GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA · PDF fileSerikali za Mitaa, uwezo wake, kazi na...

47
1 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR (Hupigwa Chapa kwa Amri ya Serikali) Sehemu ya CXXII Nam. 6489 23 Oktoba, 2014 Bei Shs. 3,000/= Imekubaliwa na Mkuu wa Posta kuwa ni Gazeti Hutolewa kila Ijumaa YALIYOMO Ukurasa Mswada wa Sheria ya Kufuta Sheria ya Baraza la Manispaa Nam. 3 ya Mwaka 1995 na Sheria ya Halmashauri za Wilaya na Mabaraza ya Miji Nam. 4 ya Mwaka 1995 na kuanzisha upya Sheria ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, Zanzibar ya Mwaka 2014, kwa madhumuni ya kuanzisha Serikali za Mitaa, uwezo wake, kazi na wajibu, muundo, mpangilio, fedha na mambo mengine yanayohusiana na hayo................................................................. 000 SEHEMU YA SHERIA Tangazo la Mswada uliyotajwa hapo chini umetangazwa katika Gazeti Rasmi hili Tangazo la Mswada Nam. :- Mswada wa Sheria ya Kufuta Sheria ya Baraza la Manispaa Nam. 3 ya Mwaka 1995 T A N G A Z O Mswada ufuatao utawasilishwa katika Mkutano wa Baraza la Wawakilishi utakaoanza tarehe 22 Oktoba, 2014 kwa shahada ya dharura na unachapishwa pamoja na Madhumuni na Sababu zake kwa ajili ya kutoa taarifa kwa wananchi. ZANZIBAR (Dkt. ABDULHAMID Y. MZEE) 23 Oktoba, 2014 Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi. Matangazo yaliyohusu maiti, kuvunjika kwa Ushirika na baadhi ya matangazo ambayo ni muhimu kwa watu kujua yanaweza kutiwa katika Gazeti. Nakala matangazo namna hiyo, zipelekwe kwa Mhariri wa Gazeti Rasmi la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar - Tanzania katika nyumba ya kupiga Chapa, Sanduku la Posta 261. Nakala zisichelewe kuliko Jumatatu kila wiki. Gazeti Makhsusi

Transcript of GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA · PDF fileSerikali za Mitaa, uwezo wake, kazi na...

1

GAZETI RASMI LA SERIKALI YAMAPINDUZI YA ZANZIBAR

(Hupigwa Chapa kwa Amri ya Serikali)

Sehemu ya CXXII Nam. 6489 23 Oktoba, 2014 Bei Shs. 3,000/=Imekubaliwa na Mkuu wa Posta kuwa ni Gazeti Hutolewa kila Ijumaa

YALIYOMO Ukurasa

Mswada wa Sheria ya Kufuta Sheria ya Barazala Manispaa Nam. 3 ya Mwaka 1995 na Sheriaya Halmashauri za Wilaya na Mabaraza ya MijiNam. 4 ya Mwaka 1995 na kuanzisha upyaSheria ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, Zanzibarya Mwaka 2014, kwa madhumuni ya kuanzishaSerikali za Mitaa, uwezo wake, kazi na wajibu,muundo, mpangilio, fedha na mambo mengineyanayohusiana na hayo................................................................. 000

SEHEMU YA SHERIA

Tangazo la Mswada uliyotajwa hapo chini umetangazwa katika GazetiRasmi hili

Tangazo la Mswada

Nam. :- Mswada wa Sheria ya Kufuta Sheria ya Baraza la ManispaaNam. 3 ya Mwaka 1995

T A N G A Z O

Mswada ufuatao utawasilishwa katika Mkutano wa Baraza laWawakilishi utakaoanza tarehe 22 Oktoba, 2014 kwa shahada ya dharura naunachapishwa pamoja na Madhumuni na Sababu zake kwa ajili ya kutoataarifa kwa wananchi.

ZANZIBAR (Dkt. ABDULHAMID Y. MZEE)23 Oktoba, 2014 Katibu wa Baraza la Mapinduzi na

Katibu Mkuu Kiongozi.

Matangazo yaliyohusu maiti, kuvunjika kwa Ushirika na baadhi ya matangazo ambayo ni muhimu kwa watu kujuayanaweza kutiwa katika Gazeti. Nakala matangazo namna hiyo, zipelekwe kwa Mhariri wa Gazeti Rasmi la Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar - Tanzania katika nyumba ya kupiga Chapa, Sanduku la Posta 261. Nakala zisichelewe kulikoJumatatu kila wiki.

Gazeti Makhsusi

2

Jina fupina kuanzakutumika.

GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR 23 Oktoba, 2014

Ufafanuzi.

MSWADAwa

SHERIA YA KUFUTA SHERIA YA BARAZA LA MANISPAA NAM. 3YA MWAKA 1995 NA SHERIA YA HALMASHAURI ZA WALAYA

NA MABARAZA YA MIJI NA NAM. 4 YA MWAKA 1995 NAKUANZISHA UPYA SHERIA YA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA

MITAA, ZANZIBAR YA MWAKA 2014, KWA MADHUMUNI YAKUANZISHA SERIKALI ZA MITAA, UWEZO WAKE, KAZI NA

WAJIBU, MUUNDO, MPANGILIO , FEDHA NA MAMBOMENGINE YANAYOHUSIANA NA HAYO

SEHEMU YA KWANZAMASHARTI YA UTANGULIZI

1. Sheria hii itajulikana kama Sheria ya Mamlaka ya Serikali za MitaaZanzibar ya mwaka 2014 na itaanza kutumika baada ya kutangazwa na Wazirikatika Gazeti Rasmi.

2. Katika sheria hii isipokuwa kama itaelezwa vyenginevyo:

“Afisa” maana yake ni mtu yeyote aliyeajiriwa na mamlaka ya mtaakufanyakazi kwa niaba ya mamlaka hiyo na inajumuisha mtumishiwa Baraza;

“Afisa aliyeidhinishwa” maana yake ni afisa aliepewa uwezo naMamlaka kwa mujibu a masharti ya sheria hii;

“Ardhi” inajumuisha ardhi iliyofunikwa na maji, vitu vyotevinavyomea ardhini, majengo pamoja na vitu vyengine vya kudumuvilivyoshikamana na ardhi;

“Baraza” maana yake ni Baraza kama lilivyoanzishwa kwa mujibuwa kifungu cha 17 cha Sheria hii;

“Baraza la jiji” maana yake ni Baraza lililoanzishwa katika eneo lamjini kwa mujibu wa Kifungu cha 18 cha sheria hii;

“Diwani” maana yake ni Diwani kama alivyotajwa ndani ya sheriaya Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Namba 11 ya 1984;

“Eneo” pale litakapotumika kuhusiana na mamlaka yoyote ya serikaliya mitaa, maana yake ni eneo ambalo mamlaka ya serikali yamtaa imeanzishwa au mamlaka ya serikali ya mitaa zimepewauwezo wa kutekeleza kazi zake kwa mujibu wa sheria hii;

“Idara” maana yake Idara iliyoanzishwa kwa mujibu wa mashartiya kifungu cha 56 cha sheria hii;

3GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR23 Oktoba, 2014

“Jengo” linajumuisha ujenzi wowote katika namna yoyote, na sehemuyoyote ya jengo;

“Kamati” maana yake ni kamati ya Baraza kama ilivyotajwa katikavifungu 51 na 53 vya sheria hii;

“Katibu” kuhusiana na mamlaka ya mtaa maana yake ni Mkurugenziwa Mamlaka ya mtaa huo;

“Mahala” inajumuisha ardhi yeyote, jengo, chumba, miundo, hema,gari, vyombo vya moto, mitaro, maziwa, madimbwi, mabwawa,michirizi au handaki likiwa la wazi au lililozingirwa ama labinafsi au kwa matumizi ya jamii;

“Mahala pa umma” inajumuisha barabara, mtaa, njia, sehemu ya kupitakwa miguu, kichochoro, barabara nyembamba, sehemuiliyotengwa, sehemu ya wazi, bustani, eleo la kuegesha gari,sehemu iliyozibwa na iliyowekwa na mamlaka ya mitaa kwamujibu wa sheria hii;

“Makamo Mwenykiti” maana yake ni msaidizi Mwenyekiti waBaraza;

“Mamlaka ya Jiji” maana yake ni Baraza lililoanzishwa katika eneola mjini kwa mujibu wa masharti ya sheria hii;

“Mamlaka ya mjini” maana yake na ikijumuisha Jiji, Manispaa auBaraza la Mji;

“Mamlaka ya Mtaa” maana yake ni mamlaka ya Baraza;

“Mamlaka ya Serikali za Mitaa” maana yake ni mamlaka yenyemipaka ya kuongoza ambayo inajitegemea na uwezo wautekelezaji wa wajumbe wa Baraza na watumishi;

“Manispaa” maana yake Baraza lililoanzishwa katika eneo la mjinikwa mujibu wa masharti ya sheria hii;

“mapato” kuhusiana na mamlaka ya mtaa, inajumuisha mfuko mkuu,viwango vyote, michango ya serikali na mapato mengineyo,yanayotokana na makusanyo ya ardhi au kazi, au kutokana navyanzo vyengine , vitavyopatikana na Mamlaka ya mtaa;

“Maudhi” maana yake ni shughuli yoyote, utendaji, kazi, tendo,uzembe au jambo ambalo athari yake juu, ndani, au chini ya ardhiambalo ni kero, lina madhara au linachafua au kuhatarisha afyaya jamii, usalama na amani ya jamii , usumbufu kwa jamii aulinaloathiri uchumi wa mtaa au wa kitaifa;

“Meya” maana yake ni kiongozi wa Jiji au Manispaa anaechaguliwamiongoni mwa Madiwani;

4

“mfanyakazi” inajumuisha afisa, mfanyakazi wa kushikizwa,waajiriwa wa muda na afisa aliyeidhinishwa;

“Mfuko wa Serikali za Mitaa” maana yake ni mfuko maalumuulioanzishwa kama ni mfuko wa ruzuku kutoka Serikali nawafadhili, ulioelekezwa moja kwa moja katika kutumika kwauanzilishaji wa maendeleo ya Serikali za Mitaa;

“Mkurugenzi” kuhusiana na Jiji, Manispaa, Mji na halmashauri yaWilaya maana yake ni Mkurugenzi aliyeteuliwa kwa mujibu wamasharti ya kifungu cha 38 cha Sheria hii;

“Mkuu wa Idara” maana yake ni Afisa aliyeteuliwa kuongoza idarazilizotajwa ndani ya vifungu vya sheria hii;

“Mwenyekiti” maana yake ni Mwenyekiti wa Baraza aliyechaguliwakwa ajili ya Baraza;

“Polisi Wasaidizi” maana yake ni mtu mwenye mafunzo ya msingiyanayofanana na ya polisi anaefanya kazi kwa niaba na chini yaudhibiti wa Mamlaka ya mtaa Zanzibar;

“Rais” maana yake ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi;

“Serikali” maana yake ni Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;

“Wadi” maana yake ni mgawanyo wa mipaka ya mamlaka ya mtaailiyowekwa kwa mujibu wa masharti ya sheria hii;

“Waziri” maana yake ni Waziri anaehusika na Serikali za Mitaa;

SEHEMU YA PILIMISINGI INAYOONGOZA

3.-(1) Mamlaka ya Serikali za mitaa ni ngazi za chini ya serikali yaZanzibar iliyo na idadi ya mabaraza ya Serikali za mitaa zilizo huru nakuanzishwa kwa mujibu wa masharti ya Sheria hii.

(2) Kuanzishwa kwa Serikali za mitaa itategemea misingi ya wamadadiliko ya uongozi wa kidemokrasia unaohitaji mgawanyiko wa mamlakana uwezo kwa ngazi ya chini ya serikali kwa kuwafikia watu.

4.-(1) Kwa masharti ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na vifunguvya Sheria hii, Waziri atapendekeza kwa Rais kuigawa Zanzibar katika idadiya Serikali za Mitaa.

(2) Mipaka ya mabaraza ya Serikali za Mitaa yatajumuisha ardhiyote na maeneo yanayofanya vijiji vya Shehia za mashamba, mitaa na maenoya shehia za mjini.

GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR 23 Oktoba, 2014

Mamlakaya serikaliza mitaa.

Eneo lamamlakayaSerikaliya mitaa.

5

(3) Mipaka ya kila Serikali ya Mtaa itaainishwa kwa mujibu wamasharti ya Sheria hii.

5.-(1) Mamlaka ya Serikali ya Mitaa itaendeshwa na watu na itafanyakazi zake kwa kuzingatia matakwa ya watu kwa kuzingatia na kufuata taratibuzilizoainishwa katika sharia hii na sheria nyengine yoyote inayotumika.

(2) Mamlaka ya Serikali ya Mtaa yatakuwa katika kila Baraza laSerikali ya Mtaa ambayo itakuwa na hadhi ya kisheria na haki ya kushitakina kushitakiwa kwa jina lake.

(3) Mamlaka ya kila Baraza la Serikali ya Mtaa yatafanywa kwakufuata demokrasia na uwakilishi wa taasisi za Serikali zilizoanzishwa kwamujibu wa masharti ya Sheria hii.

6.-(1) Mamlaka ya Serikali ya Mtaa itaongonzwa na watu na itatekelezwakwa mujibu wa matarajio ya watu kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa katikaSheria hii na Sheria nyengine zozote zinazotumika.

(2) Vyanzo vya Sheria katika mamlaka ya Serikali ya Mtaa vitakuwa:

(a) Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984;

(b) Sheria husika zinazotumika Zanzibar;

(c) Sheria ya Serikali za Mitaa;

(d) Maamuzi ya Mahakama Kuu; na

(e) Sheria ndogo ndogo za Serikali ya Mtaa husika.

7. Malengo ya Serikali ya Mtaa yatakuwa:

(a) kukuza uwezo binafsi na kuhakikisha ushirikishwaji wa watuna jamii katika kusimamia Sheria na amri na kukuzademokrasia, uwazi na uwajibikaji wa Serikali ya Mtaa;

(b) kuanzisha taasisi za Serikali ya Mtaa zinazowezekana kwaajili ya watu;

(c) kushajihisha ushiriki wa jumuiya za kijamii katika uendeshajiwa Serikali ya Mtaa;

(d) kuwezesha na kukuza elimu kwa jamii;

(e) kukuza maendeleo ya kijamii, kiutamaduni na kiuchumi;

(f) kukuza kujitegemea baina ya watu kwa kupitia uhamasishajiwa rasilimali zilizopo kwa kuhakikisha upatikanaji wahuduma kwa jamii ambazo ni endelevu;

(g) Kukuza amani, maelewano na utulivu baina ya jamii;

GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR23 Oktoba, 2014

Asili yaSerikali zaMitaa.

VyanzovyaSheria yaSerikaliya Mtaaa

Malengoyamamlakayaserikali yamtaa

6

(h) kuhakikisha ushirikishwaji wa kijinsia katika Serikali yaMtaa;

(i) kuijuulisha na kuishirikisha jamii katika kufanya maamuziyanayohusiana na matumizi ya rasilimali katika maeneo yao;

(j) kukuza usalama na afya ya mazingira; na

(k) kuhamasisha na kusaidia shughuli na mafunzo ya kada yautawala kwa wanawake, vijana, wazee na watu wenyeulemavu.

