Banana Investments Limited

8
Mbiu ya Banana Toleo la 15 , October - December 2009 Haliuzwi http:/www.banana.co.tz Banana Investments Limited Toleo la 15 October—December 2009 Www.banana.co.tz

Transcript of Banana Investments Limited

Page 1: Banana Investments Limited

Mbiu ya Banana Toleo la 15 , October - December 2009

Haliuzwi

http:/www.banana.co.tz

Banana Investments Limited Toleo la 15 October—December 2009

Www.banana.co.tz

Page 2: Banana Investments Limited

Mbiu ya Banana Toleo la 15 , October - December 2009

Haliuzwi 2

Kutokana na kukua kwa soko la bidhaa zina-

zozalishwa na kampuni ya Banana Investments

Ltd ambazo ni mvinyo wa Raha, Malkia na

Meru, kampuni imeamua kununua mitambo

mipya na ya kisasa ili kukidhi mahitaji ya

wateja wa bidhaa hizo.

Mitambo hiyo imeshawasili kiwandani na ufun-

gaji utaanza rasmi mwisho wa mwezi huu wa

tisa chini ya usimamizi wa wakandarasi kutoka

Ujerumani ambako ndiko ilikotoka hiyo mi-

tambo. Wataalamu hao watashirikiana na wa-

taalam wa hapa kwenye kampuni na kazi ya

kufunga hiyo mitambo itachukua muda wa

mwezi mmoja.

Mitambo hiyo ni ya kisasa na inajiendesha

yenyewe(Automatic). Baadhi ya mitambo

hiyo ni bottle washer, filler, crowner na la-

beler.

Imeandikwa na

Thomas Kitaly

KUTOKA KUSHOTO 1. Augustine S. Minja - Mwenyekiti 3. Beatha A. Massawe - Katibu 5. Patrick S. Mushi - Mjumbe 4. Philbert A. Mhindi - Mjumbe 2. Gerald E. Lyimo - Mjumbe

KAMPUNI KUFUNGA MITAMBO MIPYA

1. KAMPUNI KUFUNGA MITAMBO MIPYA ………..2 2. MAONESHO YA NANENANE ……………………...3 3. MIKAKATI YA KILIMO KWANZA ………………...4 4. HONGERA KWA KUPATA JIKO ..............................4 5. SERA MPYA YA MICHEZO ………………………..5 6. MATUMIZI YA KRETI ZA BIL …………………….5 7. KONA YA NAJUA HUJUI …………………………..6 8. AJIRA MPYA ………………………………………...7 9. TANZIA....................................……………………….7 10. WAFANYAKAZI WAJIUNGA NA Y’S MEN ……...7

YALIYOMO UK KAMATI YA UHARIRI KAMATI YA WAHARIRI

Moja ya mitambo ambayo imeshawasili kiwandani. Mashine hii ni ya kuoshea chupa. (bottle washer)

Page 3: Banana Investments Limited

Mbiu ya Banana Toleo la 15 , October - December 2009

Haliuzwi 3

Kama ilivyo ada kampuni ya Banana iliweza kushiriki maonesho ya kilimo ya 16 maarufu kama Nanenane yaliyofanyika katika kanda tatu tofauti. Kanda ya kaskazini yalifanyika viwanja vya TASO Themi, Kanda ya pwani viwanja vya Saba saba Morogoro na Kanda ya kati yalifanyika Dodoma. ARUSHA: Maonesho haya yalifunguliwa na Mheshimiwa Waziri wa mifugo na kilimo Ndugu John Pombe Magufuli na siku ya kilele mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Ndugu Isdori Shirima. Kampuni ya Banana Investments Ltd iliweza kuwa mshindi wa kwanza katika viwanda vinavyosindika vya-kula na kupewa zawadi ya kombe ya silver.

DODOMA:

Maonesho haya ya kilimo yalifanyika kitaifa Dodoma na yalikuwa ni ya kusisimua zaidi kwani ufunguzi wake ulifanyika na mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muun-gano Tanzania Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye alitoa msisitizo juu ya kauli mbiu ya kilimo, KILIMO KWANZA 2009. “MAPINDUZI YA KIJANI-UHAKIKA WA KILIMO NA KIPATO” Pia kwa kuboresha maonesho haya katika mkoa huu, Rais alisema kwamba maonesho haya yatafanyika ki-taifa kwa mfululizo wa miaka mitano ijayo hapo mkoani Dodoma. Siku ya kilele mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais Dr.Mohamed Shein.

