Mwongozo wa kufundisha afya katika shule na jamii … Documents/Integrated...Jumbe za usafi na...

20
Mwongozo wa kufundisha afya katika shule na jamii kupitia wafanyakazi wa afya

Transcript of Mwongozo wa kufundisha afya katika shule na jamii … Documents/Integrated...Jumbe za usafi na...

Page 1: Mwongozo wa kufundisha afya katika shule na jamii … Documents/Integrated...Jumbe za usafi na mazingira bora ina faidi watu kwa maarifa ambayo yata badilisha tabia na kuzuia uambukizaji

Mwongozo wa kufundisha afyakatika shule na jamii kupitia

wafanyakazi wa afya

Page 2: Mwongozo wa kufundisha afya katika shule na jamii … Documents/Integrated...Jumbe za usafi na mazingira bora ina faidi watu kwa maarifa ambayo yata badilisha tabia na kuzuia uambukizaji

Hati zifuatazo zimeandikwa kwa ushirikiano kati ya Partnership for child

Development (PCD) yani Ushirikiano wa Maendeleo ya Mtoto, na Serikali ya

Kenya, Taasisi ya Utafiti ya Kenya ya magonjwa (KEMRI) na International Rescue

Committee, Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na Shirika la

Chakula Duniani (WFP).

Maudhui imeanzishwa kushughulikia changamoto za afya na maarifa, mitazamo na

mazoea ya jamii la Turkana na kambi la Kakuma zinazohusiana na; tabia ya Kula,

viini vya ungojwa na maambukizi, Trachoma, Usafi wa Maji na Mazingira. Taarifa

zilikusanywa kupitia utafiti wa shule za msingi nafasihi ya mapitio ya data sekondari ili

kuhakikisha ujumbe pia kuti maanani umuhimu wa mazingiramaalum na utamaduni.

Picha ni hati miliki ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Watoto(PCD), Imperial College London.

Maelezo [email protected]

Page 3: Mwongozo wa kufundisha afya katika shule na jamii … Documents/Integrated...Jumbe za usafi na mazingira bora ina faidi watu kwa maarifa ambayo yata badilisha tabia na kuzuia uambukizaji

3

Mathumuni ya kijitabu hiki ni kupatia wafanyakazi wa afya wa kambi ya wakimbizi kakuma na

habari kuwasaidia kufundisha na kuwasiliana kuhusu madhara ya kutokula chakula bora

magonjwa yanayo wadhuru siku hizi kambini na maeneo jirani. Kijitabu hiki ni mojawapo ya

maelekezo ya kuchangia kuhusu afya ya jamii pamoja na mazingira bora ya afya, maelezo ya

lishe bora kwa madhumuni ya kuboresha afya ya jamii kambini na maeneo jirani. Kulingana na

habari zilizopatikana baada ya kukadiria mahitaji, kijitabu hiki kinapeana habari muhimu

ambayo wenyeji wanaweza kutumia kujikinga pamoja na familia zao magonjwa pamoja na

vyakula wanavyo tumia kwa lishe bora.

Kitabu hiki kita patiana elimu na hoja pia habari kuhusu uzuiaji wa magonjwa, ulaji wa lishe

bora na wakati wa kutafuta matibabu ya magonjwa yanayo wakabili. Lishe bora ina umuhimu

mkubwa kwa afya ya mama na watoto, inachangia pakubwa ukuaji wa mtoto, ukomavu wa

akili na pia kuzuia uambukizi wa magonjwa. Jumbe za usafi na mazingira bora ina faidi watu

kwa maarifa ambayo yata badilisha tabia na kuzuia uambukizaji wa magonjwa tofauti tofauti.

Mwisho, itachangia kwa habari kuhusu magonjwa na uzuiaji na pia wakati wa kuhitaji

matibabu ambayo itasaidia jamii kushughulikia afya na kuwapa nafasi nzuri kuishi kwenye

mazingira ya afya na maisha mazuri.

Kitangulizi

Page 4: Mwongozo wa kufundisha afya katika shule na jamii … Documents/Integrated...Jumbe za usafi na mazingira bora ina faidi watu kwa maarifa ambayo yata badilisha tabia na kuzuia uambukizaji

4

Kitabu hiki kina ujumbe kwa mambo manne

ambayo yanaweza kusaidia wafanya kazi wa

afya kupeana ujumbe wa afya na lishe bora

kwa wananchi wa kakuma. Kila sehemu

inaelekeza kiini cha habari, ikieleza hali ya

afya na magonjwa na njia mwafaka za

kujizuia pamoja na jamii na familia wasipate

Marathi na pia kusambaza magonjwa.

Sehemu ya mwisho inazungumzia mamboa

yote yanayoweza kusaidia uzuiaji wa

magonjwa katha na Marathi mengineyo.

Kiini cha habari zifuatazo hapa chini zinaweza

kusaidia kujumuisha jamii na kusaidia

uelewaji wa hatari za magonjwa na pia

wanacho takiwa kufanya kujizuia na lishe

isiyo faa.

Ishara na Muundo

Elimu ya lishe – Umuhimu wa lishe bora una zungumziwa kwa ufasaha,

ambapo kula chakula chenye madini yote na vyenye aina tofauti za

vyakula pamoja na kuzidisha madini bora ya afya ya watu Kaunti ya

Turkana.

Kuepuka ugonjwa wa macho – Sehemu hii inzungumzia zaidi ugonjwa

wa macho unaosababishwa na viini ambavyo vinapatikana sana ndani ya

kambi ya Kakuma. Mbinu zinaelezwa jinsi ya kuzuia ugonjwa wa macho

kutumia tahathari – SAFE (upasuaji, madawa, kuosha uso, kuboresha

mazingira).

Malaria – Ni ugonjwa mbaya ambao unsambazwa na mbu. Sehemu hii

inatujuza kuhusu vimelea (vidudu) na kueleza vile vinavyo smbazwa kwa

wanadamu, dalili na jinsi ya kutibu na pia njiwa za kujikinga kuambikizwa

na ugonjwa wa malaria.

