Ratiba Kongamano la CHAUKIDUchaukidu.org/wp-content/uploads/2019/11/Ratiba_Rasimu_Ya_3.pdfDkt....
Transcript of Ratiba Kongamano la CHAUKIDUchaukidu.org/wp-content/uploads/2019/11/Ratiba_Rasimu_Ya_3.pdfDkt....
1
Ratiba Kongamano la CHAUKIDU Chuo Kikuu cha Kyambogo
Kampala Uganda 13 - 15 Disemba 2019
2
Wadhamini
Chuo Kikuu cha Kyambogo
Bodi ya Chaukidu
3
Rais
Prof. Leonard Muaka
Chuo Kikuu cha Howard
Makamu wa Rais
Dkt. Musa Hans
Chuo Kikuu cha DSM
Rais Mtangulizi
Dkt. Mahiri Mwita
Chuo Kikuu cha Princeton
Katibu
Dkt. Beatrice Mkenda
Chuo Kikuu cha Iowa
Mjumbe
Dkt. Elias Magembe
Chuo Kikuu cha American
Mjumbe
Prof. Deo Ngonyani
Chuo Kikuu cha Jimbo MI
Mkurugenzi
Dkt. Filipo Lubua
Chuo Kikuu cha Pittsburgh
Naibu Mkurugenzi
Dkt. David Kyeu
Chuo Kikuu cha CA, Berkley
Mhazini
Mwl. Happiness Bulugu
Chuo Kikuu cha Cornell
Mjumbe
Prof. Alwiya Omar
Chuo Kikuu cha Indiana
Mjumbe
Dkt. Charles Bwenge
Chuo Kikuu cha Florida
Mjumbe
Prof. Beata Wojtowicz
Chuo Kikuu cha Polandi
Bodi ya Chaukidu
4
Mjumbe
Mwl. Abdul Nanji
Chuo Kikuu cha Columbia
Mjumbe
Dkt. Pendo Salu Malangwa
Chuo Kikuu cha DSM
Mjumbe
Dkt. Zainab Ali Iddi
Chuo Kikuu cha Taifa ZNZ
Mjumbe
Prof. Aldin Mutembei
Chuo Kikuu cha DSM
Mjumbe
Prof. Pacifique Malonga
BECOS, Rwanda
Mjumbe
Mwl. Malimi Kazi
Chuo Kikuu cha Duquesne
Mjumbe
Prof. Iribe Mwangi
Chuo Kikuu cha Nairobi
Mjumbe
Prof. Ken Walibora
Chuo Kikuu cha Riara
Mjumbe
Dkt. Hadija Jilala
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
Mjumbe
Mwl. Beatrice Ng’uono Okelo
Chuo Kikuu cha Baylor
Mjumbe
Mwl. Aidah Mutenyo
Chuo Kikuu cha Kabale
Mjumbe
Mwl. Agnes Bruhwiler
Chuo Kikuu cha Cologne
Mwakilishi wa Wanafunzi
Ndayikengurukiye Gordien
Chuo Kikuu cha Ualimu
Kamati ya Maandalizi
5
Mwenyekiti
Dkt. Charles Bwenge
Chuo Kikuu cha Florida
Mjumbe
Mwl. Beatrice Ng’uono Okelo
Chuo Kikuu cha Baylor
Mjumbe
Dkt. Kiarie Wa'Njogu
Chuo Kikuu cha Yale
Mjumbe
Mwl. Malimi Kazi
Chuo Kikuu cha Duquesne
Mjumbe
Dkt. Elias Magembe
Chuo Kikuu cha American
Mtiva - Kyambogo
Dkt. Elizabeth Kyazike
Chuo Kikuu cha Kyambogo
Mwenyekiti-Mwenza
Mwl. Aidah Mutenyo
Chuo Kikuu cha Kabale
Mjumbe
Dkt. Anne Jebet
Chuo Kikuu cha Virginia
Mjumbe
Mwl. Yunusu Lubuuka
Chuo Kikuu cha Kyambogo
Mjumbe
Mwl. Abdul Nanji
Chuo Kikuu cha Columbia
Mjumbe
Dkt. Mahiri Mwita
Chuo Kikuu cha Princeton
Mkuu wa Idara - Kyambogo
Dkt. Sarah Nabiccu
Chuo Kikuu cha Kyambogo
Ratiba ya Kongamano kwa Muhtasari
Muda (Kwa Kiswahili) Tukio Mhusika/Wahusika
Ijumaa 13/12/2019
2:00 - 5:00 Usajili Kamati Andalizi
2:00 - 2:45 Chai Washiriki Wote
2:45 - 3:00 Kuingia Ukumbini na Ukaribishaji Washiriki Wote
3:00 - 5:00 Warsha - Sehemu ya 1 Washiriki wa Warsha na Wakufunzi
5:00 - 7:00 Warsha - Sehemu ya 2 Washiriki wa Warsha na Wakufunzi
7:00 - 8:30 Chakula Washiriki wa Warsha na Wakufunzi
8:30 - 10:30 Warsha Sehemu ya 3 Washiriki wa Warsha na Wakufunzi
10:30 - 11:30 Utoaji Vyeti Washiriki wa Warsha na Wakufunzi
Jumamosi 14/12/2019
2:00 - 5:00 Usajili Kamati Andalizi
1:30 – 2:45 Chai Washiriki Wote
2:45 – 3:00 Kuingia Ukumbini Washiriki Wote
3:00 - 3:30 Kuwasili kwa Mgeni Rasmi Mgeni Rasmi na Viongozi
3:30-6:15 Ufunguzi Rasmi na Mada Elekezi ya 1 Washiriki Wote na Prof. Kimani Njogu
6:15 - 7:45 Mapumziko na Chakula cha Mchana Washiriki Wote
8:00 - 9:40 Vikao Sambamba Na. 1 Washiriki Wote
9:50 - 11:30
Hoja Pevu ya 1
Jopo la Wabobezi wa Kiswahili
Washiriki Wote
11:30 - Mapumziko na Utalii Washiriki Wote
Jumapili 15/12/2019
1:30 – 2:45 Chai Washiriki Wote
3:00 – 4:40 Vikao Sambamba Na. 2 Washiriki Wote
4:50 - 6:30 Vikao Sambamba Na. 3 Washiriki Wote
6:30 - 7:50 Chakula cha Mchana Washiriki Wote
8:00 - 8:45 Mada Elekezi ya 2 Washiriki Wote na Dkt. Ernesta Mosha
8:50 - 10:30 Vikao Sambamba Na. 4 Washiriki Wote
10:40 - 11:40 Hoja Pevu Na. 2 Washiriki Wote
11:40 - 12:30 Mapumziko Washiriki Wote
12:30 - 3:30 Usiku wa Tuzo Washiriki Wote
7
Ratiba ya Siku
Bodi ya CHAUKIDU Kutembelea Wizara ya
Jinsia, Kazi, na Maendeleo ya Jamii
3:00 - 10:00
Bodi ya CHAUKIDU Kukutana na Uongozi wa
Chuo Kikuu cha Kyambogo
8:00 - 10:00
Ijum
aa, D
isem
ba 1
3, 2
019
Ijum
aa, D
isem
ba 1
3, 2
019
8
Warsha - 8:00 Asub - 10:00 Jion
Mada ya 1: U5 Katika Ufunzaji wa Kiswahili
Dkt. Kiarie Wa'Njogu
Dkt. Wa’Njogu ni Mkurugenzi wa Programu ya Lugha za Kiafrika
katika Chuo Kikuu cha Yale, kilichopo jimbo la Connecticut, USA.
Ana shahada ya uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Jimbo Ohio, na
amekuwa mkufunzi wa masuala ya ufundishaji wa Kiswahili kama
lugha ya kigeni kwa miaka mingi sasa.
Mwl. Beatrice Ng'uono Okelo
Mwalimu Ng’uono ni mwalimu wa Kiswahili katika Chuo Kikuu cha
Baylor kilichoko Texas, Marekani. Tafiti zake zimejikikita katika
Isimu na ufundishaji wa Kiswahili na lugha nyingine za Kiafrika. Ana
tajiriba ya miaka kadhaa ya kufundisha Kiswahili kama lugha ya
kigeni kwa kutumia mbinu ya kimawasiliano na kwa kuzingatia
malengo matano maalum ya U5.
Mada ya 2: Teknolojia Katika Ufunzaji wa Kiswahili
Dkt. Filipo Lubua Dkt. Lubua ni mwalimu katika Chuo Kikuu cha Pittsburgh kilichoko
Pennsylvania, Marekani. Ana shahada ya uzamivu katika maswala ya
Teknolojia ya Ufundishaji kutoka Chuo Kikuu cha Ohio jimboni
Ohio, USA. Tafiti zake zimejikita zaidi katika maswala ya matumizi
ya kompyuta na teknolojia za kidijitali katika ufundishaji na ujifunzaji
wa lugha.
Mwl. Malimi Joram Kazi Mwl. Kazi ni mwanafunzi wa shahada ya uzamivu katika matumizi
ya Teknolojia ya Ufundishaji, Chuo Kikuu cha Duquesne kilichoko
Pennsylvania, USA. Alikuwa Mkufunzi katika Taasisi ya Elimu ya
Watu Wazima iliyoko Dar es Salaam, Tanzania. Mwl. Kazi ana ari
kubwa ya kuwasaidia walimu wa lugha kujua teknolojia rahisi
ziwezazo kutumika katika madarasa ya Kiswahili kama lugha ya
kigeni.
Iju
maa
, D
isem
ba 1
3, 2019
9
Kikao cha Bodi ya Chaukidu
Kikao cha Bodi na Chajio
11:00 - 2:30 Jioni
Ijum
aa
, Dise
mba 1
3, 2
019
10
Jumamosi 2:45Asub - 6:15Mch - Ufunguzi
Muda Tukio Mhusika/Wahusika
2:00 - 5:00 Usajili Kamati Andalizi
1:30 – 2:45 Chai Washiriki Wote
2:45 – 3:00 Kuingia Ukumbini Washiriki Wote
3:00 - 3:30 Kuwasili kwa Mgeni Rasmi Mgeni Rasmi na
Viongozi
3:30-3:40 Wimbo wa Taifa na Wimbo wa
Afrika Mashariki
Wote
3:40 – 3:50 Ukaribisho Toka kwa Wenyeviti
wa Kamati Andalizi
Dkt. Charles Bwenge &
Aidah Mutenyo
3:50 - 4:00 Salamu za Vyama na Taasisi
Marafiki
Vyama/Taasisi
Mbalimbali
4:00 – 4:10 Salamu za Mkurugenzi wa
Chaukidu
Dkt. Filipo Lubua
4.10 – 4:20 Salamu za Mtiva Mtiva
4:20 – 4:35 Burudani Aliyeandaliwa
4:35 – 5:20 Mada Elekezi ya 1 Prof. Alamin Mazrui na
Prof. Kimani Njogu
5:20 - 5:30 Salamu za Rais wa Chaukidu Prof. Leonard Muaka
5:30 - 5:40 Neno la Makamu Mkuu wa Chuo
na Ukaribisho wa Mgeni Rasmi
Makamu Mkuu wa Chuo
5:40 – 6:10 Hotuba ya Mgeni Rasmi Mgeni Rasmi
6:10 – 6:25 Picha za Pamoja na Mgeni Rasmi Makundi Matano
Yaliyoandaliwa
6:25 - 7:45 Chakula cha Mchana Wanajopo
8:00 - 9:40 Vikao Sambamba Na. 1 Washiriki Wote
9:50 - 11:30
Hoja Pevu ya 1
Jopo la Wabobezi wa Kiswahili
Washiriki Wote
na Wanajopo
11:30 - Mapumziko Washiriki Wote
J
um
am
osi
, D
isem
ba 1
4, 2
019
11
Mgeni Rasmi - Ufunguzi
Mh. Rebecca A. Kadaga (Mb)
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Uganda
12
Mada Elekezi ya 1 Ukumbi Mkuu
Mwenyekiti:
Makala- Lugha ya Kimataifa Barani Afrika:
Baina ya Kiswahili na Afrihili
Prof. Alamin Mazrui
Prof. Kimani Njogu
13
Jumamosi 8:00 - 9:40 Mch - Vikao Sambamba Na 1
Chumba cha 1
Mada: Kiswahili kwa Wageni
Mwenyekiti:
Mielekeo ya Wanafunzi wa Shule za Upili Kuhusu Ujifunzaji wa Kiswahili: Mintaarafu
Munispaa ya Kabale - Uganda
Utafiti huu unanuia kubaini mielekeo ya wanafunzi wa shule za upili kuhusu ujifunzaji wa Kiswahili:
Mintaarafu, Munispaa ya Kabale. Mielekeo huathiri mazingira ya ujifunzaji, ufundishaji na umihili wa lugha ya
Kiswahili. Malengo ya utafiti huu ni kubaini mielekeo ya wanafunzi, kutathmini uwiano kati ya mielekeo yao
na ujifunzaji wao wa Kiswahili na kuchunguza vyanzo vya mielekeo hiyo. Utafiti huu utaongozwa na nadharia
za utabia ya Skinner (1957) na nadharia ya utambuzi ya Piaget (1972). Data ya utafiti itakusanywa nyanjani
kupitia hojaji za kujazwa; maswali wazi, maswali funge na maswali vya viwango sambamba na majadiliano ya
makundi lengwa. Data itachanganuliwa kwa kutumia uchanganuzi wa kiwingidadi.
Mwasilishaji: Geoffrey Okello (Chuo Kikuu Cha Uislamu Cha Uganda-Mbale)
Lugha za Kiafrika Ziendelezwe Sambamba na Kiswahili
Kiswahili ni lugha ya mawasiliano ya Afrika mashariki. Ingawa nchini Uganda haijatiliwa mkazo, kikatiba ni
lugha ya pili rasmi . Inafundishwa katika baadhi ya shule za upili pamoja na Vyuo vikuu. Kwingine imeimarika
.
Ingawa lugha hii, inaendelea kuimarika, lugha za Kiafrika nyingine pia zinahitajika ili kusaidiana na Kiswahili.
Lugha hizi zina miundo na tamaduni zinazokaribiana , hivyo ni rahisi kutumia mfano kutoka lugha moja
(nitatumia kinyankore) kuelezea dhana fulani katika Kiswahili. Mtu akiwa anafundisha mofolojia, au sintaksia
ya Kiswahili, aweza kutumia mifano kutoka lugha yake ili kuelezea wanafunzi vizuri. Aidha, Sapir asema,
huwezi kufahamu watu bila kufahamu lugha yao. Mbinu ya uchambuzi wa maandishi itatumiwa, yaani, data
kutoka lugha ya Kinyankore zitalinganishwa na Kiswahili ili kuonyesha jinsi zinavyokaribiana.
Mwasilishaji: Yerindabo T. Innocent (Chuo Kikuu cha Kyambogo, Uganda)
Ukinzani wa Kinadharia na Kiutendaji Kuhusu Pedagojia za Ufundishaji wa Lugha za
Kigeni: Matumizi ya Tafsiri Katika Ufundishaji wa Kiswahili Nchini Uganda
Kinadharia, tafsiri katika ufundishaji wa lugha za kigeni inapingwa na baadhi ya wanazuoni kutokana na
uhusiano wake na Sarufi-Tafsiri. Jambo hili limezua mgogoro na ukinzani wa kitaaluma. Awali ufundishaji wa
lugha ulikitwa katika isimu miundo na kilichosisitizwa ni ufundishaji wa miundo ya kisarufi. Utaratibu na
mpangilio uliwekwa kwa misingi ya usasanyuzi linganuzi baina ya lugha lengwa na lugha asilia. Lengo kuu
lilikuwa kuwawezesha wanafunzi kuzungumza lugha kwa ufasaha bila kudhihirisha athari ya lugha ya kwanza.
Mwelekeo huu ulibadilika katika miaka ya 1950 na 1960 ambapo mbinu ya kimawasiliano ilichukuliwa kuwa
faafu zaidi katika ufundishaji wa lugha. Hata hivyo, utafiti uliojenga msingi wa makala haya unaonyesha kuwa
tafsiri ina nafasi kubwa katika ufundishaji wa Kiswahili katika shule za sekondari nchini Uganda. Tafsiri
haitambuliwi kama mbinu mojawapo katika mtaala. Makala haya yanajenga hoja kwamba huu ni wakati wa
muafaka wa kuikubali tafsiri kuwa mbinu mojawapo ya ufundishaji wa lugha za kigeni. Mwasilishaji: Sarah Ndanu M. Ngesu (Chuo Kikuu cha South-Eastern Kenya)
Dhima Ya Mbinu za Ufundishaji Lugha Katika Kuendeleza Umilisi wa Kuongea
wa Wanafunzi wa Kiswahili Nchini Uganda.
Nchi ya Uganda inaendeleza ufundishaji wa Kiswahili ili kuibuka na raia watakaokuwa na umilisi wa kuongea
Kiswahili ili waweze kuchangamkia fursa zinazotokana na muungano wa Afrika Mashariki. Ufundishaji wa
Kiswahili unaendelezwa katika shule za Sekondari kwa Wanafunzi ambao huanza kusoma Kiswahili katika
kidato cha kwanza. Walakini Ripoti ya UCE (2009) huonyesha kuwa wanafunzi wa Kiswahili huenda wasiwe
na umilisi wa kuongea Kiswahili mwishoni mwa masomo. Makala hii itachunguza mchango wa mbinu za
kufundisha lugha katika kuendeleza umilisi wa kuongea wa wanafunzi Uchunguzi unadhamiria kuibuka na
majibu ya maswali: Mchakato wa Ujifunzaji wa Kiswahili katika mazingira ya darasani unahusu nini? Umilisi
wa kuongea Kiswahili unaelezwa kivipi na Viwango vya umilisi wa kuongea wa wanafunzi mwishoni mwa
kidato cha nne ni vipi? Mtafiti atatumia Modeli ya Umilisi wa Kuongea iliyoasisiwa na Celce-Murcia na
wenzake (1995). Watafitiwa ni Wanafunzi ambao wamehitimu kidato cha nne pamoja na walimu wa Kiswahili
wa sekondari.
Mwasilishaji: Majariwa David (Chuo Kikuu cha Kabale)
Ju
mam
osi
, D
isem
ba 1
4, 2019
14
Jumamosi 8:00 - 9:40Mch - Vikao Sambamba Na 1 Chumba cha 2
Mada: Jopo la Kiingereza
Mwenyekiti:
Swahili Lexica on the fringe: The Design of a Bilingual Pedagogical Dictionary
The use of Swahili dictionaries, even bilingual lexica, presupposes an understanding of morphological structure
and a proficiency in analysing Swahili word forms. For learners with little or no previous experience in Bantu
languages the challenges are greater still. Therefore, the development of such understanding and proficiency is a
fundamental goal of L2 language instruction. Yet, few existing lexica manage the difficulties of Swahili (and
Bantu) lemmatisation sufficiently well and, as a result, most dictionaries do not significantly aid in this
development. The talk will focus on the development of a bilingual Swahili-Swedish (L2>L1) dictionary for
beginner students at the university level. In addition to normal uses, the dictionary is designed to function as a
pedagogical tool to be used actively in the process of language teaching, acquisition and reinforcement of
Swahili morphology, e.g., by providing more ways of identifying lemmata and discover relationships between
them.
Presenter: Niklas Edenmyr (Chuo Kikuu cha Upsala, Uswidi)
Indigenous Languages: The Way to Go in the 21st Century
The content in this paper is drawn from the findings and literature review of a Study carried out in Kabale
District, Western Uganda as a PhD study to establish the influence of Runyankore-Rukiga (RR) on English.
The study was based on the influence of Runyankore-Rukiga on English at secondary school level. The findings
indicated that the students studying Runyankore-Rukiga had a clear edge in terms of performance in English
compared to those in the same class who were not. In this paper we recognise that indigenous languages can be
used as a tool for learning altogether and better results can be realised. The paper, therefore, recommends that
indigenous languages should be taught in African schools if Africa is to cope with the needs of the 21st century.
Presenter: John Kintu (Chuo Kikuu cha Kyambogo)
Sustainable Development Goals in Africa: Windows of Opportunities for Kiswahili
Linguists in Tanzania
Head of African states, African governments and Representative officials, time and again they have been
arguing the need for African integration focusing on three agenda that are clearly stipulated to United Nations
Headquarters in New York in 2015 that sustainable Development should focus on economic, social and
environmental issues. It’s expected that all Africa states being the main actors and stakeholders should strive
to achieve such target. It is the fact that for accomplishment of those three mentioned focus, there is a need to
have a particular language that is common with traditionally African oriented. It’s from this perspectives that
the paper will have a focus on the role of Kiswahili language towards the sustainable development goals in
Africa. The objective of the study is to find out the extent of Kiswahili to African development and the reasons
of such a choice. The focus will include the Kiswahili and economic, Kiswahili and socio development and
Kiswahili with TOURISM. Presenter: Joseph Hokororo Ismail (Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Tanzania)
Ju
mam
osi, D
isem
ba 1
4, 2
019
15
Jumamosi 8:00 - 9:40Mch - Vikao Sambamba Na 1 Chumba cha 3
Mada: Kiswahili na Isimu
Mwenyekiti:
Nadharia za Isimu na Utafiti wa Kiswahili
Ufundishaji na utafiti wa sarufi ya Kiswahili umepiga hatua kubwa sana tangu miaka ya sitini na sabini.
Wataalam wa Kiswahili wamejitahidi ipasavyo kutumikiza nadharia za kiisimu katika uchanganuzi wa maumbo
na miundo ya Kiswahili. Hata hivyo, juhudi zao zinakumbwa na changamoto nyingi sana. Mojawapo ya sababu
za changamoto hizi ni kwamba nyingi za nadharia hizi zina chimbuko lake katika nchi za magharibi ambapo
hutumiwa kuchanganulia lugha zenye maumbo na miundo iliyo tofauti na ile ya Kiswahili. Nadharia hizi
zinapotumikizwa katika uchanganuzi wa lugha ya Kiswahili huzua changamoto nyingi. Karatasi hii itajaribu
kuangazia baadhi ya changamoto zinazowakumba wataalam wa Kiswahili (waalimu na wanafunzi kwa pamoja)
wanapotumia nadharia hizi kuchanganulia sarufi ya Kiswahili na mustakabali wake.
Mwasilishaji: Basilio Gichobi Mungania (Chuo Kikuu cha Nairobi)
Athari za Kituruki katika Lugha na Utamaduni wa Kiswahili
Kihistoria, kuna athari ndogo kiasi za kituruki katika lugha za Afrika Mashariki, na zile zinazopatikana zimefika
hapo kupitia wasemaji wa Kiarabu, Kiajemi, Kibulushi na lugha za Bara Hindi za Kikachi (Cutchi/Kachhchhi,
kinachojulikana kama Kikumbaro/Kibadala katika Afrika Mashariki) na Kisindi, walioajiriwa katika majeshi ya
Sultani wa Zanzibar karne ya 19 na mapema karne ya 20. Kuna maneno takriban 20 tu yenye asili ya Kituruki
katika Kiswahili; hata hivyo, machache yao ni yenye mrudio wa hali ya juu k.m. bunduki, baruti, mshikaki,
Afande! na korokoroni. Athari za Kituruki katika Afrika Mashariki zina asili yake ya mzunguko kutoka majeshi
ya Osmania (Ottoman armies), jambo ambalo laweza kuonekana katika maeneo ya kisemantiki yenye maneno-
kopwa ya Kituruki katika lugha ya Kiswahili. Nayo maneno hayo karibu yote yapatikana pia katika lugha
nyingine nyingi za Afrika Mashariki.
Mwasilishaji: Abdulaziz Yusuf Lodhi (Chuo Kikuu cha Uppsala, Uswidi)
Sababu za Upanuzi wa Maana za Maneno Katika Mazungumzo ya Kiswahili: Mifano
Kutoka Katika Vitenzi vya Kiswahili
Kila lugha huwa na maneno yenye maana zinazojulikana na kuzoeleka miongoni mwa watumiaji wake. Hata
hivyo, katika matumizi ya lugha ya kila siku, watu hujikuta wakitumia maneno kwa namna tofauti na
ilivyozoeleka katika jamii. Licha ya wazungumzaji wa lugha kutumia maneno huku wakiwa na maana
iliyozoeleka, bado wasikilizaji hujikuta wakiamua maana nyingine iliyo tofauti na makusudio ya msemaji.
Kutokana na hali hii, makala haya yanatoa ufafanuzi kuhusu suala la upanuzi wa maana za maneno unaofanyika
katika mazungumzo ya Kiswahili kwa kupambanua sababu za upanuzi huo. Kategoria ya maneno
iliyochunguzwa ni vitenzi kwa kuwa ndivyo vinavyochukuliwa kama nguzo kuu katika kukamilisha maana ya
sentensi. Utafiti huu unaongozwa na Nadharia ya Umaanilizi wa Mazungumzo ya Grice (1975). Data
ilikusanywa kwa njia ya hojaji na mahojiano na wazungumzaji nchini Tanzania. Matokeo yanaonesha kwamba
maneno yanayotumika katika mazungumzo hubebeshwa maana tofauti na makusudio ya msemaji. Sababu za
upanuzi huo ni matumizi ya maneno kitafsida, mmomonyoko wa maadili nk.
Mwasilishaji: Sikitu Elias Luvanda (TATAKI, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania)
Si Kila ‘Hapana’ ni ‘Hapana’: Uchunguzi wa Dhima za Kialami Pragmatiki 'Hapana'
Katika Kiswahili cha Mazungumzo
Makala hii inachunguza dhima za kialami pragmatiki hapana katika Kiswahili cha mazungumzo. Data
zimekusanywa kutoka katika mazungumzo yasiyo rasmi yanayofanywa na wazungumzaji wa Kiswahili katika
maeneo yasiyo rasmi kama vile kwenye vijiwe vya kahawa na vijiwe vya mamantilie na katika vipindi vya
televisheni. Kwa kutumia Nadharia ya Umuktadhaishaji ya Gumperz ya mwaka 1982, matokeo ya uchunguzi
huu yanaonesha kwamba licha ya KIPRA hapana kuwa na maana yake ya msingi ambayo ni kuashiria
kutokukubaliana na jambo, kina tabia ya kuchanuza maana tofautitofauti kulingana na muktadha kinamotumika.
Tabia hiyo hukifanya KIPRA hicho kuwa na dhima mbalimbali za kipragmatiki. Baadhi ya dhima za
kipragmatiki tulizozibaini katika makala hii ni kama vile KIPRA hapana kutumika kuashiria kuwa mzungumzaji
anatafuta jambo la kusema, anasahihisha kile kilichosemwa awali, ameshitushwa na taarifa alizozipata na
kuashiria kuwa mzungumzaji anashangaa. Kwa ujumla, makala hii inadokeza kwamba VIPRA ni vipashio vya
kiisimu vyenye utajiri wa maana katika lugha ya Kiswahili.
Mwasilishaji: Magreth J. Kibiki (Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam)
Ju
mam
osi
, D
isem
ba 1
4, 2019
16
Jumamosi 8:00 - 9:40Mch - Vikao Sambamba Na 1 Chumba cha 4
Mada: Kiswahili na Lugha Nyingine za Kiafrika
Mwenyekiti:
Kiswahili Kiinue Hadhi ya Lugha Nyingine za Kiafrika
Kiswahili ni lugha ya Kibantu ya kimsingi kwa sababu inashirikisha maandishi ya lugha ya awali ya mababu
inayoitwa "Proto-Bantu" (J.L. Doneux (1967) pamoja na lugha zote za Kibantu. Kulingana na uanishaji wa
Malcolm Guthrie(1948), Kiswahili ni Lugha ya Kibantu. Kwa hiyo kina uhusiano mkubwa kimuundo na lugha
nyingine za kiafrika za Kibantu. Lugha husababisha kushuka hadhi kwa nyingine lakini zinaweza pia kusaidiana
katika kuinua hadhi ya moja na nyingine. Makala hii itajadili jukumu la Kiswahili katika maendeleo ya lugha
nyingine za Kibantu kwenye bara la Afrika. Jinsi gani lugha hii inaweza kuokoa lugha hizi kutoweka; lakini pia
ni jinsi gani lugha hizi za Kibantu zinaweza kuwa na jukumu muhimu katika kueneza na kukuza lugha ya
Kiswahili Afrika nzima na ughaibuni. Kwa ujumla makala hii itazungumzia jukumu la Kiswahili na lugha
nyingine za kiafrika hasa za Kibantu katika kujengana na kukamilishana.
Mwasilishaji: Gordien Ndayikengurukiye (Chuo Kikuu cha Ualimu, Burundi)
Matumizi ya Lugha Katika Kuihamasisha Jamii
Lugha ni nyenzo muhimu sana katika mchakato wa uhamasishaji. Kwa kuwa lugha ni
chombo cha mawasiliano, kwa kiasi kikubwa, wanasiasa hutumia lugha katika kampeni
maalumu za kisiasa (Bakhtin, 1981; Charteris-Black, 2004, 2011; Jowett & O’Donnell,
1992). Wanasiasa ulimwenguni kote hutumia aina mahususi ya lugha ambayo huhamasisha
au kushawishi wananchi kutetea au kuunga mkono jambo au maoni fulani (Joseph,
2006). Kwa muktadha huo, lugha na uhamasishaji haviwezi kutenganishwa kwa sababu bila
ya kutumia lugha itakuwa vigumu kuhamasisha wananchi. Mtazamo wa kimseto
unaojumuisha ushawishi, utambulisho, na itikadi, unafafanua namna lugha za kienyeji
ikiwemo Kiswahili zinavyotumiwa katika uhamasishaji wa wapiga kura kwa kuegemea
muktadha halisi wa kampeni maalumu za kisiasa na kudhihirisha kwa mifano kuntu kwamba
wanasiasa hutumia aina mahususi ya lugha kuwahamasisha wanajamii kuhusu masuala ya
kijamii na ya kisiasa. Mifano itakayotumiwa katika wasilisho hili itajikita zaidi katika
kampeni za kisiasa nchini Kenya na Uganda. Mwasilishaji: Caroline Asiimwe (Chuo Kikuu cha Makerere)
Leonard Muaka (Chuo Kikuu cha Howard)
Tatizo la Mwingiliano wa Kiswahili na Lugha ya Kirundi
Lugha ya Kiswahili ina uingiliano na baadhi ya lugha za kiafrika. Kwa namna hiyo badhi ya warundi wanasikia
lugha hiyo lakini hawawezi kuitumia kwa maongezi. Ni rahisi sana kwa warundi kujifunza kiswahili kwa
sababu kuna maneno yanayorudia kutoka kirundi.Neno"dirisha" ni la kiswahili hubadirika na kuwa "idirisha"
kwa kirundi.Tofauti iliyopo ni silabi"i" inayoanzia neno "dirisha" kwa kirundi lakini maana ni moja .Pia kuna
herufi ambazo zinatamkwa visivyo kutokana na uzoefu wa matumizi ya lugha ya kirundi. Mfano neno"mtu"
kwa kiswahili na "umuntu" kwa kirundi.Warundi hutamka "mu" badala ya"m". Hitimisho ni kwamba si tatizo la
kimatamshi tu kuna tatizo la utumiaji wa maneno "kesho" na "Jana" ambayo hutumiwa kwa neno moja katika
lugha ya kirundi wakati mwingine ni maneno mawili tofauti yanayoonyesha wakati ujao na uliopita kwa
kiswahili. Kwa kuwa kirundi kina neno moja linalotumiwa kwa kuonyensha " kesho" na "Jana". Kwa kiswahili
warundi hutumia"kesho" ili kumaanisha "jana" au "kesho".
Mwasilishaji: Gabriel Niyubuntu (Chuo Kikuu cha Burundi)
Lugha za Kiafrika Kama Chemchemi za Makuzi ya Kiswahili Afrika Mashariki
Makala yanashughulikia nafasi za lugha za Kiafrika katika makuzi ya Kiswahili. Makala yanadurusu njia
mbalimbali zinazotumiwa kuunda msamiati na istilahi na mapungufu yanayobainika, pamoja na umuhimu wa
kuzingatia lugha asilia za Kiafrika kama milizamu muhimu ya kurutubisha Kiswahili. Makala yanatoa
mapendekezo ya jinsi ya kukabiliana na hali hii ili kuendeleza Kiswahili.
Mwasilishaji: Clara Momanyi (Africa Translingual Translators - ATT, Kenya)
Ju
mam
osi, D
isem
ba 1
4, 2
019
17
Jumamosi 8:00 - 9:40Mch - Vikao Sambamba Na 1 Chumba cha 5
Mada: Kiswahili na Sanaa
Mwenyekiti:
Utetezi wa Mwanamke Katika Muziki wa Kizazi Kipya
Makala hii, inalenga kubainisha utetezi wa hadhi ya mwanamke katika muziki wa kizazi kipya nchini Uganda.
Kwa muda mrefu, mwanamke amechorwa kama kiumbe duni katika mikabala mingi na kila wakati watafiti
huangazia nafasi duni ya mwanamke na udhaifu wake wala sio uwezo alionao. Mabadiliko katika mahusiano ya
kijinsia hayajamulikwa kwa kina ili kukidhi mahitaji ya wakati. Muziki wa kizazi kipya nchini Uganda
ulitokana na muziki wa asili uitwao kadongo kamu neno la Kiganda linalomaanisha gitaa moja na baadaye
uliathiriwa na mitindo ya kigeni. Makala hii itaangazia muziki teule ulioimbwa kuanzia mwaka 2009 hadi sasa
ambao unasawiri mitazamo mizuri kumhusu mwanamke na kupinga kasumba kwamba mwanamke ni mnyonge
ambaye lazima ajiegemeze kwa mwanamume ili apate kujikimu. Hivyo, nitatumia njia ya maelezo kuchanganua
matumizi ya lugha katika nyimbo teule ili kubaini utetezi wa hadhi ya mwanamke katika muziki wa kizazi kipya
nchini Uganda.
Mwasilishaji: Micah Bamugyeya (Chuo Kikuu cha Kyambogo)
Mchango wa Nyimbo Katika Kudumisha au Kupotosha Mila na Desturi za Jamii
Wimbo ni chombo muhimu katika kuhifadhi, kukuza na kueneza mila na desturi za jamii; lakini pia huweza
kuvipotosha. Umuhimu wa nyimbo ni Kuburudisha, Kuelimisha, Kudumisha/kuhifadhi mila na desturi za jamii,
kukuza na kueneza lugha...Msanii ni kioo cha jamii, hivyo anatakiwa kuwa mfano mzuri kwa hadhira yake, la
sivyio kwa kuwa anafuatwa na wengi, nyimbo zake zaweza kupotosha jamii iwapo anaenda kinyume na maadili
mema yajamiiyake. Pamoja na msaada wake mkubwa katika kudumisha/kuhifadhi mila na desturi za jamii yake,
huweza kupotosha mila na desturi za jamii kwa muda mfupi sana, iwapo msanii anakiuka sherie na kwenda
kinyume na maadili mema ya jamii yake.
Mwasilishaji: Bimenyimana Innocent (Chuo Kikuu cha Burundi, Uganda)
Mchango wa Sanaa Katika Ukuaji wa Lugha ya Kiswahili: Mifano Kutoka Katika
Mziki wa Bongo Fleva Nchini Tanzania
Katika miaka ya hivi karibuni, tumeshuhudia mijadala mbalimbali inayosisitiza matumizi ya lugha ya Kiswahili
katika shughuli mbalimbali za kijamii na kiserikali nchini Tanzania. Hii inadhihirika kupitia asasi na idara
mbalimbali zinazofanya juhudi za kuandaa makongamano, warsha pamoja na semina zinazolenga kujadili
mustakabali wa lugha ya Kiswahili. Hata hivyo, pamoja na jitihada hizo, bado mijadala hiyo haijamakinikia kwa
upekee nafasi ya sanaa katika ukuaji wa lugha sambamba na maendeleo ya jamii. Jambo hili limesababisha
mchango wa kazi za sanaa katika uenezaji wa lugha ya Kiswahili kutotazamwa kwa jicho la kipekee. Hivyo
basi, makala hii inaziba pengo hilo kwa kubainisha mchango wa Sanaa katika ukuaji wa lugha ya Kiswahili
sambamba na namna kazi hizo zinavyoweza kuchangia ukuaji wa maendeleo ya kijamii.
Mwasilishaji: Stella Faustine (Chuo Kikuu cha Dodoma)
Nafasi ya Misamiati Inayotumiwa na Waimbaji Katika Kuikuza Lugha ya Kiswahili
Tangu enzi za kale, kiswahili kimekuwa kikizungumzwa na chungu nzima ya watu katika afrika mashariki,
barani afrika na mabara mengine ulimwenguni. Kadiri miaka inavyozidi kusonga mbele ndivyo misamiati
inavyozidi kuibuka na kuchukua nafasi sahihi katika nyanja mbalimbali kutokana na matumizi yake. Misamiati
hiyo inatumiwa sana na waimbaji tofauti kwa lengo la kuukuza, kuuendeleza na kuuimarisha ubora na ladha ya
nyimbo zao wakati zinapowasilishwa kwa hadhira. Hii ni kwa sababu wameutambua umuhimu wa utangamano
unaoletwa na lugha hii adhimu katika nyanja mbalimbali za nchi husika. Misamiati hiyo ina umuhimu wake
lakini pia hatuwezi kusahau udhaifu unaoletwa na misamiati hiyo kwa hadhira kwa sababu inaweza kuendekeza
mila na desturi za jamii au ikaipotosha. Muimbaji anapopachika misamiati mipya isiyotambulika na wengi huwa
ana madhumuni ya kuburudisha na kuelimisha jamii. Jamii hiyo inaelimika wakati misamiati hiyo ni sahihi. Ila,
ikiwa anaweza kubuni misamiati ya kipekee na kuiwasilisha bila kuifanyia utafiti itakuwa ni jambo la kupotosha
jamii.
Mwasilishaji: Kaziri Alexis (Taasisi ya Ualimu)
Ju
mam
osi
, D
isem
ba 1
4, 2019
18
Jumamosi 8:00 - 9:40Mch - Vikao Sambamba Na 1 Chumba cha 6
Mada: Kiswahili, Lahaja na Mawasiliano
Mwenyekiti:
KiSheng: Tija ya Lugha za Vijana Katika Ukuzaji wa Lugha
Lahaja za Kiswahili na matumizi mengine ya lugha ya Kiswahili yasiyokubalika kama "sanifu" au
yasiyotambulika kitaaluma hupigwa vita vikali kwa njia moja au nyingine ikiwa ni pamoja na kudhalilishwa
katika sera za lugha, uchapishaji, ufundishaji na utafiti, kunyanyapaliwa katika miktadha rasmi na kutopewa
usaidizi wowote na kiserikali au kitaaluma. Pingamizi dhidi ya lahaja kongwe za Kiswahili kama Kiamu,
Kimvita, Kimakunduchi na lahaja-ibuka kama vile kiSheng hufanywa na viongozi wa serikali, wasomi, watu wa
kawaida na wengineo ambao wanaziona kama lugha potofu. Msimamo wetu hapa ni kwamba waliopotoka
katika vita hivyo ni hao wa kupinga matumizi haya ya Kiswahili tofauti na kisanifu. Madhumuni yetu hapa ni
kuonyesha kuwa Lugha haiwezi kukua na kusambaa kwingi bila kuzaa lahaja, lafudhi na matumizi mengi
mengine na kwamba ishara moja kubwa ya ukuaji wa Kiswahili ni kuwepo lahaja kongwe na lahaja mpya.
Tutadhihirisha hoja hii tukitumia data kutoka lugha kubwa kubwa duniani.
Mwasilishaji: Mokaya Bosire (Chuo Kikuu cha Oregon, USA)
Lugha na Mawasiliano: Kiswahili kwa Maendeleo ya Afrika Mashariki
Kazi ya lugha ni kusaidia wazungumzaji wake katika mawasiliano. Mawasiliano ni muhimu
sana katika maendeleo yoyoye. Nchi nyingi zilizoendelea duniani hutumia lugha
zinazoeleweka na raia wengi wa mataifa hayo. Mara nyingi lugha zinazotumika katika nchi
hizo huwa ni lugha za kwanza za raia wao. Bara la Afrika liligagwanywa kulingana na mkataba
uliopitishwa miongoni mwa nchi za Ulaya mjini Berlin Ujerumani mwaka wa 1884/1885.
Lengo la Makala yangu ni kuonyesha kwamba kikwazo kikubwa katika maendeleo ya bara la
Afrika ni ukosefu wa mawasiliano mwafaka kunakosababishwa na matumizi ya lugha za
kigeni. Kutumia lugha za kigeni katika kuendesha shughuli za maendeleo ya mataifa ya Afrika
kunasababisha kutengwa na kuachwa nyuma kwa raia wengi ambao hawajimudu katika lugha
hizo. Nitaonyesha jinsi lugha ya Kiswahili ndiyo inaweza kutumika katika mawasiliano kati ya
mataifa ya Afrika Mashariki ili kuharakisha shughuli za kimaendeleo. Mwasilishaji: Geofred Osoro Chuo (Kikuu cha Wellesley, USA)
Ju
ma
mosi
, D
isem
ba 1
4, 2019
19
Jumamosi 9:50 - 11:30 - Hoja Pevu/Kikao cha Wote Ukumbi Mkuu
Mwenyekiti:
Jopo la Wabobezi: Maendeleo ya Kiswahili Kama Taaluma na Kama
Lugha ya Mawasiliano Mapana
Prof. FEMK Senkoro
Prof. Clara Momanyi
Prof. M.M. Mulokozi
Prof. Inyani Simala
Prof. Austin Bukenya
Prof. Ruth Mukama
Prof. Mohamed Abdulaziz
Prof. Timammy Rayya
20
Jumapili - Ratiba ya Siku Kwa Ufupi
Muda Tukio Mhusika/Wahusika
2:00 - 5:00 Usajili Kamati Andalizi
1:30 – 2:45 Chai Washiriki Wote
3:00 – 4:40 Vikao Sambamba Na. 2 Washiriki Wote
4:50 - 6:30 Vikao Sambamba Na. 3 Washiriki Wote
6:30 - 7:50 Chakula cha Mchana Washiriki Wote
8:00 - 8:45 Mada Elekezi ya 2 Dkt. Ernesta Mosha
8:50 - 10:20 Vikao Sambamba Na. 4 Washiriki Wote
10:30 - 11:30 Hoja Pevu Na. 02 Washiriki Wote
11:30 - 12:30 Mapumziko Washiriki Wote
12:30 - 3:00 Dhifa na Utoaji Tuzo Washiriki Wote
Ju
mapil
i, D
isem
ba 1
5, 201
9
21
Jumapili 3:00 - 4:40 Asub - Vikao Sambamba Na 2 Chumba cha 1
Mada: Kiswahili kwa Wageni
Mwenyekiti:
Ukinzani wa Kinadharia na Kiutendaji Kuhusu Pedagojia za Ufundishaji wa Lugha Za
Kigeni: Matumizi ya Tafsiri Katika Ufundishaji wa Kiswahili Nchini Uganda
Kinadharia, tafsiri katika ufundishaji wa lugha za kigeni inapingwa na baadhi ya wanazuoni (kwa mfano, Sweet,
1845-1912; Celie-Murcia, 1979; Howatt ,1984) kwa kuhusishwa na Sarufi-Tafsiri. Watalamu hawa wanaeleza
kwamba tafsiri hudumaza umilisi wa lugha. Hata hivyo, katika karne ya 21, kuna ishara kwamba licha ya
kupingwa, tafsiri inarejea tena katika ufundishaji na ujifunzaji wa LGn. Tafiti za wataalamu Cook (2010
&2018), Martin (2013), Ito (2017), na Benzigar, (2019) zinaonesha kwamba tafsiri imeendelea kutumiwa
na walimu na wanafunzi. Utafiti uliojenga msingi wa makala hii unaonyesha kuwa tafsiri inatumika 78% katika
ufundishaji wa Kiswahili katika shule za sekondari nchini Uganda ingawa haitambuliwi kama mbinu mojawapo
katika mtaala. Walimu na wanafunzi walihojiwa walieleza kwamba tafsiri huwapa msukumo wajifunzaji,
huimarisha ujifunzaji wa msamiati na ni njia mwafaka ya kutathmini uelewa wa wajifunzaji. Makala hii
inajenga hoja kwamba huu ni wakati muafaka wa kuikubali tafsiri kuwa mbinu mojawapo ya ufundishaji wa
lugha za kigeni.
Mwasilishaji: Sarah Ndanu M. Ngesu (Chuo Kikuu cha South Eastern Kenya)
Motisha Zinazowafanya Wanafunzi wa Shule za Sekondari za Marekani Kusoma
Kiswahili: Mifano Kutoka Programu ya STARTALK ya Kiangazi
Wasilisho hili litajadili motisha zinazowasababisha wanafunzi wa shule za sekondari kujifunza Kiswahili kwa
kupitia programu ya STARTALK ya kiangazi inayoongozwa na Chuo Kikuu cha Maryland kupitia ufadhili wa
serikali ya Marekani. Kiswahili ni lugha pekee ya Kiafirika inayofundishwa kwenye progrmu hii miongoni mwa
lugha nyengine kama Kiarabu, Kichina, na kadhalika. Tutazungumza kuhusu programu moja kwenye jimbo
fulani la Marekani na tutajadili sababu zinazowahamasisha wanafunzi hawa kuanza na kuendelea kusoma
Kiswahili kwenye programu hii. Tutatumia dhana ya Dornei (1988) inayozingatia motisha za ndani na nje za
kujifunza lugha ya kigeni, na pia kazi ya Bernard (2010) inayozungumzia kuhusu uhusiano baina ya mbinu za
ufundishaji lugha, motisha, na matokeo.
Mwasilishaji: Alwiya S. Omar (Chuo Kikuu cha Indiana)
Uchambuzi wa Makosa ya Kisarufi na Kileksikoni Wanayofanya Wanafunzi
Wanaojifunza Kiswahili Kama Lugha ya Kigeni Nchini Marekani
Utafiti huu ulilenga kudadisi changamoto za kisarufi na kileksikoni zinazowakumba wanafunzi wanaojifunza
Kiswahili kama lugha ya kigeni. Ulifuata mwongozo wa Error Ananlysis Approach (Corder, 1967, 1971) ambao
hulenga kutambua makosa wanayofanya wanafunzi na hivyo kuwapa walimu miongozo ya kuboresha
ufundishaji wa lugha husika. Data zilikusanywa kutoka katika majaribio ya wanafunzi kumi na saba wa
Kiswahili nchini Marekani. Matokeo yanaonyesha kuwa vipengele vya sarufi vinavyowatatiza wanafunzi hawa
ni ngeli, matumizi ya a-unganifu na uelewa wa vitenzi vya Kiswahili ambavyo huambatanisha viwakilishi
mbalimbali. Kwa upande wa kileksikoni, wanafunzi walionekana kutatizika kutumia vitate na visawe, na
walifanya makosa mengi ya kitahajia hasa katika kuandika maneno yaliyotoholewa kutoka kwa Kiingereza.
Makosa ya sarufi changamano yalitokea miongoni mwa wanafunzi wa viwango vya juu ilhali makosa ya sarufi
ya kimsingi k.v. ngeli yalitokea zaidi miongoni mwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza. Pia, athari za lugha ya
kwanza zilidhihirika miongoni mwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza.
Mwasilishaji: Magdalyne Oguti Akiding (Chuo Kikuu cha Jimbo la Michigan)
Ugiligili wa Dhana Katika Vitabu vya Shule za Upili, Kenya
Kwa mujibu wa katika ya Kenya ya 2010, Kiswahili ni lugha rasmi na lugha ya taifa. Kama lugha rasmi,
Kiswahili hutumika katika miktadha rasmi mathalani: bungeni, mahakamani, ofisi za serikali na kwenye taasisi
za elimu. Nchini Kenya, Kiswahili hufundishwa katika viwango vyote vya elimu kuanzia shule za msingi hadi
vyuo vikuu. Katika kiwango cha upili, somo hili ni la lazima na pia hutahiniwa. Kutokana na uzito unaopewa
somo hili, walimu hujitahidi vilivyo kuwaandaa wanafunzi wao kuukabili mtihani wa mwisho wa kidato cha
nne (KCSE). Hata hivyo, katika ufundishaji wa somo hili kuna baadhi ya dhana ambazo zimetolewa fasili
tofauti jambo linaloishia kukanganya wanafunzi na walimu. Wasilisho hili linalenga kubainisha na kueleza
dhana hizi ili kuleta msawazisho wa kifasili kwa manufaa ya watumizi wa lugha ya Kiswahili. Baadhi ya dhana
hizi ni pamoja na: kirai, kishazi tegemezi, a- unganifu, sentensi sahili, kielelezo mistari na vielezi namna
vikariri.
Mwasilishaji: Shadrack Kirimi (Chuo Kikuu cha Nairobi)
Ju
mapili, D
isem
ba 1
5, 2
019
22
Jumapili 3:00 - 4:40Asub - Vikao Sambamba Na 2 Chumba cha 2
Mada: Kiswahili na Fasihi
Mwenyekiti:
Nafasi ya Fasihi ya Watoto Katika Mtaala Wenye Msingi wa Kuendeleza Vipaji 2017
Session Paper Na. 2 ya 2015 ilipendekeza kurekebisha Sekta ya Elimu na Mafunzo ili kutoa mafunzo kwa kila
mwanafunzi kwa lengo la kumkuza kwa njia kamilifu na iliyojumuishi ndiposa tuweze kupata raia waliokomaa
kiakili, kihisia na kimwili. Mtaala huu ulioanza kutekelezwa nchini miaka mitatu iliyopita, unapendekeza
umilisi wa kimsingi ambao mwanafunzi anatarajiwa kuwa nao ili kujiendeleza kimaisha. Mapendekezo haya
yote yameegemea kwenye malengo sita ya kitaifa ya elimu (KICD, 2017). Pamekuwa na mijadala mbalimbali
kuhusu namna ya kuhakikisha kuwa mtaala huu unafanikiwa katika kuyafikia malengo ya elimu kwa jumla na
malengo ya lugha ya Kiswahili. Ni katika mkutadha huu ambapo makala hii inalenga kubainisha nafasi ya fasihi
ya watoto katika kuyafikia malengo ya mtaala mpya ambao umezinduliwa nchini Kenya na unatumika katika
viwango vya chini vya shule za Msingi.
Mwasilishaji: Pamela Muhadia Ngugi (Chuo Kikuu cha Kenyatta)
Maudhui na Fani Katika ‘Poems From Kenya: Gnomic Verses in Swahili (Nassir, 1960)
Mshairi kama watunzi wengine ni kiumbe ambaye hawezi kutengwa na jamii na utamaduni anaoutungia. Katika
makala hii tutaangazia mashairi ya Ahmad Nassir bin Juma Bhalo almaarufu Malenga wa Mvita, hususan
diwani yake ya kwanza kuchapishwa, ambayo haikuangaziwa sana katika tafiti za ushairi wa Kiswahili: Poems
from Kenya: Gnomic verses in Swahili (1966). Mashairi haya yatahakikiwa kwa mikabala ya Nadharia ya
Uhistoria Mpya ambayo iliasisiwa na Stephen Greenblatt na kuendelezwa na wengine. Nadharia hii huangazia
historia ya matini kwa kuihusisha na ruwaza za utawala, jamii au itikadi za kipindi fulani. Itatuongoza katika
kuangazia lugha na matukio katika kazi ile ambayo yanaoana na muktadha wa wakati wa utunzi wake Ahmad
Nassir katika juhudi zetu za kubainisha maudhui na fani katika mashairi yake. Diwani ina mashairi hamsini na
tutatumia mbinu kusudio kuteua mashairi ambayo yatahakikiwa kimaudhui na kifani. Katika kufanya hivi,
tutashadidia alivyosema mwandishi katika utangulizi wa diwani hii: Kiswahili ni kingi.
Mwasilishaji: Rachel Maina (Chuo Kikuu cha St. Lawrence, Kenya)
Kutoka Pwani Hadi Bara: Maendeleo ya Ushairi wa Kiswahili Nchini Kenya
Historia ya ushairi wa Kiswahili inabainisha kuwa asili ya utanzu huu ni pwani ya Afrika Mashariki. Utunzi wa
mashairi ya Kiswahili ulitawaliwa na misimamo mikali ya kihafidhina – kuwa ushairi ni sehemu ya utamaduni
wa Mswahili na ulifaa kutungwa kwa kuzingatia arudhi, utamaduni na mazingira ya Waswahili. Wengi wa
washairi wa kale walikuwa mashehe ambao waliukita utunzi wao katika imani ya dini ya Kiislamu. Ushairi wa
Kiswahili ulianza kuchukua mkondo mpya wakati mabadiliko mengi ya kisiasa, kijamii na kiuchumi yalianza
kushuhudiwa barani Afrika na ulimwenguni kwa jumla. Ushairi, sawa na tanzu nyingine za fasihi, ulianza
kupanuka kimaudhui na kifani. Hadi kufikia sasa, lugha na fasihi ya Kiswahili imekuwa taaluma ya kiusomi.
Ushairi wa Kiswahili umepata umaarufu miongoni mwa wasomi kiasi cha kuufanya kukiuka mipaka
iliyowekwa na watunzi wa kale. Makala haya yanajadili mchango wa washairi na wasomi wasio na asili ya
pwani katika maendeleo ya ushairi wa Kiswahili nchini Kenya.
Mwasilishaji: Timothy Kinoti M'Ngaruthi (Chuo Kikuu cha Embu, Kenya)
Uchimuzi wa Lugha ya Kisemantiki Katika Riwaya za Kihalisiajabu
Makala haya yanachunguza dhana nzima ya uchimuzi katika kiwango cha lugha ya kisemantiki katika riwaya
za na Vita vya Mapenzi (2012) na Mzimu wa Waufi (2013) za Maundu Mwingizi. Riwaya hizi ni riwaya za
kihalisiajabu na ni riwaya ambazo kwa uwelewa wetu hazijafanyiwa utafiti, labda ni kutokana na kusheheni
masuala ya uchawi na ushirikina watafiti wa kisasa wanaona ni mambo yaliyopitwa na wakati. Ndio maana
hawajaweza kuzimakinikia. Hivyo basi, katika makala haya tutangalia jinsi riwaya hizi za kihalisiajabu
zilivyoweza kutumia lugha ya kisemantiki katika kuchimuza maudhuia mbalimbali. Kwa kuwa, umuhimu mkuu
wa lugha ni kufaulisha uwasilishaji wa maana ambapo ujumbe hubainika kutokana na maana yake na kufuatilia
ufafanuzi wa maana zilizobebwa na vipashio vya lugha vinavyohusika hivyo basi, katika makala haya
tutaangalia mbinu ambazo zinachangia uchimuzi wa uwasilishaji wa maana katika riwaya teule na jinsi mbinu
hizo zilivyoweza kuchimuza maudhui anuwai katika riwaya hizi za kihalisiajabu..
Mwasilishaji: Neema George Mturo (Chuo Kikuu Cha Tumaini Makumira, Tanzani
Ju
mapil
i, D
isem
ba 1
5, 2019
23
Jumapili 3:00 - 4:40Asub - Vikao Sambamba Na 2
Chumba cha 3
Mada: Kiswahili na Lugha za Kiafrika
Mwenyekiti:
Lugha za Asili Katika Zama za Baada-ukoloni Katika Afrika: Sera na Utekekelezaji
Kabla ya ukoloni, lugha za asili zilitumika katika jamii mbalimbali kutimiza majukumu yote ya kimawasiliano.
Wakati wa ukoloni, hali ilibadilika kwa lugha nyingi kwa sababu wakoloni walilazimisha matumizi ya lugha
zao katika nchi zetu katika nyanja muhimu kama elimu, utawala, n.k. Baada ya ukoloni, suala la lugha za asili
kwa kiasi kikubwa limepuuzwa na serikali zetu, licha ya kuwepo kwa matamko mbalimbali, mathalani: Azimio
LA Harare (Chimhundu 1997), Azimio LA Asmara (2000) na hats Sera ya Utamaduni (1997) ya Tanzania.Hivi
sasa, ukiondoa mifano michache ya lugha kama Kiswahili, Kinyarwanda, lugha chache za Afrika Kusini,
Kiyoruba, Kihausa, n.k. lugha nyingi za asili matumizi yake yamebanwa sana. Makala hii inajadili hatima ya
lugha za asili kwa kuangalia Sera zilizopo, hatua zinazipendekezwa katika maazimio, hali halisi, na majukumu
ya wataalamu kuhakikisha hatua zinazopaswa kutekelezwa zinatekelezwa.
Mwasilishaji: Kulikoyela Kahigi (TATAKI, CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM, Tanzania)
Uingizwaji wa Lugha za Kiafrika katika Mtaala wa Elimu kwa Lengo la Kuhifadhi
Utamaduni
Makala hii inajadili umuhimu wa lugha za Kiafrika kimawasiliano na kitamaduni na haja ya kuzihifadhi kupitia
Elimu. Lugha na utamaduni ni mambo yasiyoweza kutenganishwa, kwa kuwa yanategemeana. Kazi kubwa ya
lugha mbali ya mawasiliano ni kutambulisha na kuhifadhi utamaduni wa jamii fulani katika nyanja muhimu za
kimaendeleo yaani, kisiasa, kiuchumi, kielimu, kijamii na kiutamaduni. Baadhi ya lugha za Kiafrika zimeachwa
nyuma au zimesahaulika kwa muda mrefu bila mikakati ya kuziendeleza, kiasi ambacho zimeanza kufa. Kwa
mintarafu hii, makala haya yanalenga kuonesha nini kifanyike katika kuhifadhi lugha hizi kuokoa jahazi la
kupotea kwa baadhi ya lugha za Kiafrika. Mjadala wa Makala haya unategemea data zilizokusanywa kutoka
jamii mbalimbali kupitia njia ya hojaji, dodoso na usomaji wa machaapisho mbalimbali na kisha kuchambuliwa
kwa mchakato wa Tyler’s (1975) wa uendelezaji wa mtaala. Umuhimu wa makala hii utasaidia sana katika
kupanga mikakati ya kuendeleza lugha za Kiafrika ndani na nje ya Bara la Afrika.
Mwasilishaji: Mary Zacharia Charwi (Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam, Tanzania)
Ukuaji wa Kiswahili Sambamba na Lugha Nyingine za Kiafrika
Katika mpito wa historia, Kiswahili kimepiga hatua nne kubwa ambazo zimekisaidia sana kufika pale ambapo
kipo sasa, na Kiswahili sasa ndiyo lugha muhimu ya Kiafrika ambayo inaweza kuitwa lugha ya kimataifa. Hatua
hizi zote zimewatia hofu baadhi ya wasemaji wa lugha nyingine za Kiafrika (kama vile Gikuyu na Luganda,
Afrika ya Mashariki) waliodhani ya kwamba maendeleo haya makuu ya Kiswahili yatazififiza lugha zao na hata
kuziua hatimaye, hofu ambayo haina msingi kiisimu, kwani lugha haziuawi na lugha nyingine bali, kinyume
kabisa, huchangiana katika makuzi na aidha maenezi yao. Mwasilishaji: Rocha Chimera (Chuo Kikuu cha Pwani, Kenya) Target Area:
Kiswahili na Lugha Nyingine za Kiafrika: Mkabala Linganishi
Lugha ni kipengele ambacho hufungamanishwa na historia ya jamii mahususi. Jamii hizi huchunguzwa
kihistoria kwa kuegemea wazungumzaji wa lugha katika mijongeo kutoka eneo moja kwenda jingine. Lugha zao
huathiriana kwa kupitia muwasala, biashara na shughuli za kila siku. Jambo la kuhusisha lugha na historia
huibua mjadala juu ya uhusiano uliopo baina ya dhana hizi. Ili kuzifafanua dhana hizi kwa undani, makala hii
inazijadili kwa pamoja kwa kuegemea hasa historia ya lugha ya Kiswahili na lugha za Runyoro, Rutooro,
Runyankore na Rukiga. Kwa kuegemea nadharia ya Mwachano na Makutano ya Lugha za Kibantu (Massamba,
2007), makala hii inafafanua kwamba hizi ni lugha zenye mnasaba ambazo zimetokana na Mame-lugha moja.
Aidha, kwa kutumia mkabala linganishi na kigezo cha sauti mrejeo, makala inafafanua kwamba maumbo
tunayoyaona leo hii kisinkronia, yametokana na mabadiliko ya lugha na yanaweza kufafanuliwa kidikronia.
Mwasilishaji: Caroline Asiimwe (Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda)
Ju
mapil
i, D
isem
ba 1
5, 2019
24
Jumapili 3:00 - 4:40 Asub - Vikao Sambamba Na 2
Chumba cha 4
Mada: Kiswahili, Lahaja, na Uhamasishaji
Mwenyekiti:
Kiswahili Kama Lingua Franka ya Afrika Mashariki: Je, ni Baraka au ni Laana?
Hadhi ya Kiswahili katika eneo la Afrika Mashariki inatofautiana katika mataifa tofauti. Nchini Kenya,
Kiswahili ni lugha rasmi na pia ya taifa. Nchini Tanzania, ni Lugha ya Taifa na pia hutumika katika shughuli
nyingi rasmi. Ni lugha itumiwayo katika kiwango cha elimu ya msingi. Nchini Uganda, Kiswahili kimeteuliwa
kama somo la lazima katika mtaala uliozinduliwa mnamo 2017. Kilipendekezwa kama lugha rasmi ya pili ya
Uganda mnamo 2005 lakini pendekezo hilo halijapitishwa rasmi. Mnamo 2017, Bunge la Chini la Rwanda
lilipitisha sheria inayotambua Kiswahili kama lugha rasmi nchini humo. Makala haya yanatumia nchi hizi nne
za Afrika Mashariki kuchunguza maendeleo ya Kiswahili katika kipindi cha sasa na kuonyesha kama maendeleo
hayo yana matokeo chanya au hasi katika mataifa husika na eneo lenyewe. Utafiti utaongozwa na nadharia
iliyoasisiwa na Howard Gile ya makubaliano ya mawasiliano (CAT) lakini ambayo imeendelezwa katika hali
nyingi. Yatatumia mihimili yake ya mwachano na makutano. Makala yanachukulia kwamba maendeleo ya sasa
ya Kiswahili yana manufaa mengi kuliko hasara.
Mwasilishaji: Iribe Mwangi (Chuo Kikuu cha Nairobi, Kenya)
Njia Wanazotumia Wanahabari Katika Kubuni Msamiati wa Kiswahili Nchini Kenya:
Mfano Kutoka Redio Citizen na KBC Idhaa ya Taifa
Maendeleo ya haraka katika nyanja mbalimbali yamezua haja ya kubuni msamiati mpya ili kukidhi haja ya
mawasiliano. Mdee (1996), anasema kuwa uundaji wa maneno mapya ni jambo ambalo linazidi kufanyika kila
wakati maadamu binadamu anatumia lugha. Sababu za kubuni msamiati ni nyingi mathalani; kuchakaa kwa
maneno yaliyobuniwa, kukidhi haja ya utamaduni, mwingiliano wa jamii mbalimbali na pia kukua kwa kasi kwa
teknolojia ya habari na mawasiliano. Utafiti huu ulilenga kuchunguza mbinu ambazo watangazaji wa redio
hutumia kubuni msamiati katika utangazaji wao wa habari za Kiswahili nchini Kenya. Baadhi ya mbinu
zilizobainika ni pamoja na ukopaji, ufupishaji, akronimu, uhulutishaji na ubunifu. Utafiti huu unaweza
kufanikisha uarifu katika taarifa za habari na pia kuboresha lugha sanifu ya Kiswahili hasa katika mawasiliano.
Mwasilishaji: Mugambi Allam (Chuo Kikuu cha Embu, Kenya)
Thamani ya Mawasiliano Katika Ufyosi wa Kwenye Jumbe za Mitandao ya Kijamii:
Mifano ya Jumbe za WhatsApp
Makala inalenga kufafanua thamani ya mawasiliano (kama kipengele kimojawapo cha isimu-matini) kutoka
katika ufyosi unaosawiriwa kupitia jumbe za WhatsApp. Ufyosi, licha ya kubeba dhana hasi kwa jamii nyingi,
ni nyenzo maarufu inayotumika kuwasilisha dhana mbalimbali. Makala itajifunga katika ufyosi unaojielekeza
kwenye eneo la jinsi. Jumbe za ufyosi zitakazoshughulikiwa ni zile zinazogusa: a) matendo yanayotendwa na
maeneo ya siri ya mwanadamu pamoja na matokeo yanayotokana na matendo hayo; na b) Namna yoyote ya
upindishaji wa maumbile au matendo ya mwanadamu. Data zimekusanywa kupitia jumbe za WhatsApp
zilizoingia katika simu ya mwandishi. Swali muhimu linalolengwa kujibiwa na makala hii ni: Je, ufyosi
unaopatikana katika jumbe za WhatsApp unawasilisha thamani ipi ya jamii kuhusu masuala ya jinsi?
Mwasilishaji: Athumani S. Ponera (Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere, Tanzania)
Tathmini ya Mwenendo wa Uundaji wa Istilahi katika Maendeleo ya Kiswahili:
Mafanikio na Changamoto
Katika zama hizi za utandawazi, kumekuwa na juhudi mbalimbali za kuunda istilahi. Uundaji wa istilahi hizi
unaonekana kufanyika kiholela na hivyo kuzua changamoto kadhaa. Makala haya yanatathmini juhudi hizi ili
kuainisha mafanikio yaliyofikiwa pamoja na changamoto. Katika utafiti huu mdogo imebainika kwamba istilahi
za Kiswahili zinaundwa kila uchao kwa mbinu za upanuzi wa maana, ufinyazi, ufafanuzi, ukopaji, tafsiri sisi, na
kadhalika. Kumekuwa na matumizi makubwa ya Kiswahili kwenye mikutano rasmi, vyombo vya usafiri,
vyombo vya habari, ufundishaji, uchapishaji au uandishi, na kadhalika. Hata hivyo, uundaji wa istilahi
unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo ubabeli wa kiistilahi, istilahi mbovu, usambazaji na uhaba wa
makongano ya kikanda ya kuzisanifisha. Kuna haja ya kuwa na usimamizi mzuri wa istilahi ili kuwa na
mtiririko bora wa matumizi ya istilahi zinazoundwa.
Mwasilishaji: Pendo Salu Malangwa (TATAKI, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania)
Ju
mapili, D
isem
ba 1
5, 2
019
25
Jumapili 3:00 - 4:40 Asub - Vikao Sambamba Na 2
Chumba cha 5
Mada: Kiswahili na Uchumi
Mwenyekiti:
Umuhimu wa Kiswahili Katika Biashara
Mpango wa biashara ni kauli rasmi ya malengo ya biashara, sababu zinazoyafanya yakisiwe kuwa
yanawezekana, na mpango wa kutimiza malengo hayo. Aidha, inaweza kuwa na habari msingi kuhusu shirika
au kundi linalojaribu kufikia malengo hayo. Katika kutimiza ndoto hizo , inaonekana kuwa lugha ya kiswahili
imepewa kipao mbele katika jumuiya ya Afrika Mashariki na kwingineko. Malengo ya biashara yanaweza
kufafanuliwa kwa mashirika ambayo lengo lao ni faida na yale yasiyo ya faida. Mpango wa biashara za
mashirika ya faida kimsingi husisitiza malengo ya kifedha , kama vile faida ama kupata mali. Kwa mfano, hayo
mashirika ya kibiashara tunayoyazungumzia, katika jumuiya yetu ya Afrika Mashariki ili malengo yao
yatimizwe hatuna budi tutumie lugha ya kiswahili kwa ajili ya kusikilizana baina ya wananchi wa Afrika, ndiyo
maana hii lugha ya kiswahili ina umuhimu sana katika sekta ya kiswahili Afrika na kwingineko.
Mwasilishaji: Innocent Nshimirimana (Chuo Kikuu cha Ualimu, Burundi)
Kiswahili Nguzo ya Maendeleo Endelevu Katika Afrika Mashariki
kisiri yangu inalenga kuonyesha umuhimu wa lugha ya Kiswahili na jinsi lugha hii inawonekana kama nguzo ya
maendeleo ya Afrika Mashariki. Kwanza, lugha ya Kiswahili inatuunganisha na chungu nzima ya watu duniani
kote. Lugha hii hurahisisha mawasiliano kati wafanyabiashara katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Bidhaa nyingi katika sehemu hii hufanyika kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Kiswahili hustawisha maendeleo
ya kibiashara. Watu wanapoelewana kilugha, wubadilishana mawazo na fursa za maendeleo hufuata. Pili,
Kiswahili chenyewe ni bidhaa. Mimi nimeshapata hela kwa kufundisha watu tofauti lugha hii. Burundi na katika
nchi nyingine za Afrika Mashariki, wanaotaka kujifunza ni wengi na mafunzo hayo husaidia wahusika wote.
Soko la Kiswahili ni kubwa na walimu ni wachache. Kwa kufundishana lugha hii, tunainuana kiuchumi na
tunaungana kijamii, tunajenga jumuiya bora. Mwisho, Kiswahili kinatuunganisha kijamii na kiuchumi. Ni
nguzo ya maendeleo endelevu katika Afrika Mashariki na ulimwengu mzima.
Mwasilishaji: Deogratias Ndagijimana (Shule ya Sekondari ya Kigutu, Burundi)
Tathmini ya Tafsiri za Taarifa za Pembejeo Kutoka Kiingereza Hadi Kiswahili
Sekta ya kilimo nchini Kenya ni muhimu sana na huchangia kipato cha nchi. Isitoshe, wakulima wengi
wanapatikana vijijini ambapo wengi hawana umilisi wa Kiingereza. Kutokana na hili watengenezaji wa
pembejeo za kilimo hutafsiri maelekezo ya vibandiko vya pembejeo kutoka Kiingereza hadi Kiswahili ili
wakulima wengi waelewe na watumie. Ni muhimu sana kwa tafsiri za taarifa hizi kuwa sahihi kwa matumizi
bora na kuzuia watumiaji kudhurika au kuhatarisha maisha yao na ya mifugo au mimea. Makala yatatathmini
ubora wa tafsiri za Kiswahili za vibandiko hivyo ili kuona iwapo zinapasha ujumbe vilivyo. Data ya makala
haya itadondolewa kutoka kwa tafsiri za Kiswahili. Sampuli itatokana na vibandiko vya madawa ya kunyunyizia
mifugo, mashamba na ya kuua wanyama sumbufu shambani. Nadharia ya Skopos (Vermeer 1970) itatumiwa
kutathmini tafsiri zilizopo na pale ambapo kuna tatizo mapendekezo yatatolewa ili kusaidia kuendeleza
mawasiliano kupitia vibandiko hivyo. Mwasilishaji: Miriam Kenyani Osore (Chuo Kikuu cha Kenyatta, Kenya)
Uchanganuzi wa Mikakati na Mitindo Kujifunza Kiswahili Kama Lugha ya Biashara
Miongoni mwa Wafanyabiashara Jijini Kampala-Uganda
Jiji la Kampala limeibuka kuwa kimbilio la wafanyabiashara kutoka nadani nan je mwa Uganda.Utangamano
huu umefanya wafanabiashara kutumia lugha ya Kiswahili kwa sababu wateja wao hutoka sehemu mbali mbali
za ndani mwa nchi nan je ya nchi.kwa wengi ambao wanatumia Kiswahili ,wamefanikiwa kukitumia bila
kujifunza darasani.Hali hii imezua azma ya kutaka kujuwa ni mikakati na mitindo ipi wafanayabiashara jijini
Kampala hutumia kujifunza Kiswahili kama lugha ya kibiashara.Makala hii itaongozwa na mseto wa nadharia
.Yaani nadaharia ya ufuatilizi ya Krashen (1981) na Modeli ya Elimu jamii ya Gradener (1985).Utafiti
utafanyika kwa maduka ya akedi yanayopatika jijini Kampala ambao biashara tofauti tofauti huendelezwa.Vile
vile makala hii itaangazia changamoto zinazowakumba wafanyabiashara wakati wa kutumia miakakti na
mitindo ya kujifunza lugha wakati wanajifunza Kiswahili kama lugha ya kibiashara.
Mwasilishaji: Aidah Mutenyo (Chuo Kikuu cha Kabale)
Ju
mapil
i, D
isem
ba 1
5, 2019
26
Jumapili 3:00 - 4:40 Asub - Vikao Sambamba Na 2
Chumba cha 6
Mada: Kiswahili kwa Wageni
Mwenyekiti:
Ubunifu wa Kozi Fupi za Kiswahili Kama Lugha ya Kigeni Kulingana na Mahitaji
Wasilisho hili lina lengo la kuonesha mfano wa kozi fupi ya kufundisha Kiswahili kwa wageni, mbali na kozi za
kawaida kwenye vyuo vikuu. Kozi hiyo inawapa wanafunzi wanaotarajia kusafiri Afrika ya Mashariki kwa ajili
ya mafunzo ya huduma kwa jamii, au sababu nyinginezo, na ambao wana mzigo mkubwa wa krediti za masomo
mengine utangulizi wa lugha ya Kiswahili na utamaduni kabla ya kusafiri. Wasilisho litaonesha kozi fupi ya
Kiswahili inayofundishwa katika Chuo Kikuu cha Cornell kilichopo katika jimbo la New York, Marekani,
ambapo kundi la wanafunzi wanaosomea shahada ya masuala ya Afya ya Jamii na wengine wanaotegemea
kusomea shahada ya utabibu husoma kozi hii na baadaye husafiri katika Chuo Kikuu cha KCMC kilichopo
Moshi, na pia katika hospitali ya Bugando, Tanzania kwa mafunzo ya huduma kwa jamii na mafunzo ya
vitendo.
Mwasilishaji: Happiness Bulugu (Chuo Kikuu cha Cornell, USA)
Ufundishaji na Ujifunzaji wa Kiswahili kwa Wageni na Kama Lugha ya Kigeni:
Nyumbani na Ughaibuni
Mbali na kufundishwa kama lugha ya pili shuleni, vyuoni, katika vyuo vikuu na taasisi nyingine mbalimbali
katika Afrika ya Mashariki na Kati, Kiswahili kinafundishwa pia kwa wageni katika eneo hili (Afrika ya
Mashariki na Kati) na kama lugha ya kigeni katika maeneo mengine barani Afrika, na kwingineko duniani.
Ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni na kwa wageni unaendelea kukua na kuenea, si
ughaibuni tu, bali pia katika Afrika ya Mashariki na Kati, na kwingineko. Makala hii itajadili mambo
mbalimbali kuhusu ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili kwa wageni na kama lugha ya kigeni, kwa mfano: (i)
sababu za kukua na kuenea kwake; (ii) malengo yake; (iii) matokeo yake nyumbani na ughaibuni; (iv) hali yake
kufikia sasa na mustakabali wake; (v) mbinu pendekezwa ya ufundishaji; na (vi) changamoto na mapendekezo.
Mwasilishaji: Beatrice Ng'uono Okelo (Chuo Kikuu cha Baylor)
Kiswahili na Elimu: Matatizo ya Ujifunzaji na Ufundishaji wa Kiswahili Shuleni Nchini
Burundi
Ikisiri hii inalenga kubainisha matatizo yahusuyo ufundishaji na ujifunzaji wa lugha ya kiswahili shuleni. Kwa
hiyo ikisiri hii itajaribu kuweka hadharani nini kifanyike ili kuepukana na matatizo akutana nayo ajifunzaye na
afundishaye kiswahili. Kuna shida kubwa ya namna ya kufundisha kiswahili kama lugha ngeni katika shule za
msingi. Mada hii itajaribu kuonyesha mbinu ambayo inaweza kutumiwa katika kusaidia kutatua tatizo hilo.
Aidha mada hii inahusu umuhimu wa kusoma vitabu ambavyo ni hazina pekee ambayo imehifadhi mambo
chungu nzima ambayo kila mtu huhitaji katika uhai wake. Kutokana na umuhimu huo ikisiri hii itajaribu
kufichua hasara kadha wa kadha zisababishwazo na ujinyimaji wa mambo mengi muhimu yaliyomo vitabuni.
Isitoshe, wahenga hawakuacha kasema kwamba kuuliza si ujinga. Mada hii itajaribu kubainisha njia mrua ya
kupata utatuzi wa swala fulani. Njia hiyo si nyingine isipokuwa kuuliza wajuao yaani kufanya utafiti.
Mwasilishaji: Nintunze Fulgence (Chama Cha Kuendeleza Kiswahili Nchini Burundi (CHAKUKIBU)
Nafasi ya Kiswahili Nchini Tanzania na Mustakabali wa Wingilugha na Uanuailugha:
Uzoefu wa Uwandani
Kiisimujamii dunia imetawaliwa na sifa ya wingilugha. Jamii za Kiafrika hazijitengi na sifa hiyo. Tanzania ni
miongoni mwa nchi kumi na tatu (13) kwenye kundi la nchi zenye lugha zaidi ya (100) zinazofanya asilimia
75% ya lugha za ulimwengu. Uzoefu wa uwandani unaonesha ikolojia isiyo na msawazo miongoni mwa lugha
za Tanzania. Kiswahili kinatawala mandhari-lugha lakini lugha za jamii hakuna kabisa. Wingilugha ni sifa ya
kuwapo kwa lugha zaidi ya moja katika ikolojia wakati uanuailugha ni kutumika kwa lugha zilizopo katika
ikolojia. Makala hii ni matokeo ya utafiti wa mandhari-lugha uliofanyika katika Jiji la Mbeya. Kwa kutumia
nadharia ya Ubeberu wa Kiisimu, madai ya makala hii ni kwamba sera za lugha barani Afrika, zitazamwe upya
na kutilia mkazo suala la uanuailugha.
Mwasilishaji: Gervas A. Kawonga (Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa)
Ju
mapili, D
isem
ba 1
5, 2
019
27
Jumapili 4:50As - 6:30 Mch - Vikao Sambamba Na 3
Chumba cha 1
Mada: Kiswahili na Lugha Nyingine - Jopo la Mjadala Mwenyekiti:
Blogu ya Lugha na Tamaduni Zetu Katika Ukanda wa Wazungumzaji wa Kiswahili
Hapana mjadala kwamba lugha na utamaduni (wa jamii ambamo lugha husika huzungumzwa) ni vitu
vilivyoshikamana. Kwa hivyo lugha huakisi utamaduni (maisha ya kila siku ya jamii) na utamaduni huzusha
lugha. Jopo hili litazungumzia wazo la kuanzisha mradi wa BLOGU ya lugha na tamaduni za jamii mbalimbali
katika ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kati. Lengo kuu la BLOGU hii ni kuhifadhi na kutaarifu juu ya lugha
hizi na tamaduni za jamii husika. Wanajopo wataeleza na kujadili kwa kifupi kuhusu wazo la awali la mradi
huu, hatua iliyofikiwa, na uelekeo wa mradi. Katika ufafanuzi na mjadala, watatumia mifano anuai kutoka
katika jamii ambazo wanayo tajiriba ya kutosha kama wazawa au wazoefu.
Wawasilishaji:
1. Alwiya S. Omar (Chuo Kikuu cha Indiana),
2. Beatrice Mkenda (Chuo Kikuu cha Iowa)
3. Charles Bwenge (Chuo Kikuu cha Florida)
4. Filipo Lubua (Chuo Kikuu cha Pittsburgh)
5. Geofred Osoro (Chuo Kikuu cha Wellesley)
6. Hadija Jilala (Chuo Kikuu Huria-Tanzania)
7. Kawthar Iss-hack Mzee (Habari Maelezo Zanzibar)
8. Leonard Muaka (Chuo Kikuu cha Howard)
9. Mahiri Mwita (Chuo Kikuu cha Princeton)
10. Pacifique Malonga, (Chuo Kikuu cha Rwanda)
Ju
mapil
i, D
isem
ba 1
5, 2019
28
Jumapili 4:50As - 6:30 Mch - Vikao Sambamba Na 3 Chumba cha 2
Mada: Kiswahili na Fasihi
Mwenyekiti:
Matumizi ya Fasihi Simulizi Kama Mkakati wa Kuepuka Matatizo Yanayokumba Asasi
ya Ndoa: Mfano Kutoka Nyimbo za Jando za Wakamba
Lengo kuu la makala haya ni kujaribu kuonyesha kuwa, Fasihi Simulizi hasa nyimbo zina dhima muhimu
katika kutoa suluhu ya changamoto zinazokumba ndoa za kisasa katika ulimwengu huu unaobadilika. Suala la
ndoa limekuwa nyeti mno na hivyo kuwatia mbioni watunzi wa Fasihi simulizi ili kujaribu kuwachochea
wanajamii kukabiliana na changamoto hizo ambazo zinatokana na athari za kijamii kidini na kitamaduni.
Nadharia tete inayojengwa na makala haya ni kuwa, Nyimbo zinatumika na jamii inayobadilika kama mkakati
wa kutoa suluhu katika matatizo yanayochangiwa na ukale unaofifia na usasa ambao unaendelea kukita mizizi
katika jamii ya sasa. Licha ya ukiukaji wa maadili na kuacha mila miongoni mwa vizazi vya leo, nyimbo
huchangia katika kujaribu kuwaelimisha vijana umuhimu wa kuwa na maadili. Katika jamii ya Wakamba,
nyimbo hutumiwa kama chombo cha kukabiliana na masuala ya kijamii kuliko maandishi na mahubiri mengine.
Mwasilishaji: Naomi N. Musembi (Chuo Kikuu cha Jaramogi Oginga Odinga, Kenya)
Dhima ya Kimya Katika Kilongo cha Unyanyasaji Wa Kiusemi Baina ya Wanandoa
Katika Tamthilia Teule Mbili za Kiswahili
Kimya ni kipengele changamani cha mtagusano wa kiusemi chenye maana nzito na kinachochangia pakubwa
katika uendelezaji na uelewa wa mazungumzo. Binadamu hupasha habari fulani hata asiposema chochote.
Kimya kinadhihirisha hisia, mawazo na hadhi ya mzungumzaji. Mshiriki mazungumzo mwenye wasiwasi na
hofu anaweza kubaki kimya. Aidha, mwenye uwezo anayewadharau wengine huweza kutumia kimya.
Uchanganuzi wa kimya katika kilongo unategemea muktadha wa kitamaduni na kimandhari. Makala hii
inachunguza kimya katika muktadha maalumu wa unyanyasaji wa kiusemi baina ya wanandoa katika tamthilia
mbili, Machozi ya Mwanamke na Mama ee. Kwa kutumia Nadharia ya Uchanganuzi Tunduizi Kilongo wa
Kifeministi, makala hii inaonesha kwamba kimya cha wanaume kinadhalilisha na kudhihirisha mamlaka za
ubwana. Kimya cha wanawake kinathibitisha utiifu/unyonge wao kama utabaka duni. Mwanamke
aliyehamasika anatumia kimya kudhihirisha chuki, hasira na kwa jumla harakati zake za kujikombao dhidi ya
ubaguzi na ukandamizwaji wa kijinsia.
Mwasilishaji: Mutungi Boaz (Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda)
Usawiri wa Kijinsia katika Misemo ya Kwenye Daladala na Dhima zake Kiutamaduni
Lengo la makala hii ni kuchunguza usawiri wa masuala ya kijinsia katika misemo ambayo inaandikwa katika
vyombo vya usafiri hususan mabasi ya abiria maarufu kama daladala nchini Tanzania. Mojawapo ya dhamira
ambayo imejitokeza sana katika misemo ya vyombo hivyo ni usawiri wa masuala ya kijinsia. Hata hivyo,
misemo hiyo haijapewa aula miongoni mwa wahakiki wa fasihi ya Kiswahili wa masuala ya kijinsia. Makala
imekusanya data za misemo hiyo jijini Dar es Salaam. Matokeo ya awali ya utafiti huu yanaonesha kwamba
misemo mbalimbali kuhusu jinsia inapatikana katika vyombo hivyo vya usafiri; takriban yote inaandikwa na
wanaume. Misemo hii inazungumzia masuala ya kijinsia katika mambo kama vile mapenzi na ndoa, uzazi,
uchumi, vyakula, mavazi na kadhalika. Usawiri huu wa masuala ya kijinsia katika misemo hii si tu unaendeleza
utamaduni wa jamii husika kuhusiana na mambo hayo bali pia unamtweza mwanamke na kumkweza
mwanaume.
Mwasilishaji: Shani Omari (TATAKI, CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM, Tanzania
Itikadi za Kiuana Kama Zinavyobainika Katika Methali za Kisasa za Kiswahili
Makala hii inatokana na utafiti wa shahada ya uzamivu. Kiini cha makala hii ni kutathmini jinsi itikadi za kiuana
zinavyobainisha mahusiano ya kiuana katika methali za kisasa za Kiswahili. Kupitia methali za Waswahili
kiutamaduni; mila, desturi, amali, mawazo yao hufahamika na kuchukuliwa kuwa na ukweli unaokubalika na
wanajamii. Mbali na masuala tofauti yanayoangaziwa na methali katika jamii, makala hii itajikita katika suala la
itikadi za kiuana kama zinavyobainisha mahusiano ya kiuana katika methali za kisasa za Kiswahili. Itikadi za
kiuana ni uthibitisho wa hadhi za kiuana hasa kutokana na utathmini wa tofauti zake (Lorber 1994: 30). Data ya
makala hii itatokana na utafiti wa maktabani na nyanjani. Uchanganuzi wa data utaongozwa na nadharia za
itikadi, Uana na mabadiliko. Makala hii itajikita katika kutoa matokeo kuhusu mahusiano ya kiuana kama
yanavyobainika katika methali za kisasa za jamii ya Waswahili.
Mwasilishaji: Yunusu Lubuuka (Chuo Kikuu cha Kyambogo)
Ju
mapili, D
isem
ba 1
5, 2
019
29
Jumapili 4:50As - 6:30Mch - Vikao Sambamba Na 3 Chumba cha 3
Mada: Kiswahili na Utamaduni
Mwenyekiti:
Usawiri wa Mwanamke Katika Hadithi za Wakiga Kijijini Kajobe Wilayani Kabale.
Mtafiti atashughulikia usawiri wa mwanamke katika hadithi za Wakiga. Mtafiti atachunguza jinsi wahusika wa
kike wanavyowasilishwa na mwandishi. Mtafiti atatathimini jinsi utamaduni wa jamii ya Wakiga humsawiri
mwanamke, atachunguza jinsi uana wa mwanamke unaathiri wahusika wa kike katika hadithi hizi. Pia mtafiti
atachunguza mchango wa wanaume katika unyanyasaji wa mwanamke. Mtafiti atatumia nadharia ya ufeministi.
Mihimili itakayotumiwa ni kutendewa sawa kwa wanawake na wanaume, hakuna tofauti kati ya wanawake na
wanaume na tofauti ya kinjisia kati ya wanawake na wanaume kutokuwa msingi wa kimpaumbele. Mtafiti
atatumia mbinu kama muundo wa utafiti, uteuzi wa vifaa vya kukusanya data, mbinu ya tovuti na usomaji
wamatini maktabani. Miongoni mwa vitabu atakavyotumia ni; “Emicwe na Emigyenzo ya Bakiga
Ekyongyeigrwemu”, “Kigyezi ne Ebyamo Omugwa 1500”, “Oteebwa Orurimi Rwawe Ekyongeirwemu”,
“Omuzaano Oshwera Abuuza”, “Shutama Nkuteekyerereze”. Idara ya fasihi itajiongezea maarifa, wanajamii
watakaosoma tafiti hii watatambua misingi ya unyanyasaji wa wanawake, wasomi watakaoimbuka baadaye
watajipatia mada kulingana na vile nitakavyopendekeza baadaye Mwasilishaji: Kyokushaba Moreen (IUIU)
Masale: Mti wa Kitamaduni Usiovuma
Isale (Masale-wingi) ni mti wa kitamaduni unaoheshimika sana katika jamii ya Wachaga. Umaarufu wa mti huu
wa kitamaduni umeenea katika jamii za Wachaga kuanzia Machame, Rombo, Siha, Marangu, Moshi n.k. Kwa
miaka mingi mti huu umekuwa alama muhimu ya jamii ya Wachaga popote walipo. Umekuwa ukitumika katika
mambo mengi ya kitamaduni kama vile sherehe, misiba, vyakula, makazi na matambiko. Isivyo bahati, alama
hii muhimu ya kitamaduni haizungumzwi sana na hivyo haifahamiki kwa wageni wengi. Wadau wengi wa utalii
hivi sasa wanapigia chapuo suala la utalii wa kitamaduni. Hii ni kutokana na ukweli kuwa, utalii huu ni muhimu
sana na ni endelevu. Makala hii ni matokeo ya utafiti uliofanywa kwa muda wa miezi sita kuhusu mti huu
muhimu wa Wachaga. Utafiti ulihusisha watafitiwa 20; wazee wa kimila, viongozi pamoja vijana kutoka katika
maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kilimanjaro. Data zilikusanywa kwa njia ya mahojiano pamoja na ushuhudiaji.
Mwasilishaji: Shadidu A. Ndossa (Chuo Kikuu cha St. John, Tanzania
Lugha ya Utani Baina ya Timu ya Simba na Yanga: Mifano Kutoka Magazetini na
Mazungumzo ya Mashabiki
Utani ni kipera cha mazungumzo katika fasihi simulizi chenye dhima mbalimbali kwa jamii husika. Lengo la
makala hii ni kuchunguza lugha ya utani baina ya timu ya Simba na Yanga tukirejelea data kutoka magazeti ya
Kiswahili na mazungumzo ya mashabiki. Maswali tunayojibu ni: Je, vipengele gani vya lugha vinavyohusishwa
zaidi na utani? Nini umuhimu wa matumizi ya lugha hiyo ya utani katika jamii ya sasa? Data za utafiti huu
zimekusanywa kwa kusoma magazeti ya Kiswahili yanayozungumzia habari za michezo na kufanya mahojiano
na mashabiki wa timu hizo nchini Tanzania. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa habari za michezo katika
magazeti na mazungumzo hayo zimeshamiri lugha ya utani baina ya timu hizi. Lugha hii ya utani imekuwa
ikihifadhi, kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili, kuburudisha, kuelimisha na kuonya jamii. Makala pia
imebaini kuwa pamoja na kuburudisha na kuelimisha jamii, lugha ya utani imekuwa kichochea cha migogoro
baina ya mashabaki wa timu hizo.Mwasilishaji:
Mwasilishaji: Asifiwe Eliud Mwagike (TATAKI, CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM, Tanzania)
Kiswahili Katika Makongamano: Faida na Changamoto Zake
Tangu utaratibu wa makongamano ufanyike, miaka kadhaa iliyopita, bado wataalamu na washiriki wengineo wa
lugha ya Kiswahili hawajaketi ‘rasmi’ katika kutathmini faida na changamoto za makongamano yenyewe. Kama
kwamba mijadala inayofanyika inasikika katika kipindi kifupi fulani, na kupoteza mwanga wake katika siku
zinazoifuatia. Ilivyo hasa, washiriki wa makongamano haya hutoa mawazo mazito katika kuitetea na
kuiendeleza lugha hii adhimu. Lau mawazo haya yatekelezwa kivitendo, ni dhahiri kuwa nafasi ya Kiswahili
ingeimarika zaidi. Makala hii inaweka bayana faida na changamoto zinazojiri kila uchweo zihusuzo mikutano
ya makongamano haya. Lengo siyo tu kutambua mambo haya, bali iwe ni chachu ya kukaa pamoja ili kuunda
mikakati rasmi ambayo itakuwa ni dira ya muda mrefu katika utekelezaji wake kwenye mataifa mbalimbali
ulimwenguni. Mwasilishaji: Omar Salum Mohamed (Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar, Tanzania)
Ju
mapil
i, D
isem
ba 1
5, 2019
30
Jumapili 4:50As - 6:30Mch - Vikao Sambamba Na 3
Chumba cha 4
Mada: Jopo la Kiingereza
Mwenyekiti:
Reconsidering Haugen's (1983) Revised Language Planning Model with Reference to the
Teaching and Learning of Standard Kiswahili in Uganda's Lower Secondary Schools
Since the 1990s, as Uganda has been experiencing an increase in the teaching of Kiswahili in its educational
institutions across the country, the question on which Kiswahili variety(ies) to be considered in schools has
predominantly remained undecided (e.g., see, the existing language-in-education policy). Subsequently, the
widespread of various Kiswahili varieties has unceasingly and gradually cherished in schools which contrasts,
for instance, with Kaplan’s and Baldauf Jr.’s (1997:123) perspectives on schools as formal sites for the teaching
of a selected/standard variety of a given language. This theoretical article reviews postulations on the teaching
of Kiswahili, as outlined in Uganda’s language-in-education. The review intends to provide justifications to
explore Haugen’s (1983) Revised Language Planning Model, as advanced by Kaplan and Baldauf Jr. (1997)
with an aim of demonstrating how the teaching of standard Kiswahili can be re-emphasised mainly from
Uganda’s lower secondary schools where the teaching of Kiswahili is formally introduced.
Presenter(s): Caesar Jjingo (Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda)
Zainab Ali Iddi (Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar, Tanzania)
Which Language Proficiency Level is Suitable for Work for Kiswahili Language Learners? Foreign volunteers (FVs) from America, Japan, Korea, and German have started working in Tanzania in private
and public sectors since 1962. Kiswahili is the sole language that is used by FVs to communicate with most of
Tanzanians in accomplishing their duties in Tanzania. However, the study conducted by Kanigi (2016) found
that the FVs faced various language problems when using Kiswahili as a result of creating communication
breakdowns which were overcome by interpreters. This raised an interest to the researcher to find out the
proficiency level that they have reached which help them to communicate smoothly with her. The study was
guided by an interaction approach which gave an opportunity for them to interact while incorporating
negotiation strategies such as recasts, confirmation checks and clarification requests in exploring their Kiswahili
proficiency levels. They were evaluated by using American Council guideline on the Teaching of Foreign
Languages (ACTFL). The study found that the 4 FVs were in the intermediate high proficiency level. The study
suggests that, for Kiswahili learners to be able to communicate smoothly while accomplishing their duties
Tanzania, have to reach the intermediate level. Presenter: Maria Mkunde Kanigi (Chuo Kikuu cha Mzumbe, Tanzania)
Kiswahili for Unity in Diverse South Sudan
The national motto of South Sudan “Justice, Liberty, Prosperity”, has been the fundamental reason for the
previous rebellions that lasted for more than two decades and the ongoing growing tensions and bloodshed in
South Sudan. As the nation strives to rebuild itself, it is important to highlight that tensions widespread due to
the complex nature of cultural and linguistic identities of the South Sudanese. While the diverse citizens of
South Sudan, with the support of international and regional communities, hope to unite, develop, and live in
harmony with each other, there is a need to ensure that there is a language that can unite all the people as a
nation while preserving the cultural interests of the local communities. This study aims to explore how
Kiswahili can be used as a tool to assimilate and bring together the people of South Sudan, while ensuring
development at the local and international level.
Presenter: Susan Mongalla Ngbabare (Chuo Kikuu cha Ohio, USA)
Ju
mapili, D
isem
ba 1
5, 2
019
31
Jumapili 4:50As - 6:30 Mch - Vikao Sambamba Na 3 Chumba cha 5
Mada: Utafiti wa Kiswahili na Taaluma Zake
Mwenyekiti:
"Kiingereza ni Kigumu": Maoni ya Wakimbizi Kukusu Kukuza na Kuendeleza
Kiswahili Katika Jamii Zao
Wakimbizi wanaoongea Kiswahili kama lugha yao ya kwanza au ya pili wanaendelea kuongezeka katika miji
mingi Marekani. Kati yao, kuna wale wenye umri wa makamo na wazee ambao wanachukua muda mrefu
kujifunza Kiingereza. Wakati huo huo, mashirika mbalimbali kwenye miji hii hutoa huduma za ufunzaji
Kiingereza. Katika wasilisho hili, nitaongea juu ya maoni ya wakimbizi kuhusu suala la kujifunza Kiingereza,
na changamoto wanazozipitia wanapojaribu kuimudu lugha hii geni kwao. Nitajadili juu ya vikwazo
wanavyokumbana navyo na jinsi wanavyojitahidi kuvikwepa kwa minajili ya mawasiliano. Pia, nitajadili kwa
kina jinsi ambavyo Kiswahili kinaweza kukuzwa na kuendelezwa katika jamii hizi hata wakati ambapo
Kiingereza kinaendelea kutumiwa. Wasilisho hili linatokana na utafiti uliofanywa kati ya wakimbizi wa kutoka
nchi za Afrika ya Mashariki wanaoongea Kiswahili katika mji wa Pittsburgh, PA, Marekani.
Mwasilishaji: Leonora Kivuva (Chuo Kikuu cha Pittsburgh, USA)
Uhamishaji wa Kiswahili-Kiingereza: Kanuni za Kisarufi
Wazungumzaji wanaofahamu lugha ya Kiswahili na Kingereza hutumia lugha hizi kwa pamoja kwa
kuzichanganya au kuzibadilishana. Mtindo huu hujulikana kwa jumla kama uhamishaji msimbo. Hivyo basi,
lengo la kazi ni kutathmini ufaafu wa vidhibiti vya kisarufi vilivyopendekezwa na Poplack (1980) kuelezea
muundo wa uhamishaji msimbo. Matokeo ya utafiti huu yamekinza na vilevile kuoana na kanuni zilizoelezwa.
Kama ilivyopendekezwa na kanuni ya mofimu funge utafiti huu umedhihirisha kwamba, katika uhamishaji wa
Kiswahili-Kingereza, uhamishaji hauruhusiwi baina ya mofimu huru na mofimu funge. Pili, kinyume na kanuni
ya ukubwa wa kipashio imethibitishwa kuwa ni vipashio vidogo zaidi kuliko vile vikubwa ambavyo
huhamishwa. Pia, ingawa lugha ya Kiswahili na Kiingereza huwa na miundo tofauti kisarufi, maumbo kutoka
lugha ya Kiingereza huhamishwa kwa mujibu wa muundo wa lugha ya Kiswahili. Data ya uchunguzi huu
imetokana na uchanganuzi wa sentensi 50 kutoka Facebook. Mwasilishaji: Shadrack Kirimi (Chuo Kikuu cha Nairobi)
Jazanda Katika Kiswahili na Changamoto ya Dhana ya "Tamathali za Semi" Katika
Mabango na Vibonzo vya Kiswahili
Maana mbalimbali zimetolewa kuhusu tamathali za semi. Hata hivyo maana hizo zinajikita katika dhana ya
‘semi’, au ‘usemi‚’. Maana hizi hazioneshi kuwa kuna uwezekano wa dhana hiyo kujumlisha vipengele
ambavyo si vya lugha au usemi. Hata hivyo, mabango na vibonzo vyenye picha au michoro vinaonesha kuwa
dhana hiyo inaweza pia kuwamo katika nyanja ambayo si maneno au lugha ya maandishi. Je, tunaweza
kuangalia dhana hii katika upana wake na tukawa na mawazo ambayo yanaunganisha na lugha na vipengele
ambavyo si vya lugha? Kwa maana nyingine, tunaweza kusema tamathali za semi inaongelea semi zaidi kuliko
hivyo vipengele vingine? Makala hii inatoa mawazo ya kufikirisha na kuwa changamoto katika maana na
istilahi zinazotumika katika lugha na fasihi.
Mwasilishaji: Aldin Mutembei (TATAKI, CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM, Tanzania)
Nafasi ya Kamusi ya Kiswahili Sanifu Katika Utekelezaji wa Silabasi ya Kiswahili ya
Shule za Upili Nchini Kenya
Ufundjshaji wa Kiswahili katika shule za upili nchini Kenya huongozwa na silabasi ambayo imetoa mpangilio
maalum wa mada zitakazofunzwa kulingana na malengo teule. Ufundishaji huu hufanikishwa kwa kutumia
rasilmali faafu. Rasilmali hizi huhuzisha walimu waliohitimu kufundisha lugha ya Kiswahili na nyenzo
mbalimbali. Mojawapo ya nyenzo muhimu ni vitabu. Ni nadra sana kutimiza ufundishaji wa Kiswahili
pasipokurejea kamusi. Kila mwanafunzi anapojiunga na shule za upili huagizwa kujinunulia kamusi mara nyingi
ikiwa Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Toleo la tatu la Kamusi hii ya mwaka 2013 limejumuisha vipengele vingi
vya tawi la isimu, sarufi na fasihi ambavyo ni chemichemi za mada kuu za silabasi na vitabu vya kiada vya
Kiswahili. Makala hii itathmini mchango wa kamusi hii katika utekelezaji wa silabasi ya Kiswahili ya shule za
upili nchini Kenya.
Mwasilishaji: Susan Chebet-Choge (Chuo Kikuu cha Masinde Muliro, Kenya)
Ju
mapil
i, D
isem
ba 1
5, 2019
32
Jumapili 8:00 - 8:45Mch - Mada Elekezi Na. 2
Ukumbi Mkuu
Mwenyekiti:
Dkt. Ernesta Mosha
Ju
mapili, D
isem
ba 1
5, 2
019
33
Jumapili 8:50 Mch - 10:30 Jion - Vikao Sambamba Na 4
Chumba cha 1
Mada: Kiswahili na Teknolojia na Utandawazi
Mwenyekiti:
Kiswahili na Teknolojia
Lugha ya Kiswahili ni lugha ya kibantu na i miongoni mwa lugha ambazo zina kasi katika ukuaji wake. Karne
ya 21 imekuwa na mabadiliko mengi tukilinganisha na karne zilizopita.Katika mada hii nitabainisha umuhimu
wa lugha ya Kiswaili katika sekta ya teknolojia.Mada hii itachamba pia mabadiliko yanayotokana na teknolojia,
huku sababu yake ikiwa ni lugha adhimu ya Kiswahili. Pamoja na kwamba utawala na serikali za Afrika
hutumia lugha katika kuongoza ,mada hii itachambua uhusiyano uliopo baina ya njia mbalimbali zinazotumiwa
na serikali sambamba na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Aidha,makala hii itaonyesha na fasi ya
Kiswahili katika nyanja ya teknolojia nchini Burundi kwa kulinganisha na miaka iliyopita .,Pamoja na kutowa
mapendekezo ya utumiaji wa lugha ya Kiswahili katika nyanja ya teknolojia ,mada hii itazungumzia njia
mbalimbali zinazosababisha ukuaji wa lugha kupitia nyanja ya teknolojia.
Mwasilishaji: Tuyisenge Ange Merline (Shule ya Sekondari ya SOS, HG)
Utoaji Hadithi za Kidigitali Katika Madarasa ya Kiswahili
Utumiaji wa vifaa vya kielektroniki katika kufundishia na kusoma Kiswahili kwa wanafunzi wa lugha ya pili
umechangia sana katika uelewaji na ujifunzaji wa Kiswahili. Utoaji wa hadithi za kidijitali nako kumeibua
mbinu mpya katika madarasa ya lugha za kigeni. Makala hii itaangazia jinsi wanafunzi wanatumia Kiswahili
katka kutoa hadithi za kidijitali. Pia nitajadili maswali yafuatayo ya msingi, Hadithi za kidijitali ni nini? Hadithi
hizi zinaundwaje? Mwalimu anajukumu gani katika kuwasaidia wanafunzi kuunda hadithi hizi? Hadithi hizi
zinawasaidiaje wanafunzi kujifunza lugha na tamaduuni? Ni changamoto zipi zinazoibuka katika utumiaji wa
hadithi za kidijitali kujifunza lugha? Mwasilishaji: Anne Jebet (Chuo Kikuu cha Virginia, USA)
Kiswahili na Teknolojia: Changamoto na Fursa za Upatikanaji wa Matini za
Kufundishia au Kujifunzia Kiswahili Mtandaoni
Katika zama hizi za maendeleo makubwa ya teknolojia, sekta ya elimu haijabaki nyuma katika matumizi ya
teknolojia ili kufanikisha ufundishaji na ujifunzaji. Kama ilivyo kwa masomo mengine, walimu na wanafunzi
wa lugha nao wanatumia au wanatakiwa kutumia teknolojia ili kuleta ufanisi katika ufundishaji na ujifunzaji.
Mathalani, katika pedagojia, teknolojia inaweza kutumika katika utafutaji, utengenezaji, utumiaji, na usambazaji
wa matini mbalimbali (makala, picha, video nk). Mtando ndilo jukwaa ambalo walimu na wanafunzi wengi
hutumia kutafuta na kusambaza matini husika. Wakati lugha nyingi kama vile Kiingereza, Kifaransa,
kijerumani, Kichina na Kihispania zina matini lukuki za kufundishia au kujifunzia mtandaoni, bado kuna ukame
mkubwa wa matini za Kiswahili. Makala hii itaangazia upatikanaji mtandaoni wa matini za Kiswahili
zinazoweza kutumika katika ufundishaji mada mbali mbali. Aidha, mbinu za kutengeneza na kusambaza
zitapendekezwa pia.
Wawasilishaji: Filipo Lubua (Chuo Kikuu cha Pittsburgh, USA)
Malimi Joram Kazi (Chuo Kikuu cha Duquesne, USA)
Uhakiki wa Nafasi ya TEKNOHAMA Katika Kukuza Maudhui Katika Tamthilia ya
Kigogo
Fasihi ni zao la jamii na hubadilika kila uchao. Uwakilishi wa suala la TEKNOHAMA katika tamthilia za kisasa
umechukua mkondo mpya. Hii ni kwa sababu, kutokana na jinsi dunia inavyobadilika ndivyo masuala ya
kiteknolojia pia yanavyoathiri fasihi ya sasa na kuipa mguso na taathira mpya. Licha ya uwakilishi wa
TEKNOHAMA kuwa na umuhimu katika kukuza fani na maudhui katika fasihi, mchango wake katika tamthilia
ya Kigogo haujafanyiwa utafiti, suala linalomchochea mtafiti kulitafiti. Lengo kuu la utafiti huu ni kutathmini
mchango wa TEKNOHAMA katika kukuza maudhui katika tamthilia ya Kigogo ya Pauline Kea (2016). Utafiti
huu unaongozwa na Nadharia ya Uyakinifu wa Kijamii. Uteuzi wa sampuli utafanywa kimakusudi na utafiti
wenyewe ni wa muundo wa kiudhamano. Mtafiti atasoma makala mbalimbali kuhusiana na mada na kisha
kuichanganua data kwa njia ya kimaelezo. Mwasilishaji: Jackson Ndungu Mwangi (Chuo kikuu cha Laikipia, Kenya)
Ju
mapil
i, D
isem
ba 1
5, 2019
34
Jumapili 8:50 Mch - 10:30 Jion - Vikao Sambamba Na 4
Chumba cha 2
Mada: Kiswahili na Isimu
Mwenyekiti:
Alomofu za Viambishi vya Unyambuzi wa Kitenzi Katika Kiswahili Sanifu: Je,
Maumbo {-li-/-le-}, {-lish-/-lesh}, na {-lik-/-lek-} ni Alomofu za Utendea, Utendesha, na
Utendeka?
Wanaisimu waliotangulia wanabainisha kwamba {-li-/-le-}, {-lish-/-lesh-}, na {-lik-/-lek-} ni alomofu za
utendea, utendesha na utendeka katika Kiswahili. Hoja ya makala hii ni kwamba maumbo haya sio alomofu
sahihi za utendea, utendesha na utendeka. Kwa kuwa maumbo haya ni Konsonanti Irabu (KI) ama Konsonanti
Irabu Konsonanti (KIK), yanakinzana na kanuni ya Mame-Bantu kwamba kiambishi nyambuzi cha kitenzi
kinapaswa kuwa I, K, au IK. Aidha, data kutoka lahaja ama lugha nyingine za Kibantu zinaonesha kwamba
konsonanti /l/ ni sehemu ya mzizi na sio ya alomofu. Pia, kwa kuzingatia isimu historia, Kiswahili kama ilivyo
lugha nyingine za Kibantu, kimedondosha /l/ katika baadhi ya mizizi isiyonyambuliwa, lakini kinairudisha
katika mizizi nyambuzi. Data za makala hii zimepatikana kwa uchambuzi wa matini na hojaji. Kwa kuzingatia
mchakato wa udondoshaji na urudishaji wa konsonanti /l/ katika mizizi ya vitenzi, ufasiri wa data umetumia
nadharia ya Mofolojia Leksika na mkabala wa Isimu Historia Linganishi.
Wawasilishaji: Fabiola Hassan (Chuo Kikuu cha Dodoma, Tanzania)
Josephat M. Rugemalira (Chuo Kikuu cha Tumaini - Dar es Salaam, Tanzania)
Athari za Kimofosintaksia za Kikonzo katika Ujifunzaji wa Kiswahili kama Lugha ya
Pili Miongoni mwa Shule za Sekondari nchini Uganda
Tafiti nyingi kuhusu ujifunzaji wa Lg2 kama vile za Tom, Stella, na Susanne (2016) na Sarah (2019)
zimeonesha kwamba wajifunzaji wa Lg2 hufanya taksiri za kisarufi ambazo hutokana na Lg1. Lengo kuu la
utafiti huu lilikuwa ni kueleza sababu za athari hizo na kueleza mbinu za kuzitatua. Data za utafiti zilipatikana
uwandani kwa kutumia mbinu za, uchunguzi shirikishi, ushuhudiaji, matumizi ya masimulizi, insha na hojaji.
Data zilichanganuliwa kwa kutumia mbinu ya uchanganuzi matini kwa kutumia mkabala wa kimaelezo kwa
kiwango kikubwa na mkabala wa kitakwimu pale ilipohitajika. Utafiti huu uliongozwa na Uchanganuzi Taksiri
(UM) ya Corder (1967. Utafiti uligundua kuwa, Taksiri zinazojitokeza katika ujifunzaji wa Lg2 ikiwa ni za
upatanisho wa kisarufi wa nomino, virejeshi, njeo, matumizi ya ukubwa na udogoshaji, ukanushi miongoni vya
vipengele vingine vya kimofosintaksia.
Mwasilishaji: Masereka Levi Kahaika (Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda)
Muungano wa Kimofolojia Katika Vitenzi vya Kitikuu
Tunapozungumzia muungano katika vitenzi huwa tunaangazia mofimu mbalimbali zinapoungana na kuwa
mofimu moja. Kitikuu ni lahaja mojawapo kati ya lahaja za Kiswahili. Kitikuu huzungumzwa katika visiwa vya
Lamu kaskazini. Lahaja hii hudhihirisha muungano katika vitenzi vyake ambapo mofimu mbili huungana na
kuwakilishwa na mofimu moja. Crystal (2008) anafafanua muungano kama mfumo unaounganisha mizizi ya
vifundo viwili kuwa kimoja. (T.Y). Makala hii itachanganua aina mbalimbali ya miungano inayopatikana katika
vitenzi vya Kitikuu, kama vile muungano wa njeo na nafsi, hali na nafsi na hata virejeshi na njeo. Kazi hii
itatumia nadharia ya uminimalisti chini ya ukaguzi wa sifa, inayokagua mofimu mbalimbali za vitenzi katika
hatua mbalimbali. Je, mofimu moja inayosimamia uamilifu mbalimbali katika kitenzi itaweza kudhihirishwa
kwa namna gani katika nadharia hii?
Mwasilishaji: Rukiya Harith Swaleh (Chuo Kikuu cha Pwani, Kenya)
Uchambuzi wa Utoshelevu wa Taarifa za Kisintaksia za Vitenzi vya Kiswahili Katika
Kamusi za Kiswahili Sanifu
Pamoja na taarifa mbalimbali zinazopatikana kwenye kamusi, ziko pia taarifa za kisintaksia zenye lengo la
kumsaidia mtumia kamusi kutumia vizuri maneno kwa kuzingatia sarufi ya lugha mahususi. Makala hii inataka
kujua iwapo taarifa hizo zinapatikana kwa urahisi kwenye kamusi. Je, kuna vigezo gani vinavyoukiliwa wakati
wa kuingiza taarifa za kisintaksia za vitenzi vya Kiswahili kwenye kamusi za Kiswahili sanifu? Makala hii
itaongozwa na nadharia ya Eksibaa ambayo itanisaidia kutambua utoshelevu wa taarifa za kisintaksia za vitenzi
katika kamusi za Kiswahili sanifu hasa kipengele cha uelekezi wa vitenzi vya Kiswahili. Taarifa za kisintaksia
zinazopatikana kwenye kamusi zitakusanywa kwa uchambuzi wa matini, dodoso na hojaji na kuchambuliwa
kwa mkabala wa kiidadi na usio wa kiidadi. Makala hii itatathmini taarifa za kisintaksia za vitenzi zilizopo,
utoshelevu wake na kupendekeza mbinu bora za kuongeza taarifa za kisintaksia katika kamusi za Kiswahili
Sanifu.
Mwasilishaji: Gertrude Joseph (TATAKI, CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM, Tanzania)
Ju
mapili, D
isem
ba 1
5, 2
019
35
Jumapili 8:50 Mch - 10:30 Jion - Vikao Sambamba Na 4
Chumba cha 3
Mada: Kiswahili na Fasihi
Mwenyekiti:
Mchango wa Prof. Kyallo Wamitila Katika Ukuzaji wa Istilahi za Fasihi ya Kiswahili
Tunapomuongelea Kyallo Wamitila (1965-) Profesa wa fasihi wa Chuo Kikuu cha Nairobi na mchango wake
katika fasihi ya Kiswahili hatuangalii pekee uandishi wa kazi zake bunilizi, uhakiki na makala za kimataifa za
fasihi ya Kiswahili bali pia mchango wake katika ukuzaji wa istilahi za fasihi ya Kiswahili na kupelekea
kutajirisha taaluma za Kiswahili kwa Kiswahili. Lutz Diegner (2004) alihariri mchango wa Kamusi ya Fasihi
(2003) ya Wamitila ikiwa na vidahizo vipatavyo 1300 kwamba kamusi hiyo imeibua istilahi mpya, kuendeleza
zilizopo na kutoa visawe vipya kwa zile istilahi zilizokwishaundwa na kuwa hiyo ni sehemu ya mchango wa
Wamitila katika Fasihi ya Kiswahili. Mshabaha wa makala haya ni mchango wa Prof. Wamitila katika ukuzaji
wa istilahi za fasihi ya Kiswahili katika karne hii ya 21. Makala haya ni muendelezo wa utafiti wa istilahi zaidi
za Fasihi ya Kiswahili ambazo zimejidhihirisha ndani ya kazi zake za Uhakiki wa Fasihi: Misingi na Vipengele
Vyake (2002), Kamusi ya Fasihi : Isitlahi na Nadharia (2003) na Kanzi ya Fasihi: Misingi ya Uchanganuzi wa
Fasihi (2008).
Mwasilishaji: Ahmad Kipacha (Chuo Kikuu cha Nelson Mandela, Tanzania)
Dhana ya Maisha Katika Riwaya ya Sitasahau MV Bukoba na Nyaisa G Simango
Wasilisho hili linaangazia maana ya maisha kutokana na msimulizi wa Riwaya ya Sitasahau MV Bukoba na
Nyaisa G Simango aliye miongoni mwa walionusurika ajali ya majini kutoka Bukoba hadi Mwanza. Alikuwa
akiongozwa na Sergent Nico wakimpeleka mfungwa mahakamani Bukoba. Watu tele waliagaa dunia. Lilikuwa
janga kubwa kwa Afrika Mashariki na dunia nzima. Kwa kina, tunaangalia masuala yahusayo maisha, vifo vya
watu kwa idadi ya kutisha, kunusurika kwa watu wachache, mbinu za ukombozi zilizotumiwa kuopoa miili ya
wale walioagaa dunia. wakombozi waliokuja kuwakomboa baada ya janga hili, matatizo kama ukosefu wa vifaa
na uhaba wa watalamu wakushughulikia masuala ya majini. Tunaangalia mitazamo ya watu kuhusu janga
lililowafikia kama jamii nzima, msimamo wa serikali kuhusu janga hili, ripoti mbali mbali zilizotolewa na
vyombo vya habari tofauti tofauti kama, Daily News, Mtanzania na Nipashe.
Mwasilishaji: Simon Kawaida (Chuo Kikuu cha IUIU Mbale, Uganda)
Kiama cha Mahusiano Katika Riwaya ya Kiswahili: Itikadi ama Ubabe?
Dhima ya sanaa yoyote hulenga kumzindua mwanajamii kuhusu mazingira yake ili aweze kujikosoa ama
kutafuta majibu (Wafula R M 2004. Mjadala huu utalenga kuchanganua riwaya ya Kiswahili teule kwa lengo la
kuonyesha kwamba mahusiano ya kimapenzi yameingia mauti na hasa katika asasi ya ndoa. Kwa sasa asasi
husika inatishiwa kuangamizwa iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa kurejesha urazini. Asasi ambazo
zilihusika katika kudumisha mahusiano, zenyewe sasa zimetekwa nyara na nguvu za itikadi mbovu na hivyo
kuzua hali ya taharuki miongoni mwa wanajamii na hasa vijana. Dini, vyombo vya dola na misingi ya
kitamaduni sasa imekuwa butu. Uchunguzi huu utalenga kuonyesha ya kwamba mauti ya kiholela na ya kikatili
yanayoshuhudiwa kwa sasa yanaweza kukomeshwa iwapo asasi husika zinaweza kujikomboa kutoka katika
nyara zilimotekwa na kuhudumu kulingana na maadili yanayostahili. Ni hali ambayo inatishia sio tu vijana
kuingia katika mahusiano kimapenzi lakini wana ndoa na wazazi ambao tamaa yao kubwa ni kuwaona watoto wao wakiolewa na kupata vizazi vijavyo ambavyo vitarithi jamii yao. Kizazi cha kesho kinategemea hali thabiti
ya asasi za kijamii na za umma ambazo zimepewa majukumu ya kulinda ustawi wake na wanajamii.
Mwasilishaji: Leo Sanja (Chuo Kikuu cha Kenyatta, Kenya)
Mchango wa Muziki na Filamu Katika Kukuza na Kueneza Kiswahili
Katika mada hii, nitajaribu kuweka wazi nafasi ya muziki na filamu katika kukuza na kueneza Kiswahili katika
bara la Afrika na duniani kote!!! Hapo ni pamoja na kuonyesha wanamuziki wa Afrika Mashariki na wale wa
nje ya Afrika Mashariki wanaorusha nyimbo zao umuhimu wa kutumia Kiswahili katika kazi zao. Kwa hakika,
hakuna anayeweza kusema hajui kuwa muziki na filamu ni sekta ambayo ina wateja sana duniani. Aidha, kadiri
mtu asikilizapo au atazamapo nyimbo na filamu, ndivyo anatamani kuelewa kinachozungumzwa! Hivyo,
anafanya bidii ili kuelewa msamiati uliotumiwa na afanyapo hayo anakuwa anajifunza lugha!!! Kwa mantiki
hiyo, itakuwa fursa kwangu kuhimiza Wasanii wote wa Afrika mashariki na nje kurusha nyimbo na kuigiza
filamu zao na kuzipeperusha katika lugha yetu adhimu, Kiswahili.
Mwasilishaji: Eliezer Bucumi (Chuo Kikuu cha Burundi)
Ju
mapil
i, D
isem
ba 1
5, 2019
36
Jumapili 8:50 Mch - 10:30 Jion - Vikao Sambamba Na 4
Chumba cha 4
Mada: Kiswahili na Fasihi
Mwenyekiti:
Kiswahili na Ushirikishaji: Usawiri wa Wahusika Wenye Ulemavu Katika Riwaya
Teule za E. Kezilahabi na S.A. Mohamedd
Kulingana na takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa (2011), idadi ya watu wenye ulemavu wa viungo kote
duniani imefikia bilioni moja. Katika bara la Afrika, inakisiwa kuwa asilimia kumi ya Waafrika wana ulemavu
wa viungo. Mashirika ya kutetea haki na usawa pamoja na mataifa mbalimbali kote ulimwenguni yamekuwa
yakihimiza kushirikishwa kwa watu wenye ulemavu katika maswala yote ya jamii bila kuwatenga. Lengo la
makala hii ni kuchunguza usawiri wa wahusika wenye ulemavu katika riwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo (E.
Kezilahabi) na Utengano (S.A. Mohamed), ili kubainisha namna ambavyo usawiri huu umetumiwa na
waandishi husika kuwasilisha ujumbe kuhusu nafasi ya watu wenye ulemavu na ushirikishwaji wao katika jamii.
Mwasilishaji: Beth N. Mutugu (Chuo Kikuu cha Kenyatta, Kenya)
Utambulisho Mpya wa Mwafrika Kama Unavyosawiriwa Katika Riwaya za Kiswahili
Fasihi ina nafasi ya pekee katika kuumba na kujenga utambulisho mpya wa Mwafrika kupitia mahusiano ya
kijamii, utengamano wa kiuchumi na kisiasa. Hii ni kutokana na nguvu ya fasihi katika kuchunguza jamii
kuanzia kipindi cha ukoloni na hata baada ya ukoloni. Baada ya nchi za Afrika kupata uhuru wa kisiasa,
utambulisho mpya wa Mwafika kijamii na kiuchumi ni jambo muhimu ambalo linahitaji kufanyiwa kazi.
Makala hii inalenga kuonesha mchango wa riwaya za Kiswahili katika kubainisha mikakati inayotumiwa na
mataifa makubwa katika kudhoofisha utambulisho wa Waafika na kuonekana kuwa ni watu ambao hawana
utambulisho. Kazi hizi zinaweka bayana mambo ambayo yanatakiwa kushughulikiwa kupitia mbinu anwai
zinazotokana na utamaduni wa Mwafrika ili kujenga utambulisho mpya wa Mwafrika na kuwa watu ambao
wana usawa na uwezo wa kujitegemea katika kuendesha maisha yao bila kutegemea misaada kutoka mataifa
makubwa.
Mwasilishaji: Ernesta Simon Mosha (TATAKI, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania)
Matapo Katika Fasihi Simulizi
Makala hii inanuia kulijibu swali hili: Je, kuna matapo yoyote yanayojitokeza katika Fasihi Simulizi? Kabla ya
kulijibu swali hili, makala hii itaweka wazi historia fupi ya Fasihi Simulizi na sifa zake kimsingi kwa kurejelea
wataalam anuwai. Wataalam wengi wamekuwa wakishughulikia dhana ya matapo katika Fasihi Andishi. Aidha,
Fasihi Simulizi haijathaminiwa na baadhi ya wataalam. Makala hii inadhamiria kuyaweka wazi matapo ya
Fasihi Simulizi katika Kiswahili ili kubaini mchango wake kisanii kwa msaada wa fanani, hadhira na miktadha
maalum. Lengo mahsusi ni kutathmini matapo mbalimbali katika Fasihi Simulizi kwa kutumia mifano kutoka
katika mazingira.
Mwasilishaji: Kibigo Mary Lukamika (Chuo Kikuu cha MMUST, Kenya)
Kiswahili na Sanaa Katika Kuleta Umoja na Utangamano wa Afrika na Dunia
kwa Ujumla
Ni ukweli usiopingika kuwa lugha yoyote ile ni kiungo muhimu hasa katika swala zima la mawasiliano.
Lugha ya Kiswahili kama lingua franka ina mchango mkubwa katika kuleta utangamano wa wana
Afrika na baadae dunia nzima ambapo mpaka sasa Kiswahili kinachanja mbuga kukusanya mataifa yote
duniani. Sambamba na hayo Kiswahili kimeendelea kutuunganisha wana Afrika na dunia nzima kupitia
utanzu wa fasihi simulizi(sanaa).Nyimbo za injili pamoja na ile ya kizazi kipya inaendelea kukikatambulisha
vyema Kiswahili Duniani kote. Sambamba na hayo bado uwanja wa filamu au maigizo na vibonzo navyo ni
sehemu kubwa ya kukieneza Kiswahili. Licha ya kuendelea Kwa Kiswahili kupitia uwanja huu mpana wa
sanaa, bado pia kuna athari nyingi ambazo sasa zinajitokeza ambazo ni ile hali ya kukua kwa lugha ya
Kiswahili na kupotea kwa baadhi ya lugha za Kiafrika
Mwasilishaji: Levis Dotto Niyonkuru (Chuo Kikuu cha Ntare Rugamba, Burundi)
Ju
mapili, D
isem
ba 1
5, 2
019
37
Jumapili 8:50 Mch - 10:30 Jion - Vikao Sambamba Na 4
Chumba cha 5
Mada: Kiswahili na Sisasa/Utawala/Uongozi
Mwenyekiti:
Kiswahili, Usalama na Uhamiaji
Kiswahili ni lugha kamili yenye nguvu ya kupasua milima na mabonde bila kujali hali ya kiusalama. Mjadala si
vita eti usalama utoweke. Utafiti hudhihirisha kwamba Kiswahili ni lugha yenye asili, na chimbuko lake ndio
chanzo cha msafara wa kuenea kwake. Makala haya yana malengo ya kudadavua hali halisi ya Kiswahili ilivyo
hadi leo kutokana na usalama, na uhamiaji wa watumiaji wake. Umetumiwa utafiti wa aina mbili – utafiti wa
Kihistoria na utafiti wa Uchunzaji – uhamiaji wa watumiaji wa lugha ya Kiswahili kuwaelekea wale si
watumiaji wa lugha hiyo, na uhamiaji wa wasio watumiaji wa Kiswahili kuwaelekea wale ambao ni watumiaji
wa lugha hiyo ama kwa njia ya usalama tosha au kwa njia ya ukosefu wa usalama. Kwa makala haya, washiriki
wanashuhudia kukuwa na kuenea kwa Kiswahili kupitia hali ya kawaida na hali isiyo ya kawaida, na
wakishuhudia zaidi, wale waandaji wa makongamano ya Kiswahili katika Jumuiya mbalimbali.
Mwasilishaji: Mbonabuca Patience David (Chuo Kikuu cha Elimu, Burundi)
Nafasi ya Tawala za Kiafrika Katika Upangajilugha na Umuhimu wa Kiswahili
Makala haya yanalenga kuelezea uhusiano uliopo kati ya tawala za nchi za Afrika na Kiswahili katika
kuwezesha utafiti kuhusu upangaji lugha katika jamiilughaulumbi. Vilevile makala haya yatabainisha sababu za
wanaisimujamii kufanya tafiti zao katika jamiilughaulumbi. Pia makala haya yanaelezea namna gani tafiti
zinasaidia jamii katika upangajilugha. Kwasababu dhana za uwanja huu ni changamamni, tunachunguza dhana
zinazojenga hoja hii na kuzidadavua dhana hizo kulingana na mahitaji ya hoja zetu. Pia tunalenga kuonesha
mambo mbalimbali na vigezo vinavyosababisha jamiilugha kuwa jamiilughaulumbi.
Mwasilishaji: Clarah Nelson Moshi (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam)
Siasa na Lugha Nchini Kenya Enzi za Ukoloni
Makala hii imetafiti mahusiano yaliyokuwepo baina ya siasa na lugha ya Kiswahili enzi ya ukoloni wa
Mwingereza Kenya. Utafiti huu umekuwa wa maktaba na umeongozwa na malengo mawili ambayo ni kurejelea
historia ya lugha ya Kiswahili nchini Kenya na kuweza kufafanua nafasi, hadhi na mipaka ya matumizi ya lugha
tofauti tofauti mbali na kutoa fasiri za ni kwa nini kulikuwa na sera ya lugha ya aina hiyo iliyopatikana Kenya
ya kikoloni. Utafiti huu umechochewa na ukweli kuwa ni machache sana yajulikanayo kuhusu namna uwezo
alio nao mtu waweza kuathiri suala zima la mawasiliano – na katika muktadha huu – nafasi ya Kiswahili nchini
Kenya enzi ya mkoloni Mwingereza. Nadharia ya Kisosholojia iliyojikita katika mtazamo wa Kimaksi ndiyo
iliyotumika na mahitimisho ni kuwa lugha kwa jumla ina uwezo wa kujitokeza kama nembo na kwa hiyo kupitia
kwazo, hadhi na hali za kiuchumi kwa wote waliokuwa Kenya ya mkoloni Mwingereza zilijitokeza.
Mwasilishaji: Ayub Mukhwana (Chuo Kikuu cha Nairobi, Kenya)
Nafasi ya Vyama, Klabu, au Asasi za Kiswahili Katika Kukikuza Kiswahili
Vyama au asasi zinazojihusisha na ukuzaji wa lugha ya Kiswahili ni nyingi.Kwa Mfano Nchini Tanzania kuna
CHAWAKITA(Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili Vyuo vikuu Tanzania), mabaraza kama BAKIZA (Baraza
la kiswahili Zanziba), BAKITA(Baraza la Kiswahili Tanzania). Burundi kuna CHAWAKIBU (Chama cha
Wanafunzi wa Kiswahili vyuo vikuu Burundi), CHAKUKIBU (Chama cha Kukuza Kiswahili Burundi),
KLABU AMKENI TUJIFUNZE KISWAHILI, CHAWARUNDI (Chama cha Watangazaji wa Kiswahili
Burundi), RWANDA kuna CHAWAKIRWA (Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili Vyuo Vikuu Rwanda),
Kenya kuna CHAKITA (Chama cha Kiswahili Taifa). Kimataifa tuna CHAWAKAMA (Chama cha Wanafunzi
wa Kiswahili Vyuo Vikuu Afrika Mashariki), CHAUKIDU (Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani). Vyama
hivyo vinapoandaa makongamano, warsha,mafunzo ya kiswahili au kuandaa makala za kiswahili bila kusahau
ofisi za utafiti na uandishi wa vitabu tofauti, washiriki, watazamaji au wosomaji wanapata fulsa ya kukutana,
kuzungumza na kuchambua Kiswahili katika nyanja zote.Hivyo,Kiswahili kinakua kwa kasi kubwa sana kwani
njia hizon kama hamasa ya lugha.
Mwasilishaji: Leonard Nyandwi (Chuo Kikuu cha Burundi)
Ju
mapil
i, D
isem
ba 1
5, 2019
38
Jumapili 8:50 Mch - 10:30 Jion - Vikao Sambamba Na 4
Chumba cha 6
Mada: Tafsiri
Mwenyekiti:
Nadharia za Tafsiri Katika Fasihi ya Kiswahili: Mbinu, Changamoto na Mapendekezo
Makala hii inahusu Nadharia za tafsiri katika fasihi ya Kiswahili kwa kuchunguza mbinu, changamoto na kutoa
mapendekezo ya jinsi nadharia za tafsiri zinavyoweza kushughulikia tafsiri za fasihi ya Kiswahili. Lengo likiwa
ni; kubainisha mbinu za kutafsiri matini za fasihi ya Kiswahili, kubaini changamoto za tafsiri na sababu zake na
kutoa mapendekezo ya kukabiliana na changamoto hizo. Makala imetumia mifano ya riwaya ya Rosa Mistika na
data zimekusanywa kwa kutumia mbinu tatu ambazo ni usomaji wa machapisho, hojaji na usaili. Makala
inajadili kuwa matini za fasihi hufungamana na utamaduni wa jamii na hutumia sanaa ya lugha kuwasilisha
ujumbe. Kwa hiyo nadharia za tafsiri zinapaswa kuzingatia utamaduni, fani na maudhui ya kazi ya fasihi katika
tafsiri.
Mwasilishaji: Hadija Jilala (Chuo Kikuu Huria cha Tanzania)
Mandhari kama Kigezo cha Kujenga Uhalisia katika Riwaya ya Paradiso
Fasihi hufanikishwa kupitia vipengele maalum ambavyo hupitisha ujumbe uliokusudiwa na msanii wa kazi
husika. Mandhari ni mojawapo ya vipengele hivyo na muhimu sana katika kukamilisha kazi ya fasihi. Mandhari
hubainisha wapi na lini ambapo matukio ya hufanyika. Dhana ya mandhari ya mandhari basi humaanisha wakati
na mahali. Mandhari huweza kuathiri wahusika moja kwa moja kitabia na hata kupitia lugha wanayotumia. Ni
makazi maalum yaliyojengwa na mtunzi na panapotokea matukio maalum katika kazi ya fasihi. Ni jukwaa
analolitumia mtunzi ili kuwaeleza wahusika na vitendo vyao kisha kujenga maudhui. Isitoshe, matukio na
mielekeo ya kijamii humwathiri mtunzi katika uteuzi wa lugha, wahusika na maudhui. Hivyo basi, makala
yatashughulikia mandhari kama kigezo cha kujenga uhalisia kwa kurejelea riwaya ya Paradiso. Nadharia ya
uhalisia itatumiwa kwa sababu mandhari hujitokeza katika hali mbalimbali na wakati mwingine huwa ni ya
kufikirika tu. Hata hivyo sharti yawe ya kuaminika na kukubalika kwa sababu fasihi ni kazi ya kibunifu.
Mwasilishaji: Deborah Nanyama Amukowa (Chuo Kikuu cha Maseno, Kenya)
Harakati za Upiganiaji wa Haki za Mwanamke katika Tamthilia ya Kiswahili.
Kazi nyingi za fasihi zimetalii namna tofauti za unyanyasaji wa kijinsia, mwanamke akiathiriwa zaidi na
mfumo-dume wa jamii. Zipo kazi, hasa kutoka miaka ya 1980 hadi 1990 zinazomchora mwanamke kama
kiumbe aliyenyamazishwa na mwanamume na kujipata katika pingu asizoweza kujinasua. Hata hivyo, katika
miaka ya hivi majuzi kumetokea tamthilia zinazochora picha ya mwanamke aliyejikomboa kutoka kwa
minyororo ya mfumo-dume. Makala hii inajadili namna tamthilia ya Kiswahili imesawiri harakati za Kifeministi
tangu miaka ya themanini, kuonyesha mafanikio ya harakati hizo na namna ambavyo maudhui ya fasihi huakisi
mabadiliko ya jamii. Kufikia lengo hili, ninahakiki mapambano ya wanawake kwa kuchunguza maendeleo ya
mapambano hayo katika tamthilia kuanzia miaka ya 1980. Kwa kuangazia Nguzo Mama (Mhando 1982), Mama
Ee (Mwachofi 1987), Natala (wa Mberia 1997), Kigogo (Kea 2016) na nyinginezo, ninaonyesha kwamba
mafanikio aliyonayo mwanamke wa karne 21 hayatokani na mawimbi ya usasa tu, bali jumla ya jitihada
zilizoanzishwa tangu miaka ya 1980.
Mwasilishaji: Jacob Mwita (Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison, USA)
Ju
mapili, D
isem
ba 1
5, 2
019
39
Hoja Pevu Na. 2 - Uandishi Bunilizi 10:40-11:40 Jion
Ukumbi Mkuu
Mwenyekiti:
Safari ya Uandishi Bunilizi Makongomano mengi ya Kiswahili hushughulikia vipengee mbalimbali vya isimu na vya uhakiki wa fasihi. Ni
mara tukizi mno kuona mchakato wa kubuniliza ukichanganuliwa moja kwa moja. Tangu seminaa za uandishi
zilizoandaliwa Tanzania na makala za seminaa hizo kuchapishwa kwenye majuzuu mawili katika robo ya
mwisho ya karne iliyopita—mnamo mwaka 1978 na mnamo 1980 hapajawa na vikao mahsusi vinavyomulika
tajiriba ya uandishi. Kuandaliwa kwa seminaa hizo na kuchapishwa kwa makala zilizotakana nazo kulitoa
mchango mkubwa kwa vizazi vya waandishi wapya waliojifunza mengi kutokana na tajiriba na nasaha za
watangulizi wao kama vile Euphrase Kezilahabi na Said A. Mohamed. Jopo hili litaangazia tajriba ya
waandishi wanne wa Kiswahili, Pauline Keya Kyovi, Hamisi Babusa, Clara Momanyi na Ken Walibora.
Waandishi hao watajadili na kusimulia kuhusu safari ya uandishi. Miongoni mwa masuala muhimu
watakayoyazungumzia waandishi hawa ni kariha, dhamira, uteuzi na uendelezaji wa maudhui, uteuzi wa
utanzu, usukaji wa hadithi, uhusika, kuamua hadhira lengwa, urithishaji wa mikoba ya uandishi, changamoto
na nasaha ya waandishi chipukizi na watarajiwa
Wanajopo
Ken Walibora
Clara Momanyi
Pauline Keya Kyovi
Hamisi Babusa
Ju
mapili, D
isem
ba 1
5, 2
019
40
Jumapili 11:40 - 12:30Jion - Mapumziko
Ju
mapil
i, D
isem
ba 1
5, 2019
41
Jumapili 12:30 - 3:30Usik - Usiku wa Tuzo
Dhifa na Usiku wa Tuzo
Mgeni Rasmi
Mh. Janat Mukwaya (Mb) Waziri - Wizara ya Jinsia, Kazi, na Maendeleo ya Jamii
Ju
mapili, D
isem
ba 1
5, 2
019
42
Kielelezo cha Wawasilishaji
A
Abdul Nanji, 4, 5
Abdulaziz Yusuf Lodhi, 15
Agnes Bruhwiler, 4
Ahmad Kipacha, 35
Aidah Mutenyo, 4, 5, 10, 25
Alamin Mazrui, 10, 12
Aldin Mutembei, 4, 31
Alwiya S. Omar, 3, 21, 27
Anne Jebet, 5, 33
Asifiwe Eliud Mwagike, 29
Athumani S. Ponera, 24
Austin Bukenya, 19
Ayub Mukhwana, 37
B
Basilio Gichobi Mungania, 15
Beata Wojtowicz, 3
Beatrice Mkenda, 3, 27
Beatrice Ng'uono Okelo, 4, 5, 8, 26
Beth N. Mutugu, 36
Bimenyimana Innocent, 17
C
Caesar Jjingo, 30
Caroline Asiimwe, 16, 23
Charles Bwenge, 3, 5, 27
Clara Momanyi, 16, 19, 39
Clarah Nelson Moshi, 37
D
David Kyeu, 3
Deborah Nanyama Amukowa, 38
Deo Ngonyani, 3
Deogratias Ndagijimana, 25
E
Elias Magembe, 3, 5
Eliezer Bucumi, 35
Elizabeth Kyazike, 5
Ernesta Mosha, 6, 20, 32, 36
F
Fabiola Hassan, 34
FEMK Senkoro, 19
Filipo Lubua, 3, 8, 10, 27, 33
G
Gabriel Niyubuntu, 16
Geoffrey Okello, 13
Geofred Osoro, 27
Gertrude Joseph, 34
Gervas A. Kawonga, 26
Gordien Ndayikengurukiye, 16
H
Hadija Jilala, 4, 27, 38
Hamisi Babusa, 39
Happiness Bulugu, 3, 26
I
Innocent Nshimirimana, 25
Inyani Simala, 19
Iribe Mwangi, 4, 24
J
Jackson Ndungu Mwangi, 33
Jacob Mwita, 38
Janat Mukwaya, 41
John Kintu, 14
Joseph Hokororo Ismail, 14
K
Kaziri Alexis, 17
Ken Walibora, 4, 39
Kiarie Wa'Njogu, 5, 8
Kibigo Mary Lukamika, 36
Kimani Njogu, 6, 10, 12
Kulikoyela Kahigi, 23
Kyokushaba Moreen, 29
L
Leo Sanja, 35
Leonard Muaka, 3, 10, 16, 27
43
Leonard Nyandwi, 37
Leonora Kivuva, 31
Levis Dotto Niyonkuru, 36
M
M.M. Mulokozi, 19
Magdalyne Oguti Akiding, 21
Magreth J. Kibiki, 15
Mahiri Mwita, 3, 5, 27
Majariwa David, 13
Malimi Joram Kazi, 4, 5, 8, 33
Maria Mkunde Kanigi, 30
Mary Zacharia Charwi, 23
Masereka Levi Kahaika, 34
Mbonabuca Patience David, 37
Micah Bamugyeya, 17
Miriam Kenyani Osore, 25
Mohamed Abdulaziz, 19
Mokaya Bosire, 18
Mugambi Allam, 24
Musa Hans, 3
Mutungi Boaz, 28
N
Naomi N. Musembi, 28
Ndayikengurukiye Gordien, 4
Neema George Mturo, 22
Niklas Edenmyr, 14
Nintunze Fulgence, 26
O
Omar Salum Mohamed, 29
P
Pacifique Malonga, 4, 27
Pamela Muhadia, 22
Pauline Keya Kyovi, 39
Pendo Salu Malangwa, 4, 24
R
Rachel Maina, 22
Rebecca A. Kadaga, 11
Rocha Chimera, 23
Rukiya Harith Swaleh, 34
Ruth Mukama, 19
S
Sarah Nabiccu, 5
Sarah Ndanu M. Ngesu, 13, 21
Shadidu A. Ndossa, 29
Shadrack Kirimi, 21, 31
Shani Omari, 28
Sikitu Elias Luvanda, 15
Simon Kawaida, 35
Susan Chebet-Choge, 31
Susan Mongalla Ngbabare, 30
T
Timammy Rayya, 19
Timothy Kinoti M'Ngaruthi, 22
Tuyisenge Ange Merline, 33
Y
Yerindabo T. Innocent, 13
Yunusu Lubuuka, 5, 28
Z
Zainab Ali Iddi, 4, 30
44
Kongamano la 6 la Kimataifa la Mwaka 2020
Taarifa Itatolewa