8. Misingi ifuatayo ya utawala wa Mtaa itakuwa ni misingi ya kukasimuna utowaji madaraka kwa mfumo wa mamlaka ya Serikali za Mtaa katikaZanzibar:

(a) Msingi wa utoaji madaraka: endapo maamuzi na kazizitakasimiwa kwa ngazi ya chini kabisa ya Serikali yenyeuwezo;

(b) Kujitawala na Demokrasi: ushiriki wa watu wote katikakutumia haki yao ya kutoa maoni yao katika mchakato wakufanya maamuzi katika masuala ya umma;

(c) Utawala wa Sheria: kusimamia Sheria na amri na utekelezajiwake kwa utulivu na usawa na kuheshimu na kuthamini mila,maadili na thamani ya jamii;

(d) Uwazi: kujenga uaminifu baina ya Serikali na watu kwakupitia utoaji wa habari na kuhakikisha upatikanaji wa taarifasahihi;

(e) Haki: kuweka uwiayano wa mgawanyo wa rasilimali kupitiakatika maeneo ya Baraza la Serikali ya Mtaa;

(f) Usawa: kutoa huduma na fursa sawa kwa wakaazi wotewa eneo lao kwa lengo la kukuza ustawi;

(g) Upokeaji: kuongeza ushajihishaji wa wafanyakazi wa Serikalina jumuiya zisizo za Serikali katika kuwavutia watu katikautaoji wa huduma na kutunza mahitaji ya jamii;

(h) Uwajibikaji: kuhakikisha uwajibikaji wa watoa maamuzikatika mambo yote yenye maslahi ya umma; na

(i) Ufanisi na ufasaha: kuhakikisha huduma nzuri kwa jamiikupitia matumizi bora na usimamizi wa matumizi yarasilimali.

9. Mamlaka ya Serikali ya Mtaa yatakasimiwa katika ngazi za utawalana itatoa mamlaka ambapo itashirikishwa Baraza la mamlaka ya Serikali yaMtaa.

Misingi yautawalawaSerekaliya Mtaa.

GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR 23 Oktoba, 2014

kukasimumamlakayaSerikaliya Mtaa

7

10. Serikali ya Mtaa itakuwa na ngazi tatu za utawala zifuatazo:

(a) Jiji, Manispaa, Baraza la Mji na Halmashauri za wilaya;

(b) Mabaraza ya Wadi; na

(c) Baraza la Shehia.

11.-(1) Aina ya mabaraza ya Serikali ya Mtaa yanaweza kuwa kamaifuatavyo:-

(a) Mabaraza ya mjini; na

(b) Mabaraza ya vijijini.

(2) Baraza la mjini ni baraza lililoanzishwa katika mji au eneolenye mchanganyiko wa watu ambayo zaidi ya nusu ya shughuli za kiuchumisi za kilimo, zenye miundombinu yote inayohitajika na inayotumika kwa jamiina yanagawiwa kama ifuatavyo:-

(a) Baraza la jiji ambalo litakuwa ni chombo kinachojitegemea,na litakuwa na limegawiwa katika Baraza la Manispaa;

(b) Baraza la Manispaa litakuwa ni chombo kinachojitegemea,litakuwa na mabaraza ya wadi yasiyopungua kumi na tano(15) ambazo Zaidi ya nusu zitakuwa katika eneo la mjini na;

(c) Baraza la mji litakuwa ni chombo kinachojitegemea,litagawika katika mabaraza ya wadi ambapo zaidi ya nusuyatakuwa ni mabaraza ya mjini.

(3) Baraza la kijijini litajulikana kama mamlaka ya Baraza yahalmashauri liliyoanzishwa katika makaazi ya kijijini au maeneo ambayouchumi wake unategemea kilimo au uvuvi au mchanganyiko wa kiuchumi.

(4) Mamlaka ya halmashauri ya wilaya yatakuwa ni chombo chakujitegemea ambacho kitagawanywa si chini ya mabaraza kumi (10) ya wadi.

(5) Wadi, ikiwa mjini au kijijini itajumuisha si chini ya shehia mbilina kila shehia itakuwa na vijiji visivyopungua viwili kwa maeneo ya kijijinina mitaa isiyopungua miwili kwa maeneo ya mjini.

12.-(1) Kila Baraza la Serikali ya Mtaa litakuwa na mamlaka kwa mujibuwa masharti ya Sheria hii:

(2) Serikali kuu itatoa baadhi ya kazi zake kama zilivyoanishwa katikajadweli la tatu la Sheria.

(3) Waziri atarekebisha jadweli la tatu muda baada ya muda kamaatakavyoagizwa na Baraza la Mapinduzi.

GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR23 Oktoba, 2014

Ngazi yaSerikali zaMtaa

Aina yamabarazayaSerikali zaMtaa

Utoaji wamamlaka.

8 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR 23 Oktoba, 2014

(4) Kila mamlaka ya Serikali ya Mtaa:-

(a) inaweza kukasimu mamlaka yake katika ngazi nyengineyoyote ya chini;

(b) kutekeleza uwezo wake kulingana na masharti ya sheria hiina Katiba ya Zanzibar; na

(c) kuheshimu mamlaka na uwezo uliopewa na uongozi waMikoa.

SEHEMU YA TATUKUANZISHWA KWA MAMLAKA ZA SERIKALI YA MTAA

PAMOJA NA MAMBO YANAYOHUSIANA NA HAYO

13.-(1) Kutaanzishwa Mamlaka za serikali za Mitaa kwa kila MamlakaMijini na Maeneo ya vijijini.

(2) Kwa kuzingatia masharti ya kifungu kidogo cha (1) cha kifunguhiki, Mamlaka ya Mijini zitajumuisha Jiji, Manispaa na Baraza la Mji.

(3) Kwa kuzingatia Katiba ya Zanzibar, Waziri baada ya kuthibitishamapendekezo chini ya kifungu cha 4 (1) cha Sheria hii kwa amriitakayotangazwa katika Gazeti rasmini :-

(a) Orodha ya ngazi ya Serikali ya Mtaa ilizoanzishwa aukufutwa katika Zanzibar;

(b) Mamlaka zilizogawanywa au zilizounganishwa;

(c) Majina yaliyopewa serekali ya mtaa au kubadilishwa;

(4) Kila Mamlaka ya Mtaa itakuwa ni chombo chenye kujitegemeana itakuwa:

(a) endelevu na yenye muhuri wake;

(b) na uwezo wa kushitaki na kushitakiwa;

(c) kwa mujibu wa Sheria hii, itakuwa na uwezo wa kuhodhi,kumiliki, kununua na kupata ardhi, na kutoa mali yoyoteinayohamishika;

(d) kuwa na uwezo wa kufanya na kutekeleza jambo au kituchochote kama vyombo vyenye hadhi ya kisheriavinavyoweza kufanya na kutekeleza, kwa mujibu wa mashartiya Sheria hii na Sheria nyengine yoyote;

14.-(1) Waziri, kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali yaMtaa atazigawa Mamlaka ya Serikali za mitaa katika viwango vitavyotegemeayafuatayo:-

Kuanzi-shwa kwaMamlakayaSerikaliya Mtaa.

Vigezovyakuanzishamamlakaya serikaliza mitaa.

9GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR23 Oktoba, 2014

(a) Ukubwa wa eneo;

(b) idadi ya watu;

(c) uchumi wa eneo husika;

(d) maslahi ya pamoja ya jamii;

(e) ufanisi na urahisi wa utekelezaji wa shughuli za kiutawala.

(2) Vigezo bora vilivyowekwa vya uanzishaji wa Serikali ya Mtaachini ya kifungu kidogo cha (1) cha kifungu hiki, kinaweza kubadilikakulingana na hadhi ya mji na kijiji.

(3) Miundo yote iliopo ya Serikali ya Mtaa inaweza kufanyiwamapitio na kupangwa tena kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (1) na (2).

(4) Endapo Waziri atapanga madaraja ya mamlaka ya Serikali yaMtaa, atatoa notisi katika Gazeti Rasmi itakayoainisha maelezo ya msingiyanayoainishwa katika kifungu kidogo cha (1)(a-e) cha kifungu hiki.

15. Kila Amri ililofanywa chini ya kifungu cha 14 itaainisha:-

(a) jina au majina ya eneo au maeneo husika na tarehe ambayomamlaka hiyo au mamlaka hizo zitanzishwa;

(b) idadi ya wajumbe wa kuchaguliwa na kuteuliwa;

(c) mipaka ambayo mamlaka ya mtaa itaanzishwa na ambapoitatekeeleza kazi zake eneo; na

(d) muhuri wa mamlaka ya mtaa.

16.-(1) Mamlaka zote za Serikali za Mitaa zitaanzishwa kwa mujibuwa utaratibu ulioelezwa na Sheria hii.

(2) Pale itakapokusudiwa kuanzishwa mamlaka ya mtaa katika eneoau maeneo yoyote, Waziri angalau miezi mitatu kabla ya kutoa amri yakuanzisha chini ya kifungu cha 14 cha sheria hii atawajibika:-

(a) kwa notisi iliyotangazwa katika Gazeti Rasmi, atatoa notisiya nia inayoainisha mipaka ya jumla, na mambo menginekwa kadri atakavyoona inafaa; na

(b) atazitaka mamlaka zote zenye maslahi au watu walioathirikana uamuzi huo kuwasilisha kwake kwa maandishi pingamiziyoyote au maelezo mengineyo kwa namna atakayoeleza nandani ya muda atakaoutaja.

(3) Ikiwa baada ya kumalizika muda wa notisi, hakuna pingamizi aumaelezo mengine yaliyopokelewa kutoka kwa mamlaka au mtu yeyote, Waziri

YaliyomokatikaAmri yakuanzisha.

Utaratibuwakuanzishamamlakaza mtaa.

10 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR 23 Oktoba, 2014

ataendelea kutoa na kuichapisha Amri katika Gazeti Rasmi chini ya kifungucha 14 cha Sheria hii.

(4) Endapo pingamizi yoyote au maelezo mengine yamewasilishwakwa maandishi kwa Waziri kutokana na notisi aliyoitoa chini ya kifungukidogo cha (2), Waziri atawezesha kutolewa uthibitisho wa kupokelewapingamizi au maelezo hayo kwa mamlaka au mtu aliyewasilisha pingamiziau maelezo husika na atazingatia pingamizi hizo au maelezo hayo kamaitakavyoelezwa katika Kanuni.

17.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya kifungu cha 8 cha Sheria hii, Waziriatatoa hati ya kuanzishwa Serikali ya Mtaa na kutangaza katika Gazeti Rasmi.

(2) Hati itaainisha yafuatayo:

(a) jina la mamlaka ya mtaa iliyoanzishwa;

(b) idadi ya wakaazi;

(c) mahali ambapo makao makuu ya mamlaka ya mtaayatakuwepo;

(d) maelezo mengine kama ambavyo Waziri anaweza kuyatoakila baada ya muda.

SEHEMU YA NNEMUUNDO, KAZI NA UWEZO WA SERIKALI ZA MITAA

18.-(1) Kutaanzishwa Baraza la jiji , pale ambapo manispaa mbili auzaidi zipo kwenye Mkoa mmoja na zinatumia mpaka mmoja.

(2) Baraza la Jiji litakuwa na wajumbe wafuatao:-

(a) Meya wa Jiji atakae chaguliwa miongoni mwa Madiwani;

(b) Naibu Meya atakae chaguliwa miongoni mwa madiwani;

(c) Meya wa manispaa zinazounda Baraza la jiji;

(d) Madiwani wote waliochaguliwa na wananchi kutoka kwenyewadi zao;

(e) Madiwani wasiozidi watano ambao watateuliwa naWaziri,wawili miongoni mwao angalau wawe wanawake;

(3) Katibu wa Baraza atakuwa Mkurugenzi ambaye si mjumbe wa Baraza.

19.-(1)Bila ya kuathiri Sheria yeyote inayotumika Zanzibar , Baraza laJiji litakuwa na kazi zifuatazo:-

Hati yauanzi-shwaji.

Uanzi-shwaji naMuundowaBaraza lajiji.

Kazi zaBaraza laJiji.

11GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR23 Oktoba, 2014

(a) Kuendeleza, kutekeleza na kusimamia mpango mkakati wakena bajeti ;

(b) Kuandaa, kuratibu na kusimamia utekelezwaji wa mipangoya kiuchumi, kibiashara, kiviwanda na maendeleo ya kijamii;

(c) Kuongeza mapato kwa lengo la kutekeleza majukumu yake ;

(d) Kusimamia na kuratibu kazi na majukumu ya mamlaka yamanispaa ya Baraza la jiji;

(e) Kutunga Sheria ndogondogo zitakazo tumika katika maeneoyao;

(f) Kusimamia na kutathimini miradi yote ndani ya eneo lake;

(g) Kuendeleza biashara ya utalii na uwekezaji; na

(h) Kufanya kazi nyengine zozote ilizizopewa Mamlaka ya mitaakwa mujibu wa Sheria hii au Sheria nyingine yoyote.

20.(1) Kunaanzishwa Baraza la Manispaa ambalo litaundwa nawajumbe wafuatao:-

(a) Meya ambaye anateuliwa miongoni mwa madiwani;

(b) Naibu Meya ambaye anateuliwa miongoni mwa madiwani;

(c) Madiwani wote walioteuliwa na wananchi kutoka katikawadi zao;

(d) Si zaidi ya madiwani kumi (10) watakaoteuliwa na Waziri,angalau asilimia arubaini (40%) wawe wanawake;

(2) Katibu wa Baraza atakuwa ni Mkurugenzi wa manispaa ambayehatokuwa mjumbe wa Baraza.

21. Bila ya kuathiri sheria yoyote inayotumika Zanzibar, Baraza laManispaa litakuwa na kazi zifuatazo:-

(a) Kuendeleza, kutekeleza na kuratibu mpango mkakati nabajeti;

(b) Kuandaa, kuratibu na kusimamia utekelezaji wa mipango yakiuchumi, kibiashara viwanda na maendeleo ya jamii;

(c) Kuongeza mapato kwa ajili ya kurahisisha utendaji wamamlaka ya mitaa;

(d) Kutoa leseni, kuratibu na kusimamia shughuli za kibiasharakatika maeneo yao;

Kuanzi-shwa naMuundowaBaraza laManispaa.

Kazi zaBaraza laManispaa.

12 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR 23 Oktoba, 2014

(e) Kutunga Sheria ndogo ndogo zitakazotumika katika maeneoyao;

(f) Kuzingatia, kusimamia na kuratibu mipango ya maendeleo,miradi na kazi za wadi ndani ya maeneo yao;

(g) Kukagua na kusimamia miradi yote ndani ya maeneo yao;

(h) Kufanya kazi nyengine yoyote iliyopewa na mamlaka yamitaa chini ya Sheria hii au Sheria nyengine yoyote;

(i) Kusimamia uchimbaji wa mawe, mchanga, na uvunaji wambao au rasilimali nyengine za asili kamazitakavyothibitishwa na Waziri mwenye dhamana narasilimali za asili.

22.-(1) Baraza la mji litaundwa na wajumbe wafuatao:-

(a) Meya ambaye anachaguliwa miongoni mwa madiwani;

(b) Naibu meya ambaye anachaguliwa miongoni mwa madiwani;

(c) Madiwani wote wa mamlaka waliochaguliwa na wananchikutoka katika wadi;

(d) Madiwani wasiopungua kumi (10) ambao wanateuliwa naWaziri, angalau asilimia arubaini wawe wanawake.

(2) Katibu wa baraza atakuwa mkurugenzi wa mamlaka ya mji ambayehatokuwa mjumbe wa Baraza.

23.-(1)Bila ya kuathiri Sheria yeyote inayotumika Zanzibar, kila Barazala Mji, litafanya kazi katika maeneo yao kama ifuatavyo:-

(a) Kuendeleza, kutekeleza na kusimamia mipango mkakati nabajeti zao;

(b) Kuanzisha, kuratibu na kusimamia utekelezaji wa mipangoya kiuchumi, kibiashara,viwanda na maendeleo ya kijamii;

(c) Kuongeza mapato kwa lengo la kuziwezesha Serikali yaMtaa kutekeleza majukumu yake ipasavyo;

(d) Kutoa leseni, kusimamia na kufuatilia biashara zilizopo ndaniya mamlaka za Serikali ya Mtaa;

(e) Kutunga sheria ndogondogo zitakazo tumika katika maeneoyao;

(f) Kuzingatia, kusimamia na kuratibu mipango ya maendeleo,miradi na kazi za wadi zilizomo ndani ya eneo la Mamlakahusika;

MuundowaBaraza lamji.

Kazi zaBaraza lamiji.

13GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR23 Oktoba, 2014

(g) Kusimamia na kutathimin miradi yote ndani ya maeneo yao;

(h) Kusimamia uchimbaji wa mawe, mchanga na uvunaji wambao au rasilimali nyengine za asili kamaitakavyoidhinishwa na Waziri mwenye dhamana na rasilimalimza asili;

(i) kufanya kazi nyengine yoyote iliyopewa mamlaka ya mtaachini ya Sheria hii au Sheria nyengine yoyote;

24.-(1) Halmashauri ya Wilaya itakuwa na wajumbe wafuatao:-

(a) Mwenyekiti ambaye anachaguliwa miongoni mwa madiwaniwa halmashauri ya wilaya;

(b) Makamu Mwenyekiti anachaguliwa miongoni mwamadiwani;

(c) Madiwani wote waliochaguliwa na wananchi kutoka katikawadi husika;

(d) Madiwani wasiopungua kumi (10) ambao wanateuliwa naWaziri, angalau asilimia arubaini (40%) wawe wanawake.

(2) Katibu wa baraza atakuwa mkurugenzi wa mamlaka ya halmashauriya wilaya ambaye hatokuwa mjumbe wa Baraza

25. Halmashauri za wilaya zitakuwa na kazi zifuatazo:-

(a) Kuanzisha, kuratibu na kusimamia utekelezaji wa mipangoya kiuchumi, biashara, viwanda na maendeleo ya jamii ;

(b) Kuhakikisha ukusanyaji na matumizi sahihi ya mapato yaBaraza; na

(c) Kutunga sheria ndogo ndogo zitakazo tumika katika maeneoyao.

26.-(1) Bila kuathiri kazi zilizoanishwa za kila serikali ya Mtaa,mabaraza ya Serikali ya Mtaa kwa ujumla yatafanya kazi kwa mujibu wakazi zilizopewa kwa mujibu wa Sheria, kisekta, na miongozo katika eneo lamamlaka yake kama ifuatavyo:-

(a) itawajibika kuanzisha mazingira mazuri ya kazi yakiwemosehemu za afisi, vitendea kazi na vifaa muhimu vya kazikwa ajili ya utoaji wa huduma kwa wananchi;

(b) kutunga Sheria ndogondogo zitakazotumika katika maeneoyao;

(c) kukusanya mapato yatokanayo na vianzio vilivyo ainishwachini ya kifungu cha 70 cha Sheria hii;

MuundowaHalma-shauri yaWilaya.

Kazi zaHalma-shauri zaWilaya.

Kazi zajumla zamabarazaya Serikaliza mitaa.

14 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR 23 Oktoba, 2014

(d) kusafisha barabara zote, mitaa, mitaro, sehemu za kuwekeataka, masoko, vituo vya biashara, sehemu za kupumzikia,vyoo vya umma na sehemu nyengine za wazi na zisizokuwawazi; zinazotumika na jamii na usimamizi wa maeneo yakuangamiza na huduma za kutupia taka;

(e) Kumtaka mmiliki yeyote wa ardhi kuondoa uzio usiotumikaau jengo lililozidi katika barabara yoyote, mtaa au maeneoya umma;

(f) Kukuza biashara ya utalii na kuielimisha jamii kuwekezakatika nafasi zilizopo ndani ya maeneo yao;

(g) Kupendekeza kwa Mkuu wa Mkoa majina na namba zamajengo, mitaa, sehemu na kuweka kumbukumbu zake;

(h) Kuongoza, kuanzisha na kusimamia masoko ya jamii na ada;

(i) Kusaidia na kuwezesha makundi yenye mahitaji maalumu,vijana, wanawake, na watu wenye ulemavu kwa kuwapatiamikopo, fedha na uwepo wa masoko ya uhakika;

(j) Kuweka kumbukumbu za vyombo vya moto vya biashara nabinafsi, boti za uvuvi, na vyombo vyengine vyovyotevinavyofanya shughuli za baharini katika maeneo yao;

(k) Kudhibiti uchafuzi wa mazingira unaosababisha maudhi kwamtu binafsi na maudhi kwa jamii;

(l) Kusimamia na kuhakikisha upatikaniji wa huduma za kingana tiba katika vituo vya afya vya msingi na kati na kuchukuahatua muhimu za kupambana na maradhi ya mripuko;

(m) Kudhibiti uchimbaji wa mawe, mchanga, na uvunaji wambao au rasilimali nyengine za asili kamazitakavyoidhinishwa na Waziri mwenye dhamana narasilimali za asili;

(n) Kutekeleza sera ya elimu na miongozo na kusimamia skuliza Serikali za awali, msingi na kati kusimamia ubora waskuli binafsi;

(o) Kudhibiti na kusimamia shughuli za matamasha na shughulinyengine za jamii;

(p) Kufanya kazi za ukataji miti, uwekaji matuta, upandaji nauondoaji miti pembezoni mwa barabara;

(q) Kusimamia, kudhibiti na kukuza maeneo ya wazi, maegesho,bustani, majengo ya Serikali, maeneo ya kihistoria namakaburi;

15GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR23 Oktoba, 2014

(r) Kuongoza, kudhibiti na kuratibu matumizi ya ardhi kamailivyoainishwa katika mpango wa matumizi ya ardhi; na

(s) Kushughulikia mambo mtambuka ambayo yanajumuishaukingaji na udhibiti wa maambukizi ya HIV/AIDS, kuhifadhimazingira na mabadiliko ya tabia nchi, rushwa, usimamiziwa maafa, na uzingatiaji wa masuala ya kijinsia.

(2) Waziri anaweza kwa kutangaza kwenye gazeti rasmi kutungakanuni kwa utekelezaji mzuri wa kifungu hiki.

27.-(1) Baraza la jiji, Baraza la Manispaa, Baraza la Mji na Halmashauriza Wilaya zitakuwa na uwezo ufuatao:

(a) Kuingia katika mikataba;

(b) Kupanga viwango vya ada na kukusanya mapato;

(c) Kutunga Sheria ndogo ndogo au kanuni;

(d) Kuamuru na kukagua jengo lolote au biashara ndani ya eneola mamlaka yake;

(e) Kuweka vizuwizi vya kumzuia mtu yeyote au mamlakanyingine kufanya jambo lolote ambalo linaweza kuathirijamii au mamlaka ya Serikali za Mtaa.

Bila ya kuathiri kifungu kidogo cha (1) cha kifungu hiki Mabaraza ya Serikaliza Mitaa yatatekeleza uwezo mwengine wowote ulioainishwa na Sherianyengine zinazotumika Zanzibar.

28. Mamlaka za Serikali za Mitaa zinaweza kumualika mtu yeyotekuhudhuria mikutano ya Baraza ikiwa kuna haja ya kufanya hivyo.

29. Diwani atalazimika kula kiapo kwa uwazi kwa mujibu wa Jadwelila Pili (2) kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yake katika baraza naakishindwa kufanya hivyo bila sababu yeyote katika kipindi cha wiki nnebaada ya kuchaguliwa au kuteuliwa kwake, kiti hicho kitatambuliwa kuwakipo wazi.

30.-(1) Meya na Mwenyekiti watatumikia afisi kwa kipindi cha miakamitano (5) na wanaweza kuchaguliwa tena kwa kipindi chengine.

(2) Katika kipindi akiwa madarakani Meya, Naibu Meya,Mwenyekiti na Makamo Mwenyekiti wataendelea kuwa wajumbe wa Baraza.

(3) Meya, Naibu Meya, Mwenyekiti au makamu Mwenyekitiisipokuwa kama atapoteza sifa au kujiuzulu, ataendelea kutumikia ofisi zaompaka atakapo chaguliwa mrithi au kuchaguliwa tena.

Uwezowa jumlawaMabarazayaSerikali zaMitaa.

MialikokatikaBaraza.

Kiapo chaMadiwani.

Muda waMeya,NaibuMeya,Mwenye-kiti naMakamoMwenye-kiti.

16 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR 23 Oktoba, 2014

31.-(1) Nafasi ya Meya itakuwa wazi kwa kutokezea sababu zifuatazo:

(a) Kumaliza muda wake wa kazi;

(b) Kukubaliwa barua yake ya kuiuzulu na baraza,;

(c) Kuondoshwa kwa mujibu wa masharti ya Sheria hii;

(d) Ugonjwa wa akili au maradhi yaliyothibitishwa kwa taarifarasmi ya daktari na kukubaliwa na robo tatu ya wajumbe waBaraza; au

(e) Kufariki.

(2) Pale ambapo nafasi ya Meya wa Jiji, Manispaa, Baraza la Mjiiko wazi, Naibu Meya husika wa Jiji au Manispaa atakaimu nafasi hiyompaka ufanyike uchaguzi mwengine wa Meya.

(3) Nafasi iliyowazi ya Meya itajazwa ndani ya siki sitini kutokatarehe ya nafasi hiyo kuwa wazi.

32.-(1) Meya atakuwa na uwezo na kazi zifuatazo:-

(a) Kiongozi wa baraza la Jiji au Manispaa;

(b) Mwenyekiti wa baraza la Jiji au Manispaa;

(c) Muwakilishi wa jiji au manispaa katika mikutano na shereheya taifa na kitaifa;

(d) Kuitisha au kuahirisha na kuvunja vikao;

(e) Kuwa msimamizi wa maamuzi yote yanayoamuliwa naBaraza;

(f) msemaji wa Baraza la Jiji au Manispaa;

(g) Kufanya majukumu na kazi zote atakazoelekezwa chini yasheria hii au sheria nyingine.

(2) Pale endapo afisi ya Meya iko wazi au Meya hayupo au hana uwezowa kutekeleza kazi zake kutokana na sababu ya ugonjwa au sababu nyengineyoyote kazi zake zitatekelezwa na Naibu Meya.

33.-(1) Mwenyekiti atakuwa na uwezo na kazi zifuatazo:-

(a) Kiongozi wa Halmashauri ya Wilaya;

(b) Kuitisha, kuahirisha na kuvunja vikao;

(c) Kuwa msimamizi wa maamuzi yote yaliyoamuliwa naBaraza;

Nafasi yawazi yaafisi yaMeya.

Kazi nauwezo waMeya.

Kazi nauwezo waMwenye-kiti.

17GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR23 Oktoba, 2014

(d) Kuwa msemaji wa Baraza;

(e) Kuliwakilisha Baraza kitaifa; na

(f) Kufanya majukumu na kazi zote atakazoelekezwa chini yasheria hii au sheria nyingine.

(2) Pale endapo afisi ya Mwenyekiti iko wazi au hayupo au hanauwezo wa kutekeleza kazi zake kutokana na sababu ya ugonjwa au sababunyengine yoyote kazi zake zitatekelezwa na Makamo Mwenyekiti.

34. Baraza litamuondoa madarakani Meya au Mwenyekiti ikiwa:-

(a) Atatiwa hatiani kwa kosa la jinai ambalo litamuondoshea sifayakuwa mtumishi kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma;

(b) Kuugua ugonjwa wa akili au maradhi yaliyothibitishwa kwataarifa rasmi ya daktari na kukubaliwa na robo tatu ya wajumbewa Baraza; au

(c) Sababu nyengine yoyote itakayomuondoshea sifa ya kuwadiwani kwa mujibu wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar.

35.-(1) Bila ya kujali masharti yoyote ya sheria hii, Baraza linawezakupitisha azimio la kumuondosha Meya au Mwenyekiti ikiwa azimio hilolimependekezwa na kupitishwa kwa mujibu wa sheria hii au sheria nyingineyoyote.

(2) Bila ya kuathiri kifungu kidogo cha (1)cha kifungu hiki hakunaazimio litakalo pendekezwa la kumuondosha Meya au Mwenyekitiisipokuwa:

(a) miezi sita imepita tangu uchaguzi ulipofanyika wa kumchaguaMeya au Mwenyekiti;

(b) miezi mitatu imepita tokea azimio kama hilolilipopendekezwa na kukataliwa kwenye Baraza.

(3) Azimio la kumuondoa Meya au Mwenyekiti halitopitishwaisipokuwa;-

(a) Notisi ya maandishi imesainiwa na wajumbe wa Barazawasiopungua theluthi mbili na kuwasilishwa kwaMkurugenzi siku kumi na nne kabla ya kuwasilishwaBarazani;

(b) Iwapo Mkurugenzi ameridhika kwamba notisi ya azimioimezingatia masharti yaliyoainishwa katika kifungu hiki, nanotisi hiyo imeeleza sababu za azimio na imewasilishwaBarazani.

Kuondo-shwa kwaMeya naMwenyekiti

Utaratibuwakumuo-ndoaMeya auMwenye-kiti.

18 23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

(4) Endapo Mkurugenzi ataridhika na masharti ya kifungu kidogocha (3) cha kifungu hiki yametimia atawasilisha azimio lililopendekezwakatika Baraza haraka iwezekanavyo, Baraza litajadili na kuamua azimio hilokwa mujbu wa kanuni za Baraza, miiko ya kiutendaji au kanuni.

(5) Iwapo Baraza linajadili azimio lililowasilishwa, Naibu Meyaau Makamo Mwenyekiti kama itakavyokuwa ataongoza kikao na Meya auMwenyekiti kama itakavyokuwa atakuwa na haki ya kujitetea kesi yakembele ya Baraza

(6) Azimio la kumondoa Meya au Mwenyekiti litapitishwa iwapolitaungwa mkono na wajumbe wa Baraza wasiopunguwa theluthi mbili yawajumbe wa Baraza.

(7) Haraka itakavyowezekana na katika hali yoyote ndani ya sikusaba za Baraza tokea kupitisha azimio la kumuondoa, naibu Meya au makamuMwenyekiti kama itakavyokuwa atawasilisha azimio hilo kwa Waziri naMeya au mwenyekiti atatakiwa kujiuzulu katika afisi ndani ya siku saba naakishindwa kufanya hivyo ndani ya muda huo atachukuliwa kuwa amejiuzulu,na Baraza, ndani ya siku arubaini litateuwa mjumbe mwengine wa Barazakuwa meya au mwenyekiti.

36.-(1) Mjumbe wa Mamlaka ya Mtaa anaweza kujiuzulu kwa taarifa yamaandishi aliyoisaini na kuiwasilisha kwa Meya au mwenyekiti wa mamlakaya mitaa.

(2) Mtu atasita kuwa mjumbe wa Mamlaka ya Mtaa:-

(a) kwa tarehe iliyoanishwa katika notisi kama ni tarehe yakujiuzulu; au

(b) pale ambapo hakuna tarehe iliyoanishwa, kwa siku itakapopokelewa notisi .

(3) Mtu aliyejiuzulu kuwa mjumbe wa mamlaka ya Mtaa chini ya kifunguhiki, pia atasita kuwa mjumbe wa Kamati yoyote ya Baraza.

37.-(1) Baraza linawaza kuidhinisha maslahi ya Meya kutoka katikamapato yake kiwango ambacho kama itavyoona ni muafaka kwa ofisi yaMeya na kuthibitishwa na Waziri.

(2) Meya atalipwa mshahara na stahiki nyengine kamaitakavyopangwa muda baada ya muda.

(3) Meya hatakuwa Mtendaji Mkuu wa Baraza lakini atakuwa nimshauri mkuu wa Baraza.

38. Naibu Meya na madiwani wengine hawatakuwa wafanyakazi wakudumu na watalipwa mishahara na stahiki nyengine kama itakavyopangwakila baada ya muda na kuidhinishwa na Waziri.

Kujiuzulukuwamjumbe.

Maslahina poshoza Meya.

Madiwanihawata-kuwawatendajiwakudumu

1923 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

39.-(1) Kutakuwa na Mkurugenzi katika kila Baraza la jiji na Manispaaambaye atateuliwa na Rais na Wakurugenzi wa Baraza la Mji au Halmashauriza Wilaya ambaye atakayeteuliwa na Waziri kwa mujibu wa masharti yaSheria ya Utumishi wa Umma.

(2) Mkurugenzi atakuwa Mtendaji Mkuu na afisa masuuli wamamlaka za mitaa na atakuwa na majukumu na kazi za kila siku za mamlaka.

40.-(1) Mtu atakuwa na sifa za kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mamlakaikiwa:

(a) Mzanzibari;

(b) Afisa mwandamizi angalau awe na elimu ya shahada yakwanza katika fani ya Uongozi, Sheria, sayansi ya jamii,mipango, uhandisi, uchumi au fani nyengine yoyoteinayolingana na hizo kutoka katika chuo kikuukinachotambulika;

(c) asipunguwe miaka saba ya uzoefu wa kazi katika utumishiwa umma;

(d) hajatiwa hatiani na mahakama ya kisheria kwa kosa la kukosauaminifu.

(2) Mtu aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi atalazimika kuwajibika katikakazi na majukumu yake.

41.-(1) Mkurugenzi wa mamlaka ya mtaa atakuwa na kazi na majukumuyafuatayo:-

(a) atawajibika na utekelezaji wa maamuzi yote yanayofanywana Baraza;

(b) kusimamia na kuratibu shughuli za maafisa wote na idara zaBaraza;

(c) atakuwa mtunzaji wa hati zote, taarifa, rasilimali na muhuriwa Baraza;

(d) atawajibika na utekelezaji wa Sheria ndogo ndogo za Baraza;na

(e) atatekeleza kazi zote na majukumu ya kisheria anazotakiwakufanya kwa mujibu wa Sheria hii au sheria nyengine zozote.

42.-(1) Kunaanzishwa Baraza katika kila Wadi itakayojulikana kama niBaraza la Wadi.

(2) Kila Baraza la Wadi itatekeleza katika eneo lake kazi zifuatazo:-

Uteuzi waMkurugenzi

Sifa zakuwaMkuru-genzi.

Kazi namajukumuyaMkurug-enzi.

Kuanzishana kazi zaBaraza laWadi.

20

(a) kutekeleza sera, sheria, kanuni na miongozo kamaitakavyoelekezwa na Halmashauri za Wilaya;

(b) kuhamasisha jamii kwa maendeleo yao;

(c) kutekeleza, kuratibu na kusimamia mipango yote ya serikalikatika eneo lake;

(d) kusimamia afya ya jamii na mazingira;

(e) kuhifadhi na kudumisha utamaduni wa Zanzibar;

(f) kusimamia masuala ya ulinzi na usalama; na

(g) kufanya kazi nyengine yeyote iliyopewa na mamlaka chiniya Sheria hii au Sheria nyengine yoyote.

(3) Bila ya kuathiri kazi za jumla iliyopewa chini ya kifungu kidogocha (2) cha kifungu hiki, itakuwa ni kazi ya kila Baraza la Wadi katika eneolake:-

(a) kusimamia na kuboresha vyama vya ushirika katika wadi;

(b) kusimamia na kutekeleza mipango ya maendeleo;

(c) kuanzisha na kuwezesha wajasiriamali, vijana, wanawakena watu wenye ulemavu katika kupatiwa mikopo, fedha naupatikanaji wa masoko yenye uhakika;

(d) kuimarisha huduma za maktaba katika maeneo yake;

(e) kuelimisha jamii kuhusiana na Sheria na Kanuni za Serikaliza Mitaa;

(f) kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa utumiaji wa bidhaazenye hadhi na ubora;

(g) kushajihisha jamii kushiriki katika kazi za amali;

(h) kusimamia na kutekeleza sera, sheria na kanuni zinazohusianana uhifadhi wa kihistoria, mambo ya mazingira, utumiaji wamadawa ya kulevya, UKIMWI na watu wenye ulemavu;

(i) kushajihisha jamii juu ya umhimu wa ulipaji wa kodi, adana malipo mengine kwa maendeleo ya wadi;

(j) kuingiza na kujumuisha masuala ya jinsia katika miradi yamaendeleo;

(k) kuandaa kanuni na miongozo kwa utekelezaji bora wa kazizake; na

23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

21

(l) kutekeleza kazi nyengine zinazohusiana na sheria, kanuni namiongozo ya mamlaka husika.

43.-(1) Kila Baraza la Wadi litakuwa na wajumbe wafuatao :-

(a) Mwenyekiti ambae atakuwa diwani wa wadi husika;

(b) Wajumbe watatu kutoka katika kila Shehia husikawatakaoteuliwa na Kamati ya ushauri ya Shehia;

(c) Masheha wote wanaotoka katika Wadi husika ambaohawatakuwa na haki ya kupiga kura;

(d) Wataalam wasiozidi watano wanaoishi katika wadi kamawatakavyopendekezwa na Baraza la Wadi;

(e) Watu wasiozidi watano wanaoheshimika kutoka katika wadihusika watakao teuliwa na Baraza la wadi;

(f) Wawakilishi wawili wanaotoka kwenye watu wenye mahitajimaalumu, kutoka katika kila shehia zilizomo katika wadi,ambao watateuliwa na Baraza la Wadi na hawatakuwa nahaki ya kupiga kura;

(g) Wawakilishi watatu kutoka Asasi za Kiraia wawili kati yaoni wanawake, ambao hawatakuwa na haki ya kupiga kura;

(h) Mwenyekiti kutoka kila kamati ya ushauri ya Shehia ndaniya wadi;

(2) Karani waWadi atakuwa Katibu Baraza.

44. Kutakuwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wadi ambaye atakuwaDiwani wa kuchaguliwa.

45. Kutakuwa na Karani wa Baraza la Wadi ambaye ataajiriwa namamlaka ya mtaa kufanya kazi za kila siku za Wadi, atatekeleza kazi za wadiza kila siku na kuweka kumbukumbu za kila siku.

46. Mtu atastahiki kuajiriwa kuwa Karani wa Baraza ispokuwa awe nasifa zifatazo:-

(a) Awe Mzanzibari;

(b) Awe na angalau stashahada katika chuo kinachotambulika;

(c) Awe hajatiwa hatiani na mahakama ; na

(d) Awe na uwezo wa kutatua matatizo.

MuundowaBaraza laWadi.

Mwenye-kiti waBaraza lawadi

KatibuwaBaraza laWadi

Ajira nasifa zaKarani.

23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

22

47.-(1)Inaanzishwa Kamati katika kila shehia itakayojulikana kamaKamati ya Ushauri ya Shehia.

(2) Kila Kamati ya Ushauri ya Shehia itakuwa na wajumbe wafuatao:-

(a) Mwenyekiti ambae atakuwa sheha wa shehia husika;

(b) Wajumbe wasiozidi watano kutoka katika Kijiji au Mtaandani ya shehia hiyo;

(c) Watu wawili mashuhuri kutoka katika shehia ambaowatateuliwa na kamati ya ushauri ya shehia na angalaummoja wao atakua mwanamke;

(d) Wataalam wasiozidi watatu wanaoishi katika shehia kamaitakavyopendekezwa na Kamati ya Ushauri ya Shehia;

(e) Wawakilishi watatu kutoka taasisi zisizokuwa za Kiserikali, angalau wawili miongoni mwao wawe wanawake ambaohawatakuwa na haki ya kupiga kura; na

(f) Karani wa Baraza la Wadi atakuwa katibu wa kamati yaushauri wa shehia .

48. Kamati ya Ushauri ya Shehia itatekeleza kazi na uwezo ufuatao:-

(a) kusimamia na kulinda vyama vya ushirika ndani ya Shehia;

(b) kusimamia utekelezaji wa mipango ya ajira ndani ya Shehia;

(c) kuwawezesha wajasiriamali , vijana, wanawake na watuwenye ulemavu katika kuwapatia mikopo, fedha na upatikanajiwa soko la uhakika;

(d) kutoa huduma za kimaktaba katika eneo la mamlaka yake;

(e) kuielimisha jamii kuhusu Sheria na Kanuni ya Serikali ya Mtaa;

(f) kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kutumia bidhaa zenye hadhina ubora;

(g) kushajihisha jamii kushiriki katika kazi mikono;

(h) kusimamia na kutekeleza sera, sheria, na kanuni zinazohusianana uhifadhi wa sehemu za kihistoria, masuala ya kimazingira,madawa ya kulevya, ukosefu wa kinga mwilini / UKIMWI nawatu wenye ulemavu;

(i) kushajihisha jamii juu ya umuhimu wa ulipaji kodi, ada namalipo mengine kwa maendeleo ya shehia;

KuanzishanaMuundowaKamatiyaUshauriwaShehia

Kazi nauwezo waKamati yaUshauriya Shehia

23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

23

(j) kutunga kanuni; na

(k) Kutekeleza majukumu mengine yoyote yanayohusiana na sheria,kanuni na miongozo ya halmashauri za wilaya.

49. Mtu atastahiki kuwa Mjumbe wa kamati ya ushauri ya shehia ikiwa:-

(a) mzanzibari mwenye umri wa miaka 21 au zaidi;

(b) mkaazi wa shehia husika; na

(c) amehitimu anagalau elimu ya kitado cha nne.

50.-(1) Kutakuwa na Mwenyekiti wa kamati ya ushauri ya shehia ambaeatakuwa ni Sheha wa Shehia hiyo :-

(2) Mwenyekiti atakuwa na kazi zifuztazo:-

(a) kuongoza vikao vya Kamati;

(b) kwa kushauriana na wajumbe anaweza kuitisha, kuahirishana kuvunja vikao;

(c) atawajibika kusimamia maamuzi yote yatakaamuliwa naKamati;

(d) atakuwa ni msemaji wa Kamati;

(e) kutekeleza majukumu yote ya kisheria na kazi alizotakiwakizifanya kwa mujibu wa Sheria hii au Sheria nyengineyoyote.

51. Kila mjumbe wa kamati ya ushauri ya shehia atafanya kazi kwamuda wa kipindi cha miaka mitano ispokuwa atapokoma kuwa mjumbekwa kifo, kujiuzulu au kuondolewa

SEHEMU YA TANOKAMATI NA IDARA ZA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

52.-(1)Kunaanzishwa kamati katika kila MamlakayaSerikali yaMtaaambayo itajulikana kama ni Kamati ya Maendeleo ya Mamlaka ya Mtaa.

(2) Kamati ya Maendeleo yaMamlaka ya Mtaa itajumuisha wajumbewafuatao;-

(a) Mwenyekiti wa Kamati ambaye atakuwa ni Meya auMwenyekiti wa Serikali ya Mtaa;

(b) Katibu ambaye atakuwa ndiye Mkurugenzi wa Mamlaka yaSerikali ya Mtaa;

Sifa zawajumbewakamati yaushauriwashehia.

Kazi zamwenye-kiti waKamatiyaUshauriyaShehia.

Muda wamjumbewaKamati yaUshauriya Shehia

kuanzishaKamatiyaMaendeleoyaMamlakay Mitaa.

23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

24

(c) Wenyeviti wa Kamati za kudumu za Serikali ya Mtaa;

(d) Afisamipango,Mchumi, Mwanasheria, Mhasibu, Mkaguzi wahesabu za ndani ya Serikali ya Mtaa;

(e) Wajumbe wawili watakaoteuliwa na Umoja wa Taasisi zaKiraia; na

(f) Maafisa wengine wowote watakaoteuliwa na Mkurugenzikutoka Mamlaka ya Serikali ya Mtaa;

(3) Kamati za maendeleo ya Mtaa itakutana mara mbili kwa mwakana inaweza kuitisha Mikutano ya Dharura kila itakapohitajika.

53. Kamati ya Maendeleo ya Mamlaka ya Mtaa itakuwa na Kazizifuatazo:-

(a) kutekeleza sera za Mamlaka ya mtaa na kuziainishachangamoto na kutoa ushauri kwa uongozi wa wilayakuhusiana na njia mbadala za kukabiliana na matatizo hayona kuhamasisha maendeleo ya eneo husika.

(b) kusimamia na kusaidia uandaaji wa sera kwa serikali yamtaa katika maeneo yao kwa maendeleo endelevu;

(c) kuhamasisha wananchi kushiriki ,kuchangia na kusaidiamatumizi ya rasilimali, uhifadhi wa Mazingira kwamaendeleo endelevu.

(d) kuhakikisha mikakati ya utekelezaji inaendana na sera nainaleta muamko kwa mwananchi katika maeneo yao.

(e) kuhakikisha na kuanzisha ushirikiano na mahusianomiongoni mwa taasisi za Serikali kuu , Serikali za Mitaa naJumuiya zisizokuwa za kiserikali kwa madhumuni yakuimarisha mazingira na maendeleo endelevu.

54.-(1) Kwa utekelezaji mzuri wa majukumu ya Kamati za Kudumu, kilaSerikali ya Mtaa itaanzisha kamati ya kudumu kwa mujibu wa Kanunizilizotungwa chini ya Sheria hii.

(2) Bila ya kuathiri kifungu kidogo cha (1) cha kifungu hiki, Barazalinaweza kuunda Kamati maalum kama itakavyoona inafaa katika kurahisishautekelezaji wa kazi maalum kwa kipindi maalum.

55.-(1) Kila kamati itawajibika katika utekelezaji wa sera na maamuziyanayofanywa na Baraza na itakuwa na kazi zifuatazo:-

Kazi zaKamatiyamaendeleoyaMamlakaya Mtaa.

Kamati zaKudumuza Jiji,Manispaa,Baraza laMji naHalma-shauri yaWilaya.

Kazi nauwezo waKamati zaKudumu.

23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

25

(a) Kuainisha, kuchanganua na kutoa vipaumbele kulingana namahitaji ya Baraza;

(b) Kuainisha na kuwasilisha mapendekezo katika idara yamipango inayohusiana na kamati hiyo;

(c) Kuongoza na kusimamia utekelezaji wa sera na kazi za idaraya kamati husika na kushauri Idara hiyo ipasavyo;

(d) Kupokea na kutatua matatizo au malalamiko yatakayopelekwakatka Kamati kutoka Barazani;

(e) Kuanzisha mipango ya maendeleo katika maeneo yao;

(f) Kuwasilisha ripoti kwa Baraza;

(g) Kuandaa mipango ya Baraza na bajeti kwa ajili yakuthibitishwa na baraza;

(h) kuongoza na kusimamia utekelezwaji wa mipango na bajetiya baraza;

(i) kutekeleza kazi na majukumu mengine yoyote kamaitakavyoelekezwa na Baraza au sheria nyengine yeyote; na

(j) kutekeleza jukumu jengine lolote kwa usimamizi mzuri waBaraza kama itakavyoidhinishwa na Baraza.

(2) Bila ya kuathiri mashrti ya kifungu cha 54(1) cha Sheria hii kamatiza kudumu za Baraza zinaweza kusimamia zaidi ya idara moja katika kufanyakazi zake.

56. Mipango ya maendeleo ya Serikali za mtaa itakuwa na mahusiano yamojakwa moja katika sera na mipango ya maendeleo ya kitaifa.

57.-(1) Kwa utekelezaji bora wa majukumu yake, kila Mamlaka yaSerikali za Mtaa zitaanzisha idrara zisizozidi nne ambazo ni muhimu kwautekelezaji wa Kazi zake.

(2) Kila Idara ya Mamlaka ya Serikali ya Mtaa itaongozwa na Mkuuwa Idara ikiwa chini ya usimamizi wa Mkurugenzi.

58.-(1) Kila idara itawajibika kutekeleza Sera na Maamuziyatakayofanywa na Baraza na bila ya kuathiri masharti ya jumla; naitatekeleza yafuatayo:-

(a) kutekeleza mipango ya kila Kitengo cha Baraza , kusimamiana kutathmini mipango ya maendeleo ya Idara.

Mipangoyamaendeleoya Serikaliza mtaa.

Idara zaMamlakaya Serikaliza Mitaa.

Kazi zaIdara.

23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

26

(b) kutoa huduma bora kwa watu walio ndani ya mamlaka yaSerikali ya Mtaa;

(c) Kutayarisha bajeti ya mwaka ya Idara hiyo na kuwasilishakwa kamati husika ;

(d) kutayarisha ripoti kwa kamati; na

(e) kufanya wajibu mwengine wowote uliopewa na baraza.

(2) Bila ya kuathiri masharti yaliyowekwa chini ya kifungu kidogocha (1) cha Sheria hii, kila Idara inaweza kuanzisha kitengo maalum ndaniya idara kwa utekelezaji wa shughuli zake za kila siku.

59.-(1) Mkuu wa Idara atatekeleza majukumu yafuatayo:-

(a) mpango wa Baraza;

(b) kuratibu ,kusimamia na kutekeleza mpango wa Baraza;

(c) kushauri Baraza na kamati kwa mambo yanayohusika nayo;

(d) kusimamia shughuli za wafanyakazi katika Idara;

(e) kuhamasisha na kutoa ushauri wa kitaalamu katika idara;

(f) kusimamia na kutathmini mpango wa maendeleo ya Baraza;

(g) kusimamia uongozi wa Idara na kutoa taarifa kwa Mamlakahusika juu ya ukosefu wa nidhamu na utendaji mbovu kwahatua za kinidhamu; na

(h) kufanya kazi nyengine yoyote itakayopewa mamlaka.

60. Vikao na mwenendo ya Mamlaka ya Serikali ya mtaa vitafanywakama ilivyoainishwa katika jadweli la nne la Sheria hii.

SEHEMU YA SITAWAFANYAKAZI WA MAMLAKA YA SERIKALI ZA MITAA

61.-(1) Kutakuwa na wafanyakazi wa Serikali za Mitaa ambaowataajiriwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma .

(2) Kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Utumishi wa Umma,Serikali kuu au Serikali ya Mtaa inaweza kumuhamisha mfanyakazi wakekwa njia ya kuazimwa au kudumu ili kufanya kazi kwa mujibu wa Sheria auSheria nyengine yoyote inayotumika Zanzibar.

(3) Mfanyakazi aliyehamishwa kwenda kufanya kazi katika mamlakaya serikali ya mtaa, ataelekezwa, kusimamiwa na kuongozwa na Mamlakaya Serikali ya Mtaa husika.

Majukumuya Mkuuwa Idara.

23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

27

(4) Mishahara na maslahi mengineyo ya mfanyakazi yatalipwa kwamujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma, kanuni, maelekezo na miongozokama ilivyotolewa na wizara inayohusika na utumishi wa umma.

62. kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Utumishi wa Umma Mkurugenzianaweza kuteua wafanyakazi wa muda, ikiwa kama kuna haja na kuwalipamishahara na maposho kama itakavyoamuliwa na mamlaka muda baada yamuda.

63.-(1) Afisa aliyeidhinishwa wa kila Mamlaka ya Serikali ya Mtaa,atakuwa na uwezo ufuatao:-

(a) kuingia kwa wakati muafaka mahala popote ambapo ujenziunafanyika au kurekebishwa, kuhakikisha kama matakwa yakisheria kwa ujenzi huo na ruhusa ya matumizi ya ardhiimepatikana na, ikiwa hivyo , na kama masharti ya ruhusahiyo yanaheshimiwa;

(b) Kutoa na kupeleka hati za wito na amri kwa mujibu wa sheriana kanuni za mamlaka;

(c) Kuongeza mapato ya mamlaka;

(d) Kukamata bidhaa yoyote ambayo ana sababu ya maana yakuamini kwamba bidhaa hiyo ni na ya hatari au imewekwapasipofaa au ina madhara kwa umma;

(e) Kukamata mnyama asiyekuwa katika udhibit au kitu chochotekinachodhamiriwa kukiukwa kwa sheria hii na hivyokutumika kama ushahidi katika mamlaka ya Serikali ya Mtaaau kielelezo katika Mahakama ya kisheria.

(f) Kuhitaji kutolewa kwa ajili ya ukaguzi, uchunguzi auuthibitisho wa taarifa zote au hati ambazo zinawezakuhitajikakwa mamlaka;

(g) Kumtaka mmiliki waeneo au pahala na mtu mwengine yeyotehusika katika eneo au mahala hapo kumpa Afisaaliyeidhinishwa kila msaada na kufanya juhudi zote za kujibumaswali husika kuhusiana na usimamizi wa Sheria hii;

(h) Kuchukua hatua kwa mtu yeyote ambae anatangaza,anahamasisha au anasababisha kutangaza au kuhamsishabidhaa zozote au uuzaji huduma, kuuza, kuhamasisha auhuduma zilizo katika soko zilizouzwa, zilizohamasishwa aukutolewa ndani ya eneo la mamlaka kinyume na sheria hii.

(i) Kuchukua hatu adhidi ya mtu yeyote ambaya aneondoa,kubadilsha, kufuta au kusababisha kuondolewa ,kubadilisha,kufuta au kuondoa taarifa yoyote, alama, mabango na vituvyovyote vya thamani vinavyodhibitiwa chini ya sheria hii.

23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

28

(j) Kufanya jambo jengine lolote kwa maslahi na maendeleoya serikali ya mtaa kama yalivyoelezwa chini ya Sheria hiina Kanuni(2) Bila ya kuathiri kifungu kidogo cha (1) chakifungu hiki mtu yeyote anaekiuka masharti ya kifungu hikiakipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua laki mojaau kifungu kisichopungua mwezi mmoja.

64.-(1) Kila afisa aliyeajiriwa na Mamlaka wakati akishikilia ofisi yake,au ndani ya miezi mitatu baada ya kusita kushikilia ofisi hiyo, na kwa namnaambavyo kama Baraza litakavyoelekeza atafanya na kuwasilisha kwa Barazaau kama litakavyoagiza, hesabu sahihi ya fedha ya maandishi na mali zotezilizotokana na dhamana yake, na mapato na malipo yake, pamoja nastakabadhi na hati nyenginezo na kumbukumbu zinazounga mkono maingizohayo, na orodha ya watu ambao wanadaiwa kuhusiana na ofisi yake, kwakuonesha kiasi kinachodaiwa kutoka au kwa kila mtu.

(2) Kila ofisa huyo atalipa fedha zote anazopaswa kwa kulipa kwamshika fedha wa mamlaka au vyenginevyo kama mamlaka inavyowezakuelekeza.

(3) Iwapo Afisa huyo atakataa au kushindwa kufanya malipo yoyoteanayotakiwa na kifungu hiki au kuitosheleza mamlaka , mamlaka itachukuwahatua za kisheria dhidi ya Afisa huyo katika Mahakama yoyote yenyeMamlaka.

SEHEMU YA SABAMIPANGO NA MASHARTI YA FEDHA

65.-(1) Matayarisho ya mipango ya mamlaka ya serikali itazingatia njiaya ushirikishwaji, ambayo itajumuisha mipango ya idara ya mamlaka yamtaa.

(2) Mipango ya baraza itafanywa kwa mwaka, nusu mwaka namipango ya muda mrefu.

66.-(1) Kila Baraza la serikali ya mtaa litaanzisha kitengo cha mipangofedha , uchumi na maendeleo ambacho kitahusika na utoaji wote wa hudumana mipango ya uchumi na ya maendeleo ya mamlaka ya mtaa.

(2) Kitengo katika mamlaka yake itapanga utoaji wa huduma muhimuau za msingi , kuwiana na sera na mipango ya kitaifa na ya kisekta.

67. Kazi na wajibu wa Kitengo cha mipango ya fedha, uchumi namaendeleo zitakuwa:

(a) kuainisha, kuchambua na kuweka kipaombele mahitaji yaBaraza;

(b) kutayarisha bajeti na mpango wa Baraza kwa ajili yakuthibitishwa na Baraza la kutunga Sheria;

Uunga-nishaji wamipangoshirikishi

Kitengochamipangofedhauchumi namaendeleo.

Kazimajukumuya kitengochamipango ,fedha,uchumi namaendeleo.

23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

29

(c) kuongoza na kusimamia utekelezaji wa mpango na Bajeti yaBaraza;

(d) kuratibu na kusimamia shughuli za washiriki wote wamaendeleo katika utekelezaji wa miradi ya Baraza;

(e) kufanya kazi na wajibu mwengine wowote kamaitakavyopangiwa na Baraza.

68.-(1) Baada ya mpango kuidhinishwa, usimamizi, utekelzaji nautendaji wake utakuwa ni wajibu wa mkurugenzi wa Baraza.

(2) Mkurugenzi kila baada ya muda atawasilisha taarifa yamuendelezo wa Baraza na sekretarieti ya Mkoa kwa ajili ya uwajibikaji nasekreterieti ya mkoa itawasilisha ripoti wizarani na wizara ya kisekta.

69. Mamlaka ya serikali ya mtaa itapatiwa fedha kutokana na mapatoyanayotokana na mtaa, ruzuku kutoka serikalini, michango kutoka kwa jumuiaau watu binafsi, michango ya jamii na mikopo kwa mujibu wa uwezo wakekukopa au vyanzo vyengine vyovyote vilivyoidhinishwa na wizara.

(2) Kila baraza itatafuta fedha kutokana na vyanzo vyake ili kukidhimatumizi.

70. Kwa sharti la kuidhinishwa na waziri anaehusika na fedha, mamlakaya serikali ya mtaa inaweza kujipatia mapato kutokana na vyanzo vifuatavyo:-

(a) Kodi;

(i) Kodi ya mali ya Baraza;

(ii) Kodi nyenginezo kama zitakavyoidhinishwa na Sheria,taratibu na kanuni;

(b) Viwango vya mtaa

(i) Ada kwa mtumiaji huduma;

(ii) Ada ya leseni kwa mamlaka husika;

(iii) Faini za kiutawala;

(iv) Vibali;

(v) Ada na faini za mahakama;

(vi) Ada za mikataba;

(vii) Ada za mnada; na

(viii) Ada zozote nyenginezo na tozo kama zitakavyoidhinishwana sheria nyengine yoyote, taratibu na kanuni;

UtekelezajinautendajiwampangowaBaraza.

Vyanzovya fedhavyamamlakaya serikaliya mtaa.

Vyanzovyamapatoya mtaa.

23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

30

(c) Mapato ya ndani kutokana na vitega uchumi na miradi ya Baraza.

71. Kila mamlaka inaweza kushajiisha vyanzo vya mapato kutoka kwajamii katika njia zifuatazo:-

(a) mchango wa nguvu kazi;

(b) mchango wa fedha;

(c) mchango wa kitu;

72.-(1) Mamlaka ya serikali ya mtaa itashajiisha fedha kukidhi matumiziyake kwa njia ya ruzuku kutoka serikalini,wafadhili na mawakala wa ufadhilikwa mujibu wa sheria za fedha za Zanzibar.

(2) Mamlaka ya serikali ya mtaa inaweza kupokea ruzuku kutoka:-

(a) serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa njia ya:-

(i) ruzuku zenye masharti

(ii) ruzuku kamili;

(iii) Nusu Ruzuku , na

(iv) Ruzuku kutokana msaada wa serikali;

(b) ruzuku za wafadhili zinaweza kuwa:

(i) msaada wa kifedha wa moja kwa moja kutoka kwamamlaka ya serikali ya mtaa husika;

(ii) msaada wa kifedha usiokuwa wa moja kwa moja kwamamlaka husika ya serikali ya mtaa kupitia kwaMawakala wa ufadhili wa taasisi zisizokuwa zakiserikali za kimataifa na kitaifa na taasisi za kijamii,zinazofanya kazi katika eneo la mamlaka ya serikali yamtaa husika;

(iii) Msaada wa kitaalam wa mamlaka ya mtaa

(3) Ruzuku yoyote iliyotengwa chini ya kifungu kidogo cha (2) chakifungu hiki, itagawanywa kwa sekretariet ya mkoa husika kupitia akaunti yaBenki ya kila mamalaka serikali ya mtaa ambayo yatasimamiwa na mamalakaya serikali ya mtaa husika.

(4) Msaada ya moja kwa moja na isiokuwa wa moja kwa mojailiyotolewa kwa mamlaka ya serikali ya mtaa itajumuisha kama mapato yaRuzuku ya mipango ya maendeleo ya serikali ya mtaa na ratiba zilizopangwakwa ajili ya utekelezaji.

Michangoya jamii.

Ruzuku.

23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

31

73.-(1) Kwa masharti ya sheria zinazosimamia mikopo na dhamana,mamlaka ya serikali ya mtaa kama chombo kinachojitegemea kinawezakuomba mkopo kila baada ya mda kwa ajili ya shughuli za bajeti yakeiliyojipangia kulingana na uwezo wake wa kukopesheka.

(2) Kila mamlaka itahamasisha na kushajiisha uanzishaji wa taasisindogo za Kifedha ambazo zitaweza kupata huduma za mikopo kwa ajili yamiradi yake.

74.-(1) Kutaanzishwa mfuko wa maendeleo ya serikali ya mtaa, ambapomichango yote na makusanyo kwa mamlaka ya serikali ya mtaa ili kukidhimatumizi ya kimaendeleo ya mamlaka ya serikali ya mtaa italipwa.

(2) Vyanzo vikuu vya mfuko wa maendeleo ya serikali za mtaaitakuwa:-

(a) uhaulishaji fedha kutoka serikali ya mapinduzi ya Zanzibarkwa ajili ya miradi ya maendeleo ya kijamii katika ngazi yaserikali ya mtaa;

(b) fedha maalum iliyoelekezwa na serikali ya mapinduzi yaZanzibar na fedha za ziada kukidhi mapungufu ya bajeti yamamlaka ya serikali ya mtaa;

(c) misaada na michango ya ndani iliyoelekezwa kufadhili miradiya uchumi ya kijamii katika ngazi ya mtaa; na

(d) misaada na michango ya kimataifa iliyoelekezwa kusaidiamipango ya maendeleo ya serikali ya mtaa.

(3) Wizara inayohusika na fedha ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibaritaweka utaratibu na kanuni muhimu kwa ajili ya:-

(a) kuongoza hatua za ushajiishaji wa rasilimali, usimamizi,uangalizi na tathmini ya kazi za mfuko; na

(b) kuanzisha njia za kifedha na kiutawala ambazo mamlaka yaserikali ya mtaa na jumuiya za kiraia za eneo husika,zinaweza kupata fedha kutoka kwa mfuko wa serikali yamtaa.

(4) Wizara inayohusika na kamisheni ya fedha na uchumi , itaandaataratibu na kanuni muhimu za kuongoza kupitisha miongozo husika ya sera zajumuia kwa ajili ya Kamati ya mipango fedha, maendeleo ya uchumi ili :

(a) kuelekeza juu ya urejeshaji na miradi ya maendeleo yakijamii kama lengo la msingi la utoaji fedha;

(b) Kuweka vigezo vya tathmini na uteuzi wa miradiinayojitosheleza iliyowasilishwa kwa sekretarieti ya mkoailiyoombewa fedha; na

Mikopo.

Kuanzi-shwa kwamfuko wamaendeleoya serikaliya mtaa

23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

32

(c) kuishauri Kamati ya mipango fedha na maendeleo ya uchumikatika usimamizi na kanuni za maadili zinazohitajika katikausimamizi wa fedha za mradi

75.-(1) Mwaka wa fedha wa serikali za mamlaka ya mtaa utakuwa sawana mwaka wa fedha wa serikali kuu.

(2) Mkurugenzi atatayarisha na kuwasilisha bajeti ya makadirio yamapato na matumizi kwa Baraza kwa madhumuni ya kuidhinishwa kwa mudausiopungua miezi minne kabla ya kuanza kwa mwaka wa fedha na Barazalitaidhinisha makadirio ya Bajeti ndani ya siku kumi na tano tokea tarehe yakuwasilishwa kwa makadirio hayo.

(3) Mkurugenzi atawasilisha bajeti iliyopitishwa kwa sekratarietiyamkoa kwa ajili ya mapitio na kuiwasilisha kwa waziri ndani ya siku kumi natano baada ya kupokea bajeti hiyo kutoka kwa mkurugenzi.

(4) Waziri anaweza kuidhinisha na kuomba marekebisho kamaatakvyoona inafaa.

(5) Matumizi yanayotokana na makisio ya bajeti yaliyoainishwakatika bajeti ya mwaka iliyopitishwa, haitoizidi bajeti hiyo isipokuwa kwamakadirio ya bajeti ya ziada.

(6) Fedha yoyote ya ziada juu ya makadirio ya mapato na mfuko wahalali wa akiba hautotumiwa isipokuwa kwa mujibu wa sheria ya matumiziya ziada.

(7) Baada ya kupitisha bajeti , hakuna fedha itakayohaulishwa kutokakifungu kimoja cha matumizi kwenda chengine, na hakuna fedha yoyoteitakayotumiwa kwa kifungu kisichopangiwa katika bajeti bila ya idhini yabaraza na ridhaa ya waziri kupitia hatua halisi kama ilivyo katika taratibu zakupitisha bajeti ya mwaka.

76.-(1) Baada ya kuidhinishwa, utekelezaji wa bajeti utakuwa ni jukumula mkurugenzi wa baraza akisimamiwa na kitengo cha mipango, fedha namaendeleo ya kiuchumi na sekretariet ya mkoa.

(2) Katika mzunguko wa bajeti na kila hatua ya mzunguko wote wabajeti, Katibu tawala ataripoti kwa Baraza, kwa uthibitisho na uwajibikaji.

(3) Baraza litatunza madaftari yake ya hesabu ili kuweka kumbukumbuza:-

(a) Matendo yote ya fedha yaliyopokewa na kutumika;

(b) Mapato yote yaliyopakana au yaliyoingizwa lakinihajapokewa; na

(c) Matumizi yote yaliyofanywa laikini hayajalipwa.

Mwakawa fedhana bajetiyamamlaka.

Utekelezajiwa bajetiya baraza

23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

33

(4) Madaftari ya hesabu ya Baraza yatahifadhiwa na kutunzwa kwamujibu misingi na viwango vya kihasibu vinavyokubalika.

(5) Baraza litaweka na kutunza kumbukumbu sahihi za rasilimalizake zinazohamishika na zisizohamishika na madeni yaliyolipwa nayasiyolipwa.

(6) Kabala ya kumalizika kwa mwaka wa fedha, Kamati ya fedhaitaanda na kuwasilisha kwa Baraza na nakala kwa waziri ripoti ya fedha yautekelezaji wa bajeti kwa kipindi cha mwaka huo.

(7) Kamati ya Mipango,Fedha, na maendeleo ya uchumi inawezakuwasilisha bajeti ya ziada kwa Baraza la kutunga Sheria katika kipindi chamwaka wa fedha.

(8) Endapo Baraza limeshindwa kulipa mikopo yake, Waziri waFedha anaweza kutoa maelekezo kwa Baraza kurekebisha hali hiyo.

77.-(1) Mwishoni wa kila mwaka wa fedha, Serikali ya mtaa itatayarishamahesabu ya mwisho kwa mujibu wa matakwa ya Sheria hesabu ya fedhaza umma ua Zanzibar na kuwsilisha kwa mdhibiti na mkaguzi mkuu ndanikipindi kinachokubalika.

(2) Mahesabu ya Baraza ya serkali za mtaa yatakaguliwa kila mwakana mdhibit na mkaguzi mkuu wa Zanzibar au Kampuni iliyoidhinishwa namdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Zanzibar.

(3) Mkurugenzi atawezesha kuwasilishwa mbele ya Baraza,sekreterieti ya mkoa na Waziri ndani ya miezi sita kufuatia mwishono mwamwaka w a fedha ripoti ya ukaguzi wa fedha ya mapato na matumizi yote yaBaraza kwa mazingatio.

78. Mahesabu ya Mabaraza ya serikali ya mtaa yatakaguliwa kila mwakana mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu ya Zanzibar au Kampuni nyingineyoyote iliyoidhinishwa na mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu ya Zanzibar

79.-(1) Iwapo kutakuwa na ucheleweshaji wa upitishaji bajeti mwanzonoimwa mwaka wa fedha:-

(a) matumizi yataendelea huku yakisubiri kuidhinishwa kwa bajetikuu kwa mujibu wa makisio yaliyoidhinishwa mwaka uliopita,kama vile matumizi hayo yametumiwa kwa mwaka mpya wafedha;

(b) utozaji wa kodi yoyote mpya, viwango, ada na tozo, aumarekebisho yake hayatoathirika isipokuwa kwa idhini yaWaziri; na

Ukaguziwahesabu nafedha.

Ukaguziwahesabu yamamlakaya serikaliya mtaa.

Bajeti yamuda.

23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

34

(c) madeni ya Baraza na utekelezaji wa amri za mahakama , fainiau uwamuzi yataendelea kulpwa kutokana na mfuko.

80. Endapo yatatokea mazingira mapya, au jambo linalohusu ummaambalo halikuingizwa katika Kamati ya Mipango,Fedha, Uchumi namaendeleo, Mkurugenzi atawasilisha bajeti ya ziada au utengaji fedha kwaBaraza kwa ajili ya kupata idhini

SEHEMU YA NANE MAKOSA NA MASHARTI YA HATUA ZA KISHERIA

81.-(1) Kwa shari la idhini ya Mkurugenzi mashitaka au MwanasheriaMkuu, afisa sheria aliyeidhinishwa kuendesha mashtaka ya kisheria au kesiya madai anaweza, ama kwa jumla au kuhusiana na jambo maalum, kufunguaau kutetea kwa niaba mwenendo mbele ya mahakama ya kisheria.

(2) afisa sheria aliyeidhinishwa anaweza kufungua kesi kwa kuvunjwakwa sharti lolote, sheria ndogo au kanuni zilizofanywa chini sheria hii nasheria nyengine yoyote pale ambapo ukiukwaji huo umefanywa ndani yaeneo la mamalaka ya mtaa.

82.-(1) Mtu yeyote ambaye kwa madhumuni ya sheria hii:

(a) Bila ya udhuru au uhalali wa kisheria anashindwa kutii amriiliyotolewa chini ya sheria hii;

(b) Kutoa taarifa yoyote au kutoa hati yoyote ambayo ni yauwongo au ya kupotosha taarifa zake;

(c) Anazuia afisa yoyote katika utekelezaji wa kazi chini yasheria hii;au

(d) Vyenginevyo anakiuka masharti ya sheria hiiAna hatia yakosa akipataikana hatia atatozwa faini isiyopunguwa shilingimilioni moja au kifungo kwa muda wa miaka mitano auadhabu zote mbili faini na kifungo.

(2) Mtu yeyote anaefanya biashara huku usajili wake, leseni au ruhusaimesimamishwa au kufutwa chini ya sheria hii amefanya kosa na akipatikanana hatia atatozwa isiyopungua shilingi laki moja au kifungo kisichopunguamiezi miwili au adhabu zote mbili faini na kifungo.

(3) Mtu yeyote aliyeshindwa kusajili zana za kuhifadhia kwa ajili yabiashara ndani ya eneo la mamlaka ya serikali ya mtaa amefanya kosa naakipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua laki moja au kifungokisichopungua wiki mbili.

(4) Mtu yeyote ambaye ametoa leseni ya biashara au kibali ndani yaeneo la mamlaka ya serikali ya mtaa kinyume na sharti la sheria hii nakusababisha hasara ya mapato ya serikali ya mtaa amefanya kosa naataadhibiwa kwa mujibu wa sheria za fedha za umma.

Bajeti yaziada.

Mwenendowakisheria.

Makosanaadhabu

23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

35

(5) Mtu yeyote anejifanya mfanyakazi aliyeidhinishwa amefanyakosa atastahiki kutozwa faini isiyopunguwa shilingi laki tano au kifungokwa muda usiopungua mwaka mmoja.

83.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya sheria nyengine yoyote ya Zanzibar.Pale ambapo mtu anataka kusababisha maudhi kwa kusabisha hasara ndogokwa mazingira , ustawi, afya ya jamii au uchumi, afisa aaliyeidhinishwa wamamlaka ya mtaa anaweza kutoa notisi katika muundo ulioelezwa kumtakamtu huyo kukomesha maudhi hayo ndani ya muda ulioainishwa katika notisi.

(2) Notisi iliyotungwa kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (1) chakifungu hiki itaainisha aina za maudhi na hatua zinatakiwa kuchukuliwakukomesha maudhi hayo.

(3) Pale ambapo notisi iliyotolewa chini ya kifungu hiki haikutiiwamtu huyo atakuwa na hatia ya kosa na akipatikana na hatia atatozwa fainiisiyopungua shilingi laki tano au kifungo kisichopungua miezi miwili auadhabu zote mbili faini na kifungo.

84. Kwa masharti ya sheria nyengine yoyote inayotumika, mtu yoyotealiyeshindwa kuitumia na kuiendeleza ardhi ndani ya eneo la mamlaka yamtaa kwa ajili ya matumizi yaliyoidhinishwa na mpango wa maendeleo,mpango wa matuizi ya ardhi, mpango mkuu, mpango wa muundo wamakazi,mamlaka itawezesha mtu huyo kurekebisha, kubomoa au kuzuia ujenzihuo au ardhi.Isipokuwa kwamba, iwapo mtu huyo atashindwa kutii mashartiya sheria hii, sheria ndogo na kanuni zilizoundwa chini ya sheria hii,akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua shilingi laki mbili au kifungokisichopungua miezi sita au adhabuzote mbili faini na kifungo.

85. Mtu yeyote ambaye ana hatia ya kosa kinyume na masharti ya sheriana iwapo adhabu haikuelezwa, atastahiki kulipa faini isiyopungua shilingilaki moja au kifungo kisichopungua mwezi mmoja au adhabuzote mbili fainina kifungo

SEHEMU YA TISAMASHARTI MENGINEYO

86.-(1) Meya au Mwenyekiti anaweza muda hadi muda, kumuita mtupahala na kwa muda kama atakavyoamua, mkutano wa pamoja na wakaazindani ya eneo la mamlaka ya Serekali za mitaa kwa ajili ya kujadili mamboyanayoathiri wakaazi ambayo ataona kuwa yana umuhimu kwa jamii. Hakunakatika sheria hii kitakachochukuliwa kwamba kimevunja masharti ya sherianyengine yeyote kuhusiana na kufanyika mikutano ya hadhara.Ispokuwakwamba hakuna kikao kama hicho kitakachoitishwa kwa madhumuni yakukuza, kupinga au kujadili uchaguzi wa mtu yeyote kama mjumbe wa barazahilo.

87. Bila ya kujali masharti ya sheria nyengine yoyote, kitendo aumwenendo hautochukuliwa au hautoanzishwa dhidi ya afisa yeyote wamamlaka, au kwa kuzingatia kitendo chochote au mambo aliofanya au alioacha

Kero.

Matumiziay ardhiyasioru-husiwa.

Adhabuza jumla.

Mikutanoya wazi.

Ukomowauwajibikaji.

23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

36

kufanya wakati alipokuwa akifanya alifanya kwa nia njema wakati wautekelezaji wa kazi na uwezo wake aliopewa chini ya sheria hii.

88.-(1) Endapo theluthi mbili ya madiwani watawasilisha ombi kwaWaziri la kuvunjwa Baraza, Waziri ndani ya siku kumi na nne kuanzia sikualiyopokea ombi hilo, atafanya yafuatayo:

(a) kuchunguza iwapo sababu zilizoelezwa katika ombi hilozinaridhisha;

(b) iwapo uchunguzi umeonesha kuwa sababu zilizoelezwakatika ombi haziridhishi kuvunja Baraza, Waziri atalikataaombi la kuvunjwa Baraza.

(c) iwapo Waziri ana sababu za kuridhisha za kuamini kuwaBaraza livunjwe, atalivunja Baraza na ataiarifu Tume yaUchaguzi kuhusu kuwepo kwa amri kuvunjwa kwa Baraza.

89.-(1) endapo itahitajika Mamlaka ya mtaa baada ya kushauriana napolisi inaweza kuanzisha Polisi shirikishi ambao watafanya kazi katika eneolao.

(2) kazi , huduma na faida ya Polisi shirikishi zitaainishwa nakanuni zitakazotungwa kwa mujibu wa sheria hii.

90.-(1) Mawasiliano yote rasmi kwa Mamlaka ya mtaa, anuani yakeitakuwa kupitia kwa Mkurugenzi wa Mamlaka inayohusika.

(2) Mawasiliano baina ya Mamlaka za mitaa na Serekali kuu itakuwakupitia Sekreterieti ya Mkoa.

91.-(1) Serekali ya Mtaa yoyote inaweza kukubali, kuhifadhi nakusimamia mchango wa aina yoyote ulio halali, zawadi au maliinayohamishika au isiyohamishika kwa faida ya wakaazi wa eneo au sehemuya eneo husika, na inaweza kutekeleza kazi, ikijumuisha kazi za matengenezoau maendeleo, yanayotokana na au kutokea katika utekelezaji wa uwezoiliyopewa chini ya kifungu hiki.

(2) Mamlaka yoyote ya Mtaa haitokubali , bila ya taarifa ya Barazajuu ya mchango wa aina hiyo au fedha yenye thamani zaidi ya milionikumi au kwa kiwango chengine kitaekewa kumbukumbu katika kitabu chamahesabu kama itakavyoelezwa.

(3) Mamlaka ya Mtaa inaweza kupokea mchango kutoka kwamarafiki ndani au nje ya nchi, kwqa masharti kwamba taarfa ya mchangohuo iwasilishwe kwa Waziri anaehusika na mambo ya Fedha.

(4) Endapo madhumuni ya mchango au zawadi ni madhumuni ambayoMamlaka ya mtaa yamepewa uwezo wa kuzitumia fedha kwa kunyanyuakiwango, Mamlaka ya mtaa inaweza kwa kuzingatia masharti yoyote auvizuizi vilivyowekwa katika kutekeleza uwezo huo, kulipa matumizi hayo

UwezowakuvunjaBaraza

Polisiwasaidizindani yamamlakaza Mitaa.

Mawasilianobaina yaSerikaliKuu naBaraza.

MichangowaMamlakaya mtaa.

23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

37

yaliyofanywa katika kutekeleza uwezo ulitolewa na kifungu kidogo (1) chakifungu hiki nje ya mfuko mkuu.

92. Kwa mujibu wa masharti ya sheria hii,kila sheria ndogondogo,amri,taarifa au nyaraka nyenginezo zinazohitaji kuthibitishwa na Mamlakainayohusika itachukuliwa kuwa imethibitishwa ikiwa imesainiwa naMkurugenzi au afisa yeyote wa Mamlaka aliyeruhusiwa kwa niaba kwaazimio lolote la mamlaka husika.

93. Nyaraka inaweza kuwasilishwa kwenye Mamlaka kwa kuitoakwenye ofsi ya Mamlaka au kwa kuituma njia ya Posta au kwa njia yoyotenyengine ya kielektronikia.

94.-(1) Waziri anaweza kwa ujumla kutunga kanuni kwa ajili ya utekezajimzuri wa madhumuni ya sheria hii.

(2) Kanuni zitakazotungwa chini ya kifungu cha (1) cha kifunguhiki,zitatangazwa katika Gazeti Rasmi la Serekali.

95.-(1) Sheria zifatazo zinafutwa:

(a) Sheria ya Baraza la Manispaa la Zanzibar, Nam. 3 ya 1995;

(b) Sheria ya Baraza la Mji na Halmashauri ya Wilaya, Nam. 4ya 1995; na

(c) Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka ya Halmashauri yaMji na Wilaya) Nam. 3 ya 1986.

(2) Mamlaka ya Mtaa yoyote ambayo imeanzishwa auinayochukuliwa kuwa imeanzishwa na sheria zilizofutwa na ambayoilikuwepo kabla ya kuanza kutumika kwa sheria hii, itaendelea kuwepo naitachukuliwa kuwa kwa madhumuni ya sheria hii imeanzishwa auimetangazwa kwa masharti yanayohusika ya sheria hii.

(3) Mjumbe yeyote wa Mamlaka ya mtaa, Meya, Naibu Meya,Mwenyekiti au Makamo Mwenyekiti aliyechaguliwa chini ya masharti yasheria zilizofutwa, ataendelea na nafasi yake mpaka utakapofanyika uchaguzimkuu unaofuata wa Mamlaka ya Mitaa chini ya sheria hii.

(4) Leseni zote, vibali, ruhusa na hati au nyaraka nyenginezilizotolewa au kupewa na mamlaka ya Mtaa ikiwa bado zinatumika baadaya kuanza kutumika kwa sheria hii, zitaendelea mpaka tarehe ya kutumikakwa sheria hii ,itaendelea kuwa halali na kuwa na athari mpakaitakapomalizika muda wake, kusita kuwa na athari au kutumika, auzitakapofutwa na kutungwa mpya chini ya sheria hii.

(5) Watu ambao kabla ya kuanza kutumika kwa sheria hii, walikuwani wajumbe wa Baraza au kamati, wataendelea na nafasi zao na itachukuliwa

Utowajiwa taarifazamamlaka.

Nyarakaau Notisiinayo-tolewa.

Kanuni.

Kufua nakubakiza.

23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

38

kuwa wamechaguliwa kwa mujibu wa sheria hii, na wataendelea katikanafasi zao kwa muda uliobaki ispokuwa pale muda wao utakapomalizikawa kuwa wajumbe kwa mujibu sheria hii.

(6) Sheria ndogo ndogo zozote ambazo zimetungwa au zinazoendeleakutumika chini ya sheria zilizofutwa kabla ya tarehe ya kuanza kutumika kwasheria hii, zitaendelea kutumika na zitachukuliwa kuwa zimetungwa chini yamasharti ya sheria hii na zitarekebishwa au kufutwa kama zilivyotungwa.

(7) Vitu na mali zote ambazo zilikuwa zikimilikiwana Mamlaka yaMitaa mara kabla ya kuanza kutumika kwa sheria hii vitamilikiwa na Mamlakapamoja na maslahi, wajibu, malipo, majukum na amana zinaathiri mali hizo,.

(8) Shauri lolote liliopo mahakamani, maelekezo ya mahakama ,hokum au amri ya mahakama, ambazo bado zina nguvu ya kisheria dhidi yamamlaka au baraza kabla ya kuanza kutumika kwa sheria hii ambazo zinamilikiwa na Madiwani kazi na uwezo wa Baraza, itakua na nguvu ya audhidi ya baraza linalohusika ingepaswa kutekelezwa na au dhidi ya Mamlakana Baraza kabla ya kuanza kutumika kwa sheria hii.

23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

39

JADWELI LA KWANZA

[LIMEFANYWA CHINI YA KIFUNGU 13]VIGEZO VYA KUTAMBUA KIWANGO CHA BARAZA LA

SERIKALI YA MTAA1. Mamlaka ya Serikali za Mitaa yatatambuliwa kwa vigezovifuatavyo:

(a) Baraza la Jiji(i) Litakuwa na Manispaa mbili au zaidi;(ii) Uwanja wa ndege wa kimataifa na /au bandari;(iii) Miundombinu mizuri ya barabara, maji, umeme, afya,

masoko, mitaro na huduma za mawasiliano;(iv) Uwepo wa Sehemu za kujifurahishia;(v) Yenye sehemu moja au zaid za kihistoria au zenye faida

ndani ya eneo husika ;(vi) Zenye mchango mkubwa kiuchumi katika bajeti ya

Serikali.

(b) Baraza la manispaa

(i) Yenye idadi ya wakaazi kuanzia 150,000 mpaka300,000;

(ii) Angalau nusu ya idadi ya watu wanaoishi katika eneohilo wanapata Miundombinu ya barabara, maji, umeme,afya, masoko, mitaro na huduma za mawasiliano;

(iii) Kuwepo na Sehemu za kujifurahishia;(iv) Kuwa na kituo au afisi ya uendeshaji wa serikali kuu;

(c) Halmashauri ya Wilaya(i) Iwe na maeneo ya kiutendaji ya Wilaya;(ii) Uwepo wa idadi ya watu waliotawanyika ndani ya

Wilaya;(iii) Yenye Miundombinu mizuri ya barabara, maji, umeme,

afya, masoko, mitaro na huduma za mawasiliano;(iv) Uwepo wa mamalaka ya Mtaa; na

(d) Mabaraza ya Miji(i) Lazima ziwe na sifa za mjin(ii) Yenye idadi ya wakaazi kuanzia 75,000 mpaka

149,000(iii) Yenye Miundombinu mizuri ya barabara, maji, umeme,

afya, masoko, mitaro na huduma za mawasiliano;(iv) Kuwepo na Sehemu za kujifurahishia;(v) Kuwa na kituo au afisi ya uendeshaji wa serikali kuu;(vi) Faida za kihistoria za mji.

2. Mamlaka ya Mtaa yatatambuliwa kwa vigezo vifuatavvyo:

(a) Baraza la Wadi(i) Uwepo wa Diwani ndani ya wadi husika;(ii) Kuwepo na angalau shehia mbili;

23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

40

(iii) Uwepo wa Idadi ya wakaazi wasiopungua 9,000; na(iv) Uwepo wa angalau skuli moja ya msingi na/au zahanati.

(b) Baraza la shehia(i) Iwe ndani ya mipaka ya kiutawala ya shehia;(ii) Iwe na vijiji visivyopungua viwili katika maeneo ya

vijijini na mitaa isiyopungua miwili katika maeneo yamjini; na

(iii) Upatikanaji wa huduma za pamoja .

JADUELI LA PILI(LIMEFANYWA CHINI YA KIFUNGU 28)

KIAPO AU TAMKO LA UKWELI

Mimi………………………………………………………. nimechaguliwa/nimeteuliwa kuwa Diwani, ninaapa kwamba nitatumikia ofisi yangu nanitakuwa muaminifu katika kutimiza wajibu wangu kwa kadiri ya maamuzina uwezo wangu.

Kikao cha pamoja kilichoitishwa ………………………………… katikaukumbi wa Baraza la Jiji la Manispaa/ Baraza la Manispaa ya Mji/ Barazala Mji / ya …………………………………………………………..

JADWELI LA TATU(LIMEFANYWA CHINI YA KIFUNGU CHA 13) MAJUKUMU NA KAZI ZILIZOKABIDHIWA.

Fedha na maendeleo ya kiuchumi.

(a) Kuanda miupango ya kiuchumi na kijamii ya Baraza.(b) Kuandaa, kuweka na kupanga kumbu kumbu za takwimu za za

shughuli zote za kiuchumi, maendeleo na huduma za Baraza.(c) Kukuza na kushajihisha uekezaji, na kuwezesha biashara za

wawekezaji kwa mujibu wa Sheria.(d) Kushajihisha kujiwezesha, miradi ya wahisani, misaada ya

kibiashara, na kujitolea kwa jamii.(e) Kutafuta masoko na meneo ya biashara.(f) Kueneza uelewa kwa raia kwa shughuli za kiuchumi na mipango

ya kijamii.(g) Kupanga shughuli za kibiashara kwa kutoa leseni zinazotakiwa

kwa biashara za aina zote zinazifanyika katika eneo la baraza .(h) Kufanya utafiti ambao unalenga maendeleo ya Baraza na kukuza

rasili mali zake.(i) Kuanda makisio ya mapato na matumizi ya bajeti ya mwaka ya

Baraza.

23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

41

(j) Kudhibiti fedha za umma, kufungua hesabu za Baraza kwa tareheiliyoanishwa na kuwasilisha hesabu za mwisho za Baraza.

(k) Kutangaza na kuthibitisha kwa zabuni za Baraza.(l) Kupanga viwango.(m) Kusimamia na kuandaa maonesho katika baraza.

60. SHERIA NA MAMBO YANAYO HUSIANA NAYO.

(a) Kuandaa na kusambaza sheria ndogondogo, kanuni na hatua zakisheria za utekelezaji;

(b) Kuunda kanuni za ndani katika kufanya kazi za Baraza, kamatina idara zake;

(c) Kuweka viwango, afya ya jamii na mahakama;(d) kufanya ufuatiliaji wa taratibu za matakwa ya kisheria yana

husiana na mambo ya baraza kuhusu makubaliano na mikataba.

3 . KAZI ZA JAMII .

(a) kuanzishwa na kuimarisha mitaro ya maji ndani ya baraza .(b) kuanzisha miradi ya upandaji miti katika sehemu za mapumziko

na buruduni, na kusimamia uanzishaji na kutoa lesseni kwanyumba za wageni na mikahawa .

(c) Taa za barabarani na maeneo ya wazi(d) kushajihisha watu kuchangia katika kuanzisha vibaraza vya

pembeni .(e) kuimarisha barabara ndogo katika mabaraza .(f) kuweka maeneo ya vivuko na bandari kwa kushirikiana na taasi

zenye mamlaka, na kusimamia sehemu za maegesho ya ummakama ni vituo kwa ajili ya usafiri wa umma.

(g) Kusimamia maengo ya mji, kutoa ruhusa za ujenzi, kusimamiaujenzi na kutoa hati ya kukamilika kwa ujenzi na kudhibiti majengohatarishi.

(h) Kupendekeza mipango ya ardhi kwa shughuli za ujenzi, kilimo,viwanda, na uwekezaji kwa mujibu wa mpango mkuu wa baraza.

4. AFYA

(a) Kupanga mipango, kutayarisha na kutekeza mipango yakuimarisha afya ya mazingira.

(b) Kupambana na kuzaliana kwa mbu na wadudu hatarishi.(c) Kufanya usafi wa jamii na kuondosha uchafu unaotokana na

binaadamu na wanyama na takataka zitokanazo na kilimo naviwanda, kwa kukinga uharibifu wa mazingira;

(d) Kuanzisha vyoo vya umma na kuweka taratibu za matumizi nakuvisimamia na kuweka viwango kwa vyoo binafsi;

(e) Kusimamia masuala ya afya majumbani na huduma za viwandana kusimamia utekelezaji wake kwa mujibu wa viwango vyaafya vya majengo;

(f) Kuanzisha na kusimamia majengo ya machinjio ya wanyama.(g) Kuweka uzio, taa na kusimamia makaburi

23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

42

(h) Kusimamia maeneo ya vyakula na viwanji na kuzizibiti kwa kutoalesseni.

(i) Kusambaza muamko wa kiafya kwa wananchi kwa njia zoteyakiwemo maradhi UKIMWI na yasioambukiza.

(j) Kuteua wakunga kwa kuwapatia mafunzo na ufatiliaji katikautekelezaji.

(k) Kusimamia kutokomeza maradhi sugui na maradhi ya mripukokwa majibu wa mpango uliotangazwa.

(l) Kuanzisha vituo vya afya ya msingi na vituo vya urekebishaji.(m) Kutoa taarifa ya mripuko na majanga na kushiri katika kupambana

nayo.(n) Kusimamia na kuziongoza asasi za kiraia zinazotoa huduma za

afya.

5. ELIMU

(a) Kuanzisha na kusimamia skuli za msingi.(b) Kuanzisha na kusimamia madarasa ya elimu ya watu wazima

kwa kuondosha ujinga.(c) Kusimamia skuli za awali na maandalizi.(d) Kupendekeza kuanzishwa kwa skuli za Sekondari.(e) Kuunganisha kamati za wazee za skuli katika baraza.(f) Kuimarisha na kuhakikisha utekelezaji wa sera za elimu katika

ngazi ya serikali za mitaa(g) Kuweka kumbukumbu na kupendekeza katika mamlaka husika

kwa mambo yanayoaathiri elimu hususani katika masuala ya hakiza watoto na elimu kwa watoto wa kike.

(h) Kutekeleza mambo mengine yoyote iliyoithinishiwa na serikalikuu.

6. KILIMO, MALIASILI NA UTAJIRI WA WANYAMA.

(a) Kushiriki katika mipango ya uhifadhi na ulindaji wa maliasili,usalama na matumizi endelevu.

(b) Kusimamia misitu na kushajihisha upandaji wa miti.(c) Kuanzisha kinga ya moto.(d) Kuchangia katika udhibiti wadudu hatarishi wa kilimo.(e) Kuanisha, kuangalia na kuendeleza maeneo ya malisho na vituo

vya maji.(f) Kuhamamisha vikundi vya ushirika vya kilimo.(g) Kukuza shughuli za kilimo za baraza kwa kushirikiana na mamlaka

husika na kutambaza taarifa za kilimo kwa wakulima katika yabaraza.

(h) Kutoa takwimu sahihi za kulimo.(i) Kuwezesha huduma za umwagiliaji, mitaro na uhifadhi wa maji

katika kilimo cha umwagiliaji kwa kushikiana na mamlakahusika.

(j) Kuanzisha na kusimamia maeneo ya uvuvi katika maeneo yao;(k) Kukuza uanzishwaji wa miradi ya ufugaji wa ngombe, kuku na

samaki(l) Kukuza na kuimarisha mbegu za wanyama.

23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

43

7. MASUALA YA KIJAMII NA KIUTAMADUNI

(a) Kupambana na umasikini, kuwajali wazee, mayatima, wajane,watu wenye ulemavu na kupambana kwa kutoa njia sahihi zakuishi, kwa kushiriana na taasisi zinahusinana nazo;

(b) Kusherekea sherehe za kidini na kitaifa.(c) Kukuza Sanaa na utamaduni kwa kuimarisha viwango vya

wanachi na kurekebisha matendo ya wanajamii(d) Kukuza mabadiliko ya kijamii na kiutamaduni na kutumia njia

za mabadiliko ya kijamii na kiutaduni kwa kusimamia miradi yamipango ya maendeleo endelevu.

(e) kukuza miradi kibinafsi na kusimamia maendeleo yake.(f) Kuanzisha vituo vya kusimamia urekebishaji wa watoto.(g) kurekebisha vijana, michezo na vituo vya utamaduni.(h) Kuimarisha uvumilivu wa kidini na mashirikiano ya pamoja;(i) Kuanzisha sehemu za umma za maonesho, maktaba, kumbi za

mihadhara ya kitaaluma, vituo vya sinema kama ni njia yamaonesho kwa maendeleo na kukuza jamii, .

(j) Kuanzisha daftari la la rikodi za masuala ya kijamii.(k) Kuratibu ukusanyaji wa michango, misaada na ruzuku kwa

shughuli za kidini elimu, jamii, utamaduni, michezo na misaada;(l) Kuanzisha hifadhi ya nyaraka na makumbusho;(m) ukusanyaji wa matukio na mambo ya kale.

8. ULINZI NA USALAMA WA JAMII

(a) Kuangalia mikusanyiko ya kijamii kwa kuimarisha usalama wajamii.

(b) Kutoa vifaa vya kuzuia moto, mafuriko na kuanzisha kikosi chaZimamoto na uokozi;

(c) Kuweka majina ya mitaa, namba za nyumba na kuweka alama zanjia na kuchukua hatua nyengine za kiusalama kwa kuwezeshausalama wa barabarani;

(d) Kuzuia watu wasioruhusika kuchukua silaha za moto, silaha zahatari na miripuko;

(e) Kuwasilisha taarifa ya usalama katika mamlaka husika(f) Kuwasilisha mapendekezo katika taasisi husika zinazohusiana

na uzuiaji wa uhamiaji kutoka nchi jirani.

9. KAZI NYENGINEZO

(a) Kupokea wageni rasmini(b) Kutoa na kuthibishitisha hati za uongozi(c) Kutoa takwimu za shughuli za taasisi na matumizi.

23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

44

JADWELI LA NNE

(LIMEFANYWA KWA MUJIBU WA KIFUNGU CHA 59)VIKAO NA MWENENDO WA VIKAO VYA MAMLAKA ZA

SERIKALI ZA MITAA

1.-(1) Kila Baraza litakutana kwa kikao cha kawaida kila inapohitajikana angalau mara moja kwa kila miezi mitatu katika ofisi za Baraza au sehemuyoyoyte inayofaa ndani ya Mamlaka itakayoamuliwa na Baraza.

(2) Kikao cha mwanzo cha mwaka cha Baraza kitafanywa ndani yamwezi mmoja baada ya matokeo ya uchaguzi na baada ya hapo kila baada yakipindi cha miezi kumi na mbili.

(3) Kikao chengine kitafanywa kwa siku nyengine kabla ya mkutanowa mwaka kufuatana na maamuzi ya Baraza ya kikao cha mwaka au kamaKanuni za Baraza zitakavyoeleza.

(4) Mwenyekiti wakati wowote kwa ombi la maandishi lililosainiwasi chini ya theluthi mbili ya madiwani ataitisha kikao cha Baraza na sikuiliyopangwa kwa kikao hicho iwe ndani ya siku kumi na nne ya kuwasilishwakwa ombi hilo.

2.-(1) Katibu si chini ya wiki moja kabla ya muda uliopangwa wakufanyika kikao wa Mamlaka, atamuarifu kwa maandishi kila mjumbe, pahala,siku, muda wa kikao na shughuli iliyopendekezwa kufanywa katika kikaohicho.

(2) Notisi ya kikao itatolewa kwa kila diwani kwa kupewa mwenyeweau kwa kuiwasilisha katika sehemu ya makaazi yake ya kawaida, au katikaanuani ya shughuli zake. Kwa kuzingatia kwamba kutokupelekewa notisikwa bahati mbaya kwa kila diwani hakutoathiri uhalali wa kikao chochote.

3. Nusu ya wajumbe wote itafanya akidi ya kikao cha kawaida chaBaraza; na akidi ya kikao maalum cha Baraza ni theluthi mbili ya wajumbewote.

(a) Mjumbe atakaekuwa hajahudhuria vikao vitatu vya kawaida,bila ya kutoa taarifa kwa Meya au Mwenyekiti hatua zakinidhamu zitachukuliwa dhidi yake kwa mujibu wa Kanuniza Baraza zilizofanywa chini ya Sheria hii au sharia nyengineyoyote;

(b) Nafasi itakuwa wazi kwa tangazo la Tume ya Uchaguzi kwanafasi hiyo.

4.-(1) Lugha ya Baraza itakuwa ni Kiswahili kama ni lugha Rasmi aulugha ya mawasiliano na kwa ombi maalum kwa Mwenyekiti anawezakumruhusu mtu kutumia lugha ya kiingereza.

(2) Matumizi ya lugha za alama zinaweza kushajihishwa na Mabarazaza Serikali za Mitaa kwa faida za watu wenye mahitaji maalum.

Kikao chamwaka navikao vyakawaida.

Notisi zavikao

Akidi yavikao.

Lugha yaBaraza.

23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

45

5.-(1) Katibu ataweka na kutunza kumbukumbu zote za shughulizilizofanywa au zilizotokea katika mikutano yote ya Baraza.

(2) Kumbukumbu za mwenendo wa kikao cha Baraza au ya kila Kamatiyake yoyote zitandikwa kwa Kiswahili lakini zinaweza kutafsiriwa kwaKiengereza ikiwa itahitajika, na nakala zitagawanywa kwa madiwani naWaziri ndani ya wiki mbili wa kikao.

6. Wajumbe waliohudhuria katika kikao cha Baraza wanaweza kuahirishakikao na, ikiwa katika kikao chochote akidi ya kikao haijatimia kuwezakutekeleza uwezo wa Mamlaka, Mwenyekiti, ataahirisha kikao na kukipangakwa siku na tarehe atakayoiona inafaa.

7.-(1) Kila kikao cha Baraza kitakuwa wazi kwa umma na vyombo vyahabari.(2) Masharti ya kifungu kidogo cha (1) hayatotumika kwa vikaovyovyote vya Kamati vilivyoelezwa na Sheria hii.

8.-(1) Isipokuwa kama itakavyoelezwa vyenginevyo katika Sheria hii,katika kila kikao cha Mamlaka Meya au Mwenyekiti, wakiwa hawapo naibuMeya au Makamu Mwenyekiti ataendesha kikao.

(2) Ikiwa Meya, Mwenyekiti, Naibu Meya au Makamu Mwenyekitihawapo, wajumbe waliohudhuria watamteua kaimu Meya au mwenyekitikutoka miongoni mwao kuendesha kikao.

(3) Masuala yote yatakayohitaji maamuzi katika kikao chochote chaMamlaka kitaamuliwa na kwa wingi wa kura za wajumbe waliopo na iwapoya usawa wa idadi za kura Meya, Mwenyekiti au Mjumbe yeyote anaendeshakikao atakuwa na kura ya maamuzi ikijumuishwa kura yake ya kawaida.

9. Kwa Mujibu wa masharti ya sharia hii na kwa idhini ya Waziri,Baraza linaweza kutunga Kanuni za Kudumu kwa kuendesha shughuli zakena linaweza kubadilisha, kurekebisha au kufuta Kanuni.

Kumbu-kumbu zavikao.

Kuahiri-shwakwakikao.

Kikaokitakacho-fanywahadharani.

Meya auMwenye-kitikuongozavikao nakuwakura yauamuzi

Kanuni zaKudumu

23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

46

MADHUMUNI NA SABABU

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kwa mujibu wa kifungu cha 120cha Katiba ya Zanzibar ya 1984 imeazimia kuanzisha mfumo bora na waufanisi wa Serikali za Mitaa. Pia imeamua kwamba kwa mfumo wa Serikaliza Mitaa wenye ufanisi ni ule wakuwashirikisha watu katika ngazi za chini,na utakaozingatia misingi ya utoaji wa madaraka ambao ni “uhamishaji wamajukumu ya kiutawala kwa kazi maalum kwa ngazi za chini za kitaifa”.

Sheria zilizopo za Serikali za Mitaa hazijaeleza wazi na halijawezeshalengo hili, matokeo yake Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepititishaSera ya Serikali za Mitaa ya 2013, kwa utekelezaji mzuri wa sera. Serikaliimeandaa Mswada huu kwa utungwaji wa Sheria mpya ya Mamlaka yaSerikali za Mitaa ya mwaka 2014.

Mswada huu umegawika katika sehemu tisa na Majadweli manne kamaifuatayo:

Sehemu ya kwanza inahusiana na masharti ya awali, jina fupi, kuanzakutumika kwa Sheria na tafsiri.

Sehemu ya pili inahusiana na Mamlaka ya Serikali za Mitaa, maeneola Serikali za Mitaa, asili ya Mamlaka ya Serikali za mitaa, vyanzo vyasheria za Serikali za Mitaa, Malengo ya mamlaka ya Serikali za Mitaa,Misingi ya utawala ya Serikali za Mitaa, Ngazi za Serikali za Mitaa, aina zaMabaraza za Serikali za Mitaa na Utoaji wa mamlaka.

Sehemu ya tatu inahusiana na na uanzishwaji wa mamlaka ya Serikaliza Mitaa na mambo yanayohusiana nayo, vigezo vya uanzishwaji wa Mamlakaya Serikali za Mitaa, Mambo yaliomo katika tangazo la Uanzishaji, taratibuza uanzishwaji wa mamlaka za mitaa na hati za uanzishaji.

Sehemu ya nne inahusiana na uanzishwaji na muundo wa Baraza lajiji kazi zake, muundo wa Baraza la Manispaa, kazi zake, muundo wa Barazala Mji, kazi zake, muundo wa halmashauri za Wilaya, kazi zake, kazi zajumla za mabaraza ya Serikali za mitaa, uwezo wa jumla wa mabaraza zaSerikali za Mitaa, Ukaribishaji katika Baraza na kiapo cha Madiwani.

Vile vile sehemu hii inahusiana na, muda wa kukaa madarakani Meya,Naibu Meya, Mwenyekiti na Naibu Mwenyekiti, kuwa wazi kwa nafasi yaMeya, kazi na uwezo wa Meya kazi na uwezo wa Mwenyekiti, uondoshwajiwa Meya na Mwenyekiti, taratibu za kumuondosha Meya na Mwenyekiti,kujiuzulu kuwa mjumbe, mafao na maposho ya meya, madiwani si wa ajiraya kudumu, uteuzi wa Mkurugenzi, sifa za Mkurugenzi, kazi na majukumu yaMkurugenzi.

Sehemu hii pia, inahisiana na uanzishwaji na kazi za Kamati ya Ushauriya Wadi, muundo wa Kamati ya Ushauri ya Wadi, Mwenyekiti wa Baraza laWadi, Katibu wa Baraza la Wadi, Ajira na sifa za Katibu, Muundo wa Kamatiya Ushauri wa Shehia, kazi na uwezo wa Ushauri wa Shehia, sifa za wajumbewa Kamati za Ushauri za shehia, kazi za Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauriya Shehia na muda wa kazi wa mjumbe wa Kamati ya Ushauri wa shehia.

23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

47

Sehemu ya tano inahusiana na uanzishwaji wa Kamati za maendeleoza Serikali za Mitaa, kazi zake, Kamati za Kudumu za Jiji, Manispaa, Mji naHalmashauri za Wilaya, Kazi na uwezo wa Kamati za Kudumu, mpango wamaendeleo wa Kamati za Mitaa, Idara za Mamlaka za Serikali za Mitaa,kazi za Idara, majukumu ya wakuu wa Idara na vikao vya mamlaka za Serikaliza Mitaa.

Sehemu ya sita inahusiana na wafanyakazi wa Mamlaka ya Serikaliya Mitaa, wafanyakazi wasio wa kudumu, uwezo na kazi za maafisa nauwajibikaji wao.

Sehemu ya saba inahusiana na uunganishaji mipango shirikishi, kitengocha mipango, fedha,uchumi na maendeleo. kazi na wajibu wa kitengo chamipango, fedha,uchumi na maendeleo. Utekelezwaji wa mipango ya Baraza,vyanzo vya fedha vya Serikali za Mitaa, vyanzo vya mapato, michango yajamii, ruzuku, mikopo. Uansishwaji wa Mfuko wa Serikali za Mitaa. Mwakawa fedha na bajeti ya Mamlaka.Utekelezaji wa bajeti ya Baraza. Hesabu zamwisho na ukaguzi. Ukaguzi wa hesabu za Mamlaka ya Serikali za Mitaa,bajeti ya mpito na bajeti ndogo.

Sehemu ya ya nane inahusiana na utaratibu wa kisheria, makosa naadhabu, kero na matumizi ya ardhi yasiyoruhusiwa na adhabu ya ujumla.

Sehemu ya tisa inahusiana na vikao vya umma, ukomo wa dhima,uwezo wa kulifuta Baraza mapema, polisi wasaidizi wa Mamlaka ya mitaa,mawasiliano baina ya Serikali Kuu na Baraza, michango kwa mamlaka zamitaa, utoaji wa notisi kwa Mamlaka, kutoa hati au notisi, kanuni, kufutwana, kubakishwa.

ZANZIBAR (HAJI OMAR KHERI)23 Oktoba, 2014 Waziri wa Nchi- Ofisi ya Rais, Tawala za

Mikoa na Idara Maalum za SMZ

23 Oktoba, 2014 GAZETI RASMI LA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR