DIBAJI - hakikazi.org · kadhalika, mara nyingi hakuna maelewano ya awali baina ya wakusanyaji...

24

Transcript of DIBAJI - hakikazi.org · kadhalika, mara nyingi hakuna maelewano ya awali baina ya wakusanyaji...

Page 1: DIBAJI - hakikazi.org · kadhalika, mara nyingi hakuna maelewano ya awali baina ya wakusanyaji taarifa hizo na wale wanaotarajiwa kuzitumia. Hii inamaanisha kwamba bado kuna fursa
Page 2: DIBAJI - hakikazi.org · kadhalika, mara nyingi hakuna maelewano ya awali baina ya wakusanyaji taarifa hizo na wale wanaotarajiwa kuzitumia. Hii inamaanisha kwamba bado kuna fursa
Page 3: DIBAJI - hakikazi.org · kadhalika, mara nyingi hakuna maelewano ya awali baina ya wakusanyaji taarifa hizo na wale wanaotarajiwa kuzitumia. Hii inamaanisha kwamba bado kuna fursa

DIBAJI

KWA NINI TUNAHITAJI MFUMO WA NAMNA HII? 3

Kwa nini tunahitaji mfumo wa ufuatiliaji umasikini?

Nini maana ya mipango inayozingatia taarifa sahihi na kwa nini ni muhimu?

MUUNDO WA MFUMO HUU UKO VIPI? 5

Nini kilichomo kwenye Mpango Kamambe wa Ufuatiliaji Umasikini?

Ni kwa jinsi gani Mfumo wa Ufuatiliaji Umasikini unaendeshwa?

Nini maana ya Tathmini Shirikishi ya Umaskini?

NI JINSI GANI MFUMO HUU UNAWEZA KUTUMIKA? 8

Je kuna nafasi ya tawala za mikoa na serikali za mitaa kwenye mfumo huu?

Taasisi na jumuiya huru za kiraia zinaweza kuchangia vipi kwenye mfumo huu?

Ni kwa namna gani ninaweza kuingiza taarifa kwenye mfumo huu?

MFUMO HUU UTAGHARIMU KIASI GANI CHA FEDHA? 10

Nani anaugharimia mfumo huu?

Watu maskini watanufaika vipi kutokana na mfumo huu?

NI WAPI NITAPATA TAARIFA ZAIDI KUHUSU JITIHADA ZA KUONDOA UMASIKINI TANZANIA? 11

Ni wapi ninaweza kupata nakala ya Mpango Kamambe wa Ufuatiliaji Umasikini?

Nini matokeo muhimu ya kazi za Mfumo wa Ufuatiliaji Umasikini?

VIAMBATANISHO

Vipengele muhimu vya Mfumo wa Taifa wa Ufuatiliaji Umasikini 14

Muundo wa Kiutawala wa Mfumo wa Ufuatiliaji Umasikini 15

Wajumbe wataalum wa Makundi Manne ya Utendaji wa Kiufundi (TWG) 16

Orodha ya tovuti muhimu 17

Vigezo/viashiria vya kufuatilia umasikini 19

SHUKRANI

Page 4: DIBAJI - hakikazi.org · kadhalika, mara nyingi hakuna maelewano ya awali baina ya wakusanyaji taarifa hizo na wale wanaotarajiwa kuzitumia. Hii inamaanisha kwamba bado kuna fursa

Mkakati wa Kupunguza Umasikini nchini Tanzania (PRSP) ni mkakati wa muda wa kati wa kupunguzaumasikini na ni sehemu ya Mpango wa Kuzifutia Madeni Nchi Masikini (HIPC). Mkakati huu unalengakuifanya Serikali kupunguza matumizi, lakini kuelekeza zaidi nguvu na jitihada zake katika shughulizinazolenga kupunguza umasikini, na kuchukua hatua nyingine mahususi zisizohusu matumizi ya fedhazinazoweza kusaidia katika jitihada hizi za kupunguza umasikini.

Watu wengi walishiriki katika kuuandaa mkakati huu, na wengi zaidi watashiriki katika kuutekeleza nakuufanya ulete matokeo yaliyokusudiwa. Mpango huu unaorodhesha baadhi ya sababu zinazowafanyawatu wawe masikini na kupendekeza njia na hatua kadhaa za kukabiliana nazo. Mkakati wa KupunguzaUmasikini ni tofauti na mipango mingine kwani umeweka malengo yaliyo wazi na bayana na unawatakawananchi washiriki kikamilifu katika utekelezaji wake.

Kuna haja ya haraka ya kujenga uwezo wa watu mbalimbali katika kufuatilia shughuli zilizoanzishwachini ya Mkakati wa Kuondoa Umasikini. Aidha, wananchi wanahitaji kusaidia katika uchambuzi wataarifa mbalimbali zinazokusanywa na kubaini taarifa hizo zinamaanisha nini katika sera nzima yakuondoa umasikini.

Mpango Kamambe wa Kufuatilia Umasikini uliandaliwa hapo mwezi Desemba 2001 ili kuiwezesha Serikaliya Tanzania na wadau wengine kuelewa iwapo mikakati kadhaa ya kuondoa umasikini imekuwa namatokeo yaliyokusudiwa. Mpango huu unabainisha shughuli kadhaa zitakazofanyika katika kipindi chamiaka mitatu ijayo zitakazowezesha kupima kiwango cha umasikini.

Kufuatia kuandaliwa kwa Mpango Kamambe wa Kufuatilia Umasikini, Idara ya Kupunguza Umasikinikatika Ofisi ya Makamu wa Rais, imekuwa ikipokea maswali kadhaa kuhusu mfumo wa ufuatiliajiumasikini. Katika jitihada za kujibu maswali hayo, kijitabu hiki cha mwongozo kiliandaliwa. Zaidi yanakala 20,000 za kijitabu hiki (katika lugha za Kiingereza na Kiswahili) zitasambazwa nchini koteTanzania.

Tunatarajia kuwa kijitabu hiki kitatoa majibu kwa maswali tunayoulizwa mara kwa mara na kwambawahusika mbalimbali watakaopenda kupata taarifa zadi wataweza kuwasiliana nasi. Ni wazi kuwakijitabu hiki si muhtasari wa kina wa mambo yote yaliyomo katika Mpango Kamambe wa KufuatiliaUmasikini. Lengo la kijitabu hiki ni kuwasilisha masuala ya msingi kuhusu namna mfumo huo unavyofanyakazi na hivyo kuibua hamasa ya kutaka taarifa zaidi miongoni mwa watu ambao wangependa kushirikikwa njia moja ama nyingine katika jitihada za kufuatilia matokeo ya shughuli za kuondoa umasikininchini.

____________________________________R. MollelKatibu Mkuu

Ofisi ya Makamu wa Rais

Agosti 2002

Page 5: DIBAJI - hakikazi.org · kadhalika, mara nyingi hakuna maelewano ya awali baina ya wakusanyaji taarifa hizo na wale wanaotarajiwa kuzitumia. Hii inamaanisha kwamba bado kuna fursa

Siyo rahisi sana kuelezea maana ya umasikini kwasababu watu mbalimbali wana uelewa tofauti tofautiwa tatizo hili. Uelewa huo una jumuisha masualambalimbali kama:

• mtu kutokuwa na uhakika wa kupata chakula chakena matibabu;

• mtu kushindwa kumudu gharama za mavazi namakazi bora;

• mtu kukosa nafasi sawa ya kupata elimu bora nahuduma bora za afya, pamoja na na vitu vinginekama vile maji safi na salama, barabara nzuri nahuduma ya kuaminika ya usafiri wa umma;

• mtu kutotendewa haki na wafanyabiashara naviongozi wa ngazi mbalimbal i (kijiji, mitaa ,kikanda, kitaifa na kimataifa);

• mtu kutokuwa na sauti katika mambo yanayohusumaisha yake (kwenye eneo lake, kikanda, kitaifana kimataifa);

• mtu kuwa katika hatari ya kufanywa masikinikutoka na na kuwa katika kundi la watuwanaowekwa pembezoni na kunyimwa haki zao(Mathalan, walemavu, yatima, wazazi wasio nawaume au wake, wazee na watu wanaoishi naVVU/UKIMWI)

Kwa kuwa kuna njia nyingi tofa uti za kuuangaliaumasikini, pia kuna njia nyingi za kujaribu kuupunguza.Njia hizi ni pamoja na:

• kutumia vizuri maliasili zetu na vipaji vilivyopokuzalisha mali, kujipatia kipato na ajira;

• kutilia mkazo na kusaidia maendeleo ya biasharahala li ze nye kule ta ma nufaa (biasha ra ndogondogo, za kati na zile kubwa);

• kuhakikisha kuwa watu wana fursa ya kupatahuduma bora za kijamii na miundombinu;

• kuandaa mazingira bora ili watu wajisikie wakosalama kwenye makazi yao na wanaweza kuziamini

mamlaka zilizopo;

• kuwe ka mipa ngo muafaka namadhubuti ya kuwalinda watu waliokwenye makundi ha tar i za idi nayanayoweza kunyimwa haki zao zakimsingi.

3

Page 6: DIBAJI - hakikazi.org · kadhalika, mara nyingi hakuna maelewano ya awali baina ya wakusanyaji taarifa hizo na wale wanaotarajiwa kuzitumia. Hii inamaanisha kwamba bado kuna fursa

Kwa nini tunauhitaji mfumo huu?

Siyo ra hisi kupunguza uma sikini. Uma sikiniunawa husisha watu wengi, wal io katika nga zimbalimbali kwenye jamii na ambao wanakabiliwa namatatizo tofauti tofauti katika maeneo mbalimbali.Tunahitaji kufanya kazi kwa pamoja ili tusipotezemuda , nguvu na fedha kwa kutokuwa silia na nakukwamishana. Hii inamaa nisha kuwa tuna hita jikujiwekea miundo na taratibu zinazokubalika kwawote. Hii ina maana kuwa tunahitaji kuwa na MFUMOmahsusi.

Watu wengi ta ya ri wana kusa nya ta ari fa muhimukuhusiana na umasikini, lakini mara nyingi hawatumiitaarifa hizi kwa jinsi inavyotakiwa. Kazi nyingi zaukusanyaji wa taarifa hizo siyo rasmi na haziangaliimasuala ya liyopewa kipa umbele kita ifa . Hal ikadhalika, mara nyingi hakuna maelewano ya awaliba ina ya wakusa nya ji ta a rifa hizo na wa lewanaotarajiwa kuzitumia. Hii inamaanisha kwambaba do kuna fursa kubwa ya kubor esha namnatunavyokusanya taarifa hizi na namna tunavyozitumiaili tuweze kubuni na kupanga mipango inayotokana nataarifa sahihi.

Hakuna njia moja pekee ya kupima hali ya umasikiniinayoweza kushughulikia matatizo na njia mbalimbaliza kuyakabili zilizotajwa. Hivyo tutahitaji kutumianjia mbalimbali na kujitahidi kuunganisha matokeo yanjia zote hizo ili tuweze kuweka mipango yetu kwakuzingatia taarifa sahihi.

Tunahitaji MFUMO wa ufuatiliaji hali ya umasikini ilituweze kupanga na kukusanya pamoja taarifa kutokakwenye vyanzo mbalimbali, kuzichambua ili ziwezekutuongoza katika kubuni sera na mipango yetu yakupunguza umasikini. Nyingi ya sera na mipango hiihutengenezwa katika ngazi ya kitaifa. Hata hivyo,kupitia Mpango wa Mabadiliko wa Serikali za Mitaamamlaka za mikoa na wilaya zinapewa madaraka nawajibu zaidi wa kubuni sera na mipango yao yakupunguza umasikini.

Mfumo wa ufuatiliaji uma sikini utakusanya taarifakutoka kwenye vyanzo vikuu vitatu:

• Taarifa z inazotokana na mfumo za utawalazitakuwa zikikusanywa na serikali za mitaa, mikoana idara za serikali kuu (mfano taarifa kuhusu;“idadi ya wanafunzi wanaokatisha masomo yae limu ya msingi” kutoka mamlaka za elimu;“kiwango cha vifo vya watoto wachanga” kutokamamlaka za afya na kadhalika);

• Uc hunguzi rasmi uta fanywa na Kitengo chaTakwimu cha Taifa (kwa mfano, Sensa ya Watu naMakazi, Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya,Utafiti juu ya Idadi ya Watu na Afya, Utafiti wa Haliya Ajira na Nguvu Kazi, na Utafiti kuhusu Hali yaKilimo);

• Tafiti maalum zitafanywa na watafiti mbalimbaliwanaojitegemea. Tafiti hizi zitawahusisha watu wakawaida badala ya kuwatumia tu kama vyanzo vyataarifa. Matokeo ya tafiti hizi yatasaidia kufafanuasababu zita kazokuwa zinae le ze a ma badilikoya ta kayokuwa ya me jitoke za ka tika ta kwimukutoka katika vyanzo viwili vya mwanzo.

Pa moja na kukusa nya ta ari fa hizi , mfumo waufuatiliaji umasikini, utawasaidia na kuwahamasishawatu wa kawaida na viongozi kwenye maeneo yotekuchambua, kutathmini na kuzisambaza taarifa hizi.Pia mfumo huu utawahimiza wahusika wote kutumiataarifa sahihi zitakazokusanywa katika mfumo huukatika kupa nga ser a na mipa ngo madhubuti nakufanya ufuatiliaji na tathmini nzuri zaidi ya sera namipango hiyo.

4

Page 7: DIBAJI - hakikazi.org · kadhalika, mara nyingi hakuna maelewano ya awali baina ya wakusanyaji taarifa hizo na wale wanaotarajiwa kuzitumia. Hii inamaanisha kwamba bado kuna fursa

Nini maana ya upangaji unaozingatia taarifasahihi na kwanini upangaji huo ni muhimu?

Watu hupanga mipango kwa kuzingatia jins iwanavyoielewa dunia. Jinsi gani wanavyoielewa dunia,hutegemea nini wanakichofa ha mu, kwa kuzingatiatakwimu a u taa rifa wa lizona zo. Ikiwa wa tuha wa faha mu mambo me ngi na ikiwa kilewa na chokifaha mu s i sahihi, ba si ue le wa wao namipa ngo wata kayoipa nga kutoka na na ue lewa huohaitakuwa mizuri.

Ukusanyaji wa taa rifa ambao ha uja ra tibiwa nakupangwa vyema, ni bora kuliko kutokukusanya aukutafuta taarifa kabisa. Lakini hali inaweza kuwa borazaidi iwapo tutakuwa na mfumo uliandaliwa vizuri waukusanyaji wa taarifa na ambao unajumuisha taarifanyingi na za aina nyingi kwa kadri itakavyowezekana.Kwa kuutumia vye ma mfumo huo tutaweza kutoamaamuzi bora zaidi, kubuni sera nzuri zaidi na kutumiaraslimali zetu vyema zaidi katika kutatua matatizoyanayohitaji utatuzi wa haraka.

Upangaji sera kwa kuzingatia taarifa au takwimu sahihiutaihimiza na kuisaidia serikali na watumiaji wenginewa takwimu au taarifa hizo katika:

• kukusanya na kuchambua taarifa sahihi na baadayekuc ha pisha matoke o ya uc ha mbuzi huo nakuyafanyia kazi;

• kuwashawishi watu kuwa taarifa na takwimu halisina sahihi ni muhimu na ndizo zinazofaa kutumikawakati tunaposhauri kuundwa kwa sera nzuri zaidikatika jamii yetu;

• kuwa sha wishi waanda aji se ra na wana takwimukushirikiana kwa karibu zaidi. Ni jambo zuri sanapa le waandaa ji wa se ra wa naposhiriki ka tikauta ya rishaji wa mifumo ya ukusanya ji nauchambuzi takwimu na taarifa, hivyo kuzifanyataarifa hizo ziweze kutumika na kuwa na manufaa.

Wadau wengi walishiriki katika uundaji wa mfumo waufuatiliaji umasikini. Kwa hali hiyo tunaweza kuwa nauhakika kwamba takwimu na taarifa mbalimbali zilizona manufaa zitakusanywa na kuchambuliwa kwa namnainayoratibiwa, na hivyo kwa ufanisi zaidi. Taarifa naripoti za tafiti mbalimbali zitapatikana kwa urahisi nazitafikishwa kwa watu wa kawaida kwa namna ambayoitawawezesha kuzielewa kwa urahisi.

(Angalia kiambatanisho 1 kwa kuona vipengele muhimuvya Mfumo wa Taifa wa Ufuatiliaji Umasikini)

Nini kilichomo kwenye mpango kamambe waufuatiliaji umasikini?

Mpango Kamambe wa Ufuatiliaji Umasikini unawekawazi kazi zitakazofanyika katika kipindi cha miakamitatu ijayo. Huu ni mpango unaoendelea kwa sababukila mwaka unatoa mpango mpya wa miaka mitatumbele. Kila eneo katika mpango huu limewekewaghara ma yake, na ghar ama hizo kwa ujumlazimeingizwa katika bajeti ya serikali. Mpango huu piaunaelezea hatua za kujenga uwezo wa kila eneo namfumo kwa ujumla . Ha tua hii inalenga ka tikakuha kikisha kwamba kuna kuwa na watendaji wakutosha wenye ufa hamu, maa rif a na vifa avinavyohitajika kwa ajili ya kutekeleza mpango huu.Kwa maana hiyo, mfumo huu utawasaidia wadau wotekupanga sera na mipango na kufanya ufuatiliaji natathmini kwa kuzingatia taarifa na takwimu sahihiwalizopatiwa.

Mfumo wa ufuatiliaji umasikini unaendeshwavipi?

Katika warsha ya wadau iliyofanyika hapo Oktobamwaka 2000, washiriki walikubaliana kuundwa kwakamati ya kitaifa ya uendeshaji na usimamizi waufuatiliaji umasikini, ikiwa na wawakilishi kutoka kilaeneo muhimu la serikali, taasisi na jumuiya huru zaraia, wanataaluma na sekta binafsi. Aidha, warsha hiyoilipe ndekeza kuundwa kwa maku ndi manne yautendaji wa kiufundi (TWG). Makundi haya tayariyameshaundwa.

(Angalia kiamba tanisho cha pili, c he nye kiel ele zokinachoonyesha jinsi mfumo huu unavyofanya kazi).

5

Page 8: DIBAJI - hakikazi.org · kadhalika, mara nyingi hakuna maelewano ya awali baina ya wakusanyaji taarifa hizo na wale wanaotarajiwa kuzitumia. Hii inamaanisha kwamba bado kuna fursa

Kamati ya Uendeshaji wa Ufuatiliaji Umasikini iliundwaMei mwaka 2001. Mwenyekiti wa kamati hii ni KatibuMkuu katika Ofisi ya Makamu wa Rais. Kamati inawajumbe kutoka sehemu mbalimbali ikiwa ni pamojana taasisi za kitaaluma, taasisi na jumuiya huru za raia,vikundi vya kidini, mashirika ya mae nde le o yakimataifa, wizara muhimu zilizomo kwenye PRSP, nasekta binafsi.

Kazi kuu ya kamati hii ni kusimamia zoezi zima laufuatiliaji umasikini na kutoa miongozo, kupitia taarifaza utekelezaji na kupitisha mipango ya kazi za makundiya utendaji wa kiufundi. Vilevile kamati ina jukumu lakutafuta fedha ili kuwezesha utekelezaji wa mfumomzima wa ufuatiliaji umasikini kwa vitendo. Aidha,kamati hii inasimamia utayarishaji wa ripoti ya kilamwaka kuhusu hali ya umasikini nchini Tanzania.

Kamati ya kiufundi ya Mkakati wa Kupunguza Umasikini(PRS) ipo chini ya uenyekiti wa Naibu Katibu Mkuu waWizara ya Fedha. Kamati hii inajumuisha wawakilishikutoka makundi manne ya kiufundi. Kazi yake kuu nikuratibu na kuboresha mawazo ya makundi ya kiufundi,kabla hayajawasilishwa katika kamati ya uendeshaji.

Se kre tar ieti ya ufua tilia ji uma sikini ina wajumbekutoka Ofisi ya Makamu ya Rais, Wizara ya Fedha, Ofisiya Rais Mipango na Uwekezaji. Sekretarieti hii inafanyaka zi sio tu kwa Kamati ya Ue ndeshaji UfuatiliajiUma sikini na Kamati ya Kiufundi ya Mkakati waKupunguza Umasikini, bali pia kwa Kamati ya Mawaziri.

Kazi za sekretarieti hii ni pamoja na kuandaa mikutanoya kamati inazozihudumia; kuyataarifu makundi yautendaji wa kiufundi kuhusu maamuzi yaliyofikiwa nakamati hizo; kuandaa nyaraka za kamati mbalimbali; nakuratibu uandaaji wa nyaraka mbalimbali kwa ajili yakamati zote. Sekretarieti hii pia ina jukumu la kuratibumashauria no ba ina ya wada u kuhusu Mkakati waKupunguza Umasikini, na kuandaa ripoti ya mwaka juuya hali ya umasikini nchini Tanzania.

Makundi manne ya utendaji wa kiufundi ni hayayafuatayo:

• Kundi linalohusika na utafutaji takwimu autaarifa na sensaKundi hili linaongozwa na Kitengo cha Taifa chaTakwimu. Kundi hili Imeandaa mpango wa kutafuta

taarifa na takwimu mbalimbali utakaoondelea hadimwaka 2012. Mpa ngo huu wa kazi uta husishashughuli za Sensa ya Taifa ya watu na makazi,Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya, Utafiti juuya Idadi ya Watu na Afya, Utafiti wa Hali ya Ajira naNguvu Kazi, na Utafiti kuhusu Hali ya Kilimo.

• Kundi linalohusika na ukusanyaji takwimuzinazotokana wa mfumo wa utawalaKundi hili lipo chini ya uenyekiti wa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Kundi hili linajukumu la kuboresha mfumo wa se rikali kuu,ser ikal i za mikoa na za mitaa kuc ha mbua,kubadilishana na kusambaza taarifa mbalimbali.Mifumo iliyoboreshwa itawasaidia watu wengi zaidikupata taarifa muhimu na zenye manufaa, kwaurahisi zaidi.

• Kundi linalohusika na utafiti na uchambuziKundi hili linaongozwa na Ofisi ya Rais - Mipango naUbinafsishaji. Kundi hili ndilo linaloamua kuhusumaeneo ya kupewa kipaumbele na kupendekezanjia za upatikanaji fedha kwa ajili ya utafiti nauchambuzi. Aidha, kundi hili linatoa uchambuzi nakuijulisha jamii kuhusu viwango na vyanzo vyaumasikini nchini na matokeo ya sera mbalimbali zakupunguza umasikini. Mbinu tofauti za utafiti naukusanyaji taarifa zitatumika, hata hivyo mkazozaidi unawekwa katika mbinu za tathmini shirikishiza umasikini (PPA) ambazo ndizo zinazo bainishawazi jinsi watu masikini wanavyoelewa hali zao.

• Kundi linalohusika na usambazaji, uhamasishajina kujenga mwamkoKundi hili linaongozwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.Hili ndilo linaloratibu programu ya kusambazataarifa zinazopatikana kupitia mfumo mzima waufuatiliaji umasikini. Aidha, linawahamasisha nakuwafahamisha wadau mbalimbali kuhusu hali yaumasikini na hatua mbalimbali zinazofikiwa katikakukabiliana nao. Pamoja na masuala mengine, kundihili limeazimia na kujizatiti kuwafikishia wananchikatika ngazi ya chini kabisa, taarifa mbalimbali kwanjia ambayo itakuwa rahisi kwao kuzielewa nakuzitumia ili waweze kuchukua hatua mwafaka zakukabiliana na umasikini katika na maeneo aumazingira yao.

6

Page 9: DIBAJI - hakikazi.org · kadhalika, mara nyingi hakuna maelewano ya awali baina ya wakusanyaji taarifa hizo na wale wanaotarajiwa kuzitumia. Hii inamaanisha kwamba bado kuna fursa

Makundi haya ya utendaji wa kiufundi yanaratibu nakutoa mwongozo wa kazi zinazofanyika katika maeneombalimbali, na si kufanya kazi hizo yenyewe . Ni wazikuwa kama makundi haya yatakuwa makubwa mnoitakuwa ni vigumu kuyaendesha vyema. Kwa mantikihiyo, makundi haya yameundwa na idadi ndogo yawajumbe, ambayo hata hivyo inazingatia uwakilishiwenye uwiano ukiwajumuisha pia wanaharakati mahirikatika masuala ya jinsia na mazingira.

Hii inamaanisha kwamba, iwapo taasisi au jumuiya huruya kiraia ina mawazo fulani ya kuchangia katika kamatihizi, inaweza kufanya hivyo kwa kupitia mwakilishi wakatika kundi husika la kiufundi. Iwapo wewe unaonakuwa unastahili kujiunga na moja ya makundi haya,unaweza kuwasiliana mwenyekiti wa kundi husika kwakupitia Sekretarieti ya Ufuatiliaji Umasikini.

Maelezo zaidi kuhusu uanachama wa makundi hayamanne yanapatikana kwenye kiambatanisho cha tatu(3).

Nini maana y a tathmini s hirik ishi y aumasikini?

Takwimu nyingi zina zokusanywa katika Mfumo waUfuatil iaji Umasikini zimee ge mea za idi kwenyekubainisha matokeo yanayoweza kuhesabika au yale

yanayoonekana kwa macho. Takwimu hizi zinawezakutueleza mengi kuhusu mambo yanayofanyika lakini sisababu za kufanyika kwa mambo hayo. Waathirikawenyewe wa tatizo la umasikini ndio watakaowezakujibu vyema zaidi maswali kuhusu sababu za waokufanya mambo kwa namna fulani na si vinginevyo.Wao ndio wenye kujua vyema zaidi hisia walizonazo nanamna wanavyoiele wa hali ya maisha wa liyonayo.Taarifa kama hizi zinapokusanywa ndizo zinazowezakuelezea sababu za msingi zisizoweza kupimika kwanamba au kuonekana kwa macho za hali halisi iliyopo.

Tathmini shirikishi za umasikini zinatoa fursa kwa watumasikini na wale waishio katika mazingira magumuzaidi kueleza wanakifikiria nini kuhusu umasikini. Vilevile wanaweza kutoa mawazo yao kuhusu sababu zamabadiliko yanayotokea katika maisha na mazingirayao.

Watafiti wanaofanya tathmini shirikishi za umasikinihujaribu zaidi kuzungumza na mtu mmoja mmojabadala kuzungumza na kundi kubwa la watu au taasasi.Mchakato wa jumla wa tathmini shirikishi ya umasikiniumejengeka katika kuwashirikisha na kuwawezeshawatu masikini na wale walio katika makundi yanayoishikatika mazingira magumu kue le za iwa po sera namipango mbalimbali ya kuondoa umasikini imeleta auimeshindwa kuleta mabadiliko katika maisha yao.

7

Page 10: DIBAJI - hakikazi.org · kadhalika, mara nyingi hakuna maelewano ya awali baina ya wakusanyaji taarifa hizo na wale wanaotarajiwa kuzitumia. Hii inamaanisha kwamba bado kuna fursa

Mfumo wa Ufuatiliaji Umasikini ni tofauti na mifumoiliyokuwa ikitumika hapo awali kwa sababu:

• watumiaji wa ta arifa na ta kwimuzitakazopatikana wameshirikishwa katika kuamuani taarifa zipi zitafutwe na kukusanywa;

• hivi sasa watayarishaji sera, wapangaji mipango nawafadhili kwenye ngazi zote wanaelewa vyemazaidi umuhimu wa kutumia taarifa au takwimusahihi katika kutayarisha sera na mipango yakuondoa umasikini;

• kundi la utendaji wa kiufundi la uhamasishaji,uhimizaji na usambazaji limeundwa kuhakikishakuwa taarifa na takwimu zinapatikana kwa wingina kwa urahisi kwa kadri itakavyowezekana kwawadau wote na njia itakayowawezesha kuzielewataarifa na takwimu hizo kwa urahisi;

• wakati wote mfumo wa ukusanyaji, uchambuzi nausambazaji wa taarifa unafuatiliwa kwa makini nakufanyiwa mapitio na wadau mbalimbali ili kamakutakuwa na haja ya kuufanyia mabadiliko, basimabadiliko hayo yaweze kufanyika haraka.

Mfumo wa Ufua tilia ji Uma sikini umebuniwa iliujumuishe wadau wengi kadri iwezekanavyo. Katikaharakati inayoendelea dhidi ya umasikini, mfumo huuutawasaidia wale wote watakaoutumia kutumia vyemazaidi muda, rasilimali na juhudi zao. Watu wanawezakuutumia mfumo huu katika njia kuu mbili: - wanawezakuchangia na kuingiza taarifa ndani ya mfumo, na piawanaweza kutoa taarifa kutoka kwenye mfumo huu.

Je kuna nafasi ya tawala za mikoa na serikaliza mitaa katika mfumo huu?

Watumishi katika tawala za mikoa na serikali za mitaawatashirikishwa kwa karibu katika Mfumo wa UfatiliajiUmasikini kwa njia zifuatazo:

• kusaidia kutafuta na kucha mbua taa rifazilizokusanywa katika ngazi za vitongoji, mitaamikoa hadi taifa;

• kutumia taarifa zilizokusanywa katika kutayarishasera, kupanga, kufuatilia na kutathmini shughuliza kupunguza uma sikini ka tika nga zi yakitongoji/mtaa na kwenye ngazi ya wilaya;

• kuhakikisha matokeo ya ukusanyaji na uchambuziwa taarifa yanawafikia watu kwa urahisi na kwa

kiwango kikubwa na kuwahimiza kuzijadilina kuzitumia taarifa hizo.

8

Page 11: DIBAJI - hakikazi.org · kadhalika, mara nyingi hakuna maelewano ya awali baina ya wakusanyaji taarifa hizo na wale wanaotarajiwa kuzitumia. Hii inamaanisha kwamba bado kuna fursa

Watumishi wa ofisi za tawala za mikoa na serikali zamitaa watakuwa ni watendaji muhimu sana katika kaziza kundi la utendaji wa kiufundi linaloshughulikiaukusanyaji wa takwimu na taarifa kutoka katika namfumo wa utawala. Makundi mengine ya utendaji wakiufundi yanahitaji taarifa hizi ili kutoka katika mfumowa utawala ili kukamilisha ukusanyaji wa taarifa, hasaikizinga tiwa ukubwa wa nchi na muda ambaounge hitajika kukusanya ta arifa hizo zote. Ta a r i f azinazopatikana katika eneo fulani zinaweza kutumikakatika eneo husika, lakini pia waandaji sera katikangazi ya kitaifa , wanazihita ji taa rifa hizo i likulinganisha mahitaji tofauti ya watu tofauti katikamaeneo tofauti nchini.

Vilevile Mfumo wa Ufuatiliaji Umasikini utafanya kazikwa karibu na Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini waSerikali za Mitaa. Kuanzishwa kwa mfumo huu nisehemu ya Programu ya Mabadiliko katika Serikali zaMitaa . Mifumo hii miwili ina jumuisha kuwa patiawatendaji hao vifaa na mafunzo. Hii itasaidia sanakuwawezesha wafanyakazi wa mamlaka za wilaya natawala za mikoa nchini na kuwa na ufanisi zaidi katikaukusanya ji, utunza ji , ucha mbuzi na utumia ji watakwimu zina zokusanya katika mfumo wa kawa idautawala na utendaji wa serikali.

Taasisi, vikundi na jumuiya huru za raiazinaweza kuchangia vipi katika mfumo huu?

Taasisi za hiari na jumuiya huru zakiraia zimeshirikishwa katika hatuazote za utayarishaji wa Mfumo waUfua tilia ji Umasikini na zinawawakilishi katika Ka ma ti yaUendeshaji Ufuatiliaji Umasikini naha li ka dhalika ka tika makundi yautendaji wa kiufundi .

Taasisi na jumuiya huru za kiraiazita kuwa muhimu zaidi katikakute ke le za Ta thmini Shi rikishi yaUma sikini itaka yoende shwa nakusimamiwa na Kundi la Utafiti naUchambuzi na katika ka zi yakuwafikia wana nc hiita kayoe ndeshwa na Kundi laUsambaza ji, Uha ma sisha ji naUhimizaji.

Mfumo wa Ufuatiliaji Umasikini unajaribu kuwahusishawadau wengi kwa kadri iwezekanavyo. Hata hivyoufua tiliaji wa kujite gemea una ofanywa na taasis i,vikundi na jumuiya huru za kir aia nao piaunathaminiwa. Mfumo huu kwa ujumla wake, unawezakusaidi na upo tayari kuhimiza kufanywa kwa uchunguziwa kujite ge me a na kisha kuyaingiza matoke o yauchunguzi huo katika ha zina yake na kusa idiakuyasambaza.

Kundi la utendaji wa kiufundi linaloshughulikia Utafitina Uchambuzi hutayarisha na kupitia mara kwa maraprogramu ya kubainisha maeneo ya utafiti yanayostahilikupewa kipaumbele. Kiasi fulani cha fedha kimetengwakwa ajili ya kusaidia kazi za ufuatiliaji umasikinizinazofanywa na taasisi na jumuiya huru za kiraia.Fe dha hizi zina tolewa pa le a mba po ka zi hizozinaangukia katika maeneo yaliyopewa kipaumbele nakundi hili la utafiti na uchambuzi.

ZINGATIA: Fedha za Mfumo wa Ufuatiliaji Umasikini zinawezakutumika tu kusaidia miradi ya kupambana na umasikiniinayolenga katika shughuli za utafiti.

Ni jins i gani ninaweza kuingi za taarifambalimbali katika mfumo wa ufuatiliajiumasikini?

Kwa njia isiyo rasmi, ufuatiliaji umasikini hufanyika kilawakati. Watu wote, wawe masikini au matajiri, wazeeau vijana, wanaoishi mijini au vijijini, watu binafsi au

9

Page 12: DIBAJI - hakikazi.org · kadhalika, mara nyingi hakuna maelewano ya awali baina ya wakusanyaji taarifa hizo na wale wanaotarajiwa kuzitumia. Hii inamaanisha kwamba bado kuna fursa

makundi, huchukua hatua mbalimbali kulingana nataarifa na ushahidi walionao. Mfumo wa UfuatiliajiUmasikini utawasaidia watu wa aina mbalimbali kupatataarifa na ushahidi wanaouhitaji ili kufanya maamuzimazuri na yenye manufaa faida. Kadri taarifa nyingizinavyopatikana kupitia mfumo huu, ndivyo mfumowenyewe unavyozidi kuimarika na kuwa na ufanisi.

Tanzania inahitaji taarifa na ushahidi unaoonyesha jinsihali ya umasikini inavyobadilika na kuweka bayanaiwa po juhudi za se rika li za kupunguza uma sikinizimekuwa na mafanikio ama la. Mfumo huu umebuniwaili kuwawezesha wadau wote wanaoshiriki katika zoezihili kutumia vizuri zaidi muda, juhudi na rasilimali zao.

Mfumo wa Ufua tilia ji Umasikini una ka ribisha nakupokea taarifa na ushahidi uliopatikana kutokana natafiti au uchunguzi wa kujitegemea unaofanywa nawatu binafsi au taasisi mbalimbali. Iwapo utakuwa naushahidi au taarifa yoyote ambayo ungependa iingizwekatika Mfumo wa Ufuatiliaji Umasikini, tafadhali itumekwa Sekretarieti ya Ufuatiliaji Umasikini katika Ofisi yaMakamu wa Rais. Sekretarieti nayo itapeleka taarifahizo kwenye kundi husika la utendaji wa kiufundi.

Mfumo wa Ufuatiliaji Umasikini utagharimu takribanshilingi za Kitanzania bilioni 2.5 kwa mwaka. Kiasi hikicha fedha kinaweza kuonekana kuwa ni kikubwa, lakinini kiasi cha asilimia 0.6 tu ya kiasi cha shilingi zaKitanzania bilioni 516 zilizotengwa kwa ajili ya bajetiya Mkakati mzima wa Kupunguza Umasikini kwa mwaka2002/03.

Iwapo Mfumo wa Ufuatiliaji Umasikini usingekuwepo,basi ukusanyaji wa taarifa na takwimu mbalimbaliusingeweza kupangwa na kuratibiwa vyema. Kwa halihiyo, muda, jitihada na fedha nyingi zingepotea bure.Mfumo huu mpya ulioandaliwa kwa makini unamaanishakuwa tutawza kiasi kikubwa cha fedha na kupatathamani halisi ya fedha zitakazotumika.

Bajeti yenye mchanganuo wa kina wa mahitaji ya fedhakwa kila kundi kati ya makundi manne ya utendaji wa

kiufundi na kwa ajili ya utawala wa mfumo mzimaime sha andaliwa . Mae le zo za idi kuhusu sua la hiliyanapatikana katika Waraka wa Mpango Kamambe waUfuatiliaji Umasikini.

Nani anaugharamia mfumo huu?

Serikali imetoa umuhimu wa kipekee kwa shughuli zakufua tilia umasikini kama se he mu muhimu yautekelezaji wa shughuli zake. Hivyo imetenga kiasi chashilingi za Kitanzania bilioni 1.1 katika bajeti yake yamwaka 2002/2003 kwa ajili ya mfumo. Kiasi kilichobakicha shilingi bilioni 1.4 kitachangiwa na washirika wakewa maendeleo.

Watu masikini watanufaika vipi kutokana namfumo huu?

Wananchi hawatanufaika moja kwa moja kutokana nafedha zina zotumiwa c hini ya mfumo huu, baliwa ta nufa ika sa na kutoka na na kubore shwa kwataratibu za utayarishaji sera, mipango, ufuatiliaji natathmini zinazozingatia taarifa na takwimu halisi nasahihi katika ngazi ya maeneo wanayoishi, mkoa nataifa.

Pamoja na mambo mengine, mfumo huu utawapa fursawananchi kufahamu sera sera mbalimbali zinazogusamaisha yao na kiasi cha fedha kilichotengwa kwa ajilikuchochea maendeleo yao. Hivyo basi, iwapo mamboyatakwe nda kinyume na mipango na ra tiba yaute kele zaji wa mipa ngo hiyo, wananchi wata kuwakatika nafasi nzuri zaidi ya kuhoji.

10

Page 13: DIBAJI - hakikazi.org · kadhalika, mara nyingi hakuna maelewano ya awali baina ya wakusanyaji taarifa hizo na wale wanaotarajiwa kuzitumia. Hii inamaanisha kwamba bado kuna fursa

Mfumo wa Ufuatiliaji Umasikini umeundwa kwa namnainayorahisisha upatikanaji wa taarifa. Katika michacheijayo taarifa mbalimbali zitachapishwa. Taarifa hizizitapatikana katika vijitabu vidogo vidogo na ripotiambazo utaweza kuzipata katika ofisi za serikali katikawilaya au mkoa wako. Unaweza pia kupata nakala zakomwenye we kutoka kwa Se kre tarieti ya Ufuatilia jiUmasikini (anuani ya sekretarieti hiyo inaonyeshwanyuma ya jalada la kijitabu hiki). Aidha, nyingi yataarifa au ripoti zitakazotolewa zitapatikana pia katikatovuti kadha katika mtandao wa ma wa siliano yakompyuta (angalia orodha ya tovuti muhimu katikakiambatanisho cha 5) .

Ni vyema ifahamike kuwa taarifa nyingi zitapatikanapia kupitia magazeti, radio na televisheni na wakatimwingine kupitia mabango na kazi mbalimbali zawasanii wa sanaa za maonyesho. Tafadhali fuatilia kwakaribu ni nini kinachotokea katika eneo unamoishi,wilayani na mkoani kwako, na hata katika ngazi yakita ifa na uwe ta ya ri kushiriki kika milifu katikamatukio hayo.

Pia unaweza kuorodhesha jina lako na anuani yakokatika orodha ya wa tu na taa sisi zinazopele kewataarifa mbalimbali ili uweze kutumiwa taarifa kuhusuripoti mbalimbali pindi zitakapokuwa zimeandaliwa.Iwapo ungependa taarifa zaidi tuandikie kwa anuaniiliyopo nyuma ya kijitabu hiki.

11

Page 14: DIBAJI - hakikazi.org · kadhalika, mara nyingi hakuna maelewano ya awali baina ya wakusanyaji taarifa hizo na wale wanaotarajiwa kuzitumia. Hii inamaanisha kwamba bado kuna fursa

Nitapata wapi nakala ya Mpango Kamambe wa Ufuatiliaji Umasikini?

Unaweza kupata fursa ya kusoma nakala za Mpango kamambe wa Ufuatiliaji Umasikini kwenye ofisi za serikalikatika ngazi ya wilaya na mkoa. Majalada ya nakala hizo yana rangi nyekundu iliyokolea.

Ukihitaji kupata na kala yako mwe nye we , wasiliana na Sekre tarieti ya Ufua tilia ji Umasikini kwa a nuaniiliyoonyeshwa nyuma ya kijitabu hiki.

Kama umeunganishwa katika mtndao wa mawasiliano ya kompyuta unaweza kupata nakala ya bure ya mpango huokwa kufungua faili lililo katika anuani ifuatayo:http://www.tzonline.org/pdf/povertymonitoringmasterplan.pdf

12

Page 15: DIBAJI - hakikazi.org · kadhalika, mara nyingi hakuna maelewano ya awali baina ya wakusanyaji taarifa hizo na wale wanaotarajiwa kuzitumia. Hii inamaanisha kwamba bado kuna fursa

Mfumo wa kitaifa wa ufuatiliaji umasikini utakuwa na matokeo gani muhimu?

Kama matokeo ya shughuli za mfumo huu unaweza kutarajia kuchapishwa na kupatikana kwa ripotizifuatazo:

1. Ripoti ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya ya 2000/2001Ripoti hii itatoa matokeo ya takwimu kuhusu mabadiliko yanayowe za kuoneka na dha hiri(quantitative) zilizokusanywa katika Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya na kuyalinganisha namatokeo ya utafiti kama huo uliofanyika mwaka 1990/1991.

2. Ripoti ya Hali ya Umasikini na Maendeleo ya Binadamu. Ripoti hii itatoa picha ya maendeleo yaliyofikiwa katika utekelezaji wa malengo ya Mkakati waKuondoa Umasikini. Aidha, ripoti hii itaonyesha mambo muhimu yatakayojitokeza katika utafiti nauchambuzi. Ma mbo ha ya yata eleze a na kufa fanua sa babu zilizosaba bisha mabadilikoyatakayojitokeza katika taarifa na takwimu zitakazokusanywa.

3. Utafiti kuhusu Hali ya Nguvu Kazi NchiniTaarifa hii ya utafiti itabainisha mambo muhimu yatakayojitokeza kuhusu hali ya nguvu kazi nchiniTanzania na itajumuisha kipengele cha ajira mbaya kwa watoto.

4. Tathmini Shirikishi za UmasikiniTathmini hizi zitatoa picha ya matatizo halisi na hali ngumu za maisha zinazowakabili wananchi.

5. Mfumo wa Utunzaji Taarifa za Kijamii na UchumiHuu ni mfumo unaotumia kompyuta ambao ni chanzo kikuu cha taarifa za kitakwimu unaoendeshwana Kitengo cha Takwimu cha Taifa. Wadau wote wanahimizwa kuutumia mfumo huu.

6. Taarifa kwa waandaaji sera: Hizi ni ripoti maalumu zinazotumia taarifa au ushahidi kutoka katika mfumo wa ufuatiliajikuchambua na kufanya mapitio ya masuala fulani mahsusi.

13

Page 16: DIBAJI - hakikazi.org · kadhalika, mara nyingi hakuna maelewano ya awali baina ya wakusanyaji taarifa hizo na wale wanaotarajiwa kuzitumia. Hii inamaanisha kwamba bado kuna fursa

Vipengele muhimu vya Mfumo wa Taifa wa Ufuatiliaji Umasikini

Ufafanuzi kuhusu mahitaji ya taarifa:Wadau wamekubaliana juu ya viashiria muhimu vitakavyotumika katika mfumo huu pamoja navipaumbele kwa ajili ya ukusanyaji taarifa mbalimbali kuelezea sababu za hali itakayokuwaimejitokeza na hivyo kufanya takwimu kujitosheleza zaidi.

Mfumo wa kitaasisi:Kamati ya uendeshaji ya kitaifa ya mfumo wa ufuatiliaji umasikini na makundi manne ya utendaji wakiufundi yameundwa ili kusimamia na kutekeleza kazi ya mfumo. Muundo mzima wa mfumo huuunajionyesha kwenye kiambatanisho 2.

Nyenzo za ukusanyaji taarifa au takwimu:Kuna makundi mawili ya nyenzo za ukusanyaji taarifa na takwimu. Kundi la utendaji wa kiufundilinaloshughulikia utafutaji taarifa au takwimu na sensa linasimamia programu ya miaka kadhaa yaukusanyaji takwimu mbalimbali itakayotekelezwa na Kitengo cha Takwimu cha Taifa. Kundi lautendaji wa kiufundi linaloshughulikia ukusanyaji takwimu kutoka katika mfumo wa kawaida wautawala serikalini linasaidia kuweka mipango ya kuboresha na kuinua uwezo wa idara za serikali kuuna serikali za mitaa wa kuchambua na kutumia taarifa zinazokusanywa kila siku katika idara hizo.

Vipaumbele vya utafiti:Maswali ya kitafiti yatawasaidia watafiti kukusanya aina ya taarifa ambazo haziwezi kukusanywakatika ukusanyaji wa takwimu na sensa, au katika utendaji wa siku hadi siku katika utawala waserikali. Taarifa hizi ndizo zitakazo kidhi haja ya kuelezea kwa undani vyanzo na sababu za haliitakayojitokeza na masuala yanayohusu tathmini. Kundi la utendaji wa kiufundi linaloshughulikiautafiti na uchambuzi limeandaa mpango unaoweka utaratibu wa kufuatwa katika utafiti, uchambuzina tathmini shirikishi za umasikini.

Mpango wa usambazaji:Kundi la utendaji wa kiufundi linaloshughulikia usambazaji, uhimizaji na uhamasishaji limetayarishaorodha ya watu watakaotumia takwimu na taarifa zitakazokusanywa na mfumo wa ufuatiliajiumasikini. Pia limefikiria njia nzuri zaidi za kuwawezesha watu hao kupata taarifa na takwimu hizo.Miongoni mwa njia muhimu zitakazotumika katika kusambaza taarifa hizo ni ile ya kupitia Mfumo waUtunzaji Takwimu Kuhusu Hali ya Kiuchumi na Kijamii nchini Tanzania, (Tanzania Socio-EconomicDatabase) pamoja na tovuti rasmi katika mtandao wa mawasiliano ya kompyuta yenye habari kuhusuTanzania (Tanzania Online).

Kujenga uwezo:Mipango imeandaliwa ili kuhakikisha kuwa wadau wote muhimu wanaoshiriki kwenye mfumo mzimawa ufuatiliaji umasikini wanapata mafunzo na vifaa wanavyohitaji ili waweze kufanya kazi hii kwatija na ufanisi.

Gharama:Bajeti za kina kwa kila kipengele cha Mfumo wa Kitaifa wa Ufuatiliaji Umasikini na kujumuishwakatika bajeti kuu ya miaka mitatu.

Taratibu za kuchangia gharama: Sehemu ya gharama za mfumo huu italipiwa na serikali na sehemu nyingine italipiwa na wabia wamaendeleo.

14

Page 17: DIBAJI - hakikazi.org · kadhalika, mara nyingi hakuna maelewano ya awali baina ya wakusanyaji taarifa hizo na wale wanaotarajiwa kuzitumia. Hii inamaanisha kwamba bado kuna fursa

Baraza la mawaziri Kamati ya mawaziri

Kamati inayohusisha wizarambalimbali

TWG Utafutajitaarifa na sensa

TWG Utafiti nauchambuzi

Kamati ya mfukowa utafiti

Kundi la tathminishirikishi

Wizara mbalimbali

TAMISEMI

Sekreterieti yautawala ya mkoa

Mamlaka yaserikali ya mtaa

Kamati yamaendeleo ya kata

Serikali yakijiji/mtaa

TWG Mifumo yahifadhi ya taarifa

za mara kwa TWG Usambazaji

Kamati ya uendeshaji yaufuatiliaji umasikini

Kamati wa taalam ya PRS

Sekretarieti ya mfumo yaufuatiliaji umasikini

15

Muundo mzima wa mfumo wa taifa wa ufuatiliaji umasikini

Page 18: DIBAJI - hakikazi.org · kadhalika, mara nyingi hakuna maelewano ya awali baina ya wakusanyaji taarifa hizo na wale wanaotarajiwa kuzitumia. Hii inamaanisha kwamba bado kuna fursa

16

Kundi linalohusika na utafutaji takwimuna sensa

Mwenyekiti: Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha

Taifa cha Takwimu

Wajumbe:• Benki Kuu ya Tanzania• Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DFID)• Taasisi ya Mafunzo ya Takwimu ya Afrika Mashariki• Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO)• Shirika la Misaada la Japan (JICA)• Kitengo cha Taifa cha Takwimu• Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji• Chuo Kikuu Kishiriki cha Ardhi na Usanifu Majengo

(UCLAS)• Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)• Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA)• Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto

(UNICEF)• Chuo Kikuu cha Dar es Salaam• Mpango wa Chakula Duniani (WFP)

Kundi linalohusika na ukusanyaji takwimuzinazotokana wa mfumo wa utawala

Mwenyekiti: Mkurugenzi wa Tawala za Mikoa, Ofisi yaRais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Wajumbe:• Taasisi ya Mafunzo ya Takwimu ya Afrika Mashariki• Shirika la Misaada la Ireland (Irish Aid)• Mpango wa Kuboresha Serikali za Mitaa• Wizara ya Kilimo na Chakula• Wizara ya Elimu na Utamaduni• Wizara ya Afya• Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa• Wizara ya Maji na Mifugo• Wizara ya Ujenzi • Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa• Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) • Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)• Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto

(UNICEF)

Kundi linalohusika na usambazaji,uhamasishaji na kujenga mwamko

Mwenyekiti: Mkurugenzi wa Kitengo cha Ku o n d o a

Umasikini, Ofisi ya Makamu wa Rais

Wajumbe:• Shirika la CARE International • Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DFID)• HakiKazi Catalyst• HealthScope• International Data Vision• Shirika la Misaada la Ireland (Irish Aid)• Shirika la Misaada la Japan (JICA)• Mpango wa Kuboresha Serikali za Mitaa• Wizara ya Elimu na Utamaduni• Wizara ya Fedha• Wizara ya Afya• Kitengo cha Taifa cha Takwimu• Baraza la Mazingira la Taifa• Kitengo cha Kuondoa Umasikini, Ofisi ya Makamu wa Rais• Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji • Save the Children• Mtandao wa Jinsia Tanzania• Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) • Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)• Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia

Watoto (UNICEF)• WaterAid

Kundi linalohusika na utafiti nauchambuzi

M w e n y e k i t i : M kurgenzi wa Uchumi Mkuu(Macroeconomy), Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji

Wajumbe:• Benki Kuu ya Tanzania• Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DFID)• Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF)• Shirika la Misaada la Japan (JICA)• Kitengo cha Taifa cha Takwimu• Ubalozi wa Uholanzi• Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji• Kitengo cha Kuondoa Umasikini, Ofisi ya Makamu wa

Rais• Taasisi ya Utafiti wa Kuondoa Umasikini (REPOA)• Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)• Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto

(UNICEF)• Chuo Kikuu cha Dar es Salaam• Benki ya Dunia

Wajumbe katika makundi ya utendaji wa kiufundi

Page 19: DIBAJI - hakikazi.org · kadhalika, mara nyingi hakuna maelewano ya awali baina ya wakusanyaji taarifa hizo na wale wanaotarajiwa kuzitumia. Hii inamaanisha kwamba bado kuna fursa

Tanzania Onlinewww.tzonline.orgTovuti h ii ina nyaraka n yin gi mu himu ku husumaendeleo na inaonyesha anuani za tovuti nyinginembalimbali zenye habari nyingi kuhusu maendeleo.

Maelez o ya CIA kuhusu Ta n z a n i awww.cia.gov/cia/publications/factbook/geos/tz.html

ESRF www.esrftz.org Taasisi ya Utafiti wa Hali ya Uchumi na Kijamii(ESRF) ni Taasisi isiyo ya Kiserikali inayojihusisha nautafiti unaolenga katika kujenga uwezo wa kufanyauchambuzi wa masuala ya uchumi na yale ya kijamii...

Taarifa kuhusu Tanzania katika tovuti ya Benkiya Dunia www.worldbank.org/hipc/country-cases/tanzania/tanzania.htmlBenki ya Dunia hutoa mikopo na ushauri kwa zaidiya nchi 100 zinazoendelea. Benki hii inajulikanapia kama Benki ya Kimataifa ya Ufufuaji Uchumi namaendeleo. Sera, matokeo, uchumi ...

Mtandao w a Jinsia Tanzania (TGNP)www.tgnp.co.tz Mtandao huu unafanya kazi zake ukilenga katikakuleta usawa wa kijinsia; mageuzi ya kijamii nakuinua uwezo wa wanawake kushiriki kikamilifu nakuwa na usemi katika mambo yanayogusa maishayao , kij amii, kisiasa na kiuchu mi. Tovuti yamtandao h uu inaj umu isha hab ari n a taa rifamb alimb ali ikiwa ni pamo ja a shu ghu lizinazofanywa na mtandao huo kwa sasa, programuza elimu, machapisho, taarifa kuhusu ufadhili naanuani ya mtandao wenyewe.

Hakikazi Catalyst www.hakikazi.org Taasisi h ii ina lenga katika kuchangia mawaz okuhusu namna ya kuinua haki za watu wote kushirikikikamilifu katika masuala ya kijamii, kiufundi ...

Shirikisho la Vyama Vis ivyo vya Kiserika l iTanzania (TANGO) www.tango.or.tz Tovu ti hii ni mp ya! Inaj umuisha taarifa nyingikuhusu taasisi na jumuiya huru za kiraia ikiwa nipamoja na orodha ya mashirika yasiyo ya kiserikali(NGOs) programu mbalimbali za shirikisho hilo,machapisho n.k ...

Taari fa ku husu Tanz ania ka t i ka tovu ti yaShirika la Fedha la Kimataifa (IMF)www.imf.org/external/country/tza/index.htmTovuti ya IMF inaonyesha anuani ya tovuti nyingizenye taarifa muhimu mbalimbali, taarifa kuhusuI M F, Viwan go vya fe dha zin azo tolewa/riba n amachapisho ya IMF. Tovuti hiyo inajuisha pia taarifampya, viwango na kanuni mbalimbali za shirikahilo, taarifa kuhusu nchi mbalimbali na makalamaal umu. Sh irika hili linal enga katika kukuz akiw ango cha u kuaj i wa u ch umi kwa kupi tiaushirikiano wa kimataifa katika masuala ya fedhana utoaji wa mikopo na misaada ya fedha.

REPOAwww.repoa.or.tz Hii ni taasisi isiyo ya Kiserikali inayojihusisha nashughuli na ajenda za utafiti na kutoa taarifa nahabari mbalimbali kusaidia utayarishaji wa sera.

Tathmini Shirikishi za Umasikini nchini (PPA)Tanzaniawww.esrftz.org/ppa/ Tovuti hii ina kalenda ya mikutano na matukiombalimbali kuhusu umasikini. Taasisi ya Utafiti waHali ya Uchumi na Kijamii (ESRF) ni Taasisi isiyo yaKiserikali inayojihusisha na utafiti unaolenga katikakujenga uwezo wa kufanya uchambuzi wa masualaya uchumi na yale ya kijamii ...

17

Tovuti katika mtandao wa mawasiliano ya kompyuta zenye taarifa mbalimbalikuhusu umasikini nchini Tanzania ni pamoja na hizi zifuatazo:

Page 20: DIBAJI - hakikazi.org · kadhalika, mara nyingi hakuna maelewano ya awali baina ya wakusanyaji taarifa hizo na wale wanaotarajiwa kuzitumia. Hii inamaanisha kwamba bado kuna fursa

Zifuatazo ni baadhi ya nyaraka na ripoti muhimu ambazo tayari zimeshatolewa:

• Dira ya Maendeleo ya Tanzania hadi Mwaka 2025 www.tzonline.org/pdf/theTanzaniadevelopmentvision.pdf

• Waraka wa Mkakati wa Taifa wa Kupunguza Umasikini(NPES)www.tanzania.go.tz/poverty.html

• Mkakati wa Kuisaidia Tanzania (TAS)www.tzdar.or.tz/Harmonisation/TAS.doc

• Waraka wa Mkakati wa Kupunguza Umasikini (PRSP)www.tzonline.org/pdf/FinalPRSP25.pdf

• Tanzania bila umasikiniwww.hakikazi.org/eng

• Ripoti ya Maendeleo ya Utekelezaji wa Mkakati wa Kupunguza Umasikini kwa mwaka2000/01

www.tzonline.org/pdf/prspprogress01.pdf

• Mpango kamambe wa ufuatiliaji umasikiniwww.tzonline.org/pdf/povertymonitoringmasterplan.pdf

• Ripoti ya kwanza ya Maendeleo ya Tanzania bila Umasikini www.hakikazi.org/eng2

18

Page 21: DIBAJI - hakikazi.org · kadhalika, mara nyingi hakuna maelewano ya awali baina ya wakusanyaji taarifa hizo na wale wanaotarajiwa kuzitumia. Hii inamaanisha kwamba bado kuna fursa

Umasikini wa kipatoUwiano katika mahitaji muhimu ya binadamu na

umasikiniUwiano katika mahitaji muhimu maeneo ya mijini

na umasikiniUwiano wa chakula na umasikiniUmiliki mali, pato na umasikiniKundi la nguvu kazi ambalo sasa halina kazi za

kuzalishaUkuaji wa pato la ndani la jumla kwa mwakaUkuaji wa pato la jumla la ndani katika sekta ya

kilimo kwa mwaka Kiwango cha asilimia cha matengenezo ya barabara

na hali nzuri ya barabara inayohitajika

Uwezo wa binadamu Uwiano wa mtoto wa kike na wa kiume kupata

elimu ya msingiUwiano wa mtoto wa kike na kiume katika kupata

elimu ya sekondariKiwango cha umri kutoka elimu ya msingi hadi

sekondariKiwango cha kuelimika miongoni mwa watu wenye

umri wa miaka 15+Kiwango cha uandikishaji wanafunzi katika elimu

ya msingiKiwango cha watoto walioacha au walioshindwa

kuendelea na elimu ya msingiAsilimia ya idadi ya wanafunzi waliofaulu darasa la

saba katika ngazi A,B,CKiwango cha ARI kwa watoto wenye umri wa chini

ya miaka mitanoKiwango cha ugonjwa wa kuhara kwa watoto walio

na umri chini ya miaka mitanoIdadi ya watu wenye uwezo wa kupata huduma ya

maji safi

KuishiIdadi ya vifo vya watoto wachangaIdadi ya vifo vya watoto walio na umri chini ya

miaka 5Kiwango cha kuishi kwa miakaKiwango cha seropositive kwa akina mama wenye

ujauzitoWilaya zilizomo kwenye kampeni madhubuti dhidi

ya kuleta ufahamu wa ugonjwa wa ukimwi HIV/AIDS

Vifo vya watoto vinavyotokana na ujauzitoMatukio ya ugonjwa wa malaria kali kwa watoto

walio na umri chini ya miaka 5Kiwango cha watoto wenye umri wa chini ya miaka

miwili waliopata chanjo zote dhidi ya surua na DPT

Idadi ya watoto waliozalishwa na muuguzi wa afyamwenye utaalamu

Ustawi wa jamii (utawala bora)Idadi ya mahakama za mwanzo zilizopokea kesi na

kuzitolea hukumuKiwango cha wastani cha kusuluhisha mizozo ya

kibiashara

Lishe Kimo cha mtoto katika umri ulio chini ya miaka 5Uzito wa mtoto aliye chini ya umri wa miaka 5 Uzito uliozidi wa mtoto aliye na umri wa chini ya

miaka 5

Hali ya makundi yaliyo hatariniIdadi ya watoto yatima miongoni mwa watoto

waliopoIdadi ya watoto wanaoongoza familia zaoIdadi ya watoto walio katika ajiraIdadi ya watoto walio katika ajira na ambao

hawaendi shuleIdadi ya waze e wa na oishi nyumbani ambakohakuna hata mtu katika kaya mwe nye uwe zokiuchumi

Mazingira muafaka y a mae nde le okiuchumiUwiano wa akiba ya ndani kwa mwezi

19

Viashiria vya ufuatiliaji umasikini

Page 22: DIBAJI - hakikazi.org · kadhalika, mara nyingi hakuna maelewano ya awali baina ya wakusanyaji taarifa hizo na wale wanaotarajiwa kuzitumia. Hii inamaanisha kwamba bado kuna fursa

Kitengo cha Kuondoa Umasikini cha Ofisi ya Makamu wa Rais kinapenda kutoa shukrani kwa watuwafuatao kutokana na mchango wao katika kukitayarisha na kukisambaza kijitabu hiki:

• Wajumbe wa makundi yote ya utendaji wa kiufundi, hususan kundi la usambazaji, uhamasishaji na

kujenga mwamko.

• Arthur Van Diesen na Christopher Mushi wa UNDP

• Alana Albee na Kaushi Shah wa DFID

• Esther Obdam wa UNICEF

• Wafanyakazi wa Kitengo cha Kuondoa Umasikini, hususan Anna Mwasha, Paschal Assey na

Servus Sagday.

• George Clark wa Caledonia Centre for Social Development

• Emmanuel Kallonga wa Hakikazi Catalyst

• Nisha Sanghvi wa Acex Systems Ltd

• Masood Kipanya

• ColorPrint Tanzania Ltd

• Waheeda Samji na Julia Sampson wa Carpe Diem Ink

• Wengine wote ambao wameshiriki kwa njia moja au nyingine katika uchapishaji wa kijitabu hiki

________________

Dk. S. Likwelile

Mwenyekiti

Kundi la Utendaji wa Kiufundi la Usambazaji, Uhamasishaji na Kujenga Mwamko

Page 23: DIBAJI - hakikazi.org · kadhalika, mara nyingi hakuna maelewano ya awali baina ya wakusanyaji taarifa hizo na wale wanaotarajiwa kuzitumia. Hii inamaanisha kwamba bado kuna fursa
Page 24: DIBAJI - hakikazi.org · kadhalika, mara nyingi hakuna maelewano ya awali baina ya wakusanyaji taarifa hizo na wale wanaotarajiwa kuzitumia. Hii inamaanisha kwamba bado kuna fursa

Kwa Maelezo ZaidiTafadhali Wasiliana na

Sekretarieti ya Ufuatiliaji UmasikiniIdara ya Kuondoa UmasikiniGhorofa ya 2, Jengo la MaktabaS.L.P. 5380Dar-es-Salaam