Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia...

32
Kanuni za Maadili

Transcript of Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia...

Page 1: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

Kanuni za Maadili

Page 2: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

Uadilifu ndio kiungo chetu kikuu.

GuidePost

Page 3: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

Ni muhimu kujali tunavyofanya kazi. Tumejitolea kufanya kazi kwa kufuata na kuzingatia sheria zote husika kwa ukamilifu (hilo halina ubishi!), lakini pia ni muhimu, kufanya hivyo kwa kuzingatia maadili na kwa njia salama. Tunaunda thamani na kubuni imani miongoni mwa wadau wetu kwa kufanya yaliyo sahihi kila siku.

Matarajio haya yamenakiliwa kwenye Kanuni zetu za Maadili. Tafadhali chukua muda uzielewe Kanuni zetu. Endapo utajikuta katika hali mtanziko wa kimaadili, kama ilivyo kawaida kwetu sote wakati mwingine, ninakushauri uzisome Kanuni na uwasiliane na wasaidizi wowote waliotajwa. Usiogope kuuliza maswali au kuelezea dukuduku uliyo nayo. Ikiwa unawasimamia wafanyakazi wengine, kuza desturi ya wafanyakazi kuzungumza bila woga.

Ahadi ambayo tumewapa wadau wetu ni muhimu sana. Tunatarajia kila mmoja wetu atawajibikia kudumisha uadilifu wa Kampuni na kulinda urithi wetu.

Asante kwa kuendelea kujitolea kufanikisha Post.

ROBERT V. VITALERais na Ofisa Mtendaji Mkuu

POST HOLDINGS, INC. KANUNI ZA MAADILI

WENZANGU WAPENDWA:

1

Page 4: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

Wafanyakazi

YALIYOMO 6-9

01Barua kutoka kwa Rais na Ofisa Mkuu Mtendaji

04Utangulizi

05Kutafuta Mwongozo na Kuzungumza

28Mfumo wa Wafanyakazi Kuongea na Misamaha

08Utangamano na Ujumuishaji

Heshima Kazini

Usalama na Afya Kazini

09Faragha na Taarifa za Binafsi

Mitandao ya Kijamii

GUIDEPOST

Page 5: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

10-13 14-22 23-27

12Biashara ya Ndani

Kuhifadhi Nakala na Mahesabu Sahihi

13Kulinda Mali ya Kampuni na Taarifa za Siri

Kulinda Haki ya Ubunifu

18Mgongano wa Maslahi

21Ushindani wa Haki (Kutoaminika)

Kupambana na Rushwa/Ufisadi

23Kufanya Biashara Kimataifa

Kulinda Haki za Binadamu

26Ubora wa Bidhaa

Mauzo kwa Kuwajibika

Shughuli za Siasa

Kujali Mazingira

27Kushirikisha Jamii

Mawasiliano ya Nje

Wawekezaji Wateja Watumiaji na Jamii

POST HOLDINGS, INC. KANUNI ZA MAADILI

2

3

Page 6: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

Post Holdings, Inc. na washirika na kampuni zake tanzu kote duniani (“Post” au “Kampuni”) tumejitolea kufanya biashara zetu kwa njia inayofuata maadili, uwajibikaji na kwa mujibu wa kanuni na sheria zote zinazotumika. Sifa yetu ya uadilifu inatokana na maamuzi tunayofanya na jinsi tunavyoendesha shughuli zetu.

Kila mtu katika jamii ya Post ana jukumu na wajibu wa kufuata Kanuni zetu za Maadili (“Kanuni”) na kuzingatia sera na desturi za Kampuni pamoja na sheria zote zinazotumika mahali popote tunapohudumu. Katika Kanuni yetu, neno “wafanyakazi” linajumuisha waajiriwa, washirika, maofisa na wakurugenzi wa Kampuni.

Kunaweza kuwa na hali ambapo sera au sheria katika baadhi ya maeneo au katika vitengo vya biashara yetu vinaweza kuwa kali sana kushinda kanuni zilizo kwenye Kanuni zetu. Wakati mwongozo si bayana, tafuta ushauri kutoka kwa walioorodheshwa katika sehemu ya Kutafuta Mwongozo na Kuzungumza.

UTANGULIZI

GUIDEPOST

Page 7: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

POST HOLDINGS, INC. KANUNI ZA MAADILI

MAJUKUMU YA USIMAMIZIMameneja na wasimamizi wana jukumu kubwa la kuongoza kwa mfano kwa kuwa na mienendo inayofuata Kanuni zetu. Ikiwa wewe ni meneja au msimamizi, unatarajiwa:

• kuhakikisha kwamba kila mfanyakazi aliye chini yako anajua na kuelewa Kanuni na sera na taratibu husika na jinsi ya kuzitumia

• kuonyesha kwa maneno na vitendo kujitolea kwako kufuata Kanuni, sera na taratibu husika

• kuwahimiza wafanyakazi watafute ushauri au usaidizi bila woga wa kuadhibiwa au kisasi

• kuripoti haraka na kuchukua hatua dhidi ya ukiukaji, kuhakikisha kwamba hatua muafaka za nidhamu zimechukuliwa kwa ushirikiano na idara ya rasilimali watu na idara ya sheria, inavyostahili

• kukuza desturi ya kuzungumza kwa kuhakikisha kwamba unafikika na unapatikana kwa wafanyakazi wote

UCHUNGUZITunachukulia kila ripoti kwa uzito, tunachukua hatua haraka na kuchunguza kwa undani ikiwa ni muhimu. Sisi wote tunatakiwa kushirikiana kikamilifu na uchunguzi wowote endapo tutaombwa kufanya hivyo. Katika hali kama hizo, ni sharti tutoe maelezo ya kweli na kamilifu.

KUTOLIPIZA KISASIMazingira yetu yanafaa kuwa yanayowapa wafanyakazi wote ujasiri wa kuripoti matukio yoyote wanayojua au wanayoshuku kuwa hayafai au ya ukiukaji na wafanye hivyo bila kuogopa kulipiziwa kisasi. Hatua yoyote au kulipiza kisasi dhidi ya mtu yeyote ambaye kwa nia njema, ameripoti ukiukaji halisi au shaka ya ukiukaji au aliyehusika katika uchunguzi hakuruhusiwi kabisa. Soma pia Sera ya Kimataifa - Hakuna Kisasi.

Kampuni yetu hufanya kazi vizuri zaidi wakati mawasiliano ya wazi na ya kweli yanaheshimiwa na kuhimizwa. Ukijipata katika hali ngumu au inayokutia shaka, tunakuhimiza uzungumze. Ikiwa utafahamu kuwepo kwa uvunjaji wa Kanuni, sheria na kanuni za Kampuni, unatakiwa kuarifu wafuatao:

KUTAFUTA MWONGOZO NA KUZUNGUMZA

Kuripoti uvunjaji wa maadili kunataka ujasiri. Hata hivyo, kufahamu kwamba kuna uvunjaji na kukimya ni kinyume cha Kanuni zetu na hakuruhusiwi kwa sababu kunanyima fursa ya kutatua au kusuluhisha tatizo.

Ikiwa hujisikii huru kuzungumza na msimamizi wako au ikiwa msimamizi wako anahusika katika ukiukaji, piga ripoti kwa mojawapo wa walioorodheshwa hapa. Usisubiri hali iwe mbaya zaidi. Piga ripoti mara moja.

Mfumo wa Wafanyakazi Kuongea una wahudumu kutoka shirika nyingine huru. Mfumo huu unafanya kazi usiku na chana, siku saba za wiki. Tunapendekeza ujitambulishe kwa sababu kufanya hivyo husaidia kufuatilia jambo na kutoa maoni. Unaweza kuripoti bila kujitambulisha ikiwa inaruhusiwa na sheria za mahali ulipo, pia katika baadhi ya nchi, kuna aina ya masuala yanayoruhusiwa kuripotiwa kupitia Mfumo wa Wafanyakazi Kuongea. Ukiripoti, na iwe hakuna matakwa tofauti ya kisheria, wahudumu wa shirika lililopokea maoni watawasilisha hoja yako kwa idara ya Utekelezaji katika Shirika ili suala litatuliwe. Ripoti zote hushughulikiwa kwa uangalifu na haraka. Usiri na kutofichua utambulisho kutazingatiwa kwa kiwango cha juu kinachowezekana, kwa kufuata sheria na kanuni husika au utaratibu wa kisheria.

1. msimamizi wako

2. rasilimali watu

3. idara ya sheria

4. wakaguzi wa ndani

5. utekelezaji katika shirika

6. Mfumo wa Wafanyakazi Kuongea

4

5

“NIA NJEMA” ina maanisha kujitokeza na kwa ukweli na maelezo yote tuliyo nayo kuhusu tukio tunaloamini linakiuka Kanuni zetu, sera ya Kampuni au sheria. Hata kama tunashuku kwamba ukiukaji umefanyika au unafanyika, tunafaa kuzungumza. Ni sawa ikitokea kwamba ripoti tuliyopiga haikuwa kweli ilimradi tulifanya hivyo kwa nia njema. Mtu yeyote anayepiga ripoti kwa nia isiyo njema naweza kuchukuliwa hatua za nidhamu.

Kwa simu (877) 452-3658 Marekani na Kanada au kwa kutumia namba za simu kutegemea nchi unapopigia simu (angalia ukurasa wa 28) mtandaoni kwenye wavuti www.postholdings.ethicspoint.com

Page 8: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

KUFANYA KAZI PAMOJA KWA KUAMINIANA

GUIDEPOST

Page 9: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

Wafanyakazi

Ufanisi unaweza tu kupatikana ikiwa tunaheshimiana. Kila mmoja wetu ana haki ya kufanya kazi katika mazingira yasiyo na unyanyasaji, ubaguzi, ghasia na kisasi.

08 Utangamano na Ujumuishaji

Heshima Kazini

Usalama na Afya Kazini

09 Faragha na Taarifa za Binafsi

Mitandao ya Kijamii

POST HOLDINGS, INC. KANUNI ZA MAADILI

6

7

Page 10: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

GUIDEPOST

UTANGAMANO NA UJUMUISHAJI

Tumejitolea kubuni mazingira jumuishi yanayolingana na jamii ambapo tunafanya kazi na kuishi. Tunaamini kwamba utangamano unatufanya kuwa shirika bora, hutupatia mtazamo mpana, huchangia ubora wa juu wa kazi na kuimarisha mazingira yetu ya kazi. Tunaunganishwa na maadili yetu huku tukiheshimu tofauti zetu mahususi. Ni lengo letu kuhimiza na kukuza utangamano ili wafanyakazi wote wahisi kwamba wamekaribishwa, wanajumuishwa, wanathaminiwa, wanasaidiwa na wanaweza kufanikiwa.

HESHIMA KAZINI

Hatubagui wala kuwatendea wafanyakazi au wanaomba kazi kwa njia isiyo ya haki. Uamuzi wa kuajiri hufanywa kwa kuzingatia ustahili, kufuzu na utendakazi bila kuzingatia sifa nyingine kama vile kabila, rangi, dini, jinsia, taifa, usuli, uraia, umri, kuwa mwenye ulemavu, mwelekeo wa kimapenzi, utambulisho wa jinsia, hali ya kuwa mwanajeshi au mwanajeshi mstaafu na kuolewa au kutoolewa. Tunajituma kuhakikisha kwamba watu wenye sifa zinazotakikana wanaweza kukuza na kuendeleza ujuzi wao.

Kila mtu ana haki ya kufanya kazi katika mazingira yasiyo na unyanyasaji. Unyanyasaji ni tambia isiyofaa inayoathiri utendaji wa mfanyakazi au kufana mazingira ya kazi yasiwe mazuri. Unyanyasaji unajumuisha kumwendea mtu kwa namna yoyote asiyotaka kupitia maneno, kumwangalia, kumgusa

au udhalilishaji (uwe wa ngono au la) unachukiza au kufanya mazingira ya kazi yasiwe mazuri. Unyanyasaji hauruhusiwi kabisa. Ukiukaji utasababisha kuchukuliwa hatua za nidhamu, ikiwa ni pamoja na, kuachishwa kazi. Soma pia Sera ya Kupinga Unyanyasaji kwa maelezo zaidi.

USALAMA NA AFYA KAZINI

Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote. Hatufai kuruhusu vitendo visivyo salama kazini, iwe sisi ni washiriki au waangalizi tu. Ili kuhakikisha usalama wa kila mtu katika viwanda vyetu, kila mfanyakazi anatakiwa kuelewa na kufuata masharti na taratibu zote za usalama. Ukijua hali yoyote isiyo salama ya kufanyia kazi au hali yoyote inayokiuka sera ya Kampuni, sheria au hali yoyote inayoweza kusababisha hatari, unatakiwa kuripoti mara moja kwa msimamizi aliye mahali ulipo au mmoja wa walioorodheshwa katika sehemu yenye mada, Kutafuta Mwongozo na Kuzungumza.

Kazi Bila Ulevi Kufanyakazi ukiwa umelewa dawa za kulevya au pombe kunasababisha mazingira hatari isiyokubalika kwako na wengine. Tukiwa wafanyakazi, haturuhusiwi kuwa na, kutumia au kufanya kazi tukiwa tumelewa pombe, mihadarati au dawa nyingine zinazodhibitiwa. Wafanyakazi hawaruhusiwi kutenda majukumu yako wakiwa wametumia dawa zozote zinazoweza kuathiri utendakazi wao au kuwa hatari kwa usalama.

Tafadhali soma sera ya mahali ulipo kwa ushauri zaidi.

Usalama wa Binafsi Wafanyakazi hawaruhusiwi kujihusisha katika kitendo chochote kinachoweza kumfanya mtu mwingine ahofu au kutokuwa salama. Hii ni pamoja na vitisho au kitendo chochote cha ukatili, unyanyasaji au tabia ya ghasia. Huturuhusu kuwa na silaha mahali pa kazi. Marufuku hii inajumuisha maegesho ya Kampuni yanayoruhusiwa na sheria za mahali ulipo. Wafanyakazi wanatakiwa kuripoti mara moja vitisho au hofu ya ghasi kwa wasimamizi wa mahali walipo au kama ni dharura, kwa maofisa wa usalama mahali ulipo.

SWALI: Ninaamini kwamba mfanyakazi mwenza hapendezwi na utani unaohusisha masuala ya ngono yanayozungumzwa kwenye chumba cha mapumziko. Utani huo haunisumbui. Je, ninafaa kusema kitu?

JIBU: Ikiwa unaamini kwamba utani huo unachukiza mfanyakazi mwenzako, unafaa kumhimiza aongee awajulishe wanaofanya matani hayo kwamba vichekesho vyao havipendezi. Ikiwa mfanyakazi mwenzako anasita kuongea, mjulishe msimamizi au idara ya Rasilimali Watu kuhusu hali ilivyo. Sote tumejitolea kuwa na mazingira ya kazi yasiyo na unyanyasaji.

Page 11: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

POST HOLDINGS, INC. KANUNI ZA MAADILI

FARAGHA NA TAARIFA ZA BINAFSI

Wakati wa kufanya biashara yetu, Kampuni hukusanya taarifa zinazoweza kumtambulisha mtu kutoka kwa wauzaji, wateja, wanaotumia huduma, wafanyakazi na washirika wengine. Taarifa hizi zikiwa pekee, au zikiwa pamoja na nyingine zinazokusanywa, humtambulisha mtu kama vile kwa jina au pamoja na anwani au namba ya kitambulisho cha taifa. Tumejitolea kushughulikia data binafsi za watu kwa uwajibikaji na kwa kuzingatia sheria na kanuni zote husika. Tunalinda data ya binafsi ili isipotee, isitumiwe vibaya, kufikiwa na watu wasioruhusiwa au kufichuliwa, kubadilishwa au kuharibiwa.

Ingawa Kampuni inaheshimu faragha ya wafanyakazi, ina haki ya kukagua viwanda na mali zake kama vile, tarakilishi, rekodi za simu, makabati, barua pepe, faili, hati za biashara na vituo vya kufanyia kazi kwa mujibu wa sheria za mahali ulipo. Wafanyakazi hawafai kutarajia usiri wanapotumia huduma au vifaa wanavyopewa na Kampuni isipokuwa kama kuna sheria tofauti zinazotumika mahali ulipo. Pia, inapotakiwa na sheria, huwa tunawapa ilani watu ambao tunakusanya taarifa za binafsi kutoka kwako. Ilani itaeleza jinsi taarifa hizo zinatumiwa.

Tunazingatia SHERIA ZA NCHINI mahali popote tunapofanya kazi kote duniani. Tunazingatia viwango vya mishahara na saa za kazi, sheria zinazopiga marufuku ubaguzi na unyanyasaji, mwongozo wa usalama na matakwa ya usawa katika fursa za ajira. Ikiwa una dukuduku lolote kuhusu ubaguzi, unyanyasaji au kitendo kingine kinachovunja sheria, zungumza na mmoja wa walioorodheshwa kwenye Kutafuta Mwongozo na Kuzungumza.

MITANDAO YA KIJAMII

Mitandao ya kijamii inaweza kusaidia sana katika kushirikiana mawazo, kukuza biashara na kubadilishana mawazo. Kampuni hutumia mitandao ya kijamii kupigia debe bidhaa zetu na kuwasiliana na wafanyakazi, wateja, wahudumiwa, washirika wengine na umma. Tunazingatia sheria na kanuni zote zinazohusu mawasiliano ya kielektroniki. Wafanyakazi ambao hutumia mitandao ya kijamii nje ya kazi hawafai kamwe kujadili masuala ya siri ya Kampuni na hawafai kutoa maoni ambayo yanaweza kuchukuliwa kuwa ya Kampuni; wasemaji walioidhinishwa pekee ndio wanaoweza kutoa kauli kwenye mitandao ya kijamii kwa niaba yetu. Soma pia Sera ya Mitandao ya Kijamii.

8

9

TUNAUNGANISHWA NA

MAADILI YETU HUKU

TUKIENZI TOFAUTI ZETU

MAHUSUSI.

Page 12: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

TUNAFANYA KAZI PAMOJA KWA KUWAJIBIKA KWA AJILI YA WAWEKEZAJI WETU

GUIDEPOST

Page 13: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

Wawekezaji

Wawekezaji wetu wanaamini kwamba tunaweza kuleta ufanisi na thamani. Tunadumisha imani yao kwetu kwa kufanya biashara kwa kuzingatia kiwango cha juu cha uadilifu. Tunatii sheria zote husika za soko la mitaji na kanuni za Soko la Hisa la New York.

12 Biashara ya Ndani

Kuhifadhi Nakala na Mahesabu Sahihi

13 Kulinda Mali ya Kampuni na Taarifa za Siri

Kulinda Haki ya Ubunifu

POST HOLDINGS, INC. KANUNI ZA MAADILI

10

11

Page 14: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

GUIDEPOST

BIASHARA YA NDANI

Wafanyakazi hawaruhusiwi kuuza au kununu au kupendekeza uuzaji au ununuzi wa hisa za Kampuni kutegemea taarifa za ndani ya shirika walizo nazo. “Biashara ya Ndani” ni ununuaji au uuzaji wa hisa za kampuni zinazouzwa katika soko la hisa huku ukiwa na ushahidi au taarifa zisizopatikana kwa umma kuhusu anayetoa hisa hizo. Biashara ya Ndani na “udokezaji” (kumwambia mtu yeyote maelezo ya ndani ya shirika ambayo anaweza kutumia kununua au kuuza hisa) hakuruhusiwi na sera ya Kampuni pamoja na sheria za nchi nyingi. Ikiwa una shaka, taarifa unazopokea ukiwa mfanyakazi zinafaa kuchukuliwa kuwa muhimu na isiyo ya umma. Ikiwa una maswali kuhusu uuzaji au ununuaji wa hisa katika mazingira ambayo huenda yanahusisha maelezo ya faragha, wakati wa kununua au kuuza hisa, au jambo jingine linalohusu sheria husika, tafadhali wasiliana na idara ya Sheria. Soma pia Sera ya Kimataifa - Sera ya Biashara ya Ndani.

TAARIFA MUHIMU ZISIZO KWA UMMA zinajumuisha mapato, mabadiliko makuu ya faida au hasara kwa biashara, kusubiri kununua au kununuliwa, kupanua wigo au kuongeza uwekezaji, taarifa kuhusu bidhaa mpya, mashtaka yenye athari au mabadiliko katika usimamizi.

KUHIFADHI NAKALA NA MAHESABU SAHIHI

Tumejitolea kudumisha vitabu na rekodi zetu za mahesabu ya kifedha katika kiwango cha juu kabisa cha usahihi, ukamilifu na uadilifu. Tuna mifumo ya uhasibu na udhibiti wa ndani ulioundwa ili kukinga dhidi ya hasara na kuhakikisha kwamba rekodi za kampuni zinaaminika kwa ajili ya kuandaa taarifa za kifedha. Hakuna ingizo lolote la ulaghai au uongo linafaa kuwekwa kwenye vitabu, rekodi

au akaunti za Kampuni. Tunatambua kwamba wawekezaji wetu wanategemea vitabu na rekodi zetu kupata mtazamo sahihi na wenye uwazi kuhusu hali ya Kampuni.

Tukiwa wafanyakazi, ni jukumu letu kuhakikisha kwamba taarifa zilizo kwenye rekodi zetu ni kamilifu, sahihi na zinazoeleweka. Ukijua muamala wowote au mahesabu yasiyo sahihi, unafaa kuripoti suala hilo mara moja kwa mojawapo wa walioorodheshwa katika Kutafuta Mwongozo na Kuzungumza.

Kila mmoja wetu huzalisha rekodi kama sehemu ya majukumu yetu ya kawaida, kama vile ripoti za matumizi, kutayarisha zabuni, miswada na barua pepe. Ni muhimu kwa rekodi hisi kuwa sahihi na kuwekewa kumbukumbu inavyofaa. Kitu chochote kisicho sahihi kinaweza kuharibu sifa ya Kampuni na inaweza kusababisha kutoweka kwa imani waliyo nayo wawekezaji kwetu. Kwa umahususi, Kampuni hairuhusu kuomba au kusaidia kurejesha fedha kwa njia ya uongo au miamala ya kisiri isiyorekodiwa au isiyoripotiwa. Rekodi za kibiashara zinafaa kuwekwa, kuhifadhiwa na kuharibiwa kwa kufuata Sera ya Usimamizi wa Rekodi. Ikiwa unafahamu kwamba kuna rekodi zozote za kibiashara zilizo chini ya udhibiti wako zinahusika katika uchunguzi au masuala ya kisheria, hutakiwi kuzibadilisha, kuficha au kuharibu hati husika hadi utakapojulishwa hali tofauti. Hili linachukuliwa kuwa Hati ya Agizo la Kisheria. Ikiwa una maswali kuhusu iwapo rekodi fulani imewekwa chini ya Hati ya Agizo la Kisheria, tafadhali wasiliana na Idara ya Sheria.

SWALI: Nimesikia kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wenzangu kwamba Kampuni itatangaza mapato yake baadaye wiki hii na kwamba mapato hayo ni mazuri kuliko kile wachanganuzi wanatarajia. Ninajua kwamba hili litasababisha athari nzuri kwenye hisa zetu. Je, ninaweza kwenda kununua hisa za Kampuni kabla ya tangazo kutolewa kwa Umma?

JIBU: Hapana, hufai kununua hisa za Kampuni kwa sababu una maelezo yenye athari ambayo hayapatikani kwa umma. Maelezo kuhusu mapato yanachukuliwa kuwa taarifa yenye athari kwa sababu yataathiri thamani ya hisa za Kampuni na hati yatakapotangazwa, maelezo hayo yanachukuliwa kuwa yasiyo ya umma.

Page 15: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

POST HOLDINGS, INC. KANUNI ZA MAADILI

KULINDA MALI YA KAMPUNI NA TAARIFA ZA SIRI

Sote tuna jukumu sawa la kulinda na kutumia vizuri mali ya Kampuni ili kuzuia hasara, uharibifu, wizi na matumizi mabaya. Mali halisi ni pamoja na majengo, bidhaa, mitambo, rekodi, magari na fedha za Kampuni. Mali isiyo halisi ni kama vile, taarifa za siri na za kibiashara, haki ya ubunifu na mifumo ya habari ambayo pia sharti ilindwe. Kila mfanyakazi anatarajiwa kuwa mlinzi mwema wa mali yetu kwa kuitumia kwa ubora na kuilinda dhidi ya matumizi yasiyoidhinishwa. Fedha za Kampuni zinafaa kusimamiwa kwa kuzingatia sera zote husika za Kampuni.

Rasilimali za teknolojia kama vile vipakatalishi, simu za mkononi, kompyuta kibao na programu hutolewa kwa madhumuni ya kazi. Tunafaa kuwa waangalifu na tuwajibike katika kutumia rasilimali hizi kwa kwa kuzingatia

mifumo ya usalama na mikakati iliyowekwa na Kampuni ili kulinda taarifa na data ya Kampuni ili isivuje kimakosa au kufichuliwa bila kibali, kutumika vibaya, kubadilishwa visivyo au kuharibiwa. Unaweza kuruhusiwa kutumia rasilimali ya teknolojia kwa uchache na kwa njia iliyo sawa.

Huruhusiwi kabisa kutumia rasilimali ya teknolojia ya Kampuni kwa vitendo vinavyokiuka sheria, maadili au vilivyo kinyume na Kanuni au sera ya Kampuni. Kwa maelezo ya ziada kuhusu kutumia rasilimali ya teknolojia ya Kampuni, tafadhali soma Sera ya Utumiaji Unaoruhusiwa wa Teknolojia.

Katika kipindi ambacho umeajiriwa unaweza kupata taarifa fulani kuhusu Kampuni, wateja, wauzaji au washirika wake wa kibiashara au washirika wengine ambayo ni ya faragha au ya kibiashara. Taarifa za faragha inajumuisha maelezo yoyote yasiyopatikana kwa

umma ambayo yanaweza kutumiwa na washindani wetu, au ambayo yakifichuliwa, ni hatari kwa Kampuni au wateja wake. Unafaa kuchukulia taarifa za Kampuni kuwa faragha kila wakati isipokuwa kama una uelewa wa waziwazi kwamba maelezo hayo yanapatikana kwa umma. Ni sharti uchuku tahadhari inayofaa kila wakati kulinda taarifa za faragha ambazo unazopata. Shiriki tu taarifa za faragha za Kampuni na watu walio na haja ya biashara ya kufanya hivyo. Usijadili maelezo ya faragha katika maeneo ambapo yanaweza kusikilizwa kama vile migahawa, ndege, lifti au maeneo yanayotumiwa pamoja na wafanyakazi wengi kiwandani. Kwa maelezo zaidi, tafadhali soma Sera ya Kutoa Taarifa za Kampuni kwa Umma.

KULINDA HAKI YA UBUNIFU

Ni sharti tulinde haki za Ubunifu wa Kampuni yetu. Kamwe usiruhusu watu wengine kutumia ubunifu wetu bila kupata idhini inayofaa. Haki ya ubunifu inajumuisha chapa za biashara, majina, mitindo ya kufungasha, nembo, hakimiliki, uvumbuzi, hataza na siri za biashara. Haki ya ubunifu pia inajumuisha matokeo ya wafanyakazi kama vile uvumbuzi, mawazo, ugunduzi, uboreshaji, michakato, usanifu au kitu chochote unachounda kwa kutumia zana za Kampuni, kwa muda wa Kampuni kwa gharama ya Kampuni au ndani ya wigo wa kazi kazo katika Kampuni. Tunaheshimu haki za ubunifu za watu wengine jinsi tunavyoheshimu haki zetu wenyewe.

SOTE TUNA JUKUMU LA

KULINDA VIZURI NA

KUWAJIBIKIA UTUMIAJI

WA MALI YA KAMPUNI.12

13

Page 16: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

GUIDEPOST

Tunajizatiti kuwa na viwango vya juu kabisa vya

Page 17: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

POST HOLDINGS, INC. KANUNI ZA MAADILI

14

15uadilifu na haki katika kila kitu tunachofanya.

Page 18: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

TUNAFANYA KAZI PAMOJA KWA UADILIFU KWA AJILI YA WATEJA WETU

GUIDEPOST

Page 19: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

Wateja

Kudumisha ahadi yetu ya uadilifu kunajenga imani ya wateja wetu na kuimarisha sifa yetu. Shughuli yoyote tunayofanya na wateja wetu sharti iwe na usawa, na ukweli, bila mapendeleo.