MOROGORO:

Mkoani Morogoro banda letu lilitembelewa na watu wengi ambao waliweza kupata fursa ya kuonja bidhaa zetu na kupata maelezo ya kina kuhusiana na kampuni yetu na bidhaa zake kwani ilikua ni mara ya kwanza kwa kampuni ya BIL kushiriki maonesho hayo mkoani hapo. Pia katika maonesho hayo walijitokeza wateja wengi ili kufanya biashara nasi na mteja mmoja wapo alikuwa ni ndugu Richard Nkonyi. Mgeni rasmi katika maonesho haya alikuwa ni Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Mheshimiwa Dr.Hussein Mwinyi.

Katika maonesho haya kwa ujumla wake watu mbalim-bali kutoka ndani na nje ya nchi walifika katika ma-banda yetu na kuweza kuonja na kununua bidhaa bora zinazozalishwa na Kampuni ambazo ni Raha-‘Bonge la

ladha kwa bei nafuu” ,Mvinyo wa Malkia na Meru ‘Bonge la ladha kwa watu makini”

Imeandikwa na

EMANUEL NEVAVA.

MAONESHO YA KILIMO NANENANE MWAKA-2009

Kutoka kulia ni Mr. Majuva afisa masoko, mkurugenzi wa BIL wakiwa

na wateja wa Dodoma.

Bw Denis Mkojera akitoa maelezo kuhusu bidhaa za kampuni mkoani

Morogoro.

Pichani ni banda la kampuni la maonesho ya Nanenane katika vi-

wanja vya TASO Mkoani Arusha.

Page 4: Banana Investments Limited

Mbiu ya Banana Toleo la 15 , October - December 2009

Haliuzwi 4

KAMPUNI NA MKAKATI WA KILIMO KWANZA

Mtu yeyote anayepanga kuondoa umaskini hapa nchini hawezi kutenganisha dhana ya ukuzaji kilimo (Kilimo kwanza) na mkakati wa kuondoa umaskini Tanzania (Mkukuta). Huwezi kuzungumzia mkakati wa kuondoa umaskini bila kuhusisha suala la kilimo na kwenye kilimo ndipo mahali pa kuanzia ili umaskini ufutike kama ukitaka. Mkoa wa Arusha pamoja na mambo mengine um-edhamiria kuinua kilimo kwa kutumia njia za kisasa kwa sababu imebaini kwamba kuendelea kutegemea jembe la mkono hakutaleta mabadiliko yoyote katika sekta ya kilimo, ili kuinua pato la mtanzania/mkulima. Ili Kilimo Kwanza kiwe na manufaa mambo muhimu yafuatayo yatiliwe mkazo; Kuwepo na wataalamu, upatikanaji wa pembejeo, Upatikanaji wa masoko, Uboreshaji wa miundo mbinu – mfano barabara, Elimu kwa wakulima wadogo wadogo kuunda vyama vya wakulima kwa hiari, Maeneo wazi yaainishwe kwa lengo la kilimo cha mvua au um-wagiliaji na Uinishaji wa mazao kulingana na jiografia ya mahali. Sera hii ya Kilimo Kwanza ikifanikiwa itasaidia ku-punguza tofauti ya maendeleo yaliyopo vijijini na mijini na kupunguza wimbi la watu kukimbilia mjini. Aidha siri ya mafanikio katika mpango huu wa Kilimo Kwanza ni kufanya kazi kwa bidii na kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea. Kampuni inashiriki katika sera ya kilimo kwanza kwa kuingia ubia na wazalishaji binafsi au taasisi za zao la ndizi.

Chini ya utaratibu huo kampuni inaingia mkataba na baadhi ya wakulima wa migomba ambapo wataalamu wa kampuni wanatembelea wakulima hao na kuwapa ushauri jinsi ya kulima migomba kitaalam na kibiashara.

Kampuni inanunua ndizi zote zinazozalishwa na waku-lima walioko katika mpango huo kwa bei ya soko ili-yopo.

Utaratibu huu una manufaa makubwa kwa pande zote kwani unawezesha kampuni kupata ndizi zenye ubora na kwa uhakika. Na kwa upande wa wakulima unawa-hakikishia soko la bidhaa zote za ndizi anazozalisha.

Imeandikwa na

Philbert Mhindi

HONGEZA KWA KUPATA JIKO

Uongozi mzima pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya Banana Investments Ltd wanapenda kuwapa pongezi nyingi sana Bw. Adrian Anthon aliefunga ndoa na Bi. Silvestra Ngowi mnamo tarehe 08/08/2009 katika kanisa katoliki la Moshono parokia ya Kijenge jijini Arusha Siku hiyo ilikuwa ni siku ya nderemo na vifijo kwa ndugu, jamaa na marafiki wote waliohudhuria, lakini kwa upande wa kundi la makapera ilikuwa ni pigo kubwa sana kwao kwa kupungukiwa na mwanachama mwenzao. Tunakuombea kwa Mungu Ndoa yenu idumu, bila kuwa na mikwaruzo ya aina yeyote ile na maisha yenye ba-raka tele.

Imeandikwa na

Patrick Mushi

Mmoja wa wabia wetu ambae shamba lake linaonekana katika picha

hii bwana Julius Matiro wa wilaya ya Arueru mkoani Arusha

Page 5: Banana Investments Limited

Mbiu ya Banana Toleo la 15 , October - December 2009

Haliuzwi 5

SERA MPYA YA MICHEZO

MATUMIZI YA KRETI ZA BIL

Uongozi wa kampuni umepitia sera ya michezo kwa wafanyakazi na marafiki wanaoizunguka kampuni na kubadilisha baadhi ya vipengele vya sera hiyo kama ifuatavo;

Kitengo hicho cha michezo kitaendelea kuwa chini ya idara ya Public Relations ambapo idara hiyo ndio ita-ratibu michezo yote pamoja na ziara mbalimbali za kiu-talii zitakazofanywa na wafanyakazi.

Pamoja na hayo Banana sports club haitashiriki katika ligi zozote zikiwepo za kata, wilaya na mkoa. Wafanya-kazi watakao pendelea kushiriki kwenye hizo ligi kwa gharama zao wenyewe wataruhusiwa ilimradi wasitumie muda wao wa kazi.

Banana Sports Club itashiriki katika michezo ya kirafiki baina ya taasisi mbalimbali na pia timu za jirani. Lengo la marekebisho haya ya sera ni kuepusha wafanyakazi kutumia muda mwingi kwenye michezo na wakati huo-huo kukidhi haja ya wafanyakazi kujifurahisha, kujenga mshikamano na urafiki miongoni mwao, majirani na taasisi za jirani na kujenga afya zao kupitia michezo bila

kuathiri uzalishaji. Club inaandaa safari ya kutembelea mbuga za wanyama za Serengeti siku za karibuni am-bayo itakuwa ni safari ya siku tatu.

Nembo mpya ya Banana Sports Club

Imeandikwa na

Beatha Anthony

Kampuni inatumia kreti zenye nembo ya Banana Invest-ments kwa ajili ya kuweka bidhaa zake hususani Raha kwa wakati uliopo. Baadhi ya wauzaji wa bidhaa nyingine zinazowekwa kwenye chupa mfano soda, bia na bia nyingine zitoka-nazo na ndizi wamekuwa wakitumia kreti hizi kuwekea bidhaa zao.

Tunapenda kuwakumbusha wauzaji wa bidhaa za namna hii kuwa ni makosa kutumia kreti za kampuni yetu ku-

weka bidhaa za kampuni au wazalishaji wengine tofauti na zile zinazozalishwa na Banana Investments Ltd. Kreti hizi ni mali ya kampuni, na deposit anayolipa mteja wakati wa mkataba haimpi umiliki wa kreti, bali inampa haki ya kuzitumia tu. Mteja anapotumia kreti kuweka bidhaa tofauti na zile za kampuni yetu anaingiza kampuni kwenye hasara kwani anainyima fursa ya kutumia kreti hizo kwa kuwa zina-kuwa zimesheheni bidhaa tofauti wakati gari ya mauzo inapofika kwa mteja. Kampuni inaendesha msako wa watumiaji wa kreti zetu kuweka bidhaa tofauti ambapo kila anayekutwa nazo atanyanganywa bila kupewa fidia. Wauzaji wa jumla wa bidhaa zetu, na madereva wa magari ya mauzo wa-meidhinishiwa kuendesha msako huo. Watumiaji sugu watashtakiwa mahakamani.

Imeandikwa na

A Mlay.

Meneja Masoko BIL

RAHA - Bonge la ladha kwa bei nafuu

MATUMIZI YA KRETI ZA BIL

Page 6: Banana Investments Limited

Mbiu ya Banana Toleo la 15 , October - December 2009

Haliuzwi 6

Unatambua hili katika mwili wako? 1. Moyo wako hudunda mara 101,000 kila siku. Kwa

kipindi chote cha maisha yako utadunda karibu mara bilioni moja na kusukuma damu kiasi cha karibu lita milioni 400 za damu.

2. Kinywa chako huzalisha mate kiasi cha lita moja

kila siku

3. Kichwa chako kina mifupa 22

4. Kwa wastani mtu hupumua mara 23,000 kila siku

5. Kwa wastani mtu huzungumza maneno 5,000 kwa kila siku japo kiasi cha asilimia 80 mtu huzungumza peke yake pasipo kujijua.

Je Wajua?

1. Pembe ya mnyama kifaru imetengenezwa kwa ny-

wele!

2. Papa (kiongozi wa kikatoliki) aliyekuwa mdogo

kuliko wote Duniani alikuwa na umri wa miaka 11 tu

3. Fedha ya kimarekani dola ama $ ni muunganiko wa

herufi mbili U na S ambazo zinatengeneza U.S ki-fupisho cha jina la nchi ya Marekani

1. Bendera ya nchi ya Uswisi ndiyo pekee yenye

umbo la mraba

2. Nchi ya Vietnam hutumia fedha iliyo katika mfumo

wa Noti tu hawana sarafu yoyote

3. Mboni katika macho ya mbuzi yana umbo la msta-

tili

4. Samaki aina ya Pweza hawana ubongo.

Chura toka bwawa la Kihansi (Nectophrynoides as-

periginis) hapa nchini ndio chura pekee duniani ambao huzaa, wenye umbo dogo lisilozidi urefu wa inchi 3 na wenye rangi nzuri za kuvutia. Hata hivyo, kutokana na uharibifu wa mazingira na ujenzi wa mradi wa umeme wa Kihansi, vyura hawa walianza kufa. Mwaka 2001 walichukuliwa vyura 500 na kupelekwa Marekani katika mbuga ndogo ya kuhi-fadhi Amfibia Bronz Zoo jimbo la New York na Toledo Zoo jimbo la Ohio kwa idhini ya wizara ya Mazingira na Mali asili. Hata hivyo serikali iliweka mpango wa kuwarudisha kuanzia mwaka 2007 kwa awamu.

Imeandaliwa na

Michael Emanuel

kwa msaada wa mtandao (Internet)

KONA YA NAJUA HUJUI

Page 7: Banana Investments Limited

Mbiu ya Banana Toleo la 15 , October - December 2009

Haliuzwi 7

.Kampuni yetu imetikiswa na misiba ya wafanyakazi wawili ndani ya mwezi mmoja. Bibi Vumilia Lema alifariki tarehe 06/08/2009 na

kuzikwa tarehe 10/08/2009 katika kijiji cha Kifuni Kibosho, Mkoani Kiliman-jaro. Bi Vumilia aliyekua anafanya kazi katika idara ya uzalishaji ameacha mume na mtoto mmoja.

Bwana Flavian Costantine alifariki tarehe 03/08/2009 na kuzikwa tarehe 05/08/2009 kijijini kwao Kifuni

Kibosho, Mkoani Kilimanjaro. Bwana Flaviani alikua anafanya kazi katika idara ya uzalishaji.

Uongozi na wafanyakazi wa Banana In-vestments Ltd unawaombea kwa mungu

ili awalaze mahali pema peponi. AMINA.

Imeandikwa na Patrick Mushi.

TANZIA

Klabu ya kimataifa ya Y’s Men, ni kikundi cha watu

wenye imani tofauti za kidini wanaofanya kazi pamoja wakifuata mafunzo ya Yesu kristo, wakiungana na ku-saidia chama cha vijana cha YMCA. Pia kutokana na kwa kwamba hii klabu ina wanachama zaidi ya 35,000 ulimwenguni kote, hutoa fursa wa wanachama wake kusafiri nchi mbalimbali na kuweza kujipatia marafiki pamoja na ufahamu wa kimataifa ( international expo-sure).

Mnamo tarehe 29/08/2009 wafanyakazi wawili ambao ni Bw Philbert Mhindi pamoja na Shanel Kavishe wali-jiunga rasmi na club hiyo ambapo walikabiziwa uwanachama na Bw Hiyasinti Kilasara ambae ni Rais wa Afrika wa chama hicho akishirikiana na Bw Jared Musima kutoka Nairobi Kenya. Wafanyakazi hao aki-wepo

Wananchi wote wanakaribishwa kujiunga na klabu hii kwani manufaa yake ni makubwa sana hasa kwenye

ulimwengu huu wa sayansi na technolojia. Kwa maelezo zaidi angalia kwenye tovuti ya; www.ysmen.org Www.ysmentanzania.org

Imeandikwa na

Beatha Anthony.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE, AMINA .

WAFANYAKAZI BIL WAJIUNGA NA CLUB YA KIMATAIFA YA Y’S MEN

AJIRA MPYA NGUVU MPYA KAMPUNI YA BANANA

John Safiel Mshana – Fundi mitambo ya Electroniki ya

mashine (Industria Electronic Technician). Bw. John S. Mshana ana stasha-hada ya umeme wa machine za viwandani kutoka chuo cha Kili-manjaro International Institute for Telecommunications, Electronic

and Computers (KIITEC) pamoja na cheti cha Computer Software katika chuo cha Miracle Corners of the World Trust (MCWT). Pia ana uzoefu wa miaka miwili katika fani hiyo.

Godbless Elinimo Msuya - Afisa Masoko Bw. Godbless E. Msuya ana Sta-shahada ya juu ya Uhasibbu wa ushirika kutoka Chuo cha Ushirika na Biashara Moshi(MUCCoBS). Pia ana Stashahada ya Ualimu kutoka chuo cha ualimu Dar es Salaam, na ana uzeofu wa miaka 10 katika kazi hii.

Imeandikwa na

Joan Mrema.

Page 8: Banana Investments Limited

Mbiu ya Banana Toleo la 15 , October - December 2009

Haliuzwi 8

Makao Makuu Kiwanja Na. 311, Kitalu jj Oloirien Village,

P. O. Box 10123, Arusha TANZANIA

Simu: +255754224440,+255272506475 E-mail: [email protected] http:/www.banana.co.tz Dar es Salaam Depot

Ubungo Kibangu, S. L. P. 79407, Dar es Salaam

TANZANIA Simu: +255 222 774 276, +255 756 707 983

Email: [email protected] Tanga Depot Barabara ya 4,

S. L. P. 5150, Tanga TANZANIA

Simu: +255 272 646 134 Email: [email protected]

Banana Investments Limited Producers and distributors of

alcoholic and non- alcoholic beverages

BEI ZA VINYWAJI VYA NDIZI VINAVYOTENGENEZWA

NA KUSAMBAZWA NA KAMPUNI YA BANANA

RAHA

ENEO BEI YA JUMLA

INAYOPENDE-

KEZWA

BEI YA REJAREJA KWA

CHUPA YENYE UJAZO

330 ML

KANDA YA

KASKAZINI Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Singida

TZS 6,500/- KWA KRETI YA CHUPA 24

TZS 350/-

KANDA YA

MASHARIKI Mikoa ya Tanga, Morogoro, Pwani na Dar es Salaam

TZS 8,750/- KWA KRETI YA CHUPA 24

TZS 450/-

KANDA YA KATI Mkoa wa Dodoma

TZS 9,200/- KWA KRETI YA CHUPA 24

TZS 500/-

KANDA YA ZIWA Mikoa ya Mwanza na Shinyanga

TZS 6,000/- KWA CARTON YA CHUPA 12

TZS 600/-

Bei ni moja kwa nchi nzima,

Tanzania

TZS 9,000/- KWA CARTON YA CHUPA 12

TZS 1,000/- KWA CHUPA YENYE UJAZO 330 ML.

MALKIA NA MERU

Vinywaji bora vinavyotengenezwa na kusambazwa na Kampuni ya Banana