BUSINESS KISWAHILI 2. 3. 4. 5. 6. 7. GREETINGS AND INTRODUCTION SALAMU NA KUJITAMBULISHA ·...

21
BUSINESS KISWAHILI Contents 1. Greetings and introduction 2. Etiquette 3. Business vocabulary 4. Workers and titles 5. Telephoning and appointment 6. Office 7. Meeting 8. Working with the client 9. Negotiation 10. Job interview 11. Presentation 12. Marketing 13. Banking and finance 14. Immersion GREETINGS AND INTRODUCTION SALAMU NA KUJITAMBULISHA 1. My name is Juma, am glad to meet you. Jina langu ni Juma, nimefurahi kukuona 2. Would you kindly repeat your name? Naomba urudie jina lako 3. How do you do Mr. Akida? Uhaligani Bw. Akida? 4. Good morning. Habari ya asubuhi? 5. Your excellence, may I introduce to you Mr. Kamili. Mheshimiwa, naomba kukutambulishia Bwana Kamili. 6. I would like you to meet my wife Mary, this is my friend Juma. Ningependa ukutane na mke wangu Marry, huyu ni rafiki yangu Juma. 7. Maria, meet my fellow student John. Maria, kutana na mwanafunzi mwenzangu John. 8. Good bye, see you soon. Kwaheri, tutaonana hivi karibuni. 9. Have a nice weekend. Wikendi njema 10. Am going to miss you, we shall meet again.. Nitakukosa, tutaonana tena. 11. Hope to see you soon. Natumai kukuona hivi karibuni 12. Call me when you reach home. Nipigie ukifika nyumbani. 13. Have a good night.

Transcript of BUSINESS KISWAHILI 2. 3. 4. 5. 6. 7. GREETINGS AND INTRODUCTION SALAMU NA KUJITAMBULISHA ·...

Page 1: BUSINESS KISWAHILI 2. 3. 4. 5. 6. 7. GREETINGS AND INTRODUCTION SALAMU NA KUJITAMBULISHA · Nadhani, naamini 12- What exactly do you mean when you say… Chenyewe unachomanisha ni

BUSINESS KISWAHILI

Contents

1. Greetings and introduction

2. Etiquette

3. Business vocabulary

4. Workers and titles

5. Telephoning and appointment

6. Office

7. Meeting

8. Working with the client

9. Negotiation

10. Job interview

11. Presentation

12. Marketing

13. Banking and finance

14. Immersion

GREETINGS AND INTRODUCTION SALAMU NA KUJITAMBULISHA

1. My name is Juma, am glad to meet you.

Jina langu ni Juma, nimefurahi kukuona

2. Would you kindly repeat your name?

Naomba urudie jina lako

3. How do you do Mr. Akida?

Uhaligani Bw. Akida?

4. Good morning.

Habari ya asubuhi?

5. Your excellence, may I introduce to you Mr. Kamili.

Mheshimiwa, naomba kukutambulishia Bwana Kamili.

6. I would like you to meet my wife Mary, this is my friend Juma.

Ningependa ukutane na mke wangu Marry, huyu ni rafiki yangu Juma.

7. Maria, meet my fellow student John.

Maria, kutana na mwanafunzi mwenzangu John.

8. Good bye, see you soon.

Kwaheri, tutaonana hivi karibuni.

9. Have a nice weekend.

Wikendi njema

10. Am going to miss you, we shall meet again..

Nitakukosa, tutaonana tena.

11. Hope to see you soon.

Natumai kukuona hivi karibuni

12. Call me when you reach home.

Nipigie ukifika nyumbani.

13. Have a good night.

Page 2: BUSINESS KISWAHILI 2. 3. 4. 5. 6. 7. GREETINGS AND INTRODUCTION SALAMU NA KUJITAMBULISHA · Nadhani, naamini 12- What exactly do you mean when you say… Chenyewe unachomanisha ni

14. Usiku mwema.

15. Am sorry to hear about that. How are you feeling?

Nasikitika kusikia hivyo. Unahisije?

16. Unfortunately am not so well.

Kwa bati mbaya sisikii vizuri

17. Will you join us for dinner today?

Utajiunga na sisi kwa chakula cha jioni leo?

18. Here is my address, call me sometime.

Hii ni anwani yangu, nipigie wakati fulani.

ETTIQUETTE ADABU

1- Thanks

Ahsante

2- It doesn’t matter, its harmless

Haidhuru

3- Usijali

Never mind/ don’t mind

4- Nisamehe, sitarudia tena

Forgive me, I won’t do it again

5- Tafadhali, niazime kalamu yako.

Please help me with your pen.

6- Naam

Yes

7- Pole, poleni

Sorry

8- Hongera

Congraculations

9- Hebu nikuelezee.

Let me explain to you…

10- Ebu tuende kula chakula cha mchana.

Lets go for lunch

11- Nakutakia heri ya mwaka mpya.

I wish a prosperous new year

12- Ninatafuta kitabu changu.

Iam looking for my book

13- Unaweza kunisaidia na shilingi elfu kumi.

Can you help me with ten thousand?

14- Unaweza kuniambia.

Can you please tell me?

15- Ningependa….

I would like to….

16- Tafadhali useme polepole.

Please speak very slowly.

17- Ni sawa

Page 3: BUSINESS KISWAHILI 2. 3. 4. 5. 6. 7. GREETINGS AND INTRODUCTION SALAMU NA KUJITAMBULISHA · Nadhani, naamini 12- What exactly do you mean when you say… Chenyewe unachomanisha ni

It’s alright

18- Nimemaliza.

I have finished.

19- Sijui.

I don’t know.

20- Ninatafuta...

Iam searching for...

21- Unaweza kueleza zaidi?

Could you explain much more please?

22- Kweli ?

Really?

23- Tafadhali keti.

Please have a seat

24- Je, una uhakika? Tafadhali useme mambo kihususa?

Are you sure, could you be specific?

25- Unaweza kunielezea unachomanisha ukisema…?

Can you explain what you mean when you say…?

26- We require the following information.

Tunahitaji habari ifuatayo.

27- Am afraid I can’t tell you that, it is confidential.

Naogopa siwezi kukwambia, ni siri.

28- I think you should know that….

Nadhani unapaswa kuelewa kwamba…..

29- Did you know that…

Ulikuwa unajua kwamba….

30- We would like to inform you that…

Tungependa kukujulisha ya kwamba…

31- Here is the information that you required.

Hii ni habari uliyohitaji.

32- I understand what you are trying to mean.

Naelewa unachojaribu kumaanisha.

33- That’s what I exactly think

Ndivyo nafikiri hasa.

34- Am sorry but it’s impossible.

Samahani, lakini haiwezekani.

35- That depends

Inategemea.

36- Sorry we can’t meet your request.

Samahani hatuwezi kutimiza ombi lako

37- I believe…, I think…

Naamini…., nadhani…

38- Excuse me, wait for a second.

Samahani, ngoja kidogo.

39- Would you like to have another cup of tea?

Page 4: BUSINESS KISWAHILI 2. 3. 4. 5. 6. 7. GREETINGS AND INTRODUCTION SALAMU NA KUJITAMBULISHA · Nadhani, naamini 12- What exactly do you mean when you say… Chenyewe unachomanisha ni

Ungependa kunywa kikombe kingine cha chai?

40- Would you keep the sit for me?

Je, ungehifadhi kiti changu?

41- Could you do me a favor?

Ungenisaidia

BUSINESS VOCABULARY MSAMIATI WA BIASHARA

1- Buying - Kununua

2- Selling - Kuuza

3- Transportation -Usafiri

4- Storage - Uhifadhi

5- Advertising - utangazaji

6- Manufacturer - Mtengenezaji

7- Market research Utafiti wa soko

8- Balance- chenji

9- Negotiatiating abaut the price -Kujadiliana juu ya bei

10- Cash- Fedha taslimu

11- Debt - Deni

12- How much money?- Ni pesa ngapi?

13- Bei nafuu/ bei poa - Fair price

14- Bei ghali _ expensive price

15- Bei rahisi - low price

16- Bei ya jumla_ wholesale price

17- Bei ya rejareja - retail price

18- Hisa -shares

19- Mapatano ya kibiashara. -Business trasaction

20- Bei haipungui - The price doesn’t reduce

21- Uchumi - Economy

22- Kuajiri -To employ

23- Duka la nguo - Boutique

24- Mzigo- Luggage

25- Safirisha -To transport

26- Ada - Fee

27- Kutoza ada- to charge a fee

28- Kubadili pesa -To exchange money

29- Uza - Sell

30- Muuza duka_ A shop keeper

31- Mfanyakazi_ Worker

32- Dola_ Dolar

33- Fedha_ Money

34- Riba- Intrest

35- Mwajiri - Employer

36- Muuzaji - A seller

37- Bidhaa - Products

Page 5: BUSINESS KISWAHILI 2. 3. 4. 5. 6. 7. GREETINGS AND INTRODUCTION SALAMU NA KUJITAMBULISHA · Nadhani, naamini 12- What exactly do you mean when you say… Chenyewe unachomanisha ni

38- Bei- Price

39- Hebu nihesabu kiasi cha pesa ambazo utalipa.

Let me count the money that am going to pay

40- Hasara - Loss

41- Faida-Profit

42- Tafadhali lipa - Please pay

43- Kiasi - Amount

44- Hesabu - Count

45- Mteja - Customer

46- Mnunuzi - A buyer

47- Pesa za kigeni - Foreign currency

WORKERS - WAFANYAKAZI

1. Receptionist - Mpokea wageni

2. Director - Mkurugenzi

3. Manager - Meneja

4. Sales manager - Meneja wa mauzo

5. Accountant - Mhasibu

6. Advertising manager -Meneja wa kutangaza.

7. Marketing director -Mkurugenzi wa uuzaji.

8. Public relations manager –Meneja wa mahusiano na umma

9. Policeman - Askari polisi

10. Mechanic - Fundi

11. Journalist - Mwanahabari

12. Prime minister - Waziri mkuu

13. Builder - Mjenzi

14. Doctor - Daktari

15. Secretary - Katibu

16. I work in the marketing department.

Nafanya kazi katika idara ya utangazaji.

17. I work in human resources.

Nafanya kazi katika rasilimali za binadamu

18. I work in sales.

Nafanya kazi katika mauzo

19. I work in consulting.

Nafanya kazi katika ushauriano

20. I am unemployed.

Sina kazi

21. I do a part time job.

Ninafanya kazi ya muda.

22. I own a restaurant.

Nina mkahawa

23. My job is so tiring and demanding.

Page 6: BUSINESS KISWAHILI 2. 3. 4. 5. 6. 7. GREETINGS AND INTRODUCTION SALAMU NA KUJITAMBULISHA · Nadhani, naamini 12- What exactly do you mean when you say… Chenyewe unachomanisha ni

Kazi yangu inachosha na ina mambo mengi ya kushughulukia.

24. Coworkers.

Wafanya kazi wenzangu

25. Do you work fulltime?

Nafanya kazi kwa muda wote

26. My salary is fair and we get a bonus at the end of the month.

Mshahara wangu ni wa haki na tunapata nyongeza mwishoni mwa mwezi.

27. Peter got a work promotion this year.

Peter alikuzwa kazini mwaka huu

28. My friend was fired from work last week.

Rafiki yangu alifukuzwa kazini wiki iliyopita

29. I am going to quit my job.

Nitaacha kazi yangu.

30. I am planning to retire when am 40 years

Nina mpango wa kustaafu wakati nitakapokuwa na miaka arobaine.

MEETING-MKUTANO

1- It’s a very good idea, I think it will work.

Hiyo ni mbinu nzuri sana, nadhani itasaidia.

2- I think we would better leave it for the next meeting.

Nadhani tungeiachia kwa mkutano utakaokuja

3- I can see what you mean but…

Naelewa unachomanisha lakini….

4- I don’t think it’s a good idea.

Sidhani kwamba ni wazo zuri.

5- I will let you have the summary of what we have said today in few days.

Nitakupatia mhutasari wa yale tumezungumza leo baada ya siku chache.

6- Am sorry, I don’t really agree with you.

Samahani, sikubaliani na wewe hata kamwe

7- You see, what i think is..

Unaona, ninachofikiri ni…

8- I totally agree with you

Nakubaliana na we kabisa

9- In my opinion…

Kwa mtazamo wangu. .. Kwa maoni yangu….

10- That’s n unhelpful way of looking at this problem.

Hiyo ni njia isiyofaa ya kuangalia tatizo hili.

11- I think, I believe

Nadhani, naamini

12- What exactly do you mean when you say…

Chenyewe unachomanisha ni nini unaposema….

13- Could you be more specific?

Unaweza kusema mambo waziwazi?

Page 7: BUSINESS KISWAHILI 2. 3. 4. 5. 6. 7. GREETINGS AND INTRODUCTION SALAMU NA KUJITAMBULISHA · Nadhani, naamini 12- What exactly do you mean when you say… Chenyewe unachomanisha ni

14- So what you are trying to say is…

Sasa unachojaribu kusema ni..

15- The point I am trying to make is…

Jambo ambalo ninajaribu kusema ni….

16- To make a long story short…

Kwa ufupi…

17- How about if we do it like this

Vipi kama tukifanya hivi

18- How many people will be attending this meeting?

Ni watu wangapi watakaohudhuria mkutano huu?

19- To make the story short..

Kwa ufupi.

20- I have got an appointment.

Nina miadi

21- The main reason for holding this meeting is.

Sababu kuu ya kufanya mkutano huu ni..

22- Mr, chairman , treasurer, secretary

Bw. Mwenyekiti, mweka hazina, katibu

23- Let Mr Karama read us the agenda of this meeting.

Ebu Bwana Karama atusomee ajenda ya mkutano huu.

24- May we know those who have attended and those who have not attended with

permission?

25- Tunaomba kujua wale ambao wamehudhria na wale ambao hawajahudhuria kwa

ruhusa?

26- What is your contribution concerning this point?

Ni mchango upi unao kuhusu hoja hii?.

27- Mike, is there anything you would like to add?

Mike, kuna chochote ungetaka kuongeza?

28- We will be coming to that later on, Baraka you will also get the chance to speak.

Tutakuja kwa hicho baadaye, Baraka, utapata nafasi ya kuongea pia

29- In the moment, let Hamisi have his say.

Kwa sasa, Hamisi anaweza kusema.

30- I have not understood your point well.

Sijaelewa vizuri hoja yako

31- Let the secretary summarize the proposed terms.

Ebu katibu afupishe yaliyopendekezwa.

32- The meeting will be held at Serena conference hall.

Mkutano utafanyika kwenye ukumbi wa mkutano wa Serena.

33- The company president has requested that all executives and managers to attend.

Rais wa kampuni ameomba kwamba wakubwa wa kazi wote na wasimamizi

wahudhurie.

34- There is an emergency meeting at 9am tomorrow morning.

Kuna mkutano wa dharura kesho asubuhi saa tatu.

35- The meeting has been postponed to next week on Monday.

Page 8: BUSINESS KISWAHILI 2. 3. 4. 5. 6. 7. GREETINGS AND INTRODUCTION SALAMU NA KUJITAMBULISHA · Nadhani, naamini 12- What exactly do you mean when you say… Chenyewe unachomanisha ni

Mkutano umeahirishwa hadi wiki ijayo Jumatatu

36- The meeting has been rescheduled.

Wakati wa mkutano umewekwa siku nyingie.

37- The venue and time of the meeting will be informed to you in advance.

Mtajulishwa mahali na wakati wa mkutano mapema

TELEPHONING -KUPIGA SIMU

1- That’s alright.

Ni sawa

2- Sorry, wrong number

Tafadhali, namba mbovu

3- Yes, it will do well

Ndiyo, itafanya vizuri

4- I don’t have the information available now. Can you call back later?

Sina habari sasa, unaweza kunipigia baadaye?

5- I am not sure, I will find out. Can I let you know tomorrow?

Sina uhakiki, nitachunguza, ebu nikujulishe kesho?

6- Could I speak to Mr. Akida.

Naweza kuongea na Bw. Akida.

7- Mr. Smith’s office, could I speak to Mr. Mosi please.

Helo, ofisi ya Smith, ningependa kuzungumza na Mosi.

8- One moment, who is this calling?

Subiri kidogo, ni nani anayepiga?

9- Please tell Mr. Karama that we are about to deposit the money for the next order.

10- Tafadhali ambia Bw. Karama kwamba tunakaribia kuweka fedha kwa ajili ya

mzigo ufuatao..

11- Good afternoon Bruce, this is Mrs. Malika calling.

Hujambo, Bw. Bruce, huyu ni Bibi Malika anayepiga

12- My wife and I were wondering if you could join us for supper on Saturday.

Mimi na mke wangu tulikuwa tunafikiria ikiwa unaweza kujiunga na si kwa

chakula cha jioni siku ya Jumamosi.

13- We would be delighted.

Tutafurahi.

14- I want to make an appointment to see Dr. Furaha this morning please.

Ningetaka kufanya miadi ya kuonana na Daktari Furaha asubuhi hii.

15- Certainly sir, will 9:30 be alright?

16- Bila shaka Bwana, saa tatu na nusu asubuhi itakuwa sawa?

17- Yes it will do well

Ndiyo, itakuwa vizuri

18- Certainly, is Friday 11 o’clock convenient for you?

Bila shaka Ijumaa saa tano kamili itafaa?

19- The manager is out for the moment. Shall I leave him a message?

Meneja hayupo sasa. Naweza kumwachia ujumbe.

20- Am very sorry. The manager has several engagements today.

Page 9: BUSINESS KISWAHILI 2. 3. 4. 5. 6. 7. GREETINGS AND INTRODUCTION SALAMU NA KUJITAMBULISHA · Nadhani, naamini 12- What exactly do you mean when you say… Chenyewe unachomanisha ni

Samahani sana. Meneja ana shughuli kadhaa leo.

21- He is at a meeting this morning and has several appointments this afternoon.

Atakuwa kwenye mkutano leo asubuhi, na anatakuwa na miadi kadhaa mchana

huu.

22- Am sorry I will be in France then.

Samahanai nitakuwa Ufaransa siku hiyo.

23- Let us meet at the bank at 11:30pm

Hebu tukutanie kwenye benki saa tano na nusu asubuhi

24- I will call you back later.

Nitakupigia baaadye

25- Hello it’s me Sultan, can we talk.

Ni mimi Sultani, tunaweza kuongea.

26- I have sent you the data on your email, confirm and give me feedback.

Nimekutumia data kwenye barua pepe yako, tafadhali uthibitishe na unipe maoni

yako.

27- Could you ask her to call me back?

Je, unaweza kumwomba anipigie tena?

28- Does she have my name?

Je, ana nambari yangu?

29- His number is…

Nambari yake ni …

30- Is there anything else you would like to communicate?

Kuna kitu chochote ungependa kuongea?

31- The line is busy now, hold on.

32- Nambari yako iko bizi, subiri kidogo.

33- I will call you next week.

Nitakupigia wiki ijayo?

34- I’m sorry but he is away this week.

Samahani, hayuko wiki hii

35- It was cut off.

36- Simu ilikatika.

37- The network is so bad, I can’t hear what you are saying.

Mtandao unasumbua, siwezi kusikia unachosema

38- Who is speaking?

Nani anaongea?

39- Am not sure yet, I will find out. Can I let you know tomorrow?

Sina uhakika sasa, nitachunguza. Je naweza kukujulisha kesho?

40- Where are you calling from?

Unapigia wapi?

OFFICE OFISI

1- My name is Rehema, I have come to see…

Jina langu ni Rehema, nimekuja kukuona…

2- I have an appointment with you.

Page 10: BUSINESS KISWAHILI 2. 3. 4. 5. 6. 7. GREETINGS AND INTRODUCTION SALAMU NA KUJITAMBULISHA · Nadhani, naamini 12- What exactly do you mean when you say… Chenyewe unachomanisha ni

Nina miadi na wewe.

3- I will be in the office at 3pm. Let’s meet there.

Nitakuwa ofisini saa tisa mchana. Tukutane huko.

4- Our working hours are from 2am to 5pm.

Saa zetu za kazi ni kuanzia saa nane asubuhi hadi sa kumi na moja jioni.

5- Welcome to our company, how may I help you sir?

Tunakukaribisaha katika kampuni yetu, nikusaidieje?

6- Our office is on the first level room number a3.

Ofisi yetu iko kwenye chumba cha 3 gorofa la kwanza.

7- Please go around the right corridor, turn left and the first door on the left is our

offices.

Tafadhali tembelea kando ya kulia, geuka kushoto na kwenye mlango wa upande

wa kushoto ni ofisi zetu.

8- Please help me translate the sales contract into English.

Tafadhali nisaidie kutafsiri mkataba wa mauzo kwa Kiingereza.

9- Mr. Jones is not at the office now, he will be back by 1:30pm.

Bw. Johns hayuko ofisini sasa, atarudi saa saa saba na nusu mchana

10- Are you making any orders this week?

Unafanya maanunuzi yoyote wiki hii?

11- Are you working as an assistant to Mr. Jones

Je, Unafanya kama msaidizi wa Bw. Jones?

12- Please forward these documents to the secretary.

Tafadhali tuma hati hizi kwa katibu.

13- Make 3 copies on each document.

Tafadhaili tayarisha nakala tatu kwa kila hati.

14- Please lead him to the office of the accountant on the next floor.

Tafadhali mpeleke kwenye ofisi ya mhasibu kwenye ghorofa la pili

15- Could you explain to me how that mistake happened.

Unaweza kunielezea jinsi kosa hilo lilivyotokea?

16- We shall reserve a single room for each worker at the hotel.

Tutahifadhi chumba kimoja kwa kila mfanyakazi katika hoteli.

17- I will attending the seminar next week.

Nitahudhuria kongamano wiki ijayo

18- I will go with you tomorrow at approximately 5pm and will be staying for 5 days.

Nitakwenda na ninyi kesho kadri saa kumi na moja na tutaisha kwa muda wa siku

tano.

19- I would appreciate your confirmation for this reservation.

Ningependa uthibitishe kuhusu hifadhi hii.

NEGOTIATION -KUFANYA MAPATANO

1- What is the price for that machine?

Mashine hii ni bei gani?

2- The price is really high, can it be a little bit cheaper.

Page 11: BUSINESS KISWAHILI 2. 3. 4. 5. 6. 7. GREETINGS AND INTRODUCTION SALAMU NA KUJITAMBULISHA · Nadhani, naamini 12- What exactly do you mean when you say… Chenyewe unachomanisha ni

Bei iko juu sana, inaweza kuwa nafuu kidogo.

3- Our price is actually not high but it’s rational because our products are original.

Bei yetu kweli ghali, lakini ndiyo inafaa kwa sababu bidhaa zetu ni halisi.

4- The price has increased because the production costs have gone high.

Bei imeongezeka kwa sababu gharama za uzalishaji zimeenda juu.

5- The price has increased because our products are original.

Bei imeongezeka kwasababu bidhaa zetu ni halisi

6- This is very long lasting and strong, am sure you will love it.

Hii inadumu sana, ni imara, na nina uhakika utaipenda.

7- We shall be able to deliver the products to your shop next week.

Tutaweza kuleta bidhaa kwa duka lako wiki ijayo.

8- I will then give you a two year guarantee

Halafu nitakupatia dhamana ya miaka miwili.

9- We always deliver all the goods in time.

Sisi huleta bidhaa zako zote bila kuchelewa.

10- Are you making any purchase this week?

Je, unafanya ununuzi wowote wiki hii?

11- Every bag weighs exactly 50 kilograms.

Kila gunia ina uzito wa kilo hamsini kamili.

12- The products you sent haven’t reached at our store yet.

Bidhaa ambazo umetuma hazijafika kwenye stoa yetu bado.

13- If you buy a full packet I will give you a discount.

Ukinunua pakiti kamili nitakutolea punguzo.

14- You should pay a deposit of 50% today.

Unapaswa kulipa weko la asilimia hamsini leo.

15- Actually our price is still low compared to the price of other companies.

Kusema ukweli, bei bado ni nafuu ukilinganisha na bei ya makampuni mengine.

16- The dollar rate isn’t stable and that affects the price.

Kiwango cha dola si imara na hilo lanaathiri bei

17- Am sorry but I cannot continue to supply you at that price.

Ninasikitika kwamba sitaweza kuedelea kukupa bidhaa kwa bei hiyo.

18- If you were prepared to…, we might be able to…

Kama ungekuwa tayari… tunaweza kuwa….

19- We are ready to accept your offer.

Tuko tayari kukubali ununuzi wako.

20- However there will be one condition.

Hata hivyo kutakuwa sharti moja.

21- That sounds reasonable, I can agree to that.

Inasikika kuwa sababu nzuri, naweza kukubaliana na hilo.

22- I think we have reached an agreement.

Nadhani tumeafikiana.

23- Have I left anything out?

Je, kuna chochote nimeacha?

Page 12: BUSINESS KISWAHILI 2. 3. 4. 5. 6. 7. GREETINGS AND INTRODUCTION SALAMU NA KUJITAMBULISHA · Nadhani, naamini 12- What exactly do you mean when you say… Chenyewe unachomanisha ni

WORKING WITH THE CLIENT - KUSHUGULISHA MTEJA

1- Iam visiting the factory site on Monday.

Natembelea mahali pa kiwanda Jumatatu.

2- Why do you think I should put my money in the bank?

Kwa nini unadhani na lazima niweke fedha zangu katika benki?

3- But has it got any customers yet?

Je, Bado ina wateja wowote?

4- What do I do next?

Nifanye nini baadaye?

5- Why is this better than the current accounts?

Kwanini hii ni bora kuliko akaunti zote zilizo?

6- But why has your bank got many customers?

Kwa nini benki yenu ina wateja wengi?

7- We give you cheque book and we put interest on your savings monthly.

Tunakupa kitabu cha hundi na tunakuwekea riba katika akiba yako kila mwezi.

8- Thank you for your attention to this matter.

Asante sana kwa umakini wako juu ya suala hili.

9- Please fill that form, sign on it and let it be stamped.

Tafadhari jaza fomu hiyo, tia sahihi na ipigwe stempu

10- I have been your regular customer for a number of years.

Nimekuwa mteja wako wa kawaida kwa miaka kadhaa.

11- I have found your personnel so helpful.

Nimegundua kwamba wafanyakazi wako wanasaidia.

12- I would like to do business with you for a long-term.

Ningependa kufanya biashara nawe kwa muda mrefu.

13- Is it possible to supply me with two trucks every week?

Inawezekana kunipa gari mbili kila wiki

14- We shall help you and handle all the exportation process.

Tutawasaidia na kushughulikia mchakato wote wa kusafirisha

15- Communicate to our export agent.

Wasiliana na mwakilishi wetu wa mauzo ya kusafirisha nje.

16- You may deposit the money either on the dollar account or the shilling account.

Unaweza kuweka fedha ama kwenye akaunti ya dola au ya shilingi.

17- I would like to deposit money today for 200 pieces of timber.

Ningependa kuweka pesa za vipande mia mbili vya mbao.

18- When shall my products be ready if I pay the money today?

Je, bidha zangu zitakuwa tayari wakati nikilipa fedha leo?

19- You have delayed to send my products.

Umechelewa kutuma bidhaa zangu.

20- We agreed that I would receive the products by this Sunday but I haven’t yet.

Tulikubaliana kwamba ningepokea bidhaa Jumapili hii lakini bado sijapokea.

Page 13: BUSINESS KISWAHILI 2. 3. 4. 5. 6. 7. GREETINGS AND INTRODUCTION SALAMU NA KUJITAMBULISHA · Nadhani, naamini 12- What exactly do you mean when you say… Chenyewe unachomanisha ni

21- We got some challenges and we are sorry for the inconveniences caused.

Tumekuwa na changamoto fulani na tunasikitika kwa hali zozote

zilizosababishwa.

22- The goods you sent us last week were all expired.

Bidhaa zote zilizotumwa wiki iliyopita zilikuwa zimepitwa na wakati.

23- These are damaged goods.

Bidhaa hizi zimeharibika.

24- That’s an excellent point, I totally agree with you on that.

Hiyo ni wazo zuri, naafikiana nawe kabisa juu ya jambo hilo.

25- Yes I get what you are saying.

Ndiyo ninaelewa unachosema.

26- From my own perspective, it’s a little different. Let me explain.

Kulingana na mtazamo wangu, ni tofauti kidogo, hebu nikuelezee

PRESENTATION - MAWASILISHO

1- On behalf of the company, I would like to welcome you here today.

Kwa niaba ya kampuni, napenda kuwakaribisha hapa leo.

2- My name is Shujaa and am the CEO of kampala Kasino

Jina langu ni Shujaa, mimi ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampala Kasino

3- Am delighted to be here today to talk to you about…..

Nafurafihi kuwa hapa leo ili kuzungumza nanyi kuhusu….

4- I would like to introduce my colleague anne.

Ningependa kumtambulisha mwenzangu Anne.

5- I would like to take this opportunity to.

Ningependa kuchukua fursa hii…

6- I will begin with, then I will look at

Nitaanza na, basi nitaangalia

7- Next…

Ifuatayo…..

8- My talk is divided into 3 parts

Majadiliano yangu imegawanyika katika sehemu tatu

9- I would like to give you some background information about,

Ningetaka kuwapa asili ya habari kuhusu

10- Before I start, does anyone know..?

Kabla sijaanza, je, kuna yeyote anayejua…?

11- As you are all aware, as you all know…

Kama mnavyofahamu, mnavyojua……..

12- Right, let’s move on to…

Sawa, hebu tuendelee

13- This leads me to the next point which is…

Hii inatutambulishia kwenye hatua inayofuata….

14- I would now like to look at…

Sasa ningependa kuangalia …

Page 14: BUSINESS KISWAHILI 2. 3. 4. 5. 6. 7. GREETINGS AND INTRODUCTION SALAMU NA KUJITAMBULISHA · Nadhani, naamini 12- What exactly do you mean when you say… Chenyewe unachomanisha ni

15- Does anyone have any questions before I move on?

Je, kuna mtu yeyote ana maswali kabla sijaendelea

16- To sum up..

Kujumlisha

17- To summarize the main points of my talk..

Kwa muhtasari wa hoja kuu ya majadiliano yangu.

18- Just a quick recap of my main points.

Kwa kurejea haraka kwa hoja zangu

19- Is there anyone with any questions?

Je, kuna yeyote anaye maswali?

20- I will be happy to answer your questions now.

Nitafurahi kujibu mawali yenu sasa.

21- If you have questions, please don’t hesitate to ask,

Ikiwa una maswali, tafadhali usisite kuuliza

22- I would like to conclude by…

Ningependa kuhitimisha kwa…..

23- That brings me to the end of the presentation.

Huu ndio mwisho wa mawasilisho yangu

24- Thank you all for listening.

Asanteni kwa kunisikiliza

25- Thank you for your attention. It was a pleasure being here today.

Asante kwa kuwa makini, imekuwa furaha yangu kuwa hapa leo.

26- Finally…

Hatimaye….

27- After that

Baadaye………

28- Now turning to the point.

Tukiruduia kwa hoja kuu.

29- Now let’s look at

Ebu tuangalie…

30- So, in conclusion

Kwa, kuhitimisha

31- The graph shows…

Mchoro unaonyesha…

32- The aim of this presentation is to

Lengo la uwashilishaji huu ni…

33- First

Kwanza

34- Am going to talk about

Nitazungumza juu ya

35- In conclusion, we can say that

Kwa kuhitimisha, tunaweza kusema

36- As you can see from this picture.

Kama mnavyoona kwenye picha hii.

Page 15: BUSINESS KISWAHILI 2. 3. 4. 5. 6. 7. GREETINGS AND INTRODUCTION SALAMU NA KUJITAMBULISHA · Nadhani, naamini 12- What exactly do you mean when you say… Chenyewe unachomanisha ni

37- Good morning ladies and gentlemen, I welcome everyone in today’s meeting.

Hamjambo mabibi na mabwana, nawakaribisha nyote kwenye mkutano huu.

38- To express our gratitude, we shall offer a bonus to every employee.

Kwa ajili ya kutoa shukurani zetu, tutatoa nyongeza kwa kila mfanyakazi

39- I thank everyone for what you have done to make the year successful.

Nawashukuru kwa yale yote mmefanya ili kufanikisha mwaka huu

40- Best wishes for a healthy and happy new year.

Nawatakia afya njema ya mwaka mpya

41- Let’s congratulate Mr. Alex for this achievement and the best wishes for his

future in our company.

Tunampongeza Bw.Alex kwa ufanisi huu na tunakutakia mema siku zijazo katika

Kampuni yetu.

TRADE AND EXCHANGE - BIASHARA NA UBADILISHANAJI

1. I am broke, could you lend me some money.

Sina pesa, unaweza kunipa mkopo?

2. I will give you a loan of 1m.

Nitakupa mkopo wa milioni moja

3. How much interest shall you give monthly?

Unalipa kiasi gani cha riba kila mwezi?

4. The purpose of this insurance is to provide financial compensation to people.

Madhumuni ya bima hii ni kutoa fidia ya kifedha kwa watu

5. I would like to exchange shillings with dollars?

Ningependa kubadilishana shilingi na dola?

6. I would like to get a change of 1 million shillings?

Ningependa kupata chenji ya shilingi milioni moja?

7. How much is the profit that we made on this transaction?

Je, ni kiasi gani cha faida tuliyofanya katika shughuli hii?

8. The cost of making this product is high.

Gharama ya kufanya bidhaa hii ni ya juu.

9. We are not in business if we don’t make any profit.

Hatuko kwenye biashara kama hatupati faida.

10. Nations import goods they lack and export goods that they can produce

efficiently.

Mataifa huagiza bidhaa ambazo hazipo na kuhamisha bidhaa ambazo zinaweza

kuzalisha kwa ufanisi.

11. We lack enough resources to produce goods domestically.

12. Hatuna rasilimali za kutosha ili kuzalisha bidhaa nyumbani.

JOB INTERVIEW- MAHOJIANO YA KAZI

1. Ourcompany is recruiting new workers this month.

Kampuni yetu inaajiri wafanyakazi wapya mwezi huu.

2. We are looking for language specialists who will help us ease communication.

Page 16: BUSINESS KISWAHILI 2. 3. 4. 5. 6. 7. GREETINGS AND INTRODUCTION SALAMU NA KUJITAMBULISHA · Nadhani, naamini 12- What exactly do you mean when you say… Chenyewe unachomanisha ni

Tunatafuta wataalam wa lugha ambao watatusaidia katika kurahisha mawasiliano.

3. We need a leading manufacturer of pharmaceutical products based in Uganda.

Tunahitaaji mtengenezaji mkuu wa bidhaa za dawa nchini Uganda.

4. This opportunity is still available and the salary is negotiable.

Fursa hii bado ipo na mshahara ni kujadiliana.

5. Language skills and teaching experience is an added advantage.

Ujuzi wa lugha na uzoefu wa kufundisha ni faida nyingine.

6. Applicants should have a good academic background with a sound historical and

geographical knowledge.

Waombaji wanapaswa kuwa na historia nzuri ya kitaaluma na ujuzi wa kihistoria

na kijiografia.

7. You will then be allowed to sign a contract not less than two years.

Basi utaruhusiwa kusaini mkataba katika siku mbili.

8. You must be fluent in at least two European languages.

Lazima uwe na ufasaha wa lugha katika angalau lugha mbili za ulaya.

9. You must be having an experience of at least two years in the interpretation field

Lazima uwe na uzoefu wa angalau miaka miwili katika uwanja wa tafsiri.

10. All the applicants should be willing to take on the responsibility.

Waombaji wote wanapaswa kuwa tayari kuchukua jukumu.

11. We need a news reporter who is presentable and has a good speaking manner.

Tunahitaji mwandishi wa habari ambaye anayeonakana vizuri na ana mbinu nzuri

ya kuzungumza.

12. He should be able to work quickly and effectively under pressure.

Anapaswa kuwa na uwezo wa kufanya kazi haraka na ufanisi chini ya shinikizo.

13. We are pleased to announce the appointment of Mr. Peter as the vice president.

Tunafurahi ya kutangaza uteuzi wa Bw. Peter kama msaidizi wa rais.

14 Peter has been assistant manager for 6 years, she earned a master’s degree in

business administration.

Peter amekuwa msaidizi wa mkurugenzi kwa miaka sita, na alipata shahada ya

uzamili katika uchumi.

15. We are looking for an ambitious, qualified accountant aged 24-28 with several

years in the oil industry.

Tunatafuta mhasibu mwenye ujasiri mwenye ujuzi na mwenye umri wa miaka

24-28 na uzoefu wa miaka kadhaa katika kampuni ya mafuta.

16. I’m preparing to go for the job interview at 4PM.

Ninajiandaa kwenda kwa mahojiano ya kazi saa kumi.

17. My interview was successful and I will start working next week.

Mahojiano yangu yalifanikiwa na nitaanza kufanya kazi wiki ijayo

18. What is your salary expectation?

Unatarajia kiasi gani cha mshahara?

19. I am applying for a teaching job in your school.

Naomba kazi ya kufundisha katika shule yako.

20. This is a well-paying job and you will be working in shifts.

Kazi inalipwa vizuri na utakuwa ukifanya kazi kwa zamu.

Page 17: BUSINESS KISWAHILI 2. 3. 4. 5. 6. 7. GREETINGS AND INTRODUCTION SALAMU NA KUJITAMBULISHA · Nadhani, naamini 12- What exactly do you mean when you say… Chenyewe unachomanisha ni

21. I would like to work as a part time worker and later as fulltime worker after I

finish school.

Ningependa kufanya kazi ya wakati wote halafu nifanye kazi ya muda baada ya

kumaliza masomo.

22. I don’t have a driving license but I can get it anytime.

Sina cheti cha kuendesha gari lakini naweza kukipata wakati wote.

23. There is job security and you will be a satisfied with it.

Kuna usalama wa kazi na utaridhika na hilo.

24. I read your job advertisement in the newspaper and that’s why I sent in my

application.

Nilisoma tangazo lako la kazi katika gazeti na iyo sababu nimetuma maombi

yangu.

25. Please write an application letter and attach it to your CV.

Tafadhali andika barua ya maombi na uambatanishe na maelezo binafsi yako.

26. I have come along with my recommendation letter.

Nimekuja pamoja na barua yangu ya pendekezo

27. I believe in myself and I always never give up on my dreams.

Najiamimi na sikatii tamaa kwa ndoto zangu.

28. Please read through my curriculum vitae.

Tafadhali soma na upitie kwenye maelezo binafsi yangu.

29. I’m so pleased that I was called for this interview.

Ninafurahi kwamba niliitwa kwa mahojiano ya kazi.

30. I am applying for a sales manager position.

Naomba nafasi ya meneja wa mauzo.

31. Inside the envelope arze my original documents.

Ndani ya bahasha ni hati zangu za awali.

32. I graduated from Makerere University with a degree of arts with education.

Nilifuzu masomo kutoka chuo kikuu cha Makerere na shahada ya sanaa na

ualimu.

33. I am sure that my enthusiasm and experience will contribute on the job

performance.

Nina uhakika kuwa shauku yangu na uzoefu wangu utachangia makubwa katika

utendaji wa kazi.

34. I was working with a construction company for 3 years.

Nilikuwa nafanya kazi na kampuni ya ujenzi kwa miaka mitatu.

BANKING AND FINANCE - BENKI NA FEDHA

1- Your employer can pay your salary directly to your bank account.

Mwajiri wako anaweza kulipa mshahara wako kwenye akaunti yako

2. You can pay all your water and electricity bills on the phone.

Unaweza kulipia huduma za maji na umeme kwenye simu.

3. You will have the authority to withdraw your money anytime you want.

Una mamlaka ya kutoa fedha zako wakati wowote.

4. Our bank is the best in the country.

Page 18: BUSINESS KISWAHILI 2. 3. 4. 5. 6. 7. GREETINGS AND INTRODUCTION SALAMU NA KUJITAMBULISHA · Nadhani, naamini 12- What exactly do you mean when you say… Chenyewe unachomanisha ni

Benki yetu ni bora Zaidi nchini.

5. In order to save time in writing cheques, this card is accepted in many shops.

Ili kuokoa wakati wa kuandika hundi kadi hii inakubaliwa katika maduka mengi.

6. The amount is debited from your account.

Kiasi cha fedhaa kinatolewa kwenye akaunti yako.

7. You don’t have to spend a lot of time queuing in the bank.

Hutaki kupoteza muda ukipiga msururu benkini.

8. It is easy and convenient to get loans.

Ni rahisi kupata mkopo.

9. You don’t need to make an appointment with the bank manager.

Huhitaji kufanya miadi na meneja wa benki.

10. Simply call us when you want to transact any business.

Tupigie wakati wowote unaotaka kufanya biashara yeyote.

11. We are available 24 hours a day.

Sisi tuko tayari masaa 24 kila siku.

12. We don’t incur any charges on the transactions you make with our bank.

Hatuna ada yoyote tunayotoza juu ya shuguli unazofanya na benki yetu.

13. This will give you freedom over your finances and the freedom to your time as

you wish.

Hii itakupa uhuru juu ya fedhaa zako na uhuru wa kutumia wakati wako kama

unavyotaka

14. You can withdraw money anytime you want.

Unaweza kutoa pesa wakati wowote unaaotaka.

15. You cannot have this service anywhere else.

Huwezi kuwa a huduma hii popote pengine.

16. This is a unique service because it pays you high interest rate.

Hii ni huduma ya kipekee kwa sababu inakulipa kiwango cha juu cha riba .

17. The higher the balance on your account, the higher the rate of interest you can

earn.

18. Wingi wa mabaki katika akaunti yako, unaathiri kiwango cha riba unachoweza

kupata.

19. I would like to get insurance for my company.

Ningependa kupata bima kwa kampuni yangu.

20. Banks loan money and charge interest on the loans.

Benki hukopesha fedha na malipo ya riba kwa mkopo.

MARKETING - UTANGAZAJI WA BIDHAA

1- You have to do the market research very well.

Unapaswa kufanya utafiti wa soko vizuri sana.

2- We must satisfy the customers’ needs and achieve our company objectives.

Lazima tukidhi mahitaji ya wateja na kufikia malengo ya kampuni yetu.

3- You are in charge of marketing our products.

Wewe ndiye msimamizi wa utangazaji wa bidhaa zetu.

Page 19: BUSINESS KISWAHILI 2. 3. 4. 5. 6. 7. GREETINGS AND INTRODUCTION SALAMU NA KUJITAMBULISHA · Nadhani, naamini 12- What exactly do you mean when you say… Chenyewe unachomanisha ni

4- Each one plays a vital role in the success or failure in the market operation.

Kila mtu ana jukumu ya kufanya katika mafanikio au kushindwa kazi za soko.

5- The company may charge below the prices that the competitors are charging.

Kumpuni inaweza kutoza bei ya chini kuliko ya washindani.

6- There should always be a connection between the manufacturer, wholesaler

retailer and the customer.

Lazima kuwe na uhusiano kati ya mtengenezaji, muuzaji wa jumla na wateja.

7- Wholesalers generally sell large quantities of products to retailers.

Wauzaji wa jumla huuza bidhaa nyingi kwa wauzaji wa rejareja.

8- Retailers usually sell small quantities to customers.

Wauzaji wa rejareja mara nyingi huuza kwa uchache.

9- The communication between the seller and the buyer is important and should be

maintained.

Mawasliano kati ya muuzaji na mnunuzi ni muhimu na yanapaswa kuwa imara.

10- We may advertise through the newspaper.

Tunaweza kutangaza kupitia kwenye magazeti.

11- We should work together to develop a successful marketing operation.

Tunapaswa kufanya kazi pamoja ili kuendeleza uendeshaji wa masoko kwa

mfulilizo.

12- Our marketing operation should satisfy customers and achieve the company’s

objectives.

Oporesheni yetu ya uuzaji inapaswa kukidhi mahitaji ya wateja na kufikia

malengo ya kampuni.

13- What other advertising media are there besides magazines and newspapers?

Je, kuna vyombo vya utangazaji baina ya magazeti?

14- We might encounter some marketing problems in the process and we must

overcome them

Tunaweza kukutana na baadhi ya matatatizo ya uuzaji katika mchakato na ni

lazima tuyashinde

15- The products in our store is not enough.

Bidhaa kwenye stoa zetu hazitoshi.

16- The sale clerk must not be rude to customers.

Muuzaji hapaswi kuwa mkali kwa wateja.

17- The product is sold during the wrong season.

Bidhaa inauzwa wakati wa msimu usiofaa.

18- The product is of a very high quality.

Bidhaa ni bora sana

19- The price of the product increases faster than the rate of inflation.

Bei ya bidhaa huongezeka kwa kasi, zaidi kuliko kiwango cha mufumuko wa

bei.

20- Who is going to buy the product?

Nani atanunua bidhaa?

21- What is the potential to sell this product?

Nani ana uwezo a kuuza bidhaa hii?

Page 20: BUSINESS KISWAHILI 2. 3. 4. 5. 6. 7. GREETINGS AND INTRODUCTION SALAMU NA KUJITAMBULISHA · Nadhani, naamini 12- What exactly do you mean when you say… Chenyewe unachomanisha ni

22- Which type of promotion appeals to you most.

Ni aina gani ya utangazaji inayokupendeza?

23- Could it be radio, television, magazine or newspaper advertising?

Inaweza kuwa redio, televisheni, magazeti au gazeti la matangazo.

IMMERSION

Dialojia -DIALOGUE

1.Muuzaji: Bei Rahisi! Bei rahisi!

Low price! Low price!

2.Mteja: Unauza huu mkoba pesa ngapi?

How much do you sell this bag?

3.Muuzaji: Hiyo ni shilingi elfu hamsini rafiki yangu.

Its fifty thousand my friend.

4.Mteja: Huwezi kunipunguzia. Niuzie elfu thelathini hivi.

Can’t you reduce for me.you can sell it to me at only forty thousand shillings.

5.Muuzaji: Haiwezekani mtu wangu, ninapata hasara nikiuza hivyo. Ongeza

kidogo dada?

Its impossible my friend, I make a loss when I sell it like that. Just add a little money.

6.Mteja: Basi elfu arobaine na tano.

Okay forty thousand shillings.

7.Muuzaji: Tafadhali ongeza kitu kidogo, unataka nikule hasara leo? Fikisha

elfu arobaine na tano.

Please add some some money, Doyou want me to get aloss today? You can bring forty

five thousand shillings.

8.Mteja: Basi sitanunua hii, sina pesa hizo zote. Unajua uchumi ni mbaya sana

siku hizi.

Okay I wont buy this bag, I don’t have all that money. You know the economy is bad

nowadays.

9. Muuzaji: Tafadhali mtu wangu, huu mkoba ni mzuri sana. Umetoka Tanzania,

angalia. Unaweka pesa hapa, halafu unafunga hivi. Huwezi kupoteza kitu

chochote ukiwa na mkoba huu. Angalia wewe mwenyewe. Hakuna mahali

pengine utaweza kununua mkoba huu bei nafuu kama hii.

Please my friend, this bag is so nice. It came from Tanzania?see, you can keep here

you money then close like this, you can’t lose anything with this bag. Just have a look.

There is no any other place where you can get this bag at a low price.

10. Mteja; Nakwambia sina hizo pesa. Nitanunua baadaye ukipunguza bei.

Iam telling you I don’t have all that money. I will buy when you reduce for me.

11. Muuzaji: Leta elfu arobaine. Lakini utakuwa umeniumiza. Nakufanyia hivyo

kwa kuwa ni wewe mteja poa.

Bring forty thousand shillings. But you will have pressed me. Iam doing all this for

you because you are a good customer.

12. Mteja: Sawa, basi nitanunua elfu arobaini.

Page 21: BUSINESS KISWAHILI 2. 3. 4. 5. 6. 7. GREETINGS AND INTRODUCTION SALAMU NA KUJITAMBULISHA · Nadhani, naamini 12- What exactly do you mean when you say… Chenyewe unachomanisha ni

Alright, I will buy it at forty thousand shillings

13. Muuzaji: Ahsante mteja wangu. Mungu akubariki.

Thank you very much my customer. May God bless you.