Zuia Minyoo! – Sehemu hii inahusika na minyoo ya tumbo, vile

wafanyavyo mwilini, vile zina sambazwa jinsi ya kujizuia kupata minyoo na

la kufanya ukiwa umeambukizwa.

Maji, mazingira na usafio (WASH) – Sehemu hii inazungumzia

umuhimu wa kuosha mikono mara kwa mara na pia uso kuzuia magonjwa

kwa jamii. Inatufunza kitakacho tokes kukiwa hakuna maji, mazingira bora

ama usafi na pia la kufanya kutahathari na la kufanya ukiwa mgonjwa. Ina

sisitiza sana umuhimu wa kutumia choo na kuosha mikono baada ya

kutoka chooni na pia wakati wa kupika chakula.

Ishara:

1.

2.

3.

4.

5.

Page 5: Mwongozo wa kufundisha afya katika shule na jamii … Documents/Integrated...Jumbe za usafi na mazingira bora ina faidi watu kwa maarifa ambayo yata badilisha tabia na kuzuia uambukizaji

Lishe hafifu inatokea wakayi watu hawapati

chakula chenye nguvu, protein, mafuta,

vitamin na madini muhimu kutoka kwa

chakula wanacho kula. Haya madini

yanahitajika kwenye mwili ili kufanikisha,

hasa lishe duni inasababishi motto kutokuwa

inavyo hitajika na huweza pia kusababisha

unyonge na umbilikimo, pia iki tatiza uwezo

wa mtoto kusoma vizuri. Baathi ya lishe duni

zinapotokea (chini ya miaka mitano) ni

vigumu sana kurekebika. Ndio maana kuna

umuhimu wa kutengneza chakula kizuri kwa

jamii na watoto wadogo na pia kuhakikisha

watoto wanakula chakula cha kutosho.

Pamoja na hivyo, hata kama chakula ni kizuri,

kama mtu ana njaa siku yeyote ile ni vigumu

kuzingatia na kufanya mambo magumu, ni

vizuri kila familia kula chakula bora na chenye

madini muhimu.

Vyakula viwe na vitu muhimu kama vile GO,

GROW and GLOW – ‘ G Tatu. Hizi aina tatu

za vyakula vinaelezwa hapa.

Kuendelesha jamii elimu juu ya vyakula

vinavyo faa kula ina changia sana kubadilisha

tabia zao za kubadili tabia zao wale vyakula

vya kujenga miili yao

1. Ni nini lishe bora? Kwanini ni muhimu?

Lishe bora ni chakula chenye anina tatu

za vyakula; chakula cha kujenga mwili,

vyakula vya kupatia mwili nguvu,

vyakula vya kuzuia magonja.

Hizi aina tatu za vyakula vinakumbukwa kama

GO, GROW and GLOW vyakula – ‘ Gs’Tatu.

• Vyakula vya GO vyakula vyenye

kupatiana nguvu (carbohydrates kama

vile nafaka na vyakula kama mihogo, viazi

5

1: Elimu ya lishe

Baraza la kufundisha 1: Vyakula vyenye Afya

Umuhimu wa kula vyakula

vyenye afya: ‘GLOW GROW na

GO’ Ujumbe na aina tofaiti za

vyakula

Tunawezaje kuongeza uzuri

wa chakula chetu?

Uduni wa madini muhimu

Micronutrient deficiencies

Vyakula vilivyo jaza madini

muhimu wa kuvijua.

Ishara:

1.

2.

3.

4.

Page 6: Mwongozo wa kufundisha afya katika shule na jamii … Documents/Integrated...Jumbe za usafi na mazingira bora ina faidi watu kwa maarifa ambayo yata badilisha tabia na kuzuia uambukizaji

6

tamu, karoti na mafuta). Vinatupa nguvu

ya kuendelea na kazi ngumu na kwa mda

mrefu, Tusipokula vyakula vya kuongeza

nguvu mara nyingi tutakuwa na uchovu

na huwezi kufanya shughuli za kila siku.

• Vyakula vya kukua – GROW ni vya

kujenga mwili (kama nyama,

maharagwe and maziwa), Vinatu fanya

kukuwa, omekana na nguvu na wenye

afya. Usipokula vyakula vya kujenga

mwili, watoto wanaweza kuwa na mwili

mdogo sana dhidi ya umri wao.

• Vyakula vya GLOW ni vyakula vya

kukinga mwilivikiwa vime jaa vitamin

na nadini (matunda na mboga za

majani). (Vina saidia kukuza akili

(ubongo) na kufanya mwili kuwa na

nguvu na kukuwa vizuri. Vinatusaidia

kukinga magonjwa na pia husaidia baada

ya kupona ugonjwa. Tusipokula vyakula

vyakuzuia kwa wingi tunaweza kuugua

nmara kwa marana tuta pona pole pole

sana.

2. Tunaweza je kuboresha vyakula vyetu

na vitu tunavyo kula?

Ili kuwa na afya bora na pia kusaidia familia

kuwa na afya jamii wanahimizwa kutengeneza

vyakula vya nyumbani hivi:

• Tengeneza aina tofauti za vyakula kutoka

kwa vikundi vya GO, GROW and GLOW

• Ongeza ukulaji wa vitamin na madini kwa

kula matunda safi, mboga za majani. ma.

Machungwa, matunda ya njano na

mboga za majani mabichi zina lishe bora.

• Lima shamba dogo la mboga pamoja na

matunda ili yaliwe yangali mazuri.

• Himiza mama kunyonyesha watoto wao

hadi miezi sita’ Maziwa ya mama yana

lishe zote mototo ana hitaji ili kukua na

mguvu na pia kuzuia maambukizi ya

magonjwa. Kusitisha unyonyeshaji wa

motto yaweza kusababisha kukua kwa

shida na kusababisha motto apate

magonjwa katha.

• Kula vyakula kama nyama za ngombe,

mbuzi, samaki na kuku ambavyo vina

madini muhimu yanayoweza kuzuia

ukosefu wa damu. Ukiwa huna damu ya

kutosha, kuna kuwa na ukosefu wa hewa

mwilini. Hii husababisha uchovu,

usumbufu, kukosa hewa na huweza

kuzimia.

• Usipike mboga zaidi, hii ina sababisha

madini muhimu kupotea ndanin ya maji

hivyo kuharibu. Pika kidogo tuu ndio

upate madini ya sawa.

3. Kuongeza madini, kwa chakula

Madini ya aina Fulani yana hitajika kwa mwili

kwa asili mia kidogo kidogo. Ukosefu wa hayo

madini husababisha mwili kukosa vitu vya

muhimu na huwa sana kwa watoto. Kwenye

sehemu hii madini muhimu ya afya ya jamii

yana zungumziwa hapa, yanapopatikana, na

muhimu wake kwa mwili, ukosefu na jinsi ya

kuzungumzia kupitia kuongeza madini

kwenye vyakula.

4. Kutambua madini, kazi zinazofanya,

na shida zinazoletwa kwa upungufu

wake.

Madini ndani ya vyakula yana hitajika

mwilini na vitu vilivyo hai kwa maisha

yao yote. Madini hutumika kwa mambo

mengi kwa maish ya wanadamu. Madini

huchangia sehemu nyingi za maisha. Madini

inayo maslahi katika wizara ya afya ni

Vitamin A, Iodine, Zinki na iron. Ukosefu wa

haya madini kwa maisha ya kila siku yana

julikana kama Ukosefu. Ukosefu wa haya

madini husababishwa na:

• Mchanga mahali Fulani una kosa madini

Fulani.

• Vyakula vya jamii Fulani havina madini

muhimu.

• Magonjwa ya aina Fulani yana sababisha

ukosefu wa madini Fulani.

Page 7: Mwongozo wa kufundisha afya katika shule na jamii … Documents/Integrated...Jumbe za usafi na mazingira bora ina faidi watu kwa maarifa ambayo yata badilisha tabia na kuzuia uambukizaji

7

Vitamini A

Madini yaIodini

Madini yachuma

Madini yaZinc

Maziwa, mayai,

maini, mboga za majani

kama vile spinachi,

sukuma wiki na

machungwa, matunda,

karoti, malenge, viazi

tamuna papayu

Chumvi iliyo na iodini,

maziwa ya ngombe na

mayai

Nyama, samaki,

maini, spinachi,

mayai, mboga za

majani

Nyama, kuku, samaki,

maziwa, nafaka na

njugu

• Ni muhimu kwa afya ya macho na kuona

vizuri. Pia inafanya ngozi kuwa nadhifu na

yenye afya. Ina zuia kuhara, ukambe,

utapiamulo.

• Ukosefu a vitamini A husababisha kuto

ona vizuri na pia upofu wa usiku.

• Inasadia mwili katika kupumua na kukua kwa

misuli. Ni muhimu sana kwa kukua na

kuongeza nguvu ya ubongo na neva.

• Iodini hupatikana kwenye vyakula vinavyo

pandwa mchngani wenye hayo madini kwa

wingi. Mchanga usio namadini ya iodine

unapatikana sehemu za milimani.

• Ukosefu wa iodini leads husababisha ugonjwa

wa goita (uvimbe kwenye shingo).

• Inweza kuwa hali mbaya sana hasa kwa

mama wajawazito kusababisha kuzaa

watoto wenye uzani mdogo, uavia mimba na

watoto walemavu.

• Husaidia damu kuwa na afya nzuri. Kama

huli vya kutosha inasababisha ukosefu wa

damu, uchovu, uvuvu, kizunguzungu na

kuumwa na kichwa.

• Husaidi kufanya mwili kuwa na afya na

kuendeleza ukuaji wa mototo na baru baru.

• Ukosefu wa madini ya zinc ina sababisha

kutokua na magonjwa kama vile kuhara.

Baathi ya mathara yanaelezwa hapa:

Ukosefu wa madini yeyote ni vigumu san kutambua. Kuzuia ni kujaribu kula vyakula vyenye

hayo madini na chakula cha muhimu.

Aina ya madini yanapotoka Kazi yake mwilini

Page 8: Mwongozo wa kufundisha afya katika shule na jamii … Documents/Integrated...Jumbe za usafi na mazingira bora ina faidi watu kwa maarifa ambayo yata badilisha tabia na kuzuia uambukizaji

8

5. Mazungumzo juu ya kuongeza madini

kwa chakula

Ili kuzuia ukosefu wa madini kwa jamii,

vyakula Fulani vya weza kuongezewa madini

ambapo vitaminni, na madini vinachanganywa

kuongeza lishe za muhimu.

Waulize jamii kama wanajua hivi vyakula

ambavyo vimeongezwa madini.

6. Kuhakikisha umekula vyakula vilivyo

ongezwa madini muhimu

Serikali ya Kenya imesema kuna aina Fulani

ya vyakula vya vinavyo weza kuongezewa

madini:

• Unga wa ngano – umeongezwa Zinc and

chuma

• Unga wa mahindi – umeongezwa Zinc

and chuma

• Chumvi – imeongezwa Iodini

• Mafuta ya kupikia – yameongezwa

vitamini A

Kanuni: Zungumzia kuhusu ana nyingi

za vyakula ambavyo wako navyo hapo

nyumbani na uliza kama kuna vyakula

vilivyo ongezewa madini ama vyaweza

kuongezewa madini.

Eleza kwamba ni vizuri kununua vyakula ambavyo vimeongezwa madini na vitamin kila wakati

iwezekanavyo ili kuwa na afya nzuri. Pia tuangalie vile vyakula vinavyo fungwa, kama vile

chumvi, sukari, ma futa ili kuwa na afya bora nyumbani.

Eleza vyakula vyote vilivyo ongezwa

madini Kenya vina alama ya kuthihirisha.

Onyesha hiyo alama. Uliza kama

nyumbani wana chakula chenye hiyo alama

Page 9: Mwongozo wa kufundisha afya katika shule na jamii … Documents/Integrated...Jumbe za usafi na mazingira bora ina faidi watu kwa maarifa ambayo yata badilisha tabia na kuzuia uambukizaji

9

Taswira

Trachoma ni ungonjwa unaosabishwa na

vimelea na hatimaye kusababisha upofu na

huambukizwa na mikono michafu, nguo na nzi

ambao hubeba vimelea hivyo. Mapema kabla

ya maambukizi, trachoma huwa haina dalili,

lakinimaambukizi husababisha muwasho,

macho mekundu na kutoa usaa. Dalili zingine

ni kuwashwa kwa macho na kuathiriwa na

mwangaza mkali kwa macho. Vimelea

husambazwa sana na kati ya watoto wadogo

na hatimaye kusababisha upofu wa macho.

Trachomahuathiri jamii maskini, na wanaoshi

katika misongamano na pia wanaoishi bila

maji safi. Jamii zinazoishi maeneo kame na

kavu pia huathirika pakubwa. Uzuiaji wa

maambukizi huhusishwa sana na uoshaji wa

uso (ambao hupunguza uvujaji wa macho

ambayo husababisha maambukizi na pia nzi),

mazingira safi na uwepo wa maji safi

piahupunguza maambukizi.

Upofu wa macho unaweza kuzuiwa, wakati

haswa ubora wa mazingira safi umetiliwa

maanani na jamii zote. Pia unaweza kuzuiwa

kwa kutumia maji safi, kunawa nyuso na

sabuni na pia mikono. Utafiti unaonyesha

kuwa, kupunguza kunya mahali ambapo

hakuna vyoo ni muhimu katika kupunguza

maambukizi haya ya trachoma na

kipindupindu. Mikakati ya WHO ni kuangamiza

ugonjwa wa trachoma hapo mwaka wa 2020

wakitumia mikakati inayofahamika kama

SAFE (Surgery, Antibiotics, Facial cleanliness

and Envirnmental improvement).

Ni muhimu kwa jamii zinazokabiliwa na

maambukizi kufahamu jinsi ya kujikinga

kutokana na maambukizi haya sas na pia kwa

siku zijazo na lipi la kufanya iwapo

wataambukizwa. Ni muhimu pia kuzitia moyo

jamii zilizoathirika kutafuta huduma za

matibabu kwa nja ya madawa ama upasuaji

kabla ya kupofuka macho.

Maudhui

Maelezo yafuatayo yananuiwa kusaidia jamii

na elimu ya kuikinga dhidi ya trachoma.

Sehemu ifuatayo imepeana vipengele muhimu

vya afya kuhusu tabia zitakazosaidia kuzuia

maambukizi hayo.

1. Trachoma ni nini?

Trachoma ni ugonjwa wa maambukizi

ya macho unaosababishwa na uchafu

(vimelea). Hatimaye, husababisha upofu wa

macho kwani husababishakubambuka kwa

kope za macho – kwanza ugonjwa huu ndio

kiini kikuu kinachosababisha upofu ambao

hatimaye unaweza kuzuiwa.

2: SAFE from Trachoma

Trachoma ni nini?

Husambazwaje?

Tutawezaje kusitisha

ugonjwa huu?

Hutibiwa vipi ugonjwa huu?

Vipengele:

1.

2.

3.

4.

Page 10: Mwongozo wa kufundisha afya katika shule na jamii … Documents/Integrated...Jumbe za usafi na mazingira bora ina faidi watu kwa maarifa ambayo yata badilisha tabia na kuzuia uambukizaji

10

2. Trachoma husambazwaje?

Trachoma husababishwa na uchafu na

vimelea, pia trachoma inaeza ambukizwa

kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kupitia

uhusiano wa karibu hususani kwa vitu

vilivyoathirika kutokana na ugonjwa huo.

Trachoma huambukizwa haswa wakati kitu

kimegusa jicho lililoathirika na baadaye

kugusa jicho ambalo halija athirika, kwa

mfano:

• Taweli, vitambaa vya mkono na

karatasi ya chooni

• Vidole

• Nzi

3. Tutawezaje sitisha/komesha

trachoma?

Usambazaji wa Trachoma unaweza

komeshwa kupitia aina tofauti za

utendakazi.Tunafahamu SAFE.

S is for Surgery: Baadhi ya watu

walioambukizwa trachoma kwa muda mrefu

wanaweza fanyiwa upasuaji ili kurekebisha

macho yao.

A is for Antibiotics: Baadhi ya watu

walioambukizwa na vimelea hivyo wapate

madawa ili kuuwa viini hivyo.

F is for Facial cleanliness: Kuweka uso

kuwa msafi ili kuzuia nzi kubeba viini hivyo

kwa macho.

E is for Environmental improvement:

Kwa kuimarisha usafi wa shule na nyumba,

na matumizi ya vyoo, unaeweza punguza

nzi karibu na wewe na hatimaye kupunguza

uwezekano wa kupata viini

vinavyosababisha trachoma.

Upasuaji na madawa yanahitajika kwa visa muhimu, lakini tunaweza kuhusika kwa sasa ili

kuzuia ogonjwa wa trachoma. Kuweka uso na pia uimarishaji wa usafi wa shuleni na nymbani

utaweza kupunguza nafasi za uambukizaji wa trachoma.

Shughuli: Katika kiwango cha boma na pia kila mhusika ama wahusika wa boma, angalia

vitu ama shughuli ambazo zinaweza changia sana katika maambukizi ya trachoma na pia

vitu vinavyoweza kuzuia usambazaji huo.

Baadhi ya vitu hivyo ni: Nyumba safi, jiko. Matumizi ya choo ama ufukiaji wa kinyesi.

Uoshaji wa uso na usaidizi wa watoto wa changa kunawa mikono.

Unapotembea katika kila boma, angalia vitu vizuri na vibaya kwa wanajamii. Elezea athari

zilizoko,(kwa mfano uwepo wa nzi kwa nyuso za watoto) na jinsi ya kuzizuia (mfano kwa

kunawa uso na kuweka mazingara safi).

Page 11: Mwongozo wa kufundisha afya katika shule na jamii … Documents/Integrated...Jumbe za usafi na mazingira bora ina faidi watu kwa maarifa ambayo yata badilisha tabia na kuzuia uambukizaji

11

3: Malaria

Utangulizi

Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na mbu.

Huathiri mamilioni ya watu ulimwenguni

mzima na pia husababisha ugonjwa kwa

watoto na wamama waja wazito. Viini

vyenyewe hutambulikana kama Plasmodium

ambavyo huishi kwa damu. Mbu zilizoathirika

na viini hivyo husababisha ugonjwa huo

kupitia kuuma wakati inapofyonza damu.

Walioambukizwa malaria huwa wagonjwa

sana, wakiwa na homa kali, kuhara, kutapika,

kuumwa na kichwa au kuhisi baridi mwilini.

Huhisi kuchoka kwa sababu ya upungufu wa

damu mwilini kwani viini hivyo vya

plasmodium huzaana na kuongezeka mwilini.

Kwa watoto, na pia wamama waja wazito,

malaria yaweza kuwaathiri zaidi. Tiba ya

haraka ni kumeza tembe za malaria ili

kupunguza ueneaji wa viini hivyo. Watu pia

wanaweza kujikinga kwa kulala ndani ya

vyandarua kwani mbu zinazosababisha

malaria huuma usiku. Matumizi ya vyandarua

ama unyunyiziaji wa dawa kwa manyumba pia

husaidia kuuwa mbu kabla ikuume na

kusababisha madhara.

Maudhui

Agenda zifuatazo zinanuiwa kuhamasisha

jamii kuhusu athari za malaria, utoaji wa

mafunzo ya kujizuia wao na familia zao

kutokana na malaria na kugundua dalili za

malaria ili kutoa matibabu mapema.

1. Malaria ni nini?

Malaria ni ugonjwa unaosababisha kifo.

Hufanya watu kuwa wanyonge na kushindwa

na kufanya kazi ama pia kusoma vizuri, na

husababishwa na mbu. Unaposhikwa na

malaria, mtu huhisi uchovu, homa, kuumwa

na kichwa ama pia kuendesha is a killer

disease. Viini vya malaria hujulikana kama

Plasmodium na vidogo sana zaidi ya mbu.

Vinapokuwa ndani ya mwili, huongezeka na

mwishowe kumaliza chembechembe za damu

hivyo kusababisha ukosefu wa damu mwilini.

2. Huambukizwaje?

Malaria huambukizwa kupitia mbu.

Mbu aina ya Anopheles ndo huhusika sana.

Huishi katika kila nchi ote ulimwenguni

ambapo viwango vya joto ni shwari.

Wakati mwengine inaweza maanisha malaria

ni ugonjwa wa msimu. Huwa wakati wa mvua

pekee. Mbu ya kike huitaji maji kulea mayai.

Ni muhimu basi kupunguza maji

yaliyosimama karibu na nyumba na kufunika

vyombo vya maji karibu na maeneo yenu ili

kupunguza hali hii. Mbu ambayo haijaathirkia

huathirika inapouma mtu aliyeathirika.

3. Nani yuko hatarini?

Kila mtu aliyeumwa na mbu aliyeathirika

yumo hatarni, lakini watoto wachanga na

wamama waliowjswszito wamo hatarini zaidi

na wanaweza kuaga kfuatia ugonjwa huo. Ni

muhimu basi endapo mtu wa jamii yuko na

malaria umsaidie apate matibabu.

Wengine huibuwa kinga sababu ya kukaa na

viini hivyo kwa muda mrefu, hii ndio sababu

watoto na waliokuja karibuni wamo katika

hatari ya kuuguwa na malaria.

4. Hutibiwaje?

Iwapo unashuku ama unajua mtu

aliyeathirika na ugonjwa huu, ni muhimu

kupata usaidizi wa kimatibabu katika kituo

cha afya. Tiba ni kupeana dawa za malaria.

Ikiwa hali hii itasalia kama haijatibiwa,

huenda ikasababisha kifo.

Malaria ni nini?

Huambukizwaje?

Nani yuko hatarini?

Hutibiwaje?

Uzuizi wa dawa za malaria

dhidi ya kinga ni nini?

Tunawezaje kuzuia maambukizi

ya malaria?

Vipengele:

1.

2.

3.

4.

5.

6.

Page 12: Mwongozo wa kufundisha afya katika shule na jamii … Documents/Integrated...Jumbe za usafi na mazingira bora ina faidi watu kwa maarifa ambayo yata badilisha tabia na kuzuia uambukizaji

12

5. Uzuizi wa dawa za malaria dhidi ya

kinga ni nini?

Huu ni ule wakati viini vya malaria, kwa muda

hushindwa kuhisi makali ya dawa na hivyo

kuwa sugu katika kukabiliana na viini hivyo.

Mgonjwa hushindwa kupata afueni hata baada

ya kumeza tembe hizo. Hii ni hatari kwa

sababu matibabu watakayopokea

hayatawasaidia. Tukio hili linatendeka sana

ulimwenguni na sana ni kwa sababu ya dawa

duni ama kutomaliza dawa zote unapopewa

kwa matibabu. Ni muhimu kuhakikisha dawa

ni za kiwango kizuri. Ni muhimu pia

kuhakikisha na anameza kiwango sawa cha

dawa hizo alizopewa mpaka apate nafuu.

Ni muhimu pia kuhakikisha dawa zinazofanya

kazi zafanya!

6. Unaweza kujizuiaje na wengine kupata

malaria?

Kulala chini ya chandarua huzuia mbu kuuma

kwani mbu za malaria huuma usiku. Hii ni

muhimu kwa watoto wachanga katika jamii

na vile vile wamama wajawazito. Ni muhimu

pia kulala chini ya chandarua ikiwa

umeambukizwa malaria kwani huzuia mbu

kutoathirika. Vyandarua vinafaa kufunika

mwenye amelala na kuchomekezwa chini ya

godoro Mashimo ama alama zilizobuniwa kwa

chandarua hicho zafaa kurekebishwa haraka

ili kuzuia mbu. Kuvaa nguo zinazofunika

mkono na miguuwakati wa usiku pia husaidia.

