Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI...

103
Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

Transcript of Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI...

Page 1: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI

Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

Page 2: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

© HAKI YA UCHAPISHAJI

Uchapishaji wa kitabu hiki ni milki ya kiufundi ya “THE QURAN AND SUNNAH SOCIETY OF EAST AFRICA”. Kila kilichomo ndani, kwa ujumla, ni hifadhi ya qssea. Hairuhusiwi kuiga kwa njia yoyote iwayo kutoka kwa wachapishaji asili; hivyobasi uchapishaji wa kitabu hiki utahitaji ridhaa kutoka kwa muandishi. Iwapo chochote kutoka kwenye kitabu hiki kitatumiwa kama sehemu ya shirika jengine la kiufundi ama isokuwa hivyo, basi ruhusa kutoka QSSEA itahitajika.

Ruhusa inaweza kuombwa kutoka kwa:

The Qur‟an and Sunnah Society of East Africa, P. O. Box 85477, Mombasa, Kenya. Nambari ya Simu ni +254- 721473181 Ama kwa Barua Pepe (e-mail)- [email protected] web-site – www.qssea.net ISBN 978-9966-1824-0-1 Chapa ya Kwanza: Nakala 1000 [2015 / 1436]

JUMUIYA YA QUR’AN NA SUNNAH YA AFRIKA YA MASHARIKI

Page 3: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

I

MEZA YA YALIYOMO MEZA YA YALIYOMO ............................................................ I

UTANGULIZI WA MUANDISHI ................................................ IV

UTANGULIZI WA MFASIRI .................................................... VI

UTANGULIZI WA KITABU ....................................................... I

NASWAHA KWA MWENYE KUTEKELEZA „IBADA YA HAJJ .................. 1

HAPANA MADHARA, HAPANA MADHARA .................................... 9

YANAYOTANGULIZWA KUFANYWA KWA MWENYE KUHIRIMIYA.......... 12

KUHIRIMIA NA NIYA YAKE .................................................... 13

AL-MAWÂQÎT (VITUO MAALUM) ............................................ 14

AL-JUHFAH ...................................................................... 14

QARN AL-MANÂZIL .............................................................. 15

DHÂT „IRQ ....................................................................... 15

AMRI YA MTUME (صىل اهلل عليه وسلم) YA KUTEKELEZA TAMATTU‟ ............. 15

KUWEKA SHURUTI ............................................................ 16

KUSWALI KATIKA SEHEMU YA WÂDÎ AL-„AQÎQ ............................ 17

MTU KUINUA SAUTI YAKE KWA TALBIYAH ................................. 17

KUOGA UNAPOINGIA MAKKAH ............................................... 21

TWAWÂF AL-QUDÛM ......................................................... 24

(MZUNGUKO WA KUWASILI) ................................................. 24

Page 4: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

II

KUISHIKILIA SEHEMU YA BAINA YA AR-RUKN NA MLANGO ............... 27

KUTEMBEA BAINA YA AS-SWAFÂ NA AL-MARWAH ........................ 30

KUVAA IHRÂM YA HAJJ KATIKA SIKU YA TARWIYAH ..................... 36

KUELEKEA „ARAFAH .......................................................... 36

KUSIMAMA „ARAFAH .......................................................... 38

KUONDOKA „ARAFAH KWA HARAKA ........................................ 40

SWALA YA FAJR UKIWA MUZDALIFAH ...................................... 41

KURUSHA VIJIWE ............................................................. 41

KUCHINJA ...................................................................... 44

TWAWÂF AL-IFÂDHA ......................................................... 49

KUKAA MINÂ WAKATI WA USIKU ............................................ 50

TWAWÂF AL-WADÂ‟ .......................................................... 55

(MZUNGUKO WA KUAGA) .................................................... 55

MAMBO YANAYOFANYWA YA UZUSHI KATIKA HAJJ ...................... 58

BID‟AH ZA KABLA YA KUVAA IHRÂM ........................................ 62

BID‟AH ZINAZOHUSIANA NA IHRÂM, TALBIYAH, NA MENGINEYO ....... 65

UZUSHI UNAOFANYWA KATIKA TWAWÂF .................................. 66

UZUSHI UNAOFANYWA KATIKA SA‟Î ........................................ 69

BID‟AH ZINAZOFANYWA „ARAFAH .......................................... 70

BID‟AH ZINAZOFANYWA MUZDALIFAH ..................................... 72

UZUSHI UNAOFANYWA KATIKA KURUSHA VIJIWE ......................... 74

Page 5: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

III

UZUSHI UNAOFANYWA KATIKA KUCHINJA ................................. 75

SAMPULI MBALIMBALI ZA UZUSHI ........................................... 75

BID‟AH ZINAZOFANYWA KATIKA ZIYÂRAH (KUZURU KABURI LA MTUME

MADINAH) ...................................................................... 76

UZUSHI UNAOFANYWA KATIKA BAITUL MAQDIS .......................... 81

KAMUSI ........................................................................... I

Page 6: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

IV

UTANGULIZI WA MUANDISHI

Kila sifa njema ni za Allâh, tunamsifu yeye, na kumtaka msaada wake na msamaha wake. Na tunajilinda kwa Allâh kutokamana na maovu ya vitendo vyetu na nafsi zetu. Na nashuhudia yakwamba hapana mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokua Allâh peke yake pasi na mshirika yoyote na nashuhudia yakwamba Muhammad ni Mtumwa wake na mjumbe.

Amma Ba‟d:

Hamu ya kuirahisisha „ilmu ya (Dini) kwa watu wote imenipelekea mimi kwenye kuzifupisha kwa mukhtasari nukta zilizo muhimu za „Ibâda ya Hajj nilizozitaja kwenye kitabu changu

<<Hajjatun Naby (صىل اهلل عليه وسلم)>> kama ilivyopokewa na Jâbir ( رضي اهلل ,Baadhi ya riwaya muhimu zimeongezewa kwenye kitabu hiki .(عنه

ambazo asilani hazikutajwa kwenye kitabu hicho cha Hajjatun Naby

( ليه وسلمصىل اهلل ع ) au kwenye sherhe yake. Kama jinsi ilivyo hali katika

vitabu vyangu vyote, nimezitaja silsila za wapokezi wa riwaya hizi na kuziamulia daraja zake katika uswahihi na timbufi (asili) zake kwa kumpelekea msomaji kwa mukhtasari kunako vitabu vyangu vyengine vilivyokwisha kuchapishwa au ambavyo bado havijachapishwa, na

kwenye kitabu “Asili” - Hajjatun Naby (صىل اهلل عليه وسلم) – iwapo riwaya

Page 7: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

V

zimeshatajwa humo

Ili msomaji apate faida zilizokamilika kutoka katika kitabu hiki, kumeunganishwa mkia wa faharasa wa mambo ya uzushi yanayofanywa katika Hajj, „Umrah na Ziyârah (kulizuru kaburi la Mtume).

Mazao ya juhudi hizi yakaitwa <<Manâsikul Hajj Wal „Umrah juu ya miangaza ya Kitabu, Sunnah na njia ya Salaf>>.

Namuomba Allâh, mwenye rehma, mwenye huruma ayafanye matendo yangu yote yawe ni mema na kwa ajili yake peke yake pasi na mshirika na yeye katika yanayompasa.

Damascus 21st Sha‟bân, 1395H.

Muhammad Nâsir ud-Dîn al-Albâni

Page 8: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

VI

2

UTANGULIZI WA MFASIRI

Sifa zote njema ni zenye kumstahiki Allâh (هلالج لج), tunamsifu yeye, na kumtaka msaada wake na msamaha wake. Na tunajilinda kwa Allâh kutokamana na maovu ya vitendo vyetu na nafsi zetu. Na nashuhudia yakwamba hapana mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokua Allâh peke yake pasi na mshirika yoyote na nashuhudia yakwamba Muhammad ni Mtumwa wake na mjumbe.

Amma ba‟d:

Baada ya kumshukuru Allâh na kumtakia rehma Mtume wetu

Muhammad (صىل اهلل عليه وسلم), kwanza napenda kumuombea mtunzi wa

Kitabu hiki, Mwanachuoni mkubwa katika zama zetu hizi, Muhaddith,

al-„Allâmah, Sheikh Muhammad Nâsir ud-Dîn al-Albânî (رحمه اهلل) - Allâh

amzidishie malipo mema katika mizani yake hadi siku ya (سبحانه وتعاىل)

Mwisho. Kwa hakika matunda ya juhudi zake yametufaidisha mpaka nasi tukaweza kuwafikishia wenzetu wa lugha nyengine (ya kiswahili).

Dini yetu ya Uislamu inatuhimiza kujitahidi katika kutafuta „ilmu na kuitanguliza „ilmu hiyo katika kutekeleza „ibada. Na miongoni mwa „ibada ni huku kufunga safari na kwenda Makkah kuhiji au kufanya „Umrah. Usafiri huu sio kama usafiri wa aina nyengine yoyote ya ki-Utalii bali ni usafiri wa ki-„Ibada ambao ndani yake kuna mafunzo ya kimsingi. Kuanzia Niya, Mavazi, Talbiyah, na mambo mengine mengi katika yakuwajibika kuyafanya; mambo ambayo

Page 9: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

VII

Mtume Muhammad (صىل اهلل عليه وسلم) akatwambia:

« اشهك ... «.خذوا خني “Chukueni kutoka kwangu „ibâda ya Hijjah ...”

Hii ina maana yakwamba ni lazima tufanye kama jinsi

alivyofanya na kutufundisha Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) ndio „ibada yetu hiyo

ikubaliwe na kupata malipo yanayostahiki. Napenda kuwanaswihi ndugu zangu tufanyeni juhudi kukisoma kitabu hiki na kuwafundisha wengine ili tuwe na matarajio ya kupata malipo ya „ibada hiyo kutoka

kwa Mola wetu (سبحانه وتعاىل) Na hatimae sina budi kuwaombea kheri nyingi kila aliyesimama

pamoja nami katika kuhakikisha kuwa shughuli hii ya kukifasiri kitabu hiki imekamilika mpaka ikawafikia Waislamu wenye kuizungumza lugha ya Kiswahili. Ustadh wangu Abu Bilâl Athman bin Na‟mân, akiwa mbele mbele kabisa kunihimiza niifanye kazi hii ya kheri, namuombea umri mrefu wenye baraka ili azidi kunipa hima. Kwa hakika, kazi yake ya kukipitia kitabu hiki mara kadhaa kabla ya kuchapishwa imenifanya moyo wangu upate utulivu kutokana na tahkiki yake, Allâh amjazi kheri nyingi. Ama kwa majina, ndugu zangu ni wengi ambao walionihimiza kwa kila aina ya njia, nataraji mizani zao za „amali njema zitapata uzani unaostahiki kutoka kwa Mola wetu.

Ama watu wa nyumbani kwangu, nawaombea nao Allâh ( سبحانهىلوتعا ) awazidishie subra zao, na awalipe wema wenye kuzijaza mizani

zao za kheri na wazidi kunipa moyo wa kuyafanya yenye kumridhisha

Allâh ( وتعاىل سبحانه )

وــاعاىــع درــخآو ده ـــال رلل عـــال ب ـــهال ي

Page 10: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

VIII

Muhammad Awadh Salim Basawad

20th April, 2015 / Rajab 1st 1436

Mombasa, Kenya

Page 11: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

I

3

UTANGULIZI WA KITABU

Sifa zote ni za Allâh , namuhimidi na nataka kwake msaada, na nataka kwake msamaha,na tunajikinga kwake na shari za nafsi zetu, na maovu ya matendo yetu. Kwa hakika aliyemuongoza Allâh hakuna awezae kumpotosha, na aliyepotoka hakuna awezae kumuongoza, na nashuhudia kwa moyo na kutamka kwa ulimi wangu yakwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki illa Allâh. Na kwa

uhakika, Muhammad ni mja wa Allâh, na ni Mtume wake, ( صىل اهلل عليه .(وسلم

Enyi waumini mcheni Allâh ki-ukweli kweli, wala musife illa lhali mumekufa waisilamu. Enyi watu! Mcheni Mola wenu ambaye aliwaumba kutokamana na nafsi moja (Adam) na akaumba kutokamana na nafsi hiyo, mkewe (Hawâ); na akaeneza kutokamana na wawili hao, wanaume wengi na wanawake wengi. Na mcheni Allâh ambaye mwamuomba na kutaka kwake haja zenu. Na pia mcheni Allâh kwa kuunga jamaa zenu, kwa hakikka Allâh anawachunga na kuona atakwenda kuwalipa yale mnayoyatenda na kuyasema. Enyi Waumini! Mcheni Allâh na muyaseme yaliyo sawa na ukweli na mazuri, atawatengenezea matendo yenu na kuwasamehe madhambi yenu. Na anayemtwi‟i Allâh na Mtume wake, hakika huyo amefaulu.

Amma baada ya hayo yote:

Page 12: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

II

Kwa hakika maneno ya ukweli zaidi ni maneno ya Allâh, na

muongozo bora ni muongozo wa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), na uovu wa

matendo ni yale yalozushwa kwenye dini,na kwa hakika, kila lenye kuzushwa ni bid‟a, na kila bid‟a ni upotofu, na kila upotofu ni motoni.

Ndugu mu‟min wa kiume na wakike, hakika Allâh ameja‟aliya neema nyingi sana kwetu sisi, na miongoni mwa neema

zake ( وتعاىل سبحانه ) ni kuruzukia kwa kila miaka mia moja wanazuoni

wenye kuhuyisha Sunnah za Mtume wetu Muhammad (صىل اهلل عليه وسلم), na

miongoni mwa ma‟ulamaa hawa, twatarajia awe ni Mwanachuoni

huyu mtukufu, Sheikh Muhammad Nâsirud Dîn al-Albâny (رحمه اهلل),

aliyehuisha Sunnah na kufisha bid‟a nyingi kwa fadhla za Allâh na

uwezo wake ( وتعاىل سبحانه ), ambaye aliona umuhimu wa kuandika kitabu

hiki kwa ajili ya kutufunza sote waumini kuhusu sifa ya kutekeleza „Ibada ya Hajj na „Umrah, amabayo Hajj ni nguzo ya tano kwenye dini yetu ya Uislamu, kwa manhaj (njia) ya Qur‟ân na Sunnah za Mtume

.kwa ufahamu wa wema waliotangulia (صىل اهلل عليه وسلم)

Ndugu Muislamu, fahamu yakwamba „Ibada zako haziwezi kuwa njema ikiwemo „Ibada hii ya Hajj na „Umrah, hadi zikamilishe sharti mbili muhimu: Ikhlâs lillâh (utekeleze kwa kutaka radhi za

Allâh) na kufuata Sunnah za Mtume wako Muhammad (صىل اهلل عليه وسلم),

Allâh asema:

“Hawakuamrishwa illa wamuabudu Allâh kwa ikhlâs, tena

wawe ni wenye kujisalimisha Kwake na tawheed na

Page 13: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

III

wajiepusha na shirki na wasimamishe swala ,watowe zakâh,na hiyo ndiyo dini iliyo-nyooka yenye kuwapeleka

peponi”. [Al-Bayyinah 98:5]

Na Mtume kasema kwenye hadithi iliyopokewa na Imâm

al-Bukhâri kutoka kwa mama wa waumini „Âisha (رضي اهلل عنها):

رد » ذ ا ىيس ذا مرا ضدث ف أ

أ »

“Mwenye kuzua lisilokuwemo katika jambo letu hili (dini yetu), atarudishiwa mwenyewe.”

Kwa dalili hizi na nyenginezo ambazo hatukuzitaja, kukhofia kurefusha, zatuonyesha umuhimu wa ikhlâs na hatari ya riyâ‟, na umuhimu wa Sunnah na hatari za Bid‟ah. Kwa umuhimu huo, ndugu yetu fillah Abu Farida Muhammad Awadh Sâlim Basawad, alionelea umuhimu wa kukifasiri kitabu hiki bila kuongeza chochote kutoka kwake mwenyewe kwa lugha ya Kiswahili. Bali kutafsiri maneno ya mwanachuoni mkubwa, Sheikh Muhammad Nâsirud Dîn al-

Albâny (رحمه اهلل), ili tuweze kuelimika zaidi na kitabu hiki kwa ibada ya

Hajj na „Umrah. Twamuomba Allâh amlipe kila la kheri na amuongeze malipo zaidi siku ya Qiyâmah.

Nausia killa mwenye himma ya kutaka kujua „Ibada hii ya Hajj au „Umrah asome kitabu hiki, na atapata kuelimika zaidi, ili aweze kutekeleza „Ibada yake kwa ujuzi na kama alivyofanya Mtume

.(صىل اهلل عليه وسلم)

Abu Abdulmajid zeinul Abidin Bin Ali

1st May, 2015 م

ه ٢٣٤١/ رجب / ٢١

Page 14: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

1

Naswaha Kwa Mwenye Kutekeleza „Ibada ya Hajj

Vifuatavyo ni vipande vya naswaha nilivyoviweka baina ya

mikono ya ndugu zetu Waislamu wanaotaka kuitekeleza „Ibada ya

Hajj.

Mosi: Ni wajibu kwa mwenye kuitekeleza „Ibada ya Hijjah amche Mola wake, na ajitahidi kadiri ya uwezo wake asitumbukie

kwenye mambo ya haramu. Amesema Allâh ( وتعاىل سبحانه ):

“Hija ni miezi maalumu. Na anayekusudia kufanya Hija katika

(miezi) hiyo, basi asiseme maneno machafu wala asifanye vitendo vichafu wala asibishane katika hiyo Hija.”

[al-Baqarah 2:197]

Vilevile amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

« حفصق رسع يرـد، ول ضز ـي أ ح م ول ني «ذب“Mwenye kuhiji, pasi na kufanya maovu (akiwa

kwenye hajj), na asifanye upuzi, atarudi zake nyumbani akiwa hana madhambi kabisa (yaani; amesamehewa kila

kitu), kama alivyokuwa alipozaliwa na mamake.”

Mwenye kuhiji atakapofanya hivyo, hijja yake itakuwa imekamilika na kukubaliwa.

Page 15: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

2

Amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

ث » بور ىيس ل سزاء إل ال «الز ال“Hajj iliyokamilika na kukubalika haina malipo isipokuwa

Pepo.”1

Kulingana na hali hiyo, hapana budi kuwatahadharisha Waislamu, hususan wale wasioijua dini yao na walio wapotofu, dhidi ya mambo yafuatayo-:

I. Ash-Shirk (yaani; kumuwekea Allâh washirika): Mimi nimewaona watu wengi wanaofanya Hajj wakifanya ushirikina, kama vile kutaka kuokolewa na asiyekuwa Allâh, kutaka msaada kutoka kwa (waliokufa) maiti, ema miongoni mwa waliokuwa watu wema au Mitume wakiwaomba usaidizi wao mbali na Allâh na kuapa kwa majina yao kwa njia ya kuwatukuza na mambo yenye kubatilisha Hijja zao kwa hayo,

kwani Allâh ( وتعاىل سبحانه ) Amesema:

“Kama ukimshirikisha (Allâh) bila shaka amali zako zitaruka

patupu (hutazipatia thawabu japo ni amali njema).” [Az-Zumar 39:65]

II. Baadhi ya wanaotekeleza Hajj hutafuta mbinu za kujirembesha kwa kuzinyoa ndevu zao, ambalo ni jambo la ma‟asiya lililokusanya maovu (madhambi) sampuli nne niliyoyataja kwenye “Asili”.

1 Imepokewa na mashekhe wawili na wengineo kwa kuifuatiliza kutoka kwa

Abû Hurairah (رضي اهلل عنه) – na imepokewa ki-ukamilifu katika « Silsilat Al-

Ahâdîth As-Swahihah » (no. 1200) na katika « Al-Irwâ » (no. 769)

Page 16: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

3

III. Kwa hakika kuvaa pete za dhahabu kwa wanaume ni jambo la haram, hususan kitu kinachojulikana kwa jina la «pete ya uposi»; hilo ni tendo la kuwaiga watu walioteremshiwa vitabu (jambo ambalo lililoharamishwa kabisa katika Uislamu).

Pili: Wanaotaka kutekeleza Hajj wakawa hawakuleta Hady (mnyama aliyeletwa na mwenye kuhiji ili apate kuchinjwa mjini Makkah ifikapo tarehe 10th ya mwezi wa Dhul-Hijjah) pamoja nao1 itawapasa watie niya ya Hajj At-Tamattu‟ (yaani; watekeleze „Umrah kwanza, kisha ifikapo tarehe 8th ya Dhul-Hijjah, mwenye kuhiji hutia

niya ya kutekeleza Hajj). Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliwaamrisha

Maswahaba zake (ambao hawakuwa wamekuja na Hady wao) watekeleze „Umrah kwanza, kisha wavae Ihrâm kwa mara nyengine kwa kutekeleza Hajj, mpaka akakasirika sana na wale ambao waliokaidi kufanya hivyo (walipomuona yeye mwenyewe hakuwa ni mwenye kufanya hivyo, kwani yeye alikuja pamoja na Hady wake).

Akasema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

ث » م اىليا رة ف الزي إل ي «دخيج اىػ“Imeingizwa „Umrah ndani ya Hajj mpaka siku ya Qiyâmah.”

Akauliza swahaba mmoja: Jee, hukmu hii ni kwa mwaka huu

tu au ndio itakuwa milele? Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akafungamanisha

vidole vya mikono yake miwili kisha akasema:

1 Kama jinsi wanavyofanya mahujaji wengi siku hizi; ni nadra sana kumuona

mtu akija pamoja na Hady wake kama alivyofanya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم).

Yoyote mwenye kuja Hajj pamoja na Hady wake, kitendo chake hicho hakiwezi kukataliwa, kinyume cha wale ambao wasoleta Hady pamoja nao ili watekeleze Qirân au Ifrâd; kwa hakika wao wameikhalifu Sunnah ya Mtume

( وسلم عليه اهلل صىل ) hata ingawa watu hawalipendi jambo hilo, kama alivyosema

Ibn „Abbâs. Tukio hilo lilisimuliwa na Muslim (vol.4, no. 58) na Ahmad (vol.1, no.287 na 342).

Page 17: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

4

ةد »ث ل ةو لةد أ م اىليا رة ف الزي إل ي ةد دخيج اىػ

، ل، ةو ل

ةد « أ

“Imeingizwa „Umrah ndani ya Hajj mpaka siku ya Qiyâmah. Qiyâmah. (Jawabu la suala lako ni:) Laa, bali ni daima na

milele, Laa, bali ni daima na milele.”1

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alimuamrisha Fâtimah pamoja na wake

zake wote ( عنهم اهلل رضي ) wavue Ihrâm zao wote baada ya kutekeleza

„Umrah (kisha wazivae tena Ihrâm kwa ajili ya Hajj ifikapo tarehe 8th ya Dhul-Hijjah). Ibn „Abbâs kama ilivyopokewa kutoka kwake akasema:

طاف ةاليج، ذلد ضو » ، وإن ث بييك ش «رؽتخ “Mwenye kuitufu Nyumba, (na kisha akatembea baina ya Swafa

na Marwa) atakuwa ameshajifungua (ameshamaliza Ihrâm yake). Na kwa hakika hii ndiyo Sunnah ya Mtume wenu, ingawa

baadhi yenu munaichukia.”2

Kwahivyo, yoyote ambaye hakuja pamoja na Hady wake na abakie katika hali ya Ihrâm kwa ajili ya kutekeleza „Umrah katika

1 Swahîh Abî Dâwud (no. 1568, 1571) 2 Ibn „Abbâs ameyaegemeza maneno yake juu ya hadîth ya Mtume ( عليه اهلل صىل

:isemayo (وسلم

ي توب» فبال تط فهو جم رة،فإذاقدن ذاعه كم خلفحج د أ قد صفايالإنالل

وة،فقد يوال هر د كننع «حلإلنو

“Kwa hakika Allâh ameingiza ndani ya Hijja yenu hii, Ibada ya „Umrah. Kwahivyo anapoitufu Nyumba mmoja wenu na akatembea

baina ya Swafa na Marwah, atakuwa amemaliza hali yake ya kuwa na Ihrâm, isipokuwa yule aliyeleta pamoja nao Hady.” [Swahîh Abî

Dâwud No. 1573, 1580].

Page 18: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

5

miezi mitatu ya Hajj. Wale ambao watakaokuwa katika hali ya Ihrâm kwa ajili ya Hajj – emma Ifrâd au Qirân – kisha baadae wakajua kuhusu amri ya Mtume ya kutenganisha baina ya Ihrâm ya „Umrah na Ihrâm ya Hajj, watapaswa kufanya hivyo hata kama watakuwa wameshawasili Mjini Makkah na kulitufu al-Ka‟bah, na kutembea baina ya Swafa na Marwah. Kisha baadae, na wavae tena Ihrâm ifikapo siku ya tarehe 8th ya Dhul-Hijjah kwa ajili ya Hajj. Amesema

Allâh ( وتعاىل سبحانه ):

“Enyi mlioamini! Muitikieni Allâh (kwa kumtwi‟i) na Mtume wake anapokuiteni katika yale yatakayokupeni uhai mzuri.”

[al-Anfâl 8:24]1

Tatu: Tahadhari na kuwacha kulala Minâ, usiku wa kuamkia

„Arafah. Hiki ni kitendo cha wâjib alichofanya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) na

kuwaamrisha Waislamu wafanye hivyo pindi aliposema:

« اشهك ... «.خذوا خني “Chukueni kutoka kwangu „ibâda ya Hijjah ...”

