Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha...

40
MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III Moduli ya Tisa: KUTENGANISHA NA KUUNGANISHA FONIMU Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

Transcript of Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha...

Page 1: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III

Moduli ya Tisa: KUTENGANISHA NA KUUNGANISHA FONIMU

Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

Page 2: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

Moduli hii imetayarishwa kwa ushirikiano na:

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya UfundiO�si ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Taasisi ya Elimu TanzaniaChuo Kikuu cha Dodoma

Chuo cha Ualimu MorogoroChuo Kikuu cha Dar Es SalaamChuo Kikuu Huria cha Tanzania

Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu MkwawaEQUIP-Tanzania

Moduli hii imewezeshwa kwa ushirikiano na:

C.C.U ButimbaC.C.U BustaniC.C.U TaboraC.C.U NdalaC.C.U Kasulu

C.C.U KabangaC.C.U BundaC.C.U Tarime

C.C.U ShinyangaC.C.U Mpwapwa

Page 3: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

1Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DIBAJI

Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta ya elimu ili kuleta mageuzi ya kiuchumi na kijamii. Lengo la Dira ya Maendeleo ni kuwa na taifa la watu waliolelimika na jamii iliyo tayari kujifunza ku�kia 2025. Serikali ya Tanzania imethibitisha kwa vitendo kuwa Elimu ni kiambato muhimu katika kupunguza umaskini na kuimarisha maendeleo ya taifa. Kwa muda mrefu serikali imetambua kuwa “Ubora wa Elimu yoyote hauwezi kuwa bora kuliko mwalimu mwenyewe” hivyo imetilia mkazo mafunzo kazini kwa walimu kupitia mikakati mbalimbali ili kuimarisha umahiri wa walimu katika ufundishaji na ujifunzaji darasani.

Katika kuongeza ufanisi wa ufundishaji na ujifunzaji darasani, Taasisi ya Elimu Tanzania kwa kushirikiana na EQUIP-Tanzania, wameandaa moduli hii ambayo imesheheni kazi mbalimbali ambazo waalimu mtazitenda katika vikundi wakati wa mafunzo kwa kutumia mbinu ya Mafunzo ya Walimu Kazini ngazi ya shule. Mbinu hii inatambua umuhimu wa walimu kujifunza pamoja na kubaini changamoto zinazowakabili ili kupata suluhisho la changamoto za ufundishaji na ujifunzaji kwa pamoja.

Moduli hii ya Mafunzo ya Walimu Kazini, imeandaliwa ili kusaidia juhudi za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuhakikisha kuwa mbinu fanisi zinatumika darasani wakati wa ufundishaji na ujifunzaji. Moduli hii pia inawasaidia walimu kushirikishana uzoefu na umahiri katika ufundishaji na ujifunzaji darasani. Vilevile Moduli inatoa mafunzo ya ziada ikitarajiwa kuwa walimu watakuwa wamekwisha pata Mafunzo Kabilishi ya utekelezaji wa Mtaala ulioboreshwa wa kuimarisha ufundishaji wa KKK kwa wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili.

Taasisi ya Elimu Tanzania inatarajia kuwa moduli hii itawasaidia walimu kuimarisha umahiri wa ufundishaji na ujifunzaji ili kuwasaidia wanafunzi waweze kujenga uwezo unaokusudiwa wakati wa kujifunza.

Changamoto iliyo mbele yetu ni kuhakikisha kuwa tunaonyesha kwa vitendo matokeo mazuri yanayotokana na maudhui ya moduli hii wakati wa ufundishaji na ujifunzaji darasani ili kuimarisha ubora wa elimu ya shule ya msingi.

Dr. Leonard AkwilapoKaimu Mkurugenzi Mkuu,Taasisi ya Elimu Tanzania.

Page 4: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

2 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

Maelezo Muhimu kwa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

Mwongozo huu utatumika sanjari na moduli ya tisa ya mwalimu ili kumsaidia mratibu wa mafunzo kuwa na mpangilio mzuri wenye kufuata hatua kwa hatua ili kuwafanya walimu

washiriki kikamilifu katika kujifunza maudhui ya moduli ya tisa.

Mwongozo huu umegawanyika katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ambayo ni upande wa kushoto wa mwongozo unabeba maelezo ambayo mratibu wa mafunzo ya walimu kazini ngazi ya

shule atatakiwa kuyafuata wakati wa kuratibu kipindi cha kujifunza maudhui ya moduli. Sehemu ya pili ambayo ni upande wa kulia wa mwongozo unabeba maudhui yaliyo kwenye moduli ya mwalimu

ambayo watayasoma wakati wa kipindi cha kujifunza.

Wakati wa kipindi cha kujifunza, unatakiwa kufuata maelezo yanayokuongoza yaliyo upande wa kushoto wa mwongozo

huu na kuyahusianisha na maudhui yaliyo kwenye moduli ya mwalimu ambayo yapo upande wa kulia wa mwongozo huu

kama yanavyosomeka kwenye moduli ya mwalimu.

Page 5: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

3Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

MAELEKEZO NA TASWIRA KATIKA MODULI

Kuna picha na michoro mingi katika moduli. Baadhi zinajirudia mara nyingi kwa sababu zinamaanisha jambo mahususi linalotokea. Zifuatazo ni mifano ya taswira mbalimbali ambazo zinapatikana katika moduli pamoja na kile ambacho zinawakilisha:

Jadili na mwenzako: Wakati wote wa kusoma moduli, walimu wataelezwa kufanya kazi pamoja na mwalimu mwingine juu ya maswali au kazi.

Fikiri– Wawili wawili – Shirikishana: Kama ilivyo katika maelezo ya hapo juu, hapa vilevile walimu wanafanya kazi wakiwa wawili wawili. Japokuwa, hapa walimu wanatafakari mmoja mmoja kwanza juu ya swali au tatizo, halafu mwalimu anafanya kazi na mwenzake na mwishoni wanawasilisha katika kundi lote.

Jadiliana katika kikundi: Wakati mwingine walimu wataelekezwa kutafakari au kujadili maswali mbalimbali katika kikundi.

Soma: Katika kila moduli kuna “dhana kuu” ambayo kwa kawaida huwasilishwa kwa kirefu katika maelezo.

Andika: Moduli itawahamasisha walimu kuchukua maelezo na kuandika �kra zao na majibu.

Igizo: Baadhi ya mazoezi yatahitaji walimu kuigiza kazi ya KUFUNDISHA wakati wengine watapaswa kuigiza kama wanafunzi.

Page 6: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

4 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

MAELEKEZO KWA MRATIBU WA MAFUNZO YA WALIMU KAZINI

Kabla ya kuanza moduli hii, angalia ‘maelekezo muhimu’ na hakikisha kuwa wewe na walimu mnayatekeleza.

Tafadhali waambie walimu wajiorodheshe na kusaini hapa chini.

Tarehe: Shule: Wilaya: Mkoa:

Muda wa kuanza: Jina la Mratibu na sahihi yake:

Muda wa kumaliza: Jina la Mwalimu Mkuu na sahihi yake:

JINA LA MWALIMU ME / KE SAHIHI: DARASA1

2

3

4

5

6

7

8

WAAMBIE WALIMU:

“Sasa tutasoma utangulizi wa moduli hii. Tutasoma matini kwa sauti na kwa kupokezana. Baada ya mwalimu wa kwanza kusoma aya ya kwanza, atamwita mwalimu mwingine kwa jina ili asome aya inayofuata.”

Page 7: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

5Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

MODULI YA 9: KUTENGANISHA NA KUUNGANISHA FONIMU

MAUDHUI YA MODULIModuli ya 5 – 8 inahusu dhana na mbinu za KUFUNDISHA kusoma ambazo zinaendana na mabadiliko yaliyo kwenye muhtasari mpya wa darasa la kwanza na la pili. Moduli hii pia inahusu baadhi ya dhana na shughuli kama zilivyoanishwa kwenye muhtasari mpya wa darasa la kwanza na la pili. Vile vile inahusu Kutenganisha na Kuunganisha fonimu/sauti. Hizi ni njia mbili zinazowawezesha wanafunzi kutumia ujuzi wao wa foniki kusoma maneno ambayo hawayajui. Wanafunzi wanapoona maneno mageni, kwanza wanaweza kuyatenganisha kwa kuyavunja katika sauti moja moja. Baada ya kuyavunja, wanaweza kuunganisha sauti hizo kwa pamoja kubainisha namna neno linavyosomeka.

DHANA KUU1. Foniki: inaonesha uhusiano wa heru� katika utamkaji wa maneno na sauti ya lugha ya kuongea

(/s/ = “s”). Pia inajulikana kama maarifa ya uhusiano wa heru� na sauti.2. Kuhusianisha: Uwezo wa kufasiri neno kutoka kwenye maandishi kuwa matamshi, kwa kuvunja neno

katika sauti moja moja (kutenganisha fonimu) na kisha kuunganisha sauti hizo ili kutamka neno (kuunganisha fonimu).

3. Kutenganisha Fonimu: Kuvunja neno katika sauti moja moja (bata = /b/ + /a/ + /t/ + /a/)4. Kuunganisha Fonimu: Uwezo wa kusikiliza mfuatano wa sauti moja moja zinavyotamkwa na

kuunganisha sauti hizo ili kuunda neno (/b/ + /a/ + /t/ + /a/= bata).5. Heru� Mwambatano: Konsonanti mbili ambazo zinaunganishwa kutengeneza sauti za heru� moja

(ch, sh, th, dh, mw, ny)

MALENGO YA MODULIMwisho wa moduli hii, walimu watakuwa na uwezo wa:

1. Kueleza kwa nini ujuzi wa kuunganisha na kutenganisha fonimu ni muhimu katika kujifunza kusoma2. Kuongoza wanafunzi kutenganisha na kuunganisha fonimu/sauti zinazounda neno3. Kuwapima wanafunzi uwezo wa kuunganisha na kutenganisha fonimu4. Kutengeneza kadi za heru� zitakazotumika katika kutenganisha na kuunganisha sauti zinaunda neno

MAELEKEZO MUHIMU Njoo na vitu vifuatavyo:

1. Moduli ya mafunzo ya walimu kazini na kalamu2. Karatasi 10 za ukubwa wa A4 za manila kwa kila mwalimu (kama hakuna kadi za manila, tumia

karatasi iliyo wazi au bodikadi)3. Viweka alama au mkaa4. Karatasi zilizofomekwa (kama una Kivunge cha Kufundishia cha EQUIP-Tanzania)

TARATIBU ZA KUJIFUNZA KWA KILA KIPINDI1. Kutana katika sehemu tulivu yenye ubao kama

inavyoonekana katika picha2. Panga madawati/meza ili kuwezesha washiriki

wote waonane na kuongea kwa pamoja3. Waeleze walimu wawe huru kuuliza maswali

kama hawajaelewa4. Waeleze walimu kuwa msaada kwa wenzao5. Waeleze walimu kuwa wabunifu na ku�kiria dhana

watakazojifunza na jinsi zitavyohusiana na darasa lao6. Waeleze walimu waweke simu zao katika hali ya mtetemo

Page 8: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

6 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

TAFAKARI

WAAMBIE WALIMU:

“Tangu moduli ya 8, umefanyia mazoezi shughuli mbili kwenye kipindi cha kujifunza kusoma na kuandika. Orodhesha mafanikio uliyoyaona pamoja na changamoto ulizokabiliana nazo wakati wa KUFUNDISHA maudhui ya moduli hiyo darasani kwako. Una dakika 5 kwa ajili ya kazi hii.”

WAAMBIE WALIMU:

“Sasa tutajadili kwa pamoja mafanikio na changamoto katika vikundi. Kwa kila changamoto ambayo imewasilishwa tu�kiri kwa pamoja kuhusu namna ya kukabiliana nayo. Kumbuka kuandika ufumbuzi ambao unaweza kukabiliana na changamoto zilizojitokeza. Tutatumia dakika 10 kwa majadiliano.”

Page 9: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

7Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

TAFAKARI

Katika kipindi cha mwisho tulisoma kuhusu foniki. Orodhesha mafanikio uliyoyaona pamoja na changamoto ulizokabiliana nazo wakati wa KUFUNDISHA maudhui ya moduli hiyo darasani kwako.

ANDIKA PEKE YAKO (DAKIKA 5) Tafadhali andika kwenye visanduku mafanikio na changamoto ulizokutana nazo wakati wa kutekeleza mikakati hii katika darasa lako.

JADILIANA KATIKA KIKUNDI (DAKIKA 10)

1. Shirikisha wenzako kwenye kundi mojawapo kuhusu uzoefu huo. 2. Kwa kila changamoto, pendekeza namna ya kukabiliana nayo.3. Wakati wa majadiliano, andika ufumbuzi unaoendana na changamoto ulizobainisha.

Mafanikio(Elezea utaratibu uliotumia na fafanua jinsi ulivyofanikiwa)

Changamoto (Elezea utaratibu uliotumia na fafanua changamoto zake)

Njia Muhimu za Ufumbuzi(Mawazo muhimu na mahususi kwa wenzetu)

Page 10: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

8 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

UTANGULIZI WAAMBIE WALIMU:

Shughuli yetu ya leo itaanza na mchezo wa kutuchangamsha akili. Utaona majedwali mawili. Jedwali la kwanza lina alama na vitu vinavyowakilisha heru� za alfabeti (mara nyingi jina la kitu linaanza na heru� inayoliwakilisha). Jedwali la pili lina orodha ya maneno matano yanayowakilishwa na alama au vitu. Wewe na mwenzako tumia jedwali la kwanza kubainisha heru� zinazounda maneno ya jedwali la pili. Tafadhali zingatia kwamba heru� ‘A’, ‘I’, na ‘O’ hazina alama za kuziwakilisha. Neno la kwanza limeoneshwa kama mfano.

Baada ya kumaliza, utashirikisha wenzako katika kikundi kuhusu majibu yako. Usisite kuniuliza swali kama unahitaji msaada.

Walimu wanapomaliza, waambie watamke jibu kwa sauti. Hapa kuna baadhi ya majibu:

1. Sa�2. Mtu3. Jiko4. Fursa5. Yake

Page 11: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

9Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

UTANGULIZI

ZOEZI LA KUCHANGAMSHA (DAKIKA 20)

Yafuatayo ni majedwali mawili. Jedwali la kwanza lina alama na vitu vinavyowakilisha heru� za alfabeti (mara nyingi jina la kitu linaanza na heru� inayoliwakilisha). Jedwali la pili lina orodha ya maneno matano yanayowakilishwa na alama au vitu. Wewe na mwenzako tumia jedwali la kwanza kubainisha heru� zinazounda maneno ya jedwali la pili. Tafadhali zingatia kwamba heru� ‘A’, ‘I’, na ‘O’ hazina alama za kuziwakilisha. Neno la kwanza limeoneshwa kama mfano.

Jedwali la 1:

Jedwali la 2:

Page 12: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

10 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

UTANGULIZI

WAAMBIE WALIMU:

“Sasa tumemaliza, tafadhali someni swali kwa kujitegemea na �kirini kuhusu majibu yenu. Jadilini majibu yenu na mwenzako. Kisha mtashirikisha mawazo yenu kwa kundi zima.”

Baada ya kuhusianisha maneno yote, jadili swali lifuatalo pamoja na mwenzako na kisha shirikisha mawazo yako kwa kundi zima:

1. Unadhani shughuli hii inahusiana na nini?

Kama walimu wanakwama, hapa kuna baadhi ya majibu:

Jibu la 1: Tunaoanisha sauti za heru� na alama za uandishi (heru� zilizoandikwa) ili kusoma kwa sauti.

WAAMBIE WALIMU:

“Sasa tutasoma maudhui muhimu. Tutasoma matini kwa sauti na kwa kupokezana.

Baada ya mwalimu wa kwanza kusoma sehemu (kwa mfano, aya au maelezo), atamwita mwalimu mwingine kwa jina ili asome aya inayofuata.

Wakati wa kusoma weka alama zifuatazo kwenye matini unayosoma.

Weka alama ya mshangao (!) kwenye wazo unalodhani ni muhimu.

Weka alama ya kuuliza (?) kuonesha kutokukubaliana na dhana hiyo.

Weka alama ya duara (0) kuonesha kuwa dhana hiyo ni mpya kwako.”

DHANA KUU

Page 13: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

11Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

UTANGULIZI

FIKIRI – JOZISHA – SHIRIKISHANA (DAKIKA 5)

Baada ya kuhusianisha maneno yote, jadili swali lifuatalo pamoja na mwenzako na kisha shirikisha mawazo yako kwa kundi zima:

1. Unadhani shughuli hii inahusiana na nini?

DHANA KUU

Kama ilivyojadiliwa kwenye moduli 6, 7 na 8, kujifunza kusoma ni mchakato ambao unaanza kwa watoto kujua lugha ya matamshi na kujifunza namna lugha hii inavyowakilishwa kwenye maandishi. Ili wanafunzi wawe na uwezo wa kusoma maneno yalioandikwa, wanapaswa kufahamu kuwa:

Moduli hii inalenga hatua ya 3 – kuwasaidia wanafunzi kufahamu kwamba heru� zinaunda maneno yanayotamkwa na hatua ya 4 – kuwasaidia wanafunzi kusema maneno haya kwa kutamka sauti zinazoendana na heru� . Tulifanya kitu kinachofanana na hiki kwenye mchezo wa kuchangamsha.

UMUHIMU WA KUTENGANISHA NA KUUNGANISHA FONIMU (DAKIKA 45)

1. Mwalimu mmoja aanze kusoma kwa sauti. Baada ya kukamilisha sehemu (kwa mfano, aya au maelezo) amwite mwalimu mwingine kwa jina asome sehemu inayofuata.

2. Wakati unaposoma zingatia alama zifuatazo: • Weka alama ya mshangao (!) katika sehemu ambayo unaona ni muhimu.• Weka alama ya kuuliza (?) katika sehemu ambayo huelewi au hukubaliani nayo.• Weka mduara katika (o) maneno ambayo ni mapya.

• Tunaweza kuona kwamba maneno matano yameundwa na alama zinazowakilishwa na heru� tofauti (baadhi tunazifahamu).

• Tulipaswa kuusianisha alama na sauti za heru� ambazo tulizijua (kwa kutumia jedwali la 1).• Tulipojua sauti za zinawakilishwa na heru� , tuliweza kutamka neno.

1. Maneno yanayotamkwa yanaundwa na

sauti tofauti.

2. Sauti hizi zinahusiana

na heru� zinazoandikwa

3. Heru� zinaunda maneno

yanayoandikwa

4. Maneno yanayoandikwa

yanaweza kutamkwa kwa kutumia sauti zi-nazofanana na heru� .

Page 14: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

12 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU

WAAMBIE WALIMU:

“Tunaendelea kusoma matini kwa sauti na kwa kupokezana.”

Page 15: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

13Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU

Mchakato huu unafanana sana kwa wanafunzi ambao wanajifunza kusoma:

Hii ni sawa na mchezo wa Binya Vidole ambao uliusoma kwenye moduli ya 7. Tulijifunza kutenganisha neno katika kila sauti za heru� moja moja (kwa kugusa dole gumba katika kila sauti), kisha tuliziun-ganisha pamoja wakati tukitamka sauti za heru� haraka. Japokuwa, Binya Vidole ilikuwa kwa ajili tu ya maneno yanayotamkwa. Hapa, tutakuwa tunavunja neno katika sauti, lakini siyo kwa kutumia vidole vyetu. Badala yake, tutavunja sauti za maneno kupitia kwa kila silabi au heru� yake.

Namna ya Kutenganisha na Kuunganisha heru�

Mchakato wa kubaini sauti zinazaounda neno katika vipande vidogovidogo unaitwa Kutenganisha. Hivi vipande vidogo vidogo vinaweza kuwa heru� moja moja au silabi. Unaweza kuwafundisha wanafunzi wako namna ya kutenganisha kwa kutumia njia zote. Kama umekuwa ukiwafundisha wanafunzi wako sauti za heru� moja moja, unaweza ukaanza na kutenganisha sauti moja moja kwa maneno mafupi na silabi. Hapa kuna mchakato wa kuhusianisha na kuunganisha maneno mafupi:

1. Wafahamu lugha inayozungumzwa, lakini siyo lazima wajue alama zilizotumika katika lugha iliyoandikwa.

2. Wanapaswa kubaini neno kwa kugawa alama moja moja (heru�) na kuoanisha sauti wanazojua kwa kila alama. Mchakato huu unaitwa Kutenganisha.

3. Wanafunzi wanaweza kuunganisha sauti moja moja pamoja kuunda neno linalotamkwa. Mchakato huu unaitwa Kuunganisha.

HATUA YA 1: Angalia neno “duka”. HATUA YA 2: Tenganisha neno ‘duka’ katika sauti moja moja (ambayo ni utenganishaji).

/d/ /u/ /k/ /a/

Page 16: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

14 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU

WAAMBIE WALIMU:

“Tunaendelea kusoma matini kwa sauti na kwa kupokezana.”

Page 17: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

15Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU

HATUA YA 3: Tamka neno “duka” kwa sauti za heru� moja moja (ambapo ni kuunganisha).

HATUA YA 4: Tamka sauti za heru� pamoja kwa kasi ya utamkaji wa kawaida (soma kwa sauti).

Hatua za KUFUNDISHA Kutenganisha na Kuunganisha

Njia moja wapo ya KUFUNDISHA wanafunzi namna ya kutenganisha na kuunganisha maneno ni kwa kutumia kadi za heru� (ambazo utazitengeneza baadaye katika moduli hii). Hapa chini kuna hatua za kutumia kadi za heru� pamoja na darasa lako ili kuonesha namna ya kutenganisha na kuunganisha neno:

HATUA YA 1: Wanafunzi wanaangalia neno.

1. Chagua neno rahisi na chukua kadi za heru� za neno hilo. Kwa mfano, “kiti”.

2. Eleza wanafunzi wanne wajitolee – kushika kadi moja kwa kila heru�.

3. Mpe kila mwanafunzi kadi ya heru�. Waambie wazishikilie kadi zikiwa juu ili darasa zima liweze kuona neno “kiti”, usilitamke neno na usiwaulize wanafunzi hilo ni neno gani.

HATUA YA 2: Vunja neno ‘kiti’ katika sauti moja moja (ambapo ni kutenganisha).

1. Elekeza kidole kwa mwanafunzi aliyeshika kadi nyenye heru� “k” na mwambie atembee hatua moja kwenda mbele.

2. Uliza darasa, sauti ya heru� hii ni nini?. Sauti sahihi ikishatamkwa, waambie wanafunzi wote waseme /k/ kwa pamoja.

3. Fanya hivi kwa kila heru�.

/ddd/ /uuu/ /kkk/ /aaa/ “duka”

Page 18: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

16 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU

WAAMBIE WALIMU:

“Tunaendelea kusoma matini kwa sauti na kwa kupokezana.”

Page 19: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

17Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU

HATUA YA 3: Tamka neno “kiti” kuwa sauti za heru� moja moja (ambapo ni kuunganisha).

1. Mara tu sauti za heru� zote zikishatamkwa, elekeza wanafunzi kushusha kadi za heru� zao na zishikilie kwenye matumbo yao.

2. Kisha elekeza kila mwanafunzi kunyoosha kadi ya heru� yake wakati ukitamka sauti ya heru� hiyo polepole – moja baada ya nyingine: /k/ /i/ /t/ /i/

3. Waambie wanafunzi wote warudie, hakikisha wanatamka sauti ya heru� polepole: /k/ /i/ /t/ /i/

HATUA YA 4: Tamka sauti za heru� pamoja kwa kasi ya utamkaji wa kawaida (soma kwa sauti ‘kiti’).

1. Kisha simama pembeni ya waliojitolea na nyoosha kidole kuelekea kwenye heru� zao wakati ukitamka neno katika sauti ya uongeaji wa kawaida: “kiti”. Waambie wanafunzi warudie.

Umekwishamaliza kupitia mchakato wa kutenganisha na kuunganisha fonimu. Tumia mbinu hii pamoja na maneno magumu zaidi au msamiati mpya ambao unaufundisha katika kiwango cha sasa.

Namna ya Kutenganisha na Kuunganisha

Wanafunzi wanaweza kutenganisha silabi kwa njia inayofanana: Katika hatua ya 3 ‘Unganisha sauti’ ondoa sauti zilizojirudia ambazo ni ‘bbb’ na aaa ili zibaki ‘b’ na ‘a’

1 Angalia silabi

ba

2. Tenganishakatika sauti

/b/ /a/

3. Unganisha sauti

/bbb/ /aaa/

4. Tamkaharaka

“ba”

Page 20: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

18 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU WAAMBIE WALIMU:

“Tunaendelea kusoma matini kwa sauti na kwa kupokezana.”

Page 21: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

19Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU

Ukiwafundisha wanafunzi wako namna ya kutambua na kutamka silabi (kama, ba, be, bi, bo, bu), unaweza kuwaonesha namna ya kuvunja maneno marefu kuwa hizi silabi ndogo ndogo. Kwa mfano:

Wakati wanafunzi wanatenganisha neno pamoja na silabi nyingi, wanapaswa kuligawa neno katika silabi na kisha kuunganisha kila silabi pamoja. Silabi katika Kiswahili zinaundwa katika miundo tofauti:

• Irabu peke yake (mwanzoni na mwishoni mwa neno) - u|hu|ru au sa|a• Konsonanti peke yake kama ‘m’ na ‘n’ ambazo ni silabi katika baadhi ya maneno. Kama vile ‘mti’ na

‘nchi’ au /n/ mwanzoni mwa neno - m|ti au n | je• Konsonanti + irabu– na|zi• Heru� mwambatano + irabu – sha|mba

Hatua za KUFUNDISHA kutenganisha na kuunganisha silabi Unaweza pia kutumia kadi za heru� KUFUNDISHA namna ya kutenganisha maneno katika silabi. Kwa mfano, kama unataka kutenganisha neno “soma’, fuata maelekezo yafuatayo:

HATU YA 1: Angalia silabi

1. Omba wanafunzi wajitolea kadi za heru� – mmoja kwa kila heru�

2. Mpe kila mwanafunzi kadi ya heru� . Waambie washikilie kadi hizo juu ili darasa zima liweze kuona neno ‘soma’

HATU YA 2: Tenganisha silabi katika sautiUliza darasa silabi ‘so’ inaundwa na sauti gani?. Baada ya jibu sahihi, elekeza darasa zima litamke /so/ pamoja

1. Elekeza kidole kwa wanafunzi walioshikilia ’s’ na ’o’. Waambie watembee hatua moja mbele

2. Uliza darasa, silabi hiyo inaundwa na sauti gani?. Baada ya jibu sahihi kutamkwa, elekeza darasa zima litamke /so/ kwa pamoja.

3. Elekeza kidole kwa wanafunzi walioshikilia ’m’ na ’a’ na waelekeze watembee hatua moja mbele

4. Uliza darasa, silabi ‘ma’ inaundwa sauti gani? Baada ya jibu sahihi kutamkwa, elekeza darasa zima litamke /ma/ kwa pamoja.

1 Angalia silabi

bata

2. Tenganishakatika sauti

ba-ta

3. Unganisha sauti

/ba/ /ta/

4. Tamka

“bata”

Page 22: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

20 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU WAAMBIE WALIMU:

“Tunaendelea kusoma matini kwa sauti na kwa kupokezana.”

Page 23: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

21Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU

HATU YA 3: Unganisha silabi

1. Waambie wanafunzi washushe kadi za heru� zao na wazishikilie usawa wa matumbo yao.

2. Kisha elekeza kila mwanafunzi anyanyue kadi ya heru� yake wakati akitamka sauti za silabi polepole – moja baada ya nyingine: /so/…./ma/

3. Elekeza darasa lirudie, hakikisha wanatamka sauti za silabi polepole: /so/….. /ma/

HATU YA 4: Tamka “soma”

1. Kisha, simama pembeni ya waliojitolea na nyoosha kidole kwenye silabi zao na tamka neno katika sauti ya utamkaji wa kawaida: ‘soma’. Elekeza darasa lirudie neno hilo.

2. Mwisho, simama pembeni ya waliojitolea na nyoosha kidole kwenye silabi zao na tamka neno katika sauti ya utamkaji wa kawaida: ‘soma’. Elekeza darasa lirudie neno hilo.

3. Unaweza pia kutumia mbinu hii kwa maneno marefu na magumu.

Namna ya kutenganisha na kuunganisha maneno magumuMara nyingi, wanafunzi hukutana na neno lililojumuisha silabi ambazo hawajazisoma ama silabi ambazo hawakuwahi kuziona kabla. Hili linapotokea, wanafunzi wanapaswa kuvunja neno na kuwa silabi fupi na kisha kulihusianisha/kuunganisha silabi ambazo ni mpya au hawazifahamu kabisa. Kwa mfano:

1. Angalia neno jipya

Nyumbani

2. Tenganisha katika silabi

Nyu-mba-ni

3. Weka mkazo kwenye silabi

mpya ya kwanza ‘nyu’

4. Tenganisha katika sauti

/ny/ /u/

5. Unganisha

/ny/ /u/

6. Tamka

‘nyu’

7. Weka mkazo katika silabi mpya

inayofuata‘mba’

8. Tenganisha sauti

/mb/ /a/

9. Unganisha

/mb/ /a/

10. Tamka

‘mba’

11. Tamka silabi mpya kwanza

‘nyu’‘mba’

12. Tamka silabi mpya ya pili:

‘mba’

13. Tamka silabi ya tatu

‘ni’

14. Ziunganishe silabi zote tatu

/nyu/ /mba/ /ni/

15. Tamka neno

‘nyumbani’

Page 24: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

22 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU WAAMBIE WALIMU:

“Tunaendelea kusoma matini kwa sauti na kwa kupokezana.”

WAAMBIE WALIMU:

“Sasa kila mwalimu anaweza kushirikisha jambo aliloona ni muhimu, halieleweki au ni jipya. Kisha tunaweza kujadili kwa nini mbinuza kuhusianisha na kuunganisha zinaweza kuimarisha uwezo wa wanafunzi kusoma.”

Eleza kila mwalimu atoe majibu yake. Kama walimu wanakwama juu ya swali la 4, hapa kuna jibu ambalo unaweza kuwashirikisha:

Jibu la 4: Kama wanafunzi wanaweza kuvunja neno na kuwa katika sauti heru� zake (kuhusianisha), na kisha wakatamka sauti za heru� kwa pamoja (kuunganisha), wanaweza kusoma maneno ambayo hawayajui. Hivyo, ni kazi yetu kuelewa maneno haya yanamaanisha nini.

Page 25: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

23Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU

Wanafunzi wanahitaji ujuzi imara wa foniki ili kusoma maneno mapya. Hii ndiyo sababu maarifa ya sauti ya heru� mojamoja pamoja na silabi, vyote ni muhimu kwa ajili ya usomaji madhubuti.

Wanafunzi wanaweza pia kutenganisha na kuunganisha maneno pamoja na heru� mwambatano. Heru� mwambatano ni muunganiko wa heru� mbili ambazo kwa pamoja zinaunda sauti moja, na zinaweza kuunganishwa pamoja na irabu ili kuunda silabi (kama vile nyu, chu, shwa, na chwa). Muunganiko huu unaweza kutokea mahali popote katika neno.

Wanafunzi wanaweza kujifunza muunganiko wa konsonanti wakati wakijifunza silabi mpya. Wanaweza pia kuhusianisha muunganiko wa konsonanti wasizozifahamu kwa kutumia maarifa ya sauti za heru� moja moja. Baadhi ya muunganiko wa heru� za konsonanti mbili ni:

ch sh th dh gh ny vy ng mw mb

MAJADILIANO YA KIKUNDI (DAKIKA 5)

1. Maudhui gani umewekea alama ya mshangao (!)?2. Maudhui gani umewekea alama ya kuuliza (?)?3. Maudhui gani umezungushia alama ya mduara?4. Unadhani ni namna gani ujuzi wa kutenganisha na kuunganisha sauti unaweza

kuwasaidia wanafunzi kukuza uwezo wao wa kusoma.

Page 26: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

24 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

ZOEZI

WAAMBIE WALIMU:

“Sasa tutajaribu kuigiza baadhi ya mbinu za kutenganisha na kuunganisha sauti ambazo tulisoma. Kama kuna walau watu watano hapa, mwalimu mmoja atajitolea kuwa mwalimu wa darasa, na tuliobakia tutakuwa wanafunzi. Mtu mmoja ataandika heru� “n”, “j” na “e” kwenye karatasi kuu kuu na ataitumia kama kadi ya heru�. Mwalimu wa darasa ataomba watu watatu wajitolee na mtu wa mwisho atajifanya kuwa “sehemu ya darasa zima.”

Kama tuna watu chini ya 5 hapa, tunaweza kujaribu igizo lilelile pamoja na silabi kama vile “ba” au hatutakuwa na mshiriki atakayejifanya kuwa “darasa zima”.

Baada ya kufanya igizo hili, tunaweza kujaribu tena kwa maneno mengine na mtu mmoja anaweza kujaribu kuwa “mwalimu”.

WAAMBIE WALIMU:

“Tafadhali someni maswali kwa kujitegemea na �kirini kuhusu majibu. Kisha jadilini majibu na mwenzako. Halafu mtashirikisha mawazo yenu kwa kundi zima.”

Wape walimu dakika 10 kujadili na kisha waulize watoe majibu. Kama walimu wanakwama, hapa kuna baadhi ya majibu:

Jibu la 1: Mbinu hii inawasaidia wanafunzi kuunganisha heru� zilizoandikwa na sauti za heru� kwa kuona na kufanya pamoja.

Jibu la 2: Baada ya kufanya mazoezi ya kutenganisha na kuunganisha mara nyingi, andika baadhi ya maneno kwenye ubao na angalia kama wanafunzi wanaweza kuyasoma kwa sauti bila kusaidiwa.

Jibu la 3: Baada ya kubainisha wanafunzi wanaopata shida kuelewa, waweke wawiliwawili na wale wanaoelewa haraka au tenga muda na rudia zoezi mara nyingi zaidi ukiwa na wale wanafunzi wanaoelewa polepole.

Jibu ka 4: Kila unapofundisha maneno mapya darasani, fundisha kwa kutumia mbinu ya kutenganisha na kuunganisha.

Page 27: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

25Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

ZOEZI

IGIZO (DAKIKA 20) Sasa tutajaribu kuigiza baadhi ya mbinu za kutenganisha na kuunganisha sauti ambazo tulijifunza. Kama kuna watu 5 au zaidi katika kipindi chako cha mafunzo kazini (3+ walimu, mwalimu mkuu na mratibu wa mafunzo kazini), mwalimu mmoja ajitolee kuwa darasani kama mwalimu wa darasa na washiriki wengine watajifanya kuwa wanafunzi. Mtu mmoja ataandika heru� “n”, “j”, “e” kwenye vipande vitatu vya karatasi kuu kuu. Kisha mwalimu wa darasa ataomba watu watatu wanaojitolea. Mshiriki wa tano anaweza kujifanya kuwa “sehemu ya darasa zima”

Kama mko chini ya watu 5 katika kipindi chako cha mafunzo kazini, unaweza kujaribu igizo lilelile pamoja na silabi, kama “ba” ikiwa hakuna mshiriki anayejifanya kuwa “darasa”:

1. Mpe kila mwanafunzi kadi ya heru�. Waambie washikilie kadi na kuzinyanyua juu ili darasa zima lione neno “nje”. Usitamke neno na usiwaulize wanafunzi neno hilo ni nini.

2. Nyoosha kidole kwa mwanafunzi anayejitolea na aliyeshikilia heru� “n” na mwambie atembee hatua moja mbele.

3. Uliza darasa heru� hiyo inaundwa na sauti gani? Baada ya sauti sahihi kutamkwa, elekeza darasa litamke /n/ kwa pamoja.

4. Fanya hivi kwa kila heru� kwenye neno.5. Mara sauti za heru� zote zikishatajwa, waambie wanafunzi

washushe kadi za heru� zao na kuzishikilia usawa wa matumbo yao.

6. Kisha elekeza kila mwanafunzi anyanyue kadi ya heru� yake juu wakati wakitamka sauti za heru� zao polepole – mmoja baada ya mwingine: /n/…./j/…./e/

7. Elekeza darasa lirudie, hakikisha wanatamka sauti za heru� polepole : /n/…../j/……/e/

8. Mwisho, simama pembeni ya wanafunzi waliojitolea na elekeza kidole kwenye heru� zao wakati ukitamka neno kwa sauti ya uongeaji wa kawaida: “nje”. Elekeza darasa lirudie. Elekeza darasa lirudie sauti za heru� haraka haraka.

Baada ya kufanya igizo hili, kuwa huru kujaribu tena kwa kutumia neno lingine au mtu mwingine yeyote anaweza kujaribu kuwa “mwalimu”.

FIKIRI - WAWILI WAWILI - SHIRIKISHANA (DAKIKA 10) Ukishamaliza kufanya mazoezi ya mbinu ya kuhusianisha na kuunganisha, jadili maswali haya pamoja na mshiriki kisha kwenye kundi zima:

1. Mbinu hii iliwasaidiaje wanafunzi kutenganisha na kuunganisha maneno mapya?2. Unaweza kuwatambua wanafunzi ambao hawaelewi kutenganisha na kuunganisha?3. Unawezaje kuwasaidia wanafunzi wa aina hiyo wanaohitaji msaada?4. Ni wakati gani utaweza kutumia mbinu ya kutenganisha na kuunganisha katika

masomo yako?

Page 28: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

26 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

KUPANGA MKAKATI

WAAMBIE WALIMU:

“Sasa tutapanga vipindi vyetu vya kusoma na kuandika. Tutasoma maelekezo pamoja na kwa sauti. Baada ya mwalimu wa kwanza kusoma sehemu, anaweza kumuita mwalimu mwingine kwa jina ili asome sehemu inayofuata.”

Page 29: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

27Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

KUPANGA MKAKATI

KUAANDAA KIPINDI CHA “KUSOMA NA KUANDIKA” (DAKIKA 25)Ili kukuza uwezo wa wanafunzi kusoma, ni muhimu sana kwamba aweze kufanya mazoezi juu ya mbinu mpya za kusoma na kuandika alizosoma kutoka kwenye Mafunzo ya Walimu Kazini.

Kurasa zifuatazo zinajumuisha masomo ya jumla yanayoelekeza shughuli ambazo unaweza kujaribu wakati wa kipindi chako cha kusoma na kuandika (au unaweza pia kujaribu wakati wa kipindi chako cha kawaida cha Kiswahili). Pamoja na mwenzako:

1. Soma kwenye mpango wa masomo.2. Jaza nafasi zilizo wazi mahali panapohitaji hivyo.3. Jaribu masomo wakati wa kipindi cha kusoma na kuandika.

HATUA SHUGHULI ZA KUFUNDISHIA

LIZI

1. Kabla ya siku ya masomo, �kiria kuhusu sauti heru� nne au heru� mwambatano ambazo unafundisha (au �kiria kuhusu sauti za heru� ambazo wanafunzi wako wanaweza kuwa wanapata shida kuzielewa. Kwa mfano: /r/, /l/, /s/, /z/ na /mw/, /th/). Kabla ya somo, chora chati iliyoko hapa chini kwenye ubao. Hakikisha mchoro wako ni mkubwa kiasi cha kuwafanya wanafunzi wote wauone vizuri. Upande wa kushoto, andika heru� nne ambazo umechagua. Kwa kufuata mstari

“lo”. Usiandike silabi hizi kwenye ubao, zikumbuke tu. (Hatua ya maandaliza haipo kwenye hatua za somo hivyo iondolewe kwa sababu sio sehemu yake. Hii imejitokeza katika moduli zote.)

UTANGULIZI4. Waambie wanafunzi watacheza kucheza mchezo wa silabi. Kuna silabi tatu za siri kwenye

ubao na lazima watumie maarifa yao ya sauti za heru� kutamka silabi na kujaribu kubainisha zile za siri.

KUTAM-BULISH

MAARIFA MAPYA

5. Waambie wanafunzi waangalie kwenye chati na waoneshe namna ya kuunda silabi kwanza kwa kubainisha sauti za heru� zilizoko kushoto, na kisha unganisha sauti hii na sauti za irabu zilizoko juu. Unaweza kutumia mbinu ya ‘Ninafanya – Tunafanya – Mnafanya’ katika zoezi hili.

6. Anza na ‘Ninatenda’’: Elekeza kidole kwenye “r” na tamka /rrr/ polepole sana. Kisha onesha kidole kwenye “a” na tamka /aaa/ polepole.

7. Endelea na ‘Tunatenda’: Waambie watoto watamke sauti za heru� pamoja na wewe wakati unaonesha kidole kwenye heru� hizo.

8. Maliza na ‘Tunatenda Waambie watoto watamke sauti za heru� wenyewe.9. Kisha, tamka sauti za heru� pamoja kwa kasi ya utamkaji wa kawaida:/ra/. Fanya hivi pamoja

na darasa (‘Tu nafanya’) na elekeza darasa lifanye hivyo peke yake (‘Mnatenda’).

KUIMARI-SHA

10. Waambie wanafunzi kwamba ni lazima wafanye hivyohivyo kwa kila sauti za mwanzo katika heruf za kushoto kwenye chati pamoja na sauti kutoka kwenye irabu zilizoko juu ya chati.

11. Kila wakati mwanafunzi anapotamka silabi mpya, andika silabi hiyo katika kisanduku kinachohusika (angalia mfano wa “zo” kwenye ubao)

12. Kama mwanafunzi akitamka moja ya “silabi za siri”, izungushie na tangaza kwamba hiyo ni silabi ya siri. Andika jina la mwanafunzi kwenye ubao.Endelea hadi chati ikamilike na mwishoni wapongeze wanafunzi watatu ambao walibashiri silabi za siri

MWONGOZO WA SOMO LA KWANZA : Silabi ya SiriHATUA ZA KUFUNDISHA

-a -e -i -o -u

r-

z- zo

l-

mw-

Page 30: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

28 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

KUPANGA MKAKATI

(Zunguka darasani na uliza ikiwa wanafunzi wanahitaji msaada)

Page 31: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

29Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

KUPANGA MKAKATI

HATUA SHUGHULI ZA KUFUNDISHIA

KUFANYA MAZOEZI

13. Mara darasa likishakamilisha chati, cheza mchezo tena lakini kwa kutumia sauti za heru� tofauti zilizoko kushoto kwenye chati.

14. Cheza mchezo huu kwa kutumia sauti za heru� zote 24 za alfabeti na heru� mwambatano zote tofauti.

KUPIMA15. Waambie wanafunzi utatamka baadhi ya silabi kwa sauti na kwamba watapaswa

kuandika silabi hizo kwenye madaftari yao.16. Chagua silabi 5 – 6 kutoka kwenye chati. Tamka ya kwanza na wape wanafunzi muda

kuandika kwenye madaftari yao. Baada ya kusahihisha, weka kumbukumbu ya sauti za heru� ambazo wanafunzi wanapata ugumu kuzielewa. Wafundishe tena sauti za heru� zinazowatatiza kwa kutumia mbinu zilizojadiliwa kwenye moduli ya 6, 7 na 8.

HATUA SHUGHULI ZA KUFUNDISHIA

MAAN-DALIZI

1. Kabla ya siku ya somo, andika orodha ya maneno yenye silabi mbili yanayofahamika na yapatayo 6 -10

2. Kabla ya somo, changanya silabi kutoka kwenye maneno haya na ziandike ubaoni kama inavyoonekana katika kielelezo hiki hapa chini.

UTAN-GULIZI

3. Waambie wanafunzi kwamba watajifunza namna ya kuunda manenona kuchagua baadhi ya silabi mahsusi ambazo watazitumia kuunda maneno haya.

KUTAM-BULISHA MAARIFA

MAPYA

4. Waambie wanafunzi kwamba silabi zilizoko kwenye ubao zinaunganishwa kuunda maneno. Kila neno lina silabi mbili. Wapatie mfano kama vile, ka + ta = kata.

5. Waambie kwamba wanaweza kutumia silabi hizo hizo kuunda maneno kadhaa. Kwa mfano: ka + nga = kanga

6. Wanafunzi wanapaswa kufanya zoezi hili wakiwa wawiliwawili (au kundi dogo ambalo linakaa katika dawati moja) kuunganisha silabi mbili zilizoko kwenye ubao ili kutengeneza neno ambalo wanalijua.

7. Mara wakishakuja na neno, lazima waliandike kwenye madaftari yao.8. Waambie kwamba, ni mashindano ili kuona kundi gani litakuja na maneno mengi ndani

ya dakika 10 (au muda mrefu zaidi, kama ni muhimu).KUIMARI-

SHA9. Baada ya dakika 10 elekeza kila kundi liwasilishe orodha ya maneno ambayo

wameyapata. Andika majina ubaoni.10. Toa pongezi kwa kundi ambalo limekuja na maneno mengi kuliko makundi mengine.

KUFANYA MAZOEZI

11. Rudia mchezo pamoja na hii tofauti iliyowekwa kwenye silabi12. Changanya makundi ili wanafunzi wapate fursa ya kufanya mazoezi na watu wapya.

Kimkakati, weka wanafunzi wenye uwezo mzuri pamoja na wale wanaojifunza polepoleKUPIMA 13. Andika orodha mpya ya silabi kwenye ubao na waambie wanafunzi waje na maneno

mapya mengi kwa kadri wawezavyo kila mmoja kwa kujitengemea. Waambie waandike orodha hiyo katika madaftari yao.

14. Wakati unasahihisha madaftari, weka kumbukumbu ya wale wasioelewa haraka. Au, fundisha tena baadhi ya silabi na/au kutenganisha na kuunganisha silabi.

MWONGOZO WA SOMO LA PILI: Kufananisha silabiHATUA ZA KUFUNDISHA

sa ri zi

mbokaba

nata

pa

nga

du

te

Page 32: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

30 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

UTENGENEZAJI WA ZANA ZA KUFUNDISHIA

WAAMBIE WALIMU:

“Sasa tutaanza sehemu ya utengenezaji vifaa kwenye moduli hii. Tutageuka na kusoma sehemu inayofuata kwa sauti. Baada ya mwalimu wa kwanza kumaliza aya, anaweza kuita jina la mwalimu mwingine ili naye asome aya inayofuatia.”

Page 33: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

31Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

UTENGENEZAJI WA ZANA ZA KUFUNDISHIA

KUTENGENEZA KADI ZA HERUFI (DAKIKA 30)

Kadi za heru� ni nyenzo muhimu katika kufanya mazoezi ya sauti za heru� kwa kutenganisha na kuunganisha. Kadi mng’ao za heru� zinawapatia wanafunzi fursa ya:

• Kufanya mazoezi ya sauti za heru� zilizotengwa• Zinatenganisha maneno au silabi kuwa sauti zilizotenganishwa kwa vielelezo• Zinatenganisha maneno yenye silabi nyingi kwa vielelezo

Leo wewe na mwenzako mtatengeneza seti ya kadi za heru� za kutumia darasani kwako. Kwa nyongeza, utatengeneza kadi za ziada za alama za uandishi (ambazo utazitumia katika moduli zinazofuatia). Utahitaji vifaa vifuatavyo:

VIFAA VYA KADI YA PICHA

√ Viweka alama au mkaa

√ Karatasi ya manila ya A4 (karatasi 10 kwa mtu mmoja) au karatasi laini (karatasi ya daftari la kawaida, karatasi nyeupe au kisanduku cha bodi kadi, n.k.)

√ Karatasi zilizofomekwa (Kama una Kivunge cha Vifaa vya kufundishia cha EQUIP – Tanzania) √ Kalamu za rangi (kama zipo)

HATUA YA 1:Kunja karatasi na kata kadi kwa nje Kama unatumia karatasi ya A4, ikunje iwe nusu kwa upana. Kisha, fungua ukurasa na kata kwa kufuata mstari wa mkunjo. Kama unatumia vifaa laini, kata kadi kubwa kuzidi ukubwa wa mkono wako wote.

HATUA YA 2: Andika heru� ndogo kwa kila kadi Hakikisha kadi iko wima na tumia kiweka alama au mkaa kuandika kwenye heru� ndogo juu ya ¾ ya kila kadi (ili vidole vyako visizuie uonekanaji wa heru� wakati utakaposhikilia au kunyanyua juu. Andika kadi mbili za heru� kwa kila irabu kwa kuwa zinajirudia rudia ndani ya neno moja ( kwa mfano, ‘kata’ au ‘kiti’ Hakikisha unaandika kwa mwandiko wa kuchapisha, siyo wa kuviringisha. Heru� lazima ziwe kubwa na zinazoonekana vizuri ili zionekane bila shida kwa wanafunzi walioko nyuma ya darasa. Angalia hapa chini mfano wa namna ya kuandika heru�.

a b ch d e f

g h i j k l

m n o p r s

t u v w y z

sh th ng ny mw

. , ! ? “ ”

Page 34: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

32 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

UTENGENEZAJI WA ZANA ZA KUFUNDISHIA

WAAMBIE WALIMU:

“Tunaendelea kusoma matini kwa sauti na kwa kupokezana.”

Page 35: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

33Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

UTENGENEZAJI WA ZANA ZA KUFUNDISHIA

HATUA YA 3:Andika heru� mwambatano na alama za uandishi Pia tengeneza kadi sita za heru� ya mwambatano zinazofahamika (ch, sh, th, ng, ny, mw). Hizi ni heru� zilezile ambazo ulitengeneza kwenye moduli ya 7. Pia tengeneza kadi sita za alama za uandishi kwa ajili ya yafuatayo (angalia chati iliyoko hapo juu kama mfano):

1. Kituo kikuu/nukta (.)2. Kituo kidogo/ nukta mkato (,)3. Alama ya mshangao (!)4. Alama ya kuuliza (?)5. Alama 2 za kunukuu: (“) na(“)

HATUA YA 4: Fomeka kadi zako Kama umepata Kivunge cha kufundishia cha EQUIP Tanzania utaona msokoto/mviringo wa utando fomeka wenye kunata. Tafadhali rejea kwenye moduli ya 7 kama unahitaji maelekezo ya namna ya kufomeka kadi zako.

HATUA YA 5: Tumia kadi kufanya mazoezi ya kutenganisha na kuunganisha sauti za heru� kwa darasa zima Baada ya kumaliza, tumia kadi za heru� kufanya mazoezi ya mbinu ambazo ulijifunza na kuziigiza katika moduli ya leo. Kwa mfano, tumia kadi za heru� kufanya hatua za KUFUNDISHA Kutenganisha na Kuunganisha sauti za heru� kwa maneno mapya kama ‘paka’, ‘maji’, ‘tatu’, nk.

UFUATILIAJI Baada ya kumaliza moduli hii, Mratibu Elimu wa Kata, O�sa Elimu wa Wilaya na Mkaguzi wa Wilaya watafuatilia kuona kama unatumia mbinu zilizoko kwenye moduli hii katika darasa lako. Wakati wa ufuatiliaji huu, itakuwa vizuri uweze kuonesha mambo yafuatayo:

a) Elezea dhana ya kutenganisha na kuunganisha na namna inavyosaidia katika kusomab) Onesha kadi za heru� ambazo ulitengeneza wakati wa kipindic) Onesha mbinu utakayotumia pamoja na kadi za heru� kuwasaidia wanafunzi kufanya

mazoezi ya kutenganisha na kuunganishad) Onesha namna ulivyotumia mipango miwili tofauti ya masomo kuwasaidia wanafunzi

kufanya mazoezi ya kutenganisha na kuunganisha.

Page 36: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

34 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

MWISHO

WAAMBIE WALIMU:

“Walimu, tume�ka mwisho wa moduli yetu, tumia dakika kumi kutafakari somo letu la leo. Jaza fomu kurekodi tathmini yako ya moduli. Baada ya kukamilisha chomoa ukurasa huo unipatie. Tafadhali uwe mkweli katika majibu yako kwa sababu yatasaidia kuboresha Mafunzo ya Walimu Kazini ngazi ya shule hapo baadaye.” Kusanya fomu za tathmini zilizokamilishwa na walimu na uwe nazo wakati wa mkutano mwingine katika kundi la kata.

Wakati walimu wanaendelea kujaza fomu za tathmini, tafadhali tafakari kwa ujumla juu ya mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika kipindi cha siku hiyo na jaza visanduku vinavyofuata. Haya utaweza kuyajadili pamoja na Timu ya Wilaya ya Mafunzo Walimu Kazini na Waratibu wengine wa Mafunzo Walimu Kazini wa mkutano unaofuata katika kundi la kata.

MAFANIKO YA JUMLA YA KIPINDI HIKI: CHANGAMOTO ZA JUMLA ZA KIPINDI HIKI:

Shule: ______________________ Wilaya: ___________________ Mkoa:____________________

Tafakuri za Moduli # ________ Mada ya Moduli: _______________________________________

Idadi ya walimu walioshiriki : ________ Mwalimu Mkuu alishiriki : Ndiyo/Hapana

Page 37: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

35Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

MWISHO

MWISHO (DAKIKA 10)

Binafsi jaza fomu ifuatayo kuweka rekodi ya tathmini ya moduli ya leo. Baada ya kukamilisha, chomoa ukurasa huu na umpe Mratibu wako. Tafadhali uwe mkweli kwa vile mrejesho wako utasaidia kuboresha Mafunzo ya Walimu Kazi ngazi ya shule hapo baadaye.

JEDWALI LA KUTATHMINI Alama 0:

Sikubaliani kabisa na usemi huu

Alama 1: Kwa kiasi Sikubaliani

na usemi huu

Alama 2:Nakubaliana kwa kiasi na usemi huu

Alama 3: Nakubaliana Kabisa

na usemi huu

FOMU YA TATHMINI

Shule: ______________________ Wilaya: ___________________ Mkoa:_____________________

Tathmini ya Moduli: ________ Mada ya Moduli: ______________________________________

Idadi ya walimu walioshiriki: ________ Mwalimu Mkuu alishiriki: Ndiyo/Hapana

Mratibu alikuwepo kuwezesha: Ndiyo/Hapana

Soma semi zifuatazo kisha weka alama ya vema katika kisanduku husika kuonesha jibu lako:

0 1 2 3

1. Dhana kuu ya moduli ya leo ilikuwa inaeleweka.

2. Moduli hii ina mikakati mingi mizuri na yenye manufaa ambayo nitaitumia darasani kwangu.

3. Muda uliotumika kukamilisha moduli hii unafaa. Sikuhisi kwamba ni muda mrefu sana.

4. Moduli hii iliibua mjadala wa kufurahisha na tafakuri ya hali ya juu sana.

5. Violezo vya kipindi cha kusoma na kuandika vilisaidia sana. Natarajia vitakuwa rahisi kuvitumia ndani ya darasa langu.

6. Zana tulizotengeneza leo zitakuwa za manufaa sana (kama inahusika).

7. Mratibu amejiandaa kwa kipindi – amesoma vizuri moduli na ameandaa vifaa vyote vya kufundishia.

8. Mratibu anasimamia vizuri majadiliano – anajua jinsi ya kuwafanya watu wajieleze na namna ya kupata majibu.

9. Mratibu anajua namna ya kusimamia makundi – anahakikisha kuwa walimu wanatoa ushirikiano, wanashirikiana na wana hamasika.

10. Mratibu anajua jinsi ya kuwahamasisha walimu – anafuatilia kujua waliokosa vipindi au kuchelewa na kutukumbusha kwanini Mafunzo ya Walimu Kazini ni muhimu kwetu.

Page 38: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu
Page 39: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu
Page 40: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya … · Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo cha Ualimu Morogoro Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chuo Kikuu

Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule