UTUMISHINews - Tanzania · 12. Miaka Minne ya JPM: Watumishi 2,940 wanufaika na ufadhili wa masomo...

25
HABARI KWA UFUPI; Mawaziri wenye dhamana ya Utumishi na Utawala Bora Tanzania Bara na Zanzibar wakutana kuzungumzia namna ya kuboresha utoaji wa huduma kwa Umma ......uk.1 Sweden yaipongeza serikali ya Tanzania kwa kufanya vizuri katika mapambano dhidi ya rushwa........uk.4 Rais Dkt. John Pombe Magufuli aagiza vijana wenye Shahada ya kwanza waliohitimu mafunzo ya JKT “Operesheni Magufuli” waajiriwe Serikalini.........uk.16 Serikali kuwachukulia hatua kali za kinidhamu Watumishi watakaobainika kujihusisha na rushwa ya ngono..........uk.3 “Nataka nchi ya watu wenye nidhamu, wanaopendana na wachapa kazi, kila atakayepewa kazi aitekeleze ipasavyo” Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli

Transcript of UTUMISHINews - Tanzania · 12. Miaka Minne ya JPM: Watumishi 2,940 wanufaika na ufadhili wa masomo...

Page 1: UTUMISHINews - Tanzania · 12. Miaka Minne ya JPM: Watumishi 2,940 wanufaika na ufadhili wa masomo nje ya nchi.....18-19 13. Serikali yawasilisha Muswada Bungeni wa kuwa na Mamlaka

HABARI KWA UFUPI;Mawaziri wenye dhamana ya Utumishi na Utawala Bora Tanzania Bara na Zanzibar wakutana kuzungumzia namna ya kuboresha utoaji wa huduma kwa Umma ......uk.1

Sweden yaipongeza serikali ya Tanzania kwa kufanya vizuri katika mapambano dhidi ya rushwa........uk.4

Rais Dkt. John Pombe Magufuli aagiza vijana wenye Shahada ya kwanza waliohitimu mafunzo ya JKT “Operesheni Magufuli” waajiriwe Serikalini.........uk.16

Serikali kuwachukulia hatua kali za kinidhamu Watumishi watakaobainika kujihusisha na rushwa ya ngono..........uk.3

“Nataka nchi ya watu wenye nidhamu, wanaopendana na wachapa kazi, kila atakayepewa kazi aitekeleze ipasavyo” Mhe. Dkt. John

Pombe Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli

Toleo Na.11 Januari-Juni, 2020

UTUMISHI News

Page 2: UTUMISHINews - Tanzania · 12. Miaka Minne ya JPM: Watumishi 2,940 wanufaika na ufadhili wa masomo nje ya nchi.....18-19 13. Serikali yawasilisha Muswada Bungeni wa kuwa na Mamlaka

Bodi ya Uhariri:

Dira

Dhamira

Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuwa Taasisi itakayowezesha kuwa na Utumishi wa Umma uliotukuka kwa kutoa huduma bora kwa Umma na hivyo kuchangia katika kukuza uchumi, kupunguza umaskini na kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania

ifikapo mwaka 2025.

Kuhakikisha kuwa utumishi wa umma nchini unasimamiwa vizuri na kwa ufanisi kupitia usimamizi wa rasilimaliwatu,

mifumo na miundo ya kiutumishi

Dkt. Laurean NdumbaroDkt. Francis MichaelMary MwakapendaJames MwanamyotoHappiness ShayoAaron Mrikaria

1. Mawaziri wenye dhamana ya Utumishi na Utawala Bora Tanzania Bara na Zanzibar wakutana kuzungumzia namna ya kuboresha utoaji wa huduma kwa Umma ........1-2

2. Serikali kuwachukulia hatua kali za kinidhamu Watumishi watakaobainika kujihusisha na rushwa ya ngono..........3-4

3. Sweden yaipongeza Tanzania kwa kufanya vizuri katika mapambano dhidi ya rushwa...............4-5

4. Watumishi wa Umma watakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia weledi.......6

5. Taasisi za Umma zatakiwa kutekeleza mkakati wa kitaifa dhidi ya rushwa ili kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.......................7-8

6. Taasisi za Umma nchini zatakiwa kuwapatia huduma ya usafiri Watumishi wa Umma wenye ulemavu......9

7. Watendaji serikalini watakiwa kufanya majadiliano na Vyama vya Wafanyakazi ili kuimarisha ustawi wa watumishi.......................10

8. Dkt. Ndumbaro amuelekeza DED Sengerema kumfungulia mashtaka Bw. Boniventura Bwire aliyekuwa mtumishi kwa kujipatia fedha kwa udanganyifu.........11-12

9. Ufuatiliaji na Tathmini serikalini ni chachu ya utendaji kazi na uwajibikaji kwa watumishi wa umma .....................12-14

10. Taasisi za umma zapigwa marufuku kutumia kampuni binafsi katika masuala ya TEHAMA na badala yake zitumie Mamlaka ya Serikali Mtandao........14

11. Rais Dkt. John Pombe Magufuli aagiza vijana wenye Shahada ya kwanza waliohitimu mafunzo ya JKT “Operesheni Magufuli” waajiriwe Serikalini.........................................................16-17

12. Miaka Minne ya JPM: Watumishi 2,940 wanufaika na ufadhili wa masomo nje ya nchi.............18-19

13. Serikali yawasilisha Muswada Bungeni wa kuwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao ....20

14. Matukio katika picha.............................................21-22

YALIYOMO

CHUMBA CHA HABARI

uk.

Jarida hili hutolewa na; Kitengo cha Mawasiliano Serikalini ,

Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,S.L.P 670, Dodoma,

Barua Pepe:[email protected]:www.utumishi.go.tz

Page 3: UTUMISHINews - Tanzania · 12. Miaka Minne ya JPM: Watumishi 2,940 wanufaika na ufadhili wa masomo nje ya nchi.....18-19 13. Serikali yawasilisha Muswada Bungeni wa kuwa na Mamlaka

1

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya

Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman wamefanya kikao kazi kujadili namna bora ya kuboresha utoaji wa huduma kwa umma pamoja na kuimarisha Muungano ili uendelee kuwa na tija kwa wananchi.

Akifungua kikao kazi hicho, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,

Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) amesema pamoja na kujadili masuala ya kuboresha huduma pia kililenga kuimarisha muungano ili kuwaenzi kwa vitendo waasisi wa taifa letu Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume.

Mhe. Mkuchika amefafanua kuwa, katika kikao kazi hicho wameweza kubadilishana uzoefu wa namna ya kutoa huduma bora na kwa wakati kwa wananchi wa pande zote mbili za muungano ambao ndio walengwa wakuu wa huduma zinazotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Naye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman amesema wao kama mawaziri wenye dhamana ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wanataka ushirikiano wa taasisi zinazoshughulikia masuala ya kiutumishi na utawala bora uendelezwe kwa vitendo kwa ajili ya manufaa ya wananchi.

Mhe. Suleiman amesisitiza kuwa, ushirikiano huu una manufaa katika kuboresha huduma zitolewazo na taasisi za umma kwa wananchi na una tija katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa Taasisi za Umma nchini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akifungua kikao kazi cha Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chenye lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kuimarisha muungano kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Page 4: UTUMISHINews - Tanzania · 12. Miaka Minne ya JPM: Watumishi 2,940 wanufaika na ufadhili wa masomo nje ya nchi.....18-19 13. Serikali yawasilisha Muswada Bungeni wa kuwa na Mamlaka

2

Mhe. Suleiman amewataka wajumbe wa kikao hicho, kuhakikisha misingi madhubuti ya kiutendaji

iliyojengwa katika kikao kazi hicho inaimarishwa ili utekelezaji wake uwe wa vitendo na uweze kuwa chachu ya kutoa huduma

bora kwa wananchi.

Masuala yaliyojadiliwa katika kikao kazi hicho ni; kudumisha ushirikiano

katika masuala ya Ajira, Serikali Mtandao, Udhibiti wa rushwa, Usimamizi wa Maadili ya Viongozi, Mafunzo kwa Watumishi wa Umma, Utekelezaji wa Programu ya Maboresho ya Utumishi wa Umma, Maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma, Uandaaji wa Miundo na Mifumo ya Taasisi na Utawala Bora kwa ujumla.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Mohammed Aboud akichangia hoja wakati wa kikao kazi cha Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chenye lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kuimarisha muungano, kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Haroun Ali Suleiman wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akizungumza katika kikao kazi cha Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chenye lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kuimarisha Muungano kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Page 5: UTUMISHINews - Tanzania · 12. Miaka Minne ya JPM: Watumishi 2,940 wanufaika na ufadhili wa masomo nje ya nchi.....18-19 13. Serikali yawasilisha Muswada Bungeni wa kuwa na Mamlaka

3

Serikali haitosita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu

Watumishi wa Umma watakaobainika kujihusisha na rushwa ya ngono katika maeneo yao ya kazi, kwani kitendo hicho kinadhalilisha na kushusha hadhi ya utumishi wa umma nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst.), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) wakati wa kikao kazi chake na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kilichofanyika wilayani humo kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.

Mhe. Mkuchika ametoa kauli hiyo kufuatia baadhi ya Walimu wa shule za msingi wilayani Tunduru kushikiliwa na vyombo vya dola kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa ya ngono jambo ambalo halileti taswira nzuri kwa umma, ikizingatiwa kuwa Walimu wana jukumu la kuwalea wanafunzi katika maadili mema.

“Inakuwaje Mwalimu unaepaswa kuwa mfano bora wa kuigwa kimaadili unataka rushwa ya ngono kwa mwanafunzi, kitendo hicho kinamuathiri mwanafunzi husika kitaaluma na k i s a i k o l o j i a , ” M h e . Mkuchika amefafanua.

Mhe. Mkuchika ameongeza kuwa, hivi karibuni ofisi yake imesitisha ajira ya Mhadhiri mmoja wa chuo kikuu

nchini, ambaye alituhumiwa na kubainika kuwaomba rushwa ya ngono wanafunzi wa kike ili waweze kufaulu mitihani yao kwa upendeleo.

“Wanafunzi wa kike wa chuo hicho waliandika barua ya malalamiko kwenye ofisi yangu na baada ya kuwahoji na kufanya uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na vyombo vya dola ikabainika kuwa ni kweli hivyo akafukuzwa kazi,” Mhe. Mkuchika ameeleza.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na Watumishi wa Umma wilayani Tunduru wakati wa kikao kazi chake na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kilichofanyika wilayani humo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mhe. Julius Mtatiro

Serikali kuwachukulia hatua kali za kinidhamu Watumishi watakaobainika kujihusisha na rushwa ya ngono

Baadhi ya Watumishi wa Umma wilayani Tunduru wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kilichofanyika wilayani humo

Page 6: UTUMISHINews - Tanzania · 12. Miaka Minne ya JPM: Watumishi 2,940 wanufaika na ufadhili wa masomo nje ya nchi.....18-19 13. Serikali yawasilisha Muswada Bungeni wa kuwa na Mamlaka

Serikali ya S w e d e n imeipongeza

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuongoza nchi ikizingatia utawala bora hususani katika m a p a m b a n o dhidi ya rushwa.

Pongezi hizo zimetolewa na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg alipokuwa a k i w a s i l i s h a mada kuhusu uzoefu wa nchi yake katika masuala ya utumishi wa umma kwa wanafunzi na watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Kampasi ya Dar es Salaam.

Balozi Sjoberg amesema, katika nchi yao tatizo la rushwa halipo kabisa kwani Serikali iliongoza vyema mapambano dhidi ya rushwa, hivyo ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania inavyoendesha vizuri mapambano dhidi ya rushwa kwa ajili ya maslahi ya umma na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Katika mada yake, Mhe. Balozi Sjoberg amefafanua kuwa, nchini Sweden suala la Watumishi wa Umma kuwajibika kwa

wananchi limepewa kipaumbele kwani wananchi wote wanahitaji huduma sawa bila ubaguzi wa aina yoyote.

Kwa upande wake, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ameishukuru Serikali ya Sweden kwa kutambua juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano kwenye eneo la utawala bora.

“ Tu n a i s h u k u r u Serikali ya Sweden kwa

kutambua jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kuimarisha utawala bora nchini hasa katika mapambano dhidi ya rushwa,” Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema.

Aidha, katika eneo la uwajibikaji, Mhe. Dkt. Mwanjelwa ametumia fursa hiyo kuwasisitiza Watumishi wa Umma nchini kuwahudumia wananchi vizuri na kwa wakati kama Serikali inavyosisitiza kila mara.

“Ukiwa Mtumishi wa Umma, tambua wazi kuwa wewe ndio injini kwani wananchi wanahitaji huduma bora kutoka kwako, hivyo unatakiwa muda wote uwahudumie wananchi kwa uadilifu na bila ubaguzi wa aina

Sweden yaipongeza Tanzania kwa kufanya vizuri katika mapambano dhidi ya rushwa

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg wakionyesha zawadi ya ramani ya Afrika yenye nembo ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania baada ya Balozi huyo kukabidhiwa zawadi hiyo na Naibu Waziri kuonyesha ushirikiano mwema baina ya Tanzania na Sweden katika masuala ya utumishi wa umma wakati Balozi alipotembelea chuoni hapo kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya Utumishi wa Umma kwa nchi za Sweden na Tanzania.

4M h e . M k u c h i k a

a m e w a t a h a d h a r i s h a Watumishi wa Umma nchini kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) iko kazini na ina utayari wa kumshughulikia mtumishi yeyote atakayetumia cheo

chake vibaya ili kujinufaisha na rushwa ya ngono.

Aidha, Mhe. Mkuchika amesema nchi yetu imebahatika kuwa na viongozi wenye utashi wa kupambana na rushwa kuanzia Awamu ya Kwanza ya Baba wa Taifa,

Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere hadi Awamu hii ya Tano, inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye amejipambanua kwa vitendo kwa kuanzishaMahakama ya Mafisadi na Wahujumu Uchumi.

Page 7: UTUMISHINews - Tanzania · 12. Miaka Minne ya JPM: Watumishi 2,940 wanufaika na ufadhili wa masomo nje ya nchi.....18-19 13. Serikali yawasilisha Muswada Bungeni wa kuwa na Mamlaka

yoyote,” Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.

Kuhusu uhusiano uliopo kati ya Sweden na Tanzania, Mhe, Mwanjelwa amesema Nchi hizo

mbili zimekuwa na uhusiano mzuri tangu utawala wa Serikali ya Awamu ya Kwanza na uhusiano huo umeendelea kushamiri hadi sasa kwenye utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano.

“Uhusiano kati ya Sweden na Tanzania umeanza tangu mwaka 1970 walipojenga Chuo cha Utumishi wa Umma Tawi la Tabora kwa asilimia 80 na bado tumeendelea kuwa na uhusiano mzuri,”

Mhe. Dkt. Mwanjelwa a m e o n g e z a .

Mhe. Balozi Sjoberg alitembelea Chuo cha Utumishi wa Umma

Tanzania (TPSC) kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya Utumishi wa Umma kwa nchi za Sweden na Tanzania.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg wakishuhudia jinsi mashine ya kupiga chapa inavyofanya kazi mara baada ya Balozi kutembelea Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya Utumishi wa Umma kwa nchi za Sweden na Tanzania. Wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel Shindika

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Anders Sjoberg wakicheza wimbo unaosifu utendaji kazi wa Marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Awamu ya Kwanza mpaka sasa wa kwaya ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania wakati Balozi alipotembelea chuoni kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya Utumishi wa Umma kwa nchi za Sweden na Tanzania. Kushoto kwa Balozi ni Kaimu Katibu Mkuu Utumishi, Bw. Mick Kiliba.

5

Page 8: UTUMISHINews - Tanzania · 12. Miaka Minne ya JPM: Watumishi 2,940 wanufaika na ufadhili wa masomo nje ya nchi.....18-19 13. Serikali yawasilisha Muswada Bungeni wa kuwa na Mamlaka

6

Watumishi wa Umma wanaofanya kazi makao makuu ya Halmashauri za Wilaya nchini wametakiwa kutofanya

kazi kwa mazoea na badala yake wafanye kazi kwa kuzingatia weledi, ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi wanaowahudumia na watumishi wenzao wanaotoka pembezoni kufuata huduma wilayani.

Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro wakati akizungumza na Watumishi wa Halmashauri za Wilaya ya Kilombero,Ifakara Mji na Malinyi kwa nyakati tofauti, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma nchini.

Dkt. Ndumbaro amewasisitiza Watumishi hao, kuhakikisha wanawahudumia vizuri Watumishi wa Umma wanaotoka kwenye kata, tarafa na vijiji ili nao waweze kuwahudumia vizuri wananchi katika maeneo yao ya kazi.

“Hatuna budi kuwahudumia ipasavyo wananchi na watumishi wanaotumia

gharama zao kufuata huduma wilayani na kupoteza muda wao, tusiwaache waondoke

bila kupata huduma inayostahili, ” amesema Dkt. Ndumbaro.

Aidha Dkt. Ndumbaro amewashauri Watumishi wanaotaka kusoma shahada ya pili wabobee katika fani zinazoendana na shahada ya kwanza kwakuwa shahada ya kwanza ndio msingi wa taaluma walizonazo, na endapo mtumishi atajiendeleza kwa kuchukua shahada ya pili tofauti na ya kwanza atakuwa amejiendeleza katika kada tofauti hivyo kukosa fursa ya kubadilishiwa cheo (recategorization) na kukosa sifa ya kupata kibali cha mshahara binafsi.

Dkt. Ndumbaro amefanya ziara ya kikazi katika Halmashauri za Wilaya ya Kilombero, Ifakara Mji na Malinyi kuhimiza uwajibikaji, ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) aliyemtaka kuchunguza weledi wa utendaji kazi wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Malinyi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo.

Watumishi wa Umma watakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia weledi

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara na Kilombero wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani humo yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma nchini.

Page 9: UTUMISHINews - Tanzania · 12. Miaka Minne ya JPM: Watumishi 2,940 wanufaika na ufadhili wa masomo nje ya nchi.....18-19 13. Serikali yawasilisha Muswada Bungeni wa kuwa na Mamlaka

Taasisi za Umma nchini zimetakiwa kusimamia utekelezaji wa Mkakati

wa Taifa Dhidi ya Rushwa na Mpangokazi wake ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kila taasisi inakuwa na Kamati ya Kusimamia Uadilifu ili kudhibiti vitendo vya rushwa na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Agizo hilo limetolewa jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst.) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) wakati akifungua kongamano la kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu katika ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni jijini Dodoma.

Mheshimiwa Mkuchika amesema utekelezaji wa Mkakati huo umejikita kwenye sekta za kimkakati zikiwemo za Manunuzi ya Umma, Ukusanyaji wa Mapato, Utoaji

wa Haki, Maliasili na Utalii, Madini, N i s h a t i , Mafuta na Gesi, Afya, Elimu na Ardhi ambapo mkakati huo unatekelezwa katika ngazi za Kijiji/Mtaa, Kata, Tarafa, Wilaya,Mkoa na Taifa.

‘‘Kila taasisi i n a t a k i w a kuwa na Kamati ya Ku s i m a m i a

Uadilifu ili kuweza kusimamia ipasavyo utekelezaji wa mkakati wa taifa dhidi ya rushwa,’’ Mhe. Mkuchika amesisitiza.

Mhe, Mkuchika ameongeza kuwa,malengo makuu ya mkakati huo ni kuimarisha

ufanisi, uwazi na uwajibikaji wa utoaji huduma katika sekta za Umma na sekta Binafsi, ufanisi katika utekelezaji wa mikakati ya mapambano dhidi ya rushwa, kuzijengea uwezo taasisi simamizi za masuala ya Utawala Bora na kuwa na Uongozi wa Kisiasa madhubuti unaoshiriki kwa dhati katika mapambano dhidi ya rushwa.

Mhe. Mkuchika amesema, Mkakati huo wa Taifa Dhidi ya Rushwa ulizinduliwa rasmi tarehe 10 Desemba, 2016 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu.

Naye Mwakilishi wa Shirika la Mendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bw. Paul Wilson Mlemya amesema kuwa mapambano dhidi ya rushwa yanahitaji nguvu ya pamoja kati ya serikali na wananchi ili kufikia

Taasisi za umma zatakiwa kutekeleza mkakati wa taifa dhidi ya rushwa ili kuboresha utoaji huduma kwa wananchi

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akifungua Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu, katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

Baadhi ya viongozi wa Taasisi mbalimbali za Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst.) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) wakati akifungua Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu, katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

7

Page 10: UTUMISHINews - Tanzania · 12. Miaka Minne ya JPM: Watumishi 2,940 wanufaika na ufadhili wa masomo nje ya nchi.....18-19 13. Serikali yawasilisha Muswada Bungeni wa kuwa na Mamlaka

maendeleo yaliyokusudiwa.

“Rasilimali nyingi zinazopotea katika njia za rushwa zikiweza kuzuiliwa zitaleta maendeleo kwa wananchi katika sekta za elimu, afya na miundombinu kwa ujumla wake,” Bw. Mlemya amesisitiza.

Kwa upande wake, Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Mhe. Jaji (Mst.) Harold R. Nsekela amesema kuwa Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu ni muhimu kwa sababu yanatoa fursa kwa Taifa kujitathmini kama limefanya juhudi za kutosha katika kuhakikisha maadili yanazingatiwa, vitendo vya rushwa vimepungua, uwajibikaji umeongezeka na misingi ya Utawala Bora inazingatiwa.

Kongamano la Siku ya Maadili na Haki za Binadamu hufanyika Desemba 10 ya kila mwaka ambapo kwa mwaka huu, limehudhuriwa na Makatibu na Naibu Makatibu Wakuu wa Wizara, Wakuu wa Taasisi za Serikali, Viongozi wa Serikali Wastaafu na Watumishi wa Umma kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali.

Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Mhe. Jaji (Mst.) Harold R. Nsekela akizungumza wakati wa Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu, katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb)(katikati mstari wa mbele) na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (wa tatu kutoka kulia mstari wa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Taasisi za Umma, baada ya ufunguzi wa Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu, katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb)akiteta jambo na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kabla ya kufungua Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu, katika ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka.

8

Page 11: UTUMISHINews - Tanzania · 12. Miaka Minne ya JPM: Watumishi 2,940 wanufaika na ufadhili wa masomo nje ya nchi.....18-19 13. Serikali yawasilisha Muswada Bungeni wa kuwa na Mamlaka

9

Serikali imezitaka Taasisi za Umma nchini kuhakikisha zinatatua changamoto ya huduma ya usafiri kwa Watumishi

wa Umma wenye Ulemavu ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst) Mhe. George Mkuchika wakati akijibu swali la Mhe. Amina S. Mollel (Mb) (Viti Maalum) aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuwapatia huduma ya usafiri Watumishi wa Umma wenye Ulemavu.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa, ili kufanikisha azma hiyo ya Serikali, Taasisi za Umma zinatakiwa kutekeleza miongozo inayotolewa ikiwa ni pamoja na Mwongozo wa Huduma kwa Watumishi wa Umma Wenye Ulemavu wa mwaka 2008 unaoelekeza Waajiri kuwapatia huduma ya usafiri au kulipia gharama za mafuta ya kwenda na kurudi kazini kwa Watumishi wa Umma wenye Ulemavu ambao wana vyombo binafsi

vya usafiri, lengo likiwa ni kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameongeza kuwa, Waajiri ambao hawatekelezi Mwongozo huo, wanakiuka maelekezo ya Serikali kwa kuwanyima stahiki Watumishi wenye ulemavu, hivyo wakibainika watachukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa taratibu za kiutumishi zilizopo.

Serikali kupitia Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini imejipanga kufanya Ufuatiliaji wa utekelezaji wa Mwongozo huo ili uweze kufanya kazi kama ilivyokusudiwa.

Aidha, Dkt. Mwanjelwa amewakumbusha Waajiri kutoa kipaumbele cha mikopo ya vyombo vya usafiri kwa Watumishi wa Umma Wenye Ulemavu wanaokidhi vigezo vya kukopesheka ikiwa ni utekelezaji wa Waraka wa Watumishi wa Serikali Na.3 wenye Kumb.Na. C/AC.7/228/01/16 wa Juni 30, 2011 unaotoa Utaratibu wa Kukopesha Fedha Taslimu Watumishi wa Serikali kwa ajili ya kununulia Magari au Pikipiki pamoja na Matengenezo ya Magari na Pikipiki hizo.

Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akijibu maswali Bungeni jijini Dodoma.

Taasisi za umma nchini zatakiwa kuwapatia huduma ya usafiri Watumishi wa Umma wenye ulemavu

Page 12: UTUMISHINews - Tanzania · 12. Miaka Minne ya JPM: Watumishi 2,940 wanufaika na ufadhili wa masomo nje ya nchi.....18-19 13. Serikali yawasilisha Muswada Bungeni wa kuwa na Mamlaka

10Watendaji Serikalini watakiwa kufanya majadiliano na vyama

vya wafanyakazi kwa ajili ya ustawi wa Watumishi

Wa t e n d a j i katika Taasisi za Umma

wametakiwa kuwa na utaratibu wa kukutana na vyama vya wafanyakazi na kujadiliana changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi kwa ajili ya manufaa na ustawi wa Watumishi wa Umma nchini.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) wakati akifungua rasmi Mkutano wa Baraza Kuu la Nne la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma Tanzania Bara uliofanyika jijini Dodoma.

Mhe. Mkuchika amesema, ushirikishwaji wa Vyama vya Wafanyakazi katika masuala yanayohusu maslahi ya Watumishi wa Umma utasaidia kuepuka migogoro isiyokuwa ya lazima baina ya Serikali na Vyama vya Wafanyakazi.

Pia Mhe. Mkuchika amewataka wajumbe wa baraza hilo kuishauri Serikali katika masuala ya kiutumishi yanayohitaji maboresho kwa manufaa ya utumishi wa umma na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Sanjali na hilo, Mhe. Mkuchika amewataka wajumbe hao kuhakikisha wanawafahamisha watumishi kuhusu marekebisho mbalimbali yaliyofanyika katika Sheria ya Utumishi wa Umma ili kuwasaidia

watumishi kujua haki zao.

Aidha, Mhe. Mkuchika amewasisitiza Watumishi wa Umma nchini kufanya kazi kwa uadilifu na kuwa tayari kufanya kazi mahali popote kwa ajili ya kuwatumikia wananchi kwani wananchi wanalipa kodi na wana haki ya kupata watumishi w a t a k a o w a h u d u m i a .

Awali, akimkaribisha Mhe. Mkuchika kufungua mkutano wa baraza hilo, Mwenyekiti wa Baraza ambaye ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro amesema

mkutano huo pamoja na mambo mengine ulijadili

fursa ya kujadili Sheria ya Uwezeshaji wa Mfuko wa PSSSF, mabadiliko mbalimbali ya Sheria za Utumishi wa Umma na kujadili utekelezaji wa Mikataba ya Utendaji Kazi Serikalini pamoja na Miundo ya Utumishi ya Maendeleo ya Kada ya Ustawi wa Jamii ambayo ilikuwa na changamoto.

Dkt. Ndumbaro ametumia fursa hiyo

kumpongeza Mhe. Mkuchika kwa kufanya kazi kwa bidii, ufanisi mkubwa na kutoa maelekezo yanayosaidia kutatua changamoto na kero za utumishi wa umma pamoja na kushughulikia maslahi ya Watumishi wa Umma.

Naye, Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Bi. Leah Ulaya akitoa shukrani kwa niaba ya wajumbe baada ya Mhe. Mkuchika kufungua mkutano huo, amemhakikishia kuwa baraza litayafanyia kazi ushauri alioutoa na litasimama imara kushauri vema ili kuiwezesha Ofisi

ya Rais, Utumishi kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Serikali inatambua umuhimu wa kuwa na uhusiano mzuri kati yake na Vyama vya Wafanyakazi ndio maana imetunga Sheria ya Majadiliano ya pamoja katika Utumishi wa Umma SURA 105 ambayo inaunda Mabaraza ya Wafanyakazi

katika Utumishi wa Umma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst.), Mhe. George H. Mkuchika (Mb)

Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la Nne la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma Tanzania Bara wakimsikiliza Mhe. George Mkuchika (hayupo pichani)

Page 13: UTUMISHINews - Tanzania · 12. Miaka Minne ya JPM: Watumishi 2,940 wanufaika na ufadhili wa masomo nje ya nchi.....18-19 13. Serikali yawasilisha Muswada Bungeni wa kuwa na Mamlaka

11

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro amemuagiza Mkurugenzi

Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Bw. Boniface M. Magesa kwa kushirikiana na Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) kumtafuta popote alipo aliyekuwa mtumishi wa umma Bw. Boniventura Bwire na kumfikisha katika vyombo vya dola kwa kosa la kujipatia fedha za Serikali kwa udanganyifu katika kipindi cha miaka nane licha ya kufukuzwa kazi mwaka 2011.

Dkt. Ndumbaro ametoa maelekezo hayo wilayani Sengerema, wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa halmashauri hiyo chenye lengo la kusikiliza changamoto za kiutumishi zinazowakabili na kuzitatua, ikiwa ni pamoja na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao.

Dkt. Ndumbaro ameeleza kuwa, Bw. Bwire alikuwa Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe mpaka mwaka 2011 kabla ya kufukuzwa kazi mwaka 2012 na mwajiri wake

baada ya kugundulika kuwa na Stashahada ya Juu ya Uhasibu ya kughushi (advanced Diploma) ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE).

Dkt. Ndumbaro amefafanua kuwa, mtumishi huyo alighushi barua za Katibu Mkuu TAMISEMI na kufanikiwa kuhamia katika Halmashauri za Wilaya ya Ukerewe, Bariadi na hatimaye Sengerema.

“Kwa miaka nane Bw. Bwire amekuwa akifanya kazi Serikalini akiwa sio mtumishi wa umma halali baada ya kufukuzwa kazi na kuondolewa kwenye orodha ya malipo ya mishahara, na katika halmashauri zote alizohamia amekuwa akijitambulisha kama

Afisa Mapato na kufanya kazi hiyo na hatimaye kujilipa, hivyo kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu,” amesema Dkt.

Ndumbaro.

Dkt. Ndumbaro ameongeza kuwa, baada ya mtumishi huyo kuhamia Sengerema, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya

Dkt. Ndumbaro amuelekeza DED Sengerema kumfungulia mashtaka Bw. Boniventura Bwire aliyekuwa mtumishi kwa

kujipatia fedha kwa udanganyifu

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akisoma moja ya nyaraka za aliyekuwa mtumishi wa umma, Bw. Boniventura Bwire ambaye alifanya udanganyifu ili kujipatia fedha za Serikali kinyume na taratibu za kiutumishi.

Page 14: UTUMISHINews - Tanzania · 12. Miaka Minne ya JPM: Watumishi 2,940 wanufaika na ufadhili wa masomo nje ya nchi.....18-19 13. Serikali yawasilisha Muswada Bungeni wa kuwa na Mamlaka

12

Ufuatiliaji na tathmini serikalini ni chachu ya utendaji kazi na uwajibikaji kwa Watumishi wa umma

Sengerema kutokana na umakini wake aliweza kubaini kuwa, mtumishi huyo anatumia cheti cha kidato cha nne ambacho si chake hivyo akamfukuza kazi.

Dkt. Ndumbaro amesema, Mtumishi huyo baada ya kufukuzwa kazi aliwasilisha rufaa yake kimakosa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi

(CMA) badala ya Tume ya Utumishi wa Umma ambayo ndio mamlaka yake ya rufaa.

Sanjali na hayo, Dkt. Ndumbaro amesema, atawasiliana na Katibu Mkuu TAMISEMI ili afanye uchunguzi na kumtaka kumchukulia hatua stahiki mtumishi wa TAMISEMI atakayebainika kumsaidia Bw. Bwire kufanikisha azma yake ya kuiibia Serikali.

Dkt. Ndumbaro amehitimisha kwamba, mambo yote aliyoyafanya Bw. Boniventura Bwire tangu mwaka 2011 hadi sasa ni batili kwani si mtumishi wa umma halali

baada ya kufukuzwa kazi, na hakuwahi kukata rufaa kwenye mamlaka stahiki, hivyo kutokana na makosa yake kuwa ni ya jinai ameelekeza suala la mtumishi huyo liwasilishwe Jeshi la Polisi na Taasisi ya Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa uchunguzi na kulifikisha mahakamani haraka iwezekanavyo ili Sheria ichukue mkondo wake.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao.

Baadhi ya Watumishi wa Umma wilayani Sengerema wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao.

Mkurugenzi wa Idara ya

Usimamizi wa Rasilimaliwatu

Serikalini, Ofisi ya Rais, Menejimenti

ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kamishna

Msaidizi wa Polisi, Bw.

Ibrahimu Mahumi akitoa ufafanuzi wa masuala ya

kiutumishi.

Matumizi sahihi ya Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini Serikalini

yanaongeza uwajibikaji na kuboresha utendaji kazi wa viongozi na Watumishi wa Umma nchini hivyo kuwa na mchango katika maendeleo ya utumishi wa umma na taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro wakati akifungua mafunzo ya

wadau ya siku mbili yenye lengo la kuwajengea uwezo wa Ufuatiliaji na Tathmini watendaji wa Serikali yaliyofanyika jijini Dodoma.

Dkt. Michael amesema, kutokana na umuhimu wa Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini katika kuboresha

Page 15: UTUMISHINews - Tanzania · 12. Miaka Minne ya JPM: Watumishi 2,940 wanufaika na ufadhili wa masomo nje ya nchi.....18-19 13. Serikali yawasilisha Muswada Bungeni wa kuwa na Mamlaka

13

nidhamu ya utendaji kazi Serikalini, kuna haja ya mfumo huo kuwepo kisheria ili utekelezwe kwa mujibu wa sheria katika Taasisi zote za umma nchini.

Dkt. Michael amefafanua kuwa, pamoja na kuanzisha sehemu za Ufuatiliaji na Tathmini kwenye Wizara, Idara Zinazojitegemea, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, ni muhimu kwa viongozi wenye dhamana kuwa na utashi wa kisiasa katika kujenga Mfumo wa Kitaifa wa Ufuatiliaji na Tathmini ili kuongeza uwajibikaji serikalini.

Dkt. Michael ameongeza kuwa, Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini unatakiwa umguse mtumishi mmoja mmoja na taasisi kwa ujumla ambapo watumishi na taasisi hawana budi kuonyesha matokeo chanya kulingana na rasilimali zilizopo na kwa upande mwingine, wananchi wana haki ya kuiwajibisha Serikali kwa kuitaka ionyeshe matokeo chanya katika utekelezaji wa miradi mbalimbali.

Kwa upande wake, Mkurugenzi

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael akifungua mafunzo ya Ufuatiliaji na Tathmini jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Nolasco Kipanda akitoa neno la utangulizi kabla ya ufunguzi wa mafunzo ya Ufuatiliaji na Tathmini jijini Dodoma

Mkurugenzi wa “Centre for Learning on Evaluation and Results CLEAR-AA” kutoka Chuo cha Witwatersrand nchini Afrika Kusini, Prof. Dugan Fraser akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya Ufuatiliaji na Tathmini watendaji wa Serikali yaliyofanyika jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya wadau ya siku mbili yenye lengo la kuwajengea uwezo wa Ufuatiliaji na Tathmini watendaji wa Serikali wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael (hayupo pichani) yaliyofanyika jijini Dodoma.

Page 16: UTUMISHINews - Tanzania · 12. Miaka Minne ya JPM: Watumishi 2,940 wanufaika na ufadhili wa masomo nje ya nchi.....18-19 13. Serikali yawasilisha Muswada Bungeni wa kuwa na Mamlaka

14wa “Centre for Learning on Evaluation and Results CLEAR-AA” kutoka Chuo cha Witwatersrand nchini Afrika Kusini, Prof. Dugan Fraser amesema, kituo hicho kipo tayari kushirikiana na Serikali katika kuwezesha matumizi sahihi ya Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini yatakayosaidia kuboresha uwajibikaji, utoaji wa huduma bora, kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa wakati na kuimarisha Utawala Bora kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Aidha, Prof. Fraser amesikitishwa na baadhi ya watendaji wanaotumia muda mrefu kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi mbalimbali na kutoa taarifa za miradi hiyo kwa kuchelewa

na kusababisha taarifa zilizopatikana kutokuwa na mchango tarajiwa katika kufanya maamuzi.

Prof. Fraser ameweka bayana kuwa nchi isiyotumia Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini katika utekelezaji wa miradi yake husababisha kuwa na sera mbovu, wananchi kutopata haki ya kuishauri serikali au kutoa maoni juu ya utekelezaji wa miradi hiyo, na serikali husika kutekeleza programu za maendeleo bila ufanisi.

Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Nolasco Kipanda amesema kufanyika kwa semina hiyo

kunatokana na jitihada zinazofanywa na Serikali za kuwajengea uwezo wa kiutendaji wataalamu wake wa ufuatiliaji na tathmini, hivyo amewataka wataalamu hao kutumia fursa hiyo kuongeza ujuzi ili wawe na tija kwa maendeleo ya taifa.

Semina hiyo iliyokuwa na lengo la kuwajengea uwezo wataalamu wa Ufuatiliaji na Tathmini ilihudhuriwa na wadau kutoka katika Wizara, Idara Zinazojitegemea, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, Mahakama, Bunge, Tanzania Evaluation Association (TanEA) na washirika kutoka Afrika Kusini.

Taasisi za umma zapigwa marufuku kutumia kampuni binafsi katika masuala ya TEHAMA na badala yake zitumie Mamlaka

ya Serikali Mtandao

Serikali imepiga marufuku Taasisi za Umma nchini

kutumia fedha za Serikali kuzilipa taasisi binafsi ili kupatiwa huduma ambazo pia zinazotolewa na Mamlaka ya Serikali Mtandao.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) ametoa agizo hilo kwa Watumishi wa Umma na waajiri Serikalini, wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo wakati wa kikao kazi chake na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao wilayani humo.

Page 17: UTUMISHINews - Tanzania · 12. Miaka Minne ya JPM: Watumishi 2,940 wanufaika na ufadhili wa masomo nje ya nchi.....18-19 13. Serikali yawasilisha Muswada Bungeni wa kuwa na Mamlaka

15

kilichofanyika wilayani humo kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao.

Mhe. Mkuchika amefafanua kuwa, Serikali imebadili Wakala ya Serikali Mtandao kuwa Mamlaka kwa sababu hivi sasa ina wataalamu wa kutosha wa TEHAMA hivyo hakuna ulazima wa kuilipa kampuni binafsi ili kupata huduma

ya TEHAMA.

Mhe. Mkuchika alihitimisha ziara ya kikazi mkoani Ruvuma iliyokuwa na lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma, ikiwa ni pamoja na kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) mkoani humo.

Baadhi ya Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao wilayani humo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akifafanua masuala ya kiutumishi kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi chake na watumishi hao kilichofanyika wilayani humo kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.

“Kama Serikali ina

chombo chenye uwezo na weledi wa kutosha wa kutoa huduma

za TEHAMA ikiwemo mifumo ya kielektroniki

ya utoaji huduma, ni nini kinachoshinikiza Taasisi za Umma

kuendelea kuomba kupatiwa huduma hiyo na

kampuni za watu binafsi?,” Mhe.

Mkuchika alihoji.

Page 18: UTUMISHINews - Tanzania · 12. Miaka Minne ya JPM: Watumishi 2,940 wanufaika na ufadhili wa masomo nje ya nchi.....18-19 13. Serikali yawasilisha Muswada Bungeni wa kuwa na Mamlaka

16

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameelekeza vijana wote wenye elimu ya Shahada

ya Kwanza waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) “Operesheni Magufuli” kuajiriwa katika taasisi mbalimbali za serikali.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro alisema hayo wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika ofisini kwake eneo la Mtumba jijini Dodoma.

“Serikali imekuwa ikiwajengea vijana uadilifu, umoja, mshikamano, moyo wa kujitolea, moyo wa uzalendo, nidhamu

na ari ya kupenda kufanya kazi kwa kuwaingiza kwenye mafunzo ya Jeshi

la Kujenda Taifa, hivyo kwa kutambua mchango wao, Rais wa Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza wapatiwe ajira,’’ Dkt.

Ndumbaro amesisitiza.

Dkt. Ndumbaro ametaja sifa za vijana waliohitimu JKT wanaotakiwa kuajiriwa kuwa ni lazima wawe wametumikia kwa kipindi kisichopungua miaka miwili na kwamba wanatakiwa kuwasilisha taarifa zao binafsi, vyeti vya elimu, taaluma na vyeti vya kuhitimu mafunzo ya JKT katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia barua pepe ya [email protected].

Aidha, Dkt. Ndumbaro amewaasa waajiri wanaowarejesha makazini Watumishi wa Umma walioghushi vyeti vya elimu na taaluma kwa visingizio kwamba waliondolewa kimakosa au waliajiriwa kabla ya tarehe 20 Mei, 2001 kwa sifa ya Elimu ya Darasa la Saba.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli aagiza vijana wenye Shahada ya kwanza waliohitimu mafunzo ya JKT “Operesheni

Magufuli” waajiriwe Serikalini

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma kuhusu ajira kwa vijana waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa “Operesheni Magufuli” na masuala mbalimbali ya kiutumishi. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael.

Page 19: UTUMISHINews - Tanzania · 12. Miaka Minne ya JPM: Watumishi 2,940 wanufaika na ufadhili wa masomo nje ya nchi.....18-19 13. Serikali yawasilisha Muswada Bungeni wa kuwa na Mamlaka

17

“Serikali haitosita kumchukulia hatua mwajiri yeyote atakayekiuka maelekezo halali yaliyotolewa na Serikali kuhusiana na hatua zilizochukuliwa dhidi ya watumishi walioghushi vyeti,” Dkt. Ndumbaro amesema.

Akizungumzia suala la udanganyifu na upendeleo katika upandishwaji vyeo, Dkt. Ndumbaro amesema kuwa ofisi yake imebaini baadhi ya waajiri kuwasilisha

taarifa za uongo Ofisi ya Rais-Utumishi ili kuwapandisha vyeo watumishi kwa lengo la kuwanufaisha baadhi yao bila kuwa na sifa au vigezo vilivyowekwa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zinazosimamia Utumishi wa Umma.

“Ofisi yangu itaendelea kuwachukulia hatua stahiki waajiri watakaobainika kufanya udanganyifu kwa madhumuni ya kuipotosha Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili iweze kutoa vibali vya kuwapandisha vyeo watumishi isivyostahili,” Dkt. Ndumbaro amefafanua.

Dkt. Ndumbaro amewaagiza Maafisa Utumishi nchini kufanya kazi kwa

weledi kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma badala ya kuwa chanzo cha kero na matatizo ya kiutumishi.

Mkutano kati ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro na waandishi wa habari ulikuwa na lengo la kuuhabarisha umma juu ya masuala mbalimbali ya kiutumishi.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma kuhusu ajira kwa vijana waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa “Operesheni Magufuli” na masuala mbalimbali ya kiutumishi.

Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) wakati wa mkutano uliofanyika ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma.

Page 20: UTUMISHINews - Tanzania · 12. Miaka Minne ya JPM: Watumishi 2,940 wanufaika na ufadhili wa masomo nje ya nchi.....18-19 13. Serikali yawasilisha Muswada Bungeni wa kuwa na Mamlaka

18

• Viongozi 4,209 wapatiwa mafunzo ya kiutendaji

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo imefadhili watumishi 2,940 kusoma nje ya nchi katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro amesema kuwa mafunzo hayo ya muda mfupi na mrefu yamesaidia kuwajengea uwezo na ufanisi wa kiutendaji Watumishi wa Umma katika sekta mbalimbali ambazo ni vipaumbele vya maendeleo kwa Taifa na pia yameboresha utoaji huduma kwa wananchi.

“Ili kupata matokeo chanya kwenye sekta za kimkakati za Taifa ni muhimu kutumia rasilimaliwatu yenye ujuzi wa kutosha kwa kuwa ndiyo injini ya maendeleo,” Dkt. Ndumbaro alifafanua.

Sekta za kimkakati za Taifa zilizopewa kipaumbele katika ufadhili wa masomo hayo ni Kilimo, Maendeleo ya Jamii, Menejimenti ya Rasilimaliwatu, Afya ya Jamii, Nishati na Madini, Elimu, TEHAMA, Menejimenti ya Maliasili, Menejimenti ya Mazingira na Rasilimaliwatu.

Sekta nyingine zilizopewa kipaumbele ni Maendeleo ya Miundombinu, Menejimenti ya Rasilimali Fedha, Uwezeshaji wa Wanawake kupitia Ujasiriamali, Mawasiliano na Uandishi wa Habari na Menejimenti ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Wadau wa Maendeleo walioshirikiana na Serikali ya Tanzania kufadhili mafunzo hayo ni Serikali ya India, Japan, Jamhuri ya Korea, Australia, Uholanzi, Singapore, Misri na Jamhuri ya Watu wa China.

Sehemu ya Watanzania waliopata ufadhili wa kusoma Shahada za Uzamili nchini Japani wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Utumishi wakati wa hafla ya kuwaaga iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Page 21: UTUMISHINews - Tanzania · 12. Miaka Minne ya JPM: Watumishi 2,940 wanufaika na ufadhili wa masomo nje ya nchi.....18-19 13. Serikali yawasilisha Muswada Bungeni wa kuwa na Mamlaka

19

li kuhakikisha Serikali ina viongozi bora wanaofanya kazi kwa ufanisi, jumla ya

viongozi 4,209 wamepatiwa mafunzo ya kiutendaji katika maeneo ya Mawasiliano Fanisi, Uandaaji na Usimamizi wa Mpango Mkakati, Majadiliano ya Mikataba, Uongozi wa Kimkakati, Mawasiliano na Diplomasia katika Majadiliano, Maadili, Utawala Bora.

Aidha, mafunzo hayo pia yalijikita katika Uwajibikaji, Michakato ya Sera, Mitazamo na Dira, Huduma kwa Wateja, Kiongozi Muadilifu na Uongozi Binafsi na wenye Maadili, Majukumu na Mipaka, Masuala ya Itifaki, Usalama na Ulinzi wa Taifa, Utawala Binafsi, Ununuzi katka Sekta ya Umma, Hisia na Uhusiano wenye Tija kati ya Viongozi Watendaji na Viongozi wa Kisiasa, na Stashahada ya Uzamili ya Uongozi (Postgraduate Diploma in Leadership).

Hatua nyingine iliyochukuliwa na Serikali kuhakikisha viongozi wa umma wanafanya kazi kwa ufanisi zaidi ni kuwakutanisha viongozi hao na viongozi kutoka nchi mbalimbali kupitia Makongamano yanayotumika kujadili mada mbalimbali za kuboresha utendaji kazi.

Makongamano hayo yaliratibiwa na Taasisi ya UONGOZI ambapo jumla ya Mikutano 20

ya Kimataifa, Kikanda na Kitaifa ilifanyika kwa lengo la kubadilishana taarifa, maarifa, uzoefu, changamoto na kuongeza uelewa wa masuala ya Uongozi na Maendeleo Endelevu. Jumla ya Viongozi 2,430 walishiriki kutoka Tanzania na Nchi mbalimbali.

Mada zilzojadiliwa katika mikutano hiyo ni pamoja na Namna ya Kuendeleza Biashara Barani Afrika; Sera zinazohusu Mabadiliko ya Tabia Nchi; Kukuza Uwekezaji katika Sekta ya Misitu; Mafunzo kwa Viongozi wa Sasa na wa Kizazi cha Baadae; Nafasi ya Mashirika ya Umma katika Utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano; Uhuru wa Nchi, Demokrasia na Maendeleo ya Jamii Afrika; na Mikakati ya Tanzania katika Kuelekea kwenye Uchumi wa Viwanda;

Mada nyingine zilihusu Amani na Usalama kwa Afrika Jumuishi na Endelevu; Masuala ya Jinsia kutoka kwenye Nadharia Kuelekea Kwenye Vitendo; Namna ya Kujenga Uchumi Endelevu kwa Kutumia Rasilimali kwa Ufanisi; Maboresho katika Sekta ya Umma na Ugatuaji wa Madaraka; Harakati za Kujikomboa Kiuchumi kwa Bara la Afrika; Kukuza na Kuimarisha Uongozi na Viongozi Tanzania; na Rasilimali za Asili na Ujenzi wa Viwanda.

Viongozi 4,209 wapatiwa mafunzo ya kiutendaji

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza katika hafla ya kuwaaga Watanzania waliopata ufadhili wa masomo nchini Japan iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Page 22: UTUMISHINews - Tanzania · 12. Miaka Minne ya JPM: Watumishi 2,940 wanufaika na ufadhili wa masomo nje ya nchi.....18-19 13. Serikali yawasilisha Muswada Bungeni wa kuwa na Mamlaka

20

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imewasilisha Muswada Bungeni wa kutungwa kwa Sheria ya Serikali

Mtandao ya mwaka 2019 (e-Government Act, 2019) ambayo itawezesha kuundwa kwa Mamlaka ya Serikali Mtandao yenye jukumu la kuratibu, kusimamia na kuendeleza Serikali Mtandao kwa mujibu wa Sera, Sheria, Kanuni, Viwango na Miongozo ya TEHAMA iliyopo.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst.) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) alipofanya ziara ya kikazi katika Wakala ya Serikali Mtandao ili kukagua utendaji kazi wa wakala hiyo na kujionea Mfumo mpya wa Taarifa Shirikishi za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) na Mfumo wa Wazi wa Tathmini ya Utendaji Kazi wa Kieletroniki (eOPRAS) ambayo imetengenezwa na Wakala hiyo kupitia wataalam wa ndani.

Mhe. Mkuchika amefafanua kuwa, azma ya Serikali kuwasilisha Muswada Bungeni wa kubadili Wakala ya Serikali Mtandao kuwa Mamlaka ni kuwa na chombo thabiti kitakazowezesha mifumo ya TEHAMA Serikalini kufanya kazi kwa pamoja, kubana matumizi katika utengenezaji wa Mifumo ya TEHAMA kwa kutumia wataalam wa ndani na

kuwezesha ukusanyaji wa mapato Serikalini.

Mhe. Mkuchika ameongeza kuwa, Serikali imejiandaa na inaendelea kuwajengea uwezo wataalam wake wa TEHAMA nje ya nchi ili kuwa na hazina ya kutosha ya wataalam wabobevu katika eneo la TEHAMA.

Mhe. Mkuchika ameainisha kuwa, anajisikia fahari kushuhudia wataalam wa ndani wakitengeneza Mfumo mpya wa Taarifa Shirikishi za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) na Mfumo wa Wazi wa Tathmini ya Utendaji Kazi wa Kieletroniki (eOPRAS) ambayo iko katika hatua za mwisho kukamilika.

Sanjali na hayo, Mhe. Mkuchika ameridhishwa na utendaji kazi wa Kituo cha Utafiti, Ubunifu na Maendeleo ya Mifumo ya Serikali Mtandao (eGOVRIDC) kilichojengwa na Serikali jijini Dodoma kwa ajili ya kuongeza kasi ya ukuaji wa Serikali Mtandao nchini.

Utekelezaji wa Serikali Mtandao (e-Government) katika kipindi cha kuanzia mwaka 2012 hadi 2019 umeongeza ufanisi katika utendaji kazi, umepunguza gharama za utendaji na kuboresha utoaji wa huduma kwa umma kwa urahisi, haraka na gharama nafuu.

Serikali yawasilisha Muswada Bungeni wa kuwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst.) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na Wataalam wa ndani wa TEHAMA (hawapo pichani) waliotengeneza Mfumo mpya wa Taarifa Shirikishi za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) na Mfumo wa Wazi wa Tathmini ya Utendaji Kazi wa Kieletroniki (eOPRAS) ambayo inatarajiwa kukamilika hivi karibuni.

Page 23: UTUMISHINews - Tanzania · 12. Miaka Minne ya JPM: Watumishi 2,940 wanufaika na ufadhili wa masomo nje ya nchi.....18-19 13. Serikali yawasilisha Muswada Bungeni wa kuwa na Mamlaka

2121MATUKIO KATIKA PICHA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst.) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo (Mb) wakifuatilia ufunguzi wa mkutano Mkuu wa 39 wa SADC uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika kitaifa katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ACP Ibrahim Mahumi akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna wa Tume ya Maadili na Kuzuia Rushwa nchini Kenya, Bibi Rose Mghoi Machaira mara baada ya kikao kilichofanyika Ofisi ya Rais Utumishi, Mtumba, jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Watu Wenye Ulemavu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Philibert Kawemama akifungua mkutano kuhusu ushawishi na utetezi wa masuala ya watu wenye ulemavu katika ngazi ya wizara uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora jijini Dodoma. Kulia kwake ni Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Utawala, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Bi. Mwanaheri Cheyo.

Page 24: UTUMISHINews - Tanzania · 12. Miaka Minne ya JPM: Watumishi 2,940 wanufaika na ufadhili wa masomo nje ya nchi.....18-19 13. Serikali yawasilisha Muswada Bungeni wa kuwa na Mamlaka

22MATUKIO KATIKA PICHA

Afisa Utumishi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Denis Mapunda akimhudumia mteja Bi.Magreth Kiruma kutoka Shule ya Sekondari Butimba iliyoko jijini Mwanza.

Msaidizi wa Kumbukumbu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Godfrey Kajuna akimhudumia mteja Bw.Sanford Ngowi kutoka Tume ya Madini alipowasili ofisi za masijala kuwasilisha barua za ofisi ya Tume hiyo.

Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao, Dkt. Jabir Bakari akiwaeleza Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa jinsi mifumo ya TEHAMA inavyorahisisha utendaji kazi Serikalini katika ziara ya kikazi ya kamati hiyo ofisini kwake jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst.) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) (wa pili kutoka kushoto mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa baada ya kamati hiyo kuhitimisha ziara ya kikazi katika ofisi za Mamlaka ya Serikali Mtandao jijini Dodoma. Wengine ni watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na

Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA).

Page 25: UTUMISHINews - Tanzania · 12. Miaka Minne ya JPM: Watumishi 2,940 wanufaika na ufadhili wa masomo nje ya nchi.....18-19 13. Serikali yawasilisha Muswada Bungeni wa kuwa na Mamlaka

Tovuti:www.utumishi.go.tz

Ofisi ya Rais UtumishiOfisiyaRais_utumishi2019Ofisi ya Rais Utumishiutumishitzutumishitz