Vilevile inawapasa kukaa Muzdalifah usiku kucha mpaka mumalize kuswali swala ya fajr. Na iwapo utakosa kukaa usiku huo mahali hapo, jaribu usikose kuswali swala ya fajr kwani jambo la

1 Hukmu inayohusiana na Hajj at-Tamattu‟ haikhalifiani na riwaya ya „Umar na wengineo yenye kusema yakwamba Hajj al-Ifrâd ndiyo sampuli bora ya Hajj kama nilivyoyaeleza katika “Asili”. Kisha nikasoma katika maneno ya tafsiri ya Ibn Taymiyyah kuyahusu matamshi ya „Umar: „Kuitekeleza „Umrah peke yake au Hajj peke yake katika safari ya mtu.‟ Regelea katika Mjalada wa «Fatâwa» (vol. 26), kwani ni muhimu.

Page 19: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

6

kuswali swala ya fajr limekokotezwa mno na – kulingana na ma-„Ulamâ‟ – ni mojawapo ya nguzo za Hajj. Nguzo hiyo ya kukaa usiku kucha mahali hapo ni wâjib isipokuwa kwa wanawake na watu madhaifu; wao wanaruhusiwa kuondoka Muzdalifah baada ya saa sita za usiku.

Nne: Usipite mbele ya mtu anayeswali katika al-Masjidul Harâm (Mskiti Mtukufu wa Makkah) au misikiti mengine; amesema

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

ربػي، خيا »ن يلؿ أ

ىكن أ اذا غيي صلي ار بي يدي ال ال حػي ل

ر بي ن ح أ ل «يدي

“Lau anajua mwenye kupita mbele ya mwenye kuswali ukubwa wa madhambi yake, basi ingelikuwa ni bora kwake yeye

kusubiri kwa 40 (masiku, miezi au miaka) kuliko (huko) kupita mbele yake.”

Maana ya hadîth hii ni mapana sana; inamuhusu kila mwenye kuswali na wenye kupita mbele yao. Ama kuhusu hadîth zenye kuutenga Masjidul Harâm na hukmu hii, hazikuswihi.

Na inampasa kila mtu ashikamane na kuwa na Sutrah (kitu chenye urefu usiopungua kipimo cha futi moja, na kiwekwe mbele ya mwenye kuswali), kama atakuwa anaswali katika al-Masjidul Harâm au msikiti wowote mwengine, kama zilivyosema ahâdîth na riwaya chungu nzima kutoka kwa maswahaba; zote hizo zimetajwa kwenye “Asili”.

Tano: Ni juu ya wanavyuoni na wenye fadhla za „ilmu kuwafundisha Mahujjaji – kila mahali wanapowaona – „ibâda ya Hajj na hukmu zake kulingana na yanayoafikiana na Kitâb (Qur‟ân Takatifu) na Sunnah.

Lakini hatahivyo, uwajibikaji huo na usiwazuiye wao

Page 20: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

7

kutekeleza ulinganizi wa upwekeshaji waTawhîd ya Allâh, kwani huo ndio msingi wa Uislamu ambao waliotumilizwa nao Mitume na vitabu kuteremshwa. Wengi katika watu tuliowahi kuonana nao – baadhi yao wakiwa ni wanafunzi wa „ilmu – hawajui ipasavyo ufahamu wa upwekeshaji wa Allâh na upwekeshaji wa sifa zake. Kama ambavyo walivyo kwenye mughafala mkubwa juu ya kuwarudi katika Uislamu pamoja na kukhitilafiana na madh-hab zao – ili waweze kuwaunganisha neno lao na kuziweka pamoja swafu zao kwa msingi wa Kitâb na Sunnah katika „Aqîda na yanayofungamana na hukmu za kisheriya na za mafungamano baina ya wao kwa wao (mu‟âmalât) na upande wa tabia, tabiya zao, siyasa, uchumi na mengineyo katika nyanja zote za kimaisha... na kadhaalika.

Waislamu wanapaswa kukumbuka yakwamba ulinganizi wowote katika kutaka kuleta islahi ambao usiokuwa umeegemezwa juu ya njia hii iliyo nyo-oka (Kitâb Kitakatifu na Sunnah), basi hautowafaidisha Waislamu kwa chochote, bali itaongeza katika ikhtilafu zao, na kuwatia katika hizaya na udhalilifu miongoni mwao; yanayoshuhudiwa viwanjani ni ushahidi mkavu wa hayo. Wallâhul Musta‟ân.

Wakati wa Hajj hapana ubaya kuwepo na mijadala itakayofanyika kwa njia nzuri inapotokea dharura ya kuwepo. Lakini, hatahivyo, mijadala iliyokatazwa ni ile iliyo juu ya mifumo ya bâtil, ambayo haikuharamishwa wakati wa Hajj peke yake bali wakati wowote.

Mjadala huu, ambao ulioegemezwa juu ya bâtil si kama ule ambao aliouruhusu Allâh katika Qur‟ân Takatifu aliposema:

“Waite (waite watu) katika njia ya Mola wako kwa hikima na

mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora

Page 21: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

8

(siyo kwa kuwatukana wao au kutukana dini yao. Kwa njia hii huwezi kumvuta mtu).” [an-Nahl 16:125]

Lau pengine mlinganizi katika njia ya Allâh atahisi yakwamba majadiliano na mpinzani wake hayaleti natija yoyote na huyo mpinzani akiwa amepindana na kushikilia rai yake, maoni au madh-hab, na pengine huyu mlinganizi katika njia ya Allâh, Mtukufu, atahisi yakwamba mjadala wenyewe utapelekea kunako maovu, basi ni bora

kwa mlinganizi asitishe mjadala, kwani amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

« ث ل ةبيج ف ربض ال ا زخيا أ راء وإن كن مل الديد «... حرك ال

“Namuhakikishia nyumba mahali palipo bora zaidi Peponi, yule mwenye kujiepusha na ugomvi na wengine hata kama yeye yuko

katika usawa …” [Hadîth]1

1 Hii ni hadîth iliyo Hasan (nzuri), imesimuliwa kikamilifu katika «Swahîhul Jâmi‟ as-Swaghîr» (vol. 2, no. 1477), Chapa ya Al-Maktab Al-Islâmî.

Page 22: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

9

Hapana Madhara, Hapana Madhara

Mlinganizi katika njia ya Allâh anapaswa kuwa na upole na watu wote kwa ujumla na hususan mahujaji. Upole ni sifa mojawapo miongoni mwa ukarimu wa misingi ya Sheriya zetu maadamu upole

wao haukhalifu hukmu za Qur‟ân Takatifu au Sunnah za Mtume ( صىل اهلل Huu ndiwo msimamo wa kati na kati wenye uadilifu ambao .(عليه وسلم

mlinganizi katika njia ya Allâh anaopaswa kushikamana nao pasi na kujali watakayoyasema watu.

Baadi ya mambo ambayo asili yake yaruhusiwa kufanywa, na mahujaji husita kuyafanya kwa kutegemea fatwâ ambazo walizopewa na baadhi ya walinganizi katika njia ya Allâh. Kutokana na janga hilo, ningelipenda kuwatanabahisha wasomaji mambo yafuatayo:

1. Kuoga – kusiwe ni kutokana na ndoto za kujamiiyana peke yake, bali wakati wowote mtu apendapo kuoga – na kuzisugua nywele. Imepokewa katika swahihain na

kwengineko yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alifanya hivyo.

Hadîth hiyo ilipokewa na Abû Ayyûb ( اهلل عنهرضي ).1

2. Kujikuna kichwa hata kama baadhi ya nywele zitakuwa zikidondoka. Na haya pia yametajwa katika hadîth ya Abû Ayyûb. Vilevile huu ndio msimamo wa Sheikhul Islâm Ibn

Taymiyyah ( اهلل رحمه ).

1 Imepokewa kwa ukamilifu katika “Asili” (Uk. 28), na silsila yake ya upokezi imebainishwa katika al-Irwâ‟ Al-Ghalîl (no. 1019) na Swahîh Abî Dâwud (no. 1613). Ibn „Abbâs alimtuma Abdullâh bin Hanîn kwa Abû Ayyûb kuulizia

kuhusu jinsi Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alivyokuwa akiosha kichwa chake akiwa

katika hali ya Ihrâm. Wakati huo Abû Ayyûb alikuwa akioga. Aliishukisha chini nguo yake aliyokuwa amejihifadhi nayo mpaka ikafikia mahali ambapo nikakiona kichwa chake. Kisha akamuamrisha mtu aliyekuwa kando yake ammwagie maji, naye (huyo mtu) akafanya hivyo. Kisha akakisuguwa kichwa chake (kuelekea mbele na kurudisha nyuma) kwa mikono yake, kisha

akasema: “Hivi ndivyo Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alivyokuwa akiosha kichwa chake.

Page 23: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

10

3. Kuumika, hata ikibidi kunyoa nywele katika sehemu ya

kichwa. Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliumikwa katika kichwa chake

akiwa kwenye hali ya Ihrâm, na jambo hili halina budi kuhitaji kunyolewa nywele. Vilevile hii ni rai ya Ibn Taymiyyah na watu wa madh-hab ya Hanbalî lakini wakaeleza (ma-Hanbalî) yakwamba Muhrim (aliye katika hali ya Ihrâm) atapaswa kulipa fidyah (malipo ya kuwacha au kutekeleza kwa njia ya makosa jambo lolote la ki-dini, sana inakuwa kwa mfumo wa pesa, chakula au kuchinja mnyama); Lakini hatahivyo, rai zao hazina msingi wowote

kwani hazikutegemezwa juu ya dalili nzito. Mtume ( صىل اهلل عليه hakuchinja (hakutoa swadaka) baada ya kuumika (وسلم

kichwa chake.

4. Kunusa harufu nzuri na kuing‟oa kucha iliyokatika. Riwaya nyingi kuhusiana na haya zimetajwa katika “Asili”.

5. Kutafuta kivuli cha hema, kitambara, muavuli, gari au kitu

chochote mfano wake. Ilipokewa yakwamba Mtume ( صىل اهلل alifanya hivyo. Kuwabandikiza fidiya wenye (عليه وسلم

kutafuta kivuli cha vitu tulivyovitaja kwa ujumla halina dalili yoyote. Unaweza kurejea kwenye rai ya Imâm Ahmad katika «Manârus-Sabîl» (vol 1, Uk. 236). Wale wenye kung‟oa mapaa ya magari yao pindi wanapokuwa katika hali ya Ihrâm wanazingatiwa kuwa ni watu wenye kuvuka mipaka na kuvuka mipaka kumekatazwa kwenye dini yetu.

6. Kujifunga (kujizungushia) ukanda katika Izâr zao (kipande cha nguo ya chini) na kuvaa pete, kama ilivyotajwa kwenye baadhi ya athari za maswahaba. Hukmu hii pia inahusu kuvaa saa, miwani za macho na kuvaa mikoba kwenye shingo. Mambo yote haya yanaruhusiwa kulingana na hadîth

za Mtume (صىل اهلل عليه وسلم). Amesema Allâh ( وتعاىل سبحانه ):

Page 24: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

11

“Allâh anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo

mazito.” [al-Baqarah 2:185]

Kila sifa njema zinamstahiki Allâh, Mola wa walimwengu wote.

* * * *

Page 25: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

12

Yanayotangulizwa kufanywa kwa mwenye kuhirimiya

1. Imependekezwa kwa mwenye kukusudia kutekeleza Hajj au „Umrah peke yake, aoge kabla ya kuingia kwenye hali ya Ihrâm. Hukmu hii vilevile inawauhusu wanawake walio kwenye hali za ada zao za mwezi au hali ya baada ya kujifungua.

2. Wanaume wanaruhusiwa kuvaa nguo watakazo maadamu si za kuwabana na kuonyesha umbile la viungo vyao; ma-fuqahâ‟ (wanavyuoni wa fiqh) wanaziita nguo hizo “zisizoshonwa”. Wanaume wanaweza kuvaa Izâr (kipande cha nguo ya chini), ridâ‟ (kipande cha nguo ya juu) na mfano wake. Wanaweza kuvaa Na‟l ambayo ni sampuli yoyote ya champali zisizofika kwenye visigino.

3. Wanaume hawafai kuvaa kofia, kilemba, au chochote mfano wake chenye kukinga kichwa au kukigusa pasi na kizuizi. Hili ni kwa wanaume peke yao. Ama kwa wanawake, na wajiendeleze kuhifadhi nguo zao zenye kuruhusiwa kisheriya, lakini wasivae “Niqâb”1, Burqû‟, Lithâm au Mandîl juu ya nyuso zao. Vilevile

hawafai kuvaa “glovu”.2 Amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):”Muhrim

(mtu aliye katika hali ya Ihrâm) hafai kuvaa shati, kilemba, Burnus (Joho), surwale, vitambara vilivyotiwa rangi ya za‟farani, Wars au viatu isipokuwa iwapo hatoweza kupata Na‟l3.” Mtume

1 Niqâb ni kitambara chenye kusitiri sehemu za pua na uso mzima. Itakapomkurubia mwanamke niqâb yake karibu na macho yake, hapo itakuwa inaitwa “Waswasah” au “Burqu”. Inaposhukishwa chini zaidi na kusitiri ncha ya pua inaitwa “Lithâm”. Asili ya hii stara ya uso inaitwa Niqâb kwa sababu inasitiri au kufinika rangi ya uso. [Lisân al-Arab (Vol. 2. Uk. 265-266)] 2 Amesema Sheikhul Islâm Ibn Taymiyyah katika al-Mansak yake Uk. 365]: “Glovu ni stara ya mikono, kama zile wanazovaa mikononi wenye kufuga kipanga. 3 Amesema Sheikhul Islâm Ibn Taymiyyah [katika al-Mansak]: “Hujâj yoyote asiyekuwa na kitu isipokuwa viatu, hatowajibika kuvikata chini ya visigino

kwani Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliwaamrisha mahujaji wafanye hivyo mwanzo,

kisha akawaruhusu baadae katika „Arafah, wale ambao hawakuwa na hata Na‟l wavae viatu, na watakaokosa Izâr wavae surwale, na huu ndio msimamo wenye nguvu miongoni mwa rai za wanavyuoni”.

Page 26: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

13

akasema:”Mwanamke anapokuwa katika hali ya (صىل اهلل عليه وسلم)

Ihrâm hafai kuvaa Niqâb wala glovu1.” Lakini hatahivyo, mwanamke anaweza kujiziba uso wake na kipande cha kitambara akiteremshe kwenye uso wake na wala asikibane kwenye uso

wake, kama alivyosema Ibn Taymiyyah ( اهلل رحمه ).

4. Mwenye kunuiya (mke au mume) kutekeleza Hajj au „Umrah anaweza kuvaa nguo yake ya Ihrâm kabla ya kufika kwenye Mîqât (kituo maalum), anaweza hata kuvaa akiwa nyumbani kwake kama alivyofanya Mtume na Maswahaba zake. Wenye kutaka kusafiri kwa ndege hadi Makkah, wakawa hawawezi kuvaa nguo zao za Ihrâm pindi ndege ifikapo katika Mîqât kwa haraka, wanaweza kuzivaa kabla ya kuingia ndani ya ndege lakini hawaruhusiwi kuitamka Talbiyah, lakini watakapofika katika Mîqât au muda mchache tu watakapokurubia hapo ili wasije wakavuka sehemu hizo pasi na kutamka Talbiyah.

5. Muhrim anaruhusiwa kujitia mafuta mazuri au manukato yoyote yenye kunukia vizuri na yasiwe na rangi kinyume cha manukato ya wanawake; hayatakiwi kuwa na harufu lakini yawe na rangi. Yanatakiwa yote hayo kufanywa kabla ya kutamka Talbiyah. Kujitia manukato baada ya kutamka Talbiyah hairuhusiwi.

Kuhirimia na Niya yake

6. Pindi mtu aliyekusudia kuhiji au kufanya „Umrah anapofika Mîqât anatakiwa avae Ihrâm (avae nguo ziitwazo Ihrâm – na iwapo atakuwa hajatangulia kuvaa – na akatamka Talbiyah), Niya ya mwenye kutaka kuhiji au kufanya „Umrah hazitoshi, kwani kusudio lake limekuwa moyoni mwake tangu alipotoka nyumbani kwake, Talbiyah inatakiwa itamkwe ili niya ipate kuthibitika.

7. Hapana kitu chochote (katika utajo) kinachotangulia talbiyah kama vile, “Ewe Mola! Mimi nakusudia kufanya Hajj au „Umrah, basi nifanyie wepesi na unitakabalie ...”. Utajo wa sampuli hiyo si

1 Hadîth iliyoafikiwa iliyotajwa katika Swahîh Abû Dâwud.(no. 1600)

Page 27: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

14

katika maneno ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم). Hili pia linahusiana na

kuitamka niya pindi mtu anapokusudia kutawadha, kuswali au kufunga. Utajo wote wa sampuli hiyo ni uzushi ambao kwa uzushi

huo Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) amesema:

«طلىث ف انلار وك ـإن ك مدذث ةدغث وك ةدغث طلىث ... »“… Kwani kila kilichozuliwa ni bid‟ah na kila bid‟ah ni upotofu

na kila upotofu ni wamotoni.”

Al-Mawâqît (Mipaka Maalum)

8. Kuna Mawâqît tano (mipaka mitano maalum): Dhul Hulaifah, Al-Juhfah, Qarn Al-Manâzil, Yalamlam na Dhât „Irq. Hiyo ni mipaka ya watu wanaoishi karibu na sehemu hizo na wenye kuzipitia sehemu hizo wakiwa wamekusudia kutekeleza Hajj na „Umrah. Yoyote mwenye kuishi katika mahali mwa upande huo, yaani; karibu zaidi ya Makkah, anaweza kuvaa Ihrâm kutokea nyumbani kwake na watu wa Makkah huvaa Ihrâm zao Makkah.

Dhul Hulaifah ni mpaka wa watu wanaoishi Madinah, ni mji ulioko kiyasi cha Maili 6-7 kutoka Madinah, na ni mpaka wa mbali zaidi kutoka Makkah kwa kiyasi cha takriban Marâhil 10 baina yake. Mtu anaweza kufikia Mîqât hii kwa kupitia njia nyingi ambazo alizozizungumzia Sheikhul Islâm Ibn Taymiyyah katika «Fatâwa» zake. Kijiji hiki vilevile kinaitwa «Wadî Al-„Aqiq» na msikiti uliojengwa ndani yake unaitwa «Masjid ush-Shajarah». Na kwenye kijiji hicho kuna kisima ambacho watu wajinga wanakiita “Bi‟r

Ali” (Kisima cha „Ali) wakiamini yakwamba „Ali (رضي اهلل عنه) alimpiga

Jini mahali hapo, lakini hili si jambo la kweli.

Ama kuhusu Al-Juhfah: Ni mji ulioko Marâhil tatu kutoka Makkah. Ni mpaka wa watu wa Ash-Shâm (Jordan, Palestine, Syria na Lebanon) na Egypt. Watu wa Madinah pia wanaweza kuitumia njia hiyo iwapo watakwenda Makkah kwa kutumia njia nyengine.

Page 28: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

15

Amesema Ibn Taymiyyah: “Hapo (yaani; Al-Juhfah) ni mpaka wa wenye kukusudia kutekeleza Hajj wanapokuja kutoka upande wa Ash-Shâm na Egypt na miji mengine ya Magharibi. Siku hizi mpaka huu umefungwa na watu wanavaa Ihrâm zao kutoka katika mpaka mwingine ulioko kabla ya Al-Juhfah, unaitwa “Râbigh”.

Qarn Al-Manâzil au Qarn Ath-Tha‟âlib ni safari ya mchana mmoja na usiku mmoja kutoka Makkah. Ni mpaka wa watu wa Najd. Yalamlam ni safari ya nyusiku mbili kutoka Makkah – nayo ni Maili 30. Ni mpaka wa watu wa Yemen.

Na hatimaye, Dhât ‘Irq: Ni mahali kwenye mpaka wenye kuitenganisha Najd kutoka Tihâma. Ni maili 42 kutoka Makkah na ni mpaka wa watu wa „Irâq.

Amri Ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) Ya Kutekeleza Tamattu’

9. Mtu anapokusudia kuvaa Ihrâm (kwa ajili ya Hajj) ya mfumo wa Qirân na akaja pamoja na Hady wake, na aseme: «Labbaikah Allâhummah Bihajjatin Wa „Umrah» (Yâ Allâh, hapa nipo naitikia mwito wako wa Hajj na „Umrah). Iwapo mtu huyo hakuja na Hady wake – ambalo ni jambo bora, atawajibika kusema: « Labbaika Allâhummah Bi„Umrah » (Yâ Allâh, hapa nipo naitikia mwito wako wa „Umrah). Lau kama angelikusudia kufanya Hajj peke yake, atafuta niya hiyo na akusudie kufanya „Umrah badala yake, kwani

Mtume ( مصىل اهلل عليه وسل ) amesema:

ث » م اىليا رة ف الزي إل ي «دخيج اىػ

“Imeingizwa „Umrah ndani ya Hajj mpaka siku ya Qiyâmah.”

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akafungamanisha vidole vya mikono yake

miwili kisha akasema:

ضزي » د رة ف ضشثيا آل م و ةػ يي ـ ك »

Page 29: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

16

“Enyi Nyumba ya Muhammad, yoyote miongoni mwenu aliyekusudia kutekeleza Hajj na aanze na „Umrah kisha

afuatilize na Hajj1.”

Na hiyo ndiyo Hajj at-Tamattu‟.

Kuweka Shuruti

10. Mtu anapopendelea kuunganisha pamoja sharuti kwa Allâh na Talbiyah yake – ikiwa atakhofiya yakwamba yasije maradhi au khofu zikamuathiri wakati wa safari yake – anaweza kufanya

hivyo. Atasema maneno aliyotufundisha Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

« «ملي ضيد ضبصتن الي“Ewe Mola, kituo changu cha mwisho (yaani; hatima ya Ihrâm yangu) kitakuwa pale mahali upendapo kunifunga na mateso

yoyote.”2

Iwapo mtu ataunganisha sharuti hili kwa Allâh na Talbiyah yake kisha akafungika au akapatikana na maradhi au mfano wake, anaweza kumalizia Ihrâm yake ya Hajj au „Umrah na wala hatolazimika kulipa fidiya yoyote au kuirudia Hajj yake katika mwaka ufuatao, isipokuwa ikiwa Hajj yake ni ambayo iliyokuwa ya Wâjib (ya mara ya kwanza), hapo ni lazima airudie tena katika mwaka ufuatao.

11. Hakuna swala maalum inayoswaliwa pindi mtu anapovaa Ihrâm. Lakini itakapompata yeye swala kabla ya kuhirimia, akaswali kisha

akahirimia baada ya swala atakuwa amemuiga Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

wakati alipohirimia baada ya swala ya adhuhuri. Yaani; inapotokea yakwamba wakati fulani wa swala umefika, basi mtu na aitekeleze swala hiyo na kisha avae Ihrâm yake. Hii ndiyo njia

1 Tizama takhrîj yake katika “Al-Ahâdîth As-Swahîha” (no. 2469) 2 Hadîth iliyoafikiwa, Swahîh Abû Dâwud (no. 1557)

Page 30: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

17

aliyokuwa akifanya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم). Alikuwa akiswali swala ya

Dhuhr kisha ndio akivaa Ihrâm.

Kuswali Katika Sehemu Ya Wâdî Al-‘Aqîq

12. Yoyote mwenye kuvaa Ihrâm kutoka Dhul Hulaifah imependekezwa kwake aswali hapo, isiwe kwa ajili ya Ihrâm bali ni kwa sababu hapo ni mahali palipobarikiwa. Amepokea Al-

Bukhârî yakwamba „Umar (رضي اهلل عنه) amesema: “Nilimsikiya Mtume

-akisema akiwa katika sehemu ya Wâdî Al (صىل اهلل عليه وسلم)

„Aqîq:“Amenijilia mjumbe katika usiku huu wa leo kutoka kwa Mola wangu na akaniambia niswali katika jangwa hili lililobarikiwa, na useme, „Umrah ndani ya Hajj‟ kisha nivae Ihrâm

ya Hajj na „Umrah pamoja.”. Amesimulia Ibn „Umar (رضي اهلل عنه) yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliambiwa kwenye usingizi pindi

alipokuwa amejipumzisha usiku wa mwisho kwenye jangwa la Dhul Hulaifah: “Kwa hakika wewe uko katika Jangwa lililobarikiwa.”1

Mtu Kuinua Sauti Yake Kwa Talbiyah

13. Kisha Muislamu na aelekee Qiblah akiwa amesimama2 na aseme Talbiyah ya Hajj au „Umrah au zote mbili:

ػث » ا ول ش ث ل رياء ذي ذه ضش «الي

“Ewe Mola, Hajj hii imefanywa kwa dhati ya ajili yako, si kwa kujionyesha wala kutafuta sifa.”3

1 Swahîh Abû Dâwud (no. 1579), Swahîh al-Bukhârî mukhtasar (no. 761, 762), imechapishwa. Amesema al-Hâfidh katika al-Fat-h (vol. 3; Uk. 311): “Hadîth hii inaonyesha fadhla za jangwa la Al-„Aqîq na kuswali mahali hapo ni kama mfano wa fadhla za kuswali Madînah”. 2 Al-Bukhârî ameipokea kwa njia ya mu‟allaq na al-Baihaqî kwa riwaya swahîh. 3 Imepokewa na adh-Dhiyâ‟ kwa isnadi swahîh.

Page 31: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

18

14. Talbiyah ya Muislamu inatakikaniwa kuwa kama ile ya Mtume ( صىل .bila ya kuzidisha kitu (اهلل عليه وسلم

a)

ث لم » د وانليػ يم لم ليم إن ال ليم ليم ل ش ليم الييم لم يم ل ش «وال

“Tunaitikia, Ewe Mola wetu, tunaitikia, tunaitikia huna mshirika tunaitikia, hakika himdi zote na ne‟ma zote ni zako

wewe na ufalme, huna mshirika.”

b) Na ilikuwa ni miongoni mwa Talbiyah yake Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

alokuwa akiileta:

« ليم إل القي »“Mimi ni mtwi‟ifu kwako, Ewe Mola wa haki.”

15. Kujilazimisha na talbiyah ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) ni bora ingawa

kuongezea maneno mengine katika utajo uliotangulia

kunaruhusiwa kwani Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliwasikia baadhi ya

watu wakiongezea maneno mengine wakisema:

ػارج » اطو ليم ذا ال «ليم ذا اىف

“Tunaitikia Ewe Mola wa Ma‟ârij (Daraja za juu zaidi), Mola wa fadhla zote.”

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alizijuzisha lafdhi hizi. Ibn „Umar ( رضي اهلل

Page 32: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

19

:alikuwa akizidisha, akisema (عنه

و » دتاء إيلم واىػ « ليم وشػديم، واخلي ةيديم، والر“Nakuitikia, mimi ni mtwi‟ifu kwa amri zako, kheri zote ziko

kwenye mikono yako. Niya na „amali zote hutekelezwa kwa ajili yako.”1

16. Muislamu ameamrishwa apaaze sauti yake kwa Talbiyah.

Amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم): Jibrîl alikuja kunitembelea na

akaniamrisha niwaamrishe Maswahaba zangu na wale waliokuwa na mimi (katika safari yangu ya kuelekea Makkah)

tupaaze sauti zetu kwa Talbiyah2.” Akasema Mtume ( صىل اهلل عليه Hajj iliyo bora zaid ni (ile iliyofanywa kwa) kupaazwa“ :(وسلم

sauti (kwa Talbiyah) na ath-Thajju (yaani; kumwaga damu ya Hady na udh-hiya)3.” Amesema Abû Hâzim: “Walikuwa

Maswahaba wa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) wanapohirimia hawafiki

Rawhâ isipokuwa sauti zao huwa zimewakauka kwa kuzipaaza

kwa Talbiyah4.” Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) amesema: “Nilimuona Musa

akishuka ath-Thaniyyah (katika sehemu ya Makkah) (عليه السالم)

akipaaza sauti yake kwa Talbiyah”5.

17. Mtu kupaaza sauti yake anaposoma Talbiyah ni hukmu inayowahusu wote wawili, mume na mke, isipokuwa iwapo italeta fitnah (kitendo chochote kitakachofanywa na mwanamke

1 Hadîth iliyoafikiwa, Swahîh Abû Dâwud (no. 1590) 2 Imepokewa na wapokezi wa Sunan na wengineo. Swahîh Abû Dâwud (no. 1592). 3 Hadîth hasan katika Swahîh al-Jâmi‟ as-Swaghîr (no. 1112) 4 Imepokewa na Sa‟îd bin Mansûr kama ilivyotajwa katika “al-Muhalla” (vol. 7/ no. 94) kwa sanad nzuri ya wapokezi. Vilevile imepokewa na Ibn Abî Shaybah kwa sanad swahîh kutoka kwa Al-Muttwalib bin Abdullâh kama ilivyo katika al-Fat-h (vol. 3/ Uk. 324), nayo ni mursal. 5 Imepokewa na Muslim, “As-Silsilah as-Swahîhah (no. 2023).

Page 33: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

20

chenye kusisimua hisiya za mwanamume kwake). „Âisha ( رضي اهلل alikuwa akipaaza sauti yake kwa Talbiyah ambayo wanaume (عنها

walikuwa wakimsikiya. Amesema Abû „Atiyyah: “Nilimsikiya

„Âisha (رضي اهلل عنها) akisema: “Kwa hakika, mimi najua jinsi Mtume

alivyokuwa akiisoma talbiyah”, kisha akaisema (صىل اهلل عليه وسلم)

talbiyah kama ifuatavyo: “Labbayka llâhumma labbayk ...” (Ewe Mola, nakuitikia, mimi ni mtwi‟ifu kwa amri zako ...)1. Amesema al-Qâsim bin Muhammad: “Katika usiku wa kuondoka kutoka „Arafah (na kuelekea Muzdalifah), Mu‟âwiyah akamsikiya mtu akisoma Talbiyah. Akamuulizia mwenye kusoma (hiyo talbiyah).

Akaambiwa kuwa alikuwa ni mamayao waumini, „Âisha ( رضي اهلل ”.amevaa Ihrâm kwa ajili ya „Umrah kutoka At-Tan‟îm (عنها

„Âisha (رضي اهلل عنها) akasema: “Lau kama angeliniuliza mimi moja

kwa moja, ningelimueleza.”2

18. Muislamu akariri kuisoma Talbiyah kwani ni mojawapo miongoni

mwa “Nguzo za Hajj”3. Amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):”Hapana

yoyote mwenye kusoma Talbiyah isipokuwa kila kilichoko kuliani kwake na kushotoni kwake katika mawe na miti mpaka mwishoni mwa upeo wa pande zote zitasoma talbiyah pamoja naye.”4 Anahimizwa kila mmoja kuisoma talbiyah kila

1 Imepokewa na Al-Bukhârî (no. 769) [chapa ya mukhtasari], at-Twayâlisi (no. 1513) na Ahmad (vol. 6; No. 32, 100, 180, 243). 2 Imepokea na Ibn Abî Shaybah kama ilivyotajwa katika “Al-Muhallâ” (vol. 7 no. 94) na ina silsila nzuri ya wapokezi, amesema Sheikhul Islâm Ibn Taymiyyah: “Mwanamke na aipaaze sauti yake (anaposoma Talbiyah) mpaka wenzake wamsikiye, vilevile imependekezwa kukariri kuisoma kila mtu aondokapo mahali pamoja hadi pengine.” 3 Ibara hii ni kipande cha hadith kilichotajwa kwenye “As-Swahîhah (no. 828)” kama ifuatavyo, “Jibrîl aliniamrisha nipaaze sauti yangu ninaposoma Talbiyah kwani ni miongoni mwa nguzo za Hajj.” 4 Imepokewa na Ibn Khuzaymah na al-Baihaqî kwa silsila nzuri ya wapokezi kama ilivyotajwa katika “Takhrîj at-Targhîb wat-Tarhîb” (vol. 2; No. 118)

Page 34: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

21

anapopanda kilima chochote au anaposhuka kwenye bonde

lolote. Amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم): “Nilimuona Musa (عليه السالم) akishuka ath-Thaniyyah (katika sehemu ya Makkah) akipaaza sauti yake kwa Talbiyah”. Katika riwaya nyengine: “Nilimuona akipaaza sauti yake kwa Talbiyah alipokuwa akishuka ath-Thaniyyah.”1

19. Muislamu anaweza kusoma Tahlîl (kusema; Lâ ilâha illallâh; yaani Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allâh)

na Talbiyah. Amesema Ibn Mas‟ûd (رضي اهلل عنه): “Nilikuwa pamoja

na Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) katika Hijjah; hakuwacha kusoma

Talbiyah mpaka aliporusha vijiwe kwenye Jamrah; aliichanganya pamoja na Tahlîl.”2

20. Pindi Muhrim (mwenye kuvaa Ihrâm kwa Hajj au „Umrah) anapofika kwenye mipaka ya kuingia Makkah, akawa anaanza kuona nyumba za kwenye mji, hapo na awache kusoma Talbiyah3 ili aweze kutekeleza nguzo nyengine.

Kuoga Unapoingia Makkah

21. Yoyote mwenye kupata nafasi ya kuoga kabla ya kuingia Makkah na afanye hivyo na aingie Makkah wakati wa mchana kama

alivyofanya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم).4

1 Imepokewa na al-Bukhârî katika chapa ya mukhtasari ya “Swahîh” (no. 60). Amesema al-Hâfidh: “Hadîth iliyotangulia inaashiriya yakwamba kuisoma Talbiyah wakati wa kushuka kwenye sehemu za bonde ni miongoni mwa Sunan za Mitume, hususan ikiwa unashuka kwenye mabonde na kupanda kwenye sehemu za kuinuka”. 2 Imepokewa na Ahmad (vol. 1/ no. 417) kwa isnadi nzuri ya wapokezi. Akaiswahihisha al-Hâkim na adh-Dhahabi katika “Al-Hajjul Kabîr.” 3 Imepokewa na al-Bukhârî (no.779), chapa ya mukhtasari na Al-Baihaqî. Tizama katika Al-Majma‟ (vol. 3/ no. 225-239). 4 Imepokewa na al-Bukhârî (no.779), chapa ya mukhtasari, na Swahîh Abî Dâwud (no. 1630)

Page 35: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

22

22. Kisha Muhrim na aingie Makkah kwa kupitia (milima ya) Thaniyyah „Ulya; siku hizi mlango wake unaitwa Bâb al-Mu‟allât

kwani Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliingia Makkah kwa kupitia mahali

hapo1, unapoyaona makaburi kwa juu. Kisha Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

akaingia mahali patakatifu kupitia kwenye mlango wa Banî Shaybah kuwa ndiyo njia ya karibu ya kulifikia Jiwe Jeusi.

23. Vilevile Muhrim anaweza kuingia Makkah kwa kupitia njia

yoyote atakayo. Amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم): Barabara yoyote

inayokuongoza hadi Makkah ni njia zake na ni sehemu za

kuchinja.” Katika riwaya nyengine, amesema Mtume ( صىل اهلل عليه ;Njia zote zenye kukuongoza kuelekea Makkah ni zake“ :(وسلم

anaweza mtu kuingilia kwa hapa na atokeze kwa pale.”2

24. Wakati wa kuingia katika Mskiti wa Makkah, mtu (mke/mume) na asisahau kuingia kwa kutanguliza mguu wa kulia na huku aseme:

د » صوي لع م اـخص يل أةاب رمحخم ي ش و الي « الي

“Allâhumma swallî „alâ Muhammadin wasallam; Allâhumma iftah lî abwâba rahmatik”

“Ewe Mola Mswaliye Muhammad na Umsalimu; Ewe Mola nifungulie mimi mlango wa Rehma zako.”3

Au na aseme:

يطان » الش اىلدي وشيطا اىهري س وب اىػظي ذ ةالل غأ

« الرسي 1 Imepokewa na al-Bukhârî (no.780), na Swahîh Abî Dâwud (no. 1929) 2 Imepokewa na Al-Fâkihî kwa sanad iliyo hasan. 3 “Al-Kalimu at-Twayyib” cha Sheikhul Islâm Ibn Taymiyyah (Uk. 5152), kilichohakikishwa na mimi.

Page 36: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

23

“A‟ûdhubillâhil-„Adhwim wa biwajhi hilkarîm wasultwânihil qadîm minash-Shaitwânir rajîm”

“Najilinda kwa Allâh Mtukufu na kwa Uso wake Mtukufu na kwa Ufalme wake wa tangu na Sheitwani aliyefukuzwa.”1

25. Muhrim anapoliona al-Ka‟bah anaweza kuinua mikono yake ikiwa

atapenda kwani imepokewa yakwamba Ibn „Abbâs (رضي اهلل عنه) alifanya hivyo.2

26. Katika hali hii, Muhrim anaweza kumuomba Allâh kwa du‟â‟

apendayo, kwani haikuthubutu yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

alimuomba Allâh kwa du‟â‟ maalum. Anaweza kuomba kwa du‟â‟ ya „Umar, isemayo:

لم » م الص لم، و ج الص أ ا الي ا رب لم ـطيي «ةالص

“Allâhumma antas-Salâm waminkas-Salâm fahayyinâ rabbanâ bis-Salâm”

“Ewe Mola, hakika wewe ni amani na amani inatoka kwako. Basi tupe maamkuzi ya Amani …”3

1 Imepokewa na Ibn Abî Shaybah kwa sanad iliyo swahîh. Wanavyuoni

wengine wakaipokea hadith hii wakaifuatiliza kutoka kwa Mtume ( صىل اهلل عليه -lakini kwa kupitia isnad iliyo dhaifu kama ilivyoelezwa katika “Adh (وسلم

Dha‟îfah” (no. 1054) 2 Imepokewa na Al-Baihaqî (vol. 5/ no. 72) kwa isnâd iliyo hasan kutoka kwa Sa‟îd bin al-Musayyib aliyesema: “Nimesikiya kitu kutoka kwa „Umar, hakuna hata mtu mmoja aliyesikiya pamoja na mimi aliyebaki isipokuwa mimi. Nilimsikiya akisema: „Pindi Muhrim anapoliona al-Ka‟bah ...”, vilevile akaipokea kwa sanad nyengine kutoka kwa Sa‟îd bin al-Musayyib, alikuwa akisema hivi, „Amepokea Ibn Abî Shaybah (vol. 4/ Uk. 97) kutoka kwa hao wawili. 3 Na kauli ya baadhi ya mashekhe katika ta‟liq yake ya “Al-Manâsik na Az-Ziyârah” (Ibada ya Hajj na Ziyara) yakwamba du‟â‟ hii haikupokewa kutoka

Page 37: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

24

Twawâf Al-Qudûm

(Mzunguko Wa Kuwasili) 27. Kisha Muhrim atakwenda kwenye Jiwe Jeusi, alilekee kisha

aseme, “Allâhu Akbar” (Allâh ni mkubwa zaidi). Anaweza kuitamka Basmallâh [yaani; Bismillâh] (Kwa jina la Allâh); imethubutu yakwamba Ibn „Umar alifanya hivyo. Wenye kusema

yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliitamka Basmallâh katika kituo

hiki wamekosea.

28. Kisha Muhrim ataligusa Jiwe Jeusi, alibusu, na pia halafu asujudu

juu yake kwani vitendo vyote hivi vilifanywa na Mtume ( صىل اهلل عليه Umar na Ibn „Abbâs.1„ ,(وسلم

29. Iwapo Muhrim hatoweza kulibusu Jiwe Jeusi [kutokana na umati mkubwa wa watu], anaweza kuligusa tu kisha aibusu mikono yake.

30. Iwapo hatoweza kuligusa, anaweza kuliashiriya tu kwa mikono yake.

31. Vitendo vinne vya mwisho vinatakiwa kufanywa katika kila mzunguko.

32. Muhrim hapaswi kuzozana na Mahujaji wengine kwa ajili ya

kulibusu Jiwe Jeusi. Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alimwambia „Umar: “Ewe

„Umar, kwa hakika wewe ni mtu mwenye nguvu sana, kwahivyo usiwadhuru watu wanyonge unapokurubia kulibusu Al-Hajarul Aswad [Jiwe Jeusi]. Iwapo patakuwa na nafasi ya kutosha kwako, basi liguse, lau si hivyo lielekee na usome Takbir [“Allâhu Akbar” (Allâh ni mkubwa zaidi).]2

kwa Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) ni kutofahamu kwao. Nimeiswahihisha riwaya zake

katika “Al-Irwâ” (no. 1112) na ishachapishwa. 1 Imepokewa na ash-Shâfi‟î, Ahmad na wengineo. Ni hadith yenye nguvu sana kama nilivyoizungumza katika “Al-Hajjul Kabîr” [Hijjah Kubwa] 2 Imepokewa na at-Tirmidhî, Ibn Khuzaymah, Ibn Hibbân, Al-Hâkim na adh-Dhahabî. Imepokewa kikamilifu katika “Al-Hajjul Kabîr”.

Page 38: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

25

33. Kuligusa Al-Hajarul Aswad kuna fadhla kubwa. Amesema Mtume

Kwa hakika Allâh atalifufua Al-Hajarul Aswad siku“ :(صىل اهلل عليه وسلم)

ya Qiyâmah likiwa na macho mawili ya kuona na ulimi wa kumtokea ushahidi kila aliyeligusa kwa ikhlâs [kwa ajili ya

Allâh].” Akasema Mtume ( لمصىل اهلل عليه وس ): “Kuligusa (kulipangusa) Al-

Hajarul Aswad na Ar-Ruknul Yamânî [Pembe ya Yemen] hufuta

madhambi yote ya mtu.”1. Vilevile, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

amesema: “Al-Hajarul Aswad (ni Jiwe) lililotoka Peponi. Lilikuwa ni jeupe kuliko theluji, lakini likageuzwa kuwa jeusi kwa madhambi ya makafiri [wale wenye kumshirikisha Allâh].”2

34. Baada ya kuligusa Al-Hajarul Aswad, Muhrim ataanza kulizunguka al-Ka‟bah likiwa kwenye upande wake wa kushoto, na mizunguko yenyewe ifanyike kupitia ng‟ambo ya Al-Hijr. Muhrim anatakiwa akamilishe mizunguko saba, kila mojawapo ya mizunguko hiyo ianzie kutoka Al-Hajarul Aswad na imalizikie hapo. Anapolizunguka al-Ka‟bah, Muhrim anatakiwa azuiye upande mmoja wa Ridâ‟ yake [kipande cha nguo au kitambara kinachovaliwa kwenye sehemu ya juu ya mwili] chini ya kwapa yake ya mkono wa kulia alidhihirishe bega lake la mkono wa kulia, na upande mwengine wa Ridâ‟yake alifinike bega lake la kushoto. Kitendo hiki kinaitwa “Idhtwibâ‟” na inatakiwa kufanywa katika mizunguko yote saba. [Kufanya Idhtwibâ‟ ni bid‟ah kabla au baada ya Twawâf hii]. Muhrim vilevile anatakiwa afanye Ramal (mwendo mpole) katika mizunguko mitatu ya kwanza – kuanzia katika Al-Hajarul Aswad na amalizie hapohapo – na atembee mwendo wa kawaida katika mizunguko iliyobaki minne.

35. Muhrim anatakiwa aguse pembe ya Yemen katika kila mzunguko lakini asiibusu pembe hiyo. Iwapo Muhrim hatoweza kuigusa, hata asiiashirie.

1 At-Tirmidhî anaizingatia hadith hii kuwa ni hasan, haliyakuwa Ibn Hibbân, Al-Hâkim na adh-Dhahabî wanaizingatia kuwa ni swahîh. 2 Imezingatiwa kuwa ni swahîh na At-Tirmidhî na Ibn Khuzaymah.

Page 39: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

26

36. Muhrim anatakiwa aseme anapofika katika sehemu iliyoko baina ya pembe hizi mbili [Al-Hajarul Aswad na Ruknul Yamânî]:

“Mola wetu! Tupe mema duniani na (tupe) mema akhera na

utulinde na adhabu ya moto.”1 [al-Baqarah 2:201]

37. Muhrim hatozigusa pembe mbili za Shâmî kwani Mtume ( صىل اهلل عليه hakuzigusa.2 (وسلم

Kuishikilia sehemu ya baina ya ar-Rukn na Mlango

1 Imepokewa na Abû Dâwud na wengineo. Wanavyuoni wengi wameizingatia hadith hii kuwa swahîh, “Swahîh Abî Dâwud” (no. 1653). 2 Amesema Sheikhul Islâm Ibn Taymiyyah: “Kuligusa „al-Hajarul Aswad‟ (au Ruknul Yamânî) ni mtu kuzipangusa kwa mikono yake. Ama kuhusu pambizo nyengine za al-Ka‟bah, Maqâm Ibrâhîm, misikiti na kuta zake, makaburi ya Mitume, makaburi ya watu wema, chumba cha Mtume, pango la Ibrâhîm, mahali alipokuwa akiswali Mtume wetu na pasipokuwa hapo miongoni mwa makaburi ya Mitume, Jabali la msikiti wa Jerusalem ... na kadhâlika. Haifai kuzigusa wala kuzibusu sehemu zote hizi. Rai hii imeafikiwa miongoni mwa Wanavyuoni. Ama kuhusu kuvizunguka vituo vyote hivyo vilivyotajwa, hilo ni jambo la Bid‟ah katika dini, na yoyote mwenye kuamini yakwamba hayo ni sehemu ya dini atakuwa amekufuru, na atawajibishwa atubie kwa Allâh, lau hatofanya hivyo basi atastahiki kuuwawa.” „Abdir-Razzâq (no. 8940). Ahmad na al-Baihaqî wamepokea mojawapo ya riwaya bora kutoka kwa Ya‟lâ Ibn Umayyah aliyesema: “Mimi nililizunguka al-Ka‟bah pamoja na „Umar (au

„Uthmân ( عنه اهلل رضي )). Tulipoikurubia pembe iliyoko karibu na mlango wa al-

Ka‟bah, nilimshika mkono wake kumfanya aiuguse (hiyo pembe)”. Akasema, “Kwani wewe hujawahi kuitufu Nyumba pamoja na Mtume wa Allâh?” Akasema, “Kwa hakika mimi nimewahi.” Kisha „Umar akamuuliza, “Ulimuona

yeye ( وسلم عليه اهلل صىل ) akiibusu (hiyo pembe)?” Akasema (Ya‟lâ): “Sikuwahi”.

„Umar akasema: “Basi wachana na kitendo hicho. Kwa hakika, munacho kielelezo kizuri kwa Mtume wa Allâh.”

Page 40: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

27

38. Muhrim anaweza kushikilia sehemu ya baina ya ar-Rukn na Mlango wa al-Ka‟bah, akielemeza kifua chake, uso na mikono yake mahali hapo.1

39. Hakuna adhkâr maalum inayosomwa wakati wa kutufu. Muhrim anaweza kusoma Qur‟ân Takatifu au asome adhkâr yoyote

apendayo. Amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

جطق ـل » طق، ذ ال ضو ذي أ الل اف ةاليج صلة، وىك اىط

«حطق إل بي

“Kuitufu Nyumba ni swala, lakini Allâh ameihalalisha (swala hiyo) ndani yake kuzungumza, kwahivyo mwenye kuzungumza

na asizungumze isipokuwa jambo la kheri.”

Katika riwaya nyengine, amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

م » اىلك كيا ذي « ـأ

“Basi jaribuni musizungumze sana.”1

1 Kitendo hiki kimepokewa kutoka kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) kwa njia mbili,

kitu kinachofanya uhusiano kuwa mzuri na wenye nguvu kwa Maswahaba wengi waliofanya kitu hicho, kama vile Ibn „Abbâs aliyesema: “Mahali hapa ni Multazam (mahali pa kushikwa), baina ya ar-Rukn na Mlango (wa al-Ka‟bah)”. Vilevile imethubutu yakwamba „Urwa bin az-Zubeir alifanya hivyo. Riwaya zote hizi zimetajwa kwenye “Al-Ahâdîth as-Swahîhah” (no. 2138). Amesema Sheikhul Islâm Ibn Taymiyyah amesema katika kitabu chake “Mansak” (Uk. 387): “Muhrim anaweza kuishikilia Multazam – sehemu ya baina ya Al-Hajarul Aswad na Mlango wa al-Ka‟bah, aweke kifua chake, uso wake, viganja vyake na mikono juu ya mahali hapo, na amlinganie Allâh kwa lolote atakalo. Anaweza kuyafanya yote hayo kabla ya kutekeleza Twawâf al-Wadâ‟ (mzunguko wa kuaga). Baadhi ya Maswahaba walikuwa wakifanya kitendo hicho baada ya kuingia Makkah. Ikiwa Muhrim atasimama karibu na mlango na akamuomba Allâh bila ya kuishikilia na kujiegemeza kwenye Nyumba, hilo ni jambo zuri. Na anapo ondoka katika hali hii, hatosimama wala kuangalia nyuma wala kuondoka kinyume-nyume.”

Page 41: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

28

40. Haijuzu kwa mtu aliye uchi na mwanamke aliye kwenye ada yake

ya mwezi kutufu al-Ka‟bah. Amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

«ل حطف ةاليج غريان »“Haruhusiwi kuitufu Nyumba, mtu aliye uchi.”2

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alimwambia „Âisha pindi alipokuwa akitaka

kufanya „Umrah wakati wa Hijjatul Wada‟ (Hajj ya mwisho ya

kuaga) ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

ن ل تطف ةاليج »ا حفػو الاج دي أ ضت [ لي ص ل ح ]و اذػل ن

ري «تط

“Fanya kama wanavyofanya mahujaji, isipokuwa usitufu Nyumba [wala usiswali] mpaka utwahirike.”3

1 Hadith hii imepokewa na at-Tirmidhî na wengineo, na riwaya nyengine ni ya at-Twabarânî. Ni hadith swahîh kama nilivyoichambua katika “Al-Irwâ‟” (Uk. 21). Amesema Sheikhul Islâm Ibn Taymiyyah, “Haikuthubutu yakwamba

Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) alikuwa akisoma adh-kâr yoyote alipokuwa akitufu al-

Ka‟bah, wala hakuamrisha na wala hakuwafundisha Maswahaba zake kufanya hivyo.” Lakini, hatahivyo, Muhrim anaweza kumuomba Allâh kwa adh-kâr apendazo katika adh-kâr za kisheriya. Yale wanayosoma watu siku hizi chini ya chemchemi za maji halina asili yoyote katika dini. 2 Hadîth iliyoafikiwa iliyofuatilizwa kutoka kwa Abû Hurairah. Vilevile imepokewa na at-Tirmidhî kutoka kwa „Ali na Ibn „Abbâs. Imesimuliwa kikamilifu katika “Al-Irwâ‟” (no. 1102) 3Hadîth hii imepokewa na wote wawili, Al-Bukhârî na Muslim. Imefuatilizwa kutoka kwa „Âishâ katika riwaya ya Muslim na kwa Jâbir katika riwaya ya Al-Bukhârî. Imesimuliwa kikamilifu katika “Al-Irwâ‟” (no. 191)

Page 42: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

29

41. Muhrim atakapomaliza mzunguko wa mwisho atalifinika bega lake la mkono wa kulia na aelekee kwenye maqâm Ibrâhîm (kituo cha Ibrâhîm) na asome:

“Na mahali alipokuwa akisimama Ibrâhîm pafanyeni pawe pa

kuswali.” [al-Baqarah 2:125]

42. Muhrim aifanye hiyo sehemu ya maqâm Ibrâhîm iwe ni baina yake na al-Ka‟bah na aswali mahali hapo rak‟ât mbili.

43. Katika rak‟ah ya kwanza atasoma sûratul Kâfirûn (baada ya Sûratil Fâtihah), na katika rak‟ah ya pili atasoma sûratul Ikhlâs.

Na

44. Muhrim haruhusiwi kupita mbele ya mtu yoyote anayeswali mahali hapo, na asimruhusu mtu yoyote kupita mbele yake pindi anaposwali yeye. Ahâdîth nyingi zimekataza kitendo hiki (cha kupita mbele ya mwenye kuswali) pasi na kuepukwa sehemu takatifu, bali Makkah1 nzima.

45. Muhrim anapomaliza swala yake, atakwenda kwenye maji ya Zamzam akanywe hapo na ajinyunyizie kichwani mwake. Akasema

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

ا شب ل » اء زمزم ل »

1 Kwa ihsani yako, rejea katika utangulizi na “Asili” (Uk. 21, 23, 135) kwa ufafanuzi zaidi.

Page 43: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

30

“Maji ya Zamzam hunywewa kwa lile ulilolikusudia (yaani; hutosheleza mahitaji ya mtu katika chakula, kinywaji,

matibabu ...)”1

Vilevile amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

« ، تاركث، وه طػام طػ ا ]إج «[وشفاء شل “Hakika (maji ya Zamzam) ni (maji) yaliyobarikiwa na ni chakula kwa atafutae kulishwa, na ni pozo ya maradhi.”2

اء زمزم » رض ال اء لع وس خي ل ، وشفاء الص ػ طػام اىط « ذي

“Maji yaliyo bora (matamu zaidi) katika ardhi ni yale ya Zamzam. Ni chakula kwa atafutae kulishwa, na ni pozo ya

maradhi”3.

46. Kisha Muhrim atarudi tena katika Al-Hajarul Aswad, asome takbîr hapo na aliguse kama ilivyoelezwa hapo awali.

Kutembea Baina Ya As-Swafâ Na Al-Marwah

47. Kisha, Muhrim atakwenda As-Swafâ na Al-Marwah. Muda mchache tu atakapokurubia As-Swafâ, atasoma:

1 Hadîth swahîh kama wasemavyo ma-Imâm wengi. Nimeichambua katika “Al-Irwâ‟” (no. 1123) na katika as-Swahîhah (no. 883). 2 Hadîth swahîh iliyopokewa na at-Twayâlisi na wengineo. Imejadiliwa kwa kina katika “As-Swahîhah” (no. 1056) 3 Imepokewa na adh-Dhiyâ‟ katika “Al-Mukhtârah” na wengineo. Imepokewa kikamilifu katika “As-Swahîhah” (no. 1056)

Page 44: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

31

“Hakika Swafâ na Marwah (Majabali mawili yanayofanyiwa

ibada ya ku-sa‟î huko Makkah) ni katika alama za kuadhimisha dini ya Allâh. Basi anayehiji kwenye Nyumba

hiyo au kufanya „Umrah, si kosa kwake kuvizunguka (vilima) hivyo viwili; na anayefanya wema (atalipwa) kwani Allâh ni

mwenye shukrani na Mjuzi (wa kila jambo).” [al-Baqarah 2:158]

Kisha Muhrim atasema:

« ة اللا ةدأ ة

« جتدأ

“Tutaanza kwa kile alichoanzia nacho Allâh.”

48. Kisha Muhrim ataanza kwa kupanda mlima wa As-Swafâ mpaka alione al-Ka‟bah.1

49. Akiwa juu ya mlima wa As-Swafâ, Muhrim atalielekea al-Ka‟bah, ampwekeshe Allâh na amtukuze kwa kusema:

كب » أ كب الل

أ كب الل

أ « الل

1 Siku hizi si rahisi kuliona al-Ka‟bah kutoka As-Swafâ isipokuwa kwenye baadhi ya sehemu fulani. Muhrim anaweza kuliona kutoka kwenye sehemu za baina ya nguzo zilizojengewa katika ghorofa ya pili ya mskiti. Yoyote atakaeweza kuliona Al-Ka‟bah, hilo ni bora kwake, au vyenginevyo na ajaribu kadiri ya uwezo wake, na itakuwa hapana ubaya iwapo hatoweza kuliona.

Page 45: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

32

“Allâh ni Mkubwa zaidi, Allâh ni Mkubwa zaidi, Allâh ni Mkubwa zaidi.”

Mara tatu,

Kisha aseme:

« يج و د يي وي يم ول ال يم ل ل ال وضده ل ش ل إل إل اللء كدير « لع كي ش

“Lâilâha illallâh wahdahu lâ sharîka lah, lahul Mulk walahul

hamd yuhyî wayumît wahuwa alâ kulli shay‟in qadîr”. “Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allâh, peke yake, hana mshirika, ufalme ni wake, na shukrani zote

zinamstahiki yeye, Yeye ndiye mwenye kuhuisha na kufisha na ni muweza wa kila kitu.”

« زم ل إل إل الل نز وغده، وص ختده، ويم ل، أ وضده ل ش

ضزاب وضده « ال

“Lâilâha illallâh wahdahu lâ sharîka lah, anjaza wa‟dah wanaswara „abdah wahazamal ahzâbah wah‟dah.”

“Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allâh,

peke yake, hana mshirika, ametekeleza ahadi yake,

akamnusuru mtumwa wake [Muhammad (صىل اهلل عليه وسلم)] na

akawashinda makundi peke yake.”

Muhrim atayasema maneno haya mara tatu1. Muhrim anaweza kumuomba Allâh kwa maombi atakayo baina ya adhkâr.1

1 Katika “Al-Adhkâr”:

Page 46: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

33

50. Kisha Muhrim atashuka (kutoka mlima wa As-Swafâ) atembee

baina ya As-Swafâ na Al-Marwah. Amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

“Fanyeni Sa‟î baina yake kwani Allâh amewaamrisha mufanye

hivyo2.”

51. Kisha Muhrim atatembea mpaka afike kwenye „Alam (iliyowekwa) katika upande wa kulia na kushoto – inajulikana kwa jina la sehemu ya kijani – mahali ambapo Muhrim anapowajibika kukaza mwendo wake hadi afike kwenye „Alam nyengine.

Sehemu hii baina ya „Alam mbili ilikuwa – katika wakati wa

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), ni bonde la ardhi lililojaa changarawe.

Akasema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم): “Piteni „Al-Abtwah‟(sehemu iliyo

baina ya „Alam mbili) kwa mwendo wa haraka.”3[Kitendo hichi ni kwa wanaume peke yao]1

بدإلإياه ...الخلإلإلاهلل،ولنع

“Hapana mola isipokuwa Allâh. Twamuabudu yeye peke yake …” Sijaona nyongeza hii kwenye riwaya yoyote ya hadîth – emma riwaya ya Muslim wala ya mwengine yoyote. Du‟â‟ hii imetajwa kwenye ahâdîth zilizofuatilizwa kutoka kwa Jâbir. Kwahivyo usipotezwe na maneno ya mashekhe: “Imepokewa na Muslim …”! 1 Yaani ni kumuomba Allâh kwa sampuli yoyote nzuri aipendayo ya hapa ulimwenguni na kesho Akhera. Ingelikuwa ni bora kumuomba Allâh kwa

kuzisoma du‟â‟ ambazo alizokuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akizitumia. 2 Ni hadith swahîh iliyopokewa kikamilifu katika “Al-Irwâ‟” (no. 1072) 3 Imepokewa na an-Nasâ‟î na wengineo. Vilevile imepokewa kwenye “Al-Hajjul Kabîr". Nukta Muhimu: Ibn Qudâmah Al-Maqdisi amesema katika „Al-Mughnî‟ (vol. 3/ Uk. 394): “Wanawake wanapaswa kutembea kwenye Twawâf na Sa‟î yote.” Akasema Ibn Al-Mundhir: “Kuna muafaka miongoni mwa Wanavyuoni yakwamba wanawake hawapaswi kutembea haraka haraka wanapolizunguka

Page 47: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

34

Kisha Muhrim atapanda mlima wa Al-Marwah na afanye kama alivyofanya katika mlima wa As-Swafâ; ataelekea Qiblah, asome takbîr na Tawhîd (yaani aseme: Lâ ilâha illallâh) na du‟â‟ nyengine. Mpaka hapo, Muhrim atakuwa amemaliza duara moja.2

al-Ka‟bah wala kutembea baina ya Al-Swafâ na Al-Marwah, na wala hawana haja ya kufanya Idhtwibâ‟, kwani mambo haya hufanywa kuonyesha nguvu (za Waislamu kwa makafiri) na jambo hili halikuwajibishwa kwa wanawake. Wao wanastahiki kujisitiri (kitabia na adabu) wasijidhihirishe mapambo yao.” Katika “Al-Majmû‟” (vol. 8/ Uk. 75), amesema Imâm An-Nawawi yakwamba mas‟ala haya ni katika ikhtilafu baina ya wanavyuoni wa ki-Shâfi‟î, amesema: “Kuna rai mbili kuhusiana na mas‟ala haya: La Kwanza: Ambalo ndilo lenye uzito mkubwa na lililoshikiliwa na Al-Jumhûr, yakwamba wanawake hawafai kutembea haraka haraka lakini watembee kwa upole njia nzima – wakati wowote usiku na mchana. La Pili: Ikiwa mwanamke ametekeleza Sa‟î wakati wa usiku – wakati ambapo kuna watu wachache – amependekezewa atembee kwa haraka kama wanavyotembea wanaume.” Mimi (muandishi) naona yakwamba rai ya pili ndiyo yenye nguvu. Kitendo cha Sa‟î kimetokana na Sa‟î aliyoifanya Hâjar – mamake Ismâ‟îl – pindi alipokuwa akijaribu kupata msaada kwa ajili ya mwanaye aliyekuwa na kiu. Kama ilivyotajwa kwenye riwaya ya Ibn „Abbâs, „aliona kuwa mlima wa As-Swafâ ndiwo uliokuwa wa karibu awezao kuufikia, kisha akaupanda na akaelekea kwenye bonde kuona iwapo kuna mtu anayekuja. Kwa bahati mbaya hakumuona mtu yoyote. Kisha akaushuka mlima wa As-Swafâ, muda mchache alipofika kwenye bonde, akakweza pindo la rinda lake na akatembea kwa upole mpaka akavuka sehemu hiyo. Kisha akaupanda mlima wa Al-Marwah na akatizama kuona iwapo kuna mtu anayekuja. Kwa bahati mbaya hakumuona mtu yoyote. Aliendelea kufanya hivyo (yaani; kutembea baina ya As-Swafâ na Al-Marwah) kwa mara saba.” Kisha Ibn „Abbâs

akasema: “Amesema Mtume ( مصىل اهلل عليه وسل ): „Na huku ndiko kwenda Sa‟î kwa

watu baina ya Swafa na Marwah.” Imepokewa na al-Bukhârî katika “Kitâbul Anbiyâ‟. 1 Nukta ya nyongeza ya Mfasiri. 2 Kulitizama al-Ka‟bah siku hizi ni vigumu sana kutokana na jengo lililoko baina ya mlima wa as-Swafa‟ na al-Ka‟bah. Lakini hata hivyo, Muhrim na ajitahidi kadiri ya uwezo wake alielekee na asiinue macho yake na mikono yake kuelekea mbinguni kama wafanyavyo baadhi ya watu.

Page 48: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

35

52. Kisha Muhrim atapanda tena mlima wa As-Swafâ akitembea kwa mwendo wa kawaida na upole kwenye sehemu zinazostahiki, na kwa kufanya hivyo atakuwa amemaliza duara la pili.

53. Kisha atarudi tena kwenye mlima wa As-Swafâ na kisha kwenye mlima wa Al-Marwah mpaka akamilishe maduara saba – na la mwisho ambalo litakalokuwa ni kwenye Al-Marwah.

54. Muhrim anaruhusiwa kufanya mwendo wa Sa‟î kwa kutembea au kuwa juu ya kipando; la kwanza ndilo linalopendekezwa kwani

ndivyo alivyofanya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم).1

55. Muhrim anaweza kumuomba Allâh (سبحانه وتعاىل) wakati akifanya Sa‟î

kwa kusema:

كرم »غز ال

ج ال

إم أ «ربي اؽفر وارض

Rabbigh fir warham innaka antal A‟azzul-akram

“Ewe Mola tusamehe na uturehemu, hakika yako wewe ni Mtukufu na mkarimu.”

Na maneno haya yamethubutu kupokewa kutoka kwa watu wema wengi waliotutangulia.2

56. Muda mchache atakapomaliza duara la saba katika mlima wa Al-Marwah, Muhrim atapunguza nywele zake3. Kwa kufanya haya, Muhrim atakuwa amemaliza „Umrah yake na anaweza kufanya apendavyo katika mambo aliyokuwa amekatazwa kufanya wakati

1 Hii imepokewa na Abû Nu‟aim katika kitabu chake “Mustakhraj” juu ya “Swahîh Muslim”. 2 Imepokewa na Ibn Abî Shaybah (vol. 4/ no. 68, 69) kutoka kwa Ibn Mas‟ûd

na Ibn „Umar ( عنهما اهلل رضي ) kwa isnâd swahîh. Na kutoka kwa Al-Musayyab bin

Râfî‟ Al-Kâhil: Na „Urwah bin Az-Zubeir. Vilevile imepokewa na at-Twabarânî kwa isnâd dha‟îf kama ilivyotajwa kwenye “Al-Majma‟” (vol 3/ no. 248) 3 Au atanyoa iwapo muda utakaokuwa baina ya „Umrah yake na Hajj ni kiyasi cha muda mrefu ambao nywele zake zinaweza kumea tena. Al-Fat-h (vol. 3/ Uk. 444).

Page 49: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

36

alipokuwa amevaa Ihrâm. Muhrim atakaa katika hali hii mpaka siku ya at-Tarwiyah [8th Dhul-Hijjah].

57. Yoyote ambaye aliyevaa Ihrâm akawa amekusudia kufanya Hajj peke yake, na akawa hakuja na Hady wake atapaswa kumaliza

Ihrâm yake – kwa kufuatia amri ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) na kuepuka

hasira zake. Ama wale walioleta Hady watabaki katika hali yao ya Ihrâm wasimalizie hapo, lakini mpaka siku watakaporusha vijiwe katika siku ya Nahr (10th Dhul-Hijjah).

Kuvaa Ihrâm Ya Hajj Katika Siku Ya Tarwiyah

58. Katika siku ya Tarwiyah – siku ya Nane ya Dhul-Hijjah – Muhrim anapaswa avae Ihrâm na asome Talbiyah ya Hajj na afanye vitendo alivyofanya pindi alipovaa Ihrâm kwa ajili ya „Umrah alipofika kwenye Mîqât, yaani; kuoga, kujitia manukato, kuvaa Izâr na Ridâ‟ na kusoma Talbiyah ambayo isiyokoma kusomwa hadi Muhrim akimaliza kurusha vijiwe vya Aqabah.

59. Kuvaa Ihrâm katika hali hii inakuwa ni pale anapokaa Muhrim, na watu wanaoishi Makkah wanavaa Ihrâm zao Makkah.

60. Kisha Muhrim ataondoka na kuelekea Mina na aswali swala ya Dhuhr hapo, akae hapo mpaka usiku kisha aswali swala nyengine Qasran (yaani; badala ya kuswali rak‟ât 4 za „asr na „ishâ‟, Muhrim ataswali rak‟ât mbili kwa kila swala). Ataswali swala nyengine tano zilizobaki qasran, bila ya kuzijumuisha.

Kuelekea „Arafah

61. Katika siku ya „Arafah (tarehe 9th, Dhul-Hijjah), baada ya kuchomoza kwa jua, Muhrim anapaswa kuelekea „Arafah, huku akisoma Takbîr au Talbiyah kama walivyokuwa wakifanya

Page 50: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

37

Maswahaba wa Mtume ( عليه وسلمصىل اهلل ) mbele ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

na wala hakuwakatalia kitendo chao hicho.1

62. Kisha Muhrim atashukia Namira2 – sehemu karibu na „Arafah lakini hapazingatiwi kuwa katika mazingira yake – na wakae hapo mpaka jua likurubie kupinduka.

63. Jua linapopinduka, Muhrim anatakiwa ende „Uranah mahali karibu na „Arafah – na akae mahali hapo3. Hapo, Imâm hutoa khutbah inayonasibiana na hali ya hapo.

64. Kisha Imâm atawaongoza watu kwenye swala, na awaswalishe kwa kuzijumuisha Dhuhr na „Asr kwa kuzikusuru katika wakati wa Dhuhr.

65. Kutaadhiniwa muadhini mmoja kwa ajili ya swala mbili, na iqâmah mbili.

66. Hakuna kuswaliwa swala za Sunnah baina ya swala hizo (Dhuhr na „Asr)4

1 Imepokewa na Mashekhe wawili (yaani; Bukhârî na Muslim) 2 Kukaa hapo Namirah na mahali pengine baada ya hapo (paitwa „Uranah) ni jambo ambalo ni zito kulitekeleza siku hizi kutokana na umati mkubwa wa watu mahali hapo. Muhrim anaweza kupita kwenye sehemu hizi mbili akielekea „Arafah moja kwa moja; hapana neno kwa jambo hilo. Amesema Sheikhul Islâm Ibn Taymiyyah katika “Al-Fatâwa” (vol. 26/ Uk. 168): Ama

kuhusu kukaa kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) Mina katika siku ya Tarwiyah na

kulala hapo usiku mzima, na kisha kukaa kwake „Uranah – sehemu iliyoko baina ya Al-Muzdalifah na „Arafah – na kuswali swala mbili hapo na kutolewa khutbah na Imâm mpaka kutwa kwa jua, kisha kwenda hadi „Arafah, vitendo

vyote hivyo ni katika Sunnah za Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) kama wanavyoafikiana

mafuqahâ‟ wote – ingawa baadhi ya wanavyuoni hawayataji hayo na watu wengi hawayajui kutokana na mambo mengi ya uzushi yaliyotokea (yanayohusiana na Hajj na „Umrah). 3 Imepokewa na Mashekhe wawili.

4 Haikuthubutu yakwamba Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) aliswali swala za Sunnah

kabla ya Dhuhr na baada ya „Asr mahali hapa, wala kwenye safari yake yote,

Page 51: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

38

67. Yoyote ambaye hakuwahi kuswali pamoja na Imâm na aswali peke yake au aswali na Wasilamu wengine waliokosa swala pamoja na Imâm.1

Kusimama „Arafah

68. Kisha Muhrim ataelekea „Arafah na akae kwenye mawe chini ya Jabali la Rahmah ikiwa atakuwa na uwezo wa kufanya hivyo, na lau hatoweza kufanya hivyo, basi atakaa mahali popote katika sehemu ya „Arafah.

69. Anaposimama „Arafah, Muhrim anatakiwa aelekee Qiblah (upande wa al-Ka‟bah), ainue mikono yake kwa kumuomba na kumlingania

Allâh ( تعاىل و حانهسب ).

70. Na akithirishe hapo „Arafah kuleta Tahlîl (lâ ilâha illallâh) kwani du‟â‟ bora ya kuomba katika sehemu ya „Arafah ni Tahlîl, Mtume

amesema: “Du‟â‟ (maneno yaliyo) bora ambayo mimi (صىل اهلل عليه وسلم)

na Mitume wengine tuliyowahi kuyasema ni:

ء » لع كي ش د، و يم ول ال يم ل، ل ال وضده ل ش ل إل إل الل « كدير

“Lâilâha illallâh wahdahu lâ sharîka lah, lahul Mulk walahul hamd wahuwa alâ kulli shay‟in qadîr”.

“Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allâh, peke yake, hana mshirika, ufalme ni wake, na shukrani zote

zinamstahiki yeye, na ni muweza wa kila kitu.”2

wala Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) hakuswali swala yoyote ya Sunnah kwenye

misafara yake isipokuwa Sunnah ya Fajr na Witr. 1 Imepokewa na al-Bukhârî ikafuatiliwa kutoka kwa Ibn „Umar, “Mukhtasar al-Bukhârî” (no. 25, 89, 3). 2 Hadîth hasan au swahîh ina njia nyingi za upokezi, nimezipokea katika “As-Swahîhah” (no. 1503)

Page 52: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

39

71. Vilevile Muhrim anaweza kusema, wakati mwengine, du‟â‟ ifuatayo:

ا اخلي خي الخرة » «إج“Innamal khayru khayrul Âkhirah”

“Hakika kheri iliyo bora ni kheri ya akhera.”1

72. Ni katika Sunnah kwa mwenye kusimama „Arafah, kutofunga katika siku hiyo (siku ya „Arafah).

73. Muhrim ataendelea na Talbiyah yake na du‟â‟, na amlinganie

Allâh ( تعاىل و سبحانه ) kwa lolote atakalo na ajilize mbele yake ili

amfanye awe ni miongoni mwa watakao okolewa kutokamana na moto wa Jahannam na miongoni mwa wale ambao Allâh hujifakhiri mbele ya Malaika – kama ilivyotajwa kwenye hadîth:

ن » أ كث

م أ ي ا م غرـث وإ ي انلار ختدا ذي حػخق الل

ؤلء راد ا أ لئكث ذيلل: ال حتاه ة « يلد ث

“Mâ min yawmin akthara min an ya‟tikallâhu fiyhi „abdan minan Nâri min yawmi „Arafah wainnahu layadnû thumma

yubâhi bihimul Malâikah fayaqûlu: Mâ arâda hâ‟ulâi”

“Hapana siku katika masiku ambapo Allâh mtukufu, anapowaacha huru waja wengi kutoka katika Moto kuliko katika siku ya „Arafah. Hushuka karibu yao, kisha akawasifu mbele ya Malaika huku akisema: “Ni kitu gani wanachokitamani hawa?”2

Na katika riwaya nyengine, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akasema:

1 Imethubutu yakwamba Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) amesema hivyo kama

ilivyoelezwa kwenye “Asili” 2 Imepokewa na Muslim na wengineo “At-Targhîb” (vol. 2 / no. 129)

Page 53: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

40

اء، ذيلل: اجظروا إل غتادي » و الص و غرـات أ

حتاه ةأ إن اللا هذا ول يزال ساءون شػرا دب س ضت «تؾرب الش

“Innallâha yubâhi bi ahli „Arafât ahlis Samâ‟ fayaqûl: Undhurû ilâ „Ibâdî jâ‟ûnî sha‟than ghubran walâ yazâlu hâkadhâ hattâ

taghrubush shams” “Kwa hakika Allâh anawasifu watu waliosimama katika uwanja wa „Arafah mbele ya wakaazi wa mbinguni (malaika) akisema: „Watizame waja wangu; wamenijia wakiwa hali zao matimu-timu na wamechafuka kwa vumbi (kwa ajili ya kufunga safari

kwenye Nyumba yangu)1

Muhrim anatakiwa akae „Arafah mpaka kutwa kwa Jua.

Kuondoka „Arafah Kwa Haraka

74. Jua linapokutwa, Muhrim anatakiwa aondoke kwa haraka kutoka „Arafah na kuelekea Muzdalifah kwa utulivu na upole, asishindane na watu wengine kwa mwili wake, gari, kipando ... na kadhaalika. Kila Muhrim anapojipatia nafasi ya kutembea na akaze mwendo.

75. Akiwa Muzdalifah, Muhrim ataswali swala ya Maghrib – rak‟ât tatu, na swala ya „Ishâ‟ – rak‟ât mbili – kwa kuzijumuisha baada ya adhân na iqâmah.

76. Ikiwa Muhrim atatenganisha baina ya swala hizi mbili kwa ajili ya kutekeleza uwajibikaji fulani, hapana madhara katika jambo hilo.2

77. Muhrim hafai kuswali swala yoyote ya Sunnah baina ya swala hizi mbili, wala baada ya swala ya „Ishâ‟.1

1 Imepokewa na Ahmad na wengineo, imesimuliwa kikamilifu katika “At-Targhîb”

2 Imethubutu yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alifanya hivyo kama

alivyosema Ibn Taymiyyah. Vilevile imepokewa na al-Bukhârî (no. 25, 94, 801) katika Mukhtasar ya “Swahîh al-Bukhârî”

Page 54: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

41

78. Kisha Muhrim atalala mpaka alfajiri.

79. Itakapomuingilia yeye alfajiri, muhrim ataswali swala ya Fajr kwa wakati wake baada ya Adhân na Iqâmah.

Swala Ya Fajr Ukiwa Muzdalifah

80. Mahujaji wote ni lazima waswali Alfajiri katika sehemu ya Muzdalifah isipokuwa wanawake na watu madhaifu; wanaruhusiwa kuondoka mahali hapo baada ya saa sita za usiku kwa kuepuka zogo la watu.

81. Kisha Muhrim atakwenda Al-Mash‟ar Al-Harâm (ni mlima mkubwa ulioko Muzdalifah) apande hapo, aelekee al-Ka‟bah, amsifu Allâh, asome Takbîr (Allâhu Akbar). Tahlîl (Lâ Ilâha illallâh), na amuombe Allâh kwa chochote apendacho na aendelee kufanya hivyo mpaka Jua lipande juu kisawa-sawa.

82. Muhrim na akae popote apendapo katika sehemu ya Muzdalifah.

83. Muda mchache kabla ya kuchomoza kwa Jua, Muhrim anapaswa kuelekea Minâ kwa utaratibu na huku akisoma Talbiyah.

84. Anapofika Batn Muhassir, atatembea kwa upole akiweza.

85. Kisha atachukuwa njia ya katikati itakayomtokeza yeye katika Al-Jamratul Kubrâ.

Kurusha Vijiwe

86. Akiwa njiani, Muhrim ataokota vijiwe ambavyo atakavyovirusha akiwa Jamratul „Aqabah katika sehemu ya Minâ, ambapo ni mahali pa mwisho katika Jamarât (kwa uchache Jamrah) na palipo karibu na Makkah.

1 Amesema Sheikhul Islâm Ibn Taymiyyah: “Muhrim anapowasili Muzdalifah, ataswali al-Maghrib – ikiwezekana kabla ya Ngamia hajatulia. Wakishatulia Ngamia ataswali swala ya Ishâ‟. Iwapo swala hii itacheleweshwa, hapana madhara yoyote kwa hilo.”

Page 55: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

42

87. Muhrim ni lazima aelekee Jamrah na Makkah ikiwa kwenye upande wa kushotoni mwake na Minâ ikiwa kwenye upande wake wa kulia.

88. Kisha ataanza kurusha vijiwe (kwenye kuta la Jamarât), vyenye ukubwa mfano wa changarawe.

89. Kila anaporusha kijiwe, Muhrim atatakiwa asome Takbîr.1

90. Muda mchache tu baada ya kurusha kijiwe cha mwisho, Muhrim atanyamaza kusoma Talbiyah.2

91. Vijiwe havifai kurushwa isipokuwa baada ya kuchomoza kwa Jua, hata kwa wale watu madhaifu walioruhusiwa kuondoka Muzdalifah baada ya nusu ya usiku, kwani kuondoka Muzdalifah ni jambo jengine na kurusha vijiwe ni jambo jengine.3

92. Muhrim anaruhusiwa kurusha vijiwe baada ya jua kushuka mpaka usiku ikiwa ni vigumu kwake kurusha vijiwe kabla ya jua kushuka – kama ilivyopokewa katika baadhi ya hadîth.

93. Muda mchache tu baada ya Muhrim kumaliza kurusha vijiwe, ataruhusiwa kufanya kila kitu kilichokuwa ni haramu kwake pindi alipokuwa katika hali ya Ihrâm isipokuwa tendo la kujamiiyana na

1 Baadhi ya waandishi wanasema yakwamba muhrim vilevile anaweza kusema:

ورا » انب حج عل ماج « ...الل

“Allâhumma aj‟alhu Hajjan mabrûrâ”

“Ewe Mola! Ifanye Hajj yetu ni yenye kukubalika.”

Baada ya kusoma Takbir. Ibara hii haikuthubutu kuwa imesemwa na Mtume

.kama nilivyofafanua katika “Adh-Dha‟îfah” (no. 1107) (صىل اهلل عليه وسلم)2 Kama ilivyopokewa na Ibn Khuzaymah katika “Swahîh” yake: “Hii ni hadîth swahîh inayozifafanua riwaya nyengine ambazo mojawapo inayosema

yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alinyamaza kusoma Talbiyah muda mchache

tu baada ya kurusha Jamaratul „Aqabah.” Hiyo ina maana ya baada ya kurusha kijiwe cha mwisho. [Fat-hul Bârî] (vol. 3/ Uk. 426) 3 Nimeifafanua nukta hii kwa kina katika “Asili” (Uk. 80)

Page 56: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

43

mkewe. Vilevile anaweza kuvaa nguo zake za kawaida na akajitia manukato hata kabla hajachinja mnyama au kukata nywele zake.

94. Hatahivyo, anapaswa kulizunguka al-Ka‟bah siku ileile (atakapomaliza kurusha vijiwe), lau kama atapendelea kuendelea kuwa katika hali yake kama Mutamatti‟, ikiwa hakuizunguka Nyumba kabla ya usiku, atarudi zake katika hali yake ya Ihrâm; yaani atazivua nguo zake za kawaida na avae nguo za Ihrâm (Ridâ‟

na „Izâr) kwani amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم): “Siku hii ya leo

muna chaguo, lau kama mutarusha Jamrah, munaweza kumaliza Ihrâm zenu mukafanya kila kitu mulichokuwa mumeharamishiwa isipokuwa (kuingiliana) na wake zenu, lakini iwapo hamukuweza kuizunguka Nyumba kabla ya usiku, basi mutarudi tena kwenye hali zenu za Ihrâm (yaani; hali zenu mulizo hivi sasa) kabla hamujarusha Jamrah kisha mukaizunguka Nyumba.”1

1 Hii ni hadîth swahîh – kama walivyosema wanavyuoni wengi akiwa mmojawapo ni Ibn Al-Qayyim. Imefafanuliwa kikamilifu katika [Swahîh Abî Dâwud] (no. 1745). Kabla ya kuchapisha kijitabu hiki, baadhi ya wanavyuoni waliisoma hadîth hii wakashangaa mpaka wakaizingatia hadîth yenyewe kuwa ni „hadîth ngeni‟, hata baadhi nyengine wakaizingatia kuwa ni Dha‟îf – kama nilivyowahi mimi binafsi kufanya katika baadhi ya vitabu vyangu nikiizingatia isnadi ya wapokezi waliotajwa na Abû Dâwud. Ingawa Ibn Al-Qayyim akaizingatia njia hii ya hadîth kuwa ni yenye nguvu katika kitabu chake “Tah-dhîb” pamoja naye Al-Hâfidh katika kitabu chake “Talkhîs” akayaafiki hayo. Nikagundua – baadae – njia nyengine, inayozidi kuonyesha kuwa hadîth hii ina nguvu zaidi na ni swahîh. Kwa vile njia hii imeelezwa kwa marejeo ya nadra katika asili ya hadîth – yaani; “Sharh Ma‟âni Al-Athar” cha Imâm at-Twahâwî – watu wengi wameizingatia kuwa ni “hadîth ngeni” na hata kuwa ni dha‟îf kama nilivyowahi kufanya hapo mbeleni. Sababu ya pili ya wanavyuoni hawa kuidho‟ofisha hadîth hii ni kwamba baadhi ya wanavyuoni wakubwa zaidi walisema katika maandishi yao: “Sijawahi kumsikiya Mwanachuoni wa Fiqh akiyasema hayo.” Lakini hatahivyo, matamshi kama haya yanapingana na „ilmu yao ya hadîth hii, ambayo haimaanishi yakwamba hakuna hadîth hiyo. Kwa vile hadîth ipo – inapatikana, na ni jambo la kubainika waziwazi, anapaswa mtu kukinai nayo na aitendee kazi kama inavyostahiki hata kama huwenda baadhi

Page 57: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

44

Kuchinja

95. Kisha Muhrim atakwenda kwenye Manhar, Minâ na achinje mnyama wake akiwa hapo. hii ni Sunnah.

ya wanavyuoni wakawa hawaijui. Amesema Imâm ash-Shâfi‟î: “Hadîth

hukubaliwa pindi inapothibitishwa (kuwa imepokewa kutoka kwa Mtume ( صىلوسلم عليه اهلل )) hata kama baadhi ya ma-Imâm hawakutekeleza kulingana na

isemavyo. Hadîth ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) yenyewe ni dalili kivyake, hapana

(asili ya hukmu) kiwezacho kuja baada yake.”

Mimi naamini yakwamba hadîth ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) inahukumu

kitendo cha ma-Fuqahâ‟ (iwapo wamepata au wamekosa) kwani (hizo hadîth zenyewe) ndizo zenye kuzingatiwa kuwa ni asili ya hukmu zenye kuhukumu vitendo vya watu na wala zisihukumiwe (ikiwa zitathubutu kuwa ni swahîh). Wanavyuoni wengi wakubwa wametekeleza kulingana na hadîth hii (inayojadiliwa) kama vile „Umar bin az-Zubeir. Sasa ni upi msamaha wa wale wasiotekeleza kulingana na hadîth hii??

Amesema Allâh ( وتعاىل سبحانه ):

“Kwa yakini katika jambo hili mna ukumbusho kwa mwenye moyo au kwa ategaye sikio, naye mwenyewe awe hadhiri.” [Qâf: 50:37]

Kurusha vijiwe kwa Muhrim huzingatiwa kuwa ni „Îdd kama ilivyo

kwa Waislamu wengine. Hiyo ndiyo sababu ya Imâm Ahmad ( اهلل رحمه )

kupendekeza yakwamba wakaazi wa hapo (Minâ, Muzdalifah ...) waswali Minâ (swala ya „Îdd). Baadhi yao wamependekeza hili kulingana na ujumla

wa maneno ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) na baadhi nyengine wakategemea tokeo

la hitimisho tu wala sio Sunnah kwani Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) hakuwahi kuswali

Swala ya Îdd akiwa Minâ. Rejea katika Fatâwa Ibn Taymiyyah (vol. 26/ Uk. 180).

Page 58: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

45

96. Lakini hatahivyo, Muhrim anaweza kuchinja mnyama wake mahali

popote apendapo akiwa Minâ au Makkah. Amesema Mtume ( صىل اهلل :(عليه وسلم

طر » ث طريق و ه طر وك ـشاج ا ن ك ا، و ا كد نرت « ـانروا ف رضاىك

“Mimi nimechinja mahali hapa (al-Manhar) na Minâ yote ni mahali ambapo mtu anaweza kuchinja mnyama wake na vilevile Makkah yote ni mahali ambapo mnyama anaweza kuchinjwa na

Makkah nzima ni njia kwa watu ya kuingia (ndani yake), kwahivyo chinjeni wanyama wenu katika nyumba zenu.”1

97. Ni bora kwa Muhrim kumchinja mnyama wake mwenyewe kwa mikono yake iwapo itawezekana kufanya hivyo, lau si hivyo, basi anaweza kumpa mamlaka mtu mwengine amfanyie kwa niyaba yake.

98. Muhrim anatakiwa aelekee Qiblah2 anapomchinja mnyama wake, amlaze kwa upande wake wa kushoto na amkanyage kwenye upande wake wa kulia.1

1 Hadîth hii imewarahisishia Mahujaji kitendo cha kuchinja kwa kiyasi kikubwa, jambo lenye kusaidia katika kusuluhisha matatizo ya kusanyiko kubwa la ummah katika sehemu ya al-Manhar (mahali pa kuchinja) la kuilazimisha Mamlaka kuwazika wanyama wengi waliochinjwa mahali hapo (kutokana na idadi yao kubwa, mpaka pakawa hakuna wa kuwachukuwa). “Asili” (Uk. 87-88). 2 Abû Dâwud na wengineo wamepokea ahâdîth kutoka kwa Jâbir kutoka kwa

Mtume ( سلمصىل اهلل عليه و ) na imesimuliwa kikamilifu katika Al-Irwâ (no. 1138), na

al-Baihaqî akaipokea katika Sunan yake (vol. 9/ no. 285). Vilevile ilipokewa yakwamba Ibn „Umar, amependekeza yakwamba Muhrim na aelekee Qiblah anapomchinja mnyama wake. Amepokea „Abdur-Razzâq (kwenye ukusanyaji wake) (no. 8585) kwa njia nzuri ya isnâd – yakwamba Ibn „Umar hakuwahi kula katika vichinjwa ambavyo havikuchinjwa kwa kuelekezwa Qiblah.

Page 59: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

46

99. Ama kuhusu jinsi ya kumchinja Ngamia, huchinjwa haliyakuwa amefungwa mguu wake wa kushoto wa mbele, apate kusimama kwa miguu yake mitatu2, na aelekezwe Qiblah.3

100. Wakati wa kumchinja mnyama, Muislamu na aseme:

كب » أ والل مسب الل ذا الي م ولم إن ني تلتو الي »

“Bismillâhi wallâhu Akbar; Allâhumma inna hâdha minka wa laka; Allâhumma taqabbal minnî”

“Kwa jina la Allâh, Allâh ni mkubwa kabisa, Ewe Mola! Hakika fadhla hii (yaani; swadaka) inatoka kwako4, na (imechinjwa) ni

kwa ajili yako. Ewe Allâh ikubali kutoka kwangu.”5 101. Mnyama wa swadaka huchinjwa katika siku nne za „Îdd: Siku ya

Nahr (tarehe 10 ya Dhul-Hijjah), vilevile inaitwa siku kuu ya

1 Amesema Al-Hâfidh (vol. 10/ Uk. 16): “(Hivi ndivyo ilivyo) katika kumrahisishia mwenye kuchinja ashikilie kisu kwa mkono wake wa kulia na kichwa cha mnyama kwa mkono wake wa kushoto.” Vitendo vya kumlaza mnyama alale kwa upande wake wa kushoto na kumkanyaga kwa mguu wa kulia juu ya upande wake wa kulia, zote hizo mbili zimepokewa na Mashhekhe wawili kwenye swahîh zao. 2 Imepokewa katika “Swahîh Abî Dâwud” (no. 1550) na ikatiliwa nguvu na riwaya nyengine iliyofuatilizwa kutoka kwa Ibn „Umar ambayo iliyopokewa na Mashekhe wawili. 3 Hii ilipokewa na Mâlik kwa isnâd nzuri iliyofuatilizwa kutoka kwa Ibn „Umar. Katika chapa ya mukhtasar ya “Swahîh al-Bukhârî” Imepokewa kwa isnâd ya kutundikwa ya wapokezi kwa mfumo wa uhakika (no. 330). 4 Imepokewa na Abû Dâwud na wengineo kutoka kwa Jâbir. Abû Ya‟lâ amepokea riwaya kama hiyo iliyofuatilizwa kutoka kwa Abû Sa‟îd Al-Khudhrî katika “Al-Majma‟” (vol. 4/ no. 22) na ikasimuliwa kikamilifu katika “Al-Irwâ‟” (no. 1118). 5 Imepokewa na Muslim na wengineo ikafuatiliziwa kutoka kwa „Âisha na ikasimuliwa kikamilifu katika “Al-Irwâ‟”. Sheikhul Islâm Ibn Taymiyyah akaiingiza kwenye kitabu chake “Al-Mansak”: “Kama ulivyoikubali kutoka kwa kipenzi chako Ibrâhim.” Mimi sijawahi kuiona hiyo katika kitabu chochote cha Sunnah katika vitabu nilivyonavyo.

Page 60: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

47

Hajj (Yawmul Hajjul Akbar)1, na siku tatu zifuatazo (tarehe 11,

12 na 13 za Dhul-Hijjah). Amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

يق ذةص ك » يام اىتش «أ

“Kullu ayyâmit tashrîq dhab-hun”

“Siku zote za Tashrîq ni siku za kuchinja2.”

102. Muhrim anaweza kula katika alichokichinja na akachukuwa baadhi ya nyama yake nyumbani kwake kama alivyofanya

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم).

103. Muhrim amependekezwa awalishe maskini na wenye haja

kutokana na swadaka yake. Amesema Allâh ( وتعاىل سبحانه ):

“Na Ngamia (na Ng‟ombe na Mbuzi na Kondoo wa swadaka) tumekufanyieni kuwa katika alama za (dini ya) Allâh; kwa hao mnayo kheri (nyingi). Basi litajeni jina la Allâh juu yao

wasimamapo safu safu (mnawachinja); Na waangukapo ubavu, kuleni katika hao na mlishe mafakiri wanaoomba na

wanaorondearondea bila ya kuomba.” [Al-Hajj 22:36].

1 Imepokewa na al-Bukhârî kwa isnâd ya wapokezi iliyotundikwa na kwa isnâd iliyoshikanishwa na Abû Dâwud na wengineo, “Swahîh Abî Dâwud” (no. 1700, 1701). 2 Imepokewa na Ahmad na kuzingatiwa kuwa ni Swahîh na Ibn Hibbân. Mimi nadhani yakwamba ni hadîth yenye nguvu ukiizingatia njia yake ya upokezi, hiyo ndiyo sababu nikaitia kwenye”Swahîha yangu” (no. 2476).

Page 61: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

48

104. Mahujaji saba wanaweza kushirikiana kuchinja Ngamia mmoja au Ng‟ombe mmoja.

105. Yoyote asiyeweza gharama ya kuchinja Hady (mnyama) na afunge siku tatu akiwa katika kutekeleza Hajj na siku saba nyengine atakaporudi zake nyumbani.

106. Muhrim anaweza kufunga katika siku tatu za Tashriq kwani

Âisha na Ibn „Umar ( عنهما اهلل رضي ) wamesema: “Hakuna

aruhusiwaye kufunga katika siku za Tashriq isipokuwa Muhrim asiyekuwa na uwezo wa gharama ya kununua Hady.1

107. Kisha Muhrim atanyoa kichwa chake au atakata nywele zake,

chaguo la kwanza ndilo bora kwani Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

aliwaombea du‟â wenye kunyoa aliposema: “Yâ Allâh, warehemu wale walionyoa nywele zao.” Maswahaba wakasema: “Yâ Rasûlallâh, jee wale waliokata nywele zao?” Akasema tena

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم): “Yâ Allâh, warehemu wale walionyoa

nywele zao.” Mara mbili, na katika mara ya nne akasema

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم): “Na juu ya wale waliokata nywele zao.”2

108. Kinyozi na aanze kumnyoa Muhrim upande wake wa kulia kama

ilivyoelezwa katika hadîth ya Anas ( عنه اهلل رضي )3

1 Al-Bukhârî na wengineo wameyapokea haya. Imesimuliwa kikamilifu katika “Al-Irwâ‟ ul-ghalîl” (no. 964). Amesema Sheikhul Islâm Ibn Taymiyyah: “Mutamattî‟ asiyeweza kumiliki gharama ya Hady ni lazima afunge baadhi ya siku tatu kabla ya kuvaa Ihrâm yake ya Hajj katika siku ya Tarwiyah (tarehe 8th Dhul-Hijjah). Lakini rai hii ni ngeni mno, hata imefikia kukhalifu Ayah ya Qur‟ân na Sunnah. Allâh ndiye Mjuzi zaidi. 2 Imepokewa na Mashekhe wawili na wengineo kuifuatiliza kutoka kwa Ibn „Umar na wengineo. Imesimuliwa katiaka “Al-Irwâ‟” (no. 1084) 3 Imepokewa na Muslim na wengineo, vilevile imepokewa katika «Al-Irwâ‟» (no. 1085) na «Swahîh Abî Dâwud» (no. 1730). Ibn al-Humâm, mwanachuoni mkubwa katika madh-hab ya Hanafi amesema yakwamba wanavyuoni wa ki-Hanafi hawakuifuata Sunnah hii.

Page 62: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

49

109. Kunyoa nywele kunaruhusiwa kwa wanaume tu na sio wanawake. Lakini hatahivyo, wanaweza kuzikata nwele zao

kiyasi kwani Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) amesema: “Wanawake

hawaruhusiwi kunyoa nywele zao; badala yake wanatakiwa wazipunguze nywele zao (baada ya Hajj au „Umrah1). Mwanamke anaweza kufanya hivyo kwa kuzikusanya nywele zake pamoja, kisha azikate mwishoni mwake kwa urefu wa kiyasi cha ncha za vidole.2

110. Inaruhusiwa kwa Imâm atoe khutbah katika siku ya Nahr akiwa Minâ3 baina ya Jamarât4 kabla ya saa sita mchana5 awafundishe watu ibada watakiwazo kuzifanya katika siku hiyo.6

Twawâf Al-Ifâdha

111. Kisha Muhrim ataizunguka Nyumba mizunguko saba kwa namna ilivyoelezwa katika Twawâf al-Qudûm, isipokuwa hapa hatofanya Idhtwibâ wala Ramal (kutembea kwa haraka kwa hatua ndogo-ndogo).

112. Ni katika Sunnah kuswali rak‟ât mbili nyuma ya Maqâm (kituo cha Ibrâhim) kama ilivyosemwa na Az-Zuhri7, na kufanywa na

1 Imepokewa katika «AL-Ahâdîth as-Swahîhah» (no. 605) na «Swahîh Abî Dâwud» (no. 1732) 2 Amesema Sheikhul Islâm Ibn Taymiyyah: “Mtu yoyote mke/mume akipenda kupunguza nywele zake, azikusanye kwa pamoja na azikate mwishoni mwake kwa urefu wa kiyasi cha ncha za vidole. Lakini mwanamke asizidishe urefu huo.” 3 Imepokewa na al-Bukhârî na Abû Dâwud kutoka kwa kundi la Maswahaba, Tizama katika «Swahîh Abî Dâwud» (no. 1705, 1707, 1709, 1710) na «Mukhtasar al-Bukhârî» (no.847) 4 Imepokewa na Al-Bukhârî kwa isnâd ya wapokezi iliyotundikwa, na kwa iliyoshikamana na Abû Dâwud. «Swahîh Abî Dâwud» (no. 1700) na “Al-Irwâ‟ ul-ghalîl” (no. 1064). 5 Imepokewa na Abû Dâwud na wengineo. «Swahîh Abî Dâwud» (no. 1709). 6 Imepokewa na Abû Dâwud na wengineo. «Swahîh Abî Dâwud» (no. 1710). 7 Imepokewa na Al-Bukhârî kwa isnâd ya wapokezi iliyotundikwa na kwa iliyoshikamana na Ibn Abî Shaybah na wengineo. «Mukhtasar al-Bukhârî» (no. 319/ vol 1; Uk. 386).

Page 63: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

50

Ibn „Umar1 aliyesema: “Kila baada ya mizunguko saba, mtu na aswali rak‟ât mbili (nyuma ya Maqâm)2.

113. Kisha Muhrim atatembea baina ya As-Swafâ‟ na Al-Marwah – kama ilivyotangulia kuelezwa – kinyume cha Qârin na Mufrid; Sâ‟i ya kwanza inawatosheleza.

114. Kwa Twawâf hii, Muhrim ataruhusiwa kufanya mambo yote yaliyokuwa ni harâm kwake, hata kujamiiyana na mkewe.

115. Kisha ataswali swala ya Dhuhr akiwa Makkah. Amesema Ibn „Umar: “akiwa Minâ.3”

116. Kisha Muhrim atakunywa kutoka katika maji ya Zamzam.

Kukaa Minâ Wakati Wa Usiku

117. (Baada ya kutekeleza Twawâf al-Ifâdha) Muhrim atarudi tena Minâ na akae hapo kwa masiku ya Tashriq.

118. Kila siku baada ya zawâl (kupinduka kwa Jua) Muhrim atarusha vijiwe saba katika kila Jamrah (ukuta) katika Jamrât (kuta) tatu kama ilivyotangulia kuelezwa.

119. Muhrim na aanze kwenye Jamrah ya kwanza ambayo ndiyo iliyo karibu na Masjid al-Khaif, kisha ende mbele kidogo kwenye upande wa kulia asimame haliyakuwa ameelekea Qiblah na amuombe Allâh du‟â yoyote apendayo kwa kuinua mikono yake.4

1 Imepokewa na Al-Bukhârî kwa isnâd ya wapokezi iliyotundikwa na kwa iliyoshikamana na „Abdir Razzâq. «al-Mukhtasar» (no. 318). 2 Imepokewa na „Abdur-Razzâq (no. 9012) kwa isnâd nzuri ya wapokezi. 3 Mimi nadhani yakwamba huwenda aliswali kote mahali pawili, mojawapo akiwa Makkah na nyengine akiwa Minâ. Ya kwanza ilikuwa ni swala ya faradhi na hiyo ya pili ikiwa ni ya khiyari, kama ilivyowahi kutokea katika vita fulani alivyowahi kupigana.

4 Imethubutu yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alifanya hivyo kama

ilivyopokewa na Mashekhe wawili (al-Bukhârî na Muslim) na wengineo.

Page 64: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

51

120. Kisha atakuja kwenye Jamrah (ukuta) ya pili arushe vijiwe saba, halafu atasongea mbele upande wa kushoto, asimame hapo kwa muda mrefu amuombe Allâh kwa kuinua mikono yake.

121. Kisha Muhrim atarusha vijiwe kwenye Jamrah ya tatu, iitwayo Jamratul „Aqabah, akiiweka Nyumba kwenye upande wake wa kushoto na Minâ kwenye upande wake wa kulia, lakini hatosimama hapo kuleta du‟â‟ baada ya kumaliza kurusha vijiwe.

122. Katika siku ya pili na ya tatu, Muhrim atafanya kama alivyofanya katika siku ya kwanza ya Tashriq (yaani;kurusha vijiwe kwenye Jamrât Tatu).

123. Muhrim akitaka kuondoka (Minâ) baada ya kurusha vijiwe katika siku ya pili na akawa hakukaa (hapo) usiku wake kwa ajili ya kurusha vijiwe katika siku ya Tatu, anaruhusiwa kufanya hivyo.

Amesema Allâh ( وتعاىل سبحانه ):

“Na mtajeni Allâh katika zile siku zinazohisabiwa. Lakini

afanyaye haraka katika siku mbili (akarejea) basi si dhambi juu yake; na mwenye kukawiya pia si dhambi juu yake, kwa

mwenye kumcha Mungu.” [al-Baqarah 2:203]

Lakini kukaa kwa siku Tatu ni bora kwani hiyo ndiyo Sunnah (kamili).1

Riwaya zao zimefuatilizwa kutoka kwa Ibn Mas‟ûd. Yaliyowahi kupokewa kwenye baadhi ya vitabu kuhusu „Ibâdah ya Hajj yakwamba Muhrim aelekee al-Ka‟bah pindi anapokuwa akirusha vijiwe sio ya kweli na inakhalifu Sunnah swahîh kama nilivyoyaeleza katika «adh-Dha‟îfah» (no. 4864) 1 Amesema Sheikhul Islâm Ibn Taymiyyah: “Iwapo Muhrim atakaa Minâ mpaka kuzama kwa Jua (katika siku ya pili ya Tashriq), atakaa hapo usiku mzima na arushe Jamarât pamoja na watu katika siku ya Tatu.”

Page 65: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

52

124. Ni katika Sunnah kufanya „Ibâdah kwa mfumo ufuatao: Kurusha vijiwe, swadaka ya kuchinja, kunyoa au kupunguza nywele, Twawâf al-Ifâdha, na Sa‟î (kutembea baina ya As-Swafâ na Al-Marwah) kwa mutamattî‟; iwapo Muhrim atageuza mfumo huu, basi hatokuwa na madhara wala madhambi kwa hivyo. Amesema

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) kwa wale watakaobadilisha mfumo huu:

“Haina neno, haina neno.”

125. Wale watakaorusha vijiwe, lakini wakaona uzito kutekeleza

jambo hilo kwa mfumo aloutumia Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

A. Hawatokuwa na haja ya kukaa Minâ wakati wa usiku.

Amesema Ibn „Umar: “Al-„Abbâs alimuomba ruhusa Mtume ( صىل اهلل aweko Makkah wakati wa usiku badala ya kukaa Minâ (عليه وسلم

Mimi naamini yakwamba hii vilevile ni rai ya Wanavyuoni wasomi wakubwa kinyume cha Ibn Hazm aliyeshikilia rai iliyo kinyume cha hivyo katika kitabu chake, “Muhallâ”, (vol. 7/ Uk. 185). An-Nawawî akaiunga

mkono rai ya Wanavyuoni kwa kuyafasiri maneno ya Allâh (سبحانه وتعاىل):

“Lakini afanyaye haraka katika siku mbili (akarejea) basi si dhambi juu yake.”

Amesema katika “Al-Majmû‟” (vol. 8/ Uk. 283): “Hili neno, “Siku” linahusu mchana wa siku wala sio usiku wake.”. Imethubutu yakwamba „Umar na Ibn „Abdullâh walisema: „Yoyote atakayekaa Minâ katika siku ya pili mpaka Jua lichwe itambidi akae hapo usiku na arushe Jamarât pamoja na watu katika siku ya Tatu.‟” Amesema Mâlik katika kitabu chake cha “Al-Muwattâ‟”: “Amesema Ibn „Umar: „Muhrim hafai kuondoka hapo mpaka arushe Jamarât pamoja na watu kesho (yaani; katika siku ya Tatu).” Haya yamenukuliwa na Imâm Muhammad katika kitabu chake “Al-Muwattâ‟” (Uk. 233) na akasema baada ya maneno; “Sisi tunashirikiana naye (yaani; Imâm Mâlik) katika rai yake. Vilevile hiyo ndiyo rai ya Abû Hanîfah na wanavyuoni wengine kwa ujumla.”

Page 66: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

53

kwa sababu yeye alikuwa na jukumu la kuwapa Mahujaji maji.

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akamruhusu.”1

B. Wanaweza kurusha vijiwe vya siku mbili kwa siku moja.

Amesema „Âsim bin „Adiy ( عنه اهلل رضي ): “Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

aliwaruhusu wachunga Ngamia warushe vijiwe katika siku ya Nahr (tarehe 10th Dhul-Hijjah) na wachanganye urushaji wa vijiwe katika mojawapo ya siku ya pili au ya tatu.2

C. Wanaweza kurusha vijiwe wakati wa usiku. Amesema

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم): “Mchungaji anaweza kurusha vijiwe wakati

wa usiku na kuwachunga wanyama wake wakati wa mchana.”3

126. Muhrim anaweza kuzuru al-Ka‟bah na akalitufu (akalizunguka)

wakati wa nyusiku zake akiwa Minâ kwani Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

alifanya hivyo.4

127. Muhrim ni lazima atekeleze swala zake tano kwa nyakati zake misikitini awapo katika makaazi yake ya Minâ. Imependekezwa zaidi aziswali katika Msikiti wa Al-Khaif akiweza. Amesema

1 Imepokewa na Mashekhe wawili na wengineo. Imepokewa kikamilifu katika “Al-Irwâ” (no. 1079) na nikaichambua hiyo na kuifuatilia hadîth kutoka kwa Ibn „Abbâs yakwamba haikuswihi. 2 Imepokewa na wakusanyaji wa Sunnah, na kuzingatiwa kuwa ni swahîh na kundi la wanavyuoni na imesimuliwa katika “Al-Irwâ” (no. 1080) 3 Hadîth nzuri, imepokewa na al-Bazzâr, al-Baihaqi na wengineo ikafuatilizwa kutoka kwa Ibn „Abbâs. Al-Hâfidh ameizingatia isnâd yake ya wapokezi kuwa ni swahîh na imeungwa mkono kwa njia nyingi nyenginezo zilizotajwa katika “As-Swahîhah” (no. 2477). 4 Al-Bukhârî ameipokea hadith hii kwa isnâd ya kuangatika ya wapokezi (no. 287 katika chapa ya mukhtasari ya “Swahîh al-Bukhârî”), wanavyuoni wengine wameipokea kwa isnâd zilizounganishwa za wapokezi; wote wametajwa katika “As-Swahîhah” (no. 804)

Page 67: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

54

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم): “Mitume sabiini waliswali katika Masjid al-

Khaif.”1

128. Muhrim anapomaliza kurusha vijiwe katika siku ya pili au ya tatu katika siku za Tashriq atakuwa ashaimaliza „Ibâdah yake ya Hajj. Kisha atatakiwa ende Makkah na akae hapo kwa kiyasi atakachopenda Allâh. Wakati wa kukaa hapo atawajibika kuswali swala za Jamâ‟ah msikitini, bora zaidi msikiti wa Haram

kwani amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم): “Swala moja katika Msikiti

wangu wa Madinah ni sawa na swala elfu moja katika msikiti mwengine wowote isipokuwa swala katika Al-Masjidul Harâm. Swala moja katika Al-Masjidul Harâm, katika Mji wa Makkah, ni sawa na swala laki moja katika msikiti mwengine wowote.”2

129. Vilevile Muhrim anapendekezwa akithirishe kutufu (kuzunguka) al-Ka‟bah mara kwa mara na aswali hapo wakati wowote

apendapo, usiku au mchana. Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)amesema

kulihusu Jiwe Jeusi na Maqâm Ibrâhim: “Mtu atakayepangusa vitu hivyo (kwa mikono yake) atafutiwa madhambi yake. Na yoyote mwenye kuizunguka Nyumba, anapoinua mguu wake na kuukanyagia, Allâh atamuandikia Hasanah (thawabu), amfutie dhambi na amuinue daraja yake. Na yoyote atakayefanya hivyo kwa wiki nzima, malipo yake yatakuwa sawa na mwenye

kumuacha-huru Mtumwa3.” Amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

1 Imepokewa na at-Twabarâni na ad-Diyâ‟ al-Maqdisi katika “Al-Mukhtârah” na al-Mundhiri ameizingatia isnâd yake ya upokezi kuwa ni swahîh, ni kweli kama alivyosema kwani inayo njia nyengine iliyofafanuliwa kikamilifu katika “Tahdhîrus Sâjid” (Uk. 106-107). 2 Imepokewa na Ahamd na wengineo kutoka kwa Jâbir kutoka kwa Mtume

( وسلم عليه اهلل صىل ) kwa isnâd swahîh ya wapokezi. Wanavyuoni wengi

wanaizingatia hadîth hii kuwa ni swahîh. Wote wametajwa katika “Al-Irwâ” (no. 1129) 3 Imepokewa na at-Tirmidhî na wengineo. Inazingatiwa kuwa ni hadith nzuri na Ibn Khuzaymah, Ibn Hibbân, Al-Hâkim na wengineo. Imepokewa katika “Al-Mishkât” (no. 258) na “At-Targhîb” (vol. 2/ no. 120-122).

Page 68: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

55

“Enyi Banî (mwana wa..., watu wa ...) „Abd Manâf, musimkataze yoyote apendae kuizunguka Nyumba hii na kuswali ndani yake wakati wowote apendapo – usiku au mchana.”1

Twawâf Al-Wadâ‟

(Mzunguko Wa Kuaga)

130. Muda mchache tu Muhrim atakapomaliza mambo aliyokusudia kuyafanya na kuazimia kusafiri arudi zake nyumbani, anapaswa

kuizunguka Nyumba. Amesema Ibn „Abbâs (رضي هللا عنهما): “Watu

walikuwa wamezoweya kuondoka Makkah kutokea sehemu

yoyote wapendayo, kisha Mtume ( وسلمصىل اهلل عليه ) akasema:

“Haruhusiwi mtu yoyote kuondoka Makkah isipokuwa jambo la mwisho atakiwalo kufanya liwe ni kuizunguka Nyumba (yaani; al-Ka‟bah).2

131. Mwanzoni, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliamrisha yakwamba

mwanamke aliye kwenye heidh na akae Makkah mpaka atwahirike, kisha aizunguke Nyumba mzunguko wa kuaga3, lakini baadae (mwanamke) akaruhusiwa asafiri zake nyumbani

bila ya kungoja. Amesema Ibn „Abbâs: “Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

aliruhusu yakwamba mwanamke mwenye heidh anaweza

1 Imepokewa na wakusanyaji wa Sunan na wengineo. At-Tirmidhî ameizingatia kuwa ni swahîh, na vilevile al-Hâkim na adh-Dhahabi. Vilevile imepokewa katika “Al-Irwâ” (no. 481) 2 Imepokewa na Muslim na wengineo. Al-Bukhârî amepokea matamshi kama hayo. Vilevile imepokewa katika “Al-Irwâ” (no. 1086) na «Swahîh Abî Dâwud» (no. 1747). 3 Hii imethubutu katika hadith iliyopokewa na al-Hârith bin „Abdillâh bin „Aws iliyopokewa na Ahmad na wengineo. Vilevile imepokewa katika «Swahîh Abî Dâwud» (no. 1748).

Page 69: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

56

kuondoka Makkah kabla ya kufanya Twawâf al-Wadâ‟ iwapo atakuwa ashafanya Twawâf al-Ifâdhah.”1

132. Muhrim anaruhusiwa wakati akisafiri kurudi zake nyumbani, kubeba kiyasi apendacho cha Maji ya Zamzam kwani Maji hayo

yamebarikiwa. Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akijaza maji ya

zamzam katika mitungi yake na viriba vya ngozi, na alikuwa akiwamwagia maji hayo baadhi ya watu wagonjwa na akiwapa

wakinywa.2 Mara nyengine alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

akimtuma Sahl bin „Amru, Makkah, kabla ya kutekwa – akamletee kiyasi kingi awezacho cha Maji ya Zamzam. Sahl alikuwa akimletea mitungi miwili mikubwa iliyojaa Maji ya Zamzam.3

133. Muda mchache tu Muhrim anapomaliza kufanya Twawâful Wadâ‟ atatoka nje ya Al-Masjidul Harâm katika hali ya kawaida, sio kinyume-nyume. Na pia aanze kwa mguu wake wa kushoto4 na aseme:

صوي لع مد » الي إني وشي لم اليشأ

ـظيم أ »

1 Imepokewa na Ahmad kwa isnâd nzuri ya wapokezi inayoafikiana na masharuti ya Mashekhe wawili ya riwaya za kuswihi. Vilevile imepokewa katika “Al-Irwâ” (no. 1086) na imeungwa mkono na riwaya nyengine iliyofuatilizwa kutoka kwa „Âisha. Vilevile imepokewa katika «Swahîh Abî Dâwud» (no. 883). 2 Imepokewa na al-Bukhârî katika «At-Târîkh» na At-Tirmidhî kwa isnâd nzuri

ya wapokezi iliyofuatilizwa kutoka kwa „Âisha ( عنهما اهلل رضي ). Vilevile

imepokewa katika «As-Swahîhah» (no. 883). 3 Imepokewa na al-Baihaqî kwa isnâd nzuri ya wapokezi iliyofuatilizwa

kutoka kwa Jâbir ( عنه اهلل رضي ). Imeungwa mkono na riwaya nyengine

iliyopokewa katika Musannaf wa „Abdur-Razzâq (no. 2197). Ibn Taymiyyah amesema yakwamba watu wema wengi waliotutangulia (As-Salafus Sâlih) walikuwa wakibeba mitungi ya maji ya zamzam wanapo ondoka kwenda zao makwao 4 Tizama katika nukta za chini za kifungu No. 24

Page 70: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

57

“Allâhumma swalli „alâ Muhammadin wasallam; Allâhumma innî as‟aluka min fadhlik”

“Ewe Mola mfikilizie amani Muhammad; Ewe Mola hakika yangu mimi nakuomba fadhla zako.”

Page 71: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

58

Mambo Yanayofanywa Ya Uzushi Katika Hajj

„Umrah Na Ziyara

Nimeonelea yakwamba pana umuhimu kukipa mkiya kitabu hiki wa orodha ya mambo ya uzushi yanayofanywa na watu katika Hajj na ziyara ya Madinah na Baitul Maqdis (Al-Masjidul Aqswâ).

Watu wengi hawajazinduka na mambo hayo na kwahivyo hutumbukia ndani yake. Orodha ifuatayo itahudumu kama sehemu ya naswiha kwa watu hawa na tahadharisho dhidi ya kuyafanya hayo. Hii

ni kwa sababu Allâh ( وتعاىل سبحانه ) hakubali kitendo kilichokosa masharuti

mawili yafuatayo:

Kwanza: Kitendo chochote ni lazima kifanywe kwa ikhlâs kwa

ajili ya Uso Wake (عز وجل) Ya pili: Liwe ni jambo jema; yaani lifanywe kama lilivyo

kulingana na njia ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم). Ni rai iliyokubaliwa kwa

muafaka wa wanavyuoni yakwamba kitendo chochote ambacho

hakikufundishwa na Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) na ambacho hakikufanywa

kwa ikhlâs si katika Sunnah.

Sunnah imegawanywa kwa sampuli mbili: I. Suunah ya kivitendo (Sunnatu fi‟liyyah): Vitendo na maneno

ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم).

II. Sunnah ya kuacha (Sunnatu tarkiyyah): Vitendo vyote vya

„Ibâdah ambavyo Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) hakuwahi kuvifanya (wala

hakuwapendekezea wafanye).

Kwa mfano, kuadhini kwa ajili ya swala mbili za „Idd na kwa ajili ya kumzika mtu. Ingawa kuadhini ni kitendo cha „Ibâdah lakini katika

nyakati hizi makhsusi hazifai kuadhiniwa kwa sababu Mtume ( صىل اهلل عليه

Page 72: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

59

hakufanya hivyo. Maswahaba watukufu waliyafahamu haya (وسلم

kikamilifu, kwa hivyo, waliwaonya Waislamu dhidi ya uzushi wa kila aina kwa ujumla. Hudhaifah Ibn al-Yamân, kwa mfano, amesema:

“Kila „ibada ambayo Maswahaba wa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

hawakuifanya, musiifanye,”. Ibn Mas‟ûd ( عنه اهلل رضي ) amesema:

“Fuateni njia ya (Mtume wa Allâh) wala musizue (tendo la „Ibâdah) kwani kwa hakika mumetoshelezwa kikamilifu (kwa ambayo Allâh na Mtume wake waliyowaletea). Basi shikamaneni na njia (maamrisho) ya asili.”

Pongezi kwa yule aliyeafikiwa na Allâh kwa kumtakasiya Yeye

„Ibada na kufuata Sunnah za Mtume wake (صىل اهلل عليه وسلم) na wala asiwe

ni mwenye kuichanganya na bid‟ah, kwahiyo anabashiriwa kwa kutakabaliwa na Allâh twa‟a yake na kumuingiza kwenye Pepo Yake. Allâh atuja‟aliye tuwe ni miongoni ma wenye kusikiliza kauli Yake na kufuata yaliyo mazuri.

Jua yakwamba, maregeo ya bid‟ah hizi zilizoashiriwa yanaregea katika mambo haya yafuatayo:

La Kwanza: Ahâdîth dhaifu zisizofaa kunasibishwa na Mtume ( صىل اهلل wala kutumia hukmu zake kama nilivyochambua katika (عليه وسلم

«Swifat Swalâtun Nabiy» na hii ndiyo rai ya Ibn Taymiyyah na wengineo.

La pili: Ahâdîth za kuzua (mawdhû‟ah) au zisizo na asili zenye udanganyifu ambao baadhi ya Fuqahâ‟ wasoweza kuzitambua. Kama ilivyo, wao huzichukuwa hizo kuwa ni marejeo ya „ilmu na kujenga baadhi ya hukmu zao, zinazogeuka na kuwa ni uzushi mtupu katika dini.

La tatu: Hatima na mapendekezo ya baadhi ya ma-fuqahâ‟, hususan hawa katika zama zetu, ambayo yasiyokuwa na misingi ya dalili zilizo swahîh lakini wakazichukulia Sunnah za kufuatwa. Wale

Page 73: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

60

wenye fahamu zenye miangaza hawadanganyiki na uzushi huu kwani hakuna sheriya (za kufuatwa) isipokuwa za Allâh na yaliyopendekezwa na wanavyuoni walio wasomi wa kihakika (kulingana na hukmu za Qur‟ân Takatifu na Sunnah) lakini hata haya mapendekezo hayafai kuzingatiwa kama Sunnah kwani baadhi yao hayaambatani na Sunnah

za utenda-kazi za Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) – kama nitakavyo

kuyafahamisha baadae.

La Nne: Ada za ki-mila na mambo ya Khurâfât ambayo dini haikuzipa mazingatio yoyote, wala fahamu kuzielewa – hata kama baadhi ya watu wajinga wamekuwa wakiyafanya na kuzifanya kuwa ndizo hukmu zao, na hata ikiwa wale waliodai kuwa ni wanavyuoni wamewaunga mkono.

Inapasa kufahamika waziwazi yakwamba mambo ya kuzua katika dini yako katika sampuli nyingi na hatari nyingi ambayo ni yenye kutafautiana moja na jengine. Baadhi ya haya mambo ya kuzua huwenda yakampelekea mtu kwenye ukafiri na ushirikina na mengine ni mepesi kuliko hayo. Lakini hatahivyo, hata lile dogo miongoni mwa hayo mambo ya kuzua katika dini limeharamishwa. Hakuna kitu kama

“Bid‟ah ya makruhu”. Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) amesema:

«ك ةدغث طلىث ، وك طلىث ف انلار »

“Kullu bid‟atin dhwalâlah, wa kulla dhwalâlatin fîn Nâr”

“Kila bid‟ah ni upotofu, na kila upotofu (mwisho wake) ni Motoni.”

Imâm ash-Shâtibî ( اهلل رحمه ) ni miongoni mwa wanavyuoni wale

waliokuwa na utaalamu mkubwa katika kuelezea suala hili kwa kina katika kitabu chake «Al-I‟tiswâm» kutokana na utambuzi wake (mambo ya uzushi) na hatari zao juu ya Waislamu.

Page 74: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

61

Inatutosheleza sisi yakwamba amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

« « خ خ د ة ع د ي ت ض ث غ د ة ب اض ص كي خ ث ب ال ز اضخش إن الل“Innallâha Ihtajara at-tawbatu „an kulli swâhib bid‟ata hattâ

yada‟ bid‟atahû”

“Hakika Allâh ameiwekea kizuizi toba ya mwenye kufanya bid‟ah mpaka awache bid‟ah zake.”

Hadîth hii imepokewa na at-Twabarânî na adh-Dhiyâ‟ Al-Maqdisî katika «Al-Ahâdîth Al-Mukhtârah» kwa isnâd nzuri ya wapokezi, na imezingatiwa kuwa ni hadîth nzuri na al-Mundhiri.

Katika kuhitimisha, ningelipenda kuwapa wasomaji wangu kipande cha naswiha ambacho mwanachuoni mkubwa Sheikh Hasan bin „Ali Al-Barbahârî – mfuasi wa Imâm Ahmad – alichowapa wanafunzi wake: „Jitahadharini na hata mambo madogo ya uzushi; yanaweza kukuwa mpaka yawe makubwa. Kila Bid‟ah unayoiona katika Ummah huu (taifa la Uislamu) ilianza kama kitu kidogo ambacho watu wengi wakadanganyika nacho, kisha kikaanza kukuwa mpaka likawa kubwa sana ambalo watu wakaliamini kuwa ni katika dini. Kwahivyo, jitahadhari na kila unachosikiya (na kusoma) hususan ya hao (watu) wa zama zako; usiwe na pupa la kuyachukuwa mpaka uhakikishe yakwamba ni ya katika Sunnah za Mtume wa Allâh au za Maswahaba wake. Iwapo ni hivyo, yachukuwe ushikamane nayo, na wala usiyageukie mengine (yaani; mambo ya bid‟ah) usije ukatumbukia Motoni. Unatakikaniwa ujuwe - Allâh akurehemu – yakwamba hapana imani ya mtu yoyote katika Uislamu iliyokamilika mpaka afuate kwa Ikhlâs (njia ya Mtume). Yoyote mwenye kudai yakwamba kuna mambo ambayo Maswahaba wa Mtume hawakuyafikisha kwetu, basi atakuwa amewazulia urongo na hilo linapelekea kwenye kutisha kutokuwepo kwa umoja (baina ya Waislamu). Na mwenye kusema hayo amepotoka na kuwapotosha wengine, kuingiza kwenye Uislamu mambo

Page 75: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

62

yasiyokuwemo.

Allâh amrehemu Imâm Mâlik, amesema: “Ummah huu (yaani; Taifa la Uislamu) hautofaulu isipokuwa kwa lile lililowafanya kizazi cha mwanzo kufaulu. Lolote ambalo halikuwahi kuwa la dini katika zama zao halifai kuwa ni la dini milele.”

Twaziomba amani na baraka za Allâh zimshukie Mtume wetu aliyesema: “Sikuwacha kitendo chochote cha „Ibâdah kinachowakurubisha kwa Allâh isipokuwa nimewaamrisha mutekeleze. Na sikuwacha chochote chenye kuwaepusha na Allâh, na kuwakurubisha na Moto isipokuwa nimewakataza.”

Kila Sifa njema ni yenye kumstahiki Allâh, ambaye kwa ne‟ma zake hutimia mambo mema.

Bid‟ah Za Kabla Ya Kuvaa Ihrâm

1. Kujizuiya kusafiri, kuoa, kufanya kazi zako na mambo mengineyo katika mwezi wa Safar.

2. Kuvunja safari pindi mwezi unapofifia na iwapo mwezi utakuwa katika kituo cha scorpion [alama ya nane ya unajimu].

3. Kuwacha kuisafisha nyumba baada ya mtu anaposafiri.

4. Kuswali rak‟ât mbili unaposafiri kwenda Hajj na ukasoma Sûratil Fâtihah na Al-Kâfirûn katika rak‟ah ya kwanza na Sûratil Fâtihah na Ikhlâs katika rak‟ah ya pili. Atakapomaliza, atasema:

اى » « ....ج س ح م إيل و ت ش ت ا م ة ي“Allâhumma bika intasharat wa ilayka tawajjahtu ...”

Page 76: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

63

“Ewe Mola, mimi nasafiri kwa usaidizi wako na (naja) kwako nataka kuwa karibu nawe ...”

Kisha usome Aya ya Kursi, Al-Ikhlâs, Al-Falaq, na Sûrat An-Nâs ... na mengineo yaliyokuja ndani ya baadhi ya vitabu vya fiqh.

5. Kuswali swala yenye rak‟ nne.

6. Kusoma kwa yule anayetaka kwenda Hajj wakati anapotoka nyumbani kwake, mwisho za sûrat Âl-Imrân, Al-Kursi, Al-Qadr na Al-Fâtihah na kuamini yakwamba sura hizo na aya hizo zitamsaidia kukidhi mahitaji yake hapa ulimwenguni na kesho akhera.

7. Kusoma Takbîr na adhkâr nyengine kwa sauti kubwa wakati mahujaji wanapoanza safari yao na wakati watakaporudi.

8. Kuadhini wakati mahujaji wanapotoka majumbani mwao (kuwaaga).

9. Kusherehekea tukio la kulivisha al-Ka‟bah tandiko.1

10. Kuwaaga Mahujaji kwa kucheza miziki (ngoma) – kama wanavyofanya baadhi ya nchi fulani.

11. Kusafiri peke yako na kudai yakwamba anatakiwa mtu amfanye Allâh kama mwendani wake katika safari – kama wanavyoamini Masufi.

12. Kusafiri bila ya kuchukuwa furushi la kukidhi haja zako kwa madai yakwamba huu ndio msimamo wa kihakika wa kumtegemea Allâh.

13. Kusafiri kwa lengo la pekee la kuzuru makaburi ya Mitume na watu wema.

1 Bid‟ah hii imeondolewa mbali, alhamdulillâh, miaka mingi iliyopita lakini ile nyengine inayoifuata hiyo bado ingalipo. „Ali bin Al-Qâsim amesema katika Al-Bâjûrî (vol. 1/ Uk. 41): “Haifai kusherehekea tukio la kulivisha al-Ka‟bah tandiko na Maqâm Ibrâhîm na mfano wake.

Page 77: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

64

14. Kutekeleza mkataba wa ndoa na mwanamke ambaye ashaolewa iwapo amekusudia kufanya Hajj na akawa hana Mahram pamoja naye – kujifanya kuwa ni Mahram wake.1

15. Kuzindua uhusiano wa ki-undugu baina ya mume na mke ambao si Mahram na kudai yakwamba kwa njia hii atakuwa ni kama ndugu yake wa kiume au Mahram wake na anaweza kushirikiana naye juu ya msingi huu.

16. Kusafiri kwa mwanamke pamoja na kundi la wanawake “waaminifu” pasi na Mahram, au kuwazingatia Mahram wa wanawake wengine kuwa ni Mahram wake na kwa wanawake wengine pamoja naye.

17. Kuwatoza kodi Mahujaji.

18. Kuswali rak‟ât mbili mahali popote (Muhrim) anapojipumzisha kisha akasema: “Ewe Mola, pabariki mahali pangu pa kupumzika, kwa hakika Wewe ndiye mwenye kubariki sehemu zetu za mapumziko.”

19. Kusoma sûratil Ikhlâs mara kumi na moja, Al-Kursî mara moja na kila anapopumzika asome mara moja aya isemayo:

“Na hawakumhishimu Allâh kama inavyotakiwa kumhishimu.”

[Al-An‟âm 6:91]

20. Ale kitunguu cha kila ardhi atakayopita Muhrim.

21. Kusafiri katika nchi fulani au mahali fulani kwa ajili ya kupata baraka zake – ingawa hukmu ya ki-Islamu haikuzithibitisha sehemu hizo – kama vile: sehemu inayodaiwa kuwepo nyayo za Mtume

1 Bid‟ah hii na hiyo inayoifuata ndizo zenye kutisha zaidi kwani zina mbinu za kutaka kuichezea sheriya ya Uislamu na huwenda zikampelekea mtu kufanya kitendo cha uzinifu.

Page 78: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

65

katika nchi ya Jerusalem, na Masjidul-Qadam ulioko Damascus, na makaburi ya Mitume na watu wema.1

22. Kuchomoa silaha kutoka katika ala yake unapofika Tabûk.

Bid‟ah Zinazohusiana Na Ihrâm, Talbiyah, Na Mengineyo

23. Kuvaa sampuli maalum ya viatu vyenye muundo fulani na hali zijulikanazo kwenye vitabu vya fiqh.

24. Kuhirimiya kabla ya kufika Al-Mîqât.

25. Kuvaa nguo za Ihrâm kwa mtindo wa Idhtwibâ‟ kuanzia mwanzo wa Ihrâm.

26. Kuitamka niya ya Hajj au „Umrah (yaani; kusema : Nakusudia kufanya Hajj au „Umrah mwaka huu ...)

27. Kuitekeleza Hajj kimya bila ya kutamka neno lolote.

28. Kusoma Talbiyah pamoja na watu wengine kwa sauti moja (kwa pamoja).

29. Kusoma Takbîr na Tahlîl badala ya Talbiyah.

30. Baada ya Talbiyah, kusoma:

إني » ريد الز اليه يل أ غني لع ـيسي

وأ داء ـرط

أ ن وتلتي الي

يج إني ـاسػين ف الزي ـريظخم اء أذ ي ال « لم..... اشخشاةا

“Allâhumma innî urîdul Hajj fayassirhu liy wa‟a-niy „alâ arâ‟iy fardhahû; wataqabbalahû minnî. Allâhumma innî nawaytu

1 Imepokewa yakwamba „Umar ( عنه اهلل رضي ) aliwaona watu wakati wa Hajj

wakielekea kwa wingi sehemu fulani. Akaulizia kupahusu mahali hapo na

akaambiwa yakwamba hapo palikuwa ni mahali ambapo Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل )

aliwahi kukaa wakati fulani. Kisha akasema: “Kitendo hiki (yaani; kuzifanya alama za Mtume kuwa ni sehemu za „Ibâdah) kwa hakika kiliwaangamiza watu wa Kitabu. Mahali popote inapokuwajibikia swala, unatakiwa uswali.”

Page 79: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

66

adhâî farîdhatuka fil Hajj faj‟alaniy minalladhina istajâbu laka …”

“Ewe Mola, hakika yangu mimi nakusudia kufanya Hajj,

nakuomba unisalihishie na unisaidie niitekeleze kisawa-sawa na unitakabalie. Ewe Mola, nakusudia kutekeleza uwajibu ambao

ulionifaridhia, nakuomba unija‟aliye niwe miongoni mwa wenye kukuitikia ...”

31. Kwenda kwenye misikiti mengine ya Makkah na pambizoni mwake badala ya kwenda katika Al-Masjidul Harâm kama vile msikiti ulio karibu na As-Swafâ‟, Safh Abî Qabays, na Masjid Al-Mawlid na

misikiti mengine iliyojengwa kwenye athari za Mtume ( صىل اهلل عليه .(وسلم

32. Kufanya ziyara kwenye milima na sehemu nyengine za Makkah kama vile: Mlima Hirâ‟, Mlima ulioko karibu na Minâ unaodaiwa yakwamba Ismâ‟îl alikombolewa hapo ... na kadhaalika.

33. Kuswali, kwa kukusudia, katika Masjid „Âisha ulioko At-Tan‟îm , na wala si kwengine popote.

34. Kujipangusa uso na kifua mbele ya Nyumba (al-Ka‟bah) kama jinsi wafanyavyo Makristo wanapofanya maombi yao.

Uzushi Unaofanywa Katika Twawâf

35. Kuoga kabla ya kufanya Twawâf.

36. Wanaume kuvaa soksi ili wasipate kuguza sakafu ya choo na kuvaa glovu ili wasipate kuwagusa wanawake.

37. Kuswali rak‟ât mbili wanapoingia Al-Masjidul Harâm kama Tahiyyatul Masjid (maamkuzi ya Msikiti).1

1 Maamkuzi ya Al-Masjidul Harâm hufanywa kwa kuitufu Nyumba na kisha kuswali rak‟ât mbili nyuma ya Maqâm Ibrâhîm kama ilivyofanywa na Mtume

Page 80: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

67

38. Kusema, “Nakusudia kumfanyia Twawâf mtu dhaifu fulani na fulani.

39. Kuinua mkono unapoligusa Al-Hajarul Aswad kama inavyofanywa katika swala.

40. Kupiga kura kwa ajili ya kulibusu Al-Hajarul Aswad.

41. Kung‟ang‟ana na Mahujaji wengine katika kulibusu Al-Hajarul Aswad na kumtangulia Imâm katika swala, hususan anapotoa salâm, ili upatilize kwenda kulibusu Jiwe Jeusi.

42. Kuiseta Ihrâm yako unapokwenda kuligusa Jiwe Jeusi au Pembe ya Yamâni.

43. Kusema pindi unapoligusa Al-Hajarul Aswad: “Ewe Mola, (Naligusa hili) Nikiwa nakuamini Wewe na Kitabu chako.”

44. Kusema pindi unapoligusa Jiwe Jeusi: “Ewe Mola, najilinda Kwako kutokamana na kibri, ufukara, na hizaya za hapa ulimwenguni na kesho akhera.”

45. Kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto unapotufu.

46. Kusema unapokuwa mbele ya mlango wa Ka‟bah: “Ewe Mola, kwa hakika hii ni Nyumba Yako, na Haram hii ni Haram Yako, na Wewe ndiye mwenye kuieneza amani. Hapa ndipo mahali - akielekeza kidole chake kwenye Maqâm Ibrâhim - pa wale wenye kuomba hifadha Yako na Moto wa Jahannam.

47. Kumuomba Allâh haliyakuwa umesimama karibu na pembe ya „Irâq na kusema: “Ewe Mola, najilinda kwako na shaka, na ushirikina, na migogoro (na Waislamu), unafiki, tabia mbaya, na mageuko katika mali, jamii na vizazi.”

48. Kumuomba Allâh (سبحانه وتعاىل) ukiwa chini ya Al-mîzâb (kingo za maji)

ya Ka‟bah kwa kusema: “Ewe Mola niweke chini ya kivuli chako katika siku ambayo hakuna kivuli isipokuwa kivuli chako.”

Tizama katika «Al-Qawâ‟id An-Nûrâniyyah» cha Ibn .(صىل اهلل عليه وسلم)

Taymiyyah.

Page 81: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

68

49. Kumuomba Allâh haliyakuwa unalizunguka al-Ka‟bah kwa mwendo wa ramal huku ukisema: “Ewe Allâh itakabali Hajj yangu, nisamehe madhambi yangu, nilipe kheri kwa Sâ‟i yangu, nisababishie biashara zangu zitoe matunda, Ewe Mtukufu, Mwenye kusamehe.

50. Kusema katika mizunguko minne ya mwisho: “Ewe Allâh, nisamehe (madhambi yangu) na unirehemu, nisamehe uyajuayo (katika madhambi yangu). Kwa hakika wewe ndiye Mtukufu, Mkarimu.

51. Kuibusu Pembe ya Yamâni.

52. Kuzibusu Pembe mbili za Shâmi, Maqâm Ibrâhim na kuzigusa.

53. Kupangusa kuta za Ka‟bah na Maqâm Ibrâhim.

54. Kuomba baraka katika Al-„Urwah Al-Wuthqâ: sehemu za juu za ukuta wa Nyumba unaoelekea mlango wa Nyumba. Watu wengi wanadhania yakwamba yoyote mwenye kuugusa kwa mikono yake atakuwa ameishikilia imara „Urwah Wuthqâ (fundo lililofungwa kwa nguvu).

55. Baadhi watu huwacha wazi vitovu vyao na wakalala kifudifudi ndani ya Nyumba ili vitovu vyao viguse msumari ulioko katikati ya Nyumba wakidai yakwamba msumari huo ndicho kitovu (katikati ya) cha ulimwengu mzima.

56. Kufanya Twawâf wakati mvua inaponyesha wakiamini yakwamba yoyote mwenye kufanya hivyo, atasamehewa madhambi yake yote yaliyopita.

57. Kutafuta baraka kutoka kwenye maji yanayomwagika kutoka kwenye pambizo za al-Ka‟bah.

58. Kuwacha Twawâf ikiwa nguo ya mtu zimechafuka.

59. Kunyunyiza makombo ya maji ya zamzam baada ya Muhrim kuyanywa (maji hayo) kwenye kisima cha zamzam, huku akisema: “Ewe Mola, nakuomba unipe riziki kundufu, na „ilmu yenye

Page 82: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

69

manufaa, na pozo ya kila maradhi ...”

60. Kuoga kwa maji ya zamzam.

61. Kuziosha ndevu, sarafu na nguo kwa maji ya zamzam kwa ajili ya kupata baraka.

62. Kushusha pumzi kila baada ya kupiga tama la maji ya zamzam ambapo kisha mwenye kunywa huinua macho yake na kuelekea Al-Ka‟bah – kama ilivyotajwa katika baadhi ya vitabu vya fiqhi.

Uzushi Unaofanywa Katika Sa’î

63. Kutawadha kwa ajili ya kutembea baina ya As-Swafâ na Al-Marwah kwa kuamini yakwamba yoyote mwenye kufanya hivyo atalipwa hasanah elfu sabiini kwa kila hatua atakayokanyaga.

64. Kupanda Mlima wa As-Swafâ mpaka mtu aguse ukuta wake.

65. Kumuomba Allâh ukiwa unashuka kwenye mlima wa As-Swafâ kwa kusema: “Ewe Mola niongoze nipate kutekeleza kulingana na Sunnah za Mtume wako, nifishe haliyakuwa na imani ya dini yake (Uislamu), niokoe kutokamana na mitihani ya upotofu kwa Rehma zako. Wewe ndiye mwenye rehma zaidi katika wenye rehma.”

66. Kusema haliyakuwa unafanya Sa‟î: “Ewe Mola, nisamehe (madhambi yangu), nirehemu, nisamehe vitendo vyangu unavyovijua. Kwa hakika wewe ni Mtukufu, mwenye huruma. Yâ Allâh, ikubali Hijjah yangu (au „Umrah), niswamehe madhambi yangu.” Kisha useme Takbîr mara tatu.1

67. Kufanya Sa‟î mara kumi na nne (badala ya mara saba) na kumalizia As-Swafâ.

68. Kurudia Sa‟î mara kwa mara wakati wa Hajj na „Umrah.

69. Kuswali rak‟ât mbili baada ya kufanya Sa‟î.

1 Kwa hakika imepokewa yakwmba Ibn Mas‟ûd na Ibn „Umar wamesema: “Ewe Mola nisamehe madhambi yangu, nirehemu, Wewe ndiye Mtukufu, Mwenye huruma.” (no. 55)

Page 83: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

70

70. Kuendelea kufanya Sa‟î baina ya As-Swafâ na Marwah wakati ambapo swala ya faradhi inaswaliwa na kuendelea kufanya hivyo mpaka swala imalizike.

71. Kusoma du‟â‟ maalum unapofika Minâ kama ilivyotajwa katika «Al-Ihyâ‟»: “Yâ Allâh hii ni Minâ, basi nakuomba fadhla Zako kama ulivyowafadhili nazo waja wako wema.” Baada ya kutoka mahali hapo, husema: «Yâ Allâh, nija‟aliye nitoke kwa njia bora ambayo sijawahi kuitokea»

Bid‟ah Zinazofanywa „Arafah

72. Kusimama juu ya Mlima wa „Arafah tarehe 8th Dhul-Hijjah kwa saa moja kama tahadhari pasije pakapatikana makosa katika kuuona mwezi kongo wa mwezi wa Dhul-Hijjah.

73. Kuwasha mishumaa mengi katika sehemu ya Minâ usiku wa kuamkia siku ya „Arafah.

74. Kumkumbuka Allâh katika usiku wa kuamkia siku ya „Arafah kwa maneno kumi, kila mojawapo uliseme mara elfu moja: “Ametakasika Yule ambaye „Arshi Yake iko mbinguni; Ametakasika Yule ambaye makanyagio Yake yako kwenye ardhi; Ametakasika Yule ambaye njia yake iko kwenye bahari. ...” na kadhaalika.

75. Kusafiri, tarehe 8th Dhul-Hijjah, kutoka Makkah hadi „Arafah kwa mara moja.

76. Kutembea kutoka Minâ hadi „Arafah katika wakati wa usiku.

77. Kumulika taa na mishumaa juu ya Mlima wa „Arafah katika usiku wa kuamkia siku ya „Arafah.

78. Kuoga siku ya „Arafah.

79. Kusema unapokurubia „Arafah na kuuona Mlima wa Jabal Ar-Rahma:

كب » أ والل ، ول إل إل الل د لل ، وال « شتطان الل

Page 84: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

71

Subhânallâh, walhamdulillâh, walâilâha illallâh”

“Ametakasika Allâh, kila shukrani zinamstahiki Allâh, na hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allâh; na

Allâh ni mkubwa zaidi.”

80. Kuelekea „Arafah kabla ya wakati wake kufika (yaani; saa sita za mchana katika siku ya „Arafah).

81. Kusoma Tahlîl juu ya Mlima wa „Arafah mara mia moja, kuisoma

sûratil Ikhlâs mara mia moja, kisha kumtumia salamu Mtume (ملسو هيلع هللا ىلص) na kuongezea mwishoni mwake: “Na utuswalie na sisi pia, Yâ Allâh.” Mara mia moja.

82. Kunyamaza kimya katika Mlima wa „Arafah na kuwacha kuomba du‟â‟.

83. Kuupanda Mlima wa Ar-Rahma katika siku ya „Arafah.

84. Kuingia ndani ya Qubbah lililojengwa juu ya Mlima wa Ar-Rahma liitwalo “Qubbah la Âdam”, kuswali ndani yake na hata kulitufu.

85. Kuamini yakwamba Allâh hushuka katika jioni ya siku ya „Arafah juu ya Ngamia mweupe na kupeana mikono na wale waliopanda wanyama wao na kuwakumbatia wale wenye kutembea kwa miguu.

86. Kutolewa khutbah mbili na Imâm katika siku ya „Arafah na kukaa kwa muda baina ya khutbah ya kwanza na ya pili, kama ifanywavyo katika siku ya Ijumaa.

87. Kuswali Dhuhr na „Asr kabla ya kutoa khutbah.

88. Kuadhini kwa ajili ya swala za Dhuhr na „Asr katika siku ya „Arafah kabla ya Imâm hajamaliza khutbah yake.

89. Baadhi ya ma-Imâm huwaamrisha wakaazi wa Makkah baada ya kumaliza swala zao (za kufupishwa) wakiwa „Arafah wakamilishe swala zao kwa vile wao ni wakaazi wa hapo kinyume cha mahujaji wengine.

Page 85: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

72

90. Kuswali swala zisizokuwa za faradhi (swala za Sunnah) baina ya Adhuhuri na Al-„Asr ukiwa „Arafah.

91. Kusoma adh-kâr makhsusi au Du‟â‟ ukiwa „Arafah kama ile ya Al-

Khidhr (عليه السالم) iliyotajwa kwenye «Al-Ihyâ»: “Ewe

usiyeshughulishwa na chochote ...”, na sampuli nyengine za du‟â zenye urefu wa kiyasi cha kurasa tano kwa uchache.

92. Kuharakisha (kwenda Muzdalifah) kutoka „Arafah kabla ya kutwa kwa jua.

93. Kuamini yakwamba malipo ya kusimama katika uwanja wa „Arafah siku ya Ijumaa ni sawa na malipo ya kufanya Hajj mara 72.

94. Kufanywa kitu kinachoitwa “Ta‟rif” na baadhi ya watu ambao si Mahujaji; yaani wao hukutana katika wakati wa jioni ya „Arafah ndani ya misikiti, au mahali popote nje ya mji au kijiji wakimuomba Allâh, wakimkumbuka na kuinua sauti zao, wakitoa khutbah na kuimba mashairi, na kufanya mambo kama wafanyayo watu wa „Arafah.

Bid‟ah Zinazofanywa Muzdalifah

95. Kutembea kwa haraka wakati wa kukimbilia Muzdalifah kutoka „Arafah.

96. Kuoga mtu ili aupitishe usiku wake Muzdalifah.

97. Baadhi ya Mahujaji hufadhilisha kuingia Muzdalifah kwa miguu wakiamini yakwamba hii ndiyo njia ya kupatukuza mahali hapo.

98. Kusoma du‟â‟ ifuatayo unapofika Muzdalifah: “Yâ Allâh hii ni Muzdalifah ambayo unayowasababisha watu wengi tafauti kukusanyika. Twakuomba Wewe (uwatosheleze) mahitaji yetu ... na kadhaalika.” [Al-Ihyâ].

99. Kuichelewesha swala ya kutwa kwa Jua unapofika Muzdalifah na kujishughulisha na kuokota vijiwe (vya kurushwa katika

Page 86: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

73

Jamarât).

100. Kuswali swala mbili za sunnah baada ya swala ya kutwa kwa Jua (Maghrib) na kabla ya swala ya jioni („Ishâ‟), au kuiswali Sunnah hii na Sunnah ya „Ishâ‟ na witr baada ya kuswali swala mbili za faradhi (yaani; Maghrib na „Ishâ‟).

Hii ni rai ya Al-Ghazâlî.

101. Kumulika miangaza katika usiku wa kuamkia siku ya Nahr (tarehe 10th Dhul-Hijjah) na katika sehemu za Muzdalifah.

102. Kukesha usiku wa kuamkia siku ya Nahr kwa kuswali na kumtaja Allâh.

103. Kuweko Muzdalifah kwa muda mchache badala ya kuwa hapo usiku mzima.

104. Kuisoma du‟â‟ ifuatayo unapofika Muzdalifah:

« شػر الرام بقي الي لام اليج الرام و ال وال ك ةيؼ والر وح ر أ

د ا م لم نرام الطيث والص لم يا ذا اللل وال دخيا دار الص « وأ

“Allâhumma bihaqqil mash‟arul Harâm wal baytul Harâm war-Rukni wal-Maqâm, ablagha ruhu Muhammadin minnâ At-

Tahiyyâtu wassalâm wa ad-khilna dârus Salâm yâdhal jalâli wal ikhrâm”

“Ewe Mola, nakuomba kwa haki ya Al-Mash‟arul Harâm (Muzdalifa), kwa haki ya baytul Harâm (Al-Ka‟bah), Mwezi mtukufu (Dhul-Hijjah), Pembe (Al-Yamânî) na (kwa haki ya) Maqâm Ibrâhîm uzifikishe salamu zetu (Salâm) na amani kwa

roho ya Muhammad (صىل اهلل عليه وسلم) na utuingize nasi kwenye

Dârus Salâm (Pepo), Wewe ni Mola wa Utukufu na Ikrâm.1

1 Duâ‟ hii si uzushi tu bali ni kukhalifiana na Sunnah. Ndani yake muna kumlilia Allâh kwa utukufu wa Muzdalifah, Ka‟bah … na kadhaalika. Ingawaje kumlilia Allâh kunatakiwa kuwe ni kwa Majina yake na Sifa zake. Wanavyuoni wa ki-Hanafi wanalichukia jambo la mtu kulia kwa Allâh kutokana na utukufu wa sehemu hizo, kama ilivyotajwa katika «Hâshiyat Ibn

Page 87: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

74

105. Amesema Al-Bâjûrî (Uk. 318): “Ni katika Sunnah kuokota vijiwe – atakavyorusha Muhrim katika siku ya Nahr – kutoka Muzdalifah, ambavyo ni saba – na aokote vijiwe vilivyobaki kutoka katika Wâdî Muhassir.

Uzushi Unaofanywa Katika Kurusha Vijiwe

106. Kuoga kabla ya kurusha vijiwe.

107. Kuviosha vijiwe kabla ya kuvirusha.

108. Kumsifu Allâh (سبحانه وتعاىل) unaporusha vijiwe badala ya kusema

Takbir.

109. Kuongezea baada ya kusema Takbir: “(Takbir yetu ni) kwa ajili ya kumshinda Sheitwân. Yâ Allâh, ikubali Hajj yangu, ibariki Sa‟î yangu, nisamehe madhambi yangu, Mimi naamini Kitabu chako na kufuata Sunnah za Mtume wako.”

110. Kusema wakati wa kurusha vijiwe: “Kwa jina la Allâh, Allâh ni mkubwa zaidi na kwa hakika Allâh ametekeleza ahadi yake ... (mpaka aliposema) hata kama linawachukiza makafiri.”

111. Kurusha vijiwe kwa sampuli fulani; kuiwekelea ncha ya kidole cha gumba katikati ya kidole cha shahada, kisha kukiweka kijiwe juu ya ukucha wa gumba, kisha ukifyetue kidole cha gumba. Au kukunja vidole vya shahada mpaka ncha zake zizame kwenye kiungo cha gumba na mkono, kisha urushe vijiwe.

112. Kusimama kwenye umbali fulani – kwa mfano dhirâ tano kutoka kwenye Jamrah – ukitaka kurusha vijiwe.

113. Kurusha vijiwe kwa kutumia viatu ... na kadhaalika.

„Âbidîn». Tizama katika kitabu cha muandishi cha «At-Tawassul» sampuli na sheriya zake,

Page 88: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

75

Uzushi Unaofanywa Katika Kuchinja

114. Kulipa thamani ya kichinjo kwa masikini badala ya kuchinja na kudai yakwamba kuchinja wanyama husababisha israfu ya nyama kutokana na idadi kubwa ya wanyama wanaochinjwa na wachache watakaochukuliwa.1

115. Kuchinja Hady wa Tamattu‟ Makkah kabla ya siku ya Nahr.

116. Kuanzia kwenye upande wa kushoto wa kichwa wakati wa kunyoa au kuzipunguza.

117. Kunyoa nywele au kuzipunguza sehemu ya kichwa.

118. Maneno ya Al-Ghazâlî: “Ni katika Sunnah kuelekea Qiblah wakati wa kunyoa.”

119. Kusema wakati wa kunyoa nywele au kuzipunguza: “Kila Sifa njema zinamstahiki Allâh aliyetuongoza na akatune‟emesha na fadhla zake. Yâ Allâh, shungi langu liko mikononi Mwako, basi nikubalie (Hajj yangu) kutoka kwangu ...”

120. Kuizunguka (kufanya twawâf kwenye) Misikiti iliyojengwa karibu na Jamarât.

121. Kuswali swala ya „Idd Minâ katika siku ya Nahr.

122. Kuwacha kuifanya Sa‟î kwa mwenye kuifanya Hijjah ya Tamattu baada ya kuifanya Twawâf al-Ifâdhah.

Sampuli Mbalimbali Za Uzushi

123. Kusherehekea siku ya kulivisha tandiko al-Ka‟bah.

124. Kupavisha Maqâm Ibrâhîm tandiko.

1 Huu ni mmojawapo wa Uzushi unaochukiza mno kwani unatoa mapendekezo kwa rai kuliko hukmu ya Qur‟ân Takatifu na Sunnah. La zaidi ni kwamba jambo kubwa linalosababisha nyama nyingi kutairika ni ukosefu wa utekelezaji wa hukmu za njia ya Uislamu wakati wa Mahujaji wanapowachinja wanyama – kama nilivyoyagusia katika “Asili” [Uk. 87, 88].

Page 89: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

76

125. Kufunga vipande vya vitambara katika Maqâm Ibrâhîm na Minbar ya Msikiti ili zipate kutimiza mahitaji ya Mahujaji.

126. Kuandika majina ya Mahujaji kwenye kuta na nguzo za al-Ka‟bah au kuwaomba watu wengine wakufanyie hayo.

127. Kupita mbele ya mtu mwenye kuswali katika Al-Masjidul Harâm; baadhi ya Mahujaji huwenda wakapigana na wale wenye kuwazuiya wasipite mbele ya wanaoswali.

128. Kumwita aliyemaliza kutekeleza Hajj (mke au mume)– Al-Hajj.

129. Kuondoka Makkah kwa ajili ya kuvaa Ihrâm ya kufanya „Umrah.

130. Kutoka kinyume-nyume Al-Masjidul Harâm baada ya kutekeleza Twawâf al-Wadâ‟.

131. Kuipaka rangi ya chokaa nyumba ya mwenye kuhiji, kuchora baadhi ya picha juu yake na kuandika majina ya aliyekwenda kuhiji na tarehe za kurudi kutoka Hajj.

Bid‟ah Zinazofanywa Katika Ziyârah (Kuzuru Kaburi La Mtume Madinah)

Kwa hakika ni katika Sunnah kusafiri kwenda Al-Madinah kwa malengo ya kuzuru Msikiti wa Mtume na Palestine kuzuru Al-Masjidul Aqswâ (Msikiti wa mbali) – twamuomba Allâh aurudishe kwa Waislamu. Malipo ya ziyara hizi ni makubwa mno. Ni mazoweya kwa watu wengi kuzuru sehemu hizo kabla au baada ya Hajj. Lakini kwa bahati mbaya, wengi wao hufanya mambo ya uzushi mahali hapo yanayojulikanwa na Wanavyuoni. Nimehisi kuwajibika kuyaorodhesha mambo ya kuzua na bid‟ah hizo kwa ajili ya kuwaonya Waislamu dhidi ya mambo hayo. Nayo ni:

132. Kusafiri Madinah kwa lengo la pekee la kuzuru kaburi la Mtume

Page 90: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

77

(wala sio Msikiti wake)1.

133. Kutuma barua za salamu kupitia kwa Mahujaji na wageni

wanaozuru kaburi la Mtume afikishiwe Mtume (صىل اهلل عليه وسلم).

134. Kuoga kabla ya kuingia Madinah.

135. Kusema pindi unapoziona kuta za Madinah: “Ewe Mola, hii ni sehemu tukufu ya Mtume wako, ifanye iwe ni kinga kwangu kutokamana na Moto, na amani kutokamana na adhabu na mambo maovu.”

136. Kusema unapoingia Al-Madînah:

بسم اهلل، وعىل ملة رسول اهلل:

“Kwa Jina la Allâh, nikiwa juu ya mila ya Mtume wa Allâh

1 Ni katika Sunnah kusafiri kwa lengo la kuuzuru Msikiti wa Mtume. Amesema

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم): “Kusafiri kwa malengo ya kuuzuru Msikiti hakufai

isipokuwa kwa Misikiti mitatu tu: AL-Masjidul Harâm (ulioko Makkah), Al-Masjidul Aqswâ (ulioko Jerusalem) na Msikiti wangu (ulioko Al-Madinah).” Inataka ifahamike kwa ubainifu yakwamba kuna tafauti kubwa baina ya kuliona kaburi la Mtume haliyakuwa tayari uko kwenye safari ya kuelekea Madinah, na kusafiri kuelekea Madinah kwa lengo la pekee la kuzuru kaburi la Mtume. Wanavyuoni wengi walio wasomi wakubwa siku hizi hufikia kuchanganya baina ya haya mambo mawili mpaka wakasema yakwamba miongoni mwa Ma-Salafi kwa ujumla na hususan Ibn Taymiyyah amekataza kulizuru kaburi la Mtume. Huo ni urongo wa wazi. Tizama nilivyoikosoa rai ya Dr. Buti kwenye chapa ya musal-sal ya «At-Tamaddunul Islâmi» Makala yalichapishwa na offsite kwa jina la “Difâ‟un „Anil Hadith „An-Nabawî” (Kuzitetea Hadîth za Mtume).

Page 91: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

78

[Na sema: „Mola wangu! Kufanye kuingia kwangu (Madînah) kuwe ni kuingia kwema, na kutoka kwangu kuwe ni kwema

na unipe nguvu zinazotoka kwako zinazosaidia.‟”]

137. Kuliweka (mpaka sasa) kaburi la Mtume ndani ya Msikiti wake.

138. Kulizuru kaburi la Mtume kabla ya kuswali ndani ya Msikiti wake.

139. Kulielekea kaburi la Mtume haliyakuwa umeweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto – kama ifanywavyo kwenye swala - unapoingia msikitini, iwapo kaburi liko karibu naye au mbali naye na kuujaza moyo wake unyenyekevu.

140. Kulielekea kaburi unapomuomba Allâh ( وتعاىل سبحانه ).

141. Kulikusudia kaburi kwa du‟â na kutarajia kujibiwa.

142. Kutawassal kwa jaha ya Mtume unapo-omba du‟â kwa Allâh.

143. Kumuomba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akushufa‟iye.

144. Matamshi ya Ibn al-Hajj katika «Al-Mad-khal» (vol 1/ Uk. 259): “Ni miongoni mwa adabu za kulizuru kaburi la Mtume

yakwamba mtu asiyaseme mahitaji yake kwani yeye ( صىل اهلل عليه ”.anayajua mahitaji na maslahi ya kila mmoja wenu (وسلم

145. Vilevile amesema (vol 1/ Uk. 264): “Hapana tafauti yoyote

ema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) yuko hai au amekufa; yeye anaijua

hali, niya, mahitaji, dhiki na fikra za kila mtu.”!!

146. Mtu kuweka mkono wake kwenye dirisha la chumba lililojengwa juu ya kaburi la Mtume akitarajia kupata baraka. Baadhi yao huapa (kwa dirisha hilo) kwa kusema: “Naapa kwa yule ambaye juu ya dirisha lake umeuweka mkono wako.” Baadhi yao husema: “Sisi twataka shafa‟ah (uombezi) kutoka kwako Ewe Mtume wa Allâh.”

Page 92: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

79

147. Kulibusu kaburi au kuligusa au kugusa kila kilicho karibu yake katika vijiti ...na kadhaalika.1

148. Kufanya mazoweya ya sampuli fulani unapozuru kaburi la Mtume na makaburi ya wandani wake wawili (Abu Bakr na „Umar), kuwaamkua wao kwa maneno fulani na kusoma maombi fulani. Kwa mfano, amesema Al-Ghazâlî: “Muhrim na asimame mkabala wa uso wa Mtume, mgongo wake ukielekea al-Ka‟bah, auelekee ukuta wa kaburi ... na aseme: Amani ikushukie ewe Mtume wa Allâh ...,” Al-Ghazâlî ametaja salâm na du‟â ndefu.2

149. Kuswali na kulielekea kaburi.

150. Kukaa karibu au kulizunguka kaburi ili upate kusoma Qur‟ân au kuleta adh-kâr.

151. Kulizuru kaburi kila baada ya swala kumfikishia salamu Mtume

3.(صىل اهلل عليه وسلم)

1 Al-Ghazâlî ( اهلل رحمه ) amechukia kitendo hiki; amesema (vol. 1/ Uk. 244): “Ni

katika mila za kiyahudi na kinaswara (katika kuyazuru makaburi). Kwahiyo, jitahadhari na hayo.” 2 Sunnah ni kusema (unapozuru kaburi la Mtume):

ةاهللالسلمعلي كيارسلاهلل» رورح بابك السلمعلي كياأ السلمعلي كوبراكث

«عهر يا

“Amani, Baraka na rehma ziwe juu yako, Ewe Mtume wa Allâh. Amani iwe juu yako Ewe Abu Bakr, amani iwe juu yako ewe „Umar.”

Ibn „Umar ( عنه رضي اهلل ) alikuwa akifanya hivyo. Muislamu anaruhusiwa

kuongezea katika maamkuzi hayo, lakini asigande katika nyongeza. 3 Hii ni Bid‟ah, inayokwenda kinyume na hadith ya Mtume inayosema:

« فإنصلثكم حي ثهالي جم الع يعيداوصل «تب لغنلتجخذواقب

“Musilifanye kaburi langu kama sanamu wa kuabudiwa, tumeni maombi yenu (na salamu zenu) juu yangu kutoka popote mulipo,

kwani kwa hakika zitanifikia.”

Page 93: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

80

152. Kulizuru kaburi la Mtume unapoingia msikitini au kabla ya kutoka msikitini kwa wakaazi wa AL-Madînah.

153. Kupaaza sauti kila baada ya swala kwa kusema:

لم غييم يا رشل اهلل » «الص“As-salâmu „alayka yâ rasûlallâh”

“Amani zikushukie ewe Mtume wa Allâh.”

154. Kutafuta baraka kutoka kwenye vigamba vya rangi vinavyopukutika kutoka katika kuba la kaburi kunaponyesha mvua.

155. Kutafuta baraka zinazotokamana na kula tende za Saihânî zilizoko kwenye mstari uliobarikiwa baina ya Rawdhatush Sharîf (minbar na kaburi).

156. Kukata nywele zao na kuzirusha kwenye taa kubwa iliyoko karibu na kaburi.

157. Mtu kuipangusa mikono yake na mitende miwili iliyowekwa msikitini katika upande wa magharibi mwa minbar.1

158. Kuswali mara kwa mara kwenye msikiti wa zamani na kuiwacha mistari miwili ya mwanzo ambayo iko kwenye sehemu iliyo-ongezwa kwenye msikiti katika zama za „Umar na ma-Imâm wengine waliokuja baada yake.

159. Kukaa Madînah kwa muda wa wiki nzima ili aweze kutekeleza swala arubaini katika al-Masjidun Nabawi, akitarajia kupata kwa hilo, utakaso kutokamana na unafiki na kuokoka na moto.1

Watu wengi huwacha kuleta adh-kâr na du‟â za kisheriya baada ya swala hukimbilia kutekeleza Bid‟ah hii (iliyotajwa kwenye nukta hii). Allâh na amrehemu Yule aliyesema: “Kila inapoinuka Bid‟ah, Sunnah hufa.” 1 Miti hii miwili haina kazi yoyote hapo, yaliwekwa hapo kama mapambo tu na iwe ni yenye kuwavutia watu. Yameshaondolewa siku hizi, alhamdulillâh.

Page 94: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

81

160. Kuzuru baadhi ya misikiti na makaburi yaliyoko Madînah na sehemu nyengine karibu na hapo badala ya kuzuru Masjid Qubâ‟

161. Kuwaamuru Mahujaji – wakiongozwa na wale waitwao Al-Muzawwirûn – baadhi ya du‟â na adh-kâr karibu na chumba (cha kaburi la Mtume) au mbali na hapo kwa sauti kubwa na kisha Mahujaji nao warudie kwa kuitikia kwa sauti kubwa zaidi.

162. Kuzuru makaburi ya Al-Baqî kila siku na kuswali katika Masjid Fâtimah.

163. Kuzuru makaburi ya mashahidi wa (vita vya) Uhud kila siku ya al-Khamisi.

164. Kufunga vipande vya vitambara kwenye madirisha yanayoelekeana na makaburi.

165. Kutafuta baraka katika kuoga kwenye birika lililokuwa karibu na makaburi ya mashahidi.

166. Kutoka kwenye msikiti wa Mtume kinyume-nyume unapotoka kwenye kaburi.

Uzushi Unaofanywa Katika Baitul Maqdis

1 Bid‟ah hii imeegemezwa juu ya hadith dhaifu niliyoitaja katika «as-Silsilah adh-Dha‟îfah» (no. 364). Kama ilivyo, hafai mtu kutekeleza maamrisho hayo kwani swala ni kitendo cha „Ibâdah. Watu wengi walikuwa wakidhania yakwamba ilikuwa ni hadîth swahîh na wakawa wanapata tabu katika kutaka kuitekeleza, sasa kwa vile haifai wamepata afuweni (kutokana na bid‟ah hiyo). Baadhi ya wanavyuoni wanaizingatia hadîth hiyo kuwa ni miongoni mwa zilizo na nguvu, kwa vile Ibn Hibbân amemzingatia kuwa ni mtu wa kutegemewa mmojawapo wa wapokezi wake wasiojulikana. Hatahivyo, mategemezi haya ni hayakuthibitishwa na wanavyuoni wakubwa wa Al-Jarh wat Ta‟dîl.

Page 95: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

82

167. Kuzuru Baitul Maqdis (Jerusalem) kwa haraka baada ya Hajj na kusema (kwa mahujaji wengine): “Qaddasallâhu Hajjatukah” [Allâh aitakase Hajj yako].

168. Kutufu (kulizunguka) Kuba la Jabali kama wafanyavyo Mahujaji katika al-Ka‟bah.

169. Kulitukuza Jabali lenyewe kwa kulipangusa, kulibusu, kuchinja wanyama karibu nalo, kufanya kitendo chochote anachofanya Muhrim akiwa „Arafah – katika jioni ya siku ya „Arafah – na kujenga juu yake ...na kadhaalika.

170. Madai yakwamba ati kuna alama ya nyayo ya Mtume ( صىل اهلل عليه ,juu ya Jabali hili, na mabaki ya kilemba cha Mtume (وسلم

baadhi ya watu hata hudhani yakwamba Jabali hili ndipo mahali ambapo Allâh alipoweka Mguu wake.

171. Kuzuru kinachoaminika kuwa ni kitanda cha utoto cha „Îsâ‟ ( عليه .(السالم

172. Kuamini yakwamba hapo (Baitul Maqdis) ndipo itakapokuwa Swirât, Mîzân na Ukuta utakaosimamishwa baina ya Pepo na Moto, ndio ukuta huohuo uliojengwa upande wa mashariki mwa msikiti.

173. Kuitukuza silisili iliyoko na hiyo sehemu ya hapo.

174. Kuswali karibu na kaburi la Ibrâhîm.

175. Kukutana hapo (Baitul Maqdis) katika miezi ya Hajj ili wapate kuimba nyimbo fulani kwa kutumia matwari (na ngoma).

Namuomba Allâh ( وتعاىل سبحانه ) akifanye kitabu hiki kuwa ni cha

kuwasaidia Waislamu wafuate njia ya Mtume na uongofu wake. Na kutakasika ni Kwako, Yâ Allâh na kila sifa njema zinakustahiki Wewe; nashuhudia yakwamba hapana mola anayestahiki kuabudiwa kwa Haki

Page 96: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

83

isipokuwa Wewe. Nakuomba msamaha wako na natubia Kwako.

Page 97: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

i

Kamusi

„Alam :Alama ya kijani yenye kuonyesha sehemu baina ya As-Swafâ na Marwah; sehemu hii yaitwa „Abtwah.

„Aqswah (msikiti) :Msikiti ulioko Jerusalem ambao Mtume ( اهلل صىلوسلم عليه ) aliowahi kuswali ndani yake katika siku

ya safari ya usiku.

„Arafah :Mlima mpana ulioko Makkah ambao Mahujaji wote huhudhuria hapo tarehe 9th Dhul-Hijjah kuanzia kupinduka kwa jua hadi kutwa kwa jua.

„Asr :Baada ya mchana, katika wakati huu kuna swala inayopasa kuswaliwa.

„Adhân :Ulinganizi katika swala unaotangazwa kwa sauti ya juu kuashiriya yakwamba wakati wa swala umeingia.

„Abtwah :Sehemu ya baina ya As-Swafâ na Marwah inayopitwa kwa utaratibu na mtu mwenye kufanya Hajj au „Umrah.

Baitul Maqdis :Jina jengine la Masjidul Al-Aqswâ ulioko Jerusalem, unaozingatiwa kuwa ndio msikiti maarufu wa tatu mkubwa katika ulimwengu wa ki-Islamu.

Baqî’ :Makaburi ya watu wa Al-Madînah. Maswahaba wengi wa Mtume walizikwa hapo.

Batn Muhassir :Au Wâdi Muhassir; Mahali baina ya Muzdalifah na Minâ.

Bid’ah :Mambo ya Uzushi (katika dini)

Page 98: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

ii

Siku ya Nahr :Siku ya kumi ya mwezi wa Ki-Islamu katika Dhul-Hijjah. Katika siku hii, Mahujaji huchinja swadaka zao, wakanyoa (au kupunguza) nywele zao, ...

Siku ya at-Tarwiyah : Siku ya Nane ya mwezi wa Ki-Islamu katika Dhul-Hijjah. Katika siku hii, Mutamatti‟ anavaa ihrâm kwa ajili ya kutekeleza Hajj.

Siku za Tashrîq : Siku ya 11, 12 na13 za mwezi wa Ki-Islamu katika Dhul-Hijjah.

Fajr :Alfajiri, swala ya alfajiri huswaliwa katika wakati huu.

Fidyah :Malipo ya kukosea au kuwacha kutekeleza jambo la dini, sana huwa ni kwa njia ya pesa, vyakula au kuchinja mnyama.

Fuqahâ’ :Mwanachuoni msomi katika hukmu za kisheriya.

Hajarul Aswad :Jiwe Jeusi lililowekwa katika pembe moja ya al-Ka‟bah. Muhrim anatakiwa kuanza twawâf kutoka mahali hapo.

Hady :Mnyama (Ngamia, Ng‟ombe, Mbuzi, Kondoo) anayechinjwa kama swadaka na Mahujaji wakiwa Makkah.

Hajj :Kwenda Makkah kuhiji.

Hajj :Mwenye kutekeleza Hijjah.

Hasanah :Malipo yanayotolewa na Allâh kwa Waislamu wenye kufanya mambo mazuri.

Hijr :Sehemu isiyokuwa na paa ya Ka‟bah iliyoko upande wa kaskazini mwa Ka‟bah.

Idhtwibâ’ :kulifinika bega la kulia na kuweka pambizo ya Izâr kwenye (bega) la kushoto, Muhrim hufanya hivyo katika twawâf al-Qudûm peke yake.

Page 99: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

iii

Ihrâm :Hali ambapo mtu huwa ameharamishiwa kutekeleza mambo fulani ambayo ni halali kwake katika wakati mwengine. Utekelezaji wa Hajj na „Umrah unafanyika katika hali hiyo.

Imâm :Mtu mwenye kuwaongoza wengine katika swala. Vilevile ina maana ya kiongozi wa Waislamu au mtawala.

Iqâmah :matamshi yaliyopunguzwa ya adhân ambayo pindi yanaposemwa ndipo watu wanapokusanyika na kuswali.

‘Ishâ’ :Usiku, wakati ambapo swala ya usiku inaposwaliwa.

Izâr :kitambara kinachovaliwa chini ya kuino kusitiri sehemu ya chini ya mwili.

Jamaratul Kubrâ :Mojawapo ya nguzo tatu zilizojengwa kwa jiwe iliyoko Minâ; mahali ambapo Muhrim anaporushwa vijiwe; ni mojawapo ya „Ibâdah za Hajj.

Jamarât :umoja wake ... Jamrah; nguzo tatu zilizojengwa kwa jiwe iliyoko Minâ,

Jibrîl :Malaika mwenye kuteremsha vitabu vitakatifu vya Allâh kwa Mitume wake, wa mwisho wao

akiwa ni Muhammad (صىل اهلل عليه وسلم).

Ka’bah :Jengo la jiwe la mraba lililoko katika Al-Masjidul Harâm (msikiti mkubwa) mjini Makkah ambalo Waislamu wote huelekeza nyuso zao wanaposwali.

Madînah :Mji maarufu ulioko Nchini Saudi Arabia ambapo Msikiti wa Mtume ulipo.

Maghrib :kutwa kwa Jua, swala inapaswa kuswaliwa katika wakati huu.

Page 100: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

iv

Mahram :Mtu ambaye mwanamke asoweza kuolewa naye kutokana na uhusiano wao (baba, mjomba, babu, ndugu ...) au mume wake.

Makkah :Mji maarufu sana ulioko katika nchi ya Saudi Arabia ambapo Ka‟bah linapatikana hapo.

Manâsik :umoja wake ... Mansak; „Ibâdah zinazofanywa wakati wa Hajj na „Umrah.

Manhar :sehemu ambazo Muhrim anazoweza kutekeleza swadaka yake ya kuchinja, sehemu zote za Makkah ni zenye kufaa kutekeleza swadaka ya kuchinja.

Maqâm :Maqâm Ibrâhîm, iko karibu na Ka‟bah ambapo nyuma yake wale wenye kuitufu Nyumba wanapaswa kuswali rak‟ah mbili.

Marâhil : umoja wake ... Marhalah; umbali ulio sawa na Maili 24 (~44.79 km).

Marwah :Mlima ulioko Makkah, ulio karibu na Msikiti Mtukufu.

Mash’arul Harâm :Mlima ulioko Muzdalifah. Unaitwa Quzah.

Masjidul Harâm :Msikiti Mtukufu zaidi ulioko Makkah. Ka‟bah iko ndani yake.

Minâ :Sehemu iliyoko nje ya Makkah kwa umbali wa Maili tano.

Mîqât :wingi wake ... Mawâqît; sehemu zilizokuwa

chini ya maagizo ya Mtume ( اهلل عليه وسلم صىل ) kwa

watu kuhirimia, wakiwa kwenye kuelekea Makkah kutekeleza Hajj au „Umrah.

Muhrim :Mwenye kuwa katika hali ya Ihrâm kwa min-ajil ya kutekeleza Hajj au „Umrah.

Page 101: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

v

Multazam :Mahali pa kushikiliwa. Ni sehemu iliyoko baina ya mlango wa al-Ka‟bah na al-Hajarul-Aswad (Jiwe Jeusi).

Muzawwirûn :Wenye kuwafundisha watu mambo ya kufanywa na kusema wakati wa Hajj na „Umrah.

Muzdalifah : Mahali katikati ya „Arafah na Minâ ambapo Mahujaji wanapopaswa kusimama na kukaa kwa usiku mzima (Baina ya tarehe 9th na 10th Dhul-Hijjah) ili waswali swala za Maghrib na „Ishâ‟ hapo. Vilevile panaitwa Jam‟.

Na’l :Sampuli ya kiatu ambacho mwisho wake uko chini ya kisigino.

Namirah :mahali karibu na „Arafah.

Qiblah : Muelekeo ambao Waislamu wote huelekeza nyuso zao wakati wa swala, na muelekeo huo ni wenye kuelekea Ka‟bah lililoko Makkah.

Qubâ’ :Katika vijiji vya AL-Madînah, ambapo Mtume

alijenga Msikiti hapo wenye jina (صىل اهلل عليه وسلم)

kama hilo.

Ramal :Mwendo wa haraka wa hatua ndogo-ndogo unaofanywa katika mizunguko mitatu ya kwanza ya twawâf ya kulizunguka al-Ka‟bah.

Ridâ’ :Kitambara kinachovaliwa kwenye sehemu za juu ya mwili.

Rukn Yamânî :Pembe ya jengo la Ka‟ba ilioyokabiliana na Yemen.

Sa’î :Mwendo wa baina ya As-Swafâ na Al-Marwah mara saba wakati wa kufanya Hajj na „Umrah.

Swafâ :Mlima ulioko Makkah jirani mwa Masjidul-Harâm katika upande wa Mashariki.

Page 102: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

vi

Swahabah :Maswahaba wa Mtume ( وسلم صىل اهلل عليه ).

Salaf :Watangulizi wema na kila mwenye kufuata nyayo zao.

Swalât :Swala zinazotekelezwa na Waislamu kwa mara tano kila siku katika nyakati maalum.

Sheitwân :Sheitwani.

Pembe ya Shâmi : Pambizo za Ka‟bah zilizo mkabala wa Hijir.

Shawwâl :Mwezi wa kumi wa terehe za ki-Islamu.

Shirk :Ushirikina nako ni kuabudu wengine pamoja na Allâh.

Swiyâm :Kufunga wakati wa mwezi wa Ramadhân kuanzia alfajiri hadi kutwa kwa Jua.

Sunnah :Njia za kisheriya, maamrisho, vitendo vya „Ibâda na mafunzo ya Mtume ambayo yanastahiki kufuatwa na kila aliye Musilamu.

Sûrah :Mlango kutoka katika Qur‟ân Tukufu.

Sutrah :Kizuizi chenye urefu usiopungua futi moja; na ni lazima kiwe mbele ya mwenye kuswali.

Tabûk :Mji maarufu ulioko umbali wa 700 Km Kaskazini mwa Al-Madînah.

Tahiyyatul Masjid :Rak‟ât mbili zinazoswaliwa pindi mtu anapoingia msikitini.

Tahlîl :Kusema Lâ ilâha illallâh, (yaani; hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allâh).

Takbîr :Kusema: Allâhu Akbar, (yaani; Allâh Ndiye Mkubwa zaidi).

Talbiyah :Kusema, Labbayk Allâhumma labbayk (yaani; Yâ Allâh! Mimi ni mtwi‟ifu kwa amri zako, Naitikia mwito wako).

Page 103: Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida ... · Sheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI Abu Farida Muhammad Awadh Salim BasawaD

vii

Taslîm :Kusema; Assalâmu „alaykum Warahmatullâhi Wabarakâtuh; (yaani; Amani, baraka na huruma Yâ Allâh ziwe juu Yako).

Twawâf :Kulizunguka Jumba Takatifu, al-Ka‟bah, lililoko Makkah.

Thaniyyatul ‘Ulyâ : Njia inayo-ongoza hadi Makkah moja kwa moja.

Dhul-Hijjah :Mwezi wa kumi na mbili wa ki-Islamu.

Tihâmah :Sehemu inayopakana na Mji wa Najd.

‘Ulamâ’ :Wanavyuoni wasomi wa dini ya ki-Islamu.

‘Umrah :Ziyara ya Makkah ambapo mtu hutekeleza Twawâf na Sa‟î.

‘Uranah :Bonde lililopakana na „Arafah.

Uhud :Mlima maarufu ulioko Al-Madînah. Mojawapo miongoni mwa vita vikubwa vya Uislamu vilitokea hapo na kuchukuwa jina kama hilo.

Witr :Idadi ya rak‟ât isiyokuwa na mwenzi ambayo mtu humalizia nayo swala za usiku (baada ya swala ya „Ishâ‟).

Zamzam :Kisima Kitakatifu kilichoko ndani ya haram (msikiti Mtukufu wa Makkah).

Ziyârah :Kuzuru msikiti wa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم).