KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi...

36
Kuishi Kulingana na Maadili Yetu KUJALI KAZI YA PAMOJA DUNIANI MAENDELEO YANAYOENDELEA KANUNI YA MAADILI MEMA Kudumisha Viwango vya Juu zaidi vya Maadili

Transcript of KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi...

Page 1: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

Kuishi Kulingana na Maadili YetuKujali • Kazi Ya paMoja Duniani • MaEnDElEo YanaYoEnDElEa

KANUNI yA MAADILI MEMA

Kudumisha Viwango vya juu zaidi vya Maadili

Page 2: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa
Page 3: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

Kampuni ya Colgate-Palmolive kwa zaidi ya miaka 200 imeonyesha kujitolea kwa maadili na kanuni zetu imara kwa kufanya biashara kwa uadilifu na uaminifu, na kutekeleza

maadili yetu kwa kuongoza kwa heshima .

Ninajivunia kutambua adhimisho la 25 la Kanuni ya Maadili Mema ya Kampuni yetu. Tangu uzinduzi wake mnamo mwaka wa 1987, Kanuni yetu imetuongoza na seti ya kanuni ambazo zinaangazia maadili ya Colgate na viwango vilivyowekwa vinavyosimamia tabia yetu ya kimaadili. Ili kuafikiana na mabadiliko ulimwenguni na katika masoko yetu, Kanuni ya Maadili Mema huhakikiwa mara kwa mara, kusasishwa na kutolewa upya ili kuhakikisha usahihi na uelewekaji wake. Matukio katika ulimwengu wa biashara yamekuwa na changamoto zaidi au changamani na yanasisitiza umuhimu mkuu wa kutekeleza biashara katika njia ya kimaadili, inayoafikiana na sheria na inayowajibika kijamii. Kama kampuni kuu kwa kweli inayofanya kazi katika nchi nyingi ulimwenguni, sisi wote lazima tuhakikishe kwamba tabia na maamuzi yetu yanaafiki mawazo na maadili yetu kama ilivyosemwa katika Kanuni yetu ya Maadili Mema.

Kila mmoja wetu hufanya maamuzi kila siku ambayo yanaweza kuwa na matokeo ya kifedha, wanadamu, jamii au Kimaadili. Kama mjumbe wa familia ya Colgate, ni muhimu usome, ufahamu na ufuate kabisa Kanuni yetu ya Maadili Mema. Kanuni inasisitiza wajibu wa kibinafsi ambao kila mmoja wetu lazima atende kwa uadilifu na adumishe viwango vya juu zaidi vya kimaadili.

Lakini kujua kuhusu Kanuni zetu za Maadili Mema hakutoshi. Kama watu wa Colgate, tunakuza tabia ya kimaadili kupitia vitendo vyetu na maneno yetu. Tunawajibika kwa vitendo na maamuzi yetu, na tunaongea ili kupinga tabia ambayo inazozana na Kanuni yetu ya Maadili Mema, na hata pia sera zingine za Colgate.

Sifa ya Colgate imekabidhiwa kwa kila mmoja wetu. Nawashukuru mapema jinsi mnavyoendelea kujitolea kushiriki katika maadilli yetu pamoja na uongozi wenu wa maadili ambao ni muhimu katika kuendeleza mafanikio ya biashara yetu.

Ian CookMwenyekiti, Rais na CEO

UJUMBE KUTOKA KWA MWENyEKITI WETU, RAIS NA CEO

K

Page 4: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

2 Kanuni ya Maadili MEMa

KUIShI KULINgANA NA MAADILI yETUKwa kuishi kulingana na maadili yetu ya Colgate ya Kujali, Kazi ya pamoja Duniani na Uboreshaji unaoendelea, tunaunda utamaduni ambao watu wanafanya kazi kama timu, wakifanya kazi pamoja kuwadia lengo moja. Thamani tatu kuu za Colgate ni sehemu ya kila kitu tunachokifanya.

KUJALI Kampuni inawajali watu: Watu wa Colgate, wateja, wenye hisa, watumiaji, watoa huduma na wenzi wa biashara. Colgate imejitolea kutenda kwa huruma, uadilifu, uaminifu na maadili ya juu katika hali zote, kuwasikiliza wengine na kuthamini utofauti. Kampuni imejitolea pia kulinda mazingira duniani, kuboresha jamii ambazo watu wa Colgate wanaishi na kufanya kazi, na kuafikiana na sheria na masharti yote ya serikali.

KA zI yA pAMOJA DUNIANIWatu wote wa Colgate ni sehemu ya timu ya dunia, waliojitolea kufanya kazi pamoja nchini kote na ulimwenguni kote. Kampuni inaweza kufikia na kudumisha ukuaji wa faida kwa kushiriki tu kimawazo, teknolojia na talanta.

UBOREShA JI UNAOENDELEAWatu wa Colgate wamejitolea kujiboresha kila siku katika kila kitu wanachokifanya, kibinafsi na kama timu. Kwa kuelewa vyema mahitaji ya watumiaji na wateja na kuendelea kufanya kazi ili kuvumbua na kuboresha bidhaa, huduma na michakato, Colgate "itakuwa bora."

Kakika soko la leo lenye ongezeko la ushindani, maadili ya Colgate ndio msingi wa ufanisi wa watu binafsi, timu na kampuni. Ni kwa kuwaheshimu watu wengine tu na kuishi kulingana na maadili ya Colgate ndio tunatumaini kufikia matokeo bora ya biashara.

KUIShI KULINgANA NA MAADILI yETU

Page 5: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

KaMpuni ya COlgatE-palMOlivE 3

KUONgOz A KWA hEShIMA"Kuongoza kwa Heshima" ndiyo njia watu wa Colgate hutumia ili kuendeleza maadili ya Kampuni.

Kwa Kuongoza kwa Heshima, tunaunda mazingira ambapo watu wanahisi huru kutoa mapendekezo, kuchangia mawazo na kufanya michango kwenye shirika.

Kuongoza kwa Heshima huunda mazingira ambapo watu wanajali kuhusu wengine na wanafanya kazi pamoja ili kufikia uwezo wao kamili.

Kanuni za Kuongoza kwa Heshima ni:

Wasiliana Elezea mawazo waziwazi na kwa urahisi; wasikilize wengine; unda mazingira ambapo watu wako sawa kusema mawazo yao; kuza mtiririko wa maelezo kwa wakati unaofaa na unaoendelea kutoka na kuelekea kwa wengine.

Toa na Tafuta Maoni Wainue watu wote wa Colgate kwa kutoa na kutafuta maoni mema na maalum; toa mwelekeo na wasaidie watu kuzingatia kubaki imara; himiza mabadiliko mema na kuza kazi ya kipekee.

Thamini Michango ya Kipekee Thamini na utambue michango na kazi nzuri ya wengine; heshimu ubinafsi wa kila mtu; wahusishe wengine wakati wa kufanya maamuzi na kuimarisha vipaumbele. Kuwathamini watu kwa utofauti wao ndio ufunguo wa kujenga na kudumisha ufanisi katika biashara sasa na katika mustakabali.

Kuza Kazi ya pamojaJenga ahadi za malengo ya pamoja; tatua migogoro kwa njia nzuri.

Weka Mfano Kuwa mfano mzuri wa kutekeleza biashara kwa njia ya kimaadili, usimamizi bora, na kwa kuunda mazingira ya kikazi yanayopendeza na yaliyo na usawa.

KUONgOz A KWA hEShIMA

Page 6: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

KANUNI YA MAADILI MEMA YA COLGATE-PALMOLIVE

FAhARASA

Kuhusu Kanuni ya maadili Mema . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 5

Uhusiano wetu sisi kwa sisi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 6

Uhusiano wetu na Kampuni . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 8

Uhusiano wetu na Bodi ya Wakurugenzi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 14

Uhusiano wetu na wanabiashara wa nje . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 15

Uhusiano wetu na watumizi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 17

Uhusiano wetu na Serikali na Sheria . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 19

Uhusiano wetu na Jamii . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 23

Uhusiano wetu na Manzingira . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 25

Uhusiano wetu na Wanahisa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 26

Jukumu la Makubaliano . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 27

Tafuta Mwongozo na Uripoti hoja . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 28

Kielekezo cha Suala Kuu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 30

Maswali yanayoulizwa Mara kwa Mara . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 31

Page 7: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

KaMpuni ya COlgatE-palMOlivE 5

KUhUSU KANUNI yA MAADILI MEMA

Kanuni ya Maadili Mema ya Colgate inatumika kama mwongozo wa kila siku kwa mawasiliano ya biashara, ikiangaza kiwango chetu cha kanuni za tabia nzuri na maadili yetu ya kampuni. Kanuni inaonyesha wazi kila mmoja wetu kwamba njia ambayo tunatumia kufikia matokeo ya biashara yetu ni muhimu kama kufikia matokeo yenyewe. Kanuni ya Maadili Mema ya Colgate inatumika kwa watu wote wa Colgate, hii ni pamoja na Wakurugenzi, Maafisa, na wafanyikazi wote wa Kampuni na tanzu zake ulimwenguni. Wachuuzi na Wagawaji pia wako chini ya mahitaji haya kama matakwa ya Kanuni, na ni sharti ya kufanya biashara na Colgate.

Muhimu kabisa, kila mfanyakazi analo jukumu la kuonyesha utimilifu na uongozi kwa kukubaliana na masharti ya Kanuni ya Maadili Mema, Maongozo na Tabia za Biashara Ulimwenguni, Sera za kampuni na sheria zote zinazoweza kutumika. Kwa kujumuisha kabisa uadilifu na utimilifu kwa uhusiano wa biashara yetu inayoendelea na kufanya uamuzi, tunaonyesha kujitolea kwa utamaduni ambao unakuza kiwango cha uadilifu wa hali ya juu kabisa.

Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa uamuzi wetu na kwa utekelezaji wetu wa Kanuni. Kama huna uhakika, kabla hujaendelea na hatua yoyote maalum, jiulize yafuatayo:

• Ninaruhusiwa kufanya hivi?

• Je, ninaweka mfano?

• Ni sawa kuchukua hatua hii?

• Je, hatua hiyo ni ya kisheria na inalingana na Maadili ya Colgate, kanuni za Kuongoza kwa Heshima, Kanuni ya Maadili Mema, na Mwongozo wa Desturi za Biashara ya Kampuni na sera zingine?

• Nitajivunia kuripoti hatua hii kwa mtu ninayemuheshimu?

• Hatua hii itaendeleza sifa ya Colgate kama Kampuni yenye uadilifu?

• Je, ninaonyesha viwango vya juu vya uadilifu?

Ikiwa jibu lako kwa swali lolote ni HAPANA ama ikiwa una maswali yoyote ama hoja kuhusu kufafanua ama kutumia Kanuni ya Maadili au kiwango chochote kinachohusiana na Colgate, sera ama utaratibu, jadiliana hali hiyo na meneja wako, Waajiri Wafanyikazi, Shirika Kuu la Kisheria au Uadilifu wa Ulimwengu na Makubaliano.

Hakuna hatua mbaya itakayochukuliwa dhidi ya mtu yeyote kwa sababu ya kulalamika, kuripoti, kuhusika au kusaidia katika uchunguzi wa ukiukaji ulioshukiwa wa Kanuni ya Maadili Mema, isipokuwa kama madai yaliotolewa au habari iliotolewa itapatikana kuwa ya uongo kimakusudi. Kwa umbali unaowezekana, Colgate itadumisha usiri wa wahusika wote.

Kanuni inapatikana mtandaoni na imetafsiriwa kwa lugha kadhaa tofauti za nchini. Colgate inahitaji kwamba watu wote wa Colgate wasome, waelewe na wafuate Kanuni. Hata hivyo, utekelezaji haufanyiki tu. Unahitaji kujitolea kwa kila mmoja wetu. Ili kusisitiza dhamira hii, mafunzo na cheti cha Kanuni yanatolewa kwa watu wa Colgate duniani kote kila mwaka.

Page 8: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

6 Kanuni ya Maadili MEMa

Uhusiano wetu sisi wenyewe unahitaji msingi wake uwe juu ya kuaminiana na kijitolea. Tunawajibika kuwatendea wenzetu kwa heshima na hadhi.

TunajiTahidi kuwa na mahusiano mazuri.

Katika Colgate, tunajivunia kujitolea kwa nguvu kwa watu wetu na mafanikio bora sana yanoyotokana na kujitolea huko. Lakini kiwango hiki cha mafanikio kinaweza tu kufikiwa katika hali ya kuaminiana, mawasiliano ya uwazi na ukweli, na heshima. Mawasiliano yako yote na wenzako, wasaidizi wako, na wasimamizi wako yanafaa kuchukuliwa kama ushirikiano, ambapo tabia ya kila mtu inaongozwa na kujitolea kupita kiasi ili kudumisha viwango vya maadili ya hali ya juu.

Uhusiano wako na wale unaofanya nao kazi unafaa kuwa kama wa timu inayoshinda. Watu wanaofanya kazi kwa pamoja na kwa kuzingatia seti ya madhumuni ya pamoja ndio nguvu ya msukumo wa biashara yetu. Ili uhusiano wa timu hii ya nguvu kufaulu, kila mtu lazima atimize jukumu lake na awe na uhakika kwamba wenzake watafanya vilevile. Hii kumaanisha kutoa msaada unaohitajika kwa wengine, katika kila kiwango, ili kazi ifanyike. Hakuna mtu yeyote ama kitengo cha biashara ambacho kitaweka malengo yake mbele ya yale ya Kampuni.

Uhusiano wako na wale unaofanya kazi nao ama unao wasimamia unafaa kukuza uadilifu na makubaliano kwa kutoa mfano wa heshima, haki na utimilifu. Kama kiongozi, una jukumu la kuelezea kwa uwazi viwango vya utendaji kazi na kuunda mazingira yanayokuza kazi ya timu na maadili ya tabia.

Tunakuza mawasiliano ya uwazi na ukweli.

