KATIBA MPYA

40
KATIBA INAYOPENDEKEZWA Maudhui ya Msingi

description

Lugha Nyepesi

Transcript of KATIBA MPYA

Page 1: KATIBA MPYA

KATIBA INAYOPENDEKEZWA

Maudhui ya Msingi

Page 2: KATIBA MPYA

2 KATIBA INAYOPENDEKEZWA - Maudhui ya Msingi

1.0 UTANGULIZI

Mchakato wa kutunga Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umefikia hatua ya wananchi kuipigia kura Katiba

Inayopendekezwa, iliyopitishwa na Bunge Maalum tarehe 4 Oktoba, 2014. Awali, Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilitoa Rasimu ya Kwanza tarehe 3 Juni, 2013 na Rasimu ya Pili ilitolewa tarehe 30 Desemba, 2014 na kuwasilishwa kwenye Bunge Maalum tarehe 21 Februari, 2014.

Baada ya Bunge Maalum kukamilisha majukumu kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011, tunda lililozaliwa ni KATIBA INAYOPENDEKEZWA. Hatua inayofuata ni ya wananchi kuipigia kura Katiba Inayopendekezwa. Hivyo basi, kwa mujibu wa sheria, wananchi ndiyo wenye uamuzi na kauli ya mwisho juu ya upatikanaji wa Katiba Mpya.

Toleo hili linalenga kujenga na kuimarisha uelewa wa wananchi kuhusu Katiba Inayopendekezwa ili kufahamu maudhui mapya na yale yaliyoboreshwa ikilinganishwa na yaliyomo katika Katiba ya mwaka 1977, na kuwawezesha Watanzania wote kuielewa Katiba Inayopendekezwa ili kufanya uamuzi sahihi wakati wa upigaji kura ya maoni ifikapo Aprili 30, 2015.

Page 3: KATIBA MPYA

3KATIBA INAYOPENDEKEZWA -Maudhui ya Msingi

a) Alama na Sikukuu za Taifa (Ibara ya 3) Katika nchi yetu tumekuwa na alama za

utambulisho kama vile bendera, nembo na wimbo wa taifa. Hizi hazikuwahi kuwekwa ndani ya Katiba ingawaje zinatawaliwa na sheria husika. Katiba Inayopendekezwa imeziweka katika maudhui ili kuhakikisha zinafahamika vema na zinapewa ulinzi wa kikatiba. Alama hizo ni sikukuu za taifa, bendera, wimbo wa taifa. Sikukuu za taifa ni Siku ya Uhuru wa Tanganyika, Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar na Siku ya Muungano. Kuingizwa kwa mambo haya katika Katiba siyo tu kutakuza uelewa wa wananchi kuhusu alama muhimu za taifa na kuzitaja wazi, bali pia kutajenga na kukuza uzalendo wa wananchi kwa taifa lao.

Katika jamii yetu tunao watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali unaoathiri fursa zao za kupata mawasiliano kimaandishi au kwa alama. Kwa kutambua hili, kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, Katiba Inayopendekezwa inataja lugha ya alama kwa viziwi, na lugha ya alama mguso kwa viziwi wasioona kuwa lugha rasmi za mawasiliano. Hii ni hatua kubwa katika kuhakikisha kwamba ndugu zetu wenye ulemavu wanapata haki zao za aina mbalimbali ikiwamo haki ya kuwekewa mazingira imara ya kupata na kufanya mawasiliano kwa lugha muafaka kwao.

b) Lugha ya Taifa na Mawasiliano Mbadala (Ibara ya 4) Kiswahili ni hazina na tunu kwa taifa letu. Ni lugha inayobainisha

umoja na utaifa wetu. Ni lugha ambayo tunaienzi sana kama nyenzo ya kukuza mshikamano wa kitaifa na maelewano ndani ya jamii zetu. Katiba Inayopendekezwa imetambua umuhimu huu na sasa Kiswahili kinatajwa ndani ya Katiba. Kwa mnasaba huu, pamoja na kuwa lugha ya taifa, Katiba Inayopendekezwa inaelekeza Kiswahili kutumika katika mawasiliano rasmi ya kitaifa na kiserikali.

Sura ya kwanza ina maudhui ya jumla yafuatayo:

2.1 Sura ya Kwanza

Bendera ya Taifa

Nembo ya Taifa

Page 4: KATIBA MPYA

 

4 KATIBA INAYOPENDEKEZWA - Maudhui ya Msingi

c) Tunu za Taifa (Ibara ya 5)

Katiba Inayopendekezwa imeainisha tunu za taifa. Tunu ni kitu adhimu, ni kitu cha pekee, ni hidaya, ni zawadi. Ni kitu ambacho kwa muktadha wa ibara hii ni zawadi pekee kwa taifa letu. Hivyo Katiba Inayopendekezwa inazitaja tunu za taifa kwa nia ya kulitanabahisha taifa letu umuhimu wa kuzienzi na kuzilinda kama mboni ya jicho. Tunu zinazotajwa ni lugha ya Kiswahili, Muungano, utu na udugu, na amani na utulivu. Tunu hizi zitakuwa muhimili mmojawapo wa kujenga umoja na utangamano wa kitaifa.

d) Misingi ya Utawala Bora (Ibara ya 6) Mara kadhaa tumesikia kilio cha wananchi

wa ngazi zote wakitaka nchi yetu iwe imara na madhubuti katika kuweka na kuzingatia utawala bora. Ibara ya 6 inaiweka wazi misingi ya utawala bora kama masharti ya kufuatwa na viongozi na watumishi wa umma. Kuiweka misingi hii katika ibara ya 6 (na siyo ibara ya 5 inayohusu tunu za taifa) ni kuifanya iwe kipimo cha utendaji na utumishi wa umma. Huu utakuwa ni wajibu na si hiyari ya mtumishi wa umma kuamua kama anaienzi misingi hiyo au la, tofauti na kama ambavyo angeweza kuzienzi tunu zilizomo kwenye ibara ya 5, lakini zisingeweza kuchukuliwa kama kigezo cha kupima uwajibikaji na utendaji wake kwa umma endapo atashindwa kuizingatia.

Page 5: KATIBA MPYA

55KATIBA INAYOPENDEKEZWA -Maudhui ya Msingi

e) Mamlaka ya Wananchi (Ibara ya 7) Nchi yoyote inayoamini katika

demokrasia na utawala wa kisheria ni sharti itambue mamlaka ya wananchi wake. Katiba Inayopendekezwa inazingatia ukweli kwamba wananchi ndiyo msingi na chimbuko la mamlaka yote ya uendeshaji na utawala wa nchi. Katiba Inayopendekezwa inatamka wazi kuwa Serikali zote mbili yaani Serikali ya Muungano (SMT) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), zitapata mamlaka na madaraka yake kutoka kwa wananchi. Kwa msingi huu Serikali itawajibika kuhakikisha kwamba kunakuwepo mifumo thabiti inayolenga kuwashirikisha wananchi kikamilifu katika shughuli zote za uendeshaji wa taifa lao.

f) Ukuu na Utii wa Katiba (Ibara ya 9) Wakati wote wa maisha

ya taifa letu tumekuwa na ufahamu kwamba Katiba ndiyo “Sheria mama”, Katiba ndiyo chimbuko na dira ya taifa. Ndiyo msingi wa sheria zote. Katiba Inayopendekezwa inaubainisha “ukuu” huu katika ibara ya 9.

Page 6: KATIBA MPYA

6 KATIBA INAYOPENDEKEZWA - Maudhui ya Msingi

Sura ya pili inatoa dira ya mambo ambayo yataongoza maudhui ya Katiba na sheria nyingine zote zitakazotungwa ndani ya Jamhuri ya Muungano. Sura hii ina maudhui ya jumla yafuatayo:

2.2 Sura ya Pili

a) Malengo Makuu (Ibara ya 11 – 15) Lengo la ujumla la Katiba

inayopendekezwa ni kulinda, kuimarisha na kudumisha haki, usawa, udugu, amani, umoja na utangamano wa wananchi kwa kuzingatia ustawi wao na kujenga taifa huru lenye demokrasia, utawala bora, maendeleo endelevu na kujitegemea.

Pamoja na lengo la ujumla, Katiba Inayopendekezwa imebainisha kwa kina malengo mengine makuu ya Serikali katika Nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Umuhimu wa malengo haya ni kutoa dira katika kupanga na kutekeleza mikakati mbalimbali ya maendeleo ya nchi yetu.

Page 7: KATIBA MPYA

7KATIBA INAYOPENDEKEZWA -Maudhui ya Msingi

c) Sera ya Mambo ya Nje (Ibara ya 22) Kwa sasa nchi yetu inayo Sera

ya Mambo ya Nje. Katika Katiba Inayopendekezwa Sera hiyo imeboreshwa zaidi ili kuhakikisha kwamba inatekelezwa kikamilifu kwa kulinda maslahi ya taifa, kukuza maendeleo na kuleta ushirikiano wenye tija kwa nchi yetu.

Katika kuimarisha mchango wa sayansi na teknolojia, Tume ya Sayansi na Teknolojia sasa itakuwa chombo cha kikatiba cha kusimamia, kuratibu, kutafiti, na kushauri masuala ya sayansi na teknolojia nchini. Hatua hizi zote zinalenga kuweka mazingira madhubuti ya kikatiba na kisheria yatakayoongeza kasi ya maendeleo katika nchi zetu kwa kutumia sayansi, teknolojia na utafiti.

b) Dira ya Maendeleo, Mipango na Utekelezaji wa Malengo ya Taifa (Ibara ya 16 – 21) Katika taifa letu tumekuwa na mipango mingi ya maendeleo.

Mipango hii, pamoja na kuainisha mwelekeo na matarajio ya nchi yetu, haikuwahi kuwekewa msisitizo wa kikatiba. Katiba Inayopendekezwa inaainisha Dira ya Maendeleo ya Taifa. Dira ya Maendeleo ya Taifa ndiyo itakayokuwa msingi mkuu katika kutekeleza mipango yote ya maendeleo na kukuza ustawi wa taifa letu na watu wake wote.

Katika kuimarisha mwelekeo mpya wa maendeleo ya nchi yetu, Katiba Inayopendekezwa inatambua umuhimu wa shughuli za utafiti wa maendeleo kama msingi wa kukuza uchumi na kuimarisha sekta nyingine za taifa.

Nchi yetu hivi sasa inayo Tume ya Mipango ya Taifa. Chombo hiki sasa kimetambuliwa kikatiba kama chombo cha kupanga na kusimamia utekelezaji wa malengo ya kiuchumi na ya kijamii.

Page 8: KATIBA MPYA

8 KATIBA INAYOPENDEKEZWA - Maudhui ya Msingi

2.3 Sura ya Tatu

Sura hii ni mpya kabisa. Ni mara ya kwanza kuwa na vipengele ndani ya Katiba vinavyogusa rasilimali kuu za taifa letu na kuziwekea ulinzi wa kikatiba kwa manufaa

ya wananchi. Ibara za mwanzo za Katiba Inayopendekezwa zimeainisha dira na matarajio ya taifa letu katika Nyanja mbalimbali za maendeleo. Sura ya tatu inaainisha ile dhana inayokubalika duniani kote kwamba msingi mkuu wa maendeleo ya taifa lolote ni kujiletea maendeleo kwa kutumia rasilimali zake. Sura ya tatu inaainisha baadhi ya rasilimali za msingi za nchi yetu kama vile ardhi, maliasili na madini.

Page 9: KATIBA MPYA

9KATIBA INAYOPENDEKEZWA -Maudhui ya Msingi

Ardhi, Maliasili na Mazingira (Ibara ya 23 – 27) Katiba Inayopendekezwa inataja wazi

kuwa ardhi ndiyo rasilimali kuu kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi, kijamii na ustawi wa nchi na watu wake. Hivyo, Serikali zetu mbili (SMT na SMZ) zitaweka mipango bora ya matumizi endelevu ya ardhi kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Vile vile, ili kuhakikisha kwamba ardhi inawanufaisha wananchi, haki ya kumiliki ardhi inatajwa kuwa ni kwa raia wa Tanzania pekee, na mtu ambaye siyo raia wa Tanzania atakuwa na haki ya kutumia ardhi kwa uwekezaji na maendeleo mengine ya kiuchumi na makaazi.

Ifahamike vema kwamba haki ya kumiliki ardhi na mali nyingine ni ya wananchi wote. Hata hivyo, wanawake katika baadhi ya jamii zetu wamekosa kuifaidi haki hii kikamilifu. Katiba Inayopendekezwa imeona umuhimu wa kuwawekea wanawake ulinzi wa kikatiba katika eneo hili. Hivyo kwa mujibu wa ibara ya 23(2)(d) mwanamke atakuwa na haki sawa na mwanaume ya kupata, kumiliki, kutumia, kuendeleza na kusimamia ardhi. Ni kwa mara ya kwanza haki hii inatajwa kwa ufasaha wa aina yake.

Page 10: KATIBA MPYA

10 KATIBA INAYOPENDEKEZWA - Maudhui ya Msingi

Jamii yetu ina utajiri wa kuwa na makundi mbalimbali yenye mahitaji yanayotofautiana. Katiba Inayopendekezwa imetambua haki za makundi haya ya kumiliki, kutumia, kuendeleza na kuhifadhi ardhi kwa makundi ya wakulima, wavuvi, wafugaji, wachimbaji madini na makundi madogo kwa shughuli zao mbalimbali za kila siku. Haki hii itakuwa ni kwa Watanzania wote.

Hata hivyo, na kama ilivyo sasa, Serikali inaweza kulazimika kutumia ardhi au sehemu ya ardhi kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na ya kijamii yenye maslahi mapana ya nchi. Katika mazingira hayo, Katiba Inayopendekezwa inaeleza wazi kwamba Serikali itakuwa na wajibu wa kuweka utaratibu wa kisheria kwa ajili ya malipo ya fidia stahiki kwa mmiliki wa ardhi hiyo.

Page 11: KATIBA MPYA

11KATIBA INAYOPENDEKEZWA -Maudhui ya Msingi

Kuhusu maliasili za nchi, Katiba Inayopendekezwa imetamka kuwa maliasili zote za taifa ikiwa ni pamoja na madini, gesi na mafuta ni mali ya umma na zitatumika kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Kwa upande wa mazingira, Katiba Inayopendekezwa inaielekeza Serikali kuweka mipango na mikakati ya kuhakikisha matumizi endelevu, uhifadhi na usimamizi wa mazingira na maliasili kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Mazingira ni uti wa mgongo wa maendeleo stahimilivu ya nchi yeyote. Kwa kutambua hilo, Mazingira ni mojawapo ya maeneo mapya na muhimu yaliyopewa kipaumbele. Nchi yetu na nchi nyingine nyingi duniani zimeshuhudia majanga yanayotokana na mabadiliko ya tabia-nchi. Ibara hii itatoa fursa kwa wananchi na Serikali yao kuhakikisha panakuwa na mipango madhubuti ya kulinda mazingira.

Page 12: KATIBA MPYA

12 KATIBA INAYOPENDEKEZWA - Maudhui ya Msingi

2.4 Sura ya Nne

Kwa miongo kadhaa nchi yetu imekuwa na maadili ya miiko ya uongozi katika sura zake mbalimbali. Wengi watakumbuka kwamba tumewahi kuwa na waraka uliojulikana sana kama Mwongozo wa TANU; tumekuwa na miiko iliyotokana na Azimio la Arusha; tumekuwa

na taratibu za kiutumishi zinazoainisha miiko ya maadili ya uongozi. Yote haya yanadhihirisha kwamba nchi yetu na watu wake hawana ugeni katika eneo hili. Ni wazi, hata hivyo, kwamba taifa letu limekua, misingi ya haki na uhuru imepanuka, mahitaji ya leo, si mahitaji ya jana. Yote haya yamekuwa na taathira katika kusimamia na kutekeleza miiko na maadili ya viongozi. Katiba Inayopendekezwa imetambua haya. Hivyo katika Sura ya nne misingi thabiti ya miiko na maadili inawekwa.

Kuwekwa kwa misingi hii ndani ya Katiba ni jambo muhimu na la lazima. Lakini ni wazi kuwa kuwekwa kwa misingi hii ndani ya Katiba peke yake, hakutuhakikishii utekelezaji na umadhubuti tunaoukusudia. Hivyo Katiba Inayopendekezwa inaelekeza kutungwa kwa sheria mahsusi zitakazoweka kwa kina utaratibu wa kutekeleza misingi hiyo mikuu. Kwa mfano, msingi wa kikatiba umewekwa kuhusu haja ya viongozi wa umma kuwasilisha serikalini zawadi mbalimbali wanazozipata wakiwa katika utumishi wa umma. Huu ni msingi mzuri na muhimu. Lakini kwa taratibu za uandishi wa Katiba, haiwezekani kuweka maudhui ya kina ndani ya Katiba yanayohusu utekelezaji wa msingi huu. Hivyo pamoja na kuuweka mwiko huu wa maadili ndani ya Katiba itakuwa muhimu kwa sheria kutungwa ili kuelekeza utekelezaji wake kwa undani. Sheria hii itahitaji

kuainisha aina za zawadi ambazo mtumishi wa umma atapaswa kuzikabidhi serikalini; kueleza namna ya kusajili na kuweka kumbukumbu za maandishi

za zawadi hizo; kueleza zitahifadhiwa wapi, na mamlaka gani; utunzaji wake; matumizi yake baada ya kukabidhiwa kwenye mamlaka husika; zitauzwa au zitatumikaje; ndani ya muda gani; kwa manufaa ya nani, na kadhalika. Haya yote hayawezekani kukaa kwenye Katiba na ndiyo sababu Katiba Inayopendekezwa inataka maeneo yote haya yaainishwe vizuri zaidi ndani ya sheria, tofauti na kuwekwa kwenye Katiba pekee, kwani asili yake Katiba haiwezi kuweka maelekezo ya aina hii kwa kina, haiweki katazo, wala adhabu. Sheria ndiyo yenye uwezo wa kufanya yote haya.

Page 13: KATIBA MPYA

13KATIBA INAYOPENDEKEZWA -Maudhui ya Msingi

Kwa mantiki hii, sura ya nne ya Katiba Inayopendekezwa ina maudhui ya msingi yafuatayo:

a) Maadili na Miiko ya Uongozi na Utumishi wa Umma (Ibara ya 28 – 31) Hili ni eneo muhimu sana katika kukuza

na kuendeleza utawala bora. Katiba Inayopendekezwa inatambua kuwa madaraka anayopewa kiongozi wa umma ni dhamana katika kutekeleza wajibu wake. Hivyo, kiongozi wa umma atatumia madaraka yake kwa:-

i. Kuzingatia masharti ya Katiba; ii. Kuheshimu wananchi; iii. Kukuza hadhi ya taifa na kulinda

heshima ya ofisi anayoitumikia; na iv. Kukuza heshima ya ofisi kwa

wananchi

Kiongozi wa umma atapaswa kuzingatia yafuatayo:- i. Kufanya uteuzi bila ubaguzi

kwa kuzingatia uwezo, sifa na mwenendo unaofaa,

ii. Kutoa uamuzi bila kujali udugu, ukabila, udini, rushwa, na ubaguzi wa aina yoyote.

iii. Kutoa huduma pasipo upendeleo na kwa kufuata maslahi ya umma.

Page 14: KATIBA MPYA

14 KATIBA INAYOPENDEKEZWA - Maudhui ya Msingi

Kiongozi wa umma ataheshimu na kutii maadili ya uongozi wa umma na miiko ya uongozi. Katiba Inayopendekezwa inaelekeza kutungwa kwa sheria itakayoinyambua misingi hii muhimu na kutaja adhabu pale itakapokiukwa.

Kiongozi wa umma, akiwa katika kazi za ofisi au kazi binafsi au amejumuika na watu wengine atahakikisha kwamba mwenendo wake: i. Hauruhusu kutokea mgongano kati ya

maslahi binafsi na maslahi ya utumishi wa umma;

ii. Haushushi hadhi ya ofisi anayofanyia kazi; au hauruhusu matumizi ya ofisi ya umma kwa maslahi binafsi.

Page 15: KATIBA MPYA

15KATIBA INAYOPENDEKEZWA -Maudhui ya Msingi

Haki za Binadamu

Duniani kote Sura ya Haki za Binadamu ina umuhimu wa pekee. Kukaa kwake ndani ya Katiba ni kuhakikisha zinalindwa kama sehemu mojawapo ya wajibu wa dola kwa raia. Katiba Inayopendekezwa katika Sura hii imebainisha haki zote kama zilivyo

katika Tangazo la Dunia la Haki za Binadamu la Mwaka 1948. Tofauti na baadhi ya watu wanavyopotosha, haki hizi zinaweza kutiliwa nguvu mahakamani kwa mujibu wa Ibara ya 65(2) ya Katiba Inayopendekezwa. Sura ya pili ya Katiba Inayopendekezwa inataja malengo muhimu ya taifa. Malengo yamewekwa kwa nia ya kutoa dira kwa Serikali na vyombo vyake wanapopanga mikakati mbalimbali ya maendeleo. Utekelezaji wa malengo yale ni endelevu na hivyo Serikali haipaswi kufikishwa mahakamani endapo utekelezaji wake utachelewa. Hii ni kwa sababu malengo yale yanabainisha azma ya Serikali ya kuyazingatia katika utekelezaji wa mpango wa maendeleo. Hakuna Katiba yoyote duniani imeweka utaratibu wa kuifikisha Serikali mahakamani endapo malengo hayatatimia. Hivyo si sawa kusema kwamba katika eneo lile kuna haki ambazo haziwezi kudaiwa mahakamani.

2.5 Sura ya Tano

Katiba Inayopendekezwa imeingiza kizazi kipya cha haki za binadamu na kuimarisha haki za makundi maalum kama ifuatavyo:-

i. Haki za Wanawake Katiba Inayopendekezwa imewapa wanawake haki sawa na wanaume

ikiwemo haki ya kushiriki katika masuala ya kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kijamii. Katiba Inayopendekezwa imepiga marufuku vitendo vya ukatili, ubaguzi, dhuluma, udhalilishaji, unyanyasaji na mila potofu dhidi ya wanawake [Ibara za 12; na 57(b)]. Ibara hizi ni za manufaa sana kwa wanawake, hasa kwa kuzingatia kiwango kikubwa kilichopo cha matukio ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia katika baadhi ya jamii ndani ya nchi yetu.

Page 16: KATIBA MPYA

16 KATIBA INAYOPENDEKEZWA - Maudhui ya Msingi

Vile vile, Katiba Inayopendekezwa inawapa wanawake haki nyingine za msingi zifuatazo:-

• Kushiriki bila ubaguzi katika uchaguzi na ngazi zote za maamuzi [Ibara za 57 (c) na 129(4)].

• Fursa na haki ya ujira sawa na wanaume kwa kazi zenye sifa zinazofanana – [Ibara ya 57 (d)];

• Kupata huduma bora za afya ikiwemo afya ya uzazi salama [Ibara ya 57(f )];

• Haki ya kupata kumiliki mali [Ibara za 57(g), 47(1) na 23(2)]. Haki hii ni muhimu sana katika maendeleo ya wanawake hususan kwa sehemu ambazo wanawake wamekuwa wakinyimwa haki ya kumiliki mali.

• Ajira ya mwanamke kulindwa wakati wa ujauzito na anapojifungua [Ibara ya 57(e)];

• Haki ya kupata maji safi na salama [Ibara ya 51];• Haki ya kusaidiana katika matunzo na malezi

ya mtoto [Ibara ya 53(1)(g)]. Hii ni fursa ye pekee kwa wanawake ambao walikuwa wametelekezwa na wenza wao.

Sura hii inazungumzia haki za binadamu kwa ujumla wake. Zipo vile vile ibara nyingine ndani ya Katiba Inayopendekezwa zinazosisitiza haki za makundi mbalimbali wakiwemo wanawake, watoto, wachimbaji wadogo na haki za jamii wanaoishi kutegemea uoto wa asili na mazingira yanayowazunguka kwa ajili ya chakula, malazi na mahitaji mengine ya maisha. Kwa mfano katika Utangulizi wa Katiba Inayopendekezwa, miongoni mwa mambo ya kuzingatia katika misingi ya utawala bora ni usawa wa jinsia [Ibara ya 6(2)(g)]. Misingi hii ni ya muhimu sana katika kulinda, kukuza na kuendeleza haki za wanawake.

Page 17: KATIBA MPYA

 

17KATIBA INAYOPENDEKEZWA -Maudhui ya Msingi

Halikadhalika, Ibara hii inaielekeza Serikali kujiendesha kwa uwazi (Open Government) katika utekelezaji wa shughuli zake. Ibara hii inalenga kuwapa wananchi haki ya kujua nini kinaendelea ndani ya Serikali yao, uwajibikaji wake kwa wananchi na kuimarisha dhana nzima ya mamlaka ya wananchi katika kusimamia Serikali. Ibara hii ni mwendelezo wa misingi ya utawala bora ambayo inatajwa katika Ibara ya 6.Aidha, Ibara ya 214 ya Katiba Inayopendekezwa inatoa fursa kwa sekta ya habari kuanzisha tume kwa ajili ya usimamizi, uratibu na utoaji huduma kwa wananchi.

ii. Haki ya uhuru wa habari na vyombo vya habari (Ibara ya 40) Katiba Inayopendekezwa inatoa haki na

uhuru wa mtu na vyombo vya habari kutafuta, kupata, kutumia na kusambaza habari na taarifa sahihi. Ibara hii inaondoa malalamiko ya muda mrefu ya wanahabari na wamiliki na vyombo vya habari ya kutokuwa huru katika utekelezaji wa kazi na majukumu yao ya kila siku.

Page 18: KATIBA MPYA

18 KATIBA INAYOPENDEKEZWA - Maudhui ya Msingi

iii. Haki za wafanyakazi na waajiri (Ibara ya 45) Katiba Inayopendekezwa imebainisha

haki za wafanyakazi mahali pao pa kazi. Jambo hili litaondoa manung’uniko ya wafanyakazi kuonewa na waajiri, kupewa ujira usiostahili kulingana na kazi wanazozifanya na kuachishwa kazi bila kufuata utaratibu. Hivyo, haki hii sasa inalindwa na kupewa nguvu ya kikatiba. Kwa upande mwingine, haki za mwajiri pia zimeainishwa.

iv. Haki za wakulima, wafugaji, wavuvi na wachimba madini (Ibara ya 46) Kwa mara ya kwanza katika taifa letu, Katiba

Inayopendekezwa imeyatambua makundi madogo madogo ya wakulima na wafugaji, wavuvi na wachimba madini ambayo mara kwa mara yamekuwa yakiathiriwa na migogoro ya ardhi. Kimsingi, makundi yote hayo yana maslahi yanayofanana na kushabihiana kwa kiasi kikubwa. Kutokana na hali hii migogoro imekuwa ikizuka mara kwa mara kwa sababu tu ya kugombania maslahi hayo. Katiba Inayopendekezwa kwa kutambua na kuzingatia ukweli huo, inazitaja na kuzitambua haki za makundi hayo kwa nia ya kuhakikisha kwamba maslahi yao yanalindwa.

Page 19: KATIBA MPYA

 19KATIBA INAYOPENDEKEZWA -Maudhui ya Msingi

v. Haki ya mazingira safi, afya, na maji salama (Ibara ya 50 -51) Hili ni eneo jipya katika muktadha wa haki mbalimbali

zinazotambuliwa duniani hivi sasa. Katika siku za nyuma Mahakama iliwahi kutafsiri haki ya kuishi kuwa inajumuisha haki ya mazingira safi, afya, na maji salama, lakini haikuwahi kuwekwa ndani ya Katiba au sheria. Haki hii sasa inawekewa misingi thabiti ya utekelezaji, Katiba Inayopendekezwa inazibainisha haki hizi waziwazi na kuelekeza mamlaka ya nchi kuhakikisha kwamba wananchi wanajengewa utaratibu utakaowawezesha kuishi katika mazingira safi na salama; wanapata maji safi na salama kwa ajili ya kujenga jamii iliyo na afya bora.

Page 20: KATIBA MPYA

 

20 KATIBA INAYOPENDEKEZWA - Maudhui ya Msingi

vii. Haki na wajibu wa vijana (Ibara ya 54) Ibara hii ni mpya na ni mara ya kwanza kuwekwa

kikatiba. Katiba Inayopendekezwa inatambua haki za vijana na wajibu walionao kwa jamii. Katiba Inayopendekezwa inaielekeza Serikali kuhakikisha kwamba vijana wanawekewa mazingira mazuri ya kuwa raia wema na kupatiwa fursa za kushiriki kikamilifu katika masuala ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Sambamba na hilo, Katiba Inayopendekezwa inaielekeza Serikali kuanzisha Baraza la Vijana la Taifa. Baraza hili litakuwa muhimu sana kwa vijana kutoka katika makundi mbalimbali ya jamii kupata jukwaa la kupaza sauti zao, kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili na kushirikiana na Serikali katika kuzikabili.

vi. Haki za mtoto (Ibara ya 53) Haki za mtoto zimekuwa sehemu

ya sheria mbalimbali za nchi yetu. Pamoja na kuwepo kwa Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009, Katiba Inayopendekezwa imeimarisha misingi ya kuzitambua haki za mtoto kikatiba. Jambo hili limetokana na hali halisi ya mazingira wanayokabiliana nayo watoto katika nchi yetu. Katiba Inayopendekezwa inalenga kuhakikisha kwamba zinakuwepo sheria mahsusi za kuwalinda watoto dhidi ya ubaguzi na unyanyasaji wa aina zote.

Page 21: KATIBA MPYA

21KATIBA INAYOPENDEKEZWA -Maudhui ya Msingi

 

viii. Haki za watu wenye ulemavu (Ibara ya 55) Kwa kipindi kirefu watu wenye ulemavu wamekuwa

wakikabiliwa na changamoto mbalimbali. Pamoja na kuweka mazingira mazuri ya kuwawezesha kupata haki ya mawasiliano [Ibara ya 4(4)], Katiba Inayopendekezwa imeainisha haki mahsusi za watu wenye ulemavu. Baadhi ya haki hizo ni: haki ya kuheshimiwa, kutambuliwa na kulindwa dhidi ya vitendo vinavyoshusha utu wa mtu mwenye ulemavu. Vitendo hivyo ni pamoja na ubaguzi, uonevu, ukatili na mila potofu.

 

Vile vile, Katiba Inayopendekezwa inaelekeza kwamba watu wenye ulemavu wana haki ya kupata elimu kwa kutumia vifaa maalum na kushiriki katika nafasi za uwakilishi na shughuli za kijamii, kuwekewa miundombinu na mazingira yanayofaa yatakayomwezesha kwenda anapotaka, kutumia vyombo vya usafiri, kupata habari, kutumia lugha ya alama, alama mguso, maandishi ya nukta nundu, maandishi yaliyokuzwa, kupata ajira, kufanya kazi na kupata huduma bora za afya na uzazi salama. Kutambulika kwa kundi hili kikatiba ni fursa nzuri ya kuhakikisha kwamba taifa letu linaondokana na vitendo ambayo vina sura ya ukatili, ubaguzi na unyanyapaa, na badala yake kuwapa fursa ya kujiendeleza kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Page 22: KATIBA MPYA

ix. Haki za makundi madogo katika jamii (Ibara ya 56)

Katiba Inayopendekezwa inaweka masharti ya ulinzi wa haki za makundi madogo ikiwa ni pamoja na baadhi wanajamii wenzetu wanaoishi kwa kuwinda, kukusanya matunda na mimea mingine ya asili. Katiba Inayopendekezwa inaainisha haja ya kujenga mazingira yatakayoyawezesha makundi haya kushiriki katika uongozi wa mamlaka za nchi, kupata fursa maalum za elimu, kujiendeleza kiuchumi, kupata ajira na kutengewa maeneo ya ardhi ambayo kwa desturi makundi hayo huyatumia kwa makaazi na kupata riziki ya chakula.

 

22

x. Haki ya wazee (Ibara ya 58)

Wazee ni hazina ya taifa letu. Katiba Inayopendekezwa inatambua umuhimu huu wa wazee katika jamii. Ndani ya Katiba Inayopendekezwa wazee wanapewa fursa ya kushiriki katika shughuli za kimaendeleo na kijamii, kupata huduma mbalimbali na kulindwa dhidi ya vitendo vya ukatili. Kupitia Katiba Inayopendekezwa kutawekwa miundombinu na mazingira bora yatakayowawezesha kwenda wanakotaka na kutumia vyombo vya usafiri wa umma kwa gharama nafuu.

KATIBA INAYOPENDEKEZWA - Maudhui ya Msingi

Page 23: KATIBA MPYA

 

23KATIBA INAYOPENDEKEZWA -Maudhui ya Msingi

xi. Haki za Wasanii (Ibara ya 59)

Kama zilivyo haki nyingine nyingi, ni mara ya kwanza Katiba inazianzisha haki za wasanii. Katiba Inayopendekezwa inaonyesha hivyo katika Ibara ya 59. Haki hizi zinajumuisha haki-miliki ambazo zitawasaidia kulinda kazi zao za ubunifu, ufatifi na hatimaye kukuza Sanaa, taaluma, ubunifu na ugunduzi kwa manufaa yao binafsi na taifa kwa jumla. Hili ni kundi muhimu katika kukuza fursa za ajira kwa vijana na kuiletea sifa na heshima nchi yetu kwa kutumia Sanaa na ubunifu wao. Ni kundi ambalo lina uwezo mkubwa wa kuitangaza nchi yetu katika Nyanja za kiuchumi, kiutamaduni na kijamii. Hivyo, Katiba Inayopendekezwa inajenga mazingira mazuri ya kundi hili kuthaminiwa, kuendelezwa na kulindwa.

Page 24: KATIBA MPYA

 24 KATIBA INAYOPENDEKEZWA - Maudhui ya Msingi

Sura ya sita ina maudhui ya jumla yafuatayo:-

2.6 Sura ya Sita

a) Uraia katika Jamhuri ya Muungano (Ibara ya 70 – 71)

Suala la uraia limetamkwa kwenye Katiba Inayopendekezwa. Katiba Inayopendekezwa imebainisha aina za uraia katika Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kuwa ni uraia wa kuzaliwa na uraia wa kuandikishwa.

b) Hadhi maalum ya watu wenye asili au nasaba ya Tanzania (Ibara ya 72)

Katiba Inayopendekezwa inatoa nafasi kwa mtu yeyote mwenye asili au nasaba ya Tanzania na ambaye alikoma kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano kwa kupata uraia wa nchi nyingine, kuwa na hadhi maalum atakapokuwa katika Jamhuri ya Muungano. Hii itawafanya watu wenye sifa hizo kupata stahili na fursa ambazo ni tofauti na zile za wageni wawapo ndani ya nchi ya asili yao.

Page 25: KATIBA MPYA

 25KATIBA INAYOPENDEKEZWA -Maudhui ya Msingi

Sura ya saba ina maudhui ya jumla yafuatayo:

2.7 Sura ya Saba

a) Mahusiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (Ibara ya 77)

Katika kuhakikisha kwamba changamoto za Muungano zinapatiwa ufumbuzi wa kudumu, Katiba Inayopendekezwa inaweka utaratibu wa mahusiano baina ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa lengo la kukuza umoja, na kulinda maslahi ya Taifa na maendeleo ya wananchi.

b) Wajibu wa viongozi kulinda Muungano (Ibara ya 78)

Katiba Inayopendekezwa imetambua wajibu wa pekee wa viongozi wakuu wa nchi kuulinda na kuutetea Muungano. Viongozi hao ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Rais wa Zanzibar. Katika kutekeleza majukumu yao, viongozi hao wanapewa jukumu la kuhakikisha kuwa wanatetea, wanalinda, wanaimarisha na kudumisha umoja wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Page 26: KATIBA MPYA

26 KATIBA INAYOPENDEKEZWA - Maudhui ya Msingi

Sura ya nane ina maudhui ya jumla yafuatayo:-

2.8 Sura ya Nane

a) Hadhi ya Rais wa Zanzibar (Ibara ya 99)

Katiba Inayopendekezwa imerejesha hadhi ya Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Suala hili linajibu na kutatua changamoto ya muda mrefu kuhusu nafasi na hadhi ya Rais wa Zanzibar katika Muungano. Awali katika Hati ya makubaliano ya Muungano Rais wa Zanzibar alipewa hadhi na nafasi ya kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

b) Idadi ya Mawaziri (Ibara ya 115)

Kwa mara ya kwanza inapendekezwa kuwepo kwa ukomo wa idadi ya mawaziri kikatiba. Hivi sasa kuundwa kwa Wizara na uteuzi wa mawaziri hakuongozwi na sheria yoyote. Katiba Inayopendekezwa imeweka ukomo wa idadi ya mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano isiyozidi arobaini. Ni dhahiri kwamba jambo hili litaipunguzia Serikali gharama za uendeshaji na kurahisisha usimamizi wa shughuli za Serikali.

 

Page 27: KATIBA MPYA

27KATIBA INAYOPENDEKEZWA -Maudhui ya Msingi

c) Wananchi kuihoji Serikali (Ibara ya 116)

Muundo wa Bunge unaopendekezwa ni ule ambao mawaziri wanatokana na wabunge. Katiba Inayopendekezwa inaendeleza utaratibu huu. Huu ni utaratibu unaohakikisha kwamba Serikali inawajibika moja kwa moja kwa wananchi. Ni utaratibu unaowawezesha wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi kupata fursa ya kuisimamia Serikali kupitia maswali Bungeni na kuhoji utendaji wake. Utaratibu huu unaakisi vizuri falsafa iliyomo kwenye Ibara ya 7 ambayo inaeleza kwamba msingi wa mamlaka yote ya nchi ni wananchi wenyewe.

 

Page 28: KATIBA MPYA

28 KATIBA INAYOPENDEKEZWA - Maudhui ya Msingi

Sura ya tisa ina maudhui ya jumla yafuatayo:-

2.9 Sura ya Tisa

a) Uhusiano na Uratibu wa Mambo ya Muungano (Ibara za 127 – 128)

Katiba Inayopendekezwa inaimarisha Muungano wetu kwa kuanzisha Tume ya Usimamizi na Uratibu wa Mambo ya Muungano. Chombo hiki, pamoja na mambo mengine, kitakuwa na jukumu la kukuza na kuratibu ushirikiano baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Mojawapo ya malengo ya uratibu huu ni kuimarisha ushirikiano na uhusiano baina ya Serikali hizi mbili na kukuza kiwango cha utoaji huduma kwa wananchi wote.

Kwa utaratibu wa sasa ipo Kamati inayoshughulikia masuala ya Muungano ambayo inaongozwa na Makamu wa Rais. Kwa Katiba Inayopendekezwa chombo hiki sasa kitakuwa na nguvu ya kisheria na hivyo kuweka mfumo madhubuti zaidi wa kushughulikia changamoto za Muungano na pia kuratibu masuala mengine yanayohusiana na ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar kwa ujumla wake.

Page 29: KATIBA MPYA

29KATIBA INAYOPENDEKEZWA -Maudhui ya Msingi

a) Muundo wa Bunge – Ibara ya 129.

Katiba Inayopendekezwa imeweka ukomo wa idadi ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano. Idadi ya wabunge imetajwa kutopungua mia tatu arobaini (340) na kutozidi mia tatu tisini (390). Hatua hii itasaidia sana kudhibiti ongezeko la majimbo ya uchaguzi na hivyo kupunguza gharama za uendeshaji. Idadi inayotajwa itajumuisha wabunge wote wanaotoka Tanzania Bara na wale wanaotoka Zanzibar. Katiba Inayopendekezwa inamtaka Rais kuteua watu watano kutoka katika kundi la watu wenye ulemavu kuwa wabunge. Hii ni fursa nzuri ya kuhakikisha kwamba kundi hili muhimu linapata uwakilishi wa uhakika Bungeni.

Sura ya kumi ina maudhui ya jumla yafuatayo:

2.10 Sura ya Kumi

Page 30: KATIBA MPYA

30 KATIBA INAYOPENDEKEZWA - Maudhui ya Msingi

Sura ya Kumi na Mbili ina maudhui ya jumla yafuatayo:

2.11 Sura ya Kumi na Mbili

a) Mahakama ya Juu (Ibara ya 171 – 174) Mahakama ya Juu ya Jamhuri ya Muungano

ndiyo itakuwa chombo cha mwisho cha utoaji haki nchini. Hiki ni chombo kipya ndani ya Katiba Inayopendekezwa na imeongezwa ili kupanua wigo wa utoaji haki na kukifanya kuwa chombo chenye mamlaka ya mwisho katika kutatua mashauri ya aina mbalimbali nchini. Chombo hiki pia kitakuwa na mamlaka ya kushughulikia mashauri yanayohusu matokeo ya uchaguzi wa Rais na kusikiliza mashauri baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuhusu tafsiri ya Katiba.

Page 31: KATIBA MPYA

31KATIBA INAYOPENDEKEZWA -Maudhui ya Msingi

a) Tume ya Utumishi wa Umma (Ibara ya 210 – 212) Katiba Inayopendekezwa inaanzisha Tume ya

Utumishi wa Umma ambayo itakuwa chombo cha juu chenye mamlaka ya nidhamu na uratibu wa mambo yote ya utumishi wa umma katika Jamhuri ya Muungano. Pamoja na kazi zake nyingine, Chombo hiki kitahakikisha kwamba kunakuwepo uwakilishi na uwiano mzuri wa watumishi wa umma kutoka Tanzania Zanzibar na Bara.

Sura ya Kumi na tatu ina maudhui ya jumla yafuatayo:

2.12 Sura ya Kumi na Tatu

Page 32: KATIBA MPYA

32 KATIBA INAYOPENDEKEZWA - Maudhui ya Msingi

• Mgombea huru (Ibara ya 216) Katiba Inayopendekezwa inaanzisha

utaratibu wa kuwa na mgombea huru katika nafasi mbalimbali za uchaguzi kwa ngazi zote. Hili ni jambo jipya linaloonesha kukua na kukomaa kwa demokrasia katika nchi yetu.

• Tume Huru ya Uchaguzi (Ibara ya 217 – 223) Katiba Inayopendekezwa imeanzisha

Tume Huru ya Uchaguzi. Kuanzishwa kwa chombo hiki kunatoa majawabu ya changamoto na maswali ya muda mrefu kuhusu uhuru wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kusimamia na kuendesha chaguzi hapa nchini.

Sura ya Kumi na Nne ina maeneo mapya ambayo hayamo katika Katiba ya Mwaka 1977 maeneo haya ni:

2.13 Sura ya Kumi na Nne

Page 33: KATIBA MPYA

33KATIBA INAYOPENDEKEZWA -Maudhui ya Msingi

a) Chombo cha Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Ibara ya 249) Kwa mara ya kwanza nchini, Katiba Inayopendekezwa inaelekeza

kuanzishwa kwa chombo cha kikatiba cha kuzuia na kupambana na rushwa. Lengo ni kuhakikisha nchi yetu inakuwa na chombo huru na chenye nguvu ya kupambana na rushwa ili kujenga taifa lenye uadilifu na kuimarisha utawala bora.

Sura ya Kumi na Tano ina maudhui ya jumla yafuatayo:

2.14 Sura ya Kumi na Tano

Page 34: KATIBA MPYA

34 KATIBA INAYOPENDEKEZWA - Maudhui ya Msingi

SEHEMU YA TATU

3.0 UTATUZI WA CHANGAMOTO ZA MUUNGANO

Sehemu hii ya waraka ni mahsusi kwa ajili ya kubainisha namna ambavyo changamoto za Muungano zimepatiwa ufumbuzi ndani ya Katiba Inayopendekezwa.

Tangu kuasisiwa kwa Muungano wetu mwaka 1964, kumekuwepo na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa Mambo ya Muungano. Changamoto hizo zimekuwa zikishughulikiwa na tume na kamati

mbalimbali zilizokuwa zinaundwa katika vipindi tofauti vya uongozi wa nchi yetu. Miongoni mwa tume na kamati hizo ni Tume ya Jaji Nyalali (1991), Kamati ya Amina Salum Ali (1992), Kamati ya Shellukindo (1994), Kamati ya Jaji Mark Bomani (1995), Kamati ya Shamhuna (1977), Kamati ya Jaji Kisanga (1998), Kamati ya Ramia (2000) na Kamati ya Pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (2006).

Aidha, hadi mchakato wa kuandika Katiba mpya unaanza, changamoto kubwa zilizokuwa zinaendelea kutafutiwa ufumbuzi ni kama ifuatavyo:

• Utafutaji na uchimbaji mafuta na gesi asilia;• Ushirikiano wa Zanzibar na taasisi za nje;• Ajira kwa watumishi wa Zanzibar katika taasisi za

Muungano;• Rais wa Zanzibar kuondolewa kuwa Makamu wa

Rais wa Jamhuri ya Muungano;• Orodha ya mambo ya Muungano kuongezeka

kutoka mambo 11 mpaka 22;• Uwezo wa SMZ kukopa ndani na nje ya nchi; na• Maamuzi kuhusu utatuzi wa changamoto za

Muungano kukosa nguvu za kisheria.

Page 35: KATIBA MPYA

35KATIBA INAYOPENDEKEZWA -Maudhui ya Msingi

Katiba Inayopendekezwa imejielekeza kutatua changamoto hizo kama ifuatavyo:

a) Kuanzishwa kwa Tume ya Mambo ya Muungano Ibara ya 127 ya Katiba Inayopendekezwa inaanzisha Tume ya Usimamizi na Uratibu wa mambo ya

Muungano. Tume hii, pamoja na mambo mengine, itakuwa na jukumu maalum la kuwezesha uratibu na ushirikiano wa sera, sheria, mipango na mikakati baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Uratibu huu utasaidia sana kubainisha changamoto zozote zitakazojitokeza katika kutekeleza shughuli za Muungano. Itakumbukwa kwamba hivi sasa ipo Kamati inayoongozwa na Makamu wa Rais ya kushughulikia changamoto na masuala mengine ya Muungano. Kamati hii haikuanzishwa kikatiba, hivyo ipo mifano ambayo utekelezaji wa maamuzi ya Kamati ulitegemea sana uhusiano mzuri kati ya watendaji na taasisi husika za pande zote mbili. Uhusiano mzuri na utashi wa kisiasa ni mambo muhimu. Hata hivyo, Katiba Inayopendekezwa imeona hii haitoshi. Hivyo, mojawapo ya malengo ya kuanzishwa kwa Tume hii ni kujenga misingi imara ya kikatiba ya utekelezaji wa shughuli za Muungano na kuyapa nguvu ya kisheria maamuzi mbalimbali yatakayotolewa na Tume hii.

Page 36: KATIBA MPYA

36 KATIBA INAYOPENDEKEZWA - Maudhui ya Msingi

b) Nafasi na hadhi ya Rais wa Zanzibar

Kwa mujibu wa Hati ya Makubaliano ya

Muungano, Rais wa Zanzibar alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Hata hivyo, kufuatia mabadiliko mbalimbali yaliyotokea katika nchi yetu, hususani kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992, nafasi ya Rais wa Zanzibar kama Makamu wa Rais iliondolewa. Baada ya mabadiliko mbalimbali ya kisiasa na kikatiba (hususan kwa upande wa Zanzibar, na uzoefu uliopatikana wa namna bora zaidi ya kuimarisha Muungano wetu), Katiba Inayopendekezwa inarejesha nafasi ya Rais wa Zanzibar kama Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano kupitia Ibara ya 99(b).

Page 37: KATIBA MPYA

37

c) Ushirikiano na uhusiano wa Zanzibar na Taasisi za Kimataifa

Jambo hili ni miongoni mwa mambo ambayo

yalionekana kuwa moja ya changamoto zilizoukabili ustawi wa Muungano na maendeleo ya pande zote mbili za Muungano wetu. Katiba Inayopendekezwa inatambua umuhimu huu na haja ya kuimarisha mamlaka ya Zanzibar kwa mambo yasiyo ya Muungano yanayohusu Zanzibar. Katiba Inayopendekezwa inajibu hoja hii kupitia Ibara ya 76. Kwa mujibu wa ibara hii, Zanzibar itakuwa na uwezo na uhuru wa kuanzisha uhusiano au ushirikiano na jumuiya au taasisi yoyote ya kikanda au kimataifa kwa mambo yanayoihusu.

KATIBA INAYOPENDEKEZWA -Maudhui ya Msingi

Page 38: KATIBA MPYA

38 KATIBA INAYOPENDEKEZWA - Maudhui ya Msingi

d) Uwezo wa Zanzibar kukopa ndani na nje ya nchi Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 1977, inaweka mamlaka ya kukopa

nje ya nchi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Katika muktadha wa kuimarisha uwezo na uhuru wa Zanzibar kwa shughuli za maendeleo yake, Katiba Inayopendekezwa katika Ibara ya 261 inatoa mamlaka kwa SMZ kukopa fedha ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano bila ya kulazimika kupitia Serikali ya Muungano. Kwa minajili hii, endapo mkopo husika utahitaji dhamana, basi Serikalii ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania itatoa dhamana kwa mkopo unaoombwa. Ni wazi utaratibu huu utarahisisha sana upatikanaji wa mikopo kwa maendeleo na ustawi wa Zanzibar.

e) Orodha ya Mambo ya Muungano Muungao wetu ulianza kwa kuainisha mambo 11 ambayo ndiyo yaliyokuwa

msingi wa ushirikiano kati ya iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Hadi leo ushirikiano umekua na kufikia mambo 22. Katika kipindi cha miaka takriban hamsini ya Muungano wetu mahitaji na mazingira yamebadilika. Pande zote mbili za Muungano zimejiimarisha kwa namna mbalimbali katika maendeleo yao. Kwa kuzingatia ukweli huu, Katiba Inayopendekezwa inaainisha masuala 16 badala ya 22 ya sasa [Ibara ya 74(3)]. Miongoni mwa mambo yaliyopunguzwa ni suala la utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia ambalo kipekee lilionekana kuwa changamoto kubwa katika ustawi na maendeleo ya taifa letu.

Page 39: KATIBA MPYA

39KATIBA INAYOPENDEKEZWA -Maudhui ya Msingi

f) Ajira katika Taasisi za Muungano Mojawapo ya changamoto zilizojitokeza katika uhai wa Muungano

wetu ni suala la ajira ya wananchi wa pande zote mbili katika taasisi za Muungano. Pamoja na Tume ya Utumishi wa Umma kuwa na jukumu la ujumla katika eneo hili, Katiba Inayopendekezwa katika Ibara ya 128(1)(f ) na 128(3) inataja wazi kwamba Tume ya Usimamizi na Uratibu wa Mambo ya Muungano itakuwa vile vile na jukumu la kusimamia uwakilishi wa pande zote mbili za Muungano ndani ya ajira ya utumishi wa Jamhuri ya Muungano. Aidha, Tume itaweka utaratibu utakaowezesha uteuzi wa viongozi na watumishi katika taasisi au Wizara za Muungano kufanyika kwa kuzingatia uwakilishi wa pande zote mbili za Muungano. Hii ni hatua muhimu ya kuleta uwiano murua, kupata mchango chanya wa wananchi wote katika ajira na kuuimarisha Muungano wetu.

Page 40: KATIBA MPYA

Tanzania Women Cross-Party Platform (T-WCP ULINGO)P.O Box 65454, Dar es SalaamEmail: [email protected]

Tel: +255 784 600416