Dkt. John Pombe Joseph MAGUFULI - TANESCO

6
TANESCO MITANDAONI AGOSTI 2020 1 “Tunayaangaza maisha yako” Dkt. John Pombe Joseph MAGUFULI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MIAKA 5 Mafanikio Sekta ya Nishati ya Umeme Upanuzi wa kituo cha kuzalisha umeme kwa gesi Kinyerezi I megawati 185 Kituo cha kuzalisha umeme kwa gesi Kinyerezi II megawati 240 Mradi wa kufua umeme kwa maji Julius Nyerere megawati 2115 2 1 3 1 Miradi ya kufua umeme Julius Nyerere Mw 2115, Kinyerezi Extension I 85, Kinyerezi II Mw 240 Miradi ya njia ya kusafirisha umeme Iringa - Shinyanga, Makambako - Songea, Lindi - Mtwara Umeme Vijijini 2 3 03 Toleo NA. Jarida la Mitandaoni

Transcript of Dkt. John Pombe Joseph MAGUFULI - TANESCO

Page 1: Dkt. John Pombe Joseph MAGUFULI - TANESCO

TANESCO MITANDAONI AGOSTI 2020 1

“Tunayaangaza maisha yako”

Dkt. John Pombe Joseph

MAGUFULIRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MIAKA 5

Mafanikio Sekta ya Nishati ya Umeme

Upanuzi wa kituo cha kuzalisha umeme kwa gesi Kinyerezi I megawati 185

Kituo cha kuzalisha umeme kwa gesi Kinyerezi II megawati 240

Mradi wa kufua umeme kwa maji Julius Nyerere megawati 2115

2

1

3

1 Miradi ya kufua umeme Julius Nyerere Mw 2115, Kinyerezi Extension I 85, Kinyerezi II Mw 240

Miradi ya njia ya kusafirisha umeme Iringa - Shinyanga, Makambako - Songea, Lindi - Mtwara

Umeme Vijijini

2

3

03

Toleo NA.

Jarida la Mitandaoni

Page 2: Dkt. John Pombe Joseph MAGUFULI - TANESCO

TANESCO MITANDAONI AGOSTI 2020 2

“Tunayaangaza maisha yako”

GENERATION  2115 MW

JULIUS NYERERE HYDROPOWER PROJECT“Tunayaangaza maisha yako”

Wataalamu wakiendelea na kazi ya kuchoronga mwamba kwa kutumia mashine aina ya Tunnel Boring Machine (TBM) inayotumia umeme.

Miaka Mitano ya Rais Magufuli kutimiza ndoto ya Mwl. Nyerere

#JN-HPP Mw 2115|

Tumeshuhudia katika kipindi cha miaka mitano cha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt.

John Pombe Magufuli ndoto ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere ya kuwa na umeme katika mto Rufiji inakwenda kutimia kwa vitendo

Ni zaidi ya miaka arobaini tangu kufanyika kwa upembuzi yakinifu kuhusiana na ujenzi wa mradi huu wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) utakaozalisha megawati zipatazo 2115.

Akihutubia katika hafla ya uwekaji saini kati ya TANESCO na Kampuni ya Arab Contractors ikiwa na ubia na Kampuni ya Elsewedy Electric zote za nchini Misri Ikulu Jijini Dar es Salaam Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, alisema mradi wa JNHPP ulianza tangu enzi za Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K Nyerere miaka ya 70, ambapo upembuzi yakinifu ulifanyika kati ya mwaka 1976 na 1980.

Mheshimiwa Rais aliweka jiwe la msingi Julai 26, 2019 kuashiria kuanza kwa ujenzi wa mradi ambapo utekelezaji upo katika hatua mbalimbali.

Ujenzi wa njia ya kuchepusha maji (Diversion Tunnel) uchimbaji wake umekamilika kazi inayofanyika hivi sasa ni ya kuimarisha miamba kwa uwekaji wa zege na kusuka nondo.

Kazi ya uwekaji zege awamu ya kwanza katika sakafu kwenye njia ya kuchepusha maji imefika mita 269 kati ya mita 703.76.

Aidha, kazi ya ujenzi wa eneo la lango (Water Intake) la kuingilia maji kwenda kwenye mitambo ya kufua umeme inaendelea na unatarajiwa kukamilika Februari 2022.

Mhandisi Dismas Mbote, Mhandisi wa ujenzi njia za maji pamoja na Bwawa kwenye Mradi wa Julius Nyerere amesema utekelezaji wa njia hiyo ulianza Mwezi Oktoba 2019.

Aliongeza kuwa kazi ya uchimbaji wa lango imekamilika kwa kuchimbwa kina cha mita 53 ambapo hivi sasa kazi inayoendelea ni uondoaji wa kifusi na uchimbaji wa mahandaki matatu yatakayotumika kupitisha maji kwenda kwenye mitambo ya kufua umeme.

Njia ya kuchepusha maji ya kwanza itakuwa na urefu wa mita 350, ya pili mita 410 na la tano mita 570 hadi kwenye mitambo ya kufua umeme.

Aidha, utekelezaji wa eneo la kufua umeme (Power house) hatua ya uchimaji ipo mita 64 kutoka usawa wa bahari, kazi inayoendelea ni ujenzi wa kingo za bwawa kuzuia maji ili kuendelea na uchimbaji hadi mita 39 juu ya usawa wa bahari.

Inaendelea Uk 3

Leo tunaposaini mkataba huu ni zaidi ya miaka arobaini, tunatekeleza kwa kutumia fedha za ndani kiasi cha shilingi Trilioni 6.558 ambazo ni za walipa kodi ”, alisema Dkt. Magufuli

Page 3: Dkt. John Pombe Joseph MAGUFULI - TANESCO

TANESCO MITANDAONI AGOSTI 2020 3

“Tunayaangaza maisha yako”

JNHPP MW 2115| ujenzi Bwawa la kufua umeme kukamilika mwanzoni mwa 2022

Kazi ya ujenzi wa bwawa la kufua umeme ukianza mwezi Oktoba 2019 katika kipengele cha uchimbaji eneo la bwawa

na maandalizi mengine.Akiongelea hatua mbalimbali za utekelezaji

upande wa ujenzi wa bwawa Mhandisi Victor Kutinah ambaye Mhandisi Bwawa alisema ujenzi wa bwawa unatatajiwa kukamilika mwanzoni mwa mwaka 2022.

Aliongeza maeneo mengine ya awali katika ujenzi wa bwawa ambayo yamekamilka ni gallery na uchimbaji wa njia ya kuchepusha maji.

Aliongeza, ili kujenga bwawa maji yanatakiwa kuchepushwa ambapo uchimbaji wa mahandaki (Diversional tunnel) ya kuchepushia maji umekamilika kwa asilimia 100 kazi inayoendelea ni kuimarisha miamba.

Katika uimarishaji wa miamba inasukwa nondo na kumwagwa zege.

Aidha yanaendelea maandalizi ya ujenzi kituo cha kupokea na kusambaza umeme (Switch yard) ambapo utafiti wa udongo na miamba kwenye eneo hilo umeshafanyika lakini pia eneo limeshasafishwa kwa ajili ya ujenzi kuanza.

Kituo cha kupokea na kusambaza umeme kunatarajiwa kukamilika mwezi Mei 2022.

Hakuna kulala, Wataalamu na mafundi wakiendelea na kazi ya kusuka nondo kwenye njia ya mchepusho (tunnel) kwa ajili ya kumwaga zege la kuimarisha miamba kabla ya zoezi la kuchepusha maji.

Gallery ni handaki ambalo litatumika kwa ajili ya ukaguzi wa bwawa ikiwa ni pamoja na kuondoa maji yanayozidi ili kulinda kuta za bwawa ”,Mhandisi Kutinah.

#JN-HPP Mw 2115|

Page 4: Dkt. John Pombe Joseph MAGUFULI - TANESCO

TANESCO MITANDAONI AGOSTI 2020 4

“Tunayaangaza maisha yako”

Katika kuhakikisha unafanyika uwekezaji mkubwa katika Sekta ya Nishati ya Umeme nchini, mbali ya kuwekeza

katika miradi ya kufua umeme kwa kutumia gesi, lakini pia imeendelea na uwekezaji wa miradi ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi.

Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa maji wa Kinyerezi II ni mradi wa aina yake nchini kwani inatumia Teknolojia mpya na ya kwanza nchini yenye hatua mbili za kufua umeme (Com-bined cycle).

Kinyerezi II inazalisha umeme kwa kutumia gesi na mvuke.

Aprili 3, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alikizindua kituo cha Kinyerezi II na kuwashukuru Wafanyakazi wa TANESCO kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuhakikisha huduma ya umeme inapatikana.

Mradi wa Kinyerezi II Megawati 240 ulibuniwa ili kuongeza uwezo wa kufua umeme kutokana na gesi asilia na hivyo kuimarisha na kuongeza uwezo wa gridi ya Taifa katika kusafirisha na kusambaza umeme nchini.

Katika hatua nyingine Serikali imeendelea na utekelezaji wa ujenzi wa Kinyerezi I Extension ambayo itazalisha megawati 180.

Mradi wa Kinyerezi I Extension una hatua tatu ambazo ni upanuzi wa kituo, kuunganisha mradi wa Kinyerezi I na Kinyerezi I Extention pamoja na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme Gongo la Mboto.

Takribani asilimia 84 ya mradi wa Kinyerezi I Extension imekamilika na mradi unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Desemba mwaka huu.

Eneo la Kinyerezi linamiradi mikubwa minne ambayo ni mradi wa Kinyerezi I, Kinyerezi II, Kinyerezi I Extension ambao upo katika hatua ya utekelezaji.

Miradi mingine ni Kinyerezi III ambao upo kwenye hatua ya upembuzi yakinifu na Kinyerezi IV.

Vituo vya Kuzalisha umeme kwa kutumia gesi vinachangia megawati 892 kwenye gridi ya Taifa ambayo ni sawa na asilimia 51.54.

Aidha, katika kuhakikisha TANESCO inajiendesha Serikali ilizima vituo vya kuzalisha umeme vya IPTL, AGRECCO na SYMBION, kuzimwa kwa mitambo hiyo Serikali imeokoa kiasi cha shilingi Bilioni 719 kwa mwaka.

Kinyerezi I Extension/Kinyerezi II

Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Kituo

cha Kuzalisha Umeme cha Kinyerezi II kabla ya kukizindua.

Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akizindua Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa kutumia gesi cha Kinyerezi II.

Mnahangaika kwa kweli kwa kazi nzuri, mimi nafikiri Mhe. Waziri na Bodi ya Wakurugenzi mkipata mabakibaki ya kuwaongeza mshahara msisite, mimi sina tatizo na Wafanyakazi hawa wamefanya kazi nzuri”, Dkt. John Pombe Magufuli

Aprili 3, 2018, Kinyerezi - Dar es Salaam

Mhandisi Stephen Manda, akitoa maelezo ya Mradi wa Kinyerezi II kwa Waziri wa

Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani (kulia) kabla ya kuwasili kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuzindua Kituo cha Kinyerezi II. Wa

kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO Dkt. Alexander

Kyaruzi na Mkurugenzi Mtendaji TANESCO Dkt. Tito Mwinuka.

KINYEREZI

Page 5: Dkt. John Pombe Joseph MAGUFULI - TANESCO

TANESCO MITANDAONI AGOSTI 2020 5

“Tunayaangaza maisha yako”

Katika kipindi cha miaka mitano miradi mbalimbali kusafirisha umeme imetekelezwa, kutekelezwa kwa miradi

hiyo kumeimarisha hali ya upatikanaji wa umeme pamoja na kuunganisha baadhi ya Mikoa na grid ya taifa hivyo kuondokana na umeme wa mafuta.

Ujenzi wa njia hizo za kusafirisha umeme Serikali imeokoa kiasi cha shilingi Bilioni 15.3 kwa mwaka kwa kuunganisha Mikoa ya Lindi, Mtwara, Njombe na Ruvuma na gridi ya Taifa na kuzima mitambo ya kutumia mafuta kwenye Mikoa hiyo.

Miradi mikubwa ya kusafirisha umeme ambayo imekamilika ni Njia za Kusafirisha umeme za Iringa - Shinyanga, Makambako - Songea na Lindi - Mtwara.

Aidha, miradi mingine ya kusafirisha umeme ipo katika hatua ya ujenzi, Mradi wa Kusafirisha umeme kutoka Singida – Arusha – Namanga kV 400, Mradi wa Njia ya kusafirisha Umeme kutoka Bulyanhulu – Geita kV 220.

Mwingine ni Mradi wa kuunganisha Mikoa ya Kigoma na Katavi katika Gridi ya Taifa ambayo Oktoba 11, 2019 Mheshimiwa

Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli aliweka jiwe la msingi.

Ujenzi wa njia hizi za umeme umekua ukienda sambamba na zoezi la umeme Vijijini na kwa mujibu wa Waziri wa Nishati hadi kufikia mwezi Aprili 2020.

Umeme Vijijini

Ongezeko la vijiji vilivyounganishwa umeme kutoka Vijiji 2018 kwa mwaka 2015 hadi kufikia jumla ya Vijiji 9112 vilivyounganishwa umeme hadi kufikia mwezi Aprili 2020 sawa na ongezeko la vijiji 7,094.

Aidha, hadi kufikia mwezi Aprili, 2020 jumla ya Wilaya na Halmashauri 36 za Tanzania Bara vijiji vyake vyote vimefikiwa na ujenzi wa miundombinu ya umeme.

Vitongoji na maeneo ambayo hayajafikiwa na miundombinu ya umeme yataendelea kupelekewa umeme kuanzia mwezi Juni, 2020.

katika kipindi cha mwezi Januari, 2016 hadi Machi 2020, jumla ya Taasisi 11,164 zimeunganishiwa umeme ikilinganishwa na Taasisi 4,036 zilizokuwa zimeunganishiwa kufikia mwezi Desemba, 2015.

Ongezeko hilo linafanya jumla ya Taasisi zilizounganishiwa umeme kufikia 15,200, kwa mwaka wa fedha 2020/21 jumla ya shilingi Bilioni 297.43 zimetengwa kwa ajili ya kusambaza umeme Vijijini.

Kuongezeka kwa idadi ya Watumiaji umeme “Energy access” kutoka asilimia 35 hadi asilimia 85, hali hii imechangizwa sana na ushushaji wa gharama za kuunganishwa umeme kutoka sh. 177,000/= hadi sh. 27,000/= tu.

Njia za Kusafirisha Umeme

USAFIRISHAJI UMEME

BODI YA UHARIRI:

Mwenyekiti:Dkt. Tito E. MwinukaMkurugenzi Mtendaji TANESCO Mhariri Mkuu: Johary KachwambaMeneja Uhusiano

Wachangiaji:Grace KisyombeYasini SilayoSalama KasamaluSamia Chande

Msanifu wa kurasa:Henry Kilasila

Page 6: Dkt. John Pombe Joseph MAGUFULI - TANESCO

TANESCO MITANDAONI AGOSTI 2020 6

“Tunayaangaza maisha yako”

TANESCO kukuza Uchumi Mikoa ya Katavi na KigomaKutokana na Serikali kuwaamini

wataalamu wa ndani (Watanzania) katika kutekeleza na kusimamia

Miradi mikubwa na ya kimkakati, TANESCO imedhamiria kuinua uchumi wa Mikoa ya Magharibi kwa kuhakikisha inapata umeme wa kutosha, uhakika na gharama nafuu kwa kutumia Wataalamu kutoka TANESCO.

Wataalamu wa kitanzania wameonesha uwezo kwa kusimamia na kutekeleza miradi mbalimbali ukiwemo Mradi wa kimkakati wa kufua umeme kwa maji wa Julius Nyerere Mw 2115.

Safari ya kuhakikisha Mikoa ya Katavi na Kigoma ambayo ipo Kanda ya Magharibi inapata umeme wa uhakika ilianza Oktoba 11, 2019 baada ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuweka jiwe la msingi kuashiria kuanza kwa utekelezaji wa mradi wa upelekaji umeme wa gridi ya Taifa Mikoa ya Kigoma na Katavi.

Kama ilivyo dira ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ya kuiona Tanzania ni nchi ya Viwanda, TANESCO inaiona ni dira ambayo itatukomboa Watanzania wote kwa uwepo wa umeme mwingi na wa kutosha.

Kutokana na ukweli kwamba nishati ya umeme ni uchumi na ni kichocheo cha maendeleo, Wananchi wanatakiwa kuchangamkia fursa ya kufika kwa umeme wa gridi ya Taifa katika Mikoa ya Katavi na Kigoma kwa kufungua biashara ambazo zitawaongezea vipato vyao.

Kwa kutambua umuhimu wa nishati ya umeme katika kukuza vipato vya Watanzania Bodi ya Wakurugenzi TANESCO, imefanya ziara ya kikazi lengo likiwa kukagua miradi ya kusafirisha umeme Mikoa ya Katavi na Kigoma lakini pia na vituo vya kupoza na kusambaza umeme.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO Dkt. Alexander Kyaruzi alisema lengo la ziara ya Bodi ni kutaka kujiridhisha uhitaji mkubwa wa umeme kwa Mikoa ya Katavi na Kigoma hivyo Bodi kuweza kutoa uelekeo.

“Bodi imefika kuona mahitaji ya umeme

kwenye Mikoa hii na kutafuta suluhu ya haraka”, alisema Dkt. Kyaruzi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Katavi Mhe. Juma Homera akiwa kwenye kikao na Bodi ya Wakurugenzi TANESCO aliwaomba kuhakikisha umeme wa gridi unafika Mkoa wa Katavi kwa haraka kutokana na wawekezaji wengi kuonesha nia ya kufungua viwanda, pamoja na upatikanaji wa soko la chakula Kongo DRC.

Alisema, tayari wawekezaj i wengi wameonesha nia akitolea mfano viwanda vya sukari, maji, kuchakata mpunga na mahindi lakini pia ujenzi wa Bandari kubwa ya Kalema.

“Pia kiwanda cha kuchakata Pamba, uwekezaji wa krasha, ujenzi wa kiwanda cha nguo na ujenzi wa Reli kwenda ziwani Kalema”,

alisema Mhe. Homera.Miji ya Katavi na Kigoma ni miongoni

mwa miji inayopata maendeleo kwa kasi hivyo uhitaji wa umeme wa gridi kwenye Mikoa hiyo ni mkubwa.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye ameipongeza Bodi na Menejimenti ya TANESCO, alisema kupatikana kwa umeme wa uhakika Mkoa wa Kigoma kutawawezesha Wananchi kukuza vipato vyao.

Mhandisi Sana Idindili ambaye ni Meneja Mwandamizi Kanda ya Magharibi akitoa taarifa kwa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO alisema Mkoa wa Katavi unapata huduma ya umeme kupitia vyanzo viwili vya jenereta zinazo tumia mafuta kufua umeme katika Wilaya za Mpanda na Mlele na umeme wa gridi ya Taifa kutokea nchini Zambia kupitia Mkoa Rukwa.

Gharama za uzalishaji umeme kwa Mkoa wa Katavi kwa unit moja ni wastani wa shilingi 750.

Aliongeza kuwa, kwa upande wa Mkoa wa Kigoma unapata huduma ya umeme kupitia vyanzo vitatu ambavyo ni Kigoma mjini, Kasulu na Kibondo na vituo vyote vinazalisha umeme kupitia mafuta. Gharama ya kuzalisha umeme kwa wastani unit moja ni shilingi 649.4.

Umeme utakao patikana kupitia gridi ya Taifa ni wa uhakika na unapatikana kupitia vyanzo mbalimbali ikiwemo maji na gesi.

Kampuni Tanzu ya TANESCO ya ETDCO

ndio itakayohusika na ujenzi wa Njia Kuu ya Kusafirisha kutoka Tabora hadi Katavi na Kutoka Tabora hadi Kigoma.

Wataalamu wa TANESCO watahusika na ujenzi wa vituo vya kupoza umeme vya Ipole, Inyonga, Mpanda, Urambo na Nguruka.

GRIDI KUFIKA MIKOA YA KATAVI/KIGOMA

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Juma Homera akiwa kwenye kikao na Bodi ya Wakurugenzi TANESCO .