KANUNI ZA MAADILI YA UTENDAJI KATIKA UTUMISHI...

32
KANUNI ZA MAADILI YA UTENDAJI KATIKA UTUMISHI WA UMMA Kanuni hizi zimetungwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa katika kifungu cha 34 cha Sheria ya Utumishi wa Umma ya Mwaka 2002 pamoja na Kanuni ya 65 (1) ya Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2003. 1

Transcript of KANUNI ZA MAADILI YA UTENDAJI KATIKA UTUMISHI...

KANUNI ZA MAADILI YA UTENDAJIKATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kanuni hizi zimetungwa na Waziri waNchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti yaUtumishi wa Umma kwa mujibu wa

mamlaka aliyopewa katika kifungu cha 34cha Sheria ya Utumishi wa Umma ya

Mwaka 2002 pamoja na Kanuni ya 65 (1)ya Kanuni za Utumishi wa Umma za

Mwaka 2003.

1

TABIA NA MIENENDO YAKIMAADILI

1. Ili Utumishi wa Umma uwe wenye ufanisi na wa kuheshimika, watumishi wanapaswa kuzifuata Kanuni za Maadili ya Utumishi pamoja na kuwa na tabia na mwenendo unaozingatia mambo yafuatayo:

1. Kutoa Huduma Bora2. Utii kwa Serikali3. Bidii ya Kazi4. Kutoa Huduma Bila Upendeleo5. Kufanya Kazi kwa Uadilifu6. Kuwajibika kwa Umma7. Kuheshimu Sheria8. Matumizi sahihi ya Taarifa

2

3

KutoaHuduma Bora

KUTOA HUDUMA BORA

2. Watumishi wa Umma wanapaswakutambua kwamba wana wajibu wakutoa huduma bora kwa umma. Katikakutimiza wajibu wao, wanapaswa piakuzingatia yafuatayo:

a) Kuifahamu vema na kuiheshimu Kanuni hii ya Maadili.

b) Kuweka malengo halisi ya kazi ilikuwawezesha kufikia kiwango chajuu kabisa katika utendaji wao wa kazi.

c) Kuwa wabunifu, wavumbuzi na sikuzote kujibidisha kuongeza viwangovya utendaji kwa kujiongezea maarifana ujuzi.

d) Kutumia misingi ya haki, badala yaupendeleo, katika utoaji wa huduma.

e) Kuwa msafi na kuvaa nguo za heshimazinazokubalika mahalipa kazi.

4

f) Kujitahidi kudumisha uhusiano mzurimahali pa kazi na utendaji kazi wapamoja kwa:

(i) kutoa maelekezo ambayo ni wazi; sahihi na ya kueleweka;

(ii) kuepuka kufanya vitendo viovu aukutamka maneno yanayolenga kuwaaibisha watumishi wa ngazi moja, za chini yao au wa vyeo vya juu;

(iii) kuepuka matumizi ya lugha mbaya, matusi, utani na hasira katika utendaji wa kazi;

(iv) kutafakari ipasavyo maoni rasmi yanayotolewa na watumishi wengine na hata walio chini yao;

(v) kufanya mikutano ya watumishi mara kwa mara;

(vi) kuhakikisha kwamba watumishi walio chini yao wanaweka male- ngo halisi ya kazi, kufuatilia utendajiwao mara kwa mara na kuwa-himiza kuongeza uwezo na ujuzi wao katika utendaji;

5

(vii) kutoa taarifa za tathmini ya utendaji kwa watumishi bila upendeleo;

(viii) kutoa sifa au tuzo kwa watu-mishi wenye utendaji bora na kuwaadhibu wenye utendaji duni;

(ix) kuwaheshimu watumishi wenzaopamoja na kuheshimu haki zao,hasa haki za faragha wanapo-shughulikia taarifa zao za siri na binafsi.

6

7

Utii kwaSerikali

UTII KWA SERIKALI

3. (1) Watumishi wa Umma wanapaswa kuitii Serikali iliyopo madarakani.

(2) Kwa hiyo, Watumishi wa Umma wanatakiwa kutekeleza sera na maelekezo halali yanayotolewa naMawaziri na viongozi wao wengine wa Serikali.

