TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA

23
SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA Na Prof Handley Mpoki Mafwenga [PhD, MSc, LLM, MBA, PGDTM, ATM, LLB, ICSA(UK)] Mshauri wa Sera za Uchumi, Bajeti na Kodi Wizara ya Nishati na Madini [TMAA]

Transcript of TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA

Page 1: TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA

SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA

Na Prof Handley Mpoki Mafwenga [PhD, MSc, LLM, MBA, PGDTM, ATM, LLB, ICSA(UK)]

Mshauri wa Sera za Uchumi, Bajeti na Kodi Wizara ya Nishati na Madini [TMAA]

Page 2: TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA

UTANGULIZI

Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) ulianzishwa tarehe 2 Novemba, 2009 chini ya Sheria ya Wakala wa Serikali, Sura ya 245 Kupitia Gazeti la Serikali Na 362 .

Lengo la Wakala ni kuhakikisha, Serikali inapata mapato stahiki kutoka kwenye shughuli za uzalishaji na biashara ya madini nchini, kupitia usimamizi na ukaguzi thabiti wa shughuli hizo, na kuhakikisha kuwa shughuli hizo zinafanyika kwa kuzingatia uhifadhi na utunzaji thabiti wa mazingira katika maeneo ya migodi.

Page 3: TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA

MAJUKUMU YA WAKALA

Kukagua na kuhakiki uzalishaji

na mauzo ya madini

Kusimamia na kukagua shughuli za

utunzaji wa mazingira

Kukagua na kuhakiki hesabu za fedha za

migodi

TMAA

Page 4: TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA

UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA WAKALA

1. Ukaguzi wa Kiwango na Ubora wa madini yanayozalishwa na kuuzwa na wachimbaji wakubwa

.

Lengo: kuhakikisha kwamba Serikali inapata takwimu sahihi za madini yanayozalishwa na kuuzwa nje; thamani yake halisi na mrabaha unaostahili kulipwa.

Page 5: TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA

UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA WAKALA

Page 6: TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA

MIGODI MIKUBWA INAYOKAGULIWA NA TMAA

Tulawaka

Geita

Golden Pride

Buzwagi

TanzaniteOne

North Mara

Bulyanhulu

Shanta Chunya

Williamson

Ngaka

= Migodi hii imesimamisha uzalishaji

MAZAO YANAYOZALISHWA NA MIGODI MIKUBWA: Mikuo ya dhahabu

(Bulyanhulu, Geita, North Mara, Buzwagi na New Luika).

Makinikia ya shaba (Bulyanhulu na Buzwagi).

Almasi (Williamson) Tanzanite

(TanzaniteOne). Makaa ya Mawe

(Ngaka).

Page 7: TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA

UKAGUZI MKAKATI

1. Kazi ya Ukaguzi Mkakati (strategic auditing) katika machimbo ya madini ya ujenzi na viwandani kwa kutumia “Hati ya Mauzo ya Madini” inafanyika kwa kushirikiana na Ofisi za Madini za Kanda.

Ukaguzi huu hutekelezwa kwa:

Kuweka vituo vya ukaguzi kwenye njia kuu ziendazo na zitokazo kwenye maeneo ya uchimbaji.

Kukusanya “Hati za Mauzo” zinazotolewa na wachimbaji kila wanapofanya mauzo.

Kutunza na kuchambua takwimu za mauzo katika kanzidata na kukokotoa mrabaha stahiki.

Kufuatilia malipo ya mrabaha kwa kushirikiana na Ofisi za Madini husika.

Page 8: TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA

2. Ukaguzi kwa wachenjuaji wa marudio ya dhahabu wanaotumia kemikali ya sayanaidi (vat leaching):

inaendelea…

Unafanyika kwa kuweka Wakaguzi na matumizi ya lakiri (security seals) katika maeneo ya mitambo ya uchenjuaji wa marudio (elution plants) 6 iliyopo Jijini Mwanza na 11 iliyopo Geita.

UKAGUZI MKAKATI

Page 9: TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA

UDHIBITI WA UTOROSHAJI NA BIASHARA HARAMU YA MADINI

Kazi hii hutekelezwa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, TRA, TAA, Idara ya Madini na Usalama wa Taifa kwa:

Kufanya ukaguzi kupitia madawati maalum yaliyopo katika viwanja vya ndege vya Julius Nyerere (Dar), Kilimanjaro na Mwanza.

Kutoa elimu kwa umma kuhusu sheria na taratibu za kuingiza na kusafirisha madini nje ya nchi.

Kuimarisha ushirikiano na vyombo vingine vya serikali.

