Tanzania Ijayo, Document No. 7, Ufugaji Wa Kisasa Na Biashara Kubwa Ya Mazao Ya Mifugo Yetu

4
1 TANZANIA IJAYO: UFUGAJI WA KISASA NA BIASHARA KUBWA YA MAZAO YA MIFUGO YETU BIASHARA YA MAZAO YA NG’OMBE DUNIANI Mazao makuu ya ng’ombe (cattle) ni: (i) NYAMA: beef (adult cattle) na veal (calves) na sehemu nyingine za ng’ombe zinatumika kwa chakula; (ii) MAZIWA (maziwa ya ng’ombe- diary milk na mazao makuu mengine ni: butter-siagi, yogurt-mtindi and cheese-jibini); na (iii) NGOZI (hides and skins - leather, viatu, mabegi, nguo, mikanda, viti na sofa) ndiyo mazao muhimu ya biashara kwa soko la ndani na kwa masoko ya kimataifa. Tanzania inalazimika kufanya ufugaji wa kisasa, unaotumia sayansi, teknolojia na ubunifu (science, technology and innovation) kwa sababu watu bilioni 7.3 (2015), bilioni 8.1 (2025), bilioni 9.6 (2050) na bilioni 10.9 (2100) wengi wao watahitaji maziwa ya ng’ombe, nyama na mazao mengine ya mifugo ya aina mbalimbali. Takwimu zinaonyesha kwamba kwa zaidi ya miaka 50, uzalishaji wa nyama Duniani UMEONGEZEKA MARA NNE, kutoka tani milioni 78 kwa mwaka hadi kufikia tani milioni 308 kwa mwaka kati ya Mwaka 1963 na 2014; na wastani wa utumiaji wa nyama kwa mtu mmoja Duniani (consumption per capita) kwa sasa unakadiriwa kuwa kilo 42.9 kwa mwaka. IDADI YA MIFUGO TANZANIA Tanzania inakadiriwa kuwa na ng’ombe (cattle) milioni 23 na asilimia 97 (97%) ya ng’ombe hao wanafugwa kiasilia (indigenous). Sensa ya Mwaka 2012, inaonyesha kwamba kwa Mwaka 2007/08, nchi yetu ilikuwa na idadi ya mashamba makubwa ya ufugaji kama ifuatavyo: kuku-mashamba 494,866; ng’ombe 120,014; mbuzi 24,193; na kondoo 14, 609. Idadi ya mashamba makubwa ya mifugo, kwa wakati huo, hayakuzidi 700, 000. IDADI YA MIFUGO NA ENEO LA MALISHO DUNIANI Mwaka 2013, idadi ya ng’ombe Duniani ilikadiriwa kufikia bilioni 1.5 ikiwa ni ongezeko la asilimia 54 (54%) ya idadi iliyokuwepo Mwaka 1963. Kati ya Mwaka 2008 na 2013, idadi ya kondoo Duniani ilikardiriwa kuwa bilioni 1.1 na mbuzi milioni 881.6. Nchi zenye ng’ombe wengi Duniani ni: (1) India– milioni 329.6; (2) Brazil- milioni 209.8; (3) China- milioni 104.2; (4) USA- milioni 89; na (5) Umoja wa Ulaya- milioni 84.8. Idadi ya kuku Duniani wanaofugwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu wameongezeka kutoka bilioni 4.1 hadi bilioni 21.7 kati ya Mwaka 1963 na 2013. Mifugo ndiyo inakisiwa kutumia eneo kubwa la ardhi Duniani (pasture and land dedicated to the production of feed), ikitumia takribani asilimia 80 (80%) ya ardhi yote itumiwayo kwa

description

Tanzania Ijayo, Document No. 7, Ufugaji Wa Kisasa Na Biashara Kubwa Ya Mazao Ya Mifugo Yetu

Transcript of Tanzania Ijayo, Document No. 7, Ufugaji Wa Kisasa Na Biashara Kubwa Ya Mazao Ya Mifugo Yetu

  • 1

    TANZANIA IJAYO: UFUGAJI WA KISASA NA BIASHARA KUBWA

    YA MAZAO YA MIFUGO YETU

    BIASHARA YA MAZAO YA NGOMBE DUNIANI

    Mazao makuu ya ngombe (cattle) ni: (i) NYAMA: beef (adult cattle) na veal (calves) na

    sehemu nyingine za ngombe zinatumika kwa chakula; (ii) MAZIWA (maziwa ya ngombe-

    diary milk na mazao makuu mengine ni: butter-siagi, yogurt-mtindi and cheese-jibini); na (iii)

    NGOZI (hides and skins - leather, viatu, mabegi, nguo, mikanda, viti na sofa) ndiyo mazao

    muhimu ya biashara kwa soko la ndani na kwa masoko ya kimataifa.

    Tanzania inalazimika kufanya ufugaji wa kisasa, unaotumia sayansi, teknolojia na ubunifu

    (science, technology and innovation) kwa sababu watu bilioni 7.3 (2015), bilioni 8.1 (2025),

    bilioni 9.6 (2050) na bilioni 10.9 (2100) wengi wao watahitaji maziwa ya ngombe, nyama na

    mazao mengine ya mifugo ya aina mbalimbali. Takwimu zinaonyesha kwamba kwa zaidi ya

    miaka 50, uzalishaji wa nyama Duniani UMEONGEZEKA MARA NNE, kutoka tani milioni 78

    kwa mwaka hadi kufikia tani milioni 308 kwa mwaka kati ya Mwaka 1963 na 2014; na

    wastani wa utumiaji wa nyama kwa mtu mmoja Duniani (consumption per capita) kwa sasa

    unakadiriwa kuwa kilo 42.9 kwa mwaka.

    IDADI YA MIFUGO TANZANIA

    Tanzania inakadiriwa kuwa na ngombe (cattle) milioni 23 na asilimia 97 (97%) ya ngombe

    hao wanafugwa kiasilia (indigenous). Sensa ya Mwaka 2012, inaonyesha kwamba kwa

    Mwaka 2007/08, nchi yetu ilikuwa na idadi ya mashamba makubwa ya ufugaji kama

    ifuatavyo: kuku-mashamba 494,866; ngombe 120,014; mbuzi 24,193; na kondoo 14, 609.

    Idadi ya mashamba makubwa ya mifugo, kwa wakati huo, hayakuzidi 700, 000.

    IDADI YA MIFUGO NA ENEO LA MALISHO DUNIANI

    Mwaka 2013, idadi ya ngombe Duniani ilikadiriwa kufikia bilioni 1.5 ikiwa ni ongezeko la

    asilimia 54 (54%) ya idadi iliyokuwepo Mwaka 1963. Kati ya Mwaka 2008 na 2013, idadi ya

    kondoo Duniani ilikardiriwa kuwa bilioni 1.1 na mbuzi milioni 881.6. Nchi zenye ngombe

    wengi Duniani ni: (1) India milioni 329.6; (2) Brazil- milioni 209.8; (3) China- milioni 104.2;

    (4) USA- milioni 89; na (5) Umoja wa Ulaya- milioni 84.8.

    Idadi ya kuku Duniani wanaofugwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu wameongezeka kutoka

    bilioni 4.1 hadi bilioni 21.7 kati ya Mwaka 1963 na 2013.

    Mifugo ndiyo inakisiwa kutumia eneo kubwa la ardhi Duniani (pasture and land dedicated to

    the production of feed), ikitumia takribani asilimia 80 (80%) ya ardhi yote itumiwayo kwa

  • 2

    kilimo: Hekta bilioni 3.4 zinatumika kwa ufugaji (grazing) and theluthi moja ya ardhi inayofaa

    kwa kilimo Duniani inatumika kuzalisha chakula cha mifugo (The sector uses 3.4 billion

    hectares for grazing and one-third of global arable land to grow feed crops).

    Livestock is the worlds largest user of land resources, with pasture and land

    dedicated to the production of feed representing almost 80% of the total

    agricultural land.

    UZALISHAJI WA NYAMA DUNIANI

    Mwaka 2012, nyama ya takribani tani milioni 304 ilizalishwa Duniani (produced worldwide);

    na makadirio ya wastani wa matumizi ya nyama yalikuwa kilo 42.8 kwa kila mmoja wetu kwa

    mwaka (consumption per capita) kwa wakati huo kwa nchi zinazoendelea ikiwa ni kilo 33.4

    kwa mtu mmoja kwa mwaka, na kwa nchi zilizoendelea ikiwa ni wastani wa kilo 76.2 kwa mtu

    mmoja kwa mwaka. Kwa Mwaka 2014, FAO ilikadiria ongezeko la uzalishaji wa nyama

    Duniani kufikia jumla ya takribani tani milioni 311.6. FAO inakadiria kwamba ifikapo Mwaka

    2050 (Idadi ya watu Duniani inakadiriwa kuwa bilioni 9.6), uzalishaji wa nyama Duniani

    utafikia tani milioni 455.

    WAUZAJI WAKUBWA WA NYAMA DUNIANI

    Brazil na India kwa pamoja ziliuza nyama kwa kiasi cha asilimia 40 (40%) ya nyama yote

    iliyouzwa Duniani kote (2013). Uuzaji mkubwa Duniani kwa Mwaka 2013 ilikuwa kama

    ifuatavyo: (1) Brazil iliuza takribani tani milioni 1.85 (20.17% ya mauzo ya Dunia nzima), (2)

    India tani milioni 1.77 (19.26% ya mauzo ya Dunia nzima), (3) Australia tani milioni 1.59

    (17.38%), (4) USA tani milioni 1.17 (12.79%) na (5) New Zealand, tani 528,000 (5.77% ya

    mauzo Dunia nzima). Kwa upande wa Afrika, muuzaji mkubwa Duniani alikuwa ni Afrika

    Kusini (namba 22 Duniani) - iliuza tani 13,000 (0.14% ya mauzo ya Dunia nzima).

    UZALISHAJI WA MAZIWA YA NGOMBE DUNIANI

    Uzalishaji wa maziwa Duniani unakisiwa KUONGEZEKA ZAIDI YA ASILIMIA 50 (50%)

    kutoka tani milioni 482 Mwaka 1982 hadi kufikia tani milioni 754 Mwaka 2012. India ndiyo

    inaongoza kwa kuzalisha maziwa mengi kuliko nchi zote Duniani, inazalisha karibu asilimia 16

    (16%) ya maziwa yote ya Dunia, ambayo ni takribani tani milioni 122 kwa mwaka. India

    inafuatiwa na USA, China, Pakistani na Brazil. OECD na FAO wanakisia kwamba kati ya

    Mwaka 2010 na 2020 uzalishaji wa maziwa utaongezeka kwa kiasi cha tani milioni 153.

    UTUMIAJI WA MAZIWA DUNIANI

    Inakadiriwa kwamba kila mmoja wetu (Jumla ya watu bilioni 7.3 Duniani) anatumia wastani

    wa takribani kilo 108 za maziwa kwa mwaka. Takwimu zinaonyesha utumiaji wa maziwa

  • 3

    Duniani kwa kikanda ni kama hivi: (1) Asia: 39% ya utumiaji wa maziwa Duniani, (2) Ulaya

    (Europe) 29%, (3) Amerika Kaskazini 13%, (4) Amerika Kusini 9%, (5) Afrika 6%, (6)

    Amerika ya Kati (ikiwemo Mexico) 3%, na (7) Oceania (Australia, New Zealand , n.k.) 1%

    BIASHARA YA NGOZI (HIDES & SKINS)

    Ngozi za aina mbalimbali zinatokana na wanyama wanaochinjwa au kuuawa. Kati ya Mwaka

    2008 na 2013, FAO inakadiria uchinjaji kwa mwaka ulikuwa hivi: kondoo 542.5 milioni na

    mbuzi milioni 426.6.

    Afrika inakadiriwa kuwa na asilimia 15 (15%) ya jumla ya ngombe na takribani asilimia 25

    (25%) ya kondoo na mbuzi wote Duniani. Hata hivyo, mbali ya wingi huo wa mifugo, Afrika

    inazalisha asilimia 8 (8%) tu ya ngozi za ngombe na takribani asilimia 14 (14%) tu ya ngozi

    za kondoo na mbuzi Duniani - Idadi ya ngozi zinazozalishwa Duniani inakadiriwa kuwa

    takribani milioni 240 kwa mwaka.

    MTAJI MKUBWA WA UFUGAJI WA KISASA KUTOKA KWENYE UCHUMI WA GESI

    ASILIA: Kama ilivyo kwenye KILIMO na UVUVI wa kisasa, UFUGAJI wa kisasa wenye lengo

    la kuuza mazao ya mifugo yetu kwenye soko la ndani na masoko makubwa ya nje, tunahitaji

    vitu vitano muhimu sana: (i) ardhi ya malisho kwa wafugaji, (ii) matumizi makubwa ya

    sayansi, teknolojia na ubunifu - wataalamu na taasisi zao za mafunzo na utafiti wa kaliba ya

    juu, (iii) rasilimali fedha, (iv) viwanda vya kuthaminisha (value addition) na kukamilisha

    utengenezaji wa mazao ya mifugo yetu, na (v) sera na sheria za kustawisha ufugaji na

    wafugaji.

    Nchi 10 bora kwa uzalishaji mwingi wa Gesi Asilia Duniani ni: (1) USA, (2) Russia, (3) Iran,

    (4) Canada, (5) Qatar (GDP per capita: US$ 98,986), (6) Norway (GDP per capita: US$ 100,

    579), (7) China (GDP per capita: US$ 6,959), (8) Saudi Arabia (GDP per capita: US$ 24, 953),

    (9) Algeria (GDP per capita: US$ 5,606) na (10) Netherlands (Uholanzi). Kwa hiyo Uchumi wa

    Gesi Asilia ni muhimu sana kwa upatikanaji wa mitaji ya uhakika ya kuboresha na kukuza

    Uchumi wa Mifugo nchini mwetu (Tanzania - GDP per capita: US$ 719).

    Ushirikiano na mpangilio unaotekelezeka vizuri kati ya Uchumi wa Mifugo na Kilimo; na

    Uchumi wa Gesi Asilia, Viwanda na Huduma (services) ndio utakaokuza uchumi wetu kwa

    zaidi ya 10% kwa mwaka, boresha na kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja, na hatimae

    kutokomeza umaskini wetu na kutufanya tuwe nchi ya kipato cha kati ifikapo Mwaka 2025

    (Dira yetu ya Maendeleo).

    Document No. 7

    Tarehe: 18 March 2015

  • 4