OFISI YA RAIS - Mwalimu Wa Kiswahili
Transcript of OFISI YA RAIS - Mwalimu Wa Kiswahili
OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MKOA WA DAR ES SALAAM
MTIHANI WA UTAMILIFU KIDATO CHA SITA 2020
KISWAHILI -2
Msimbo: 121/1
Muda: Saa 3.00 ljumaa, 04 Disemba, 2020 Asubuhi
MAELEKEZO
1. Karatasi hii ina maswali nane (8) katika sehemu A na B 1.
2. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na kila swali
Sehemu A ina alama arobaini (40) na sehemu B ina alama sitini (60) 3.
Simu za mkononi haziruhusiwi katika chumba cha mtihani A.
Andika nanmba yako ya mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako 5. cha kujibia
Mtihani huu una kurasa 3 zilizochapishwa
SEHEMU A: (ALAMA 40) Jibu maswali yote katika sehemu hii
"Hadithi ni utenzi wa fasihi simulizi wenye dhima kubwa kwa jamil" Fafanua bayana Fani ya 1.
Utenzi huu. (hoja tano)
2. Ushairi na ngonjera ni tanzu za fasihi simulizi zenye kufanana na kutofautiana. Bainisha
hoja tatu za kufanana na hona mbili za kutofautiana kwa tanzu hizo.
Fafanua mambo matano (5) muhimu yanayopaswa kuzingatia ili kuwepo kwa uhuru wa 3.
mwandishi wa kazi za kifasihi nchini Tanzania.
Bainisha kwa kutoa mifano dhahiri vipengele vya kisanaa vilivyotumika katika shairi 4.
lifuatalo. Walivyosema wahenga, sifa ya mke tabia
Si kule kuvaa kanga, kwa sura ukavutiya Utuni akijitenga, hadhi yake humpoteya
Sura njema sio pambo, sifa ya mke tabia
Kinompa taadhima, ukinaifu na haya,
Utifu na huruma, hata uhodari piya,
Kigezo cha mke mwema, sifa niliwatajiya,
Sura njema sio pambo, sifa ya mke tabia.
Pia awe mtulivu, asiwe kiruka njiya,
Ufedhuli na uovu, kama yake mazoweya,
Usijipe maumivu, ukiowa utaliya
Sura njema ni kipambo, sifa ya mke tabia.
Awe kama malaika, mzuri kupindukiya,
Tabia zikipotoka, si vizuri kusogeya,
Utakuja fedheheka, tahadhari nakwambiya
Sura njema ni kipambo, sifa ya mke tabia
2
Sehemu B (Alama 60) Jibu maswali matatu (3) kutoka sehemu hii
Swali la tano (5) ni la lazima
ORODHA YA VITABU VYA SWALI LA 5-8
USHAIRI
Uchungu Tamu TheobaldA. Mvungi Fungate ya Uhuru Mohamed.S. Khatibu
Kimbunga Haji Gora Haji
Mapenzi Bora Shaaban Robert
RIWAYA
Kufikirika Shaaban Robert
Mfadhili Hussein Tuwa
Vuta Nkuvute Shafi Adam Shafi
Usiku utakapokwisha- Mbunda Msokile
TAMTHILIA
Kivuli kinaishi Saidi Mohamed
Kwenye ukingo wa Thim Ebrahim Hussein
Nguzo mama Penina Muhando
Morani Emanuel Mbogo
"Ushairi ni msingi mzuri sana wa kujenga jamii yenye maadili mema kwa vizazi nyote" 5. Thibitisha usemi huo kwa kutoa hoja nne kwa kila Diwani katika Diwani mbili ulizosoma.
6. Matumizi ya Taswira katika ushairi huonesha ukomavu na umahiri wa mwandishi. Onesha
ukweli wa kauli hii kwa kutoa hoja nne (4) kwa kila kitabu katika Diwani mbili ulizosoma
"Mtindo ni kipengele muhimu sana katika utanzi wa riwaya kwani hufanya kazi ya 7
mwandishi kufikisha ujumbe aliokusudia kwa jamii lengwa" Thibitisha usemi huu kwa
kutoa vipengele vinne kwa kila kitabu katika riwaya mbili ulizosoma.
Tamthiliya nyingi ni za machungu kutokana na ujumbe mzito unaobebwa kwa jami. 8. Fafanua dai hili kwa kutoa hoja nne zinazodhihirisha machungu kwa kila kitabu kati ya
tamthilia mbili ulizosoma.
3