Guide To Kumlisha mtoto zaidi kadiri anavyokua Kumbuka ... · Kati ya umri wa miezi 6 na miaka 2...

2
Kati ya umri wa miezi 6 na miaka 2 mtoto bado huhitaji maziwa ya mama kila siku ili kupata nishati na virutubishi muhimu. Kama mtoto hanyonyeshwi atahitaji kikombe 1 au 2 vya maziwa mengine kila siku mpaka atimize miaka miwili au zaidi. Kama maziwa hayapatikani mpe mtoto milo miwili ya ziada. Epuka kumpa mtoto vinywaji ambavyo havina virutubishi kwa mfano chai, kahawa, soda na vinywaji vya rangi na sukari (juisi bandia). Mpe mtoto maji ya matunda halisi (juisi) kwa kiasi. Maziwa freshi ya wanyama na maji anayopewa mtoto lazima yachemshwe. Mpe mtoto maji safi na salama kila siku kukidhi kiu yake. Daima tumia kikombe kilicho wazi kumlishia mtoto. Usitumie chupa au vikombe vyenye mifuniko yenye vitundu vidogo kwani ni vigumu kuvisafisha. Kuongezeka uzito ni kiashiria cha afya bora na hali nzuri ya lishe. Endelea kumpeleka mtoto kwenye kliniki ya watoto kila mwezi ili kuchunguza afya, kupata chanjo na kufuatilia ukuaji na maendeleo yake. Mtoto akiwa mgonjwa apewe milo midogo mara kwa mara pamoja na vinywaji kwa wingi ukijumuisha maziwa ya mama. Mhimize mtoto ale vyakula vya aina mbalimbali hasa vile ambavyo anavipendelea. Mara mtoto apatapo nafuu au kupona ongeza kiasi cha chakula na idadi ya milo. Guide To Ulishaji wa Mtoto Baada ya Miezi Sita Kumbuka: Kumlisha mtoto zaidi kadiri anavyokua Both technical and financial support for the development of this brochure was provided by the Quality Assurance Project (QAP), managed by University Research Co., LLC (URC), under USAID Contract Number GPH-C-00-02-00004-00. September 2005 Anza kumpa mtoto chakula cha nyongeza anapotimiza miezi 6 Nini: Uji au chakula kilichopondwa vizuri Mara ngapi: Mara 2 kila siku Kiasi gani: Mlishe vijiko vya chakula 2-3 kila mlo Umri wa miezi 7 – 8 Nini: Chakula kilichopondwa Mara ngapi: Mara tatu kwa siku Kiasi gani: Mlishe theluthi mbili (2/3) ya kikombe kila mlo (kikombe 1=mls 250) Umri wa miezi 9 – 12 Nini: Chakula kilichokatwa vipande vidogo vidogo au kilichopondwa na vile ambavyo mtoto anaweza kushika mwenyewe. Mara ngapi: Mara 3 kila siku pamoja na asusa moja. Kiasi gani: Mlishe robo tatu (3/4) ya kikombe kila mlo (kikombe 1=mls 250) Umri wa miezi 12 – 24 Nini: Vyakula vinavyoliwa na familia, vikatwe- katwe au kuponda kama inahitajika. Mara ngapi: Mara 3 kila siku pamoja na asusa mbili Kiasi gani: Mlishe kikombe kilichojaa kila mlo (kikombe 1=mls 250)

Transcript of Guide To Kumlisha mtoto zaidi kadiri anavyokua Kumbuka ... · Kati ya umri wa miezi 6 na miaka 2...

Page 1: Guide To Kumlisha mtoto zaidi kadiri anavyokua Kumbuka ... · Kati ya umri wa miezi 6 na miaka 2 mtoto bado huhitaji maziwa ya mama kila siku ili kupata nishati na virutubishi muhimu.

✽ Kati ya umri wa miezi 6 na miaka 2 mtoto badohuhitaji maziwa ya mama kila siku ili kupatanishati na virutubishi muhimu. Kamamtoto hanyonyeshwi atahitaji kikombe1 au 2 vya maziwa mengine kila siku mpakaatimize miaka miwili au zaidi. Kama maziwahayapatikani mpe mtoto milo miwili ya ziada.

✽ Epuka kumpa mtoto vinywaji ambavyo havinavirutubishi kwa mfano chai, kahawa, soda navinywaji vya rangi na sukari (juisi bandia). Mpemtoto maji ya matunda halisi (juisi) kwa kiasi.

✽ Maziwa freshi ya wanyama na maji anayopewamtoto lazima yachemshwe. Mpe mtoto majisafi na salama kila siku kukidhi kiu yake.

✽ Daima tumia kikombe kilicho wazi kumlishiamtoto. Usitumie chupa au vikombe vyenye mifunikoyenye vitundu vidogo kwani ni vigumu kuvisafisha.

✽ Kuongezeka uzito ni kiashiria cha afya bora nahali nzuri ya lishe. Endelea kumpeleka mtoto kwenyekliniki ya watoto kila mwezi ili kuchunguza afya, kupata chanjona kufuatilia ukuaji na maendeleo yake.

✽ Mtoto akiwa mgonjwa apewe milo midogo mara kwa marapamoja na vinywaji kwa wingi ukijumuisha maziwa ya mama.Mhimize mtoto ale vyakula vya aina mbalimbali hasa vile ambavyoanavipendelea. Mara mtoto apatapo nafuu au kupona ongezakiasi cha chakula na idadi ya milo.

Guide To

Ulishaji waMtoto

Baada ya Miezi Sita

Kumbuka:Kumlisha mtoto zaidi kadiri anavyokua

Both technical and financial support for the development of this brochure was provided by theQuality Assurance Project (QAP), managed by University Research Co., LLC (URC), under USAID

Contract Number GPH-C-00-02-00004-00. September 2005

Anza kumpa mtoto chakula chanyongeza anapotimiza miezi 6Nini:Uji au chakula kilichopondwa vizuriMara ngapi:Mara 2 kila sikuKiasi gani:Mlishe vijiko vya chakula 2-3 kila mlo

Umri wa miezi 7 – 8Nini:Chakula kilichopondwaMara ngapi:Mara tatu kwa sikuKiasi gani:Mlishe theluthi mbili (2/3) ya kikombekila mlo (kikombe 1=mls 250)

Umri wa miezi 9 – 12Nini:Chakula kilichokatwa vipande vidogovidogo au kilichopondwa na vile ambavyomtoto anaweza kushika mwenyewe.Mara ngapi:Mara 3 kila siku pamoja na asusa moja.Kiasi gani:Mlishe robo tatu (3/4) ya kikombe kilamlo (kikombe 1=mls 250)

Umri wa miezi 12 – 24Nini:Vyakula vinavyoliwa na familia, vikatwe-katwe au kuponda kama inahitajika.Mara ngapi:Mara 3 kila siku pamoja na asusa mbiliKiasi gani:Mlishe kikombe kilichojaa kila mlo(kikombe 1=mls 250)

Page 2: Guide To Kumlisha mtoto zaidi kadiri anavyokua Kumbuka ... · Kati ya umri wa miezi 6 na miaka 2 mtoto bado huhitaji maziwa ya mama kila siku ili kupata nishati na virutubishi muhimu.

Chepesi namaji maji

Uzito mzuri

Baada ya Miezi Sita

Nahitaji kufahamu nini?✽ Mpe mtoto chakula laini ulichomwanzishia, kijiko kimoja au viwili

vya chakula mara mbili kila siku. Ongeza uzito, kiasi na aina zavyakula taratibu kadiri mtoto anavyokua. Kwa kuanzia, chakulacha mtoto kiwe laini, lakini kisiwe chepesi au cha majimaji sana.

Mtoto anapoanza kula✽ Ni muhimu kumnyonyesha mtoto

maziwa ya mama pekee maraanapozaliwa hadi anapotimiza umriwa miezi sita. Hii ina maanakwamba mtoto asipewe maziwamengine yoyote, vyakula au vinywajiikiwa ni pamoja na maji.

✽ Baada ya miezi 6 maziwa ya mamapekee hayatoshelezi mahitaji yamtoto. Hivyo mtoto aanze kulishwataratibu vyakula vya aina mbalimbaliili aweze kukua vizuri.

✽ Maziwa ya mama bado huendeleakuwa sehemu muhimu ya chakulacha mtoto mpaka atimize angalauumri wa miaka miwili.

✽ Wakati wa kumlisha mtoto mwenyeumri kati ya miezi 6 na 12, daimampe maziwa kwanza kabla yakumpa chakula kingine.

✽ Mtoto ana tumbo dogo hivyohuweza kula chakula kidogo kwamara moja ni vyema alishwe marakwa mara.

✽ Kama mama ana virusi vya UKIMWI,inawezekana ikawa bora zaidikumwachisha mtoto kunyonyamaziwa ya mama anapotimiza umriwa miezi 6 na kumpa aina nyingineya maziwa yanayofaa. Ni muhimuaombe ushauri kwa mtoa hudumawa afya ili apewe maelezo zaidi.

Utayarishaji na uhifadhi salamawa chakula cha mtoto:

✽ Kadiri mtoto anavyozoea kula na kutafuna, aanze taratibukula vyakula vilivyopondwa na vigumu kiasi.

✽ Boresha uji au chakula cha mtoto kwa kutumia maziwa,karanga zilizokaangwa au mbegu nyingine za mafuta.

✽ Pamoja na vyakula vikuu kama uji, wali, ndizi naviazi vya kuponda, pia mtoto huhitaji vyakula vyaasili ya mikunde, nyama, kuku, samaki au mayaikila siku. Mboga za majani na matundahumpatia virutubishi muhimu.

✽ Ni muhimu kumpatia mtotomafuta na sukari kwa kiasi ilikuongeza kiasi cha nishatikwenye chakula. Mafuta piahusaidia usharabu wa baadhiya vitamini na huongeza ladhaya chakula.

✽ Matumizi ya unga wa kimeaau vyakula vilivyochachushwahuongeza ubora uyeyushwajiwa chakula na usharabu wavirutubishi.

✽ Mama na walezi waoshe mikonoyao kwa sabuni na maji ya kutoshayanayotiririka kabla ya kutayarishachakula na kumlisha mtoto. Vile vilebaada ya kwenda chooni au kum-hudumia mtoto aliyejisaidia. Mikonoya mtoto ni lazima ioshwe pia.

✽ Vyombo vyote vilivyotumika kutaya-risha chakula na kumlishia mtoto kablaya kuvitumia vioshwe kwa sabuni namaji yanayotiririka. Vihifadhiwe vikiwavimefunikwa. Epuka kutumia chupa yakumlishia mtoto au vikombe vyenyetundu dogo kwani ni vigumu kuvisafisha.

✽ Tayarisha chakula katika mazingira safina kifunikwe ili kuzuia wadudu nauchafu. Mtoto anapaswa kuwa nachombo chake cha kulia chakula. Nimuhimu kumlisha mtoto chakula marabaada ya kutayarishwa. Mtoto asipewemabaki katika mlo unaofuata.

✽ Mtoto ajifunze taratibu kulamwenyewe. Hata hivyo, inabidiasimamiwe na mtu mzima au mtotomkubwa ili kuhakikisha amekulachakula cha kutosha na chakulakinabakia kuwa safi.