BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA...

258
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI Kikao cha Tano – Tarehe 5 Februari, 2018 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa tukae, Katibu. NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: KIAPO CHA UAMINIFU Mhe. Dkt. Adelardus Lubango Kilangi NAIBU SPIKA: Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- MHE. MOSHI S. KAKOSO - K.n.y MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.

Transcript of BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

1

BUNGE LA TANZANIA____________

MAJADILIANO YA BUNGE___________

MKUTANO WA KUMI

Kikao cha Tano – Tarehe 5 Februari, 2018

(Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Naibu Spika (Mhe. Tulia Ackson) Alisoma Dua

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa tukae, Katibu.

NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE:

KIAPO CHA UAMINIFU

Mhe. Dkt. Adelardus Lubango Kilangi

NAIBU SPIKA: Katibu!

NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU MEZANI:

HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI

Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:-

MHE. MOSHI S. KAKOSO - K.n.y MWENYEKITI WAKAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU:

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge yaMiundombinu kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

2

MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA - K.n.y MWENYEKITIWA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI:

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati naMadini kuhusu shughuli za kamati kwa mwaka 2017.

NAIBU SPIKA: Katibu!

NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU MEZANI:

MASWALI NA MAJIBU

Na. 55

Changamoto Zinazowakabili Walemavu

MHE. OSCAR R. MUKASA aliuliza:-

Watanzania wenye ulemavu wanakabiliwa na kerombalimbali za kimaisha ikiwemo ukosefu wa ajira kama ilivyokwa Watanzania wengine, aidha, zipo changamoto za jumlakama vile kijana mwenye ulemavu wa ngozi asiye na ajiraana changamoto ya mahitaji ya kujikimu na pia anachangamoto za kipekee za mahitaji ya kiafya na kiusalama.

Je, Serikali inatoa kauli gani kuhusu umuhimu wakuwatazama vijana wenye ulemavu mbalimbali kwa namnaya pekee na kama zipo sera na mikakati ya kiujumla kwavijana wote nchini?

NAIBU SPIKA: Ofisi ya Waziri Mkuu sijui nani anayejibumaswali.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, WATU WENYEULEMAVU: Mheshimiwa Naibu Spika, niko hapa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Ikupa Alex, Naibu Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu, Walemavu.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

3

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, WATU WENYEULEMAVU alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuunaomba kujibu swali la Mheshimiwa Oscar Rwegasira Mukasa,Mbunge wa Biharamulo Magharibi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua vijanawenye ulemavu kuwa ni kundi mojawapo miongoni mwaWatanzania wenye ulemavu nchini ambalo linakabiliwa nachangamoto mbalimbali zinazorudisha nyuma maendeleoyao. Mojawapo ya changamoto hizo ni ukosefu wa ajira,huduma za afya, uwezo mdogo wa kuyamudu mahitaji yakujikimu, umaskini na changamoto ya kiusalama.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kutambua umuhimuwa kundi hili la watu wenye ulemavu wakiwemo vijanawenye ulemavu, Serikali iliunda Baraza la Taifa la Watu WenyeUlemavu ambalo kazi yake kubwa ni kutoa ushauri kwaSerikali na wadau mbalimbali wanaohusika na masuala yawatu wenye ulemavu juu ya namna bora ya kushughulikiachangamoto zao, kuzijumuisha zile za kundi la vijana wenyeulemavu.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, Serikali imeendeleakuunda Kamati za Wenye Ulemavu kuanzia ngazi ya Mkoa,Halmashauri ya Wilaya, Kata na Mtaa/Kijiji. Kazi kubwa yaKamati hizi ni kuhakikisha kuwa masuala ya watu wenyeulemavu yanazingatiwa katika mipango yote ili kuondoa kerombalimbali wanazokumbana nazo ikiwa ni pamoja namasuala yanayohusu elimu, ajira, afya na mikopo yauwezeshaji wananchi kiuchumi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo, nichukue pia fursahii kuwakumbusha na kuwahimiza Wakurugenzi waHalmashauri zote nchini kusimamia ipasavyo utekelezaji wasuala hili ambalo liko kisheria na pia ikizingatiwa kuwamaagizo kadhaa yamekwishatolewa kwa maneno na kwamaandishi.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

4

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kwa kushirikiana nawadau mbalimbali imeendelea kuboresha vyuo vya mafunzoya ufundi vya watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kuajiriwana kijiajiri na kupata ujuzi mbadala wa kumudu maisha yao.

MHE. OSCAR R. MUKASA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru na naishukuru Serikali kwa majibu yake, ninamaswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, moja natambua jitihadaza Serikali za kuweka mfumo kwa aji l i ya kuwafikiawalemavu, lakini suala la mfumo ni moja na suala la kufikishahuduma wanazohitaji kwa maana ya kuwafanyia upendeleochanya (positive discrimination) ni lingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni kwa namna ganiSerikali sasa imeweza kuwafikishia rasilimali fedha na rasilimalimafunzo watu wenye ulemavu kwenye vikundi vyao, tofautina kuwajumuisha kwenye vikundi vingine ambapo mahitajiyao mahususi hayawezi kutimizwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwa namna gani na kwakiwango gani Serikali inadhani inaweza kuwapatia nafuukwenye yale mambo ya msingi kwa mfano Bima ya Afya.Tuchukulie mfano mlemavu wa ngozi akipata ruzuku kwenyebima ya afya una uhakika wa kuhakikisha anakingwa kwabima, kitu ambacho anakihitaji kama Watanzania wenginelakini yeye anakihitaji zaidi? Nakushukuru sana.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya WaziriMkuu, Ulemavu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, WATU WENYEULEMAVU: Mheshimiwa Naibu Spika, kabla sijajibunimpongeze sana kwa jinsi ambavyo anafuatil ia nakushughulikia masuala ya watu wenye ulemavu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanzalinauliza ni jinsi gani Serikali imeweza kuwapatia vikundi vyawatu wenye ulemavu fedha. Niki-refer kwamba swali lake

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

5

lilikuwa linauliza kwa habari ya vijana; kuna mfuko wamaendeleo ya vijana ambao mfuko huu unawawezeshavijana.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nielezee kidogokwamba kinachotakiwa kufanyika ni kwamba vijanawanatakiwa wajiunge kwenye vikundi, wakishajiungakwenye vikundi mbalimbali, kwenye maeneo yalipowanatakiwa pia kuwe na SACCOS. Kwa hiyo, kama Serikalitunapeleka hela kwenye zile SACCOS halafu baada yakupeleka hela kwenye zile SACCOS vile vikundi vinapewakupitia zile SACCOS.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kufanya hivyo kikubwaambacho kinapatikana kwenye hivi vikundi ni kwambawakati ule wa kurejesha wanatakiwa warejeshe riba yaasilimia 10. Katika hiyo riba ya asilimia 10, asilimia tano inabakikwenye kikundi husika, asilimia mbili inabaki kwenyeHalmashauri na asilimia tatu inaenda Serikalini. Kwa hiyo, hiyoni njia mojawapo ambayo kama Serikali tunavipatia hivivikundi fedha lakini pia kuna hii mifuko ya uwezeshaji kiuchumiwananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kikubwaambacho ninapenda niongelee hapa, nitoe wito kwaHalmashauri mbalimbali wawahamasishe watu wenyeulemavu kujiunga kwenye vikundi, kwa sababu hizi hazitolewikwa matu mmoja mmoja. Wawahamasishe watu wenyeulemavu kujiunga kwenye vikundi, yakiwepo makundi yavijana lakini pia na makundi mengine ambayo sio ya vijanaili waweze kunufaika na hizi fedha ambazo zinatolewa naSerikali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia ameongelea kwaupande wa afya, kwa upande wa afya ametolea mfanowa watu wenye ualbino. Kwa upande wa watu wenyeualbino tayari Serikali imekwisha kuziagiza Halmashaurikwamba zinapoagiza dawa kutoka MSD zihakikishezinajumuisha mafuta ya watu wenye ualbino katika madawaambayo wanaagiza. (Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

6

Mheshimiwa Naibu Spika, jingine la pili ameongeleakwamba kwanini Serikali haitoi bima ya afya kwa watu wenyeulemavu. Niseme wazi kwamba Serikali, hicho ni kituambacho kama Serikali tunakichukua, hatuna specifickwamba hii ni bima ya afya kwa ajili ya watu wenye ulemavu.Lakini watu wenye ulemavu wasiokuwa na uwezowanatibiwa baada ya kutambulika kwamba hawa watuhawana uwezo wa kugharamia mahitaji yao. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kabla sijampanafasi Mheshimiwa Ally Saleh ya kuuliza swali la nyongeza,naomba maswali ya nyongeza yawe mafupi ili wengi tupatefursa ya kuuliza maswali. Ukishauliza swali refu leo hii nitakuwanatakata hapa kwa sababu Waheshimiwa Wabungemnaotaka kuuliza mpo wengi, sasa mkitumia muda mrefukujieleza muda wote unaisha kwenye maelezo, wenginekwenye swali la nyongeza unataka utoe na mfano.Mheshimiwa Ally Saleh.

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante. Jana tu nilimpongeza Waziri Mkuu kwenye twitterkwa tamko lake ambalo limesema kila Wizara na Idara itoetaarifa kila mwaka imetenga kiasi gani kwenye kuimarishahuduma kwa watu wanaoishi na ulemavu. Nafikiri hili nitamko zuri sana na linafaa kupongezwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, je, Serikali imejipangaje,utaratibu huu tutaanza kuuona katika mwaka huu wafedha? (Makofi)

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, WATU WENYEULEMAVU: Mheshimiwa Naibu Spika, utaratibu huu kamaSerikali tumeu-plan kwamba uanze kuonekana katika bajetiya mwaka huu wa fedha. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Sasa mmeshaona mifano hapa, ninyiambao bado mmesimama. Mheshimiwa Badwel swali lanyongeza.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

7

MHE. OMARY A. BADWEL: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi na niweze kuuliza swali dogola nyongeza.

Kwa kuwa hawa walemavu ili waweze kupata hiziajira na huduma zingine mbalimbali ni lazima wapiti shule,vyuo na taasisi zingine ili waweze kukubalika katika hili eneola ajira. Sasa kwa kuwa wanapitia katika shule mbalimbaliambazo zina matatizo mengi na inawafanya wasiwezekupata elimu vizuri kwa mfano Shule ya Viziwi Kigwe ambayohakuna maji kwa muda mrefu na shule ile ni ya kitaifa nainachukua wanafunzi wengi.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuwapelekea majiwanafunzi wa shule ya wasiosikia Kigwe? (Makofi)

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, WATU WENYEULEMAVU: Mheshimiwa Naibu Spika, kama Serikali nisemekwamba hilo tumelichukua na kwa sababu ni sualamtambuka, tutafanya mawasiliano ndani ya Serikali kwamaana Wizara ya Maji ili tuweze kuona jinsi gani tunawezatukapeleka maji katika Shule ya Kigwe, ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tutaendeleena Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mheshimiwa Daimu Iddi Mpakate,Mbunge wa Tunduru Kusini sasa aulize swali lake.

Na. 56

Kituo cha Afya Mtina

MHE. DAIMU I. MPAKATE aliuliza:-

Katika Jimbo la Tunduru Kusini kuna vituo vitatu vyaafya ambapo Kituo cha Afya Mtina kina zaidi ya miaka 30hakijafanyiwa ukarabati na pia hakuna wodi ya wazazi.

Je, ni lini Serikali itajenga wodi ya wazazi katika kituohicho na kufanya ukarabati ili kiweze kutoa huduma borakwa wakazi wa Kata za Nasya, Semeni, Nyerere, Angalia na

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

8

wakazi wa Kata ya Mchesi, Vijiji vya Likumbula, Tuwemachona Namasakata?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba kujibu swali laMheshimiwa Daimu Iddi Mpakate, Mbunge wa Tunduru Kusinikama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Wilaya yaTunduru ina vituo vitano ambapo vituo vya afya viwili vipokatika Jimbo la Tunduru Kusini na vitatu katika Jimbo laTunduru Kaskazini. Kituo cha Afya Mtina kilianzishwa mnamomwaka 1970 na kimekuwa kikiendelea kutoa huduma zakujifungua na huduma za matibabu ya kawaida kwa kipindichote. Kwa sasa chumba cha kupumzikia akina mamabaada ya kujifungua kimetengwa ndani ya wodi ya kawaidaya wanawake. Serikali kupitia wadau wa maendeleo (WalterReed Program) waliweza kufanya ukarabati wa jengo la tibana matunzo (CTC) kwa wagonjwa wanaoishi na virusi vyaUKIMWI.

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa msingi wa wodiya wazazi katika Kituo cha Afya Mtina unaendelea kupitiafedha za Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo laTunduru Kusini ambapo kiasi cha shilingi milioni nne zilitolewa.Aidha, Halmashauri katika bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 imetenga kiasi cha shilingi milioni 10 kwa ajili ya ukarabatina kuboresha Kituo cha Afya Mtina.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, katikakuboresha huduma za afya kwa wananchi wa Tunduru,Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/2018 imeipatiaHalmashauri ya Wilaya ya Tunduru kiasi cha shilingi milioni400 kwa ajili ya ukarabati wa Kituo cha Afya Mkasale kilichopokatika Jimbo la Tunduru Kusini. Aidha, Halmashauri inajengawodi mbili za upasuaji katika Hospitali ya Wilaya, nyumba yamganga katika zahanati ya Naikula, ukarabati wa nyumba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

9

mbili za watumishi katika Kituo cha Afya Mchoteka nakuendeleza ujenzi wa zahanati ya Legezamwendo kupitiamapato yake ya ndani. Serikali itaendelea kuboresha vituovya kutolea huduma za afya kwa kadri fedhazitakavyopatikana.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Daimu Iddi Mpakate, swalila nyongeza.

MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Naibu Spika,asante na Mheshimiwa Naibu Waziri asante kwa majibumazuri. Kwa kuwa kituo hiki kinahudumia zaidi ya Kata Tano,Kata ya Mtina, Lukumbulem Mchesi, Masakata naTuwemacho.

Je, ni lini sasa Serikali itaona umuhimu wa kuboreshakituo hiki ili kiweze kutoa huduma za upasuaji kwa wakinamama na wajawazito?

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kampeni ya mwaka2010 Rais wa Awamu ya Nne alitoa ahadi ya kujenga kituocha afya katika Kata mbili za Nalase ambazo zipo katika Mjimmoja na Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru imekuwainatenga kila mwaka na mpaka sasa imeishia kujenga msingitu. Je, ni lini Serikali itaona haja ya kutimiza ahadi ile ya Raiswa Awamu ya Nne ili wapate kituo cha afya pale Nalasi?Ahsante.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): MheshimiwaNaibu Spika, naomba uniruhusu nimpongeze kwa dhati jinsiambavyo Mheshimiwa Mpakate anapigania kuhakikishakwamba wananchi wake wanapata huduma ya afya iliyobora. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali la kwanzaameuliza lini, na unaweza ukaona nia njema ya Serikali jinsiambavyo inahakikisha huduma ya afya inapatikana na hasakatika ujenzi wa vituo vya afya katika kata husika. Hii ndiomaana katika Halmashauri yake tumeanza na hiyo Kata ya

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

10

kwanza na hiyo kata nyingine kwa kadri pesaitakavyopatikana. Nia njema ya Serikali ni kuhakikisha vituovya afya vinajengwa katika kata zote.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la pili, nikweli kwamba kuna ahadi iliyotolewa na aliyekuwa Rais waAwamu ya Nne kwamba vingejengwa vituo vya afya katikakata mbili alizozitaja na yeye mwenyewe amekiri kwambakatika hizo kata mbili kazi ambayo imefanyika mpaka sasahivi ni ujenzi wa msingi. Naomba nimuombe MheshimiwaMbunge kwa kushirikiana na wananchi aendelee kuwahimizaujenzi sio msingi tu, hebu waendelee kujenga mpaka kufikiausawa wa lenta na Serikali itaenda kumalizia ujenzi huo.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Qulwi Qambalo swali lanyongeza.

MHE. QAMBALO W. QULWI: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru, Wilaya ya Karatu ina zaidi ya umri wa miaka 20na haina hospitali ya wilaya. Hivi sasa uongozi wa wilayaunakamilisha taratibu za kupata eneo kwa ajili ya ujenzi wahospitali hiyo. Je, Serikali iko tayari sasa kuanza kutenga fedhakatika bajeti inayokuja ili kuanza ujenzi wa hospitali hiyo?(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,TAMISEMI, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): MheshimiwaNaibu Spika, kwamba Serikali iko tayari kuanza kutenga, niana azma ya Serikali ni kuhakikisha kwamba ujenzi wa Hospitaliza Wilaya unafanyika katika Wilaya 64 zote ambazo hatunahospitali za Wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kama ambavyo yeyemwenyewe amesema katika swali lake, ndiyo wameanzakutenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya.Naomba tuongeze kasi ya kutenga hilo eneo, lakini pia

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

11

kutokana na Halmashauri yenyewe kwa sababu ni hitaji letu,tuanze kutenga pesa na Serikali ije kumalizia.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Kakoso.

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Naibu Spika,nishukuru kwa kunipa nafasi hii, kwa kuwa Kituo cha Afyacha Mwese ni cha muda mrefu sana, kina zaidi ya miaka 40hakijafanyiwa ukarabati wa aina yoyote na Serikali iliahidikukikarabati kituo hicho. Je, Serikali ni lini itapeleka fedhakwa ajili ya kituo hicho ili kiweze kuwasaidia wananchi waKata hiyo ya Mwese?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,TAMISEMI majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): MheshimiwaNaibu Spika, kuhusiana na Kituo cha Afya Mwese ambachoni cha muda mrefu, je, ni lini Serikali itakuwa tayari kutengapesa ili kufanya ukarabati?

Mheshimiwa Naibu Spika, utakubaliana kwamba nikiu ya Waheshimiwa Wabunge wengi wangependa vituo vyaafya viweze kukarabatiwa, na ndiyo maana Serikali kwa kujuaumuhimu huo tumeanza na vituo vya afya 205, si haba.Naomba Mheshimiwa Mbunge avute subira awamu kwaawamu na kwa kasi tunayoenda nayo naamini muda si mrefuna kituo cha afya cha kwake kitapata fedha.

MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana, Serikali imesema kwamba itakarabati vituo205 kikiwemo pia na Kituo cha Afya cha Malya, ninapendakujua Mheshimiwa Waziri, ni formula gani mnayotumiakupelekwa kwa baadhi ya vituo vya afya shilingi milioni 500na vingine milioni 400 wakati mlichagua kwamba vituo vyote205 vikarabatiwe kwa pamoja. Ni formula gani mnayotumia?Lakini ni l ini pesa zingine ambazo mliahidi kwambamtapeleka shilingi milioni 500 kwa kila kituo, kwa nini 400 nakwa nini 500? (Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

12

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,TAMISEMI majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): MheshimiwaNaibu Spika, ni formula gani ambayo inatumika katikakupeleka kupeleka fedha katika vituo vya afya sehemunyingine milioni 500 sehemu nyingine milioni 400?

Mheshimiwa Naibu Spika, formula zipo nyingi, kwanzaya kwanza inategemea na source of funding, ni nani ambayeameleta fedha ili ziweze kwenda kwenye kituo cha afya.Lakini pia formula nyingine ni namna ambavyo ukarabatiunaohitajika, kuna baadhi ya maeneo ni majengo machachetu ndiyo ambayo yanaongezwa kiasi kwamba ikipelekwashilingi milioni 400 inatosha kabisa kuweza kufanya ujenzi uleukakamilika. Kwa hiyo, inategemea source lakini pia naukarabati ni kwa kiasi gani unakwenda kufanyika katikaeneo husika.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto, Mheshimiwa Hawa Mchafu Chakoma, Mbunge waViti Maalum sasa aulize swali lake.

Na. 57

Matibabu Bure kwa Mama Wajawazito

MHE. HAWA M. CHAKOMA aliuliza:-

Je, Serikali ilimaanisha nini kusema kuwa matibabuni bure kwa kinamama wajawazito?

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waAfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto naomba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

13

kujibu swali la Mheshimiwa Hawa Mchafu Chakoma, Mbungewa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, mama wajawazito ni mojaya makundi maalum wanaostahili kupata huduma zamatibabu bure kama ilivyoainishwa katika Mwongozo waUchangiaji wa Huduma za Afya wa mwaka 1997. Aidha,mwongozo umeweka bayana kuwa akina mamawajawazito ni haki yao kupewa huduma zote bila malipona sio zile tu zinazohusu huduma za ujauzito.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwongozouliopitiwa mwaka 2009/2010, imetamkwa bayana kuwahuduma ya afya kwa mama wajawazito ni bure ikiwa namaana kwamba mara tu mwanamke anapokuwa naujauzito, huduma zote kuanzia kliniki ya ujauzito, paleatakapougua maradhi yoyote pamoja na huduma yakujifungua, sanjrari na kumuona daktari, kupatiwa vipimo,kupewa dawa na kufanyiwa upasuaji pale utakapohitajikakufanyiwa hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, ili kuondoa adhakwa wananchi, Wizara imeanzisha utaratibu wa kutengabajeti itakayotumika kwa aji l i ya ununuzi wa vifaavinavyohitajika wakati wa kujifungua (delivery parks), deliveryparks hizo watapewa akina mama wajawazitowanapokaribia kujifungua ili wawe wanatembea na vifaahivyo. Hii itapunguza kero kwa akina mama kujinunulia vifaavyao wao wenyewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, Serikali inazikumbushahalmshauri kusimamia kikamilifu utekelezaji wa sera hii ili akinamama wajawazito wapate huduma za matibabu burekama Mwongozo wa Uchangiaji wa Mwaka 1997 na Sera yaAfya ya Mwaka 2007 inavyoelekeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, wananchiwanaombwa kutoa taarifa kuhusu hospitali zinazotoza fedhakwa ajili ya matibabu kwa akina mama wajawazito ili hatuastahiki ziweze kuchukuliwa.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

14

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Hawa Mchafu Chakoma,swali la nyongeza.

MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Naibu Spika,ninakushukuru, pamoja na majibu mazuri ya MheshimiwaNaibu Waziri, sasa naomba nimuulize maswali mawilimadogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Naibu Waziriatakubaliana na mimi ni kwa muda mrefu sasa Sera yaMatibabu Bure kwa mama wajawazito ya mwaka 2007imeendelea kuwabagua akina mama wanaopatamiscarriage kwa kuwatoza gharama za kusafishwa.

Je, Serikali haioni kwamba hii ni ajali kama ajalinyingine, hivyo basi akinamama hawa ambao walikuwawana kiu ya kupata watoto wanastahili kufarijiwa kwakusafishwa bila malipo? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, ni ipi sasakauli ya Serikali juu ya mabadiliko ya kisera ili ianze kuwa-include akina mama wanaopata miscarriage na waleambao mimba inatunga nje ya kizazi kuanza kupatamatibabu bure na sio kuwaweka kwenye group (orodha) yamagonjwa ya akina mama ambayo kimsingi yanalipiwa kwaasilimia 100? Ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto majibu.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, swalilake la kwanza lilikuwa limejielekeza kwa nini akina mamaambao mimba zao zinaharibika ama kwa lugha ya kitaalammiscarriage, kwa nini nao wasipate matibabu bure?

Mheshimiwa Naibu Spika, katika jibu langu la msinginilisema kwamba huduma za akinamama wajawazitokuanzia mwanzo wa mimba mpaka mwisho ni bure, hiiinakwenda sambamba na tiba ambayo inaambatana na

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

15

mimba kuharibika. Ninaomba tu niseme kwamba hudumahii ni bure kwa mujibu wa sera yetu lakini kama suala hilihalitekelezeki kama inavyotakiwa katika sera niseme tukwamba tutalichukua na kutoa maelekezo katika mamlakahusika ili sasa hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini sambamba na hilo,sasa hivi Serikali tunafanya mapitio ya Sera ya Afya, tutawekautaratibu mzuri wa kuweza kulisimamia jambo hili.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Joseph Selasini, swali lanyongeza.

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru, akina mama wengi wajawazito wanapatamadhara na kufariki hasa wanapokuwa na referral kutokazahanati kwenda vituo vya afya na hospitali.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuboresha hudumaya ambulance ili hawa akina mama wanapopata matatizovijijini waweza kufikishwa haraka kwenye vituo vya afya nazahanati?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto majibu.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwelitunatambua kwamba kumekuwa na changamoto yakuwasafirisha akina mama wajawazito kwenda katikasehemu za kupata huduma, na kwa kiasi kikubwa kwa kwelikumekuwa na muitikio mkubwa sana wa akinamamakujifungulia katika vituo vya afya, hivi tunavyoongea sasahivi ni zaidi ya asilimia 60 ya akina mama wajawazitowanajifungulia katika vituo vya afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini sambamba na hilo,Serikali imeendelea kuboresha vituo vya afya na fedha kamaalivyosema Naibu Waziri TAMISEMI, zaidi ya vituo 205vimefanyiwa maboresho kwa kujenga theater, wodi ya akina

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

16

mama kujifungulia ili hizi huduma za kujifungulia ziweze kuwakaribu zaidi. Lakini sambamba na hilo, Serikali imeendeleakutoa magari (ambulance) katika vituo vya afya na hospitaliza wilaya, na kadri muda unavyokwenda tutakuwatunaziongeza ili tuweze kufikia vituo vyote.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, akinamamammesimama, nadhani swali hili tuwasikie akina babawatutetee akina mama, si ndiyo jamani? (Makofi)

Mheshimiwa Emanuel Mwakasaka.

MHE. EMANUEL A. MWAKASAKA: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza,tatizo la akina mama kujifungua mara nyingi wakatimwingine linaletwa pia na matatizo ya baadhi ya ma-nurseambao huwa wanawanyanyapaa akina mama wenzaowanapotaka kujifungua.

Sasa sijui Serikali ina mpango gani au huwa inachukuahatua gani kuwadhibiti hawa akinamama ambao wanatabia za kuwanyanyasa akina mama wenzao wanapotakakujifungua? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto majibu.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika,tumekuwa na tatizo la baadhi ya watoa huduma kutoalugha zisizokuwa sahihi kwa wagonjwa ambao wanafikakatika hospitali, na hili ni jambo ambalo ni kinyume kabisana maadili na taaluma za afya ikiwa ni pamoja na ma-nurse.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeendelea kuimarishamabaraza yetu na hivi karibuni, wiki iliyopita tu, MheshimiwaWaziri alitoa kauli ya kuhakikisha kwamba watoa hudumawote, ikiwa ni pamoja na madaktari na ma-nurse ,wanakuwa wanatoa huduma nzuri ambayo inazingatiamaadili na miiko ya kazi ambayo wanayo.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

17

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naendeleakulisisitiza hilo, na tumeendelea kuimarisha mabaraza yetuna tumeanza kuchukua hatua kwa wale ambao wanakiukataratibu hizo.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Joseph Mkundi, swali fupi.

MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Naibu Spika,kumekuwa na mkanganyiko katika utaratibu wa upatikanajiwa vitambulisho kwa wazee ili waweze kupata huduma zaafya ambapo baadhi ya maeneo wazee hawa wamekuwawanatakiwa kuchangia baadhi ya gharama.

Sasa Serikali inaweza kutoa kauli ni upi wajibu wahalmashauri na upi wajibu wa wazee hawa ili wawezekupata vitambulisho ili wapate huduma za afya bure?(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mkundi, swali hili tulikuwatunatetewa akina mama, au unamaanisha akina mamawazee? Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, ni agizola Serikali kwamba Halmashauri zitoe vitambulisho vya wazeeili waweze kutambulika kirahisi wanapokwenda kutafutamatibabu ya afya. Na hii inaendana na Sera ya Afya yamwaka 2007 ambayo inasema kwamba wazee watapatamatibabu bure.

Mheshimiwa Naibu Spika, vitambulisho hivi vinapaswavitolewe bure kwa sababu halmshauri zinagharamia.Inawezekana kwamba zile gharama ndogondogo kamaupigaji wa picha ambazo wanatakiwa wazee naowazigharamie ambayo sio gharama kubwa sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunapendakusema tu kwamba gharama ya kitambulisho ni bure naHalmashauri zinatakiwa zigharamie hilo.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

18

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana Mheshimiwa Constantine John Kanyasu, Mbunge wa GeitaMjini sasa aulize swali lake.

MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa swali lakwangu ndio linafuata.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Yahaya Omary Massare,Mbunge wa manyoni Magharibu.

Na. 58

Watumishi na Viongozi wa Halmashauri WaliostaafuZamani Kupatiwa Kadi za Bima ya Afya

MHE. YAHAYA O. MASSARE aliuliza:-

Sasa hivi baadhi ya watumishi wa Halmashauri kamavile Wakurugenzi na wengine wanapostaafu hupatiwa kadiya bima ya afya pamoja na familia zao.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuwapatia kadi kamahizo watumishi na viongozi wa Serikali waliostaafu kabla yautaratibu huo kuanzishwa ikizingatiwa kuwa wengi waowalilitumikia Taifa hili kwa uadilifu na uaminifu mkubwa?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto majibu.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waAfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, naombakujibu swali la Mheshimiwa Yahaya Omary Massare, Mbungewa Manyoni Magharibi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambuamchango wa wastaafu waliowahi kuwa watumishi naviongozi wa Umma katika maendeleo ya Taifa hili. Kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

19

sababu utaratibu wa kuwapatia bima ya afya wastaafuwaliowahi kuwa viongozi na watumishi wa Umma ni kupitiaSheria ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Sura Namba 395,Toleo la Mwaka 2015 kwa kuzingatia vigezo na mashartiyafuatayo:-

(i) Mstaafu husika lazima awe alikuwa mwanachamamchangiaji wa mfuko kabla ya kustaafu.

(ii) Mstaafu awe amefikisha umri wa kustaafu kwa hiarimiaka 55 au kwa lazima au miaka 60.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, kupitia utaratibu huu,wanachama wastaafu wanaokidhi masharti na vigezovilivyoainishwa, hupatiwa bima ya afya inayomuwezeshakupata huduma za matibabu yeye mwenyewe pamoja namwenza wake hadi mwisho wa maisha yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuzingatia uhitaji wahuduma za afya na changamoto za upatikanaji wa hudumahizi kwa wastaafu na wananchi wengine walio nje yautaratibu huu, mfuko umeweka utaratibu wa kujiunga kwahiari kupitia utaratibu wa mwanachama binafsi.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Yahaya Omary Massareswali la nyongeza.

MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi hii niulize swali la nyongeza,pamoja na majibu mazuri sana ya Serikali nina maswali mawiliya nyongeza. Pamoja na majibu haya mfuko huu unatambuatu viongozi na watumishi wa umma, lakini watumishi wasekta za kisiasa kama Wabunge na viongozi wenginehawapo katika mfumo huu. Je, Serikali sasa iko tayarikuwaingiza watumishi wa kisiasa wakiwemo Wabunge katikautaratibu huu ambao unafikia miaka 55 au 60 wawezekupatiwa kadi za afya na wawe ni wanachama?

Mheshimiwa Naibu Spika, na kama Serikali inakubali,je, ni lini utaratibu huu utaanza?

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

20

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto majibu.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika,Wabunge ndio wanatunga sheria na nataka nimuombe sanaMheshimiwa Massare, kama jambo hili kwa umuhimu wakealipitishe katika Tume ya Utumishi wa Bunge lijadiliwe halafusasa lifikishwe Serikalini kwa taratibu nyingine kufuatwa.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Maida Abdallah.

MHE. MAIDA HAMAD ABDALLAH: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali mojala nyongeza.

Je, Serikali inaweza kutuambia ni kwa nini wazeekama baba na mama wa Mbunge hawakuwekwa miongonimwa wategemezi katika bima ya afya?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto majibu.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwamujibu wa taratibu wa Sheria ya Bima ya Afya, inatambuayule mwenye kadi, mwenza wake na watoto wake,wategemezi wengine; baba, mama, walezi, wale wako njeya utaratibu huo. Kwa hiyo, niendelee kuwasisitizaWaheshimiwa Wabunge kwamba changamoto hii na sisitumeiona, tunaendelea kuitafakari kuangalia jinsi bora zaidiya kuweza kulifanyia kazi ili hawa nao waweze kunufaika.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Salome Makamba swali lanyongeza.

MHE. SALOME W. MAKAMBA: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali lanyongeza.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

21

Mheshimiwa Waziri, tunafahamu kwamba sekta zisizorasmi zinachangia sana Pato la Taifa na wengi wao wakokwenye hatari ya kupata ajali na magonjwa kama watu wabodaboda. Serikali ina mpango gani wa kurasimisha nakuwaweka katika mpango wa bima ya afya sekta isiyo rasmi,hasa vijana wetu wa bodaboda? Ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto majibu.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikalitunatambua kwamba sekta isiyo rasmi nayo ina mchangomkubwa sana katika ukuaji na kuchangia katika uchumi wanchi yetu, lakini sisi kupitia bima ya NHIF na CHF tunatambuamakundi haya na kwa kupitia vikundi vyao kuna mfumo wabima ambao wanao ambao wanaweza kukata kwa kupitiavikundi vyao. Lakini hata hivyo, kwa mtu mmoja mmoja sasahivi tunakuja na utaratibu wa CHF iliyoboreshwa ambayonayo itakuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kutoa hudumakwa mtu mmojammoja ambaye atakuwa anahitaji.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tutaendelea,Mheshimiwa Constantine John Kanyasu Mbunge wa GeitaMjini sasa aulize swali lake.

MHE. CONSTANTINE J. KANYASU: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru sana, naomba swali langukwa niaba yawananchi wa Geita Mjini lijibiwe.

Na. 59

Uhaba wa Dawa na Madaktari - Hospitali ya Rufaa yaMkoa wa Geita

MHE. CONSTANTINE J. KANYASU aliuliza:-

Liko tatizo la uhaba wa dawa na madaktari katikaHospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

22

Je, Serikali inachukua hatua gani kuhakikisha kuwadawa na Madaktari wa kutosha wanakuwepo?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto majibu.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waAfya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto naombakujibu swali la Mheshimiwa Kanyasu Constantine John,Mbunge wa Geita Mjini kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kumbukumbu zilizopoWizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watotozinaonyesha kuwa Hospitali ya Mkoa wa Geita ilipandishwahadhi kutoka iliyokuwa Hospitali ya Wilaya ya Geita na kuwaHospitali ya Rufaa ya Mkoa kuanzia mwaka wa fedha 2017/2018. Hata hivyo, kutokana na idadi kubwa ya walengwawa huduma kwenye hospitali hiyo, hospitali ya Wilaya yaGeita imekuwa ikipata mgao mkubwa wa fedha zakununulia dawa, vifaa tiba na vitendanishi kuliko hospitaliza Mkoa isipokuwa Hospitali ya Mkoa wa Tanga na ile yaMkoa wa Kagera.

Mheshimiwa Naibu Spika, kufuatia hali hiyo, Hospitaliya Geita katika mwaka wa fedha 2015/2016 ilitengewa fedhaza Kitanzania shilingi 141,939,184 na katika mwaka wa fedha2016/2017 ilipokea kiasi cha shilingi 278,666,525 kiasi ambachoni takribani mara mbili ya mgao wa mwaka wa fedha 2015/2016. Katika mwaka wa fedha 2017/2018, Hospitali hii baadaya kupandshwa hadhi kuwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa,mgao wake umeongezeka na kufikia fedha za Kitanzaniashilingi 368,287,841; hadi kufikia mwezi Desemba 2017, Hospitalihii ilikuwa imepokea kiasi cha milioni 168,609,586.94 kwa ajiliya kununua dawa kupitia bohari ya dawa. Hali ya upatikanajiwa dawa kwa sasa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa waGeita ni asilimia 90 kwa zile dawa muhimu.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

23

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa kuna jumla yaMadaktari Bingwa 451 nchi nzima. Wizara imeweka utaratibuwa kutoa ufadhili wa masomo ya Uzamili kwa MadaktariBingwa kila mwaka wa fedha kwa uwiano wa wanafunzi100 ndani ya nchi na 10 nje ya nchi. Jumla ya madaktari 236wanaendelea na masomo na tunataraji ndani ya miakamitatu watakuwa wamehitimu na kurudi vituoni. Wizaraimeanzisha utaratibu wa kuwatawanya Madaktali Bingwaili kuweka uwiano katika Mikoa yote nchini na sasa jumla yaMadaktari Bingwa 74 ambao walikuwa wakifadhiliwa naWizara walihitimu masomo ya udaktali bingwa kwenye fanimbalimbali, taratibu za kuwapandisha vyeo nakuwatawanya kulingana na uhitaji katika Mikoa zinaendelea.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Constantine John Kanyasuswali la nyongeza.

MHE. CONSTANTINE J. KANYASU: Mheshimiwa NaibuSpika, ninamshukuru Naibu Waziri kwa majibu yake mazuriingawa hakuwa na takwimu kabisa kwenye eneo lamadaktari maana yake amekili upungufu uliopo nilioutaja.

Mheshimiwa Naibu Spika, Hospitali yetu ya Rufaa yaMkoa wa Geita inahudumia takribani wagonjwa 400 kila siku.Na mwaka jana wakati Waziri wa Afya amefanya ziarakwenye Hospitali hiyo aligundua kwamba mpaka wakatitunatoka kwenye bajeti tulikuawa bado tunaichukuliaHospitali ya Geita kama Hospitali ya Wilaya, haikuwa kwenyeHospitali za Mkoa na ndiyo sababu mpaka leo pale tunaspecialist mmoja ambaye ni surgeon hatuna kabisaPhysiotherapy Doctor, hatuna mtu wa mionzi, hatunagynaecologist, hatuna mtu wa usingizi kwa sababu ilikuwainachukuliwa kama Hospitali ya Geita.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa swali langu kwa kuwatumeongeza vituo vingine vya Nyamkumbu na Kasambatumejenga theater kwa ajili ya upasuaji na kuna wataalamwengi wamezagaa ambao wanaomba ajira. Ni lini Wizara

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

24

italeta wataalamu wanaoweza kukudhi kiwango chaHospitali ya Mkoa?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili katikaHospitali yetu ya Mkoa wa Geita ambapo nimesema hatunawataalam tuna ujenzi wa Hospitali ya Mkoa baada yakuchukua Hospitali ya Wilaya ambayo tulifanya kuwa Hospitaliya Mkoa, tunajenga Hospitali y Mkoa, lakini speed ni ndogo.Nini kauli ya Serikali ili kuifanya ile Hospitali ya Halmashauriirudi kwa wananchi na huduma ziweze kupungua gharamayake?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa AfyaMaendeleo ya Jamiii Jinsia Wazee na Watoto majibu.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, swalilake la kwanza ilikuwa ni kuhusiana na idadi ya wataalam.Ni kweli lazima nikiri katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa waGeita kuna changamoto kubwa sana ya Madaktari Bingwana hilo sisi tumeliona kama nilivyojibu katika swali langu lamsingi. Ni kwamba tunaendelea kuhakikisha kwambatunafanya training ya kutosha Madaktari Bingwa na palewatakapopatikana basi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geitatutaipa kipaumbele kuongeza idadi ya Madaktari Bingwa iliwaweze kutoa huduma pale.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini swali lake lingine lapili lilikuwa lina husiana na kwa nini sasa Serikali isiongezemkono wake katika ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa naile iliyokuwepo pale iweze kurudi kuwa Hospitali ya Wilaya.

Naomba nimkumbushe Mheshimiwa Mbunge nikwamba mwishoni mwa mwaka jana Serikali il ifanyamaamuzi ya kuziondoa Hospitali za Rufaa za Mkoa kutokangazi za Serikali za Mitaa na kuzipeleka Serikali Kuu. Jukumuhilo sasa na sisi tumelipokea, tumekabidhiwa rasmi na miminimuhaidi tu Mheshimiwa Mbunge sasa na sisi tutajielekezanguvu zetu kuhakikisha kwamba tunazijenga na kuziboreshaHospitali za Rufaa za Mkoa.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

25

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Maftah swali la nyongeza.

MHE. MAFTAHA A. NACHUMA: Mheshimiwa NaibuSpika, asante sana nilikuwa naomba kuuliza swali la nyongezakwamba sasa hivi Tanzania kuna dawa hizi ambazo zinaitwatressa medicines ambazo zinatolewa kwenye Hospitali zaRufaa ama Hospitali za Mikoa tu na kwamba kule vijijinikwenye Zahanati na Vituo vya Afya hizi dawa hazitolewi zamagonjwa kama BP, magonjwa HIV, Kifua Kikuu sasa swalilangu; nilikuwa naomba kujua kwa sababu wananchiwanapata tabu sana kusafiri umbali mrefu kwenda kutafutadawa hizi kwenye Hospitali za Mikoa na Hospitali za Rufaa.

Je, Serikali ipo tayari hivi sasa kufundisha wale MedicalAssistant’s kule vijijini ili dawa hizi ziweze kutolewa kule vijijini?Ahsante sana.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, majibu.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza nianze kwa kutoa ufafanuzi, tumapoongelea sualala tressa medicines tuna maanisha kwamba ni dawa zilemuhimu na ambazo sisi zina tusaidia katika sekta ya afyakubaini na kuangalia kwamba zile dawa muhimu zipo. Tressamedicines sio dawa ambazo unasemasijui kwa lugha yakitaalam mnasemaje kwamba ni dawa ambazo ni muhimuambazo zilikuwa zinatakiwa kutotolewa katika sehemu fulanitressa medicine ni general term ambayo sisi tunaitumiakuhakikisha kwamba tunazibaini na kuzipatia zile dawamuhimu kule ambapo tunazo.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa labda niendelee kwakusema kwamba sasa hivi ndani ya Serikali na mwanzonimwa mwezi huu tumetoa mwongozo wa utoaji wa dawakatika ngazi mbalimbali. Mwongozo huu kwa jina la kitaalamtunaitwa standard treatment guedline hapo siku za nyumakila ngazi i l ikuwa inajitolea dawa holela na kadriwalivyokuwa wanaiona. Na hii changamoto tulikuwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

26

tunaipata sana katika Hospitali kubwa makampuni ya dawayana kuja yanamwambia mtoa huduma andika dawa hiiwakiwa wanampa na yeye motisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati sisi Serikalitunaagiza dawa nyingi kwa pamoja unakuta sasa mgonjwaanaandikiwa dawa anaambiwa dawa hazipo. Serikaliimeongeza sana bajeti ya dawa kutoka bilioni 30 mwaka2015/2016 kufikia bilioni takribani 270 katika mwaka wa 2017/2018 ni zaidi ya mara tisa ndani ya miaka miwili. Kwa hiyo,hali ya upatikanaji wadawa sasa hivi nchini ni nzuri sanapamoja na hizi tressa medicines.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lako lingine lanyongeza ilikuwa sasa kutokana na mwongozo huu,umeweka utaratibu dawa gani kwa ugonjwa gani zitakuwazinapatikana na kwamba hivyo vituo vya afya vitatakiwakuzingitia dawa gani na kutoa matibabu kwa kulingana naule mwongozo wa utoaji dawa ambao kama na sisi Serikalitumetoa. Tunatambua kwamba baadhi ya maeneo ambayotunachangamoto ya watumishi tunaendelea kutoa mafunzoil i na wale watumishi waweze kutoa tiba kwa walewagonjwa wanaofika pale ambapo hamna madaktari kwakuzingatia miongozo ambayo na sisi tutakuwa tumewapa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Taska Mbogo swali lanyongeza.

MHE. TASKA R MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante naomba kuuliza swali la nyongeza.

Kwa kuwa matatizo ya Mkoa wa Geita yanafananana matizo ya Mkoa wa Katavi. Mkoa wetu wa Katavi haunaHospitali ya Mkoa na hauna pia Hospitali ya Rufaa.

Je, ni lini sasa Serikali itamaliza ujenzi wa Hospitali yaMkoa wa Katavi na kuleta Madaktari Bingwa wa magonjwambalimbali kama upasuaji wa macho, meno kwa sababusiku nyingine watu wanavimba ufizi wanashindwa kupasua?Ahsante.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

27

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa AfyaMaendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto majibu.

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, bahatinzuri Mkoa wa Katavi nimeutembelea ikiwa ni sehemu yaMikoa 12 ambayo nimetembelea ndani ya miezi minne tangunimeteuliwa kuwa Naibu Waziri. Nimeiona changamoto hiyokatika Mkoa wa Katavi, lakini kama nilivyojibu katika swalalangu la msingi ni kwamba sasa hivi Serikali imechukuamajukumu ya kuendesha Hospitali za Rufaa za Mikoa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ninachokuombaMheshimiwa Taska Mbogo na Wabunge wengine wa Mkoawa Katavi ni kuendelea kuihimiza Serikali yetu ya Mkoakuhakikisha kwamba wanatenga eneo na kuanza maandaliziya awali na sisi kama Serikali tutaendelea kujipangakuhakikisha kwamba tunajenga Hospitali ya Rufaa ya Katavi.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tunaendeleana Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, MheshimiwaMaryam Salum Msabaha Mbunge wa Viti Maalum sasa aulizeswali lake.

Na. 60

Kituo cha Afya cha Kambi ya Migombani Unguja

MHE. MARYAM SALUM MSABAHA aliuliza:-

Majengo ya Kituo Afya cha Kambi ya Jeshi MigombaniUnguja ni chakavu na pia ni siku nyingi sana.

Je, ni lini Serikali itajenga kituo hicho ili kiwe cha kisasana kiendane na wakati?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Mamboya Ndani ya Nchi kwa niaba ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi laKujenga Taifa, majibu.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

28

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANO YA NCHI (K.n.y.WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Maryam Salum Msabaha, Mbunge wa VitiMaalum kwa niaba ya Waziri wa Ulinzi wa Jeshi la KujengaTaifa kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Kituo cha Afya cha Jeshicha Migombani Zanzibar ni moja ya vituo vya tiba ambavyohuanzishwa katika kila Kikosi cha JWTZ ili kutoa huduma yamwanzo ya tiba kwa Wanajeshi na familia zao, watumishiwa umma ikiwa ni pamoja na wananchi wanaishi jirani kablaya kupelekwa katika hospitali za rufaa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni, kweli majengo ya kituohicho na vituo vingine vya JWTZ yamechakaa na kwa sababuni ya muda mrefu. Kutokana na uchakavu huo wa Kituo chaKambi ya Migombani na sehemu nyingine, ni matazamio yaWizara kuvi karabati upya vituo vyote katika mwaka wafedha 2018/2019 kadri hali ya upatikanaji wa fedhaitakavyoruhusu.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Maryam Msabaha swali lanyongeza.

MHE. MARYAM SALUM MSABAHA: Mheshimiwa NaibuSpika, asante kwa kuwa haya maswali tumekuwa mara kwamara tunauliza na hakuna utekelezaji. Je, naomba kumuulizaMheshimiwa Naibu Waziri nusu mwaka wa fedhaunakwishwa. Ni majengo mangapi yamekarabatiwa kwaupande wa Zanzibar na ni vituo vingapi vya kambi vya Kambiza Jeshi kwa upande wa Zanzibar vimekarabatiwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili kwa kuwa hivivituo vya afya tunavyoviulizia ambavyo vipo kwenyemakambi ya Jeshi havihudumii tu majeshi na familia zao,zinahudumia pia na jamii zilizowazunguka na hasa hichi kituonilichokiulizia kiko sehemu ambapo ajali zinatokea mara kwamara.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

29

Je, Serikali ina mikakati gani kuhakikisha vituo vyotevya majeshi vinapata dawa kwa wakati muafaka na sitahikizinazofaa kwa wakati muafaka? Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Mamboya Ndani ya Nchi kwa niaba ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi laKujenga Taifa.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANO YA NCHI (K.n.y.WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA): MheshimiwaNaibu Spika, kama ambavyo nilivyojibu katika majibu yamsingi kwamba kwa bajeti ya mwaka 2018/2019 Serikaliimeazimia kuvifanyia ukarabati vituo vyote ikiwemo vyaZanzibar na kikiwemo hiki cha kwenye Brigedi ya Nyuki,Migombani. Kwa hiyo, mwaka wa fedha 2018/2019 badohaujaisha kadri ambavyo fedha kama ambavyo nimesemazitapatikana basi vituo hivi pamoja na hiki cha Migombanivitafanyiwa ukarabati. Sambamba na kuvipatia hudumanyingine muhimu kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa kwahatua za awali.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini ikumbukwe kwambavituo hivi kwa kawaida vinatumika kwa ajili ya kutoahuduma za awali kabla ya kuweza kuwapeleka wagonjwawenye matibabu makubwa katika Hospitali za Kikanda kwaupande wa Zanzibar ikiwemo Hospitali ya Jeshi ya Bububu.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tutaendeleana Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano. MhehimiwaJoel Mwaka Makanyaga Mbunge wa Chilonwa sasa aulizeswali lake.

Na. 61

Kurejesha Utaratubu wa Kuweka Matuta Barabara Kuu

MHE. JOEL M. MAKANYAGA aliuliza:-

Serikali imefanya kazi kubwa kujenga mtandao wabarabara za kiwango cha lami nchini, kipindi cha nyuma

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

30

barabara kuu zilikuwa zinawekwa matuta ili kudhibiti ajali,lakini hivi karibuni Serikali imefuta utaratibu wa kuwekamatuta kwenye barabara hizo na hivyo kuwa chanzokikubwa cha ajali zinazosababisha majeruhi, ulemavu na vifo.Kwa mfano, eneo la Buigiri, Wilaya Chamwino lina ajali nyingikutokana na barabara kukosa matuta.

(a) Je, Serikali haioni kuwa kuna umuhimu wakurejesha utaratibu wa kuweka matuta kwenye barabara?

(b) Kama utaratibu wa matuta hauwezekani, je,Serikali haioni kuwa kuna haja ya kuyaondoa matuta yotekwenye barabara kuu ili kuondoa malalamiko ya wananchikwa viongozi wao kwenye maeneo ambayo hayanamatuta?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waUjenzi Uchukuzi na Mawasiliano, naomba kujibu swali laMheshimiwa Joel Mwaka Mwakanyaga kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kabla sijatoa majibu yaswali namba 61 la Mheshimiwa Joel Mwaka MakanyagaMbunge wa Chilonwa, lenye sehemu (a) na (b) napendakutoa maelezo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wakala waBarabara Tanzania (TANROADS) imekuwa ikichukua hatuambalimbali za kuboresha usalama barabara na kurekebishasehemu hatarishi kwenye barabara kuu na barabara za mikoanchi nzima ikiwemo barabara ya Morogoro - Dodoma eneola Buigiri i l i kupunguza ajali za barabarani. Hatuazilizochukuliwa na Serikali kupunguza ajali za barabarani nipamoja na kuweka au kurudisha alama zote muhimu zabarabarani ikiwemo za kudhibiti mwendo, kuweka michoroya barabarani na kurekebisha kingo za madarajazilizoharibika, uwekaji wa matuta na kadhalika kamailivyokuwa ikifanya kipindi kilichopita.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

31

Katika mwaka wa fedha 2017/2018 TANROADSitaendelea kuweka vivuko vya watembea kwa miguu (zebracrossing) na alama zote muhimu nchini pale tutakapohitaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kutoa maelezoya awali napenda sasa kujibu swali la Mheshimiwa JoelMwaka Makanyaga Mbunge wa Chilonwa, lenye sehemu (a)na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli ajali za barabaranizina sababisha majeruhi, ulemavu na vifo kwa watu wetuikiwa ni pamoja na kusababisha hasara kubwa kiuchumi kwaTaifa letu. Moja ya njia ambayo Serikali imekuwa ikitumiakupunguza ajali kwenye baadhi ya sehemu ni kuwekamatuta ya barabarani. Hata hivyo, napenda kulieleza Bungelako Tukufu kuwa, kiutaalam hairuhusiwi kuweka matutakwenye barabara kuu. Aidha, matuta yaliyowekwa katikabarabara kuu yaliwekwa kwa lengo la kupunguza ajali zabarabarani kama njia ya mpito. Wizara inafanya utafitikupata njia mbadala ya kupunguza ajali kabla ya uondoshajiwa matuta hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati wa mpito, Serikaliinaendelea kurekebisha matuta ambayo yalijengwa bilakuzingatia viwango vilivyomo kwenye Mwongozo wa Wizarawa Usanifu wa Barabara (Road Geomentric Manual ya 2011)kulingana na upatikanaji wa fedha.

Aidha, inapobainika kuwa kuna haja ya kuwekamatuta kwenye barabara, matuta hayo yatawekwakulingana na viwango vilivyoainishwa kwenye mwongozohuu.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Joel Makanyaga swali lanyongeza.

MHE. JOEL M. MAKANYAGA: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru kwa majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Waziri,lakini pamoja na majibu hayo mazuri naomba niulize swalimoja la nyongeza.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

32

Mheshimiwa Naibu Spika, Buigiri ni eneo linalojulikanakwamba kuna Shule ya Watoto Wasiona kabisa na wenginewana uono hafifu. Je, Serikali haioni kwamba kuna kilasababu ya kulishughulikia suala hili la usalama barabaranikatika eneo la Buigiri kwa umuhimu na haraka ili kuondokanana tatizo la ajali pale Buigiri?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE):Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba kuna kituo kwaajili ya wasioona sehemu za Buigiri kama alivyozungumzaMheshimiwa Mbunge. Kiutaratibu tunategemea sehemuzenye mahitaji maalum kama hayo kuwe na watu ambaowanawaongoza wanaovuka barabara ili wasiweze kupataajali. Lakini hata hivyo, nimshauri na kumueleza MheshimiwaMbunge kwamba Serikali tutaendelea kutafuta utaratibumzuri wa kuhakikisha kwamba watu wenye mahitaji maalumkama hao wanapokuwa wanavuka na kutumia barabarazetu wanasaidiwa ili wasiweze kupata madhara.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Joseph Kizito Mhagamaswali la nyongeza.

MHE. JOSEPH K. MHAGAMA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsantekwa kupata nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Naomba nimuulize Waziri, kwa vile imethibitikakwamba baadhi ya ajali zinazotokea barabarani auzinasababishwa na ubovu wa barabara, au zinasababishwana ukosefu wa alama mahususi za barabarani jukumuambalo amekebidhiwa wakala wa barabara yaaniTANROADS. Je, Serikali ina mpango gani wa kuiwajibishaTANROADS pale ambapo sababu ya ajali inaonekana nikutotekeleza wajibu wa wakala huyo? Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano majibu.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

33

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE):Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba kuna ubovu wabarabara na Serikali imekuwa ikiendelea kufanya jitihada zakurekebisha ubovu huo kuhakikisha kwamba barabara zetukuu na barabara za mikoa zimapitika kila wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitoe wito tu kwaWatanzania wenzetu, kumetokea tabia ya hivi karibuniwananchi kuchukua hatua wenyewe ya kuweka matutabarabarani na hicho kimekuwa ni chanzo kimojawapo chaajali mbalimbali kwa sababu wanapoweka matuta bilakuwashauri au bila kuwaambia TANROADS ina maana yalematuta yanakuwa hayana alama na magari yanapokujayanafika, yanavamia yale matuta na kusababisha ajali.Niwashauri Watanzania, tunawaomba wasiweke matutabarabarani bila kuviambia vyombo husika vinavyohusika nabarabara ili kuweka alama kuwaonyesha maderevakwamba kuna tuta mbele wanakokwenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwambie tu MheshimiwaMbunge Ndugu yangu Joseph Mhagama kwamba TANROADSwanajitahidi sana kufanya kazi zao kwa uadilifu na kwaumakini wa hali ya juu kuzingatia usalama wa Watanzania.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Fatma Toufiq swali lanyongeza.

MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kwa kunipa fursa hii kuweza kuuliza swali lanyongeza. Kwa kuwa kumekuwa na tatizo la uwekaji kiholelawa matuta kwenye baadhi ya barabara za mitaani na hivyokusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa vyombovya moto na ikizingatiwa kwamba wananchi hawa hawanautalaam wowote. Je, Serikali ina mkakati gani wakukabiliana na kadhia hii? Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano majibu.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

34

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE):Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyokuwa namuelezaMheshimiwa Joseph Mhagama, ninatoa wito kwaWatanzania, barabara hizi zinajengwa kwa gharama kubwasana ya pesa za Watanzania. Tunapoweka matuta bilavyombo vinavyohusika hasa TANROADS kufahamu tunaharibubarabara zetu ambazo tumezijenga kwa gharama kubwasana. Kitu ambacho Serikali tunakifanya, tunapanga mkakatiwa kuwasiliana na Wizara ya mambo ya ndani kitengo chausalama barabarani kutoa elimu ya kutosha kwa wananchinamna ya matumizi bora ya barabara bila kuleta ajali kwaWatanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunawaomba sanaWatanzania wasijichukulie maamuzi ya kuweka matutabarabarani hata kwa kugongwa kwa mbuzi tu isipokuwawawasiliane na taasisi zinazohusika tusaidie kama kunaumuhimu wa kuweka matuta tutaweka, lakini kwa utaratibuambao unaeleweka.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Rhoda Kunchela swali lanyongeza.

MHE. RHODA E. KUNCHELA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante, changamoto zilizopo katika Jimbo la Chilonwalinafanana kabisa na changamoto zilizopo katika Wilaya yaMpanda, Mkoa wa Katavi.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi kuna ujenzi ambaounaendelea kutoka katika Mkoa wa Tabora barabara yaInyonga - Ipole kuelekea Mpanda. Barabara hii inajengwalakini wakandarasi hawaweki alama za ujenzi kwamba kunamadaraja yanajengwa, kuna mashimo yamechimbwa najambo hili limekuwa linasababisha ajali nyingi kwa wakaziwa Mpanda, kwa wakazi wa Mkoa wa Katavi.

Nini tamko la Serikali kuhakikisha inatoa maekelezokwa hawa wakandarasi ili kupunguza ajali za barabaranikatika Mkoa wa Katavi?

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

35

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzina Mawasiliano majibu.

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO:Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kumjibu MheshimiwaMbunge swali lake la ujenzi wa barabara ya kutoka Katavimpaka Tabora. Ni kweli Serikali tumeanza ujenzi wa barabarahiyo na hatua tunayokwenda nayo sasa ni hatua yamobilization yaani makandarasi kwa sasa wanakusanyavifaa vya ujenzi katika maeneo hayo, bado kabisa kazi yaujenzi haijaanza. Mara itakapoanza kazi ya ujenzi tutawekaalama kuhakikisha kwamba watumiaji wote wanaotumiabarabara hiyo wako salama.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tutaendeleana Mheshimiwa Mussa Bakari Mbarouk, Mbunge wa TangaMjini sasa aulize swali lake.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Ahsante Mheshimiwa NaibuSpika, kwa niaba ya watu wangu wa Tanga ambaonawapenda sana na wao wananipenda sana, naombaswali lao namba 62 lijibiwe.

Na. 62

Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kisasa-Tanga

MHE. MUSSA B. MBAROUK aliuliza:-

Tanga kuna uwekezaji wa bomba la mafuta tokaHoima - Chongoleani, viwanda mbalimbali vya saruji, vivutiovya utalii vya Amboni Caves, Magofu ya Tongoni na SaadaniNational Park:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga kiwanja chandege kikubwa na cha kisasa katika Jiji la Tanga?

NAIBU SPIKA: Unawanunulia soda kila siku nini hao?Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilianomajibu.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

36

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, naomba kujibu swali laMheshimiwa Mussa Bakari Mbarouk, Mbunge wa Tanga Mjiniambaye anapendwa sana na wapiga kura wake kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kiwaja cha ndege chaTanga ni miongoni mwa viwanja 11 nchini vilivyofanyiwaupembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa kugharamiwa naBenki ya Dunia kupitia mradi wa Transport Sector SupportProject. Viwanja vingine vilivyofanyiwa upembuzi yakinifu nausanifu wa kina ni Lake Manyara, Musoma, Iringa, Songea,Kilwa Masoko, Lindi, Moshi, Njombe, Simiyu na Singida.

Mheshimiwa Naibu Spika, usanifu huu ulikamilikamwezi Juni, 2017 na ulihusisha usanifu wa miundombinu yaviwanja hivi kwa ajili ya upanuzi na ukarabati ili kukidhimahitaji ya sasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeanzamajadiliano na Benki ya Dunia ili kupata mkopo wakugharamia ukarabati na upanuzi wa baadhi ya viwanjahivi kwa kuzingatia mapendekezo ya report ya upembuziyakinifu na usanifu wa kina ambao ulizingaia mambombalimbali ikiwa ni pamoja na ukuaji wa shughuli za uchumi,utalii na mahitaji ya usafiri wa anga. Katika upembuzi yakinifuna usanifu wa kina huo, kiwanja cha ndege cha Tanga nimiongoni mwa viwanja vilivyopewa kipaumbele kwamahitaji ya ukarabati hivyo katika majadiliano ya awali, Benkiya Dunia imeonesha nia ya kugharamia ukaratabi wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi unaopendekezwautahusisha mradi wa barabara ya kuruka na kutua ndegepamoja na barabara ya kiungio kwa kiwango cha lami.Ukarabati wa maeneo ya maegesho ya ndege, ujenzi wajengo kubwa la kisasa la abiria pamoja na miundombinuyake, usimikaji wa taa pamoja na mitambo ya kuongozea

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

37

ndege. Baada ya ukarabati unaopendekezwa kiwanjakitakuwa na uwezo wa kuhudumia ndege aina ya ATR 72yenye uwezo wa kubeba abiria 70 au ndege za kufanana nahiyo na kitaweza kutumika kwa saa 24.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa majadiliano katiya Serikali na Benki ya Dunia yanaendelea yakiwemo mapitioya awali ya report za miradi inayopendekezwa pamoja namaandalizi ya taarifa mbalimbali zinazohitajika kabla yamkataba wa mkopo kusainiwa na baadae kutangazwazabuni.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mussa Mbarouk swali lanyongeza.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante, kabla sijauliza swali langu la nyongeza kwanzaniipongeze timu yangu ya Coastal Union ya Tanga ambayoimepanda daraja mwaka huu, lakini pia niwapongeze timuya African Sports kwa kubakia katika ligi daraja la kwanza.Maswali yangu ya nyongeza ni kama ifuatavyo:- (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kufuatia ukarabatiunaofanywa na ambao ulishawahi kufanywa uwanja wandege wa Tanga, katika eneo la Magomeni kuna nyumbazaidi ya 228 ambazo zilifanyiwa evaluation mwaka 2008 lakinimpaka leo hawajalipwa. Lakini pia kuna nyumba nyingine802 ambazo nazo zinahitajiwa kuvunjwa ili kupanua uwanjaule wa ndege.

Sasa je, nataka kujua, Serikali ni lini itawalipaWananchi wale fidia ili kuweza kufanya ukarabati huumkubwa unaotakiwa kufanywa kufuatia ufadhili wa Benkiya Dunia?

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini jambo la pili, kwakuwa Jiji la Tanga sasa hivi route za ndege zimeongezeka nakuna shughuli nyingi za mipango ya kiuchumi amabzozinafanyika. Je, ni lini Bombadier itaanza kwenda Tanga?Ahsante.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

38

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbarouk hivi juzi ulikuwepoMorogoro? Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi naMawasiliano majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE):Mheshimiwa Naibu Spika, nyumba zote ambazo zilifanyiwaevaluation kwa ajili ya malipo ya fidia, shughuli za fidiazinafanyika na evaluation imekwishafanyika na tunafahamuidadi ya pesa zinazodaiwa lakini tuko kwemnye uhakikikupitia Wizara ya Fedha ya kulipa fidia hiyo, kwa hiyo, wakatiWizara ya Fedha itakapomaliza kupitia fidia hiyo, malipoyatafanyika kwa watu ambao wataathirika na upanuzi wauwanja wa ndege huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili, Bombadieritaanza lini safari za kwenda Tanga, kiutaratibu Bombadierwanafanya biashara pamoja na kutoa huduma kamamashirika mengine ya ndege kwa hiyo, hilo tutalichukua,tutawapelekea ATCL basi waje wafanye tathmini ya masualaya soko, usalama na mambo mengine ambayo yanahusikakabla ya kupeleka ndege kufanya shughuli za safari za uwanjahuo wa Tanga, ahsante.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge mnanipawakati mgumu sana, Mheshimiwa Gekul naomba ukae unamaswali mengi tayari kwenye hii karatasi tafadhali.Mheshimiwa Kunti Majala.

MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru, Mheshimiwa Waziri, wananchi wa Kata yaMakole, Manispaa ya Dodoma walisitishiwa uendelezaji wanyumba zao kwa ajili ya upanuzi wa uwanja wa ndege uliokohapa wakati huo kuna wananchi wa Kata ya Msalato 89wanaidai Serikali tangu mwaka 2005.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilitaka kujua wananchi waMsalato watalipwa lini lakini pili wananchi wa Makolewaliositishiwa uendelezaji wa nyumba zao…

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

39

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Kunti wewe ni swali lanyongeza linaulizwa moja na umeshauliza. MheshimiwaNaibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE):Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba kumekuwepo naupanuzi wa uwanja wa ndege au tutautumia sasa hivi hapaDodoma na wananchi wa Makole madai yao ya fidiayanashughulikiwa kupitia Wizara ya Fedha na sasa hivi Wizaraya Fedha wako kwenye uhakiki wa kuhakikisha kwambawanalipa hayo madai yao wakati watakapomaliza uhakiki.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbunge wa Segerea swalila nyongeza.

MHE. BONNAH M. KALUWA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante, nilitaka nimuulize Mheshimiwa Waziri kutokana natamko lake la juzi, Jimbo la Segerea katika Kata ya Kipawakuna wananchi 1,800 wanasubiri malipo tangu mwaka 1992na juzi alisema kwamba waondoke. Sasa nilitaka nimuulizeMheshimiwa Naibu Waziri ni lini sasa atawafanyia malipo yaowatu wa Kata ya Kipawa, Mtaa wa Kipunguni na wanahusikavipi kuondoka kabla hawajalipwa malipo yao?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE):Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba kuna wananchiwanatakiwa wapishe eneo la uwanja wa ndege wa JuliusKambarage Nyerere International Airport ambao walivamiamiaka ya nyuma, lakini Serikali ya Awamu ya Tano iliamuakwamba walipwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, kati ya hao kuna wananchi59 ambao tayari wamekwishapokea malipo yao kwa ajili yakupisha upanuzi wa uwanja huo. Tunaowazungumza naambao nilitoa agizo waondoke ni hao wananchi 59 na bado

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

40

naendelea kusisitiza kwamba hao wananchi 59 ambao tayariwamekwishakupokea malipo yao ya fidia, wanatakiwawaondoke wapishe upanuzi wa uwanja wetu wa ndege.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nikiri kwamba kunabaadhi ya wananchi ambao hawajalipwa kwa sababumbalimbali, kuna baadhi walifungua kesi na kuna wengineambao hawajafungua kesi lakini hawakuridhika na fidia, haobado tunaendelea kutafuta utaratibu mwingine wakuwashawishi kwa njia moja au nyingine ili waweze kupishaupanuzi wa uwanja huo wa ndege.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Esther Matiko swali lanyongeza kwa kifupi.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana. Mkoa wa Mara una shughuli nyingi sanaambazo zingeweza kuliongezea Taifa letu uchumi kwamaana ya utalii, tuna Ziwa Victoria lakini pia makumbushoya Baba wa Taifa. Katika majibu yake Naibu Waziriametueleza kwamba wamefanya usanifu pia kwenyeuwanja wa ndege wa Musoma, ningependa kujua uwanjawa ndege wa Musoma na wenyewe upo kati ya viwanjavilivyopewa priority maana yake umetaja Tanga tu kamandiyo umepewa kipaumbele na unaanza kukarabatiwa?Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO (MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE): Kwenyejibu langu la msingi wakati najibu kuhusu uwanja wa ndegewa Tanga nilieleza viwanja 11 ambavyo vimeshafanyiwaUpembuzi yakinifu na usanifu wa kina na uwanja wa Musomaukiwemo. Ni kweli kwamba viwanja vyote vimepewakipaumbele kinacholingana na pesa itakapopatikana kamanilivyoeleza tutafuta mkopo kutoka Benki ya Dunia, pesaitakapopatikana basi viwanja vyote vitapewa kipaumbelekujengwa kwa sababu tunahitaji viwanka vyote vya Mikao

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

41

viwe na kiwango kizuri ambacho ndege yoyote inawezaikashuka, ahsante.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tutaendeleana Wizara ya Maliaisli ya Utalii, Mheshimiwa Dkt. RaphaelMasunga Chegeni, Mbunge wa Busega sasa aulize swali lake.

Na. 63

Migogoro ya Ardhi na Mipaka

MHE.DKT. RAPHAEL M. CHEGENI aliuliza:-

Migogoro ya ardhi na mipaka ya vijiji na hifadhi badoimeendelea kuwa tatizo sugu licha ya kuwepo kwa ahadina kauli mbalimbali na Serikali.

Je, mgogoro wa Pori la Akiba Kijereshi na Sayankakatika Wilaya ya Busega utatatuliwa lini?

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waMaliasili na Utalii, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt.Raphael Masunga Chegeni, Mbunge wa Busega kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Pori la Akiba la Kijereshi lenyeukubwa wa kilometa za mraba 65.7 ililtangazwa rasmi natangazo la Serikali Na. 215 la mwaka 1994. Pori hilolilikabidhiwa rasmi kwa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamaporimwaka 2005 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji waHalmashauri ya Wilaya ya Magu. Pori la Akiba la Kijereshilimepakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa upande waKaskazini na Kijiji cha Lukungu upande wa Mashariki,Mwamalole, Mwakiroba, Kijilishi, Igwata na Muunganoupande wa Kusini Mashariki mwa pori hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, uvamizi wa mapori hayaya akiba kwa kilimo, makazi na ufugaji umesababisha

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

42

ongezeko la matukio ya wanyamapori kuharibu mazao nakudhuru wananchi. Aidha, hali hii imesababisha migogorobaina ya wananchi na mamlaka ya usimamizi wawanyamapori.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kutatua migogoro katiya wakulima, wafugaji na maeneo ya hifadhi nchini Serikaliimechukua hatua mbalimbali. Wizara kwa kushirikiana nawananchi imetambua na kuweka mipaka kwenye maeneoya hifadhi ikiwemo Pori la Akiba la Kijereshi na Hifadhi yaMsitu wa Sayanka. Hadi mwisho wa Januari, 2018 jumla yavigingi 74 vimesimikwa katika pori la Akiba Kijereshi, Aidha,katika Hifadhi ya Msitu wa Sayanka jumla ya vigingi 67vimesimikwa, hatua hii imesaidia kupunguza migogoro yamipaka kati ya wananchi na hifadhi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, tatizo lililobakikwa sasa ni baadhi ya wananchi kutaka kulima na kuanzishamakazi ndani ya Hifadhi ya Misitu ya Sayanka na wenginekutaka kulima ndani ya mita 500 kutoka mpaka wa Pori laAkiba la Kijereshi kinyume cha Sheria ya Misitu naWanyamapori.

Wizara kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Wilayaya Busega na Halmashauri ya Wilaya ya Busega inaendeleakutoa elimu na kufanya vikao na mikutano na wananchiwanaozunguka Pori la Akiba Kijereshi. Mikutano hiyo inalengakuwakumbusha wananchi umuhimu wa uhifadhi nakuepusha kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita 500kutoka mpaka wa pori la Akiba. Katazo hilo ni kwa mujibuwa Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori Namba 5 ya mwaka2009. Aidha, Serikali inatoa wito kwa wananchi kuachakuvamia maeneo ya hifadhi ili kudumisha uwepo wabioanuai kwa faida yetu ya sasa na vizazi vijavyo. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Raphael Chegeni swalila nyongeza.

MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru sana na napenda nipongeze majibu ya

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

43

Mheshimiwa Naibu Waziri lakini nina maswali mawili madogoya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, majibu haya yamejikitakuelezea taarifa ambayo siyo sahihi, kwa sababu migogoromingi imekuwa ikichochewa na uhamishaji wa mipaka nandiyo malalamiko ya wananchi katika maeneo husika, kwavile Serikali imekuwa ikihaidi muda mrefu kwamba kuwe nampango shirikishi kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii, TAMISEMIna Wizara ya Ardhi ili kuainisha mipaka vizuri zaidi, kituambacho kitaondoa migogoro na migongano iliyopo.

Je, ni lini sasa Serikali kupitia majibu haya, kwa sababusuala hili siyo mara ya kwanza au ya pili kuuliza hapa Bungeni,ni lini Serikali itakaa na wananchi wa maeneo husika ilikutatua mgogoro wa namna hii?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili MheshimiwaNaibu Waziri aliyekuwepo wakati ule Engineer Ramo Makanialitembelea maeneo husika yaliyotajwa kwa maanakwamba pori la Akiba la Kijereshi kwa wananchi wa kijiji chaKijereshi, Mwakiloba, Lukungu na Mwamalole na akajionemwenyewe kwamba wananchi wana haki kwa kilewanachokizungumza, vilevile alikwenda Pori la Akiba laSayanka akajionea mipaka imehamishwa wananchiwamekuwa miaka yote wanalima kabla ya mipakakuwekwa. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri uko tayari sasa kujaujionee uhalisia huu na uondokane na taarifa potofu ambazozinazotolewa na wataalam wako? Ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasilina Utalii majibu.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaNaibu Spika, kabla ya kujibu naomba niitumie nafasi hiikumpongeza sana kwa kazi nzuri ambayo amekuwaakiifanya kwa kweli akina Masunga na Hasunga nadhani nimachachari sana, hongera sana Mheshimiwa Mbunge.(Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

44

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa naomba nijibu maswaliyake. Kuhusu matatizo na migogoro mbalimbali ambayo ipokatika maeneo mengi, ni kweli kabisa tumebaini kwambakuna migogoro mingi ambayo aidha, imesababishwa nakutokushirikisha vizuri wananchi ama kutokana na sababumbalimbali ama kuongezeka kwa idadi ya watu katikamaeneo mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imechukua hatuambalimbali katika maeneo mengi, kwanza tuliunda Kamatiya Kitaifa shirikishi ambayo ilishirikisha Wizara mbalimbaliambayo sasa imebainisha maeneo mbalimbali yenyemigogoro na hivi sasa ipo katika hatua ya mwisho yakubainisha na kutoa ushauri ili tuweze kufanya uamuzi nimaeneo yapi Serikali iweze kuyaachia kwa wananchi namaeneo yapi yabaki chini ya hifadhi. Baada ya taarifa hiyokukamilika hivi karibuni nadhani kwamba taarifa hiiitatolewa Bungeni na Wabunge wote watapata nafasi yakuweza kujua.

Kuhusu kukaa na wananchi wa Jimbo la MheshimiwaChegeni mimi naomba nimuambie tu kwamba Serikali tukotayari kukaa na wananchi ili kuweza kupitia mipaka hatuahadi hatua, mimi nimuahidi baada ya Bunge hili tutakaa nayetutapanga kwamba ni lini twende tukawatembelee ili nanijir idhishe kabisa kwamba madai anayoyasema nawananchi wanayoyasema kweli yanahusu hiyo mipaka nakama mipaka imesogezwa basi tuweze kuchukua hatuastahiki katika maeneo haya aliyoyataja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Grace Kiwelu swali lanyongeza.

MHE. GRACE S. KIWELU: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika majibu ya NaibuWaziri amesema Kamati ya Kitaifa iliyoundwa, ninapendakujua ni lini Kamati hiyo itakamilisha taarifa hiyo na kuiletandani ya Bunge ili matatizo hayo yaweze kukoma?(Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

45

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasilina Utalii majibu.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaNaibu Spika, kama nilivyosema kwamba Kamati ya Kitaifaambayo ilikuwa inashirikisha zaidi ya Wizara tano iliundwakupitia maeneo mbalimbali na kupitia nchi nzima kuonamigogoro ambayo iko katika maeneo mbalimbali. Kamatihiyo imeshatoa tayari matokeo ya awali ambayoyamebainisha kila kitu ni maeneo gani ambayo yapo kwenyematatizo, baadhi ya maeneo ambayo yamebainishwa nipamoja na vijiji 366 viko ndani ya hifadhi.

Kwa hiyo, basi juzi tumekaa na hiyo Kamati imetoatena draft nyingine tumetoa maelekezo ni imani yangu ndaniya kipindi cha miezi miwili, Kamati hiyo itakamilisha kabisahiyo taarifa na itawasilishwa kwa Waheshimiwa Wabungena kutoa taarifa kamili.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Boniphace Mwita Getereswali la nyongeza.

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swalila nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Jimbo la Bunda naVijiji vya Honyari, Kihumbu, Maliwanda, Sarakwa, Kyandegempaka wao kati ya pori la Akiba la Gruneti na MheshimiwaNaibu Waziri amesema hapa kutoka mpaka wa Mto Lubanakwenda kwa wananchi ni mita 500 ningependa kujua kutokampaka mto Lubana kwenda porini ni mita ngapi?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasilina Utalii, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaMwenyekiti, ni kweli kabisa katika hili eneo la Gruneti kunamipaka ambayo ipo lakini itakuwa ni vigumu sana kumpataarifa kamili umbali uliopo kati ya huo mto na hilo eneo

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

46

analolisema. Kwa hiyo naomba nitumie nafasi hii kuwambiakuwa nitakaa nae, tutaenda kutembelea hilo eneo ili tuonekwamba kuna umbali wa mita ngapi ambazo zinahusisha.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Innocent Bashungwa swalila nyongeza.

MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru kwa kuniona. Kuna mgogoro kati ya Porila Akiba la Kimisi na maeneo ya Rweizinga – Mguruka katikaKata ya Bwelanyange, mwaka jana Bunge liliielekeza Serikaliiende katika hayo maeneo na kutatua migogoro hii, lakinimpaka hivi sasa Serikali haijafika.

Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa kujua ni liniMheshimiwa Waziri utaambatana na mimi ili tuende kwenyeKata ya Bwelanyange maeneo ya Rweizinga na Mguruka ilikushirikisha wananchi katika kuweka mipaka mipya kati yapori la Akiba la Kimisi na Kata ya Bwelanyange? Nashukuru.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasilina Utalii, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaNaibu Spika, ni kweli kabisa katika maeneo aliyoyatajakulikuwa kuna matatizo na wananchi walikuwa namalalamiko kuhusu mipaka na naomba nimhakikishiekwamba niko tayari wakati wowote mwezi wa Machi,mwaka huu nitatembelea katika Mkoa wa Kagera natutakapokuwa huko basi tutapata nafasi ya kwenda kupitiana kuongea na wananchi juu ya mipaka hiyo yote aliyoitajakatika maeneo ya Bwelanyange na maeneo mengine yotealiyoyataja.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleaMheshimiwa Goodluck Asaph Mlinga, Mbunge wa Ulanga,sasa aulize swali lake.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

47

Na. 64

Hitaji la Eneo la Kilimo kwa Wananchiwa Jimbo la Ulanga

MHE. GOODLUCK A. MLINGA aliuliza:-

Sehemu kubwa ya Jimbo la Ulanga imezungukwa naHifadhi ya Selous Game Reserve hivyo kufanya wananchi waKata za Mbuga, Ilonga, Kataketa na Lukunde kukosamaeneo ya kilimo.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuwapatia wananchiwa maeneo hayo maeneo ya kilimo?

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waMaliasili na Utalii, naomba kujibu swali la MheshimiwaGoodluck Mlinga, Mbunge wa Ulanga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Pori la Akiba Selouslilianzishwa kati ya mwaka 1896 na 1912 na Serikali ya Kikoloniya Wajerumani. Wajerumani waliligawa pori hilo katikamaeneo manne ambayo ni Ulanga, Kusini, Muhoro naMatandu. Mnamo mwaka 1951 pori hili lilisajiliwa rasmi kwaGN Na. 17 chini ya Fauna Consveration Ordinance CAP. 302.

Mheshimiwa Naibu Spika, Pori la Akiba la Selous nimuhimu sana kiuchumi, kiikolojia na kiutamaduni siyo tu kwaTaifa letu bali pia Kimataifa. Pori linaliingizia Taifa fedha zaKitanzania na za kigeni kupitia utalii, lina misitu ya Ilindimainayosaidia upatikanaji wa maji, linachangia kudhibitimabadiliko ya tabia ya nchi na makazi na mazalia ya viumbehai wakiwemo wanyamapori, samaki na viumbe wengine.Kutokana na umuhimu huo Umoja wa Mataifa umelitambuaeneo hili kuwa urithi wa dunia. Sambamba na hilo Serikali yaKikoloni ilianzisha pori tengefu la Kilombero mwaka 1952 ilikuunganisha mfumo wa kiikolojia katika maeneo hayo awili.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

48

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kutatua changamoto zamatumizi ya ardhi katika maeneo yaliyotajwa, Serikaliinatekeleza mpango wa Kilombero na Lower Rufiji WetlandsEcosystem Management Project, mradi huu unahusishakutatua matatizo ya mipaka ya vijiji na mapori ya hifadhiyaliyo katika Wilaya ya Ulanga, Malinyi na Kilombero pamojana kuwawezesha wananchi kumiliki ardhi kupitia hati milikiza kimila.

Aidha, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo yaMakazi kupitia mradi wake wa Land Tenure SupportProgramme (LTSP) inaendelea kuhakiki mpaka wa poritengefu la Kilombero ambalo ni sehemu ya Wilaya ya Ulangana kupima ardhi ya vijiji kwa ajili ya urasimishaji wa ardhikwa wananchi na hatimaye kupata hati za kumiliki. Serikaliinaamini kuwa kupitia miradi hii miwili changamoto yamatumizi ya ardhi kwa shughuli za kilimo, ufugaji na makazizitatatuliwa kikamilifu.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Goodluck Mlinga, swali lanyongeza.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kwa nafasi yapekee napenda nikipongeze Chama changu cha Mapinduzikwa kutimiza miaka 41 ya utawala bila kung’oka, na kwautendaji huu tuna miaka 41 mbele.

Mheshimiwa Naibu Spika, Waziri atakuwa shahiditangu hili pori lianzishwe ni miaka mingi sasa na watuwameongezeka kwa kiasi kikubwa, sheria hizi zilizoanzishamapori ndiyo sheria hizi hizi zilizoanzisha vijiji, inapotokeamaeneo wanayoishi wananchi yakagundulika madiniwananchi wanatolewa, lakini wananchi wanapohitaji kulimamaeneo ya mapori wanaambiwa sheria zizingatiwe. Kwanini sheria ziko bias upande mmoja kwa kuwaonea wananchiambao ni wanyonge?

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

49

(b) Mheshimiwa Waziri tulikuwepo nae Ulanga wikimbili zilizopita ameona jiografia ya Ulanga ilivyo ngumumaeno yote ya matambalale ambayo wananchi wanawezawakalima ni Mapori Tengefu, ni Hifadhi na Bonde la mtoKilombero, naomba busara zitumike ili wananchi wapatemaeneo ya kilimo kwa sababu wameongezeka kwa kiasikikubwa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasilina Utalii majibu.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaNaibu Spika, ni kweli kabisa wakati tunapata Uhuru idadi yawananchi wa Tanzania ilikuwa haizidi milioni tisa na ardhiilikuwa hivi, lakini miaka karibu 56 ya Uhuru wananchi waTanzania wameongezeka kwa kiwango kikubwa sana, sasatuko karibu milioni 52 lakini ardhi haijaongezeka. Kwa hiyonaomba nimuambie Mheshimiwa Mbunge kwambakutokana na ongezeko la watu ndiyo maana kumekuwa napresha kubwa sana katika maeneo yaliyohifadhiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo naombanimhakikishie kwamba sheria zilizotungwa sio kwamba zikobias, sheria ziko vizuri kabisa, sheria zinaainisha maeneoyaliyohifadhiwa, maeneo ambayo yanafaa kwa makazi,maeneo yanayofaa kwa ufugaji, maeneo yanayofaa kwakilimo kwa hiyo hili lazima tulisimamie ipasavyo. Siyo kwambasheria zinapendelea labda kitu fulani na Serikali yetuitaendelea kuhakikisha kwamba wananchi wanapatiwamaeneo ya kulima yale yanayostahili na yale yaliyohifadhiwayaendelee kuhifadhiwa kwa mijibu wa sheria.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nijibu swali lakela pili ni kweli kwamba tutatumia busara kubwa sana katikakuhakikisha kwamba wananchi wa Jimbo hili la Ulangawanapata eneo la kulima, kufuatia hatua hiyo na ziaraambayo tumeifanya hivi karibuni kama alivyosema yeyemwenyewe Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii ameundaKamati ya Wajumbe 22 kwa sababu ya ukubwa wa Bondelenyewe la Kilombero lilivyo ili kuweza kubainisha, kuweza

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

50

kupitia maeneo yote na waone ni maeneo gani yahifadhiwe,maeneo gani yatafaa kwa kilimo ili kusudi wananchi wapatekuelekezwa ipasavyo. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Kuchauka swali lanyongeza.

MHE. ZUBER M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kwa kunipa nafasi nami niulize swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, vijiji vya Mpigamiti pamojana Kikulyungu ni vijiji ambavyo vimepakana na hifadhi yaSelous katika Halmashauri ya Wilaya ya Liwale, lakini kunamgogoro mkubwa sana wa ardhi kati ya Kikulyungu pamojana Selous.

Je, ni lini Mheshimiwa Waziri utaweza kutatuamgogoro huu ambao umedumu zaidi ya miaka 10 na watutayari washapoteza maisha?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasilina Utalii majibu.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaNaibu Spika, ni kweli katika eneo hili kuna migogoro mingina kuna eneo kubwa ambalo kwa kweli kuna matatizo.Naomba nikuhakikishie hata jana nilikuwa karibu na pori laSelous katika maeneo ya Mbwande nikishughulikia matatizoambayo yanafanana na namna hii. Kwa hiyo, katika eneolako hili la Mpigamiti pamoja na Kikulyungu ambako kunamatatizo naomba niseme kwamba ninalichukuatutaendelea kulifanyia kazi na tutashirikiana na wewe ilikuweza kutafuta ufumbuzi wa hili tatizo ambalo limedumukwa muda mrefu kusudi wananchi wa eneo lako wapatekufaidika na wapate kufurahi. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Felister Bura swali lanyongeza.

MHE. FELISTER A. BURA: Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

51

nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo lanyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, takribani zaidi ya vijiji 12vinavyozunguka Pori la Akiba la Mkungunero hawafanyi kaziya kilimo kwa sababu ya mgogoro mkubwa ambaoumedumu zaidi ya miaka 10, kati ya wafanyakazi wa pori laAkiba la Mkungunero na wakulima wanaozunguka pori lile.Suala hil i l imeshafika Serikalini, lakini hakuna hatuazinazochuliwa. Wabunge wa Majimbo Mheshimiwa JumaNkamia na Mheshimiwa Dkt. Ashatu wanapata shida sanawakati wa kampeni na hata wakati wa kuwatembeleawananchi wao.

Je, ni lini sasa matatizo haya yatakwisha mpaka halisiwa pori la Mkungunero litabainishwa ili wakulima walewafanye kazi yao kwa uhuru na kwa amani?(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasilina Utalii majibu.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaNaibu Spika, ni kweli kumekuwa na tatizo la muda mrefu lavijiji hivi 12 katika pori la Akiba la Mkungunero ambapowananchi walikuwa wanagombania mipaka, hil i nimojawapo ya eneo ambalo Kamati ya Kitaifa imeyapitia nawenyewe tumeipitia tumeona kweli kuna mgogoro ambaounatakiwa kutatuliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitumie fursa hiikumuomba Mheshimiwa Felister Bura kwamba katika hili eneoSerikali iliagiza kwamba maeneo yote yenye migogoroyawekewe mipaka na muda wa mwisho ulikuwa ni tarehe31 Desemba, 2017. Hivi sasa tunafanya tathmini kupitiamaeneo yote sio tu katika eneo hili la Mkungunero, katikamapori yote ya akiba na mengine yote kuangalia baada yakuweka mipaka na vigingi katika haya maeneo ni maeneoyapi ambayo yana migogoro, ni maeneo kiasi ganitunatakiwa tuyaachie ama tuendelee kuyahifadhi nawananchi watafutiwe maeneo mengine.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

52

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya haya yotekukamilika basi Waheshimiwa Wabunge watajulishwa nahatimae tutajua kabisa kwamba wananchi sasawatatatuliwa haya matatizo na hili tatizo la Mkungunero navijiji hivi 12 vyote vitakuwa vimepata ufumbuzi wa kudumu.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana Wizara ya Kilimo. Mheshimiwa Peter Joseph Serukamba,Mbunge wa Kigoma Kaskazini, swali lake litaulizwa kwa niabana Mheshimiwa Stanslaus Mabula.

Na. 65

Bei ya Kahawa Ikilinganishwa na Gharama za Uzalishaji

MHE. STANSLAUS S. MABULA (K.n.y MHE. PETER J.SERUKAMBA) aliuliza:-

Bei ya kahawa ni ndogo ikilinganishwa na gharamaza uzalishaji.

(a) Je, Serikali ina mpango gani wa kupandisha beiya zao la kahawa?

(b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidiawakulima kwa kuwapatia ruzuku?

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waKilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Peter JosephSerukamba, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, lenesehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, bei ya kahawa dunianiikiwa ni pamoja na kahawa ya Tanzania hutegemea beikatika masoko mawili ya rejea duniani ambayo ni Soko laBidhaa la New York (New York Commodities Market) kwakahawa ya Arabica na Soko la London International FinancialFutures and Options Exchange kwa kahawa ya Robusta.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

53

Mheshimiwa Naibu Spika, mwenendo wa bei katikamasoko hayo huathiri moja kwa moja bei kwa nchi zotewazalishaji wa kahawa ambapo mwenendo huo pia huathiribei katika soko la mnada wa kahawa na bei ya wakulimaTanzania. Bei ya kahawa katika masoko ya rejea pia hutokanana kiasi kilichopo na mahitaji (demand and supply) yakahawa duniani kwa wakati husika. Aidha, kwa kuwawanunuzi hununua kahawa kwa bei ya mwali pwani (FOB)ambayo hujumuisha bei ya mkulima na gharama, zao zaununuzi kwa hivyo bei ya kahawa haizingatii kabisa gharamaza uzalishaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, zao la kahawa piahukabiliwa na ada na tozo mbalimbali ambazo huongezagharama za kufanya biashara na hivyo kusababishawanunuzi wengi kwenda kununua kahawa katika nchi jiraniambako hakuna ada na tozo nyingi na hivyo kutoa bei nzuriukilinganisha na bei za ndani. Hali hiyo husababisha wakulimakutorosha kahawa nje ya nchi ili waweze kupata bei nzuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali haiwezi kupandishabei ya kahawa kwa kuwa bei hiyo hutokana na masoko rejeaya dunia. Hata hivyo, Serikali inatekeleza mikakati mbalimbaliya kuwaongeza kipato wakulima. Mikakati hiyo ni pamojana kufuta ada na tozo zipatazo 17 katika sekta ya kahawaili kumpunguzia mkulima mzigo wa malipo ambayowanunuzi huweka kwenye gharama zao za ununuzi;kuongeza ushindani katika mnada kwa kuwaondoawanunuzi wa kahawa vijijini ili wakanunue kahawa mnadanikwa ushindani, kuimarisha, kufufua na kuanzisha Vyama Vikuuvya Ushirika katika kila Mkoa unaolima kahawa na Vyamavya Msingi kwa maana ya AMCOS katika kila kijiji ili kukusanyakahawa ya wakulima, wanachama na kuipeleka mnadani.Aidha, AMCOS zimehamasishwa kuanzishwa viwanda vyakuchakata kahawa ili kupata kahawa bora na yenye bei nzurina kuimarisha usimamizi kwa zao la kahawa katika ngazina hatua zote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali huwapatia wakahawa ruzuku kwa kupunguza bei ya miche bora ya

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

54

kahawa inayozalishwa na Taasisi ya Utafiti wa KahawaTanzania, vilevile Mamlala za Serikali za Mitaa zinazolimakahawa nchini zimeagizwa zote kuanzisha bustani zakuzalisha miche bora kulingana na mahitaji ya wakulima waona kuigawa bure na pia kuhakikisha inapandwa nakutunzwa. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Stanslaus Mabula, swali lanyongeza.

MHE. STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa Naibu Spika,pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri,naomba nimuulize maswali mawili madogo ya nyongeza.

Moja, kwa kuwa tunafahamu kwamba soko lakahawa bei yake imekuwa ikipanda na kushuka, Serikalihaioni sasa umuhimu wa kuanzisha ruzuku maalum kwa ajiliya wakulima wa kahawa ili hata soko linapoporomkamkulima asipate maumivu sana kwenye upande wa mauzo?(Makofi)

Pili, tunaamini kwamba Vyama vyetu vya Ushirikavinayo nafasi kubwa sana ya kuhakikisha wakulima wan chihii wananufaika. Ni nini mkakati wa Serikali kuhakikishaVyama vya Ushirika vinaimarika na kuwa msaada kwawakulima? Ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimomajibu.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza kuhusu ruzuku katika bei ya mazao. Naomba nisemekwamba bei ya ruzuku kwa upande wa Serikali, sisi tunatoamazao yote katika standardization na vilevile tutaangaliasiku zijazo kuhusu Vyama vya Ushirika kama vinafanya vizuribasi tutaoa hiyo standardization na ruzuku katika vyama namazao yote yanayohusika.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake (b) nikuhusu Vyama vya Ushirika. Serikali tumejipanga kuhakikisha

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

55

kwamba tunafanya total transformation, vilevile operationskatika Vyama vya Ushirika. Ni kweli vingi havifanyi vizuri natumeangalia kabisa vingine hata havifanyiwi mahesabu lakinikama Serikali, kama nil ivyosema tumefanya totaltransformation kuhakikisha kwamba Vyama vya Ushirikavitakuwa vinafanyiwa mahesabu, vitakuwa vinafanyiwaukaguzi ili tuweze kupata bei nzuri na mazao bora.

Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabungewote naomba niwataarifu kwamba hivi majuzi mweziuliopita Tume ya Vyama vya Ushirika imeundwa na tayariimeshaanza kazi. Nashukuru. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Sixtus Mapunda, swali lanyongeza.

MHE. SIXTUS R. MAPUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa kunipa na mimi nafasi ya kuuliza swali lanyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri,naomba niulize swali dogo tu la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, moja kati ya matatizoyaliyosababisha wakulima wapate shida sana na zao lakahawa kuporomoka ni utendaji mbovu wa hivyo Vyamavya Msingi na Vyama vya Ushirika. Mwaka huu tunakwendakwa mara ya kwanza kwa kuwa na Chama Kikuu cha Ushirikana Mkoa ambacho kitanunua kahawa kwa niaba yawakulima.

Je, Serikali imejiandaa vipi kuwaandaa WatendajiWakuu wa Vyama vya Msingi kwa sababu tumebakiwa namuda mchache na uwezo wao unaweza ukawa ni mdogohuko nyuma walishatuletea hasara, kwa mfano, Mbinga,hoteli ya Mbiku, ma-godown, viwanja na majengo yote yakokwa Msajili wa Hazina….

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Sixtus, umeshauliza swalimoja. Mheshimiwa Naibu Naibu Waziri wa Kilimo majibu.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

56

kwanza naomba nichukue fursa hii kumpongeza sanaMheshimiwa Mbunge kwa jinsi ambavyo amekuwa akifuatiliasana katika suala zima la Vyama vya Ushirika hususan katikaJimbo lake la huko Mbinga.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Jimbo la Mbingana lenyewe limekuwa likilima sana zao hili la biashara lakimkakati la kahawa na ni kweli naomba nikiri kwambavyama vingine vya ushirika vimekuwa havifanyi vizuri. Lakinikama nilivyomjibu Mheshimiwa Mbunge Stanslaus Mabula,katika maswali yake mawili ya nyongeza ni kwamba Serikaliimejipanga sawasawa kufanya total transformation katikasuala zima la Vyama vya Ushirika na tumejipanga kuingiakwa miguu miwili. Tutakuwa tunafanya mafunzo yamahesabu na vilevile kuhakikisha kwamba ukaguzi utakuwaunafanyika kwa kina ili tuweze kupata mazao bora ambayopia yatakuwa yanatupatia bei nzuri. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Gimbi Masaba swali lanyongeza.

MHE. GIMBI D. MASABA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kunipa nami nafasi ya kuuliza swali lanyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa tatizo la KigomaKaskazini linafanana kabisa na tatizo la wananchi wa Mkoawa Simiyu kwa wakulima wa pamba. Katika Mkoa wa Simiyukumezuka wadudu waharibifu wanaoharibu zao la pambana mahindi na hitaji la dawa za wakulima hawa ni sawa nachupa milioni moja na laki nne, lakini mpaka sasa wakulimahawa wamepatiwa chupa 350 tu ni sawa na asilimia 25.(Makofi)

Je, Serikali ina mpango gani wa haraka kuwasaidiawakulima hawa ili kuhakikisha kwamba mazao hayohayaharibiki? Ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimo,majibu.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

57

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika,kwa niaba ya Serikali naomba nimpongeze sana MheshimiwaGimbi Masaba kwa swali lake la kuhusu pamba pamoja nawakulima wa zao la pamba na Waheshimiwa Wabungewote ambao wanatoka katika Mikoa inayolima pamba.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa habari njema naombaniseme tu kwamba Serikali tumejipanga kuhakikisha kwambazao la pamba ambalo mdudu wa kweleakwelea pambambegu zake zinaharibika. Serikali imeshatoa shilingi bilionitatu tayari kuhakikisha kwamba mpango huu wa dharurana tatizo hili la dharura linafanyiwa kazi na vilevile shirika laFAO limeshatupatia US dollar milioni 250 kwa ajili ya kutatuatatizo hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo naombaniwahakikishie kabisa wakulima wa pamba kwamba tatizohili litatatuliwa hivi karibuni. Ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tutaendeleana Mheshimiwa Pauline Phillip Gekul sasa aulize swali lake.

Na. 66

Ushuru wa Mazao

MHE. PAULINE P. GEKUL aliuliza:-

Halmashauri ya Mji wa Babati inaidai NFRA ushuru wazaidi ya shilingi milioni 90 katika kipindi cha mwaka 2014/2015.

Je, ni lini fedha hizo zitalipwa?

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waKilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Pauline PhilipoGekul, Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini, kama ifuatavyo:-

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

58

Mheshimiwa Naibu Spika, katika msimu wa ununuziwa nafaka mwaka 2014/2015 Wakala wa Taifa wa Hifadhiya Chakula (NFRA) ulinunua tani 1,127.826 za mahindi zenyethamani ya shilingi 6,063,913,000 kutoka kwa wakulima navikundi vya wakulima katika Mji wa Babati. NFRA ilipaswakulipa kwa Halmashauri ya Mji wa Babati ushuru wa shilingi181,917,390 ambazo ni asilimia tatu ya thamani ya mahindiyaliyonunuliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha2014/2015 Wakala ulilipa ushuru wa mazao kwa tani 4,400,000zenye thamani ya shilingi 66,000,000 na kubaki na deni nadeni la ushuru wa mazao kwa tani 7,727.686 zenye thamaniya shilingi 115,917,390.00. Hata hivyo, kutokana na ufinyu wabajeti wakala ulishindwa kulipa kiasi chote cha ushuru kwawakati kutokana na kuongezeka kwa ununuzi wa mahindizaidi ya melengo yaliyopangwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha2015/2016 Wakala ulilipa deni lote la ushuru wa mazao kwaHalmashauri ya Babati kwa awamu mbili ambapo tarehe 10Agosti, 2015 ulilipa shilingi 23,000,000 na kumalizia deni lashilingi 92,917,390 tarehe 27 Januari, 2016. Aidha, kwa sasaWakala umelipa ushuru wa mazao kwa Halmashauri zoteilikonunua mahindi na hakuna deni lolote kuhusu ushuru wamazao.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Pauline Gekul, swali lanyongeza.

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri kulitendeahaki swali langu maana yake ni swali la muda mrefu miakamitatu, lakini hizo fedha tumeshazipokea na tumezisahau.

Hata hivyo, nina maswali mawili ya nyongeza; swalila kwanza, Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa kuwa NFRAwalipewa eneo la kujenga godown au kiwanda katikaHalmashauri ya Mji wa Babati kwa ajili ya kuchakata mahindiyetu kuongezea thamani, pamoja na kuwapa kiwanja hicho

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

59

au eneo hilo zaidi ya heka sita mpaka leo mwaka wa tatuNFRA hawajafika kujenga godown kiwanda hicho. Naombanifahamu ni lini NFRA watafika katika Halmashauri ya Mji waBabati kujenga kiwanda hicho?

Swali la pili, kwa kuwa wananchi wetu wengi katikaMkoa wa Manyara na katika Halmashauri ya Mji wa Babatimsimu huu wa kilimo cha mahindi hawajapata pembejeoza kilimo, hawajapata mbegu na mbolea, wamelazimikakupanda mahindi ya mwaka jana waliyovuna mashambani,mbegu hawajapatiwa. Mbegu zilizopo zinauzwa kwa bei yajuu kilo mbili shilingi 12,000.

Naomba nipate kauli ya Serikali ni kwaninihampunguzi bei ya mbegu za mahindi ili wananchi wetuwaweze kupanda mbegu hizo badala ya kuwaachia sasawanapanda mahindi ya mwaka jana? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Kilimo,majibu.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika,awali ya yote pia na mimi naomba nimpongeze kwa dhatikabisa Mheshimiwa Mbunge kwa jinsi ambavyo kamaalivyosema amekuwa akifuatilia jambo hili tangu miakamitatu i l iyopita. Vilevile naomba nichukue fursa hiikuwapongeza wananchi wote wa Jimbo la Babati Mjini kwajinsi ambavyo wanafuatilia na kuzingatia umuhimu wa kilimona vilevile kuweza kutoa ardhi kwa ajili ya kujenga mradihuu wa maghala.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu hiyo ninaombanitamke hapa mbele ya Bunge lako Tukufu kwamba mradihuu tayari umeshakamilika na ninamuagiza Mtendaji Mkuuwa NFRA kuanza kazi mara moja ifikapo mwisho wa mweziwa tatu. Huu mradi unagharimu milioni 8000. Kwa hiyo,Mtendaji Mkuu wa NFRA hili ni agizo, mwezi wa tatu mwishonimradi huu uanze kazi mara moja kwa ajili ya kuongezathamani ili wananchi hawa wa Babati waweze kupata ajirana thamani ya mazao yao pia iweze kuongezeka.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

60

Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la pili,Mheshimiwa Mbunge ameuliza suala zima la mbegu. Katikasuala zima la mbegu, sisi kama Serikali mbegu huwazinakusanywa na makampuni binafsi na ndiyo maanaunakuta bei inakuwa ni kubwa, lakini kupitia Wakala wetuwa Taifa wa Mbegu tumeanzisha mpango mahsusi wakuhakikisha kwamba tutakuwa tunazalisha mbegu ambayoinaitwa hybrid kwa ajili ya kuboresha ili iweze kuwa na beipungufu.

Vilevile tunashirikiana na makampuni binafsi kwa ajiliya kuhakikisha kwamba wakulima wetu wanapata mbegubora na kwa bei nafuu.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. MheshimiwaZubeda Hassan Sakuru, Mbunge wa Viti Maalum, swali lakelitaulizwa kwa niaba na Mheshimiwa Susan Lyimo.

Na. 67

Baadhi ya Shule na Vyuo Kutokidhi Matakwa ya Sheria

MHE. SUSAN A. J. LYIMO (K.n.y MHE. ZUBEDA H.SAKURU) aliuliza:-

Baadhi ya Shule na Vyuo nchini vinaendelea kudahiliwanafunzi pamoja na kutokidhi matakwa ya sheriambalimbali.

(a) Je, Serikali inachukua hatua gani kudhibiti vyuona shule zinazoendelea kudahili wanafunzi huku zikiwa namapungufu?

(b) Je, mpaka sasa ni vyuo vingapi na shule ngapizilizofutiwa usajili kwa kutokukidhi matakwa ya kisheria.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIAalijibu:-

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

61

Mheshimiwa Naibu Spika, wa niaba ya Waziri waElimu, Sayansi na Teknolojia, naomba kujibu swali laMheshimiwa Zubeda Hassan Sakuru, Mbunge wa Viti Maalum,lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Elimu, Sayansi naTeknolojia ina taratibu za kudhibiti ubora wa elimu namafunzo yanayotolewa shuleni na vyuoni kupitia Idara yaUdhibiti Ubora wa Shule katika maana ya shule za msingi,sekondari na vyuo vya ualimu. Baraza la Taifa la Elimu laUfundi (NACTE) kwa vyuo na taasisi zinazotoa elimu ya katina Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kwa taasisi zinazotoa elimu yajuu. Shule na vyuo vinavyobainika kukiuka taratibu za utoajielimu na mafunzo huchukuliwa hatua mbalimbali ikiwa nipamoja na kusitisha udahili wa wanafunzi, kusitisha programuzitolewazo, kupunguza idadi ya wanafuzni waliozidi na kufutausajili wa taasisi husika.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2017/2018Serikali imefuta usajili kwa shule saba za awali na msingi nashule moja ya sekondari. Vilevile vituo 16 vilivyokuwavimedahili wanafunzi wa elimu ya awali na msingi kabla yakusajiliwa viliagizwa kuwatawanya wanafunzi hao kwakuwapeleka katika shule zilizosajiliwa na kufunga vituo hivyo.Katika mwaka 2016/2017 Serikali kupitia NACTE ilifanya uhakikikatika vyuo na taasisi 103 za elimu ya ufundi ambapo vyuona taasisi 31 zilibainika kuwa na mapungufu na hivyo kufutiwausajili.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha katika mwaka 2017/2018 uhakiki mwingine ulifanyika katika vituo, vyuo na taasisi454 za elimu ya ufundi ambapo jumla ya vyuo na taasisi 59za elimu ya ufundi zilibainika kuwa na mapungufu na hivyowalitakiwa kurekebisha mapungufu ndani ya kipindi cha miezimitatu kuanzia tarehe Mosi Februari, 2018. Chuokitakachoshindwa kurekebisha mapungufu yaliyobainishwandani ya kipindi kilichopangwa kitafutiwa usajili.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa vyuo vikuuSerikali kupitia TCU ilifanya uhakiki wa vyuo vyote vya elimu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

62

ya juu nchini kati ya mwezi Oktoba, 2016 na Januari, 2017 ilikuhakiki ubora wa elimu inayotolewa vyuoni. Taarifa yauhakiki ilionyesha mapungufu katika baadhi ya vyuo, kufuatiataarifa hiyo TCU kwa mwaka wa masomo 2017/2018 ilisitishaudahili wa wanafunzi wa Programu za Afya na Uhandisikwenye vyuo vitano. Vilevile TCU ilisitisha udahili katikaprogramu zote kwa mwaka wa kwanza kwa vyuo 14, aidha,katika mwaka huo wa masomo TCU imedhibiti na kuzuiavyuo vikuu kudahili wanafunzi katika programu ambazohazijapata ithibati zipatazo 75 katika vyuo vikuu 22.

NAIBU SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Susan AnselmLyimo swali la nyongeza.

MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru. Pamoja na jitihada za kudhibiti ubora wa elimuhapa nchini ikiwa ni pamoja na kuanzia shule ya awalimpaka vyuo vikuu, naishukuru Serikali kwa juhudi hizo kwasababu siku zote Upinzani tumekuwa tukizungumzia suala laubora wa elimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninataka kujua ni nini hatmaya wanafunzi katika vyuo vile ambavyo vimefutiwa usajiliwakiwa tayari wanaendelea na masomo? Kwa mfano,unakuta vijana hao tayari walishalipa ada lakini na mudawao. Je, Serikali inatuambia nini au inawaambia niniwanafunzi ambao tayari walikuwa kwenye masomo lakiniwakaondolewa?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili ni kweli kwambahuu ukaguzi ni mzuri sana lakini kumekuwa na ubaguzimkubwa kwenye ukaguzi kwa maana ya shule za msingi zaSerikali na zile za private, hali inayopelekea kuwa na doublestandard, kwa sababu wanafunzi wa shule za private kilamwanafunzi anatakiwa alipe shilingi 5000 kwa ajili ya ukaguzi,lakini wanafunzi wa shule za Serikali ni bure. Hamuonikwamba kwa ubaguzi huu ndiyo inayopelekea kuporomokakwa elimu hasa kwenye shule za Serikali na ndio sababukunakuwa na matokeo mabaya? (Makof)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

63

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia majibu.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu uwezekano wa wanafunziwanaondelea na vyuo kuathirika na hatua ambazotunachukua wakati wa kuhakikisha kwamba kuna uborakatika vyuo vyetu.

Naomba tu nimhakikishie Mheshimiwa Mbungekwamba kila wakati tunapochukua hatua tunahakikishakwamba wanafunzi hawataathirika lakini ifahamike kwambakwa sababu tokea awali vyuo hivyo vinafahamu kuhusuutaratibu ambao wanatakiwa wafuate, pale tatizolinapotokea maana yake wenyewe watatakiwa kurejeshagharama hizo kwa wanafunzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile kuhusiana na tofautialiyotaja ya ada ya ukaguzi kati ya shule za Serikali na zile zawatu binafsi, Serikali haioni kwamba tofauti hiyo ina atharizozote zile katika ubora wa elimu. Ni utaratibu tu ambaoumewekwa wa kuhakikisha kwamba hiyo ada inalipwa lakinihatuoni kwamba shilingi 5000 kulipa kwa shule binafsikwamba ina athari katika ubora wa elimu.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunamaliziaswali la mwisho Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Mwanne Ismail Mchemba, Mbunge wa VitiMaalum, sasa aulize swali lake.

Na. 68

Ujenzi wa Nyumba za Askari Polisi na Magereza

MHE. MWANNE I. MCHEMBA aliuliza:-

Hali ya nyumba za Polisi na Magereza nchini ni mbovusana.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

64

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga nyumba zaaskari hao?

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waMambo ya Ndani ya Nchi, napenda kujibu swali laMheshimiwa Mwanne Ismail Mchemba, Mbunge wa VitiMaalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli hali ya makazi kwaAskari wetu siyo nzuri, hata hivyo Serikali imekuwa ikifanyajitihada mbalimbali kwa kushirikiana na wadau mbalimbaliwa maendeleo na kwa kutumia rasilimali zilizopo katikamaeneo husika kujenga makazi mapya na kufanya ukarabatiwa majengo yaliyopo.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika bajeti ya mwaka2017/2018 Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 12.3 fedhaza maendeleo kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa makazi yaaskari wetu katika maeneo mbalimbali nchini.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mwanne Mchemba swalila nyongeza.

MHE. MWANNE I. MCHEMBA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kwa kunipa nafasi na mimi niulize maswali madogoya nyongeza kama ifuatavyo:-

Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa NaibuWaziri, pamoja na jitihada zote zinazofanywa na Serikalikutatua tatizo la makazi ya askari. Je, kwa kipindi hiki cha2017/2018 Mkoa wa Tabora umetengewa kiasi gani?

Swali la pili, kwa kuwa hivi karibuni kumekuwa nawimbi kubwa la wakimbizi kutoka Congo na kwa kuwa hivikaribuni pia wamesema kwamba baadhi ya wakimbizi walewametawanyika katika Mkoa wa Kigoma inawezekanawakaja na Mkoa wa Tabora. Je, Serikali inatoa kauli ganikwa sasa?

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

65

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Mamboya Ndani ya Nchi, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nichukue fursa hiikumpongeza sana Mheshimiwa Mwanne Mchemba kwa swalilake zuri la pili la nyongeza kutokana na changamoto yamfumuko wa Wakimbizi ambao wanaingia nchini kutokaDRC hasa kutoka katika maeneo ya Kivu kutokana nachangamoto ya hali ya usalama nchini DRC. Kabla sijatoaufafanuzi wa swali lake hilo la pili nimjibu kwamba kwa bajetiambayo nimeizungumza ya maendeleo ambayo nilisema nitakribani bilioni 12.3 ya mchanganuo mbalimbali ikiwemoshilingi bilioni 7.2 ya Magereza ni fedha ambazo zimetengwakwa maendeleo nchi nzima.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa Jeshi laMagereza hakuna utaratibu wa sub vote kwenye Jeshi hiloingawa Jeshi la Polisi ipo lakini kwa ujumla kwa mwaka huuwa fedha hakuna fedha ambayo imetengwa kwa ajili yamradi wa maendeleo kwa Tabora specifically, lakini kwasababu tunatambua kwamba kuna maeneo mengi nchiniambayo kuna majengo mengi ya Polisi ambayo yapo katikahatua za mwisho kukamilika, kwa mfano, kule Mtambaswala- Mtwara, Njombe, Mabatini Mwanza, Musoma na kadhalika,kwa hiyo fedha hii ya maendeleo mwaka huu tunatakatuilekeze katika majengo ambayo tayari yapo katika hatuaza mwisho kukamilika kabla hatujaanza miradi mipya.

Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue fursa hii sasakuweza kuzungumzia hoja yake ya pili muhimu ya wimbi lawakimbizi kutoka DRC. Mpaka hivi naomba nitoe taarifarasmi kwamba Wakimbizi ambao wametoka DRC kuingianchini tokea Januari wanakadiriwa kufika zaidi ya 2,500 nakatika hao takribani wakimbizi 1,960 tayari wameshakuwawamehifadhiwa katika Kambi ya Wakimbizi Nyarugusu nawengine 300 na zaidi wapo kwenye vituo vya kupokeleaWakimbizi. Changamoto ambayo amezungumza yakwamba kuna baadhi ya wakimbizi ambao wamekuwawana desturi aidha ya kutoroka kwenye makambi kutoka

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

66

DRC na kuingia mitaani ama kupita njia za panya kuingianchini kwetu kwa kisingizio cha machafuko DRC.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nitoe kauli ifuatayo,jambo la kwanza nataka nitoe angalizo ama onyo kali kwawakimbizi kama hao kuacha desturi hiyo. Tumeshatoamaelekezo katika vyombo vyetu vya usalama nchinikuhakikisha jambo la kwanza kwa Idara ya Uhamiajikuendelea kufanya msako kwa kushirikiana na vyombovingine vya dola, ikiwemo Jeshi la Polisi hasa katika Mkoawa Kigoma ambao una changamoto kubwa sana yawakimbizi, hii inadhihira na takwimu ambavyo zipo kwamwaka jana.

Mheshimiwa Naibu Spika, takribani asilimia 30 yawahamiaji haramu waliokuja Tanzania wametokea katikaMkoa wa Kigoma. Kwa hiyo, tumewekeza nguvu nyingi sanakatika Mkoa wa Kigoma kuhakikisha kwamba inadhibitiwimbi la wahamiaji haramu kuingia. Vilevile tumetoamaelekezo kwa Idara ya Wakimbizi ambayo ipo chini yaWizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuhakikisha kwambainafanya uhakiki na kuimarisha ulinzi katika makambi yetuhasa Kambi ya Nyarugusu ambayo ndiyo kambi ambayoinapokea wakimbizi kutoka DRC ili kuhakikisha kwamba walewote ambao watakiuka sheria na utaratibu wachukuliwehatua kwa mujibu wa sheria ya wakimbizi kwa kushtakiwaili baadaye sheria ichukue mkondo wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, hiyo ndiyo kauli ya Serikalikuhusiana na swali lake la pili.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, muda wetuumekwenda tumefika mwisho wa kipindi chetu cha maswalina majibu.

Waheshimiwa Wabunge, nichukue fursa hii kwanzakabisa kabla ya matangazo kumpongeza sana MwanasheriaMkuu wa Serikali na nimpe salamu za Mheshimiwa Spikaanakukaribisha sana Bungeni na tunaamini kwambatutaweza kufanya kazi kwa pamoja. (Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

67

Waheshimiwa Wabunge, pia nitambue kurudi kwaMheshimiwa Waziri Mkuu ili msije mkaanza kumpelekea hojaMheshimiwa Mwakyembe. Mheshimiwa Waziri Mkuuamesharejea kwa hivyo yupo Bungeni.

Waheshimiwa Wabunge, matangazo tuliyonayo yawageni tutaanza na wageni walioko Jukwaa la Spika naoni wageni sita wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaowamekuja kushuhudia akiapishwa ambao ni viongozi kutokaOfisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakiongozwa naNaibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Ndugu Paul JoelNgwembe, karibu sana Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Pia ameongozana na Katibu Mtendaji wa Tume yaKurekebisha Sheria Ndugu Casmir Kyuki, pia familia yaMwanasheria Mkuu wa Serikali ikiongozwa na mke wakeNdugu Natalia Kilangi, karibuni sana. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, tunao pia wageni watanowa Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe ambaye ni Waziriwa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambao niMadiwani wawili na Wenyeviti wawili wa Vitongoji,wakiongozwa na Mzee Adamson Mwakabwale huyoanatoka Kata ya Kajunjumele na Ipyana, karibuni sana.(Makofi)

Tunao pia wageni wa Waheshimiwa Wabunge nahuyu ni mgeni wa Mheshimiwa George Lubeleje ambaye nimwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nayeanaitwa Ndugu Mariam Mapunda, karibu sana.

Tunao pia wageni waliotembelea Bunge kwa ajili yamafunzo kundi la kwanza ni wageni 35 ambao ni watumishiwa kristo wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God kutokaMkoa wa Dodoma, karibuni sana. Tunao pia Mapadri nanekutoka Seminari ya Shirika la Damu ya Yesu wa Kanisa Katolikiwa Mkoani Dodoma, karibuni sana. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, tangazo lingine linatokakwa Mheshimiwa Susan Lyimo ambaye ni Makamu Mwenyekiti

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

68

wa Umoja wa Wabunge Wanawake Tanzaniaanawatangazia Wabunge wote wanawake kuwa leo tarehe5 Februari, 2018 kutakuwa na semina kwa ajili WabungeWanawake wote. Semina hiyo itafanyika katika Ukumbi waMsekwa mara tu baada ya kuahirishwa Kikao cha Bungekuanzia saa 7.00 mchana. Waheshimiwa Wabungewanawake mnaombwa kuhudhuria. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge tangazo lingine linatokaIdara ya Kamati za Bunge..., Mheshimiwa Makamu Mwenyekitinadhani wanaume wanataka kualikwa ndiyo minong’onohiyo. (Kicheko)

Waheshimiwa Wabunge, tangazo lingine linatokaIdara ya Kamati za Bunge na mnatangaziwa WaheshimiwaWabunge wote kuwa fomu za kuomba kupangiwa Kamatiza Kudumu za Bunge zinapatikana sehemu ya mapokezi yaUkumbi huu wa Bunge.

Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge mnaombwa kilammoja kuchukua nakala yake ya fomu ili aweze kujaza nazote zirejeshwe hapo hapo mapokezi kabla ya tarehe 10Februari, 2018. Hii ni kuzingatia masharti ya Kanuni ya 116(7)ya Kanuni za Bunge kuhusu ukomo wa ujumbe katika Kamatiza Kudumu za Bunge ifikapo mwisho wa Mkutano huu waKumi wa Bunge. Kwa hiyo, mnakumbushwa kuchukua fomuna kuzijaza.

Waheshimiwa Wabunge, kabla hatujaendelea kwaleo sitazitaja hapa, lakini kuna Wizara ambazo majibu yakeya msingi ni marefu sana na uzuri watendaji wako hapa,ambao ndio watayarishaji wa hayo majibu watusadiekupunguza urefu wa majibu wasitoe historia ndefu sana, kwasababu maswali huwa yanakuwa yameulizwa jambomahsusi. Kwa hiyo, tusitoe historia kwenye hayo maswali. PiaWaheshimiwa Wabunge mnaoweka mazingira magumusana Mawaziri pamoja na Kiti hapa kwenye kuyakataamaswali yenu mapya mnayoyauliza ambayo hayakuwepokabisa kwenye swali la msingi.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

69

Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge naomba sanatusome yale maswali kama hukuliona kabla ukifika hapasoma swali linahusu nini. Swali linahusu wodi ya wazazi,unauliza dawa. Swali linahusu jengo unauliza mbegu sasatafadhali ama swali linahusu majengo wewe unazungumziakitu tofauti. Sasa kuliko kuwaambia Mawaziri hawajajibusawasawa kwa sababu na sisi tunasikiliza hapa majibu niafadhali maswali yetu yaulize kitu mahsusi ambachokinahusika na swali la msingi ili Mbunge usiambiwe umeulizaswali ambalo halihusiki, pia wizara isilazimike kujibu jamboambalo halikuwa limeulizwa kwenye swali la msingi. Maswaliyote ya nyongeza yanatokana na maswali ya msingi namajibu yaliyotolewa na upande wa Serikali.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kusema hayotutaendelea na ratiba yetu. Katibu.

MWONGOZO WA SPIKA

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Bobali.

MHE. HAMIDU H. BOBALI: Mheshimiwa Naibu Spika,ninakushukuru kwa kunipa nafasi hii ya kutoa Mwongozowangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, natumia Kanuni ya 47sambamba na masharti yake yaliyopo kwenye Kanuni ya 48.Ikikupendeza unaweza ukaamua, aidha Bunge lijadili kamaitakupenda ama Serikali itoe majibu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi yetu sisi haifuati misingiya dini, lakini sisi wananchi tunaoishi kwenye hii nchi tunadini zetu na dini zimegawanyika katika madhehebumbalimbali, ukiingia kwenye dini ya kiislamu ina madhehebumengi na ukienda kwenye dini ya kikristo ina madhehebumengi. Viongozi wetu wamekuwa wakilitambua na kulijuahili.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa naomba Mwongozowako kwa nini kwa upande wa dini ya kiislamu Serikali

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

70

imekuwa ikifanya kazi na ikitambua taasisi au dhehebu mojatu linaloitwa BAKWATA ikiacha madhehebu mengine. UkiachaBAKWATA, taasisi hii inayoitwa BAKWATA, lakini taasisi zinginezote hata zikiwa na shughuli zake kubwa zimekuwahazitambuliki na wakati mwingine hata ushiriki wa viongoziwakubwa wa Kiserikali hawaonekani. Kwa hiyo nilikuwanaomba mwongozo wako kwamba je hivi BAKWATA ndiotaasisi pekee iliyopewa mamlaka na Serikali ya kuwasemeawaislamu wa nchi hii?

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba mwongozo wako.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mtolea.

MHE. ABDALLAH A. MTOLEA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi nimesimama hapakwa hisani ya Kanuni ya 68(7).

Mheshimiwa Naibu Spika, Kiti chako mara kadhaakimekuwa kikiri kwamba kuna idadi kubwa sana ya maswaliya Waheshimiwa Wabunge na muda ambao upo kwa ajiliya kujibu hautoshi kwa maswali yote kupata nafasi. Kwamaelezo hayo tulitegemea kwamba kigezo kitakachokuwakinatumika kwa kujibu maswali ni ile first in, first out.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo nilikuwa najaribu kupitiamaswali ambayo yameulizwa hapa nikagundua kwambaswali kwa mfano la Mheshimiwa Goodluck Mlinga aliulizasiku nyingi sana, Mheshimiwa Pauline Gekul aliuliza mwaka2016, Mheshimiwa Constantine Kanyasu aliuliza mwaka 2016,Mheshimiwa Daimu Mpakate hakumbuki, lakini MheshimiwaMussa Mbarouk aliuliza Novemba 2017. Kwa uchacheukiangalia utagundua kumbe kigezo siyo first in, first out.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba mwongozo wakokwanza tujue ni kigezo gani kinatumika kupanga maswali iliyaweze kujibiwa? Pili kwa nini hatupati acknowledgementletter pale tunapopeleka maswali angalau tuambiwekwamba, swali lako limepokelewa, lipo kwenye mchakato,siku likipata nafasi litajibiwa. Angalau tuwe na kitu cha

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

71

kuonesha kwamba, swali langu lipo maana hivi tunavyokaa,mimi binafsi nina maswali sita toka mwaka 2016hayajajibiwa. Sasa nashindwa kujua kwamba, hayo maswaliyameshatupwa kapuni au yapo kwenye foleni ya kusubirikujibiwa au la?

Mheshimiwa Naibu Spika, pia maswali mengineyanapokaa mwaka mzima yanapoteza ule umuhimu wake.Linapoletwa kuja kujibiwa hapa yale majibu yanakuwa tenasiyo relevant kwa wakati ambao tuliuliza. Kama muda wakujibu maswali ni mdogo kwa nini basi, isiangaliwe baadhiya maswali au maswali ya muda mrefu yajibiwe kwamaandishi kwa sababu haya maswali mengine tunatumwana wananchi, sasa unapokaa mwaka mzima haliulizwi nahuna majibu inaleta mchanganyiko na mengine tunatumwana Mabaraza yetu ya Halmashauri kwamba fuatilia hili. Sasakwa nini basi tusijibiwe hata kwa maandishi?

Mheshimiwa Naibu Spika, je, baada ya muda ganiMbunge atambue kwamba swali langu sasa litakuwalimetupwa kapuni na halitaulizwa tena ili kama anawezaaandike tena au achukue maamuzi mengine?

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Mwongozo wako.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge nimeombwamwongozo na Mheshimiwa Bobali na pia MheshimiwaMtolea. Nitaanza na Mheshimiwa Bobali ambayeamesimama akiomba Mwongozo halafu akataja Kanuni ya47 na Kanuni ya 48.

Maelezo aliyoyatoa Mheshimiwa Bobaliamezungumza kuhusu nchi yetu kutokuwa na dini nakwamba wananchi wake ndio wenye dini na hilo ni waziwote tunalifahamu, na ameeleza katika dini hizi kwambayako madhehebu mbalimbali.

Mheshimiwa Bobali anaomba Mwongozo wangukwamba kwa nini, Serikali inaitambua BAKWATA pekee kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

72

upande wa waislamu na kwamba madhebu mengine hatayanapokuwa na matukio makubwa Serikali haishiriki kwenyematukio hayo. Pia ameuliza kwamba je, BAKWATA ndichochombo kinachowasemea waislamu wote hata waleambao madhehebu yao hayapo chini ya BAKWATA?

Waheshimiwa Wabunge, Mwongozo unaombwachini ya Kanuni ya 68(7) kwa jambo ambalo limetokeamapema Bungeni na mapema ilishatafsiriwa kwamba nimapema siku hiyo. Jambo hili aliloliomba Mheshimiwa Bobalikutolewa Mwongozo na Kiti hapa halijatokea hapa Bungeni.Kwa hiyo, kama anahitaji Bunge hili kutoa maelezo kuhusujambo hilo atumie Kanuni inayohusika na afuate utaratibuunaotakiwa. Mwongozo unaombwa kwa jambo lililotokeaBungeni mapema.

WNimeombwapia Muongozo na Mheshimiwa Mtoleakuhusu maswali. Mheshimiwa Mtolea ametoa maelezo kwakirefu, kwa kufupisha tu amezungumza kwamba maswalimengine yanachukua muda mrefu zaidi na yako maswaliambayo yalikuja siku nyingi na hayajasikika na WaheshimiwaWabunge hawana hakika kama hayo maswali bado iko sikuyatapangiwa ama hapana. Ametoa mfano wa maswaliyaliyoulizwa leo ambayo mengine ni ya muda mrefu na kwahivyo, majibu yanavyotolewa leo mambo mengineyalishafanyika zamani.

Sasa ameuliza kuhusu vigezo vya kupangwa maswalina pia namna gani ya kutambua kwamba, maswaliyamepokelewa, ikiwa Mbunge hapewi maandishi yoyotekwamba sasa swali lako limepokelewa. Pia, ameulizakwamba ni baada ya muda gani ukipita hatajua kama swalilake litajibiwa ama halitajibiwa.

Waheshimiwa Wabunge, Bunge linapopokea maswaliya Wabunge kuna vitu vingi ambavyo huangaliwa, si kwalengo la kuzuia maswali yasijibiwe, lakini ni Bunge linatakakujiridhisha na vile vitu vinavyoulizwa. Wakati mwinginemaswali yanakuwa yakilingana ya Mbunge mmoja namwingine, kwa hiyo, hawawezi wote kupewa fursa ya kuuliza

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

73

maswali yanayolingana, lakini jambo kubwa la msingi nikwamba maswali yanachukua muda mrefu.

Waheshimiwa Wabunge, katika maswali kuchukuamuda mrefu, nadhani yeye amesema ya kwake ni ya mwaka2016 na hii ni 2018 naamini kwamba ni yote maana hujaeleza,nimeshawahi kukusoma hapa ukiwa na swali la msingi, sijuihilo utakuwa ulileta lini, lakini huenda una maswali mengina mengine hayajajibiwa. Sasa ili upate majibu mahsusikuhusu maswali yako wewe inabidi uende kwenye Kitengochetu kinachoshughulikia maswali ili uone utaratibu wa hayomaswali yako.

Waheshimiwa Wabunge, kama ambavyo alivyokirimuomba muongozo, Waheshimiwa Wabunge tuko 393 kilamtu anapeleka maswali idadi anayoona yeye inafaa. Sasayako maswali mengine kuuliza vitu ambavyo pengineKikanuni ama kisheria haviruhusiwi, kwa hiyo, hayo hayawezikuja, lakini yale ya jumla ambayo yanaruhusiwa kuja, idadiya maswali ni kubwa kuliko fursa zinazojitokeza.

Hata hivyo, niwaombe Waheshimiwa Wabungeambao pengine walishaleta maswali mengi sana hukonyuma na hakuna hata moja lililopata nafasi, basi waendewapate kujua kama hayo maswali yote yameruhusiwaKikanuni kwa hivyo, yatapangiwa muda ama yako yaleambayo hayako sawa Kikanuni, kwa hiyo hayatawezakuwepo ili Wabunge hao waweze kuleta maswali mapya.

Waheshimiwa Wabunge, kwa hiyo, Mwongozowangu ni kwamba Mheshimiwa Mtolea pamoja na Wabungewengine wenye hoja kama yake waende kwenye Kitengochetu kinachopokea hayo maswali ili waweze kutolewaufafanuzi wa maswali yao yamefikia wapi.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kusema hayotutaendelea na ratiba iliyo mbele yetu. Katibu.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

74

NDG. JOSHUA CHAMWELA – KATIBU MEZANI:

HOJA ZA KAMATI

Bunge lipokee na Kukubali Taarifa ya Kamati ya Kudumuya Bunge ya Miundombinu kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017 na Kamati ya Kudumu ya Nishati na

Madini kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017

NAIBU SPIKA: Tutaanza na Mheshimiwa Mwenyekiti waKamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, MheshimiwaProfesa Norman Sigalla King.

MHE. PROF. NORMAN A. S. KING – MWENYEKITI WAKAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU:Mheshimiwa Naibu Spika, Taarifa ya Utekelezaji wa Shughuliza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kwa Kipindicha Januari, 2017 hadi Januari, 2018.

Mheshimiwa Naibu Spika, Sehemu ya Kwanza nimaelezo ya jumla. Kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu zaBunge, Kanuni ya 117(15), Toleo la Januari 2016, naombakuwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu taarifa ya Mwaka yaShughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinukwa kipindi cha Januari 2017 hadi Januari 2018.

Mheshimiwa Naibu Spika, mtiririko wa Taarifa hiiumegawanyika katika maeneo makubwa manneyafuatayo:-

(a) Sehemu ya Kwanza – maelezo ya jumla.

(b) Sehemu ya Pili - uchambuzi wa matokeo yautekelezaji wa majukumu ya Kamati.

(c) Sehemu ya Tatu - maoni, mapendekezo na ushauriwa Kamati.

(d) Sehemu ya Nne - hitimisho.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

75

Mheshimiwa Naibu Spika, majukumu ya Kamati; kwamujibu wa Kanuni za Bunge, Nyongeza ya Nane, Kanuni ya6(8), Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imepewajukumu la kuisimamia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi naMawasiliano. Katika kusimamia Wizara hiyo, Nyongeza yaNane, Kanuni ya 7(1) ya Kanuni za Bunge Toleo la Aprili, 2016imeainisha majukumu ya Kamati kama ifuatavyo:-

(a) Kushughulikia Bajeti ya Wizara inayoisimamia.

(b) Kushughulikia Miswada ya Sheria na Mikatabainayopendekezwa kuridhiwa na Bunge iliyo chini ya Wizarahusika.

(c) Kufuatilia Utendaji wa Mashirika ya Umma yaliyochini ya Wizara inayoisimamia.

(d) Kushughulikia Taarifa za Utendaji za kila mwakaza Wizara husika.

(e) Kufuatilia utekelezaji unaofanywa na Wizara kwamujibu wa Ibara ya 63 (3)(b) cha Katiba.

Mheshimiwa Naibu Spika, shughuli zilizotekelezwakatika kipindi cha mwaka 2017/2018; katika kipindi chakuanzia Januari 2017 hadi mwezi Januari 2018, Kamatiilitekeleza majukumu yake kwa njia ya kufanya vikaombalimbali pamoja na ziara kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, vika; vikao vyakushughulikia taarifa za utendaji wa Mashirika na Taasisi zilizochini ya Wizara ambayo Kamati inaisimamia; Vikao hivyovilihusisha Mamlaka ya Bandari Tanzania – TPA, RailwayHolding Company – RAHCO, Mamlaka ya Viwanja vyaNdege Tanzania – TAA, Kampuni ya Meli Tanzania – MSCL,Wakala wa Barabara Tanzania – TANROADS, Bodi ya Usajiliwa Makandarasi, Bodi ya Usajili wa Wahandisi, TEMESA,Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Mfuko wa Mawasilianokwa Wote, Kampuni ya Simu Tanzania, Tume ya TEHAMA naShirika la Posta.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

76

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, pia Kamati ilifanya ziara,ilipata fursa ya kutembelea mikoa karibu 22 ya Tanzania Bara;kujionea jinsi Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote unavyopelekamawasiliano katika maeneo yaliyoko pembezoni. Mikoailiyotembelewa ni pamoja na Tanga, Kilimanjaro, Arusha,Manyara, Dodoma, Singida, Tabora, Mwanza, Simiyu, Mara,Pwani, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe, Mbeya, Songwe,Rukwa, Katavi, Kigoma, Kagera na Geita.

(c) Mheshimiwa Naibu Spika, pia Kamati ilipata nafasiya kushiriki uzinduzi wa ujenzi wa reli ya kisasa (standardgauge) kutoka Dar es Salaam – Morogoro, uwekaji wa jiwela msingi kwa ajili ya kuongeza kina cha Bandari ya Dar esSalaam Gati Namba Moja mpaka Saba, Bandari ya Mtwarapia uzinduzi wa barabara mbalimbali zikiwemo Msata –Bagamoyo na katika Mikoa mingine ya Singida, Tabora,Kigoma, Kagera na Geita na daraja la Furahisha MjiniMwanza. Aidha, Kamati ilihudhuria uzinduzi wa viwanja vyandege vya Tabora na Bukoba pamoja na kiwanja cha ndegecha Chato na uzinduzi wa Hostel za Chuo Kikuu zilizojengwana TBA.

(d) Mheshimiwa Naibu Spika, pia Kamati iliendeleana kuchambua na kujadili Bajeti ya Wizara Ujenzi, Uchukuzina Mawasiliano. Sekta ya Ujenzi Fungu 98, Sekta ya UchukuziFungu 62 na Sekta ya Mawasiliano Fungu 68.

(e) Mheshimiwa Naibu Spika, pia Kamati ilifanya vikaovya kuchambua Miswada ya Sheria na Mikataba ya Kimataifailiyopendekezwa kuridhiwa. Katika kipindi cha mwakammoja, Kamati ilichambua Miswada na Mikataba ifuatayo:-

i. Muswada wa Sheria ya Reli Tanzania ya mwaka2017.

ii. Azimio la Bunge la kuridhia Itifaki ya Nyongeza yaTano ya mwaka 1994, Itifaki ya Nyongeza ya Sita ya Mwaka1999, Itifaki ya Nyongeza ya Saba ya mwaka 2004, Itifaki yaNyongeza ya Nane ya mwaka 2008 na Itifaki ya Nyongeza yaTisa ya mwaka 2016 ya Katiba ya Umoja wa Posta Duniani.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

77

iii. Muswada wa Sheria ya Shirika la MawasilianoTanzania wa mwaka 2017.

iv. Muswada wa Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzaniawa mwaka 2017.

Mheshimiwa Naibu Spika, uchambuzi wa matokeoya utekelezaji wa majukumu ya Kamati. Katika utekelezajiwa majukumu yake, Kamati ilipata fursa ya kupitia nakuchambua utekelezaji wa Bajeti ya Wizara hii kwa mwakawa fedha 2016/2017 pamoja na mapendekezo na makadiriokwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Bajeti ya mwaka wafedha 2017/2018, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilianoiliidhinishiwa shilingi trilioni 4.5. Mgawanyo wa fedha hizikatika kila Sekta ni kama ifuatavyo:-

i. Shilingi 1,929,707,714,000/= Sekta ya Ujenzi;

ii. Shilingi 2,569,073,208,000/= Sekta ya Uchukuzi; na

iii. Shilingi 18,104,139,000 Sekta ya Mawasiliano.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati imebaini kuwamwenendo wa Bajeti inayotengwa kwa ajili ya Sekta hii nimzuri na umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka. Hivyo,Kamati inaipongeza Serikali sana kwa kuipa Sekta yaMiundombinu kipaumbele.

Mheshimiwa Naibu Spika, Sekta ya Uchukuzi, Mamlakaya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA); Mamlaka ya BandariTanzania ina majukumu ya kuendeleza bandari, kuendeshashughuli za bandari, kutangaza huduma za bandari,kushirikisha na kusimamia sekta binafsi katika uendeshaji wabandari. Mamlaka hii inamiliki na kusimamia Bandari Kuu zaDar es Salaam, Tanga, Mtwara pamoja na Bandari Ndogoza Kilwa Masoko, Kilwa Kivinje, Kwale, Lindi, Mikindani, Mafia,Pangani na Bagamoyo. Vilevile, Mamlaka ya BandariTanzania (TPA) inamiliki bandari kadhaa za Maziwa Makuukama Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

78

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati imeelezwakwamba, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania – TPAinakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo:-

a. Uwezo mdogo wa kuhudumia meli kubwainayotakana na kina kifupi katika bandari ya Dar es Salaampamoja na Tanga.

b. Uchakavu wa miundombinu ya bandari nchini.

c. Uwepo wa bandari bubu na ushindani wa bandarizingine kama vile za Beira-Msumbiji, Mombasa-Kenya naDurban-Afrika Kusini.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na changamotohizo, Kamati inaipongeza Serikali kupitia Mamlaka ya BandariTanzania kwa kuanza kutekeleza baadhi ya ushauri wakekama ifuatavyo:-

(i) Mgongano uliokuwepo kwa tozo za hifadhi zamizigo (Warehouse Rent) inayotozwa na Mamlaka ya MapatoTanzania (TRA) na Storage Charges zilizokuwa zinatozwa naBandari umerekebishwa.

(ii) Pia Himaya ya Forodha kwa Pamoja (SingleCustoms Territory) kwa mzigo wa Congo, Kamati imejulishwakuwa Serikali imetoa notice ya muda wa mwezi mmoja, ilikuvunja Mkataba huo ambao umekuwa ukileta utata nakupunguza motisha kwa wafanyabishara wa Congo kutumiaBandari ya Dar es Salaam.

(iii) Aidha, Serikali imefuta Kodi ya Ongezeko laThamani (Value Added Tax-VAT) kwa huduma zitolewazo namawakala kwenye mizigo inayosafirishwa kwenda nchi jirani(VAT on transit goods).

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuboresha nakuongeza ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam, Kamatiimejulishwa kuwa hatua mbalimbali za utekelezaji zimefikiwakama ifuatavyo:-

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

79

(i) Kuhusu ujenzi wa Gati Namba Moja hadi Saba nagati la kushushia meli za magari; Mkandarasi yupo katikaeneo la kazi na kwa sasa imefanyika kazi kwa asilimia 15.

(ii) Kuhusu kuongeza kina na upana wa lango lakuingilia meli, kazi hii ipo katika hatua mbalimbali zakutangazwa kwa ajili ya kumpata Mkandarasi na Mtaalammwelekezi.

(iii) Ujenzi gati Namba 12-14; utekelezaji wa ujenzi wagati hizi utafanyika katika awamu ya pili ya maboresho naupanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam. Kwa sasa Serikali badoipo kwenye majadiliano na wafadhili ili kufanya upembuziyakinifu wa namna bora ya kuhamisha Kurasini Oil Jet namiundombinu yake kwa ajili ya kupisha ujenzi wa magatihayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati ukarabati naupanuzi wa bandari ya Dar es Salaam unaendelea; ni vyemaSerikali ikaanza pia ukarabati wa bandari nyingine muhimukama vile Bandari ya Tanga, Bandari ya Mtwara, Bandari yaMwanza, Bandari ya Kigoma na Bandari ya Ziwa Nyasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa reli; Kamati inatoapongezi kwa jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ilikufufua na kuimarisha mtandao wa reli nchini. Miongonimwa juhudi hizo ni pamoja na kuendelea na ujenzi wa reliya kati kwa kiwango cha kisasa (standard gauge). Hivyo,katika kuendeleza juhudi hizo mnamo mwezi Septemba,2017, Serikali ilileta Muswada wa Sheria ya Reli wa 2017 ambaomoja kati ya majukumu yake ilikuwa ni kuanzisha Shirika jipyala Reli (Tanzania Railway Corporation – TRC) ambalo pamojana mambo mengine, litakuwa na jukumu la kusimamia,kuendeleza miundombinu ya Reli na kutoa huduma za usafiriwa reli.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mipango ya Sektaya Uchukuzi ya mwaka 2017/2018, miongoni mwa malengoyaliyowekwa kuhusu kuimarisha miundombinu ya reli nchinini pamoja na kuendelea na ujenzi wa reli ya kisasa. Hivyo,Serikali kwa kutambua umuhimu wake imetenga karibu bilioni900 kwa ajili ua jambo hilo.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

80

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati imejulishwa kuwaujenzi wa reli hii umegawanyika katika sehemu tanozifuatazo:-

(i) Dar es Salaam – Morogoro, kilometa 205, ujenziumeshaanza.(ii) Morogoro – Makutupora, kilometa 336, mradi unatarajiwakuzinduliwa mwezi Februari, 2018.(iii) Pia Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya Makutupora –Tabora, kilometa 295.(iv) Tabora – Isaka kilometa 133.(v) Isaka – Mwanza kilometa 250.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu ujenzi wa reli yakisasa katika maeneo mengine nchini kwa kiwango chakisasa (standard gauge), ujenzi wa reli ya kutoka Mtwara hadiMbaba Bay na matawi yake kuelekea Liganga naMchuchuma kilometa 1,092 upembuzi yakinifu umekamilika.Vilevile reli ya kutoka Tanga – Arusha – Musoma yenye urefuwa kilometa 1,108 na Arusha kilometa 438, shughuli zaupembuzi yakinifu na usanifu wa awali zimekamilika.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na maendeleomazuri katika mradi wa ujenzi wa reli hii ya kisasa, mradi huuunakabiliwa na changamoto zifuatazo:-

i. Usajili wa raia wa kigeni katika bodi za taalumanchini, yaani wafanyakazi wa reli.

ii. Upatikanaji wa maeneo ya ujenzi (ardhi) nje yamaeneo yanayomilikiwa na RAHCO.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kampuni ya Ndege yaTanzania – ATCL; Kamati imejulishwa kuwa pamoja na ndegembili mpya aina ya Dash 8 Q400 kwa sasa, Kampuni inamilikindege tatu ambazo zinafanya ziara zake ndani ya nchi.Kamati imejulishwa kuwa mwezi Julai, 2018; Serikaliinategemea kupokea ndege zingine mbili ambapo moja niDash 8 Q400 na nyingine ni ndege kubwa aina ya Boeing 787yenye uwezo wa kubeba abiria 262.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

81

Mheshimiwa Naibu Spika, Sekta ya Ujenzi Wakala waBarabara Tanzania (TANROADS); jukumu kubwa la wakalahuu ni kuhudumia mtandao wa barabara ambaounakadiriwa kuwa na urefu wa jumla ya kilometa 35,000ambapo kati ya hizo, kilometa 12,786 ni barabara Kuu, nakilometa 22,214 ni barabara za mikoa. Lengo ni kuwezeshabarabara ziweze kupitika kwa urahisi na hatimaye kusaidiaukuaji wa uchumi, kama ilivyofafanuliwa katika Mpango naMikakati ya Kitaifa na Kimataifa, ikiwemo Dira ya Taifa yaMaendeleo 2015, Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano naMikakati ya Kisekta.

Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikio hayoWakala wa Barabara anakabiliwa na changamotombalimbali zikiwemo:-

(a) Kutokutolewa kwa wakati fedha za miradi yamaendeleo hali inayosababisha kazi zilizopangwa kwabaadhi ya miradi kutotekelezwa ama kutekelezwa kwa kiasikidogo;

(b) Msongamano wa magari barabarani hasa Jiji laDar es Salaam, na miji mingine inayokuwa kwa kasi, kamavile Jiji la Mbeya, Mwanza na Arusha;

(c) Baadhi ya wasafirishaji kuendelea kuzidisha uzitowa mizigo kwenye magari na kusababisha uharibifu wabarabara; na

(d) Uwezo mdogo wa wakandarasi wa ndani katikautekelezaji wa miradi mikubwa ya ujenzi wa barabarakutokana na kukosa mitaji vifaa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu matuta barabarani.Licha ya Wakala wa Barabara (TANROADS) kuahidi kuendeleakurekebisha matuta makubwa, ili kuyaweka katika viwangovilivyoainishwa katika mwongozo wa Wizara kuhusu usanifuwa barabara wa mwaka 2011, bado kumeendelea kuwapomatuta makubwa hasa katika barabara kuu ambapoyamekuwa chanzo cha uharibifu wa barabara, kwani magari

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

82

yenye mizigo hulazimika kwenda mwendo mdogo; hivyouzito kuwa mkubwa na kusababisha barabara kutitia.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, matuta barabaraniyamekuwa yakisababisha mizigo kuhama na kuelemeaupande mmoja; jambo ambalo wakati mwingine limekuwachanzo cha ajali kwa magari mengi ya mizigo. Pia matutahusababisha myumbo wa matairi (wheel alignment) hivyokuchochea ubovu na kuongeza uwezekano wa ajali.

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa viwanja vyandege nchini umeendelea kutekelezwa chini ya Sekta ya Ujenzina Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS). Kamatikatika kutekeleza majukumu yake imebaini kuwa ujenzi waviwanja vya ndege umeendelea kwa kasi kubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kulikuwepo nachangamoto ya kupatikana kwa fedha kwa wakati kwa ajiliya ujenzi wa viwanja ndege nchini. Hata hivyo, Kamatiimejulishwa kuwa upatikanaji wa fedha kwa ajili ya ujenziwa viwanja vya ndege kwa sasa ni mzuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu ujenzi wa jengo laabiria (Terminal III) katika Kiwanja cha Kimataifa cha JuliusNyerere, mkataba ulisainiwa 18 Aprili, 2013. Hadi kufikiaDesemba, 2017; utekelezaji wa kazi ulifikia asilimia 68 ambapokazi zilizoendelea ni kuezeka na kumalizia kazi za kusimikamitambo ya umeme, viyoyozi na utandazaji wa nyaya namabomba.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi wa ujenzi wa kiwanjacha ndege cha Mwanza ulianza mwezi Oktoba, 2012 naulipangwa kukamilika mwezi Septemba, 2014. Hata hivyo,hapo awali mradi huu ulikuwa ukikabiliwa na changamotoya upatikanaji wa fedha kwa wakati hivyo kusababishautekelezaji wake kuwa ndogo. Lakini sasa hali ya fedhaimetengamaa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu ujenzi wa kiwanjacha ndege cha Songwe mkoani Mbeya ulianza mwaka 2000

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

83

ambapo ujenzi umekuwa ukitekelezwa kwa awamukulingana na upatikanaji wa fedha. Kiwanja hiki ni muhimusana kwa wakazi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na hatawasafiri kutoka nchi jirani za Zambia na Malawi. Tangukiwanja hiki kilipofunguliwa rasmi mwaka 2012 kumekuwepona ongezeko kubwa la abiria na ndege. Hata hivyo, pamojana umuhimu mkubwa wa kiwanja hiki, mradi huu piaumekuwa ukitekelezwa kwa kasi ndogo, jambolinalosababisha mradi kutokukamilika kwa wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, pamoja nachangamoto hizo katika ujenzi wa kiwanja hiki, Kamati tokamwaka 2016 imekuwa ikishauri mara kwa mara umuhimuwa kuwekwa kwa taa za kuongozea ndege ambazozitasaidia ndege kutua nyakati za usiku na hata mchanawakati wa ukungu mkubwa. Hali kadhalika kuwekwa kwauzio kuzunguka mipaka yote ya kiwanja ili kuongeza usalamawa kiwanja na kuepuka uvamizi na wananchi wa maeneojirani kukatiza katika maeneo ya kiwanja.

Mheshimiwa Naibu Spika, kiwanja cha ndege chaKigoma. Pamoja na kuwa mradi huu upo mingoni mwamiradi inayogharamiwa kwa mkopo kutoka Benki yaUwekezaji ya Ulaya, Kamati imejulishwa kuwa ilikubaliwakuwa kabla ya fedha za mkopo kuanza kutoka Serikali iweimeshalipa fidia kwa wananchi wote watakaothiriwa naukarabati na upanuzi wa kiwanja hiki.

Mheshimiwa Naibu Spika, sekta ya mawasiliano,Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania yaani TCRA. Serikalikupitia TCRA imeweka mfumo wa kusimamia mawasilianoya simu ambao umechangia kuongeza ufanisi katikautekelezaji wa Sheria na Kanuni zilizopo katika udhibiti wamawasiliano, ikiwa ni pamoja na kuhamasisha mabadilikoya teknolojia ili kuongeza ubora wa huduma na kuendanana kasi ya mabadiliko yanayotokea. Mfumo wa TTMS pamojana mambo mengine mpaka kufikia Desemba, 2017umewezesha mambo yafuatavyo:-

(a) Kuhakiki mawasiliano ya simu za ndani;

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

84

(b) Mfumo wa kubaini simu za ulaghai;

(c) Mfumo wa kuhakiki mapato yatokanayo nahuduma za mawasiliano;

(d) Kudhibiti uhalifu katika mitandao;

(e) Uanzishwaji wa maabara ya kisasa ya kiuchuguziya kidijitali; na

(f) Kuweka viwango vipya vya mwingiliano baina yamitandao ya simu nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mfuko wa Mawasiliano kwaWote (UCSAF) ulianzishwa kwa lengo la kupeleka hudumaya mawasil iano maeneo yasiyokuwa na mvuto wakibiashara. Mwezi Oktoba, 2017 Kamati ilipata nafasi yakutembelea maeneo mbalimbali ili kujionea ikiwa hudumaza mawasiliano zinapatikana katika sehemu hizo ambazominara imejengwa. Katika ziara hiyo, Kamati ilitembeleatakribani mikoa 20 ya Tanzania Bara na Kamati ilibainichangamoto zifuatazo;-

(a) Serikali za Mikoa, Wilaya pamoja na wananchihawajui uwepo wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote nakwamba miradi hiyo ya ujenzi wa minara inatoka kwenyeruzuku ya Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote.Dhana iliyoko maeneo mengi ni kuwa minara inajengwa naMakampuni ya simu yenyewe, hivyo mchango wa Serikalikatika kusambaza mawasiliano hautambuliki.

(b) Pamoja na kuwa makampuni yamepewa mashartiya kuwajibika katika kutoa huduma za jamii katika maeneoyanayofanya shughuli zake za kibiashara kwa kiasi kiasikikubwa makampuni haya yamekuwa hayatoi huduma hizi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa minara kwakutumia Kampuni ya TTCL ulikuwa ukisuasua kwa siku zanyuma, hata hivyo baada ya Kamati kufanya ziara ya ukaguziwa minara mwaka wa jana, TTCL imekamilisha miradi yake

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

85

yote iliyokuwa inadaiwa na Mfuko wa Mawasiliano kwaWote.

Mheshimiwa Naibu Spika, migogoro ya ardhi Katikamaeneo mengi ambayo Kamati imetembelea minarayamebainika wazi kuwa na migogoro ya umiliki wa maeneohusika. Pia kumekuwa na changamoto ya wizi wa vifaa vyaminara kama vile mafuta, betri na nyaya aina ya fiber. PiaMinara mingi iliyojengwa inatumia umeme wa jua (solarpower), hii inasababisha nyakati za usiku hasa kipindi chamvua maeneo mengi kuwa na mawasiliano hafifu kwasababu jua haliwaki kipidi kirefu. Makampuni pia yanajengaminara pasipo kuweka huduma za kijamii kama choo,kibanda cha mlinzi na huduma zingine za msingi kwenyemaeneo ya mnara.

Mheshimiwa Naibu Spika, Sehemu ya Tatu nimapendekezo na ushauri wa Kamati. Kamati inapongezaSerikali kwa kuona umuhimu wa kuendeleza miundombinunchini ambapo bajeti ya mwaka 2017/2018 Serikali iliendeleakuongeza tengeo la fedha katika sekta ya miundombinu hadikufikia shilingi trilioni 4.5.

Mheshimiwa Maibu Spika, hii inaonyesha kwa kiasikikubwa serikali imezingatia umuhimu wa kuharakiashamaendeleo katika nchi yetu kwani miundombinu ndiyoitawezesha tija na utendji bora wa sekta nyingine. Hata hivyopamoja na shabaha nzuri ya serikali katika masula yamiundombinu kamati inazizitiza fedha kutolewa kwa wakatiili kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo nakuepuka limbikizo la madeni.

Mheshimiwa Naibu Spika, sekta ya uchukuzi; Mamlakaya Bandari Tanzania; kwa kuwa Mamlaka ya Bandari Tanzaniandiyo mamlaka iliyopewa jukumu la kusimamia jukumu labandari nchini; na kwa kuwa mamlaka hii inayo miradi mingiya ujenzi na ukarabati wa bandari ambapo kwa sasamamlaka ipo katika hatua ya kuboresha na kufanyaukarabati wa bandari kama vile Mtwara na ujenzi wamagati pamoja uchimbaji wa kina katika Bandari ya Dar es

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

86

Salaam; kwa hiyo basi Kamati inaishauri Serikali kamaifuatavyo:-

(a) Asilimia 20 ya mapato ya bandari yabaki bandariniili kuwezesha Mamlaka ya Bandari Tanzania iweze kutekelezabaadhi ya miradi kama vile miradi ya ujenzi wa bandari yaKalema, Kigoma na Mtwara ambayo jumla inagharimubilioni 20, wakati mapato ya bandari kwa mwaka ni wastaniwa bilioni 270;

(b) Kuharakisha mchakato wa ununuzi wa flow metermpya kwa ajili ya upimaji wa mafuta yanayoingia Bandariya Dar es Salaam. Kamati ilitembelea bandari na kuonatatizo la kutokuwepo na flow meter na hivyo kutokujua kwauhakika kiwango cha mafuta kinachoingia Bandari ya Dares Salaam. Ni rai ya Kamati kuwa flow meter inunuliwe kwaharaka. Hivi tunavyoongea sasa tatizo hil i badohalijashughulikiwa; na

(c) Kuunganisha zabuni za ujenzi wa bandari yaKigoma il i kuweza kupata mzabuni mwenye uwezoatakayefanya kazi hiyo; kwani imekuwa ikitangazwa marakadhaa bila kupata mzabuni kutokana na gharama yamaandalizi (mobilization) kuwa kubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa reli nchini; kwakuwa Serikali imeonyesha nia dhati ya kujenga reli ya Katikatika kiwango cha kisasa (standard gauge) ambapo mradihuu umeanza tangu mwezi Aprili, 2017na unatekelezwa kwaawamu tano; na kwa kuwa katika uhalisia tawi la kutokaTabora – Kigoma - Uvinza - Msongati na Kaliua - Mpanda -Kalema ndilo lenye mizigo mingi inatoka na kwenda nchijirani kama vile DRC Kongo Burudi na Ruanda. Hivyo basikamati inaishauri serikali ifuatavyo:-

(a) Reli hii ijengwe kwa kuzingatia faida za kiuchumina kipaumbe zaidi kiwekwe katika tawi la Tabora, KigomaTabora – Kigoma - Uvinza - Msongati; Kaliua – Mpanda –Kalema na Tabora – Mwanza.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

87

(b) Kuwapeleka kwenye mafunzo zaidi wataalamuili kuweza kuhudumia miundombinu za treni za kisasainayoendelea kujengwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mamlaka ya Viwanja vyaNdege Tanzania (TAA); kwa kuwa kumekuwa ya migogoromingi ya uvamizi wa maeneo ya viwanja vya ndege, na kwakuwa utatuzi wa migogoro hiyo umekuwa ukigharimu Serikalifedha nyingi kulipa fidia na kuchelewesha baadhi ya miradiya ujenzi wa viwanja hivyo; hivyo basi kamati inashauriifuatavyo:-

(a) Kuhakikisha kwamba TAA inapata hati za viwanjakwani Kamati imejulishwa kuwa viwanja vya ndege vinanetu ndivyo vyenye hati miliki kati ya viwanja 58 vinavyomilikiwana mamlaka ya viwanja vya ndege. Bado kuna haja yakuhakikisha kuwa viwanja vingine vimebaki vinapimwa nakupatiwa hati miliki;

(b) Ili kuepuka ongezeko la gharama za ujenzi ni vemaserikali ikakamilisha miradi ya ujenzi wa viwanja vya ndegevilivyoanza vikiwemo viwanja vya ndege vya Julius Nyererevya Terminal Three na Kiwanja cha Ndege cha Mwanza naKiwanja cha Ndege cha Songwe na kulipa fidia kamainavyotakikana.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kampuni ya Ndege ATCL.Kwa kuwa serikali imeonyesha nia ya dhati ya kufufu kampuniya Ndege Tanzania; na kwa kuwa biashara ya ndege inahitajimikakati mikubwa ya biashara ili kuweza kuingia katika sokola ushindani, Kamati inashauri ifuatavyo:-

(a) ATCL ij itangaze kwenye vyombo rasmi vyakimataifa ambavyo huonyesha safari za ndege dunia nzima.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, kampuni hii sasaijipange kuingia katika soko kwa kujitangaza katika vyombovya habari, majarida na vipeperushi mbalimbali, kujali watejana kuwa na bei nafuu ili kuhakikisha abiria wengi wanatumiandege hizi.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

88

Mheshimiwa Naibu Spika, Sekta ya Ujenzi, Wakala waBarabara Tanzania (TANROADS); kwa kuwa Wakala Barabaranchini (TANROADS) ndio waliokabidhiwa jukumu la ujenzi naukarabati wa barabara nchini, na kwa kuwa pamoja najitihada za Serikali kujenga barabara maeneo mbalimbalihivyo basi Kamati inashauri ifuatavyo:-

(a) Kuhakikisha inaunganisha miji yote na mikoailiyosalia kama vile mkoa wa Katavi – Kigoma, Katavi –Tabora, Kigoma – Kagera, Njombe - Makete - Mbeya kwabarabara za lami ili kufungua fursa za maendeleo katikamaeneo hayo.

(b) Ukarabati wa baadhi ya barabara za mikoa iliyokatika hali isiyoridhisha na kutopitika na hasa wakati wamvua na kuadhiri shughuli za kiuchumi na kilimo.

(c) Pia matuta madogo madogo ya barabaranimaarufu kwa jina la rasta na matuta makubwa yasiyo nakiwango yaondolewe kwa kuwa yanasababisha ajali nauharibifu wa magari. Aidha, matuta yabaki sehemu zenyeumuhimu tu na yawe na kiwango maalum. (Makofi)

(d) Kununua mizani ya kisasa ambayo ina uwezo wakupima uzito wa magari huku yakiwa kwenye mwendo(weight in motion). Kamati inaendelea kushauri kwambamizani hii ya kisasa ifungwe pia katika maeneo mengine yenyekusababisha msongamano mkubwa wa kupima magari;kwa mfano, Himo – Moshi, Mizani ya Mikese Morogoro,Kihonda, Morogoro, Makambako na Kwa Mpemba nikitajakwa uchache.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu kupunguzamsongamano katika Jiji la Dar es Salaam; kwa kuwa Serikaliimeonyesha nia ya kupunguza msongamano katika jiji la Dares Salaam kwa kuweka barabara za juu (flyovers) eneo laTazara na Ubungo na kwa kujenga barabara za michepuko;na kwa kuwa msongamano katika jiji la Dar es Salaamumekuwa ukisababisha adha kubwa, kwa hiyo basi kamatiinashauri serikali yafuatayo:-

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

89

(a) Barabara za juu maarufu kama flyovers zijengwehasa katika makutano ya barabara kuu zenye msongamanomkubwa kama vile Magomeni, Morocco na Mwenge.

(b) Wadau kama mifuko ya jamii inawezakushirikishwa katika kujenga barabara za kulipia.

(c) Pia kukamilisha ujenzi wa barabara zinazosaidiawakazi kufika maeneo yao bila kupita katikati ya Jiji la Dares Salaam ikiwa ni pamoja na kukamilisha barabara zakutoka Goba-Madale-Wazo Hill, Goba–Kimara-Ardhi-Makongo nakadhalika.

(d) Pia barabara za mitaani yaani Wingroads nazozifunguliwe kwa kuwekwa lami kwani zitapunguzamsongamano kwa kiasi kikubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Sekta yaMawasiliano; Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA); kwakuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ilianzishwa kwalengo la kusimamia mawasiliano nchini, na kwa kuwakumekuwepo changamoto mbalimbali zinazotokananaukuaji wa Technolojia hivyo basi kamati inashauri serikaliifuatavyo:-

(a) Kuendelea kudhibiti mawasiliano ya ulaghai nahatimaye kupunguza vitendo viovu vinavyofanyika kupitiamitandao na ili kuimarisha usalama wa watu mali zao.

(b) Mamlaka ya Mawasil iano Tanzania kwakushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania kuharakishakutafuta uvumbuzi wa namna bora ya kupata taarifa zamakusanyo ya simu za ndani kwa kutumia mitambo ya TTMCili serikali iweze kutoza kodi stahiki kutokana na miamala yafedha inayofanyika kupitia simu za mkono. Kuendeleakuchelewesha kulitekeleza suala hili kunazidi kuikosesha nchikodi stahiki kutokana na makapuni haya ya kutoza kodi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mfuko wa Mawasilianokwa Wote (UCSAF); kwa kuwa mfuko huu ulianzishwa wa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

90

lengo la kupeleka mawasiliano sehemu sizizokuwa na mvutowa kibiashara na kwa kuwa kamati bado hairidhishwi nakasi ya utekelezaji wa miradi wa usambazaji wa mawasilianosehemu hizo hivyo basi Kamati inashauri Serikali yafuatavyo:-

(a) Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA kuwekamasharti ya kutoa leseni kwa makampuni ya simu pamojana masharti mengine iwe kupeleka mawasiliano katikamaeneo ya pembezoni kama mchango kwa jamii(Corporate Social Responsibility).

(b) Kuhakikisha Makampuni ya simu yanatoa kiwangokilichopangwa cha asilimia 0.9 kama tozo za huduma (ServiceLevy Rate).

(c) Katika maeneo ambayo vijiji vimetoa ardhi burekwa ajili ya ujenzi wa minara; basi makampuni husikazichangie/ itoe ruzuku kwa kijiji husika kila mwaka.

(d) Mahakama na vyombo vingine viambata kamavile Jeshi la Polisi, watoe kipaumbele na kuharakisha kutoahaki kwenye masuala ambayo yanagusa umma moja kwamoja. Kuchelewa kutoa haki kwani kunacheleweshautekelezaji wa miradi hiyo.

(e) Halmashauri na Serikali za vijiji zitoe ushirikiano wakutosha na wa haraka pale ambapo maeneo yanahitajikakwa ajili ya ujenzi wa minara ili kuweza kurahisisha kupatamawasiliano kwa haraka.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi wa anuani za makazina misimbo ya posta; kwa kuwa mradi huu una manufaamakubwa kwani utawezesha kuwepo kwa utambulisho wamakazi ya watu na makampuni na hatimaye kurahisishashughuli zote za kijamii, kiuchumi na kisiasa; na kwa kuwautekelezaji wa mradi huu umekuwa ukisuasua; kwa hiyo basi,Kamati inashauri Serikali yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara husika ikiwemo Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makaz; TAMISEMI na Ujenzi,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

91

Uchukuzi na Mawasiliano zikae na kuona namna nzuri yakuharakisha mradi huu muhimu unatekelezwa haraka na kwaufanisi mkubwa na pia fedha kwa ajili ya utekelezaji wamradi huu zitolewe kama zilivyoidhinishwa na kwa wakati ilimradi huu ukamilike.

Mheshimiwa Naibu Spika, hitimisho, Kamatiinaendelea kusisitiza kuwa, ili Sekta ya Ujenzi, Uchukuzi naMawasiliano na Idara zake zote ziendelee kufanikiwa nilazima uteuzi na ajira za watendaji zifuate weledi, jamboambalo Kamati inaamini limezingatiwa. Pili, watendaji wataasisi hizo na dodi wasiingiliwe na watunga sera baliwapimwe kwa uzalishaji wao.

Mheshimiwa Naibu Spika, narudia; pili, watendaji wataasisi hizo na bodi wasiingiliwe na watunga Sera baliwapimwe kwa uzalishaji wao. (Makofi)

Tatu, sheria na taratibu zinazowekwa kwenye taasisizinazofanya biashara zifasili malengo mama ya taasisi hizo.Kama ni sheria au taratibu swali liwe uwepo wa sheria autaratibu hizo zinasaidia kuongeza ufanisi na faida katika taasisihizo?

Mheshimiwa Naibu Spika, hili likizingatiwa tutakuwana nafasi ya kuwahukumu watendaji na bodi kwa haki.

Mheshimiwa Spika, shukrani, napenda kukushukuruwewe binafsi kwa kunipa nafasi ya kuwasilisha Taarifa yaKamati yangu mbele ya Bunge lako Tukufu. Aidha, kwanamna ya pekee sana napenda kumpongeza na kumshukuruWaziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano rafikiyangu, Mheshimiwa Profesa Makame Mbarawa Mnyaa (Mb)akishirikiana na Naibu Mawaziri Mheshimiwa EngineerAtashasta Nditiye, (Mb) na Mheshimiwa Elias Kwandikwa.(Makofi)

Aidha, Kamati inawashukuru Makatibu Wakuu waWizara hii, Mhandisi Joseph Nyamuhanga kwa maana Sektaya Ujenzi, Mhandisi Dkt. Leonard Chamuriho - Sekta ya

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

92

Uchukuzi), Mhandisi Dkt. Maria Sasabo Sekta ya Mawasilianopamoja na Naibu Katibu Mkuu Ndugu Angelina Madete…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, muda wakoumekwisha naomba umalizie hoja yako na pia kulielezaBunge kwamba taarifa hii iingie kwenye Taarifa Rasmi zaBunge.

MHE. PROF. NORMAN A. S. KING – MWENYEKITI WAAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante napenda kuwashukuru Katibu nawasaidizi wake wote.

Mheshimiwa Spika, baada ya kueleza shughulizilizotekelezwa na Kamati maoni na ushauri sasa naombakutoa hoja kwamba Bunge lipokee lijadili na kuikubali taarifaya mwaka ya shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge yaMiundombinu kwa kipindi cha Januari, 2017/2018 pamoja namaoni na ushauri katika taarifa hii

Mheshimiwa Spika naomba kutoa hoja.

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA KAMATI YAKUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU KWA KIPINDI CHA

JANUARI 2017 HADI JANUARI 2018 – KAMAILIVYOWASILISHWA MEZANI

SEHEMU YA KWANZA

1:0 MAELEZO YA JUMLA1.1 Utangulizi

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu zaBunge, Kanuni ya 117 (15), Toleo la Januari 2016, naombakuwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu Taarifa ya Mwaka yaShughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinukwa kipindi cha Januari 2017 hadi Januari 2018.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

93

Mheshimiwa Spika, mtiririko wa Taarifa hii umegawanyikakatika maeneo makubwa manne yafuatayo:-

a. Sehemu ya I- Maelezo ya Jumla (Utangulizi);

b. Sehemu ya II- Uchambuzi wa Matokeo ya Utekelezaji waMajukumu ya Kamati;

c. Sehemu ya III- Maoni, Mapendekezo na Ushauri wa Kamati;na

d. Sehemu ya IV- Hitimisho

1.2 Wajumbe wa Kamati

Mheshimiwa Spika, Naomba kuwatambua Wajumbe waKamati hii kama ifuatavyo:-

1. Mhe .Prof. Norman Adamson Sigalla King, Mb – Mwenyekiti2. Mhe. Moshi Seleman Kakoso, Mb - M/ Mwenyekiti3. Mhe. Asha Mshimba Jecha, Mb - Mjumbe 4. Mhe. Abbas Ali Hassan Mwinyi, Mb ,, 5. Mhe. James Francis Mbatia, Mb ,,6. Mhe. Mansoor Shanif Hirani, Mb ,,7. Mhe. Anna Richard Lupembe, Mb ,,8. Mhe. Saul Henry Amon, Mb ,,9. Mhe. Ahmed Mabkhut Shabiby, Mb ,,10. Mhe. Quambalo Willy Qulwi, Mb ,,11. Mhe. Hawa Mchafu Chakoma, Mb ,,12. Mhe. Halima Abdallah Bulembo, Mb ,,13. Mhe.Dkt. Chuachua Mohamed Rashid, Mb ,,14. Mhe. Mary Deo Muro, Mb ,,15. Mhe. Zubeda Hassan Sakuru, Mb ,,16. Mhe. Bhagwanji Maganlal Meisuria, Mb ,,17. Mhe. Dua William Nkurua, Mb ,,18. Mhe. Musa Rashid Ntimizi, Mb ,,19. Mhe. Lathifah Hassan Chande, Mb ,,20. Mhe. Raphael Japhary Michael, Mb ,,21. Mhe. Ritta Enespher Kabati, Mb ,,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

94

22. Mhe. Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka, Mb ,,23. Mhe. Emmanuel Adamson Mwakasaka, Mb ,,24. Mhe. Charles Kitwanga, Mb ,,25. Mhe. Zuberi Mohammed Kuchauka, Mb ,,26. Mhe. Rukia Kassim, Mb ,,27. Mhe. Dkt. Pudenciana W. Kikwembe, Mb ,,

1.3 Majukumu ya Kamati

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge,Nyongeza ya Nane, Kanuni ya 6(8), Kamati ya Kudumu yaBunge ya Miundombinu imepewa jukumu la kuisimamiaWizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Katika kusimamiaWizara hiyo, Nyongeza ya Nane, Kanuni ya 7(1) ya Kanuni zaBunge Toleo la Aprili, 2016 imeainisha majukumu ya Kamatikama ifuatavyo:-

a) Kushughulikia Bajeti ya Wizara inayoisimamia;

b) Kushughulikia Miswada ya Sheria na Mikatabainayopendekezwa kuridhiwa na Bunge iliyo chini ya Wizarahusika;

c) Kufuatilia Utendaji wa Mashirika ya Umma yaliyo chini yaWizara inayoisimamia;

d) Kushughulikia Taarifa za Utendaji za kila mwaka za Wizarahusika; na

e) Kufuatilia Utekelezaji unaofanywa na Wizara kwa Mujibuwa Ibara ya 63 (3) (b) ya Katiba.

1.4 Shughuli zilizotekelezwa katika Kipindi cha Mwaka2017/2018

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanzia Januari 2017hadi mwezi Januari, 2018 , Kamati ilitekeleza majukumuyake kwa njia ya kufanya vikao mbalimbali pamoja na ziarakama ifuatavyo:-

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

95

a) Vikao vya kushughulikia taarifa za utendaji wa Mashirikana Taasisi zilizo chini ya Wizara ambayo Kamati inaisimamia;Vikao hivyo vilihusisha Mamlaka ya Bandari Tanzania-TPA,Railway Holding Company-RAHCO , Mamlaka ya Viwanja vyaNdege Tanzania- TAA, Kampuni ya Meli Tanzania- MSCL,Wakala wa Barabara Tanzania- TANROADS,Bodi ya Usajili waMakandarasi, Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Tanzania ElectricalMechanical and Electronics Services Agency-TEMESA,Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania-TCRA, Mfuko waMawasiliano kwa Wote-UCSAF, Kampuni ya Simu Tanzania-TTCL, Tume ya TEHAMA, Shirika la Posta Tanzania;

b) Ziara- Kamati ilipata fursa ya kutembelea Mikoa ishirini namiwili (22) ya Tanzania Bara; kujionea jinsi Mfuko waMawasiliano kwa Wote unavyopeleka Mawasiliano katikamaeneo yaliyoko pembezoni. Mikoa iliyotembelewa nipamoja na Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Dodoma,Singida, Tabora, Mwanza, Simiyu, Mara, Pwani, Lindi, Mtwara,Songea, Njombe, Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi, Kigoma,Kagera na Geita;

c) Kamati pia ilipata nafasi ya kushiriki uzinduzi wa ujenzi wareli ya kisasa (Standard Gauge) kutoka Dar es Salaam –Morogoro, uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya kuongezakina cha Bandari ya Dar es Salaam Gati Na. 1-7, Bandari yaMtwara pia uzinduzi wa barabara mbalimbali zikiwemoMsata – Bagamoyo na katika Mikoa mingine ya Singida,Tabora, Kigoma, Kagera na Geita na daraja la Furahisha –Mwanza. Aidha, Kamati ilihudhuria uzinduzi wa viwanja vyandege vya Tabora na Bukoba pamoja na kiwanja cha ndegecha Chato (Geita).

d) Vikao vya kuchambua na kujadili Bajeti ya Wizara Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano; Sekta ya Ujenzi Fungu 98, Sekta yaUchukuzi Fungu 62, Sekta ya Mawasiliano Fungu 68;

e) Vikao vya kuchambua Miswada ya Sheria na Mikataba yaKimataifa iliyopendekezwa kuridhiwa. Katika kipindi chamwaka mmoja, Kamati ilichambua Miswada na Mikatabaifuatayo;-

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

96

i) Muswada wa Sheria ya Reli Tanzania ya Mwaka 2017 (TheRailways Bill, 2017);

ii) Azimio la Bunge la kuridhia Itifaki ya Nyongeza ya Tano yaMwaka 1994, Itifaki ya Nyongeza ya Sita ya Mwaka 1999, Itifakiya Nyongeza ya Saba ya Mwaka 2004, Itifaki ya Nyongeza yaNane ya Mwaka 2008 na Itifaki ya Nyongeza ya Tisa ya Mwaka2016 ya Katiba ya Umoja wa Posta Duniani;

iii) Muswada wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzaniawa Mwaka 2017 (The Tanzania TelecommunicationsCorporation Bill, 2017);

iv) Muswada wa Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania waMwaka 2017 (The National Shipping Agencies CorporationBill, 2017)

SEHEMU YA PILI

2.0 UCHAMBUZI WA MATOKEO YA UTEKELEZAJI WAMAJUKUMU YA KAMATI

2.1 Bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Mheshimiwa Spika, katika utekelezaji wa majukumu yake,Kamati ilipata fursa ya kupitia na kuchambua utekelezaji waBajeti ya Wizara hii kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017; pamojana Mapendekezo na Makadirio kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

Mheshimiwa Spika, katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2017/2018, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano iliidhinishiwashilingi trilioni 4.5 (4,516,885,061,000). Mgawanyo wa fedhahizi katika kila Sekta ni 1,929,707,714,000 Sekta ya Ujenzi,2,569,073,208,000 Sekta ya Uchukuzi na 18,104,139,000 Sektaya Mawasiliano.

Kamati imebaini kuwa mwenendo wa Bajeti inayotengwakwa ajili ya Sekta hii ni mzuri na umekuwa ukiongezeka

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

97

mwaka hadi mwaka. Hivyo, Kamati inaipongeza Serikali kwakuipa Sekta ya Miundombinu kipaumbele.

2.2 Sekta ya Uchukuzi

2.2.1 Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania-TPA

Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Bandari Tanzania inamajukumu ya kuendeleza bandari, kuendesha shughuli zabandari, kutangaza huduma za bandari, kushirikisha nakusimamia Sekta binafsi katika uendelezaji za uendeshaji wabandari. Mamlaka hii inamiliki na kusimamia Bandari Kuu zaDar es Salaam, Tanga na Mtwara pamoja na bandari ndogoza Kilwa Masoko, Kilwa Kivinje, Kwale, Lindi, Mikindani, Mafia,Pangani na Bagamoyo. Vilevile, Mamlaka ya BandariTanzania inamiliki bandari kadhaa za maziwa makuu kamavile Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa.

Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Bandari licha ya kutoahuduma kwa mizigo inayoingia na kutoka ndani ya nchi; piainahudumia nchi za Burundi, Rwanda, DR Congo, Uganda,Zambia, Malawi na Zimbambwe.

Kamati imeelezwa kwamba, Mamlaka ya Usimamizi waBandari Tanzania-TPA inakabiliwa na changamotombalimbali zikiwemo:-

a) Uwezo mdogo wa kuhudumia meli kubwa na kina kifupikatika bandari ya Dar es Salaam pamoja na Tanga;

b) Uchakavu wa miundombinu ya bandari nchini; na

c) Uwepo wa bandari bubu na ushindani wa Bandari zinginekama vile Beira-Msumbiji, Mombasa-Kenya na Durban-AfrikaKusini.

Mheshimiwa Spika, pamoja na changamoto hizo, Kamatiinaipongeza Serikali kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzaniakwa kuanza kutekeleza baadhi ya ushauri wake kamaifuatavyo;-

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

98

i) Mgongano uliokuwepo kwa tozo za hifadhi za mizigo‘’Customs Warehouse Rent’’ inayotozwa na Mamlaka yaMapato Tanzania-TRA na ‘’Storage Charges’’ zinazotozwana Mamlaka ya Bandari Tanzania-TPA ambapo yalikuwayanatozwa kwa pamoja. Kamati imejulishwa kuwa tozo hizisasa zimewekewa utaratibu ambapo Mamlaka ya Bandariitakuwa inatoza kwa muda wa siku thelathini tu (30) mzigoukiwa bandarini. Shehena itakayokaa zaidi ya siku hizo nakupelekwa kwenye hifadhi (yard) za Mamlaka ya MapatoTanzania ndio zitatozwa ’’Storage Charges’’;

ii) Kuhusu Himaya ya Forodha kwa Pamoja (Single CustomsTerritory) kwa mzigo wa Congo, Kamati imejulishwa kuwaSerikali imeanza kutekeleza kwani imetoa ‘’notice’’ ya mudawa mwezi mmoja ili kuvunja Mkataba huo ambao umekuwaukileta utata na kupunguza motisha kwa wafanyabisharawa Congo kutumia Bandari ya Dar es Salaam; na

iii) Aidha, Serikali imefuta kodi ya ongezeko la thamani (ValueAdded Tax-VAT) kwa huduma zitolewazo na mawakalakwenye mizigo inayosafirishwa kwenda nchi jirani (VAT ontransit goods);

Mheshimiwa Spika, katika kuboresha na kuongeza ufanisi wabandari ya Dar es Salaam, Kamati imejulishwa kuwa hatuambalimbali za utekelezaji zimefikiwa kama ifuatavyo:-

i) Kuhusu ujenzi wa gati namba 1 hadi 7 na gati la kushushiameli za magari (RoRo berth); Mkandarasi yupo katika eneola kazi na kwa sasa kazi imefanyika kwa asilimia kumi natano (15%);ii) Kuhusu kuongeza kina na upana wa lango la kuingilia meli,kazi hii ipo katika hatua za kutangazwa zabuni ya awali kwaajili ya kumpata mkandarasi na Mtaalam mwelekezi; naiii) Ujenzi gati namba 12-14; utekelezaji wa ujenzi wa gati hiziutafanyika katika awamu ya pili ya maboresho na upanuziwa Bandari ya Dar es Salaam. Kwa sasa, Serikali bado ipokwenye majadiliano na wafadhili ili kufanya upembuzi yakinifuwa namna bora ya kuamisha Kurasini Oil Jet na miundombinuyake kwa ajili ya kupisha ujenzi wa magati hayo.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

99

Mheshimiwa Spika, wakati ukarabati na upanuzi wa bandariya Dar es Salaam unaendelea; ni vyema Serikali ikaanza piaukarabati wa bandari nyingine muhimu kama vile bandariya Tanga, bandari ya Mtwara, bandari ya Mwanza, bandariya Kigoma, bandari ya ziwa Nyasa.

2.2.2 Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL)

Mheshimiwa Spika, kuhusu Kampuni ya Huduma za Meli-MSCL;Kampuni hii inakabiliwa na changamoto ya uchakavu waMeli kutokana na kutokufanyiwa matengenezo makubwakwa wakati na hivyo kusababisha gharama kubwa. Mfano,MV Butiama ambayo haifanyi kazi tangu mwaka 2010, MVVictoria nayo haifanyi kazi toka mwaka 2014 na MV Liembaambayo inafanya kazi lakini kwa kusuasua.

Wakati Kamati ilipokuwa ikifuatilia utatuzi wa changamotohii ilijulishwa kuwa, Serikali imetenga shilingi bilioni 24.496(24,496,000,000) katika Mwaka wa Fedha 2017/2018 kwa ajiliya kununua meli mpya mbili (2) ambazo moja ni kwa ajili yakubeba abiria na mizigo Ziwa Tanzanyika na ya pili ni kwaajili ya kubeba abiria na mizigo katika Ziwa Victoria. Aidha,fedha hizo pia zitatumika katika ukarabati wa MV Victoria,MV Liemba, MV Butiama, MV Umoja na MV Serengeti.

Mheshimiwa Spika, Kamati imejulishwa kuwa fedha hizozimeshatolewa tangu Agosti, 2017 na utekelezaji wa miradihii uko katika hatua mbalimbali. Kamati inampongezaMkurugenzi mpya wa MSCL kwa hatua alizochukuwa zakufuatilia uendeshaji wa meli na sasa mapato yameanzakuongezeka.

2.2.3 Ujenzi wa Reli

Mheshimiwa Spika, Kamati inatoa pongezi kwa jitihadambalimbali zinazofanywa na Serikali ili kufufua na kuimarishamtandao wa reli nchini. Miongoni mwa juhudi hizo ni pamojana; kuendelea na ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango chakisasa (Standard Gauge). Hivyo, katika kuendeleza juhudi hizomnamo mwezi Septemba, 2017, Serikali ilileta Mswada wa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

100

Sheria ya Reli, 2017 ambao moja kati ya madhumuni yakeilikuwa ni kuanzisha Shirika jipya la Reli (Tanzania RailwayCorporation-TRC) ambalo pamoja na mambo menginelitakuwa na jukumu la kusimamia, kuendeleza miundombinuya Reli na kutoa huduma za usafiri wa Reli.

Katika mipango ya Sekta ya Uchukuzi ya Mwaka 2017/2018,miongoni mwa malengo yaliyowekwa kuhusu kuimarishamiundombinu ya reli nchini ni pamoja na kuendelea na ujenziwa Reli ya kisasa. Hivyo, Serikali kwa kutambua umuhimuwake imetenga shilingi bilioni 900(900,000,000,000.00).

Mheshimiwa Spika, Kamati imejulishwa kuwa ujenzi wa relihii umegawanyika katika sehemu kuu tano ambazo ni:-

i. Dar es Salaam –Morogoro (km 205) -ujenzi umeshaanza;

ii. Morogoro-Makutupora (km 336)- mradi unatarajiwakuzinduliwa mwezi Februari,2018;

iii. Makutupora-Tabora (km 295), Tabora-Isaka (km 133) naIsaka –Mwanza (km 250)- Serikali inatafuta fedha kwa ajili yaujenzi wa vipande hivi;

Mheshimiwa Spika, kuhusu ujenzi wa reli ya kisasa katikamaeneo mengine nchini kwa kiwango cha kisasa (StandardGauge), ujenzi wa reli ya kutoka Mtwara hadi Mbaba Bay namatawi yake kuelekea Liganga na Mchuchuma (km 1, 092)upembuzi yakinifu umekamilika.

Vilevile, Reli ya kutoka Tanga- Arusha-Musoma (km 1,108), kwakipande cha Tanga- Arusha (km 438) shughuli ya upembuziyakinifu na usanifu wa awali zimekamilika.

Mheshimiwa Spika, pamoja na maendeleo mazuri katikamradi wa ujenzi wa reli hii ya kisasa, mradi huu unakabiliwana changamoto zifuatazo:-i. Kuchelewa kupatikana kwa fedha kwa ajili ya ufuatiliaji nausimamizi kwa upande wa RAHCO kama watekelezaji waMradi;

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

101

ii. Matumizi kutokea mfuko wa uendelezaji Reli;iii. Usajili wa raia wa kigeni katika bodi za taaluma nchini; naiv. Upatikanaji wa maeneo ya ujenzi (ardhi) nje ya maeneoyanayomilikiwa na RAHCO.

2.2.4 Kampuni ya Ndege ya Tanzania-ATCL

Mheshimiwa Spika, Kamati imejulishwa kuwa pamoja nandege mbili mpya aina ya Dash 8 Q400. Kwa sasa, Kampuniinamiliki ndege tatu (3) ambazo zinafanya ziara zake ndaniya nchi. Kamati imejulishwa kuwa mwezi Julai, 2017; Serikaliinategemea kupokea ndege zingine mbili ambapo moja niDash 8 Q400 na nyingine ni ndege kubwa aina ya Boeing 787yenye uwezo wa kubeba abiria 262.

2.3 Sekta ya Ujenzi

2.3.1 Wakala wa Barabara Tanzania- TANROADS

Mheshimiwa Spika, Wakala wa barabara ulianzishwa kwataarifa ya Serikali iliyotolewa kwenye Gazeti la Serikali Na.293 mwaka 2000 chini ya kifungu 3(1) cha Sheria ya Wakalawa Serikali Na. 30 ya Mwaka 1997. Jukumu kubwa la wakalahuu ni kuhudumia mtandao wa barabara, ambaounakadiriwa kuwa na urefu wa jumla ya kilometa 35,000;ambapo kati ya hizo, kilomita 12,786 ni barabara kuu, nakilometa 22,214 ni barabara za Mikoa. Lengo ni kuwezeshabarabara ziweze kupitika kwa urahisi na hatimaye, kusaidiaukuaji wa uchumi wa nchi, kama ilivyofafanuliwa katikaMpango na Mikakati ya Kitaifa na Kimataifa, ikiwemo Diraya Taifa ya Maendeleo 2015, Mpango wa Taifa wa MiakaMitano na Mikakati ya Kisekta.

Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikio hayo Wakala waBarabara unakabiliwa na changamoto mbalimbalizikiwemo:-

a. Kutokutolewa kwa wakati fedha za miradi ya maendeleohali inayosababisha kazi zilizopangwa kwa baadhi ya miradikutotekelezwa ama kutekelezwa kwa kiasi kidogo;

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

102

b. Msongamano wa magari barabarani hasa jiji la Dar esSalaam, na miji mingine inayokuwa kwa kasi, kama Mbeya,Mwanza na Arusha;

c. Baadhi ya wasafirishaji kuendelea kuzidisha uzito wa mizigokwenye magari na kusababisha uharibifu wa barabara;

d. Uwezo mdogo wa Makandarasi wa ndani katikautekelezaji wa miradi mikubwa ya ujenzi wa barabarakutokana na kukosa mitaji ya kutosha pamoja na mitamboya kisasa; na

e. Ongezeko la gharama za ujenzi, ambazo ni kikwazo kwaujenzi wa nyumba za kutosha za gharama nafuu kwa ajili yamakazi ya watumishi wa umma.

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na migogoro na mvutanokutoka kwa wananchi mbalimbali unaotokana na wasiwasiwa kutolipwa fidia au kulipwa fidia kwa kiasi kidogoambacho hakiendani na hali ya uchumi wa sasa; jambo hililinasababisha wananchi kugoma kuondoka katika maeneoya miradi; na kusababisha kuchelewa kuanza kwa miradi.

Aidha, changamoto kubwa katika ujenzi wa barabara kwasasa imekuwa uvamizi wa barabara, uliofanyika miakailiyopita ambapo wananchi walikuwa wakijenga katikamaeneo ya hifadhi za barabara bila kujali Sheria ya barabaraNamba 13 ya Mwaka 2007.

Ni rai ya Kamati kwamba, vyombo vya usimamizi wa Sheriaya barabara kuwa macho wakati wote na endapokutaonekana mtu anajenga ndani ya hifadhi ya barabaraazuiwe na abomolewe mapema kuliko kumwacha nakusababisha misuguano baadaye.

Mheshimiwa Spika, kuhusu matuta barabarani, licha yaWakala wa Barabara (TANROADS) kuahidi kuendeleakurekebisha matuta makubwa, ili kuyaweka katika viwangovilivyoainishwa katika mwongozo wa Wizara kuhusu usanifuwa barabara wa mwaka 2011, bado kumeendelea kuwapo

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

103

matuta makubwa hasa katika barabara kuu ambapoyamekuwa chanzo cha uharibifu wa barabara, kwani magariyenye mizigo hulazimika kwenda mwendo mdogo; hivyouzito kuwa mkubwa na kusababisha barabara kutitia. Aidha,matuta barabarani yamekuwa yakisababisha mizigokuhama na kuelemea upande mmoja; jambo ambalowakati mwingine limekuwa chanzo cha ajali kwa magarimengi ya mizigo. Pia, matuta husababisha myumbo wamatairi hivyo kuchochea ubovu na kuongeza uwezekanowa magari.

2.3.2 Barabara za Jiji la Dar es Salaam

Mheshimiwa Spika, Kamati inaipongeza Serikali kwa juhudimbalimbali zinazofanywa katika kuhakikisha jiji la Dar esSalaam linakuwa halina msongamano mkubwa wa magari.Juhudi zilizofanyika ni pamoja na ujenzi wa miundombinu yamabasi yaendayo kasi (BRT), kujenga barabara za juu (flyovers)katika eneo la TAZARA na maaandalizi ya ujenzi wa barabaraza juu (Interchange) katika eneo la Ubungo pamoja nakukamilisha barabara nyingine za kupunguza msongamanokatika jiji la Dar es Salaam. Sehemu barabara hizo ni pamojana Ardhi-Makongo- Goba, na Goba- Madale –Wazo Hill.

Mheshimiwa Spika, ni ukweli usiopingika kuwa Jiji la Dar esSalaam limekuwa likikabiliwa na msongamano mkubwa wamagari unaotokana na sababu mbalimbali zikiwemo ofisinyingi za umma kujengwa sehemu moja na kusababishawakazi wa jiji kuwa na uelekeo mmoja, ubovu wa barabaraza mlisho (feeder roads), utegemezi usafiri wa barabara kwakiasi kikubwa, uduni wa huduma za usafiri wa umma naongezeko kubwa la idadi ya magari ikilinganishwa na uwezowa barabara.

Aidha, msongamano huu unaendelea kujitokeza katika majijimengine kama vile Mwanza, Mbeya na Arusha, na sasaManispaa Dodoma na sababu zikiwa ni ongezeko kubwa laidadi ya magari ikilinganishwa na uwezo wa barabara. Ni

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

104

lazima sasa kuweka mipango kabambe ya kuongezabarabara za michepuko katika majiji haya ili kuepusha nakupunguza msongamano kwani unaathari nyingi zakiuchumi, kijamii na kimazingira.

2.3.3 Mizani za Barabarani

Mheshimiwa Spika, moja kati ya majukumu ya TANROADS niujenzi na utunzaji wa barabara, kudhibiti uzito wa magari ilikuhakikisha barabara zinadumu kwa muda mrefu. Hatahivyo, pamoja na jukumu hilo bado changamoto imekuwani uharibifu wa barabara unaosababishwa na magarikubeba mizigo yenye uzito mkubwa. Kwa Mfano, magarimengi ya aina ya fuso kwa wastani yanatakiwa kubeba mzigousiozidi tani 3.5, lakini mengi yanazidisha na kubeba mizigohadi tani 8. Hali hii ni hatari sana kwani mara nyingiyamekuwa yakisababisha ajali pamoja na uharibifu wabarabara kwani matairi yake ni membamba ambapohuchimba barabara na kusababisha mabonde.

Mheshimiwa Spika, ili kukabiliana na changamoto ya magariyanayobeba mizigo kupita kiasi kinachostaili, mizani ndichochombo muhimu sana katika udhibiti uzito wa magariambayo husababisha uharibifu wa barabara. Kamatiinaipongeza Serikali kwa kuendelea kuongeza za udhibiti wauzito wa magari na sasa kuna mizani 38 ya kudumu, mizani22 zinazohamishika na mizani moja (1) inayopima uzito wamagari yakiwa kwenye mwendo.

2.3.4 Ujenzi wa Viwanja vya Ndege Nchini

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa viwanja vya ndege nchiniumeendelea kutekelezwa chini ya Sekta ya Ujenzi na Wakalawa Barabara Tanzania (TANROADS). Kamati katika kutekelezamajukumu yake imebaini kuwa ujenzi wa viwanja vya ndegenchini umeendelea kwa kasi kubwa.Aidha, Kamati imejulishwa kuwa, ushauri wa Kamatikuhakikisha kuwa viwanja vyote vinakuwa na Hati Miliki

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

105

umeanza kutekelezwa. Hata hivyo, kati ya viwanja hamsinina nane (58) vinavyomilikiwa na Mamlaka ya Viwanja vyaNdege- TAA, viwanja vilivyofanikiwa kupata Hati Miliki nivinane (8) tu. Kamati imejulishwa kuwa viwanja vingine kumi(10) viko kwenye mpango wa kupata Hati Miliki mwaka huu.

Mheshimiwa Spika, Kulikuwepo na changamoto yakupatikana fedha kwa wakati kwa ajili ya ujenzi wa viwanjandege nchini. Hata hivyo, Kamati imejulishwa kuwaupatikanaji wa fedha kwa ajili ya ujenzi wa viwanja vyandege kwa sasa ni mzuri.

2.3.5 Ujenzi wa Viwanja vya Ndege

a) Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha JuliusNyerere Dar es Salaam

Mheshimiwa Spika, kuhusu ujenzi wa jengo la tatu la abiria(terminal III) katika Kiwanja cha Kimataifa cha Julius Nyerere,mkataba ulisainiwa 18 Aprili, 2013.

Hadi kufikia Desemba, 2017; utekelezaji wa kazi ulifikiaasilimia 68 ambapo kazi zinazoendelea ni kuezeka nakumalizia kazi za kusimika mitambo ya umeme, viyoyozi nautandazaji wa nyaya na mabomba.

Mheshimiwa Spika, mradi huu unakabiliwa na changamotozifuatazo;-i. Upatikanaji wa fedha; Kamati imejulishwa kuwa Wizara yaFedha na Mipango inaendelea kufwatilia taratibu zaupatikanaji wa fedha za ndani; pamoja na kuangalia fedhaza mkopo wa masharti nafuu;

ii. Changamoto nyingine ni Kodi ya Ongezeko la Thamani(VAT) na ushuru wa bidhaa. Kwa mujibu wa Mkataba vifaavya ujenzi kwa ajili ya mradi huu vilisamehewa Kodi yaOngezeko la Thamani (VAT). Hata hivyo, Sheria Mpya ya Kodiya Ongezeko la thamani (VAT) ya Mwaka 2014 iliyoanzakutumika mwaka 2015 ilifuta msamaha wa Kodi ya VAT katikamradi huu.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

106

b) Kiwanja cha Ndege cha Mwanza

Mheshimiwa Spika, Kiwanja cha Ndege cha Mwanza ndichoKiwanja kikubwa cha Ndege kwa eneo la Kanda ya Ziwa.Kutokana na umuhimu wake; Serikali imekuwa ikikiendelezaKiwanja hiki kwa kukipanua ili kiweze kukidhi mahitaji mengiya sasa ya wakazi wa Kanda ya Ziwa na hatimae ndegekubwa za Kimataifa kutua. Mradi wa Ujenzi wa Kiwanja hikiulianza mnamo mwezi Oktoba 2012 na ulipangwa kukamilikaMwezi Septemba, 2014. Hata hivyo, hapo awali mradi huuulikuwa ukikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa fedhakwa wakati hivyo kusababisha kasi ya utekelezaji wa mradikuwa ndogo.

c) Kiwanja cha Ndege cha Songwe

Mheshimiwa Spika,Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege chaSongwe Mkoani Mbeya ulianza mwaka 2000 ambapo ujenziumekuwa ukitekelezwa kwa awamu kulingana naupatikanaji wa fedha. Kiwanja hiki ni muhimu sana kwawakazi wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na hata wasafirikutoka nchi jirani za Zambia na Malawi. Tangu Kiwanja hikikil ipofunguliwa rasmi mwaka 2012 kumekuwepo naongezeko kubwa la abiria na ndege.

Hata hivyo, pamoja na umuhimu mkubwa wa Kiwanja hiki,mradi huu pia umekuwa ukitekelezwa kwa kasi ndogo jambolinalosababisha mradi kutokukamilika kwa wakati.

Aidha, pamoja na changamoto hizo katika ujenzi waKiwanja hiki, Kamati toka mwaka 2016 imekuwa ikishaurimara kwa mara umuhimu wa kuwekwa kwa taa zakuongozea ndege ambazo zitasaidia ndege kutua nyakatiza usiku na hata mchana wakati wa ukungu mkubwa. Halikadhalika, kuwekwa kwa uzio kuzunguka mipaka yote yaKiwanja ili kuongeza usalama wa kiwanja na kuepukauvamizi na wananchi wa maeneo jirani kukatiza katikamaeneo ya Kiwanja.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

107

d) Kiwanja cha Ndege cha Kigoma

Mheshimiwa Spika, Kiwanja cha Ndege cha Kigomakilianzishwa mwaka 1954. Serikali imekuwa ikifanya jitihadambalimbali ili kuhakikisha kuwa miundombinu ya Kiwanjahiki inaboreshwa na kuweza kutoa huduma zakuridhisha.Ukarabati wa Kiwanja hiki unafanyika kwa awamukulingana na upatikanaji wa fedha. Katika mwaka wa fedha2017/2018 utekelezaji ulikuwa wa awamu ya pili ambapolinahusisha ujenzi wa jengo la abiria, mnara wa kuongezeandege, ukarabati wa maegesho ya ndege na usimikaji wataa za kuongozea ndege.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kuwa mradi huu upo mingonimwa miradi inayogharamiwa kwa Mkopo kutoka Benki yaUwekezaji ya Ulaya, Kamati imejulishwa kuwa; ilikubaliwakuwa kabla ya fedha za mkopo kuanza kutoka, Serikali iweimeshalipa fidia kwa wananchi wote watakaothiriwa naukarabati na upanuzi wa Kiwanja hiki. Baadhi ya wananchiwamekuwa na madai ya kupunjwa fedha za fidia na baadhiya maeneo yao kurukwa katika zoezi la ulipaji fidia lililofanyikamwaka 2013. Hata hivyo, tathimini imefanyika upya nakuanisha mahitaji ya ziada ili kulipa madai hayo.

2.4 Sekta ya Mawasiliano

2.4.1 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

Mheshimiwa spika, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania- TCRAilianzishwa chini ya Sheria Na. 12 ya Mwaka 2003 ya Udhibitiwa Mawasiliano Tanzania baada ya kuunganishwa kwailiyokuwa Tume ya Utangazaji Tanzania na Tume yaMawasiliano Tanzania-TCC. Madhumuni ya kuanzishwa kwaMamlaka hii ni kusimamia Makampuni ya Mawasiliano nchiniyakiwemo Makampuni yanayotoa huduma za Simu,Utangazaji, Intaneti, Posta na Usafirishaji wa Vifurushi.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TCRA imeweka mfumo wakusimamia mawasiliano ya simu, ambao umechangiakuongeza ufanisi katika utekelezaji wa Sheria na Kanuni

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

108

zilizopo katika udhibiti wa mawasiliano, ikiwa ni pamoja nakuhamasisha mabadiliko ya teknolojia ili kuongeza ubora wahuduma na kuendana na kasi ya mabadiliko yanayotokea.

Mfumo wa TTMS; pamoja na mambo mengine, mpaka kufikiaDesemba 2017 umewezesha kufanya yafuatayo:-

a) Kuhakiki Mawasiliano ya Simu za NdaniKatika kipindi cha Julai hadi Desemba, 2017; TCRA iliendeleakusimamia uendeshaji wa mfumo wa mawasiliano ya simuza ndani za kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine (localoff-net traffic) na kuwezesha kupatikana kwa takwimu za idadiya dakika zilizotumika pamoja na idadi ya simu zilizopigwa.

Aidha, katika kipindi hiki TCRA iliendelea kusimamiauendeshaji wa mfumo wa mawasiliano ya simu za ndani(local on-net traffic) na kuiwezesha TCRA kujua idadi yamawasiliano ya simu za ndani zilizopigwa pamoja na idadiya dakika zilizotumiwa na wateja katika maongezi ya simuyaliyofanyika ndani ya mtandao mmoja.

b) Mfumo wa Kubaini Simu za UlaghaiTCRA iliendelea na zoezi la kuzitambua na kuzifungia nambaza simu ambazo zimekua zikiingiza mawasiliano ya simu zakimataifa kwa njia za ulaghai, na kusababishia Serikalipamoja na watoa huduma upotevu wa mapato. Katikakipindi cha Julai hadi Desemba, 2017 TCRA ilifanya zoezi lakuwatafuta wahalifu na ilifanikiwa kuwakamata wahalifuwatatu wenye asili ya Somalia na kuwafikisha kwenyevyombo vya Sheria kwa kosa la kuingiza mawasiliano ya simuza kimataifa kwa njia za udanganyifu.

c) Mfumo wa kuhakiki Mapato yatokanayo na Hudumaza MawasilianoHadi Decemba 2017, TCRA iliendelea na uboreshaji wa Mfumowa TTMS kwa kufunga mfumo wa kuhakiki mapatoyatokanayo na huduma zote za mawasiliano (sauti, datana jumbe fupi, miamala ya kifedha, pamoja na mapatoyatokanayo na huduma za ziada zinazotolewa na watoahuduma hapa nchini. Kazi zifuatazo zilikuwa zimeshafanyika:

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

109

a) Kusimikwa kwa vifaa kwa upande wa watoa huduma(Vodacom, Tigo, Airtel, Viettel, Zantel, Smile, Smart, TTCL naSimbanet ambavyo vinavyokusanya taarifa ya huduma zamawasiliano yanayofanyika;

b) Kufungwa kwa vifaa vya kuchakata taarifa kutoka kwawatoa huduma katika kituo cha kusimamia Mfumo wa TRAshapa TCRA;

c) Kufungwa kwa Mfumo wa kuchakata taarifa (dataprocessing) na kuonesha taarifa mbalimbali za matumizi(dashboard) na mapato ya Makampuni ya watoa hudumahapa TCRA; na

d) Kusimikwa kwa mfumo wa kuonesha taarifa mbalimbaliza mapato yatokanayo na huduma za Mawasiliano.

d) Uhalifu katika MitandaoMheshimiwa Spika, mabadiliko ya mara kwa mara yateknolojia yamechangia kukuwa kwa Sekta ya Mawasilianokwa kasi kubwa. Mabadiliko haya yamekuja na changamotombalimbali za usalama na uhalifu katika mitandao.Changamoto hizi ni pamoja na ulaghai, utapeli, wizi n.k.Kamati ilijulishwa kuwa, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzaniainaendelea kudhibiti vitendo hivi kwa kujenga uwezo kwawatumishi wake; pamoja na kushirikiana kwa karibu navyombo vya ulinzi na usalama.

Aidha, katika kipindi cha 2017, TCRA iliratibu na kuwezeshamafunzo ya uchunguzi wa vifaa vya kieletroniki namawasiliano (Digital forensic Training) kwa kuvishirikishavyombo vingine vya ulinzi na usalama kwa lengo lakukabiliana na ongezeko la uhalifu katika mitandao.

e) Uanzishwaji wa Maabara ya Kisasa ya Kiuchuguziya Kidijitali

Mheshimiwa Spika, Kamati ilijulishwa kuwa katika kipindi chaJulai-Desemba, 2017; Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,imeanzisha maabara ya kisasa ya kidijitali ya uchunguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

110

(digital forensic Lab) pamoja na usimikaji wa vifaa na mifumombalimbali ili kusaidia kukabiliana na wimbi la makosa yakimtandao na kurahisisha utendaji wa kazi.

f) Kuweka viwango vipya vya mwingiliano baina yaMitandao ya Simu NchiniMamlaka ya Mawasiliano Tanzania imekamilisha kazi yakuchunguza na kubaini gharama halisi za muingiliano yamitandao ya simu (cost –based interconnection Rates) bainaya mitandao ya simu nchini. Uchunguzi huo ulifanywa kwakusaidiwa na mtaalamu mwelekezi (M/s Incyte Consulting)ambapo alipendekeza viwango vya muingiliano kwa kipindicha miaka mitano ijayo (mwaka 2018-2022) kamainavyooneshwa katika jedwali. Viwango hivyo vitatumikakwa muda wa miaka mitano kuanzia 1 Januari 2018 hadi 31Desemba 2022.

Jedwali lifuatalo linaonesha; Viwango vya muingiliano yamitandao ya simu kwa Shilingi kwa Dakika

Chanzo; Taarifa ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, 2018

2.4.2 Mradi wa Postikodi na Simbo za Posta

Mheshimiwa spika, mradi wa anuani za makazi ni muhimusana kwani utarahisisha shughuli zote za kijamii, kiuchumi nakisiasa kuweza kufanyika kwa urahisi na kuokoa muda.Miongoni mwa huduma zitakazorahisishwa na kuwapo kwamfumo huu ni pamoja na; huduma za umeme, gesi, maji,mabenki, ulinzi na usalama, huduma za dharura kama zimamoto ,magari ya wagonjwa, pamoja na wasambazaji wavifurushi.

Maelezo / Mwaka 2018 2019 2020 2021 2022 Gharama za mwingiliano wa simu za maneno kwa dakika kwa Shilingi ya Tanzania.

15.6 10.4 5.2 2.6 2.0

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

111

Mheshimiwa Spika, changamoto kubwa inayoukabili mradihuu ni ujenzi holela na kutokuwa na maridhiano juuupatikanaji wa majina ya mitaa.

Vilevile, changamoto nyingine kutokuwa na fedha zakutosha, kutokuwapo kwa takwimu halisi za idadi yabarabara/mitaa katika kata, uharibifu wa miundombinukama vile nguzo za majina ya mitaa na vibao vya nambaza nyumba hata sehemu zilizopangwa.

Mheshimiwa spika, Kamati hairidhishwi na kasi ya utekelezajiwa mradi huu ukilinganisha na umuhimu wake kwa Taifa.Vile vile fedha zinazotengwa kwa ajili ya kutekeleza mradihuu zimekuwa hazitolewi kwa wakati. Katika mwaka wafedha 2017/2018 Serikali imetenga shilingi bilioni 3(3,000,000,000.00), kwa ajili ya uendelezaji wa mradi katikamji wa Dar es Salaam, Zanzibar, Mwanza na Mbeya. Hatahivyo, hadi kufika mwezi Decemba, 2017 Fedha hizo zilikuwabado hazijatolewa.

2.4.3 Shirika la Posta TanzaniaMheshimiwa spika, shirika hili linahitaji mtaji ili liwezekujiendesha kibiashara na kukabiliana na ushindani uliopona changamoto ya soko katika sekta ya posta. Kamatiimejulishwa kuwa Serikali imeendelea kufanyia kazichangamoto ya Shirika hili ili liweze kujiendesha ikiwa nipamoja na kulipa madeni mbalimbali. Aidha, shirikalimeshatoa kiasi cha shilingi billion 6.7 mpaka mweziDisemba, 2017 kwa ajili ya kulipa pension za wastaafu waShirika la Posta na Simu la Afrika Mashariki kwa niaba yaSerikali kwa makubaliano ya kurejeshewa fedha hizo naSerikali.

Mheshimiwa Spika, kutokana na ushauri wa Kamatiuliotolewa 2016/2017, Serikali imefanikisha yafuatayo:-

i) Ofisi ya Msajili wa Hazina inaendelea kulipa deni la shilingibillion 6.7 la wastaafu ambao ajira zao zilianzia kwalililokuwa Shirika la Posta na Simu la Afrika Mashariki. Hadikufikia Novemba 2017, Serikali imeshalipa shilingi billion 2.7;

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

112

ii) Wizara ya Fedha na Mipango inaangalia uwezekano wakuweza kuliondoa Shirika hili kwenye Mashirika ya Ummayanayosubiri kurekebishwa ili liweza kuwa na sifa ya kupatamikopo kutoka taasisi mbalimbali za fedha;

iii) Shirika kuweza kutoa huduma ijulikanayo kama postamlangoni kufikisha barua, nyaraka na vipeto hadi mtejaalipo. Huduma hii imeanza kutolewa katika maeneo ambayomiundomninu ya postikodi imekamilika; maeneo hayo nikama Arusha (kata 8), Dodoma( kata 8) na Dar es salaam(kata 32).

2.4.4 Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)

Mheshimiwa spika, Mfuko wa Mawasiliano kwa Woteulianzishwa kwa lengo la kupeleka huduma ya mawasilianomaeneo yasiyokuwa na mvuto wa kibiashara. Hata hivyo,kwa kuzingatia ukubwa wa nchi yetu na muda ambao mfukohuu umekuwepo toka kuanzishwa kwake, Kamati badohairidhishwi na kasi ya utekelezaji wa mradi wa usambazajiwa mawasiliano sehemu zisizokuwa na mvuto wa kibiasharahasa vijijini. Kamati imebaini kuwa, moja ya sababu ya kuwana kasi ndogo ya utekelezaji wa mradi huu ni kwa kuwaMakampuni makubwa ya simu bado hayajahimizwa vyakutosha kupanua huduma zao katika maeneo yasiyokuwana mvuto wa kibiashara kama mojawapo ya uwajibikajiwao kwa jamii (corporate social responsibility).

Mheshimiwa Spika, mwezi Oktoba, 2017; kamati ilipatanafasi ya kutembelea maeneo mbalimbali ili kujionea ikiwahuduma za mawasiliano zinapatikana kwa sehemu ambazominara ilijengwa na makampuni ya simu kwa kutumia ruzukukutoka Mfuko wa Mawasiliano. Katika ziara hiyo, ambayoKamati ilitembelea takribani Mikoa 20 ya Tanzania Bara,Kamati ilibaini changamoto zifuatazo;-

a) Serikali za Mikoa, Wilaya pamoja na wananchihawatambui uwepo wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote;na kwamba, miradi hiyo ya ujenzi wa minara ni kwa ruzukuya Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote. Dhana

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

113

iliyoko maeneo mengi ni kuwa minara inajengwa naMakampuni ya ya simu yenyewe; hivyo mchango wa Serikalikatika kusambaza mawasiliano hautambuliki kabisa;

b) Pamoja na kuwa Makampuni yamepewa masharti yakuwajibika katika kutoa huduma za jamii; katika maeneoyanayofanya shughuli zake za kibiashara, kwa kiasi kikubwaMakampuni haya yamekuwa hayatoi huduma hizi;

c) Ujenzi wa minara kwa kutumia Kampuni ya TTCL ulikuwaukisuasua kwa siku za nyuma, hata hivyo baada ya Kamatikufanya ziara ya ukaguzi wa minara mwaka jana; TTCLimekamilisha miradi yake yote iliyokuwa inadaiwa na UCSAF;

d) Migogoro ya ardhi; Katika maeneo mengi ambayo Kamatiimetembelea minara yamebainika wazi kuwa na migogorodhidi ya umiliki wa eneo husika.

e) Wizi wa vifaa vya minara kama vile mafuta, betri na nyayaaina ya ‘’fiber’’;

f) Minara mingi iliyojengwa inatumia umeme wa jua (solarpower), hii inasababisha nyakati za usiku hasa wakati kipindicha mvua maeneo mengi kuwa na mawasiliano hafifu kwasababu jua haliwaki kipidi kirefu;

g) Makampuni yanajenga minara pasipo kuweka hudumaza kijamii kama choo, kibanda cha mlinzi na huduma zingineza msingi kwenye maeneo la mnara.

2.4.5 Tume ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano-TEHAMA

Mheshimiwa Spika Tume ya Teknolojia ya Habari naMawasiliano ilianzishwa kwa amri ya Rais kupitia tangazo laSerikali na 532 la mwezi Novemba 2015. Majukumu yakekukuza TEHAMA, kukuza uwekezaji katika maeneo yakimkakati ya uzalishaji wa bidhaa za TEHAMA nchini, kufanyautafiti na kushauri masuala ya TEHAMA.Majukumu mengineni uendelezaji wa miundombinu nchini; pamoja na kukuzana kuvutia uwekezaji kwenye sekta ya TEHAMA, il i

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

114

kutengeneza ajira na kuweza kuchangia katika shughuli zakijamii na kiuchumi.

Kamati imejulishwa kwamba katika Afrika Mashariki; Tanzaniandiyo nchi iliyochelewa kuwa na taasisi ya TEHAMA. Nchi zaAfrika Mashariki zimekuwa na taasisi za TEHAMA tangu mwaka2006-2008. Kamati imejulishwa kuwa nchi kama Kenyaimeshafikia mahali wanaendesha kilimo kwa TEHAMA. Kamatiimebaini kuwa, ikiwa Serikali itaweka mkazo kwenye sektahii tunaweza kupiga hatua haraka katika kuwaleteamaendela wananchi wa Tanzania.

SEHEMU YA TATU

2.0 MAPENDEKEZO NA USHAURI WA KAMATI

2.1 Bajeti ya Miundombinu

Mheshimiwa Spika, Kamati inaipongeza Serikali kwa kuonaumuhimu wa kuendeleza miundombinu nchini ambapokatika Bajeti ya Mwaka 2017/2018; Serikali iliendelea kuongezatengeo la fedha katika sekta ya Miundombinu hadi kufikiajumla ya shilingi shilingi trilioni 4.5 (4,516,885,061,000). Hiiinaonesha kwa kiasi kikubwa Serikali imezingatia umuhimuwa kuharakisha maendeleo katika nchi yetu kwanimiundombinu ndiyo itawezesha tija na utendaji bora wa sektazingine. Hata hivyo, pamoja na shabaha nzuri ya Serikalikatika masuala ya miundombinu, Kamati inasisitiza fedhakutolewa kwa wakati ili kuharakisha utekelezaji wa miradiya maendeleo na kuepuka limbikizo la madeni.

2.2 Sekta ya Uchukuzi

2.2.1 Mamlaka ya Bandari Tanzania

Mheshimiwa Spika, kwa Kuwa, Mamlaka ya Bandari Tanzaniandiyo Mamlaka iliyokasimiwa jukumu la kusimamia bandarinchini;

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

115

Na kwa Kuwa, Mamlaka hii inayo miradi mingi ya ujenzi naukarabati wa bandari ambapo kwa sasa Mamlaka yaBandari ipo katika hatua ya kuboresha kwa kufanyaukarabati bandari kama vile Mtwara na ujenzi wa magatipamoja na uchimbaji wa kina katika Bandari ya Dar esSalaam;

Kwa hiyo Basi, Kamati inaishauri Serikali yafuatayo;-

a) Asilimia ishirini (20%) ya mapato ya bandari yabakibandarini ili kuwezesha Mamlaka ya Bandari Tanzania iwezekutekeleza baadhi ya miradi kama vile miradi ya ujenzi wabandari ya Kalema, Kigoma na Mtwara ambayo inagharimutakribani shilingi bilioni 20 wakati mapato ya bandari kwamwaka ni shilingi bilioni 270;

b) Wafanyakazi wapewe nafasi ya kwenda kujifunza katikaBandari zingine zinazofanya vizuri ili kuweza kufahamuwenzao wanachokifanya na hatimae kuweza kubaini mbinuza ushindani na bandari zingine katika biashara;

c) Kuendelea kushughulikia changamoto zingine zinazoikabiliMamlaka ya Bandari, ili Bandari iweze kufanya vizuri zaidi nakuweza kushindana na nchi zingine shindani;

d) Kuharakisha mchakato wa ununuzi wa flow meter mpyakwa ajili ya upimaji wa mafuta yanayoingia Bandari ya Dares Salaam. Kamati ilitembelea bandari na kuona tatizo lakutokuwepo na flow meter, na hivyo kutokujua kwa uhakikakiwango cha mafuta kinachoingia bandari ya Dar es Salaam.Ni rai ya Kamati kuwa ‘’flow meter’’ inunuliwe kwa haraka.Hivi tunavyoongea sasa tatizo hili bado halijashughulikiwa;na

e) Kuunganisha zabuni za ujenzi wa bandari ya Kigoma ilikuweza kupata mzabuni mwenye uwezo atakayefanya kazihiyo; kwani imekuwa ikitangazwa mara kadhaa bila kupatamzabuni kutokana na gharama ya maandalizi (mobilization)ya miundombinu.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

116

2.2.2 Ujenzi wa reli nchini

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, Serikali imeonesha nia ya dhatiya kujenga upya Reli ya Kati katika kiwango cha kisasa(standard gauge); ambapo mradi huu umeshaanza tangumwezi April, 2017 na unatekelezwa kwa awamu tano;

Na kwa Kuwa, katika uhalisia Tawi la kutoka Tabora- Kigoma-Uvinza- Msongati na Kaliua-Mpanda-Kalema ndilo lenyemizigo mingi inayotoka na kwenda nchi za jirani kama vileDR Congo, Burundi na Rwanda;

Kwa hiyo Basi, Kamati inaishauri Serikali yafuatayo:-

a) Reli hii ijengwe kwa kuzingatia faida za kiuchumi nakipaumbele zaidi kiwekwe katika tawi la Tabora – kigoma -Uvinza- Msongati; Kaliua – Mpanda –Kalema; na Tabora-Mwanza;

b) Kuwapeleka kwenye mafunzo zaidi wataalam ili kuwezakuhudumia miundombinu ya treni za kisasa inayoendeleakujengwai;

2.2.3 Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania-TAA

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, kumekuwa na migogoromingi ya uvamizi wa maeneo ya viwanja vya ndege;

Na kwa kuwa, utatuzi wa migogoro hiyo umekuwaukiigharimu Serikali fedha nyingi kulipa fidia na kucheleweshabaadhi ya miradi ya ujenzi wa viwanja vya ndege;

Kwa Hiyo Basi; Kamati inaishauri Serikali,

a) Kuhakikisha inapata hati za Viwanja vya Ndege kwaniKamati imejulishwa ni kuwa viwanja vya ndege vinane (8)vimeshapatiwa hati miliki kati ya viwanja hamsini na nane(58) vinavyomilikiwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege,bado kuna haja ya kuhakikisha kuwa viwanja vinginevilivyobakia vinapimwa na kupatiwa hati miliki pamoja na

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

117

kuwekwa uzio ili ili kujiepusha na uvamizi wa maeneo jamboambalo huleta migogoro na wananchi na kusababishaSerikali kuingia gharama kubwa kwa ajili ya fidia;

b) Aidha, kuongeza udhibiti na ulinzi katika Viwanja vyaNdege vilivyopo Mikoani hasa vilivyopo mpakani kama vileMtwara, Kigoma na Kagera il i kuepuka viwanja hivikupitishwa biashara haramu;

c) Ili kuepuka ongezeko la gharama za ujenzi; ni vyema Serikaliikakamilisha miradi ya ujenzi wa viwanja vya ndegevilivyoanza vikiwemo; Kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere(Terminal III), Kiwanja cha Ndege cha Mwanza na Kiwanjacha Ndege cha Songwe; na

d) Kuharakisha ulipaji wa fidia kwa wananchi waliopishaujenzi wa viwanja vya ndege kama kama vile Kiwanja chaNdege cha Julius Nyerere (Terminal III) Kiwanja cha Ndegecha Mwanza na Kiwanja cha Ndege cha Songwe.

2.2.4 Kampuni ya Ndege ya Tanzania-ATCL

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, Serikali imeonesha nia ya dhatiya kufufua Kampuni ya Ndege ya Tanzania;

Na kwa kuwa, biashara ya ndege inahitaji mikakati mikubwaya kibiashara ili kuweza kuingia katika soko la ushindani;

Kwa hiyo Basi, Kamati inaishauri Serikali yafuatayo:

a) Kuwa na mikakati ya kitaifa ya kuhakikisha kuwa ATCLinakuwa na uwezo wa kushindana na kutengeneza faida;

b) TCL iangaliwe kama Kampuni ya kibiashara na sio kutoahuduma; na

c) ATCL ijitangaze kwenye vyombo rasmi vya Kimataifaambavyo huonyesha safari za ndege dunia nzima. Aidha,Kampuni hii sasa ijipange kuingia katika soko kwa kujitangazakatika vyombo vya habari, majarida na vipeperushi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

118

mbalimbali, kujali wateja na kuwa na bei nafuu ili kuhakikishaabiria wengi wanatumia ndege hizi.

2.3 Sekta ya Ujenzi

2.3.1 Wakala wa Barabara Tanzania-TANROAD

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, Wakala wa Barabara nchini-TANROADS ndio wamekabidhiwa jukumu la ujenzi naukarabati wa barabara kuu nchini;

Na kwa Kuwa, pamoja na jitihada za Serikali kujengabarabara; bado maeneo mengi nchini barabara zakehazipitiki hasa wakati wa masika;

Kwa hiyo Basi, Kamati inaishauri Serikali yafutayo;-

a) Kuhakikisha inaunganisha Miji yote Mikuu na Mikoa iliyosaliakama vile Mikoa ya Katavi- Kigoma, Katavi-Tabora, Kigoma-Kagera na Njombe-Makete-Mbeya kwa barabara za lami ilikufungua fursa za maendeleo katika maeneo hayo;

b) Kukarabati baadhi ya barabara za Mikoa zilizo katika haliisiyoridhisha na kutopitika hasa wakati wa mvua na kuathirishughuli za kiuchumi na kijamii;

c) Wizara ya Ujenzi isimamie Sheria za barabara kwa kutoaelimu kwa wananchi kwa kutumia vyombo vya habari kamaruninga, magazeti na redio. Pia kufanya mikutano na kuwekaalama zitakazoonesha mwisho wa eneo la barabara;

d) Kuendelea na ujenzi wa barabara za lami hasa maeneoyanaochochea Uchumi wa Taifa letu kama vile maeneo yenyevivutio vya utalii, kilimo na viwanda na madini;

e) Matuta madogo madogo ya barabarani maarufu kwajina la rasta na matuta makubwa yasiyo na kiwangoyaondolewe kwa kuwa zinasababisha ajali na uharibifu wamagari. Aidha matuta yabaki sehemu zenye umuhimu tu nayawe na kiwango maalumu;

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

119

f) Kamati imekuwa ikishauri na inaendelea kushauri kwambaili kuilinda miundombinu yetu hasa alama za barabara nareli; upo umuhimu mkubwa wa kutungwa kwa Sheria yakudhibiti uuzaji wa chuma chakavu ili kunusuru miundombinuyetu iliyogharimu fedha nyingi na kwa usalama wa watumiajiwa barabara zetu; na

g) Kununua mizani ya kisasa ambazo zinauwezo wa kupimauzito wa magari huku yakiwa kwenye mwendo (Weight inMotion). Kamati inaendelea kushauri mizani hizi za kisasazifungwe pia katika maeneo mengine yanye kusababishamsongamano mkubwa wa kupima magari Mfano, Himo-Moshi, Mizani ya Mikese- Morogoro, Kihonda-Morogoro,Makambako kwa mpemba n.k.

2.3.2 Ujenzi wa Viwanja vya Ndege

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, Wakala wa BarabaraTanzania umepewa jukumu la ujenzi wa Viwanja vya Ndegenchini;

Na kwa kuwa, bado kuna changamoto kubwa ya uboreshajina ujenzi wa viwanja vya ndege;

Kwa hiyo Basi, Kamati inashauri Serikali yafuatayo;-

a) Kuhakikisha inamaliza kwa wakati malipo ya fedhayaliyoidhinishwa ya kuendeleza viwanja vya ndege nchinihususan Kiwanja cha ndege cha Mwanza, Songwe naMtwara. Vile vile, kuweza kulipa fidia kwa viwanja vya ndegevya Julius Nyerere International Airport- JNIA, Mwanza, Bukoba,Msalato, Kigoma, Shinyanga, Songwe, Sumbawanga, n.k; na

b) Kuharakisha kutekeleza awamu ya pili ya ujenzi wa jengola tatu (Terminal III) la abiria katika kiwanja cha Kimataifacha Julius Nyerere ili mradi huu uweze kukamilika. Aidha,Kamati inashauri wakati ujenzi wa jengo la tatu unaendelea,ni vyema kuendelea kuboresha mifumo ya jengo la pili laabiria linalotumika sasa ili kuwa na muonekano mzuri nakuleta taswira nzuri ya nchi; na

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

120

c) Kuhakikisha viwanja vya ndege vinawekewa uzio kwaniviwanja vingi havina uzio jambo linalohatarisha usalama.

2.3.3 Kupunguza msongamano katika Jiji la Dar esSalaam

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, Serikali imeonesha nia yakupunguza msongamano katika jiji la Dar es Salaam kwakuweka barabara za juu (flyovers) eneo la TAZARA na Ubungona kwa kujenga barabara za michepuko;

Na kwa kuwa, msongamano katika jiji la Dar es Salaamumekuwa ukisababisha adha kubwa;

Kwa hiyo Basi, Kamati inashauri Serikali yafuatayo:-

a) Barabara za juu maarufu kama (flyovers) zijengwe hasakatika makutano ya barabara kuu zenye msongamanomkubwa kama vile, Magomeni, Morocco, Mwenge. Wadaukama Mifuko ya Hifadhi ya Jamii inaweza kushirikishwa kwakujenga barabara za kulipia.

b) Kukamilisha ujenzi wa barabara zinazosaidia wananchikufika maeneo yao bila kupita katikati ya Jiji la Dar es salaam,ikiwa ni pamoja kukamilisha barabara kutoka Goba-Madale-WazoHill, Goba –Kimara, Ardhi-Makongo-Goba n.k. Piabarabara za mitaani (ring roads) nazo zifunguliwe kwakuwekwa lami kwani zitapunguza msongamano kwa kiasikikubwa;na

2.4 Sekta ya Mawasiliano

2.4.1 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania-TCRA

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, Mamlaka ya MawasilianoTanzania ilianzishwa kwa lengo la kusimamia mawasilianonchini;

Na kwa Kuwa, kumekuwepo changamoto mbalimbalizinazotokana na ukuaji wa teknolojia;

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

121

Kwa Hiyo Basi, Kamati inashauri Serikali yafuatayo:

a) Kuendelea kudhibiti mawasiliano ya ulaghai na hatimayekupunguza vitendo viovu vinavyofanyika kupitia njia yamtandao na ili kuimarisha usalama wa watu na mali zao;na

b) Kuendelea kukabiliana na changamoto za kukua kwateknolojia ya habari na mawasiliano na changamoto zakekama vile uhalifu mitandaoni unaojumuisha kashfa kwawatu, usambazaji wa picha zisizostaili hivyo kuharibu maadili,mila na desturi zetu. Aidha, Mamlaka ya MawasilianoTanzania-TCRA iendelee kuisaidia Jeshi la Polisi katikakutekeleza sheria ya Cyber Crime na kuwabana wahalifu;na

c) Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwa kushirikiana naMamlaka ya Mapato Tanzania kuharakisha kutafuta ufumbuziwa namna bora ya kupata taarifa za makusanyo ya simu zandani kwa kutumia mtambo wa TTMS ili Serikali iweze kutozakodi stahiki kutokana na miamala ya fedha inayofanyikakupitia simu za mkononi. Kuendelea kuchelewa kulitekelezasuala hili kunazidi kuikosesha nchi kodi stahiki kutokana naMakampuni haya kutotozwa kodi stahiki;

2.4.2 Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote-UCSAF

Mheshimiwa Spika, kwa Kuwa, mfuko huu ulianzishwa kwalengo la kupeleka mawasiliano sehemu zisizokuwa na mvutowa kibiashara;

Na kwa Kuwa, Kamati bado hairidhishwi na kasi ya utekelezajiwa mradi wa usambazaji wa mawasiliano sehemu hizo;

Kwa Hiyo Basi, Kamati inashauri Serikali yafuatayo:-

a) Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania-TCRA kuweka mashartiya kutoa leseni kwa Makampuni ya Simu pamoja na masharti

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

122

mengine iwe kupeleka mawasiliano katika maeneo yapembezoni kama mchango wa kijamii (Corporate SocialResponsibility);

b) Kuweka mpango wa uwiano wa mawasiliano nchi nzimahasa maeneo ya mipakani ambapo mara nyingi watu katikamaeneo hayo hupata mawasiliano ya nchi jirani jamboambalo linawakosesha haki ya kukosa taarifa za nchi yao;

c) Kuhakikisha Makampuni ya simu yanatoa kiwangokilichopangwa cha 0.9% kama tozo za huduma (services LevyRate) i l ikuongeza uwezo wa kifedha kwa Mfuko waMawasiliano kwa Wote kumaliza shida ya mawasiliano vijijini;

d) Katika maeneo ambayo vijiji vimetoa ardhi bure kwa ajiliya ujenzi wa minara; basi Kampuni husika ichangie/ itoeruzuku kwa kijiji husika kila mwaka;

e) Mahakama na vyombo vingine viambata kama vile jeshila Polisi, kwenye watoe kipaumbele na kuharakisha kutoahaki kwenye masuala ambayo yanagusa umma moja kwamoja, kutoa haki kwani ucheleweshwaji wa kesi hasazinazohusu ujenzi wa minara ya simu, unacheleweshamaendeleo katika maeneo husika;

f) Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote kuhakikisha Makampuniya simu yanapopewa fedha na Serikali kwa ajili ya ujenzi waminara yanafanya kazi hiyo katika muda uliopangwa na kwakiwango kizuri kinachotarajiwa;

g) Halmashauri na Serikali za vijiji zitoe ushirikiano wa kutoshana wa haraka pale ambapo maeneo yanahitajika kwa ajiliya ujenzi wa minara il i kuweza kurahisisha kupatamawasiliano kwa haraka;

h) Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote utoe elimu kwawananchi ili wajue umuhimu na uwekezaji unaofanywa naSerikali katika kuleta maendeleo hususan katika ujenzi waminara ya mawasiliano ili wananchi watoe ushirikiano waulinzi ili vifaa vya minara view salama; na

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

123

i) Kuongeza rasilimali watu kwenye Mfuko wa Mawasilianokwa Wote ili Mfuko uweze kusimamia ipasavyo kwa kukaguana kutembelea maeneo ambayo Serikali imewekeza fedhakwa ajili ya ujenzi wa minara na kuhakikisha kazi hiyoimefanyika na mawasil iano yanapatikana kamailivyokusudiwa; na

j) Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote ufanye kazi kwakushirikiana kwa karibu na Wakuu wa Mikoa na Wilaya iliwaweze kufahamu miradi ujenzi wa minara inayofadhiliwana Serikali inayojengwa katika maeneo yao.

2.4.3 Mradi wa Anuani za Makazi na Misimbo ya Posta

Mheshimiwa Spika, kwa Kuwa, mradi huu unamanufaamakubwa kwani utawezesha kuwepo kwa utambulisho wamakazi ya watu na makampuni na hatimae kurahisishashughuli zote za kijamii, kiuchumi na kisiasa;

Na kwa Kuwa, utekelezaji wa mradi huu umekuwa ukisuasua;

Kwa Hiyo Basi, Kamati inashauri Serikali yafuatayo;-

a) Wizara husika ikiwemo Ardhi, Nyumba na Maendeleo yaMakazi; TAMISEMI na Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano zikaena kuona namna nzuri ya kuhakikisha mradi huu muhimuunatekelezwa haraka na kwa ufanisi mkubwa; na

b) Fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu zitolewe kamazilivyoidhinishwa na kwa wakati ili mradi huu ukamilike.

SEHEMU YA NNE3.0 HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, Kamati inaendelea kusisitiza kuwa, iliSekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Idara zake zoteziendelee kufanikiwa ni lazima uteuzi na ajira za watendajizifuate ueledi jambo ambalo Kamati inaamini limezingatiwa.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

124

Pili, watendaji wa Taasisi hizo na Bodi wasiingiliwe nawatunga Sera bali wapimwe kwa uzalishaji wao.

Tatu, sheria na taratibu zinazowekwa kwenye taasisizinazofanya biashara zifasili malengo mama ya taasisi hizo;kama ni sheria au taratibu swali liwe uwepo wa sheria autaratibu hizo zinasaidia kuongeza ufanisi na faida katika taasisihizo?

Mheshimiwa Spika, hili likizingatiwa tutakuwa na nafasi yakuwahukumu watendaji na bodi kwa haki.

3.1 Shukrani

Mheshimiwa spika, napenda kukushukuru wewe binafsi kwakunipa nafasi ya kuwasilisha Taarifa ya Kamati yangu mbeleya Bunge lako Tukufu. Aidha, kwa namna ya pekee napendakumpongeza na kumshukuru Waziri wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame MbarawaMnyaa (Mb) akishirikiana na Manaibu Mawaziri Mhe.Eng.Atashasta Nditiye, (Mb) na Mhe. Elias Kwandikwa, (Mb).Aidha, Kamati inawashukuru Makatibu Wakuu wa Wizara hiiEng. Joseph Nyamuhanga (Sekta ya Ujenzi); Eng. Dkt. LeonardChamuriho (Sekta ya Uchukuzi), Eng. Dkt. Maria Sasabo (Sektaya Mawasiliano); pamoja na Naibu Katibu Mkuu Ndg.Angelina Madete. Kamati pia inawashukuru Wakuu wa Taasisi,Wakurugenzi na wafanyakazi wote ambao wameipa Kamatiushirikiano mkubwa. Ni kwa ushauri na utaalam waoumeiwezesha Kamati kutekeleza majukumu yake nakuwasilisha taarifa hii leo katika Bunge lako tukufu.

Mheshimiwa Spika, vile vile nachukua fursa hii kumshukuruKatibu wa Bunge Stephen Kagaigai kwa kuiwezesha Kamatiwakati wote ilipokuwa inatekeleza majukumu yake. Aidha,shukrani za pekee ziende kwa Mkurugenzi wa Idara za Kamatiza Bunge Ndg. Athuman Hussein, Mkurugenzi Msaidizi Ndg.Dickson M. Bisile, Makatibu wa Kamati Ndg. Hosiana Johnna Ndg. Richard Masuke. Vilevile, nawashukuru pia watendajiwote wa Ofisi ya Bunge kwa ushirikiano wao wa kuiwezeshaKamati yangu kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

125

3.2 HojaMheshimiwa Spika, baada ya kueleza shughuli zilizotekelezwana Kamati, Maoni na Ushauri, sasa naomba kutoa Hojakwamba Bunge lipokee, lijadili na kuikubali Taarifa ya Mwakaya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinukwa kipindi cha Januari 2017 hadi Januari 2018 pamoja naMaoni na Ushauri katika Taarifa hiyo.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

Prof. Norman Adamson Sigalla King, MbMwenyekiti

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu 05 Februari, 2018

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Naibu Spika,naafiki.

NAIBU SPIKA: Hoja imeungwa mkono, nilikuwanaangalia ni wangapi wamesimama nisije nikasemaimeungwa mkono kabla haijaungwa. Ahsante sanaMwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge tunaendelea; sasatutamsikia Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Nishati naMadini, Mheshimiwa Deogratias Ngalawa, Mbunge waLudewa.

MHE. DEOGRATIAS F. NGALAWA – MAKAMUMWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATINA MADINI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa Kanuniya 117(15) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari,2016 naomba kuwasilisha taarifa ya Kamati ya Kudumu yaBunge ya Nishati na Madini kuhusu utekelezaji wa majukumuya Kamati katika kipindi cha mwezi Januari, 2017 hadi Januari,2018.

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na muda kuwamfupi sintaweza kusoma taarifa yote, hivyo naomba taarifayote pamoja na sehemu ambazo sitazisoma iingie katikaKumbukumbu Rasmi za Bunge (Hansard).

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

126

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi cha Januarihadi Desemba, 2017 Kamati imetekeleza majukumumbalimbali ya kikanuni, kama ilivyoainishwa katika kanuniya 7(1) ya Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za BungeToleo la Januari 2016.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati i l itumia njiambalimbali kutekeleza majukumu yake kikanuni, ikiwa nipamoja na ukaguzi wa miradi ya maendeleo, kupokea nakujadili taarifa mbalimbali kwa Wizara pamoja na taasisi zakena kupata mafunzo na semina mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati ilitekeleza matakwaya Kikanuni ya 98 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo laJanuari, 2016 kwa kufanya ziara za ukaguzi wa miradimbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Wizara yaNishati na Madini. Ziara hizo zilifanyika katika Mikoa wa Dares Salaam, Tanga na Geita kwa lengo la kukagua utekelezajiwa miradi mbalimbali ya maendeleo chini ya Wizara yaNishati na Madini iliyotengewa fedha na kupelekwa fedhakwa mwaka wa fedha wa 2016/2017. Miradi iliyokaguliwana kamati yako kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ni kamailivyoonyeshwa katika jedwali la taarifa hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika ukaguzi huo, Kamatiilibaini changamoto kadhaa zinazochangia kuzolota kwautekezaji wa miradi katika maeneo mbalimbali hasayaliyokaguliwa na Kamati.

Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto kubwailiibainika kuwa katika ukaguzi wa miradi yote ni ukosefu wafedha za miradi ya maendeleo. Kielelezo namba moja nanamba mbili vinatoa ufafanuzi kuhusu mchanuo waupatikanaji wa fedha za miradi ya maendeleo,zilizoidhinishwa kwa mwaka husika pamoja na ufafanuzi waupatikanaji huo kwa asilimia.

Mheshimiwa Naibu Spika, miradi ya sekta ya madiniiliyokaguliwa na Kamati ni kama ifuatavyo:-

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

127

Mheshimiwa Spika, Mgodi wa Dhahabu wa Buckreef,Kamati ilibaini kwamba licha ya leseni zote za uchimbajiwa utafiti kukabidhiwa kwa kampuni ta TANZAM hakuna kaziyoyote iliyokwishafanyika katika kuendeleza mgodi huo tangukampuni hiyo ingie mkataba na STAMICO. Kamati inaishauriSerikali kuwa makini inapoingia ubia katika miradi ya sektaya madini ili kuepuka wabia wa aina hii ambao hawazingatiiushauri wa mbia mwenza (STAMICO) jambo linalosababishahasara zisizo na msingi.

Mheshimiwa Spika, Migodi ya Wachimbaji WadogoWaliopata Ruzuku ya Serikali, Geita (Blue Reef Mining naMgusu Mining). Katika Mkoa wa Geita jumla ya wachimbajiwadogo saba wamenufaika na ruzuku ya Serikali vikiwemovikundi vya wajasiriamali wanaoshughulika katika maeneoya wachimbaji wadogo. Katika ziara ya ukaguzi wa migodiya wachimbaji wadogo waliopata ruzuku Kamati iliridhishwana utendaji wa wachimbaji wadogo watatu tu kati ya sabawaliopata ruzuku ambao wameendeleza shughuli zao zauchimbaji katika maeneo yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na mafanikio hayokwa baadhi ya wanufaika Kamati ilibaini changamotokubwa ya usimamizi wa fedha usioridhisha kwa wachimbajiwadogo. Aidha, wanufaika hao wa ruzuku kwa namna mojaama nyingine hawakutumia fedha hizo kwa malengoyaliyokusudiwa na Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, migodi ya wachimbaji wakati (Busolwa Mining na Nyarugusu Processing Plant). Mgodiwa Busolwa Mining ni mgodi unaomilikiwa na Mtanzania(mzawa) kwa asil imia 100 na Kamati i l i j ionea jinsiinavyoendesha shughuli zake kwa kutekelezasheria na kanunimbalimbali ikiwa ni pamoja na kulipa kodi zote za Serikali.Tangu mgodi huo uanze mwaka 2014 umeshalipa kodi kiasicha shilingi bilioni 120; mrabaha bilioni 562; kodi ya zuio lamwaka 2017 shilingi bilioni 20 na service levy shilingi bilioni 48.Pamoja na mgodi huo kuendesha shughuli zake kwa ufanisiKamati ilibaini kwamba unakabiliwa na changamoto yaufinyu wa eneo hasa la kutupia mabaki yatokanayo na

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

128

shughuli za mgodi (TSF). Ni mapendekezo ya Kamati kuwamaombi ya mgodi huo kupatiwa eneo lingine yashughulikiwemapema ili kusaidia kuongeza uhai wa mgodi huo ambaoumeajiri zaidi ya Watanzania 300.

Mheshimiwa Naibu Spika, sekta ya madini; sekta yavito ya Tanzanite. Kamati inampongeza kwa dhati kabisaMheshimiwa Spika kwa hatua yake ya kuunda KamatiMaalum iliyoshughulikia masuala ya uchimbaji, usimamizi, nabiashara ya madini ya Tanzanite na kubaini changamotonyingine mbalimbali hususan katika usimamizi wa biasharakwa ujumla. Mkataba wa ubia katika ya Tanzanite One,Tanzania Limited na Serikali, kupitia Shirika la Madini nchini(STAMICO), haukutoa fursa kwa Serikali kupata faida,kutokana na kuwepo kwa vipengele kadhaa kandamizi kwaSerikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati inapendakuipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniailiyoongozwa na Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kwakuamua kujenga ukuta kuzunguka eneo la mgodi ili kuongezaudhibiti wa biashara ya Tanzanite na kupunguza utoroshwajiwa madini hayo ambao ulikuwa ni changamoto kubwakatika kudhibiti mauzo. Aidha, Kamati inaunga mkonojitihada zinazoendelea za kushughulikia kwa kina mkatabahuo baina ya TML na STAMICO kwa kutumia sheria mpya zarasilimali ambazo zinaruhusu kurejea makubaliano hasi katikamikataba ya ubia ili Taifa liweze kunufaika na madini hayaya Tanzanite.

Mheshimiwa Naibu Spika, sekta ya madini nchiniimeendelea kukabiliwa na changamoto nyingi hasa katikasuala ukusanywaji wa kodi za Serikali. Sekta hii imekuwaikichangia asilimia nne tu katika pato la Taifa, mchangoambao ni kidogo sana ikilinganishwa na ongezeko lauzalishaji katika sekta hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inamiliki mgodimmoja tuu kwa asilimia mia moja ambayo ni Mgodi waStamigold kupitia Shirika la STAMICO. Mgodi huu licha ya

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

129

kuajiri Watanzania zaidi 700 bado kumekuwa na jitihadandogo za Serikali katika kuusaidia katika masuala ya msingikwa lengo la kuundeleza. Baadhi ya masuala hayo ya msingini pamoja na kama ilivyoorodhwa hapo chini.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati inampongezaMheshimiwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. JohnJoseph Magufuli kwa maamuzi ya kuigawanya Wizara yaNishati na Madini na kuwa Wizara mbili tofauti. Hii itachangiakwa kiasi kikubwa kuongeza ufanisi wa kiutendaji kwaWizara. Aidha, Kamati inaipongeza Wizara ya Madini kwakasi walioanza nayo katika utatuzi wa changamotombalimbali ikiwemo hii ya uzalishaji wa madini ya dhahabupamoja na malalamiko mbalimbali ya wananchiwanaozunguka maeneo ya migodi katika ulipwaji wa fidia.Pia Kamati inaipongeza Serikali na Bunge kwa ujumla kwakufanya mabadiliko katika Sheria ya Madini ya mwaka 2010ambayo yanaanzisha kamisheni mpya itakayosimiwa nakuratibu sekta ya madini kwa ufanisi.

Mheshimiwa Naibu Spika, sekta ndogo ya gesi, Kamatihaikuridhirishwa na mahusiano ya ubia wa kuendeleza miradiya gesi asilia inayotekezwa na TPDC, Pan Africa Energy,Songas, pamoja na TANESCO. Kamati iliona kuna haja yaBunge kuingilia kati ya kupata vyema ufafanuzi wa ziada ilikuweza kuishauri Serikali juu ya mikataba na mahusianobaina ya wabia hawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati inampongeza sanaMheshimiwa Spika binafsi kwa kuunda Kamati Maalumambayo imeshughulikia masuala ya maendeleo na matumiziya sekta hii ya gesi asilia nchini na namna ambavyo matumiziya gesi asilia yatasaidia kuongeza mapato katika nchi yetukupitia Kamati hiyo Bunge litaweza kuwa na uelewa wakiwango cha juu na kupata namna bora zaidi ya kuishauriSerikali katika sekta hii ya gesi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maoni ya jumla kuhusuutekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

130

2016/2017 kutokana na ziara ya ukaguzi wa miradi yamaendeleo Kamati ilitoa maoni yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na ukaguzi wamiradi Kamati ilitoa maoni yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, moja; utekelezaji wa bajetikwa Wizara ya Nishati na Madini haukuwa wa kuridhisha kwakuwa fedha zilizotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleohazikuwasil ishwa kwa wakati, na miradi minginehaikupelekewa fedha kabisa. Miradi mingi ya REA katikaawamu ya pili haikukamilika kutokana na kasoro mbalimbalikama vile uainishaji wa maeneo bila kuzingatia vijiji navitongoji ambavyo tayari vina wananchi wengi na ufungajiwa mashine umba (transformer) nyingi kutokizi mahitaji yaeneo husika.

Mheshimiwa Nabu Spika, Serikali iangalie upya namnabora ya kuwasaidia wachimbaji wa kati kwa kuwapatiamaeneo ya kutosha kwa kuwa wameonesha nia ya dhati yakuendeleza sekta ya madini. Ruzuku iliyotolewa na Serikalikupitia Wizara ya Nishati na Madini kwa wachimbaji wadogowadogo haikusimamiwa vizuri na hivyo kushindwa kuletatija kwa wananchi waliokusudiwa. Aidha, Serikali inapaswakutoa elimu ya kutosha kwa wachimbaji juu ya ruzukuwanazopokea kutoka kwa Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na mipango mizuriya TPDC katika kuendeleza sekta ya gesi asilia nchini, ni lazimaSerikali iwekeze fedha za kutosha katika miradi ya gesi ilikuharakisha azma ya nchi yetu kuingia katika uchumi waviwanda na Serikali itenge fedha za kutosha na kuzipelekakwa wakati kwenye miradi ya kimkakati kama vile Mgodiwa Makaa ya Mawe Kiwira, ambao mpaka sasa hakunashughuli zozote za uendelezaji wa mgodi huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ziara za mafunzo na seminakwa wajumbe wa Kamati ni kama ilivyoonyeshwa katikajedwali.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

131

Mheshimiwa Naibu Spika, kazi mahsusi zilizotekelezwana Kamati ni kuwa Kamati ya Nishati na Madini katika kipindicha mwaka mzima imetekeleza majukumu kamainavyoonesha kwenye taarifa hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, utekelezaji wa majukumuya Wizara kwa ujumla. Ili kujiridhisha na utekelezaji wa bajetiKamati ilipokea na kujadili taarifa ya upatikanaji wa fedhana utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa kipindi cha nusumwaka cha Julai hadi Desemba 2017. Katika mwaka 2017/2018 iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini ilitengewa jumlaya bilioni 998.34. Hadi kufikia tarehe 31 Desemba 2017 Wizarailikuwa imepokea jumla ya shilingi bilioni 222.53, sawa naasilimia 44.58 ya lengo la bajeti ya nusu mwaka wa fedha2017/2018 ambayo ilikuwa ni shilingi bilioni 499.17. Kati yafedha hizo shilingi bilioni 198.66 ni za miradi ya maendeleo,na sawa na asilimia 42.33 ya lengo la fedha ya maendeleokwa kipindi hicho cha nusu mwaka ambayo ilikuwa ni shilingibilioni 469.32 na shilingi bilioni 11.74 ni kwa ajili ya matumizimengineyo (OC) ambayo ni sawa na asilimia 81.44 ya lengola nusu mwaka ambalo lilikuwa ni shilingi bilioni 14.74.

Katika fedha za maendeleo zilizoidhinishwa kwamwaka 2017/2018 jumla ya shilingi bilioni 21.78 zilikuwa kwaajili ya sekta ya madini ambapo shilingi bilioni 14.7 ni fedhaza ndani na shilingi bilioni 7.83 ni kutoka nje.

Mheshimiwa Naibu Spika, uchambuzi wa matokeoya utekelezaji wa majukumu ya Kamati ya Nishati na Madini;ili kubaini utekelezaji wa majukumu ya Wizara hizo Kamatiilipokea taarifa kutoka Wizara ya Nishati na Wizara ya Madinizilizohusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara hizo pamojana hali ya upatikanaji wa mafuta nchini. Aidha, taasisizifuatazo ziliwasilisha taarifa kwenye Kamati na kujadiliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Wakala wa NishatiVijijini (REA), Kamati ilibaini changamoto kadhaa ambazozimekuwa kikwazo katika utendaji kazi wa Wakala huu.Baadhi ya changamoto hizo ni kama zilivyoainishwa katikajedwali hili.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

132

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati inaipongezaSerikali kwa juhudi na hatua mbalimbali zilizochukua nainazoendelea kuchukua kusambaza umeme vijijini. Aidha,Kamati inatoa rai kwa Waheshimiwa Wabunge kuendeleakushirikiana na Serikali katika maeneo ambayo badoyanahitaji maboresho katika utekelezaji wa miradi hii ya REAAwamu ya Tatu.

Mheshimiwa Spika, kuhusu Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO); Kamati ilipokea na kujadili taatifa ya utekelezajiwa hali ya upatikanaji wa fedha za miradi ya maendeleohadi kufikia Desemba, 2017 Kutoka Shirika la Umeme TANESCOambalo linatekeleza majukumu ya kuzalisha, kufua,kusafirisha, kusambaza na kuuza umeme nchini. Pamoja naTANESCO kudai kiasi cha fedha katika kipindi hicho cha kufikiaDesemba 2017, TANESCO ilikuwa inadaiwa na wazabuni kiasicha shilingi bilioni 913. Katika taarifa hiyo Kamati ilibainichangamoto zilizoonesha katika taarifa hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa uande wa Kampuniya Uendelezaji wa Joto Ardhi nchini (TGDC); katika mwaka2017/2018 jumla ya shilingi bilioni 36.7 zilitengwa na Serikalikwa ajili ya kampuni ya TGC kwa ajili ya miradi ya maendeleona matumizi mengineyo. Hadi Desemba 2017 Kampuniilikuwa imepokea kiasi cha shilingi bilioni 1.35 sawa na asilimia44.78 ya fedha zilizotengwa kwa kipindi cha nusu mwaka.Aidha, ni vyema kuzingatia kwamba fedha zote za ndanizinatoka kampuni mama TANESCO. Pamoja na jitihadambalimbali zinazofanywa na TGDC katika kuendeleza nishatihii ya joto ardhi bado zipo changamoto kadhaa kamazilivyooneshwa katika jeswali hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Shirika la Maendeleoya Petroli Tanzania (TPDC); katika kipindi hiki cha nusu mwakaJulai/Desemba 2017 TPDC imeweza kukusanya jumla ya shilingibilioni 161.41 sawa na asilimia 55 ya malengo ya nusu mwakaya kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 295. 47 fedha zilizotengakukutumika katika kipindi cha Julai hadi Desemba, 2017 nishilingi bilioni 3.1. Hadi kufikia Desemba 2017 shilingi bilioni2.1 sawa na asilimia 67 ya lengo zilitumika katika kutekeleza

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

133

miradi mbalimbali ya maendeleo. Pamoja na jitihadambalimbali zinazofanywa na shirika hili katika ukusanyaji wamapato kutoka vyanzo vingine bado inakabiliwa nachangamoto kama zilivyoainishwa katika taarifa hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Chuo cha Madini;kwa mwaka fedha 2017/2018 chuo hakikutengewa fedhakwa ajili ya shughuli za maendeleo, hata hivyo, miradi yamaendeleo ya chuo hiki imetelezwa kupitia vyanzo vinginevya fedha wakiwemo wabia wa maendeleo. Pamoja namafanikio mbalimbali ambayo Kamati i l ielezwachangamoto kubwa ni kama zilivyoainishwa kwenye taarifahii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Wakala wa JiologiaNchini; hadi kufikia Desemba 2017 Wakala ulikuwa umepokeajumla ya shilingi milioni 642.57 sawa na asilimia 27.5 kwa ajiliya matumizi ya kawaida. Aidha, Wakala ulikuwa umepokeashilingi bilioni 2.53 kwa ajili ya utekelezaji wa utafiti kwenyeMradi wa SMMRP, hata hivyo, licha ya majukumu hayo mazitoaliyonayo GST changamoto ni kama zilivyoainshwa hapokatika taarifa hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Shirika la Madini laTaifa; kuanzia mwezi Julai hadi Desemba 2017 Shirika lilikuwalimepokea shilingi bilioni 1.66 sawa na asilimia 12 ya fedhazilizoidhinishwa kwa ajili ya kipindi cha nusu mwaka 2017/2018. Shilirika limekwama kwa kiasi kikubwa kutekelezamajukumu ya msingi ya kuendeleza sekta ya madini kutokanana changamoto kama zilivyoainishwa katika taarifa hii.

Mheshimiwa NaibuSpika, kwa upande wa sektandogo ya mafuta na hali ya upatikanaji wa mafuta nchini;pamoja na mafanikio ya Serikali ya kuanzisha Wakala waUingizaji Mafuta kwa Pamoja Nchini sekta hii badoinakabiliwa na changamoto kama zilivyoainishwa katikataarifa hii.

Mheshimiwa Spika, kuhusu hali ya upatikanaji waumeme nchini; ili kufikia azma ya nchi yetu kujenga uchumi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

134

wa viwanda ni lazima miradi mingi ya umeme ipelekewefedha kama ilivyopangwa, sambamba na miradi ya REAinayotekelezwa nchi nzima. Aidha ukarabati wamatengenezo wa mitambo ya kufua umeme ni jambomuhimu katika kuimarisha upatikanaji wa umeme nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuchambua utekelezaji wamaoni na ushauri wa Kamati kuhusu bajeti ya Wizara kwamwaka wa fedha 2016/2017 na mchakato wa bajeti waWizara kwa mwaka wa fedha 2017/2018. Katika bajeti yamwaka 2016/2017 miradi mingi haikuweza kukamilikakutokana na ukosefu wa fedha za kuendeleza miradi. Niushauri wa Kamati kwamba bajeti iliyotengwa ya miradi yamaendeleo itolewe yote na kwa wakati, na kuwe nausimamizi mzuri wa fedha hizo ili ziweze kuleta tija. Aidha,Kamati inaendelea kusisitiza Serikali kufanyia maoni kufanyiakazi maoni na ushauri wa kamati kwa manufaa ya Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, sehemu ya tatu ya taarifahii ni maoni na mapendekezo na nianze na maoni ya Kamati.Baada ya kupokea taarifa mbalimbali ya Wizara ya Nishatina Wizara ya Madini ziara za ukaguzi wa miradi pamoja nakukutana na wadau wa sekta zote mbili za nishati na madiniK amati ina maoni yafuatayo:-

(i) Fedha za miradi ya maendeleo zinapaswakuwasilishwa kwa wakati kwani kutopatikana kwake kwawakati kunaathiri utekelezaji wa miradi iliyokusudiwa.

(ii) Serikali iendelee kutafuta na kubuni vyanzo vinginembalimbali vya mapato.

(iii) Serikali itekeleze kwa ukamilifu miradi mipya yausafirishaji na usambazaji umeme na kupanua gridikwenye maeneo ambayo hayajaunganishwa kwenye Gridiya Taifa.

(iv) Serikali iimarishe doria katika njia za umemepamoja na kuhamasisha wananchi kushiriki ulinzi wamiundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

135

(v) Serikali iwekeze katika vyanzo vingine vyakuzalisha nishati mbadala. Aidha, kuwekeza zaidi katikanishati jadidifu ambayo uzalishaji wake ni nafuu na rafiki kwautunzaji wa mazingira kutasaidia kuongeza nishati yaumeme.

(vi) Serikali inapaswa kupunguza tozo nyingi za taasisikwenye bei ya Mafuta ili kumpunguzia mizigo mwananchi/mtumiaji.

(vii) Serikali kuwekeza katika uvumbuzi wa teknolojiaya hali ya juu ili kuweza kushindana na nishati mbadala,kama vile nishati jadidifu (renewable energy) na hata miradiya LNG kwa nchi nyingine kama Msumbiji ni tishio kwabiashara ya gesi na mafuta kwa siku za usoni. Hivyo basi,Serikali inapaswa kuwekeza miradi ya gesi asilia mapemaiwezekanavyo.

(viii) Fedha za miradi ya REA zinapaswa kuwasilishwakwa wakati ili kuepuka ongezeko la gharama kutokana naucheleweshaji au ukamilishaji wa miradi hiyo.

(ix) Miradi ya REA Awamu ya Tatu hasa miradi yadensification izingatie utekelezaji wa maeneo yaliyorukwakatika awamu ya kwanza na awamu ya pili ya utekelezajiwa miradi ya REA.

(x) Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC)liwezeshwe kupata pesa za kujiendesha na sio kutegemeafedha kutoka Serikali Kuu ambazo huchelewa na hivyokuathiri utekelezaji wa miradi mbalimbali ya uendelezaji wagesi asilia. Aidha, Serikali iangalie namna itavyoweza kutatuachangamoto ya madeni ya taasisi zake katika shirika hili.

(xi) Serikali iangalie namna ya kulikwamua Shirika laMadini la Taifa (STAMICO) pamoja na migodi inayosimamiwana shirika hili ili shirika liweze kusimama na kujiendeshakibiashara.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

136

(xii) Serikali iweke utaratibu mzuri wa ufungaji wa flowmeters ili iweze kupata takwimu sahihi wakati wa upakuajiwa mafuta.

(xiii) Wakala wa Jiolojia nchini iendelee kufanya utafitiambao una tija na kuwafikia wananchi hasa elimu za utafitiwa maafa na majanga.

(xiv) Serikali iangalie namna ya kuiwezesha Wakalawa Jiolojia nchini kua ndio mtafiti pekee wa masuala yamadini na kuweza kutoa takwimu zitakazohifadhiwa kwamanufaa ya taifa. Hatua hiyo itapunguza watafiti wenginewa nje ya nchi kuja kufanya utafiti kwa muda mrefu bilakutoa takwimu na kuharibu maeneo ya nchi kwa shughuliza uchimbaji. (Makofi)

(xv) Wachimbaji wa kati na wadogo wadogowapewe kipaumbele na Serikali ili waweze kuendeleza sektaya madini kwa maendeleo ya uchumi wa Taifa letu.

(xvii) Serikali ilisaidie Shirika la TANESCO kujikwamuana madeni mengi ambayo yanalifanya lishindwe kujiendesha.

(xviii) Bunge lipewe Bajeti ya kutosha ili kuliwezeshakutekeleza makujuku yake ya kikatiba na kikanuni, hasakufanya ukaguzi katika miradi mbalimbali inayotekelezwana Serikali ili liweze kuishauri Serikali ipasavyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuelezea shughulizilizotekelezwa na Kamati, naomba kutoa mapendekezo yaKamati kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Wakala wa Nishati Vijijini;kwa kuwa, miradi mingi ya REA imeshindwa kukamilika kwawakati kutokana na kucheleweshwa na kutolewa chini yakiwango kwa fedha zilizokusanywa kutoka kwenye tozo zamafuta na kiasi kilichoidhinishwa na Bunge lako.

Na kwa kuwa, hali hiyo imesababisha ongezeko lagharama za miradi husika kutokana na sababu mbalimbali

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

137

ikiwemo fidia kwa wakandarasi na kupanda kwa thamaniya dola hapa nchini;

Kwa hiyo basi, Bunge linaishauri Serikali kutoa fedhaza miradi ya REA na zipelekwe kwa wakati na kwa kiwangocha kutosha ili miradi iliyokusudiwa itekelezwe kwa wakatina hivyo kuepusha Serikali kulipa gharama za fidia kwawakandarasi zinazochelewesha miradi yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, urukwaji wa maeneomuhimu ya huduma za kijamii katika miradi; kwa kuwamaeneo mengi ya kijamii na kiuchumi katika vijiji na vitongojivingi yalirukwa wakati wa utekelezaji wa miradi ya awamuya kwanza na ya pili ya utekelezaji wa mradi wa umemevijijini.

Na kwa kuwa hali hiyo ilikwamisha kufikiwa kwamalengo ya mradi, kuibua malalamiko kutoka kwa viongoziwa maeneo husika kwa madai ya kutoshirikishwa, pamojana kusababisha kero kwa wananchi hasa kwenye maeneoyaliyorukwa.

Kwa hiyo basi, Bunge linaishauri Serikali ihakikishemaeneo ya kijamii na ya kiuchumi yanapewa kipaumbelekatika utekelezaji wa miradi ya awamu ya tatu. Aidha,viongozi wa maeneo ambayo mradi utapita washirikishwekikamilifu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Miradi mingi yaREA iliyotekelezwa katika awamu ya kwanza na ya piliilibainika kukosa usimamizi mzuri.

Na kwa kuwa hali hiyo ilisababisha miradi hiyokutekelezwa kwa kiwango duni ikiwa ni pamoja na ununuziwa vifaa na mashine umba (transformer) zisizo na uboraunaokidhi viwango.

Kwa hiyo basi, Bunge linaishauri Serikali kuhakikishakunakuwa na usimamizi madhubuti katika utekelezaji wamiradi ya REA.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

138

Mheshimiwa Naibu Spika, Shirika la Ugavi la UmemeTanzania; kutokana na uchambuzi wa Taarifa mbalimbalizilizowasilishwa mbele ya Kamati kuhusu TANESCO, Kamatiina mapendekezo yafuatayo:-

(i) Bunge linaishauri Serikali kuchukua hatua za harakana madhubuti ili kupata ufumbuzi wa madeni ili kuiwezeshaTANESCO kuepuka na kujiendesha kwa hasara.

(ii) Wateja wengi kutolipa ankara za umeme kwawakati; kwa kuwa TANESCO imebainisha kuwepo kwawateja wengi wanaochelewa au kutolipa ankara za umemekama inavyotakiwa.

Na kwa kuwa, hali hiyo inachangia kupunguza uwezowa kifedha wa TANESCO na hivyo kuathiri utendaji nauendeshaji wa shughuli za Shirika.

Kwa hiyo basi, Bunge linaishauri Serikali iingilie kati nakuhakikisha wadeni wote wa TANESCO (ikiwemo Serikali nataasisi zake) wanalipa ankara zao kikamilifu nawatakaoshindwa waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Mheshimiwa Naibu Spika, uharibifu wa mitambo yakufua umeme; mitambo mingi ya kufua umeme imekuwaikiharibika na kushindwa kufanya kazi kutokana nakutokufanyiwa matengenezo kwa wakati. Kuharibika kwamitambo hiyo mara kwa mara husababisha kukosekana kwaumeme wa uhakika nchini jambo linaloigharimu TANESCOna Taifa kwa ujumla.

Mheshimiwa Naibu Spika, Bunge linaishauri Serikalikutenga na kupeleka fedha za kutosha kwa TANESCO ilikuiwezesha kuifanyia matengenezo mitambo ya kufuaumeme na hivyo kuepusha adha ya ukosefu wa umeme wauhakika kwa wananchi na hasara kwa Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu uchakavu wamiundombinu ya kusafirishia umeme unachangia kupoteaumeme mwingi njiani. Upotevu huo unaathiri kwa kiasi cha

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

139

umeme kinachowafikia watumiaji, na hivyo kuikoseshamapato TANESCO na kuathiri uzalishaji katika uchumi nchini.Bunge linaishauri Serikali kutenga fedha za kutosha ilikuiwezesha TANESCO kufanya matengenezo rekebishi(rehabilitation) katika vituo na miundombinu ya kusafirishiaumeme nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Shirika la PetroliTanzania (TPDC), Kamati ina mapendekezo yafuatayo:-

(a) Shirika linakabiliwa na madeni mbalimbali kutokakwa wadau mbalimbali. Shirika pia linaidai Taasisi ya TANESCOambao ndio mlaji/mnunuaji mkubwa wa gesi.

(b) Bunge linashauri Serikali kuweka utaratibu mahsusiwa kumaliza madeni haya ya taasisi hizi za kiserikali; aidha,kuangalia namna bora ya kuendelea kupeana huduma.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu uzalishaji wa gesinyingi kuliko Inavyonunuliwa; TPDC haina uwezo wa kujengamiundombinu ya kusambazia gesi inayozalisha na hivyokushindwa kulifilia soko la watumiaji. Hali hiyo inasababishaTPDC kushindwa kuuza gesi na hivyo kukosa mapatoyatakayoiwezesha kujiendesha kibiashara kama ilivyokusudiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Bunge linaishauri Serikalikuiwezesha TPDC kutekeleza mradi wa usambaza gesi katikaMkoa wa Dar es Salaam kwa kujenga miundombinu yakusambaza gesi kwa watumiaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, ufinyu wa bajeti kwashughuli za TPDC; bajeti inayotengwa na Serikali kwa ajili yaTPDC ni ndogo na fedha zake hazipatikani kikamilifu na kwawakati. Hali hiyo inachangia kuikwamisha TPDC katikautekelezaji wa shughuli zake.

Bunge linaishauri Serikali kuipatia TPDC bajeti yakutosha na kuiwezesha kutekeleza majukumu yake ya msingikama inavyotakiwa.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

140

Mheshimiwa Naibu Spika, Chuo cha Madini Dodomakinakabiliwa na ukosefu wa fedha kutokana na kutotengewafedha za maendeleo katika bajeti iliyopita. Hali hiyoinasababisha chuo kushindwa kukarabati miundombinu yamafunzo ili kiweze kuongeza udahili wa wanafunzi katikafani za ufundi mchundo na ufundi sanifu katika sekta yamadini. Bunge linaishauri Serikali kukiwezesha chuo hiki kwakukitengea bajeti ya kutosha.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wakala wa Jiolojia nchini...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MHE. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa kengele ya piliimeshagonga kwa hiyo omba yaingie yote, nadhaniulishaomba mwanzoni, kwa hiyo hitimisha hoja yako.

MHE. DEOGRATIAS F. NGALAWA – MAKAMUMWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATINA MADINI: Mheshimiwa Naibu Spika, hitimisho, napendakutoa shukrani zangu za dhati kwa Mheshimiwa Spika, JobNdugai, Mheshimiwa Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson, naWenyeviti wote wa Bunge kwa ushirikiano wenu kwa Kamatiyangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuwashukuruWajumbe wote wa Kamati ya Nishati na Madini, kwaushirikiano wao wakati wa kutekeleza majukumu ya Kamati.Kwa heshima kubwa naomba kuwatambua kwa majina yaokama na yaingie katika Hansard.

Pia ninatoa pongezi kwa Wizara ya Nishati…

MHE. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa naomba utoe hoja.

MHE. DEOGRATIAS F. NGALAWA – MAKAMU WENYEKITIWA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI:Baada ya kusema hayo, sasa naomba Bunge lako Tukufuliipokee na kuijadili taarifa hii na hatimaye kukubali maoni

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

141

na ushauri wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati naMadini.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja.(Makofi)

TAARIFA YA SHUGHULI ZA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGEYA NISHATI NA MADINI ZILIZOTEKELEZWA KATIKA KIPINDI

CHA KUANZIA JANUARI, 2017 HADI JANUARI, 2018 – KAMAILIVYOWASILISHWA MEZANI

____________

SEHEMU YA KWANZA

1.0 UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 117 (15) yaKanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari 2016, naombakuwasilisha Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishatina Madini, kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Kamati katikakipindi cha Januari, 2017 hadi Januari, 2018.Kutokana na muda kuwa mfupi, sitaweza kusoma taarifayote, hivyo naomba taarifa yote, pamoja na sehemuambazo sitazisoma iingie katika Kumbukumbu Rasmi zaBunge “Hansard”.

1.1 Majukumu ya Kamati

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Januari hadiDisemba, 2017, Kamati imetekeleza majukumu mbalimbaliya kikanuni kama ilivyoanishwa katika Kanuni ya 7 (1) yaNyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo laJanuari, 2016. Pamoja na majukumu mengine Kamatiimetekeleza majukumu ya msingi yafuatayo :-

a) Kushughulikia Bajeti ya Wizara ya Nishati na Wizara yaMadini;

b) Kushughulikia Taarifa za Mwaka za Utendaji wa Wizara yaNishati na Wizara ya Madini pamoja na;

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

142

c) Kufuatilia utekelezaji wa Majukumu ya Wizara hizo.

1.2 Njia zilizotumika kutekeleza majukumu ya Kamati

Mheshimiwa Spika, Kamati i l itumia njia mbalimbalikutekeleza majukumu yake kikanuni, ikiwa ni pamoja naukaguzi wa miradi ya maendeleo, kupokea na kujadili taarifambalimbali kwa Wizara pamoja na taasisi zake, na kupatamafunzo na semina mbalimbali.

1.3 Ziara za ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo 2016/2017

Mheshimiwa Spika, Kamati ilitekeleza matakwa ya Kanuniya 98(1) ya Kanuni za kudumu za Bunge Toleo la Januari, 2016kwa kufanya ziara za ukaguzi wa miradi mbalimbali yamaendeleo inayotekelezwa na Wizara ya Nishati na Madini.

Ziara hizo zilifanyika katika Mikoa ya Dar es Salaam, Tangana Geita kwa lengo la kukagua utekelezaji wa miradimbalimbali ya maendeleo chini ya Wizara ya Nishati na Madiniiliyotengewa fedha na kupelekewa fedha kwa mwaka wafedha 2016/2017.

Mheshimiwa Spika, Miradi iliyokaguliwa na Kamati yako kwamwaka wa fedha 2016/2017 ni hii ifuatayo:-

i) Miradi ya Umeme Vijijini katika Wilaya ya Tanga;

ii) Miradi ya Umeme Vijijini katika Wilaya ya Geita;

iii) Mradi wa Umeme wa Gesi wa Kinyerezi I Extension (MW185);

iv) Mradi wa Umeme wa Gesi wa Kinyerezi II (MW 240);

v) Ukarabati wa Kituo cha kufua Umeme cha Hale;

vi) Mradi wa Umeme wa Bulyanhulu – Geita KV 220;

vii) Mgodi wa Dhahabu wa Buckreef;

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

143

viii) Migodi ya Wachimbaji wadogo waliopata Ruzuku yaSerikali; na

ix) Migodi ya Wachimbaji wa kati.

Mheshimiwa Spika, katika ukaguzi huo Kamati ilibainichangamoto kadhaa zinazochangia kuzorota kwautekelezaji wa Miradi katika maeneo mbalimbali hasayaliyokaguliwa na Kamati. Changamoto kubwa iliyobainikakatika ukaguzi wa miradi yote ni ukosefu wa fedha za miradiya maendeleo.

Kielelezo Na. 1 na Na. 2 vinatoa ufafanuzi kuhusu mchanganuowa upatikanaji wa fedha za miradi ya maendeleozilizoidhinishwa kwa mwaka husika pamoja na ufafanuzi waupatikanaji huo kwa asilimia.

MWENENDO WA UPATIKANAJI WA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA KIPINDI

CHA MIAKA MITANO KUANZIA 2013/2014 HADI 2017/2018

Kielelezo: 1

MWAKA KILICHOIDHINISHWA (Tsh. Bilioni)

KILICHOTOLEWA

(Tsh. Bilioni) %

2013/2014 1,100 614 55.82

2014/2015 957.2 271.57 28.37

2015/2016 502.3 579 115.27

2016/2017 1,056 698.61 66.17

2017/2018 938.32 198.66 21.17

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

144

1.4 Miradi ya Sekta ya Madini iliyokaguliwa na Kamati

1.4.1 Mgodi wa Dhahabu wa Buckreef

Mheshimiwa Spika, Mgodi wa Dhahabu wa Buckleef uliokomkoani Geita, una Leseni ya Uchimbaji Mkubwa (SpecialMining License) SML Na. 04/92 na unamilikiwa kwa mkatabawa ubia (Joint Venture Agreement)ulioingiwa mwaka 2011kati ya Serikali kupitia STAMICO na Kampuni ya TANZAM 2000.

Kupitia mkataba huo, STAMICO inamiliki asilimia 45 naTANZAM 2000 inamilki asilimia 55 ya hisa. Kwa mujibu wamkataba huo TANZAM 2000 ina jukumu la kutafuta fedha zakuendesha Mgodi (Operator) wakati jukumu la STAMICOlilikuwa kuhamishia Leseni zake 12 kwa Kampuni hiyo.

Kamati ilibaini kwamba, licha ya Leseni zote za uchimbajina utafiti kukabidhiwa kwa Kampuni hiyo, hakuna kaziyeyote iliyokwishafanyika katika kuendeleza Mgodi huo tanguKampuni hiyo iingie Mkataba na STAMICO.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

145

Mheshimiwa Spika, pamoja na Kampuni kuripoti kuwaimekamilisha ufungaji wa Mtambo mpya wa kuchenjuliadhahabu, Kamati inasikitishwa na kitendo cha mbia huyokutozingatia ushauri wa STAMICO kuhusu aina ya mtambounaofaa kutumika katika eneo hilo, hatua ambayoinaisababishia Serikali hasara. Kamati inaishauri Serikali kuwamakini inapoingia ubia katika miradi ya sekta ya madini ilikuepuka wabia wa aina hii ambao hawazingatii ushauri wambia mwenza, (STAMICO) jambo linalosababisha hasarazisizo za msingi.

Kamati haikuona jitihada zozote za mbia huyo za kuendelezaMgodi kama walivyokubaliana kwenye Mkataba. Vilevile,Kamati imesikitishwa na usimamizi mbovu wa STAMICO katikaMgodi huo licha ya kuwa na mashapo yenye uhakika wakuzalisha dhahabu na kuliingizia Taifa mapato. Ni mtazamowa Kamati kwamba, hatua stahiki zichukuliwe ili kurekebishakasoro ambazo zimebainika katika ubia huo.

1.4.2 Migodi ya Wachimbaji Wadogo waliopata Ruzukuya Serikali-Geita (Blueleef Mining na Mgusu Mining)

Mheshimiwa Spika, katika awamu zote mbili za malipo,jumla ya Shilingi 8,071,000,000/= zimetolewa na Serikali kwakuratibiwa na Wizara ya Nishati na Madini, na jumla yaWachimbaji Wadogo 115 wamenufaika kwa kupata ruzukuhizo katika mikoa mbalimbali. Katika awamu ya kwanza yamalipo, kiwango cha juu kwa kila mnufaika kilikuwa ni Dolaza Kimarekani 50,000 na awamu ya pili kiwango cha juucha mnufaika kilikuwa ni Dola za Marekani 100,000. Kwamaoni ya Kamati, viwango hivyo vya fedha ni vikubwaikilinganishwa na usimamizi mdogo unaotolewa na Wizaraya Madini.

Katika Mkoa wa Geita jumla ya Wachimbaji WadogoWadogo Saba (7) wamenufaika na ruzuku ya Serikali,vikiwemo Vikundi vya Wajasiriamali wanaoshughulika katikamaeneo ya wachimbaji wadogo. Katika ziara ya ukaguziwa Migodi ya wachimbaji wadogo waliopata ruzuku, Kamatiiliridhishwa na utendaji wa wachimbaji wadogo watatu (3)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

146

tu kati ya Saba (7) waliopata ruzuku ambao wameendelezashughuli zao za uchimbaji katika maeneo yao.

Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikio hayo kwa baadhiya wanufaika, Kamati ilibaini changamoto kubwa yausimamzi wa fedha usioridhisha kwa Wachimbaji Wadogo.Aidha, Wanufaika hao wa ruzuku kwa namna moja amanyingine hawakutumia fedha hizo kwa malengoyaliyokusudiwa na Serikali.

Kwa kuwa, katika awamu zote mbili za utoaji wa ruzukukwa Wachimbaji Wadogo kumekuwa na kasoro mbalimbalikwenye matumizi na usimamizi wa ruzuku hizo, Kamatiinaishauri Serikali kufanya tathmini (evaluation) ya fedha hizokabla haijaanza awamu nyingine ili kuhakiki na kutatuachangamoto nyingi ambazo zipo kwa sasa.

1.4.3 Migodi ya Wachimbaji wa Kati (Busolwa Mining naNyarugusu Processing Plant)

Mheshimiwa Spika, Kamati ilifanya ziara ya ukaguzi waMigodi ya Busolwa Mining na Nyarugusu Processing Plant,iliyopo Mkoa wa Geita. Lengo la ziara lilikuwa ni kujifunzajinsi Wachimbaji wa Kati wanavyoendesha shughuli zao nakubaini mchango wao katika mapato ya Serikali.

Busolwa Mining ni Mgodi unaomilikiwa na Mtanzania, yaanimzawa kwa aslimia mia moja, na Kamati ilijionea jinsiunavyoendesha shughuli zake kwa kutekeleza Sheria naKanuni mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kulipa kodi zote zaSerikali. Tangu Mgodi huo uanze kazi mwaka 2014,umeshalipa kodi kiasi cha shilingi bilioni 120, Mrabahashilingi Bilioni 562, kodi ya zuio kwa mwaka 2017 shilingiMilioni 20 na Service Levy shilingi Milioni 48.

Pamoja na mgodi huo kuendesha shughuli zake kwa ufanisi,Kamati ilibaini kwamba, unakabiliwa na changamoto yaufinyu wa eneo hasa la kutupia mabaki yatokanayo nashughuli za Mgodi yaani (TSF). Ni mapendekezo ya Kamatikuwa, maombi ya Mgodi huo kupatiwa eneo lingine

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

147

yashughulikiwe mapema ili kusaidia kuongeza uhai wa Mgodihuo ambao umeajiri zaidi ya Watanzania 300.

1.5 SEKTA YA MADINI

1.5.1 Madini ya Vito ya Tanzanite

Mheshimiwa Spika, pamoja na Kamati kutoa maoni namapendekezo yake kuhusu madini ya Tanzanite, badoutekelezaji wake ulikua wa kusua sua sana kwa upande waSerikali. Changamoto ya usimamizi usioridhisha katika mgodihuu umesababisha Taifa kupoteza mapato mengi sana.Migogoro ya muda mrefu kati ya wachimbaji wadogowadogo (mitobozano), utoroshwaji wa madini ya Tanzanitenje ya nchi ya Tanzania ambapo madini hayo yalikuayanasafirishwa kama madini ghafi, jambo ambalo ni kinyumena matakwa ya Sheria ya Madini ya Mwaka, 2010.Mheshimiwa Spika, kwa umahiri wako wa kuzingatiachangomoto hizo za muda mrefu katika madini hayo, Kamatiinakupongeza kwa dhati kabisa kwa hatua yako ya kuundaKamati Maalum iliyoshuhulikia masuala uchimbaji, usimamizina biashara ya madini ya Tanzanite na kubaini changamotonyingine mbalimbali hususani katika usimamizi na biasharakwa ujumla.

Mkataba wa ubia kati ya Tanzanite One (T) Ltd na Serikalikupitia Shirika la Madini nchini STAMICO haukutoa fursa kwaSerikali kupata faida kutokana na kuwepo kwa vipengelekadhaa kandamizi kwa Serikali kikiwepo kipengelekinachotamka kuwa faida itakayogawanywa kwa wabiaitakuwa ni faida mabaki (residual net profit) ambayo kimsingitangu kuanza kwa mkataba huo tarehe 20 Juni, 2013 faidahiyo haijawahi kupatikana kutokana na gharama kubwa zauendeshaji. Faida mabaki ni faida ambayo inapatikanabaada ya kutoa gharama zote za moja kwa moja zauzalishaji na gharama zisizo za moja kwa moja kutoka katikamauzo.

Mheshimiwa Spika, Kamati inapenda kuipongeza Serikali yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

148

Rais John Pombe Magufuli, kwa kuamua kujenga ukutakuzunguka eneo la mgodi ili kuongeza udhibiti wa biasharaya Tanzanite na kupunguza utoroshwaji wa madini hayo,ambao ulikuwa ni changamoto kubwa katika kudhibitimauzo. Aidha, Kamati inaunga mkono jitihada zinazoendeleaza kushughulikia kwa kina Mkataba huo baina ya TML naSTAMICO kwa kutumia sheria mpya za rasilimali ambazozinaruhusu kurejea makubaliano hasi katika mikataba yaubia, ili Taifa liweze kunufaika na madini haya ya Tanzanite.

1.5.2 Madini ya Dhahabu

Mheshimiwa Spika, Sekta ya Madini nchini imeendeleakukabiliwa na changamoto nyingi hasa katika suala laukusanyaji wa Kodi za Serikali. Sekta hii imekuwa ikichangiaasilimia 4% tu katika pato la Taifa, mchango ambao ni kidogosana ikilinganishwa na ongezeko la uzalishaji katika Sektahiyo.

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na malalamiko mengi kutokakwa Wawekezaji nchini hasa kwenye sekta ya Madini,wakiidai Serikali marejesho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani(VAT returns) ambayo kiutaratibu inapaswa kulipwa baadaya Migodi kukamilisha hesabu zao na kuwasilisha TRA. Serikalihaijalipa fedha hizo kwa Migodi hiyo kwa madai ya kuwepochangamoto kadhaa ambazo il ikuwa inazifuatil ia il ikujiridhisha kabla ya kuzilipa. Kamati inaishauri Serikali kutatuachangamoto hizo ili Migodi hiyo iweze kulipwa fedha hizo.

Mheshimiwa Spika, Serikali inamiliki mgodi mmoja tu kwaasilimia mia moja ambao ni Mgodi wa Stamigold kupitiaShirika la STAMICO. Mgodi huu licha ya kuajiri Watanzaniazaidi ya mia saba (700), bado kumekuwa na jitihada ndogoza Serikali katika kuusaidia katika masuala ya msingi kwalengo la kuuendeleza. Baadhi ya masuala hayo ya msingi nipamoja na:-

1. Serikali kutousaidia Mgodi kupata fedha za kufanyautafiti katika leseni zinazozunguka eneo hili ili kuongeza uhaiwa mgodi;

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

149

2. Mgodi haujasaidiwa kupata msamaha wa kodi yamafuta na vipuli vya uendeshaji kama ilivyo kwa migodimingine ya wawekezaji nchini;

3. Kukosekana kwa Mining Development Agreement(MDA) kwa muda mrefu kunaukwamisha Mgodi kujiendeshakibiashara kama ilivyo kwa Migodi mingine nchini;

4. Mgodi huu unakabiliwa na deni kubwa kutoka kwaWazabuni mbalimbali wanaotoa huduma katika Mgodi huo.Kamati inaishauri Serikali kuingilia kati deni hilo ili kuepushashughuli za Mgodi huo kusimama na kusababisha hasarakubwa.

Kamati inampongeza Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, kwamaamuzi ya kuigawanya Wizara ya Nishati na Madini nakuwa Wizara mbili tofauti. Hii itachangia kwa kiasi kikubwakuongeza ufanisi wa kiutendaji kwa Wizara hizi.

Aidha, Kamati inaipongeza Wizara ya Madini kwa kasiwaliyoanza nayo katika utatuzi wa changamoto mbalimbaliikiwemo hii ya uzalishaji wa Madini ya Dhahabu pamoja namalalamiko mbalimbali ya wananchi wanaozungukamaeneo ya migodi kama vile Mgodi wa North Mara hasamaeneno ya Nyamichele katika vijiji vya Nyakunguru,Murwambe, Matongo na Nyamongo katika ulipwaji wa fidiazao. Hata hivyo, juhudi hizo zitakuwa na tija iwapoWananchi wa maeneo hayo ambao wameteseka tokamwaka 2012 wakidai kulipwa fidia ya maeneo yao kutokaMgodi wa North Mara, watalipwa stahiki yao ili wawezekujikwamua na hali mbaya ya kiuchumi inayosababishwana kutoendeleza maeneo yao yaliyofidiwa na mgodi.

Mheshimiwa Spika, Kamati inaipongeza Serikali na Bungekwa ujumla kwa kufanya mabadiliko katika Sheria ya Madiniya Mwaka 2010 ambayo yanaanzisha kamisheni mpyaitakayosimamia na kuratibu sekta ya madini kwa ufanisi.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

150

1.6 SEKTA NDOGO YA GESI

Mheshimiwa Spika, Gesi Asilia iligundulika nchini mwaka 1974ambapo ugunduzi wa kwanza ulibainika katika Kisiwa chaSongo Songo na kufuatiwa na ugunduzi mwingine mwaka1982 katika eneo la Mnazi Bay (Mtwara). Gesi asilia hiyohaikuendelezwa kwa kuwa ilionekana kutokuwa na manufaakiuchumi. I l i kuhakikisha nchi inanufaika na gesiiliyogunduliwa, miaka ya 1990 Serikali ilifanya tafiti zakuangalia namna bora ya kutumia gesi asilia hiyo. Utafiti wamwaka 1991 ulionesha kuwa na ti ja kiuchumi hivyoikaonekana ni bora gesi asilia isafirishwe hadi Dar es Salaamkwa ajili ya kutumika viwandani pamoja na kuzalisha umeme.

Mheshimiwa Spika, tangu kugundulika kwa gesi hiyo hapanchini, jumla ya Viwanda 41 na Taasisi 2 vimekwishaunganishwa katika mtandao wa matumizi ya gesi asilia.Kamati inaipongeza Serikali kwa kuendeleza miradi yakuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia. Miradi hiyomikubwa inayotarajiwa kukamilika ifikapo Juni, 2018inakusudiwa kuongeza zaidi ya Megawati 425 kwenye Gridiya Taifa, na hivyo kupunguza tatizo la upungufu wa umemenchini.

Aidha, Kamati haikuridhishwa na mahusiano ya ubia wakuendeleza miradi ya gesi asilia inayotekelezwa kati ya TPDC,PANAFRICAN ENERGY, SONGAS pamoja na TANESCO. Kamatiiliona kuna haja ya Bunge kuingilia kati na kupata vyemaufafanuzi wa ziada ili kuweza kuishauri Serikali juu yamikataba na mahusiano baina ya wabia hao.

Mheshimiwa Spika, Kamati inakupongeza sana wewe binafsikwa kuunda Kamati Maalum ambayo imeshuhulikia masualaya maendeleo na matumizi ya sekta hii ya gesi asilia nchinina namna ambavyo matumizi ya gesi asilia yatasaidiakuongeza mapato katika nchi yetu. Kupitia Kamati hiyo,Bunge litaweza kuwa na uelewa wa kiwango cha juu nakupata namna bora zaidi ya kuishauri Serikali katika sekta hiiya gesi.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

151

1.7 Maoni ya Jumla kuhusu Utekelezaji wa Miradi yaMaendeleo kwa mwaka wa Fedha 2016/2017

Mheshimiwa Spika, kutokana na ziara ya ukaguzi wa miradiya maendeleo Kamati ilitoa maoni yafuatayo:-

i) Utekelezaji wa Bajeti kwa Wizara ya Nishati na Madini,haukuwa wa kuridhisha kwa kuwa Fedha zilizotengwa kwaajili ya miradi ya maendeleo hazikuwasilishwa kwa wakatina miradi mingine haikupelekewa fedha kabisa;

ii) Miradi mingi ya REA katika Awamu ya Pil ihaikukamilika kutokana na kasoro mbalimbali kama vileuainishaji wa maeneo bila kuzingatia vijiji na vitongojiambavyo tayari vina wananchi wengi, na ufungaji waMashine Humba (Transformer) nyingi kutokidhi mahitaji yaeneo husika;

iii) Serikali iangalie upya namna bora ya kuwasaidiaWachimbaji wa Kati kwa kuwapatia maeneo ya kutosha kwakuwa wameonesha nia ya dhati ya kuendeleza Sekta yaMadini;

iv) Ruzuku iliyotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Nishatina Madini kwa Wachimbaji Wadogo Wadogo,haikusimamiwa vizuri na hivyo kushindwa kuleta tija kwaWananchi waliokusudiwa. Aidha Serikali inapaswa kutoaelimu ya kutosha kwa wachimbaji juu ya ruzukuwanazopokea kutoka kwa Serikali;

v) Pamoja na Mipango mizuri ya TPDC katikakuendeleza Sekta ya Gesi asilia nchini, ni lazima Serikaliiwekeze fedha za kutosha katika miradi ya Gesi ili kuharakishaazma ya nchi yetu kuingia katika uchumi wa viwanda; na

vi) Serikali itenge fedha za kutosha na kuzipeleka kwawakati kwenye miradi ya kimkakati kama vile Mgodi wamakaa ya Mawe wa Kiwira ambao mpaka sasa hakunashughuli zozote za uendelezaji wa mgodi huu.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

152

1.8 Ziara za mafunzo

Mheshimiwa Spika, baadhnishai ya Wajumbe wa Kamatiwalipata fursa ya kusafiri kwenda nchini Marekani kwa ajiliya kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu sekta za Nishatihususani Umeme wa Upepo (Wind Energy). Lengo la ziara hiiilikuwa ni kuwajengea uwezo Wajumbe wa Kamati katikamasuala ya uzalishaji wa umeme kwa kutumia vyanzovingine ambavyo ni rahisi na vinapatikana katika mazingirayetu.

Mafunzo hayo yamekuza uelewa kwa Wajumbe kuhusumasuala ya kuzalisha Umeme kwa njia ya upepo na hivyokuwasaidia kutoa ushauri kwa Wizara ya Nishati kuhusuuzalishaji wa umeme kwa njia ya upepo. Umemeutakaozalishwa kutokana na upepo utakuwa wa gharamandogo, na hivyo utauzwa kwa bei nafuu na utakuwa wakuaminika.

Mheshimiwa Spika, katika ziara hiyo Wajumbe walipatawasaa wa kukutana na wadau mbalimbali katika sekta zaNishati. Aidha, walitembelea maeneo mbalimbali ambakoumeme wa njia ya upepo unazalishwa, na kuweza kujengauelewa zaidi juu ya uzalishaji wa umeme huu pamoja nagharama za utumiaji. Aidha, Wajumbe walipokea ushaurijuu ya kutoa vipaumbele vya wawekezaji mbalimbali ikiwani pamoja na kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji katikasekta ya Nishati. Nishati ya umeme wa upepo ni rafiki kwamazingira

1.9 Semina kwa Wajumbe wa Kamati

Mheshimiwa Spika, katika kuendelea kuwajengea uwezoWajumbe wa Kamati yako, Ofisi ya Bunge iliandaa seminaelekezi kupitia mradi wa Legislative Support Programunaonfadhiliwa na Mpango wa Maendeleo wa Umoja waMataifa (UNDP), kuhusu masuala ya kutunga Sheria pamojana Kanuni mbalimbali. Mafunzo haya yamekua muhimu sanakatika kuongeza uelewa kwa Wajumbe wa Kamati.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

153

Pia Wizara ya Nishati na Madini kupitia taasisi ya TPDC naTGDC iliwapatia Wajumbe wa Kamati, semina ya siku mojakuhusu Miradi ya mpango wa matumizi ya gesi asilia pamojana uendelezaji wa nishati ya joto ardhi nchini. Lengo la seminahiyo, l i l ikuwa ni kuwawezesha Wajumbe wa Kamatikufahamu vyema mpango mkakati wa gesi asilia nchinipamoja na matumizi ya nishati ya jotoardhi.

Mheshimiwa Spika, Taasisi isiyo ya kiserikali ya NaturalResource Government Institute (NRGI) imekuwa ikiandaasemina za mara kwa mara kwa lengo la kuwajengea uwezoWajumbe wa Kamati katika sekta hizi muhimu za madini,mafuta na gesi. Semina hizo pia zimekuwa zikilengakufafanua sheria mbalimbali zinazohusu udhibiti na ukusanyajiwa mapato katika sekta hizi kwa maendeleo ya uchumiwetu.

Mheshimiwa Spika, vilevile, Kamati yako ilipata mafunzokuhusiana na matumizi ya Umeme wa Upepo kupitiakampuni ya Wind East African Energy ambayo ilitoa mafunzojuu ya matumizi ya umeme wa upepo ikianisha faida nanamna ya kuutumia umeme huu.

Kamati pia ilipata mafunzo kuhusiana na matumizi yarasilimali kupitia taasisi ya OXFAM, ambayo yalijikita yalijikitakatika uchambuzi wa sekta ya uchimbaji wa madini, gesiasilia na kutunza mazingira.

Mheshimiwa Spika, kupitia mafunzo hayo Wajumbe waKamati ya Nishati na Madini, wamepata uelewa mpanakuhusu sekta hizi muhimu wanazozisimamia kwa kuelewavyema mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kutekelezamajukumu yao ya kushauri na kuisimamia Wizara ya Nishatina Wizara ya Madini.

1.9.1 KAZI MAHSUSI ZILIZOTEKELEZWA NA KAMATI

Mheshimiwa Spika, Kamati ya Nishati na Madini katika kipindicha mwaka mzima imetekeleza majukumu yafuatavyo:-

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

154

i) Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo iliyotengewa Fedhakwa mwaka wa Fedha 2016/2017;

ii) Kupokea na Kuchambua utekelezaji wa maoni naushauri wa Kamati kuhusu bajeti ya Wizara kwa Mwaka waFedha wa 2016/2017 pamoja na uchambuzi wa Bajeti yaWizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/2018;

iii) Kupokea Taarifa ya nusu Mwaka ya upatikanaji waFedha na utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa mwakawa Fedha 2017/2018 na;

iv) Kupokea na kujadili Taarifa za utendaji wa Taasisimbalimbali zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Wizara yaMadini.

1.9.2 Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara kwa Ujumla

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza majukumu yake,Kamati ilitaka kujiridhisha kuhusu utekelezaji wa majukumuya Wizara kwa kurejea Hati idhini ya Serikali Na. 144 ya tarehe22 Aprili, 2016 (Government Instrument). Lengo lilikuwa nikuoanisha bajeti inayotengwa, iliyopokelewa, matokeo yautekelezaji wa bajeti na matarajio ya wananchi kwa Serikaliyao.

Ili kujiridhisha na utekelezaji wa Bajeti, Kamati ilipokea nakujadili taarifa ya upatikanaji wa fedha na utekelezaji wamajukumu ya Wizara kwa kipindi cha nusu mwaka (Julai –Disemba, 2017). Katika mwaka 2017/18 iliyokuwa Wizara yaNishati na Madini ilitengewa jumla ya Shilingi bilioni 998.34.Hadi kufikia tarehe 31 Desemba, 2017 Wizara ilikuwaimepokea jumla ya Shilingi bilioni 222.53 sawa na asilimia44.58 ya lengo la bajeti ya nusu mwaka wa fedha 2017/18ambayo ilikuwa ni shilingi bilioni 499.17.

Kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 198.66 ni za miradi yamaendeleo sawa na asilimia 42.33 ya lengo la Fedha zamaendeleo kwa kipindi hicho cha nusu mwaka ambalolilikuwa ni shilingi bilioni 469.32, na Shilingi bilioni 11.74 ni

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

155

kwa ajili ya matumizi mengineyo (O.C) ambayo ni sawa naasilimia 81.44 ya lengo la nusu mwaka ambalo lilikuwa nishilingi bilioni 14.74.

Katika Fedha za maendeleo zilizoidhinishwa kwa mwaka2017/18 jumla ya shilingi bilioni 21.78 zilikua kwa ajili ya sektaya madini ambapo shilingi bilioni 14.7 ni fedha za ndani nashilingi bilioni 7.83 ni kutoka nje.

SEHEMU YA PILI

2.0 UCHAMBUZI WA MATOKEO YA UTEKELEZAJI WAMAJUKUMU YA KAMATI YA NISHATI NA MADINI

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza majukumu yake yakusimamia utendaji wa Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini,Kamati ilipokea taarifa mbalimbali zinazohusu Wizara yaNishati na Wizara ya Madini pamoja na sekta ndogo yaMafuta nchini.

Ili kubaini utekelezaji wa majukumu ya Wizara hizo, Kamatiilipokea taarifa kutoka Wizara ya Nishati na Wizara ya Madinizilizohusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara hizo pamojana hali ya upatikanaji wa mafuta nchini. Aidha, Taasisizifuatazo zilizowasilisha taarifa kwenya Kamati na kujadiliwa;

2.1 Wakala wa Nishati Vijijini ( REA)

Mheshimiwa Spika, Kamati ilipokea na kujadili taarifa yaWakala wa Umeme vijijini kuhusu utekelezaji wa miradi yaumeme pamoja na upatikanaji wa fedha za miradi hadikufikia Disemba, 2017.

Katika mwaka wa Fedha wa 2017/18 Serikali imetengashilingi bilioni 469.09 kwa ajili ya Mfuko wa Nishati Vijijini.Kiasi cha shilingi bilioni 234.54 kilitarajiwa kupokelewakwenye mfuko kutoka kwenye vyanzo mbalimbali katikakipindi cha Nusu mwaka (Julai – Disemba, 2017). Hata hivyo,hadi kufika Disemba, 2017, kiasi cha shilingi bilioni 190.58

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

156

(sawa na asilimia 81.26) ndiyo kilikuwa kimepokelewa kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya REA Awamu ya Tatu.

Aidha, Kamati ilibaini changamoto kadhaa ambazozimekuwa kikwazo katika utendaji kazi wa Wakala huu.Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na:-

a) Mwitikio mdogo wa wateja kuunganishiwa umemekwenye maeneo ambayo ujenzi wa miundombinuumekamilika;

b) Msamaha wa kodi kwa vifaa vya miradi ya nishatibado ni changamoto;

c) Baadhi ya maeneo kurukwa wakati wa kupelekaumeme, hasa katika maeneo muhimu kama Zahanati, Shulena maeneo mengine ya kijamii;

d) Baadhi ya mashine za utekelezaji wa miradi kua nivifaa duni na kutokukodhi mahitaji ya maeneo husika. Mfanoni mashine humba (Transformer) katika baadhi ya maeneozimebainika kuharibika mara kwa mara au kuwa na uwezomdogo wa kufanya kazi; na

e) Ushirikishwaji mdogo wa Viongozi pamoja naWananchi katika maeneo ya miradi hasa wakati wauainishaji wa vijiji/vitongoji.

Mheshimiwa Spika, Kamati inaipongeza Serikali kwa juhudina hatua mbalimbali ilizochukua na inazoendelea kuchukuakusambaza umeme vijijini, Aidha, Kamati inatoa rai kwaWaheshimiwa Wabunge kuendelea kushirikiana na Serikalikatika maeneo ambayo bado yanahitaji maboresho katikautekelezaji wa miradi hii ya REA Awamu ya Tatu.

2.2 Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)

Mheshimiwa Spika, Kamati ilipokea na kujadili taarifa yautekelezaji na hali ya upatikanaji wa Fedha za miradi yamaendeleo hadi kufikia Disemba, 2017 kutoka Shirika la

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

157

Umeme (TANESCO) ambalo linatekeleza majukumu yakuzalisha/kufua, kusafirisha,kusambaza na kuuza umemenchini. Katika kipindi cha mwezi Julai hadi Disemba, 2017,TANESCO imeunganisha wateja wapya 105,844 kati ya 124,990waliotarajiwa kuunganishwa katika kipindi hicho. Idadi hiyoni sawa na asilimia 85 ya lengo.

Shirika hilo lilikusanya shilingi bilioni 730 kutokana na mauzoya umeme na michango ya wateja wapya walioombakuunganishiwa umeme (consumer contribution). Kiasi hichoni sawa na asilimia 84 ya lengo ambalo lilikuwa ni kukusanyashilingi bilioni 866. Hadi kufika tarehe 31 Disemba, 2017 Shirikalilikuwa linadai Wateja wake (Serikali na Taasisi zake pamojana wateja binafsi) kiasi cha shilingi bilioni 277.4. Kati ya denihili wateja binafsi wanadaiwa shilingi bilioni 83.8 na Serikalina taasisi zake pamoja na shirika la umeme Zanzibar (ZECO)wanadaiwa shilingi bilioni 193.7.

Mheshimiwa Spika, pamoja na TANESCO kudai kiasi hichocha fedha, katika kipindi hicho cha kufikia Disemba, 2017,ilikuwa inadaiwa na Wazabuni kiasi cha shilingi bilioni 913.

Katika mwaka wa Fedha 2017/18, Serikali ilitenga shilingibilioni 293.41 kwa ajili ya maendeleo kwa TANESCO. Hadimwezi Disemba, 2017 jumla ya shilingi 42.13 sawa na asilimia14 ya fedha zilizotengwa tayari zilikuwa zimepokelewa naTANESCO kutoka Serikalini.

Katika taarifa hiyo Kamati ilibaini changamoto zifuatazo:-

a) Madeni ya TANESCO yanasababisha kuzorota kwautendaji wa shirika. Aidha, madeni yameendelea kuongezekana hakuna jitihada zozote za Serikali za kusaidia kumalizamadeni haya;

b) Gharama kubwa za uzalishaji wa umeme kwakutumia mafuta hasa kwenye maeneo ambayohayajaunganishwa na gridi ya Taifa;

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

158

c) Wateja wengi zikiwemo Wizara na Taasisi za Serikali,kutolipa ankara za umeme kwa wakati hivyo kuathiriutekelezaji wa majukumu ya shirika;

d) Uharibifu wa mara kwa mara wa mitambo ya kufuaumeme unaosababisha mitambo hiyo kuzimwa kwa mudamrefu, kunaligharimu shirika na Taifa kwa ujumla kwakukosekana kwa umeme wa uhakika katika maeneo mengihapa nchini;

e) Ukosefu wa umeme wa kutosha kutokana na Serikalikushindwa kuwekeza kwenye mitambo ya kuzalisha umemekwa muda mrefu licha ya ongezeka kwa mahitaji ya umemenchini; na

f) Upotevu wa umeme kutokana na uchakavu kwamifumo ya usafirishaji na usambazaji wa umeme.

2.3 Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Nchini (TGDC)

Mheshimiwa Spika, Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhinchini ilisajiliwa mwezi Disemba, 2013 na kuanza kazi Julai,2014. TGDC ni kampuni tanzu ya TANESCO na inamilikiwa naSerikali ya Tanzania kwa asilimia mia moja (100%). Kampunihii ina jukumu la kuharakisha uendelezaji wa nishati yajotoardhi nchini ili kuchangia kukuza uchumi na kuongezaajira.

Katika mwaka 2017/18 jumla ya shilingi bilioni 36.7 zilitengwana Serikali kwa ajili ya kampuni ya TGDC kwa ajili ya miradiya maendeleo na matumizi mengineyo. Hadi Disemba, 2017Kampuni ilikuwa imepokea kiasi cha shilingi bilioni 1.35 sawana asilimia 44.78 ya fedha zilizotengwa kwa kipindi cha nusumwaka. Aidha, ni vyema kuzingatia kwamba, fedha zoteza ndani zinatoka kampuni mama ya TANESCO.

Pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanywa na TGDC katikakuendeleza nishati hii ya joto ardhi, bado zipo changamotokadhaa zikiwemo:-

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

159

a) Kukosekana kwa sheria mahususi ya Jotoardhi nchini;

b) Gharama kubwa za kulipia leseni za umiliki wamaeneo ya kufanyia kazi, ikizingatiwa kwamba TGDChaijawa na chanzo cha fedha za kulipia leseni;

c) Upatikanaji wa fedha za miradi ya Jotoardhi; na

d) Uhaba wa wataalam wenye ujuzi stahiki katika sokola ajira nchini.

2.4 Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)

Mheshimiwa Spika, Kamati ilipokea na kujadili taarifa yautendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC).Katika uchambuzi huo ilibainika kwamba, ugunduzi wa gesinchini bado haujawanufaisha wananchi kwa kiwango chakuridhisha.

Katika kipindi hiki cha nusu mwaka (Julai – Disemba, 2017)TPDC imeweza kukusanya jumla ya shilingi bilioni 161.41 sawana asilimia 55 ya malengo ya nusu mwaka ya kukusanyakiasi cha shilingi bilioni 295.47. Fedha zilizotengwa kutumikakatika kipindi cha Julai hadi Disemba, 2017 ni shilingi bilioni3.1. Hadi kufikia Disemba, 2017, shilingi bilioni 2.1 sawa naasilimia 67% ya lengo zilitumika katika kutekeleza miradimbalimbali ya maendeleo.

Aidha, kutolipwa kwa wakati kiasi cha shilingi bilioni 398.69ambazo Shirika linawadai wateja wake, kunaliathiri shirikakatika utekelezaji wa majukumu yake ipasavyo. Pamoja najitihada mbalimbali zinazofanywa na shirika hili katikaukusanyaji wa mapato kutoka vyanzo vingine, badolinakabiliwa na changamoto zifuatazo;

a. Ukosefu wa soko la uhakika na la kuaminika la gesiinayozalishwa nchini;b. Bajeti ndogo inayotengwa kwa Shirika ambayoinalifanya shirika lishindwe kutekeleza majukumu yake muhimukwa Taifa hasa uwekezaji na utafiti wa gesi na mafuta nchini;

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

160

c. Kucheleweshwa kwa fedha za maendeleokunakwamisha utekelezaji wa miradi. Mfano, mradi wakusambaza Gesi asilia katika mkoa wa Dar es Salaam;

d. Uendelezwaji wa rasilimali watu unaotokana nakupungua kwa mikataba ya utafiti wa mafuta na gesi,kumesababisha kupungua kwa fedha za mafunzo (Annualtraining fees) zilizokua zinatokana na mikataba hiyo. Hali hiiimerudisha nyuma shughuli za uendeshaji wa rasilimali watukatika shirika hasa ukizingatia kuwa sekta hii inahitaji utaalamna teknolojia ya hali ya juu.

e. Ushindani katika sekta ya gesi kutokana na mataifambalimbali pamoja na vyanzo mbadala vya nishati.

2.5 Chuo cha Madini (MRI)

Chuo cha Madini ni chuo cha ufundi kilichoanzishwa kwaajili ya kupata mafundi sanifu wa kada ya kati ili kusaidiautafiti wa madini nchini, pamoja na kutoa ushauri elekezi(consultancy) katika sekta za madini, mafuta na gesi.

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa Fedha wa 2017/18 Chuohakikutengewa fedha kwa ajili ya shughuli za maendeleo.Hata hivyo miradi ya maendeleo ya chuo hiki imetekelezwakupitia vyanzo vingine vya fedha, wakiwemo wabia wamaendeleo. Aidha, hadi kufikia tarehe 31 Disemba, 2017Chuo kilikuwa kimepokea jumla ya Shilingi Milioni 144.34 tusawa na asilimia 11.48 ya bajeti iliyoidhinishwa kwa mwaka2017/18. Utolewaji huu wa fedha hauridhishi kwaniunakwamisha maendeleo ya chuo hiki muhimu kwa Taifakwa ajili ya Mafundi sanifu na Mafundi Mchundo ambao nimuhimu sana kwa maendeleo ya sekta hii ya Madini.

Pamoja na mafanikio mbalimbali ambayo Kamati ilielezwa,changamoto kubwa zifuatazo zilibainika:-

a) Bajeti ndogo isiyokidhi mahitaji ya msingi ya chuo;

b) Kucheleweshwa kwa Fedha za bajeti iliyoidhinishwa;

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

161

c) Upungufu wa ofisi za watumishi, ukumbi wa mikutanona mihadhara;

d) Uhaba wa wakufunzi katika fani za uhandisi nausimamizi wa mazingira migodini, masomo mtambuka nasayansi za mafuta na gesi;

e) Hakuna sehemu za kutosha za wanafunzi waokufanyia mafunzo kwa vitendo na;

f) Kukosekana kwa ulinzi madhubuti katika kampasi yaNzega, hivyo kusababisha uvamizi kutoka kwa wachimbajiwadogo na wizi wa mara kwa mara katika kampasi hiyo.

2.6 Wakala wa Jiolojia nchini (GST)

Mheshimiwa Spika, Wakala wa Jiolojia nchini ana majukumuya kukusanya, kuchambua, kutafsiri, kutunza takwimu nataarifa mbalimbali za kijiosayansi (jiolojia, jiokemia najiofizikia), kutengeneza na kusambaza ramani, takwimu nataarifa mbalimbali zinazoainisha kuwepo kwa ainambalimbali za miamba nchini.

Vilevile, wakala hufanya uchunguzi wa kimaabara kwasampuli mbalimbali za miamba, madini, maji, mimea naudongo kwa ajili ya tafiti mbalimbali nchini na kuratibuutokeaji wa majanga kama vile matetemeko ya ardhi,milipuko ya volkano, maporomoko ya ardhi, mionzi asili n.k.

Hadi kufika Disemba, 2017 wakala ulikuwa umepokea jumlaya shilingi milioni 642.57 sawa na asilimia 27.5 kwa ajili yamatumizi ya kawaida. Aidha, wakala ulikuwa umepokeashilingi bilioni 2.53 kwa ajili ya utekelezaji wa utafiti kwenyemradi wa SMMRP.

Hata hivyo, licha ya majukumu haya mazito waliyonayo GST,changamoto zifuatazo zimekuwa kikwazo katika utekelezajibora wa majukumu yake:-

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

162

a) Kuathirika kwa ukusanyaji wa maduhuli kutokana nakupungua kwa shughuli za utafutaji na uchimbaji madininchini;

b) Kutopatikana kikamilifu na kwa wakati kwa fedhazilizoidhinishwa kwenye bajeti na kunaathiri utekelezaji washughuli zilizopangwa na wakala, mafunzo, ukosefu wawatumishi na vitendea kazi;

c) Upungufu wa wataalam wenye taaluma stahiki kamavile wakemia, wajiolojia, wahandisi jiolojia na maslahi duni;na

d) Mabadiliko ya teckonolojia na maendeleo makubwaya jiosayansi duniani yanaongeza gharama za uendeshaji wakazi za wakala.

2.7 Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)

Mheshimiwa Spika, Kamati ilipokea na kujadili taarifa yautekelezaji wa majukumu ya STAMICO. Shirika hili la madinilimepewa jukumu la kusimamia sekta ya madini kwa kufanyatafiti na uwekezaji katika migodi ya madini kama zilivyokampuni zingine kwa niaba ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, kuanzia mwezi Julai hadi Disemba 2017,shirika lilikuwa limepokea shilingi bilioni 1.66 sawa asilimia12 ya Fedha zilizoidhinishwa kwa ajili ya kipindi cha nusumwaka 2017/18.

Shirika limekwama kwa kiasi kikubwa kutekeleza majukumuya msingi ya kuendeleza Sekta ya Madini kutokana nachangamoto zifuatavyo:-

a) Ukosefu wa Fedha, na hivyo kukwamisha shughuli zashirika na kushindwa kuanzisha miradi mingine;

b) Uwekezaji uliofanyika katika miradi mingi haujaanzakutoa faida. Mfano, ni Mgodi wa Tanzanite One, Stamigold/Tulawaka, Kiwira n.k;

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

163

c) Shirika kukabidhiwa majukumu mengi licha ya bajetindogo inayotengwa kwa mwaka; na

d) Ukosefu wa Mikataba katika migodi ya Stamigold naKiwira kunakwamisha migodi hiyo kukopesheka.

2.8 Sekta Ndogo ya Mafuta na hali ya upatikanaji waMafuta nchini

Mheshimiwa Spika, Kamati ilipokea na kujadili taarifambalimbali zilizowasilishwa na Wizara pamoja na wadau waSekta ndogo ya mafuta nchini kuhusu mfumo mzima wauingizaji wa mafuta pamoja na maendeleo ya sekta hiyo.Katika taarifa hizo Kamati il ipata uelewa wa hali yaupatikanaji wa mafuta nchini pamoja na changamotozinazoikabili sekta hiyo.

Pamoja na mafanikio ya Serikali ya kuanzisha Wakala wauingizaji wa mafuta kwa pamoja nchini, Sekta hii badoinakabiliwa na changamoto zifuatazo:-

a) Uwezo mdogo wa mita za upokeaji mafuta (flowmeters), hali inayosababisha mita hizo kushindwa kwendana kasi inayokubalika ya kushusha tani 1200 kwa saa nabadala yake imekuwa ikishusha mafuta kwa kasi ya tani 400kwa saa;

b) Ukosefu wa Matanki makubwa ya kuhifadhia mafuta(Farm Tanks) baada ya kupakuliwa kutoka Melinikunasababisha hasara kwa Makampuni yanayoingiza mafutapamoja na kuikosesha Serikali mapato;

c) Gharama kubwa ya uwekaji wa Vinasaba (Tsh. 12kwa lita) ikilinganishwa na nchi jirani kama Kenya gharamani Tsh. 1 kwa lita na Uganda Tsh. 2 kuna muongozea mzigomwananchi; na

d) Tozo za Taasisi mbalimbali za Serikali kwenye bei yamafuta ni mzigo kwa Wafanyabiashara wa Sekta ya mafuta.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

164

Mheshimiwa Spika, ukosefu wa matanki ya kuhifadhia Mafutayaani (Farm Tanks) ni changamoto kubwa. Hata hivyo,Kamati inapenda kuipongeza Serikali kwa hatuazinazoendelea za utekelezaji wa mradi huu ikiwa ni pamojana mchakato wa kubadilisha kanuni ya uagizaji wa mafutakwa pamoja (The Petroleum (Bulk Procument) Regulationsya mwaka 2017 ili kuingiza vipengele vya upokeaji wa mafutasehemu moja (Single Receiving Terminal).

2.9 Hali ya Upatikanaji wa Umeme nchini

Mheshimiwa Spika, hali ya upatikanaji umeme nchini badoni changamoto katika baadhi ya maeneo hasa mkoa waDar es Salaam, ambako umeme umekua si wa uhakika naumekua ukikatika mara kwa mara na hivyo kuathiri wananchikatika uendeshaji wa shughuli za kiuchumi. Tatizo lamiundombinu chakavu limechangia hali duni ya upatikanajiwa umeme wa uhakika.

Hata hivyo, Katika maeneo mengine hususani vijijini,mafanikio ya kupatikana umeme yameonekana kwa kiasikikubwa kutokana na ukamilishwaji wa miradi mingi ya REAawamu ya kwanza na awamu ya pili.Kwa sasa nchi yetu ina uwezo wa kuzalisha MW 1300 namatumizi ya juu kabisa ya nchi yetu yameweza kufikia hadiMW 1041. Matumizi haya yanakadiriwa kuongezeka siku hadisiku kutokana na mahitaji ya nishati hii kukua kwa kasi nchini.Mahitaji haya ya umeme yanapaswa kabisa kuendana nakasi ya ukamilishaji wa miradi mingi ya Umemeinayotekelezwa hapa nchini. Kamati inaishauri na kuitakaSerikali kupeleka fedha katika miradi yote ya umeme ili iwezekukamilika kwa wakati na kufikia malengo ya wizarailiyojiwekea ya kufika MW 5000 ifikapo 2021.

Mheshimiwa Spika, ili kufikia azma ya nchi yetu kujengauchumi wa viwanda ni lazima miradi mingi ya umemeipelekewe fedha kama ilivyopangwa, sambamba na miradiya REA inayotekelezwa nchi nzima. Aidha, ukarabati namatengenezo ya mitambo ya kufua umeme ni jambomuhimu katika kuimarisha upatikanaji wa umeme nchini.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

165

2.9.1 Kuchambua utekelezaji wa maoni na ushauri waKamati kuhusu Bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 na mchakato wa bajeti wa Wizara kwa Mwaka waFedha 2017/2018

Mheshimiwa Spika, Kamati ilipata fursa ya kuchambuautekelezaji wa maoni na ushauri wa Kamati kuhusu Bajeti yaWizara ya Nishati na Madini kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 pamoja na kuchambua Bajeti ya Wizara hiyo kwaMwaka wa Fedha 2017/2018.

Katika bajeti ya mwaka wa Fedha 2016/2017 miradi mingihaikuweza kukamilika kutokana na ukosefu wa Fedha zakuendeleza miradi.

Mheshimiwa Spika, Kama ilivyoelezwa kwenye taarifa yaKamati ilivyowasilishwa Bungeni mnamo tarehe 19 Juni, 2017tunaipongeza Serikali kwa kutenga bajeti ya kutosha katikamiradi ya maendeleo hususani miradi ya umeme itakayosaidiawananchi kupata umeme wa uhakika katika maeneo mengiya nchi na kuwezesha dhana ya uchumi wa viwandakutekelezeka kwa vitendo. Hata hivyo hadi kufika Januari,2018 pesa zilizopelekwa katika miradi ya maendeleo ni shillingibilioni 198.66 sawa na asilimia 42.33 ya fedha zilizopangwakupokelewa katika kipindi cha nusu mwaka 2017/18.

Ni ushauri wa Kamati kwamba, bajeti iliyotengwa ya miradiya maendeleo itolewe yote na kwa wakati na kuwe nausimamizi mzuri wa fedha hizo ili ziweze kuleta tija. Aidha,Kamati inaendelea kusisitiza Serikali kufanyia kazi maoni naushauri wa Kamati kwa manufaa ya Taifa.

SEHEMU YA TATU

3.0 MAONI NA MAPENDEKEZO

3.1 Maoni ya Kamati

Mheshimiwa Spika, baada ya kupokea taarifa mbalimbaliza Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini, ziara za ukaguzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

166

wa miradi pamoja na kukutana na Wadau wa sekta zotembili za Nishati na Madini, Kamati ina maoni yafuatayo;

a) Fedha za miradi ya maendeleo zinapaswakuwasilishwa kwa wakati, kwani kutopatikana kwake kwawakati kunaathiri utekelezaji wa miradi iliyokusudiwa;

b) Serikali iendelee kutafuta na kubuni vyanzo vinginembalimbali vya mapato. Aidha, kutegemea Serikali Kuupamoja na wafadhili pekee kunakwamisha utekelezaji wabaadhi ya miradi ya maendeleo;

c) Serikali itekeleze kwa ukamilifu miradi mipya yausafirishaji na usambazaji umeme na kupanua gridi kwenyemaeneo ambayo bado hayajaunganishwa kwenye gridi yataifa;

d) Serikali iimarishe doria katika njia za umeme pamojana kuhamasisha wananchi kushiriki katika ulinzi wamiundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme;

e) Serikali iwekeze katika vyanzo vingine vya kuzalishanishati mbadala. Aidha kuwekeza zaidi katika nishati jadidifuambayo uzalishaji wake ni nafuu na rafiki kwa utunzaji wamazingira kutasaidia kuongeza nishati ya umeme;

f) Serikali inapaswa kupunguza tozo nyingi za taasisikwenye bei ya Mafuta ili kumpunguzia mizigo mwananchi/mtumiaji wa mafuta;

g) Serikali kuwekeza katika uvumbuzi wa teknolojia yahali ya juu ili kuweza kushindana na nishati mbadala, kamavile nishati jadidifu (renewable energy), na hata miradi yaLNG kwa nchi nyingine kama Msumbiji ni tishio kwa biasharaya gesi na mafuta kwa siku za usoni. Hivyo basi Serikaliinapaswa kuwekeza katika miradi ya gesi asilia mapemaiwezekanavyo ili kutoa huduma ya uhakika na kuteka sokomapema;

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

167

h) Fedha za miradi ya REA zinapaswa kuwasilishwa kwawakati, ili kuepuka ongezeko la gharama kutokana nakucheleweshamukamilishaji wa miradi hiyo;

i) Miradi ya REA Awamu ya Tatu hasa miradi yaDensification izingatie utekelezaji wa maeneo yaliyorukwakatika Awamu ya Kwanza na Awamu ya Pili ya utekelezajiwa miradi ya REA;

j) Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini TPDC liwezeshwekupata pesa za kujiendesha na sio kutegemea Fedha kutokaSerikali Kuu ambazo huchelewa na hivyo kuathiri utekelezajiwa miradi mbalimbali ya uendelezaji wa gesi asilia. Aidha,Serikali iangalie namna inavyoweza kutatua changamotoya madeni ya taasisi zake katika shirika hili;

k) Serikali iangalie namna ya kulikwamua Shirika laMadini la Taifa (STAMICO) pamoja na migodi inayosimamiwana shirika hili ili shirika liweze kusimama na kujiendeshakibiashara;

l) Serikali iweke utaratibu mzuri wa ufungaji wa FlowMeters ili iweze kupata takwimu sahihi wakati wa upakuajiwa mafuta;

m) Wakala wa jiolojia nchini iendelee kufanya utafitiambao una tija na kuwafikia wananchi hasa kuhusu elimuza utafiti wa maafa na majanga;

n) Serikali iangalie namna ya kuiwezesha wakala wajiolojia nchini kua ndio mtafiti pekee wa masuala ya madinina kuweza kutoa takwimu zitakazohifadhiwa kwa manufaaya Taifa. Hatua hiyo itapunguza watafiti wengine wa nje yanchi kuja kufanya tafiti kwa muda mrefu bila kutoa takwimuna kuharibu maeneo ya nchi yetu kwa shughuli za uchimbaji;

o) Wachimbaji wa Kati na Wadogo wadogo wapewekipaumbele na Serikali ili waweze kuendeleza sekta ya madinikwa maendeleo ya uchumi wa Taifa letu;

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

168

p) Serikali ilisaidie Shirika la TANESCO kujikwamua namadeni mengi ambayo yanalifanya lishindwe kujiendeshakikamilifu;

q) Bunge lipewe Bajeti ya kutosha ili kuliwezeshakutekeleza makujuku yake ya kikatiba na kikanuni, hasa yakufanya ukaguzi katika miradi mbalimbali inayotekelezwana Serikali ili liweze kuishauri Serikali ipasavyo.

3.2 Mapendekezo

Mheshimiwa Spika, baada ya kuelezea shughulizilizotekelezwa na Kamati, naomba kutoa mapendekezokama ifuatavyo:-

3.2.1 Wakala wa Nishati Vijijini (REA)

a) Hali ya upatikanaji wa Fedha za Miradi ya REA kwa wakati

Kwa kuwa, miradi mingi ya REA imeshindwa kukamilika kwawakati kutokana na kucheleweshwa na kutolewa chini yakiwango kwa fedha zilizokusanywa kutoka kwenye Tozo zaMafuta na kiasi kilichoidhinishwa na Bunge lako;

Na kwa kuwa, hali hiyo imesbabsha ongezeko la gharamaza miradi husika kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemofidia kwa wakandarasi na kupanda kwa thamani ya dolahapa nchini;

Kwa hiyo basi, Bunge linashauri fedha za miradi ya REAzipelekwe kwa wakati na kwa kiwango cha kutosha ili miradiiliyokusudiwa itekelezwe kwa wakati na hivyo kuiepushaSerikali kulipa gharama za fidia kwa wakandarasiinaochelewesha malipo yao.

b) Urukwaji wa maeneo muhimu ya huduma za kijamii katikaMiradi

Kwa kuwa, maeneo mengi ya kijamii na kiuchumi katika vijijina vitongoji vingi yalirukwa wakati wa utekelezaji wa miradi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

169

ya awamu ya kwanza na ya pili ya utekelezaji wa mradi waumeme vijijini,

Na kwa kuwa, hali hiyo ilikwamisha kufikiwa kwa malengoya mradi, kuibua malalamiko kutoka kwa viongozi wamaeneo husika kwa madai ya kutoshirikishwa, pamoja nakusababisha kero kwa wananchi hasa kwenye maeneoyaliyorukwa,

Kwa hiyo basi, Bunge linaishauri Serikali ihakikishe maeneoya kijamii na ya kiuchumi yanapewa kipaumbele katikautekelezaji wa miradi ya awamu ya tatu. Aidha, viongoziwa maeneo ambayo mradi utapita washirikishwe kikamilifu.

c) Utekelezaji wa Miradi ya REA awamu ya tatu

Kwa kuwa, Miradi mingi ya REA iliyotekelezwa katika awamuya kwanza na ya pili ilibainika kukosa usimamizi mzuri,

Na kwa kuwa, hali hiyo ilisababisha miradi hiyo kutekelezwakwa kiwango duni ikiwa ni pamoja na ununuzi wa vifaa namashine humba (Transformer) zisizo na ubora unaokidhiviwango,

Kwa hiyo basi, Bunge linashauri Serikali kuhakikisha kunakuwana usimamizi madhubuti katika utekelezaji wa miradi ya REAawamu ya tatu.

3.2.2 Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO)

Mheshimiwa Spika, kutokana na uchambuzi wa Taarifambalimbali zil izowasilishwa mbele ya Kamati kuhusuTANESCO, Kamati ina mapendekezo yafuatayo:

a) Madeni

Kwa kuwa, Shirika la Ugavi wa Umeme (TANESCO) linakabiliwana madeni mbalimbali kutoka kwa Wazabuni na Serikali nataasisi zake, na madeni hayo yamekuwa yakiongezeka,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

170

Na kwa kuwa, hali hiyo imeifanya TANESCO ishindwekujiendesha na kutekeleza majukumu yake kikamilifu,

Kwa hiyo basi, Bunge linaishauri Serikali kuchukua hatua zaharaka na madhubuti ili kupata ufumbuzi wa madeni hayoili kuiwezesha TANESCO kuepukana na kujiendesha kwahasara.

b) Wateja wengi kutolipa Ankara za umeme kwa wakati

Kwa kuwa, Taarifa za TANESCO zimebainisha kuwepo kwawateja wengi wanaochelewa au kutolipa Ankara za umemekama inavyotakiwa,

Na kwa kuwa, hali hiyo inachangia kupunguza uwezo wakifedha wa TANESCO na hivyo kuathiri utendaji na uendeshajiwa shughuli za Shirika,

Kwa hiyo basi, Bunge linashauri Serikali iingilie kati katikakuhakikisha wadeni wote wa TANESCO (ikiwemo Serikali naTaasisi zake) wanalipa Ankara zao kikamilifu nawatakaoshindwa waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

c) Uharibifu wa Mitambo ya kufua umeme

Kwa kuwa, mitambo mingi ya kufua umeme imekuwaikiharibika na kushindwa kufanya kazi kutokana nakutokufanyiwa matengenezo kwa wakati,

Na kwa kuwa, kuharibika kwa mitambo hiyo mara kwa marahusababisha kukosekana kwa umeme wa uhakika nchinijambo linaloigharimu TANESCO na Taifa kwa ujumla,

Kwa hiyo basi, Bunge linaishauri Serikali kutenga na kupelekafedha za kutosha kwa TANESCO ili kuiwezesha kuifanyiamatengenezo mitambo ya kufua umeme na hivyo kuepushaadha ya ukosefu wa umeme wa uhakika kwa wananchi nahasara kwa Taifa.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

171

d) Uchakavu wa miundombinu ya kusafirishia umeme

Kwa kuwa, uchakavu wa miundombinu ya kusafirishia umemeunachangia kupotea kwa umeme mwingi njiani,

Na kwa kuwa, upotevu huo unaathiri kiasi cha umemekinachowafikia watumiaji, na hivyo kuikosesha mapatoTANESCO na kuathiri uzalishaji katika uchumi wa nchini,

Kwa hiyo basi, Bunge linashauri Serikali kutenga fedha zakutosha ili kuiwezesha TANESCO kufanya matengenezorekebishi (rehabilitation) katika vituo na miundombinu yakusafirishia umeme nchini.

3.2.3 Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)Mheshimwa Spika, kuhusu Shirika la Maendeleo ya PetroliTanzania (TPDC), Kamati ina mapendekezo yafuatayo:

a) Madeni

Kwa kuwa, Shirika linakabiliwa na madeni mbalimbali kutokakwa wadau mbalimbali.

Na kwa kuwa, Shirika pia linaidai Taasisi ya TANESCO ambaondio mlaji/mnunuaji mkubwa wa gesi,

Hivyo basi, Bunge linashauri Serikali kuweka utaratibumahususi wa kumaliza madeni haya ya Taasisi hizi za kiserikali.Aidha, kuangalia namna bora ya kuendelea kupeanahuduma.

b) Uzalishaji wa Gesi nyingi kuliko inavyonunuliwa

Kwa kuwa, TPDC haina uwezo wa kujenga miundombinu yakusambazia gesi inayozalisha na hivyo kushindwa kulifilia sokola watumiaji,

Na kwa kuwa, hali hiyo inasababisha TPDC kushindwa kuuzagesi hiyo na hivyo kukosa mapato yatakayoiwezeshakujiendesha kibiashara kama ilivyo kusudiwa,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

172

Kwa hiyo basi, Bunge linashauri Serikali kuiwezesha TPDCkutekeleza mradi wa kusambaza gesi katika Mkoa wa Dares Salaam, kwa kujenga miundombinu ya kusambaza gesikwa watumiaji.

c) Ufinyu wa bajeti kwa shughuli za TPDC

Kwa kuwa, bajeti inayotengwa na Serikali kwa ajili ya TPDCni ndogo na fedha zake hazipatikani kikamilifu na kwawakat,

Na kwa kuwa, hali hiyo inachangia kuikwamisha TPDC katikautekelezaji wa shughuli zake,

Kwa hiyo basi, Bunge linashauri Serikali kuipatia TPDC bajetiya kutosha na kuiwezesha kutekeleza majukumu yake yamsingi kama inavyotakiwa.

3.2.4 Chuo cha Madini Dodoma (MRI)Kwa kuwa, Chuo cha Madini kinakabiliwa na ukosefu wafedha kutokana na kutotengewa fedha za maendeleo katikabajeti iliyopita,

Na kwa kuwa, hali hiyo inasababisha chuo kushindwakukarabati miundombinu ya mafunzo ili kiweze kuongezaudahili wa wanafunzi katika fani za ufundi mchundo naufundi sanifu katika sekta ya madini,

Kwa hiyo basi, Bunge linashauri Serikali kukiwezesha chuohiki kwa kukitengea bajeti ya kutosha na kukipatia fedhakwa wakati. Aidha Serikali iangalie uwezekano wa kukifanyachuo hiki kishirikiane na taasisi nyingine za kitaaluma ilikuendeleza taaluma hizi adhimu nchini.

3.2.5 Wakala wa Jiolojia nchini (GST)Kwa kuwa, Wakala wa Jiolojia nchini imepewa jukumumuhimu la kukusanya, kuchambua, kutafsiri na kutunzataarifa mbalimbali za kijiosayansi, kwa lengo la kuliwezeshaTaifa kufanya maamuzi sahihi kuhusu matumizi ya ardhi(earth),

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

173

Na kwa kuwa, ufinyu wa bajeti kwa Taasisi hiyo kunachangiakwa kiasi kikubwa kuathiri utekelezaji wa majukumu hayona hivyo kusababisha Taifa kukosa taarifa za msingi kuhusianana jiolojia ya nchi,

Kwa hiyo basi, Bunge linashauri Serikali kuiwezesha kibajetiGST ili itekeleze kwa ufanisi majukumu yake, ambayoyanahusisha pia kufanya tafiti mbalimbali kuhusu majanga(matetemeko ya ardhi, milipuko ya Volkano na maporomokoya ardhi), ili kuiliwezesha Taifa kukabiliana nayo.

3.2.6 Sekta Ndogo ya Mafuta

Mheshimwa Spika, kwenye Sekta ya Mafuta nchini, Kamatiina mapendekezo yafuatayo:

a) Uwezo mdogo wa mita za upokeaji mafuta (flowmeters)

Kwa kuwa, mita za kupokelea mafuta zina uwezo mdogowa kupokea mafuta,

Na kwa kuwa, hali hiyo inasababisha mita hizo zishindwekwenda kwa kasi inayokubalika wakati wa kupakua mafuta,

Hivyo basi, Kamati inashauri Serikali kufanya marekebishokwenye mita za upokeaji mafuta ili ziweze kuendana na kasiya upokeaji mafuta itakayowezesha kushusha tani 1200 kwasaa badala ya tani 400 kama ilivyo sasa.

b) Umuhimu wa Matenki ya Kuhifadhia Mafuta

Kwa kuwa, Serikali haina sehemu moja ya kupakulia mafutayaani Single Storage Terminal, ambayo ingekuwa ndio kitovucha upakuaji wa mafuta,

Na kwa kuwa, kukosekana kwa sehemu hiyo kumesababishakuripotiwa kwa matukio ya hujuma kutoka kwa makampuniya mafuta nchini,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

174

Kwa hiyo basi, Bunge linashauri Serikali kuharakisha utekelezajiwa mpango wa kuwa na sehemu moja ya kupakulia mafutayaani Single Storage Terminal jambo ambalo litaiwezeshaSerikali kuwa na udhibiti wa kutosha katika upakuaji wamafuta.

4.0 HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, napenda kutoa shukrani zangu za dhatikwako Mhe. Job Ndugai, Spika, Mhe. Dkt. Tulia Akson, NaibuSpika na Wenyeviti wote wa Bunge kwa ushirikiano wenukwa Kamati yangu.

Mheshimiwa Spika, napenda kuwashukuru Wajumbe wotewa Kamati ya Nishati na Madini, kwa ushirikiano wao wakatiwa kutekeleza majukumu ya Kamati. Kwa heshima kubwanaomba kuwatambua kwa majina yao kama ifuatavyo:-

1. Mhe. Deogratius Ngalawa, Mb M/Mwenyekiti2. Mhe. Joyce Bitta Sokombi, Mb Mjumbe3. Mhe. Mohamed Juma Khatib, Mb Mjumbe4. Mhe. Bahati Ali Abeid, Mb Mjumbe5. Mhe. Susan limbweni Kiwanga, Mb Mjumbe6. Mhe. Ally Mohamed Keissy, Mb Mjumbe7. Mhe. Vedastus Mathayo Manyinyi, Mb Mjumbe8. Mhe. Yussuf Kaiza Makame, Mb Mjumbe9. Mhe. Katani Ahmad Katani, Mb Mjumbe10. Mhe. Zainab Mussa Bakar, Mb Mjumbe11. Mhe. Haroon Mulla Pirmohamed, Mb Mjumbe12. Mhe. Bupe Nelson Mwakang’ata, Mb Mjumbe13. Mhe. Mwantakaje Haji Juma, Mb Mjumbe14. Mhe. Daimu Iddi Mpakate, Mb Mjumbe15. Mhe. Desderius John Mipata, Mb Mjumbe16. Mhe. Maryam Salum Msabaha, Mb Mjumbe17. Mhe. Catherine Valentine Magige, Mb Mjumbe18. Mhe. Oscar Rwegasira Mukasa, Mb Mjumbe19. Mhe. Kiza Hussein Mayeye, Mb Mjumbe20. Mhe. Dustan Luka Kitandula, Mb Mjumbe21. Mhe. Innocent Lugha Bashungwa, Mb Mjumbe22. Mhe. Wilfred Muganyizi Lwakatare, Mb Mjumbe

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

175

23. Mhe. John Wegesa Heche, Mb Mjumbe24. Mhe. Anne Kilango Malecela, Mb Mjumbe

Pia ninatoa pongezi kwa Wizara ya Nishati na Wizara yaMadini pamoja na Viongozi wake, Waziri wa Nishati Mhe.Dkt. Medard Matogolo Kalemani (Mb), Naibu wake Mhe.Subira Khamis Mgalu, pamoja na Waziri wa Madini, Mhe.Angellah Jasmine Kairuki pamoja na Manaibu Waziri wakeMhe. Stanslaus Haroon Nyongo (Mb), a Mhe. Dotto MashakaBiteko (Mb), na Watendaji wote wa Wizara hizi mpya kwaushirikiano walioutoa katika kipindi hiki, ambao umeiwezeshaKamati kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee napendakumshukuru Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai kwaushirikiano wake kwa Kamati. Pia namshukuru Mkurugenziwa Idara ya Kamati za Bunge, Ndg. Athuman Hussein,Mkurugenzi Msaidizi Ndg. Michael Chikokoto pamoja naMakatibu wa Kamati hii, Ndg. Mwanahamisi Munkunda naNdg. Felister Frank Mgonja kwa kuratibu vyema shughuli zaKamati na kuhakikisha Taarifa hii inakamilika kwa wakati.

Baada ya kusema hayo, sasa naomba Bunge lako Tukufuliipokee na kuijadili Taarifa hii na hatimaye kukubali maonina ushauri wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati naMadini.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

Mhe. Deogratius Ngalawa, MbM/Mwenyekiti

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na MadiniFebruari, 2018

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Naibu Spika,naafiki.

NAIBU SPIKA: Hoja imeungwa mkono, ahsante sanaMheshimiwa Mwenyekiti.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

176

Waheshimiwa Wabunge, tumefika mwisho wamawasilisho sasa tutaanza michango. Nimepata majinakadhaa hapa mbele ya wachangiaji kutoka Chama chaMapinduzi, Chama cha Demokrasia na Maendeleo naChama cha Wananchi (CUF). Sasa majina kidogo yamezidikwenye uwiano, kwa hiyo muda ambao WaheshimiwaWabunge mtapangiwa kuchangia tutakuwa tukiangaliatunao muda kiasi gani. Tutaanza na Mheshimiwa CharlesKitwanga, atafuatiwa na Mheshimiwa Maryam Msabaha.

Nimekumbushwa hapa na Katibu, wachangiajidakika 10.

MHE. CHARLES M. KITWANGA: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Vilevilenimshukuru Mwenyezi Mungu kwa jinsi ambavyo amekuwamwema pamoja na matatizo niliyopa sasa ni mzima kabisa.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu wa Spika, nianze kwanza kwakuipongeza sana Serikali kwa uamuzi wake wa kuhakikishakwamba inajenga miundombinu itakayowezesha uchumiwetu kupaa. Serikali imejikita katika kuhakikisha kwambatunakuwa na reli, tunakuwa na viwanja vya ndege,tunakuwa na barabara na tunakuwa na mashirika ambayoyanaweza kweli kweli kuonekana kwamba ni mashirikaambayo yana nia ya kuonesha kwamba tunajenga uchumiwa viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, na kikubwa ambachonikiseme ni jinsi ambavyo Serikali imeweka kipaumbelekuhakikisha kwamba inatumia fedha zake za ndani. Hilinilisisitize kwa sababu kuna watu hapa wanasema kwambakukopa si fedha za ndani. Hicho ni chanzo kingine katikakuhakikisha kwamba unajipatia pesa katika Serikali yako.Aidha, unaweza ukakusanya ushuru, unakusanya pesa nakupata revenue. Vilevile unaweza ukakopa ukapata hizo pesana baadaye utalipa kwa kutumia pesa zako za ndani. Kwahivyo kukopa ni pesa zako za ndani.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

177

Mheshimiwa Naibu wa Spika, pamoja na pongezi hizoniangalie tu namna ambavyo tunaweza tukahakikishakwamba uchumi wetu unapaa kwa haraka sana. La kwanzani linkages. Tunapojenga reli, tunapopanua bandari ni lazimatuangalie ni kwa namna gani hiyo bandari itawezakuharakisha uchumi wetu. Huwezi kuwa na bandari iliyo nzurihalafu mizigo inafika huna mahala pa kuiweka. Kwa hiyo,dry ports ziwekewe umuhimu unaolingana na jinsi ambavyotunapanua bandari zetu, ikiwemo dry port ya pale Fela katikaJimbo la Misungwi.

Mheshimiwa Naibu wa Spika, vilevile niipongezeSerikali kwa kuweka umuhimu wa pekee katika kuhakikishakwamba Shirika letu la Simu la TTCL l inaimarishwa.Nizungumzie umuhimu uliopo kwa Shirika la TTCL na tuangalieni kwa namna gani Serikali iliangalie shirika hili kwa umuhimuwa kipekee.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo hii tukiingia vitani Airtelwakaondoka, Vodacom wakaondoka na mashirika ya binafsiyakaondoka tutawasiliana vipi? Ni vyema tukaona huuumuhimu na tukaweka nguvu sahihi ya kuhakikisha kwambaShirika letu la Simu la TTCL linapewa kila msaada na isiwemsaada tu wa pesa au vifaa kwa sababu matatizo mengineyanatokana na namna ya uendeshaji, na hili nitajaribukulizungumzia na nitoa ushauri kwa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu wa Spika, ushauri wa kwanza nikuhusu usimamizi na katika kusimamia niombe Serikaliiangalie uwezekano wa kuwa na mfumo wa eyes on handsoff. Serikali isiingilie ingilie haya mashirika hasa hasa yaleambayo Serikali imeya-own kwa asilimia kikubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, sioni kwa nini kama Serikaliimejenga ikaweka bodi imara na bodi yenyewe ikaajiriMkurugenzi au Mtendaji Mkuu imara, na kukawa na mfumomzuri wa mawasiliano kila siku Katibu Mkuu au Waziri aendekuweka mkono wake kwenye shirika hilo. Yeye Waziri, KatibuMkuu na Wizara mama ihangaike na kuhakikisha kwambatuna sera zilizo sahihi na hizo sera zinajengewa mfumo wa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

178

utekelezaji na hao wajumbe wa Bodi pamoja na menejimentiyake kuweza kutekeleza ile sera ambayo Serikali ingependaitekelezwe.

Mheshimiwa Naibu wa Spika, vilevile kujengwemahusiano mazuri ya mawasiliano. Sioni kwa nini kamamenejimenti wanakaa kila wiki kwa vyovyote vilewataitaarifu bodi kinachoendelea labda kila quarter, lakiniBodi nayo iwajibike kumweleza Waziri na Katibu Mkuu ninikinachoendelea kwenye shirika hilo angalau kwa mudaambao watakuwa wamejipangia. Hapo kila mtu atakuwaametekeleza wajibu wake yake bila kumwingilia mwingine.Tunaangalie vilevile nilikuwa nakizungumzi issue ya linkage,hii ni kitu muhimu sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa unakuta tunahangaikakutengeneza reli, reli inapokuwa inajengwa kutoka Dar essalaam kuja Morogoro unaweka reli ya umeme. UkishafikaMorogoro kuja Dodoma kwanza tofauti ile standard gaugena ile reli iliyopo zinatofautiana. Sijui unaanza kupakua hiyomizigo uweke kwenye ile reli nyingine ile ya zamani na vichwavile vya … Mimi nadhani kuwe na mpango ambao unakuwani wa jumla utachukua muda, lakini mnakuwa na umuhimuwa kusema kwamba tutajenga reli kutoka Dar es Salaammpaka Kigoma, tutajenga reli kutoka Dar es Salaan mpakaMwanza.

Mheshimiwa Naibu wa Spika, kitakachokuwepo paleni kwamba kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoroitachukua muda huu; na kutoka Morogoro kwenda Dodomaitachukua muda huu na Dodoma kwenda Mwanza aukwenda Kigoma itachukua muda huu. Na katika muda huolazima kuwe na mipango thabiti ambayo tunasemakwamba hiyo ni transition period ambayo itakuwainaeleweka kwa wafanyabiashara na watu wenye viwandanchini ambapo watakuwa na matarajio yanayoeleweka, namipango hii ifuatwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, maana kwanzanimeipongeza Serikali kwa namna ya kutafuta revenue.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

179

Hakuna sababu ya kuanza kujenga nusu nusu wakati hujuikinachofuatia na huna mpango wa kupata hela. Ni vyemaukawa umejipanga kwamba nikitoka Dar es Salaam kufikaMorogoro nitakuwa nimepata hela za kutoka Morogorokwenda Dodoma na nikianza kujenga kutoka Morogorokwenda Dodoma nitakuwa nimepata hela za kutokaDodoma kwenda Tabora. Tusiwe na mipango ya zima moto.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nisisitize hili la usimamizi wataasisi na ili watu wengi hatuliwekei umuhimu na hatujuimadhara yake. Sielewi kwa nini kwa mfano TCRA ambayoni shirika ambalo kwa vyovyote vile kulingana na sources zafunding yake lazima litajitegemea. Kwa hiyo, palekinachotakiwa ni kuwa na bodi ambayo ni imara yenye watuwenye kuwaza mawazo mapana. Yale yaliyoko kwenyeutaratibu au kwenye sheria TCRA hayo ni ya kawaida, mtuyeyote anaweza akayafanya.

Mheshimiwa Naibu Spika, these people should thinkbeyond that na tunahitaji watu wanaoweza ku-think beyondthat, na hicho ndicho kinatupa tatizo. Watanzania wengitunajaribu kuwaza leo nitakula nini na jioni nitakula nini.Tukitaka kuendelea ni lazima tuwaze leo tutakula nini, keshokuna nini, kesho kutwa chakula kitapatikana wapi na wikiijayo nini tufanye. Haya mawazo ya kuwaza leo hii, halafukesho hujui, kesho inapofika ndipo unaanza kuwaza,tuondokane nayo.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

MHE. CHARLES M. KITWANGA: Kengele hiyo? Ni yakwanza? (Kicheko)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Kitwanga ahsante sanakwa mchango wako, umeshamaliza muda wako, ahsantesana. Mheshimiwa Maryam Msabaha atafuatiwa naMheshimiwa Innocent Bashungwa, dakika chache kamazitabaki tutamalizia na Mheshimiwa George Malima Lubeleje.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

180

MHE. MARYAM SALUM MSABAHA: Ahsante sanaMheshimiwa Naibu Spika, nami kwa kunipatia fursa hii niwezekutoa nami maoni yangu, nami pia ni mjumbe wa Kamati,mengi tumeshayachangia kwenye Kamati; na yale mazuripia tuliyoishauri Wizara na Serikali pia wayachukue kwamustakabari wa Wizara ya Nishati na Madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeona haya mamboyanavyokwenda katika hii Wizara na hii Wizara haijawahikumuacha mtu salama. Tumeona migogoro mingi ambayoimetokea kwenye hii Wizara ya Nishati na Madini, mpakaMheshimiwa Rais akachukua jukumu la kutenganisha hiziWizara zikawa Wizara mbili.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kuna mambombalimbali ambayo yamefanyika kwenye Kamati hizi.Tumeona yale masuala ya makinikia, mambo ya michangayalivyokwenda, sasa Watanzania wengi bado wanahoji piawanataka angalau wapate taarifa kile ambacho tulikuwatunakidai kiko wapi na ni kitu gani tulichonufaika nachompaka sasa hivi. Si vibaya sana tukitoa taarifa tukawaambiaWatanzania kama kipindi kile tulivyokuwa tumewashirikishanamna tulivyokuwa tunaibiwa kwenye masuala ya migodi.Kwa hiyo, niiombe Serikali na Wizara itoe taarifa ili wananchiwajue ni kiasi gani tulichokipata mpaka kwa sasa hivi kwasuala lile la mchanga. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna hili suala la wachimbajiwadogo wadogo; hawa wachimbaji wadogo wadogohuwa kuna wachimbaji ambao wanapatiwa ruzuku naSerikali. Lakini umeangalia katika suala letu la taarifailivyotoka umeona ni namna gani ni wachimbaji wachachesana ambao wamepata ruzuku ya Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, niishauri sana Serikali naBunge lako Tukufu kuhusu hii Serikali ya wachimbaji wadogowadogo, tuangalie humu ndani kwa kina hizi pesazimekwenda wapi, huku tukianza kuangalia tukichimbuakwa kina kuna vitu vingi sana vimefichika huku kwawachimbaji juu ya hizi ruzuku zilizotolewa kwa Serikali kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

181

ajili ya kuwafikia wachimbaji wadogo wadogo. Umeona ninamna gani wamepata wale wachimbaji, waliopata niwatatu. Sasa tuangalie zile pesa ambazo zil ikuwazimetengwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo wadogo hizifedha zimekwenda wapi? Na kama zimeishia kwenye mifukoya watu au kama watu wamepiga deal basi naomba hayamasuala yafuatiliwe kwa kina zaidi ili tuzidi kugundua huuuozo ambao uko kwenye Kamati ya Madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu GST, hawa niwataalam na endapo tungekuwa tumewatumia vizuri hatahawa wawekezaji wanaokuja kwa kweli wasingewezakuvamia maeneo kabla hawajapata utafiti.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tuangalie hii bajetiambayo tunaitenga katika hii Wizara, hizi taasisi zinafikiwaau zinapelekwa kwa wakati? Sasa kama vitu kama hivi hawaGST hawawezeshwi kwa wakati, sasa tuangalie ni namnagani hii Wizara tuwawezeshe hawa GST kabla wachimbajihawajaenda kuvamia maeneo wafanye kama utafiti kamakweli huko wanakoenda kuchimba kuna madini auwanaenda kufanya uharibifu wa mazingira. Hata kamawawekezaji wamekuja hawa wafanye kwanza utafiti wakutosha na waangalie pale kuna madini kiasi gani iliwaruhusu wawekezaji sasa nao wachimbe yale madini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuangalie wataalam ninamna gani Serikali sasa mnaweza kuwapa kipaumbele ilituangalie tunadhibiti haya madini tunayosema tumeibiwakwa siku nyingi yawanufaishe Watanzania kwa ujumla.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna mambo mengi sanakuhusiana na masuala ya REA. Niipongeze Serikali kwa hayamasuala ya REA, lakini bado kijijini kuna tatizo sugu sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, umeme unapotolewautakuta wale wafanyabiashara au mtu ana shule yake, aumtua ana uwezo, basi wanaruka vijiji vya wale watu ambaohawana uwezo. Niombe hao watu wakusanywe kwapamoja umeme kama unapita usibague huyu ana uwezo,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

182

huyu hana uwezo, ili wapate wote kwa wakati muhafakahayo yanatotakiwa kwenye umeme wa REA.

Mheshimiwa Naibu Spika, tuje kwenye madeni yaTANESCO. Hili Shirika limekuwa likijiendesha sana kwa hasara,kama ulivyoona tulivyotoa maoni yetu kwenye Kamati yetu.Tuangalie na hawa wadaiwa sugu wanachukuliwa hatuagani na Serikali ili wapate kulipa. Hata kama ni taasisi zaSerikali basi tuhakikishe ni namna gani wanarejesha hayamadeni TANESCO ili TANESCO iweze kujiendesha.

Mheshimiwa Naibu Spika, hii Kamati yetutumechambua mambo mengi mazuri yaliyoongelewa humukwenye Kamati, naomba yachukuliwe, lakini sana sana pianiende kwenye suala la barabara. Kuna barabara hiziambazo tumekuwa tukizi jenga, lakini barabara hizitunazijenga kwa gharama kubwa halafu zinaharibika kwamuda mchache. Sasa niulize Serikali hawa wakandarasiwanaohusika na hizi barabara wanachukuliwa hatua ganiendapo zile barabara zinaharibika kwa kipindi ambacho nicha… na watoe guarantee kama hizi barabarawanazozijenga zitachukua muda gani, na zikiharibika kablaile guarantee haijaisha basi wachukuliwe hatua.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia tuangalie suala labandari. Tuangalie bandari hizi bandari bubu ambazo nitatizo, kuna vitu vingi sana vinapita kwenye bandari bubu.Sasa tunazidhibiti vipi hizi bandari bubu ili tuache kupitisha,ziache kupitisha mizigo, vitu vya haramu na mambo mengineili wale ambao wanakwepa kodi nao wadhibitiwe ili zile kodizirudi Serikalini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na suala Bandariya Dar es Salaam kwenda Zanzibar bado kuna malalamikosana kwa wafanyabiashara ambao wanatoka Zanzibar.Kumekuwa na changamoto kubwa sana kwenye suala hilila wafanyabiashara wa Zanzibar. Unakuta umelipia mzigowako Zanzibar, ule mzigo ukifika tena pale bandariniunakuwa-charged ushuru. Unakuta umetoka na kiporo(mfuko) chako kidogo, labda ni kiporo cha mchele au vitu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

183

vyako vidogo vidogo umenunua unapeleka Zanzibar, kwahiyo ukifika pale unachajiwa ushuru. Sasa tuangalie ni namnagani ili suala la Muungano kuhusu masuala ya bandari ninamna gani sasa tuliweke ili pande zote mbili zinufaike,upande wa Zanzibar wasilalamike na upande wa TanzaniaBara usilalamike. Tusiwe kule tumeshalipa kodi wakija tenahuku wanalipa kodi.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda waMzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa MaryamMsabaha, Mheshimiwa Innocent Bashungwa.

MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kutoamchango wangu. Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungukwa kunijalia afya njema nikaweza kusimama mbele ya Bungelako Tukufu kutoa mchango huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze na suala la REA, nakatika hili suala la REA nianze kwa kuipongeza Serikali. KupitiaREA Serikali inafanya kazi nzuri ya kuwapelekea vijijini hudumahii muhimu katika maendeleo ya Watanzania. Pamoja najitihada nzuri za kupeleka umeme vijij ini kupitia REA,changamoto za REA ukiziangalia kwa kwa undanizinasababishwa na mambo makubwa mawili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la kwanza, miminipo kwenye Kamati ya Nishati na Madini, tumekuwatukiishauri Serikali zile tozo za kutoka kwenye mafuta kwendakwenye mfuko wa REA zimekuwa ring-fenced lakinikumekuwa kuna mkwamo, ile hela haiendi moja kwa mojakwenye mfuko ili iweze kwenda kwenye REA kuhudumiausambazaji wa umeme vijijini.

Kwa hiyo, nipende kuiomba Serikali wakatiwanafanya wind up tusikie upande wa Serikali ni lini hiiautomation ya transfer ya hela, kwa sababu mwananchiakienda kununua mafuta kwenye sheli (Shell/Petrol Station)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

184

ile tozo inatozwa pale pale analipa cash, sasa kwaninikunakuwa kuna mkwamo? Kwa nini hii hela isiende mojakwa moja kwenye mfuko wa REA ili wakala wa REA wawezekusambaza umeme vijijini bila kusuasua? Pia kwenye REAhapo hapo kwa upande wa TANESCO ukiangalia TANESCOna REA wanavyofanya kazi ni sawa na treni ambayo inamabehewa mengi lakini ina kichwa cha treni ambachouwezo wa engine yake ni mdogo sana.

Mheshimiwa MNaibu Spika, kichwa cha engine niupande wa TANESCO; TANESCO ina madeni makubwaimefika kwenye point ambapo inaweza ika-collapse kwasababu inadaiwa na inashindwa kutoa huduma ya umemenchini kwa sababu ya madeni makubwa zile cost zamaintenance zimekuwa accumulative. Kwa hiyo, ile speedya REA kusambaza umeme vijijini inakwamishwa na TANESCOkushindwa kufanya majukumu yake kwa sababu haina pesa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nipendekeze Serikali ifikemahali idara zile za REA ambazo zinahusika na kusambazaumeme vijijini tuvi-merge na REA ili ule ufanisi wa REA zileidara ambazo zipo upande wa TANESCO ambazo zinahusikana huduma za umeme vijijini viwe-merged kwenye REA iliREA iendelee kufanya kazi vizuri kama inavyofanya; halafuTANESCO inayobaki iendelee kutoa huduma ya umememaeneo ya mjini. Tukifanya hivyo wananchi wetu vijijiniwatapata umeme vizuri bila kusua sua na upande wa mijiniTANESCO itajikita kutoa umeme mjini. Hii itatupeleka kwenyedhamira ya kwenda kwenye uchumi wa viwanda na kwendakwenye uchumi wa kati. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili ambaloningependa kulizungumza ni miradi mikubwa ambayoWatanzania wanaisubiri kwa hamu kubwa sana yakutufikisha kwenye uchumi wa viwanda. Miradi hii ni pamojana Mradi wa Stigler’s Gauge ambao ni mradi mkubwa sana.Ninamshukuru Rais Magufuli na Serikali ya Awamu ya Tanokwa kulisimamia hili. Mradi wa Standard Gauge Railway nimradi mkubwa sana, Tanzania itakuwa kama Ulaya miradihii ikitekelezwa. Hata hivyo sisi Bunge tunatakiwa tuwe

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

185

sehemu ya kui-facilitate Serikali iweze kutekeleza miradi hiikwa kasi ya haraka sana kwa sababu Watanzania wanasubirimiradi hii kwa hamu kubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nipende kupendekezakwa mikopo ya nje ambayo inaweza ikawezesha Serikalikutekeleza miradi hii. Ifike mahali tuangalie mechanism yaBunge ya kuwa na oversight kwa Serikali lakini bilakuikwamisha Serikali katika kuwa na wigo wa kwendakukopa mikopo ya bei nafuu. Wakati tunajadili Kamati yabajeti hapa kulikuwa kuna hoja kwamba kwa nini Serikaliimekopa additional ya shilingi bilioni 1.46 kabla ya kujaBungeni.

Sasa nipende kupendekeza kwamba Serikali mje namechanism ambayo itatufanya sisi ile checks and balanceyakuisimamia Serikali inakuwepo. Lakini Serikali badomnakuwa na freedom pale fursa inapojitokeza ya kukaa nahizi Development Financial Institutions, kukaa na walewanaoweza kutupa mikopo ya bei nafuu kwa ajili ya miradiya bei nafuu kama Stigler’s Gauge na SGR muweze kufanyahivyo kwa sababu hakuna Serikali ambayo inadhamira yanjema na Watanzania kama Serikali ya Awamu ya Tano. Sasakwanini tuwe sehemu ya kikwazo badala ya kui-facilitate iliiweze kutoa maendeleo ambayo tumewaahidi Watanzaniakwa kasi ambayo Serikali inataka twende. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nichangie kuhusu upandewa sekta ya madini hasa hasa wachimbaji wa kati nawadogo. Kwa miaka mingi tumeona watu wanaochukuahizi Special Mining Licenses, tumehangaika nao, lakini kwasababu ya uchanga wa sekta na taasisi zetu kuendeleakuzijengea uwezo tumekuwa na changamoto kubwa sanaya kupata fair share ya tax collection.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nipendekupendekeza kwamba Serikali ifike mahali jitihada zotetuzipeleke kwenye hawa wachimbaji wa kati ambaotukiweza kuwa-facilitate wataweza kutengeneza ajira humuhumu nchini na pia yale mapato ambayo wanayapata

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

186

yatawekezwa hapa hapa Tanzania, badala ya kuendeleakuangaika na ku-facilitate wawekezaji wakubwa waKimataifa ambao wanafanya tax planning, madini yetuyanaenda kodi hatuzioni, wanatuachia mapango tu kwenyenchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naamini Serikali kwa sababuipo katika ku-reform il i kuhakikisha resources za nchizinawanufaisha Watanzania jambo hili nadhani limefikamahali pake. Tumetembea kwenye mikoa ambayoinachimba dhahabu wachimbaji wa kati wana uwezomkubwa sana. Teknolojia za dunia sasa hivi zinaweza zikawaadopted na hawa wachimbaji wa kati wakawezakuisimamima migodi vizuri lakini pia wakaajiri Watanzaniana mapato wanayopata yanabaki hapa hapa nchini.

Kaka yangu Mheshimiwa Lubeleje ameniomba dakikachache nimuachie kwa hiyo naomba niishie hapo iliMheshimiwa Lubeleje kaka yangu uweze kutumia hizo dakika.Nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana, Mheshimiwa GeorgeMalima Lubeleje

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Naibu Spikanakushukuru sana kwa kunipa nafasi, na nimshukuru sanaMheshimiwa Mbunge kwa kunipa hizi dakika tano. (Makofi)

Kwanza kabisa nizungumzie REA. REA awamu yakwanza, REA awamu ya pili usimamizi wake haukua mzurindiyo maana miradi mingi ilikwama. Kwa mfano kuna vijijivya Tambi, Nambori, kijiji cha Saa Zima, kijiji cha Igoji Mojana Igoji Mbili, tayari nguzo zipo na nyaya zipo lakinitransformer hakuna. Kwa hiyo nilikuwa naomba sana katikaREA hii ya awamu ya tatu waweke transformer ili wananchiwaweze kupata huduma.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine, kuna vijijiambavyo havijafikiriwa kabisa kupata umeme. Kijiji chaKiboriani, Ngaramilo, Mkanana, Chamanda pamoja na

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

187

Iwondo hazijapelekwa nguzo wala nyaya. Kwa hiyo naombasana hii REA awamu ya tatu wawakumbuke basi wapateumeme.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la tatu, kukatikakatika kwa umeme Mji wa Mpwapwa na maeneo mengineimekuwa ni kero kubwa sana, kila wakati kwa siku umemeunaweza kukatika mara mbili/tatu. Sasa kwanza unawezakupata hasara ukaunguza vitu kwenye fridge, lakini pili kwasababu wananchi wanalipa bill kwa hiyo lazima huduma yaumeme iwe nzuri. Sasa kisingizio cha TANESCO kwamba kwasababu ya mvua na kuna baadhi ya nguzo zipo kwenyemabwawa, nguzo zingine zimeoza.

Mimi nashauri wabadilishe nguzo zote zile ambazozimeoza. Kama inawezekana nguzo ziwekwe za chumaambazo haziwezi kuoza, haziwezi kuliwa na mchwa hiiinaweza kusaidia sana ili wananchi waweze kupata hudumaya umeme Wilaya ya Mpwapwa na Mkoa wa Dodoma kwaujumla. Kwa hiyo ya kwangu yalikuwa ni hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwakunipa nafasi, ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Lubeleje.

Waheshimiwa Wabunge, nitasoma majina yawachangiaji wetu wa mchana kabla hatujaendelea,Mheshimiwa Dunstan Kitandula, Mheshimwa Anna KilangoMalecela, Mheshimiwa Hawa Ghasia, Mheshimiwa BonifaceGetere Mwita, Mheshimiwa Dkt. Rashid Chuachua,Mheshimiwa Menrad Kigola, Mheshimiwa John Heche,Mheshimiwa Marwa Ryoba, Mheshimiwa Zuberi Kuchauka naMheshimiwa Kiza Mayeye.

Waheshimiwa Wabunge, hao ndiyo watakuwawachangiaji wetu wa mchana, baada ya kusema hayonasitisha shughuli za Bunge mpaka saa 11:00 jioni leo.

(Saa 7.00 Mchana Bunge lilisitishwa hadi saa 11:00 Jioni)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

188

(Saa 11.00 Jioni Bunge lilirudia)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa tukae.

Waheshimiwa Wabunge, tutaendelea nawachangiaji wetu ambao nilikuwa nimewataja asubuhikabla hatujatoka na tutaanza na Mheshimiwa DustanKitandula, atafuatiwa na Mheshimiwa Zuberi Kuchauka,Mheshimiwa John Heche ajiandae.

MHE. DUNSTAN L. KITANDULA: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru kwa kunipa fursa hii ili nami niwezekuchangia kwenye hotuba mbili hizi za Kamati; Kamati yaMiundombinu lakini vilevile Kamati ya Nishati na Madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa ya Kamati yaMiundombinu imesisitiza umuhimu wa kuimarisha barabarazetu. Katika ule ukurasa wa 37, anazungumzia umuhimu wakuunganisha makao makuu ya mikoa kwa mikoa. Vilevilekatika ukurasa wa 38, naomba kunukuu kipengele (d),anasema, kuendelea na ujenzi wa barabara za lami hasamaeneo yanayochochea uchumi wa Taifa letu kama vilemaeneo yenye vivutio vya utalii, kilimo, viwanda na madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika eneo hili, napendaniikumbushe Serikali, imekuwa ikitoa ahadi nyingi kwabarabara za namna hii hasa katika Mkoa wa Tanga naupande kwa Kilimanjaro. Ipo barabara inayounganisha Mkoawa Tanga na Kilimanjaro lakini ni barabara ya kimkakatimaana inapita kwenye maeneo muhimu ya ukuzaji wauchumi, utalii na viwanda. Ni barabara kutoka Tanga –Mabokweni – Maramba - Mtoni Bombo - Mlalo - Same.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo hili kwanza linagusausalama wa nchi yetu, maana ni eneo la mpakani lakinivilevile kiutalii ni eneo ambalo ukitokea ukanda wa Tangampaka kule Same unazungumzia kuunganisha utalii kutokaMombasa, Saadani na Mbunga ya Mkomazi ambayo inaanziaupande wa Mkinga inakuja mpaka Mlalo, inakuja mpakaSame tunaelekea Kilimanjaro na maeneo ya namna hiyo.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

189

Kwa hiyo, rai yangu, barabara hii imekuwa ikipewa ahadikwa muda mrefu, ni wakati sasa upembuzi yakinifu ufanyikebarabara hii iwekewe utaratibu wa kuwekewa lami. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nikitoka kwenye taarifa yaKamati hiyo, sasa nizungumzie taarifa ya Kamati ya Nishati.Nataka niipongeze Serikali kwa kazi kubwa inayofanya kwakupeleka umeme vijijini kupitia mradi wa REA. Tulipoanza naREA I tulifanya makosa lakini ilikuwa ni sawasawa tufanyemakosa kwa sababu tulikuwa tunajifunza. Tumekwenda REAII hali kadhalika tumefanya makosa, yapo tuliyorekebishalakini bado kuna makosa tumefanya katika usimamizi wamiradi ile.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tumeingia REA III,hatuna nafasi ya kufanya makosa kwa sababu tulishapatafursa ya kufanya majaribio na ku-test jinsi yakwenda.Tunakwenda kwenye REA III tumekubaliana kwamba kila kijijikitakachoguswa tuhakikishe hakuna kitongoji kinaachwa.Naisihi sana Serikali tusije tukarudia makosa ya REA I na REA IIya kuacha baadhi ya vitongoji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nasema hivi kwa sababuzipo changamoto tumeanza kuziona. Kule Jimboni kwangukwenye maeneo ya Kidiboni, Kitongoji cha Chakachanikimesahaulika. Ninayo ahadi kwamba kitafanyiwa kazinaiomba Serikali ilikumbuke hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tulipofanya REA I tuliachabaadhi ya sekondari, Sekondari za Reanzoni, Duga naKigongoi. Tunapokwenda sasa kwenye REA III kwa sababusekondari hizi zipo jirani na maeneo haya basi tuhakikishetunaziingiza kwenye mpango ili ziweze kupatiwa umeme.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine natakakuzungumzia deni la TANESCO. Ukienda ukurasa wa 23,Kamati inasema, madeni ya TANESCO yanasababishakuzorota kwa utendaji wa shirika. Aidha, madeniyameendelea kuongezeka na hakuna jitihada zozote zaSerikali za kusaidia kumalizika madeni haya.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

190

Mheshimiwa Naibu Spika, hii siyo hali nzuri, TANESCOina madeni makubwa. Ukienda kwenye ukurasa uleinaonesha kwamba deni la TANESCO limefikia bilioni 913 nakatika hizo takribani bilioni 200 ni madeni yanayotokana nataasisi za Serikali. Naisihi sana Serikali ije na mkakati maalumwa kuhakikisha deni hili la TANESCO linalipwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye Kamati tuliwahikuletewa taarifa kwamba Serikali ina mpango wa kukopafedha Benki ya Dunia ili tulipe madeni haya. Naisihi sanaSerikali yangu isiende kukopa Benki ya Dunia ili tulipe madenihaya, tutafute njia nyingine za kulipa madeni haya. WenzetuAfrika Kusini wana mzigo mkubwa sana kutokana na ESKOMinashindwa sasa kufanya kazi, inakuwa mzigo hata kwa nchizinazopata umeme kutokana na Shirika la Umeme la SouthAfrica. Tusije tukaingia kwenye mtego huo wa kusababishatukapata umeme kutoka Afrika Kusini ambao bei yake ni ghali.Tuisaidie TANESCO iweze kutupatia umeme kwa bei ya chini.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nawaomba tujifunze kwawenzetu wa Ghana. Wenzetu Ghana waliamua kuanzishaenergy bond na katika kufanya hivyo wameweza kukusanyadola milioni 750 ambazo zinaelekezwa katika sekta yaumeme. Kama tunataka kuisaidia TANESCO tuangalie optionhii, tujifunze wenzetu walifanya nini, tuone kama tunawezakuleta energy bond, wananchi wanunue bond hizo na tuwezekusaidia Shirika letu la TANESCO liondokane na mzigo wamadeni.

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo lingine natakakuipongeza sana Serikali kwa uamuzi wake thabiti wakuamua kuja na Mradi wa Umeme wa Mto Rufiji, ni hatuakubwa ya kimapinduzi, tumechelewa. Wenzetu Ethiopiawameamua kuwa energy hub saa hizi wanazungumziakuzalisha megawatt 10,000 kutokana na chanzo cha Mto Nile.Sisi tutumie mto huu vizuri kuwekeza ili tuweze kupataumeme wa uhakika ili ndoto yetu ya kuwa na uchumi waviwanda iweze kutimia. (Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

191

Mheshimiwa Naibu Spika, nafahamu tuko katikahatua za mwanzo ambazo utekelezaji utaanza hivi karibuni.Naipongeza Serikali kwa kuanza utekelezaji huu kwa kutumiabajeti za Wizara mbalimbali ili hatua za mwanzo ziwezekutekelezwa. Rai yangu, Bunge hili lishirikishwe ipasavyo,Wabunge wa Bunge hili wapate semina ya nguvu ili kujengauelewa wa pamoja ili tutakapokuja kuleta bajeti ya mradihuu iweze kupita kwa urahisi tukiwa kitu kimoja, tukiwatunaelewana kwamba jambo hili ni jambo la kitaifa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,nakushukuru sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Tunaendelea naMheshimiwa Zuberi Kuchauka atafuatiwa na MheshimiwaJohn Heche na Mheshimiwa Marwa Ryoba ajiandae.

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi jioni hii ya leo ili nami niwezekuchangia Kamati hizi mbili. Awali ya yote nizipongezeKamati zote mbili kwa uwasilishaji wa umakini kabisa na kazinzuri iliyofanywa na Kamati hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, naomba nielekezeushauri kwa Serikali. Serikali ya Awamu ya Tano au Serikali yaChama cha Mapinduzi hebu tupunguze umakiniunaotupelekea kutokuwa makini. Kwa mfano, mradi huu wareli ya standard gauge tumesaini mwaka mmoja na Kenya,Kenya wamemaliza lakini sisi kwa sababu ya umakinitumechelewa mpaka leo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Bandari ya Dar es Salaamyuko mwekezaji pale alileta ombi lake la kujenga grainterminal miaka kumi na moja (11) imekwisha mpaka leohaijajengwa amekwenda Msumbiji amepewa miaka miwiligrain terminal inafanya kazi. Tanzania tuko makini mno,huu umakini ndiyo unaotupozea muda na kuonekana tukonyuma. Naomba hilo mlichukue kama ni changamoto.(Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

192

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa niende kwenye hotubaza Kamati mbalimbali. Kamati zote ambazo zimeshawasilishahapa taarifa zake, tatizo hili la upatikanaji wa fedha kilaKamati lazima iguse. Tunalo tatizo kwenye Serikali ya Chamacha Mapinduzi ya utoaji wa pesa, pamoja na kwambatulipopitisha bajeti Wizara nyingi zilikuwa zinalalamikiwakwamba pesa hazitoshi lakini hata zile kidogo zilizotengwabado haziendi kwa wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo hili l imekuwalikigharimu sana miradi yetu ya maendeleo kukwama. Miradimingi hapa ambayo leo hii haijatekelezwa tatizo kubwa niupatikanaji wa pesa. Sasa hatuelewi tatizo hili ni nini na dawayake ni nini, ni tatizo sugu kwa mimi ninavyoliona.

Mheshimiwa Naibu Spika, ufanisi wa bandari hasanikianzia na bandari yetu ya Dar es Salaam. Kabla sijaingiakwenye Bunge hili Gati namba saba, moja na mengine tangumwaka 2008 linatajwa mpaka leo lipo kwenye vitabu tu.Mnaendelea kutuchafulia makaratasi tu Gati namba tatu ,namba nne hatuelewi nini kinachoendelea. Tunawaombenisana sana wote sisi tuna uchungu na nchi hii hebu tufanyekazi tuache kufanya kazi kwa mazoea.

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa viwanja vyandege. Nashukuru Serikali imetuletea takwimu hapa, viwanjavingi vinaonekana vinataka kufanyiwa ukarabati, lakini hivikweli tunajenga hivi viwanja hivi kwa mikakati ya kiuchumiau kukidhi matakwa ya kisiasa? Kwa sababu mimi kamaungeniuliza mikakati ya kiuchumi ningekutajia viwanja kamacha Mtwara, Kigoma, Songwe - Mbeya na hicho cha Mwanzaambacho mmekikazania.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo kubwa zaidi hatunavipaumbele, tuna viwanja hapa tumeviandika lukuki lakinimwisho wa mwaka vyote hivi hakuna kilichokwenda. Hivikwa nini hatuwezi kuamua tu mwaka huu tunashughulikana kiwanja namba A, mwaka mwingine namba B ili twendekuliko kurundika viwanja vya ndege lukuki ambavyo vyotehivi mwisho wa siku hatuwezi kuvifanyia kazi. (Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

193

Mheshimiwa Naibu Spika, Bodi ya Wakandarasi kwamujibu wa sheria ndiyo mlezi wa wakandarasi lakini hivi kwelibodi hii inalea wakandarasi hasa hawa wazawa,tunawajengea uwezo kiasi gani? Mikakati ya kuwajengeauwezo wakandarasi hawa wadogo tunayo, mbonahaieleweki? Mimi naiomba Serikali ya Chama cha Mapinduzisisi wote nchi hii ni ya kwetu, wote ni wazalendo na hayatunayashauri kwa uzalendo mkubwa sana, naombamyachukue. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye Kamati pametajwasera ya kuunganisha mikoa yetu kwa barabara, mikoakadhaa imetajwa, lakini nisikitike tu Mwenyekiti wangualisahau tu, Mkoa wa Lindi na Morogoro hajautaja. Lindi naMorogoro unaunganishwa kwenye Wilaya ya Liwale naWilaya ya Mahenge na hili tumelipigia kelele sana lakinikwenye vitabu hivi bado halijaweza kuonekana.Nawaombeni sana jambo hili ni la muhimu sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, upande wa Mfuko waMawasiliano kwa Wote (USCAF). Huu Mfuko wa Mawasilianokwa Wote kwa mujibu wa taratibu unachangiwa namakampuni mbalimbali ya simu, hatujapata malalamikokwamba makampuni haya hayajawahi kuchangia lakinitunapata malalamiko (USCAF) wana uhaba wa pesa. Sasauhaba huu wa pesa unatoka wapi, iwapo haya makampuniyanachangia? Maana ukienda kuwauliza wanasema miradimingi haitekelezwi kwa sababu ya pesa lakini source zile zapesa zinapatikana kwamba hawa wanachangiwa nakampuni za simu na zinachangia. Kwa nini pesa hiziSerikali hamtaki kuwapa hawa watu wa Mfuko waMawasiliano kwa Wote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile mimi niende upandewa madini...

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Kuchauka nakuongezadakika moja, muda wako mnagawana na Mheshimiwa KizaMayeye, kwa hiyo, malizia hoja yako.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

194

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Naibu Spika,niangalie tu upande madini, kule kwetu Mtwara kuna Kandaya Mtwara ambayo ofisi yake moja iko Nachingwea, lakiniHalmashauri ya Wilaya ya Liwale ina madini na soko lake likoNachingwea. Sisi watu wa Halmashauri wa Wilaya ya Liwaletunapataje faida zaidi ya kuachiwa yale mashimo iwaposoko la madini liko Nachingwea na mratibu wa Kanda yukoNachingwea. Naomba Mheshimiwa Waziri atufafanulie hililimekaaje. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipanafasi hii. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Tunaendelea naMheshimiwa John Heche, atafuatiwa na Mheshimiwa MarwaRyoba Chacha na Mheshimiwa Anne Kilango Malecelaajiandae.

MHE. JOHN W. HECHE: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana kwa nafasi hii ya kuchangia ili niwezekusema kidogo kuhusu hoja zilizoko mbele yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kati ya matatizo makubwaambayo nchi yetu imekuwa ikikabiliwa nayo ni ufisadimkubwa unaolelewa na Serikali hii ya CCM. Ufisadi huuumekuwa kwenye miradi mbalimbali ya Serikali na kilamipango inayopangwa ukiangalia ndani yake unakuta kunamkono wa kifisadi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2010 mpakamwaka 2013/2014, kulikuwa na msukumo mkubwa sanakuhusu suala la gesi kule Kusini. Msukumo wa hali ya juu kwelikweli, wananchi kule wakapigwa, wakawekwa ndani,likapelekwa mpaka Jeshi, watu wakawa tortured kwelikweli.Wakati ule hapa Bungeni kikaingizwa kitu tunaambiwakwamba sasa tunataka ku-shift kutoka kutumia umeme wahydropower tunakwenda kwenye umeme wa gesi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hiyo ni Serikali ya Kikwetena il ikuwa ni mipango ya Serikali ya Kikwete. Watu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

195

wakalazimishwa kule likajengwa bomba pesa zikakopwakwa walipa kodi maskini wa nchi hii wakawekewa kitu kwakubambikiwa. Wananchi wa Kusini hawakukubali lakinimkatumia nguvu nyingi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, leo baada ya miaka mitatu,minne tume-shift tena tunaambiwa sasa tunakwenda kwenyeStieglers Gorge. Serikali iliyoingia hii sasa na yenyewe inatafutajinsi ya kupiga, tutapigia wapi, sasa tupigie kwenye StieglersGorge. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, bomba la gesi lililojengwakwa gharama kubwa kweli kweli matumizi yake tumeambiwakwenye Kamati ni mpaka sasa ni asilimia sita tu peke yakena tuliaminishwa na Watanzania wakaaminishwa kwambasasa hatutaki tena kutumia umeme wa maji kwa sababu isnot anymore reliable. Sasa umeme unaoaminika ni umemewa gesi.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa Serikali hiihii, ya Chamakilekile, Rais aliyeko ndiye alikuwa Waziri kwenye Serikalihiyohiyo, alikuwa kwenye Baraza la Mawaziri linalopangamipango, leo amekuja anatuambia sasa tunaenda StieglersGorge. Stieglers Gorge haijawahi kuingia kwenye bajeti.Ukisoma kitabu cha bajeti cha mwaka jana hakuna kitutulichojadil i kuhusu Stieglers Gorge. Hakuna pesazilizopangwa kwa sababu Bunge hili ndilo lipo kwa niaba yawananchi kupanga mipango na ku-authorize matumizi yapesa kwa niaba ya wananchi wa nchi hii ambao ndiyowalipa kodi. Bunge hil i halikuwahi kupanga hichokinachoitwa Stieglers Gorge. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sawa ni mradi mzuri na wotetunautaka, lakini kama tuliwekeana utaratibu na kamamwaka juzi tu tumechukua pesa za walipa kodi tukapelekakwenye bomba, kwa nini tusi-utilize bomba kwa matumiziya asilimia mia moja kabla hatujahamia kwenye hikikinachoitwa Stiglers Gorge? Kama siyo kwamba kuna wingula kaufisadi kapya kanatengenezwa hapa kwa sababu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

196

ufisadi uliokuwepo sisi hatukugusa? Kwa nini leo tunachukuapesa wakati bomba hili tunalitumia kwa asilimia sita pekeyake? (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nafikiri ni lazimaSerikali ije hapa na majibu, iwaambie Watanzania kwambagesi tuliyowaaminisha miaka miwili, mitatu, iliyopita kwaSerikali hii hii ya Chama kilekile ni nini kimeikumba gesi. Kwanini gesi inatumika kwa asilimia sita na sasa tunahama tenakurudi kwenye hydro ambayo tuliwaambia wananchikwamba haiko reliable kwa sababu mvua zetu haziaminiki.

Mheshimiwa Naibu Spika, hili bwawa tumeambiwajuzi kwenye semina tarehe 3 lina urefu wa kilometa 100 yaanikama unatoka Chalinze mpaka Dar es Salaam na upanawake ni kilometa 25. Mimi ninachotaka kutoka hapa Waziriatuambie hizo pesa ambazo angalau wamefikiria kwambawanataka kuzitoa kwa ajili ya ujenzi wa hili bwawa,wanakadiria kutoa shilingi ngapi na kwenye bajeti ipi nawaliipitisha wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu wamesemawithin three months tayari kutakuwa na mobilizationinafanyika pale kwa ajili ya kuanza kujenga bwawa. Sasahuyo aliyewapitishia hizo hela ni nani? Nani anatoa mamlakaya pesa nyingi hizo kupitishwa kinyemela hivyo bila Bungehili? Ni nini kazi ya Bunge hili ambalo wananchi maskini kilasiku wanatoa kodi, wanajinyima kwelikweli, mama zetuhawawezi hata kununua vidonge lakini wanalipa kodikutulipa sisi mamilioni ya pesa tukae hapa tujadili mipangoyao na hatufanyi hiyo kazi, tuna haja gani ya kuendelea kuwahapa? Tunataka Waziri atuambie. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tuje kwenye REA. Mwakajana tulizindua kitu kinaitwa REA wakaja wakandarasi naNaibu Waziri wakati ule sasa hivi Waziri rafiki yangu kweli,tulikuwa naye pale Bunda. Wakaja wakandarasiwakatuaminisha kwamba kufikia Desemba, kwa mfano,miradi ya densification, Waziri ni rafiki yangu na yeye yuko

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

197

hapa atathibitisha ninachokisema, kwamba densificationDesemba umeme unawaka. Kwanza ilikuwa Oktobabaadaye ikasemekana sijui imekuwaje Desemba.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo tunazungumza maeneokwa mfano ya Sirari kwenye mji ambao una population yawatu 45,000, hawana umeme pale. Hata mradi wadensification wenyewe tulioahidiwa hakuna kitu wala hakunahata nguzo zilizopelekwa mpaka sasa hivi mradi tulioambiwaDesemba utakuwa umewaka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hizi pesa za REA MheshimiwaWaziri ziko wapi? Kwa sababu hizi pesa siyo za bajeti walasio za nini, ni pesa za walipa kodi maskini ambapo kila sikutunanunua petrol tunakatwa Sh.50. Mama kijijini kuleakinunua mafuta ya taa mnamkata pesa au hizi pesa tenamnachukua mnaenda kununulia Madiwani wakati hizi pesazinatakiwa zilete umeme? Zinaenda wapi pesa ambazo zikoring-fenced? Pesa ambazo zinatolewa kabisa zikiwa namatumizi, mtu anaenda kununua mafuta anajua matumiziyake ni kwamba zituletee umeme wa REA, ziko wapi na nikwa nini haziendi kwenye REA? Nataka Waziri atuambie hizopesa ziko wapi? (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, leo wamesema TANESCOinadaiwa na sisi wote ni wajumbe tunajua TANESCOinadaiwa. TANESCO hiyo ambayo inadaiwa iko hoi,wameenda tena kubomoa na jengo lake linalokadiriwakufikia bilioni 54, sijui ni la kwake au walikuwa wamepangaau nini. Yaani mgonjwa ambaye yuko mahututi kwelikwelianaweza kufa sasa wamenyang’anya hadi sehemu ya kulalaananyeshewa na mvua. Sasa hawa hivi mipango yao niipi? Ni kwenda mbele au wanaenda mbele hatua mbili,wanarudi kumi na tano nyuma wanajipongeza? Kwa sababusasa hivi wamedhibiti vyombo vya habari, wanadhibiti hataWabunge kuongea, wakiongea tu wanashughulikiwa yaaniwao wenyewe wanajifungia wanafanya maamuzi ambayomiaka mitatu ijayo mbele au kwa sababu wanajua mwaka2020 hawarudi sasa wanataka tukiingia Serikalini tusikutechochote hapa. (Makofi/Kicheko)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

198

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu kama leowanakwenda kukopa kwenye benki za kibiashara kuwekezakwenye mradi mkubwa kama wa Stieglers Gorge wanalipajehizi pesa? Kama siyo kwamba wanataka Serikali itakayokujaishindwe kufanya kazi yake? (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa NaibuSpika, Taarifa.

MBUNGE FULANI: Kaa chini.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Heche kwanza kengeleimegonga, kwa hivyo, muda wako umekwisha. MheshimiwaMlinga amemaliza kuchangia, kwa hiyo huwezi kumpataarifa. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, kwa hiyo, tunaendelea naMheshimiwa Marwa Ryoba Chacha atafuatiwa naMheshimiwa Anne Kilango Malecela, Mheshimiwa HawaAbdulrahman Ghasia ajiandae.

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Naibu Spika,nikushukuru sana. Naomba niseme machache kuhusu Kamatihii ya Miundombinu na hii ya Nishati.

Mheshimiwa Naibu Spika, huwa naona kunaWabunge wamejiuzulu Ubunge wao na Madiwani etiwanamuunga mkono Magufuli kwamba amefanya mambomazuri sana katika nchi hii. Huwa nakaa najiuliza mpaka leosijapata majibu, kwamba Magufuli amefanya mambomakubwa kwelikweli. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, nikachukulia sample yaMkoa wangu wa Mara mpaka leo haujaunganishwa nabarabara ya lami na Arusha ambayo Muasisi wake ni Nyerere

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

199

mwenyewe. Nyerere akafa akawaachia wengine kuongozanchi hii mpaka leo na Magufuli amekuwa na historia ya kuwaWaziri wa Wizara hiyo kwa muda mrefu sana. Mwaka 2013wameanza kutengeneza barabara ya kuunganisha Mkoa waMara na Mkoa wa Arusha wakaanza na kilometa 50. Imepitamiaka sita kilomita 50 hazijakwisha hata kilometa sita tuwameshindwa kumaliza. Hiyo ndiyo Serikali ya CCM, nijiuzululeo nimuunge mkono wakati barabara imemshinda. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2016/2017ikatengwa shilingi bilioni 20 kwenye barabara hiyo, upandewa Mara bilioni 12 upande wa Arusha bilioni nane. Upandewa Arusha wakatangaza tenda wameshaanza kulima.Upande wa Mara bilioni 12 kipande cha Mugumu - Natampaka sasa hivi wanaendelea kutangaza tenda, bajeti ya2016/2017. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi Ryoba niko tayarikujiuzulu kuwaunga mkono, lakini mbona sioni sababu yakuwaunga? Nipeni sababu ya mimi kujiuzulu kuwaungakama barabara ndogo tu ya kuunganisha Mkoa wa Marana Arusha imewashinda. Kwa hiyo, bado, bado sana. Kwahiyo, niwaambie wananchi wa Mkoa wa Mara adui yao niCCM na Magufuli. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi leo mkoa ambaoametoka Muasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius KambarageNyerere hata Uwanja wa Ndege hakuna. Hakuna uwanjawa ndege wa maana Mkoa wa Mara. Nani leo, Waziri gani,Mbunge gani wa CCM asimame hapa aniambie Mkoa waMara haustahili kuwa na Uwanja wa Ndege tena wenyehadhi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2016/2017 ilitengwabilioni mbili kwenye Uwanja wa Chato, baadaye nikasikiabilioni 39.15 zimetokea wapi mbona hatujawahi kuzionakwenye bajeti mniambie! Kama kweli mnampenda MwalimuJulius Kambarage Nyerere, unachukua bilioni 39 unapelekaChato kuna nini? (Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

200

Mheshimiwa Naibu Spika, samahani MheshimiwaWaziri wewe ni rafiki yangu lakini naongea mambo ya kitaifakidogo inauma. Pale ambapo anatokea Muasisi wa Taifahata uwanja wa ndege na barabara hakuna. Leo Mkoa waMara kwa mfano hakuna Jimbo hata moja ambapowanakunywa maji safi na salama, hakuna! Asimame yeyotehapa aniambie Mkoa wa Mara kuna Jimbo lenye chujio,wapi? Tarime wanakunywa matope, Musoma Mjiniwanakunywa jinsi yalivyo, wanaugua amoeba na minyoohivyo hivyo, sasa ninyi niwaunge kwa lipi, si mnisaidie?(Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, unajua nilikuwa napitakwenye hiki kitabu cha Kamati ya Miundombinu, ninyiWajumbe wa Kamati mniambie, nimesikia mmeitishampewe taarifa ya Uwanja wa Chato, Waziri amegomakuwaletea na umetumia bilioni 39! Kwenye kitabu humunaangalia naona viwanja vingine, hivi uwanja wa Chatounajengwa au haujengwi na kama unajengwa kwa ninihaumo humu? Wajumbe wa Kamati nataka majibu, kwanini hauko humu? Wabunge nataka majibu kwa nini haukohumu? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, halafu mkandarasianayejenga huo uwanja unajua ni nani? Ni yule ambayeameshindwa kumaliza zile kilometa 50 pale Mkoa wa Mara,ndiyo amepewa Mayanga nani mwingine si ndiyo huyo? Kisarafiki yake na nani, Magufuli, ooh haya, twende kazi. (Makofi)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU): MheshimiwaNaibu Spika, mwongozo.

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba niendelee…

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU): MheshimiwaNaibu Spika, mwongozo.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

201

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Marwa naomba ukae,Mheshimiwa Jenista.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU): MheshimiwaNaibu Spika, pamoja na kuheshimu sana mchango waMheshimiwa Mbunge lakini naomba nitumie Kanuni ya 68(1)ya Utaratibu na Kanuni ya 68(7) ya Mwongozo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye Kanuni ya 68(1) yaUtaratibu, Mheshimiwa Mbunge anayo hoja ambayoimewekwa mbele yetu na inachangiwa, lakini anapoendeleana mchango wake ameendelea kugusa pia Kanuni ya64(1)(b) na (d) na nitazisema hizo Kanuni ambazo nimezitajahapa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ya kwanza Kanuni ya64(1)(d), Kanuni hiyo inatukataza kabisa katika kutumiamaneno ndani ya Bunge ili kulishawishi Bunge kuamua jambololote ama kuwashawishi Wabunge waelewe jambo hilolakini kwa kutumia jina la Rais, hiyo inakatazwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Marwa hapaanajaribu kuliaminisha Bunge kwamba mchakato wa tendaambayo inaendelea katika uwanja wa Chato, mkandarasiamepewa kazi hiyo eti tu kwa sababu ni rafiki wa MheshimiwaRais. Kwa hiyo, hiyo siyo sahihi na hiyo ni kuvunja Kanuni.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile ukienda katikaKanuni ya tisa (9), kila Mbunge atalisemea jambo ambaloliko katika mjadala tu na jambo ambalo Mheshimiwa Ryobaamelizungumza sasa hivi, ameendelea kudai kwambatunaendelea na shughuli hizi za michakato ya miradi lakinitunachokifanya ni kuendelea kuwanyanyasa wananchi waMkoa wa Mara, jambo ambalo si la kweli. Mawaziriwatakaposimama watatoa mifano ya namna gani Serikaliyetu ya Chama cha Mapinduzi imefanya mambo makubwasana katika Mkoa wa Mara na mikoa mingine katika nchi hiiya Tanzania. (Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

202

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naombaMwongozo wako kwa sababu mchangiaji anaendeleakuvunja Kanuni na kadri anavyoendelea kushangiliwa yeyeanaendelea kuvunja Kanuni. Kwa hiyo, nilikuwa naombamwongozo wako ili kanuni hizi zisiendelee kuvunjwa. (Makofi)

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa NaibuSpika...

NAIBU SPIKA: Naomba ukae Mheshimiwa Msigwa.

Waheshimiwa Wabunge, Mheshimiwa JenistaMhagama ametoa maelezo kwa kirefu kiasi kuhusu…

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tuwetunasikilizana, tusipende kuropoka kila wakati, tafadhali.Mheshimiwa Khenani, mimi nazungumza na weweunazungumza, unataka kufanya nini?

Waheshimiwa Wabunge, Mheshimiwa Jenistaamesimama akiitaja Kanuni ya 68(1) na Kanuni ya 68(7) lakinipia Kanuni ya 64(1)(b) na (d). Kanuni ya 68 inatakaMheshimiwa Mbunge anayesimama na kusema kuna Kanuniinavunjwa ataje Kanuni inayovunjwa, Mheshimiwa Jenistaametaja Kanuni ya 64 akisema inavunjwa na MheshimiwaMarwa Ryoba Chacha katika mchango wake.

Kwa mujibu wa Kanuni ya 68(4), Spika anaweza kutoauamuzi papo hapo juu ya jambo la utaratibu ama kuahirishakutoa uamuzi huo mpaka baadaye na pale anapoonainafaa fasili ya (5) anaweza akatuma jambo hilo kwenyeKamati ya Kanuni ili iweze kumshauri. Kanuni ambayoMheshimiwa Jenista anasema imevunjwa ni Kanuni ya 64(1)(b)ambayo inazungumza kuhusu mambo yasiyoruhusiwaBungeni na mojawapo inazungumzia Mbungehatozungumzia jambo ambalo haliko kwenye mjadala napia (d) inasema hatatumia jina la Rais kwa dhihaka katika

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

203

mjadala au kwa madhumuni ya kutaka kulishawishi Bungekuamua jambo lolote kwa namna fulani.

Waheshimiwa Wabunge, nimesikiliza maelezo yaMheshimiwa Jenista lakini pia nimesikiliza mchango waMheshimiwa Ryoba Chacha kwa sababu sisi kama Bungetulishatunga sheria ya namna ya kufanya michakato na watukupewa zabuni kwa hivyo si sawasawa kwamba kuna mtuamepewa zabuni kwa urafiki labda tu kama Mbunge anaoushahidi na kama upo nitautaka huo

Waheshimiwa Wabunge lakini kwa kuwa sinao hapambele na haujawasilishwa kwangu Mheshimiwa RyobaChacha nitakuruhusu uendelee lakini hayo manenouliyozungumza kuhusu mchakato kwamba amepewa rafikiwa Mheshimiwa Rais kujenga kiwanja cha ndege Chatoutayafuta halafu tutaendelea na mjadala. Kwa hiyo uyafutehalafu uendelee na mjadala.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa NaibuSpika, naomba Mwongozo.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Msigwa unazijua taratibu,siwezi kukuruhusu wewe kuongea kabla sijamaliza hoja mojana Mbunge mmoja. Kwa hiyo, kaa tumalize ile hoja halafuutapewa nafasi.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa NaibuSpika, mbona hatugombani, nilikuwa naomba tu Mwongozowako.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Msigwa naomba ukae.Mheshimiwa Ryoba naomba ufute hayo maneno halafuuendelee na mchango wako.

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba nifute, lakini ujumbe umefika. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Ryoba, naomba ukae.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

204

Waheshimiwa Wabunge, tutaendelea na nilimtajaMheshimiwa Anne Kilango Malecela atafuatia naMheshimiwa Hawa Abdulrahman Ghasia. (Makofi)

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Naibu Spika,si nimefuta niendelee na dakika zangu, what is wrong?

MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Naibu Spika…

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Naibu Spika…

MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza naomba nichukue nafasi hii kushukuru kupata nafasihii ya kuongea. Naomba niseme neno dogo kidogo, hataunapoamua kumnyonga mnyonge lakini mpe haki yake.Serikali ya Chama cha Mapinduzi Awamu ya Tano inafanyakazi nzuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba tuzungumze kwatakwimu, tuwe tunazungumza kwa takwimu. Kwanzanazungumzia Kamati ya Nishati na Madini, nazungumziaupande wa madini sasa. Serikali ya Awamu ya Tano yaMheshimiwa Rais Magufuli imefanya mambo makubwamawili na mambo haya yamewavutia Madiwani wenginewanakuja wenyewe. (Makofi)

WABUNGE FULANI: Ahaaa.

MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Naibu Spika,jambo la kwanza kudhibiti madini yasipotee na jambo la pilini upande wa ukusanyaji wa pesa za madini. Serikali ya CCMya Awamu ya Tano kwa kipindi hiki cha mwaka 2017/2018nusu tu…

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MHE. ANNE K. MALECELA: Basi mnyamaze niseme.Kipindi nusu tu tuhatujafika mwaka 2018, Serikali imekusanyaasilimia 80.4 ya makusanyo ya mwaka mzima. Lengo ilikuwamwaka 2017/2018, Serikali ikusanye bilioni 194.397 hadi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

205

mwaka 2018 Desemba lakini Serikali hii imekusanya bilioni156.311 sawa na asilimia 80, sasa utasema hiyo Serikaliinacheza? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, msiwasikil ize hawa,tumewazoea, sisi tunaangalia kazi inayofanywa na wananchiangalieni vizuri Serikali ya Awamu ya Tano inachapa kazi.Ningeshangaa sana Serikali inavyochapa kazi iungwe mkonona hawa, ningeshangaa, lazima hawa wakasirike. Kwa hiyo,msipate tabu Waheshimiwa Wabunge, twendeni kazini.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, twende kwenye suala laREA, nipongeze Bunge la Kumi ndilo lilikuja na hii tozo ambayoimeleta manufaa kwa nchi yetu. Naomba nikubali kwambajambo lolote linapoanza lina changamoto, huwezi kuanzajambo mara ya kwanza ukalifanya kwa asilimia 100, maraya pili ukalifanya asilimia 100, kidogo kidogo REA itasimama.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitoe takwimu,mwaka 2008 umeme vijijini ulikuwepo kwa asilimia 2.2 tukabla ya kuwa na REA. Ilipofika 2015 umeme vijijini ukafikiaasilimia 21.02, hayo ni madogo jamani? Serikali inachapakazi, sasa. (Makofi)

MBUNGE FULANI: (Aliongea bila kuwasha kipaza sauti)

MHE. ANNE K. MALECELA: Nyamaza. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2015 mpakaDesemba, 2017 angalieni Serikali ya Awamu ya Tanoinavyochapa kazi, umeme vijijini umefikia asilimia 49.5. Sasanajiuliza hivi hamuyaoni hayo, wenzetu mna macho gani,tafuteni miwani. Serikali inachapa kazi jamani Wabunge waCCM tujivune. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimpongezeMheshimiwa Naibu Waziri Subira Mgalu, anajitahidi sana. Wikiiliyopita alikwenda Kilimanjaro, nampongeza sana, kuangalia

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

206

matatizo yaliyotokana na REA I na REA II. Kwa hiyo, Serikaliinafahamu kwamba kuna changamoto, alikwenda Mwanga,Rombo na akaja Same.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimemshangaa, Kata yaVulha, Kata ambayo Mawaziri wachache sana wanafika,amefika Subira. Kule kuna mradi wa REA II, nilipambana nayosana ile, Serikali ikapeleka umeme kule lakini haikumaliza.Mheshimiwa Waziri amekwenda kuangalia na amekwendakuwahakikishia wananchi kwamba REA III inakwendakumalizia, Serikali inafanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa WaheshimiwaMawaziri, Waziri wa Nishati pamoja na Naibu Wazirimlikwenda Kilimanjaro lakini kuna Wilaya ina matatizo sananaomba nisimame hapa niiombee umeme kule ambapohaujafika, Wilaya ya Siha. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Siha kuna Katamoja ambayo ina vij i j i vinne, hiyo Kata inaitwaDonyomurwakna. Kuna vijiji vinne kwenye kata hii, vijiji viwilivina umeme na vijiji viwili bado umeme haujafika. (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba niseme kitu kimoja, waacheni hawa, hakuna Serikaliambayo inaweza ikafanya mambo yote kwa wakati mmoja,haipo duniani. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Haipo.

MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Naibu Spika,kwa hiyo, naiombea Wilaya yangu ya Siha kwamba vile vijijiambavyo Mheshimiwa Waziri nimekuletea kimaandishiuhakikishe vinapata umeme na Alhamisi ya wiki hii nahamiaSiha. Naomba Watanzania wawe na uhakika kwamba Sihalitakuwa Jimbo la Chama cha Mapinduzi.

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

207

MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba niwahakikishe Watanzania kwamba CCM inashindaSiha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja,ahsante sana. (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Hawa AbdulrahamanGhasia, atafuatiwa na Mheshimiwa Boniface Mwita Getere,Mheshimiwa Kiza Mayeye ajiandae.

MHE. HAWA A. GHASIA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi na mimi ya kuzungumza.Nianze kwa kuwapongeza Wenyeviti wote wa Kamati kwataarifa nzuri sana waliyowasilisha lakini pia bila kumsahaudada yangu Mheshimiwa Anne Kilango Malecela kwa hotubayake nzuri sana ambayo ameimalizia hivi punde. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuipongeza sanaSerikali yangu ya Awamu ya Tano na Serikali ya Chama chaMapinduzi kwa kazi nzuri sana ambayo imefanya. Kuna watuambao wanakaa wanasema tangu uhuru hatujafanyachochote, siwezi kuwakatalia kwa sababu wengi ni watotowa miaka ya 80 na 90. Sisi ambao tumezaliwa tukiwatunapita katika Mto Rufiji tukivuka kwa pantoni na sasa hivitunapita katika Daraja la Mkapa katika Mto Rufiji tunajuawapi tulikotoka na kazi gani Serikali ya Chama cha Mapinduziimefanya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda niipongeze Wizaraya Miundombinu kwa kazi kubwa sana inayoifanya katikakupanua bandari zetu. Katika taarifa na hata hivi karibunimimi mwenyewe nimeshuhudia uzinduzi wa upanuzi waBandari ya Dar es Salaam pamoja Bandari ya Mtwara. Kazikubwa sana inafanyika kule kuhakikisha kwamba kuleMtwara tunaongeza Gati namba mbili ambalo litakuwa naurefu wa mita 300. Nina uhakika kabisa baada ya hapo

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

208

korosho zetu na mizigo yetu ya Mtwara itakuwa inapita bilamatatizo yoyote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niipongeze Serikali yaAwamu ya Tano kwa kuanza ujenzi wa barabara kwakiwango cha lami kutoka Mtwara - Newala - Masasi. Sasahivi tayari mkandarasi yupo kazini, anajenga kipande chaMtwara - Mivata zaidi ya kilometa 50. Niiombe Serikali yangukile kipande kilichobaki basi mkandarasi mwingine sawa naahadi ya Mheshimiwa Rais wetu Dkt. John Joseph PombeMagufuli alivyoahidi kwamba vipande vyote vilivyobakivitatafutiwa wakandarasi, hivyo tutafutiwe wakandarasikwa sababu sisi Wabunge wa Chama cha Mapinduzi kaziyetu kuunga mkono bajeti yetu ya Serikali ya Chama chaMapinduzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunaomba ilemiradi yetu itekelezwe na wale ambao wanaikataa bajetiwasishangae katika maeneo yao kuona mpaka sasahivi hakuna kinachofanyika kwa sababu hakuna bajetiwaliyoipitisha kwa ajili ya miradi katika maeneo yao.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niunge mkono ujenzi wareli kwa kiwango cha standard gauge ambao unaendeleasasa hivi kutoka Dar es Salaam kuja Morogoro na pia kutokaMorogoro hadi Makutupora. Pia suala la ujenzi wa viwanjavya ndege, naipongeza sana Serikali yangu na naipongezasana kwa kulifufua Shirika letu la Ndege kwa kununuabombardier zile ambazo kwa kweli wote bila kujali vyamatunazipanda na tunazitumia kila siku. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hapa nina changamotomoja tu ambayo nataka kuishauri Wizara ya Miundombinu,ndege zetu hizi zinalala au zina-park saa 10.00 au saa 11.00.Tatizo kubwa sana bombardier zinaweza kutua Uwanja waSongwe, Kigoma, Mtwara, Bukoba na Songea lakini viwanjahivi vingi havina taa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimuombe Waziriwa Miundombinu ahakikishe kwamba viwanja hivi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

209

vinawekwa taa ili ndege zetu hizi ziweze kutumika kwa ufanisizaidi. Tunaweza kwenda Mtwara hata saa 4.00 au saa 6.00usiku kama uwanja una taa lakini unakuta ndegezinakimbizana na jua, jua likizama na zenyewe zina-park. Piaviwanja hivi tukiweka taa tunaongeza hata usalama kwandege ambazo zinapita katika anga za kimataifa kukiwana matatizo ya kutaka kutua wawe na viwanja mbadalavya kuweza kutua.

Mheshimiwa Naibu Spika, Viwanja vyetu vingivinakosa sifa ya kuweza kutua usiku kwa sababu ya ukosefuwa taa. Kwa hiyo, nimwombe Mheshimiwa katika bajetiinayokuja ahakikishe viwanja vyote ambavyo bombardierinatua basi viwekewe taa ikiwemo pamoja na Kiwanja chaMtwara. (Makofi)

MHE. MAFTAH A. NACHUMA: Mheshimiwa Naibu Spika,taarifa.

T A A R I F A

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Maftah, Taarifa.

MHE. MAFTAH A. NACHUMA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante. Naomba kumpa taarifa Mheshimiwa Hawa Ghasiaanayezungumza hivi sasa kwamba viwanja hivi viwekee taa.Taarifa ninayompa ni kwamba juzijuzi tumeweza kumsikiaMheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniaakiwa anazungumza kwamba Kiwanja cha Mtwarakimetengewa shilingi bilioni 41 kwa ajili ya kukarabati nakuweka taa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa ninayompa kwambaaisisitize tu Serikali zile pesa ziweze kuletwa kweli kwa ajili yakukarabati taa za Uwanja wa Ndege wa Mtwara. Ahsante.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, taarifa hiyoinaonekana mnaipokea kwa niaba ya Mheshimiwa HawaGhasia. Mheshimiwa unaipokea taarifa hiyo? (Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

210

MHE. HAWA A. GHASIA: Mheshimiwa Naibu Spika,taarifa naipokea, ni kweli hizo pesa Mheshimiwa Raisamesema lakini lazima nikumbushe kwa sababu viwanjavilivyo kwenye huo mpango ni vingi, kwa hiyo, Waswahiliwanasema lazima kamba kila mtu anavutia kwake. Kwahiyo, naikubali taarifa na mimi namsisitiza Waziri kwambazile pesa zilizotengwa hizo taa ziwekwe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niendelee naupande wa Wizara ya Nishati. Nataka nizungumzie deni laTANESCO. Deni la TANESCO ni la historia, tunalo kwa mudamrefu kwa sababu muda mrefu shirika letu l i l itakakubinafsishwa. Sasa yale madeni tukisema tuiachie TANESCOyenyewe iweze kuyalipa sidhani kama tunaitendea haki.Naishauri Serikali yangu ione uwezekano wa kuisaidiaTANESCO kulipa yale madeni ili iweze kujikwamua na kuwezakutekeleza majukumu yake kwa uhakika.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kwambaTANESCO inadai taasisi za Serikali lakini na yenyewe inadaiwana taasisi kubwa ambayo inaidai TANESCO ni TPDC. TPDCinashindwa kutekeleza miradi yake mingi kwa sababuinapeleka gesi TANESCO na TANESCO anashindwa kulipa naTPDC naye anachukua gesi kwa watu. Kwa hiyo, naombaTANESCO isaidiwe kama tunataka ikimbie, tukiiacha yenyeweitakwenda kila siku ikitambaa. Kwa hiyo, nataka tuiwezesheTANESCO kwa yale madeni aidha Serikali iyachukue autuwasaidie kuyalipa au tuwasaidie kukopa ili wawezekujiendesha kwa tija.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ambalonataka nichangie ni kwamba tuwe na gas master plan aumpango kabambe wa matumizi ya gesi kwa sababu sasahivi kila mwekezaji anaweka kiwanda eneo ambaloanalitaka yeye. Sidhani kama Serikali itakuwa na uwezo wakumpelekea kila mtu gesi pale ambapo amejenga kiwanda.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tukitenga maeneomaalumu, tukaonyesha mpango kabambe wetu kwamba

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

211

bomba la gesi litapita katika maeneo haya na yeyoteanayetaka kutumia gesi akaweke kiwanda chake katikamaeneo hayo, nina uhakika kabisa kwamba ndani ya mudamfupi tutakuwa na uwezo wa kuwafikishia gesi katikaviwanda hivyo. Bila kuwapa maelekezo kila mtu akajengaanapotaka mwenyewe, tutakuwa na gesi nyingi lakinitutashindwa kuitumia kwa sababu gharama ya kuwafikishiawatu gesi itakuwa ni kubwa zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda nimalizie kwakuiomba Wizara ya Miundombinu kuunganisha barabara yakutoka Mtwara - Kilambo kwa kiwango cha lami kwa sababubarabara hii inatuunganisha na nchi majirani zetu Msumbiji.Ni Sera ya Taifa kwamba barabara za Kitaifa ziunganishwekwa kiwango cha lami. Natambua kwamba tayari kwaupande wa Mtambaswala tumeunganisha lakini watu wengizaidi wanatumia kivuko cha Kilambo kwa ajili ya kwendaMozambique kwa sababu ndiyo njia fupi zaidi kuliko upandemwingine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie kwa kuiombaSerikali wakati wa bajeti mara nyingi hapa tumekuwa nautaratibu wa watu kukataa kila bajeti, lakini inapokujawakati wa utekelezaji walewale walioikataa bajeti ndiyowanakuwa wa kwanza kulalamika kwamba kwaohaijapelekwa. Mheshimiwa Rais aliomba kula kwa wananchina alikuwa na ahadi zake na Wabunge tuliomba kura kwawananchi tulikuwa na ahadi zetu. Kwa hiyo, zile ahadi zetututakuja kuulizwa sisi 2020 tumetekeleza kwa kiasi gani.(Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Hawa Ghasia,muda wako umekwisha. Mheshimiwa Boniface Mwita Getereatafuatiwa na Mheshimiwa Kiza Mayeye, Mheshimiwa AkbarAjali ajiandae.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

212

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi na mimikuchangia. Kwanza nawashukuru Wenyeviti wa Kamati,Mawaziri wote wa Wizara hizi tatu na Watendaji wao naManaibu Waziri kwa kazi nzuri ambayo wanatufanyia.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuchangia nijielekezekwenye Wizara ya Nishati. Wizara ya Nishati kuna maeneomawili; kuna eneo la Densification na eneo la REA III, lakiniyote inatoka kwenye REA. Kasi ya utendaji kazi waWakandarasi katika Jimbo la Bunda kwa upande wadensification ni mdogo sana, ninavyozungumza hapa, wakosite lakini wanaenda pole pole sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, REA katika vijiji, kasi yakenayo imekuwa ndogo ingawa Mheshimiwa Waziri anafanyakazi kubwa sana ya kuanzisha hii miradi katika maeneombalimbali. Nami wakati fulani namhurumia, anatembeasana, lakini Wakandarasi wanaenda slow sana. Sasa, sijui niupungufu wa hela au ni nini, sielewi.

Mheshimiwa Naibu Spika, namwomba MheshimiwaWaziri sasa awahimize hawa Wakandarasi katika maeneona hasa Wilaya ya Bunda, hususan Jimbo la Bunda katikamaeneo ambayo Mheshimiwa Waziri alikuja akafanyauzinduzi wa Mradi wa REA III katika eneo la Maiwanda katikaJimbo la Bunda. Kwa hiyo, nafikiri ni vizuri Mheshimiwa Waziriakahimiza wakaja kwenye kutenda hiyo kazi vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika REA kuna mambohuwa siyaelewi vizuri. Moja, ni kitu kinaitwa kilometa. Unakutakuna upungufu kati ya watu wa survey ya TANESCO na surveyya Mkandarasi, TANESCO ukiwauliza, nani amefanya surveyya kumpa Mkandarasi aende kujua Kijiji ‘A’ kila kilometa tatu,kina kilometa moja na Kijiji ‘B’ kinawekewa transfoma mbilina Kijiji ‘A’ kinapewa transfoma tatu au kilometa mbili. Sasaukiuliza TANESCO, wanasema ni REA; ukiuliza REA, wanakujana takwimu, hawahusishi wanakijiji wale kujua toka mwanzokwamba kijiji hiki kitapata kilometa mbili au mtandao waumeme wa kilometa mbili na transfoma tatu na voti ngapi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

213

katika hiyo transfoma. Kwa hiyo, hilo nalo ni tatizo liko hapa,Mheshimiwa Waziri naomba uliangalie vizuri ili tuwezekwenda vizuri katika suala hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala la Wizara yaMiundombinu. Kuna masuala ya barabara ya lami kutokaNyamswa kwenda Bunda na kutoka Bunda kwenda Brambana Bramba kwenda Kisorya, imechukua muda mrefu sana.Kwa hiyo, tunaomba Mheshimiwa Waziri anayehusika awezekuiangalia kwa makini zaidi kwenye hiyo barabara. Kunabarabara ambayo inatoka Sanzati kwenda Mgeta na Mgetakwenda Nata, nayo tunaomba Mheshimiwa Wazirianayehusika aweze kuiangalia vizuri hiyo barabara.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kusema mamboyafuatayo:-

Kwanza, ni kumpongeza Rais wetu wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John PombeMagufuli kwa kazi nzuri anayoifanya kwenye Mkoa wa Mara.Sisi Mara hatuna upungufu wa kupata Rais, tumewahi kupataRais miaka 24, kwa hiyo, hatuwezi kulalamika kwamba Raisamefanya nini kwa miaka miwili iliyokuwepo hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimewahi kwenda Indiakumshuhudia mtu anafanyiwa operesheni; kuna opereshenindogo na kubwa. Operesheni kubwa ni zile zinazohusishamatumbo kwa ndani; unatoa labda figo na vitu vingine.Mtu yeyote atakayekatwa kisu kwa operesheni kubwa lazimaagune na lazima arushe miguu. Kwa hiyo, ninachoonawenzangu hapa wanarusharusha miguu, naona kamaoperesheni ya Mheshimwia Dkt. Magufuli imewafikia. Kwahiyo, sioni matatizo ya namna hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza MheshimiwaRais kwa mambo yote anayoyafanya. Kwanza, ni kutupaMkoa wa Mara shilingi bilioni 10 za uwanja wa ndege. Kwamara ya kwanza Rais, Mheshimiwa Dkt. Magufuli akiwamadarakani, juzi Waziri Mkuu ametua pale na ndege kubwa.Sasa tunamlaumuje kwa mambo haya? Tunapozungumza,

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

214

site watu wanaendelea na kazi. Tunamshukuru MheshimiwaRais kwa kutuletea Mkoa wa Mara shilingi bilioni nne kwaajili ya Hospitali ya Kongwa ambayo imekuwepo toka mwaka1975. Inaendelea kufanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Niabu Spika, kwa hiyo, sisi Maratunamlaumu kwenye jambo gani? Kwa hiyo, mambomengine yapo, yanaendelea. Naona watu wanarusha miguutu, lakini hali ya hewa ni nzuri. Kwa hiyo, namshukuruMheshimiwa Rais pia kwa kudhibiti rushwa, kuweka nidhamuya kazini, kudhibiti wazembe na wala rushwa, kutoa elimubure, kuanzisha miradi mikubwa ya Stigler’s Gorge na miradimingine inayoendelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tunachokiona hapani kitu kimoja; wenzetu wameshaona Messi wa CCM niMheshimiwa Dkt. Magufuli. Kwa hiyo, ni lazima mshikeshikemiguu. Wana-CCM lazima tukae tayari kumlinda Messi wetuasiumizwe, asilete madhara katika mambo hayo. Kwa hiyo,nafikiri kwamba haya ni mambo ya msingi ya kufanya, lakininaomba Wizara zinazohusika ziangalie Jimbo la Bunda.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

NAIBU SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Kiza Mayeye,atafuatiwa na Mheshimiwa Akbar Ajali na MheshimiwaMendrad Kigola, ajiandae.

MHE. KIZA H. MAYEYE: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante. Napenda nikushukuru kwa kunipa nafasi hii ya leo.Nikiwa kama Mwanakamati wa Kamati ya Nishati na Madini,napenda kuipongeza Kamati ya Nishati na Madini kwa kazinzuri ambayo wameifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nianze kuongeleasuala la TANESCO. TANESCO ni taasisi ambayo tunaitegemea

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

215

katika nchi yetu, lakini imeshindwa kufanya kazi yake ipasavyokwa sababu ya haya madeni. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niongelee suala la Kigoma.Mpaka leo mikoa hii ya Magharibi ambayo ni Katavi, Kigoma,tunatumia umeme wa dizeli ambao kwa namna moja amanyingine unasababisha hasara kubwa kwa Serikali yetu. Sasanaiomba Serikali ijitahidi kadri inavyoweza, kwa sababutayari wameanza mpango huu wa Gridi ya Taifa, basi mikoahii ya Magharibi, Kigoma na Katavi tuweze kuingia katikaGridi ya Taifa haraka inavyowezekana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia niongelee suala lawachimbaji wadogo wa madini. Wachimbaji wadogowengi wa madini ni vijana wa Kitanzania ambao wengiwameamua kujishughulisha wasiingie katika wizi na wafanyekazi. Naiomba sasa Serikali iwasaidie vijana hawa, iwasaidieelimu, iwasaidie vifaa. Leo tumeona vijana wengiwamekuwa wakifunikwa na vifusi katika migodi kwa sababuhawana uelewa wanapoingia kule chini. Kwa hiyo, naiombaSerikali ijitahidi kadri inavyoweza itoe elimu kwa vijana hawa.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine niongeleekuhusu REA. Naipongeza sana Serikali, pamoja na kufanyakazi vizuri katika REA II lakini kuna changamoto ambazozimejitokeza. Naomba wanapokwenda katika REA IIIwajitahidi changamoto zile zisirudie. Kwa sababu tumeonavijiji vingine umeme unapita barabarani, lakini hauendi katikahospitali na shule. Umeme unakwenda Kijiji ‘A,’ lakini unarukaunakwenda Kijiji ‘C’, Kijiji ‘B’ kinakosa umeme. Kwa hiyo,naiomba sana Serikali, pamoja na kazi nzuri ambayowanafanya katika Mradi huu wa REA, REA III iende vizuri navijiji vyote vipate umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niongelee suala la Chuohiki cha Madini cha MRI. Tunahitaji wasomi ambaowamebobea katika suala zima la madini. Leo Tanzaniatunatengeneza Tanzanite, lakini Tanzanite hii ambayotukiipeleka katika Soko la Dunia ambayo imechachuliwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

216

hapa Tanzania, inaonekana haina hadhi sawa na ile ya Indiaau South Africa. Naiomba sasa Serikali iwasomeshe watu,iwapeleke nje, wakapate ujuzi ili kesho Tanzanite yetu hiiionekane sawa na ile ya India au ya South Africa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho kabisa, Waswahiliwanasema mnyonge, mnyongeni haki yake mpeni.Nampongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania kwa kuweka ukuta huu Mererani ambaounalinda madini yetu ya Tanzanite yasiweze kuibiwa. Leomadini yetu hayataweza kuibiwa, yatatoka na yatapelekwamoja kwa moja kwa asilimia 100 na hakuna wezi ambaowatapitisha tena haya madini kwa njia ya chocho. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,naomba kuunga mkono hoja. Ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, huyu Mbungemmeona amemalizia na kuunga mkono hoja. Hizi hoja ni zaWenyeviti wa Kamati. Sasa sisi Wabunge kama hatuziungimkono, sijui tunasubiri nini? Wengine walikuwa wanasemaWaziri ajibu; hizi hoja ni za Kamati zetu, ndiyo zimeletwa hapa.Kwa hiyo, tukumbuke tu hilo Waheshimiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Akbar Ajali, atafuatiwa na MheshimiwaMendrad Kigola na Mheshimiwa Subira Mgalu ajiandae.

MHE. AJALI R. AKBAR: Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza nachukua nafasi hii kukushukuru wewe kwa kunipanafasi hii. Mchango wangu umegawanyika katika maeneomawili. Kama hoja za Kamati zilivyozungumza, maana yakeMawaziri wanashauriwa kwamba miundombinu ifanye kazikufuata utaratibu ule ambao kwa kweli unashauriwa naKamati, nashauri miundombinu ishirikiane na Wizara nyingine.Kwa sababu leo TCRA haitaki kushirikiana na Halmashauriambazo zipo huko Wilayani.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama tunavyofahamukwamba sasa hivi tunaenda kwenye bajeti, Halmashaurinyingi zinakuwa hazina mapato, lakini minara ya simu ipo

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

217

katika Halmashauri zote, lakini Service Levy inakuwa hailipwikatika Halmashauri husika. Kwa hiyo, naomba Wizara ishinikizeTCRA itoe takwimu ambazo ni sahihi ili Halmashauri ipatekutoza Service Levy. Kwa sababu leo minara ya simu inalipaService Levy bila kuwa na habari, lakini TCRA ina uwezo wakujua kwamba ni simu kiasi gani zinakuwa zinaingia kwa kilamnara.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziriatakapokuja hapa atueleze, je, kulipa Service Levy ni sheriaau mtu analipa kwa hiari yake? Kwa sababu kuna baadhiya makampuni hayalipi kabisa na mengine yanalipa kwakiwango kidogo sana. Kwa hiyo, Wizara ya Miundombinuiishinikize TCRA isaidie Halmashauri ili Halmashauri iwezekutoza ule ushuru kutegemeana na simu ambazotunazitumia kutoka hayo maeneo ambayo yapo.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, kama vile ambavyonimezungumza kwamba Wizara ishirikiane na Wizaranyingine, vilevile tumezungumzia hapa kuhusu Wizara yamiundombinu. Ukiangalia sana kwa mfano kule Mtwara, leoni eneo ambalo kwa kiasi kikubwa sana wanalima korosho.Kwa asilimia karibu 70 ya export ya korosho inalimwa Mtwara,lakini ukienda kuangalia kule, zile barabara zote za Kitangali,Mtopwa, Luagala na Nanyamba, zimebaki mashimo.Mapato yetu ya Export Levy, kwa mfano mwaka huutumepata shilingi bilioni 140 na hizo fedha huwa zinapatikanakila mwaka. Hizo fedha asilimia 65 zinakwenda kule kwa ajiliya kuboresha zao la korosho, lakini zi le barabarahaziboreshwi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tuangalieuwezekano wa miundombinu kwa kushirikiana na Wizara yaKilimo kuona ni namna gani zile fedha ambazo zinapatikanazinakwenda kuboresha zile barabara ambazo zinahusianana mambo ya kilimo.

Mheshimiwa Naibu Spika, haiwezekani leo zile fedhazote ambazo ni asilimia 65 zinaondoka halafu asilimia 35zinakwenda katika Mfuko Mkuu. Nasema kwamba kama kila

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

218

mwaka tungeamua sisi Mtwara tutumie tu Export Levy, basibarabara zote za Mtwara zingekuwa na lami. Sasa sisihatutaki lami, tunataka angalau kifusi kiwepo katika zilebarabara ambazo zinatumika na ambapo magari makubwayanakuwa yanapita kule.

Mheshimiwa Naibu Spika, namwomba sanaMheshimiwa Waziri kwamba katika bajeti yake inayokuja, basiashirikiane na Wizara ya Kilimo na Wizara ya Kilimo vilevileiangalie uwezekano, ni namna gani watajitoa kusaidia zilebarabara zao? Wasiangalie tu kupata zile fedha asilimia 35ambazo zinakwenda kwenye Mfuko Mkuu na asilimia 65ambazo zinaenda kwenye Bodi. Waangalie namna ganiwananchi wananufaika kwa barabara zao kuwa bora? Isiwekama maeneo ambayo wanachimba madini, watuwanachukua yale madini wanaondoka halafu wanaachamashimo. Namwomba sana Mheshimiwa Waziri afanyejitihada za kushirikisha maeneo yote hayo mawili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la tatu nizungumziekuhusu REA. Mtwara ni eneo ambapo gesi inatoka kwa wingisana, lakini mpaka leo kuna tatizo kubwa sana la umeme.Okay, sisi hatuna shida kuhusu umeme, lakini hawa wananchiwana shida ya maji. Leo maji ule umeme unaopatikanaMtwara, hauwezi kusukuma maji kwa kiwango kikubwa. Kwahiyo, namwomba sana Mheshimiwa Waziri ule umeme uliopoMtwara hautoshi, achukue hatua za dharura ili ahakikishekwamba ananunua mashine za dharura ili tuweze kupatamaji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi leo hii huwezi kupatamalalamiko ya maji kwa kuwa mvua zinanyesha. Itakapofikiamwezi wa tatu it is a crisis, itakuwa ni war. AsitakeWaheshimiwa Wabunge wa Mtwara, Nachingwea au Lindituje tuombe hapa chini ya dharura, kwa sababu itakuwa nitatizo kubwa sana kupita kiasi. Kama gesi ipo Mtwara,inawezekana vipi umeme ukosekane? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nachukua nafasi hiikumwomba sana Mheshimiwa Waziri afanye jitihada zote za

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

219

kuleta mashine mpya za gesi aende akafunge katika stationya Mtwara. Nakuomba sana Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Naibu Spika, huo ndiyo ulikuwa mchangowangu wa leo. Ahsanteni sana na naunga mkono hoja.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa MendradKigola, atafuatiwa na Mheshimiwa Subira Mgalu naMheshimiwa Stanslaus Nyongo ajiandae.

MHE. MENDRAD L. KIGOLA: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru sana kwa kunipa nafasi hii ili nami niweze kutoamchango kwenye Kamati hizi mbili; Kamati ya Miundombinuna Kamati ya Nishati na Madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa, nianzekutoa pongezi nyingi sana kwa Serikali. Kuna watu wenginewamekuwa wanachangia; kwanza, nimesikitika sana kwasababu kuna kitabu hapa ambacho ni taarifa ya Kamati.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukienda ukurasa wa 12 kunakipengele kidogo, wameeleza vizuri Serikali imefanya nini?Imeeleza vizuri kabisa, kwamba katika miundombinu;ukichukua kipengele kimoja, sitaki nichukue vitu vingi, kwamfano pale kwenye ujenzi wa reli na tulishaongea ili nchiiweze kusonga mbele, uchumi wa Taifa ukue ni lazimatuhakikishe kwamba tumeimarisha usafiri wa reli. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hapa nilikuwa nasomakwamba Serikali katika mipango yake mizito kuna ujenzi wareli wa Dar es Salaam – Morogoro kilometa 205; kuna ujenziwa reli kutoka Morogoro – Makutupora kilometa 336; kunaujenzi wa reli Makutupora – Tabora kilometa 295; kuna Tabora– Isaka, kilometa 133; kuna Isaka – Mwanza, kilometa 250;halafu mtu mwingine anasema haoni. Jamani, hayo nimaendeleo makubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ndugu zangu WaheshimiwaWabunge, tukitaka uchumi wa nchi uendelee lazima Serikali

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

220

ijikite kwenye miundombinu ya reli ili tuweze kusafirisha mizigomizito kwenye reli zetu na barabara za lami tuweze kusafirishamabasi yetu na magari madogo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tulishasema ndani ya Bungehili, Serikali imefanya mambo mengi sana na tunayaona kwamacho. Nami kama Mbunge, naiunga mkono Serikali naiendelee na mikakati mizuri. Tunategemea kwamba tukifikamwaka 2020 nadhani maswali mengi sana yatakuwayamejibiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika ujenzi wa barabarakuna barabara nyingine zina changamoto. Naishukuru sanaSerikali kwamba kwenye mipango ile ya Serikali ilishawekwatayari. Kuna barabara moja ambayo wanaisema kila sikuna huko kuna viwanda vingi na tumesema nchi yetu ni yaviwanda; kuna barabara ile ya Mafinga – Mgololo kilometa84. Naiomba Serikali kama ilivyokuwa imeahidi, basiutekelezaji wake ukianza kwenye bajeti inayokuja nitafurahisana.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine, kuna barabaraile ya Nyororo mpaka pale Mtwani. Hiyo barabara ikiwekwakiwango cha lami itatusaidia sana kwa sababu kule kunaviwanda vingi sana halafu maeneo yale mvua zinanyeshasana kiasi kwamba magari makubwa yanashindwa kupitana kusafirisha ile mizigo mizito. Kwa hiyo, naiomba Serikali,katika ukanda huu wa Kusini, ikitujengea zile barabara zalami, basi itakuwa imefanya vizuri ili wenye viwanda vikubwawaweze kusafirisha mizigo yao. Vile vile hii barabara tunajuakabisa tuna kiwanda kikubwa cha Mgololo ambachokinatengeneza karatasi kule, kinashindwa kusafirisha mizigomizito, kwa hiyo, itakuwa imetusaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nikienda kwenye nishati namadini kwa sababu muda ni mdogo; kwanza, nitoe pongezikwa Serikali. Natoa pongezi kubwa sana kwa MheshimiwaWaziri wa Nishati na Madini. Kwa kweli alifanya ziara kwenyeJimbo langu na aliongea na wananchi na kupongeza sana.Alichokiongea siku ile, utekelezaji wake umeanza. (Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

221

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo moja la Watanzania,unataka kitu kifanyike mara moja, siku moja; lazima kuwekuna hatua. Mimi nampongeza Waziri, sasa hivininavyoongea mkandarasi yuko site, kama alivyoongea.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba Serikali, bahatinzuri ameandika kwenye ripoti yake; kuna maeneo yaleambayo yalirukwa. Katika survey kuna vitongoji vinginevimerukwa, naomba vile vitongoji ambavyo vimerukwaviweze kupewa survey tena ili viweze kupewa umeme kwasababu wananchi wanalalamika, wanajua kamahawatapewa. Nakuomba kwenye majumuisho yakouwaambie wananchi kwamba yale maeneo yote ambayoyalikuwa yamerukwa, hayakufanyiwa survey kwambamtafanya survey na watapewa umeme kama kawaida.

Mheshimiwa Naibu Spika, zile gharama za uingizajiumeme, naomba kwenye majumuisho tuwaambie wananchizijulikane vizuri. Kwa sababu kuna watu wengine wanasemaile ya 177,000 kuna wengine kuna ile 27,000, kwa hiyo, inaletamchanganyo kidogo. Sasa naomba Mheshimiwa Wazirianapotoa majumuisho, aliweke sawa hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna watu wenginewameanza kuchangia, wanasema wachangie fedha yanguzo. Yaani mtu anataka aweke umeme pale, anaambiwana TANESCO kwamba achangie fedha fulani. Mwananchimmoja alisema anaambiwa achangie Sh.500,000 kwa ajiliya nguzo. Namwomba Mheshimiwa Waziri hili aliweke sawa,kwamba zile nguzo ni bure au kuna watu wenginewanatakiwa wachangie pale? Tunaona tunapatamchanganyiko sisi Wabunge tunaulizwa maswali ya namnahiyo. Kwa hiyo, leo tunategemea Mheshimiwa Waziri atupemajumuisho, masuala ya nguzo tuhakikishe kwamba kamani bure ijulikane watu wanapelekewa bure.

Mheshimiwa Naibu Spika, halafu kuna shule nyingi tuzimerukwa. Kwa hiyo, tunaomba Mheshimiwa Waziri, zile

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

222

Taasisi hasa shule, Zahanati na Vituo vya Afya, basi kamakuna exemption ya kuweka umeme kwenye hizi Taasisi, basiMheshimiwa Waziri tunaomba majumuisho tuelezwe vizuri iliwananchi waelewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana nanaunga mkono hoja. Ahsante sana.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana.

MICHANGO KWA MAANDISHI

MHE. RHODA E. KUNCHELA: Mheshimiwa Naibu Spika,kuhusu wachimbaji wadogo wadogo; taarifa ya Kamati,imejikita na kuonesha faida na hasara zilizojitokeza wakatipesa za ruzuku zinatolewa kwa hawa vijana na vikundi vyao.Bado naona kuna haja ya Serikali kuhakikisha inazisimamiapesa hizi za ruzuku kwa wanufaika wa ruzuku hizi na kuwapasemina za kutosha.

Mheshimiwa Naibu Spika, mfano tu Mkoa wa Katavileo baadhi ya vijana (vikundi vya wachimbaji wadogowadogo) katika machimbo ya Isula, Milomo, Kapanda, Ibindi,Mtisi, Kampuni na Stalika, vijana hawa hawajapata mafunzona hivyo mikopo au ruzuku chache zilizopatikana walizitumiakwa matumizi yao binafsi.

Mheshimiwa Naibu Spika, uchache wa pesa ya ruzukukwa wachimbaji wadogo wadogo, Kamati imeshauriiongezwe kwa usimamizi maalum.

Mheshimiwa Naibu Spika, mazingira na manyanyasokwa vibarua wa wachimbaji wadogo wadogo; hawawanafanya kazi katika mazingira magumu sana bila waajiriwao kuwapatia vitendea kazi vyenye usalama katikamazingira magumu. Je, Serikali ina wachukulia hatua ganiwachimbaji hawa wanaoajiri hawa vibarua hususan katikamachimbo ya Ibindi, Kapanda, Mtisi na maeneo menginekama Isulamilomo?

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

223

Mheshimiwa Naibu Spika, vibarua hawawananyanyaswa na kunyimwa mishahara yao na wakihojikuhusu maslahi yao wanafukuzwa kazi kwa sababuwamehoji. Je, Serikali hii ya CCM imeshindwa kusimamiaunyanyasaji huu kwa vibarua wa wachimbaji wadogowadogo?

Mheshimiwa Naibu Spika, uchache wa utoaji waleseni kwa wachimbaji wadogo wadogo, usumbufuwanaopata wachimbaji hawa wanapofuatilia leseni zaokuna urasimu mkubwa sana kupitia Maafisa Madini waWilaya na Mikoa pamoja na Kamishna wa Kanda wa Madini,ni kwa nini leseni hizi zinatolewa kwa usumbufu mkubwa nakusababisha wachimbaji hawa kushindwa kufanya kazi zaona kupelekea kuporwa machimbo yao kumbewanacheleweshwa ili wanyang’anywe machimbo yao. Je,Serikali hamwoni kwamba jambo hili linakwamisha uchumi,nini mkakati wa Serikali wa kuhakikisha inaongeza watumishiwa madini i l i kuondoa usumbufu huu wa gharamawachimbaji kusafiri kutoka wilaya moja kwenda wilayanyingine, mkoa kwa mkoa, kufuatilia leseni zao. Maoni yaKamati yazingatiwe pia.

Mheshimiwa Naibu Spika, umeme wa REA Vijijini,changamoto za umeme vijijini ni kubwa na kama Kamatiilivyoshauri Serikali ihakikishe inasimamia uwekaji wa umemekatika vijiji vyenye vipaumbele si kubagua vijiji na kuvirukabaadhi ya vijiji hili jambo si sawa. Serikali iliangalie jambo hilikwa sababu upatikanaji wa umeme vizuri unapelekeauchumi kukua.

Mheshimiwa Naibu Spika, upatikanaji wa umemekatika Mikoa na Miji mfano, Dar es Salaam; mpaka sasaumeme Mkoa wa Dar es Salaam bado ni tatizo na Mikoamingine kama Katavi, Mbeya na Rukwa bado tatizo nikubwa. Je, Serikali haioni haja ya kuhakikisha Taifa linapataumeme wa uhakika, maji ya kutosha halafu ndio mjipangekwa ajili ya mabadiliko ya uchumi wa viwanda, Je, Serikalihaioni kuwa mnafanya kiini macho kuelekea uchumi waviwanda?

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

224

MHE. SILAFU J. MAUFI: Mheshimiwa Naibu Spika,nampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt. John Joseph Pombe Magufuli kwa uongoziwake wa kuwathamini wananchi kwa maendeleo yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Serikali kuonainapunguza gharama ya uzalishaji wa umeme kwa kutumiamafuta, kama ilivyo mikoa kadhaa ya nchi ikiwemo Mkoawa Rukwa, Katavvi na kadhalika. Tunaomba kuunganishwana gridi ya Taifa kwa sasa takribani mikoa yote. Mfano Rukwatunatumia mafuta na umeme wa kutoka Zambia. Hii harakatiya kuanzisha viwanda tunahitajika kuwa na umeme wakutosha na kukidhi haja.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mikoa ya Kusini kuna nafakaza kutosha, tunahitaji kuziongeza thamani, hivyo umeme nimuhimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia umeme REA III ufikishwekwenye vijiji na vitongoji vyote nchini, kwa hatua ya sasa,ikamilishwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuunga hojamkono.

MHE. MARY D. MURO: Mheshimiwa Naibu Spika,nipende kupongeza Kamati ya Nishati na Madini kwa taarifana kwa utendaji ambao umepelekea kudhibiti mianya yautoroshaji wa rasilimali yetu ya madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa kuiombaSerikali kuharakisha uchakataji wa gesi yetu ili iwezekupunguza shida ya nishati hii ambayo inasababisha ukatajimiti holela na hivyo kusabisha uharibifu wa mazingira.

Mheshimiwa Naibu Spika,nishauri Serikali kuharakishaulipaji fidia kwa wananchi mahali ambako miradi ya umemeinapita kwani imesababisha umaskini kwa jamii paleambapo wameweka X na kushindwa kulipa hivyokusababisha wananchi kushindwa kuendeleza.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

225

Mheshimiwa Naibu Spika, nishauri Serikali kupunguzaurasimu kwa wawekezaji wa miradi ya madini kwanikunawakatisha tamaa wawekezaji hao.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nishauri Serikalikuwawezesha wachimbaji wadogo wadogo kwa kuwapahitaji la muda mrefu kwani wameshindwa kupata patokubwa kutokana na vifaa duni wanavyotumia katikauchimbaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, nishauri Serikali kuangaliakwa upya juu ya Shirika la TANESCO kwa kulipunguzia mzigowa kufufua umeme, kusafirisha na kuuza kunakopelekeautendaji ambao ni mgumu na usiokuwa mzuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, nishauri elimu kwawachimbaji wadogo ili kusaidia kuwezesha kuchimba kwatija.

Mheshimiwa Naibu Spika, nishauri Serikali kulipamalipo ya TANESCO kwani inapunguza utendaji waTANESCO.

Mheshimiwa Naibu Spika, nishauri Serikali kujengamatenki ya Serikali ya kupokelea mafuta ili kudhibiti kwaurahisi upotevu wa mafuta unaopelekea Serikali kukosa kodihalisi ya mafuta hayo.

MHE. LUCIA M. MLOWE: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba kuchangia katika hoja hii kama ifuatavyo:-

Kwanza, naipongeza Kamati kwa ufuatiliaji wa miradimbalimbali na kwa ripoti nzuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, bei za gesi ziko juu sanampaka wananchi wanashindwa kununua gesi hiyo. NaombaSerikali ione ni namna gani bei zinapungua na kuwawezeshakununua kwa bei nafuu. Kwa namna nyingine watuwataendelea kuharibu mazingira kwa kukata miti hovyo kwaajili ya kutengeneza mkaa na kutumia kuni kwa ajili ya kupikia.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

226

Mheshimiwa Naibu Spika, Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO); nashukuru Serikali inajitahidi kupeleka umemehadi vijijini, lakini kuna tatizo limezuka la kukatika umemekila mara. Mfano, Mjini Njombe na baadhi ya maeneo hapaDodoma hasa eneo la Kisasa umeme unakatika mara kwamara.

Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba Serikali ionenamna gani inarekebisha miundombinu ya umeme ili usikatikemara kwa mara, iimarishe miundombinu kama transformerna nguzo na waya wa muda mrefu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Shirika la Maendeleo yaPetroli (TPDC); bei za mafuta zinapanda kila kukicha hiiinatokana na kuwa tunategemea kutoka nje maana sisihatuna matanki kwa ajili ya kuhifadhi mafuta hayo. NaiombaSerikali iweke matanki yake kwa ajili ya kuhifadhi mafutahaya ili bei ishuke.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ina madeniTANESCO; hii inasababisha uendeshaji unakuwa mgumu naShirika limekuwa likijiendesha kwa hasara. Serikali iwachukuliehatua watu wenye madeni sugu lakini pia Serikali yenyeweilipe madeni yake

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Naibu Spika,nachukua fursa hii kukushukuru wewe kwa kunipa nafasi hiiya kutoa mchango wangu katika taarifa ya shughuli zaKamati hii. Aidha, napenda kuwapongeza Wajumbe waKamati wote kwa kuandaa na kuiwasilisha kwa umakinikabisa taarifa hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuchangia taarifahii napenda kuchangia yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa usambazajiumeme vijijini; napenda kuwapongeza Serikali yetu kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

227

hatua na spidi nzuri ya kuwapelekea wananchi wa vijijinihuduma hii. Umeme kwa sasa sio tena luxury ila ni kitumuhimu kwa maendeleo ya nchi hii na wananchi. Hata hivyo,bado inaonekana kuwa kasi ya usambazaji umeme haiendisawa na kasi ya matumizi au uungaji wa huduma hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu katika sualahili Serikali iendelee kuwaelimisha wananchi wa vijijiniumuhimu wa huduma. Ni vyema vikaundwa vikundi vyakitaalam na kuwezeshwa il i waweze kwenda vij i j inikuwaelimisha wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia ni vyema kukawa namsamaha wa gharama za kuunga umeme kwa wateja waawali ili kuwahamasisha kujitokeza kwa wingi wananchi wavijijini.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.

MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Naibu Spika,napenda kuwapongeza Kamati ya Nishati na Madini kwataarifa nzuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na utekelezaji mzuriwa miradi ya REA, naungana na Kamati kupendekezakuwepo kwa usimamizi mzuri wa hii miradi ili iwe endelevukitaalam. Usambazaji kwa maeneo ya viji j ini, wayazinawekwa umbali mrefu na pia miundombinu ya nguzo zakawaida ni changamoto kutokana na mazingira ya vijijini.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kazi nzuriinayofanywa na REA, napendekeza Serikali iwe na mkakatiwa kuimarisha wataalam wa TANESCO ili waendane naongezeko na kasi ya usambazaji wa umeme kwa mpangowa REA. Kutokana na ongezeko la usambazaji wa umemekumesababisha kuzorota kwa huduma za dharura(emergency) hasa katika maeneo ya vijijini.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

228

MWENYEKITI: Tunaendelea na Mheshimiwa NaibuWaziri wa Nishati, Mheshimiwa Subira Mgalu; atafuatiwa naMheshimiwa Stanslaus Nyongo, Naibu Waziri wa Madini; naMheshimiwa Naibu Waziri Mheshimiwa Nditiye ajiandae.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana kwa nafasi uliyonipa nami niwezekuchangia taarifa ya Kamati ya Nishati. Awali ya yote,namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kibali chake nakuniwezesha kusimama ndani ya Bunge lako. Pia naishukurusana Kamati yetu ya Nishati na Madini kwa taarifa yake nzuriambayo iliwasilishwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile nawashukuru sanaWaheshimiwa Wabunge kwa michango yao mizuri hasakatika Sekta yetu ya Nishati kwa kuwa natambua kabisa nawao wana tambua kwamba sekta yetu ni mtambuka nawezeshi kwa sekta nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, zimejitokeza hoja nyingi,lakini naomba nijielekeze kwenye hoja ya umeme vijijini; nahapa naomba nijieleke kwenye miradi kama ambavyoWaheshimiwa Wabunge wamesema, kwamba miradi kunamiradi ya REA II ambayo pengine haikukamilika kwa namnamoja ama nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nilitaarifu Bungelako Tukufu kwamba Serikali imeshughulikia na ninavyosemasasa, Wakandarasi mbalimbali wameteuliwa kwa ajili yakutekeleza miradi REA II ambayo ilikwama. Hapa nasemeakwa Mkoa wa Kilimanjaro na Singida.

Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru sanaMheshimiwa Mbunge, Mama Anne Kilango Malecela nanimtaarifu katika Jimbo la Siha, Jimbo la Siha peke yakelilibakiwa na vijiji vitano tu ambapo REA II sasa ndiyovinakamilisha. Ndiyo maana naamini Mbunge yulealishawishika baada ya kuona Jimbo zima umeme upokasoro vijiji vitano, ambapo kama alivyosema Mheshimiwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

229

Mbunge, Mama Anne Kilango Malecela, Mkandarasi Njalitayupo site na anaendelea na kazi ya kukamilisha upungufuuliojitokeza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo, mikoambalimbali yote ambayo ina upungufu kwenye REA II,naomba nitaarifu Bunge lako Tukufu kwamba Wakandarasiwale walikuwa hawajamaliza kazi katika kipindi chauangalizi. Kwa hiyo, nawathibitishia, katika kipindi chauangalizi ni kwamba Wakandarasi watamaliza upungufuuliojitokeza; na kwenye REA III tunawaahidi kwambaupungufu hautajitokeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nilithibitishie Bungelako Tukufu kwamba Serikali ya Awamu ya Tano chini yauongozi wa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwenyesuala la nishati vijijini imejipanga vizuri. Ndiyo maana sasatumeanza safari ya vijiji vilivyosalia 7,873 na Wakandarasi. Nikweli kipindi cha miezi sita walikuwa na survey, lakinisambamba na hilo Wakandarasi katika kipindi hicho chotewalikuwa wameagiza vifaa.

Mheshimiwa Naibu Spika, mtakubaliana namikwamba Mikoa mbalimbali ambayo tumefanya ziaraWakandarasi wameanza kazi. Ninaposimama leo kusemandani ya Bunge lako Tukufu, yapo maeneo vijiji vimeshawashaumeme. Kwa mfano, Mkoa wa Geita, Rukwa, Tanga, Pwanina mikoa mingine, Wakandarasi wapo site na wanaendeleana kazi. Ndiyo maana tarehe 13 tulikutana nao tukawapamaelekezo mbalimbali ya namna ya kuanza miradi hii kwakasi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nalithibitishiaBunge Tukufu kwamba tumepokea changamoto ambazozimeelezwa. Tuwataarifu tu kwamba Wizara hii chini ya Waziriwangu tumejipanga vizuri katika usimamizi. Ndiyo maanakwa sasa ngazi ya Mkoa yupo Engineer pekee kwa ajili yamiradi ya REA; ngazi ya Wilaya yupo Technician kwa ajili yamiradi ya REA; na ngazi ya Kikanda yupo mtu wa REA kwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

230

ajili ya kusimamia miradi hii tu. Kwa hiyo, hii yote imefanywaili kuboresha usimamizi na kuona changamoto ambazolizijitokeza REA Awamu ya Pili hazijitokezi tena.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nilithibitishie Bungelako kwamba kwa sasa hata miradi ya Densfication ambayolengo lake ni kuvifikia vijiji 305 inaendelea vizuri katika maeneombalimbali. Sambamba na hilo, hata mradi huu ambaounaendana sambamba na REA III, huu wa Msongo wa KV400 wa Mikoa ya Iringa, Dodoma, Shinyanga na Tabora naounaendelea vizuri ambapo vij i j i 121 vitafikiwa namiundombinu ya umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niseme kamaambavyo Mheshimiwa Mama Anne Kilango amesema, ndaniya miaka miwili ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano,imeongeza usambazaji umeme kwa asilimia 28 miaka miwili;naamini na ninawathibitishia, kwa miaka ambayotumejipanga 2018/2019, 2019/2020 vijiji vyote vilivyosalia 7,873vitapata umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie; tulitoa maelekezokwamba kisirukwe Kijiji chochote, Kitongoji chochote, Taasisiya Umma yoyote, iwe Sekondari, iwe Shule ya Msingi, iweZahanati. Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge wamesema hilona sisi ndiyo mwongozo ambao tumetoa na nawaombaWakandarasi wafanye kama ambavyo Serikaliimewaelekeza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwanafasi hii, nawashukuru Waheshimiwa Wabunge wotena tunawaahidi Utumishi uliotukuka. Ahsanteni sana.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa StanslausNyongo, Naibu Waziri wa Madini atafuatiwa na MheshimiwaNaibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, MheshimiwaAtashasta Nditiye na Waziri Mheshimiwa Dkt. Kalemaniajiandae.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

231

NAIBU WAZIRI WA MADINI (MHE. STANSLAUS H.NYONGO): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwakunipa nafasi hii jioni ya leo. Kwanza kabisa natoa shukraniza dhati kabisa kwa Kamati ya Nishati na Madini kwa kazinzuri walioifanya. Kamati ya Nishati na Madini kipekee kabisatumekuwa tukipokea mchango mkubwa, ushauri maelekezombalimbali kutoka katika Kamati hii. Kwa kweli ushauri waotunaupokea na ni ushauri mzuri na tutaendelea kushirikianana Kamati hii kwa maana kuisukuma Sekta hii ya Madini iwezekusonga mbele.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile nawashukuru sanaWaheshimiwa Wajumbe 14 waliochangia, wametoamichango mizuri michango yenye mashiko. Namshukuru namama yangu Mheshimiwa Anne Kilango kwa complementaliyotupa. Kweli kabisa kwamba Wizara yetu imekuwaikikusanya maduhuli kwa hali ya juu. Tunapambana usiku namchana kuhakikisha tunakusanya maduhuli ambayotunayapeleka katika Mfuko wa Serikali na Watanzania wotewaweze kupata fedha au kupata huduma mbalimbalikutokana na makusanyo tunayokusanya kutoka katikaWizara yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli tunakusanyakwa kiasi kikubwa na ni mfano tuseme wa kuigwa kwasababu mpaka hapa tulipo tuko katika nusu ya mwaka wafedha wa kibajeti. Tumekusanya zaidi ya asilimia 80.4 yamaduhuli. Tunashukuru sana mama kwa kuliona hilo natunashukuru kwa pongezi ulizotupa; na tutaendelea kukazamsuli kuhakikisha kwamba tunaendelea kukusanya maduhuliili Watanzania wote waweze kupata huduma kutokana namapato yanayopatikana katika Sekta ya Madini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, michango mingiimeongelewa, nami napenda kuungana na waliochangiahasa katika ukurasa wa tano wa taarifa ya Kamati kuhusianana mradi wa Buckreef. Ni kwamba STAMICO iliingia mkatabana Buckreef na kampuni ya TAZAM 2000 wakatengenezaKampuni ya Bacliff ambapo STAMICO wanashikilia asilimia45.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

232

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kama ilivyosemaKamati tumelitazama hili, huyu mbia kwa kweli havutii natumeamua kuangalia kwa namna nyingine ambapoSTAMICO inawabidi wakae chini na wanasheria waweze ku-review mkataba huu ili tuweze kuangalia na ikiwezekanatutafute mbia mwingine ili STAMICO wahakikishe kwambayule mbia atayepatikana basi aweze kufanya kazi vizuri nauchimbaji uendelee na Serikali iweze kujipatia kipato. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna hoja nyingine ambayoimeongelewa kuhusu pesa za ruzuku pamoja na pesa zamikopo zilizokuwa zinatolewa na Wizara. Kweli kabisakwamba kuna watu walikuwa wanapokea ruzuku kutokaSerikalini, yaani kutoka Wizara ya Madini kupitia Benki ya TIB,walikuwa wanapata fedha kwa ajili ya kuendeleza migodi.Ilikuwa ni fedha maalum kwa kuendeleza wachimbaji. Kunawachimbaji wengine walifanikiwa, wamefanya vizuri sana.Kuna wachimbaji wengine wamekwama, lakini inaonekanakabisa walikuwa na juhudi za kufanya vizuri lakiniwamekwama. Wachimbaji wengine walichukua zile fedhana kwenda kuzitumia kwa matumizi mengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna wachimbaki tisa kwataarifa tulizonazo. Napenda kuchukua nafasi hii kuwaelezakwa mara mwisho, nilitoa tamko nikiwa Singida, warudishehizo fedha. Nachukua nafasi kusema kwamba nimetoa tenatamko la mwisho, wala sina haja ya kutoa siku nyingi, nikwamba ndani ya hizi siku 14 zinazofuata, wajisalimishewenyewe, wazirudishe hizo fedha kwa sababuwamewanyima Watanzania wengine kuweza kupata fedhahizo na kufanya shughuli za uchimbaji wakaweza kuendelezaSekta hiyo ya Madini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala la wachimbajiwadogo, Wizara imejipanga vizuri, sasa hivi tumeshatengazaidi ya heka za mraba laki 238 kwa ajili ya kuwapawachimbaji wadogo waweze kuchimba, lakini tunahakikishakwamba wachimbaji hao wadogo wakae ndani ya vikundi,tuwatambue tuwarasimishe wachimbe ili na Serikali nayo

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

233

iweze kukusanya kodi, maduhuli na Halmashauri husikaziweze kupata ushuru wa huduma (Service Levy).

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala la GSTlimezungumziwa. GST ndiyo Taasisi pekee ambayo inawezaikafanya kazi vizuri kwa maana ya kufanya tafiti mbalimbalina kuweza kuwasaidia wachimbaji wadogo kuwapatiamaeneo ambayo tayari yameshafanyiwa utafiti, yana taarifaza kutosha kwa maana maeneo ambayo yana dhahabu yakutosha au madini mengine ambayo tayari yamefanyiwautafiti wa kutosha ili kuepusha wachimbaji kuchimba kwakubahatisha. Tumejipanga na GST na kuja kuleta taarifa hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kumalizia. Kwamigogoro iliyopo, tunaifanyia kazi na hasa ule mgogoro waNorth Mara na watu wa Nyamongo, maongezi yanaendelea.Taratibu zinafanyika na makundi yote tunayashirikisha.Tunachotaka ni Serikali itatue mgogoro wa Nyamongo iliwachimbaji waendelee na wananchi waendelee na shughulizao za ujenzi wa Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, namalizia kwa kusemakwamba Kamati imeshauri kwamba kuna wachimbaji waKitanzania tuwape maeneo, akiwepo mchimbaji waBusolwa. Tunahakikisha mchimbaji huyo tunampa eneo iliaongeze muda wa mgodi, Watanzania waneemeke na ajirakatika mgodi huo na Serikali tuendelee kupata kodi kutokakatika mgodi huo kwa sababu mgodi huo unafanya kazi.Hakuna haja ya kumnyima eneo ambalo tunadhani Serikalitunaweza tukampa na kukamsaidia mchimbaji mdogo nawa kati.

Mheshimiwa Naibu Spika, Watanzania wengine wotewanaotaka kuwekeza katika Sekta ya Madini, tuko tayarikuwasaidia kuwapa maeneo mazuri wachimbe na tutawezakuwasaidia kwa namna ambayo watatoa ajira kwaWatanzania wengine…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

234

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Nyongo.Mheshimiwa Atashasta Nditiye, Naibu Waziri wa UjenziUchukuzi na Mawasiliano, halafu Mheshimiwa Dkt. Kalemani,tutamalizia na Mheshimiwa Waziri Profesa Mbarawa.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwanafasi ya kuweza kuchangia hotuba ya Mwenyekiti waKamati ya miundombinu. Kwanza nachukua nafasi hiikuwashukuru sana Wajumbe wote wa Kamati yaMiundombinu kwa taarifa yao nzuri kabisa ambayo imetupamwongozo kama Serikali katika kutekeleza majukumu yetu.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nawashukuru Wajumbewote kwa ushauri mbalimbali ambao mmeendelea kutupatiaambao umetuimarisha katika kutekeleza majukumu yetu.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa muda wenyewesiyo rafiki sana, nitajikita moja kwa moja kwenye suala laMamlaka ya Viwanja vya Ndege. Tulipata maelekezo naushauri mzuri sana kutoka kwa Kamati kuhusu namna yakuweka mipaka kwenye viwanja vyetu ambavyo kwa kwelivinavamiwa. Nakiri ukweli kwamba viwanja vyetu vingi sanavinavamiwa na Watanzania aidha, kwa kujua au wakatimwingine kwa kutojua. Tumeendelea kuwasiliana namamlaka zinazohusika kuhakikisha kwamba viwanja vyetuvinabaki salama.

Mheshimiwa Naibu Spika, nachukua nafasi hiikuwashauri Watanzania, kabla hawajafanya maendelezo yasehemu yoyote waliyopata nafasi ya kiwanja karibu na Taasisiza Kiserikali ni vizuri sana wakawasiliana na mamlakazinazohusika kabla ya kuweka maendelezo ya kudumu. Kwaupande wetu Serikali, sasa hivi tunajiandaa na tunatengenezaKitengo maalum cha Real Estate kwa mamlaka ya viwanjavya ndege ambacho kitafanya kazi ya kufuatilia viwanjavyetu vyote kubaini mipaka yetu yote na kufuatilia kupata

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

235

hati. Kwa sababu bila kutengeneza Kitengo hicho cha RealEstate tutapata matatizo kidogo katika kufuatilia hizo hati.

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie kidogo kuhusuMamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Nashukuru sanakwa pongezi ambazo Kamati wametupatia, tunazipokeakama Serikali na tunakiri kwamba TCRA kwa kweli inafanyakazi nzuri sana kuhakikisha kwamba ina-regulate masualaya mawasiliano hapa nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, naendelea kuishauri TCRAna tunaielekeza kabisa kwamba wale wamiliki waving’amuzi binafsi ambao wanatakiwa watoe channel zabure kwa Watanzania watekeleze. Kama hawatatekelezakwa wakati unaotakiwa, basi TCRA ijipange kuwachukuliahatua stahiki ili Watanzania waendelee kupata huduma zafree chanel kama leseni ya wale watoa hudumainavyowataka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitajikita vilevile kwa sualala TTCL. Kwanza nitoe shukrani za dhati kwa ushauri wakuimarisha TTCL ambao umetolewa na Kamati.Tunawashukuru kwanza kwa hatua mliyoichukua ya kui-support Serikali katika uanzishaji wa Shirika la MawasilianoTanzania (TTCL). Tunawashukuru kwa jinsi ambavyommeendelea kuipigania iweze kuwa imara. Huo ni moyo wakizalendo ambao kwa kweli sisi Serikali tunaunga mkono;na tunaishukuru sana Kamati kwa jinsi ambavyomnaipambania TTCL.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi TTCL inatengenezamuundo wa shirika. Baada ya hapo shirika limeshafunguliwakama Shirika la Umma. Hivi sasa inaendelea na shughuli zakimkakati. Kwa mfano, sasa hivi ninayo furaha kueleza Bungelako Tukufu kwamba kuna mkakati ambao TTCL unaendeleanao wakishirikiana na TANROAD wa kuhakikisha mizani yoteTanzania inawekewa vifaa maalum au inaunganishwa namkongo wa Taifa kuhakikisha kwamba malipo yoteyanayofanyika magari yote yanayopita yanaonekana kuanziaMakao Makuu ya TANROAD na hata Wizarani.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

236

Mheshimiwa Naibu Spika, kupitia mradi huutunategemea kutekeleza kwa awamu mbili. Awamu yaKwanza tumeanza na Vituo 19. Mpaka sasa hivi ninapoongeaVituo 14 vimeshaunganishwa na mkongo wa Taifa, ambapokila gari inayopita inaonekana lakini ina uzito unaoongezekaunaonekana. Kwa maana hiyo, hata chargewanayochangiwa kikawaida inaonekana moja kwa mojakwenye mitandao.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunategemea kwakutekeleza mradi huu, mapato ya Serikali hayatapotea, lakiniile human intervention tutaipunguza kwa kiwango kikubwasana. Kwa sababu ni kweli kwamba kupitia kwenye mizaniSerikali tumekuwa tukipoteza mapato. Njia rahisi kabisaambayo tumeona ni ya kutufaa ni kuanzisha hii systemambapo TTCL wameonesha uwezo mkubwa sana katikakuitekeleza.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile mfumo huu utawezaku-share na mifumo mingine ya TANROADS ambapo ni mifumokama ya fedha, mifumo ya emails, hata rasilmali watu. Katiya vituo hivyo tunaamini kabisa tutakapoingia awamu yapili tutatekeleza na vituo vingine vitakavyofuata il ikuhakikisha kwamba mapato yote ya Serikali hayapoteikupitia mizani.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Nditiye muda wakoumekwisha. Ahsante sana kwa mchango wako. MheshimiwaDkt. Kalemani, Waziri wa Nishati. (Makofi)

WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, naminiungane na wenzangu kushukuru sana kwa kunipa fursa hiiili niweze kuchangia Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Nishatina Madini, lakini kwa upande wa Nishati. Kwanza,nampongeza Mheshimiwa Naibu Waziri, ameeleza kwa kiasi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

237

fulani mipangilio yetu kuhusiana na miradi ya umeme vijijini.Nami nampongeza sana Mheshimiwa Naibu Waziri wangu.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa, naishukurusana Serikali ya Awamu ya Tano jinsi inavyotoa pesa zakutosha katika kutekeleza miradi ya REA awamu ya tatu. Kwatakwimu tulizonazo katika kipindi kama hiki, mwaka wafedha 2015/2016, tulipata asilimia 78.8 katika kipindi kamahiki cha miradi ya REA awamu ya tatu. Katika kipindi chamwaka 2016/2017, tulipokea asilimia 79.3, kwa hiyo,tuliongeza asilimia moja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitoe taarifa mbele yaBunge lako Tukufu katika kipindi hiki cha nusu ya mwaka,tumepokea asilimia 81.3. Kwa niaba tu ya Wizara yangu nawengine, nichukue nafasi hii kuishukuru sana Wizara yetuinavyoshirikiana na Wizara ya Fedha pamoja na Serikali yaAwamu ya Tano. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niwape tu uhakikawananchi na Waheshimiwa Wabunge kwamba kwautaratibu huu, tuna uhakika mkubwa kwamba miradi hiiitatekelezwa kwa asil imia mia moja ndani ya mudamliotupatia na sisi tutafanya kazi kwa nguvu zote kuhakikishakwamba kazi inakamilika kwa wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumetaja mikoa ambayotumeshaanza kutekeleza, lakini nichukue nafasi hii kuwaelezawananchi na Waheshimiwa Wabunge, mpaka sasatumeshawasha umeme vijiji 24 chini ya mpango huu mpyawa REA awamu ya tatu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru sanaMheshimiwa Heche. Nitoe tu taarifa kwamba kwenye Jimbolake tumeshawasha Kijiji cha Nyangere kwenye Jimbo lake.Kwa hiyo, tayari tumeshamwashia umeme kwenye ile awamuya tatu. Hata kule Butiama tumeshawasha umeme Masusura;kule Mwanza tumeshawasha Ipanga na Nguge; Geitatumeshawasha Nyangomango; kule Mtwara tumewasha

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

238

Nalingo; kule Arusha tunawasha Didigo; tunakwendakuwasha kijiji hadi kijiji. Kwa hiyo, nitoe taarifa kwambatunakwenda vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumze kidogo kwenyesuala la madeni ya TANESCO. Nami nawapongezaWaheshimiwa Wabunge kwa kuunga mkono kwamba Shirikaletu kwa kweli linahitaji kupewa msukumo wa aina yake.Nazipongeza pia Taasisi za Serikali ambazo zil ikuwazinadaiwa kwa kiasi kikubwa, zimeanza kulipa madeni yake.Kwa hiyo, nawapongeza sana Waheshimiwa Wabunge jinsimnavyosukuma kwenye Halmashauri zenu, kiasi ambachosasa tumeanza kupata mapato mazuri kutoka kwenye Taasisiza Maji, Jeshi letu, Mambo ya Ndani na Taasisi nyingine zaSerikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, mpaka sasa deni kidogolimepungua. Lilikuwa shilingi bilioni 297, sasa limebaki shilingibilioni 277. Kwa hiyo, ni maendeleo makubwa. Nawaombatu Waheshimiwa Wabunge kupitia kwenye taasisi zetu, basituendelee kuliunga mkono Shirika letu ili liweze kuwahudumiavizuri na kwa asilimia ambazo wananchi wetu wanamatarajio nalo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumze kidogokuhusiana na mradi wa Stieglers. Mheshimiwa Hecheamezungumza kwamba tumeanza kuutekeleza. Niseme tu,utekelezaji wa mradi wa aina yoyote una hatua zake. Hatuaya kwanza ya kawaida ya kutekeleza mradi ni maandaliziya mradi. Hatua ya pil i ni kufanya matayarisho yamiundombinu wezeshi kutekeleza mradi; na hatua ya tatu niya kujenga mradi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa tunachofanya nikuandaa na kutayarisha mazingira wezeshi ya kuutekelezamradi huo kabambe. Ndiyo maana hivi sasa kwa upandewa miundombinu ya umeme tumeanza kujengamiundombinu ya umeme kupitia Shirika letu la TANESCOambalo bajeti yake ilipita katika mwaka wa fedha huu

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

239

tunaoendelea nao. Shilingi bilioni 7.7 zilipitishwa kwa ajili yamiradi ya Morogoro; na mradi unaojengwa sasa kwenda kuleni kupitia bajeti ya Serikali kupitia TANESCO. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hapo tutafanyautaratibu na tunaendelea na utaratibu sasa wa kutangazatenda. Tutakapoukamilisha, ndipo sasa tutajua ni kiasi ganina utekelezaji wa mradi huo utaanza na taratibu za kawaidaza kibajeti kuja kwenye Bunge lako Tukufu zitafuatwa.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, niseme tukwamba bado maandalizi yanaendelea, lakini nawaombawananchi na Waheshimiwa Wabunge tuunge mkono juhudiza Serikali za Mheshimiwa Rais za kuujenga mradi huu kwasababu utatutoa kwenye shida za upungufu wa umeme nakuwa na umeme wa uhakika wa kujenga uchumi waviwanda tunaotarajia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo,nizungumze kidogo kuhusiana na miradi ya umeme kuleMtwara na Lindi. Nawapongeza sana WaheshimiwaWabunge wa Mtwara na Lindi kwa jinsi ambavyo mweziNovemba tulikuwa na shida kidogo, lakini tuliunganapamoja, mwezi Novemba Mtwara tulibaki na mashine tatuzinazofanya kazi hadi kufika Novemba, 2017. Hata hivyo,nitoe taarifa kwa Waheshimiwa Wabunge kwamba hivi sasamashine zinazofanya kazi kwa Mtwara na Lindi, mashine zotesasa tisa sasa zinafanya kazi. Zimekarabatiwa, zinafanya kazivizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niungane na MheshimiwaMbunge wa Mtwara kwamba mliomba mashine mbili mpya,tumeshazileta na zimeshaanza kufungwa. Ni matarajio yetundani ya miezi miwili nazo zitakamilika. Kwa hiyo, Mtwarana Lindi tutaanza kupata umeme wa megawatts nne zaziada. Kwa hiyo, naipongeza sana Serikali yetu naWaheshimiwa Wabunge mnavyotuunga mkono katikajitihada hizi.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

240

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu ya muda tuniseme; kweli kabisa katika Mikoa ya Ruvuma na Mtwaratuna changamoto ya miundombinu, lakini tunaendeleakukarabati na kujenga miundombinu mingine mipya. KatikaMikoa ya Sumbawanga, Kigoma pamoja na Katavi ni kwelitunatumia mafuta mazito kwa sasa, lakini Serikali Tukufukupitia Bunge hili katika bajeti ya mwaka huu mlituidhinishiashilingi bilioni 13.2 kwa ajili ya kujenga umeme mkubwa wakilovolts 400 wa kutoka Sumbawanga kwenda Mpanda,Kigoma, Nyakanazi, Geita mpaka Bulyanhulu. Hivi sasautekelezaji umeshaanza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kipande cha Geita –Nyakanazi, Mkandarasi yuko site ameshaanza ujenzi; kwakipande cha Bulyahkhulu kwenda Geita Mkandarasi yuko site,ameshaanza ujenzi na kwa kipande cha kutoka Mbeyakwenda Sumbawanga, Mkandarasi taratibu za kwanza zakufanya survey anakamilisha; na kufika Julai mwaka huuataanza ujenzi rasmi. Kwa hiyo, upande wa Sumbawanganapo utapata umeme mkubwa wa kilovolts 400 kwa ajili yaujenzi wa uchumi wa viwanda vyetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, labda la mwisho kwasababu ya muda nizungumze kidogo kuhusiana na suala labei za umeme wa REA pamoja na TANESCO. Bei ya umemekijijini ni Sh.27,000/= basi, hakuna bei zaidi ya hapo. Kwa miradiya TANESCO ambayo iko katika Mitaa na katika Halmashauriza Mijini ni Sh.177,000/= basi. Hizi ni bei ambazo Serikali kwakiasi kikubwa imechangia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nichukue nafasihii bado kuipongeza Serikali. Hakuna nchi kwa nchizinazoendelea zenye gharama ya umeme Sh.27,000/= hatavijijini, hakuna. Tanzania ni bei yetu ya kwanza. Kwa hiyo,naipongeza sana Serikali kwa utaratibu huo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hakuna mteja anayelipianguzo. Ni vizuri nikaliweka bayana suala hili. Gharama zaumeme wananchi tunachangia. Gharama ya kununua nguzomoja ni Sh.200,000/= hadi Sh.250,000. Sasa kama ingekuwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

241

ni kulipia nguzo ingekuwa gharama kubwa sana.Kinachofanyika ni kutoa huduma kwa umbali wa hudumazinazoweza kupewa kwa mteja, lakini siyo kulipa nguzo. Kwahiyo, nguzo hazilipiwi, ni kuchangia juhudi za Serikali katikakutandaza umeme.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,nimalizie tu na kusema kwamba, kwa vile sasa hivitunatekeleza miradi ya umeme vijijini, niwaombe sanaWaheshimiwa Wabunge, lengo letu ni kupeleka umeme kijijikwa Kijiji, Kitongoji kwa Kitongoji, nyumba kwa nyumba,taasisi kwa taasisi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nawaombaWaheshimiwa Wabunge katika Taasisi za Ummamuwashawishi na kuwashauri Wenyeviti wa Halmashauriwaanze kutenga fedha kidogo ili kuzifikishia taasisi zetuumeme. Haipendezi na siyo matarajio ya mradi, nguzokuning’inia karibu na Taasisi ya Umma halafu Taasisi ya Ummaisipate umeme ndani ya nyumba. Kwa hiyo, nichukue nafasihii kuwaelekeza na kuwashauri Waheshimiwa Wakurugenziwalipo waanze kufanya hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho nachukua nafasihii kuwaagiza Wakandarasi popote walipo,tumeshawaelekeza, mwisho wa kuanza kazi ambaohawajaanza ni tarehe 2 Machi, lakini kwa kiasi kikubwawameshaanza kutekeleza.

Mheshimiwa Naibu Spika, nachukua nafasi hiikukupongeza kwa kunipa nafasi hii. Ahsante sana. Nashukurukwa kunisikiliza (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa ProfesaMakame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi naMawasiliano.

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO:Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote nami napendakuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

242

rehema kwa kutujaalia kufanya shughuli zetu tukiwa na afyanjema.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuishukuru sanaKamati yangu ya Miundombinu kwa taarifa nzuri na kwamwongozo mzuri. Nachukua fursa hii kuunga mkono taarifaya Kamati ya Miundombinu. Naomba niwahakikishie tuKamati yetu kwamba maelekezo yote waliyotoatutayatekeleza kwa maslahi ya Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzina Mawasiliano katika mwaka wa fedha 2017/2018,tulitengewa shilingi trilioni 4.5. Fedha hizi tumezitumia kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa Sekta ya Uchukuzi kwaupande wa Bandari; Bandari yetu ya Dar es Salaam imeanzakuimarika vizuri kwa sababu sasa hivi tumeongeza uadilifumkubwa na tumejipanga katika kuboresha miundombinu.Kwa taarifa tu, katika mwaka wa fedha 2016/2017, tani milioni14.7 zilipita kwenye Bandari ya Dar es Salaam. Katika kipindicha miezi minne kutoka Julai mpaka Septemba, miezi mitatu,quarter ya mwanzo, mizigo ya nchi za jirani imeongezekakutoka tani milioni 1.16 mpaka tani milioni 1.479. Hiiimetokana na kujipanga vizuri na wafanyakazi wetu kufanyakazi kwa uadilifu mkubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa mapato,mwaka 2016/2017, Bandari ya Dar es Salaam au Bandari zotezilitengeneza karibu shilingi bilioni 734.9 wakati matumiziyalikuwa shilingi bilioni 446. Salio lilikuwa ni shilingi bilioni 288.Kwa quarter ya kwanza kuanzia mwezi Julai mpakaSeptemba mwaka 2017/2018, Bandari ya Dar es Salaamimekusanya mapato ya shilingi bilioni 207.5 wakati matumizini shilingi bilioni 67. Inaonesha sasa Bandari ya Dar es Salaamimejipanga kuhakikisha kwamba hata matumizi yenyewewanapunguza kwa kiasi kikubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, matokeo yake ni kwambapato halisi ni shilingi bilioni 139.6. Hii ina maana, kama

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

243

tutaendelea namna hii, itakapofika mwisho wa mwaka wafedha huu, bandari itaweza kuwa na mapato halisi takribanshilingi bilioni 450. Haijawahi kutokea katika historia ya bandarizetu za Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mambo haya yote hayakujabure, yamekuja kutokana na miundombinu ambayo sasa hiviinaendelea hapo Bandari ya Dar es Salaam. Tukianzia Bandariya Dar es Salaam sasa hivi, tuna mradi mkubwa wauboreshaji wa gati ya kwanza mpaka gati namba sabaambayo tutatumia takriban shilingi bilioni 336. Kazi kubwainayofanyika ni kuongeza kina cha maji kwenye bandari hiyo,pia na kuboresha bandari yenyewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, mara baada ya ukarabatihuo, tutahakikisha sasa meli kubwa zenye uwezo wakuchukua kontena 19,000 za tani 20 zinaingia Bandari ya Dares Salaam bila matatizo yoyote. Tunaamini tukifanya hivyo,tutaweza kushindana na bandari zote zilizopo katika maeneoya jirani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hatukusimama hapo tu,lakini hata Bandari ya Mtwara tuna mradi ambao sasatunajenga gati jipya lenye urefu wa mita 350 ambalo lenyewelitagharimu shilingi za Kitanzania bilioni 149 na Mkandarasiyuko kwenye site na kazi inaendelea. Hatukusimamia hapo,lakini tumeendelea na ujenzi wa matishari ambayo tuyatumiakwa ajili ya kupeleka mizigo katika bandari zetu za kule Kyelana maeneo mengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kuna mradi wa ununuziwa scanner ambapo tayari sasa scanner nane zimefika Dares Salaam. Kwa mara ya kwanza katika Bandari ya Dar esSalaam mwaka huu tumeingiza scanner maalum kwa ajiliya reli. Pia tumeingiza scanner nyingine nne (mobile scanners)pamoja na scanner nyingine tatu ambazo gharama yake nishilingi bilioni 52.2. (Makofi)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

244

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu flow meter, kazitunaendelea nayo ya utaratibu wa ununuzi wa flow meterna hivi karibuni manunuzi hayo yatakamilika.

Mheshimiwa Naibu Spika, huwezi kuwa na Bandariimara kama huna usafiri wa barabara imara. Kwa kulijuahilo, Serikali ya Awamu ya Tano tumeanza ujenzi wa reli yakiwango cha standard gauge. Awamu ya kwanza imeanzaDar es Salaam mpaka Morogoro yenye urefu wa kilometa300. Treni hii ni ya kipekee katika nchi za Afrika ya Masharikina Kati. Treni hii itatumia umeme na itakuwa inakwendamwendokasi wa kilometa 160 kwa saa. Itakuwa na uwezowa kubeba tani milioni 17 kwa mwaka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huu utagharimutakribani shilingi za Kitanzania trilioni 2.7. Jumatano hii Munguakipenda, Wajumbe wa Kamati ya Bajeti na Kamati yaMiundombinu watatembelea eneo la ujenzi; na nawatakaWajumbe hawa watembelee usiku, ndiyo unaona raha yaujenzi, siyo mchana. Pale watu wanafanya kazi saa 24 kwawiki, siku saba.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitafurahi kamaninavyosema; na nimemwalika hapa Mheshimiwaatembelee lakini atembelee usiku, siyo mchana, kwa sababuusiku ndiyo utaona ile raha ya ujenzi wenyewe. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeanza awamu ya pili.Awamu ya pili inaanzia Morogoro mpaka Makutupora yenyeurefu wa kilometa 442. Wiki iliyopita Serikali ililipa advancepayment, yaani malipo ya awali dola za Kimarekani milioni215 sawa na shilingi bilioni 483. Wakati wowote mwezi huututaweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa kutoka Morogorompaka Makutupora ili kazi iendelee. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2020 ifikapo mweziJuni, Watanzania wataanza kufurahia treni ya kisasa kutokaDar es Salaam mpaka Dodoma ambapo sasa watatumia

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

245

masaa mawili na nusu mpaka masaa matatu kutoka Dar esSalaam mpaka Dodoma. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kazi haikuishia hapo tu,tunaendelea na mpango wa kuanzia Makutupora mpakaTabora, Tabora - Isaka, Isaka – Mwanza. Tunatoka Tabora –Kigoma – Uvinza - Msongati. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wiki mbili zilizopita, wenzetuwa Rwanda walikuja hapa na tuliweka makubaliano sasaya kujenga reli ya kisasa kutoka Isaka mpaka Kigali yenyeurefu wa kilometa 521 na tunategemea jiwe la msingilitawekwa mwezi Oktoba mwaka huu, kwa vile tumejipangavizuri kuhakikisha kwamba Bandari ya Dar es Salaamtunaiboresha kwa miundombinu ya aina yoyote ili kuhakikishakwamba mambo yanakwenda vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa usafiri waanga; ili anga zetu ziwe salama tunajipanga tunanunua radarnne za kisasa ambapo radar moja itafungwa Dar es Salaam,moja itafungwa Mwanza, moja itafungwa Mbeya nanyingine itafungwa Kilimanjaro. Hiyo imegharimu takribanshilingi za Kitanzania bilioni 63. Tunafanya hivyo kwa sababutunapoteza mapato mengi kwenye sehemu ya madini, watuwanaingia na ndege ndogo hatuwezi kuona.

Tunaamini sasa, tukiweka radar hizo za kisasa ndegeyoyote itakayoingia Tanzania hasa ndege hizi za kiraia,tutaweza kuiona na tutakusanya mapato yanayostahili.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa viwanjavya ndege; tunaendelea na ujenzi wa jengo la abiria paleDar es Salaam ambalo litakuwa na uwezo wa kuchukuaabiria milioni sita ikilinganishwa na jengo la abiria terminal IIlenye uwezo wa kuchukua abiria milioni mbili na nusu. Jengohili litagharimu shilingi takriban bilioni 560 litakapomalizika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa wakati mmoja kwenyejengo lile zitaweza kukaa ndege 22 kwa wakati mmoja. Kwakweli ni jengo la kisasa ambapo kazi inaendelea na ujenzi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

246

umefika asilimia 70. Kwa upande wa Mwanza, tumetengatakriban shilingi bilioni 110 ambapo tunajenga runway namaegesho mengine kuhakikisha kwamba uwanja waMwanza sasa unakuwa uwanja wa Kimataifa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa uwanjawa Shinyanga tumetenga shilingi bilioni 49.18 na Mkandarasitumeshampata kwa ajili ya ujenzi. Kwa upande wa uwanjawa Sumbawanga tumetenga shilingi bilioni 55 na Mkandarasitumempata. Kwa upande wa uwanja wa Songwe vile viletumetenga bilioni 17 na kazi inaendelea. Uwanja wa Musoma,Songea na Iringa tayari tunahangaika kuwatafutaWakandarasi kuhakikisha kwamba nako mamboyanakwenda vizuri. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Waziri.Naona kwa sababu umeshataja viwanja vyote vya ndegehapo, Waheshimiwa Wabunge tumeshakuelewa. Kwa hiyo,muda wetu umekwisha. Naona bado umesimama, nakupadakika moja.

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO:Mheshimiwa Naibu Spika, naomba tu niwahakikishieWaheshimiwa Wabunge kwamba Serikali hii imejipangakuunganisha mikoa yote ya Tanzania kwa kiwango cha lami.Sasa hivi kuna mradi unaendelea kutoka Katavi mpakaTabora ambapo Serikali itatumia shilingi bilioni 770. Huu nimradi mkubwa na tutajenga barabara ya kisasa. Pia kunamradi unaendelea baina ya Katavi na Kigoma, Kigoma -Kagera, Kigoma - Tabora na mengineyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana nanaunga mkono hoja ya Kamati yangu ya Miundombinu.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Waziri kwahabari njema hizo. Waheshimiwa Wabunge, sasa nitawaita

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

247

watoa hoja, tutaanza na Mheshimiwa Profesa NormanSigalla, Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu ili ajeahitimishe hoja yake.

MHE. PROF. NORMAN A. S. KING - MWENYEKITI WAKAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU:Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nawashukuru sanaWaheshimiwa Wajumbe wote ambao wametoa michangoyao. Naomba uniruhusu niwatambue kwa majina hasa waleambao wameandika, kwa sababu wale ambaowamechangia hapa ndani wote mliwaona.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kumshukuruMheshimiwa Ritta Kabati, Mheshimiwa Shelukindo,Mheshimiwa Oran Njeza, Mheshimiwa Juma Othman Hija,Mheshimiwa Aida Joseph Khenani, Mheshimiwa Eng. RamoMakani, Mheshimiwa Rhoda Edward Kunchela, MheshimiwaSilafu, Mheshimiwa Mashimba Ndaki, Mheshimiwa Mary DeoMuro, Mheshimiwa Lucia, Mheshimiwa Zainab na MheshimiwaLucy Owenya.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuwekakumbukumbu sawasawa, nadhani ni Mheshimiwa Shekilindibadala ya Mheshimiwa Shelukindo. Umetaja Shelukindohapo, nadhani ni Mheshimiwa Shekilindi. Sasa sema ilikumbukumbu rasmi za Bunge ziwe na jina linalotuhusu kwasasa.

MHE. NORMAN A. SIGALLA KING - MWENYEKITI WAKAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU:Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na michango mingi yaWabunge pia nichukue nafasi hii kipekee kuwapongezaMawaziri kwa maana Waziri Mheshimiwa Profesa Mbalawapamoja na Naibu wake kwa michango yao kwenye hoja hii.Nitoe ufafanuzi katika mambo machache. KwanzaWaheshimiwa Wabunge wote waliochangia wameipongezaSerikali ya Chama cha Mapinduzi kwa kazi kubwa inayofanya,nasi tunapokea pongezi hizo. Pia wengi wameongeleaumuhimu wa kuunganisha barabara za lami, nashukurukwamba Mheshimiwa Wazirri amefafanua vizuri jambo hilo.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

248

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kuna hoja ya kuangaliauwezekano wa kuunganisha barabara za mikoa, nashukuruMheshimiwa Waziri pia ametoa ufafanuzi mkubwa kwenyehilo. Pia kuna hoja ya uwanja wa Chato na pia hoja yakujenga uwanja Mkoa wa Mara; nafikiri haikujibiwa na nivizuri nitoe ufafanuzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni vizuri WaheshimiwaWabunge na Bunge lako lifahamu; mimi nimeshiriki kwenyeuwekaji wa jiwe la msingi uwanja wa Chato. Shilingi bilioni39 zilizotajwa ni gharama za ujenzi mradi ukikamilika.Kilichofanyika Chato ni kuweka jiwe la msingi. Kuhusu fedhaza bajeti kwa mwaka huu wa fedha kwa mfano, 2018/2019,wale Wajumbe watakaokuwa kwenye Kamati yaMiundombinu wataona bajeti hiyo. Kinachoonekana sasa nikama vile umeshajengwa. Haujajengwa, tulichofanya nikuweka jiwe la msingi. Hilo ni la kwanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, pia aliuliza vizuri rafikiyangu, Mbunge wa Sengerema kwamba kwa nini uwanjahaujajengwa Mkoa wa Mara? Je, kwa nini Serikali inapelekanguvu upande wa Chato?

Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabunge naBunge lako Tukufu, ni vizuri watu wafahamu, mpaka MwalimuNyerere anatoweka tarehe 14 Oktoba, 1999 viwanjaambavyo vilikuwa vimejengwa Tanzania hii ni vichache sanana hasa viwili vikubwa ni uwanja wa KIA na uwanja wa Dares Salaam. Viwanja vingine vya Kigoma na Tabora nakwingineko, wote tulikuwa tunatua na ndege kwa mashaka,siyo kwa kujengwa. Kwa hiyo, lawama ziende kwa nani?

Mheshimiwa Naibu Spika, Rais Dkt. Magufuli ameingiawakati Mheshimiwa Rais wetu Mwasisi wa nchi hiialishaondoka katika nchi hii. Kwa hiyo, siyo sawa hata kidogokwa hekima yote ile kupeleka lawama kwa Rais wa Awamuya Tano wakati, Rais wa Awamu ya Pili alikuwepo, ya Tatualikuwepo, ya Nne alikuwepo na muda huo viwanjahavikujengwa kwa sababu ya uwezo wa uchumi kuwamdogo.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

249

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu utangazaji wa tendalabda nayo niifafanue kidogo. Ni vizuri Bunge lako Tukufulikafahamu, utangazaji wa tenda wa viwanja au miradimingine ya Serikali imegawanyika katika sehemu kuu mbili;unaweza ukafanya kitu kinachoitwa open tender kwamaana ya kwamba unatafuta Mkandarasi wa ujenzi wauwanja au jambo lolote ndani ya Serikali au restricted tender.

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati gani unatumiarestricted tender? Ni pale ambapo Wakandarasi ambao tayariunao wanafanya miradi mingine; unataka mradi mwingineunaofanana na kazi ambazo tayari Wakandarasi wapo,unataka utekelezwe. Badala ya kupoteza muda kufanyaopen tender, unafanya kitu kinachoitwa restricted tender, kwamaana ya kwamba unachagua katika wale ambao tayariwapo na unaangalia nani mwenye bei ndogo halafuunampa kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Procurement Act iko wazina wala siyo kwamba ni jambo linafanywa kwa kificho, likowazi kwenye kufanya hivyo, kwa hiyo, chochoteutakachofanya katika hivyo, ni sahihi. Kwenye Halmashaurizetu tunafanya hivyo na kwenye Serikali Kuu tunafanya hivyopia.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitumie dakikachache kupongeza kwa dhati taasisi ambazo Kamati hiiinazisimamia. Nianze na taasisi kama TCRA; siwezi kuzitajazote 37 na CEOs kokote waliko wajue kwamba nazitaja hizitu kama mfano. TCRA, Kamati iliagiza kwamba watekelezeutaratibu wa TTMS ili tuwe na hakika ya mapato ambayoSerikali inapata. Wameshirikiana na wenzao wa TRA na sasakazi inafanyika vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati ilielekeza TPAkwamba wajaribu kurekebisha kero za Bandari ya Dar esSalaam ikiwa ni pamoja na ucheleweshaji na sikuzinazochukuliwa katika kupakua na kupakia pamoja na tozombalimbali. TPA wamerekebisha jambo hilo na sasa mamboyamekwenda vizuri.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

250

Mheshimiwa Naibu Spika, wanaoagiza mizigo kwakutumia Bandari ya Dar es Salaam kwa sasa watakuwa nimashuhuda kwamba hata vitu vilivyokuwa vinanyofolewakwenye magari au kwenye magari tunayoagiza, sasa hivi wizihuo haupo tena. Pongezi sana kwa TPA pongezi sana kwaCEO wa TPA pia.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia Tanzania BuidingAgency (TBA) ambayo ndiyo taasisi iliyopewa madaraka yakujenga miradi mbalimbali ya Serikali na hasa majengo,imefanya kazi nzuri sana. Kwa mfano, imejenga hostel paleChuo Kikuu Dar es Salaam. Gharama za kampuni ya Kichinailiyokuwa ime-tender ilikuwa shilingi bilioni 80 kumaliza mradiule. Wao wametumia shilingi bilioni 10. Pia ukienda kwa mradiwa hostel za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ndiyo kamahivyo, lakini ukienda mradi mwingine kama wa Ihungo,wengine wali-tender shilingi bilioni 60, lakini wao wamemalizakwa shilingi bilioni 11. Wameenda hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nenda Mlonganzila, hivyohivyo; wamekwenda wakitekeleza miradi mingi kwa kaributen percent of the entire total ukilinganisha na Wakandarsiwengine. Lazima tuwapongeze sana TBA na CEO wake kwakazi kubwa na nzuri wanayofanya katika kutekeleza miradimbalimbali. Unakuja bodi za Wakandarasi na za Wahandisi;wote wamefanya kazi nzuri sana. Wakandarasi ambaowamekuwa wakizembea kutimiza viwango wameondolewakwenye roster ya Wakandarasi Tanzania. Ni kazi nzuri sanainayofanywa na taasisi hizi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikitaja MSL pale Mwanza,ameteuliwa Kaimu Mkurugenzi. Kwa muda mfupi tu wa miezimichache aliyokaa, ameweza kuifanya meli ya MV. Liembaambayo ilionekana kama haifai pale Kigoma na ilikuwainaripotiwa kwamba imeleta hasara kila trip ya shilingi milioninne. Yeye kwa trip moja ameweza kusimamia na kupatashilingi milioni 15. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika na Waheshimiwa Wabungewa Bunge lako Tukufu, kwa hiyo, hii inaonesha kwamba kuna

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

251

vitu viwili muhimu ambavyo lazima Wizara hii iendeleekufanya. Moja, ni uteuaji kwa kufuata weledi wa Watendajiwanaosimamia taasisi mbalimbali zilizo chini ya Wizara hii;lakini pili, kufuatilia kwa makini ili kuona jinsi gani ambavyotunaweza kuisaidia Tanzania na Serikali kwa ujumla kupatamaendeleo. Ndiyo maana nimesema nizitaje taasisi kwauchache.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,nitakuwa nimekosa fadhila kama nisiporudia kusemanashukuru sana Waheshimiwa Wabunge wa Bunge hili kwamichango yao kutoka pande zote kwa vyama vyote.Michango yenu imekuwa ya muhimu sana na tumeichukua,tutazidi kuisheheni na kuiweka vizuri ili kwamba kwenye vikaovijavyo tuweze kuisaidia Serikali yetu kutekeleza mipangoyake.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,naomba sasa kutoa hoja kwamba taarifa ya utekelezaji yashughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinukwa kipindi cha Januari, 2017 hadi Januari, 2018 sasaipokelewe na Bunge lako Tukufu kama taarifa rasmi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja.(Makofi)

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Naibu Spika,naafiki.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, hojaimeungwa mkono. Sasa nitawahoji.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Hoja ya Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge yaMiundombinu kuhusu Shughuli za Kamati kwa

Mwaka 2017 Iliridhiwa na Bunge)

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

252

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa walioafiki wameshinda.Kwa hiyo, mapendekezo na maoni yaliyotolewa na Kamatihii sasa ni mapendekezo ya Bunge. Kwa hiyo, Serikali iyachukueyote kama yalivyo.

Waheshimiwa Wabunge, sasa namwita MheshimiwaDeo Ngalawa, Mheshimiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishatina Madini.

MHE. DEOGRATIUS M. NGALAWA – MWENYEKITI WAKAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI:Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza napenda kukushukuruwewe binafsi kwa kunipa ruhusa ya kuja kuongelea mambombalimbali ambayo Waheshimiwa Wajumbe wameyajadilikuhusu taarifa ya utekelezaji wa Kamati ya Kudumu ya Bungeya Nishati na Madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, wachangiaji katika Kamatihii, wamechangia Waheshimiwa Wabunge 23. Kwa kuongeawamechangia Waheshimiwa Wabunge 16 na kwa maandishiwamechangia Waheshimiwa Wabunge saba. Napendaniwataje Waheshimiwa Wabunge wote ambaowamechangia hasa kwa maandishi kwa sababu hawawalioongea wameonekana hapa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabungewaliochangia kwa maandishi ni Mheshimiwa Lucia MichaelMlowe, Mheshimiwa Mary Deo Muro, Mheshimiwa Oran Njeza,Mheshimiwa Juma Othman Hija, Mheshimiwa ZainabMndolwa Amir, Mheshimiwa Rhoda Edward Kunchela namwisho ni Mheshimiwa Silafi J. Maufi.

Mheshimiwa Naibu Spika, wachangiaji wengi katikataarifa hii ya Kamati walijikita sana kwenye maeneo yamadeni. Walijikita pia kwenye maeneo ya mradi wa umemewa maji wa Mto Rufiji ambao tunaita Stieglers Gorge, miradiya REA I, REA II na REA III bila kusahau Densification Project.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile walizungumziamatumizi ya gesi kwa maana ya kuwepo kwa master plan ili

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

253

kuweza ku-utilize gesi ambayo ipo kwa sasa ambayoinatumika kwa kiasi kidogo. Pia walizungumzia Taasisi ya GST,elimu kwa wachimbaji, ruzuku kwa wachimbaji wadogo,makusanyo ya maduhuli na suala zima la biashara yaTanzanite.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kwa kifupiwazungumzaji wengi wameipongeza Serikali ya Chama chaMapinduzi kwa utekelezaji mahiri wa miradi yetu mingiambayo inatekelezwa sasa na Serikali hii ya Awamu ya Tano.Wachangiaji wengi waliojikita katika madeni hasa yaTANESCO na TPDC ukiangalia lengo lao kubwa lilikuwa nikuzifanya hizi taasisi mbili ziweze kujiendesha bila kutegemearuzuku au mkono wa Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, hoja zilijikita zaidikatika kuhakikisha kwamba wanayasaidia mashirika hayamawili ya TANESCO na TPDC kuondokana na ule mzigo wamadeni na hasa TANESCO. Kwa sababu deni la TANESCOwadaiwa na wadai unakuta kwamba TANESCO badoanabaki kuwa na deni kubwa. Kwa hiyo, nguvu zilielekezwanyingi kwa wachangiaji wengi kuona kwamba hili shirika laTANESCO, Serikali iweze kuhakikisha kwamba inalisaidia iliiweze kujiendesha yenyewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa eneo la TPDC; pia TPDCana madeni, lakini madeni ambayo TPDC anayo ni madenimachache kuliko madeni ambayo yenyewe inadai. Hataukijaribu kuiangalia TPDC kwa undani na kwenye maelezoya taarifa yetu, unakuta kwamba TPDC bado inabaki na helanyingi kiasi ambacho yenyewe inaweza ikajiendesha. Kwahiyo, michango mingi ilikuwa inaonesha kwamba TPDC inamzigo mkubwa na Serikali inatakiwa kuingiza mtaji mkubwaili kuhakikissha gesi ile ambayo inatumika itengenezewemiundombinu ya kutosha kwa sababu gesi inayozalishwa ninyingi kuliko ambayo inatumika sasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wajumbe wenginewalijikita sana kwenye mradi wa umeme wa maji wa MtoRufiji naamini kwamba hii Mheshimiwa Waziri na baadhi ya

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

254

Wajumbe waliizungumzia kwa kina kwamba huu mradi siyokwamba umeanza, ila upo katika maandalizi ya kuanza.Sasa na ni vizuri mara nyingi mradi kabla hujaingia kwenyeile process yenyewe kuufahamu, kabla haujaileta bajeti hapa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, bajeti itakujawakati tayari kila kitu kipo kwenye table na vitu hivyovinakuwa vinaonekana. Kwa hiyo, sisi kama Kamatitunaipongeza Serikali kwa hatua ambazo inazichukua kwasababu umeme huu wa stieglers Gorge utatuletea Megawati2100 na vilevile itaendana sambamba na linkage ambayoinawekwa na philosophy ya nchi kwenda kwenye uchumiwa viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kulikuwa na miradi yaumeme wa REA. Wachangiaji wengi wamezungumziaupungufu ambao umefanyika katika mradi wa REA awamuya kwanza na REA awamu ya pili; na mara nyingi ni kulekurukwa kwa baadhi ya vijiji. Umeme unatoka kijiji hiki hapa,kinaruka unaenda kwenye kijiji kingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukijaribu kuangalia, wengiwameshauri kwamba ule upungufu ambao tayariumeshaonekana katika hii miradi ya REA I na REA II maanayake ni kwamba sasa kwenye REA III yafanyike maboresho.Bahati nzuri Serikali imekuja na utaratibu wa DensificationProject ili kuweza ku-clear upungufu wote ambao umefanyikakatika REA I na REA II na bahati nzuri baadhi ya Wakandarasitayari wameshapewa tender na wapo site wanafanya kazihii ya marekebisho.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna matumizi ya gesi;wachangiaji wengi wameona kwamba gesi iliyopo ambayoinazalishwa na TPDC ni nyingi. Kwa hiyo, kuna haja sasa yaSerikali kutengeneza miundombinu wezeshi ya kuifanya TPDCiweze kupeleka gesi maeneo mbalimbali na hususan kwenyemajumba yetu. Kwa hiyo, hiyo master plan itaonesha maeneoambako gesi inapita na hata kama wawekezaji watakuja,maana yake watatumia ile master plan ambayo ipo. Vilevilewachangiaji wengine walizungumza kwamba kuna baadhi

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

255

ya nchi jirani ambazo na zenyewe zinaenda na mifumo hii.Kwa hiyo, maana yake TPDC iwezeshwe ili kuweza kuingiakwenye soko la kiushindani la Kimataifa, kwa sababu gesiiliyopo ni nyingi na watumiaji ni wachache.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia limeongelewa kuhusuGeological Survey of Tanzania (GST) kwamba ndio iwe mtafitipekee wa madini Tanzania na in case kama kuna wawekezajiwa uchimbaji, basi wapate consent au washirikiane na taasisihii katika kufanya utafiti huo. Kwa sababu inaonekana baadhiya taasisi za nje zinafanya hujuma ya kufanya tafiti kwa mudamrefu kiasi ambacho hata zile taarifa nchi inakuwa hazina.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo, kwa kuiunganisha naGST kwa kupata consent ya GST maana yake ni kwamba,nchi kwanza itapunguza ule urasimu ambao unafanywa napia nchi itakuwa na clear picture ya maeneo ambayo yanamadini na vilevile itawafanya baadhi ya wachimbaji wetuwadogo na wa kati kutokutumia gharama zao nyingi katikakuwekeza mahali ambako hawana uhakika wa madiniambako yapo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naamini kwambaGST ikishakuwa mbele ya wachimbaji wetu wa kati na wachini, maana yake ni kwamba mtu ataenda kuwekeza naatakopa mikopo benki kwa ajili ya uwekezaji huu akijua pichahalisi na hali halisi ya madini iliyopo.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia limezungumziwa sualala elimu kwa wachimbaji. Elimu kwa wachimbaji ni muhimuna hata sisi Kamati tumesisitiza hilo kwa sababu kuna atharinyingi ambazo zinatokea kule kwa sababu ya kukosa uelewana kukosa elimu ya kutosha juu ya maeneo hayo,kunakuwepo na athari nyingi na ajali nyingi, kwa mfanokuangukiwa kwa vifusi na vitu vya namna hiyo. Hayoyameelezwa, nasi kama Kamati tuliona jambo hili ni lamuhimu kupewa kipaumbele.

Mheshimiwa Naibu Spika, lilizungumzwa pia suala laruzuku kwa wachimbaji wadogo. Hapa pia lilizungumzwa

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

256

na suala la elimu na ndiyo maana unaona hata kwenye ripotiya Kamati na Wajumbe walipokuwa wanachangia, kunabaadhi ya pesa za ruzuku ambazo Serikali imepeleka, lakiniilienda kufanya kazi ambayo haikukusudiwa. Watu waliendakuelekeza kwenye maeneo ambayo hawakuyaombea. Kwahiyo, hapa upatikane usimamizi wa kutosha ili kuhakikishakwamba hela inayotolewa na Serikali inasimamiwa nainafanya klengo lililokusudiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia katika upande wamadini kuna makusanyo ya maduhuli. Napenda kuipongezaWizara ya Madini kwa ukusanyaji wa maduhuli asilimia 84 yalengo ambalo ni la mwaka mzima kwa kukusanywa ndaniya nusu mwaka. Kwa hiyo, kama Kamati tunaipongeza,iendelee na utaratibu huo. Vilevile wapo walioipongezaSerikali kwa kuchuka hatua kuhusu utoroshwaji na ubadhirifuambao unapatikana kwenye madini yetu ya Tanzanite.Serikali imeshachukua hatua kubwa ya kujenga ule ukuta napia kupitia mikataba ambayo inaonekana inaitia hasara nchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa ujumla, WaheshimiwaWabunge wengi waliochangia kwenye Kamati yanguwameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kaziinayozifanya, ni kazi njema, ina nia njema na imeoneshauzalendo mkubwa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa hili namaendeleo ya watu wake wote.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuchukua hatuahii kukupongeza wewe, Mawaziri wote, kuwapongezaWabunge wote waliochangia kwenye Kamati yangu nanaomba sasa taarifa hii ya utekelezaji ya Kamati ya Kudumuya Nishati na Madini ipokelewe na Bunge lako na kuwa nitaarifa rasmi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja.(Makofi)

MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA: Mheshimiwa NaibuSpika, naafiki.

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

257

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Waheshimiwa Wabunge,hoja imeungwa mkono. Sasa nitawahoji.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Hoja ya Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge yaNishati na Madini ukuhusu Shughuli za Kamati

kwa Mwaka 2017 Iliridhiwa na Bunge)

NAIBU SPIKA: Walioafiki wameshinda. Kwa hiyo, hayoni maoni na mapendekezo ya Bunge kwa Serikali. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, kwanza nichukue fursa hiikuwashukuru sana Kamati ya Miundombinu na Kamati yaNishati na Madini kwa kazi nzuri sana waliyoifanya kwa niabayetu sote ambao hatuko kwenye Kamati hizo, wamefanyakazi nzuri, wameshirikiana vizuri na Serikali, ndiyo maanatumewasikia hapa Mawaziri wakikubaliana na maoni namapendekezo ya Kamati na kwamba yote watayafanyiakazi.

Waheshimiwa Wabunge, kama ambavyonimeshawahoji, haya siyo maoni tena wala mapendekezoya Kamati. Kwa upande wa Serikali taarifa hizi mbili za Kamatizimeshakubaliwa na Bunge. Kwa hiyo, hayo ndiyo Maazimioya Bunge kwa Serikali, kwa maana ya kwamba Bunge sasalimeshaamua mambo gani linaishauri Serikali na mambogani l ingependa yafanyike il i kuhakikisha kwambatunawaletea maendeleo wananchi wetu.Kwa hiyo,nawaombe upande wa Serikali mzichukue taarifa hizi zaKamati, myapitie maoni yaliyoko humo na pia mapendekezoyaliyoko humo kwa sababu Bunge limeshahojiwa na hayondio mapendekezo ya Bunge na pia maoni ya Bunge.

Kwa upande wa Nishati na Madini na pia kwaupande wa Miundombinu, Bunge limeshafanya kazi yake yakikatiba ya kuishauri Serikali na maoni yake yapo kwenye hizotaarifa za Kamati. Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge, hatasisi ambao hatuko kwenye Kamati hizo, niwashukuru sana

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

258

kwa kazi nzuri mliyoifanya ya kuweza kuchangia kwamaandishi, lakini pia kuchangia humu ndani ili kuwezakuweka vizuri maoni haya ili Serikali iweze kujua nini chakufanya. Kwa hiyo, nawapongeza sana kwa kazi nzuri.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kusema hayo,niwakumbushe tu, huwa tunakumbushana kila wakati,tumeshafika nusu ya kipindi chetu cha Bunge lakini badohatufuati kanuni. Sijajua kama ni kwa makusudi ama nikwamba tunasahau. Waheshimiwa Wabunge wengiwananyanyuka humu ndani wakielekea kila mahaliwapendako, wananyanyuka wapendavyo kama wakokwenye mkutano wa hadhara hivi; lakini kanuni zetuzinatueleza nini cha kufanya unaponyanyuka kutoka sehemumoja kwenda nyingine.

Sasa tukifika nusu namna hii, halafu bado hatufuatihizo taratibu na siyo jambo zuri kwamba kiti kinakwambiarudi ulipokuwa il i ukafuate utaratibu wa namna yakunyanyuka na namna ya kurudi humu ndani. Tufuateutaratibu na nadhani ni mambo hayo kwa sababu hayatiliwimkazo, ndiyo maana wakati mwingine tunaona tunawezakujibizana ama kuzungumza namna tunayotaka humundani.

Hili Bunge tunapoliita wenyewe Bunge letu Tukufu nilazima sisi wenyewe tulipe hiyo hadhi, hatuwezi kuwatunanyanyuka kama tuko darasani ama tuko mahaliambapo hapana utaratibu. Tufuate utaratibu ili akilini kwetutujue kwamba hili ni jengo la namna gani na tuweze kutoahiyo heshima ambayo tunaipa sisi wenyewe kwenye kanuni.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kusema hayo,naahirisha shughuli za Bunge mpaka siku ya kesho Jumanne,tarehe 6 Februari, 2018, saa 3.00 asubuhi.

(Saa 1.30 Usiku Bunge liliahirishwa mpaka Siku ya Jumanne,Tarehe 6 Februari, 2018, Saa Tatu Asubuhi)