FUNGUO ZA Wajibu wa KUMLINDA DAVID Mifumo ya ... ZA KUMLINDA DAVID DHIDI YA UKATILI Wajibu wa Mifumo...
Transcript of FUNGUO ZA Wajibu wa KUMLINDA DAVID Mifumo ya ... ZA KUMLINDA DAVID DHIDI YA UKATILI Wajibu wa Mifumo...
FUNGUO ZA
KUMLINDA DAVID
DHIDI YA UKATILI
Wajibu wa
Mifumo ya Kitaifa
ya Ulinzi watoto
“ Nilipokuwa mtoto,baba yangu wa kambo
alikuwa akitumia dawa za kulevya, na mama yangu
akiwa hayupo,alikuwa akinipapasa na kunigusa
sehemu zangu za siri. Sikufahamu kilichokuwa
kinaendelea. Nilikuwa mtoto tu, mwenye umri wa
miaka sita.
Alikuwa akiniambia kwamba jambo hili liwe siri kati yetu
sisi wawili na kwamba nisimwambie mtu yeyote. Wakati mwingine alikuwa
akinifanyia vitendo ambavyo vilikuwa vinaumiza.
Nilisikia aibu na sikupenda watu wengine wanione,
kwahiyo nilijificha.
”- David –
Zifuatazo ni funguo za
mfumo wa kitaifa wa
ulinzi wa watoto
Mifumo ya ulinzi wa watoto ni muhimu ili kuzuia na kushughulikia aina zote za uonevu dhidi ya watoto, ukiwemo unyanyasaji wa kijinsia na unyonyaji, kutojali, utandikwaji wa viboko, watoto wanaofanya kazi za hatari, ajia ya watoto katika vikundi vya kivita, ndoa za mapema na vitendo vingine vya kimila vyenye madhara.
Mkakati wa kitaifa unahakikisha
kwamba mpango tendaji wa kuzuia hali kama
iliyomtokea David unakuwepo.
Mkakati wa
Kitaifa
Mkakati wa kitaifa,
sera au mpango
tendaji wa kuzuia
ukatili dhidi ya
watoto wenye
makusudi halisi na
ya muda maalum na
mkakati wa
utekelezaji ni lazima
uandaliwe.
Mkakati wa kitaifa unahakikisha kwamba mpango tendaji wa
kuzuia hali kama iliyomtokea David upo.
Mkakati wa kitaifa, sera au mpangotendaji wa kuzuia ukatili dhidi ya watoto, wenyemakusudi halisi na wa muda maalum, pamoja na mkakati wa utekelezaji ni lazima viandaliwe.
MKAKATI
WA KITAIFA
“ Hatimaye nilimwambia rafiki yangu yaliyonitokea
na akanishawishi nimweleze mwalimu
wangu. Mwalimu wangu alikuwa na wakati mgumu kuniamini mwanzoni lakini
pia alinieleza kwamba kitendo alichonifanyia
baba yangu si sawa na ni kinyume na sheria.
”
MFUMO WA
KISHERIA
Sheria za kitaifa ni lazima zizuie aina zote za ukatili dhidi ya watoto katika mazingira yote ikiwemo majumbani, na ni lazima zitekelezwe na kufuatiliwa kwa namna inayoleta matokeo.
“Mwishoni walimu wangu walinisindikiza kituo cha Polisi
kutoa taarifa kuhusu yale yaliyotokea. Polisi walimwita
mwanaume mmoja kutoka katika idara ya huduma za jamii,
Bob, ambaye ndiye aliyekuwa mtu niliyekuwa nawasiliana nae.
Alinisindikiza kwa daktari na alizungumza na mama yangu.
Mama yangu alipata mshtuko mwanzoni, lakini baadae
alikasirika sana na baba yangu wa kambo. Aliamua tukakae na
bibi kwa muda. Bob alikubaliana na uamuzi huu.
”
SHIRIKA
LINALORATIBU
Shirika linahusika na uratibu ngazi ya taifalinawajibika katika utekelezaji wa mkakati wa kitaifa na inabidi liwe na uwezo wa kuzihusisha na kuziratibu sekta za serikali (ustawi wa jamii, afya, elimu, haki, n.k..) na kuzihusisha asasi za kiraia, mashirika ya kimataifa, familia na watoto kwa njiailiyo salama.
“Katika miezi iliyofuata nilipata msaada mkubwa kutoka kwa Bob na wengine, ikiwemo kwenda kumwona
daktari mara kwa mara. Mnasihi wangu aliniomba nisimulie yale
yaliyonitokea kwa kuchora picha. Wakati mwingine nilikuwa nalia na
kupiga makelele na sikuona raha yoyote ya kuishi.
Mwanzoni sikutaka baba yangu wa kambo aadhibiwe kwani nilihisi kuwa
mimi ndiye niliyesababisha yaliyotokea. Lakini baada ya
kuzungumza na Bob, nilielewa na kukubali kwamba baba yangu wa
kambo anahitaji kuadhibiwa na pia kusaidiwa kutambua kwamba
kitendo alichonifanyia kilikuwa ni kosa.
”
HUDUMA ZA KUZUIA
NA KUSHUGHULIKIA
MASUALA ZA MAHALI
HUSIKA
Ngazi ya serikali ya mahali inayo wajibu wa kwanza wa kuhakikisha kuwepo kwa huduma zinazofikika, zenye kujali watoto, zinazozuia kutokea kwa hali fulani, zenye mwitikio ambazo zinajumuisha utoaji wa taarifa, pamoja na taratibu za kutoa rufaa na programu za uponyaji, urekebishaji na kuingizwa upya katika kundi.
“Baada ya muda fulani baba yangu wa kambo alipelekwa mahakamani.
Sikutaka kukutana naye mahakamani kwahiyo Bob
alihakikisha kwamba niliweza kuwaeleza majaji kile kilichotokea
kwa kutumia kinasa sauti cha video. Nilielezwa kwamba baba
yangu wa kambo atafungwa hela kwa miaka 5.
Sikuona tena aibu, lakini nilimkumbuka baba yangu wa
kambo na mambo mazuri tuliyofanya pamoja, kama kwenda
kuona wanyama nilipokuwa mdogo.
”
MFUMO WA
SHERIA WENYE
KUJALI WATOTO
Serikali inaanzishamfumo maalum wa kisheria wenye kulengawatoto ambaounahakikisha kwamba watoto wanaweza kutoa taarifa kuhusu ukatiliwanaofanyiwa na kwamba wakosajiwanachukuliwa hatua za kisheria.
“Baada ya miezi kadhaa, nilianza kujisikia vizuri,
kwa msaada wa Mnasihi wangu, Bob aliniuliza
ningependa kufanya nini na ni kwa njia gani
angeweza kunisaidia. Nilitaka kurudi shule na
pia nilitaka kwaeleza watoto wengine kuhusu
uonevu wa kijinsia. Nilianzisha klabu ya
watoto.
”
Inabidi Serikali iwasikilize wasichana na wavulana na kuwahusisha watoto moja kwa moja katika uundaji na utekelezaji wa sera (na programu) zinazoshughulikia ukatili ambao watoto wanafanyiwa. Vitendo vya watoto wenyewe vya kushughulikia ukatili inabidi viungwe mkono.
USHIRIKI WA
WATOTO
Acha ukatili
dhidi ya watoto
“Klabu yangu ya watoto ilianza kuwahamasisha watoto na watu wazima
kuchukua hatua dhidi ya uonevu wa watoto, na kuishawishi Serikali ifanye
mambo mengi zaidi. Kwa kuwa mara nyingi watu hawapendi kuzungumzia uonevu wa
kijinsia, Serikali ya mitaa haikuwa tayari kabisa kulikubali wazo hilo.
Lakini baada ya muda, Serikali iliamua kuanza kampeni ya kutoa taarifa. Magazeti
ya mahali yalitoa makala ili kuwapa taarifa walimu na wazazi wengine kuhusu uonevu
wa kijinsia.
”
Umma wenye uelewa na unaounga mkono jitihada husika unatakiwa uhusishwe katika jitihada za kuzuia madhara kwa watoto na kushughulikia masuala ya ulinzi wa watoto katika jamii zao, maeneo wanakoishi na katika jamii nzima.
UMMA WENYE
UELEWA NA
UNAOUNGA
MKONO JITIHADA
MABADILIKO
YANAHITAJI
UJASIRI
“Kutokana na shinikizo kutoka asasi za kiraia , baadhi ya shule
zilianza kuingiza suala la uonevu wa kijinsia katika mitaala ya
mafunzo ya walimu, na shule na taasisi nyingine zinazoshughulikia
watoto zilianzisha vifungu vya ulinzi wa watoto. Wataalamu wote wanaoshuhgulikia watoto walipata
taarifa na mafunzo kuhusu uonevu wa kijinsia ili waweze
kutambua mtoto ambaye yuko hatarini.
Kama walimu wangelikuwa wamepata mafunzo wangelitambua
kwamba kuna jambo ambalo halikuwa sawa katika maisha yangu. Kwa mfano, mwalimu
wangu shuleni angegundua kwamba wakati mwingine nilikuwa
najificha na kulia na angeweza kutambua tatizo ni nini.
”
Wataalamu wote wanaofanya kazi na au wanaowashughulikia watoto kama vile polisi, walimu, wafanyakazi wa serikali, walezi, maafisa wa mahakama, wataalamu wa afya na wafanyakazi wa jamii, ni lazima wapatiwe mafunzo kuhusu jinsi ya kutambua ukatili, kutoa rufaa na kuhakikisha matunzo na usiri.
Hatua za kuzuia ukatili kama vile kutoa taarifa, kampeni na mafunzo kuhusu haki za watoto na ulinzi na msaada kwa wazazi na walezi vinapaswa kutolewa.
WAFANYAKAZI
WANAOJITOA
KWA MOYO
“Rasilimali zaidi zilihitajika kuhakikisha kwamba watoto wote nchini wanalindwa zaidi kutokana
na aina zote za ukatili.
Miaka michache baadae, kutokana na ushawishi wa asasi za kiraia,
Serikali iliongeza bajeti ili kuzisaidia familia kwa ukamilifu
kutoa malezi bora zaidi kwa watoto wao na kuzuia uonevu wa
aina zote.
”
Rasilimali za kutosha na zinazostahili zinapaswa kutolewa ili kukomesha aina zote za ukatili dhidi ya watoto.
RASILIMALI ZA
KUTOSHA
“Serikali iliamua pia kuweka viwango kwa ajili ya malezi
mbadala ya watoto na kuanzisha mfumo wa
ufuatiliaji ili kuhakikisha kwamba wataalamu
wanaowashughulikia watoto na wnaofanya kazi na watoto
wanafuata taratibu sahihi.
”
Serikali inawajibika kuhakikisha kwamba huduma na jitihada vinasimamiwa kisheria na kufuatiliwa kwa ufanisi.
VIWANGO, SHERIA,
UFUATILIAJI NA
USIMAMIZI
“Jambo ambalo bado linakosekana ni mfumo
unaofahya kazi wa kukusanya data ambao unaisaidia
Serikali kufanya makadirio ya ukubwa wa tatizo, idadi ya
watoto waliopata msaada na idaadi ya watoato
waliosaidiwa kurudia hali ya kawaida. Serikali imejitoa
kutekeleza suala hili na kwa msaada wa baadhi ya
wafadhili tunatarajia mfumo huu utaanzishwa mapema.
Hivi sasa nina umri wa miaka 20 na mambo mengi
yamebadilika katika nchi yangu. Licha ya mambo yote ambayo Serikali na wengine wamefanya, wapo baadhi ya
watoto ambao bado wanaonewa kijinsia. Hivyo ni
lazima tuendelee kupigania haki ya watoto ya ulinzi.
”
Kila nchi inapaswa kuanzisha mfumo wa ukusanyaji data unaoratibiwa mahali pamoja, ambao unahakikisha upatikanaji wa taarifa za kila wakati kuhusu ukubwa wa tatizo pamoja na uelewa kuhusu masuala ya ulinzi wa watoto na njia zinazofaa za kushughulikia suala hilo.
MIFUMO YA
UKUSANYAJI DATA
Funguo zinazohakikisha
kuwepo kwa mfumo wenye
ufanisi wa ulinzi wa watoto
Hadithi ya David ni ya kutunga. Inaeleza hali za watoto wengiduniani kote. Kwa bahati mbaya, katika nchi nyingi, si mara zotekunakuwa na mwitikio na huduma zenye ufanisi, kama ilivyo katika kisa cha David. Hadithi hiiilitungwa kuonyesha jinsi ambavyomifumo ya ulinzi wa watoto inaweza kuzuia na kushughulikia aina zote za ukatili dhidi ya watoto.
Maandishi yameandikwa na Catherine Kates,
Roberta Cechetti na Lena Carlsson.
Usimamizi wa Mradi na Catherina Kates na
Roberta Cechetti.
Mpango wa Ulinzi wa Watoto
Shirika la Save the Children
Mei 2011
Kwa taarifa zaidi:
Tovuti: resourcecentre.savethechildren.se
Barua pepe: [email protected]
Imechapishwa na Pazzini Stampatore Editore
Verucchio (RN) Italia
Imechapishwa kwenye karatasi
zilizorejeleshwa
DIRA NA DHIMA YA SHIRIKA LA SAVE THE CHILDREN
SISI NI shirika la watoto linalojitegemealinaloongoza duniani .
DIRA yetu ni dunia ambamo kila mtotoanapata haki ya kuishi, kulindwa, kuendelezwa na kushiriki.
DHIMA yetu ni kuhamasisha mafanikiokatika namna dunia inavyoawatendeawatoto, na kufanikisha mabadiliko ya mara moja na ya kudumu katika maisha yao.
Mfumo wa Sheria