Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · AIDS Foundation, EnCompass...
Transcript of Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu na virusi … · AIDS Foundation, EnCompass...
PROGRAMU YA ELIMU RIKA KWA
AJILI YA KUPUNGUZA HATARI ZA
KIFUA KIKUU NA VIRUSI VYA
UKIMWI KATIKA MAGEREZA
NCHINI TANZANIA
KIJITABU CHA MWONGOZO KWA
WAELIMISHA RIKA
JULAI 2017
Kitabu hiki kimeweza kutolewa kwa msaada wa watu wa Marekani kupitia Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa
Kupunguza UKIMWI (PEPFAR) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) chini ya Mkataba wa Ushirika
namba AID-OAA-A-14-00046. Yaliyomo ni wajibu wa programu ya AIDSFree na si lazima kuwa yanawakilisha mawazo ya shirika
la USAID, PEPFAR au Serikali ya Marekani.
PROGRAMU YA ELIMU RIKA
KWA AJILI YA KUPUNGUZA
HATARI ZA KIFUA KIKUU NA
VIRUSI VYA UKIMWI KATIKA
MAGEREZA NCHINI
TANZANIA
KIJITABU CHA MWONGOZO
KWA WAELIMISHA RIKA
JULAI 2017
AIDSFree
Programu ya kuimarisha mikakati kabambe ya kudhibiti UKIMWI
(AIDSFree) ni mkataba wa miaka mitano unaofadhiliwa na Mpango wa
Dharura wa Ukimwi wa Rais wa Marekani (PEPFAR) na Shirika la Umoja
wa Mataifa la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) chini ya Mkataba wa
Ushirika -OAA-A-14-00046. AIDSFree inatekelezwa na Taasisi ya Utafiti na
Mafunzo ya JSI na washirika Abt Associates Inc., Elizabeth Glaser Pediatric
AIDS Foundation, EnCompass LLC, IMA World Health, Umoja wa
Kimataifa wa VVU / UKIMWI, Jhpiego Corporation, na PATH. AIDSFree
inasaidia na kuendeleza utekelezaji wa mikakati ya PEPFAR kwa kujenda
na kuendeleza uwezo wa kitaalam na kutoa ushauri wa kitaalam kwa
USAID, serikali za nchi husika na watekelezaji wa miradi ya UKIMWI katika
ngazi ya wilaya, mkoa na kitaifa.
Recommended Citation
Programu ya kuimarisha mikakati kabambe ya kudhibiti UKIMWI
(AIDSFree). 2017. Elimu rika kwa ajili ya kupunguza hatari za kifua kikuu
na virusi vya ukimwi katika magereza nchini Tanzania: Kijitabu cha
mwongozo kwa waelimisha Rika: Julai 2017. Arlington, VA: Programu ya
AIDSFree.
AIDSFree Tanzania Uniformed Services
JSI Research & Training Institute, Inc.
Plot No. 2 Mkwawa Road, Oyster Bay
P.O. Box 9263
Dar es Salaam, Tanzania
SHUKRANI
Shukrani zetu za dhati kwanza ziwaendee watu
wa Marekani kupitia Msaada wa Shirika la USAID
la Serikali ya Marekani kwa kufadhili utolewaji wa
Kijitabu hiki
AIDSFree/JSI inatoa shukrani kwa Uongozi wa
Magereza Tanzania, hasa Dkt. Juma Malewa,
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania
kwa kuidhinisha na kupitisha utungaji na
uchapishaji wa Kijitabu hiki. Tunamshukuru
Bwana Ali Abdalla Ali, Kamishna wa Chuo cha
Mafunzo Zanzibar aliyefunga rasmi mafunzo ya
majaribio ya Kijitabu hiki.
Tunatambua ushiriki na mchango uliotolewa na
waakilishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo na
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Taasisi za
kiserikali na zisizo za kiserikali na maafisa 54 wa
magereza hususan Dkt. Wilson Rugamba,
Mganga Mkuu wa Jeshi la Magereza, Dkt.
Richard Mwankina (Mrakibu Mwandamizi wa
Gereza la Ukonga ), Dkt. Juma A. Mwaibako
(Mrakibu, Gereza la Ruanda, Mbeya), Dkt. Hilda
Mmari (Mrakibu Msaidizi wa Magereza – Makao
Makuu), Dkt. Abdilatif Mkingule (Inspekta,
Ukonga Chuo), na Dkt. Dotto Pakacha (Inspekta,
Gereza la Segerea). Mapendekezo yao
yamesaidia kukiboresha Kijitabu hiki.
Shukrani za pekee ziwaendee Dkt. Beati Mboya,
Mkurugenzi Mkazi wa AIDSFree/Tanzania na Dkt.
Peter Maro, Mkurugenzi maswala ya kiufundi
kwa uongozi wao katika hatua mbali mbali
zilizochangia kuwepo kwa chapisho hili.
Tunatambua juhudi za Dkt. John Gulaka, Afisa wa
Uhusiano-Magereza wa AIDSFree/JSI katika
hatua mbali mbali za mchakato wa kukiandaa
Kijitabu hiki. Kwa wataalam wetu Bwana Ignatio
Chiyaka na Bi. Zuki Mihyo, Kijitabu hiki
hakingeweza kuwepo bila mchango wao kwenye
kuandaa yote yaliomo na kujumuisha maoni na
mapendekezo ya wadau husika wakiwemo
Uongozi wa Jeshi la Magereza Tanzania.
Msingi wa Kijitabu hiki umetokana na Kitabu cha
PharmAccess cha Waelimishaji Rika kwa Majeshi
ya Polisi, Magereza na Uhamiaji cha Mwaka
2013.
vii
YALIYOMO
Vifupisho ........................................................... ix
Utangulizi .......................................................... 1
Jinsi ya kutumia kijitabu hiki ............................ 2
Namna ya kuanza ............................................ 2
Somo 1: Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu
na VVU ............................................................... 5
Kipindi 1.1: Ufahamu juu ya VVU na
UKIMWI ............................................................... 6
Somo 2: Viwango vya HATARI ya
maambukizi ya VVU kwenye magereza .... 63
Kipindi 2.1: Viwango vya hatari ya maambukizi
ya VVU ................................................................ 64
Somo 3: Kifua kikuu na VVU: Matibabu,
huduma na msaada ........................................ 115
Kipindi 3.1. Huduma za upimaji VVU ........... 117
viii
Kipindi 3.2: Kifua kikuu, VVU: matibabu,
huduma, na msaada ........................................ 154
Kipindi 3.3: Kuzuia maambukizi ya VVU kutoka
kwa mama kwenda kwa mtoto ...................... 170
Somo 4: Kuvunja ukimya kuhusu kifua kikuu
na VVU. .............................................................. 178
Kipindi 4.1: Kutambua aina za shutuma katika
magereza ........................................................... 179
Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU
na Kifua kikuu .................................................. 203
Kipindi 5.1: Kukabiliana na hali ya kuwa
na VVU................................................................ 204
Orodha ya maneno ......................................... 222
Mirejeo ............................................................... 233
ix
VIFUPISHO
UKIMWI upungufu wa kinga mwilini
WAVIU watu waishio na virusi vya ukimwi
SOSPA toleo maalumu la sheria ya makosa
ya kujamiiana 1998
VVU virusi vya ukimwi
x
1
UTANGULIZI
Malengo ya programu hii ni kusaidia kubadili
tabia miongoni mwa wafungwa na wafanyakazi
wa magereza ili kupunguza hatari ya VVU na
kifua kikuu kwa kuwaelimisha juu ya mambo
yanayochangia na kuhamasisha matumizi ya
huduma za afya zipatikanazo. Waelimisha rika
kwa wafungwa na wafanyakazi wa magereza
watatoa mafunzo ili kuhakikisha wenzao
wanapata elimu, manufaa na ujuzi wa namna ya
kupambana na VVU na kifua kikuu mahali
popote iwe gerezani ama nje ya gereza. Kitabu
hiki kimetungwa kwa ajili ya matumizi ya
waelimisha rika kwa wafungwa na wafanyakazi
wa magereza na kimetengenezwa mahususi kwa
ajili ya kukidhi mazingira ya gerezani. Ingawa,
masomo yanaweza kupangwa kwa namna fulani
ili kutumiwa pia na wanufaikaji wengine ikiwemo
polisi.
2
Jinsi ya kutumia kijitabu hiki
Kitabu hiki kinawapa waelimisha rika shughuli na
maelezo muhimu kwa ajili ya kutoa mafunzo ya
VVU na kifua kikuu kwa wafungwa na
wafanyakazi wa magereza. Waelimisha rika
watatumia njia mbalimbali kuwashirikisha wenzao
kwenye majadiliano, michezo, michezo ya
kuigiza, pamoja na maswali na majibu. Mafunzo
haya yametengenezwa kwa ajili ya makundi
madogo madogo ya washiriki wasiozidi 20. Kila
kundi linapaswa kukamilisha masomo yote tano
yaliyo kwenye ratiba. Ratiba ya mafunzo inaweza
kupangwa kwa kuzingatia shughuli za kila siku za
magereza na uwepo wa wafanyakazi wa
magereza kwa ajili ya kusimamia nidhamu ya
wafungwa.
Mwongozo huu una masomo matano. Kila somo
lina utangulizi kwa ufupi sambamba na maelezo
ya kina na ya uhakika. Masomo yanahusisha
mada zifuatazo:
3
1. Maelezo ya msingi kuhusu VVU na UKIMWI
2. Tabia hatarishi kwa maambukizi ya kifua
kikuu na VVU gerezani
3. Matibabu ya kifua kikuu na VVU, huduma, na
msaada
4. Kuvunja ukimya juu ya kifua kikuu na VVU
5. Kuishi kwa matumaini ukiwa na kifua kikuu
au VVU
Namna ya kuanza
Kabla ya kufundisha chochote au kuongoza
majadiliano ya kikundi, soma na pitia mwongozo
huu ili kutambua na kuelewa kwa kina mada na
maelezo yaliyomo. Maandalizi haya yatamsaidia
mwelimisha rika kuongoza majadiliano kwa
ufanisi na kujibu maswali yoyote ambayo
yanaweza kujitokeza.
Maelezo yaliyomo kwenye mwongozo huu
yanakwenda sambamba na malengo ya serikali
ya Tanzania kuzuia maambukizi ya VVU na kifua
4
kikuu pamoja na kuzuia maambukizi nyemelezi
miongoni mwa wafungwa na watu waishio na
VVU, na hivyo kuboresha afya zao. Mwongozo
huu unatoa maelezo muhimu kwa wakati
muafaka.
Orodha ya maneno na maana zake imetolewa
mwishoni mwa mwongozo huu kwa ajili ya
kuwasaidia waelimishaji kuyatumia
wanapofafanua maneno magumu.
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
5
SOMO 1: ELIMU YA MSINGI
KUHUSU KIFUA KIKUU NA
VVU
Lengo
Kukuza kiwango cha elimu ya msingi kuhusu
kifua kikuu na VVU miongoni mwa wafungwa na
wafanyakazi wa magereza.
Madhumuni ya Mafunzo
Mwisho wa somo hili, washiriki watakuwa na
uwezo wa:
Kueleza maana ya kifua kikuu, VVU na
UKIMWI.
Kuelezea dalili na ishara za kifua kikuu, VVU,
na UKIMWI.
Kueleza namna ambavyo kifua kikuu na VVU
vinaweza kuenezwa uraiani na gerezani.
Kueleza namna ugonjwa unavyoendelea.
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
6
Kueleza mambo ya uhakika kuhusu kifua
kikuu, VVU, na UKIMWI nchini Tanzania kwa
ujumla na hasa kwenye magereza.
Kuelezea uhusiano baina ya kifua kikuu na
VVU gerezani.
Kipindi 1.1: Ufahamu juu ya VVU na
UKIMWI
Dakika 60
Kipindi 1.1: Mazoezi:
Kuelewa VVU na UKIMWI
VVU na UKIMWI ukweli/uongo
Ueneaji wa VVU na magonjwa ya ngono
Uhusiano kati ya VVU na jinsia
Mwisho wa kipindi washiriki watakuwa na uwezo
wa:
Kueleza maana ya VVU na UKIMWI
Kutokomeza imani za upotoshaji kuhusu
UKIMWI
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
7
Kueleza namna ambavyo VVU vinaenezwa
Kueleza hatua tano za dalili za UKIMWI.
Zoezi 1.Kuelewa VVU na ukimwi
Dakika 20
Hatua 1: Utambulisho
Jitambulishe kwa jina na uzoefu wako wa
shughuli za uwezeshaji wa kifua kikuu na
VVU (ukiwa nao). Eleza majukumu yako
kama mwelimishaji rika. Wakaribishe
washiriki kwenye majadilianao yao ya kwanza
juu ya kifua kikuu na VVU. Waombe
wajitambulishe. Kwa kifupi eleza mada kwa
ajili ya majadiliano.
Tambua kwamba kipindi hiki kinaweza kuwa
cha kibinafsi na chenye hisia kali. Ndani ya
kundi panaweza kuwepo na washiriki wenye
VVU au wenye rafiki wa karibu au
wanafamilia wanaoishi na VVU au UKIMWI.
Wakumbushe washiriki kwamba si vibaya
kuachana na swali na wahimize kutoa
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
8
maelezo yale tu ambayo wanajisikia vizuri
kuyatoa. Kama hawajisikii vizuri kuzungumzia
mambo haya kwenye kundi
kubwa,wanaweza kuzungumzia kwenye
makundi madogo madogo ama wawili wawili
au kutochangia kabisa.
Hatua 2: Taratibu za mafunzo
Taja kanuni hizi muhimu
Usiri: Heshimu maelezo binafsi ya kila
mshiriki. Jaribu kujizuia kutoa maelezo nje ya
kikundi lakini ikiwa utafanya hivyo, toa
maelezo ya ujumla pasipo kutumia majina ya
washiriki.
Heshima: Mheshimu kila mtu kwenye kikundi.
Hii inamaanisha kutowashambulia wengine
(kwa maneno au matendo) na kuwa muwazi
na mwepesi wa kuhisi mitazamo ya wengine.
Kumbuka kutumia kauli ya “MIMI”. Inavutia
zaidi kusema “vizuri kwa mimi binafsi,
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
9
ninahisi kwamba….” Badala ya kusema,
“Hapana, umekosea, ukweli ni kwamba…”.
Uangalifu: Sikiliza wanachokizungumza
wengine. Hutaishia kujifunza kitu fulani tu
bali utawafanya wengine wajisikie kuwa huru
zaidi.
Uwazi: Washawishi wengine kuzungumzia
uzoefu wao wenyewe, pasipo
kuwazungumzia wengine. Chukua tahadhari.
Usiwe mwoga wa kuzungumza kwa uwazi
bila ugomvi, kutukana ama kuwa mtu
asiyejali hisia za wenzake.
Hatua 3: Maswali na majibuvvu na UKIMWI
ni nini?
Swali: VVU ni nini?
Jibu: VVU maana yake ni virusi visababishavyo
upungufu wa kinga kwa binadamu. Virusi hivi
hushambulia mfumo wa kinga wa mwili ambao
huulinda mwili dhidi ya magonjwa.
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
10
Hatua 4: Utangulizi
VVU na UKIMWI nchini Tanzania kulingana na
“Ripoti ya Kuzuia VVU na UKIMWI 2016”(AVERT
2017)
Watu milioni 1.4
wanaishi naVVU
Asilimia 4.7 ya
watu wazima
wana maambukizi
ya VVU
Maambukizi
mapya 54,000 ndani ya mwaka 2015
Vifo 36,000 vyenye uhusiano na UKIMWI
viliripotiwa mwaka 2015
Asilimia 53% ya watu wazima wenye VVU
wanapata tiba ya kupunguza makali
UKIMWI ni nini?
UKIMWI maana yake ni upungufu wa kinga
mwilini. Kuambukizwa virusi vya ukimwi
hupelekea kudhoofika kwa mfumo wa kinga.
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
11
Jambo hili humfanya mtu aliye na VVU
kushambuliwa kwa urahisi na magonjwa ambapo
mtu asiye na maambukizi ya VVU huenda
asingepatwa au angepona kwa urahisi. VVU
hushambulia na kuharibu chembechembe za
mfumo wa kinga zijulikanazo kama CD4 ambazo
hupambana na maambukizi. Kupungua kwa
chembechembe za CD4 huufanya mwili
kushindwa kupambana na maambukizi na
baadhi ya saratani. Pasipo matibabu, VVU
vinaweza kuharibu taratibu mfumo wa kinga na
hatimaye kukua na kuwa ugonjwa unaoitwa
UKIMWI.
Hatua baada ya dalili za awali
Waambie washiriki kwamba mtazungumzia
hatua za ugonjwa zinazojitokeza baada ya
dalili za awali: maambukizi makali ya VVU,
kukua na kuongezeka kwa VVU bila
kuonesha dalili, na UKIMWI.
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
12
Hatua 1: Dalili kali za VVU
Ndani ya wiki 1–4 baada ya maambukizi, virusi
vimeanza kusambaa, na mtu anaweza
kukumbana na mlolongo wa dalili zijulikanazo
kama dalili kali za VVU. Dalili katika hatua hii
zaweza kuwa pamoja na homa, kuumwa kichwa,
maumivu ya miguu, kuwashwa kooni, kukua kwa
fundo limfu, uchovu, ukurutu mwilini, maumivu
na kuuma kwa viungo , kuharisha, kubadilika kwa
tabia ya ulaji, na kichefu chefu. Hatua hii
hujulikana kitaalamu kama “acute retroviral
syndrome” au “acute primary HIV infection,” na
dalili hizi zinaweza kutokea kwa kuwa mwili wako
unakuwa ukipambana na virusi. Ni mwitikio wa
asili wa mwili dhidi ya VVU. Katika kipindi hiki
kiwango kikubwa cha virusi huzalishwa. Katika
hatua hii ya maambukizi makali ya VVU, mtu
anakuwa katika hatari kubwa ya kueneza VVU
kwa wapenzi ama watumiaji wenza wa madawa
ya kulevya kwa kutumia sindano kutokana na
kuwepo kwa kiwango kikubwa cha VVU kwenye
mishipa yao ya damu. Kwa hiyo ni muhimu
kuchukua hatua za kupunguza hatari za kueneza
virusi.
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
13
Hatua 2VVU Kukua na kuishi mwilini bila
kuonekana:
Baada ya hatua ya maambukizi makali ya VVU,
ugonjwa huhamia kwenye hatua ijulikanayo
kama “kukua na kuishi kwa VVU mwilini bila
kuonekana.” Kipindi cha virusi kutoonekana
maana yake ni kipindi ambapo virusi vinaishi na
kukua ndani ya mwili wa mtu pasipo kuonesha
dalili zozote. Katika hatua ya ukuaji wa virusi
pasipo kuonekana, watu wenye VVU huwa
Chembechembe za CD4 ni chembechembe za damu
zinazofanya kazi kubwa ya kuulinda mwili dhidi ya
maambukizi. Virusi hutumia chembechembe hizi za
CD4 (mara nyingi huitwa chembechembe-T au
chembechembe –T saidizi) kuzaliana zaidi na kuenea
kote mwilini huku zikiharibu chembechembe hizo za
CD4. Baada ya hapo mwitikio wa kinga utaanza
kupunguza kiwango cha virusi mwilini hadi kufikia
kiwango fulani thabiti mwilini mwako. Wakati huu
chembechembe mpya za CD4 zitaanza kuongezeka,
lakini huenda zisifikie kiwango cha chembechembe za
CD4 zilizokwishaharibiwa.
Chembechembe za CD4 ni nini?
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
14
hawaoni dalili zozote labda zile ndogo ndogo
sana. Hatua hii mara nyingine huitwa “dalili za
maambukizi ya VVU” au “maambukizi sugu ya
VVU.” Eleza kwamba katika hatua hii, VVU bado
vinazaliana na kuongezeka kwa kiwango kidogo
sana, lakini bado vipo hai. Ikiwa utakuwa kwenye
matibabu ya kupunguza makali, unaweza kuishi
kwenye hatua hii kwa miongo kadhaa, kwa kuwa
matibabu husaidia kuwepo kwa kiwango kidogo
cha virusi.
Hatua 3: Ukimwi
Hatua ya mwisho ya maambukizi ya VVU
hutokea pale ambapo mfumo wa kinga unakuwa
umeharibiwa vibaya na virusi na mtu huwa katika
hatari kubwa zaidi au huwa hatarini kupatwa na
maambukizi mazito na hatari zaidi au magonjwa
ya bacteria na ukungu magonjwa ambayo
vinginevyo angeweza kupambana nayo
(“maambukizi nyemelezi”). Idadi ya CD4
inaposhuka chini ya 200 kwa kiwango cha
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
15
milimita za mchemraba za damu, yaani (200
chembechembe/mm3), unahesabiwa kuwa sasa
una UKIMWI. Kwa mtu mwenye mfumo wa kinga
imara, idadi ya CD4 huwa ni chembechembe
500–1,650 kwa milimita za mchemraba. Vile vile
utahesabiwa kuwa una UKIMWI ikiwa utapatwa
na ugonjwa nyemelezi mmoja ama zaidi, bila
kujali idadi ya CD4 zako.
Dalili za UKIMWI
Kupungua uzito ghafla
Homa za mara kwa mara au kutokwa na
jasho usiku
Uchovu wa kupindukia na usioelezeka
Kuendelea kuvimba kwa tezi za limfu kwenye
kwapa, kinena, au shingo
Kuharisha kwa zaidi ya wiki moja (uharo
usiosikia dawa)
Kuwashwa mdomoni, njia ya haja kubwa, na
sehemu za siri
Kukohoa pasipo kukoma
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
16
Majibu yenye rangi nyekundu, kijivu, pinki,
ama zambarau juu ya au chini ya ngozi au
ndani ya mdomo, pua au kope za macho.
Kupoteza kumbukumbu, unyonge, na
maradhi mengine ya nyuroni.
Magonjwa makubwa makubwa
Tofauti ya VVU na UKIMWI ni ipi?
Mtu mwenye maambukizi ya VVU anaweza kuwa
na afya njema kwa miaka kadhaa bila ya kuwa na
ishara au dalili za maambukizi mwilini. Mtu
mwenye virusi bila ya dalili ni “mtu anayeishi na
VVU” au “mwenye maambukizi ya VVU”.UKIMWI
ni hatua ya mwisho ya maambukizi na si kila
mwenye VVU hufikia hatua hii. Baada ya mtu
kuambukizwa VVU kwa kipindi fulani (mara
nyingi kwa miaka mingi), dalili zinazosababishwa
na virusi huanza kujitokeza. Katika hatua hii, watu
wenye VVU huwa na uwezekano mkubwa wa
kupatwa na maambukizi nyemelezi. “UKIMWI” ni
ufafanuzi wa kidaktari unaowalenga watu wenye
VVU wanaosumbuliwa na ambukizi moja au
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
17
maambukizi kadhaa mahususi, ikiwemo kifua
kikuu, saratani kwa kiasi kidogo, macho, ngozi,
na hali ya mfumo wa neva.
Zoezi 2. VVU zoezi la Kweli/Uongo
Dakika 20
Hatua 1: Zoezi
Eleza kwamba mtafanya zoezi la kutolea
ufafanuzi upotoshaji kuhusu VVU na
UKIMWI. Waambie washiriki kwamba
utasoma maelezo na kama wanaamini ya
kwamba maelezo ni ya“UKWELI” wasimame;
na kama wanaamini kuwa maelezo ni ya
“UONGO” wakae. Hakikisha maelekezo
yanaeleweka vizuri. Soma maelezo mara
moja au mbili. Waruhusu washiriki wajibu.
Waombe waelezee kwa nini wanaamini ya
kuwa maelezo ni ya KWELI/UONGO na
jadilianeni
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
18
Muongozo wa majibu:
MAELEZO KWELI/UONGO
1. Unaweza
kuambukizwa VVU
kwa kung’atwa na
mbu
UONGO: Imethibitishwa
kwamba VVU haviwezi
kuenezwa kwa njia hii.
2. Kufanya mapenzi
kinyume na maumbile
ni moja kati ya njia
hatari zaidi kwa
ueneaji wa VVU.
KWELI: Kufanya mapenzi
kinyume na maumbile ni
hatari zaidi katika ueneaji
wa VVU kuliko namna
nyingine yoyote ya
kujamiiana. Wakati wa
kujamiiana kwa njia hii,
mboo inaweza kuchana
ngozi laini njia ya haja
kubwa, jambo ambalo
litaviwezesha virusi kuingia
kwenye mishipa ya damu.
3. Watu wanaweza
kuambukizwa VVU
ikiwa watafanya
mapenzi mdomoni na
KWELI: VVU vipo kwenye
shahawa za mtu mwenye
maambukizi. Hivyo, VVU
vinaweza kuenezwa ikiwa
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
19
MAELEZO KWELI/UONGO
mtu mwenye
maambukizi ya VVU
shahawa zitaingia
mdomoni mwa mtu.
Hatari ya kuambukizwa
VVU unapofanya mapenzi
mdomoni huongezeka
ikiwa kuna vidonda
mdomoni. Hatari yaweza
kupunguzwa kwa kuvaa
kondomu na kuhakikisha
hakuna shahawa
zinazoingia mdomoni
mwa mwenza wako.
Kibaiolojia inawezekana
VVU kuenezwa kwa
kufanya mapenzi
mdomoni na mwanamke
mwenye VVU, lakini jambo
hili linadhaniwa kuwa ni
kwa kiasi kidogo. Kutumia
kinga kama kondomu au
kiwambo cha meno wakati
wa kufanya mapenzi
mdomoni kunaweza
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
20
MAELEZO KWELI/UONGO
kuzuia kueneza zaidi kwa
VVU, magonjwa mengine
ya ngono, na homa ya ini.
Kiwambo cha meno ni
kipande mraba
chembamba cha mpira au
silikoni ambacho huwekwa
juu ya meno wakati wa
kufanya mapenzi
mdomoni.
4. Zinapotumiwa kwa
usahihi, kondomu
zinaweza kuwakinga
wanaume na
wanawake kutokana
na maambukizi ya
VVU.
KWELI: Kondomu hutoa
ulinzi dhidi ya VVU,
magonjwa mengine ya
ngono, na mimba
zisizotarajiwa. Zikitumiwa
mara kwa mara kwa
usahihi, kondomu ni moja
kati ya njia bora zaidi za
kujikinga na VVU.
5. Dawa maalumu
zinaweza kutibu
maambukizi ya VVU.
UONGO: Hadi sasa,
hakuna tiba wala chanjo
kwa maambukizi ya VVU.
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
21
MAELEZO KWELI/UONGO
Ijapokuwa, kuna vidonge
vinavyoweza kupunguza
uzalianaji wa virusi ndani
ya mwili wa mtu aishiye na
VVU. Vile vile kuna dawa
zinazosaidia kukinga ama
kutibu maambukizi
nyemelezi
yaliyosababishwa na VVU.
6. VVU ni ugonjwa
unaowaathiri
makahaba na
wanaume
wanaofanya nao
mapenzi peke yake.
UONGO: Mtu yeyote
anaweza kuambukizwa
VVU.Hatari ya mtu kupata
VVU haina uhusiano na
jinsi mtu alivyo, bali tabia
aliyo nayo.
7. Ukiishi na mwenza
mmoja tu, huwezi
kuambukizwa VVU.
UONGO: Watu walio
waaminifu kwa wenza wao
bado wanaweza kuwa
katika hatari ya kupata
VVU ikiwa wenzi wao
wanashiriki kufanya
mapenzi ama kuchangia
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
22
MAELEZO KWELI/UONGO
nyembe na watu wengine
wenye maambukizi.
8. Watu wenye
magonjwa ya ngono
(maambukizi
yaenezwayo kwa njia
ya kujamiiana) wapo
katika hatari kubwa ya
kuambukizwa VVU
kuliko wale wasio na
magonjwa ya ngono
ikiwa watafanya
mapenzi na mtu
mwenye maambukizi
ya VVU.
KWELI: Magonjwa ya
ngono sehemu za siri
huvipa VVU njia rahisi ya
kupenya kwenye mishipa
ya damu.
9. Mtu anaweza
kupona VVU kwa
kufanya mapenzi na
bikira.
UONGO: Bikira hawana
uwezo wowote wa
kuwaponya watu wenye
maambukizi ya VVU. Hadi
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
23
MAELEZO KWELI/UONGO
sasa bado hakuna tiba
kwa VVU.
10. Huwezi kupata
VVU kwa sababu tu
unaishi kwenye
nyumba moja na mtu
mwenye ugonjwa.
KWELI: Kuishi kwenye
nyumba moja na mtu
mwenye VVU hakuwezi
kuwaweka hatarini wale
wanaoishi nae; VVU
havienezwi kwa migusano
ya kawaida ndani ya
familia.
11. Wakati wote
unaweza kutambua
kama mtu ana VVU
kwa mwonekano
wake.
UONGO: Watu wengi
wanaoambukizwa VVU
hawaoneshi dalili yoyote
ya ugonjwa kwa miaka
mingi. Ingawa, virusi
vinakuwepo mwilini mwao
na vinaweza kuenezwa
kwa watu wengine.
12. VVU vinaweza
kuenezwa kutoka kwa
mtu mmoja mwenye
KWELI: Kuchangia sindano
wakati wa utumiaji wa
madawa ya kulevya
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
24
MAELEZO KWELI/UONGO
VVU kwenda kwa mtu
mwingine pale
wanapochangia
sindano wanapotumia
madawa ya kulevya.
kunabeba hatari kubwa
sana ya ueneaji wa VVU.
Damu yenye maambukizi
hupitishwa kwa urahisi
kutoka kwa mtu mmoja
kwenda kwa mtu
mwingine kupitia sindano
yenye maambukizi au
vifaa vingine vilivyotumika
kuandaa au kujidunga
madawa.
Hatari kwa wanaume
na wanawake
kuambukizwa VVU
huongezeka pale
ambapo pana
magonjwa ya ngono
mahali ambapo
kiwango cha VVU kiko
juu.
KWELI: Magonjwa ya
ngono kwa wanawake
hayatambuliwi kwa urahisi
na mara nyingi huisha
pasipo kuchunguzwa.
Magonjwa ya ngono
sehemu za siri huvipa VVU
njia rahisi kuingia kwenye
mishipa ya damu.
Unyanyapa kwa wanawake
pia ni kikwazo ambacho
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
25
MAELEZO KWELI/UONGO
kinawavunja moyo
wanawake kutafuta
matibabu ya kutosheleza.
Zoezi 3: Jinsi VVU na magonjwa ya ngono
yanavyoenezwa
Dakika 10
Hatua 1: Maswali na majibi—uenezwaji wa
VVU
Swali: VVU vinaenezwaje?
Jibu: VVU haiambukizwi kwa urahisi kama surua
au homa ya mafua. Kwa mfano, virusi kama
surua na homa ya mafua huenezwa kwa njia ya
hewa kwenye maeneo yenye vizuizi palipo na
watu wenye maambukizi. VVU huishi kwenye
majimaji ya mwili ya mtu aliyeambukizwa kama
vile damu, shahawa, majimaji kabla ya shahawa,
uke, uteute kwenye njia ya haja kubwa, na
maziwa ya mama. VVU vinahitaji kuingia kwenye
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
26
mwili wa mtu. Hivyo basi, VVU vinaweza
kuenezwa kwa njia zifuatazo:
Kufanya ngono na mtu mwenye maambukizi
Kuongezewa damu au mazao ya damu na
mtu mwenye maambukizi ya VVU
Kuchangia matumizi ya sindano, mabomba
ya sindano, na vitu vyenye ncha kali vilivyo
na bacteria na mtu mwenye maambukizi ya
VVU
Kutoka kwa mama mwenye VVU kwenda
kwa mtoto wakati wa ujauzito, kuzaa ama
kunyonyesha.
Uwepo wa maambukizi yatokanayo na ngono
(kotokwa maji maji, vidonda, na miwasho )
huongeza hatari ya kupata na kueneza VVU. Hii ni
kwa sababu watu wenye VVU wenye maambukizi
ya magonjwa ya ngono wana kiwango kikubwa cha
VVU kwenye ute wa sehemu zao za siri na/au kwa
kuwa kuingia kwa virusi kumerahisihwa kutokana na
uwepo wa michubuko kwenye mucosa
Jinsi magonjwa ya ngono huongeza hatari ya kupata na
kueneza VVU
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
27
Hatua 2: Eleza
Zungumzia magonjwa ya ngono
Hatua 3: Maswali na majibu
Swali: Jinsi gani VVU havienezwi?
Jibu:
Maji maji mengine mwilini kama, machozi,
mate, jasho, matapishi na mkojo
Migusano binafsi: busu kavu mdomoni
pasipo na vidonda, kukumbatiana, kushikana
mikono, kusalimiana kwa kushikana mikono.
Mikusanyiko kijamii: wakati wa kazi, shuleni,
kwenye sinema, mgahawani.
Hewa au maji: chafya, kukohoa, kuogelea
bwawani/madimbwi
Vifaa: kalamu, vyoo, taulo, mashuka, sabuni,
vifaa vya kulia chakula, mavazi.
Wadudu: kung’atwa na mbu ama wadudu
wengine
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
28
Hatua 4: Maswali na majibu—upunguzaji wa
ueneaji wa vvu
Swali: Ueneaji wa VVU unawezaje kupunguzwa?
Jibu: “Mpango mkakati wa UNAIDS 2016–2021”
(ukurasa.58) eneo la matokeo 4, ili kupunguza
ukosefu wa usawa katika upatikanaji wa huduma
na bidhaa, umezitaka serikali za kitaifa kutoa
kipaumbele kwenye upatikanaji wa huduma za
kinga za VVU kwa makundi maalumu, ikiwemo
watu wanaotumia madawa ya kulevya na wakazi
wenza, ili kupunguza kwa haraka kwa kuwakinga
na kusimamia haki za watu wote kupata huduma
za kutosha zenye ubora wa juu bila ubaguzi.
Kupunguza hatari kwa vijana na makundi
maalumu kupata VVU na madhara yake kwenye
maeneo yote yenye maambukizi ni jambo
muhimu katika kutokomeza ugonjwa wa UKIMWI
(2016).
Ikiwa wewe ni mfanyaji mapenzi, kuna mambo
kadhaa muhimu unayopaswa kuchukua ili
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
29
kupunguza hatari ya kuambukizwa VVU.
Kutojamiiana ni njia mojawapo ya kuzuia kupata
au kueneza VVU. Ikiwa huwezi kuacha
kujamiiana, tumia kondomu (ya kiume ama kike)
wakati wote ufanyapo mapenzi kwenye uke, njia
ya haja kubwa ama mdomoni. Inapotumiwa
wakati wote na kwa usahihi kondomu za kiume
na kike njia bora zaidi katika kuzuia kuzuia VVU.
Shughuli mbalimbali za kimapenzi vile vile
zinabeba viwango tofauti vya hatari ya VVU.
Ngono kinyume cha maumbile pasipo kutumia
kondomu au ngono ya kulazimisha ni njia hatari
zaidi kwa ueneaji wa VVU kwa kuwa hupelekea
kuchanika kwa kuta za uke na njia ya haja kubwa:
Usichangie sindano, bomba za sindano na
vifaa vingine vyenye ncha kali na mtu yeyote
ikiwa unatumia madawa ya kulevya.
Pata matibabu ya VVU ikiwa wewe ni mama
mjamzito unayeishi na VVU ili kupunguza
hatari ya kumwambukiza mtoto wako wakati
wa ujauzito, kuzaa na kunyonyesha.
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
30
Hakikisha kwamba mazao ya damu
unayopokea yamefanyiwa uchunguzi wa
VVU.
Vaa vifaa vya kujikinga (Kama glavu na
miwani ya kuzuilia vumbi) na safisha mikono
baada ya kushika damu na maji maji
mengine (hasa kwa wataalamu wa huduma
za afya au watoa huduma).
Tumia dawa za kurefusha maisha au kinga ili
kujikinga na uwepo wa maambukizi (ikiwa
inapatikana) ikiwa upo katika hatari ya
kupata maambukizi ya VVU.
Jitolee mwenyewe, katahiriwe hospitalini
Punguza idadi ya watu unaofanya nao
mapenzi. Unapokuwa na idadi kubwa ya
wapenzi unajiongezea nafasi ya kupata
mpenzi mwenye VVU au ugonjwa mwingine
uenezwao kwa njia ya ngono.
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
31
Hatua 5: Elezea
Elezea “mapenzi salama” kwenye magereza
Majadiliano kuhusu mapenzi salama
hayatawezekana kwa kuwa magereza ni
mahali wanapokaa wafungwa kulingana na
jinsia zao wenyewe. Kwa sababu hii
hawawezi kuzungumzia mapenzi salama
kwa watu wenye jinsia moja, lakini elimu hii
itawasaidia watakapomaliza kutumikia
vifungo vyao na kurudi majumbani mwao
au katika jamii.
Mapenzi salama katika magereza
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
32
Zoezi 4: Uhusiano baina ya VVU na jinsi
Dakika 10
Hatua 1: Eleza
Kijamii jinsi imefafanuliwa, kwa kuzingatia zaidi
majukumu ambayo wanaume na wanawake
huyafanya katika jamii.Jinsi inaweza kufanya
jambo kubwa katika kupandikiza ufuasi. Kwa
pamoja jinsia na jinsi hutoa uzoefu wa kipekee
kwa wanaume na wanawake waishio na VVU.
Kwa hiyo kuelewa desturi za jinsi na ukosefu wa
usawa wa jinsi ni muhimu katika kupunguza
hatari ya VVU miongoni mwa wanaume na
wanawake, wavulana na wasichana. Ijapokuwa
kuwa mambo yanayofanana baina ya vihatarishi
vya VVU na tabia katika jinsi mbalimbali, tofauti
zipo na baadhi ya watu huambukizwa zaidi
kuliko wengine.
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
33
Hatua 2: Maswali na majibu
Swali: Kuna mtu anayeweza kutupa mfano wa
namna ambavyo majukumu ya kijinsi
yanavyoweza kuathiri uwezo wa mwanamke
kutumia dawa.
Jibu: Wanawake wanaweza kukumbana na
changamoto nyingi na vikwazo inapokuja suala
la afya zao wenyewe na ustawi wao. Wengi
wanaishi kwenye mazingira ya uonevu,
wanakumbana na unyanyapaa na ubaguzi katika
jamii, ukosefu wa amana za kiuchumi na huduma
za kiafya na mara kwa mara wao ndio watoa
huduma wa kwanza katika familia. Changamoto
hizi zinachangia kwa kiasi kikubwa uwezo wao
wa kumwona daktari, kufuata dawa, kunywa
dawa, kupumzika na kushusha kiwango cha
msongo wa mawazo.
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
34
Hatua 3: Hitimisho
Swali: Hivyo, nini kifanyike kuhusu jambo hili?
Jibu: Tukumbuke kwamba jinsia zetu, umri,
hadhi katika jamii zetu, nakadhalika ni mambo
yanayobadilika ambayo yanaweza kumfanya kila
mmoja wetu kuwa na kiwango tofauti cha hatari,
uzoefu na uwezo wa kupata huduma na fursa.
Kipindi 1.2 Ufahamu juu ya Kifua Kikuu
Dakika 110
Kipindi 1.2: Mazoezi
Utangulizi juu ya kifua kikuu na ugonjwa
Ueneaji wa kifua kikuu
Kifua kikuu kisichoonekana na ugonjwa
wa kifua kikuu
Jinsi ya kuchunguza kifua kikuu
Mambo ya uhakika na upotoshaji kuhusu
kifua kikuu
Maambukizi ya kifua kikuu na
changamoto za ugonjwa magerezani.
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
35
Madhumuni ya kipindi
Mwisho wa kipindi hiki, washiriki wataweza:
Kuelezea aina mbili za kifua kikuu
Kuainisha kifua kikuu kulingana na sehemu
ya mwili iliyoathiriwa
Kufuta dhana ya upotoshaji kuhusu kifua
kikuu
Kuelezea namna ambavyo kifua kikuu
kinaenezwa
Kuorodhesha viashiria na dalili za kifua kikuu
Kuelezea tofauti baina ya maambukizi ya
kifua kikuu yasiyoonekana na ugonjwa wa
kifua kikuu.
Kuelezea uhusiano baina ya kifua kikuu na
maambukizi ya VVU.
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
36
Zoezi 1. Utangulizi kuhusu maambukizi ya
kifua kikuu na ugonjwa
Dakika 10
Hatua 1: Eleza—kifua kikuu na vvu
VVU na kifua kikuu ni muunganiko hatari mno.
Kila ugonjwa huufanya ugonjwa mwingine uenee
haraka zaidi. VVU huufanya mfumo wa kinga wa
mwili kuwa dhaifu na mtu mwenye VVU halafu
akaambukizwa kifua kikuu huwa katika nafasi
kubwa kuugua ugonjwa wa kifua kikuu kuliko
yule mwenye kifua kikuu asiye na VVU.
Hatua 2: Elezakifua kikuu nchini tanzania
Shirika la afya ulimwenguni limeitaja Tanzania
kama nchi yenye mzigo mkubwa wa kifua kikuu
(TB), na moja kati ya nchi zenye mzigo mzito wa
kifua kikuu na VVU. Mnamo mwaka 2013,
wagonjwa 64,000 wa kifua kikuu waliripotiwa na
asilimia 83 (53,120) ya wagonjwa hawa walikuwa
wamepatiwa ushauri nasaha na kupimwa VVU.
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
37
Katika kundi hili, asilimia 39 (20,717) walikutwa
wakiwa na maambukizi ya VVU. Mwezi Aprili
2016 kulikuwa na takribani wagonjwa 295 wa
kifua kikuu mapafuni katika kila watu wazima
100,000 katika Tanzania (International
Organization for Migration in Tanzania 2016).
Serikali imeweka kipaumbele kutolewa kwa
pamoja kwa huduma za kifua kikuu na VVU ili
kupunguza mzigo wa magonjwa haya. Kwa hiyo,
watu waishio na VVU wanaotumia vidonge vya
kupunguza makali wana nafasi nzuri ya
kupambana na maambukizi ya kifua kikuu. Utoaji
wa huduma hizi pamoja utahakikisha pia
upatikanaji wa matibabu ya kifua kikuu na VVU
kwa kiwango kikubwa zaidi.
Hatua 3: Jadili
Kifupisho “TB” kinamaanisha nini?
Unadhani ni jambo gani husababisha kifua
kikuu?
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
38
Hatua 5: Elezavipi na kwa nini
Kifua kikuu kinasababishwa na bakiteria
wanaoitwa Mycobacterium tuberculosis. Kwa
kawaida bakiteria hawa hushambulia mapafu,
lakini bakiteria wa kifua kikuu wanaweza
kushambulia sehemu yoyote ya mwili ikiwemo
figo, uti wa mgongo na ubongo. Si kila
aliyeambukizwa na bakiteria wa kifua kikuu
huugua. Hivyo basi, kuna namna mbili zenye
uhusiano na kifua kikuu: maambukizi ya kifua
kikuu yasiyoonekana na ugonjwa wa kifua kikuu.
Ikiwa hautatibiwa vizuri, ugonjwa wa kifua kikuu
unaweza kuwa ugonjwa wa kifo. Wote wenye
hali fulani kiafya inayodhoofisha mfumo wa kinga
vile vile huwa hatarini kupata kifua kikuu.
Maziringira yanayowafanya watu kuwa katika
hatari kubwa ya kuathiriwa haraka na ugonjwa
wa kifua kikuu ni pamoja na:
Maambukizi ya VVU
Matumizi mabaya ya madawa
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
39
Silikosisi/asbestosi: ugonjwa wa mapafu
unaosababishwa na kuvuta hewa iliyo na
madini ya silika ambayo ni sehemu ya
mchanga, miamba na mawe yenye madini
kama vile kwazi. Baada ya muda, kuwepo
katika mazingira yenye chembechembe za
silika husababisha makovu kwenye mapafu,
ambayo yanaweza kuathiri uwezo wa mtu
kupumua.
Ugonjwa wa kisukari (aina ya 2): ugonjwa
sugu wenye kiwango cha juu cha sukari
(glukosi) isivyo kawaida kwenye damu.
Ugonjwa mkali wa figo
Uzito mdogo wa mwili
Saratani
Matibabu kama vile corticosteroids au
upandikizaji wa viungo.
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
40
Zoezi 2: Ueneaji wa kifua kikuu cha mapafu
Dakika 20
Hatua 1: Eleza: kifua kikuu cha mapafuni
nchini Tanzania
Idadi ya waathirika wa kifua kikuu cha mapafuni
katika Tanzania iliripotiwa kuwa watu 295 kati ya
watu 100,000, kulingana na hotuba ya bajeti ya
mwaka 2014/2015 ya waziri wa afya. Kifua kikuu
cha mapafuni ni moja kati ya maambukizi
nyemelezi kwa wengi miongoni mwa watu
waishio na VVU. Karibu asilimia 39 ya wagonjwa
wa kifua kikuu nchini Tanzania wameambukizwa
VVU (WHO 2012).
Hatua 2: Chemsha bongo
Wagawe washiriki katika makundi ya watu 3
au 4 na acha wajadili njia ambazo kifua kikuu
kinaenezwa kwa dakika 5. Yaombe makundi
yawasilishe majibu yao.
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
41
Kuvuta hewa yenye
matone madogo sana ya
erosoli ambayo hutolewa
pale mtu mwenye PTB
ambukizi anapokohoa,
piga chafya, tema mate,
zungumza au imaba.
Namna kifua kikuu cha
mapafu kinavyoweza enezwa
Hatua 3: ElezaNamna kifua kikuu cha
mapafu kinavyoweza enezwa
Mtu anapovuta hewa
iliyou na bakiteria
wanaosababisha kifua
kikuu cha kwenye
mapafu, bakiteria
wanaweza kukaa
kwenye mapafu na
kuanza kuzaliana.
Kifua kikuu cha
mapafu
kinaambukizwa, maana yake bacteria wanaweza
kuenezwa kwa watu wengine. Kifua kikuu kwenye
sehemu nyingine za mwili, kama vile, figo au uti
wa mgongo hakiambukizi. Eleza zaidi kwamba
kuna aina mbili za kifua kikuu: (1) kifua kikuu
ndani ya mapafu, ambacho kinaambukiza, na (2)
kifua kikuu nje ya mapafu, ambacho
hakiambukizi.
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
42
Hatua 4: Maswali na majibu: kwa nini kifua
kikuu cha mapafu ni ambukizi
Swali: Kwa nini wanadhani kifua kikuu cha
mapafu ni ambukizi?
Jibu: Kifua kikuu ndani ya mapafu kimo
mapafuni. Kinaenea pale mtu mwenye kifua
kikuu ambukizi anapotoa hewa nje iliyo na
bacteria wa kifua kikuu halafu mtu mwingine
anawavuta ndani bakiteria waliopo kwenye hewa
hiyo. Mtu mwenye maabukizi ya kifua kikuu cha
mapafu hutoa bakiteria zaidi pale anapofanya
vitendo kama kukohoa au kucheka. Kifua kikuu
nje ya mapafu hakiambukizwi kwa watu wengine
kwani kipo katika sehemu nyingine za mwili na
sio kwenye mapafu. Watu wenye ugonjwa wa
kifua kikuu cha mapafu wana uwezekano
mkubwa wa kuueneza kwa watu wanaokuwa nao
kwa karibu kila siku, ikiwemo wanafamilia, rafiki,
wafanya kazi wenzao na wafungwa.
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
43
Hatua 5: Fuatilia
Angalia kama washiriki wana maswali
Hatua 6: Fafanua zaidi
Kuna aina nyingine ya kifua kikuu inayoitwa
bovine TB ambayo ipo zaidi Tanzania. Bovine TB,
au Kifua kikuu cha mifugo, kinaweza kuambukiza
zaidi kwa wanyama, wakiwemo binadamu.
Bovine TB husababishwa na bacteria wajulikanao
kitaalamu kama Mycobacterium bovis (M. bovis)
ambao ni sehemu ya aina ya wadudu
wanaoambukiza kifua kikuu wajulikanao kama
Mycobacterium tuberculosis complex.
Hatua 7: Uliza
Mnadhani zipi ni dalili na viashiria vya kifua
kikuu?
Pitia majibu yaliyoorodheshwa kwenye boksi.
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
44
Viashiria na dalili za kifua kikuu
Kujisikia kuumwa au
dhaifu
Kupungua uzito
Homa za jioni na
kutoka jasho jingi usiku.
Kukohoa kwa zaidi ya
wiki mbili
Maumivu ya kifua na
kukohoa damu.
Zoezi 3: Maambukizi ya kifua kikuu
kisichoonekana na ugonjwa wa kifua kikuu
Dakika 10
Hatua 1: Eleza
Bakteria wa kifua kikuu wanaweza kuishi mwilini
bila ya wewe kuugua. Hii hujulikana kama
maambukizi ya kifua kikuu yasiyoonekana. Kwa
watu wengi ambao wanawavuta bacteria wa
kifua kikuu na kuambukizwa, mwili huwa na
uwezo wa kupambana na bacteria ili kuwazuia
wasikue. Watu wenye maambukizi ya kifua kikuu
kisichoonekana:
Hawana dalili
Hawajisikii kuumwa
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
45
Hawawezi kueneza bacteria wa kifua kikuu
kwa wengine
Mara nyingi huonekana kuwa na
maambukizi ya kifua kikuu kwa kipimo cha
kuchunguza athari kwenye ngozi au kipimo
cha damu.
Wengi huugua ugonjwa wa kifua kikuu ikiwa
hawatapatiwa matibabu kwa ajili ya
maambukizi ya kifua kikuu kisichoonekana.
Hatua 2: Taja
Watu wengi wenye maambukizi ya kifua kikuu
kisichoonekana hawataugua ugonjwa wa kifua
kikuu. Kwa watu hawa, bacteria wa kifua kikuu
hubaki mwilini bila kuwa na madhara kwa kipindi
chote cha maisha bila kusababisha ugonjwa.
Lakini kwa watu wengine, hasa wale wenye
mifumo dhaifu ya kinga kutokana na maambukizi
ya VVU, bakteria huweza kuleta athari, kuzaliana,
na kusababisha ugonjwa wa kifua kikuu.
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
46
Bakteria wa kifua kikuu huwa na athari ikiwa
mfumo wa kinga hautakuwa na uwezo wa
kuwazuia kukua. Bakteria wa kifua kikuu
wanapokuwa na athari (wanapoongezeka mwilini
mwako), hii huitwa ugonjwa wa kifua kikuu. Watu
wenye ugonjwa wa kifua kikuu ni wagonjwa.
Wanaweza vili vile kueneza bacteria kwa watu
wanaokuwa nao kila siku, hasa kwa kifua kikuu
cha kwenye mapafu. Baadhi ya watu hufikia
kupatwa na ugonjwa wa kifua kikuu mapema
mara baada ya kuambukizwa (ndani ya wiki
kadhaa) kabla hata ya mifumo yao ya kinga
kupambana na bakteria. Watu wengine
wanaweza kuanza kuugua baada ya miaka
kadhaa pale ambapo mifumo yao ya kinga
inapokuwa dhaifu kwa sababu nyingine.
Uwezekano wa kuugua ugonjwa wa kifua kikuu
ni mkubwa kwa watu wenye VVU ukilinganisha
na wale ambao hawana maambukizi. Watu
wenye mifumo dhaifu ya kinga, hasa wale wenye
maambukizi ya VVU, wana hatari kubwa ya
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
47
kupatwa na ugonjwa wa kifua kikuu kuliko watu
wenye mfumo wa kinga usio na maambukizi.
Zoezi 4: Tofauti kati ya kifua kikuu
kisichoonekana na kifua kikuu cha kwenye
mapafu
Dakika10
Hatua 1: Maswali na majibu
Swali: Ni nini tofauti kati ya kifua kikuu
kisichoonekana na kifua kikuu cha kwenye
mapafu?
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
48
Jadili na pitia majibu yaliyopo kwenye
jedwali hapa chini.
MTU MWENYE
MAAMBUKIZI YA KIFUA
KIKUU KISICHOONEKANA
MTU MWENYE KIFUA
KIKUU NDANI YA
MAPAFU
Hana dalili Dalili zaweza kuwa:
Kikohozi kibaya
kinachochukua wiki
3 au zaidi
Maumivu kifuani
Kukohoa damu au
makohozi
Udhaifu au uchovu
Kupoteza uzito
Kukosa hamu ya kula
Homa za baridi
Homa
Kutoka jasho usiku
(kupita kiasi)
Hajisikii kuumwa Kwa kawaida hujisikia
kuumwa
Hawezi kueneza bacteria Anaweza kueneza kifua
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
49
MTU MWENYE
MAAMBUKIZI YA KIFUA
KIKUU KISICHOONEKANA
MTU MWENYE KIFUA
KIKUU NDANI YA
MAPAFU
wa kifua kikuu kwa
wengine
kikuu kwa wengine
Kwa kawaida matokeo ya
kipimo cha TB kwenye
ngozi ama damu
huonesha kuwa ana
maambukizi ya TB
Kwa kawaida matokeo
ya kipimo cha ngozi
ama damu huonesha
kuwa ana maambukizi
ya kifua kikuu.
Kipimo cha x-ray ya kifua
hakina shida na makohozi
hayana maambukizi.
Anaweza kuwa na
kipimo cha x-ray ya
kifua kikionesha tatizo,
au makohozi
yakaonesha
maambukizi.
Anahitaji matibabu ili
kuzuia kifua kikuu ndani ya
mapafu
Anahitaji matibabu kwa
ajili ya kifua kikuu ndani
ya mapafu
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
50
Zoezi 5: Uchunguzi wa kifua kikuu
Dakika 20
Hatua 1: Maswali na majibu
Swali: Nani anapaswa kupimwa kifua kikuu?
Jibu: Wale ambao wapo kwenye hatari kubwa
zaidi ya kuambukizwa na bakiteria wa kifua kikuu
ikiwemo:
Watu wanaoishi kwa karibu na mtu mwenye
ugonjwa wa kifua kikuu (kama, wanafamilia,
wafungwa)
Watu kutoka kwenye nchi ambazo zina
kiwango kikubwa cha kifua kikuu
Watu wanaoishi au kufanya kazi kwenye
mazingira hatarishi (kwa mfano: magerezani,
vituo vya kutolea matibabu ya kifua kikuu)
Watoa huduma za afya wanaowahudumia
wagonjwa walio katika hatari zaidi ya
ugonjwa wa kifua kikuu.
Watoto wachanga, watoto, vijana walio
pamoja na watu wa zima walio kwenye hatari
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
51
zaidi ya maambukizi ya kifua kikuu
kisichoonekana au ugonjwa wa kifua kikuu.
Wenye VVU au wagonjwa wa UKIMWI.
Watu walio katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa
wa kifua kikuu
Wajawazito wenye
VVU
Watu wenye
maambukizi ya VVU
Watu waliopata
maambukizi ya
bakteria wa kifua
kikuu miaka miwili
iliyopita
Watu ambao
hawakupata
matibabu ya kifua
kikuu vizuri hapo
zamani
Watoto wachanga na
watoto wadogo
Watu wanaojidunga
madawa ya kulevya
Watu wanaoumwa
magonjwa mengine
yanayodhoofisha
mfumo wa kinga
Watu wenye umri
mkubwa
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
52
Swali: Ni nani aliye katika hatari zaidi ya kupatwa
na ugonjwa wa kifua kikuu?
Jibu: Eleza kwamba vipimo ya kifua kikuu kwa
ujumla huwa havihitajiki kwa watu waliopo
kwenye hatari ndogo ya maambukizi ya bacteria
wa kifua kikuu.
Hatua 2: Maswali na majibuUpimaji wa
ugonjwa wa kifua kikuu
Swali: Je mnafahamu jinsi ugonjwa wa kifua
kikuu unavyopimwa?
Jibu: Elezea aina mbalimbali za vipimo kwa
maambukizi ya kifua kikuu:
Kipimo cha kifua kikuu kwa njia ya ngozi
(kipimo cha uchunguzi cha mantoux)
Kipimo cha kifua kikuu kwa njia ya damu
Makohozi (mchanganyiko wa mate na uteute
uliokoholewa kutoka kwenye njia ya
upumuaji, hasa kama matokeo ya
maambukizi au magonjwa mengine na mara
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
53
nyingi huchunguzwa kwa kutumia darubini ili
kusaidia uchunguzi wa kitabibu.
Hatua 3: Eleza
Mtoa huduma za afya anapaswa kuchagua ni
kipimo gani cha kifua kikuu anapaswa kutumia.
Vigezo katika kuchagua kipimo gani kitumike ni
pamoja na sababu ya kufanya vipimo, uwepo wa
vipimo, na gharama. Kwa ujumla, haishauriwi
kumpima mtu kwa vipimo vyote viwili yaani
kipimo cha kifua kikuu kwenye ngozi na kile cha
damu.
Zoezi 6: Ukweli na upotoshaji kuhusu kifua
kikuu cha kwenye mapafu
Dakika 15
Hatua 1: Eleza
Waambie washiriki kwamba utasoma
maelezo na kama wanadhani maelezo ni
UKWELI wahamie upande wa kulia, na kama
wanadhani ni UPOTOSHAJI wahamie
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
54
kushoto. Kama hawajui, wasihame. Hakikisha
washiriki wameelewa maelekezo.Muulize
mshiriki mmoja ama wawili kutoa maelezo
kwa nini wanadhani maelezo ni ukweli au
uongo. Tumia ufunguo wa majibu (chini)
kwani una maelezo ya kina ambayo unaweza
kuhitaji kuwashirikisha washiriki ikibidi.
Ukweli na upotoshaji kuhusu kifua kikuu cha kwenye
mapafu
MAELEZO MAJIBU
Kifua kikuu cha kwenye
mapafu hutokea
kwenye jamii masikini
tu.
UPOTOSHAJI Kifua kikuu
cha kwenye mapafu
unaweza kumpata mtu
yeyote. Ingawa, watu
fulani wapo katika hatari
kubwa Zaidi ya kupata
kifua kikuu cha mapafu
kushinda wengine. Kama
mtu anatambua
vihatarishi, inaweza
kupunguza uwezekano
wa mtu kupata kifua
kikuu cha mapafu.
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
55
MAELEZO MAJIBU
Kwa kawaida matibabu
ya kifua kikuu cha
kwenye mapafu
huchukua miezi 6–8.
KWELI: Matibabu ya
kifua kikuu cha kwenye
mapafu kwa kawaida
huchukua miezi 6–8 na
yanaweza kufikia hadi
miezi 12 kwa kesi
maalumu.
Hakuna tofauti kati ya
ugonjwa wa kifua kikuu
cha mapafu na
maambukizi ya kifua
kikuu.
UPOTOSHAJI: Mtu
mwenye maambukizi ya
kifua kikuu haambukizi
kwa kuwa wadudu
hawana athari ama
hawaonekani. Mtu
hatambui kama
ameambukizwa kwa
kuwa hakuna viashiria
wala dalili
zinazoonekana. Mtu
mwenye kifua kikuu cha
mapafu ameathirika kwa
namna ya tofauti kabisa.
Mtu mwenye kifua kikuu
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
56
MAELEZO MAJIBU
cha mapafu anaweza
kuambukiza na ana
viashiria na dalili.
Kama mtu anakohoa
naweza kupata kifua
kikuu cha mapafu.
UPOTOSHAJI: Kifua
kikuu cha mapafu
hakikoholeki kwa urahisi.
Unalazimika kuwa karibu
kabisa na mtu mwenye
kifua kikuu cha mapafu
kwa muda mrefu (kwa
kawaida masaa mengi
au siku nyingi, kama vile
gerezani). Unapaswa
kutambua dalili za
ugonjwa ili uweze
kutafuta matibabu
mapema iwezekanavyo.
Kifua kikuu cha kwenye
mapafu ni ugonjwa
unaoambukiza na
unaweza kuenezwa kwa
njia ya hewa.
KWELI: Kifua kikuu cha
kwenye mapafu ni
ugonjwa ambao
unaenezwa kutoka kwa
mtu mmoja kwenda kwa
mwingine kwa njia ya
hewa wakati wa
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
57
MAELEZO MAJIBU
kukohoa, kupiga chafya,
kucheka, kuimba, kupiga
makelele na hata
kuzungumza. Ikiwa mtu
mwenye maambukizi
anakohoa ama kupiga
chafya, vijidudu
husambaa hewani
ambapo vinaweza
kuvutwa na wale
waliopo katika eneo hilo.
Kama mgonjwa
anakamilisha matibabu,
kwa kawaida huwa
amepona.
KWELI: Kama hakuna
usumbufu kwenye
matibabu na
yamefuatwa kama
ilivyoelekezwa kwa
kipindi husika, kwa
kawaida unakuwa
umepona kifua kikuu
cha mapafu.
Kumbuka: Kukamilisha
matibabu maana yake ni
kumaliza kozi ya
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
58
MAELEZO MAJIBU
matibabu ya kifua kikuu
ndani ya mapafu na
kufanyiwa uchunguzi wa
kifua kikuu na madaktari
ili kuthibitisha uponyaji.
Zoezi 7: Kifua Kikuu Magerezani
Dakika 10
Hatua 1: Eleza
Kuzuia ueneaji wa kifua kikuu ni moja ya
changamoto kubwa kwenye maeneo ya
magereza hasa pale kunapokuwa na
msongomano wa watu.
Hatua 2: Jadili
Ni changamoto zipi zinazojitokeza wakati wa
kukabiliana na maambukizi ya kifua kikuu katika
magereza?
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
59
Hatua 3: Eleza
Kuna changamoto nyingi: binafsi, kijamii na
kiutamaduni, sera, na mazingira, ikiwemo
zifuatazo:
Upungufu wa mbinu za kuthibiti maambukizi
na uwepo wa kiwango kidogo cha huduma
za afya kutokana na ufinyu wa rasilimali.
Wafungwa mara nyingi hutenganishwa
kwenye vizimba ama sehemu ya wagonjwa
bila ya kufanyiwa vipimo vya kiafya
(Wagonjwa wa kifua kikuu hutengwa).
Mlundikano, lishe hafifu, na ukosefu wa hewa
ya kutosha.
Idadi ndogo ya wafanyakazi wa afya.
Upungufu wa rasilimali kuendesha uchunguzi
wa kiafya na kununua madawa.
Kutofuata masharti ya matibabu miongoni
mwa wakazi wenza.
Hatari kubwa miongoni mwa wafungwa
kupata usugu wa kifua kikuu (kwa mfano,
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
60
wadudu wa TB kupata usugu kutoka kwenye
dawa mbalimbali za TB) kutokana na
kutofuata masharti, ingawa utumiaji wa dawa
chini ya uangalizi wa mtoa huduma ukiwa
umezingatiwa kila siku.
Zoezi 8: Uhusiano kati ya VVU na kifua
kikuu
Dakika 15
Hatua 1: Mapitio
Waambie washiriki kuwa tumezungumzia
VVU, kifua kikuu, na madhara ya VVU
kwenye mfumo wa kinga wa mwili wa
binadamu.
Hatua 2: Jadili
Jinsi gani maambukizi ya VVU yanaweza
kumwathiri mtu mwenye maambukizi ya kifua
kikuu.
Pokea maoni machache.
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
61
Hatua 3: Eleza
VVU huongeza kasi ya maambukizi ya kifua kikuu
kuwa ugonjwa wa kifua kikuu kwa kuwa VVU
hudhoofisha mfumo wa kinga. Ukiwa una
maambukizi ya VVU una nafasi kubwa ya kupata
kifua kikuu kuliko mtu asiye na maambukizi ya
VVU. Bakteria wa kifua kikuu wana nafasi kubwa
ya kuwa na madhara na kushambulia mapafu na
sehemu nyingine za mwili.
Hatua 4: Maswali na majibu
Swali: Watu wafanyeje ikiwa wana VVU na kifua
kikuu ndani ya mapafu?
Jibu: Wanalazimika kupata matibabu moja kwa
moja pasipo kuchelewa ili kupunguza kuugua
zaidi. Kila mmoja anapaswa kutumia dawa zake
kwa usahihi kabisa kama daktari au mtoa
huduma za afya alivyowaelekeza.
Somo 1. Elimu ya msingi kuhusu kifua kikuu na VVU
62
Hatua 5: Fafanua zaidi
Vidonge vya kifua kikuu ni vikali sana. Vinaweza
kutibu kifua kikuu, hata kwa watu wenye VVU
kwa baadhi ya watu. Kumbuka, Vidonge vya
kifua kikuu hufanya kazi vizuri pale tu ambapo
hutumiwa kulingana na maelekezo ya mtoa
huduma za afya.
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
63
SOMO 2: VIWANGO VYA
HATARI YA MAAMBUKIZI YA
VVU KWENYE MAGEREZA
Lengo
Kukuza elimu juu ya vihatarishi vya VVU katika
maeneo ya magereza
Dhamira
Mwisho wa somo hili, washiriki wataweza:
Kutambua na kuelezea viwango tofauti vya
vihatarishi vinavyochochea hatari ya
maambukizi ya VVU katika magereza.
Kuainisha jinsia na kuchunguza namna gani
desturi za kijinsia zinauhusiano na
maambukizi ya VVU.
Kueleza tofauti kati ya kuchukua tahadhari ya
VVU na kukabiliana na hatari za VVU
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
64
Kutambua viwango vya hatari ya VVU
kutokana na tabia mbalimbali za kimapenzi
Kutambua majukumu ya kijinsia
yaliyopangwa na jamii kwa ajili ya wanaume
na wanawake.
Kulinganisha njia mbalimbali zilizopo za
kujikinga na VVU
Kipindi 2.1: Viwango vya hatari ya
maambukizi ya VVU
Masaa 2, dakika 15
Kipindi 2.1: Mazoezi
Utangulizi juu ya ngazi tatu za hatari za
VVU
Jinsi na jinsia
Jinsi, jinsia na VVU: Kuchukua tahadhari
na kukubaliana na hatari
Kiwango cha hatari
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
65
Igiza kama mwanaume, igiza kama
mwanamke
Kufanya maamuzi kuhusu jambo
linalofaa na lisilofaa
Zoezi 1: Ngazi tatu za Viwango vya hatari
vya VVU
Dakika 10
Vifaa vinavyohitajika:
Karatasi kubwa za kuandikia, ubao wa chaki
Hatua 1: ElezaViwango vya hatari
Wafahamishe washiriki kwamba kuna ngazi
tatu za hatari za VVU:
Ngazi ya mtu binafsi
Ngazi ya familia
Ngazi ya jamii
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
66
Elezea zaidi kuhusu vihatarishi vya VVU:
Viwango vina uhusiano na mambo ambayo
huwaweka watu kwenye hatari ya
maambukizi ya VVU.
Vihatarishi vya VVU katika viwango vya mtu
binafsi, familia, na jamii na mifano ifuatayo
kwenye jedwali hapa chini:
NGAZI YA MTU
BINAFSI
NGAZI YA
FAMILIA
NGAZI YA JAMII
Elimu (kwa
mfano,
Kutokuwa
kabisa au
kuwepo na
kiwango
kidogo cha
elimu)
Mtazamo
(kwa
mafano.,
Mila za
kitamadu
ni na
imani
Miiko.
Mila za
kijamii (kwa
mafano,
wajibu na
majukumu ya
wanaume na
wanawake)
Sera za
serikali
Siasa/uimara
wa kisiasa
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
67
NGAZI YA MTU
BINAFSI
NGAZI YA
FAMILIA
NGAZI YA JAMII
dhana ya
uwanaume
miongoni
mwa
wanaume
ambayo
inapelekea
tabia
hatarishi,
dhana ya
uwanawake
miongoni
mwa
wanawake
inayozuia
majadiliano
kuhusu
mapenzi
salama)
Umri (kwa
Rasilimali
(kwa mfano;
ukosefu wa
vifaaa vya
kujifungulia
kwa
wafungwa
wajawazito).
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
68
NGAZI YA MTU
BINAFSI
NGAZI YA
FAMILIA
NGAZI YA JAMII
mfano,
wakazi
wenza vijana
mara nyingi
huwa katika
hatari kubwa
kimwili,
kiakili, na
ukatili wa
kijinsia
kutoka kwa
wakazi
wenza
wakubwa)
Matendo ya
kimapenzi
yasiyo
salama
Kuchangia
vitu vyenye
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
69
NGAZI YA MTU
BINAFSI
NGAZI YA
FAMILIA
NGAZI YA JAMII
ncha kali
(kama,
nyembe)
Ukosefu wa
elimu (kwa
mfano,
ukosefu wa
elimu
kuhusu
namna
ambavyo
VVU
huenezwa)
Matumizi
mabaya ya
madawa ya
kulevya na
pombe.
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
70
Hatua 2: ElezaGerezani
Nchini Tanzania, tafiti zinaonesha uwepo wa
kiwango cha juu cha VVU (asilimia 6.7) ndani ya
magereza ukilinganisha na watu wazima
Mazingira ya kizuizi na msongamano ambayo
mara nyingi hupelekea msongo, wasiwasi,
fadhaa, na unyanyasaji, ikiwemo unyanyasaji
wa kimapenzi.
Baadhi ya wafungwa wa kiume wanaweza
kukumbana na unyanyasaji wa kimapenzi na
kushiriki shughuli za mapenzi yasiyo salama
na wanaume wengine kwa kubadilishana vitu
ama huduma, kitu kinachoongeza hatari kwao
kuambukizwa VVU.
Magonjwa ya ngono, kama herpes, chlamydia,
kaswende, au gono yapo miongoni mwa
wakazi wenza, huongeza hatari yao kwa VVU.
(Serekali ya Muungano ya Tanzania 2010)
Mazingira hatarishi kwa VVU ndani ya magereza
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
71
kwingineko (asilimia 5.1)(Das and Horton, 2016)
kutokana na mazingira hatarishi ambayo ni
pamoja na: (tazama boksi la bluu).
Tanzania imetia sahihi na kuridhia hati zote rasmi
za haki za binadamu, sheria na sera za kimataifa
(umoja wa kimataifa) na kikanda kuhusu uzuiaji
wa VVU, zinazotoa idhini ya kuwapima watu VVU
kwa hiari, wakiwemo wafungwa walio katika
magereza.
Hatua 3
Kwa kina, jadili nini kifanyike ili kupunguza
mazingira haya hatarishi kwenye magereza.
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
72
Zoezi 2: Jinsi na Jinsia
Dakika 20
Vifaa vinavyohitajika:
Karatasi kubwa ya kuandikia na ubao
Maandalizi ya awali:
Andaa alama mbili moja iandikwe “jinsia” na
nyingine iandikwe “jinsi” kwa ajili ya zoezi hili.
Hatua 1: Eleza
Ingawa wafungwa hukaa kwenye vyumba
vidogo kulingana na jinsia zao, ni muhimu
kwao kuwa na taarifa kuhusu usawa wa
kijinsi, vurugu zenye misingi ya kijinsi, na
ukatili wa kijinsia. Elimu hiyo inaweza
kuwasaidia wafungwa baada ya kutumikia
vifungo vyao kuendeleza mila sahihi za kijinsi
na usawa wa kijinsi, ikiwa ni pamoja na
kupambana na ukatili wenye misingi ya
kijinsi.
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
73
Hatua 2: Uliza na jadili maswali yafuatayo:
Jinsi maana yake ni nini?
Jinsi humaanisha sifa za kibaiolojia na
kimaumbile za wanaume na wanawake ambazo
hazibadiliki isipokuwa kwa upasuaji. Mifano ya
sifa za jinsia ni:
Viungo vya mwili: uume, uke, matiti,
korodani
Maumbile: mzunguko wa hedhi, uzalishaji
manii
Muundo wa kijenetiki: kromosomu XX na XY.
Jinsia maana yake ni nini?
Jinsia humaanisha kazi, haki, majukumu, fursa,
heshima, mipaka, matarajio na wajibu wa mtu
uliopangwa na jamii.
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
74
Sifa za jinsi ni:
Hutofautiana miongoni na ndani ya
tamaduni
Hubadilika baada ya muda
Kazi na matarajio hupangwa kulingana na
jinsia, umri, ukabila, dini, na sababu nyingine
za kitamaduni
Huwahusu wanaume, wavulana, wanawake,
na wasichana; si wanawake pekee.
Hatua 3: Eleza
Baadhi ya mila za jinsi na ukosefu wa usawa wa
kijinsi huwaweka wanaume, wavulana,
wanawake, na wasichana katika hatari mbalimbali
za kupata maambukizi ya VVU:
Wanaume na wavulana wameathiriwa na
matarajio ya jinsi ambayo yanaweza
kuhamasisha tabia za kujihatarisha, kupinga
upatikanaji wa huduma za afya na kwa kiasi
kidogo kujipangia kazi zao kama wenza na
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
75
wanafamilia. Kwa wasitani, kiwango cha
upimaji VVU na kupata matibabu ni mdogo
miongoni mwa wanaume ukilinganisha na
wanawake. Kote mashariki na kusini mwa
Afrika, kuna tofauti kubwa ya utumiaji na
unufaikaji wa huduma kati ya wanaume,
wavulana, wanawake, na wasichana.
Wanaume na wavulana hupata huduma za
afya kwa kiwango cha chini sana
ukilinganisha na wanawake na wasichana.
Asilimia 54 ya vifo vya watu wazima vyenye
uhusiano na UKIMWI vilitokea miongoni
mwa wanaume mashariki na kusini mwa
ukanda wa Afrika (makadirio ya UNAIDS
2016). Huduma za afya haziwafikii wanaume
wengi kusini mwa jangwa la Sahara, na hii
huchangia sana wanaume kuhitaji na
kutumia kwa kiasi kidogo huduma za VVU
katika kanda hizi. Matarajio ya wanaume
kuanza matibabu ni madogo sana, na mara
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
76
nyingi hutegemewa kuwa na kiwango cha
chini cha CD4 wanapoanza na kukatiza
matibabu na kupoteza ufuatiliaji, hivyo
kufikiwa kwa kiasi kidogo kupungua kwa
virusi vya ukimwi ( Sonke Gender Justice
and Men Engage, 2017).
Ukosefu wa usawa wa kijinsi na usiri wa
ukatili wa wenza zinaweza kuwazuia
wanawake na wasichana, hasa wanawake
vijana kujikinga wenyewe dhidi ya VVU.
Nchini Tanzania, wanawake wameathirika
mno na VVU, Tanzania ina wanawake
690,000 wenye miaka 15 na zaidi waishio na
VVU. Kulingana na Utafiti wa Viashiria vya
VVU/UKIMWI na Malaria Tanzania Mwaka
2011–12, (TACAIDS et al. 2011) maambukizi
ya VVU kwa wanawake yalikuwa asilimia 6.2,
ukilinganisha na asilimia 3.8 ya wanaume.
Wanawake wenye umri wa miaka 23–24
walikuwa na uwezekano wa kuishi na VVU
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
77
mara mbili zaidi ya wanaume wa umri huo.
Wanawake huathiriwa mapema, kwa kuwa
wana wapenzi wakubwa na huolewa
mapema. Lakini pia wanakumbana na wakati
mgumu kujadiliana kuhusu mapenzi salama
kwa sababu ya ukosefu wa usawa wa kijinsi.
Nchini Tanzania asilimia 35 ya wanawake
inaaminika wamekumbana na ukatili wa siri
kwa wapenzi. Utafiti kutoka Tanzania
unaonesha kuwa huku wanawake
wakitegemewa kuwa watiifu kwa wapenzi
wao hata kama wapo kwenye mahusiano
mabaya, wanaume wanashawishiwa
kujihusisha na mapenzi ya ziada
yasiyosalama.
Hatua 3: Zoezi la jinsi na jinsia
Eleza kwamba sasa tutashiriki katika
shuughuli ya pamoja ili kujifunza zaidi
maneno jinsi na jinsia.
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
78
Onesha alama mbili ambazo zimetengwa
kwa umbali wa fiti kadhaa. Moja ina
neno“jinsia” lililoandikwa juu yake, na
nyingine ina neno “jinsi.”
Soma sentensi moja moja na uwaombe
washiriki kuhamia kwenye alama ambapo
wanadhani sentensi inaegemea yaani jinsia
au jinsi. Baada ya kila mmoja kuhama,
endelea kwa kumwomba mtu mmoja
aliyesimama upande mmoja wa chumba
aeleze kwa nini waliamua kusimama upande
huo. Uliza ikiwa wengine wangependa
kuchangia sababu zao. Waulize kundi jingine
kwa nini wameamua kusimama chini ya
alama waliyopo. Baada ya kufanya hivyo kwa
muda soma sentensi inayofuata.
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
79
MAELEZO YA JINSIA AU JINSI MAJIBU
Wanawake huzaa watoto Jinsi
Wasichana ni wapole na wakimya Jinsia
Wavulana ni werevu na thabiti Jinsia
Wanawake hunyonyesha watoto Jinsi
Wanaume ni vichwa vya familia
zao
Jinsia
Wanaume huanzisha mapenzi kwa
wenza wao
Jinsia
Wanaume wana akili kuliko
wanawake
Jinsia
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
80
Zoezi 3: Jinsi, jinsia, na VVU: Kuchukua
tahadhari, kukabiliana na hatari
Dakika 20
Vifaa vinavyohitajika:
Karatasi kubwa za kuandikia au ubao wa
chaki
Hatua 1. Utangulizi
Andika neno “hatari” kwenye karatasi ya
ubaoni au kwenye ubao wa chaki. Andika
maelezo yao ya ufafanuzi kwenye karatasi ya
ubaoni/ubao wa chaki. Fikieni muafaka
kuhusu maana ya neno hatari (tazama
kisanduku)
Maana ya hatari:
Hatari ni uwezekano au tishio la kupata
maambukizi (VVU, TB, n.k.), uharibifu, jeraha, deni,
upotevu, au matukio yoyote yanayoweza kuzuiwa
kwa kuchukua hatua stahiki.
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
81
Hatua 2: Uliza
Waombe washiriki watoa mifano ya
mazingira ambayo wanaweza au mtu
wanayemjua, au watu wengine huchukua
tahadhari au hukabiliana na hatari za VVU
Hatua 3: Maswali ya kujadiliana:
Kuhusiana na VVU, ni nani anayechukua
tahadhari zaidi, mwanaume au mwanamke?
Kwa nini?
Kuhusiana na VVU, ni nani anayekabiliana na
hatari zaidi, mwanaume au mwanamke? Kwa
nini?
Nini faida na hasara za kuchukua tahadhari
na kukabiliana na hatari hizi kwa wanaume
na wanawake?
Ni mambo gani mengine yanayoathiri
tahadhari za VVU ambazo watu huchukua
na ambazo watu hukabiliana nazo?
Hatari hizi zinaweza kupunguzwa vipi?
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
82
Hatua 4: Eleza
Wanawake hukumbana na hatari zaidi za
maambukizi ya VVU ukilinganisha na wanaume
kwa sababu ya mila za kijamii na kiutamaduni
(jinsi) na sababu za kibaiolojia (jinsia) (tazama
sanduku chini):
MILA ZA KIJAMII NA
KIUTAMADUNI (JINSIA)
SABABU ZA
KIBAIOLOJIA (JINSI)
Wanawake mara
nyingi hawana nguvu
na maamuzi katika
maisha yao ya
kimapenzi.
Wanawake
hawatarajiwi kujadili
au kuamua kuhusu
mapenzi; jambo hili
huchukuliwa kama ni
kazi ya mwanaume.
Wanawake
wanaweza kuhisi
Wanawake wana
uwezekano
mkubwa wa kupata
VVU kutokana na
kitendo chochote
kimoja cha kufanya
mapenzi kwa
sababu shahawa
hubaki ndani ya
uke kwa muda
mrefu baada ya
kujamiiana, na
hivyo kuongeza
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
83
MILA ZA KIJAMII NA
KIUTAMADUNI (JINSIA)
SABABU ZA
KIBAIOLOJIA (JINSI)
kwamba hawawezi
kuuliza au kusisitiza
kutumia kondomu au
njia yoyote ya
kujikinga.
Wanawake
wanaweza kujisikia,
ingawa hawawezi
kukataa kufanya
mapenzi hata kama
wanajua wanajiweka
katika hatari ya
kupata mimba au
kuambukizwa
magonjwa ya ngono
au VVU.
Baadhi ya wanawake
hujihusisha kwenye
mahusiano ya
kimapenzi kupata,
uwezekano wa
kuambukizwa. Pia
kuna virusi vingi
kwenye shahawa
kuliko kwenye
majimaji ya ukeni.
Kuta za uke ni laini
sana na zinaruhusu
vitu kupenya, na
kuruhusu VVU
kupenya, na ngozi
ngozi laini ya ukeni
ni rahisi zaidi
kupata michubuko
au kuchanika kuliko
ngozi ya kawaida.
Wanawake wapo
katika hatari zaidi
ya kupata VVU
wakati wa
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
84
MILA ZA KIJAMII NA
KIUTAMADUNI (JINSIA)
SABABU ZA
KIBAIOLOJIA (JINSI)
pesa, simu, chakula,
au namna nyingine
za hadhi na ulinzi.
Wanawake
wanaweza
kukumbana na
namna nyingi za
mizozo kutokana na
unyonge wao katika
jamii, na kuongeza
hatari za maambukizi
ya VVU.
Wanawake ambao
huwaambia wenza
wao kwamba wana
ugonjwa wa
ngono/VVU
wanaweza
kukumbana na ukatili
wa kimwili, kiakili, au
kujamiiana kuliko
wanaume kwani
shahawa zinaweza
kusalia ndani ya
uke kwa siku
kadhaaa baada ya
kujamiiana, wakati
wanaume
hujihatarisha na
majimaji yenye
maambukizi ya
VVU tu wakati wa
kujamiiana.
Wanaume ambao
hawajatahiriwa
wana uwezekano
mkubwa wa
kuambukizwa VVU
ukilinganisha na
wale waliotahiriwa.
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
85
MILA ZA KIJAMII NA
KIUTAMADUNI (JINSIA)
SABABU ZA
KIBAIOLOJIA (JINSI)
hisia au kuachwa.
Wanawake
wanaweza kudai
matakwa ya
kimapenzi kwa
wenza wao kuzuia,
kuzomewa, kuachwa,
kupigwa, au kuuawa.
Wanawake pia
wanategemewa
kuwa na mahusiano
ya kimapenzi na au
kuolewa na wazee,
ambao wana
uwezekano mkubwa
kuwa na VVU.
Wanaume
wanahimizwa
kufanya mapenzi
kadri iwezekanavyo,
Uume haupo
kwenye hatari
kubwa ya
kusababisha
maambukizi kwa
sababu inakingwa
na ngozi ngumu
ukilinganisha na
uke ambao una
sehemu kubwa
inayoweza
kuruhusu
maambukizi ya
VVU toka kwenye
shahawa.
Unapokuwa na
magonjwa ya
ngono ambayo
hayajatibiwa
kunaongeza
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
86
MILA ZA KIJAMII NA
KIUTAMADUNI (JINSIA)
SABABU ZA
KIBAIOLOJIA (JINSI)
bila kufundishwa jinsi
ya kujilinda
wenyewe, na hivyo
kuongeza hatari
kwao kuambukizwa
VVU.
Kiashiria kikuu cha
uanaume na
mafanikio ni kuwa na
wapenzi wengi wa
kike kadri
iwezekanavyo. Kwa
wanaume waliooa na
wale ambao
hawajaoa, wapenzi
wengi ni jambo
linalokubalika
kiutamaduni.
Wanaume wanaweza
kudharauliwa na
uwezekano wa mtu
kupata VVU.
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
87
MILA ZA KIJAMII NA
KIUTAMADUNI (JINSIA)
SABABU ZA
KIBAIOLOJIA (JINSI)
kutaniwa kama
hawataonesha
kwamba
watachangamkia
fursa zozote ama
zote za kimapenzi.
Ushindani husisitizwa
kwa wanaume
kuonesha ni nani
aliye mkuu na bora.
Kiashiria kingine cha
uanaume ni kuwa na
uthubutu kwenye
mapenzi, ikiwemo
kutotumia kondomu
(matumizi ya
kondomu
huchukuliwa kama ni
ishara ya udhuru na
ni udhaifu).
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
88
MILA ZA KIJAMII NA
KIUTAMADUNI (JINSIA)
SABABU ZA
KIBAIOLOJIA (JINSI)
Wanaume wengi
wanaamini kuwa
kondomu
hupunguza raha ya
mapenzi au ni
kiashiria cha ukafiri
na uzinzi.
Matumizi ya
kondomu vile vile
yanakinzana na kile
kinachoonekana
kama kiashiria
muhimu cha
uanaume—kuwa na
watoto wengi
iwezekanavyo.
Zoezi 4: Viwango vya hatari mchezo wa
kadi
Dakika 25
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
89
Vifaa vinavyohitajika:
Kadi zilizoandikwa “vielelezo” Andika yafuatayo
kwenye kila kadi: Kuacha kabisa, kupiga
punyeto,mapenzi kwenye uke-bila kondomu,
kumkumbatia mtu mwenye VVU, Kupiga busu,
mapenzi makavu-bila kondomu, Kuchua,
Mwanaume aliyetahiriwa akijamiiana na
mwanamke, Kumnyonya mwanaume uume kwa
kutumia kondomu, Kumnyonya mwanamke
ukeni bila kondomu, watoto wachanga kunyonya
kwa mama mwenye maambukizi ya VVU,
Mapenzi kinyume na maumbile—bila kondomu
Kadi zilizoandikwa “kadi za hisa”: Andika
viwango kwenye kadi za hisa kwa mfano.
Hatari kubwa zaidi, Hatari kidogo, Hatari
kiasi, Hakuna hatari yenye uhusiano na
ueneaji wa VVU.
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
90
Hatua 1: Fahamisha
Wafahamishe washiriki kuwa wanakwenda
kukamilisha zoezi linaloangazia tabia
zilizobeba hatari za kuambukiza VVU.
Weka kadi zenye tabia za kimapenzi
kuelekea chini kwenye kitita (tazama orodha
chini) halafu waombe washiriki kuchukua
kadi na kuiweka ukutani/sakafuni kwenye
kipengele sahihi, “Hatari kubwa” “Hatari
kidogo” “Hatari kiasi” na “ Hakuna hatari”
kuhusiana na ueneaji wa VVU
Kuachana na mapenzi kabisa
Kupiga punyeto
Mapenzi ukeni-bila kondomu
Kumkumbatia mtu mwenye VVU
Kupiga busu
Mapenzi makavu—bila kondomu
Kuchua
Mwanaume aliyetahiriwa akifanya mapenzi
na mwanamke
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
91
Kumnyonya uume mwanaume kwa kutumia
kondomu
Kumnyonya mwanamke ukeni bila kutumia
kondomu
Watoto wachanga kunyonya kwa mama
mwenye maambukizi ya VVU.
Mapenzi kinyume cha maumbile-bila
kondomu.
Baada ya kadi zote kuwa ukutani/sakafuni,
waombe washiriki wapitie mahali ambapo
kadi zimewekwa. Halafu waombe wajitolee
kusema kama:
Hawakubaliani na mahali kadi zote
zilipowekwa
Hawaelewi uwepo wa kadi zote mahali zilipo
Walipata wakati mgumu kuweka kadi zote.
Hatua 2: Jadili
Jadili uwepo wa baadhi ya kadi, hasa zile
zenye utata kuhusu hatari, au kadi ambazo
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
92
zimewekwa dhahiri mahali pasipo sahihi.
Anza kwa kuwauliza washiriki kwa nini
wanadhani kadi iliwekwa kwenye kipengele
fulani. Pitia vipengele hapa chini kama huna
uhakika mahali ambapo tabia fulani
inapaswa kuwapo.
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
93
Hatari za ueneaji wa VVU kutokana na shughuli
za mapenzi
HAKUNA
HATARI
HATARI
KIDOGO
HATARI
KIASI
HATARI
KUBWA
Kuachan
a na
mapenzi
Kupiga
punyeto
Kumkum
batia
mtu
mwenye
VVU
Kupiga
busu
Kuwaza
tendo la
kimapen
zi
Kuchua
Kufanya
mapenzi
kwenye
uke kwa
kondomu
Kumnyony
a mboo
mwanaum
e mwenye
VVU- kwa
kutumia
kondomu
Kufanya
mapenzi
mdomoni
na
mwanamk
Wato
to
wach
anga
kuny
onya
kutok
a
kwa
Mwa
namk
e
mwe
nye
VVU
Map
enzi
Map
enzi
ukeni
—
bila
kond
omu
Map
enzi
kinyu
me
cha
mau
mbile
- bila
kond
omu
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
94
e mwenye
VVU
Kutumia
vidole/mik
ono/vitu
vilivyosafis
hwa kabla
ya
kuchangia
kinyu
me
cha
mau
mbile
kwa
kutu
mia
kond
umu
na
vilaini
shi
Map
enzi
maka
vu-
bila
kond
omu
Hatua 3: Uliza
Waombe washiriki watazame tabia zilizopo
kwenye vipengele vya “Hatari kidogo” na
“Hakuna hatari”. Weka msisitizo kwenye
dhana ya kwamba baadhi ya tabia za
kimapenzi zenye kufurahisha zina hatari
kidogo au hazina hatari kabisa.
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
95
Hatua 4: Hitimisha
Hitimisha na sisitiza kwamba hatari
hutegemea mazingira ya tabia au sababu
zingine. Hizi ni pamoja na mila za jinsio,
ikiwa kama mwenza ameambukizwa au la,
ikiwa kama mtu ni/si mtoaji au mpokeaji wa
tabia za kimapenzi, na ugumu wa kufahamu
ikiwa kama mwenza wa mtu
ame/hajaambukizwa VVU.
Kiwango cha hatari kwa kiasi kikubwa kwa tabia
hizi kitatofautiana kulingana na sababu kadhaa.
Hizi ni pamoja na mila na ukosefu wa usawa wa
kijinsia, ikiwa kama mwenza ni/si mwathirika wa
VVU, ikiwa kama mtu ni/si mtoaji au mpokeaji wa
tabia za kimapenzi, historia ya kimapenzi na hali
ya VVU kwa kila mwenza, na matumizi sahihi ya
kondomu. Kwa mapenzi ya mdomoni, uwepo wa
vidonda, au fizi zinazotoa damu kunaweza
kuongeza hatari ya kuambukizwa VVU kwa
mtoaji.
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
96
Zoezi 5: Igiza kama mwanaume, igiza kama
mwanamke
Dakika 40
Vifaa vinavyohitajika:
Karatasi ya ubaoni au ubao wa chaki
Hatua 1: Uliza
Waulize washiriki kama wamewahi kuambiwa
“kuigiza kama mwanaume” au “kuigiza kama
mwanamke.” Wape nafasi ya kuchangia
baadhi ya uzoefu ambao mmoja wao
ameusema au kitu kinachofanana kwao. Kwa
nini mtu kasema hili? Jambo hili linamfanya
mshiriki ajisikie vipi?
Hatua 2: Sema
Tutatazama kwa kina zaidi aya hizi mbili. Kwa
kuzichunguza, tunaweza kuanza kuona namna
ambavyo jamii inatambua maana ya kuwa
mwanaume au mwanamke.
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
97
Hatua 3: Chunguza “kama mwanaume”
Kwa herufi kubwa, chapa kwenye kipande
cha karatasi ya ubaoni maneno, “Igiza kama
mwanaume.”
Waombe washiriki kuchangia mawazo yao
kuhusu maana ya maneno haya. Andika
mawazo haya kwenye karatasi ya ubaoni au
ubao wa chaki
“Igiza kama mwanaume”
Kuwa shupavu
Usilie
Wakoromee watu
Usioneshe hisia
Walinde watu
wengine
(wanawake na
watoto)
Pambana na
utakayokabiliana
nayo maishani ,
usionyeshe uwoga
Kuwa bosi
Ingiza kipato
Miliki wapenzi/wake
zaidi ya mmoja
Safiri kutafuta ajira
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
98
Hatua 5: Jadili—“kama mwanaume”
Ni kwa namna gani jambo hili linawafanya
washiriki wajisikie kutazama orodha hii ya
matarajio ya kijamii?
Kunaweza kuwako na mipaka kwa
mwanaume kutazamiwa kutenda namna hii?
Kwa nini?
Ni hisia zipi wanaume hawapaswi
kuzionesha?
Ni kwa namna gani “kujifanya mwanaume”
kunaathiri mahusiano ya mwanaume na
mwenza na watoto wake?
Ni kwa namna gani mila za kijamii na
matarajio ya “kuigiza kama mwanaume”
yana matokeo hasi kwenye afya ya uzazi na
mapenzi kwa mwanaume?
Je inawezekana wanaume kutoa
changamoto na kubadili majukumu yaliyopo
kulingana na jinsi?
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
99
Hatua 6: Chunguza “kama mwanamke”
Sasa kwa herufi kubwa, chapa kwenye
kipande cha karatasi ya ubaoni maneno,
“Igiza kama mwanamke.”
Waombe washiriki kuchangia mawazo yao
kuhusu maana ya maneno haya. Andika
mawazo haya kwenye karatasi ya ubaoni au
ubao wa chaki.
“Igiza kama mwanamke”
Usioneshe hisia
Kuwa mwangalizi
Kuwa mrembo, ila
usiwe mrembo sana
Kuwa nadhifu, ila
usiwe nadhifu sana
Kuwa mkimya
Kuwa mke mwema
Kuwa mwaminifu
Kuwa mnyenyekevu
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
100
Hatua 7: Jadili
Ni kwa namna gani jambo hili linawafanya
washiriki wajisikie kutazama orodha hii ya
matarajio ya kijamii?
Kunaweza kuwako na mipaka kwa wanawake
kutarajiwa kujimudu kwa namna hii? Kwa
nini?
Ni kwa namna gani “kuigiza kama
mwanamke” kunaathiri mahusiano ya
mwanamke na mwenza na watoto wake?
Ni kwa jinsi gani mila za kijamiii na matarajio
ya “kujifanya mwanamke” yana matokeo hasi
kwenye afya ya uzazi na mapenzi kwa
mwanamke?
Je wanawake wanaweza kuishi kinyume cha
mambo haya?
Je inawezekana wanawake kutoa
changamoto na kubadilisha majukumu
yaliyopo kulingana na jinsia?
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
101
Hatua 8: Hitimisha
Hitimisha zoezi hili kwa kueleza kwa ufupi
baadhi ya majadiliano na kuchangia mawazo
yoyote ya mwisho. Swali la mwisho laweza
kuwa kama ifuatavyo:
Shughuli hii ni njia nzuri ya kuelewa maana ya
mila za jinsi. Lakini kumbuka kuwa hizi mila za
jinsi zinaweza pia kuathiriwa na matabaka,
utamaduni, kikundi fulani, na tofauti nyingine.
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
102
Ujumbe ambao wanaume wanaupata kutokana
na “kuigiza kama mwanaume” ni pamoja na:
• Kuwa shupavu na usilie
• Kuwa mwingizaji wa kipato
• Jisimamie na usirudi nyuma
• Fanya mapenzi unapohitaji
• Wanawake ni vitu fulani kuwa navyo—mali
Jumbe hizi na majukumu kulingana na jinsi
kufuatia “kuigiza kama mwanaume” zina
matokeo (madhara) yafuatayo kwenye
mitazamo ya wanaume na uume:
Wanaume wanathaminiwa zaidi kuliko
wanawake.
Wanaume wanaogopa kudhuriwa na
kuonesha hisia zao.
Wanaume wanahitaji uthibitisho mara zote
kwamba wao ni wanaume kweli.
Wanaume hutumia mapenzi kuthibitisha
kuwa wao ni wanaume kweli.
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
103
Wanaume hutumia nguvu kuthibitisha kuwa
wao ni wanaume kweli.
Ujumbe ambao wanawake wanapata kutokana
na “kuigiza kama mwanamke” ni pamoja na:
Kutoonesha hisia na kukaa kimya
Kuwa waangalizi na wajenzi wa nyumba
Jifanye mrembo, ila usiwe mrembo sana
Kuwa nadhifu, ila usiwe nadhifu sana
Fuata miongozo ya wanaume
Mtunze mmeo—mpe starehe ya mapenzi
Usilalamike
Jumbe hizi na majukumu kulingana na jinsi
kufuatia “kuigiza kama mwanamke” vile vile
yana matokeo (madhara) yafuatayo kwenye
mitazamo ya wanawake na uke:
Mara nyingi wanawake hawajiamini
Wanawake huthaminiwa kwanza kama
mama na si kama watu
Wanawake huwategemea wenza wao
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
104
Wanawake wana maamuzi kidogo kuliko
wanaume kuhusu maisha yao kimapenzi
Wanawake wameathirika zaidi na VVU na
UKIMWI na ukatili
Mila za jinsi zisizo na manufaa huongeza hatari
ya magonjwa ya ngono na VVU na mimba
zisizotarajiwa, na hutengeneza vikwazo
vikubwa kwa maendeleo ya wanawake kijamii,
kiuchumi, na kisiasa.
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
105
Zoezi 6: Kufanya maamuzi kuhusu jambo
linalofaa na lisilofaa
Dakika 30
Hatua 1: Eleza
Tutatazama mchakato wa kufanya maamuzi
sahihi kwa kujitambua ili kujikinga na VVU.
Eleza kwamba watapewa orodha iliyo katika
namna tofauti na wanapaswa kuonesha kwa
matamshi au kwenye karatasi kama hatua
iliyochukuliwa ilikuwa “sahihi” au “si sahihi”
Hatua 2: Fafanua
Toa maana ya maneno haya: “kufaa” na
“kutofaa.”
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
106
Kufaa Kutofaa
“Kufaa inamaanisha
kitendo au mwitikio
unaostahili, sahihi, au
unaoendana na
mazingira ya uzuiaji VVU
na mila za jinsia na
usawa kama
ilivyojadiliwa katika
shughuli zilizotangulia.
Kutofaa inamaanisha
kitendo au mwitikio
usiostahili, usio sahihi, na
usioendana na mazingira
ya uzuiaji wa VVU na
mila za jinsi na usawa
kama ilivyojadiliwa katika
shughuli zilizotangulia.
Hatua 3: Soma
Kariri hadithi ya kwanza (ukurasa unaofiuata)
halafu washiriki waseme wapi panafaa na
wapi hapafai na kwa nini.
Hatua 4: Jadili
Kufungua mjadala wa ukweli kuhusu
mapenzi inaweza kuwa jambo gumu lakini ni
mhimu.
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
107
Watu wenye madaraka wasitumie vibaya
nafasi zao kuwalazimisha wengine kutenda
kinyume na matakwa yao.
Watu wanapaswa kuheshimu haki za
wengine kuchagua kama wanataka kufanya
mapenzi na kufanya mapenzi salama kwa
kutumia kondomu za kike au kiume.
Ili mradi tabia za kimapenzi ni jambo la
maridhiano pasipo kuumiza au kujeruhi,
wengine hawapaswi kuingilia.
Wapange washiriki wawili wawili halafu
wape eneo la kujadili na kuamua kama
linafaa au halifai. Wape dakika 10 kufanya
hivyo na elezea kwa kifupi kila eneo.
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
108
Simulizi za Matukio
Tukio 1: Kumtembelea daktari
Afisa magereza ameambiwa na daktari kuwa ana
kifua kikuu, ambayo ni maambukizi nyemelezi ya
kawaida kwa wale waishio na VVU. Daktari
akashauri kwamba wote wawili afisa magaereza
na mwenzi wake wapate ushauri nasaha na
kupima VVU. Afisa magereza akamweleza
mpenzi wake kuwa kikohozi chake kisichoisha
kinasababishwa na hali mbaya ya ubaridi baada
ya muda kitaisha.
Haifai: Afisa magereza ana wajibu wa
kumfahamisha mwenza wake ukweli kuhusu
mkutano wake na daktari na kumpa nafasi
mwenza wake kujilinda na kushughulika na
uwezekano wa kuwa mwathirika wa VVU.
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
109
Tukio 2 : Fadhaa za magonjwa ya ngono
Mfungwa ambaye hivi karibuni ameachiliwa
kutoka gerezani amekutana na binti/kijana
mtaani na kuanza mahusiano naye kimapenzi.
Siku moja
wakati
akioga,
binti/kijana
aliona
kidonda
chekundu kwenye sehemu zake za siri. Anaona
soni sana kuzungumza na mwenzi wake lakini
alimpeleka hospitali ili kupata vipimo na
kumweleza dakitari kuhusu kidonda.
Haifai: Ni muhimu kabisa kumfahamisha mpenzi
wako kuhusiana na ugonjwa wowote wa ngono
(VVU au vinginevyo) unaoutambua ili aweze
kuchunguzwa. Hii si kwa ajili ya afya zao tuu,
lakini pia kwa ajili ya afya ya jamii nzima kwa
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
110
sababu ugonjwa ukitibiwa mapema, ndivyo
unavyoweza kudhibitiwa mapema na kupunguza
uwezekano wa kuwaambukiza wengine.
Tukio 3: Hakuna zawadi ya bure
Afisa magereza amekuwa akimchumbia
msichana anayeuza machungwa na mayai
sokoni. Alinunua vitafunwa vyake kila mara
alipomwona, pamoja na kumpa zawadi ndogo
ndogo. Alikuwa na usongo wa kufanya mapenzi
nae. Jioni moja walipigana busu na alimtomasa
matiti yake. Mzuka ulimpanda sana lakini binti
alisema hayuko tayari. Alimsukuma binti chini,
akamkandamiza mikono yake chini na
akajilazimisha hadi akazama ndani yake.
Haifai: Afisa magereza huwenda alifikiri binti
“alipaswa kumpa”mapenzi kwa kuchukua chakula
na zawadi lakini hakuwa na haki ya kumbaka.
Ubakaji huongeza hatari ya maambukizi ya VVU
kwa kuwa wabakaji mara chache sana hutumia
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
111
kondomu na kitendo cha kutumia nguvu kufanya
ubakaji hupelekea kuchanika kwa kuta za uke au
njia ya haja kubwa.
Tukio 4: Matumizi mabaya ya cheo
Siku moja, mwalimu mkuu katika chuo cha
mafunzo katika gereza alimwomba mmoja wa
wanafunzi wake wa kike kubaki baada ya vipindi
kwisha na kumwambia kwamba alitaka
kujadiliana naye kuhusu maendeleo yake
kitaaluma. Baada ya vipindi msichana alibaki na
mkuu wa chuo alimsifia sana kuhusu uzuri wake.
Kitendo hicho cha kumsifia kilimchukiza sana
msichana, lakini hakusema chochote kwa kuwa
alikuwa mwalimu wake. Mwalimu alipoona
kwamba msichana hajafurahi, alimwambia awe
makini sana, kwani matokeo ya maendeleo yake
kitaaluma yalikuwa mikononi mwake, na
alimwomba msichana kwenda nyumbani kwake
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
112
jioni ile, kitu ambacho msichana alitii kwani
aliogopeshwa kuwa hatafaulu mitihani yake.
Haifai: Mwalimu hakupaswa kutumia cheo chake
au nafasi yake kumtisha msichana mdogo.
Ingawa msichana alikwenda nyumbani kwa
mwalimu, ilikuwa ni kwa sababu ya vitisho
kwamba uhalali wa matokeo yake kitaaluma
ungeharibiwa kama asingefuata alichoambiwa na
mwalimu kufanya.
Tukio 5: Tabia za kutowajibika
Afisa magereza alihamishwa kwenda gereza la
wilaya ambapo alidhani angepaswa kwenda bila
ya mke wake na watoto ili kuepusha usumbufu
kwao kuhusiana na mambo ya shule na familia.
Afisa alikaa peke yake katika makazi yake mapya.
Siku moja, alipokuwa baa, alikutana na
mwanamke na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi
ulioendelea kwa kipindi fulani. Pamoja na kuwa
Afisa alikuwa ameoa na akijua kuwa mwanamke
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
113
huyu alikuwa na mpenzi mwingine, hakuona hili
kama ni tatizo. Mwanamke alisisitiza kutumia
kondomu, lakini Afisa hakuona umuhimu wa
kondomu, na baadaye baaada ya mda
mwanamke aliacha kusisitizia.
Haifai: Pamoja na kwamba wote wawili
walikuwa wawazi kuwa wana wapenzi wengi
lakini hawakuwajibika kwa kufanya mapenzi
yasiyo salama, jambo ambalo haliwaweki wao tu
katika hatari lakini pia linawaweka wenzi wao
wengine katika hatari ya maambukizi ya VVU,
ambao huenda hawafahamu kuwa wenzi wao
walikuwa wakifanya mapenzi na watu wengine,
na mapenzi yasiyo salama.)
Tukio 6: Woga usiotakiwa
Mfungwa ajulikanaye kama Victor alihamishiwa
kwenye chumba kimoja kidogo kutokana na umri
wake mdogo ukilinganisha na wengine ambao
walionekana mabingwa na wenye kupenda
Somo 2: Viwango vya na vihatarishi vya maambukizi ya VVU
magerezani
114
kutaniana. Victor alikuwa mpole na mwenye aibu
na mara nyingi alipendelea kukaa peke yake.
Kwa tabia hiyo wenzake walimtania kwa kumwita
mwanamke nakadhalika. Siku moja wenzake
walimzunguka, wakamsukuma, na kumvua
suruali yake ili kuthibitisha kama kweli alikuwa
mwanaume au la. Mmoja wao alimshika kwa
nguvu na kumtisha.
Haifai: Ingawa walikuwa ni wakazi wenza wa
kiume, ukandamizaji na matendo mabaya
yanaweza kutokea kutokana na tofauti ya nguvu
za mamlaka. Waelimisha rika wanapaswa
kujadiliana na wafungwa nini kinapaswa
kufanyika kwenye tukio kama hili na taratibu
zinazopaswa kufuatwa katika kuripoti tukio kama
hili.)
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
115
SOMO 3: KIFUA KIKUU NA
VVU: MATIBABU, HUDUMA
NA MSAADA
Lengo
Kupata maelezo ya msingi kuhusu kinga,
matibabu, huduma, na msaada wa Kifua
kikuu na VVU.
Dhamira za mafunzo
Mwisho wa somo hili, washiriki wataweza:
Kueleza umuhimu wa kujua hali yako ya kifua
kikuu na VVU.
Kueleza maana ya upimaji VVU wa hiari na
ule unaoasisiwa na mtoa huduma.
Kuelezea umuhimu wa huduma za upimaji
VVU.
Kujadili dawa za kupunguza makali na
mahali pa kupata huduma na msaada.
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
116
Kuonesha kwa vitendo jinsi ya kutumia
kondomu za kike na kiume.
Kueleza kwa kifupi upatikanaji wa matibabu
mengine kwa matatizo mtambuka ya kiafya
kama vile, maginjwa ya ngono, maambukizi
kwenye njia ya uzazi, na maambukizi
nyemelezi.
Kueleza maana ya maneno kinga ya
maambukizi ya VVU kutoka kwa mama
kwenda kwa mtoto na kutokomeza
maambukizi ya VVU kutoka kwa mama
kwenda kwa mtoto.
Kutoa maelezo ya msingi jinsi ya kumtunza
mama mwenye VVU na mtoto.
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
117
Kipindi 3.1. Huduma za upimaji VVU
Dakika 145
Kipindi 3.1: Mazoezi
Kuelezea maana ya maneno
Ufunguzi kuhusu upimaji wa VVU
Kweli/Uongo kuhusu upimaji VVU
Upimaji wa VVU kwa ujumla
Upimaji wa VVU gerezani
Matumizi ya kondomu za kike na kiume
Dhamira
Mwisho wa kipindi hiki washiriki wataweza:
Kufafanua upimaji wa hiari na ulioasisiwa na
mtoa huduma
Kueleza umuhimu wa kujua hali ya VVU
Kujadili umuhimu wa huduma za kupima
VVU
Kuonesha kwa vitendo jinsi ya kutumia
kondomu za kike na kiume
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
118
Zoezi 1: Kueleza maana ya maneno
muhimu
Dakika 30
Shirika la afya duniani lilibadilisha maneno yao
mwezi wa saba 2015 kutoka “ Ushauri nasaha na
upimaji wa VVU” kuwa “Huduma za upimaji wa
VVU,” na nchi zinafuata inavyostahili zinapokuwa
zinahuisha miongozo yao. Maneno huduma za
upimaji wa VVU yanatumika kujumuisha huduma
zote zinazopaswa kutolewa pamoja na upimaji
wa VVU: ushauri nasaha (maelezo ya ushauri
nasaha kabla na baada ya kupima);
zilizounganishwa na huduma stahiki za kinga,
matibabu na usimamizi na huduma zingine za
kliniki na na msaadali; na kushirikiana na huduma
za maabara ili kusaidia uthibiti wa ubora na
utolewaji wa majibu sahihi.
Hatua 1
Waambie washiriki kuwa watatumia dakika
takribani 30 au chini yake wakitazama baadhi
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
119
ya maneno muhimu ambayo watakuwa
wakiyatumia katika kipindi hiki na kwa muda
mrefu baada ya kozi.
Chaguo 1
Kwa kutumia karatasi ya ubaoni iliyoandaliwa
yenye vifupisho vyote, ligawe kundi katika
timu mbili. Waambie washiriki kwamba
watacheza mchezo wa vifupisho.
Wafahamishe kuwa vifupisho hivi
vimeandikwa kwenye karatasi ya ubaoni
ambayo mtaifungua mchezo utapoanza.
Taja kuwa kila kikundi kitachagua mwakilishi
ambaye atachagua kifupisho kimoja na
kuwaambia wanakikundi maana yake.
Atakapopatia kundi litapata alama 2 lakini
akikosea kundi litapoteza alama 2. Waambie
kuwa watapeana zamu mpaka vifupisho
vyote vitakapokwisha.
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
120
Chaguo 2
Waalike washiriki kukaa wawili wawili na
kuchukua kipande cha karatasi. Wafahamishe
kwamba utatamka kifupisho ili wao waandike
kwa kirefu kama pea. Kwa ufafanuzi zaidi
ziunganishe pea mbili ili ziweze
kusahihishiana pale unapokuwa ukitoa
majibu sahihi kama yalivyotolewa kwenye
kisanduku cha maneno kulia kwako
Hatua 2: Pongezi
Pongeza kundi
zilizopata majibu
kwa usahihi zaidi.
Zoezi 2:
Utangulizi
kuhusu upimaji
wa VVU
Dakika 20
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
121
Hatua 1: Eleza
Katika kipindi hiki tutatazama/zungumza mambo
kadhaa ya huduma za uchunguzi, uangalizi,
matibabu, na msaada, ikiwemo upimaji VVU wa
hiari, upimaji VVU ulioasisiwa na mtoa huduma
na kuzuia maambukizi ya VVU toka kwa mama
kwenda kwa mtoto.
Hatua 2: Tamka
Shabaha mpya duniani 90–90–90 zinatoa wito
kwamba asilimia 90 ya watu waishio na VVU
kufanyiwa uchunguzi, asilimia 90 ya watu wenye
VVU waliofanyiwa vipimo kupatiwa dawa za
kupunguza makali ya virusi vya ukimwi, na
asilimia 90 ya wale wanaotumia dawa za
kupunguza makali wanalazimika kuwa na
kiwango kidogo cha virusi ifikapo 2020. Asilimia
90 ya kwanza (upimaji wa VU), ni muhimu
kwenye asilimia 90 ya pili (kuanzishiwa dawa za
kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI
miongoni mwa watu waishio na VVU), na
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
122
matokeo ya msingi ya asilimia 90 ya tatu
(kupungua kwa virusi miongoni mwa watu
wanaotumia dawa za kupunguza makali virusi
vya ukimwi), ambayo huboresha matokeo ya
wateja na kuzuia ueneaji wa VVU. Huku ikiwa ni
jambo muhimu kupata watu wengi zaidi
kufanyiwa vipimo na kufanikiwa kuwafikisha
kwenye huduma za matibabu na uangalizi, ni
muhimu kwamba kiwango cha ongezeko
kisididimize ubora wa huduma.
Hatua 3: Zoezi la kikundi
Zoezi hili linazingatia faida na hasara kwa
mtu kujua hali yake ya VVU.
Kabla ya kuanza zoezi, waulize washiriki
kama wanafikiri ni lazima kujua hali zao za
VVU.
Wapange washiriki katika makundi ya watu 4
ili waweze kujadili na kuorodhesha faida na
hasara za mtu kujua hali yake ya VVU.
Wape washiriki dakika 10 kufanya hivyo.
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
123
FAIDA MAELEZO
Ishi kwa mda
mrefu
Mpaka sasa dawa za kupunguza
makali zimeweza kuimarisha afya
za watu waishio na VVU, na kwa
kiasi kikubwa zimesaidia
kurefusha maisha kuanzia miaka
5–20. Inawezekana pia kuongeza
kipindi ambacho mfungwa
mwenye maambukizi anaweza
kuishi kwa kubadili mfumo wa
maisha na kupata matibabu ya
maambukizi nyemelezi. Kwa
mfano, kujiepusha na hatari
zaidi, kupunguza unywaji wa
pombe, na kula vizuri kunasaidia
kurefusha maisha.
Kunamaliza
wasiwasi
kuhusu hali
yako
Kupima VVU kunaondoa
wasiwasi kwamba
umeambukizwa au la. Wale
wenye wasiwasi kuhusu tabia zao
za zamani wanaweza kupata
nguvu mpya ya maisha kwa
kutambua hali zao.
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
124
FAIDA MAELEZO
Kuanza
kujikinga upya
Kutambua kuwa hujaambukizwa
VVU kunakupa wewe mwanzo
mpya ulio safi ambao kwao
kunaweza kujengwa utamaduni
wa kufanya mapenzi salama.
Kumbuka kwamba robo tatu ya
watu waliopima
hawajaambukizwa.
Kuweka
mipango ya
maisha yako
yaliyobaki
Kwa wapenzi wachanga, kupima
pamoja kabla ya kuoana
kunawawezesha kutambua ya
kuwa wanaweza kupata watoto
ambao hawajaambukizwa ikiwa
wataendelea kujikinga na
maambukizi. Wale
watakaogundua kuwa
wameambukizwa VVU
wanaweza sasa kupanga maisha
yao yaliyobaki. Inaweza kuwa ni
miaka mingi ijayo kabla
hawajaanza kuugua na hatimaye
kufariki. Wakati huo huo,
wanaweza kuwakinga wenza
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
125
FAIDA MAELEZO
wao na maambukizi na kuzuia
maambukizi ya VVU kutoka kwa
mama kwenda kwa mtoto.
Wanaweza pia kupanga
dhamana za hapo baadaye kwa
familia zao kwa kuandaa usia na
kuweka mipango ya kifedha.
Hatua 4: Wahakikishie
Washukuru washiriki kwa ushiriki wao na
eleza kuwa mara tutapoelewa ukweli kuhusu
VVU tutaweza kupunguza ueneaji wake na
kuishi kwa mda mrefu, maisha yenye afya.
Pia tunaweza kujilinda na kuwalinda wengine
kutokana na maambukizi ya VVU kwa kwa
kupunguza vihatarishi tunazokumbana nazo
gerezanni na mara baada ya kutoka. Kama
mwelimisha rika, unaweza kuwahakikishia kuwa
kama mwongozo wa kitaifa kuhusu VVU
utafuatwa na wafungwa na wafanyakazi wa
magereza tunaweza kupunguza hatari nyingi za
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
126
maambukizi ya VVU magerezani na kusaidia
upimaji wa VVU.
Zoezi 3: Kueleza maana ya ushauri nasaha
na upimaji wa hiari na ushauri nasaha na
upimaji wa VVU ulioasisiwa na mtoa
huduma
Dakika 20
Hatua 1: Dadisi
Waulize washiriki wanafikiri nini tofauti kati ya
upimaji VVU hiari na ulioasisiwa na mtoa
huduma?
Hatua 2: Elezea jedwali lifuatalo
USHAURI NASAHA NA
UPIMAJI WA HIARI
USHAURI NASAHA NA
UPIMAJI WA VVU
ULIOASISIWA NA MTOA
HUDUMA
Mtu huchagua
kutafuta vipimo.
Mtu anatafuta huduma za
matibabu, halafu upimaji
unapendekezwa na
kufanywa na daktari kama
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
127
USHAURI NASAHA NA
UPIMAJI WA HIARI
USHAURI NASAHA NA
UPIMAJI WA VVU
ULIOASISIWA NA MTOA
HUDUMA
sehemu ya mashauriano.
Huduma
pasipokuweka jina au
huduma za siri
zinaweza kutolewa.
Huduma zitolewazo ni za
siri na hutunzwa kwenye
kumbukumbu za hospitali
ili kuhakikisha
mwendelezo wa huduma.
Lengo la msingi
limejikita katika kuzuia
ueneaji wa VVU kwa
kutathimini hatari,
kupunguza hatari, na
upimaji.
Lengo la msingi ni
kuwatambua watu
walioambukizwa VVU na
kuwaunganisha na
huduma za kinga,
uangalizi na matibabu.
Maridhiano kwenye
maandishi au alama
za vidole kwa
wasiojua kuandika na
kusoma huhitajika.
Maridhiano ya mdomo
huhitajika na yanapaswa
kutunzwa kwenye
kumbukumbu za
mgonjwa.
Mtumiaji wa kwanza Mtumiaji wa kwanza wa
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
128
USHAURI NASAHA NA
UPIMAJI WA HIARI
USHAURI NASAHA NA
UPIMAJI WA VVU
ULIOASISIWA NA MTOA
HUDUMA
wa matokeo ya
vipimo ni mteja,
anayetumia taarifa
kufanya maamuzi
binafsi ya maisha
yake.
matokeo ya vipimo ni
mtoa huduma za afya
kufanya uchunguzi sahihi
na kutoa matibabu sahihi.
Hatua 3: Faida za upimaji wa vvu ulioasisiwa
na mtoa huduma
Waulize washiriki wanafikiri ni zipi faida za
upimaji wa VVU ulioasisiwa na mtoa
huduma?
Elezea yafuatayo:
Hhuwasaidia wataalamu wa afya kuwatibu
wateja wao kwa usahihi kwa kuwatambua
wale wanaohitaji matibabu/au program za
uzima mapema.
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
129
Huwasaidia watoa huduma za afya
kuboresha huduma za matibabu zitolewazo
kwa wateja wao na kupunguza ugonjwa na
vifo.
Inasaidia kupunguza unyanyapaa katika
jumuiya kama magerezani kwa kufanya
upimaji wa VVU kuwa ni jambo la kawaida.
Hatua 4: Sisitiza
Sisitiza kwamba bila kujali ni njia gani ya
upimaji imetumika, kanuni tano za upimaji
wa VVU zinapaswa kufuatwa. Waulize
washiriki “kanuni za upimaji wa VVU” ni nini.
Washiriki wanaweza kujibu au unaweza
kueleza kanuni hizi tano kama ifuatavyo:
KANUNI ZA
UPIMAJI WA
VVU
MAELEZO
Ushauri
nasaha
Ushauri nasaha ni majadiliano
baina ya mshauri wa VVU aliyepata
mafunzo na mteja anayetafuta
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
130
KANUNI ZA
UPIMAJI WA
VVU
MAELEZO
kupunguza kupata na kueneza
VVU kupitia:
- Maelezo: Mteja hupokea
maelezo kuhusu ueneaji na
namna ya kujikinga na VVU na
maana ya matokeo ya vipimo
vya VVU. Watu ambao hupima
na kuonekana hawana
maambukizi ya VVU wanapaswa
kupata maelezo ya afya kwa
kifupi juu ya matokeo ya vipimo
vyao.
- Ushauri nasaha na kinga ya VVU:
Wateja hupokea msaada ili
kutambua tabia hatarishi
mahususi zinazopelekea kupata
au kueneza VVU na kupiga hatua
ya kupunguza hatari hii.
Mpaka leo tafiti hazijaonesha
kwamba kutoa ushauri nasaha kwa
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
131
KANUNI ZA
UPIMAJI WA
VVU
MAELEZO
mda mrefu kunahitajika au
kunamanufaa zaidi. Isitoshe, utoaji
ushauri nasaha kwa mda mrefu
baada ya vipimo kwa watu ambao
hawakukutwa na maambukizi
unaweza kuelekezwa kwingine
rasilimali zilizotengwa kwa ushauri
nasaha ambazo zinahitajika na
wale waokutwa na VVU, wale
ambao majibu yao bado hayana
hitimisho, na wale waliokutwa
katika mahusiano ambayo mmoja
wao ana VVU na mwingine hana
VVU
Kuridhia Mtoa vipimo amekupatia maelezo
ya kina ili uweze kufanya maamuzi
sahihi kwa kujitambua kuhusu ikiwa
kama unataka kupima au la, ikiwa
ni pamoja na uhuru wa kukataa
kupima. Maelezo yanapaswa
kugusia, vipimo vinahusisha nini,
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
132
KANUNI ZA
UPIMAJI WA
VVU
MAELEZO
majibu tarajiwa, na uwezekano wa
matokeo yatokanayo. Upimaji wa
lazima haufai.
Usiri Kile unachokijadili na mshauri
kitabaki kuwa siri yenu wawili.
Mshauri hataweza kumwambia mtu
mwingine yeyote mlichokijadili au
nini matokeo ya vipimo vyako.
Usahihi Watu wote ambao vipimo vyao
vinaonesha wana VVU wanapaswa
kupimwa tena ili kuthibitisha vipimo
vyao kabla ya kuanzisha huduma
na matibabu ya VVU.
Mshikamano Kutoa huduma za upimaji VVU
mahali ambapo hakuna upatikanaji
wa huduma, au uunganishwaji
dhaifu kwenye huduma, ikiwepo
dawa za kupunguza makali ya
virusi vya ukimwi, una manufaa
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
133
KANUNI ZA
UPIMAJI WA
VVU
MAELEZO
kidogo kwa wale wenye VVU.
Zoezi 4: Upimaji VVU: Zoezi Kweli/Uongo
Dakika 15
Hatua 1: Zoezi
Waelezee washiriki kuwa utataja orodha ya
maelezo. Ungependa wao wasimame ikiwa
maelezo ni KWELI, au wakae ikiwa
wanadhani maelezo ni UONGO. Waambie
kuwa utawauliza waeleze sababu za majibu
yao.
MAELEZO JIBU (KWELI/UONGO)
Upimaji pasipo
kutumia jina
maana yake
unapewa namba
na hakuna
KWELI: Kutuliza hofu na
kupunguza unyanyapaa
baadhi ya huduma za upimaji
haziwahitaji wale walifanyiwa
vipimo kutoa majina yao.
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
134
MAELEZO JIBU (KWELI/UONGO)
anayejua jina lako
unapopimwa.
Sampuli ya damu zao
hutambuliwa kwa kutumia
namba pekee. Huduma za
upimaji wa VVU zinapaswa
kuwa siri, maana yake kile
ambacho mtoa huduma na
mteja wanajadili hakitatolewa
kwa mtu yeyote bila ya
ridhaa ya mtu anayepimwa.
Usiri unapaswa kuheshimiwa,
lakini usiruhusiwe kutilia
mkazo siri, unyanyapaa, au
fedheha.
Mtu akigundulika
kuwa na VVU
baada ya kufanya
vipimo ya lazima
basi moja kwa
moja hufukuzwa
kazi.
UONGO: Upimaji wa hiari
unathaminiwa na watu wenye
VVU hawapaswi kufukuzwa
kazi. Ingawa, baadhi ya
waajiri huhitaji wafanyakazi
kupima kabla ya kwenda
kufanya kazi nje ya nchi. Mtu
anayekutwa na maambukizi
ya VVU kwa kawaida
huruhusiwa kuendelea
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
135
MAELEZO JIBU (KWELI/UONGO)
kufanya kazi lakini haruhusiwi
kusafiri nje ya nchi.
“Kipindi cha
mficho” ni kipindi
ambacho kinga
dhidi ya VVU
huenda isionekane
kwenye damu ya
mtu
aliyeambukizwa.
KWELI: Huchukua hadi kati ya
miezi mitatu hadi sita kwa
kinga ya VVU kuonekana
kwenye damu. Ushauri siku
zote kwa kila anayepima VVU
na kujikuta hana maambukizi
ni kupima tena baada ya
“kipindi cha miezi mitatu” si
sahihi. Marudio ya upimaji
yanahitajika kwa wale tu
ambao matokeo ya vipimo
vyao yanaonesha
hawajaambukizwa ambao
wameripoti hivi karibuni
(miezi mitatu iliyopita) au
uwepo katika hatari
enderevu. Kwa watu wengi
ambao hawana maambukizi
ya VVU baada ya kupima,
upimaji kwa mara nyingine
kufanya uamuzi wakati wa
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
136
MAELEZO JIBU (KWELI/UONGO)
kipindi cha mficho si lazima
na inaweza kupoteza
rasilimali.
Wale wanaokutwa
bila maambukizi ya
VVU baada ya
kupima hawapaswi
kujizuia na tabia
hatarishi hapo
baadaye
UONGO: Mtu anaweza
kujiingiza katika mahusiano
hatari ya kimapenzi pasipo
kuambukizwa. Lakini hii
haimaanishi kuwa
hawataambukizwa kwenye
shughuli zao za kufanya
mapenzi yasiyo salama
zinazofuata
Kila mmoja
anapaswa
kupimwa.
KWELI: Upimaji wa VVU ni
njia ya kujikinga, kupata
matibabu, uangalizi, na
huduma zingine za msaada
dhidi ya VVU. Uelewa wa
watu juu ya hali zao za VVU
kupitia huduma za upimaji ni
muhimu kwenye mafanikio ya
kupambana na VVU. Wigo
wa upimaji VVU miongoni
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
137
MAELEZO JIBU (KWELI/UONGO)
mwa watoto ni mdogo.
Mbinu zinahitajika kuongeza
uchunguzi wa mapema kwa
watoto wachanga na
kuwaunganisha kwa wakati
watoto wachanga
watakaogundulika kuwa na
VVU kwenye matibabu na
huduma. Mbinu za ziada
zinahitajika kuongeza
utumiaji wa huduma za
upimaji VVU miongoni mwa
wanaume, ikiwemo utolewaji
wa huduma za upimaji VVU
katika maeneo ambayo
yanafaa zaid na kukubalika
na wanaume, na kubadili njia
za kuwahimiza upimaji wa
wenza wa wanaume katika
maeneo ambapo kuna
uwepo mkubwa na kwa
wapenzi na wenzi wa
wanaume na wanawake
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
138
MAELEZO JIBU (KWELI/UONGO)
wenye VVU kwenye maeneo
yote. Kuyafikia makundi
maalumu ya watu, kama vile
wakazi wenza, ni jambo la
kupewa kipaumbele.
Kama mtu
atagundulika kuwa
na VVU mtu huyu
anapaswa
kuwaeleza wenzi
wake wote kuhusu
majibu ya vipimo.
KWELI: Ingawa kuweka wazi
kwa wapenzi, wanafamilia
wenye msaada, na
wafanyakazi wa afya, mara
nyingi kuna manufaa, hii
inapaswa kufanywa na au
kwa ridhaa ya mtu
aliyepimwa. Ushauri nasaha
kwa wateja wenye VVU
inapaswa kujadili majibu
yanayowezekana kuwekwa
wazi, na hatari na manufaa
ya kuweka wazi, hasa
miongoni mwa wanandoa na
wapenzi. Wape ushauri ili
kusaidia kuweka wazi kwa
pamoja. Wanandoa na wenzi
wanapaswa kupewa ushauri
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
139
MAELEZO JIBU (KWELI/UONGO)
nasaha na upimaji wa hiari
pamoja na msaada wa
kuweka wazi kwa pamoja.
Mshauri anapaswa kutazama
hatari za vurugu za ndani za
wapenzi na kujadili hatua
zinazowezekana ili
kuhakikisha usalama wa
kimwili wa mteja hasa
wanawake ambao
wamegundulika kuwa na
VVU.
Mtu wa kwanza
kwa wanandoa
kugundulika na
VVU ndiye aliyeleta
virusi kwenye
familia.
UONGO: Wakati ambapo
mtu anajua kuwa ana
maambukizi ya VVU hauna
uhusiano na muda
alioambukizwa. Baada ya
kipimo kuonesha uwepo wa
VVU, unapaswa kuhimiza na
kuwapima wenzi, watoto, na
wanafamilia wengine wa
mteja. Jambo hili linaweza
kuwa mmoja mmoja, vipimo
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
140
MAELEZO JIBU (KWELI/UONGO)
kwa wapenzi, kupima kwa
pamoja, au kumfahamisha
mwenza kwa ridhaa.
Zoezi 5: Upimaji wa VVU uraiani na
magerezani
Dakika 30
Hatua 1: ElezaUpimaji wa VVU
Kupima VVU ni njia pekee na muhimu kujua
kama una VVU. Ikiwa una VVU, ni jambo
muhimu kutambua ugonjwa. Jambo hili
litakupa nafasi nzuri ya kupata matibabu na
huduma unazohitaji ili kuishi kwa afya.
Unapokwenda kupima VVU, utakuwa na
nafasi kuzungumza na mtu aliyepata
mafunzo, hivyo unaweza kuuliza swali lolote
amabalo unaweza kuwa nalo. Mtu
anayekupima atakupatia maelezo jinsi
ambavyo vipimo vinafanyika na jinsi
utavyopata majibu.
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
141
Kutegemeana na aina ya kipimo,
utachukuliwa sampuli ndogo ya damu
kutoka mkononi mwako, au tone la damu
kutoka kwenye kidole chako. Kuna baadhi ya
vipimo hufanyika kwa kutumia maji maji
yanayopatikana kuzunguka fizi.
Kuna aina mbalimbali za vipimo vya VVU.
Baadhi ya vipimo vya VVU huonesha uwepo
wa virusi halisi kwenye damu (kipimo cha
antijeni) na vipimo vingine huonesha kinga
za VVU zinzofanya kazi ya kupambana na
VVU. (kipimo cha kinga).
Ikiwa vipimo vitaonesha kuwa una VVU,
inamaanisha una maambukizi ya VVU. Ikiwa
vipimo vitaonesha kuwa huna VVU, maana
yake huna maambukizi ya VVU. Kwa baadhi
ya vipimo utahitaji kufanyiwa vipimo vya
ufuatiliaji ikiwa majibu ya yataonesha kuwa
una maambukizi ya VVU.
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
142
Hatua 2: Maswali na majibu kipindi cha
mficho
Swali: Kipindi cha mficho maana yake nini?
Jibu: Kipindi kuanzia ulipoambukizwa VVU
mpaka pale ambapo mwili utatoa kinga ya
kutosha kwa VVU itakayoweza kuonekana kwa
kutumia kipimo cha kinga ya VVU hujulikana
kama kipindi cha mficho. Watu wengi huweza
kutengeneza kinga ya VVU ndani ya miezi mitatu
mara baada ya kupata maambukizi ya VVU.
Lakini kipindi cha mficho kinaweza kutofautiana
kulingana na kipimo cha VVU kilichotumika. Kwa
ujumla, mtu yeyote mwenye matokeo hasi
kupitia kipimo cha kinga ya VVU ndani ya miezi
mitatu ya uwezekano wa kuwa na VVU,
anapaswa kupima tena baada ya miezi mitatu.
Hatua 3: Maswali na majibuupimaji wa
VVU
Swali: Kipimo cha antijeni ni nini?
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
143
Jibu: Kipimo cha antijeni hugundua antijeni za
VVU (sehemu ya virusi) kwenye damu. Kipimo
cha antijeni kinaweza kugundua maambukizi ya
VVU kabla ya kinga ya kutosha ya VVU
haijatolewa ili kuweza kugunduliwa kwa kipimo
cha kinga ya VVU.
Swali: Inachukua mda gani kupata majibu ya
vipimo vya VVU?
Jibu: Matokeo ya haraka ya kipimo cha kinga ya
VVU yanaweza kutolewa ndani ya dakika 15–30.
Ingawa, inaweza kuchukua siku kadhaa au wiki
kadhaa, kutegemeana na aina ya kipimo
kilichotumika. Katika Tanzania matokeo chanya
ya kipimo cha VVU ni lazima yathibitishwe kwa
kipimo cha uthibitishaji.
Swali: Watu waliopo nje ya gereza wanaweza
kwenda kupima wapi?
Jibu: Watoa huduma za afya wanaweza
kukufanyia vipimo vya VVU. Vipimo vya VVU vile
vile vinapatikana katika hospitali nyingi, kliniki za
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
144
matibabu, vituo vya afya vya jamiii, vituo vya
ushauri nasaha na upimaji kwa hiari, na mashirika
ya huduma za UKIMWI.
Hatua 4: Maswali na majibu—vipimo vya
VVU gerezani
Swali: Ukiwa gerezani vipimo vya VVU hufanyika
vipi?
Jibu: Vipimo vya VVU hutolewa katika vituo vya
afya vya magereza ikiwemo huduma za kliniki za
ushauri nasaha na upimaji kwa hiari
zinazotembea ambazo hutembelea maeneo ya
magereza. Ingawa, upimaji wa lazima kwa
wafungwa ni kinyume cha maadili na hauna
ufanisi, upimaji unapaswa kuwa wa hiari
ukiambatana na ushauri nasaha kabla na baada
ya kupima. Matokeo yanapaswa kutolewa kwa
wafungwa na mfanyakazi wa afya ambaye
anapaswa kuhakikisha kutunza siri za kihospitali.
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
145
Hatua 5: Maswali na majibu—bada ya
kugundua ugonjwa
Swali: Je unapaswa kufanya nini ikigundulika una
VVU au hauna maambukizi ya VVU?
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
146
Ufanye nini ikiwa
huna VVU
Kuachana kabisa na
shuguli za mapenzi
ni njia bora zaidi
kuzuia kupata VVU.
Kuepuka maambukizi
huja pale unapokuwa
mwaminifu kabisa
kwa mpenzi mmoja,
inayohitaji wewe na
mpenzi wako
anagalau kupima
VVU kila mmoja, kwa
anagalau miezi
mitatu tofauti; na
mkiamua kufanya
mambo ya mapenzi
ya ndani ya(uke,
mdomo, na njia ya
haja kubwa)
kwamba mtumie kwa
usahihi kondomu ya
kike au kiume.
Ufanye nini ikiwa una VVU.
Kitu cha kwanza ambacho
kliniki itakifanya ni kupima
kiwango cha CD4.
Watachukua damu kutoka
kwako itakayopelekwa
maambara ili kupima idadi ya
seli za CD4 kwenye ujazo wa
mililita moja ya damu. Hii
itakusaidia kujua mfumo wako
wa kinga una afya kiasi gani.
Inapendekezwa kuwa watu
wenye VVU wapime viwango
vya CD4 zao kila baada ya
miezi sita. Pia unaweza
kuhitaji kipimo cha kutaza
wingi wa virusi utapoanza
kutumia ARVs na mara
nyingine baadaye kupima
upunguaji wa virusi kwa
kutumia dawa za ARVs
(ufanisi).Unapokuwa tayari na
salama kufanya hivyo, ni
muhimu kuweka wazi kwa
mwenzi wako kuwa una VVU
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
147
Zoezi 6: Matumizi ya kondomu za kike na
kiume
Kuzuia ueneaji wa VVU
Dakika 30
Hatua 1: Eleza
Eleza kwamba hii ni fursa kwa ajili yao
kujifunza au kuchangia taarifa kuhusu jinsi ya
kutumia kondomu ya kiume na kike kwa
ufasaha kama njia ya kujikinga na VVU.
Kuzungungumzia kuhusu kondomu kwenye
maeneo ya gerezani inaweza kuwa ni jambo
gumu. Ingawa, ni muhimu kuweka wazi kuwa
kondumu hazitagawiwa magerezani.
Hairuhusiwa na sheria za Tanzania. Kwa hiyo ni
muhimu kupata taarifa hizi kuhusu kondomu
kwani zitawanufaisha mara baada ya kumaliza
kifungo au kuachiliwa kutoka gerezani kwa
mfano, mahabusu.
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
148
Eleza kuwa kondomu hutoa kinga
madhubuti dhidi ya VVU ikiwa itatumika kwa
usahihi na wakati wote. Ingawa kondomu
zimezuiliwa gerezani, wafungwa wanaweza
kutumia kondomu mara baada ya kutoka
gerezani.
Hatua 2: Uliza
Kwa kunyosha mikono wangapi wamewahi
kutumia kondomu? Nani anaweza kueleza hatua
za namna ya kutumia kondomu ya kiume
kuanzia mwanzo hadi mwisho?
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
149
Hatua 3: Hatua jinsi ya kutumia kondomu ya
kiume
Jinsi Ya Kutumia Kondomu Ya Kiume
Kata pakiti ya kondomu kwa
kufuata alama pembeni mwa
pakiti. Unapofungua pakiti ya
kondomu usitumie kucha wala
meno.
Iweke kondomu kwenye ncha ya
uboo halafu ikunjue kuelekea
chini ya urefu wa uboo kwa
kuisukuma chini kwenye mzingo
wa duara wa kondomu.Valisha
kondomu kwenye uboo ukiwa
bado umesimama. Minya chuchu
ya kondomu katikati ya kidole na
kidole gumba cha mkono mmjoja
(Ukiacha nafasi nchani ili
kukusanya shahawa au manii).
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
150
Baada ya kufanya mapenzi na
kukojoa, shikilia mzingo wa
kondomu halafu toa uboo nje
kabla haujalala. Ifunge kondomu
katika kifundo kwenye manii au
shahawa.
Itupe kondomu iliyotumika mahali
salama. Kama vile kondomu ya
kike, kamwe usiidumbukize
chooni kondomu ya kiume.
Inaweza kuziba choo chako na
haiozi. Ifunike kwenye tishi halafu
itupe kwenye pipa la takataka au
kwenye choo cha shimo.
Hatua 4: Orodhesha
Jadili mambo magumu zaidi tunayokabiliana
nayo wakati wa kutumia kondomu. Waombe
washiriki kupendekeza ni namna gani
changamoto hizi zinaweza kutatuliwa.
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
151
Baadhi ya matatizo ya kawaida mara zote ni
pamoja na:
Kujaribu kuiviringisha kondomu kuelekea
chini wakati ikiwa “nje—ndani.”
Kondomu haikunjuki kuelekea kote chini.
Kondomu haijawekwa sawa kwenye kielelezo
Mtumiaji hana utulivu wakati akifungua pakiti
au hutumia meno kuifungua.
Hewa kwenye chuchu haijatolewa
Kamwe usitumie mafuta ya mgando kama
Vaseline®
au mafuta ya taa kama kilainishi
wanapotumia kondomu.
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
152
Jinsi Ya Kutumia Kondomu Ya Kike
Fungua pakiti ya kondomu. Chana
moja ya mapengo mwishoni na
usitumie mkasi wala kisu. Kwani
hutaki kuiharibu kondomu. Shikilia
sehemu ya juu ya kondomu na
wakati huo huo sukumiza sehemu ya
ndani ya duara, huku sehemu ya
wazi ikining’inia.
Utagundua kwamba kuna duara
mbili kwenye kondomu ya kike,
tofauti na kondomu ya kiume. Duara
ya nje, ambayo ipo wazi, huenda nje
ya kondomu. Duara ya ndani
huenda ndani na husaidia kushikilia
kondomu juu wakati wa tendo la
ndoa. Sukumiza sehemu ya ndani,
duara iliyofungwa.Mara baada ya
duara kuonekana ndefu na
nyembamba, sasa ipo tayari
kuingizwa ndani ya uke.
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
153
Tafuta sehemu ya faragha na iingize
sehemu ya ndani, sukumiza duara
ndani ya uke wako. Kama ni mara ya
kwanza kuingiza kisodo au kufanya
mapenzi, itakuchukua mda kabla
hujawa mzoefu wa kuisokomeza
hapo. Kiasi kidogo cha kilainishi
kinaweza kusaidia mambo kwenda
shwari. Unaweza kutumia kidole cha
kati kuisukuma ila hakikisha
haijageuzwa. Duara ya nje inapaswa
kubaki nje ya uke. Uko tayari
kwenda! Ukiwa tayari, hakikisha
unamwongoza mpenzi wako
kuingiza uboo kwenye kondomu.
Hakikisha haingizi pembeni au kwa
bahati mbaya kuikosa kabisa kwa
namna yoyote
Safisha. Ukishamaliza, geuza duara ya nje mara
kadhaa ili kuifunga halafu ivute nje taratibu. Kama
ilivyo kwa kondomu ya kiume, kamwe usitupe
kondomu ya kike kwenye choo cha maji. Inaweza
kuziba choo chako na haiozi. Ikunje kwenye tishu na
uitupe kwenye pipa la takataka au choo cha shimo.
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
154
Kipindi 3.2: Kifua kikuu, VVU:
matibabu, huduma, na msaada
Dakika 40
Kipindi 3.2: Mazoezi
Matibabu ya vvu na maambukizi
nyemelezi
Matibabu ya mgonjwa mwenye
maambukizi ya vvu
Dhamira
Mwisho wa kipindi, washiriki wataweza:
Kueleza kwa kifupi uwepo wa matibabu kwa
matatizo mengine ya kiafya, ikiwemo,
magonjwa ya ngono, maambukizi ya njia ya
uzazi, na maambukizi nyemelezi.
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
155
Zoezi 1: Matibabu ya VVU na maambukizi
nyemelezi
Dakika 40
Hatua 1: Eleza
Waambie washiriki kwamba sasa watajadili
matibabu ya maambukizi tuliyokwisha
kujadili kama VVU, kifua kikuu, magonjwa
mengine ya ngono, na maambukizi ya njia
ya uzazi.
Hatua 2: Maswali na majibu—maambukizi
Swali: Tunajikinga vipi na magonjwa ya ngono?
Chukua mawazo machache
Jibu: Njia bora ya kujikinga na magonjwa ya
ngono ni kuzuia kuupata. Katika hatua hii ya
kwanza ya kujikinga, uwezekano wa kupata
magonjwa ya ngono unaweza kupunguzwa kwa:
Usianze kufanya mapenzi mapema (kwa
vijana wadogo)
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
156
Kupunguza idadi ya wapenzi
Kutumia kondomu kwa usahihi na wakati
wote
Utambuzi wa haraka na kupata matibabu
sahihi ya ugonjwa wa ngono
Swali: Maambukizi njia ya uzazi inamaanisha
nini?
Jibu: Maambukizi kwenye njia ya uzazi ni
maambukizi yaliyopo kwenye mkondo wa
sehemu za siri. Huwaathiri wanaume na
wanawake. Baadhi ya katika njia ya uzazi (kama
vile kaswende na gono) huambukizwa kwa njia
ya kujamiiana lakini mengi yao hayaambukizwi
kwa njia hiyo (kama maambukizi ya fangasi). Njia
bora ya kushughulikia ugonjwa wa ngono ni
kutafuta matibabu mara moja.
Hatua 3: Maswai na majibu—matibabu ya
VVU
Swali: VVU hutibiwa vipi?
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
157
Unaweza usiwe na mda wa kupitia maswali
yote yafuatayo. Pitia maelezo kwa ufupi
kuhusu dawa za kupunguza makali ya virusi
vya UKIMWI kwenye ukurasa ufuatao.
Jibu: Maambukizi ya VVU hutibiwa kwa kutumia
dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI
Swali: Nini maana ya dawa za kupunguza makali
ya virusi vya ukimwi?
Jibu: Ni dawa zinazotumika kutibu mambukizi ya
VVU. Watu wanaotumia dawa za kupunguza
makali hutumia muunganiko wa madawa
(yaitwayo HIV regimen) kila siku. Kuna
muunganiko mbalimbali wa madawa. Dawa za
kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI
zinapendekezwa kwa kila mtu mwenye
maambukizi ya VVU. Dawa za kupunguza makali
ya ukimwi haziwezi kuponyesha kabisa VVU, bali
huwasaidia watu kuishi kwa mda mrefu, maisha
yenye afya. Dawa za kupunguza makali ya virusi
vya ukimwi pia hupunguza hatari ya kueneza
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
158
VVU kwa mtu mwingine. Nchini Tanzania, kwa
watu wazima na vijana wadogo, hatua ya
mwanzo (ya kwanza) madawa ya regimen ni
miongoni mwa miunganiko ifuatayo ya dawa
tatu: (1) (tenofovir (TDF) + lamivudine (3TC) +
efavirenz (EFV); (2) zidovudine (AZT) +
lamivudine (3TC) + lopinavir/ritonavir (LPV/r); or
(3) abacavir (ABC) + lamivudine (3TC) +
nevirapine (NVP).
Dawa za kupunguza makali ya virusi vya
UKIMWI kwa kifupi
Dawa za
kupunguza makali
ya virusi vya
UKIMWI ni utumiaji
wa dawa za VVU
kutibu maambukizi
ya VVU.
Inapendekezwa kwa
kila aliyeambukizwa
na VVU, na husaidia
Toleo jipya la
miongozo ya
kimataifa
linapendekeza
kutumia dawa mara
baada ya
kugundulika na VVU
(“Pima na Tibu”) kwa
kuanza matibabu
mapema
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
159
watu wenye VVU
kuishi kwa muda
mrefu, maisha
yenye afya.
Watu wenye VVU
wanapaswa kuanza
kutumia dawa
kulingana na
mwongozo wa
kitaifa wa usimamizi
wa VVU/UKIMWI.
Kwa watu wenye
VVU wenye hali
zifuatazo. Ni
muhimu sana
kuanza matumizi ya
mara moja
mwanamke akiwa
na mimba
Magonjwa fulani
yenye uhusiano na
maambukizi ya VVU
kama vile utando
yatapunguza hatari
ya VVU na matatizo
ya kiafya yasiyo na
uhusiano na VVU
miongoni mwa watu
wenye VVU na
UKIMWI Na
itapunguza wingi wa
virusi kwa kiwango
kisichogundulika na
hivyo kupunguza
hatari ya kuenea
kwa VVU.
Ufanisi wa dawa
hutegemea ufuasi
mzuri wa dawa—
kutumia dawa kila
siku kama
ulivyoelekezwa na
mtoa huduma wa
afya. Kabla ya
kuanza kutumia
dawa, ni muhimu
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
160
mdomoni, herpes
simplex, mkanda wa
jeshi, dalili kiunoni,
kansa ya mlango wa
kizazi, na kifua
kikuu.
kukabiliana na
maswala yoyote
yatakayoathiri makali
ya dawa.
Swali: Tiba ya virusi vya UKIMWI hufanya kazi
vipi?
Jibu: VVU hushambulia na kuharibu seli za CD4
kwenye mfumo wa kinga ambazo hupambana
na maambukizi. Seli zikiwa chache, ni vigumu
kwa mwili kupambana na maambukizi na aina
fulani za saratani. Dawa huzuia VVU kuongezeka
(kuzaliana wenyewe), kitu ambacho hupunguza
kiwango cha VVU mwilini ingawa haiondoi VVU
vyote mwilini. Uwepo wa VVU wachache mwilini
huupatia mfumo wa kinga nafasi ya kuponyesha
na kuzalisha seli za CD4 zaidi. Hata kama bado
mna kiasi fulani cha VVU mwilini, mfumo wa
kinga una nguvu za kutosha kupambana na
maambukizi na magonjwa yajulikanayo kama
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
161
maambukizi nyemelezi kama vile kifua kikuu,
homa ya mapafu, na kansa ya mlango wa kizazi.
Maambukizi nyemelezi ni maambukizi ambayo
hutokea mara kwa mara na huwa makubwa zaidi
kwa watu wenye mfumo dhaifu wa kinga, kama
vile watu waishio na VVU. Kwa kupunguza
kiwango cha VVU mwilini, dawa za VVU
zinaweza pia kupunguza hatari ya kueneza VVU
kwa mtu mwingine.
Swali: Ni wakati gani muafaka kuanza kutumia
dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi?
Jibu: Watu wenye maambukizi ya VVU
wanaostahili wanapaswa kuanza dawa mapema
iwezekanavyo. Watoa huduma za afya
watashirikiana na wagonjwa ili kuona nani
anastahili kulingana na mwongozo wa kitaifa.
Kwa watu wenye hali zifuatazo, ni muhimu sana
kuanza kutumia dawa mara moja: Ujauzito na
magonjwa fulani yenye uhisiano na maambukizi
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
162
ya VVU kama utando mdomoni, mkanda wa
jeshi, au kansa ya malango wa kizazi.
Kulingana na Mwongozo Wa Kitaifa Wa
Kusimamia VVU Na UKIMWI Toleo 5 (Wizara ya
Afya na Maendeleo ya Jamii, Tanzania [MOHSW]
2015), dawa zinapaswa kuanzishwa kwa watu
wote wenye kifua kikuu na maambukizi ya
uhusiano na VVU, bila kujali hatua za kliniki za
WHO au kiwango cha seli za CD4. Matibabu ya
kifua kikuu yanapaswa kuanza kwanza,
yakifuatiwa na matibabu mapema iwezekanavyo,
ndani ya wiki mbili za awali baada ya kuanza
matibabu ya kifua kikuu.Watu wenye VVU wasio
na ishara wala dalili za uwepo wa kifua kikuu
wanastahili kupata dawa za kujikinga za
isoniazid. Jitihada zote zinapaswa kufanyika
kupambana na maambukizi nyemelezi. Msisitizo
unapaswa kuwekwa katika utambuzi wa
mapema, matibabu, na rufaa, pakiwa na ulazima.
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
163
Kumbuka: Mwongozo mpya unapendekeza
kuanzisha dawa kwa wagonjwa wote mapema
mara maambukizi ya VVU yanapothibitishwa
kuwepo. (“Pima na Tibu”). Serikali inaweza
kutengeneza miongozo mipya kulingana na
kiwango cha utayari wao (usambazaji wa
madawa, uwezo wa maabara, rasilimali watu,
fedha, nakadhalika).
Swali: Nini faida za kutumia dawa za kupunguza
makali ya ukimwi?
Jibu: Baadhi ya faida za dawa za kupunguza
makali ya virusi vya UKIMWI ni pamoja na:
Watu wenye VVU wanaotumia dawa
wanaweza kuishi kwa mda mrefu
ukilinganisha na wale wasiotumia dawa.
Watu wanaotumia dawa wana magonjwa
machache yenye uhusiano na VVU
ukilinganisha na wale wasiotumia dawa.
Kwa kuwa watu wanaotumia dawa kama
ilivyoelekezwa wana afya bora, huenda
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
164
hospitali mara chache na huepuka gharama
nyingine za kiafya.
Wakiwa na afya njema, watu wanaotumia
dawa wana muda zaidi kukamilisha malengo
na dira za maisha yao.
Wakiwa na afya njema, watu wanaotumia
dawa wanaweza kuzitunza familia zao vizuri
zaidi.
Wakiwa na afya njema, watu wanaotumia
dawa wanaweza kuishi kama kawaida.
Kwa kuwa watu wanaotumia dawa wana kiasi
kidogo cha VVU ndani ya miili yao, wana
nafasi ndogo ya kueneza VVU kwa watu
wengine.
Hatua 4: Maswali na majibukuishi kwa
kutumia dawa za kupunguza makali
Swali: Sababu kubwa ya dawa kuota usugu na
matibabu kutofanya kazi ni nini?
Jibu: Ufuasi hafifu wa dawa huongeza hatari ya
dawa kuota usugu na matibabu kutofanya kazi.
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
165
Kutumia dawa kila siku kama ilivyoelekezwa,
ijulikanavyo kama “ufuasi,” ni muhimu sana kwa
dawa kuweza kufanya kazi. Baadhi ya watu
huacha kutumia dawa kama ilivyoelekezwa kwa
kuwa hupatwa na madhara ya pembeni, au kwa
kuwa wanajisikia kuwa na nguvu na wenye afya
na kudhani hawahitaji dawa tena. Baada ya
muda, japo, bila ya dawa, VVU huongezeka tena
mwilini na watu huanza kuugua. Isitoshe, kuna
uwezekano kwamba dawa hizo hizo za
kupunguza makali zisimsaidie tena huyu mtu
mara atakapotaka kuanza matibabu tena kwa
kuwa VVU mwilini watakuwa wameshatengeneza
usugu kwa dawa hizo. Wanaweza wakaanza
kutumia aina nyingine ya dawa, lakini inaweza
kuwa ni vigumu sana kuzipata na /au kukumbwa
na madhara ya pembeni kuliko ulipokuwa
ukitumia dawa za mwanzo. Uenezaji wa kirusi
kinachopelekea usugu wa dawa za VVU kwa njia
ya mapenzi ni jambo linalowezekana pia. Usugu
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
166
ni sababu ya msingi kwa nini matibabu yanaweza
yasifanye kazi.
Swali: Ni kwa muda gani dawa za kupunguza
makali ya virusi vya UKIMWI humwezesha mtu
mwenye maambukizi kuishi?
Jibu: Watu wengi wanaotumia dawa kama
ilivyoelekezwa huishi maisha ya kawaida na
huugua kwa vipindi sawa na watu wasio na
maambukizi ya VVU.
Swali: Changamoto za dawa za kupunguza
makali ya UKIMWI ni zipi?
Jibu: Uwezekano wa hatari za dawa ni pamoja
na madhara ya pembeni (madhara yoyote ya
dawa, kemikali, au dawa nyingine ambazo ni za
nyongeza kwa ajili ya madhara mahususi, hasa
madhara ambayo ni ya kudhuru au yenye
maudhi) yanayosababishwa na dawa za
kupunguza makali au dawa nyingine ambazo
mtu mwenye VVU anazitumia. Asili ya madhara
ya pembeni inategemeana na sehemu ya mwili
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
167
ambako dawa imekusudiwa kutibu au namna
ambayo mwili unashughulika na dawa.
Dawa za kupunguza makali ni matibabu ya
muda mrefu—mtu analazimika kutumia
dawa kila siku kama ilivyoelekezwa na mtoa
huduma za afya. Ufuasi hafifu—kutotumia
dawa kila siku na kama ilivyoelekezwa—
huongeza hatari ya dawa kuota usugu na
matibabu kutofanya kazi.
Dawa nyingi za kupunguza makali humezwa
mara moja kwa siku, pamoja na au bila ya
chakula. Baadhi humezwa mara mbili kwa
siku au zinapaswa kumezwa pamoja na
chakula.
Baadhi ya aina za dawa za kupunguza
makali zinaweza kuwa na madhara ikiwa
zitamezwa pamoja na vidonge vingine au
wakati wa mimba. Ni muhimu kuzungumza
na mtoa huduma za afya kuhusu dawa
zingine unazotumia na mfahamishe kama
una mimba.
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
168
Dawa za kupunguza makali zinaweza
kusababisha matatizo mengine. Baadhi ya
matatizo yanaweza kutatuliwa baada ya wiki
kadhaa za utumiaji, matatizo mengine
yanahitaji ushauri wa daktari au wataalamu
wa afya.
Ikiwa dawa hazimezwi kila siku kama
ilivyoelekezwa, dawa hazitafanya kazi vizuri
na mtu anaweza kuugua. Watu ambao dawa
hazifanyi kazi kabisa wanalazimika
kubadilisha na kupata aina nyingine ya dawa,
lakini machaguzi yao ya dawa hapo baadaye
yatakuwa yamepungua.
Ikiwa unapata matibabu kutibu matatizo
mengine ya kiafya au kinzamimba (uzazi wa
mpango), ni muhimu kumfahamisha daktari
wako. Baadhi ya dawa za kupunguza makali
(kama, efavirenz, nevirapine) huingiliana na
baadhi ya madawa ya uzazi wa mpango.
Kutumia madawa ya kulevya (kama bangi,
cocaine, ecstasy, na kadhalika) pia kunaweza
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
169
kusababisha dawa kuacha kufanya kazi
vizuri.
Swali: Madhara ya pembeni ya kawaida ya dawa
za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI ni
yapi?
Jibu: Madhara ya pembeni ya dawa yanaweza
kutofautiana kulingana na dawa na mtu
anayetumia dawa hizo. Watu wanaotumia aina
moja ya dawa wanaweza kuwa na madhara ya
pembeni tofauti kabisa. Madhara ya pembeni ya
kawaida ni pamoja na:
Maumivu ya kichwa, kizunguzungu cha mara
kwa mara, ambayo huenda yasiwe makubwa
sana.
Kuvimba kwa mdomo na ulimi au kuharibiwa
kwa ini, ambayo inaweza kutishia maisha
Ukurutu mwilini kote
Ganzi miguuni
Matatizo ya figo (hasa kwa matumizi ya
tenofovir)
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
170
Ndoto za ajabu (hasa kwa matumizi ya
efavirenz)
Kipindi 3.3: Kuzuia maambukizi ya
VVU kutoka kwa mama kwenda kwa
mtoto
Dakika 30
Kipindi 3.1: Mazoezi
Utangulizi kuhusu kuzuia na kukomesha
maambukizi ya VVU kutoka kwa mama
kwenda kwa mtoto
Dhamira za mafunzo
Mwisho wa kipindi, washiriki wataweza:
Kueleza maana ya maneno kuzuia
maambukizi ya VVU kutoka kwa mama
kwenda kwa mtoto na kukomesha
maambukizi ya VVU kutoka kwa mama
kwenda kwa mtoto
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
171
Kutoa maelezo ya msingi jinsi ya kumtunza
mama mwenye VVU na mtoto
Zoezi 1: Utangulizi kuhusu kuzuia
maambukizi kwenda kwa mtoto
Dakika 30
Hatua 1: Anza
Waulize washiriki wanaelewa nini kuhusu kuzuia
na kukomesha maambukizi.
Hatua 2: Eleza
Eleza kuwa kuzuia inamaanisha kuzuia
maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda
kwa mtoto na kukomesha inamaanisha
kukomesha maambukizi ya VVU kutoka kwa
mama kwenda kwa mtoto.
Hatua 3: Maswali na majibumaambukizi ya
VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Swali: Maambukizi ya VVU kutoka kwa mama
kwenda kwa mtoto maana yake ni nini?
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
172
Jibu: Maambukizi kutoka kwa mama kwenda
kwa mtoto ya VVU hutoka kwa mama aliye na
VVU kwenda kwa mtoto wake wakati wa ujauzito,
kuzaa, (hujulikana pia kama uchungu wa uzazi
na kujifungua), au wakati wa kunyonyesha (kwa
njia ya maziwa ya mama). Maambukizi ya VVU
kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto vile vile
huitwa maambukizi ya perinatal ya VVU.
Maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa
mtoto ni njia ambayo mara nyingi watoto
wachanga huambukizwa VVU.
Swali: Unadhani maambukizi ya VVU kutoka kwa
mama kwenda kwa mtoto yanaweza kukingwa?
Jibu: Ndiyo
Hatari za maambukizi ya VVU kutoka kwa
mama kwenda kwa mtoto ni ndogo pale
ambapo
Wanawake wenye
VVU wanapopata
dawa wakati wa
Watoto waliozaliwa
na wanawake
wenye VVU
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
173
ujauzito na
kujifungua na katika
mazingira fulani,
kuzaa kwa upasuaji
uliopangwa (mara
nyingine hujulikana
kama C-section).
hupokea dawa za
VVU kwa kipindi
cha wiki sita baada
ya kuzaliwa na
kunyonya maziwa
ya mama kwa miezi
sita halafu
anaachishwa
Hatua 4: Eleza
Wizara ya afya na ustawi wa jamii imeridhia njia
bora kuzuia maambukizi ya VVU kwa watoto
wachanga na watoto wadogo ili kufikia lengo la
kutokomeza maambukizi toka kwa mama
kwenda kwa mtoto. Mbinu ni pamoja na hizi
zifuatazo:
Kinga za awali za maambukizi ya VVU kwa
wanawake wenye umri wa kuzaa na wenza
wao.
Kuzuia mimba zisizotarajiwa kwa wanawake
wenye VVU
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
174
Kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa
wanawake waathirika kwenda kwa watoto
wachanga
Kutoa matibabu, huduma, na msada kwa
wanawake wenye maambukizi ya VVU,
watoto wao wachanga na familia zao.
Hatua 5: Maswali na majibu—wanaume na
nafasi yao katika kuzuia maambukizi ya vvu
toka kwa mama kwenda kwa mtoto
Swali: kuna faida gani
za kuwashirikisha
wanaume kwenye
kuzuia maambukizi
toka kwa mama
kwenda kwa mtoto?
Jibu: Ushahidi unaonesha kwamba wanaume
wanapounga mkono huduma za afya kwa
wanawake:
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
175
Utumiaji wa huduma za kuzuia na kupata
matibabu ya VVU kwa wanawake na watoto
huongezeka.
Matokeo kiafya huboreka.
Kuna ongezeko na ufuasi wa matumizi ya
dawa.
Kuna ongezeko la upimaji na matibabu
miongoni mwa wanaume.
Unyanyapaa hupungua.
Hatua 6: Maswali na majibu—lengo
Swali: Nini lengo la kuzuia maambukizi ya VVU
toka kwa mama kwenda kwa mtoto nchini
Tanzania?
Jibu: Lengo ni kuzuia maambukizi ya VVU
kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na kutoa
matibabu kwa wajawazito wote wenye
maambukizi ya VVU na watoto wao wenye VVU
wanaohudhuria afya ya mtoto na uzazi na
huduma za kuzuia maambukizi ya VVU toka kwa
mama kwenda kwa mtoto katika vituo vya afya
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
176
gerezani. Hili linaweza kufikiwa kwa kutoa
huduma za upimaji wa VVU kwa wanawake
wajawazito ikifuatiwa na kuwapa mbinu kwa
wanawake wenye VVU kuzuia maambukizi wima
ya VVU kwa watoto wao wachanga.
Hatua 7: Fupisha
Kutokomeza maambukizi ya VVU toka kwa
mama kwenda kwa mtoto nchini Tanzania
kunahitajika:Jitihada endelevu ili kuzuia
maambukizi mapya miongoni mwa
wanawake, na kuboresha upatikanaji wa
huduma za uzazi wa mpango miongoni
mwa wanawake waishio na VVUKuboresha
upatikanaji wa huduma kabla ya kujifungua
na wahudumu wenye ujuzi wakati wa kuzaa
kwa wanawake wote, bila kujali mali, hali, na
makazi.
Uharakisha upanuzi wa huduma za kuzuia
maambukizi ya VVU toka kwa mama kwenda
kwa mtoto zenye ubora wa juu kwenye
Somo 3: Matibabu ya Kifua Kikuu na Virusi vya UKIMWI
177
huduma zote kabla ya uzazi na vituo vya
kujifungulia na kuimarisha uwepo wa
huduma kwa kuzishirikisha jamii na vituo vya
afya.
Ubora na mwendelezo wa huduma kwa
wakati muafaka kwa mama na mtoto.
Ushirikishwaji wa wanaume kwenye jitihada
za kuzuia maambukizi ya VVU toka kwa
mama kwenda kwa mtoto ni hatua muhimu
ya kuweza kuwapima VVU wanaume.
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU
Magerezani
178
SOMO 4: KUVUNJA UKIMYA
KUHUSU KIFUA KIKUU NA
VVU
Lengo
Kukuza elimu na ujuzi wa mawasiliano kwa
mfungwa ili aweze kuripoti shutuma zenye
uhusiano na kifua kikuu na VVU miongoni mwa
wafungwa wenzake.
Dhamira za mafunzo
Mwisho wa mafunzo, wafungwa na wafanyakazi
wa magereza wataweza:
Kuelezea na kutambua aina za shutuma
kwenye magereza.
Kuzungumzia shutuma za kimwili au
kimapenzi kwa uwazi zaidi.
Kueleza maana na manufaa ya mawasiliano
kwa wenza.
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU
Magerezani
179
Kutambua njia za asili na zenye ufanisi za
mawasiliano kwa mwenza miongoni mwa
wakazi wenza na wafanyakazi wa magereza.
Kuelezea njia za kutoa taarifa na kutafuta
huduma miongoni mwa wakazi wenza.
Kutambua changamoto kuu na njia za
kuzitatua.
Kipindi 4.1: Kutambua aina za
shutuma katika magereza
Saa 2, Dakika 5.
Kipindi 4.1: Mazoezi
Aina za shutuma katika magereza
Kuzungumzia shutuma za kimwili na
kimapenzi
Jinsi ya kuvunja mazoea ya ukimya
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU
Magerezani
180
Zoezi 1: Aina za shutuma katika magereza
Dakika 20
Vifaa vinavyohitajika
Ubao wa chaki au karatasi za kuandikia
ubaoni
Maandalizi ya awali
Ikiwezekana washirikishe baraza la magereza
katika mjadala huu.
Hatua 1: Fafanua
Wafahamishe washiriki kuwa wafungwa
wanaweza kukumbana na uonevu wa kimwili au
kimapenzi na aina nyingine za vurugu na
kuonewa na wafungwa wenzao na wafanyakazi
wa magereza na kushindwa kutoa taarifa ya
uonevu kwa kuhofia ulipizaji kisasi.
Endelea kueleza kwamba wafungwa vile vile
wanaweza kukumbana na mambo ya kutendewa
vibaya, kudhihakiwa, lugha zisizi na adabu, na
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU
Magerezani
181
uongo wa kupindukia kutoka kwa wafungwa
wenzao. Wafanya kazi wa magereza wanaweza
kutumia kauli za vitisho kama njia ya
kuwaogopesha au kuwavunja moyo wafungwa
wenza ili kuwafanya watii kanuni na taratibu za
magereza
Hatua 2: Jadili
Eleza kwamba majadiliano haya yatatoa
mwanga juu ya haya mambo hivyo
wafungwa pamoja na wafanyakazi wa
magereza wanaweza kutatua mambo haya.
Matukio ya unyanyasaji kwa kiasi kikubwa
husababishwa na sababu za kimazingira na
mahali kama vile umati mkubwa/msongamano,
usimamizi hafifu, nguvu ya madaraka ambayo
inaweza kutengeneza fursa kwa aina mbalimbali
za unyanyasaji. Madhara ya unyanyasaji wa
kimwili na kimapenzi yanaweza kuwa pamoja na
majeraha, ugonjwa, kujiumiza mwenyewe,
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU
Magerezani
182
msongo wa mawazo, na ugonjwa wa akili.
Sababu hizi zinaweza kutatuliwa na kuzuiwa kwa
kuongeza usimamizi thabiti na kwa wafanyakazi
wa magereza kuzungukia vizimba na program
za elimu rika na uhamasishaji. Usimamizi usio
thabiti kutoka kwa maafisa wa magereza huleta
mianya kwa wafungwa kujiingiza kwenye vurugu
na kuwatendea vibaya wengine. Si rahisi
kufuatilia shutuma za unyanyasaji au uonevu
miongoni mwa wafungwa wenye maelezo
yasiyijitosheleza hasa kuhusu shutuma za
unyanyasaji wa kimapenzi miongoni mwa
wafungwa wenzao. Hali hii imekuzwa na mazoea
ya ukimya na ukosefu wa, au upungufu wa, njia
za ufuatiliaji na uwekaji kumbukumbu za
shutuma hizo katika vizimba vya magereza.
Uwekaji wa kamera na vibonyezo hisishi kwenye
vizimba kunaweza kusaidia kufuatilia unyanyasaji
na tabia za vurugu miongoni mwa wafungwa.
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU
Magerezani
183
Hatua 3: Chemsha Bongo
Wapange washiriki wawili wawili kwa ajili ya
chemsha bongo halafu waombe wajadili na
kuandika aina gani za unyanyasaji wa—
kimwili, hisia na kimapenzi—ambao hutokea
katika magereza. Wape takiribani dakika 10.
Hatua 4: Maoni
Waombe washiriki kuchangia aina za
unyanyasaji walizoziainisha.
Hatua 5: Mapitio
Eleza maneno kwenye jedwali hapa chini:
NENO MAANA
Ukatili: Shirika la afya duniani (WHO)
linaeleza ukatili kuwa ni “matumizi
ya nguvu za kimwili au madaraka
kwa kukusudia, kutishwa au kwa
uhalisia, dhidi ya mtu mwenyewe,
mtu mwingine, au dhidi ya kikundi
au jumuiya ambayo huenda
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU
Magerezani
184
NENO MAANA
yakasababisha au yakawa na
uwezekano mkubwa sana wa
kusababisha majeraha, kifo,
madhara ya kisaikolojia, maendeleo
mabaya au unyimaji” (Krug et al.
2002). maneno “Matumizi kwa
kukusudia” ni ya msingi mno
ambayo yanatofautisha vurugu na
madhara na majeraha ya
kutokukusudia.
Madaraka: Uwezo wa kufanya jambo fulani
pamoja na kusimamia na
kuwashawishi watu wengine na
matendo yao. Madaraka yanaweza
kutumiwa kwa njia chanya na hasi
pia. Unyanyasaji unaweza kutokea
iwapo madaraka yatatumika kwa nia
ya kudhulumu au kupata fadhila
kutoka kwa mtu asiye na nguvu kwa
kubadilishana faida au ahadi.
Ukosefu wa usawa wa madaraka
kati ya watu unaweza kufanywa kwa
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU
Magerezani
185
NENO MAANA
mabavu au kwa vitisho. Miundo ya
madaraka yaweza kuwa halisi au ya
kutambua. Miundo ya madaraka
yaweza kuwa; kuwa na madaraka,
uwezo wa kufanya maamuzi, au
umiliki wa chakula, pesa, au silaha.
Ridhaa: Maana yake ni kufanya uchaguzi
sahihi wa kufanya jambo fulani kwa
uhuru na kwa hiari. Hakuna ridhaa
pale ambapo makubaliano hufikiwa
kwa njia ya vitisho, nguvu, au njia
nyingine za lazima, utekaji nyara,
ulaghai, udanganyifu, uwakilishi
mbaya. Kutishia au kuzuilia au
kuahidi kutoa fadhila ili kupata
ridhaa ya mtu ni matumizi mabaya
ya madaraka. Matendo yote ya
ukatili na unyanyasaji wa kimapenzi
hutokea bila ya ridhaa stahiki. Hata
kama mtu atasema ndiyo wakati wa
moja ya matendo haya, si ridhaa
ikiwa alisema kwa kushinikizwa—
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU
Magerezani
186
NENO MAANA
yaani mkosaji alitumia nguvu fulani
au vishawishi ili kumshawishi
mhanga kusema ndiyo.
Ukatili wa
kimwili:
Inamaanisha matumizi ya nguvu
kwa kukusudia yenye nia ya
kusababisha kifo, ulemavu,
majeraha, au madhara mengine.
Matendo ya ukatili ni pamoja na
kukwaruza, kusukuma, kutupa,
kukwida, kung’ata, kukaba, kutikisa,
kupiga kofi, kupiga ngumi,
kuunguza, na matumizi ya silaha,
vizuizi, au ukubwa wa mwili wa mtu
au nguvu dhidi ya mtu mwingine.
Ukatili wa
kimapenzi:
Inamaanisha matumizi ya nguvu
kumlazimisha mtu kushiriki mapenzi
kinyume cha ridhaa yake, jaribio au
kukamilisha kitendo bila ya ruhusa
yake au kuelewa, au mwingiliano wa
ukatili wa kimapenzi. Vitendo vya
ukatili wa kimapenzi ni pamoja na,
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU
Magerezani
187
NENO MAANA
usumbufu wa kimapenzi, ubakaji,
jaribio la ubakaji, ubakaji kwenye
ndoa, unyonyaji, ukatili wa watoto
kimapenzi/uzinzi wa maharimu,
vitendo vya kimapenzi (bila-
kuingiliana kimapenzi), ukahaba a
kulazimishwa, ukahaba wa watoto,
na biashara za mapenzi.
Unyanyasaji wa kimapenzi na ukatili
huambatana na tabia
hatarishi.Hatari ya ueneaji wa VVU
huongezeka wakati wa ukatili wa
kimapenzi kwa kuwa nguvu nyingi
hutumika, au kitendo cha
kulazimisha ambacho kinaweza
kusababisha kuchanika kwa ngozi
au ngozi nyembamba na hivyo
majimaji kuweza kupenya.
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU
Magerezani
188
Hatua 6: Uliza
Waombe washiriki wataje baadhi ya njia za
kuzungumzia ukatili wa kimapenzi kwa
ujumla.
Hatua 7: Tafakari
Jadili na washiriki kwa nini ni vigumu
kuzungumzia ukatili kwenye mazingira ya
magereza na uandike kwenye karatasi ya
kuandikia ubaoni au kwenye ubao wa chaki.
Mazoea ya kukaa kimya yaweza kuwa ni moja ya
sababu zinazopelekea ugumu wa kuzungumzia
ukatili katika magereza.
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU
Magerezani
189
Zoezi 2: Kuzungumzia ukatili wa kijinsia na
kimwili: Kuvunja mazoea ya ukimya
Dakika 45
Hatua 1: Eleza
Sema kwamba uongozi wa magereza nchini
Tanzania umejipanga kuhakikisha uwepo wa
usalama kwa wafungwa. Ingawa, kama ilivyo
kwenye magereza mengi ulimwenguni (Dennehy
na Nantel, 2006), Magereza ya Tanzania
yanakumbana na changamoto nyingi za uongozi
mbaya, matumizi mabaya ya madaraka, na ukatili
ambazo menejimenti ya magereza inajaribu
kuzishughulikia. Kama ilivyojadiliwa kwenye
shughuli zilizotangulia, eleza kwamba, wafungwa
wanaweza kukumbana na ukatili wa kimapenzi,
kimwili na namna nyinginezo za ukatili ndani ya
magereza kutoka kwenye mikono ya wafungwa
wengine ama wafanyakazi wa magereza wasio
waaminifu.
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU
Magerezani
190
Kwenye baadhi ya matukio wafungwa na
wafanyakazi wanaamini ya kwamba
kinachoendelea nyuma ya ukuta wa gereza,
hasa, ukatili wa kimapenzi, haupaswi kuwekwa
wazi kwa umma. Mitazamo kama hii hutambulika
kama “Mazoea ya ukimya,” ambayo,
isiposhughulikiwa, inaweza kupelekea
kuongezeka kwa matukio ya ukatili wa
kimapenzi, kimwili, na ukatili mwingine ndani ya
magereza. Kutoshughulikia mazoea ya ukimya
kunadumisha na kuendeleza tabia za ukatili
ambazo zinaongeza hatari ya kifua kikuu,, VVU,
na magonjwa ya ngono, na hivyo kuwadhuru
wafungwa na maofisa wa magereza (Dannehy
na Nantel, 2006 uk. 177)
Hatua 2: Maswali na majibu—mazoea ya
kukaa kimya
Swali: Mazoea ya kukaa kimya maana yake
nini?”
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU
Magerezani
191
Wape nafasi washiriki wakupe maoni yao
wenyewe kabla hujawaelezea.
Jibu: ”Mazoea ya ukimya” (Martin 2002) maana
yake ni hali ya wafungwa, wafanyakazi, au
uongozi kutokuwa tayari kuzungumzia kwa
uwazi matukio ya uvunjifu wa sheria, ukiukaji wa
miiko, au yenye utata, kama vile ukatili wa
kimapenzi. Mazoea ya ukimya yamejengwa
katika kanuni zisizozungumzika.
Wafungwa wengi hushabihia mazoea ya ukimya
kwa sababu ya woga wa kulipiza kisasi na
kwamba wengine huenda wasiwalinde mara
baada ya kuvunja ukimya. Wangeweza
kuhatarisha nidhamu kuliko kukiuka mazoea ya
ukimya ndani ya gereza. Lakini ukimya huu si
sahihi kwani unawalinda wakosaji, hasa kwa kuwa
lengo la magereza ni kuhakikisha usalama na
mazingira salama kwa watu kupitia usimamizi
unaofaa na maofisa wanaowasimamia.
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU
Magerezani
192
Uwepo wa tabia zinazokiuka maadili, matumizi
mabaya ya madaraka, kufunika mambo
kunaweza kupelekea magereza kuwa mahali
hatari kuishi na kufanya kazi kwa kuruhusu
makundi ya watu kutumia kanuni wanavyopenda
wao pasipo kuwajibishwa. Jambo hili hupelekea
hasira, kuvunjika moyo, na mara nyingine huzuni
na ugonjwa wa akili
Hatua 3: Eleza
Ili kushughulikia mazingira yasiyo salama
yaliyosababishwa na ukatili wa kimapenzi na
namna nyingine za ukatili, mazoea ya ukimya
yanapaswa kushughulikiwa kwa kuhakikisha
wafungwa wanaelewa tofauti kati ya kuaminiana,
na kutii adhabu kwa ujumla. Kwa kutambua
kuwa, uaminifu ndani ya kikundi ni muhimu
katika kuimarisha umoja, kukuza usalama, na
kujenga uaminifu, kutii dhamira za magereza za
kuhakikisha usalama, ulinzi, na mazingira wezeshi
ni muhimu zaidi.
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU
Magerezani
193
Hatua 4: Ufupisho
Fupisha kwa kusema kwamba ni muhimu kwa
wafungwa kuvunja mazoea ya ukimya kwa
kuzungumzia ukatili gerezani, ikiwemo ukatili wa
kimapenzi. Serikali ya Tanzania ina vyombo,
program na miradi kadhaa, ambayo inadhibiti
unyanyasaji wa kimapenzi na ukatili. Ikiwemo
“toleo maalumu la Sheria ya makosa ya
kimapenzi ya mwaka1998 ambayo inaweka wazi
aina mbalimbali za makosa ya jinai yenye
uhusiano wa ukatili wa kijinsi, ikiwemo ubakaji,
mashambulizi na maudhi kimapenzi, ukahaba,
ukeketaji, na biashara ya mapenzi.
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU
Magerezani
194
Hatua 5: Funga somo
Wape nakala (ikiwa zipo). Kama hakuna,
soma nakala zifuatazo kwa washiriki:
Toleo maalumu la Sheria ya makosa ya
kimapenzi Tanzania (SOSPA)
Mnamo mwaka 1998 bunge la Tanzania lilipitisha
Toleo Maalumu la Sheria ya Makosa ya
Kimapenzi (SOSPA)(Serikali ya Muungano wa
Tanzania 1998) ili kulinda “heshima na uadilifu
wa wanawake na watoto,” iliyotambulisha
makosa mapya kama vile maudhi kimapenzi,
unyanyasaji kimapenzi, na usafirishaji wa
binadamu.
SOSPA Ni chombo kikuuu cha kitaifa kinachotoa
idhini kupambana na ukatili wa kijinsi na namna
nyingine za unyanyasaji wa kimapenzi. Inatoa
adhabu kali na haki ya kupata fidia kwa wahanga
wa ukatili.
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU
Magerezani
195
SOSPA imerasimisha ubakaji kuwa ni kosa la jinai
na inatoa adhabu kali kwa mbakaji.
SOSPA imeingizwa kwenye sheria za adhabu za
Tanzania. Sheria za adhabu sura 16, Toleo jipya,
imeweka wazi yafuatayo:
Kifungu 130, sura 16, kinaeleza kuwa, ni kosa
kwa mwanaume kumbaka msichana au
mwanamke. Mwanaume atakuwa ametenda
kosa la ubakaji ikiwa atashirikiana mapenzi
na msichana au mwanamke ambaye si mke
wake, au kuwa mkewe ambaye ameachana
naye; au bila ya ridhaa yake kufanya jambo
hili wakati wa kufanya mapenzi; au kwa
ridhaa yake, pale ambapo ridhaa
imepatikana kwa mabavu, vitisho, au
kumweka katika hofu ya kifo au majeraha
Mtu yeyote anayejaribu kubaka anatenda
kosa la kujaribu kubaka na, isipokuwa kwa
mambo yaliyoainishwa kwenye kifungu
kidogo cha 3, anastahili kifungo cha maisha
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU
Magerezani
196
gerezani ikiwa kosa lake litathibitishwa, na
kwa namna yoyote ile anastahili kifungo jela
kwa si chini ya miaka 30 pamoja na au bila
ya adhabu ya viboko.
Mtu yeyote ambaye, anakusudia
kusababisha maudhi kimapenzi kwa mtu
yeyote kwa kutamka neno lolote au sauti,
kufanya ishara ya mwili, au kuonesha neno
lolote au kitu kwa nia kwamba neno hilo au
sauti isikike, au ishara ya mwili au kitendo
ionekane na mtu mwingine, mtu huyu
anatenda kosa la shambulizi kimapenzi.
Ikithibitika, anastahili adhabu ya kifungo
gerezani kwa kipindi kisichozidi miaka
mitano, faini isiyozidi shilingi 300, 000, au
vyote viwili faini na kifungo.
Mtu yeyote ambaye, kwa kujifurahisha
kimapenzi, anafanya kitendo chochote, kwa
kutumia sehemu zake za siri au kutumia
vibaya sehemu nyingine yeyote ya mwili wa
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU
Magerezani
197
binadamu au kitu chochote katika tundu
lolote au sehemu ya mwili ya mtu mwingine
yeyote, iwe kitendo ambacho hakijumuishi
ubakaji chini ya kifungu 130, ametenda kosa
kubwa la unyanyasaji wa kimapenzi.
Zoezi 3: Mazoezi ya jinsi ya kuvunja
ukimya
Dakika 60
Vifaa vinavyohitajika
Ubao wa chaki au karatasi ya kuandikia
ubaoni
Maandalizi ya awali
Soma na elewa kipengele hiki.
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU
Magerezani
198
Hatua 1: Jadili
Fungua kwa kusema kwamba kwa namna
nyingi gereza ni kama mji mdogo.
Katika mji huu wafungwa ndio raia. Na kama
ilivyo katika mji wako na mji wangu, raia wa
gerezani wanapaswa kuwekwa mahali salama na
pa uhakika. Hili hufanyika kwa kuwapa makazi
ambayo yanakidhi viwango vya afya ya jamii,
huduma za afya kitabibu na kiakili ambazo
zinakidhi viwango vya kitaifa, vyakula ambavyo
vina mahitaji ya msingi ya lishe, na misaada
mingine ili kusaidia urejeaji wenye mafanikio
kwenye jamii zao.
Ingawa, kama ilivyo kwa miji midogo, magereza
hayawezi kwa ufanisi huku kukiwa na mazoea ya
ukimya. Tunahitaji kuvunja mazoea ya ukimya
kwa sababu inadidimiza lengo la uwepo wa
magereza: “Kutoa huduma rekebishi kwa
kutengeneza maisha ya kirafiki na thabiti na
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU
Magerezani
199
mazingira ya kazi kwa ajili ya wafungwa na
wafanyakazi wasimamizi wa magereza.” (Smith
na Yarussi 2007)
Hatua 2: Eleza
Ukali wa aina yoyote ile, hasa ukatili wa kijinsia, ni
aina kubwa zaidi ya ukiukwaji wa haki za
binadamu katika mazingira rekebishi. Ukatili wa
kijinsia miongoni mwa wafungwa na au kati ya
wafanya kazi wa magereza pia ni jambo la
kiusalama na ulinzi kwa:
Kuhatarisha usalama, ulinzi na afya za
wafungwa na wafanya kazi
Kuongeza hatari ya kupata na kueneza VVU,
magonjwa ya ngono, na maambukizi
yanayohusiana.
Kupunguza uaminifu na motisha miongoni
mwa wafungwa na wafanyakazi gerezani.
Kupunguza heshima miongoni na baina ya
wafungwa na wafanya kazi.
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU
Magerezani
200
Kutishia usalama na ulinzi wa vituo vya
magereza.
Kudhuru mahusiano ya kifamilia
Kujenga mtazamo hasi kwa umma juu ya
magereza.
Kudumisha tabia za ukatili ndani na nje ya
magereza.
Hatua 3: Maswali na majibu—wakati
tunpovunja mazoea ya ukimya
Swali: Ni wakati gani tungeweza kusema
mazoea ya ukimya yamevunjwa?
Chukua maoni machache
Jibu: ”Wafungwa huhakikishiwa usiri mara baada
ya kuripoti matukio ya ukatili wa kimapenzi
kuwaepusha na maudhi au kisasi kutoka kwa
wakosaji. Pasipo na kamera zinazotazama,
walalamikaji wanapaswa kuruhusiwa kuonesha
ushahidi wa kimwili kuhusu kesi za unyanyasaji
wa kimwili na kimapenzi. Tekinolojia inaweza
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU
Magerezani
201
kusaidia kuvunja mazoea ya ukimya kwa kuwa
wafungwa na wafanyakazi wanajua kuwa kamera
zinatazama matendo na tabia zao.
Hatua 4: Maelezo
Mfumo wa mawasiliano unaathiri sana namna
ambavyo wafungwa wanavunja mazoea ya
ukimya. Kwa mfano wafungwa wa kiume na kike
wanaweza kutofautiana tabia zao na mfumo wa
mawasiliano, hata kama hawajawahi kukumbana
na ukatili katika mazingira ya magereza. Ingawa,
ni mhimu kwa wafungwa kujua kwamba
endapowamewahi kunyanyaswa kimapenzi,
kushambuliwa, au kuudhiwa na wafungwa
wenzao au wafanya kazi, wana haki ya kuripoti
kosa kwa usalama, kwa siri, na bila ya kutaja jina.
Mfungwa anaweza kutoa taarifa zote au kuminya
kiwango cha taarifa anazozitoa kadri anavyoona
yafaa. Ingawa, kadri taarifa nyingi zinapotolewa,
ndivyo itavyopelekea mfanyakazi wa magereza
Somo 4: Kuvunja Ukimya Kuhusu Kifua Kikuu na VVU
Magerezani
202
kuchukua hatua dhidi ya mkosaji na kumweka
mhanga na wafungwa wengine salama.
Hatua 5: Shauri
Mfungwa yeyote akikumbana na
unyanyasaji wa kimapenzi, uonevu au
kupigwa bila sababu halali anatakiwa atoe
taarifa kwa uongozi wa gereza mara moja.
Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu
203
SOMO 5: KUISHI KWA
MATUMAINI UKIWA NA VVU
NA KIFUA KIKUU
Lengo
Kuwajenga washiriki kiakili, kwa hisia, kiroho, na
kimwili jinsi ya kukubaliana na kuishi na kifua
kikuu na VVU.
Dhamira za mafunzo
Mwisho wa somo hili washiriki wataweza:
Kusema umuhimu wa ufuasi mzuri na kuishi
maisha yenye afya.
Kueleza madhara ya kifua kikuu na VVU,
kimwili, kisaikolojia, kijamii, kitabia, na
kiuchumi miongoni mwa wafungwa na
familia zao.
Kubainisha njia za kupunguza unyanyapaa,
na ubaguzi dhidi ya watu wenye VVU.
Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu
204
Kueleza jinsi ya kuwasaidia watu waishio na
VVU na magonjwa nyemelezi.
Kipindi 5.1: Kukabiliana na hali ya
kuwa na VVU
Dakika 60
Kipindi 5.1: Mazoezi
Utangulizi kuhusu kuishi kwa matumaini
ukiwa na VVU na TB.
Kupunguza unyanyapaa na ubaguzi
dhidi ya watu waishio na VVU
Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu
205
Zoezi 1: Utangulizi kuhusu kuishi kwa
matumaini ukiwa na VVU na TB
Dakika 30
Vifaa vinavyohitajika
Jadili maswali yaliyopo kwenye karatasi ya
ubaoni au ubao wa chaki
Vipeperushi vinavyoelezea kuishi kwa
matumaini ukiwa na VVU gerezani
(ikiwezekana)
Maandalizi ya awali
Andika maswali ya kujadili (tazama hatua ya
3 chini) kwenye karatasi ya ubaoni au ubao
wa chaki
Hatua 1: Eleza
Kutambua ya kuwa una maambukizi ya VVU
kutabadili maisha yako ghafla. Unaweza
kukumbana na wigo mpana wa hisia—wasiwasi,
Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu
206
kupoteza, majonzi, huzuni, kukanwa, hasira,
mashaka. Haijalishi ni kwa kiasi gani daktari na
marafiki wanakuhakikishia, namna ambavyo
vidonge vina ufanisi mkubwa sasa na
zitakavyokuwa hapo baadaye, udogo wa
madhara kimwili yatokanayo na kiwango kidogo
cha maambukizi yaliyopo mwilini mwako kwa
sasa, au ni jinsi gani unapaswa kujiandaa kiakili
na kimawazo, uhitaji wako wa msaada itakuwa
jambo bora. Maswala kisaikolijia yanayowakumba
watu wengi wenye VVU hutofautiana. Matumaini
na matarajio ya maisha yako ya baadaye,
mahusiano yako, na mwenendo wa maisha yako
yote yatahitaji mabadiliko fulani ili kukufanya
uweze kukabiliana na hali ya kuwa na VVU na
kuishi maisha mazuri yenye afya.
Majadiliano haya yanalenga kujadili na kuibua
mbinu na njia za namna ambavyo mtu anaweza
kukabiliana na hali ya kuthibitika kuwa na
maambukizi ya Kifua Kikuuau VVU gerezani
Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu
207
mahali ambapo rasilimali zinaweza kuwa chache
na kuna hatari ya ukatili, unyanyapaa na ubaguzi.
Hatua 2: Jadili
Yapatie makundi ya watu wanne wanne maswali
yafuatayo kwa ajili ya majadiliano:
Nini maana ya kuishi kwa matumaini ukiwa
na Kifua Kikuu na VVU gerezani?
Mfungwa au mfanyakazi wa magereza
anaweza kufanya nini ili kuishi kwa
matumaini akiwa na maambukizi?
Ni jinsi gani mafanyakazi wa magereza au
mfungwa anaweza kumjali mtu aishie na
VVU gerezani?
Wafanye au wasifanye nini ili kuonesha
kujali?
Hatua 3: Maelezo
Eleza kwa kifupi majibu kwa maswali haya
pamoja na washiriki.
Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu
208
Gawa vipeperushi vifuatavyo (ikiwa vipo).
Kama havipo, soma baadhi ya njia muhimu
kuonesha kuwajali watu wenye VVU
magerezani.
Wafungwa waishio na VVU wanapaswa wajitahidi
kuiweka miili yao kuwa na nguvu, kwa kuhusisha
yafuatayo:
Kula mlo uliokamilika au kuongeza kiwango,
kila inapowezekana, ikiwemo vyakula vyenye
virutubisho ambavyo vina protini, vitamini,
na wanga. Ukosefu wa virutubisho
utachangia sana kuharibiwa kwa mfumo wa
kinga wa mwili. Mlo kamili huupatia mwili
nguvu za kuweza kupambana na magonjwa.
Vyakula vya asili vinafaa zaini kuliko vile vya
kwenye makopo na vyakula vilivyosindikwa.
Mboga mboga zina madini na vitamin
mahususi kwa ajili ya mwili kustawi .Chakula
kinapaswa kusafishwa na kupikwa vizuri
Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu
209
kabla ya kuliwa ili kuulinda mwili kutokana na
magonjwa yatokanayo na vyakula.
Kuwa mkakamavu kwa kufanya mazoezi na
kupata muda wa kutosha kulala. Mazoezi ya
viungo yatapunguza msongo na uvunjikaji
moyo na kuchangia kupata afya njema na
uvumilivu.
Kujiunga au kuunda vikundi saidizi na
wafungwa wenzio ambao wana VVU
Kuzungumza na wafungwa wengine kuhusu
upimaji wa ugonjwa.
Kutafuta ushauri wa kidakitari pale mtu
anapojisikia kuumwa, au kuwa na msongo,
na kufuata ushauri, ikiwemo kutafuta ushauri
wa kidaktari, nasaha, na kijamii.
Ukiwa kwenye matumizi ya vidonge fuata
maelekezo ya dawa uliyoandikiwa. Kuwa na
rafiki wa matibabu ambaye utakumbushana
naye muda wa kunywa vidonge.
Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu
210
Usivute sigara na usitumie dawa bila ya
maelekezo ya daktari.
Kuzungumza na mtu unayemwamini kuhusu
hisia zako.
Kumwambia mtu fulani unayemwamini
kwamba una VVU.
Njia za kuwahudumia watu waishio na VVU
gerezani
Usijitenge na wafungwa wenzio au
wafanyakazi wa magereza. Jenga urafiki. Ishi
kama ambavyo mmekuwa mkiishi kabla.
Usibadilike kwa sababu tu unajua mtu fulani
ana maambukizi ya VVU.
Tambua hisia zao. Usiwafanye wafadhaike
kutokana na hisia zao. Ni sawa kulia
wanapolia na kucheka wanapocheka. Ni
jambo zuri kiafya kutoa hisia kuliko kuziweka
moyoni. Kuweka hisia mbaya moyoni
husababisha msongo na msongo
Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu
211
husababisha madhara kwenye mfumo wa
kinga.
Ikiwezekana waalike kwenye matembezi
unapopata nafasi ya kufanya mazoezi. Kuwa
mwangalifu na nguvu za miili yao.
Usiwaruhusu kufanya vitu ambavyo hawana
nguvu za kutosha kuvifanya.
Wasaidie kuweka mambo yao sawa. Watu
wengi waishio na VVU hawapendi kufanya
vitu vigumu kama kuandika wosia au
kuziambia familia zao kuhusu ugonjwa wao.
Washirikishe kwenye sikukuu za kidini au za
asili au sherehe ikiwa inawezekana.
Jitolee kuwahudumia watu wenye VVU ili
daktari wa magereza aweze kupumzika.
Ikiwa ni mfanya kazi wa magereza, wasaidie
baadhi ya majukumu ili kurahisisha maisha.
Ni sawa kuzungumzia ugonjwa wao, lakini
kuwa mwepesi wa kuhisi. Wafungwa
wenzako au wafanyakazi wa magereza
Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu
212
wanaweza kuchagua siku ya kuzungumza.
Itategemea na namna ambavyo anajisikia
siku hiyo.
Kama ilivyo kwa mtu mwingine yeyote, watu
wenye VVU wana siku nzuri na mbaya. Katika
siku nzuri watendee kama ilivyo kawaida.
Katika siku mbaya watendee kwa kuwajali
zaidi na huruma.
Kujali kunaweza kuoneshwa pasipo maneno.
Huhitaji kuzungumza muda wote.
Wahimize kufanya maamuzi kwa muda
mrefu iwezekanavyo kwa ajili yao. Mtu
anapoumwa, maamuzi mengi hutolewa
kwao, hivyo basi waruhusu wafanye
maamuzi mengi iwezekanavyo.
Zingatia ahadi zako ikiwa utawaahidi watu
waishio na VVU. Usiwaambie utawaona
kesho huku ukijua kuwa kesho hutaweza
kuonana nao.
Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu
213
Kuwa tayari kuona watu waishio na VVU
wakikasirika pasipo na sababu.
Hawajakukasirikia wewe. Wamekasirishwa na
kile kinachoendelea kwao na kutokuwa na
uwezo wa kukishughulikia.
Usiwafanyie kile ambacho bado wana uwezo
wa kukifanya.
Jaribu kuwa na mtazamo chanya.
Kwa kujenga urafiki unaleta mwanga kwenye
mazingira yenye giza nene.
Zoezi 2: Punguza unyanyapaa na ubaguzi
dhidi ya watu waishio na VVU
Dakika 30
Vifaa vinavyohitajika
Karatasi ya ubaoni au ubao wa chaki
Maandalizi ya awali:
Andika maswali(tazama hatua 3 chini)
kwenye karatasi ya ubaoni au ubao wa chaki.
Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu
214
Hatua 1: Eleza
Uliza washiriki nini maana ya unyanyapaa na
ubaguzi dhidi ya watu waishio na VVU.
Chukua maoni machache.
Hatua 2: Eleza
Unyanyapaa Ubaguzi
Unyanyapaa maana yake
ni tabia isiyopendeza au
isiyoya heshima ambayo
mtu au kikundi kinakuwa
nayo ambayo hupelekea
kushuka kwa hadhi ya
mtu au kikundi hicho
katika macho ya jamii.
Unyanyapaa unaweza
kuletwa na mwonekano
mwilini, kama vile, dalili
za ugonjwa
zinazoonekana, au
mtazamo hasi kwa kundi
Ubaguzi unaweza
kuelezewa kwa
kujumuisha mtazamo
hasi au tabia fulani au
vitendo. Mara nyingi
huelezewa kama ni
utofauti unaojengwa
kuhusiana na mtu
unaopelekea
kutendewa bila haki na
bila kuthibitisha kwa
misingi ya uhusika wao,
au kuchukuliwa kama
wanahusika katika kundi
Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu
215
fulani la watu au mtu fulani. Kwa mfano
unyanyapaa unaweza
kusababisha madhara
na ubaguzi
unaoelekezwa kwa
watu ambao kweli, au
wanahisiwa tu kuwa na
VVU, na vikundi vya
kijamii na watu
wanaoishi nao
Hatua 3: Zoezi
Wagawe washiriki kwenye makundi matano
na wape kila kundi hadithi moja. Waeleze
washiriki kuwa watajadili maswali yafuatayo:
Kwa maoni yako, unadhani kwa nini katika
hadithi hii watu wameonesha tabia hizo?
Unadhani nini kifanyike ili kupunguza
unyanyapaa na ubaguzi?
Unadhani ni nani anaweza kuwasaidia watu
wanaonyanyapaliwa au kubaguliwa?
Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu
216
Hadithi 1
Siku moja afisa Mapendo
aliporudi nyumbani
kutoka kwenye
majukumu alikuta mke
wake akilia. Baada ya
kumwuliza kwa nini
analia, mkewe alisema ametoka kliniki ya uzazi
na ameambiwa kuwa ana VVU. Baada ya kusikia
haya, afisa Mapendo alighadhabika sana na
kuanza kumfokea mke wake, akisema kuwa
amepata maambukizi ya VVU kutoka kwa
mwanaume mwingine nje ya ndoa, na hivyo
hastahili kuendelea kuishi nae. Kwa hiyo,
alimtolea vitu vyake ndani ya nyumba na
kumfukuza nyumbani.
Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu
217
Hadithi 2
Jane ni muuguzi
katika gereza
mkoani mwanza.
Amefanya kazi pale
kwa zaidi ya miaka
10. Anafanya kazi
kwa bidii anapotoa huduma kwa wagonjwa
wake. Mara zote anapogundua kuwa mgonjwa
ana maambukizi ya VVU, huhakikisha kuwa
anapomhudumia anavaa glavu na barakoa ili
kuikinga pua yake, hata kama mgonjwa hana
vidonda ambavyo vinaweza kusababisha
maambukizi.Mara nyingi mgonjwa anapogundua
jambo hili huchukizwa.
Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu
218
Hadithi 3
Mariam ni mke wa
mfungwa
aliyefunguliwa
gerezani hivi
karibuni. Ana shiriki
katika vikundi vya ushirika wa kukopa na kuweka
katika mji wake. Anashirikiana vizuri na wenzake
kwenye shughuli zao za kila siku. Miezi miwili
iliyopita yeye na mmewe walikwenda kliniki
kupima VVU, na wote waligundulika kuwa na
maambukizi ya VVU. Tokea wakati huo
wanachama wenzake kwenye kikundi
wamemtenga na hawashirikiani naye tena
kwenye shughuli zao za kikundi kwa kuhofia
kuwa nao wangeweza kuambukizwa VVU. Hali hii
inamsikitisha Mariam na inatishia hali ya uchumi
wa familia yake.
Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu
219
Hadithi 4
Salum ni mfungwa anayetumikia kifungo cha
miaka mitano gerezani. Anaishi na VVU na
amekuwa akitumia vidonge vya ARV kwa miaka
miwili. Kwa kipindi chote hicho amejitahidi
kuficha vidonge vyake ndani ya vitu vyake, lakini
siku moja mfungwa mwenzake alivikuta na
alianza kumzungumzia na kufikia hatua ya
kumtenga wakati wa chakula. Baada ya muda
Salum aligundua kuwa wenzake walikuwa
wakijiweka kando na yeye, hivyo aliamua kueleza
hali halisi lakini waliendelea kumcheka na
kumtenga.
Hadithi 5
Shida alifunguliwa kutoka gerezani. Alikuwa na
furaha kubwa kurudi nyumbani kuungana tena
na familia, mke, na watoto wake. Alipokuwa
gerezani Shida alipima VVU na aligundulika kuwa
navyo. Aliudhika sana kuhusu namna ambavyo
atakwenda kumweleza mke wake kwa kuwa
Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu
220
hakutaka kuharibu siku yake ya furaha, hivyo
aliendelea kuficha na usiku huo alifanya mapenzi
na mkewe bila ya kutumia kondomu.
Hatua 4: Eleza kwa kifupi
Toa fursa kwa kila kundi kujadili hadithi yao
kwa kina.
Hatua 5: Jadili
Swali: Tunawezaje kupunguza unyanyapaa na
ubaguzi dhidi ya watu waishio na VVU?
Jibu: Kuendeleza mbinu/njia zinazoshughulikia
sababu kuu za unyanyapaa na makundi
maalumu ya waathirika, ikiwemo wafungwa.
Zifuatazo ni baadhi ya njia tunazoweza kujaribu
na kupunguza unyanyapaa katika ngazi ya kisera
na kijumuiya.
Kuzishirikisha jamii kuthibitisha kutoa msaada
kwa watu waishio na VVU (kwa mfano.
Somo 5: Kuishi kwa matumaini ukiwa na VVU na Kifua kikuu
221
biashara katika jamii, mashirika ya kijamii,
mashule, na viongozi wa jumuiya).
Kukuza uongozi katika jamii kwa watu
waishio na VVU.
Kukuza mbinu za kiafya kwa jamii kuhusu
kinga na huduma ya Kifua Kikuu na VVU.
Kuendelea kutoa elimu kuhusu mambo
yenye kuhusiana na Kifua Kikuu na VVU.
222
ORODHA YA MANENO
CD4: Aina ya chembechembe –T ambazo
huukinga mwili dhidi ya maambukizi na kuutunza
mfumo wa kinga. VVU hushambulia
chembechembe za CD4 moja kwa moja, na
kuhatarisha mfumo wa kinga.
Daraja: Kikundi cha watu waliowekwa pamoja
kulingana na viwango vyao vya mali na/au kazi
wanazofanya katika uchumi.
Dhuluma: Kujenga maoni thabiti mara nyingi
maoni hasi kuhusu kitu fulani au mtu fulani
(kitengo cha kikundi cha watu) bila ya kuwa na
elimu ya kutosha au uchunguzi wa mambo kwa
kina.
Haki za binadamu: Haki za binadamu ni za watu
wote na hazitofautishwi. Kanuni ya kiulimwengu
ya haki za binadamu ndio msingi wa sheria za
kimataifa za haki za binadamu zilizotiliwa mkazo
katika azimio la kimataifa la haki za binadamu la
mwaka 1948, na zimeelezewa katika mikutano,
223
maazimio na maamuzi mbalimbali ya haki za
binadamu za kimataifa. Haki za binadamu
zinarithiwa kwa wanadamu wote, bila kujali
utaifa, makazi, jinsia, taifa au asili ya kabila, dini,
lugha, au hali nyingine.
Imani: Maoni thabiti na mara nyingi hutokana na
misingi ya kidini na au kanuni za kiutamaduni.
Jinsia: Kazi, haki, majukumu, fursa, mipaka,
matarajio, stahili, na majukumu yanayotambuliwa
kijamii. Jinsi hutofautiana miongoni na ndani ya
tamaduni na inaweza kubadilika baada ya muda
fulani. Majukumu ya jinsia huzingatia, jinsia, umri,
kabila, dini, na sababu zingine za kiutamaduni.
Jinsi: Sifa za kibaiolojia na kimaumbile za
mwanaume na mwanamke ambazo hazibadiliki
bila ya kufanya upasuaji. Mfano wa viashiria vya
jinsi: viungo: uume, uke, matiti, korodani;
maumbile: mzunguko wa hedhi, utengenezwaji
wa shahawa; muundo wa kijenetiki: kromosomu
XX na XY.
224
Kujamiiana: Tabia zote za maisha ya watu
kimapenzi, ikiwemo fikra, na hisia, shauku, tabia,
na sura.
Maambukizi yanayoenezwa kwa ngono: Kundi la
maambukizi ambalo mara nyingi huenezwa kwa
njia ya mwingiliano wa mapenzi yasiyo salama na
mtu mwenye maambukizi.
Madaraka: Uwezo wa kufanya jambo fulani
pamoja na kusimamia na kuwashawishi watu
wengine na matendo yao. Madaraka yanaweza
kutumiwa kwa njia chanya na hasi pia.
Makundi maalumu: Watu wanaotumia madawa,
malaya, wasenge, watu wa jinsia mbili, madereva
wa masafa marefu, wachimbaji madini,
wafungwa, na watoto wa mitaani ni makundi
maalumu. Makundi maalumu yana uwezo
mdogo sana wa kupata huduma zinazostahili,
pia yana kiwango kikubwa cha hatari ya kupata
na kueneza VVU, na viwango vikubwa vya
kukumbwa na mauti na /au ugonjwa kwenye
225
maeneo yenye magonjwa ya
mlipuko/kuambukiza ukilinganisha na makundi
mengine katika jamii.
Mapenzi kinyume na maumbile: Mapenzi katika
njia ya haja kubwa, bila kujali jinsi za washiriki.
Neno hili hutumiwa vibaya kwa kuchanganywa
na ubakaji, ambayo hushindwa kutofautisha
mapenzi ya lazima bila ya ridhaa. Mapenzi
kinyume na maumbile ni jinai pale tu inapokuwa
imelazimishwa.
Mapenzi salama: Hujulikana pia kama “mapenzi
yenye kinga,” humaanisha kupunguza hatari za
maabmbukizi au mimba, mara nyingi kwa
kufanya mapenzi kwa kutumia kondomu ya kike
au kiume au kwa kutafuta njia mbadala za
ushirikiano wa mapenzi.
Mateso: Adhabu kali za kimwili au mateso kiakili
yaliyofanywa chini ya mamlaka ya sheria.
Haijumuishi maumivu au mateso yanayotokana
na, asili, au matukio ya vizuizi kisheria.Ubakaji wa
226
wafungwa umetambuliwa kama mfumo wa
mateso na kitengo maalumu cha umoja wa
mataifa kinachoshughulikia mateso. Hii ni kesi
bila kujali kitendo kimefanywa na mfungwa au
mfanyakazi wa magereza. Matendo mepesi ya
unyanyasaji wa kijinsi yanaweza kujumuisha,
ukatili, unyama, au kuwatendea vibaya. Kamati ya
umoja wa mataifa inayoshughulikia mateso
wakati wote imekuwa ikipambana na ukatili wa
kijinsi dhidi ya wafungwa na imetoa wito kwa
serikali kuchukua hatua thabiti kushughulikia
jambo hili.
Mila: Mfumo au mpangilio wa tabia
unaokubalika na kuchukuliwa kuwa ni “jambo la
kawaida” katika jamii au ndani ya kikundi kwenye
jamii.
Mitazamo: Maoni, mawazo na hisia za mtu
kuhusu kitu au jambo fulani.
Sera: Mpango, au mfumo wa utendaji wa serikali,
chama cha siasa, au biashara uliokusudiwa
227
kushawishi na kufikia maamuzi, matendo, na
mambo mengine, kama vile sera za serikali
kwenye elimu, afya (ikiwemo VVU), au usawa wa
jinsi, sera ya kampuni kuhusu ajira na mafunzo
au rasilimali watu/wafanyakazi.
Ridhaa: Mmakubaliano ya hiari bila ya matumizi
ya nguvu. Hakuna ridha pale ambapo mkosaji
anatumia vibaya nafasi ya madaraka kumfanya
mhanga “kukubali” kitendo cha mapenzi. Hakuna
ridhaa huru ikiwa kulihusisha, ulaghai,
udanganyifu na ujanja. Sera zina malengo ya
jumla na malengo maalumu na taratibu
zinazoweka mfumo au njia za utendaji
zilizochaguliwa miongoni mwa njia nyingine kwa
kuzingatia mazingira fulani ili kutoa mwongozo
na kutambua maamuzi ya sasa na ya baadaye.
Sheria: Mifumo ya usimamizi, na mbinu za
kurekebisha maovu zinaweza kutungwa na
chombo chenye mamlaka; sheria hujenga
muundo wa siasa, uchumi na historia ya nchi kwa
ujumla kwa kufanya kazi kama msuluhishi wa
228
mahusiano kati ya watu. Zinatungwa na
husimamiwa na katiba za nchi na zina mfumo au
seti ya kanuni zilizotungwa na serikali za miji,
taifa, au nchi ambazo husimamiwa na taasisi za
kijamii kuongoza mienendo. Sheria zilizotungwa
na serikali hutumika kutoa mwongozo wa namna
ambavyo jamii zinapaswa kuwa, kama vile, sheria
zinazokataza kuendesha huku ukiwa umelewa,
wizi, kuua, kutumia madawa, au kumiliki bunduki.
Ubaguzi: Huelezewa kuwa huenda ikajumuisha
yote mawili mtazamo hasi au tabia fulani au
kitendo. Mara nyingi huelezewa kama tofauti
inayotengenezwa kuhusu mtu inayosabaisha mtu
huyu kutendewa isivyofaa pasipo na haki kwa
misingi ya uhusika wake ama kuhisiwa kuhusika
katika kundi fulani. Kwa mfano, unyanyapaa
unaweza kusababisha madhara na ubaguzi moja
kwa moja kwa mtu ambaye kweli, au anahisiwa
tu kuwa na maambukizi ya VVU, na makundi
katika jamii na watu wanaoshirikiana nao katika
jamii.
229
Ubakaji: Kitendo chochote cha upenyezaji bila ya
ridhaa kwenye uke, njia ya haja kubwa, au
mdomoni. Neno hili halibagui jinsi, wote
mwanamke na mwanaume wanaweza kubakwa.
Uenevu: Kwa kawaida hutolewa kama asilimia,
kama vile, uenevu wa VVU ni jamii yenye
maambukizi ya VVU katika kipindi fulani.
Ukatili: Shirika la afya duniani linaelezea ukatili
kama ni “matumizi ya nguvu au madaraka kwa
makusudi, kutishia au kufanya kweli, dhidi ya mtu
mwenyewe, mtu mwingine, au dhidi ya kikundi
au jamii ambapo kunaweza kupelekea
uwezekano mkubwa wa majeraha, kifo, madhara
kisaikolojia, maendeleo mabaya, au unyimaji.”
Neno” matumizi ya kukusudia” ni kiungo
muhimu ambacho kinatofautisha ukatili na
majeraha au madhara ambayo hayakukusudiwa.
Ukatili kimwili: Matumizi ya nguvu kwa kukusudia
wenye nia ya kusababisha kifo, ulemavu,
mejeraha, au madhara mengine. Vitendo vya
230
ukatili wa kimwili ni pamoja na kukwaruza,
kusukuma, kutupa, kukwida, kupiga, kukaba,
kutikisa, kupiga kofi, kupiga ngumi, kuchoma, na
matumizi ya silaha, vizuizi, au kutumia ukubwa
wa mwili wa mtu au nguvu dhidi ya mwingine.
Ukatili wa kijinsia: Kudhuru kimwili, kimapenzi, au
kisaikolojia kwa mwanaume au mwanamke
inayomlenga mtu kwa misingi ya jinsi yake.
Ukosefu wa usawa wa kimamlaka kati ya
wanaume na wanawake unachangia kwa kiasi
kikubwa ukatili wa kijinsia.Ukatili wa kijinsia
unalenga kudumisha ukosefu wa usawa wa
kijinsia na/au kusisitiza wajibu wa kimila wa jinsia
kwa wanaume na wanawake.
Ukatili wa kimapenzi: Matumizi ya nguvu
kumlazimisha mtu kushiriki tendo la kujamiiana
kinyume cha ridhaa yake, jaribio au kukamilisha
kitendo bila ya ridhaa au uelewa wake, au
mwingiliano mbaya wa kimapenzi. Vitendo vya
ukatili wa kimapenzi ni pamoja na usumbufu
kimapenzi, ubakaji, jaribio la ubakaji, ubakaji
231
ndani ya ndoa, unyonyaji, unyanyasaji wa watoto
kimapenzi/ngono, vitendo vya mapenzi (bila
upenyezaji) umalaya wa kulazimishwa, umalaya
kwa watoto, na biashara ya mapenzi.
Unyanyapaa: Mtazamo wa kijamii kuwa mtu au
kikundi hakifai au ni cha hali ya chini.
Unyanyapaa unaweza kutokana na sifa za
kimwili, kama vile, dalili za ugonjwa
zinazoonekana, au kutokana na mtazamo hasi
unaoelekezwa kwenye kikundi fulani cha watu au
mtu.
Unyanyasaji: Matumizi ya kitu au kumtendea mtu
isivyostahili, kwa kumdhuru, au kinyume cha
sheria.
Unyanyasaji wa kijinsi: Aina yoyote ya
mwingiliano wa kimapenzi isiyotakiwa kama vile,
kulazimisha busu, kulazimisha, ulawiti, umalaya,
au upekuzi mbaya. Unyanyasaji wa kijinsia
huendekezwa na shauku ya kutumia mabavu,
232
amri, na utawala-si mapenzi au tamaa. Mkosaji
anaweza kutumia nguvu au vitisho.
Usiri: Makubaliano au uwakilishi unaoweka wazi
kwamba taarifa hazitatolewa. Kuwa na uwezo wa
kuzungumza kwa usiri ni muhimu kwa wahanga
wengi wa unyanyasaji wa kijinsia, na mara nyingi
panakuwa hakuna usiri kwa waathirika.
Utamaduni: Imani, desturi, na mzoea ya jamii au
kikundi ndani ya jamii (kama vile utamaduni wa
vijana) na tabia za jamii zilizopatwa.
Wakala wa mabadiliko: Tukio, shirika, vifaa, au,
mara nyingi, mtu anayetenda kama kichocheo
cha mabadiliko.
233
MIREJEO
AVERT. 2017. “HIV and AIDS in Tanzania.”
http://www.avert.org/professionals/hiv-around-
world/sub-saharan-africa/tanzania.
Das, Pamela, and Richard Horton. 2016. “On
Both Sides of the Prison Walls—Prisoners and
HIV.” The Lancet 388 (10049): 1032–33.
doi:10.1016/S0140-6736(16)30892-3.
Dennehy, Kathleen M., and Kelly A. Nantel. 2006.
“Improving Prison Safety: Breaking the Code of
Silence.” Washington University Journal of Law &
Policy 22: 175–185.
http://openscholarship.wustl.edu/law_journal_law
_policy/vol22/iss1/14.
International Organization for Migration (IOM).
2016. “Fighting Tuberculosis in Tanzania,” April
15, 2016, Tanzania: Migration for the Benefit of
All [website]. https://tanzania.iom.int/press-
releases/fighting-tuberculosis-tanzania.
234
Joint United Nations Programme on HIV/AIDS
(UNAIDS). 2014a. The Gap Report.
http://www.unaids.org/sites/default/files/media_a
sset/UNAIDS_Gap_report_en.pdf
Joint United Nations Programme on HIV/AIDS
(UNAIDS). 2014b. On the Fast Track to End AIDS:
UNAIDS 2016–2021. Geneva, Switzerland:
UNAIDS.
http://www.unaids.org/sites/default/files/media_a
sset/20151027_UNAIDS_PCB37_15_18_EN_rev1.p
df.
Joint United Nations Programme on HIV/AIDS
(UNAIDS). 2016. Global AIDS Update 2016.
Geneva, Switzerland: UNAIDS.
http://www.unaids.org/sites/default/files/media_a
sset/global-AIDS-update-2016_en.pdf.
Krug, Etienne G., Linda L. Dahlberg, James A.
Mercy, Anthony B. Zwi, and Rafael Lozano.
World Report on Violence and Health. Geneva,
Switzerland: World Health Organization, 2002.
235
http://www.who.int/violence_injury_prevention/vi
olence/world_report/en.
Martin, Keith L. “Cracking the Code of Silence.”
Prisonerlife.com. July 6, 2002.
https://www.prearesourcecenter.org/sites/default
/files/library/crackingthecodeofsilence7-6-
2002.pdf.
Mills Edward J., Nathan Ford, and Peter
Mugyenyi. 2009. “Expanding HIV Care in Africa:
Making Men Matter.” The Lancet 374 (9686):
275–276. doi:10.1016/S0140-6736(09)61348-9.
Office of the United Nations High Commissioner
for Human Rights (OHCHR). 2005. Human Rights
and Prisons: A Compilation of International
Human Rights Instruments Concerning the
Administration of Justice. Professional Training
Series No. 11 Add.1.
https://www.un.org/ruleoflaw/files/training11Add
1en.pdf.
Smith, Brenda V., and Jaime M. Yarussi. 2007.
Breaking the Code of Silence: Correction
236
Officers' Handbook on Identifying and
Addressing Sexual Misconduct. Washington, DC:
NIC/WCL Project on Addressing Prison Rape and
National Institute of Corrections.
https://s3.amazonaws.com/static.nicic.gov/Librar
y/022473.pdf.
Sonke Gender Justice Network and MenEngage.
2012. Addressing HIV and Sexual Violence in
Correctional Services Facilities: A Guide for
Working with Members of the Correctional
Department of Correctional Services.
http://detentionjusticeforum.org.za/wp-
content/uploads/2013/09/Sonke-and-Just-
Detention-International-Addressing-HIV-and-
Sexual-Violence-in-Correctional-Facilities-Guide-
for-Correctional-Staff.pdf.
Sonke Gender Justice and MenEngage. 2017.
“Men and HIV in the ESA Region.” Sonke Gender
Justice. Accessed January 25.
http://www.genderjustice.org.za/publication/men
-hiv-esa-region/.
237