Guide to the Public Housing Tenancy Agreement - Swahili

30
Mwongozo wa Mkataba wa Makazi ya Umma wa Upangaji Swahili

Transcript of Guide to the Public Housing Tenancy Agreement - Swahili

  • Mwongozo wa Mkataba wa Makazi ya Umma wa UpangajiSwahili

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    TAARIFA MUHIMU Tafadhali soma mwongozo huu kabla ya kusaini Mkataba wa Makazi ya Umma wa Upangaji

    Mkataba wa Makazi ya Umma wa Upangaji ni hati ya kisheria ambayo inaelezea haki na wajibu wako kuhusu mali (nyumba na ardhi karibu na nyumba).

    Hii ni msaada wa mwongozo tu, haimufungi mtu kisheria.

    Mwongozo huu unakusaidia kuelewa vizuri Mkataba wa Makazi ya Umma wa Upangaji.

    Hii siyo Mkataba wa Makazi ya Umma wa Upangaji na haifanyi kuwa sehemu ya Mkataba wa Makazi ya Umma wa Upangaji.

    Kama unahitaji ushauri juu ya haki zako na wajibu kama mpangaji, tafadhali pigia Kitengo cha Watumiaji cha Mkoa wa Kaskazini kwa (08) 8999 1999 or 1800 019 319 kabla ya kuweka sahihi kwenye Mkataba wa Makazi ya Umma wa Upangaji.

    Kama una matatizo ya kuelewa mwongozo huu, tafadhali muulize Afisa wako wa Huduma kwa Mteja ili akusaidie au kupanga Mkalimani kwa ajiri yako kabla ya kusaini Mkataba wa Makazi ya Umma wa Upangaji.

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    1. Maombi na kutimiza matakwa Sisi (Makazi) na wewe (mpangaji) lazima kuzingatia Sheria za Makazi ya Upangaji na Sheria ya Makazi.

    Kuna sera kwa ajili ya makazi ya umma. Sera huelezea kwa undani zaidi haki zako na wajibu na sheria ya Makazi juu ya kuishi katika makazi ya umma.

    Unawajibika kutambua sera yoyote tunayokuambia inahusiana na upangaji wako. Kama una maswali yoyote unaweza kuuliza afisa makazi. Unaweza kujifunza zaidi kuhusu sera zetu kwenye tovuti yetu: www.housing.nt.gov.au

    http://www.housing.nt.gov.au

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    2. Misaada ya Masharti ya Upangaji Mkataba inakuwezesha kuishi katika nyumba kwa tarehe ziliyoandikwa katika Mkataba (ukurasa 1) isipokuwa sisi au wewe

    ukimaliza Mkataba mapema.

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    3. Kodi Kodi inatakiwa wiki angalau 1 mapema. Kodi inakatwa siku ya Jumatatu. Kodi lazima kulipwa na malipo ya moja kwa moja

    kutoka Centrelink au benki au moja kwa moja kwa amana yako katika akaunti yetu. Kodi inaweza kulipwa mda wowote (kwa mfano kila wiki, wiki mbili au kila mwezi).

    Tunaweza kuwaambia Centrelink au benki yako kuhusu mabadiliko yoyote ya kodi yako.

    kodi yako inaweza kubadilika, tutakuambia mabadiliko yoyote.

    Utalipa kodi ya soko kama inavyoonekana kwenye Mkataba yako Upangaji. Kama unastahili kwa marupurupu basi kiasi unahitaji kulipa kitakuwa chini.

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    4. Dhamana Sisi tutaweka amana ya usalama (dhamana) wakati wewe wanaoishi katika nyumba.

    Kama kuna matengenezo yoyote, kusafisha au fedha bora zinadaiwa na sisi wakati ukitoka nje ya nyumba, tunaweza kubaki na baadhi au fedha yote ya dhamana.

    Mfano 1: sisi tunaweza kutunza fedha ya dhamana kuchukua nafasi ya kufuli kama hujarudisha funguo yako wakati wa kuondoka. Mfano 2: tutatunza dhamana ya fedha za kulipia kuweza kuchukua takataka zozote zilizobaki juu ya mali wakati wa kuondoka.

    Kama hakuna fedha tunazokudai wakati kuondoka nyumbani kwako, sisi tutarudisha fedha zako ndani ya siku 7 za kazi.

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    5. Huduma na gharama Kama nyumba yako ina meta inayojitegemea ni lazima kulipa matumizi ya maji ukitoa punguzo lolote tunalokupa.

    Kama nyumba yako ina meta inayojitegemea ni lazima kulipa gharama za umeme na gesi katika nyumba yako.

    Kama nyumba yako haina meta inayojitegemea, tunalazimika kulipa kwa ajili ya huduma zote.

    Ni lazima kulipa kwa viwango vya wote, kodi au mashtaka mengine kwa ajili ya mali.

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    6. Habari unazotoa Ni lazima utupe habari sahihi na za ukweli.

    Mfano wa 3: Kama ukipata kazi, ni lazima utwambie juu ya badiliko la mshahara. Mfano wa 4: Kama mtu akihamia au nje ya makazi yako, ni lazima utwambie kuhusu mabadiliko hayo.

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    7. Matumizi ya majengo yako Eneo lazima kutumika kama nyumbani kwako pa kuishi. Usipatunze bila sababu kwa uchafu Tuambie kuhusu matengenezo yoyote yanayotakiwa kwenye nyumba. Lazima wasiliana na ofisi ya eneo lako kwaa 1800 104 076

    kuripoti matengenezo. Tuambia kuhusu madhara yoyote au kama unadhani uharibifu wowote unaweza kutokea kwenye nyumba yako. Ni lazima

    kuwasiliana na ofisi ya eneo lako kwa 1800 104 076 kuripoti uharibifu. Mfano 5: Ni lazima kutoa taarifa kama maji yanavuja maana yanaweza kusababisha kiasi kikubwa cha uharibifu wa nyumba na unaweza kutakiwa kulipia maji ya ziada.

    Usijenge au kubadilisha chochote kwenye nyumba yako bila ruhusa ya maandishi. Kwa mfano 6: kama unataka kujenga nyumba ya nyuma ni lazima kupata ruhusa kwa maandishi kutoka kwetu.

    Usisumbue majirani wako.Mfano 7: Kuliza sauti kubwa zinasumbua majirani.

    Usitumie nyumba yako kwa shughuli za kinyume cha sheria. Mfano wa 8: kutunza vitu vilivyoibiwa nyumbaji au sehemu yoyote kwenye nyumba ni kinyume cha sheria.

    Lazima upime na kusafisha kengele ya moshi katika nyumba angalau kila baada ya miezi 12. Lazima kutuambia kama kengele ya moshi haifanyi kazi na ni lazima turudishie nyingine. Lazima kuacha kuifanya kengele ya moshi isifanye kazi. Wasiliana na ofisi ya eneo lako kama huna uhakika nini cha kufanya.

    Lazima kupata kibali chetu kubadili kufuli na kutupa ufunguo haraka kama unaweza, isipokuwa tukikwambia vinginevyo. Lazima usitukane matusi au vurugu kwa watu wengine.

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    8. Dhima ya uwakilishi wako Kama ukiruhusu mtu kutembelea nyumba yako na wao kufanya kitu chochote ambacho si sambamba na matumizi yako

    ya nyumbani (sehemu 7 hapo juu), unahusika isipokuwa ni kitendo cha unyanyasaji wa majumbani au familia.

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    9. Mkataba wa Tabia Zinazokubalika Shirika la Makazi linachukulia baadhi ya tabia ya kutokuwa za ustarabu. Tabia zisizokuwa za ustarabu ina maana kwamba

    ni tabia za matusi au vurugu, au ambazo zinajenga kero kwa watu wanaoishi karibu na wewe. Pia znahusisha uvunjaji wa sheria, ubaya au uharibifu.

    Kama wewe, wageni au watu waliotajwa katika mkataba wa upangaji wanaenenda katika njia ambayo shirika la Makazi linaamini kuwa siyo tabia nzuri, tunaweza kukutaka wewe kuingia katika Mkataba Kubadili Tabia.

    Mkataba Tabia Zinazokukubalika ni makubaliano kati ya wewe na Shirika la Makazi ambayo unakubaliana kwamba huwezi kujiingiza katika tabia zisizofaa katika sehemu ya nyumba na sehemu yoyote ndani ya mita 50 ya nyumba. Makubaliano ni halali kwa kipindi cha muda fulani.

    Kama huingia moja au kama wewe ukivunja Mkataba wa Tabia ya Kukubalika tunaweza kuangalia jinsi ya kumaliza upangaji wako.

    Kama ungependa msaada wa jinsi ya kusimamia wageni wako au watu wengine wanaoishi na wewe, wasiliana na ofisi ya eneo lako kwa msaada.

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    10. Mamlaka maalum ya watumishi wa umma wa Usalama wa Makazi Sisi hutumia watumishi wa umma wa Makazi ya Usalama ili kukusaidia kutatua tabia zizizofaa katika makazi ya umma.

    Kutoa taarifa ya tabia zisizofaa wakati wa masaa ya kazi, wasiliana na watumishi wa umma wa Usalama wa Makazi kwa 1800 685 743.

    Kama mambo ni ya haraka au unaita nje ya masaa ya kazi, tafadhali wasiliana Polisi juu ya 131 444.

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    11. Wakaaji wanaotambulika Wakaaji wanaotambulika ni watu ambao umetwambia kuwa wataishi nawe nyumbani. Wewe unahusika kwa tabia zao.

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    12. Matakwa yetu ya jumla Tutahakikisha kuwa nyumba yako inastahili kwa ajiri ya kuishi, salama, na safi kwa kiasi kikubwa wakati unahamia.

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    13. Vyumba zilizo wazi Una haki ya nyumba kuanzia tarehe ya mwanzo ya Mkataba wa Nyumba.

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    14. Kufurahia ukimya Unaweza kutarajia kufurahia ukimya wa nyumba yako bila kulazimika kusumbuliwa na sisi.

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    15. Kuweza kwetu kuingia kwenye nyumba Tunaweza kuja kwenye nyumba yako kuweza:

    Kukusanya kodi

    Kufanya ukaguzi

    Kufanya matengenezo

    Kuangalia kama matengenezo yamefanyika

    Kuandaa ripoti ya mazingira

    Kuonyesha nyumba kwa mpangaji au mununuzi anayetarajiwa

    Ni lazima kufuata sheria za Sheria Makazi ya Upangaji kuhusu mda gani tunaweza kuingia na kiasi gani cha mda wa ujumbe ni lazima kukupa kabla ya kuingia.

    Tunaweza kuingia nyumba yako kwa ajili ya dharura au kama tunafikiria kama kuna uharibifu au uwezekano wa uharibifu.

    Tunaweza kuingia nyumba yako kama wewe ukitutaka au kuturuhusu sisi.

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    16. Ukarabati na matengenezo Sisi tutadumisha nyumba yako katika hali nzuri ya kutengeneza. Tunaweza kukuuliza kulipa gharama za kurekebisha

    uharibifu unaosababishwa au kuruhusiwa na wewe.

    Kama hatuwezi kurekebisha matengenezo ya dharura ndani ya siku 14 unaweza kuuliza Mahakama husika kututaka kutufanya hivyo.

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    17. Ulinzi wa nyumba yako Ni lazima tuulize ruhusa yako kabla ya kubadilisha kufuli. Kama tukibadilisha kufuli bila ruhusa yako, tutakupa ufunguo.

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    18. Dhamana ya uwakilishi wetu Matendo ya watu kwa niaba yetu yanatakiwa kuchukuliwa kama matendo yetu.

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    19. Bima Tunahusika kwa bima ya nyumba.

    Hatuhusiki kwa vitu unavyovimiliki au kukata bima ya vifaa vyako.

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    20. Fidia Hauwezi kutulalamikia au kuomba fidia wakati wewe au mtu unayehusika naye wakati akivunja mkataba. Hii inajumuisha:

    Uzembe au matendo ya kinyume cha sheria.

    Uharibifu au upotevu wa jengo.

    Maumivu au kifo ambacho kimetokea ambapo wewe au mtu ambaye unahusika kwake ameshidwa kuhusika au kuchangia inavyotakiwa.

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    21. Ukomesaji Kama wewe una tatizo la kudumisha upangaji wako, Shirika la Makazi linawezakukusaidia, au kukuelekeza kwnye huduma

    mbalimbali za msaada. Uliza Afisa makazi kwa msaada.

    Unaweza kusitisha Mkataba huu kwa kutupatia taarifa ya siku 14.

    Tunaweza kukomesha Mkataba huu kwa kutoa taarifa ya siku 42.

    Kama wewe una deni zaidi ya siku 14 ya kodi tunaweza kuhitaji wewe kulipa kiasi cha deni kwa tarehe tunayokupangia. Kama una shida kulipia huduma za kodi, tafadhali wasiliana na ofisi ya eneo lako mara moja kujadili jinsi ya kuingia katika mkataba wa kulipa kiasi hicho cha deni.

    Kama hulipi kodi unayodaiwa tunaweza kutafuta kumaliza upangaji wako. Tafadhali wasiliana na ofisi ya eneo lako ili kujadili jinsi gani tunaweza kukusaidia.

    Kama ukivunja muda wa Mkataba tunaweza kukuuliza uweze kurekebisha. Kama ukishidwa kurekebisha, tunaweza kutafuta kumaliza upangaji wako.

    Sisi au wewe unaweza unawea kusimamisha Mkataba kwa taarifa ya siku 2 kama nyumba yako haijawa tayari kupatikana kwa zaidi ya siku 3 kutokana na mafuriko au kuishi katika nyumba ni tishio kwa afya za watu au usalama au haistahili kwa kuishi.

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    22. Kurudisha nyumba Mwisho wa mkataba wako unalazimika kurudisha nyumba kwetu katika hali nzuri na usafi unaostahili.

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    23. Kutelekezwa majengo na bidhaa Kama tunafikiri kwamba umetelekeza nyumba yako na hujalipa kodi, tunaweza kuchukua milki ya nyumba yako au kutuma

    ombi kwa mahakama kuchukua milki ya nyumba yako.

    Kama ukiacha bidhaa nyumbani baada ya kuitelekeza, tutaharibu mali yoyote ambayo iko chini ya thamani ya gharama ya kuhifadhi na kuuza.

    Bidhaa ambayo ni ya thamani zaidi kuliko gharama ya kuhifadhi na kuziuza itaweza kuhifadhiwa kwa muda wa siku 14. Tutakujulisha uweze kuvikusanya.

    Kama ukija na kuchukua bidhaa, unahitaji kutulipa gharama kwa ajili ya matangazo, kuondolewa na kuhifadhi.

    Kama huwezi kuchukua bidhaa, tutavihifadhi kwa siku 30 na kisha kuviuza.

    Wakati sisi tunauza bidhaa, tutabaki na kiasi cha gharama cha kutangaza, kuhifadhi na kuuza bidhaa yako. Tunaweza pia kuweka fedha yoyote ambayo wewe deni kwetu. Tutakupa fedha yoyote itakayobaki.

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    24. Utoaji taarifa Wakati tunataka kukwambia chochote, tutakwambia wewe binafsi au kukutumia taarifa kwa barua.

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    25. Mazoezi Hauruhusiwi kukodisha nyumba yako kwa mtu mwingine bila ruhusa yetu ya maandishi.

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    26. Mikataba ya Makazi iliyopita Mkataba huu unarudiria Mkataba wa mara ya mwisho mbao ulisaini na sisi.

    Kama ulisaini Mkataba huu na kubaki katika nyumba hiyo tutatumia Hali ya Ripoti zilizopo kama ushahidi wa hali ya nyumbanilabda kama tukiandaa mwingine mpya. Tutakukaribisha uwepo wakati tunakagua nyumba.

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    27. Tofauti Mkataba wa makazi unaweza kubadilika tu kama sisi wote tukikubaliana kwa maandishi.

  • Guide to the Public Housing Tenancy Agreement

    28. Ufafanuzi na tafsiri Sehemu hii inatoa maelezo na maana ya maneno muhimu na misemo yaliyotumika ndani ya Mkataba wa Upangaji.

    Button 15: Button 16: Button 17: Button 100: Button 19: Button 99: Button 21: Button 98: Button 23: Button 97: Button 25: Button 96: Button 27: Button 95: Button 29: Button 94: Button 31: Button 93: Button 33: Button 92: Button 35: Button 91: Button 37: Button 90: Button 39: Button 89: Button 41: Button 88: Button 43: Button 87: Button 45: Button 86: Button 47: Button 85: Button 49: Button 84: Button 51: Button 83: Button 53: Button 82: Button 55: Button 81: Button 57: Button 80: Button 59: Button 79: Button 61: Button 78: Button 63: Button 77: Button 65: Button 76: Button 67: Button 75: Button 73: Button 74: Button 72: