MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe?...

68
UKIMWI na Jamii Inayoabudu Mwili Mmoja KITABU CHA 2 USHIRIKIANO WA MAKANISA YA NORDIC – FOCCISA AFRIKA KUSINI ANGOLA BOTSWANA DENMARK FINLAND ICELAND LESOTHO MALAWI MSUMBIJI NAMIBIA NORWAY SWAZILAND SWEDEN TANZANIA ZAMBIA ZIMBABWE

Transcript of MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe?...

Page 1: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

UKIMWI na Jamii Inayoabudu

MwiliMmojaKITABU CHA 2

USHIRIKIANO WA MAKANISA YA NORDIC – FOCCISA

AFRIKA KUSINI ANGOLA BOTSWANA DENMARK FINLAND ICELAND LESOTHO MALAWI MSUMBIJI NAMIBIA NORWAY SWAZILAND SWEDEN TANZANIA ZAMBIA ZIMBABWE

Page 2: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

UKIMWI NA Jamii inayoabudu

MwiliMmojaKITABU CHA 2

Mwili Mmoja Kitabu cha 1 kina makusanyo ya mitazamo

kuhusu changamoto, kwa ajili ya kanisa na unyanyapaa un-

aohusiana na UKIMWI.

Mwili Mmoja Kitabu cha 2 kimejikita katika maombi, utarati-

bu wa ibada, kuabudu na kujifunza Biblia, ikichanganyikana

na shuhuda binafsi kutoka kwa watu waishio na UKIMWI. Vi-

tabu vyote (cha Kwanza na cha Pili) vimetolewa katika lugha

za Kiingereza, Kireno, Kiswahili na Kinorwejiani.

Ushirikiano wa NORDIC FOCISSA ni uhusiano wa pamoja baina ya

mabaraza ya makanisa kumi na moja ya Kusini mwa Afrika na ma-

baraza ya makanisa ya nchi za Kaskazini mwa Ulaya.

Ushirikiano wa Makanisa Kusini mwa Afrika na Ulaya Kaskazini

(Nordic Foccisa) inato shukrani zake kwa NORAD na DANDA/ Dan-

Church Aid kwa uhisani wao kuusaidia Mradi huu.

MHARIRI Elizabeth Knox-Seith, DanChurchAid

MRATIBU Jan Bjarne Sødal, Baraza la Kikristo, Norway

BODI YA UHARIRI Precious Mwewa, Mwandishi wa Labari,

Zambia. Mch. Japhet Ndlovu Baraza

la Makanisa nchini, Zambia. Mch. Elias

Zacarias Massicame, Baraza la Makanisa,

Msumbiji. Jan Bjarne Sodal, Baraza la

Kikristo, Norway. Mch. Birthe Juel Chris-

tensen, DanChurchAid, Denmark.

MSHAURI WA NJE Gillian Paterson

WATAFSIRI George Mwita - CUAHA, Edwin Msiri - Tan-

zania Development Mates. Ivan Chetwynd

(Kiingereza na Kinorwejiani). Melodien na

Tony Winch (Kireno)

MPIGA PICHA Ulrik Jantzen, Das Büro, Copenhagen

WANAMITINDO Beauty Chandra na Preben Bakbo Sloth,

wanaharakati VVU+

MICHORO YA KITAALAMU Anne Mousten na Kit Harding

MPIGA CHAPA Jonsson Grafisk, Copenhagen

IMETOLEWA NA Ushirikiano wa Makanisa ya Kaskazini na

Kusini (NORDIC-FOCCISA)

ISBN 978-82-7941-031-7

© © Baraza la Kikristo, Norway, [email protected]

JINA LA AWALI LA KITABU One Body (Mwili Mmoja)Kitabu hiki si cha kuuza au kutumiwa kwa malengo ya kibiashara. Maandishi yanaweza kunukuliwa au

kurudufiwa, ili mradi upendeleo unatolewa kwa mwandishi na mtoaji wa kitabu hiki.

NAKALA ZA TOLEO LA KISWAHILI KITABU CHA KWANZA NA CHA KITABU PILI ZINAWEZA KUAGIZWA KUTOKA:

Jumuia ya Kikristo Tanzania Simu +255 262324445 email: [email protected]

Baraza la Kikristo Norway Simu +47 23081300 email: [email protected]

NAKALA ZA TOLEO LA KIINGEREZA ZINAWEZA KUAGIZWA TOKA:

Baraza la Kikristo Norway Simu +47 23081300 email: [email protected]

Baraza la Makanisa Zambia Simu 260-1-229551-224622 email: [email protected]

Page 3: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

UTANGULIZI 1

Mwili Mmoja

USHIRIKIANO WA MAKANISA YA NORDIC – FOCCISA

UKIMWI NA Jamii inayoabudu

Mafunzo ya Biblia, Liturjià na Hadithi Binafsi Kutoka Kusini na Kaskazini

KITABU CHA 2

Page 4: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

2 UTANGULIZI

UTANGULIZI

Kuabudu Katika Namna Tofauti

DENMARK Hali Halisi

DENMARK Yubile ya Maono kwa Kanisa

ZAMBIA Kuvunja Ukimya na Fedheha

NORWAY Unyanyapaa na Utu

NORWAY Mahali Salama kwa Mazungumzo

NORWAY Biblia Kitabu Kitakatifu

ZAMBIA Kujifunza Biblia

KANISA

ZAMBIA Kanisa Lenye Huruma

MSUMBIJI Kuwakumbatia Waliosahauliwa

DENMARK Kutengeneza Jumuia Mpya Zenye Tumaini

NORWAY Kuwa Mwili Mmoja

NORWAY Mwanamke Aliyekuwa Apigwe Mawe

DENMARK Pumziko Lenye Tumaini

UJINSIA WA BINADAMU

ZAMBIA Ubaba, Jinsia na Yesu

ZAMBIA Ujinsia – Kipawa na Wajibu

NORWAY Nani Anayediriki Kurusha Jiwe la Kwanza

DENMARK Maana, Kifo na Upotevu

SURA ZA MUNGU

DENMARK Imani

ZAMBIA Matendo ya Uponyaji ya Yesu

DENMARK Sura Nne za Mungu

ZAMBIA Mungu Anayesamehe

ZAMBIA Mungu wa Uumbaji

NORWAY Mwanamke Mlemavu

ZAMBIA Hakuna Hukumu

NORWAY Utaratibu wa Ibada Kwa Vituo

DENMARK Juu ya Ukaribu

DENMARK Mungu anayetugusa

DENMARK Kuwasha Mishumaa

DENMARK Sala Siku ya UKIMWI Duniani

3

5

6

10

12

14

16

18

21

22

24

26

29

30

33

34

36

40

43

44

46

48

49

50

52

54

58

60

62

64

Page 5: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

UTANGULIZI 3

NA JAPHET NDLOVU, BARAZA LA MAKANISA LA ZAMBIA

JAN BJARNE SØDAL, JUMUIA YA KIKRISTO YA NORWAY

BIRTHE JUEL CHRISTENSEN, DANCHURCHAID – DENMARK

ELIAS MASSICAME, JUMUIA YA KIKRISTO YA MSUMBIJI

Tangu mwanzo Wakristo wengi wamechukulia kuabudu kama

tendo muhimu la utambulisho wao. Wanathiolojia wengi wa

Kikristo wamemfasili binadamu kama homo adoran: yaani ki-

umbe ambaye asili yake ni kuabudu. Hii ina maana kwamba

kumwabudu Mungu ndiyo kiini cha kuwa mwanadamu. Ni kati-

ka ibada zetu – roho za maisha yetu katika jumuia – tunapoweza

kuwasiliana na kumleta Mungu katika maisha binafsi.

Kama sehemu muhimu katika mradi wa pamoja juu ya

mtazamo wa kithiolojia kuhusu VVU na UKIMWI wa Jumuia

za Kikristo Kusini mwa Afrika na Nchi za Ulaya za Nordic –

FOCCISA – tumekuwa tukishughulikia masuala ya Liturjia na

kujifunza Biblia. Katika Biblia na kupitia mafunzo ya Biblia na

kwa kutengeneza majaribio kiliturujia, tumegundua vyanzo na

msukumo mpya. Hii inaonyesha uhitaji wa njia sahihi ambao

kwa pamoja unaleta neno la Mungu katika maisha yetu, katika

mtazamo wa VVU na UKIMWI na katika uhalisi wa changamoto

na mahitaji ambayo ugonjwa umeleta.

Liturjia ya kanisa imejengeka katika uzoefu wa jumuia fulani.

Kwa ujumla jumuia hizi zinaonyesha uzoefu tofauti na hali za

kimaisha – vijana na wazee, matajiri na masikini, wenye afya

na wagonjwa, wanaume na wanawake, wenye VVU na wasio na

VVU, familia na waseja, watu wanaoteseka kwa kukosa amani

na walio na amani, wale wenye furaha na wale wenye huzuni.

Liturjia ya kanisa inaonyesha ibada ya jumuia yote, kwa hiyo

kuabudu lazima kuwe ni kwa kubadilika ili kuweza kugusa

changamoto mbalimbali zinazowakabili wanadamu. Ni lazima

pia kuwe na majumuisho: ili kwamba kwa kuongea kuhusu au

kumwelezea Mungu, ni lazima tuelewe umuhimu wa kukwepa

unyanyapaa au hali za kutengana na lugha tunazotumia. Tume-

jaribu kuchunguza kanuni hizi katika liturjia na mafundisho

yetu ya Biblia, ili kufanya zikubalike kadiri inavyowezekana.

Tumefanya maamuzi yakini kutengeneza kitabu chenye

shuhuda binafsi kutoka kwa watu waishio na VVU na UKIMWI,

kutoka Kaskazini na Kusini mwa dunia. Shuhuda hizi zinaamsha

maswali muhimu juu ya kutambua, au kuelewa upya, imani

Kuabudu Katika

Namna Tofauti

Page 6: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

4 UTANGULIZI

ya Ukristo. Matumaini yetu ni kwamba kitabu chote kitatoa

sehemu ya jibu – angalau uradhi wa kuanzisha kwa pamoja

Liturjia na mafunzo ya biblia, kama sehemu ya changamoto

ambayo makanisa yanapitia dunia nzima, katika nyakati hizi

za UKIMWI.

Ushirikiano Kati ya Kusini na Kaskazini

Mradi huu ulitengenezwa na Jumuia tano za nchi za Nor-

dic na nchi kumi na moja za Kusini mwa Afrika chini ya

kivuli cha ushirikiano wa Kikanisa (NORDIC-FOCCISA),

ulipewa msukumo na makanisa nchini Zambia, Msumbiji,

Norway na Denmark ikiwa na lengo la kukuza mtazamo

wa kithiolojia katika masuala yaliyosababishwa na maam-

bukizi ya VVU.

Katika kitabu hiki, utajua njia za kutumia nyakati za UKIM-

WI, Liturjia, mafunzo ya biblia, ibada au hali zozote. Njia hizi

ni pamoja na shuhuda binafsi, mafundisho ya biblia, liturjia,

mashairi na fikra mbalimbali. Hizi zimeandikwa au kuanda-

liwa na watu waishio na VVU au UKIMWI au wanaohusiana

nao kwa karibu na ambao wanatambua kuwa rasilimali zili-

zopo hazilingani na mahitaji ya makundi yao au makanisa

kwa wakati huu.

Kitabu hiki kimelengwa kwa watu katika jumuia za chini

(mitaa), katika kaskazini na kusini pia, walio na majukumu

ya kufundisha, kuhubiri, kuabudu na kazi nyingine za mi-

kusanyiko ya waumini. Uhitaji ni mkubwa, katika utoaji wa

elimu ya Biblia na liturjia kwa ajili ya matumizi katika wakati

wa VVU na UKIMWI. Hata hivyo, desturi zetu kiliturjia ziko to-

fauti sana, na hatujifanyi kuwa makusanyo yaliyomo katika

kitabu hiki yanatosha sana kuelezea mahitaji yote yaliyopo.

Badala yake mradi huu unaonyesha uzoefu wa Kikristo ulio

tofauti kiasili kuhusiana na VVU na UKIMWI.

Dhamira Tatu

Malengo, kama ilivyo katika kitabu cha kwanza katika mtiririko

huu, yapo katika dhamira tatu kama zilivyoainishwa na uzoefu

wa VVU.

1) Kujumuisha Kanisa

2) Kujamiiana

3) Mfano ( au sura ya) wa Mungu

Tulichokifanya ni kuleta pamoja viini vya dhamira yetu kwa

kutumia vipengele vya Biblia, na kujiuliza namna Liturjia au

elimu ya Biblia inavyoweza kuwa katika mtazamo wetu – kama

ilivyoonyeshwa katika kitabu cha kwanza – juu ya kujamiiana,

kanisa na mfano au sura ya Mungu. Kwa hiyo, maandiko,

yanatofautiana kutokana na hali halisi ya eneo yalipoandikwa.

Hatuonyeshi kuwa hizi ni njia pekee ambazo maandiko ya

Biblia yanaweza kutumika. Hii itatofautiana kutokana na hali

na mazingira ya wale wanaoyatumia. Malengo yamekuwa ni

kuwa makusanyo haya ya maandiko yaonyeshe umoja kadiri

ya namna tulivyoitwa: Hali ya kuwa katika namna tofauti ya

mwili mmoja wa Kristo tunaouita Kanisa.

Unaweza kutumia maandiko haya kadiri unavyotaka. Una-

karibishwa kuchagua, kuchukua au kubandika katika namna

unavyoona inafaa katika desturi na mazingira yako.

Tunatumaini kuwa maandiko haya yatahamasisha na kukuza

mitazamo zaidi, itakayosababisha kuanzisha kwa liturjia mpya

na elimu ya Biblia katika masuala yanayohusu VVU na UKIMWI.

Zaidi ya yote ni matumaini yetu kuwa utaratibu tulioutumia

katika kutoa maandishi haya, utapanda mbegu ndogo ambazo

zinaweza kusababisha kuanzishwa kwa mikusanyiko ya pamo-

ja makanisani, kidunia, kitaifa pamoja na kimitaa au kifamilia.

Kokote tunakotoka, vyovyote tulivyo, iwe tuna VVU au ha-

tuna, tunategemeana ili kuwa kama tulivyo kwa namna Mungu

alivyodhamiria tuwe – Mwili Mmoja katika Kristo.

UTANGULIZI

Page 7: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

UTANGULIZI 5

Ninaogopa....

Ninajiogopa mimi mwenyewe, ninauogopa ugonjwa nilionao.-

Kwani itatokea lini, itatokea lini?

Kifo cha taratibu, au labda cha haraka na bila maumivu?

Watu...

Wale wasionionyesha upendo

Wale wasionipa ulinzi ninaohitaji.

Tatizo la kifedha...

Ambapo hakuna msaada unaoweza kuonekana

Hufanya maumivu kuwa makali zaidi.

Wote wananitazama na kutikisa vichwa vyao...

“Hata hivyo unaenda kufa”

“Hatujui mbele hali itakuwaje”

“Una bima ya maisha?”

“Sithubutu kukupenda, Je kama ukifa na kuniacha!”

“Je ukiniambukiza?”

Ninataka kujiua...

Nitafunga kamba kuzunguka shingo yangu

Nitajirusha

Nitameza vidonge,

lakini labda kesho,

katika makutano ya barabara

au ndege ya kijeshi kuangukia katika sebule yangu

Hapana....

Nimetahadharishwa.

Tahadhari ambayo watu wachache tu hupata.

Je inanifanya mimi kuwa wa pekee?

Kitu cha pekee?

Inanifanya niogope

- lakini pia mwenye furaha.

Imenifundisha kupenda maisha

Na kuyathamini

Badala ya kuishi tu.

Sasa nahitaji kuishi

Nahitaji kuujua upendo.

Nahitaji kujua usalama.

Niamini....

Nifanye msikivu

Sikiliza sauti yangu ya ndani.

Sauti.

Hufanya ninyenyue kichwa changu juu

Na kutabasamu juu ya hatima yangu.

Inanifanya niishi kwa matumaini

Na kuniambia ni vyema,

maisha yangu yatakuwa mafupi kuliko ya wengine

Lakini labda mazuri zaidi?

Ninatumaini....

DORTHE, AISHIE NA VVU, DENMARK

Hali Halisi - Nina VVU

Page 8: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

6 UTANGULIZI

NA PREBEN BAKBO SLOTH

Ukiwa kijana unatakiwa kuangalia mbele, kutengeneza mipan-

go, kuwa na maono na kuota ndoto. Kuangalia mateso na kifo

cha awali kwa kawaida hatuvioanishi na ujana. Lakini kuwa na

VVU katika umri wa miaka 24 hubadilisha mtazamo wako. Kwa

kuongeza, katika maongezi yetu, daktari aliniambia nina kama

miaka mitano iliyosalia ya kuishi. Wakati ujao ukawa ni tishio,

kupanga kukawa hakuna maana, maono ikawa ni ukwepaji,

ndoto – kufikirika na matumaini ya uongo.

Kuadhiriwa na mtu ambaye hakujali kukuambia ukweli, iliku-

wa ni pigo langu kubwa kuwaamini watu wengine. Nitawezaje

kuwaamini wengine, wakati imani yangu imesalitiwa kabisa

kiasi cha kunipa virusi hatari? Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-

tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea

na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

sababisha kujidharau na hisia ya kutojijali na iliwavunja mioyo

watu wengine.

Wakati huo wafuasi wengine wa mrengo wa kulia wa ka-

nisa walikuwa wakihubiri kuwa VVU na UKIMWI ni adhabu

Ushuhuda Kutoka Kwa Mhanga

Wa Siku Nyingi

kutoka kwa Mungu juu ya maisha ya dhambi. Nikiwa nime-

pooza tayari na mshtuko wa kuhukumiwa kifo, haikuwa ra-

hisi kutoyaweka mahubiri yao moyoni, kupokea hukumu hii

ya Mungu mimi binafsi, kujitwika mabegani mwangu na ku-

jaribu kukubali namna hii ya hukumu takatifu ya ajabu. Na

ndivyo ilivyokuwa mimi, na alama ya kifo ya VVU juu yangu,

iliyobandikwa na hasira ya Mungu, katika hali ya mgogoro

(wa ugonjwa) unaoandamwa na aibu na kujihukumu, niliona

haiwezekani kutaka msaada kutoka kwa mtu mwingine. Si-

kudhubutu kumwendea yeyote kumshirikisha taabu zangu,

kwa sababu nilikwisha ridhia kuwa kila mtu hatonijali, kama

vile Mungu alivyokwisha fanya.

Huwezi kumdanganya Mungu, lakini watu unaweza kujaribu.

Matokeo yalikuwa ni kuishi miaka miwili na siri yangu moyoni.

Miaka miwili ya mateso kisaikolojia, kiroho na kimhemuko. Mia-

ka miwili ya kudanyanya, visingizio na kunyamaza. Miaka miwili

iliyonichukua mbali, mbali sana na marafiki na familia yangu,

kwenye baridi na giza la upweke. Nililikimbia kanisa ambamo

nilikuwa mshirika, kwa kuwa nilipambana na kutengwa.

Yubile ya Maono K

Page 9: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

UTANGULIZI 7

UTANGULIZI

Mfano Mpya wa Mungu

Ilikuwa ni baada ya miaka miwili ya kwanza nilipothubutu ku-

tafuta msaada, kujihatarisha kwa kuwa wazi kuhusu hali yangu

kiafya, kujua kama VVU ni adhabu kutoka kwa Mungu na kufi-

kiria mimi kama mfano wa Mungu. Mungu aliongea nami pia,

kwa kutumia picha zilizoniambia kwa uwazi kuwa ninaweza

kutoka kanisani, lakini Mungu hataniruhusu niondoke. Nilipata

nyumba ya kiroho katika kusanyiko dogo mjini Copenhagen.

Hapa nilipewa hamasa, walinielewa, walinikubali na kunijali.

Nilikutana na watu wengine wenye UKIMWI, hali iliyoanzisha

mchakato wa uponyaji ambao haujamalizika mpaka leo, miaka

kumi na tano. Nilijua kuwa hakuna kitu, hata VVU na UKIMWI,

kinachoweza kunitenganisha na Upendo wa Mungu (Warumi

8:38). Katika mazingira ya kushirikishwa na kupendwa hisia ya

hukumu na aibu haraka ilitoweka.

Mahubiri kuhusu upendo wa Mungu usio na masharti na

ushirika unaojali uliumba sura mpya ya Mungu kwa ajili yangu.

Sura ambayo niliweza kujiona na kupata nguvu. Taratibu imani

yangu kwa watu wengine na kwangu ilianza kujengeka.

Mchakato kufikia kujiheshimu na ujasiri ndani yangu na kwa

wengine ulichukua miaka mingi na ulifanikishwa kwa uvumili-

vu, upendo na uelewa wa watu wote ndani na nje ya kanisa, na

uzoefu wa hali inayojirudia ya kutojisikia kuachwa na Mungu

Uzima Huuliza Maana

Maswali mengine mengi na matatizo yameacha makovu katika

miaka kumi na nane iliyopita. Woga wa kujisikia mdhaifu, woga

wa maumivu, woga wa kifo, hali ya kujisikia kukata tamaa na

kutokuwa wa maana baada ya kupoteza marafiki wengi na

kuachwa, kutoamini maisha ya mbele nk. Wakati mwingine

imekuwa ni vigumu kuwa na malengo hata ya muda mfupi,

bila kutaja kuwa na maana katika maisha katikati ya maumivu,

hasara na mateso. Ni katika miaka minne tu iliyopita nime-

tambua kuwa kama maisha na kifo yana maana, basi mateso

lazima yana maana pia. Bila kuamini katika maana, au uhiari

wa kutafuta maana, ningelikwisha kata tamaa, ningeona kila

kitu hakina maana na kumegeka kiroho na kiakili. Kwa hakika

ni uzima pekee ndio huuliza maana na ni lazima nijibu. Nijibu

kwa kutafuta na kupata maana, maana katika hatua tofauti ka-

tika maisha ziletazo majibu.

Kuzungumza na Mungu, maombi na kumtafakari, katika ku-

angalia maisha yangu ndani ya injili na kitabu cha Zaburi, kuku-

tanika na kuzungumza katika kanisa na kukutanika na wengine

walio na UKIMWI imekuwa ni vyombo vya Mungu katika mcha-

kato huu wa uponyaji.

Jumuia ya kanisa na kukutana na wakristo wengine imekuwa

ni msaada usio na kifani. Wamesaidia kujenga daraja kutoka

mauti hadi uzima, kutoka katika kuvunjika hadi kutovunjika na

kutoka kujichukia hadi upendo.

Kanisa lina UKIMWI

Mpambano wangu na kanisa na ujumbe wake, mara baada ya

kuambukizwa, ilikuwa ni kusikia ujumbe wa kuhukumiwa. La-

kini “ kuhukumu ni kuficha upendo wa Mungu”, kama mchun-

gaji Carina Wøhlk alivyosema wakati fulani katika siku ya

UKIMWI duniani. Ni kwa nini kanisa, au angalau sehemu yake,

ni msemaji wa hukumu? Ninaona mifano mingi ndani ya Biblia

kuwa umbo halisi la tabia ya Mungu juu ya wanyonge, walio ka-

tika hatari na waliotengwa ni kuwaingiza kundini, kuwapenda

na kuwajali. Na kama ulivyomtendea mmoja wa wanafamilia

yangu, umenitendea mimi – kwa mema au mabaya.

Kwa Paulo kulinganisha kanisa kama mwili katika akili, wakati

mwingine huwa ninaona kama baadhi ya wanathiolojia na wa-

tafsiri wa maandiko ni meno, nami ni sehemu ya ute ambao

mwili unataka kuutoa! Lakini wakati sehemu moja ya mwili

ina UKIMWI, mwili wote huumia, na kwa hiyo kanisa lote lina

UKIMWI. Kanisa ni lazima lionyeshe huruma kwa kujali, kama

linataka kuishi kufuatana na mtazamo wa Paulo. Kama halitaki

kufanya hivyo, basi lijiite kitu kingine, kwa sababu limekuwa

chanzo cha kuvunja moyo, kukatisha tamaa na mateso.

ubile ya Maono Kwa KanisaDENMARK

Page 10: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

8 UTANGULIZI

Kukosa Makazi

Nimekuwa nikiwa na kanisa, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Den-

mark, kama nyumba yangu ya pili. Kwa namna ile ile nilivyoifa-

hamu nyumba yangu mwenyewe, nilizoea maisha ya kanisani,

ibada na lugha zake na nilijisikia kuwa nyumbani. Lakini nili-

pogundua katika moja ya nyumba zangu siwezi kusema mau-

mivu na mateso yanayohusiana na kuishi na VVU, ghafla niliji-

sikia kutokuwa nyumbani katika nyumba yangu mwenyewe.

Wakati mwingine maumivu na mateso yamekuwa ni makali

kiasi kwamba nimelazimika kuzungumza na mtu yeyote, na

wakati imani ya ujasiri wangu inapokutana na ukimya na chu-

ki mbaya iliyofichika, najisikia kukosa makazi katika nyumba

yangu mwenyewe. Ningejigawa. Kama ningeweza kujigawa ili

kupata sehemu ya mwili wangu yenye afya, inayofanya vizuri,

inayoheshimika, basi ingekuwa ni maumivu kidogo kuiacha

nyumba na kubakia kama ulivyo na ukiwa na maumivu – lakini

usiye na makazi.

Kusikia wanafamilia yangu na washirika wa kanisa wakisema

wamejisikia kudhalilika kwa sababu yangu iliniongezea hali hii

ya kujisikia kutokuwa na makazi.

Kanisa linapowakataa watu wenye VVU kwa namna hii, wa-

natakiwa wawe na imani kubwa au uzoefu mkubwa wa dini

vinginevyo wanaweza kumwacha kumwamini Mungu. Lakini

si matokeo yanayojulikana kwa kanisa.

Kuwa Mtu Mkamilifu

ndani ya Nyumba ya Mungu

Mungu aliumba watu wakamilifu. Roho, nafsi na mwili. Na

kwa hiyo ndani ya nyumba ya Mungu mtu mkamilifu lazima

aangaliwe na pia kumjali. Kwa asili, hii inajumuisha ushauri wa

kichungaji, uongozi wa kiroho, maombi nk. – lakini kwa mtu

mwenye magonjwa yanayonyanyapaliwa kama VVU na UKIM-

WI, haitoshi kujua tu kuwa unaweza kwenda kanisani na mata-

tizo yako ya kiroho.

Kanisa ni lazima litoe taarifa za jumla na zisizo na mwisho

kuwa watu wenye VVU wanakaribishwa. VVU, UKIMWI, kuja-

miiana, unyanyapaa nk, ni lazima kila wakati kuwa kwenye

ajenda za kanisa – siyo tu kuihusianisha na Siku ya UKIMWI

Duniani.

Kwa bahati ninaona makanisa katika sehemu nyingine za du-

nia ambayo yanaishi nje ya maono yao ya Ufalme wa Mungu,

katika ibada zao na jumuia zao. Lakini kukiwa na watu millioni

arobaini duniani wenye VVU hili ni hitaji la muhimu. Katika hali

hii kanisa lazima lijitoe katika fikra zilizozoeleka na kupooza,

kunyanyasa na thiolojia ya matengano na mila iliyozoeleka.

Kama tawi la mwaka wa sherehe wa Agano la Kale – japo hili

linaweza kuwa halijawekwa katika vitendo – kanisa linaweza

kutangaza mwaka wa sherehe, wakati wa sherehe na mahali

pa sherehe.

Itaweza kuleta furaha na uhuru kutoka katika kujihukumu na

aibu – kwa kuonyesha kujali na kukubali watu walio na VVU.

Sherehe itahusisha maombi kwa ajili ya msamaha kwa miaka

mingi ya kuzembea kufanya hivi. Kutakuwa sherehe kwa ajili

ya jamuia ambayo kila mtu huchukuliwa kwa usawa: ambapo

busara, uzoefu na hekima ya watu wenye VVU inathaminiwa

na kutumiwa. Sherehe kwa ajili ya watu ambao wamewekwa

huru kutokana na mateso yaliyowafanya kupooza. Sherehe

kwa sababu tunaweza kuanza kuishi maisha yenye ubora.

Sherehe kwa kuiona heshima ya watu wenye VVU ikikua na

uwezo wao ukionekana kwa faida ya kila mtu.

Ujasiri

Wapi kanisa litapata ujasiri wa kufanya haya yote? Nadhani

inatubidi tuanze kuchunguza hisia zetu – na si hizia zetu za

mapenzi tu. Pia maumivu, huzuni, simanzi na hasira vinaweza

kuwa hali ya mabadiliko ya hali ya akili inayoweza kutuunga-

nisha na watu wengine na jamii zinazotuzunguka. Ni lazima

tuchunguze mahitaji ya watu wenye VVU, tusikilize maoni yao

na tutafute njia na namna ya kuyatatua.

Lazima tuombe kwa ajili ya ushujaa, kumtumaini Mungu na

sisi wenyewe pia, kwa ajili ya imani ambayo roho wa Mungu

atatupa ili kufanya maono ya sherehe ya kumbukumbu iti-

mie: chumba chenye wingi wa matarajio maishani na uhuru

na matumaini, pamoja na kuta zenye upendo, kujali, heshima

na imani.

Kama kazi yote ya kanisa inaweza kwa moyo wa uwazi na

kuaminiana, kama Kaka Roger wa Taizé alivyosema, basi watu

wenye VVU hawataogopa kuliendea kanisa.

Page 11: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

UTANGULIZI 9

TumainiTuna tumaini la mbingu mpya na nchi mpya, ambamo amani inaishi, ambapo pumzi ya Mungu ndiyo uzima na hutengeneza up-

inde wa mvua wenye rangi na maumbo tofauti. Tuna tumaini la mbingu na nchi mpya, ambamo upendo unaishi, ambamo roho ya

Yesu Kristo itoayo uzima hukaa ndani ya watu na kati ya watu, ambamo mateso yameteswa, kifo kimekufa na kaburi li wazi kama

lilivyokuwa asubuhi ya Pasaka. Tuna tumaini la mbingu mpya na nchi mpya, ambamo furaha inaishi, ambamo Roho Mtakatifu wa

Mungu anaendelea kuumba upya ibada kwa wanadamu na tumaini lisilozuilika la maisha bila mipaka.

Amen.

Mwili wa UlimwenguLazima nitubu kwa sababu nadhani mara nyingi kanisa ni hodari kujiweka katika upande ambao unaegem-

ea mawazo ya umma – na kwa kufanya hivyo linapuuza wajibu wa asili lililokuwa nao kama taasisi na nguvu

kwa ajili ya mema. Wajibu wa kanisa ulikuwa ni kuwaendea watu na kuonyesha kuwa inawezekana kufikiri

tofauti. Kwamba kulikuwa na njia mbadala namna ya kuwaangalia watu, na mtazamo wa uhai.

Wewe ni Mkristo hasa, uliye na imani ya kutosha na ninajisikia mshirika halali wa kanisa, kama unaishi na

UKIMWI kama ambavyo unaweza kuwa na kansa au kifua kikuu au ugonjwa mwingine wowote. Ninaweza

kuelewa kuwa baadhi ya watu wanajisikia kuwa kanisa haliwakaribishi – na hilo linanitia huzuni, kwa saba-

bu kanisa limepuuza wajibu wake na kukwepa jukumu lake la asili la kuwa mahali pa kukutanika wanyonge

na waliokataliwa na jamii.

Kama kanisa linatakiwa kuwa la watu wote, lazima limjumuishe kila mmoja, hata wale wanaoishi na VVU

– na wanaweza kupatikana katika makundi yote ya jamii. Hakuna anayekwepa. Kanisa la pamoja linaweza

kukusanya kila mtu katika mbawa zake. Hii ni changamoto kubwa kwa kanisa wakati huu, kuonyesha kwa

mapana namna linavyoweza kuwafikia wengi. Kuonyesha kuwa siyo mahali pa kukutana kwa wanaojulika-

na na wanathiolojia. Kwamba ni mahali ambapo watu wanaweza kuja na kupata faraja, nguvu na ongezeko

wanalohitaji kuwawezesha kukua kiakili, kiroho na kimwili. Hii inajumuisha si kwa wagonjwa tu, bali pia

kwa walio karibu nao.

Tatizo la UKIMWI ni la kila mahali kwa watu wote. Hitaji hili la kibinadamu ndilo kanisa linatakiwa kuliti-

miza na hakuna shaka kwamba hamasa ipo kutokana na amri ya Yesu kuhusu upendo. Kuna nafasi kwa ajili

yetu sote ndani ya maneno hayo na haitakiwi kuhukumiana sisi kwa sisi.

USHUHUDA WA JESPER, ALIYEKUFA KWA UKIMWI, DENMARK

UTANGULIZI

Page 12: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

10 UTANGULIZI

Kupima na Kuishi kwa Matumaini

NA JOY LUBINGA, MRATIBU WA DUARA ZA MATUMAINI

Siyo rahisi kukabiliana na ukweli kuwa karibuni au baadaye

nitakufa kwa sababu nimeathirika kwa ugonjwa usio na tiba.

Japokuwa siku moja nilikuwa na ujasiri na kwenda kupima na

nikaonekana nimeathiriwa na VVU.

Mimi ni mjane wa miaka 52 ninayeishi na VVU. Nilipima mwaka

2003. Nina watoto watano – wote wa kike- wana umri kati ya mi-

aka 3 hadi 13, na ninamwangalia mpwa wangu ambaye wazazi

wake walikufa kwa UKIMWI.

Mume wangu alichunguzwa na kuonekana ana kifua kikuu

mwaka 1998. Baadaye alionekana kuwa na homa ya uti wa

mgongo inayosababishwa na fangasi, na madaktari waliniambia

alikuwa na UKIMWI na angekufa wakati wowote au kuwa kichaa.

Habari hii ilinifanya nitetemeke sana kwa sababu nilihisi kuwa

ninaweza kuwa na VVU. Siku moja nilipokuwa nimerudi nyum-

bani kutoka kazini, ninakumbuka watoto wangu walivyoniam-

bia kuwa baba yao alikuwa hajaamka kutoka kitandani. Niliingia

na kumuuliza jinsi alivyokuwa akijisikia. Aliangalia pembeni.

Huu ulikuwa mwanzo wa ugonjwa wa muda mrefu, alikwenda

kila mara hospitali mpaka alipokufa tarehe 5 September 1998.

baada ya kuambiwa alikuwa na kifua kikuu, alipoteza tumaini na

alitumia dawa za kifua kikuu kwa muda mfupi. Ninahisi kuwa hii

ndiyo sababu iliyofanya afe mapema.

Tangu hapo maisha yangu yaliendelea kama kawaida. Niliishi

na watoto wangu, na kuwasaidia kwa mahitaji ya msingi ambayo

waliyahitaji kwa ajili ya shule. Haikuwa rahisi. Lakini nilijitahidi

kwa kiasi fulani. Wazo la kupima halikunijia kwa sababu sikuwa

na dalili za ugonjwa wowote.

Kupima na Kuonekana Nimeathirika

Mwaka 2003 kitu fulani kilinitokea nikiwa ofisini mwangu

kilichonisumbua kwa kuwa sikukubaliana nacho. Hii ilikuwa ni

mwanzo wa maumivu yasiyoisha ya kichwa, kukosa hamu ya

kula na kupoteza uzito. Si kuwa na furaha na nilipoteza uzito

ghafla. Nilionekana mbaya kwa sababu nilipata vipele miguuni

na usoni. Sikuweza kuvaa nguo fupi. Mpaka pale afya yangu

ilipoanza kuzorota ndipo nilipokumbuka madaktari walinia-

mbia mume wangu alikuwa na UKIMWI. Hili lilinifanya niende

kupima VVU.

Kuonekana nimeathirika halikuwa jambo la kushtusha kwan-

gu. Lakini lilikuwa ni pigo kubwa kwangu kukabiliana na uk-

weli kwamba sasa nilikuwa ninaishi na VVU. Kitu cha kwanza

nilichofikiria ilikuwa ni kifo, na ukweli kuwa ningeweza kuacha

watoto wangu wakiwa yatima. Wazo hili daima limeniletea hu-

zuni na mtu wa kwanza kumshirikisha habari hizi alikuwa ni

binti yangu mkubwa. Tulilia pamoja na alinipa maneno mengi

ya matumaini na kunitia moyo.

Baada ya hapo nilifanya vipimo vyote vya muhimu. Mwanzoni

kiwango changu cha chembechembe nyeupe za damu (CD4)

kilikuwa 314 ambacho hakikuwa kibaya kutokana na muundo

wa Zambia. Lakini kwa sababu ya wasiwasi mwingi, zilishuka

na kuwa 119 katika muda mfupi – ndani ya mwezi mmoja hivi.

Nilishauriwa kuanza matibabu ya kupunguza makali ya VVU na

kurefusha maisha. Kwa kuwa matibabu haya yalikuwa ghali,

niliamua kumshirikisha hali hii ngumu bosi wangu, Katibu Mkuu

wa Baraza la Makanisa la Zambia. Alinisaidia kupata dawa kupi-

tia ufadhili wa serikali. Kwa hakika nilisaidiwa. Nilipopimwa na

kuonekana na VVU nilikuwa na uzito kwa kilo 51, lakini sasa

nina uzito wa kilo 90. Na chembechembe nyeupe za damu

(CD4) zangu zimeongezeka na kuwa 470. Ninamwona daktari

kila mwezi kwa ajili ya uchunguzi na kujitunza mwenyewe kwa

sababu ninajua hali yangu.

Nimewashirikisha watu wengi hadithi yangu, si kwamba ni-

napenda kuwa na VVU au ninaifurahia hali hii - lakini nimeona ni

muhimu kuwatia nguvu wengine wanaojikuta katika hali kama

iliyonikuta. Nimenyanyapaliwa na kukataliwa katika maisha. La-

kini ninajua kwamba Mungu ananipenda. Ana nafasi ya mwisho

katika maisha yetu na hakika ameahidi kuungana nasi ili kuvunja

unyanyapaa, ukimya na fedheha ya VVU na UKIMWI.

Kuvunja Ukimya na FedhehaZAMBIA

Page 13: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

UTANGULIZI 11

NA ACKIM SAKALA, MTENDAJI KATIKA DUARA ZA MATUMAINI, ZAMBIA

Nilianza kuugua mwaka 1998. Nilikuwa na maumivu makali

ya tumbo, madaktari hawakuweza kujua kilichokuwa kikisa-

babisha maumivu. Niliwekwa katika matibabu ya vidonda vya

tumbo japokuwa sikuwa navyo. Kabla ya hapo mwaka 1995 –

nilimpoteza rafiki wa karibu. Alikufa akiwa mwembamba sana

na dalili zote za UKIMWI. Baadaye, mwaka 1996 nilipoteza rafiki

mwingine katika namna hiyo hiyo.

Katikati ya mwaka 2003 nilionyesha dalili zote kama za rafiki

zangu waliokwisha fariki. Ni wakati huo nilipoamua kuchukua

hatua. Kati ya mwaka 1998 na 2002 nilishapoteza uzito kutoka

kilo 70 hadi kilo 41. Nilishapata malaria za mara kwa mara, ku-

toka jasho usiku na vipele – hizi ni baadhi ya dalili.

Upimaji

Ilikuwa ni June 2002 wakati nikiwa mjini nilipoona Kituo Kip-

ya cha Upimaji na Ushauri ambapo kitu fulani kiliingia akilini

mwangu. Niliamua kwenda kupima. Nilipitia katika ushauri,

upimaji na kuonekana nimeathiriwa na VVU.

Nikiwa nashuka ngazi baada ya kupima nilipata kwikwi iliyodu-

mu muda wa siku sita, usiku na mchana. Nilichunguzwa na nika-

onekana nilikuwa na kifua kikuu na nikaanza tiba ya kifua kikuu

kuanzia mwezi June 2002 mpaka Februari 2003. Nilishaongeze-

ka uzito hadi kilo 65. Mtu niliyekuwa nimemweleza hali yangu

baada ya kupima alikuwa ni mke wangu. Baadaye niliwaambia

dada na kaka zangu na rafiki wachache niliowaamini. Tangu ni-

lipopimwa nikawa mgonjwa sana. Mke wangu alizingatia katika

kunihudumia, lakini ninajua kwa hakika alikuwa akiogopa kuam-

bukizwa. Baada ya miezi sita alikwenda kupima VVU. Tangu hapo

amekuwa akienda kupima kila baada ya miezi mitatu. Bahati, kila

mara amekuwa anaonekana kutokuwa na VVU.

Kuishi Kwa Uwazi Kama Familia

Haijawa rahisi kuishi na virusi. Nilizaliwa June 24, 1961, katika

familia ya watoto tisa – wanne wa kiume na watano wa kike.

Baada ya kuoa tulipata watoto watano, watatu wa kike na wawili

wa kiume. Mkubwa kwa sasa ana miaka 16 na mdogo ana mi-

aka 4. Miaka miwili ya kwanza sikuwaambia watoto wangu

chochote, lakini baada ya kupata mazoezi kimatibabu mwaka

2004 niliamua kuwa wazi kuhusu hali yangu. Niliombwa kue-

leza kidogo kuhusu maisha yangu katika kituo cha televish-

eni cha taifa, na kabla ya hapo niliwapeleka binti zangu wawili

wakubwa katika ushauri. Hivi ndivyo hali yangu ilivyowekwa

wazi kwa watoto wangu. Ninaelewa haijawahi kuwa rahisi kwa

binti zangu walio shule za sekondari kuwa na baba aliye na

VVU – kama ambavyo haikuwa rahisi kazini kwangu na katika

jumuiya yangu. Lakini ilinilazimu kukumbana na unyanyapaa

na fedheha na kusaidia kuvunja ukimya kwa kuongea kuhusu

hali yangu kwa uwazi.

Matibabu

Nilianza kupata matibabu ya kurefusha maisha (ART) kwa sa-

babu nilipata kifua kikuu. Baada ya miezi minne niliambukiz-

wa homa ya uti wa mgongo. Miezi sita baadaye, nilipokwenda

kupimwa chembechembe nyeupe za damu (CD4) zilikuwa

chini hadi 270 lakini nilipokwenda kupima miezi sita baadaye

kipimo kilionyesha 324. Hivi karibuni nitakwenda kwa ajili ya

kipimo kingine, na ninatumaini zitakuwa zimeongezeka kwa

kuwa ninajisikia mwenye afya nzuri zaidi kuliko pale mwanzo.

Baada ya kuwa nje ya kazi kwa mwaka mmoja, nimerudi katika

kazi yangu ya ualimu na kama mwamuzi wa mpira wa miguu.

Tabia ya Maisha Yangu Leo

Kwa sasa ninaishi maisha yenye kujali. Ninaamini mimi ni uum-

bwaji wa Mungu na kwamba ninaishi kwa makusudi ya Mungu.

Ninaamini ninaweza kusaidia kuvunja ukimya ndani ya kanisa

na katika jumuiya kwa sababu ya nafasi yangu kama mwalimu

katika jamii.

Ninaweza kuongea kuhusu hali yangu ndani ya kanisa na katika

umma kupitia Duara za Tumaini, mtandao ulioundwa na Ba-

raza la Makanisa la Zambia. Kupitia Duara za Tumaini ninapata

masaada wenye thamani na mahitaji yangu binafsi yanatimiz-

wa. Sote tunajaribu kuvunja unyanyapaa na fedheha na kutiana

moyo kuwa wazi juu ya hali zetu ili kuwasaidia wengine.

Ujasiri wa Kuwa Wazi

Ni mtandao wa kusaidia watu waishio au walioathiriwa na VVU na

UKIMWI. Vikundi vya masaidiano vimeundwa katika jiji lote la Lusaka,

na kazi itatawanywa katika miji mingine ya Zambia pia. Kwa kawaida

vikundi hukutana katika makanisa na mikusanyiko ya kiroho, lakini

pia hata majumbani. Kazi hii ilianzishwa na Baraza la Makanisa la Zam-

bia. Joy Lubina ni mshauri wa saikolojia ya jamii na Ackim Sakala ni

mwalimu. Wote wawili wanajulikana vyema kati umma wa wazambia

kwa sababu wamekuwa na ujasiri wa kuwa wazi kuhusu hali zao. Kupi-

tia mikutano mingi katika mtandao wa kiimani wa makanisa na katika

mahojiano ya televisheni na redio pamoja na magazeti wanawashauri

na kuwatia moyo wengine kuvunja ukimya na unyanyapaa juu ya VVU/

UKIMWI.

Ushuhuda

Duara za Tumaini

Page 14: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

12 UTANGULIZI

Katika kuitikia wito juu ya mtazamo wa kithiolojia kuhusu un-

yanyapaa unaohusiana na VVU na UKIMWI, Baraza la Kikristo la

Norway liliwaalika watu waishio na VVU kuhudhuria katika ma-

jadiliano. Waliungana na wafanyakazi kutoka katika makanisa,

seminari na taasisi zingine za Kikristo. Majadiliano yalifanyika

Aksept, katikati ya jiji la Oslo mahali lilipo kanisa la wale walio-

athirika kwa VVU na UKIMWI. Mikutano ya namna hii iliendelea

kwa miezi kadhaa, katika makundi madogo na makubwa. Mita-

zamo ifuatayo inafafanua mtiririko wa maongezi tuliyoshirik-

ishana Oslo na ni jaribio la kushirikishana yale yaliyojitokeza

katika majadiliano yetu. Yanaeleza uzoefu kuhusu unyanyapaa

na uhitaji wa kuelewa nini maana ya kuwa mwanadamu.

Mazingira ya Unyanyapaa

Nchini Norway, watu waishio na VVU wanakumbana na un-

yanyapaa kwa mapana sana. Japokuwa tabia za unyanyapaa

hazionyeshwi kwa maneno, ziko dhahiri kwa wale waishio na

VVU. Mtu mmoja alisema “watu wanakuchukulia tofauti: wa-

nakukwepa na wanakusengenya. Ujumbe hupokelewa vyema

kama vile ambavyo ungesemwa kutoka juu ya mapaa ya ny-

umba.” Hata katika taasisi za afya, “mahali ambapo tunatege-

mea kupata utaalamu na kupokelewa bila upendeleo,” kume-

kuwepo taarifa za mara kwa mara za wagonjwa wenye VVU

wanaoachwa katika foleni au kukataliwa huduma za upasuaji.

Kwa mujibu wa muathirika wa ubaguzi wa aina hii “inatokea,

kwa sababu macho, mioyo na fikra zao zimefungwa!”

Kwa mujibu wa watu waishio na VVU, uzoefu wa unyanya-

paa katika jamii mara nyingi umesababishwa na kujinyanya-

paa, ambako husababisha kufichika kwa hali zao kwa wengine.

Wakati mwingine woga huu wa kukataliwa hauwezi kuthibit-

ishwa na watu wengine wanaweza kuonyesha hisia zisizotara-

jiwa za upendo na kukubalika katika kueleza hali zao kuhusiana

virusi. Hata hivyo kinyume chake ni kweli. Mama mmoja akase-

ma anaogopa kusema na anajisikia hawezi kuwaambia rafiki

zake kuwa mwanae wa kiume ana VVU kwa sababu anaogopa

“kupoteza heshima yake.” Kuna woga wa kujihalalishia kuwa

watoto watanyanyapaliwa, au kwamba mtu atapoteza misaa-

da inayohitajika ya marafiki na familia yake.

Hivyo “ katika hali ya kutoaminika wapo wengi ambao hu-

jitenga, wakikaa nyumbani bila kutoka nje”: hali ya mahusiano

inayoweza kuwa useja wa kujitengenezea, inayoweza kusaba-

bisha kufadhaika na wakati mwingine kujiua.

Mawazo, Uzoefu na Mtazamo Juu ya

Watu Waishio au Walioathirika kwa VVU

Unyanyapaa na UtuNORWAY

Utambulisho na Lawama

Masuala ya utambulisho yanaoneka kuwa na utata hasa yan-

apohusu VVU. Hii kwa sehemu ni kwa sababu ya dalili za la-

wama zinazoambatana nayo. Kama mshiriki mmoja alivyose-

ma. “Ninaposema nina VVU, ninasikia sauti inayosema, ‘kwa

nini unavyo?’ Tofauti na kansa, VVU inaonyesha kuwa ni kitu

ulichojitakia.” Kwa kukumbana na mitazano hii, kuishi na VVU

kunaweza kumfanya mtu akaweka moyoni sura anayoumbiwa

na wengine, na kuigeuza kuwa ni sahihi juu yake mwenyewe.

Hivyo virusi kuwa kielelezo cha utambulisho wa mtu. “Kusema

kuwa mtu ana VVU ni kitu tofauti na kusema mtu anaishi na

VVU au ni VVU halisi, akasema mtu mmoja. “Ndiyo”, mwingine

akakubali: “Hiyo ni tofauti yenye maana sana kwa sababu ‘ni’

inahusika na utambulisho wa jumla wa mtu; ambapo kama

ukisema una virusi, inakuwa kitu tofauti na wewe, kitu ulicho-

nacho na siyo namna ulivyo. Hii ina maana kuwa haifungamani

na utambulisho wako.” “Ina maana kuwa” akasema mwingine,

“Lugha hiyo ni muhimu, pamoja na jinsi tunavyozungumza

kuhusu sisi wenyewe.”

Kutengwa

Kadiri mazungumzo yalivyoendelea, iliendelea kuonekana dha-

hiri kuwa uzoefu wa watu wenye VVU ulitoa mwanga katika mta-

zamo wetu na maana ya kuwa mwanadamu katika jamii yetu.

“Siwezi kumwambia yeyote nina VVU kwa sababu ninaogopa

watanihurumia” alisema mtu mmoja; watahusiana nami ka-

tika njia tofauti; watakuwa waangalifu kile wanachoniambia.”

“Ninajisikia mdogo sana.” Alisema mshiriki mwingine. “Kama

wangeweza kubaini kuwa mimi ni mtu halisi mwenye malengo

na mwenye rasilimali: lakini vyote wanavyoona ni virusi.” Wa-

shiriki walieleza juu ya ukuta wa kutofahamu wanaokumbana

nao kila wakati wanapojaribu kueleza kuwa hata wao ni wana-

damu wenye mahitaji ya kawaida ya kibinadamu. Washiriki wen-

gi walielezea hisia za kudharauliwa na kuhukumiwa.

Hii ni kwa sababu watu wanaangalia zaidi virusi (ambavyo ni

vya kibaolojia) na kutolea sababu zenye utashi (si za kibaiolo-

jia). Si kwamba watu wenye VVU ni watenda dhambi kidogo

kuliko wengine, lakini pia si watenda dhambi wakubwa kuliko

wengine. Uovu na ubaya vinaishi duniani, na sote tuna uovu

na ubaya. Hiki ndicho tulichonacho kimsingi, alisema mshiriki

mmoja. “Lakini tatizo ni kwamba kuna mfano au sura kamili-

fu ambayo watu hudhani ni lazima wafanane nayo,” alisema

Page 15: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

UTANGULIZI 13

mshiriki mwingine; ‘ kutwisha mzigo wa ubaya kwa watu fulani

ni njia ya kulinda ‘sura kamilifu’ tunayopenda kuwa nayo juu

yetu wenyewe. Na ndipo sura hizi timilifu na maumbo zinaleta

ugumu kwetu sisi kujiona na kuwaona wengine kama tulivyo:

tunaumba makundi yasiyo sahihi na kupoteza mawasiliano

na maisha yetu wenyewe, kwa mwelekeo wetu wenyewe ku-

fanya yaliyo sahihi na mabaya.’ Kama suluhisho wale wanao-

taka kurejesha maadili katika jamii huanzisha visingizio vya

“kubeba dhambi”, kama ilikuwa; na kama ikitokea tusikatae

ukweli kuhusu jamii, tunakataa kitu cha muhimu kuhusu sisi

wenyewe kama wahusika.”

Mfumo Gonganishi

Makundi haya bandia huumba tofauti kati ya watu. “Lakini

tatizo ni, ‘alisema mshiriki mmoja’, pia yanasababisha tofauti

hata ndani ya watu. Hivyo mmoja anakwepa kujihusisha yeye

mwenyewe na watu wengine kama tulivyo (au walivyo). Am-

bapo mifumo gonganishi hutokea.: mtu anasema kitu hiki, na

mwindine anafanya au kuishi kwa namna tofauti. Jambo am-

balo ni unafiki. Watu wanaliona hili, na ndiyo sababu baadhi ya

watu wanaacha kwenda kanisani. Lakini ‘kuwa mwanadamu’ ina

maanisha ni kujifunza kuwa sisi wenyewe, si kuendana na sura

halisi ambayo hata hivyo ni bandia. Tusilazimishane kuwa kama

sisi wenyewe na tusihukumiane kwa sababu ya kuwa tofauti.”

Hivi ‘kuwa tofauti’ ina maana gani, basi? ‘Tofauti ina maanisha

kutoweka kwa wazi kutoka sura halisi ya kawaida tuliyonayo

wote, katika mazingira yetu ya ndani. Tukihusianisha sura hii

na mwanadamu halisi, hivyo tumeelemea katika kufanya hu-

kumu zisizo sahihi juu ya wale wasioikubali. Na tunajiweka

mbali nao. Lakini fulani ana mapungufu katika ubinadamu

kwa sababu tu ni wa tofauti.” Kuna utofauti mkubwa miongoni

mwetu, kwa namna ile ile kwamba kuna tofauti ndani ya kila

mtu na kila mmoja miongoni mwetu.

Hofu na Kukataa

Upinzani mwingi juu ya nini ni tofauti ni matokeo ya

hofu.”Lakini kila mtu anaogopa kitu fulani,” Alisema mtu

mmoja. “inahusiana na kuishi. Tunaogopa vitu vinavyotishia

maisha yetu. Na tunajitahidi kukiweka kando chochote ki-

nachotishia maisha yetu.” “Lakini woga mwigi unahusiana na

ujinga, na upendeleo,” alisema mwingine. “Sote tuna upen-

deleo na kukata tamaa. Lakini ni lazima nikubaliane na ukweli

huu na nifanye kitu fulani kuhusu hiki, kama kurekebisha mi-

tazamo yangu mibovu au kuchunguza mapendo yangu.”

Kwa uhakika ni kwamba kuhukumiana kwa sababu ya tofauti

zetu ni kukataa ukweli thabiti kuhusu hali za kibinadamu,

ambao ni kuwa sisi sote tu tofauti, lakini kwa namna fulani,

sisi sote ni sawa.

Biblia yenyewe imetumika mara nyingi kuridhia ubaguzi.

“Kwa mfano, ‘Wamebarikiwa walio maskini wa roho’ wakati

fulani imeonekana kama ujumbe unaoonea unaowaambia

maskini au watu wanaoteseka, ‘kwa kuwa unavyoteseka au

ukiwa maskini hapa duniani, basi utakwenda mbinguni utaka-

pokufa.’ Lakini pengine maana yake ni kwamba, kwa sababu

ya mateso yao, upendeleo maalum hutolewa kwa wale walio

katika mazingira magumu, wagonjwa au waliobaguliwa au

- kwa namna yetu – kuishi na VVU au UKIMWI.”Ni kama ma-

cho yao yamefunguliwa na kuona kitu cha muhimu.” ‘Mtu

hulazimishwa kujishughulisha yeye mwenyewe, kunyenyua

mawe mazito yeye mwenyewe, kama yalivyo na kutafuta

kilichojificha chini yake.”

Hivyo Agano Jipya limekuwa ni maandiko ya kinabii

na ukombozi, ikiongelea udhaifu wetu na uwezo wetu,

dhambi zetu na mazuri, kufanana kwetu na tofauti zetu: na

kusisitiza kuwa yote haya ni sehemu ya nini maana ya kuwa

mwanadamu.

UTANGULIZI

Page 16: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

14 UTANGULIZI

Mahali Salama kwa MazungumzoUmuhimu wa kuwa na sehemu salama kwa mazungumzo mara

kwa mara umesisitizwa. Mjini Oslo, Aksept, kituo kwa ajili ya

yeyote aliyeathirika kwa VVU, mfululizo wa maongezi ulifanyi-

ka kati ya watu walioambukizwa VVU na walioathirika kwa VVU

na UKIMWI kwa namna moja au nyingine. Wazo na hamasa ya

kufanya aina hii ya mazungumzo ilitokana na mtaala wa ma-

fundisho kuhusu mbinu za Kujifunza Biblia iliyotengenezwa

katika kituo cha Ujamaa kilichopo Piertermartzburg, Afrika

ya Kusini. Mazungumzo yaliendelea kwa miezi kadhaa, katika

makundi madogo na makubwa. Kutokana na uzoefu katika

mazungumzo haya – yote hasi na chanya – tulifikia katika mi-

tazamo ya msingi na mashaka yaliyo muhimu ili kufanya maz-

ungumzo haya kuwezekana. Vipengele hivi vifuatavyo vimeo-

nyeshwa kwa mifano kwenye mikutano yetu Oslo.

1. Kuanza kwa Uzoefu

Katika mazungumzo yetu tulifikia katika uzoefu halisi wa maisha

ya watu waliotengwa na kunyanyapaliwa jinsi yalivyokuwa na

kipaumbele tangu tulipoanza. Lakini mara nyingi, wakati mta-

zamo wetu wa kualika jumuia katika mazungumzo ya aina hii

katika Kanisa na miradi ya kithiolojia, imekuwa ni rahisi kuweka

ajenda za mikutano ambazo hazikidhi uzoefu halisi na mahitaji

ya msingi ya washiriki. Katika kujaribu kulikwepa hili, tuliandaa

mkutano wa kwanza kwa misemo mitatu ya ufunguzi.

I. Unyanyapaa ni dhambi

II. kujamiiana ni kuzuri

III. Kanisa lina UKIMWI

Wanawake wawili wenye UKIMWI walitoa madokezo ya utan-

Baadhi ya Madokezo kwa Vitendo

Uzoefu kutoka kwenye kundi Lililopo Oslo

gulizi na waliulizwa kujibu maswali yafuatayo: “Unadhani ajenda

ya kanisa juu ya UKIMWI ni nini?” na “Nini iwe ajenda ya kanisa

kuhusu UKIMWI?”

2. Kutengeneza Nafasi Salama

Tulipokutana kwa mara ya kwanza, tulichelewa kuanza mku-

tano, ili kuona kama wengi wa wale waliokuwa wamesaini kuja

kama wangekuja. Wengi hawakuonekana. Kulikuwa hali ya

kusita. Tutakuta mtazamo gani kwenye kikundi? Washiriki wen-

gi walikuwa hawajamwambia yeyote kuwa walikuwa na VVU.

Lakini ilikuwa wazi walipojieleza wao wenyewe, waliokuwepo

pale kwa sababu ya kazi zao katika kanisa na waliokuwepo pale

kwa sababu VVU ilikuwa sehemu ya maisha yao wenyewe. Huu

ulikuwa mwanzo usio sawia, ingeweza kutisha kwa baadhi na

ilisisitiza umuhimu wa kuwa na nafasi salama.

3. Mahali

Sehemu ya mkutano wetu haikuwa isiyo eleweka. Majadiliano

yetu daima yalifanyika Aksept. Hili limekuwa ni muhimu katika

kutengeneza mfumo salama kadiri inavyowezekana kwa wale

waliosema juu ya uzoefu wao wenyewe katika kuishi na VVU.

4. Washiriki

Ili kuumba ujasiri mkuu kwa ajili ya kushirikishana uzoefu,

mkutano wa pili ulikuwa wa siri, hasa kwa watu waishio na

VVU. Baadaye tuliruhusu mazungumzo kwa washiriki wengi

zaidi, lakini pia tulikuwa na vikundi vidogo vya mazungumzo

ambapo watu wangelizungumza zaidi juu ya mawazo yao na

Page 17: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

UTANGULIZI 15

Mahali Salama kwa Mazungumzouzoefu. Katika Pietermaritzburg zaidi wanafanya kazi katika

vikundi vidogo vya watu waishio katika mazingira magumu,

kwa sababu wamejijengea ujasiri binafsi wa kuongea.

5. Muwezeshaji

Wajibu wa muwezeshaji ni muhimu katika kuweka mazingira:

a) Kusimamia na kupangilia majadiliano

b) Kuhakikisha kuwa kila mtu anayetaka anapewa wasaa wa ku-

shirikisha

c) Kuhakikisha kuwa washiriki wanaruhusiwa kuvunja miiko

6. Kanuni za Msingi

Kanuni zilizo wazi ziliwekwa kwa ajili ya mazungumzo: ni

lazima usikilize, uhusudu na kuonyesha kuheshimu kili-

chosemwa, na siyo kushambulia au kuteketeza yale ambayo

wengine wameyasema. Inaweza kuchukua muda kwako

kutambua nini ni cha muhimu zaidi na kile unachodhani.

Hii hudhaniwa kabla kuwa unajua kuwa utakachosema haki-

takuwa kiini cha kukosoana.

7. Muda

Inachukua muda kutengeneza mahali salama. Na kundi imara

linalokutana mara nyingi daima litatengeneza ujasiri kuliko

kundi ambapo watu huja na kuondoka.

8. Mazingira ya Kukiri

Ya msingi na mara nyingi husahaulika! Lakini mawazo yetu, mi-

tazamo na kushirikishana uzoefu unatakiwa kuthibitishwa na

wengine, tunatakiwa kusikia kuwa yale tunayosema ni sawa au

mazuri au mengine sahihi.

9. Malumbano – Ushiriki Hai

Ukimya unaweza kuwa lugha ya uwezo. Ilitokea mmoja wa

washiriki katika mikutano yetu anayefanya kazi katika kanisa,

aliyekuwa kimya sana alipoulizwa na mmoja wa wanawake

waliokuwa wazi kuhusu maisha yake: “Unafikiri nini?” Jinsi

alivyojibu ilionyesha dhahiri kuwa alishangaa iwapo ukimya

ulikuwa unaficha aina fulani ya ukosoaji.

10. Mifumo ya Utawala

Katika mazingira kama ya VVU na UKIMWI kuna hatari ya kuwa

na ajenda ya siri. Mikutano na majadiliano inaweza isikidhi

matarajio. Uwepo wa mtu mwenye mamlaka katika jamii

au kanisa mara nyingi unaweza kuwafanya watu wengine

kuchukua tahadhali kuhusu yale wanayosema. Je ni salama

kutamka mambo ambayo kanisa mara nyingi linayahukumu

au kulikosoa kanisa kwa nguvu?

11. Kushirikishana

Taratibu, baada ya mikutano kadhaa, ujasiri ulianza kuimarika.

Tofauti miongoni mwetu zilikuwa ndogo na mazungumzo

yetu yakawa kwa undani zaidi. Tulishirikishana mawazo na

maswali, matukio katika maisha yetu, imani, kukata tamaa na

hatari. Kuwa na VVU au kutokuwa na VVU – kimsingi tulikuwa

watu tunaotafuta kitu kizuri kwa ajili ya maisha yetu na maku-

sanyiko yetu.

•KutokakwenyeMalengohadimaandiko

Katika aina hii ya kujifunza Biblia, hatuchagui maandiko yoyote, lakini yale tunayoona muhimu katika utaratibu wa

kushughulika na uzoefu wetu binafsi au masuala yanayohusiana.

•MamlakayaAndiko

Biblia mara nyingine imetumiwa kukandamiza au kuhalalisha ukandamizaji. Ile tu kuwa kitabu cha Kidini, ina

mamlaka kwa watu wengine kiasi kwamba wakati mwingine inawafanya watu kukaa kimya kuhusu maisha yao

binafsi. Hivyo inatakiwa kuelezwa na kutumiwa kwa uangalifu – uangalifu ulio na asili katika Injili yenyewe.

•MwenziwaTatukatikaMazungumzo

Andiko la Biblia linaweza kuwa na kazi ya kuwa mwenzi wa tatu katika mazungumzo wakati mnashirikishana.

Kila mmoja wa washiriki kwenye majadiliano alikuwa na hadithi yake na uzoefu. Ukweli unaweza kuoneka-

na kama upuuzi. Hadithi ya Biblia “kwa sehemu ya tatu” inaweza kuwa hadithi halisi ambayo inaweza kutoa

mwanga katika maisha yetu na kuleta matumaini, au kudhihirisha matumaini ambayo yapo tayari.

Kutengeneza nafasi kwa ajili ya Utaratibu wa Kujifunza Biblia

Watu wengi wamepata uzoefu hasi kwa namna ambavyo Biblia imekuwa ikitumika. Ni

kitabu kilichofungwa kwa baadhi yao. Lakini katika mazingira salama, maandiko ya

Biblia yanaweza kuanzishwa na kuonekana ya maana. Vipengele vya muhimu katika

njia tunazotumia ni:

NORWAY

Page 18: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

16 UTANGULIZI

Hatua ya Kwanza Katika Maisha Yetu

Biblia ni kitabu kitakatifu kwa Wakristo wote. Ni muhimu

katika maisha ya binafsi ya Mkristo na katika kuielewa

jamii. Wengi wanaamini kuwa wale waliosoma Biblia wana

aina fulani ya kanuni inayofungua maandiko mbalimbali

na kwamba haijalishi namna wanavyoyaelewa maandiko.

Tunaelewa kuwa ufahamu wa kithiolojia ni muhimu ka-

tika kujifunza Biblia, lakini tunaamini pia kuwa uzoefu

wetu wa kila siku ni muhimu kwa kuelewa ujumbe uliomo

katika maandiko ya Biblia. Wakristo Amerika ya Kusini na

Afrika ya Kusini wametufumbua macho juu ya umuhimu

kwa watu wa kawaida katika kusoma Biblia. Kanuni ya

msingi ya kujifunza biblia ni kuiainisha Biblia na maisha

ya kila siku kwa kila mmoja wetu, kwa ushawishi kuwa

kuna uhusiano kati ya yale Biblia inasema na yale watu

wanakumbana nayo.

Utaratibu unaoelezewa hapa umesimamia katika tara-

tibu zinazotumika katika kituo cha Ujamaa kilichopo Pi-

etermaritzburg, Afrika ya Kusini. Vikundi vya kujifunza

Biblia huko vimepangwa kutokana na tofauti za watu,

pamoja na watu waishio na VVU na UKIMWI. Hawa wana-

jifunza Biblia kwa kufuata uzoefu wa watu wenye VVU.

Kwa njia hii maandiko ya Biblia yanatoa mtazamo mpya

na wa ndani. Tunaamini utaratibu wao wa kujifunza bib-

lia unaweza kutusaidia kuangalia kwa uwazi mahusiano

yaliyomo kati ya maandiko ya biblia na VVU na UKIMWI na

unyanyapaa.

Mafunzo ya Biblia Yanayomhusisha Mtu

Kama kiongozi wa kikundi cha kujifunza Biblia, jukumu lako

zaidi ni kama muwezeshaji na si mwalimu. Washiriki wasiele-

kezwe maana ya andiko. Wafike katika maana ya andiko kuto-

kana na mazingira yao. Baadhi ya watu hudhani wanajua zaidi

ya wengine! Na kuna wengine wasioamini kuwa tafsiri zao

wenyewe zina umuhimu wowote. Kwa mfano: “Wewe ni mc-

hungaji, huwezi kutueleza maana ya andiko hili?” Ni muhimu

kuwa uweke wazi kwa washiriki wote kuwa uzoefu wao ni

muhimu katika kuelewa andiko. Uchunguzi wa maandiko ya

Biblia si njia inayotakiwa kufuatwa kwa ubinafsi. Ni suala la

tabia katika kusoma Biblia. Kadiri unavyozoea na kuridhika

na utaratibu huu wa kujifunza Biblia, unaweza kujiweka huru

kutoka kwenye maswali. Uchunguzi wa maandiko ya biblia un-

aweza kuelezwa kama tabia nne unapojifunza maandiko:

1. Kusoma Biblia katika mtazamo wa mazingira ya wasomaji

wenyewe na changamoto zinazowakabili.

2. Kusoma Biblia pamoja na wengine.

3. Kusoma Biblia kwa ufasaha na kwa undani.

4. Kusoma Biblia ukiwa na wazo la kufanya siku ya kila mtu na

mabadiliko kijamii.

Tabia Nne za Msingi1. Soma Biblia katika

Mazingira ya Msomaji Mwenyewe

Utaratibu unaotumika hapa ni wa jumla na unaweza kutumi-

ka kwa mada yoyote inayokufurahisha. Tunashauri kuanza

majadiliano kwa maswali yanayosaidia kila mtu katika kundi

kushirikisha uzoefu ambao utaweza kukusaidia kuelewa

ujumbe wa maandiko ya biblia. Kuhusu VVU na UKIMWI

kama mada, kuna watu ambao hawajui ni kwa namna gani

ilivyo kuishi na VVU. Japokuwa unaweza ukawa huna VVU

wewe mwenyewe, tunaamini kuwa unao uzoefu ambao un-

aweza kuutumia.

2. Soma Maandiko Mkiwa Pamoja

Baada ya kushirikisha uzoefu unaohusiana na mada, someni

maandiko ya Biblia. Ni muhimu mkisoma kwa pamoja, kwa

sauti. Kusoma kwa pamoja kunakuwezesha kuielewa kama

kikundi.

Ni vyema kuchagua maandiko ambayo yanahusiana kwa

karibu na mada kadiri inavyowezekana. Inawezekana uka-

ona kuwa Biblia haijishughulishi na mwelekeo wa mada

Utaratibu katika

Kujifunza Biblia

Biblia Kitabu KitakatifuNORWAY

UTANGULIZI

Page 19: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

UTANGULIZI 17

unayofikiria. Kwa mfano VVU havikuwapo nyakati za Biblia.

Lakini kunyanyapaliwa na kutengwa na kuuliza dhambi ya

nani imesababisha magonjwa ni mambo ambayo yaliku-

wapo.

3. Soma Maandiko

Kwa Umakini Na Kwa Kina

Baada ya kusoma maandiko pamoja, mnaweza kuuliza-

na maswali ambayo yatawasaidia kuingia katika andiko.

Mshiriki mmoja aandike maneno ya msingi katika karatasi

kubwa na kuzibandika katika ukuta. Kwa njia hii kila kitu kili-

chosemwa kitasikika na kuangaliwa kwa umakini.

Kwanza, baadhi ya maswali ya jumla:

• Maandikoyanahusunini?

• Makusudi na malengo yapi yameshughulikiwa katika

maandiko?

• Nini kilikustusha sana kuhusu maandiko haya? Halafu

chunguza maandiko kiundani:

• Naniwanahusikakatikahadithihii?

• Tunajifunzaninikuhusuwahusikakatikahadithihii?

Tumia muda katika maswali haya na ruhusu muda fulani kwa

ajili ya vitu fulani vilivyotajwa ili kuamsha mawazo mapya

kwa wengine. Unaweza kumuuliza mtu kueleza kwa undani

zaidi Kuhusu kile alichosema. Lakini usithubutu kusema si

sahihi. Kila mmoja wetu tunaangalia kwa miwani ambayo

maisha yetu na uzoefu vimetupa.

Wakati mwingine inaweza kusaidia ikiwa washiriki

wataachwa kujadili baadhi ya maswali katika jozi au kuy-

atafakari kila mmoja peke yake kwa kipindi kifupi kabla ya

kushirikisha majibu yao kwa kikundi chote.

Inaweza kuwa na msaada pia kwa kuangalia uhusiano kati

ya mtu katika maandiko, pia kijamii, kisiasa, kidini na kiu-

chumi

• Mahusianoyawatuuliowasomayanahusunini?

• Wanachukulianajewaokwawao?

• Jewanamahusianotimilifu?

Unapokuwa umeelewa yote haya unaweza kujaribu kudha-

ni ni nini mtu katika maandiko anafikiri kuhusu maisha na

kuhusu Mungu. Ikiwa unaangalia katika moja ya vitabu vya

injili. Unaweza pia kuangalia namna Yesu anavyomwelezea

Mungu katika maandiko katika maswali.

• NiniuelewakuhusuMungualionaomtu?

• Nininikiletachotumaininamwangakatikamaandiko?

Baada ya kuwa umeyachunguza maandiko ya Biblia kwa

umakini, ni muhimu

Ukiyageukia maisha yako na hali zako mwenyewe.

• Nani miongoni mwetu ana uzoefu unaoendana au ulio

sawa na mtu aliye katika maandiko?

• Tunahusianajesisikwasisikatikahalizanamnahii?

• Tuhusianevipisisikwasisi?

Unapoongea kuhusu hali za siku za leo, unaweza kukagun-

dua kuwa ni muhimu kurudi katika maandiko na kuangalia

yanasema nini. Hii inasaidia kufungua mazungumzo kati ya

maandiko na hali zetu wenyewe. Unaweza kupata ufafanuzi

katika uzoefu wako wewe mwenyewe ambao ghafla utaku-

saidia kuona mambo mapya katika maandiko na kitu fulani

kipya kuhusu wewe.

4. Soma Maandiko Ukiwa na

Matazamio ya Kubadilika

Usomaji wa Biblia haukomi mpaka pale unapoona kile unachowe-

za kufanya kuleta matumaini katika maandiko katika siku za leo.

• Tunawezakufanyaninikukomeshadhulumaleo?

• Tunawezaje kuboresha maisha kwa wale wasio tendewa

haki?

Wakati mwingine mabadiliko ya muhimu sana ni pale am-

bapo malengo yanaletwa na kujadiliwa. Nyakati nyingine in-

aweza isieleweke nini unachoweza kufanya. Lakini unaweza

kupiga hatua kidogo kuyaboresha maisha ya mtu fulani. Un-

aweza kufanya kitu kutengeneza hali ya uwazi kuhusu kitu

ambacho kimekuwa kigumu kukiongelea, pingana na tabia

zisizofaa, anzisha mradi au anza kuwa na mawasiliano na

watu unaojua wanapambana na maisha yao.

Page 20: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

18 UTANGULIZI

Utaratibu wa VitendoZAMBIA

Kujifunza Biblia

Hatua zifuatazo zinaweza kufuatwa katika mifumo tofauti ya ku-

jifunza Biblia. Lakini mambo matatu mara nyingi ni ya muhimu:

1. Maisha ya Kiroho – Kukosekana hili husababisha kukosekana

kwa majadiliano kitaaluma.

2. Kutumia Akili – Kukosekana kwa nidhamu kiakili na kufikiri

kwa kina husababisha “mawazo mazuri” yasiyo na msingi, pia

mitazamo isiyo sawia.

3. Utashi – kukosekana kwa utashi wa kutii kunasababisha ku-

tojifunza kwa vitendo.

1. Soma Maandiko Kwa Uangalifu

Fanya uchunguzi wa awali. Soma kipengele mara kadhaa, iki-

wezekana katika tafsiri tofauti. Andika kila wazo litakalokujia.

Amua aina ya uandishi kama ni shairi, nathari, historia au hoja.

2. Kujifunza kwa Undani

Jaribu kuandika katika sentence moja kusudi la muhimu lili-

lomo katika fungu la maandiko.

3. Kugawanya Maandiko

Tafsiri za kisasa zimewekwa katika aya. Lakini inawezekana

kuzigawanya aya hizi

4. Miunganiko

Maandiko mengi yameunganika. Ni lazima tujaribu kuvumbua

maunganiko kati ya aya. Maneno “sasa basi” na “basi” ni mfano

wa hili: Warumi 6:1 na 8:1.

5. Vielelezo

Tunahitaji vielelezo kutusaidia katika mawazo yaliyofupishwa,

kama mifano ya Yesu na namna alivyotumia maneno kama

mwanga, chumvi nk.

6. Marudio

Mwalimu yeyote mzuri anajua thamani ya marudio. Zingatia

mlinganyo uliomo katika Zaburi: Ushairi katika Biblia ni wa mar-

udio; mwandishi anaeleza ukweli katika njia moja na pia ukweli

huo huo katika mfumo mwingine. Mfano Zaburi 42:1-2

7. Mhusika

Wakati mwingine tabia hutajwa ili kusisitizia pointi. Jaribu

kutafuta zaidi kuhusu mtu huyo. Tofauti inaweza kuonekana

miongoni mwa wahusika, kwa mfano Mafarisayo na watoza

ushuru, Luka 18:9-14.

8. Mtazamo Wetu Kwa Masuala Ya Kisasa

Iwapo tunaiamini Biblia mtazamo wetu utakuwa tofauti ku-

toka kwa ule wa wengine wengi. Kwa mfano hatutashawi-

shika na hali au mazingira. Tutaichukulia biblia kama ni

sahihi katika hali zetu za sasa. Masuala fulani yameshughu-

likiwa kwa uwazi. Matatizo mengine hayajashughulikiwa –

tunatakiwa kuanzisha utaratibu tofauti wa kujifunza juu ya

matatizo haya.

9. Kutafuta Kanuni

Kukuongoza kufikia Majibu

Kama wakristo ni lazima tuambatanishe maisha yetu

kwa Kristo, hivyo tutapata miongozo kwa masuala yenye

utashi kwa asili ya Mungu na kwa lipi Mungu amelidhi-

hirisha kuhusu makusudio yake kwa ajili yetu. Vipengele

vifuatavyo vinaweza kuunda mfumo ambao utatuwezesha

kufikia hitimisho kuhusu matatizo mengi yanaotokea siku

za leo:

Upendo wa Mungu – Kumbukumbu la Torati7:6-8 Warumi 5:6-11

Haki ya Mungu - Kumbukumbu la Torati32:4, Warumi 3:21-26

Utakatifu wa Mungu – Mathayo 5:48

Mungu ni Muumbaji – Mwanzo 1:2, Zaburi 8:5-8

Mungu ni Mtunzaji – Mathayo 6:25-33

Mungu ni Mkombozi – Waefeso 1:7

Mungu ni Hakimu – Mathayo 25:31 – 46

Sisi ni watumishi wa ulimwengu – Mwanzo 1:28-30

Tunategemeana sisi kwa sisi – Mwanzo 4:9-11, Walawi 19:18

10.Jinsi ya Kutumia Kanuni

Kwanza kusanya taarifa nyingi kadiri inavyowezekana

kuhusu tatizo la kushughulikia na amua kanuni ipi

ya biblia inahusika. Soma kwa uangalifu vifungu vya

maandiko vinavyoonekana kuoana. Tengeneza wasaa

kwa mazingira yanayobadilika tangu nyakati za Biblia.

Iwapo kanuni inaonekana yenye kukinzana, kwanza

angalia tafsiri yako. Kama bado kuna mikinzano amua

kanuni ipi ni ya juu. Kumbuka kutofautisha kwa uan-

galifu kati ya mawazo yako mwenyewe na mafundisho

ya Biblia.

Page 21: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

UTANGULIZI 19

Kwa maana mwili si kiungo kimoja bali ni vingi.

Mguu ukisema kwa kuwa mimi si mkono, mimi si

wa mwili, je! Si wa mwili kwa sababu hiyo? Na sikio

likisema kwa kuwa mimi si jicho, mimi si la mwili,

je! Si la mwili kwa sababu hiyo? Kama mwili wote

ukiwa jicho ku wapi kusikia? Kama wote ni sikio

ku wapi kunusa? Bali Mungu amevitia viungo kila

kimoja katika mwili kama alivyotaka. Lakini kama

vyote vingekuwa kiungo kimoja mwili ungekuwa

wapi? Lakini sasa viungo ni vingi, ila mwili ni mmo-

ja. Na jicho haliwezi kuuambia mkono , sina haja

na wewe, wala kichwa hakiwezi kuiambia miguu

sina haja na ninyi. Bali zaidi sana vile viungo vya

mwili vidhaniwavyo kuwa vinyonge zaidi vyahita-

jiwa zaidi. Na vile viungo vya mwili vidhaniwavyo

kuwa havina heshima, viungo vile twavipa heshima

zaidi, na viungo vyetu visivyo na uzuri vina uz-

iri zaidi sana. Kwa maana viungo vyetu vilivyo na

uzuri havina uhitaji; bali Mungu ameuungamanisha

mwili, na kukipa heshima heshima zaidi kile kiungo

kilichopungukiwa, ili kusiwe faraka katika mwili,

bali viungo vitunzane kila kiungo na mwenziwe. Na

kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia na-

cho, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote

hufurahi pamoja nacho.

1KORINTHO 12:14-26

Mwili Mmoja

Page 22: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

20 KANISA

Page 23: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

KANISA 21

au walioathiriwa na VVU na UKIMWI. Kwa nyakati fulani, Sakra-

ment imekataliwa kwa watu waishio na VVU, ibada za mazishi

zimekataliwa kwa watu waliokufa kwa UKIMWI na hatujawafariji

wasio na matumaini. Tunakiri kuwa kanisa limekataa wakati li-

lipotakiwa kukumbatia na kuhukumu lilipotakiwa kuonyesha

upendo, huruma na uangalizi. Tunatubu dhambi hizi. Kwa hiyo

tunajiweka sisi wenyewe katika kukubali kwa uaminifu kuvunja

ukimya, kusema kwa uwazi na kwa ukweli kuhusu kujamihiana

VVU na UKIMWI. AMINA.

6. Kutangaza Msamaha na Neema

K: “Hili ni Agano nitakalo agana nao baada ya siku hizo, asema

Bwana: Nitaweka sheria zangu katika mioyo yao na kuziandika

katika akili zao, sitazikumbuka dhambi zao na matendo yao

maovu milele.” Waebrania 10:16-17.

7. Wimbo wa Kusifu na Shukrani

8. Ombi la Ufunguzi wa Neno la Mungu

K: Mungu baba yetu neno lako ni taa kwa miguu yetu, bila hiyo

tunapotoka. Fungua macho yetu na masikio yetu ili tuweze

kuona na kujua siri zilizofichwa katika neno lako. Baba, tu-

fundishe kupitia neno hili. Katika jina la Yesu Kristo tunaomba.

AMINA.

9. Kusoma Neno

1 Korintho 12:14 – 26

10. Mahubiri

• Huuniwitokwakanisadunianzimakukubalikuwajangala

VVU na UKIMWI ni kama lake;

• Kanisa lisikubali tu kuwa VVU vipo katikati yake, bali litoe

kwa ukamilifu na kukubali kwa uwazi na kuwajali kwa up-

endo walioathirika na kuathiriwa.

11. Maombi Baada ya Mahubiri

12. Wimbo wa Kufunga

13. Baraka

W: Mungu baba mwenye huruma na upendo atukuzwe milele

na milele kupitia Yesu Kristo Bwana wetu. AMINA.

ZAMBIA

Kanisa Lenya HurumaLiturjia

Katika kanisa la “Reformed” nchini Zambia mchungaji mmoja

ambaye ni mratibu wa VVU/UKIMWI, aliunda liturjia hii na kui-

tumia kwa baadhi ya vikundi vya watu waishio na VVU nchini

Zambia.

K = Kiongozi

W = Wote

1. Wito Kwa Ajili ya Kuabudu

K: Bwana apewe sifa! Asifiwe, O watumishi wa Bwana, Lisifiwe

jina la Bwana! Libarikiwe jina la Bwana kuanzia wakati huu na

milele.

Kaka na Dada katika Yesu Kristo: Tumekutanika leo mbele za

Mungu baba yetu mwenye huruma na upendo. Kwa hiyo kwa

mioyo ya unyenyekevu tumwabudu kwa maombi, nyimbo na

sifa. AMINA

2. Nyimbo za Sifa

3. Maombi ya Ufunguzi

W: Mpendwa Mungu, Tunalitukuza na kulisifu jina lako kwa

sababu ya upendo na ulinzi unaotupa kila siku katika maisha

yetu. Asante kwa upendo na ulinzi unaoendelea kutupa hata

leo.

Bwana tumekutanika kudai kupotea kwa asili ya kanisa lako

katika ulimwengu huu ulio katika maumivu kwa sababu ya

janga la VVU na UKIMWI.

Bwana kama kanisa tumekuwa kimya kwa masuala ya VVU na

UKIMWI na kwa kufanya hivyo tumejitenga na huduma yako

na watu wako walioathiriwa na ugonjwa huu. Tunaomba msa-

maha wako.

Bwana tunakuomba kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo

kubadili mafundisho yetu na matendo kwa kaka na dada zetu

walioathirika au kutoathirika kwa VVU. Tupe moyo usiohu-

kumu bali unaopenda na kujali. Katika jina la Yesu tunaomba.

AMINA.

4. Wimbo

5. Toba ya Pamoja

W: Tunakiri na kukubali kuwa sisi kwa namna fulani tu-

mechangia unyanyapaa na ubaguzi na kwamba makanisa yetu

hayajawa salama au mahali pa ukaribisho kwa watu waishio

KANISA

Page 24: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

22 KANISA

Agano la Kale linatuambia kuwa watu waliokuwa na ukoma

na kifua kikuu walisahauliwa na kutengwa na jamii ambamo

waliishi (Walawi 13). Jamii kwa ujumla imerithi tabia hii ya ku-

nyanyapaa watu wanaoteswa na magonjwa yanayochukuliwa

kuwa sugu. Lakini Bwana ni ndiye mwangalizi wa majira yote

na sehemu kwa sababu anajua ali za watu wake katika magon-

jwa na afya njema.

Ni kwa sababu hii kanisa lazima lifanye kazi na watu walio-

athiriwa au kuathirika kwa VVU na UKIMWI ili kuwasaidia kuwa

na imani, kwa kuwa ni kwa imani milima huhamishwa, dhoruba

hupoozwa na miujiza kutendeka. Ni muhimu kuwakumbusha

wale wanaoteseka kuwa ni Mungu pekee ndiye anayeweza ku-

kubali hali zote za kibinadamu na kwa kufanya hivyo tutawasa-

dia kuponya hali zao za kiroho. (Waebrania 10:39). Kwa mtaza-

mo huu imani huja kama silaha muhimu, ambayo ni muhimu

na imara katika kuelewa changamoto ya VVU na UKIMWI. Biblia

inatueleza kuwa Ayubu aliteseka sana lakini uvumilivu wake

katika imani ulimfanya kumshinda mwovu.(Ayubu 1:14-21)

Katika maandiko, injili ya Yohana 8:1-11 inaelezea kisa kati

ya Yesu Kristo na mwanamke aliyezini. Ukweli kwamba Yesu

hakuruhusu mwanamke apigwe mawe ni ishara iliyo wazi ya

ulinzi na kuwaangalia watu waliokataliwa na jamii.

Mfano mwingine uliotolewa na Yesu Kristo unapatikana ka-

tika Injili ya Mtakatifu Mathayo 8:1-3. Hapa ni pale Yesu alion-

yesha upendo kwa kumgusa mtu mwenye ukoma, aliyekuwa

ametengwa kufuatana na sheria ya Musa.

Kwa kumgusa mwenye ukoma Yesu Kristo alionyesha up-

endo alionao kwa kila mtu bila ubaguzi na alivunja desturi za

kukataliwa na kubaguliwa kwa wanaoteseka kwa ukoma.

Tukiongelea kithiolojia, katika mfano huu Yesu Kristo ameo-

nyesha kuwa ugonjwa na udhaifu wa kibinadamu hauwakilishi

matakwa ya Mungu.

Katika baru yake kwa Warumi 3:10, Paulo anaonyesha ukweli

dhahiri kwa wakristo wote kwa kueleza, “ hakuna mtu liye safi.

Hata mmoja.” Kwa upande mwingine, Isaya 6:5 pia inaonge-

za, “Maana hata mimi ni mtu nisiye na midomo iliyo safi na

ninaishi kati ya watu wasio safi.” Kwa hiyo tendo la kusafisha

midomo hutokea kama ishara ya shukrani kwa Mungu. Ni kwa

neema yake tunachukuliwa kama wasafi. Hatuna haki ya kuwa-

cheka wengine. Hii ndiyo maana kuwanyooshea vidole watu

wenye VVU na UKIMWI si haki bila kujali namna au sababu ya

kuathirika kwao.

Mfano mwingine wa Yesu Kristo unapatikana katika Injili ya

Marko 10:46-52. Hapa kipofu Batimayo, mwana wa Timayo

aliyekuwa ametengwa na jamii yake katika mji wa Yeriko, baa-

da ya kusikia kuwa Yesu wa Nazareti alikuwa akipita, alianza

Mtazamo Wa Kibiblia:

Ugonjwa, Unyanyapaa Na Wajibu Wa Kanisa

Kuwakumbatia WaliosahaulikaMSUMBIJI

Page 25: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

KANISA 23

kupiga kelele: “Yesu mwana wa Daudi Unihurumie!” Bila ku-

jali mwitikio wa wafuasi wa Yesu na umati wa watu uliokuwa

unamfuata, Yesu alisimama na kumwita Batimayo na kufanya

aone tena.

Leo hii, Batimayo anamwakilisha dada au kaka aishiye na VVU

na UKIMWI. Na kanisa na viongozi wake wameitwa kufungua

macho yao, kufikiri na kusikia sauti ya Batimayo, ambaye kati-

ka jamii ya leo ni watu waishio na VVU na UKIMWI, ambao wito

wao kwa matendo ni kwa kanisa na jamii kwa ujumla.

Upendo na huruma vinaonyesha huduma ya Yesu na anaku-

wa wa muhimu juu ya wote wale walioitwa kwa jina lake Kristo.

Kwa hiyo, kama wakristo tumeitwa kupenda na si kuhukumu.

Yesu mwenyewe alitupa mfano kwa namna alivyoonyesha up-

endo na huruma kwa wale waliokuwa wakiteseka nyakati zake.

Kwa yesu, Upendo lazima uonyeshwe katika “pendaneni ninyi

kwa ninyi kama unavyojipenda mwenyewe” na hurumia “ kwa

kusudio na kuteseka na mwingine”.

Ni wajibu wa kanisa kuwa karibu na watu waishio na VVU na

UKIMWI, ili weweze kuuona uso wa Mungu. Kanisa lina wajibu

wa kuwafanya watu waishio na VVU na UKIMWI kuelewa kuwa

Mungu anampenda kila mtu. Ndiyo maana alimtoa mwanaye

Yesu Kristo, ili kwamba wale wanaoamini kupitia yeye wasian-

gamizwe bali wawe na uzima wa milele.

KANISA

Kanisa limeitwa kuwa sauti ya kinabii na taasisi

inayoponya, kama sehemu ya safari ya kupiga

vita unyanyapaa na kubaguliwa. “Café Ecuméni-

co” ni jina lililotolewa kwa mradi unaoleta watu

wenye au walioathiriwa na VVU na UKIMWI, uon-

gozi wa kanisa, mtandao wa wachungaji walio

katika mapambano na VVU na UKIMWI na vyama

vya kijamii. Malengo yake makuu ikiwa ni kuli-

fanya kanisa kuwa wazi na sehemu salama kwa

mitazamo ya kawaida na mijadala juu ya VVU na

UKIMWI.

Mara moja kila mwezi, watu hukutana ku-

jadiliana masuala yanayohusu VVU na janga la

UKIMWI. Wanakutana chini ya mradi wa Kuzuia

na kuondoa VVU na UKIMWI, kwa ubia na Baraza

la Kikristo la Msumbiji, Mtandao wa Wachungaji

katika Kupambana na VVU/UKIMWI katika jiji na

jimbo la Maputo, chama cha watu waishio na VVU

na UKIMWI kilichopo katika eneo liitwalo ‘Caniço

Residential Area’ na World Relief.

Kwa sasa kuna zaidi ya wanachama 140 kati-

ka Chama cha watu waishio na VVU na UKIMWI

pale Polana Caniço Residential Area na kama 30

watumishi wa kanisa wanachama wa Mtandao

wa Wachungaji katika Kupambana na VVU na

UKIMWI. Wanahusika katika nafasi muhimu ka-

tika kuunda mtandao wa masaidiano. Baadhi ya

wachungaji wanatoka katika makanisa ambayo

si wanachama wa Baraza la Kikristo la Msumbiji,

inayoleta changamoto mpya katika “Café Ecu-

ménico’.

Mgahawa wa Kiekumenia

Page 26: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

24 KANISA

NA CARINA WØHLK

Katika kipindi cha miaka michache, kusanyiko la watu wa-

chache ambao wanaishi au wameathirika kwa VVU na UKIMWI

limeundwa ndani ya kanisa la Roho Mtakatifu katika jiji la Co-

penhagen, ambako kuna kituo kinachojishughulisha na VVU

na UKIMWI. Uanzishwaji halisi wa kusanyiko ulitokea sambam-

ba na faragha kwa ajili ya watu wenye VVU na UKIMWI mwaka

1999. Kusanyiko limeongezeka haraka na kimya – pamoja na

kusanyiko la kuabudu na kusanyiko lingine maalum liabudulo

usiku.

Juhudi za kuanzisha kusanyiko la wenye VVU zilianzishwa na

watu wenye VVU wenyewe. Walisema wanahitaji kuabudu na

kukusanyika katika mazingira ya Kikristo. Ombi lao linaeleweka

ninapofikiria kuhusu upweke ambao mara nyingi ninauona ku-

husiana na huu ugonjwa hatari na unaounda desturi fulani. Ka-

tika ushauri wangu wa kichungaji, nimekutana na seti mbili za

matatizo yanayohusiana na upweke: hiari na usio wa hiari.

Upweke wa hiari unatokea kwa watu wenye VVU, kutokana

na matatizo mengi ya kijamii na viwewe vinavyohusiana na

ugonjwa walionao, wamechagua kujitenga na jamii. Wanata-

futa maisha yao ya pekeee na jamii zao bila mahusiano yoyote

ili kukwepa kupoteza mengi.

Upweke usio wa hiari ni tatizo la watu wenye VVU ambao wa-

mekataliwa na kutengwa na jamii kwa sababu ya kuwa na VVU.

Wamesukumwa mbali na hawajaribu kutafuta mahusiano na

jamii kwa kuogopa kulaumiwa na kutupwa.

Kuushinda Upweke

Katika Warumi 14:7-8 Paulo anaandika, “Hatuishi kwa ajili

Ushauri wa Kichungaji na Kazi za Kikanisa Miongoni

mwa Watu Waishio na VVU na UKIMWI

yetu wenyewe na hatufi kwa ajili yetu wenyewe. Kama tukiis-

hi, tunaishi kwa ajili ya Bwana na kama tukifa tunakufa kwa

ajili ya Bwana: Kwa hivyo sasa, iwapo tunaishi au kufa, sisi ni

wa Bwana.”

Maneno haya yanaweza kuongelea moja kwa moja juu ya

upweke ambao watu wengi wenye VVU wanauona – kama

ukumbusho kutoka kwenye injili kwamba hatujatengwa,

hata kama wakati fulani inaonekana hivyo.

Kwa jinsi ninavyoona, kanisa lina mchango kiasi fulani ku-

wezesha kuushinda upweke. Katika Ukristo, wanadamu

wote wameumbwa kwa sura ya Mungu na wana thamani in-

ayolingana.Tunaishi kwenye mwili mmoja. Mtiririko huu wa

mawazo una maana kuwa unaunganika na kutegemeana na

wanadamu wengine. Tunategemeana, ili maisha yaendelee.

Lakini kwa hakika kuna tabia, hata katika kanisa kuwa kudha-

ni baadhi ya watu ni bora zaidi kuliko wengine na hii ni tishio

kwa kanisa.

Mwaka mmoja uliopita, baada ya safari yangu Zambia amba-

po nilijionea kwa mara ya kwanza ukubwa wa janga, nilihubiri

katika Kanisa la Roho Mtakatifu. Katika mahubiri yangu nilitu-

mia usemi “kanisa lina UKIMWI” ili kuhamasisha mshikamano

na roho ya uwajibikaji kwa wakristo. Usemi huu ulionekana

ni wa makosa. Wasikilizaji walisikia kitu kimoja tu; kwamba

kanisa linaumwa na kwamba ugonjwa unahusiana na ngono.

Lakini msisitizo wangu ulikuwa na hakika ni kwamba VVU

na UKIMWI unatuhusu sisi sote. Janga la UKIMWI ni changa-

moto kwetu sisi sote. Kama wakristo ni lazima tuhusike na

maumivu ambayo kaka na dada zetu katika kristo wanapitia.

Lazima tuonyeshe huruma na kuwajibika kama tunataku ku-

towesha janga hili.

Kutengeneza Jumuia Mpya Zenye Tumaini

DENMARK

KANISA

Page 27: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

KANISA 25

Iwapo tutakuwa pamoja, tunaweza kuuondoa ugonjwa na

chuki miongoni mwetu. Kanisa linatakiwa kujifungua kwa ajili

ya kusanyiko linaloweza kumkumbatia kila mmoja. Na katika

kusanyiko hili tunaweza kusababisha uwezekano wa kuwa

wazi, kama vile tulivyo.

Kuanzisha Mtandao wa Sharika

Kusanyiko la wenye VVU katika Kanisa la Roho Mtakatifu ni

mfano wa mtandao wa kijamii na kiroho kwa ajili ya watu wali-

oathirika kwa VVU na UKIMWI. Kwa kuanzia, mtandao ulikuwa

dhaifu na wa kificho. Huduma mara ya kwanza zilitolewa kwa

watu wenye VVU tu, kwa sababu wanachama wake hawakuta-

ka kujulikana. Kulikuwa hali ya kutengwa, lakini sababu iliku-

wa uzoefu uliokuwepo wa kuhukumiwa na Wakristo wenzao.

Kadiri muda ulivyokwenda, Wakristo wenye VVU wameweza

kuaminiana na kuwa wazi. Wameanza kujisikia huru na kuan-

za kuaminiana na kutegemeana kuhusuana

na wahudumu na kusanyiko lote ndani ya

kanisa.

Leo hii, ibada ni kwa wote walioathiriwa

na VVU/UKIMWI na si kwa wale walioam-

bukizwa tu. Hii ina maana kwamba wale

walioathiriwa, familia zao na marafiki, wa-

fiwa, walioajiliwa kati kazi inayohusiana na

masuala ya UKIMWI nao wanakaribishwa.

Kusanyiko la wenye UKIMWI halijafikia ki-

wango ambacho litaweza kugonga kengele

na kufungua milango wazi, lakini malengo

yamekuwa ni kuchangamana.

Mara nne kwa mwaka, Januari, Aprili, Julai na Oktoba, ibada

kwa wenye VVU huchukua sura ya Sakramenti takatifu ikifu-

atiwa na chakula cha pamoja. Ni muhimu kwamba mikusa-

nyiko hii iwavutie washiriki wengi – kwa kawaida zaidi ya 20.

Wanafanya aina mbili cha kusanyiko – mezani pa Bwana za

katika meza ya chakula.

Washiriki wanapata wasaa wa kuhusiana - na watu wengine

na Mungu. Alama ya muhimu kwa Ukristo, msalaba, unatuo-

nyesha umuhimu wa kutoka nje kwa ajili ya uzima.

Wanadamu wanahitaji msingi ulio imara na mahusiano ya

karibu. Hii inatumika si kwa wale wenye VVU, ambao wame-

poteza sana na mahusiano yaliyovunjika, kukataliwa sana,

ndiyo, pengine hata hisia za kuwa wamekataliwa na Mungu.

Ni matumaini yangu kuwa, kadiri muda unavyoenda, kuta-

kuwa na utashi mwingi kila mahali kuwakumbatia wale wais-

hio na VVU na UKIMWI. Tunahitaji Kusanyiko la Kikristo lililo-

wazi lenyewe.

Page 28: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

26 KANISA

Katika mazungumzo Oslo, Noway, yaliyowahusisha watu

waishio au walioathirika kwa VVU, moja ya mambo ya muhimu

ilikuwa kwamba ‘sisi sote ni wabeba mazuri na maovu.’ Tu-

natengeneza makundi yasiyo sahihi na kutosema kweli

kuhusu sisi wenyewe ikiwa tunabebesha mizigo ya uovu watu

wengine. Japokuwa tu watu tofauti kama watu sote ni sehemu

ya mwili mmoja. Hii ni sehemu ya liturjia hii. Maneno ya utan-

gulizi na malalamiko ni nukuu za mazungumzo. Ni vyema ku-

wafanya watu tofauti wengine kusoma maandiko tofauti.

K = Kiongozi

M = Msomaji

W = Wote

1. Utangulizi

K: Unachomfanyia mwingine, unajifanyia mwenyewe na sisi

sote. Katika ufahamu wa ndani, sisi ni mtu mmoja. Mwili

mmoja. Tunapomharibu mtu mmoja, tunaharibu kitu fu-

lani ndani yetu pia na kama madhara kitu fulani katika ubi-

nadamu. Lakini hii haimanishi kuwa sisi wanadamu tunafa-

nana. Kunatofauti kubwa miongoni mwetu, katika njia sawa

kwamba tofauti ipo ndani ya kila mtu kati yetu.

2. Wimbo

3. Malalamiko

Wasomaji wawili kutoka nyuma ya madhabahu:

W: Lini, Ee Bwana Utanisahau milele?

M1: Ni kama vile watu wananikwepa, wananisengenya,

wananichukulia kama vile ni wa tofauti. Wanadhani nime-

haribikiwa. Nimetengwa.

M2: Sithubutu kumweleza mtu ye yote kuwa nina VVU, kwa

sababi sifahamu wengi watalipokeaje.

M1: Nimeumizwa na kuchoshwa kwa maswali mengi! Ni

hitaji la kibinadamu kuwa na mwandani; Nina mahitaji pia,

hamu ya kuwa na watoto, hamu ya kuwa na mume.

M2: Baadhi ya watu wanaona virusi pekee, hawanioni mimi!

M2: Ninaogopa sana kukataliwa au kuvunjwa moyo. Sid-

hubutu kuwa katika mapenzi.

M2: Kwa nini inaonekana kama vule Mungu anakasirika ni-

napojitahidi kufanya vizuri?

M1: Nimemtafuta Mungu anayenipenda, asiyenihukumu

na ambaye anaweza kunisaidia kukubali VVU na kuwa huru

kuokana na mashutumu. Sikumpata kanisani. Umekuwa ni

utafiti wa upweke.

W: Mpaka lini, Ee Bwana? Utanisahau milele?

4. Ukiri wa Pamoja Ulio Sahihi

Soma kutoka upande mmoja wa madhabahu:

M: Tunakiri kwamba sisi ni sehemu ya vyote alivyoumba

Mungu na aliviona kuwa ni “vizuri sana” kwamba sote tu-

nasehemu katika ya vizuri hivyo na ndani yetu uzuri unakaa.

Tunakiri kwamba mtu wentu wa ndani, na miili yetu pia, ma-

hitaji yetu na hamu yetu vyote ni sehemu ya sura ya Mungu

ndani yetu.

Tunakiri kuwa sote tuna thamani na kwamba tuna thamani kwa

sababu sote ni uumbaji wa Mungu, kwa sababu tupo na tunaishi

5. Kimya au Wimbo

6. Uthibitisho wa

Kushiriki Katika Uharibifu

Soma kutoka upande mwingine wa Madhabahu:

M: Tunakiri kushiriki katika kuunda makundi na kutenga baa-

dhi ya watu wakati tunawaingiza wengine.

NORWAY

Kuwa Mwili Mmoja

Liturjia

KANISA

Page 29: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

KANISA 27

Tunakiri hisia zetu, kwamba tunaogopa yale yasiyozoeleka

na kwamba tumechangia tabia ya watu kujiona wametengwa,

wamenyamazishwa na kubaguliwa.

Tunakiri kuwa tumejihusisha zaidi na hadhi ya mtu na kuwa

tofauti zaidi kuhusu hali zao za ndani, umuhimu wao na ubi-

nadamu wao wa kawaida.

Tunakiri kuwa kuwa mara nyingine tunaona baadhi ya watu

au vikundi fulani vya watu kuwa ni waovu na kwamba hat-

uoni kuwa sisi ni sehemu ya uovu na wema.

Tunakiri kutotenda haki kuwa wenye nguvu, afya na mata-

jiri kati yetu wanapewa kipaumbele, wanahudumiwa vizuri

na kwa njia hiyo tunapata hata zaidi.

Tuangalia kwa huruma, tusamehe, tusafishe na tufanye wa-

takatifu.

7. Kimya au Wimbo

8. Ukiri kwa Usawa Wetu Kibinadamu

Soma kutokea katikati ya madhabahu

M: Tunakiri kuwa sehemu yetu ya ubinadamu imeumizwa

na kujeruhiwa, i uchi na kudhalilika.

Tunakiri kuwa tu sawa kibinadamu. Ambapo hakuna hata

mmoja aliye juu au chini ya wenzake, hakuna aliye mwema

au mbaya zaidi ya wengine. Tunakiri kuwa sisi ni tofauti,

aina na maumbile tofauti ambayo vyote ni sehemu ya ubi-

nadamu mmoja: kwamba sisi ni sehemu ya mwili mmoja,

kanisa moja – ambako wa mwisho ni wa kwanza na ambako

nguvu ni ya yule aliye mnyonge.

9. Ukiri Kwa Upendo wa Mungu

K. Unapendwa, zaidi ya unavyofahamu – unapendwa, umesa-

mehewa na kukombolewa.

10. Kusoma Maandiko

Luka 13:10-17

11. Ukiri wa Imani

W: Tunaamini katika Mungu aliye Upendo;: aliyetuumba kwa

upendo; anayeteseka tunapoteseka na aliye kazini duniani

kwa ajili ya mema.

Tunaamini katika Mungu ambaye hatumi magonjwa au

mateso mengine kama adhabu kwa dhambi.

Tunaamini katika Yesu Kristo, aliyejichukulia miili na damu

yetu; aliyetuonyesha namna Mungu alivyo; anayewaweka

watu juu ya sheria na kanuni; atusafishaye na kutuweka

huru kufuata njia ya upendo.

Tunaamini kuwa Yesu Kristo hawezi kumilikiwa au kutawa-

liwa na yeyote na kudhibitiwa na sheria na taratibu.

Tunaamini katika Roho Mtakatifu ambaye hatuondoi ka-

tika miili yetu au maisha ya duniani na ambaye hawafanyi

baadhi ya watu waumini wazuri kuliko wengine.

Tunaamini kuwa sote ni sehemu ya kanisa, na kwamba

sote ni jumuia inayong’ara, katika kanisa hili hakuna hata

mmoja ambaye kwa maana amewekwa nje, katika kanisa

hili watu hupata msaada kukubali na kujipenda wenyewe na

kupenda jirani zao.

Tunaamini katika kanisa ambalo halinyanyapai, halibagui,

halitengi au kumhukumu yeyote.

Tuamwamini Mungu. Msaada kwa kutoamini kwetu.

12. Kutafakari Maandiko

Hapa ni baadhi ya miongozo:

Katika Luka 13:10-17 tunakutana uso kwa uso na Mungu

ambaye anapinga mamlaka na kulegeza vifungo vya watu

waliofungwa. Ni Mungu ambaye si tu kwamba yuko kazini

nyakati za kazi kuanzia saa tatu hadi kumi na moja, ie ndani

Page 30: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

28 KANISA

ya taratibu fulani, bali ni nguvu ambayo haifungwi au ku-

dhibitiwa. Mungu mwenyewe huvunja taratibu za maandiko

kwa sababu watu na huruma ni muhimu sana kuliko sheria.

Lengo la sheria ni muhimu sana kuliko utii kwa sheria fu-

lani. Asili ya Mungu ni Upendo na makusudi yake kutokana

na maneno yake na matendo ni kulegeza vifungo, kuwai-

nua waliokandamizwa na kuwaweka watu huru; Mungu

anaponya na kuokoa.

Kisa hiki na hadithi zingine kuhusu Yesu zinaweza kuku-

saidia kuondoa mitazamo ya Mungu inayomhusisha na

ukandamizaji, kulipiza visasi na kuadhibu, na badala yake

kuelekeza katika kiini hasa cha injili – Upendo wa Mungu

kwa ajili ya kila mtu.

Ukristo na injili vina umuhimu kiasi kwamba nyakati fulani

zinaonekana kuwa havijatumika ipasavyo. Vinaweza kuwa

vyombo vizuri vyema sana kwa maisha yetu: vinaweza ku-

tuweka huru na kutusafisha katika kila kitu ndani yetu na

mazingira yetu yanayo tukandamiza. Yanaendana na hali

ya kutokuwa mkamilifu kibinadamu, inayoumba hukumu

na fadhaa na ambayo huwashusha watu chini. Vina sisitiza

umuhimu wa kujipenda na kuwapenda majirani.

13. Maombi ya Mwombaji

• Munguwakilamwanadamu,tupeuwezonaujasiriku-

tambua na kukataa kila aina ya unyanyapaa, kutengwa

na kubaguliwa. Tusaidie kupinga upendeleo na tupe

uwezo wa kutambua uwepo wako ndani ya kila mtu.

Ndani ya mioyo yetu tunawaleta kwako wale ambao

tunawafahamu wanapitia hali ya kutengwa.

• Mungu wa Upendo, jifunue kwetu na tusaidie kush-

uhudia kwako kwa ukweli. Tuondoe na vishawishi ku-

tumia vibaya ili kuwaumiza wengine, au kuhudumiwa

badala ya kuhudumia Tusaidia kushirikiana upendo

ulioleta kwetu na kujitahidi kuondoa mitazamo mi-

bovu kuhusu wewe.

• Mungu, chanzo cha maisha na uzima, tusaidie kuic-

hunga miili yetu, maisha yetu na sisi wenyewe. Tupe

ujasiri na nguvu ya kupingana na dharau, ubaguzi

na ukatili kwa wanawake, na kukomesha udhalimu

unaotokea ndani na nje ya ndoa. Daima tusaidie ku-

waangalia watu wenye upungufu kuliko sisi na kuon-

gea kuhusu VVU kwa lungha zinazoonekana kuwa za

heshima, upendo, msamaha na urafiki.

• Mungu wa Utatu, zifanye sehemu zetu za kukutani-

ka mahali pa kujumuika wote, ambapo ujuzi wetu na

thamani ya kila mtu unathaminiwa. Tusaidie kuwa vile

ambavyo ndani yetu tayari tuko: wanachama wa mwili

mmoja. Tusaidie kumwona mtu kabla ya sheria, virusi

na ugonjwa. Tunaomba kwa ajili ya kanisa linaloweza

kufanya maisha kuwa mazuri na yanayowezekana kwa

ajili yetu sote, linaloweza kuwa mkondo wa nguvu

zako za uponyaji humu duniani.

14. Maombi ya Baraka na Kutawanyika

K: Bwana awabariki na kuwatunza.

Bwana awaangazie uso wake na awarehemu; Bwana awasame-

he na kuwapa amani yake.

Mwende kwa amani: kwa ujasiri na furaha; mkielewa kuwa

mnapendwa; daima mkielewa na kila mahali kwamba ninyi ni

mwili wa Kristo.

Mwende kwa amani na mmtumikie Bwana wa uzima.

Page 31: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

KANISA 29

Mwanamke Aliyekuwa Apigwe MaweWakati tunatafakari juu ya kuhusishwa kwa kanisa inakuwa

muhimu Pia Kuangalia na kuchunguza sababu za msingi kwa

nini unyanyapaa na kubaguliwa kunachukua nafasi katika jamii

zetu na unajisikiaje ikiwa wewe ndiye unayenyanyapaliwa.

Funzo hili la Biblia pamoja na hadithi ya Zakayo katika Luke

19:2-10, inaweza kutusaidia kufanya hili

1. Soma Andiko Kimtazamo wa Hali

yako na Changamoto Zinazokukabili.

• Unawezakusemakuhusuwakati ambaoulitendewa isivyo

haki?

• Aukuhusuwakatiambaoulilaumiwakwasababuyajambo

ambalo hukutenda?

• Ulitakaninikifanyikaulipoonakuonewa?

2. Soma Andiko Pamoja

Soma hadithi ya mwanamke ambaye ilikuwa apigwe mawe,

Yohana 8:1-11, pamoja. Hili linaweza kuwa andiko lenye nguvu

sana, hasa awaliokandamizwa. Hisia kali zinaweza kuibuka un-

apofanyia kazi andiko hili.

3. Soma Andiko kwa Umakini na kwa Undani

Andika maneno ya muhimu kwenye ubao. Jiulize maswali ya

jumla kuhusu andiko kwanza.

• Andikolinahusunini?

• Ninikimekushtuakuhusuandikohili?

• Nivipiandikohililinahusiananakutendewaisivyohaki?

Halafu angalia kwa undani kwenye andiko:

• Tunamkutananikatikahadithi?

• Tunajifunzaninikuhusuwatukwenyeandiko?

Inaweza kusaidia pia kuangalia mahusiano ya watu katika

andiko, pia katika mtazamo wa kijamii, kisiasa, kidini na kiu-

chumi. Kwa mfano:

• Unadhaniwaandishiwalimtendeajemwanamke?

• UnadhanikwaniniwaandishiwalimletamwanamkekwaYesu?

• Unadhaniwaandishiwalimkamatamwanamkewapiwakati

akifanya uzinzi?

• UnadhaniKwaninihatusikii lolotekuhusumwanaumeali-

yekuwa akifanya naye uzinzi?

• Unadhani kwa nini hakuna amri inayosema mwanaume

apigwe mawe?

• NiniYesuanakifanyaanapokutananawaandishinamwan-

amke?

• Kwaniniwaandishiwanaondokabilakumpigamawemwa­

namke?

• NiniYesuanadhihirishakuhusuMungu?

Baada ya kuwa umelichunguza andiko kwa uangalifu, ni

muhimu kuangalia maisha na hali yako mwenyewe.

• Unawezakujionakwenyeandiko?

• Unajionaukiwananani?

• Je,uliwahikupitiahalikamahiyo?

• Naniunadhanianapitiahalikamahiyoleo?

4. Soma Andiko Ukiwa na

Mtazamo wa Kufanya Mabadiliko

Kujifunza Biblia hakumaliziki mpaka unapokuwa umeona kile

unachoweza kufanya kuleta tumaini lililo kwenye andiko ka-

tika siku zetu za leo.

• Tunawezakufanyaninikuwazuiawatuhasawanawake,ka-

tika aina hii ya ukandamizaji?

• Tunawezaje kufanya maisha bora kwa watu wanaopitia

ukandamizaji huu?

NORWAY

Jamii ilikuwa inapanga kumhukumu mwanamke aliyekuwa amekutwa akifanya

mapenzi nje ya ndoa; mwanaume aliyekuwa naye ilikuwa asihukumiwe.

Walimleta kwa mwalimu aliyekuwa mjini wakati huo. Mwalimu hakupinga

mpango wao. Kwa urahisi alisema yeyote asiye na dhambi awe wa kwanza

kurusha jiwe. Mmoja baada ya mwingine, kuanzia mkubwa hadi mdogo,

waliondoka. Kwa hiyo jaribio la kugawa na kutenga lilitenguliwa, siyo kwa

muujiza, lakini kwa ufunuo wa msingi ambao wote tunashiriki. Kwa njia hii

sote ni mwili mmoja.

ANGALIA YOHANA 8:2-11

KANISA

Kujifunza Biblia Kuhusu Unyanyapaa

Page 32: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

30 KANISA

NA CARINA WØHLK

Pumziko ama kurudi nyuma kunaweza kuelezewa kama mka-

kati wa kujitoa. Kijeshi neno hili halina maana ya kushindwa.

Inaweza kuonyesha haja ya kusimama na kufikiri juu ya hali

fulani iliyojitokeza.

Kuwa na mapumziko ni desturi ya muda mrefu ndani ya ka-

nisa. Neno pumziko ndani ya kanisa lina maana kuwa ni wakati

na mahali kwa ajili ya ukimya na kutafakari, Pumziko ni wasaa

wa kujitoa ili kupumzika na kukusanya nguvu.

Yesu Kristo mwenyewe anatupa uwezekano wa kuwa na

pumziko. Katika Marko 6:31 Yesu anawaambia wanafunzi

wake, “ Twendeni mahali pasipo na watu tukapumzike”. Yesu

mwenyewe anatafuta wasaa wa kutafakari - hebu fikiria busta-

ni ya Getsemane. Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na

hamu ya kuwa na mapumziko na nguvu na mtazamo ambao

vinaweza kuwapa watu wa dunia ya leo.

Tangu mwaka 1991 nimeshirikiana na rafiki kutoka Chama

cha Kitaifa cha Kilutheri cha UKIMWI katika kuwa na mapum-

ziko kwa ajili ya watu walioathiriwa kwa VVU na UKIMWI – hii

ni kusema kuwa wale walioambukizwa pamoja na ndugu na

jamaa wa wanaoishi na VVU au waliokufa kwa UKIMWI. Ma-

pumziko hufanyika katika kituo cha mapumziko kaika mazin-

gira muafaka.

Changamoto mojawapo inoyohusiana na mapumziko ime-

kuwa ni kutafuta uhusiano sahihi kati ya mazungumzo na

utulivu. Mapumziko ya kwanza yalifanzika katika ukimya, na

tulitumia sauti zetu pale tulipoomba na kuimba. Kwa baadhi

ya washiriki hii iliwasababishia wasiwasi. Mmoja wa washiriki

alijisikia kama vile akili imenyenyuliwa na hakujua namna ya

kuendana na hisia na mawazo ya wasiwasi yaliyomjaa.

Ukimya

Ilikuwa wazi kwangu kuwa watu wengi wenye VVU wanauhu-

sisha ukimya pamoja na kifo. Watu wanaoishi katika mazingira

ya kutengwa na upweke kwa sababu ya hali zao ki-VVU wana-

Kuonyesha Upendo na Uangalizi katika

Mazingira Muafaka Kiroho

hitaji kuongea na si kuwa kimya. Ni muhimu sana kushirikiana

na kukutana na wenye virusi. Kwa kuangalia hali zao wenyewe

kwa wengine, watu wenye VVU wanaweza kujifunza mikakati

mipya ya kuondoa ugonjwa.

Miaka ya hivi karibuni tumetengeneza uwiano kati ya maon-

gezi na ukimya katika njia maalum. Tumehakikisha kuwa tuna-

weza kutumia njia mbili zilizo zoeleka. Ya kwanza ni katika ma-

ongezi na nyingine ni kwa wale wanaohitaji ukimya na ambao

wanahitaji kuangalia zaidi mhitaji yao ya ndani. Kuongezea

kila mshiriki ana njia moja ambayo anaweza kuitumia kutafuta

amani na ukimya.

Tunawapa motisha washiriki kuwa wawe kimya katika kipindi

kuanzia kuanzia ibada ya jioni mpaka wakati wa kifungua ki-

nywa asubuhi inayofuata. Siku ya mwisho kabla ya ibada ya

kufunga tunakula kifungua kinywa kimya, tunawasiliana kwa

tabasamu, kukumbatiana na ishara.

Mbiu ya Pumziko

Mbiu ya mapumziko kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa

“Mwanga katika giza”, “Ujasiri kuishi”, “Wasiwasi au woga”,

“Ukaribu”, “Furaha ndani ya uzima” “Makosa na msamaha”, na

“Ifanyike”. Kila mwaka baada ya pumziko fomu maalumu ya

kutathmini hutumwa na tunawaomba washiriki kupendekeza

mbiu kwa ajili ya mwaka ujao. Kwa njia hii washiriki wenyewe

kwa hamasa wanaijaza na kuamua kuyaweka mambo ya mu-

himu katika form.

Pumziko lina mbiu maalum. Hufanyika mwishoni mwa wiki,

kuanzia ijumaa mchana mpaka jumatatu saa sita mchana.

Vifungu viwili vya maandiko katika Biblia vinavyohusiana na

mbiu ya mwaka huo huchaguliwa. Vifungu hivyo hujadiliwa,

kimoja Jumamosi na kingine Jumapili.

Pumziko hufungwa Jumatatu kwa ibada na sakramenti. Hu-

duma hii hukusanya mawazo na hisia kwa msisitizo na mazun-

gumzo kwa mbiu ya mwaka husika imetekelezwa.

Sakramenti na matumizi ya amani ki-liturjia katika ibada hu-

Pumziko Lenye TumainiDENMARK

KANISA

Page 33: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

KANISA 31

sisitiza wajibu wa pumziko la kuumba kusanyiko. Washiriki

wanaweza kwenda njia tofauti wakijua kuwa hawajaachwa pe-

keyao. Mungu yuko pamoja nao – na kuna wengine wanaoshi-

riki uzoefu wao na kuusambaza nchi nzima.

Siku mbili nzima tunazozitumia kwenye pumziko zina vi-

pindi vitatu vya kuabudu katika muundo wake: maombi ya

asubuhi, tafakuri juu ya maandiko ya Musa na kusoma jioni.

Mambo haya matatu ndiyo ya lazima kufanyika kwa kila siku.

Kuwa pamoja katika pumziko, peke yake inatosha. Ni muhimu

kwamba mpango mzima usiwe wa kuchosha. Ni lazima kufikiri

hitaji la washiriki la kupumzika na mlo pamoja na dawa. Kwa

kuongeza ni lazima kuwe wasaa wa maongezi na matembezi.

Ibada yenye Msisimko

Kila mwaka kati ya watu 20 na 30 hushiriki katika pumziko –

Mashoga na wasio mashoga walio na VVU, familia, marafiki na

wale waliopoteza wapendwa wao kwa UKIMWI. Kwa ufupi Ma-

pumziko ni wasaa wa muhimu na ibada yenye msisimko wa

roho kwa wale wenye VVU na familia zao. Fomu nyingi za tath-

mini kwa miaka mingi zimethibitisha umuhimu wa mapum-

ziko, kiroho na kijamii.

Labda faida kubwa ya mapumziko haya ni kwamba zimetia

nguvu uanzishwaji wa jamii zinazomwabudu Mungu kwa ajili

ya watu waishio au walioathirika kwa UKIMWI. Baada ya pum-

ziko la kwanza, wazo lilitolewa la kuwa na huduma kwa washi-

riki. Kwa miaka jamii hii imeongezeka na ina watu 30.

Hamu inayojirudia mwaka baada ya mwaka kwa ajili ya ma-

pumziko na jamii ya wanaoabudu walioathirika kwa VVU na

UKIMWI inasisitiza namna ilivyo muhimu kwa kanisa kuwaku-

bali kundi hili la watu katika ibada zake. Kanisa la kikiristo ni

lazima lifike kwa wanyonge ili kuwavuta katika Upendo.

Sijawahi kudhani kuwa imani ni kuhusu kile una-

chofanya kanisani. Imani ni sehemu ya maisha

yako, maisha yako ya kila siku. Wala sijawahi ku-

fikiri kuwa unaweza kuwasiliana na Mungu kwa

kuomba kabla ya kwenda kulala au kuomba nee-

ma kabla ya kula. Maombi ni wasaa mzuri sana tu-

lionao katika kuwasiliana na Mungu kwa ukaribu,

na inaweza kutumiwa katika hali zote na nyakati

zote – mchana na usiku. Nafikiri inapendeza sana

kuomba kwa pamoja kanisani – kwa mfano kuse-

ma sala ya Bwana- lakini nafikiri ni muhimu kuwa

na mahusiano binafsi na Mungu.

Ninajisikia huzuni ninapoona watu wanaopayu-

ka kwa sauti zao kufanya maombi hapa na pale

au hebu tukae chini na tukunje mikono yetu na

ooh, ni kwa namna gani imani yetu ni kubwa au

sisi ni wakristo safi. Ni muhimu kukumbuka kuji-

tunza kila wakati, katika mazingira yoyote uliyo-

mo, katika maisha yako yote.

Sisemi kuwa maombi ni ya thamani au kwamba

hakuna nguvu ya kutosha kuwa katika uelewa

kuwa mtu fulani anaomba kwa ajili yako na

kwamba upo katika mawazo ya watu kwa nam-

na ya upendo. Nimeona matunda ya hili – lakini

kwa ajili ya mahusiano yako binafsi na Mungu, ni

muhimu usijifariji mwenyewe kuwa ni kitu una-

choweza kufanya unapopiga magoti pembezoni

mwa kitanda chako kabala hujazima taa.

Ni wasaa tulionao kila wakati na ni kitu ninach-

okiona kuwa cha thamani sana na muhimu pale

ninapoimba. Nafikiri ni katika kuimba nimekuwa

na ukaribu zaidi, ukaribu sana na Mungu. Nimejisi-

kia kuwa kuimba imekuwa ni njia yangu ya kuomba

– njia yangu ya kukiri imani yangu. Baadhi ya watu

huiita ushuhuda na wanaruhusiwa kufanya hivyo.

Imani haina kitucha kufanya juu ya ufafanuzi. Ima-

ni hakika ni kitu rahisi na kilicho kimya na kilmelala

pale kama uzi katika maisha yangu.

USHUHUDA WA JASPER, ALIYEKUFA KWA UKIMWI, DENMARK

Wimbo Ulio Kimya

Page 34: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

32 UJINSIA WA BINADAMU

Page 35: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

UJINSIA WA BINADAMU 33

Utangulizi

Kwa kirahisi tu, ngono ni tofauti ya kimaumbile baina ya wa-

nawake na wanaume. Inahusu ukweli kuwa tunazaliwa wa-

nawake ama wanaume. Kwa upande mwingine, ujinsia unahu-

su hisia za kijinsia, tabia zake na mahusiano yake. Ni uhusuano

baina ya wapenzi wawili ama wale wanaotarajia kuwa wapenzi.

Lakini katika jamii mbalimbali, suala la ujinsia linalolinganishwa

na dhambi limejengeka ndani ya maadili ya kiutamaduni.

Mtazamo wa Kibiblia

-Mwanamke aliyekamatwa akizini

katika hadithi hiyo tunaona jinsi dhambi ya kujamiiana ili-

vyosimikwa katika utamaduni na desturi za Kiebrania. Ma-

farisayo waliitunza sheria ya Musa, yaani torati. Walimleta

mwanamke waliyemkamata akizini ili kumjaribu yesu. Jibu

lake kwa maswali yao liliwapa changamoto kubwa washitaki

wake. Yesu akasema, yeyote kati yenu asiye na dhambi awe

wa kwanza kumtupia jiwe. Alimlinda yule mwanamke. Was-

hitaki wake waliondoka mmoja baada ya mwingine wakiwa

wamevunjika. Yesu akamwagiza yule mwanamke asifanye

dhambi tena naye akasamehewa.

• Jetunafanyajekwawalewanaoshutumiwaleo?

• Jetunawapachangamotoileilewaliopatawenzetu?

• Jetunasameheamabadotunabebamitazamoileile?

Tafakuri

• Tungependakujua kwanini yulemtualiyehusikana tukio

hilo hakuwa na wasi wasi wowote.

• Kwamawazoyetuwenyewedhambininini?

• Jewanawakewanaonekanakuwajibikazaidinadhambiza

kujamiiana kuliko wanaume?

• Je tunatambua kuwa ujinsia wa kibinadamu ni maadili ya

kiutamaduni yanayoamuliwa na desturi

• Je ujinsia ni kipawa toka kwa Mungu ama laana toka kwa

Shetani?

• Ujinsiaunafaidaganikwawanaumenawanawake?

Hitimisho

Hadithi kutoka Yohana 8:3-11 inazungumzia hadhi: “Musa al-

ituamuru tuwapige mawe wanawake wa jinsi hii.” Uanaume

na hali zinazofanana zimeshamiri katika kanisa leo. Dhambi

ya ujinsia imenyanyapaliwa kama DHAMBI ILE. Yesu aliwapa

changamoto wanaume wa Kiebrania katika jibu lililotolewa.

Yesu alifahamu shabaha yao katika kuwabagua wanawake.

Tunamsikia Yesu akisema:

• UjinsianikipawakutokaMungu–Mwanzo1:27­28

• Ujinsiaunabebadarakafulani

• Unahitajikuwajibikakikamilifukwawatuwajinsiazote

• Zaidi ya yote unahitaji kupendana (Efe 5:25­32; Col.

3:12-13)

Maadili ya kijamii na mafao yake yamejengwa katika mitaza-

mo iliyojengeka kwa wengi katika jamii ambazo kwa upande

mwingine zinaendeleza mifano ya watu kama wababe na

wenye nguvu, na wanawake ama wasichana kuonekana kama

wale wasio na nguvu, na hii inategemea majukumu ya kanisa

kuondosha udhalimu wa kijamii na ubaguzi wa kijinsia.

UJINSIA WA BINADAMU

Ubaba, Jinsia na Yesu

Kujifunza Biblia Juu ya Ujinsia wa Binadamu, Unyanyapaa na VVU

ZAMBIA

Nitatoa mkono wangu na mguu ili kuwa na kikundi cha Mduara wa Matu-

maini. Ninaweza kuwashirikisha watu hawa siri zangu za ndani kabisa na

bado wakanipenda. Nilipougua kwa mara ya kwanza ilikuwa ni kikundi

hiki kilichonipa nguvu ya kuendelea mbele. Katika kundi hilo tulionge-

lea juu ya maisha na pia tulipata mgeni aliyekuja kutufundisha juu ya

lishe, vipengele vya sheria, tiba mbadala na programu nyingi zingine. Ni-

lipomsikia mwezeshaji akielezea hadithi yake jinsi alivyogundua yuna

VVU, nilijiweka katika nafasi yake na kumwelewa. Hii ilinipa nguvu kuta-

mbua kuwa sikuwa peke yangu. Maisha yangu yaliokolewa kutokana na

hili. Ndiyo maana najua ni jinsi gani hili ni muhimu kwa watu wengine.

MJUMBE WA MDUARA WA MATUMAINI KITONGOJI CHA GARDEN

Page 36: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

34 UJINSIA WA BINADAMU

Ujinsia - Kipawa na wajibuUtaratibu huu wa ibada uliandaliwa na kutumiwa na Duara

za Matumaini huko Busokolo mjini Lusaka, Zambia. Duara za

matumaini ni vikundi vya misaada kwaajili ya wanoishi na VVU

na UKIMWI.

K: Kiongozi

M: Msomaji

1. Msafara na nyimbo zikiimbwa.

2. Salamu na Ukaribisho wa Wageni

K: Ndugu kaka na dada zangu, tumekusanyika hapa leo kush-

erehekea uzuri wa uumbaji wake Mungu na huu ndio uzuri

wa ujinsia wetu. “Kwa hiyo Mungu aliumba wanadamu kwa

mfano wake.Kwa sura na mfano wake aliwaumba; mwanaume

na mwanamke aliwaumba….Kisha Mungu akaona kila kitu ali-

chokitenda kuwa ni chema.” Kwa hiyo, kwa maombi na sifa fikra

na matendo, tumwabudu Mungu wa milele. Amina

3. Somo la Ufunguzi

I Korintho 7:3-12

4. Wimbo wa Sifa

5. Maombi ya Kufungua

K: Mtakatifu Mungu uliye hai

Ambaye tumetokana na mkono wako wa kiufundi

Tunakushukuru kwa kipawa hiki cha ujinsia,

Tunakushukuru kwa kazi zako kuu,

Utuongoze ili tuweze kuikubali miili yetu

Na kwamba tuweze kuuelezea ujinsia wetu katika njia ya ku-

wajibika zaidi.

Tuongoze kukubali kuwa sisi ni hekalu la Roho Matakifu

Utusamehe tunapoupungukia na kuupunguzia makali uum-

baji wako

Utufundishe ili tusitumie vibaya uwezo wetu wa kuvutia ki-

mapenzi

Utupe ujasiri wa kupinga mifumo yote inayogeuza miili ya bi-

nadamu kwa biashara

Kwa Roho wako, utuwezeshe kufurahia ujinsia wetu

Tunaomba kwa Jina la Yesu Kristo

K: Sasa tuzingatie kwa muda kidogo na kuleta mbele ya mawa-

zo yetu mabaya ambayo tumeyatenda katia eneo la ujinsia.

6. Sala ya Toba

K: Katika nafasi zetu na katika majukumu kama watu binafsi

– baba, mama, walezi wa kiroho, viongozi wa vijana n.k. hatu-

jafikiria na kuyafanya yale yote tunayopaswa kuyafanya kuelezea

uzuri na fumbo la ngono, ujinsia na mahusiano mazuri. Kwa wingi

tumedumu katika mambo hasi yanayohusu ngono na hivyo kuu-

pagaisha ujinsia. Mungu tunaomba msamaha wako.

7. Wimbo

8. Masomo Mwanzo

1:27, 2:24

9. Mwongozo wa Mahubiri

a. Utangulizi

Wakati mamilioni ya watu wanaishi ama wameathiriwa kibin-

afsi na VVU na UKIMWI, ugonjwa huu ni mojawapo ya matatizo

makubwa sana katika zama zetu. Taasisi za kidini kwa ujumla na

makanisa yote kwa pamoja yana nafasi kubwa ya kupambana na

kuenea kwa ugonjwa huu kutoka mtu mmoja kwenda mwing-

ine. Mungu aliumba wanadamu wakiwa na hisia zenye nguvu

za ujinsia ambazo wanadamu wanaweza kuzitumia vizuri ama

vibaya. Hisia hizi zenye nguvu zinaweza kubebwa maishani na

kufanyiwa kazi kwa njia ya kuwajibika. Kazi moja ya kanisa ni ku-

zungumzia juu ya maadili na uwajibikaji na kusaidia kupunguza

mazingira hatarishi kupitia elimu. Ukristo umenyanyapaa ngono

na kuifanya dhambi juu ya dhambi zote na kumbe imani ya Kibib-

ZAMBIA

Utaratibu wa Ibada juu ya Ujinsia

UJINSIA WA BINADAMU

Page 37: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

UJINSIA WA BINADAMU 35

lia inaielewa dhambi kuwa ni dhambi.

Tunaposherehekea ujinsia wetu, tunafanya yafuatayo:

• Tunakubali kwamba Mungu aliwaumba wanadamu wote –

waume kwa wake – katika sura ya Mungu, na kwa kufanya hivyo

alitupa kipawa cha kuthaminiwa, kufurahiwa na kuenziwa.

• Kuukubaliujinsiakamasehemumaalumyautambulishowetu

inadumisha ushirikiano baina ya watu na kuleta starehe.

• Tunakumbushwakuwapamojanauwezowakuboreshamap-

enzi na furaha katika uhusiano wa kibinadamu ujinsia un-

awaweka watu wazi baina yao wenyewe na pia mbele ya nguvu

za kijamii

b. Mafunzo yaliyotolewa

• Uumbaji wa wanadamu kama mwanaume na mwanamke

haukuwa wa kubahatisha;

• Kujamiiana katika ndoa ulikusudiwa na Mungu kutoa ma-

funzo ya kisaikolojia, kimwili, kihisia, na ukamilifu wa kijamii

na kiroho, zaidi ya kuzaa na kuongezeka tu.

• Ikiwa familia ya Kikristo haiwezi kutoa majibu kwa vijana

chipukizi, basi itawapoteza hao kwa watu wengine wataka-

oweza. Ikiwa kanisa litakaa kimya, nalo litawapoteza pia.

Ujinsia wa mwanadamu kwa hakika ni kipawa toka Mungu amabacho Kina-

paswa kufurahiwa na wapenzi wawili. Kipawa cha ujinsia kinaendelea ku-

wepo ndani tya watu wanaosihi na VVU na kinatakiwa kutumika na si kukan-

damiza. Ujinsia ni uumbaji wa ajabu wa Mungu, na unapaswa kufurahiwa na

wote wanaoshi na VVU na wale wasio navyo.

DUARA ZENYE A MATUMAINI

Ujinsia wa kibinadamu

10. Maombi

• OmbakwambaMunguatupehekimakufundishakuhusu

kile kilicho sawa na salama juu ya ngono, matendo ya ku-

jamiiana, na mahusiano kwa kuzingatia VVU na UKIMWI

• Kuwaombeawanawakenawatotowaliodhalilishwa

• Kutoa shukrani kwa ajili ya uongozi wa Mungu, ulin-

zi, na nia kwamba tuishi maisha yenye maendeleo na

manufaa.

11. Matoleo - Huku nyimbo ikiimbwa

12. Sala ya kuombea Matoleo

13. Baraka ya Kufunga

K: Bwana Mungu wa amani mwenyewe awatakase ninyi nyote

kikamilifu; na roho zenu nafsi na mwili zihifadhiwe bila lawa-

ma hata kuja kwake Bwana Yesu Kristo. Neema ya Bwana wetu

Yesu Kristo iwe pamoja nanyi Amina.

14. Wimbo wa Kutawanyika

Page 38: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

36 UJINSIA WA BINADAMU

Nani Anayediriki Kurusha Jiwe la Kwanza?

Kutoka kujifunza Biblia Yoh 8:2-11

Kila mwaka ibada katika Siku ya UKIMWI duniani ndani ya Kanisa

Kuu la Kilutheri mjini Oslo Norway, hutayarishwa huko Aksept -

Kituo cha Kimisheni cha Kanisa Jijini Oslo kwa wote wale ambao

wameathiriwa na VVU. Mwaka 2002 mahubiri yaliandaliwa kwa

kushirikiana na wateja wa Aksept. Ifuatayo ni taarifa ya mchaka-

to na mahubiri yaliyotolewa katika ibada hiyo.

Unyanyapaa, ubaguzi, na ujinsia

Mchakato ulianza kwa wasaa wa kubungua bongo kutafuta

masomo na maandiko ambao ulionekana kuwa wa kufaa uli-

fanyika kwa wakati muafaka na ulioenda sambamba na wale

walioshiriki mijadala husika. Kumbukumbu toka katika mikutano

hiyo iliweka msingi wa kuandika mahubiri hayo. Shabaha ilikuwa

kuendesha mazungumzo baina ya wanadamu na Mungu - ma-

hubiri yanayosikiliza, yanayoelewa, yanayofariji na yanayoleta

changa moto. Mbinu iliyotumika inaweza kuwa msaada kwa ku-

pata mfano wa mahubiri na hata kuwa mahubiri yenyewe. Zaidi,

inatupatia undani wa kufikiri na hata kufanya mazungumzo kati

ya wale walioathirika kwa VVU, mchungaji na kifungu cha Biblia.

1. Kubungua bongo kwa mara ya kwanza:

Watu wanaoishi na VVU walioko Aksept walipata fursa ya kuku-

tana mara mbili kwa kazi ya kikundi na kusema kitu juu ya kile

wanachodhani kuwa ni muhimu kuelezea katika siku ya UKI

WI Duniani mwaka huu. Asubuhi ya kwanza ilikuwa pamoja na

“mjadala wa mwanzo juu ya maadili, dini, na falsafa kituoni.

Hizi ni baadhi ya kumbukumbu zilizonakiliwa daftarini

Matakwa na fikra juu ya ibada

• ujinsiaungekuwasomokuumwakahuu

• kanisalimehamishwambalisananaukwelilinapozungum-

zia ngono

• hatamsimamowetukuhusuujinsianimgumukuutekeleza

• ingelikuwasahihikuendeshaibadayamsetoyamadhehebu

yote ya kidini katika siku kama hii! VVU na UKIMWI umetu-

athiri sote.

Tunataka kusema nini kwa Mungu, Mahubiri yanaweza kuwa

kama mazungumzo kati ya Mungu na wanadamu

• hitajiladawayakuukomeshaUKIMWI

• kukubalikazaidikutokawatuwengi.NilazimaMunguafun-

gue macho ya watu

• hajayakupatamtuwakumpenda.WalewenyeVVUwanahi-

taji kupata nafasi ya kupenda.

• mzigomoyonikwawatotowanaozaliwanaVVU

• Kwaninimimi?nivigumukuikubalihadhiyamtu;kugha-

sighasi mtu humkasirisha!

• haja ya kumsaidia mhusika kurejea mahala pa kazi. Watu

bado wanakutana na ubaguzi

Wale wanaoishi na VVU hawaundi kikundi cha watu wenye

NORWAY

Page 39: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

UJINSIA WA BINADAMU 37

ya UKIMWI Duniani yanaweza kufuata mwelekeo kwamba wale

wote wanaoishi na VVU si waaminifu kwa wake ama waume

zao. Hii yenyewe ni mtazamo wenye kunyanyapaa.

4. Mahusiano yanayowezekana

Kwa upande mwingine, kifungu kinachokoza vyama vingi. Ka-

tika mkutano wa pili, majuma mawili yaliyofuata, tafakuri ili-

fanywa kwa kifungu toka Yohana 8:2-11.

Mwanamke huyu alikuwa tayari amekwisha hukumiwa na

wale watu waliomleta kwa Yesu. Hao Mafarisayo na Waandi-

shi walikuwa na hatia gani? Je waliiona akisi yao wenyewe

ndani ya mwanamke yule? Lazima tujikague wenyewe kabla

ya kuhukumu wengine.

Waandishi na Mafarisayo walionyesha mtazamo hafifu kue-

lekea wanawake. Je mwanamke yule anajua nini kinachoende-

lea? Mwanaume naye, Je yuko wapi? Inawezekana hakufanya

kitu chochote kabisa. Alikuwa ni mwathirika tu katika jamii ili-

yomilikiwa na wanaume. Je mwanamke huyo alikuwa na VVU?

Je alikuwa ameshitakiwa kwa kumuambukiza mtu? je mwana-

mke alijiamulia mwenyewe kujihusisha na shughuli iliyokuwa

imetengwa kwa ajili ya wanaume? Je alikuwa akifanya biashara

ya ngono? Ama alikuwa mwanamke aliyempenda mwanaume

na akawa mwathirika wa ndoa ya nguvu. Kuna kila uwezekano

hapa. Kifungu hakituelezi chochote kuhusu mwanamke yule.

Naye hasemi chochote cha kujitetea.

Tunajifunza zaidi kuhusu wanaume waliompeleka kwa Yesu.

Walitaka kumtega mtego Yesu, ama kwa kumlazimisha aifuate

sheria na kanuni au kuthibitisha kuwa alikwisha jitenga na ka-

nuni, sheria na desturi za Kiyahudi. Wanathiolojia na watauwa

waliifahamu sheria, walikuwa mafundi katika hiyo. Kulingana

na sheria, mwanamke yule alipaswa kupigwa mawe! Nao wali-

kuwa tayari kufanya hivyo. Je walikuwa wamemwelewa vibaya

Yesu wakidhani kuwa yu upande wao?

Lakini wanaume hawa walikuwa na nini katika dhamiri zao?

Kwa nini walikuwa na hamaki sana? Je walikuwa kinyume na

wanawake walioendesha maisha yao wenyewe ya kujamii-

ana? Je walikuwa ni wandume waliokuwa wamefadhaishwa

na mambo? Je walikuwa wametimiza matendo mangapi ya

udhalilishaji wa ujinsia? Hatuelezwi chochote lakini tunaweza

kutumia dhana zetu....

Kifungu hiki kinaangaliwa kwa kuhusiana na VVU na kinan-

yanyapaa jinsi kilivyo: VVU havihitaji kuzungumziwa pamoja

na kutokuwa mwaminifu. Zaidi ya hayo ngono si pekee inay-

asilia moja ama kabila moja. wanawake na wanaume, vijana

kwa wazee, wenyeji wa Norway na wageni, mashoga na wasio

mashoga, n.k.

Katika Siku ya UKIMWI Duniani dhamira mbili kuu zilijitokeza:

). Unyanyapaa/ ubaguzi na

2.Ujinsia. Katika mkutano wa kwanza tulifanya kazi kutafuta

kifungu cha Biblia kitakachokuwa msingi wa kutafakari juu

ya maudhui haya mawili. Hivyo ilipendele zwa kufanya rejea

kwa Wasamaria - Wasamaria walikuwa kundi lililonyanyapaliwa

na kubaguliwa wakati wa Yesu. Lakini kuna rejea chache zina-

zohusika na ujinsia katika kifungu kile. Wimbo wa Sulemani

pia ulitajwa, lakini hautaji chochote juu ya unyanyapaaji. Ha-

timaye tuliishia na hadithi juu ya mwanamke aliyepatikana na

zinaa.

2. Yoh 8:2-11 Inasomwa

3. Mwanamke aliyepatikana na Zinaa

Hatukuwa tumeridhika na kifungu hiki pia, kwa sababu kiliun-

ganisha ujinsia na utendaji dhambi. Kifungu hicho pia kingewe-

za kuonekana kama kinanyanyapaa; kwa nini ni mwanamke

tu peke yake aliyekamatwa katika tendo hilo? Nini kilimtokea

mwanaume yule (lazima tudhanie kuwa kuna mwanaume ali-

yehusika)? Pia, mashirika na vyama katika siku kama hii, Siku

UJINSIA WA BINADAMU

Unyanyapaa awali ya yole, ni mfumo wa kulin-

da. Inaunganishwa na fikra kuwa kuna kitu am-

bacho hakipo sawasawa kinachotutisha. Mara

nyingi; kitu ambacho hatukijui ama cha kigeni.

Hofu yetu yaweza kuwa na sababu kamili ama

yaweza kuwa haina msingi wowote. Hata hivyo,

tumejitungia mawazo na mifano juu ya vile tu-

navyoviamini kuwa ni hatari. Haya ni mawazo

ambayo huenda hatuyaelewi vilivyo, kwani un-

yanyapaa hujenga mizizi yake katika fahamu

zetu zizlizolala –katika mitazamo na mawazo

tulio nayo, lakini tusiyoyazungumzia na hata

kuyakubalia. Ili tuweze kuhakiki sura hizi, tu-

nahitaji utashi na ujasiri wa kujaribu misima-

mo yetu dhidi ya ukweli, na kuzifanyia tathmini

ukizipima na mtazamo wetu juu ya ubinadamu

tunaodai kuwa nao. Lakini huu unaweza kuwa

mchakato wenye shida nyingi hivyo fursa zina-

zojitokeza zinahitaji kuimarishwa kwa maku-

sudi kabisa na nafasi salama zikipatikana

KUTOKA TAFAKURI ZA KITHIOLOJIA MJINI OSLO

Page 40: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

38 UJINSIA WA BINADAMU

ngono. Wengi wanatazamia kukutana na mtazamo wa jinsi hii

hata katika sekta ya huduma ya afya. wapo wengi walio na VVU

ambao hawatadiriki kufanya ngono na wengine kwa sababu ya

kuogopa kuwaambukiza wengine, pia wanafikiri hawafai tena na

hakuna atakayetaka kufanya ngono na yule ambaye ana VVU.

Wengi wameeleza juu ya matukio yanayofanana kiasi fulani

na lile la mwanamke katika kifungu cha Biblia. Wengine wameji-

weka wazi kwenye vyombo vya habari kwa kuwa walijiachia we-

nyewe na kufanya ngono na mtu fulani, lakini tofauti na hadithi

hii leo watu wapo tayari kuliko kawaida kutupa mawe, hasa kwa

kuwatwika majukumu makubwa watu wanaoishi na VVU zaidi

ya wale wasio navyo. Je mawe haya hufananaje?

“Umepata kile unachokistahili.” “Usinikaribie!” Umeleta aibu

katika ukoo wako!” hii ni baadhi ya ya jinsi mawe hayo ‘yalivyo’,

na yanauma zaidi ya mawe halisi.

Sababu kubwa ya kuwanyanyapaa watu wanaoishi na VVU ni

kuwa VVU vimeunganishwa na mambo mengi ambayo yame-

kwisha kuhukumiwa kuwa ni dhambi katika utamaduni wetu:

ujinsia, ukahaba, matumizi ya madawa ya kulevya, ushoga,

uasherati, na kadhalika.

Watu wametupa mawe katika mazingira ya jinsi hiyo kwa karne

nyingi, ijapokuwa kuna hadithi kama ile ya Yohana Sura ya 8.

6. Wanadamu kama Viumbe wenye Ujinsia

Je tufanye nini ili tuondokane na hawa wenye uchu wa kuy-

atupa mawe yao? Tunawapata hao ndani yetu wenyewe, ikiwa

tutazichunguza nafsi zetu.

Huenda inasaidia kuzungumzia ujinsia katika njia iliyo wazi na

ya moja kwa moja kama inavyowezekana si tu kwa jinsi inavy-

opaswa kuwa ama jinsi gani mtu anavyotaka kuwa.

Ujinsia si kile kitu alicho nacho mtu: ni vile mtu alivyo. Ujinsia

ni jambo kubwa na gumu ikiwa pamoja na VVU ama bila VVU.

Ni vigumu mtu kuishi katika viwango vyake vya kimaadili. Ujinsi

unajumuisha yote mafanikio na mapungufu. Ni jambo la kimb-

ingu na pia linafadhaisha. Linaweza likawa na utata nje ama

ndani ya ndoa. Hakuna furaha itakayokuwa bora zaidi, hakuna

itakayokuwa wazi zaidi.

Ni vigumu kuzungumzia juu ya ujinsia wa mtu binafsi, yote

hasa kuhusu nyakati za furaha na zile nyakati ambazo mtu an-

gependa zisitokee. Inauma sana kujisaliti mwenyewe, kwa sa-

babu wapo watu wamesimama mstarini tayari kutupa mawe.

Wengi ambao wana VVU wanapitia ukweli kwamba virusi vy-

UJINSIA WA BINADAMU

oleta maambukizi ama kueneza ugonjwa. Lakini kila kitu ki-

nachohusika na ngono tayari kina hatia. Dhambi kwa hakika

inakuwa dhana potovu katika mantiki hii kwa sababu ngono

yenyewe si dhambi. Lakini ngono inapata ugumu tunapoingi-

za VVU. Ngono ilikuwa na ugumu hata kabla ya VVU watu wen-

gine wameacha kufanya ngono baada ya kupata VVU. Mwana-

mke katika kifungu hicho alihukumiwa na jamii yake yote, na

sisi pia tunahukumiwa na jamii yetu nzima. Mtu ameondolewa

haki yake ya kuishi kwa kuwa tu ana VVU. Watu wanasema

“wamepata kile walichokistahili”: “Ni hukumu ya Mungu”, bado

unasikia wachungaji na mashehe wakizungumza namna hiyo.

Mmoja katika kikundi alisikia kisa cha mwanamke aliyeuawa

kwa sababu ya uzushi usio na kweli!

Dhambi ni nini? Ni kwa jinsi gani tutauhudumia “Ujinsia ulio

mzuri”. Ni vibaya wakati wengine wanapoelezea na kuamua

dhambi ni kitu gani. Inapaswa kuwa jukumu la mtu binafsi,

kwa sababu kile ambacho wengine wanaamini kuwa si sawa

chaweza kuwa sawa kwa mwingine. Je vipi kuhusu wale am-

bao bado hawajaolewa? Lakini kutokuwa mwaminifu ni dham-

bi; kwani daima mtu mmoja huumia mwishoni.

Je ina maana gani kutupa mawe leo? Ni matendo ya huku-

mu, kujiweka juu ya wengine na kuwatenga wengine. Nchi 183

hazitoi vibali vya kuingia nchini kwa watu wenye VVU. Lakini

tumewahukumu pia wale waliotuambukiza? Je tumewatolea

taarifa? Ama sivyo? Ngono ni tukio ambalo wahusika wote

wawili wanawajibika wakati uhusiano ni wenye usawa. Itaku-

waje ikiwa utakamatwa katika hali ya kufanya ngono, na labda

ukimwambukiza mwingine na VVU “Kama ningejua nimem-

wambukiza mwingine nimpendaye - ningeweza kuimudu hali

hiyo.”

Je mwanamke alipokea jibu? Je amesaidiwa? Hata nami si-

kuhukumu! Haya ni maneno yenye maana sana. “Nenda na

usifanye dhambi tena.” Je hiyo ina maana hakuna ngono tena?

Ama ina maana: “Ondoka hapa na uishi maisha ya ‘kawaida’

kuanzia sasa? Ondoka na ujitunze mwenyewe; epuka ubaya,

usiruhusu mtu akudhuru tena.”

Je ni kipi kinacholeta mabadiliko katika mitazamo? Ufahamu,

ujuzi wa mtu binafsi:”Ingeweza kuwa mimi.”

5. Ubaguzi

Kuna mambo mengi ambayo tunaweza kuyatambua. Watu we-

nye VVU mara nyingi wanakutana na mtazamo huu: usifanye

Page 41: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

UJINSIA WA BINADAMU 39

enyewe vimekuwa ni ishara ya usafi katika ujinsia; inafunua

dhana kwamba mtu husika hakuishi maisha yaliyonyooka.

Kana kwamba kila mtu huishi maisha hayo.

7. Unyanyapaa na Ubaguzi

Ni jambo la kuzingatia kwamba Kanisa ambalo limerithi ha-

dithi hii ya mwanamke aliyepatikana na kosa la zinaa halijawe-

za kuwaelimisha waumini wake na kubadili utamaduni wake

wa kuhukumu, angalau kuupunguza kidogo. Badala yake,

tunayo historia ya kanisa ambapo watupa mawe wamepewa

uhuru wa kufanya mambo yao watakavyo. Wakati umefika

ambapo tabia hii ya unyanyapaaji na ubaguzi itambulike kwa

jinsi ilivyo, yaani kama dhambi kinyume cha Mungu na injili.

Kama ujinsia ni zaidi ya kuzaa tu - na ndivyo ilivyo - basi lazima

uwe kitu ambacho kila mmoja ana haki nacho, si kwa wateule

wachache tu - bila kusahau umuhimu wa kuwajibika. Hapa

pawe mahala pa kuanzia kwa mazungumzo yote juu ya jinsi

tunavyoweza kuishi pamoja kama viumbe wenye ujinsia. Na

tutakaposhirikisha kila mmoja katika hili ndipo tutakapoweza

kuondoa mipaka ile ya ubaguzi tuliyojiwekea. Na inaenda bila

kusema kuwa hii lazima ijumuishe watu ambao wanaishi na

VVU.

Unyanyapaa upo wazi. Watu wanaoishi na VVU wamekata-

liwa vibali vya kuingia nchini katika nchi 183 za dunia, mad-

aktari wa meno wamekataa kuwatibu, marafiki wao wame-

wasuta hata wafanyakazi wenzao mahala pa kazi. Yote haya

yanajengeka na kuwa mitazamo kinyume cha ujinsia ambayo

yanalingana na kutupiwa mawe.

8. ”Hata mimi sikuhukumu!”

Hii ndiyo injili: “Hata mimi sikuhukumu.” Baada ya kulibaini

hili: kwamba hakuna mtu aliye bora kuliko wengine inapokuja

katika maisha ya ujinsia, nini hatua ya baadaye? Sisi tutaishije

pamoja katika katika maisha yetu ya ujinsia? Tutawezaje ku-

zuia kuumizana? Tutawezaje kumheshimu kila mmoja? Tut-

awezaje kuvumilia fumbuzi zingine, na kadhalika?

Yesu alimwambia yule mwanamke hatimaye kuwa - “usitende

dhambi tena.” - hii haina maana kufanya ngono siku zijazo.

Zaidi ni suala la kujiangalia mwenyewe kwa siku zijazo. Hii ni

changamoto! Hatutaukwepa mjadala juu ya haki na kile kisicho

haki. Lakini tunaepushwa na unafiki ambao watu wengine ni

bora kuliko wengine katika eneo hilo.

Je ina maana gani kuwa binadamu? Kuwa

na VVU ama kutokuwa navyo, maisha

yote na maisha ya kila mmoja ni maisha

yaliyo hatarini, kila maisha ni maisha

yaliyowazi. Ndani ya tofauti zote, kila

mtu yu tupu na katika maana halisi ya

neno, amejeruhiwa.

Tunakumbushwa juu ya hili kila mara.

Hata hivyo, tunajaribu kulikataa, na

kuliweka mbali, tunajaribu kujishawi-

shi wenyewe na wengine kwamba tuko

salama, wazima na sisi si wa kufa.

Ushirika wa kweli unawezekana tu pale

watu wanapokuja pamoja na kutambua

kuwa kila maisha yao binafsi yapo wazi

kwa jambo lolote - si kama ufahamu tu

lakini kama taarifa ya uwazi unaom-

kabili mtu yeyote kuweza kukutana na

jambo lolote yumkini hata kupata maje-

raha.

Kisha ipo nafasi ya kukutana baina

yetu, tupo katika ngazi moja na hivyo

tunaweza kuzungumza.

KUTOKA TAFAKURI ZA KITHIOLOJIA MJINI OSLO

Page 42: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

40 UJINSIA WA BINADAMU

NA ELIZABETH KNOX-SEITH

Katika utamaduni wa magharibi, kifo huonekana kama tukio

la kushindwa – na kuwa mgonjwa, yaani kuwa katika hatari ya

kufa, kunakuwa kulingana na ufahamu wa ndani namna moja

isiyo ya kupendeza sana ya adhabu. Kwa kuwa tumejaribu sana

kutokomeza kifo kama sehemu mojawapo ya mzunguko wetu

wa maisha, hivyo kuwa mgonjwa, ambayo ni kama kuwa katika

mchakato wa kufa kunakuwa tishio katika utu wetu wa ndani.

Ni lazima tusife: chochote na kitokee sisi ni lazima tuishi –

milele ama kwa muda mrefu tunaoweza. Hili lenyewe hugeuza

ugonjwa kuwa tukio la kushindwa.

Ili tuweze kuelezea kuwa kifo ni sehemu asilia ya mzunguko

wa maisha yetu mara nyingi tumetafuta sababu binafsi za mtu

kuwa mgonjwa. Tunasema, ni mtu mwenyewe ndiye aliyeko-

sea, aliyeshindwa kimaadili. Mtu huyu amefuata tabia ambayo

ni sahihi na haki kama ataugua. Ugonjwa na kifo una maana nzi-

to sana katika utu wetu wa ndani kwani vyote vinaashiria kuwa

hatuna haki ya kuishi. Pale mateso yanapotufikia, yanatuambia

japo si moja kwa moja kuwa tumepoteza maana yetu kama wa-

nadamu, yaani haki yetu ya kuishi.

Kwa njia moja, namna hii ya kufikiri inafanya vitu kuwa rahisi

kwa wote wanaoishi na wote wenye afya. Wale wanaoumwa wa-

naweza, ikiwa tu watabadili mtindo wao wa kuishi na kuachilia

wanayoyaita kuwa ni “makosa”, matumaini ya kupata tena haki

yao ya kuishi na hivyo kupona kutoka ugonjwa walio nao – na

wale walio na afya njema wanaweza wakati ule ule kwa ushindi

kutangaza kuwa wale wanaoishi maisha yenye haki na sahihi

nao watapewa haki ya kuishi milele

Lakini ugonjwa kama UKIMWI unaumbua udhaifu ambao kila

mwanadamu na kila jamii hata ile iliyo duni kabisa inaupitia

wanapokaribiwa na ukweli kama vile kifo. Katika maudhui ya

kukata tamaa UKIMWI huchipua swali, kwa nini mimi? Kwa nini

mimi nifikiwe na haya? Kwa nini mimi nipoteze maisha? UKIMWI

umeweka wazi kuwa kifo kinaweza kuingia katika umri wowote

na kwamba tiba ya kisasa haithibitishi ongezeko la maisha ya

milele. Na kama swali halinihusu mimi, linaweza kumhusu kaka

yangu, dada yangu, rafiki yangu wa kike, rafiki yangu wa kiume,

mwanangu ama dada yangu, baba yangu ama mama yangu.

Ikiwa mtu fulani aliye karibu yetu akaangukia eneo la hatari basi

swali hilo huwa halisikiki tena katikati ya maumivu tulio nayo

Kweli zilizopo katika

sura nzima ya UKIMWI

Maana, Kifo na Upotevu

KUJAMIIANA

DENMARK

Page 43: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

UJINSIA WA BINADAMU 41

– uwezekano wa kumpoteza huyo “fulani” unakuwa ndiyo kig-

ezo kitakachotawala juhudi za dhati za kutafuta maana halisi ya

mambo hayo yote.

Kuambiwa Ukweli

Taarifa ya kuambiwa kwamba una VVU huleta mshutuko kwa

karibu kila mtu kwani ni kama pigo kubwa ambalo hubadili

maisha yao kabisa. Kila mmoja ambaye amekwisha pima

VVU na UKMIWI anajua jinamizi ambalo mtu hupitia, hasa

pale mtu anaposubiri majibu yake. Hata mtu angejaribu ku-

jiandaa namna gani kupokea majibu hayo imekuwa vigumu

kujiandaa. Hata kwa wale wanaofikiri kwamba hatari ya kua-

mbukizwa ni ndogo kusubiri ni zoezi ambalo wangependa

kutokuwa nalo. Haishauriwi pia kuchukua vipimo ikiwa hauna

mtandao wenye nguvu unaokuzunguka. Kukabiliwa na hatari

ya kupata maambukizi ya VVU ni kukabiliwa na maswali ya

msingi mengine bado kufikiriwa, na kama utaachwa peke

yako ukiwa na matarajio mbalimbali na mashaka mengi ya-

nayohusika inaweza kukuletea madhara binafsi.

Shauku ya kuhukumu ni sehemu maarufu ya mfumo wa ki-

hisia kuhusu VVU na UKIMWI, yote kwa wote walioambukizwa

na kwa familia zao. Je majirani wasema nini ikiwa watagundua

ya kwamba mwanangu….? Je mama na baba yangu watase-

ma nini, ikiwa watafahamu kuwa nime….? Daima nimekuwa

binti mzuri …..Je watafikiri nini sasa….?

Picha zinacheza mbele ya macho ya akili zetu mara tu ma-

zungumzo yanapogeukia VVU na UKIWMI – na swali litaka-

oulizwa ambalo daima haliulizwi kwa sauti ni, Je ameam-

bukizwa namna gani?

Ngono bado ni eneo ambalo limezungukwa na fumbo, ma-

tarajio na hofu - na hakuna mipaka katika mawazo ambayo

hufufuliwa na hoja kama hii hasa pale mtu anapogundua

kuwa mtu aliye karibu nao ameambukizwa.

Maswali ya hatia siku zote hubakia nyuma tu – na hivyo

ni muhimu kumkamata ngombe dume katika pembe zake

na kusema hilo haliwezekani kutofautisha baina ya “hatia”

na “wahanga wa VVU’ wasio na hatia. Wote wamo katika

mtumbwi ule ule, bila kujali wameambukizwaje. Kwamba

mtu anaweza kuwa na uzoefu binafsi wa hatia na fedheha

unaohitaji kushughulikiwa, ni jambo lingine – lakini uzoefu

huo unaweza kuwa na ugumu pia, tena bila kuzingatia vi-

rusi vilipatikanaje. Mama atakayeruhusu mtoto wake apewe

damu kabla damu hiyo haijapimwa, anaweza kuwa na mzigo

mkubwa sana kuubeba wa hatia – na ni lazima asaidiwe kwa

namna ile ile ambayo yule aliyeambukizwa na mpenzi wake

wa kiume angehitaji kusaidiwa ili kushughulikia hasira anay-

oweza kuwa nayo dhidi ya mpenzi wake na nafsi yake. Ma-

tukio ya kujisikia hatia na kuona aibu mara nyingi ni matokeo

ya kutoikubali hasira. Huyo ni ngombe dume mwingine

anayepaswa kukamatwa pembe, na hiyo inahitaji juhudi za

kutosha –lakini huwa ni amani sana pale ngombe dume huyo

anapokuwa ameondoshwa njiani. Mafahali wanaweza kuon-

gozwa kwa kuzikamata pembe zao kwa wakati muafaka,

lakini hiyo ina maana ya kuwepo mapambano daima. Kama

wataruhusiwa kubaki hasara itakayopatikana itakuwa sawa

na ile katika duka la vyombo vya udongo.

Shauku kwamba watu wote wana uzoefu kutokana na

kuogopa yasiyojulikana, kifo na njia ile ambayo ugonjwa

husika utafuata, mara nyingi kwa muda mrefu. Kwa mtu

aliye na VVU, kisichojulikana hujulikana, ama kitajulikana

hatua moja baada ya nyingine na muda ukiendelea. Kwa ka-

waida wale ambao wapo karibu ya watu wenye VVU hujikuta

wakiwa na shauku kubwa kuliko hata wahanga wenyewe,

hasa kwa sababu wao wenyewe hawaupitii mchakato huo

na wanaweza kudhania tu jinsi gani yalivyo mateso hayo.

Hofu ya kitu gani kitatokea ni kubwa zaidi kuliko hofu aliyo

nayo mtu wakati jambo limekwisha tokea na linaendelea ku-

wepo – na kwamba watu wengi wanaoishi na VVU wanaweza

kusema sambamba kuwa ni nafuu wanapozifikia awamu

za ugonjwa waliougopa hapo awali. Hii haina maana kuwa

shauku inapotea- daima kuna kitu kipya kinachoweza kuto-

kea: awamu mpya za ugonjwa unaoambaa katika upeo wa

maisha halisi huku ukileta tishio japo kwa mbali.

Kuishi na VVU na UKIMWI ni tendo jepesi la kuweka uwiano

baina ya uwezo wa kuachilia mambo na uwezo wa kudhibiti

– si tu katika ujinsia bali katika maisha pia. Hili ni tendo la ku-

jenga uwiano ambalo linaboresha ufahamu wa mtu wa nini

maana ya kuwa binadamu.

Uzoefu wa upendo, kukubalika na msaada baina ya vikundi vya huduma

ambapo upendo wa Mungu hudhihirika inaweza kuwa nguvu kubwa ya

uponyaji. Uponyaji unalelewa pale makanisa yanaposhiriki maisha ya kila

siku mahali ambapo watu hujisikia salama kusimulia habari na shuhuda

zao. Kupitia ibada za kweli, makanisa husaidia watu kuingia eneo la upon-

yaji la Mungu. Makanisa yana huduma muhimu sana katika kuhimiza ma-

jadiliano na changanuo za habari, kusaidia kutambua matatizo na kuunga

mkono ushiriki kuelekea mabadiliko yenye maendeleo katika jumuia.

JAPHET NDHLOVU

´

Page 44: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

42 SURA ZA MUNGU

Page 45: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

SURA ZA MUNGU 43

Kuwa sehemu ya matumaini ya

Kiulimwengu katikati ya mateso

Hii ilikuja yenyewe tu. Nilijitenga mwenyewe katika nyumba

moja mikoani na nikaanza kipindi kirefu cha maombi. Nilitaka

kuomba - na maisha katika utu wangu wa ndani yakaanza,

kama inavyokuwa unapoanza kuomba. Huu ni ulimwengu

wa ndani ambao unaendelea kujifungua wenyewe na kuleta

hali ya ushirikiano. Nilishi katika hali yangu ya hofu ya kufa na

kupata maambukizi ya UKIMWI na pole pole nikaanza kugund-

ua kuwa haikuwa sababu yangu kupata ugonjwa huo. Haikuwa

sababu kwamba nilistahili adhabu. Nimeupata ugonjwa huu

kwa sababu zingine kabisa.

Hivyo nilipata nguvu mpya ya kisaikolojia na nafasi ya kuto-

sha pia. Niligundua kuwa nimeendelea kuwa na furaha zaidi?

Maombi yaliwezesha furaha ipatikane na niliweza kukusanya

nyenzo mbalimbali na nguvu ambazo ningetumia kwa muda

uliobaki.ilikuwa kama chemichemi ya furaha ilikuwa ikitiririka

ndani yangu. Sasa nilikuwa nimekutana na kitu kingine na kama

Mkristo ningeweza kusema kikawaida kabisa kuwa nimekutana

na Yesu Kristo ama Mtakatifu. Mungu alinigusa, aliugusa moyo

wangu, ….na aliufungua moyo wangu,ili kwamba niweze kusi-

kia furaha ya msingi katika kuwa hai, furaha ya kuwa mwanad-

amu na kuishi na wanadamu wengine. Hofu yangu ilipungua,

na sasa ikiwa nitakufa ama nitaugua kukawa na maana kidogo

sana. Hakunisumbua tena. Cha maana zaidi kikawa hali iliyopo

kwa sasa kwani nilikuwa nimekutana na ulimwengu wa ndani

uliokuwa umejaa na vingi sana, na hii ikanipa nguvu zaidi na

uwezo wa kuishi, kiasi kwamba mipango yangu kwa ajili ya

siku zijazo ikaanza tena kuwa na maana.

Imani yangu ya ndani kabisa ni kuwa, watu wote wana-

oteseka, watahusika na kubeba maumivu ya ulimwengu wote

– mateso ambayo Kristo aliyapitia, hasa alipoona dhambi zote

ulimwenguni katika historia yote – zote mara moja. Imani

yangu ni kuwa kila mwanadamu anayeteseka hushiriki katika

kubeba mateso haya ya pamoja, ambayo wanadamu wote wa-

nashirikiana. Kwangu mimi, hii ina maana kwamba katika sabu-

ri niliyo nayo na ugonjwa wangu ninashiriki katika mateso haya

ya kiulimwengu. Hivyo kwa njia moja ninayashiriki mateso ya

Kristo, hii inanipa nguvu na furaha kubwa.

USHUHUDA WA BJARNE, ALIYEKUFA KWA UKIMWI

ImaniNimekuwa muumini kwa muda mrefu kadiri ninavyokumbuka,

lakini kama vile ilivyo kwa watu wengi imani yangu imepitia awa-

mu mbalimbali na migogoro mbalimbali.

Kwa muda mrefu kabla sijaambukizwa na VVU, nilipitia kipindi

kizima cha kuchanganyikiwa kuhusu dini, na sikuwa na uzoefu

mwingi wa maisha ya kihisia. Baada ya kugundua kuwa nina VVU

kidogo ama zaidi nimerejea tena kule nilikoanzia. Nimewahi

kuwa na mashaka na mtazamo wangu wote juu ya Kristo, mta-

zamo wangu kama fikra niliyonayo. Lakini katika kipindi hicho

cha migogoro ya kimaisha ndipo nilipogundua ya kuwa nilikuwa

nina VVU. Tangu hapo nimerejea kwa namna fulani katika imani

niliyokuwa nayo wakati wa utoto. Ninakumbuka matukio kadhaa

nikingali mtoto, moja ni uhusiano wenye kina pamoja na Yesu.

Uhusiano wa jinsi hiyo umenipatia nguvu –na ni chanzo cha mai-

sha mapya ya kupumzika katika imani yangu.

Baada ya kugundua kuwa nina VVU, nilipitia vipindi kadhaa vya

mitafaruku ya kihisia. Mawazo juu ya dhambi na hatia moyoni,

kama inavyotokea kwa wengi wetu – kujisikia kwamba mimi ndiye

niliyeusababisha ugonjwa huu. Kisha fedheha iliyofuata baadaye

kama matokeo ya hali hiyo. Nilipambana na hali hiyo kwa mwaka

mmoja na vita hiyo ilinifanya nijione mtu wa kuogofya sana.

Nilikuwa nimejilaumu sana mwenyewe. Nilikuwa na hak-

imu ndani yangu, ambaye daima aliniambia nimejisababshia

mwenyewe ugonjwa ule. Kwa mwaka wote ule nilizidi kujisikia

fedheha, mwenye hatia na mwenye dhambi. Ingawa niliende-

lea, kupambana na hali zote hizo. Nilikosa baraka ya ushirika wa

Kikristo ambao ungenisaidia kushinda hatia, fedheha na dhambi

moyoni mwangu. Ina sumbua sana pindi unapogundua vema ya

kwamba una VVU kwani unaanza kupata dalili ndogo ndogo hapa

na pale, na hiyo hukuvunja pole pole.

Nilimaliza mapambano yangu ndani ya mwaka mmoja kwa

juhudi zangu mwenyewe. Yote kwa sababu nilikosa na mtu wa

kunisaidia kufanya hivyo.

Maombi

Maombi yamenisaidia katika vipndi vyote vya shida yangu.

Nilipogundua ya kuwa nina VVU, mchakato ulianza, na katika

hatua fulani niligundua kuwa yanipasa nianze kuomba tena.

SURA ZA MUNGU

DENMARK

Page 46: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

44 SURA ZA MUNGU

NA JAPHET NDHLOVU

Matukio ya Kibiblia juu ya uponyaji alioufanya Yesu inajumuisha

maelezo ya kutosha juu ya watu walioponywa, na jinsi walivy-

oupokea uponyaji huo. Mwanamke yule asiyekuwa safi na

mwenye hali duni, mwenye ukoma aliyedhalilishwa na kudhi-

hakiwa, mtu yule aliyepooza na kutengwa, omba omba asi-

yeona – hawa wote walikutana na kukumbatiwa na upendo wa

ajabu toka kwa Mungu. Mara tu baada ya kujisikia kupendwa

na kukubalika, hali hii huwa tishio kwa wenye nguvu waliopo,

desturi, na watu ambao wamewapuuza, kuwakataa, na hata

kuwakandamiza.

Baada ya mahubiri ya Petro kwa watu zaidi ya wakati wa

Pentekoste mlemavu mmoja mwenye umri wa miaka 40 ali-

yelala langoni mwa Hekalu aliponywa. Naye Petro akatangaza

kuwa nguvu ya Yesu ya ufufuo ambayo ilifanya kazi kurejesha

mambo yote, ilimponya yule mlemavu na kwamba huyu Yesu

alipaswa kuabudiwa kama Bwana juu ya wote. Watawala we-

nye hofu wakawakamata Petro na Yohana. Walielewa kwamba

uponyaji huu si jambo jema la kawaida tu lililotendeka, bali

changamoto dhidi ya mamlaka yao, na wito mpya wa utii na

shambulio kwa mfumo uliopo.

Uzito aliokuwa nao Yesu alipokabiliana na magonjwa una-

tolewa kielelezo katika kisa cha uponyaji wa mtu aliyekuwa na

mkono uliolemaa (Mk 3:1-6). Uponyaji huu unapata umuhimu

katika siku ya Sabato, kwani katika fikra ya Kiebrania kutom-

ponya mtu yule kungemwacha katika hali inayokaribia kufa.

Mapambano dhidi ya ugonjwa ni mapambano ya kuwaokoa

wale ambao wameumizwa na nguvu ya mauti na hatari zake.

Kwa kuwa ugonjwa unapingamana na nguvu ya muumba ya

kuokoa, lazima urekebishwe na uumbaji kurejeshwa. Yesu ni

mkombozi ambaye rehema za Mungu zinapatikana. Kilicho

kipya katika huduma yake ni kwamba wenye kunufaika na hu-

ruma za Mungu si viongozi wa kidini na wasomi wa sheria lakini

ni wale wanaochukuliwa kama walio nje, masikini, walemavu,

wagonjwa, na wale waliofiwa. Yesu alijiweka huru kufikiwa na

kila mmoja aliyemhitaji, akipuuza mipaka iliyozoeleka na hivyo

kuwatambua rasmi wale waliotupwa na ulimwengu kwa saba-

bu moja hadi nyingine. Kwa utaratibu wa kudumu alikutana na

watu katika maeneo yao ya kuhitaji na kuyashughulikia mahi-

taji hayo. Yesu anaelezwa kama mpiganaji, ambaye mara kwa

mara kwa nguvu alizo nazo anapingana na mamlaka yale am-

bayo yamewaweka watu katika hali ya unyonge. Chochote kile

kilichowafunga watu lazima kikabiliwe na nguvu inayowezesha

hayo kuharibiwa. Kwa jinsi hiyo wagonjwa waliponywa, wale-

mavu wakapewa nguvu mpya ya utendaji na walionyanyaswa

kufunguliwa.

Wakati yesu alipowakaribisha wagonjwa na walemavu kwa

mikono meupe aliwasilisha mfano wenye nguvu kwa wafuasi

wake. Namna ambayo makanisa na washirika wake wanakabili-

ana na changamoto ya VVU na UKIMWI ni kielelezo cha kiwango

cha umakini walio nao katika kumfuata Yesu. Itikio lenye up-

endo na huruma - la mikono iliofunguliwa- linatakiwa toka

kwa watu wa Mungu. Ni daraka ambalo Yesu Kristo alilitoa, kwa

mfano maelezo juu ya Hukumu katika Matt 25:31-46. Zaidi,

itikio kama hilo ni ishara ya neema na upendo wa Mungu, si

katika maudhui ya UKIMWI tu bali kwa jumuia yote kwa ujumla.

Inatangaza kwa ajili ya wote kusikia na kuona kwamba utawala

wa Mungu unaanza kutambulika na kuanza kupata sura yake

duniani.

Kuwakubali katika upendo wale wanaoishi na VVU inatangaza

kuwa nguvu ya Mungu ya kuokoa inachukua hatamu dhidi ya

mauti na nguvu yake ya kuharibu. Huruma kwa hakika ndiyo

wito wa awali walio nao watu wa Mungu katika janga lililosaba-

bishwa na wimbi la VVU na UKIMWI.

Ni ufahamu gani wa undani ambao imani ya Kikristo inatupa-

tia katika hatua hii ya ukomavu wa kuwepo kwa UKIMWI. Baa-

dhi ya maandiko ya Agano Jipya yanaashiria kile tunachoamini

kuwa lazima kijumuishwe katika harakati kamilifu za Kikristo za

kupinga ukimya, fedheha, na unyanyapaa kwani haya yote ya-

nahusishwa na maambukizi ya VVU na UKIMWI, hatua ambayo

ni muhimu leo kama ilivyokuwa mara tu baada ya UKIMWI ku-

tambuliwa.

Matendo ya Uponyaji ya Yesu

tafakuri ya BibliaZAMBIA

Page 47: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

SURA ZA MUNGU 45

Labda, hakuna ugonjwa ambao ulikuwa wa kutisha sana ka-

tika Palestina ya karne ya kwanza kama vile ukoma. Ukoma ulie-

nea polepole hadi kuufanya mwili uchukize na hivyo kunyang-

anywa umahiri wake. Kupata maambukizi hayo kulimaanisha

kutengwa ili kutogusana na mtu yeyote asiye na ukoma; ukoma

si tu haukuwa na tiba bali pia ulikuwa ni hatari.

Alipokutana na mwenye ukoma katika barabara kuu ya Gal-

ilaya, Yesu angeliweza kutamka neno la uponyaji kutokea

mbali, kama alivyofanya katika matukio mengine (k.m.Luka

7:1). Lakini Yesu alichagua kuunyosha mkono wake na kum-

gusa mwenye ukoma huku akimponya. Kwa kufanya hivyo,

Yesu alizipinga desturi za kijamii na pia kutoujali ukoma katika

hali yake halisi. Aliamua kuhatarisha afya yake na kibali chake

mbele ya jamii kwa kuweka mikono yake juu ya mtu aliyechoka

na maisha.

Kwa nini Yesu alitenda kwa namna hii isiyokubalika kiafya na

kijamii? Marko anatueleza ya kuwa Yesu alifanya hivyo kwa

sababu alisukumwa na huruma kwa tatizo la mwenye ukoma

yule.

Uponyaji wa mwenye ukoma yule haukuwa tendo lililojiten-

ga. Huruma iliambatana na maisha na huduma ya Yesu. Mara

kwa mara aliguswa na huruma alipoiona njaa, alipouona ujinga,

ugonjwa, na hata alipokiona kifo. Kwa hiyo Yesu alikamatwa

na huruma wakati alipowaona watu wa kawaida katika hali ya

kupoteza shabaha ya maisha na kuwa kama “kondoo wasio na

mchungaji” (Math 6:34), wagonjwa na wasioona wakiwa mion-

goni mwa makundi ya watu (Math 14:14; 20:34), na huzuni ya

wale waliopoteza wapendwa wao (Luka 7:13; Yohana 11:35).

Bila kubakia tu katika eneo la hisia, huruma ya Yesu ilijieleza

yenyewe katika utendaji wake ndani ya huduma yake. Kuto-

kana na huruma yake aliwafufua wafu (Yohana 11; Luka 7:14),

aliwafundisha watu wengi (Marko 6:34), na kuponya wagonjwa

(Math 14:14; 4:23; 9:23; 9:35; 19:2)

Katika kuwahudumia wenye shida Bwana Yesu hakuogopa

kugusana nao. Alikamata mikono ya wagonjwa (Marko 1:31;

Math 9:25) na wale waliofungwa na shetani (Marko 9:27). Vid-

ole vyake viliwagusa wasioona (Math 20:34; Yohana 9:6; Math

9:29), viziwi (Marko 7:33), na wasiosema (Marko 7:33). Cha

kushangaza kabisa zaidi ya yote, Yesu aliwagusa wenye ukoma

– wale waliotengwa wa enzi zake (Math 8:3; Marjo 1:41; Luka

5:12-13), na hivyo kuonyesha kina cha huruma yake.

Huruma ya Yesu haikuwa na mipaka, ilivuka rafiki zake wote

na hata kuwazunguka maadui zake. Akitarajia hatimaye ku-

kataliwa kwake katika taifa alilolipenda, Yesu aliulilia mji wa Ye-

rusalemu (Math 23:37). Wakati wa kukamatwa kwake alipenda

kumponya askari ambaye sikio lake lilikuwa limejeruhiwa ka-

tika purukushani iliyotokea (Luka 22:51). Yesu pia aliomba Baba

yake ajibu kwa rehema na msamaha kwa maaskari waliokuwa

wakimsulubisha (Luka 23:34). Kwa kufanya hivyo,Yesu aliishi

katika yale aliyofundisha, kwamba huruma zielekezwe kwa

mtu yeyote bila kubagua, kama mfano ule wa Baba wa mbin-

guni (Math 5:43-45). Kama mmoja wa wafuasi wake wa awali

alivyosema baada ya kuyatafakari maisha ya Yesu, “Kwani una-

ijua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo kwamba ingawa alikwa

tajiri lakini kwa ajili yetu akawa maskini ili kwamba kwa umas-

kini wake tuwe matajiri” (2 Kor 8:9).

Kulingana na Agano Jipya, Yesu si mfano mkubwa wa hu-

ruma peke yake. Muhimu zaidi, yeye anabeba moyo wa

huruma wa Mungu wa Biblia. Dhamira ya Mungu mwenye

huruma, inayoibuliwa kutokana na ufunuo wake mwe-

nyewe, inapatikana katikati ya imani ya jumuia ya Kiebra-

nia, baada ya kulifunua jina la kimungu kwa Musa mlimani

Sinai, Yahweh alijieleza mwenyewe kama “Mungu mwenye

neema na huruma, si mwepesi wa hasira, mwenye upendo

na mwaminifu” (Kut 34:6). Mungu huyu anawahurumia

watu katika taabu zao, si kwa sababu ya sifa zao za kibi-

nadamu ila kwa sababu ya upendo wa Mungu na rehema

zake nyingi. Tukumbuke kuwa Mungu ni mwenye neema

hata katikati ya dhambi na uasi wa kibinadamu. Mungu

hakika ni mwenye neema na rehema katika mazingira

haya ya UKIMWI. Huruma za Mungu zinatungoza kufikia

utendaji wa kimungu unaoonyeshwa Yatika Yesu Kristo.

SURA ZA MUNGU

Page 48: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

46 SURA ZA MUNGU

Tokea tukio la kwanza la kujitokeza kwake, VVU na UKIMWI dai-

ma umetafsiriwa kama adhabu toka kwa Mungu. Watu wengi

wenye VVU wameikubali tafsiri hii, na hii huongeza mateso

juu ya mateso. Dhana kwamba VVU na UKIMWI ni adhabu toka

kwa Mungu inaashiria sura asilia ya Mungu kama nguvu inay-

oadhibu na kukaripia.

Katika mafunzo ya Biblia yanayofuata tutazingatia visa vinne

toka Agano Jipya vinavyotupatia mbadala wa sura ya Mungu

yenye upendo na maendeleo.

Msingi wa kawaida wa visa hivi vinne ni kuwa vina akisi sura

ya Mungu katika mwendo. Mungu husogea na huweza ku-

sogezwa. Mungu si mgumu na si aliye mbali. Hukutana nasi

hapa, na pale tulipo.

LUKA 15:11-32

Mfano wa Mwana Mpotevu

Mungu anayekimbia na kukutana nasi

Hadithi ya Mwana mpotevu inatuonyesha sura yenye nguvu

ya Mungu kupitia mtazamo na matendo ya Baba. Mungu ndiye

anayetukumbatia – kwa dhati na kwa ukarimu. Anakimbia ku-

tujia na kutuzungushia mikono yake, kama vile hadithi inavy-

osema hivyo ndivyo baba anavyofanya. Na kinachomhimiza

ni ile nguvu ya upendo aliyonayo. Mwana mpotevu ni kielel-

ezo cha wale wanadamu walioko chini udongoni na pia nje ya

ulingo. Hii inaweza kumtokea mtu yeyote. Na mambo men-

gi yanaweza kutufanya tuzame chini kwa kuvunjika moyo.

Maana inayotolewa na hadithi hii katika injili ni kuwa Mungu

hutupa uwezekano wa maisha mapya, yanayopewa kielelezo

na uzoefu tulioupata na undani wa kifahamu tulioupata katika

safari yetu kuelekea chini. Kipo kituo cha mageuzi katika kila

mgogoro wa kimaisha, na kwetu sisi pia hata pale tulipovuruga

fursa zilizojitokeza kwa ajili yetu, zaidi kwetu tena hata pale

tunapoona aibu juu ya maamuzi na makosa yetu.

Hadithi hii inatupa matumaini kwamba tunaweza kuendelea

kuishi maisha yetu pamoja na hayo yote yanayotupata – na

kwamba yupo Mungu na wapo wanadamu ambao wanasubiri

kutukaribisha jinsi tulivyo – bila kujali hali yetu ya kiafya na

VVU ama historia ya maisha yetu.

Maswali ya Kufikiria

• LiniMungualikujanakukutananawekatikaharakatizamai-

sha yako?

• Unawezakujifananishanananizaidi­mwanampotevuama

kaka yake mkubwa ambaye anadhani hakutendewa vizuri

na babaye?

• Nanikatiyaoyukombalikabisanababayao?

• Kunauhusianoganikatiya“msamaha”na“haki”?

LUKA 24: 13-35

Simulizi ya Safari kulekea Emmau

Mungu anayetembea kando yetu

Huzuni huleta ganzi katika fahamu zetu. Hivi ndivyo ilivyo-

tokea kwa wanafunzi baada ya Yesu kufa. Ni wagumu kusiki-

liza, akili zao zimepumbaa, wasioona vizuri na walioyumba

na kwenda mbali. Hawatambui kuwa Bwana aliyefufuka

anatembea kando yao.

Hadithi hii inaelezea sura ya Mungu aliyeshinda mateso ili

aweze kuchukuliana nasi katika huzuni yetu. Yeye anatem-

bea katika barabara mbaya pamoja nasi – bila kutuacha tu-

poteze lengo na mwamko. Hutubeza ili atuwezeshe kuona

mambo yote katika mtazamo mpya. Upendo wake wenye

nguvu unatufanya tuweze kuukabili ulimwengu unaotuzun-

guka – na kuendelea na maisha yetu. Anatutia moyo na ku-

tupa changamoto ya kuishi. Hukutana nasi kwa maneno na

kwa vitendo.

Sura hii ya Mungu imepewa maana yake na dhana ya Agano

La kale ya Mungu aliye Imanueli, yaani Mungu pamoja nasi.

Ndiyo. Mungu yu pamoja nasi, na amekuja na kukaa nasi. Yu

karibu – hata pale tunapotoa machozi ma kukasirika kwa ku-

toonekana kwake.

Maswali ya kufikiria

• Marangapi katikamaishayakoumejisikia kwambaulitele-

kezwa?

• Je inawezekana sura hii ya Mungu kuwa mfano mzuri

kwetu?

• JeinawezekanakweliMungualiyetembeakandokandoyetu

atatufundisha jinsi ya kutembea pamoja na wanadamu wen-

zetu wenye mahitaji?

• Je sura ya Mungu anayetembea pembeni mwetu inaleta

maana gani kwa wale wanaokufa na UKIMWI?.

• WanafunziwalimtambuaYesualipoumegamkatewakatiwa

Kujifunza Biblia

Sura Nne za MunguDENMARK

SURA ZA MUNGU

Page 49: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

SURA ZA MUNGU 47

chakula cha jioni. Je sakramenti ya Chakula cha Bwana ina

maana gani kwa watu wenye huzuni?

YOHANA 13:1-17

Hadithi ya Yesu akiwaosha miguu wanafunzi wake

Mungu anayeinama chini kutugusa

Hadithi ya Yesu akiwaosha miguu wanafunzi wake inatupa

picha ya Mungu aliye tayari kupiga magoti ili aweze kutu-

karibia. Utayari huu unafunuliwa katika kufanyika kwake

mwili, ambapo Mungu Mwana anainama chini kutoka mbin-

guni hadi chini, na katika tukio hilo kabla tu ya matukio ya

Ijumaa Kuu na Pasaka, ambapo Yesu anainama kuwahudu-

mia wanafunzi wake. Kwa njia hii anaonyesha unyenyekevu

na utayari kwa kugusana nao.

Watu wengi wenye VVU ni wahanga wa chuki na hofu ya

kugusana kimwili. Wanajisikia kuwa ugonjwa wao unawal-

izimisha kwenda magotini na kwamba watu wengine wa-

nawadharau na kujitenga nao. Yesu akiwa tayari kunyoosha

mkono wake na kuwagusa na kuwainua walio wanyonge ni

mfano mzuri kwa Wakristo binafsi na hata kwa kanisa kwa

jumla.

Maswali ya Kufikiria

• Jeliniilikuwamarayamwishokwakokupigamagotiilikum-

fikia mtu mwingine?

• Je umewahi kuwa, ama unahisi kuwa umekuwa mwenye

hofu ya kuwagusa wengine?

• JeunafikirininijuuyasurayaMunguaikwachiniameinama

na kukushika miguu na mikono?

• JesurayaainahiyoyaMungu inamaanaganikwawenye

VVU na UKIMWI?

YOHANA 9:1KK

Uponyaji wa mtu aliyezaliwa akiwa asiyeona

Mungu anayejinyoosha kutufikia na kutuponya

Katika kisa hiki cha uponyaji, Yesu anaondoa muunganiko wow-

ote kati ya hatia na hatima. Kwa kufanya hivyo pia anaondoa sura

ya Mungu kama yule anayehukumu ama kuadhibu, yeye anayet-

upatia tunachokistahili. Badala yake, katika uponyaji peke yake,

anachora picha halisi ya Mungu anayetufikia kwa nia ya kutuka-

milisha

Wakati wanapokutana na yule asiyeona, wanafunzi wanakuwa

na tahadhari. Wanatafuta mtu wa kumtupia lawama. Watu wengi

wenye VVU wanakutana na hali ya jinsi hiyo yenye utata wa ki-

maadili hata pale wanapojifungua na kueleza hali ya ugonjwa

walio nao. Uonevu wa kawaida ni ule ambapo wale wenye VVU na

UKIMWI wametengeneza vitanda vyao, na sasa ni lazima wavila-

lie. Katika hadithi hii Yesu anaweka wazi kuwa hatupati kile tuna-

chokistahili. Hadithi hii ya Injili ni moja tu kati ya nyingi zilizomo

katika Agano Jipya kuhusu uponyaji. Watu ambao wanumwa sana

wanahitaji kupewa matumaini, lakini matumaini bandia yanaweza

kuleta maumivu makubwa. Hata hivyo hakuna uwezekano kwa

wale wenye UKIMWI kuponywa, lakini matumaini yanayoletwa

na Injili, ni sura na mfano wa Mungu mwenye upendo ambaye

anaweza kutupatanisha sisi katika ukweli wa ugonjwa na kutupa-

tia nguvu ya kuishi – bila kujali yote yaliyopo.

Maswali ya Kufikiria

• Jeunaamini kamakunauhusianobainayakile tunachoki-

fanya na kile kinachotutokea?

• Jewakatiwamiujizaumekwisha?

• Jeupatanishonaugonjwamkubwaunawezakuletaupon-

yaji wa kiroho?

Page 50: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

48 SURA ZA MUNGU

Mungu Anayesamehe1. Utangulizi

Katika tamaduni nyingi za kiafrika, kama si zote uhusiano baina

ya mtoto na mzazi hauwezi kuvunjwa kirahisi na kitu chochote.

Hata dhambi na kifo haviwezi kusitisha uhusiano wa aina hiyo.

Tunapohusisha mambo haya na Mungu muumbaji wa vyote

wakiwemo wanadamu., tunagundua kuwa hakuna kinachowe-

za kututenga na upendo wa Mungu. Je VVU na UKIMWI vinaweza

kututenga na Mungu jinsi hiyo mwenye kusamehe.

2. Tafakuri

Katika kujifunza kwa upana kifungu hicho – ambacho kinawe-

za kusomwa mara nyingi kutoka tafsiri mbalimbali ili kuweza

kukielewa vizuri na kuukubali mfano huo – maswali yafuatayo

yanaweza kusaidia:

a. Maswali yanayohusu kifungu chenyewe:

• OnyeshajinsimfanohuuunavyojibuhojayaMafarisayoka-

tika Luka 15:2

• Baba, Mwana na Roho wanapenda kufanya nini na kuona

nini kinatendeka?

• Kamayulemtotoaliyemdogokatikakisachetuangejihukumu

mwenyewe. Je! Baba angeweza kumpokea tena nyumbani?

• Je mfano wa mwana mpotevu unatufundisha nini juu ya

uhusiano wetu na Mungu?

• JeMafarisayowalitarajikujifunzaninikutokananakisahiki

cha kusisimua.

b. Maswali yanayohusiana na VVU na UKIMWI:

• Jeunaonamwelekohuohuokatikajuhudizetuzakukabili

maambukizi ya VVU?

• Je kuna wakati ambapo tunawadharau wale wanaoishi na

VVU kama watoto ambao wamepotea?

• Je huenda tunawaangalia kama wenye dhambi waliopata

maambukizi ya virusi kwa kuendesha maisha ya kutojali

chochote

• Tutatambuajechanzochamaambukizinakwanininilazima

tufahamu, je si kwa sababu zile zile za kutoa lawama.

• Je Mungu anaangalia watu wanaoishi na VVU na UKIMWI

kama wakosaji ambao hawawezi kusamehewa?

c. Jinsi kifungu kinavyohusika na mazingira yetu:

• Jetunawezakuionatabiaaliyokuwanayokakamkub-

wa katika kisa chetu miongoni mwa jamii ya Kikristo

katika kuendekeza ukimya, fedheha, na unyanyapaa

unaohusishwa na maambukizi ya VVU?

• Hebu angalia herufi zilizotajwa katika kifungu na

somo gani linaweza kutolewa humo na kulitumia ka-

tika mapambano dhidi ya unyanyapaa unaombatana

na VVU.

• Tunapatakanunizipitokakatikavifungu?

• Jinsi gani Kanisa linaweza kuwa chemichemi ya up-

endo na ukarimu?

Mfano wa Mwana mpotevu

Kujifunza Biblia Luka 15:11-32

ZAMBIA

Page 51: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

SURA ZA MUNGU 49

SURA ZA MUNGU

Katika semina ambayo iliendeshwa katika ukumbi wa Mt. Pau-

lo UCZ Kabwata mjadala ulifanyika ukijumuisha kundi la watu

walioishi na VVU. Wote hawa ni wanachama wa mtandao wa

kuhudumiana unaojulikana kama Mduara wenye Matumaini.

Ifuatayo ni kumbukumbu ya majibu yao juu ya vifungu kadhaa

vya Biblia.

LUKA 15:1-11

Kondoo aliyepotea na Sarafu iliyopotea

Kifungu kilisomwa na kundi lote kutoka tafsiri mbalimbali

za Biblia ili kupata maana halisi ya kifungu kile.

Baada ya kukisoma kifungu washiriki walipewa changamo-

to ni kwa jinsi gani watajisikia kama waishio na VVU endapo

kifungu kingesomwa mbele yao.

Yafuatayo ni majibu:

• Kujisikiamsamaha–Munguhusamehe

• Kujisikiaupendo–Mungunipendo

• Kujisikiakukaribishwa–Mungunimkarimu

•Kujisikiakuombasanabaadayakupitiamatatizo.Lazima

tukumbuke kuwa yupo Mungu mwenyezi wa kumpelekea

maombi yetu. Kifungu kinatupatia hisia za kuwa na uhakika

kiasi kwamba hata baada ya kupitia matatizo ama magumu

yupo Mungu wa kutusamehe daima tunapochukua hatua

zinazostahili.

Wengine walidhani ya kuwa kifungu kilileta hali ya kujisikia

kuhukumiwa tayari – mtu mmoja alisema: “ unapokisoma

kifungu hiki kwa mara ya kwanza utadhani sasa unahuku-

miwa hasa ikiwa umeishi maisha yasiyokuwa na tahadhari

tena yaliyohususisha ngono.”

Kundi lilithibitisha ya kwamba wamejifunza Mungu yupo

ili kusamehe na kuwasaidia kuanza maisha maisha mapya

ambapo hawataangalia jinsi walivyopata ugonjwa bali kuishi

maisha yasiyo na majuto.

MWANZO 27-28

Mungu anaumba Mwanadamu kwa sura yake

Kifungu kilisomwa kutoka tafsiri tofauti za Biblia ili kuielewa

kwa udani maana yake.

Baada ya kusoma kifungu hicho tena, washiriki waliulizwa

nini kilikuwa kinaendelea katika fikra zao walipokuwa wak-

isikiliza kifungu hicho. Yafuatayo ni majibu waliyotoa:

• Mungunimkuu

• Mungunimwenyezi

• MungunimuumbahatakamatunaVVU,nayeametubari-

ki

• Tumeumbwa kwa sura ya Mungu na hivyo tunafanana

na Mungu na yote tunayoyapitia tuyaache mikononi mwa

Mungu kwani yeye ni muumba wetu. Muumba huyu anajua

na kuvielwea virusi hivi sana.

-Tunapaswa kuwa na shukrani na daima kumwomba Mungu

na kuendelea kumshukuru kwa maisha yetu.

Jambo lingine waliloliona wanachama ni kuwa ikiwa Mungu

ni muumba wetu –kwa nini tupitie mateso mengi – kwa nini

tuwe na VVU? Kwa nini asiviondoe virusi toka kwetu?

Mungu wa Uumbaji ZAMBIA

Masomo mawili ya Biblia

Sikuwahi kabisa kupitia maisha yaliyokamilika kama

nilivyofanya baada ya kugundua ya kuwa nina VVU.

Ili kukutana na nafsi yako mwenyewe - ni vigumu, ni

kazi kubwa, kitu ambacho ungependa kukiepuka kama

ungeweza, na tunahitaji msaada wa kila moja wetu

katika safari yote. .

USHUHUDA WA RONNY, ALIYEKUFA KWA UKIMWI, DENMARK

Page 52: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

50 SURA ZA MUNGU

Katika mijadala mjini Oslo, iliyowahusisha watu wanaoishi na

VVU ama kuathirika, kifungu hiki cha Biblia kikawa muhimu

sana kwa uelewa wetu juu ya kile kinachomaanisha kumwona

mtu kando yetu na kutopagawa na amri na taratibu za kisheria.

Miongozo ifuatayo inaweza kusaidia kujifunza kifungu hiki.

1. Soma kifungu kwa kuzingatia mazin-

gira yako mwenyewe na changamoto un-

azozikabili:

Kabla ya kusoma kifungu cha Biblia uulize maswali kadhaa juu

ya jinsi washiriki wanavyomchukulia Mungu kuwa ni nani na

jinsi gani mazingira tofauti ya maisha yanavyoweza kutupatia

sura tofauti ya Mungu. Kwa mfano:

• JeunawezakutuelezawakatiambapoulifikiriMunguame-

kuadhibu? Ulifanya nini?

• Je umewahi kujisikia ya kuwa Mungu anakupenda pale

tu unapokuwa unastahili hivyo ama kamaunazitii amri za

Mungu?

• Je pamewahi kuwepo mazingira ya aina nyingine ambapo

ulikosa uhakika wa upendo wa Mungu, ukifikiria kuwa Mungu

anaweza kuwa amekasirika kidogo ama mgumu kumwamini?

Turuhusu washiriki wafikirie juu ya jambo hili kwa muda kabla

hatujaanziasha mjadala wa vikundi. Ili kuweka mambo katika

wepesi wa kutokuwaogofya wengine unaweza kuanza kwa

kuwaeleza juu ya tukio ambalo unadhani huenda lilikuwa ad-

habu ya Mungu. Jaribu kuwasaidia watu kuelewa mifano na

sura tofauti tunayobeba pamoja nasi daima. Unaweza pia ku-

ziandika sura tofauti zilizotajwa katika karatasi pana ya ubaoni,

kwa mfano: Mungu anayekasirika; Mungu mwenye hali zina-

zobadilika; Mungu anayehukumu na kuendelea.

2. Kisome kifungu hicho kwa pamoja

Soma hadithi juu ya mwanamke mlemavu katika Luka 13:

10-17. kila mmoja asome sentensi ama andiko moja.

3. Kisome kifungu kwa ufasaha na kwa kirefu

Andika maneno ya msingi katika karatasi. Uliza maswali

ya jumla juu ya kifungu hiki.

• Kifunguhichokinahusunini?

• Ninikinakugusajuuyakifunguhiki?

• Dhamiraganizimokatikakifunguhiki?

Kisha angalia kwa makini katika kifungu:

• Unakutanananinikatikahadithi?

• Tunajifunzaninijuuyakifunguhiki

Inaweza pia kuwa na msaada mkubwa kuangalia mahu-

siano baina ya watu katika kifungu hicho, pia kutoka

katika mitazamo ya kijamii, kisiasa, na kiuchumi.

• Je viongozi wa sinagogi wanahusiana vipi na mateso

ya mwanamke?

• JeYesuanahusianavipinaviongoziwasinagogi?

• JeYesuanahusianavipinaSabato?

• Je viongozi wa sinagogi wanahusiana vipi na maisha

ya binadamu, hasa kulingana na alichosema Yesu?.

• Je watu tofauti waliokuwepo walisema nini mwisho-

ni?

• KunathiolojiaganiyaYesuyauelewawaMungukatika

kifungu?

• Unajisikiajekulinganishanakifungu?

Baada ya kufanya kazi kwa karibu pamoja na kifungu

hicho cha Biblia, ni vizuri kwamba myaangalie maisha

yenu na mazingira yenu.

• Jeunawezakuitambuahalialiyokuwanayoyulemwa-

namke?

• Je umewahi kukutana na matukio kama yale yaliom-

tokea yule mwanamke?

• Je kitu gani kingine unachodhani kinafanana na hali

aliyokuwa nayo yule mwanamke?

• JeUnahusianavipinanawenginewanaofanananaye

siku hizi

Mwanamke MlemavuNORWAY

Kujifunza Biblia kutoka Luka 13:10-17

Page 53: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

SURA ZA MUNGU 51

4. Soma kifungu ukiwa

na wazo la kubadili mambo

Masomo ya Biblia yaliyowekwa katika mazingira ya ma-

hali hayamaliziki hadi utakapoona kile ambacho unaweza

kufanya kuleta upeo wa matumaini katika kifungu katika

siku zetu za leo.

• Nanianayefanyamawasilianohayoamawapitunapata

sura ya Mungu ambayo Yesu anaiwakilisha leo?

• Tutapambana namna gani dhidi ya sura zinazopoto­

shwa za Mungu.

• Tutawezaje kueneza sura ya Mungu ambayo Yesu

ameleta?

• Tutafanyaje maisha kuwa bora kwa watu walio katika

hali kama ile aliyomo yule mwanamke?

Tafakuri

Mazungumzo mjini Oslo juu ya kifungu hiki yanaweza kupewa

muhtasari ufuatao;

Ukweli kwamba Yesu aliponya watu siku ya Sabato umekuwa

na maana kwa kuelewa moja ya sifa maalu sana za Mungu.

Hapa tunakutana na Mungu anayepinga mamlaka na kufun-

gua vifungo vya wale waliofungwa.

“Ni Mungu yule ambaye si tu anapatikana kwa shughuli kati

ya saa 3 asubuhi na saa 11 jioni, bali yeye ni nguvu isiyoweza

kuwekewa mipaka ya utendaji.”

Katika hadithi hii tunaona Mungu mwenyewe akivunja kanu-

ni za maandiko ”kwa sababu Mungu ameweka watu na huruma

juu ya sheria. Kile ambacho Yesu amekimaanisha ni kwamba

kusudi la sheria ni muhimu sana kuliko kufuata vipengele bi-

nafsi vya sheria yenye sura ya kutobatilika.” Au kama mshiriki

mmoja alivyosema , “Ni asili ya Mungu kupenda, na kusudi

la maneno na vitendo vyake ni kufungua vifungo vya watu,

kuwainua waliokandamizwa, kuweka huru waliofungwa, na

kuponya na kuokoa.”

SURA ZA MUNGU

Page 54: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

52 SURA ZA MUNGU

SURA ZA MUNGU

Hakuna Hukumu ZAMBIA

Mungu ni muumbaji mwenye upendo wa kudumu. Mungu ni Mungu anayesa-

mehe. Ijapokuwa mtu anaweza kuwa na VVU, tunajua kwamba Mungu anatu-

penda na anatuhudumia. Kwa kuwa yeye ni muumba wetu tumekubali hali

zetu za kiafya na kuendelea kumtafuta katika maisha yetu yote. Si wale wa-

naoishi na VVU ama Mungu anayestahili kulaumiwa kwa ugonjwa huo kuto-

kea. Upendo wa Mungu na kazi zake zinaweza kuwa zimedhihirishwa kupitia

walio baina yetu wanaoteseka. Mungu ni Mungu mwenye upendo kwa sababu

tuliumbwa kwa mfano wake na kubarikiwa naye. DUARA ZA MATUMAINI, ZAMBIA

K - Kiongozi

W- Wote

1. Ukusanyaji wa watu

muziki ukichezwa

2. Wito wa kuabudu

K: Bwana anasema “Mimi ndiye nikuponyaye…uniangalie mimi

nawe utapona.”

Marafiki, tumekutana hapa mbele za Mungu mwenyezi, yeye

anayejali na mwenye huruma. Kwa hiyo kupitia maombi na sifa

na nyimbo tumwaabudu Mungu anayeishi milele na mwenye

upendo mwingi. Amen.

3. Nyimbo za Sifa

4. Sala ya kufungua

K: Baba, upendo wako unafanya kazi kupitia uumbaji wote.

Mwana wa Mungu, katika mfano wako tutafanywa wapya. Roho

mtakatifu, umeyagusa maisha yetu kwa matumaini. Pokea

ibada yetu, utuchukue tena tukutumikie mbele zako: utuweke

huru ili tukutukuze leo.

Bwana, katika uwepo wako tunakubali sehemu yetu katika

dunia ambayo imechoshwa na maumivu. Katika zama zetu hizi

tunakutana na maumivu kwa njia mbalimbali. Tunapokutana

leo, wengi wanateseka kwa sababu ya wimbi la VVU na UKIMWI.

Watu wanaoishi na VVU wananyanyapaliwa. Tunakuomba Bwa-

na kwamba utatutumia sisi kama vyombo ambavyo upendo

wako unaweza kutiririka kuwafikia kaka zetu na dada zetu wa-

naoishi na VVU.

Bwana mwenye rehema, pale ambapo tumewanyanyapaa

rafiki zetu na pia sisi kwa sisi, utusamehe na uhuishe upendo

wako ndani ya mioyo yetu ili kwamba tuweze kuonyesha kujali

na huruma kwa wale wanaoishi na VVU.

Utuongoze katika ibada hii. Tunaomba tukutane na ushirika

wa kweli baina yetu nawe na baina yetu sisi kwa sisi.

Utusikie katika Jina la Mwanao Bwana wetu Yesu Kristo. Amina.

5. Maombi ya Toba

K: Bwana mwenye neema, kwa toba yetu yote ya imani ambayo

hutoweka utendaji unapohitajika, tumekiri kuwa tunakupenda na

kwamba tunapendana sisi kwa sisi lakini bila shaka haikuwa hivyo.

W: Tusamehe tunaomba

K: Utusamehe kwa kutokutii kwetu

W: Tumeshiriki maonevu, ukatili, na unyanyapaa dhidi ya wale

miongoni mwetu wanaoishi na VVU, kwa hivyo kuwanyanganya

watu maisha yenye uzima tele na tumaini ulilotupa ndani ya Mwa-

nao Yesu Kristo.

K: Kama jumuia yenye imani kwa Mwanao, hatujawaonyesha kaka

zetu na dada zetu wema wako.

Page 55: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

SURA ZA MUNGU 53

W: Uturehemu eeh Bwana

K: Kama Kanisa, hatujawa na upendo baina yetu kama vile Kristo

alivyotupenda: hatujasameheana kama tulivyosamehewa; hatu-

jajitolea kutumikia ulimwengu ulioharibika kwa upendo.

W: Tunakiri kuwa dhambi yetu kama kanisa katika jina la Bwana ali-

yejaa neema: Amina

6. Tamko la Msamaha

K: Marafiki, katika Yesu Kristo, hapa tuna uthibitisho wa upendo

wa ajabu wa Mungu. Ilikuwa wakati tukingali wenye dhambi

Yesu alikufa kwa ajili yetu. Pokea rehema za Mungu kwa Jina la

Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu.

W: Neema ya ajabu jinsi gani ilivyo tamu ile sauti iliyoniokoa

fukara kama mimi, nilikuwa nimepotea hapo awali lakini sasa

nimepatikana, nilikuwa nisiyeona lakini sasa ninaona

7. Maombi na ufahamu zaidi

K: Bwana mwenye neema, neno lako linatupatia uzima tele

katikati ya maumivu na mateso. Lnaleta matumaini wakati tu-

mekata tamaa. Naomba uturuhusu sisi kuisikia sauti yako leo

tunaposoma neno lako takatifu na tunaomba liponye kuvun-

jika kwetu moyo. Katika Jina la Yesu Kristo tunaomba. Amina!

8. Somo kutoka maandiko matakatifu

Yohana 8:1-11

9. Mwongozo wa Mahubiri

• walimuwasheriawalimletamwanamkenamtuanaweza

kushangaa yuko wapi mwanamume aliyekuwa akizini

naye. Sheria ya Musa ilihitaji kuuwawa kwa wote wawili na

si mwanamke peke yake [law 20:10, Kumb. 22:22]

• Waalimu washeria walitaka kumwaibisha yule mwanam-

kena kumnyanyapaa. Jambo ambalo ni baya sana kuli-

fanya. Wale walioambukizwa VVU hawapaswi kunyanya-

paliwa.

• Baadhiyetutunatendakanakwambahatujawahikufanya

dhambi siku za nyuma na kufikiri kuwa kaka zetu wanaoi-

shi na virusi wamefanya dhambi zaidi yetu. Sisi nasi ni

wenye dhambi pia.

• Yesu hakumhukumu lakini alionyesha huruma na kwa

neema kubwa alimwambia asitende dhambi tena.

10. Maombi

Kwa uchaguzi wako mwenyewe.

11. Nyimbo ya kufunga

12. Maombi ya Kufunga

W: Neema ya Bwana wetu Yesu, Upendo wa Mungu baba

na ushirika wa roho Mtakatifu, uwe nasi leo na siku zote.

Amina!

Page 56: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

54 SURA ZA MUNGU

“Ndani yake tunaishi

tunatembea na kuwa na uzima”

Utaratibu wa Ibada Kwa VituoNORWAY

Ibada hii ni matokeo ya mazungumzo yaliyofanyika Oslo juu ya

unyanyapaa wa watu wanaoishi na VVU. Inatarajiwa kwamba

ibada yote itajumuisha mahubiri yatakayoelezea sura ya Mun-

gu na fikra juu ya ubinadamu.

Utangulizi wa Utaratibu

wa Ibada na maandalizi yake

Utaratibu wa Ibada sio mwongozo ulionyooka wa ibada. Wakati

mwingi wa ibada wale ambao watapenda wanaweza kutafuta

nafasi ya kwenda katika vituo mbalimbali katika chumba kile.

Vituo hivyo mbalimbali vinahusika na maisha ya binadamu na

kile kinachofanyika mbele za Mungu ambaye ametuumba,

ametukubali, na kutuweka huru.

Ibada hii kimsingi si ile ya kawaida, kwa hiyo ni muhimu

kwamba waabuduo waandaliwe mapema ili kwamba wawe

na mawazo ya kile ambacho watakishiriki. Maandalizi haya

yanaweza kufanyika katika vipindi vya mwanzo vya ibada,

vijalida vya kanisa na kadhalika. Hii ina maana ya kuwafanya

watu wasijisikie ya kutengwa ama kubaguliwa. Ni muhimu ku-

weka agenda kwa ibada ambayo inaelezea dhana iliyo nyuma

yake pamoja na maendeleo yake. Ibada hii ina mambo yanay-

ofanana na vituo asilia vya Msalaba.

Vituo vilivyotajwa hapa ni mapendekezo yetu. Vinapaswa

kuandaliwa kabla ya ibada. Kwa kuwa wanahitaji nafasi ya

kutosha unaweza kuongeza ama kupunguza idadi kulingana

na matakwa ya mahali mlipo na nafasi zilizopo. Katika maz-

ingira mengi, idadi ya vituo vilivyoorodheshwa inaweza isiwe

halisi. Kwa hiyo tunashauri ya kwamba ufanye uchaguzi. La-

kini kituo tulichokiita Mahali pa Ajabu lazima kiingizwe, ni

bora sana kwanza kutafuta namna asili za kuelezea jambo

zitakazotuwezesha kupata alama kwa vituo mbalimbali. Tu-

meandaa mapendekezo kadhaa ya rangi yatakayoweza kuju-

muishwa kwa kutundika vipandev ya nguo zilizofumwa uku-

tani ama kuzilaza chini. Pia inawezekana kuruhusu vipande

vyembamba vya nguo hizo vitoke katika vituo hadi Mahali pa

Ajabu. Kuwepo pia na Biblia iliyo wazi katika kila kituo, hasa

ikiwa imefunguliwa katika moja ya vifungu vya Biblia vilivyo-

pendekezwa. Kwa nyongeza kifungu kilicho kifupi kinaweza

kuandikwa katika karatasi na kuninginizwa juu ama kuwekwa

pembeni karibu na Biblia. Hii itasaidia kuona kituo kinamaan-

isha nini. Hatushauri watu kutumia vikaratasi vidogo vyenye

gundi. Muhimu sana: fanya mambo rahisi na yanayoweza

kutendeka. Haya tuliotoa ni ushauri tu, si mambo ya lazima:

mazingira ya mahali lazima yazingatiwe na hayo yataashiria

kile utakachopenda kujumuisha.

Pia tumeshauri mahali utakapoweka vituo hivyo mbalim-

bali katika chumba. Sehemu hizi pia zinategemea ucha-

guzi wako. Uwezekano mwingine ni kuendesha ibada hiyo

yote nje. Mlango wa kuingia “kanisani” unaweza kutumika

pia kama eneo la madhabahu. Lakini si wazo zuri kuwa na

vituo vingine ndani na vingine nje ya jengo. Hii itaweza

kutafsiriwa kana kwamba vituo vingine ni muhimu zaidi

ya vingine.

Shule ama jumba la parokia linaweza kutumika kama mahala

pa kuabudia. Maandalizi ya ibada yanaweza kuwa nafasi nzuri

ya kuendesha warsha inayowahusu vijana na watu wazima.

Muda unaweza kutumika kutafakari juu ya vituo na namna ya

kuvifikia, kushughulikia umoja wa ibada, kuandaa ramani na

kutengeneza vituo, na labda kutafuta njia mbadala ya kuvitolea

utambulisho. Unaweza, kwa mfano, kuambatanisha, uzoefu

binafsi na visa vingine katika baadhi ya vituo. Ni muhimu haya

nayo yawekwe kwa kifupi.

SURA ZA MUNGU

Page 57: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

SURA ZA MUNGU 55

• Mahali pa manunguniko na malalamiko

Uchungu, mawe, giza na rangi zinazon’gaa. Karibu na mlango

wa kuingilia nyumba ya ibada. Zab 22:2

• Mahali pa mazungumzo

Uwezekano wa kutua mizigo; toba. Pamewekwa nyuma ya

eneo la kuabudia. Viti vimepangwa viwili Viwili. Meza zikiwa

na vikombe na chai ya moto. Mawe yakiwa na mishumaa inay-

owaka juu yake. Rangi ya kijani iliyoiva sana. Yohana 3: Niko-

demo alikuja usiku kwa Yesu ili kusema……

• Mahali pa Ushirika

Pamewekwa nyuma pembeni mwa chumba. Mshumaa un-

aowaka umewekwa katikati ambapo watu wanaweza kuketi

katika mduara wakizunguka mwanga. 1 Kor 12;12-26 (mst.

13);Filipi 2:1.

• Mahali pa kicheko na furaha

Ukiambata moja ya kuta za nje. Manjano, rangi nyingi nyingi,

pua nyekundu, ama mchoro wa msanii. Mwanzo 18:12; I Kor

1:27a..

• Mahali pa mwili na Ujinsia

kuchua miguu ama mikono. Rangi zinazovutia kiupendo-

pinki, maua, mitandio, shela iliyoandaliwa vizuri. Wimbo wa

Sulemani Wimb.4:1; Luka 7:38b

• Mahali pa thamani

Lulu, nyota, kibahri. Kutoka Isaya 45:3: “ Nitawapa ninyi hazina

gizani na katika utajiri wa maeneo ya maficho. Ili ujue kwamba

ni mimi Bwana ninayekuita kwa Jina lako”.

• Kijito cha maji

Ni kisima. Katika kituo cha ubatizo, ukiwa na mimea iliyohifa-

dhiwa katika chungu, na mti. Mkondo wa maji wa kumwagilia

maua; maji baridi ya kunywa; karai la kuoshea. Rangi ya kiba-

hari na kijani. Yohana 4:14; Ubatizo wa Yesu, Ufunuo 22:1 , 17;

Zab 42:1

• Mahali pa uwazi na maumivu

Katikati, kuelekea nyuma ya eneo la kuabudia. Kitambaa cha

kufumwa rangi nyekundu (damu ya mzee) Uwezekano wa ku-

soma shairi na vifungu vingine. Yeremia 30:17.

• Mahali pa Ajabu

Ni mahali pa mageuzi, hamasa ya maisha na nguvu. Katikati ya

sehemu ya kuabudu. Kuna mkate na divai. Rangi zote zaweza

kukusanywa hapa..

• Mahali pa maombezi na kuwasha mishumaa

Njiani kuelekea eneo la madhabahu. Fursa ya kuwasha mshu-

maa na kuandika sala za maombezi katika vijikaratasi. Chungu

ama chombo kinachofanana. Rangi ya matumaini. Filipi 4:6

• Mahali pa Mapumziko

Mbele ya madhbahu. Rangi nzito zenye joto, mito ya vitanda,

blanketi, magodoro. Math 11:28

• Mahali pa Mapambano

Nyuma ya madhabahu, ikiwezekana sambamba na ukuta

kuelekea madhbahuni. Mabango, karatasi ukutani za kuandi-

kia. Rangi za mapambano. Zambarau. Ephe 6:12

Vituo

Page 58: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

56 SURA ZA MUNGU

1. Msafara

Wakati nyimbo inayostahili ikiimbwa. Washiriki wanabeba divai

na mkate [mmoja], maji kwa ajili ya vijito vya maji na mshumaa

kwa ajili ya kila kituo. Kila mtu mmoja awe na mshumaa mmo-

ja, unaobebwa katika mikono iliyofumbwa. Msafara utaelekea

madhbahuni.

2. Salamu pamoja na Neno fupi la Biblia

• Mdo17:24­25;27b–28

• Watu walio na mishumaa wataenda kwenye maeneo yao

rasmi ama baada ya salamu au ama wakati wa utambul-

isho pale kila kituo kitakapokuwa kinatajwa. Tunapofanya

hivyo, vituo vilivyoko karibu vitajwe mwanzoni, ili kwamba

ushirika uone kwamba pale ndipo wabeba mshumaa wana-

pokwenda. Baada ya hapo vifuate vituo vilivyopo mwishoni

mwa eneo la kuabudia.

3. Wimbo

4. Utangulizi

Maneno ya ufunguzi na maelezo ya chumba. Andaa mazin-

gira ya kiusalama ukizingatia kile kitakachotokea. Mambo ya

kutaja:

• Hakiyakuwakitukizima

• “TazamaMtuyule”,wekanafasikwaajiliyamaishayoteam-

bayo yanasaidiwa na Mungu

• Vituovyotevinatajwa,amanamtufulanianayesimuliatukio

lililotokea linalomuunganisha na kituo kimojawapo kati ya

hivyo, ama kwa kuchukua baadhi ya mawazo kutoka katika

mahubiri yaliyoandikwa mwishoni mwa orodha hii ya ibada

ilyopendekezwa. Ikiwa wabeba mshumaa wameelekea kati-

ka vituo vyao, basi wasimame pale kituo chao kitakapotajwa

huku wakiendelea kubeba mshumaa wao.

• Waeleze watu kwamba wanaweza kuendelea kukaa kimya

katika maeneo yao, au kwenda hadi vituo vyo vyote wa-

navyohitaji. Hakuna sababu ya kwenda kwenye vituo vingi

iwezekanavyo. Ni vema kusiskiliza hisia zako.

• Tangaza kama ibada ya Ushirika Mtakatifu itakuwepo ama

karamu ya chakula chenye upendo ama kitu kingine cho-

chote kufuatia ziara hadi vituo hivyo.

• KilakituKIFANYIKEmachonipaMungu,katikanyumbayake

na kimwelekee Mungu anayetukubali na aliyetuumba jinsi

tulivyo.

• Sala ya kuhitimisha Utangulizi Asante sana, kwamba

tunaweza kuwa watu tuliokamilika nyumbani mwako: wewe

muumba wetu: wewe Yesu, ambaye unatukubali na uliyetu-

weka huru: wewe Roho Mtakatifu, unayetoa na kufanya

upya maisha ndani yetu.”

5. Toba ya Imani

Pendekezo Kanuni ya Nicea

6. Muziki

Muziki wa ala ama wenye kuongoza kutafakari

7. Ziara kutembelea Vituo

Angalau kwa nusu saa: ama tukiwa kimya na muziki wa mbali

ukichezwa, ama katika ukimya ikiwa hilo haliogopeshi. Ikiwa

ukimya utachaguliwa, inaweza kuwa vizuri zaidi kuvunja

ukimya mara mbili ama tatu kwa kutumia nyimbo za kuta-

fakari. Hii inajenga hisia za ushirikiano katika chumba kizima

wakati watu wakitembelea vituo kadhaa.

8. Ushirika Mtakatifu au Mlo wa Upendo

Wakati watu wametawanyika chumbani, ibada inaendelea. Watu

wanaweza kubakia pale walipo.

• WakatikunaUshirikaMtakatifu:msherehekeajianapigama-

goti karibu na mkate na divai katika mlolongo wa kati wa viti

karibu na Mahali pa Ajabu na unaweza kuanza moja kwa moja

na maneno maalum ya kuendesha ibada hiyo: Usiku ule ali-

posalitiwa….”

• KuonyeshanaIsharayaAmani:“Tusalimianenisotekatikaup-

endo wa Yesu/ “Amani ya Bwana wetu iwe pamoja nanyi.”

• UgawajiwamezayaBwanaunaanziaMahalipaAjabu.Wale

wanaopenda wanaweza kupokea Ushirika Mtakatifu. Mkate

ambao umebarikiwa [si kuwekwa wakfu] unaweza kugawan-

ywa kwa wale ambao hawatarajii kupokea Ushirika. Ugawaji

huo unaweza kufanyika kimya kimya ukiambatana na nyim-

bo za kutafakari.

9. Sala ya Bwana, Baraka ya kufunga na kutawanyika

Kila mmoja anakusanyika katika katika duara ndani ya du-

ara. Sala ya bwana inasemwa kwa pamoja, kisha Mchungaji

anatamka Baraka ya Kufunga Ibada

10. Wimbo wa kuongoza msafara wa kutoka

Utaratibu wa Ibada

SURA ZA MUNGU

“Ndani yeke tunaishi,

tunatembea na kuwa na huo uzima”

Page 59: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

SURA ZA MUNGU 57

Tupo hapa. Tumekuja kusimama mbele za Bwana ndani ya

uwepo wake Yeye Aliye Mtakatifu. Tumeupa kisogo ulimwengu.

Ulimwengu ulio laini, mgumu, usio na haki, uliojaa anasa na

wenye kupendeza. Tumesimama hapa, tukiangalia kwa uhakika

nje. Lakini “Ulimwengu” haujatupa sisi visogo. Sie tungali tu-

meubeba pamoja nasi, na ndani yetu fadhaa na hasira bado

zinakoroga mambo chini chini. Kutaka na kushindwa bado zi-

nashindana baina yao ili kutupotosha tusitafute kukutana na

Yeye Aliye Mtakatifu. Inawezekana mwili wetu huu wa kibinada-

mu unaweza kukumbuka uzoefu wa usiku ule ingawa roho zetu

zina mwelekeo wa kulisahau hilo, ya kwamba kujivunia mambo

mazuri yaliyopita jana inahatarisha unyenyekevu ama kuleta

fedheha kwa wale wanaotishia heshima yetu binafsi.

Tunajaribu kuwa kamili na tunaamini kuwa hii ni sawa na

kusema tuwe kamili katika hali ile tunayopaswa kuwa nayo tun-

apomkaribia Mungu…ama je si hivi ndivyo inavyopaswa kuwa?

Je kuwa kamili si kukubali tofauti zilizopo za mema na mabaya?

Je si mtu binafsi kujipatia haki ya kuwa sehemu ya uumbaji na

pia kuwa sehemu ya ulimwengu unaoendelea kuhangaika?

Ni pale tu tunapolikubali hili na kupeleka Kanisani vyote vile tu-

livyo navyo kama wanadamu, ndipo tunapoweza kukutana na Yeye

Aliye Mtakatifu. Hapo tunatoa nafasi kwa neema, kukaribishwa

tena kwa Mungu na furaha. Kila kitu kinawezekana kwa Mungu.

Katika ibada hii tutaruhusiwa kuwa vile tulivyo, yaani bin-

adamu. Ndani ya kila mmoja wetu kuna vyumba vya kutosha,

na leo kuna vyumba vingi katika nyumba hii ya Bwana. Wakati

mwingine ni vile vyumba vyenye furaha na shukrani ndivyo

vinavyotawala nafasi zilizopo ndani yetu. Ikiwa hivyo ndivyo

ilivyo kwako leo basi mfuate mbeba mshumaa hadi sehemu

ya furaha na kicheko. Ikiwa kwa upande mwingine ikiwa hii ni

siku ambapo chumba cha aibu na hasira kinatawala, basi ufuate

mbeba mshumaa mwingine hadi sehemu ya malalamiko na

manunguniko. Ikiwa mwili wako utahama kati ya kuwa na haja

ya kuguswa na haja ya kupumzika, basi utembelee vituo vyote

kile cha mwili, ujinsia na uhisia – na mahali pa mapumziko. Ama

ikiwa upo katika kipindi cha maisha yako unapoona kuwa kila

kitu kimekauka ndani yako, kana kwamba unazunguka ovyo

katika uwanda ulio kame, hivyo basi ufuate mbeba mshumaa

hadi kisima chenye maji yenye uhai au usafiri hadi mahali pen-

gine panapofaa ambapo utaweza tena kuinuka katika umaarufu

wako. Ama uchukue njia itakayokutoa toka sehemu ya mazun-

gumzo, ambapo unaweza kujifungua na kujiachilia mwenyewe

kwa mambo yote yanayokuzuia usikutane na wengine, hadi se-

hemu ya ushirikiano ambapo utapokea nguvu kwa kutiwa moyo

na wenzako. Kutoka hapo unaweza kuendelea mbele zaidi, ama

kwa wengine katika sehemu ya maombezi yenye kuombeana

na uwashaji wa mishumaa, ama unaweza kujitupa mwenyewe

uwanjani kupigania maisha bora katika mahali panapohusika.

Mwisho, fuata barabara inayoongoza kutoka vituo vyote hadi

MAHALI PA AJABU ambapo tunainua mikono yetu kama vyombo

vitupu na kupokea mkate na divai, ujasiri wa kuishi na nguvu ya

kutoka na kwenda ulimwenguni – pamoja na Mungu.

Namna hii tunakuwa salama. Tukiwa ndani ya nyumba ya Mungu

tukionana ana kwa ana na yeye Aliye Mtakatifu, tunaweza kuwa

vile tulivyo. Kila kitu kinawezekana kufanyika - kwa Mungu.

Kaa kimya kwa muda na ujisikie kile unachokihitaji leo. Labda

inatosha kutembelea kituo kimoja – ama utapenda kukaa tu ka-

tika viti vya kanisani wakati wote? Chochote ambacho ni sahihi

kwako bado ni sahihi tu.

Katika nyumba ya Mungu tupo huru.

Ndani ya Nyumba ya Mungu tunaishi nakutembea na kupata

uhai wetu.

Mahubiri Yaliyopendekezwa

Page 60: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

58 SURA ZA MUNGU

Kila mwaka wakati wa majira ya baridi, kipindi cha faragha huan-

daliwa kwa ajili ya watu wanaoishi na VVU na UKIMWI pamoja

na wapendwa wao. Watu huja pamoja kutafakari, kuomba,

kuzingatia na kusaidiana – kwa ukimya na pia kwa kushuhudi-

ana. Huu ni mfano wa utaratibu wa ibada ya pamoja:

1. Nyimbo

2. Sala ya Asubuhi

Tuombe,

Mungu Bwana wetu

Tunakushukuru kwa ukimya huu

Katika ulimwengu uliojaa kelele na purukushani.

Asante kwa sababu upo hapa

Bwana, uende pamoja nasi katika siku mpya iliyo mbele yetu.

Hatujui ikiwa siku hii itangaa na kupendeza

Ama itakuwa imezingwa zingwa na iliyo chungu.

Lakini tunaamini na kutumaini kuwa wewe ni Mungu wa upendo,

Kwamba utaenda pamoja nasi kila siku hadi mwisho wa nyakati,

Ndiyo,hadi ndani ya umilele usio na mwisho,

Kwamba unatupenda na kutusaidia bila kujali kinachotokea.

Utusaidie tuwe na muda mzuri wa maombi leo

Utujalie kuyasikia mapigo ya moyo wako. Amina!

3. Somo la Biblia

: LUKE 24:13-35

4. Kutafakari

Tunaweza kufuata njia nyingi katika maisha yetu. Tunaweza

kuchukua njia kuu ama zile za pembeni. Tunaweza kuchukua

njia za mkato ama kuchukua mizunguko. Tunaweza kupotea

na kukengeuka. Tunaweza kusimama katika njia panda na ku-

kosa fikra ya kuchagua mwelekeo wa kufuata.

Tunaweza kufuata njia nyingi katika maisha yetu. Kati ya hizo

zingine hutuongoza katika njia isiyo na mpenyo wa kutokea.

Nyingine hutufikisha pale tunapotaka kufika. Na kisha vipo vijia

ambavyo hatujawahi kukanyaga miguu yetu, njia ambazo haz-

ijapitiwa, maeneo yenye fursa ambazo bado kuvumbuliwa.

Hapo zamani palikuwepo mtu aliyefikia mwisho wa safari

yake – mbinguni. Pamoja na Bwana aliona maisha yake yak-

ipita. Alifurahi alipoona nyakati za kupendeza na alilia alipoo-

na nyakati za kusiskitisha. Lakini aligundua ya kwamba katika

nyakati zote njema, kulikuwa na fungu lingine la nyayo pem-

beni mwa zile zake, kana kwamba kulikuwa na mwingine. La-

kini katika nyakati mbaya kulikuwa na nyayo za miguu miwili

zikipasua njia katika safari ya maisha.

Yule mtu alimwangalia Bwana na kumwuliza kwa kumkaripia,

“kwa nini ulikuwa nami tu pale kila kitu kilipokuwa rahisi nami

nikiwa na furaha? Kwa nini hukutembea nami wakati mambo

yalipokuwa mabaya zaidi?” Bwana akaligusa shavu lake na-

kumwambia “ Mtoto wangu mpendwa, wakati maisha yako

yalipokuwa hayavumiliki tena sikutembea pembeni mwako

bali nilikubeba.

Tunaweza kufuata njia nyingi katika maisha. Lakini muhimu

zaidi ya njia tunazochukua ni watu wanaotembea pembeni

mwetu, wenzetu tulio nao katika safari yetu. Yesu Kristo si tu

kiongozi wetu bali yeye ni mwenzetu. Hatua kwa hatua anat-

uongoza na anatusaidia katika mizigo yetu pale inapotuele-

mea. Yeye atatutegemeza, na kutuinua na kutuweka mabegani

mwake na kutubeba ikiwa tutwekwa chini kwa lazima. Amina!

5. Nyimbo

6. Amani

Amani ya Mungu inapokelewakwa kukumbatiana katika up-

endo wa kindugu.

Mwongozo wa Ibada wakati wa Faragha

Sala ya Asubuhi

Juu ya UkaribuDENMARK

Page 61: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

SURA ZA MUNGU 59

Sala ya Mchana

1. Nyimbo

2. Maombi

Kama ilivyo kwa wanafunzi wako njiani kwenda Emmaus.

Nasi daima tunashindwa kuona

Kwamba ni wewe Yesu, uliyejiunga nasi safarini. Lakini pale

macho yetu yanapofunguka

Tunagundua kuwa ilikuwa ni wewe uliyeongea nasi siku

zote

Hata kama wakati mwingine tulikugeuka na hatukusikia

neno lolote ulilosema.

Lakini hiki ni kielelezo cha imani tuliyonayo kwako: kwamba

tujaribu kupenda na kusamehe pamoja na wewe

Ijapokuwa tumekuwa na mashaka, kwa sababu ya imani

yetu, wewe Yesu umekuwepo hapa daima, upendo wako

ukiwaka kwa kina kirefu ndani ya mioyo yetu.

Shukrani zetu zimfikie Mungu!

Amina!

3. Kusoma na Kutafakari

Luka 24:13 –35 ikisomwa polepole.

4. Ukimya Mfupi

Washiriki wanachagua neno ama sentensi kutoka masomo,

inayosambazwa kama kitambaa kilichorembwa kwa rangi

mchanganyiko na kutandikwa kanisani sakafuni.

5. Ukimya

6. Nyimbo

7. Baraka ya Haruni

hii itasomwa wakati wote wameshikana mikono: Bwana tu-

bariki na ututunze. Bwana ifanye sura yako in’gae juu yetu

na uwe na neema juu yetu. Bwana ainue hari yake juu yetu

na atupatie amani! Amina!

SURA ZA MUNGU

Pale ulipoketi Ukiwa na magamba ya

fedheha na uchafu

Wa mikono yako iliyo tupu bali imejawa na

makovu

Juu ya nafsi yako tupu na yenye makovu

Unasimulia hadithi yako na unahesabu

hasara uliyopata

Yule mtu aliyekuacha ama mtoto ambaye

ilibidi umwache

Sumu iliyofurika ndani ya mwili wako

Mto uliojaa ambao hakuna anayeweza

kuuzuia

Ambao hautaki kukoma katika kunguruma

kwake

Huku ikizipiga na kuharibu kingo zako zote

laini

Unasema nataka kufa Mimi sisemi kitu

Nina nyoosha mkono wangu na kuushika

mkono wako ulio mgumu na usio na raha

Sala ya Mchana

Kukaa Kimya na Kusikiliza

Page 62: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

60 SURA ZA MUNGU

NA CARINA WØHLK

Tumeogopa sana kugusana sisi kwa sisi. Ninyi mlio na VVU kwa

kiwango kikubwa mmekutana na hofu hii ya kutokuwa karibu

na wenzenu katika mwili na nafsi yako – vyote pale wale wa-

sioambukizwa wamejiweka mbali nawe katika wasiwasi wao na

kutokujua kwao, na wakati ambapo ninyi wenyewe mmewasu-

kuma wengine mbali nanyi kwa sababu mmekuwa na uoga wa

kupuuzwa na kukataliwa.

Tumeogopa sana kugusana sisi kwa sisi, kwa sababu kugu-

sana kimwili kunaanika udhaifu wetu na utofauti wetu. Hivyo

tunawapiga butwaa watu kwa mbali badala ya kuwaruhusu

watukaribie. Tunajiepusha kushirikiana na wengine. Mara

chache sana tumejitokeza mbele na kueleza habari zetu hu-

susan kuwa sisi ni akina nani. Hii inahitaji kujisikia kwa dhati

ndani yetu na ndani ya wengine pia, inahitaji ukaribu kwa Mun-

gu anayetukumbatia na na anayetupenda kupita mipaka yote

ya ufahamu.

Katika faragha hii tumeangalia asili na umuhimu wa ukaribu.

Mbali na pilika pilika za maisha ya kila siku tumezingatia maneno

na fikra. Tumezungumza lugha ya maombi na tumekutana kila

mmoja na mwenzake katika ukimya. Sasa tunataka kutembea

kidogo na wanafunzi katika barabara inayoelekea Emmaus –ili

tuweze kudaka na kuelewa vizuri ukaribu wa kimungu.

Hadithi ya Emmaus inatupeleka hadi wakati na mahali – mahali

penye utupu – baada ya jeuri ya msalaba wa Kalvari.wawili kati

ya wanafunzi wa Yesu, wawili kati ya marafiki wawili wapendwa,

wapo njiani kuelekea katika kijiji cha Emmaus. Walikuwa katika

hali ya masikitiko makubwa huku wakienda. Ingawa ilikuwa ikin-

gali ni mchana, wao bado walikuwa gizani kabisa. Hawakuweza

kuiona njia ya kuepuka maumivu yao. Kwa niniYesu, ambaye

alikuwa mwema sana, kuufikia mwisho mbaya wa aina hii? Je

hakuwa ameahidi ya kuwa atakuwepo pale kwa ajili yao? Na kisha

anaenda akiwa amewatelekeza bila kujali. Hawaelewi chochote –

yaani hata yote yale ambayo imemlazimu Yesu kutaabika kwayo.

Hawaoni maana yoyote katika kisirani hiki.

Wanafunzi wa Yesu wamepotea. Wajipoteza wenyewe katika

kujisikia kwao kupoteza. Wamempoteze mtu waliyempenda.na

pia wamepoteza imani yao katika maneno yake. Wasingeweza

Mahubiri katika Ibada ya Faragha

Luka 24:13-35

kuamini tena ya kwamba yeye alikuwa yule aliyesema kuwa

ndiye –mkombozi na Mwana wa Mungu matarajio yao yote na

matumaini waliyokuwa nayo yalitoweshwa.

Walimfuata mtu waliyeamini kuwa ni njia ya kwenda mbingu-

ni – na kwamba njia hiyo ghafla imebadilika na kufikia mwisho

wake. Wamechanganyikiwa na kukata tamaa. Wameondoka

Yerusalemu kwa huzuni na mshangao. Mino’ngono ilidai japo

kwa ukweli fulani kuwa kaburi la Yesu lilikuwa tupu. Lakini hiyo

ilionekana kuwa si kitu cha kuamini, kwani kilikuwa chema

sana kuwa cha kweli.

Ghafla, mtu wa tatu alifika katika eneo la tukio. Huyu alikuwa

ni Bwana aliyefufuka, Yesu Kristo. Tunalijua hilo. Lakini wa-

nafunzi hawakumtambua. Yote wanayoyaona ni mgeni tu.

Hawakukatishwa tamaa wanachokiona ni njonzi.

Mtu aliwauliza kwa nini wapo chini sana. Wanaonekana kana

kwamba wamepoteza rafiki yao wa karibu…wanafunzi wal-

imweleza nini kilitokea Yerusalemu siku chache zilizopita. Wa-

namweleza jinsi ndoto zao zote zilivyoharibika na kuanguka

na sasa zimelala chini ya msalaba.

Kwa uwezo mkubwa, yule mtu anawatafsiria unabii wa kale.

Anawaelezea jinsi ilivyoandikwa katika maandiko kuwa im-

empasa Mwana wa Mungu ateswe na kisha kuchukuliwa juu

katika utukufu. Anajaribu kuweka sawa maoni ya wanafunzi

juu yamambo yaliyotokea. Wanapokaribia kijiji walichokuwa

wakienda, yule mgeni alitangulia mbele kidogo kana kwamba

alikuwa akiendelea. Lakini wanafunzi, waliofurahia kuwa naye

na pia maneno yake yenye ufahamu, walimwomba akae na

kula pamoja nao. Wakati wa chakula, muujiza ulitokea. Mag-

amba yalidondoka kutoka katika macho ya wanafunzi.

Kwa muda mfupi tu wakati Yesu akiumega mkate, Karamu ya

Bwana ikawa imefanyiwa marejeo – lakini kwa namna nyingine.

Sasa imekuwa wazi kuwa yule anayetoa ndiye anayepewa.

Yesu Kristo amekufa na kufufuka. Mwili wake na damu yake

ni moja pamoja na mkate na divai.Ni katika ushirika huu wa

kila siku, na si barua isiyo na uhai inayowapa wanafunzi imani

katika ufufuo. Ni kule kuambatana, na si mazungumzo, kina-

chofungua akili zao. Wanafunzi wanamwona Yesu akiwa hai

katika mwili kule barabarani, lakini haiwaingii vizuri. Wanasi-

Mungu anayetugusaDENMARK

“Bwana, uwe pamoja nasi hapa,

karibu yetu wakati siku inapochomoza

na jua na mwanga wa nyota unapozizima

katika virindi vya giza la usiku.

Roho yako isituache kabisa hadi

utakapotupokea mbinguni”

Anima!

B.S. INGEMAN, NO. 366. KATIKA KITABU CHA NYIMBO CHA KIDENMARK CHA 1966

Page 63: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

SURA ZA MUNGU 61

kia anapotafsiri maandiko. Lakini hawamsikilizi kwa makini. Si

kwamba wana mioyo migumu tu, bali wao ni wagumu kusikia

na wazito kujifunza.

Ni wakati ule tu wanapokuwa wanajiandaa kula, muda wana-

poketi pamoja na Yesu chakulani, ndipo wanapogundua nam-

na gani mateso na utukufu vinaelea katika hadithi hii .Ufunuo

ni kuwa na macho yako wazi.

Katika furaha ya kutambuliwa, Yesu anatoweka. Njia zao

lazima zipishane kwa sasa, lakini wanafunzi hawasumbuliwi

tena na wasiwasi wa kutenganishwa na Yesu. Wamemwona na

kugundua kuwa yeye ni nani. Wamemtambua na kumkubali

kuwa yeye ni Mwana wa Mungu. Na kwamba anawaweka huru

warudie maisha yao na uhusiano na watu wengine. Mitume

waliokuwa wamekufa ganzi sasa wamepata nguvu mpya na

kuwa watendaji.

Hali za kimaisha ambazo hazitabiriki pia hazibadiliki haraka,

lakini si ilivyo kwa imani ya wanafunzi. Hawana majuto tena.

Hawapotezi mwelekeo tena. Sasa wanaweza kuiona maana ya

kile kilichotokea.

Hadithi ya safari kuelekea Emmaus ni hadithi ya mchakato wa

huzuni. Wanafunzi wanaenda katika safari ya ndani na ile ya nje.

Wanasafiri kutoka mashaka na kukata tamaa hadi utendaji.

Tunapowapoteza wale tuliowazoea, wakati vitu vinapopo-

romoka badala ya kuendelea mbele, wakati mioyo yetu inapo-

vunjika na hakuna kitu cha kutushikilia, tunaelemewa na hisia

za kutokuwa na maana na kukata tamaa. Tunakuwa kama wale

wanafunzi wawili wakielekea Emmaus. Tunajiona wapweke

na tuliotelekezwa na Mungu, na ndipo tunaililia mbingu “kwa

nini?”

Lakini hata hivyo hatuwezi kuiona maana mahali pasipo na

maana, ingawa pia hatuwezi kujenga mshikamano pale palipo

na maanguko, hatukuachwa peke yetu. Ipo njia ya kushinda

mateso. Yesu Kristo atajiunga nasi katika njia hiyo – hata pale

tunapomwona kama mgeni tu.

Yeye atatutoa kutoka katika giza la mashaka na kukata tamaa.

Atatupa ufahamu wa ndani ili tuweze kuiona hali yetu waziwa-

zi. Atatumwagia upendo wake na kutujaza matumaini. Matu-

maini huleta nuru katika maisha. Matumaini huyaona maisha

yetu jinsi yalivyo – wakati huo huo ikiangalia mianya ya kuleta

mabadiliko.

Tunaogopa sana kugusana sisi kwa sisi. Lakini tunaye Mungu

anayetugusa kwa uzuri wake mkubwa sana wa milele. Tu-

naogopa sana kukaribiana. Lakini tunaye Mungu ambaye huta-

ka tugusane naye: Mungu ambaye – kwa maana halisi- huja

ndani ya ngozi yetu, kwa sababu anatupenda.

Tunaogopa sana kugusana sisi kwa sisi. Lakini katika maisha

yetu na uhusiano baina yetu, Mungu huja karibu – hata kama

hatutaki chochote kutoka kwake na kinachomhusu. Yeye huja

karibu kwa upendo unaovuka mipaka yetu na kutuelemea kwa

nguvu zake. Amina!

Mpendwa Mungu Baba,

Asante sana kwa kuwa leo tulikuwa hapa

pamoja nawe na kila mmoja wetu

katika faragha hii.

Tunaomba:

Uiweke mioyo yetu tayari kuupokea

upendo.

Uyaweke macho yetu wazi

Kupokea ufunuo wako

Tuimarishe katika imani

Kwa kuwa wewe ni Bwana

Juu ya uzima na mauti

Juu ya walio hai na walio wafu pia

Wewe ambaye u sala moja mbali,

Uwe karibu nasi daima!

Amina!

Na sasa tuombe kwa muda mfupi tukiwa kimya…

Sasa mnaweza kusimama, na pamoja na mitume tunajiombea

na kumwombea kila mmoja.

Neema ya Bwana wetu Yesu kristo, Upendo wa Mungu Baba, na

ushirika wa Roho Mtakatifu

Uwe pamoja nasi sote

Amina!

SURA ZA MINGU

Page 64: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

62 SURA ZA MUNGU

Mungu, uliumba ulimwengu mmoja,usio na mipaka na migawanyiko.

Tunatubu hakika kwamba ni kwa sababu yetu ulimwengu umepasuka na kumeguka.

Tusaidie kurejesha umoja ulimwenguni,

Na utuunganishe katika mapambano ya kuwapatia watu wote wenye VVU fursa sawa na haki wanazopate watu wengine.

Mungu, tunaomba kwa ajili ya nchi zile ambazo mamlaka yamefumba macho yao na kutouoona ukweli unaodhihirishwa na VVU na UKIMWI.

Tupatie ujasiri wa kuziweka wazi, ili kwamba hakuna mwingine yeyote anayehitaji kutolewa kafara katika madhabahu ya kukataa.

Tunauwasha mshumaa kwa ajili ya umoja wa wanadamu wote.(Mshumaa unawashwa)

Mungu tupatie ujasiri ili tufanyie kazi umoja

Mungu wewe ambaye ni chanzo cha utu na heshima yetu.

Utuonyeshe wajibu tulionao kwa kila mmoja wetu.

Utusaidie kujenga ulimwengu ambapo hakuna atakayefaidika na mateso na huzuni ya watu wengine,

ulimwengu ambapo watafiti, wazalishaji wa madawa na sisi wenyewe tutakuwa makini kufahamu wajibu wetu wa kimaadili.

Mungu tunaoomba kwa ajili ya ulimwengu ambapo maisha ndio hoja kubwa –si takwimu na faida.

Tunawasha mshumaa kwa ajili ya vipaumbele sahihi katika jamii. (Mshumaa unawashwa)

Mungu utupatie ufahamu wa ndani kutendea kazi haki

Mungu, wewe uliyetuumba sawa bila kujali shughuli zetu za kutafuta maisha, ngazi za kijamii, utaifa ama mielekeo yetu ya ujinsia.

Utuunganishe dhidi ya mipaka yote ya kijamii tuliyoiweka.

Tunaomba kwa ajili ya waliojiajiri kutoa huduma ya ngono wanaonyonywa na kuishi chini ya ugumu wa kazi yao.

Tunaomba kwa ajili ya wale wote wanaopambana kwa ajili ya haki ya kujilinda wenyewe dhidi ya VVU.

Hao tunaomba wasikilizwe na kwamba wapate wasemaji wenye nguvu na ndugu halisi katika mapambano.

Tunawasha mshumaa kwa ajili ya dunia ambayo haitakuwa na sisi na wao.(Mshumaa Unawashwa).

Mungu tupatie mshikamano ili tuwe sauti kwa wasio na sauti.

Kuwasha Mishumaa

Page 65: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

SURA ZA MUNGU 63

Mungu, unatuhudumia na umetuita tumtumikie kila mmoja bila kuhesabu gharama.

Imarisha mwelekeo wetu na utayari wetu kumhudumia kila mmoja wetu.

Tunaomba kwa ajili ya waajiriwa katika sekta za afya na za kijamii na kwa waliojitolea wanaofanya kazi miongoni mwa watu wanaoishi na VVU.

Wasaidie kujua kuwa wanakutumikia wewe, Oh Bwana Mungu, na uwape ustahimilivu.

Tunawaombea marafiki, jamaa na wapenzi wa wale ambao wana VVU, na wale waliofiwa kutokana na UKIMWI.

Tunawasha mshumaa kwa ajili ya faraja kwa wale wanaomboleza. (mshumaa unawashwa)

Mungu utupe moyo wa huruma wa kuwahudumia wale wanaoteseka.

Mungu, umetuumba sisi sote kwa mfano wako na umetufanya kuwa waumbaji wenza wa ulimwengu wenye haki.

Utusaidie katika mapambano dhidi ya ubaguzi, ujinga, na upumbavu,

ili kwamba muda mfupi ujao tuweze kuona milima na mabonde ya ulimwengu unaowapatia heshima inayostahili wote wanaoishi na VVU.

Mungu, uwakaribie wale ambao wamepoteza ajira zao, marafiki wao, familia na wapenzi wao kwa sababu ya hali yao ya VVU.

Tunawasha mshumaa huu kwa ajili ya ulimwengu tukiwa na heshima na taadhima kwa watu wote. (Mshumaa unawashwa)

Mungu utupatie dira tutakayowashirikisha

Wale waliopoteza matumaini yole.

Mungu ambaye unatujua na kuyasikia maumivu yetu:

Tunajua kwamba hakuna kitakacho tutenganisha na upendo wako.

Tunaomba kwa ajili ya watu wote walio na VVU na wote ambao wameathiriwa na UKIMWI.

Ambao wanaishi na shauku nyingi, wakiwa na majonzi na kujisikia kupotelewa.

Mungu uliyeumba watu wote katika mfano wako, utusaidie kuwapo pale walipo wenzetu wanaoteseka.

Tunawasha mshumaa kwa ajili ya dunia ambapo tunashirikiana mateso na kuchukuliana mizigo. (Mshumaa unawashwa)

Mungu tupe upendo wako wa ziada ili tuweze kuelewa kwa kina zaidi maumivu na mategemeo ambayo ni sehemu ya binadamu.

Kumpenda Mungu

Tumeshirikiana na wewe katika

maumivu yetu na kupoteza kwetu.

Wewe ni tumaini letu

Katika mateso yetu na kuhitaji kwetu

Tunaomba tupate amani katika kuamini

kwamba wewe ni mwenye uwezo

miongoni mwa walio wadhaifu.

Utuonyeshe basi kuwa nguvu

zako zinaweza kudhihirika katikati

ya udhaifu wetu usio na kifani

Page 66: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

64 UTANGULIZI

BabaYetu Uliye Mbinguni

Katika siku hii ya UKIMWI Duniani

tunakuja kwako na kila kitu

kinacho tuponda ponda na kutusukuma

Tunaomba:

Uwe pamoja na wanao na binti

wala wote wanaoishi na VVU na UKIMWI.

Watoto wamekuwa yatima,

wanawake wamekuwa wajane.

Vizazi vinatoweka.

Mungu utupe nguvu ya kukabili

wimbi la UKIMWI katika

upana na ukubwa wake

Tuinue juu,

ili tuweze kwenda ulimwenguni

na kupambana dhidi ya UKIMWI

na ubaguzi wenye jeuri kubwa.

Tusaidie kukabiliana na kujitangazia haki kwetu

binafsi na mawazo yetu yasio sahihi kuhusu VVU

na wale walioambukizwa.

Fungua mioyo yetu kwa

ajili ya mabadiliko na upatanisho.

Katika wema wako Mungu

wape mapumziko wale

waliofariki kutokana na

kwa wale wanaoishi na na VVU

Hili tunaliomba katika

Jina la Yesu Kristo

Bwana wetu.

Sala Siku ya UKIMWI Duniani

Page 67: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-

Mwili Mmoja ilianzishwa kwa pamoja na Kikundi cha Kuweka

Mikakati kilichokutana Lusaka 2004.

Kutoka Zambia: Japhet Ndlovu, Joy Lubinga, Munalula

Akakulubelwa, Rose Malowa. Kutoka Msumbiji: Dinis Matso-

lo, Elias Massicame. Kutoka Norway: Jan Bjarne Sodal, Estrid

Hessellund, Steinar Eraker. Kutoka Denmark: Carina Wøhlk,

Birthe Juel Christensen. Kutoka EHAIA: Sue Parry

WALIOCHANGIA KITABU CHA 2

ZAMBIA

Mch. Japhet Ndhlovu, Katibu Mkuu wa wa Baraza la Makanisa

nchini Zambia. Akishirikiana na Duara za Tumaini. Joy Lubinga

Mshauri Nasaha Masuala ya Akili na Jamii, Duara za Tumaini.

Ackim Sakala. Mwalimu, Mwana harakati UKIMWI+. Duara

za Tumaini. Askofu Luckson Chibuye, Mch. Pearson Banda.

Mratibu VVU na UKIMWI kutoka Kanisa la Reformed, Zambia.

MSUMBIJI

Mch. Elias Zacarias Massicame, Mratibu wa Kitaifa wa VVU/

UKIMWI katika Baraza la Makanisa Msumbiji akishirikiana

na Mch. Dinis Matsolo, Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa

Msumbiji

DENMARK

Mch. Birthe Juel Christensen, Afisa Habari, DanChurch Aid.

Denmark. Mch. Carina Wøhlk, Chama cha Taifa cha UKIMWI

cha Kilutheri. Preben Bakbo Sloth, HIV+ activist. Elizabeth

Knox-Seith, Mwana Soshiolojia Mtamaduni

NORWAY

Jan Bjane Sodal, Mratibu wa Mradi wa VVU/UKIMWI wa

Baraza la Kikristo Norway akishirikiana na watu waishio

au walioathiriwa na VVU wanaokutana Aksept – Kituo cha

kanisa Mjini Oslo. Norway: Helge Fisknes, Oslo City Mis-

sion. Steinar Eraker, former pastor at Aksept, Mch. Elisabeth

Tveito, Mjumbe wa Bodi katika Baraza la UKIMWI Norway,

Mhariri-mwenza, na Estrid Hessellund, wa Toleo ‘Positive:

Branding, Sexuality, HIV and AIDS. Verbum, Norway, 2005

uk 16 na 29’

TUNASHUKURU KWA RUKHSA YENU YA KUTUMIA

YALIYOMO KTIKA TOLEO HILI LA SASA

MwiliMmoja

Page 68: MwiliMmoja - norgeskristnerad.no · Nitaurudishaje ujasiri wangu ka-tika maamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemea na kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yali-