18 Mgongano wa Maslahi

21 Ushindani wa Haki (Kutoaminika)

Kupambana na Rushwa/Ufisadi

23 Kufanya Biashara Kimataifa

Kulinda Haki za Binadamu

16

17

POST HOLDINGS, INC. KANUNI ZA MAADILI

Page 20: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

MGONGANO WA MASLAHI

Kila mmoja wetu ni lazima achunge asiwe na athari, maslahi au uhusiano ambao unaweza kuhitilafiana na maslahi ya Kampuni yetu. Hii ina maana kwamba shughuli zetu za binafsi, kifedha au za kibiashara sharti zisiathiri uwezo wetu wa kufanya uamuzi sahihi kwa niaba ya Kampuni. Ili kudumisha sifa yetu, usijiweke katika hali zinazoweza kuibua hata dhana kwamba kuna mgongano wa maslahi.

Sehemu zinazofuata zinaeleza baadhi ya matukio ya kawaida ambayo yanaweza kusababisha mgongano wa maslahi.

Ajira ya Nje Kazi unayofanya nje ya Kampuni ni lazima isiathiri vibaya utendakazi wako kazini au kusababisha mgongano wa maslahi. Sera ya Kampuni hairuhusu kufanya kazi au kutoa huduma kwa mshindani yeyote, mteja au muuzaji bila kibali cha idara ya Rasilimali Watu.

Mbali na ajira ya nje, shughuli za kibinafsi kama vile kuwa na biashara unayofanya katika muda wako, zinaweza kusababisha mgongano wa maslahi ikiwa biashara hiyo ina shughuli zinazoshindana na maslahi ya Kampuni au zinatoa picha mbaya kwa Kampuni. Kwa sababu hiyo, ikiwa unahusishwa kikamilifu au kwa sehemu na biashara fulani, biashara hiyo hairuhusiwi kuiuzia Kampuni au mshindani wa kampuni wa sasa au anayeweza kuwa mshindani, mteja au muuzaji wa kampuni bila kufichua uhusiano huo na kupata kibali.

Maslahi ya Kifedha Tunaheshimu uhuru wako wa kuwekeza katika kampuni nyingine ilimradi maslahi yako ya kifedha hayaathiri uamuzi au shughuli unazofanya kwa niaba ya Kampuni na haidhuru sifa ya Kampuni. Hakuna mfanyakazi au wanafamilia yake (ilivyofafanuliwa hapa chini) anafaa kuwa na uwekezaji mkubwa katika biashara yoyote inayotaka kufanya biashara na Kampuni au mshindani yeyote wa Kampuni, isipokuwa kama umiliki huo umefichuliwa na kupatikana hausababishi mwingiliano wa maslahi. Hata hivyo, kumiliki kiasi kilicho chini ya 5% ya thamani ya hisa (au zaidi ya 5% katika bima ya ubia au uhusiano kama huo usio wa hiari, mipangilio usiyoagiza) au kuwa na hisa katika kampuni inayouza hisa kwa umma kunaruhusiwa.

GUIDEPOST

SWALI: Ninazingatia kutafuta kazi ya muda mfupi katika duka lililo karibu nami. Duka hilo huuza baadhi ya bidhaa za Kampuni yetu. Je, hilo litakuwa mgongano wa maslahi kwa Kampuni?

JIBU: Mradi kazi ya muda unayofanya haikuzuilii kutumia muda na juhudi zako katika kazi yako ya Kampuni na kwa vile huhusiki katika ununuzi wa bidhaa ambazo duka linauza, hakutakuwa na tatizo.

Page 21: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

Kufanya Kazi na Familia Hatupendi mgongano wa maslahi kati ya mahusiano yetu ya binafsi na ya kikazi. Kanuni ya kawaida ni kwamba, hatukuruhusu kumsimamia moja kwa moja mtu wa familia. Katika matukio ambapo mtu wa familia anafanya kazi katika idara au eneo sawa, majukumu ya kazi na muda wa ziada utatolewa kwa kuzingatia vigezo vyenye usawa. Uamuzi unaohusu malipo na tathmini ya utendakazi utashughulikiwa na mtu asiye na uhusiano. Mgongano wa maslahi au uwezekano wa mgongano unaweza kutokea katika hali ambapo mtu wa familia anafanya kazi au anahudumia mshindani, mteja au muuzaji. Ripoti hali zozote unazotilia shaka kwa msimamizi wako mara tu unapofahamu hali yoyote inayoweza kusababisha mgongano wa masilahi ili kuepuka kuwa na mgongano wa maslahi na mtu wa familia.

Ni muhimu kueleza kama kuna uhusiano wowote wa kifamilia unoingiliana na kazi. Kufanya hivyo hutusaidia kuzuia kutokea kwa mgongano wa maslahi na hulinda sifa ya watu binafsi na Kampuni.

MTU WA FAMILIA ni pamoja na mkeo au mumeo, mtoto, ndugu, mzazi, mtoto au mzazi wa kambo, pamoja na mavyaa, bavyaa, mkaza mwana, wifi na mtu yeyote anayeishi na wewe.

18

19

KILA MMOJA WETU NI LAZIMA ACHUNGE

ASIWE NA ATHARI, MASLAHI AU UHUSIANO

AMBAO UNAWEZA KUHITILAFIANA NA

MASLAHI YA KAMPUNI YETU.

POST HOLDINGS, INC. KANUNI ZA MAADILI

Page 22: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

Fursa za Biashara ya Kampuni Hatufai kamwe kushindana na Kampuni au kutumia taarifa, mali au nafasi zetu katika Kampuni kujinufaisha binafsi. Tunatarajiwa kukuza maslahi ya Kampuni na hatufai kamwe kujinufaisha na fursa tunazounda tukiwa waajiriwa wa Kampuni. Vivyo hivyo, hatufai kamwe kumsaidia mtu au kumruhusu kujinufaisha kwa kuchukua fursa ya biashara au uwekezaji kwa manufaa ya binafsi, hao ni pamoja na wanafamilia au marafiki.

Uanachama katika Bodi au Kamati Ingawa tunahimiza kushiriki katika mashirika ya taaluma na shughuli za jamii, ni muhimu kwamba ushiriki wetu usidhuru sifa ya Kampuni au kutuzuia tusifanye kazi zetu. Si lazima wafanyakazi wapate kibali cha kuwa katika bodi ya mashirika yasiyo ya faida ilimradi shughuli za mashirika hayo hayaathiri vibaya au kuingiliana na majukumu ya Kampuni. Kibali cha mapema cha idara ya Utekelezaji katika Shirika kinahitajika ili kuhudumu katika bodi ya wakurugenzi wa mashirika mengine.

Zawadi na Burudani Kutoa au kupokea zawadi na burudani kunataka kuzingatiwa kwa kina. Ingawa tabia ya kutoa na kupokea zawadi inaweza kukuza uhusiano bora wa kibiashara, kuna uwezekano wa kuwa mgongano wa maslahi au kuonekana kuwa na mgongano. Kwa sababu hiyo, tunajukumu la kuhakikisha kwamba zawadi au burudani yoyote inayotolewa au kupokelewa inaruhusiwa na Kanuni zetu na sera au sheria zozote husika. Haturuhusu kabisa kutoa au kupokea zawadi au burudani yoyote, iwe ni moja kwa moja au kupitia watu wengine kwa lengo la kushawishi uamuzi wa kibiashara au kuathiri uwezo wa kufanya uamuzi huru.

Zawadi yoyote tunayotoa au kupokea katika mahusiano ya kibiashara haifai kuwa na thamani ya kifedha, isiwe ya mara kwa mara na itimize matakwa yote yaliyo kwenye sera yetu, ikiwa ni pamoja na sera ya mahali ulipo na Sera yetu ya Kupambana na Rushwa/Ufisadi. Ni muhimu kukumbuka kwamba kile kinaweza kuchukuliwa kuwa wastani kwa mujibu wa sheria na desturi za sehemu moja kinaweza kuwa ubadhirifu mahali pengine. Zawadi zinazokubalika ni vitu vinavyoweza kugusika kama vile

vilivyo na nembo ya kampuni, mikoba ya zawadi au vyakula maalum. Zawadi zisizokubalika ni pamoja na: • Zawadi ya pesa au sawa na pesa• Zawadi inayotolewa ili kupokea faida

ya binafsi au ushawishi wa kibiashara• Zawadi zinazokiuka sheria, za ngono

au zinazokiuka maadili yetu• Zawadi kwa maofisa wa serikali

GUIDEPOST

SWALI: Je, kuna tofauti gani kati ya zawadi ya biashara na burudani?

JIBU: Zawadi ni vitu vya thamani kama vile safari, malazi vyakula au burudani wakati mwenyeji hayuko, ukarimu ni pale mwenyeji yuko.

SWALI: Muuzaji alinipa zawadi ghali wakati wa mkutano wa kibiashara. Sikutaka kumuudhi kwa hivyo nilikubali zawadi hiyo. Je, nifanye nini?

JIBU: Unafaa kuripoti kuhusu zawadi hiyo mara moja kwa idara ya Utendakazi katika Shirika na uombe kuelekezwa. Kutegemea na hali zilizopo na thamani ya zawadi, tunaweza tukakuomba kurudisha zawadi hiyo au kuomba ruhusa ya muuzaji aliyekupa ili uikabidhi kwa shirika lisilo uhisani.

Page 23: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

Kumpa chakula au zawadi ndogo kwa ofisa wa serikali inaweza kuwa kinyume cha sheria. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu kutagusana na maofisa wa serikali hapa chini kwenye Kupambana na Rushwa/Ufisadi.

Ukarimu wa kibiashara, ikiwa ni pamoja na vyakula na burudani, haujapigwa marufuku ikiwa marudio na matukio yake yanaeleweka na yanahusu utendaji wa biashara za Kampuni na kufuata sera husika.

Ikiwa huna uhakika ikiwa zawadi au ukarimu unazidi kiwango kinachokubalika, unaweza kuwasiliana na idara ya Utekelezaji katika Shirika kwa mwongozo. Kuwa na zawadi au kukubali ukarimu unaoweza kuathiri unahitaji idhini ya Ofisa wa Utekelezaji katika Shirika.

USHINDANI WA HAKI

Tunatakiwa kuzingatia sheria za ushindani na kutoaminika katika nchi nyingi tunakofanya biashara. Sheria kama hizi zinanuiwa kudumisha ushindani wa haki na sera yetu inatutaka tufuate kikamilifu sheria za ushindani zinazotumika katika maeneo tunakohudumu. Hufai kutangamana na washindani. Hata hivyo, tunaelewa kwamba kuna matukio ya kutangamana na washindani ambayo hayawezi kuepukika kama vile wakati wa makongamano yanayohusu tasnia au miungano ya vyama vya wafanyakazi. Katika matukio hayo, wafanyakazi wanatakiwa kuwa waangalifu wanapowasiliana au kutangamana na washindani.

Sheria za ushindani zinatukataza kufanya makubaliano na washindani ambayo yanaweza kudumaza biashara. Mifano

ya shughuli zinazokatazwa ni pamoja na: kupanga bei, kudhibiti uzalishaji, kudanganya katika zabuni na kugawanya masoko, wateja, maeneo au rafu za kuuzia. Kukubali kupunguza uzalishaji au mauzo au kutofanya biashara na wateja au wauzaji fulani pia hakuruhusiwi. Si lazima makubaliano yawe rasmi au kwa maandishi ili yawe ya kisheria.

Sheria za ushindani ni changamano na huenda zikawa tofauti kati ya nchi mbalimbali. Ukikubali kupokea taarifa za faragha au za kibiashara kuhusu mshindani, ni sharti uifahamishe idara ya Sheria mara moja. Soma Sera ya Kimataifa - Sera ya Kutii Sheria za Ushindani.

KUPAMBANA NA RUSHWA/UFISADI

Kuzuia, kutambua na kuripoti rushwa na ufisadi ni jukumu la kila mtu anayefanya kazi katika Kampuni. Tunataka kudumisha imani kati yetu na washirika wetu wa kibiashara. Imani hiyo inapatikana kwa ubora ikiwa sisi wote tutafanya shughuli zetu kwa kuzingatia maadili na uaminifu bila kujali shinikizo za kibiashara tulizo nazo wakati huo. Huwa hatuamui kushiriki rushwa au tabia nyingine za ufisadi.

Hatutoi wala kupokea rushwa. Hatuombi wala kukubali rushwa. Hatufanyi malipo ya kulainisha mambo au kuwaruhusu watu wengine wafanye hivyo kwa niaba yetu.

20

21

POST HOLDINGS, INC. KANUNI ZA MAADILI

UKARIMU WA KIBIASHARA,

IKIWEMO VYAKULA NA BURUDANI,

HAUJAPIGWA MARUFUKU IKIWA

HAIJIRUDIIRUDII SANA.

Page 24: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

RUSHWA ni malipo au “kitu chochote cha thamani” kinachotolewa ili kuathiri au kupongeza uamuzi wa biashara au kitendo cha serikali. Rushwa inaweza kutolewa kwa kutumia kitu “chochote cha thamani,” ikiwemo pesa, fursa za biashara, kupendelewa, kupata taarifa za faragha, fursa za ajira, zawadi, vyakula, burudani (kwa mfano tiketi za kuhudhuria michezo) au michango kwa mashirika yasiyo na faida.

Malipo ya kulainisha mambo, ambayo pia huitwa “chai” au “kupaka mafuta” hufanywa ili kuharakisha utaratibu na masuala ya kawaida kama vile kutoa kibali, kufungua au kufunga maji au umeme, kuondoa bidhaa forodhani, kukubali visa au kutoa ulinzi wa polisi. Ingawa malipo hayo huwa kawaida ya biashara katika baadhi ya nchi, yanasalia kuwa kinyume cha sheria katika nchi nyingi. Huruhusiwi kutoa malipo ya kulainisha mambo isipokuwa katika hali ambapo upo katika hatari ya kuumizwa, ambapo unaruhusiwa kutoa malipo ya kulainisha, lakini ni sharti uripoti kwa idara za Sheria na Utendakazi wa Shirika mara moja.

Kutangamana na Maofisa wa Serikali Sheria zinazohusu kutangamana na maofisa wa serikali ni changamano ni inafaa kuangaliwa kwa makini.

Mtagusano wetu na ofisa wa serikali haufai kumfanya atumie vibaya wadhifa wake namna inayonufaisha Kampuni. Sheria na kanuni za kupambana na ufisadi zinadhibiti zawadi, ukarimu, burudani na safari zinazoweza kutolewa kwa maofisa wa serikali.

Zawadi za ofa zisizo na thamani kama vile bidhaa zilizo na nembo ya Kampuni au nembo ya mojawapo ya bidhaa zetu, inaweza kupewa ofisa wa serikali kama ishara ya ukarimu ili kukuza uhusiano mwema, lakini zawadi kama hizi zinafaa kuwa ndogo na hazifai kutolewa ili kuathiri kitendo au uamuzi au kupendelewa. Kampuni inaweza ikalipa ada zisizo ghali zinazohusiana na ukarimu, burudani na safari wakati gharama kama hizo zinahusiana na matangazo, maonyesho au ufanyaji mifano ya bidhaa za Kampuni au zinazohusiana na utekelezaji au utendaji wa mkataba. Ikiwa malipo kama hizi yatafanywa kwa ajili ya maofisa wa serikali, ni sharti yaidhinishwe na idara ya Sheria au Utekelezaji katika Shirika. Maofisa wa Serikali ni Pamoja na:

• Ofisa au mfanyakazi yeyote wa serikali, shirika, wizara au idara ya serikali (katika ngazi yoyote)

• Mtu yeyote anayehudumu kwa njia rasmi kwa niaba ya serikali (katika ngazi yoyote)

• Ofisa au mfanyakazi yeyote wa kampuni inayomilikiwa kikamilifu au kwa sehemu na serikali (k.m kampuni inayomilikiwa na serikali)

• Chama cha siasa au ofisa wa chama chochote cha siasa au mgombea katika wadhifa wa kisiasa

• Ofisa au mfanyakazi katika ofisi ya kimataifa ya umma kama vile Umoja wa Mataifa

• Wanafamilia ya waliotajwa hapa juu

Tunahudumu katika nchi nyingi kote duniani ambapo kuna nyakati ambapo sheria na desturi za nchi husika zinaweza kukinzana na Kanuni zetu au sera za Kampuni. Ikiwa huna uhakika wa sheria, kanuni au sera ya kufuata, tafadhali soma Sera ya Kupambana na Rushwa/Ufisadi na utafute ushauri kutoka idara ya Sheria au Utekelezaji katika Shirika.

GUIDEPOST

Page 25: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

KUFANYA BIASHARA KIMATAIFA

Tunafuata kanuni zote zinazosimamia shughuli za biashara yetu kimataifa. Wafanyakazi wanaohusika katika mauzo, masoko, usambazaji au usafirishaji wa bidhaa, ikiwa ni pamoja na uhawilishaji wa teknolojia, katika mipaka ya kimataifa sharti wafahamu sheria husika na sera za nchi walipo zinazohusu vikwazo vya biashara ya kimataifa.

Kama raia wa kimataifa, tunatii vikwazo vyote vya kiuchumi na sheria zinazopinga ususiaji. Vikwazo vya kiuchumi ni nidhamu inayowekwa na nchi moja au zaidi kwa nchi, kundi au mtu binafsi. Vikwazo vinaweza kujumuisha aina kadhaa za vizingiti vya biashara, ushuru wa forodha, na vikwazo vya miamala ya kifedha. Tunazingatia vikwazo vyote kila wakati tunapofanya biashara. Pia tunazingatia sheria zinazopinga ususiaji, sheria hizo zinakataza kampuni kushiriki au kuhusika katika baadhi ya ususiaji wa kimataifa. Ukipokea ombi linalokutaka ushiriki katika ususiaji wa watu binafsi, kampuni au nchi, wasiliana na idara

ya Sheria au Utendakazi katika Shirika kwa sababu huenda tukatakiwa kuripoti maombi kama hayo kwa mamlaka za usimamizi.

Tunafuata sheria zote zinazopiga marufuku utakatishaji wa fedha au kufadhili vitendo haramu. Hatuwezi kuhusika katika miamala yoyote inayohusisha fedha zinazotokana na vitendo vya uhalifu kama vile ulaghai au ugaidi. Utakatishaji wa pesa ni kuficha asili ya pesa zilizopatikana kwa njia haramu, kwa kawaida kupitia kupitisha fedha hizo katika benki za kimataifa ua biashara halali.

Ukiukaji wa sheria zozote zilizotajwa katika sehemu hii ya Kanuni unaweza kusababisha adhabu mbaya ya kesi ya madai na jinai kwa Kampuni na mfanyakazi. Isitoshe, sheria hizi ni changamano na vikwazo vinavyohusiana

na miamala ya biashara ya kimataifa hubadilika bila ilani. Ikiwa una maswali yoyote kuhusu sheria hizi, tafadhali wasiliana na idara ya Sheria au Utendakazi katika Shirika haraka iwezekanavyo.

KULINDA HAKI ZA BINADAMU

Tukiwa shirika rai wa kimataifa, tumejitolea kulinda haki za binadamu kwa kila mtu. Tunazingatia sheria zote za mishahara na saa za kazi katika utendaji wetu wote. Tuna sera inayopiga marufuku kabisa ajira ya watoto, ajira ya lazima na tabia za ulanguzi wa binadamu. Tunatarajiwa washirika wetu wa kibiashara, wakiwemo wauzaji, washauri, wakandarasi na wakandarasi wasaidizi kuzingatia viwango sawa.

22

23

SHERIA ZA USHINDANI NI CHANGAMANO

NA HUENDA ZIKAWA TOFAUTI KATI YA

NCHI MBALIMBALI.

POST HOLDINGS, INC. KANUNI ZA MAADILI

Page 26: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

KUFANYA KAZI KWA KUJITOLEA KWA AJILI YA WATEJA WETU NA JAMII ZETU

GUIDEPOST

Page 27: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

Watumiaji na Jamii

Tumejitolea kuwapa wateja wetu chaguo salama, nafuu na za ubora wa juu kabisa. Tunajihusisha katika jamii tunakofanya kazi na kuishi.

26 Ubora wa Bidhaa

Mauzo kwa Kuwajibika

Shughuli za Siasa

Kujali Mazingira

27 Kuhusisha Jamii

Mawasiliano ya Nje

24

25

POST HOLDINGS, INC. KANUNI ZA MAADILI

Page 28: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

UBORA WA BIDHAA

Tunajitahidi kila wakati kuzalisha bidhaa za ubora wa juu katika zote tunazounda. Wafanyakazi wanaohusika katika kuandaa, kutayarisha, kufungasha au kuchambua bidhaa wanatarajiwa kufahamu viwango, sera na michakato ya Kampuni inayohusu kushughulikia bidhaa mahali walipo. Pia wafanyakazi wanatarajiwa kufuata michakato yote bora inayohusu kanuni na sheria za usalama wa vyakula. Ni sharti tufanye shughuli zetu kwa namna inayolenga kudumisha uadilifu na ubora wa bidhaa za Kampuni.

MAUZO KWA KUWAJIBIKA

Tunajivunia bidhaa zetu na tunaelewa umuhimu wa kuwa na uwazi na usahihi katika matangazo na ufungashiaji wetu. Tunataka kuhakikisha kwamba mikakati yetu ya mauzo inafuata sheria na kanuni zilizopo pamoja na sera za mahali ulipo.

SHUGHULI ZA SIASA

Sote tuna haki ya kuunga mkono harakati za siasa tunazojichagulia wenyewe, lakini shughuli hizo za kisiasa zifanyike kwa muda na rasilimali zetu binafsi. Hatufai kamwe kutumia muda na rasilimali za Kampuni katika shughuli za siasa. Hatufai kuwashurutisha wafanyakazi wenza kuunga mkono misimamo fulani.

Katika baadhi ya majimbo au mikoa, ni marufuku kuwachangia wagombea wa viti vya jimbo, mkoa au serikali za mitaa. Hakuna michango yoyote kutoka Kampuni inaruhusiwa bila kibali cha Bodi ya Wakurugenzi au wawakilishi wake.

KUJALI MAZINGIRA

Tumejitolea kufanya biashara yetu kwa namna inayodumisha ubora wa mazingira huku tukiboresha ustawi wa jamii ambako tunahudumu. Kila mmoja wetu ana jukumu la kujali kuhusu athari tunazoacha kwenye mazingira. Tunaweza kufanya hivyo kwa:

• Kufuata sheria husika za mazingira• Kutoa ripoti kuhusu umwagikaji,

kuvuja au utokaji usioidhinishwa• Kuwa waangalifu tunapotumia nishati

na maji• Kuwauliza wauzaji na washirika wa

biashara kufuata viwango fulani vya biashara

• Kujitolea kuzima taa, kutumia karatasi kidogo na kurejeleza

GUIDEPOST

Page 29: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

26

27

KILA MMOJA WETU

ANA JUKUMU LA

KUJALI KUHUSU

ATHARI TUNAZOACHA

KWENYE MAZINGIRA.

POST HOLDINGS, INC. KANUNI ZA MAADILI

KUSHIRIKISHA JAMII

Wafanyakazi wetu na biashara yetu huchangia muda, vipaji na rasilimali za kifedha kusaidia katika kuleta tofauti kwenye jamii tunakoishi na kufanya kazi. Kujitolea kwetu kuwahudumia wengine ni sehemu muhimu ya uraia wetu wa kimataifa wa kuwajibika ni inaonekana kwenye maadili yetu.

MAWASILIANO YA NJE (UVUMBUZI KWA UMMA)

Wafanyakazi hujikuta wakiulizwa maswali kuhusu biashara yetu na watu wa nje. Wafanyakazi walioteuliwa pekee ndio wanaoweza kujibu maombi hayo. Lengo la mawasiliano ya nje ni kuhakikisha kwamba ujumbe unaowasilishwa umeandaliwa vizuri ukiwa na taarifa sahihi. Kifa mfanyakazi anatakiwa kufahamu Sera ya Kutoa Taarifa za Kampuni kwa Umma.

SWALI: Nimepigiwa simu na kituo cha redio cha mahali ninapoishi wakiniuliza kuhusu thamani ya lishe katika moja ya bidhaa zetu. Ninaielewa bidhaa hii. Je, ni sawa nikimjibu aliyepiga?

JIBU: Hapana. Wafanyakazi walio na idhini pekee ndio wanaoweza kujibu maswali kutoka kwa wanahabari. Pia ni muhimu kutahadhari kwa sababu mpiga simu anaweza kuwa amedanganya kwa lengo la kupata taarifa za Kampuni kwa njia ya ulaghai.

Page 30: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

Ukisikia au kuona kitu unachoamini kuwa ni kinyume cha sheria au kinakiuka Kanuni yetu – Usinyamaze! Ripoti dukuduku zozote ulizo nazo kwa meneja au msimamizi wako, Idara ya Rasilimali Watu, Idara ya Utekelezaji katika Shirika, Idara ya Sheria, Wakaguzi wa Ndani au Mfumo wa Wafanyakazi Kuongea.

TUMIA MFUMO WA WAFANYAKAZI KUONGEA:

• Hitilafu za uhasibu na ukaguzi• Michakato ya usalama wa kuandaa chakula• Rushwa, ufisadi au malipo haramu• Hatari kwa usalama na mazingira• Mgongano wa maslahi• Wizi au ulaghai• Ubaguzi na unyanyasaji• Ghasia kazini (wakati usio wa dharura)

MISAMAHAMsamaha wowote wa kutotumia Kanuni hii unahitaji ruhusa kwa maandishi kutoka kwa Ofisa Mkuu wa Utekelezaji, au katika baadhi ya matukio (ikiwa ni pamoja na kwa mkurugenzi au ofisa yeyote mkuu), kibali cha Bodi ya Wakurugenzi kinahitajika. Ikiwa inahitajika kisheria, misamaha itatolewa mara moja.

*Namba za Mfumo wa Wafanyakazi Kuongea zinaweza kubadilishwa wakati wowote. Unaweza kupata maelezo ya hivi karibuni zaidi kwenye www.postholdings.com.

Unaweza kufikia Mfumo wa Wafanyakazi Kuongea kwenye tovuti www.postholdings.ethicspoint.com au kwa kupiga simu ukitumia namba zifuatazo kulingana na mahali ulipo.

Kila mfanyakazi ana wajibu wa kufanya kazi kwa uadilifu na kwa kufuata Kanuni yetu ya Maadili.

NCHI MSIMBO WA KUTUMIA NAMBA YA SIMU BILA MALIPO

Kanada 877-452-3658

Uchina 400-600-0569

Ujerumani 0-800-225-5288 888-225-7389

Ayalandi 00-800-222-55288 888-225-7389

Kenya Tovuti pekee: www.postholdings.ethicspoint.com

Uholanzi 0800-022-9111 888-225-7389

Afrika Kusini 080-020-4430

Uhispania 900-99-0011 888-225-7389

Uswizi 0-800-890011 888-225-7389

Muungano wa Falme za Kiarabu

8000-021 888-225-7389

Uingereza 0-800-89-0011 888-225-7389

Marekani 877-452-3658

28

Page 31: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

Idara ya Utekelezaji katika Shirika lina jukumu la msingi la kuhakikisha uzingatiaji wa Kanuni ya Maadili. Idara ya Utekelezaji katika Shirika hufanya

kazi kwa karibu sana na idara za Sheria, Ukaguzi wa Ndani, na Rasilimali Watu katika ngazi ya Shirika na katika kila kitengo cha biashara ili kuhakikisha

kwamba kuna uzingativu wa Kanuni ya Maadili katika Kampuni nzima na huunga mkono sera na taratibu. Unaweza kuwasiliana na idara ya Utekelezaji katika Shirika kwa baua pepe [email protected] au kwa sanduku

la posta Marekani 2503 S. Hanley Road, Saint Louis, Missouri 63144.

Page 32: Kanuni za Maadili - Post Holdings · 2019-03-16 · USALAMA NA AFYA KAZINI Hali Salama za Kufanyia Kazi Tumejitolea kuwa na mazingira salama ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wote.

Post Holdings, Inc. 2503 South Hanley Road St. Louis, MO 63144 www.postholdings.com

October 2018