Himiza fikira za ubunifu na utungaji na ikiwa wewe ni msimamizi, watendee wasaidizi wadogo kama watu binafsi, ukiwapa uhuru unaohitajika wa kufanya kazi zao. Toa maoni ya kuendelea kuboresha utendaji kazi.

Uhusiano wako na msimamizi wako unafaa uwe wa heshima na uaminifu. Wewe na msimamizi wako ni timu moja iliyo na lengo la kufikia malengo yaliowekewa kwa kitengo chako na Kampuni. Unajukumu sawa na msimamizi wako kuhakikisha kwamba mawasiliano kati yenu ni ya uwazi na ukweli. Chukua hatua mara nyingi kama iwezekanavyo. Kuwa mbunifu katika kutatua shida. Ushirikiano na ubunifu wako ni muhimu kufikia malengo ya kitengo chako na Kampuni.

TunaThamini waTu wa ColgaTe kama mTaji weTu mkubwa.

Kujitolea kwa Colgate kutunza watu kunajitokeza wazi katika mahali pa kazi kupitia kwa mipango mingi iliyoundwa kukuza na kutuza mafanikio ya watu binafsi na ya timu. Unahimizwa kujiendeleza zaidi uwezavyo na utoe usaidizi wa maana kwenye mafanikio ya Kampuni. Mwishowe, ni bidii ya watu walio na vipawa na ujuzi ulimwenguni kote wanaowezesha mafanikio ya biashara yetu. Haswa, katika maswala ya ajira:

• Ni sera, desturi na hamu ya Colgate kutoa nafasi za ajira kwa watu wote wanaohitimu kwa msingi wa usawa. Kampuni haitabagua dhidi ya mwajiri yeyote au mwombaji wa ajira kwa sababu ya umbari, rangi, dini, jinsia, utambulisho wa jinsia, asili ya kitaifa, jamii, umri, mwelekeo wa jinsia,

UhUSIANO WETUNA KILA MMOJA

Page 9: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

KaMpuni ya COlgatE-palMOlivE 7

ulemavu, hadhi ya ndoa, hali ya uzee au sifa yoyote ile inayolindwa na sheria yeyote katika hali na masharti ya ajira. Hii inajumuisha, lakini haijazuiliwa kwa, kuajiri, kuandikwa kazi, kupandishwa cheo, kuhamishwa, fidia, mafunzo, kushushwa cheo au kupigwa kalamu.

• Hatuwatumii watoto wadogo kufanya kazi. Kuwafanyisha watoto wadogo kazi hufafanuliwa kama kuajiri mtu yeyoye mwenye umri mdogo kuliko umri uliopitishwa na sheria katika mamlaka ya sheria husika. Hata hivyo, hakuna wakati wowote tutakapoajiri tukijua mtu yeyote mwenye umri chini ya miaka kumi na sita (16).

• Tunadumisha mazingira ya kujumuisha ya kufanya kazi na kufikia ubora kwa kuvutia na kuhifadhi watu kutoka misingi yote ya jamii katika mahali petu pa kazi.

• Tunatoa mafunzo, masomo na kutoa nafasi za kupata vyeo zitakazoruhusu ukuzaji na kuendeleza kikazi kwa watu wote wa Colgate.

• Tunatekeleza tathmini za utendaji kazi zinazotoa maoni wazi na ya usahihi. Utaratibu huu unahimiza mazungumzo na mawasiliano ya njia-mbili na usimamizi wa kiwango cha juu kupitia tathmini za utendaji kazi.

• Tunalipa utendaji wa kazi na kugundua na kutunuku mchango unaofanywa na watu binafsi na timu ambazo zinazidi kazi zao za kawaida kupitia mipango kama ya Mpango wa Tuzo wa Mwachanachama Unaweza Kuleta Mabadiliko.

• Tunapiga marufuku unyanyasaji wa kingono au wowote ule wa watu wa Colgate na mtu yeyote katika mahali pa kazi ama unapofanya biashara yoyote ya Kampuni.

• Tunajitahidi kuepuka mapendeleo ama kuonekena kwa mapendeleo katika mahali pa kazi kulingana na sera na utaratibu iliyochukuliwa na Kampuni.

• Tunajitahidi kuondoa hatari zinazowezekana kutoka mahali pa kazi na kufuata sheria za usalama na afya na viwango vyote husika vya kazini.

• Tunasaidia kuhifadhi mazingira salama, yenye afya na uzalishaji, kwa watu wote wa Colgate na wengine wote, kwa:

– kuzuia umiliki, matumizi, uuzaji au uhamishaji wa dawa zisizo halali ama vifaa vya madawa kwa kutumia mali au wakati wa Kampuni;

– kuzuia kufanya biashara ya Kampuni ukiwa umelewa;

– kuzuia umiliki au utumizi wa silaha au risasi katika majengo ya Kampuni au unapofanya biashara ya Kampuni kulingana na sheria ya hapa. Umiliki wa silaha unaweza kuruhusiwa kwa wafanyakazi wanaolinda usalama wakati umiliki huu umethibitishwa kuwa muhimu ili kuimarisha usalama wa wafanyakazi wa Kampuni;

– kuzuia vitendo vyovyote ambavyo vinaweza kuchukuliwa kama vya uhasama, kutishia, kushusha hadhi au vitisho, na

– kuhitaji kwamba usaidizi wowote wa mihadarati au utumizi mbaya wa pombe, mzozo au kumiliki silaha kinyume cha sheria kuripotiwa kwa wasimamizi mara moja.

Mmoja wa wafanyikazi wenzangu alituma kichekesho kisichofaa kwangu na kwa wafanyikazi wengine. Niliona inakera, lakini sijui kama ninapaswa kuwasiliana na mfanyakazi mwenzangu na hoja yangu.

Katika Colgate-Palmolive, tumejitolea kudumisha mazingira ya kazi ya kitaalamu ambapo watu wote wa Colgate wanashughulikiwa kwa heshima na uadilifu. Kwa hivyo, tabia ya kukera au isiyofaa haikubaliwi. Kama unahisi wasiwasi kuongea na mfanyakazi mwenzako moja kwa moja, tafadhali wasiliana na Meneja wako, Waajiri Wafanyakazi au Maadili na Makubaliano Duniani kwa msaada.

S:J:

Page 10: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

8 Kanuni ya Maadili MEMa

Kama watu wa Colgate, tunajitahidi kuambatana na sera za Colgate huku tukiweka jitihada kuendeleza utendaji wa kampuni. Tunatambua imani na uaminifu tuliokabithiwa na tunatekeleza kwa unyofu na wima katika hali zote ili kuhifadhi imani na uaminifu huo. Tunajiepusha na migogoro yeyote potovu na haribifu kwa kampuni.

Tunaepuka mgongano wa maslahi.

Uamuzi wako ndio moja kati ya mali ya thamani yako kubwa. Unapaswa kuepuka shughuli yoyote, mapendeleo au uhusiano ambao unazozana au unaonekana kutishia uwezo wako wa uamuzi huru katika maslahi bora ya Kampuni. Migongano inaweza kutoka katika hali nyingi. Haiwezikani kuzitaja zote hapa, na daima haitakuwa rahisi kutofautisha kati ya shughuli nzuri na isiyo nzuri. Ukiwa na wasiwasi, wasiliana na meneja wako, Waajiri Wafanyi kazi au Shirika la Kisheria Duniani kabla ya kuchukua hatua yoyote. Mwongozo unaofuata hutumika kwa hali nyingi za kawaida za mgongano:

Uwekezaji

Usifanye uwekezaji wowote unaoweza kuathiri uamuzi wako wa kibiashara. Sera za Kampuni zinakataza watu wa Colgate kumiliki hisa ama kuwa na hamu ya kumiliki katika Kampuni inayoshindana na ama inayofanya biashara na Colgate. Kizuizi hiki hakitumiki kwa kumiliki viwango vidogo (kwa ujumla chini ya 1%) vya hisa za Kampuni inayouza hisa kwa umma ila tu uwekezaji huo usiwe wa kiwango kinachoweza kuunda dalili ya mzozo wa upendeleo. Ikiwa ulifanya uwekezaji usiokubaliwa kabla ya kuungana na Colgate, toa ripoti ya ukweli kwa Shirika la Kisheria Duniani.

Familia

Mjulishe Meneja wako na uchukue idhini kutoka kwa Kitengo chako ama Mkubwa na Shirika la Kisheria Duniani kabla ya kufanya biashara kwa niaba ya Colgate na Kampuni yoyote ambayo wewe ni memba wa familia wa karibu ama una hamu kama hiyo ambapo unaweza kufaidika kutokana na matendo yako ama matendo yao.

Kazi Zingine

Usimfanyie kazi mshindani ukiwa bado unafanyia Colgate kazi ama kumfanyia kazi, ama kutoa huduma yoyote kwa, mtu yeyote wa tatu ambaye anaweza kuathiri utendaji kazi ama uamuzi juu ya kazi. Usitumie wakati wa Kampuni, ama vifaaa na bidhaa kwa kazi ya nje ambayo haina uhusiano na kazi yako hapa Colgate bila ruhusa kutoka kwenye kitengo chako au Mtendaji mkubwa.

Binafsi

Ingawa tunagundua na kuheshimu haki za watu wa Colgate kushirikiana kwa uhuru na watu wanaopatana nao katika mazingira ya kikazi, lazima tufanye uamuzi mzuri ili kuhakikisha uhusiano huo hauaathiri vibaya utendaji wa kazi, uwezo wa kusimamia wengine katika mazingira ya kazi.

UhUSIANO WETUNA K AMpUNI

Page 11: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

KaMpuni ya COlgatE-palMOlivE 9

Tabia ya mahali popote pa kazi inayotokana na uhusiano wa kimapenzi ama urafiki kati ya wafanyikazi unaweza kuwa mbaya kama tabia hiyo inaleta hali isiyo sawa katika mazingira ya kufanya kazi. Mapendeleo ama kufanya uamuzi wa biashara kwa msingi wa hisia, kiapo cha utii, ama urafiki badala ya maslahi ya Kampuni hayakubaliwi. Watu wanaojipata katika uhusiano wa kibinafsi ama urafiki wanafaa kutumia uamuzi mwema na hisia.

Kuwa na ufahamu wa ukweli kwamba memba mwingine wa nyumba yako anaweza kuajiriwa kwa kiwango ambacho kinaweza kuunda ama kuonekana kama kuunda mzozo wa mapendeleo. Ikiwa hali hii itatokea, muone meneja wako ama mshauri wa sheria wa kitengo chako kwa mwongozo.

Bodi

Pata idhini kutoka kwa Rais ama Afisa Mkuu Mtendaji, na Washauri wa Jumla kabla ya kukubali kutumikia Bodi ya Wakurugenzi ama Bodi kama hiyo kwa biashara ya nje ama chombo cha serikali. Kutumikia Bodi la shirika la wataalamu au lisilo la faida linalohusiana na kazi, lazima kuidhinishwe mapema na Kitengo chako au Mtendaji mkubwa.

Nadhari Zingine

Tunajitahidi kudumisha mazingira mema ya kazi ambayo yanaangazia maadili ya Kampuni yetu na kukuza mahusiano dhabiti ya kufanya kazi. Ijapokuwa migongano ya maslahi mara kwa mara hutokea kutokana na kushughulika na wahusika wa nje, migongano au mwonekano wa mgongano huenda pia ukasababishwa na maingiliano ya kindani. Wale wetu wanaowadhibiti wengine lazima wawe waangalifu sana ili kuhakikisha kwamba hali hazijatokea ambazo zinaweza kuoneka kwa wengine kama mapendeleo au mgongano wa maslahi unaowezekana.

Kama utajikuta katika hali halisi au inayowezekana ya mgongano wa maslahi, mara moja lazima uripoti kwa meneja wako ili hali hiyo iweze kuhakikiwa na kutathmini vizuri. Kampuni itashirikiana na wewe ili kushughulikia hali na kutambua suluhu inayofaa.

Tunalinda siri za mauzo ya kampuni na maelezo ya kisiri.

Siri za kuuza za Colgate, habari za wamiliki wengine na data ya ndani ni mali ya thamana sana. Ulinzi wa mali hii, pamoja na kutunza siri, kunachukua jukumu muhimu katika kukua kwetu na uwezo wa kukamilisha. Siri ya kuuza ni habari inayotumika pamoja na biashara ya Colgate ambayo haijulikani kwa ujumla ama kujulikana kwa urahisi, na ambayo hatua zimechukuliwa ili kutunza usiri Hata hivyo, habari za wamiliki wengine, lazima zilindwe pia.

Siri za kuuza za Colgate na habari za wamiliki wengine zinaweza kuwa na fomula yoyote, muundo, kifaa ama habari inayotumika katika biashara yetu na inayoipa Colgate fursa ya kupata faida zaidi ya washindani wake. Siri za kuuza za Colgate na habari zingine za wamiliki sio za hali ya kiufundi kila wakati. Zinaweza pia kujumuisha uchunguzi wa biashara, mipango ya bidhaa mpya, mipangilio ya hila, habari za fedha ama bei ambazo hazijachapishwa, orodha ya wafanyikazi, wateja na wauzaji, na habari kuhusu mahitaji ya mteja, mapendeleo, tabia za biashara na mipango. Hata bila kukamilika orodha hii inadokeza sehemu kubwa ya

Hivi karibuni nilipokea idhini ya meneja wangu ya kuchukua kazi ya pili ya kuuza mali isiyohamishika ili kuongezea mapato yangu. Je, ninaweza kutumia simu yangu ya kazini kuwasiliana na wateja wangu au kutumia mashine ya kunakili ili kutoa nakala za maelezo ya orodha za mali wakati wa saa za kufanya kazi?

Hapana. Matumizi yako uliyoyakusudia ya mali ya Kampuni ni ya faida yako ya kibinafsi tu, hayahusiani na kanuni ya biashara ya Kampuni, na yanaweza kuchukuliwa kuwa yanaingiliana na uwezo wako wa kufanya majukumu yako yanayohusiana na kazi. Ijapokuwa matumizi wastani ya kibinafsi yanaruhusiwa, yanapaswa kuzuiliwa na yasiingiliane na utendaji kazi wa majukumu yako ya kikazi.

S:

J:

Page 12: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

10 Kanuni ya Maadili MEMa

habari inayotakikana kulindwa. Habari ya siri za kuuza na wamiliki wengine sio lazima ifae kupata hati ya kumiiliki, lakini haiwezi kujulikana kwa jumla na umma.

Wajibu wako kuhusu siri za kuuza za Colgate na maelezo mengine ya faragha ni:

• Kutofichua maelezo haya kwa watu wengine wa Colgate au wahusika wengine isipokuwa kwa misingi wa "kutaka kujua" au "kutaka kutumia" na, katika hali hizo, na uteuzi wa siri na mbinu zingine za kulinda data kama vile ulinzi wa nywila au usimbaji fiche, kama inavyofaa; na sio kufichua maelezo haya.

• Kutohusika na wahusika wengine kushughulikia maelezo haya bila hakiki inayofaa ya usalama na vidhibiti vya teknolojia vya maelezo vya wahusika wengine.

• Kutochapisha au kujadili maelezo haya kwenye tovuti zinazopatikana kwa umma au tovuti za midia ya jamii.

• Kutotumia habari hii kwa faida yako au kwa faida isiyoidhinishwa ya watu nje ya Colgate.

• Kuchukua hatua zingine zote zinazofaa ili kulinda siri za uuzaji za Colgate na maelezo ya siri kulingana na Mwongozo wa Desturi za Biashara za Kampuni.

Ikiwa utawacha kazi Colgate, wajibu wako wa kulinda siri za kuuza za Colgate na maelezo mengine ya siri utaendelea hadi habari hiyo itajulikana na umma au Colgate haiichukulii tena kuwa siri ya kuuza au ya wamilki. Unapaswa pia kukumbuka kwamba mawasiliano, masuala yaliyochapishwa, habari za elektroniki, nakala ama rekodi aina yoyote, utaratibu maalumu wa ufahamu, njia maalum za Colgate kufanya mambo, – ikiwa ya kisiri au la – yote ni mali ya Kampuni na lazima yabakie Colgate. Kwa kweli, ujuzi wa kibinafsi uliopatikana ama kuboreshwa kazini ndio tu mali ya kibinafsi ya yule aneyeondoka. Ikiwa una swali kama habari fulani ni ya umiliki ama ya siri ya kuuza, wasilliana na na Shirika la Kisheria la Duniani.

Tunalinda daTa ya kibinafsi.

Tunaheshimu haki za siri za kibinafsi za wafanyikazi wetu, watumiaji, wateja, watoa huduma na watu wengine ambao Colgate ina uhusiano wa kibiashara. Ni sera ya Colgate kukusanya, kuchakata, kutumia na kubakia na maelezo ya kibinafsi kutoka kwa wafanyikazi, watumiaji, wateja, watoa huduma na watu wengine kama inavyofaa tu na kulingana na sheria za nchi ambazo tunafanya biashara, ikiwa ni pamoja na sheria zinazohusiana na ukusanyaji na matumizi ya maelezo ya kibinafsi ya watoto wadogo, na kuchukua hatua zote zinazofaa za kulinda maelezo hayo.

Kama sehemu ya ajira yao na ya Colgate, huenda wafanyikazi wakatoa maelezo mengine ya kibinafsi kwa Kampuni, kama vile anwani za nyumbani na barua pepe, maelezo ya familia kwa malengo ya faida, na maelezo mengine ya kibinafsi. Tunatumia maelezo hayo kwa sababu zilizotolewa kwetu tu, isipokuwa mfanyakazi akubalie matumizi mengine, na kama inavyofaa kwa malengo ya biashara na kulingana na sheria za nchini.

Vivyo hivyo, watumiaji wanapohusiana na Colgate, kupitia maombi ya maelezo ya bidhaa au kuhusika katika mashindano ya Kampuni, kwa mfano, huenda wakatoa maelezo ya kibinafsi, kama vile majina, anwani za mtaa na anwani za barua pepe, kwa Kampuni. Tunatumia maelezo hayo kwa sababu zilizotolewa kwetu tu, isipokuwa mtumiaji aruhusu matumizi mengine, na kama inavyofaa kwa malengo yetu ya kuhifadhi rekodi. Ni sera yetu kutoshiriki maelezo ya kibinafsi ya mtumiaji na wahusika wengine, isipokuwa yakihitajika ili kutoa huduma kwa wateja wetu na kulingana na sheria na masharti husika.

Wakati wa mahusiano ya biashara na Colgate, wateja, watoa huduma na watu wengine wanaweza kutoa maelezo ya kibinafsi, kama vile majina, namba za simu, namba za faksi, anwani za mtaa, anwani za barua pepe, kwa Kampuni. Tunatumia maelezo kama hayo kwa sababuzilizotolewa kwetu tu na kama inavyofaa kwa malengo ya kuhifadhi rekodi. Ni sera yetu kutoshiriki maelezo ya kibinafsi ya wateja, watoa huduma na

Page 13: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

KaMpuni ya COlgatE-palMOlivE 11

watu wengine na wahusika wengine, isipokuwa itakapohitajikai katika muktadha wa uhusiano wa biashara na kulingana na sheria na masharti husika.

Sheria zinazohusiana na siri ya mtumiaji zinakuzwa na kurekebishwa mara kwa mara. Tumejitolea kufuatilia sheria za siri na viwango vinavyobadilika na tunaweza, mara kwa mara, kukuza sera maalum husika. Kwa maelezo zaidi kuhusu ulinziwa data ya kibinafsi, tafadhali wasiliana na Shirika la Kisheria la Duniani.

TunafuaTa sera za wanahabari na vyombo vya habari.

Maombi ya habari za fedha ama biashara kuhusu Colgate kutoka kwa vyombo vya habari, wanahabari, jamii ya fedha ama umma yanapaswa yaelekezwe kwa Makamu wa Rais, Mawasiliano ya Shirika au Makamu wa Rais, ama Uhusiano wa Wakekezaji. Maombi ya habari ama mawasiliano kutoka kwa tume ya Usalama na Ubadilishanaji, Soko la Hisa la New York ama warekebishaji wengine na wasimamizi wa ulimwenguni kote lazima yaelekezwe kwa Wanasheria. Ni muhimu kwamba mfanyakazi yeyote asijibu swali lolote kama hilo ama kuwasiliana wenyeye kwa wenyewe kwasababu majibu yoyote ya kuputosha, ama yasiofaa ama habari ya kukanusha, inaweza kusababisha kuenea kwa utangazaji usiofaa na unaweza kudhuru msimamo halali wa Kampuni.

Sera hii haitumiki kuuliza hadharani habari ya fedha, kama ya Kila Mwaka na Ripoti za Robo Mwaka, ama shuguli za ukuzaji wa Kampuni hadharani.

Maombi ya mahojiano na mtu yeyote wa Colgate yanayohusiana na Kampuni au shughuli zake au/na kutolewa kwa habari yeyote kwa wanahabari lazima yaangaliwe na kupitishwa na Makamu wa Rais, Mawasiliano ya Shirika au Makamu wa Rais ama Mahusiano wa Wawekezaji. Mahojiano yanayoanzishwa na Kampuni pia lazima yaidhinishwe kabla ya kupanga kukutana na vyombo vya wanahabari.

Kwa habari zaidi kuhusu maongozi ya Kampuni ya kutunza habari za siri, tafadhali rejea kwa “Maongozo ya Ununuzi na Uzaaji wa Amana wa Colgate-Palmolive na Kuhifadhi Habari za Siri” na “Maongozi ya Colgate-Palmolive ya Kutunza Habari za Wamiliki Wengine na Kuheshimu Habari za Wamiliki Wengine,” zinazopatikana katika Maongozi ya Biashara ya Kampuni.

Tunadumisha ripoTi na rekodi za kuTegemewa.

Hali halisi ya kifedha ya Kampuni yetu na matokeo ya shughuli zake lazima zinakiliwe kulingana na mahitaji ya sheria na kwa ujumla ikubaliwe na kanuni za jumla za kuhesabu (GAAP). Sera ya Kampuni na sheria pia, inahitaji Colgate kutunza vitabu, nakala na akaunti zinazoangazia kwa usahihi na usawa hali ya mapatano ya biashara na utoaji wa mali ya Kampuni.

Uadilifu wa rekodi za akaunti ya Kampuni na kumbukumbu za uhasibu msingi wake ni usahihi na ukamilifu wa maelezo ya kawaida yanayosaidia maandishi kwenye vitabu vya hesabu vya Kampuni. Kila mtu anayehusika katika kuunda, kuchakata na kurekodi habari kama hizo anawajibika uadilifu wake. Kila uhasibu ama kiingilio cha fedha kinapaswa kuangazia haswa yale yaliyofafanuliwa na maelezo ya usaidizi. Hakufai kabisa kuwa na ufichaji wa habari kutoka (ama kwa) usimamizi, ama kutoka kwa wakaguzi wa hesabu wa ndani ya Kampuni ama wakaguzi wa hesabu wa kibinafsi.

Hakuna malipo kwa niaba ya Kampuni ambayo yataruhusiwa ama kufanywa kwa nia ya uelewano kuwa kila sehemu ya malipo hayo ni ya kutumiwa kwa sababu yoyote ila tu ile iliyoelezewa kwa hati za kuunga mkono malipo. Hakuna maandishi ya uwongo ama ya kupotosha yataruhusiwa kuwekwa katika vitabu ama rekodi za Kampuni kwa sababu yoyote, na hakuna fedha, mali ama akaunti ya Kampuni itathibitishwa, patikana ama kuhifadhiwa kwa sababu zozote zile ila tu kama fedha hizo, mali ama akaunti imeangaziwa

Page 14: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

12 Kanuni ya Maadili MEMa

vyema kwenye vitabu na rekodi za Kampuni. Hakuna fedha za shirika ama mali ztaruhusiwa kutumiwa kwa sababu yoyote isiyo halali ama isiyo sawa. Wasimamizi na wengine wanaosimamia uandalizi wa habari za fedha lazima wahakikishe kwamba sera za shirika la fedha la Colgate zimefuatwa. Mapato na matumizi yanapaswa kutambuliwa vizuri na kwa wakati unaofaa.

Mali na dhima inapaswa kurekodiwa vizuri na kuthaminiwa inavyostahilika. Kwa kuongezea, wale wanawajibika kwa au wanahusika kujaza viingilio na tume ya Ulinzi na Ubadilishanaji na viingilio vinavyotakikana kwa sheria inayotumika ama mawasiliano na jamii ya biashara na fedha wanapaswa kuhakikisha kwamba viingilio hivyo na mawasiliano vinahusisha kufichuliwa kuliokamilika, kulio na haki, kulio na usahihi, kulio wa wakati unaofaa, na kunaoeleweka. Ikiwa utapata kufahamu uwezekano wa kusahaulika, uwongo ama kutokuwa sahihi katika uhasibu ama maandishi ya fedha, kwenye data ya kawaida inayosaidia maandishi kama hayo, ama katika tume ya Usalama na Ubadilishanaji ya Colgate ama hitilafu yoyote katika uthibiti wa kindani, lazima utoe ripoti mara moja kwa meneja wako ama mshauri wa sheria wa kitengo chako. Unaweza pia kuona Idara ya Maadili na Makubaliano ya Ulimwengu kuhusu mambo haya kwa kutumia njia ya kutojulikana na ya kisiri.

Tunalinda mali ya ColgaTe.

Mali ya Kampuni, vifaa ama huduma lazima zitumiwe kwa sababu zinazofaa na zilizoidhinishwa. Wizi wa pesa, mali ama huduma haukubaliwi kabisa. Vifaa vya Colgate, mifumo, kadi za mkopo za shirika na utoaji huduma lazima zitumike kwa nia ya kufanya biashara ya Colgate peke yake kwa sababu zilizoruhusiwa na Usimamizi. Una wajibu wa kibinafsi kulinda mali ya Colgate uliyoachiwa, lakini pia kusaidia kulinda mali ya Colgate kwa ujumla. Unapaswa kuwa macho kwa hali yoyote ama ajali inayoweza kusababisha hasara, utumiaji mbaya ama wizi wa mali ya Kampuni na ni lazima uripoti habari zote kama hizo kwa meneja ama Idara ya Usalama ya Shirika kwa haraka unapofikiwa na habari hizo.

Ni maofisa fulani na wafanyikazi wengine wakubwa ambao wanaruhusiwa kufanya makubaliano yanayoathiri Kampuni. Hautakiwi kufanya ahadi zinazoathiri mali ya Kampuni ila tu kama zimeruhusiwa vizuri. Ikiwa unahitaji kuhakikisha mamlaka yako ama ya mtu yeyote ya kufanya makubaliano na Kampuni, unapaswa kumuona mkurugenzi wa fedha wa kitengo chako ama wa kitengo chako.

TunaTumia rasilimali ya habari za Teknolojia na midia ya jamii kwa kuwajibika.

Lazima tutumie Nyenzo za Teknolojia ya Maelezo na Midia ya Jamii ya Colgate kwa kuwajibika na kwa njia inayolingana na Kanuni na Mwongozo wote mwingine wa Kampuni, ikiwa ni pamoja na Mwongozo wa Desturi za Biashara za Kampuni na/au Mwongozo juu ya Kutumia Nyenzo za Teknolojia ya Maelezo na Midia ya Jamii.

Nyenzo za Teknolojia ya Maelezo ya Colgate hujumuisha vifaa, programu na huduma zote za sasa na za mustakabali ambazo hukusanya, huhifadhi, na huwasilisha na kuchakata data ambayo inamilikiwa,

Je, nifanye nini nikiulizwa kuchelewesha kupata gharama zingine hadi kipindi kingine? Kwa mfano, kama tu atanifafanulia kwamba "maadamu zirekodiwe mwaka huu wa mapato, hatufanyi kitu chochote kibaya," hiyo ni kweli?

Hapana. Kuchelewesha kwa kujua gharama kutakuwa desturi ya kupotosha, isiyokubaliwa na ni ya kinyume cha sheria. Kila shughuli ya kibiashara na kifedha, hata kama ndogo, lazima iripotiwe kwa usahihi na uaminifu. Udanganyifu wowote wa waraka au rekodi ya Kampuni ni kosa baya na linaweza kusababisha ukomeshaji wa ajira.

S:

J:

Page 15: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

KaMpuni ya COlgatE-palMOlivE 13

inapangishwa au kutolewa na Colgate.

Kwa kuongezea, Nyenzo za Teknolojia ya Maelezo ya Colgate hujumuisha maunzi, programu au huduma ya mwajiri au muhusika mwingine kwa umbali ambapo zinatumiwa ili kufikia au kuingiliana na Nyenzo za Teknolojia ya Maelezo ya Colgalte.

Nyenzo za Teknolojia ya Maelezo ya Colgate, na hata pia Midia ya Jamii, inapaswa kutumiwa kwa njia ya heshima na ya kitaalamu kwa malengo ya biashara ya Colgate isipokuwa kwa malengo yaliyozuiwa na yanayofaa ya kibinafsi. Kwa kuongezea, matumizi yafuatayo yamekatazwa:

• Unyanyasaji, ubaguzi, ujumbe ambao ni wa matusi, utapeli, ama ujumbe wa kutisha, pamoja na zile zinazotumika na kukera umbari, dini, asili ya kitaifa, jamii, rangi, ngono, kitambulisho cha jinsia, umri, uraia, hali ya uzee, hali ya ndoa, ulemavu au tabia nyengine yoyote iliyolindwa na Sheria.

• Usambazaji usioidhinishwa wa faragha au maelezo ya siri ya uuzaji ya Colgate au majadiliano yasiyoidhinishwa ya biashara ya Kampuni au michakato ya kindani kwenye tovuti yoyote ya nje.

• Kusababisha ama kukubali ukiukaji wa usalama ama kuvurugwa kwa mtandao wa mawasiliano ama/na kufichua vibaya nywila yako kwa wengine ili kuwakubalia kutumia nywila yako.

• Matumizi yoyote mengine yaliyokatazwa na Mwongozo wa Desturi za Biashara ya Kampuni au Mwongozo wa Kutumia Nyenzo za Teknolojia ya Maelezo na Midia ya Jamii.

Isipokuwa kama inavyozuiwa na sheria husika, Colgate inahifadhi haki ya kufuatilia, kufikia na kuhakiki Nyenzo zote za Teknolojia ya Maelezo ya Kampuni katika hali zinazofaa kulingana na uamuzi wa Kampuni na kulingana na sheria husika. Haki ya kampuni ya kufuata, kufikia na kuhakiki Nyenzo zote za Teknolojia ya Maelezo ya Kampuni inafikia hadi biashara na hata pia maelezo ya kibinafsi yaliyoundwa, kuhifadhiwa au kupitishwa kwa kutumia Nyenzo za Teknolojia za Maelezo ya Kampuni, na pia hujumuisha tovuti za Midia za Jamii zilizotembelewa kupitia Nyenzo za Teknolojia za Maelezo ya Kampuni. Wafanyikazi wanapaswa wasitarajie faragha kuhusiana na biashara hiyo au maelezo ya kibinafsi.

Colgate ina haki ya kuzuia au kuondoa upatikanaji wa mtumiaji yeyote au matumizi ya Nyenzo ya Teknolojia ya Maelezo ya Colgate wakati wowote, kwa sababu yoyote ile, bila ilani ya mapema, isipokuwa inapokatazwa na sheria.

Mara kwa mara mimi hutembelea tovuti za blogu nikipumzika nyumbani, na wiki iliyopita, niligundua maoni kutoka kwa mfanyakazi wa zamani akifafanua masaibu yake na Kampuni yetu kwa njia mbaya sana. Hii ilinikasirisha sana. Ninaweza kujibu maoni haya?

Huwezi kujibu maoni kwa niabaa ya Kampuni. Hata hivyo, uko huru kujibu kwa msingi wa kibinafsi, bora uwe haukiuki mwongozo wa Kampuni juu ya kutumia Nyenzo za Teknolojia ya Maelezo na Midia ya Jamii na haufichui maelezo ya siri au ya mmiliki wa Kampuni. Unahimizwa sana pia kuleta suala hili kwa meneja wako au Mwajiri Wafanyikazi.

S:

J:

Binti yangu na mimi wakati mwingine tunatumia kompyuta yangu ndogo ya Kampuni ili kufikia Mtandao. Hivi karibuni aliniuliza kama yeye na rafiki yake wanaweza kutumia kompyuta yangu nikiwa nje ya mji wiki hii. Je, ni sawa kuwapa maelezo ya kuingia na nywila?

Hapana. Maelezo ya kuingia na nywila husaidia kuweka Nyenzo zetu za Teknolojia ya Maelezo salama. Haupaswi kufichua maelezo haya kwa mtu yeyote. Pia, haushahuriwi kuweka maelezo ya kuingia au nywila kwenye kompyuta yako au kuziweka katika mfuko wako wa kompyuta. Kwa kuongezea, unaweza kulinda vyema data ya Kampuni dhidi ya watumiaji wasiodhinishwa kwa kubadilisha nywila zako mara kwa mara. Zaidi, wajumbe wa familia hawapaswi kutumia kompyuta yako ndogo ya Kampuni kwa matumizi ya kibinafsi.

S:

J:

Page 16: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

14 Kanuni ya Maadili MEMa

Tumefanikiwa kuwa na kikundi cha watu wa kipekee wanaotoa huduma kwenye Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni, inatoa ushauri, mwongozo, na uongozi ambao ni muhimu sana kwa mafanikio yetu yanayoendelea. Ujuzi wao wa pamoja kwenye biashara, masomo na huduma ya umma, ujuzi wa kimataifa, mafanikio ya kimasomo, maadili ya tabia na anuwai, Bodi letu ya Wakurugenzi inatoa maono thabiti ya biashara ya Kampuni.

Tuna bodi la wakurugenzi ambalo liko huru, lina uzoefu na liko anuwai.

Kujitegemea kunakuza uadilifu na uwajibikaji. Ni sera ya Colgate kuwa na Bodi la Wakurugenzi ambalo kwa asili lina wakurugenzi wanaojisimamia. Wakurugenzi wote wanaohudumia kamati ya Bodi la Wakurugenzi ambalo husimamia ukaguzi, fidia na uongozi na maswala ya kujitegemea. Hakuna ukurugenzi wa kufungiana, na ni sera ya Kampuni kuwa hakuna yeyote wa wakurugenzi wa kujitegemea atakayepokea malipo yoyote ya ushauri, sheria ama malipo yoyote ya kutokuwa – Mkurugenzi kutoka kwa Kampuni.

Tunakuza mawasiliano ya moja kwa moja na uwazi na bodi.

Nje na ndani ya chumba cha mikutano, wakurugenzi wa Colgate wanawasiliana moja kwa moja na mara kwa mara na usimamizi wa Kampuni. Wakurugenzi wakuu mara kwa mara huungana na wakurugenzi wakati wa mikutano kwa wakati wao usio rasmi, na kwa pamoja wanashughulika kikamilifu kwa mazungumzo ya mambo ya biashara. Katikati ya mikutano ya bodi iliyopangwa, wakurugenzi hualikwa pia, na mara kwa mara huonana na meneja wakiwa na maswali na maoni. Matokea ya mazingira ya uwazi na waaminifu yanaangazia utamaduni wa biashara ya Colgate unasaidia bodi kuchukua usukani katika maendeleo na muundo wa muongozo wa biashara ya Kampuni.

TunajiTolea kuwa na uongozi bora zaidi wa kampuni.

Bodi ya Colgate imekuwa kiongozi katika kusaidia kubuni uongozi bora wa Kampuni. Ni moja wapo ya kanuni bunifu ya maadili mema kuongoza shughuli zote za biashara na kukuza mikakataa ya Bodi na kamati zake, Colgate imeweka shughuli bora zaidi za uongozi wa Kampuni katika karne mbili zilizopita, ambazo zinaendelea kuboreshwa na kuandaliwa. Bodi la Colgate iko katikati ya sera hizi na linaamini kwamba uongozi mwema wa biashara unaambatana na unasaidia sana mafanikio yetu ya muda mrefu.

Kwa maelezo zaidi ya majadiliano ya mpango wa uongozi wa Kampuni ya Colgate, tafadhali angalia “Maongozi ya Bodi la Colgate-Palmolive kwa Masuala Muhimu Muhimu Ya Kusimamia Usimamizi,” ambayo yanapatikana kwenye tovuti ya Kampuni.

UhUSIANO WETU NABODI yETU yA WAKURUgENzI

Page 17: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

KaMpuni ya COlgatE-palMOlivE 15

Kila mmoja wetu anawajibika jinsi vile tutakavyoonekana kwa wagawaji na wateja. Ni muhimu kwamba tudumishe sifa yetu ya uaminifu na ukweli tunapofanya biashara na makundi hayo.

Tunawashughulikia waTeja na wauzaji kwa uadilifu.

Lengo letu katika kufanya shughuli za biashara ni kuhakikisha vyanzo vinavyoaminika. Ni muhimu kuwa na uaminifu unaposhughulika na wateja kwa uhusiano mzuri wa kudumu. Kwa hivyo, tunatazama wagawaji wetu kama washirika wetu na tunatarajia wapate faida ya maana. Tunawapa wagawaji wetu watarajiwa upendeleo sawa na unaofaa. Uamuzi unafanywa kwa kigezo cha madhumuni kama vile bei na ubora pia uaminifu na uadilifu wa muuzaji. Kutoa ama kupata kiinikizo, mlungula au malipo kama hayo hairuhusiwi.

Hatutoi mapendeleo ya kibinafsi kwa wateja, posho la cheo, usaidizi wa kuuza, ama hali kama hiyo; tunashughulikia wateja wetu wote kwa msingi wa biashara ulio sawa. Shughuli za wateja na wauzaji zinajadiliwa katika sehemu ya Kanuni hii namajukumu yeto yako chini ya sheria ya ushindani/kutokiritimba.

Kanuni ya Maadili Mema ya Watoa huduma kwa Colgate inapatikana kwa lugha kadhaa kwenye tovuti ya Kampuni chini ya sehemu ya "Fanya Kazi na Sisi" ya Watoa Huduma.

haTuToi zawadi ama kupokea zawadi zisizofaa.

Haikubaliwi kutoa au kupokea zawadi, malipo au faida zingine za kibinafsi ili kushawishi, au ambazo zinaweza kuonekana kushawishi uamuzi wowote wa biashara. Kama unakusudia kutoa au kupokea zawadi, malipo au faida zingine ambazo ni zaidi ya thamani ya ($50 USD), lazima uwasiliane na Shirika la Kisheria Duniani au Maadili na Makubaliano Duniani kwa idhini kabla ya kufanya hivyo. Pia, zingatia kwamba huenda ukakubali zawadi tu ya thamani ya kifedha kutoka kwa chanzo kimoja mara moja kwa kila kalenda ya mwaka. Kama kitakuwa kidendo cha aibu Kampuni kutokubali zawadi fulani ambayo inaweza kuzidi thamani ya kifedha rasmi, basi kukubali kwako zawadi hiyo kunapaswa kuripotiwa kwa Shirika la Kisheria Duniani ambalo litakusaidia kubainisha hatua inayofaa. Kwa kuongezea, usipange au usipokee zawadi, au faida zingine ambazo ni zaidi ya kifedha rasmi kwa dhamani kwa niaba ya mjumbe wa karibu wa familia kutoka kwa mtu yeyote ambaye Kampuni ina uhusiano naye wa biashara unaoendelea au angependa kuanzisha uhusiano wa kibiashara. Fuata sheria hii: usikubali kamwe zawadi au huduma kama itakudhoofisha au itaonekana kukudhoofisha. Hii haijumuishi burudani ya mara kwa ara ya biashara, ambayo inaweza kurudishwa , au zawadi ya thamani rasmi pekee.

Unafaa uwe makini kwamba kuna sheria maalumu zinazo ongonza tabia inayofaa kwa shughuli za serikali, serikali ya mtaa ama serikali ya nje ambayo haikubaliani na sheria za shughuli za kampuni zisizo za serikali. Kwa ujumla, unaweza kukosa kutoa ama kupeana zawadi kwa wafanyakazi wa serikali yo yote, kiinua mgongo ama kitu cho chote cha thamani, kama lishe ama safari ila tu kama imeshapitishwa na Shirika la Kisheria Duniani.

UhUSIANO WETU NAMAShIRIKA yA NJE yA BIAShARA

Page 18: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

16 Kanuni ya Maadili MEMa

Watoa huduma na wauzaji wa Colgate wanapaswa wakati wote kushauriwa juu ya mahitaji ya kufuata Kanuni wakati wafanyakazi na sisi au wakabiliane na uwezekano wa kupoteza biashara yetu kwa kushindwa kufanya hivyo. Kwa kuongezea, tunapaswa kuheshimu na kufuata sera za wateja au watoa huduma kwa umbali ambapo hazitapingana na sera zetu wenyewe.

Tunaheshimu siri za uuzaji na habari za siri za wengine.

Ni sera ya Colgate kutokiuka kimaksudi haki za ufahamu wa kiakili wa mali ya wengine. Pia ni sera ya Kampuni kuheshimu siri za uuzaji au habari za wamiliki za watu wengine. Hii haswa ni muhimu ikiwa unafahamu siri za uuzaji na habari za wamiliki za mwajiri wa zamani. Ikiwa maswali yoyote yatatokea katika eneo hili, shauriana na Shirika la Kisheria Duniani.

Ikiwa mtu ye yote nje ya Kampuni atakukujia na uvumbuzi, ugunduzi ama wazo, ni muhimu kuilinda Kampuni kutokana na Ukiukaji ama madai ya kifedha, haswa kwa hali spesheli ambapo juhudi zetu ama za washauri wetu zimewahi kufikia uvumbuzi kama huo, ugunduzi ama maoni, tunayotaka kutumia kwa bidhaa ya Kampuni. Usiruhusu watu wa nje kufichua habari zozote za uvumbuzi wao, ugunduzi ama wazo lolote jipya. Rejea maoni yote ambayo hayajatafutwa, bila kuyafichua, kwa Idara ya Maswala ya Watumizi katika eneo lako ili wayashughulikie kulingana na utaratibu wa Kampuni.

Kwa habari zaidi kuhusu habari za kulinda wengine, tafadhali rejea kwa “Maongozi ya Colgate-Palmolive ya Kulinda Habari za Wamiliki wa Kampuni na Kuheshimu Habari za Wamiliki za Wengine,” ambazo zinapatikana katika Maongozi ya Shughuli za Kampuni.

Kama sehemu moja ya kazi yangu, ninafanya mipango ya mikutano, safari na warsha nyingi za biashara. Sasa, hoteli ya humu nchini ambapo mimi huhifadhi vyumba imenipatia wikendi isiyokuwa na malipo ya adhimisho la harusi yangu. Ni wazo nzuri sana. Ninaweza kukubali?

Hapana. Kukubali toleo hilo litafanya iwe vigumu kwako kuonekana usiyekuwa na mapendeleo wakati unapopanga malazi ya baadaye ya hoteli. Hata kuonekana kwa mgongano huo wa maslahi hakufai na kunapaswa kuepukwa kwa kukataa toleo hilo kwa heshima.

S:

J:

Hivi karibuni nilitoka kwa kampuni shindani na nikajiunga na Colgate. Nilidhania inaweza kusaidia timu yangu mpya kwangu kuandika waraka mdogo unaoonyesha kila kitu ninachokumbuka kuhusu mipango na mbinu za biashara za mwajiri wangu wa zamani. Je, hili ni jambo nzuri la kufanya?

Itakuwa vibaya sana, na pengine kinyume cha sheria, kwako kushiriki maelezo ya kisiri au ya mmiliki ya mwajiri wako wa awali. Hupaswi kutoa maelezo yoyote yasiyokuwa ya umma uliyoyapata ulipokuwa ukifanya kazi na mshindani, na kama utawahi kuulizwa kufanya hivyo, unapaswa kuripoti hali hiyo kwa kitengo kinachofuata cha usimamizi, Waajiri wafanyakazi, Shirika la Sheria Duniani au Maadili na Makubaliano Duniani.

S:

J:

Page 19: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

KaMpuni ya COlgatE-palMOlivE 17

Sifa yetu imejengwa juu ya ubora na usalama wa bidhaa zetu. Kujitolea kwetu kwa ubora na usalama ni muhimu kuendeleza ukuaji na mafanikio ya Kampuni yetu.

Tunaweka viwango vya juu zaidi kwa bidhaa zeTu.

Tumejitolea kuhakikisha kwamba watumizi wanaweza kuamini bidhaa za Colgate kwa utegemeaji, ubora na utendaji wa kiwango cha juu. Pamoja na kutumikia mamilioni ya watu katika masoko tunayofanyia kazi, ni lazima tujitahidi kila wakati kutengeneza bidhaa zetu kwa njia nzuri zaidi ili ziweze kuwa bei nafuu kwa nambari kubwa zaidi ya watumizi.

Bidhaa zinazouzwa na Colgate sio lazima tu zitimize viwango vya usalama vilivyowekwa na sheria, lakini pia mara kwa mara viwango kali zaidi vya Kampuni. Tunahusika katika vipindi tofauti ili kutoa usaidizi wa haraka kwa watumizi wakati bidhaa imeharibiwa ama imetumiwa vibaya au bandia. Afya ya mtumizi, usalama na maslahi ni ya muhimu kwetu na kama mfanyakazi wa Colgate ni jukumu lako kupiga ripoti maswala yoyote unayokumbana nayo yanayohusiana na ubora ama usalama wa bidhaa kwa kiongozi wa kitengo cha biashara.

Tuna mwiTikio kwa waTumizi.

Kwa sababu biashara yetu ni bidhaa za utumiaji, mafanikio yetu yanategemea kuridhika kwa mtumizi, uaminifu na maslahi mema. Tunaweza kufikia vizuri malengo yetu na kutumikia mahitaji ya watumiaji kwa kufuata kipindi thabiti, cha haki na nyeti na cha kujali mawasilainao ya watumiaji.

Tunagundua umuhimu wa kuterejea na kuhakukisha mwitikio kwa mahitaji ya watumiaji na mapendeleo ya bidhaa zetu. Tunaamini kwamba maoni ya watumiaji, hoja na maswala yanayowasilishwa kwenye Kampuni kuhusu bidhaa zetu ni njia muhimu ya kupata habari. Mahitaji ya watumiaji hubadilika kila wakati, kwa hivyo lazima tusikize kila wakati kila wanachotaka na tutumie ubunifu wetu kutosheleza mahitaji haya yanyobadilika.

Wakati mtumiaji anawasilisha kutotosheka, tunashughulikia shida hiyo kwa haraka, kwa utaratibu na haki, na tunafanya hima kudumisha na kupata tena ukarimu wa mtumiaji na kuendelea kwa ununuzi wa bidhaa za Colgate.

kuTangaza kweTu ni sahihi.

Hali moja iliyo muhimu sana katika biashara yetu ni kutangaza. Kutangaza kunafaa kuwa na ubunifu na ushindani, lakini kwa wakati huo huo, uwe wa ukweli na sahihi, sio wa potosha na kwa kila mara uwe unalingana na sheria. Kutangaza kwetu lazima pia uepuke na kueleza vibaya watu kwa misingi kama ya umbari, dini, asili ya taifa, rangi, jinsia, msingi wa jinsia, umri, uraia, mwelekeo wa jinsia, hali ya uzee, hali ya ndoa ama ulemavu au tabia nyingine yoyote inayolindwa na sheria. Utangazaji unabuni zaidi ya taswira ya bidhaa. Inajenga sifa yetu ya utegemeaji, kutegemewa na uaminifu.

UhUSIANO WETUNA WATUMIA JI

Page 20: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

18 Kanuni ya Maadili MEMa

Pia, tunatahadhari katika uchaguzi wa vyombo vya habari ambavyo ujumbe wetu unaonekana. Haturuhusu matangazo yetu kuonekana kwenye vipindi vya televisheni ama kwenye vyombo vye habari vinayofanya kiiua mgongo au kutumia vurugu, ngono ama tabia zingine zisizokubalika na jamii ama kuathiri sana sifa za bidhaa za Kampuni yetu.

Tunaangalia viwango vya haki vya kibiashara kwa kuunda, kutumia na kuchagua utangazaji, alama za uuzaji, na miundo ili bidhaa zetu zifanikiwe kwa nguvu ya ubora wake na sifa yetu, kuliko kwa nji ya kuiga ama kuuza kwa ukarimu wa washindani wetu. Haki ya biashara inahitaji:

• Kufuata vikali mahitaji ya sheria ya kawaida kuhusiana na ukiukaji wa alama za biashara na mashindano yasiyo na haki.

• Kuepukana na kuiga alama za biashara zinazojulikana, misemo, mada za utangazaji, na michoro inayotumika na kampuni za kimataifa naya mikoa na za mitaa ya karibu na mbali.

Kwa majadiliano zaidi juu ya maongozi ya Utangazaji wa Kampuni, angalia “Maongozi ya Utangazaji wa Colgate-Palmolive” na “Taarifa ya Sera ya Makazi ya Utangazaji wa Colgate-Palmolive” yanayopatikana katika Maongozi ya Shughuli za Biashara za Kampuni.

Page 21: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

KaMpuni ya COlgatE-palMOlivE 19

Tunatii sheria zote zinazodhibiti biashara ya Colgate. Kwa kweli, ni sera yetu kuenda mbele zaidi ya sheria na kufuatilia moyo wake. Fanya tabia ya kuwasiliana na Sheria iwapo ukiwa na shaka.

Tunakubaliana na sheria za mashindano/ kuTokukiriTimba

Ni sera ya colgate kuwa wafanya kazi wote wafuate kabisa sheria za mashindano (yanayojulikana kama sheria za kutokukiritimba Marekani (U. S.) ya kila nchi na eneo ambapo Colgate inafanya biashara. Sababu ya sheria ya kushindana ni kulinda utaratibu wa mashindano kusaidia watumiaji. Sheria ya mashindano huhakikisha kwamba Kampuni zinashindana kupata biashara kwa kupeana bei za chini, bidhaa bunifu na huduma bora na sio kuingiliana na nguvu za soko za mahitaji na upeanaji. Sheria za mashindano pia zinalinda kampuni kutokana na uporaji au vitendo visivyo vya haki na kampuni tawala ili uwanja wa mashindano uwe wazi na wa haki kwa wote. Colgate inaunga mkono malengo ya sheria za mashindano. Tunaamini kwamba Colgate inafanya vyema katika soko la mashindano.

Karibu kila nchi inatumia sheria za ushindani. Ni jukumu letu kuelewa sheria za mahali tunapoenda kufanya biashara na kutafuta mwongozo kutoka kwa kitengo cha biashara cha ushauri wa kisheria au Shirika la Kisheria Duniani kama inavyohitajika. Lazima tuambatane na moyo wa sheria husika.

Sheria za mashindano ulimwenguni kote haziruhusu mikataba ya sasa au kati ya washindani watarajiwa inayoweza kuadhiri mashindano. Ufunguo wa makubaliano ni kujitegemea. Colgate lazima ijitegemee katika shughuli za biashara yake – kuweka bei, vipunguzo, ukuzaji, hali za ununuzi, wasambazaji na wagawaji, na kuchagua bidhaa za kutoa na ngapi za kuuza. Ni muhimu kukumbuka kuwa mkataba usio halali sio lazima uwe rasmi ama hata wa maandishi. Unaweza kuwa mkataba wa mazungumzo ama umehitimiswa kutoka kwa sababu ya biashara ama maoni ya hati. Mkataba pia sio lazima ufaulu kutekelezwa ili usiwe halali.

Sheria za mashindano pia zinatoa vizuizi fulani kwa uhusiano na mteja na wasambazaji. Katika nchi nyingi, jaribio lolote la kunyanyasa haki za wateja ama wasambazaji kuamua bei, sheria na masharti ya uuzaji, ama kuweka vizuzizi visivyofaa kuzuia haki ya kufanya kazi huru linakiuka sheria za mashindano.

Matokeo ya Colgate na watu wake kutokubaliana na Sheria za mashindano ni makubwa sana. Ukiukaji wa sheria fulani za mashindano unaweza kusababisha faini, kufungwa kwa watu binafsi wanaohusika, ama hata faini nzito zaidi kwa Kampuni. Hata hivyo, hata kusipokuwepo kuhukumiwa kwa mhalifi, sheria za umma zinaweza kutumiwa kuokoa uharibifu na ada ya wakili.

Unapokuwa na shaka lolote kuhusu hatua yakufikiria inaweza kutokea chini ya sheria za mashindano, unapaswa kuwasiliana na Shirika la Kisheria Duniani.

Kwa habari zaidi juu ya masuala ya mashindano/ kutokukiritimba, tafadhali rejea kwa “maongozi ya kimataifa ya Colgate-Palmolive,” ambayo inapatikana katika Maongozi ya Shughuli za Biashara za Kampuni.

UhUSIANO WETU NASERIK ALI NA ShERIA

Page 22: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

20 Kanuni ya Maadili MEMa

Tunakubaliana na sheria za usalama.

Kwa wakati unaweza kuwa na habari kuhusu Colgate ama Kampuni za uuzaji uuma ambazo zinafanya biashara na Colgate ama zinajadiliana yasiyojulikana na umma kama (“isiyo-ya uuma”) - kama matokeo ya kifedha au ya shughuli, uwezekano wa kunua, au uwekezaji, mipango ya uuzaji au kuletwa kwa bidhaa mpya.

Habari inachukuliwa kuwa sio ya umma mpaka itakapofichuliwa wazi kwa umma kama, ikiwa habari hiyo imefunuliwa kwa umma na wakati wakutosha umepita kwa usalama wa soko kuelewa habari hiyo. Ikiwa habari isiyo ya umma ni ya ukweli, hiyo ni, habari ambayo mdadisi busara atatilia maanani wakati wa kufanya uamuzi wa uwekezaji – chini ya sheria zinazotumika za usalama na sera za Kampuni:

• Ni lazima usiuze kwa akaunti yako mwenyewe ama kwa akaunti ya mtu mwengine katika hisa, ama amana zingine za Kampuni (Colgate au nyingine) ambayo habari isiyo – ya umma inahusiana nayo.

• Usihimize au kulazimisha wengine, kwa msingi wa habari zisizo za umma kama hizo kuhusika katika hisa, bondi ama rusuku nyingine kama hizo za Kampuni.

• Usifichue habari zisizo za umma kama hizo kwa watu nje ya Colgate.

• Lazima ujadili maelezo kama hayo yasiyo ya umma na mtu wa ndani wa Colgate isipokuwa wawe na hitaji la kujua maelezo kama hayo.

Watu wa Colgate wanaofahamu habari zisizo za umma kuhusu Colgate wanapaswa kuwa na uwangalifu ili kuhifadhi kwa ujasiri na lazima wasifanye uuzaji katika hisa za Colgate, bondi ama ruzuku yoyote ya Kampuni nyingine inayohusika kabla ya habari zisizo za umma itangazwa kwa umma na kwa wakati unaofaa baada ya muda baadaye. Kizuizi kama hiki kinaendelea kwa shughuli za chaguo za hisa na maamuzi ya kuwekeza katika au kuuza hisa za Colgate katika mipango ya faida ya Kampuni.

Ikiwa utaiacha Colgate, uwajibikaji wako kuhifahdi usiri wa habari zisizo za umma kama hizo utaendelea hadi habari hiyo itakapofunuliwa wazi kwa umma.

Ukiwa una swali kuhusu kama habari ni za "muhimu" au zimefichuliwa kabisa kwa umma, lazima uwasiliane na Shirika la Kisheria Duniani au ujiepushe kuuza katika eneo la rusuku lililoathirika ama kufunua habari hiyo hadi utakapoelezwa kwamba habari hiyo sio muhimu ama imefunuliwa kwa umma na imeeleweka.

Mwenzi wa biashara alinieleza kuhusu mkutano ambao unafanywa na mmoja wa washindani wetu wa moja kwa moja wakati wa mkutano wa mambo ya meno. Ningependa kuhudhuria mkutano wao, lakini ninaogopa hawataniruhusu wakijua nimetoka kampuni shindani. Ninaweza kuhudhuria iwapo niweke kitambulisho changu siri?

Hapana. Sio vizuri kujificha ili usijulikane ili upate maelezo kutoka kwa mshindani. Unapaswa kuwasiliana na Shirika la Kisheria Duniani kabla ya kuhudhuria mkutano wowote wa mshindani, kwa sababu mikutano kama hiyo inaweza kuibua masuala ya kutokukiritimba.

S:

J:

Nimegundua kwamba siwezi kununua hisa za Kampuni kulingana na maelezo ya kindani, lakini ninaweza kushauri mmoja wa familia au rafiki kufanya hivyo?

Hapana. Utakuwa ukikiuka sheria za biashara ya kidani kama vile ungekuwa ukinunua hisa wewe mwenyewe. Kwa kuongezea, mtu uliyemshauri anaweza kuwa anakiuka sheria kama atajua mapendekezo yako yalikuwa ya maelezo ya kindani.

S:J:

Page 23: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

KaMpuni ya COlgatE-palMOlivE 21

haTuToi msaada wa kisiasa.

Hakuna fedha ama mali ya Kampuni inyoyoweza kutumika kwa misaada ya vyama vya kisiasa au mgombeaji, akiwa wa serikali, wa mtaa, Marekani (U. S.) ama ngambo. Msaada wa kisiasa unajumuisha wa moja kwa moja (kama, pesa) ama msaada wa aina yoyote, Msaada usio wa-pesa unajumusiha ununuzi wa tiketi za mchango, msaada wa bidhaa, kazi ya kujitolea kwa watu wa Colgate katika wakati wa kawaida wa biashara na utumizi wa vifaa vya Colgate kwa kusaidia mchango ama sababu za kisiasa. Ikiwa unalo swali kuhusu msaada usio wa – pesa, tafadhali wasiliana na Shirika la Kisheria Duniani.

Kampuni hairuhusiwi kulipa ama kumrudishia pesa mtu yeyote wa Colgate ama mtu anayehusika na Kampuni (pamoja na washawishi wa nje), wanaohusika moja kwa moja au la, kwa hali yoyote, kwa msaada wa kisiasa ambao mtu anakusudia kutoa ama ameshatoa.

Watu binafsi wa Colgate watabaki huru kufanya msaada wa kibinafsi kwa wagombeaji ama vyama watakavyo chagua. Msaada wa kibinafsi ni jukumu na mzigo wa mtu binafsi. Colgate haitakubali jukumu lolote au uwajibikaji kwa heshima ya msaada wa kibinafsi. Zaidi, msaada wa kibinafsi hautafanywa kwa lengo la kusaidia Colgate ama moja wapo ya Kampuni inayoshughulikia kwa kupata ama kuhifahdi biashara.

Kama vile makampuni mengi ya kimataifa, Colgate inahusika na hulipa malipo ya kila mwaka kwa mashirika kadhaa ya biashara na viwanda nchini Marekani. Ili kusaidia kuhakikisha kwamba mashirika haya ya biashara hayatumii sehemu yoyote ya malipo haya yaliyolipwa na Colgate kwa michango ya kisiasa, Afisa Mkuu wa Maadili na Makubaliano wa Colgate hufahamisha mashirika ya kibiashara ya Marekani kila mwaka juu ya sera yetu ya kuzuia michango kama hiyo na uhitaji kila shirika la biashara kuhusika katika mchakato wa cheti cha kila mwaka. Kujifunza zaidi, tafadhali rejea sera yetu ya michango ya kisiasa, ambayo inaweza kupatikana katika sehemu ya Usimamizi ya tovuti ya www.ColgatePalmolive.com.

Tunashughulikia wengine kwa uadilifu.

Ni sera ya Kampuni kwamba watu wa Colgate lazima wafuate kabisa sheria zote husika za kutotoa hongo duniani kote na lazima wasihusike katika hatua zozote za hongo. Kwa hivyo, haupaswi kutafuta kushawishi uamuzi au tabia ya mhusika yeyote wa nje ambaye unaweza kuwa unafanya biashara ya Kampuni naye kwa kuahidi zawadi au faida zingine, au na ushawishi wowote usio wa kisheria.

Kwa kuongeza, sheria zingine za kushawishi zinaweza kuhitaji uwandikishaji wa Kampuni ama watu na ripoti kama mshawishi ikiwa mtu wa Colgate atawasiliana na mfanyakazi wa serikali kwa sababu ya kuathirii au upitishaji ama hatua nyingine rasmi. Ikiwa unahusika na shughuli zozote kama hizi, ni lazima uwajulishe Shirika la Kisheria Duniani.

Kujitolea kwa Colgate kushughulika kisheria na kwa uadilifu na serikali inatumika uliwenguni kote. Sera ya Kampuni, Desturi ya Shughuli za Ufisadi za Nje ya Marekani na sheria za kutotoa-hongo kama hizi ulimwengini kote haziruhusu watu ama ajenti wao kutoa au kutaka kutoa pesa ama kitu chochote cha thamani- ikiwa pesa taslimu au la, ama ikiwa kwa moja kwa moja au la, kupitia kwa wengine- kwa afisa wa nje (kama, mfanyakazi wa serikali ya nje, chama cha kisiasa cha nje, ama mwanachama rasmi, ama mgombeaji rasmi wa kisiasa wa nje) kushawishi kuwa rasmi kuathiri desturi yoyote ya serikali ama uamuzi, ama kusaidia Kampuni kupata au kuhifadhi biashara.

Ili kuhakikisha kuwa haukeuki kiwango hiki, ni sera ya Kampuni kuwa, isipokuwa malipo yoliyokubaliwa na sheria, (kwa mfano, Malipo ya leseni au kibali yanayotakikana), hakuna malipo, burudani, au zawadi au vitu vingine vyovyote vitatolewa kwa maafisa wa kigeni, moja kwa moja au la, isipokuwa iwe imeidhinishwa kwa mapema na Shirika la Kisheria Duniani kama agizo halali chini ya sheria za Marekani na zingine husika.

Kuwa wa moja kwa moja na mwenye ukweli unaposhughulika na kuwasiliana na wafanya kazi wa serikali. Taarifa yoyote inayofahamika au ya uongo kimaksudi kwa wafanyakazi wa serikali (mazungumzo

Page 24: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

22 Kanuni ya Maadili MEMa

au maandishi) na haswa taarifa yoyote chini ya kiapo, inaweza kufunua Kampuni na watu wake kwa kisasi kibaya.

Kuzidi wafanyikazi wa kawaida au wa serikali, kumbuka kwamba katika nchi nyingine wafanyakazi wa serikali wanaweza kujumuisha wahadhiri wa chuo kikuu, waalimu wa shule, madaktari wa meno, madaktari wa wanyama, madaktari na wafanyakazi wa vyombo vya habari vya serikali.

Kwa maelezo zaidi ya maongozi ya sera za kampuni katika sehemu hizi, angalia “Maongozi ya Colgate-Palmolive katika Desturi ya Shughuli za Ufisadi za Marekani” “Maongozi ya Uhusiano wa Biashara na Wakuu wa Serikali na Colgate-Plamolive”, yanayopatikana katika Maongozi ya Shughuli za Biashara ya Kampuni.

TunadhibiTi rekodi kulingana na sheria.

Tunakubaliana na sheria na kanuni zote zinazohusiana na udhibiti wa rekodi za Kampuni (pamoja na hati na data za kielektroniki).

Ikiwa kuna udadisi wa serikali ama mashitaka ambayo hayajakamilika unayofahamu ama yalioripotiwa kwako, wasiliana na wanasheria mara moja. Ikiwa lazima uhifadhi rekodi zote zinazoweza kuhusika kwenye mashtaka, ama ni muhimu kwa mashtaka, ama zinazousika kwa udadisi, bila kuzingatia mahitaji ya programu ya kuhifahdi rekodi. Usiharibu ama kubadilisha rekodi kama hizo, kwani kuharibu vibaya kwa rekodi kunaweza kuwa na matokeo mabaya – pamoja na adhabu ya umma na /wahalifu kwa Kampuni na kwako binafsi. Ikiwa una swali kama rekodi Fulani inahusiana na udadisi au mashitaka, wasiliana na Shirika la Kisheria Duniani kabla ya kutupa rekodi hiyo.

Tunakubaliana na kanuni za uuzaji za kimaTaifa.

Katika shughuli za nyumbani na za ngambo, Kampuni inakubaliana kabisa na sheria zote zinazotumika – haswa sheria za Marekani - zinazoongoza mahuduli na mahuruji na shughuli za biashara na watu wasio wa Marekani. Sheria hizi zinahusisha vizuizi kwenye aina za bidhaa ambazo zinaweza kuhuduliwa kwenda Marekani (U. S.) na njia ya kuhuduli. Zinazuia pia kusafirisha nje kuenda kwa, na biashara zingine nyingi, nchi kadhaa kama kushirikiana na kuhusika katika ususaji wa nje wa nchi ambazo hazijasusiwa na Marekani. Watu wa Colgate lazima wafanye shughuli za Kampuni ili kukubaliana kabisa na sheria za nchi ambapo wanashughulika; hata hivyo, kuna wakati ambapo kunawezakutokea mzozo kati ya sheria ya nchi moja na zile za Marekani ama sera ya Kampuni. Kuwa mwangalifu wa mzozo kama huu, unapaswa kumjulisha meneja wako na uwasiliane na Shirika la Kisheria Duniani.

Kwa maongozi ya maelezo zaidi juu ya sheria hizi na nchi zinzohusika, angalia “Maongozi ya Kimataifa ya Colgate-Palmolive ya biashara”, inayopatikana katika “Maongozi ya Shughuli za Biashara za Kampuni”.

Ninafahamu kwamba kuna sheria ambazo zinazuia hongo kwa maafisa wa serikali. Lakini sheria hiyo pia inazuia hongo kwa watu ambao sio maafisa wa serikali?

Kuna sheria dhidi ya hongo ambazo zinazuia hongo kati ya wahusika binafsi wa kibiashara; k.m., hongo ya kibiashara. Sheria hizi ni muhimu pia - na zinatekelezwa kabisa - kama zile zinazozuia hongo kwa maafisa wa serikali.Daima kumbuka kwamba sera ya Kampuni na sheria za nchini zinakataza kumhonga yeyote anayefanya kazi ya Kampuni, awe afisa wa serikali au mtu binafsi.

S:J:

Ninawezaje kubainisha muda ambao lazima niweke rekodi za Kampuni na ni wakati ninapoweza kuzitupa?Angalia tovuti ya intraneti ya Usimamiaji Rekodi za Kampuni katika OurColgate.com > Tovuti za C-P > Sheria na Masharti au wasiliana na Msimamizi wako wa nchini wa Rekodi (inapotumika).

S:J:

Page 25: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

KaMpuni ya COlgatE-palMOlivE 23

Kampuni inajitahidi kuwa mjumbe anayechangia katika jamii ya ulimwengu. Sisi ni raia wa kila eneo ambapo tunafanyia kazi, na kama raia binafsi, tunalo jukumu la kuunga mkono afya, elimu na maslahi ya jamii.

Tunahusika kaTika kusaidia wa kujiTolea kaTika jamii na maeneo ya mTaani.

Kupitia dunia nzima, ni lengo letu kuhusika katika miradi ya kuendeleza ukuzaji na maslahi ya watu wa jamii. Miradi kama hii inajumusha kuhusika kwa michango ya ufadhili, na kuchukua jukumu kwa kuwasaidia maskini, walioumia na wasiokuwa na makaazi katika saa za mchafuko wa dunia. Tunazingatia sana vijana, haswa elimu ya vijana. Colgate inaamini kuwa uwekezaji unaowekwa kwa watoto utatusaidia wote kwa siku zijazo za kesho. Hii ndio sababu Kampuni inadhamini mipango ya kusoma, ubunifu wa ushauri, mashindano ya riadha na shughuli zingine za vijana duniani kote. Juhudi hizi hukuza moyo wa kushindana na mafanikio kwenye vijana.

Kampuni pia inahimiza watu wake kuhusika kwa wakati wao wenyewe katika shughuli za mtaani za kusaidiana.

Tunafanya kazi na serikali kwenye masuala yanayohusika na biashara yeTu.

Kampuni iko na matawi katika nchi zaidi ya 200. Ni sera yetu kufanya kazi kwa ushirikiano na serikali ya mitaa na serikali ya nchi. Wakati mwingi, maswala yanayoathiri shughuli zetu yanaweza kutokea. Baada ya uzingatiaji wa makini, Kampuni itatoa maoni na mapendekezo kwa serikali juu ya maswala kadhaa kuunga malengo yetu na mahitaji ya biashara.

TunakaTaa shughuli za kuTumia vibaya na hali isiyo ya kibinadamu kaTika kazi.

Colgate hairuhusu matumizi mabaya ya kazi kwa watoto, unyonyaji wa watoto, na njia yoyote nyingie ya kuwatendea vibaya wafanyakazi haikubaliki. Pia, ni sera ya Colgate kutofanya kazi na msambazaji ama kontrakta anayejulikana kufanya kazi kwa njia ya kuwatendea vibaya mfanyakazi ama kuwanyanyasa watoto, ghadhabu ya kimwili, unyanyasaji wa wanamake, kutumikia kwa kulazimishwa na njia nyngine yoyote ya unyanyasaji. Hakuna unyanyasaji wa watoto ama sheria za kikazi unaokubalika na Kampuni, na ikiwa ukiukaji wa sera zetu utajulikana na Kampuni, ni fursa ya kukuukomesha uhusiano wa biashara mara moja.

Tunaonyesha kujiTolea kweTu kwa haki za kiibinadamu ulimwenguni.

Colgate imejitolea kuheshimu haki za kibinadamu uliwenguni kote. Hadi mwisho, Colgate inashughulika na kufafuta kufanya kazi na washirika wanokuza viwango vifuatavyo:

UhUSIANO WETUNA JAMII

Page 26: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

24 Kanuni ya Maadili MEMa

• Nafasi sawa kwa waajiriwa wote katika viwango vyote bila kujali umbari, dini, jinsia, kitambulisho cha jinsia, asili ya kitaifa, jamii, umri, mwelekeo wa jinsia, ulemavu, hadhi ya ndoa, hali ya uzee au tabia yoyote nyingine inayolindwa na sheria katika sheria au mashari yoyote yale ya ajira;

• mahali pa kazi penye usalama unaolinda afya na mazingira;

• kulipa wafanyakazi malipo ambayo yatawawezesha kufikia mahitaji ya muhimu, na kuwapa wafanya kazi fursa ya kuboresha vipawa, ujuzi na uwezo wao;

• kuheshimu uhuru wa kushirikiana kwa wafanyakazi; na

• kufanya kazi na serikali na jamii tunazofanya biashara nazo ili kuboresha maslahi ya elimu, kitamaduni, kiuchumi, na hali ya jamii katika jamii hizo.

Page 27: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

KaMpuni ya COlgatE-palMOlivE 25

Mazingira masafi ni muhimu kwa Colgate sio tu kwasababu ni kitu cha busara kufanya lakini kwasababu inafanya ufahamu mzuri wa biashara. Hoja yetu ya kutia juhudi zetu kulinda sayari yetu inazingatia kufanya kazi kwa njia iliyosalama kwa mazingira inayolinda ulimwengu wetu kwa vizazi vijavyo.

TumejiTolea kwa uendelezaji na uwajibikaji wa kijamii.

Katika Colgate, uendelezaji ni muhimu kwa mafanikio ya Kampuni. Imewekwa mizizi kwenye dhamani za utunzaji wa Colgate, kazi ya pamoja na kuendeleza uboreshaji. Lengo letu ni kwa Watu, Utendaji kazi na Sayari.

Kwa kuongeza, tunajitolea kutimiza lengo letu la kuendeleza ulimwengu na kuhakikisha kuwa biashara ya Colgate inakua kila wakati na kwa uwajibikaji na faida kwa wale tunaowahudumia, pamoja na wafanyakazi, washikadau wetu na wawekezaji ulimwenguni tukikuza maslahi ya vizazi vijavyo.

Kwa miaka michache iliyopita, ahadi yetu ya uendelezaji na uwajibikaji wa jamii imeongezeka kwa kuwa tumejumuisha vumbuzi hizi katika shughuli zetu za biashara, Njia hii iliyojumuishwa imetia nguvu vumbuzi zetu za uendelezaji na majukumu ya kijamii na utendaji kazi wa biashara yetu, kutusaidia kuajiri na kudumisha vipaji bora, kuboresha mahusiano yetu na washikadau, na kutoa nafasi mpya za uvumbuzi. Pengine muhimu zaidi, ahadi hii imewafurahisha na kuwahusisha watu wa Colgate duniani kote.

Sera zetu za uendelezaji na mipango zimetolewa kwa muhtasari ili uweze kuangalia katika sehemu ya "Kutenda Karama Zetu" ya tovuti ya www.ColgatePalmolive.com

Tunalinda na kuTunza mazingira yeTu.

Kampuni imejitolea kulinda mazingira. Kwa hivyo, ni lazima kila mtu akubaliane na barua na moyo waa sheria na kanuni zinazotumika kwa mazingira na sera za jamii zinazowakilisha. Hakuna mtu au meneja katika Kampuni mwenye ruhusa kuhusika katika tabia isiyokubaliana na sera hii, kuongoza, ama kuidhinisha, ama kuruhusu tabia yoyote kama hii na mtu mwingine.

Tutakuza mawasiliano ya uawazi na umma na tutatafuta ushirika unaoendelea na unaozalisha katika jamii tunayofanyia kazi. Tutaendelea kushiriki habari na watumiaji kuhusu sera za mazingira na tutafanya kazi na viongozi wa jamii na wengine wote wananoshiriki katika kujitolea kwetu kulinda mazingira kwa vizazi vijavyo.

Katika uliwengu wetu unaoendelea kubadilika, Colgate inatoa kipaumbele kufanya kazi kwa njia ya uwajibikaji na ya heshima. Juhudi hizi zimesababisha kuwa na ongezeko la utendaji bora na faida za kifedha kwa Kampuni. Tunajua kwamba bado kuna mengi yakufanywa. Mipango yetu inayoendelea ya kupunguza alama ya mahusiano ya mazingira itabaki kuwa sehemu muhimu ya kutoa, kupakia na usambazaji wa bidhaa zetu.

Kwa habari zaidi kuhusu sheria za mazingira zinazotumika kwenye kampuni na sera zinazohusiana na Kampuni na utaratibu, tafadhali angalia katika “Sera ya Mazingira, Afya ya Kikazi & Usalama wa Colgate-Palmolive,” inayopatikana katika Maongozi ya Shughuli za Biashara za Kampuni.

UhUSIANO WETU NAMAzINgIRA

Page 28: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

26 Kanuni ya Maadili MEMa

Tunajitahidi kuhudumia mahitaji ya wawekezaji wetu na kuwasaidia kujenga thamani ya uwekezaji.

Tunashikilia uongozi mzuri wa biashara ili kulinda dhamana ya wawekezaji weTu.

Uongozi wa kibiashara wa sera na mipango ya Kampuni, ambayo kanuni ya maadili mema ni sehemu muhimu sana, na inatumika kama njia muhimu ya kulinda wawekezaji. Katika miaka ya hivi karibuni “mapambano” yamepitishwa na baraza kuu, ya SEC wa soko la hisa la NewYork, na warekebishaji na wasimamizi wengine kote ulimwenguni ili kukuza uadilifu wa biashara ambao umekuwa zoezi la Colgate kwa muda mrefu. Wawekezaji wengine wamehudumiwa vizuri na bodi lakujitegemea, linalohusisha wakurugenzi wa kujitegemea wanaosimaimia maswala ya ukaguzi, malipo na uongozi. Kamati ya kurekebisha kila wakati mikakati ya uongozi unafafanua wazi jukumu na uwajibikaji na uongozi wa biashara ya Kampuni.

Kwa maelezo zaidi juu ya mpango wa uongozi wa biashara wa Kampuni, tafadhali tazama “Maongozi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Maswala Muhimu ya Uongozi wa Kampuni na Kamati Aandalizi na Kamati ya Fedha , zote ambaozo zinapatiakana katika tovuti ya Kampuni.

Tunadumisha mipango ya nguvu ya ukaguzi ili kuongeza ujasiri wa wawekezaji.

Kampuni imejitoela kwa ubora, uadilifu an uwazi wa ripoti za fedha. Kujitolea huku kunaonyeshwa katika sera za muda mrefu za kampuni na utaratibu pamoja na ukaguzi wa ndani inayoangalia udhabiti wa kifedha ulimwenguni, kamati ya wakaguzi wakujitegemea, na kamati ya wakaguzi wakujitegemea ambao wanajukumu kubwa la kusimamia sehemu hizi. Ili kuongeza ufanisi wa rasilmali hizi, watu wa Colgate wanatakikana kuhusika katika mawasiliano ya ukweli na haki na ubadilishanaji huru wa habari na ukaguzi wa nje na ndani na kamati ya wakaguzi.

Kwa habari zaidi kuhusu kazi muhimu za wakaguzi wa ndani wa Kampuni, wakaguzi wa kujitegemea na Kamati ya Wakaguzi, tafadhali tazama “Mkataba wa Kamati ya Wakaguzi wa Kampuni ya Colgate-Palmolive” ambayo inapatikana katika tovuti ya Kampuni.

Tunawajulisha wenye hisa habari kuhusu maendeleo ya kampuni.

Kila mwaka wenye hisa wanaitwa kuhudhuria mkutano wa kila mwaka wa Kampuni ambapo maendeleo ya Kampuni wa mwaka uliopita tizamwa na wenye hisa wanapewa fursa ya kuuliza maswali kwa usimamizi mkuu wa Kampuni. Katika miezi yakuingilia, washikadau wanaweza kuangalia tovuti ya Kampuni www.colgate.com, kwa maelezo zaidi juu ya uzinduzi wa hivi karibuni wa bidhaa, na matokea ya karibuni ya fedha na maendeleo ya biashara.

UhUSIANO WETUNA WAWEKEzAJI

Page 29: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

KaMpuni ya COlgatE-palMOlivE 27

Kuwa na kanuni ya maadili mema iliyoandikwa haitoshi – viwango vya tabia ni lazima viwasilishwe kwa na kufuatwa na wale ombwa kufuata.

mawasilianao na uwazi ni muhimu.

Kwa kukubali ajira na Colgate, kila mmoja wetu anawajibika na makubaliano na viwango vya tabia, na sheria na kanuni zote na maongozi yenye maelezo zaidi inayopatikana katika maongozi ya shughuli za biashara na katika sera zingine, utaratibu na maongozi yanayoandaliwa na Kampuni na tanzu zake, vitendaji kazi na divisheni. Meneja wanalo jukumu la kuwasilisha viwango hivi kwa wale wanaofanya kazi nao, kuhakikisha kwamba wanavielewa na kuvifuata, na kuunda mazingira ambapo watu wanaweza kujadiliana huru masuala ya uadilifu na sheria.

idara ya uadilifu na makubaliano ya ColgaTe ulimwenguni inasimamia makubaliano

Makubaliano na Kanuni ya Maadili Mema na Mwongozo wa Desturi za Biashara utasimamiwa na Idara ya Maadili na Makubaliano Duniani. Idara huripoti kwa Afisa Mkuu Mtendaji/Mwenyekiti wa Bodi na Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi wa Bodi la Wakurugenzi wa Colgate kuhusiana na kuanzishwa, kutekelezwa kwa Kanuni ya Maadili Mema na mipango husika.

Habari inayoripotiwa kwa idara ya Maadili na MakubalianoDuniani au kupitia kwa njia nyingine, kwa usahihi, kuwasilishwa kwenye msingi wa usiri wa Kamati ya Ukaguzi.

UWA JIBIK A JI WAM A K U B A L I A N O

Page 30: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

28 Kanuni ya Maadili MEMa

TAFUTA MWONgOzO NA URIpOTI hOJAunahimizwa kuTafuTa mwongozo.

Kanuni hii haiwezi kutoa majibu yaliyo na maelezo kwa maswali yote. Kwa hivyo mwishoe lazima tutegemee ujuzi na kuelewa kwa kila mmoja kwa yale yanayopaswa kufuatwa kwa viwango vya juu vya Kampuni, ikiwa pamoja na hisia za wakati unaofaa kutafuta mwongozo unaofaa wa tabia.

Wakati mwingi, unapaswa kuleta maswali kuhusu mwongozo yaliyoelezwa katika kanuni kwa kumfahamisha moja kwa moja meneja au Shirika la Kisheria Duniani, ambaye anaweza kuelekeza maswala hayo kwa wakubwa wake, wakili mwingine katika Shirika la Kisheria Duniani, Idara ya Maadili na Makubaliano Duniani, au idara ya Kuajiri Wafanyakazi katika kitengo fulani. Unaweza pia kuwasiliana na viwango vya juu vya usimamizi ama Idara ya Uadilifu na Makubaliano wewe mwenyewe – moja kwa moja ama kupitia kitengo cha haraka cha Kanuni ya Maadili Mema ya Colgate-Palmolive (iliyojulikana awali kama mawasiliano ya moja kwa moja), kama ilivyofafanuliwa hapa chini.

lazima uripoTi ukiukaji unaoshuku.

Ikiwa unajua ama una sababu nzuri ya kushuku ukiukaji wa Kanuni ya maadili mema ama mwongozo wowote wa kampuni, unapaswa kuripoti mara moja kwa meneja wako au Shirika la Kisheria Duniani. Kwa njia nyingine, unapaswa kusikia huru kuenda kwa kiwango cha juu cha usimamizi ama kwa Idara ya Uadilifu na Makubalianao bila woga wa kuulizwa maswali. Colgate haitalipiza kisasi dhidi ya mtu yoyote atakayeripoti habari kuhusu ukiukaji kwa nia njema, ama mtu anayehusika katika uchunguzi wowote, ama kesi inayoendeshwa na Kampuni ama Serikali, isipokuwa kama habari hizo zimepatikana kuwa za uwongo na maksudi ya kudanganya. Kampuni itachukua hatua zote kuficha kitambulisho cha mtu na habari ya siri ambayo ametoa na itafichuliwa kwa msingi wa kutaka kujua wakati huo ufichuzi ni:

• Hauwezekani kuepuka ili kufanya uchunguzi mzuri na kuchukua hatua inayofaa

• Au vinginevyo kunahitajika na sheria zinazohusika.

unaweza kuwasiliana na kiTengo Cha maadili na makubaliano duniani ya ColgaTe-palmolive.

Lengo la Kitengo cha Maadili ya Colgate-Palmolive ni:

• Kuwapa watu wa Colgate ushauri na kuwasaidia kufafanua jinsi Kanuni ya Maadili mema inaweza kutumika kwa hali fulani.

• Kuwapa watu njia nyingine ya mawasiliano ili watu walete habari kuhusu ukiukaji wa sheria, ama shughuli zinazozozana na Kanuni ya Maadili ya Kampuni.

Huenda ukawasiliana na Maadili na Makubaliano Duniani kupitia Kitengo chetu cha Maadili ya Colgate-Palmolive masaa 24 katika 1-800-778-6080 (Marekani Kaskazini) au 1-212-310-2330 (simu ambayo mpokeaji anailipia kutoka maeneo yote

nje ya Mareka Kaskazini).

Unaweza pia kuwasiliana na Maadili na Makubaliano Duniani kupitia barua-pepe ya kawaida au faksi. Anwani ya kutuma ni:

Global Ethics and Compliance Colgate-Palmolive Company 300 Park Avenue, 8th Floor

New York, NY 10022Anwani ya siri ya barua pepe ni: [email protected]. Namba ya simu ya faksi ya siri ni: 1-212-310-3745.

Page 31: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

KaMpuni ya COlgatE-palMOlivE 29

Tunakuhimiza uwasiliane na Uadilifu na Makubaliano ili kuuliza maswali kuhusu, ama kuripoti ukiukaji wowote unaoshukiwa wa Kanuni ya Maadili mema. Ukiukaji wote ulioripotiwa utachunguzwa haraka. Ni muhimu kwamba watu wanaoripoti wasifanye uchunguzi wao binafsi kwani unaweza kusababisha maswala magumu ya kisheria. Kuchukua hatua mwenyewe kunaweza kuzua mizozo katika uchunguzi na unaweza kuiathiri vibaya sana Colgate nakujiathiri mwenyewe.

Tunakuhimiza kujijulisha unapopiga simu ili kusaidia uchunguzi na kufuatilia. Wakati sheria za kawaida zinaruhusu, unawezakutoa habari kama mtu asiyejukilikana. Kuna sheria katika nchi nyingine ambazo zinakataa aina ya habari unazoweza kuripoti kupitia kwa nambari ya haraka. Kama sheria hizi zinaweza kutumika kwenye hali yako, mwakilishi wa Uadilifu na Makubaliano ya Ulimwengu atakuelekeza kwa mtu katika biashara yako ambaye anaweza kukusaidia na swali lako au hoja.

Kwa sababu ya uchunguzi wa ukiukaji ama ukiukaji wa kushukiwa wa Kanuni ya Maadili mema ama Maongozi ya Shughuli za Biashara, inawezekana kuelekeza data ya kibinafsi iliyochukuliwa kutoka nchi moja au nyingine. Kwa kuendelea, ukiukaji wa kushukiwa ama haswa wa kanuni ya maadili mema ama Mwongozi wa Shughuli za Biashara unaweza kusababisha kuwe na ripoti inayofanywa na Idara ya Uadilifu na Makubaliano ya Ulimwengu ambayo inaweza kuwa na data ya kibinafsi. Katika hali kama hizo, data ya kibinafsi inayotumiwa na wafanyakazi wa Kampuni na wanabiashara wa Colgate katika shughuli za Idara ya Uadilifu na Makubaliano ya Ulimwengu kuchunguza ripoti hiyo, lakini tu kwa muda mfupi kama itakavyotakikana kwa sababu hii (na baadaye data hiyo ya kibinafsi itaondolewa ama itawekwa kama inavyotakikana na sera ya Kampuni ama na sheria).

haTua za kinidhamu zinaweza kuChukuliwa.

Sera ya kampuni ni "kutohimili kabisa" tabia yoyote ambayo inakiuka Kanuni ya Maadili Mema au Mwongozo wa Desturi za Biashara. Hii inamaanisha kwamba wakati tokeo la ukiukaji limethibitishwa, hatua inayofaa italingana na hali na jinsi ukiukaji utakavyochukuliwa. Vivyo hivyo, Kampuni inakusudia kuzuia tukio la tabia isiyolingana na Kanuni au Mwongozo wa Desturi za Biashara na kukomesha tabia yoyote kama hiyo ambayo inaweza kutokea punde tu inapowezekana baada ya utambuaji wake. Watu wa Colgate wanaokiuka Kanuni au Mwongozo wa Desturi za Biashara huenda wakachukuliwa hatua za nidhamu, hadi kujumuisha kusitishwa, kulingana na sheria ya nchini.

kanuni inaTumika kwa shughuli zoTe za waTu wa ColgaTe na kampuni.

Kanuni inatumika kwa kila mtu anayefanya kazi na Kampuni ya Colgate-Palmolive na kampuni zake tanzu, ikiwa ni pamoja na maafisa, na hutumika pia kwa wakurugenzi na mawakala wa Kampuni kulingana na sheria husika. Nakala za Kanuni, zinazopatikana kutoka kwa Idara ya Maadili na Makubaliano Duniani, zinapaswa kupewa watu au mashirika yaliyobaki na kuidhinishwa kushughulikia kwa niaba ya Kampuni katika maeneo ambayo Kanuni inatumika. Watu wa Colgate duniani kote wanaonyesha kujitolea kwao kwa makubaliano na viwango vya uadilifu vya Kampuni kwa kuhusika katika mafunzo na vyeti vya Kanuni ya Maadili Mema kila mwaka.

Page 32: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

30 Kanuni ya Maadili MEMa

Bodi la Wakugurenzi wa Colgate . . . . . . . . . . . 14

Faragha ya Data . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 10

Haki za Kibinaadamu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 23

Hatua ya Kinidhamu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 29

Kanuni ya Maadili Mema ya Watoa huduma . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 15

Kitengo cha Maadili . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 28

Kufanyisha Watoto Wadogo Kazi . . . . . . . . 7, 23

Kujitolea na Kutoa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 23

Kuripoti Ukiukaji Unaoshukiwa . . . . . . . . . . . 28

Kutohimili Kabisa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 29

Kutolipiza Kisasi . . . . . .ndani ya jarida la nyuma

Kuzuia hongo/FCPA . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 21

Kuzuia Unyanyasaji . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 7

Maelezo ya Siri ya Wengine . . . . . . . . . . . . . . . 16

Maelezo Yetu ya Siri . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 9

Maombi ya Vyombo vya habari . . . . . . . . . . . . 11

Mapendeleo . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 7, 9

Mashirika ya Biashara na Viwanda . . . . . . . . . 21

Mazingira Salama ya Kufanya kazi . . . . . . . . . . 7

Mgongano wa Maslahi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 8

Michango ya Kisiasa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 21

Rekodi Sahihi za Kifedha . . . . . . . . . . . . . . . . . 11

Sheria ya Biashara ya Kindani/Amana . . . . . . 20

Sheria za Ushindani/Kutokukiritimba . . . . . . 19

Siri za Uuzaji . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 9, 16

Ubora na Usalama wa Bidhaa . . . . . . . . . . . . . 17

Uendelezaji/Uwajibikaji wa Kijamii . . . . . . . . 25

Ulinzi wa Mali ya Kampuni . . . . . . . . . . . . . . . 12

Usahihi wa Utangazaji . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 17

Usimamiaji Rekodi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 22

Vidhiviti vya Maduhuli/Mahuruji . . . . . . . . . . 22

Vyanzo vya IT/Midia ya Jamii . . . . . . . . . . . . . 12

Wasiliana Nasi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 28

Wateja Wetu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 15

Watumiaji Wetu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 17

Zawadi na Burudani . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 15

KANUNI yA MAADILI MEMA FAhARASA

Page 33: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

KaMpuni ya COlgatE-palMOlivE 31

MASWALI yANAyOULIzWA MARA KWA MARA

S: Ni wapi ninaweza kupata Kanuni ya Maadili Mema ya Colgate?

J: Unaweza kuipata kwenye OurColgate.com na hata pia tovuti ya nje ya Colgate ya www.ColgatePalmolive.com. Kama huwezi kufikia mtandao, unaweza pia kupata nakala kutoka kwa Waajiri Wafanyakazi mahali popote ulimwenguni. Kanuni hiyo inapatikana kwa lugha 40.

S: Nitajuaje viwango vipi vinavyotumika katika eneo la kazi?

J: Colgate inaafikiana na sheria na masharti yote kila mahali tunapofanya kazi. Kwa kuongezea, kunaweza kuwa na sera na desturi maalum za Kampuni ambazo zinashughulikia suala hili. Anza na Kanuni ya Maadili Mema - hakikisha kumuuliza meneja wako, Mwajiri wa wafanyakazi, Maadili na Makubaliano Duniani, au Shirika la Kisheria Duniani kama haupatii jina unalolitafuta.

S: Je, Kanuni ya Maadili Mema inatumika kwa nani?

J: Wafanyi kazi wote wa Colgate katika viwango vyote lazima wafuate Kanuni ya Maadili Mema. Hakuna ubaguzi.

S: Na nikikiuka sera ya Kampuni kwa bahati mbaya?

J: Wafanyi kazi wote wanajukumu la kuhakikisha kwamba hatua zao zinalingana na Kanuni ya Maadili Mema. Hii ndiyo sababu tunakuomba upitie na uhakikishe Kanuni ya Maadili Mema kila mwaka, na ukamilishe mafunzo yoyote yanayohitajika ambayo umepewa. Unatarajiwa pia kuleta maswali au hoja zozote kwa meneja wako, Maadili na Makubaliano Duniania, au Shirika la Kisheria Duniani. Ukichukua hatua ambazo hazilingani na tabia zilizofafanuliwa katika Kanuni au Sera nyingine za Kampuni, kusema kwamba ulikuwa na nia nzuri au kwamba hukujua hatua zako hazikufaa hazitakulinda dhidi ya hatua za kisheria au matokeo ya kisheria.

S: Meneja wangu alinieleza nifanye kitu ambacho ninadhania ni kinyume cha sheria. Je, nifanye nini?

J: Unapaswa kuongea na meneja wako ili uhakikishe kwamba unaelewa ombi. Kama, baada ya mazungumzo hayo, ikiwa bado una wasiwasi, unapaswa kuwasiliana na Maadili na Makubaliano Duniani katika Kitengo cha Maadili ya Colgate-Palmolive au Shirika la Kisheria Duniani ili uripoti hoja zako:

Kitengo cha Maadili ya Colgate-Palmolive [email protected]

1-800-778-6080 (Marekani Kaskazini) 1-212-310-2330 (simu ambayo mwenye kupigiwa anailipia kutoka nje ya Marekani Kaskazini)

1-212-310-3745 (Fax)

Page 34: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

32 Kanuni ya Maadili MEMa

Kumbuka, haikubaliwi kamwe kuvunja sheria, bila kujari ni nani aliyekuambia ufanye hivyo. Usihatarishe kazi yako au sifa za Kampuni kwa kufanya kitu ambacho ni kinyume cha sheria au si cha kimaadili.

S: Ni wapi ninaweza kwenda kwa mafunzo juu ya maswali ya ziada yanayohusiana na makubaliano na maadili?

J: Wasiliana na Waajiri Wafanyakazi wa eneo lako, Elimu na Mafunzo Duniani, Shirika la Kisheria Duniani au Maadili na Makubaliano Duniani.

S: Je, Kanuni hii ya Maadili Mema ni ya siri?

J: Hapana, tunafanya Kanuni yetu ya Maadili Mema ipatikane kwenye tovuti yetu na tunatoa nakala unapoomba.

S: Je, tunatarajia watoa huduma wetu kufuata Kanuni ya Maadili Mema ya Colgate?

J: Tunatarajia watoa huduma wetu kuonyesha kiwango hicho sawa cha juu cha maadili ambacho tunafuata katika kampuni. Kampuni ya Colgate-Palmolive imekuza Kanuni ya Maadili Mema ya Watoa Huduma, ambayo inapatikana kwa lugha kadhaa na inaweza kupatikana kwenye tovuti ya Kampuni yetu chini ya sehemu ya "Fanya kazi na Sisi" ya Watoa huduma.

Page 35: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

KaMpuni ya COlgatE-palMOlivE 33

sera ya kuTolipiza kisasi

Ni sera na desturi ya Colgate kudumisha viwango vya juu zaidi vya kimaadili na kuunda eneo la kazi huru pasipo na tabia isiyofaa au ya kinyume cha sheria ambayo watu wanahimizwa kushiriki hoja zao na Kampuni bila woga wa kulipiziwa kisasi. Vivyo hivyo, katika Colgate, hakuna hatua yoyote mbaya itakayochukuliwa dhidi ya mfanyakazi yeyote, mfanyakazi wa zamani, wakala au mhusika mwingine kwasababu ya kulalamika kuhusu, kuripoti, au kuhusika katika au kusaidia katika uchunguzi wa ukiukaji unaohisiwa wa Kanuni ya Maadili Mema ya Kampuni, sera ya Kampuni au sheria husika, isipokuwa madai au maelezo yaliyotolewa yanaopatikana kuwa ya uwongo unaojulikana. Kwa umbali unaowezekana, Colgate itadumisha siri ya malalamiko yote. Madai yote ya ulipizaji kisasi yatachunguzwa, na kama inafaa, hatua ya

kinidhamu itachukuliwa, ikiwa ni pamoja na kusitishwa kwa ajira.

JIFUNZE • TENDA • ONGEA

Unaweza kuwasiliana na Maadili na Makubaliano Duniani kupitia Kitengo chetu cha Maadili kiko wazi masaa 24

Colgate-Palmolive 1-800-778-6080 (Marekani) au 1-212-310-2330 simu ambayo mwenye kupigiwa anailipia

(Kimataifa), au kupitia barua ya kawaida, barua pepe au faksi

Maadili na Makubaliano Duniani Colgate-Palmolive Company 300 Park Avenue, 8th Floor

New York, NY 10022

[email protected]

001-212-310-3745 (faksi)

Page 36: KANUNI yA MAADILI MEMA - Colgate...Kuafikiana na Kanuni ni rahisi kuhakikisha kwa kutumia uamuzi unaofaa na kutafuta mwongozo wakati maswali jitokeza. Kila mmoja wetu anawajibika kwa

D12-128 5/12

MawasilianoyaKampuni300ParkAvenueNewYork,NY10022-7499