8

9

Bidii yaKazi

BIDII YA KAZI

4. Watumishi wa Umma wanapaswa kufanya kazi kwa bidii na nidhamu ya hali ya juu. Vilevile, wanapaswa kuonyeshakwamba wanaheshimu na kujali wajibu wao kwa kufanya yafuatayo:

a) Kutumia maarifa, ujuzi na utaalamu wao ili kupata ufanisi wa upeo wa juu katika utendaji wao wa kazi;

b) Kutimiza wajibu wao na kwa kufanyakazi kwa ufanisi wa kiwango cha juu nakuzikamilisha katika muda unaotakiwa;

c) Kuepuka mwenendo mbaya ambaoutaathiri ufanisi katika utendaji kazi;

d) Kuwa tayari kufanya kazi katika kituo chochote cha kazi atakachopangiwa; na

e) Kufika sehemu ya kazi kwa muda uliopangwa na kuzingatia muda rasmi wa kufanya kazi.

10

11

Kutoa HudumaBila Upendeleo

KUTOA HUDUMA BILAUPENDELEO

5. (1) Watumishi wa Umma wanayo haki ya kidemokrasia ya kuwa wanachama wa chama chochote cha siasa. Vilevile, wanayo haki ya kuvipigia kura vyama vyao pamoja na viongozi wao wakati wa uchaguzi mkuu.

(2) Watumishi wa Umma wanaweza kushiriki katika masuala ya siasa katika vyama vyao ilimradi kwa kushiriki kwao hawataonyesha upendeleo katika utendaji wao wa kazi.

12

(3) Hata hivyo, Watumishi wa Umma wanapaswa kuzingatia masharti yaliyowekwa katika ushiriki wao katika masuala ya siasa:-

a) Hawaruhusiwi kufanya wala kuji-husisha na masuala ya siasa wakatiwa saa za kazi au mahali pa kazi;

b) Kutoa huduma kwa upendeleo kutokana na msimamo wao wa kisiasa; na

c) Kutumia taarifa au nyaraka za kiofisi wanazopata kutokana na utumishi wao kwa umma kwa manufaa ya vyama vyao.

(4) Watumishi wa umma wanayo haki yakuwasiliana na viongozi au wawakilishiwao wa kisiasa ilimradi wanazingatiayafuatayo:

a) Waepuke kutumia ushawishi wa kisiasa kuingilia mgogoro wa kikazi baina yao na serikali;

13

b) Waepuke kutumia ushawishi wa kisiasa kwa manufaa yao binafsi ambayo sio sehemu ya sera za Serikali.

(5) Watumishi wa Umma wanayo haki ya kuabudu na kushirikidini yoyote wanayoipenda ilimradikwa kufanya hivyo hawavunji sheria zilizopo. Hata hivyo, kwa kuwa Serikali haina dini, hairuhusiwi kuhubiri imani za diniwakati wa kazi na mahali pa kazi.

14

15

Kufanya Kazi kwa Uadilifu

KUFANYA KAZI KWA UADILIFU

6. (1) Watumishi wa Umma wanapaswa kutumia madaraka waliyokabidhiwa kwa kuzingatia mipaka ya madarakayao na hawapaswi kutumia madara-ka hayo kwa manufaa yao binafsi,kuwapendelea marafiki na jamaazao au kuwakandamiza wengine.

(2) Watumishi wa Umma wanapaswakusimamia vizuri fedha na mali yaumma waliyokabidhiwa na niwajibu wao kuzuia uharibifu,upotevu au ubadhirifu usitokeekutokana na uzembe au manufaa yamtu binafsi au kundi fulani.

(3) Watumishi wa Umma wanapaswakutumia rasilimali za umma kwamanufaa ya umma. Rasilimali zaumma ni pamoja na mitambo, vifaavya ofisi, simu, kompyuta, mashine zakunakili kwa picha, huduma za umma (kama vile umeme, maji, usafiri n.k.),majengo na vifaa vinginevyo

16

vilivyonunuliwa kwa fedha zaSerikali au kutolewa msaada kwaSerikali. (Gharama anazorejeshewamtumishi na Serikali au gharama zahuduma za nyumbani kwa baadhiya watumishi kama vile: simu,maji, umeme huhesabiwa kama ni sehemu ya mali ya umma).

(4) Watumishi wa Umma wanapaswakuwa waaminifu na kutumia mudawa kazi kutekeleza wajibu wao. Hawaruhusiwi kutumia muda wakazi kwa shughuli zao binafsi aukwa mapumziko isipokuwa kama wamepewa idhini ya kufanya hivyo.

17

(5) Watumishi wa Umma hawaruhusi-wi kuwaomba au kuwaagiza watu-mishi walio chini yao kuwafanyiakazi zao binafsi ambazo hazinauhusiano na kazi zao za utumishiwa umma.

(6) Watumishi wa Umma wanatakiwa,kwa utaratibu uliowekwa, kuwatayari kutangaza kwa waajiri waoau mamlaka yoyote halali mali walizo-nazo, za waume au wake zao namali za ndugu wanaowategemeaendapo watatakiwa kufanya hivyo.

(7) Watumishi wa Umma wanapaswakuepuka tabia ambayo inavunjaheshima ya utumishi wao kwaumma hata wanapokuwa nje yamahali pa kazi. Tabia inayoweza kuvunja heshima ya utumishi waumma ni pamoja na matumizi yamadawa ya kulevya, ulevi, kukopakwa kiwango ambacho hawawezikurejesha, mwenendo mbaya nakujihusisha na vitendo vyovyoteviovu mbele ya jamii.

18

(8) Watumishi wa Umma wanapaswakuepuka kutoa zawadi zisizo halali,kuomba, kulazimisha au kupokearushwa kutoka kwa mtu yeyoteambaye waliwahi kumhudumia, wanayemhudumia au wanayetarajiakumhudumia ama kwa kufanyahivyo wao wenyewe au kwa kum-tumia mtu mwingine.

19

(9) Kwa mujibu wa Kanuni hii, rushwani mapato yasiyo halali ambayoyamepatikana kutokana na matu-mizi mabaya ya ofisi au madarakaaliyokabidhiwa mtumishi.

(10) Watumishi wa Umma au familiazao wanapaswa kuepuka kuomba,kupokea au kutoa zawadi ambazo zitaonekana kwamba zinalengakuathiri uadilifu wao.

(11) Watumishi wa Umma wanapaswa kuepuka kutoa zawadi kwa watu-mishi wenzao.

(12) Kwa mujibu wa Kanuni hii, vituvifuatavyo havihesabiwi kamazawadi yenye mwelekeo wa rushwa:-

a) vitu vidogovidogo vyenye thamani ambavyo vimetengenezwa mahususi kwa kutolewa kama zawadi. Vitu hivyo ni pamoja na kadi za salamu, vikombe vya washindi wa mashindano mbalimbali,

20

kalenda, vitabu vya kumbukumbu za kila siku (shajara), kalamu n.k.;

b) kitu chochote ambacho mtumishi wa umma analipia au kufanya marejesho kulingana na thamani yake;

c) kitu chochote ambacho kimelipiwa na Serikali.

(13) Zawadi yoyote ambayo haipokwenye maelezo yaliyotanguliahapo juu, inapaswa kukabidhiwakwa mwajiri na mtumishi aliye-pokea kwa maandishi. Mwajiri ana-paswa kukiri kupokea zawadi kuto-ka kwa mtumishi na kuingiza kati-ka rejesta ya zawadi zilizokabidhi-wa kwake. Serikali itatoa zawadihizo kama hisani kwa jumuiya aushirika lolote.

21

(14) Watumishi wa Umma wanaoachakazi au kustaafu katika utumishi waumma, wanapaswa kuepuka kutu-mia madaraka waliyokuwa nayowalipokuwa katika utumishi waumma kwa kuomba au kupokeahuduma ya upendeleo katika utu-mishi wa umma kwa faida yaobinafsi au watu wengine.

(15) Mtumishi aliyeacha kazi au kustaa-fu aepuke kumwakilisha mtu aushirika lake Serikalini ili apewehuduma kwa masuala ambayoyalikuwa chini ya madaraka yakealipokuwa katika utumishi.

22

23

Uwajibikaji kwa Umma

UWAJIBIKAJI KWA UMMA

7. (1) Watumishi wa Umma wanapaswakuwahudumia wateja wao na watu-mishi wenzao kwa heshima.Vilevile, wanapaswa kuwahudumiakwa makini zaidi wananchi wenyemahitaji ya pekee kama vile wazee,wanawake, watoto, maskini, wagonjwa,wenye ulemavu na kundi lolote lawatu ambao wapo katika halingumu.

(2) Watumishi wa Umma ambaowanaombwa na wananchi kutoaufafanuzi au maelekezo juu yamasuala yatokanayo na sheria,kanuni na taratibu za serikali wana-paswa kushughulikia mahitaji yawananchi hao haraka kwa uwazi na bila upendeleo.

(3) Watumishi wa Umma wanapaswakutekeleza wajibu wao wakijihesabukwamba wao ni watumishi wa umma.

24

25

KuheshimuSheria

KUHESHIMU SHERIA

8. (1) Watumishi wa Umma wanapaswakuzifahamu, kuzizingatia na kuzifuataipasavyo sheria, kanuni na taratibu zakazi.

(2) Watumishi wa Umma wanapaswakutumia sheria, kanuni na tarati-bu zilizopo katika kutekelezawajibu wao na wakati huo huokutambua kasoro ambazo zinahi-taji marekebisho.

(3) Watumishi wa Umma wanapaswakuepuka kumnyanyasa mwananchiau mtumishi mwenzao kwa misingi ya jinsia, kabila, dini, itikadiza kisiasa, utaifa, utamaduni,kuoa au kuolewa au ulemavu.

(4) Watumishi wa Umma waepuke kuwana mahusiano yoyote ya kimapenzimahali pa kazi na wakati wa kazi.Vilevile, wanapaswa kuepuka tabiayoyote ya unyanyasaji wa kijinsia.

26

Matendo ya unyanyasaji wa kijinsiani pamoja na:

a) kulazimisha mahusiano yakimapenzi au upendeleo wa kimapenzi na mtu yeyote;

b) vitendo vya kubaka, kunajisi aushambulio lolote la aibu;

c) vitendo vya makusudi ambavyohavikubaliki kama vile kugusana,kufinyana, kupapasana, kusuguanaau kushikana kwa nguvu sehemuyoyote ya mwili, nywele au hata nguo;

d) kutoa masengenyo, ishara, sautifulani fulani, utani, matamshi yoyoteyanayolenga jinsi au kiungo cho-chote cha mwili wa mtu.

27

e) kusaidia au kupokea upendeleo, ahadiau zawadi kutokana na kukubalikuwa na uhusiano wa kimapenzi;

f) kuangalia, kuonyesha au kugawa vitu kama vile picha, filamu,machapisho katika vijarida ambayohuonyesha matukio au vitendo bayanavya mahusiano ya kimapenzi auambayo huvunja maadili mema sehemu ya kazi au wakati wa kazi.

(5) Watumishi wa Umma ambaowanaombwa na viongozi wao wakazi kuvunja Sheria au Kanuni zaMaadili ya Utendaji katika Utumishiwa Umma au Kanuni za Maadili yaKazi za Kitaalamu wanapaswa kutoataarifa kwa kutumia taratibu za Serikalizilizopo za kushughulikia malalamiko.Iwapo mtumishi ataona vigumu kutu-mia taratibu zilizopo katika sehemuyake ya kazi, malalamiko yanawezayakaelekezwa moja kwa moja kwaKatibu Mkuu, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Ummaambaye atashughulikia malalamikohayo ipasavyo.

28

29

Matumizi Sahihi ya Taarifa

MATUMIZI SAHIHI YA TAARIFA

9. (1) Watumishi wa Umma hawaruhusi-wi kutoa kwa watu wasiohusikataarifa za Serikali, ama za siri au zakawaida, ambazo wamezipokeakutoka kwa watu wengine kwakuaminiwa tu lakini bila idhini.Kwa kuzingatia utunzaji wa siri zaSerikali, watumishi hawaruhusiwi piakutoa taarifa za Serikali kwa watuwasiohusika hata baada ya kuachakazi katika utumishi wa umma.

(2) Watumishi wa Umma hawaruhusi-wi kupotosha au kuzuia utekelezajiwa sera na mipango ya Serikalikwa kutoa taarifa kwa watu bilaidhini kabla sera na mipango hiyokutangazwa rasmi kwa umma.

(3) Watumishi wa Umma hawaruhusi-wi kutumia nyaraka au taarifa zaSerikali wanazozipata katikakutekeleza wajibu wao kwa manu-faa yao binafsi.

30

(4) Taarifa za Serikali zitatolewa kwavyombo vya habari na maafisawenye madaraka ya kufanya hivyokwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.

(5) Watumishi wa Umma watatoa taari-fa za Serikali wanazotaka zipelekwe kwenye vyombo vyahabari kupitia kwa maofisa wao wahabari, mawasiliano na elimu aukupitia kwa wakuu wao wa kazi.

Dar es Salaam,Tarehe 11 Januari, 2005

MARY M. NAGU (Mb)Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

AnwaniS.L.P. 2483, Dar es Salaam

Barua pepe: [email protected]: www.estabs.go.tz

31