kikafiri anavaa mavazi
yao na wala havai mavazi ambayo alikuwa akivaa katika mji wa watu wake.
Je, huku ni kujifananisha [nao]?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio. Atazingatiwa kuwa anajifananisha nao. Isipokuwa tu ikiwa kama
ataogopa lau akibaki katika mavazi yao - anaogopa asije kupata madhara au
mali yake - atavaa mavazi yao ili kuepukana na shari yao. Katika hali hii
kapewa ruhusa. Ama ikiwa na amani na wala haogopi na kafanya hilo ili
kujifananisha nao, hili halijuzu.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/8216_0.mp3
11. Kuvaa Nguo Yenye Picha Ya Kafiri?
Swali:
Ipi hukumu ya kumtukuza kafiri? Kama kuvaa picha yake kwenye kifua na
mfano wa hayo?
´Allaamah al-Fawzaan:
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
15
Haijuzu kuvaa picha hata ikiwa ni ya Muislamu. Muislamu mzuri mwenye
msimamo haijuzu kwake kuvaa picha kwenye kifua chake. Hili ni Haramu.
Vipi tusemeje ikiwa ni ya kafiri?
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/8229
12. Inajuzu Kuwapenda Wazazi Ambao Ni Makafiri?
Swali:
Je, Muislamu atakuwa mwenye kupata madhambi kwa mapenzi ya
kimaumbile kuwapenda wazazi wake makafiri, au mke wake myahudi au
mkristo?
´Allaamah al-Fawzaan:
Asimpendi kafiri. Hata kama atakuwa ni mzazi wake, au baba yake au kaka
yake. Anasema (Ta´ala):
ه ورسوله ولو كانوا آ ادا اللـا ون من ه واليوم الخر يواد م أو باءهم أو أبناءهم أو إخوانه لا تجد قوما يؤمنون باللـا
عشيرتهم
"Hutokuta (ee Muhammad صلى هللا عليه وآله وسلم) watu wanaomuamini Allaah na
Siku ya Mwisho (kuwa) wanawapenda wale wanaopinzana na Allaah na
Mtume Wake, japo wakiwa (ni) baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au
jamaa zao." (58:22)
Anatakiwa kumchukia kafiri, chuki ya kidini kwa ajili ya Allaah (´Azza wa
Jalla). Hata akiwa ni katika jamaa wa karibu sana kwake.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/8877.mp3
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
16
13. Kuwapenda Na Kuwanusuru Makafiri Yanapokutana
Swali:
Urafiki unaomtoa mtu katika Uislamu je, ni lazima uwe na mambo mawili;
kuwapenda na kuwanusuru?
´Allaamah al-Fawzaan:
Kukiwa kuna kuwapenda na kuwanusuru, huku ni kuritadi. Ama ikiwa ikiwa
ni moja wapo kati ya hayo - mapenzi bila ya kuwapenda - hili ni dhambi
kubwa katika madhambi makubwa na ni khatari kwa mtu. Au kuwanusuru
bila ya kuwapenda, hili pia ni khatari. Lakini halifikii katika kiwango cha
ukafiri.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/5096.mp3
14. Kumpenda Mke Kafiri Kwa Dini Yake
Swali:
Kuna shubuha wanaitumia baadhi ya watu pale wanaposema kuwa Dini
inaamrisha kumpenda mke. Vipi sasa ikiwa mke atakuwa ni myahudi au
mkristo. Je, huku si kuwafanya marafiki na kuwapenda makafiri?
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
17
´Allaamah al-Fawzaan:
Ikiwa anampenda kwa ajili ya Dini yake, itakuwa ni kufanya naye urafiki.
Ama ikiwa anampenda kwa ajili ya uke, haya ni mapenzi ya kindoa na wala
sio mapenzi ya kidini.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/5097.mp3
15. Kuwasifia Manaswara Na Mayahudi Kwamba Wanachunga Ahadi
Swali:
Wasemaje kwa yule anayewasifia manaswara na mayahudi kwa kuwa
wanachunga ahadi na wanajua kufanya kazi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Yeye anawasifu kwa kuwa wanachunga ahadi na wala haoni kufuru waliomo
mpaka awasifu? Wako na kufuru, na wala hakuna baada ya kufuru dhambi
nyingine. Haijuzu kuwasifu. Haijuzu kuwasifu nao wako na kufuru na ndio
aina kubwa ya dhambi na Shirki na Ilhaad. Yote haya wako nayo. Haya ni
maslahi ya kidunia yao na wala hayana uhusiano wowote na Dini wala Imani,
wanafanya hayo kwa maslahi ya dunia yao.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/8203
16. Atakayejifananisha Na Makafiri Basi Yeye Ni Katika Wao
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
18
Swali:
Kauli ya Mtume (صلى هللا عليه وسلم):
"Yule mwenye kujifananisha na watu, basi yeye ni katika wao."
Je, ina maana ni katika wao kihakika? Akijifananisha na makafiri anakuwa
kafiri kabisa?
´Allaamah al-Fawzaan:
Anasema Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) kuhusu
Hadiyht hii:
"Dogo tuwezalo kusema ni dalili ioneshayo uharamu wa kujifananisha [na
makafiri], hata kama uinje wake inaonesha dalili kuwa ni kufuru."
Kujifananisha kunatofautiana; kuna wakati inakuwa kufuru, Fisq na maasi.
Inatofautiana kutokana na aina zake.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/8186
17. Kutabasamu Na Kumkumbatia Kafiri
Swali:
Ipi hukumu ya kutabasamu kwa kafiri, kupeana naye mikono na
kukumbatiana naye?
´Allaamah al-Fawzaan:
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
19
Haijuzu kutabasamu kwa kafiri. Lakini akikusalimia unamrudishia. Kama
alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
"Msianze kuwasalimia mayahudi na manaswara. Na wakiwatolea Salaam,
warudishieni kwa kusema: "Wa ´alaykum."
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/8177
18. Tafsiri Sahihi Ya Aina Za Kufanya Urafiki Na Makafiri
Swali:
Kuna ambao wanasema "Kufanya urafiki na makafiri kunakuwa kwa sampuli
tatu:
1) Kufanya urafiki nao kikamilifu pasina mipaka kabisa." Hii ni kufuru
inayomtoa mtu katika Uislamu.
2) "Kwa ajili ya kuhifadhi maslahi maalum na hakuna kinachopelekea kufanya
hivyo kama kuwa na khofu na mfano wake." Hili ni Haramu na sio kufuru.
3) "Mtu kufanya hivyo kwa ajili ya kuwa na khofu kwa makafiri na mfano
wake." Hukumu ya hilo inajuzu, kwa sharti kufanya urafiki huku iwe kwa
uinje tu na si moyoni. Je, mgawanyo huu ni sahihi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio. Haya ndio tuliyoyasema katika darsa yetu leo. Haya ndio jumla ya
tuliyoyasema katika darsa yetu.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/7312.mp3
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
20
19. Kuita Nchi Ya Kikafiri Kuwa Ni Nchi Rafiki
Swali:
Inajuzu kuita nchi ya kikafiri kuwa ni "nchi rafiki" au kumwita kafiri kuwa ni
"rafiki yangu"?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hili halijuzu. Kwa kuwa rafiki maana yake ni mapenzi. Hawi rafiki ila yule
unayempenda.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/91.mp3
20. Wanaosema "Heshimuni Dini Ya Kinaswara Na Kiyahudi"
Swali:
Kupitia kampeni hii kumejitokeza ambao wanalingania kuheshimu Dini tatu
kukiwemo na unaswara na uyahudi, pamoja na kujua kwamba - kama
ulivyosema - ya kuwa Dini zao zimefutwa na Uislamu sio katika Dini yao?
´Allaamah al-Fawzaan:
Sisi tunaheshimu asli ya Dini; Dini ya ´Iysa na Muusa (´alayhimus-Salaam).
Na tunaheshimu kitabu chake Tawrat. Tunaheshimu asli. Na tunaheshimu
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
21
Dini za Mitume wote kwa jumla. Dini za Mitume tunaziheshimu. Ama Dini
zilizofutwa na zilizobadiliwa, sisi hatuziheshimu. Kwa kuwa haziwi Dini tena.
Asli ya Dini ndio sahihi, kutoka kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa). Sisi tunaheshimu
Dini ya Muusa na ´Iysa.
ا ب ق اق ويعقو والسباط وم ولوا آمنا ه وما أنزل إلينا وما أنزل إلى إبراهيم وإسماعيل وإس ى ا أوتي موس اللـا
بهم بيون من را وعيسى وما أوتي النا
"Semeni: “Tumemwamini Allaah na yaliyoteremshwa kwetu na
yaliyoteremshwa kwa Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quwb na al-
Asbaatw na aliyopewa Muwsaa na ‘Iysaa na waliyopewa Manabii kutoka kwa
Mola wao." (02:136)
Na nguzo sita za Imani: "Kuamini Allaah, Malaika Wake, Mitume Wake na
Mitume Wake... " Tunaamini vitabu vyote na Mitume wote. Ama Dini
zilizofutwa na kubadilishwa, sisi hatuziheshimu. Sisi hatuishii kumtetea
Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) peke yake. Wallaahi
naapa lau kama kuna yeyote atakayemponda ´Iysa (´alayhis-Salaam)
msimamo wetu utakuwa kama msimamo wa Mtume Muhammad (Swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam). Wallaahi naapa lau kama kuna yeyote
atakayemponda Muusa (´alayhis-Salaam) basi msimamo wetu utakuwa kama
msimamo wa tunavyomtetea Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa
sallam). Hatutofautishi baina ya yeyote katika wao. Hili sio khaswa kwa
Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), bali hili
msimamo wetu ni kwa Mitume wote, tunawatetea, tunawaheshimu na
tunawaamini (´alayhimus-Swalaat was-Salaam).
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/8166
21. Kwanini Wastaajabu Kwa Teknolojia Walio Nayo Makafiri
Swali:
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
22
Ipi hukumu ya mwenye kukithirisha kustaajabu kwa mayahudi, elimu zao,
mafanikio yao na kuona wako na haki kwa hayo, je huku ni kuritadi au
kuwafanya ni marafiki na ipi nasaha zako kwa watu hawa?
´Allaamah al-Fawzaan:
Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anamwambia Mtume Wake:
نيا لنفتنهم في ياة الد نهم زهرة ال عنا به أزواجا م نا عينيك إلى ما متا ه ول تمدا
"Na wala usikodolee macho yako kwa yale Tuliyowastareheshea baadhi ya
watu miongoni mwao, (kwani) hayo ni mapambo ya maisha ya dunia tu."
(20:131)
نيا ياة الد بهم بها في ال ه ليعذ ما يريد اللـا ون وتزهق أنفسهم وهم كافر فل تعجبك أموالهم ول أولدهم إنا
"Basi isikupendezee mali zao, na wala watoto wao. Hakika Allaah Anataka
kuwaadhibu kwayo katika maisha ya dunia, na zitokelee mbali nafsi zao
(katika mauti) na hali wakiwa makafiri." (09:55)
نيا وتزهق أ بهم بها في الد ه أن يعذ ما يريد اللـا م وهم كافرون نفسه ول تعجبك أموالهم وأولدهم إنا
"Na wala isikupendezee mali zao, na watoto wao. Hakika Allaah Anataka
kuwaadhibu kwayo duniani, na zitokelee mbali nafsi zao (katika mauti), na
hali wao ni makafiri." (09:85)
ورزق ربك خير وأبقى
"Na riziki ya Mola wako ni bora zaidi na ni yenye kubakia." (02:131)
Haijuzu kwa mtu kustaajabu kwa yaliyo kwa makafiri na kusema hawa ndio
wako katika haki. Na kama wangekuwa hawako katika haki wasingelifikia
teknolojia hii. Ewe ndugu! Huku ni kuwavuta pole pole. Usistaajabu kwa
mazuri ya dunia walio nayo kwa kuwa haya ni katika kuwavuta pole pole.
Hili ni jambo lipo katika Qur-aan, limetajwa katika Qur-aan. Allaah
Kamkataza Mtume Wake asistaajabu kwa walio nayo makafiri na asidokolee
macho yake kwa walio nayo.
ورزق ربك خير وأبقى
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
23
"Na riziki ya Mola wako ni bora zaidi na ni yenye kubakia." (02:131)
Riziki ndogo iliyo ya Halali ni bora kuliko vya dunia vingi, mali na maendeleo
pamoja na kufuru. Kuwa na pato kidogo pamoja na Imani na kushikamana na
Dini ni bora kuliko kupata dunia yote pamoja na kufuru.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/8160
22. Kukubaliana Na Makafiri Juu Ya Kitu Cha Shirki
Swali:
Atakayekubaliana na makafiri kwa uinje na si kwa undani na bila ya
kuchukia, kufuru yake inakuwa ndogo?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana. Atakapokubaliana nao kwa uinje bila ya kuchukia hata kama si kwa
undani, anakuwa kama wao. Akakubaliana nao juu ya kumshirikisha Allaah,
juu ya kwamba Masiyh ni mwana wa Allaah na wala hapingi hili, akasema hii
ni dini yao na ´Aqiydah yao na Dini zote ni sawa, kila mmoja ashikamane na
la kwake. Huyu anaritadi kutoka katika Dini ya Kiislamu.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/860.mp3
23. Kuleta Kicheko Na Makafiri
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
24
Swali:
Ipi hukumu ya kuleta kicheko na kuwa na tabia nzuri pamoja na makafiri? Je,
hili linaingia katika kufanya nao urafiki na kuwapenda?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio. Ikiwa kuleta kwako kicheko pamoja nao ni kwa mapenzi, hili linaingia
katika kufanya nao urafiki. Kwa kuwa kitendo cha nje huafiki kitendo cha
ndani cha kuwapenda. Kule kuleta kwako kicheko pamoja nao, hili bila ya
shaka ni aina moja wapo ya kuwafanya marafiki.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/861.mp3
24. Kuangalia Mazoezi Ya Makafiri Kwenye TV Na Kutamani Washinde
Swali:
Watu wengi siku hizi wamepewa mtihani kwa kuangalia mazoezi (michezo),
wanaishaji´isha, kuitolea mali na kutamani ishinde. Na huenda kati yao
kukawa makafiri. Hili linaweza kuingia katika kufanya urafiki na makafiri na
kuwapenda?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ikiwa anapenda kafiri ashinde - hata kama sio mazoezi - huku ni kuwapenda.
Ikiwa anapenda ashinde hata kama sio mazoezi, huku ni kufanya nao urafiki.
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
25
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/8156
25. Ibara Ya Kusema "Makafiri Ni Waislamu Bila Ya Uislamu"
Swali:
Ibara hii tunaisikia kwa wale ambao wanastaajabu kwa makafiri, wanasema:
"Ni Waislamu bila ya Uislamu."
´Allaamah al-Fawzaan:
Haya ni maneno machafu. Sio Waislamu. Bali wao ni makafiri. Tunawaita
"makafiri" kama Alivyowaita Allaah (´Azza wa Jalla).
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/8155
26. Kumpenda Raisi Wa Nchi Ambaye Ni Kafiri
Swali:
Sisi ni vijana tunaishi katika nchi moja wapo ya Ulaya. Wametupa fatwa
baadhi ya watu ya kwamba ni wajibu juu yetu kumpenda raisi wetu
anayehukumu nchi hiyo, pamoja na kuwa ni kafiri. Akasema "mtampenda
mapenzi ya kimaumbile". Upi usahihi wa maneno haya?
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
26
´Allaamah al-Fawzaan:
Haya ni maneno machafu. Huku ni katika kufanya nao urafiki. Haijuzu kwa
Muislamu kumpenda kafiri. Hata kama kafiri atakufanyia wema, haijuzu
kumpenda. Isipokuwa tu utamlipa nawe wema, kumlipa wema kwa wema
wake. Lakini asimpende kwa hilo. Na kwa ajili hiyo, ndio maana baba ambaye
ni kafiri ni wajibu kwa mtoto amtendee wema kwa ajili tu ya kulipiza wema
na wala asimpende moyoni mwake. Amchukie kwa ukafiri wake huku
akimtendea wema kwa kuwa ni mzazi wake na ana haki juu yake.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/1306.mp3
27. Ni Kupi Kujifananisha Na Makafiri?
Swali:
Kipimo ni kipi kwa kujifananisha na makafiri? Je, ni kwa yale ambayo ni
maalum kwako au ni kwa kila kinachotoka kwao?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ni kujifananisha nao katika mambo ya ´Ibaadah zao, hili halijuzu.
Kujifananisha nao katika mambo ya kiada ambayo ni maalum kwao; katika
mavazi yao, utembeaji wao na mfano wa hayo.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/1943_0.mp3
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
27
28. Kuwapenda Makafiri Pamoja Na Kuwasaidia Dhidi Ya Waislamu Na
Uislamu
Swali:
Kuwapenda makafiri bila ya kuwasaidia dhidi ya Waislamu ni dhambi kubwa
katika madhambi makubwa au ni kufuru inayomtoa mtu katika Uislamu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Tumekwishasema hili ya kwamba kuwapenda makafiri bila ya kuwa pamoja
na kupenda huko kitendo dhidi ya Waislamu na Waislamu ya kwamba ni
Haramu na ni dhambi kubwa katika madhambi makubwa. Ama kuwapenda
makafiri pamoja na kupenda huko kukawa na kuwasaidia [dhidi ya
Waislamu], huku ni kuritadi kwa wazi.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/2031.mp3
29. Uwajibu Wa Kuchukia Makafiri Na Ukafiri Wao
Swali:
Kuna mtu leo kaandika makala kwenye gazeti la Riyaadh ya kwamba
kuchukia makafiri ni jambo la wajibu, na anadai yeye ya kwamba wajibu ni
kuchukia kufuru na sio kuchukia makafiri. Je, kauli yake ni sahihi na vipi
kumjibu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
28
Sisi tunachukia kufuru na mwenye kufuru hiyo, sisi tunachukia yote mawili.
Kauli yake ya kwamba ni wajibu kuchukia kufuru na asichukiwe mtu,
upambanuzi huu ni batili.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/2898.mp3
30. Hukumu Ya Kusema Dini Zote Ni Sawa Twamuabudu Mungu Mmoja
Swali:
Yapi maoni yako kwa ibara hii:
"Waislamu na wakristo ni ndugu katika ulimwengu wa kiarabu na ´Ibaadah
zote ni kwa Mungu Mmoja"?
´Allaamah al-Fawzaan:
Haya maneno ni ya batili. Haya maneno ni ya batili.
كمون أفنجعل المسلمين كالمجرمين ما لكم كيف ت
”Je, Tuwajaalie Waislamu kama wakhalifu? Mna nini! Vipi mnahukumu?”
(68:35-36)
Muislamu hawezi kuwa sawa na kafiri. Kamwe! Na ambaye atawafanya kuwa
sawa, basi na yeye ni kafiri kama wao. Mwenye kusema Uislamu na kufuru ni
sawa, huyu ni kafiri. Kwa kuwa hakuukanusha ukafiri bali ameukubali na
kuufanya ni kama Uislamu. Allaah Atukinge. Ikiwa anajua alisemalo na
kakusudia jambo hili, anakuwa kafiri. Na kama ni mjinga, ni wajibu kwake
kukaa kimya na asome kwanza kabla ya kuongelea masuala haya ya khatari.
Uislamu haulingani na dini yeyote katika ardhi; sawa ikiwa ni uyahudi,
unaswara na nyenginezo. Hakuna dini ya sahihi isipokuwa Dini ya Uislamu
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
29
ambayo katumwa nayo Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa
sallam). Na ikawa ni wajibu kwa watu wote duniani kumfuata. Yule
asiyemfuata Mtume huyu ni kafiri, mkaidia, kwa kuwa Allaah (Ta´ala)
Kawaamrisha walimwengu wote kumfuata Mtume huyu.
وما أرسلناك إل كافة للناس
"Na Hatukukutuma (ee Muhammad صلى هللا عليه وآله وسلم)isipokuwa (ni Mtume
Wetu) kwa watu wote." (34:28)
ه إليكم جميعا ها النااس إني رسول اللـا قل يا أي
"Sema (ee Mtume Muhammad صلى هللا عليه وآله وسلم): “Hakika mimi ni Mtume wa
Allaah kwenu nyinyi nyote." (07:158)
Yule mwenye kusema Uislamu na kufuru ni sawa, huyu ikiwa ni mjinga basi
kakosea na ni juu yake kutubia na asome kabla ya kuongea. Na ikiwa kasema
hiyo kwa ujuzu ni kafiri, kwa kuwa kafanya haki na batili kuwa sawa.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/8139
31. Kafiri Anajijongeza Kwangu Na Kusema "Ndugu Yangu", Nifanye Nini?
Swali:
Naishi na mtu ambaye ni mkristo na ananambia: "Ewe ndugu yangu, sisi ni
ndugu." Na anakula na kunywa na sisi. Inajuzu kufanya hivi na lipi la wajibu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Lililo la wajibu ni kujiweka nae mbali na wala usiishi nae. Kwa kuwa ni adui
wa Allaah, Mtume Wake na ni adui wako. Kuishi kwako pamoja nae, na
kucheka nae, na kufanya nae urafiki na kutangamana nae hili linapingana na
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
30
al-Walaa´ wal-Baraa´. Ni juu yako kujitenga nae. Na akikwambia: "Ndugu
yangu".Mwambie: "Muongo wewe, wewe sio ndugu yangu." Wewe ni ndugu
wa Shaytwaan. Wewe sio ndugu yangu. Haijuzu kuchukulia sahali katika
masuala haya.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/8136
32. Kubusu Kichwa Cha Mzazi Asiyeswali
Swali:
Inajuzu kubusu kichwa cha mmoja katika wazazi wawili ikiwa anaswali
wakati fulani au haswali kamwe?
´Allaamah al-Fawzaan:
Haijuzu kufanya hivyo. Kwa kuwa hili ni katika mapenzi, kumbusu ni katika
mapenzi. Haijuzu kubusu kichwa chake. Lakini lisifanye hili kutomtendea
wema. Kumfanyia wema katika mambo ya kidunia. Ama kumdhihirishia
mapenzi, kama kumbusu kichwa na mfano wa hayo, hili halijuzu.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/13267_0.mp3
33. Kusoma Elimu Ya Dini Katika Miji Ya Makafiri
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
31
Swali:
Je, linaingia katika hali ulizotaja kutafuta elimu ya kidunia - kama ilivyo
katika Hadiyth ya Jariyr (Radhiya Allaahu ´anhu)?
´Allaamah al-Fawzaan:
Makusudio ni kutafuta elimu ya kidunia. Ama kutafuta elimu ya Kishari´ah
haijuzu kuitafuta katika miji ya makafiri. Elimu ya Kishari´ah haijuzu
kuitafuta katika miji ya makafiri. Hili halijuzu. Linalojuzu ni elimu za kidunia
tu; elimu ya uhandisi, utabibu n.k., elimu za kidunia ndio zinazotafutwa kwa
makafiri ikiwa hazikupatikana katika miji ya Waislamu. Ama elimu ya
Kishari´ah haijuzu kuitafuta katika miji ya makafiri, na wala haijuzu kusoma
kwa makafiri. Hawakuangamia Waislamu ila pale walipoanza kuwasomesha
watoto wao elimu ya Kishari´ah kwa makafiri ambao wanawatatiza katika
Dini yao na´Aqiydah yao. Halijuzu hili.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/12975.mp3
34. Tofauti Kati Ya Nchi Ya Kiislamu Na Ya Kikafiri
Swali:
Baadhi ya ndugu yanatofautiana sana katika kupambanua kati ya nchi ya
kikafiri na nchi ya Kiislamu. Ni kipi kipimo?
´Allaamah al-Fawzaan:
Nchi ya kikafiri ni ile ambayo inahukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah.
Namna hii ndivyo walivyosema wanachuoni. Kwamba nchi ambayo
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
32
haihukumu kwa Shari´ah ya Allaah, huzingatiwa ni nchi ya kikafiri. Hali
kadhalika miji ambayo kunadhiri alama za Shirki, kama manasamu na
hayakatazwi wala kuvunjwa, hii pia huzingatiwa ni mji wa kikafiri.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/4106
35. Kuvaa Nguo Yenye Msalaba
Swali:
Ni nini hukumu ya kuvaa msalaba au picha ya msalaba?
´Allaamah al-Fawzaan:
Halijuzu hili. Kuvaa msalaba haijuzu kwa hali yoyote ile. Kwa kuwa Mtume
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa haachi nyumbani kwake kitu
katika msalaba isipokuwa anakivunja. Halijuzu hili. Msalaba ni lazima
uondoshwe kwenye nguo, saa, gari au kitu kingine chochote. Ni lazima
kuuondosha. Kwa kuwa ni alama ya manaswara, msalaba ni alama ya
manaswara. Na manaswara wanaabudu msalaba.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/11150.mp3
36. Kumtembelea Kafiri Ambaye Ni Mgonjwa Kwa Lengo La Da´wah
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
33
Swali:
Vipi kumtembelea kafiri wakati ni mgonjwa?
´Allaamah al-Fawzaan:
Kumtembelea wakati ni mgonjwa, ikiwa makusudio ni kumfanyia Da´wah
katika Dini ya Allaah, pengine akakubali Uislamu na akafa ni Muislamu, hii ni
fursa nzuri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimtembelea myahudi
na akamlingania katika Uislamu akasilimu naye alikuwa juu ya kitanda
anataka kukata roho, akafa hali ya kuwa ni Muislamu. Na akamtembelea ami
yake Abu Twaalib na kumlingania katika Uislamu, akamwamia: "Sema
"hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah." Ikiwa lengo la
kumtembelea kafiri mgonjwa ni ili kumlingania katika Uislamu, hili ni jambo
zuri.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/7625.mp3
37. Ufaransa Imepiga Marfuku Kuvaa Hijaab, Tuhame?
Swali:
Waislamu wanawake Ufaransa wamekatazwa kuvaa Hijaab. Je, unawanasihi
kufanya Hijrah kuhamia katika nchi hii au wafanye nini?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hata kama hawakuwakataza kuvaa Hijaab. Pale ambapo wanaweza kufanya
Hijrah itakuwa ni wajibu. Haijuzu kwa Muislamu kubaki katika nchi za
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
34
makafiri naye anaweza kufanya Hijrah. Kwa kuwa Allaah Kawapa matishio
makali wale ambao wameacha kufanya Hijrah ilihali wanaweza kuhama.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/4087
38. Kuishi Katika Miji Ya Kikafiri Pamoja Na Kudhihirisha Dini
Swali:
Baadhi ya Madu´aat wamesafiri kwenda katika miji ya kikafiri na kuishi huko,
tunapojadiliana nao wanasema: "Waislamu walifanya Hijrah kuhamia
Habashah na ilikuwa ni nchi ya kikafiri na Najaash alikuwa akiwapa haki zao
na kuwatetea, na sisi huku hatudhulumiwi, ni bora kuliko nchi nyingi za
Kiislamu." Kauli hii inakubaliwa?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hili itategemea na kiasi ya hali itavyokuwa. Ikiwa mji watokapo
wanakandamizwa na kupewa mitihani kwa Dini yao na wakapata mji
ambapo wanadhihirisha Dini yao na wala hakuna yeyote anayewaudhi,
wanaweza kuhamia mji huyo hata kama itakuwa ni nchi ya kikafiri. Ikiwa
wanaweza kudhihirisha Dini yao. Najaash aliwapa uwezo Waislamu na uhuru
wa kuweza kufanya Da´wah, mpaka hata yeye mwenyewe (Rahimahu Allaah)
akasilimu kwa sababu ya Da´wah yao.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/5556.mp3
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
35
39. Makafiri Ni Ndugu Zetu Kibinaadamu
Swali:
Mwenye kusema makafiri ni ndugu zetu wa kibinaadamu na si katika Dini. Je,
maneno yake haya ni sahihi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Haitoshi kiubinaadamu. Wala mtu hasemi hivi kwa kutaka kuwapaka mafuta
au kupata hisia zao. Mtu hasemi hivi. Inatakiwa kusema wao ni maadui wetu
wala mtu hasemi ndugu zetu wa kibinaadamu. Bali mtu anatakiwa kusema ni
maadui wetu. Ikiwa ni maadui wetu katika Dini, udugu wa kibinaadamu
utafidisha nini? Utafidisha nini? Fir´awn alikuwa pia binaadamu. Au sio? Je
alikuwa pia ndugu yetu? Haitakikani kusema hivi.
Chanzo: http://alfawzan.ws/node/1875
Tarehe: 1431-04-14/2010-03-29
40. Kwa nini Sisi Tu Ndo Twavaa Mavazi Ya Makafiri Wao Hawavai
Mavazi Yetu?
Swali:
Je, ni sahihi kwa mwenye kusema ya kwamba kuvaa Kanzu katika miji ya
kimagharibi kama Amerika na kwenginepo, huchukuliwa ni katika kutafuta
umaarufu?
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
36
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana, sivyo. Mtu avae nguo za kawaida. Kwa nini wao wanapokuja kwetu
hawavai mavazi yetu? Sisi tu ndo tukiHuu ni udhalili kwetu. Mavazi ya
kawaida usiyaache ewe ndugu. enda kwao tunavaa mavazi yao.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/taxonomy/term/117
41. Hukumu Ya Kusema Mayahudi Na Wakristo Ni Ndugu Zetu
Swali:
Ipi hukumu kwa yule asemaye:
"Ndugu zetu mayahudi na wakristo"?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio, ni wandugu zake yeye, ni wandugu zake yeye. Lakini sisi sio ndugu
zetu. Sisi tunajitenga nao mbali. Ama kwa yule asemaye ni ndugu zake, basi
watakuwa ndugu zake kweli isipokuwa kama atatubu kwa Allaah ('Azza wa
Jalla) kwa kauli hii chafu. Na kama hatotubia basi watakuwa ndugu zake
kweli.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/taxonomy/term/117
42. Hukumu Ya Kujiita Majina Ya Makafiri
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
37
Swali:
Ipi hukumu ya mwenye kujiita kwamajina ya baadhi ya makafiri?
´Allaamah al-Luhaydaan:
Akiitwa kwa majina ya baadhi ya makafiri, dogo tuwezalo kusema ni kwamba
hii ni aina ya kujifananisha nao. Na Mtume Anasema:
"Mwenye kujifananisha na watu, basi yeye ni katika wao."
Tunamuomba Allaah Atukinge. Kipi kinachomkataza kuitwa majina ya
Kiislamu na waislamu. Na lau angeenda katika vitabu angepata majina mengi
sana. Hakuitwa majina ya baadhi ya makafiri isipokuwa ni kwa sababu
amevutika nao.
Chanzo:
http://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.scholarsubject&schid=3098
1&subjid=31339
43. Kuongea Lugha Za Makafiri Pasina Haja
Swali:
Je, kuongea lugha ya makafiri kunaingia katika Hadiyth "Mwenye
kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao."?
´Allaamah al-Fawzaan:
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
38
Kuiongea wakati wa haja, hakuna neno. Ama kuiongea pasina haja, hili
limeharamishwa. Kwa kuwa kuna kujifananisha na kuihama lugha ya
kiarabu.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/alldroos?tid_1=240
44. Kuvaa Nguo (Jezi) Yenye Jina Au Picha Ya Kafiri
Swali:
Mwenye kuvaa wanayovaa makafiri na kukawa nyuma ya mgongo wake
katika vazi lake jina la kafiri na wala hanuwii kujifananisha na mtu huyo au
watu hao katika kuvaa huko...
´Allaamah al-Fawzaan:
Huku ni kumuadhimisha kafiri. Maadamu anavaa nguo yenye jina la kafiri au
picha yake, huku ni kumuadhimisha kafiri. na wala halijuzu hili. Dogo
tuwezalo kusema ni kwamba ni haramu. Na ikiwa anamuadhimisha,
kunakhofiwa akaritadi kabisa.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/alldroos?tid_1=240
45. Kuvaa Suruwali Ni Kujifananisha Na Makafiri
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
39
Swali:
Yapi maoni yako kuvaa suruwali? Na je, inajuzu kuivaa?
´Allaamah Rabiy´ al-Madkhaliy:
Kuvaa suruwali kuna kujifananisha na makafiri.
Chanzo: http://subulsalam.com/catplay.php?catsmktba=355
46. Maandamano Ni Kujifananisha Na Makafiri Kikamilifu
Imaam Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy:
Haya maandamano... ambayo tulikuwa tukiyaona kwa macho yetu wakati
Ufaransa ilipokuwa inatawala Syria, na tulikuwa tukiyasikia katika miji
mingine na sasa tumeyasikia [tena] Algeria. Lakini Algeria imezidi miji
mingine kwa upotevu huu na kujifananisha huku [na hawa makafiri]. Kwa
kuwa tulikuwa hatuoni wasichana pia wanashiriki kutoka nje kwenye
maandamano, jambo ambalo kikamilifu ni kujifananisha na makafiri na
makafiri wa kike. Kwa sababu ndio tunayoyaona kwenye picha na TV na
redio,wanatoka maelfu ya makafiri wakiume na wakike mchanganyiko, sawa
ikiwa ni wa Ulaya, Syria au wengine. Wanasongamana wanawake na
wanaume na huenda hata sehemu za mbele zikagusana na makalio. Huku ni
kujifananisha na makafiri kikamilifu, nako ni kutoka wasichana na wavulana
kutoka nje na kuandamana.
Jambo lingine ni kwamba haya maandamano kuna kujifananisha na makafiri
wazi wazi kwa kupinga au kuonesha kwao hasira zao kwa baadhi ya kanuni
ambazo viongozi wao wamewawekea, nitaongezea kitu kimoja. Haya
maandamano ya kiulaya ambayo waislamu wamekuja kuyaiga kichwa
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
40
mchunga, siyo njia ya Kishari´ah kwa kutengeneza hukumu na kutengeneza
jamii.
Kuanzia nukta hii yanakosea makundi na mapote yote ya Kiislamu ambayo
hayafuati njia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika
kutengeneza jamii. Jamii haibadilishwi kwa nidhamu za Kiislamu kwa fujo,
maneno mabaya na maandamano. Bali [jamii inabadilishwa] kwa utulivu na
kueneza elimu kati ya waislamu na kuwalea na Uislamu huu hadi malezi haya
yalete matunda, hata kama litapatikana hili baada ya kipindi kirefu.
Fataawa Juddah (12)
47. Hukumu Ya Kushiriki Sikukuu Za Makafiri Na Kuwapongeza
Swali:
Ipi hukumu ya kuwapa pongezi (hongera) makafiri kwa sikukuu zao na
kushiriki katika sikukuu zao?
´Allaamah al-Fawzaan:
Tunamuomba Allaah afya! Haijuzu kushiriki na manaswara katika sikukuu
zao wala kuwapa pongezi wala kuhudhuria.
وا كراما وا باللاغو مر ور وإذا مر والاذين ل يشهدون الز
"Na wale wambao hawatoi ushahidi wa uongo." (25:72)
Na uongo ni sikukuu za mashirikina, kushudia na kuhudhuria. Hakuna
kuhudhuria, kuwasaidia na wala kuwapa pongezi. Hata sikukuu za Bid´ah
ambazo zipo kwa Waislamu, kama sikukuu ya Maulidi na mfano wa hayo
katika sikukuu za Bid´ah haijuzu kwa mtu kushiriki wala kuhudhuria wala
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
41
kuwapa pongezi wala kuwasaidia wala asile katika chakula ambacho
wametayarisha khaswa kwa ajili ya hizo sherehe.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/alldroos?tid_1=240
48. Kula Pamoja Na Kafiri Na Kumpa Swadaqah
Swali:
Ipi njia nzuri tunayotakiwa kuifuata katika kuwalingania makafiri ambao
wako pamoja nami kazini? Je, naweza pia kula pamoja naona kuwapa
Swadaqah?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ndio, hakuna neno. Waweza kula nao na wao wakala nawe katika [chakula]
kinachoruhusiwa. Kuwapa Swadaqah ya Zakaah haijuzu. Ama [Swadaqah] ya
kujitolea [ya kawaida] hakuna ubaya kwa hilo. Khaswa ikiwa kwa hili
walenga kuwaingiza katika Uislamu
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/alldroo...
49. Jinsi Ya Kutangamana Na Makafiri Katika Shirika Unapofanya Nao Kazi
Swali:
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
42
Vipi ntatangamana na makafiri? Kwa kuwa wanachanganyika nami kazini
kila siku.
´Allaamah al-Fawzaan:
Ukipata kazi nyingine mbali nao ndio bora. La sivyo, fanya kazi yako na
waache katika kazi yao. Kila mmoja afanye kazi yake.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/alldroo...
50. Mwanamke Kafa Baba Yake Mdogo Kafiri
Swali:
Kuna baba mdogo wa mwanamke kafa ambaye alikuwa ni kafiri. Je inajuzu
kwa mwanamke kuhudhuria janaza yake
´Allaamah al-Fawzaan:
Hapana, watahudhuria makafiri! Watamsimamia makafiri na si Waislamu.
Lakini kukiwa hakuna mtu katika makafiri, anaweza kumsimamia - yaani
akamuosha akamkafini na akamzika mahala pa mbali na si katika makaburi
ya Waislamu. Haifai kumuosha kwa kuwa kuosha ni ´ibaadah na haifai kwa
kafiri. Mzingire kwenye kitu na amzike mahala mbali na njia [manyumba].
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/alldroo...
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
43
51. Kuvaa Nguo Za Makafiri Za Kumalizia Masomo
Swali:
Sisi ni mjumuiko wa wanafunzi tunaenda Thanawiy na karibu madrasah yetu
yatafanya hafla ya kumaliza madrasah na wametuomba kuvaa nguo za
kumaliza madrasah. Ni nguo zinazovaa watu wa magharibi wamalizapo
masomo. Je inajuzu kwangu kuvaa nguo hizi katika hafla hii?
´Allaamah al-Fawzaan:
Vaa nguo katika nguo za Waislamu na usivae nguo za makafiri. Vaa nguo za
Waislamu zenye kusitiri nzuri na usivae katika nguo za makafiri. Usiwaige
makafiri
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/alldroo...
52. Hukumu Ya Muislamu Kuwa Na Urafiki Na Makafiri
Swali:
Ipi hukumu ya kufanya urafiki na makafiri na ipi sura ya kufanya nao urafiki?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy
Ufanyaji urafiki na makafiri unalioharamishwa na kukubaliana na dini yao, na
kupenda dini yao. Akimpenda Muislamu mkristo kwa ukristo wake na
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
44
myahudi kwa uyahudi wake, na mwenye kuabudu moto kwa hilo basi hapo
atakuwa kama wao. Na urafiki kama huu umeharamishwa.
ه منهم نكم فإنا ومن يتولاهم م
"Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao."
(05:51)
Ama urafiki wa kikazi tu; kununua na kuuza, na kubadilishana mambo yenye
manufaa, na kazi makafiri kwa Waislamu. Hakika si katika urafiki hata ikiwa
Muislamu atafanya kazi kwa kafiri ili apate mshahara wake. Hakuna ubaya.
Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliweka mfanya kazi siku ya
kuhama kwake kwenda Madiynah mtu ambae alikuwa ni kafiri ili amuoneshe
njia ya kwenda Madiynah na akampa mshahara wake. Jambo hili kuhusu
urafiki linahitajia ufafanuzi. Ataejenga nao urafiki na akawapenda kwa dini
yao anakufuru. Kwa dalili ya Aayah hii:
ه منهم نكم فإنا ومن يتولاهم م
"Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao."
(05:51)
Ama urafiki kwa maana kufanya nazo kazi katika jambo la maslahi tu, hakuna
ubaya na wala si katika jambo limelokatazwa.
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=...
53. Kumuomba Kafiri Msaada Kwa Kitu Anachokiweza
Swali:
Inajuzu kuwaomba makafiri msaada kwa wayawezayo?
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
45
´Allaamah al-Fawzaan:
Wakati wa haja na dharurah hakuna ubaya. Unapokuwa katika safari na
wewe unahitajia msaada huwezi kumwambia nisaidie? Hili ni jambo linajuzu.
Hili ni jambo mubaha.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/alldroo...
54. Kumualika Jirani Kafiri Katika Walima
Swali:
Inajuzu kumualika jirani kafiri mnaswara katika walima wa ndugu yangu
nikitarajia ni njia ya yeye kuingia katika Uislamu?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hakuna ubaya kumuita kafiri kula chakula, na kuitikia wito wake akikuita
kwenda kula chakula naye ni jirani yako au ndugu yako, hakuna ubaya kwa
hilo. Masuala ya kula chakula na kuitikia mwaliko wake hili sio katika
kufanya nae urafiki. Hili ni katika kuamiliana nae katika mambo ya kidunia,
na huenda ikawa ni njia ya kumfanyia Da´wah, na khaswa ikiwa ni jirani yako
yuko na haki zake hata kama ni kafiri. Anasema Allaah (Jalla wa ´Alaa):
ب والاحب بالنب وبالوالدين إحسانا وبذي القرب واليتامى والمساكني والار ذي القرب والار الن واعبدوا اللـه ول تشركوا به شيئابيل وما ملكت أيانكم وابن الس
”Na mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni ihsaan wazazi wawili na jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini na majirani wa karibu na majirani walio mbali, na rafiki wa ubavuni na msafiri na waleiliyowamiliki mikono yenu ya kulia.” (04:36)
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
46
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/alldroos?tid_1=240
55. Kuwapa Mkono Wa Pole Makafiri Wanapofiwa
Swali La Kwanza:
Kiongozi wa upotofu kafariki Papa Johanna. Je inajuzu kusema mafikio yake
ni Motoni kwa kuwa kafa katika kufuru na ipi hukumu ya kutoa taazia
[mkono wa pole]...
´Allaamah al-Fawzaan:
Kipi kikujulishacho kwamba kafa katika kufuru? Usilenge. Usilenge moja kwa
moja kwamba kafa katika kufuru. Haijuzu kumshuhudia yeyote Pepo wala
Moto ila yule aliyemshuhudia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa
sallam). Usilenge moja kwa moja kwamba kafa katika kufuru. Allaah Anajua
zaidi. Hivyo ndo maana usilenge kwamba ni katika watu wa Motoni. Hii ndo
kanuni kwamba hashuhudiwi mtu maalumu. Ama makafiri, manaswara na
mayahudi kwa ujumla ni motoni. Ila kusema Johanna [Paulo] ataingia motoni
ni kosa. Watakiwa kusema Kuna uwezekano akaingia motoni. Allaah Anajua
zaidi. Unaweza pia kusema ikiwa kafa katika ukafiri basi ataingia motoni na
ikiwa alikufa kwa kufanya Tawbah ataingia Peponi. Usilenge kitu ila kwa
dalili.
Swali La Pili:
Na ipi hukumu ya kutoa taazia (mkono wa pole) kwa makafiri wanapokufa?
Uwajibu Wa Kuwachukia Makafiri Na Kutofanya Nao Urafiki
47
´Allaamah al-Fawzaan:
Mtu (haijuzu) kutoa taazia kwa makafiri. Mtu anatoa taazia kwa kafiri kwa
muumini. Ikiwa ndugu yake muumini (muislamu) kafa, unatoa taazia kwa
muumini. Ama kutoa taazia kwa kafiri haijuzu kufanya hivyo.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/alldroos?tid_1=240
Swalah na salaam zimwedee mbora wa Mitume, na ahli zake na
Maswahabah zake ajmaa´iyn