Ni muhimu kuzuia watoto wachanga kwa

kutumia njia hii.

Dawa ya kufukiza ni kemikali inayoweza

kuuwa mbu au kupunguza maisha ya mbu a

hivyo kuuma watu wachache. Vyandarua na

kunyunyuzia vyumba na dawa hizi mwishowe

husaidia kuzuia mbu kutouma. Dawa hizi za

kemikalli zinafaa kunyunyiziwa kila baada ya

miezi 6 hadi mwaka mmoja.

Ikiwa una chandarua cha kudumu. kinafaa

kubadilishwa bssds ys miaka 3.

Mbu aina ya Anopheles hupenda kuishi kwa

maji, ziwa, kidimbwi, na pia mosquitoes like

to breed in water, lakes, ponds and even little

pools of water made in potholes and ditches.

Ikiwezekana hakikisha ya kuwa hakuna maji

yaliyotulia karibu na nyumba.

Shughuli : Uliza mwenye nyumba kama wana vyandarua vya mbu?Uliza

kuonyeshwa. Elezea tofautikati ya LLIN na chandarua kinachostahili kutibiwa kila

baada ya mwaka.

Ikiwa kuna mashimo kwa chandarua elezea sababu ya mashimo hayo na jinsi

yanaweza kurekebishwa.

Onyesha njia nzuri na mwafaka ya kulala kwa chandarua hicho. (completely covered

and with the edges of the net tucked into the mattress).

Uliza mwenye nyumba walichokuwa wakifanya kwa kitanda usiku uliopita? Elezea

umuhimu wa kujifunika usiku, kuwa kwa nyumba na kuzuia kuumwa na mbu wakati

wa msimu.

Page 13: Mwongozo wa kufundisha afya katika shule na jamii … Documents/Integrated...Jumbe za usafi na mazingira bora ina faidi watu kwa maarifa ambayo yata badilisha tabia na kuzuia uambukizaji

Taswira

Soil-transmitted helminths (STH) ni minyoo

ambazo huishi kwa tumbo na husambazwa

kupitia mchanga, mikono, na wakati

mwenginekupitia kwa chakula ambacho

hakijapikwa vizuri ama kusafishwa vizuri na

huwa na mayai ya Minyoo. Maambukizi

husababisha uchovu, kuumwa na tumbo na

kufura kitambi. Baada ya muda Minyoo hizo

huchangia kutohudhuria shule na matokeo

duni na pia kiwango cha chini cha lishe kwa

ukuaji na maendeleo. Kwa watu wazima, kuna

shida ukuaji na uwezo wa kufanya kazi na

kubidika katika utendaji majukumu ya siku

kwa siku kwani Minyoo huishi kwa tumbo na

hula chakula kilichonuiwa hivyo basi kudorora

kiafya na kutokuwa vyema.

Maudhui

Zifuatazo ni ajenda za mafunzo kwa lengo la

kuwafahamisha wanachama wa jumuiya

hatari ya maambukizi ya vimelea minyoo, na

njia ambazo wanaweza kujilinda na kulinda

familia kupitia tabia ya usafi na jinsi ya

kuvunja mzunguko wa kuambukizwa. Lengo

la ujumbe wa afya ni muhimu kusaidia

kuzingatia kuwa natabia ya usafi.

1. Minyoo ni nini?

Elezea wanajamii kwamaba Minyoo huishi

kwa tumbo na kuzuia chakula na madini

kufika katika sehemu zinazostahili za miili

ya watot. Maambukizi na Minyoo

huwafanya kuchoka, kuumwa na tumbo na

kuwafanya kuhisi wanyonge. Kwa watoto.

maambukizi huzuia ukuaji na pia

huzuia kutohudhuria shule na hatimaye

kupata matokeo duni. Kwa watu wazima,

na pia watoto, mambukizi husababisha

ugumu wa kufanya kazi vyema za siku

baada ya siku. Kuna aina tatu ya

maambukizi ya STH: hookworm,

roundworm, and whipworm.

13

4: ZUIA minyoo!

Minyoo ni nini?

Huambukizwaje?

Tunawezaje kusitisha tatizo

hili la minyoo?

Maana ya Echinococcus jinnsi

ya kuizuia

Vipengele:

1.

2.

3.

4.

Page 14: Mwongozo wa kufundisha afya katika shule na jamii … Documents/Integrated...Jumbe za usafi na mazingira bora ina faidi watu kwa maarifa ambayo yata badilisha tabia na kuzuia uambukizaji

14

2. Huambukizwaje?

Elezea kwamba Minyoo hutaga mayai

ambayo hutoka kwa tumbo kupitia kinnyesi

na kuambukiza watu wengine kupitia ngozi,

chakula na mikono ambayo haikusafishwa

vizuri baada ya kugusa mayai yaliyo kwa

kinyesi.

Mayai ya Hookworm huanguliwa kwa kinyesi

na kutmbea mahali mtu alitupa kinyesi kupitia

kwa miguu.

Mayai ya Roundworm na whipworm huganda

kwa mikono na chakula kutoka nje. Kula

kutumia mikono chafu ama kuweka mikono

michafu husababisha maambukizi.

3. Tunawezaje kusitisha tatizo hili la

minyoo?

Minyoo zinaweza kuzuiwa kwa njia tofauti:

1. Kutumia choo kila mara

2. Kunawa mikono baada ya kutumia

choo, kuosha motto na baada ya kula.

3. Kuvaa viatu.

4. Kupokea matibabu ya Minyoo mara

moja kila mwaka.

Elezea kuwa utumizi wa choo huzuia watu

wengine kukanyaga kinyes na hatimaye

kuambukizwa hookworm, na pia hueka

kinyesi mbali na watu wengine na mikono.

Mayai ya wadudu wengine hukaa kwa muda

mrefu katika mazingira, hii inamaanisha

yanaweza kuchukuliwa kwa urahisi bila

ufahamu wa kujua umegusa kinyesi

Eleza umuhimu wa kunawa mikono:kunawa

mikono na sabuni baada ya kuenda choo

huangua mayai ya wadudu hawa endapo

yataganda kwa mikono na hivyo kuifanya

mikono kuwa salama kucheza na marafiki

ama kula. Minyoo yengine huishi kwa

mchanga, kwa hivyo ni vizuri kunawa mikono

baada ya kucheza na mchanga ama kutoka

shambani.

Kuvaa viatu pia huzuia maambukizi ya

hookworm ambazo huishi kwa mchangana

karibu na nyumba pia. Zinaweza kuganda

kwa ngozi na kutambaa ndani, kabla ziingie

kwa tumbo.

Kupokea matibabu mara moja kila mwaka

huangamiza minyookatika mwili na hatimaye

kupunguza idadi ya Minyoo. Madawa haya ni

salama na unahitaji tu tembe moja! Tembelea

kituo chako cha afya upate matibabu.

4. Echinococcus na jinsi ya kuizuia

Echinococcus ni aina nyingine ya Minyoo

ambayo kwa kawaida haishi kwa binadamu,

bali huishi kwa mbwa na ng’ombe, kondoo na

mbuzi pia huwa na Minyoo hizi. Kwa kawaida,

njia ya maambukizi huwa ni kati ya mbwa na

wanyama wanaofugwa, wakiambukiza kupitia

nyama ya ng’ombe ama mbuzi (kupitia kwa

mbwa) na kutokakwa kinyesi cha mbwa

ikirudi kwa ng’ombe. Wakati mwengine, watu

huambukizwa kwa kula kinyesi cha mbwa ka

bahati mbaya na hatimaye kusababisha

ugonjwa wa hydatid. Hii hutokea kutokana na

uchafu, mikono michafu ama kunywa maji

kutoka kwa kidimbwi kilichowachwa wazi.

Ugonjwa huu ni vigumu kupata matibabu kwa

hiyo ni vyema mtu kujikinga kwa mara ya

kwanza. Njia za kuzuia maambukizi haya ni

kama ifuatavyo:

• Kunawa mikono kabla ya kugusa chakula

kila mara

• Kutibu maji yaliyochotwa kutokakwa

kidimbwi kilichowachwa wazi kabla ya

kunywa.

Page 15: Mwongozo wa kufundisha afya katika shule na jamii … Documents/Integrated...Jumbe za usafi na mazingira bora ina faidi watu kwa maarifa ambayo yata badilisha tabia na kuzuia uambukizaji

Taswira

Uhaba wa maji na usafi duni wa kiafya yote

haya yamesababisha maambukizi kupitia

uchafu kama vile kinyesi. WASH yaani Water,

Sanitation and Hygiene ni muhimu katika

kuzuia magonjwa kwa hali kama vile

kuharisha trachoma na maambukizi ya

wadudu. Kwa muktasari, maji safi huzuia

usambazaji wa magonjwa yanayohusiana na

maji kama vile kuharisha na kipindupindu.

Kuharisha ni baadhi ya magonjwa matatu

ambayo husababisha vifo kwa watoto.

Vile vile, usafi wa maji huzuia usambazaji wa

magonjwa kama vile trachoma na magonjwa

mengine yanayosababishwa na wadudu.

Maambukizi ya

magonjwa haya

yanaweza kutokea

kupitia hali duni za

kiafya kwa sababu ya

uhaba wa maji safi ya

kuosha.

Mbinu za usafi, kama vile kuongeza

matumizi ya vyoo inaweza kusaidia kuweka

kinyesi na vitu vingine vinavyosababisha

maambukizi mbali na watu na hivyo kuzuia

nzi kuzaa. Kinyesi kwa mara nyingi huweka

mayai ya wadudu na pia uchafu. Hookworm

kwa mfano hupatikana kwa kinyesi na

inaweza kusambazwa kupitia kutembea kwa

kinyesi na kutonawa mikono kabla ya kula na

kutayarisha chakula.

Mabadiliko kuhusu

huduma za WASH ni

lazima ziambatane na

mabadiliko ya

mapendekezo kuhusu

afya, ambayo ndo

maana elimu ya afya na

habari ni muhimu.

Unawaji wa kawaida wa mikono baada ya

kutumia choo na kabla ya kutayarisha chakula

unaweza kupuguza mizigo mingi ya

magonjwa na athari zake.

Maudhui

Agenda za mafunzo zifuatazo zimelenga

kuhamasisha wahusika wa jamii kuhus njia

ambazo wanaweza kujikinga wao pamoja na

jamii zao kutokana na vimelea na viini

vinavyosababisha maambukizi. Kiini kikuu cha

ujumbe wa afya ni vipi maambukizi ya

vimelea na viini vinaweza kuafikiwa kupitia

uoshaji wa mikono, matumizi ya vyoo safi na

uvaaji wa viatu.

1. Kwa nini uwekaji wa mikono na nyuso

ni muhimu?

Magonjwa mengi husababishwa na uchafu

ama viini ambavyo husambaa kupitia kwa

mikono michafu na mazingira machafu.

Magonjwa haya ni Minyoo, trachoma na

kipindupindu.

Elezea jamii na wenye nyumbas: Viini vingi

huwa kwa kinyesi na inaweza kukupea

ugonjwa iwapo utakula ama kunywa kwa

bahati mbaya. Huwa ni vidogo mno, kwa hiyo

hatuwezi kuviona na ni muhimu mtu kuwa

muangalifu.

Kwa nini uwekaji safi wa

mikono na nyuso ni muhimu?

Kuharisha ni nini na ni vipi

inaweza kutibiwa?

Ni vipi tunaweza kudumisha

usafi wa mikono nyuso?

Wakati muhimu wa

kutekeleza uoashaji a mikono

Jua lini na vile utaweza

kutibu maji kabla ya kunywa.

Vipengele:

1.

2.

3.

4.

5.

15

5: Maji na Usafi wa Mazingira and wa mwili

Page 16: Mwongozo wa kufundisha afya katika shule na jamii … Documents/Integrated...Jumbe za usafi na mazingira bora ina faidi watu kwa maarifa ambayo yata badilisha tabia na kuzuia uambukizaji

16

Viini i vinaweza kukusababisha ukawa

mgonjwa na kufanya tumbo kuwa na shida na

hatimaye kuharisha. Viini hivi ni vimelea na

Minyoo ambavyo ni vidogo mno. Huanza

kidogokwa kimo na hatimaye kukuwa kwa

urefu wa zaidi 35cm

E lezea jamii kwa vile viini viko kwa mchanga

ni muhimu kuepuka yafuatayo:

• Matumizi ya choo kumaanisha watu

hawatagusa kinyesi

• Kunawa mikono kumaanisha hutashika

viini au hata kula na mikono chafu.

• Kuweka choo kuwa kisafi kumaanisha

hutabeba uchafu unapoenda choo

• Kutoenda choo ama kunya karibu na maji

husambaza viini kupitia kwa maji.

• Kuvaa viatu.

Hatua hizi pia ni muhimu kwa kuzuia

trachoma: kujiweka msafi na nyumba yako

na shule itaondoa nzi ambazo husababisha

kuenea kwa trachoma.

2. Kuharisha ni nini na ni vipi kunaweza

kutibiwa?

Uliza mwenye jamii jinsi anavyoeza kuelezea

ya kwamba kuna kuharisha ?

Eleza kwamba: DKuharisha hutokana na

kula chakula ama maji machafuyaliyo na viini

hivyo. Kunaweza sababishwa na kutumia

mikono chafu.

Dalili za kuendesha ni kama kunya damu,

ama kutoa choo laini kwa siku kwa muda wa

siku tatu.

Husababisha kuishiwa na maji mwilini. Watoto

wachanga wanaweza poteza uhai sababu ya

kuishiwa na maji mwilini.

Lipi la kufanya ikiwa kuna mtu katika jamii

ambaye anaharisha?

Eleza kwamba: Ni muhimu kuhakikisha

kwamba mgonjwa anakunywa maji mengi na

kula chakula kilicho na madini ili kustiri

upotevu wa maji mwilini. Kwa

kawaidakikombe kimoja (250ml) cha maji

kwa kila kipindi.

Oral Rehydration Therapy pia husaidia na

endapo atakuwa mgonjwa sana, ORS pia

husaidi mwili.

Eleza njia ya kutengeza ORS nyumbani

ukitumia yafuatayo:

• Vijiko 6 vya sukari.

• Kijiko ½ teaspoon chumvi.

• Litre moja ya maji masafi yaliyotibiwa.

Elezea pia ni muhimu kuhakikisha ya kwamba

vipimo ni kamili.

Page 17: Mwongozo wa kufundisha afya katika shule na jamii … Documents/Integrated...Jumbe za usafi na mazingira bora ina faidi watu kwa maarifa ambayo yata badilisha tabia na kuzuia uambukizaji

17

3. Jinsi ya kuweka uso na mikono yako

kuwa safi

Eleza jinsi ya kunawa mikonos:

1. Loa mikono yako na maji safi

2. Weka sabuni kwa mikono yote

3. Sunza mikono ukitumia maji safi

Ikiwa sabuni haipo, tumia jivu Kunawa uso

fanya hivyo pia.

4. Ni wakati gani unafaa kunawa mikono

na uso?

• Wahusika wote wa jamii wanapaswa

kunawa nyuso zao kila siku kupunguza

athari za kupta trachoma.

• Unafaa kunawa mikono na sabuni ama

jivu baada ya kuenda chooni ili kupunguza

viini.

• Unafaa kunawa mikono kabala ya kula

chakula ama kutayarisha chakula kuzuia

maambukizi.

• Mikono inafaa kusafishwa baada ya

kubadiliisha mtoto.

• Mikono inafaa kusafishwa kabla ya

kunyonyesha.

5. Kunywa maji masafi

Maji yaliyochotwa kutoka kwa mto ama

kidimbwi kilichowazi yanafaa kutibiwa kabla

ya matumizi ili kupunguza viini na uchafu na

hatimaye kuifanya kuwa salama. Kwa mfano:

• Kuchemsha maji: maji yanafaa kuwa

yakichemka kwa muda wa dakika 10.

• Kutibu na aquatabs, PUR.

• Kutumia chlorine: 1/8 yakijiko kidogo

cha unga huo kwa lita 10 za maji. Unga

huo unafaa kuwa mkavu na kuhifadhiwa

kwa mkebe uliofunikwa. Maji na Chlorine

yanafaa yatulie kwa muda wa dakika 30.

• Kuua vini vya ungojwa vilivyomo

ndani ya maji kwa kutumia nguvu za

miali ya jua: Jua hua na miyale ambayo

pia huaribu viini vinavyosababisha

maradhi. Acha maji yatulie kwa chupa

kwa muda masaa matano.

Page 18: Mwongozo wa kufundisha afya katika shule na jamii … Documents/Integrated...Jumbe za usafi na mazingira bora ina faidi watu kwa maarifa ambayo yata badilisha tabia na kuzuia uambukizaji

18

Maelezo

Page 19: Mwongozo wa kufundisha afya katika shule na jamii … Documents/Integrated...Jumbe za usafi na mazingira bora ina faidi watu kwa maarifa ambayo yata badilisha tabia na kuzuia uambukizaji

Maelezo

19

Page 20: Mwongozo wa kufundisha afya katika shule na jamii … Documents/Integrated...Jumbe za usafi na mazingira bora ina faidi watu kwa maarifa ambayo yata badilisha tabia na kuzuia uambukizaji

Partnership for Child Development

Imperial College London

School of Public Health

Norfolk Place

London

W2 1PG

www.schoolsandhealth.org

@schoolshealth