Simbegwire anavipenda, na kila mmoja akala hadi akashiba. Baada ya kula watoto wakaenda kucheza huku...

18
Simbegwire Simbegwire Rukia Nantale Benjamin Mitchley Matteo E. Mwita swahili nivå 5

Transcript of Simbegwire anavipenda, na kila mmoja akala hadi akashiba. Baada ya kula watoto wakaenda kucheza huku...

Page 1: Simbegwire anavipenda, na kila mmoja akala hadi akashiba. Baada ya kula watoto wakaenda kucheza huku watu wazima wakiongea. Simbegwire akajisikia furaha na jasiri. Akaamua kuwa si

SimbegwireSimbegwire

Rukia Nantale Benjamin Mitchley Matteo E. Mwita swahili nivå 5

Page 2: Simbegwire anavipenda, na kila mmoja akala hadi akashiba. Baada ya kula watoto wakaenda kucheza huku watu wazima wakiongea. Simbegwire akajisikia furaha na jasiri. Akaamua kuwa si

Simbegwire alihuzunika mama yake alipofariki.Baba yake alijitahidi kumtunza mwanaye.Taratibu wakaanza kuwa wenye furaha tena, bilaya Mama Simbegwire. Kila asubuhi walikaa nakupanga mipango ya siku inayofuata. Kila jioniwaliandaa chakula cha jioni pamoja. Baada yakuosha vyombo, baba yake Simbegwirealimsaidia kufanya kazi zake za shule.

2

Page 3: Simbegwire anavipenda, na kila mmoja akala hadi akashiba. Baada ya kula watoto wakaenda kucheza huku watu wazima wakiongea. Simbegwire akajisikia furaha na jasiri. Akaamua kuwa si

Siku moja baba yake Simbegwire alirudinyumbani kwa kuchelewa. “Mwanangu ukowapi?” aliita. Simbegwire alimkimbilia baba yake.Alisimama ghafla baada ya kumwona baba yakeakiwa ameshika mkono wa mwanamke. “Natakaukutane na mtu muhimu, mwanangu. Huyu niAnita,” alisema huku akitabasamu.

3

Page 4: Simbegwire anavipenda, na kila mmoja akala hadi akashiba. Baada ya kula watoto wakaenda kucheza huku watu wazima wakiongea. Simbegwire akajisikia furaha na jasiri. Akaamua kuwa si

“Hujambo Simbegwire? Baba yako amenisimuliamengi kukuhusu,” alisema Anita. Lakinihakutabasamu wala kumpa Simbegwire mkono.Baba yake Simbegwire alijaa na furaha.Aliongelea jinsi maisha yatakavyokuwa mazuriwatatu hao wakiishi pamoja. “Mwanangu, nimatumaini yangu kuwa utamkubali Anita kuwamama yako,” alisema.

4

Page 5: Simbegwire anavipenda, na kila mmoja akala hadi akashiba. Baada ya kula watoto wakaenda kucheza huku watu wazima wakiongea. Simbegwire akajisikia furaha na jasiri. Akaamua kuwa si

Maisha ya Simbegwire yakabadilika. Hakuwa namuda tena wa kukaa na baba yake asubuhi. Anitaalimpa kazi nyingi za nyumbani zilizomchoshasana kiasi cha kushindwa kufanya kazi zake zashuleni jioni. Alikuwa anaenda moja kwa mojakulala baada ya chakula cha jioni. Faraja pekeealiyokuwa nayo ni blanketi lenye rangi nyingialilopewa na mama yake. Baba yake Simbegwirehakugundua kwamba binti yake alikuwa hanafuraha.

5

Page 6: Simbegwire anavipenda, na kila mmoja akala hadi akashiba. Baada ya kula watoto wakaenda kucheza huku watu wazima wakiongea. Simbegwire akajisikia furaha na jasiri. Akaamua kuwa si

Baada ya miezi michache, baba yake Simbegwirealiwaambia kwamba ana mpango wa kusafiri.“Itanibidi nisafiri kikazi,” alisema. “Lakini najuahakutakuwa na tatizo.” Uso wa Simbegwireulijawa huzuni, lakini baba yake hakugundua.Anita hakusema lolote. Hakuwa na furaha.

6

Page 7: Simbegwire anavipenda, na kila mmoja akala hadi akashiba. Baada ya kula watoto wakaenda kucheza huku watu wazima wakiongea. Simbegwire akajisikia furaha na jasiri. Akaamua kuwa si

Mambo yakawa mabaya kwa Simbegwire.Aliposhindwa kumaliza kazi au alipolalamika,Anita alimpiga. Wakati wa chakula cha jioni Anitaalikula chakula kingi, na kumwachia Simbegwiremakombo. Kila usiku Simbegwire alikuwa analia,huku akilikumbatia blanketi la mama yake.

7

Page 8: Simbegwire anavipenda, na kila mmoja akala hadi akashiba. Baada ya kula watoto wakaenda kucheza huku watu wazima wakiongea. Simbegwire akajisikia furaha na jasiri. Akaamua kuwa si

Asubuhi moja, Simbegwire alichelewa kuamka.“Wewe mtoto mvivu,” Anita aliita kwa kelele.Akamvuta Simbegwire kutoka kitandani. Blanketilake zuri likanasa kwenye msumari na kuchanikavipande viwili.

8

Page 9: Simbegwire anavipenda, na kila mmoja akala hadi akashiba. Baada ya kula watoto wakaenda kucheza huku watu wazima wakiongea. Simbegwire akajisikia furaha na jasiri. Akaamua kuwa si

Simbegwire alikasirika sana. Akaamua kutorokanyumbani. Akachukua vipande vya blanketi lamama yake. Akachukua na chakula na akaondokanyumbani. Akaifuata barabara aliyopita babayake.

9

Page 10: Simbegwire anavipenda, na kila mmoja akala hadi akashiba. Baada ya kula watoto wakaenda kucheza huku watu wazima wakiongea. Simbegwire akajisikia furaha na jasiri. Akaamua kuwa si

Ilipofika jioni alipanda mti mrefu karibu na kijitona akaandaa kitanda kwenye matawi ya mti.Alipokuwa analala akaimba “Maama, maama,maama, umeniacha. Umeniacha na haukuruditena. Baba hanipendi tena. Mama unarudi lini?Uliniacha.”

10

Page 11: Simbegwire anavipenda, na kila mmoja akala hadi akashiba. Baada ya kula watoto wakaenda kucheza huku watu wazima wakiongea. Simbegwire akajisikia furaha na jasiri. Akaamua kuwa si

Asubuhi iliyofuata, Simbegwire aliimba ule wimbotena. Wakina mama walipokuja kufua nguo zaowalisikia wimbo wa huzuni kutoka kwenye mtimrefu. Wakafikiri ni upepo unatikisa matawi yamti na wakaendelea na kazi zao. Lakini mamammoja akasikiliza ule wimbo kwa makini.

11

Page 12: Simbegwire anavipenda, na kila mmoja akala hadi akashiba. Baada ya kula watoto wakaenda kucheza huku watu wazima wakiongea. Simbegwire akajisikia furaha na jasiri. Akaamua kuwa si

Mama huyo akaangalia juu ya mti. Alipomwonamsichana na vipande vya blanketi la rangi, akalia,“Simbegwire, mtoto wa kaka yangu!” Wakinamama wengine wakaacha kufua na wakamsaidiaSimbegwire kushuka toka juu ya mti. Shangaziyake akamkumbatia na kumfariji.

12

Page 13: Simbegwire anavipenda, na kila mmoja akala hadi akashiba. Baada ya kula watoto wakaenda kucheza huku watu wazima wakiongea. Simbegwire akajisikia furaha na jasiri. Akaamua kuwa si

Shangazi yake Simbegwire akampeleka nyumbanikwake. Akampatia chakula, akampeleka kitandanina akamfunika na blanketi la mama yake. Usikuule Simbegwire akalia alipokwenda kulala. Lakiniyalikuwa machozi ya furaha. Alijua shangazi yakeatamtunza.

13

Page 14: Simbegwire anavipenda, na kila mmoja akala hadi akashiba. Baada ya kula watoto wakaenda kucheza huku watu wazima wakiongea. Simbegwire akajisikia furaha na jasiri. Akaamua kuwa si

Baba yake Simbegwire aliporudi nyumbani,alikikuta chumba chake kikiwa tupu. “Ninikimetokea, Anita?” aliuliza kwa simanzi. Anitaakaelezea kuwa Simbegwire alitoroka. “Nilitakaaniheshimu,” alisema. “Labda nilikuwa mkalisana.” Baba yake Simbegwire aliondokanyumbani na akaelekea kwenye kijito. Akaendakwenye kijiji cha dada yake kuuliza kamaamemwona Simbegwire.

14

Page 15: Simbegwire anavipenda, na kila mmoja akala hadi akashiba. Baada ya kula watoto wakaenda kucheza huku watu wazima wakiongea. Simbegwire akajisikia furaha na jasiri. Akaamua kuwa si

Simbegwire alikuwa anacheza na binamu zakealipomwona baba yake akija kwa mbali. Aliogopakuwa baba yake angekuwa amekasirika, naakakimbilia ndani ya nyumba ili ajifiche. Babayake alimwendea na akamwambia, “Simbegwireumempata mama mzuri. Anayekupenda nakukuelewa. Najivunia kuwa nawe naninakupenda.” Walikubaliana kuwa Simbegwireangeishi na shangazi yake kwa muda woteatakaotaka.

15

Page 16: Simbegwire anavipenda, na kila mmoja akala hadi akashiba. Baada ya kula watoto wakaenda kucheza huku watu wazima wakiongea. Simbegwire akajisikia furaha na jasiri. Akaamua kuwa si

Baba yake alikuwa akimtembelea kila siku.Mwishoe akaja na Anita. Akampa mkonoSimbegwire. “Nisamehe, nilikosea,” akalia.“Utanipa nafasi kujaribu tena?” Simbegwirealimwangalia baba yake aliyekuwa na uso wawasiwasi. Baadaye akamwendea Anita taratibu naakamkumbatia.

16

Page 17: Simbegwire anavipenda, na kila mmoja akala hadi akashiba. Baada ya kula watoto wakaenda kucheza huku watu wazima wakiongea. Simbegwire akajisikia furaha na jasiri. Akaamua kuwa si

Wiki iliyofuata, Anita aliwaalika Simbegwire,binamu zake, na shangazi yake kwa ajili yachakula. Anita akaandaa vyakula vyote ambavyoSimbegwire anavipenda, na kila mmoja akala hadiakashiba. Baada ya kula watoto wakaendakucheza huku watu wazima wakiongea.Simbegwire akajisikia furaha na jasiri. Akaamuakuwa si muda mrefu atarejea nyumbani kuishi nababa yake na mama yake wa kambo.

17

Page 18: Simbegwire anavipenda, na kila mmoja akala hadi akashiba. Baada ya kula watoto wakaenda kucheza huku watu wazima wakiongea. Simbegwire akajisikia furaha na jasiri. Akaamua kuwa si

Barnebøker for NorgeBarnebøker for Norgebarneboker.no

SimbegwireSimbegwireSkrevet av: Rukia Nantale

Illustret av: Benjamin MitchleyOversatt av: Matteo E. Mwita

Denne fortellingen kommer fra African Storybook (africanstorybook.org) og ervidereformidlet av Barnebøker for Norge (barneboker.no), som tilbyr barnebøkerpå mange språk som snakkes i Norge.

Dette verket er lisensiert under en Creative Commons Navngivelse 3.0 Internasjonal Lisens.