MWONGOZO ELEKEZI - BRAC€¦ · huru kuwasiliana nasi kwa njia ya barua pepe ifuatayo LEADtzf@gmail...

12
MFUKO WAS UWEKEZAJI WA MRADI WA LEAD MWONGOZO ELEKEZI

Transcript of MWONGOZO ELEKEZI - BRAC€¦ · huru kuwasiliana nasi kwa njia ya barua pepe ifuatayo LEADtzf@gmail...

Page 1: MWONGOZO ELEKEZI - BRAC€¦ · huru kuwasiliana nasi kwa njia ya barua pepe ifuatayo LEADtzf@gmail .com au tembelea ofisi ya tawi lililo karibu nawe. Kumbuka mfanyakazi wa BRAC hawezi

MFUKO WAS UWEKEZAJI WA MRADI

WA LEAD

MWONGOZO

ELEKEZI

Page 2: MWONGOZO ELEKEZI - BRAC€¦ · huru kuwasiliana nasi kwa njia ya barua pepe ifuatayo LEADtzf@gmail .com au tembelea ofisi ya tawi lililo karibu nawe. Kumbuka mfanyakazi wa BRAC hawezi

BRAC MAENDELEO TANZANIA Mfuko wa Uwekezaji wa Mradi wa LEAD Mwongozo Elekezi – Awamu ya Pili Kurasa Na 1 hadi 11

YALIYOMO

1. Mfuko wa Uwekezaji wa Mradi wa Kuwezesha Kimaisha kupitia 2

Maendeleo ya Kilimo na Mifugo (LEAD)

2. Hatua za Maombi za mfuko wa uwekezaji wa mradi wa LEAD 2

2.1 Hatua Nne: Kupitia, Kuchambua, Uchaguzi, na Kupewa mkopo 2

2.2 Kuzipata fomu na kutuma maombi yako na nyaraka ambatanishi 3

3.Vigezo vya kukidhi kupata mkopo wa Mfuko wa uwekezaji wa mradi 5

wa LEAD

4. Fomu ya maombi 5

4.1 SEHEMU A: Kampuni Yako 5

4.2 SEHEMU B: Mradi wa Biashara yako 7

4.3 SEHEMU C: Taarifa za kifedha 9

4.4 SEHEMU D: Nyaraka Ambatanishi 11

Page 3: MWONGOZO ELEKEZI - BRAC€¦ · huru kuwasiliana nasi kwa njia ya barua pepe ifuatayo LEADtzf@gmail .com au tembelea ofisi ya tawi lililo karibu nawe. Kumbuka mfanyakazi wa BRAC hawezi

BRAC MAENDELEO TANZANIA Mfuko wa Uwekezaji wa Mradi wa LEAD Mwongozo Elekezi – Awamu ya Pili Kurasa Na 2 hadi 11

1. Mfuko wa Uwekezaji wa Mradi wa Kuwezesha Kimaisha kupitia Maendeleo ya Kilimo na Mifugo (LEAD) BRAC Maendeleo Tanzania kupitia mradi wa Kuwezesha Kimaisha kupitia

Maendeleo ya Kilimo na Mifugo (LEAD) imeanzisha Mfuko wa uwekezaji ambao ni

fedha maalumu kwa ajili ya kuwekeza kwenye mnyororo wa thamani wa kuku na

mahindi nchini Tanzania. Fedha hizi zimegawanywa katika sehemu kuu mbili

ambazo ni ruzuku (40%) na mkopo(60%)

Mjasiriliamali anaweza kuomba mtaji kati kuanzia dollah za Kimarekani 5,000

hadi 30,000 ambazo ni kama Shillingi za kitanzania kuanzia 8,000,000 hadi

50,000,000. Ifahamike kuwa kiasi kinachoombwa kisizidi asilimia hamsini ya

thamani ya uwekezaji wa biashara yako (jumuisha mali na thamani ya biashara).

2. Hatua za maombi ya mfuko wa uwekezaji wa Mradi wa LEAD

2.1 Hatua nne zinazofuatwa wakati wa maombi ya mkopo ni Kupitia, Kuchambua, kuchagua, na Kutoa mkopo

Mfuko wa uwekezaji wa mradi wa LEAD ni chombo cha kuelekeza na kutoa mkopo kwa

utaratibu mzuri na usawa Makampuni mbalimbali yanakaribishwa kutuma maombi yao

ambayo yanaonyesha mawazo na mipango ya biashara mizuri .ili kuweza kufanikiwa

kupata mkopo Kanuni zimewekwa na kutangazwa, ikijumuisha sifa za kupata mkopo,

hatua za kuchagua, na namna ya kutathmini maombi yaliyotumwa . Bodi ya pamoja

inayohusisha watu tofauti iitwayo Kamati Maalumu ya Ushauri wa Kiufundi (Technical

Advisory Committee) – inayojumuisha 1) mwajiliwa mmoja wa BRAC Maendeleo

Tanzania, 2) Mjasiliamali na mwekezaji wa kujitegemea mwenye uzoefu kutoka eneo

husika la utekelezaji, na 3) mwangalizi kutoka nje – atasimamia mchakato na kutoa

maamuzi kwa uwazi kuwa nani atapata mkopo ,ili kuondoa mwingiliano wa kimaslahi. Lengo ni kutoa mkopo kwa makampuni ambayo yana uhitaji na watatumia kwa ufanisi ili

kutambua Nyanja pana za kupunguza umaskini na kuwawezesha maskini; na kufanya

yote haya kwa uwazi. Katika sera kwa ujumla ya lengo la mfuko wa uwekezaji wa mradi

wa LEAD ni kutangaza mawazo mapya ambayo yatachochea kukua kwa uchumi wa

vijijini nchini Tanzania, kuboresha kipato cha kaya na kutengeneza fursa mpya katika

kuleta mabadiliko endelevu kwenye soko ambayo yatawasadia.

Mfuko wa uwekezaji wa mradi wa LEAD upo wazi kwa makampuni binafi

yanayojiendesha kifaidana yamefikia kiwango fulani cha ukuaji lakini hawana

uwezo wa kupata mikopo kutoka kwenye taasisi za kifedha. Mfuko huu ni

mahsusi kwa mnyororo wa thamani wa mahindi na kuku.

Page 4: MWONGOZO ELEKEZI - BRAC€¦ · huru kuwasiliana nasi kwa njia ya barua pepe ifuatayo LEADtzf@gmail .com au tembelea ofisi ya tawi lililo karibu nawe. Kumbuka mfanyakazi wa BRAC hawezi

BRAC MAENDELEO TANZANIA Mfuko wa Uwekezaji wa Mradi wa LEAD Mwongozo Elekezi – Awamu ya Pili Kurasa Na 3 hadi 11

Hatua nne (4) za mfuko wa uwekezaj ni kama ifuatavyo;-

Kupitia Maombi

Kuchambu

a

Kuchagua

Kutoa

• Awali maombi yanafanyiwa upembuzi ili kuhakikisha waombaji wanakidhi vigezo • Uchambuzi wa kiushindani kwa waombaji waliobaki wenye vigezo utafanywa na kamati ya

uthibitishaji kwenye ngazi ya kitaifa

• Waombaji waliopata alama za juu watafanyiwa tathmini na kutembelewa na wafanyakazi

wa BRAC Maendeleo Tanzania waliopo karibu nae, ambao watajiridhisha kwa kuona

eneo analo fanyia biashara na kumfanyia tathmini ya kampuni na taarifa za kifedha. • Waombaji bora kutoka ngazi ya kitaifa hadi ngazi ya chini maombi yao

yakishapitiwa na kufanyiwa tathmini yatapelekwa kwa kamati kuu ya ushauri

na ufundi ili kuwachagua washindi. • Kupitisha ruzuku na mkopo • Kutoa mkopo kwa waombaji waliochaguliwa. • Kumb. Waombaji ambao hawajafanikiwa kuchaguliwa watajulishwa kwa maelezo

sababu kuu ambazo zimesababisha maombi yao yakataliwe. 2.2 Upatikanaji wa fomu za maombi, utumaji pamoja na nyaraka za kuambatanisha. Upatikanaji wa fomu za maombi

Fomu za maombi zinapatikana kwenye tovuti yetu ambayo ni tanzania.brac.net (maombi

kwa njia ya mtandao yanahimizwa) au kutoka katika tawi la BRAC Maendeleo Tanzania

lililo karibu nawe. Mara baada ya kujaza maombi yako na kuwa na nyaraka za

kuambatanisha tutumie maombi hayo kabla ya tarehe ya ukomo ya kupokea maombi.

Ujazaji wa fomu

Kuweza kujaza fomu za maombi rejea mwongozo elekezi uliotolewa. Mwongozo

elekezi una taarifa muhimu kuhusu aina ya taarifa tunazozi hitaji katika kufanyia

tathmini maombi yako. Kama una maswali au wasiwasi wowote unapojaza fomu yako, tafadhari kuwa

huru kuwasiliana nasi kwa njia ya barua pepe ifuatayo LEADtzf@gmail .com au

tembelea ofisi ya tawi lililo karibu nawe. Kumbuka mfanyakazi wa BRAC hawezi na

hapaswi kujaza/kukujazia fomu ya maombi lakini atakupatia maelekezo na

mwongozo namna ya kujaza pia kukupatia majibu ya maswali yako. Kutuma maombi na Nyaraka Ambatanishi

˃ Kutuma kwa njia ya mtandao, tafadhari tuma maombi na nyaraka za

kuambatanisha kwenye barua pepe hii [email protected]. Tafadhari andika

neno MFUKO WA UWEKEZAJI WA MRADI WA LEAD kama kichwa cha habari.

Page 5: MWONGOZO ELEKEZI - BRAC€¦ · huru kuwasiliana nasi kwa njia ya barua pepe ifuatayo LEADtzf@gmail .com au tembelea ofisi ya tawi lililo karibu nawe. Kumbuka mfanyakazi wa BRAC hawezi

BRAC MAENDELEO TANZANIA Mfuko wa Uwekezaji wa Mradi wa LEAD Mwongozo Elekezi – Awamu ya Pili Kurasa Na 4 hadi 11

Mwisho wa kupokea maombi yako na nyaraka za kuambatanisha ni tarehe 13 Mei,

2015 saa 9 mchana muda wa Afrika Mashariki. Maombi yote yatakayotumwa

baada ya tarehe na mudauliotajwa hapo juu hayatapokelewa.

˃ Kupeleka maombi katika ofisi za BRAC, peleka maombi yako na nyaraka zote

ambatanishi kwenye ofisi ya tawi la BRAC lililo karibu nawe, ambapo tarehe ya

mwisho ni 13 Mei, 2015 saa 9 mchana muda wa Afrika Mashariki. Maombi yote

yatakayopelekwa baada ya tarehe na muda uliotajwa hapo juu hayatapokelewa.

Yafuatayo ni matawi ya ofisi za BRAC Mikoani.

Mkoa/Wilaya Ofisi ya Tawi Arusha Ngaramtoni na Kimandolu

Dar es Salaam Gongo la mboto na Tegeta

Dodoma Ipagala, Miyuji, Kikuyu na Kondoa Kilimanjaro Pasua, Himo, Mwika, Mkuu, Tarakea, Machame,

Masama na Sanyajuu

Iringa Kihesa, Ruaha na Mafinga

Manyara Babati, Galapo, Katesh

Mara Bunda, Tarime na Kamunyonge

Mbeya Mbalizi na Nzovwe

Morogoro Msamvu na Kilosa

Mwanza Nyegezi na Kirumba

Shinyanga Kahama

Singida Manyoni Tabora Ipuli na Kanyenye

Tanga Korogwe, Pongwe na Nguvumali

Zanzibar Darajabovu na Bububu

Mfuko wa uwekezaji wa mradi wa LEAD utakujulisha kupokea maombi yako kwa

kukutumia barua pepe au kukupigia kwenye namba ya simu ambayo/ambazo

utakuwa umeijaza/umezijaza kwenye fomu ya maombi.

Timu ya mfuko wa uwekezaji wa mradi wa LEAD itawasiliana nawe ili kukupatia

maelezo ya ziada, hivyo hakikisha barua pepe na namba za simu unazotoa ni sahihi

ili tuweze kukupata.

3. Vigezo stahiki vya mfuko wa uwekezaji wa mradi wa LEAD kuna wigo mpana zaidi kwa wajasiliamali binafsi ambao wamejikita katika biashara

kwenye sekta ndogo ya mahindi na kuku kwani wanakidhi vigezo vya kutuma maombi . Hii

inajumuisha;- wazalishaji na wauzaji wa pembejeo, wasafirishaji, wasindikaji na wamiliki

wa mashine. Makampuni ambayo yanasisitizwa ni yale yanayotaka kuanzisha au kuongeza

uzalishaji na uzambazaji wa vifarangaau chakula cha kuku; pia wazalishaji, watengenezaji

na wasambazaji wa pembejeo za kilimo na mifugo kama: mbegu, mbolea,

Page 6: MWONGOZO ELEKEZI - BRAC€¦ · huru kuwasiliana nasi kwa njia ya barua pepe ifuatayo LEADtzf@gmail .com au tembelea ofisi ya tawi lililo karibu nawe. Kumbuka mfanyakazi wa BRAC hawezi

BRAC MAENDELEO TANZANIA Mfuko wa Uwekezaji wa Mradi wa LEAD Mwongozo Elekezi – Awamu ya Pili Kurasa Na 5 hadi 11

viuatilifu, zana na vifaa, wasindikaji , wafanyabiashara, na sekta binafsi zinazotoa

huduma kama wauzaji pembejeo za kilimo na mifugo, wasindikaji wa mayai na

nyama, watoa huduma za kuhifadhia (maghala) na wasafirishaji. Pia tunahimiza

sana kwa yeyote mwenye wazo la kibunifu na ambalo linafaa katika mradi

hususani katika mnyororo wa thamani wa mahindi na kuku.

Watakao stahili kupata mkopo, ni wale ambao mawazo yao ya biashara yana

matokeo chanya kwa jamii ya wakulima maskini waliopo vijijini hapa Tanzania.

kwani wataongeza ubora na upatikanaji wa huduma bora, pembejeo, kununua

mazao kwa bei nzuri au kuwapatia uhakika wa masoko.

Maombi yako kufanyiwa kazi unapaswa kutimiza vigezo vifuatavyo:

Ni kwa ajili ya makampuni na sekta binafsi zinazojiendesha kifaida (makampuni

binafsi yanayojiendesha kifaida Ubia na kampuni nyingine , au biashara za watu

binafsi ). Mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali hayastahili kuomba.

Makampuni kutoka eneo lolote nchini Tanzania yanaruhusiwa kuomba, lakini

mradi wa kibiashara lazima utekelezwe kutoka kwenye mikoa 15 kama ifuatavyo:

Dar es Salaam, Zanzibar, Kilimanjaro, Arusha, Dodoma, Manyara, Morogoro, Tanga,

Iringa, Mbeya, Mwanza, Shinyanga, Tabora, Mara, na/au Singida

Waombaji wote ni lazima biashara zao ziwe zimesajiliwa na zina leseni.

Waombaji wote lazima waonyeshe ukomavu wa kifedha (taarifa za kibenki za biashara, mfumo wazi wa uhasibu, na walau miaka miwili ya akaunti ya fedha).

Waombaji wote lazima wawe wanajishughulisha na mnyororo wa thamani

wa kuku au mahindi.

Pia mambo yafuatayo ni muhimu kuyazingatia katika kutuma maombi yako: Mfuko wa uwekezaji wa mradi wa LEAD umelenga kufanikisha kutoa mikopo kwa

usawa. Maombi ambayo makampuni yanatoa sehemu kubwa kugharamia mradi

kwa vyanzo vyao (pamoja na chanzo cha tatu cha uwekezaji), na mambo

mengineyo yakiwa sawa, basi yatapewa kipaumbele zaidi.

4. Fomu ya Maombi

4.1 Sehemu A: Kampuni Yako Sehemu hii ina kazi kuu mbili, kutupatia taarifa ambazo zitatusaidia kuyafanyia

kazi maombi yako, kututhibitishia kuwa kampuni yako inakidhi vigezo stahiki vya

mfuko wa uwekezaji wa mradi wa LEAD na kutonyesha uwezo wa kampuni yako.

(A1-A21) - Vipengele hivi vinatoa taarifa za msingi kuhusu kampuni yako, namna

gani tunaweza kukupata/kuwasiliana nawe, nani mhusika mkuu wa kuwasiliana

nae au meneja wa biashara. Tafadhari toa taarifa kama idadi ya waajiriwa wako,

kipato kwa mwaka na taarifa za usajiri wa biashara yako.

(A22) - Kipengele hiki kinaelezea shughuli zako kuu za kibiashara kwa sasa, ni

bidhaa gani unazo uza kwa sasa na huduma unazotoa.

Page 7: MWONGOZO ELEKEZI - BRAC€¦ · huru kuwasiliana nasi kwa njia ya barua pepe ifuatayo LEADtzf@gmail .com au tembelea ofisi ya tawi lililo karibu nawe. Kumbuka mfanyakazi wa BRAC hawezi

BRAC MAENDELEO TANZANIA Mfuko wa Uwekezaji wa Mradi wa LEAD Mwongozo Elekezi – Awamu ya Pili Kurasa Na 6 hadi 11

(A23) - Hapa chini ni mfano wa aina ya taarifa na maelezo muhimu

yanayotakiwa kufafanuliwa.

Mfano: Bidhaa na huduma zinazotolewa

(A24) - Orodhesha mtandao wako wa usambazaji

Mji/Miji husika na mkoa/mikoa ambayo unauza bidhaa zako au unatoa huduma

Jina la msambazaji au wakala ambaye anayeuza bidhaa zako

(A25) - Elezea changamoto ambazo kampuni yako inakumbana nazo hususani za

kiundeshaji na kiutawala.

(A26) - Orodha na 1) Matumizi ya kampuni yako kwa miezi miwili iliyopita na 2)

Jumla ya mauzo yako ya miezi miwili iliyopita.

Chini hapa ni mfano wa aina ya taarifa na maelezo muhimu ya kufafanuliwa kwa

kipengele cha A26.

Mfano: Mauzo ya mwezi

Page 8: MWONGOZO ELEKEZI - BRAC€¦ · huru kuwasiliana nasi kwa njia ya barua pepe ifuatayo LEADtzf@gmail .com au tembelea ofisi ya tawi lililo karibu nawe. Kumbuka mfanyakazi wa BRAC hawezi

BRAC MAENDELEO TANZANIA Mfuko wa Uwekezaji wa Mradi wa LEAD Mwongozo Elekezi – Awamu ya Pili Kurasa Na 7 hadi 11

Mfano: Matumizi ya mwezi

(A27) - Orodhesha mali za kuduma za kampuni na zako binafsi, bila kizuizikwenye

ardhi, magari, nyumba na mashine.

4.2 Sehemu B: Mradi wako wa kibiashara

(B1-B3) - Katika sehemu hii, toa taarifa za msingi kuhusu mradi wa biashara yako. Elezea mradi wa biashara yako kwa maneno matatu au chini ya maneno

matatu (mfano: uzalishaji wa vifaranga, usindikaji wa mahindi, utengenezaji wa chakula cha kuku, au usindikaji wa nyama ya kuku)

Bainisha ni sehemu gani nchini Tanzania mradi wako wa kibiashara utatekelezwa Bainisha wazo lako la kibiashara kama lipo kwenye sekta ndogo ya kuku

aumahindi

(B4) - Eleza kwa kifupi wazo lako la biashara unalotaka kuongeza kwenye biashara

yako ya sasa, inaweza kuwa kukuza biashara zaidi ya hapo ulipofikia sasa au wazo jipya ambalo litaendana na shughuli za biashara yako ya sasa. Tafadhali usirudie

taarifa ambazo umekwisha zieleza kwenye vipengele vingine kwenye hii fomu. Muundo wa biashara yako ukoje?

Ni jinsi gani bidhaa/huduma zako zitawafikia wateja?

kwa nini unafikiri wazo lako la kibiashara litafanikiwa?

Ni jinsi gani bidhaa/huduma yako italifikia soko? Ni jinsi gani utaingiza fedha kutokana na wazo lako jipya la biashara?

(B5) - Elezea hatua utakazochukua kutekeleza mradi wako wa kibiashara, ikijumuisha

shughuli zote muhimu utakazofanya (Mfano : kuwekeza, kukarabati, kuweka mitambo,

manunuzi, kuajiri wafanyakazi wa kudumu au wa muda mfupi na leseni zinazohitajika)

Page 9: MWONGOZO ELEKEZI - BRAC€¦ · huru kuwasiliana nasi kwa njia ya barua pepe ifuatayo LEADtzf@gmail .com au tembelea ofisi ya tawi lililo karibu nawe. Kumbuka mfanyakazi wa BRAC hawezi

BRAC MAENDELEO TANZANIA Mfuko wa Uwekezaji wa Mradi wa LEAD Mwongozo Elekezi – Awamu ya Pili Kurasa Na 8 hadi 11

(B6) - Elezea umelenga wateja gani katika biashara yako (jumuisha miji na mikoa

ambapo utakuwepo). Pia elezea nini mpango wako katika kukuza wigo wa wateja

na kuwavutia wateja, ikihusisha kuzitangaza na kuzitafutia masoko bidhaa au

huduma zako.

(B7) - Mradi wa LEAD umelenga kuongeza kipato kwa wakulima na wafugaji

wadogo wadogo takribani 100,000. Kwa kuwezesha wajasiliamali kupitia mfuko

wake wa uwekezaji, mradi wa LEAD unatarajia kuwatanufaisha wakulima

kutokana na kuboresha na kuongeza bidhaa au huduma zinazotolewa na

wajasiliamali . Elezea ni jinsi gani mradi wa biashara yako utawanufaisha

wakulima na wafugaji wadogo wadogo na jinsi utakavyoshirikiana nao. (B8) - Kwa kutumia jedwari lililopo, elezea uzoefu wa biashara yako katika kutekeleza mradi huu wa kibiashara, uwezo wake wa sasa na rasilimali zilizopo. Ni kwa muda gani kampuni inajishughulisha na biashara /au kampuni ina

mpango gani kuongeza uelewa kwa shughuli zilizopangwa?

Ni wafanyakazi wangapi kwa sasa unao ambao watafanya kazi kwenye mradi wa biashara?

Uzoefu katika usimamizi ngazi ya utawala na wafanyakazi wako ukoje? Ni vifaa vipi, mashine gani, miundombinu, mali ghafi na/au ardhi iliyopo?

(B9) - Elezea changamoto na viatarishi ambavyo unadhani vinaweza kujitokeza

katika utekelezaji wa mradi wa biashara yako na umejipanga vipi

kukabiliana/kupunguza changamoto na viatarishi ulivyojitaja. .

(B10) - Katika mradi wa biashara ulioupanga kuutekeleza, wataje washindani

wako wakuu na bei za bidhaa au huduma zao.

Mfano: Washindani wa kampuni katika mradi wa biashara ya kuzalisha chakula chakuku

NA eleza jinsi utavyoweza kutofautisha bidhaa au huduma zako kutoka kwa

washindani wako.

Page 10: MWONGOZO ELEKEZI - BRAC€¦ · huru kuwasiliana nasi kwa njia ya barua pepe ifuatayo LEADtzf@gmail .com au tembelea ofisi ya tawi lililo karibu nawe. Kumbuka mfanyakazi wa BRAC hawezi

BRAC MAENDELEO TANZANIA Mfuko wa Uwekezaji wa Mradi wa LEAD Mwongozo Elekezi – Awamu ya Pili Kurasa Na 9 hadi 11

Ni kwa kiwango gani muundo wa biashara yako ni mzuri kuliko

washindani wako?

Muundo wako utawafikishia wateja bidhaa kwa gharama/bei nafuu?, kama ndio, ni kwa jinsi gani ?

Utatengeneza bidhaa/huduma bora kukidhimahitaji ya soko kwa njia

tofauti? (mfano: vifungashio au usambazaji)?

4.3 Sehemu C: Fedha (C1) – Tafadhari tengeneza jedwari lenye maelezo kuhusu bajeti pendekezwa kwa mradi wa biashara yako kwa miezi 12. Mishahara Vifaa vya kununua

Mali ghafi Gharama za uendeshaji(kodi, umeme, maji, mawasiliano nk)

Usafirishaji

Matangazo Ada, nk......

Mfano: Bajeti ya kampuni inayoanza mradi wa biashara ya uzalishaji wa chakula cha kuku

Page 11: MWONGOZO ELEKEZI - BRAC€¦ · huru kuwasiliana nasi kwa njia ya barua pepe ifuatayo LEADtzf@gmail .com au tembelea ofisi ya tawi lililo karibu nawe. Kumbuka mfanyakazi wa BRAC hawezi

BRAC MAENDELEO TANZANIA Mfuko wa Uwekezaji wa Mradi wa LEAD Mwongozo Elekezi – Awamu ya Pili Kurasa Na 10 hadi 11

Page 12: MWONGOZO ELEKEZI - BRAC€¦ · huru kuwasiliana nasi kwa njia ya barua pepe ifuatayo LEADtzf@gmail .com au tembelea ofisi ya tawi lililo karibu nawe. Kumbuka mfanyakazi wa BRAC hawezi

BRAC MAENDELEO TANZANIA Mfuko wa Uwekezaji wa Mradi wa LEAD Mwongozo Elekezi – Awamu ya Pili Kurasa Na 11 hadi 11

(C2) - Jumla ya fedha zinazohitajika ili kutekeleza mradi wa biashara yako (yaani

makadirio yako ya jumla ya bajeti)

(C3) - Jumla ya fedha kwa ajili ya mradi unazoweza kutoa kutokana na rasilimali

zako mwenyewe. Mfano: Katika C2 wazo lako la mradi litagharimu shilingi 60,060,000/=

kutekelezeka, unaweza kutoa shilingi 33,160,000/= kutokana na rasilimali fedha zako mwenyewe.

Mfuko wa uwekezaji wa mradi wa LEAD unatarajia wewe kuchangia fedha

taslimu kutokana na rasilimali yako mwenyewe kuwekeza katika mradi

(C4) - Jumla ya fedha kwa ajili ya mradi wa biashara zitakazotolewa kutoka chanzo

cha tatu (washirika wenu, na benki, taasisi nyingine za fedha, au NGO)

(C5) - Jumla ya fedha za mradi unazoomba kutoka BRAC Mfano: kipengele cha C2 wazo lako la mradi litagharimu 60,060,000

kutekelezeka, katika kipengele C3 umejaza kuwa utawekeza Tsh 33,160,000 kutoka kwenye rasilimali fedha zako. Katika kipengele C4 kama hukubainisha chanzo chochote cha tatu cha fedha. Hivyo kiasi cha fedha zinazoombwa kutoka BRAC kitakuwa (60,060,000 – 33,160,000) = shilingi 26,900,000/=

Fedha inayoombwa ni kuanzia shilingi 8,000,000/= hadi shilingi 50,000,000/=

Kiasi cha fedha kinachoombwa hakipaswi kuwa zaidi ya asilimia 50 ya thamani ya

uwekezaji wako wa sasa (ikiwa ni mali pamoja na 'thamani ya biashara yako)

(C6) - Katika jedwali lifuatalo jaza taarifa zote za mkopo ambao kampuni yako

imepata huko nyuma.

(C7) - Elezea taarifa za kifedha za biashara yako zinavyosimamiwa na nani anayehusika.

Tafadhali saini na andika tarehe husika kukiri kuwa taarifa ulizotoa katika maombi haya ni za kweli na sahihi.

4.4 Sehemu D: Nyaraka za kuambatanisha Mwisho, tumia orodha hii uliyotolewa na hakikisha una ambatanisha vivuli

vya nyaraka ambatanishi zilizoainishwa.

Maombi yote yatakayotumwa bila viambatanisho kama 1) Usajiri wa

biashara na 2) taarifa za kibenki na/au taarifa za fedha kwa njia ya simu

kwa miezi 3 iliyopita HAYATAKUBALIWA.

MWISHO WA MWONGOZO ELEKEZI