Kuchukua hatua kali za kisheria kwa wanaobainika.

Page 10: TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA

Kuhakiki kumbukumbu, taarifa na nyaraka mbalimbali

Kuhakiki mauzo ya madini, gharama halisi za uwekezaji na uendeshaji kama zilivyobainishwa kwenye taarifa za migodi

Kuchambua taarifa za upembuzi yakinifu za migodi

Kuhakiki usahihi wa ritani za kodi za migodi

UKAGUZI NA UCHAMBUZI WA HESABU ZA FEDHA ZA MIGODI

LENGO: kukusanya taarifa sahihi za kodi na tozo mbalimbali za migodi mikubwa na ya kati na kuziwasilisha TRA na vyombo vingine husika vya Serikali. Kazi hii hufanywa kwa:

Page 11: TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA

Kukagua shughuli za usimamizi na utunzaji wa mazingira katika maeneo ya migodi

Kuhakiki uwepo wa dhamana ya utunzaji na ukarabati, wakati wa uhai wa mgodi na baada ya mgodi kufungwa

Kuhakiki utekelezaji wa Mipango ya Usimamizi wa Mazingira na uzingatiaji sheria na kanuni

Kuhakiki bajeti na matumizi ya migodi kwa ajili ya utunzaji na ukarabati wa mazingira

Kazi hiyo hufanyika kwa:

USIMAMIZI NA UKAGUZI WA MAZINGIRA MIGODINI

LENGO: kuhakikisha kuwa shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini zinafanyika kwa kuzingatia uhifadhi na utunzaji thabiti wa mazingira katika maeneo ya migodi.

Page 12: TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA

Kasoro zinazojitokeza mara kwa mara katika ukaguzi wa mazingira:

USIMAMIZI NA UKAGUZI WA MAZINGIRA MIGODINI inaendelea…

Page 13: TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA

SHUGHULI ZA MAABARA

Wakala una Maabara ya kisasa ambayo hutoa huduma za utambuzi na uchunguzi wa madini mbalimbali.

• Maabara inatumika kufanya uchunguzi wa sampuli za madini kutoka migodi mikubwa ili kujua ubora, kiasi na thamani ya madini yanayozalishwa na mrabaha stahiki;

• Maabara pia hutumika kutoa huduma za uchunguzi wa sampuli za madini kutoka katika taasisi mbalimbali za Serikali na watu binafsi kibiashara.

Page 14: TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA

CHANGAMOTO ZILIZOPO

• Kuongeza Fungamanisho la Sekta ya Madini na Sekta nyingine za Uchumi.

• Miundombinu kwenye Maeneo ya Migodi.

• Uvamizi unaofanywa na Wachimbaji Wadogo kwenye Maeneo yenye Leseni.

• Ulinzi na Usalama kwenye Maeneo ya Wachimbaji Wadogo.

• Uchafuzi wa Mazingira unaosababishwa na Uchimbaji Mdogo.

Page 15: TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA

1. Baadhi ya migodi mikubwa kuendelea kulipa kodi ya mapato

Kwa kipindi ambacho Wakala umekuwa ukifanya ukaguzi katika migodi mikubwa (2009 – 2014), jumla ya Shilingi bilioni 527.8 zimelipwa na migodi mikubwa kama kodi ya mapato.

2. Mapunjo ya kodi na tozo mbalimbali kulipwa Serikalini na migodi baada ya kubainika kutolipwa

Kwa kipindi cha kuanzia Januari, 2012 hadi Machi, 2014 jumla ya Shilingi bilioni 8.89 zimelipwa na migodi mikubwa na ya kati kama mapunjo ya kodi na tozo mbalimbali zikijumuisha mrabaha, kodi ya zuio, ushuru wa huduma, SDL na PAYE.

MAFANIKIO YALIYOPATIKANA

Page 16: TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA

3. Kuongezeka kwa malipo ya mrabaha:

Katika kipindi cha Juni 2011 hadi Machi 2014, Wakala umewezesha Serikali kukusanya mrabaha wa jumla ya Shilingi bilioni 3.6 kutokana na ukaguzi wa madini ya ujenzi na viwandani. Kiasi hiki ni kikubwa ikilinganishwa na kiasi kilichokuwa kinakusanywa kabla ya ukaguzi kuanza. Kwa mfano, Ofisi ya Kanda ya Mashariki ilikuwa inakusanya wastani wa Shilingi milioni 3 kwa mwaka kabla ya ukaguzi wa TMAA kuanza mnamo Julai 2011.

Kupitia ukaguzi kwa wachenjuaji wa marudio ya dhahabu wanaotumia kemikali ya sayanaidi (vat leaching), jumla ya Kilo 409.9 za dhahabu zenye thamani ya Shilingi bilioni 22.6 katika kipindi cha mwezi Julai 2013 hadi Machi 2014,. Mrabaha uliolipwa ni Shilingi milioni 901.1.

inaendelea…

MAFANIKIO YALIYOPATIKANA

Page 17: TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA

4. Serikali kupata mrabaha na takwimu sahihi za madini yanayozalishwa na migodi mikubwa nchini

Kupitia kaguzi mbalimbali, jumla ya Dola za Marekani milioni 437 zimekusanywa na Serikali kama mrabaha katika kipindi cha kuanzia Mwaka 1998 hadi 2013.

5. Udhibiti wa Utoroshaji wa Madini na Ukwepaji wa Mrabaha

Tangu Wakala uanze kukagua wasafiri na mizigo katika viwanja vya ndege mwezi Julai 2012 hadi Machi 2014, jumla ya matukio 43 ya utoroshaji madini yenye thamani ya takriban Shilingi bilioni 15.72 yameripotiwa katika viwanja 3 vya ndege.

6. Kuboreshwa kwa mazingira migodini

Mazingira katika maeneo ya migodi yameboreshwa kufuatia kaguzi zilizofanywa na TMAA. Aidha, ajali zitokanazo na matumizi ya sayanaidi zimepungua kwa wachimbaji wadogo.

inaendelea… MAFANIKIO YALIYOPATIKANA

Page 18: TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA

Malipo ya Kodi na Mrabaha Yaliyofanywa na Kampuni za Uchimbaji Mkubwa wa Madini, Mwaka 2000 - 2013

(Shilingi Bilioni)

* Kodi nyingine zinajumuisha: Stamp Duty, Import Duty, Excise Duty, Income Tax & Local Government Levy na hazijumuishi Ushuru wa Barabara.

Year Corporate

Tax

PAYE SDL WHT *Other

Taxes

Total Taxes

Paid

Total

Royalty Paid

Grand

Total

2000 0 3.88 0.86 4.71 0.39 9.85 4.45 14.30

2001 0 7.23 1.13 4.86 0.35 13.57 7.65 21.22

2002 0 10.68 1.69 5.40 1.64 19.41 11.41 30.82

2003 0 12.79 1.66 5.45 2.19 22.09 16.44 38.53

2004 0 8.33 2.44 5.32 4.86 20.95 20.59 41.54

2005 2.31 13.05 8.87 7.50 5.44 37.16 22.34 59.50

2006 1.75 11.78 2.49 3.35 2.84 22.21 30.38 52.59

2007 1.44 22.28 3.76 3.26 3.44 34.18 31.40 65.58

2008 0.88 44.01 7.55 5.61 9.23 67.27 33.72 100.99

2009 3.21 52.64 9.78 7.87 8.67 82.16 44.42 126.58

2010 21.38 49.92 11.32 13.14 4.87 101.16 71.55 172.71

2011 137.16 90.30 19.5 12.26 26.26 287.93 98.13 386.06

2012 299.85 87.45 19.32 67.64 46.81 528.35 117.66 646.01

2013 24.67 87.32 19.25 36.63 22.25 197.44 116.64 314.08

Total 492.65 501.66 109.62 183.00 139.24 1,443.73 626.78 2,070.51

Page 19: TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA

Kiasi cha Dhahabu Kilichozalishwa na Mrabaha Uliolipwa na Wazalishaji Wanaotumia Teknolojia ya Vat Leaching

(Geita na Mwanza)

Page 20: TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA

Kiasi cha Dhahabu Kilichozalishwa na Kuuzwa na Migodi Mikubwa 7 Nchini (2000 – 2013, Wakia Milioni)

Page 21: TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA

Kiasi cha Mrabaha Uliolipwa na Migodi Mikubwa 7 ya Dhahabu Nchini, Mwaka 2000 – 2013 (Dola Milioni)

2000 2001 2002 2003 2004 2005 2006 2007 2008 2009 2010 2011 2012 2013

32.8

7.5 3.5

10.6

14.4 17.3

19.0

23.4 24.3 27.3

46.9

64.7

74.1

70.8

Page 22: TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA

22

KUVUTIA MITAJI YA UWEKEZAJI (FDI) KATIKA SEKTA 1998 – 2012 (USD Million)

FDI A

mo

un

t (U

SD M

illio

n)

g Total FDI Inflows g FDI in Mining

Page 23: TEITI -WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA-MWANZA

ASANTENI KWA

KUNISIKILIZA